Simulizi : Kimbia, Kimbia! [Run Nigger, Run!]
Sehemu Ya Pili (2)
“Hadi hapo naona mtafaruku uliendelea kuwepo pamoja na kunieleza Henry alikuwa na tabia ya kuja hapa mara kwa mara na akionyesha mambo yalikuwa ni shwari.” Hughes alisema kwa namna kama alitoa maoni.
Sasa walikuwa barazani, kwani lile kabati la pili lilikwishakaguliwa na hakukuwa na chochote cha maana walichoona zaidi ya kuona nguo za kiume ambazo walihisi zilikuwa za yule mtu aliyekutwa barazani.
“Sidhani kama mtafaruku ulikuwepo kwa hawa watu, kwani kama ungekuwepo basi huyu Henry asingekuwa na uhusiano mwema na huyu jamaa, au…aah, Afande unaonaje hili?”
“Utajuaje? Vipi kama alikuwa na hasira za ndani ambazo zilikuwa hazijafikia muda wa kuripuka? Yawezekana haya ni matokeo ya mripuko! Nasema tu, kwani kitabia binadamu ni mgumu sana kumuelewa hupatikanaje afikishwapo katika mazingira fulani yasiyo ya kawaida.”
“Hapo sina la kuchangia.”
“Ahsante kwa ushirikiano,” Hughes alisema. Aliendelea tena, “kabla ya kuagana ningeomba unielekeze nyumbani kwa baba mwenye nyumba.”
Baada ya kuelekezwa kwa baba mwenye nyumba ambaye kwa bahati mbaya alikuwa amesafiri kikazi mikoani, Inspekta alichukua vijana wapatao sita hivi ili kuongozana hadi nyumba aliyokuwa akiishi huyo Henry kwa kufuatisha maelezo waliyopata kutoka kwa mama mmoja aliyekuwa mpangaji katika nyumba hiyo ya baba mwenye nyumba; na pia alimuagiza Afande Kanyengele afuatilie kituo cha taxi alichokuwa akifanyia mtuhumiwa Obrien ili kupata habari zaidi ikiwa ni pamoja na kujitahidi kuweza kupafahamu nyumbani kwake.
Walikubaliana wakutane ofisini kwa Hughes majira ya jioni ili kujua kila mtu alipata habari gani zaidi.
***
Wawili hao walikutana jioni hiyo kama walivyokubaliana, lakini Kanyengele ndiye alimkuta Hughes akimsubiri.
“Umefikia wapi?” Hughes aliuliza huku akiikodolea bahasha iliyokuwa imeshikiliwa mkononi na Kanyengele.
“Nimeweza kupajua anapoishi.”
“Hivyo mlifika?” Hughes aliuliza tena.
Kanyengele alisema baada ya kutulia kwa sekunde chache, “afande inaonyesha ulikuwepo uhusiano wa karibu sana kati ya huyu dereva pamoja na Marehemu!”
“Endelea.”
“Kuna picha ambazo wamepiga pamoja katika mikao inayoonyesha licha ya kuwa marehemu alikuwa ni mteja wake wa kudumu, pia zaidi hawa walikuwa!”
“Na kingine tulichoona. Ile nyumba wanauza pombe haramu…na hiki kinanifanya tena nione ipo haja ya kufikiri zaidi kwani sidhani mtu wa aina ya marehemu hangeweza kuwa mfikaji hapo nyumbani kwa Obrien!”
“Kwanini unadhani asiweze?”
“Kwanza huwezi kufika kwa usafiri wa aina yoyote…the guy lives in slams and the lady doesn’t resemble going those places! (jamaa anaishi sehemu zisizopimwa wakati marehemu hafanani na kuwa mfikaji wa huko!)”
“Hivyo unataka kusemaje?”
“Nina imani hatupo mbali sana na jibu sahihi, lakini hadi hapa naona bado tumefungwa tusifike…ninahisi tu, au pengine nitahisi vingine nikijua wewe unazo taarifa zipi zingine.” Kanyengele alijibu huku akimpatia Hughes bahasha.
Hughes aliipokea bahasha.
“Bosi, ulimpata Henry?”
Ukimya uliotokea kwa sekunde kadhaa uliondolewa na Hughes kwa kurejesha tena mazungumzo huku akiendelea kuzitazama picha, kwani tayari alikwishafungua ile bahasha aliyopewa na Kanyengele, “uhusiano unaosema hapa wala siuoni…huyu akiwa mteja wake wa kudumu si vibaya kupiga picha za mikao ya namna hii.”
“Kulingana na taarifa tulizopokea mtaani na zile za kazini kwake, bado nitashangazwa sana endapo tutabaini marehemu alikuwa akifika kwa Obrien!” Kanyengele alikoleza hoja zake.
“Sioni kushangazwa huku ni habari sana, kwanza kuzikuta picha huko si sababu tosha marehemu alikuwa akifika huko…what if they used to meet somewhere else for their love making you’re pondering over? (vipi kama walikuwa wakikutana kwingine kufanya mapenzi yao?)” Hughes alisema huku mkono wake wa kulia ukichezea shavu lake la kulia huku macho yake yakikodolea picha moja ambapo marehemu Brigitte alikuwa kapiga picha akiwa kamkalia mapajani Obrien huku kavalia kisketi kifupi sana kiasi mapaja yake makubwa yalijianika wazi.
Hughes alijisemea moyoni, ‘kilikuwa kiumbe ambacho hata mimi ningetamani nishiriki ukandamizaji! Duh, mapaja kama mama mkwe…uuh!’
“Hujanielewa.” Kanyengele alisema tena huku akichekacheka. Tayari mawazoni alimsoma bosi wake kutokana na jinsi alivyokuwa akizikodolea picha za marehemu kwa namna za ulaghai huku akishuhudia pia macho yake yakilegea zaidi akimiminwa uroho fulani!
Hughes aliinua kichwa na kumtazama Kanyengele kwa sekunde mbili tatu hivi kwa macho yaleyale malegevu, na kisha aliendelea kuziangalia picha zile.
Macho yake yalikuwa ulafi mtupu!
“Sitashangazwa tukijua marehemu hakuwahi kufika kwa Obrien hata kama tukibaini walikuwa pia ni wapenzi. Hapa najaribu kuona kama kunaweza kuwa na uhusiano ambao utaweza kuhusishwa na mauaji haya! Pengine Obrien ahusiki?”
“Hizi picha…ebu tuwaachie wataalamu wazipitie.” Hughes alisema kama vile hakutilia maanani maoni ya Kanyengele ingawaje moyoni yalikusanywa kama taarifa muhimu.
“Kumbe ni vipi?” Kanyengele aliuliza kishauku.
“Tuache hili kwanza,” Hughes alinyamaza kidogo kabla ya kuendelea tena kwa mwendo wa kubadilisha somo, “unajua hatukuweza kumpata Henry!”
“Hakupatikana?”
“Habari ni kuwa, eti aliondoka nyumbani kwake asubuhi sana, na wala hakuaga yeyote!”
“Mmh, afande…hapa!” Kanyengele alisema, na safari hii mshangao wake ulifanywa kwa kukepuakepua macho.
“Hatahivyo, tuliisachi nyumba…nimechukua baadhi ya picha zake na kuzisambaza ili kazi ya kumsaka ianzwe.” Aliendelea kusema Hughes baada ya kunyamaza kwa sekunde tano hivi, “pia ofisi imeletewa taarifa kuhusu ugomvi fulani ambao ulifanyika usiku wa kuamkia leo huko sinza katika baa ya de-paradise.”
Kanyengele alitulia kimya akisikiliza kwa makini huku mikono yake ikishikashika kama ilivyokuwa desturi yake kufanya hivyo kila anapohisi kupatiwa habari mpya.
“Inadaiwa ugomvi ulitokana na mtu mmoja aliyemvamia marehemu na wenzake waliokuwa wakistarehe katika baa hiyo.”
“Mizunguko yenye miamba mingi imeanza…hii kesi itakuwa miongoni mwa kesi nzito sana, maana hapa unasema umepata taarifa za kutokea ugomvi unaomuhusisha marehemu!” Kanyengele alisema kimshangao tena huku bado akiichezea mikono.
“Hatahivyo, mtoa taarifa aligoma kutoa address yake kwa kudai kuhofia usalama.”
“Usalama wake? Kesi hii…mmh, kazi ipo!” Kama kawaida yake, Kanyengele alisema kimshangao.
Hughes aliacha kuziangalia picha zile; na kwa muda alimkazia macho Kanyengele kabla ya kuanika nje tabasamu lake huku macho yake yakilegea.
“Mmh?”
“Napenda shangaa zako, kwani huwa ndio mwanzo wako katika kuweza kuchapakazi kisawasawa. Ndio napenda sana kufanyakazi na wewe nikijua vitendawili vingi wavifungua. I like your style, make it up!”
Kanyengele hakujibu zaidi ya uso wake kufunguka tabasamu pana kiasi hadi meno yake meupe mithili ya sufi iliyosafishwa yaliachwa kuonekana kitambo.
***
MOJA YA VIVUTIO vya de-paradise ilikuwa ni upigaji wa nyimbo zilizopata kuvuma zamani kuanzia za kiafrika hadi zile za kizungu zikichanganywa kwa ustadi mzuri sana kiasi cha kufanya wateja wengi kufurahishwa zaidi. Kwa ujumla wengi walivutwa na ubora wa huduma; na kama zilitokea dosari, basi hizo zilikuwa mara chache sana huku jitihada za wazi zikifanywa katika kuhakikisha makosa hayarudiwi.
John Hughes na Kanyengele walifika baa hiyo kunako majira ya saa nne usiku ikiwa ni agenda yao katika kuweza kupata taarifa zaidi kuhusiana na ugomvi uliotokea usiku wa jana.
Watu hawakuwa wengi.
Hughes alitegemea hili kutokana na siku hiyo (jumatatu) kuwa ya kazi.
Muziki tulivu, ukipigwa si kwa sauti ya juu ulikoga nyoyo za idadi kubwa ya waliofika hapo.
“Habari yako. Sijui nikuhudumie nini tafadhali?” Hughes alisemeshwa na muhudumu aliyemfuata mezani ambako alikuwa ameketi peke yake, kwani walikubaliana na Kanyengele waketi tofauti huku kila mmoja akijaribu kufanya upepelezi kivyake.
Hughes alimtazama muhudumu huyo kuanzia chini akipanda juu hadi alipoliacha tazamo usoni pake.
Aliushika mkono mmoja wa muhudumu ambaye hakufanya matata yoyote katika kumgomea, “una sauti nzuri. Nimeipenda sana.”
“Nashukuru.” Muhudumu alijibu huku akikwepesha macho yake baada ya kuushuhudia utazamaji wa Hughes.
Ili aweze kutoa huduma, muhudumu alirudia swali.
“Nilikuja kunywa, lakini naona huduma nyingine unaweza pia kuifanya kama utajali.” Hughes alinyamaza kidogo kabla ya kuendelea tena, “niletee kili baridi.”
“Naomba pesa.”
Hughes aliacha kuushika ule mkono, kisha aliitoa pochi katika mfuko wa kulia wa suruali yake na ndipo alichomoa noti ya alfu kumi na kumpatia huku akisema, “hivi unalala hapahapa baa?”
“Kwanini unaniuliza?”
“Samahani…anyway, kaniletee bia.”
Muhudumu alitoa mguno wa kicheko huku akianza kuondoka.
“Kazi na ukandamizaji.”
Hughes alimtazama kwa nyuma huku akikubali hakuwa miongoni mwa ‘mali’ zilizomtia kiwewe; lakini kwakuwa alikuwa kazini, basi aliona ulikuwepo umuhimu wa ‘kumbamiza’ endapo ingebidi ili kuweza kulainisha kazi zake.
Ndani ya dakika moja tangu mhudumu kuondoka, alijikuta akishangazwa baada ya kushtukia akisimamiwa na mtu mmoja aliyeonekana alikuwa ni miongoni mwa mfanyakazi wa baa hiyo.
Mtu huyo aliyebeba kikapu kidogo alimuuliza John Hughes iwapo ni yeye ndiye aliyeagizia bia aina ya Kilimanjaro.
Badala ya kujibu, Hughes aliuliza huku akimtazama kwa macho yenye ishara za kudadisi kwa kufichaficha, “where is the lady I sent for?”
“Samahani bro, ni wewe uliagiza?” Mtu yule alikazia swali lake la awali badala ya kujibu swali la Hughes.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni baridi?” Hughes alijibu kwa kuuliza huku akijiuliza moyoni kwanini yule dada hakurudi; na pia alijiuliza ni kwanini huyo mtu alionekana kukwepa kujibu swali lake.
“Pia nimeleta chenji yako.” Mtu yule alisema huku akiiweka bia mezani.
Mara, Hughes aliinuka kwa ghafla mithili jambo fulani lisilopendeza lilimchota…
John Hughes alifanya kuinuka mithili ya mtu asiyependezwa na jambo fulani…ulikuwa mkwara!
Lakini mtu yule hakushtuka; macho yake yalizalisha utalii wa kumtazama machoni huku akiumauma midomo!
Chupa ya pombe ilikuwa tayari mezani na glasi yake.
“Niliyemtuma ndiye ahudumie!” Hughes alisema kwa kuzianika wazi hasira zake ambazo kwa ndani haikuwa sahihi kwamba hivyo zilijitokeza.
“Dada amepata udhuru. Ameitwa na bwana wake.”
“Si yupo kazini lakini?”
“Bwana wake ni mteja wa kudumu, hatuwezi kumkataza kuwa naye…samahani mzee!”
Hughes alirudi kuketi.
“Karibu mzee.” Yule mtu alitoa opener na kuanza kuifungua pombe huku akisema zaidi, “jisikie upo kwako.”
“Ningejisikia nipo kwangu kama ungeniitia dada! Nimempenda na yeye anajua…usimzibie riziki!”
Mtu yule alitoa chenji, na kisha aliondoka bila kujibu.
Hughes aliitoa simu yake na kumtumia meseji Kanyengele ambapo aliandika maandishi haya, “how do u make outta der? Dem watchas! (mambo yaendaje hapo? Wanatutazama tayari!)”
Huges alipomaliza bia yake, yule muhudumu wa kiume alikuja tena mezani na kuuliza iwapo alihitaji kuongezewa pombe nyingine.
“Keti kwanza.” Hughes alisema kwa kujiamini.
Yule mtu hakupinga; aliketi.
“Kwanini hupendi nipate raha katika baa yenu?” Hughes aliuliza huku akimtupia mtu yule tazamo kwamba hakuwa akifanya masihara.
“Raha ya mteja ni kipimo cha huduma zetu. Biashara zetu ni kwakuwa tunakuwepo pale mteja apatapo raha!”
“Sasa, mimi namtaka yule demu…niletee hiyo raha!”
“Umejibiwa mteja! Huyo ni mali ya mteja mwingine!”
“Nihitaji nipewe mwingine?”
“Samahani, mteja.” Yule mtu alijibu huku akianza kusimama, “huduma zetu ni vinywaji na vitafunwa; mengine, hapa si mahala.”
“Ebu keti.” Hughes alibadilisha sauti yake na kuwa yenye kufanya maombi, “Kitu kingine nahitaji ambacho wewe ndiye unihudumie kwasababu ni wajibu ufanye.”
Mtu yule aliketi tena bila kusema lolote.
“Sijui cheo chako, lakini nimejua wewe ni sehemu ya wafanyakazi wa hii baa ambao mpo makini.” Hughes alisema tena kwa sauti yenye kila dalili za amri.
“Kwahiyo?” Yule mtu aliuliza bila kuonyesha mshangao.
“Nakubali unaweza kuwa hunijui, lakini ninaamini unaifahamu kazi yangu na ndio maana umemuondosha yule dada asinihudumie.”
“Nakusikiliza.”
“Let’s hit the target.” Hughes alianza kusema tena kwa sauti ya upole, “hapa ulitokea ugomvi jana usiku.”
“Ugomvi? Hapa? Mmh, wewe nani kwanza?” Mtu yule alionyesha kushangazwa kidogo ingawaje baadaye alitulia na kurejea katika kawaida yake.
Hughes alitoa kitambulisho, “mimi ni polisi.”
Mtu yule hakujibu wala hakushtuka; alitabasamu.
“Nipo kazini na unapaswa kunieleza. Jana kulitokea ugomvi gani hapa?”
“Skliza askari,” Yule mtu alisema kwa ukali kidogo huku akitumbua hata macho yake, “hii ni baa ambapo ugomvi si jambo la ajabu sana kutokea! Siwezi kukumbuka kuna ugomvi gani ulitokea, kwani ni ugomvi mkubwa ndio uongozi hujulishwa na hasa pale tunapokuwa tumepata hasara!”
“Ugomvi ulikuwa mmoja tu jana, tena mkubwa. Huwezi kusema hukumbuki.”
Mtu huyo alieleza kimkato kwamba hakuwahi kupata taarifa za kutokea ugomvi hapo jana usiku ingawaje alikiri kutokuwepo nyakati fulani.
“Didn’t see quarrels nor hear it…nothing yo!” Mtu yule alijibu kwa kujirejesha katika hali za utulivu.
“Ndio maana nilihitaji kuhojiana na yule muhudumu ambaye najua ni mfanyakazi wa kawaida ambaye anaweza kuwa alikuwepo hiyo jana usiku wakati wote…but for sure, I like that lady with her breathtaking voice a woman needs in bed.”
Yule mtu alicheka!
Hughes akashangaa!
“Nimeelewa! Dada alidai unamtongoza na yeye hapatikani huko. Hiyo ndiyo sababu ya kuomba asikuhudumie! This is highly regarded bar!” Mtu yule alisema huku akisimama, “sorry, I’m too wrapped up! Ukinihitaji fika kesho saa za kawaida, utanikuta.”
Hughes hakutaka kusema; isipokuwa alimtazama mtu huyo aliyeanza kuondoka taratibu kwa mwendo wa maringo wa kutojali.
Tazama zake zilikuja kukatishwa na sauti ya dada mmoja aliyetokeza mezani kwake kwa namna ileile ya ghafla kama alivyotokea huyo mtu.
“Mzee unahitaji kinywaji gani?”
Hughes alimtazama kwanza dada huyu ambaye hakika alikubali alivutia kiasi chake hasa pale alipotuma macho yake katika miguu yake.
“Those TBL!”
“Nini?”
“Umejaliwa mama!”
“Mmh?” Bado dada huyo aliuliza kwa hali ya mshangao kidogo, kwani dhahiri hakuelewa nini Hughes alimaanisha.
“Miguu mama! Ya bia mamah…ooh, Gosh…had ‘em babe!”
Ndipo mshangao ulimtoka dada huyo na kumfanya kuguna kidogo kabla ya kuchanua tabasamu huku akimtupia Hughes swali katika kujifanya hakujali aliyoambiwa, “Kinywaji gani babah?”
“Sihitaji.” Hughes alijibu akichekacheka huku bado ukodozi wake ukifinyanga mtazamo ashki.
Dada huyo alipotaka kuondoka, Hughes alimzuia kwa kumshika mkono huku akisema, “haraka ya nini mrembo? Mimi ni mteja wako wakati wote.”
Dada huyo hakugoma kushikwa; na hata pale mkono wake ulipokuwa ukikandwakandwa, pia hakugoma zaidi ya kutazama pembeni huku akimimina nje tabasamu lililopendezeshwa kwa legevu za macho.
Naam, macho legevu yalikutana!
Na kila mmoja alijua kuyachezea!
“Hivi itawezekana nikihitaji uwepo hapa ili unipatie huduma hadi jogoo awike? Ndio, unavyotazama napenda. Unavyotabasamu, napenda zaidi. Napenda hili joto linalofukuta katika mkono wako.” Hughes aliwahi kusema maneno mengi kabla ya kujibiwa.
“Nipo kazini,” Dada huyo alianza kusema huku bado kakwepesha tazamo zake, “sidhani kama itawezekana kwasababu nipo kwa ajili ya wateja wote. Halafu…umesema hauhitaji huduma!” Dada huyo alisema kwa sauti tulivu, na kisha alivuta mkono wake katika harakati za kuhitaji kuachiwa.
Hatahivyo, hakutumia nguvu kuutoa mkono huo; lakini hali hiyo ilifanya Hughes aupeleke mkono wake mwingine kusaidia ubinyaji huku akijaribu kumlegeza kwa maneno, “Dada! Sauti yako, mwili wako na sasa hili joto ndivyo vinafanya nihitaji!”
“Baba wewe, mbona una mambo?”
Hughes alicheka!
Dada huyo akajikuta pia akicheka ingawaje yeye alifanya kwa chati huku ule mkono wake ambao haukushikwa ukipelekwa kuuziba mdomo wake!
Eti dada alificha asionekane alicheka!
Dada alifurahishwa huku akijua kuvutika taratibu; akivutika, ndivyo yeye pia akijua aliwinda…
“Skliza bibie…Je, yawezekana nikalipia wewe kuketi na mimi ili tunywe na kuburudika kwa raha zetu? Nafikiri inawezekana, ebu fanya hili. Wee mkubwa unajua!”
‘Hii inaweza kuwa bingo…lakini, mwee…kazi naipenda!’ Dada huyo aliwaza kwa muda; kisha ndipo alianza kujibu kwa mwendo wa kujiumauma huku akihakikisha sauti yake imechongwa kuendelea ‘kuvuta’ kama ni kweli ilichangia kumtetemesha mtu na ubaba wake, “ni…” alianza kusema, “hapana…unajua utaratibu ni…mmh, lakini…eeh, si unajua…?”
Hughes alimkatisha huku akiacha kumshika mkono wake na huku pia akiitoa pochi yake mfukoni, “kabla hujasema, ebu niletee kili baridi. Na wewe nunua ili nifurahi kuona koo lako linavyozungumza linapoingiza khabari!”
“Ahm…?”
“Kwanza hujanieleza unaitwa nani. Nitafurahi mdomo wangu ukuite jina lako kabla hujaenda kuniletea kinywaji.” Hughes alikatiza tena huku akitoa noti ya alfu tano na kumpatia.
“Sema Sozy inatosha.” Dada alijibu huku akipiga hatua taratibu.
“Jina zuri kulitamkia kitandani.”
Suzan alipiga hatua mbili tatu hivi, kisha alisimama na kugeuka kumtazama Hughes kwa sekunde chache kabla ya kugeuka tena na kuanza kuondoka huku akiamini alisindikizwa na macho-uchu; na kwakweli, alifurahia sana kusindikizwa hivi, kwani ndivyo huko nyuma alihakikisha ‘yalitetemeshwa kimtindo’!
Hatahivyo, kufurahia huko hakukumtoa asitambue haikuwa sahihi kulegeza ‘dhibiti zake’ kwasababu hapo bosi wake ndiye aliagiza akatoe huduma baada ya kuelezwa alimchoropoa muhudumu mwenzake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipofika kaunta, mara alishtukia akigongwa begani; akageuza shingo bila kuusumbua mwili…
“Sozy. Anasemaje mteja?”
Alikuwa ni meneja wake.
“Aah, anavijimambo sana!” Suzan alianza kusema huku sasa akigeuka mzimamzima, “eti anaomba alipie huduma ya kuketi na mimi hadi majogoo…Bosi unasemaje?”
“Unamjua?”
“Kwani vipi bosi? Si mteja tu!”
“Yule ni nyoka!”
Suzan alishtuka na kusema, “ati?”
“Usihofu, anataka kujua habari za ugomvi wa jana…akikuuliza mueleze ugomvi uliletwa na wateja ambao hatuwafahamu na hatuhitaji kuwajua.”
“Bosi, kwanini usiseme naye? Mimi si msemaji wajua, sheria za kazi nazijua!”
“Usijali. Fanya nisemavyo. Ni sheria nikiagiza. Ninakuamini ndio maana nilikuchagua. Pia, nimekupa likizo, nenda kamnywe hata ukipenda kalale naye…but tomorrow, kazi kama kawa.”
Tabasamu likamkunjuka Suzan; na ndivyo punde kidogo, huko mawazoni mwake aliuona uso wa Hughes wenye macho yaliyokuwa yakitazama kimahaba, yakimtazama huku kama vile yakisema yalimuita!
Hayo macho kama vile halikadhalika yalitabanaisha kwamba hata kitandani yalimuita kwa raha zao!
John Hughes alijua meneja wa baa ndiye alimleta Suzan baada ya kuamini angeweza kuhojiana naye kiaina bila kuhatarisha mambo ambayo alihisi hakutakiwa kufikishwa kuyajua; na ndivyo, aliruhusu kwanza akaletewe kinywaji huku akifahamu meneja wake angemuulizia hukohuko na kumuagiza nini cha kufanya baadaye.
Susan aliporudi Hughes hakushangaa kuona mfuko wa kubebea vinywaji ukiwa na chupa mbili za bia na glasi mbili, isipokuwa ndivyo alisema kwa kukunjuka tabasamu pana zaidi, “nadhani hata kibali umepata, au?”
“Mteja usikonde, nipo ili jogoo atakapowika tutakuwa tumejifungia wapi na nini tukitenda…ndio, jogoo akiwika na wewe nijue uwikavyo!” Suzan alisema huku akizifungua bia zote baada ya kuziweka mezani; na alipomaliza kummiminia glasi ya pombe ndipo alisema tena, “niruhusu nirudishe kikapu.”
Badala ya kujibu, Hughes alitania kabla ya kuachia pumzi za kinamna ambazo Suzan alizisikia, “mwili watetemeka!”
Susan alilembua tena macho huku akinyanyuka, kisha alimtazama kidogo Hughes kabla ya kukwepa kumtazama kwa namna alitambawa na aibu wa mahaba.
Bado, Hughes alihema akiilembesha sanaa ya mvuto!
Taratibu, Susan akaanza kuondoka, akisema, “ukitetemeka, tetemesha!”
“Sisimsha bibie!”
Akiwa bado karibu, Susan alisimama; lakini bila kugeuka alijibu, “wasisimsha!” Kisha aliendelea kuondoka huku akijua ‘kutetemesha’ kiasi alifuatisha vyema mapigo ya mziki uliokuwa ukipigwa kwa sauti ya chini kiasi.
‘Mmh! Huu ni usanii katika sanaa!’ Hughes alijisemea huku sasa akisisimshwa kikwelikweli.
***
Mwangaza wa jua uliendelea kumpiga Deborah Evans hapo kitandani alipokuwa amelala kiasi cha kuzalisha sumbufu fulani ambazo zilifanya aanze kujigeuzageuza. Pia, sauti ya luninga ilichangia kumsumbua kwa jinsi ilivyomtikisa masikioni.
Wakati uchovu ukikazana kutawala mwili wake, ndivyo sumbufu hizo zilisababisha mwili kujituma kuamka; na ndivyo macho yake makubwa yalianza kuamka kivivuvivu kabla ya hatimaye kuweza kujilazimisha kuketi kitandani.
Ndivyo wakati akiketi kitandani, shuka aliyojifunika iliporomoka hadi mapajani mwake na kumuacha mtupu maeneo yote ya juu kiasi nywele zake zikijilaza ovyo mabegani kwani zilikuwa nyingi sana.
Mwili bado ulichoka.
Akikapua macho, alitazama dirishani ambapo pazia jepesi liliweza kumjulisha alichelewa kuamka, kwani tayari kulipambazuka. Mara kidogo, alibadilisha tazamo hilo na kuligandisha juu ya kikabati cha kitanda.
Alijitikisa kichwa kujaribu kufukuza kizunguzungu kilichokuwa bado kikimchafua. Baadaye kidogo, alisogeza mkono wake wa kushoto na kuishika simu yake ya mkononi ambayo haikuwa imezimwa. Akaibeba.
“Mmh! Ni kweli, nimechelewa!” Alisema mara baada ya simu kumthibitishia, ndipo kisha hata aliachia miayo huku mkono wake mmoja ukijipeleka karibu na mdomo kufanya kama vile ulikuwa ukitaka kuuziba.
Siku hiyo ilikuwa Jumanne saa 4.00.
Baada ya kuketi kitandani kwa takriban dakika mbili hivi, ndipo Deborah alijitoa ndani ya shuka kwa kuivuta pembeni kidogo.
Na ndivyo, mtupu kamili alibakizwa!
Macho mawili tu yakijua!
Macho yake mwenyewe yakijua!
Ndiyo alijitazama akibinyabinya matiti yake yaliyokuwa makubwa kiasi kabla ya kuiteremsha miguu yake ili kukanyaga sakafuni. Kisha, taratibu alianza kuongoza njia kuelekea bafuni.
Huko hakukaa sana kama ilivyo desturi yake; kwani alijifanyia usafi kwa mwendo wa haraka na kisha kurejea chumbani na kuketi kitandani. Bado alidharau kuiangalia runinga ijapokuwa masikio hayakuzuiwa kusikiliza.
Huku akikunjuka tabasamu, aliusogeza mto wake pembeni…pochi ndogo ikaonekana!
Tabasamu likaongezeka!
Akafurahi!
Taratibu mkono wake wa kulia ulijisogeza na kuishika pochi ile.
Aliifungua…
Kasi ya furaha ikaongezeka!
Mkono ukapelekwa; na huo ulichoropoa kimzigo fulani…burungutu!
Fedha!
Pumzi zilimbana kwa sekunde huku moyo ukisisimshwa sana…akazibusu!
Akizidi kufurahi!
Akifurahi alipata!
Akifurahi alibahatika!
Naam, alifurahi sana!
Alifurahi huku moyo wake ukiizungumza furaha yake kwamba asingethubutu kumkataa ‘buzi’ aliyempatia burungutu hilo hata kama kwa kufanya hivyo ingekuwa ni kuhatarisha uhusiano wake na mchumba wake!
Kwa mara ya kwanza naye alijiwa na mawazo ya kusaliti penzi lake kwa George Bofy, mwanaume aliyekiri alimpenda kwa dhati akiahidi hata wakati mmoja hasingethubutu kumsaliti!
Sasa alifanya!
Sasa alisaliti!
Ndivyo hata alijikuta akisema kwa sauti huku raha ikizidi kumtambaa mwilini, “ooh George! Please, nisamehe mpenzi kwani hii ni adimu nisiyokubali niiachie kwasababu tu nakupenda!”
Wakati akisema maneno hayo, ndivyo pia mawazo yake yalisukumwa katika kukumbuka maneno aliyoelezwa na ‘buzi’ hilo. Maneno hayo yalijirudiarudia katika kupeleka jitihada za kumtawala asirejeshwe nyuma kutomsaliti mpenzi wake ambaye ni hakika alimpenda.
Buzi lake lilipata kumueleza haya: kwamba, kila binadamu ni fursa kwa ajili ya mwingine kwakuwa ni binadamu ndiye mjengaji wa fursa na wala si Mungu kama wengi wanavyofikiria!
‘I’m your opportunity, don’t stand loosing! (mimi ni fursa yako, usiipoteze!)’ Aliikumbuka kauli hii ya buzi hilo.
Furaha aliyokuwa nayo ilifanya hata ajikute akijiangalia kwa muda kwa mwendo wa kuutalii mwili wake; na hasa alitazama kiuno chake chembamba kilichobebwa na matako makubwa kiasi.
“Mimi ni fursa yako vilevile, ndio ni sehemu ya raha zako…usiichezee ukaikosa! Wapo wanaitamani, wasiipate!” Alisema kwa kujiamini huku akiinuka na kuanza kutembea mithili alikuwa katika mashindano ya kuonyesha uzuri wa umbo lake.
Alijivuta hadi mlangoni, na kisha aligeuka kwa madaha na kurejea tena kitandani huku akichekacheka kwasababu mawazo yake yalimpatia msukumo sahihi kwamba ni hakika yeye pia ni miongoni wa wanawake wenye kuvutia sana kiasi cha kuweza kuwa fursa tamu mbele ya mwanaume yoyote aliyebahatika kupewa nafasi ya kuutalii na kuufaidi vilivyo mwili wake.
“Mwanaume yoyote hapa kafika!” Alijisifia kwa sauti huku akizikumbuka tazama za kilafi za dereva wake ambaye alijua alikuwa akimtamani isipokuwa alikuwa akiogopa ‘kuzoza’ ili asimwage unga.
‘Ningekuwa mchunaji, hakika ningeweza hasa!’ Alijisemea tena huku bado akichezea mwili wake ambao hapo uliibuka kuwashwa, ukitetemeka kuhitaji.
Simu ya mkononi ilipolia, aliitazama bila kuijibu wala kuisogelea kujua ilitoka kwa nani; bado rabsha za kuuchezea mwili hazikusimamishwa ijapokuwa hakufanya kwa sana, kwani hapo mikono yake ilikuwa ikichezea matiti yake huku akijisemea, ‘utapwita baba!’
Simu ililia tena!
Baada ya sekunde kadhaa ndipo aliibeba na kuitazama…
Alikuwa dereva wake.
Kabla ya kuipokea simu, hisia zake ziliacha alama huenda kaka yake hakurudisha gari kama ilivyotakiwa.
“Ni aje Thalmus? Mambo?”
“Pole dada!” Sauti ya dereva ilisema.
“Wanipa pole? Ya nini? Wewe…?” Aliuliza huku akikunja uso kidogo huku mshangao ukianza kumvamia.
“Samahani.” Thalmus alimkatiza, “samahani dada. Nimegutushwa sana na habari nilizosoma katika gazeti la leo…yaani, siamini kwamba inawezekana hujui bado!”
“Habari gani? Au gari langu…?”
“Ni kuhusu kaka yako.” Sauti ya Thalmus ilimkatisha taratibu. “Pole!”
Deborah alikapua macho bila kusema chochote. Huku mawazo yakianza kusafiri huku na huko.
“Kaka yako yu mahututi hospitali!”
“Wasema?” Deborah alisema kwa sauti ya juu kiasi alitoka kitandani na kusimama tuli huku akihemahema.
Lile burungutu la fedha likaanguka chini; wala hakujali kuliokota…na wala hakuangaika kulitazama!
“Mkewe amechinjwa! Kaka ni mahututi sana, alipigwa risasi tatu! Moja imetoboa mashavu yote!”
Ukimya ukatanda zaidi ya dakika huku sauti ya kwiki ikisikika kuanza kuchukua nafasi pana katika kuvuma…
“Dada?” Sauti ya Thalmus iliita ukimya ulivyozidi kusonga sana.
“Nipitie mara moja!”
“Sina usafiri. Labda tukutane…?”
“Huna usafiri kivipi? Gari si…?” Deborah alimkatisha usemi kabla ya kujikuta yeye pia akikatizwa.
“Sijaletewa gari kama ulivyonijulisha katika simu.”
***
Hisia zilimueleza Deborah kugeuka nyuma, lakini si kwamba hivyo zilieleza kwa kumjengea tafsiri kwamba huko nyuma yake kulikuwa na ishara zisizopendeza!
Huo haukuwa mwendo!
Bali, isipokuwa hizo zilimvuta kama jambo la kawaida tu kwa mtu kuamua kufanya hivyo!
Lakini pengine ‘chale zake’ zilisema!
Hapo alikuwa tayari akiwa ametoka nyumbani kwake na akizidi kuzivuta hatua kuelekea kituo cha taxi ambacho hakikuwa mbali sana na kwake.
Mawazoni mwake bado kulijawa wasiwasi kuhusu hali ya ndugu yake Marlon huku akihisi pengine matatizo yao ya kimapenzi ndio yalipeleka hali hiyo kwamba mwenzake aliuawa na yeye kujeruhiwa vibaya.
‘Who did it?’ Alijiuliza huku akigeuza kichwa chake ili kuangalia huko nyuma.
Wakati akikirejesha kichwa chake kutazama mbele ndipo tazamo lake katika kuangazaangaza lilijikuta likisimamisha zoezi lake la kujigeuza!
Macho yaliona!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na ndivyo, mzimamzima, akageuka!
Upande wa kushoto wa barabara ya Idrissa ya kutokea kituoni, pale mbele ya nyumba yake aliona gari moja dogo.
Gari hilo lilikuwa limesimama hapo.
Mtu mmoja mrefu na mwembamba, aliyevalia shati jeupe na suruali nyeusi alitoka ndani ya gari hilo huku kichwa chake kikionekana kupepesapepesa.
Kwa harakaharaka, Deborah alianza kuzipiga hatua kurudi nyumbani kwake huku akijaribu kujiuliza iwapo alilijua gari lile au aliwahi kuliona mahala popote. Hatahivyo, hakujiuliza kwamba alihofu.
Hakuwa na hofu; na ndivyo hakujua kama ilitakiwa kuwepo basi ni wapi ingetokea.
Ndio, yote ni kwakuwa alijiamini aliishi safi, akiishi bila kujenga uadui na mtu.
Hivyo ndivyo hata mwili wake ulizidisha kasi ya kutembea kwake ili kuweza kumuwahi mtu huyo ambaye alijenga tafsiri angekuwa ni mgeni wake; lakini hatahivyo, bado sehemu kubwa ya mawazo yake ilijazwa na ule wasiwasi wa uzima wa nduguye Marlon Evans.
Mtu yule aligeuka aliposikia sauti kali huko mbele yake; pia aliacha kufungua mlango wa dereva. Hapo alikuwa katika utayari wa kuondoka baada ya kuhakikisha hakukuwa na mtu katika nyumba ya Deborah.
“Kaka! Kaka!” Deborah alipiga kelele zaidi huku sasa akizidisha zaidi haraka ya mwendo wake.
Mtu yule alipomuona Deborah alitabasamu, akasimama hapohapo katika mlango wa gari lake huku akisema moyoni, ‘atakuwa ndiye.’
Deborah alipomfikia alitoa salamu kwanza huku akihemahema kutokana na mwendo aliofanya.
“Samahani kwa kukusumbua, hatahivyo nashukuru wewe ni mtu mwenye kujali.” Mtu yule ambaye alikuwa ndiye afande Kanyengele alisema kwa sauti tulivu.
Bado walisimama hapo nje.
“Nilipotazama nyuma niliona gari hili, ndipo nikahisi ni ugeni wangu pengine…ok. Karibu ndani.” Deborah alisema huku akianza kutoka kuelekea katika mlango wa nyumba.
“Usijali. Nisicheleweshe shughuli zako, tutaongea hapahapa.”
“Si vizuri mgeni kumfikishia nje.”
“Dada usijali.”
Deborah aliitikia kwa kichwa, na kisha alisogea hapo katika gari.
“Samahani…naona unalia hivi! Una matatizo?” Kanyengele aliuliza kidadisi.
“Ni kweli…we acha tu!”
“Ni nini?”
“Ni mambo ya kifamilia…enhe, hivi mwenzangu ni nani?”
“Wewe ndiye Deborah Evans?”
“Hujanijibu.” Deborah alikaza macho kuashiria alihitaji kujibiwa kwanza.
“Mimi ni askari, Juma Kanyengele.”
Wasiwasi ukampata Deborah, lakini haukuwa kwamba ulimpata kwakuwa kule kuelezwa mtu huyo alikuwa ni askari; bali aliingizwa kupata wasiwasi akihisi hapo aliletewa taarifa mbaya zaidi kuhusu kaka yake!
“Enhe…nashukuru.” Deborah alichelewa kujibu, na alijibu huku hali za wasiwasi zikijichora usoni mwake.
Kanyengele alisoma hili, lakini hakuonyesha kujali.
“Wewe ndiye Deborah Evans?”
Deborah aliitika kwa kichwa huku mdomo wake ukipelekwa chini kidogo kusaidia ukubali wake ni yeye alikuwa.
“Kwanza pole na yaliyompata kaka.”
“Bado sijajua hali yake, kwani ni hii asubuhi ndio nilipata taarifa.” Deborah alisema kwa majonzi.
“Asubuhi hii ndio umejua?” Kanyengele aliuliza kimshangao kama ilivyo desturi zake aanzapo kuhisi kitu.
“Dereva wa gari langu alinijulisha…na hapa nakwenda kumuona hospitali…ooh, my bro! What got him?”
Afande Kanyengele alifikiri kidogo na kisha ndipo aliomba ampatie lift hadi hospitali wakati akiendelea kumhoji ndani ya gari.
Deborah alikubali.
Hivyo, walipanda gari.
Kanyengele alimjulisha Deborah hali yote ilivyokwenda kuhusu walivyowakuta Marlon na marehemu Brigitte asubuhi ile ya jumatatu.
“Hapa nimetoka kituo cha kuegesha magari huko kimanga-mawenzi.” Alisema zaidi Kanyengele, na sasa waliingia barabara ya morogoro kwani walipitia njia ya kutokezea barabara ya morocco.
Deborah aliendelea kusikiliza; na tayari machozi yalikuwa yakimtoka, kwani sasa alidhihirisha ni hakika ndugu yake alipigwa risasi na akiwa mahututi sana hospitalini.
“Tulipokea taarifa kaka yako alikuwa na gari lako jumapili. Ni kweli?”
Deborah aliitika kwa kichwa kabla ya kujibu kwa mdomo, “Alipita hapa jumapili majira ya saa moja hivi. Akaniomba gari, nikampatia kwa makubaliano jumatatu awahi alfajiri kumpatia dereva wangu ili asimcheleweshe kufanya kazi zake.”
“Unaye dereva kumbe?”
“Gari yangu ni taxi.”
Kanyengele alikohoa kidogo, akapunguza mwendo kiasi na kisha alianza kusema tena, “gari imekutwa na alama za damu kwenye kiti cha dereva.”
Deborah alishtuka!
“Pia mlinzi wa kituo cha kuegesha magari anasema alimuona Marlon akiwa amelowa damu katika shati lake, na akielekea kuwa mtu mwenye wasiwasi uliochanganyika na hasira.” Kanyengele aliendelea tena kwa kugeuza kichwa chake kumtazama Deborah huku akimtupia swali, “dada huna habari yoyote pengine kaka yako alikuwa na ugomvi na mtu hivi?”
“Hapana…sijui!”
Kanyengele alitaka kugusia habari za De-paradise, lakini aliamua kutogusa hadi kama Deborah angeashiria kujua kama sio kuzisema kabisa. Hivyo aliuliza tena, “Marlon aliomba gari kwa ajili gani? Hakusema sababu?”
“Hakusema sababu zaidi ya kuniomba kwa kusisitizia.”
“Hivi hujui lolote kuhusu alikuwa na mtafaruku na marehemu Brigitte?”
Huku akizidi kutoa machozi, Deborah alijibu, “Afande naomba niache kwanza…nina machungu sana!”
Kanyengele alinyamaza.
Dakika zilipita kama tatu hivi, na tayari walikuwa wakipinda kona ya kuiingia barabara ya united nation. Hapo Kanyengele aliufukuza ukimya kwa kusema kimsisitizo, “skiliza. Jikaze tuhojiane, kwani kuzidi kuchelewa kupata taarifa ndio fursa nzuri sana ya muuaji kumrahisishia asiweze kujulikana.”
“Aliyetenda haya, alipanga kuwaua wote. Ndio, hata kaka yako ilikuwa auawe! Ni bahati ya mtende kwamba hadi sasa anapumua…please, give us support!” Alisisitizia tena Kanyengele.
Deborah hakusema!
“Haya…nipatie unachojua kuhusu mtafaruku wa kaka yako na marehemu. Najua unajua!”
Taratibu, mwishowe Deborah alifungua kinywa chake akijibu kwa kuonyesha masikitiko makubwa, “Brigitte alimmaliza kaka.”
Kanyengele hakumuelewa Deborah.
Ndivyo alimuuliza kwa kukurupuka, “Unasema alimmaliza?”
“Ndio.”
“Bado sikuelewi.”
“Baada ya kaka kupata matatizo ya kiuchumi, ndipo Brigitte alianza visa huku akimtaka asiwe akilala kwake kwa kutumbukiza madai nduguze walimchukia!”
“Mmh…mbona kaka yako bado aliishi na marehemu hukohuko tabata?”
“Si kweli afande. Kaka aliacha kuishi kwa Brigitte kama miezi sita hivi iliyopita ingawaje bado wakati kadhaa alikuwa akilala huko. Nakuambia hadi napata taarifa asubuhi hii, bado najua walikuwa ni wapenzi ingawaje najua pia walikuwa hawaishi kukwaruzana mara kibao!”
Huku akihakikisha sauti yake ilitoka kwa taratibu na bila kuashiria alizalisha alama za kutokubaliana na maelezo ya Deborah, Kanyengele alieleza bado hakuuona utofauti wa Marlon kulala kwa marehemu na utofauti wa kuishi naye pamoja. Ndio, kichwani kwake, alisimamisha ukubali kwamba hadi walipokumbwa na balaa hilo lililopelekea kuchinjwa kwa Brigitte wawili hao walijulikana waliishi pamoja kama wapenzi wa kudumu.
“Ok…ebu…ooh, kwani kaka anaishi wapi hivi sasa?” Kanyengele alimalizia kueleza kwa kutumbukiza swali.
“Kaka anaishi nyumbani, upanga.” Deborah aliendelea kujibu, “Lakini kwakuwa ni kweli anampenda sana Brigitte, tena kwa muda wa miaka mingi sana, basi ndivyo kaka hujikuta akijirudisha na kulala huko kwa siku kadhaa kabla ya kukosana tena!”
“I, see.”
“Brigitte hajui kupenda zaidi ya kupenda uchumi wa mwanaume mwenye kujua kujiruhusu kutoboka vyema!”
Kanyengele aliamsha mazungumzo tena, lakini safari hii hata sauti yake ilizungumza mshangao aliokuwanao “hivi…inavyoo…aah, tuseme muuaji alikuwa na chuki kubwa dhidi ya wote wawili…yaani, kama vile kaka yako na marehemu hawakuwa na mtafaruku! Don’t you see this?”
“Hapana…I won’t swallow it! Mtafaruku ulikuwepo, kwasababu mimi binafsi nimeshiriki mara kadhaa kuwapatanisha! Despute was there!”
“Really?”
“Absolutely yes! Ila nina wasiwasi na mzazi mwenziwe…siamini kama ni mtu mwema kiasi hicho! Nahisi tu…lakini, jaribuni kumtazama huyu jamaa! Naona hasira mbaya sana zipo ndani mwake.”
Kanyengele hakujibu.
Deborah aliendelea kusema zaidi, “Familia ilijaribu mara nyingi kumuonya kaka kuhusu huyu jamaa…haiwezekani asifanye chochote kibaya huku ukimtazama unaziona ishara ni kichaa aliyempenda Brigitte…sometimes, I accept a woman is not only a fun to play with, but also a dangerous animal could turn out to one’s dismay! (wakati mwingine, mwanamke si wakuchezea kwani anaweza kuwa hatari bila kutarajia!)”
Kanyengele aliuliza akitaka kujua ni jamaa gani Deborah alijaribu kumuhusisha na skendo hili.
“Si Henry! Bado hamjamjua?”
“Hajulikani alipo!” Kanyengele alijibu huku akihisi kuvutwa kiasi na mitazamo ya Deborah.
“Tujue…ndio, jana alikuwa wapi. Ndio, kwanini haonekani?” Deborah alisema kimsisitizo, “I bet, he’s the one…his eyes warned it all!”
Kanyengele hakujibu.
“Unajua mtu aliyeumizwa sana huku akijazwa hofu huweza hatimaye kuwa na hasira kubwa kabla ya chuki mbaya sana kumchota! Na chuki hiyo inaweza kumtupa mtu huyo katika kutenda jambo baya sana ilimradi hasira ijimalize! This man…hapana!”
***
Siku tano tangu kuripotiwa mauaji ya Brigitte, ndipo Henry Kipekecho alikamatwa akitokea shinyanga alikodai alikwenda kufanyiwa usaili wa kazi katika kiwanda kimoja.
“Unaweza kuthibitisha ulikwenda kufanya interview?” Hughes alimuhoji Henry wakiwa chumba cha mahojiano.
“Take it, nitafuatilia yote. Na nikijua unasema uongo, hakika nitakuumiza huku kupona kwako kukiwa ni matokeo ya kufanikiwa kuibashiri namba yangu ya kazi! Unasikia? Be afraid to drag me going rough!” Hughes aliweka ‘mkwara’ huku akiizunguka meza taratibu bila kumtazama Henry aliyekuwa kanyon’gonyea kwa hofu.
Wakati Henry akiitikia kwa kuchangia kutingisha kichwa chake, Hughes hakuonyesha kujali kujibiwa huko zaidi ya kuacha kuzunguka na kusogea mezani katika kiti chake ambapo aliichukua simu yake ya mkononi.
Alimtupia tazamo fupi Henry kabla ya kuketi huku akiunganisha simu hiyo na waya wa ‘headphone’ uliokuwepo mezani hapo; na baada ya kuuweka masikioni ndipo alianza kubonyeza namba kadhaa huku akimtupia swali bila kumtazama, “wajua upo hapa kwanini?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Henry hakujibu, lakini tayari alitetemeka kwa hofu.
“Nakuuliza!” Hughes alimuuliza tena kwa sauti baada ya kusimama na kuanza kumfuata huko upande wa pili wa meza alipokuwa ameketishwa.
Alipomfikia, alimuinamia na kumtingisha kichwa kwa nguvu kudhihirisha hali za shari ziliingizwa.
“Eeh? Nasema na wewe!”
“Hapana afande!” Henry alijibu kwa uoga; isitoshe, machozi yalianza kumlengalenga!
Hughes alimuachia na kisha akarudi katika kiti chake, akaketi na kutulia mithili hakuwa yule aliyekuja mbogo.
Mara simu yake ilisema!
“Nataka kujua kama tayari mmepatiwa majibu…aah, unasema jina lake…eeh? Aah…that’s is to say alikwenda?....ok, ok!” Inspekta aliiondoa ile headphone masikioni; na vyote, pamoja na simu akaviweka mezani.
“Ukweli wako ndio utakaokusaidia. Ukidanganya, hakika mabaya zaidi yatakupata.” Hughes alisema huku akimtazama Henry akionyesha alama za utiifu kwa kuinamisha kichwa chini.
“Ok. Tuchukulie ni kweli hujui kwanini ulikamatwa. Mimi nitakuambia, lakini nitafanya kwa njia ya kukuuliza.” Aliendelea kusema, “nieleze, unajua lipi kuhusu mkeo?”
“Sina mke.” Henry alijibu kinyonge.
“Kabisa unasema hivyo!”
“Nilikuwa naye, lakini tuliachana.”
“Who?” Hughes aliuliza kwa kutoa sauti kubwa kidogo, lakini bado alama za upole ziliendelea kujichora usoni.
“Mmh…Brigitte.”
“Ok! Ok!” Hughes alisema kwa kutabasamu huku akinyanyuka tena na kuanza kutembea tembea.
“Nakuuliza tena. Nini unaelewa kuhusu Brigitte?”
“Siamini nilichoelezwa.”
“Huamini? Nani aliyekueleza hicho usichoamini?”
“Afande roho inaniuma sana kama ni kweli ndivyo hivyo nilivyoelezwa na askari walionikamata kituoni nikiwasili jijini hapa!” Henry alisema na hata sura yake ilidhihirisha alikuwa ndani ya majonzi licha pia alionyesha vilevile alichotwa ndani ya hofu zake!
Hughes alirudi tena kuketi.
“Ni kwamba, Brigitte amekutwa amechinjwa kinyama huko nyumbani kwake jumatatu ya terehe 21. Hiyo ni siku wewe ulisafiri…or you went there to firm your strong alibi! (Au ulikwenda huko ili kutengeneza ushahidi uhusiki!)”
“Sasa nieleze. Jumapili ya tarehe 20 mwezi huu hukufika nyumbani kwa marehemu?” Hughes alihoji.
“Nilikwenda.”
“Ulikwenda au ulifika?”
“Nilifika afande.”
“Saa ngapi?” Hughes aliuliza tena kwa kumkazia macho yake ambayo hatahivyo yalishindwa yasilembue.
“Majira ya jioni.”
“Ulimkuta nani?”
Henry alinyamaza kidogo kabla ya kuanza kujibu. Naam, mawazoni aliwaza habari fulani.
kabla ya kuanza kujibu. Naam, mawazoni aliwaza habari fulani.
“Nilimkuta Brigitte peke yake. Mumewe alikuja baadaye.”
“Mumewe?” Hughes aliuliza kwa kujenga usoni alama kubwa za kwamba ni kweli aliingia kushangaa; lakini, hatahivyo, kabla ya Henry kuanza kumjibu aliongeza swali, “nani huyo?”
“Marlon Evans.”
Hughes alitingisha kichwa kabla ya kumtupia swali jingine, “Je, ni kweli mlitoka pamoja?”
“Tulimuacha Marlon.”
“Fafanua.” Hughes alisema tena.
Henry alifafanua usemi wake kwa kueleza marehemu alitaka kumpatia lifti kwakuwa gari ilikuwa ije kumfuata nyakati hizohizo alizokuwa akiaga.
“Mimi nilipewa lifti hadi kituo cha mwenge.” Henry aliweka msisitizo kukazia maelezo yake.
“Unaweza kuitambua hiyo taxi?”
“Naweza kujaribu.”
Hughes alimtazama kabla ya kumtupia swali jingine, “na dereva wake unaweza kumtambua?”
“Naweza.”
Hughes alitabasamu, akavuta faili lake na kuandika; na baada ya hapo, alianza kuhoji zaidi, “ebu nieleze habari yote ilivyokuwa.”
Henry hakueleza kila kitu, na hivyo alifanya kwa kuhofu pengine angejikuta akituhumiwa ni mshiriki. Ndio, hivyo alifikiri kutokana na ukweli kumganda kwamba kama asingempelekea Marlon ‘habari zile’, basi bila shaka hadi leo hii Brigitte angekuwa yu hai!
Ubaini huu ulimuuma sana!
Ulimtisha sana!
Hivyo, alieleza ‘habari’ hadi kufikia aliposhushwa mwenge akidai ndipo alipanda ‘daladala’ na kurejea nyumbani; pia alizificha zile habari zilizosababisha asononeshwe vile kiasi cha kuamua kurudi kwa Marlon!
“Marehemu alikuwa anakwenda wapi? Hakuwahi kukueleza hili?”
Akifikirifikiri, Henry alijibu, “nakumbuka Brigitte alisema walikuwa wanakwenda baa ya De-paradise. Mimi siijui hiyo baa.”
“Mbona unajibu kwa kufikirifikiri?” Hughes alimtupia swali hili kwa kumkazia macho kama vile alihisi alilambishwa uongo kwa baadhi ya maelezo. Kiasi kidogo sana cha ulembuzi wa macho yake kilisimama kuonyesha nguvu zake licha ya kufukuzwa sana; isipokuwa ile mistari michache iliyojichora pajini kwake ilinena wazi yeye hapo hakupatikana kwa masihara.
“Unajua,” Henry alijitetea, “najaribu kukumbuka mazungumzo yake na dereva…sikuwa sehemu ya mazungumzo yao kwa nafasi pana niweze kusema wote watatu tulikuwa ndani ya mazungumzo ya pamoja.”
“Ok. Alikwenda kuonana na nani?” Hughes aliuliza tena huku akibadilisha utazamaji wake na kuufanya katika namna za kawaida katika kutazama.
“Alimfuata mpenzi wake mwingine…inaelekea dereva wake atakuwa anajua mengi. Nadhani wanajuana sana!”
“Hukusikia jina la huyo mpenzi likitajwa?” Hughes aliuliza tena baada ya kutulia kimya kwa sekunde kadhaa.
“Ni Edwin!”
“Ok! Ok!”
“Tushirikiane, nitakusaidia uondoke ndani ya balaa hili endapo nitathibitisha uhusiki.” Hughes alizungumza kwa upole na hata tazama zake zilikubali kwamba sasa alimuonea huruma kwasababu kwa kiasi kikubwa alijikuta akiingizwa kumuamini.
“Marlon alimfuata Brigitte kule baa...na sijui alizipata wapi habari kwamba mpenzi wake alikuwa huko pamoja na huyo awara yake.” Hughes alijulisha kwa sauti ya utulivu.
“Nilim…atch? I see!” Henry alijikuta akiropoka ingawaje aliweza kusitisha alichotaka kuzungumza baada ya kukumbuka kumbe habari zingine alikubali asizieleze.
Hughes alishtushwa na mkurupuko huo wa ghafla wa Henry, lakini hakuuonyesha bayana; na ndivyo alitulia kwa nusu dakika hivi akiruhusu mawazo yake kujadili maelezo aliyopewa kwa harakaharaka ili kuona endapo kuna namna iliyojificha ambayo ingeweza kufananishwa na ujio wa mkurupuko huo.
...Wakati huo, macho ya Henry yalipapasa kidogo, kabla kichwa hakijainama chini katika jitihada za kujaribu kuficha wasiwasi ulioanza kumsumbua tena.
Hughes aliinuka na kujiondoa katika meza huku akimtazama Henry ambaye bado aliinamisha kichwa chini akionyesha dhahiri kujawa na dalili za wasiwasi ambao akitaka kuufanya bila mafanikio usiweze kuonekana.
Hughes aliacha kumtazama, kisha akaanza kutembea kuizunguka meza huku mawazo yake yakimkumbusha alivyofundishwa jinsi ilivyokuwa ngumu kujua tabia ya mwanadamu kutokana na kujichanganya kwake kwa sana, na ndivyo akiutazama uelewa wake kwamba kati ya viumbe vyote ulimwenguni vyenye kuumiza vichwa kuvijua ni mwanadamu anayeongoza!
Huku akitembea aligeuka kidogo na kumtazama Henry, kisha tena aligeuza mbele tazamo zake akiendelea kuizunguka meza taratibu.
‘Hakika ni ngumu sana kumjua binadamu!’ Alijisemea, ‘Henry pia? Nadanganywa? Au?’
Aligeuka tena!
Mara…macho yao yakagongana!
Akasimama; akatabasamu kidogo kabla ya kurejea tena kutomtazama huku akigeuka pia; ndivyo huko mawazoni mwake alizungumza kimasikitiko, ‘I’m fooled!’
Hughes alikubali kuchanganya kwa mwanadamu si kwamba kumuelewa ni kazi isiyowezekana; lakini ndivyo alikiri ilikuwa ni kazi nzito sana hasa kuweza kujua tabia zake. Na aliendelea kukubali pia ilikuwa ni shughuli ngumu pia kuelewa vyanzo vyake mwanadamu!
Kwanini Binadamu ni mgumu hivyo?
“2” Sasa alimkaribia Henry kwa nyuma huku akimshuhudia jinsi asivyotulia, akishuhudia uhisi fulani kwamba huyo alitamani ageuke kwasababu hapo tayari hofu zilikwishamvamia!
Ndivyo Hughes alitaka!
Ndivyo alihisi tabia zake za hofu ndizo zisimame kuongoza kuhojiwa!
Ndivyo alipenda mwendo huo ukamate kasi, kwani alifahamu ungeweza kujenga hali za uropokaji wake kujifunua zaidi!
Ndivyo alipenda kwakuwa hakuwa na namna nyingine ya kumlazimisha kuweza kujifunua kikamilifu, kwani habari za kutesa alijua ilikuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu na hatari sana kwa mustakabali mzima wa maisha yake iwapo angebainika kama angeamua ndio uwe muongozi wa mahojiano hayo!
Ndivyo, alipumua pumzi ya matumaini!
Alipomfikia, alimgusa kichwani. Akageuza kichwa chake huku akisogezea mdomo karibu na masikio yake kabla ya kumsemesha kwa kuachia sauti ya kunon’gona, “tafadhali nitazame vizuri.”
Kisha alimuacha na kwenda kuketi kiti cha mbele ambacho kwanza alikigeuza ili kuhakikisha zaidi walitazamana…hakumsemesha bado.
Hughes alimtazama huku bado akijisemea kuhusiana na ule utalii wake wa ndani ya mawazo yake kuhusiana na habari za mwanadamu na tabia zake, ‘hii dhana ni sahihi kabisa, kwani nazidi kukubali mwanadamu amekuwa akichanganya sana kuweza kumuelewa kutokana na hali za zake za kubadilika mara kwa mara aidha akiwa ndani ya mazingira yaleyale na, au hata awapo katika mazingira tofauti…ndio, binadamu amekuwa haeleweki awapo hivi ni kwa ajili ipi na awapo ndani ya mazingira fulani anabadilika kwa kuvutwa na nini na kwa sababu gani.’
‘Nakuona Henry, nakiri ni muafaka kusema mwanadamu hubadilika kwa sababu anayo desturi ya kubadilika. Nataka nichezee mabadiliko yako ili uweze kunifunulia yote…bado yapo unaficha! Nataka nielezwe, nahitaji wewe ndiye useme.’Alijisemea zaidi Hughes huku macho yake yakiendelea kusaili mwili wake na kubadilika kwake katika kujua huko alipotaka Henry asogee kama ni ndivyo alikuwa akisogea.
“Unajua unanishtua?” Hughes alirejesha mahojiano huku akitazama pembeni kwa makusudi.
Henry hakujibu.
Ndipo Hughes alivuta zaidi kiti chake hadi kumfikia, akamshika kichwa chake kwa mikono yake miwili na kumtikisa huku akimuuliza kwa ukali, “unasema nini? Ulitaka kusema nini? Sema upesi!”
“Hapana afande!”
“Hapana nini?” Hughes alifoka tena.
Henry alinyamaza huku hofu ikimkwida maradufu.
Hughes akaacha kumtikisa huku akiruhusu kuhema kwake kulivyomjia mara. Kidogo tena, alisema, “if playing alibi, I’ll bring it to dead! (Iwapo unajifunika uhusiki, nitakuumbua!)”
Henry alikepuakepua macho!
“Nimegundua husemi yote, ninahisi ipo namna unahusika na sakata hili. Did you kill her?” Hughes alifunua zaidi ukali wake ili kuhakikisha ulitikisa si chini ya kiwango cha alivyohitaji.
“Hapana!”
Henry alitetemeka!
“Hapana nini?”
“Sikumuua.”
“Lakini ulishiriki…eeh, sema!”
“Ahm…aah…unajua…sikush…?”
“Usijigongegonge! Nataka unijibu kwa uwazi…nakuuliza tena…uliua au ulishiriki kumuua Brigitte?” Hughes alimkatiza Henry kuendelea kusema.
Jasho lilianza kumtoka Henry huku akizidi kutetemeka maradufu. Bado alijibu kwa kugomagoma akikataa katakata kwamba hakuua na wala hakushiriki kufanya unyama huo.
Hughes alitishia tena kwa kumbusha ule mkwara aliomueleza katika awali ya mahojiano; ndio, alimueleza alikuwa akijitafutia matatizo zaidi endapo angeendelea kufanya masihara kwa kusema uongo huku akijua.
Hughes aliinuka, akaipanda meza na kushuka upande wa pili; kisha alikifuata kiti chake na kuketi huku bado akipumua kuonyesha alikasirika sana. Lakini mawazoni hakukasirika hivyo huku bado akimsoma sana Henry katika zilezile jitihada zake za kujaribu kuona ukweli wa maneno yake ulikuwa ukivuta wapi!
Huku akiziona ishara za hofu kumuandama Henry, ndivyo aliamua kufungua kinywa chake kwa kusema kwa namna kama vile hakukuwepo hali isiyopendeza muda mchache uliopita baina yao, “Marlon yupo hospitali. Yeye pia alidhuriwa.”
Hughes aliyatazama kwa makini macho ya Henry, kwani bado aliacha nafasi za kuhakikisha alizichunguza kauli zake.
“Huyo Edwin hayupo nchini muda mrefu.” Hughes alisema huku akihisi mawazo ya Henry kuzidi kuchafuka.
“3” Henry alijikuta akianza kusema kwa majonzi huku machozi yakimtoka, “Ndugu yangu…ooh, afande nisaidie tafadhali.” Aliendelea, “afande natumbukia ndani ya matatizo kwa kuonewa…nilishauri, sikusikilizwa! Najuta kwanini nilipeleka habari!”
Hughes alimtazama kwa makini huku bado ile taadhari kwamba mwanadamu huishi kwa kuificha halisi ya tabia zake, lakini akitupwa ndani ya mazingira fulani mwanadamu huyohuyo anaweza kujifunua kwa tabia zingine ambazo zinaweza kumpeleka katika kuyatoa nje yote yaliyofichwa ndani mwake.
‘He’s like coming…ooh, come come crony!’ Hughes aliomba moyoni akihisi ujio wa mabadiliko fulani katika tabia zenye kuonekana za Henry huku akizitegemea hizo ndizo zingemtumbukiza hata ashindwe kuacha asiropoke.
Henry alikiri kwa kujieleza taratibu, kwamba bado hakuweza kusema yote aliyokuwa akifahamu huku akisisitiza hakuhusika na mauaji.
Mdomo wa Hughes uliicheza tabasamu huku moyoni akisema, ‘now that you come…blow out man!’
Ndivyo Hughes alimueleza Henry, “You’re duty bound to tell it all.” Sauti yake iliibua upya upole wake, “Ukweli wako ni nafasi za kupona. Bali uongo wako ni kujitumbukiza zaidi matatizoni.”
Ndipo Henry aliamua kusema, akisema yote!
Hakuficha tena!
“4” Alisema Hughes baada ya kuona Henry alimaliza kusema ambayo hakusema huko awali, “Utakuwa ni mtu wa ajabu sana ambaye hapa nathibitisha. Lakini kama ni kweli haya usemayo…anyway, ni hivi pia…” Aliendelea zaidi kwa kumtupia swali, “je, wamjua Edwin?”
“Simjui. Ila Marlon alinielezea.”
“Alikuelezea nini?”
“Kwamba ndiye aliyempindua.”
“I’see!” Hughes alishika tama.
Henry hakusema tena, alitulia kimya.
Hata zile hofu zilikimbia na kumuacha akichapwa na majonzi makubwa aliyokuwanayo akifikiri uchungu mkali alioupata marehemu wakati akichinjwa!
Henry alimuwahi Hughes kwa kumtupia swali, “yaani, Marlon alifikia hatua ya kumuua Brigitte?”
Hughes hakujibu, bali alirudia maelezo yake ya awali, kwamba, Edwin hakuwepo nchini kwa zaidi ya miezi miwili hadi wakati huo. Lakini alifanya kwa namna ya kuuliza.
“Si kweli afande! Hapa ipo namna…na ndio maana nimeamua niseme yote ninayojua ili muuaji au wauaji waweze kujulikana bayana!” Henry alisema. Baada ya kitambo kifupi, aliendelea tena kusema huku akionekana kuwa ndani ya shangaa zake huku pia akionekana kufikirifikiri, “Haiwezekani afande, labda huyo ni Edwin mwingine…lakini, ebu…mmh?”
Hughes aliendelea kumsoma huku akizidi kukubali sasa binadamu huyu alijifunua kwa kujiachia wazi jumlajumla.
“Afande…mmh, umesema alikuwepo mwanamke mwingine huko baa wakiwa na pamoja na Brigitte?”
“Una maana gani?” Hughes aliuliza huku akimakinisha zaidi kichwa chake bila kujua ni kwanini hivyo alijikuta akijiweka tayari tayari.
“Jambo lingine nimekumbuka,” Henry alieleza, “unajua wakti tukiwa ndani ya ile teksi, nilimsikia Brigitte akimuagiza dereva waende kwanza nyumbani kwa rafiki yake aitwaye Jane. Huyu nadhani walikuwa pamoja.”
“Very good.” Hughes alijibu huku midomo ikimchezacheza kwa furaha; na kidogo tena aliendelea kusema, “Huyu muhimu sana! Wamjua!”
“Kama ndiye, namjua. Hata anapoishi ninapajua.”
“Really?”
“Kama sivyo ningesema.”
Hughes alinyoosha mikono yake, akaishika ya Henry, akatabasamu zaidi.
‘You give the impression without a smell of blood! (Sioni ukinuka damu!)’
II
John Hughes alirejea nyumbani kwake majira ya saa tano usiku na kumkuta Lana Job amelala ambaye tayari miezi sita hii ya ujauzito ilianza kumsumbua kwa kumfanya kujihisi uchovu kila mara na hivyo kuwa mlalaji mapema tofauti na desturi zake.
Mlango ulipofunguliwa, pua zake zilivuta hewa tofauti!
Zilinusa harufu nzuri!
Mnuko mzuri wa marashi!
Kabla hajashangaa alimuona mfunguzi ambaye alifanya asite kushangazwa zaidi ya kuanza kutengeneza ukubali, kwamba, harufu ya marashi ilikuwa maridhawa!
“Karibu mume wetu! Karibu Baba Doris!” Mama mkwe alisema huku uso wake ukiwa tayari umekunjuka furaha na akimtazama Hughes kwa kumbandikia tazamo la usingizi, tazamo kwamba mwili ulitayarishwa kwa habari za kitandani…those, bedroom eyes!
Hapo, mama mkwe alivalia nguo nyepesi iliyobana ikionyesha alama za maungo yake ya ndani. Matiti yake makubwa ambayo hayakulala sana yaliitutumua nguo yake kiasi michoro ya midomo ya chuchu ilijijenga vyema kwa kuchungulia chini kidogo…
Huku mshawasha wa mwili uliitika, ndivyo pia ulisindikiza kuitikia salamu ya mkwewe kwa kutikisa kichwa chake huku mdomo ukiicheza tabasamu!
Mama mkwe alibandua taratibu tazamo lake huku akigeuka kuanza safari ya kurejea chumbani; na kwa mwendo huo Hughes alifanywa msindikizaji huku macho yake yakikwapua ukodoaji!
Made himself a window shopper!
Hughes alitazama ‘kasheshe za mbingiriko’ zilizokuwa zikitupwa na mama mkwe kupitia ‘ule mbinuko wake’ uliojua vilivyo kunyanyasa pindi ulipotakiwa kufanya!
Kweli, mkwe alitikisa hasa!
‘Kinomanoma’ alitikisa!
Kwamba, kama alifanya, basi alijua kutayarisha huku akihakikisha akitembea taratibu kwa kuzalisha madaha yaliyofichwa kidogo; na pengine hivyo alifanya hadi kuhakikisha macho ya Hughes yaliposhindwa kumtazama kutokana na kutoweza kuonekana baada ya kukaribia chumba chake.
“That’s a gallop!” Hughes alisema kwa sauti ya chini wakati alipokuwa akifungua mlango wa chumbani.
Alimkuta mkewe kajimwaga kitandani bila kujifunika; na isitoshe, akiwa hakuvikwa chochote!
Tena, huyo alilala chali!
Miguu ikiwa imetupwa huku na kule!
Hughes alivuta pumzi zake kwa nguvu kabla ya kuanza kumsogelea…na alipomfikia, akambusu!
Alibusu tumbo huku moyo wake ukisema, ‘na akiwa dume, mchezo huu tutauzika kabisa!’ Na zaidi, mikono ilipapasa tumbo hilo huku ikibinyabinya kwa kwa tahadhali sana ili kuhakikia hakuvuruga usingizi wa mkewe, kisha alinon’gona Sasa alisema, lakini kwa sauti ndogo sana ya kunon’gona huku akipandisha uso katika shavu lake. “ni vizuri watoto kuachana miaka nane.”
Taratibu…alimbusu kwa mwendo uleule wa kuhakikisha hakuvuruga usingizi wake.
“2” Hakukaa sana chumbani, kwani mara baada ya kuvua nguo zake alijifunga taulo na kisha ndipo alitoka akielekea chumba cha kuogea.
Korido lilikuwa ukiwa uliojaa ubaridi mwepesi uliokuwa bado umejichanganya na ile harufu ya manukato ya mama mkwe.
Alipofikia mlango wa chumba cha mkwewe, hapo alijikuta akisimama kwa muda kabla ya kuendelea tena na safari yake huku akitingisha kichwa.
Alipofika huko, alifungua mlango wa maliwatoni na kuingia ndani; isipokuwa alishangaa kidogo, kwani pua zilikamata uwepo mkubwa zaidi wa harufu!
Harufu ileile!
“Mama alijua kujipaka!” Alijisemea huku akielekea ulipo mlango wa bafu.
Huko ulikutwa wazi ukiwa umeegeshwa.
Basi, ndivyo aliusukuma kidogo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kisha aliingia ndani…
Lakini…mara!?
Ndio, mara alihisi mlango ukifungwa nyuma yake huku pua zake zikimkubalisha kwamba harufu ya marashi ilikuwa imezidi maradufu kutema cheche zake!
Kabla hajageuka, hisia zake zilitaka kuamini habari fulani, lakini akili iligoma huku sauti ya mguno ikimtoka!
Akageuka mwili mzima!
Mamaa…?
Alishikwa bumbuwazi!
Alikubali asiamini alichokiona!
Taulo ikadondoka!
Na ndivyo, macho mawili mengine hayakusita kuzama kuviangalia vifichwa!
Alitamani kupiga kelele, lakini alishindwa kufanya hivyo bila kuzijua sababu za kutokufanya hivyo!
Kidogo akatulia, akainua mikono yake na kuyafikicha macho yake ili kuona labda alikuwa ndotoni…
Hapana!
Hapana!
Ndio…alijihakikishia huko hakuwepo!
Akili ilielekea ukubalini, ikibaini ilikuwa ni kweli alichokiona kilikuwa!
‘Huwezi kukiona kisichokuwapo, lakini kisichokuwapo huuona uliopo!’ Mawazo yalitengeneza msingi wa ukubali wake na kuurusha huko akilini.
Tena zaidi, hicho ‘kitazamwa’ kiliuthibitisha uhai wake kwa kumjibu kwa njia ya ulembuzi wa macho yake; na hata midomo yake iliuthibitisha uhai, kwani iliicheza tabasamu!
Kwamba, aliona kilikuwa!
Kwamba, aliona alikuwa!
***
Ni kwamba, mle bafuni kulikuwa na macho manne yakitazamana, mawili kati yao yalikuwa yakitoa tazamo la kufurahia hali; na wakati yale macho mengine yalianika mtazamo fulani!
Mtazamo wa kushangaa!
Mtazamo wa aibu!
Mtazamo wa kutoamini!
Tuseme tazamo hizo zilikuwa ni viumbe wawili waliokuwa wakitazamana ambapo mmoja akifurahia, na mwingine bado akishangaa!
Binadamu walikuwa!
Mwanaume alikuwa!
Mwanamke alikuwa!
Naam, Hughes alishangazwa kumkuta mwanamke mle bafuni kwa namna akimsubiri mtu!
Kumsubiri mtu bafuni?
Na si hivyo tu, kwani alishindwa kuyaamini macho yake yalipozidi kumtambulisha kwa kumhakikishia kuwa binadamu huyo aliyemkuta mle bafuni hakuwa mwingine bali alikuwa ndiye yuleyule mnyemelea ambaye hapo alikuwa mtupu huku akichekelea!
Eti mama Lana!
Hatahivyo, si kwamba Hughes alipatwa na mshangao jinsi ‘chakula’ kilivyoletwa, la hasha, mshangao wake haukuwa huko; kwani, kwake hali kama hizi hazikuwa habari ngeni hata kidogo! Ndio, alikuwa mzoefu wa hali hizi hasa akikumbuka enzi za utoto wake jinsi dada zake wakubwa walivyokuwa wakimgombania ‘kupigishwa kwata’ huku akiikumbuka pia baadhi ya ‘mijimama’ iliyopata kumjia ikidai ilitaka kuujua ‘ukubwa-gogo’.
Kilichopelekea ashikwe na mshangao, ni huu mwendo wa mkwewe kutaka kuwa mchafuzi wa haki ya bintiye! Kwamba, eti kule ‘kubakwa na dada zake’ aliona hakukuwa habari mbaya kama huu mwendo!
Eti, mwendo huu aliona ndio ulikuwa!
Yaani, amdunge sindano mkwewe?
Batili tupu!
Lakini kwa upande wa mama mkwe, hali hiyo ya kuwa mtupu hivyo wala haikumshangaza, kwani hapo alifurahi kumuona mkwewe ambaye naye alikuwa mtupu baada ya taulo yake kudondoka!
“Mwanangu. Macho yangu yasione ukinikatili, kwani hii ni nafasi adimu mithili ya kumpata nguva baharini.” Mkwe alianza kuzungumza; na alifanya kwa sauti ya puani.
Hughes alikuwa tayari kamficha ‘fahari ya mkewe’ kwa kumgeuzia mgongo mkwewe; na pia aligeuka ili kukwepesha tazamo lake lisimsukume mahala ambapo hatimaye angeshindwa kuwa mlinzi imara!
Taratibu, mama alisogea!
Tena alisogea!
Tena na tena akasogea…
Naam, alisogea hata miili iligusana!
Mkubatiwa akakumbatiwa huku akishangaa akifanywa!
Hatahivyo, ‘mkumbatiwa’ akataka kuzuia ile mikono, lakini akaishia kushindwa ingawaje hivyo hakushindwa kwamba alizidiwa nguvu; bali ni kwamba, hivyo alishindwa kwakuwa alijikuta akishindwa tu basi!
Na si kushindwa tu, hata alianza kutetemeka sana huku wote wakipokea ujotojoto!
Hatimaye, Hughes alijikaza kusema ingawaje hivyo alifanya kwa aibu sana, “mama Lana! Kwanini unanifanyia mambo haya? Watafuta nini kwangu?”
Wala mkwewe hakujali, kwani ndivyo alizidisha kumtomasa kwa kumchezea kifuani akizisukasuka nywele za hapo huku pia akihakikisha mgongo ulisuguliwa vilivyo na kupitia matiti yake.
“Hujui mimi ni mume wa mwanao?” Hughes aliuliza tena huku akiendelea kuruhusu kujibakisha mtazamaji wa yote aliyokuwa akitendewa.
“Hujasema uongo Baba Doris. Lakini, si wajua penzi halina mipaka! Usinidanganye hujui!” Mama mkwe alijibu huku bado mikono yake ikifanya utundu wake.
“Huu si utamaduni!”
“Ni kweli huu si utamaduni, lakini huwezi kukataa huu ni matokeo ya kukupenda! Na hapa siondoki, bali nimekujua umenijua!”
Hughes alishusha pumzi nzito.
Mama mkwe alisema zaidi, “elewa nilikupenda tangu nilipokuona mara ya kwanza! Naomba hayo mengine tuyaweke kando ili tuweze kupumuliana. Sifurahi uondoke hukupewa.”
Lakini muda kidogo, mkwe aliacha kumkumbatia!
Akageuka…
Akasogea katika mlango na kuufunga!
Kisha aligeuka tena, Hughes akasogelewa tena!
Safari hii mama mkwe aliizungusha mikono yake kwa kuipeleka kule ambapo Hughes alijitahidi pasifikiwe! Hapo mikono yake ilikutana, ikagusana na mikono ya Hughes iliyokuwa imeweka ulinzi imara ingawaje haikujua kuondosha au kufukuza!
Mkwe alifungua kinywa chake tena kwa kusema, “mpenzi wangu, naomba tugeukiane ili kila mmoja apate fursa ya kutalii.” Mama mkwe alisema kwa sauti nyororo huku mikono yake ikiibinyabinya mikono ya Hughes iliyohakikisha ulinzi bado ulikuwepo hapo patakatifu.
“Nini mama?” Hughes alilalama tena.
“Nahitaji raha Baba! Wewe ni raha wangu!” Mama mkwe aliendelea kusema, “hakika ukikipata nipendacho ukipate ndivyo nitakuwa nimepewa halikadhalika.”
Mama wa mtu alianza kuhemahema!
“Lakini mama...?”
“Mwanaume vipi? Nikikupa ni raha, hutosikia uchungu!” Hughes alikatishwa usemi.
“Mama, si vizuri. Ni dhambi hii!” Hughes aliendelea kulalamika, bado sauti yake alihakikisha ilikuwa ndogo sana; na hakujua alifanya hivyo kwa sababu gani.
“Mwanaume usitake kunichekesha. Hivi unataka kuniambia hapo ulipo hujawahi kufanya dhambi?”
“Tunafanya dhambi, lakini hii imezidi…hapana!”
Huku bado akihemahema mama mkwe hakujibu kwanza; kwani alikuwa kama vile aliingizwa kufikiri.
“Mwanaume nisikilize.” Alianza tena kusema huku mikono yake sasa ikianza kumchezea mashavu, “Wote hutenda dhambi hata manabii walitenda pia!”
“Wewe!” Hughes alijikuta akiropoka kimshangao, kwani kauli hiyo ya mama mkwe sasa aliona ilikuwa ikisogea hatua mbaya zaidi katika kukejeli Wateule.
“Andiko linasema Mfalme Daudi aliwahi kumchukua mke wa jemedari wake na kulala naye. Na si hivyo, hata alimfanyia hila jemedari huyo kwa kumpeleka mbele ya vita na kisha kuachwa auawe kwa makusudi. Tena Andiko hilohilo linasema huyo mwanamke ndiye mama wa Mfalme Suleiman!” Mama mkwe alinyamaza kidogo na kisha aliendelea huku akiirudisha mikono yake kule ulinzi ulipokuwa bado imara, “Mfalme Suleiman alikuwa na zaidi ya wanawake alfu moja, wakati wanawake zaidi ya mia tatu wakiwa ni vimada. Isitoshe, alifikia kuiabudu miungu waliokuwa wakiabudu wanawake zake hao kwa sababu alivutwa na raha za mapenzi yao.”
Hughes alipumua pumzi nzito tena!
“Ndivyo si ajabu hapa ukijua kushindilia kwa raha zetu wenyewe! Ndio, hatupo peke yetu…halafu, Bwana ni mwema na mwingi wa kusamehe!”
Mama mkwe alivuta pumzi zake tena na kisha akazishusha kabla ya kuanza kusema kwa kubana pua, “ewe mwanaume! Hii haitakuwa dhambi ya ajabu sana. Wapakwa mafuta walifanya dhambi, na walisamehewa! Sisi pia tutasamehewa, kwani Bwana anaelewa mwili ni dhaifu…ndivyo acha upewe raha zake!”
Hughes hakujibu neno; alihema zaidi huku mawazoni akizinguliwa sana, kwani kila upande wa mawazo yake ulitamani ndio uibuke mshindi!
Kutamakia…ndivyo ilikwenda; Hughes alianza kupandwa na ‘mshawasha’ huku akisisimka zaidi!
Naam, alianza kuhisi kutamani sana!
Alihisi ukomavu wa mkwewe ungekuwa darasa nzuri kwa kwa kuwatembelea wengine ili simba ajue kuunguruma vilivyo!
Ndivyo taratibu uzalendo ulikuwa ukimpita pembeni, huo ukimuacha akifungwa pingu na yule mdudu; kwamba, huo ulimuachwa akipandwa na yule mzuka wa ngono ambaye hakupenda apande kwa ajili ya mkwewe!
Ndio, alikuwa hataki apandwe, lakini sasa alipandwa!
Ndio, shetani wa ngono aliingia kumdhibiti!
Ndio, huyo alimchota mzima mzima!
Na wakati huo maneno ya mama mkwe yaliendelea kutupa mivuto na shawishi zake na hivyo kuzidisha kasi ya Hughes kutweta mithili alitoka marathon!
“Kwanza, namsaidia binti kutokana na hali aliyonayo. Namsaidia ili usitoke nje ukanaswa na wengine. Nasaidia utulizwe humuhumu huku nikihakikisha unaendelea kumpenda mkeo ambayo ni sehemu za raha zangu.”
***
Mara Hughes aliacha kuweka ule ulinzi kwa kuiondoa mikono yake; lakini ndivyo kwa wakati huohuo aliishika kwa nguvu mikono ya mkwewe na kuisukuma!
Mkwe akashangaa!
Alishangaa huku akirudi nyuma!
Hughes aligeuka na kumtazamana mkwewe!
Mkwe alitazama huku hisia za kumuumiza moyoni zikifukuzana kujijaza mawazoni mwake, kwani alihisi kuziona ishara za kushindwa vita…lakini kumbe hakujua!
Ndio, mkwe hakujua kwamba alifanikiwa kumvuta Hughes ambaye sasa alikuwa akirejea kuwa ‘mraruzi’ aliyekuwa akitazama ‘shambulizi lake’ huku akifurahi kugeuka kuwa yuleyule mlafi asiyejua kuacha kula!
Pamoja na mama mkwe kujihisi kuelekea ushindwani, lakini pia zilikuwepo hisia fulani zilizomfanya ajione alikuwa mithili ya mbwa aliyejikuta akiwa ndani ya himaya ya chatu mkubwa mwenye njaa!
Mawazo ya Hughes sasa yalikuwa ni uraruzi, akizidi kusogea kukubali kwamba hapo alifikishwa ili amtende vilivyo mkwewe kama mwenyewe alivyotamani avunwe!
Ndio, hapo alihitaji amegewe!
Alihitaji raha ya kuku kudonoadonoa!
Yote hayo, ‘muandaliwa’ aliamshwa!
Hata alijisemea, ‘ndio, kuku na mayai yake natafuna!’
***
Lakini ndani ya dakika moja hivi, mama mkwe aliziona ishara zilizomjulisha haikuwa kweli alirushwa vile kwamba alishindwa vita kutokana na kule kutafsiri jinsi mikono yake na yeye mwenyewe aliposukumwa kwa nguvu kuzuiwa kumshikashika mkwewe!
Ndio, sasa alin’gamua yaliyokuwamo wakati huo mawazoni mwa mume wa bintiye…akafurahi sana!
Akichekelea kindanindani!
Tena alifurahi, sasa walitazamana!
Akifurahi sasa alikuja!
Akifurahi alikuja kumuibuwa!
Akifurahi alishinda huku akihofu angedundwa zaidi ya hisia zake kulingana na maelezo ya binti yake alivyokuwa akimjulisha kuhusu upigaji wa mkwewe ulivyokuwa habari nzito sawasawa na ukubwa wa mpiganaji mwenyewe!
Ndio, hapo alipigania kujifikisha ikiwa ni hitimisho la matokeo ya kuvutwa kulikoletwa na ule ujulisho, kwani alimpenda akitamani avunwe ili yeye pia afaidi kama bintiye alivyokuwa akiburudishwa kwa kuachwa hoi!
Macho ya Hughes yalianza kubadilika, yakitumbua mithili ya fisi mwenye njaa atazamapo mfupa, kwani sasa alitaka auone na kuutalii mwili mzima wa mkwewe kwakuwa tayari aliutamani na akitaka sana kuuchezea kuliko jambo lolote lile ndani ya wakati huo. Naam, hapo alitaka kuutalii mwili wake kabla ya kuitwa yeye ni miongoni waliofikishwa; na ndivyo kwa juujuu, yaani, kwa haraka haraka, alianza kwa kuutazama mwili ambapo ndani ya sekunde zisizozidi kumi hivi tayari tazamo lake lilizalisha tafsiri kwamba yeye pia angeweza kuwa radha nzuri kutokana na mvuto wa umbo lake hata katika umri aliokuwa nao!
Ndipo tazamo rasmi lilianza mara!
Hatua kwa hatua!
Ngazi kwa ngazi!
Hughes aliyapandisha macho juu kidogo, na tazamo likagandishwa katika kichwa; na kuanzia hapo, tazamo lilianza kuteremka chini taratibu hata likaifikia ile pua iliyochongoka utadhani ilikuwa ni pua ya mkewe mwenyewe (Lana) kwa jinsi ilivyomfanana.
Tazamo lile liliendelea kusafiri tena, hilo lilisafiri kwa kupiga hatua ndogo tu kabla ya kutulia bila kusogea. Hapo ilionekana midomo iliyokuwa ikichezacheza huku ikimetameta. Midomo ile ilikuwa milaini sana kiasi ilikuwa na uwezo wa kumvuta ‘mtafunaji’ ili kuhitaji kufaidi motomoto za busu.
Alijilamba huku macho yake yakishuka taratibu hadi katika kifua cha mkwe...hapo hapo, mapigo ya moyo yalizidisha kasi kiasi almanusura udenda ulitaka kumtoka kama siyo kuuwahi kuuvuta na kuumeza!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment