Simulizi : Uhasama
Sehemu Ya Pili (2)
Siku iliyofuata, Mata alienda hadi hospitali kuulizia maendeleo ya ndugu yake kama walivyo ekti, na kufika hadi kwa daktari.
“Kwahiyo jana uthiku hakuthumbua kabitha?" Mata alimuuliza daktari baada ya kuambiwa hali ya Moto ilivyokuwa.
“Ndio hakusumbua kabisa, inabidi leo uondoke nae maana hali yake ni nzuri, na nitamuandikia dawa za kutuliza maumivu, mkitoka mtapitia katika dirisha la dawa, muzichukue"
“Athante dokta, ninawedha kuondoka nae?"
“Yeah, unaondoka nae"
“Haya dokta kadhi njema"
Baada ya kuagana na dokta, alitoka katika ofisi ya dokta na kuelekea hadi katika chumba alicholazwa Moto.
“Vipi, kadhi umekamilisha?" Mata aliuliza kwa pupa huku akitabasamu akijua kazi imekwisha.
“Subiri nitakuelezea tukifika nyumbani"
“Thatha thi uniambie mara moja tu?"
“Mata, mbona una haraka hivyo?"
“Haya twende"
Walianza safari ya kuelekea nyumbani kwa Mata, walipitia kwenye dirisha la dawa na kupewa dawa kama walivyoambiwa na daktari, wakapitia na mapokezi na kulipa gharama zote.
Baada ya kulipa gharama zote, walitoka nje na kupanda kwenye gari, ili waondoke zao, wakati wapo ndani ya gari wakashauriana wampigie simu na Mrutu ili wakutane nyumbani kwa Mata, walipofika wakaingia hadi ndani, na baada ya muda mfupi Mrutu nae akaingia, baada ya kusalimiana wote wakamtaka Moto awaelezee imekuaje huko hospitali.
“Dah! Yani hamuwezi amini yule mtoto nahisi alipangiwa asife pale hospitali"
“Embu acha kuzunguka mbuyu, tuelezee imekuaje"
“Ok, achaniwaelezee ilivyokuwa. Wakati....."
Moto aliwaelezea kila kitu, mwanzo hadi mwisho.
“Kwahiyo huku fanikiwa kumuua?" Mata alimuliza swali la kipumbavu.
“Mata unataka nikuambie mara ngapi?"
“Aaah!!! Nimechanganyikiwa ndugu yangu"
“Eeeee basi ndo hivyo, sasa sijui tunafanya nini tena" Moto aliongea.
“Hapa hakuna chengine cha kufanya dhaidi ya kumuua tu"
“Ndio lazima afe, sasa hiyo njia ya kumuua ndio ipi tena"
“Itabidi tupange mpango mwengine" Mata alisema.
“Sasa huo mpango mwengine ni upi?" Mrutu aliuliza.
“Tutapanga baadae, kwanza sasa hivi mimi nina usingizi, jana usiku sijalala kabisa kwajili ya hofu"
“Hofu ya nini?" Mata aliuliza.
“We unadhani kufumaniwa unataka kumchoma mtu sindano ya sumu ni mchezo?"
“Kwani umegundulika?" Mata aliuliza.
“Hata kama, ila ndio hivyo sijapata usingizi, halafu pia ndio mara yangu ya kwanza kulala hospitali, hata hiyo pia imechangia nisipate usingizi" Moto aliongea huku akielekea katika chumba kimoja wapo cha hiyo nyumba ya Mata.
“Wewe nenda kalale, ila ukiamka uthithahau kutandika kitanda"
“Utatandika mwenyewe bwana" Moto aliongea huku akifunga mlango.
“Sasa Mata, acha na mimi niende dukani kwangu, maana nimemuacha yule kijana wangu mwenyewe, halafu si unajua pale muda mwengine wateja wanajaa Sasa acha basi mimi nikamsaidie"
“Haya bwana we nenda, hata hivyo mimi mwenyewe pia najiandaa kuondoka hapa kuelekea kadhini, maana kuna kadhi dha watu thija dhimalidhia"
******************************
Majira ya mchana, yalimkuta Inspekta Ganjo, akielekea katika hospitali aliyolazwa Hemedy, alienda hadi katika chumba alicholazwa Hemedy, akamkuta akiwa amekaa.
Hemedy alimsalimia Inspekta Ganjo, baada ya salamu, Insepekta Ganjo akamuuliza hali yake inaendela vipi, Hemedy akamjibu kuwa sasa hivi ana unafuu, wakati wakiendelea na maongezi, Nesi Maria akaingia na kumuambia Inspekta Ganjo anaitwa na daktari, Inspekta Ganjo aliinuka na kwenda kwa daktari.
“Hali ya mwanao sasa hivi inaendelea vizuri" Daktari alianzisha maongezi baada ya salamu.
“Nashkuru daktari, kwahiyo ni lini mutamruhusu?"
“Nimekuita hapa ili nikuambie kuwa leo ndio tutamruhusu kuondoka, baada ya kuona hali yake kidogo imetengemaa"
“Kwahiyo mutamruhusu sasa hivi au?"
“Sasa hivi itabidi uondoke nae, na nimemuandikia dawa nyengine za kukausha kabisa vile vidonda, chukua hii karatasi(huku akimpa karatasi iliyo andikwa dawa) mtapitia pale kwenye dirisha la dawa"
“Na malipo?"
“Mkifika pale mapokezi mtaambiwa kila kitu"
“Asante dokta, mungu akubariki"
“Amina, na wewe pia"
Baada ya kuagana, Inspekta Ganjo alienda katika chumba alichokuwemo Hemedy, na kumchukua na kuondoka nae, wakati wakiwa kwenye kordo wakielekea katika dirisha la dawa, walikutana na nesi Maria.
“Haaa!!! Kwani ndio umeruhusiwa kuondoka leo?" Nesi Maria aliuliza.
“Ndio nimeruhisiwa, kwani wewe ulitaka ni baki hadi lini?"
“Hapana, nilikuwa nauliza tu, ila kama umeruhusiwa pia sio mbaya"
“Basi ndio hivyo"
“Sawa, ila nitakuona lini tena mdogo wangu, unajua mimi tayari nishakuzoea?"
“Usija dada maria, mi mbona nitakuja kukutembelea siku yoyote tu"
“Haya safari njema"
Baada ya kuagana, walienda hadi katika dirisha la dawa na kumalizia mapokezi, baada ya kukamilisha kila kitu, waliondoka hadi kituoni.
Walimuhoji maswali kwamba ilikuaje kuaje. Hemedy aliwaelezea jinsi tukio lilivyotokea hadi yeye kuponea chupuchupu, aliwaelezea hadi alipo bambikiwa zahma la uwizi, na kunusurika kifo kwa mara ya pili, baada ya kutokea kwa polisi.
“Hao watu waliovamia nyumbani kwenu, ukiwaona unaweza ukawajua?" Inspekta Ganjo alimuuliza.
“Ndio nawajua, tena...(Hemedy ikawa anataka kusema kwamba flash ya tukio zima pia anayo, ila akakumbuka aliambiwa na Goda kuwa hiyo flash asimpe mtu akae nayo yeye mwenyewe, akaghairisha kusema hivyo) Na wajua nikiwaona" akamalizia.
“Koplo Taure, inabidi umpigie simu baba yake mdogo aje amchukue mwanae, akakae nae ikiwa sisi tunaendelea na uchunguzi, tena mpigie sasa hivi"Inpekta Ganjo alimuambia Koplo Taure.
Koplo Taure alimpigia simu Mrutu na kumuambia aje kituoni. Baada dakika ishirini, Mrutu alifika hadi kituoni hapo.
“Ndio bwana Mrutu, mwanao huyo hapo, itabidi wewe uwende nae nyumbani, huku sisi tukiendelea na uchunguzi"
“Sawa, na vipi kuhusu gharama zake hospitali"
“Kuhusu gharama usijali, mimi nishamlipia, kwahiyo wewe kilicho baki ni kuondoka nae tu"
“Nashkuru, acha mimi niende nae"
Baada ya hapo, Mrutu aliaga na kuondoka na Hemedy kuelekea nae nyumbani kwake. Walipofika Mrutu, akamkaribisha Hemedy nyumbani kwake, akamuonyesha chumba atakacho lala, baada ya kumuonyesha kila kitu, Mrutu alitoka hadi nje ya chumba alichompa Hemedy huku akitabasamu.
“Kazi imekwisha, nammaliza leo leo"
Mrutu aliongea hivyo na kutoka hadi nje ya nyumba yake na kwenda kusikojulikana.
“Tobi"
“Mkuu"
“Nenda kaniitie Tito mara moja"
“Sawa Mkuu"
Kijana mwenye mwili mkubwa kutokana na kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma aliejulikana kwa jina la Tobi, alienda alipo agiziwa na Mzee mwenye mvi zilizoanza kuota kwenye nywele zake.
Baada ya muda si mrefu alirudi na kijana mwenzie aliekuwa na mwili mkubwa kama yeye, wote wakasimama mbele ya Mzee mwenye nywele zilizo anza kuota mvi.
“Mkuu" wote waliongea neno hilo.
“Tito?" Mzee mwenye nywele zilizoanza kuota mvi aliita.
“Mkuu" Kijana mwenye mwili mkubwa aliejulikana kwa jina la Tito aliitikia.
“Unaweza ukaniambia kwanini mzigo wakati naondoka niliuwacha mwingi, ila sasa nimerudi nakuta mzigo umepungua na nikiangalia mahesabu naona siyaelewi kabisa, kwanini imekuwa hivi?"
“Mkuu, unachoongea ni kweli kabisa, kuna mtu alitaka mzigo nikampa, ila aliniambia kuwa pesa ataniletea baada ya wiki mbili, ila sasa naona ni mwezi na nusu huu hajaleta bado"
“(huku akiinuka na kuipiga meza iliyokuwepo mbele yake kwa gazabu) Nime kukataza mara ngapi kutoa mzigo bila ya kupewa pesa? Wewe unazijua biashara zetu hizi, kutapeliana ni jambo la kawaida, halafu wewe unaenda kutoa mzigo bila ya kupewa pesa?"
“Mkuu, ila nimefanya hivyo kwa mtu ambae tunamuamini sana na hata wewe pia umeruhusu kuwa akija hata kama akiwa hana pesa tumpe mzigo pesa ataleta siku yoyote"
“Ni nani huyo?" Mzee mwenye nywele zilizo anza kuota mvi aliuliza.
“Ni Mrutu Mkuu"
“Kwahiyo Mrutu na yeye ameamua kunitapeli?"
“Sijajua Mkuu, kwasababu pia sio kawaida yake kuchelewa kuleta pesa baada ya kumpa mzigo"
“Nenda kamfuate na umuambie kuwa tunataka pesa yetu, au kama hana pesa, basi mwambie akupe mzigo wetu"
“Sawa Mkuu"
“Ok, Tito nenda nilipo kutuma, na Tobi wewe nenda kaendelee na kazi"
“Mkuu" walisema wote kwa pamoja na kuondoka.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika ngome ya Mzee mwenye nywele zilianza kuota mvi, anaejulikana kwa jina la Mr Bakari Haneni.
Mr Bakari Haneni, alikuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya, alichangia sana kuwaharibu vijana wa Tanga kwa kuwauzia madawa hayo hatari ambayo serikali ilipiga vita kila siku.
Kwa wakati huo alikuwa yupo katika jengo la gorofa mbili lililochakaa kwa kuachwa na wakoloni miaka mingi iliyopita, lililokuwa maeneo ya mwambani kando kando ya bahari ya hindi.
Mr Bakari Haneni, alikuwa ni mtu katili sana, kuua kwake ni jambo jepesi kuliko kufumbua na kufumba kope ya jicho lake, alikuwa na walinzi wanao lilinda jengo hilo zaidi ya hamsini, na kila mlinzi mmoja alikuwa na silaha kali, alikuwa akiwakamata vijana wadogo hasahasa wakiume kwajili ya kufanya kazi ya kufanga madawa ya kulevya kwenye vipakti vidogo vidogo.
Alikuwa ni tajiri mkubwa tu katika mkoa huo wa Tanga kupitia biashara hiyo ya madawa ya kulevya, alikuwa anamiliki nyumba moja ya gorofa iliyokuwepo maeneo ya Raskazone, anamiliki Hoteli za nyota tatu, moja ilikuwa maeneo ya kwaminchi na nyengine ilikuwa pangani, alitembelea magari ya kifahari ya kila aina.
Akiwa hadharani alionekana ni mtu mwema sana, alipeleka misaada katika vituo vya kulelea watoto yatima mbalimbali vilivyopo katila mkoa huo wa Tanga, alionekana ni mtu mwema sana mbele ya watu, kuna waliosema kwamba Mzee huyo akiamua kugombe ubunge kwa mkoa wa Tanga kwa chama chochote kile, basi atapita bila pingamizi lolote, kutokana kuwa watu walimpenda kwa kujitolea kwake.
Ila kwa upande mwengine, alikuwa ni katili na aliuwa watu bila sababu yoyote, alikamata vijana wadogo na kwenda kuwatumikisha katika ngome yake kwa kuwafanyisha kazi za kufunga madawa ya kulevya, na ikionekana kati ya hao vijana mmoja wapo akianza kusinzia tu kutokana na kuathiriwa na madawa hayo wanayo yafunga, aliuliwa na kwenda kutupwa katika shimo na mwisho huchomwa moto, ilikuwa sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuingia halafu utoke nje ya ngome hiyo, waliokuwa wakipelekwa katika ngome hiyo waliishia kufa na maiti zao huchomwa moto mpaka kuwa majivu, pamoja na yote hayo, serikali ilikuwa haijui chochote kuhusiana na ukatili aliokuwa akiufanya Mzee huyo.
* * * *
“Hallow"
“Niambie Mrutu"
“Shwari, sijui nani mwenzangu?"
“Tito, Mr Tito hapa naongea"
“Ohhhh!!! Tito, samahani ndugu yangu, simu yangu ilpotea na nimenunua simu nyengine na hata laini pia nimenunua nyengine, sikuweza kuirinyuu kwasababu kitambulisho nilicho sajilia nacho pia kili potea"
“Sawa, mbona sasa kimya? Mwezi huu na nusu hujarudisha pesa zetu halafu pia mawasiliano na sisi umekata, eeeh kuna nini?" Tito alimuuliza kwa upole kabisa kilichomkumba Mrutu hadi ikawa harudishi pesa zao.
“Hapana kaka, nilipatwa na msiba wa kaka yangu halafu pia nimekabidhiwa mimi nimlee mwanae aliemuacha ndio maana ukaona nipo kimya ila ningekuja maskani tuje kuyamaliza, ila usijali pia kwa hilo siku si nyingi nitakucheki ili nirudishe pesa zenu"
“Hakuna tatizo ila naomba unitafute wewe usitake hadi nikutafute mimi maana Mkuu alikasirika kweli ila tulivyomuambia kuwa ni wewe ndio umechukua mzigo, kidogo hapo akapunguza hasira zake ila fanya urudishe pesa za watu au rudisha mzigo kabla Mkuu hajatoa amri mbaya juu yako"
“Usijali nitafanya hivyo hivi karibuni tu"
“Hakuna shaka Bwana Mrutu"
Mrutu alipogundua kuwa anaongea na mtu alieamua kupoteza mawasiliano nae kwa makusudi, kutokana na kudaiwa pesa alizo chukua mzigo wa watu wa madawa ya kulevya, alianza kupatwa na hofu, hakuelewa mtu huyo namba yake iliipata vipi.
Mrutu pamoja na kuwa na duka la spea za magari lililo muingizia pesa nyingi, ila pia aliona haitoshi, baada ya kushawishiwa kuwa kazi ya kuuza madawa ya kulevya ina hela sana, akashawishika na biashara hiyo haramu, akaamua na yeye aanze kuuza madawa ya kulevya.
Akakutanishwa na Tito kwa mara ya kwanza, akaomba kuelekezwa biashara inavyoenda, akaelekezwa vizuri na yeye akanunua mzigo mdogo kwajili ya kuanza nao, bahati ikawa kwake akaumaliza wote.
Akazidi kushawishika na biashara hiyo baada ya kuona imemletea faida kubwa, akamtafuta tena Tito akaomba amuongezee tena mzigo, safari hii aliomba apewe mwingi zaidi ya ule wa mwanzo baada ya kuona ule wa mwanzo faida umemletea kubwa.
Baada ya kufanya biashara sana na Tito, akafanikiwa kuwa mteja mkubwa kuliko wote kwasababu yeye alikuwa anachukuwa mzigo mkubwa sana, ilikuwa akichukua karibia nusu ya mzigo unaokuja, ndipo hapo Mr Bakari Haneni akataka kumuona huyo mteja wake anaechukua nusu ya mzigo anawo uleta, akakutanishwa nae katika hiyo ngome yake, na Mrutu ikawa ndio mtu wa kwanza wa kawaida kuingia na kutoka katika ngome hiyo akiwa na uhai wake.
Alipo aminiwa sana ikawa na yeye akija bila pesa anapewa mzigo bila ya wasiwasi wowote na yeye akimaliza mzigo au hata kama hajaumaliza basi anarudisha pesa ya watu ndipo hapo Mr Bakari Hanaeni alipo muamini na yeye.
Ila toka alipo chukua mzigo mara ya mwisho bila ya kutoa pesa kwanza kama kawaida yake, basi tangia siku hiyo hakurudisha tena pesa ya watu na wala hakupatikana tena kwenye simu, ndipo hapo hasara ilipoonekana na Tito alipo ambiwa amfuatilie.
Mrutu alichukua mzigo kama kawaida yake bila ya kutoa pesa kwanza akiahidi kuwa ataleta baada ya kufikisha mzigo katikati ila baada ya kuuchukua mzigo ule yakamkuta makubwa baada ya kumkabidhi kijana wake anaemuamini kuusambaza, akapotea nao na asijue alipo elekea na kujikuta akidaiwa pesa nyingi bila kujua atazitolea wapi, akaamua kupoteza mawasiliano na Tito afikirie atazipata vipi pesa za watu ili alipe mzigo uliopotea na kijana wake.
Ndipo hapo alipo shawishika tena kwa mara ya pili baada ya kuambiwa wamuue kaka yake na familia nzima ili wachukue mali zote halafu wagawane wao, hapo ndipo alipoona anaweza kuokoka na kundi lile hatari la Mr Bakari Haneni, akapanga atakapo pata mgawo wake wa mali za kaka yake walie amua kumuua ili wazichukue, akapanga kurudisha pesa za watu halafu achane na biashara hiyo, aliwa puuza wale waliosema“Muda hamsubiri mtu" akawapuuza na wale waliosema“liwezekanalo leo lisingoje kesho"
Akawa anaingoja kesho ili aache, ikiwa uwezekana wa kuacha leo ukiwa upo, akawa ameshachelewa kwa kuigoja kesho, sasa amepigiwa simu na yule mtu aliemkimbia kwa kupoteza nae mawasiliano ili mpaka mpango wao ukitimia ndipo arudishe pesa za watu, biashara hiyo aliifanya kwa siri sana hata wakina Mata walikuwa pia hawajui kwamba anafanya biashara kama hiyo.
***************************
“Mkuu, kuna kesi nyingi sana za kupotea kwa watoto huko mitaani" Koplo Taure aliongea.
“Hili jambo lipo, na kuna mafaili mengi yenye kesi kama kama hii,(akamuangalia Koplo Taure kwa umakini) nakukabidhi hii kesi uifuatilie wewe na ninakupa wiki tatu uwe umeshanipa majibu ya hao watoto wanaopotea wanakwenda wapi, umenisikia?" Inspekta Ganjo alisema.
“Mkuu" Koplo Taure aliitikia kwa ukakamavu wa kijeshi.
“Kuanzia sasa hii kesi ipo mikononi kwako wewe, chukua mafaili yote yanayo husika na kesi kama hii, ukae nayo wewe ofisini kwako. Unaweza kwenda"
“Mkuu" Koplo Taure alipiga salut na kuondoka katika ofisi ya Inspekta Ganjo.
*******************************
“Ok, Tito nipe taarifa”
“Mkuu, kazi imefanyika kama ilivyopangwa”
“Ndio nataka unieleze sasa”
“Wale vijana walio enda kuupokea mzigo wamekuja nao bila tatizo na ule mzigo uliobakia, pia tume uuza wote, kwahiyo sasa hivi tuna huu mzigo mpya tu”
“Ok, na vipi kuhusu huyu nani huyu.......”
“Mrutu”
“Yeah, yeah, na yeye ulimfuatilia kama nilivyo kuagiza?”
“Ndio mkuu”
“Amekuelezaje kuhusu kupotea kwake na mzigo wetu mwezi mzima”
“Amenieleza mambo mengi, amesema kwamba alipatwa na msiba wa kaka yake na anavyodai kuwa ameachiwa mtoto wa kaka yake amlee yeye ndio maana ikapelekea hadi kutooneka mwezi mzima"
“Kwahiyo hiyo ndio ilimpelekea kutoweza kutoa taarifa?”
“Hapana Mkuu, amesema pia alipoteza simu ndio maana pia hakuwa na mawasiliano na sisi"
“Kwhiyo hakusema kwamba pesa yetu ataileta lini?"
“Hakusema siku maalumu ila alisema siku si nyingi atakuwa tayari ameshaleta"
“Naona tayari ameanza kupoteza uaminifu, ila mimi nampa wiki moja tu, asipoleta pesa yetu, basi mimi nitajua cha kufanya, wewe nenda kaendelee na kazi"
“Sawa Mkuu"
**********************************
Ni majira ya usiku, katika nyumba ya Mrutu, Mrutu alionekana, akiinuka katika kitanda chake, aka kaa hapo hapo kitandani, akawa kama anafikiria kitu, mara akasimama, alikuwa amevaa pensi, juu alikuwa yupo tumbo wazi, akaiyendea droo yake, akaivuta kwa mbele na kuchukua bastola yake, akaenda kwenye mlango wa kutokea katika chumba chake na kuufungua, alipotoka nje ya mlango wa chumba chake, akaenda hadi kwenye mlango wa chumba alicho lala Hemedy, bahati nzuri ikawa kwake, mlango ulikuwa upo wazi, akazama hadi ndani, akamkuta Hemedy akiwa amelala, hakutaka kupoteza muda, akamuendea hadi pale kitandani na kumuwekea bastola ya kifua upande wa moyo, bila kufikiria mara mbili akamfyatulia risasi iliyozama hadi ndani ya kifua changa cha Hemedy....
“Maaamaaaa!!!!"
Hemedy alishtuka kutoka usingizini, kutokana na ndoto alioiyota muda mfupi, alipiga kelele za kumuita mama yake alie kuwa kaburini, alikuwa akihema haraka haraka kama mtu alietoka kukimbia umbali mrefu, huku majasho yakimtoka, kelele zake zilimfikia Mrutu alie kuwa katika chumba chake na kumfanya aje mbio mbio hadi katika chumba alicho lala Hemedy.
“Vipi, mbona kelele tena usiku huu, una nini?"
“Ndoto, nimeota ndoto baba"
“Ndoto gani?"
Hemedy alishindwa amuelezee vipi Mrutu hiyo ndoto aliyoiyota, ikiwa muhusika mwenyewe ndio huyo huyo, alizidi kuwa na wasiwasi baada ya kumuona alivyo muota ndivyo alivyo kuja, Mrutu alikuwa ameshika bastola na amevaa pensi ile ile aliyo muota nayo na juu alikuwa yupo tumbo wazi, hakujua amuelezeea au asimuelezee, akabaki kimya tu huku akiwa kamkodolea macho baba yake huyo mdogo.
“Wewe si nakuuliza, hiyo ndoto iliyo kufanya hadi ukapiga kelele ni ndoto gani?"
“Nimeiota ile siku wazazi wangu walipo uliwa na wale watu waliotuvamia" Hemedy aliamua kudanganya, ghafla machozi yalianza kumtoka, alianza kulia chini chini, ikabidi Mrutu alimsogelee na kuanza kum'bembeleza.
“Nyamaza mwanangu usilie, kumbuka kuwa kila mtu atakufa katika huu ulimwengu, wazazi wako wametangulia, inabidi uwaombee mungu awalaze mahali pema huko walipo, inabidi usahau ili mambo mengine yaendelee"
“(huku akimkumbatia Mrutu" inaniuma kila nikiwakumbuka wazazi wangu"
“Najua kwamba inauma, ila inabidi ujikaze, kwasababu wewe sio wa kwanza kufiwa na wazazi wote wawili, kuna wenzako wazazi wote wawili wamekufa na sasa hivi wapo mitaani tu huko hawajui pakwenda, ila shukuru mungu kwasababu umepata mtu wa kukulea, kwahiyo usilie sana hadi uka kufuru mungu" Mrutu alimuonea huruma Hemedy, ila hakuwa na jinsi ya kufanya, kwasababu waliyo yataka tayari yameshatokea, alibaki tu akim'bembeleza, alifanya hivyo kama dakika mbili, Hemedy akanyamaza.
“Haya lala mwanangu"
“Sawa baba"
“Halafu kuanzia kesho inabidi nikupeleke shule, ukaendelee kusoma, kwasababu huo muda uliokaa nyumbani ni mwingi sana"
“Sawa" Hemedy alisema huku akijifunika shuka.
Baada ya kuhakikisha Hemedy tayari ameanza kupitiwa na usingizi, Mrutu alinyanyuka na kuichukua bastola yake, aliiyangalia na kumuangalia Hemedy.
Ni kweli alipanga siku hiyo amuue Hemedy, ila kuna kitu kama huruma hivi kilimuingia kwenye moyo wake, hapo ndipo alipo amini kuwa damu nzito kuliko maji, lakini kwa upande mwengine hakuwa na jinsi, ilibidi Hemedy afe ili ushahidi upotee kabisa, kwakuwa yeye alishindwa kumuua Hemedy, akapanga kazi hiyo ata waachia wakina Moto ili waitekeleze.
Akaondoka chumbani kwa Hemedy, akaenda chumbani kwake ili kuitafuta kesho yake. Akaenda kulala.
************************
Siku iliyofuata Mrutu alimpeleka Hemedy shuleni kwao, akamueleza mwalimu wake yote yaliyo mkuta Hemedy, mwalimu alisikitika sana, alimsikitikia Hemedy ambae kwa wakati huo alikuwa ni yatima, ila na yeye alikuwa kama wengine tu waliosikitishwa na vifo hivyo, sikitiko lake halikuwa na uwezo wa kuwarudisha wazazi wa Hemedy duniani, akamruhusu Hemedy kwenda darasani.
Baada ya kukamilisha kila kitu Mrutu akaondoka shuleni hapo na kwenda dukani kwake, akapanga hatokaa sana dukani ili awapigie simu wakina Moto, wapange ni jinsi gani ya kumuua Hemedy.
****
Koplo Taure siku hii alipanga kuanza upelelezi wa kesi alizopewa na Inspekta Ganjo za kupotea kwa watoto mitaani, baada ya kupewa ruksa ya kutoka kituoni muda huu wa mchana, aliwasha gari yake na kwenda hadi katika nyumba ya mmoja wapo aliye leta kesi ya kupotelewa kwa mtoto wake, alipofika aliteremka kwenye gari na kwenda hadi mlangoni, akapiga hodi, baada ya sekunde kadhaa akasikia michakacho ya hatua za mtu kutokea ndani, akajua mwenyeji ndio anakuja, akasubiri.
“Za saa hizi?" Koplo Taure, alianzisha maongezi baada ya mlango kufunguliwa, alitokea msichana, Koplo Taure alivyo muangalia tu alijua kuwa huyo atakuwa ni mfanyakazi wa humo ndani.
“Nzuli tu" Msichana huyo alijibu kwa lafudhi ya kabila la kisambaa, Koplo Taure alitabasamu na kuendelea.
“Baba au Mama sijui nimewakuta?"
“Yupo Mama tu Baba hayupo"
“Sawa, pia sio mbaya, naomba uniitie"
“Haya subili nikamuite"
Yule msichana aliingia ndani na kumuacha Koplo Taure hapo hapo nje, baada ya dakika mbili alirudi tena.
“Anakuambia upite ndani"
Koplo Taure aliingia ndani ya nyumba hiyo, akalakiwa na sebule safi iliyopendezeshwa na vitu vya thamani vilivyowekwa kwenye sebule hiyo, akachagua sofa moja kati ya mengi yaliyo kuwepo katika sebule hiyo, akakaa juu yake, alianza kupitisha macho kwenye sebule hiyo huku na huko, ilimradi tu iwe kama wengi wafanyavyo wanapokuwa ugenini kwa mara ya kwanza, baada ya muda alitokea mwanamke mtu mzima kidogo.
“Karibu" Alisema mwanamke huyo huku akikaa katika sofa jengine tofauti na lile alilo kaa Koplo Taure.
“Asante" Koplo Taure alijibu.
“Wewe ni nani na nikusaidie nini?"
“Bilashaka wewe ndio mzazi wa Hassani Dupe?"
“Ndio ni mimi"
“Mimi ni polisi kutoka katika kituo cha polisi Mabawa(Huku akimuonyesha kitambulisho) Nimekuja hapa nataka nikuulize maswali mawili matatu kuhusiana na kupotea kwa mtoto wako na ninaomba unipe ushirikiano wa kutosha ili nipate mwanga wa kujua ni wapi pakuanzia kumtafuta mtoto wako na sio wako tu, hii kesi ya kupotea kwa watoto zipo nyingi sana kituoni kwetu na vituo vyengine vya polisi, kwahiyo naomba unijibu kila nitakalo kuuliza"
“Ndio niko tayari, uliza tu"
Koplo Taure alitoa kijidaftari na kalamu ili aanze kuandika maelezo atakayo yatoa mwanamke huyo.
“Mwanao ana umri gani?"
“Ana miaka kumi na saba"
“Tangu mwanao apotee ana muda gani hadi sasa?"
“Ni wiki tu"
“Unaweza ukanieleza alipotea potea vipi?"
“Iyo siku wakati ndio mara ya mwisho kumuona, aliniaga anakwenda uwanjani kwenda kuangalia mpira, basi tokea siku hiyo ndio sikumuona tena mwanangu mimi(akianza kulia) mwanangu sijui wamempeleka wapi jamani, kwani amewakosea nini hadi wakamfanyia hivyo, mwanangu mwenyewe ndio huyo huyo mmoja tu sina mwengine mimi, eeee mungu mlinde mwanangu uko ali...." Hakuweza kuendelea tena kutokana na kilio cha uchungu wa mwana, ikabidi Koplo Taure afanye kazi nyengine ya kum'bembeleza.
“Dada nyamaza basi tuendelee"
“Mwanangu mimiiii, Hassani wewe upo wapi mwananguuuuu"
“Wanawake bwana!!!" Koplo Taure alijisemea kimoyo moyo“aaah!! ila uchungu wa mwana aujuae mzazi muache alie kwanza" ikabidi amsubirie hadi atakapo nyamaza ndipo waendelee na maongezi yao. Baada ya Dakika tano mwanamke yule alinyamaza mwenyewe, akajifuta machozi kwa kutumia kanga yake, na kumuangalia Koplo Taure.
“Wakati unanieleza maelezo yako, kuna sehemu ulisema kwamba hujui aliwakosea nini hadi wakamfanyia hivyo mwanao, ni wakina nani hao?"
“Mimi si wajui"
“Kwani huko uwanjani ana kawaida ya kwenda kila siku kwenda kuangalia mpira?"
“Hapana, wameanza kwenda hivi juzi juzi tu, walikuwa wanasema kwamba wanaenda kuangalia sijui ligi sijui mambo ya mpira mimi, ila walikuwa wanaenda kuiyangalia timu yao ikicheza"
“Kwani alikuwa akienda na wenzake?"
“Ndio wapo wanne, wanaoenda huko uwanjani kwenda kuangalia mpira"
“Kwahiyo amepotea na hoa wenzake?"
“Hapana, mmoja wao aliwakimbia hao watekaji"
“Huyo mmoja wao alie kimbia ninaweza nikampata ili anieleze tukio zima lilivyokuwa?"
“Hapana, wazazi wake wamemuamisha mji na yeye ndio aliekuja kutoa taarifa hizo za kutekwa kwa wenzake"
“Alisemaje, unaweza ukanielezea?"
“Yeye alisema kwamba wakati wanarudi huko mpirani, njiani walikutana na gari iliyopaki pembeni, kwenye hiyo gari kuna mwanaume mmoja aliwaita wote, walipofika pale kwenye ile gari, ghafla milango ikafunguliwa wakatokea wanaume wengine wanne na kuwashikilia kila mmoja wake, ila huyo mmoja ambae kapona kwenye huo utekaji, yeye alifanikiwa kuwatoroka na kukimbia na yeye ndie aliekuja kutupa hizo taarifa"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa, hiyo gari hajamiambia kuwa niya rangi gani au labda kama namba zake za gari amezishika?"
“Alivyosema yeye, hiyo gari ilikuwa ni ya rangi nyeusi ila namba za gari ndio hakuzishika"
“Unaweza ukanielekeza huo uwanja wa mpira mahali ulipo?"
“Mbona sio mbali sana na hapa nyumbani, ni hapo mbele tu, kuna mtaa mmoja upo hapo mbele kuna nyumba ina fremu za maduka, kwa mbele kidogo tu ndipo utauona huo uwanja"
“Hakukuja watu au labda mtu mwengine kuja kukuhoji kama hivi?"
“Hapana wewe ndio wa kwanza kuja hapa"
“Sawa, asante Dada, acha mimi nikaendelee na kazi, nikiwa na shida na wewe nitakutafuta"
“Haya kaka, lakini naomba unitafutie mwanangu, maana mtoto mwenyewe ndio huyo huyo mmoja tu"
“Usijali Dada, kwavile jeshi la polisi limeamua kufuatilia basi lazima watapatikana tu"
“Haya kaka karibu tena"
Baada ya kutoka katika nyumba ya mhanga mmoja wapo aliepotelewa na mtoto, Koplo Taure alienda hadi hapo uwanjani tukio lilipotokea, alipofika alipaki gari pembeni na kuangalia angalia hapo kama dakika tano, alipoona hakuna cha maana aliwasha gari na kuondoka.
Akiwa yupo kwenye gari yake akitembea tembea mitaani, akapita katika shule anayo soma Hemedy, bahati nzuri ndio akawakuta wanafunzi mida hiyo ndio wanatoka shuleni hapo, kwambali alimuona Hemedy akitoka ndani ya shule hiyo, akapaki gari pembeni na kumuita, Hemedy alipoona kuwa alie muita ni Koplo Taure, akenda hadi kwenye hiyo gari, Koplo Taure akampa ishara apande na yeye bila kubisha, akazunguuka upande wa pili na kupanda kwenye gari.
Wakasalimiana na Koplo Taure akaomba kumpeleka Hemedy hadi nyumbani kwao(nyumbani kwa Mrutu) hapakuwa na pingamizi lolote safari ikaanza huku wakiwa wanapiga stori.
*****************************
“Hapana bwana leo zamu yenu kuja kwangu"
“Thawa kama ndio unavyotaka, thatha umemtaarifu na Moto?"
“Moto nimeshampigia simu tayari akasema tukutane huko huko kwangu, yani hapa ilikuwa ndio nakutaarifu wewe tu"
“Bathi thawa, acha mimi nijiandae nije"
Baada ya kuongea na Mata, Mrutu alimuachia duka mfanya kazi wake, akafunga safari hadi nyumbani kwake, alipokuwa njiani, gari yake ilipata pancha, hakuwa na jinsi ikabidi aiyache kwa fundi na yeye akanza safari ya kwenda kwa miguu nyumbani kwake, bahati ilikuwa kwake kwasababu hapakuwa mbali sana na nyumbani kwake, baada ya robo saa akawa tayari ameshafika kwake akawakuta Moto Na Mata wanamsubiria.
“Mbona upo kwa miguu, gari yako ipo wapi?" Mata aliuliza.
“Imenipatia pancha nikaona niiyache kwa fundi, na wewe mbona sioni gari yako, ipo wapi?" Mrutu alijibu na yeye akauliza.
“Mimi gari yangu ameondoka nayo mdogo wangu baada ya kunileta hapa kwako"
“Poa basi tuingieni ndani"
Wote watatu wakaingia hadi ndani, Moto na Mata wakakaa sebuleni wakimsubiria Mrutu aliengia chumbani kwake mara moja.
Wakati huo huo Koplo Taure na Hemedy walikuwa tayari wamefika nyumbani kwa Mrutu.
“Sasa si unaenda kubadilisha nguo halafu tunaenda nyumbani kwangu au sio?"
“Itabidi iwe hivyo kwasababu sina chakufanya hapa, ngoja nikabadilishe nguo halafu tunaondoka wote"
“Sasa Baba yako akirudi halafu akikuta wewe haupo, utamuambiaje utakapo rudi?"
“Nita muambia nilikuwa na wewe"
“Haya poa basi fanya haraka mimi nakusubiri. au twende wote huko huko ndani"
Koplo Taure akashuka kwenye gari yeye na Hemedy, wakaongoza kuingia ndani ya nyumba ya Mrutu, kwakuwa Mrutu alimuachia Hemedy funguo yake ili atapo wahi kurudi shule asipate tabu ya kumsubiri hadi yeye atakapo rudi, hivyo Hemedy alikuwa na funguo yake, akafungua geti na kuingia hadi ndani ya uzio wa nyumba hiyo, wakawa wanauelekea mlango wa kuingia ndani ya nyumba hiyo, Hemedy akatayarisha funguo ili afungue mlango huo.
“Au twende tu hivi hivi Anko Taure" Hemedy aliacha kufungua mlango na kumgeukia Koplo Taure.
“Kwanini?"
“Nahofia kama akirudi halafu akakuta sipo anaweza akazingua, lakini kama nikirudi na nguo za shule hatoweza kuzingua"
“Akikuuliza mbona umechelewa wewe utamjibu nini?"
“Nitamuambia kuwa leo tumecheleweshwa kutolewa, halafu pia si hatuto kaa sana, kwahiyo wewe usijali"
“Au kama vipi acha mimi nikuache tu, siku nyengine ukipata muda mzuri nitakupeleka nyumbani kwangu"
“Hapana twende wote leo"
“Kwanini unang'ang'ania twende leo, au unadhani sito kupeleka nyumbani kwangu?"
“Hapana sio hivyo, ila sasa mimi nitabaki na nani hapa, nyumba yote hii nikae pekeangu, sitoweza kumsubiria Baba mdogo hadi atakapo rudi"
Alisema hivyo kwa kuwa hakuliona gari la Mrutu hapo kwenye maegesho, kwahiyo akadhani labda huenda ikawa bado hajarudi.
“Haya poa twenzetu"
Wakaanza safari ya kuondoka hapo, wakaenda kwenye gari na kuelekea nyumbani kwa Koplo Taure, walipo fika wakaingia ndani kwavile Hemedy bado hajala, ikabidi Koplo Taure atoke nje ya nyumba yake na kwenda katika banda la chipsi lililokuwa karibu na nyumba yake, akanunua chipsi vipimo viwili, baada ya kupatiwa chipsi zake na kulipa, akarudi nyumbani kwake, akampatia Hemedy mfuko mmoja wa chipsi na yeye akabaki na mmoja, wakawa wana kula, baada ya kumaliza kula wakaendelea na stori nyengine.
Raskazoni, Katika nyumba ya Mr Bakari Haneni. 10:20 Jioni.
Ilionekana gari aina ya Verosa ikikunja kona ya upande wa kulia kuashiria kuwa inataka kuingia katika jumba hilo linalo milikiwa na Mr Bakari Haneni muuzaji wa madawa ya kulevya, gari hiyo ilipofika karibu na geti la kuingilia humo ndani, geti lilijifungua lenyewe na kufanya gari hiyo kuingia humo ndani, likaenda hadi katika maegesho ya magari kwenye jumba hilo, wakashuka Tito na Tobi kwenye hiyo gari wakiwa mikononi mwao kila mmoja amebeba briefcas nyeusi.
Ghafla wakasikia sauti ya kupigwa kwa mluzi walipo tafuta sauti hiyo inatoka wapi ndipo macho yao yalipotua juu ya nyumba hiyo ya gorofa na kumuona Bosi wao Mr Bakari Haneni akiwa amekaa kwenye kiti cha thamani kilicho tengenezwa kwa mbao huku pembeni kukiwa na wanawake wawili wanao mpepea, akawaonyesha ishara ya kuwaita na wao bila pingamizi walianza kwenda mdogo mdogo, wakatumia ngazi kufika huko juu alipo bosi wao.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naona Mkuu upo huku juu unaangalia mandhari ya bahari ya hindi na kupata upepo wake mwanana tu" Tito alianzisha mazungumzo baada ya kufika mbele ya bosi wao.
“Nina wasiwasi gani wakati kila ninacho kitaka nakipata bwana" akanyamaza kidogo na kuwa angalia wale wanawake“tupisheni kidogo ila mmoja kati yenu alete vinywaji hapa"baada ya kuondoka kwa wale wanawake, akawageukia wakina Tito na kuwaambia wakae kwenye viti vyengine vilivyokuwepo hapo hapo, baada ya dakika kadhaa vinywaji vikaletwa ikawa sasa kila mmoja ana kinywaji chake.
“Enhee nipeni habari vijana wangu"
“Kazi imekamilika, walikuwa wanataka kutuchezea mchezo ambao sisi tumeuanza kabla yao, wameushindwa na kukimbia"
“Imekuaje?" Mr Bakari Haneni aliuliza.
“Tumekubaliana tufanye biashara ya kiamani, ila baada ya makabidhiano wao wakajifanya wajuaji, wakataka kutudhulumu, yani wachukue mzigo wetu na pesa zao, ila wakawa wameingia choo cha kike, hawakujua kwamba wanafanya biashara na watu ambao biashara hizi tumezianza kabla hatuja toka kwenye matumbo ya mama zetu, kibao kika wageukia wao, wakakimbia wameacha pesa zao na mzigo wetu na vyote viwili tukaondoka navyo sisi"
“Safi sana, kwahiyo mmeondoka na mzigo wetu na hela zao?" Mr Bakari Haneni akauliza tena kama hajasikia kile alicho ambiwa.
“Ndio, tumeondoka navyo vyote"
“Safi, embu nionyesheni"
Wakafungua briefcas walizo kuja nazo na kumuonyesha bosi wao, alitabasamu na kuwapa ishara ya kuzifunga na wao wakazifunga.
“Safi sana vijana wangu, mnajua kwamba ninawaamini kuliko kijana yoyote nilie wahi kuwa nae, kwasababu kazi zangu mnazifanya kwa umakini mkubwa sana"
“Ila sasa Mkuu, mimi naona kama vile hawatokubali kushindwa, lazima tu walipize" Tobi alisema
“Hahaha mimi najiamini sana, kwanza hawana taarifa zozote kuhusiana na sisi, halafu wao wana mtandao mdogo sana kwahiyo hawawezi kushindana na mimi hata kidogo" Mr Bakari Haneni alijigamba.
“Tuachaneni na hayo, vipi kuhusu pesa zetu kwa Mrutu?" Aliuliza tena.
“Dah!! Mkuu yule mtu bado mimi sija muelewa kabisa yani" Tito alijibu.
“Kwanini?"
“Yani kila nikimpigia simu ananiambia nimvumilie tu, kila siku hilo ndio jibu lake, sasa mimi nashindwa kumuelewa"
“Naona sasa ameamua kuvunja uaminifu kabisa"
“Hapo ndio nashindwa kuelewa Mkuu"
“Halafu si umesema kwamba ana mtoto ambae anamlea?"
“Ndio Mkuu?"
“Basi itabidi huyo mtoto atekwe mara moja halafu tuone sasa kama hatoleta pesa zetu" Mr Bakari Haneni alisema.
“Ila Mkuu je kama asipo mfuatila huyo mtoto, si itakuwa tumefanya kazi ya bure tu, kwanza mtoto mwenyewe sio wake ni wa kaka yake ambae sasa ni marehemu"
“Hilo nyie lisimipe wasiwasi, tukimteka huyo mtoto halafu asipo mfuatilia sisi tunamuua tu huyo mtoto halafu tutajua jinsi gani ya kurudisha pesa yetu, yule ni mtoto mdogo sana kwangu kwanza kazi yenyewe tumefundisha sisi"
“Kama ni hivyo hakuna tabu, sisi tupe amri tu ni lini tuka mchukue, kazi rahisi sana hiyo" Moyo alisema.
“Msijali tumuangalie kwa hizi siku mbili, asipo leta pesa zetu, basi haina budi hiyo kazi kufanyika"
“Sawa Mkuu"
“Kwanza mmenifurahisha baada ya kurudi na mzigo wetu na hizo pesa za wale wapumbavu, sasa chakufanya sasa hivi, chukueni milioni Tano mkagawane, nataka vijana wangu mufurahi na nyie"
Baada ya kuongea hivyo Tito alifungua briefcas moja iliyo kuwa na vibunda vya noti za elfu kumi kumi, akachukua kibunda kimoja, na kuifunga briefcas, wakaaga na kuanza safari ya kwenda kufurahi kama walivyo ambiwa, wakashuka ngazi hadi chini na kuiyendea gari yao waliyokuja nayo na kutoka hadi ya nyumba hiyo, wakashika uwelekeo wa Hospitali ya Bombo, baada ya kuivuka hospitali ya Bombo, mbele kidogo wakakunja kulia kuingia Hobours club, wakaenda kuimalizia siku yao hapo.
Nyuma kidogo, muda ambao Koplo Taure na Hemedy walivyo ghairisha kuingia ndani ya nyumba ya Mrutu..
Mrutu aliengia ndani ya chumba chake, baada ya muda kidogo akatoka hadi sebuleni alipo waacha Moto na Mata.
“Vipi, mbona kama vile mnashangaa shangaa kuna nini?" Mrutu aliwauliza swali hilo baada ya kuwaangalia wakina Mata usoni na kuona wakiwa kama kuna kitu wanakitafakari vichwani mwao.
“Thio hivyo, ila kuna thauti dha watu tume dhithikia wakiongea ongea thatha ndio tuna jiulidha nidha kina nani"
“Hizo sauti mumezisikia wapi?"
“Huko nje"
“(akauwendea mlango wa kutokea nje, akaufungua na kuangaza angaza, akarudi tena ndani) Nyie mna matatizo mbona huku nje hakuna watu?"
“Bathi labda itakuwa tumethikia vibaya, lakini tume dhithikia kabitha yani"
“Eti Moto ni kweli hata wewe umeziskia hizo sauti za watu?"
“Ndio, hata mimi pia nimezskia"
“Walikuwa wanaongea nini?"
“Hatuja sikia vizuri walichozungumza zaidi ya minong'ono tu"
“Basi tuachaneni na hayo, tuendelee na yaliyo nifanya nimiite hapa, ni hivi Hemedy ninae hapa nyumbani" Mrutu alidhani labda akiwaambia taarifa hiyo wenzake watafurahia lakini ndio kwanza kila mmoja akawa yupo katika hali yake ile ile ya kawaida.
“Huyo Hemdy ndio nani?" Mata aliuliza.
“Aaaaaah!!!!!! Kwahiyo mnataka kuniambia hamumjui Hemedy leo hii??
“Tungemjua tunge kuuliza? Embu acha uswahili basi tuambie ni nani? Moto aliongea.
“Sawa, Hemedy si huyu mtoto wa marehemu mzee Mheshimiwa"
“Kwahiyo unaponae hapa nyumbani kwako?" Mata aliuliza kwa mshangao ulio changanyikana na furaha.
“Ndio, nipo nae hapa nyumbani"
“Usha muua.....aaah ushamuuliza kuhusu hiyo flash kama anayo yeye?" Moto aliuliza kwa wahka.
“Hapana bado sijamuuliza"
“Halafu si umesema yupo hapa kwako? Isije ikawa anatusikia tunacho zungumza" Moto alionyesha wasiwasi wake.
“Hapana, ameenda shule bado hajarudi"
“Ila sio yeye kweli aliekuwa anaongea hapoa nje?" Moto alipo sema hivyo Mrutu na Mata wakashtuka, Mrutu akainuka haraka akaenda nje kwenda kuangalia vizuri, akaizunguka nyumba nzima ila hakuona mtu, akatoka hadi nje kabisa ya uzio huko napo pia hakuona mtu, ikabidi arudi tu hadi sebuleni walipo wenzake.
“Tusijitie presha bure kwanza hajarudi shule bado na kama ingekuwa ni yeye aliekuwa akiongea hapo nje sasa itakuwa alikuwa akiongea na nani? na kwanini asiingie ndani?"
“Thatha kama akirudi shule halafu akitukuta je itakuaje?" Mata aliuliza.
“We nawe una muhofia mtoto mdogo yule, si ndio hapo tutakapo muulia hapa hapa" Moto alisema.
“Aaa aaa!!!! Hapa kwangu sitaki afe mtu, sitaki kesi mimi" Mrutu aliongea.
“Sasa wewe ulikuwa unataka afie wapi?" Moto aliuliza.
“Afe popote lakini sio hapa kwangu, sitaki kesi mimi"
“Sawa, halafu kwanini huja muuliza kama ile flash yenye video la tukio zima kama anayo yeye?"
“Nitamuuliza vipi, wakati mtoto mwenyewe nimekabidhiwa jana tu"
“Basi tumsubirini hapa hapa akirudi tutamuhoji kama anayo yeye, au nyie mnasemaje?"
“Je kama hiyo flash yeye hana?" Mata aliuliza.
“Hamna jinsi zaidi ya kumuua tu na..."
“Lakini sio hapa kwangu" Mrutu alimkatisha Moto.
“Hafi hapa kwako bwana"
“Haya tumsubirini nahisi muda si mrefu atarudi kutoka shule"
Wakakubaliana wamsubirie Hemedy hapo hapo kwa Mrutu. Wakamsubiri.
Muda ambao wana msubiri Hemedy arudi shule ili wamuhoji maswali yao, ndio muda ambao Koplo Taure na Hemedy ndio wapo kwenye gari wanakuja nyumbani kwa Mrutu, baada ya mwendo wa dakika kadhaa, walifika nyumbani kwa Mrutu, wakateremka wote kwenye gari na kuliendea geti, wakazama hadi ndani.
“Mimi nilikuambia atakuwa bado hajarudi, si unaona hata gari yake haipo" Hemedy alimuambia Koplo Taure huku wakiuwelekea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo.
“Kwahiyo ndio unanisuta?" Koplo Taure alimwambia Hemedy huku akicheka.
“Hapana sikusuti ila wewe ulikuwa m'bishi, hukutaka tu nikae nyumbani kwako ndio maana ukani harakisha hivi"
“Hahahahah wewe dogo mpumbavu sana, sasa mimi nikuharakishe kwa kipi hasa, wewe si ulisema tusichelewe kurudi kwa kumuhofia baba yako"
Hemedy hakusema kitu, muda huo alikuwa anatia ufunguo kwenye kitasa, mlango ukakubali akaufungua, ulipofunguka, akapigwa na butwaa baada ya kutupa macho yake kwenye masofa yaliyokuwepo hapo sebuleni, akabaki ameganda tu mlangoni, Koplo Taure baada ya kuona Hemedy ameganda mlangoni haingii ndani, akataka kujua ni kipi alichokiona Hemedy humo ndani na yeye akapenyeza kichwa kuchungulia hapo sebuleni......
“Vipi, mbona mnanishangaa hivyo?" Mrutu aliwauliza wakina Hemedy waliokuwa bado mlangoni wameganda wakimshangaa yeye.
“Umefika saa ngapi hapa nyumbani?" Hemedy aliuliza.
“Mimi mbona nimefika muda tu, nimekusubiri kweli naona hutokei, kwani shule ndio mnatoka(akaangalia saa iliyokuwepo hapo ukatani) saa kumi na mbili?" Mrutu akajibu na yeye akauliza.
“Hapana nilikuwa kwa anko Taure, ila shule tumetoka tangia saa tisa na nusu" Alijibu na kuondoka hapo mlangoni ambapo alikuwa ameganda akimshangaa Mrutu, aliingia ndani na kumfanya Koplo Taure na yeye kuingia ndani, akaenda kukaa katika sofa moja wapo.
“Mbona gari sijaiona hapo nje?" Hemedy aliuliza huku akielekea mlango wa chumbani kwake.
“Gari nimeiacha kwa fundi, imepata pancha wakati naja hapa nyumbani"
Hemedy baada ya kusikia hivyo akafungua mlango wa chumba chake na kuingia humo ndani.
“Niambie Mrutu"
“Shwari, vipi kaka"
“Safi tu, kumbe ulikuwa upo nae huyu tangia muda wote?"
“Ndio, nilikuwa nipo nae tangu anatoka shule"
“Ulienda nae wapi?"
“Nimeenda nae nyumbani kwangu tu, kuna muda tulikuja hapa tukakuta nyumba tupu haina mtu, ndipo hapo aliponiambia tuondoke wote"
“Mliingia hadi humu ndani?"
“Ndio tulifika hadi hapo nje ila hatukuingia ndani, ndipo alipo niambia tuondoke tu, aisee ila huyu dogo ni mjanja sana, unajua alikataa kabisa kubadilisha nguo za shule kwa kuhofia eti akirudi unaweza ukamuuliza alikuwa wapi"
“Hahahah huo sio ujanja ni upumbavu, sasa alicho hofia ni nini, wakati mimi nimempa uhuru wa kufanya chochote ila tu asivuke mipaka"
Hemedy alifika hapo sebuleni na kujumuika nao, wakaendelea na maongezi yao hadi pale Koplo Taure alipoaga na kuondoka zake, Hemedy na yeye akaingia chumbani kwake kwenda kujisomea.
Turudi nyuma kidogo muda ambao Hemedy na Koplo Taure ndio wanaingia kwenye nyumba ya Mrutu.
“Nahisi itakuwa ndio huyo hapo ana rudi, maana nasikia sauti ya geti kufunguliwa" Aliongea Mrutu.
“Mbona nasikia kama kuna mtu anaongea nae" Moto alipoongea hivyo, Mrutu akainuka na kwenda hadi dirishani na kumuona Hemedy ameongozana na Koplo Taure, alichanganyikiwa hakujua afanye nini kwa wakati huo, aliwaona wakizidi kuukaribia mlango wa kuingia hapo ndani, akatoka fasta dirishani hapo na kuwaendea wakina Moto ambao walikuwa katika sintofahamu, hawakujua ni kwanini mwezao amechanganyikiwa kiasi hicho, ikawalazimu wasubiri awaambie ni kipi kilicho mchanganya hivyo.
“Askari, polisi" Nyoyo za kina Mata zilipa “Paaaa!!!!!" baada ya kusikia neno Askari, na wao wakachanganyikiwa hawakujua wafanye nini, Mata alichukua mto wa sofa akajifunika nao usoni na kupelekea wenzake wamcheke kimya kimya.
Mrutu akaona akiendelea kupoteza muda hapo watakutwa na itakuwa mambo mengine, wao hawakumuhofia Koplo Taure ila walimuhofia Hemedy anaweza akawataja kwa askari huyo na kusababisha mengine, Mrutu akawachukuwa na kuwapeleka hadi chumbani kwake, akawafungia humo na yeye akawahi kurudi sebuleni na kutulia kwenye sofa, baada ya sekunde kadha ndipo mlango ulipofunguliwa na Hemedy kupigwa na butwaa baada ya kumuona Mrutu yupo ndani ikiwa yeye alidhani labda itakuwa bado hajafika.
Turudi sasa muda huu.
Baada ya Koplo Taure kuondoka na Hemedy kuingia chumbani kwake, Mrutu aliwafuata wakina Moto na kuwatoka nje ya nyumba hiyo.
“Thatha thi tuende tukamuhoji yule dogo kule ndani?" Mata aliuliza.
“Hapana nyie nendeni mimi nitawatafuta tupange jinsi gani ya kukamilisha huu mpango"
“Kwanini tuthiimalidhe hii kadhi thatha hivi?" Mata aliuliza.
“Mbona Mata wewe ni mbishi? Kwani mimi sinimewaambia nyie nendeni halafu tutapanga jinsi gani ya kukamilisha hii ishu"
“Haya kama ndio unavyotaka acha thithi tuende ila uthithahau kumuuliza kama hiyo flash anayo"
“Msijali nitafanya hivyo"
Baada ya kuagana na wakina Mata, alirudi ndani na kupitiliza hadi chumbani kwake, akafikiria atumie mbinu gani kumuhoji Hemedy ili ajue kinacho wasumbua“Lakini yule ni mtoto mdogo hawezi kunishinda maarifa, ngoja nikamuite" baada ya kuwaza hivyo aliinuka akenda chumbani kwa Hemedy, akamkuta bado anajisomea“Embu njoo sebuleni mara moja" alivyomuambia hivyo akatoka hadi sebuleni na kumsubiri Hemedy baada ya dakika mbili Hemedy nae akaja pale sebueleni, akaka kwenye sofa jengine tofauti na lile alilo kaa Mrutu.
“Embu naomba unielezee tukio zima lilivyotokea hadi kupelekea vifo vya wazazi wako" Mrutu akanzisha mazungumzo.
Hemedy akatulia kama kama sekunde thelathini, akanza kumuelezea.
“Tulikuwa tumekaa sebuleni, mara ghafl........" akamuelezea tukio zima lilivyokuwa, alipo maliza kumuelezea akanza kulia, ikabidi Mrutu ambembeleze, baada ya muda akatulia.
“Ila si unajua kama ile nyumba ina kamera za ulinzi?" Mrutu akamuuliza swali la kimtego.
“Ndio najua"
“Mbona kunasiku nilienda kwenye kile chumba cha kuongozea kamera ili nichukue ushahidi wa video ya tukio lakini nikakuta ile video haipo?" Mrutu alimuuliza swali jengine la kimtego baada ya lile la kwanza kufanikiwa.
Hemedy hakujua amuambie ukweli au amfiche kama alivyoambiwa na Goda, akabaki njia panda asijue amjibu kitu gani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi sijui" akajibu kiufupi.
“Sasa nani ambae kaichukua ile video wakati kile chumba ni cha siri, ingekuwa Goda ni mzima ningesema labda ni yeye ndie kaichuku au kuna mtu mwengine ambae Baba yako alimuonuesha kile chumba?"
“Sijui"
“Mbona kila kitu hujui, we mtoto ni mpumbavu nini? Au wewe ndio umeichukua ile video halafu unanificha?" Mrutu aliongea kwa hasira na kumfanya Hemedy aanze kuogopa, baada ya kuona anakaripiwa sana akaanza kulia huku akisema neno moja tu kwamba hajui. Ikabidi Mrutu ashushe sauti yake na kumbembeleza tena Hemedy.
“Usione hivi mwanangu ni hasira tu zile kwahiyo nyamaza tutawapata tu wauwaji wa wazazi wako, ok nenda kaendelee na kusoma acha mimi niandae chakula cha usiku"
Hemedy alinyanyuka na kwenda chumbani kwake, akakaa juu ya kitanda na kuanza kufikiria yaliyotokea muda mfupi ulio pita.
“Mbona kila kitu hujui, we mototo ni mpumbavu nini? Au wewe ndio umeichukua ile video halafu unanificha?"
Maneno hayo yalijirudia kichwani mwake na kuyafikiria mara mbili mbili“Kwanini anigombeshe namna hii ikiwa tayari nimemuambia kuwa video sinayo mimi? Aaaa! lakini huwenda ikawa anataka kunisaidia kweli kuwatafuta wauwaji wa wazazi wangu, sasa sijui nimpee au nikae nayo tu" akainuka na kwenda kwenye kabati la nguo zake, akafungua kabati na kuitoa flash na kwenda nayo kwenye kitanda, akakaaa“ Sasa mimi hii flash nitaitumia vipi kuwapata wauwaji wa wazazi wangu, acha tu nimpe, siku akiniuliza tena nitampa" baada ya kuwaza hayo, akaiweka flash kwenye meza yake ya kusomea na kuendelea kusoma.
Koplo Taure baada ya kutoka nyumbani kwa Mrutu, akafikiria aende wapi kuimalizia siku hiyo, ndipo alipo pata wazo la kwenda baa ila hakujua ataenda baa gani, baada ya kuwaza kwa muda mfupi, akatoa simu yake na kuingia sehemu ya majina, akatafuta kwa sekunde kumi, alipo lipata jina alilo kuwa analitafuta, akapiga na kusubiri kwa sekunde kadhaa, akaanza kuongea, “Hellow, mimi mzima sijui wewe, ok nataka nikutane na wewe leo hii, sasa hivi ndio, hobours club?, basi poa mimi ndio naelekea hivi, ok" akakata simu baada ya kumaliza kuongea na huyo alie mpigia, akaenda nyumbani kwake, akaoga na kubadilisha nguo, alivaa tisheti nyeupe na jinzi nyeusi, chini akavaa all star nyeupe kumechisha na tishet aliyoivaa, akaenda kwenye kioo na kujiangalia, akatoa tabasamu baada kujigundua amependeza yeye mwenyewe alijisifu“Utafikiri sio Askari vile” akajisemea mwenyewe na kujipigia salut, akacheka na kutoka nje na kupanda kwenye gari yake, akaelekea sheli, akaongezea mafuta kiasi kwenye gari yake, baada ya kutiliwa mafuta akaenda alipo ahidiana na mtu alieongea nae kwenye simu muda mfupi uliopita, akafika hadi hobous club na kukuta baa hiyo imechangamka kwa kuwa na watu wengi siku hiyo, akapaki gari kwenye maegesho, akushuka na kuyaangalia mandhari hayo vizuri, akapiga hatua kuiyendea meza ambayo ilikuwa iko tupu haina watu, akavuta kiti na kutulia hapo.
Baada ya muda kidogo alioneka msichana mrembo alievalia kileo zaidi, akiingia kwenye baa hiyo, karibia wanaume wengi waliokuwemo kwenye baa hiyo walimkodolea macho mnyange huyo na yeye kama alijua vile kwamba anaangaliwa, alitembea kwa mapozi haikujulikana alikuwa anafanya kusudi au ndivyo anavyotembea, maana alitembea kama vile hataki, ila kwambali akasikia sauti ya mluzi ukipigwa, akageuka huku na huko kuangalia ni wapi ulipotokea, akaachia tabasamu baada ya kumuona aliemfuata, akapiga hatua kumuendea Koplo Taure, alipofika Koplo Taure akainuka na kuachia tabasamu huku akimpa mkono mrembo huyo ambae alifanikiwa kuwapumbaza wanaune karibia wote kwenye baa hiyo, bila ajizi aliupokea mkono wa Koplo Taure, Koplo Taure nae bila ya kuongea lolote akauwinua mkono wa mrembo huyo na kuupeleka hadi mdomoni kwake na kuubusu, mrembo huyo aliishia kutabasamu tu.
“Karibu" Koplo Taure baada ya kuuachia mkono wa mwanamke huyo, akavuta kiti chengine na kumkaribisha mwanamke huyo.
“Asante" alijibu akiwa bado tabasamu lipo usoni mwake, kisha akaka kwenye kiti alichokaribishwa.
Muhudumu alifika katika meza yao, wote wawili wakaagiza soda aina ya fanta kusindikiza maongezi yao.
“Kwajinsi ulivyo pendeza mtu anaweza akabisha akiambiwa kuwa wewe ni askari" Koplo Taure alianzisha maongezi.
“Mbona hata kwako pia ni hivyo hivyo, nilikusahau kwa muda baada ya kukuona, leo ndio nimeamini kuwa zile gwanda za polisi wala hazikupendezi, ukizivaa zinauficha uzuri wako, wewe ni handsome sana, najivunia kuwa na wewe"
“Hata mimi najivunia kuwa na wewe Jesca, nina sababu zaidi ya milioni za kujivunia kuwa na wewe, unajua kwamba uzuri wako umewafanya wanaume wengi waliokuwepo hapa kukuangalia wewe hadi nikapata kijiwivu kidogo".
Wakaendelea na mazungumzo yao hawa maaskari wawili wanaofanya kazi kituo kimoja.
Tito na Tobi walikuwa bado wapo kwenye baa hiyo hiyo wakiendelea kunywa pombe baada ya kupewa pesa na bosi wao na kuja kuimalizia siku yao hapo, tangia saa kumi na mbili jioni, walikuwa hapo hadi muda huu wa saa tatu usiku bado wanaendelea kunywa.
“Oyaaaaa Tiiitoooo" Tobi alimuita Tito kwa sauti kubwa baada ya pombe kumkaa kichwani.
“Nambieeee Tobiii" Tito nae alijibu kwa sauti ya kilevi.
“Unamuona yule demuu"
“Yuko wapiii?"
“Yulee kulee aliekaa na yuleeee boyaaa"
“Ndio nimewaona, sii wale kule waliokaa kwenye meza ileee paleee"
“Ndio hao hao, sasa mimi namtakaaa yule demu, natakaa niondoke naee nikamto**** nimuache yule boya akilia pekeake pale"
“Nakwaminia Tobiii, nenda kamporee yuleee booyaa, kwanzaa wewee una helaaa, hawezi kuchomoaaa kabisaa"
“Poa mwanangu acha mimi niendeee nikamchukue yuleee demuuu tuondokeee naeee au wewe unasemajeee?"
“Hivyoo hivyoo tu"
Tobi aliinuka kwa kupepesuka na kwenda kwenye meza waliyokaa mtu na mpenzi wake, alitaka kwenda kufanya vurugu amchukue msichana alie kaa na mtu wake.
“We boyaaa, mbona umekaaa na demu mzuriiii halafu unaonekana mchomvuu tu, mademu hawa ni wakwetu sisi, wee kapuku utampeleka wapiii mtoto mzuriiii kamaa huyuuu, embuu nipishee nimchukue mimi"
Tobi alianza kuropoka baada ya kuifikia meza ya wapenzi wale, ila katika watu wale wawili hakuna hata mmoja aliemsemesha, wote wakawa kimya wakimuangalia mlevi huyo anavyo ropoka.
“Yaanii mimi naongeaaa na wewe boyaa halafu unajifanya hunisikii, kwanza unanijua mimi ni nani? Eeeeeee si nakuuliza wewe fala, unanijuaa mimi ni nanii?"
Bado watu wale walikaa kimya tu wakimsikiliza anavyoropoka, si kwamba huyo anaeitwa boya alikuwa akimuogopa huyu mlevi, hakuwa akimuogopa bali alikuwa anasubiri afanye kitendo chochote cha kijinga ili amuonyeshe kazi.
“Naona hunijui mimi vizuri shogaa wewe, oyaaa Tito(akamgeukia Tito) mimi namfanyia huyu fala kum*****ke" alivyoongea hivyo akarusha ngumi iliyoenda usawa wa uso wa huyo jamaa, ila jamaa aliyona akaikwepa, Tobi baada ya kuona ngumi yake imekwepwa akarusha kofi lilioenda usawa wa shavu la huyo jamaa, jamaa akarudi nyuma kidogo na kuudaka mkono wa Tobi, akafanya kama vile anakamua nguo, Tobi akapiga kelele za uchungu huku akikunja sura yake, jamaa baada ya kuona ameridhika na adhabu hiyo aliyompatia, akauwachia mkono wake na kutulia pale pale kwenye kiti, akimsubiria afanye kitendo chengine cha kipumbavu amuadhibu tena.
Tukio lote hilo lilikuwa likishuhudiwa na Koplo Taure na Afande Jesca, walikuwa kimya wakiuwangalia mchezo mzima.
“Yani wewe mse**** ndio umenifanyia hivi, hujui kama unachezaa na mtu hatariii"
Akachukua chupa ya bia iliyokuwepo hapo mezani na kuivunja chini, akabakiwa na kipande cha chupa, ikawa anamfuata jamaa kwa kasi ili akamchome na hicho kipande cha chupa, Jama baada ya kuona akimlegezea sana huyu mgeni asiekuwa na adabu anaweza akamdhuru kweli, akainuka kwenye kiti tayari kupambana na huyu mgeni asie na adabu, akapanga kumfundisha adabu, Tobi alikuja mbio mbio huku akipepesuka, kipande cha chupa akikielekeza mbele tayari kwa kumchoma nacho cha tumbo jamaa, Jamaa baada ya kuona Tobi anamletea kipande cha chupa usawa wa tumbo lake, akasogea pembeni kidogo na kuupiga teke mkono wa Tobi uliokuwa umeshika kipande cha chupa na kufanya kipande hicho kiruke pembeni, akampiga ngumi mbili za uso za haraka haraka, na kumfanya Tobi mikono yake yote miwili aipeleke usoni mwake, baada ya sekunde kumi na tano, akatoa mikono usoni na kumuangalia jamaa aliekuwa bado kasimama akimsubiria afanye kitendo chengine cha kipumbavu.
“Haaaa!!!! Yani umenipiga ngumi zakooo halafu bado umesimama mbele yanguuu, naona hunijui vizuri, mimi sishindwi kukuua hapa hapa na hakuna atakae nifanya chochote, nakuua halafu naendaa mwenyewe polisi, na ninakuambia nitatokaa tuu, wewee unamjua Mr Bakari Haneniii? sasa yule mimi ndio bosi wangu, nakuua halafu huko polisi najakutolewa usiku huu huu, subiri nikuonyeshe kwamba mimi sitaniii ninapoongea"
Tito muda wote akimuangalia mwenzake anavyoleta vurugu hapo, ila baada ya kumsikia Tobi anamwambie yule jamaa asubiri ili amuonyeshe akajua moja kwa moja anataka kutoa bastola, akainuka ili amuwahi kabla haja haribu, ni kweli kama alivyowaza ndivyo Tobi alivyotaka kufanya, akapeleka mkono wake ubavuni mwake akitaka kuchomoa bastola ila kabla hajaitoa Tito aliwahi kumzuia.
“Tito niachee ni muonyeshe huyu fala, nasemaaa niaacheeeee, niacheeee, hawezi kunipiga halafu mimi nikamuangalia tu"
“Tobi twenzetuuu utaharibu, sio mahala pake hapaa, embu twende achana na huyo boyaa" Tito aliongea hivyo huku akimvuta Tobi watoke nje ili waende zao.
“Nakwambiaje, nitakutafutaaa tuu kum*****ko, yani wewe ni boyaa tuu, nishakumaki sura nitakutafutaaa nakwambiaa" Tobi aliendelea kutukana huku akikokotwa na Tito hadi kwenye gari yao na kuingia humo, Tito alikamatia usukani wa gari hiyo na kuanza safari ya kuondoka hapo.
Koplo Taure na Afande jesca waliliona tukio lote hadi pale Tobi alipotaka kuchomoa bastola pia waliishudia bastola iliyokuwepo kiunoni kwa Tobi baada ya kupandisha shati alilovaa ili aichomoe, wakapanga wakiondoka na wao wa waungie tela ilikujua mwisho wao ni wapi.
“Kila sehemu ninapokuwa, basi ujue nipo kazini, acha tuwafuate" alisema Koplo Taure na kunyanyuka kwenye kiti na kuianza safari ya kuwafuata wakina Tito akifuatiwa na Afande Jesca kwa nyuma, kwa kuwa walishalipia vinywaji walivyotumia, kwahiyo hakukuwa na mtu alie wasumbua, wakaenda kwenye gari aliyokuja nao, wakaingia wote wawili na kuianza safari ya kuwafuata wakina Tito.
“Wale watu mimi nina mashaka nawo, nahisi sio watu wakawaida" Koplo Taure aliongea huku akiendesha gari mbio ili kuwawahi wakina Tito ambao walikuwa wakielekea njia ya Mkwabi Supermakert baada ya kuivuka Toyota.
“Hata mimi pia nimewaza hivyo hivyo"
“Halafu wamenitia wasiwasi baada ya kusema kwamba ni watu wa Mr Bakari Haneni"
“Sasa hapo wasiwasi wako upo wapi, kwani umefikifia nini baada ya kusema wao ni watu wa Mr Bakari Haneni, kumbuka yule ni tajira na ana watu wengi wanaomfanyia kazi yeye?"
“Kuna hali ambayo si ya kawaida nimeiyona ila usijali nitakuambia"
Waliendelea kuwafuta nyuma nyuma mpaka pale walipo lipita jengo la Club Lavida Loca na kukunja kushoto lilopo jengo la Uhamiaji(Migration) na kuelekea ilipo garden ya uhuru park, waliipita uhuru park na kuifuata Hosteli, walinyoosha moja kwa moja wakaipita round about ya mabanda ya papa wakanyoosha moja kwa moja, wakakipita kituo cha polisi mabawa na kunyoosha hadi chuo cha komesho na kukunja kulia kuelekea majengo, mbele kidogo baada ya kuvuka tuta, wakakunja kushoto kabla hawajaufikia msikiti wa majengo, wakaenda mbele kidogo na kusimama nje ya nyumba nyeupe yenye geti jekundu, Tito akashuka na kuliendea geti la nyumba hiyo na kulifungua lote, akarudi tena kwenye gari na kuliingiza ndani ya nyumba hiyo, akaliweka kwenye maegesho na kushuka, akaliendea geti na kulifunga vizuri na kurudi kwenye gari na kumkuta Tobi akiwa bado amesinzi kwa pombe alizo kunywa, akamkokota hadi ndani ya nyumba hiyo na kumpeleka katika chumba kimoja wapo, akamuingiza humo na kumlaza kitandani na yeye akatoka hadi kwenye chumba chengine na kujitupa kitandani, ili aisake kesho yake, Aka lala.
“Ntaendelea kuwafuatilia kesho" Koplo Taure aliongea hivyo huku akigeuza gari baada ya kuikariri nyumba waliyo ingia watu hao, akaendesha gari taratibu akiufuata uelekeo wa nyumbani kwake.
“Si tunaenda kulala wote leo?" Koplo Taure alimuuliza Afande Jesca.
“Ukalale na nani?"
“Si na wewe kipenzi changu"
“Na hivyo videmu vyako vya mtaani kwenu, utavilaza wapi?"
“Aaa!! Jesca unajua kabisa hakuna mwengine anaeweza kumpa furaha Sentaure zaidi yako wewe, sasa ni vipi unizushie kuwa nina wanawake wengine? Mimi nakupenda wewe tu na hilo mwenyewe unajua"
“Ndio maneno yenu hayo, hamna lolote nyie wanaume"
“Kwa hapo sikupingi ni kweli hatuna lolote juu ya wale tunao wapenda kama mimi ilivyo kwako wewe. sasa vipi ombi langu la kulala nawewe usiku wa leo?"
“Kwani lazima?"
“Hapana mimi sikulazimishi ila moyo wangu ndio unanilazimisha nikulazimishe, naomba usikatae, kwasabau ukikataa utanifanya usiku wa leo ni uone mkubwa"
“Na kesho kazini je?"
“Kuhusu kazini usijali, tutatega alamu ili ituamshe asubuhi, lakini kwa sasa nomba uufanyie kazi mwili wangu"
“Kwenda uko(huku akimpiga kofi lisilo uma kwenye bega lake)Eti uufanyie kazi nwili wangu, utanilipa?"
“Usijali kuhusu hilo, nitakupa mshahara mzuuri wa penzi naamini utaufurahia huo mshahara"
“(akaingiwa na aibu za kike) Maneno yako hayo"
“Maneno yangu yana nini?"
“Mmh! Basi tuache"
“Sawa, lakini si umenikubalia ombi langu?"
“Nahofia nitachelewa kazini kama nikiamkia kwako, yani nikitoka kwako niende tena kwangu nikajiandae niende kazini, si nitachelewa jamani"
“Basi usijali, hapa tunapitia kwako, unachukua nguo zako za kazi halafu tunaenda kwangu, asubuhi ukiamka tunajiandaa kisha tunaondoka wote au wewe unasemaje?"
“Mmmmh!!! Mwanaume king'ang'anizi wewe, haya twende"
Koplo Taure aliendesha gari huku akitabasamu muda wote“ huna lolote, wakati wewe mwenyewe ulikuwa pia unataka, sema umeamua kuleta viunzi ambavyo nimeweza kuviruka vyote" alijisemea maneno hayo kimoyo moyo.
“Lione uko, linafurahia tu tabia mbaya"
Afande Jesca alisema maeno hayo baada ya kumuona Koplo Taure akitabasamu mwenyewe, ila hakujibu kitu akaendelea nasafari hadi kwa Afande Jesca, wakashuka wote na kuingia ndani ya nyumba hiyo ya kupanga anapoishi Afande Jesca, walipofika ndani ya chumba chake, Afande jesca akachukua nguo zake za kazi na kuziweka kwenye mkoba wake, akachukua na vipodozi na kuvitia kwenye mkoba,(“wanawake bwana, huyu ata akiambia aende eneo lililotokea ujambazi, anaweza akachuku wanja akidhani ni bastola. acheni wanawake waitwe wanawake")Koplo Taure alijisemea baada ya kumuona Afande Jesca akikusanya vipodozi vyake na kuvitia kwenye mkoba.
“Twende" Afande Jesca baada ya kumaliza kila kitu akamuambia Koplo Taure.
“Wapi?"
“Unajua Sentaure usinizingue, nitaghairisha sasa hivi"
(huna uwezo wa kughairisha)alijisemea kimoyo moyo “Tendwe, mpenzi usije ukanuna bure, nikakikosa nilicho kiomba"
Wakatoka nje ya nyumba hiyo, wakapanda kwenye gari kuelekea nyumbani kwa Koplo Taure, walipofika nje ya nyumba hiyo, Koplo Taure akashuka kwenye gari na kwenda kufungua geti, baada ya kufungua akarudi tena kwenye gari ili aliingize ndani.
“Jianaume ji bahili hili, kwani kama ungeweka mlinzi ungepungukiwa wapi kwenye mshahara wako?" Afande Jesca alisema hivyo baada ya Koplo Taure kurudi kwenye gari.
“Kuna mlinzi mmoja muda si mrefu nataka nimuweke ndani humu"
“Nani?"
“Wewe"
“Nyooo!!!!! Nani umuweke mlinzi?"
“Sijamaanisha uwe mlinzi wa getini, bali nataka nikuoe kabisa ili uwe mlinzi wa nyumba yangu"
“Nenda uko, wewe ndio muowaji? Labda yesu arudi"
“Kwahiyo huniamini au?" Koplo Taure aliongea hivyo huku akipaki gari kwenye maegesho ya nyumba hiyo, akashuka kwenye gari ili akafunge geti.
“Ndio sikuamini"
Baada ya kufunga geti, alirudi hadi upande alipokuwa Afande jesca, akafungua mlango wa gari na kumnyoshea mkono Afande Jesca.
“Karibu nyumbani kwetu mke wangu mtarajiwa"
Afande alitabasamu na kuupokea mkono wa Koplo Taure, wakaongozana hadi ndani ya nyumba hiyo, Afande Jesca akabaki kushangaa shangaa mandhari ya sebule hiyo, sio kwamba hakuwahi kuja katika nyumba hiyo, la hasha! Aliwahi kuja karibia mara tatu, ila alishangaa shangaa ilimradi tu iwe basi, wakaongoza hadi chumbani kwa Koplo Taure, walipofika huko, wakaingia bafuni, ambapo lilikuwepo humo humo ndani, walipotoka wakaenda hadi kitandani, Koplo Taure akanza uchokozi wake wa kikubwa.
“Mmh mmh!!! Mbona unaharaka hivyo? Nenda kazime taa kwanza"
KoploTaure kusikia hivyo, akachomoka mbio kama Usain Bolt wa kwenye mashindano ya marathon, sekunde moja ilikuwa nyingi, ikawa tayari amezima taa. mpaka hapo mimi mwandishi sikuweza kuona tena nini kiliendelea baada ya giza kutawala humo chumbani, ila nilichoweza kusikia hapo ni sauti ya kama vile mtu anakula muwa hivi, ila sikutaka kujipa imani hiyo moja kwa moja maana sikuona muwa wowote ndani humo, nikaona isiwe tabu, nikaondoka mdogo mdogo hadi gheto kwangu, nikapanga kuwafuatilia tena asubuhi patakapo kucha. Nikaondoka zangu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*********************************
Nyumbani kwa Mrutu. 12:30 Asubuhi.
Mrutu baada ya kuhakikisha Hemedy ameshajiandaa kwaajili ya kwenda shule, wakaongozana hadi kwenye gari na kuianza safari ya kuelekea shule anayosoma Hemedy, walipofika shule, wakashuka kwenye gari na kuelekea moja kwa moja katika ofisi za shule hiyo kwajili ya kuonana na mwalimu anaewasimamia wanafunzi kwa kila kitu.
“Ndio mwalimu, nataka kuanzia leo hii huyu mwanangu na yeye awe analetwa na kurudishwa kwa gari ya shule, maana mimi sina muda wa kumleta na kumrudisha kila siku" Mrutu aliongea hivyo baada ya salamu na kukaribishwa kwenye kiti ofisini humo.
“Kwahilo usijali, maana huyu aliacha kupanda gari ya shule baada ya baba yake kutaka mwanae amlete na kumrudisha kwa gari yake, sasa kwavile wewe mwenyewe ndio umeamua apande gari ya shule, hakuna tabu, chamsingi ni kuelekeza huo mtaa anao kaa kwa sasa ili aletwe na arudishwe"
Mrutu akamuelekeza mtaa anaokaa, baada ya kuona mwalimu ameujua vizuri, akaaga na kuondoka, akarudi nyumbani kwake kwaajili ya kuijianda kwenda dukani kwake, alipofika akajiandaa vizuri, ila kabla hajatoka kwenda dukani kwake, akaenda katika chumba anacho lala Hemedy, sijui ni kipi kilichomfanya aende ila alienda hadi chumbani humo, akaangaza angaza macho yake chumbani humo, ila ghafla macho yake yakatua kwenye meza ya kujisomea ya Hemedy, akaona kijidude flani kipo hapo juu ya meza, akaiyendea hiyo meza hadi karibu yake, akakuta ni flash ndio ipo hapo juu,(flash hii ndio ile wakina Murutu wanayoitaka kutoka kwa Hemedy) akaichukua na kuigeuza geuza“hii flash ya nini?" alijiuliza mwenyewe, baada ya kuona amekosa jibu, akaona isiwe tabu, akatoka nayo hadi sebuleni na kuiyendea tv ya hapo sebuleni, akaiwasha na kuwasha na deki, ili aijaribu hiyo flash ajue ni ya nini......
Ghafla simu yake iliyokuwa mfukoni mwa surualia aliyoivaa iliita, akaacha kuichomeka flash kwenye deki, akaitoa simu kwenye mfuko na kuangalia nani aliepiga, akaona ni mfanya kazi wake ndio anampigia, akaipokea.
“Enhee!! Niambie kolo"
“Bosi, embu njoo dukani mara moja" sauti iliyotoka kwenye simu iliongea hivyo.
“Kuna nini?"
“Kuna watu hapa mimi siwaelewi wanachokizungumza, labda uje mwenyewe ndio unaweza ukawaelewa"
“Wanataka nini hao watu?"
“Bosi wewe njoo ndio utawaelewa, wanadai wanataka kulifunga hili duka"
“Haya poa nakuja" Mrutu baada ya kusikia kuwa watu hao wanataka kulifunga duka lake, kidogo akachanganyikiwa.
“Wanakuambia ufanye haraka"
Mrutu hakujua watu hao wanao mtaka yeye ni wakina nani na wanataka nini, ikabidi aache alichokuwa anataka kufanya ili kuwahi dukani kwake, akaiyacha flash juu ya deki na kuizima tv na deki, na kuondoka hapo ili awahi dukani kwake.
Baada ya dakika ishirini, akawa tayari amefika dukani kwake, akapaki gari pembeni na kushuka, akaenda hadi dukani na kukuta kuna sura ngeni za watu wa tatu wamesimama hapo dukani kwake.
“Za saa hizi jamani" alianza na salamu baada ya kuwafikia.
“Nzuri, wewe ndio mmiliki wa duka hili?" Jamaa mmoja kati ya hao watatu alimuuliza Mrutu.
“Ndio, ndio ni mimi"
“Ok, duka lako halija lipiwa kodi ya mapato ya TRA, na kwanini umechelewa kulipa hadi muda huu, au hamkutangaziwa?" Hadi hapo akajua kwamba watu hao ni watu wa TRA.
“Dah!! Nduguzangu mambo mengi ndio yamenifanya nisahau yote, ila mimi sina kawaida ya kuchelewa kulipa kodi"
“Sawa, sasa sisi tunalifunga hili duka hadi hapo utakapo lipa kodi, ndipo tutakapo lifungua tena" Yule jamaa aliongea hivyo huku akielekea kwenye geti la duka hilo ili kulifunga, ila mrutu akamuwahi na kumzuia.
“Sasa jamaa si tuzungumze kwanza?"
“Tuzungumze kitu gani? Wewe hujui umechelewa kwa muda gani kulipia kodi?"
“Najua nimechelewa, ila si nimekuambia kuwa nina mambo mengi ndio yamenifanya nichelewe kulipa kodi"
“Haya zungumza nakusikiliza"
Mrutu hakutaka maneno mengi, akaingia dukani na kutoka na kiasi cha pesa na kumpatia, Jamaa akazitia mfukoni pesa alizopewa.
“Na ukalipie kabla hatuja rudi tena" Jamaa akasema hivyo huku akiondoka dukani hapo akifuatiwa na wenzake, wakapanda kwenye gari yao na kutokomea zao.
Mrutu akashusha punzi ndefu(huu mkosi wa asubuhi asubuhi)akawaza huku akiingia ndani ya duka lake.
*******
Mtaa wa Majengo. 2:30 Asubuhi.
Koplo Taure alikuwa ndani ya gari lake akisubiri lindo lake alilolianza tokea jana usiku, alikuwa amepaki gari yake mbali kidogo na nyumba ya wakina Tito, akiwasubiria watoke ili awafuatilie tena, yeye mwenyewe hakujua kwanini amepatwa na hamu ya kuwafuatilia watu hao aliowaona jana usiku kwa mara ya kwanza, “Duh!! Najipa kazi ambayo haina maana yoyote, sasa kwanini nawafuatilia hawa watu? Ila acha niifuate nafsi yangu inavyotaka, huenda ikawa watu hawa wanalaziada" alijiwazia mwenyewe.
Baada ya dakika kadhaa aliwaona wakitoka na gari yao na yeye akaiwasha ya kwake ili kuwafuatilia, akawaona wakiingiza gari barabarani wakielekea kule kule kwa jana walipo toka, akawa yupo nyuma ya gari mbili zilizofuatana, ila zile gari mbili baada ya kufika Hosteli zikakunja kuelekea chumbageni, sasa akawa yupo nyuma ya gari ya kina Tito, akaona akiendelea kuwafuata hivyo hivyo wanaweza wakamshtukia, akalipita gari lao na kwenda hadi Toyota kuwasubiria, akapaki pembeni kujaribu bahati yake kama kweli na wao watapita na njia hiyo hiyo, bahati ikawa kwake baada ya kuwaona wanatokea na njia ya jengo la Tanesco, akawasubiri hapo hapo Toyota, walivyofika wakampita na kuelekea na njia ya kuelekea Hospitali ya Bombo, akaendelea kuwafuata nyuma hadi walipoipita Hospitali ya Bombo akawa bado yupo nyuma yao.
“Oya Tobi, unaiyona hiyo gari hapo nyuma?" Tito alimuuliza Tobi.
“Ndio naiyona"
“Hii gari imeanza kutufuatilia tokea tunatoka home"
“Aaa!! Mimi basi nimeanza kuiyona tangia tupo Toyota"
“Basi jua kuwa tunafuatiliwa, sasa wewe embu ishike namba zake, halafu tutajua nini chakufanya"
Tobi baada ya kusikia hivyo, akageuka nyuma na kuanza kuzisoma namba za gari ya Koplo Taure, alipozikariri, akarudisha shingo yake mbele.
“Sasa skia, hapa tunajifanya kama tunaingia kwa Mkuu halafu tuone yeye atafanya nini"
Aliposema hivyo akawasha endiketa za kulia kuashiria kuwa anataka kukunja.
Koplo Taure baada ya kuona lindo lake linataka kuingia katika nyumba ya Mr Bakari Haneni, akalipita gari la kina Tito na kunyoosha moja kwa moja kama anaenda Beach ya Raskazoni.
Wakina Tito baada ya kuona ile gari iliyokuwa inawafuata imenyoosha na wao wakaghairisha kuingia kwenye nyumba ya Bosi wao, wakalifuata gari la Koplo Taure kwa kasi baada ya kuliona limekunja mbele kabisa kwenye kituo kidogo cha polisi, kipindi hicho geti la nyumba ya Mr Bakari Haneni lilikuwa tayari limeshajifungua, ila baada ya wakina Tito kughairisha kuingia likajifunga lenyewe.
Wakina Tito waliendesha gari kwa kasi ilikuliwahi gari la Koplo Taure, wakafika na wao kwenye kituo kidogo cha polisi, wakapiga kona kuingia kulia, ila bahati haikuwa kwao baada ya kutoliona gari la Koplo Taure, maana hapo kulikuwa na njia mbili sasa hawakujua gari hiyo imeingilia na njia ipi, wakageuza gari na kurudi walipotoka, wakafika kwenye nyumba ya Bosi wao Mr Bakari Haneni na kuingiza gari ndani baada ya geti kujifungua.
Walipeleka gari sehemu ya maegesho na kushuka garini humo, wakaanza kuelekea ndani ya nyumba hiyo, walipofika sebuleni walimkuta bosi wao akiwa amekaa kwenye sofa moja wapo kati ya mengi yaliyopangwa kwa ustadi mzuri uliopendezesha sebule hiyo.
“Mbona vijana wangu, mlikuja hadi getini halafu ghalfa mkaondoka, mlienda wapi?"
“Mkuu, kuna mpumbavu alikuwa anatufuata nyuma"
“Sijakuelewa Tito, embu fafanua vizuri"
“Kuna gari ilikuwa ikitufuatilia"
“Sasa nyie mlijuaje kama hiyo gari ilikuwa ikimifuata nyie, je kama ilikuwa na safari zake?"
“Hapana Mkuu, hiyo gari ilianza kutufuata tangia tunatoka home"
“Imeishia wapi hiyo gari?"
“Wakati tunataka kuingia humu ndani, ndipo ikatupita na sisi tukaghairisha kuingia humu ndani, ilituifuatilie ila mbele kule ikatupotea"
“Ila mumewajua ni wakina nani wanaomifuatilia?"
“Hapana Mkuu, ila tumezimaki namba zake"
“Safi, ila hadi sasa hamjawafikiria kuwa ni wakina nani waliokuwa wanamifuatilia?"
“Sina uhakika, Ila mimi nina wasiwasi huenda ikawa ni wale tulio wachukulia pesa zao na mzigo wetu jana baada ya kutaka kutuletea ujanja ujanja" Tobi alisema.
“Huenda ikawa ndio hao, na kama ndio itakuwa mmefanya kosa kubwa sana kupajua hapa na kumijua nyinyi kuwa ni watu wangu"
“Dah!!! Kweli, sasa tufanyeje Mkuu"
“Hakuna namna nyengine zaidi ya kuwatafuta na kuwapoteza wote katika uso wa hii dunia, kabla hawajaleta madhara ya aina yoyote"
“Sawa Mkuu" wote wawili waliitikia.
“Vipi lakini, maskani iko salama kule" Mr Bakari Haneni aliuliza kuhusu jengo lao zinapoendelea shuhuli zao za madawa ya kulevya.
“Mkuu, hatukufika ila tumempiga simu Yuni, anasema kila kitu kipo shwari".
Wakiwa wanaendelea na maongezi yao, muda huo Koplo Taure ndio alikuwa anaingia kituoni, alivyoshuka kwenye gari akaenda mapokezi na kumkuta Afande Jesca akiendelea na kazi.
“Mbona umechelewa hivyo?" Afande Jesca alimuuliza Koplo Taure baada ya kufika hapo alipo.
“Dah!!! We acha tu, wamenishtukia kwamba nawafuatilia, ila nimejihakikishia kuwa ni watu wa Mr Bakari Haneni"
“Imekuaje kuaje, embu nielezee"
“Hata sijui, ila walivyofika kwenye nyumba ya Mr Bakari Haneni, mimi nikawapita ila nilivyofika mbele nikawaona wakinifuata kwa kasi, nikaiingiza gari yangu kwenye kile kituo kidogo cha polisi, ndipo hapo nilipowaona wakihangaika kunitafuta baada ya kunikosa wakarudi zao na kuingia kwenye nyumba ya Mr Bakari Haneni, ndipo na mimi nikaondoka zangu"
“Duh! Umenifanya niwe na wasiwasi baada ya kuona hutokei kabisa"
“Usijali mamii, ndio nimerudi mume wako" Koplo Taure aliongea hivyo huku akielekea ndani ya kituo hicho ilipo ofisi yake.
Nnje ya jengo la TRA. 8:15 Mchana.
Alionekana Mrutu akitoka ndani ya jengo hilo, alikuwa ameenda kulipa deni analo daiwa duka lake, baada ya kufika kwenye maegesho ya magari, akaliendea gari yake nakuingia humo, akatoa simu yake na kumpigia Mata.
“Haloo" aliongea baada ya simu yake kupokelewa.
“Ndio Mrutu, niambie" upande wa pili ulisikika.
“Safi tu, upo kazini kwako sasa hivi?"
“Hapana, nipo nyumbani, leo thijaenda kadhini"
“Basi poa nakuja"
Akakata simu na kuingia tena sehemu ya majina, akatafuta kwa sekunde saba, alipolipata hilo jina analotafuta akapiga.
“Ndio Moto, uko wapi wewe?" aliongea baada ya simu kupokelewa.
“Mimi nipo maskani tu, vipi kuna ishu yoyote imetokea?"
“Hapana, ila naomba tukutane kwa Mata sasa hivi"
“Poa"
Alipokata simu, akawasha gari na kuelekea nyumbani kwa Mata, alivyofika akashuka kwenye gari na kuingia ndani ya nyumba ya Mata, akamkuta anakata kata matunda hapo sebuleni.
“Naona mzee unataka kuutia mwili wako vitamini kwa matunda"
“Nataka kuutia mwili wangu au miili yetu? Kama ingekuwa nataka kula pekeangu ningeyaficha haya matunda halafu nathubiri mkiondoka ndio nayala, uthinitie uchoyo bwana"
“Sawa basi yakate kate ili tule wote" aliongea hivyo huku akichukua kipande cha chungwa.
“Aaa!! Mrutu mbona unaandha kula kabla mimi thijakula?"
“We kama hujakula acha mimi nianze kula. Hajakuja bado huyu Moto?" alisema hivyo huku akienda kukaa kwenye sofa jengine.
“Bado hajafika, ila nahith..." kabla hajamalizia sentensi yake, mlango ukafunguliwa na Moto akaingia ndani, moja kwa moja akaenda kwenye sahani ya matunda iliyokuwa imewekwa chini mbele ya Mata aliekuwa akiendelea kumenya matunda mengine, akachukua kipande cha nanasi na kurudi nacho hadi kwenye sofa jengine.
“Nyie vipi? Mbona kila anaekuja anachukua tu halafu anakula, mnajua mimi thijakula kituchochote kati ya hivi nilivyo vimenya? Ohooo!!! Hamtokula thatha hivi" Mata aliongea.
“Acha zako wewe embu menya matunda tule"
“Haya nyie nifanyeni bwege tu"
“Ok, tuachaneni na hayo, ni hivi jana yule dogo nilimuhoji vizuri tu kuhusu ile video, akasema yeye hajui ni nani ambae kaichukua"
“Halafu Mrutu bwana, sasa wewe umeongea kiistarabu unadhani anaweza akakuambia ukweli, ulitakiwa umkazie sura" Moto aliongea huku akiikwepesha miguu yake na maji maji yaliyokuwa yanatoka kwenye kipande cha nanasi alicho kishika.
“Nyie hamjui tu, ila nimemkazia sana tu mpaka akalia, lakini akasema yeye hajui. halafu iweje nimkazie sana, kwani yeye anajua kama mimi pia nipo kwenye huu mchezo"
“Dah!!! Thatha tunafanyaje?"
“Inabidi afe tu ili tupoteze ushahidi kabisa, unajua inaweza ikatokea siku tukakutana nae sehemu mbaya halafu akatuletea matatizo, maana sidhani kama itakuwa sura zetu amezisahau"
“Hapo kweli, thatha tutatumia njia gani ya kumuua?"
“Inabidi tumteke, tukamuulie mbali" Moto aliongea,
“Halafu nimekumbuka kitu, wakati asubuhi nataka kutoka nyumbani kuelekea dukani, kuna flash niliiyona chumbani kwa yule dogo kwenye meza yake ya kujisomea, ila sikupata muda wa kuicheki baada ya kupigiwa simu na yule kijana wangu wa kazi"
“Sasa wewe hiyo flash unahisi ina nini au labda unahisi itakuwa ni hiyo flash yenye ile video?"
“Hata mimi nimehisi hivyo. sasa ngoja nikaichukue ili tuje kuiyangalia wote hapa" akanyanyuka kwenye sofa na kuiyendea sahani yenye matunda na kuchukua kipande cha nanasi na kuondoka nacho, akatoka nje na kupanda kwenye gari yake na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake, kwenda kuichukua flash yenye video ya tukio zima walilolifanya wakina Mata nyumbani kwa marehemu Mzee Mheshimiwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ENDELEA....
Hemedy muda huo alikuwa kwenye basi la shule akirudishwa nyumbani kwao(nyumbani kwa Mrutu) walipofika nje ya geti, akashuka kwenye gari la shule na kufungua geti, akaingia ndani sebuleni, akaaza kupiga hatua kuelekea chumbani kwake, ila kabla hajaufikia mlango wa chumbani kwake, akarudi nyuma kidogo baada ya kuona kitu juu ya deki alichokifananisha, akaiyendea deki, alaipofika akaiyona ile flash yake yenye video “mmh!! hii flash si nimeiyacha ndani, imefuata nini hapa, huyu itakuwa ni bamdogo, sijui tayari ameshaiyona hii video, mamaa sijui itakuaje kama tayari ameshaiona" alijisemea mwenyewe.
Akaona asipotumia ujanja anaweza akaadhibiwa kwa kosa lakudanganya, akaichukua ile flash, akaenda nayo chumbani kwake, akaificha chini ya godoro lake la kulalia, akatoka tena nje ya chumba chake, akakiendea chumba cha Mrutu na kujaribu kufungua mlango akaona mlango umefungwa“hajarudi bado" hivyo hivyo akiwa na nguo zake za shule ba begi lake, akafunga milango yote vile vile alivyokuta na kutoka nje ya nyumba hiyo na kupotelea huko.
Muda si mrefu naye Mrutu, akafika nyumbani hapo na kuingia hadi ndani sebuleni, akaiyendea deki alipoiyacha ile flash asubuhi, ila cha ajabu hakuikuta, akaanza kuitafuta, akainua deki, akaangalia kwenye tv, akaanagalia kwenye masofa, akaliendea kabati la vyombo na kuitafuta kote huko lakini hakuiyona, ikabidi atulize akili kwanza“ hii flash imeenda wapi? mbona kote huko siyoni, ila asubuhi nakumbuka niliiacha hapa hapa kwenye deki, au itakuwa Hemedy kaichukua? lakini hapana Hemedy yeye si yupo shule, sasa ataichukua vipi? au amesharudi" akaanza kumuita Hemedy huku akienda katika chumba chake, alipofika akafungua mlango akaingia ndani, lakini nako hakumkuta Hemedy, ikabidi aanze kuitafuta humo humo chumbani kwa Hemedy akatafuta kila sehemu lakini hakuiyona“ Duh sasa ni nani ambae kaichukua ile flash, au Hemedy kaichukua?" akapata wazo la kuangalia nguo za Hemedy za shule, lakini nazo pia hakuziona, akajua Hemedy bado hajarudi shule, akatoka hadi sebuleni na kukaa hapo akivuka kumbukumbu vuzuri ya wapi aliiweka ile flash.
Hemedy baada ya kuzurura mitaani kwa nusu saa nzima, akaona arudi nyumbani huwenda ikawa tayari baba yake mdogo amerudi kutoka kazini, akapanga kama asipomkuta basi asiingie ndani mpaka atakapo rudi, baada ya kufika karibu na nyumba yao, akaliona gari ya Mrutu imepaki nje ya geti, akajua tayari amesharudi, akaingia ndani na kumkuta Mrutu amekaa sebuleni.
“Shikamoo baba" Hemedy alimsalimia Mrutu.
“Marahaba, ndio unarudi shule sasa hivi?"
“Ndio"
“Nyumbani ulirudi kufuata nini baada ya kukupeleka shule asubuhi?" Mrutu aliuliza swali la kimtego ili kumnasa Hemedy, Hemedy naye kama alijua vile kwamba ana tegwa, akajua akijibu hovyo tu itakuwa tayari ameshanaswa.
“Hapana, mimi sijarudi nyumbani toka unipeleke shule na ndio ninarudi sasa hivi"
Hemedy akajibu kiufundi na kumfanya Mrutu ashushe pumzi nyingi.
“Mbona mimi kunawakati nilikuja shuleni kwenu na kuambiwa kuwa umerudi nyumbani"
Hemedy alicheka kimoyo moyo baada ya kuona baba yake huyo mdogo ameishiwa maswali ya kimitego.
“(kwa staili hiyo wala huwezi kunitega kamwe)alijiwazia mwenyewe, Hapana bamdogo kweli mimi sijatoka nje ya eneo la shule"
“Kwahiyo walimu wako waongo?"
“Itakuwa, kwasababu mimi sijatoka hata nje ya darasa, muda wote nilikuwa nipo darasani"
Mrutu akaishiwa pozi, hakujua am'bane vipi tena, hakuwa na swali jengine la kumuuliza, ikabidi tu amruhusu Hemedy kwenda kubadilisha nguo, baada ya kubadilisha nguo, Hemedy alirudi sebuleni hapo.
“Sasa skia, hapa sebuleni kuna flash yangu imepotea, kwahiyo kama utaiyona naomba unirudishie maana ina taarifa zangu za kikazi"
“Sawa, hakuna shida" hadi hapo Hemedy akajidhihirishia kuwa Mrutu bado hajaiyangalia ile flash.
“Basi chukua hii(akampa noti ya shilingi elfu tano)utanunua chakula ukitakacho, mimi leo sitopika na sasa hivi kuna sehemu naenda mara moja"
Baada ya kumuaga Hemedy, akatoka nje na kupanda kwenye gari yake, akaanza safari ya kwenda nyumbani kwa Mata, baada ya ya dakika kumi na tano akawa tayari amefika, akashuka kwenye gari na kuingia ndani.
“Vipi? Mbona umekuja huna furaha?" Moto alimuuliza huku akiwa ana lamba kokwa la embe.
“Kwanza mbona mimi hamjaniwekea matunda, yani mmeyala yote nyie pekeenu?"
“We si umechelewa mwenyewe, ila tumekubakishia, yale pale juu ya friji kwenye ile sahani" Mrutu akaenda hadi kwenye friji na kuichukua sahani yenye matunda na kwenda nayo kwenye sofa na kukaa.
“Enhee!! Hiyo flash iko wapi?" Mata aliuliza.
“Dah!! Yani ile flash imepotea katika mazingira ya kutatanisha, sijaiyona sehemu nilipoiyacha" Mrutu aliongea hivyo huku akila ubale wa embe.
“Au labda yule dogo aliporudi shule aliichukua" Moto aliongea.
“Hapana sio yeye, maana yule dogo alipo rudi shule alinikuta naitafuta"
“Thatha itakuwa imeenda wapi, au wewe athubuhi ulipoenda dukani kwako, ndipo dogo alipo ichukua?"
“Mata, yule dogo nimempeleka mwenyewe hadi shule, na aliporudi pia nikajaribu kum'bana lakini haonyeshi kabisa kama alirudi nyumbani wakati mimi sipo"
“Bathi hapo ndipo ninapo amini kwamba nyumba yako ina majini, na unatakiwa umuite shekh haraka thana, aje kuipigia kithomo kabla mambo hayajazidi kuwa makubwa, maana thiku unawedha ukalala nyumbani kwako na athubuhi ukajikuta ume lala juu ya bahari"
“Hahahahha!!!! Kwanini umesema hivyo Mata?" Mrutu alicheka baada ya Mata kusema hivyo.
“Hili tukio la leo nikiliunganisha na lile la jana ndio napata picha kamili kwamba nyumba yako ina majini"
“Tukio lipi hilo la jana?" Mrutu akauliza huku akianza kuingiwa na wasiwasi.
“Jana thi tulithikia minong'ono ikitokea nje wakati tumekaa pale thebuleni kwako, halafu ulivyo enda kuangalia hukukuta mtu yoyote, thatha wewe udhani kuwa hiyo ni hali ya kawaida"
“Hahahah!!!! Mata bwana, kumbe ndio hivyo? Ile minong'ono ilikuwa ni ya yule dogo na yule Askari aliekuja nae"
“Hapana, mimi thi themei wakati walipokuja wale, ila nathema mwandho kabitha, wakati ndio tuna ingia ingia pale kwako"
“Hata ile mingong'ono ya mwanzo ilikuwa pia ni wao" Mrutu alipoongea hivyo, Mata na Moto macho yao waliyatoa pima, wakabaki wamemkodolea macho Mrutu.
“Vipi mbona mmeganda hivyo?" akawauliza.
“Kwahiyo unataka kutuambia kuwa maongezi yote yale waliyasikia?" Moto aliuliza.
“Hapana, hawakufika karibu na dirishani"
“Thatha kwanini waliondoka na hawakuingia ndani?" Mata aliuliza.
“Walienda nyumbani kwa yule askari, embu tuacheni na mada hii, turudini kwenye mada iliyotufanya tukutane hapa" Mrutu aliwakatisha na kuwarudisha kwenye mada yao ya mwanzo.
“Ok, tunafanyaje thatha?" Mata aliuliza.
“Itabidi tumteke tukamuulie maporini huko" Moto alitoa rai yake.
“Tatizo lako Moto hufafanui, watakiwa utuambie tuna mtekaje tekaje, sio useme tu tunamteka tunamteka, embu fafanua basi" Mrutu aliongea.
“Sawa, acha nifafanue, ni hivi wewe leo itabidi uchelewe kurudi nyumbani kwako, halafu yeye kule si atabaki pekeake, basi mimi na Mata hapa, tutaenda hadi pale kwako na kumchukua halafu tunaondoka nae, tunatafuta msitu wowote kisha tuna maliza kazi huko huko, au nyie mnasemaje?" Moto alihitimisha ufafanuzi wake.
“Hiyo itakuwa ni njia mbaya upande wangu" Mrutu alionyesha wasiwasi wake.
“Kwanini umesema hivyo?" Moto aliuliza.
“Unadhani akishapotea katika mazingira ya kutatanisha kama hayo, mimi si nitaitwa kusaidia polisi upelelezi, aa aa!!! Aise hiyo njia mimi sijaiafiki kabisa"
“Hata mimi pia thijaiafiki kabitha" Mata nae aliongea.
“Sasa basi toeni mawazo yenu" Moto aliongea.
“Subirini mimi apa niwaambie. leo usiku nitatoka nae kwenda popote pale na gari yangu, halafu tutawasiliana kuwa naelekea wapi, tukiwa katika matembezi, nyinyi matakuja na gari yenu na kutuzibia njia kwa mbele, mimi si nitasimama, basi nyie mnakuja na bastola, mnatuteka wote wawili halafu mtamchukua yeye na kuondoka nae ndipo hapo mtakapo enda kumfanya chochote, na mimi huku nyuma ntajifanya kukimbia polisi kwenda kutoa taarifa, huo ndio utakuwa mpango mzuri, ambao utatufanya tusishtukiwe na yoyote" Mrutu alihitimisha mpango wake na kuwaangalia wenzake aone watasema nini.
“Hapo sawa, lakini utakapoenda huko polisi kutoa taarifa hiyo, je wakikuuliza unawajua waliyomiteka wewe utasemaje?" Moto aliuliza.
“Mimi nitawaambia kuwa walijiziba nyuso zao na maksi, kwahiyo sikuweza kuwaona usoni"
“Basi sawa kama mpango ndio huo, mimi binafsi nimeuafiki, sijui Mata yeye ni vipi"
“Hata mimi pia nikopamoja na nyinyi" Mata nae aliunga mkono wazo la Mrutu.
“Sawa kama mpango ndio huo na vipi kuhusu zile mali, maana na mimi nataka nitembelee gari bwana nshachoka kutembea kwa miguu"
“Hilo tutalishuhulikia baada ya kumaliza kwanza hili" Mrutu alijibu.
“Lakini thi zipo thalama kabitha mali dhetu tarajiwa?" Mata aliuliza.
“Ziko salama, leo tu kabla sijaenda TRA nilipitia katika ofisi zote na kukuta kazi zinaendelea kama kawaida, si unajua mimi ndio nazisimamia mali zote za marehemu"
“Basi kama ni hivyo shwari, maana nilivyokuwa na usongo na hela yani nikipata mgawo wangu, naacha kabisa hii shuhuli ya ujambazi, nisije nikajikuta siku naingia kwenye vyombo vya dola na maisha yangu yakamalizikia jela, nataka na mimi niwe raia mwema" Moto aliongea.
“Sasa si bora uingie kwenye vyombo vya dola kuliko kuingia mikononi mwa raia wenye hasira kali" Mrutu aliongea hivyo huku akiinuka na kuuendea mlango wa kutokea.
“Vipi, mbona unaondoka tena Mrutu, unaenda wapi?" Mata alimuuliza.
“Acha mimi niwaache, kuna sehemu nataka kwenda mara moja"
“Poa, lakini uthithahau bathi kuukamilisha mpango tulioupanga"
“Msijali" Mrutu aliongea hivyo huku akiufunga mlango na kuondoka zake nyumbani hapo kwa Mata, akiwaacha Moto na Mata wakiendelea na maongezi mengine, akawasha gari kutokomea zake.
Katika ngome(maskani) ya Mr Bakari Haneni. 11:07 Jioni.
Tito na Tobi waliingiza gari katika lango la jumba hilo la zamani, ililoachwa na wakoloni miaka mingi iliyopita, lilikuwa likilindwa masaa ishirini na nne na watu wenye bunduki, waliokuwa wakitembea tembea huku na huko, jumba hilo lilikuwa limezungukwa miti mingi iliyotengeneza msitu mdogo, walipoingia ndani ya jumba hilo, wakashuka kwenye gari na kunyoosha hadi ndani ya jengo hilo, wapanda ngazi na kufika katika gorofa ya pili, wakaingia kwenye chumba kikubwa kilicho fananiana kama ukumbi flani kilichokuwepo gorofa ya pili ambayo ilikuwa ndio mwisho wa jengo hilo, huko kulikuwa na kundi la watoto wenye umri kati ya miaka kumi na tano hadi ishirini, wakifunga madawa ya kulevya kwenye vipakti vidogo vidogo, wengine walikuwa wamesinzia na kukaa chini kabisa huku udenda ukiwatoka, ulikuwa ni unyanyasaji na udhalilishaji ila kati ya hao wote hakuna aliewajali watoto hao.
Tito na Tobi walitoka katika ukumbi huo na kuelekea kwenye chumba chengine huko huko kwenye gorofa ya pili, walivyoingia wakakuta watu, wanayapanga madawa hayo yaliyokuwa tayari yamefungwa kwenye vipakti vidogo vidogo, walikuwa wakiyapanga kwenye maboksi yaliyokuwemo chumbani humo, wakatoka katika chumba hicho na kushuka chini kwa kutumia ngazi, huko wakaelekea katika ukumbi nwengine na kukuta kundi la vijana wanafanya mazoezi, baada ya kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, wakatoka nje na kupanda kwenye gari yao na kutokomea zao mjini.
Nyumbani kwa Mrutu. 3:02 Usiku.
“Sasa Hemedy embu jiandae mara moja tukatembee" Mrutu alimwambia Hemedy.
“Wapi?" Hemedy aliuliza.
“We kajiandae twenzetu au wewe unaona raha kukaa nyumbani tu kila siku?"
“Hapana"
“Basi kama ni hivyo kajiandae twenzetu. au ujiandae nini? twenzetu tu hivyo hivyo"
“Hivi hivi?"
“Eeeee!!! Hivyo hivyo pia vinatosha, kwanza hatuendi kukaa sana, muda si mrefu tutarudi"
Baada ya kuongea hivyo, walitoka nje na kupanda kwenye gari, ili wakatembee kama Hemedy alivyojua, hakujua kuwa baba yake mdogo anania mbaya na yeye, kama angejua nini kimepangwa juu yake, wala asingeitamani hiyo safari, kwavile, usilolijua ni sawa na usiku wa giza, basi kwa hemedy pia kulikuwa ni usiku wa giza, hakuweza kuona mbele hata hatua moja, baada ya yote safari ya kwenda kumuua Hemedy ikaanza.
Nyumbani kwa Inspekta Ganjo. 2:32 Usiku. Nusu saa nyuma.
“We Taure, mbona hadi saa hii hujaenda kumchukua Hemedy?" Inspekta Ganjo alimuuliza Koplo Taure.
“Mzee namalizia kupanga hivi viti mara moja" Koplo Taure alimjibu Inspekta Ganjo.
“Nenda bwana mara moja, hivyo viti muachie Jesca avipange yeye" Inspekta Ganjo alimuambia.
“Sawa" Koplo Taure alijibu na kuacha kupanga viti.
“Jesca, embu vipange hivyo viti haraka, muache Taure amfuate Hemedy, aje kusherehekea na watoto wenzake"
Nyumbani kwa Inspekta Ganjo, usiku huo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa mjukuu wake wa kike, anaeitwa Hilda. wanafunzi wenzake anaosoma nao walialikwa kuja kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mwenzao.
Koplo Taure baada ya kuambiwa hivyo, akatoka nje akapanda kwenye gari yake na kwenda kumfuata Hemedy nyumbani kwao, dakika ishirini na tano ikawa tayari ameshafika nyumbani kwa Mrutu, bahati nzuri ndio akawakuta wanatoka, akabidi aweke gari pembeni na kushuka, akaipigia mkono gari ya Mrutu, nae akasimama, akawafuata,Mrutu akashusha kioo cha malango wa gari ili kumsikiliza Koplo Taure.
“Niambie Mrutu" Koplo Taure aliongea hivyo huku akimpa tano(salamu iliyozoeleka kwa vijana) kupitia kwenye kwenye kioo cha mlango kilicho shushwa.
“Freshi tu" Mrutu nae alijibu na kugonganisha mkono wake kwenye mkono wa Koplo Taure.
Hemedy nae alimsalimia Koplo Taure, baada ya kuijibu salamu ya Hemedy, akaendelea kuongea na Mrutu.
“Mnaelekea wapi sasa hivi?" Koplo Taure aliuliza.
“Tunaenda kutembea tembea tu" Mrutu alijibu.
“Wapi?"Koplo Taure aliuliza.
(huyu vipi, mbona maswali mengi) alijiwazia mwenyewe. “tunaenda kula msosi wa usiku, maana leo nimechoka kupika" Mrutu alijibu tu hiyo basi, lakini alishayachoka maswali ya Koplo Taure.
“Basi kama ndio hivyo, nilikuwa namuomba huyo dogo, maana Inspekta Ganjo anamuita nyumbani kwake"
“Kuna nini usiku huu"
“Kuna sherehe ya kuzaliwa kwa mjukuu wake, sasa alikuwa anamuhitaji akajumuike na wenzake"
“Sasa.. Lakini.. Hajakula bado huyu, subiri kwanza tukale halafu utakuja kumchukua"
“Lakini ni muhimu, Inspekta anamtaka aende kwenye hiyo sherehe, halafu kama hajakula, mbona hata huko pia chakula kipo kingi tu, ataenda kula"
“Baba, acha niaende tu" Hemedy aliongea.
Hadi hapo Mrutu hakuwa tena na chakupinga, labda angesingizia kuwa kesho atachelewa shule, lakini kesho yenyewe ilijuwa ni wikiendi, kwahiyo hakukuwa na shule, akabaki hajui aseme kitu gani, hakuwa na jinsi akamkubalia Hemedy aende na Koplo Taure. Hemedy akashuka kwenye gari, akaingia ndani haraka kwenda kubadilisha nguo, baada ya dakika kumi alirudi akiwa tayari ameshapendeza, alikuwa amevaa jinzi nyeusi na juu akavaa tisheti ya njano aliyo iziba na kikoti cheusi alichokifungua zipu kwa mbele na kufanya tisheti aliyoivaa iyonekane kwa mbele na mikono ya kikoti hicho aliipandisha juu kidogo na kichwani akavaa kofia aina ya cape nyusi aliyoigeuza nyuma kupaleta mbele na chini kabisa akavalia raba za rangi ya njano zenye upapi mweusi. sio siri alikuwa amependeza sana, halafu ukiachana na alivyopendeza, pia alikuwa na sura nzuri, sura ambayo mzazi wowote angetamani mwanae wakiume awe na sura kama ya Hemedy, tungekuwa tupo ulaya tungemuita “Handsome boy" ila kwavile tupo Bongo, basi tunamuita “Mtanashati".
Mrutu mwenyewe baada ya kumuona alikubali, maana hakuwahi kumuona akiwa amependeza namna hiyo, akabaki tu kujisikitikia,(Dah!!! Sasa kwanini nataka kumfanyia ubaya mwanangu mwenyewe, hivi kweli ninaweza nikaruhusu afe ikiwa uwezo wa kumuepusha na hicho kifo ninao? Sijui, lakini tutaona) Mrutu alijiwazia mwenyewe, wakati huo Hemedy alikuwa akipanda kwenye gari ya Koplo Taure.
“Mrutu, kama vipi na wewe tuongozane sote" Koplo Taure aliongea hivyo huku akielekea kwenye gari yake upande wa dereva.
“Hapana nyie nendeni tu, mimi kuna sehemu naenda sasa hivi"
Koplo Taure aliingia kwenye gari yake na kuiwasha.
“Dogo kwajinsi leo ulivyopendeza, sidhani kama huko tunapoenda patatosha" Koplo Taure aliongea hivyo huku akiigeuza gari.
“Kwanini?"
“Aiseee!!!! Umependeza sana, yani kama hutoodoka na demu mmoja basi ujue utaondoka nao wote"
“Hahaha!! Anko bwana, sasa kwani itakuwa ndio nimependeza pekeangu, si wapo watu wengi ambao watukuwa wamependeza tena zaidi yangu mimi"
“Wapo waliopendeza, ila wote umewazidi, subiri mwenyewe utaenda kujionea huko, hivi dogo una demu wewe"
“Mmmmh!! Anko mimi hayo mambo wala siyajui kabisa"
“Basi huku lazima ukaondoke na mmoja"
Waliendelea stori huku wakielekea nyumbani kwa Inspekta Ganjo, baada ya dakika kadhaa ikawa tayari wameshafika, Koplo Taure akaingiza gari ndani ya nyumba hiyo na kulipaki sehemu ya maegesho, wakashuka kwenye gari na kuanza kuelekea sehemu ilipo pangwa sherehe hiyo ifanyike, sasa hivi kulikuwa kumechangamka baada ya watoto wengi kuhudhuria sherehe hiyo, ni kweli kama Koplo Taure alivyomuambia Hemedy, kulikuwa kuna watoto wengi wa kiume waliopendeza lakini kati ya hao wote hakuna aliemfikia Hemedy kwa kupendeza, watoto hao walikuwa na umri kati ya miaka kumi na mbili hadi kumi na sita, Koplo Taure na Hemedy wakiwa wanapiga hatua kuelekea vilipo viti ili nawao wakakae kama watu wengine walivyofanya, watu wote wakageuza shingo zao kuwaangalia wao, hasa hasa Hemedy ambae alikuwa mgeni machoni mwao, maana hao watoto wote, walikuwa wanasoma shule moja na mjukuu wa Inspekta Ganjo, na Hemedy yeye hakuwa akisoma shule wanayosoma wao, wakabaki wakimshangaa tu hadi alipoenda kukaa kwenye kiti kimoja wapo, sio kwamba walimshangaa kwakuwa ni mgeni machoni mwao, La hasha!! Bali walimshangaa kutokana na jinsi alivyopendeza.
“Dogo si nimekuambia kuwa lazima uwafunike watu wote hapa? Si unaona wanavyokuangalia?" Koplo Taure alimwambia Hemedy.
“Duh!! We acha tu hadi mwenyewe naona aibu" Hemedy alisema.
“Unamuona yule demu kule mbele anavyokuangalia?"
Hemedy akaangalia huko alipoelekezwa na kukuta kweli kulikuwa na msichana wa makamo yake anamtolea macho, macho yao yalipogongana, yule msichana akatoa tabasamu lililo mfanya Hemedy kuondoa macho yake haraka na kuangalia pembeni kwa aibu.
“Sasa sio yule tu, unawaona na hao wawili huko pembeni yako wanavyokuangalia"
Hemedy akapeleka macho yake huko alipoelekezwa tena na kukuta kuna wasichana wengine wawili wakimwangalia yeye, akarudisha macho yake na kuangalia mbele tu.
“Yani hapa lazima uondoke na demu tu, maana sio poa wanavyo kutolea macho"
Hemedy hakujibu kitu akabaki akitabasamu tu, alivyotabasamu ndipo hapo uzuri wake ulipoongezeka, ama kwa hakika Hemedy alikuwa ni Handsome boy, hata mimi nilitamani angekuwa ni mdogo wangu tu kwajinsi nilivyo mkubali, sio mimi tu hata wewe msomaji ungefanikiwa kumuona nadhani ungekubaliana na mimi, ngoja kwanza nikuelezee kidogo muonekano wake, alikuwa ana sura flani hivi, sio nene sana wala sio nyembamba sana, nikimaanisha alikuwa na sura ya saizi ya kati, sura yake ilibeba pua ilichongoka kwa mbele kidogo na kufananiana kama za wale watu wa Uganda na alikuwa na macho mazuri, hakuwa mweupe sana na wala hakuwa mweusi, bali alikuw na rangi ya chocolate na hakuwa mfupi sana wala hakuwa mrefu sana bali alikuwa na urefu wa wastani na zile nguo alizovaa ndio zikazidi kuongeze uzuri wake, nadhani hadi hapo, itakuwa tayari ushapata picha Hemedy jinsi alivyo, japokuwa kwa uchache sana.
“Sasa skia dogo, acha mimi nimfuate Mzee nikamwambie kwamba tayari umeshakuja, maana alisisitiza lazima na wewe pia uwepo"
“Poa, mimi utanikuta hapa hapa"
“Sawa, lakini angalia usije ukasababisha ungomvi hapa, ukaharibu shuhuli ya watu"
“Hahahaha!!! Anko bwana!"
Mrutu aliinuka na kwenda ndani ya nyumba hiyo, akakutana Inspekta Ganjo, akamueleza kwamba ameshakuja na Hemedy, Inspekta Ganjo, akafurahi na kumruhusu akaendelee na shuhuli nyengine, wakati anatoka akakutana na Afande Jesca, wakaongozana wote na kwenda hadi kwenye viti, sehemu ambayo alimuacha Hemedy.
“Mambo mtoto?" Afande jesca, alimsalimia Hemedy baada ya kufika.
“Poa" Hemedy alijibu.
“Heee!!! Huyu mtoto mbona kama vile namjua ila sikumbuki nimemuona wapi?" Afande Jesca aliongea hivyo huku akimwangalia Hemedy usoni.
“Kwani humkumbuki huyu?" Kaplo Taure alimuuliza.
“Hapana, sikumbuki nilimuona wapi?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nilimleta kituoni siku ile..." Kabla hajamalizia sentensi yake, Afande jesca akamkatisha.
“Basi, basi, nishamkumbuka, duh! kumbe ni mzuri hivi? Siku ile wakati unamleta pale kituoni alikuwa usoni ana vidonda vidonda, lakini leo ndio namuona vizuri. Anaitwa nani vile.."
“Hemedy" Koplo Taure akajibu.
“Anhaaaa!!! Kumbe ndio huyu Mkuu aliokuambia ukamchukue?"
“Ndio, embu tulia kwanza naona kama vile shuhuli ndio inataka kuanza"
Ni kweli shuhuli ilikuwa ndio inaanza, Msema chochote, alimaarufu kama “MC" alisogea mbele na kuanza kuwaambia watu kuwa shuhuli ndio inaanza na muda huo, mwenye shuhuli ndio anatoka ndani kwahiyo watu wajiandae kumpokea.
Baada ya dakika moja, watu waliambiwa wasimame na kumuimbia nyimbo ya kumtakia furaha ya kuzaliwa binti huyo.
“Happy birthday to you, happy birthday to yo, happy birthday ni ya Hilda, happy bithday to youuu"
Watu wote waliimba wimbo huo baada ya kutoke binti huyo mdogo, kati ya umri wa miaka kumi na mbili au kumi na tatu, alikuwa amependeza kushinda wote kwa mavazi aliyoyavaa na sio mavazi tu hata kwa sura alikuwa ni mzuri sana, siwezi kumuelezea kwasababu ninaweza nikachukua karibia page tano, nikiwa bado na muelezea tu, ila jua kwamba alikuwa ni mzuri.
Akaenda kukaa kwenye kiti kilicho pambwa na maua mazuri na mbele yake kulikuwa na meza iliyojaa kila aina ya vinywaji ila ni vile ambavyo havileweshi. Watu wakakaa kwenye viti baada ya mwenye sherehe kukaa, zikafuata ratiba nyengine.
********
Baada ya kuchukuliwa Hemedy na Koplo Taure, Mrutu hakuwa na jinsi, akawapigia simu wakina Mata, ili kuwauliza wako wapi na kuambiwa kuwa wote wawili, wapo nyumbani Mata, wanaisubiria taarifa yake ili wakakamilishe kile walichopanga.
Ila Mrutu akawaambia wamsubirie hapo hapo nyumbani kwa Mata na yeye anakuja, wakamshangaa na walipomuuliza kwanini yeye aliwajibu wamsubiri tu watajua huko huko, hawakuwa na jinsi ikabidi wamsubiri. Mrutu aliwasha gari yake kwa safari ya kuelekea nyumbani kwa Mata, baada ya dakika kadhaa, ikawa tayari ameshafika, akapaki gari na kuingia ndani ya nyumba hiyo, akawakuta Mata na Moto wamekaa kwenye masofa wanamsubiri.
“Haya vipi tena, mbona tulivyopanga thivyo, thi tulipanga utupigie thimu ili thithi tuje kumalidha kadhi, haya mbona umekuja wewe huku?" Mata alimuuliza.
“Yani nahisi yule dogo umri wake wa kuishi bado ni mrefu" Mrutu aliongea.
“Kivipi sasa, embu tufafanulie" Moto aliongea.
“Yani ni hivi...." akawahadithia ilivyokuwa.
“Dah!!!! Thatha tunafanyaje?" Mata aliuliza.
“Mimi hata sijui pia tunafanyaje" Mrutu alisema.
“Yule dogo, leo ndio siku yake ya mwisho kuvuta pumvi" Moto aliongea.
“Kivipi?" Mrutu aliuliza.
“Inabidi akafe huko huko kwenye hiyo sherehe" Moto aliongea.
“Tutamuuaje, embu fafanua"Mrutu aliongea.
“Tutavamia pale pale kwenye hiyo sherehe na kumuua halafu tunaondoka zetu"
“Mmmh!!! Mbona kama vile hiyo ni njia ngumu?" Mrutu alionyesha wasiwasi wake.
“Nyie kama kwenu hiyo kazi ni ngumu basi niachieni mimi nitaifanya, chamsingi ni kuondoka sasa hivi na kuelekea huko"
“Mimi nitakuwa pamoja na wewe" Mata aliongea.
“Sawa, lakini kuna anaepajua nyumbani kwa yule Inspekta?" Mrutu aliuliza.
“Mimi napajua ndio" Mata alijibu.
Baada ya kukubaliana na mpango huo, wote wakainuka na kutoka nje, wakapanga watumie gari ya Mata na dereva awe ni Mrutu ili Mata na Moto, watakapo vamia sherehe hiyo na kufanya mauaji ya Hemedy, watakapo toka waingie kwenye gari na kukimbia. Wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Inspekta Ganjo, dakika ishirini ikawa wameshafika, wakapaki gari nje ya geti la nyumba ya Inspekta Ganjo, Moto na Mata wakaweka bastola zao vizuri na kujiandaa kuelekea ndani ya nyumba hiyo ilipo sherehe ya mjukuu wa Inspekta Ganjo, ili kumuua Hemedy na Kutokomea zao.
Ndani ya nyumba ya Inspekta Ganjo, sherehe ilikuwa inaendelea kama kawaida, wakati huo ndio ulikuwa ni wakati wa kula chakula, watu wote walijipanga katika mstari mmoja kulekea sehemu iliyoandaliwa kwajili ya chakula, Hemedy na yeye alikuwa pia katika mstari huo, yeye alikuwa mtu wa mwisho kabisa kwenye huo mstari.
Wakati watu wanaendelea kupata chakula, ghafla watu wote wakageuza shingo zao nyuma baada ya kuskia kishindo kama cha mtu alieanguka, walipoangalia nyuma ya mstari huo, wakapigwa na butwaa baada ya kumuona mtu wa mwisho kabisa kwenye mstari huo akigalala chini na kutulia kimya.
ENDELEA....
“Jamani msiogope, hiyo ni hali ya kawaida ambayo huyo mtu anayo, kwahiyo nyie endeleeni kupanga mstari, sisi acha tumuondoe hapo" Inspekta Ganjo aliongea hivyo huku akimfuata yule mtu aliekuwa amevaa nguo za kiulinzi, alikuwa ni mlinzi wa nyumba hiyo, alieenda kupanga mstari nyuma ya Hemedy baada ya kuona watu wote wamepanga mstari kwajili ya chakula, alikuwa ni mgonjwa wa kifafa na ndio huo uliomuangusha hapo, Inspekta Ganjo akifuatiwa na vijana wawili, wakaenda kumtoa pale alipoanguka na kumpeleka kwenye bustani ya nyumba hiyo.
Hemedy kipindi hicho alikuwa yupo mbali kidogo na mstari huo kwa hofu baada ya mtu huyo kuanguka nyuma yake, alitandwa na hofu kuu, hakujua mlinzi huyo alifika saa ngapi nyuma yake, akabaki ameduwaa tu hadi pale alipoondolewa hapo na kupelekwa kwenye bustani ya nyumba hiyo.
Watu wakapanga tena mstari kwajili ya kwenda kupata chakula. kila mmoja alipopewa chakula chake, alienda kukaa kwenye kiti na kuendelea kula msosi huo.
Hemedy nae ikafika zamu yake ya kupewa chakula, alipopata akaenda nacho kwenye kiti chake na kumkuta Koplo Taure na Afande Jesca wakiendelea kula chakula, naye akaka na kuanza kula.
“Dogo, kumbe uko vizuri" Koplo Taure aliongea huku akila kipaja cha kuku.
“Kwanini?" Hemedy aliuliza.
“Nimekuona pale umeruka kama mcheza kareti baada ya yule mtu kuanguka nyuma yako"
“Yani nyie acheni tu, nimeshtuka pale, almanusura moyo wangu utoke nje kwa hofu, maana kwa kile kishindo nilijua kumetua bomu la nyuklia nyuma yangu" Hemedy alijibu na kumfanya Afande Jesca atabasamu, tabasamu ambalo lilielekea cheko.
“Sasa wewe ni kipi kilichokufanya hadi ukashtuka vile" Koplo Taure alimuuliza.
“Anko wewe unadhani kile kishindo ni cha kawaida? Mimi nilidhani labda malaika mtoa roho za watu kanishukia kuja kuichukua roho yangu"
Hadi hapo Afande Jesca na Koplo Taure walikuwa wanacheka kwa sauti kubwa na kufanya watu wengine wawageukie wao ila hilo halikuwafanya waache kucheka.
“Dah!! Kumbe wewe mtoto una vituko namna hii?" Afande Jesca aliongea hivyo huku akimalizia kucheka.
“Hapana sio hivyo, mimi kile kishindo ndio kimenishtua, maana nilikuwa nataka niparamie ukuta nikimbie zangu"
“Sasa wewe unaweza kumkimbia malaika mtoa roho?" Afande Jesca aliongea.
“Kumkimbia haiwezekani, ila ukijaribu unaweza ukafanikiwa"
Wakati huku ndani watu wakiendelea na kula, kule nje wakina Moto bado wanafikiria ni jinsi gani ya kuingia humo ndani.
“Mimi nilijua tu kwamba hiii njia itakuwa ni ngumu" Mrutu aliwaambia wenzake.
“Hapana hii njia sio ngumu bali kuingia humo ndani ndio kugumu" Moto aliongea huku akiwa anaangalia ukuta wa nyumba hiyo nyumba.
“Sasa tutafanyaje?" Mrutu aliuliza.
“Subirini mimi nikaruke ukuta niingie humo ndani, maana itakuwa geti limefungwa" Moto aliongea hivyo huku akifungua mlango wa gari ili atoke, ila Mrutu akawahi kumzuia.
“Sikiliza Moto, usitake kufanya mambo ya kitoto, kumbuka hii nyumba ni ya Inspekta sasa hujui humo ndani kuna askari wangapi, usije ukaingia halafu ukashindwa kutoka, kisha ikapelekea upate matatizo wewe au sote" Mrutu alimwambia Moto.
“Sasa tufanyeje?" Moto aliongea huku akiufunga mlango wa gari vizuri.
“Hapa hakuna namna nyengine zaidi ya kuondoka, huyu dogo yupo, tutampata siku yoyote" Mrutu aliongea hivyo huku akiwasha gari.
“Basi poa twendeni" Moto alijibu kiunyonge.
Mrutu aliondoa gari mahala hapo kuelekea nyumbani kwa Mata, Mrutu alikuwa bado anasita kumdhuru Hemedy, japokuwa alijua Hemedy ni tatizo kwao lakini hakupenda afe, alitamani kuwaambia wenzake wabadilishe maamuzi lakini hakujua atawanzaje, ikiwa Hemedy amepona kuawa kama hivyo, basi yeye alishukuru sana, alitamani kila siku wamkose kama hivyo ili Hemedy aendelee kuishi. Walimuacha Moto geto kwake na wao kuendelea na safari yao, walipofika nyumbani kwa Mata, Mrutu alichukua gari yake na kuondoka hapo kuelekea kwake maana usiku pia ulishakuwa mkubwa, alipofika kwake akaingiza gari ndani na yeye akaelekea moja kwa moja hadi chumbani kwake na kujitupa kitandani. “bwana eee mi siogi, kwanza nilioga ile saa kumi na mbili, sasa sahii nioge tena ili iweje" alijiwazia mwenyewe na kuvua nguo haraka haraka na kujitupa tena kitandani akiusaka usingizi. Kwa mbali aliskia simu yake ikiita kipindi hicho alikuwa ndio usingizi unamnyemelea, akainuka huku akisonya kwa kukatishwa usingizi wake usiku huo, akaichukua simu yake na kusoma jina la anaempigia“Afande Taure" jina lilosomeka hivyo, akaipokea.
“Niambie Afande" Mrutu aliongea.
“Mrutu, nilikuwa nakujulisha kwamba Hemedy hatorudi huko kwahiyo atalala huku huku"
“Anhaa!!! Basi sawa hakuna shida"
“Haya poa usiku mwema" Simu ikakatwa na Mrutu kurudi tena kitandani kuusaka usingi kwa mara nyengine, baada ya muda, akalala.
Nyumbani kwa Inspekta Ganjo, baada ya sherehe kuisha, watu walianza kuondoka mmoja mmoja kuelekea makwao, ila Hemedy yeye hakuruhusiwa kuondoka na Inspekta Ganjo akamtaka alale hapo hapo, waliobakia waliondoa ondoa viti vyote na vitu vyengine vilivyotumika kwenye sherehe hiyo, baada ya kuondoa kila kitu, wakaingia ndani ya hiyo nyumba na kila mmoja akaenda kulala, sebuleni wakabakia Hemedy, Koplo Taure, Afande Jesca, Inspekta Ganjo na Hilda.
“Hemedy" Inspekta Ganjo aliita.
“Nam! Babu" Hemedy nae aliitikia.
“Aaa!!!! Usiniite babu bwana, mimi na baba yako, baba yako alikuwa ni mkubwa kwangu, alinipita mwaka mmoja, sasa wewe utaniitaje babu, we niite baba tu, anaetakiwa kuniita babu ni huyu Hilda hapa. Unajua mimi na baba yako tulikuwa marafiki sana kipindi hicho tunasoma, tulipomaliza ‘form six', mimi nikajiunga na jeshi baba yako akaendelea kusoma, wakati anasoma mimi huku nikaajiriwa kwenye jeshi la polisi, sikutaka kupoteza muda nikaoa, baada ya mwaka mmoja nikapata mtoto wa kike, mtoto huyo alipozaliwa, uzao wake ukaondoka na maisha ya mke wangu, nikabakia na mwanangu ambae niliachiwa na mke wangu, sikutaka tena kuoa mke mwengine, nikaamua nimlee mwanangu.
Baba yako alipomaliza chuo, akaajiriwa kwenye bandari, nikamshawishi aowe ila yeye akajifanya m'bishi, mwenyewe alidai hadi ajiajiri mwenyewe, baada ya miaka tisa ya kuajiriwa bandarini ndipo alipofungua miradi yake na yeye ndio akaoa, wakati huo mimi mwanangu alikuwa na miaka kumi na nane. Baada ya miaka miwili mbele, baba yako na mama yako, ndipo walipo kupata wewe, na mimi mwanangu katika kurukaruka kwake, akapata mimba, na yeye baada ya kumzaa huyu(akamuonyeshea kidole Hilda) na yeye akafa kama mama yake baada ya kujifungua, kwahiyo hapa nimebakiwa na huyu mjukuu wangu ndio kila kitu kwangu, nampenda kama ninavyojipenda mimi"
Inspekta Ganjo baada ya kutoa historia fupi ya maisha yake yeye na Mzee Mheshimiwa, akawaambia Hemedy na Hilda kuwa wao ni ndugu japokuwa hawakutoka katika ukoo mmoja yani undugu huo umeunganishwa kwa urafiki wa wazazi wao.
Akawaambia wapeane mikono ishara ya kufahamiana, Hemedy na Hilda walipeana mikono kwa sekunde tano na kila mmoja akaachia mkono wa mwenzake, kwakuwa muda ulikuwa umeenda sana, ikabidi Koplo Taure na Afande Jesca waage na kuondoka zao, wakawaacha Inspekta Ganjo, Hemedy na Hilda wakiendelea na stori, Hemedy alipopata nafasi ya kuongea basi aliwachekesha na kuwafanya hata wasahau kama huo ni usiku wanahitajika wakalale, baada ya kukaa sana sebuleni hapo ikabidi Hemedy aonyeshwe chumba cha kulala na kila mmoja akaingia katika chumba chake kwajili ya kwenda kuitafuta kesho yake.
* * * *
Siku iliyofuata Inspekta Ganjo, aliinuka kama kawaida yake saa kumi na mbili na nusu, akajiandaa kwenda kazini, baada ya kumaliza kujiandaa, akaingia chumba alicholala Hemedy na kumkuta bado akiwa amelala, aliishia kutabasamu tu baada ya kukumbuka vituko vya Hemedy, akafunga mlango na kuwaendea wafanya kazi wa nyumba hiyo, akawaachia maagizo flani flani na kuondoka zake.
Kange. 7:17 Mchana.
“Kwa huu muda tulio waacha unatosha kabisa kulipiza kisasi, nahisi wanadhani tumewaogopa kwa kile walicho tufanyia, sasa ni hivi muda wowote ule tutakapo waona popote pale, lazima walipe kwa walicho tufanyia" Kijana mmoja mwenye macho ya paka aliongea kuwaambia wenzake wawili.
“Doze, unajua kwamba wale watu wana kundi kubwa?" Kijana mwengine mwenye mwili mwembamba alimuambia kijana wa mwanzo kuongea mwenye macho ya paka, alietajwa kwa jina la Doze.
“Haaa!! Kwahiyo Tosh na wewe unawaogopa wale wapumbavu?" Doze alimwambia kijana wa pili kuongea alietajwa kwa jina la Tosh.
“Hapana, si maanishi hivyo" Tosh aliongea.
“Sasa maana yako ni ipi? Wakati tayari ushaonyesha uoga juu ya wale wajinga" Doze alisema.
“Mimi nilikuwa namaanisha kwamba, tusiwaingilie hovyo hovyo, tunaweza tukageukiwa sisi kama siku ile" Tosh aliongea.
“Hapo nimekupata, nilidhani na wewe tayari ushaanza kuwaogopa wale wajinga"
“Wale hawatusumbui tena, bora tayari tumepajua sehemu wanayopenda kwenda kunywa, tutawafuata na kuwaulia mbali tu"
“Hapana, wale hatuwaui kwanza, wale tunawateka halafu tunawaambia wampigie simu bosi wao, aturudishie pesa zetu la tunawaua watu wake, sasa akisharudisha pesa zetu ndio tutajua tuwaue au tuwaache" Kijana mwengine wa tatu, aliekuwa kimya muda wote, alienyoa para na kufanya chogo lake litokeze kwa nyuma, nae akaongea.
“Kiku, unauhakika tukiwateka wale watu, yule mzee ataturudishia pesa zetu?" Tosh aliuliza.
“Lazima arudishe, kwasababu yule mzee wale watu ndio watu wake anaowategemea kwa kila kitu, kwahiyo lazima arudishe tu"kija mwenye chogo, alietwa Kiku alijibu.
“Halafu sikutegemea kama yule mzee anafanya biashara zile" Tosh alisema.
“Sasa hivi hakuna kumuamini mtu, watu wengine wanafanya wema kwa watu ili kulinda maovu yao yasigundulike, sasa wewe unadhani ni nani amabe ukimwambia kuwa mzee yule anafanya biashara kama ile ambayo serikali inaipiga vita kila siku, atakubali, hakuna ambae atakae kuamini hata kidogo" Kiku alisema.
“Kwahiyo hii ishu tunaianza lini?" Doze aliuliza.
“Ikiwezekana ianze leo, hamjui tu jinsi gani ninauchungu wa kuchukuliwa pesa zetu na mzigo wao, hawajui zile pesa sisi tumezitoa wapi, halafu wao wanakuja kuzichukua kirahisi rahisi tu" Kiku aliongea kwa uchungu.
“Kama ni hivyo fresh, itabidi leo tukawatege pale kwenye ile club wanayopenda kwenda kunywa, lazima tuwatie mikononi tu" Tosh aliongea.
“Kama ni hivyo hakuna noma, acha kwanza mimi niwaache, kuna demu mmoja naenda kumshuhulikia mara moja, kwahiyo tutakutana baadae" Kiku aliongea huku akiinuka kwenye sofa alilokaa.
“Oya Kiku, angalia lakini huyo demu asije akakulegeza, ukashindwa kuifanya hii ishu baadae" Doze alimwambia hivyo huku akicheka.
“Usijali, naenda kupunguza maji kidogo tu, maana mwili wangu nahisi kuna uzito umeongezeka" Kiku aliongea hivyo huku akiufunga mlango wa nyumba hiyo.
Nyumbani kwa Inspekta Ganjo. 11:09 Jioni.
Hemedy baada ya kushinda kwa kutwa nzima nyumbani kwa Inspekta Ganjo, akataka kuondoka ili aelekee nyumbani kwao, lakini aliekewa pingamizi kubwa na watu waliokuwepo kwenye hiyo nyumba ya Inspekta Ganjo la kuondoka hapo, kila mmoja akataka abaki hapo hapo, kwa jinsi walivyo muhusudu kwa muda waliokaa nae, aliwachekesha, aliwafurahisha kwa kila namna, alifanya wampende ghalfa kutokana na uchesi wake, lakini nae akasimamia msimamo wake kuwa ni lazima aondoke hapo aelekee kwao, baada ya kumlazimisha sana, akakubali kubaki, lakini akawaambia kwamba ni lazima aongee na baba yake mdogo ili nae ajue atasema nini kuhusu kubaki hapo hadi wikiendi itakapo isha. Wakampigia simu Inspekta Ganjo, wakamuambia kuwa wanataka kubaki na Hemedy nyumbani hapo hadi kesho yake ndipo aondoke, Inspekta Ganjo akawakubalia, wakamuambia kuwa Hemedy amesema anataka kupata ruksa ya baba yake mdogo kuhusu kubaki hapo. Inspekta Ganjo nae akamwambia Koplo Taure ampigie simu Mrutu aongee nae kuhusu ombi la Hemedy, Koplo Taure nae akampigia simu Mrutu na kumuambia alivyoambiwa na Inspekta Ganjo, Mrutu hakuwa na pingamizi akamkubalia Hemedy akae hapo hadi kesho yake. Koplo Taure akarudisha majibu kwa Inspekta Ganjo na Inspekta Ganjo nae akamruhusu Hemedy akae nyumbani kwake hadi hapo kesho.
Walifurahi baada ya kuruhusiwa kubaki na Hemedy hadi hapo kesho, ikabidi mfanya kazi mmoja wa kiume anaempeleka na kumrudisha Hilda shule, achukue gari na kuenda na Hemedy hadi nyumbani kwa Mrutu, walipofika Hemedy aliingia ndani chumbani kwake, akaoga na kubadilisha nguo, baada ya hapo alirudi tena kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani kwa Inspekta Ganjo ikaanza.
Hobours Club. 4:30 Usiku.
Tito na Tobi, walienda kwenye club hiyo walioyozoea kuenda kunywa hapo, wakaenda kwenye meza iliyokuwepo gizani kidogo na kukaa, waliagiza pombe na kuanza kunywa mdogo mdogo huku wakiendelea na stori zao.
Kwenye meza nyengine iliyokuwa mbali na meza waliyokaa wakina Tito, kulikuwa kuna watu watatu wamekaa wakiwaangalia wao.
“Sasa tunafanyaje, windo letu lilepale tayari limeshafika" Tosh aliongea kuwaambia wenzake.
“Tusiwe na wasiwasi, tusubirini kwanza kama lisaa limoja, walewe ndipo tutakapo enda kuwateka" Kiku aliongea.
Baada ya kukubaliana hivyo, wakawaacha wakina Tito kwa lisaa limoja ndipo wakawateke. Baada ya kuwasubiri sana, ndipo walipoamua wawafuate na kuwateka. Doze na Kiku, waliinuka na kuwaendea wakina Tito kwenye meza yao, walipofika wakachomoa bastola zao na kila mmoja akamuekea mtu wake bastola ya mbavu, Doze alimuwekea bastola ya mbavu Tito na Kiku alimuwekea bastola Tobi.
“Mnatakiwa mtulie hivyo hivyo, mkifanya ujinga wowote, basi bastola hizi zitatawanya mbavu zenu" Kiku aliwaambia, alipoona wametulia akaendelea.
“Haya wekeni bastola zenu juu ya meza na msifanye ujinga wowote utakao mfanya malaika mtoa roho, aje hapa ikiwa mwenyewe amepumzika huko juu kwa mungu" Kiku aliwaambia hivyo, Tito na Tobi wakazitoa bastola zao na kuziweka juu ya meza, Doza akazichukua na kuzichomeka kiunoni kwenye jinzi yake aliyoivaa.
“Haya inukeni taratibu kabisa, kumbukeni kosa moja la mmoja wenu linaweza likamshababishia na mwenzake kifo, kwahiyo tunaomba mtulie na mfuate tunachotaka, haya inukeni taratibu" wakainuka na kusubiria amri nyengine, kipindi hicho Tito alikuwa anatafuta mbinu ya kujinasua kutoka kwa hao watu wasio wajua.
“Haya, tunaanza kuondoka taratibu, kama vile marafiki kumbe ni maadui wakubwa tu, kumbukeni kosa moja litawagharimu maisha yenu" Kiku aliendelea kuwaonya, wakaanza kutembea taratibu, ila baada ya kupiga hatua mbili mbele, ghafla.....
“Haya, tunaanza kuondoka taratibu, kama vile marafiki kumbe ni maadui wakubwa tu, kumbukeni kosa moja litawagharimu maisha yenu" Kiku aliendelea kuwaonya, wakaanza kutembea taratibu, ila baada ya kupiga hatua mbili mbele, ghafla Tito akajaribu bahati yake ya kutaka kujiokoa, akamsukuma Doze, na kwakuwa Doze hakujiandaa na tukio hilo, akajikuta akipepesuka na kwenda hadi chini na bastola aliyoishika ikaanguka mita chache mbele yake, Tito alivyotaka kuiwahi, akajikuta akitulizwa na ngumi moja ya pua, akanza kuona mawenge, akahisi kama vile kuna kimiminika kikitoka katika pua zake na churuzikia mdomoni mwake, hakujua ni nini hadi pale alipopeleka mkono wake puani akagusa kidogo na kuuangalia, na kukuta ni damu ndio ambayo inatoka katika pua yake, akataka kujua ni nani huyo aliefanya hivyo, ndipo hapo alipotupa macho yake mbele yake na kumuona mtu mwengine tofauti na wale wawili waliowateka.
Tosh akaiyokota bastola iliyoanguka na kumpa Doze bastola yake na yeye akaondoka hapo kuelekea nje kwenye gari lao na kuingia humo.
Doze na Kiku, waliwaongoza wakina Tito kama vile hakuna kitu kinachoendelea, watu wengine waliokuwepo hapo club wala hawakujua kwamba watu hao wana kitu wanafanyiana, walitoka nje ya club hiyo na kuelekea kwenye gari lao walilokuja nalo, wakatoa kamba ngumu na kuwafunga wakina Tito mikono yao kwa nyuma, kisha wakawaingiza kwenye gari.
“Nyie si mlikuwa mnajifanya wajanja kututapeli pesa zetu na mkaondoka na mzigo wenu? Haya sasa tutauona ujanja wenu, lazima mtalipa tu kwa mlio tufanyia" Kiku aliongea hivyo na kumuambia Tosh aondoe gari kuondoka hapo na kutokomea kuelekea wanapopajua wao, hadi hapo wakina Tito wakawa tayari wameshajua walio wateka ni wakina nani.
Baada ya dakika ishirini, wakafika katika jumba moja lililochoka ila lilikuwa na milango na madirisha yake, wakawaingiza humo na kuwafungia kwenye viti vilivyokuwepo humo humo ndani, wakawafunga kwa kamba ngumu kiasi ambacho zile kamba zikawa zinawaumiza kwa jinsi zilivyokazwa.
“Kuanzia sasa nyumbani kwenu patakuwa ni hapa, kwahiyo tunamiomba mufurahie maisha mapya" Tosh aliongea hivyo huku akiwacheka.
“Tosh, embu tuwasachi hawa, huwenda wakawa na kitu chengine cha kujitetea" Doze aliongea hivyo huku akiwafuata, aliwapekuwa kila sehemu na kutoa visu,sigara, pesa na simu zao na kuvitia mfukoni mwake.
“Ok, mnaweza mkapiga stori wenyewe kama mtapenda kufanya hivyo" Kiku aliongea.
Baada ya kuhakikisha wamewaweka katika hali ambayo hawezi kujinasua hapo, wakaondoka na kutokomea zao wanapopajua wao.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Oya Tito, tunafanyaje ili kujiokoa hapa?" Tobi alimuuliza Tito huku akijaribu kujitingisha aone kwamba anaweza kutoka hapo alipo fungwa ila aliishia kujiumiza tu na hizo kamba alizofungwa nazo.
“Hapa hatuwezi kutoka, tusubirie tu tuone watatufanya nini" Tito aliongea hivyo huku akitafuta pozi la kujiweka vizuri, maana alisikia maumivu mara mbili, maumivu ya kukazwa na kamba na maumivu ya pua yake iliyoadhibiwa na Tosh. Kwakuwa hawakuwa na la kufanya, wakabaki wametulia tu.
*******************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment