Search This Blog

Monday 24 October 2022

SIRI ILIYOTESA MAISHA YANGU - 3

 

    Simulizi : Siri Iliyotesa Maisha Yangu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Mpaka saa nne na nusu iliyofuata Dk. Ian alikuwa bado hajapiga simu kama alivyoahidi kufanya baada ya kuingia Dar es Salaam, Caroline alitakiwa  kanisani saa saa tano kamili ambako ndoa yake ingefungwa! hofu na wasiwasi wake ulirejea tena  na alishindwa kuelewa ni wapi alikokuwa daktari wake!

    Magari tayari yalikuwa nje ya nyumba yao, watu walishapanda  na matarambuta yalipigwa ni Caroline peke yake aliyekuwa akisubiriwa, alikuwa amegoma kabisa kutoka ndani kwenda kanisani! Hali yake haikuwa nzuri siku hiyo,alijisikia dalili kama za siku za nyuma!

    Ilikuwa ni siku ya saba bila kutumia dawa ya kuzuia kifafa! Na kwa mujibu wa maelezo ya daktari wake kama zingepita siku saba bila kutumia dawa hiyo ilikuwa ni lazima aanguke! Alitakiwa kunywa dawa hiyo maisha yake yote.

    Siku hiyo ya harusi ndiyo ilikuwa siku yake ya saba tangu amalize dawa zake, hivyo alijua kwa vyovyote kama angediriki kwenda kanisani ni lazima angeanguka kifafa mbele za watu na huo ndio ungekuwa mwisho wa uhusiano wke na Reginald kitu ambacho kwa hakika hakukitaka kitokee, alikuwa tayari harusi iahirshwe lakini asianguke kifafa mbele ya Reginald   alielewa ni kiasi gani  aliuchukia  ugonjwa huo.

    “Mwanangu twende tu labda leo hutaanguka inawezekana hizo siku saba zitakwisha saa sita  ya usiku!  Si unajua siku mpya huanza saa sita usiku? Twende tu mwanangu ukafunge ndoa yako ninaamini hutaanguka! Wala usiwe na wasiwasi tusipokwenda kabisa itakuwa aibu?”

    “Mama ni heri aibu ya kutokwenda kanisani si aibu ya kuanguka kifafa kanisani!”

    “Hapana Caroline, nakuomba mwanangu unyanyuke twende tu!”

    Kwa sababu ya heshima na utii aliokuwa nayo  kwa mama yake ingawa kwa shingo upande Caroline alinyanyuka kitandani alikokuwa amekaa akilia na kulinyoosha vizuri vazi lake la harusi lililokuwa limejikunya mwilini mwake.

    Alitoka hadi nje  na kuingia ndani ya gari, msafara mrefu ulianza kuondoka kuelekea kanisa la Mtakatifu Joseph ambako harusi ilipangwa kufungwa! Macho yake yalikuwa bado yakibubujikwa na machozi, ilikuwa tayari saa tano na nusu ikiwa  nusu saa baada ya muda uliopangwa.

               **************

    Reginald alifika kanisani saa nne kamili asubuhi na kuanza kumsubiri bibi harusi mtarajiwa afike lakini hadi saa nne na nusu  waliyopanga kukutana Caroline alikuwa  hajaonekana, alianza kuingiwa na hofu juu ya jambo lililotokea hadi asitokee kanisani mpaka muda huo!

    “Au amebadili mawazo yake nini?”Reginald alimuuliza mpambe wake.

    “Sidhani ila nina uhakika kutakuwa na tatizo  naomba tu isije kuwa ajali!”

    “Sasa mbona hatokei!

    Kila mtu ndani ya kanisa alianza kuhisi jambo  baya lilikuwa limetokea, ilipofika saa tano kamili bila bibi harusi kutokea mawazo ya wengi yalianza kuhisi Reginald alikuwa ameachwa katika mataa! Ilikuwa ni aibu kubwa iliyopelekea Reginald kuanza kutokwa na machozi, alishindwa kuelewa ni kosa gani alilomfanyia Caroline mpaka kufikia uamuzi wa kulipa kisasi kibaya namna hiyo! Mpambe wake alimbembeleza wakati akilia na kumpa moyo kuwa lazima Caroline angefika!

    Dakika chache baadaye walisikia matarumbeta yakipigwa nje ya kanisa na msafara ulionekana kuwasili, ilikuwa furaha kubwa mno kwa Reginald aliruka na kuanza kukimbia kwenda nje,  mpambe wake alimfuata kwa nyuma, nje ndani ya gari lilopambwa vizuri alimwona Caroline akiwa katikati ya akinamama wawili shingo yake ikiwa imelala begani kwa mama mmoja,   alipomwangalia vizuri  mama huyo Reginald alimfahamu, alikuwa shangazi yake na Caroline! Alisogea hadi karibu kabisa na gari hilo.

    “Shangazi  poleni na matatizo mbona mmechelewa?’Aliuliza Reginald lakini hakuna aliyejibu swali lake.

    “Mama nasikia kizunguzungu! Nasikia kizunguzungu siwezi kushuka garini nitaanguka!”Alisema Caroline wakati mama yake wakijaribu kumshusha garini.

    “Jitahidi mwanangu!”

    Caroline alijitahidi kama mama yake alivyomwomba na kwenda moja kwa moja hadi ndani ya kanisa ingawa kizunguzungu kiliendelea kumsumbua! Kwa kuwa alikuwa amechelewa padri alianza moja kwa moja shughuli ya kufungisha ndoa!

    “Reginald unakubali kumuoa Caroline?”

    “Ndiyo nakubali!” Reginald aliyajibu maswali yote kisha kumvalisha pete Caroline, padri akamgeukia Caroline na kumuuliza maswali yale yale lakini hakujibu kitu chochote alibaki ameduwaa! Kizunguzungu kilikuwa kikizidi kumbana.

                                             ***********************

    “Excuse me!”(Samahani) Ilikuwa ni sauti ya mzungu nyuma akimuuliza mtu aliyesimama mlangoni  mwa kanisa kama alimfahamu Caroline.

    “Yeah!She is the one getting married today!”(Ndiye yeye anayeolewa leo!)

    Bila kusita  Dk. Ian alianza kukimbia kuingia ndani ya kanisa alijua msaada wake ulihitajika sana kuokoa jahazi, kwa hakika aliamini Caroline alikuwa katika wakati mgumu.

    Je harusi hii itafanyika? Kifafa kitazuiliwa?Fuatilia wiki ijayo.







    Baada ya kupata maelezo kutoka kwa mtu aliyemkuta mlangoni Dk. Ian alianza kuingia ndai ya kanisa la St. Joseph akikimbia, alipita katikati ya viti vilivyojaa watu na kwenda hadi mbele, kanisa lilikuwa kimya watu wakimsikiliza padri aliyekuwa akiendesha ibada hiyo.

    Mami ya watu walifurika kanisani siku hiyo kushuhudia caroline akiolewa, Dk Ian alijua ni kiai gani alihitajika ili kunusuru harusi hiyo na kumwepusha caroline na aiba iliyokuwa mbele  yake, wakati akipita watu wote kanisani waligeuka na kumwangalia, walionyesha mshangao kumwona mzee wa kizungu akikimbia katikati ya kanisa walikuwa wamebakiz kama hatua tatu kutoka mahali waliposimama caroline, Reginald wapambe wao pamoja na kuingiza mkono wake wa kulia mfukoni mwa koti lake na kutoa kichupa kidogo na kukishika kwa mkono wa kushoto kisha akaingiza tena mkono wake katika mfuko wake mwingine wa koti na kutoa bomba la sindano.

    Aliyafanya yote hayo kwa haraka huku watu kanisani wakimshuhudia, lakini walishindwa kuelewa ni nini alichotaka kufanya! Alikinyanyua kichupa juu na kulichomeka bomba la sindano ndani yake na kuanza kuyavuta maji yaliyokuwemo kwa kutumia bomba alipomaliz alikirudisha kichupa mfukoni na kuanza kumsogelea caroline aliyekuwa akiyumbayumba.

    Kabla hajamfikia alishtuka kumwona caroline akianguka chini na kulala chali, alianza kutupa miguu yake huku na kule hewani, mwili wake ulikakamaaa na mapovu mengi yalianza kumtoka mdomoni, kilikuwa kifafa! Mama  na baba yake walishika mikono vichwani mwao ilikuwa ni aibu kubwa mno kwa upande wao.

    Minong’oni ilianza kusikika kanisani.

    “Bibi harusi ana kifafa yalianza kusikika kila mahali kanisani! Watu walinyanyuka vitini mwao na kuanza kusogea madhabahuni kushuhudia kama walichokisikia kilikuwa na ukweli ndani yake, kanisa zima lilitawaliwa na vurugu, kufikia hapo haikuwa harusi tena bali fujo.

    “Caroline! Caroline! Caroline kumbe kweli una kifafa sasa kwanini nilipokuuliza ulikataa!” Alisema Reginald akipiga kelele ilikuwa ni aibu kubwa kwake pia.

    Alipofikiria gharama alizokuwa ameingia katika maandalizi ya harusi hiyo roho ilimuuma sana, alijua kwa hakika asingeweza kuoa msichana mwenye kifafa maishani mwake, Reginald alipiga magoti chini  na kuanza kumtingisha caroline sakafuni, caroline hakushtuka alikuwa amelala chini mwili wake ukiwa umekakamaa!

    Profesa Kadiri baba yake caroline alishindwa kuvumilia kuona jinsi mtoto wake alivyokuwa akitingishwa sakafuni, alimfuata Reginald akamshika na kumnyanyua.

    “niachie mzee nyei si mlijua mtoto wenu ana kifafa lakini mkataka kunitapeli? Sasa Mungu amewaaibisha!Nirudishieni mahari yangu sasa hivi!”Reginald alifoka.

    “kijana hebu naomba uwe mtulivu kidogo mahari yako utapata acha kwanza tushughulikie hili tatizo la mtoto!”

    “Haiwezekani!”Reginald aliendelea kufoka huku akilia machozi, alimkaba profesa Kadiri shati! Padri na watu wengine waliokuwepo walikwenda na kumshika wakimzuia asifanye fujo ndani ya nyumba ya Mungu lakini hakusikia.

    “Kijana mbona leo umekuwa siyo mstaarafu?”

    “Nataka mahari yangu mimi niondoke hapa, nikatafute mwanamke mwingine wa kuoa haraka!” alisema Reginald.

    Kauli hiyo ilimuudhi sana profesa Kadiri na kumfanya atoke mbio hadi kwenye gari lake lililokuwa nje na aliporejea alikuwa na kitabu kidogo mkononi mwake! Kilikuwa kitabu cha hundi za benki.

    “Kijana unanidai shilingi ngapi?”

    “Shilingi milioni moja na nusu!”

    “Hakuna zaidi ya hapo?”

    “Hakuna wewe nipe tu hizo zinatosha!”

    “Utapokea hundi maana leo ni Jumamosi benki zimekwishafungwa!”

    “Nipe tu!”

    Profesa kadiri aliinama na kuandika hundi ya shilingi milioni moja na nusu mbele ya padri na kumkabidhi Reginald wapambe wake walishangilia na kumbeba Reginald juu juu na kutoka naye nje ya kanisa, watu wengi waliobaki vitini baada ya  timu ya Reginald kuondoka walikuwa ni ndugu na marafiki wa familia ya caroline peke yao.

    Ilikuwa huzuni kubwa na watu wengi ndani ya kanisa walisikika wakilia, wengi walimwonea huruma caroline, nje miungurumo ya magari ilisikika ishara kuwa msafara wa Reginald na ndugu zake ulikuwa ukiondoka.

    Padri alibaki amesimama bila kujua la kufanya, harusi ilikuwa imevunjika baada ya bibi harusi  kuanguka kifafa ndani ya kanisa! Hakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya kuwapa pole wazazi wa  caroline na ndugu zake wengine pole, lilikuwa ni jambo la kusikitisha sana!Katika miaka yote ishirini aliyofanya kazi ya Mungu hilo ndilo lilikuwa tukio la kwanza kwa padri Slivinus Urio aliyekuwa akiifungisha ndoa hiyo.

    Dk. Ian alisimama mahali pale kimya kabisa, hakujua kitu gani angefanya, kuchelewa kwake kulikuwa kumesababisha matatizo, ndani ya moyo wake aliamini kama angewahi kufika Tanzania angemwepusha caroline na aibu iliyokuwa imempata! Alijisikia vibaya ndani ya nafsi yake, ingawa hakuifahamu lugha ya kiswahili hali aliyoiona pale ndani ya kanisa ilimuonyesha wazi kuwa harusi ilikuwa imevunjika na hilo ndilo lilimuumiza moyo zaidi.



    Dk. Ian alikuwa mzaliwa wa Newzealend kutoka katika familia ya mfanyabiashara maarufu nchini humo, Smith William! Baba yake alikuwa miongoni mwa raia wa nchi hiyo waliopigana vita vya pili ya dunia na ilipokwisha baba yake alijikuta nchini Canada na kuamua kuanzisha maisha yake katika nchi hiyo jeshini alifanya kazi kama daktari wa jeshi la Canada.

    Mwaka 1949 akiwa nchini Canada alimuoa binti wa tajiri maarufu nchini humo aliyeitwa Richard Mond!Mzee huyo alimiliki viwanda vya vyuma, hoteli nyingi za kitalii, alikuwa na mashamba makubwa ya ngano na kahawa! Alikuwa mtu aliyeheshimika sana nchini humo.

    Tajiri huyo aliamua kumpa Smith mtoto wake baada ya kumponyesha ugonjwa wa kuvimba viungo uliomsumbua kwa miaka mingi na kutumia tiba nyingi bila mafanikio.

    Smith alimponyesha kwa wiki mbili tu kwa furaha aliyokuwa nayo tajiri Richard aliamua kumpa Smith binti yake Christine awe mke wake! Smith hakuamini maana Christine  alikuwa ni mwanamke mzuri.

    Baada ya ndoa yake tajiri Mond alimkaribisha Smith kuishi naye nyumbani kwake, aliwapa nyumba nzuri  ya kifahari kuishi, alimfanya kuwa daktari wa familia yake na miaka miwili baadaye mwaka 1951 Dk. Smith na mkewe Christine walipata mtoto wa kwanza waliyemwita Ian!

    Dk. Smith  alitaka mtoto wake awe daktari bingwa kama yeye, ili kutimiza hilo alimpeleka katika shule zilizofundisha masomo hayo  na mwaka 1977 alipata digrii yake ya kwanza ya utabibu kutoka chuo kikuu cha Montreal na alisoma katika chuo  hichohicho digrii mbili zaidi na kuwa daktari bingwa na magonjwa  ya ubongo katika umri mdogo wa miaka 26.

    Tajiri Mond na mke wake walifariki katika ajali mwaka 1983 na kuiacha mali yote mikononi mwa binti yao na mumewe smith!Maisha yakabadilika na wakajikuta tayari ni mamilionea Dk. Smith alitajirika ghafla! Lakini nao pia hawakuishi muda mrefu sana walikufa miaka miwili baadaye kwa ajili ya gari  vilevile na kuiacha mali yote mikononi mwa mtoto wao pekee Ian Smith.

    Wakati hayo yanatokea Ian alifanya kazi katika hospitali ya rufaa ya Montreal alilazimika kuacha kazi ya udaktari na kuwa mfanyabiashara lakini alisaidia wagonjwa pale alipotakiwa kufanya hivyo! Alijipatia sifa kubwa sana katika kutibu wagonjwa wenye kifafa, hivyo wagonjwa wengi walimfuata nyumbani kwao kwa ushauri,hivyo ndivyo walivyofahaimiana na Caroline!

    Miaka mitatu baadaye biashara baadaye biashara hiyo ilimuongezea utajiri mara tatu zaidi, watu walishindwa kuelewa ni kwanini hali hiyo ilitokea lakini siri kubwa ya utajiri wake ilikuwa ni kujiunga na kundi la mafia, alilitumia kundi hilo kufanya biashara yake ya madawa ya kulevya na kuwavamia watu usiku na kuwaibia mali zao.

    Ni shughuli hizi haramu ndizo zilimfanya Ian atajirike zaidi hakuna mtu aliyefahamu siri hii zaidi ya watu aliofanya nao kazi! Kwa nje Dk, Ian alionekana mtu mwema na aliyesaidia watu wenye shida lakini kwa ndani alikuwa muuaji, mtu asiye na huruma aliyeua mke wake wa kwanza, Doroth kabla hata ya kuzaa naye mtoto baada ya mwanamke huyo kutoboa siri ya kazi yake Dk. Ian kujikuta matatani! Isingekuwa pesa zake angenyongwa.

    Wiki mbili baada ya kutoka mahabusu alikokuwa amefungiwa mke wake alikutwa ufukweni mwa bahari akiwa amekufa baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha! Hakuna  upelelezi uliofanyika kufuatia hongo alilolitembeza kwa wakuu wa polisi! Hakutaka tena kuao baada ya  tukio hilo kwa kuogopa siri zake kuvuja, aliishi maisha ya upweke yaliyojaa faragha na usiri wa hali ya juu.



    Caroline alizinduka na kuangalia huku na kule kanisani! Alimwona mama yake akilia machozi, kumbukumbu kuwa alikuwa kanisani kufunga ndoa zilimwijia lakini hakumwona Reginald mahali pale! Kumbukumbu za kizunguzungu alichokipata pia zilimwijia na alipojipapasa alikuta kipande cha mti kikiwa katikati ya meno yake! Aliwekewa kipande hicho kilichofungwa na kitambaa kila alipoanguka ili kuzuia kuuma ulimi.

    “Padri yupo wapi Reginald?”

    “Reginald………..!” Padri alishindwa kumalizia sentensi yake.

    “Tufungishe basi ndoa tuondoke?”

    Kwa kauli hiyo ilibidi padri amsogelee caroline na kuanza kumweleza juu ya kila kitu kilichotokea, caroline alilia machozi kwa uchungu! Kwa mara nyingine tena kifafa chake kilikuwa kimwaibisha!

    Mara ghafla alishtukia kitambaa kikipita usoni kwake na kumfuta machozi yake alipogeuka kuangalia nyuma yake alimwona Dk.Ian.

    “I’m sorry caroline! Very sorry for being late!All these is because of me!”(Nisamahe caroline, nisamehe  kwa kuchelewa yote haya ni kwa sababu yangu!) alisema Dk.Ian akiwa amemkumbatia caroline, aliyekuwa akilia mfululizo.

    “My husband to be has left me because I’m epileptic! Who is gonna marry me?”(Mume wangu mtarajiwa ameniacha kwa sababu nina kifafa nani atania sasa?”

    “Don’t worry!(Usiwe na wasiwasi!)

    “I wil never be happy again!”(sitakuwa na furaha tena!)

    “It is my fault caroline! For that reason your happiness Is my responsibility!”(Ni makosa yangu caroline kwa sababu hiyo nina wajibu mkubwa wa kukufanya uwe na furaha!)

    “Yeah!(ndiyo!)
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “How?”(Kivipi?)

    “I’m going to marry you(Nitakuoa!)

    “Marry me?when?(kunioa mimi? Lini?)

    “Today and right now!”(Leo tena sasa hivi)

    “Your’re jocking Ian?”(Unanitania Ian!

    Akiwa ameumia moyoni mwake kwa yaliyotokea ingawa aliahidi kutooa kabisa maishani mwake alijikuta akimfuata padri na kumweleza alichotaka kufanya ndani ya kanisa wakati huo! Padri alishangazwa na uamuzi huo na kuwaita wazazi wa Caroline pamoja na caroline mwenyewe  na kuongea nao.

    Caroline hakuwa na kipigamizi  watu waliobaki kanisani walitangaziwa juu ya bahati iliyokuwa imejitokeza kila mtu aliruka na kushangilia, ndoa ikawa imefungwa hakun aliyekuwa tayari kuamini kilichotokea caroline hakulia tena alifurahi kuolewa na mtu aliyekifahamu kifafa chake na aliyekuwa na tiba ya tatizo hilo.

    Harusi hiyo ilifuatiwa na tafrija ya nguvu iliyofanyika katika hoteli ya sheraton kwa gharama za Dk. Ian hapakuwahi kuwa na tafrija kubwa kiasi hicho katika historia ya jiji la Dar es salaam watu walikunywa na kula hadi kusaza, muda wote wa harusi hiyo caroline alionekana kucheka na kufurahi hakuwa na machozi tena.

    Majira ya saa 8:30 usiku waliondoka ukumbini kwenda kulala katika vyumba vya juu ya hoteli hiyo sheraton. Walikaa katika hoteli hiyo kwa wiki mbili kwa gharama za Ian. Wakaondoka kwenda Canada reginald alipoanza kuwafanyia fujo akidai kuwa caroline alikuwa mke na alimtaka aondoke naye.

    Caroline akawa ameondoka Tanzania kwenda Canada kwa mara ya pili lakini safari hiii akiwa mke wa mtu tajiri kuliko watu wote katika nchi hiyo, alijua maisha yalikuwa raha mustarehe baada ya hapo asingelia tena wala kuishi kwa majonzi! Lakini kitu kimoja tu hakukifahamu Dk. Ian alikuwa muuaji!

    Je nini kitaendelea Canada? Je huo ndio mwisho wa matatizo ya Caroline? Fuatilia wiki ijayo!













    N

    i wanaume wengi ?waliomwacha katika ?maisha yake sababu ya  ugonjwa wa kifafa aliozaliwa nao,  aliwachukia wanaume wote waliomnyanyasa kwa sababu ya ugonjwa isipokuwa mwanamume mmoja tu naye alikuwa Harry!  Ndani ya nafsi yake bado Caroline alimpenda Harry, alimfikiria karibu kila siku iliyopita! Harry alikuwa moyoni mwake na alikuwa tayari kumsamehe kama angekuja na kumwomba msamaha.

     Lakini Harry hakufanya hivyo,  baada ya kumwacha Caroline wakati huo wakisoma wote katika shule ya sekondari ya  Arusha hakudiriki  hata siku moja kumtafuta Caroline, kumpigia simu  wala kumwandikia kadi! Hapakuwa na mawasiliano yoyote kati yao tangu Caroline ahamishwe na wazazi wake Arusha, jambo lililomuonyesha Caroline wazi kuwa Harry alimchukia na alimchukia sababu ya kifafa.

    Pamoja na kuyafahamu hayo yote bado Caroline  alimpenda Harry na aliamini siku moja  wangekutana na kuurudisha tena uhusiano wao, hakumtaka mwanaume mwingine yeyote maishani mwake hilo ndilo aliloamini Caroline.

                ****************

    Baada ya  Caroline kuachana  na  Harry katika shule ya sekondari ya Arusha na yeye kuhamia shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani, kijana huyo alimalizia kidato cha nne na baadaye kuendelea na kidato cha sita katika shule hiyohiyo.

    Alipomaliza kidato cha sita alichukuliwa na baba yake aliyekuwa raia wa Uingereza na kwenda nchini humo ambako alijiunga na chuo kikuu cha Manchester Air zone Institute kwa ajili ya masomo ya  Urubani na ufundi wa ndege, yalikuwa ni masomo ya miaka  mitano na alimaliza na kupata digrii yake.

    Maisha yake yalikuwa mazuri kwa sababu baba yake  alikuwa na uwezo mkubwa kipesa! Alipata kila alichotaka, alibadilisha wasichana wazuri kadri alivyotaka! Hata siku moja hakuwahi kumkumbuka Caroline, ilikuwa ni kama hakuwahi kukutana na msichana wa aina hiyo maishani mwake! Alimchukia Caroline na hakupenda kabisa kuwa na uhusiano na msichana mwenye kifafa na hata kusikia habari zake.

    Kazi yake ya kwanza aliyopata baada ya kumaliza chuo kikuu ilikuwa ni katika shirika la ndege lililoitwa Air One, huko aliajiriwa kama rubani na fundi wa ndege. Hakukaa sana shirika hilo akaamua kuhamia nchini Marekani ambako aliajiriwa na shirika jingine kubwa la ndege lililoitwa USD Airlines, lilimiliki ndege nyingi na Harry alikabidhiwa ndege aina ya Boeing 737 iliyosafiri kwenda katika nchi za Mashariki ya kati kutokea Marekani.

    Ilikuwa ni kazi ngumu kiasi kwamba robo tatu ya maisha ya Harry yalihamia kwenye ndege, kila siku kwake ilikuwa safari na alipopata nafasi ya kupumzika ilikuwa ni kulala na alipoamka alioga na kuingia safarini tena! Maisha yake yote yalihamia angani  ni mara chache sana alikuwa nchi kavu. Sababu ya kazi nyingi hata siku moja hakuwahi kumkumbuka Caroline katika maisha yake ingawa Caroline bado aliteseka.

                *****************

    “Ian kweli umenioa?”

    “Ni kweli huamini Caroline?”

    “Sio rahisi kuamini!”

    “Naomba uelewe hivyo! Niliumia sana ulipoachwa kanisani na  nilijilaumu sana kukucheleweshea dawa, aibu yote uliyoipata ilikuwa ni sababu yangu ndio maana nimeamua kukuoa Caroline nataka uwe na furaha katika maisha yako”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Utaniweza kweli na kifafa changu?”

    “Ninalijua  sana tatizo lako lakini bado nimeamua kukuoa, hivyo wasiwasi ondoa!”

    Waliendelea kuongea wakiwa ndani ya ndege ya shirika la ndege la British Airways wakielekea Copenhagen nchini Dernmark baada ya kutoka hapo ndege ilitegemewa kuruka moja kwa moja hadi  Ottawa nchini Canada, huo ndio ungekuwa mwisho wa safari yao na ni hapo ndipo maisha mapya ya Caroline yangekuwa! Mpaka wakati huo alikuwa bado haamini pamoja na kuhakikishiwa  na Dk. Ian kuwa kweli  alikuwa ameolewa.

    Walitua kwenye uwanja wa ndege wa Ottawa saa kumi na mbili na nusu ya jioni, walipotoka nje ya uwanja Caroline alishangazwa na mapokezi yaliyokuwepo uwanjani hapo! Kulikuwa na magari  aina ya benzi ya rangi nyeusi  yapatayo ishirini yote yakiwa yamekuja kuwapokea wao.

    Watu waliowapokea wote walivaa suti nyeusi pamoja na tai!  Walipendeza na walionekana ni watu wenye uwezo lakini wote Walipiga magoti na kuwasalimia Dk. Ian na Caroline! Kwa Caroline yote yaliyokuwa yakitokea yalikuwa ni ndoto, hakuamini hata kidogo kuwa ingekuwa kweli! Hakuwahi kuwaza wala kutegemea kuwa siku moja angepigiwa magoti na mzungu akisalimiwa.

    “This is my wife Caroline..... Caro  meet  Mr Lead, my assitant!”(Huyu ni mke wangu anaitwa Caroline.....Caro kutana na msaidizi wangu anaitwa  bwana Lead!) Dk. Ian alimtambulisha Caroline kwa mzee mmoja wa makamo na baada ya utambulisho huo mzee huyo alipiga magoti chini na kumsalimia Caroline akiwa ameinamisha kichwa.

    Ilikuwa ni kama mbinguni, mambo aliyokuwa akifanyiwa alizoea kuyaona   akifanyiwa Malkia Elizabeth kwenye luninga na hakuwahi kufikiri siku moja angefanyiwa yeye. Waliongozwa na kupelekwa moja kwa moja kwenye gari la kifahari benzi la milango minane lililokuwa limewekwa tayari kwa ajili yao, matarumbeta yalilia kila upande wa uwanja huo na wapiga picha walikuwa na kazi ngumu kurekodi kila kilichokuwa kikiendelea.

    Ndani ya gari Caroline alimkumbatia Dk. Ian na kumpiga mabusu mfululizo usoni akimshukuru kwa kila kitu alichomfanyia.

    “Thank you Ian! Thank you again and again!  I thank you a milion times!”(Asante Ian! Asante tena na tena na asante mara milioni moja zaidi!)

    “For what!”(Unanishukuru kwa nini?) Dk. Ian aliuliza.

    “Thank you for making me a Queen in my life!”(Asante kwa kunifanya  Malkia katika maisha yangu!)

    “Take it easy!”(Usijali!)

    Msafara wa magari uliondoka kuelekea nyumbani kwa Dk. Ian katika eneo la matajiri mjini humo, kilometa kama kumi kutoka uwanja wa ndege gari lilikata kulia na kuingia kwenye ngome kubwa ya rangi nyeupe! Ndani ya ngome hiyo kulikuwa na uwazi mkubwa uliopandwa nyasi na maua mazuri ya kupendeza, magari yalizidi kusonga mbele yakipita katikati ya bustani za maua! Caroline hakuwa kuona sehemu nzuri kama hiyo maishani mwake na hakutegemea  sehemu kama hizo zilikuwepo duniani.

    Mbele kama kilometa moja na nusu walisimama mbele ya jumba kubwa la kifahari  wanawake wengi walijipanga nje ya jumba hilo wakiwa wamevaa nguo nyeupe na wakiwa vikawa vidogo vya rangi ya Kahawia wakipepea hewani! Caroline alizidi kushangaa, mlango ulifunguliwa na wote wawili waliteremka na kusimama, wanawake wanne waliwafuata na kuanza kuwapepea wakiwaongoza kuingia ndani ya nyumba.

    “Oh! Thanks God, at last I can relax, the only thing troubling me is this man, Harry Robertson! How can I get him  off my mind and enjoy life with my beloved husband?”(Oh! Nakushukuru Mungu mwisho sasa napumzika, kitu kimoja tu kinanisumbua ni huyu mwanaume, Harry ninawezaje kumtoa kabisa akilini mwangu nikaendelea kufaidi maisha   na mume wangu?) Aliwaza Caroline wakati akiishangaa nyumba ya Dk. Ian, ilijaa vioo na marumaru kila sehemu.

    Walipitiliza moja kwa moja hadi chumbani ambako walioga na baadaye kujitupa kitandani, kwa mara ya kwanza katika maisha yake Caroline alilifaidi tendo la ndoa kwa hiari yake.

    “Welcome into my life Caroline this is going to be your home forever!”(Karibu katika maisha yangu Caroline hapa ndio patakuwa nyumbani kwako milelel!)

    “Thank you Ian for making me happy! I love you!”(Asante Ian kwa kunifanya niwe na furaha tena! Ninakupenda!)

    “I love you too and I promise to love you forever!”(Nakupenda pia na ninaahidi kukupenda milele!)

             **************

    Yalikuwa maisha mapya kwa Caroline,maisha yaliyoonekana kuwa ya furaha siku zote, alikipata kila alichokitaka yakiwemo matibabu ya ugonjwa wake! Katika muda wa miezi mitatu tu aliyokaa nchini Canada ugonjwa wake ulipona kabisa, hakuanguka tena. Kila mtu katika familia yake alimheshimu   Caroline, aliitwa Queen!

    Asubuhi aliamshwa kitandani, aliogeshwa alipigishwa mswaki, alivalishwa nguo, kitu pekee alichofanya ni kula chakula! vingine vyote vilifanywa na wafanyakazi wa nyumbani kwake, kila alikokwenda alipewa ulinzi. Maisha ya Caroline yalikuwa ya Kifalme, machozi na huzuni zote alizowahi kuwa nazo zilifutika aliishi maisha ya raha mustarehe.

    Pamoja na raha zote hizo bado  Harry aliendelea kuwa kichwani mwake, alimuwaza na kumfikiria kila siku! Alimuota akiwa usingizini na kuna wakati badala ya kumwita Ian kwa jina lake alimwita Harry!  Bado alitamani kuonana naye na aliamini hilo lazima lingetokea maishani mwake. Kadri siku zilivyozidi kupita mawazo juu ya Harry yaliongezeka na kumkosesha raha.

    Alipowasiliana na  ndugu zake Arusha  akitaka kujua mahali alikokuwa Harry aliambiwa aliondoka miaka mingi kwenda Ulaya kwa baba yake na haikujulikana mama yake alikuwa wapi kwa wakati huo, hakuna mtu aliyejua Harry alikuwa ulaya katika nchi gani! Ilibidi Caroline kwa utajiri wa mume wake aamue kumtafuta Harry huko huko Ulaya. Alikwenda katika ofisi za shirika moja binafsi la upelelezi na kuwaeleza shida yake.

    “Nataka mmtafute popote pale duniani kwa gharama yoyote na mimi nitalipa!”

    “Hiyo ni kazi ndogo kwa kuanzia utatulipa dola za Kimarekani milioni tano!”

    “Pesa siyo tatizo! Ninachohitaji ni kumwona Harry kabla sijafa!”

    “Hilo litafanyika!”

    Caroline aliandika hundi ya kiasi hicho cha pesa, picha na taarifa  muhimu za Harry  na kuwakabidhi, kazi ya kumsaka Harry dunia nzima ilianza, kwanza wapelelezi  walitumwa Arusha Tanzania.

               ****************

    “Woooow! I cant believe it! Is it mine?”(Woooow! Nashindwa kuamini! Kweli ni yangu?)

    “Yeah it is yours! Dont you remember that to day is 23rd August?”(Ndiyo ni yako! Umesahau kuwa leo ni tarehe 23 mwezi wa nane?)

    “What happens with 23rd August?”(Kwani nini hutokea tarehe 23 mwezi wa nane?)

    “Your birthday darling!And this Aeroplane is your birthday present! I want to make you the happiest woman on earth”(Sikukuu yako ya kuzaliwa mpenzi na hii ndege ni zawadi yako, nataka kukufanya mwanamke mwenye furaha kuliko wote duniani!)

    Caroline aliruka kwa furaha na kumkumbatia mume wake huku akilia machozi, Ian hakuwa amemtaarifu  juu ya kumnunulia ndege kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.

    “I want you to go to Miami  beach for a month long vacation! Go there and relax! I just need to have another Pilot who will be flying you jet!”(Nataka uende Miami ukapumzike kwa mwezi mmoja, ninachohitaji sasa hivi ni rubani mpya atakayekuwa anarusha hii ndege yako!)

    Wiki moja baadaye matangazo ya rubani mpya aliyekuwa akitakiwa na tajiri Ian Smith kwa ajili ya kuendesha ndege ya mke wake yalitangazwa katika redio, televisheni, magazeti na kwenye mtandao wa Internet! Marubani sehemu mbalimbali duniani walisoma matangazo hayo. Miongoni mwa marubani waliosoma tangazo hilo alikuwa Harry ambaye kwa wakati huo hakuwa na kazi baada ya shirika la ndege la USD Airlines kufilisika. Alifurahi kupita kiasi na siku ya usaili alikuwa  miongoni mwa wasailiwa waliofika katika ofisi ya tajiri Ian.

    Je nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.

    Nawapenda Mayatima wote  na ninawaeleza wazi kuwa hawana sababu ya kujisikia wanyonge kwa sababu  ya hali zao! MUNGU ANAYAJUA MAISHA YETU.











    M

    arubani wapatao 210 ?walifurika mbele ya ofisi ?za Dk. Ian Smith asubuhi ya siku hiyo kwa ajili ya kufanyiwa usaili, kati ya marubani hao wote alitakiwa   rubani mmoja tu  kwa ajili ya kuirusha ndege ya Caroline mke wa tajiri Dk. Ian, ilikuwa ni kazi ngumu kupita kiasi kuipata nafasi hiyo.

    Kila mtu  alibeba makabrasha vyeti mbalimbali  kuonyesha yeye ndiye alikuwa  rubani bora kuliko  wengine, Harry alisimama nyuma kabisa ya kundi hilo akiwa  mwenye mawazo mengi, hakuwa na uhakika wowote  wa kushinda katika kinyang’anyiro hicho, aliona hakuwa na sifa za kutosha kuipata nafasi hiyo.  

    “I worked with Kenya Airways for 5 years, later i joined British Airways where I also did another 10 years as a Pilot! Those days the wages wasn’t good so had to quit! What about you?”(Nilifanya kazi na Shirika la Ndege la Kenya kwa miaka 5, baadaye nilijiunga na Shirika la ndege la Uingereza ambako nilifanya kazi kwa miaka 10,  wakati huo malipo hayakuwa mazuri ilibidi niache kazi! Vipi wewe?)

    “I worked with Brazillian Airways for 4 years....... it wasn’t pay  and left it for American Airlines where I’m an Imployee up this moment, I love Canada my country,  need to come back and work here!”(Nilifanya kazi na shirika la ndege la Brazil kwa miaka 4, .......ilikuwa hailipi ikabidi niondoke na kujiunga na shirika la ndege la Marekani ambako nafanya kazi hadi leo hii, naipenda Canada nataka kurudi nyumbani nifanye kazi hapa!)

    Harry aliysikia maongezi yote  ya wazee wawili waliokuwa mbele yake  wakiwa wamebeba brifkesi zao mikononi, walionekana wana elimu ya kutosha kuhusu mambo ya urubani! Hata kama ni yeye angekuwa anatafuta marubani ni lazima angewapa wazee hao,  kamwe asingempa kazi mtu mwenye elimu na uzoefu kidogo kama aliokuwa nao yeye! Harry alikata tamaa, wazo la kutaka kuondoka lilimwijia kichwani  lakini alipingana nalo na kuamua kujaribu.

    “I’m gonna try it! It doesn’t matter I loose or gain, at least  I gave  it a trial!”(Nitajaribu haijalishi nitapata au sipati ili mradi nimejaribu!) aliwaza Harry, alitaka sana kupata  kazi hiyo ili ajikwamue tena kimaisha, alikuwa amechoka kukaa    bila kazi nchini Marekani! Aina ya ndege aliyotakiwa kuaendesha pia ilimvutia, katika maisha yake alitamani sana kuendesha ndege ya aina hiyo, ilikuwa ni aina mpya kabisa ya ndege.

    “Sijui huyo mkewe yupo vipi mpaka kanunuliwa ndege ya kisasa namna hii? Lazima atakuwa bonge ya kifaa kinachomchanganya akili tajiri Ian!” Aliwaza Harry!

    “Hivi huyo mke wa Ian ni mtu wa hapa Canada?” Harry aliwasikia  wazee waliokuwa mbele yake wakiendelea na maongezi yao, alisogea   kimya kimya hadi karibu yao ili asikie jibu la swali hilo, alitamani sana kumfahamu mwanamke huyo!

    “Hapana nasikia  ni Mwafrika!”

    “Alitokea nchi gani?”

    “ Sina uhakika alitokea nchi gani, ila niliwasikia watu wakisema ni mtu wa Afrika Magharibi lakini kuna wengine wanadai ametoka Tanzania  huko Afrika ya Mashariki, kwa kweli sina jibu zuri la nchi anayotoka!”

    “Ni mwanamke mwenye bahati sana, anaitwa nani?” Harry aliyaingilia kati mazungumzo yao na  wazee hao waligeuka nyuma kuangalia ni nani alikuwa akiwasemesha, walionekana kutofahamu kama kulikuwa na mtu kasimama nyuma yao akiwasikiliza.

    “Kwa kweli jina lake silifahamu!”

    “Huwa anaonekana lakini?”

    “Siyo rahisi  kumwona mimi nimezaliwa hapahapa Ottawa na ninaishi katika jiji hilihili lakini hata siku moja sijawahi kumtia machoni, analindwa  kupita kiasi!”

    “Aisee!” Harry aliitika kwa mshangao.

    Baadaye usaili ulianza marubani walianza kuingia mmoja baada ya mwingine katika chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo, marubani waandamizi wa mashirika matatu  makubwa ya ndege duniani, British Airways, Lufhthansa, United Airlines walikuwa ndani ya chumba hicho kuongea na rubani mmoja baada ya mwingine wakitafuta rubani mmoja tu kati ya marubani wote waliojitokeza, ilikuwa ni kazi ngumu na maswali yalikuwa magumu, Harry alisimama nyuma kabisa akitetemeka  na moyo wake ulidunda kwa nguvu, hakujiamini hata kidogo alihofia kila mtu aliyekuwepo mahali pale.

    “Harry Robertson!”msichana mmoja aliyesimama mlangoni aliita na Harry alitembea kwa haraka kuelekea mlangoni ambako aliingia hadi ndani! Macho yake yalipambana na nyuso za wazee wawili waliovaa mavazi ya Kirubani.

    “Naitwa rubani Rose  B. Kipya!  Ninatokea British Airways na huyu hapa ni rubani Reuben Kip kutoka Lufhthansa na aliyekaa kwenye kona ni rubani Martin Jackson kutoka United Airlines,  kabla hatujakufanyia usaili, sijui mwenzetu unaitwa nani?”

    “Ninaitwa rubani Harry Robertson!”

    “Ndiyo Harry, elimu yako katika masuala ya urubani ni ipi?”

    Harry alianza kuielezea elimu juu ya masuala ya urubani kisha akakabidhi vyeti vyake vyote, rubani Rose akavipokea  na kuanza kuvikagua, alisoma  huku akitingisha kichwa, kisha akanyanyua uso wake kumwangalia, alionekana kutokuwa na neno la kuongezea! Akavichukua vyeti vyake na kuwakabidhi marubani wenzake, nao wakaanza kuvitupia macho! Wote walipomaliza kuviangalia walinyanyua nyuso zao na kuonekana kukubali  kitu fulani ndani ya nafsi zao! Tabasamu zilionekana katika nyuso zao ziliashiria ushindi kwa Harry!

    “Jamani kuna mtu ana suala la nyongeza?” Rubani Rose aliyeonekana kuwa kiongozi wa usaili huo aliuliza.

    “Mimi ninalo!” Alijibu rubani Martin.

    “Haya uliza?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kitu gani cha kwanza unachoweza kufanya kama ndege imeleta hitilafu angani na kuanza kushuka kwa kasi kuelekea baharini au ziwani?”

    “Ni kuachia hewa ya oksijeni  itoke ya kutosha na kuhakikisha  abiria wote wamefunika pua zao mipira ya hewa hiyo midomoni na puani, kuhakikisha ndege haichomi ncha ya kichwa chake  kwenye  maji bali kutua taratibu juu ya maji!”Alimaliza Harry.

    “Sina swali zaidi , unaweza kuondoka!” Alisema rubani Martin huku akicheka.

    Hadi jioni ya saa kumi na mbili siku hiyo bado usaili ulikuwa ukiendelea, mtu wa mwisho kufanyiwa aliingia ofisini saa 1:30 usiku! Marubani walikuwa bado wapo nje ya ofisi wakisubiri matokeo yao, wasaili walikuwa wamechoka sana kiasi cha kushindwa kutoa majibu siku hiyo, waliomba wasailiwa wote wafike ofisini hapo saa nne siku iliyofuata kupata majibu yao, masaa yaliyokuwa mbele yao yalikuwa ni kama miaka kumi zaidi ya kusubiri, hawakuwa wavumilivu kiasi hicho kila mtu alitamani kufahamu ukweli siku hiyo hiyo.

    “Hatuwezi kutoa majibu leo!”Alisema rubani Rose B.Kipya kwa hasira, alionekana amechoka kuliko wengine wote, isitoshe alionekana ni mama asiye na huruma hata kidogo alikuwa na moyo wa kishupavu kama mwanaume akiamua kitu ameamua.

                 ******************

    “Vipi usaili umemalizikaje?Umepata rubani?”

    “Ndiyo nimepokea ripoti kama dakika ishirini zilizopita, inavyoonekana ilikuwa kazi ngumu sana!”

    “Lakini mmempata rubani?”

    “Hapana majibu yatatoka kesho!”

    “Jamani tafadhali msiniletee rubani kijana sana, nataka rubani mzee au makamo kidogo!”

    “Darling lakini hiyo inategemea sana na elimu ya mtu!”?“Iko wapi hiyo ripoti? Naomba niione kidogo, majina yao  yanaweza kunionyesha nani atanifaa!”

    “Hii hapa!” Dk. Ian alimkabidhi Caroline makaratasi yote ya majina  na akaanza kupitia jina moja baada ya jingine, akiwa kimya kabisa! Mbele kidogo alishtuka na kusimama wima mikono ikiwa kichwani, Dk. Ian hakuwepo  wakati huo alikuwa chooni akijisaidia! Caroline aliona jina kama la mtu aliyemfahamu, hakuwa na uhakika kama kweli mtu huyo alikuwa  yeye, Harry Robertson!

    Lilikuwa jina la mwanaume wake wa kwanza, aliyemkataa sababu ya kifafa! Aliweka chini karatasi la majina na kuanza kuchambua nakala za vyeti na  maelezo yao mengine ili kuangalia kama jina hilo lilikuwa la mtu aliyemfahamu na aliweka wapelelezi binafsi wamtafute duniani kote, mwanaume aliyehisi alimpenda kuliko mwanaume mwingine yeyote duniani! Ilichukua kama dakika tatu zaidi kuviona vyeti vya Harry na tayari Dk. Ian alisharejea kutoka chooni.

    “Vipi tena unatafuta kitu gani humo darling?”

    “Kuna mtu jina lake limenivutia nataka kuangalia vyeti vyake!”

    “Nani?”

    “Harry Robertson!”

    “Nilijua tu huyo utamfurahia sababu ni mwafrika mwenzako!”

    “Ni mwafrika?”

    “Ndiyo lakini ni kijana mdogo sana kitu ambacho  wewe hupendi!”

    “Nimevutiwa nae sana nipo tayari kumchukua, kifupi kesho wasaili wakija waeleze  ninayemtaka  ni huyo Harry peke yake, wengine waondoke zao!”

    “Sawa darling!” Aliitikia Dk. Ian, pamoja na ukatili wake wote kwa Caroline hakuwa na neno, alimpenda kupita kiasi na alikuwa tayari kumfanyia lolote alilotaka. Siku  iliyofuata matokeo yalipotoka jina la Harry Robertson ndilo lilitangazwa kuwa  mshindi,.Harry aliruka juu na kushangilia, aliona hiyo kama bahati ya ajabu, hakujua ilikuwa ni mipango ya Caroline.

    Hakuamini jibu hilo, ilikuwa ni furaha kubwa mno kwake kupata kazi tena! Aliamini ndoto yake ya kuendesha ndege kubwa ilikuwa imetimia! Alishindwa kuelewa ni kitu gani hasa kilichofanya ashinde, hakutaka kukubali kuwa yeye ndiye alikuwa  rubani bora kuliko wengine wote.

    Wakati akifurahia hivyo aliitwa ofisini ambako kwa mara ya kwanza alikutana na  tajiri Dr. Ian Smith na kusalimiana nae, alisaini mkataba wa kazi kwa miaka mitatu na kuruhusiwa kuondoka kurejea  nchini Marekani, akitakiwa   kuwa kazini wiki moja baadae. Aliahidiwa nyumba nzuri, gari zuri la kutembelea siku zote ambazo angekuwa safarini!  Kwa  mambo hayo   kila kitu alichohitaji katika maisha yake angekipata, kitu kimoja tu hakikutajwa katika mkataba wake nacho ni msichana mzuri! Hicho ndicho alichohitaji zaidi baada ya kuanza kazi.

    Harry alikuwa kijana hodari wa ngono, alipenda vimwana kuliko kitu kingine chochote, alibadili wasichana kama nguo, kila msichana mzuri duniani alitaka awe wake, alipenda  kutembea na wasichana wenye  majina  kuliko. Sura yake ya kuvutia ilimfanya awapate wasichana  kirahisi, wasichana wengi walivutiwa na muonekano wake na pia kazi aliyoifanya! Kwa mshahara na marupurupu aliyoahidiwa kwa kuendesha ndege ya mke wa Dr. Ian alikuwa na uhakika wa kuwachanganya wasichana  wote wa Canada kama kachumbari.

              ****************

    Caroline  alitamani sana kumwona mtu aliyekuwa na jina kama la mpenzi wake wa kwanza! Alipoambiwa kuwa  Harry aliondoka kurejea Marekani alisikitika sana! Alipoulizia kama  kulikuwa na picha  alizoacha aliambia hakuna, alizidi kuumia. Wiki moja aliyopewa Harry kabla ya kuanza kazi aliiona kubwa mno!  Na alishindwa kuelewa ingeifikia vipi! Alitamani sana kumwona Rubani mwenye jina la Harry  alishindwa  kuwa na uhakika kama Harry huyo ndiye Harry aliyemtafuta!

    Siku za  kusubiri Harry arudi kuanza kazi zilikuwa za mateso makubwa kwa Calorine, alibadilika na kuwa mtu mwenye mawazo na huzuni kila siku pamoja na zawadi ya ndege aliyonunuliwa, Dr. Ian aliigundua hali hiyo,  siku zote hakupenda  kumwona Caroline akisikitika, alitaka kumpa furaha maishani mwake, aliamini mateso na huzuni  alizozipata maishani mwake zilitosha  na hakutaka aendelee kuishi katika mateso hayo?

    “Usihuzunike mke wangu,  kwanza nataka Rubani akirejea tu uende  kwenye nyumba yetu  huko Miami Beach ukapumzike kwa mwezi mmoja! Unahitaji muda fulani kukaa peke yako na  kustarehe, nitakufuata baada ya mwezi huo mmoja! Sawa?”

    “Sawa lakini Rubani yupo wapi?

    “Atakuja tu!”

    “Mbona anazidi kuchelewa?”

    “Lini tulimpa wiki moja!”

    “Wiki moja ilikuwa kubwa mno! Mngempa siku tatu tu!”

    “Vumilia tu mama!”

    ***************

    Caroline alipakia kabisa mizigo yake ndani ya ndege tayari kwa safari. Siku ambayo Rubani angewasili kutoka Marekani, kila kitu alichokihitaji akiwa Ufukweni  Miami  kilikuwa ndani ya ndege   aliyekuwa  akisubiriwa alikuwa ni Rubani Harry Robertson peke yake, Caroline alikuwa na hamu sana ya safari hiyo, na si safari tu bali alitaka sana kukutana  na mtu mwenye jina sawa na mwanaume aliyempenda  kuliko wote, mpaka wakati huo aliamini bila kifafa wangekuwa bado wako pamoja!

    “Ngriii! Ngriiii! Ngriii!” Ulikuwa mlio wa simu pembeni mwa kitanda alipojilaza Caroline akimuwaza Harry! Alinyanyuka  kinyonge na kuinyanyua simu.

    “Hallow nani?”

    “Dr. Ian!”

    “Ndiyo Darling!”

    “Taarifa nzuri!”

    “Taarifa gani?”

    “Rubani kaja!”

    “Hakyanani?” Aliuliza kwa mshangao Caroline na alinyanyuka kitandani na kuanza kurukaruka kwa furaha!

    “Ndiyo na tayari nimeshamtaarifu juu ya safari yenu dakika chache zijazo atakuwa ndani ya ndege akikusubiri!”

    “Kweli?”

    “Ndiyo!”

    “Usichelewe kumtaarifu!” Alijibu Caroline tayari sura yake ilisharejewa na furaha iliyopotea! Aliona dakika zikienda taratibu sana, alitaka sana kumuona Harry!

    Nusu saa baadae mlango wa chumba ulifunguliwa akaingia Dr. Ian na kumwamsha Caroline kitandani akamwomba ajiandae kwa safari ya kwenda Miami kwani Rubani  alikuwa akimsubiri ndani ya ndege, Caroline alinyanyuka kwa furaha na wote wawili walitembea hadi  uwanjani ambako ngazi zilishushwa, Caroline na Dr. Ian wakakumbatiana na kupigana mabusu ya kwaheri.

    “I will miss you!” (Nitakukumbuka sana) Dr. Ian alimwambia mkewe.

    “Me too!” (Hata mimi pia!) Alisema Caroline.

    Baadae waliachiana na akaanza kupanda ngazi kuingia katika ndege, ilikuwa ndege kubwa kuliko zote alizowahi kupanda, aliamini kweli mume wake alimpenda na alishangaa ni kwanini mawazo yake yalikuwa bado yapo kwa Harry!

    Aliingia ndani ya ndege na kukaa, mtumishi ndani ya ndege alimfuata na  kumfungia mkanda wake vizuri,   dakika chache baadae ndege iliacha ardhi na kupaa angani! Hali ilipotulia  Caroline alishindwa kuvumilia na kujikuta akiufungua mkanda wake na kuamua kwenda kwenye chumba cha Rubani, mpaka wakati huo wote walikuwa bado hawajaonana uso kwa uso! Alipoufungua mlango tu Harry aligeuka nyuma, macho yao yakagongana.

    “Haaaaa! Harry ni wewe!”

    “Jamani Caroline kumbe wewe ndiye mke wa Dr. Ian?”

    “Ndiyo ni mimi lakini bado nakupenda Harry kwa muda mrefu sana nimekutafuta bila mafanikio!” Alisema Caroline na kuinama akimbusu Harry mdomoni.

    Machozi yalikuwa yakimtoka kwa furaha aliyokuwa nayo ghafla ndege ikaanza kwenda mrama! Ikiyumba kutoka  upande  mmoja hadi mwingine.

    Je, nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.













    “No! No! No, Caroline no! Acha tafadhali! Utasababisha ajali mbaya  na sote tutakufa, acha Caroline acha!” Aliendelea kupiga kelele Harry akimsukuma Caroline aliyekuwa amemwangukia miguuni na kumkumbatia akimpiga mabusu  yasiyo na idadi usoni na shingoni, kwa furaha aliyokuwa amepata Caroline alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa, hakuelewa   kitu alichokuwa akikifanya kilikuwa cha hatari kupita kiasi.

    “Tafadhali niachie Caroline ndege itaanguka!”Harry alizidi kupiga kelele lakini Caroline hakujali aliendelea kumkumbatia kwa furaha bila kujua alikuwa akipoteza mwelekeo wa ndege na kuifanya izidi kuyumba zaidi.

    Ghafla mbele yake  Harry aliona maji mengi! Ilikuwa ni habari, ndege ilikuwa ikielekea majini alijua  bila kufanya jambo  kwa haraka ndege  ingetumbukia majini na huo ndio ungekuwa mwisho wao!  Akili yake ilifanya kazi kwa haraka, nguvu nyingi zikamwijia mwilini mwake akafanikiwa kumsukuma na kumwangusha Caroline pembeni, akaanza kuhangaika  ili kuidhibiti ndege iliyokuwa kwa mita chache  kuyafikia maji.

    Kwa utaalam aliokuwa nao  alifanikiwa  kuikatisha kona na baadaye kuiwezesha kuelekea  tena  angani! Hata yeye hakuamini kilichotokea, alipoona hivyo Caroline aligundua alikuwa amesababisha hatari na hofu ikaanza kumwingia moyoni mwake, kila mtu kati yao alibana pumzi akiomba muujiza utokee,  ndege ilipofika juu  Harry alifanikiwa kuituliza na kuendelea na safari yao.

    “Flight no 13 where are you?”(Ndege namba 13 upo?)

    “ I’m back on the communication track, we were facing some technical problems,   right now were ok!”(Nimerudi katika mawasiliano, nilipotea kidogo sababu ya matatizo ya kiufundi lakini hivi sasa tuko salama)

    “Oh! My God we lost the touch with your plane!”(Oh! Mungu wangu tulipoteza kabisa mawasiliano na ndege yako!)

    Yalikuwa ni maongezi kati ya Harry na watu waliokuwa ndani ya chumba cha mawasiliano cha ufuatiliaji wa safari za ndege za tajiri Ian Smith, kwa muda kidogo walipoteza mawasiliano  kati yao na ndege iliyombeba Caroline kwenda Miami.

    Harry alishusha pumzi huku akitabasamu, hakuamini kama alikuwa amefanikiwa kuidhibiti tena ndege hiyo walipambanisha macho yao na wote wakatabasamu, ndani ya mioyo yao kulijaa furaha isiyoelezeka.

    “You wanted us to die after we have just met?”(Ulitaka tufe mara baada ya kukutana?)

    “No!  You know  how much I love you,  cant kill you”(Hapana! unajua  nakupenda kiasi gani, Harry siwezi kukuua)

    “Then why did you disturb the move?”

    “Sorry Harry,  just got outta  my cells, it was a surprise! I didnt know you were the pilot”(Samahani harry, nilipagawa nilipokuona, kilikuwa ni kitu cha kushtua sana, sikutegemea wewe ndiye rubani niliyetafutiwa!)

    “Lets not talk a lot here, do it once were in Miami! all I  can t tell you is I love you Caroline and did regret for what I did, please for give me!”(Tusiongee mengi hapa tutaongea  tukitua Miami, ila ninachoweza kukueleza ni kuwa nakupenda sana Caroline, nilijuta sana kwa niliyokufanyia tafadhali nisamehe!”

    “Let the gone go! This is a new chapter of love and harmony!” (Yaache yaliyopota hiki ni kipindi cha mapenzi na amani!) Alijibu Caroline huku akicheka, ilikuwa si rahisi kuieleza furaha aliyokuwa nayo moyoni mwake, ilikuwa ni kama ndoto kukutana na Harry tena! Hakumuwazia kabisa Dk. Ian kichwani mwake.

                  ************

    Ndege yao ilitua katika kiwanja cha ndege cha nyumbani kwao huko Miami, saa 12:30 jioni,  tajiri Ian alimiliki eneo la hekari 120  katika ufukwe huo aghali duniani! Ni watu matajiri tu waliokuwa na maeneo katika ufukwe huo, tena maeneo yenyewe yalikuwa madogo mno,mtu mwenye eneo kubwa alikuwa tajiri Ian Smith peke yake.

     Nyumba yao ilikuwa umbali wa meta 2000 kutoka mahali ndege yao ilipotua. Walikuta idadi ya watu wapatao ishirini wakiwasuburi eneo hilo,  waliposhuka   ndani ya ndege  msichana mwenye mwamvuli alimfuata Caroline na kumfunika kwa juu ili asiungue na jua  na  alimwomba amfuate  kumpeleka kwenye  gari lililokuwa  maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kumpokea.

    “Wait! Why are you so much hurried?”(Subiri kwanini una haraka kiasi hicho?) Caroline alimwambia msichana aliyekuwa amemfunika mwamvuli tena kwa sauti ya ukali.

    “I’m sorry madame!”(Nisamehe mama!)

    “Haaaaaarry!” Caroline  aliita baada ya kumkemea msichana huyo.

    “Yes mom!”Ndiyo mama)   Harry aliitika kwa heshima zote, hakutaka mtu yeyote agundue kilichoendelea kati yake na Caroline jambo ambalo kwa hakika alijua lingeweza kuhatarisha  usalama wa maisha   pamoja na kazi yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Please come with me!”(Tafadhali nifuate!) Caroline alimwamrisha na Harry alikwenda mbio hadi mahali alipokuwa.

    “Hebu nifuate na tangu sasa  unapoongea na mimi kitu chochote unisemeshe kiswahili ili hawa watu  wasielewe  sawa mpenzi?”

    “Sawa kipusa changu!” Alijibu Harry na wote walicheka na kuongoza hadi kwenye gari ambako mlango wa gari ulifunguliwa na msichana aliyewekwa tayari kwa kazi hiyo, Caroline akaingia ndani akifuatwa nyuma na Harry! Dereva aliyekuwa ndani ya gari aliwaamkia kwa heshima zote na gari likaanza kuondoka.

    “Douglas!”Caroline alimwita dereva   aliyekuwa akiwaendesha.

    “Yes mom!”(ndiyo mama!)

    “Meet Harry the new pilot in our company, he is gonna be flying my new jet!…..Harry this is Douglas Sagawalla a senior drive in our company!”( Douglas kutana na  Harry, rubani mpya katika  kampuni yetu, yeye atakuwa anairusha ndege yangu .....Harry huyu ni dereva wetu wa siku nyingi anaitwa Douglas Sagawalla!)

    Harry na Douglas walishikana mikono na kukaribishana huku gari ikiendeshwa taratibu kutoka uwanja wa ndege  kuelekea  kwenye nyumba yao iliyokuwa nyuma ya kilima kilichopambwa na majani mengi ya kijani.

    Walipoifikia nyumba gari liliegeshwa  na wote wakashuka, Harry alikuwa amepigwa na mshangao mkubwa kwani katika maisha yake yote pamoja na kutembea nchini nyingi  duniani Harry hakuwahi kuona nyumba ya kifahari kama iliyokuwa mbele yake, ilijengwa kwa mawe ya marumaru za kung’aa na iliezekwa vioo! Alipoingia ndani ya nyumba hiyo ndiyo alizidi kushangaa zaidi,  kila kitu alichokiona ndani ya nyumba hiyo kilikuwa kigeni maishani kwake.

    “Caroline,  mumeo ni tajiri sana eh!”

    “Kwanini?”

    “Nyumba hii ni nzuri mno!”

    “Ahsante!”

    “Lakini utakubali  kuwa na mimi tena wakati umeshazoea kuishi maisha ya kifahari?”

    “Ninachotaka katika maisha yangu ni furaha hata kama nitalala chini, nakupenda Harry kuliko mwanaume mwingine duniani, nipo tayari   kuacha vyote hivi kama utataka iwe hivyo!” Yalikuwa maneno ya Caroline ambayo Harry  hakuyaamini hata kidogo ilikuwa si rahisi mwanamke kuacha mali na raha zote alizokuwa nazo kwa sababu ya mwanaume masikini kama yeye!

    Tayari ilishatimu saa 1:10,   ndani ya nyumba hiyo walipokelewa na watumishi wa ndani na wote wakaketi vitini, wasichana wawili walioonekana kama wahindi wekundu walijitokeza na kuwanza kumpepea Caroline kwa kutumia vikawa. Alikuwa ni kama Malkia ndani ya himaya ya mumewe, yote hayo yalimshangaza Harry.

    “Hebu mmoja wenu aende akampepee yule mgeni  wangu pale,  hapa mmoja tu ananitosha!” Aliamuru Caroline.

    Kauli hiyo ilimfanya mmoja wa wasichana hao kuondoka na kwenda kuanza kumpepea Harry mara moja,  Harry alizidi kushangazwa na  yote yaliyotokea ndani ya nyumba  hiyo,  ni  mara ya kwanza katika maisha yake alijisikia Mfalme, hakuwahi kufanyiwa mambo kama  hayo maishani  mwake, saa  nzima baadaye Caroline aliwafukuza wasichana  waliokuwa wakiwapepea  pamoja na wafanyakazi wengine wote ndani ya nyumba yake, wakabaki wao wawili tu!

    “You can just go to bed, I will be ok!”(Nendeni tu mkalale sitakuwa na tatizo lolote!) aliwaambia wafanyakazi wake.

    “Thank you madame! Will he sleep in the visitors lounge so that we can go and make the bed ready?”(Ahsante mama je mgeni atalala kwenye chumba cha wageni ili tukakitayarishe kitanda chake?)

    “Just go I will handle that!”(Nendeni tu hilo nitalishughulikia!)

    Baada ya wafanyakazi kuondoka Caroline bila woga wala kumfikiria mume wake Ian, aliyemnusuru katika matatizo aliyokuwa nayo ya kuachwa na wanaume sababu ya kifafa! Alinyanyuka kwenye kiti  alichokaa na kuhamia katika kiti alichokaa Harry, lilikuwa kochi la kukaliwa na watu wawili! Aliuzungusha mkono wake  wa kulia begani kwa Harry! Kumbukumbu zote za yaliyotokea  wakiwa katika shule ya sekondari ya Arusha zilimwijia kichwani mwake, Caroline alishindwa kuvumilia na kujikua akimwaga machozi mfululizo.

    “Ha! Mbona unalia tena?”

    “Nimekumbuka ulivyonifanyia shuleni Arusha, ulinidhalilisha sana Harry tena mbele ya wasichana wako eti  sababu nilikuwa na kifafa!”

    “Caroline…Caroline…..Caroline….. tafadhali sana nisamehe, nimekwisha kuomba msamaha, hebu kubali kunisamehe na usahau  yaliyopita!”

    “Sawa Harry lakini….!”

    “Nisamehe mpenzi!” Alisema tena Harry na kumkumbatia Caroline, tayari walikuwa wakibembea katika anga za mahaba. Dakika chache zilizofuata bila kujitambua walijikuta wapo kama walivyozaliwa na yaliyoendelea kati yao yalikuwa ya kuhatarisha maisha yao kama tajiri Ian Smith angeufahamu ukweli huo!

    “I missed you!”(nilikukumbuka sana!)

    “Me too, Caroline, cant you believe me?”(hata mimi pia Caroline hauwezi kuniamini?)

    “No body can make me feel   the way you do! My old man cant do it like this! Ohoooooo!” Caroline alizidi kulia  kimahaba akiwa katikati ya mikono ya Harry.

    Harry hakuyaamini macho wala akili yake kuwa mwanamke aliyekuwa amelala naye kitandani alikuwa Caroline! Mke wa  mtu tajiri kupita kiasi duniani, Ian Smith. Ni kweli alimfahamu Caroline tangu shuleni lakini aliyekuwa naye kitandani hakuwa Caroline aliyemzoea.

     Harry alijua jambo  alilofanya lilikuwa ni hatari na alihofia sana  lakini kwa upande mwingine  jambo hilo  lilikuwa njia ya  yeye kujipatia utajiri kwani wakati wowote  kwa kumtumia Caroline angeweza kuchota mamilioni ya pesa katika akaunti za tajiri Ian na kutajirika, alimshukuru Mungu kumkutanisha na Caroline tena.

    “Kila kitu hupangwa na Mungu! Unafikiri nisingekuacha ungempata vipi tajiri Ian, ilikuwa ni lazima nikuache ili ukutane na mtu mwingine!”

    “Ni kweli, lakini elewa bado nakupenda  sana Harry sidhani kama katika maisha yangu nitampenda mwanaume mwingine kama ninavyokupenda wewe!”

    “Najua! Hebu kwanza nieleze vizuri kuhusu kifafa chako!”

    “Sina tena kifafa!”

    “Kweli?”

    “Ndiyo!”

    “Ilikuwaje?”

    “Ian alinitibu!”

    “Kwani yeye daktari?”

    “Ndiyo!      Watu wengi sana wamepona!”

    Siku hiyo hawakulala mpaka asubuhi, Caroline akimsimulia Harry yaliyotokea katika maisha yake, aibu zote alizozipata kutonana na ugonjwa wa kifafa mpaka kufikia kitendo cha kuachwa kanisani siku ya harusi na tena mbele ya padri.

    “Pole sana!”

    “Hivyo ndivyo ilivyo lakini nimekwishasahau!”

    “Pamoja na hayo yote hivi sasa unaishi maisha mazuri au siyo?”

    “Ndiyo lakini mume wangu ni mzee sana ninahitaji kuwa na kijana kama wewe ndiyo maana nataka wewe uendelee kuwa rubani wangu siku zote ili uzibe mapengo  yaliyopo kwa Ian, ndiyo Ian ni tajiri  lakini mimi kama mwanamke ninahitaji zaidi ya mali na chakula!”

    “Usiwe na wasiwasi nitaziba mapengo yote ili mradi uniahidi kuficha siri!”

    “Umeoa Harry?”

    “Bado!”

    “Safi kabisa, Mungu alikutunza kwa ajili yangu!”

                 *************

    Mwezi mmoja ulikatika Harry na Caroline wakiishi ufukweni kama mke na mume, Caroline alifaidi maisha kupita kiasi! Ian alipopiga simu akitaka kuungana na mkewe kama walivyoahidiana Caroline alikataa.

    “No! Not now, I need to be alone for another month Ian!”(Hapana! Ninahitaji kuwa peke yangu kwa mwezi mwingine mmoja!)

    “Why?”(Kwanini?)

    “No reasons but I need to be alone!”(Hakuna sababu lakini nahitaji kuwa peke yangu!)

    “Ok! But take great care of yourself! How is Harry?”(Sawa! Lakini uwe mwangalifu sana! Harry anaendeleaje?)

    “Doing fine, he is a good boy! Good than any body else in your company!”(Hajambo, ni kijana mzuri nafikiri kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya kampuni!)

    “Sure?”(Kweli?)

    “Yeah!”(Ndiyo!)

    Wafanyakazi wote ufukweni walishangazwa na hali iliyoonekana kati ya Harry na Caroline, hawakuonekana kuwa kama  mtu na bosi wake, picha iliyoonekana kati yao ilikuwa ni  ya mtu na mpenzi wake walishangazwa na kitendo cha  watu hao wawili  kutembea wakiwa wameshikana viuno! Kuogelea pamoja na kulala  katika nyumba moja wakati nyumba ya wageni ilikuwepo pembeni.

    Kilichowafanya wawe na uhakika zaidi ni kitendo cha wafanyakazi wote kuondolewa ndani ya nyumba kila ilipotimia saa moja jioni jambo ambalo halikuwa kawaida kabisa ya kila wageni walipokuja kukaa katika nyumba hiyo kutoka Canada au kwingineko kokote duniani.

                   ************

    Thomson alikuwa mmoja wa wafanyakazi katika nyumba ya tajiri Ian Smith, kabla ya kubla ya kuhamishiwa  Miami aliishi nchini Canada akifanya kazi katika nyumba ya Dk. Ian. 

    Pamoja na kuwa mfanyakazi lakini alikuwa rafiki mkubwa na mpelelezi wa tajiri Ian, alishirikiana na Ian mara nyingi katika  mauaji, ni yeye aliyewatilia sumu katika chai wafanyabiashara wanne wa Kijapani walipokuja na mamilioni ya dola  ufukweni   iami kuongea biashara na Ian Smith! Wakafa na maiti zao kuzamishwa baharini, hakuna mtu aliyefahamu kilichotokea  na pesa zote walizokuwa nazo zilichukuliwa na Ian kwa sababu hiyo Ian alimwamini  Thomson kuliko mfanyakazi mwingine yeyote.

    Thomson alikuwa miongoni mwa watu walioshangazwa na tabia ya mke wa bosi wake pamoja na rubani na kuamua kufuatilia nyendo zao taratibu hakutaka kufanya haraka  asije kushtukiwa.

    Ilikuwa ni katikati ya usiku, Thomson alikuwa nyuma ya dirisha la chumba cha kulala cha nyumba ya tajiri Ian, alisikia sauti za watu wakiongea, alipotupa macho ndani kupitia katikati ya mapazia aliwaona Harry na Caroline wakiwa wamekumbatiana.

    “Caroline!”

    “Naam!”

    “Unanipenda kweli?”

    “Ndiyo nakupenda sana!”

    “Upo tayari kuacha vyote kwa ajili yangu?”

    “Ndiyo!”

    “Hakika?”

    “Ndiyo!”

    “Basi hakuna haja ya kurudi tena kwa Ian, tuondoke zetu kesho!”

    “Kwenda wapi?”

    “Nitakueleza  mbele ya safari tutakwenda wapi!”

    “Kweli?”

    “Ndiyo!”

    “Lakini Ian siyo mtu mzuri sana harry atatuua kama tumeamua hivyo ni lazima twende mahali ambako  kwa hakika hatatupata!”

    “Hawezi kutupata!”

    “Huko tutaishije?”

    “Tutaiuza ndege hii na tutapata mamilioni ya dola, tutabadili sura zetu na kuishi maisha ya  raha mustarehe na Ian atatutafuta maisha yake yote bila kutupata au wewe unaonaje?”

    “Sawa tu!”

    Thomson alizidi kuchungulia dirishani na kuyasikia maneno waliyokuwa wakiongea, hakuelewa chochote  sababu waliongea kwa  kiswahili! Lakini hilo halikuwa kikwazo kwake, aliyoyaona kwa macho yalitosha! Roho ilimuuma sana kuona mke wa bosi  na rafiki yake wake anachezewa kiasi hicho, alitamani aikamilishe kazi  ya kuwateketeza wote wawili  kwa moto ndani ya nyumba hiyo  lakini alishindwa kufanya hivyo kwa sababu ilikuwa ni lazima awasiliane na tajiri Ian na kumweleza juu ya alichokishuhudia.

    Alinyata na kwenda hadi nyumbani kwake ambako alinyanyua simu na kuanza kuzungusha namba za Canada nyumbani kwa mzee Ian!

    “Hallow Ian Hapa!”

    “Ndiyo shikamoo mzee!”

    “Unasemaje Thomson mbona simu usiku huu?”

    “Mzee kuna jambo ambalo kwa kweli ni lazima nikueleze  ingawa sitakiwi kabisa kufanya hivyo!”

    “Jambo gani hilo?”

    “Siyo siri mama analala chumba kimoja na rubani wake, nimewaona kwa macho yangu sasa hivi wapo chumbani wakifanya mapenzi!”

    “Una  uhakika?”

    “Asilimia mia moja!”Alijibu Thomson na simu ikakatwa, hiyo ilitosha kuonyesha ni hasira kali kiasi gani  aliyokuwa nayo Ian kwa wakati huo! Thomson alimfahamu vizuri sana Ian, alipofanya hivyo ilimaanisha vifo vya watu.

                     **********

    Mwili wa Ian ulikuwa umevimba alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Miami asubuhi hiyo, kila mtu alishangaa ni kwa nini safari hiyo ilikuwa ya dharura kiasi hicho kawaida yake kabla ya safari alitoa taarifa siku mbili kabla ya safari yake.

    “They have to die! A very bad death!(Ni lazima wafe kifo kibaya sana!)

    Je nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo utamu ndio sasa umeanza.















    Ilikuwa ni hali ya mawingu ?na ukungu katika anga  ?yote ya Miami asubuhi hiyo katika kipindi hicho cha mwaka, baridi ilitanda kila mahali,ndege ya Caroline ilikuwa ikikatiza katikati ya  mawingu kuelekea mahali ambako Caroline   hakupafahamu! Ni Harry peke yake ndiye aliyeelewa mahali walikokuwa wakielekea.

    Pamoja na hali hiyo bado Caroline hakuonyesha wasiwasi wowote, alimwamini Harry kupita kiasi, asubuhi ya siku hiyo   alikuwa ameamua kumwacha kabisa mzee Ian, mtu aliyemponya kifafa na kumtoa katika umasikini akamfanya   kuwa Malkia! Maisha ambayo Caroline hakuwahi kuyafikiria yangetokea katika uhai wake.

    Ni mzee Ian ndiye alifuta machozi na huzuni katika maisha ya Caroline, lakini alikuwa akimwacha  kwa sababu ya Harry! Kijana mwenye sura nzuri ya kuvutia,  mpenzi wa  kwanza katika Maisha yake, aliyemwonyesha nini ilikuwa maana ya kupendwa  na umuhimu wa mapenzi katika maisha ya mwanadamu!

     Lakini ni Harry huyo huyo ndiye aliyemwacha Caroline sababu ya kifafa miaka mingi   wakisoma katika  shule ya sekondari huko Arusha nchini Tanzania!  Caroline hakuwahi kuumia kama kipindi hicho katika maisha yake ilikuwa kidogo tu achanganyikiwe.

    Shule ilimshinda ikabidi ahamishiwe Dar es Salaam, wazazi waliamua kumuondoa Arusha ili kumuepusha na huzuni pamoja na aibu aliyoipata baada ya kuachwa na Harry! Lakini yote hayo Caroline hakuyajali na hakutaka kuyakumbuka, alimpenda Harry aliamini  bila yeye yasingekuwa kamili.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Caroline alimpenda Harry kupindukia na alifanya  yote aliyokuwa akitenda kuufurahisha moyo wake, hakutaka kufikiria mara mbili wala kuuona ubaya na hatari ya jambo alilokuwa akilifanya, alitaka kuwa na furaha katika maisha yake hata kama furaha hiyo ingedumu kwa wiki mbili tu! Ni Harry  peke yake   aliyekuwa hiyo furaha  aliyoitafuta na si kitu kingine chochote. Pamoja na kuolewa na mwanaume mwenye mali na tajiri   bado  maisha yake hayakuwa na furaha.

    “Harry I missed my period!”(Harry sikupata siku zangu za mwezi huu)

    “Sure?”(Hakika?)

    “Yeah!”(Ndiyo!)

    “You’re kidding Caroline!”(Unatania Caroline)

    “Nope!”(Hapana!)

    “Then that’s  good news,  eventually we’re gonna have our first baby  girl(Basi hiyo ni habari njema hatimaye tunapata mtoto wetu wa kwanza wa kike!)

    “You like baby girls isn’t?”(Unapenda watoto wa kike au siyo?)

    “Most men do like baby girl!”(Wanaume wengi hupenda watoto wa kike!)

    “Me too!”(Mimi pia!)

    “Caroline are you sure  you  pregnant? Don’t make me euphoric for nothing!”(Lakini una uhakika  una mimba? Usinifanye nifurahi kupita kiasi kumbe hakuna kitu!)

    “Ok! Lets give it one week more!”(Basi acha tuipe tena wiki nyingine moja zaidi tuangalie!)

    Ndege ilizidi kukatisha katikati ya mawingu, Caroline akiwa amekaa kando ya Harry aliyekuwa akiendesha ndege hiyo kwa kasi ya ajabu lakini kwa uangalifu! Hakuonekana kuwa  mtu mwenye  hofu moyoni mwake hata kidogo, lakini ndani ya akili ya Caroline kulijaa mahangaiko kisawasawa, alimfahamu vizuri Dk. Ian na alijua kabisa jambo walilokuwa wakilifanya lilikuwa ni la hatari kubwa! Alijua ni kiasi gani Dk Ian alimpenda na pia kiasi gani angekasirika baada ya kuambiwa kuwa mke wake alitoroka na mtu mwingine, mbaya zaidi alitoroka na ndege ya kifahari ya pesa nyingi aliyomnunulia siku chache kabla  kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.

    Caroline alijua mbele yake kulikuwa na kifo! Alijua  ni kiasi gani kitendo cha kuua kilikuwa kidogo  kwa Dk. Ian! Alipomwangalia Harry alimhurumia ingawa yeye hakuonekana kujali kitu chochote,  Caroline aliamini kitendo walichokuwa wakifanya kilimaanisha kufungua milango ya kaburi ili wadumbukie ndani!

    “Harry where are we flying to!”(Harry  hivi tunaelekea wapi!)

    “I will let you know!”(Nitakujulisha baadaye!)

    “I need to know!”(nahitaji kufahamu!)

    “Don’t worry darling we are going to hide somewhere in a very wonderful place! Where Dk. Ian will never see us again!”(Usiwe na wasiwasi mpenzi, tunakwenda kujificha mahali pazuri ambapo  Dk. Ian hatatuona tena!)

    “You sure of what you talking ‘bout’?” (Una uhakika na kitu unachokiongelea?)

    “Positively sure!” (Uhakika wa nguvu!)

    “Mind you, Dr Ian is a dangerous person Harry, I know   he doesn’t joke, he is so mean! Once he says kill, he means it! And I know thats what he is going to say”(lakini kumbuka Dk. Ian ni mtu hatari sana Harry! Namfahamu vizuri, ni mtu ambaye humaanisha ayasemayo, akisema ua hatanii na ninajua hicho ndicho atasema baada ya kusikia nimetoroka na wewe!) Alisema Caroline.

    “Don’t worry Caro, he wont see us even if he uses a Microscope!”(Usijali Caroline, hatatuona hata kama atatumia darubini!) Alijibu Harry huku akicheka na baadaye walipigana mabusu kwa midomo yao laini na safari ikaendelea.

    Kwa masaa karibu matano yaliyofuata ndege ilizidi kukatisha mawingu kuelekea mahali ambako Caroline hakupafahamu,  alikuwa usingizini na katika usingizi huo alimwota Dk. Ian! Alikuwa amefungwa kamba akimwagiwa mafuta ya petroli mwili mzima ili achomwe moto, Dk. Ian alisimama mbele yake akifurahia kitendo hicho, baada ya kulowanishwa vizuri  na petroli Dk. Ian alikabidhiwa kiberiti,  akachomoa  njiti moja  na kuiwasha kisha akamtupia  Caroline mwilini mwake, akashika moto na kuanza kuungua, alipiga kelele akiomba msaada lakini hapakuwa na  mtu wa kumsaidia!

     Ghafla Caroline alizinduka usingizini   akipiga kelele, macho yalikuwa yamemtoka na mwili wake wote ulikuwa ukitoka jasho jingi!

    “Vipi Caroline?” Harry aliuliza baada ya kumwona Caroline akishtuka na kuketi.

    “Ndoto tu!”

    “Ndoto? Ndoto gani  ya kukushtua namna hiyo?Umeota unadumbukia shimoni nini? Maana hizo ndizo huwa ndoto za kutisha zaidi!”

    “Afadhali ingekuwa hiyo ya kudumbukia shimoni!”

    “Kwani umeota ndoto gani?”

    “Nimemwota Dk. Ian!”

    “Anafanya nini?”

    “Amewaamuru watu wake wanimwangie mafuta ya petroli halafu yeye akanilipua na kiberiti!”

    “Ah wapi!” Harry alisema huku akicheka.... “hilo ni jambo lisilowezekana kabisa, hiyo ni ndoto tu! Atakupata wapi Dk. Ian!”

    “Unasema tu Harry! Si ajabu ipo siku atanipata kweli, na si ajabu wewe hautakuwepo siku hiyo!”

    “Kwanini unasema hivyo Caroline?” Aliuliza Harry akionyesha huzuni kubwa.

    “Sababu sikukuona katika ndoto yangu!”

    “Nope!(Haiwezekani)

    Nusu saa baadaye Caroline alipotupa macho yake nje kupitia dirishani aliuona msitu mkubwa kupita kiasi, hiyo ilimwonyesha kuwa  walikuwa wakijiandaa kutua, mbele kidogo waliona uwazi mkubwa usio na miti, kilikuwa ni kama kiwanja cha ndege  kilichokuwa katikati ya pori, hakupaelewa mahali pale palikuwa ni wapi! Ndege ilizidi kushuka chini kuelekea ardhini, Harry akiwa kimya kabisa akili yake ilikuwa imeishia kwenye mtambo wa kuendeshea ndege.

    “Harry unatua porini?”

    “Tunatua kwa muda tu ili tupumzike kisha tutaendelea  na safari yetu!”

    “Una uhakika na uwanja huu?”

    “Unaonekana hauna matatizo si ajabu uliwahi kutumika siku za nyuma!”

    “Harry lakini inaweza kuwa hatari kwanini tusiendelee mbele mpaka kwenye mji wowote mkubwa ndio utue?”

    “Naogopa kutua katika viwanja vikubwa  huko nina hakika Dk. Ian atatukamata!” Alijibu Harry akizidi kuipeleka ndege  taratibu ardhini ambako alifanikiwa kutua bila matatizo! Kilikuwa ni kiwanja cha ndege kamili lakini alishindwa kuelewa ni watu gani waliokitumia.

    Baada ya kutua ardhini alifungua mlango na kuruka  hadi ardhini Caroline akimfuata kwa nyuma, walikuwa   katikati  kabisa ya pori! Hapakuwa na dalili ya watu kuishi mahali pale, palitisha kupita kiasi.

    “Harry hapa mahali sio pazuri! Ni bora tuondoke!”

    “Kwanini?”

    “Mwili wangu unachezwa na machale! Tutapata matatizo makubwa hapa!”

    “Wewe  ni muoga  sana Caroline, niamini mimi! Unapokuwa na mimi tafadhali punguza wasiwasi!”

    “Sawa lakini.....!” Kabla hajamaliza sentensi yake  alishtukia Harry akipiga kelele, mshale wenye ncha kali ulikuwa umepenya kwenye bega lake la kushoto.

    Harry alianguka chini  akipiga kelele, damu nyingi zilikuwa zikimtoka  kwenye mkono wake, Caroline alilala chini karibu kabisa na Harry, alipoinama tu mshale ulipita mahali alipokuwa amesimama na kusimama wima kwenye bodi la ndege yao! Hiyo ina maana asingelala mshale ungezama mwilini mwake. Hofu kubwa ilimwingia Caroline moyoni, hakuamini kama mishale ile ilitoka kwa wafuasi wa Dk. Ian! Ilikuwa si rahisi afahamu walikuwa mahali pale, Harry alizidi kulia akiomba msaada.

    “Unaona sasa Harry! Nilikuambia hapa sio mahali pazuri palinitisha mimi!”

    “Nisaidie Caroline!”

    “Nifanye nini sasa?”

    “Ungoe huu mshale!”

     “Acha nijaribu lakini sina uhakika kama nitaweza!” Alijibu Caroline na kujaribu kuuvuta mshale huo  huku Harry akilia kwa maumivu lakini ilishindikana kuutoa. Damu nyingi ziliendelea kumbubujika.

    “Nifanye nini sasa?”

    “Basi te...na nas...ikia mw...ili unai...shiwa ngu...vu! Nina wasiwasi mshale huu una sumu!” Alijibu Harry kwa sauti ya chini huku akikakatakata maneno na baadaye alikaa kimya.

    “Harry! Harry! Harry!” Caroline aliita lakini Harry aliendelea kuwa kimya.

    Ghafla kundi kubwa la watu waliovaa nusu uchi wakiwa wamefunikwa na kitambaa kidogo  mbele kuficha sehemu zao za siri walijitokeza wakiwa wamevuta pinde zao tayari kuachia mishale, walitembea hatua za taratibu wakiisogelea ndege na waliimba wimbo ambao Caroline alishindwa kuuelewa ulikuwa katika lugha gani!     Watu hao walivaa kofia kubwa za mikeka vichwani mwao kiasi kwamba haikuwa  rahisi kuziona nyuso zao  lakini kwa kuwaangalia ngozi za miili yao  Caroline aliweza kuwafanananisha na wazungu au wahindi wekundu!

    Akili ya Caroline ilimrudisha moja kwa moja katika filamu  ya The Vietnam war, aliyowahi kuiangalia miaka mingi kabla, alihisi watu wale walikuwa Wavietnam! Alishtuka na kuogopa zaidi alipokumbuka jinsi walivyowaua maaskari wa Kimarekani katika filamu hiyo.

    Watu wasiopungua mia tano waliizunguka ndege  ya akina Caroline na  wengine ishirini kati yao walisogea mbele kuwafuata Caroline na Harry mahali walipolala,walivuta pinde zao kama watu waliokuwa wakisubiri amri ili waachie mishale iliyokuwa katika pinde hizo!Kwa haraka haraka  alipohesabu Caroline alikadiria mishale isiyopungua kumi na moja ingeingia mwilini mwake, alilia kwa uchungu na alipomwangalia Harry aligundua alikuwa hajitambui tena.

    “Hogree magrii tanui!” Caroline alisikia sauti hiyo kutoka kwa mtu mwenye ndevu nyingi aliyesimama nyuma ya watu hao ishirini, wakazidi kuzivuta pinde zao! Akajua mwisho wa maisha yake umefika.

              ***************

    Dakika ishirini na tano baada ya ndege ya Caroline kuruka kutoka Miami, ndege ya Dk. Ian ilitua ufukweni na kupokelewa na  Thomson pamoja na wafanyakazi wengine! Dk. Ian alikuwa akilia machozi na rangi ya ngozi yake ilibadilika kwa sababu ya hasira, mmoja wa wafanyakazi alishangaa kumwona Dk. Ian akilia, tangu aanze kazi kisiwani hapo hakuwahi  hata siku moja kumwona Dk. Ian akilia, hakuwa kufikiri iko siku angeyaona machozi ya mtu tajiri kama huyo.Sababu ya mambo hayo alijikuta akitabasamu! Hakutegemea Dk. Ian angemwona lakini bahati mbaya alikishuhudia kitendo hicho.

    Kwa hasira aliyokuwa nayo alimgeukia kijana huyo na kuanza kumuuliza maswali ni kitu gani kilimfanya acheke katika kipindi hicho cha majonzi!

    “Why are you laughing you sonofabitch! Do you think I want to buy your teeth?”(unacheka nini wewe mtoto wamalaya! Unafikiri nataka kununua meno yako?) Aliuliza Dk. Ian kwa hasira.

    Kila mfanyakazi aliyekuwepo uwanja wa ndege aligundua hasira aliyokuwa nayo Dk. Ian, wote walitetemeka kusikia akimtukana mwenzao kiasi hicho na hawakujua ni kitu gani kingempata, bila kuchelewa kijana huyo alianguka miguuni kwa Dk. Ian na kuanza kumlamba miguu akimwomba msamaha.

    “Forgive me sir! You are the most respected man on the planet, I didnt  intend to make you annoyed!”(Nisamahe bwana! Wewe ndiye mtu unayeheshimika zaidi duniani, sikufanya makusudi kukukasirisha!) Alisema kijana huyo lakini badala ya Dk. Ian kumsamehe alichomoa bastola yake mbavuni na kummiminia risasi zisizo na idadi damu nyingi zikamtoka, baada ya shughuli hiyo Dk. Ian alianza kutembea kuondoka eneo hilo.

    “Burry his body immediately, Thomson come  with  me to my house for a  meeting! Where is Caroline’s plane?”(Ufukieni mwili wake haraka wewe Thomson nifuate kwenye nyumba yangu  ili tufanye mkutano! Iko wapi ndege ya Caroline?)

    “They   left  twenty minutes ago!”(Wameondoka dakika ishirini zilizopita!)

    “To?”(Kwenda wapi?)

    “They  said goodbye to nobody!”(Hawajamuaga mtu!)

    “These people are tired of living! they cant get out of my hand, why didnt you kill them”(Watu hawa wamechoka kuishi! hawawezi kunitoroka mimi! Kwanini hukuwaua) Alisema Dk. Ian kwa hasira huku machozi yakimtoka! Siku hiyo hata Thomson alitishwa na hali aliyokuwa nayo tajiri yake hata siku moja hakuwahi kumwona Dk. ian akiwa na hasira kiasi hicho.

    “I hastated!”(Nilisita!) Alijibu Thomson akimfuata Dk. Ian kwa nyuma.

    Je nini kitatokea? Harry amekufa? Na nini kitatokea mahali walipo Harry na Caroline?  Watu gani wamewateka? Je, Dk. Ian atafanikiwa kuwapata? Fuatilia wiki ijayo.













    S

    iku hiyo hiyo Dk. Ian aliitisha ?mkutano wa haraka   na ?kuanza kugawa majukumu ya kuwasaka Caroline na Harry popote walipokimbilia duniani, aliamini wasingeukwepa mkono wake uliosambaa dunia, kupitia mtandano wa Mafia!

    “Nilijitoa Mafia sasa narudi sababu ya hawa mbweha wawili na nitawapata tu!” Alifoka kwa hasira  Dk. Ian mbele ya wafanyakazi wake waliokusanyika  ndani ya nyumba yake, hali ilikuwa mbaya na ilimtisha karibu kila mtu aliyekuwepo katika mkutano huo, wafanyakazi wote hawakuwahi kumwona Dk. Ian akiwa amekasirika kiasi hicho. Walishindwa kuelewa ni nini kingewapata Caroline na Harry kama wangekamatwa.

    “Yaani kweli Caroline pamoja na wema wote niliomfanyia amenitoroka tena na ndege niliyomnunulia mwenyewe kwa mamilioni ya dola? Haiwezekani lazima  nimpate!  Na siku akipatikana nitamchinja kwa mkono wangu mwenyewe!”

    “Usijali mzee,  atapatikana wala usiwe na wasiwasi hiyo sisi ni kazi yetu!”

    Baada ya mkutano huo Dk. Ian alipiga simu kwa kila mwakilishi wa Mafia katika mabara yote duniani, akianzia na Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Asia, Ulaya, Afrika na mengine  na kuwajulisha kuwa alikuwa amerejea tena  rasmi katika Umafia na alitaka watu waliotoroka na ndege yake wakamatwe haraka iwezekanavyo na kuuawa bila serikali ya nchi yoyote kufahamu!

    “Sitaki muwataarifu polisi, kazi hii   haitushindi, watafutwe kimya kimya  hadi wapatikane, ikibidi kuilipua ndege  wote wafe hata hivyo ndege ikiungua siyo tatizo sana kwangu!”

    “Sawa bosi!” Ndiyyo alivyoitikiwa na karibu kila mtu mwakilishi aliyempigia simu.

    Msako huo haukutangazwa katika chombo chochote cha habari wala polisi hawakufahamishwa juu ya kutoroka kwa Caroline na Harry, hivyo ndiyyo Mafia walifanyavyo kazi zao! Wakuu wa mabara wa Mafia waliwataarifu wakuu wa nchi mbalimbali juu ya msako huo  na katika muda wa masaa 12 tayari taarifa hizo zilishafika  katika kila  nchi duniani.

    Mawakala wa Mafia katika viwanja vyote vya ndege walikuwa na taarifa hiyo, kila ndege iliyoingia katika viwanja vyote dunia nzima ilirekodiwa na taarifa zilitolewa makao makuu ya Mafia, huko Milano Italia na baadaye kupelekwa kwa Dk. Ian ambaye tayari alisharudi Canada kutulia akisubiri taarifa, hasira yake ilizidi kuongezeka kadri dakika zilivyozidi kusonga mbele bila Caroline na Harry, alikuwa na hamu kubwa ya kuwapata   na kuwaonyesha yeye alikuwa ni mtu wa aina gani.

    “Nitamuua vibaya sana huyu mwanamke na hata huyo mwanaume wake nilishaacha kuua lakini sasa narejea!”

     Kila mara Dk. Ian alijiuliza ni kitu gani ambacho Caroline alikikosa kwake mpaka kuamua kutoroka na rubani  aliyempa kazi yeye mwenyewe, kwake ilikuwa ni aibu kubwa kushindwa  na mfanyakazi wake.

    “Hivi huyu Harry ni nani  mpaka aninyang’anye mimi mwanamke niliyempenda kiasi hiki?” Aliwaza  Dk. Ian kisha akanyanyuka na kwenda kwenye kabati ambako alichukua faili lenye maelezo  ambayo  Harry aliyatoa wakati wa kutafuta kazi ya Urubani kwenye kampuni yake! Aliyasoma hadi mwisho lakini alionekana kutoelewa kitu chochote, wazo  lilimwijia kichwani na kuamua kuwapigia simu watu wa kituo cha upepelezi binafsi cha  Investigation& Scrutiny Centre.

    “Hallow!”

    “Yeah!”

    “Can I help you?”(Naweza kukusaidia?)

    “ Can I  speak to the boss!”(Naweza kuongea na bosi wako?)

    “Hold on!”(Subiri!)

    Dakika kama mbili baadaye Dk. Ian alisikia sauti nzito kutoka upande wa pili, alipojitambulisha   mtu aliyepokea alionekana kutetemeka, alionyesha wazi hakuwahi kupokea simu kutoka kwa mtu tajiri kama Dk. Ian.

    “Dr. Ian the Rich?”(Dk. Ian tajiri?)

    “Yeah!”(Ndiyo!)

    “What can I do for you sir?”(Nikusaidie nini mzee?)

    “I just need to know  the depth of one person!”(nataka kujua undani wa mtu mmoja!)

    “Name him and we shall tell you everything in a minute!”(Tutajie ni nani na tutakueleza kila kitu juu yake katika muda wa dakika moja!)

    “Harry Robertson!”(Ni Harry Robertson!)

    “His profession?”(Kazi yake?)

    “A pilot!”(Ni rubani!)

    “Give me ten minutes sir and I will get back to you with every information that you need!”(Nipe dakika kumi nitakupigia!)

    “Ok!”(Sawa!) Dk. Ian alijibu na kukata simu.

    Hazikutimia dakika kumi,  kilikuwa ni kiasi cha kama dakika saba tu baadaye simu ikaita, Dk. Ian hakutegemea kama simu hiyo ingeweza kuwa inatoka kampuni ya upepelezi ya Investigation& Scrutiny Centre, alipoipokea  alishangaa na kukutana na sauti nzito  aliyoongea nayo mara ya mwisho!?”Yes! We have found him!”(Ndiyo tumempata!)

    “Sure? Then tell me about him!”(Hakika? Basi niambieni kila kitu juu yake!)

    “He was born Tanzania  28 years ago, went to school in the same country, he later joined a university where  he did his pilot course, he was employed by the following companies  USD Airlines as a pilot, quit the job and eventually employed by you  a few days ago!”(Alizaliwa Tanzania miaka 28 iliyopita, alisoma katika nchi hiyo hiyo,  lakini baadaye alijiunga na chuo kikuu ambako alisomea mambo ya uendeshaji wa ndege, amefanya kazi katika kampuni ya USD Airlines  na baadaye aliacha kazi na hatimaye ameajiriwa na wewe siku chache zilizopita!)

    Dk. Ian hakuyaamini masikio yake, halikuwa jambo rahisi hata kidogo taarifa za watu kupatikana kirahisi kiasi hicho! Alishindwa kuelewa watu hao walifanya kazi namna gani, ni kweli aliyekuwa akiongelewa  alikuwa ni Harry! Ni baada ya maelezo hayo ndiyo jina Harry lilifunuka katika kumbukumbu zake, alikumbuka kumsikia mke wake akilitaja mara kwa mara! Alihisi ni Harry huyo huyo ndiye alitoroka na mke wake baada ya kuwakutanisha alipompa kazi kama rubani.

    “Lazima watakuwa wanafahamiana, wote waliishi Tanzania! Haiwezekani lakini nitawapata tu!”

                   ***********

    Ndege ya Caroline ilitafuwa kila kona ya dunia bila kupatikana, haikuonekana  katika mitambo ya setilaiti  pamoja na Rada, Mafia walishindwa kuelewa mahali Harry na Caroline walipojificha, Dk. Ian alizidi kuchanganyikiwa. Ilikuwa si rahisi kuwaona katika mitambo kwani ndege  yao ilikuwa katikati ya msitu ya Cambodia, na walikuwa chini ya ulinzi  mkali wa Wavietnam!

    Walikuwa wakihojiwa  na maongezi kati yao yalikuwa si ya kuelewana kwa sababu kila mtu hakuielewa lugha ya mwenzake vizuri,  Caroline na Harry waliongea kiingereza lakini Wavietnam nao waliongea lugha yao,  katika kile kilichoonekana kama amri kutoka kwa mkubwa wao  walifungwa kwa kamba  na kuning’inizwa mitini vichwa chini miguu  juu na viboko vilianza kupita miilini mwao! Walilia kupita kiasi kufuatia mateso hayo, waliachwa mtini kwa karibu saa nzima wakiteseka.

    “Harry unaona sasa uliyoyasababisha?”

    “Nisamehe Caroline, hata hivyo huu si muda  muafaka wa  kutupiana lawama!”

    “Bila wewe haya yote yasingetokea Harry!”

    “Sawa laki……!”Kabla hajamaliza  Harry sentensi yake Harry alishtukia kiboko kikipita  katikati ya mgongo wake.

    “Hey! Where are you  from? Are you Americans?”(He! Nyie ni akinanani? Nyie ni Wamarekani?)

    Wavietinam waliwachukia sana Wamarekani na hilo wote wawili walilielewa  vizuri, kama wangediri kutamka walikuwa Wamarekani  mbele ya Mvietnam huo ndio ungekuwa  mwisho wa maisha yao! Walishangaa kusikia sauti ya mtu akiongea Kiingereza lakini iliwapa matumaini kuwa angalau sasa wangeweza kujieleza vizuri.

    “Answer my question are you Americans?”(Jibu swali langu nyie ni wamarekani?)

    “NO! No! We’re not!”(Hapana! Hapana! sisi sio!)

    “Who are you?”(Nyie ni akinanani?)

    “We are Canadians can’t you see the mark on the plane?”(Sisi ni Wacanada huoni alama kwenye ndege yetu!?)

    “You’re lucky to be Canadians other wise…….!”(mna bahati kuwa wacanada vinginevyo……!) Alisema mtu huyo na  baadaye kuongea lugha ya Kivietinam ambayo Harry na Caroline hawakuielewa lakini walishtukia wakifunguliwa kamba na kushushwa kutoka mtini  na kulazwa chini , baadaye walibebwa  juujuu na kupelekwa  hadi kwenye kibanda kilichokuwa karibu kabisa na eneo hilo ambako kupewa uji, miili yao haikuwa na nguvu kabisa lakini baada ya kunywa uji huo walijisikia vizuri. Mzee mmoja mwenye ndevu nyingi aliingia na kuanza kuwapaka vitu kama kinyesi cha ng’ombe katika vidonda walivyokuwa navyo miguuni, siku hiyo hawakutoka ndani ya kibanda  hicho kilichooneka kuwa mahabusu walilala bila kusemeshana hadi usiku wa manane Caroline alipomwamsha Harry aliyekuwa akikoroma usingizini.

    “Harry tafadhali hebu nieleze ukweli tutaondokaje  mahali hapa?”

    Harry alikaa kimya kwa muda wa kama dakika tatu bila kujibu kitu, alionekana kuwa katika mawazo Fulani.

    “Harry niambie tutaondoka vipi hapa?”

    “Tutaondoka tu ila tunahitaji kupanga mikakati!”

    “Ipi?” Caroline aliuliza.

    “Mpaka sasa sijaifahamu ila tutaondoka!”

    “Na ndege?”

    “Ndiyo kwanini tuiache ndege yetu?”

    Usiku huo wa manane waliongea mengi juu ya maisha yao, hofu ya Caroline juu ya Dk. Ian  bado iliendelea kumsumbua pamoja na Harry kumtia nguvu,  alijua siku moja  ni lazima angeiingia mikononi mwake na kuuawa kikatili! Upande mwingine wa moyo wake ulijaa majuto lakini hakutaka kumwonyesha Harry hali hiyo.

    “Nimekwishakueleza kuwa  Dk. Ian hatatupata hata kitokee nini!  Tatizo lako wewe huniamini, kwanza tukitoka hapa kazi yetu  ya kwanza itakuwa ni kubadilisha hizi sura zetu na ndege tutaiuza na kupatka mamilion ya dola tunaweza hata kuamua kurejea Tanzania,   nina ndoto za kuwa Rais wa nchi hiyo  kama ikitokea  nikawa na pesa baada ya hapo Dk. Ian atanikamata vipi wakati nitakuwa nalindwa na dola?”

    “Kweli? Lakini mbona unajiongelea mwenyewe wakati tuko wawili?”

    “Samahani nilipitiwa”

               ***************

    Asubuhi kulipokucha wote wawili waliwaamshwa na kuwapelekwa  mbele ya  kiongozi wao aliyeitwa Wung  huko walihojiwa  maswali mengi   juu yao na kurudishwa tena katika kibanda chao ambako walifungiwa na kuendelea kuhudumiwa kwa kla kitu,  kwa wiki nzima walibaki katika mahabusu ndani ya kambi ya Vietnam!  Ilionekana hapakuwa na namna yoyote ambayo wangeweza kujiokoa, hawakuruhusiwa kutoka katika chumba chao usiku na mchana! Caroline alichoka kukaa ndani alitaka kuwa huru, walikuwa ni kama wafungwa.

                     ************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog