Search This Blog

Friday, 28 October 2022

KISASI - 3

 









    Simulizi : Kisasi

    Sehemu Ya Tatu (3)







    “KITU KIKUBWA KINACHOTUOGOPESHA SI KWAMBA TUNA MAPUNGUFU AU KWAMBA HATUJAKAMILIKA. WOGA WETU MKUBWA NI KWAKUWA TUNA NGUVU KUPITA KAWAIDA. HUO NI MWANGA WETU, NA WALA SIO GIZA LINALOTUOGOPESHA MDA WOTE. MUDA MWINGINE TUNAJIULIZA ‘MIMI NI NANI MPAKA NIWE MWENYE KIPAJI, NGUVU, MWEREVU AU MWENYE AKILI NYINGI?’ LAKINI TUNASAHAU KUJIULIZA KWANI ‘MIMI NI NANI MPAKA NISIWE VYOTE HIVYO?’. MAISHA NI KWA WALE WAAMINIO UZURI WA NDOTO ZAO, NI KWA WALE WAOTAO NA KUFANYA JUHUDI YA KUZIBADILI NDOTO ZAO KUWA KWELI. Unaweza kama Ukiamua,,WEWE NDO WA KUJIPANGIA MAMBO MENGI UYATAKAYO. Hii ni sehemu ya TISA



    Inawezekanaje mtu amfukie mwenzake akiwa mzima, tena mama yake,,,looh! Nikajiuliza mara mbili mbili lakini sikuelewa kabisa huyu Khajat alikuwa mtu wa aina gani, nilijaribu sana kufikiria huyu msichana ni wa aina gani lakini bado akili yangu ilirudi nyuma tena na kutafakari iweje msichana wa aina hiyo japo sijamuona awe na roho ya kiume namna ile. Nilitulia nikimsikiliza Patrick wakati akiendelea kusimulia.

    **PATRICK**

    Niliganda, nilikuwa nimetumbua macho nisijue nini cha kufanya kwakweli. Sikuelewa nini fundisho pale, sikujua ni kwa vipi mtu anaweza kuwa mnyama vile. Khajat alikuwa na macho makavu kabisa. Hakuwa akicheka wala hakusomeka usoni mwake.

    “Patrick wewe ni mwanaume au mwanamke?” aliniuliza huku akinitazama kwa hasira.

    “Kwanini unaniuliza swali la kipuuzi hivyo” nilimuuliza huku nikimtazama usoni.

    “Kwanini unakuwa muoga kiasi hicho hasa kwa kitu ambacho hufanyi wewe” aliongea huku akilia, nilielewa kabisa uchungu aliousikia, lakini hiyo haikunizuia mimi kushangaa kitendo kile cha kinyama kilichotendwa na mwanamke. Nilimvuta na kumkumbatia kwani alikuwa amezidisha kulia. Sikutaka kumuonyesha kabisa kuwa yeye ni mnyama kwa kiasi kile ambacho kilikuwa ni ukweli. Tangu nizaliwe hii ndio mara ya kwanza naona kitu cha ajabu vile. Ilikuwa ni kitu ambacho ningekuja kumsimulia hata mtoto wangu. Haikuwa kawaida kabisa kwakweli, ni kitu ambacho hata msikilizaji wa simulizi hii atakubali kuwa si kawaida.

    “Patrick niliteswa sana, niliteseka katika umri ambao nilitakiwa kupata upendo. Sikuwa na hatia lakini nilibakwa na kuteswa nikiwa na umri wa mtoto. Nilianza kuingiliwa kimwili hata kabla sijaota maziwa kifuani mwangu. Nilikuwa mdogo sana lakini nilikomazwa. Nililia usiku na mchana lakini sikusikilizwa na huyu mwanamke. Kwanini alinitesa kwa makosa ya mama yangu? Je hastahili leo kulipa kwa ubaya alionifanyia? hii ni adhabu yake na adhabu ni malipo halali kwa mkosaji, hata mimi niko tayari sasa kwa kupewa adhabu kama itabidi kupewa” aliongea huku akiendelea kuongea. Hakika sikuwa na la kusema wala kufanya, nilibaki nikiwa nimemkumbatia huku moyo wangu ukitafuta neno la kumwambia lakini sikulipata. Bado nilikuwa nikitafakari hasa ni nini anajisikia yule aliyewekwa ndani ya lile shimo.

    “Patrick, kitu kilichonifanya niwe hai mpaka leo ni hii siku, nilikuwa nikimuomba mungu aniweke hadi siku hii ya leo ili niweze kumaliza lililo moyoni mwangu” aliniambia na kujiachilia toka kwangu kisha aliondoka na kuingia kwenye gari. Nilikuwa bado mimi nimesimama pale kwenye ile sehemu aliyofukiwa yule mama. Machozi yalinitoka nilipolitazama lile kaburi. Nilikuwa namuogopa sana Khajat kwa sasa, hakuwa mtu wa kawaida. Ni bora adhabu ya dada yake Felly aliyompa mchumba wake kuliko adhabu hii ya kumfukia mtu akiwa hai.

    “Tuondoke Patrick”. Nilisikia sauti ya Khajat ikisemesha, nilipogeuka alikuwa ameshawasha gari tayari akinisubiri. Taratibu niliingia kwenye gari huku akili yangu ikiwa imechanganyikiwa kwa niliyoyaona. Khajati akawasha gari na tukaondoka.

    “Nipeleke hotelini nikapumzike Khajat”. Nilimweleza huku nikivuta pumzi, lakini nilishangazwa na yeye kuipita hoteli niliyofikia na kuendelea na safari.

    “Khajat nimekuambia unishushe hotelini”. Nilimueleza hayo lakini alikataa mimi kwenda kulala hotelini.

    “Huwezo kwenda kulala hotelini wakati mimi nina nyumba kubwa, hivyo utalala kwangu Patrick”. Aliongea hayo na kuzidi kukanyaga mafuta.

    “Hey Khajat embu acha masihara, mimi nitaendaje kulala kwako?”. Nilimuuliza hayo lakini hata hivyo hakuonekana kujali swali langu.

    “Patrick hatuna cha kujadili hapo” aliongea hayo na muda huo tayari tulikuwa tumefika kwake. Tulishuka akaingia ndani na kisha alinionyesha chumba cha kulala mimi na yeye alitoka nje ila kwa mbali nilimsikia akiongea na simu;

    “Kwahiyo amesema hawezi kutoa ni la kwake?” aliongea hivyo kisha alikaa kimya akisikiliza mtu wa upande wa pili wa simu na kuanza tena kuongea.

    “Nipe niongee nae” alisema tena na hapo nilimsikia akifoka tena.

    “Mpe huyo kijana hilo begi, unataka maelekezo ya aina gani ndo utoe. Acha upuuzi. Taarifa zote alizokupa hazikutoshi mpaka utake nini zaidi, nikikata simu nategemea huyo kijana awe ameshaondoka hapo na hilo begi, kinyume cha hapo anza kuandika upya barua ya kuomba kazi sehemu nyingine”. Alimaliza na kukata simu kisha alipiga tena simu nyingine ambayo alikuwa akiongea kwa upole.

    “Habari yako kipenzi”. Aliongea na kunyamaza kidogo.

    “Hapana unajua shughuli ni nyingi sana lakini nilikuona siku moja na kitumbo chako sema nilikuwa kwenye gari na wewe ulikuwa uneingia ofisini kwako, hahaa” aliongea na kutoa kicheko kilichoonyesha kabisa kuwa alikuwa akijilazimisha.

    “Hapana siumwi ila nataka kuonana na wewe kesho, nina shida ya kitu fulani nilitaka tuongee”. Mh! Niliguna nakusogea mlangoni nijue alikuwa anaongea na nani.

    “hapana sio ugonjwa, ni mamabo tu ya kawaida”. Alimaliza na kilichofuata ilikuwa ni salamu ya usiku mwema. Niliyatafakari maneno machache aliyokuwa ameongea na hii simu ya pili aliyopiga nikagundua wazi alikuwa anaongea na Pamela,,uuf nilichoka, sikujua angeongea nae nini.

    Nilioga na nilipomaliza tayari chakula kilikuwa tayari na Khajat alikuja kunigongea kisha nilishuka na kwenda mezani. Alikuwa amevaa nguo yake nzuri ya kulalia lakini usoni alionekana kama mtu ambaye hakuwa tayari kulala.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Khajat unafikiria nini”. Nilimuuliza kwakuwa hakuwa anakula vizuri.

    “Nahisi yule mwanamke nimemuwahisha sana, alitakiwa ateseke sana kabla ya kufukiwa kama vile”. Mh! Macho yalinitoka kweli, niliogopa kuona huyu ni mtu wa aina gani ambaye pamoja na adhabu kubwa isiyo ya kibinadamu aliyompa yule mwanamke lakini yeye bado hakuridhika, alikuwa bado na hasira ya kufanya makubwa zaidi.

    “Khajat!!” nilijikuta nikiita na kushangaa.

    “Patrick, mimi nina roho mbaya kuliko shetani. Mtu akinifanya niumie na kujuta kuzaliwa huwa lazima nimfanye ajute na yeye kukutana na mimi. Niliteseka na kuumia kama wao wanavyoumia”. Mh! Hata kama lakini sio kuwa mkatili hivyo, nilijisemea moyoni.

    “Naelewa, lakini achana na hayo mambo kwasasa, umeshamaliza kulipa kisasi sasa acha kuwaza zaidi”. Nilijitahidi kumuonysha kuwa lile jambo lilikuwa la kawaida japo hata kwenye macho yangu yeye mwenyewe aliona kuwa nilikuwa nina uwoga. Sio kwamba mimi sikuwa katili, hapana, ni kwakuwa tu mimi sikuwa katili wa kiasi kile.

    “Kesho nataka kwenda kuongea na Pamela kuhusu wewe na yeye. Nafahamu kwanini dada yangu alifanya hivyo. Felly ni mtu muungwana sana, ana huruma na sikuzote Felly amekuwa akimpenda sana Pamela ila aliumizwa tu na namna ambavyo Pamela alifanya”. Aliongea na kunyanyuka kabla sijasema chochote, alikwenda akafungua mlango na kijana mmoja aliingia.

    “Ukiwa unatumwa kitu, uwe unajua na namna ya kujieleza, sio unalegeza mdomo na kuogopa kuongea, wewe ni askari wa aina gani unaletewa Kiswahili kirefu na mtumishi wa kawaida unalegea. Weka begi hapo chakula kipo pale kama unataka kula kama huli basi kesho, makabrasha yote niyakute mezani kwangu saa moja asubuhi, kinyume cha hapo kila kazi kesho utafanya mwenyewe”. Aliongea mfululizo na huyo jamaa alisimama kwa ukakamavu kweli.

    “Sawa mkuu”. Yule jamaa alijibu nakufunga malango kisha aliondoka.

    “Patrick ukimaliza nenda kapumizike, mimi niko ‘TV ROOM’ naangalia filam” aliongea hayo huku akiendelea kupanda ngazi kuelekea juu. Nyumba yake ilikuwa ni ndogo lakini ilikuwa ni ghorofa iliyobuniwa vizuri na kusanifiwa vizuri.

    ******

    Ilikuwa asubuhi tulivu sana, haikuwa ni siku ya kazi. Niliamka mapema sana na kuambua kwenda na Khajat mazoezi, tulikimbia umbali kwa kilomita kumi toka pale nyumbani kwake, na huko tulikuta sehemu yenye kama msitu mdogo hivi. Kulikuwa na kambi ya jeshi.

    “Usiogope Patrick, lazima ujifunze mambo mengi sana yatakayokusaidia baadaye”. Sikumuelewa Khajat alichoniambia lakini sikuhangaika kumuuliza kwakuwa nilishamfahamu kuwa yeye huwa hatoagi ufafanuzi kwa maneno bali kwa matendo, hivyo nilijikaza na kuingia kwenye ile kambi.

    “Oooh Kapten Janeth, habari”. Alimsalimia dada mmoja aliyeonekana kuwa na yeye alikuwa kwenye mazoezi ndani ya lile jengo kubwa lililokuwa kama linatisha hivi.

    “Salama mwalimu wa mafunzo, hahaa” walicheka na kukumbatiana, nilichotambua kwa haraka ni kuwa yule dada na Khajat walikuwa ni marafiki wa siku nyingi waliosoma shule moja, na pia niligundua Khajat ni mwalimu, sikujua ni mwalimu wa nini lakini nilivuta subira kidogo ili nijue ukweli wa kila kitu.

    “Huyu anaitwa Patrick, ni mpenzi wangu,,Patrick huyu ni mwanafunzi wangu, ni rafiki yangu na pia ni mtu wa karibu sana baada ya Felly”. Aliongea hayo na mimi sikutaka kuonyesha mshangao kutambulishwa kama mpenzi kwakuwa nilijua atakuwa amesema hivyo kwasababu yoyote nzuri aliona inafaa.

    “Nashukuru kukufahamu Patrick”. Janeth alinipa mkono na mimi nilimsalimu na hapo tulianza kuondoka kuelekea upande wa pili wa lile jengo.

    “Ulimaliza salama?” Janeth alimuuliza Khajat.

    “Yeah, nilifanikiwa lakini bado nahisi ile adhabu haikumfaa sana”. Aliongea Khajat.

    “Ulimpa adhabu gani?”. Aliuliza Janeth.

    “XT3 na KM3”. Alitaja vitu ambavyo sikuvifahamu lakini sikutaka kushangaa.

    “He! Khajat, wewe!”. Janeth alishangaa na kusimama.

    “Janeth katika mapambano, silaha yoyote inaweza kufanyakazi nzuri dhidi ya adui iwapo tu utakuwa umejua lengo la mapigano, hiyo ndiyo kanuni niliyowafundisha”. Aliongea na kumshika mkono Janeth ikiwa ni ishara ya kumwambia waondoke.

    “Lakini kwa mtu wa kawaida tena dhaifu kama yule huwezi kutumia hata 1 au 2 wala huwezi tumia XT au KM, du! Khajat, nimekuogopa aisee, sijawahi kuona hata mtu akifanyiwa hayo kwakweli”. Aliongea Janeth na hiyo ilinipa moyo na kujioa kumbe sio muoga kwani hata Janeth mwenyewe alikuwa akishangaa.

    “Nafurahi kuona unashangaa, hii inamaana nimejitahidi kulipa kisasi kitakatifu”. Aliongea hayo Khajat na Janeth alikaa kimya kama aliyepigwa na butwaa. Tulikuwa tumeshafika kwenye chumba chenye silaha na hapo alichukua bunduki moja ndefu na mimi alinipa bastola ndogo na kuanza kunifundhisha namna ya kushika na kupiga. Tulifanya zoezi hilo kwa muda wa lisaa limoja kisha tulitoka nje na tulipofika pale aliondoka na kuniacha nikiwa na Janeth tukiongea.

    “Janeth XT3 ndio nini?”. Nilimuuliza Janeth wakati Khajat hayupo, ila kabla hajanijibu nilisikia sauti ya Khajat ikijibu swali lile, alikuwa yuko nyuma yangu tayari na alianza kunielezea.

    “XT3 inasimama badala ya ‘xtreme Torture namba tatu’ hii ni kutesa kulikopitiliza, kwenye mafunzo ya kijeshi, hii hupewa gaidi asiyetaka kutaja sehemu ambapo kitu cha kudhuru watu kipo na kinahatarisha uhai wa watu kwa wakati huo na ni cha haraka, adhabu za hapa ni kama kuchoma sindano ya maumivu makali, kuchoma mishipa kwa bisibisi, kumchoma mtu kwa moto wa gesi, kukata vidole au kung’oa kucha, kukata sehemu yenye nyama na kuchomeka waya zenye shoti ya umeme. Kama jambo si la haraka unatumia XT1 ambayo huwa ni kumpiga, kumtishia kuwaumiza awapendao, kumpiga shoti za kawaida au kumpiga sehemu zinazomletea maumivu, kama anachelewa kusema na jambo ni la hatari kidogo unatumia XT2 inayojumuisha, kuua mtu mwingine mbele yake ili kumletea woga, kumuingizia waya puani na kuzidi kuusukuma kama haongei, kumuwekea kitambaa usoni na kumimina maji huku ukikibana ili maji yaingie puani na kumfanya asipumue, kumvisha mfuko wa lastiki kufunika uso wake ili ashindwe kuvuta pumzi na mengine. Umeridhika?” aliniuliza na sikuwa na cha kusema kwakuwa maswali yalizidi kuwa mengi.

    “KM3 inasimama badala ya ‘Kilingi method namba tatu’ hii ni mbinu ya kuua. Kwenye hii wanafanyiwa watu kama magaidi, walioua watu wengi sana, watu kama kina Osama na wengine, inajumuisha, kuua kwa kumfukia mtu akiwa mzima huku umemfunga gesi ilia pate maumivu makali kabla hajafa, kuna kumfunga jiwe na kumtosa baharini akiwa mzima, kuna kumkata kiungo kimoja baada ya kingine huku ukimtundikia drip ya damu na kumpiga sindano ya kumpa nguvu ili asife haraka, kuna kumchoma sindano ya kumfanya aoze na kutoka wadudu akiwa mzima, tuishie hapo”. Alimaliza na kumuambia Janeth ampe usafiri ili turudi kwa gari. Niliogopa sana, maswali niliyokuwa nayo ni juu ya ualimu wa Khajat, ilikuwaje Khajat alikuja Fiji na kupata kazi, Khajat alikuwa ni afisa uhamiaji iweje sasa awe ni mtu anayejua mambo ya kijeshi, je Khajat alimfundisha Janeth wapi, yalikuwa ni baadhi tu ya maswali mengi yaliyokisumbua kichwa changu. Sikuwa na muda wa kuuliza lolote kwakuwa hakuonyeshe kutaka maswali.

    “Ngriii,,,ngriii”. Mlio wa simu yangu ulisikika ukiita, nilipoitazama alikuwa ni Pamela.

    “haloo” niliipokea kisha niliitikia.

    “Habari Pamela” ilikuwa salamu iliyofuata kabla ya yeye kuongea. Sauti yake ilikuwa ya kinyonge sana, alionekana hakuwa na raha kabisa na hiyo ilinifanya nijisikie kunyong’onyea.

    “Salama mpenzi, nahisi kukumis Patrick, naomba urudi nyumbani, sitaki tuongelee tena hilo jambo nimeelewa na sitaki ukae mbali na mimi” aliongea bila kung’ata maneno.

    “Nimekumis pia Pamela, nitarudi nyumbani” nilimueleza huku Khajat akionekana kutabasamu. Niliongea nae kidogo na kukata simu.

    “Inapendeza sana kama ameamua yaishe, unajua nyie mmejaliwa maisha sasa, mnakaribia kupata mtoto. Mnatakiwa muwe karibu sana pamoja.” Aliongea Khajat huku akitabasamu. Niliona jinsi ambavyo aliyatamani yale maisha lakini alionekana bado alikuwa na kitu cha kutekeleza.

    “Ndio, ila nina changamoto kubwa sana ndani yangu”. Nilimueleza hayo lakini hata hivyo hakujibu zaidi ya kucheka tu na kukanyaga mafuta, baada ya dakika chache tulifika nyumbani, nilikwenda kuoga na yeye pia na baada ya muda mfupi tulikutana tena mezani kwaajili ya chai.

    “Khajat…..” nilitaka kuongea lakini nilikatishwa na kudakia kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nataka kujua umejua wapi mambo yale na wewe ni nani. Ndo swali ulilotaka kuuliza si ndio?” aliniuliza huku akinitazama kwa kutabasamu.

    “Ndio” nilimjibu huku nikijiweka tayari kwa kumsikiliza.

    “Nilipotoroka kule Bombay, nilikuja huku kumfata Felly, nilikuwa mtoto wa miaka 9, nilikuwa naitwa Roshan, ila mimi nilibadili na kujiita Khajat ambalo ni jina la yule mwanamke niliyemfukia, lengo likiwa ni jina hilo linikumbushe jukumu la kulipa kisasi nililojiwekea siku ikifika. Baada ya kuja huku nilianza shule na nilikuwa kila ninachokifanya nakifanya kwa hasira sana na hiyo ilinisaidia kufanya mambo mengi kwa makini na usahihi, nilipomaliza elimu ya sekondari, Felly alikuwa tayari ni mpelelezi, hivyo aliniuliza ninachotaka kufanya au nataka kwenda chuo. Nikaamua kwenda chuo cha jeshi na huko nikajifunza mambo mengi, baadaye waliona juhudi yangu na nikachaguliwa kujiunga na mafunzo zaidi ya kijeshi na baadaye walinipeleka Cuba kwenda kusoma shahada ya sayansi ya kijeshi na mambo ya ujasusi. Niliporudi nilikuwa mwalimu kwenye chuo cha kijeshi, ni hayo”. Alimaliza kuongea na kunywa funda moja la chai.

    “Sasa ilikuwaje tena ukawa kwenye idara ya uhamiaji?” nilimuuliza tena kwakuwa sasa alionekana akijali mimi kumfahamu.

    “Huku uhamiaji nilikuja kwakuwa sikutaka kwenda kwenye operesheni za kivita, nia yangu ni ili nisijekufa huko kabla aliyecheza na maisha yangu hajawajibika kwa makosa yake, hivyo nilichagua kuja uhamiaji ila kwa kitengo cha jeshi cha kudhibiti uingiaji wa magaidi na madawa ya kulevya, wakati huo nilikuwa nikijipanga kwa kilichotokea”. Aliongea na mpaka hapo nilikuwa nimebakiwa na swali moja tu.

    “Sasa kama huyu Bi Khajat alikuwa India, ilikuwaje wewe ukampata na kumtesea huku au ilikuwaje yeye kuwa huku, au ulimfata?” nilimuuliza kisha alicheka na kuanza tena kuongea.

    “Nilianza mawasiliano na Bi Khajat mika 6 iliyopita kwa njia ya mtandao, tulikuwa marafiki lakini muda wote hakujua kama ni mimi na hata picha nilizokuwa nikimtumia zilikuwa ni za mama mmoja marehemu. Tulijadili mambo mengi sana na baadaye nilimwambia aje kunitembelea na yeye alikubali kuja. Nilimtumia barua ya mwaliko na niliwasiliana na uhamiaji wa kule nao walimkamilishia kila kitu. Niliingia gharama za kumtumia tikiti ya ndege na pesa nyingine kwaajili yake, hivyo kama mwezi hivi uliopita alipanda ndege na kuja alipofika pale uwanja wa ndege nilikwenda kumpokea nikimueleza kuwa mimi ni mtoto wa huyo mama aliyekuwa anawasiliana naye na nilitumwa kumchukua. Hakuwa amenijua hivyo nilimchukua mpaka nyumbani kwangu hapa na nilimuhudumia kila kitu alipotulia ndipo nilimueleza ukweli mimi ni nani na mambo mengine yalifata.” Aliongea huku akionyesha kufurahishwa zaidi na jinsi alivyomkamata.

    “Mh! Aisee, hiyo nimeipenda, mimi sina swali lingine kwakweli ila nataka Pamela akishajifungua nirudi kwanza nchini kwangu nikajue mambo yanaendaje kule, nahisi si sawa mimi nikiendelea kuvumilia dhuluma hii.” Niliongea huku nikitazama juu.

    “Najua inavyokuuma ila kila kitu kitakuwa sawa. Kila mtu atalipa kwa kadiri alivyofanya.” Alisisitiza Khajat na hapo tulimaliza chai na safari ya mimi kurudi kwa Pamela ilianza. Baada ya muda nilikuwa nimeshafika na kupokelewa na Pamela.

    “Oooh Patrick, nisamehe mpenzi kwa kutokukuelewa mapema.” Alinikimbilia na kunikumbatia. Nilikuwa njia panda kwa mambo mengi sana, kwanza sikujua ni upi mwisho wangu au malengo yangu na Pamela, sikujua nini kitafata baada ya yeye kujifungua. Sikujua nampenda au vipi, sikuwa naelewa maana ya chochote kilichokuwa kikitokea.

    “Hapana Pamela, kosa lilikuwa langu na ulikuwa na haki ya kuchukia na kunipa adhabu ndogo uliyonipa”. Niliongea nae na kisha tuliingia ndani.







    “Maisha hutupa changamoto ili kupima ujasiri wetu na utayari wetu wa kubadilika, katika muda huo, hakuna nafasi ya kujifanya kwamba hakuna linalotokea au kusema kuwa hauko tayari kuipokea hiyo changamoto. CHANGAMOTO HAZISUBIRI UTAYARI WAKO. Maisha hayaangalii nyuma, ni kama sheria mpya inayotungwa juu ya jambo fulani, huwa inaanzia pale iliposainiwa. Wiki moja ni zaidi ya muda wakutosha tunaohitaji ili kuamua kama tunakubali mwisho wetu tuupanga au la”Japokuwa unaweza pia kuhutaji kwenda mbele kwenye maisha yako, lakini unaweza kukuta umeweka mguu mmoja kwenye ‘break’. Nini thamani ya maisha kama tunaamua kwenda mbele kwa mashaka ya kukanyaga breki. Ili uwe huru, lazima ujifunze kusahau na kuacha mambo mengine yaende. Acha kuumizwa na machungu yaende, sahau. Tupa woga kulee, achana na kuzisumbukia na kukumbuka maumivu yako ya zamani. Nguvu unayotumia kujihusisha na maumivu yako na maisha yako ya zamani ndiyo inayokuvuta nyuma na kukufanya usisonge mbele. KUBALI KUANZA UPYA. HII NI SEHEMU YA KUMI.



    Basi ndugu mwandishi mimi nilikaa kama nimepigwa na butwaa hivi. Nilitokea kumpenda sana Khajat lakini nilimuogopa sana. Ukioa mwanamke kama huyu unatakiwa kuwa makini na kila ufanyacho kwakuwa muda wowote na popote anaweza kukufanya kitu kibaya. Hii simulizi iliachiwa usiku kucha. Na sasa ilikuwa inaelekea saa nane za usiku. Bado nilikuwa macho nikisikiliza redio nione nini kinafuata, ILIKUWA HIVI.

    MWEZI MMOJA MBELE.

    ***PATRICK****

    “Hongera sana Patrick ni mtoto wa kiume, muda si mrefu tutakuruhusu uingie ndani.” Ilikuwa kama miujiza vile, alizaliwa mtoto wa kiume, asante mungu, nilijisemea moyoni nikiwa pale nje ya kile chumba alichokuwa ameingizwa Pamela jana usiku.

    “Patrick ujue ilishindikana kabisa Pamela kujifungua kwa njia ya kawaida kwakuwa cevix zake zilikuwa hazijatanuka vizuri, hivyo ilibidi tumpasue, kwahiyo mkeo amezaa kwa uapasuaji.” Ilikuwa sauti ya dokta Anderson ikinipa taarifa. Khajat na Felly walikuwa pembeni yangu nao wakisubiri kumuona mtoto aliyeletwa duniani. Nilikuwa na jukumu sasa la kulea familia, nilikuwa tayari sasa ni baba wa mtoto wa kiume.

    “Asante sana dokta Anderson, nilipopata taarifa niliona ni vyema kukatisha safari yangu na kurejea tena kumtizama Pamela na mtoto wetu.” Wakati huo nilikuwa nimekatiza safari yangu ya kikazi baada ya kupata taarifa kuwa Pamela alikuwa amepatwa na uchungu wa kujifungua na alipelekwa hospitali. Tulikaa pale nje kwa muda kidogo na walipomaliza mambo yao walituruhusu kuingia.

    “Ooooh Pamela, hongera mpenzi, sasa tuko watatu na sio wawili tena” nilimsogelea pale kitandani na kumbusu.

    “Asante sana Patrick, hongera na wewe, nakupenda sana Patrick.” Alisema Pamela, ila neno ananipenda lilizidi kuniumiza kwakuwa sikuwa nafahamu hisia zangu juu yake, nilikuwa nimevurugwa na mambo mengi sana na sikujua nishike lipi niache lipi.

    “Nakupenda pia Pamela.” Niliongea huku nikionyesha kabisa kuwa nilikuwa na wasiwasi na nilichokiongea, wakati huo Pamela alikuwa akinitazama kwa makini sana.

    “Usijali Patrick kila kitu kitakuwa sawa mpenzi.” Alisema Pamela na kunifanya nishangae kwanini alisema vile, pengine aligundua kabisa kuwa sikuwa sawa na ile kauli yangu, pengine aligundua nilichokuwa nikikiwaza.

    “Niko sawa mbona Pamela.” Nilijikosha kwa kujichekesha, lakini alitabasamu akiashiria kuwa nisimdanganye.

    “Alafu embu sogea karibu.” Aliniambia na hapo nilimsogelea na alinitazama macho yangu kisha alimwita nesi mmoja aliyekuwa pale ndani ya chumba kile.

    “Lailath naomba ukamcheki Patrick wingi wa damu, naona macho yake ni meupe sana.” Loo! Alikuwa anajali sana siku zote alikuwa akihakikisha kuwa afya yangu iko sawa hasa ukizingatia kuwa yeye alikuwa daktari.

    ******

    Tulirudi nyumbani na maisha yaliendelea kama kawaida. Siku zilienda na mwezi ulikatika sasa. Siku moja nikiwa natoka kazini mchana na kwenda kwenye chakula cha mchana nilikutana na mtu amabye aliponiona alikimbia karibu avunjike mguu.

    “Dany, habari yako?” nilimsalimu mtu huyu na baada ya kugeuka na kuniona alishtuka na kuanza kukimbia.

    “Mamaaaa,,,mzimuuu” alipiga kelele huku akikimbia kama mwehu, nilijitahidi kumfata nyumanyuma lakini kadiri nilivyokuwa nikimfata ndivyo alivyozidi kukimbia na hapo niliamua kumuacha tu. Niliketi chini na kulia sana kwakuwa kile kilichotokea sio tu kuwa kilinifadhaisha na kuniaibisha lakini kilinipa picha ya ubaya niliofanyiwa.

    “Patrick mbona umekaa chini?” nilishtushwa na sauti ya msichana ikiniuliza swali lakini niliponyanyua macho juu alikuwa ni Khajat na nilipotazama kwa mbali nilimuona na Felly nayeye akija upande ule. Nilinyanyuka na kujikung’uta kisha nikazuga kama vile hakuna kilichotokea.

    “Nilikuwa nasikia kizunguzungu nikaamua kukaa hapa kidogo.” Nilijaribu kudanganya ili angalau niepushe maswali zaidi.

    “Hapana Patrick huwezi kusema ni kizunguzungu wakati macho yako yanaonekana kama vile ulikuwa ukilia.

    “Kuna kitu kimetokea hapa ila nitakimaliza tu usijali.” Nilimjibu na kujifuta machozi kisha waliongozana na mimi kuelekea ofisini kwangu. Tulipofika mlangoni tulisimama nje tukiongea maneno mawili matatu lakini nilipotazama kwa ndani kupitia vile vioo sikuona mtu hata mmoja ofisini. Nilishtuka nikatazama vizuri pale mlangoni kile kibao cha mlango kilikuwa kimegeuzwa na kusomeka CLOSED, nikashtuka nani anayeweza kufungwa ofisi wakati mimi sipo.

    “Patrick rudi nyuma usiusogelee mlango njoo huku.” Khajat alinivuta mkono na kunisogeza mpaka lilipokuwa gari lake.

    “Felly, kuna uhalifu unafanyika kule ndani.” Aliongea Khajat na kuniambia niingie ndani ya gari nitulie. Niliona Felly akifungua gari yake kule nyuma na kutoa bastola mbili na moja alimpa Khajat, kisha walikuja tena kwenye gari na kuniuliza.

    “Mlango mwingine wa kuingilia ndani ya ofisi zenu uko wapi?” aliuliza Felly.

    “Hakuna mlango hapo zaidi ya huo, mlango mwingine ni mpaka uzunguke kwenye lile ghorofa kubwa ukapitie ghorofa ya pili ndio kuna ngazi ya kushuka kutokea chini.” Nilimueleza hayo Felly lakini kabla hajamaliza kunisikiliza Khajat alidakia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimeona ndani kuna jamaa wanne na wote wana silaha, sasa kuna liledirisha pale linaweza kutupelekea kwenye ‘ventilation’ tukapita hivyo mpaka ndani kisha tutashukia kwenye huo mlango anaosema Patrick.” Alimwambia Felly na kwa pamoja niliona wakiondoka taratibu, waliingia kwenye kile kidirisha na baada kama ya dakika tano nilisikia mlio wa risasi na watu huku nje walianza kukimbia, nilishuka kwenye gari na kuanza kukimbilia kule ndani kuangalia kama kuna jinsi naweza kusaidia. Nilipofika karibu na mlango alitoka mmoja wa wale wahalifu na kuanza kukimbia na mimi nilianza kumkimbiza, nilikimbia na mwendo wa mita mia tatu mbele nilimkaribia na kumpiga mtama kisha alianguka chini, alipokuwa anageuka ajitetee nilishtuka kuona buti likipita mdomoni kwake na kumfanya ateme damu, nilipotazama ni nani nilitabasamu kwakuwa alikuwa ni Felly.

    “hahaa” nilijikuta nikicheka yule jamaa alishikwa akapelekwa mpaka pale ofisini na maaskari walikuwa wameshafika wakawachukua na kuondoka.

    “Nyie hamfai kuolewa, hahaa” niliwatania na kuingia ndani ya ofisi walipokuwa wamekusanyika wafanyakazi wote.

    “Jamani poleni sana kwa yaliyotokea, kwa kipekee na niaba ya kampuni niwashukuru Felly na Khajat kwa msaada wao mkubwa uliofanikisha wote hapa kuwa hai lakini kuzuia fedha na mali zetu zisiharibiwe. Kampuni itaangalia namna ya kuonyesha jinsi inavyothamini walichokifanya. Naomba kwasasa wakati nawasiliana na wenzangu wa utawala, kila mtu amalizie kazi zake ndani ya nusu saa mfumo mzima wa kompyuta utazimwa na kazi kwa leo tutakuwa tumemaliza.” Nilimaliza kuongea na wafanyakazi na hapo mimi pamoja na kina Khajat tulikuwa pale nje kwaajili ya kutoa kwanza maelezo ya awali na hatua nyingine za kipolisi ziliendelea.

    **JIONI YAKE**

    Tulikuwa nyumbani na wakina Khajat walikuja kumuona mtoto kama kawaida yao ya kuja kila jioni kumtembelea Pamela, nilikuwa bado nikichanganywa na lile swala la pale ofisini lakini zaidi lilikuwa swala la Dany.

    “Jamani, kuna kitu kimetokea leo kimenifadhaisha sana lakini nahitaji pia msaada wenu wote wa mawazo na namna yeyote.” Niliwaambia kabla ya kuendelea.

    “Baba Cris na wewe, swala la kazini siumeshasema jamani na polisi watafatilia.” Aliongea Pamela aliyekuwa amenogewa na maongezi waliyokuwa wakiyafanya pale. Nilinyanyuka na kwenda dirishani nikifikiri nawezaje kuliongelea hivyo na nilipopata namna niligeuka na kuongea nao;

    “Sio swala la kazini, ni tukio lililotokea mda mfupi kabla ya tukio la kuvamiwa kwa ofisi.” Niliongea kwa upole na pamela alikaa kimya anisikilize.

    “Ndio lililokufanya ukae pale chini si ndio?” aliuliza Felly.

    “Ndio, ndilo lililonifanya nikae pale chini na kulia.” Niliongezea na hapo nilihisi machozi yakinitoka lakini niliyazuia.

    “Patrick umelia leo?” aliuliza Pamela.

    “Nini kilitokea?” aliuliza Khajat

    “Nilimuona kijana mmoja anaitwa Dany, Daniel Mfangavo, huyu ndiye alikuwa ‘bestman’ wangu. Huyu ndiye aliyekuwa rafiki yangu wa siku nyingi sana, nilipomuona nilimuita aliitika na kugeuka, nilikwenda kwa furaha na kujaribu kumpa mkono lakini alianza kukimbia huku akisema mimi ni mzimu. Nilijaribu kumfata ili niweze kumuelezea lakini ikashindikana kwakuwa watu walikuwa wakishangaa na mwishowe nilimuacha akatokomea. Imeniuma sana kwakuwa sasa nimepata picha halisi kuwa huko Tanzania mimi nitakuwa kituko mbele za watu siku wakiniona.” Niliwaeleza hayo huku nikiwa bado na maruweruwe ya kilichotokea pale.

    “Kwahiyo ni Mtanzania?” aliuliza Khajat.

    “Ndio ni Mtanzania, na itakuwa yupo huku kwa biashara au kikazi labda.” Nilimjibu huku akili yangu bado ikikumbuka tatizo lililotokea. Mimi na Dany tulijuana mda mrefu sana toka kipindi nikiwa kidato cha pili na toka pale tulikuwa marafiki wakubwa sana na tulibahatika hata kuwa ndugu. Maisha yangu na Dany yalikuwa ni kama mtu na kaka yake. Tuliishi vizuri sana na mpaka yeye anafikia umri wa kuoa mimi ndiye nilikuwa msimamizi wa ndoa yake na pale mimi nilipooa yeye ndiye aliyekuwa msimamizi wa ndoa yangu. Undugu wangu na Dany ulizidi hata undugu wangu na Mark ambaye alikuwa ni ndugu yangu wa damu.

    “Kesho asubuhi itanibidi nikafatilie kwenye makabrasha ya ofisi za uhamiaji na kama kuna taarifa yoyote basi tutajua alipo na mimi nitamfata kwaajili kuongea naye na kumuelimisha kabla ya wewe kuongea naye.” Aliongea Khajat na mjadala wa hilo ulikuwa umefungwa mpaka kesho yake. Khajat alikuwa ni mtu wa vitendo zaidi kuliko maneno, alikuwa kama dada yake, hakuwa anapenda kuongea sana juu ya mambo ambayo ipo njia ya kuya fahamu bila nadharia nyingi kuhusishwa.

    “Hilo nadhani Khajat atalikamilisha, ila Patrick kuna kitu kingine inabidi ukifahamu na uwe makini sana kuelewa na uwe na moyo mgumu.” Aliongea Felly na hapo macho yalinitoka.

    “Njoo ukae mpenzi.” Aliniambia Pamela ambaye alionekana kama kufahamu anachotaka kusema Felly. Mapigo ya moyo yalizidi kunienda mbio, nilijua kabisa Felly huwa anaongea kuhusu Mary tu kwakuwa amekuwa akijielekeza sana katika kufanya Uchukuzi wa namna mbinu za kunihujumu ulivyofanyika. Nilitegemea tena kusikia kuna baya lingine limetokea. Hivyo nilikaza moyo na kwenda kuketi pale karibu na Pamela aliyekuwa amenishikilia vilivyo.

    “Baada ya habari kupelekwa na Mary akishirikiana na Mark kuwa umefariki na mwili wako haujapatikana, taharuki ilitanda ndani ya familia na nje ya familia yako. Hali hiyo ilikuwa mbaya sana hasa kisa kizima na mafanikio uliyoyafikia kuwashika wengi sana. Taharuki hii ilipelekea vifo viwili, cha kwanza ni cha mama yako mzazi aliyefariki kwa shinikizo la damu baada ya kupata taarifa ya kuwa umefariki, alifariki akiwa nyumbani kwenu na kifo kingine ni cha baba yako aliyepooza baada ya kupata ile taarifa. Baba yako alitaka kuagiza uchunguzi binafsi ufanyike juu ya kifo chako lakini kuna siku alikutwa amefariki. Taarifa ya madaktari inayopatikana kwenye tovuti ya hospitali inayoitwa Regency iliyopo huko Tanzania inaonyesha kuwa alifariki kwa kukosa hewa. Lakini kwa maelezo ya Pamela ambaye nilimuonyesha ile taarifa ya daktari inaonekana kuna habari zinakosekana kwenye taarifa ile. Ukiangalia ile taarifa, (akamtuma Pamela ailete kwenye ngamizi yake, na ilipokuja aliendelea kuelezea), kuna namba za kurasa hazionekani sawia. Kwamfano kwenye taarifa inayoonyesha kuwa alikuwa ameishiwa pumzi na ndio chanzo cha kifo chake, kwenye kurasa ya 5 ilitakiwa ifate kurasa ya 6 na 7 ndio ije kurasa ya 8, ila taarifa ina kurasa namba 1 mpaka 5 kisha inafata 8 mpaka 9. Hii inamaana kuwa kurasa ya 6 na 7 imechomolewa. Je kurasa hizo zinahusu nini? Ndilo lilikuwa swali la msingi lililonifanya sasa niombe ushauri wa kidaktari kwa Pamela ili kujua kitu gani kilichomolewa kwenye hiyo taarifa. Sasa alichoeleza Pamela ni kwamba kwenye ile kurasa ya tano inaishia kwa kueleza tu kuwa marehemu aliishiwa pumzi, lakini kurasa za nyuma hazionyeshi kama marehemu alikuwa na pumu, au kwamba alikuwa sehemu isiyokuwa na hewa, hivyo swali la kujiuliza ni je marehemu alikosa pumzi au alikoseshwa pumzi? Majibu yote haya mawili yanaweza kujibiwa kwa njia ya kitaalamu ya kidaktari, mfano kwenye karatasi zilizochomolewa Pamela anasema zitakuwa zinaelezea mazingira ya mgonjwa kukosa hewa, lakini pia kurasa ya nane ambayo ni muendelezo wa kurasa zilizochomolewa zinaonyesha kuwa kuna neno linamalizia na ‘mto’ au ‘kabali’. Hii kwa maneno mengine ni kwamba hilo tatizo la kukosa hewa linaweza kuwa limesababishwa na marehemu kubanwa na mto ambao Pamela anasema ni njia rahisi ya kumkosesha mtu pumzi ambao kwa dakika kumi tu humfanya mtu kukosa hewa na kufariki, kwa maelezo ya Pamela ambayo hata hivyo yanashabihiana kabisa na sehemu ya taarifa, anasema kuwa mtu akibanwa na mto usoni na kwa mkandamizo mkubwa inamfanya mtu kukosa dakika 1 hadi ya 3 na kuanzia dakika ya 4 mpaka ya saba kitendo cha kukosa hewa huaribu ubongo na mfumo wa taarifa na kusababisha hadi mfumo wa hewa huaribika kabisa na dakika zinazopata huwa ni kupoteza uhai. Hayo yote ni kweli na yanathibitishwa na sehemu ya taarifa hiyo iliyochomolewa ambayo niliipata baadaye ikitoka kwa mtu anayejiita dokta Muya kwenda kwa Mary na pia kutoka kwa Mary kwenda kwa Mark na baadaye kutoka kwa Mark kwenda kwa mtu mwingine anayeitwa Paul, taarifa hiyo ilionyesha kuwa ni kweli mzee wako alifariki kwa kukoseshwa hewa na alikutwa pingili zake za uti wa mgongo za shingoni zinazounganisha na fuvu la kichwa zikiwa haziko sawa, hii inamaana kuwa kulikuwa na kujitetea wakati akizibwa pua na mdomo na kwakuwa mkandamizo ulikuwa mkubwa ilisababisha shingo yake kucheza na ndio moja ya vitu vilivyoharakisha kifo chake. Taarifa hiyo toka kwa dokta kwenda kwa Mary ilikuwa imeambatana na ujumbe uliosema ‘tayari imeondolewa kwenye mfumo wa kompyuta na kijana anasubiri pesa yake’, ujumbe huo ulijibiwa na Mary kwenda kwa dokta Muya kuwa ‘malipo nimeyafanya muda sio mrefu, shilingi laki 5 utampa na shilingi milioni moja utaweka vocha’. Baada ya kufanya mawasiliano hayo, Mary alipokea ujumbe toka kwa Mark ambaye hati yake ya kusafiria inaonyesha hakuwa Tanzania wakati huo, ujumbe ulikuwa ukisema ‘umefanya kazi nzuri beb, namalizia kufanya packaging ya kontena moja la mwisho kisha wakishapakia mimi nitarudi na British Airways kesho’. Baada ya ujumbe huo Mary siku hiyohiyo alimtumia ujumbe huyo mtu anayeitwa Paul, ujumbe huo ulisomeka ‘kazi ya taarifa imekwisha na tayari milioni moja imetumwa kwako na secretary wangu, sasa nataka kazi ya yule P.I uikamilishe leo, waambie na kina Jof na malipo yao ya laki 6 kila mmoja yatafanywa leo jioni. Mkimaliza hiyo hatutaenda Arusha nataka tuanze kujipanga kwa Master plan, you should all be set, Buberwa ataleta schematic kisha tutapanga ni ambush au ni nini.’ Ilimaliza sehemu ya ujumbe huo, ujumbe huu umezua maswali mengi moja ikiwa ni hao kina Jof na Paul wanakazi gani inayoitaji mchoro na mpango. Hilo nimekosa majibu yake ya kiundani.” Alimaliza kuongea Felly na wakati huo mimi nilikuwa nimejawa na hasira na sikujua nilie au iweje.

    “Kwahiyo wazazi wangu wote wawili wamefariki?” nilijikuta nikiuliza swali ambalo majibu yake nilikuwa nayo tayari.

    “Ndio” alijibu Pamela. Machozi yalinitoka na nikajihisi kabisa kuwa nilikuwa ninaota.

    “Je kwanini walimuua baba yangu?” nilimuuliza Felly aliyekuwa akinitazama.

    “Baba yako alikuwa amemuajiri mtu kufatilia ukweli wa kifo chako, sasa ilikuwa ni ngumu sana taarifa kutopatikana kama baba yako angefatilia ndio mana wakamuua, lakini mawasiliano ya Mary na Paul yamemtaja yule mpelelezi binafsi kama ndiye anayefata kwenye orodha pale waliposema P.I yani Private Investigator. Na kuna baadhi ya mambo nimefatilia inaonyesha kuwa Mary anahisa kwenye kampuni ya Alsad Drilling Company iliyopo Urusi, hisa hizi alirithishwa na baba yake, na pia anamiliki kampuni nyingine mbili Msumbiji na nyingine iko Afrika ya kusini, kazi za kampuni hizi hazijulikani wazi na pia usajili wa kampuni hizo una utata kwani inaonekana kwenye kila nchi imesajiliwa kama kampuni tanzu ya kampuni inayoitwa Mary and Unique Supplies lakini kiukweli hakuna kampuni kama hiyo. Mfano kwenye muongozo wa kampuni ya Afrika ya kusini kwenye kifungu cha biashara za kampuni inaonyesha ni kampuni inayohusika na utoaji wa ushauri kwa wachimbaji wa madini na mambo ya chemikali za migodini, inaonekana pia kampuni hii inamakao yake makuu Pritoria na Maputo, lakini kwenye miji hiyo hakuna ofisi hata moja inayomilikiwa na Kampuni hizi. Hii inafanya wasiwasi uwepo juu ya kazi za Mary.” Aliongea Felly aliyeonekana kuwa makini sana na kile alichokuwa akikieleza.

    “uuf.” Nilishusha pumzi na kumgeukia Pamela aliyeonekana kuwa mnyonge sana, nilimtazama na yeye aliangalia chini.

    “Nini kingine ambacho sikifahamu hapa Felly.” Nilimuuliza Felly.

    “Ambacho hakifahamiki hapa nadhani ni nia ya yote haya na huo mpango mkubwa Mary aliomwambia Paul angeufanya. Haifahamiki kwanini Mark alishiriki kwenye kusababisha yote haya, na kingine ambacho hukifahamu ni kwamba baba yake na Mary alifariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari akiwa anatokea sehemu inaitwa Arusha. Na huyo Dany unayemuongelea anamagari yake kumi ya kitalii aliyoyakodisha kwenye kampuni ya GEOMARY ambayo inamilikiwa na Mark na Mary, hivyo kukuona wewe huku kunaweza kupeleka picha mbaya Tanzania na pengine tutategemea lolote, lakini kabla ya chochote kutokea sisi tutafanya namna ya kuwahi. Nimeshafanikisha kutega mawasiliano yote ya Mary na Mark ya barua pepe na hapo ni pa kuanzia tu. Khajat atafatilia ya Dany na tukifanikiwa kumpata yeye ndo atatusaidia.” Alisema Felly. Nilikaa kimya tu sikujua cha kusema niliamua kushukuru lakini nilichokuja pia kugundua kumbe Pamela alikuwa pia akiwalipa kama motisha ya kufanya kazi hiyo, nilifarijika lakini kazi kubwa ilikuwa ni je nini kitafata????





    Nimeshafanikisha kutega mawasiliano yote ya Mary na Mark ya barua pepe na hapo ni pa kuanzia tu. Khajat atafatilia ya Dany na tukifanikiwa kumpata yeye ndo atatusaidia.” Alisema Felly. Nilikaa kimya tu sikujua cha kusema niliamua kushukuru lakini nilichokuja pia kugundua kumbe Pamela alikuwa pia akiwalipa kama motisha ya kufanya kazi hiyo, nilifarijika lakini kazi kubwa ilikuwa ni je nini kitafata????http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Unafikiri kuwa kwakuwa hakupendi basi wewe huna thamani. Unafikiri hivyo kwakuwa tu hakutaki tena, na kwamba yuko sahihi, kwakuwa mawazo yake na Hukumu yake juu yako iko sahihi. Kama amekufukuza na kukupiga basi wewe ni takataka. Unahisi yeye ni wako kwakuwa unataka uwe wake. Hapana usifanye hivyo. Ni neno baya sana kusema ni WAKO. Hasa unavyolitumia kwa mtu unayempenda WEWE. Mapenzi hayatakiwi kuwa hivyo. Umeshawahi kuona jinsi mawingu yanavyopenda mlima? Hujizungusha pembeni yake na kuna wakati huwezi kuuona mlima kwakuwa tu mawingu yameufunika. Lakini unajua kuwa ukienda juu ya mlima utaona kilele chake? Na hii ni kwakuwa mawingu hayafuniki kilele cha mlima. Kilele cha mlima huonekana kwa juu kwakuwa mawingu hukiachia, haikifuniki. Huuacha mlima uweke kichwa chake juu, huru bila kuwa na kitu cha kuuficha juu au kuusonga. HUWEZI KUMILIKI MTU. Huwezi kupoteza usichokuwa nacho. Kuna muda jifunze kuwa mbinafsi ili kuzuia kuumia na wale uwapendao.” HII NI SEHEMU YA KUMI NA MOJA,



    **PATRICK**

    Kuna mambo nilikuwa nikiona hayawezkutokea kwa binadamu wa kawaida. Kuna mambo mengine niliona ni kama simulizi za kusadikika na kwamba hayawezi kumtokea mtu kabisa. Kila mtu ni kipofu wa kesho yake, laiti kama ningejua nini kitanitokea katika maisha yangu basi pengine ningetumia uwezo wangu na pesa zangu zote kuzuia haya yasitokee. Maswali yalikuwa ni mengi sana, swali kubwa ni kwamba Mary alikuwa na mpango gani na mimi. Mark anahusikaje toka mwanzo kabisa wa mapenzi yangu na Mary. Majibu yalikuwa ni machache na yasiyo ya kuaminika kabisa kwa maswali yote niliyojiuliza. Dany angepatikana ndiye pengine angeweza kunipatia majibu machache kati ya mengi niliyoyawaza.

    *******

    Kesho yake asubuhi nilikwenda kazini kama kawaida na nilipofika pale maaskari na maafisa upelelezi walikuwa wakinisubiri kwaajili ya kumalizia upelelezi wa awali. Tulikaa pamoja na kuzungumza na walipomaliza waliondoka na mimi niliendelea na kazi.

    “Ngriiiiiiiii,,,ngriiiiii.” Simu yangu ilikuwa ikiita na nilipoitazama nilikuta ni Khajat.

    “Hallow Khajat.” Nilimsalimu huku nikitabasamu kama vile aliniona.

    “Hallow Patrick, kuna Maswali nilitaka kukuuliza kwanza.” Aliongea na kusikika kama alikuwa akichapa kitu kwenye kompyuta.

    “Sawa uliza nakusikiliza.” Nilijiweka tayari kujibu maswali yake sawia.

    “Ulisema Dany anaitwa nani jina lake kamili?” Aliuliza na kunyamaza kidogo.

    “Daniel Mfangavo.” Nilimjibu na yeye alikuwa kama anaandika.

    “Je inawezekana ndio yeye anaitwa Daniel Fredrick?” aliniuliza tena na mimi nilikaa kwa muda nikitafakari kama anaweza kuwa yeye.

    “Ndio, jina la baba yake ni Fredrick Mfangavo.” Nilimjibu na yeye aliendelea kuuliza.

    “Je unafahamu jina la mke wake?” aliuliza swali hilo ambalo lilikuwa jepesi kwangu kwakuwa mke wa Dany alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana toka kipindi tukiwa sekondari.

    “Ndio, anaitwa Catherine Cathbert.” Nilimpa jibu lakini akaonekana kama kuguna vile.

    “Umesema Catherine Cathbert?” aliniuliza tena na kunyamaza kidogo.

    “Ndio, vipi kwani?” nilimuuliza tena. Kwa vyovyote nilijua kuwa kuna kitu hakipo sawa.

    “Subiri kidogo usikate simu.” Aliniambia hayo na nilisikia kupitia simu kama vile akibonyeza vitufe vya simu kama ishara ya kwamba alikuwa akipiga simu, kisha baada ya muda kidogo nikasikia akiongea kwenye simu.

    “Hivi uliniambia umekutana na jina Catherine Cathbert?” alimuuliza huyo aliyekuwa akiongea naye kwenye simu, ikaonekana kama vile ameshapata jibu la swali alilouliza na kisha aliendelea.

    “Ni mke wa Dany, hivyo endelea kuanzia hapo.” Alimaliza kuongea na nikasikia akikata simu.

    “Patrick.” Alirudi tena kwenye simu tuliyokuwa tukizungumza na kuniita na nilipoitika hakunipa muda wa kumuuliza chochote bali aliendelea na maswali.

    “Dany na Mary walijuana lini?” aliniuliza na nilikuwa nikisikia kabisa akiandika kwenye kompyuta.

    “Aah Dany alimjua Mary wakati nilipoanza mahusiano na Mary na si kabla ya hapo.” Nilimjibu na hapo Khajat aliniambia nisubiri kidogo, alipomaliza kuandika aliongea tena.

    “Dany anafanya biashara gani?” aliniuliza tena na hapo sikuwa na ushahidi na biashara anayofanya kwa sasa lakini nikijuacho ni kwamba Dany alikuwa ni meneja wa hoteli kubwa jijini Dar es Salaam na alikuwa akimiliki kampuni ya utalii ambayo hata hivyo ilikuwa ni ndogo sana ambayo nilikuwa na mpango wa kuja kuiunganisha na kampuni yangu niliyotegemea kufungua hapo baadaye.

    “Ni meneja wa hoteli na anamiliki kampuni ya utalii.” Baada ya kumjibu aliendelea tena na maswali.

    “Urafiki wenu na Dany ulikuwaje.” Aliuliza swali jingine.

    “Alikuwa ndiye mtu ambaye alijua siri zangu zote, kila kitu kwenye maisha yangu yeye ndiye alijua na kila kitu chake aliniambia. Ni rafiki yangu mkubwa na ninayemuamini kama nilivyokuwa nikimwamini mama yangu.” Baada ya hapo Khajat aliniulizwa swali la mwisho.

    “Je mpaka sasa kwa walioko Tanzania ni nani unamuamini sana?” sikuwa nimemuelewa vizuri sana.

    “Sijakuelewa swali lako.” Nilimuomba alirudie tena swali hilo.

    “Kuacha mimi, Pamela na Felly, nani mwingine unamuamini?” lilikuwa swali gumu sana lakini sikuwa na namna zaidi ya kueleza ukweli wa hisia zangu.

    “Namuamini sana Dany, ni kwa vile tu hajajua ukweli kuwa niko hai na nimehujumiwa sana, na ninajua kama akijua ukweli atatusaidia kurudisha kila kitu changu.” Nilimueleza hayo kisha aliniaga na kukata simu.Baada ya muda kidogo Pamela alikuja pale kazini na alipita moja kwa moja mpaka ofisini kwangu, nilijiuliza ni kwanini alikuja ofisini kwa muda ule lakini nilituliza akili ya kujiuliza baada ya yeye kunieleza nia yake ya kuja pale.

    “Ni mekuja kukuambia kuwa tunaenda na Felly sehemu fulani hivi kuna rafiki yangu nampeleka akamuone ilikumsaidia kwaajili ya mambo yake kisha tutawahi kurudi.” Alineleza hayo lakini moyoni nilikuwa na wasiwasi sana juu ya walikokuwa wanatakiwa kwenda.

    “Lakini sio hatari huko mnakokwenda Pamela?” nilimuuliza na kuonyesha dhahiri wasiwasi wangu kitu kilichoonekana kumvunja moyo.

    “Sio hatari Patrick, ingekuwa hatari wala nisingethubutu kabisa kwenda, najua nimetoka hospitali muda si mrefu sana na ninatakiwa nipumzike angalau miezi mitatu lakini huku tuendako ni muhimu zaidi kwa Felly kukamilisha uchunguzi wake ili jioni atupe mrejesho wa alichokuwa akikifanyia uchunguzi.” Alijitahidi kunishawishi na mimi sikuwa na kitu cha kupinga. Alikaa pale kidogo na Felly alikuja.

    “Hey Patrick najua utakuwa na wasiwasi, atakuwa sawa ili mradi yuko na mimi, ananifikisha kwa huyo mtu kisha nitampa dereva amrudishe.” Aliongea Felly na hapo waliondoka. Kwenye majira ya saa tisa mchana kazi zilikuwa zimekwisha na Khajat alikuja kunifata pale ofisini.

    “Patrick nimefanikiwa kujua kujua Dany alipo sasa nataka twende wote ila utajificha sehemu nakuwekea hivi vidude masikioni utakuwa ukisikia nikiongea nae na hata wewe utaweza kuniambia chochote kama ukitaka, nataka nimfate kwanza mimi nimjue vizuri kisha tutaangalia kitu kingine cha kufanya.” Aliongea Khajat na hapo aliniwekea kidude fulani hivi kama kifungo na kuongea kisha nilimsikia kupitia kile kidude, akawasha gari na sasa tukaondoka mpaka kwenye bar moja maarufu sana pale Fiji, tulipofika Khajat alishuka na kuniambia nimfate. Tukaenda mpaka kwenye sehemu fulani kulikuwa na kona ya kupumzikia watu na pale tukakutana na dada mwingine ambaye sikuwa namfahamu.

    “Vipi yuko wapi?” Khajat alimuuliza yule dada.

    “Nimeshamtengea sehemu ya peke yake yuko kwenye ile kona pale una muona?” yule dada akamuonyesha Khajat.

    “Patrick, Dany ni mdhaifu wa nini mana kila mtu anaudhaifu wake.” Aliniuliza Khajat na kunifanya nicheke.

    “Dany anapenda sana wanawake.” Nikamjibu huku nikiendelea kucheka.

    “Najua Dany ni mdhaifu wa wanawake lakini unajua ni mdhaifu wa sehemu gani ya mwanamke?” aliuliza tena Khajat na kunifanya akili yangu irudi nyuma na kukumbuka kipindi tukiwa shuleni. Kabla ya Dany kuwa na Cathe alikuwa akimpenda sana msichana mmoja aliyekuwa akiitwa Anjela, sio kwamba alikuwa akimpenda sana, hapana alikuwa akimtamani zaidi, kilichokuwa kinamfanya amtamani Anjela ni mapaja yake meupe, na kila mara alikuwa akiniambia hilo. Hata mama yake Dany kabla ya kufarikim kipindi Dany akiwa shule ya msingi aliwahi kusema mwanae ni mbaguzi sana hata marafiki huwa anapenda weupe tu. Hivyo ugonjwa wa Dany ni mapaja meupe.

    “Anapenda sana mapaja hasa meupe kama yako.” Nilimjibu Khajat na yeye alicheka kisha aliniambia nimsubiri pale. Akaondoka na yule msichana na baada kama ya dakika kumi alirejea pale. Alikuwa kapendeza sana ndani ya sketi fupi sana iliyoacha mapaja yake nje.

    “Kama hivi.” Aligeuka huku na huko ili nimtazame.

    “hahaa, ndio kama hivyo, umependeza sana.” Nilimwambia Khajat na yeye alicheka na kukonyeza.

    “Sasa, mimi nitaenda kuonana na Dany pale. Wewe utakuwa hapa utasikiliza anayoniambia kama ni ya kweli ama la kama ikitokea nimemuuliza kitu unachokijua, uwe mvumilivu inaweza kuchukua zaidi hata ya masaa 8 kuwa na mazoea nae. Ukiona tumeondoka nitakupa ishara na wewe utakuwa na huyu dada hapa atakuongoza kila kitu na sehemu ya kwenda, nataka kujua vitu vingi sana kwake hivyo itachukua muda.” Aliongea Khajat.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sawa, hilo kwangu mimi sio tatizo.” Nilimwambia na hapo alianza kufikicha macho yake mpaka yakawa mekundu kabisa.

    “Khajati ndo unafanya nini hivyo.” Nilimuuliza kwa mshangao, macho yake yalikuwa mekundu kama vile alikuwa akilia.

    “Hii ni sehemu ya mchezo, nitakie mafanikio basi.” Alicheka wakati akijibu.

    “Nakutakia mafanikio mema.” Aliondoka pale na nilimuona akielekea kwenye ile meza aliyokaa Dany. Sikujua alikuwa anataka kufanya lipi na lipi, sikuelewa kabisa angefanyaje ili kufanikisha hayo aliyoyakusudia. Nilikuwa nimekaa pale nikitamani sana kuongea na Dany, huyu jamaa ni rafiki yangu sana, tulianza wote kutafuta maisha na kutembeza wasifu wetu kila sehemu kabla ya kuamua kujiajiri wenyewe. Mara zote nilikuwa nikikaa kwao na yeye akikaa kwetu. Dany hakuwa na mama kwakuwa mama yake alishafariki toka yeye akiwa shule ya msingi hivyo nyumbani kwao walikuwa watoto wa kiume tu lakini pia wawili walifariki kwa ajali kipindi tukiwa wakubwa kabisa, hivyo Dany alibaki kuwa peke yake. Hivyo mimi ndiye nilikuwa ndugu yake wa kipekee kabisa.

    “Dada unalia nini?” Nilishtuka na kusikia sauti ikiuliza swali hilo. Mh! nikaguna na kutazama kule alikokuwa Khajat. Nikaona Dany akiwa karibu naye na Khajat alikuwa ameinama akilia. Sikujua imetokeaje.

    “Khajat mbona unalia nini kimetokea.” Nilimuuliza Khajat kwakuwa nilijua angenisikia kupitia kile kidude alichoniwekea.

    “Niko sawa usijali hakuna tatizo lolote.” Alinijibu na mimi nilisikia nikamuelewa lakini jibu alilonipa liliendana na swali alilouliza na Dany hivyo Dany alidakia.

    “Hakuna tatizo wakati unalia dada, nambie nini tatizo naweza kukusaidia.” Dany alidakia na kuonyesha nia ya ukaribu.

    “Nyie wanaume ni nyoka kabisa, nimempenda alaf leo anakuja kuniacha pasipo sababu, kwanini jamani?” Khajat alizidi kulia mpaka ikabidi mimi nitoe kile kidude nicheke kwanza. Dany ikabidi aanze kumbembeleza pale mpaka Khajat akanyamaza. Nikarudisha tena kile kidude sikioni ili niweze kusikia yanayojiri.

    “Usijali maisha ndivyo yalivyo, haimaanishi mmoja kukufanyia hivyo basi wote ni ndivyo walivyo. Kuna muda lazima ujifunze kuacha mtu aondoke kama hataki kukuthamini, ujifunze kujali zaidi furaha yako kuliko ya mtu asiyejali ya kwako. Kuna muda lazima mambo fulani yatokee ili dunia izunguke. Maisha yataenda kama utajifunza kuwa mbinafsi muda mwingine.” Aliongea Dany kwa busara ya hali ya juu.

    “Uuf angalau nina jisikia nafuu kwasasa, naomba muite muhudumu nataka pombe kali.” Aliongea Khajat na hapo Dany alimuita muhudumu na kumuagizia amletee pombe kali. Dany hakuwa mnywaji toka zamani sasa sikujua itakuwaje hapo kwenye kunywa ila Khajat alimlazimisha kunywa na muda si muda niliona wakikumbatiana na kupigana mabusu. Dany alishaanza kulewa na kuongeaongea. Muda ulizidi kwenda na mimi nilikaa pale tu nikisubiri maelekezo yoyote. Nikamuona Khajat akitoka pale na kuelekea chooni kisha aliniambia nimfate, muda huo giza lilikuwa limeshaingia. Nilikwenda mpaka choo cha wanawake.

    “Patrick wewe unatakiwa sasa uende nyumbani, Felly anakuja hapa utaondoka akishafika, nenda akae na Pamela.” Aliongea hayo na mimi sikuwa na pingamizi kwakuwa nilikuwa nimechoka.

    “Sasa na wewe unavyokunywa pombe hivyo siutashindwa kufanya kazi?” nilimuuliza huku nikimtazama.

    “Hahaaa, hizi kazi nimefanya kwa miaka mingi sana Patrick, hata ninywe ndoo nzima pale silewi, atalewa yeye, kwenye ile glasi ninayotumia nimeweka kidonge cha kukata kilevi, hivyo mimi pale nakunywa pombe tu isiyo na kilevi ila yeye ndiye anayekunywa yenye kilevi ndo mana unamuona hajielewi. Felly ameshafika fanya uende.” Aliniongelesha na tuliagana akaondoka, bado aliniambia kuwa nitamsikia kupitia kile kidude nisikitoe. Nikaondoka mpaka nyumbani na nikiwa njiani nilisikia bado Khajat akimsisitiza Dany wakalale. Kwasauti ya Dany niliyoisikia ni kama vile alikuwa kalewa sana. Baadaye nilisikia tena sauti ya Khajat ikimuelekeza Felly namba ya chumba na hoteli waliyokuwa wakienda na Felly alimwambia CC2 italetwa kwenye chakula na muhudumu kisha anajua cha kufanya ili wafanye kazi kwa ukaribu. Sikuwa nimeelewa ni nini na mimi ikabidi niingilie.

    “Hey CC2 ndo nini nyie watu.” Niliuliza na nilisikia sauti ya Khajat ikicheka.

    “Ni Coca kete mbili, coca ndiyo mmea unaotumika kutengenezea madawa ya kulevya ya kokein.” Alinijibu na hata kabla sijauliza chochote waliendelea na mazungumzo yao na baada ya muda mfupi sikusikia kitu tena kwa maana ya kwamba mawasiliano nao yalikatika.

    Nilifikia nyumbani na tulikaa na Pamela na mtoto wetu Cris na hadi tunaenda kulala hakukuwa na taarifa yoyote toka kwa Khajat wala Felly na kwakuwa kesho yake haikuwa siku ya kazi basi wao walikuwa wa kwanza kufika kwetu asubuhi na kutuchukua mpaka kwa Felly kwakuwa kule ndio kulikuwa na vifaa vya uhakika vya kutufanya tuelewe vizuri watakayokuwa wanatuambia.

    “Twendeni kule chini nikatumie ile kompyuta kubwa.” Aliongea Felly na hapo tulishuka ngazi na kwenye kwenye chumba kilichokuwa chini ya ardhi.

    “Ataanza kuongea Khajat kisha mimi nitamalizia.” Aliongea Felly.

    “hahaa aanze dogo sio.” Nilitania na wote walicheka.

    “Hahaa, sawa bhana, ila dogo sasa hivi ni Cris.” Walicheka tena wote na Khajat alianza kuongea.

    “Jana nilianza kazi ya kumtafuta Dany na nikagundua ameingia nchini kwa biashara, amekuja kufatilia magari ya kitalii aliyonunu kwenye kampuni moja iliyoko huku. Nikabahatika kupata namba yake ya simu aliyoitumia kumpigia afisa mmoja wa uhamiaji na ndipo nilipotafuta eneo ambapo ile namba ipo kwa wakati huo, nikaenda na Patrick mpaka pale na nilifanikiwa kumpata Dany zaidi ya vile nilivyotarajia. Baadaye Patrick ulipoondoka mimi nilikwenda na Dany hotelini na nilifanikiwa kumuwekea dawa na hapo alilala kabisa. Hivyo mimi na Felly tulipata muda wa kupekuwa kompyuta yake na simu na kutambua mawasiliano yake mengine.” Alimaliza Khajat na Felly alidakia.

    “Katika kutafuta Dany, jana nilikuta mawasiliano ya barua pepe toka kwa mtu anayeitwa Catherine kwenda kwa Mary, ujumbe ulikuwa ukieleza juu ya kuingiza magari yake kwenye mzunguko wa kampuni yake kama vile walivyo ahidiana, hii ilikuwa ni mwezi mmoja toka baba yako afariki, lakini ujumbe huo ulijibiwa na ulisomeka kama ifuatavyo ‘nakumbuka shem, tena najua unadai mengi sana na asante kwa uvumilivu wako, kesho nitamu assign mtu atakuja kuyaingiza kwenye payroll na wewe utatuma vijana wako wayalete’ sehemu ya ujumbe huo ambao ulisomeka hivyo ulikuwa kwenye anuani ya cathe.co@gmail.com na uliandikwa kwa mchanganyiko wa lugha ya kingereza na Kiswahili na Pamela ndiye aliyetusaidia kutafsiri maneno ya Kiswahili. Ujumbe huo pia ukajibiwa tena kwa lugha ya kingereza kuwa ‘thanks, though it was a great pain but atlist we have accomplished the mission’ (asante, japokuwa yalikuwa ni maumivu makubwa lakini angalau tumekamilisha mpango), swali nililojiuliza lilikuwa ni huo mpango ulikuwa upi? Na pia aliyetuma barua pepe hii alikuwa ni nani, je ni Dany au ni Catherine, jibu lilikuwa ni dogo tu, kama Cathe ndiye angekuwa ametuma ule ujumbe basi Mary asingemwita shemeji, hivyo aliyetuma ule ujumbe alikuwa ni Dany. Baadaye siku hiyo hiyo ile anuani ya barua pepe ilituma ujumbe kwa mtu aliyeitwa Paul akimwambia ‘nilitambulishwa kwako na Mary, nimefurahia kazi yako ya nje na ya ndani. Nategemea kufanya kazi na wewe ikitokea kuna ulazima’, ujumbe uliishia hapo na Paul aliujibu. Hapa kumbuka kuwa Paul ni yule ambaye Mary alimtumia ujumbe kumwambia juu ya kukamilika kwa mpango wa kuchomoa zile karatasi lakini zaidi kumwambia ajiandae kwa mpango mkubwa utakao fata. Hivyo mpaka hapa Paul ndiye kijana wa kazi za kihalifu wa Mary. Kuna wasiliano pia ya Mary kwenda kwa Paul akimwambia ‘tembea juu ya nyayo za Mark, subiri ujumbe wenye G na O itakuwa ni red light and when it turns green, you know what to do, mind you, this is the master plan, after this we will be done with all the shit and you will go back to Al Hamid for the Pritoria event”(itakuwa ni taa nyekundu, na ikibadilika kuwa ya kijani, unajua cha kufanya, nikukumbushe kuwa huu ndo mpango mkubwa, baada ya hili tutakuwa tumemaliza upuuzi wote na utarudi kwa Al Hamid kwaajili ya tukio la Pritoria), huu ulikuwa ujumbe toka kwa Mary kwenda kwa Paul uliotumwa siku tatu kabla ya leo, meneno ya Kiswahili tumepata tafsiri toka google. Pia kwa kipindi cha nyuma kuna ujumbe ulitoka kwa Dany kwenda kwa Mary na hiki ni kipindi kile Mary akiwa bado yuko huku, ujumbe huo ulikuwa ukisomeka ‘Hey Mary, you didn’t bring me up t speed for two day, is there a prob? Setup is in place, green code to you.’ (Hey Mary, hujanipa taarifa kwa siku mbili, kuna tatizo lolote?, mazingira yako sawa, unaweza kuendelea) maneno yaliyotumika hapa ya green code na mengine ni maneno ambayo hutumiwa na watu wenye mafunzo ya kijeshi au wapelelezi au majasusi au majambazi wenye uelewa wa lugha za kijeshi. Hii ikanipa wasiwasi sana, nikaendelea kutafuta mawasiliano mengine ambayo yalikuwa kati ya Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Alsad Drilling Company ya Urusi na Mary akimuelekeza kuwa atakuwa tayari kununua hisa zote na kuihamishia kampuni hiyo nchini Tanzania baada ya kukamilisha mpango wa kumuondoa mtu ambaye ni kikwazo, ujumbe unamueleza jinsi alivyofurahishwa na mbinu aliyompa ya kufungua kampuni Maputo na Afrika ya kusini ila pia anashukuru kwa zile sanduku za silaha zilizofanikiwa kumfikia bila tatizo na hivyo ameimarika na sasa yuko tayari kwa kazi baada ya vijana wake kumaliza mafunzo. Hizo ni habari chache tu, lakini kubwa ni kwamba tunaye Dany hapa ndani.” Felly alifungua mlango mmoja uliokuwa pale ndani na nikamuona Dany akiwa amefungwa kwenye kiti na mdomo wake ukiwa umefungwa pia, alikuwa na majeraha kiasi usoni.

    “Dany!!” nikamsikia Pamela akimwita kwa mshangao.

    “Unamjua?” Nilimuuliza Pamela.

    “Huyu ndiye aliyenibaka yeye na ndugu zake kipindi kile nikiwa nafanya kazi kwao.” Sikujua cha kusema, Khajat aliufunga ule mlango na kutugeukia tena.

    “Kibaya zaidi ni kwamba leo asubuhi Mary amemtumia Dany ujumbe kuwa tayari wameshafanikiwa kumuua MARK usiku wa leo na sasa wako huru kuendelea na mambo mengine.” Aliongea Khajat.





    “Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa. Kanuni ya mafanikio katika lolote binadamu afanyalo huwa ni KUWA NA MPANGO THABITI, mpango hukueleza ni wapi unataka kufika na kwa kiasi gani. Mipango ya mafanikio yetu hupangwa na vichwa vyetu pamoja na fikra tulivu zinazotawala mioyo yetu, ukiwa na mpango kinachofata ni MKAKATI, hii huwa ni njia ya utekelezaji wa mpango wako. Ukijua uendako ni rahisi sana kupata njia ya kukupeleka huko, hata kama utachelewa kiasi gani lakini ni rahisi sana kufika huko. Maisha hayana kanuni maalumu wala haikuhitaji uwe na elimu kubwa sana ili ufanikiwe katika maisha, unachotakiwa tu ni kujitambua, kuweka mipango, kutafuta mkakati, kuweka vipaumbele, kujiamini na kusimamia unayoyaamini, UKIMALIZA YOTE HAYO KIKUBWA NI UWE NA HAMU KUBWA YA KUFANIKIWA INAYOZIDI WOGA WAKO WA KUSHINDWA. MAISHA MAZURI NI WEWE TU KUYATAFUTA.” HII NI SEHEMU YA KUMI NA MBILI

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wengi najua watatokea sana kumpenda Khajat, kwenye hii simulizi nilitamani sana Khajat asikike akisimulia, japo sikujua kingereza lakini nilikuwa nina uhakika sauti yake tu ingenieleza Khajati ni mtu wa aina gani. Usiku niliuona mfupi hasa ukizingatia muda huo ilikuwa ikielekea saa 9 usiku, na kipindi kilikuwa kinaisha saa kumi na mbili kasoro ili kupisha idhaa ya Kiswahili ya shirika la utangazaji la Uingereza. Kwenye sehemu hii ya kumi na moja ndiyo niliona ni kwa namna gani Khajat alikuwa si mtu wa mchezo. Pia nikagundua kuwa Felly ni mpole sana ambaye huongozwa na hisia na hisia hizo humfanya ashindwe kumtesa mtu. Lakini bado najiuliza huyu Mary ana mashetani gani,,unajua nini mwandishi? Patrick aliendelea kusimulia hivi;







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog