Search This Blog

Monday 24 October 2022

PATASHIKA - 5

 









    Simulizi : Patashika

    Sehemu Ya Tano (5)









    Vivian alikuwa anashindana na nafsi yake kama ama awaeleze wenzie yale aliyoambiwa na Mwasumbi ama asiwaeleze. Lakini mwisho wa siku akawa amekata shauri kutowaambia.

    “Kabla sijaachana na Mwasumbi, alivuta kwa nguvu nywele chache toka kichwani kwake na kunipatia, alisema ana hakika ipo siku nitazihitaji.” Vivian aliamua kuwaambia hilo maana hakuona kuwa lilikuwa na taarifa yoyote kuhusiana na habari ya silaha aliyokuwa ameambia na Mwasumbi.

    “Ziko wapi hizo nywele? Yule Mzee ana akili sana, sasa nakubali kuwa anaweza kuwa baba yangu, sikuwahi kumpenda Paul, hakukuwa na mvuto wowote wa baba na mwana kati yangu mimi na yeye. Huyu Mwasumbi kwa namna mnavyonisimulia na matendo yake huyu anaweza kuwa ni baba yangu huyu...” Milka alisema, lakini akakatizwa na Vivian.

    “We, Milka hebu angalia hicho kinywa chako hicho kisije kikaponza kichwa, watu hawachaguagi baba, baba huchaguliwa na mama pale mama anapoamua kuzaa na mwanaume alomridhia...” Vivian alisema, kwa namna ya kumuonya Milka juu ya kauli aliyokuwa ameitoa kuhusu Mzee Paul.

    “Ziko wapi hizo nywele?!” Hellen alimkatiza Vivian kuonyesha kuwa hakuwa amezingatia onyo lake. Japo kutokana na maelezo yote ilikuwa inaelekea kuwa yeye peke yake ndiyo mtoto halisi wa Paul lakini tangu siku ile aliponusurika kunyongwa kule shambani, Hellen amekuwa na chuki ya ajabu dhidi ya Mzee Paul. Hivyo lolote baya lililosemwa au kupangwa dhidi ya Mzee Paul lilikuwa likiifurahisha na kuiburudisha nafsi yake. Hivyo onyo la Vivian kwa Milka kuhusu kauli mbaya ya Milka juu ya Mzee Paul hakulipenda hata kidogo.

    “Hizi hapa!” Vivian alisema huku akiwa anafungua saa yake ya mkononi. Alizitoa zile nywele na kuwakabidhi wenzie.

    “Sikilizeni, kama nilivyosema hapo awali, huyu Mzee Mwasumbi ana akili sana na kweli anastahili kuwa Luteni wa Jeshi. Unajua inawezekana hakuwa na hakika juu ya maisha yake, na alijua kuwa Vivian angetaka kuthibitisha kama kweli yeye ni mtoto wake. Hivyo hizi nywele zinaweza kutumika kupima vinasaba vya yule Mzee na kulinganisha na vya mtoto..." Kabla Milka hajamaliza maelezo yake, Hellen akadakia.

    “Nakubaliana na wewe Milka, naona na wewe una akili kama baba yako Mwasumbi. Kweli hilo ndiyo lengo halisi la yeye kukupatia hizi nywele. Ila nami nina wazo la kuchangia...” Hellen alisema kwa sauti ya kushadadia

    “Sema tu.” Milka alijibu kwa haraka kwa ile sauti ya kushabikia pia. Vivian alikuwa akiwaangalia na kuwasikiliza.

    “Hakuna ajuaye hatima yetu, inawezekana sote tukatoka salama na kuendelea na maisha yetu ya kawaida au pia inawezekana hatutoka hapa salama. Lakini pia, inawezeka baadhi tukatoka salama na wengine tukaishia hapa.” Hellen aliongea lakini kauli yake ilikatishwa na Milka aliyelalamika.

    “Aaaah! shostito, acha kutuchuria basi, we sema unalotaka kusema hayo mambo ya kufa wakati wengine ndiyo tunataka tukitoka hapa tukaanze kuyafaidi maisha wala halikubaliki. Sema unachotaka kusema, kama kufa tungekufa siku ile kule Kijijini.” Milka aliongea.

    “Ninachotaka kusema ni kuwa, wote tufanye kama Mzee Mwasumbi alivyofanya, tutoe nywele zetu na tuziweke kwenye mafungu matatu kama tulivyo, kila unywele mmoja wa mmoja wetu tuuweke na kipande cha nywele ya Mzee Mwasumbi. Halafu kila mmoja awe na hayo mafungu matatu, ili akifanikiwa kutoka hapa salama afanye hivyo vipimo. Manaonaje?” Hellen alimalizia maelezo yake.

    “Wazo zuri Hellen, nadhani tufanye hivyo.” Vivian aliafiki.

    “Wewe naye una akili sana usije kuwa mtoto wa Mwasumbi pia, maana anaonekana alikuwa kiwembe sana yule mtu.” Milka alisema.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aaah! mimi bwana nimechukua akili za mama yangu, alikuwa na akili sana yule, ndiyo maana nadhani alishindwa kuishi na mtu kama Mzee Paul.” Hellen alisema kwa kujitapa.

    “Unamaanisha nini? Ina maana mama Maganga aliyeweza kuishi na Mzee Paul alikuwa mjinga?” Vivian alihoji kwa sauti ya kuonya kwa mara nyingine. “Utamuweza huyu, si anaongea tu bila kufikiri saa nyingine.” Safari hii Milka lilimgusa kwa vile mama yake alikuwa amesemwa, hivyo akaunga mkono onyo la Vivian.

    “Haya tuyaache hayo, tusijeanza rushiana ngumi wenyewe kwa wenyewe bure.” Vivian alisema tena. Baada ya hapo walizigawa zile nywele katika mafungu matatu na kuziweke alama ili kujua ipi ilikuwa ya nani. Kisha kila mmoja wao akapewa aina tatu za nywele ili azitumie pindi ikihitajika.

    Maisha yao yaliendelea hivyo kwa wiki kadhaa, wakajikuta wamezoeana. Waliongea wakamaliza yakuongea, waliangalia muvi hadi wakachoka. Hatimaye maisha ndani ya nyumba hiyo yakawa mchoko mkubwa kwao. Yule Bibi aliendelea kuwapikia na kuwapa huduma. Jambo moja liliwashangaza, hawakujua ni saa ngapi na namna gani yule Bibi aliletewa chakula cha kuwapikia. Ila walikuta tu yule Bibi anabadilisha mapishi kila siku na vinywaji vikiongezeka kwenye friji.







    MWASUMBI ALIREJEWA na fahamu taratibu kama zilivyokuwa zimemtoka. Aliweza kuyasikia mapigo ya moyo wake jinsi yalivyokuwa yakilazimishwa taratibu na mzungunguko hafifu wa damu. Alifumbua macho na kujaribu kutambua alikuwa wapi, lakini nguvu ya giza lilokuwa limetanda kila mahali ilimzidi macho yake. Hakuweza kuona chochote. Alijaribu kujitingisha, hapo akasikia ule mlio wa mbao kusuguana. Mlio wa kitanda kilichochoka. Alijaribu kupapasa aligundua kuwa alikuwa amelala juu ya mkeka. Akataka kuinuka, lakini maumivu makali toka kila sehemu ya mwili wake ilimzuia kuinuka. Baada ya dakika chache macho yake yakawa yameshazoea giza, alikodoa kwa nguvu zaidi huku akidhani kuwa kukodoa sana ndiyo kuona. Hatimaye akagundua kuwa alikuwa ndani ya chumba au nyumba. Aliweza kuona mwanga hafifu ulioweza kupenya kwa wembamba kama michirizi kwenye kuta za nyasi za chumba au nyumba aliyokuwa. Hatimaye alikuwa na hakika kuwa alikuwa ndani ya chumba cha nyasi baada ya kujitahidi na kufanikiwa kugusa sehemu ya ukuta wa chumba hicho – vidole vyake vilikutana na nyasi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Khoo khoo...aaaar!” Ilikuwa ni sauti ya kukohoa toka upande wa nje wa sehemu aliyokuwepo. Sauti ilionyesha dhahiri kuwa aliyekuwa anakohoa alikuwa na umri uliokwenda sana. Mwasumbi alijaribu kukumbuka tukio la mwisho wakati akipambana na Sophia.

    Alichokumbuka ni kuwa, mara baada ya kuwa ameachana na Vivian, alibana sehemu huku akiwatayari kwa lolote. Nia yake ilikuwa ni kupambana na yeyote yule, alijua wazi kuwa KAPTEN na Paul wangecharuka kama nyuki mara baada ya yeye kuwawahi na kumchukua Maganga. Kwao ilikuwa kama kupokonywa tonge mdomoni.

    Akiwa amejituliza kwenye kichaka fulani kilichokuwa jirani na nyumba moja ya nyasi eneo lile, aliweza kumwona Mzee mmoja aliyekuwa akiendesha baiskeli kuelekea barabarani. Ilikuwa inaelekea kuwa saa tisa alasiri wakati hayo yalipoanza kutokea. Wakati Mzee yule alipokaribia kuingia barabarani lilitokea tukio ambalo lilimsisimua Mwasumbi. Kwa nukta ya kwanza aliona Ua Jekundu likianguka mbele ya baiskeli ya yule Mzee, wakati yule Mzee anatafakari nini kilikuwa kinatokea na kuliangalia lile ua jekundu pale chini. Ghafla alikuja mtu aliyekuwa anajiviringisha kwa sarakasi kama kimbunga cha kiangazi. Mwasumbi alifanikiwa kutambua kuwa yule mhusika alikuwa ni mwanamke kwa jinsi mtikisiko wa nyonga zake na makalio ulivyokuwa pindi alivyokuwa akiruka. Lakini alishindwa kutafsiri jinsi yule msichana alivyompiga yule Mzee, kwani alipofikia mahali pale yule Mzee alipokuwa amesimamisha baiskeli yake akitaka kuokota lile ua, yule msichana alisimamia mikono na kwa kutumia miguu aliishika shingo ya yule Mzee na kuivunja. Hata risasi zilizotoka kwenye Bastola ya Mwasumbi ziliishia kuzikosakosa buti za yule msichana. Awali Mwasumbi alikuwa amejiandaa kumtetea yule Mzee, alijua fika kuwa yule mtu aliyekuwa akienda kumshambulia yule Mzee angetumia moja ya staili zilizozoeleka, hivyo shabaha yake ilikuwa imekadiria eneo ambalo kichwa kingekuwepo wakati huo. Staili hiyo ya uuaji ilimfanya Mwasumbi mara moja amkumbuke Sophia. Mwasumbi alijiweka sawa kwa pambano. Wakati macho yake yakiwa kwa Sophia maarufu kwa jina la Ua Jekundu, mara akasikia mchakacho tokea mgongoni kwake. Akahisi kitu kinakuja, alikwepa kwa kasi na kulipisha teke lililokuwa limepigwa na mtu tokea nyuma. Mwasumbi alijipindua na kuachia teke kali lililompata yule mtu ubavuni. Akaongeza jingine ambalo lilimpeleka chini. Hapo hakutaka kusubiri, aliachia risasi iliyolenga moyo na kumuua yule jamaa. Kabla hajakaa sawa walitokea wengine wawili. Mwasumbi alichomeka bastola kwenye mkanda wake. Akawa tayari kukabiliana nao, kitendo cha yule wa kwanza kumnyatia bila kummaliza ilikuwa taarifa tosha kwa Mwasumbi kuwa watu hao walimtaka akiwa hai. Hivyo alijua kuwa yeye alikuwa na nafasi na uhuru mzuri wa kuwamaliza kuliko wao, alielewa kuwa walikuwa na wakati mgumu kuliko yeye. Ndiyo siri ya mchezo, mtu anayetakiwa kumshika mwenzie huku kukiwa na sharti la kumbakiza hai huwa na wakati mgumu zaidi kuliko yule anayewindwa. Hapo likatokea pambano moja safi sana, lilibadilika toka mpango wa kutekana nyara na kuwa kufa na kupona. Kila mmoja alitumia uwezo na mbinu zake. Hadi mpambano unakwisha wale jamaa walikuwa maiti ambazo bado zilikuwa za moto zikiwa zinalilia pumzi iliyozitaliki. Mwasumbi alikuwa hoi lakini alijua hakuwa na muda wa kujipooza wala kupumzika. Wakati akitembea taratibu toka sehemu aliyokuwepo, mara akasikia mlio wa kitu kama jani likidondoka. Hakutaka kugeuka kuangalia, alishajua huyo angekuwa nani na kama akigeuka tu angekuwa ameshaingia kwenye mahesabu ya adui, alijirusha pembeni wakati pigo la aina yake la mkono wa Sophia likipita kwa kasi kama upanga uliopiga hewa. Mwasumbi aliachia mapigo manne mfululizo, mawili yalimpata Sophia, lakini mawili yalikwepwa.

    “KAPTEN anakuhitaji, sijatumwa kukuua, ila ukinilazimisha unajua nini naweza kufanya.” Alisema Sophia kwa sauti ya kike ya kikatili.

    “Haiwezekani, ama nife au ufe, maana kwa vyovyote nitaishia kufa au kuua.” Mwasumbi alisema huku akijiweka sawa tayari kwa mpambano. Alikuwa anamjua Sophia, alijua nguvu zake na udhaifu wake. Akakumbuka kuwa walianza hii kazi pamoja mara baada ya kufanikiwa kumshawishi ajiunge na kundi lao la kuzitafuta karatasi zilizo na kanuni ya kutengenezea silaha. Sophia akabaki kwenye upande wa kuua na kushambulia wakati yeye Mwasumbi na Paul wakiwa kwenye upande wa kimkakati zaidi huku wote wakitumiwa na KAPTEN bila kujuana. Kapten alikuwa bosi wao wote wawili walipokuwa Dar es salaam na aliwaweka Katunguru makusudi. Alijua uwezo wa Sophia kuwa hakuwa mtu wa masihara hata kidogo.

    “Okay, chukua au acha…!” Sophia hakumalizia kauli yake, alijipindua kwa staili ya kipekee na kuachilia mapigo mfululizo kwa Mwasumbi. Mwasumbi alitumia uwezo wake wote kuyaona na kujikinga lakini hatimaye mengi yakaanza kumwingia.

    “Hebu niambie, Maganga umempeleka wapi?” Sophia aliuliza huku akiwa amejaa ghadhabu.

    Japo alikuwa taabani, Mwasumbi alijua fika kuwa kama angesema tu angehalalisha kuuawa na Sophia. Maana sababu pekee ambayo ingewafanya watu hawa waendelea kumuacha hai ingekuwa ni kutaka kujua Maganga alipo.

    “Si..si..sijui..muulize Mr M” Mwasumbi alisema. “Hebu acha kunichezea, unajua fika kuwa Paul hajui lolote na kwa uzembe alioufanya na yeye anakabiliwa na kifo huko aliko!” Sophia alisema huku akiongezea vipigo kuelekea kwa Mwasumbi.

    Mwasumbi sasa alikuwa taabani kabisa. Lakini Sophia aliendelea kutoa kipigo kikali. Alijua fika kwa mtu mzoefu kama Mwasumbi ili aweze kutoa siri lazima umpeleke katikati ya hali ya kifo na uzima, huku nafsi ikiachiwa nguvu ndogo sana ya kuamua, ndipo angeweza kuropoka.

    Wakiwa katika hali kama hiyo, Mwasumbi akajikuta anapoteza uwezo wa kufikiri na akawa hajielewe elewi, mara akaanza kuropoka vitu asivyovijua. Wakati hali hiyo ndiyo ambayo Sophia alikuwa akiisuburi, maana alijua katika hali hiyo angeweza kuyapata mawazo yaliyoko sirini mwa Mwasumbi maana midomo yake sasa ilikuwa ikiropoka yaliyoko moyoni. Kumbukumbu ya mwisho kabisa ambayo Mwasumbi aliweza kuidaka kwa mbali aliweza kusikia sauti kama ya inzi wengi sana, hakuelewa walitoka wapi. Hiyo ndiyo ilikuwa kumbukumbu ya mwisho, hakuweza kukumbuka kilichofuata. Sasa alijikuta yuko kwenye hiyo nyumba ya nyasi. Akiwa bado yuko pale kitandani, aliweza kuona kitu kama mlango kikifunguka, lakini ukubwa wa mwanya huo haukutosha kuitwa mlango wala dirisha lakini kwa vile ulikuwa ardhini na kuunganika na sehemu ya paa, Mwasumbi aliamua kuutambua kama mlango. Mara akaingia mtu, alijua ni mtu kwa vile aliona miguu miwili na mikono, lakini giza halikumruhusu kuweza kuiona sura ya mtu aliyekuwa ameingia. Mtu huyo alisogea hadi pale alipokuwa amelala. Aliingiza mkono chini ya uvungu, akatoa kiberiti, akawasha koroboi ambayo mwanga wake sasa ulifanikiwa kulifukuza giza lililokuwa limetanda. Sasa aliweza kuiona vema sura ya mtu aliyekuwa mbele yake, alikuwa Mzee aliyekuwa na nywele na ndevu nyingi nyeupe. Yule Mzee alipomsogelea Mwasumbi karibu zaidi huku vidole vyake vikavu vilivyokuwa vikitetemeka vikiwa vinatomasa majeraha ya Mwasumbi kwa mtindo wa kuyakagua, ndipo alipoweza kusikia harufu kali toka kwa huyo Mzee. Mzee huyo alikuwa akitema mate mara kwa mara. Aliendelea kutomasa majeraha ya Mwasumbi baada ya dakika kadhaa, alichukua mkoba fulani na kutoa mikebe midogo midogo. Mwasumbi aliendelea kujifanya hajui kinachoendelea ili kujipa nafasi ya kujua nini kilikuwa kikiendelea. Yule Mzee alifungua baadhi ya mikebe na kuanza kuchukua ungaunga toka kwenye hiyo mikebe na kuyapaka majeraha yaliyokuwa mwilini mwa Mwasumbi. Maumivu yaliyoletwa na zile dawa, yalimfanya Mwasumbi ajinyonge nyonge kwa uchungu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Oooooh umeshaamka!” Alisema yule Mzee kwa sauti ya kukoroma.

    “Niko wapi hapa?” Mwasumbi aliuliza badala ya kujibu.

    “Usiogope uko salama, maana yule mwanamke siku ile alikuwa anataka kukua kabisa!” Alisema yule Mzee.

    “Mwanamke yupi?” Mwasumbi alijifanya kuuliza japo alijua yule Mzee alikuwa akimwongelea Sophia.

    “Yule uliyekuwa unapambana naye. Alikuzidi nguvu kabisa, sema nikaingiwa na huruma nikaamua nikuokoe.” Alisema yule Mzee huku akiwa anafungasha dawa zake na kuzirudisha kwenye mkoba wake.

    “Unajua sikumbuki chochote kilichotoke, naomba uniambie Mzee!” Mwasumbi alisema ili aweze kuunganisha matukio.

    “Nilimwona jinsi alivyomuua Mzee Magesa, yule Mzee aliyekuwa akiendesha baiskeli. Nikaona jinsi ulivyopambana na wale wengine, kisha ulivyojaribu kupambana naye lakini akakuzidi nguvu. Sikupenda jinsi alivyokuwa akikutesa, nikaamua kukusaidia.” Alisema yule Mzee.

    “Sasa ulinisaidiaje, maana siamini kama uliweza kukabiliana na yule muuaji?” Mwasumbi alihoji kwa mshangao.

    “Ha ha ha ha!, nilituma askari wangu, askari wangu huwa hawashindwi kabisa.” Alisema yule Mzee huku akicheka na kukenua meno yake ambayo yalikuwa ya njano huku fizi zake zikiwa zimefunikwa na ukoko mzito wa njano.

    “Una askari wewe Mzee?” Mwasumbi alihoji kwa mshangao zaidi.

    “Ndiyo, hata hapa tulipo ndiyo wanaotulinda, maana baadaya kufanikiwa kumfukuza siku ile alipotaka kukua, yule mwanamke amerudi hapa Kijijini zaidi ya mara tano, ameshakagua kila mahali na kuua watu kadhaa lakini wiki ya pili hii sasa askari wangu hawajamruhusu kukaribia hili eneo hadi amekata tamaa maana sijamwona kwa hizi siku nne.” Alisema yule Mzee kwa kujitapa.

    “Sikuelewi Mzee, ni kweli inaonekana umenisaidia maana nipo hapa na nimeona ukiwa unanipa dawa, ila suala la askari wako hapo sikuelewi, labda kama utafafanua kidogo.” Mwasumbi alikuwa mpole.

    “Unajua shida yenu ninyi vijana mnadharau sana jadi yenu. Kwa namna nilivyoona mnapambana kwa ustadi mkubwa, kama mngechanganya ule uwezo wenu na uwezo wetu wa jadi hakuna ambalo lingeshindikana. Hebu tulia halafu sikiliza kwa makini uniambie unasikia nini?” Mzee alisema huku safari hii akiwa anamenya kipande cha Muhogo. Mwasumbi alijituliza na kujitahidi kusikiliza kama alivyoambia. Naam! Alisikia mlioa wa kitu kama nzi, na mara hiyo akakumbuka kuwa alisikia mlio kama huo mara ya mwisho kabla hajapotelewa na fahamu.

    “Nasikia mlio kama wa nzi wengi, nakumbuka siku ile kabla sijapoteza fahamu nilisikia huo mlio pia. Sasa huo mlio una uhusiano gani na wewe kuniokoa miye au askari unaosema?” Hatimaye Mwasumbi alisema. Huku akisikia kichwa kikiwa kinagonga kwa mbali.

    “Hao ni nyuki na ndiyo askari wangu. Hao ndiyo niliowatuma kumfukuza yule mwanamke siku ile. Kwa jinsi alivyokuwa anapigana hakuna mtu angeweza kumshinda, ila hakuna mtu anaweza kusimama na kupigana na askari wangu. Unajua kwa nini Nyerere alifanikiwa kwenye utawala wake na hata kwenye vita yake dhidi ya Idd Amini?” Alisema yule Mzee huku akijitapa.

    “Sijui, ila nashangaa unaposema nyuki ndiyo askari wako, wewe uliwezaje kuwaamuru nyuki?” Mwasumbi alisema kwa mshangao.

    “Ndiyo maana nimekuuliza…” Kauli ya yule Mzee ilikatizwa na sauti ya mlio wa bati tokea nje. “Ingia!” Yule Mzee alisema. Mara akaingia binti mmoja akiwa na ndoo kichwani. Aliingia kimyakimya, akaitua ile ndoo, halafu akapiga magoti, akainama mbele ya yule Mzee. Mzee hakujibu kitu aliendelea kutafuna muhogo wake huku mlio wa mmeng’enyo wa ule mhogo ukifika hadi kwenye masikio ya Mwasumbi. Yule binti alitoa vyungu vinne toka ndooni. Kisha akatoka nje ambapo alikuwa ameacha kikapu kingine, alikiingiza ndani. Toka ndani ya kile kikapu alitoa sufuria iliyokuwa imejaa vipande vya papai lililomenywa. Kisha akatoa kidumu cha maji. Aliinua kile kidumu cha maji akapiga magoti akiwa amejiweka tayari kumnawisha yule Mzee. Yule Mzee alipukuta mikono yake, kisha akanawa. Binti aliondoka.

    “Inabidi ule vizuri, hapa kuna samaki aliyechemshwa, chungu kingine kina uji wa mtama, kingine kina supu ya mlenda iliyochangwanywa na majani ya maboga na maharage mabichi, hiki kingine kina ugali wa ulezi uliopikwa kwa maziwa. Kwa vile tunakula ulezi ni vema tukamaliza kwa haya mapapai ili kuweka tumbo sawa tusije hangaika tukienda chooni. Kumbuka hujala kwa uhakika kwa muda mrefu, nimekuwa nikitumia njia za kienyeji kukupa chakula, ila sasa unatakiwa ule ili upate nguvu.” Alisema yule Mzee huku akisogeza vile vitu jirani na kilipokuwa kichwa cha Mwasumbi. Akaanza kumlisha na kumnywesha.

    “Nilikuwa nasema unajua nini kilimsaidia sana Nyerere kwenye uongozi wake na Vita ya Kagera? Nyerere alikuwa jirani na viongozi wa dini na wataalamu wa jadi kama sisi. Wewe unadhani kwa nini viongozi wengi walikuwa wakimwogopa Nyerere na kuwa waadilifu? Wengi waliogopa ile fimbo yake, ndiyo maana walimwita Mzee Kifimbo. Lakini pia kwenye ile vita ya Kagera, silaha kama hii niliyo nayo hapa vilitumika sana, ndiyo maana hadi leo Waganda huamini kuwa Watanzania ni wachawi sana, kumbe ni ufundi tu kama huu.” Alisema yule Mzee huku akiwa anajitafuna. Alikuwa akila na wakati huohuo kumlisha na kumnywesha Mwasumbi. Baada ya maelezo hayo ya yule Mzee, Mwasumbi alikuwa kimya tu akitafuna chakula. Ilikuwa wazi kuwa alikubaliana na wazo la yule Mzee kuhusu umuhimu wa yeye kula ili arejewe na nguvu zake za kawaida. Hivyo alijitahidi kufanya kila awezavyo kula ule mchanganyiko wa chakula aliokuwa ameletewa. Wakati huo huo alikuwa akiwaza mambo mengi yaliyokuwa yakipita kichwani kwake. Alimuwaza Maganga, alimuwaza Vivian, hakuwa na hakika kama alifanikiwa kufika mikononi mwa watu waliokuwa wakimsubiri. Lakini pia, alijisikia faraja alipokumbuka jinsi Sophia alivyokuwa amesema kuhusu Paul, ina maana KAPTEN alikuwa ameamua kumuua Paul baada ya kugundua kuwa ameshindwa kazi aliyokuwa amepewa.



    * * *



    Mwasumbi aliendelea kuwa hapo kwa siku kadhaa akiwa anapata matibabu. Sasa alikuwa na uwezo wa kutembea mwenyewe na kufanya mazoezi mepesi. Kibanda walichokuwepo, kama alivyosema Mzee kilikuwa kikilindwa na nyuki wengi sana waliokuwa wakiruka hapo muda wote. Mbali kidogo na hicho kibanda kulikuwa na vibanda kadhaa ambavyo walikuwa wakiishi wake wa Mzee na watoto. Aliyeleta chakula siku ile alikuwa ni mmoja kati ya wake zake. Umri wa yule msichana ulitosha kuwa mjukuu wake.

    Cha kushangaza familia ya yule Mzee iliweza kuja na kufanya chochote katika eneo la kile kibanda bila nyuki kuwasumbua. Huo ndiyo ufundi ambao muda wote yule Mzee alikuwa akijisifia mbele ya Mwasumbi kuwa nao.

    Siku moja wakiwa katika maongezi ya kawaida na mambo mbalimbali mara yule Mzee akauliza swali.

    “Treni senta echi ndiyo nini?” Mzee alimgutua Mwasumbi toka katika mawazo yake.

    “Unasemaje Mzee?” Mwasumbi alihoji maana hakuelewa.

    “Dakika za mwisho kabla sijatuma nyuki wangu kumfukuza yule mwanamke ulikuwa ukipiga kelele huku ukisema hayo maneno. Sasa sielewi ulikuwa ukimaanisha nini. Pia, ulipokuwa ukizindukazinduka ulikuwa ukisema train…sijui treni…sijui trening senta echi...”

    “Ooooh my God! Ndivyo nilivyosema! Tayari Maganga yuko hatarini. Lazima nielekee huko Training Centre H. Maana kama Sophia alinisikia nikisema hivyo na akamwambia KAPTENI mara moja watajua Maganga alipo.” Mwasumbi alisema huku akiwa ameshasimama. Alikuwa amehamaki sana.

    “Maganga ndiyo nani na KAPTEN ndiyo nani?” Mzee alihoji. Mwasumbi hakuonekana kuwa tayari kuongelea yale mambo.

    “Halafu kuna redio yako hapa ila miye imenishinda kuiwasha.” Mzee alisema huku akiinama chini ya kitanda. Alivuta kitu kama boksi, kisha akatoa kitu na kumkabidhi Mwasumbi. Mwasumbi alikipokea, ilikuwa ni Redio Call. Mwasumbi aliiwasha na kutafuta chaneli fulani.

    “Ndiyo Afande!”

    “Luteni Mwasumbi hapa.”





    “Sema Afande, nilikuwa nimeanza kupata wasiwasi sasa.” Ulijibu upande wa pili.

    “Nilipata dhoruba kiasi. Vipi vipusa viko salama?” Mwasumbi alihoji.

    “Yap Comrade, viko salama, nimevihifadhi Section 14 M, hadi hapo nitakapopata maelekezo yako zaidi…” Mwasumbi hakutaka kusubiri kusikia zaidi. Ile kujua kuwa wale wasichana walikuwa salama ilikuwa ahueni. Alizungusha na kuhama ile chaneli. Akaipata chaneli nyingine.

    “Mwasumbi hapa!” Mwasumbi alijitambulisha baada ya kuwa ameipata chaneli aliyoitaka.

    “Mmbando hapa!”

    “Afande inatakiwa kuimarisha ulinzi Training Centre H, kuna uwezekano mkubwa KAPTEN na timu yake wameshapajua na wanaweza kushambulia muda wowote toka sasa!” Mwasumbi alitaarifu.

    “Uko wapi Luteni?”

    “Niko sehemu moja inaitwa Kasomeko katikati ya Katunguru na Kamanga!” Mwasumbi alisema.

    “Asante Luteni, nitafanyia kazi hiyo sasa hivi!” Jenerali Mmbando alisema kisha akazima ile Radio Call na kuacha upande wa Mwasumbi ukikoroma.



    ******



    “Okay, kama mlivyosikia, watu wetu wako Section 14 M, Sophia sasa hivi chukua vijana wako nataka ukawachukue wale wasichana halafu uwapeleke nyumba salama, Kawekamo, hapo wataalamu wetu watawafanyia kazi. Mimi na Paul tutaelekea Training Centre H. Hii ni nafasi ya Paul kurekebisha makosa na kumpata Maganga. Nina imani bado watakuwa hawajamsafisha kichwa na hivyo anajua kuwa wewe ni baba yake mzazi. Na kama Mwasumbi alishapata fursa hiyo basi haina shida, yule Padre mwanafunzi hawezi kuwa na madhara yoyote. Kama mjuavyo Training centre H haina mawasiliano yoyote ya kwenda nje. Hivyo Jenerali Mmbando analazimika kutuma taarifa hii kwa njia ya mtu na labda kuongeza ulinzi zaidi au kumhamisha Maganga toka pale. Hakuna namna nitakubali makosa safari hii, tunachotakiwa ni kuwa mbele ya Jenerali Mmbando kivitendo, akifika akute tumeshamaliza kazi.” KAPTEN alisema mara baada ya kuwa amesikia ile sentesi ya mwisho ya Mwasumbi wakati akiongea na Jenerali Mmbando.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * *



    Wakati KAPTEN akitoa maagizo hayo kwa vijana wake, Jenerali Mmbando naye alikuwa akifanya vivyo hivyo kwa mtu wake wa siri aliyeko Mwanza.

    “… Mambo mawili, tuma watu wakammalize Mwasumbi. Sihitaji uniulize sababu, hii ni amri na ni kwa usalama wa Taifa. Halafu Kesho asubuhi nataka unipe orodha ya vijana wako safi kumi na tano. Watu hao nataka waelekee Training Centre H, kwa ajili ya kuongeza ulinzi na mimi nitakuja kesho jioni nitaelekea huko kadhalika. Sikiliza, hakikisha unafanya hii kazi kwa siri ya hali ya juu na umakini mkubwa.” Mmbando alipomaliza maelezo hayo hakutaka kusubiri maswali. Alikata simu kisha akaminya namba nyingine. “Ndiyo afande!” Ulijibu upande wa pili.

    Akabonyeza namba nyingine “Ndiyo Comrade!” Ulisema upande wa pili. “Sikiliza kwa makini, kesho jioni nataka uende Training Centre H, kuna kipuri nataka ukakichukue halafu ukipeleke sehemu salama. Kipuri kiko white room, neno la siri ni Maganga.” Kadhalika kama hapo awali, alipomaliza maelezo yake alikata simu. Kisha akashusha pumzi ndefu na kuwasha sigara yake.

    “Kazi imeanza!” Mmbando alijisemea huku akipuliza moshi wa sigara hewani.

    * * *

    Siku moja majira ya jioni wakati Vivian, Milka na Hellen wakiwa sebuleni, walisikia sauti za vishindo vikitokea nje, mara wakasikia mlio wa risasi. Wote wakakimbia kila mmoja kwenda kujificha alipojua. Milka hakujificha mbali sana na ilipokuwa sebule, hivyo aliweza kuona yule mwanajeshi wa kike akiingia pale sebuleni kwa stahili ya sarakasi huku akikwepa risasi kadhaa zilizokuwa zikimwandama. Risasi moja iliyomkosa yule mwanajeshi wa kike ilitua jirani na mguu wa Milka na kumfanya atoe ukelele wa hofu. Alipopiga kelele risasi zilikoma, halafu ghafla akaona Ua Jekundu, likianguka sakafuni jirani na alipokuwa amesimama. Kisha akamwona msichana mmoja akitokezea akiwa amevalia sare za jeshi. Yule msichana aliyetupa Ua aliendelea kutembea taratibu kwa kujiamini kuelekea sehemu ambayo kulikuwa na korido iliyokuwa ikielekea viliko vyumba vya nyumba hiyo. Alipofika kwenye kona ili aingie kwenye ule uwazi uliokuwa unaelekea vilipo vyumba, alipigwa teke la shingoni. Akageuka kwa kasi huku akijipangusa pale alipokuwa amepigwa.

    Alijikuta anatazamana na yule mwanajeshi wa kike. Huyu msichana mwingine alikuwa ni Sophia ama Au Jekundu kama alivyozoeleka. Sophia alimtazama yule mwanajeshi wa kike halafu akaanza kuachia mapigo mazito ya kung-fu ambayo yule mwanajeshi wa kile yalimshinda kabisa. Ikawa wazi kichwani kwa Sophia kuwa alikuwa anapambana na mtu ambaye hakuwa kwenye ngazi yake. Hivyo hakutaka kupoteza muda, alifyatua teke la kupeleka na kurudisha yule mwanajeshi wa kike alitoa mlio wa maumivu na kuanguka chini kama gunia ambalo halijajazwa vema maharage.

    “Njooni hapa kabla sijaanza kuwauwa mmoja mmoja!” Sophia alitoa amri. Kwanza kilipita kimya kabla ya Hellen kujitokeza, alikuwa akitetemeka kwa woga. Milka alifuata, Vivian alikuwa wa mwisho.

    “Nifuateni, mkileta tabia za kike mtamfuata huyo mnayemwona hapo chini!” Sophia alisema huku akipiga hatua kutoka ndani. Alitembea hivyo hadi walipofika nje ambako walikuta gari limepaki. Waliingizwa ndani na gari likaondolewa. Sophia alikuwa ameandamana na wanaume wengine wawili, Milka na Hellen waliweza kuwatambua wale wanaume kuwa ndiyo wale waliokuwa wakiteketeza Kijiji chao siku ile ya mwisho walipokuwa Kijijini kabla ya wao kupoteza fahamu kutokana na moto ule mkubwa.

    Mara hii walijua wazi kuwa walikuwa kwenye mikono hatari zaidi, walitazamana wakabetuliana midomo, hawakuwa na muda wa kuongea.

    “TAFUTA.” Sophia alisema huku akiwa ameweka radio ya upepo. Alikuwa amekaa kwenye kiti cha abiria, mwanaume mmoja alikuwa akiendesha gari na mmoja alikuwa nyuma ya viti walivyokuwa wamekaa Hellen, Vivian na Milka. Lilikuwa gari aina ya Noah.

    "Niko na warembo wako hapa, ndiyo tunaelekea safe house." Sophia alisema.

    “Kazi nzuri.” KAPTEN alisema na kuizima ile redio.

    Baada ya kuizima ile Redio Call, alitoa simu yake ya kiganjani, akaminya namba kadhaa kisha akasubiri kuongea.

    “Kuna bidhaa zetu muhimu sana katika hii operesheni, kuna hisia kuwa zinaweza kuwa na ufunguo wa kutufikisha sehemu ambayo tunaitaka. Hivyo kwa siku hizi tatu wataanza kulishwa dawa ili kama wana alama zozote mwilini ziweze kujitokeza. Hivyo tuonane pale safe house baada ya siku tatu toka leo ili kuchunguza miili yao…” Hiyo ilikuwa sehemu ya maelezo ya KAPTEN alipoongea na mtu aliyekuwa upande wa pili wa simu. Alimwangalia Mzee Paul aliyekuwa amekaa kiti cha pembeni na pale alipokuwa. Walikuwa kwenye gari wakielekea Section Centre H. Walikuwa wakifukuzana na muda ili kuwahi kumchukua Maganga kabla timu ya Jenerali Mmbando haijaenda kumchukua kama alivyokuwa ameshauri Luteni Mwasumbi akiwa kule kwenye ile nyumba ya Mzee mfuga nyuki. Kama alivyokuwa amemwambia, KAPTEN alikuwa akimpa Mzee Paul nafasi ya mwisho ili kufanikiwa kukamilisha kazi yake ya kumkabidhi Maganga, kazi ambayo alikuwa ameshindwa dakika za mwisho kule Kijijini ambapo alizidiwa ujanja na Luteni Mwasumbi. Gari hili lilikuwa la kijeshi na wao walikuwa wamevalia kijeshi.

    Eneo hilo lilikuwa porini sana, ukifika sehemu kilipo Chuo cha Ualimu Butimba, unaingia kwa ndani zaidi, ni sehemu ambayo ilisemwa kuwa ni hifadhi maalum ya miti adimu kwa ajili ya utafiti wa madawa yaani Medical Research. Kulikuwa na walinzi wa siri, ambao waliweza kuona hiyo gari likiwa linaingia kwenye hilo pori, lakini kwa vile lilikuwa la kijeshi hawakulitilia shaka sana. Gari lilizidi kukata msitu kuelekea sehemu ambapo kulikuwa na jengo kubwa la kijani. Walipokuwa umbali fulani walisimamisha gari.

    Wakati gari hilo likiwasili, Maganga alikuwa ametoka kuoga, alijikagua mwili wake kama alivyokuwa akifanya siku zote. Alivaa nguo nyepesi kisha akaenda kujilaza kitandani. Ilikuwa ni saa tano na nusu asubuhi. Maganga tayari alikuwa ni mtu aliyejikinai, mwili wake ulikuwa umeshakufa ganzi na nafsi yake kuota kutu. Ile hali ya kujali na kuzingatia mambo aliyokuwa amejijengea kwa muda mrefu kutokana na mafunzo ya Upadri ilikuwa imeshamtoka, alikuwa ameshakaa katika jengo hilo kwa siku zaidi ya arobaini. Ilikuwa ni sehemu ambayo ilikuwa imeshamkinai kuwepo kama ambavyo Milka, Vivian na Hellen walivyokuwa wamekinai kukaa kwenye ile nyumba waliyokuwa wamepelekwa na yule mwanajeshi wa kike.

    Akiwa amejipumzisha kitandani mara akasikia vishindo vya watu vikija upande ule wa chumba. Kutokana na ratiba yake, ulikuwa ni muda wa yeye kupumzika hadi hapo saa nane na nusu muda ambao wangekuja madaktari maalumu kwa ajili ya kuuchunguza na kuupekua pekua mwili wake. Hivyo kusikia vishindo vya watu ilimshangaza sana, katika jumba hilo wahusika walioneka kujua na kujali muda. Akiwa bado anawaza mara mlango ukafunguliwa.





    Wa kwanza kuingia alikuwa ni KAPTEN, ambaye alibaki kwenye mwimo wa mlango, alimtazama Maganga kwa muda bila kusema wala kufanya lolote. Macho yao yalipokutana, aliyaangalia macho ya Maganga kwa jinsi yalivyokuwa mekundu na kuonekana kuchoka, huku kukiwa na kitu fulani katika macho hayo ambacho mtu ambaye ni Padri mtarajiwa asingeweza kuwa nayo. Uso wa KAPTEN ulikuwa kama una mshangao fulani, lakini hakuuliza, alipiga hatua tatu mbele, ndipo Mzee Paul naye akajichomoza. Alipomwona Maganga, Paul alitabasamu kisha akapiga hatua kukimbilia pale alipokuwa Maganga, kuona hivyo Maganga alijiinua pale kitandani. Mzee Paul alipofika pale kitandani alimkumbatia Maganga kwa nguvu, lakini haikuchukua muda mrefu alimwachia. Alitambua mabaidiliko, hakuwa amekumbatia ule mwili wa Maganga anayemfahamu, huu ulikuwa mwili wa jitu na si Padri mtarajiwa.

    “Maganga, pole sana kwa yote yaliyokupata.” Mzee Paul alisema.

    “Yapi hayo!?’ Maganga alihoji kama asiyewajua watu wote waliokuwa mbele yake na wala hakujua nini kilikuwa kimetokea.

    “Wewe hujui, jinsi ulivyochukuliwa Kijijini na kuwekwa kwenye hii nyumba?” Mzee Paul alisema.

    "Hatuna muda zaidi, watafika muda si mrefu kutoka sasa, mchukue mwanao tuondoke. Imekuwa jambo jema tumemkuta akiwa hai." Sauti ya KAPTEN iliunguruma. Maganga aligeuka akamwangalia KAPTEN.

    “Huyu ni nani?” Maganga alimwuliza Paul.

    “Ni mtu aliyejitolea kunisaidia kukutafuta wewe baada ya kupotea.” Paul alijibu.

    “Hana jina?” Maganga aliuliza tena kwa sauti kavu, sauti ambayo ilimshangaza Paul na kumkera kwa wakati mmoja. Alihisi ile sauti ilikuwa na dosari fulani lakini hakuwa na muda wa kuchunguza zaidi.

    “Hayo majibu yenu mtajibishana tukishatoka hapa, kwa sasa hebu tuondokeni haraka.” KAPTEN alisema tena, wakati huu sauti yake ikiwa na amri ndani yake. Sauti hii Maganga aliifananisha na wale watu ambao huja usiku na kumfanyisha mafunzo magumu na ya kikatili.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akajikuta ameanza kumchukia huyo mtu na mara hiyo hiyo maneno aliyosoma kwenye ile karatasi aliyoandikiwa na mama yake aliyoichukua chini ya mtungi yakamjia kichwani kwa kasi "Paul na Mwasumbi wako kwenye misheni moja japo hawajui....sijui yupi aliye upande wako.” Maneno hayo yalimfanya awe na hadhari na Paul. Alisimama, akavaa mavazi yake ya mazoezi ambayo yalikuwa mazito kisha akaongozana nao kuanza kutoka mule ndani. Maganga alishangaa kukuta maiti za wanajeshi waliokuwa na silaha zikiwa zimetapakaa maeneo waliyokuwa wakipita. Walipofika nje walikimbia kuelekea pale walipokuwa wameegesha gari lao. Hata kabla hawajafika lilipokuwa gari lao, mara wakasikia mlio kama wa Inzi.

    “Nyuki, tukimbie kurudi ndani hadi wapite, ni hatari sana hawa.” KAPTEN alisema, ilibidi wakimbie kurudi ndani japo walikuwa wamebakiza hatua chache kulifikia gari lao. Kwa vile gari lao lilikuwa la wazi hawakuona kuwa ni busara kuliondoa huku wakiwa wanafukuzwa na nyuki, hivyo ingemaanisha kujitakia vita ambayo hawakuwa wanajua kuipigana. Walikimbia kwa kasi, wakati wanakimbia, nyuki wakiwa wanawakimbiza walishangaa jinsi Maganga alivyokimbia kwa staili ya ajabu sana na kuwaacha wao wakiwa wanafukuzana na wale nyuki. KAPTEN na Paul walikuwa ni wanajeshi safi sana, ambao wamekuwa kwenye misheni na kazi kwa muda sasa lakini namna Maganga alivyokuwa mwepesi na kukimbia iliwaacha vinywa wazi. Walifanikiwa kuingia ndani na kufunga mlango, waliendelea kusikia sauti ya wale nyuki kwa dakika kadhaa. Baadae kukawa kimya. Walitoka tena kuelekea lilipokuwa gari lao. Hapo walishikwa na mshangao mwingine, walikuwa wamewaacha vijana wawili kwenye lile gari, lakini walikuta maiti zao zikiwa na mishale iliyowauwa.

    "Daaah! hawa wameshambuliwa saa ngapi tena!” Alihoji huku akipanda kwenye gari. Aliliwasha, Maganga na Paul waliingia viti vya nyuma kisha KAPTEN akaliondoa gari kwa kasi.

    Moja kwa moja safe



    ***********



    ILIKUWA SIKU YA PILI, usiku wa saa moja na nusu, Vivian, Lilian na Hellen walikuwa wamejilaza kando ya bwawa la kuogelea ndani ya safe house ambayo inamilikiwa na KAPTEN ikiwa maeneo ya mlima wa Kawekamo nje kidogo ya jiji la Mwanza. Hawakuwa na la kuongea, hawakuwa na la kuulizana, walishaongea yote, walishaulizana na kujibizana yote walipokuwa kwenye ile nyumba waliyokuwa wamewekwa na yule mwanajeshi wa kike. Kwa sasa hawakuwa wanajua majaaliwa yao, tangu wameingia kwenye hii nyumba walikuwa wakichomwa sindano asubuhi na jioni. Miili yao ilikuwa imeanza kubadili rangi na kuwa ya jabu ajabu tu. Ulinzi ulikuwa mkali sana, walinzi walikuwa wakibadilishwa kila baada ya saa sita. Wakiwa kando ya hilo bwawa mara Hellen alishtuka kama aliyeona kitu, alijiinua akamwangalia kwa makini mlinzi mmoja aliyekuwa akitembea kuja upande huu waliokuwepo. Ndiyo alimkumbuka.

    “Haaaah!, namjua yule mwanaume!” Hellen alimwambia Vivian aliyekuwa amejilaza kando yake.

    “Yupi?” Vivian aligutuka.

    “Yule pale!” Alisema huku akitaka kuinua mkono ili kuonyesha.

    “Wewe hujajifunza tu, hapa hutakiwi kupayukapayuka wala kunyooshea watu mikono, utakuja kukatwa hiyo chingo, shauri zako. Kwani huwezi kusema bila kuonyesha kidole?” Vivian alisema huku akiusukumia chini mkono wa Hellen.

    “Usimwangalie wala usijifanye unamjua, nisimulie kwanza.” Vivian alionya.

    “Nakumbuka huyu mwanaume nililala naye usiku mmoja kabla sijaja Mwanza. Yeye ndiye niliongea naye kwa mara ya mwisho juu ya hamu yangu na kiu yangu ya kutaka kumjua baba yangu. Jamani kumbe na yeye yuko kwenye huu mtandao? Ukweli ni kwamba huyu mwanaume hakuwa tu mteja wangu wa kawaida, tulikuwa tunapendana sana alikuwa ananiridhisha sana kitandani." Hellen alisema huku akijishika shika.

    “Kweli?” Vivian alisaili.

    “Haswa!, hata siamini kwa kweli kama Machumu anaweza kuwa kwenye kundi hili la hatari.” Hellen alisema.





    “Kwa nini usiamini, kwani alikuambia anafanya kazi gani?” Vivian alihoji zaidi wakati huo yule mlinzi alikuwa ameshapita na walikuwa wakimtazama mgongo wake tu. Alikuwa amebeba silaha nzito.

    “Mimi nilikuwa najua kuwa yeye ni askari polisi. Sasa ndiyo napata mwanga, maisha anayoishi Machumu, vitu anavyofanya si vya mtu anayelipwa mshahara wa askari, anaishi maisha ya kifahari sana, khaaaaa!” Hellen alisema kwa mshangao.

    “Ngoja, si anazunguka kwa hivi, akipita hapa tena mwite kwa sauti ya chini halafu tuone kitakachojiri.” Vivian alishauri.

    “Akhaaa! mimi nimeshamuogopa siwezi bwana asije nipiga risasi bure!” Hellen alisema kike kike.

    “Hawezi, hawajawekwa hapa kutuua wamewekwa hapa kutulinda, muite tu tuone! Kama tumepangiwa kufa tutakufa tu, kama tumepangiwa kupona tutapona tu.” Vivian alisema kwa sauti ya kusisitiza.

    “Haya nyamaza huyo hapo amekaribia.” Hellen alinong'ona.

    “Machumu…” Hellen aliita. Yule mlinzi akageuka akamwangalia Hellen huku bado akiwa anatembea. Hakusema neno japo uso wake ulionyesha mshtuko na mshangao fulani, lakini hata hivyo aliendelea kutembea. Vivian na Hellen wakabaki wametazamana.

    “Amekutambua unaona alivyoshangaa!”Vivian alisema.

    “Mmmh! inawezekana, au kashindwa kuelewa yupi ni yupi, si unajua jinsi mimi na wewe tunavyofanana.” Hellen alisema.

    “Kwa kweli lazima kuna kitu, maana mnavyofanana, hata mimi siku ile nimekuona kwa mara ya kwanza pale Kijijini tukiwa na Maganga nilidhani u Vivian, mnafanana sana. Kwa kweli kuna haja sana ya kuutafuta ukweli toka katika maelezo ya Mwasumbi.” Alisema Milka ambaye alikuwa kimya muda wote akiwasikiliza Hellen na Vivian.

    Yule mlinzi aliendelea kutembea bila kugeuka, wale wasichana waliendelea kumwangalia huku wakijifanya kuwa hawana habari naye. Kulikuwa na walinzi wangine sita, wote wakiwa na silaha. Hatimaye mzunguko wa yule mlinzi ukawa unamleta tena sehemu waliyokuwa wamejilaza wale wasichana pembeni ya bwawa. Akiwa anatembea kwa mwendo ule ule wasichana wote watatu walikuwa wakimwangalia. Taratibu alinyanyua mkono hadi kinywani kwake kwa kutumia kidole cha shahada akawaonyesha ishara kuwa wanyamaze kimya. Ishara hiyo aliifanya kwa kuweka kidole juu ya kuta za mlango wa mdomo. Kama ilivyokuwa mwanzo hakusimama akaendelea na mwendo wake ule ule.

    “Unaona, amekutambua, ametuambia tunyamaze.” Milka alisema kwa kunong'ona.

    “Tufanye kama alivyotaka.” Vivian alisema. Hellen hakuwa na la kusema alikuwa kimya akiwa ameshikwa na butwaa. Hiyo mada ikaishia hapo wakaendelea na mambo mengine.

    Giza lilipoanza kuingia, kila mmoja alienda kuchukua nguo zake wakavaa. Wakatoka eneo hilo la bwawa la kuogelea wakaingia ndani. Usiku huo kuna jambo likawa limetokea, Vivian alikuwa ameenda chooni, katika shughuli za chooni ndipo kwa bahati mbaya au nzuri aliingiza mkono mfukoni, huko vidole vyake vikagusa kitu. Karatasi! Aliivuta na kuifunua, ilikuwa ndogo tu na yenye maandishi machache. “Nimekutambua, hakikisha hulali, saa nane usiku.” Mapigo ya moyo ya Vivian yakabadilika, vidole vikaanza kutetemeka. Aliona hii ndiyo ilikuwa nafasi pekee. Alielewa kuwa ujumbe ule kwa vyovyote ulikuwa umeandikwa na yule mlinzi-Machumu na mlengwa alikuwa ni Hellen. Alishindwa kuelewa kama amshukuru Mungu au la. Hakutaka kujua hiyo karatasi iliwekwaje na muda gani, hilo halikuwa na maana kwa wakati huo. Alikifinyanga kile kikaratasi na kukitupia mdomoni.

    Akakitafuna taratibu, aliondoka chooni, hakutambua kuwa hakuwa amejisaidi haja ndogo wala kubwa. Maana baada ya kukipata kile kikaratasi na kukisoma, alivuta suruali na kuivaa. Haja zikawa zimetoweka.

    Asubuhi ya siku iliyofuata ilikuwa ya patashika kubwa kwenye hiyo nyumba. Walipoamka Milka na Hellen hawakumwona Vivian, kwanza walianza kutafuta kimyakimya hawakumwona. Hawakujua wamwulize nani hadi pale walipoulizwa. Waliamriwa kuingia kwenye chumba fulani ambako walikutana na KAPTEN na Sophia wakiwa wanawangoja, Milka na Hellen hawakuchelewa kujua kuwa watu waliowaita walikuwa ni wenye hasira nyingi.

    "Nataka mniambie yule mwenzenu amekwenda wapi. Kushindwa kufanya hivyo mtauawa kifo cha mateso sana!" KAPTEN alisema kwa sauti isiyokuwa na chembe ya utani.

    “Nadhani sisi ndiyo tuwaulize mmempeleka wapi mwenzet....” Kabla hajamaliza kusema Milka alipokea kofi kali sana tokea nyuma yake. Alienda chini huku akitoa kilio kikali cha maumivu na hofu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shenzi, huko kwenye mafunzo ya usista ndiyo mlifundishwa kuwajibu watu hivyo?” Sauti ilisema toka nyuma yake. Milka aliitambua ile sauti, akageuka. Uso wake ukawa unatazamana ana kwa ana na Mzee Paul.

    “Baba una....” Kabla hata hajamaliza kauli yake, mlio mkubwa wa bunduki ulisikika wote wakatazamana.

    “Mr M, hebu kaangalie kuna nini?” KAPTEN aliamuru.

    “Sawa Afande!” Mzee Paul alijibu. Milka na Hellen wakatazamana huku Milka akiwa bado anatomasa shavu lake kwa sababu ya lile kofi. Mara milio zaidi ya risasi ilisikika. KAPTEN na Sophia walikimbilia nje toka kwenye kile chumba walichokuwa.

    “Mwasumbi yuko hapa, Maganga haonekani.” Sauti ya Mzee Paul ilisikika ikipiga kelele.

    “Sophia, Mwasumbi asitoke hapa hai. Mr M, hakikisha Maganga hapotei.” KAPTEN alitoa amri. Kisha milio ya risasi ikaendelea kurindima, vilio vilisikika, sauti za kutisha na kutukana kwa hasira vilisikika pia.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog