Simulizi : Kisasi
Sehemu Ya Nne (4)
**PATRICK**
Kizunguzungu cha fikra kilinikamata, kila nililoelezwa pale lilikuwa ni kama mchezo wa maigizo au ndoto za alinacha, Dany anahusika kwenye kusuka mpango wa mimi kuuawa? Haikuwa kitu rahisi sana kukiamini hasa kwa kuwa Dany alikuwa ni rafiki zaidi ya ndugu. Alikuwa ni rafiki ambaye kama angekatwa mikono yote miwili mimi ningeweza kukata mkono wangu mmoja nimpatie ilimradi tu wote tuwe na angalau mkono mmoja. Nilijikuta nikilia sana kwakuwa hata kumuuliza nini kilisababisha yote hayo ilikuwa ni kitendawili. Toka tulipokutana shule ya sekondari ya St. Thomas kula Tabora miaka ile tukiwa kidato cha pili mimi nikiwa nimehamia pale na kumkuta yeye akiwa amehamia pia toka shule ya Trust iliyoko jijini Dar. Siku hiyo ya kwanza tu tukawa marafiki kama tulijuana miaka mingi, kwakuwa tulikuwa ni watundu sana ilikuwa rahisi sana kufahamika, wasichana wote shuleni pale walitujua hasa kwakuwa tulikuwa wageni lakini waongeaji kuliko wenyeji. Dany alikuwa na kipaji cha kuimba, alikuwa na sauti nzuri sana ya kuimba, mimi nilikuwa na kipaji cha uandishi wa hadithi na makala za kielimu pamoja na kuigiza. Tulipofikisha mwezi mmoja toka tuhamie Dany akiwa na mwezi mmoja na wiki tulipeleka barua kwa mkuu wa shule juu ya kuanzisha gazeti la shule ambalo lilikuwa ni karatasi kubwa ya mita mbili iliyokuwa na vipande vya makala mbalimbali, hadithi na katuni pamoja na habari zilizojiri pale chuoni, mkuu wa shule alituelekeza kuwa tuliandae alione kwanza na sisi tuliandaa tukawashirikisha wanafunzi wengine wenye kujua habari za michezo na wanaofahamu mambo ya sanaa za muziki wa nje pamoja na mwalimu mmoja wa sayansi ambaye alikuwa anaandika makala za afya. Gazeti hili lilikuwa libandikwe kwenye ubao mkubwa wa matangazo na lingesomwa na kila mtu ambaye angetaka. Tulifanikiwa katika hili, tukajulikana sana pale shule na kupendwa na kila mtu wakituita mapacha. Tulianzisha kundi la kuhimiza matumizi ya kingereza mda wote na kuliita English Club, likakua na tukaanza kupata mialiko toka mashule mengine, tuliandika muswada (script) kitabu cha THINGS FALL APART cha Chinua Achebe na kuanza kufanya mazoezi ya kukiigiza kitabu kile kwa zaidi ya mwezi, tulishirikisha watu wa vidato mbalimbali, tukapata udhamini wa bodi ya shule walioahidi kutuletea kampuni ya kutengeneza maigizo hayo. Tulifanikiwa kuigiza na kutolewa kwenye CD ule mkanda ulioitwa Things Fall Apart ambao baadaye ulitumika kufundishi kwa karibu shule nyingi za seminari na mashule mengine. Wazazi wetu wakajuana na sasa tulikuwa zaidi ya ndugu. Dany kwetu alikuwa ni kama mtoto wao na vivyo hivyo mimi kwao. Kwakuwa mama yake na Dany alifariki kipindi Dany akiwa shule ya msingi hiyo ilimfanya Dany kuwa mnyonge mda wote lakini baada ya kukutana na mimi kila kitu kilikuwa poa. Nilipotenda kosa basi ujue na Dany alikuwepo, nilipokuwa na majonzi tulikuwa pamoja, tulitumia pesa pamoja na tulifaidika na kila tulichokianzisha. Sisi tulikuwa chanzo cha upendo kwa wanafunzi wengine, tukiwa shuleni sio tu tulikuwa wabunifu ila tulikuwa njema sana darasani. Mara zote tulikuwa tukibadilishana namba mbili na tatu, tulipofika kidato cha tatu tulibuni kipindi kimoja tulichokiita jumamosi ya burudani na pia Usiku wa vipaji. Shuleni ilikuwa ni kusoma kuanzia jumatatu hadi jumapili, hivyo tulikuwa tunachoka sana lakini baada ya kukaa na kutafakari nilimwambia Dany tubuni kitu tukiite Jumamosi ya burudani, basi tuliandaa andiko tukapanga kuwa siku ya jumamosi badala ya kwenda kujisomea usiku basi wanafunzi wote wakusanyike kwenye ukumbi wa mikutano na kisha jukwaani kutakuwa na mziki na watu watapanda kwaajili ya kucheza kwa wale wanaoweza kucheza, wale wanaoweza kuimba wataimba, na wale wenye vichekesho na burudani nyingine watafanya hivyo, Jumamosi ya burudani ilikuwa inaanza saa 1 jioni na kuisha saa 4 na nusu usiku. Pia Usiku wa Vipaji lilikuwa ni tamasha la vipaji vya uigizaji, mitindo na uimbaji pamoja na vichekesho na uchezaji ngoma, hii ilikuwa ni kwaajili ya kuendeleza vipaji vya wale waliokuwa navyo, usiku wa vipaji ulikuwa ufanyike kila mwisho wa muhula, yani siku moja kabla ya kwenda nyumbani na zawadi zingetolewa. Mkuu wa shule alikubali yote haya. Kikundi chetu cha kingereza kilitanuka zaidi na kuwa English and Computer Club, yote haya yalituunganisha kama wanafunzi. Baada ya kumaliza shule wanafunzi hawakujizuia kutoa machozi kwa wale tuliowaacha, tulitengeneza Jarida kubwa lenye kuonyesha matukio mengi sana tuliyofanya pale shuleni. Hakika ilikuwa kumbukumbu tosha. Maisha yaliendelea na kidato cha tano nilichaguliwa kwenda Benjamini Mkapa na Dany alichaguliwa kwenda Azania. Mda mwingi tulisoma pamoja na tulikuwa tunapokezana wiki hii Dany alikuwa anavaa sare za shule za Benja na kuja kusoma shuleni kwetu kwakuwa hakukuwa na ufuatiliaji sana na vivyo hivyo na mimi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Dany aliwahi kuumwa na kupungukiwa damu, nilikaa hospitali mwezi mzima sikwenda shule kuhangaika na ndugu zake. Hayo yalikuwa maisha yetu na Dany, mtu ambaye alishiriki kila aina ya maisha yangu, mtu ambaye nilimuamini na kumpenda kama ndugu yangu na zaidi hata ya ndugu. Nilichopata kilikuwa chetu sote na alichopata yeye kilikuwa chetu sote. Mtu ambaye nilikuwa namthamini kuliko hata Mark. Hakuna siri ya maisha yangu ambayo yeye hakuijua, tulitoroka wote shule, tuliadhibiwa pamoja, alipogombana na Catherine mimi ndiye niliyekuwa msuluhishi, mimi nilipogombana Fatima yeye ndiye alikuwa msuluhishi. Tulichukua wasichana marafiki na tulikuwa makini kila mmoja kuhakikisha mwenzake haumizwi. Leo hii huyu Dany ambaye alijitolea kugharamia safari yangu ya mapumziko baada ya ndoa yangu na Mary, safari iliyogharimu zaidi ya milioni 15 ndiye mmoja wa watu waliopanga kifo changu, Dany aliyekuwa msimamizi wa ndoa yangu leo hii ndiye anafanya haya, huyu Dany ambaye nilitoa pesa yangu ya faida ya miezi minne ya kampuni yangu kugharamia harusi yake yote iliyogharimu milioni 55 ndiye yeye adui wangu wa leo. Alifikiria nini wakati akiyafanya haya? Nini kilimpata? Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo ningependa anijibu.
“Patrick!” aliita Khajat.
“Unatakiwa sasa ujikaze, muda wa kufanya maamuzi ndio huu, muda wa kukaa na kulia au kutafakari umwekwisha sasa, katika maisha ya binadamu kuna muda wa kutafakari na muda wa kutenda. Ukiwa mtu wa kutafakari muda wote utakuwa unachelewa kwenye kila jambo. Adui ni adui tu hata awe baba yako. Akishajigeuza na kuwa adui basi hakuna kufikiri tena juu yake zaidi ya kutenda kama ulivyopanga kutenda iwapo ungemkamata adui. Najua Dany kakuumiza sana, najua pia Pamela leo na yeye kakutana na adui yake lakini wote lazima mjifunze kukaza mioyo.” Aliongea Khajat aliyekuwa tayari ameshafungua mkoba wake na kuuweka pale mezani, alivaa gloves tayari na alikuwa ameshikilia kifaa cha kukatia kucha maarufu kwa lugha ya kigeni kama Nail Cuter.
“Patrick unahitaji kwenda kwenye mazishi ya ndugu yako?” aliuliza Felly.
“Sidhani kama ipo haja ya mimi kwenda kumzika, nataka kujua mambo mengi sana kabla sijarudi Tanzania, nataka kujua kwanini haya yote yametokea.” Nilimwambia Felly na wakati huo bado nilikuwa nimekaa nikitazama ule mlango ambao Dany alikuwapo.
“Felly, tunapoteza muda. Mtu Patrick kama hautakuwa na roho nyepesi naomba usikae hapa na Pamela pia. Tunataka kujua vitu vingi toka kwa Dany na bahati mbaya mimi si mtu wa kuhoji kwa maneno mengi, hivyo kama kuna yeyote kati yenu anaogopa damu basi aende akakae na Cris chumbani.” Aliongea Khajat huku akiwa na sura yenye kutabasamu. Alitutazama na Pamela bado alikuwa akilia lakini alisema yuko tayari kuona damu ya Dany na hiyo ingempa nafuu kiasi kwa machungu aliyokuwa akisikia.
“Khajat, unataka kumfanyaje.” Aliuliza Felly.
“Nampa XT 1, itamfaa, nia yangu ni kumfanya ajute sio kuchukua tu taarifa toka kwake, nafahamu hata nikimpiga kofi atasema ila nataka ateseke kwanza kabla ya kumkabidhi Patrick amfanye atakacho.” Aliongea Khajat huku akikata kucha na kile kikata kucha.
“Hii ndiyo kazi niliyojitolea maisha yangu kuisomea na kuifanya kwa moyo. Niliisomea kwakuwa niligundua kuwa mimi ni kati ya watu wachache duniani ambao hawata kwenda mbinguni lakini pia ni kati ya watu wachache ambao wako tayari kufa muda wowote na hivyo nafanya lolote kubwa ili nikiwa sipo nikumbukwe.” Aliongea Khajat na kufungua ule mlango kisha Dany alitolewa pale kwenye kile kisehemu alichokuwa amefungwa. Khajat na Felly wakamfunga kwenye kiti kingine vizuri na kama mikono pamoja na miguuni na sehemu nyingine, kisha Khajat alimvua shati na kumtoa ile Solotape mdomoni.
“Dany, umemuona rafiki yako.” Khajat alimwambia Dany lakini Dany hakunitazama usoni.
“Dany nilikukosea nini?” Nilimuuliza huku machozi yakinitoka lakini bado hakujibu wala kunitazama.
“Patrick usihangaike kumuuliza, muda ukifika atajibu yote hata yale ambayo hujamuuliza.” Aliongea Khajat kwa kujiamini. Muda huo Felly alikuwa pembeni kimya akiwa anaipekua bado ile laptop ya Dany.
“Unamjua Pamela? Yule pale uliyeshiriki kumbaka wewe na ndugu yako na kisha baba yako naye alimuingilia, na hata alipofukuzwa na kuitwa Malaya nyie mlichekelea.” Alimuuliza swali hilo pia hakujibu. Khajat akamrudishia tena ile solotape mdomoni ili asiweze kuongea au kutoa sauti.
Dany alikuwa bado ameangalia chini na kila nilipokuwa nikimtazama nilikumbuka sana kipindi cha urafiki wetu, hiyo ilinifanya nizidi kutoa machozi, Khajat alikuwa ametoka kidogo na aliporudi alikuwa ameshikilia chupa ya pombe kali na mkono mwingine alikuwa na Spirit ya kuweka kwenye kidonda, alifungua mkoba wake na kutoa chupa la damu kisha alilitundika ukutani na kuvuta ule mrija kisha akamchoma Dany na kuruhuru damu ianze kuingia nilimuona Dany akiwa anatetemeka kwa hofu na wakati huo mimi nilihisi woga wote umeondoka na hata ningeambiwa nimfanye chochote kwa wakati huo ningefanya, alikuwa si rafiki tena. Khajat akamimina ile pombe kali na kunywa glasi moja kisha alimtazama Pamela aliyekuwa ametoa macho kusubiri kuona kilichokuwa kikiendelea.
“Dany najua kuwa uko tayari kusema yote, lakini muda wa kusema wewe bado haujafika, hivyo usihangaike kufikiria kuwa sasa ni muda wa kujibu maswali, hapana huu ni muda wa majuto.” Khajat alivuta kiti na kukaa karibu yake kisha alichukua kitambaa na kumfuta Dany lile jasho kifuani, akamwaga ile pombe kali iliyokuwa kwenye ile glasi na kuchukua ile mashine ya kukatia kucha akaanza kumbana nayo Dany kifuani na kukata nyama kidogokidogo kama vile alikuwa anakata kucha. Pamela alishindwa kuvumilia na kuamua kuondoka pale lakini mimi nilikaa nikishuhudia jinsi Dany alivyokuwa akiteseka. Nilimtazama alivyokuwa akilia kama mtoto nikatamani kumuonea huruma lakini huruma haikuja. Khajat anaroho ngumu kuliko mtu yeyote niliyewahi kumuona duniani. Pamoja na damu nyingi kumtoka Dany lakini Khajat hakuwa anaogopa kitu, mdomo ulikuwa umevungwa na hakuweza kuongea chochote japo alizidi kulia. Ile mashine ya kukata kucha ilikuwa ikifinya na kukata kinyama kidogo sana kitu kilicholeta maumivu makali, nilimtazama na taswira ya tulivyokuwa shule ikanijia. Dany alikuwa amelowa kwa damu, Felly alikuwa makini kwenye kazi zake na wala hakuwa na wasiwasi wowote, kwake ilikuwa ni kama jambo la kawaida sana. Baada ya kuhakikisha kuwa ile glasi ndogo imejaa vile vinyama vidogo vya kifuani kwa Dany, Khajat alinyanyuka na kuchukua kitambaa kisha akamwagia Spirit kwenye vile vidonda hali iliyosababisha Dany apige kelele mpaka kupoteza fahamu. Na baada ya hapo Khajat alivua zile ‘gloves’ na kumfata Felly pale alipo. Mimi nilikuwa bado niko pale nikitizama.
“Patrick, hiyo ni adhabu ndogo sana niliyompa na ni kwakuwa sioni adhabu nyepesi zaidi ya hiyo. Usihofu hatakufa kwakuwa damu inaingia mwilini kwake na tulimpima mwanzoni hata shinikizo la damu wala ugonjwa wowote wa mwili hivyo sio rahisi afe kabla ya wewe kulipa kisasi.” Aliongea Khajat huku akinitazama.
“Inabidi kumuhoji sasa, mtengenezee yale maji umuashe, kuna vitu hapa natakiwa nimuulize kwanza ili tujue kama Patrick anaweza kusafiri kwenda Tanzania au la.” Aliongea Felly akimwambia Khajat na baada ya hapo Khajat aliondoka kuelekea juu, nilitoka na kumfuata nyuma.
“Patrick huna moyo wa kiume kabisa, ni bora ungekuwa muumini wa kanisa. Lakini sikulaumu ni kwakuwa pengine unaamini sana dini, lakini nitafanya yote badala yako.” Aliongea Khajat huku akinitazama.
“Khajat, kuna muda utajua roho yangu ilivyo, kwasasa nataka kujua kwanza sababu ya kila jambo. Naelewa kabisa ninachotakiwa kufanya ila lazima kwanza nijue chanzo cha yote ni nini, nani alianzisha haya, yalianza lini na wamepanga kwenda mpaka wapi.” Nilimuambia Khajat ambaye hata hivyo alinitazama na kukubaliana na mimi japo alionekana kabisa kuwa hakuamini maneno yangu.
“Anaweza kuishi kwa muda gani?” nilimuuliza Khajat.
“hana kitu cha kumfanya afe kwa muda huu, ile adhabu ni ndogo. Mimi naelewa kanuni za mateso, yule pale nimeshtua mishipa yake lakini hiyo sio shida. Damu yake ipo kawaida kwakuwa inaingia mwilini na tulivyomfunga mwili wake hauchezi sana, tukimalizana naye tutamtundikia drip ya maji ilia pate nguvu zaidi. Atakuwepo mpaka mwisho wewe usijali.” Alinijibu na tulikuwa tumeshafika juu na kumkuta Pamela akiwa amelala kwenye kochi.
“Pamela.” Nilimuita na yeye alishtuka.
“Patrick, sitaki kumuangalia yule mbwa, alininyanyasa sana na kunitesa. Ni kwakuwa nilikuwa sina wazazi ndio mana aliona mimi naweza kuwa ni shimo la choo la wao kuweka uchafu wao na kuondoka si ndio? Waliniumiza sana, familia nzima waliniigilia bila ridhaa yangu, walinibaka na kuniita Malaya, kisha kunipa elfu 45 kwa kazi zote nilizofanya kwa miezi hiyo? Tena nafukuzwa eti nitawaua watu mule ndani kwa ukimwi? Yani wao wanibake alafu mimi ndo niwe wa kuwaambukiza ukimwi? Kweli jamani?” Pamela alikuwa akiongea huku akilia kitu kilichomfanya Khajat atokwe na machozi. Mimi sikuwa na la kusema nilibaki kumkumbatia tu.
“Pamela, usilie, kila kitu kitalipwa sawa na maumivu yako.” Aliongea Khajat na kufungua jokofu kisha alitoa pilipili mbichi kwenye mfuko, zilikuwa ni zaidi ya pilipili 50 kwenye ule mfuko. Nilimuacha Pamela pale na kumfata Khajat aliyekuwa akielekea jikoni.
“Za nini hizo?” nilimuuliza Khajat ambaye tayari alikuwa ameziweka kwenye mashine ya kutengenezea juice na kuanza kuzisaga.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni dawa ya kumuamsha.” Aliongea Khajati huku akiongeza maji kiasi na baada ya dakika 1 ilikuwa imeshakuwa kama juice nzito. Ilikuwa ni kali kiasi cha kutufanya wote tuliokuwa pale tukohoe kasoro Khajat peke yake aliyekuwa kawaida. Alishuka na ile pilipili kwenye kibakuli kisha tulipofika pale chini alivaa gloves nyingine mpya na miwani kubwa ya kuzuia ile pilipili isiingie machoni. Dany alikuwa bado amepoteza fahamu lakini Khajat alipopeleka lile bakuli kwenye pua ya Dany alianza kupiga chafya, na hapo alizinduka. Khajat alichukua ile pilipili na kuimwaga kwenye vile vidonda vya vya Dany na hapo alilia mpaka sasa huruma ilinijia. Nilihisi uchungu aliousikia Dany pale alipokuwa amekaa na hakuwa na jinsi ya kusema tena. Khajat aliitoa ile solotape na sasa Dany aliongea.
“Patrick nisamehe ndugu yangu, nateseka Patrick naomba mwambie aniache. Khajat inatosha naomba unisafishe naumia sana.” Aliongea Dany huku akilia kwa uchungu na mwili wake kutetemeka.
“Subiri maswali kabla sijakuvuruga zaidi. Unachotakiwa kusema hapa ni ukweli wa kila jambo ili ufe ukiwa umesema ukweli na sio kuomba msamaha na kutaka kuachwa. Elewa kuwa hapa ulipofika ndo mwisho, mbegu ya watu wote wanaofanya wengine waishi kwa tabu duniani ni lazima imalizwe kabisa ili waishi watu wanaoweza kufata taratibu za kibinadamu. Kwenye maisha ulikuwa una nafasi ya kuleta furaha kwa kila aliyekutendea wema, kama ulishindwa unachostahili ni adhabu ambayo sio wewe utapanga.” Aliongea Khajat kwa hasira na kumsindikiza na ngumi nzito ya sikio iliyomfanya Dany atoe jicho kama vile aliona pepo.
“Nisamehe Khajat.” Aliongea Dany.
“Nitazame vizuri usoni, unahisi mimi ni mtu wa kusamehe? Nasamehe makosa ya kawaida ya kibinadamu ila sio ya kijasusi, Swali la kwanza, mpango wa kumpoteza Patrick ulianza lini?” Aliuliza Khajat na Dany alikuwa kimya kama vile akifikiria. Khajat ahakusubiri alirudi nyuma na kuchukua ile mashine ya kukatia kucha kisha alipeleka pale kwenye kidonda na kuvuta tena nyama kisha kukata, huku akimtazama. Dany alilia kwa sauti kubwa.
“Ilianza kabla ya Mary kurudi Tanzania.” Alijibu na hapo nilishtuka ilikuwaje mpaka mpango huo ukaanza mapema hivyo.
“Nani alisuka mpango huo kabla ya hapo.” Aliuliza Khajat.
“Alikuwa ni Mary, lakini baadaye nilikuja kukutanishwa na mtu wa tatu ambaye alikuwa ni Mchungaji Priscus Mjata, ambaye ndiye aliyewafungisha ndoa Patrick na Mary na ndiye mshiriki wa kibiashara wa Mary, Mr. Ruyega ambaye alikuwa ni dereva wa Patrick na pia Mark alikuja kuunganishwa baadaye.”
“Mwingine nani?” Khajat aliuliza.
“aahh,,,mhh” Dany alianza tena kung’ata maneno, alishtuliwa na ngumi nyingine ya uso iliyofanya damu zianze kumtoka puani, wakati huo mimi nimesimama kimya nasikiliza tu.
“Na,,,na,,,na mama yake Mark ambaye baadaye tulikuja kujua kuwa yeye na Mary ndio walikuwa wanausuka huu mchezo toka siku nyingi.”
“Mama yake Mark!!!!” nilishangaa na kujikuta nimepigwa na butwaa.
Lisha mbwa wote chakula sawa kwakuwa hujui yupi atakuokoa wakati wa hatari. Inawezekana katika kuwalisha mbwa ukawa ukimpendelea mmoja au hata kuwa pendelea wa aina fulani tu, lakini katika kuenenda kwako ukakutana na hatari ukiwa na mbwa wote. Wale uliowalisha na kuwapendelea wakanenepa na kunawiri wakakukimbia kwakuwa walikuwa na nguvu za kukimbia, uliwalisha mpaka wakawa wajinga na wavivu wa akili yao, hawakujua tena kuwa wakila wanatakiwa wakulipe kwakuwa walinzi wako na watetezi wako. Wale ambao hukuwalisha, hukuwapendelea au kuwajali wakabaki na wewe wakitamani kukutetea, lakini wakuwa walikonda kwa upendeleo wako uliowanyanyapaa na kuwatenga, wakawa hawana tena nguvu hata ya kukupigania na kukutetea. UTAKUFA HAPO. Majuto ni mjukuu, ni mjukuu ambaye hutokea wakati wa dakika za mwisho kabisa za Tumaini finyu lililobaki kwenye mishipa ya damu. Kumjua mtu au kutokumjua hakukupi sababu ya kumdharau au japo kumuamini sana. Maisha ni kitendawili ambacho wachache hukitegua kwa wakati husika. USIMDHARAU MTU KWA KILE ULICHONACHO AMBACHO YEYE HANA. KILA MTU NI MUHIMU KWAKO, NI MUDA TU HAUJAFIKA WA KUONA UMUHIMU WAKE KWAKO”…………..HII NI SEHEMU YA KUMI NA TATU.
Ndugu mwandishi, mpaka hapa ilikuwa tayari ni saa kumi kasoro, ile CD iliendelea kuchezwa na sauti ya Khajat ikasikika ikisimulia, yeye alikuwa akisimulia kwa lugha ya kingereza, lakini kuna msichana ambaye alikuwa akitafsiri nahisi anaweza kuwa ni Pamela au mtu mwingine yeyote, masimulizi yake yalikuwa hivi.
**Khajat**
>>MIAKA MINGI ILIYOPITA<<
Kila aina ya binadamu anayedhaniwa kuwepo duniani ujue yupo. Muda wa maisha ukifika basi unaweza kubahatika kukutana naye. Maisha ya ukatili nilijifunza kipindi nikiwa jela ya watoto, ni siku hiyo nilipoamka na kugundua kuwa nilikuwa nikionewa. Nikajiuliza sana kosa langu mimi ni nini mpaka yule mama anifanyie haya yote, lakini sikujua. Inawezekana labda nilikuwa mtukutu lakini yawezekanaje mimi niwe mtukutu kipindi cha udogo wangu tena wakati namuogopa yule mama kupita ukoma? Kila siku asubuhi tulikuwa tukienda kupigwa viboko viwili na yule askari wa kiume, lakini cha kushangaza sikuzote aliniweka mimi wa mwisho na wote walivyomaliza kuchapwa mimi niliachwa bila kuchapwa. Hakuwa ananieleza sababu ya yeye kuacha kunipa ile adhabu ambayo ilikuwa ni lazima kwa kila mtoto kupewa adhabu ile. Siku moja alikuja kunifata tukiwa ndani na kunitoa nje, niliogopa sana lakini hiyo haikuwa sababu ya mimi kukataa kutoka nje.
“Nataka nikupe kazi, na ukifanikisha nitakupa zawadi itakayokufanya ufurahi maishani.” Alinieleza huku akijaribu kunishawishi, nilikuwa mdogo lakini nilikuwa ni muelewa sana na mwepesi kufikiri.
“Kazi gani.” Nilimuuliza kwa ile sauti yangu ya kitoto.
“Nataka ukamuue mtu.” Aliniambia hukua akinitazama kwa macho makali.
“Nani?” nilimuuliza na mimi, yule askari alishangaa sana kwakuwa alitegemea pengine ningekataa au ningetetemeka ila haikuwa hivyo, nilikuwa tayari nimeshachafuka roho. Nakumbuka nikiwa na miaka mitatu ndo nilianza kupigwa, nilikuwa mdogo sana lakini kumbukumbu za kile kipigo zilinijia siku zote za maisha yangu, nilikuwa silali kwa raha kwakuwa ndoto zilizidi kujirudia kwenye kichwa changu, nikiwa na miaka mitano ndipo nilibakwa na katika miaka hiyo ndipo nilifinywa na mama sehemu zangu za siri na kupata kidonda, nilishindwa kwenda shule lakini hiyo haikutosha akanitafutia kosa na kuamua kunipeleka jela ya watoto, huko pia kuna kipindi tulichanganywa pia nikabakwa, nashukuru mungu kile kidonda kilikuja kupona. Maisha ya jela yalinitengeneza kuwa mtu mpya kabisa.
“Nataka ukamuue mtoto mwenzake, anayekaa kitanda cha karibu na wewe, kisha ukitoka humu ndani nitakupa kiasi kikubwa cha pesa.” Aliniambia yule askari. Nilimuuliza sababu ya kumuua lakini alinijibu majibu ambayo sikuwa naona kama yanasababu yoyote ya kumuua yule mtoto ambaye naye anapata shida pale kama mimi, nikamkubalia na kweli akanipa sumu nikamuwekee na mimi niliipokea lakini nilizunguka na kumuwekea yeye ile sumu kwa kuichomokeka kwenye sigara yake, ilikuwa ni sumu ya unga ambayo nilitakiwa kwenda kuipaka kwenye mto wa yule mtoto kisha akivuta ingemfanya aanze kutoka damu puani akiwa amelala kisha angefariki, hivyo nilikwenda kupunguza ujazo ya ile sigara yake kisha nikachomeka ule unga kidogo kwa ndani na kurudisha majani ya ile sigara kisha alipokuja kuvuta alianza kutoka damu puani na mpaka alikufa pale ofisini nikiwa nachungulia. Hiyo ndiyo siku niliyogundua kuwa nina uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo. Nilipotoka niliendelea na shule kidogo lakini wakati huo nilikuwa pia nikifanya kazi na kikundi kidogo cha majambazi waliokuwa wakinipitisha madirishani wakati wa kuiba, nilikuwa na akili shuleni na hakuna mtu ambaye angeamini kuwa mimi nilikuwa mtu hatari katika udogo wangu. Nilifanya yote haya kwakuwa nilihitaji pesa za kugharamia maisha yangu, sikuwa na mtu wa kunisaidia, mama alikuwa akinitesa sana, kuna mtoto wa mtaa wa kumi kutoka pale kwetu alikuwa akiteswa na yeye na wazazi wake wa kumzaa kwakuwa tu alizaliwa akiwa taahira, iliniuma kwakuwa kila mra nilikuwa nikipita wakati natoka Naporill kulekule Bombay nilikuwa nikimuona akilia, huruma ilinijia na siku moja usiku nilikwenda kwao nikapita dirishani na kuingia mpaka kwenye chumba cha wazazi wake, alikuwepo baba yake akiwa amelala hoi, nilipitisha kisu kwenye koo lake na kuondoa maisha yake.Niliua sana katika udogo wangu, hasa watu wote waliokuwa wakifanya maisha ya watu kuwa magumu. Hata wale majambazi waliokuwa wakinituma na kuniingiza dirishani nilikuja kuwaondoa duniani baadaye. Nilikuwa hatari sana. Nilipopata pesa ya kuja kwa Felly, nilikwenda uwanja wa ndege wa Chhatrapati Shivaji na kuingia upande wa mizigo kisha nilikuja Fiji. Maisha yangu ya nyuma niliyaacha Bombay nchini India lakini nilikuja kuyaimarisha kwakuwa mwema tu kwa kila mtu na mbaya sana kwa wale wanaowafanya wengine waishi maisha magumu. Niko tayari hata mimi kuadhibiwa kwa lolote kama matendo yangu yatamchukiza yeyote, huo ndo msemo niliokuwa nikijiambia kila siku. Nilikwenda kwenye shule ya jeshi, baadaye walinichukua na nilikwenda mafunzo mbalimbali, lakini kubwa ni mafunzo ya kutesa na kuua. Sijafundishwa kulenga mguu, sijafundishwa kulenga kichwa, nimefundishwa kuua kwa mkono.
**SASA**
Patrick alikuwa ni kinyume cha mimi. Namaanisha nilikuwa mkatili sana, lakini Patrick alikuwa ni mpole na mwema sana. Wema wake sikuuchukia lakini uliniudhi muda mwingine. Alikuwa na imani za kidini zilizomfanya kuwa mtu wa kusamehe jambo kubwa lililohitaji msamaha wa mauti kwa aliyekosa.
“Mama yake Mark alihusikaje kwenye hili?” nilishtuliwa na sauti ya Felly aliyekuwa bado akiendelea kumuuliza Mark maswali. Nilimtazama Patrick alikuwa amekaa akisikiliza huku machozi yakiendelea kutoka. Nikamtamza Dany alikuwa anawasiwasi sana kila nilipomkaribia.
“Mama yake Mark aliambiwa na Mary kipindi bado akiwa Marekani kuwa kuna mpango wa kupata pesa nyingi sana kama atakuwa tayari. Na yeye alisema ndiyo yuko tayari, kipindi hicho Mary alikuwa Urusi kwenye biashara zake. Baadaye Mary alinipigia simu na kuniambia kuhusu mpango wa kupata pesa, nilikubaliana naye na yeye aliniambia kuwa anakuja http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Tanzania ili tuweze kupanga kila kitu. Siku aliyokuja alianza kwakuniambia kuwa anataka afungue kampuni ya magazeti, kampuni kubwa ambayo itakuwa na mtaji mkubwa sana, alaf baadaye ndio tutafanya huo mpango aliokuwa nao, tulikuwa na mama yake na Mark. Lakini kesho yake mama yake na Mark aliniita na kuniambia kuwa mpango uliopo ni wa kuichukua kampuni ya Patrick na Mary ameshapanga kila kitu mpaka kufanikisha kuichukua. Nilikataa lakini siku hiyo nilipokuwa nataka kwenda kwa Mark kumwambia, nilipigiwa simu na Mary, akaniambia niende benki nikatoe pesa kiasi cha laki nne kisha niende kuonana naye kuna jambo anataka nimsaidie. Nilimuuliza pesa ni za nini akasema nifanye hivyo ndo niende kwake. Sikuwa na wasiwasi, nikaelekea ATM na kutoa pesa, nikaingia kwenye gari na kuondoka nikiwa njiani nikakumbuka sikuangalia nilibakiwa na shilingi ngapi kwenye akaunti yangu kwakuwa nilitakiwa kuwa na pesa nyingi kwaajili ya kuagiza mzigo. Nilipoitazama ile karatasi yenye kuonyesha salio nilikuwa na milioni 45, lakini ninavyokumbuka akaunti yangu ilikuwa na milioni 5 tu, hapohapo simu ya Mary ikaingia na mimi nikapokea, wakati huo nilikuwa nimeegesha garo pembeni ya barabara.
“Dany usiwe mjinga, tumeletwa duniani ili tuishi kwa muda mfupi kisha tufe. Mgao wako umeuona nadhani, nahitaji jibu lako sasa, utaingia kwenye huu mchakato au ukose pesa hizo milioni 40 na uhai wako.” Nilisikia sauti ya Mary upande wa pili wa simu ikiniambia, ghafla nikatetemeka na sikuwa tayari kuchukua ile pesa.
“Mary sihitaji pesa yako.” Nilimjibu lakini alikaa kimya kidogo na kuongea tena.
“Sawa Dany, hakuna mtu anayeweza kulazimishwa kuchukua pesa hata siku moja, mimi sina muda huo pia, pesa inatafutwa sasa ukipewa ukaikataa basi hutakiwi kulazimishwa, kata simu alaf nitafanya mchakato wa kuirudisha kwenye akaunti yangu, wakati huo wewe mpigie simu mkeo mkeo umuage kwakuwa leo ndo mwisho wa wewe kuvuta pumzi yako.” Aliniambia hivyo na mimi niliona masihara, nikacheka lakini kilichofata kilinifanya nione kuwa sio kawaida.
“Unacheka nini, nimekuambia kata simu Dany umpigie mke wako, dakika tano zinakutosha sana kusema yote. Tazama kifuani kwako kisha uelewe ninachokisema.” Alisisitiza na mimi nilipotazama kifuani niliona taa nyekundu kama tochi vile mtu alikuwa akinimulika, sikutaka kuongea tena nikakata simu na kuwasha gari ili niondoke lakini sikuweza kwakuwa nilisikia risasi ikipenya kwenye kioo cha upande wa kushoto na kabla sijatafakari simu iliita nikaona ni Mary akipiga, nikapokea.
“Shusha kioo.” Nikasikia sauti ya Mary ikiniambia hayo, na mimi nikashusha huku nikitetemeka. Nilipomaliza kushusha aliniambia niangalie upande wa kulia wa barabara na nilipoangalia nilimuona akiwa kwenye BMW. Kisha aliwasha taa na risasi nyingine tena ilikuja na kupiga upande wangu karibu kabisa na sikio langu. Niligundua kuwa ile risasi ilitoka mbele kabisa kama umbali wa mita mia moja hamsini kutoka pale nilipo. Hivyo nikawa napanga kurudisha gari nyuma ili nichomoke kwa kasi lakini sikuweza kwakuwa nyuma kulikuwa na magari mawili yamepaki pande mbili za barabara.
“Huna pa kwenda Dany, kifo au ukae kwenye familia yangu.” Alieleza Mary, sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kumkubalia, nikakubali kushirikiana naye. Lakini alichosema kitu cha kwanza kwa mtu yeyote anayefanya kazi na yeye ni usiri. Sikujua kama Mary ni mtu mwenye nguvu vile. Alikuwa ni msichana mzuri lakini alikuwa na nguvu ya kufanya atakalo. Mfano kuna siku Mary alimpiga risasi mfanyakazi wake kwakuwa tu alikuwa anaongea na simu na kumtajia mtu kuwa bosi wake ni mkali. Hii yote iliniogopesha na sikuwa na jinsi. Hivyo kwenye mpango huu tulikuwa watu wanne, mimi Mary, mama yake na Mark, na Mark ambaye alikuja kuingizwa baadaye. Sisi tulikuwa wasikilizaji tu wa mipango ya Mary na tulichotakiwa kufanya ni kufungwa mkono. Baadaye Mary alinipeleka mpaka Urusi kwenye kampuni ambayo alikuwa na hisa nyingi, akanitambulisha kwa watu ambao wengi walionekana kama majasusi, na walikuwa wakimuogopa sana. Tukaja mpaka hapa Fiji kwenye kampuni ya Hawadh Shipping Agency ambayo ni kampuni pia ambayo yeye anamiliki asilimia kubwa sana ya ‘share’, akanikutanisha na Hawadh ambaye ndiye mwenye kampuni na Gibson ambaye alinitambulisha kama mkurugenzi wa kampuni ya Katapila. Nilichokuja kugundua ni kwamba Mary anaogopeka na anamtandao mkubwa, lakini sikujua kamwe atawezaje kuchukua mali za Patrick mpaka siku aliporudi Tanzania na kudai kuwa Patrick amefariki. Niliamini kabisa kwa maelezo yake, jinsi alivyoleta zile picha na habari za kwenye magazeti pamoja na Mark alivyokuwa akisema. Sikushtuka pia baada ya baab yake Patrick alipouwawa kwakuwa nilijua tu ni mpango pengine wa kuficha yote tuliyopanga. Mary alituaminisha kuwa Patrick hayuko hai. Nilijua ndio mpango umekamilika baada ya sasa Mary kuwa mmiliki wa ile kampuni na mali zote ambazo Patrick aliziacha, ndio maana hata siku ambayo nilimuona Patrick nilikimbia.” Aliongea Dany lakini nilihisi kama kuna kitu natakiwa kukijua zaidi.
“Kwahiyo Mary ana kazi gani hasa?” Felly aliendelea kumuuliza.
“Kwa kweli sijui, alinikutanisha na watu tu lakini sikuwahi kumuuliza anafanya kazi gani nyingine zaidi ya ile ya kampuni ya Patrick na ile ya majarida anayotoa.” Dany alijitahidi sana kuongea kwa ile sauti yake iliyojaa maumivu.
“Umesema ulikutana na Hawadh ambaye ni mmliki wa Hawadh Shipping Agency, je huyo Hawadhi yukoje?” Felly aliendelea kumuuliza.
“Ni kijana tu wa miaka 35 hivi.” Alijibu Dany.
“Na wewe ulikuja huku kuonana na Hawadhi?” aliuliza Felly.
“Hapana nilikuja kwa shughuli zangu lakini nikiwa huku Mary alinipigia simu nionane na Hawadhi kuna vitu atanipa nimsaidie kuvisaini.” Alijibu Dany.
“Je unafahamu kuwa Mary husafirisha Biskuti kuja Australia?” aliuliza Felly.
“Hapana sifahamu.” Alipojibu Felly alinigeukia.
“Umechoka Khajat? Naona nadanganywa na wewe upo hapa. Dany anaelewa sana juu ya usafirishaji wa biskuti toka Tanzania unaofanya na Hawadh Shipping Agency ya Tanzania na ndiyo kampuni iliyomsaidia kusafirisha hata magari yake. Hawadh walisafirisha konteza za futi arobaini za biskuti miezi sita iliyopita na nyaraka zilizoandikwa ziliandikwa kwa jina na Priscila Michael, mzigo uliandikwa kuwa ni wa Hawadh Enterprise, kiwanda mzigo ulipotoka kinaitwa ni Priscila Food Industrirs, hii kampuni ni kweli ipo lakini inauwezo mdogo sana, nataka uniambie nini kinatengenezwa na ni vitu gani ulikwenda kuweka sahihi.” Aliongea Felly na mimi nilimsogelea Dany nikiwa nimeshikilia kisu mkononi. Dany hakuwa tayari kusema, nilimtsha lakini hakuwa tayari kusema lolote.
“Siwezi kusema chochote, Mary ni mnyama zaidi ya mnavyodhani. Hakuna kati yenu atakayemuweza hata kumfikia. Nikisema chochote hapa basi familia yangu itakuwa hatarini. Sina cha kuwaambia zaidi ya hicho nilichosema.” Nilimtazama usoni nikaona ni kweli hawezi kusema kwakuwa anamuogopa Dany lakini dawa yake niliijua. Kabla sijanyanyuka pale, Patrick alikuja na kunipora kile kisu kisha akamchoma Dany kwenye mkono lakini aliishia kulia tu, hakuweza kujibu chochote. Niligundua kuwa Dany anajaribu kujitoa kama vile ahusiki na kwamba alilazimishwa.
“Nakuhimiza ujibu swali alilokuuliza Felly kabla sijatoka hapa.” Nilimwambia Dany lakini alikuwa kimya tu akilia. Kwa hatua hiyo inamaana Dany alikuwa ameshayazoe maumivu. Nilipanda mpaka juu na kuchukua mashine za kizamani za kusagia nyama yani zile za kutumia mikono kuzungusha, nilipofika pale nilimkamata Dany mkono na kuingiza vidole vyake viwili kisha nilichanganya na vipande viwili vya nyama ili kuiweka mashinde sawa na hapo nikaisukuma, Dany alilia sana kwa uchungu lakini niliisukuma na kuvisaga nusu kicha niliviweka chumbi iliyomfanya akojoe kabisa.
“Niendelee?” nilimuuliza huku nikimtazama.
“Hapana, zile kontena hazisafirishi biskuti, ni unga wa pembe za ndovu ndio zinasagwa na kuwekwa kama biskuti ili isishtukiwe bandarini.” Alijibu kwa haraka huku kamasi na machozi yakimtoka.
“Na Mary kwasasa yuko wapi.” Nilimuuliza na hapo alikaa kimya lakini nilipompelekea maishine ile aliongea.
“Usidhani yanayokutokea sasa, au yale uliyopitia ndiyo yatakayoonyesha wewe utakuwa mtu wa aina gani hapo baadaye. Haijalishi umetoka kwenye familia ya aina gani na wala haijalishi maisha yako ya sasa yakoje. Lakini uamuzi wako utakaoufanya sasa juu ya nini unataka kukitilia mkazo na nini maana ya vitu fulani kwako, aina ya mafanikio uyatakayo na jinsi ambavyo utafanya ili kuyafikia ndicho kitakachokupa mwanga wa mtu wa aina gani utakuwa. Kila kitu duniani chenye mafanikio kilianzishwa na mtu mmoja tu. Wazo huwa kichwani kwa mtu mmoja nayeye anaposhirikisha wengine bado tunahesabu kuwa yeye ndiye aliyeleta jambo hilo. Kila mtu mwenye mafanikio alikuwa na ndoto kabla, akazichambua ndoto zake na kuziishi huku akifanya kila njia kuzileta kwenye uhalisia. WEWE UNANAFASI YA KUFIKA PALE UTAKAPO KAMA UTAACHA KUJIDHARAU.” Hii ni sehemu ya KUMI NA NNE.
Ilikuwa sasa ni saa 10 kamili usiku, Khajat alikuwa amemaliza kusimulia na kuelezea historia yake mpaka alipofika. Ndugu mwandishi katika maisha ya kawaida ya binadamu nilijifunza kumbe kuna muda watu wabaya wanatengenezwa na matendo ya binadamu wengine. Khajat alitengenezwa na matendo ya yule mwanamke aliyefukiwa akiwa hai, ila sasa Felly alianza kusimulia na yeye. Alikuwa akiongea kwa lugha ya kingereza lakini kulikuwako na mtu pembeni akitafsiri. Ilikuwa hivi;
***FELLY***
>>MIAKA MINGI ILIYOPITA<<
Kwenye maisha nilijifunza kujitegemea toka nikiwa mtoto kabisa. Kipindi ambacho nilikuwa binti aliyetakiwa kupata malezi ya wazazi ndiyo muda ambao nilikuwa mtaani nikitafuta maisha yangu mwenyewe. Mafanikio katika maisha niliyapima kwa matendo yangu ya kila siku na jua lilipozama. Kisichokuua kitakukomaza, niliamini hivyo na kila jua lilipozama nilipiga goti na kumwambia mungu nashukuru kwa pumzi na kama ikikuendeza naomba kesho tena nivute pumzi. Maisha magumu ya kulelewa na mama wa kambo baada ya mama yetu kufariki ndiyo yaliyoniondoa nyumbani. Kipigo kilichopitiliza kilinifanya mtumwa ndani ya himaya ya baba yangu, nikaamua kuingia mtaani wakati huo nikiwa na miaka saba na Khajat akiwa na mwaka mmoja. Hiyo pia ni mwaka mmoja toka mama afariki na kumuacha http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Khajat akiwa na siku chache. Sikumchukia yule mwanamke kwakuwa tu hakutuwekea sumu lakini nililiacha hilo mikononi mwa Khajat kuamua akikua. Nikiwa na miaka kumi na kipindi hicho bado nikiwa shuleni nilifanikiwa kupanda meli ya mizigo na kujificha kwenye masanduku. Nilikaa siku tatu bila kula, lakini baadaye nilishindwa na kujitokeza kwa wale mabaharia. Niliwaeleza kwa nini nilikuwa naondoka India, walinielewa na nilipewa kazi ya kupika Mboga kila siku ndani ya ile meli, walikuwa watu wakarimu sana. Nilitegemea pengine wangeweza kunibaka lakini haikuwa hivyo. Baada ya mwezi mmoja tulikuwa tumefika Australia na meli ilikuwa ikienda kutia nanga kisiwa cha Fiji. Hivyo na mimi nilifika mpaka Fiji na kushuka. Nahodha wa ile meli ambaye nakumbuka alikuwa ni mzungu, akanipa namba yake ya simu na pesa kiasi fulani kisha aliniagiza kwenda kwa mama mmoja ambaye ni dada yake anayeishi SUVA, nilikwenda bila kusita mpaka kule na yule mwanamke tayari alikuwa na maelezo juu yangu hivyo alinipokea.
Nilichokuja kugundua kuhusu yule mwanamke ni kwamba alikuwa haniamini kabisa, alaf pia alikuwa ni mjane ambaye aliachwa na mumewe aliyekuwa ni nahodha, mpaka mumewe anafariki hawakuwa wamebahatika kupata mtoto na kwenye ile nyumba aliishi peke yake na mbwa wake. Mara kwa mara alitegesha kiasi kikubwa sana cha pesa maeneo ambayo alijua kabisa ningeona. Mara zote hizo nilikuwa nikiona na kuzichukua kisha nilimpatia. Alikuwa akifanya majaribio mengi lakini baada ya miezi mitatu aligundua mimi si aina ya msichana aliyemtarajia. Nilianzishwa shule na muda wote huo nilisoma kwa bidii sana. Nilikuwa nikimuwaza sana Khajat na nilipanga kumfata siku nikishafanikiwa kuweka maisha sawa. Nilisoma na kuhitimu vizuri elimu ya sekondari na baadaye nilijiunga na jeshi kisha nilikwenda kusoma chuo kikuu, ambapo ndipo nilikutana kwa mara ya kwanza na Pamela na akawa rafiki yangu mkubwa, baadaye nilianza kujitegemea, yule mama alifariki na kuniachia ile nyumba ambayo nilikuja kuikabidhi kwa kanisa ili walelee watoto yatima. Nilikuja kusoma shahada ya pili ya mambo ya upelelezi wa makosa ya jinai kisha nikawa mwalimu wa mafunzo ya upelelezi jeshini, wakati huo Khajat ndio alikuwa amekuja kwangu na kunihadithia yote yaliyomkuta.
Nilifanya kazi ofisi za jeshi baadaye nilihamishiwa ofisi za polisi Fiji ambapo nilikuwa mkuu wa kitengo cha upelelezi na baadaye nilikwenda Cuba kusomea mambo ya kivita na uchunguzi wa mauaji. Nilipomaliza nikapelekwa ofisi ya usalama. Hii yote iliwezekana kwakuwa yule mama alinitafutia urai wa Fiji nikiwa bado sekondari, na hata Khajat alipofika kitu cha kwanza nilianza kuhangaika ilia pate uraia. Maisha yalikuwa mazuri, ni kama gari linavyoenda sawia pale matairi yake yanapokuwa sawa, na inapokuwa kwenye mteremko, huenda haraka na bila kuhitaj mafuta mengi, hivyo ndivyo maisha yetu yalivyoanza kwenda sawia pale ambapo hisia zetu, akili zetu na maono yetu yalikuwa yametulia. Sikuwahi kuwa na mwanaume au kufanya mapenzi mpaka nilipofika miaka 29, nilikutana na mwanaume aliyeziinua hisia zangu, alikuwa ni kama teja kwakuwa madawa ya kulevya yalikuwa yamemuathiri. Sikuwa na mwanaume kwakuwa sikuona umuhimu wao, nilikuwa mtu wa mazoezi tu na kufikiria mafanikio yangu. Nilikuwa mbinafsi na hii ilikuwa ni njia ya kuzuia kuumizwa. Nilimchukua yule kijana, nikampeleka kwa daktari ambaye nilionyeshwa na Pamela, akatibiwa kwa pesa zangu mpaka akaona kabisa. Nikamleta nyumbani kwangu, akacheza na mwili wangu kwa kadiri alivyotaka, nikampa pesa kwa kadiri alivyotaka. Nilimpenda sana kwakuwa nilijua wanaume wengi waliniogopa, alitoa bikra yangu na kumaliza woga wangu. Nikamtafutia kazi jeshini, nikamuingiza kwenye darasa langu la karate nililokuwa nikiwafundisha wanajeshi wa baharini. Akawa ameiva. Nikaanza kuchunguza mienendo yake nikagundua anawanawake wengine, sikuwahi kumuuliza, nilijua bado anahitaji muda wa kubadilika. Lakini hakuwa anabadilika, nikamuonya mara nyingi akawa akiitika lakini hakuwa akitekeleza. Ikaniuma sana lakini bado nilimpa muda nikiamini angebadilika lakini ilikuwa tofauti, kuna muda alilala nje akidai yuko kambini lakini nilimfatilia na kumkuta akifanya mapenzi na mwanamke mwingine, nilikuwa dirishani siku hiyo, sikuongea chochote bali nilirudi nyumbani. Aliporudi kesho yake nilimwambia kuwa nimemuona na kumuomba ajirekebishe, badala yake akafoka na kunipiga, nilimtazama tu kwakuwa nilijua nikisema nimpige na mimi ningeweza kumuua. Baadaye alianza kujirekebisha ila bado alikuwa akiendelea na mambo mengine, siku niliyokuja kugundua alimlazimisha Pamela kufanya naye mapenzi tena kwa kumnywesha pombe ndipo niliona huo ndo uwe mwisho sasa wa wema wangu kwake, niliiba bomu dogo nikiwa kambi ya jeshi na kuondoka nalo mpaka nyumbani, kipindi hicho alikuwa akienda kwenye kulinda Amani Iraq. Nilikuwa nampangia vitu vyake kwenye begi. Haikuwa rahisi kwangu lakini niliona kabisa kuwa sikumuhitaji kwangu na kwenye hii dunia, hivyo nililishonea lile bomu vizuri kwenye begi chini na kulitegesha masaa mengi nikijua kabisa litalipuka akiwa ameshafika. Na ndicho kilichotokea. Sidhani kama nitakuwa tena na mwanaume, na hata nikiwa naye najua nitamuua kinyama siku akifanya upuuzi, niliamua kuishi kama mwanaume tu lakini nimekuja kugundua nimekuwa zaidi ya mwanaume.
>>SASA<<
Dany alitueleza mengi aliyoweza kutueleza lakini kwenye maelezo yake bado niliona kuna vitu vingi sana kuhusu Mary bado hatujavijua. Kikubwa kilichonisumbua kilikuwa ni kwanini amemfanyia mumewe vile, je ilikuwa ni pesa tu ama? Lakini hatukujua lolote kabisa. Tuliamua kumuweka Dany apatiwe matibabu akiwa palepale kwangu huku tukiendelea kusubiri siku Mary anayokuja Fiji, tulikaa zaidi ya wiki mbili lakini Mary hakuwa ametokea wala kupiga simu.
“Khajat tunafanyaje? Maana naona kama tumekwamba sehemu.” Nilimuuliza Khajat wakati huo ikiwa ni wiki ya pili na siku tatu toka siku Dany aliyosema kuwa Mary angekuja wiki iliyofuata. Hatukujua lakufanya zaidi lakini tulikuwa na lengo la kumkamata Mary na kumfanya chochote ambacho tungekiwaza kwa muda huo.
“Mfatilie Hawadh umlete hapa nyumbani, yeye ndiye atatusaidia kujua yaliyobaki.” Aliniambia Khajat, lakini Hawadh hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa ni mtu katili sana na aliyejulikana na kuchukiwa na wengi lakini hiyo haikunipa shida sana kwakuwa Hawadh anapenda sana wanawakem na katika kufanya uhalifu au mauaji au hata upelelezi ni rahisi sana kumpata mwanaume ambaye anapenda wanawake, hakuna upelelezi rahisi kama mwanamke kumpeleleza mwanaume anayependa ngono. Kanuni kwa watu kama hawa ni tatu tu, mpe anachotaka kwa kiwango kikubwa ili uivuruge akili yake, mbili, mfanye akuone wewe ni mtu wa kawaida ila unayemfaa, tatu weka mihemko pembeni kisha mpeleke unapotaka wewe. Ndicho nilichomfanyia Hawadh. Baada ya kumtafuta kwa siku nzima hatimaye niligundua alikuwa Kansaz Casino iliyokuwa Vulpatra kama kilomita 30 kutoka kwangu, nilivaa kama wahudumu wale wa ile kasino lakini nguo yangu ilikuwa tofauti kwakuwa niliiweka mpasuo mpaka juu kabisa na nilipotembea au kuinama kidogo ilikuwa ikionyesha nguo yangu ya ndani. Nilipofika pale niligundua alipokuwa amekaa na alikuwa amekuja na walinzi watatu waliokuwa wamesimama karibu yake. Haraka nilimuwahi muhudumu aliyekuwa akimuhudumia pale na kuchukua vile vinywaji kisha nilimpelekea, kwa manjonjo kabisa nilimfungulia na aliponitazama nilijua kabisa alinitamani nikaondoka na kudondosha funguo niliyokuwa nimeshika kisha kwa makusudi niliinama kuiokota na kumpa muda wa kunitamani zaidi. Niliponyanyuka nilimkonyeza na kama alijua vile alisimama na kunifuata.
“Binti habari yako.” Tulikuwa tumesimama kwenye korido wakati akinisemesha.
“Salama, unahitaji nini nikusaidie.” Niliongea huku nikijiachia kwake na kuondoka, nia yangu ni yeye ajue tu kuwa sikuwa nafahamu wadhifa wake na hivyo nilimuona kama mteja wa kawaida tu ambaye hakuhitajika kupapatikiwa sana.
“Wewe ni muhudumu mpya hapa?” aliniuliza huku akinifata.
“Ndio, nimetoka Jorpradigo Casino.” Nilisogea mbele na kufungua malango wa chumba fulani na yeye aliingia, bila hiyana nilijifanya kama vile sikumuona na kuavua nguo zangu zote mpaka ya ndani mbele yake kisha nilimgeukia, alikuwa ametoa macho na mdomo ukiwa wazi, nilichukua nguo nyingine kwenye begi langu dogo na kuanza kuvaa taratibu huku nikimtazama, kisha nilimsogelea na kumuomba alifunge mkanda wa brazia yangu. Alifanya hivyo lakini nilishamsoma kabisa kuwa alikuwa ni dhaifu sana. Nilipomaliza alikuwa bado amesimama pale.
“Unakwenda wapi?” aliniuliza.
“Muda wangu wa kazi umekwisha naelekea kwangu.” Nilimuambia huku nikimpita na kwenda kwenye mlango lakini kabla sijafungua, alinifata na kunisimamisha.
“Naweza kuwa na wewe kwa usiku mzima?” aliniongelesha huku akionekana kuzidiwa sana.
“Ndio, njoo KLPC 34, SUVA BRIDGE, lisaa limoja kuanzia sasa. Njoo mwenyewe, sipendi kulindwalindwa, kama unataka raha waache walinzi wako nyumbani.” Nilimwambia hayo na bila kumpa muda wa kujibu niliamua kuondoka, sikuwa nimempa namba yangu ya simu. Niliondoka moja kwa moja mpaka nyumbani nikamweleza Khajat na yeye alikubali kuondoka na mimi. Tulikwenda mpaka bali na Khajat alikuwa ameshatega kamera na kila kitu kwenye hoteli moja iliyokuwa pale, kisha alipokuja mimi niliingia naye kwenye ile hoteli baada ya kuhakikisha kuwa alikuwa mwenyewe. Baada ya kuingia nae nilimuwekea madawa ya kulevya kwenye kinywaji na alipokunywa tu alikuwa tayari ameshalewa, madawa niliyomuwekea yalikuwa ni tofauti sana na yale mengine ya kulevya, hii ilikuwa ni ya kipolisi iliyokuwa na nguvu ya kuuharibu ubingo na kumfanya mtu aseme chochote bila kujijua. Hivyo baada ya hapo Khajat aliingia kule chumbani na tulianza kupekua simu yake na kukuta mawasiliano yake na Mary wiki tatu zilizopita juu ya kuingia kwa kontena la biskuti mwezi ujao. Hakukuwa na mawasiliano mengine kati yake na Mary. Hivyo Khajat alipoingia ilikuwa ni kumuhoji tu ili kama kuna analolijua basi atueleze.
“Khajat, hakuna kumtesa huyu.” Nilimuambia Khajat na yeye alikubali. Nilisema hivyo kwakuwa kama tungeweza kumfanya chochote basi ingekuwa ngumu sana kwa sisi kumaliza tuliyoyaanzisha.
“Hawadhi.” Khajat alimuita kwa sauti ya chini na yeye aliitika kwa sauti ya chini kama vile mlevi.
“Mary anakuja lini Fiji.” Khajat alimuuliza lakini Hawadh hakujibu.
“Hawadh nakuuliza Mary au Priscila analeta lini lile kontena la biskuti huku Fiji.” Alimuuliza tena na kwa mbali kabisa Hawadh alianza kujibu.
“Ameshakuja, yuko huku toka jana anamtafuta Dany.” Alijibu kwa sauti ya kilevi.
“Dany yuko wapi kwani.” Nilimuuliza nikiwa na nia ya kujua kama anafahamu chochote juu ya Dany.
“Dany hajaonekana, itakuwa amekimbia na pesa za mzigo.” Alijibu tena huku akiwa bado anarembua macho kama vile anasinzia.
“Mary amefikia wapi.” Nilimuuliza tena lakini hakuonekana kufahamu.
“Sio rahisi kujua Mary anapofikia ila natarajia kuonana nae siku yoyote akinipigia simu.” Mpaka hapo hatukuwa tunahitaji tena maelezo mengine toka kwa Hawadh, nilimpa maji yanye glucose yaliyomfanya atapike na ile dawa ikakata akarudi kama kawaida.
“Tumefanya vya kutosha Hawadh mapaka umelala, sasa naomba tukaoge kisha tuondoke.” Kwakuwa alikuwa bado hajielewi vizuri niliharakisha mambo na tukaenda kuoga kama vile kuna tulichokifanya, baada ya hapo tulitoka nje. Akaniandikia hundi ya dola elfu 3 na yeye aliondoka kwenda kwake. Tulirudi moja kwa moja mpaka kwa Pamela na wao walikuwa bado hawajalala. Tukawachukua na kwenda nao mpaka kwangu ili wakalale huko. Tulipofika nyumbani baada ya kufungua tu na kwenda kule chini aliko Dany ambaye alikuwa tayari ameanza kurudi katika hali nzuri japo alikuwa ndani ya sindano ya usingizi, tukasikia sauti ya simu ya Dany ikiita, tulipoiangalia alikuwa ni Mary, haraka Pamela alimchoma sindano nyingine ya kumuamsha, alipoamka tu alikuwa bado hajakaa sawa. Ujue Khajat ni mtu ambaye hapendi kucheleweshwa, simu ilikuwa imeshakatika na sasa ilikuwa ikiita kwa mara ya pili lakini Dany bado alikuwa na maruweruwe, Khajat alimpiga ngumi moja ya uso na akili ya Dany ilikaa sawa, nilimwonea huruma kwa mara ya kwanza kwani ile ngumi ilimfanya alie na damu za pua zianze kumtoka.
“Sikiliza Dany, ukijifanya wewe ni mfu hapa, nitakuzika kabla pumzi yako haijafika mwisho. Ni lazima ufe ila muda wako bado haujafika hivyo jiweke kama binadamu.” Khajat alimsemesha Dany huku akimkazia macho na Dany alinyamaza kulia na kutingisha kichwa kama ishara ya kwamba amemuelewa Khajat.
“Sasa Mary anapiga simu hapa, ukionyesha dalili yoyote ya kumtaarifu kuwa uko sehemu yenye hatari ujue wakati unakata simu utakuwa umekata pia koo lako na mkeo atakishuhudia kichwa chako kikiwa kwenye begi, hivyo mwambie uko Side Villa Motel, akikuambia muonane sema sawa. Maneno tofauti na hayo basi uhesabu kuwa mke wako ni mjane.” Khajat alimaliza kumtahadharisha na ile simu ilipokelewa na kuwekwa sauti ya juu ili wote tusikie.
“Hallo Mary.” Aliitikia Dany.
“Yes Dany, please may I speak to my husband please?” (Ndio Dany, naweza kuongea na mume wangu tafadhali?) aliongea Mary kwa sauti ya kejeli. Nilimtazama Patrick alikuwa amejaa hasira mpaka machozi yalianza kumtoka.
“I don’t Understand what you talking about.” (sielewi unachokiongea) Dany alijifanya kama vile hakuwa anaelewa vizuri alichokuwa anaongea Mary. Mary alipiga simu na kuongea kwa lugha ya kingereza kwa makusudi kabisa.
“Dany, am not a kid, hand the phone to Patrick.”(mimi sio mtoto Dany, mpe Patrick simu.) Kabla hata Dany hajajishauri Patrick alikuwa ameshaongea.
“What do you want.” Ilikuwa ni sauti ya Patrick ikimuliza Mary.
“Patrick mimi si mjinga, na sijafurahia kuwa kwako hai, ila nakupa mambo mawili uachague moja, kaburi au uhai. Huyo afisa uhamiaji anayeitwa Khajat hatakusaidia sana kwakuwa unahitaji jeshi la watu mia 200 kuniangamiza. Kaa mbali na njia nipitayo na wewe utaishi kwa Amani mume wangu. Dunia hii si mapenzi tu, dunia ina mengi, mwache Dany huru kisha wewe endelea na maisha yako, usifatilie kuhusu mimi na umwambia huyo mwanamke wako Khajat ajali zaidi maisha yake. Hakuna wa kuangamiza ndoto zangu.” Alimaliza Mary na hapohapo Khajat alichukua ile simu.
“You don’t know me well Mary.” (Hunijui vizuri Mary), aliongea Khajat lakini kabla hajaendelea alikatizwa na kicheko cha Mary.
“Khajat, a senior migration office with no, HA/MO/2345. You kidnaped Dany three weeks ago, you drive a black escalade, you are single, 5.5 feet. Is that not you sweatheart?”(Khajat, ni afisa wa uhamiaji ngazi ya juu, namba yako ni HA/MO/2345. Ulimteka Dany wiki tatu zilizopita. Unaendesha gari nyeusi aina ya escalade, hujaolewa, una urefu wa futi 5.5, je sio wewe mpenzi?) Aliongea Mary, mimi nilikuwa kimya.
“Mary, am more that what you have read about me, the difference between you and me is that, you take life of the innocent people for you greed, I serve the life of the innocent people by taking the life of the guilt one. I don’t need an army to take you down and slaughter you, I just need me, and one smart woman. I will catch you because when you pressed the button to dial Dany’s number is when you put your life in jeopardy. So gather you men.”(Mary, mimi ni zaidi ya yale ulioyasoma kuhusu mimi, tofauti kati yangu na wewe ni kwamba wewe unaua watu wasio na hatia kwa uroho wako, ila mimi naokoa maisha ya watu wasio na hatia kwa kuua wenye hatia. Sihitaji jeshi kukukamata na kukuchinja. Najihitaji mimi mwenyewe na msichana mmoja timamu. Nitakukamata kwakuwa muda uliompigia Dany simu ndipo ulipoweka maisha yako hatarini. Kwaiyo kusanya watu wako) Aliongea Khajat na kukata simu.
Nitakukamata kwakuwa muda uliompigia Dany simu ndipo ulipoweka maisha yako hatarini. Kwaiyo kusanya watu wako) Aliongea Khajat na kukata simu.
*****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kifo ni hatua ya mwisho wa muda wa binadamu katika dunia, haijalishi ni muda gani utachukua hapa duniani ila jua tu kwamba ipo siku na wewe utakufa. Cha kujiuliza ni kitu gani katika maisha kitakutambulisha baada ya kifo chako? Ni kitu gani kitamfurahisha muumba wako pale utakapokuwa ukifanyiwa hesabu ya mema uliyoyafanya kama shukrani ya pumzi kwa muumba? Kuna muda wa kila kitu, kuna starehe za ujana na shida za uzeeni. Kufa Hakuhitaji uwe mgonjwa au upate ajali, ili ufe inahitajika SIKU YAKO IWE IMEFIKA. Inaumiza sana kufiwa na mtu uliyempenda au mtu aliyewahi kukufanya ucheke ama kujifunza kitu. Lakini hiyo haitufanyi tusahau kuwa wote tutakufa. Muda wetu katika dunia hii una kikomo, na huwa kifo ni mshangao kwetu hasa afapo mtu ambaye hatukutegemea. Ni kama kupanda ngazi usiku wa giza nene, ufikapo sehemu na kudhani kuwa kuna ngazi nyingine mbele lakini unashangazwa na kujikuta ukitembea hewani na kuanguka, giza litakufumba macho na hutaamka tena. KILA MUDA NI MUDA WA KUJIWEKA SAWA KWA MUUMBA. TAFUTA KITU CHA KUIFANYA JAMII YAKO IKUKUMBUKE, TAFUTA KITU CHA KUMFANYA MUUMBA WAKO AJISIKIE FARAJA KUKUPOKEA.” ULALE SALAMA NGWEA.HII NI SEHEMU YA KUMI NA TANO.
**KHAJAT**
Nilikuwa nimeshamaliza na mambo ya kazini na sasa nilikuwa tayari kwenda kuonana na Felly ili tupange zaidi juu ya mikakati ya kumuweka Mary kwenye mikono yetu. Tulikubaliana kabisa kuwa hakuna kumtoa Dany. Kitendo cha Mary kumtaka Dany inaonyesha anafahamu mengi juu ya Mary na sasa ndio alikuwa amefungua dirisha la mateso ya Dany. Nilikuwa nimeagiza vifaa zaidi ili Dany aeleze yote anayotakiwa kueleza. Niliagiza mashine ya kukamulia miwa ambayo iliwahi kumfanya Gervace Harv kusema juu ya bomu walilolitega Indovoa karibu kabisa na soko kubwa la Suva, mashine ile inasehemu ya kuingiza mua kisha hukamuliwa na makapi hutupwa pembeni. Baada ya wanajeshi wa Fiji kushindwa kupata majibu ya maswali yao kutoka kwa Gervace ambaye alikuwa ni gaidi aliyetumiwa na nchi za Saudia tuliitwa kikosi chetu kwaajili ya kwenda kutafuta lile bomu. Mara zote Gervace alipokuwa akipigwa ili aseme alikataa na kusema hata mnipige vipi mimi niko tayari kufa na sitasema chochote. Nilimuomba mkuu wa kikosi anipe nafasi ya kuonana na Gervace ila alinikatalia. Nilifikiria kazi nzito ya kutafuta kitu usichojua kilipo nikaamua kumtoroka na kwenda kule alikokuwa amewekwa nikawaomba wale wanajeshi waliokuwa wanamlinda waniruhusu nionane naye na wao waliniruhusu, nikaomba ile mashine ya miwa iliyokuwa karibu na pale kambini iletwe ndani na wale wanajeshi waliileta kimya kimya, nilimtazama Gervace usoni nikamuuliza bomu liko wapi ila hakusema, alichoniambia ni kwamba baba yake aliuawa na jeshi kwakuwa tu alitoa siri za wakuu wa jeshi kufuja mali za ununuzi wa silaha. Lakini pamoja na kwamba alikuwa akilipa kisasi alikuwa ameshakosea kutega bomu litakaloua watu, nilimsihi kwa sauti ya upole lakini hakusikia. Ile mashine ilipokuja nilimuuliza tena lakini aliishia kunitemea mate. Nikaukamata mkono wake na kuuingiza ndani ya ile mashinekisha nikawasha, ilianza kuminya vidole vikawa kama chapati na hata haikufika mbali tayari alikuwa ameshasema bomu lilipo. Nilikuwa katili sana lakini kama kuna mungu basi atanisamehe, ila adhabu hii itamkuta Dany kama ataamua kukaa kimya bila kuusema ukweli wote bila kuacha chochote. Haijalishi kwamba yeye sio gaidi au ni mtu wa kawaida tu, kitendo cha yeye kushiriki kuua na kudhulumu nguvu ya mtu tayari ni ugaidi uliostahili adhabu kali ambayo sio kifungo cha maisha bali maumivu makali na ya muda mrefu kabla ya kufa.
Nilitoka vizuri nje ya ofisi na nilikwenda mpaka kwenye gari yangu, nilipofika nilifungua mlango na kuingia ndani kisha nikawasha gari, ila kabla sijaingiza gia nikasikia sauti ya mtu ikitaja jina langu kwenye kiti cha nyuma, nilipogeuka tu nilikutana na kitu kilichopulizwa usoni kwangu na hapohapo nilipoteza fahamu. Sikujua ni kitu gani na ni nani aliyefanya vile. Nikaja kushtuka nikiwa nimefungwa kila sehemu kwa kamba ngumu, mbele yangu kulikuwa na mwanamke ambaye niliweza kuitambua sura yake kwakuwa niliiona kwenye picha. Alikuwa ni Mary.
“Habari yako Khajat.” Alinisemesha kwa dharau huku akinitazama machoni, hasira zilinipanda na nilikuwa nasubiri afanye makosa ya kunifungua zile kamba. Nilipomtazama usoni tayari nilikuwa nimeshamsoma kuwa ni mtu katili mwenye sura ya malaika.
“Unataka nini kwangu.” Nilimuuliza huku nikiendelea kumtizama usoni.
“Nataka kumuonyesha Patrick kuwa wewe huwezi chochote, una mpotezea muda wake na kumuhatarishia maisha yake zaidi.” Aliongea huku akitabasamu, nilizidi kumtazama usoni ili kujua ni ipi nia yake.
“Hutapata chochote unachokitaka.” Nilimsemesha kwa kujiamini na hiyo ilimfanya acheke kisha aliondoka pale na kurudi tena akiwa na mikasi, alikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa ni mzungu aliyejichora mwili wake. Sikujua alitaka kufanya nini lakini sikutaka kumuonyesha woga ili asinitawale.
“Mfungue izo kamba.” Alimwambia yule mzungu na yeye alinisogelea na kutaka kunifungua kamba.
“Nakushauri kama unataka kufanya chochote basi usinifungue hapa.” Nilimwambia Mary na yeye alicheka kisha alinitazama usoni kwa dakika mbili.
“Khajat, mimi ni zaidi ya hili tabasamu unaloliona usoni mwangu, Roland mfungue kamba tuone atafanya nini.” Aliongea Mary na yule kijana alinifungua kamba, aliponiachia nilikuwa nimesimama nikimtazama Mary alitaka kufanya nini;
“Chukua simu mpigia Patrick mwambie amlete Dany Villa Bridge baada ya nusu saa.” Aliniambia akiwa ameukunja uso wake kama vile alikuwa akinitisha, bado nilikuwa sijajua uwezo wa Mary, lakini pia hakuonekana kama ni mtu wa kutishwa kirahisi.
“Sipigi simu popote na humpati huyo Dany, fanya lolote unalotaka, na mimi na wewe tumemalizana hapa.” Nilimwambia hivyo na kuondoka, sikufika popote nilipigwa teke mgongoni lililonifanya nianguke chini, nilivyojigeuza nikakutana na ngumi nyingine ya shavu na kiatu kilinikanyaga shingoni, nilikuwa bado kama nina maruweruwe hivi na nilivyotazama vizuri nikakuta ni Mary ndiye aliyenipiga;
“Usinifanye nikakuua mapema.” Aliniambia huku akinitazama kwa sura yenye kuonyesha kuwa alikuwa akimaanisha. Nilichokuwa nakifanya sio kupigana na Mary, nia yangu ilikuwa kuujua uwezo wa Mary na alikuwa na ujuzi gani kwenye mambo anayoyafanya. Nilijigeuza vizuri na kumtazama kisha nilimpelekea ngumi ya uso iliyomfanya aanguke pembeni, nilikuwa haraka na kunyanyuka na yeye alikuwa amejibinua haraka na kukaa sawa, niliitazama miguu yake alivyoiweka na ngumi alivyokunja nikajua kuwa Mary alikuwa ni mtaalamu wa karate, kijana wake wa kizungu alikuja mbio na kutaka kunivamia ila niliwahi na kuibetua meza akakutana nayo na hiyo ikamfanya akae chini kwa maumivu, Mary aliniwahi palepale na kuja na teke ambalo hata hivyo nilikuwa nimeliona na kumpisha akutane na ukuta, nilichokifanya nilimuwahi yule kijana pale chini na kumshika shingo kisha nikaivunja mbele ya Mary ambaye alikuwa bado yuko pale chini. Mary alitoa macho, nikamfata pale alipo na kuzishika nywele zake kisha nikamnyanyua, wakati napanga kumpiga ngumi ya tumbo yeye alikuwa ameshaniwahi na kichwa kilichonipeleka tena chini na hapo aliniwahi na kunifunga mikono kwa pingu.
“Nitakuua lakini sio sasa, hivyo usinilazimishe Khajat.” Aliniambia hivyo huku akininyanyua na kuniweka kwenye kile kiti. Kisha na yeye aliketi chini kwakuwa alikuwa tayari amechoka, alinyanyua simu na kupiga;
“yeah, njoo ndani.” Aliongea maneno machache tu na hapo alikuja mtu mwingine ndani, wa sasa hivi alikuwa ni mwafrika ambaye inaonekana alikuwa ni Mtanzania kwakuwa lugha waliyoongea ilikuwa inaendana kabisa na ile ambayo Patrick na Pamela wanayoongeaga. Hapo walikuwa tayari wamenifunga kwani sikuelewa walichokuwa wanasema. Lakini baada ya muda mfupi yule jamaa alionoka na kurudi na simu yangu, kisha Mary alisogea karibu yangu na kunisemesha.
“Uko tayari kupiga simu au nipige mimi?” alinisemesha lakini mimi sikumjibu, alinitazama huku akitabasamu.
“Ujue Khajat umemuua kijana wangu mmoja, sijui kwanini unahisi sitaweza kukuua na wewe hata sasa hivi, sijui kitu gani kinakufanya uone kuwa ninaweza kuwa na huruma na wewe,mh! ni hili tabasamu langue e? tabasamu hili limeua wengi sana, wengi hulitazama juujuu, tabasamu langu litakuua wewe pia muda ukifika hivyo kwa sasa chukua simu nifanyie kwanza kazi yangu.” Alinitazama huku akiendelea kutabasamu. Alikuwa na tabasamu lililoficha unyama wake, alionekana mpole lakini alikuwa muuaji.
“Sipigi simu, usinitishie kufa kwakuwa mimi ni marehemu siku nyingi sana. Hakuna jipya unaloweza kunifanya mimi, hakuna maumivu mapya unayoweza kunipa ambayo sikuwahi kuyapata kabla, kama unataka kuyaona machozi yangu hapo sawa ila kama unahitaji majibu ya maswali yako jua kabisa hapa hutayapata.” Nilimwambia na yeye alizidi kunitolea tabasamu. Akachukua mkazi mmoja uliokuwa pale mezani kisha akanisogelea taratibu.
“Khajat, nikupe simu upige?” aliniongelesha tena huku akiniwekea ule mkazi kwenye kidole changu cha mwisho, ulikuwa ni mkasi wa kukata vyuma, akauweka katikati ya ukucha wangu, nilimtazama usoni na kumtemea mate, kilichofata yalikuwa maumivu makali na jasho, alikuwa amenikata na niliona sehemu ya kidole changu ikiwa nusu, kipande alichokikata kilikuwa kimedondoka chini. Nililia sana kwakuwa nilisikia maumivu na hapo alichukua kitambaa anifunge ili kuzuia damu ile isitoke, nikakataa kufungwa kitambaa ikiwa ni ishara ya kumuonyesha kuwa sikuwa naogopa kufa, walinishika mkono kwa nguvu na yule jamaa aliyekuwa naye alifanikiwa kunifunga mkono ule na hivyo damu ilikuwa ikitoka kidogo lakini maumivu niliyasikia mpaka shingoni. Hakuishia hapo bado alinilazimisha niongee na Patrick lakini nilimkatalia, nilichojifunza ni kwamba Mary hakuwa anamjua Felly wala hakuwa na taarifa kuwa Patrick alikuwa na mtoto huku. Hii kwa maneno mengine ilionyesha kuwa intelijensia ya Mary ni dhaifu na hii ilikuwa nafasi nzuri ya mimi na Felly kumsaka iwapo ningefanikiwa kutoka nikiwa mzima. Alinipiga sana lakini baada ya yeye kuchoka aliamua kutoka nje, nilijifanya nimezimia na alipokuja alinipiga makofi lakini nilijikaza na kujifanya nimelegea.
“Itakuwa maumivu yanamfanya mishipa ya fahamu inaleta shida, mchome sindano ya diclofenac kisha leta ile drip ya glucose umpe, tunaondoka hapa baada ya lisaa limoja, ila wewe utatangulia Villa Bridge na Hasheem, mkifika pale mtakaa upande wa juu wa daraja lile mkiwa na silaha, eneo lile halina watu wanaopitapita, mtakapo muona Dany basi hapohapo ua mwingine yeyote utakayemuona, hakikisha kama mkimuona Patrick basi asitoke kwenye mdomo wa bunduki akiwa hai. Hakuna kuacha alama, tutafanya kama tulivyofanya ya Urusi, tupo watatu tu, ni wewe Hasheem na mimi, yeyote mwingine atakayekuja atakufa, hata huu mzoga tutaua pale ambapo Dany atakuwa upande wetu.”alimwambia yule jamaa wakati huo mimi nilikuwa bado nilikuwa nimejifanya kama nimezimia. Akachukua simu yangu na nikamsikia akitafuta namba kisha alipiga akaweka sauti kubwa ili yule jamaa na yeye asikie.
“Khajat uko wapi muda wote huo?” sauti ya Patrick ilisikika, nikatamani sana kuzungumza na kumuambia asiongee lakini hiyo haikuwezekana kwakuwa ingeharibu kila kitu.
“Ni Mary hapa, sikiliza Patrick najua unapafahamu Villa Bridge, nikukute pale ukiwa na Dany baada ya lisaa limoja, kinyume na hapo huyu Malaya wako atakufa kwakuwa hata hivyo amebakiza muda mchache sana kabla hajafa. Nimesema baada ya lisaa na ninaanza kuhesabu sasa hivi, ukichelewa dakika moja tu utakuta kichwa chake pale.” Alimaliza kuongea na kukata simu kabla hata Patrick hajaongea chochote kisha akamwambia yule jamaa anifungue na kunipeleka nje, alinifungua na kunitoa ile drip, kisha alinibeba na Mary alibeba bastola yake akawa akimfata yule jamaa aliyenibeba, nilijilegeza kabisa kama vile nimezimia kweli, kwakuwa Mary aliponiteka pale ofisini aliondoka na gari langu basi alilitumia hilohilo kwenda Villa Bridge, akamwambia yule jamaa aniweke kwenye buti ya gari kisha niliwekwa mule na yeye alikuwa nje nikawa nasikia akiongea na yule jamaa.
“Mna uhakika huyu mwanamke yuko peke yake?” alimuuliza yule jamaa.
“Ndio bosi, hakuna mtu mwingine anayeshirikiana naye.” Alijibu na hapo nikawa pia nimegundua kuwa kumbe alituma watu kunipeleleza ambao hata hivyo hawakuambulia kujua mengi zaidi.
“Sawa ila mkifika pale kuweni makini, kuna kona mbili katika lile daraja, juu kule kwenye mona ya kwanza ukikaa unaona mashariki mwa barabara, na kona ya pili unaona pia magharibi kwa ile barabara, ukikaa kona hii hapa na unaweza kuwa na uwezo wa kulenga mita mia tano, hivyo kwa bastola hizi hamuwezi kufikisha kwenye usawa huo iwapo mtu atatokea kuwa usawa huo, sasa mtatumia KNT-308 sniper riffle ambayo inaweza kulenga mita 800, itakuwa na risasi tatu tu, hatuendi kuvamia, tunaenda kubadilishana mzigo ila tukiwa na lengo la kuchukua mizigo yote na kusafisha. Hivyo risasi chache zikitumika itasaidia zaidi, kwenye risasi tatu unatakiwa utumie moja ikiwezekana kwakuwa Patrick ni mtu laini sana, siwapi risasi nyingi ili kuzuia isijekuwa kama ya Urusi. Mkiacha mtu akakimbia basi mmoja kati yenu lazima afe, tangulia mkiwa kwenye nafasi zenu mniambie nikakuwa kilomita moja karibu.” Walimaliza kuongea na hapo sikuelewa nifanye nini, nilisikia Mary akiondoka upende waliokuwepo na kuja nyuma ya gari, nikajiweka sawa na alipokuja alikuta bado nimezimia, akanishika shingoni kisha akafunga buti na kuingia kwenye gari na kuliwasha. Kule kwenye buti kulikuwa na kofia yangu ya pikipiki na hapo niliivaa kabisa tayari kwa lolote, gari ilikuwa ikikimbia kwa spidi kama 130 hivi, nikawa nahesabu kwa kukadiria kilomita, ilipofika sehemu nikafungua mlango wa buti wa chini kisha nikajitupa na huku Mary akiendelea na safari, hakuweza kuniona kwakuwa alikuwa kwenye kasi na mimi nilichokifanya nikukimbilia sehemu kuliko kuwa na simu za barabarani, nikampigia simu Felly;
“Felly mko wapi?” nilimuuliza Felly aliyeonekana kama amechanganyikiwa hivi.
“Oooh Khajat, mzima.” Alinisemesha na kuonekana kama alisimamisha gari.
“Niko sawa, msiende tena nimefanikiwa kutoroka ila nataka uje haraka barabara ya Capricon sasa hivi ili tuwahi mbele ya Mary tuangalie cha kufanya, uko na nani?” nilimuuliza wakati huo roho ya hasira imenijaa na nilikuwa natamani kuona damu ya mtu ikimwagika.
“Niko na Dany kwenye gari na niko mita mia 5 kutoka hapo ulipo.” Nilitazama kwa mbali na kweli niliona gari kwa mbali sana ikiwa imepaki, baada ya muda kidogo walikuja pale na nilimkaba Dany na kuzuia hewa isipite kooni ili apoteze fahamu kisha nilimfunga mikono na miguu na kumuingiza kwenye buti.
“Nipe funguo Felly.” Nilimuomba Felly funguo kwakuwa niliona kama atanichelewesha na yeye wala hakubisha alinipatia funguo, muda huo kidole kilikuwa kimeanza kuuma sana kwakuwa nilikitonesha pale nilipojitupa na maeneo mengine ya mwili pia yalikuwa yakiniuma lakini kwa hasira niliyokuwa nayo niliyapuuzia.
“Tunapita porini ndio kuna njia ya mkato, tukifika mita mia 5 tutaweka gari kichakani na hapo itabidi tuende kwa mguu na kwakukimbia, utakwenda kona ya mashariki na mimi nitakwenda kona ya magharibi kule juu ya daraja, kila upande una kijana mmoja kwenye Rifle hivyo unatakiwa uwe makini sana, ukimshtua na akifyatua risasi tutakuwa tumeharibu, hatuendi na bastola, utatumia kisu tu au mkono.” Nilimaliza kutoa maelezo na Felly alikuwa tayari ameshanielewa, nilivuta mafuta na kupangua gia, tulipiga msituni na vichaka vyote tulivilaza chini, kwa mwendo ule ikatuchukua dakika 25 kuliona daraja kwa mbali, hakukuwa na dalili yoyote ya gari kwa mbali na nilipochukua darubini na kutazama juu ya daraja niliweza kuhakikisha kuwa wapo watu wawili, walikuwa wamevaa kama wanajeshi na mmoja alikuwa mashariki na mwingine magharibi, nilimpa Felly na yeye aliwaangalia kisha tulianza kukimbia kuelekea kwenye daraja. Daraja hili ni daraja la treni juu na chini lilikuwa linapitisha magari, ila mara nyingi hakukuwa na magari yakipita wala treni kwakuwa ile barabara ilikuwa imehamishwa kwa wakati huo. Tulifika mpaka karibu na daraja na kuamua kuanza kutambaa na tumbo na Felly alikuwa upande wa pili akifanya hivyo. Nilifanikiwa kufika nyuma kabisa ya yule jamaa wa kwanza ambaye ndiye alinibeba kuniingiza kwenye gari.
“Hey.” Nilimshtua na aliposhtuka na kugeuka alikutana na kisu kilichopita kwenye koo lake. Nilimuona Felly akimvizia yule jamaa, na yeye alimshika bega na alipogeuka alikutana na ngumi iliyonifanya nicheke japo nilikuwa na maumivu, ilikuwa ngumi nzuri iliyotua kwenye pua na kumfanya adondoke kama mzigo. Hapohapo na simu ya yule mmoja ilianza kuita.
“Hallo, niambieni kama kuko sawa ili nije.” Aliongea Mary.
“Mary, this is just the beginning, I will catch you and kill you ASAP, your men are down, get prepared sweatheart.”(Mary huu ni mwanzo tu, nitakukamata na nitakuua muda si mrefu, vijana wako wamekufa, jitayarishe mpenzi) Nilimwambia na kukata simu.
“Nitakupenda siku zote. Pale nywele zangu nyeusi zitakapokuwa nyeupe bado nitakupenda. Pale ngozi yako laini ya usichana itakapokaliwa na ngozi iliyojikunja ya uzee bado nitahitaji kukushika. Pale sura yako itakapokuwa na makunyanzi unapotabasamu bado nitakupenda, pale ambapo kila chozi ulilolitoa litakuwa limeacha alama kwenye sura yako mimi nitabaki kukupenda. Nitakuthamini daima, yote ni kwakuwa nilikuwa na wewe wakati wote ukipitia hayo. Nitashiriki maisha yako, nitashiriki machozi yako, na nitakupenda mpaka pale pumzi itakapochoka kuishi ndani yako au ndani yangu. Nilikupenda kabla na nitakupenda baada. Pale utakapoamua kwenda na kusema mimi sio faraja yako nitakuwa tayari kukuangalia ukiondoka kwakuwa nia yangu ni wewe uwe na furaha hata bila mimi. Kila mtu anahitaji faraja na upendo, niko tayari kukupenda kama nijipendavyo. Siku zote, miaka yote NITAKUPENDA, na hiyo ni kwakuwa tu KUKUPENDA WEWE NI AMANI YA MOYO WANGU.” HII NI SEHEMU YA KUMI NA SITA
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**KHAJAT**
Nilikuwa nina hasira sana na Mary kwakuw alinikata kidole. Toka nimeteswa nikiwa India hakuna mwanamke amewahi kunitesa au kunipiga au hata kunidharau, Mary alikuwa ndiye msichana wa kwanza kunidharau na kunimudu kwa muda mfupi. Japo sikukaa naye pale ndani kwa muda mrefu lakini nilikuwa nimegundua kabisa kuwa Mary sio mtu wa kawaida. Ni mwanamke ambaye atakuwa na historia ndefu sana ambayo nilitamani sana kuijua. Alikuwa ni mwanamke ambaye anaonekana kabisa kuwa hababaishwi wala haogopeshwi na kitu lakini pia hakatishwi tamaa. Mary sio mtu wa kupaniki, sio mtu wa hasira kama mimi, ilikuwa ngumu sana kujua kama amekasirika au la kwakuwa alitoa tabasamu muda wote.
******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment