Simulizi : Uhasama
Sehemu Ya Tano (5)
Majira ya usiku nyumbani kwakina Hilda. Baada ya kumaliza kula, Anti yao aliwaaga na kwenda kulala huku akiwaacha vijana hao wakiangalia luninga iliyokuwa hapo sebuleni. Hemedy nae alimuaga Hilda na kuingia chumbani kwake kwajili ya kwenda kulala na yeye, alipofika, akavua nguo na kubakiwa na bukta tu, akaingia chooni, choo ambacho kilikuwa humo humo chumbani, alipotoka huko alikuwa akijifuta maji kuashiria alitoka kuoga. Ila ghalfa aliganda kama anataka kupigwa picha baada ya kumuona Hilda akiwa kitandani kwake amekaa huku akimuangalia yeye kwa tabasamu pana usoni mwake.
“Wewee! Umefuata nini chumbani kwangu?" Hemedy alimuuliza huku akiwa bado ameganda vile vile na taulo lake mkononi.
“Mbona muoga hivyo? Embu njoo tulale bwana" Hilda aliongea hivyo huku Akitabasamu, akajilaza kitandani na kumfanya Hemedy akose cha kusema, akapiga hatua na kuiendea henga, kisha akaliweka taulo juu yake na kubakiwa na bukta na kwenda kitandani alipolala Hilda, akamuangalia kwa muda, kisha na yeye akajiweka juu ya kitanda hicho, wakawa wanaangaliana bila kujua ni kipi kinachowafanya waangaliane hivyo.
Katika kuangaliana hiyo, ikapekea hisia flani ziwakumbe kwenye miili yao na kujikuta wakianza kushikana shikana baada ya kusogeleana. Walifanya hivyo hadi pale Hemedy alipo panda juu ya banati huyo na kujikuta akitaka kufanya kitu ambacho sio akili yake iliyomtuma kufanya hivyo, alianza kutalii kwenye mwili wa binti hadi alipofika sehemu ambayo binti hakuruhusu kirahisi Hemedy ainyemelee. Nilipoona hivyo, nikageuza macho yangu kuangalia pembeni huku nikiwaacha wenyewe wakiendelea kuminyana, huyu akitaka kufanya kitu falani na huyu akikataa kitu hicho kisifanyike.
Baada ya dakika thelathini, nikageuka kule walipo baada ya kusikia sauti ya kilio cha Hilda, hapo nilishuhudia mashuka yakiwa yamepambwa kwa damu huku Hilda akiwa analia ameegamia kwenye ukuta ambao umeachiana na kitanda kwa milimita moja, akiwa amejifunika shuka kuanzia kwenye kifua kuja chini.
“Hemedy ndio umenifanya nini hivi? Kumbe unaroho mbaya kiasi hichi? Hujui kama mwenzako nilikuwa naumia? Haya ona sasa umenitoa ushichana wangu bila ridhaa yangu, umenimwaga damu yangu pasi na huruma halafu eti unajifanya unanipenda. muongo hunipendi wewe hihihiiii”Haa!! Ilishangaza Hilda kusema eti ametolewa usichana wake bila ridhaa yake, kama ni hivyo, sasa ni kipi kilichomfanya hadi akataka kulala kitanda kimoja na rijali Hemedy, sijui alitaka wachekeane tu hapo kama matahira? Aaa!! Lakini hayakuwa yakinihusu hayo.
“Hilda nisamehe, sikujua kama nitakuumiza kiasi hichi, hayakuwa malengo yangu kukutoa damu kiasi hichi" Hemedy aliongea hivyo huku akiwa amekunja mikono yake ishara ya kuomba msamaha. Wakati huo alikuwa amekaa mwisho kwenye ukingo wa kitanda huku mguu mmoja akiwa ameuning'iniza chini huku mwengine ukiwa juu ya kitanda akiwa ameukunja.
“Muongo, muongo Hemedy. Mimi si nilikuambia kuwa unaniumiza lakini wewe ukajifanya hunisikii. Haya sasa umenisababishia tatizo ambalo sijui pia nitalisovu vipi" Hilda aliongea huku akiwa anaendelea kulia, ila safari hii hakuwa akilia kama mwanzo, sasa hivi alikuwa akilia kilio cha chini chini.
“Tatizo gani hilo?" Hemedy aliuliza kwa wahka.
“Leo nipo katika siku za hatari Hemedy!" La haula!! Hemedy macho yalimtoka pima mithili ya mtu aliekutana na mala
“Leo nipo katika siku za hatari Hemedy!" Hemedy macho yalimtoka pima mithili ya mtu aliekutana na malaika mtoa roho uso kwa uso.
“La...la...lakini mimi sijamwagia ndani" Hemedy aliongea hivyo huku dhahiri akionekana akiwa na aibu ilichanganyikana na uoga.
“Hujamwagia ndani kitu gani........? Sina nakuuliza?" Hilda aliongea kwa kufoka na kumfanya Hemedy akose cha kusema na kubaki kimya tu utafikiri hakusikia hilo swali aliloulizwa.
“Subiri tuone, kwani mwezi ni mbali, na sijui kama ikiwa hivyo itakuaje jamani. Ila yote umeyataka wewe Hemedy, sijui nitatembeaje masikini mimi. Hemedy umeniumiza sana yani" Hilda aliongea kwa malalamiko, ila muda huu hakuwa akilia.
Akamsogelea pale alipo“ Hilda kama ambavyo damu yako imemwagika mbele ya macho yangu, ndivyo ambavyo nitakavyo utunza upendo wangu kwako, sitoruhusu hata kwa sekunde utoe chozi lako eti kisa nimekuacha au nimekusaliti. Nakupenda Hilda na wewe huna haja ya kunijibu kwamba unanipenda pia, hii damu ambayo imetoka limelijibu hilo neno" Akamfuta machozi kwa kutumia vidole vyake kisha akampiga busu moja la kwenye paji la uso. Bilashaka Hilda yale maumivu yote aliyasahau hapo hapo, maana alikuwa ni mwenye kutabasamu tu baada ya kuyasikia maneno hayo.
“Nipishe huko niende zangu" Hilda aliongea hivyo, akajinyanyua hapo alipo huku akiwa bado ameshikilia shuka lisimdondoke mwilini mwake. Hemedy alikuwa akimuangalia tu muda wote huku akitabasamu.
“Fumba macho yako nivae nguo zangu. Lione linatabia mbaya tu kuchungulia wenzake" Hilda aliongea hivyo baada ya kushuka kitandani na kumuona Hemedy anamuangalia tu muda wote. Akageukia ukutani na kumfanya binti huyo aliachie shuka alilojiziba nalo na kuvaa nguo zake, baada ya hapo alianza kupiga hatua za kudema dema kama mtoto mdogo anaefundishwa kutembea huku akigugumia kwa sauti za puani. Sauti hizo zilimfanya Hemedy ageuke na kumkuta ndio anataka kufungua mlango wa kutoka.
“Sasa Hilda na haya mashuka je?" Hemedy aliongea hivyo huku akiyasontea mashuka kidole. Hilda akageuka na kumuangalia yeye.
“Yatandike halafu ulale hivyo hivyo" kisha akafungua mlango na kuondoka zake. Hemedy aliyatoa mashuka hayo na kuyaweka kwenye deli lake la nguo chafu, akachukua mengine na kuyatandika, kisha akajibwaga hapo kitandani chali. Ila ghafla alikurupuka baada ya kukumbuka kitendo alichotoka kukifanya muda mfupi, moja kwa moja akaelekea chooni.
* * * *
“Kwanini lakini unanichukia kwa kosa ambalo si la kweli? Hutaki hata kuniona kwa kosa la kupangwa ili mimi na wewe tuachane Hawa? Mwenzako najihisi furaha pale ninapokuona hata kama unanichukia. Hawa lile tukio usingelipa maamuzi ya papo kwa hapo bila hata ya kulifikiria na kuniuliza ilikuaje. hukutakiwa kuchukua maamuzi ya haraka namna ile, tena kwa kutaka kuniumiza, ukaamua ukaanzishe mapenzi na Babel kwa haraka ili tu nafsi yangu iume, nakupa pongezi kwa hilo kwasababu umefanikiwa kwa asilimia mia kuumiza moyo wangu dhaifu, nakupa hongera kwa kunifanya nitoe machozi kila mara ninapokufikiria, nakupa pongezi kwa kunifanya hata nisahau kula au kuoga pale inaponijia picha yako usoni kwangu. Laiti ungejua kwamba huyo ulieamua kuwa nae kwasasa hana nia nzuri na wewe, wallah usingejaribu hata kumuita jina lake achana na kuwa nae karibu tu. Hawa tambua hakuna mwanaume akupendae kwa dhati zaidi yangu mimi, hao wote wanataka kuuchezea tu moyo wako na kuuacha ukibubujikwa na machozi ambayo kwangu itakuwa ni mfadhaiko mkubwa kwenye mtima wangu. Hawa naomba niwe muokozi wa moyo wako, naomba urudishe imani yako kwangu. Bado Nakupenda Hawa wangu" Ramah alikuwa akilalamika mbele ya mnyange huyo wakati wakiwa shule kwenye eneo la kutupa takataka asubuhi hiyo walipokutana wote wakiwa na vindoo vilivyokuwa na mataka baada ya kuyamwaga kwenye shimo.
“Ramah tambua kwamba mapenzi yetu yaliisha siku ile ile nilipokufumania ukiwa na yule mwanamke wako mkitaka kufanya uchafu wenu kule nyuma ya vyoo. Ramah umenifanya nilie zaidi yako wewe unaelia kilio cha kuigiza mbele yangu eti ukitegemea utairudisha imani yangu kwako, moyo wangu ni mgumu sana kumsamehe mtu alienitenda kimapenzi, nenda kawafuate hao hao wazindaki wenzako wamapenzi, hao ndio ambao utakao endana nao ila sio mimi tena" Hawa aliongea huku akimuangalia kijana huyo kwa nyodo huku mdomo wake akiwa ameupindisha mthili ya mgonjwa wa kifafa.
“Hawa tambua hujui ukijuacho, siku ukija kujua kuwa ukijuacho ulikuwa hukijui, utakuwa umeshachelewa, ila hata kama utakuwa umechelewa, basi tambua akupendae kwa dhati yupo na anakusubiri na kukukaribisha muda wowote" Ramah alipoongea hivyo, akaondoka huku akimuacha banati huyo akiyafikiria maneno hayo ya mwisho.
“Aaa!! Hana lolote kaishiwa na maneno" Aliongea mwenyewe kwa sauti ya chini na kuondoka hapo kuelekea huko anakotakiwa awe. Sio kwamba Hawa hakuwa akimpenda tena Ramah, la hasha! Bali alitaka na yeye apate maumivu kama yale aliyoyapata yeye kipindi anamfumania.
Hilda alijitahidi kumbembeleza rafiki yake aachane na Babel arudiane na Ramah huku akimkumbusha kuwa Babel ni pendapenda wala hana mapenzi ya kweli naye, ila yeye aling'ang'ania msimamo wake kuwa hatoweza kumsamehe Ramah kwa kile alichomfanyia.
“Lakini mboma Hilda unanilazimisha nirudiane na Ramah wakati amenitenda nikiwa naona kabisa?" Hawa alimuuiza hivyo Hilda wakati wakiwa kantini wakipata chakula.
“Wewe hujui Hawa, ule ulikuwa ni mchezo tu wa kuwaachanisha wewe na Ramah. Lakini hakuna ukweli wa aina yoyote kwa unachokifikiria" Hilda aliongea.
“Hilda wewe unasema hivyo kwa vile hujawaona walichokuwa wanafanya kule nyuma ya vyoo na yule mwanamke wake, naamini kama ingekuwa umeona wala usingethubutu kuniambia maneno hayo"
“Sikiliza Hawa nikuambie. Ule ulikuwa ni mpang....." Hilda alikatishwa na sauti kali ya Hawa.
“Hawa tutagombana sasa hivi, maana naona unapenda unione nikilia kila muda. Ohooo, we endelea tu kuniambia hayo mambo" Hawa alionekana dhahiri akiwa amekasirishwa na maneno ya Hilda aliekuwa akimtaka aachane na Babel arudiane na Ramah.
“Mmh! Basi shosti tusije kugombana bure kwa mambo ambayo hayana ulazima kwangu" Hilda aliongea hivyo huku akijifuta mdomo wake kwa kitambara baada ya kumaliza kula. Wakachukuana kuondoka hapo kuelekea darasani.
* *
Siku hiyo Babel alimchukua Hawa na kwenda nae Mikadi Beach kwenda kufurahia nae. Ndio, alikuwa na haki ya kumfanyia binti huyo chochote anachokitaka ili mradi na yeye apate anachokitaka. Hakuanzia kwa binti huyu tu kufanya hivyo, bali ni kwakila binti ambae ataingia kwenye mikono yake, lazima amfanyie vitu vingi ilimradi apate kile anachokitaka kisha hapo amtelekeze na kumuacha akilia pekeake. Hiyo ndio ilikuwa tabia yake, yupo radhi apoteze kiasi kikubwa cha pesa lakini na yeye apate kile akitakacho. Na alikuwa na msemo wake kuwa akipita mara moja basi harudii tena. Kinachomtia ujeuri ni mali za baba yake ambae kwake alikuwa na mtoto huyo huyo mmoja tu, alikuwa akimpenda kupita maelezo, alimuachia gari atembelee nalo kila sehemu anayotaka kuenda na sio kumuachia gari tu, hata kiasi cha pesa atakachoomba pia hupewa.
Na siku hii alikuwa na Hawa kwenye ufukwe huo wakifurahia, sio kwamba alikuwa akimpenda sana mnyange huyo, laa! Alikuwa na lake aliatakalo na akishalipata basi humuacha akimlilia pasi na kumuonea huruma.
“Hawa unajua mimi nakupenda sana" Babel aliongea hivyo wakati wakiwa wamekaa kwenye viti katikakati yao pakiwa na meza iliyochafuliwa kwa vyakula na vinywaji mbalimbali.
“Najua baby kuwa unanipenda na ndio maana unafanya kila uwezalo ili kunifurahisha" Hawa aliongea hivyo huku aking'ata paja la kuku aliekaangwa kwa ustadi mkuu.
“Sasa kwanini wewe hunipendi?" Babel aliuliza swali liliomfanya Hawa aache kutafuna nyama hiyo na kumuangalia yeye.
“Kwanini?" Hawa alimuuliza.
“Kwasababu kila ninapokuambia tufanye mapenzi wewe unanizungusha” Haa!! Inamaana kufanya mapenzi ndio kipimo cha kumpenda mtu? Sio mimi tu nilie jiuliza hilo swali, hata Hawa na yeye pia alijiuliza lakini akakosa jibu sahihi la swali hilo.
“Baby wala usijali, ipo siku tu utakuwa na mimi kitanda kimoja" Hawa aliongea hivyo huku akiwa na mashaka na mtu huyo.
“We kila siku ni mtu wa kuniambia hivyo hivyo tu nisijali, hujui kama mwenzako nashindwa kuvumilia, sasa kama usiponipa wewe unadhani nani mwengine atanipa. acha zako bwana we kama hunipendi niambie" Babel aliongea kwa ghadhabu kiasi kwamba hata Hawa pia alishangaa, kisha akainuka hapo na kuanza kuondoka.
“Jamani mpenzi unaenda wapi sasa?" Hawa nae alipoongea hivyo, akachukua pochi yake iliyokuwa juu ya meza na kuondoka kumfuata mwanaume huyo anapoelekea huku wakiviacha vyakula vikiwa vingi juu ya meza.
* *
Siku zilipita na kidato cha nne wakamaliza kufanya mitihani yao, wakawa sasa wakijiandaa kusherekea mahafali yao siku moja inayofuata. Siku ya jumamosi ndio siku ambayo ilipangwa mahafali hayo, walikuwa na shamrashamra za maandalizi hayo. Wahenga hawakukosea kuusema ule msemo wa ‘siku hazigandi' na nikweli siku hiyo haikuganda. Siku hiyo ikapita na kuingia siku iliyosubiriwa na wanafunzi wengi wa shule hiyo. Siku ya mahafali ya kidato cha nne.
Shamrashamra ziliendelea ndani ya ukumbi, wanafunzi walioteuliwa kwaajili ya kuhakikisha ukumbi unakuwa wa kupendeza, waliifanya kazi yao ipasavyo, hadi majira ya saa nane mchana, ikawa kila kitu kipo kama kilivyopangwa, ikawa unasubiriwa muda tu wa shuhuli hiyo kuanza na muda wenyewe ulikuwa ni saa kumi za jioni. Wanafunzi hao wakarudi nyumbani kwaajili ya kujiandaa ili muda utakapofika warudi wakiwa wamependeza.
Majira ya saa kumi, wanafunzi wengi walionekana wakiingia shuleni hapo wakiwa wamependeza kuliko kawaida, kila mmoja hakutaka kuwa nyuma siku hiyo kwa kutokelezea, kila mmoja alivaa vile alivyoona kuwa vitampendeza siku hiyo, hawakuwa wanafunzi tu, hata wazazi pia walihudhuria kwenye mahafali hayo. Wanafunzi waliowekwa kwaajili ya kuwapokea na kuwaelekeza sehemu inapofanyika sherehe hiyo, walikuwa wakipishana kuwapeleka wazazi sehemu husika.
Muda ulipofika, wanafunzi wote na wazazi walikaa sehemu iliyopangwa kwajili yao huku walimu na mgeni rasmi wakikaa sehemu yao. Mahafali yalianza kwa kusomwa sala fupi kisha ikafuatiwa na risala iliyosomwa na huyo huyo mwanafunzi. Baada ya hapo ratiba nyengine zikaendelea. Wanafunzi wa kidato cha nne walioyofanya vizuri kwenye mtihani uliopita kabla wa taifa, walipewa zawadi mbalimbali kulingana ufaulu wao.
Baada ya zoezi hilo lililochukua saa nzima kuisha. Ikafutia burudani zilizopangwa kutolewa na wanafunzi, walianza wao kidato cha nne kutoa burudani zao za mashari ya kuwaaga wenzao, kisha likafuatia igizo la vijana wa kidato cha pili na cha kwanza. Baada ya wao kutoka, wakafuatia mapacha nao wakawachekesha watu waliohudhuria hapo kwa nafasi yao, na wao wakamaliza na kuingia Hemedy. Wanafunzi wote walilipuka kwa shangwa na makofi yalichagizwa na vifijo na mbinja baada ya kijana huyo kupanda kwenye jukwaa.
Alipofika hapo, akakamata kipaza sauti na kuanza na salamu. Kisha akatoa hadithi iliyowafanya watu wazisahau kama sio kutozikumbuka kabisa shida zao na matatizo kwa kucheka kila anapoweka kituo. Hadithi hiyo ilichukua dakika kumi na tano akamaliza na kushuka kwenye jukwaa huku akisindikizwa na makofi ya pongezi.
Ilibakia burudani ya mwisho, burudani ya kuimba, walianza vijana wawili, wakaimba wote kwa pamoja na akafuatia na yule binti nae pia akaimba kisha akashuka baada ya kumaliza. Akawa bado Ramah kupanda kwenda kuimba. Akanyanyuka sehemu aliyokuwa amekaa na kuanza kupiga hatua kuelekea juu ya jukwaa. Wanafunzi waliokuwepo darasani siku ile wao ndio waliompigia makofi huku wengine wakishangwaza na kitendo hicho cha kusikia kuwa Ramah na yeye pia ni muimbaji. Alipofika juu ya jukwaa na yeye akatoa salamu kama walivyofanya wenzake kisha akaliweka koo lake sawa tayari kwa kuimba.
“Baby kama ujana yote nilokupa, tayari nilikupa moyo wangu ili ukae naoo. Leo upendo unanifanya nilie, machozi yafunga mboni zangu nashindwa kutazama. Pendo langu umelizima kamshumaa, umenidharau, umeninyima hata heshima. ×2. Kama wamekuambiaa, mi nakuzinguaa, amini na siku moja ukweli utaujua. Hutofurahiaa, penzi bandiaa, lakweli lipo kwangu na we hujaridhiaaa aaaa.
Bado naamini, nitakuwa na wewee, japo thamini, ila chagua langu wee. Bado naamini, nitakuwa na wewe, japo thamini, ila nitakuwa na wewee, one day.
Kama ni kosa mi kukupenda wewe semaga unanichukiaaa, marafiki wanasemaga, alifichiki pendo mamiyoo, nikikuona mwenzioo, najawa na furaha nakufikiria sanaa aaaa.
Pendo langu umelizima kamshumaa, umenidharau, umeninyima hata heshima. ×2. Kama wamekuambiaa, mi nakuzinguaa, amini na siku moja ukweli utaujua. Hutofurahiaa, penzi bandiaa, lakweli lipo kwangu na we hujaridhiaaa aaaa.
Bado naamini, nitakuwa na wewee, japo thamini, ila chagua langu wee. Bado naamini, nitakuwa na wewe, japo thamini, ila nitakuwa na wewee, one day”.
Ramah aiimba kwa ustadi mkubwa na kwa hisia kali sana, akifuatisha biti ya nyimbo hiyo iliyowekwa kwenye muziki uliokuwa humo ndani ya ukumbi. Watu wote walimpigia makofi huku wengine wakidiriki kwenda kumtunza kabisa kwa jinsi alivyoiimba nyimbo hiyo ya msanii maarufu hapa nchini anaeitwa Ibrahnation nyimbo hiyo aliita NAAMINI. Ilikuwa ni nyimbo nzuri iliyowafanya watu wanaoijua kuenda nae sawa wakati akiwa akiimba huku wakitingisha vichwa taratibu kwenda kulia na kushoto.
Watu wote walilipuka kwa shangwa huku wakimpigia makofi wakati akiwa anashuka. Akaitwa na mgeni rasmi na kuenda kupeana nae mkono huku wakipiga picha ya pomoja, hapo akapeana mikono na walimu wote waliokuwa kwenye meza hiyo huku wakipambwa na matabasamu usoni mwao, kisha akarudi sehemu alipokuwa amekaa yeye Hemedy na Hilda.
Hawa nyimbo hiyo ilimfanya aingiwe na ubaridi wa ghafla mwilimi mwake, kwa mara ya kwanza alijutia uamuzi wake wa kuachana na kijana huyo. Sio kwamba eti kwavile alikuwa na kipaji cha kuimba ama kwavile alipongezwa na watu wote hapo ukumbini? Laa hasha! Bali ni kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa kijana huyo, aliamua kuachana nae ili tu na yeye apate maumivu kama aliyoyapata yeye wakati akiwa anamfumania.
Kama wamekuambiaa, mi nakuzinguaa, amini na siku moja ukweli utaujua. Hutofurahiaa, penzi bandiaa, lakweli lipo kwangu na we hujaridhiaaa aaaa........
Maneno hayo kwenye hiyo nyimbo aliyoiimbaa Ramah, yalijirudia kwenye ubongo wake na kumfanya moyo wake uzidi kumuuma.
Kama ni kosa mi kukupenda wewe semaga, unanichukiaaa, marafiki wanasemaga, alifichiki pendo mamiyoo, nikikuona mwenzioo, najawa na furaha nakufikiria sanaa aaaa.
Alipo yakumbuka na maneno hayo, akashindwa kuvumilia kukaa hapo ndani, akatoka nje ya ukumbi mbio mbio huku akiwa ameweka kitambara chake usoni ili kuyazuia machozi yanayomtoka yasionekana na watu wengine. Babel nae baada ya kumuona Hawa ametoka nje akiwa kwenye hali hiyo na yeye akatoka kumfuata huko huko.
ENDELEA
“VIPI MPENZI, mboma umetoka ukumbini haraka namna hii huku unalia? Au ni yule boya ndi....." Babel alimfuata Hawa aliekuwa yupo nje ya ukumbi kwenye mti ameuigamia. Ila alikatishwa na sauti kali ya Hawa.
“Niache usinishike. Nani mpenzi wako?" Hawa aliongea kwa hasira na kumfanya kijana huyo amshangae sana.
“Nini Hawa kimekukuta? Mbona sikuelewi?" Babel aliongea huku akijaribu kumshika mkono, ila mkono wake ulipangulia kwa hasira.
“Nimekuambia usiniguse. Kahaba wa kiume wewe" Hawa aliongea hivyo na kumfanya Babel ashikwe na hasira za ghafla kwa kutukanwa tusi hilo na mwanamke huyo. Akainua kono lake la kushoto na kulivutia kasi kutaka kulipeleka kwenye shavu la mnyange huyo, ila kono lake liliishia kati baada ya kuzuia na mtu alietokea hapo ghafla.
“Mmh mmh!! Umeona wapi mwanamke akapigwa namna hii? We kama hakutaki usimlazimishe, nenda kawapige hao hao makahaba wenzako uliozoea kuwapiga lakini sio huyu" Hemedy ndie aliezuia kono la Babel lisitue kwenye shavu la Hawa. Aliongea hivyo huku akilirusha kwa pembeni kono hilo. Kitendo hicho Babel alikitasfiri ni dharau kama sio udhalilishaji mbele ya mwanamke.
Hemedy alimfuata Hawa aliekuwa yupo pembeni akilia na kumyanyua. Babel alishindwa kuzizuia hasira zake, akataka kwenda kumvaa pale pale alipo Hemedy, ila alijikuta akizuiwa na kundi la wenzake lililokuwa limefika hapo baada ya kumuona mwenzao ametoka nje kumfuata Hawa huku Hemedy nae akitoka nje. Wakajua tu huko hakutakuwa na usalama kama ikiwa na Hemedy ametoka nje, ikabidi na wao watoke.
Babel alikuwa aking'ang'ania kuchomoka kwenda kumvaa Hemedy kwenye mikono ya wenzake waliomshika barabara huku wakimsihi atulize munkari maana walimjua kijana huyo hakawii kufanya fujo sehemu yoyote ile.
Hemedy baada ya kufanikiwa kumnyamazisha Hawa aliekuwa akilia muda wote. Alimuongoza kuingia nae ndani ya ukumbi, alimpeleka hadi kwenye meza waliyokuwa wamekaa wao watatu na kumuunganisha na yeye akawa wanne. Kipindi chote hicho, Ramah wala hakuwa na habari nae, alikuwa akichezea simu tu hakuangalia sehemu yoyote, hata pale Hawa alipotoa salamu, yeye alijifanya kutoisikia salamu hiyo. Alikuwa ‘busy' na simu yake.
Hawa akawa hana raha hata tangu afike hapo, japokuwa Hemedy na Hilda wajitahidi kumsemesha na kumfurahisha, lakini kama alikuwa akitabasamu, basi hazizidi hata sekunde tano anakuwa amenyamaza na kuwa vile vile uso wa mashaka. Walijitahidi kuongea stori ambazo walimshirikisha na Ramah, lakini yeye alikuwa akiwajibu kwa kichwa tu na kuendelea na kucheza na simu yake. Hawakuwa na jinsi zaidi ya kutulia na kuendelea kuangalia shuhuli inavyoendelea. Wanafunzi wengi hasa wa kike walikuja wakitaka picha na Ramah na yeye alipiga nao bila ajizi, kitendo hicho kilimuuma sana Hawa, akatamani angekuwa na uwezo wa kuwakataza watu hao wasipige na Ramah picha, lakini angeanzia wapi ikiwa yeye na huyo kijana wamenuniana? Asingeweza kamwe!.
Tena kibaya zaidi alipokuja Shamsa kupiga picha nae, hapo nafsi ilizidi kumuuma huku akimkata jicho kali huyo binti. Ukafika muda wa chakula, watu wote walienda kuchukua chakula na kuenda kukaa kwenye meza zao wakiendelea kula. Ramah hakutaka hata kuinuka hapo alipokaa, ikambidi Hemedy ndio afanye kazi ya kumletea chakula Rafiki yake maana alijua dhahiri amechukizwa na kitendo cha yeye kumleta Hawa kwenye meza yao, lakini yeye lengo lake halikuwa baya, alichotaka yeye ni kuwafanya watu hao wawe karibu tena.
Baada ya kumaliza kula, mgeni rasmi aliondoka, na muda huo ukawa ni muda wa kucheza muziki kuimalizia sherehe hiyo. Wanafunzi waliinuka na kuanza kucheza vile ambavyo kila mmoja ametaka kucheza, wengine walicheza wawili wawili huku wengine wakicheza pekeyao, kuna wengine walicheza chibe chibe wakati huo muziki wala haukuruhusu kucheza hivyo ili mradi kila mmoja aifurahishe nafsi yake tu. Kuifurahisha nafsi kucheza chibe chibe wakati muziki hauendani na staili hiyo! Mmmh!
Hemedy na Hilda waliinuka kwenye viti walipokaa na kwenda mbele kuungana na wenzao kucheza muziki huo. Kwenye meza wakabakia Ramah na Hawa ambapo kila mmoja alikuwa kimya. Hawa kila akitaka kuliita jina la Ramah alijikuta akishindwa kufanya hivyo, akabaki kimya na kumuangalia kijana huyo akiendelea kuichezea simu yake. Ni kama vile Ramah alijua kuwa banati huyo atataka kumuita, akachomeka visikiliza muziki masikioni mwake na kuendelea kuichezea simu yake. Ajabu hii! Ni dhahiri hakuwa akitaka maongezi yoyote na binti huyo ndio maana alichomeka visikilizia muziki masikioni mwake.
Ilikuwa ni jambo la ajabu kusikiliza muziki kwa staili hiyo wakati humo ndani kulikuwa kukipigwa muziki kwa sauti kubwa. Ila yeye alifanya hivyo kuashiria kuwa hataki maongezi na binti huyo. Walikaa hivyo hadi pale Hilda na Hemedy waliporudi na kuungana nao tena huku wakiwaacha wengine wakiendelea kucheza muziki.
“Jamaa mbona umetulia tu hutaki kwenda kucheza hata kidogo rumba" Hemedy aliongea hivyo huku akikivuta kiti kwa mbele baada ya kukaa.
“Jamani twenzetuni mi nishachoka kukaa hapa" Ramah aliongea hivyo huku akianza kunyanyuka kwenye kiti alichokaa.
“Mbona mapema hivyo kaka" akaangalia saa yake ya mkononi. “Saa moja hii na nusu, mapema sana mzee" Hemedy aliongea.
“Kichwa kinaniuma, kwahiyo nataka kuwahi nyumbani" Ramah aliongea hivyo, kipindi hichi alikuwa tayari amesimama kando ya kiti akiwaangalia hao wenzake.
“Sawa, twenzetuni" akamuangalia Hawa kisha akasema. “Vipi Hawa na wewe unabaki au tunaenda wote?" Hemedy alimuuliza hivyo na kumfanya Hawa aitikie kwa kichwa kuashiria na yeye pia anaondoka. Wote wanne wakaondoka na kuenda nje ya ukumbi huo. Hawa alishangaa sana baada ya kumuona Ramah akielekea kwenye gari moja wapo kati ya mengi yaliyokuwa yamepaki hapo. Ilikuwa ni gari aina ya Harrie yenye rangi nyeusi, ilionekana bado mpya kabisa.
Ramah akatoa funguo na kufungua milango ya hiyo gari, kisha akaingia upande wa dereva akiwaacha Hilda na Hemedy wakiingia siti za nyuma. Kitendo hicho kilimfanya Hawa agande nje asijue aingie au arudi tu ukumbini. Hemedy kuona hivyo, akashuka kwenye gari na kumfungulia Hawa mlango wa mbele, kisha Hawa akaingia na kutulia kwenye siti kimya na safari ikaanza baada ya Hemedy kuingia kwenye gari.
Ramah akaweka muziki wa Justin Baby ulioitwa Sorry kwa sauti ya kawaida na kuwafanya Hilda na Hemedy kule nyuma kuufuatisha huku wakikumbatiana na kupigana mabusu kabisa huku wakionekana wakiwa na furaha kupita maelezo. Ramah muda wote alikuwa akitabasamu baada ya kuwaona watu hao kupitia kioo kilichokuwa mbele yake kwa juu.
Wakamuacha Hawa nyumbani kwao na wao wakaelekea nyumbani kwakina Hilda. walipofika wakashuka wote na kuingia ndani ya hiyo nyumba, wakamkuta Anti yao akiwa yupo sebuleni amekaa akibadilisha chaneli kwenye luninga. Walimsalimia wote na kukaa nae hapo kwa muda, kisha Ramah akaaga na kuondoka zake akiwaacha wenzake kila mmoja akiingia kwenye chumba chake.
* * * *
Jumatatu ilifika na wanafunzi wa kidato cha tatu hadi cha kwanza walienda shule huku wa kidato cha nne baadhi yao sana wakiwa wameenda shule kukamilisha yale ambayo hawakuyakamilisha kabla. Hemedy na Hilda walipanga siku hii wawapatanishe Ramah na Hawa kivyovyote vile, walijua wote wanapendana lakini hawawezi kusameheana hivi hivi pasi na kupata mtu wa kuwapatanisha. Wakafikiria wakaona kwa hapo shule haitokuwa vizuri kufanya hivyo, wakapanga wawakutanishe kiujanja sehemu nyengine tofauti na hiyo. Coco Beach wakaona sehemu hiyo itafaa sana kuwakutanisha watu hao kiujanja.
“Jamaa leo nataka tuende Coco tukainjoi, ila leo inabidi uwende na gitaa, nataka nikusikie ukiimba huku ukipiga gitaa. Si unakumbuka kuna siku nilikuambia hicho kitu?" Hemedy alimuuliza Ramah.
“Usijali kaka nakumbuka, nitafanya hivyo" Ramah aliongea.
“Basi mida flani ya jioni jioni tutakupitia hom kwenu tuelekee huko" Hemedy aliongea.
“Mtanipitia wewe na nani?" Ramah aliuliza.
“Jamaa si mimi na Hilda?"
“Sawa"
Hemedy alimaliza kuyaweka sawa Kwa Ramah na kumuachia kazi Hilda nae kumshawishi Hawa hadi akubali kuenda huko. Haikuwa kazi kubwa sana kwa Hilda kumshawishi Hawa, alikubali na kuahidi atatokea huo muda uliopangwa. Wakamaliza hivyo huku wakiwa na furaha ya kufanikiwa kuwashawishi watu hao bila wenyewe kujua.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Majira ya saa kumi na nusu jioni, Hemedy na Hilda walienda kwakina Ramah kwaajili ya kuelekea huko walipopanga, wakamkuta Ramah akiwa tayari ameshajiandaa, kilichofuatia hapo ni kuchukua ufunguo wa gari na wote kuingia humo safari ya kwenda huko walipopanga ikaanza. Baada ya muda wakawa wamefika na leo hii walienda kwenye miamba ya mawe mwisho kuenda kuweka kambi. Wakashuka kwenye gari na kukaa kwenye miamba hiyo au tuseme mawe makubwa mbali kidogo na yanapoishia mawimbi ya maji ya bahari, Wakakaa hapo. baada ya kupiga stori kwa muda mfupi, wakataka Ramah awaimbie huku akipiga gitaa, na yeye bila ajizi akaanza kufanya hivyo. Muda wote Hilda alionekana akichezeachezea simu yake huku akiangalia huku na huko, ni kama vile kulikuwa kuna kitu anakitafuta hivi.
Baada ya dakika tano, alioneka Hawa akija mahala hapo akiwa amependeza kupita kawaida. Ramah baada ya kumuona aliacha kupiga gitaa na kumtazama yeye kwa mshangao. Sio kwamba alikuwa akimtazama kwa jinsi alivyopendeza, hapana, alikuwa akimtazama kwa kujiuliza mtu huyo amefuata nini hapo? Hata kwa Hawa pia ilikuwa ndio hivyo hivyo, akabaki amesimama tu akimuangalia kijana huyo anavyomkodolea macho.
Hilda baada ya kuona amesimama tu pasi na kuja hapo walipo, akamuita na kumfanya binti huyo kupiga hatua za kinyonge kuenda mahala hapo, alipofika alikaribishwa na kukaa sehemu hiyo akiwa hana amani kabisa, akawasalimia wote na safari hii Ramah pia aliitikia salamu hiyo.
Wakasitisha zoezi la kuimba wakawa wanapiga stori za kawaida, muda kidogo, Hemedy na Hilda waliaga na kusema wanaenda kununua chochote kitakacho sindikiza maongezi yao. Wakabaki wenyewe wawili hapo, wakawa hawajui waongeleshane au wakae kimya tu hivyo hivyo. Kimya kikavunjwa!.
“Hilda" Ramah aliita baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kuongea chochote.
“Naam" Hilda nae aliitikia.
“Bado tu unanichukia?" Ramah aliongea hivyo na kumfanya ashindwe kulijibu hilo swali kwa mdomo, badala yake akalijibu kwa kutikisa kichwa kulia kwenda kushoto na kushoto kwenda kulia akimaanisha hapana.
“Kwanini uliamua kunichukia pasi na kunisikiliza nilichokuwa nataka kukuambia?"
“Nisamehe mpenzi. Ni hasira tu zile ndo zilinifanya niwe vile"
“Umeamua nini kuhusu mimi?"
“Ramah mi bado nakupenda, naomba tuweke tofauti zetu pembeni na tuendeleze mapenzi yetu, yale yaliyopita tuyaache, tuangalie yajayo" Hawa aliongea kwa upole.
“Sasa ni vipi utakuwa na mimi wakati umenifumania kwa macho yako?"
“Hapana Ramah mi bado nakupenda. Shamsa alinifuata leo akaniambia kila kitu na nimejuta sana baada ya kusikia kuwa kumbe ulikuwa tu ni mpango wa Babel kunipata mimi. Ila naomba unisamehe kwa yale maneno niliokuwa nakuambia" Hawa aliongea hivyo huku machozi yakimtoka. Ramah alimvutia karibu yake na kuanza kumfuta machozi.
“Hawa niliwahi kukuambia sitoruhusu machozi yako yatoke ikiwa mimi nipo karibu na wewe. Nakupenda Hawa, karibu tena katika himaya ya moyo wangu" Akampiga busu la mdomoni na kumuangalia usoni, hapo kila mmoja alitabasamu na kukumbatiana tena. Baada ya kuachiana, Hawa akaomba aimbiwe nyimbo, Ramah akachukua gitaa na kuanza kuvuta nyuzi moja moja kwa ustadi mzuri huku akimuangalia Hawa usoni.
“............labda nyayo zako zimekutana na mengi. Ukasema tena kupenda sipendi, sipendi. Ni mimi swahiba wako, fundi mjenzi, nitalinda na kutunza penzi, penzi. Kudhulumiwa na kutangatangaa, kwa kilio na machozi. Mi jahazi na nshatia nangaa, sing'atuki hata waje kwa ndumba. Baby tembea naomba uje, ooh na penzi langu uje uonje......”
Hiyo ilikuwa ni baadhi ya mistari aliyokuwa Ramah akimuimbia Hawa. Hakika Hawa alijiskia faraja sana na kukiri kimoyomoyo kuwa Ramah alikuwa akimpenda kweli tofauti na alivyokuwa na Babel. Kwa Ramah alikuwa nae zaidi ya miezi miwili sasa lakini hakuwahi kumgusia chochote kuhusu kufanya mapenzi. Ila kwa Babel hata wiki haijaisha lakini kijana yule alikuwa ni mwenye kuhitaji kufanya tendo hilo.
Majira hayo Hemedy na Hilda walikuja hapo huku Hilda akiwa ameshika mifuko miwili ya nailoni mikononi mwake. Walimkuta Hawa akiwa amemuigamia Ramah huku akiimbiwa nyimbo. Hemedy alipiga makofi mengi huku Hilda yeye akipiga vigelegele. Kitendo hicho kilifanya watu hao wageuke nyuma na kuwaona wenzao wakiwa na furaha ya ajabu.
“Sasa je, mlikuwa mnachukiana bure, halafu kumbe nyote mnapendana, waone vile walivyo tahayari, Kama mmefumaniwa kichochoroni mkifanya niniliu" Hemedy aliongea hivyo huku na yeye akikaa. Aliposema hivyo wote wakawa ni wenye kucheka tu. Hilda akaifungua ile mifuko na kutoa vichupa vya plastiki vilivyokuwa na juisi ya embe ndani yake. Akampa kila mmoja cha kwake na yeye akakaa hapo na kuendelea na stori nyengine.
* *
Siku za mitihani zilipowadia, wakafanya mitihani hadi pale walipomaliza yote na kufunga shule kwa mwezi mmoja na wiki moja. Hapo wakawa huru zaidi, likizo hiyo waliitumia kufurahia mapenzi yao, lakini hawakusahau kusoma sana kwajili ya kidato cha nne. Likizo hiyo ikaisha na kufungua tena shule, sasa walikuwa kidato cha nne, hawakutaka kufanya mchezo hata kidogo na darasa hilo, wakapunguza mitoko na kuwa ni wenye kujisomea kila mara.
* * * *
Zilianza sekunde, zikafuata dakika, yakafuata masaa na kuenda kwenye miezi. Wakawa sasa wamebakiza mwezi mmoja kufanya mtihani wa mwisho, hapo ikawabidi wayasahau mapenzi yao na kuamua kukazana na kusoma. Mwezi nao ukaisha na siku za mitihani zikafuata. Wakafanya mitihani yao kwa wiki moja tu kutokana na wao kuwa kwenye masomo ya sanaa huku wakimuacha Hawa akiendelea na mitihani kwasababu yeye masomo yake ni ya biashara.
Walimaliza mitihani yao na kufanya mahafali hapo shule, siku hiyo ilikuwa ni huzuni sana kwao kuachana na marafiki zao walizoeana nao sana, walipiga picha nyingi za ukumbusho. Lacho, Shebe na Mnama, majira hayo walikuwa wameacha bifu na watu hao baada ya kuwafuata kipindi kirefu na kutaka waache tofauti zao na kutaka kushirikiana pamoja kama wanafunzi. Ramah na Hemedy walikubali na kuanzia hiyo siku hiyo wakawa wapo pamoja huku bifu lao wakilisahau. Lakini Babel yeye hakutaka suluhisho hata kidogo na watu hao, alichokuwa akitaka yeye bifu liendelee hadi pale afe yeye au wafe wao.
Wakapiga picha za pamoja kama ukumbusho, mahafali yalipoisha, wakawa na wao wameondoka shuleni hapo kabisa kabisa.
Baada ya wiki moja kupita tangu wamalize shule. Ramah akawajia wenzake na taarifa iliyowafanya wanyong'onyee na kuingiwa na mfadhaiko mkubwa kwa taarifa hiyo. Taarifa iliyomfanya Hawa kulia kila muda huku akiwa haamini hata hiyo taarifa. Akaomba iwe ni ndoto au iweni mzaha tu wa Ramah kutaka kuwainjoi wenzake, lakini aliwahakikishia hivyo baada ya kuwatolea kitu kilicho wafanya waamini.
Taarifa yenyewe ni kwamba, Ramah anahitajika akasomee nchi za nje elimu yake iliyobakia. Kwahakika taarifa hiyo ili wafanya marafiki zake waingiwe na ubaridi wa ghafla kwenye miili yao. Mwanzo walidhani ni mzaha tu wa rafiki yao, ila aliwahakikishia kwa kuwatolea tiketi ya ndege inayotakiwa asafiri siku mbili zijazo. Hapo Hawa hakuweza kujizuia kulia, alilia sana huku akisema kuwa Ramah anamuacha mwenye hajui ataishije baada ya yeye kuondoka.
Ikabidi wachukue wasaa huo kumfariji na kumbembeleza mwenzao hadi pale alipotulia kabisa. Kuanzia muda huo hakutaka kabisa kuwa mbali na Ramah akifurahia uwepo wake mwisho mwisho.
Siku ya safari ilifika, wakamsindikiza uwanja wa ndege huku wakiongozana na baba yake Ramah. Walipofika wakashuka wote na kumsindikiza hadi sehemu ambapo walitakiwa waishie hapo maana huko mbele ni kwaajili ya wasafiri tu. Hapo Ramah aliwakumbatia wote ishara ya kuwaaga, alipofika kwa Hawa, hakutaka kumuachia hata kidogo huku bado akiendelea kulalamika akisema haamimi kama kweli anaondoka huku akimuacha yeye pekeake.
Ukafika muda ambao wasafiri wanatakiwa waingie kwenye ukaguzi kwaajili ya safari. Ramah akaondoka huku akitembea kinyume nyume akiwapungia mkono. Ghafla Hawa alichomoka hapo alipo na kumfuata Ramah na kwenda kumrukia kwa kumkumbatia, nusura waanguke. Hapo wakajikuta wote wanalia na kuahidiana kuonana tena mungu akipenda. Waliachiana na Ramah akaondoka na kuingia ndani ya chumba cha ukaguzi. Hemedy jicho moja lilimtoka chozi na kumfanya alifute kabla halijafika chini. Hawa alikuja na kumkumbatia Hemedy huku akilalamika kuwa Ramah amemuacha mwenyewe.
Walikaa hapo hadi pale ndege ilipoiacha anga ya Tanzania na kuingia katika anga ya kimataifa. Kisha na wao wakaondoka uwanjani hapo kuelekea walipotoka. Hawa hakuwa na furaha hata kidogo, kuondoka kwa kipenzi chake kuenda kusomea nchi za nje, tena hata yeye mwenye pia hajui kuwa anaenda kusomea nini wala anaenda kusomea wapi. Lilimuuma sana ila hakuwa jinsi kwasababu ilikuwa ni lazima watengane tu kivyovyote hata kama isingekuwa kwa safari.
* *
Majibu yao ya kidato cha nne yakatoka baada ya miezi mitatu kupita, wote walifaulu vizuri kuendelea na masomo yao, hata Ramah pia alifaulu, ila ndio hivyo hakuwepo nchini. Kibaya zaidi Hawa yeye alifaulu mbeya huku wenzake wakifaulu hapo hapo Dar. Wakatengana kwa mara ya pili, Hawa alizidi kushikwa na uchungu, akajiona hivi hivi wenzake wanamtenga, ila kwa vile masomo ndio yanayo watenganisha, hawakuwa na budi zaidi ya kutengana.
Hawa akaenda mbeya huku Hemedy na Hilda wakibaki Daresalam. Walifaulu shule ya sekondari Tambaza na kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na cha sita hapo. Japokuwa maisha ya kusoma wakiwa wapweke bila ya wenzao yaliwagubika, ila ndio hivyo sasa hawakuwa na jinsi zaidi ya kusoma tu wakiwa wenyewe. Walianza kusoma katika shule hiyo wakiwa wageni kama wenzao. Miezi mitatu mbele, walipata marafiki wapya shuleni hapo japokuwa hawakuwa na ladha kama za wale waliotoka nao katika elimu ya upili. Walisoma kwa bidii huku kila mmoja akiwa na ndoto zake.
Mwaka huo ukaisha, ukaingia mwaka wa pili na sasa walikuwa wakimalizia mwaka wa mwisho shuleni hapo, walikuwa wapo kidato cha sita. Mwaka huo nao ukaisha wakiwa wamemaliza kidato hicho cha mwisho. Wakawa sasa wanasubiri matokeo yao baada ya kumaliza elimu hiyo.
* * * *
“Dah! Mwanangu hii kazi hata sijui itaisha lini, nishachoka kuifanya mimi" Kanu aliongea hivyo kumuambia Asu wakati wakiwa kwenye Cafe moja maeneo ya Msimbazi wakipata staftah asubuhi hiyo.
“We acha tu! Ila sasa tutafanyaje wakati sisi ni vibaraka tu" Asu aliongea.
“Hata kama, lakini na sisi pia tunahitaji mapumziko jamaa. Nina muda mrefu nalala usingizi wa mashaka mashaka tu"
“Inabidi tumuombe mkuu aweke vijana wengine wa zamu wa kuifanya hii kazi, maana ni muda mrefu sana tunaifanya pekeetu"
“Hivi Asu unaweza ukaniambia kuwa Mkuu anampango gani na yule dogo? Na huyo anaesema kila siku Kiongozi ni nani?”
MAAJABU! Ina maana hata hawa vijana hawajui wanamlinda Hemedy kwasababu gani? Na hata huyo anaesemwa ni Kiongozi hata wao pia hawamjui?" UTATA!.
“Ndugu yangu hata sijui, ila nahisi ni......" Asu alikatishwa sentensi yake na simu yake iliyokuwa ikiita. Akaitoa mfukoni na kuingalia juu ya kioo ilisomeka jina Mr Kaoneka. “Mkuu" alitamka kwa sauti ndogo kisha akaipokea.
“Sawa Mkuu" alitamka neno hilo moja na kuitoa simu sikioni mwake ikiwa tayari ishakatwa.
“Mkuu anatuita" Alisema neno hilo, kisha akanywa chai iliyokuwa kwenye kikombe.
“Duh! Nishachoka mimi" Kanu alitamka kwa ghadhabu kiasi.
Walipomaliza kula. Wakalipa na kutoka nje ya hiyo Cafe. Wakapanda kwenye gari lao na safari kuelekea huko Mkuu wao alipowahitaji. Walitumia nusu saa tu, kisha wakapaki gari lao nje ya jengo moja refu, wakashuka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuingia humo. Walipofika ndani ya jengo hilo, wakapanda lifti iliyowapeleka flow ya juu ya jengo hilo, huko wakatoka kwenye chumba cha lifti baada ya kujifungua na kuanza kuifuata korido ndefu iliyokuwa mbele yao. Mwisho kabisa wa hiyo korido. Wakaingia kwenye chumba kimoja na kumkuta Mkuu wao (Baba yake na Ramah) akiwa amekaa kwenye kiti chake cha kuzunguuka akiwatazama wao. Akawapa ishara ya kukakaa na wao wakafanya hivyo.
“Nimekuiteni hapa kuna jambo nataka niwaambie" Akatulia baada ya simu yake ya mezani kuita, akaiangalia kwa muda halafu akainyanyua na kuiweka sikioni mwake, kisha baada ya dakika, akaitoa sikioni na kuiweka mahala pake. Kisha akawa anawaangalia tu machoni vijana hao pasi na kusema chochote. Kitendo hicho kilidumu kwa dakika moja, simu yake ya mkononi ikaita, akaichukua na kuipokea kisha akaiweka sauti kubwa na kuiweka juu ya meza akiwa ameilaza upande wa spika ukiwa juu.
“Mr Kaoneka" Sauti ya kwenye simu iliita, lakini muitwaji wala hakunyanyua mdomo wake kujibu. Akakaa kimya, kisha sauti hiyo ikaendelea.
“Nadhani wale vijana sasa wamemaliza shule, ila kinachotakiwa, waishie hapo hapo kidato cha sita, yani wasiendelee tena na elimu yoyote. Unachotakiwa sasa hivi ni kufanya mpango kivyovyote vile waingie JKT na baada ya kumaliza mafunzo hayo, moja kwa moja waingie jeshi la polisi" Mtu wa upande wa pili aliongea.
“Kiongozi sijakuelewa. Kwani wapo wangapi wanaotakiwa? Naona kwenye maelezo yako umeingiza ‘uingi' wakati mimi namjua mmoja tu" Mr Kaoneka aliongea.
“Aaah! Samahani Mr Sijakuambia kitu. Ni kwamba nimeona hata yule binti anafaa kuwepo kwenye huo mpango, kwahiyo ndio maana nikasema unatakiwa kufanya kila uwezalo waingie JKT kisha hapo wakimaliza mafunzo, moja kwa moja waingie kwenye jeshi la polisi" Akatulia kidogo ili kusubiri maneno hayo yamuingie vizuri Mr Kaoneka. Kisha akaendelea.
“Fanya hicho kitu haraka iwezekanavyo. Halafu wakimaliza mafunzo wanatakiwa wakalitumikie jeshi la polisi mkoa wao, mkoa wa Tanga. Baada ya hapo kazi itakuwa ni nyepesi sana kwasababu kwa miaka hiyo, yule kijana atakuwa pia hana tena kisasi na mtu yoyote. Kwasababu hiyo kazi iliyoko mbele yake haihitaji mtu nwenye kisasi"
“Sawa Kiongozi nimekuelewa, hilo jambo ni dogo sana kwa upande wangu, nilazima likamilike"Mr Kaoneka aliongea.
“Mr, tambua nakutegemea sana kwenye jambo hili, na ndio maana ulipotoa wazo hili miaka nane iliyopita viongozi wote waliopita waliliunga mkono na kukuachia wewe hii kazi kwasababu umeaminika sana. Sasa pasije pakatokea uzembe wa aina yoyote na kusababisha mpango ulioanzia kwa viongozi wenzangu waliopita ukaja kuharibika kwangu. Utanifanya nionekane mzembe sana kwenye uongozi wangu na mimi sitaki hicho kitu kije kunitokea.
“Ondoa shaka. Nitahakikisha kila kitu kinaenda sawa" Mr kaoneka alipoongea hivyo, simu ikakatwa na kuwaangalia vijana wake.
“Najua hamjui ni kwasababu gani mnamuwekea ulinzi yule kijana. Hata hivyo hampaswi kujua, mnachotakiwa nyie ni kufanya kama vile ambavyo nawatuma basi. Aaa, nadhani nyote mmemsikia Kiongozi alivyosema japokuwa hamumjui na hampaswi kumjua kwa sasa. Amesema kuwa ulinzi kuanzia sasa muuweke kwa wote wawili, yani yule kijana na yule binti. Tumeelewana?" Mr Kaoneka aliongea kisha akawauliza.
“Ndio mkuu tumekuelewa" walijibu wote kwa pamoja.
“Najua mmeichoka hii kazi, lakini sasa hamna budi kuifanya na pia tu niwaambie kitu, muda si mrefu mtapumzika kwa muda kwasababu wale vijana wanatakiwa waende JKT, kwahiyo huko watakuwa chini ya ulinzi wa wakufunzi wao. Wakishatoka huko moja kwa moja wataenda kulitumikia jeshi la polisi, sasa hapo nyie hamtokuwa na kazi sana ya kuwalinda kwasababu watakuwa wanaweza kujilinda wao wenyewe ila nyie mtakuwa mkihakikisha usalama wao kwa uchache sana. Yule kijana akimaliza kisasi chake kwa wale watu waliomuulia familia yake, basi hapo ndio itakuwa mwisho wa kazi yenu na kuanzia hapo mtakuwa mkilipwa mshahara pasi na kufanya kazi yoyote hadi vifo vyenu, Kwsababu mmefanya kazi kubwa sana. Najua mtajiuliza nimejuaje kwamba ni lazima alipize kisasi cha vifo vya familia yake, na hilo pia hampaswi kujua.... Mnaweza kwenda" Mr Kaoneka alipoongea hivyo, akachukua faili lililokuwa juu ya meza yake na kuanza kulifunuafunua hapo pasi na kuwatazama hao vijana walioko mbele yake.
Vijana hao baada ya kuona mkuu wao ameshika kazi nyengine, wakajinyanyua hapo na kuanza kuondoka humo ndani na kutokomea wanapopajua wao.
* *
Wiki mbili mbele. Hemedy na Hilda walienda JKT kwaajili ya mafunzo. Kwa fikra zao walijua wamechaguliwa kwenda huko, ila haikuwa hivyo, hawakujua kuwa huo ulikuwa ni mpango uliopangwa wao kwenda huko. Baada ya miezi kadhaa mbele. Walihitimisha mafunzo hayo na kutakiwa wachukue mafunzo mengine kwaajili ya jeshi la polisi. Walishangaa sana ila hawakuwa na la kupinga kutokana na kulazimishwa sana na mkufunzi wao.
“Mpenzi unajua hichi kitu kinanishangaza sana. Eti tupelekwe JKT muda ambao wenzetu tayari wameanza kama mwezi mmoja nyuma, halafu na sisi nasi tuchaguliwe kuenda. Halafu kilichonishangaza zaidi tulipo lazimishwa kuchukua mafunzo ya jeshi la polisi" Hemedy alikuwa akimuambia Hilda.
“Hata mimi pia hili jambo limenishangaza sana ila ndio hivyo sasa hakuna budi, inabidi tufuate tu"
“Duh! Ila mimi nahisi kuna namna hapa" Hemedy aliongea.
“Kwanini unahisi hivyo?"
“Haiwezekani kila kitu tulazimishwe lazimishwe tu"
“Mmmh!!"
Baada ya kumaliza mafunzo ya JKT. Walienda kwenye mafunzo mengine ya jeshi la polisi kwa miezi sita, baada ya hapo wakaambiwa wajiandae kuenda kulitumikia jeshi la polisi mwezi mmoja unaofuata.
“Kwahiyo na nyie mnaenda kuwa askari?" Anti yao aliwauliza huku akijiweka vizuri hapo sebuleni kwenye sofa.
“Ndio hivyo Anti. Hata hatujui imekuajekuaje hadi tukafikia huko" Hemedy aliongea.
“Lakini huenda ikawa juhudi zenu mazoezini ndio zimemifanya mkapelekwa huko" Anti aliongea.
“Lakini mimi hayakuwa malengo yangu kuwa askari" Hemedy aliongea.
“Hata kama, huenda ikawa juhudi zenu zimewafanya wakuu wenu wamione mnafaa ndio maana wakamichukua, kwahiyo msilalamike sana"
“Lakini mimi Anti siwezi hizo kazi za vurugu vurugu" Hilda aliongea.
“Unaziweza ndio maana ukachaguliwa, au unadhani hao wenzako walioweza wameanzaje?" Anti aliongea.
“Lakini hii sio ha...." Hemedy alikatisha sentensi yake baada ya simu yake iliyokuwa pembeni ya sofa alilokalia kuita, akapeleka macho kwenye kioo na kuichukua ile simu, akawa anaiyangalia tu bila kuipokea.
“Mbona hupokei simu?" Hilda aliuliza, ni dhahiri alishaanza kushikwa na wivu baada ya kuona Hemedy haipokei ile simu na badala yake anaiangalia tu, akainuka pale alipokaa na kuenda kuipokonya ile simu na kuingalia kwenye kioo kwa muda, huku akiwa ameitumbulia macho kama vile Hemedy alipokuwa ameitumbulia macho.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“I.G.P!" Hilda alisema kwa sauti ndogo huku akiiangalia hiyo simu.
“Anataka nini tena huyo babu yenu?" Anti aliwauliza.
“Hatujajua. Subiri niipokee" Hemedy aliongea hivyo na kuichukua simu kwenye mkono wa Hilda na kuipokea. Akaongea nae kidogo, kisha simu ikakatwa na wenzake wakabaki wakimtazama yeye awaambie ni kipi mtu huyo alikuwa anataka.
“Anasema amepewa taarifa za sisi kuwa askari wa Tanga, akapongeza tu na kusema anatusubiri Tanga" Hemedy alisema.
“Mbona kapewa taarifa mapema hivyo? Au ndio taratibu za kijeshi hizo?" Anti aliuliza.
“Siwezi jua, lakini amesema pia tumepangiwa kwenye kituo chake" Hemedy aliongea.
“Haya jitahidini wanangu, msiikatae hiyo kazi" Anti yao aliongea hivyo huku akiinuka na kuingia chumbani kwake.
* *
“Jamani umebadilika Hawa hadi nakuonea wivu" Hilda aliongea kumuambia Hawa wakati wakiwa Hotelini siku ya pili baada ya Hawa kurudi kutoka shule.
“Mbona hata nyie pia mmebadilika, tena ndio mmezidi kupendeza jamani" Hawa aliongea.
“Vipi lakini masomo huko ulipoenda?" Hemedy alimuuliza.
“Hivyo hivyo tu shemu tumesoma, halafu si unajua tena ugenini kule, nilikuwa nimeboreka kweli yani" Hawa aliongea.
“Unaenda chuo gani kusoma?" Hemedy alimuuliza.
“Namikimbia tena ndugu zangu naenda huko Kenya Nairobi kusoma. Na nyie nanyi?"
“Sisi kwetu kumetokea magumashi ambayo hatuyaelewi, ambiwa na sisi tumekuwa askari" Hemedy aliongea na kumfanya Hawa ashangae.
“Nyote wawili au?" Hawa aliuliza.
“Ndio sote, yani hapa tunapokuambia, baada ya siku ngapi tu tunaenda Tanga" Hemedy aliongea.
“Lakini sio mbaya, hiyo ni bahati sana, yani kumaliza ‘form six' tu mmepata kazi, kuna wenzanu wamefika hadi chuo lakini bado hawajapata kazi" Hawa aliwaambia.
“Mi mbona nishakubaliana nayo, ila kimbembe kipo kwa huyo rafiki yako hapo" Hemedy aliongea.
Huku akimsukuma begani “Nani aliekuambia kuwa mimi nimeikataa hiyo kazi?" Hilda aliongea.
“Kwahiyo hapa nimekaa na maaskari? Afadhali mmeniambia mapema, ninaweza nikafanya kosa hapa mkanichukua bila huruma" Hawa aliongea na kuwafanya wenzake wacheke.
“Hapana bwana, bado hatujawa askari rasmi ila mafunzo tunayo, sasa usije ukashangaa tutakuadhibu bila ya kukupeleka kituoni" Hemedy aliongea.
“Hivi jamani Ramah mnamawasiliano nae?" Hawa aliwauliza.
“Mmmh! Ramah tangu aondoke sijawahi kuwasiliana nae kwa njia yoyote ile" Hemedy aliongea na kumfanya Hawa anyongee.
“Kwani wewe unaenda lini chuo?" Hilda alimuuliza.
“Kesho kutwa ndio naenda"
* *
Tanga. Uwanja wa ndege majani mapana. 6:30 Mchana.
Hemedy na Hilda kwa mara ya kwanza tangia waondoke katika mji huo ndio wanarudi leo. Walitoka hapo uwanjani na kuanza kupiga hatua ndogo ndogo huku wakiwa wanashangaa shangaa mandhari ya hapo. Hilda aliachia begi lake alilokuwa akiliburuza na kumkimbilia babu yake aliekuja kuwapokea hapo, alipofika akamkumbatia huku wote wakiwa na furaha ya aina yake kukutana tena baada ya kuondoka kwa miaka mingi.
Hemedy alilichukua begi la Hilda akalivuta pamoja na lakwake kuelekea kule walipo. Alipofika akamsalimia na kuwaongoza kwenye gari alilokuja nalo.
“Yani huyu mjukuu wako hajaacha tu kudeka kwako. Tangu tupo Dar alikuwa akikusema sana utafikiri hatutofika" Hemedy aliongea hivyo wakiwa ndani ya gari kuelekea nyumbani.
“Sasa jamani Hemedy hujui kama huyu ni babu yangu na nina muda mrefu sijamuona, kwahiyo lazima ni deke kwake" Hilda nae aliongea.
“Hata kama lakini ushakuwa wewe" Hemedy aliongea.
“Umeona wapi mtoto kwa mzazi akikuwa?"
Waliendelea na maongezi kwenye gari hadi pale walipofika nyumbani. Ikawa shangwe nyengine kwa wale wafanyakazi ambao walikuwa ni wazamani nyumbani hapo huku wale wapya wakiwa ndio kwanza sura hizo wanaziona. Ikaandaliwa sherehe ya kuwakaribisha tena watu hao nyumbani. Maandalizi yalifanywa haraka haraka na kuwaalika baadhi ya watu waliokuwa wakiwajua vijana hao.
Koplo Taure ambae kwa sasa amepanda cheo hadi kuwa Inspekta huku Inspekta Ganjo akiwa ni I.G.P (Inspekta Generalal wa Polisi) na Afande Jesca akipanda cheo hadi kuwa Sajenti. Watu hao walihudhuria hapo na ikawa ni furaha nyengine ya kuonana tena baada ya kupoteana kwa miaka tisa. Mrutu nae alikuja na kuungana na wenzake kuwakaribisha wageni hao. Ikawa ni furaha tu muda wote, wakala wakanywa hadi kufikia majira ya usiku sherehe hiyo ndio ikaisha na kila mmoja kurudi alipotoka huku Hemedy akiondoka na Mrutu.
Walipofika nyumbani kwao Hemedy akawa ni mwenye kuyashangaa mazingira ya hiyo nyumba. Alikumbuka mambo mengi sana ya nyuma. Aliwakumbuka wazazi wake, alimkumbuka na mfanyakazi wao ambae yeye alimchukulia kama kaka yake, akabaki ameganda hapo ndani ya uzio wa nyumba hiyo.
“Anko na mimi nataka uniogesha na hayo maji kama unavyo yaogesha haya maua" Hemedy alimuambia Goda kipindi hicho alikuwa akimwagilia maji bustani za hapo nyumbani.
“Na wewe unataka kuoga kama ninavyo yaogesha haya maua?" Goda alimuuliza huku akiwa anaendelea kumwagilia maji bustani hiyo.
“Ndio Anko" Hapo Goda alimuelekezea mbomba wa maji Hemedy na kuanza kumwagia maji yeye, Hemedy akawa anapiga kelele huku akielekea ndani ya nyumba hiyo, alipofika mlangoni akampamia mama yake aliekuwa anatoka nje baada ya kusikia kelele zake.
“Goda nini tena mbona nasikia kelele?" Mama yake alimuuliza Goda huku akiwa amekishika kichwa cha Hemedy aliekuwa amemkumbatia yeye.
“Muulize huyo mwanao kilichomfanya hadi akawa anapiga kelele ni nini" Goda aliongea huku akicheka na kuendelea kumwagilia maji bustani.
“Eti Hemedy ni kipi kilichokufanya ukapiga kelele?" Mama yake alimuuliza huku akiwa anamuangalia usoni.
“Anko mchokozi" Hemedy aliongea hivyo na kumfanya mama yake acheke na kumvuta kuingia nae ndani. Ila ghafla alichomoka kwenye mkono wa mama yake aliekuwa kamshika na kukimbilia kule alipo Goda, kisha akampiga kofi na kuanza kukimbia kuelekea kule aliposimama mama yake. Ila Goda aliwahi kumkimbilia na kunyanyua juu na kufanya Hemedy apige kelele kumuita mama yake huku akiwa anacheka.
Kumbukumbu hiyo ilimrejea kichwani mwake baada ya kuiona hiyo bustani, bila kutarajia machozi yalianza kumtoka pasi na kilio cha mdomo. Mrutu alipomuona hivyo, akamfuata na kuingia nae ndani huku akiwa anambembeleza. Waliingia sebuleni na kukaa kwenye masofa. Hemedy akawa anapitisha pitisha macho kwenye hiyo sebule na kuona kuna baadhi ya vitu vimebadilishwa ikiwemo masofa.
Hapo Mrutu alimuuliza za huko atokako na stori nyengine kama hizo. Baada ya hapo kila mmoja aliingia kwenye chumba chake kwenda kupumzika, hawakuwa na haja ya kula tena kwasababu kule kwa IGP Ganjo wamekula.
Siku mbili mbele, walikuwa wameanza kazi rasmi kwenye kituo ambacho IGP Ganjo anafanya kazi. Siku hiyo ndio walikuwa wakikabidhiwa mavazi na kila kitu cha jeshi ili kuwa askari rasmi. Cheo cha Ukonstebo ndio cheo walichokuwa nacho wao. Cheo cha mwanzo kabisa katika jeshi la polisi. Walianza kazi rasmi hapo.
Mwaka mmoja kupita. Hemedy alipandishwa cheo kiajabu ajabu pasi na yeye kuelewa. Akawa sasa ni Koplo Hemedy huku Hilda akiwa katika cheo chake kile kile cha Ukonstebo. Ilimshangaza kila askari aliesikia hicho kitu lakini ndio hivyo hawakuwa na cha kupinga.
“Unajua Hilda mimi sielewi kabisa nimepandaje cheo kwa mwaka mmoja tu, wakati mimi najua kutoka cheo kimoja hadi kwenda chengine inachukua miaka mitatu, tena hadi uwe na bidii katika kazi ndio unapandishwa cheo. Sasa mimi kwangu hata sijui imekuaje yani" Koplo Hemedy alimuambia Konstebo Hilda wakati wakiwa katika ofisi ya Koplo Hemedy.
“Niajabu kweli lakini inabidi ushukuru kwasababu kupanda cheo kila askari anatamani"
“This is ‘wonder’!" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiinuka kwenye kiti alichokaa na kuanza kupiga hatua kutoka ndani ya ofisi hiyo.
“Sasa unaenda wapi Hemedy?" Konstebo Hilda alimuuliza.
“Naelekea hom, kwani hujui kama muda ushaisha hapa!"
“Oooh! Basi subiri tuongozane wote ukani ‘drop' nyumbani"
Wakatoka nje wote na kuingia kwenye gari la Koplo Hemedy alilopewa na Mrutu. Wakaanza safari ya kutoka hapo kituoni kuelekea nyumbani kwakina Konstebo Hilda, walipofika akashuka na kuingia ndani kwao akimuacha Koplo Hemedy akielekea kwenye nyumba yake aliyopanga. Hakutaka kuishi na Mrutu nyumba moja, alihofia anaweza akabanwa banwa kwenye mambo yake ndio maana akaamua apangishe nyumba nzima aishi yeye mwenyewe. Hata pale alipotaka kuishi mwenyewe, Mrutu alitaka kumpa ile nyumba yake aliyokuwa akiishi zamani yeye na ikiwa imepengishwa, lakini pia alikataa na kudai anataka kuanza maisha yake yeye kama yeye.
Alipofika kwenye hiyo nyumba anayoishi iliyoko maeneo ya Msambweni, akaingiza gari ndani na yeye kuingia ndani ya nyumba hiyo. Ilikuwa ni nyumba yenye hadhi kiasi ambayo kijana yoyote angetamani kuishi hapo. Akaingia chumbani kwake na kuliendea kabati na kulifungua, huko alionekana akichangua changua nguo zilizomo humo ndani. Alifanya hivyo kwa dakika kumi na alipokosa alichokuwa anakitafuta, akakaa kitandani na kuanza kufikiria.
Akainuka tena na kuliendea begi lake la nguo na kulifungua, kisha akaanza kutoa nguo moja baada ya nyengine na kuziweka chini. Begi lilipokuwa tupu, akaanza kufungua zipu moja baada ya nyengine kwenye begi hilo. Wakati akiwa anafungua zipu na kutia mkono wake kwenye sehemu hizo, akawa kama kuna kitu amekishika kwa ndani, akakivuta na nje na alipokiangilia, aliachia tabasamu baada ya kuipata flash aliokuwa akiitafuta. Akaiendea ‘laptop' yake, akaichukua na kuenda kukaa nayo kitandani. Akaiwasha na baada ya dakika moja ikawa tayari imewaka.
Akaichomeka flash na iliposoma akaifungua kwenye mafaili yake na kuliendea faili moja lililoandikwa 13/06, akalifungua. Kwa mara ya kwanza tangu apewe flash hiyo na marehemu Goda ndio anaifungua siku hiyo. Hapo akakutana na video moja tu na kuifungua. Hapo ilianza kumuonyesha video wakati kipindi hicho wakiwa sebuleni wakipiga stori na familia yake hadi pale walipoingia watu wasiowajua na kuiteketeza familia yake huku wakiondoka na briefcase iliyokuwa na nyaraka za mali za baba yake...
Machozi yalikuwa yakimtoka alipomaliza kuiangalia hiyo video. Akaifunga ‘laptop' yake bila ya kuizima na kuanza kulia tu pasi na kupata wakumbembeleza, alilia sana hadi pale alipoona panatosha. Akachukua simu yake na kumpigia baba yake mdogo.
“Niambie Afande, hahaha!!" Sauti ya Mrutu ilisikaka kwenye spika za simu ya Koplo Hemedy baada ya simu kupokelewa.
“Baba kesho nataka unipeleke yalipo makaburi ya wazazi wangu" Koplo Hemedy wala hakupokea heshima hiyo aliyopewa kwa furaha kama ambavyo Mrutu amefanya.
“Kuna nini tena?" Mrutu aliuliza swali la kibwege huku ikionekana dhahiri amehamanika huko alipo.
“Nataka nikayaone" Koplo Hemedy alijibu kwa ufupi.
“Sawa. Kesho nikipata muda mzuri nitakucheki halafu tutaelekea huko" Mrutu aliongea.
“Sawa" alijibu na kukata simu.
* *
Siku iliyofuata Mrutu na Koplo Hemedy walikuwa ndani ya gari wakielekea huko walipozikwa wazazi wake. Kwavile walikuwa kwenye gari lao binafsi, walitumia saa moja na nusu kufika huko. Walipofika kwanza waliwasalimia baadhi ya ndugu zao huku Mrutu akiwa ndie anaemtambulisha Koplo Hemedy, maana yeye hakuwa akiwajua hata mmoja. Baada ya kuwasalimia hao ndugu zao, walienda moja kwa moja hadi kwenye shamba lao ambalo ndipo makaburi hayo yapo.
Koplo Hemedy alilia sana mbele ya makaburi hayo ya wazazi wake yaliyokuwa yamepekana, alilia sana kiasi kwamba Mrutu na yeye akajikuta akidondosha chozi. Hakutaka kumbembeleza wala kumsogelea pale alipopiga magoti kwenye hayo makaburi, alichofanya yeye ni kumuacha tu hadi pale aliponyamaza mwenyewe na kutulia vile vile akiwa amepiga magoti.
“Baba na Mama yangu huko mlipo mungu awalaze mahali pema. Najua hamkufa kwa mipango ya mungu, ila mmekufa kwa mipango ya wanadamu wenye mioyo dhalimu waliotaka kuchukua mali zenu. Kwa hilo wamefanikiwa, wameniacha sijarithi chochote kutoka kwenu. Labda nilichorithi ni kisasi ambacho kimeishi ndani ya moyo wangu tangu mlipotoweka kwenye ulimwengu huu. Naahidi mbele yenu kulipa kisasi kwa kuwaondoa mmoja baada ya mwengine kwa mikono yangu kama vile ambavyo wameziondoa roho zenu. Nawajua na ushahidi ninao"
Mrutu alishtuka baada ya kusikia maneno hayo ya mwisho aliyoyatamka Koplo Hemedy. Hakuelewa mtu huyo aliongea hivyo kutokana na uchungu alionao au amemaanisha aliochoongea. “Ina maana anawajua hadi sasa waliowaua wazazi wake?.... Lakini hapana hawezi kuzikumbuka zile sura, alikuwa ni mdogo sana. Sasa ni vipi aseme anawajua?... Mrutu alijiwazia mwenyewe bila ya kupata majibu ya hicho anachokiwaza. Ikabidi amuulize.
“Hemedy u..u...unawajuaje waliowaua wazazi wako wakati tukio hilo limetokea zamani sana?" Mrutu alimuuliza huku akiwa na hofu nyingi iliyomkumba ghafla.
“Flash yenye ile video ninayo" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akimuangalia Mrutu usoni. Mrutu baada ya kusikia hivyo, alijikuta akipigwa na butwaa lililoonekana waziwazi na Koplo Hemedy..
“Ile video si nilikuuliza ukasema haunayo wewe?" Mrutu alimuuliza huku akioneka dhahiri anawasiwasi mwingi kupita maelezo.
“Nilikuwa nataka nije kuwatafuta mwenyewe, sikutaka mtu yoyote anisaidie kwa hili"Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiinuka pale chini.
“Sa..sasa mimi baba yako mdogo si nipo? Nitakusaidi kwa hilo. Chamsingi ni kunionyesha hiyo flash na mimi ili niwajue hao watu" Mrutu aliongea.
“Hapana, wewe tulia hii kazi nitaifanya mwenyewe na nitawapata tu kivyovyote" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akianza kupiga hatua kuondoka hapo makaburini.
“Lakini mimi baba yako nipo, nitakusaidia kwa hilo, kwasababu huwezi jua hao watu wana hatari kiasi gani" Mrutu aliongea hivyo huku akimfuata Koplo Hemedy kule anakoelekea.
“Baba kumbuka wale waliouliwa ni wazazi wangu, mimi ndio nina uchungu kuliko mtu yoyote yule, ninapokuambia uniachie mimi naomba ufanye hivyo maana sihitaji mtu wa kunisaidia katika hili" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiwa kamgeukia.
“Sawa, lakini naomba na mimi pia niwaone" Mrutu aliongea kwa kulalamika.
“Sawa" aliongea hivyo na kugeukia mbele na safari ya kuondoka hapo ikaanza. Walirudi tena kijijini na kuwaaga wenyeji wao na wao wakaondoka. Njiani Mrutu alikuwa na mawazo mengi kupita maelezo, hakujua afanye nini ili kuliepuka hilo balaa lililopo mbele yao. Hapo ndio akajua kwamba siku zao za kufurahi uraiani zinakaribia kuisha kama sio kufika kabisa. Akawaza kama ikiwa hiyo flash ndiyo yenyewe basi aongee na wenzake waone watafanya nini.
Safari yao iliishia nyumbani kwa Koplo Hemedy na wote wakashuka kwenye gari na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Koplo Hemedy alimletea ‘laptop' na flash, kisha akamuekea ile video na kumfanya Mrutu ashtuke tena baada ya kuzishuhudia sura za wenzake zikionekana waziwazi kwenye hiyo video, akabaki kutetemeka tu na kumfanya Koplo Hemedy asimuelewe hata kidogo kwa hicho kitendo. Mrutu aliirudia tena kwa mara ya pili ile video kisha akaaga na kuondoka hapo.
Safari yake iliishia nyumbani kwa Moto na kumkuta mtu huyo akiwa ndio anaamka muda huo kutoka usingizini. Wakachukuana na kukaa sebuleni.
“Kaka kuna tatizo kubwa sana limejitokeza na tusipoliwahi basi litatuwahi sisi" Mrutu aliongea hivyo na kumfanya Moto asimuelewe alichoongea.
“Sijakuelewa mimi hata kidogo. Tatizo lenyewe ni lipi?" Moto alimuuliza.
“Hemedy karudi na sasa anataka kulipa kisasi" Mrutu aliongea.
“Hemedy yupi na hicho kisasi ni kipi?" Moto aliongea hivyo akionekana dhahiri kutomkumbuka mtu huyo kama sio kutomjua kabisa.
“Hemedy yule mtoto wa marehemu Mheshimiwa mulie muulia wazazi wake"
“Karudi vipi, na anataka kulipa kisasi kwani bado anatukumbuka?" Moto aliongea kikawaida sana, alijua huo ni wasiwasi wa Mrutu, alijua kwamba sura zao hadi kwa wakati huo zitakuwa zimefutika katika kumbukumbu ya yule mtoto waliemuulia wazazi wake.
“Ile flash yenye ile video anayo na leo akanionyesha na sura zenu zimeonekana bila chenga" Mrutu alipoongea hivyo. Moto akashtuka mithili ya mtu alieletewa taarifa za kifo cha mtu anaemjua.
“Eeee!! Kaka uko ‘serious' au unatania?" Moto aliuliza huku akiwa macho kayatoa kama mtu alieona kitu cha kutisha.
“Wala sipo katika matani na ninavyokuambia yule mtu sasa hivi ni askari polisi, na kwavile amesema atawatafuta wauwaji wa wazazi wake, basi ujue lazima afanye hivyo na lazima atamipata tu"
“Ni askari?" Moto alizidi kuchanganyikiwa.
“Ndio ni askari na ana cheo cha Ukoplo"
“Sasa tutafanyaje?" Moto aliuliza, dhahiri alionekana kuchanganywa na hiyo taarifa.
“Ndio nimekuja kwako hapa tujue tunafanyaje"
“Inabidi tumuue, tumtumie watu watakao muua tu" Moto aliongea.
“Kwani hakuna njia nyengine zaidi ya hiyo ya kumuua?" Mrutu alimuuliza.
“Sasa unadhani tutufanya njia gani nyengine? Inabidi afe tu hakuna namna nyengine hapo"
“Tutafute njia nyengine bwana lakini sio kumuua" Mrutu alipinga.
“Basi iseme hiyo njia, sio unasema tutafute njia nyengine halafu hujui pia hiyo njia ni ipi"
“Acha mimi niende, halafu baadae nitakutafuta tujue tunafanyaje" Mrutu aliongea hivyo huku akinyanyuka kwenye sofa alilokaa.
“Sawa wewe nenda ila jua hakuna njia nyengine salama zaidi ya hiyo" Moto aliongea hivyo huku akiigamiza mgongo wake kwenye sofa.
“Kwani Mata hajarudi bado huko alipoenda?" Mrutu aliuliza hivyo huku akiwa ameshika kitasa cha mlango akitaka kuufungua atoke nje.
“Hajarudi bado, ila jana nimeongea nae akasema kesho ndio anarudi"
Mrutu aliposikia hivyo, akafungua mlango na kutoka nje ya nyumba hiyo na kuelekea anapopajua yeye.
“Huyu jamaa ndie alieleta pingamizi hadi yule mtoto hatukumuua tangia kitambo, sidhani kama yote yangetokea haya kama angekufa muda ule" Moto aliongea pekeake baada ya Mrutu kuondoka nyumbani kwake. Akachukua simu na kupigia namba anayoijua yeye na kuiweka sikioni.
“Safi... leo nataka tukutane kwenye ile baa yangu kuna kazi nataka niwape, saa mbili usiku" Alipoongea hivyo, akakata simu na kujiinua kwenye hilo sofa na kuingia ndani.
“Watu tunatiana presha tu saa hizi" Alimalizia maneno hayo akiwa anaufunga mlango wa chumbani kwake.
Majira ya usiku kwenye baa ya Moto ilioko maeneo ya Sahare, palionekana pamechangamka kwa mishemishe za walevi na wasiokuwa walevi waliojumuika kwenye baa hiyo. Kwenye meza iliyokuwa mbali kidogo na zilipo meza nyengine, kulikuwa kuna watu watatu wamekaa kuizunguka meza hiyo, mmoja wao alikuwa ni Moto huku wale wawili hatujapata bado kuwaja.
“Sasa wazee wa kazi nimemiita hapa kuna kazi nataka niwape" Moto aliongea kuwaambia hao watu aliowaita wazee wa kazi.
“Tunakusikiliza mkubwa" Jamaa mmoja wapo aliongea.
“Kuna mtu nataka katika hizi siku mbili awe yupo tayari kwa mazishi na ninaamini hilo nyie mnaliweza" Moto aliongea.
“Ni mwanaume au mwanamke?" Jamaa aliuliza.
“Ni mwanaume, tena kijana mdogo tu" Moto aliongea.
“Kazi rahisi sana hiyo, tulidhani ni mwanamke, kidogo angechelewa kufa" Jamaa aliongea.
“Kwanini?" Moto aliuliza.
“Kwasababu tusingemuacha hivi hivi kabla ya kifo chake, ila kwavile ni mwanaume, basi itakuwa ni rahisi tu. Chamuhimu ni wewe kutupa ‘information' ya huyo mtu halafu utuambie unataka kwa muda gani awe tayari kwa mazishi basi" Jamaa aliongea.
Moto alitoa simu yake na kuiminyaminya kisha akawapa watu hao hiyo simu. “Mtu mwenyewe ndio huyo hapo" Mrutu aliongea.
“Hahahah!! Mtoto mwenyewe kumbe ni mzuri namna hii?" Jamaa mwengine ambae alikuwa kimya muda wote, aliongea hivyo baada ya kuiona picha ya Koplo Hemedy.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni askari huyo" Moto aliwaambia.
“Huyu hatakama angekuwa komandoo wala sisi asingetupa shida kamwe" Jamaa wa mwanzo aliongea.
“Tuambie anapatikana wapi ili hiyo kazi tuifanye kesho" Jamaa wa pili aliongea.
Mrutu aliwaelekeza sehemu anapopatikana Koplo Hemedy na na kila kitu kuhusiana na yeye, yani muda anaorudi nyumbani na vitu vyengine kama hivyo. Haikujulikana vyote amevijulia wapi, ila ndio hivyo aliwaambia watu hao. Baada ya kumaliza kuwaelekeza, wakaelewana kiasi cha pesa kutokana na hiyo kazi, kisha jamaa hao wakaondoka wakimuacha Moto akitafuta viwanja vyengine vya kuenda kujirusha usiku huo maana alijua kazi imefika mikono salama.
* * * *
Siku iliyofuata. Koplo Hemedy alitoka kwenye nyumba yake na kupanda kwenye gari lake. Akalitoa nje na kushika njia ya panda ya msambweni na kutokea mabanda ya papa. Akaachana na ‘round about’ na kushika uelekea wa njia ya mkuu wa mkoa. Akanyoosha na njia hiyo hadi pale alipoiona Nyinda Hotel mbele kidogo akapaki gari kwenye jengo moja liliokaribu na Hotel hiyo kisha akashuka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo.
“Mambo mrembo" Koplo Hemedy alimsalimia binti aliemkuta mapokezi baada ya kufika hapo. Usoni mwake alipambwa na tabasamu huku akiwa funguo yake ya gari akiizungusha zungusha kwenye kidole chake cha shahada.
“Poa. Nikusaidie nini?" Binti huyo alijibu na kuuliza akiwa na yeye amepambwa na tabasamu usoni mwake.
“Kuna shida mbili nataka unisaidie, ila moja utanisaidia baada ya kuimaliza nyengine" Koplo Hemedy aliongea huku akiwa bado na tabasamu usoni mwake.
“Ok, nakusikiliza" Binti huyo alijibu huku akiwa ameweka pozi la kusikiliza hizo shida.
“Kwanza Mr Mata nimemkuta?" Koplo Hemedy aliuliza.
“Bosi hayupo amesafiri ila leo ndio anakuja"
“Sawa, asante kwa ushirikiano wako. Nikutakie kazi njema, acha mimi niende nitarudi kesho kuja kumuona" Koplo Hemedy alipoongea hivyo, akaanza kupiga hatua kuondoka hapo, ila alipofika mbele kidogo kama hatua tano, akageuza na kurudi pale mapokeza.
“Samahani, nilikuambia nina shida mbili lakini nimekutajia moja, ila pia nilikuambia nitakuambia shida ya pili baada ya kuimaliza ya kwanza. Lakini ya kwanza sikuifanikisha ila kesho nitakaporudi tena ‘ofcourse' nitakuambia" Alipoongea hivyo akaanza tena kupiga hatua kutoka humo akimuacha binti huyo akimuangalia mpaka pale alipopotea kwenye upeo wa macho yake.
Koplo Hemedy baada ya kutoka nje ya jengo hilo, akapanda kwenye gari lake na kurudi na njia ile ile aliyokuja nayo, ila sasa alipofika njia panda ya Msambweni, alinyoosha moja kwa moja hadi kituo cha polisi Mabawa. Alipofika kituoni hapo, akashuka kwenye gari na kuingia ndani hadi kwenye ofisi yake ilipo.
Majira ya saa nane mchana, alitoka kituoni hapo na kuingia kwenye gari lake na safari ya kurudi nyumbani kwake ikaanza. Wakati akiwa barabarani kuelekea nyumbani kwake, kuna pikipiki kubwa juu yake wakiwa wamepanda watu wawili lilikuwa likimfuata nyuma pasi na yeye kujua. Aliongozana nalo hadi alipofika nje ya geti la nyumba yake, akashuka kwenye gari na kwenda kufungua geti kisha akarudi tena garini na kuliingiza ndani, akarudi tena kufunga geti na akaelekea moja kwa moja ndani ya nyumba hiyo.
Huku nje wale wale watu waliokuwa wamevaa ‘Helment' vichwani mwao, walikuwa wapo mbali kidogo na ilipo nyumba ya Koplo Hemedy, wakaonekana kama wanashauriana kitu, kisha wakawasha pikipiki lao na kuja hadi nje ya geti la nyumba ya Koplo Hemedy. Wakashuka na kuvua makofia hayo, hapo ndipo sura zao zilipoonekana, walikuwa ni wale watu waliokuwa jana wakipewa kazi ya kumuua Koplo Hemedy na Moto.
Mmoja akagonga geti kipindi hicho Koplo Hemedy alikuwa yupo sebuleni amevua fulana na kubaki tumbo wazi huku akiwa anamenya matunda. Sauti ya kugongwa kwa geti aliisikia, akaipuuzia kwa mara ya kwanza ila ikajirudia tena. Ikambidi aache alichokuwa anafanya na kuinuka hapo hivyo hivyo tumbo wazi na kwenda getini kujua ni nani anaegonga. Alipofika akafungua geti dogo na kukutana na ngumi nzito ya uso ilimfanya kurudi nyuma huku mikono yake akiwa ameiweka usoni mwake.
Jamaa hao wakaingia ndani haraka na kumpiga teke la tumbo na kumfanya Koplo Hemedy agugumie kwa maumivu hayo. Jamaa mmoja akachomoa bastola na kumnyooshea yeye. Koplo Hemedy kuja kuitoa mikono yake usoni aangalie ni wakina nani hao waliomvamia. Alikutana na domo la bastola likimuangalia yeye. Akapatwa na hofu, hakuzijua hizo sura na wala hakuwahi kuziona sehemu yoyote ile. Akabaki akiwa anatetemeka kwa hofu maana alijua vyema kazi ya kifaa hicho hakina mas'hara hata kidogo.
“Ongoza njia ukafie ndani ya nyumba yako" Jamaa huyo aliemnyooshea bastola, alimuambia hivyo na kumfanya Koplo Hemedy kurudi ndani huku akiwa mikono ameiweka juu. Waliingia kwa staili hiyo hiyo hadi sebuleni.
“Geuka nyuma ushuhudie kifo chako kinavyoenda kukukuta punde tu" Jamaa alimuamrisha Koplo Hemedy na kumfanya ageuke nyuma kitaratibu kabisa. Jamaa huyo baada ya kuona Koplo Hemedy ameguka kuwaangalia wao. Akamuangalia mwenzake usoni na mwenzake akampa ishara iliyomfanya jamaa huyo kuiondoa usalama bastola aliyoishika huku akianza kuminya ‘triger' tayari kuruhusu risasi itoke kwenye tundu la bastola hiyo.
.
“Usipige risasi, utajaza nzi, hiyo haina kiwambo cha kuzuia sauti" Jamaa mwengine alimuambia yule mwenzake alieshika bastola. Ikabidi wamuamrishe Koplo Hemedy akae kwenye sofa, sofa lilelile ambalo mwanzo alikuwa amekaa juu yake akimenya matunda kabla haijagongwa hodi. Hilo likawa ni kosa pasi na wao kujua. Akarudi kinyume nyume na kukaa, miguu yake akaibananisha kwa chini kuificha ile sahani ambayo ina matunda na kisu kwa juu.
Wale jamaa mmoja wapo yule ambae hakushika bastola akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye kordo inayotenganisha vyumba vya hiyo nyumba, walitaka kabla hawajamuua Koplo Hemedy, waisachi hiyo nyumba na kuchukua chochote kinachobebeka kwa urahisi halafu waondoke nacho. Yule jamaa aliekuwa akienda vyumbani, alipofika kwenye kona ya kuenda kwenye kordo ya kuingia vyumbani, yule mwenzake huku nyuma alikuwa akimuangalia yeye huku akiwa amemnyooshe bastola Koplo Hemedy.
Koplo Hemedy akaona hiyo ndio bahati ya mtende, hakutaka kuichezea hata kidogo. Pale pale akapeleka mkono wake wa kulia chini akakivuta kile kisu na kukirusha kwa ustadi mkubwa hadi kwenye mkono wa yule alieshika bastola. Jamaa alitoa ukelele wa maumivu huku bastola ikimdondoka chini, ukelele huo ulimfanya yule mwenzake kuchungulia haraka kutaka kujua ni kipi kilichomfanya mwenzake akapiga kelele namna hiyo. Alipochungulia alikutana na kipande cha chungwa lilichomenywa na kukatwa katikati. Kipande hicho kilimpiga kwenye macho na kumfanya jamaa aanze kulia kama mtoto mdogo kwa macho yake kupata uchungu wa maji maji yenye ladha ya ugwadu ya chungwa.
Koplo Hemedy haraka akainuka pale na kuiwahi bastola iliyokuwa chini, kisha akampiga yule jamaa aliekuwa kaishika ngumi ya taya na kumfanya jamaa akunje sura na kumfanya afananiane na nyani mzee. Kabla hajakaa sawa, akampiga na ngumi nyengine mbili zaa mbavu. Yule jamaa kule aliepigwa kipande cha chungwa cha macho. Alikuja mbio huku akiwa bado anapepesa pepesa macho, akawa anarusha ngumi za kibwege kumuendea Koplo Hemedy. Ila zote alizihepa na kumpiga ngumi moja ya mdomo, Jamaa akainama kwa maumivu, hapo akampiga dochi moja la kidevu na kumfanya atoe mguno kama wa mbuzi aliepigwa kigongo cha kichwa wakati akila mahindi ya watu.
Dochi hilo alilopigwa lilimfanya aende kutua chini chali. Jamaa mwengine akampiga Koplo Hemedy teke la mgongo na kumfanya aende mbele kidogo huku ile bastola alioishika ikimtoka na kuangukia pembeni, akageuka na teke aina ya ‘yoko' alilolipiga kwa kuuzungusha mguu na kuja kumpiga jamaa huyo la shingo na kwenda kujipigiza kwenye ukuta. Yule jamaa alielala chini baada ya kupigwa dochi la kidevu, pale alipoangukia ndio pale kile kisu kilipoanguakia, akakiokota na kuinuka nacho kwa kummendea Koplo Hemedy aliekuwa akidili na yule mwenzake.
Koplo Hemedy alikuwa akimuona kupita kioo cha kabati la vyombo lililokuwa mbele yake, akawa anamsubiri afike karibu yake amuonyeshe kazi. Yule jamaa baada ya kudhani hajaonekana kwa hilo analotaka kulifanya, akachomoka kwa kasi huku kisu akikiweka mbele kwajili ya kumchoma nacho Koplo Hemedy cha mgongo. Hapo Koplo akasogea pembeni na kumfanya jamaa apite mazima kisha Koplo akamsindikiza na teke la mgongo na kumfanya jamaa kwenda kuingiza uso wake kwenye kioo cha kabati la vyombo.
Akapiga kelele kwa maumivu huku kisu akikiachia bila kupenda na kuanza kurusha mikono yake kwa kiwewe huku kichwa chake kikiwa ndani ya kabati baada ya kupenyeza kwenye kioo. Yule jamaa mwengine, akainuka pale ukutani na kuchomoa mchuma wa pazia na kwenda nao mbio mbio huku akipiga kelele kama mwehu domo likimtoka udenda ulichanganyika na damu, dhamira yake ilikuwa ni kumpiga na huo mchuma Koplo Hemedy aliekuwa nyuma ya yule mwenzake aliezamisha kichwa kwenye kioo cha kabati pasi na kukitoa. Yule jamaa alieshika mchuma aliuvuta kwa nguvu zake zote kutaka kumpiga nao Koplo wa kichwa, ila Koplo aliinama na kuufanya mchuma huo upite kwa kasi na kwenda kumpiga mwenzake wa mgongo.
Yule jamaa aliezamisha kichwa kwenye kioo cha kabati, baada ya kupigwa mchuma huo kwenye mgongo wake kwa nguvu. Alijikuta akikichomoa kichwa chake bila kupenda kwenye vioo hivyo kwa maumivu ya huo mchuma uliotua kwenye mgongo wake. Lahaula!! Sura yake ilitisha kwa kuingalia kama una moyo mwepesi, sura nzima ilikuwa na vipande vipande vya vioo, akabaki akipiga kelele kama mwehu huku mikono yake akiirusha rusha hewani. Yule jamaa mwengine baada ya kumuona mwenzake akiwa katika hali hiyo, alijikuta kwa mshtuko akiuachia ule mchuma na kumsogelea mwenzake pale alipo. Koplo aliuokota ule mchuma na kumpiga nao wa mgongo na kumfanya jama huyo ajikunje na kukaa chini bila kupenda. Kisha hapo akaiokota bastola iliyokuwa chini yake na kuwaelekezea watu hao.
“Haya inukeni taratibu hapo mlipo na mkae pale mbele" Koplo Hemedy aliwaamrisha hivyo na kuwafanya watu hao wakae sehemu walipoelekezwa huku kila mmoja akiugulia maumivu yake hasahasa yule aliechomwa na vipande vya vioo usoni mwake.
“Wewe kichwa, haya mtoe mwenzako hivyo vioo usoni mwake, na umtoe taratibu" Jamaa huyo aliebatizwa jina la ‘kichwa' alifanya kama alivyoambiwa. Wakati akimtoa hivyo vipande vya vioo mwenzake, yule jamaa mwengine alikuwa akipiga kelele za nguvu kwa maumivu, zoezi hilo lilichukua dakika moja na kuisha. Kisha Koplo Hemedy akaliendea kabati hilo hilo lililovunjwa, akatoa kichupa ambacho ndani yake kilikuwa na dawa aina ya spiriti, akakifungua na kuenda kumiminia yule jamaa yote usoni mwake. Jamaa alipiga kelele ambazo sidhani kwamba katika maisha yake alishawahi kupiga kelele kiasi hicho. Alikuwa akipiga kelele huku mikono yake ikiwa karibu kabisa na uso wake, hakuelewa aushike uso wake au auache tu. Mikono ilikuwa ikimtetemeka mithili ya kifaranga kilichomwagiwa maji ya baridi.
Baada ya dakika tano, jamaa akatulia huku akiwa bado analia chini chini. Koplo Hemedy muda wote alikuwa akiwaangalia tu pasi na kuwafanya chochote. Alipoona jamaa katulia huku akiugulia maumivu yake chini chini. Akachukua simu yake na kuipiga namba anayoijua yeye kisha akaiweka sikioni.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Njoo nyumbani kwangu na askari wawili, sasa hivi" alikata simu na kuwaangalia jamaa hao walivyogwaya kwa kusikia habari za askari, wakajua tayari jela inawahusu, hawakuwa na namna ya kufanya. Wakabaki hapo chini wametulia kimya na hofu imewatanda mioyoni mwao kama watoto wakiume wanao subiria kutairiwa. Walionywa kuwa huyo wanaetaka kuenda kumuua ni askari lakini wao wakajibu jeuri baada ya kuonyeshwa picha ya kijana mwenye sura nzuri na ya upole, wakajua ni lelemama tu kama walivyo vijana wengine wenye sura kama hizo.
Baada ya dakika kumi, kuliingia askari watatu ndani humo, walipofungua mlango wa hapo sebuleni, walipigwa na butwaa baada ya kuwaona watu wawili wakiwa wamekaa chini na kwenye miili yao hakutamaniki kwa damu huku mmoja sura yake ikiwa nyekunde mithili ya nyama ya kitimoto.
“Afande vipi tena, mbona hali hii?" Askari mmoja alimuuliza Koplo Hemedy baada ya kutoielewa hali hio.
“Hao jamaa kuna kitu walikitaka kutoka kwangu, lakini sasa kimewageukia wao. Embu wakusanyeni tuondoke nao" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiingia chumbani kwake, aliporudi alikuwa amevaa fulana tayari na kuwakuta watu hao wakiwa tayari wanapingu mikononi mwao. Wakawatoa humo ndani na kuwapeleka kwenye gari la polisi lililopaki nje ya nyumba hiyo. Wakawatia kwenye gari hilo wao na pikipiki lao na safari ya kuenda kituoni ikaanza huku Koplo Hemedy akienda na gari lake.
Walipofika walishushwa mzega mzega hadi katika chumba cha mahojiano na kufungwa kamba ngumu kwenye viti. Koplo Hemedy alikaa kwenye kiti kilichokuwa kimewaangalia wao. Akawatazama kwa muda huku akiwatolea tabasamu, tabasamu la kejeli kisha akaanza kuwauliza maswali.
“Wewe kichwa, unaitwa nani jina lako halisi?" Koplo Hemedy alimuuliza. Ila jamaa akabaki kumuangalia tu kwa kiburi. Koplo Hemedy akatabasamu na kumuuliza swali hilo hilo yule mwengine ambao alipata maswahibu ya kuchomwa na vioo vya kabati. Ila jamaa na yeye akajifanya kiburi kama vile alivyokuwa mwenzake. Koplo kuona hivyo, akaona akiendelea kuwachekea watazidi kumletea kiburi. Bila kutarajia, jamaa yule aliepata maswahibu ya kuchomwa na vioo. domo lilimlegea mithili ya chupi saizi sitini na tisa kwa kimbaumbau baada ya kupokea ngumi nzito juu ya domo hilo. Akapiga kelele kama kichaa alieona fuko la makande jalalani likiokotwa na mbwa yatima mwenye njaa.
“Sudi....sudi. Naitwa Sudi Afande, nisamehe sana" Jamaa alibwabwaja huku domo likitoa damu iliyochanganyikana na ute kama misekure ya kwenye muvi ya ‘Uwanja wa Dhambi' wale wahenga kama mimi ndio watakuwa wanaijua hii muvi.
“Huna baba wewe?" Koplo Hemedy alimuuliza huku akitabasamu.
“Khalfani. Masudi Khalfani" Jamaa lilitaja huku likilia kama mtoto mdogo alienyang'anywa puto na mwenzake.
“Nyumbani kwangu mmefuata nini?"
“Kukuua Afande, tusamehe sana, nisamehe sana"
“Nani aliemituma?"
“Moto. Mtu mmoja anaitwa Moto Afande" Koplo Hemedy hakuwahi kulisikia hilo jina wala hakujua mmiliki wa hilo jina ni nani.
“Ni nani na anaishi wapi?"
“Ni kijana mmoja anaemiliki baa inayoitwa Fire iliyoko kule Sahare Afande na anapoishi sipajui" Jamaa alijibu huku udenda ukimtoka mdomoni mwake.
Alitia huruma kumtazama!
Akamgeukia na yule mwengine, akamuuliza jina lake, lakini akaonekana bado kiburi kimemjaa. Koplo Hemedy akatoka humo huku akiwa ametabasamu na aliporudi alikuwa ameongozana na askari mmoja wapo aliemuita kule nyumbani kwake. Mkononi alikuwa ameshika rungu kubwa kama la yule mchekeshaji wa bongo anaeitwa ‘Pembe' ila rungu hili lilionekana kushiba kilo nyingi tofauti na lile. Alipofika hapo, akamfungua pingu yule jamaa kiburi na kumuamuru yule askari mwengine aishike mikono ya jamaa huku akiwa ameilaza juu ya meza iliyokuwa mbele yake. Askari huyo alishika mikono hiyo barabara na kuilazisha juu ya meza kwa nguvu.
Kisha hapo Koplo Hemedy alianza kuvipiga viganja vya mikono vya huyo jamaa. Mbona kiburi kiliisha? Alikuwa akilia kama mtoto huku akiomba asamehewe, lakini ndio kwanza Koplo Hemedy wala hakujali hizo kelele, yeye aliendelea kuliinua juu hilo rungu na kulitulisha juu ya viganja vya huyo jamaa kiburi hadi pale alipotaja jina lake ndio Koplo akaacha kufanya hivyo.
“Mwinyiheri Afande. Mwinyiheri Mbwana" Jamaa alitaja majina yake huku akiwa mikono ameining'iniza kwa mbele mithili ya yale mazombi ya kwenye muvi ya ‘Wrong Turn' viganja vilikuwa havitamaniki kwa kupondwa na hilo rungu. Akajutia ubishi wake, akajutia kumvamia mtu aliedhani ni nyoronyoro baada ya kumuona kwenye picha, zaidi ya yote, akajutia kuifanya hiyo kazi.
“Anhaa!! Kumbe unaweza kuongea bila tabu. Sasa kwanini umetaka yakukute yote hayo wakati kumbe uwezo wa kujibu ulikuwa unao?" Koplo Hemedy alimuuliza maswali kama yale aliyomuuliza yule mwenzake na kujibu vilevile. Baada ya kuridhika na kuwahoji kwa siku hiyo. Akawachukua na kuwapeleka sero kisha yeye akaondoka kuelekea nyumbani kwake.
Alipfika alimkuta Konstebo Hilda akiwa na yeye ndio anafika hapo. Akamuelezea kila kitu kilichomkuta na kumfanya Konstebo Hilda kushangaa sana huku akimpapole mpenzi wake. Wakaingia wote sebuleni na Konstebo Hilda akashangaa mazingira ya hapo yalivyokuwa hovyo. Ikambidi achukue jukumu la kuisafisha sebule hiyo huku Koplo Hemedy akiingia chumbani kwake. Alipotoka alikuwa ameshika ‘laptop' mkononi mwake na kwenda kukaa nayo kwenye sofa, kipindi hicho sebule hiyo ilikuwa ishamaliza kufanyia usafi. Konstebo Hilda akaenda kukaa kwenye sofa alilokaa Koplo Hemedy. Hapo Koplo Hemedy kabla hajaiwasha hiyo ‘laptop', akamuambia mpango wake wa kuwasaka wauwaji wa wazazi wake. Kisha akaiwasha na kuiangalia wote ile video. Sasa alikuwa ameikopi humo humo ndani ya ‘laptop'.
Wakati wakiwa wanaiangalia hiyo video. Koplo Hemedy aliona kitu chengine kilichomshitua kwenye hiyo video. Akawa anairudia rudia mara nyingi sehemu moja hadi pale alipoulizwa kunanini na mpenzi wake.
“Hembu muangalie huyu mtu kwa umakini anavyolitamka hili neno" Koplo Hemedy alimjibu. Video hiyo haikuwa na sauti bali ni picha mjongeo tu. Na sehemu hiyo ni ile baada ya kumuua baba yake na Koplo Hemedy, Moto alipomuambia Mata amuambie Mrutu aweke gari vizuri ili waondoke pale. Hapo Hemedy alianza kuvuta kumbukumbuka kabla ya yeye kuzimia baada ya kushuhudia kifo cha baba yake.
“Mshtue MRUTU aweke gari sawa tuondoke kabla nzi hawaja kuja". Hayo ndo maneno ya mwisho kuyasikia kabla hajazimia. Na nikweli baada ya kuyakumbuka akafananisha maneno hayo na huo mdomo wa Moto unavyoongea akakuta vikiendana sawa kabisa, tena bila kurefusha wala kufupisha.
“Ina maana Baba mdogo pia alishiriki katika kifo cha wazazi wangu?" Alijiuliza swali hilo na kumfanya Konstebo Hilda asimuelewe hata kidogo.
“Hapana, haiwezekani" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiwa amebananisha meno yake kwa gadhabu ya hali ya juu.
“Mpenzi nini, mbona sikuelewi? Baba yako mdogo ameshiriki vipi kwenye kifo cha wazazi wako?" Konstebo Hilda alimuuliza hivyo huku akiwa anamuangalia usoni.
“Ameshiriki ndio, ameshiriki na uhakika ninao" Akamgeukia usoni na kumuambia. “Kama unataka kuamini haya, embu fuatiliza maneno haya na huu mdomo wa huyu mtu kwenye hii video ndio utaamini"
“Mshtue MRUTU aweke gari sawa tuondoke kabla nzi hawaja kuja" Koplo Hemedy aliongea kwa sauti maneno hayo na kumfanya Konstebo Hilda kuyafuatiliza na kwa kuuangalia mdomo wa huyo mtu kwenye hiyo video na kukuta yameendana sawa kabisa. “Mmmh!" akaishia kuguna tu na kumuangalia mpenzi wake usoni.
“Hilda siamini hata kidogo. Yani bamdogo Mrutu anaweza kushiriki kumuondoa kaka yake duniani kisa mali tu. Halafu eti mahakamani akadai eti kuwa mali hazikuwa ni za baba" Alipofika hapo kuna kumbukumbu nyengine ikamjia kichwani mwake. Akakumbuka siku ile alipomuona baba yake huyo mdogo akiwa ameongozana na wauwaji wa wazazi wake wakiingia kwenye nyumba yake. Siku ile alidhani watu hao wanampango wa kumuua baba yake mdogo pia ila leo amejidhihirishia mwenyewe kuwa baba yake mdogo alikuwa yupo kwenye mapango na wauwaji hao.
“Subiri niende huko huko kwake" aliongea hivyo huku akinyanyuka hapo. Konstebo Hilda akataka kuungana nae, ila alikatishwa na simu iliyotoka kwa IGP Ganjo akimtaka kituoni kwa muda huo. Hakuwa na la kupinga, akaondoka hapo huku akimuacha Koplo Hemedy akiondoka kuelekea kwa Mrutu.
Nyumbani kwa Mrutu. Mrutu alimuita Moto hapo nyumbani kwake baada ya kupata njia nzuri ya kumdhibiti Koplo Hemedy, asiwagundue au asifanikiwe kwa kuwapata wao. Moto alifika hapo baada ya nusu saa kuitwa na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Akaenda kukaa kwenye sofa sebuleni alipokuwa amekaa Mrutu akimsubiri yeye.
“Kaka naona unatembea na basotla kila sehemu?" Mrutu alimuuliza hivyo Moto aliekuwa ameitoa bastola yake kiunoni na kuiweka juu ya sofa baada ya kumsumbua pale alipokaa.
“Si unajua tena ulinzi popote. Duniani hakuna wema kaka” Moto aliongea huku akiiangalia bastola yake utafikiri ndio anaiyona kwa mara ya kwanza.
“Duh! Ni Kweli”
“Niambie kaka umepata mpango gani wa kumdhibiti huyo dogo" Moto aliongea hivyo huku akijua anamzuga Mrutu tu maana alishatuma watu kumuua Koplo Hemedy.
“Njia nimeipata baada ya kufikiria sana na ninzu....." Wote walishtuka baada ya mlango wa sebuleni kufunguliwa kigadhabu. Macho yao wakayapeleka hapo na kumkuta Koplo Hemedy akiwaangalia kwa hasira kuu. Macho yaliwatoka pima mithili ya mjusi kafiri aliebanwa na mlango baada ya kujua hasimu wao ndie alieingia hapo. Moto akawahi kuichukua bastola yake na kumuelekezea Koplo Hemedy.
Koplo Hemedy alipigwa na taharuki baada ya kumshuhudia baba yake mdogo akiwa na muuwaji wa wazazi wake. Ndio lazima sura aikumbuke si ametoka kuiona kwenye ile video muda si mrefu? Akabaki akiwa hajui afanye nini. Machozi yalianza kumtoka taratibu huku akiwa bado amesimama hapo hapo mlangoni haamini macho yake kama baba yake mdogo angeweza kumuua kaka yake kisa mali tu, akajikuta akianza kupiga hatua za taratibu akiwaendea wao. Ila alisimamishwa na ukelele wa Moto aliekuwa amemnyooshea bastola yeye.
“Simama hapo hapo mbwa wewe na leo nakuua mbele ya baba yako mdogo" Moto aliongea hivyo huku akiwa kasimama macho akiwa kayakaza kumuangalia Koplo Hemedy.
“Moto unataka kufanya nini tena nyumbani kwangu? Hujui kama hiyo ni kesi, tena itaniangukia mimi mwenye nyumba, acha hizo bwana!" Mrutu aliongea hivyo huku akiwa na yeye amesimama. Hapo Koplo Hemedy alivyosikia jina la mtu huyo alieitwa ‘Moto' akajua ndio huyo huyo aliewatuma wale watu kuja kumuua nyumbani kwake, akazidi kupandwa na hasira na mtu huyo.
“Mimi nataka nipoteze ushahidi kabisa, huyu mtu alitakiwa afe tangu zamani ila wewe ukajifanya kumkingia kifua, sasa leo namuua mbele ya macho yako" Moto aliongea huku bado bastola amemuelekezea Koplo Hemedy.
“Usitake kuchukua maamuzi ya haraka haraka, embu subiri tuyaongee tuyamalize kaka" aliongea hivyo huku akimfuata Koplo Hemedy pale aliposimama. “Mwanangu embu kaa chin..."
“Nani mwanao, tena toka mbele yangu muuaji mkubwa wewe" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akimsukuma Mrutu. Msukumo huo ulimfanya akampamie Moto aliekuwa nyuma yake na Moto bila kutarajia, aliminya ‘trigger' na risasi ikaenda kupiga kwenye bega la Mrutu. Hapo hapo Koplo Hemedy akamuwahi kwa teke la mkono na bastola ile ikaenda hewani. Moto akabaki kuiangalia bastola ile kule juu na kuisubiria ishuke ili aidake. Koplo Hemedy baada ya kumuona mtu huyo ameinua shingo yake kuangalia juu ilipo bastola. Akampiga ngumi mbili za haraka haraka za kwenye koromelo na kumfanya Moto arudi nyuma huku akiwa ameishika shingo yake. Jambo la kuvuta punzi na kumeza mate akiona kabisa hivi hivi vikimsaliti.
Wakati akirudi nyuma alimpamia Mrutu aliekuwa amelala chini kwa maumivu ya bega lake na kujikuta na yeye akienda chini. Koplo alimruka Mrutu na kumfuata Moto aliekuwa chini akigaagaa huku akiwa ameishika shingo yake. Alipofika pale alipo, alimshika kola ya shati alilovaa na kumuinua juu, kisha akampiga vichwa vitatu vya pua na kuifanya pua hiyo ipinde kwenda kushoto huku ikitoa damu kwenye tundu zote mbili. Akamuinua tena na kumpiga ngumi zisizo na idadi za kifua na kumfanya acheue damu kama sio kutapika kabisa.
Akamuinua tena huku akiwa analia kwa hasira na kumpiga ngumi nyingi za uso, na alipokuja kumuachia uso wote ulikuwa hautamaniki kwa damu kama nyama ya kuku buchani. Akamfuata pale chini alipolala na kumpiga ngumi moja ya nguvu ya mdomo. Halikuwa swala la kubisha au kupinga kwamba bwana huyo hata kama akipona hapo basi atakuwa ni kibogoyo. Meno yalipukusutika kama punje za mahindi kwenye gunzi huku domo likitoa damu iliyochanganikana na ute kama ng'ombe alierogwa.
Koplo Hemedy aliiende bastola iliyokuwa chini kwa hasira na kumuelekezea Moto kwa wakati huo alikuwa amepiga magoti akiomba msamaha pasi na kuongea. Ataongeoaje wakati domo linavuja damu mithili ya bomba la mvua? Tena sehemu hii ndio ile ile alipompigia mama yake na Koplo bastola ya shingo. Koplo Hemedy alipokumbuka hilo, wala hakuna mshauri nahasa wa kumshauri hilo lililoko kichwani mwake na yeye akashaurika. Hapo hapo akampiga risasi ya shingo na kumfanya Moto atoe macho kwa taharuki ya kukutana na malaika mtoa roho kwa mara ya kwanza tangu azaliwe.
Akamuongezea risasi nyengine mbili za kifua, na Moto akabaki mdomo wazi huku akionekana kama vile kuna kitu anataka kusema, lakini alijikuta akifumbwa mdomo na risasi aliyopigwa mdomoni, akaenda chini na kutulia kimya akiwa hawezi tena kunyanyuka. Atanyanyukaje wakati roho yake imeshaagana na mwili muda mfupi uliopita? Koplo Hemedy akabaki kulia tu kwa uchungu huku akiwataja wazazi wake akiwa amepiga magoti chini.
Mrutu muda wote alikuwa ameshika bega lake sehemu lilipo jeraha alilopigwa risasi na hayati Moto huku akiwa haamini hata kidogo kwa anayoyaona, alikuwa ameacha mdomo wazi huku akimuangalia Moto pale chini alipolala pasi na kuwa na roho yake kwa jinsi mwili wake ulivyo chafuliwa. Muda huo huo Konstebo Hilda aliingia humo ndani huku akiwa ameongozana na askari watano wenye silaha mikononi mwao.
Konstebo Hilda alimkimbilia Koplo Hemedy pale alipo na kumuangalia kama yupo salama huku wale askari wengine wakiitoa maiti ya Moto huku wengine wakimchukua Mrutu mzega mzega hadi kwenye gari la polisi. Konstebo alimuinua Koplo Hemedy pale chini alipo na kutoka nae nje, huko walikuta gari la polisi limeshaondoka hapo na wao wakaingia kwenye gari alilokuja nalo Koplo Hemedy hapo na kuondoka kuelekea kituoni.
“Koplo, unauhakika kwamba yule marehemu ndie alieuwa wazazi wako akishirikiana na wenzake akiwemo baba yako mdogo?" IGP Ganjo alimuuliza hivyo baada ya kuwa nae ofisini kwake.
“Mkuu uhakika ninao na ushahidi pia ninao" Koplo Hemedy alimuambia IGP Ganjo hivyo wakati huo alikuwa ameshanyamaza kulia.
“Unaweza ukanipa huo ushahidi, maana hii kesi ya mauwaji itakuhusu kama ukiwa hauna ushahidi kwa hicho unachosema" IGP aliongea na kumfanya Koplo Hemedy kumtolea flash yenye video kisha IGP akaichomeka kwenye Kompyuta yake na kuiangalia kwa umakini hiyo video.
“Hapa kidogo ninayo njia ya kukusaidia kwa kukuokoa na hilo zahma mahakamani.... Unajua Koplo kama usingekuwa na huu ushahidi, basi hii kesi ingekuangukia wewe na wala usinge weza kuchomoka mikononi mwa sheria" akamrudishia flash yake na kumuambia.
“Umesema bado wangapi?" IGP alimuuliza.
“Bado watatu mkuu na mmoja nimeshapajua ofisini kwake" Koplo Hemedy alijibu.
“Embu ngoja kwanza mara moja" IGP aliongea hivyo, kisha akasimama na kuliendea kabati la kuhifadhia mafaili, akachangua changua na kurudi na faili moja, akaliweka juu ya meza na kulifunua, humo ndani kulikuwa na picha nyingi nyengine za kutisha zilizojaa damu na majeraha mengi kwenye miili hiyo ya kwenye hizo picha. Akaanza kuangalia picha moja baada ya nyengine hadi pale alipopata picha mbili zenye taswira zilizokuwa zimechafuka kwa damu na majeraha. Akaziangalia vizuri na kumuomba Koplo Hemedy ile flash tena na kuichomeka kwenye kompyuta yake, kisha akasema.
“Hawa watu wawili kwenye hii video yako ndio hawaapa kwenye hizi picha. Walikutwa wamekufa kwenye daraja la Amboni miaka sita iliyopita" Akamuangalia usoni Koplo Hemedy huku akitabasamu.
“Najua unajiuliza nimewakumbukaje hawa watu baada ya kuwaona kwenye hii video. Ila iposiku na wewe utakuja kujua mimi nimewakumbukaje kama sio kuwajua hawa watu kwenye hii video yako... Hawa watu wameshakufa zamani na muuwaji hajapatikana hadi leo, sasa kumebakia mtu mmoja tu na ndio huyo mwengine kwenye hii video, na bilashaka ndio huyo uliesema unapajua anapofanyia kazi. Nitatuma askari wakamkamate na wamlete hapa kituoni" IGP aliongea.
“Lakini mkuu naomba nikamchukue mwenyewe huyu" Koplo Hemedy aliongea.
“Hapana Koplo, ukienda wewe unaweza hata kumuua kwa hasira ulizokuwa nazo kwa mtu huyo, ni bora waende askari wengine wamlete halafu atahukumiwa na mahakama lakini sio kumuua" IGP aliongea.
“Mkuu nakuahidi sitomfanya chochote hadi namleta hapa kituoni, kwahiyo nakuomba nimfuate mwenyewe Mkuu" Koplo Hemedy aliongea kwa kulalamika na kumfanya IGP Ganjo kumuangalia usoni kwa muda, kisha akasema.
“Unajua Koplo hiyo ni kesi ya mauwaji ikiwa utamuua. Lakini kwa vile wewe ni askari na unazijua sheria, basi mimi nakuruhusu uwende ila chunga sana usije ukaingia pabaya"
“Sawa mkuu" aliongea hivyo kisha akainuka na kupiga salut.
“Unaenda wapi?"
“Naenda kuongea na yule mtuhumiwa alieshiriki kwenye mauwaji ya wazazi wangu" Koplo Hemedy aliongea hivyo na kumfanya IGP kumruhusu aende. Akatoka na kwenda kwenye sero aliyomo Mrutu na kumchukua hadi kwenye chumba cha mahojiano.
“Hivi ni kweli bamdogo umeshiriki kwenye mauwaji ya wazazi wangu. Umeshiriki kuiondoa roho ya kaka yako kisa mali tu?" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku dhahiri akionekana anaweza kulia muda wowote kuanzia hapo.
“Nisamehe sana mwanangu ni tamaa tu zile ndio zimeniponza na ninajuta sanaa" Mrutu aliongea huku akilia, kipindi hichi kwenye bega lake kulifungwa bendeji kwenye lile jeraha lake.
“Tamaaa, tamaa wakati baba yangu nakumbuka alikuwa akikupa chochote unachotaka hadi nikadhani mmelazaliwa tumbo moja kumbe mama tofauti. Au nikwavile hujazaliwa na mama nae?" Koplo Hemedy aliongea kwa hasira huku akimuangalia Mrutu kwa macho ya gadhabu.
“Hapana sio hivyo mwanangu, zile zilikuwa ni tamaa tu na ushawishi, lakini sikuwa na uwezo wa kufanya hivyo" Mrutu aliongea huku akilia sasa.
“Ok, ok. Na vipi kuhusu siku ile mahakamani ukasema kuwa zile mali hazikuwa ni za baba, kuna ukweli wowote hapo?" Koplo Hemedy alimuuliza.
“Hapana zile zilikuwa ni ‘trick' tu kutaka kuzichukua zile mali, lakini hakuna ukweli wowote kwa kile kilichoongelewa pale mahakamani siku ile"
“Mko wa ngapi katika ule mpango wenu?"
“Tulikuwa watatu na mmoja ndio huyo uliemuua. Nisamehe sana Hemedy niko tayari kutoa ushahidi wote mahakamani mali zote zirudi mikononi mwako"
“Nasikitika kukuambia dhalimu wewe kuwa kifungo cha maisha kina kuhusu, subiri apatikane na huyo mwenzako, mtaenda kujibu mahakamani" Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiinuka kwenye kiti na kuondoka hapo huku akimuacha Mrutu akimuomba msamaha bila kikomo.
Majira ya usiku nyumbani kwa Koplo Hemedy, alikuwa yupo sebuleni kwake akiwa amekaa akiminyaminya ‘laptop' yake. Hapo alionekana Konstebo Hilda akitokea jikoni na kuja kukaa karibu na Koplo Hemedy.
“Mume wangu chakula tayari, twende mezani tukale" Konstebo Hilda pamoja na kuwa ni askari, lakini sauti yake nzuri haikubadilika, ilikuwa ni ileile iliyochagizwa na mirindimo ya kipwani.
“Subiri kwanza nimalizie hapa nakuja sasa hivi" Koplo Hemedy aliongea hivyo pasi na kumuangalia mwanamke huyo usoni. Hapo Konstebo Hilda alionyesha kukasirika akabaki kuvimbisha mashavu yake kama chura mwenye mimba huku akiwa kageukia pembeni. Koplo Hemedy baada ya kumuangalia kwa jicho pembe na kumuona katika hali hiyo. Akaacha anachokifanya na kupitisha mkono wake kwenye kiuno laini cha mnyange huyo mdogo kabisa mwenye kumiliki miaka ishirini na moja tu hadi sasa.
“Ukinuna wewe kwenye moyo wangu ni msiba. Haijalishi ni kwa kiasi gani lakini na kuahidi kukupa mahaba. Yale ya wazee wa zamani naamini utashiba. Nakupenda mke wangu wewe ndio mama mimi baba".
Koplo Hemedy alipoongea hivyo, Konstebo Hilda kule alipoelekezea uso wake akajikuta akitabasamu, tabasamu ambalo limetoka chini ya uvungu wa moyo wake kwa maneno hayo. Koplo Hemedy baada ya kuona mpenzi wake hajageuka huku upande wake. Akaendelea.
“Wewe ndie mwezi wangu, usiku waangazia.
Ewe ndie taa yangu, mwanga wanimulikia.
Wewe ndie nuru yangu, wewe ndio langu pazia.
Nisamehe mke wangu, kukuudhi sikupenda.
Nakupenda wewe wangu, kwengine siwezi kwenda”.
Hapo Koplo Hemedy alimbeba kwa kupitisha mkono wake wa kushoto kwenye shingo ya mnyange huyo huku wakulia ukikamata nyuma ya magoti na kumfanya binti huyo arushe rushe miguu huku akicheka. Alimbeba na kwenda nae kwenye meza ya chakula na kumuweka kwenye kiti na yeye akikaa kwenye kiti chengine. Muda wote Konstebo Hilda alikuwa na tabasamu usoni mwake huku akimuangalia kijana huyo kwa jicho ambalo lilionyesha akihitaji kitu fulani.
Waliendelea kula huku kila mmoja akiwa kimya huku wakiangaliana kwa zamu, ni vijiko tu ndo vilisikika hapo vikipigana vikumbo na sahani. Walipomaliza kula waliingia chumbani baada ya kuhakikisha kila kitu wamekiweka sawa huko nje.
* * * *
Siku iliyofuata wakajianda wote na kuelekea kituo chao cha kazi, walipofika Koplo Hemedy alimuacha Konstebo Hilda hapo na yeye kuondoka hapo baada ya kusaini na kuelekea kwenye kampuni ya Mata. Dakika kumi na tano zilitosha kumfikisha. Alipofika akapaki gari nje na yeye akaingia ndani na mapokezi akamkuta mwanamke yule yule aliekuweko jana.
“Habari ya leo mrembo?" Alisabahi huku usoni tabasamu likimjaa.
“Safi tu, za tangu jana?" Mwanamke huyo alijibu na kuuliza akiwa na yeye anatabasamu usoni mwake.
“Nzuri tu, sijui huyu jamaa nimemkuta?"
“Aaa bosi bado hajakuja, ila hii ndio mida yake ya kuja. Unaweza ukamsubiri hapo kwenye hilo sofa" Mwanamke huyo aliongea hivyo na Koplo Hemedy akaenda kukaa kwenye sofa lililokuwa hapo. Baada ya nusu saa baadae, aliingia Mata alionekana mwili wake kuridhika na hela. Alifika hapo mapokezi na kumsalimia ‘secretary' wake.
“Bosi halafu kuna mgeni huyo hapo alikuwa anakusubiri" mwanamke huyo aliongea huku akimsontea kidole Koplo Hemedy. Muda wote huo Koplo Hemedy alikuwa akitabasamu tu baada ya kujidhihirishia kuwa mtu aliemfuata ndio huyo hapo mbele yake.
“Karibu ofithini huku" Mata aliongea hivyo kumuambia Koplo Hemedy. Ilionekana dhahiri hakumjua hata kidogo. Hata hivyo atamjuaje wakati alivyomuacha na sasa hivi alivyo ni tofauti? Wakaongozana wote hadi ofisini kwake, alipofika akamkaribisha kwenye viti vya wageni huku yeye akikaa kwenye kiti chake cha kuzunguuka.
“Karibu bwana nani kumbe...?" Mata aliongea hivyo huku akimuangalia mgeni huyo machoni mwake.
“Hemedy... Hemedy Muheshimiwa Bhachu au kwenye kazi yangu wananiita Koplo Hemedy" Koplo Hemedy alikuwa akiongea kwa tabasamu huku huyo anaeongea nae akiwa macho kayatumbua kama mtu aliekutana na mzuka wa Nsyuka macho kwa macho baada ya kusikia jina la mtu huyo.
Aligwaya kwa si kitoto!!.
“U...umethema unaitwa nani?" Mata alimuuliza huku hofu, woga, wasiwasi na hamaniko vikiwa pamoja nae.
“Haina haja ya kurudia jina, nadhani hadi hapo ushanijua mimi ni nani" Koplo Hemedy aliongea.
“Unataka nini hapa ofithini kwangu?" Mata alijifanya kukaza wakati dhahiri uoga ulionekana waziwazi usoni mwake.
“Nimekuja kukuchukua tuende kituoni kisha mahakamani ukajibu mashtaka uliyodhani umeyakimbia miaka kadhaa nyuma"
“Sikilidha kijana, nitakupa petha kiathi chochote ukitakacho halafu uniache" Mata alijaribu kumshawishi.
“Hicho kiasi chochote cha pesa unachotaka kunipa nitakipata endepo utasimama pale kizimbani ukisomewa mashtaka yako, utakapo hukumiwa basi itapitishwa na hukumu ya kurudishiwa mali zangu zote ambazo mmezidhulumu"
“Kijana nitakupigia kelele dha mwidhi thatha hivi" Mata aliongea huku akiinua simu ya ofisini kwaajili ya kuita walinzi waje kumtoa Koplo Hemedy. Ila mkono wake ukagandamizwa hapo hapo juu ya hiyo simu na mkono ngangari wa Koplo Hemedy, akabaki akigugumia kwa maumivu huku akijaribu kujinasua, ila hakuweza.
“Sikuja kukuua na usinilazimishe kufanya hivyo kama ambavyo nimefanya kwa yule mwenzenu mnaemuita Moto" Macho ya Mata yalitoka nje sentimita tano na kurudi tena ndani kwa mshtuko alioupata kusikia taarifa hiyo.
“Una...unathema umemuua Moto?" Mata aliuliza huku uoga ukiongezeka mara dufu.
“Ndio nimemuua na sasa yuko monchwari akisubiria ndugu zake waje kuuchukua mwili wake na nitafanya hivyo na kwako kama utaleta ubishi wa aina yoyote... Au sijui nikuue tu na wewe ilinitimize roho mbili kuziondoa duniani.... Unajua kuua raha sana, acha kwanza nikuue halafu nikupeleke kituoni ukahifadhiwe huko kisha mwili wako upelekwe mahakamani kwenda kujibu mashtaka, naamini hiyo itakaa poa sana au wewe unasemaje?"
“Hapana kijana wangu uthiniue, nitakupa hata mali dhote, nithamehe thana" Mata aliongea huku akilia, ukumbuke wakati huo mkono wake bado unaadhibiwa kwa kuminyizwa juu ya simu ya mezani sijui ndio ya ofisini.
“Wewe mbona uliwauwa wazazi wangu huku unacheka, si inaonekana kitendo kile kilikufurahisha, acha na mimi leo nifurahi kwa kuitoa roho yako hapa ofisini kwako, hata hivyo litakuwa ni jambo zuri kwasababu nitakuwa naitoa roho yako kukiwa hakuna mtu yoyote anaeshuhudia kitendo hicho zaidi ya mimi na wewe tu"
“Nithamehe kijana, thirudii tena, mwendhio nina familia, nina mke na mtoto mmoja, sasa unadhani ukiniua mimi familia yangu itaishije" Maneno hayo yalimtia gadhabu Koplo Hemedy na kumfanya auachie ule mkono wake aliougandamiza kwenye simu na kumpiga ngumi mbili za jicho la kulia. Jicho hilo lilivimba kwa juu kidogo huku kwa ndani likibadilika rangi na kuwa jekundu kama limepakwa ‘lipstick'. Kisha akaivuta kwa mbele tai yake na kuufanya uso wake uje mzima mzima kwa mbele, hapo akampiga ngumi nyingi za uso na uso huo ukawa umevimba huku unatoa damu kama maji ya shukayo kwenye maporomoko.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mlivyoniulia wazazi wangu mlitegemea mimi niishije, niishi wapi? Au unaongea tu kwavile wewe ndio umefanya vile. Mmenifanya ninusurike kifo kwa kutaka kuchomwa moto bila hatia na raia waliodhani mimi ni mwizi kwa kutanga tanga usiku pasi na kujua nielekee wapi. Halafu unakuja kuniambia eti nikuonee huruma unafamilia, kwani mimi niliishije bila familia baada ya kuniulia wazazi wangu? nataka huyo mwanao na yeye ajekuishi bila familia kama vile ambavyo mimi nimeishi" Alikuwa akiongea kwa uchungu mkubwa sana huku chozi likimdondoka. Akakishika kichwa cha Mata na kukipigiza kwenye meza mara nyingi na alipokiachia......!
Ajuae ni mungu na mimi nilieshuhudia.
Akamuinua na kuanza kumtoa nje huku akiwa ameishika tai aliyoivaa akawa anaivuta kwa mbele na kumfanya Mata afananiane na mbuzi anaegoma kupelekwa machinjioni. Akamvuta hivyo hivyo na kumtoa ndani ya hiyo ofisi. Wafanyakazi wote walipigwa na butwaa huku wafanyakazi wakike wakipiga kelele za hofu baada ya kuiona hali hiyo aliyonayo bosi wao. Yule ‘secretary' wake alizidi kuchanganyikiwa baada ya kuishuhudia sura aliyonayo Koplo Hemedy sio ile aliyokuwa nayo hapo wakati anaingia. Aliingia kwa sura nzuri yenye tabasamu zuri, lakini sasa liletabasamu halikuwepo wala ule uzuri pia haupo.
Alikuwa sura ameikunja kama mtu akunjavyo nguo akitaka kuziweka kabatini huku akimvuta Mata tai yake kumtoa nje. Alijua kabisa kuwa hiyo sio sheria na hata huyo anaemfanya hivyo akiamua kumshtaki basi anakesi ya kujibu, wafanyakazi walitoka nje kumshuhudia bosi wao anavyotolewa nje mkukumkuku na mtu wasiemjua. Ikabidi mfanyakazi mmoja wa kiume ajitoe kimasomaso kumfuata Koplo Hemedy.
“Kaka vipi, mbona huyu mtu hivi tena, kuna nini?" Jamaa huyo aliongea. Koplo Hemedy kwa ghazabu alizokuwa nazo hakutaka hata kuongea, akamtolea kitambulisho cha kazi na kumuonyesha.
“Hata kama ni askari, lakini sio haki kumchukua mtuhumiwa hivi hai hai namna hii" Jamaa aliongea.
“Huyu nimekuja kumchukua kistaarabu, ila yeye akataka kuniitia mimi mwizi, sasa ndio nikaona nimfunze adabu kwanza" Koplo Hemedy alivyoongea hivyo, akamfunga pingu na kumtia kwenye gari lake, safari ya kuelekea kituoni ikaanza. Njia nzima Mata alikuwa akilia huku akiomba msamaha, lakini Koplo wala hakutaka kumsikiliza.
Walifika kituoni, akamshusha na kumuingiza ndani, huko akamkabidhi kwa askari mwengine amuhoji maana anaweza akamuulia hapo hapo kituoni kwa ghadhabu alizokuwa nazo, akaenda ofisini kwa IGP.
“Mkuu tayari nimemleta" aliongea hivyo baada ya kukakamaa kwa heshima.
“Yupo wapi?" IGP alimuuliza.
“Yupo chumba cha mahojiano na Koplo Kindo"
“Sawa, nenda kaendelee na kazi na inabidi kesi zao tuzipeleke mahakamani haraka iwezekanavyo kwa sababu ushahidi upo"
“Sawa Mkuu" akakakamaa na kuondoka hapo ofisini.
Siku nne mbele walipelekwa mahakamani kwenda kujibu mashtaka yao. Muda wote huo Mata alikuwa haamini kwamba ndio wanaenda mahakamani na alijua kuchomoka haiwezekani kwasababu ushahidi wa kueleweka upo, tena video bora hata kama ingekuwa ni maelezo angeweza kupinga. Lakini ilikuwa ni sura yake ile ile, ataanzaje kuikataa, labda aseme wapo mapacha au autumie ule msemo kuwa duniani wawili wawili. Lakini ndio afanane kila kitu na yeye?
Mahakama ile ile waliyotumia kudhulumu mali za watu, ndio hiyo hiyo wanayoenda kuhukumiwa. Mahakama ya Chumbageni, ndio mahakama wanayoenda kusomewa mashtaka yao. Walifikishwa na kuingizwa katika chumba cha washtakiwa wanaosubiri muda wao wa kupanda kizimbani ufike waende. Walikaa hapo kwa nusu saa ndio muda wao ukafika. Waliingizwa ndani ya mahakama na kupandishwa vizimbani na kuanza kusomewa mashtaka yao.
Wakaulizwa kwamba wanayapinga au laa! Hawakuwa na namna ya kupinga wakati ushahidi upo wa kujitosheleza. Hapo wakasomewa tena mashtaka ya kudhulumu mali na hapo pia hawakupinga. Ukafika muda wa kutoa hukumu. Hakimu akasoma vifungu vya sheria na kutoa hukumu kwa watu hao.
“............wana hukumiwa na mahakama kifungo cha maisha kwa kosa la kuua kwa kukusudia na kudhulumu mali za watu kwenye mahakama tukufu bila mahakama kujua. Mali zote walizokuwa wakizimiliki, zitataifishwa na kurudishwa kwa mshtaka bwana Hemedy Muheshiwa Bhachu kuanzi hivi sasa" Hakimu akagonga nyundo kuashiria Hakuna tena la mjadala.
Zilisikaka sauti za vilio kutoka kwenye mabenchi ya watu waliokuja kusikiliza hizo kesi. Alikuwa ni mwanamke wa makamo na mtoto mmoja wa kiume ndio walikuwa wenye sauti hizo za vilio baada ya hukumu hiyo kupita.
Mke na mtoto wa Mata ndio waliokuwa wakilia kwa uchungu baada ya kichwa cha familia kuhukumiwa kifungo hicho. Koplo Hemedy pamoja na kuwa na tabasamu kwa hukumu hiyo, lakini aliingiwa na roho ya huruma baada ya kuwaona watu hao wakilia, akajua moja kwa moja ndio hiyo familia ya Mata maana baba yake mdogo hakuoa wala hakuwa na mtoto. Akatamka mbele ya mahakama kuwa ameiachia familia ya Mata nyumba wanayokaa na fuso mbili za kazi ili kujikimu kipindi hicho ambacho Mata atakuwa yupo gerezani akitumikia kifungo chake.
Mahakama haikupinga hivyo kutokana na yeye ndie mwenye hizo mali. Kesi hiyo ikaisha na watu hao wakapelekwa gerezani huku wakimuacha Koplo Hemedy uraiani akiwa na mali nyingi sanaaa. Baada ya siku mbili walipewa taarifa kuwa Mata alikufa huko jela kwa ugonjwa wa moyo. Ikawa ndio mwisho wake huku familia yake ikihuzunika.
Koplo Hemedy baada ya kukabidhiwa mali zake zote zilizokuwa zikimilikiwa na wale watu watatu, yani Mata, Moto na Mrutu. Akaziuza zote ila alibakisha ile showroom ya magari na kuiongezea kuwa kubwa zaidi. Akafungua na kampuni kubwa ya kusafirisha mizigo mikubwa kutoka hapo Tanga kwenda kwenye mikoa mengine na nchi jirani. Akawa sasa anaishi kwenye nyumba iliyoachwa na wazazi wake huku akiwa na Konstebo Hilda.
* *
Siku moja wakati IGP Ganjo akiwa ofisini kwake. Simu yake ya mezani iliita, aliitazama kwa sekunde kadhaa na kuipokea.
“Bilashaka naongea na IGP Makame Ganjo kutoka mkoa wa Tanga kituo cha polisi Mabawa?" Sauti nzito ya upande wa pili iliongea. IGP akajiuliza hii sauti ni ya nani? Maana hakuwahi kuisikia hata siku moja, ila hakupata jibu.
“Ndio ni mimi ila sijajua naongea na nani?" IGP aliuliza.
“Ok, hii ni simu kutoka Ikulu Daresalam" Mtu wa upande wa pili alijibu na kumfanya IGP kuchoka ghafla. Alichoka ndio. Akajiuliza inakuaje simu kutoka ikulu ije kwake wakati kuna wakubwa zake, sasa ni vipi ije kwake? Kwanza alidhani ni masihara, akaitoa hiyo simu sikioni na kuiangalia, akidhani itampa jibu lolote kwa hayo aliyokuwa akijiuliza. Akairudisha tena sikioni na kusikiliza pasi na kusema kitu.
“Kesho asubuhi unatakiwa uende uwanja wa ndege wewe na wale wajukuu zako, yani Hemedy na Hilda. Mkifika hapo mtakuta kuna ndege inawasubiri kuwaleta huku. Najua huamini ila sasa hivi atakuja mtu hapo ofisini kwako kukuletea barua. Asante kwa kunisikiliza. Fanya kama barua itakavyo kuelekeza" Simu ikakatwa na kumuacha IGP Ganjo asielewe ni kipi kilichotokea hadi kuwa hivyo? Na ni kwanini aitwe yeye na Koplo Hemedy na Konstebo Hilda? Baada ya dakika ishirini za kujiuliza maswali. Mlango wake ukagongwa na kumruhusu huyo mgongaji aingie. Aliingia kijana nadhifu alievaa suti safi, ilikuwa ni sura ngeni kwake hakuwahi kuiona hata mara moja. Akamruhusu akae na yeye akakaa. Wakasalimiana kidogo na mtu huyo akatoa bahasha na kumkabidhi IGP. Kisha akaaga na kuondoka.
IGP mikono ilikuwa ikimtetemeka kwa hofu baada ya kushuhudi nembo ya uhuru ikiwa juu kwenye hiyo bahasha pembeni yake pakiandikwa jina lake. Akaifungua na kuanza kusoma, kilichoandikwa humo ndani hakikuwa na tofauti yoyote na vile alivyoambiwa, ila huku msisitizo ulitumika zaidi, chini kabisa kulikuwa na saini ya Raisi. Hapo ndipo alipoamini kuwa ni kweli. Hapo hapo akawaita Koplo Hemedy na Konstebo Hilda ofisini kwake, walipofika hakutaka kuwaambia chochote, aliwakabidhi hiyo barua na kukaa kimya akisubiri wamalize kuisoma.
Iliwachukua dakika moja tu kuisoma na askari hao wakabaki kumuangalia mkuu wao kwa macho ya mshangao na ya kuuliza. Kunanini mbona hivi? Ila walipata jibu kupitia macho ya IGP kuwa. Sijui hata mimi pia nipo kwenye koma.
Siku iliyofuata asubuhi. Walienda uwanja wa ndege na kupokelewa na yule kijana alieleta barua jana, akawaongoza hadi kwenye ndege moja ndogo na kuwaingiza humo na safari ya kuelekea huko wanakotakiwa ikaanza. Walitumia saa moja kufika katika uwanja wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere. Ndege hiyo ikapaki sehemu maalumu na watu hao wakashuka na kuongozwa kupelekwa kwenye gari mbili za Ikulu zilizokuwa zikiwasubiri hapo uwanjani.
Muda wote walikuwa bado na maswali mengi vichwani mwao. Hawakujua huko wanaenda kufanya au kufanywa nini? Maana sio rahisi kwa askari wa kawaida kupelekwa tu Ikulu kirahisi rahisi. Walifunguliwa geti baada ya kufika na gari hizo zikaenda kupaki sehemu maalumu. Wakashuka huku wakishangaa shangaa mazingira ya humo ndani jinsi yalivyokuwa ya kupendeza. Hapo akaja mtu mwengie aliewataka wamfuate huko anapoelekea yeye, huyu alikuwa ni mwanamke alikuwa ndani ya suti safi ya kike.
Akawaongoza hadi katika mlango mmoja kati ya mingi waliyoipita huko nyuma. Walipofika hapo akawaambia wasubiri muda si mrefu mlango utafunguliwa na wao waingie humo. Kisha yeye akaondoka akiwaacha watu hao wakimuangalia pasi na kuelewa chochote hadi muda huo... Mlango ulifunguka na wakaingia ndani kama walivyoambiwa. Hapo Konstebo Hilda na Koplo Hemedy walipata mshtuko baada ya kumuona Baba yake na Ramah akiwa amekaa na Raisi wa nchi wakiwaangalia wao. Wakakaribishwa wakae kwenye viti wakiwa na mshangao wao hivyo hivyo na wao wakafanya hivyo.
“Najua bado mnajiuliza kwanini mmeitwa hapa. Ila tambueni kuna kazi maalumu mnayotakiwa kuifanya baada ya nyie vijana kutoka mafunzoni" Mr Kaoneka alipoongea hivyo, akamgeukia Raisi na akatakiwa aendelee. Kisha akasema...
“Hemedy wewe tulikuwa tunakufuatilia tangia ukiwa mdogo mwenye umri wa miaka saba baada ya kukaa kikao na Raisi wa nchi wa kipindi hicho na kuona kuna ulazima wa kuunda kitengo cha siri kitakacho fanyia kazi taifa hili baada ya kuona matukio mengi makubwa ya kiuhalifu na ugaidi kushamiri hapa nchini. Tukakaa kikao cha watu watatu tu, ikiwa ni pamoja na mimi na mshauri wa Raisi wa kipindi hicho ambae kwa sasa ni marehemu na Raisi wa kipindi hicho ambae kwa sasa ameshastaafu. Kikao hicho kilikuwa kikizungumzia juu ya usalama wa taifa hili. Tukaona kuna umuhimu wa kutengeneza ama kuunda kitengo cha siri sana kitakacho fanyia kazi taifa hili hapo baadae. Ndipo ikatubidi kutafuta vijana wadogo wenye akili nyingi na uelewa wa haraka na ukakamavu na ujasiri ambao tutawatengeneza waje kukitumikia kitengo hicho. Tukaona tutafute vijana hao katika mikoa tofauti. Tukaanzia hapa Dar, tukaenda na Arusha, tukafuata Mwanza, Tukaenda Tanga na kumalizia na Zanzibar. Huko kote tumetafuta kijana mmoja mmoja. Tukafanikiwa kupata wanaume watatu na wakike wawili. Wakike tumewapata Dar na Mwanza, ila huyo wa mwanza alifariki muda tu, ndipo tukaamua tumeweke huyu Hilda akakave sehemu ya huyo aliekufa. Nadhani mlishangaa sana baada ya kumaliza ‘form six' mkatakiwa kuenda JKT kisha mkapelekwa jeshini moja kwa moja bila kuelewa. Hiyo yote ilikuwa ni mipango yetu na hata pale wewe Hemedy ulipopandishwa cheo kwa mwaka mmoja tu pia ilikuwa katika mipango yetu..." Akatulia kidogo kuwaangalia watu hao na kuwaona wapo katika usikivu mkubwa. Kisha akaendelea. “Nadhani hapo mshaelewa ni kwanini mmeitwa Ikulu. Hamna budi kukubali kwenda kwenye mafunzo ya ujasusi miaka sita nchi za mbali, hata hivyo mtakuwa mnatetea Taifa lenu na watu wake zidi ya wahujumu wanaotaka kuihujumu nchi hii. Je mko tayari kwa hilo? Kwasababu hatuwezi kuwalazimisha" Mr Kaonekana aliwafafanulia sababu ya wao kuitwa Ikulu kisha akawauliza swali.
Koplo Hemedy na Konstebo Hilda walimuangalia babu yao na kukuta akiwa na tabasamu kuu usoni mwake, kisha akainua kichwa juu chini ishara ya kuwaambia wakubali. Na vijana hao wakakubali kuwa wapo tayari kulitumikia taifa lao kwa njia hiyo. Hapo Mkuu wa nchi na Mr Kaoneka waliachia tabasamu usoni mwao. Kisha Mr Kaoneka akasema.
“Napenda sana vijana wenye kujitolea kwa taifa lao bila kulazimishwa. Wenzenu wawili wameshatangulia kwenda mafunzoni jana. Na kesho ndio mtaondoka nyie halafu kesho kutwa ataondoka huyo mmoja aliebakia. Huko mafunzo yataanzia Korea, halafu mtaenda na Japan, mtamalizia na China kwa bara la Asia. Kisha Mtaenda Marekani na Urusi kisha Mtamalizia na Cuba. Hadi hapo mtakuwa mmeiva kwa kila sekta ya ujasusi. Mafunzo hayo yata chukua miaka sita hadi kumalizika kisha hapo ndio mtarudi Tanzania mkiwa tayari mpo vizuri kukitumikia kitengo tulichokipa jina la TSSI yani Tanzania Secret Service Investigation. Mtakaporudi ndio mtapangwa kutokana na juhudi na umakini mtaouonyesha huko ndio mtapangwa wa kwanza ni nani hadi watano. Yani atapatikana TSSI 01 hadi TSSI 05, hadi hapo mimi sina tena chakusema, labda nimuachie Kiongozi hapa kama analolote la kusema amiambie" Alimaliza Mr Kaoneka.
“Mimi namiambia tu juhudi na umakini ndio vitu vinavyo hitajika huko ili ufaulu vizuri. Huku kuandaliwa nyie hakukuanza leo wala jana. Mpango huu ulianzi kwa Raisi wa awamu ya pili Dr. Hussein Molito. Yeye ndie alikaa chini na huyu Mr Kaoneka na kujadiliana ni vipi watalilinda taifa lao wakiwa pamoja na mshauri mkuu wake ambae kwa sasa ni marehemu. Mpango huo ukaendelea hadi kwa Raisi wa awamu ya tatu naye akajulishwa hadi wanne na wa tano sasa niko mimi wa awamu ya sita. Hata mimi pia nimefurahi kuona vijana mnakuwa wazalendo na nchi yenu pasipo kulazimishwa. Nashkuru sana na ninawatakia safari njema na mafunzo mema" Alimaliza kuongea Mheshimiwa Raisi Alex Kileo na wakaitiwa mtu wa kuwapeleka hotelini kwenda kupumzika.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyofuata, walitolewa hotelini na kupelekwa moja kwa moja uwanja wa ndege kwa safari ya kwenda huko mafunzoni. Ilikuwa ni furaha kwa wote kwa kuajiriwa katika kitengo hicho cha siri serikalini. Njia nzima IGP Ganjo alikuwa akiwaasa sana huko wanapoenda wasifanye mchezo na wawe makini sana na mafunzo hadi pale yatakapo kamilika.
Walifika uwanja wa ndege na kufanya taratibu zote. Kisha wakasubiri muda wa kuondoka hiyo ndege ufike. Muda ulipofika waliingia ndegeni na kumuacha IGP Ganjo na Mr Kaoneka kuwanyooshea mkono wa kwaheri na ndege ikapotelea mawinguni. IGP Ganjo na Mr Kaoneka walipeana mikono na IGP akapanda ndege kwaajili ya kurudi Tanga....
MWISHO
0 comments:
Post a Comment