Search This Blog

Thursday, 27 October 2022

UHASAMA - 3

 









    Simulizi : Uhasama

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Siku iliyofuata. Kituo cha Polisi Mabawa. 3:00 Asubuhi.



    “Unakumbuka nimekupa muda gani wa kukamilisha ule upelelezi kuhusu kupotea kwa watoto mitaani?" Inspekta Ganjo alimuuliza Koplo Taure.



    “Ni wiki tatu Mkuu" Koplo Taure alijibu.



    “Umefikia wapi hadi sasa hivi katika upelelezi wako?"

    Inspekta Ganjo alimuuliza Koplo Taure swali ambalo hakujua alijibu vipi, maana hakuwa amefikia popote katika kupeleleza chanzo cha kupotea kwa watoto mitaani.



    “Mkuu, lakini si umenipa muda wa kupeleleza? Subiri muda ukifika halafu ukiona sikuletei majibu ndio uniulize" Koplo Taure alijitutumua na kujibu hivyo, japokuwa hakutakiwa kumjibu hivyo mkuu wake, lakini hakuwa na jibu la kumpa litakalo mridhisha mkuu wake. Inspekta baada ya kusikia jibu Koplo Taure, alitabasamu tu.



    “Najua hujafika popote katika upelelezi wako ndio maana ukanijibu hivyo"



    “Hapana Mkuu, hukutakiwa kuniuliza sasa hivi, ungeniuliza baada ya ule muda ulionipa kuisha, halafu ikiwa sijakuletea ripoti zozote"



    “Nikuulize swali?" Inspekta Ganjo alimdhihaki Koplo Taure kwa kumuuliza hivyo, eeeee!!! alimdhihaki kweli, kwasababu tangia mwanzo alimuuliza maswali pasi na kumuuliza kwamba amuulize swali, ikiwa hilo lenyewe pia lilikuwa ni swali.



    “Ndio Mkuu" Koplo Taure alijibu kwa unyenyekevu.



    “Niliwahi kukupa kesi ya kupeleleza vifo vya familia ya Mzee Mheshiniwa, baada ya siku mbili, nikakuuliza swali hili hili ambalo leo umejifanya umelitolea sababu, labda nikukumbushe kidogo, nilikuuliza umefikia wapi katika upelelezi wa vifo vya familia ya Mzee Mheshimiwa, wewe kunajibu ukanipa, unaweza kulikumbuka lile jibu ulilonipa?"



    “Ndio nalikumbuka" Koplo Taure alijibu.



    “Ulini jibu vipi?"



    “Nilikuambia kuwa, sijui nianziea wapi"



    “Eeeewalaa!!!! Hivyo hivyo hujakosea. Sasa mbona leo hii nakuuliza swali kama lile la siku ile halafu wewe unanijibu kuwa bado muda wa kukuuliza swali hilo?"



    “Mkuu, kumbuka lakini siku ile hukunipa muda wa kuukamilisha ule upelelezi, lakini kwenye kesi hii ya kupotea kwa watoto mitaani, umenipa muda" Koplo Taure alijibu kiunyenyekevu, maana alijua kuwa Mkuu wake tayari ameshakasirika kwa lile jibu alilompa.



    “Anhaaa!!! Naona leo umetumia akili sana kujibu maswali yangu, ungekuwa hiyo akili unayoitumia kujibu maswali yangu, ungeitumia kwaajili ya upelelezi, naamini ungekuwa unafanikiwa katika kazi zako na pia kama cheo pia ushapandishwa"

    Inspekta Ganjo alimdhihaki Koplo Taure kwa maneno ya kejeli kama hayo, Koplo Taure alichukia lakini hakuwa na jinsi, kwavile aliemuambia hivyo ni mkuu wake, akabaki kimya tu.



    “Ok, acha nikupe mwanga kidogo, mchunguze Mr Bakari Haneni nyendo zake, kuanzia safari zake na kila anachokifanya.... Unaweza kwenda kuendelea na mapumziko yako, nakutakia jumapili njema" Inspekta Ganjo, alivyomuambia hivyo Koplo Taure, akamruhusu aende, Koplo Taure akainuka na kukakamaa kwa heshima kisha akaanza safari ya kuondoka katika ofisi ya mkuu wake, alipoufikia mlango, akaskia ameitwa, akageuka na kumuangalia Inspekta Ganjo.



    “Kuwa makini na huyo mtu unaeenda kumfuatilia, ila baada ya muda niliokupa nahitaji ripoti kamili kuhusu kesi niliokupa ya kuifuatilia" Alipo muambia hivyo, akavuta faili lililokuwa mezani kwake na kuanza kulipekuwa pekuwa, Koplo Taure alivyoona hivyo, akafungua mlango na kuondoka kituoni hapo kuelekea nyumbani kwake, alipofika akapitiliza hadi kitandani na kulala chali akiangalia dari la chumba hicho.



    “Kwanini ameniambia nimchunguze Mr Bakari Haneni? Na kwanini ameniambia niwe makini... hapo ndipo ninapoamini kuwa Mr Bakari Haneni sio mtu mzuri japokuwa anaoneka ni mtu mzuri, nikiunganisha na tukio la wale watu niliowaona kule club na walipoingia kwenye nyumba ya Mr Bakari Haneni, Hahahah!!! nimetumia akili sana kuwafuatilia wale watu japokuwa mkuu yeye anaona mimi sifanyi kazi kwa ufasaha, acha nisijiumize sana kichwa kwa kufikiria, nitaanza kumchunguza kesho" alijiwazia mwenyewe na kuchukua simu yake, akaingia upande wa majina, alipolipata jina analotaka kulipiga, akapiga.



    “Haloo" sauti tamu ya kike ikaskika kwenye spika za simu ya Koplo Taure.



    “Duh!!! Hivi kweli kwa sauti hii, inaweza ikamuhoji muhalifu na ikampa majibu yote inayo muuliza?" Koplo Taure aliongea.



    “Hahaah! Kwanini?"sauti ya upande wapili ikacheka halafu ikauliza.



    “Unataka kujua kwanini nimesema hivyo?" Koplo Taure aliuliza kwenye swali.



    “Ndio"sauti ikajibu.



    “Basi njoo nyumbani kwetu mara moja" Koplo Taure aliiyambia sauti iliyotoka kwenye simu yake.



    “Poa, nakuja sasa hivi" sauti ilijibu na simu ikakatwa, Koplo Taure akaisubiri sauti aliyoongea nayo ije nyumbani kwake.

    Baada ya nusu saa, sauti ilibisha hodi katika geti la nyumba yake, akatoka nje haraka haraka ili kwenda kuiwahi sauti isije kuondoka, baada ya kulifikia geti lake, akalifungua na kuonekana mtu mwenye sauti iliyoongea kwenye simu. Alaaa!! Kumbe alikuwa ni Afande Jesca ndio mwenye sauti ile nzuri iliyoskika kwenye simu ya Koplo Taure, wakaingia wote hadi chumbani kwa Koplo Taure.



    “Mkuu leo kanipa kazi nyengine ya kumfuatilia Mr Bakari Haneni" Koplo Taure aliongea huku akikaa kitandani.



    “Ana nini nae?" Afande Jesca aliongea huku akikaa kitandani karibu ya Koplo Taure.



    “Sijui, ila kaniambia nimchunguze tu"



    “Huenda ikawa kuna kitu amekiona kwake"



    “Labda" Koplo Taure aliongea hivyo huku akipitisha mkono kwenye kiuno cha Afande Jesca.



    “Unataka kufanya nini wewe mwanaume?" Afande Jesca alimuuliza baada ya kuona mkono wake ameupeleka kwenye kiuno chake.



    “Hujui ninachokitaka kukifanya?" Koplo Taure aliongea hivyo huku akimlaza kitandani.



    “Aa aa!!! Sentaure kwa leo haitowezekana" Afande Jesca aliongea hivyo huku akimtoa Koplo Taure alieanza kumlalia kwa juu.



    “Kwanini?"



    “Nipo katika siku"

    Koplo Taure baada ya kusikia hivyo, aliishiwa pozi na kujiweka kando, akamuangalia Afande Jesca kwa jicho la “una bahati, maana leo nilivyo kupangia" akayapeleka macho yake juu na kuangalia dari la chumba hicho. Alitahayari!

    ******

    Muda wa jioni, nyumbani kwa Inspekta Ganjo, Hemedy alijiandaa kuondoka katika nyumba hiyo ili alelekee nyumbani kwao, lakini bado watu wa hapo walitaka aendelee kuwepo kwajinsi walivyo mzoea kwa muda mfupi, ila ndio hivyo sasa hawakuwa na jinsi ikabidi wamruhusu aondoke, mfanyakazi wa kuendesha gari akajiandaa kumpeleka Hemedy kwao, na kila kitu kilipokamilika Hemedy akaenda kwenye gari na kukaa tayari kwa safari, mara ghafla Hilda nae akaja mbio mbio kutokea ndani akataka na yeye amsindikize Hemedy nyumbani kwao, hakuna ambae alim'bishia, wakamruhusu na yeye kupanda, akakaa siti za nyuma, ikabidi Hemedy na yeye ahamie siti za nyuma alipo kaa Hilda, Hilda akaishia kutabasamu tu baada ya kumuona Hemedy amekuja kukaa siti za nyuma.



    Safari ikaanza ya kumpeleka Hemedy nyumbani kwao, huku nyuma aliwaacha wafanyakazi wa Inspekta Ganjo na huzuni nyingi sana kwa kuondoka kwake, walishamzoea kwa muda mfupi waliokaa nae, aliwafurahisha kwa vituko vyake na kufanya watamani kukaa nae pamoja kila siku, ila ndio hivyo hawakuwa na jinsi, walimuacha aende. Baada ya dakika kadhaa walifika nyumbani kwa Mrutu na kumuacha Hemedy akashuka kwenye gari na kumfanya dereva ageuze gari ili warudi nyumbani kwao. Hilda alihuzunika sana kuchana na Hemedy, alitamani hata kumuambia babu yake kuwa amuombe Hemedy waishi wote nyumbani kwao, ila akajua hata akimwambia ombi lake halito kubaliwa, kwasababu Hemedy anaishi na baba yake mdogo, akabaki akimpungia mkono na Hemedy akampungia mkono, wakaagana hivyo na Hemedy akaingia ndani ya nyumba yao.



    Katika jumba walilofungia wakina Tito. 3:25 Usiku.

    Tosh na wenzake, waliingia kwenye hilo jumba baada ya kuwaacha wakina Tito kwa siku nzma bila ya kuwaletea chakula, walipoingia katika chumba hicho, waliwakuta wakiwa wamechoka, shingo zao wamezilaza kwenye mabega yao, haikujulika ni kwaajili ya uchovu wa kutulia sehemu moja au ni njaa.

    Tosh akawaendea hadi mbele yao na kuwainua shingo zao, akawaangalia kwa sekunde kadhaa halafu akawaachia na kurudi nyuma kidogo waliposimama wenzake.



    “Kitakacho miokoa hapa ni kitu kimoja tu, tunataka kuongea na bosi wenu aturudishie pesa zetu ndipo na sisi tutakapo miachia, kwahiyo sasa hivi nataka mnitajie namba za bosi wenu ili tumpigie" Tosh aliongea ivyo huku akitoa simu tayari kuandika namba zitakazo tajwa.



    “Haya, mmoja wenu anitajie haraka hizo namba" Tosh aliongea hivyo lakini hakuna hata mmoja kati ya hao wawili alietaja hizo namba, ikabidi arudie tena kuwaambia kuwa wataje namba za bosi wao lakini hakuna hata mmoja aliethubutu kunyanyua mdomo wake kutaja namba za Mr Bakari Haneni.



    “Kumbe nyie jeuri eee, basi hiyo jeuri yenu itakwisha sasa hivi" Tosh alipoongea hivyo akachomoa bastola yake na kuwaelekezea.

    “Paaa!!! Paaaa!!! Milio ya risasi ilisikika na kuwafanya wakina Doze kushtuka, Tito na Tobi wakaachia tabasamu lililo mshangaza Tosh...







    “Mnacheka nini nyie wajinga?" Tosh aliwauliza wakina Tito waliotabasamu baada ya kuwaona Doze na Kiku walivyoshtuka baada ya Tosh kupiga risasi pembeni ya kina Tito.



    “Sio kwamba nimewakosa kwa bahati mbaya, hapana mimi huwaga sikosagi ninapotaka kutoa uhai wa mtu na risasi, nimefanya hivyo kwa makusudi ili niwaonyeshe kuwa hii bastola niliyoishika ina risasi nyingi tu, kwahiyo kama naamua kumiua nina miua bila tabu, sasa narudia kwa mara ya mwisho, mnataja namba ya bosi wenu ama hamtaki kutaja? Na msipotaja kwa amani basi mjue mtataja kwa maumivu, si shindwi kutumia nguvu bale inapobidi" Tosh aliwachimba mkwara wakina Tito.

    Bado wakina Tito waliendelea kuweka ngumu, hawakutaka kutaja namba ya Mr Bakari Haneni, haikujulikana kwamba wanategeana kutaja au wameamua wasiitaje kwa ujeuri. Wote wawili walikaa kimya.



    “Naona sasa, mmependa nitumie njia nyengine tofauti na ile ya amani niliowapa. Ok sio mbaya kwavile nyie ndio mnavyotaka basi subirini nitumie njia mnayoitaka" Tosh alioongea hivyo, akatoka humo ndani, baada ya dakika mbili akarudi na kifaa flani cha kutobolea mbao za madirisha kwajili ya kuweka nondo, mimi jina lake limenitoka kidogo, nadhani hadi hapo itakuwa ushakijua hicho kifaa.



    Akaenda nacho hadi mbele yao na kusimama nacho, wakina Tito hawakujua Tosh anataka kuwafanya nini na wakina Doze pia hawakujua Tosh anataka kuwafanya nini mateka wao, wakakaa kimya waone kitakachoendelea.



    “Si mmekataa kutumia njia ya amani? Sasa subiri nitumie njia ambayo mmeichagua nyie" Tosh baada ya kuongea hivyo, akamuita Kiku hapo mbele na kumuambia aushike mkono wa Tobi vizuri sehemu ya kiganja chake. Kiku akakishika kiganja cha mkono wa Tobi kwa nguvu, maana Tobi alikuwa analeta tabu, baada ya kuhakikisha kiganja kimenyooka vizuri, Tosh akasogea karibu na Tobi na kukikita kile kifaa cha kutobolea matundu kwenye mbao za dirisha, akakikita kwenye kiganja cha Tobi.



    “Subiri nikutoboe wewe kidogo, maana mwenzako nilimpa adhabu kule club alipotaka kuleta unja wake wa kike, nataka huu mkono wako wa kulia niutoboe tundu katikati ili hatakama utakapotaka kula chakula, basi kitokee kwenye hili tundu" Tosh aliongea hivyo huku akianza kukizungusha kile kifaa kwenye kiganja cha Tobi, mwanzo alivumilia ila baada ya maumivu kukolea, akapiga kelele za kuomba msamaha.



    “Hapana usiniombe msamaha mimi, omba msamaha kiburi chako kilichokufanya ukae kimya kutaja namba za bosi wako" Tosh aliongea hivyo huku akiendelea kukizungusha kile kifaa kwenye kiganja cha Tobi hadi damu zikaanza kutoka lakini hilo halikumfanya Tosh aache kukizungusha kile kifaa.



    “Basiiiiiiiii, achaaaaaa, natajaaaaa, natajaaaa, achaaaaaa!!" Tobi alipiga kelele baada ya maumivu kumfikia hadi kwenye moyo, ikabidi Tosh aache kukizungusha kile kifaa.



    “0652358545, Aaaaaaaahh!!!!" Tobi alitaja namba ya bosi wake haraka haraka huku akiwa bado ana maumivu kwenye kiganja chake.



    “We fala hebu rudia tena kuitaja hiyo namba, usiitaje kama vile nimekulazimisha kuitaja" Tosh aliongea hivyo huku akiitoa simu yake mfukoni tayari kuandika namba zitakazo tajwa na Tobi.

    Tobi akazirudia tena kuzitaja namba za Mr Bakari Haneni kwa utaratibu kabisa huku akigugumia kwa maumivu.



    “Huoni sasa namba umezitaja kwa njia ya maumivu, wakati nilikupa njia ya amani kabisa, aah!!! Lakini sikulaumu sana kwasababu hiyo ndio njia ulioipenda" Tosh aliongea hivyo, akawageukia wenzake na kuwaangalia kwa macho ya (tufanye nini sasa maana namba tunazo) wenzake wakamuelewa na kumpa ishara ya kuzipiga hizo namba, Tosh akazipiga hizo namba na simu ilipo anza kuita,akaiweka sauti ya nje.



    “Haloo" Sauti nzito ya upande wapili ilinguruma kwenye spika za simu.



    “Naongea na tajiri mwenye roho nzuri mbele za watu kumbe ni mmoja wa watu anaechangia kuwaharibu vijana kwa kuwauzia madawa ya kulevya?" Tosh alimuuliza hivyo huyo mtu wa upande wa pili, moja kwa moja akajua kuwa anaongea na Mr Bakari Haneni ndio maana akaongea hivyo, mtu wa upande wa pili alikaa kimya kama sekunde ishirini.



    “We ni nani?" mtu wa upande wa pili aliongea.



    “Unaongea na mtu mwenye akili nyingi kuliko wewe uliowatuma vijana wako wapumbavu kuja kutupora pesa zetu na kuondoka na mzigo wenu"



    “Unataka nini kwangu? Na vijana wangu unao hapo?" Mr Bakari Haneni aliongea kwa hasira.



    “Mmh mmh!!!!! Tuliza hasira zako wewe mzee, ninachotaka mimi, uturudishie pesa zetu na mzigo wetu, vitu ambavyo vijana wako waliondoka navyo vyote baada ya kutaka kufanya biashara" Tosh aliongea hivyo.



    “Watu wangu unao hapo?" Mr Bakari Haneni aliongea.



    “Yeah, nipo nao hapa tuna piga stori" Tosh aliongea hivyo huku akiwaangalia wakina Tito walioyokuwa wanayafuatilia maongezi hayo.



    “Embu wape simu niongee nao"



    “Ohooooo!! Kumbe unataka kuongea na vibaraka wako? haya hawa hapa" Tosh alimpa simu Tobi aliekuwa bado anagugumia kwa maumivu.



    “Mkuu, tusaidie kwa njia yoyote, tunateseka huku" Tobi aliongea baada ya kuwekewa simu karibu na mdomo wake.



    “Mko wapi, mko sehemu gani?"



    “Mkuu, wasikilize wanachotaka, tunateseka huku" Tobi baada ya kuongea hivyo, Tosh akaiondoa simu na kuendelea kuongea yeye.



    “Ok, utatupa mizigo yetu au tuwapoteze vijana wako?"



    “Hapana, msifanye hivyo, nitamipa pesa zenu" Mr Bakari Haneni aliongea.



    “Sio pesa tu na tunataka na yale madawa"



    “Sawa, sasa nitamipatia vipi hivyo vitu mniachie vijana wangu?"



    “Kesho saa tisa alasiri, njoo pekeako karibu na chuo cha Utumishi kilichopo huku kange, baada ya hapo tutakupa maelekezo ya nini ufanye ili kutupatia mizigo yetu" Tosh alimuambia.



    “Hapana mimi sitoweza kuja, kuna safari nataka kwenda, kwahiyo sitopata muda wa kuja huko, ila nitatuma vijana wangu waje" sio kwamba Mr Bakari Haneni ana safari kama alivyosema, laa hashaa!!! Hakuwa na safari ya aina yoyote ila alikuwa na uoga na watu hao asio wajua.



    “Pia sio mbaya, ila kama utatuma vijana wako basi wasizidi wawili, tafadhali zingatia maelekezo ninayokupa, ukifanya kinyume na haya maelekezo basi ujue utajuta, na ninakuambia tena utajuta wewe na kundi lako"



    “Sawa, hakuna shaka nitafanya kama mnavyotaka, ila nanyie msije mkatugeuka, kwasababu hata mimi sishindwi kufanya chochote kibaya juu yenu, kwahiyo naomba tufanye makabidhiano ya amani" Mr Bakari Haneni na yeye aka kaza ili asionekane kwamba amewaogopa watu hao.



    “Hahahahaha!!! Mzee unaoneka unajiamini sana, ok, sio mbaya ndio inavyotakiwa, tumekuelewa na wewe pia usije ukatugeuka kwasababu na sisi hatushindwi kufanya chochote kibaya juu yako na watu wako, sasa utafanya kama tulivyo kuagiza, usiku mwema" Tosh baada ya kuongea hivyo akakata simu na kuwageukia wenzake.



    “Tayari tumeshamaliza, kwahiyo tuwapeni chakula hawa mbwa wale, maana inavyooneka wana njaa sana"

    Doze akafungua begi alilokuja nalo na kutoa mifuko miwili iliyokuwa na chakula ndani, Tosh akawanyooshea bastola na kumuambia Kiku awafungue kamba walizo wafunga ili wapate kula, Kiku akawafungua na kuwafanya wakina Tito wawe huru, mistari ya kukazwa na kamba ilionekana kwenye miili yao sehemu waliyofungwa na kamba hizo, baada ya kufunguliwa kwenye viti hivyo walisimama juu ili kunyoosha miili yao iliyokaa kwa siku nzima bila kujigeuza upande wowote.



    Tosh alikuwa bado amewanyooshea bastola kwaajili ya kuwalinda wasifanye kitendo chochote cha kipuuzi, walipojinyoosha wakakaa tena kwenye viti, ndipo Kiku alipo wapa mifuko yenye chakula kila mmoja wake, wakaifungua na kukuta ni wali na nyama ya kuku, walianza kula hata kabla hawaja nawa kwa jinsi walivyokuwa na njaa, Tobi yeye alitumia mkono wa kushoto kula, kwasababu mkono wake wa kulia ulikuwa umeadhibiwa kwa kuchomwa na kile kifaa cha kutobolea mbao za madirisha, walikula haraka haraka kutokana na njaa ilivyo washika.



    Kiku akawatolea maji safi na kuwapa kila mmoja chupa yake, walikula hadi wakashiba na kushushia na maji waliyopewa, baada ya kumaliza kula kila kitu, wakafungwa tena kamba ila safari hii hazikukazwa sana kama mwanzo ila zilifungwa kwa uangalifu mkubwa.



    “Ok, mtalala kwenye hii nyumba yenu mpya kwa usiku huu wa mwisho halafu kesho ndio mtajua hatma yenu, usiku mwema waungwana" Tosh aliongea hivyo na kutoka na wenzake katika chumba hicho walichowafungia wakina Tito na kutoka nje kwenye jumba hilo.



    “Sasa tukishapata mizigo yetu halafu tunafanyeje?" Doze aliuliza huku akifungua mlango wa nyuma wa gari na kuingia ndani.



    “Kama watakuja kiwema, itakuwa haina haja ya kuwaletea tabu ila kama wakitaka mapambano itabidi tupambane nao" Kiku aliongea huku akikaa siti za mbele upande wa abiria.



    “Itabidi iwe hivyo, hatuto jali kama ana kundi kubwa au laa" Tosh aliongea hivyo huku akiondoa gari kwenye jumba hilo na kutokomea zao walipo pajua wao.



    **************************



    Siku iliyofuata. Nyumbani kwa Mata 1:30 Asubuhi.



    “Mnajua kila siku tunavyomuacha huyu dogo ipo siku anaweza kutuumbua" Moto aliongea na kuwaambia wenzake.



    “Thatha njia za kumuulia kila thiku ndio dhina shindikana, yani kila tukipanga vinatokea vikwadho, hadi nashindwa kuelewa tutumie njia gani ambayo haitoshindikana"



    “Yani leo lazima iwezekane tu kwasababu mimi nshachoka kila siku kuzungushana na kitoto kidogo kama kile" Moto aliongea kwa gadhabu.



    “Kila mmoja kachoka kuzungushana nae, cha mthingi ni kutafuta njia rahithi ya kumuua ili tupotedhe ushahidi kabitha"



    “Leo tunaenda kumteka akitoka shule, naamini njia hii itakuwa rahisi sana"



    “Tuna mtekaje yani?" Mata alimuuliza.



    “Itabidi tumteke akiwa yupo kwenye gari la shule, hiyo itakuwa ni njia rahisi kwasababu hakuna atakae tusumbua wakati tunamteka" Moto aliongea.



    “Hakuna atakae tuthumbua kivi yani?" Mata alimuuliza.



    “Yani ni hivi, mimi na wewe Mata tutaliteka gari la shule, halafu tunaingia ndani ya gari hiyo na kutoka na mtu wetu moja kwa moja hadi kwenye gari yetu halafu tunaondoka nae tuna enda kumuulia mbali huko" Moto aliwaambia wenzake.



    “Na Mrutu nae kwenye gari, yule dogo thi atamuona Mrutu? Mata aliuliza.



    “Hapo inabidi tuchague Mrutu avae maksi usoni au yule dogo tukishamtoa kwenye gari la shule ndio tumvishe maksi ili asimuone Mrutu"



    “Hapo itakuwa poa thana, au wewe unathemaje Mrutu, maana tangia tuandhe kuongea wewe hukutia neno lolote" Mata aliongea na kumuambia Mrutu.



    “Mi sina neno, kama mpango ndio huo basi fresh" Kiukweli Mrutu hakupenda Hemedy afe ndio maana hakuwa na raha kama mwanzo wala pia hakutaka kuchangia chochote katika maongezi hayo.



    “Basi sawa, itabidi saa tisa kamili tuwe maeneo ya shule tukimsubiria yule dogo ili tutimize mpango wetu haraka" Moto aliongea hivyo na kufunga kikao hicho na kila mmoja akenda kazini kwake ila Moto yeye hakwenda popote zaidi ya kwenda maskani kwake maana yeye hakuwa na kazi maalumu ya kufanya.



    Katika shule anayosoma Hemedy. 9:30 Alasiri.



    Walioneka wanafunzi wakitoka katika geti la shule hiyo, wengine walienda katika magari yaliyo wafuata na wengine walienda kwa miguu nyumbani kwao kwakuwa sio mbali na shule hiyo, baada ya dakika kadhaa, gari la shule lilitoka katika geti hilo huku likiwa limewabeba wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, na Hemdy pia alikuwa ni mmoja wapo aliekuwepo katika gari hilo.



    Liliongoza njia kuelekea majumbani kwa watoto hao, ila kabla halijafika mbali, likapungiwa mkono na wakina Moto na dereva wa gari hilo akalisimamisha pembeni ili kuwasikiliza watu hao. Mata alitoa bastola na kumuweka chini ya ulinzi dereva wa gari hilo na Moto yeye akatoa bastola na kuzama ndani ya gari hilo ili akamtoe Hemedy aondoke nae.



    Mrutu alibaki kwenye gari akiwasubiri wenzake wakamilishe huo mpango ili waondoke zao. ila ghafla akaona gari ya polisi ikija mbio mbio upande ambao gari ya shule lime paki, gari ya polisi ikawasha endiketa ishara ya kutaka kusimama upande huo huo lilipokuwa gari la shule, Mrutu hakujua afanye nini ili wajiokoe na hilo zahma litakalo wakumba muda mfupi ujao, Mata pia aliliona hilo gari la polisi likija upande huo, Moto nae aliliona hilo gari kupitia katika kioo cha mbele cha gari hiyo ya wanfunzi, gari hilo la polisi lilikuwa likija kwa kasi sana huku likiacha vumbi kwa nyuma....







    Mrutu akawapigia honi wenzake kuashiria kuwa waondoke, Moto na Mata waliiyelewa ile honi ina naama gani, wote wawili wakaacha wanachokifanya na kuanza kukimbilia kwenye gari lao, walipofika wakaingia ndani haraka haraka na Mrutu akaigeuza gari na kuiyondoa kuipeleka njia tofauti na ile gari ya polisi inapokuja, aliyondoa kwa kasi sana na alipofika mbele kidogo, akakunja kona almanusura aiangushe gari, baada ya kuiweka sawa, akapotelea huko huko.



    Gari ya polisi ilipofika karibu na ile gari ya shule, ilifunga breki za nguzu na kusimama pembeni kidogo na gari ya shule.

    Akashuka koplo Taure na kumfuata dereva ambae bado hadi muda huo alikuwa ameganda kwa uwoga wa kunyooshewa bastola kwa mara ya kwanza tangu alipotoka katika tumbo la mama yake.



    “Za saa hizi kaka?" Koplo Taure alimsalimia baada ya kumfikia.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sa..safi tu kaka" dereva alijibu.



    “Vipi, mbona kama vile haupo kawaida?"



    “Majambazi" alijibu kwa ufupi.



    “Sijakuelewa, majambazi wana nini?" Koplo Taure alimuuliza.



    “Wamenivamia"



    “Unajua mimi sikuelewi kabisa unachokizungumza, embu nyoosha maelezo" Koplo Taure alimwambia hivyo, baada ya kumuona hamuelewi.



    “Nimevamiwa na majambazi"



    “Wapi?"



    “Hapa hapa sasa hivi, ndio wale waliondoka na gari mbio kuelekea huko nyuma" Dereva alimwambia Koplo Taure, baada ya kusikia hivyo, akamwambia amsubiri hapo hapo asiondoke, akawahi kwenye gari yake na kuanza kuwafukuzia wakina Mata ambao hadi sasa washatokomea zao wanapopajua, Koplo Taure kwakuwa aliiyona ile gari ilipokunja na yeye alipofika hapo kwenye kona akakunja ila apofika mbele kidogo hakuona hata dalili ya vumbi, akageuza gari na kurudi hadi pale iliposimama gari ya shule.



    “Walikuwa wanataka nini?" Koplo Taure alimuuliza dereva baada ya kushuka kwenye gari na kumfuata.



    “Sijui, walikuja wawili hapa, mmoja akaniwekea bastola mimi na mwengine akaingia humu ndani ya gari"



    “Baada ya hapo?" Koplo Taure alimuuliza dereva baada ya kuona hajamalizia maelezo yake na kujiangalia kwenye suruali yake, ikabidi Koplo Taure aipeleke shingo yake hadi ndani ya gari sehemu alipokaa dereva na kuona kwenye suruali ya dereva huyo kuna maji maji chini ya mkanda“Mkojo"alijisemea mwenyewe na kutabasamu kisha akarudisha shingo yake nyuma.



    “Hawakufanya chochote, ila waliondoka baada ya kuona gari ya polisi inakuja"



    “Kwahiyo hawakukuambia chochote?"



    “Ndio, hawakusema kitu chochote"



    “Wewe unahisi walikuwa wana taka nini?"



    “Afande, kusema ukweli mi sijui chochote"



    “Sawa, ila mimi kuna mdogo wangu namtaka humu kwenye gari" Koplo Taure akabadilisha mada na kuongea kilichomleta hapo.



    “Lakini kwanini usimsubiri hadi akifika nyumbani ndio ukamchukue?"



    “Hapana, ni muhimu niondoke nae sasa hivi"



    “Anaitwa nani?"



    “Hemedy, Hemedy Mheshimiwa" Dereva akamgeukia utingo wake na kumuambia amuite Hemedy, baada ya sekunde kadhaa, Hemedy akashuka nje ya gari hilo na kuenda upande wa dereva, upande ambao Koplo Taure alikuwa amesimama, alipofika akamsalimia na kutulia.



    “Mkubwa, ni huyu hapa, asanteni, mnaweza kuendelea na safari yenu" Koplo Taure aliongea hivyo huku akiondoka na Hemedy kuelekea kwenye gari alilokuja nalo.



    “Sasa, kaka unaenda nae wapi huyo dogo?" Dereva aliuliza huku akichungulia kwenye kioo cha mbele ya gari hilo.



    “Nyie, endeleeni na safari yenu, nitampeleka mimi nyumbani kwao" Koplo Taure aliongea hivyo huku akingia kwenye gari baada ya Hemedy kuingia, akawasha gari na safari ya kuelekea kituoni ikaanza.



    Muda huo huo, ndio ulikuwa muda ambao, Mr Bakari Haneni, aliahidiana na Tosh, kupeleka pesa na mzigo wa madawa ya kulevya ili apewe watu wake. Mr Bakari Haneni hakuwa mzembe kiasi hicho, eti apeleke pesa na mzigo halafu awachukue watu wake kijinga jinga hivyo, hakutaka kukubali huo upumbavu, akapanga kupeleka kundi lake likakafanye mashambulizi baada ya kukabidhiana mizigo aliyoombwa na watu hao. Akampigia simu Yuni, mmoja kati ya watu wake wanaolinda ngome yake.



    “Njoo nyumbani kwangu mara moja, njoo na watu kama kumi hivi wenye silaha, haraka nawasubiria" Alipoongea hivyo akakata simu na kuwasubiria vijana wake aliowaita. Baada ya nusu saa, gari aina ya Hiace iliingia katika nyumba ya Mr Bakari Haneni, ikapaki sehemu maalum ya kupaki magari katika nyumba hiyo, na hao vijana walishuka na kuelekea katika moja ya bustani ya nyumba hiyo alipokuwa amekaa bosi wao, walipofika wakajipanga mstari na kumuangalia bosi wao. Mr Bakari Haneni aliwapitishia macho mmoja baada ya mwengine alipofika kwa wa mwisho, macho yake akayaleta kwa kijana aliesimama katikati ya vijana hao.



    “Yuni, nadhani unajua kwamba Tito na Tobi wametekwa kama jana nilivyokuambia" Mr Bakari Haneni aliongea hivyo kumuambia huyo kijana wa katikati, ambae alikuwa mrefu halafu mweupe mwenye macho makubwa na mwili mkubwa.



    “Ndio Mkuu" akajibu kiukakamavu.



    “Sasa basi, wale wajinga leo ndio ile siku ya kuwakomesha, haiwezekani wacheze na mimi hata kidogo, kwahiyo nataka mukawafunze adabu ikibidi muwauwe pia kama itawezekana, halafu murudi na wenzenu na mizigo yetu. Mmenielewa?"



    “Ndio Mkuu" wakaitikia wote.



    “Sasa ni hivi, Yuni utapanda na kijana mmoja kwenye gari nyengine tofauti na hiyo gari mliyokuja nayo nyie ndio ambao mtaenda kukabidhiana nao hiyo mizigo, halafu baada ya hapo hawa wengine watawashambulia ghafla baada ya nyinyi kuwa mbali nao, mtajua jinsi gani ya kujipanga wenyewe ila ninachotaka mrudi na mizigo yangu na wenzenu" Mr Bakari Haneni aliwaambia vijana wake.



    “Hakuna tatizo mkuu, tutarudi kama ulivyotuagizia" Yuni alijibu.



    “Sasa subiri nikupe namba zao ili mkifika muwasiliane" alimpa namba za Tosh. Baada ya hapo akaendelea.



    “Sitaki mrudi kama mnavyoondoka, nataka mrudi na wenzenu na mizigo yetu, halafu hakikisheni hamdhuriki hata kidogo, kwasababu nyote bado nawataka"

    Mr Bakari Haneni alivyoongea hivyo akawaruhusu waende na wao wakapnda kwenye gari walilo kuja nalo. Yuni na kijana mmoja wao wakapanda kwenye toyota mark 11 grand na safari ya kuelekea katika chuo cha utumishi kilichokuwepo kange ikaanza.



    Baada ya dakika thelathini, wakawa wamefika mbali kidogo na kilipo chuo cha Utumishi. Wakasimamisha gari pembeni, ili wapange ni jinsi gani ya kufanya.



    “Sasa nyie mtaenda mbele kabla yetu sisi, mtakipita kile chuo na kusimama kwa mbali kidogo, halafu sisi tutaenda kusimama pale pale chuoni walipotuelekeza, kwahiyo sisi tukishakabidhiana mizigo, mtatusubiri tukishafika mbali kidogo, ndipo na nyie mtakapo anzisha mapambano, naamini hadi hapo itakuwa tayari tushawazidi, kwasababu wao itakuwa hawaja jiandaa, halafu baada ya hapo sisi tunachukua mizigo yetu, kisha tunapotea haraka sana" Yuni aliwaambia wenzake. Alipoona wote wapo kimya wakimsikiliza yeye, akaendelea.



    “Kumbukeni, Mkuu ametuambia kwamba, turudi kama tulivyoondoka upande wetu, akimaanisha asipungue mtu hata mmoja katika hii kazi na tusirudi kama tulivyoondoka, akimaanisha turudi na wenzetu na mizigo yetu" Yuni alipoongea hivyo akawaambia wale waliokuwepo kwenye Hiace watangulie mbele halafu na wao wafuatie. Ikawa kama walivyopanga, baada ya kuondoka kwa ile Hiace baada ya dakika kumi na wao wakafuatia.



    Tosh na Doze walikuwa kwenye gari wamekaa wakiwasubiri wageni wao, gari yao waliipaki pembeni kidogo ya chuo hicho.

    Waliiyona Hiace iliyowapita muda mchache uliopita, ila hawakuitilia maanani sana, hawakuwafikiria kuwa watakuwa ndio hao wageni, kwasababu wageni wao waliwaambia wasimame chuoni hapo na hiyo Hiace ilipapita chuoni hapo. Baada ya dakika kumi na tatu, waliiyona gari aina ya mark 11 grand ikisimama karibu na chuo hicho.



    “Oya Tosh nahisi jamaa itakuwa ni hao hapo, embu jaribu kuwapigia simu" Doze alimwambia Tosh awapigie simu hao wageni wao wanaotaka kukutana nao.



    “Wao pia namba yangu si wanayo, watatu pigi..." kabla hajamaliza sentensi yake, simu yake iliita, akaipokea.



    “Haloo" Tosh aliongea baada ya kupokea simu.



    “Tumefika, mko wapi nyie?" sauti ya upande wa pili iliongea.



    “Ndio mko kwenye hiyo mark 11 grand?" Tosh aliuliza.



    “Ndio"



    “Haya, shukeni na mizigo yetu, halafu si manaiyona hii gari hapa pembeni yenu?"



    “Ndio, tunaiyona"



    “Shukeni, mmje na mizigo yetu hadi kwenye hiyo gari"



    “Hapana, hatuwezi kufanya biashara hiyo, kwanini tusishuke wote, sisi na nyie"



    “Pia sawa, shukeni na sisi tushuke" Tosh alipoongea hivyo, akasubiri kwanza walioko kwenye ile gari waliposhuka na wao ndipo wakashuka.



    “Mbona hatuwaoni watu wetu, wako wapi?" Yuni alionea huku akiangaza angaza upande wa pili waliopo wakina Tosh waliokuwa wameshuka kwenye gari mikono mitupu.



    “Msiwe na wasiwasi, leteni mizigo yetu, halafu ndio mtawaona watu wenu, si tumeamua kufanya biashara ya amani, sasa kinachomiogopesha ni nini?" Tosh alimuuliza Yuni.



    “Hata kama, ila ni vizuri zaidi tukiwaona watu wetu"



    “Ok, watu wenu wapo kwenye gari ya nyuma yetu, kwahiyo mnaweza kuja tufanye makabidhiano"



    Baada ya kukata simu, Yuni na kijana aliongozana nae, waliwafuata wakina Tosh waliokuwa wakiliendea gari ya nyuma yao ili wakafanye makabidhiano, walipokutana kwenye hiyo gari iliyodaiwa kuwa Tito na Tobi wamo. Tosh akataka briefcas walizoshika wakina Yuni zifunguliwe, zilipofunguliwa kwenye briefcas ya kwanza kulikuwa na vibunda vya noti za elfu kumi zimepangwa kwa ustadi mzuri. Tosh alipoona alitabasamu na kuamuru ilifunguliwe na hiyo nyengine nayo ilikuwa na vipakti vya madawa ya kulevya vilivyo jaa kwenye hiyo briefcas.



    Baada ya kuhakikisha kila kitu ndicho, akawafungulia mlango wa gari hiyo na kuwatoa wakina Tito wakiwa wamefungwa kamba, baada ya kuwatoa wakawafungua kamba na kuwaruhusu waondoke nao baada ya wao kukabidhiwa mizigo yao.



    Baada ya makabidhiano kwenda sawa, Tito, Tobi, Yuni na kijana mwengine walianza safari ya kuliendea gari lao ili waondoke na wenzao kwenye ile Hiace wafanye yao.

    Wakina Tosh wao hawakuwa na habari kwamba ilipangwa wageukwe, zile briefcas wakaziingiza kwenye ile gari nyengine ambayo alikuwa Kiku ndio anaiendesha, na wao wakaanza kuiyendea gari yao ili waondoke zao. Ila ghafla Doze alikoswa koswa na risasi iliyopita sentimita chache kwenye sikio lake, ikabidi ajirushe upande wa nyuma wa gari aliyokuwemo Kiku.

    Tosh baada ya kuona tukio hilo yeye alikimbia hadi kwenye gari alilokuja nalo huku akikoswa koswa na risasi, alipofika aliingia moja kwa moja upande wa dereva na kuwasha gari ili aondoke zake, risasi bado ziliendelea kupigwa na kufanya vioo vya hiyo gari kuvunjika, ila yeye hakujali alichotaka kwa wakati huo ni kuokoa uhai wake tu, akawasha gari na kuliondoa hapo kwa kasi huku akisindikizwa na risasi zilizopasua kioo cha nyuma.



    Wale watu kwenye ile Hiace baada ya kuona gari moja tayari imeondoka, wakaamisha mashambulizi kwenye hii gari iliyobakia, walipiga risasi hiyo gari, inavyooneka watu hao hawakuwa na mafunzo yoyote ya kutumia bunduki maana walijipigia tu bila ya kulenga shabaha, waliipiga risasi gari na kuipelekea kuifanya chujio kwa matundu ya risasi.

    Doze baada ya kuona Tosh ameondoka na gari walilokuja nalo, akaona akichelewa tena na gari hii ambayo ndani yake yupo Kiku itamuacha, kwavile alikuwa ubavuni mwa gari hiyo, akafungua mlango wa nyuma na kuingia humo, Kiku baada ya kuona Doze ameingia ndani, akaondoa gari kwa kasi kiasi kwamba nusura nusura akauvamie mti uliokuwa mbele yake baada ya kupata upenyo mzuri akatokomea zake.



    Wale watu baada ya kuona watu wao wamekimbia na wao wakapanda kwenye gari yao na kuanza kuwakimbiza huko huko walipoelekea. Wanafunzi wachuo hicho waliposikia milio ya risasi hawakujua wakimbile wapi wakabaki wakifukuzana humo humo ndani ya chuo. ili kuwa kama vile wanaangalia muvi jinsi mapigano hayo yalivyokuwa yakiendelea hapo nje ya chuo hicho.



    Kituo cha polisi.



    Baada ya kufika kituoni, akaweka gari kwenye paking ya hapo, na kushuka, akanza kuelekea ndani huku akifuatiwa na Hemedy kwa nyuma, wakaongozana hadi kwenye ofisi ya Inspekta Ganjo na kuingia humo. Hemedy alipoingia humo akamsalimia Inspekta Ganjo na kukaa kwenye kiti.



    “Habari za shule?" Inpekta Ganjo, alimuuliza.



    “Nzuri tu" Hemedy alijibu.



    “Unasoma lakini?"



    “Ndio, nasoma"



    “Vizuri, nimemtuma huyu aje kukuchukua kule shule, ngoja kwanza. hivi watu waliofanya mauwaji ya wazazi wako ukiowaona unawakumbuka?" Inspekta Ganjo alimuuliza.



    “Ndio, nikiwaona nawakumbuka" Hemedy alijibu.



    “Sawa, Koplo Taure mpeleke akawaone" Inspekta Ganjo alipoongea hivyo, Koplo Taure akamchukua Hemedy na kutoka nae nje ya ofisi na kwenda nae kwenye selo walipo hao alioambiwa kuwa akawaangalie kuwa ndio wauwaji wa wazazi wake.



    “Wale pale watatu, embu waangalie kama ndiwo" Koplo Taure alipomuambia hivyo, Hemedy akakaza macho baada ya kuangalia vizuri, akapigwa na butwaa, ikabidi afikiche macho yake kwa kutoamini anachokiona mbele yake.



    “Haaaaaa!!!!! Na wewe pia upo?" Hemedy aliuliza Kwa hamaki baada ya kumuona mtu alie mshangaza sana kumuoma mahala hapo.









    “Dogo, sijakuleta hapa uje kuwauliza watu maswali, embu waangalie wale watu watatu kule mwisho, ndio hao au sio?" Koplo Taure alimwambia Hemedy baada ya kuona amemshangaa mtu huyo aliekuwa pembeni ya watu watatu waliokuwa wamekaa mwisho kabisa ya ukuta wa selo hiyo.



    “Hapana, wale sio na wala pia siwajui" Hemedy alijibu huku akiwa bado macho yake ameyagandisha kwa yule mtu aliekuwa amekaa pembeni ya wale wengine.



    “Una uhakika?" Koplo Taure alimuuliza.



    “Ndio"



    “Haya twende" Koplo Taure aliondoka na Hemedy hadi katika ofisi ya Insepekta Ganjo.



    “Enhee! Kasemaje, ndiwo au?" Inspekta Ganjo aliongea hivyo baada ya watu hao kuingia katika ofisi yake.



    “Amesema siwo" Koplo Taure aliongea hivyo huku akikaa kwenye kiti kilichopo humo ofisini.



    “Eti Hemedy, wale watu sio waliofanya mauaji ya wazazi wako?" Inspekta Ganjo alimuuliza Hemedy.



    “Hapana sio wale, mimi nawajua nikiwaona" Hemedy alijibu.



    “Sawa, nilimtuma huyu aje kukuchukua shuleni kwenu ili uje kuwaona hawa watu kama ndio au sio, kwasababu hawa watu wamefanya tukio la mauwaji kwenye familia flani siku ya leo, sasa ndio tumefanikiwa kuwakamata, sisi tukawashuku kuwa huenda ikawa ndio hawa waliofanya mauwaji ya wazazi wako pia"



    “Hapana, sio wale" Hemedy alisema.



    “Basi kama sio, hakuna tatizo(akamgeukia Koplo Taure) mpeleke nyumbani kwao huyu"

    Koplo Taure alitoka na Hemedy nje ya kituo hicho, wakapanda kwenye gari ya polisi na safari ya kwenda nyumbani kwa kina Hemedy ikaanza.



    “Anko" Hemedy alimuita Koplo Taure wakiwa ndani ya gari.



    “Sema dogo"



    “Hivi yule mtu mwengine aliekaa pembeni ya wale mnaosema majambazi kule selo, ana kesi gani yule?" Hemedy aliuliza.



    “Kwani unamjua yule mtu?"



    “Ndio namjua yule"



    “Umemuona wapi?"



    “Yule ni daktari aliekuwa katika ile hospitali nilipoenda kulazwa mara ya pili, aliwahi kunichoma sindano ya dawa, aah aliniumiza, yani kanichoma sindano inauma, halafu sasa ananichoma huku anacheka ikiwa mwenzake mimi nime kasirika"



    “Anhaa!!! Yule ana kesi yake ya kumpiga mkewe hadi kumjeruhi, kwahiyo ndio ameletwa hapa na majirani zake, maana alikuwa amekunywa pombe zilizompelekea kumpiga mkewe hadi kumzimisha"



    “Dah!! Kumbe ana roho mbaya hadi kwa mkewe"



    Koplo Taure alipaki gari nje ya nyumba ya Mrutu baada ya kufika.

    Hemedy akashuka na kumuaga Koplo Taure kisha akaingia ndani ya nyumba hiyo, Koplo Taure akageuza gari na kurudi kituoni.



    * * * *



    Kundi la Mr Bakari Haneni baada ya kuwafukuza wakina Kiku na Doze, waliwakosa na kuamua kurudi nyumbani kwa Bosi wao, baada ya mwendo mrefu kiasi kutoka Kange hadi Raskazone, wakafika na kuingiza gari zao ndani ya nyumba hiyo, wakashuka na kumfuata Bosi wao aliekuwa bado yupo pale pale kwenye bustani amekaa.



    “Vipi? Mbona sura zenu hazina furaha kama siku nyengine ninapo waagiza mkafanye kazi na kufanikiwa, kwanza vijana wangu wapo wapi?"



    “Wale pale ndio wanashuka kwenye gari" mtu mmoja katika kundi hilo aliongea huku akiwanyooshea kidole wakina Tito waliokuwa ndio wana shuka katika gari aliloenda nalo Yuni na yule kijana mwengine, na wao wakaongozana na kwenda hadi mbele ya bosi wao na kusimama mstari mmoja kumuangalia bosi kama walivyofanya wenzao.



    “Embu njoeni hapa mbele yangu vijana wangu"

    Mr Bakari Haneni alipoongea hivyo Tito na Tobi walienda mbele yake na kusimama.



    “Dah!! Aise!! Hawaja waumiza lakini(aliongea hivyo huku akiwaangalia angalia vijana hao) Tobi wamekutoboa na nini hapa kwenye mkono?"



    “Mkuu, wale watu wana roho mbaya sana na ni lazima walipe kwa hili, hapa wamenitoboa na kifaa flani cha kutobolea matundu kwenye mbao za madirisha" Tobi aliongea kwa ghazabu za waziwazi.



    “Ila hawaja waumiza sehemu nyengine yoyote?"



    “Hapana Mkuu, walitulaza tu na njaa siku moja na kutufunga kwenye viti kiasi kwamba hatukuweza kujitikisa kwenda popote" Tito alijibu.



    “Sawa, mmekuja na mizigo yetu?"

    Mr Bakari Haneni alimgeukia Yuni na kumuuliza swali hilo.



    “Hapana Mkuu" Yuni alijibu.



    “Kwanini?" Mr Bakari Haneni aliuliza huku hasira zikianza kumpanda.



    “Mkuu, wale watu walikuwa pia wamejiandaa, haikuwa kama vile sisi tulivyodhani, baada ya kukabidhiana wao wakanza kuturushia risasi, ikabidi sisi tujifiche na kuanza kurushiana risasi na wao, ila wao baada ya kuona tuna wazidi wakapanda kwenye gari yao na kukimbia na tukawaunganishia ila hatukuweza kuwapata"



    Yuni alidanganya maana alimjua mtu huyo hakuwa na masihara pindi akutumapo kazi halafu usiikamilishe kama yeye anavyotaka, ndio maana akatumia uongo huo ili kumpoza hasira na kweli hasira zilipungua na kuwa katika hali ya kawaida.



    “Lakini nyote si mmerudi salama?"



    “Ndio Mkuu" wakaitikia wote.



    “Ok, nyie wengine mnaweza kwenda mkaendelee na kazi, Tito na Tobi bakini hapa kwanza" Alipoongea hivyo lilekundi lote likaondoka na kwenda kwenye ile Hiace na kutoka ndani ya nyumba hiyo kuelekea kwenye ngome yao.



    “Hiyo sehemu mlipofungiwa mnapajua?"

    Mr Bakari Haneni aliwauliza watu hao baada ya lile kundi kuondoka.



    “Ndio Mkuu, tunapajua" Tito alijibu.



    “Inabidi mkafanye shambulizi la kushtukiza ikiwezekana kuwateka kabisa na kuwapeleka kwenye ngome yetu ili wakalipe kwa walichokifanya"



    “Mkuu, ila mimi sidhani kama lile jumba walilotufungia kwamba itakuwa ndio maskani kwao" Tito aliongea.



    “Kwanini?"



    “Kwasababu pale walikuwa wanakuja na kuondoka tu, nahisi lile jumba walilikodisha au wamelitumia tu kwa muda kutokana na mimi nilivyo wasoma"



    “Ok, itakuaje ili kuwapata, maana wameodoka na mzigo wetu na pesa zao, hiyo ni hasara kubwa sana"



    “Mkuu, wale tuna kuhakikishia ndani ya wiki hii hii watakuwa mikononi mwetu na kuwaleta mbele yako"



    “Nitafurahi kama itakuwa hivyo, nawaamini sana vijana wangu wa kazi"



    “Mkuu wewe usijali"



    “Sawa, nendeni katika nyumba yenu, atakuja daktari kuja kumitibu baada ya nyie kufika halafu kesho nitawahitaji hapa Asubuhi"



    Baada ya kusikia hivyo waliondoka na kwenda katika gari na kupanda na safari ya kuelekea katika nyumba yao iliyokuwa maeneo ya majengo waliyopewa na bosi wao ikaanza.



    * * * *



    “Duh!!! Yani ilikuwa kama vile muvi la kizungu kwajinsi wale wajinga walivyoturushia marisasi yao" Kiku aliongea hivyo kuwaambia wenzake baada ya kufanikiwa kuwatoroka wakina Yuni na kundi lake. Wakati huo walikuwa wapo katika nyumba yao waliyoifanya kama maskani yao ya kufanya na kupanga mambo yao mengi.



    “Halafu huyu mjinga aliniacha na gari sijui alitaka waniue wale wajinga wenzie" Doze aliongea kwa utani.



    “Asa mimi nakuona hutokei, unadhani mimi ningefanyaje kama sio kuondoka pale" Tosh aliongea.



    “Embu tuachaneni na hayo, kwanza tunafanyaje maana yale magari wameyaharibu hasa hasa upande wa vioo na tena ile gari nyengine tumeiazima sio yetu" Kiku aliongea.



    “Kwani vioo si vinabadilishwa tu, tuna badilisha halafu tunalitoa gari la watu" Tosh aliongea.



    “Hata hivyo pesa tunazo nyingi tu, hata akitaka tumnunulie gari nyengine pia uwezo huo tunao" Doze aliongea.



    “Ila kumbukeni wale wajinga hawatokubali lazima watatutafuta tu kwahiyo tunapokuwa sehemu yoyote tuwe makini tusijiachie" Kiku aliongea.



    “Au kama ikiwezekana na sisi pia tuwawinde popote pale tutakapo waona tuwauwe tu kabla hawaja tuanza sisi" Tosh aliongea.



    “Hapo Tosh umeongea, inabidi tuwawahi kabla hawaja tuwahi" Doze aliongea.



    “Embu kwanza fungua hiyo mizigo yetu tuhakikishe kama ni yenyewe isije ikawa tumeuziwa mbuzi kwenye gunia" Kiku alipoongea hivyo, Tosh akazifungua zile briefcacas na wote macho yao yakatua ndani ya mikoba ile, wakahakikisha ni kweli yale yalikuwa ni madawa ya kulevya origino kabisa na pesa halali kwa matumizi zilizokuwepo katika mkoba mwengine, baada ya kuhakikisha wakaifunga mikoba ile na kuendelea na maongezi yao mengine ambayo hayakuwa na ulazima kuyaandika katika hii hadithi yetu.



    * * * *



    Wakina Mrutu baada ya kukimbia na gari yao wakaenda moja kwa moja nyumbani kwa Mata.



    “Dah!!! Aithee yani yule mtoto ana mungu kweli yani" Mata aliongea hivyo baada ya kukaa kwenye sofa ndani ya nyumba hiyo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “We acha tu mimi tayari kashanichosha, yani kila tunapo mpangia mipango basi anaikwepa hata sijui pia tufanyeje" Moto aliongea kwa masikitiko kana kwamba hivyo wanavyotaka kufanya ni sawa tu.



    “Kwandha imekuaje lile gari la polithi likaja pale hai hai?" Mata aliwauliza wenzake kama vile kuna ambae anajua lile gari lilifuta nini pale, ikawa ameuliza swali la kipumbavu kwa upande wangu mimi muandishi sijui wewe msomaji.



    “Sasa Mata, nani ambae anajua kwamba lile gari limefuata nini pale, au umekosa maneno ya kuongea ndio maana" Moto aliongea.



    “Bathi tuachane na hayo, vipi kuhuthu yule dogo, maana kesho kutwa Mrutu anataka kwenda kuchukua barua ili tuende mahakamani tukachukue mali dhetu"



    “Yule dogo twendeni tukammalize huko huko nyumbani kwa Mrutu sasa hivi" Moto aliongea.



    “Nshasema nyumbani kwangu sitaki afe mtu" Mrutu aliongea kwa gadhabu, si kwamba kachukia Hemedy kufa nyumbani kwake, laa hasaa!! Bali hakutaka kabisa habari hizo za kuuliwa kwa mwanae huyo.



    “Hapana hatumuui hapo kwako, bali tuna mteka na kuondoka nae" Moto aliongea hivyo akidhani kuwa mwenzao amekasirika kutokana na sababu hiyo.



    “Ok, twendeni bathi thatha hivi tuka ifanye hiyo kadhi maana kesho kutwa tu tunachukua mali dhetu"

    Kikao hicho kikafungwa na safari ya kwenda kwa Mrutu ikaanza, baada ya dakika kadhaa ikawa tayari wameshafika nje ya nyumba ya Mrutu.



    Kipindi hicho Hemedy alikuwa yupo sebuleni anaangalia Tv, kwa mbali alisikia sauti ya geti likifunguliwa, kwakuwa hapo alipokaa kuna dirisha la kuweza kumuonyesha nje ya sebule hiyo, akapanda juu ya sofa na kufungua pazia la dirisha hilo, akawaona watu watatu wakiingia ndani ya nyumba hiyo, wawili kati yao hakuwajua vizuri, ila mmoja wao akamjua kuwa ni baba yake mdogo, ila wapofika karibu na mlango wa kuingilia ndani ndipo hapo alipo pigwa na butwaa baada ya wawili kati ya hao watu kuwajua vizuri na kuwakumbuka haswaaa kuwa ndio hao walio muulia wazazi wake.



    Hakujua watu hao wamejuana vipi na baba yake mdogo hadi kufuatana hadi hapo nyumbani, (au itakuwa wamemteka na yeye nini?) alijiuliza mwenyewe lakini akapingana na hilo baada ya kuona watu hao wapo kiurafiki zaidi na baba yake mdogo, akashindwa kuelewa, akabaki ameduwaa tu, baada ya sekunde tano akainuka hapo na kukimbilia chumbani kwake.



    “Huyu dogo yupo, si unaona hata Tv inawaka inavyoelekea yupo humu humu ndani" Moto aliongea baada ya kuingia sebuleni hapo.



    “Thatha tumthubirie au tumtafute" Mata aliongea.



    “Atafutwe tufanye haraka tuondoke, oya Mrutu embu mfuate chumbani kwake ukamuangalie" Moto aliongea hivyo, Mrutu hakuwa na namna ya kupinga, akaenda hadi katika chumba anacholala Hemedy na kuingia humo ndani, alipoingia alipigwa na butwaa kwa alichokikuta humo ndani, hakuelewa imekuaje hadi ikawa hivyo, akabaki na kuduwaa tu asielewe nini afanye..







    “Huyu mtoto yupo wapi?" Mrutu alijiuliza mwenyewe baada ya kutomuona Hemedy humo chumbani kwake, akanza kumtafuta kila sehemu ila alimkosa na kuamua kutoka kurudi sebuleni.



    “Humo chumbani dogo hayupo bwana na sijui kaelekea wapi" Mrutu aliwaambia wenzake baada ya kufika sebuleni hapo.



    “Umemuangalia hadi chooni huko" Moto aliongea huku akiinuka kwenye sofa alilokaa.



    “Ndio, kote huko nimemuangalia ila sija muona. we unataka kwenda wapi mbona umeinuka?" Mrutu alijibu na kumuuliza Moto baada ya kumuona ameinuka kwenye sofa.



    “Subiri mimi nikamcheki huko nje, nakuja sasa hivi" alipoongea hivyo akafungua mlango na kutoka nje. Mrutu akanza kuwa na wasiwasi hakujua Hemedy yupo wapi, akapatwa na wasiwsi zaidi baada ya kuona Moto anatoka nje kwenda kumtafuta huko uani, alidhani labda huenda Hemedy akawa yupo huko huko uani, akapanga endapo Hemedy akiletwa na Moto kutoka huko uani basi alete pingamizi lolote ili mradi tu Hemedy asife. Baada ya dakika tatu akarudi sebuleni hapo.



    “Haya vipi?" Mata alimuuliza.



    “Hayupo" alijibu huku akikaa kwenye sofa.



    “Nahisi itakuwa ametoka kidogo ila atarudi muda si mrefu kwahiyo tumsubirini" Moto aliongea hivyo huku akiinuka kwenye sofa na kuliendea friji lililo kuwepo hapo hapo sebuleni na kuchukua soda na kurudi nayo kwenye sofa, akaifungua na kuinywa pafu moja.



    “Mrutu na wewe unazingua, kwanini huweki hata pombe bwana, we unatuwekea masoda haya ya kunywa wanafunzi" Moto aliongea.



    “Mimi siweki pombe, si unajua kuwa mimi ni muislamu, sasa nitawekaje pombe kwenye nyumba yangu"



    “Acha zako wewe nani aliekuambia kuwa waislamu hawanywi pombe, halafu pia wewe kama haunywi unatakiwa utuwekee sisi wageni" Moto aliongea.



    “Kwanza mimi sinywi pombe halafu sitoweza kuziweka katika nyumba yangu, kwani wewe kama unataka kunywa pombe, si unywe huko unapotoka halafu ukija hapa uwe tayari ushapendeza"



    “Unajifanya muislamu safi kumbe huna lolote" Moto aliongea hivyo huku akiipiga pafu kubwa ile soda, ikabakia nusu.



    “Sio muislamu safi, ila si unajua kuwa sisi wengine hatukuzoea hivyo vitu" Mrutu alijibu lakini moyoni mwake alikuwa anaombea Hemedy asirudi muda huo huko alipoenda.



    “Anakudanganya tu huyo, kwadha tangu lini akanywa pombe" Mata aliongea.



    “Mimi huwaga nanywa siku moja moja nikiamua" Moto alijibu.



    “Basi hapa kwangu siweki pombe mimi"

    Waliendelea na mazungumzo yao huku wakivuta muda Hemedy arudi huko alipoenda ili waondoke nae, wawili kati yao wakiombea Hemedy arudi ili watimize azma yao, mmoja wao aliombea Hemedy asirudi ili wasiitimize azma yao.



    Baada ya kukaa kwa muda mrefu nyumbani hapo kwa Mrutu, maana walikaa takribani masaa matatu bila Hemedy kutokea hadi muda huo wa saa tatu na nusu usiku wakaamua tu waage ili waondoke zao.



    “Subirini niwasindikize hadi hapo nje nika nunue msosi maana leo nimechelewa kupika msosi" Mrutu aliongea.



    “Kwahiyo hukutaka kupika kwaajili yetu, ulidhani labda tutakumalizia chakula chako" Moto aliongea hivyo huku akiuelekea mlango wa kutokea nje.



    “Hapana sio hivyo, nyie wenyewe mnajua kwamba tulikuwa wote hapa tunapiga stori kiasi kwamba hadi nimesahau kupika" Mrutu aliongea hivyo huku na yeye akitoka nje baada ya Moto kutoka huku akifuatiwa na Mata nyuma yake. Walitoka nje ya nyumba hiyo, Moto na Mata walipanda kwenye gari na kuondoka nyumbani hapo na Mrutu nae alielekea kwenye kibanda cha mgahawa kwenda kuangalia chakula.



    Hemedy kule chumbani kwake alitoka ndani ya kabati ambalo halikuwa na kitu chochote ndani yake, alikuwa amejifungia ndani ya kabati ili kujilindia roho yake kwa watu hao walio muulia wazazi wake, alipokuwa ndani ya kabati alikuwa akiskia tu minong'ono hakuskia kile ambacho kina ongelewa kwa ufasaha zaidi, ila baada ya kuona kimya ndipo akaamua atoke ndani ya kabati hilo kutokana na joto alilokuwa akilipata.



    Akanyata hadi mlangoni kwake na kutega sikio vizuri ili aweze kusikia chochote kitakachoongelewa sebuleni hapo, kimya. akafungua mlango na kutoa kichwa akachungulia vizuri na kuona sebule ikiwa tupu, akarudi katika chumba cha baba yake mdogo na kujaribu kuufungua mlango ila akaona mlango umefungwa, “atakuwa ametoka nao wale watu" alijiwazia mwenyewe, akatoka nje ya nyumba hiyo na kwenda katika mti uliokuwa mbali kidogo na nyumba hiyo, akatulia hapo.



    Baada ya kujibanza hapo kwenye mti kwa dakika tano, akamuona baba yake mdogo akirudi na mifuko miwili, akamsubiria aingie ndani baada ya dakika mbili na yeye akaingia.



    “We ulikuwa wapi masaa yote" Mrutu aliekuwa yupo kabatini akitoa sahani, alimuuliza swali hilo Hemedy alieingia humo sebuleni.



    “Nilikuwa hapo jirani kwa rafiki yangu" Hemedy alijibu kwa uoga.



    “Haaa!!! Yani wewe umekuja mtaa huu hata wiki hujamaliza tayari ushapata rafiki, mbona muongo we dogo"



    “Kweli baba mimi nilikuwa hapo jirani tu"



    “Sawa, ila siku nyengine usikae kwa watu hadi muda huu, umeniskia?" Mrutu hakuweza kumgombesha sana, kwasababu yeye mwenyewe pia amefurahi baada ya wakina Mata kumkosa mwanae huyo kwa mara nyengine “hahahah!! hapo ndipo ninapo amini kuwa huyu dogo analindwa na mungu asiuawe, eeee mungu mlinde hivi hivi" alijiwazia mwenyewe huku akimpa sahani Hemedy.



    “Sawa nimekuelewa" Hemedy alijibu huku akipokea sahani aliyopewa na Mrutu, akachukua mfuko mwengine uliokuwa umebakia juu ya meza baada ya mwengine kuchukuliwa na Mrutu, akamimina chakula hicho ndani ya sahani, kilikuwa ni pilau na nyama za kuku, na yeye akaenda kwenye meza akakaa na kuanza kula, baada ya kumaliza kula alimuaga baba yake huyo na kwenda chumbani kwake, akabadilisha nguo na kuvaa nguo zake alizozoea kulalia nazo ambazo zilikuwa ni track suti, akazima taa na kujitupa kitandani, hapo mawazo yote yalikuwa kwa wale watu waliomuulia wazazi wake. “kumbe bamdogo anajuana nao, au na yeye anashirikia nao? Hapana haiwezi kuwa hivyo. lakini sasa mbona yupo nao, au na yeye wanataka kumuua, mmhh!! itabidi nimuambie kuwa wale watu ndio walio waua wazazi wangu, sijui nika muambie sasa hiviii? Aagh nitamuambia kesho" aliendelea kuwaza hadi pale alipopitiwa na usingizi na kulala. Akalala.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * * * * * * * * *



    Siku iliyofuata. Nyumbani kwa Mr Bakari Haneni. 2:45 Asubuhi.



    Gari ya kifahari aina ya Jaguar ilitoka katika nyumba hiyo na kuelekea barabara ya hospitali ya Bombo, ikanyoosha moja kwa moja, ikaipita Regal Naivera Hoteli. “kuna nyuki anatufuata nyuma yetu" Mr Bakari Haneni alimwambia hivyo dereva wake ambae pia ni mlinzi wake baada ya kuona gari aina ya Breves lililokuwa likiifuatilia gari hiyo nyuma yake tangia anatoka nyumbani kwake.



    “Twende PSPF tukasimame pale, halafu tumuone yeye ataenda wapi"

    Wakaipita Toyota na kwenda kusimama mbele kidogo katika jengo la PSPF lililokuwa likiangaliana na jengo la Tanesco, gari ikapaki katika maegesho ya jengo hilo, “subiri mimi nizuge kuingia humu ndani, wewe endelea kumuangalia ataishilizia wapi baada ya sisi kusimama hapa" alimwambia hivyo mlinzi wake kisha akashuka kwenge gari na kupotelea ndani ya jengo hilo.



    Ile gari iliyokuwa ikiwafuata nyuma, ilikuwa ni gari ya Koplo Taure, baada ya kuona windo lake limesimama katika jengo hilo, yeye akaenda mbele kidogo kwenye Car Wash iliyokuwa karibu na garden, akapaki hapo na kuelekeza macho yake katika jengo aliloingia Mr Bakari Haneni.



    Baada ya dakika ishirini, alimuona Mr Haneni akitoka katika jengo hilo na kuingia katika gari alilokuja nalo, aliiyona gari hiyo ikigeuza na kurudi kule kule ilipotoka na yeye akaingiza gari barabarani ili kuendelea kulifuatilia windo lake.



    “Hivi hili gari linalo tufuata unaweza ukalijua?" Mr Bakari Haneni alimwambia dereva wake huku akiwa amegeuza shingo yake kuliangalia gari la Koplo Taure kupitia kioo cha nyuma.



    “Hapana Mkuu, silijui" dereva alijibu.



    “Ok, sio mbaya, muache atufuatilie" Mr Bakari Haneni alipo ongea hivyo, akarudisha shingo yake mbele.



    “Subiri nizikariri namba zake za gari" Mr Bakari Haneni aligeuza tena shingo yake na nyuma, akazikariri namba za gari ya Koplo Taure, wakati huo walikuwa tayari wamefika katika nyumba yake, dereva akaingiza gari ndani na kuipeleka katika maegesho na kusimamisha.



    Koplo Taure baada ya kuona windo lake limeingia katika nyumba hiyo, yeye akageuza gari na kurudi kituoni..



    Mr Haneni, akashuka kwenye gari baada ya kupakiwa sehemu maalumu ya kupaki magari katika nyumba hiyo na kuingia sebuleni mwa nyumba yake na kuwakuta Tito na Tobi tayari wameshafika nyumbani hapo.



    “Vijana wangu karibuni, mmefika saa ngapi hapa?" Mr Bakari Haneni aliongea hivyo huku akikaa katika sofa.



    “Tumefika kama dakika kumi tu zilizopita" Tobi alijibu.



    “Vizuri. wakati natoka hapa nyumbani kuna gari ilikuwa inanifuata nyuma, ili kujipa uhakika zaidi, nikamuambia dereva wangu aipaki gari yetu katika jengo la PSPF halafu mimi nikashuka nakuingia ndani ya jengo hilo ili kuzuga tu, baada ya kutoka nikamuona mfuatiliaji amepaki gari yake pale Car Wash karibu na ile garden, ikabidi tu ni ghairishe safari yangu na kuamua kurudi hapa" Mr Bakari Haneni aliongea.



    “Kwahiyo huyo mfuatiliaji ameishia wapi?" Tito aliuliza.



    “Sijui, ila nilikuja nae hadi hapo nje ya geti, sasa sijui ananisubiria au kaamua aondoke zake"



    “Kwahiyo huyo mfuatiliaji huju mjua kuwa ni nani?" Tito aliuliza.



    “Sijamjua ila namba zake za gari nimezikariri ni T 946 RKK"



    “Mkuu, huyo mtu aliekufuatilia wewe ndio huyo huyo alietufuatilia sisi siku ile" Tobi alisema kwakua yeye ndie aliezikariri namba za gari ya Koplo Taure siku ile alipo wafuatilia kutoka Majengo kwenye nyumba yao hadi hapo nyumbani kwa Mr Bakari Haneni.



    “Kama ndio huyo huyo mtu mmoja alienifuatili mimi na nyinyi, basi inavyoelekea kuna kitu anataka akichunguze kwetu, sasa nasema hivi, mkiliona popote gari hilo, hakikisheni mtu mwenye gari hilo mna mkamata mnakuja nae mbele yangu au kama ataleta tabu basi mnaweza kumalizana nae huko huko ila vizuri mkija nae hapa ili nimuone"



    “Hakuna shaka Mkuu" waliitikia wote kwa pamoja.



    “Ok, Tito vipi kuhusu Mrutu na Mzigo wetu, maana tumempa muda wa kutuletea pesa zetu lakini ameamua kuuchezea mwenyewe au unataarifa zozote kuhusu yeye?"



    “Hapana Mkuu, sina taarifa zozote kutoka kwake, wala pia hajaleta pesa zetu"



    “Safi, watu wakaidi kama hawa ndio nawapenda, sasa sikia si umesema yule mtoto wa kaka yake anaemlea yeye?"



    “Ndio mkuu"



    “Basi huyo mtoto namtaka leo hii hii akiwa hai, fanya unachoweza"



    “Usijali Mkuu, hilo limepita"



    “Kwanza naona maskani watoto wakufanya kazi wamepungua kwahiyo namtaka na huyo mtoto nae akasaidiane na wenzake kufanya kazi"



    “Hakuna shaka Mkuu"



    “Jana daktari niliemuagizia alikuja kwenu?"



    “Ndio Mkuu"



    “Vipi hali ya mkono wako Tobi?"



    “Mkuu, leo kidogo afadhali, viganja ninaweza kuvikunja" Tobi alijibu.



    “Hawa washenzi, itabidi walipe kwa walicho kifanya, ila kwanza leo nendeni mkaniletee huyo mtoto halafu hayo mambo mengine yatafuata baadae"



    “Sawa Mkuu"

    Waliitikia wote kwa pamoja na kutoka nje sehemu walipo paki gari yao, wakaingia na kutoa gari nje ya nyumba hiyo.



    “Tutampata wapi huyu mtoto?" Tobi alimuuliza Tito.



    “Usijali, huyo dogo mimi namjua tangu ana kaa na wazazi wake hadi sasa anakaa na Mrutu, ila kwa Mrutu sipajui inabidi tumfuate shuleni kwao naamini hapo hatuwezi kumkosa" Tito alijibu.



    “Anasoma shule gani?"



    “Anasoma pale EBEN-ENZER ENGLISH MEDIUM SCHOOL"



    “Lakini sasa hivi bado mapema sana, watakuwa bado hawajatoka shule"



    “Kwasasa bado hawajatolewa ndio, inabidi sasa hivi tutafute sehemu tuvute muda, kwenye saa nane nane hivi, tunaenda kwenye ile shule, tutamsubiri akitoka na gari ya shule basi hiyo ndio nafasi, tutamchukua humo humo kwenye gari na kuondoka nae"



    “Sasa hivi tuna elekea wapi kuuvuta huo muda?"



    “Kwasasa twenzetu Mikanjuni Pazuri tukapate maji maana nina siku kama nne hivi sijapata yale mambo halafu pia itakuwa rahisi kwasababu Mikanjui Pazuri na ile shule sio mbali sana kwahiyo hapo itakuwa afadhali kidogo" Tito alipoongea hivyo, aliongeza spidi ya gari ili kuwahi kwenye baa hiyo.



    * *



    Majira ya saa tisa na nusu alasiri, wanafunzi wanaosoma katika shule ya EBEN-ENZER walitolewa shuleni hapo ili kila mmoja aelekee nyumbani kwako, wale waliokuwa wakiletwa na kurudishwa na gari ya shule wao walipanda katika gari hiyo na walipotimia gari ilianza kutoka shuleni hapo na kuingia barabarani.



    Kama siku ya jana alipo simamishwa na watu asiowajua na leo pia ilikuwa ni hivyo hivyo, dereva anaendesha gari ya shule alipigwa mkono na mtu aliesimama katika ya barabara akimtaka asimamishe gari, kwakuwa mtu huyo alisimama katikati ya barabara dereva hakuwa na jinsi zaidi ya kusimamisha gari, hofu, wasiwasi, uoga vyote vilimpata dereva huyu kwa wakati mmoja, maana alijua watu hao ndio wale wale waliokuja jana na kumtaka asimamishe gari bila ya kujua walikuwa wanataka nini.



    Tito alishuka kwenye gari walilokuja nalo na kuingia katika gari ya shule, wakati huo Tobi yeye amesimama mbele ya gari hiyo bila ya kuongea chochote, Tito alipoingia ndani ya gari hiyo akaanza kumuangalia mwanafunzi mmoja baada ya mwingine, wanafunzi hao hawakuwa na hofu na mtu huyo kwasababu hawakujua kuwa alifuata nini ndani ya gari hilo, wao wakabaki kumuangalia anatafuta nini.

    Tito macho yake yalitua katika sura ya Hemedy, Akatabasamu na kuanza kumfuata sehemu alipokuwa amekaa.







    ENDELEA....



    Alipomfikia akamshika mkono na kumuinua, ila Hemedy akagoma kuinuka na kujaribu kuutoa mkono wa mtu huyo asie mjua, Tito alipoona Hemedy anataka kuleta tabu, maana kitendo hicho aliona kama vile ni upotevu wa muda, ni kitendo cha sekunde mbili tu, jikono lenye jiganja jikubwa mithili ya shepe, lilitua katika uso usio na hatia wa hemedy, wanafunzi wote waliokuwemo ndani ya gari hilo walitaharuki kwa kupiga mayowe hafifu ya kuwaita mama zao bila kupenda waliposhuhudia tukio hilo, walianza kupatwa na wasiwasi na mtu huyo alievamia gari yao. Hemedy kipindi hicho viganja vya mikono yake aliviweka juu ya uso wake huku akilia, aliona giza na nyotanyota kutokana na kutohimili uzito wa hilo kofi alilozawadiwa.



    “Unafikiri nimekuja kucheza na wewe hapa? Embu inuka tuondoke" Tito aliongea hivyo huku akimuinua tena, safari hii hakuleta tabu maana alihofia kipigo chengine zaidi ya hicho alichopewa.



    Akamtoa nje ya gari hiyo na kumpeleka kwenye gari walilokuja nalo, wakati yote yakiendelea, dereva na utingo wake waliwekwa chini ya ulinzi na Tobi kwa kuwanyooshea bastola, kama kawaida yake dereva wa gari hilo na leo pia alijikojolea kama alivyojikojolea jana yake. Tobi baada ya kuona windo lao wameshalitia mikononi, akaacha kuwaweka chini ya ulinzi watu hao na kuelekea kwenye gari yao kwa mwendo wa haraka, alipofika ndani ya gari alimkuta Hemedy akiwa amefungwa kamba za mikono na mdomoni amebandikwa gundi la plastiki liliweza kumdhibiti vizuri kutopiga kelele, akabaki kugugumia huku machozi yakimtoka, hakuelewa watu hao ni wakina nani na wanataka nini kwake, akabaki kusali kimoyo moyo akimuomba mungu wake amnusuru na balaa lolote litakalo enda kumtokea. Gari liliondolewa kwa kasi kubwa na kutokomea pasipojulikana.



    Dereva wa gari ya shule baada ya kuganda kwa muda mrefu akiwa bado kaduwaa kwa matukio yanayomtokea, hakuelewa anamkosi gani maana ni mara ya pili hii kufuatwa na watu asio wajua tena wakiwa ni tofauti tofauti, akafikiria kuacha kazi hiyo lakini hapo hapo akakinzana na wazo hilo, hakuwa na kazi nyengine je atakula nini endapo akiachana na kazi hiyo?, umri wake umekwenda hakuwa na uwezo wa kufanya kazi ngumu je atafanya kazi ipi nyepesi zaidi ya hiyo?.



    Akachukua simu yake na kupiga polisi, akawataarifu kwa ufupi tukio hilo na kuambiwa asubiri hapo hapo watakuja muda si mrefu, wakati huo watu walioona tukio hilo wakaanza kujisogeza eneo hilo na kumuuliza dereva maswali ya kimbea ili wapate ya kwenda kuwaeleza wasio shuhudia tukio hilo. watu hao wametungwa jina na kuitwa “redio vifua".



    Baada ya dakika kumi, gari ya polisi iliwasili eneo hilo, polisi walishuka kwa mbwembwe nyingi utafikiri walikuwa wanaenda vitani. Askari mmoja almanusura ateguke mguu kama si kuvunjika kabisa baada ya mguu wake kukwama kwenye bodi ya gari hiyo, kama sio mazoezi aliyoyachukua kipindi akiwa depo, leo hii angeaibika mbele ya raia waliokuwa eneo hilo.

    Koplo Taure alimfuata dereva wa gari la shule na kumsabahi.



    “Na leo tumekutana tena sehemu hii hii, enhee, embu nieleze kwa ufupi tukio lilivytokea" Koplo Taure alianzisha maongezi.



    “Dah!! Afande hata sijui nikueleze vipi, nahisi nina mkosi mimi sio bure, itabidi niombe ruhusa mara moja ili niende nyumbani kwetu ndipo nije kuendelea na kazi hii" Dereva alijibu kwa masikitiko utadhani ni mwenye kuonewa sana.



    “Leo wamekuja watu wengine tofauti na wale wa jana, mmoja akatuweka chini ya ulinzi mimi na utingo wangu, halafu mwengine akaingia humu ndani na kwenda kumchukua yule mtoto uliemfuata jana"



    Koplo Taure hakuamini masikio yake baada ya kusikia hivyo, akafikiria kwamba kuwa mtu anaedhania ndie huyo aliechukuliwa na watu hao wasiojulikana, ikabidi aulize vizuri, na kuhakikishiwa kuwa ndie huyo huyo mtoto aliekutana nae katika mazingira ya kifo na kujenga nae urafiki hadi kumchukulia kama mdogo wake wa kuzaliwa nae tumbo moja, mtoto anaemhusudu kuliko mtoto yoyote yule, eti ndio ametekwa na watu hao wasiojulikana.



    Ikabidi amuambie dereva awapigie simu uongozi wa shule na kuwataarifu tukio hilo ili walete dereva mwengine kwaajili ya kuwapeleka watoto hao majumbani kwao, halafu yeye aambatane na polisi hao kuelekea kituoni kwaajili ya kutoa maelezo kamili. Dereva alifanya kama alivyoambiwa na baada ya dakika tano akaja dereva mwengine na baadhi ya walimu wa shule hiyo, wakaelezwa kwa ufupi tukio lilivyotokea na baada ya hapo dereva na utingo wakachukiliwa na kuanza safari wakiwa na polisi hadi kituoni.



    Walipofika fika wakapelekwa katika chumba maalumu kwajili ya mahojiano. Koplo Taure akatoka humo na kwenda kumpa taarifa Insepekta Ganjo. Inspekta baada ya kusikia taarifa hiyo alichanganyikiwa kwasababu hata yeye pia ana mhusudu sana mtoto huyo wa marehemu rafiki yake, wakatoka wote hadi katika chumba cha mahojiano na kuanza kuwahoji watu hao.



    “Mimi nilimuona mtu akiwa amesimama barabarani huku akinipungia mkono, tukio hilo likanikumbusha la jana maana hata jana pia nilifanyiwa hivyo hivyo na watu nisiowajua kama hivi leo ilivyokuwa, na sikua na jinsi ikabidi nipaki gari pembeni ili kumsikiliza shida yake mtu huyo huku nikiwa na wasiwasi huenda ikawa huyu wa leo akawa kama yule wa jana, baada ya kusimamisha gari akaja hadi upande niliopo na kuniamuru nitulie vile vile nilivyokuwa huku akinitishia maisha kuwa nikifanya jambo lolote basi ndio itakuwa ni tiketi yangu ya kuelekea mbinguni, akamuita na na huyu utingo wangu na kutuweka pamoja wote" akameza mate na kuendelea. “walikuwa wawili, huyo mwengine akaingia ndani ya gari letu akatoka na Hemedy na kumuingiza kwenye gari lao, yule alietuweka sisi chini ya ulinzi akaondoka mbio baada ya kumuona mwenzake tayari ameshaingia kwenye gari walilokuja nalo na kutokomea zao" Dereva akamaliza kutoa maelezo yake.



    “Walielekea na njia ipi baada ya kufanya tukio?" Koplo Taure alimuuliza.



    “Walielekea na njia hii ya Tairi Tatu hadi hapo sikujua tena walipooelekea"



    “Unaweza ukaikumbuka gari hiyo ni ya aina gani na namba zake za usajili?" Koplo Taure alimuuliza.



    “Ile gari ni Alteza nyeusi na ina namba za usajili zilizosomeka T 196 YRN" Dereva alijibu.

    Koplo Taure aliposikia maelezo ya hiyo gari alishtuka, ila akajifanya kukausha ili Mkuu wake asijue mshtuko wake, akabaki kujiuliza gari hiyo aliiyona wapi? Maana hizo namba na maelezo ya gari hiyo havikuwa vigeni kwake, ni kama vile alishawahi kuliona hilo gari ila tatizo linakuja aliliona wapi hilo gari?.



    “Watu hao walikuwa na silaha wote? na zilikuwa ni zaina gani?" Koplo Taure alimuuliza.



    “Sijui kama wote walikuwa na silaha ila mimi nimemuona nayo huyo alietuweka sisi chini ya ulinzi, na pia siijui ni ya aina gani kwasababu mimi sio mzoefu na majina ya bunduki"



    “Sawa, ukiwaona unaweza ukawajua kwa sura?"



    “Ndio, hata sasa hivi wakija mimi nitawajua" Dereva alijibu kwa kujiamini.



    Hadi hapo Koplo Taure hakuwa na swali jengine la kuongeza, akamgeukia mkuu wake na kumkuta akiwa na sura ya mfadhaiko, haikueleweka imesababishwa na mawazo ya kutekwa kwa Hemedy ama ni vipi? Inspekta Ganjo aliinuka bila kusema chochote na kutoka ndani ya chumba hicho akimuacha Koplo Taure asijue afanye nini na watu hao, na yeye hakuwa na jinsi. Akawaruhusu waondoke huku akiwaambia kuwa wakiihitajika kituoni hapo wasisite kuja kwaajili ya kufanya uchunguzi mwengine kama kutahitajika kufanya hivyo, wakaaga na kuondoka zao.



    Koplo Taure akakusanya karatasi za maelezo aliyokuwa akiyaandika na kuziweka katika faili, akatoka na kwenda katika ofisi yake ilipo na kukiendea kiti kilichokuwa nyuma ya meza kubwa iliyo kuwa na makabrashi machache yaliyopangiliwa vizuri upande wa kulia juu ya meza hiyo, akakaa kwenye kiti na kuanza kutafakari maelezo aliyopewa na dereva wa gari ya shule.



    “Ile gari ni Alteza nyeusi na ina namba za usajili zilizosomeka T 196 YRN"

    “Hii gari sio ngeni katika fikra zangu, ila sasa sijui nimeiyona wapi?" akapiga kichwa chake kwa kofi hafifu kidogo ili kurejesha kumbukumbu ya kile anachokifikiria, akalaza kichwa chake kwenye meza kwa sekunde kadhaa, alipokuja kukiinua sura ilipambwa kwa tabasamu, “Ni vijana wa Mr Bakari Haneni ndio wenye gari hii"

    Mawazo yake yalikatika baada ya kuingia mtu humo ndani, mtu huyo alipiga salut na kumuambia kuwa anahitajika na Inspekta katika osifi yake, akatoweka baada ya kufikisha taarifa hiyo akimuacha mtaarifiwa akijizoa zoa kwenye kiti alichokuwa amekaa, akainuka na kuanza kuelekea ilipo ofisi ya mkuu wake.



    “Ndio mkuu" Koplo Taure aliongea hivyo huku akiwa amesimama mbele ya mkuu wake. Akapewa ishara ya kukaa na yeye akafanya hivyo.



    “Umepata wazo gani kuhusiana na hii kesi ya kutekwa kwa Hemedy?" Inspekta Ganjo alimuulizia huku akimuangalia kwa macho makavu yasio na mzaha hata kidogo.



    “Mkuu, naomba uniachie kwa siku ya leo, kesho nitakupa jibu"Koplo Taure aliongea kwa unyenyekevu, maana alishajua kuwa akijibu vibaya huenda yakamkuta makubwa ambayo hakuyatarajia, alijua kuwa mkuu wake ni mwenye kumhusudu sana huyo mtoto.



    “Sawa, na vipi kuhusu ule mshtuko wako pindi ukiwa unamuhoji yule dereva wa gari ya shule alipokutajia namba za gari iliyo mteka Hemedy?"

    Koplo Taure hakutarajia kuwa mkuu wake alimuona pindi akishtuka wakati wa mahojiano yake na dereva, alidhani mshtuko wake aliuficha mbele ya mkuu wake kumbe ulionekana dhahiri.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mkuu, yale maelezo yake aliyotoa yule dereva wa gari ya shule kuhusu gari iliyomteka Hemedy, ni kwamba hiyo gari mimi naijua na hata watu wake pia nawajua, ila sina uhakika kuwa ndio watu walio mteka Hemedy"



    “Watu hao ni wakina nani?"



    “Ni vijana wa Mr Bakari Haneni" Koplo Taure alijibu.



    “Na kwanini umesema huna uhakika kuwa ndio watu waliomteka Hemedy?"



    “Kwavile bado sina usibitisho kwahilo, ila mara nyingi nimewaona wao ndio wanaiendesha hiyo gari"



    “Sawa, nadhani umebakisha wiki moja ili unipe ripoti ya uchunguzi wako ulipofikia kuhusu kupotea kwa watoto mitaani. Sasa basi, naomba kesi hizo uziambatanishe na hii ya kutekwa kwa Hemedy, ndani ya wiki hii nataka uniletee majibu yatakayo niridhisha"



    “Sawa, Mkuu"

    Koplo Taure aliruhusiwa kuondoka katika ofisi hiyo ya mkuu wake, akaelekea moja kwa moja katika ofisi yake ama yao na kukiendea kiti chake na kukaa hapo, macho akayaelekeza juu ya dari na kuangalia huko huku akiwaza afanye nini ili apate ufumbuzi wa hilo jambo.



    * * * *



    Majira hayo, yalimkuta Mrutu akiwa dukani kwake, alikuwa akiongea na simu, akili yake na sikio lake moja, vilikuwa amevipa utulivu ili kusikiliza kile anachoambiwa kwenye simu hiyo, mara ghafla akaanza kubadilika, alionekana kama mtu anaeanza au aliechanganyikiwa, maana aliongea na simu hiyo huku akitetemeka, alipomaliza kuongea na simu, akamuachia duka msaidizi wake na yeye kutoka nje na kuiyendea gari na kuingia humo, akalitoa gari hilo kwa mwendo wa kasi ya wastani, akishika barabara ya mabanda ya papa, akanyoosha na barabara hiyo hadi alipo ipata Duga Mwembeni, akakunja kushoto na kushika barabara ya Tanga Beach, alipofika Mikanjuni Transifoma akakunja kulia na kuitafuta Tairi Tatu, alipofika hapo akakunja kushoto, akatembea kidogo hadi katika shule ya EBENENZER ENGLISH MEDIUM SCHOOL, alipofika hapo akapaki gari pembeni na kuingia ndani ya shule hiyo, akanyoosha moja kwa moja hadi katika ofisi ya mkuu wa shule kwa mwendo wa haraka.



    “Karibu Mr Mrutu, karibu ukae" alikaribishwa na sauti ya mwana mama aliekuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguuka, mwili wake ulikuwa upo ndani ya suti ya kike ya gharama, alipachika miwani ya macho huku mkononi akiwa ameshika kalamu anaizungusha zungusha.



    “Asante mwalimu" Mrutu alisema hivyo huku akikaa kwenye kiti.



    “Habari zako?" Mwalimu alianzisha maongezi kwa salamu.



    “Salama tu. Mwalimu naomba unipe hiyo taarifa vizuri, ilikuaje kuaje?" Mrutu alimuuliza mwalimu huyo huku akimtolea macho huku mikono yake iliyokuwa juu ya meza ikitetemeka.



    Mwalimu huyo alimuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akamuambia“Ni hivi, mtoto wako Hemedy Muheshimiwa Bhachu, ametekwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari ya shule wakati akipelekwa nyumbani na wenzake"



    “Kwahiyo hamjui amepelekwa wapi?" Mrutu aliuliza swali la kipumbavu. haikujulikana ni kwasababu Hemedy ametekwa au ni uoga wa kutekwa kwa mtoto huyo.



    “Kiukweli hadi sasa hivi hatujui lolote, ila tumewaachia polisi wakifanya uchunguzi, naamini kwa vile jambo hili limefika polisi basi tutampata tu mwanao, na...." Alikatisha maneno yake baada ya kuona simu ya Mrutu ikiita.

    Mrutu baada ya kuitoa simu yake mfukoni,aliangalia ni nani anaempigia, baada ya kulisoma jina akapokea simu huku akitetemeka zaidi. Alisikiliza kwa sekunde kadhaa. Kisha akaropoka kwa sauti kubwa.



    “Nooooo!! Msimfanyie hivyoo!!"







    Simu ilikatwa na kumuacha Mrutu akitetemeka huku akipambwa na jasho lililokuwa likimtiririka, ni dhahiri kwamba kiyoyozi kilichokuwa kikifanya kazi ndani ya ofisi hiyo, hakikumsaidia kwa lolote, maana jasho lilizidi kumtiririka tu pasi na kukoma.



    “Vipi Mr Mrutu?" Mwalimu alimuuliza hivyo baada ya kuiyona hali ya kuchanganyikiwa iliyomtokea ghafla mtu huyo.



    “Mwalimu acha mimi niende nitakutafuta baadae"

    Mrutu aliinuka bila kusubiri jibu lolote kutoka kwa mwalimu huyo, akatoka mbio mbio hadi ndani ya gari na kutulia akimuacha mwalimu akiwa mdomo wazi pasi na kujua nini aongee. Akatoa simu na kuipiga namba aliyotoka kuongea nayo muda si mrefu.



    “Haloo" alianza kuongea baada ya kuona simu imepokelewa.



    “Sikiliza Mrutu, tulikupa muda mwingi wa kurudisha pesa zetu, ila muda wote huo umeuchezea, kwasasa hivi tupo njiani tukimpeleka mwanao maskani, tukifika huko tutakupigia simu ili uongee na mkuu mwenyewe" sauti ya upande wa pili iliskika ikiongea hayo.



    “Jamani, msifanye hivyo mimi pesa zenu nitamirudishia, ila mwanangu muacheni"

    Ni kweli Mrutu aliongea kwa uchungu mkubwa na alimaanisha alichoongea, kama ingekuwa ana roho ile ile aliyokuwa nayo mwanzo basi angeshukuru maana ingekuwa wamerahisishiwa kazi ya kumpoteza mtoto huyo, ila kwasasa roho yake imebadilika na kujikuta hataki Hemedy adhurike kwa chochote kile.



    “Sisi tumetumwa tu kufanya hivi, hatuna maamuzi mengine, kama unapenda huyu dogo asidhurike kwa chochote, subiri tukifika ukiongea na mkuu ndio utajua ni jinsi gani ya kumshawishi ili amuachie huyu dogo"

    Simu lilikatwa na kumuacha Mrutu akitokwa na chozi kwenye jicho lake moja huku jengine likijiandaa kufanya hivyo maana tayari lilishaanza kutoa ishara hiyo.



    Mrutu hakujua afanye nini kwa wakati huo, akabaki akitetemeka na jicho la pili tayari lilishaanza kufanya kama vile lilivyofanya lile jengine, akajikuta bila kupenda akianza kulia, alilia kwa dakika kadhaa kisha hapo akanyamaza na kuchukua simu yake ili ampigie Mata.



    Simu ilipopokelewa akamuuliza yupo wapi kwa wakati huo, akaambiwa kuwa ndio anajiandaa kutoka kazini kwake, akamuambia kuwa yeye atamkuta nyumbani kwake, alipomaliza kuongea na mtu huyo, akampigia na Moto na kumuambia wakutane nyumbani kwa Mata, baada ya hapo akakata simu.



    Hakujua atawaambia nini, maana watu hao hawakujua kuwa mwenzao anafanya biashara nyengine ya kuuza madawa ya kulevya na hapo ana UHASAMA na tajiri wake anaemuuzia madawa hayo. Akapanga kuificha ishu hiyo, hakutaka wenzake wajue kwamba yeye anafanya biashara hiyo, akapanga kuwaeleza kilichomkuta Hemedy ila atageuza maneno ili aonekane yeye hana hatia hadi kupelekea mtoto huyo kutekwa, ila hata hivyo akajua akiwaelezea hayo, basi wenzake watafurahi kwasababu wao wenyewe walikuwa wanataka wamuue mtoto huyo, kwahiyo hapo itakuwa wamerahisishiwa kazi.



    “Nitajua huko huko nini chakufanya, siwezi kuikosa damu yangu"



    Alijiwazia mwenyewe huku akiiwasha gari yake, na kuondoka mahala hapo na kuelekea nyumbani kwa Mata. Dakika kumi na tano, zilitosha kabisa kumfikisha sehemu hiyo, akapaki gari lake nje ya nyumba na kushuka humo. Moto nae alikuja dakika hiyo hiyo na kusalimiana, wakatafuta sehemu ya kukaa wakiwa wanamsubiri mwenyeji aje, baada ya dakika kadhaa, Mata nae alifika hadi hapo, akashuka na kuwapa salamu, akaenda kufungua geti na kuingiza gari yake ndani, Mrutu yeye hakufanya hivyo maana alijua hawezi kukaa humo ndani kwa muda mrefu, wakaingia wote hadi subuleni na kukaa kwenye masofa yaliyokuwepo mahali hapo.



    “Enhee!! Tuambie unajipya gani mwendhetu?" Mata alianzisha maongezi.



    “Hemedy ametekwa" Mrutu alijibu kiufupi.



    “Ametekwa na nani?" Moto aliwahi kuuliza.



    “Siwajui na ametekwa leo wakati wakiwa ndani ya gari la shule wakirudishwa nyumbani"



    “Kwahiyo ametekwa na wendhake?" Mata aliuliza.



    “Hapana, wamemteka pekeake, yani walivyosimamisha gari la shule, wakamchukua yeye na kuondoka nae"



    “Mimi namuombea wakamuue kabisa huko huko walipompeleka" Moto aliongea hivyo huku akiurudisha mwili wake na nyuma kuegemea sofa alilokalia, Mrutu alimkata jicho la chuki hadi wenzake hao wakamshangaa.



    “Vipi kaka, mbona unamuangalia jamaa kwa jicho hilo?" Mata alimuuliza baada ya kuona hajamuelewa kwanini amemkata jicho wakati ameongea kitu ambacho wao wenyewe walikuwa wanataka wakifanye kwa mtoto huyo. Sasa ni vipi mwenzake alipoongea hivyo yeye amemuangalia kwa jicho baya la kuchukizwa na kauli hiyo.



    “Tatizo nyie hamjui mnachokiongea ndio maana mnasema hivyo"



    “Ndio utuambie thatha ili tujue" Mata aliongea.



    “Hao watu waliomteka huyo dogo, wanataka pesa ili wamuachie" Mrutu aliongea kauli ambayo ili wafanya wenzake wacheke sana kwa kumshangaa mwenzao.



    “Kwahiyo hicho ndicho kilichokufanya hadi ukaniangalia kwa jicho baya namna hiyo hadi ukanifanya niogope? Sasa hapo tatizo nini, si unawaachia tu wamuulie tu huko huko maana hata hivyo itakuwa wameturahisishia kazi ambayo kila siku sisi tulikuwa tunatamani tuimalize" Moto aliongea hivyo huku akimalizia na kicheko cha furaha. Hakujua tu jinsi gani Mrutu anachukizwa na kauli zake, akatamani hata kumrukia na kumpiga makofi mawili ila akazizuia hasira zake mbele ya mtu huyo anaeongea maneno yanayo mchoma.



    “Halafu kuna jambo nataka niwaambie" Mata aliongea hivyo na kuwafanya wenzake wamuangalie, alipoona wote wapo kimya wanamsikiliza yeye akaendelea.



    “Ni hivi, leo nimeenda mahakamani kufungua kethi ya madai, ndipo wakanipa karatathi hii hapa(akaitoa kwenye bahasha na kumpa Mrutu) wameniambia wiki ijayo ndio kethi hii itathomwa" Mrutu aliwaambia hivyo wenzake, Moto nae akaichukua karatasi hiyo na kuisoma.



    “Uliwaambiaje ulipofika mahakamani?" Mrutu alimuuliza.



    “Mimi niliwaambia kuwa nimekuja kufungua kethi ya kudai mali dhangu, wakaniuliza nadai kwa nani, nikawaeledhea kwa ufupi kuwa namdai marehemu Mheshimiwa Bhachu, walishangaa na kutaka ushahidi, mimi nikawatolea ile kopi ya karatathi aliyoandika marehemu ile siku tuliyomuua, hapo ndipo waliponipa karatathi hiyo na kuniambia watampelekea barua mthimamidhi wa mali hizo ambae ni wewe muda wowote kuanzia muda huo"



    “Kwahiyo unataka kuniambia wiki ijayo tunachukua mali zetu" Moto aliongea hivyo huku akiwa na tabasamu lililo karibia kucheka, inavyooneka taarifa hiyo imeusuuza kabisa moyo wake.



    “Ndio,(akamgeukia Mrutu na kumuambia) kuhuthu huyo dogo wewe usimuwadhie maana hata thithi tulikuwa tunataka tumuue ila hao watu bila kujua wameturahithishia kadhi, wewe achana na huyo dogo wiki ijayo tunachukua mali dhetu halafu tunagawana na kila mmoja anakuwa tajira maana mali hidho ni nyingi thana"



    “Acheni basi mimi niwaage nielekee nyumbani" Mrutu alisema hivyo huku akiinuka.



    “Hakuna shaka, wewe nenda tu" Mata alisema hivyo na Mrutu akaondoka.



    “Unajua mimi simuelewi kabisa huyu Mrutu" Moto alimwambia hivyo baada ya kuona Mrutu ameshaondoka.



    “Achana nae, lile ni wenge tu la kutekwa kwa yule dogo, ila atatulia tu, kwahiyo wewe usiwe na shaka nae"



    * * * *



    Gari ya kina Tito, iliingizwa kwenye lango la ngome ya Mr Bakari Haneni, ngome hiyo ilionekana kulindwa kwa ulinzi mkali, walinzi hao walijua nini wanafanya maana walikuwa makini kuliko umakini wenyewe, walikuwa wameshika silaha kali kali huku wakiranda nazo kila sehemu kwa mtindo wa kupishana, yani huyu akienda huku basi mwingine anaenda kule alipotoka mwenzie.



    Gari hiyo ilipakiwa sehemu na kushuka watu hao huku wakiwa wamemshika Hemedy, walimfungua kamba na gundi walilomuweka mdomoni na kumuacha awe huru kutembea mwenyewe, hofu, wasiwasi, uoga na kutetemeka vyote hivyo vilimshika baada ya kuona eneo hilo lilivyo, aliona watu waliokuwa makini muda wote wakitembea huku na huko huku wakiwa wameshika bunduki kubwa kubwa, yeye mambo hayo alizoea kuyaona kwenye picha za video za kizungu.



    Aliongozwa kutembea kuelekea ndani ya jengo hilo la zamani, akiwa na uoga mwingi alienda tu bila kupenda maana alihofia kuleta tabu zitakazo sababishia kupokea kipigo kingine kutoka kwa watu hao wasio taka kucheka hata mara moja, hata hivyo alijua hata kama atafanikiwa kuwakimbia watu hao wawili pia asinge weza kutoka ndani ya ngome hiyo inayilindwa kwa ulinzi mkali, akapanga kutii kile atakacho ambiwa ili aone mwisho wake.



    Walienda ghorofa ya pili ya jengo hilo na kuingia katika chumba kimoja wapo ambacho Mr Bakari Haneni alikifanya kama ni ofisi yake akiwa sehemu hiyo, waliingia ndani ya chumba hicho na kumkuta bosi wao akiwasubiri, walimuweka Hemedy mbele yao huku wao wakiwa wamesimama nyuma yake.



    “Safi sana vijana wangu, mtoto mwenyewe ndio huyu?" Haikueleweka ameuliza hivyo kwa mamlaka aliyokuwa nayo au alitaka uhakika zaidi maana hakukuwa na mtoto mwengine aliyeagiza aletwe zaidi ya huyo.



    “Ndio mkuu" walijibu wote kwa pamoja.



    “Sawa, mumewasiliana nae yule mjinga?"



    “Ndio mkuu, tumempa tu taarifa ya kuwa mwanae tunae sisi kwahiyo yeye asihangaike kumtafuta"



    “Sawa, embu mpigie tena uongee nae"

    Tito akatoa simu na kumpigia Mrutu, alipoona inaita akaiweka sauti kubwa ili wote wasikilize kitakachoongelewa hapo.



    “Haloo" ilisikika sauti ya Mrutu kwenye simu, Tito alimuangalia bosi wake na kupewa ishara ya kuendelea kuongea.



    “Sikiliza Mrutu, tumekupa muda mwingi wa kurudisha pesa zetu ila wewe umeuchezea kwahiyo tutakuletea maiti ya huyo dogo uizike mwenyewe pindi atakapo kufa kwa kuathiriwa na madawa ya kulevya, maana ataenda kusaidiana na wenzake kufanya kazi ya kuyafunga madawa hayo" Tito aliongea hivyo.



    “Hapana jamani msifanye hivyo, mimi pesa zenu nitamirudishia wiki ijayo, haki ya mungu vile naapia, nitazirudisha kweli"



    “Mrutu umechelewa sana kwa hilo, subiri tu nikupe uagane na mwanao vya mwisho"

    Akamuwekea simu Hemedy karibu, Hemedy alianza kulia huku akimtaka baba yake amsaidie kumtoa mikononi mwa watu hao.



    “Hemedy usilie mwanangu, nitakutoa tu kwa watu hao, subiri nifanye mpango niwape wanachotaka, utatoka tu"



    Ni dhahiri kilio cha Hemedy kilimfanya Mrutu ajione ni mwenye hatia sana kwa jambo hilo ndio maana akaongea kwa uchungu mkubwa, akimpa moyo kuwa ataachiwa muda si mrefu japo kuwa hakuwa na uhakika wa jambo hilo, alijua kuwa ukiingia katika ngome hiyo si rahisi kutoka ukiwa na uhai wako, labda yatoke majivu ya mwili pindi ambapo utakapokuwa mwili umechomwa moto na majivu hayo yatoke kwa njia ya kupeperushwa na upepo.

    Mr Bakari Haneni alimpaishara Tito aliekuwa bado ameshika simu iliyokuwa ikitoa sauti ya Mrutu, naye aliiyelewa ishara hiyo na kuirudisha simu hiyo karibu yake.



    “Tunakupa siku Nne za kurudisha pesa zetu na zikipita hizo siku tutakuletea maita ya mtoto wako hadi mlangoni kwako ikiwa ipo katika hali ya kupendeza machoni mwako, maana tutavibadilisha viungo vyake nikimaanisha miguu tutaishonea sehemu za mikono na mikono tutaishonea sehemu za miguu huku kichwa chake tukikitenganisha na kiwiliwili, naamini hali hiyo utaipenda, na nina kusisitiza tu, ole wako uwaambie polisi chochote, ukifanya kinyume na maagizo tunayokupa basi jiandae kupokea mwili wa huyu dogo kisha utaupokea na mwili wako mwenyewe ukiwa hauna uhai, nikutakie kazi njema" Tito aliongea kauli za kutisha kiasi ambacho Hemedy alikuwa akitetemeka kwa uoga kama simu mbovu iliyoweka mtetemesho pindi ikiita, hakutaka kusubiri atajibu nini alikata simu na kusubiri maelekezo mengine kutoka kwa bosi wake.



    “Mpelekeni kwa IBILISI akampumzishe, inavyooneka amechoka sana huyu mtoto"



    “Sawa mkuu" walijibu na kumtoa Hemedy kwenye chumba hicho na kumpeleka kwenye chumba kingine kilichofanana na chumba cha kulalia ila humo hakukuwa na kitanda zaidi ya godoro lilowekwa chini ya mkeka huku juu ya godoro hilo kukiwa na mtu alielala juu yake kichwa na kiwiliwili amevielekeza upande wa pili.



    “Ibilisi tumekuletea mwanadamu umfundishe maovu ila kwa sasa bosi amesema apumzike kwanza" Tito aliongea hivyo na kufanya huyo mtu alietambulika kwa jina la Ibilisi ageuze shingo yake na kule sauti hiyo ilipotoka.

    La haulaa!!!! Mtu huyo alifanana kabisa na jina hilo aliloitwa kutokana sura lake jeusi utadhani amepaka oili chafu usoni, alitisha kumtazama kutokana sura lake lilivyobaya, almanusura Hemedy afe kwa mshtuko uliompata baada ya kuona sura la jitu hulo lililofananiana na mazombi yale ya kwenye picha ya WRONG TURN. Kwahakika hata mimi muandishi na kiri hilo kwamba jitu hilo lilikuwa na sura ambayo sikuwahi kuiyona katika ulimwengu huu, naamini kwamba angeamua kuekti muvi za kutisha angepiga hela kuliko kawaida kutoka na jinsi alivyo, subiri nikupe picha kidogo jinsi alivyo, alikuwa na ngozi nyeusi mithili ya giza la kaburini japo kuwa sijawahi kufika huko, sura lake lilikuwa ni baya la kuogofya huku likipambwa na macho mekunde mithili ya nyanya mbivu, kichwani hakuwa na nywele hata moja, naamini mtoto aliezaliwa leo akimuangalia anaweza kupoteza maisha bila ya kutamka neno lolote kwa ubaya wa sura hilo, alitisha, aliogopesha, kwa kumuangalia tu sura yake ilitangaza roho mbaya aliyokuwa nayo.



    Baada ya kumleta Hemedy kwenye chumba hicho, wakaondoka huku wakimuacha Hemedy akiwa bado ameganda akimuangalia mtu huyo wa kutisha, sio kwamba alikuwa akimuangalia kwa kupenda, la hasha! Bali alikuwa bado amepigwa na butwaa kwa kuona zombi mtu laivu bila chenga mbele yake, jitu hilo likaanza kumsogelea huku likimtolea tabasamu la karaha lililozidi kuongeza ubaya wa sura lake, tabasamu hilo ndilo lililomgutusha Hemedy aliekuwa bado ameduwaa, tabasamu hilo lilipambwa na meno ya njano kama unga wa binzari, kwahakika hakufaa hata kukaribia kutabasamu maana ndio alizidi kutisha hadi kuwashinda wale walioekti muvi za kutisha za kizungu, akamsogelea Hemedy hadi karibu kabisa, Hemedy alinza kukohoa sana baada ya harufu ya mdomo ya jitu hilo kumuingia puani mwake...







    JITU hilo lilicheka sana huku likirudi nyuma kidogo baada ya kuona Hemedy ameshindwa kuvumilia harufu iliyotoka mdomoni mwake, ilielekea alifanya kusudi kabisa kufanya vile maana alirudi nyuma ili kumpa Hemedy apate nafasi ya kupata hewa nzuri.



    “Karibu sana dogo, karibu kitandani upumzike" liliongea kwa sauti baya ya kushangaza, sauti yake ilifanana kabisa na zile spika kubwa za muziki zinazowekwa kwenye klabu (Bass) na kufanya Hemedy azidi kuogopa kwa kuhisi kuwa amekutana na malaika mtoa roho.



    “Naona unanjaa sana suburi nikakuletee chakula" aliongea hivyo baada ya kumuona mtu anaemuongelesha amekaa kimya pasi na kuongea chochote. Aliinuka pale kwenye lile godoro na kufanya Hemedy aone kitu chengine cha kustaajabisha kwa mtu huyo. Alikuwa ni mrefu kupita kawaida na mwili mkubwa uliyojengeka kimazoezi. Alitoka ndani humo na kumuacha Hemedy pekeake, safari hii alikaa chini kwenye pembe ya ukuta miguu akiwa ameikunja na mikono yake akiwa ameifumbata kwenye magoti yake huku kichwa chake amekilaza juu ya mikono yake, alikuwa analia huku akimuita mama yake mzazi, hakujua amefanya nini hadi kutekwa na watu hao, akaanza kumfikiria baba yake mdogo ana nini na watu hao hadi kudaiwa pesa za watu na kupelekea akachukuliwa yeye, aligutushwa na sauti ya m'buruzo wa kitu chini ya sakafu ya kwenye chumba hicho, akainua kichwa ili ajue ni nini hicho, sura yake ilipambwa na machozi yaliyotiririka mashavuni na kuangukia juu ya sakafu hiyo, mbele yake alikuta sahani ya chakula imewekwa na lile jitu la kutisha, akakiangalia chakula hicho kilikuwa ni ugali na samaki mkubwa aliekaangwa vizuri pembeni pakiwa na mchuzi wa samaki mwingine aliechanganywa humo, macho yake akayapeleka kwa jitu hilo la kutisha na kulikuta likitoa tabasamu la kuogofya Hemedy akayatoa macho yake haraka kwa jitu hilo maana aliiliogopa sana, jitu hilo halikusema kitu likatoka ndani humo na kumuacha Hemedy mwenyewe.



    Alibaki akikiangalia hicho chakula, japo kuwa alikuwa na njaa ila hakutaka kula akihofia maisha yake huenda kimewekwa sumu, aliinuka pale alipokaa na kwenda kwenye mlango wa chumba hicho akijaribu kuufungua na kukuta ukiwa umefungwa kwa nje, akarudi pale alipokaa mwanzo na kukaa mtindo ule ule na kuanza kulia akidai anaonewa kwahiyo anataka uhuru wake.



    * * * *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mrutu alikuwa amekaa sebuleni kwake majira ya usiku, akiwaza ni jinsi gani atafanya ili amtoe mtoto huyo asiye na hatia mikononi mwa wale mabaazazi, hakujua atafanya nini, akapanga kuwashirikisha polisi ila aliogopa vile vitisho alivyopewa, aliogopa kuupokea mwili wake ukiwa hauna uhai kama alivyoambiwa na pia aliogopa kuupokea mwili wa mwanae ukiwa umebadilishwa viungo, vyote hivyo vilimchanganya, akawa amebaki hajui nini chakufanya ili balaa hilo lipite, ‘nitauza duka langu kisha niwarudishie pesa zao' akawaza afanye hivyo, ‘hapana siuzi duka, ila nitakopa benki kisha niwarudishie pesa zao halafu tukishagawana hizo mali, naenda kuwalipa benki pesa zao, yes, hiyo ndio njia nzuri zaidi' alitokwa na tabasamu la matumaini lililo fanya ajisikie amani ya moyo.



    ila tabasamu lake lilizima ghafla kama mshumaa upulizwapo na upepo, baada ya kukumbuka sehemu ambayo Hemedy amepelekwa.



    “Katika ngome hii si rahisi mtu asie husika kuingia na kutoka akiwa na uhai wake, ila kwako imekuwa bahati sana mkuu kukuamini na kuruhusu utoke ukiwa na uhai wako, wote wanaoingia hapa huwa hawatoki na mwisho wao ni kufa kisha miili yao kwenda kuchomwa moto kwenye shimo lile paleee"



    Aliyakumbuka maneno hayo aliyowahi kuambiwa na Tito kwa mara ya kwanza kuingia ndani ya maskani(ngome)ya Mr Bakari Haneni, kipindi hicho alikuwa anasindikizwa kutolewa katika ngome hiyo ndipo alipoambiwa maneno hayo.



    ‘Nitafanya nini?' ndio swali lililotawala kichwani kwake kwa wakati huo, ile tabasamu lilikuwa tayari limepotea kitambo usoni kwake, uso wake ulipambwa na mashaka yalio changanyikana na uoga, ukweli ni kwamba, Mrutu alikuwa akijuta kwa kila kosa alilowahi kulifanya katika maisha yake, hakuwahi kufikiria kuwa kazi hiyo ingeweza kuja kumuadhibu kwa mawazo kiasi hicho.

    ‘Nitawarudishia pesa zao halafu ndio nitajua nifanye nini pindi wakigoma kumtoa mwanangu' alihitimisha mawazo yake na kauli hiyo, akaondoka sebuleni hapo kuelekea chumbani kwake kulala huku akiacha Tv na taa ya hapo vikiwaka vyote kwa pamoja.



    Siku iliyofuata. 12:42 Asubuhi. Mtaa wa Majengo Msikitini.



    Koplo Taure aliweka kambi kuwinda windo lake, hiyo sehemu aliyokaa hapakuwa mbali na nyumba na kina Tito, aliweza kuona kila kitu kwa nje kwenye nyumba hiyo, alipanga siku hiyo awafuatilie tena ili ajue wanapoenda baada ya kuamka, ila bahati haikuwa kwake, kwasababu alisubiri sana hadi akachoka, akiangalia saa yake ya mkoni ilimuonyesha ni saa tatu na nusa asubuhi na yeye alikuwa hapo tangia saa kumi na mbili asubuhi, akahisi labda watu hao hawakuwa wamelala kwenye nyumba hiyo au watakuwa wamechoka sana kutokana na sababu zao wanazozijua wao wenyewe, akakata tamaa na kuwasha gari lake na kuelekea kituoni, kwa vile mtaa huo na kituoni kwake hapa kuwa mbali, ili mchukua dakika nne tu kufika kituoni.



    Muda ambao Koplo Taure anafika kituoni, ndio muda ambao wakina Tito wanatoa gari lao kwenye nyumba yao na kuelekea kwenye mjengo wa bosi wao ulioko mtaa wa Raskazoni, walipofika waliingiza gari ndani ya mjengo huo na kuweka gari kwenye maegesho, wakashuka na kuelekea juu kwenye ghorofa ya pili ya jengo hilo ambapo bosi wao alikuwa amekaa kwenye kibaraza cha sehemu hiyo akiangalia mandhari ya bahari ya hindi.



    “Karibuni vijana wangu" aliwakaribisha wakae kwenye viti vyengine vilikuwa sehemu hiyo na kuwagiza wahudumu walete chai ili wanywe kwa pamoja, baada ya dakika kadhaa ililetwa chai ya nguvu iliyo ambatana na vitafunwa ghali, kila mmoja akashika nafasi yake na kuanza kunywa chai hiyo. Baada ya muda walimaliza na wafanyakazi wa nyumba hiyo wakaondoa vyombo vilivyotumika hapo na kuwaletea vinywaji laini ili kusindikiza maongezi ya watu hao.



    “Mnjaua muda wote sikunywa chai, nilipanga niwasubiri nyie ili tunywe wote maana sikuwahi kushiriki chakula cha pamoja na nyie hata siku moja"

    Waliongea maongezi mengi ya kazi yao hiyo ambayo hayakuwa na ulazima kuyaandika hapa. Baada ya kuongea sana Tito akaomba kumuuliza swali bosi wake, akaambiwa aulize tu asiwe na shaka.



    “Hivi wewe familia yako iko wapi? Maana sijawahi kumuona mke wako wala mtoto wako humu ndani, kila nikija nakuta wafanya kazi na walinzi tu wajengo hili" Tito aliuliza.



    “Aaaa!!! Mimi katika maisha yangu nilibahatika kuoa mwanamke mmoja tu miaka kumi na tatu iliyopita, tuka kaa mwaka mmoja ndipo mke wangu akashika mimba, baada ya miezi tisa mke wangu alijifungua watoto wawili mapacha wa jinsia tofauti, mkubwa alikuwa ni wakiume na mdogo ni wakike, watoto hao tukawapa majina wa kiume tulimuita Ata na wakike tulimuita Atu, baada ya kufikisha miaka saba watoto hao nikawaamisha nchi kwenda kusoma shule na hapo hapo wafunzwe mapigano, na watarudi hapa nchini wakiwa na miaka ishirini na tano, kwa sasa wanamiaka kumi na mbili. Nataka nifanye makubwa sana hapa nchini hapo baadae wanangu wakirudi na ndio maana nimewapeleka Urusi kwenda kusoma na kufundishwa kupambana, najua kwa miaka watakayo kaa huko, wakirudi hapa watakuwa wameiva kwa mapigano ya ngumi na kulenga shabaha, hahahha!!! Tanzania Tanzania, nchi ya kwetu hii, lazima miaka ijayo niwe tajira sana zaidi ya hapa nilipo kupitia watoto wangu" Alihitimisha kutoa historia fupi ya familia yake na mipango yake mibaya ya baadae juu ya nchi hii.



    “Na mke wako je? Mbona sijawahi kumuona hata siku moja au ameenda na wanae kuishi nao huko huko Urusi?" Tito aliumuuliza.



    “Mke wangu nilimuua mwenyewe kwa mikono yangu nilipokuja kumfumania na mlinzi wangu mmoja wakifanya mapenzi chumbani kwangu, yeye nilimnyonga kwa mikono yangu na huyo mlinzi nilimuua kifo cha kistaarabu sana, yeye nilimkata kata kila kiungo huku akiwa na uhai wake, halafu ndio nikamchinja na nyama zake nikazipika supu nikawapa mbwa wangu wafurahie. et jamani hicho si ni kifo cha kistaarabu kabisa?"



    Haaaa!!! Yani kumkatakata mtu kiungo kimoja kimoja akiwa mzima halafu kumchinja na nyama zake kuzipika supu na kuwapa mbwa, hicho ni kifo cha kistaarabu?

    Nilistaajabu sana na sio mimi tu hata Tito na Tobi pia walistaajabu ila waliitikia tu kwa kuwa bosi wao ndio amewauliza swali hilo.



    “Kwahiyo sasa hivi umeamua kuishi mwenyewe tu?" Tobi alimuuliza.



    “Ndio sitaki tena kuongeza familia zaidi ya wanangu tu, kwasababu hao ndio najua watakuja kunisaidia baadae"



    “Ila lakini watoto wako umewapa miaka mingi sana ya kuishi huko nje, huoni kama wakirudi watakuwa wamekusahau baba yao?" Tobi aliuliza.



    “Hapana, tuna wasiliana sana kwenye mtandao wa Skype kwahiyo siwezi kuwasahau wala wao hawawezi kunisahau mimi"

    Waliendelea na maongezi yao hadi pale wakina Tito walipotaka kuondoka nyumbani hapo kwa bosi wao, wakataka kuelekea baa kwenda kunywa.



    “Hakuna shaka nyie nendeni ila mimi sasa hivi naelekea maskani kuna mambo naenda kuyaweka sawa" Mr Bakari Haneni aliongea hivyo huku akipeana mikono na watu wake.

    Wakatoka na na kuingia kwenye gari yao, wakatoka nje ya nyumba hiyo na kuelekea walipopanga kwenda, walipofika Toyota, wakaona kuna gari nyuma yao ikiwaungia, walipoliangalia vizuri wakaligundua ni gari ambalo sio mara ya kwanza kuwafuatilia.



    “Unajua nini Tito, leo tubadilishe baa, tuelekee Tanga Pazuri, kule ni mbali, hapo ndipo tutakapopata uhakika zaidi kwamba ni kweli hili gari linatufuatilia sisi au laa"



    Tito aliliunga mkono wazo la Tobi na kuelekea baa ya Tanga Pazuri iliyokuwa maeneo ya Kwaminchi, kuna sehemu walikuwa wakiangalia nyuma kuliangalia hilo gali hawakuliona na sehemu nyengine waliliona, wakajua huyo anaewafuatilia alijua wapi wanaelekea, ndio maana huyo mfuatiliaji alikuwa akiwafuatilia kwa kuwachanganya.



    Baada ya mwendo mrefu kiasi walifika kwenye baa hiyo na kupaki gari lao nje ya baa hiyo na wao wakaingia ndani, wakatafuta sehemu iliwawezesha kuona nje ya baa hiyo, waliliona gari iliyokuwa ikiwafuatilia ikipaki mbali kidogo na wao walipopaki gari yao, ila hawakuona mtu yoyote alieshuka kwenye gari hiyo.



    “Itakuwa anatutega ili tuondoke aendelee kutufuatilia, si unaona hataki kushuka" Tobi aliongea hivyo huku akiangalia gari hiyo.



    “We subiri tu, asiposhuka tuta mfuata pale pale" Tito alisema kwa kujiamini.



    “Halafu unajua hili gari sio mara ya kwanza kutufuatilia, si unalikumbuka?"



    “Ndio nalikumbuka, hili gari si ndio lile la siku ile lililokuwa likitufuatilia toka kule hom hadi kwa mkuu halafu likatupita mazima kuelekea na Raskazoni Beach, na tulipolifuata likatupotea tena. Nalikumbuka sana na leo lazima tumjue huyu mwenye gari hili"



    Wakati wakiwa wanaendelea kulijadili gari la Koplo Taure. Kuna gari jengine lilikuja na kupaki mbali kidogo na lilipo gari lao, na watu wa gari hilo pia hawakushuka kwenye hilo gari, ila wakina Tito hawakulitilia maana sana gari hilo wao wakabaki kulichunguza gari la Koplo Taure.



    Baada ya kukaa kwa dakika nyingi bila kushuka mtu yoyote kwenye lile gari lililokuwa likiwafuatilia, wakakata shauri kuwa wamfute pale pale na kumshusha kilazima mtu au watu waliokuwepo kwenye gari hilo, kwavile walishalipia vinywaji walivyotumi japokuwa hawakuvimalizia, wakaanza kuondoka kulifuata gari hilo, kama hatua tano Tobi alirudi hadi kwenye meza waliokuwa wamekaa, akamalizia kinywaji chake na kukimalizia na cha Tito halafu akaondoka kuambatana na Tito aliekuwa akimsubiri, wakaenda hadi katika gari la Koplo Taure na kumgongea kioo cha mbele upande wa dereva.



    Koplo Taure hakujua afanye ili kujiepusha na hao watu maana alishajua kuwa wamemgundua, akapanga kuondoa gari kwa ghalfa ila akaona kwenye kioo mdomo wa bastola ukimuangalia yeye, akajua tayari ameshakamatika, hakuwa na jinsi, akafungua mlango wa gari taratibu na kushuka kabisa kwenye gari lake, Tito alikuwa bado amemnyooshea bastola safarii hii alimnyooshea bastola ya kichwa.



    “Tulia hivyo hivyo, usijaribu kufanya ujanja wowote, bastola yangu iko tayari kutii kile nitakacho iamrisha, haya niambie wewe ni nani na kwanini unatufuafuatilia?" Tito alimuonya na kumuuliza swali.

    Koplo Taure hakujua afanye ili kujiokoa na hilo zahma, Tito alipoona Koplo Taure yupo kimya, akaiondoa usalama bastola aliyoishika na kubaki huru kwamba ikiminywa trigger basi ubongo wa Koplo Taure unamwagika sekunde hiyo hiyo.



    “Kwahiyo Jamaa ndio umegoma kuongea?"Tito alimuuliza hilo swali huku akiwa ametabasamu. Ila Koplo Taure akabaki kimya pasi na kujibu chochote.



    Ghafla kulisikika mlio wa bunduki huku ukiambatana na kumwagika kwa ubongo na kuwafanya watu waliokuwa katika baa hiyo kutaharuki na kuanza kukimbia huku na huko kila mmoja akijaribu kuokoa roho yake...







    Ilikuwa ni mshike mshike eneo hilo, watu walikimbia kutoka katika baa hiyo kila mmoja kukimbilia sehemu yake ili kuokoa roho yake. Tito ndie aliekumbwa na taharuki zaidi baada ya kuona mwili wa rafiki yake Tobi upo chini huku kichwa kikiwa mfano wa matapishi ya mgonjwa wa homa ya malaria, kilikuwa kimepasuka na kufanya ubongo uliochanganyikana na damu vyote vikiipamba ardhi ya eneo hilo na kuifanya iwe ni yenye kutisha kuiyangalia. Koplo Taure muda huo alikuwa nyuma ya gari lake amejificha baada ya kutokea shambulizi hilo la kushtukiza.



    Tito hakutaka tena kuganda sehemu hiyo, maana alijua kufanya hivyo ni kujihatarishia uhai wake, hakutaka kimtokee kama kilicho mkuta mwenzake, alichofanya yeye ni kujibu mashambulizi huku akikimbia upande ulipo gari lake huku akirusha risasi upande ulipo gari lao, hilo la kujibu mashambulizi kidogo lilimsaidia, maana wavamizi hao walikuwa wakirusha risasi huku wakijificha nyuma ya gari lao. Tito alifika haraka kwenye gari lao na kuingia ndani, akajaribu kuitia funguo kwenye swichi ila akajikuta akipeleka funguo sehemu nyengine, akajaribu tena kwa mara ya pili, mara hii alifanikiwa na kuiwasha gari na kuliondoa sehemu hiyo kwa kasi kubwa almanusura agonge lori la mafuta lililokuwa likija upande huo, aliondoa gari huku akisindikizwa na risasi hafifu za wavamizi hao.



    Koplo Taure baada ya kuona windo lake moja limekimbia huku jengine likiwa limebakia mwili dhalili ulio lala chini pasi na uhai, akazunguuuka upande wa pili wa gari lake na kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma na kurukia kwenye siti za mbele upande wa dereva na kuwasha gari ili kumfukuzia Tito aliekuwa mbali kwa wakati huo, aliondoa gari mbio kumuungia Tito alipoelekea.



    “Shitii!!, tumewakosa wote, ila sio mbaya huyu mmoja tuliemkosa tutampata siku nyengine, hawawezi kutuchezea mchezo wa kifo kutaka kutuua wakati tulikubaliana tufanye makabidhiano ya amani" Tosh aliongea kwa ghadhabu baada ya kuwakosa wakina Tito waliotaka kuwaua kipindi kile walipofanya makabidhiano ya pesa na madawa ya kulevya na watu kule kange.



    “Oya Tosh, tusepeni maana wazee hawakawii kuja hapa halafu ikawa kazi nyengine ya kuwakwepa" Kiku aliongea hivyo huku akiingia kwenye gari walilokuja nalo hapo. Gari hili ndio lile wakina Tito ambalo hawakulitilia maanani sana lilivyokuja eneo hilo. Wakaingia wote watatu kwenye gari lao na kutokomea kusikojulikana wakiuacha mwili wa Tobi eneo hilo ukiwa umelala chini.



    Polisi walikuja baada ya dakika kumi kutokea tukio hilo, wakachukua maelezo kwa raia walioshuhudia tukio hilo, kisha wakaondoka na mwili wa Tobi kwenda kuufanyia harakati za kuuzika maana haukuwezekana kukaa hata kwa siku moja kwa jinsi ulivyo haribika, baada ya hapo usubirie adhabu au raha za kaburini kama ambavyo viongozi wa kiimani wasemavyo.



    Koplo Taure alikuwa yupo nyuma ya gari la Tito alie kuwa akiendesha gari huku akiwa analia kwa kushuhudia kifo cha rafiki yake, hilo lilimpa wepesi Koplo Taure kumfuatilia bila yeye mwenyewe kujua maana hakuwa makini kuangalia nyuma, yeye alikuwa anachotaka kwa wakati huo afike maskani kwao na kumueleza bosi wake mkasa mzima, na hilo ndio lilikuwa ni kosa maana alikuwa akimpeleka Koplo Taure maskani kwao bila yeye kujua.



    Aliipita Mwambani Beach na kulitafuta pori ambalo ndani yake ndio kuna ngome yao, kipindi hicho Koplo Taure alikuwa bado akimfuatilia ila sasa aliongeza umakini zaidi, hakuwa karibu nae, maana alihofia kugundulika mapema kupelekea adhma yake kushindwa kutimia, ikiwa yupo mbali nae ila akikunja kona humuwahi na kuendelea kumfuatila taratibu. Kwa mbele kidogo aliweza kuliona jengo kubwa likiwa ndani pori hilo lililozungukwa na miti mikubwa mikubwa, akasimamisha gari na kushuka haraka, akatafuta sehemu ambayo alikuwa akiliona gari la Tito vizuri na kufuatilia kila tukio kwa mbali, aliona gari hilo likiingizwa katika geti kubwa la chuma na geti hilo likafungwa tena, alitembea kwa kunyata hadi karibu na uzio uliozungushia kwenye jengo hilo, akatafuta mti mrefu uliokuwa mbali kidogo na uzio huo na kuupanda, hapo aliweza kushuhudia ulinzi mkali uliokuwa eneo hilo, akayasoma mazingira ya eneo la ndani, aliweza kuwaona watu waliokuwa makini muda wote wakizunguka huku na huko wakiwa wameshika silaha kali ambazo zilipaswa kutumiwa na jeshi ila sio watu wa kawaida kama hao. Aliporidhika kuyasoma mazingira hayo, akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo kuelekea kituoni.



    Huku ndani ya jengo hilo, Tito aliposhuka kwenye gari, akaongoza njia ya kuingia ndani ya jengo hilo huku akilia kama mtoto mdogo, walinzi walimshangaa lakini hakukuwa na hata mmoja aliethubutu kumsimamisha na kumuuliza kulikoni, kila mlinzi alikuwa makini na kazi yake. Alifika katika ofisi ya bosi wake na kuingia bila ya hodi, na kumkuta bosi wake huyo akiwa na mwanamke waliokuwa wanafanya wanachokijua wao ndani humo.



    “Tito, ni nini unafanya, ni tabia gani hiyo kuingi...." Mr Bakari Haneni aliongea kwa ghazabu huku akipandisha suruali yake, alikatishwa kauli na sauti ya kilio cha Tito, ikabidi amuambie yule mwanamke atoke nje mara moja kisha hapo atamuita pindi akimaliza maongezi na kijana wake, waje kuendelea na kile walichokikatisha.



    “Enhe!!, niambie mbona umekuja huku unalia, kuna nini na Tobi yupo wapi?" Mr Bakari Haneni alimuuliza maswali hayo baada ya yule mwanamke kutoka humo ndani.



    “Amekufa, Tobi amekufa mkuu" Tito aliongea hivyo huku akilia na kumuacha bosi wake akiwa amegwaya kwa taarifa hiyo.



    “U...una..unasemaje?"Aliuliza kwa kigugumizi wakati hakuwa nacho kabla.



    “Tobi ameuliwa mkuu"



    “Nani kafanya hivyo, nani aliefanya huo upumbavu, niambieeee" Mr Bakari Haneni aliongea kwa ghadhabu huku akimtingisha Tito utadhani yeye ndio amefanya mauwaji ya Tobi.



    “Mkuu, siwajui waliofanya hivyo, na sikubahatika kuwaona vizuri"



    Mr Haneni akabaki akiwa ametahayari kwa taarifa hiyo, hakujua aulize nini tena, maana alikuwa na maswali ya kuuliza mengi ila hakujua aanze na lipi kati ya hayo mengi, akatuliza kichwa chake na kutaka aelezewe imekuaje Tobi afe wakati wametoka kuagana muda si mrefu, kipindi hicho macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira mithili ya taa za gari za nyuma pindi lichunapo breki.



    “Tulipoondoka pale kwako, tulipanga tuelekee baa kama tulivyokuaga, ila nyuma yetu kulikuwa kuna gari lililokuwa likitufuata..." akamuhadithia ilivyokuwa hadi kumuweka chini ya ulinzi Koplo Taure, “ndipo hapo niliposhudia Tobi akianguka chini huku kichwa chake kikitawanyishwa kwa risasi, mimi kuona hivyo, nikakimbilia kwenye gari nakuondoka kuja huku" Tito alimaliza kusimulia huku akijifuta kamasi zilizokuwa zikitoka kwenye tundu za pua yake.



    “Kwahiyo mwili wake umeuacha hapo hapo?" Alaa!!! Mr Bakari aliuliza swali la kijinga haikueleweka ni kwasababu ya taharuki juu ya kifo cha Tobi au ni hasira alizokuwa nazo.



    “Ndio mkuu, unadhani labda ningewezaje kuondoka na mwili wake wakati mashambulizi bado yalikuwa yakiendelea" Tito alijubu kwa ghadhabu kiasi kwa swali hilo la kijinga aliloulizwa.



    “Ok, ok, wewe nenda kapumzike halafu mimi nitajua nini chakufanya, ila kesho asubuhi uwe hapa"

    Baada ya kuambiwa hivyo Tito aliondoka na kuelekea ilipo nyumba yao waliyopewa na bosi ila kwa sasa alikuwa peke yake, hakujua mwili wa rafiki yake itakuwa upo wapi kwa wakati huo, akapanga kurudi kule kule ili akaangalie kama ataweza kuupata mwili huo ila akajua kurudi kule ni kuyafuata matatizo kwa mara nyengine, akalipinga wazo hilo na kuingia nyumbani kwake.



    Mr Bakari Haneni hakuwa tena na hamu na yule mwanamke kwa taarifa hiyo aliyopewa punde tu, akaamrisha mwanamke huyo auawe, sio kwamba auawe eti kwakuwa hawakufanya kile walichopanga kukifanya. la hashaa!. Ila ilikuwa ni lazima auliwe hata kama wangefanya kile walichokuwa wanataka kufanya, bila kuhoji wala kuuliza swali, mwanamke huyo aliuliwa kwa kifo cha kidhalili sana ambacho hakikufaa kufanywa na mwanadamu alieumbwa kwa udongo huu dhaifu tunao tembea juu yake kila kukicha, watu hao waliopewa jukumu la kumuua, walimuingilia kimwili hadi kupelekea kifo chake ila hawakukoma kufanya hivyo bali waliendelea hadi pale waliporidhika wenyewe na kuupeleka mwili huo katika shimo tayari kwa kuchomwa moto.



    Koplo Taure alipofika kituoni, moja kwa moja alielekea katika ofisi ya mkuu wake na kuingi humo.



    “Mkuu, katika uchunguzi wangu, nimefanikiwa kujua wale vibaraka wa Mr Bakari Haneni gari lao lililo tumika kumteka Hemedy, kujua wanapoenda kwenye ngome yao" Koplo Taure aliongea kwa pupa baada ya kuruhusiwa kuongea.



    “Mmh mmh!!!, embu jaribu kuongea taratibu na pangilia maneno ili nikuelewe vizuri" Insepekta Ganjo alimuambia hivyo.



    “Ni hivi, leo katika uchunguzi wangu wa kulifuatilia lile gari lililomteka Hemedy, nimefanikiwa kujua mahali kwenye ngome yao na nina hisi hapo ndipo Hemedy alipohifadhiwa"



    “We si umesema hunipi taarifa yoyote hadi utakapoisha muda niliokupa? Sasa ni vipi uje kunipa taarifa hizo, au tayari ushaikamilisha kazi niliyokupa?" Inspekta Ganjo alimuuliza kwa kumtahariza utafikiri hiyo taarifa aliyoletewa sio nzuri kwenye masikio yake.



    “Hapana mkuu, nimekuambia hivi, ili unipe kikosi kitakachonisaidia kwenda kuivamia ile ngome, maana kuna ulinzi mkali na wakimakini, sitoweza kwenda pekeangua pale"



    “Sawa, ulikuwa unataka watu wangapi na ni lini utafanya huo uvamizi?"



    “Ni kesho mkuu na nilikuwa naomba askari kama ishirini tukasaidiane hiyo kazi"



    “Askari ishirini?" Inspekta Ganjo aliuliza kwa tahamaki.



    “Ndio mkuu, kwasababu hiyo ngome inalindwa kwa umakini zaidi, sio ya kuiingia kwa mchezo mchezo"



    “Ok, nitakupa Askari hao ila muwe makini zaidi"



    “Sawa mkuu"



    “Unahisi hiyo ngome ni nani mmiliki wake?" Inspekta Ganjo alimuuliza swali la kimtego, kwa akili za kawaida unaweza ukasema swali hilo ni la kawaida lakini haikuwa hivyo.



    “Hapana siwezi jua kwasababu sina ushahidi wowote na siwezi kumuhisi mtu yoyote" Koplo Taure ni kama vile alijua kuwa anategwa, maana alilijibu swali hilo kwa ufasaha kama vile ambavyo Inspekta alitaka lijibiwe. Inspekta akatabasamu baada ya kusikia jibu hilo,‘kidogo sasa hivi akili yako inakuwa, na ukiendelea kufanya kazi kwa akili, utakuja kupanda cheo kwa urahisi kabisa' alijiwazia mwenyewe na kumruhusu aende akapumzike, na yeye akasimama na kupiga salut ya heshima na kutoka ofisini humo kuelekea nyumbani kwake.



    * * * *



    Siku iliyofuata. 3:26 Asubuhi.



    Polisi waliovalia mavazi ya kikazi kazi zaidi walikuwa kwenye magari mawili ya polisi aina ya ‘defender' wakiwa na silaha kali kali zikiwepo mabomu ya machozi huku vifuani mwao wakiwa wamevalia vazi lisiloweza kuruhusu risasi kupenya likiwa limezunguka hadi mgongoni, vichwani mwao wamevalia makofia magumu yenye vioo kwa mbele yasio ruhusu risasi kupenya kichwani, magotini na viwiko vya mikono walikuwa wamevalia vazi flani la sponji ili hata kama wakitua sehemu ambazo walihitajika kuruka basi wasiumie, huku miguuni wakiwa wamevalia buti kubwa mithili za wale wakata majani ila hizo zilikuwa ni za kijeshi zaidi. Uzito wake mtoto wa miaka kumi hainui. Kiufupi walitisha na walipendeza kwenye vazi hilo, Koplo Taure yeye alikuwa amevaa kama hao askari wengine ila yeye hakuvaa sare za jeshi la polisi, yeye alikuwa amevalia nguo za kiraia.



    Walipokamilika wote, safari ikaanza huku wakiukumbuka msemo walio ambiwa na Insepekta Ganjo kuwa umakini katika kazi ndio unahitajika kuliko kutumia nguvu, kwa mwendo waliokuwa wakienda nao, dakika kumi na tano zilitosha kuwafikisha karibu na ngome hiyo, wakashuka kwa haraka na kila mmoja akaangalia upande wake huku wakisikiliza maelekezo kutoka kwa koplo Taure, walikuwa wakisikiliza maelekezo huku wakiwa wamempa mgongo Koplo Taure aliekuwa katika katika yao.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ina bidi tujigawe watano watano. Watano wa mwanzo wataenda nyuma ya jengo hili na watano wengine wataenda upande wa kushoto na wengine wataenda upande wa kulia na sisi sita tuliobakia tutaenda upande wa mbele wa jengo hili, umakini katika kazi ndio unahitajika, hakikisheni kila mmoja anamlinda mwenzake, kuingia humo ndani, tutapitia kwa kuruka ukuta huo, kupitia kwenye hii miti iliyokuwa karibu na ukuta huo, watu hao wanaolinda ngome hii wapo makini sana, kwahiyo sisi tunatakiwa kuwa makini zaidi yao, sidhani kama wamejua kwamba leo watavamiwa ila nauhakika tutafanya shambulizi la ghafla litakalo waacha wakibabaika, kuingia ndani ya ngome hii tunatakiwa kuingia sawa, nadahini kila mmoja ana saa yake hapa, kwahiyo baada ya dakika tano kuanzia sasa, wote tunatakiwa tuwe ndani ya jengo hili, hawa walinzi wa mwanzo tunatakiwa tuwauwe kwa kutumia visu au roba, hatutakiwi kutumia risasi maana mlio wake utawafanya hao wengine wajiandae na hapo ndio kutakuwa na ugumu wa hii kazi. Narudia tena, umakini katika kazi ndio unahitajika. Go ahead, step by step, make sure you become protecter of your friend". (Tunaenda hatua kwa hatua, hakikisha unakuwa mlinzi wa mwenzako).



    Baada ya maelekezo hayo kila mmoja akashika nafasi aliyopewa, watano wakaenda nyuma ya jengo hilo, watano wakaenda kulia mwa jengo hilo, watano wakaenda kushoto mwa jengo hilo na sita waliobaki wakaenda mbele ya jengo hilo. Walienda kwa mtindo wa kupishana. Wanyuma kabisa anawahi mbele na wanyuma anaefuatia anawahi mbele ya yule wa kwanza halafu anaebaki nyuma pia anafanya hivyo hivyo, walienda kwa mtindo wa miguu ya jongoo. Walipofika karibu na ukuta huo, kila mmoja akapanda katika mti uliokuwa mbali na mwenzake na kuwafanya wafanane na tumbiri wanaovamia shamba la watu la ndizi. Wakiwa huko juu waliweza kuona eneo la ndani na jinsi kulivyokuwa na ulinzi mkali kuliko wao walivyodhani, hapo ndipo kila mmoja akaongeza umakini zaidi kuliko ule wa mwanzo waliokuwa nao, kila mmoja akabaki kuyasoma mazingira ya humo ndani ili muda waliopanga kuingia humo utakapofika ajue anatua sehemu gani.



    Muda waliopangiana ulipofika kila mmoja akaruka na kutua juu ya ukuta huo kwa ustadi wa hali ya juu, kiasi kwamba hakukusikika kishindo cha aina yoyote, hapo wakaanza kutambaa ili kuwafikia walinzi waliokuwa wakiranda chini ya ukuta huo, kwa kuwahesabu kila ukuta ulikuwa na walinzi nane na wao waliku watano watano, wakapeana ishara na kuruka kwa pamoja huku kila mmoja akimuwahi mtu wake, wale watatu waliobakia, walikuwa bado wameduwaa kwa tukio hilo hadi wanapata akili ya kushambulia, wakashangaa wakiwa hawana uhai na kubaki chini wakigaagaa na kushika visu viilivyozama shingoni mwao.



    Upande wa mbele sehemu walipoingilia wakina koplo taure, walifanya kama walivyofanya wenzao ila kwao mlinzi mmoja alibahatika kukimbilia ndani huku akipiga mayowe ya kuomba msaada, kufika tu ndani jengo hilo, akakutana na Tito aliekuwa anatoka baada ya kusikia kelele hizo, akamtuliza mlinzi huyo na kumuuliza kulikoni, akaambiwa kuwa wamevamiwa, Tito hakuwa na muda wa kuuliza mvamizi ni nani, akatoa simu yake na kumpigia Mr Bakari Haneni kumpa taarifa hizo.



    “Sasa nyie chakufanya ni kuwa makini zaidi, hao wavamizi watajuta kuingia kwenye ngome yangu, subirini nafanya kitu sasa hivi, nyie msiwe na wasi kabisa" alijibu hivyo Mr Haneni na kukata simu...







    Haikueleweka amesema hivyo kutokana na hasira au uoga wa kuvamiwa kwa ngome yake, maana hakuwa na chakufanya kama alivyosema, akabaki akitetemeka tu, hakujua wavamizi hao ni wakina nani, akaitwaa simu yake na kumpigia Tito ili ajue wavamizi hao ni wakina nani, jibu alilopewa lilimfanya aingiwe na uoga mkubwa kiasi kwamba akitishwa kidogo tu basi ndio utakuwa mwisho wa maisha yake, maana alipewa taarifa kwamba wavamizi hao ni jeshi la polisi ndio lililovamia ngome yake.



    Taarifa hiyo ilimchanganya kiasi kwamba kwa mara ya kwanza tangia atengeneze hiyo nyumba yake aiyone ni ndogo, maana hakutulia sehemu moja, mara aende chumbani mara arudi sebuleni mara afungue friji kisha kulifunga tena bila kuchukua chochote ndani humo, alikuwa amechanganyikiwa si masihara, na kilichomfanya kuchanganyikiwa kiasi hicho ni vile jamii ilivyokuwa ikimchukulia ni mtu mwema mwenye kusaidia kila mtu mwenye shida, mwenye kupeleka misaada kila siku kwenye vituo vya kulelea watoto yatima, hadi wengine wakadiriki kusema kwamba mtu huyo kama ataamua kugombea ubunge kwa chama chochote, basi atapita bila pingamizi lolote, sasa iweje leo hii maovu yake yaje kujulikana kwamba yeye ndie anasababisha upotevu wa watoto mitaani kwa kuwateka na kwenda kuwafanyisha kazi za kufunga madawa ya kulevya, jamii itamchukuliaje?, raia wenye hasira kali si wata muua kwa kipigo cha mbwa mdokozi.



    Hakutaka yote hayo yamtokee, akapata wazo la ghafla kuwa ahame nchi na kwenda mbali hadi pale zahma hilo litapopita, akapiga simu uwanja wa ndege wa Tanga kwamba anaweza akapata ndege ya kukodisha, jibu alilopewa lilimfurahisha, hakutaka kusubiri, akachukua simu na kumpigia Tito simu kumuuliza hali inaendeleaje huko, na kupewa majibu mabaya kuwa wanazidiwa na jeshi hilo lililofanya shambulizi la kushtukiza, akamuachia maagizo kuwa wajitahidi kupambana nao na mambo yakiwa sawa basi amjulishe kwa njia ya emal, akamdanganya kuwa yeye anajaribu kutafuta namna ya kutoa msaada ila alimuambia kuwa wajitahidi kadri ya uwezo wao, alijiandaa kwa kutaka kuhama nchii hii.



    Huku kwenye ngome mambo yalikuwa yamewiva, ilikuwa ni mtafaruku, kila aliekuwepo ndani ya jengo hilo, alikuwa akitafuta jinsi ya kujiokoa mwenyewe. Milio ya risasi ilisikia kila kona ya jengo hilo, ni hivyo tu kwamba jengo hilo liko mbali kabisa na makazi ya watu, lakini ingekuwa ni patashika na kwa raia pia, maana sehemu hiyo haikutofautishwa na uwanja wa vita, japokuwa walinzi wa jengo waliona kabisa wamezidiwa ila hawakutaka kuacha kupambana, walijitolea kufa na kupona hadi mwisho wa mpambano huo. Wale walinzi waoga ndio walikuwa wakiuliwa hovyo hovyo, maana walikuwa wakikimbia huku na huko wakitafuta sehemu ya kutokea, ila bahati haikuwa kwao, kila pande wanayokimbilia walipigwa risasi na kugaagaa chini kama kuku mwenye ugonjwa wa kideri.



    Mmoja kati ya hao walinzi waoga waliokuwa wakikimbia pasi na kuelewa waende wapi, aliuparamia ukuta uliozungurushiwa kwenye jengo hilo ili akimbie, ila bahati haikuwa kwake, alitunguliwa na risasi mbili za mgongo, hakuwa na budi kuachia ukuta huo na kujiacha kutoka huko juu kuja chini, akiwa yupo hewani kabla hajua tua chini, hakuwa akiamini macho yake kwamba na yeye leo anakufa, alipotua chini, hakubahatika hata kumuita shangazi yake mahali hapo, ikawa roho na mwili vimeshatenganishwa zamani na risasi zilizo zama kwenye mwili wake.



    Wale walinzi waliobakia wote wakawa wapo ndani ya jengo hilo wamejificha kwa tahadhari, huku nje kulibakia na askari waliokuwa nao wamejificha kwenye mapipa ya maji yaliyokuwepo eneo hilo, hadi kipindi hicho hakukuwa na asakari hata mmoja aliedhurika wala kufa kwenye mpambano huo, walikuwa makini na wakilindana wenyewe kwa wenyewe, kipindi hicho hakukuwa na upande uliokuwa ukirusha risasi kwenda popote, kulikuwa kimyaa utafikiri hakukuwa na mpambano uliokuwa umetokea muda si mrefu. Koplo Taure alikuwa akiwapanga askari wake kwa kutumia ishara ili waweze kuingia ndani ya jengo hilo.



    Wawili walitoka mbio na kuenda kubana katika mlango mkuu wa kuingilia ndani humo, wakachungulia kwa umakini na kukuta eneo la ndani ya jengo hilo lililokuwa na ukubwa mithili ya uwanja wa mpira wa kikapu likiwa halina mtu yoyote zaidi ya machuma ya kufanyia mazoezi yaliyokuwa eneo hilo, wakawapa ishara wenzao na askari watano wakaenda haraka na kuwapita wale wawili waliokuwa pale mlango, wakazama ndani na kujibanza ukutani, ghafla zilitoka risasi pasipojulikana na kuwafanya askari hao kuuwahi mlango wa kutokea, askari wote watano walijeruhiwa vibaya maeneo mbali mbali ya miili yao, ila walifanikiwa kutoka nje na kupokelewa na wenzao, wakawahifadhi sehemu salama na kupatiwa huduma ya kwanza na askari mwenye utaalamu na tiba.



    Koplo Taure akaamrisha kila askari afunike uso wake kwa kofia maalumu za kuzuia sumu yoyote inayosambaa kwa hewa, na askari wakafanya hivyo na Koplo Taure akaamrisha kupigwe mabomu ya machozi ndani humo, ni kitendo cha dakika moja tu, mabomu ya machozi kama ishirini yalikuwa yametapakaa ndani ya jengo hilo na kupiga mabomu mengine sita ya moshi mzito na kufanya eneo hilo kuwa kama vile ni usiku kutokana moshi huo kutanda eneo lote, wakawasha tochi zao walizozifunga kwenye vichwa vyao na kuzama ndani ya jengo hilo, ndani humo kulisikika kelele za vikohozi kila upande, walichofanya askari hao ni kuzifuatilia kelele hizo na kuwashika kama kuku kwenye banda lao, waliwatoa walinzi kumi na moja, na kuwafunga pingu huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.



    Hiyo ilikuwa ni sehemu ya chini ya jengo hilo, wakahitajika kupanda juu ili kufika juu ya ghorofa ya pili ya jengo hilo, walipanda kwa umakini mkubwa huku moshi ukipungua taratibu na mabomu ya machozi waliyoyapiga mwanzo yakipungua kasi, walipofika sehemu ya juu ya jengo hilo, walikutana na ujia mrefu ulio tenganisha vyumba, ikawa askari hao wana kazi ya kufungua chumba kimoja baada ya chengine kwa tahadhari kuu, walihofia yasije yakawakuta kama yaliyo wakuta wenzao watano, baadhi ya vyumba hawakukuta kitu zaidi ya magodoro yaliyopangwa chini ya sakafu na vyumba vyengine walikuta maboksi ya madawa ya kulevya yamepangwa vizuri.



    Walijigawa watatu watatu kwenda upande tofauti tofauti, wakiendelea kusachi vyumba hivyo vilivyokuwa vingi kwenye flow hiyo, askari watatu walikiendea chumba kimoja kwa uangalifu na kujibanza pembeni ya mlango wake, walipeana ishara na mmoja akarudi nyuma kidogo na kuuenda mlango huo kwa kasi kubwa kwa kuupiga teke moja na kupelekea mlango huo ufunguke. Risasi zilirushwa kutokea ndani ya chumba hicho bila mpangilio, bahati yake askari huyo aliwahi kuruka pembeni, na hapo risasi zikaachwa kupigwa na kuwa kimya cha ghafla, askari hao wakapeana ishara na mmoja akatoa kitu mfano wa kiazi na kukirusha ndani humo, dakika hiyo hiyo watu waliokuwa ndani ya chumba hicho wakaanza kukohoa kwa nguvu huku walinzi hao wakiziachia bunduki zao na kufikicha macho yao, askari hao watatu wakazama haraka na bila kuuliza wakaanza kumimina risasi kwa walinzi hao.



    Walinzi walikufa huku wakiwa bado wana utamani uhai, walikuwa wapo sita, ndani ya chumba hicho mbele kulikuwa na mlango mwengine ila huu haukuwa umezibwa na kitu chochote, ulikuwa wazi tu, askari hao wakausogelea kwa umakini na kuufika karibu yake na kutulia, ikawa kila mmoja hataki kuchungulia ndani humo akihofia uhai wake, baada ya kutulia kwa sekunde ishirini, mmoja akajitoa kimasomaso na kuchungulia, alikuta kundi la watoto likiwa limejikunyata sehemu moja huku wengine watatu wakiwa wamelala chini hawajiwezi kwa kuathiriwa na madawa ya kulevya, akawaambia wenzake kwamba pako salama waingie tu na wao wakafanya hivyo, wakawapa ishara ya kutopiga kelele watoto hao na kuanza kuwaongoza njia kuwatoa ndani humo huku wale watatu wakiwabeba wao, waliwatoa hadi nje kabisa ya jengo hilo na kukuta gari la hospitali limeashafika hapo kitambo kwaajili ya kutoa msaada kama kutahitajika hivyo, wale watoto walikuwa wapo ishirini na nne, wakaingizwa baadhi yao kwenye gari hilo na wengine wakaingizwa kwenye gari la polisi, kwajili ya kuwapeleka hospitali ili kutibiwa kutokana na kuathiriwa na madawa ya kulevya.



    Maiti zilizozagaa huko nje, zilichukuliwa zote na kuwekwa sehemu moja, bunduki zilizokuwa zikitumiwa na watu hao pia zilikusanywa na kuwekwa sehemu moja, na wale waliokutwa ndani ya jengo hilo, walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi Chumbageni na kuhifadhiwa humo.



    Huko ndani ya jengo hilo, Koplo Taure alifika katika chumba kimoja wapo, na kuufungua mlango kwa tahadhari, alipoingia ndani alimkuta Hemedy akiwa amewekwa chini ya ulinzi na jitu la kutisha kiasi kwamba Koplo Taure alihisi jitu hilo ni mzimu.



    “Ukifanya ujinga wowote, huyu dogo namuua kwa risasi, unachotakiwa sasa hivi ni kupambana na mimi ili kuokoa uhai wako na wa huyu dogo, najua siwezi kutoka salama humu, kwahiyo nataka nife na wewe, chakufanya ni kutoka ndani ya chumba hiki na kuingia kwenye hiko chumba kinachofuata, chumba hicho kina sehemu nzuri na kubwa tu ya kupambana" Ibilisi kama tumjuavyo, alipomaliza kuongea hivyo, akampa ishara Koplo Taure atoke humo na kuingia kwenye hicho chumba chengine kwajili ya kupambana, na yeye akafanya kama alivyoambiwa, na jitu hilo nalo, likamfunga Hemedy kamba za miguu na mikono na kumuacha humo humo yeye akaelekea katika chumba alichokuwa Koplo Taure, akampa ishara atoe risasi katika bastola alioishika na yeye akafanya hivyo na kuzitupa pembeni, ikawa ni mkono kwa mkono.



    Wakabaki wakiangaliana kama majogoo yaliyotoka kupigana vita ya kugombania mtetea. Koplo Taure akapewa ishara ya kumfuata mtu huyo na yeye akamfuta kwa mapigo ya tik taka yaliyotua kifuani mwa jitu hilo, mapigo hayo hayakumuathiri kwa chochote zaidi ya kumrudisha nyuma tu kidogo na kumfanya jitu hilo lijifute vumbi kifuani mwake huku likitoa tabasamu la kuogofya kwa macho ya mwanadamu wa kawaida, Koplo Taure akajitayarisha kwa pigo jengine na kurusha ngumi za haraka haraka zilizo hepwa na jitu hilo kwa ustadi mkubwa.



    Akarudi tena nyuma kujipanga, alijua kuwa jitu hilo, likovizuri kwenye mapigano na lilikuwa liko makini sana, aliwaza kuwa akifanya mchezo basi ndio itakuwa ni mwisho wa maisha yake, akajipanga upya na kulifuata tena, safari hii alikuwa akilipiga mateke ya ugoko na buti lake la kijeshi, mbinu hiyo ili msaidia, lakini haikumsaidia hivi hivi, maana jitu hilo lilikuwa likirusha na ngumi nzito zilizokuwa zikimkosa kosa Koplo Taure, jitu lilipoona ngumi zake anazorusha hazifanikiwi lengo, likaanza kitumia nguvu.



    Likamshika Koplo Taure na kumuinua juu kisha lika mtupa na ukutani, hakika pigo hilo lilitosha kumnyong'onyeza Koplo, maana hakuweza hata kuinuka kwa maumivu aliyoyapata, likamfuta tena pale alipo huku likitoa sauti ya kukera kama ile ya muungurumo wa radi pindi mvua inyeshapo, likamuinua juu, safari hii alipanga kumvunja kiuno kwa kumpigisha kwenye goti lake, Koplo japokuwa hakuwa na nguvu, ila aliona akifanya mchezo basi pigo hilo kama si kuondoka na maisha yake basi litamfnya atembelee kiti cha walemavu daima, hakutaka yote yamkute, ndio maana akutumia ujanja wa kumng'ata kwenye mshipa wa shingo kwa nguvu.



    Jitu lilipiga kelele za maumivu huku likimuachia na kupiga magoti huku likishikilia shingo yake, akaona sasa hiyo ndio nafasi ya kuliua jitu, akalipiga ngumi za kichwa za haraka haraka, likaenda na chini, hapo lilipokea mabuti yenye kilo nyingi, yasiokuwa na idadi ya kichwa, hadi ikawa linatoka damu za pua na mdomo, Koplo alihakikisha tayari jitu hilo limekufa ndipo na yeye alipoacha na kutoka kwenye chumba hicho na kuingia kwenye chumba alichoachwa Hemedy. Alipofika alimkuta Tito amemuweka chini ya ulinzi Hemedy kwa kumnyooshea bastola ya kichwa.



    “Hamuwezi mkanichukua hata mara moja, najua kwamba nilazima nife, lakini siwezi kufa pekeangu, ni lazima nife na huyu mtoto, (akamuangalia Hemedy aliekuwa amempigisha magoti chini na kumuambia) dogo sali sala zako za mwisho, maana unaenda kufa muda si mrefu" Tito alimaanisha kusema hivyo, maana muda huo huo aliitoa usalama bastola yake na kusubiri aiamrishe tu ifanye kile anachokitaka.



    ‘Paaaa!!' mlio wa risasi ulijirudia rudia ndani ya chumba hicho na kumfanya Koplo Taure apigwe na butwaa kubwa kwa kitendo hicho huku Tito akitoa tabasamu.







    Tito alitoa tabasamu la karaha lililochanganyikana na damu iliyokuwa inatoka mdomoni mwake kutokana na kupigwa risasi iliyozama kichwani kwake, Koplo Taure akageuka nyuma na kukuta ni askari ndie aliempiga risasi Tito alietaka kumuua Hemedy, hawakuongea kitu, Koplo Taure alimchukua Hemedy na kutoka nae nje ya jengo hilo.



    “Huyu nae ameathiriwa na madawa ya kulevya?" aliuliza hivyo daktari aliekuwa eneo hilo.



    “Hapana huyu ni mzima, labda apimwe aangaliwe kama anatatizo lolote" alijibu Koplo Taure na kumkabidhi Hemedy kwa daktari huyo, yeye na askari wengine, wakarudi tena ndani ya jengo na kuanza kupekuwa chumba kimoja baada ya chengine, walitoa maboksi mengi ya madawa na bunduki nyingi zilizohifadhiwa katika chumba kimoja na kuziingiza ndani ya magari yao, wakakusanya na maiti zilizokuwa zimezagaa eneo lote hilo na kuzitia kwenye gari, walipoona hakuna chengine chakufanya, wakalizungushia jengo hilo utepe na kuondoka eneo hilo.



    Walipofika kituoni, Koplo Taure akanyoosha hadi katika ofisi ya Mkuu wake na kuingia.



    “Koplo, hakuna muda wa kupoteza, chukua askari muwahi uwanja wa ndege, Mr Haneni anataka kutoroka, nimepewa taarifa hizo na askari wa huko nilie muweka kunipa taarifa juu ya safari za mtu huyu atakapotaka kuondoka kwa kutumia ndege, anataka kuondoka na ndege ya kukodi, kwahiyo wahini kabla hajafika uwanjani hapo, maana akifika tutakuwa tayari tumeshamkosa" Insepekta Ganjo alimuambia hivyo baada tu ya kuingia kwenye ofisi yake.



    Koplo Taure alitoka mbio na kuwataka askari wapande kwenye gari ili wamfuatilie Mr Bakari Haneni, bila kuuliza wakapanda kwenye magari na safari ya kumfukuzia mtu huyo ikaanza. Magari yaliendeshwa kwa kasi kiasi kwamba ilitisha na iliogopesha kwa kuangalia, yalikuwa yakifika sehemu ya kona, matairi hutoa sauti za malalamiko, dakika kadhaa, wakawa wameshafika eneo la sabasaba, wakaliona gari la Mr Bakari Haneni aina ya Jaguar kwa mbali, likiendeshwa kwa kasi, gari hilo Koplo Taure alilijua vyema kutokana kuna siku aliwahi kulifuatilia, akajua ndani ya gari hilo ndimo alipo Mr Bakari Haneni, wakaongeza mwendo ili kuliwahi.



    “Ongeza mwendo, polisi waanakuja" Mr Haneni alimwambia dereva wake baada ya kuona magari ya polisi kwa mbali yakija kwa kasi.



    “Sasa mkuu, unadhani tutawakimbia vipi wakati wameshajua kuwa tunaenda uwanja wa ndege, lazima watukamate tu" dereva alimjibu.



    “Nimekuambia ongeza mwendo weweee" aliongea kwa ghadhabu huku akiwa bado shingo yake ameigeuza nyuma kuwaangalia polisi hao wanaokuja kwa kasi ya ajabu. Kwavile na yeye alikuwa ni mtumishi tu, hakuwa na jinsi, akaongeza mwendo na kufanya gari hilo likimbie mithili ya mshale ulioachiwa na muwindaji kwenda kumchoma swala wa nyikani.



    Polisi nao hawakukubali kuachwa kizembe na gari hilo, na wao wakaongeza mwendo ya magari yao kiasi kwamba magari hayo yakikanyaga hata punje ya mchanga yanaweza kuanguka. Ikawa ni mshikemshike kwenye barabara hiyo, magari yote yalikuwa yapo kasi kupita maelezo. Mr Haneni alipoona magari hayo yana karibia kuwafikia, akachomoa bastola yake na kuanza kushambulia, polisi nao hawakutaka kushambuliwa kizembe wakati na wao pia silaha wanazo, na wao wakaanza kushambulia gari hilo lililokuwa mbali kidogo na wao.



    Wakati wa kushambuliana, gari la Mr Haneni likapigwa risasi ya tairi na kupelekea gari hilo likose muelekeo kutokana na kasi lililokuwa nayo, likahama njia na kwenda nje ya barabara na kugonga mti uliokuwa pembeni ya barabara hiyo na kupelekea ajali kubwa iliyoikumba gari hilo baada ya kuugonga mti huo kwa ubavuni na gari hilo kupenduka mara mbili.



    Polisi waliwahi mahala hapo na na kukuta damu zimezagaa kwenye gari hilo, walijitahidi kuwatoa watu hao na kufanikiwa, ila dereva akawa hana tena uhai baada ya kipande cha kioo cha mbele kuja kumchoma kwenye shingo. Mr Haneni alikuwa na hali mbaya, alikuwa akitoa mabonge ya damu mdomoni mwake, wakamchuku yeye na dereva wake ambae kwa sasa ni maiti na kuwapeleka hospitali ya Bombo, dereva alipelekwa monchwari huku Mr Haneni akipelekwa chumba cha matibabu kwajili ya kwenda kuwahiwa kabla hali yake kuwa mbaya zaidi na kupelekea kifo, walimuweka kitandani huku akiwa na pingu mkononi iliyo fungwa kwenye kitanda hicho.



    Koplo Taure baada ya kufika kituoni, alihitajika kwenye ofisi ya mkuu wake na kuelekea huko.



    “Safi sana Afande, naona sasa unaonyesha juhudi katika kazi, na hivyo ndivyo inavyotakiwa askari awe, ukiendelea kufanya kazi kwa kutumia akili kama hivi ulivyofanya naamini utapanda cheo kwa haraka zaidi, enhee, nipe taarifa, kazi imeendaje huko" Inspekta Ganjo aliongea hivyo huku akiwa amepambwa na tabasamu usoni mwake.



    “Tumeifanya kazi kwa ukamilifu, sote tumerudi wazima, japokuwa kuna askari watano wamejeruhiwa, ila kwa uwezo wa mungu, watarudi katika hali ya kawaida kwasababu majeraha yenyewe sio makubwa"



    “Kuna ambao mmewakamata katika tukio hilo?"



    “Ndio mkuu, tumewapeleka kituo cha chumbageni"



    “Katika jengo hilo, ni shughuli gani iliyokuwa ikifanywa?"



    “Ni kufunga madawa ya kulevya, kulikuwa na watoto wengi waliokuwa wakiifanya kazi hiyo, ila wote tumewapeleka hospitali ya Bombo"



    “Na vipi kuhusu Hemedy, nae mmemkuta pia?"



    “Ndio mkuu, nae tumempeleka hospitali japo kuwa hakuwa katika watoto hao waliathiriwa na madawa hayo, ila yeye tumempeleka kwa uchunguzi kama anatatizo lolote"



    “Huyu Haneni nae, mmemkamatia wapi?"



    “Tumemkamata sabasaba kwa mbele kidogo, baada ya gari lake kupata ajali kwa kugonga mti, dereva wake amekufa hapo hapo ila yeye hali yake ni mbaya na tumempeleka hospitali"



    “Sawa, sasa hivi chukua askari watano, muende katika nyumba yake mkasachi kila sehemu,(akafungua droo iliyopo hapo katika meza yake na kutoa bahasha) na hiki nikibali cha kusachi nyumba yake, kama ikiwa walinzi wake watahitaji kibali" Akamkabidhi na kumruhusu aende.



    Koplo Taure akatoka nje na kuchukua askari watano na kuingia kwenye gari safari ya kwenda kwenye nyumba ya Mr Bakari Hanein ikaanza.

    Walipofika nje ya jumba hilo, waligonga geti na kufunguliwa na mlinzi wa getini, baada ya kujitambulisha kuwa wao ni askari, wakaruhusiwa kuingia ndani na kuanza kueleza shida yao.



    Jumba hilo lilikuwa na ulinzi mkali kutoka katika kampuni flani inayoshuhulika na maswala hayo ya ulinzi, kama walivyotabiri, walinzi hao walitaka kibali na kuonyeshwa, walipo kihakiki vizuri, ndipo waka waruhusu polisi hao kusachi. Walianzia flow ya chini ya jumba hilo, wakaangalia vyumba vyote ila hawakukuta kitu, wakapanda flowa ya juu, pia wakaangalia vyumba vyote pia hawakukuta kitu, ila kuna chumba kimoja kilikuwa kimefungwa, wakawaita walinzi kadhaa wa jumba hilo na kuwauliza chumba hicho kina nini, mbona kimefungwa tofauti na hivi vyengine, wakajibu hawajui chochote kuhusiana na hilo.



    Ikabidi watumie nguvu kufungua chumba hicho, wakapanga kuvunja mlango ili waingie ndani humo, baada ya kuminyana na mlango huo kwa dakika kadhaa, ndipo ukatii kufunguka kwa kuvunjwa. Wakaingia ndani ya chumba hicho, kilioneka kama stoo hivi, maana kilikuwa ni kikubwa kilichojaa makorokoro mengi ikiwemo na maboksi kadhaa, wakafungua maboksi hayo na kukuta ni madaya ya kulevya ndio yamehifadhiwa humo, walinzi wenyewe walishangaa, maana hawakuwahi kufikiria kama bosi wao anafanya biashara hiyo haramu inayopingwa duniani kote.

    Wakayachukua maboksi hayo, kama ushahidi wa kumfungia Mr Haneni mahakamani pindi akipata nafuu, wakaondoka nayo kuyapeleka kituoni.



    Mrutu alipewa taarifa ya kupatikana kwa Hemedy na kwenda moja kwa moja hadi hospitali kumuangalia, Kwavile hakukuwa na tatizo lolote alilokutwa nalo, aliruhusiwa kuondoka siku hiyo hiyo akiwaacha wenzake wakiendelea kutibiwa, akaondoka na Mrutu hadi nyumbani kwake, Mrutu muda wote alikuwa na furaha isiyo kifani baada ya kumpata mwanae huyo kirahisi tofauti na vile yeye alivyodhania.



    Walipofika nyumbani, alimuuliza maswali mawili matatu kuhusiana na hali yake na kilichomkuta huko, alimuambia kila kitu kilichomtokea hadi kukutana na jitu la kutisha, Mrutu alicheka sana baada ya kusikia hivyo, maana hata yeye pia alimjua huyo mtu wa kutisha kama Hemedy mwenyewe alivyomuita. Mrutu alipata wazo, alijua Hemedy kuishi hapo ni kuendelea kuyaweka maisha yake hatarini kutoka kwa kina Mata wanaotaka afe, akapanga kumuomba Inspekta, Hemedy akaishi kwake kwa kisingizio cha huenda ikawa kuna wengine wanao muwinda huyu mtoto, akampigia simu Koplo Taure ili ampe namba za Insepekta, hilo halikuwa tatizo, akapewa na kuzipiga muda huo huo, akamueleza kama alivyopanga na Inspekta alikubali bila kinyongo Hemedy akaishi nyumbani kwake.



    Baada ya kuongea na Inspekta, Mrutu akampa taarifa hiyo Hemedy aliekuwa chumbani kwake akioga, alifurahi sana baada ya kuambiwa akakae kwa Inspekta maana hata yeye pia alipapenda kutokana na kupata watu wa kuongea nao tofauti na hapo kwa baba yake mdogo, alijiandaa haraka haraka na kuchukua nguo zake kwenda kuyaanza maisha upya kwa Inspekta Ganjo, hakusahau flash yake, aliichukua pia.

    Alipokamilisha kila kitu, wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Inspekta, dakika ishirini zilitosha kuwafikisha nyumbani hapo na kuingia ndani ya nyumba hiyo.



    “Haaa!! Medy!"



    Ilikuwa ni sauti ya Hilda mjukuu wa Inspekta baada ya kumuona Hemedy akiingia nyumbani kwao, alitoka mbio na kuja kumdandia Hemedy mithili ya nyani alieona mgomba wenye ndizi mbivu zenye kutamanisha, bila kumjali Mrutu aliekuwa amesimama akiangalia tukio, hata hivyo Hilda hakujua kwamba mtu huyo ni baba yake mdogo na mtoto huyo, alichojali yeye ni kuidhihirisha furaha yake baada ya kumuona mtu alietokea kumhusudu vibaya mno, baada ya dakika moja ndipo alipomuachia na kuanza kusalimiana nae, Hemedy nae akachukua nafasi hiyo kumtambulisha mtu huyo kuwa ni baba yake mdogo, hapo ndipo Hilda alipozinduka kutoka kwenye ndimbwi la furaha na kuingiwa na aibu kwa tukio alilolifanya mbele ya mtu huyo, akamsalimia na yeye, akapokea begi la nguo alilokuwa analiburuza Hemedy na kuingia ndani ya nyumba hiyo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wafanyakazi wa nyumba hiyo, walipomuona Hemedy walifurahi sana kiasi kwamba wakamfanya Mrutu ashangae kwa furaha ya kumuona mwanae, alijilaumu kwa mara nyengine kwa kutaka kumuua mtoto huyo anaependwa na watu kutokana na ucheshi wake, hata yeye mwenyewe pia alikuwa akimpenda sana tu, ila ameamua kumhamisha kwake ili kumlinda na kifo.

    Watu wa nyumba hiyo walifurahi zaidi baada ya kuambiwa kuwa mtoto huyo amekuja kuishi kabisa kwenye nyumba hiyo, furaha yao ilipelekea hadi kupanga kufanya kijisherehe cha kizushi ili kumkaribisha mgeni walietokea kumhusudu kuliko mgeni yoyote aliewahi kufika nyumbani hapo.



    Wakaandaa mazingira ya sherehe hiyo haraka haraka huku wakimsubiria Inspekta arudi kutoka kituoni ili waje kusherehekea wote sherehe hiyo iliyozushwa siku hiyo hiyo, wafanya kazi wa kike walipika vyakula mbali mbali kwa haraka na kwa ustadi mkubwa kuliko walivyowahi kupika kabla, baada ya maandalizi yote kuisha, wakawa wana msuburi Inspekta aje ili waungane wote kwenye sherehe hiyo, muda huo wa kumsubiri Inspetka, Hemedy alikuwa akiwapiga stori ambazo ziliwafanya muda wote meno yao yawe nje kwa vicheko.



    Baada ya saa moja kupita, Inspekta aliingia ndani ya nyumba hiyo huku akifuatiwa na Koplo Taure na Afande Jesca, walipewa taarifa ya sherehe hiyo iliyozuka ndio maana wakaja na vinywaji ili sherehe izidi kupamba, Afande Jesca alipoingia sebuleni hapo, alikumbatiana na Hemedy huku akimpa pole kwa maswahibu yaliyo mkuta. Walifurahi wote kwa pamoja huku wakila na kunywa, japokuwa sherehe hiyo haikupangwa kabla ila ilipendeza na kuoneka kama iliyopangwa muda mrefu tu.



    Baada ya kufurahi sana hadi usiku wa saa nne, Mrutu aliaga na kutaka kuondoka nyumbani hapo, muda huo huo nae Koplo Taure aliga na kuondoka wakiambatana watatu yani Koplo Taure, Mrutu na Afande Jesca na kila mmoja alielekea kwake, isipokuwa Koplo Taure na Afande Jesca walielekea sehemu moja. Waliobaki waliendelea kupiga stori hadi pale Inspekta alipoenda kulala na kuwaacha wengine wakiendelea na maongezi yaliyonogeshwa na Hemedy hadi majira ya saa tisa usiku, waliondoka mmoja mmoja kwenda kulala japokuwa hawakutaka kufanya hivyo, ila iliwalazimu kufanya hivyo kutokana na siku inayofuta ni wenye kuhitajika kufanya shuhuli za hapo nyumbani.



    * * * *



    Siku nne zikapita huku Hemedy akiendelea kuishi nyumbani hapo kwa Inspekta, alipewa uhuru wa kufanya chochote hadi akajihisi yupo nyumbani kwao.



    Kesi ya Mr Bakari Hanein ilipangwa kusomwa wiki hiyo hiyo kutokana na ushahidi wote kukamilika, watoto walioathiriwa na madawa ya kulevya kiasi fulani walipata ahueni na kukutana na familia zao, wazazi wao walitoa machozi ya furaha kukutana na watoto wao huku wakikilaani kitendo cha Mfahari huyo kuwateka watoto wao na kwenda kuwatumikisha kazi zisizofaa kwa jamii, watoto hao waliruhusiwa kurudi majumbani kwao huku wakisubiria siku ya kusomwa kesi ya Mr Haneni kwenda mahakamani kutoa ushahidi.



    Kesi ya Mr Bakari Haneni iliambatana na ya Mata kwenda kudai mali zake kwa marehemu Mheshimiwa Bhachu kama mwenyewe alivyodai. Kipindi hicho Mr Haneni hali yake na yeye iliridhisha kutokana na kuwa hakupata majeraha makubwa mwilini mwake, akatolewa hospitali na kupelekwa kituo cha polisi cha chumbageni kwajili ya kusubiri siku ya hukumu yake.



    Siku mbili zilipita na siku hii ilikuwa ndio siku ya kusomwa kesi yake huku ikiwa ndio siku ya Mata kwenda kudai mali zake mahakamani, bahati nzuri au mbaya kesi zote hizo mbili zilihitajiwa kusikilizwa katika mahakama moja, mahakama ya chumbageni. Mata alijiandaa kwajili ya kwenda mahakamani huku Mrutu nae akijiandaa kwenda mahakamani kama msimamizi wa mali hizo, huku nae Mr Haneni akiandaliwa kupelekwa mahakamani kwajili ya kesi yake.



    Watu wote hao walikutana mahakamani hapo kwajili ya kesi zao ila kwa Mr Haneni yeye alihifadhiwa katika chumba maalumu kilichopo mahakamani hapo kwajili ya watuhumiwa wanaosubiri kusomewa kesi zao kwa siku hiyo. Umati wa watu ulijaa mahakamani hapo kwajili ya kushuhudia kesi ya Tajiri huyo aliewashangaza wengi baada ya kuisikia kesi yake.



    Kesi nyengine ilianza kusomwa mahakamani hapo, baada ya kesi ya kwanza ikafuatia ya Mata, nae akaenda kusimama kizimabani kudai haki yake kama alivyosema, Mrutu alisimama upande wa mdaiwa, na Moto nae alikuwa amekaa kwenye mabenchi yaliyokuwemo ndani ya mahakama hiyo akishuhudia kila kinachoendelea.



    Huko nje ya mahakama, Inspekta Ganjo aliongozana na Hemedy kutaka kuingia ndani ya mahakama hiyo, ili kwenda kushuhudia kesi hiyo inayodaiwa kuwa ni kesi ya madai ya mali za baba yake aliekuwa kaburini, hata yeye pia ilimshangaza taarifa hiyo ya kuwa zile mali hazikuwa ni za baba yake wakati yeye alijua fika ni za baba yake, hata hivyo pia alihitajika kuwa kama shahidi yeye akiwa na watoto wengine waliotekwa na kundi la Mr Bakary Hanein kwajili ya kutoa ushahidi.



    Wakiwa wapo mlangoni wa kuingilia ndani ya mahakama hiyo, Hemedy alipigwa na bumbuwazi baada ya kumuona mtu alie mshangaza kuwepo humo ndani ya mahakama, akabaki akiwa ameganda mlangoni akimshangaa mtu huyo, hata mtu huyo alipomuona Hemedy, pia alibaki na mshangao akiwa haamini kwamba huyo mtoto anaemshangaa amemfananisha au ndie yeye, Inspekta Ganjo hata yeye pia aliuona mshangao wa Hemedy akijiuliza mtoto huyo ameona nini kinachonfanya kuwa katika mshangao huo...







    “Hemedy!! ni wewe kweli?" sauti ya mtu huyo, iliuliza kwa hamaki baada ya kutoamini macho yake, akataka kuamini kwa kuuliza kabisa.



    “Nesi. Nesi Maria!!" ni kama vile waliambia watajane majina yao, wote waliuliza kwa hamaki na mshangao wa wazi wazi.



    Nesi Maria alienda hadi pale mlangoni ambapo watu hao walikuwa bado wamesimama, akasalimiana na Inspekta maana mtu huyo pia ni mwenye kujuana nae tangia kipindi kile Hemedy alipopelekwa hospitali kwa mara ya pili kwenda kutibiwa baada ya kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali wakidhani ni mwizi. Nesi huyo ndie aliepewa kazi ya kumhudumia Hemedy kipindi chote alipokuwa hospitali pale, na kutokea kumhusudu sana kutokana na ucheshi wake usio kera na kutamani muda wote awe nae pamoja na leo hii wamekutana tena kwa mara nyengine baada ya kupoteana kwa takribani miezi miwili.



    Akamuomba Inspekta atoke na Hemedy nje wakasalimiane vizuri, na yeye bila kipingamizi akawaruhusu waende, hata kilichowafanya watake kuingia ndani ya mahakama hiyo pia walikisahau, akaingia Inspekta pekeake huku Hemedy akitoka na nesi Maria nje, kama angemtilia maanani yule aliekuwa kizimbani amesimama na kumuangalia vizuri, bila shaka pangetokea jambo jengine ambalo lingewashangaza wengi mahakamani hapo, ila ndio hivyo, hakumtilia maana mtu huyo na yeye akatoka na nesi huyo nje ya mahakama hiyo.



    “Umekuja kufanya nini hapa?" nesi Maria alimuuliza Hemedy swali hilo baada ya kuongea nae kwa dakika tatu.

    Hapo ndipo Hemedy alipokumbuka ni kipi kilichomleta mahakamani hapo, hata hivyo akajiambia mwenyewe kuwa, baba yake mdogo yupo, yeye ndie atakae jua nini chakufanya huko ndani.



    “Mimi nimekuja kusikiliza kesi, je wewe umekuja kufanya nini?" akajibu na kurudisha swali lile kwa Maria.



    “Hahahah!! We Medy umekuja kusikiliza kesi gani wewe, haya lakini, hata mimi pia nimekuja kusikiliza kesi ya huyu tajiri Haneni, na wewe pia umekuja kusikiliza kesi hiyo hiyo?"



    “Ndio"



    Wakati wakiwa bado wanaendelea kupiga stori. Huko ndani mambo yaliwiva baada ya Mrutu kukubali kuwa mali hizo hazikuwa ni za marehemu kaka yake bali yeye alikuwa ni kama msimamizi tu wa mali hizo, akapigilia msumari kauli yake kusema kwamba, marehemu kaka yake, alishawahi kumuambia hicho kitu kuwa mali hizo sio zake ila kuna tajiri ambae yupo nje ya nchi hii ndio amemuachia kuwa kama msimamizi kwa miaka mingi sana iliyopita, ili ushahidi ukamilike zaidi, wakatoa ile karatasi ambayo walimshurutisha marehemu andike kuwa mali sio zake na kutia saini yake kabisa ambazo kwa sasa ziko mbili baada ya kuzipiga kopi, na kopi alibaki nayo Mrutu na ile halisi aliichukua Mata.



    Kutokana na kuwa ushahidi umekamilika na pia Mrutu kukiri hilo jambo kuwa mali hazikuwa ni za kaka yake, basi hapakuwa tena na mlolongo mkubwa zaidi ya kukabidhiwa Mata mali hizo, kwa hakika isingewezekana hata kidogo kuwadhania kuwa walikuwa wakicheza mchezo mchafu mahakamani hapo, kwa jinsi Mata alivyo vaa, bila shaka ungesema ni kama mfanyakazi wa benki kuu ya dunia au ni mkurugenzi wa kampuni fulani kubwa nchi za nje, alikuwa amevaa suti ghali ya rangi ya kijivu ikinogeshwa na tai nyeupe iliyokuwa ikioneka kwa uchache kifuani mwake, huku chini akiwa amevaa viatu vikali vilivyo ng'arishwa kiwi kiasi kwamba viliumiza macho wakati vikipigwa na mwanga wa jua ukiwa unaviangalia na vilikuwa mithili ya kioo kwajinsi vilivyoweza kuonyesha taswira mbalimbali zilizokuwa zikioneka.



    Alikabidhiwa mali zote mahakamani hapo na Mrutu akatia saini yake kwenye karatasi fulani aliyopewa na karatasi hiyo hiyo ikapita kwa Mata na yeye apia akatia saini yake, ikawa hadi hapo, Mrutu amekwisha kabidhi mali hizo kwa Mata na kesi yao ikaisha hapo na kila mmoja akaondoka kivyake.



    Huku nje ya mahakama hiyo, Maria na Hemedy walikuwa wakihitimisha maongezi yao, baada ya ule muda wa kesi ambayo iliwafanya kuwa mahakamani hapo kufika, nesi Maria alijaribu kumuuliza kuwa Hemedy ana simu ili aweze kupata mawasiliano nae, lakini jibu alilopewa lilimnyong'onyeza baada ya kujibiwa kuwa hana simu, hakutaka tena kupotezana na mtoto huyo tena, ila hakuwa na jinsi ilibidi iwe hivyo maana Hemedy hakuwa na simu kweli, wakachukuana wote kwa pamoja na kuingia ndani ya mahakama hiyo ili kuisikiliza kesi ya Mr Haneni.



    Ukafika ule muda uliokuwa ukisubiriwa na wengi mahakamani hapo, muda wa kusomwa kesi ya Mr Bakari Haneni, watu walitulia kimya huku wakisubiri mfahari huyo aletwe kizimbani kusomewa mashtaka yake, baada ya dakika tano, akaingizwa ndani humo, kila mmoja alikuwa akimuangalia kwa chuki kuu huku wakitamani akishasomewa mashtaka yake na hukumu ikipita, basi waachiwe mtu huyo wamfanye kile ambacho kwao kitapunguza machungu kwa kiasi fulani kwenye mioyo yao.



    Akapandishwa kizimbani na kuanza kusomewa mashataka yake na kuulizwa kuwa amekubaliana na hilo au anapinga hayo mashtaka? Chaajabu akataka uletwe kwanza ushahidi wa mashtaka hayo, wakaletwa watoto wote waliokuwa wametekwa na vijana wa tajiri huyo na kukiri kwamba tajiri huyo walishawahi kumuona kwenye ngome waliokuwa wametekewa na yeye ndie mkuu wa kikosi kile, pia uliletwa ushahidi uliopatikana nyumbani kwake wa madawa ya kulevya, na kama hiyo haitoshi, pia alishtakiwa kwa kufanya mauwaji ya watu wengi sana kwa siri, baada ya ushahidi wote huo kuletwa mbele yake, akaulizwa tena kama ana chakupinga kutokana na mashtaka hayo.



    Chakushangaza, akayakubali mashtaka hayo, ikimaanisha kwamba, amekubali madawa ya kulevya yaliokutwa nyumbani ni yake, amekubali ni kweli yeye ndie aliekuwa akiwateka watoto na kwenda kuwafungia katika ngome yake na kuwafanyisha kazi hatari na mbaya ya kufunga madawa hayo, amekubali kuwa ni kweli alishaua watu wengi sana bila makosa ya aina yoyote, kila mtu aliekuwa mahakamani hapo alishikwa na ghadhabu kwa mtu huyo, watu wote walitamani hata mahakama itoe hukumu ya kuachiwa mtu huyo kwao ili wamfunze adabu kwa kile alichokifanya, watu wote wakasubiri waone hakimu atatoa hukumu gani kwa mfahari huyo.



    Hakimu aliwaambia kuwa wawaachie nusu saa ya kwenda kujadili na baraza la mahakama kuhusu hukumu ya mtu huyo, wakachukuana baraza la mahakama na kuingia katika chumba flani kilichopo hapo hapo mahakamani na kwenda kujadili hukumu hiyo. Baada ya nusu saa, walitoka wote na kila mwana baraza alikaa katika sehemu aliyokaa mwanzo wakimuacha hakimu akienda kaa katika sehemu yake.



    “Mmm mmm!!" Hakimu alijikohoza kidogo kuweka koo lake vizuri ili aweze kusema hukumu hiyo, kisha akaendelea baada ya kuona mahakama nzima ipo kimyaa kiasi kwamba hata kishindo cha sisimizi kiliweza kusikika pindi atembeapo ndani au nje ya mahakama hiyo kwa muda huo.



    “.............baraza la mahakama limekaa na kujadili juu ya hukumu ya Mr Bakari Haneni kwa makosa yanayomkabili, kwakua ushahidi umeonekana na hata yeye mwenyewe pia amekiri ilo, mahakama inampatia adhabu ya kifungo cha maisha na kazi nzito mpaka pale atakapo fikisha umri wa miaka sitini na tano, ndipo adhabu ya kufanya kazi nzito itaisha ila kifungo kitaendelea hadi kifo chake" hakimu alihitimisha adhabu ya mkwasi huyo na kugonga nyundo akimaanisha kwamba adhabu imepita.



    Watu wengine walilipuka kwa furaha huku wengine wakishikwa na ghadhabu kutokana na adhabu aliyopewa, wao walitaka mahakama itoe hukumu ya kunyongwa kwa mtu huyo, ikiwa hukumu hiyo kwa nchi ya Tanzania ilishafutwa zamani sana. Watu waliotaka Mr Haneni anyongwe walianzisha vurugu mahakamani hapo na kufanya kusiwe na maelewano tena, watu hao walitaka kumfuata mfahari huyo hapo hapo kizimbani ili wamtoe na kumuadhibu wenyewe, ila kwajitihada za jeshi la polisi lililokuwa mahakamani hapo, waliwazuia watu hao na kumtoa mkwasi huyo huku wakiwa wamewadhibiti watu hao vizuri, pamoja na hayo pia hawakuacha kumzibiti mkwasi ili asiweze kuwatoroka askari.



    Askari walifanikiwa kumtoa nje ya mahakama ili wampakize kwenye gari la wafungwa tayari kumpeleka katika gereza la Maweni. Watu ndio walizidi kuchachamaa wakiwataka askari hao wawaachie mtu huyo wamuadhibu wenyewe, kipindi hichi watu ndio waliongezeka zaidi kiasi kwamba asakari waliona dhahiri wanaenda kushindwa na watu hao, ikabidi waombe msaada kwa askari wengine, na kwavile kituo cha polisi hakikuwa mbali na mahakama hiyo, askari walikuja haraka wakiwa wengi kama kumbikumbi kipindi cha mvua, mikononi mwao wakiwa wameshika mabomu ya machozi huku wengine wakiwa wameshika viboko.



    Walipofika hapo hawakutaka kuuliza kuna nini wala nani na nani ana nini, walichofanya wao ni kutembeza kipigo huku wakiwazawadia na mabomu ya machozi, hilo lilisaidia, maana kila mmoja alikimbia kwa njia yake huku wakitoka machozi kama mtoto mchanga alieachishwa ziwa na mama yake ingali muda bado wa kufanya hivyo, baada ya sekunde thelathini katika uwanja huo wa mahakama hapakuwa na raia yoyote aliesalia hapo. Wasubiri nini wakati walishapata kile walichokitaka kutoka kwa askari hao? Kipigo ndicho walichokuwa wakikitaka, ni wazi kwamba walijua wakianzisha fujo mahali hapo, basi jeshi la polisi haliwezi kuwachekea tu kwa wanachokifanya, ilikuwa ni lazima watulize ghasia kwa namna yoyote ile. Gari la magereza liliondoka na wafungwa waliotoka kuhukumiwa siku hiyo, kuelekea gereza la maweni kwajili ya kuwapeleka wafungwa hao kuanza maisha mapya sehemu hiyo, Mr Haneni alikuwa ni mmoja wa wafungwa hao wanaopelekwa.



    Mata na wenzake walipotoka mahakamani, walielekea moja kwa moja nyumbani kwa Mata, walipofika nyumbani hapo, kila mmoja alichukua nafasi yake sebuleni hapo huku akiwa na uso wenye tabasamu kuu.



    “Thiamini, thiamini kabitha kama leo hii nimekuwa tajiri, dah mungu mkubwa thana" Mata aliongea kwa furaha.



    “We acha tu, hunishindi mimi, yani hapa natamani tugawane hata sasa hivi, yani nikipata hizi hela, kwanza nanunua nyumba Kwaminchi maana eneo lile nalitamani sana kuishi, halafu nanua gari kali la kutembelea kisha natafuta mtoto mzuriiii nimuweke ndani, maana nishachoka maisha haya ya ubachela" Moto aliongea hivyo kwa furaha hadi jino lake la mwisho lililokuwa bovu likaoneka.



    “Ila kumbukeni ile nyumba ya kaka na yale magari yaliokuwepo pale nyumbani havipo katika mgawo, hapa tutagawana zile sheli za mafuta na ile showroom ya magari basi" Mrutu aliongea hivyo.



    “Hivyo vitu havina tatizo, tunalijua hilo kuwa zile ni mali za urithi, kwahiyo vile utajua wewe mwenyewe au sivyo Mata" Moto aliongea.



    “Ndivyo"



    “Halafu wakati natoka pale mahakami, nilimuona yule dogo, kumbe na yeye pia alikuwa ametekwa na kundi la Mr Haneni" Moto haikuelewa aliuliza au aliongea.



    “Dogo yupi?" Mata alimuuliza.



    “Hemedy, mtoto wa Mrutu hapa, ambae tulitaka tumuue" Moto alijibu, Mrutu roho ikampiga paaa!! Akajua tayari Hemedy ameoneka na kinachofuta hapo ni mipango ya kumuua ndio itakayoongelewa.



    “Anhaa!!! Thatha tunamfanyaje huyu mtoto, au tumuache tu maana kama ni mali thithi tayari tumeshazipata haina haja tena ya kumuua, au kuna haja ya kufanya hivyo?" Mata aliongea na kuuliza swali.



    “Inabidi afe, kwasababu uhai wake ni hatari kwetu, anazijua sura zetu yule" Moto aliongea, Lakini alimfanya Mrutu achukukie kupita maelezo kwa kauli hiyo.



    “Oya, sikilizeni niwaambie, yule dogo hafi, sasa afe kwasababu gani wakati mali tayari tunazo sisi?" Mrutu aliongea kwa ghadhabu kiasi kwamba wenzake pia wakamshangaa.



    “Kumbuka yule dogo anazijua sura zetu lakini, anaweza akatuona sehemu mbaya halafu ikawa ni hatari kwetu" Moto aliongea.



    “Wewe unasema anazijua sura zenu, una uhakika gani na hilo? Hapana yule dogo hafi na kama akifa labda nisijue nini kimemuua la sivyo tutaleteana Uhasama wenyewe kwa wenyewe" Mrutu alizidi kuongea kwa ghadhabu huku akiwa macho yake ameyatoa kuwaangalia watu hao, aliogopesha, alitishia, yani kama angekuwa akimuangalia mtoto anaekataa kunywa dawa, basi kwa macho hayo angekunywa dozi nzima kwa siku moja, alifanya hivyo kuwaonyesha msisitizo wa kile alichokisema.



    “Mmmhh!! Basi kaka hatokufa kama unavyotaka" Moto aliamua kumshusha hasira kwa kumuambia maneno hayo, kwahilo alifanikiwa, maana mrutu alirudi katika hali aliyokuwa nayo mwanzo.



    “Ok, thatha vipi, kuhuthu kugawana hidhi mali?" Mata aliwauliza wenzake swali hilo, haikujilikana aliuliza hivyo ili kupotezea mada iliyopita au ni kiherehere cha kutaka wagawane mali hizo.



    “Sasa hivi muda umeenda sana, natakiwa niwepo dukani maana yule msaidizi wangu anaumwa, kwahiyo anataka akapumzike, mambo hayo tutayaongelea siku nyengine, ila acheni mimi niende" Mrutu aliaga na kuondoka mahala hapo na kuwaacha wawili.



    “Unajua mimi huyu Mrutu simuelewi kabisa yani na sio leo tu tangia muda naona kabadilika sana yani" Moto aliongea.



    “Mimi mwenyewe nilikuwa namuona muda tu hadi nikashikwa na hofu kwamba mahakamani anawedha kutubadilikia"



    “Ila bwana mimi siwezi kumuacha yule dogo hai, nitamuua kwa njia yoyote ile, tena wala asinitishe kabisa, mimi mwenyewe mtemi vile vile kama yeye anajifanya mtemi, tena asituchimbie biti, ohoooo! mimi nilikuwa namuangalia tu pale anavyoongea kwa kibesi" Moto aliongea sana, nahisi yote hayo kwasababu Mrutu alikuwa hayupo, ila kama angekuwepo sidhani kama angeweza kuongea yote hayo.



    “Hata mimi nakubaliana na wewe ni ladhima tumuue tu"



    * * * *

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Inspekta Ganjo na Hemedy baada ya kuondoka mahakamani walielekea moja kwa moja hadi nyumbani kwake, wao waliwahi kuondoka baada ya kuona vurugu linaanza pale mahakamani, Ganjo yeye ni askari polisi, kwahiyo alijua ni nini kitafuta baada ya vurugu lile, ndio maana akawahi kuondoka akiwa na Hemedy mapema. hata kama yeye ni Inspekta, lakina askari wale wasingeweza kumgundua mapema, kwahiyo na yeye kichapo kingemuangukia bila kujali cheo chake.



    Siku hiyo ikapita, ikangia siku nyengine na siku hii mpya ilikuja na taarifa ya kuwa Hilda anahitajika Daresalam kwa Mkuu wake(mdogo wake na Inspekta Ganjo) mwanamke huyo alimuhitaji Hilda akaishi nae kutokana yeye hakubahatika kuwa na mtoto, kwasababu hakuwa kizazi kutokana na matatizo ya kiafya. Inspekta hakupinga, akamtaarifu Hilda taarifa hiyo, ila ilipingwa vikali akidai hawezi kuondoka na kumuacha Hemedy hapo, kwahakika mtoto huyu alikuwa ni mwenye kumhusudu mtoto mwenzie kupita maelezo.



    Inspekta akamueleza mdogo wake taarifa hizo, kwakuwa mwanamama huyo alitaka sana Hilda akaishi kwake, basi akaomba kama kuna uwezekano Hilda aje na huyo mtu aliedai hawezi kuondoka na kumuacha, taarifa hizo akafikishiwa Hemedy na yeye akakubali kuondoka ila akataka kwanza apewe taarifa hizo baba yake, hilo halikuwa tatizo, Mrutu alifikishiwa taarifa hizo na yeye akazipokea kwa furaha na kuruhusu Hemedy aondoke hata siku hiyo hiyo, alikuwa na furaha kwasababu alijua hiyo itamuweka Hemedy salama na wakina Moto wanaotaka kumuua.



    Taratibu zikafanywa haraka haraka pamoja na kuwaombea uhamisho wa shule watoto hao, baada ya kila kitu kukamilika, siku ya safari ilipofika, watoto hao wakasafirishwa kuelekea katika mji huo pendwa wa Daresalam, masaa sita yalitosha kuwafikisha katika mji huo, wakashuka kwenye basi walilopanda, walikuja kupokelewa hapo stendi ya mabasi Ubungo na kijana. Akawapakiza kwenye gari yake na safari ya kuelekea Kinondoni, sehemu ilipokuwa nyumba ya huyo mkuu wake Hilda ikaanza.



    Hapo hapo stendi kulikuwa kuna gari aina ya Nisan Murano, iliyopakia mahala hapo, ndani yake kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wakimuangalia Hemedy kila alichokuwa anakifanya mahala hapo kabla hajaondoka na kijana huyo aliekuja kuwapokea, baada ya kuondoka gari lililokuja kuwachukua watoto hao, ndipo kijana mmoja akainua simu yake na kupiga namba anazozijua yeye, kisha simu akaiweka sikioni kusikiliza upande wa pili.



    “Ndio mkuu, ameondoka na gari iliyokuja kuwachukua hapa stendi" aliongea kijana huyo.



    “Sawa, endeleeni kumfuatila kila nyendo zake mtoto huyo, msije mkafanya uzembe kama ule mlio ufanya kule Tanga, kuweni makini na mtoto huyo, kiongozi atakasirika kama alivyokasirika mlipofanya uzembe hadi akatekwa na wale vijana wakati yupo katika basi la shule" ilisikika sauti yenye mamlaka upande wa pili.



    “Tuna kuhakikishia mkuu hakuna uzembe wowote mwengine utakao tokea" alijibu kijana huyo.



    “Sawa, nawaamini kwahilo, naamini kazi itakuwa rahisi kuliko vile alivyokuwa kule Tanga, kwahiyo namitakia kazi njema" simu ilikatwa na vijana hao wakawasha gari na kuanza kulifuatilia gari lililokuja kuwapokea wakina Hemedy







    ENDELEA..



    Vijana hao waliendelea kulifuatilia gari lililokuja kuwapokea wakina Hemedy, walilifuatilia hadi lilipoingia katika nyumba moja kubwa ya rangi nyeupe na wao wakapaki gari yao mbele kidogo na nyumba hiyo na kutulia hapo. Huko ndani ya nyumba hiyo, walishuka kwenye gari na kuanza kuingia ndani ya nyumba huku mabegi yao yakiletwa na kijana alieenda kuwapokea stendi, waliingia sebuleni na kukaa hapo baada ya kutomkuta mtu yoyote mahali hapo, baada ya sekunde kadhaa alitokea mwanamke wa makamo, mwanamke huyo alikuwa ni kibonge, mfupi, mwenye rangi ya maji ya kunde, Hilda alipomuona mwanamke huyo, aliinuka kwenye sofa alilokaa na kwenda kumkumbatia kwa furaha.



    “Za safari wanangu?" aliwauliza swali hilo baada ya Hilda kumuachia kumkumbatia.



    “Salama tu, shikamoo" walijibu wote kwa pamoja.



    “Marahaba. Haya niambie za huko" aliongea mama huyo huku akichezea nywele za Hilda aliekuwa amekilaza kichwa chake kwenye mapaja yake wakiwa wamekaa kwenye sofa jengine, tofauti na lile alilokaa Hemedy.



    “Nzuri tu, hatujui za hapa" Hilda alijibu, mwanamke huyo alikuwa na furaha ya hali ya juu baada ya Hilda kuwa nyumbani kwake, mtoto huyo alimtaka tangia mama yake alipofariki, ila Inspekta Ganjo, aliweka ngumu kwa kudai asubiri kwanza akue kue, na leo hii yupo nyumbani kwake alikuwa na furaha ya aina yake.



    “Baba na wewe unaitwa nani?" Mkuu wake Hilda alimuuliza Hemedy.



    “Hemedy, Hemedy Bhachu Mheshimiwa" alijitambulisha Hemedy majina yake yote matatu utafikiri aliambiwa afanye hivyo.



    “Karibu baba, karibu jisikie upo nyumbani"



    Waliendelea na maongezi hadi pale chakula kilipokuwa tayari na wote watatu wakaelekea mezani kwenda kula. Walipomaliza kula, kila mmoja akaonyeshwa chumba atakachokitumia hapo, na kila mmoja aliingia katika chumba alichopewa kwenda kufanya anayoyajua yeye mwenyewe.

    Siku mbili mbele, Hilda na Hemedy, walienda kuanza shule, darasa lile lile la tano waliloishia huko Tanga.



    Tanga. Nyumbani kwa Mata. Saa 6:00 Mchana.



    Siku hii walikutana tena kwajili ya kupanga mipango yao ya kuuza mali zao.



    “Inabidi tuziuze hizi mali kama tulivyo kubaliana, kisha tugawane pesa zitakazo patikana" Mrutu aliongea.



    “Hilo ndio la muhimu, sasa mtu wa kununua vitu vyote hivyo, atapatikana wapi?" Moto aliongea.



    “Mimi kuna tajiri mmoja nimempata, anatokea Arusha, amethema atanunua hizo sheli dha mafuta, ila akathema akija kuziangalia hidho sheli, bathi ataangalia na hiyo showroom ya magari, kama ataikubali, bathi atainunua nayo" Mata aliongea.



    “Huyo tajiri umempatia wapi?, asije akawa ni tapeli" Mrutu aliongea.



    “Huyo nimempata mtandaoni, baada ya kutoa tangadho kwenye webthite yangu, ndipo akachukua namba yangu na akathema kesho kutwa atakuja huku Tanga kuja kudhicheki hidho kampuni"



    “Basi sio mbaya, ili mradi kila kitu kiende sawa"



    Wakafunga kikao chao na kila mmoja akaondoka zake kuelekea anapopoajua yeye huku wakiisubiria hiyo siku atakayo kuja huyo tajiri kutoka Arusha kuja kununua hizo kampuni.



    Siku mbili hazikuwa nyingi, siku ya siku ikafika na kweli huyo tajiri alikuja na kutaka kuonyeshwa hizo kampuni, safari hii walikuwa wote watatu, wakimtembeza tajiri huyo aliekuwa akitembea na ulinzi wake, walimpeleka kila sehemu zilipo kampuni hizo na kumuonyeasha kila kitu, baada ya kuzunguka masaa kadhaa, wakatafuta sehemu nzuri itakayo wawezesha kuongea kwa kina kuhusu malipo.



    Wakaonelea swala hilo wakaliongelee katika hoteli, wakachagua hoteli moja tulivu sana, iliyokuwa pembezoni ya bandari ya Tanga, NYUMBANI HOTELI ndio hoteli waliochagua kuliongelea swala hilo. Wakafika hadi hapo na kuchagua sehemu moja tulivu kwaajili ya maongezi hayo.



    “Ndio mabwana, kampuni nimeziona na zote nimezipenda na nipo tayari kuzinunua" Aliongea Tajiri huyo baada ya kukaa sehemu ambayo kwao wameiyona ni nzuri kwa maongezi yao.



    “Ndio hivyo, dhote dhipo kamili, hakuna hata kitu kimoja kilichopungudhwa"



    “Mmiliki halali wa zile kampuni ni nani?" Tajiri huyo aliwauliza.



    “Ni mimi" Mata alijibu.



    “Ok, naomba nione hati miliki, ili nijiridhishe nafsi" aliongea tajiri huyo na kumfanya Mata aufungue mkoba aliokuja nao hapo, akatoa makaratasi na kumkabidhi, alipojiridhisha, akayarudisha makatasi yale kwa Mata. Baada ya hapo, wakaelewana bei kuwa kampuni zote wataziuza kwa kiasi gani, baada ya maelewano zikafuta taratibu nyengine za kuuziana kampuni hizo, mambo yalifanywa haraka haraka, wakawekewa pesa zao walizozihitaji kwenye benki waliyoitaka na kuanzia hapo, hawakuwa na chao tena, labda chao kilikuwa ni hizo pesa tu.



    Baada ya kila kitu kuenda kikamilifu, wakachukuana wenyewe watatu na kuongozana hadi nyumbani kwa Mata huku nyuso zao zikiwa na bashasha kila muda.



    “Zile pesa ni nyingi sana, kwahiyo huo mgawo naomba ufanyike leo leo, kwasababu panaweza kutokea mmoja wetu akaingiwa na tamaa na kutaka kuzichukua pekeake" Mrutu aliongea kuwaambia wenzie.



    “Ulichoongea ni chamaana sana, kama vipi hii ishu tuifanye hata sasa" Moto aliongea.



    “Haaa!! Yani petha dhimewekwa leo benki halafu dhikatolewe leo leo, kwandha haitowedhekana kutoa petha nyingi kiasi kile kwa wakati mmoja"



    “Hilo tunalijua, yani hapa chakufanya ni kupangiana kila mmoja atachukua kiasi gani kwenye zile pesa, kisha tunaenda kuzihamisha tu kila mmoja kwenye akaunti yake, naamini hilo litakuwa jepesi zaidi kuliko kuzitoa halafu tuanze kugawana" Mrutu aliongea.



    “Sasa mimi ambae sina akaunti benki nafanyaje?" Moto aliuliza.



    “Si unafungua akaunti tu halafu ndio unaziamisha kwenye akaunti hiyo" Mtutu alimjibu.



    “Hapo sawa" alikubali na wakaanza kupangiana kila mmoja atachukua kiasi gani kwenye hizo pesa, waligawana sawa sawa, baada ya hapo, wakaongozana hadi benki, huko walifanya kama walivyopanga, kilikuwa ni kitendo cha nusu saa tu, kila kitu kikawa sawa, na kila mmoja akafa kivyake.



    Mrutu kipindi hichi alikuwa anaishi katika nyumba ya marehemu kaka yake, ile nyumba yake aliipangisha na kuhamishia makazi kwenye nyumba hiyo ya ghorofa mbili. Alipotoka benki, akanyoosha moja kwa moja hadi katika nyumba hiyo na kuingia ndani, akaenda hadi katika chumba alichokuwa akilala kaka yake na mke wake, chumba hicho ndio alikifanya ni chumba chake kwa wakati huo, alipofika ndani ya chumba hicho, akakaa kitandani na kuangalia mandhari ya chumba hicho utafikiri ndio mara yake ya kwanza kuingia humo, chumba hicho kilikuwa kina vitu vichache ila vilikuwa ni vya thamani ya hali ya juu.



    Baada ya kupepesa macho yake kwa muda mrefu, macho yake yakatua katika ukuta wa chumba hicho, kulikuwa na picha moja yenye taswira mbili zilizokuwa na tabasamu kwenye nyuso zao, sura hizo zilikuwa ni Mheshimiwa Bhachu na mke wake wakiwa wapo pamoja kwenye picha hiyo. Mrutu aliiyendea picha hiyo na kuishika ikiwa bado ipo hapo hapo ukutani.



    “Pumzikeni kwa amani kaka na shemeji huko mlipo, zile zilikuwa ni tamaa za pesa tu zilizonikumba kipindi kile, japokuwa kaka yangu ulilkuwa unanipa kiasi chochote ninachokitaka kwako, ila sikuridhika nikataka na mimi niwe kama wewe, ndipo niliposhawishika kukufanyia ubaya kaka yangu bila kosa lolote, nikashiriki kuitoa roho yako na ya mke wako, tulipanga tumuue na mwanao ila hilo limeshindikana hadi sasa nipoongea haya, nakiri mbele ya picha yako, nitamtunza mwanao hadi kifo chake au kifo changu, naamini kwa kufanya hivyo, mtanisamehe kwa yote niliyoyafanya juu yenu, pumzikeni kwa amani na mungu amiweke mbali na adhabu zake" aliongea hayo huku machozi ya uchungu yakimtiririka kwenye macho yake, aliigeuza ile picha upande wapili ili kuziziba taswira za watu hao, maana kila akiiangalia picha hiyo, anaona kama vile zile taswira zina msuta na kumlaumu kwa kile alichokifanya, alijitupa kitandani kuusaka usingizi japo kuwa usiku bado haukuingia.



    * * * *







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog