Search This Blog

Monday 24 October 2022

MKONO WA SHETANI - 4

 

    Simulizi : Mkono Wa Shetani

    Sehemu Ya Nne (4)





    Hakuna kipya alichokiona ndani ya tovuti hiyo. Tovuti hiyo ilikuwa ni ya Kampuni la utalii la LIVE VIEW REAL AFRICA ambalo lilikuwa linajitangaza kwa mambo mbalimbali ya utalii. Alisoma mambo mengi kuhusiana na kampuni hiyo. ‘Hakuna chochote cha kunisaidia’ Jacob aliwaza. Lakini imekuwaje mpaka hawa jamaa wakawa na anuani hii? Jacob alijiuliza.

    Hapo ndipo akapata wazo la kuangalia wamiliki wa kampuni hiyo. Hapo macho yakamtoka. Mwili wote ukawa wa baridi pale alipoiona sura ya Dr. Don kuwa ndiye mkurugenzi wa Kampuni hiyo. Jacob hakupata shida kukumbuka kuwa sura hiyo ndio yule mzungu ambaye alikuwa akijiuliza atampata wapi.

    Sauti ambayo hakujua ilikuwa imetokea wapi ilinong’oneza “mlango ndio huu ila kuwa makini” Jacob aliiangalia kushoto na kulia ili aone aliyemnong’oneza ndipo alipogundua kuwa ni roho yake tu. Jacob alichukua muda mrefu zaidi kusoma juu ya LIVE VIEW REAL AFRICA. Baada ya kuridhika na alivyoyapata, alitumia masaa yaliyobaki katika siku hiyo kwa ajili ya furaha na Regina wake.

    Msululu wa magari yaliyokuwa yakisubiri ruhusa ya kupita ulikuwa mrefu sana. Gari ya Jacob Matata ilikuwa karibu na yalipo majengo ya DIT. Hakuwa na haraka asubuhi hiyo. Ndani ya kichwa chake kulikuwa na mambo mawili tu siku ya hiyo; Live View Real Africa na Dr. Don’. Alikuwa na uhakika kuwa hapa ndipo kwenye siri yote. Taa za kijani ziliwaka kuashiria upande wao upite.

    Baada ya kuwa amefika sehemu ambayo alikuwa amepanga kwenda, Jacob aliiegesha gari lake upande wa pili wa barabara iliyokuwa mbele ya jengo moja. Jengo hili lilisomeka LIVE VIEW REAL AFRICA Co. Ltd. Aliyatuma macho yake mpaka kwenye majengo hayo. Aliyasanifu kwa macho kana kwamba alikuwa anayakariri.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lilikuwa ni jengo lenye ghorofa tatu. Chini kulitumika kama ofisi na maduka mbalimbali. Aliangalia watu waliokuwa wakiingia na kutoka kwenye majengo hayo.

    Alikaa hapo takribani masaa matatu akiruhusu macho yake na akili yake kuchunguza vizuri eneo hilo na watu wake.

    Alipofika saa sita na dakika tano, Jacob aliwasha gari na kuondoka. Aliingia kulia na kushika barabara ya posta. Aliingiza gari lake ndani ya kituo cha mafuta jirani na posta mpya. Aliiacha gari hapo na kuingia posta. Hapo alichukuwa kitabu cha orodha ya simu. Alianza kuangalia namba mbalimbali za mkoa wa Dar. Macho yake yaligota kwenye namba ya Live View Real Africa Co.Ltd. Alichukua namba zake za simu na kutoka nje. Kwa pale nje aliiendea sehemu ya kupigia simu, mara baada ya kulipia alienda kupiga.

    “Live View Real Africa tukusaidiea nini “ aliuliza mtu aliyepokea simu.

    “Nahitaji kuongea na Meneja tafadhali” Jacoba aliomba .

    “Samahani, kwa sasa meneja yuko nje ya ofisi!

    “Atarudi saa ngapi? Jacob aliuliza na kuongeza” maana nina miadi naye!

    “Hajaacha maagizo yoyote” ulijibu upande wa pili na kukata simu.

    Jacob hakupoteza muda zaidi. Baada ya dakika tatu alikuwa anaegesha gari pale alipokuwa ameegesha awali kabla ya kwenda posta.

    Aliangalia pande zote, baada ya kuhakikisha kuwa hakukuwa na gari karibu, alivuka barabara akaelekea zilipo ofisi za Live View Real Africa.

    “habari za kazi mzee” Jacob alimsalimia mzee mmoja aliyekuwa amekaaa chini ya mti uliokuwa pembeni kidogo ya ofisi hizo.

    “aa kazi wapi kijana shida tu! Wote wakacheka

    “mzee naomba kukuuliza, hivi wewe ni mwenyeji eneo hili hasa ofisi hizi? Jacob aliuliza huku amemkazia macho yule mzee.

    “aa hakuna mwenyeji zaidi yangu eneo hili, kwani unamtafuta nani?

    “nilikuwa napenda kujua kama bosi wa hizi ofisi amesharudi toka safari” Jacob aliuliza huku akionyesha mkono kuelekea zilio ofisi za LIVE VIEW REAL AFRICA.

    “kwani alikuwa amesafiri? Aliuliza yule mzee kwa mshangao kidogo.

    “ndio, jana niliwasiliana naye akasema kuwa angetoka kidogo” Jacob aliongopa.

    “Mmhh mbona leo nimemwona anaingia ofisini……. Alisema yule mzee. Kabla hata hajamaliza aligeuza na kusema “tena huyo hapo ndio anatoka” alisema huku akionyeshea kidole kwa jamaa mmoja mwenye asili ya kiasia.

    “Basi mwache, mi nitamsubiri hapa” Jacob alisema huku akitoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi yule mzee.

    “ooh asante kijana, Mungu akuongezee” alisema yule mzee lakini Jacob hata hakusikiliza maana macho yake yalikuwa yameongozana na yule mtu ambaye ndio ametambulishwa kuwa ni bosi wa ofisi za Live View Real Africa.

    Kwa jinsi alivyoonekana, Jacob alitambua kuwa yule mhindi hakuwa ameenda mbali. Hivyo akaamua atafute sehemu moja nzuri ili abane na kumsubiri, bosi wa Live View Real Africa.



    Dakika tatu tu baada ya kuondoka yule mhindi, gari moja aina ya Range Rover ilipaki mbele ya ofisi hizo. Walishuka vijana wanne. Wote waliingia ndani ya ofisi hizo. Nywele za Jacob zilisimama wakati alipowaona wanaingia ndani ya jengo hilo. Lakini alipuuzia na kujituliza. Kama alivyokuwa amefikiria, haikupita muda mrefu yule mhindi akawa amerudi. Akasubiri mpaka alipoiingia ndani ya ofisi ndipo na yeye akasimama.

    “naomba kuonana na meneja” Jacob alisema mara baada ya kuwa amefika mapokezi.

    “nimwambie nani na unatokea wapi” aliuliza yule dada wakati akiinua simu ili kumtaarifu meneja wake juu ya ugeni huo. Sauti ya yule dada ilimtambulisha Jacob kukwa ndiyo yule aliyoisikia pale posta. Alishangaa kwa nini alipewa taarifa za uongo.

    Kuna kitu tu lazima! Jacob aliwaza.

    “Mwambie Jacob, mkurugenzi wa kituo cha kulele watoto yatima cha NEZAR” Jacob aliongopa tena. Baada ya kuongea na bosi wake, yule dada alimruhusu Jacob kuingia ili kumwona. Sekunde kadhaa baadaye, Jacob aligonga mlango ambao alielekezwa kuwa ni wa meneja.

    “pita mlango uko wazi” ilisema sauti toka ndani.

    “asante sana” alisema wakati tayari akiwa ndani

    “karibu uketi” alisema yule mhindi ambaye macho yake yalionyesha ishara fulani ambayo Jacob hakuielewa haraka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akiwa anakaa tu, mara walitokea watu wawili mlangoni, wengine wawili nyuma ya pazia ambalo lilikuwa limening’inia nyuma ya kiti cha yule meneja. Hivyo adadi yao jumla ikawa wanne na yule meneja wa tano huku Jacob akiwa wa sita. Wote wanne walikuwa wameshikilia bastola zilizokuwa na viwambo vya kuzuia sauti. Kutokea kwao ilikuwa kama kufumba na kufumbua.

    “tulia hivyo hivyo, usitingishe hata kidole chako” Mmoja kati ya wale waliokuwa nyuma yake alimwamuru.

    Jacob akajua tayari yumo mikononi mwa adui tena. Wakati akili yake inafikiri nini cha kufanya, ghafla akasikia kitu kama sindano kinamchoma shingoni. Giza nene likaanza kuingia machoni mara uwezo wa kufikiri ukampotea. Hakujua ni nini kilikuwa kinaendelea baada ya hapo.



    * * *



    Kitendo cha Jacob kuwafyeka vijana wake, kilimwuma sana Dr.Don hivyo baada ya kuwapokea wale wapiganaji maalum kutoka Marekani waliokuwa mbuga za wanyama Mikumi, kulimfanya apange upya namna ya kumpata Jacob.

    “Nafikiri wote mmeona jinsi huyo mdudu alivyofanya”. Dr. Don aliendelea kuwataadhalisha wale makomandoo.

    “wasi wasi wangu ni mmoja, sina uhakika kama Jacob hakupata nafasi ya kuwahoji wale vijana aliowaua. Aliwahoji au hakuwahoji lakini ili tuwe salama, tuchukulie kuwa aliwahoji na hivyo Jacob anajua baadhi ya mambo yetu. Kilichopo ni yeye kutafutwa.

    Nimesambaza picha za Jacob kwa wakuu wa ofisi zetu mbalimbali za biashara. Hivyo muwe tayari maana popote atakapoonekana nitapewa taarifa haraka, nanyi mtatakiwa kwenda kumchukua. Maana najua atataka kutembelea na kuhoji vituo vyetu.”



    Kwa vile maafisa utawala wote wa mashirika yaliyoko chini ya Dr.Don walikuwa wamepewa picha za Jacob, macho ya yule mhindi yalimtambua mara moja wakati akimhoji yule mzee. Hivyo kule alikoelekea yule mhindi alipiga simu kumtaarifu Dr. Don juu ya ujio wake ofisini hapo. Pia alitoka ofisini ili kuvuta muda wa wale wapiganaji maalum kuja. Watu wanne walioshushwa na ile Range, ndio hasa waliomweka Jacob katikati.



    * * *



    Mpaka wakati fahamu zinamrudia Jacob Matata alijikuta yuko ndani ya giza. Alipotaka kujitingisha ndipo alipogundua alikuwa amefungwa vizuri kwenye kitu chembamba mfano wa kitanda. Alikadiria kitanda hicho kuwa na ukubwa kama wa jeneza.

    Alipotaka kugeuza kichwa, kilikuwa kizito sana. Baadaye macho yalipozoea giza ndipo alipoweza kuona vizuri ndani ya chumba hicho. Kilikuwa ni chumba kidogo kiasi kuwa usingeweza kuweka vitanda viwili. Alipoangalia pande zote hakuweza kuona mtu. Alikuwa peke yake. Ndani ya chumba hicho hamkuwa na kitu zaidi ya kile kitu ambacho kilitumika kumfungia.

    Alijaribu kufikiria mahali hapo ni wapi lakini hakufanikiwa maana hakuwa na kumbukumbu yoyote zaidi. Aliweza kukumbuka pale alipoingia ndani ya ofisi za Live View Real Africa. Watu wanne wenye bastola walikuwa wamejificha ndani ya ofisi walipo mteka mmoja alimpiga na kitu kichwani. Hapo ndio ulikuwa mwisho wa kumbukumbu zake.

    Jacob alitumia muda huo kufikiria mambo mbalimbali alijua fika kuwa alitakiwa kutumia akili na nguvu zaidi kama kweli alitaka kuona Shirika la JEPA na wananchi wanaupata ukweli juu ya upotevu wa mamilioni ya dola.

    Ndani ya chumba palikuwa kimya kabisa. Milio ya ndege huku nje ilionyesha kuwa eneo hilo lilikuwa porini au nje kabisa ya jiji. Alikaa ndani ya chumba hicho katika hali hiyo kwa muda mrefu. Hakukuwa na dalili yoyote ya mtu kuja. Baadae akaona kitu kimemulika ndani ya chumba ilikuwa ni miale ya jua. Ilianza kutokea juu kabisa ya chumba ambapo kulikuwa na kitundu kidogo cha kuingizia hewa. Hii ilionyesha kuwa ndio kwanza jua lilikuwa linachomoza. Ndiyo!! ilikuwa ni asubuhi. Kutokana na jinsi walivyokuwa wamemfunga damu haikuweza kutembea vizuri mwilini. Hivyo mwili ulianza kufa ganzi, baada ya muda taratibu fahamu zilimtoka tena.

    Mara hii kelele za funguo zilizokuwa zikifungua mlango ndizo zilizomzindua. Sauti za watu zilisikika nje ya chumba. Jacob akajifanya bado hajarudiwa na fahamu. Mlango ulifunguliwa kabla hajaingia mtu ndani taa zenye mwanga mkali sana ziliwashwa. Kwa vile alikuwa ndani ya giza kwa muda mrefu, taa zile zilimuumiza macho.

    Kama makadirio ya Jacob yalivyokuwa, watu wanne waliingia ndani. Bila kusema neno walisimama pale alipokuwa amefungwa Jacob. Alipowatazama akagundua kuwa hawa watu si wale walioshiriki katika zoezi la kumteka nyara.

    Mara wote waliinama kila mmoja alishika upande wa kile kijitanda alichokuwa amefungiwa Jacob. Walikinyanyua na kuanza kutoka nacho nje. Jacob aliendelea kuonekana kama mtu ambaye bado alikuwa hajarudiwa na fahamu.

    Wakati wamefika kwenye korido la kijumba hicho ghafla wote wanne walikuwa wameanguka chini. Risasi zilizokuwa zimepigwa toka upande usiojulikana ziliwamaliza wote. Jacob hakuwa na namna yoyote ya kujitetea kwa hiyo wakati wanaanguka walikiachia kile kitanda naye akadondoka chini kama mzigo. Jacob akawa amesubiri aone ni nani na kwa nini aliamua kufanya hivyo.





    “Jacob!” Iliita sauti niliyoitambua kuwa ni ya kike. Haikuwa ngeni kwake.

    “Amanda!” Aliita baada ya kutambua sauti hiyo ilikuwa ya nani.

    “Tufanye haraka, wako kule wanatusubiri,” Amanda alisema huku akiwa tayari amemfungua. Amanda ni msichana ambaye yuko Ofisi Fukuzi pamoja na Jacob. Jacob hakujua ni jinsi gani huyu dada alipata taarifa za yeye kuwa pale.

    “Inabidi tuondoke hapa haraka, maana wenzao na hawa jamaa wako kule barabarani, na gari wanawasubiri hawa. Wakiona wamechelewa wanaweza kupata wasiwasi na kuja huku.” Alieleza Amanda ambaye wakati huu alikuwa ameweka chini kibegi kidogo na kutoa dawa fulani ambazo alimpa Jacob. Baada ya muda mfupi ile hali ya kufa ganzi na uchovu wa Jacob ilitoweka.

    “Hebu nieleze, ni nini kinaendelea?” Jacob alihoji wakati akinyoosha viungo vyake.

    “Sawa bosi, hawa jamaa wanne hapo chini walikuwa wamekuja kukuchukua ili wakupeleke kwenye gari liko pale barabarani. Wale jamaa waliokuteka kule Live View Real Africa ndio wako ndani ya gari wanasubiri upelekwe. Ungepelekwa wapi na kufanya nini mie sijui. Namna gani nimekufikia na nimejua uko hapa nitakueleza baadae ila sasa tufikirie nini cha kufanya.” Amanda alisema wakati huo huo wakiwa wanaelekea nje. Baada ya kufika nje, Jacob aliangalia pande zote za eneo hilo. Nyumba hiyo ilikuwa karibu na kilipo kiwanda cha Wazo Hill. Moshi uliokuwa angani uliashiria hivyo.

    “Mambo mengine baadaye, sasa hivi twende tukapambane nao,” Jacob aliamuru akiwa tayari kwa mapambano.

    “Lakini hali yako bado si nzuri bosi…”

    “Ukiwa na wanaume wa saizi yetu usiwe unasema maneno kama hayo,” Jacob alisema huku akiongoza kufuata kinjia ambacho kilikuwa kinaelekea kule barabarani.

    Jacob alikiangalia kijumba alichokuwa amewekwa ndani. Ilikuwa nyumba ndogo tu yenye korido ya kuelekea chumbani. Ilikuwa na chumba kimoja tu na ilikuwa imefanywa kwa mfano wa msalaba, yenye kuta za mawe na milango ya chuma. Mlango mmoja ulikuwa ni wa kuingilia ndani ambapo ungekutana na korido ya kuelekea chumbani na mlango mwingine ukiwa ni wa kuingilia kile chumba alichokuwa amefungiwa Jacob. Chumba hicho kilikuwa na matundu madogo sana kwa juu. Bila shaka ni ya kuingizia hewa kwa vile kijumba hicho hakikuwa na dirisha hata moja.

    “Ili wasituone kwa urahisi ni vizuri tupitie njia hii huku, kisha tuwashambulie kwa ghafla.” Amanda alishauri.

    “Umekuja na gari yako?”

    “Ndiyo,” alijibu Amanda.

    “Bora tuwasubiri hapa, maana wakiona wenzao wamechelewa wataamua kuja. Japo si wote watakaokuja, lakini kwa kiasi fulani tutakuwa tumewapunguza.”

    Wazo hili la Jacob liliafikiwa na Amanda ambaye alisifia tu.

    “Sawa mwanaume, ndio maana adui zako wanahara.”

    “Hao!” Jacob alipiga kelele.

    “Wapi bosi?” Amanda aliuliza.

    “Ingia ndani,” Jacob aliamuru na wote wakakimbilia ndani.

    “Wewe utakaa nyuma ya mlango huu wa kwanza, mimi nitaingia ndani ya chumba walichokuwa wamenifungua,” Jacob alitoa maelekezo.

    Tayari walikuwa wameshafika, walikuwa wawili.

    “Huyo kichaa habebeki?” sauti ilihoji kwa dhihaka na kufuatiwa na kicheko.

    “Huyu kichaa kawa mzito sijui tayari ni maiti,” Jacob alijibu ili kuondoa wasiwasi.

    “Nani huyo anayejifanya ana sauti nzito siku hizi, ni wewe Kizito?” mmoja alipata wasiwasi na sauti ya Jacob. Wote wawili walikuwa wakitembea kwenye korido, hivyo kabla Jacob hajajibu, mmoja tayari alikuwa kwenye mlango wa kuingilia chumbani. Jacob alimpa risasi moja ya begani mara kikasikika kishindo cha mwingine akianguka. Tayari Amanda alikuwa ameshafanya mambo.

    Wakati Jacob anataka atoke ili amsogelee yule jamaa aliyempgia risasi ya bega, jamaa alijitahidi na kuichukua bastola yake iliyokuwa imeanguka kando yake. Akajishindilia idadi kubwa ya risasi. Bastola yake haikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti, hivyo eneo lote likarindima kwa mlio wa zile risasi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jacob na Amanda kwa pamoja walitoka nje bastola zao zikiwa mikononi. Wakakimbilia barabarani lakini kabla hawajafika wakasikia mlio wa gari likiondoka kwa kasi. Bila shaka jamaa walishasikia milio ya zile risasi.

    “Gari lako uliegesha mbali toka hapa?” alihoji Jacob, ilhali wakizidi kukimbia kuelekea barabarani.

    “Si sana ila haitakuwa rahisi kuwawahi.”

    “Sawa, twende haraka kuna sehemu nataka tuwahi kufika.”

    Bastola zao zikiwa bado mikononi walikimbia kuelekea lilipokuwa gari la Amanda. Walipishana na baadhi ya magari. Madereva wa magari hayo walionekana kuwashangaa. Jacob alikamata usukani na kuonda gari kwa kasi ambayo ilimshangaza hata mwenyewe.

    “Gari lako zuri sana ni jepesi.”

    “Mtaliano huyo!” alisema Amanda kwa furaha baada ya gari lake kusifiwa. Mbele walikutana na magari ya polisi yakielekea kule walikokuwa wakitoka.

    “Raia wema wameshatoa tarifa,” alisema Amanda ambaye muda wote alikuwa akishangaa jinsi Jacob alivyojua kulitumia lile gari. Jacob mwenyewe hakuwa na muda wa kujibu bali aliongeza mwendo.

    “Angalia isije ikawa badala ya kuwawahi hao jamaa tukajimaliza wenyewe,” alisema mara baada ya kuona Jacob akizidi kuongeza mwendo.



    Mtu mmoja tu ndiye alifanya Jacob akimbize gari kiasi kile. Alikuwa ni ufunguo wa mambo. Ni mtu muhimu ambaye Jacob aliamini kuwa muda mfupi ujao angekuwa marehemu. Mtu huyo si mwingine ila ni meneja wa LIVE VIEW REAL AFRICA.

    Nimjue aliye nyuma ya mambo haya yote, bila shaka, yule meneja ataweza kunifikisha! Aliwaza Jacob Matata wakati akipangua gia kwa kupunguza mwendo na kukata kushoto. Aliegesha sehemu ya kuegeshea magari. Alikuwa amefika ofisi za Live View Real Africa, kabla ya kutoka ndani ya gari alitupia macho upande wa pili wa barabara. Gari lake lilikuwa palepale alipoliacha jana kabla hajatekwa. Jacob aliazima simu ya Amanda ili ampigie mtu.

    “Hallow Toni, gari langu liko mtegoni naomba ulinasue na kuliweka mahali salama ikiwezekana,” Jacob alisema mara baada ya kupiga simu mahali. Hakusubiri jibu kutoka kwa huyo mtu aliyeitwa Toni.

    “Angalia usalama nyuma yangu, kuna mtu nahitaji kumchukua hapa,” alisema Jacob huku akifutika vizuri bastola yake tayari kwa kutoka ndani ya gari.

    “Nani unayemhitaji?” Amanda alihoji.

    “Nahitaji kumhoji meneja wa hizi ofisi maana kwa vyovyote ana uhusiano na hawa watu.” alisema Jacob huku macho yake yakiwa yamaelekea kwenye mlango wa kuingilia ndani ya ofisi hizo. Huku akimrudishia Amanda simu yake, “Najua kuwa hawa jamaa waliokimbia huko Wazo Hill watapeleka taarifa kwa Dr. Don. Kutokana na umakini ulioonyeshwa na Dr. Don katika kuficha nyendo zake, mtu wa kwanza kuuawa ili kufuta nyayo zake ni meneja wa hizi ofisi. Wanajua fika kuwa mara nitokapo huko, nitakuja ili nimhoji na hivyo itakuwa hatari 77 Japhet Nyang’oro Sudi



    kwao. Hivyo mimi nataka nimhoji kabla hajauawa.” Neno la mwisho lilisemwa na Jacob wakati tayari akiwa nje ya gari.

    Hatua zake za kikakamavu hazikuchelewa kumfikisha sehemu ya mapokezi ya ofisi hizo.

    “Meneja nimemkuta?” aliuliza Jacob baada ya kufika mapokezi na kusalimia.

    “Meneja hajafika leo.”

    “Aah! Nilikuwa nimesahau, alisema atakuwa nyumbani leo,” Jacob aliongopa.

    “Yuko nyumbani, si unapafahamu kwake?”

    “Ndiyo, jana alinielekeza lakini nimepasahau.”

    “Yuko Oysterbay nyumba, namba. 018.”

    “Ooh! Asante sana,” Jacob alishukuru na kuondoka.

    “Vipi?” Amanda aliuliza wakati Jacob anawasha gari na kuliondoa kwa kasi huku vijana waliokuwa eneo hilo wakishangilia.

    “Mtu wetu leo hajafika kazini, yuko nyumbani kwake maeneo ya Oysterbay nyumba namba 018. Ndiko tunakoelekea.”

    Alipofika Oysterbay, alipunguza mwendo ili kuruhusu macho yao kuweza kusoma namba za nyumba ambazo zilikuwa zimeandikwa kwenye mageti.

    “Itakuwa mtaa unaofuata hapo juu,” alisema Amanda ambaye tangu jana alipopewa taarifa za kufuatilia nyendo za Jacob na kuangalia usalama wake amekuwa na furaha sana. Furaha yake inatokana na kuwa miongoni mwa watu wanaomhusudu sana Jacob Matata. Amekuwa kwa muda mrefu akitafuta siku ambayo angefanya kazi bega kwa bega na Jacob. Hivyo alipopokea amri toka kwa Bi. Anita ikimtaka kufanya kazi na Jacob, Amanda alifurahi sana. Kwa hiyo pamoja na kufanya naye kazi alikuwa akitaka kujifunza mengi toka kwa Jacob na wakati huohuo kumwonesha kuwa wapo wanawake hatari kama yeye.

    “Hiyo hapo, acha niegeshe pale mbele,” Jacob alisema wakati wakiipita hiyo nyumba na kwenda kuegesha mbele kidogo.

    “Fanya kinachotakiwa kufanyika kwa wakati,”Jacob alisema wakati akiteremka kwenye gari. Amanda alielewa na kutingisha kichwa kuonyesha kuitikia.

    Mpaka hapo Jacob akawa na uhakika kuwa leo hii alikuwa hatua moja mbele ya adui. Hivyo hakuwa na wasiwasi kuwa adui angekuwa anamsubiri hapo nyumbani kwa meneja.

    “Nahitaji kuonana na bosi wako,” Jacob alimwambia mlinzi aliyekuwa katika lango kuu la kuingilia ndani.

    “Nimwambie nani?”

    “Mwambie Mr. J.M. Masaga.”

    Yule mlinzi aliinama ili apige simu kwa bosi wake ambaye inaonyesha alikuwa ndani. Lakini hakumalizia hata kubonyeza namba alizokusudia kwenye simu. Pigo la kareti la kiganja cha Jacob lilitua sawasawa kwenye paji la uso wa yule mlinzi na kuikata pumzi ya uhai wake papohapo. Pamoja na kuwa kazi ilikuwa ngumu, lakini Jacob alielewa kuwa siku za kuupata ukweli zilikuwa zinayoyoma. Jambo moja hakuwa na uhakika nalo, je pesa zilizoibwa zilikuwa ndani ya Tanzania au tayari zilikuwa nje ya nchi?

    Nchi inamwangalia yeye, Ofisi Fukuzi inamwangalia yeye, pia taaluma yake inamtaka aitetee na kuiletea sifa zaidi. Kwa hali kama hiyo, Jacob hakuwa na muda wa kuzungumza na mlinzi kama huyo. Alipohakikisha ameuweka mwili wa huyo mlinzi sehemu ambayo hata wakija askari mia wasingeweza kuuona, Jacob alipiga hatua za kuingilia ndani ya jumba hili la meneja wa LIVE VIEW REAL AFRICA.

    Mr. Ambish Jitilake, hakuwa na sababu hasa iliyomfanya asiende kazini siku hiyo. Mr. Ambish ana asili ya Asia. Ni Mhindi. Yeye ndiye meneja wa LIVE VIEW REAL AFRICA. Tangu alipoajiriwa na Dr. Don, miaka kama kumi iliyopita amekuwa hana raha na kazi yake. Lakini pia hakujua ni kitu gani kilimfanya aendelee kung’ang’ania kazi hiyo. Elimu yake ingemwezesha kupata ajira sehemu nyingine kwa haraka na urahisi zaidi. Nini sasa kilimfanya aendelee kufanya kazi na mtu asiyeeleweka kama Dr. Don? Pesa? Hapana. Vitisho? Hapana, Cheo? Hapana. Sasa ni nini?, Hakuwa na jibu.

    Dr. Don amekuwa akimpa Mr. Ambish amri na kazi ambazo zilikuwa ni nje ya majukumu yake. Mr. Ambish hakujua Dr. Don alikuwa akiishi wapi. Hakujua ni wapi ilikuwa ofisi ya Dr. Don, pia ni mara chache sana walikuwa wakikutana. Mawasiliano yao mengi waliyafanya kwa njia ya simu, faksi na njia nyinginezo. Lakini Dr. Don ni mkurugenzi na Mr. Ambish ni meneja.

    Usiku wa kuamkia siku hii, Mr. Ambish alimpokea kijana aliyedai kuwa ametumwa toka kwa Dr. Don. Alikuja na orodha ya majina na picha za watalii ambao wangewasili kesho yake jioni. Lakini tofauti na watalii wengine picha zote za watalii hao zilikuwa na alama ya ‘X’. Mr. Ambish alitakiwa kuandaa gari tu la kuwapokelea na kuwatembeza watalii hao. Dereva na watu wengine wa kuwahudumia wangeandaliwa na Dr. Don mwenyewe. Sababu hasa ya Dr. Don kufanya hivyo haikujulikana. Mambo kama haya ndiyo humfanya meneja huyu ashindwe kumwelewa mkurugenzi wake. Hapo kazi huwa ngumu.

    Dr. Don hakuwa anataka Mr. Ambish aujue undani na kazi zake haramu. Alifanikiwa. Mr. Ambish hakujua chochote kibaya cha Dr. Don zaidi ya amri na maagizo yaliyokuwa yakimtatanisha mara kwa mara.

    Nyumba hii alikuwa akiishi peke yake. Mtu mwingine ni mlinzi ambaye hakuwahi hata kuingia ndani. Ni wakati Mr. Ambish anajiandaa kuweka zile picha na majina ya watalii ndipo alipohisi kuna mtu anatembea sebuleni. Alisikiliza kwa makini zaidi. Ni kweli kulikuwa na mtu. Ni nani? Mr. Ambish alijiuliza, kama ni mgeni, kwa nini mlinzi hajanitaarifu na ameingiaje ndani?

    Aliitupa kitandani ile bahasha iliyokuwa na vitu alivyokuwa anaangalia. Kabla mkono wake haujagusa kitasa cha mlango wa chumba, tayari mdomo wa bastola ulikuwa ukimtazama.





    “Tulia na geuka uingie ndani” iliamuru sauti ya Jacob ambaye tayari alikuwa ameshafanikiwa kuingia ndani.

    Mr. Ambish alipomwangalia Jacob alimtambua.

    Alitambua kuwa ndiye aliyekuja kuchukuliwa ofisini kwake na watu waliokuwa wametumwa na Dr.Don.

    “Bana kubwa mimi pana… hapana jua sababu Don nataka ua wewe” Mr. Ambish aliropoka bila kujua alikuwa anaongea na nani. Jacob aliweka bastola yake na kumsogelea Mr. Ambish. Kuona hivyo Mr. Ambish akapata ujasiri mpya.

    “Jina lako nani? Aliuliza Jacob

    “Jina lnagu iko takia nini bana? alibisha

    “Bana iko fanya nini mie, wewe taka ua mimi bure” alilalamika mhindi huyu baada ya kupokea kofi toka kwa Jacob.

    “Sina haja ya kukuua maana najua huna makosa, ila nataka ujibu maswali yangu yote, na mara hii ukibisha sitatumia mkono, bali nitasambaratisha ubongo wako kwa risasi. Lazima ujue kuwa ukiuza Utumbo usiogope nzi” alionya Jacob wakati anamalizia kusema, Mr.Ambish akatupia macho yake kwenye saa iliyokuwa ukutani. Mara moja Jacob akatambua hiyo ilimaanisha nini.

    “Simama mikono ikiwa juu na kisha tangulia nje.”

    Kwa muda mfupi tu huo Jacob alikuwa ametambua kuwa Mr. Ambish hakuwa mzoefu wa mchezo huu wala kutumia silaha ila alihisi anazo habari ambazo zingeweza kumsaidia.

    “Vipi umeamua twende nae? Amanda alihoji hali akitia gari moto.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Inaonesha jamaa zake wanaweza kuja hapa muda si mrefu tokea sasa” alieleza Jacob ambaye alikuwa amekaa nyuma na mateka wake. Muda huo pia alitumia kuangalia vilivyokuwa ndani ya bahasha iliyokuwa chumbani kwa Mr. Ambish .

    “Vipi hiyo bahasha ina chakula chochote” alihoji Amanda.

    “Tena kizuri sana” alijibu Jacob ambaye alionyesha kufurahia kuzipata zile picha na taarifa za kuja kwa wale watalii.

    “Wapi utatumia kumtapisha jamaa yako” aliuliza Amanda katika lugha ambayo bila shaka isingeeleweka kwa urahisi na Mr. Ambish ambaye wakati huu ngozi yake ilikuwa nyekundu.

    “Kimara mwisho” alisema Jacob.

    Amanda alikuwa mzuri sana katika uendeshaji. Baada ya dakika kadhaa tu walikuwa Kimara, walitumia ubabe kupita njiani.

    “Ingia kushoto pale mbele utaona gereji imezungushiwa uzio wa mabati. Ingia ndani” Jacob alijua gereji hii haitumiki kwa muda mrefu

    “nafikiri itakuwa ni sehemu nzuri ya kumtapisha” aliongeza.

    “Jina lako nani” Jacob alirudia swali lake, Mahojiano yalikuwa yakifanyikia ndani ya gari. Jacob aligundua kuwa Mr. Ambish alikuwa anaogopa sana silaha, hivyo wakati huu mdomo wa Bastola ulikuwa katikati ya paji la uso wa mhindi huyo.

    “naitwa Ambish Jitilake”

    “Mimi iko meneja ya Live View Real Africa”

    “Nani mmiliki wa hiyo kampuni?

    “yeye naitwa Dr.Don Keller”

    “Ni nani waliokuja kuniteka ndani ya ofisi yako jana?

    “mimi pana jua”

    “kama huwajui kwa nini uliniruhusu watumie ofisi yako?

    “Dr. Don yeye sema mimi niwaruhusu” alijibu baada ya kusita kidogo.,

    “Kwa nini alikuamuru hivyo?

    “Mimi pana jua”

    “Je unajua kitu kingine kinachomilikiwa na Dr. Don”

    “Yeye ana Kampuni mingi, hata ile Afri Afri Mich Co.Ltd ni ya yeye.

    “Ofisi za Dr.Don ziko sehemu gani?

    “Mimi pana jua”

    “Unafikiri ni kwa nini Dr. Don alitaka kuniua?

    “Yeye hajaniambia mimi ni nini nafanya yeye iko taka ua wewe” mpaka hapo Jacob hakuona uongo wowote ndani ya macho ya yule mhindi wakati wa mahojiano.

    “Habari za hawa watu na picha zao ni nani aliyekuletea? Jacob alisema huku akituma ile bahasha.

    “Dr. Don natuma kijana moja jana usiku”

    “watu hawa watafika lini na ndege gani?

    “Watafika kesho na ndege ya shirika la ndege la ufaransa?

    Jacob alimtupia macho Amanda ambaye alionyesha kuwa hakuna cha ziada. Wote wawili waliridhika na maelezo ya huyo meneja ambaye alionyesha wazi kutokuwa mshirika katika uovu wa Dr. Don zaidi ya kuwa meneja wa kampuni la utalii la Live View Real Africa Co.Ltd. Walianza safari ya kuelekea kituo cha Polisi cha kati.



    * * *

    “Mkuu wa kituo yupo? Aliuliza Jacob alipofika mapokezi na kumkuta askari wa zamu.

    “Una shida gani? Aliuliza badala ya kujibu.

    “Pita ndani” alisema mara baada ya kuona kitambulisho cha Jacob. Watu kama hawa huwa ni adimu nyakati ambazo nchi imo katika wakati mgumu kama huu. Hivyo wakuu wengi wa idara hutamani hata kuwaona tu.

    “Nikusaidie nini mzee? Alisema mkuu huyo msaidizi wa kituo mara tu alipomwona Jacob. Alimkumbuka, kwani ni siku chache tu kabla ya kitu cha Inspekta Ezron ambaye ndye alikuwa mkuu wa kituo hiki, Jacob alikuwa amekuja kituoni hapo ili kuonana na Inspekta Ezron. Hivyo hakuwa mgeni machoni pa mkuu huyo wa kituo.

    “Kuna raia mwema mmoja ndani ya gari hapo nje nahitaji umweke chini ya ulinzi mkali ambao ni hewa tu inaweza kuupenya na si vinginevyo” Jacob alisema huku akiinuka kutoka nje.

    “Sawa mzee” alijibu yule askari huku akiinuka na kuanza kumfuata Jacob kuelekewa ilipokuwa gari.

    “Asihojiwa, asipigwe, wala asiumizwe na kuteswa kwa namna yoyote ile. Akipotea ni bora na wewe upotee. Usifanye chochote juu yake mpaka upokee maelezo toka kwangu. Kintume na nilivyokuagiza utajua ni kwa nini Gundi hainati kwenye chupa yake ”

    Maelezo hayo ya Jacob yalizingatiwa sana na yule Afisa wa Polisi. Alilisikia sana jina la Jacob na hivyo hakutaka kuingia matatani na mtu kama Jacob.



    * * *



    “Wakati tunapanga nini cha kufanya, hebu sasa ukanieleze ilikuwaje ukaweza kufika sehemu ile niliyokuwa nimefungwa” Jacob alisema wakati wanatoka ndani ya eneo la kuegeshea magari la kituo cha kati cha jiji la Dar es salaam tayari kuelekea nyumbani kwa Jacob.

    “Pitia hapo gereji ya AZ kisha tuchukue gari jingine ndipo tuelekee kwangu” Jacob alisema. Amanda hakujua ni kwa nini Jacob aliamua wafanye hivyo. Alitii na kufanya kama alivyoamriwa.

    “Eeh hebu nieleze ulifanyaje mpaka ukawa mkombozi wangu katika mazingira kama yale? Jacob alimwuliza Amanda. Wakati huu wote wawili pamoja na Regina walikuwa wamejipumzisha mara baada ya kuwa wamepata chakula cha usiku. Regina alikuwa amejiegemeza kifuani kwa Jacob. Hapa walikuwa nyumbani kwa Jacob.

    “Mkurugenzi Bi. Anita alipata taarifa za vifo vya kutisha vilivyokuwa vimetokea. Kifo cha Inspekta, meneja wa Benki, mhudumu wa Benki, wafanyakazi wa ofisi ya mkurugenzi wa shirika la JEPA, Bwana Makia Kimisa, vilimfanya agundue kuwa ilihitajika uongezewe nguvu.

    Hivyo juzi usiku alinitaarifu juu ya uamuzi wa ofisi Fukuzi kuniteua mimi kuwa msaidizi wako katika operasheni hii. Jana asubuhi ilibidi niwahi ili kuanza kufuatilia nyendo zako.

    Wakati unaenda Live View Real Africa mpaka inatokea unatekwa nyara mimi nilikuwa shahidi wa yote.” Amanda alisema huku muda mwingi macho yake yakimwangalia Regina. Alikuwa kama mtu anayemwambia “unafaidi sana dada”

    “Mpaka hapo nimeshakuelewa, asante kwa kazi nzuri. Ila tuna kazi kubwa zaidi usiku huu” alisema Jacob huku akichezea nywele za Regina, mpenzi wake. Kisha akaongeza “sasa hivi ni saa mbili usiku, saa nne itatukuta tuko kwenye moja ya majengo ya ofisi hizi tunaweza kuambulia lolote linaloweza kutufikisha alipo Dr. Don. Tutaanzia pale Live View Real Africa Co. Ltd na kisha Af Afri Afri Mich Co.Ltd. Hivyo kwa masaa haya mawili yaliyobaki tunaweza kupumzika huku tukijiweka sawa kiakili maana hatujui ni nini tutakutana nacho huko. Regina atakuonyesha sehemu ya kupumzika wakati mimi nitaingia stoo kuangalia vitendea kazi vinavyoweza kutusaidia” Jacob alipomaliza kueleza Regina aliinuka na kuelekea chumba kingine.

    “Okay, dear karibu ndani ujipumzishe” alisema mara baada ya kurudi sebuleni.



    ***



    Saa tatu na nusu usiku iliwakuta Jacob na Amanda wakiwa wanachagua silaha. Ndani ya ghala hili la Jacob kulikuwa na silaha za kila aina na za kisasa kabisa.

    “chagua silaha ambayo unafikiri inaweza kukusaidia kupambana na mtu ambaye ni komandoo.” Jacob alimwambia Amanda wakati wakiwa wanaendelea kuchagua.

    “Komandoo zaidi yako ni nani” Amanda alisema.

    “nilivyopambana na Dr. Don siku ile nilijua kuwa yule mtu yuko kwenye ngazi ya ukomandoo tena wa kufuzu kwa alama za juu” Jacob alihasa ili kumwonyesha Amanda kuwa mtu waliyekuwa wanaiendea himaya yake ni wa namna gani.

    “pamoja na hayo yote bosi, kwa kazi uliyoifanya Israel naamini wewe ni zaidi ya komandoo hivyo sina wasiwasi ninapokuwa na wewe.” Alisema Amanda wakati huu akiwa anaweka baadhi ya silaha ndani ya mavazi yake. Jinsi alivyokuwa akificha silaha zake, ilitosha kujulisha Jacob kuwa dada huyo hakuwa wa kawaida.

    Amanda ni msichana aliyekuwa ameaminika kuwa na shabaha kali kuliko watu wote ndani ya ofisi Fukuzi. Lakini mwenyewe alikuwa ananyoosha mikono kwa Jacob. Inasemekana kama kuna adui ishirini basi Amanda alihitaji risasi ishirini ili kuwamaliza wote. Kupoteza shabaha ilikuwa ni ndoto.

    Saa nne kasoro dakika kumi tayari walikuwa ndani ya gari kwa safari ya kwenda Afri Afri Mich Co.Ltd. Kila mmoja alikuwa katika hadhali na morali ya juu. Amanda alikalia usukani.



    * * *



    Alifahamu kuwa Jacob ni hatari lakini hakudhani ni hatari kiasi hicho. Alifikiria juu ya uwezekano wa kuwa amehujumiwa na makomandoo alioletewa, lakini wazo hilo alilitupilia mbali.

    “Mtu mmoja, mmoja tu! Dr. Don alijikuta akijisemea. Alishindwa kuoanisha mtiririko wa matukio. Tangu wameanza mchezo huu yeye amekuwa hatua moja mbele ya Jacob. Lakini kitendo cha Jacob kumteka yule meneja wa Live View Real Africa, ilimaanisha kama si Jacob kuwa hatua mbele basi sasa wako sambamba.

    Ni hayo yaliyomfanya Dr. Don awe ofisini mpaka dakika hii ambapo ni muda ambao Jacob na Amanda walikuwa wanachagua silaha, za kufanyia kazi usiku huo. Aliazimia kuongeza hadhali na umakini katika mipango na kazi zake. Alimwona Jacob kama mzimu na si mtu wa kawaida. Mpaka wakati huu ulinzi aliokuwa ameuweka kwenye jingo hili la Afri Afri Mich Co.Ltd ni wa kutisha ghorofa ya pili ya jingo hili ndipo ilipokuwa ofisi yake.

    Ndani ya ofisi hiyo ndimo alipokuwa amehifadhia mamilioni ya dola. Pesa ambazo zilikuwa zimeiweka nchi pabaya mpaka wakati huo. Baada ya kupanga mipango yake na kuhakikisha ulinzi katika eneo lote la kuzunguka jengo, Dr. Don aliingia ndani ya gari na kutokomea.



    Wakati akiondoka eneo hilo, kulikuwa na kila dalili ya mvua kunyesha. Aliposhika barabara ya Alli hassani Mwingi macho yake yaliona gari. Gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa taratibu sana. Tayari mvua ilikuwa imeanza, japo haikuwa kubwa. Alipata wasiwasi juu ya gari hii akapunguza mwendo ili aangalie ndani.



    “Mvua kama hizi kwa nyakati kama hivi zina faida na hasara zake” alisema Jacob Matata ambaye alikuwa amekaa pembeni na kumwachia Amanda usukani. Walikuwa wanakaribia kushika barabara ambayo ingewapeleka yalipo majengo ya Afri Afri Mich Co.Ltd. Waliadhimia waanzie hapo.



    “aah nani huyo asiyejua kutumia taa, anapishana na gari huku akiwa ameweka full light” Amanda alilalamika wakati anapishana na gari la Dr. Don. Dr. Don alifanya hivyo makusudi kabisa alitaka kuwaona waliokuwa ndani ya gari. Mwendo wa gari na upande ambao gari hiyo ilikuwa ikielekea vilimpa wasiwasi. Kwa uzoefu wake katika mambo ya ujasusi ulimwezesha kutilia mashaka gari hiyo. Dar es salaam ya sasa mtu hawezi kuendesha gari taratibu kiasi hicho katikati ya jiji tena muda kama huu! Dr. Don. aliwaza

    Kipindi wanapishana, kwa vile hakupunguza mwanga wa taa za gari lake, hakupata shida kuitambua sura ya mpelelezi Jacob Matata akiwa kiti cha mbele cha gari hilo, akiendeshwa na msichana mmoja. Mara moja nywele zikamsimama japo alikuwa na kipara. Jasho ikamtoka japo mvua ilikuwa ikinyesha, akili yake ikaelekea kwenye mamilioni ya dola za kimarekani ndani ya ofisi yake.



    Mambo mawili aliyawaza kwa wakati mmoja. Kila mkono uliamua kufanya jambo moja. Wa kushoto ulizungusha usukani ili kugeuza gari, wa kulia ulitoa simu na kubonyeza namba kadhaa. Mdomo uliongea huku gari ikiwa tayari imeshageuzwa na kuanza kurudi ofisi za Afri Afri Mich Co.Ltd.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mwendo kidogo aliweza kuliona lile gari walilokuwamo kina Jacob. Bado lilikuwa likienda taratibu kama ilivyokuwa alipopishana nao. Mkono wa kushoto uliendelea kuendesha na mkono wa kulia ulikuwa umeshikilia silaha tayari. Bunduki hii aliyokuwa ameshikilia Dr. Don ni moja kati ya silaha hatari kabisa. Ilikuwa ni maalumu kwa kulipulia. Ina uwezo wa kubeba mabomu manne hadi kumi. Huweza kuyarusha hadi umbali wa kilomita moja.

    Tayari alikuwa analisogelea gari la kina Jacob na Amanda na wakati huohuo gari hilo lilikuwa inakaribia mnara wa simu aliokuwa amesema. Mnara huo ulikuwa mkabala na jengo la Afri Afri Mich Co.Ltd.

    Alikuwa na uhakika kuwa Jacob na mwenzie wangejifanya kupita mbele ya jengo hilo ili kuangalia hali ya ulinzi ilivyo. Ndilo maana aliamini gari hilo lingefika kwenye mnara wa simu. Hapo walinzi wangelishambulia kwa urahisi tokea ndani ya kuta za jengo hilo.

    Gari la kina Jacob na Amanda lilipokaribia zaidi ule mnara, Dr. Don aliinua bunduki yake maalumu, aliitoa nje kwa kupitia dirishani. Wakati kidole cha shahada cha mkono wa kulia kikiwa tayari kufyatua mara eneo lote la katikati ya jiji lilikuwa giza. Umeme ulikuwa umekatika, hata hivyo aliweza kuziona taa za gari alilolitaka.

    Gari lilipofika mnara wa simu, ghafla likawa limesambazwa vipandevipande na kuacha moto mkubwa kutanda eneo hilo. Mabomu yaliyorushwa na Dr. Don na vijana wake yalikuwa yamelisambaratisha vibaya gari alilokuwa amepanda Jacob na Amanda.

    Badala ya kusimama Dr. Don alipita eneo hilo kwa kasi. Hakuona sababu ya kusimama hapo. Hakuhitaji maswali toka kwa polisi.

    * * *

    Upande wa Jacob na Amanda, ilikuwa kama sinema. Jacob aliona sababu ya kufuatilia pale Amanda alipolalamika juu ya taa za gari walilopishana nalo, Jacob aliona si vibaya kugeuza kichwa na kuangalia lilikuwa gari gani, japo mvua ilikuwa inanyesha lakini aliweza kugundua kuwa lile gari lilipunguza mwendo mara tu lilipowapita.

    Jacob Matata alimwamuru Amanda apunguze mwendo zaidi. Akarukia viti vya nyuma macho yake yakiwa yanalichunguza gari la Dr. Don kwa makaini zaidi. Ni wakati gari la Dr. Don lilipogeuza ndipo Jacob akawa na uhakika kuwa ndani kulikuwa na mtu ambaye si rafiki yao.

    “Kaa tayari kwa lolote kuna kiumbe anataka mchezo nasi.”

    Alimtahadharisha Amanda ambaye hata hivyo badala ya kushtuka ndio kwanza akawa mtulivu kwenye usukani. Wimbi la nyuma halizamishi chombo alinong’ona.

    Macho ya Jacob yaliweza kushuhudia gari hilo lilipowakaribia. Dr. Don alipotoa mkono nje ulioshiklia silaha yake ndipo Jacob aliporukia mbele tena.

    Kukatika kwa umeme ilikuwa kama sherehe kwa Jacob.

    “Nyosha usukani, nikihesabu hadi tatu turuke nje kwa pamoja na kuliacha gari likienda”

    “Moja… mbili… tatu…”Hata kabla Jacob hajamaliza wote wawili walikuwa wameshatua nje. Wakati wametua ndipo waliposhuhudia gari lao likisambaratishwa vipandevipande.

    “Ulijuaje?” aliuliza Amanda.

    “Baadaye! Tubane mahali ili eneo liwe shwari,” alisema Jacob.

    Mvua ilikuwa imeongezeka sana wakati huo. Lakini mvua hiyo haikuwazuia watu wa eneo hilo kusikia kishindo. Mlipuko wa gari la kina Jacob ulikuwa mkubwa. Watu walianza kumiminika kwenda katika eneo hilo. Japo walinyeshewa na mvua lakini hali hiyo haikuwazuia kujazana hapo.

    “Tutumie fursa hii kuvuka barabara na kuingia jengo hili,” alisema Jacob na wote wakatembea kuvuka barabara kuelekea jengo la Afri Afri Mich Co.Ltd.

    “Wewe pitia upande wa kushoto mimi wa kulia, tutakutana nyuma ya jengo na hapo tutajaribu kuingia,” Jacob alishauri na wote wakatawanyika.

    Wingi wa kelele za watu na kisha baadaye ving’ora vya Polisi viliwasaidia sana Jacob na Amanda kuingia ndani ya jengo hilo bila ya kushtukiwa na walinzi. Jacob alikuwa wa kwanza kuvuka ukuta. Aliangaza pande zote. Giza lilikuwa totoro, lakini tayari macho yalikuwa yameshazoea giza. Hakuona mtu yeyote eneo hilo. Alimwashiria Amanda ili aruke. Amanda aliruka kwa mtindo uliomshangaza Jacob.

    “Inaonekana walinzi wote wamekaa sehemu moja ili kujikinga mvua,” Jacob alimwambia Amanda ambaye alikuwa anaweka vizuri bastola yake.

    “Kajibanze kwenye kona ile mimi nitaelekea upande huo wa kushoto.Yeyote atakayetokezea upande huu wa kulia ni halali yako, na atakayekuja huko niliko, basi ndio itakuwa kiama chake. Ila uwe mwangalifu,” Jacob alisema huku akielekea upande alioutaja. Nguo zote zilikuwa zimeloanishwa na mvua. Baridi ilikuwa imeanza kuvamia miili kwa fujo.

    Hii ilikuwa fursa nzuri kwa Jacob na Amanda kwani kelele za mvua, watu na ving’ora vya polisi eneo la ajali vilifanya walinzi wasiwe na wasiwasi wowote. Wakati huu walikuwa wamejikusanya kwenye banda moja lililokuwa mbele ya jengo upande ule aliokuwa akielekea Jacob Matata.

    Jacob aliweza kuliona hilo banda, ila hakujua kama ndimo walimokuwamo walinzi wakipiga simulizi za hapa na pale. Wakati anakaribia sehemu moja iliyokuwa na dirisha akasikia nyayo za mtu zikija upande ule aliokuwapo. Akajibanza usawa wa ukuta kwa staili ya buibui.

    Macho yake yakawa yamemwona huyo mtu aliyekuwa anakuja. Alikuwa amevalia sare huku akiwa ameshiklia SMG yake. Alipofika usawa aliokuwapo Jacob, Jacob alirusha bastola yake upande mwingine. Yule askari akageuka kuangalia kilipotokea kishindo. Ni wakati huo ambapo Jacob aliruka na kumpiga kabali yule mlinzi. Kabali hiyo haikumwachia hata chembe ya pumzi mlinzi huyo. Akalegea na kwenda chini bila hata ya kutoa kelele. Akamvuta na kumsimamisha kwa kumwegesha ukutani. Alipiga hatua kuelekea lilipokuwapo lile banda na akiwa kama hatua sita hivi kulifikia ndipo aliposikia sauti za watu wakiongea na kucheka tokea ndani ya hilo banda.

    Kwa vile banda hilo lilikuwa limetengenezwa kwa mabati, matone ya mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha yalifanya ndani ya banda kuwe na kelele na hivyo kuwafanya wale walinzi waongee kwa sauti ili kusikilizana.

    Hakuwa na kizuizi chochote kulifikia banda hilo. Alitembea mpaka alipofika jirani kabisa na dirisha la banda hilo na hapo alitega sikio na kuweza kusikia walichokuwa wakiongea.

    “Hata sijui lile gari lilikuwa la nini na la nani?” mmoja aliuliza.

    “We mshikaji vipi, sie mradi kesho tutapokea posho zetu inatosha. Haya mengine mwachie bosi mwenyewe.” Vicheko! Kwa vile eneo lote lilikuwa giza, isingekuwa rahisi kwake kuona idadi na watu waliokuwa ndani. Ila kwa kukadiria kulikuwa na zaidi ya watu kumi.

    ”Hivi uliona gari lake lilivyopita kasi mara baada ya shambulio?” Mmoja aliuliza.

    “Aah wapi bwana, yeye alikuwa ameshaondoaka,” mwingine alibisha.

    “Mimi aliponipigia simu alisema tulishambulie lile gari yeye anakuja. Lakini tulipolishambulia yeye alipitiliza halafu baadaye akanipigia simu na kunitaarifu kuwa kuna watu wawili wanakuja. Hao wangetusaidia kujibu maswali ya polisi kama wangeingia ili kutuuliza. Ndio wale jamaa mliowaona wameingia,” alieleza huyu aliyeonekana kuwa ni kiongozi wao. 105 Japhet Nyang’oro Sudi





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog