Sehemu Ya Pili (2)
MIAKA ISHRINI NA TANO BADAE
Mauji ya kutisha tena ya aina moja yalikuwa yakizidi kushika kasi siku hadi siku katika vitongoji vya mitaa ya isevya,.watu wengi hususani wazee walikuwa wakipoteza maisha yao katika mtindo wa aina moja.walichinjwa vichwa kwa kutenganishwa na kiwiliwili,. Hali ya sinto fahamu ilikugubika mji wa tabora,.mauji yale yalikuwa ni gumzo nchi nzima,.hakuna aliye jua anaye fanya mauwaji yale ni nani,.kila siku ziendazo kwa mungu aliokotwa mwili wa mtu ukiwa hauna kichwa,.cha kushangaza zaidi muuaji aliondoka na kichwa na kuacha mwili,. Hali ilikuwa tete, lakini hakuna aliye jua kama Raymond Fambo ndiye muhusika wa ule uhalifu,. Hofu kubwa ilitawala mji wa tabora,.homa ya matukio ya mauwaji ilivyozidi kuwa kubwa ndivyo takwimu za mauaji zilivyozidi kuongezeka siku hadi siku,. Afisa wa polisi mkoa wa tabora hakupata usingizi hata tone,alikuwa na kazi kubwa kuhakikisha anatoa msukumo wa ziada kwa watendaji wake wa chini kuhakikisha muuaji anakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria,. lakini wapi. Hakuna aliyejua sababu za matukio yale ni nini, kila mtu alisema lake,.hisia za watu wengi ziliwapeleka katika imani za kishirikina,.pamoja na hisia hizo kwa mamia ya wananchi bado lawama nyingi zilielekezwa kwa jeshi la polisi kwa kushindwa kuzuia matukio yale,. Ndani ya jeshi la polisi hali ilikuwa tete mabosi hawakukaa maofisini mwao kimuhemuhe cha kumsaka muawaji kilipamba moto kila kukicha,. Raymond Fambo,aliendelea kufanya mauaji kwa wazee kwa siri kubwa, hakuna watu aliowachukia mkoani tabora kama rika hilo la wazee,.ilikuwa ni kisasi,tena kisasi alicho jiapiza muda mrefu kukifanya,.kisasi dhidi ya mauaji ya mama yake mpendwa aliye uawawa kwa mapanga kwa imani za kishirikina wakati akiwa angali mtoto,.aliamini wazee aliowaua ndio kizazi kilicho husika na mauwaji ya mama yake,.shida na mateso aliyoyapata utotoni mwake aliapa kuteketeza vijana hao wa zamani mpaka pale ubongo wake utakapo sema basi!. Kwa zaidi ya wiki tatu bado hakukamatwa wala kuhisiwa mtu hata mmoja dhidi ya matukio yale yaliyo kuwa yanendelea,. Jijini Dar es salama,wizara ya mambo ya ndani Ispekta jeneral wa polisi{I.G.P} Ernest Kamkuru azidi kuchanganyikwa pale taarifa za matukio ya mauwaji zilivyo zidi kushika kasi pasi na taarifa yeyote ya kukamatwa kwa muuwaji wa vifo vile, Siku hii akiwa katika ofisi yake nadhifu,macho yamemwiva,huku mishipa ya kichwa ikiwa imemsimamaa mwili wake ulikuwa umefura kwa hasira za nyati, pamoja na uwepo wa feni iliyokuwa ikizunguka kwa kasi lakini bado jasho jingi lilimtoka mwilini mwake. Kila baada ya dakika mbili alinyanyua mkono wake wa kushoto na kuitazama saa yake ya mkononi na kadiri muda ulivyo zidi kuyoyoma ndivyo hasira yake ilivyo zidi kuongezeka mara dufu, Alinyanyua mkonga wa simu ya mezani na kupiga namba Fulani kisha akaiweka simu sikioni, Simu iliita upande wa pili kwa sekunde chache kisha ikapokelewa kwa nidhamu na sauti nyembamba ya kike,. “koplo anna kutok….” “KEEP QUIAT MWANAMKE!.” Ispekta Ernest alimkatisha kwa sauti ya ukali yenye mikwaruzo mizito kooni kama kwamba alikuwa anakohozi katika koo lake “hao watu nilio waita wako wapi mpaka dakika hii.?” alisema Ernest kwa ukali. “Samahani afande taarifa zilizopo ni kwamba afande kilanga yupo njiani anakuja akitokea gongo la mboto, lakini kwa bahati mbaya barabarani kuna foleni ndefu hali inayo pelekea kuto wasiri kwa wakati hadi dakika hii, ila afande Babra yeye kisha wasiri ndio kwanza kapandisha ngazi kuja ofisini kwako muda mfupi uliopita”. alijibu yule dada kupitia simu,. Dakika hiyohiyo Kabla Ispekta Ernest hajatia neno mlango wa ofisi yake ulisukumwa na ispekta Babra akatokeza. alikuwa ni mwanamke mrefu mweusi mwenye matiti makubwa na mwili wenye nguvu zile za kiafrika,alisimama kikakamavu na kusaluti huku akiwa anatiririkwa jasho mwili mzima, I.G.P Ernest alimtizama kwa ghadhabu kuu zaidi kisha akasema, “Hivi ninyi mnadhani mimi ni mjomba wenu!. Yanii mimi nawaita,mpaka mjishaue shaue ‘ndo’ mje siyo? Haya, hilo jenzako liko wapi?” Alisema ispekta Ernest,lakini kabla hata Babra hajajibu mlango wa ofisi ile ulisukumwa taratibu na mara Kilanga akatokeza, “Heee! hivi ninyi ni majini watu!., I.G.P alizidi kuhamanika kwa hasira, “mara gongo la mboto, mara katika foleni mara,..ninyi vipi? mmenizoea kiasi cha kuniona mimi mjomba wenu siyo?,. Alibwata kwa sauti ya ukali kwelikweli, Si kilanga wala Babra aliye mjibu, I.G.P aliwatizama kwa zamu wale askari wake huku akihema kwa kasi na kufanya kifua chake kipande na kushuka wakati akivuta pumzi na kuzitoa nje.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Abubakar Kiranga” I.G.P aliita kwa sauti yenye kiburi huku akiwa kisha hamisha macho yake kwa wale askari wake alio waamini, sasa alikuwa akitizama pembeni midomo yake ikiwa imenuna kama kwamba amenyweshwa mkojo wa mlevi, “Ndiyo afande” aljibu Kilanga kwa heshima na sauti ya kikakamavu, “Babra frances” “Ndiyo afande” “Nawatuma tabora mkaniletee muuwaji wa vikongwe” Alisema I.G.P kisha akatulia macho yake madogo yakiwa yanatizama pembeni. Kilanga na Babra wakatazamana kwa mshangao huku kilanga akimeza funda la mate, ubaridi Fulani ukapenya katika maungo yake. Msinitumbulie macho ninyi viumbe.! Kati yenu hakuna asiye jua juu ya matukio ya mauwaji ya kuchinjwa shingo dhidi ya wazee yanayo endelea kule tabora!. Alisema kwa sauti ya ukali huku akihamisha macho yake kwa kasi na kuwatizama askari wale wawili, Nimekwisha ongea na kamanda wa polisi mkoa wa tabora juu ya ujio wenu na nimemweleza file lote la mauwaji ya vikongwe kuanzia kesho litakuwa chini yenu,namaanisha kesho asubuhi sitaki kusikia harufu yenu hapa jijini,alisema tena kibabe huku akiwa kawatumbulia macho yake makali, “Kuna swali” aliuliza baada ya kuzungumza, “Kwanini umetuteuwa sisi na siyo c.i.d wengine afande” Babra aliuliza swali la kipuuzi!. Come on askari!! Wewe ulitaka nimteuwe nani? Nimekuteuweni kwakuwa nimejisikia kukuteuwa,shenzi taipu,sifa tu!. miaka yote hujui kama ninyi ndio chaguo langu nambari moja katika kazi nyeti kama hizi. Alisema I.G.P huku macho yake madogo yakitoka katika hali ya ukali na kuwa katika mshangao. Ukimya wa nukta kadhaa ulichukua nafasi kabla ya I.G.P kuwaruhusu kwa mara nyingine kuondoka. Babra na Kilanga waliondoka katika ofisi ya I.G.P wakiwa na mori kubwa ya kazi kutokana na sababu mbili ama tatu,kwanza ni kule kuaminika mbele ya bosi wao ambae ndiye mkuu wa jeshi la polisi nchini pili ni kule wao kuonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutatua kesi ambazo mara nyingi huwa ngumu na kuwashinda askari wengi, sasa leo jukumu lililokuwa mbele yao ni kumtafuta muuwaji wa mauwaji ya vikongwe yanayo endelea kule tabora, Katu hakuna mtu kati yao aliyejua kama ile kesi ingepelekea kuharibu kabisa muelekeo wa maisha yao kwa miaka mingi!. ********************************************
Wakati tume ya kipelelezi ikiundwa kibabe jijini dar es salam,.upande wa pili mkoani tabora Raymond Fambo alikuwa akijianda chumbani kwake kwa ajili ya kutoka, Kiharisia ilikuwa ni mvao wa mtoko wa kazi,.kazi maalum yenye kuupoza hasira yake na donge lake la moyo.,kazi aliyo ifanya pasina shaka kuwa ni kisasi cha mauwaji ya mama yake,. Basi Alivaa jinsi yake ya blue, shati la langi jekundu lililo mkaa vema,kofia kubwa ya pama na groves za mikono., Alijitazama mala mbili katika kioo cha kabati leke la nguo,.alipo lidhika na muonekano wake aliinama chini ya uvungu wa kitanda na kutoa viatu vukubwa buti za rangi ya kaki kisha akatia miguu yake ndani ya viatu,. naaaam!. hapo muenekano wake wa kazi ukawa umekamilika,. Alitoka chumbani kwake na kuingia katika moja ya chumba alicho kifanya kama stoo katika nyumba yake..ilikuwa ni stoo isiyo kua na vitu vingi ndani zaidi ya jokofu kubwa na godoro jipya la tanform,. Raymond alichukua kisu kikubwa chenye makali ya uhakika kilicho kuwa juu ya jokofu ile na kukichomeka katika ala yake kisha akakipachika kiunoni kisha taratibu pasina haraka taratibu akauendea mlango,. “kumekucha muda wa kazi” alijisemea moyoni akifungua malango na kutoka nje,. Alitembea kwa mguu kutokea mtaa ule wa nyumbani kwake mpaka stendi ya mabasi ya mkoani,hapo madereva baiskeli walikuwa wengi, kimwenekano alikuwa ni mtu aliyehitaji usafiri,. wale madereva wakamzonga,. “kweli nahitaji usafiri lakini siyo wa baiskeli,mimi si wakupanda baiskeli” alisema Raymond huku akiwasha sigara yake kwa kibiriti cha gesi na kuvuta kwa mkupuo na kutoa moshi mwingi puani na mdomoni mwake,. Wale madereva waliondoka wakinung’unika moyoni kwa kukosa rizki kwa kukataliwa na mtu yule mwenye muonekano wa majivuno sijui kwa umaridadi aliokuwa nao ama ni nini!!. Dakika kumi na mbili badae alikuja dereva pikipiki iliyo kuwa inaendeshwa na kijana mrefu mweupe akiwa amevaa suruali ya jinsi na tshert nyeusi na shuka jekundu la kimasai, “oyaaa twendzaoo” alisema yule dereva aliyeitwa Richard,. Raymond alipanda kisha safari ikaanza,. Walipita katika shule ya sekondari ya uyui na kukatisha kushoto wakashika njia ndogo ya vumbi wakazidi kuvuta mafuta,. “vipi kwa hapa” Rchard aliuliza,.baada ya kwenda mwendo wa kilomita takribani mbili na nusu,. “Hapa hapa panatosha” Alijibu Raymond,. Usikawie basi sisi unajua washenzi hawa sasa hivi wameweka ulinzi kila kona”alisema Richard; Sikawii mzee mwenyewe,. huyu wa leo mrembo sana” alijibu Raymond huku akitelemka katika pikipiki na kutembea kwa mguu umbali wa nusu kilomita,. ilionekana safari yake imefika mwisho mbele ya nyumba ndogo ya udongo na makuti,wakati huo ilikuwa ni saa mbili na dakika mbili usiku,.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment