Search This Blog

Monday, 24 October 2022

KIMBIA, KIMBIA! [RUN NIGGER, RUN!] - 5

 

     







    Simulizi : Kimbia, Kimbia! [Run Nigger, Run!]

    Sehemu Ya Tano (5)







    Obrien alijibu kwa kuitikia kwa kichwa; lakini kabla Daktari hajatokomea aliwahi kuuliza swali ambalo hatahivyo tayari njozi aliyoota ilikwishamjulisha, isipokuwa hapo alitaka uhakikisho zaidi ili kukazia mazingira yakujikuta sasa akiwa amefungwa pingu tofauti na jinsi alivyoletwa katika chumba hicho, “samahani Daktari. Hivi nilipatwa na nini hadi kufikishwa hapa hospitali…sikumbuki hili!”

    “Ok! Kifupi hapa uliletwa kutokana na ajali mbaya sana uliyopata huko tabata…usijali sana, endelea kupumzika.” Daktari alijibu, na baada ya kitambo kifupi aliondoka.

    Nesi alimtayarishia vidonge na maji kama alivyoagizwa. Na wakati huohuo, aliingia askari ambaye alianika hali kwamba hakuwa mtu wa masihara; kwanza, askari yule alimtazama nesi na kumkenulia meno yake, na kisha ndipo akamsogelea Obrien huku akimtazama kwa dharau; na hata alipomfikia hakumsemesha zaidi ya kutoa funguo za pingu mfukoni mwa suruali yake!

    Ndipo mikono ya Obrien ikafunguliwa!

    “Nashukuru” Obrien alijibu huku akijitahidi kuiweka hofu yake pembeni angalau kwa muda.

    Askari hakuitika!



    “Kunywa hizi dawa.” Nesi alimpatia Obrien glasi ya maji pamoja na vile vidonge.

    “Ugua pole. Nitarudi baadaye kukucheki zaidi.” Nesi yule aliendelea kusema, “tafadhali pumzika na usitake kusumbua kichwa chako kwa sasa. Ni muhimu kama daktari alivyokujulisha.”

    Nesi alimuaga, na kisha akamgeukia yule askari na kusema huku akiondoka taratibu, “unajua Daktari kaagiza mgonjwa asisumbuliwe.”

    Askari yule alikenua tena meno yake na kisha alisogea pembeni ya mlango kilipokuwepo kiti na kuketi.

    Hapo ukimya ukatanda kwa muda, na hata ulipelekea kumfanya Obrien arejeshwe tena ndani ya ulimwengu wake wa mawazo kuhusu ile ndoto ambayo ndio ilimjulisha hapo alikuwa wapi na ni nini hasa kilimsibu; na isitoshe ile hofu iliyokuwa imeanza kuondoka ilianza kurejea tena, na ndivyo pia ilikuwa kadri macho yake yalivyomuona askari huku akitambua sasa alifungwa pingu ndivyo (hofu) ilishika kasi huku kichwa kikimuuma utadhani ‘inskoskaz ya msolopogaz’ ilimparuza kiaina!

    Hakika, kichwa kilimgonga sana huku mawazo mengine lukuki yakimjia bila mpangilio; lakini, hatahivyo, kadri muda ulivyojongea ndivyo hatimaye utaratibu fulani ulianza kumjia ndani ya mawazo yake ambapo huo ulisimama kama mpokeaji na mratibu wa taarifa zote zilizokuwa zikizidi kumiminika, kwamba hapo ndipo kumbukumbu halisi ilijiunda kwa kasi ya taratibu katika kumkumbusha, kumjulisha, kumhakikishia kweli ya halisi na kila kilichopelekwa ambacho huko kabla alijua huku akijitambua…

    ‘Nakubali nilipata ajali…lakini huko nilipokimbia ni kweli nilishiriki ule unyama?’ Alizungumza mawazoni kama uhakiki kwamba kwa kiasi fulani alikubali huku kwa kiasi kingine aligoma kujipokea alitenda!



    *****

    Huku akimuogopa askari, Obrien alijikakamua kumuuliza askari yule, “Afande nafahamu unajua kuhusu habari zangu. Please, nisaidie nijikumbuke vizuri. Nisaidie, kwani mambo mengine yananishangaza na kunitisha sana hasa hili jambo la kufungwa pingu huku nikidhihirisha nipo chini ya ulinzi. Eeh? Whom I scuffled against? Tell pal!”

    Askari alimtazama kwa dharau bila kuonyesha alisikia alichoulizwa; na muda kidogo tena, alichomoa kitabu mfukoni mwake na kufungua karatasi kadhaa kabla ya kuanza kusoma.

    “Please, help me knowing what I tussled over. (Tafadhali nijulishe nilikorofisha nini.)” Obrien alisema tena kwa kuongeza sauti yake lakini katika hali za utulivu.

    Askari aliinua kichwa chake, kisha alijibu taratibu kabla ya kuzama tena katika kitabu chake, “damu zimeanza mapema kukudhuru!”

    Obrien alishtuka!

    “Nini? Damu? Eeh…niliua?”

    “Sijui nikujibuje, yaelekea ubongo wako bado unamushkeli kadhaa. Hatahivyo, kama nilivyokueleza, damu za watu hizo! Oho, uuaji una mwisho wake…utaulipia!” Askari alijibu bila kumtazama.

    “Afande ni kweli naumwa, lakini si kwa kiwango cha kushindwa kujua jambo! That’s why napenda nifahamu ukweli zaidi...ila elewa kupata ajali si uuaji kama mtu hukufanya kwa makusudi…ooh, I remember that kid! Maskini…how’s he?”

    Askari aliinua kichwa chake tena, na kisha aliachia shari ya tazama ikitafsirika waziwazi!

    “Nisai…?”

    “Hey, close your gob lest I come up my most! (funga mdomo nisikasirike!)” Askari alikatiza kwa sauti ya ukali.

    Obrien aliona, aliijua maana!

    Na ndivyo aliufyata mdomo!

    Na alitetemeka sana akishika tafsiri kwamba alikuwa hatarini, kwamba ilikuwa ikisubiriwa apate nafuu ndipo aanze kuhojiwa kabla ya kupelekwa mahakamani kwa mashtaka; ndio, alielewa angepelekwa huko kama utaratibu wa kumfunga kama sio kuhukumiwa kifo kwa hatia ya kufanya mauaji!

    Ndivyo alisikitika sana!

    Akisikitika kwanini alikimbia!

    Akisikitika pia alisababisha ajali ambayo hapo bado hakujua kama yalikuwepo mashtaka mengine kwamba alisababisha hasara kwa baadhi ya mali ikiwa ni pamoja na kusababisha maumivu au vifo kwa watu kadhaa!

    Ndio, alisikitika sana, akiumia moyoni, akizidiwa na nguvu za hofu iliyozidi kumchota!

    Lakini, hatahivyo, hakujua maumivu na hofu hizo zilikuwa zikitengeneza hasira fulani yenye kuzaa!

    Ndio, hakujua sehemu fulani ya mawazo yake ilisimama kama historia ambayo ndiyo ilikuwa mtengenezaji wa tafsiri zilizovutwa na hisia kali kiasi cha kuzalisha maumivu na hofu zile huku hasira ikivimba taratibu ikinyemelea kushika hatamu!

    Ndivyo historia hiyo ilisema ikianika habari iliyonyakuliwa juujuu mithili ya mwewe anyakuapo kifaranga…Naam, habari ikawa wazi...



    *****

    Kwamba, Michelle Obrien aliikumbuka tarehe 20/08/1989; na hata asubuhi ya siku iliyofuatia pia aliikumbuka akihakikisha njonzi yake haikukosea sana!

    Ndivyo, aliacha kumtazama askari, akizivuta tena kumbukumbu zake, akafumba macho mithili alihitaji kupumzika kidogo; na hapo, macho ya mawazo yakaona nyumba moja chakavu…

    Hiyo akaitambua.

    Home!

    Lakini kabla hajasogezwa katika kufikiri zaidi, mara alijihisi akiwa ndani ya gari akiendesha huku simu ya mkononi ikiita!

    Simu hiyo ilikuwa chini ya mziki wake katika chumba kidogo kilichokuwa jirani na eneo la ‘gear’ ya gari; lakini simu hiyo iliunganishwa na waya wa ‘microphone’ iliyokuwa daima masikioni mwake. Na iliporuhusu sauti kutoka, alimsikia mteja wake wa kudumu akimjulisha alimtaka amfuate nyumbani kwake ili kumchukua kwa safari ya sinza, De-paradise.

    Mteja alikuwa Brigitte Wingly.





    ****

    Askari alitikisa kichwa pale tazamo zake zilipoacha kwa muda kuangalia kitabu alichokuwa akisoma kiitwacho ‘ I stalk Me’, ndio, alijikuta akitikisa kichwa baada ya kumuona Obrien akitabasamu huku kafumba macho yake, hata alisema kwa sauti ya chini, “not normal.”

    Ndivyo kabla ya kurejea tena katika kitabu chake kilichotungwa na ‘huyuhuyu mtunzi wako’, askari alijikuta akikubali pia inawezekana hata Obrien pia alikuwa akijitafuta kama muhusika katika hiyo riwaya alivyokuwa akijinyatia katika kujifukuza ili hatimaye aweze kujikamata na hata ikiwezekana ajisweke lupango!



    ****

    Mara tena…hali ilibadilika; kwamba, Obrien aliwaza akiamshwa na mchumba wake; na ndivyo kumfanya abaini alilala kwa ‘mshikaji wake’ usiku wa kuamkia tarehe 21/08/1989.

    “Mpenzi ulisema nikuamshe ikifika saa kumi.”

    “Mbona bado giza?” Usingizi uliokuwa bado na nguvu za kumchukua Obrien ulifanya aulize hivyo.

    Mpenzi wake aliyeitwa Ailin Chris alimuelekeza kutazama saa ya ukutani mara baada ya kuwasha taa yenye mwanga mkubwa.

    Obrien alipoangalia, aliishia kuitikia kwa kichwa; na kisha ndipo alijitoa kitandani.

    Alichukua khanga na kuvaa huku Ailin akimtazama kwa macho ambayo yaliachia utazamaji wenye ishara kwamba kuna kitu alihitaji akiseme au alihitaji atimiziwe kwanza; lakini kwakuwa Obrien hakumtazama, hakuweza kujua.

    “Mpenzi, haki yangu vipi?”

    Hapo Obrien alishtuka na kugeuka nyuma, kwani tayari alikuwa katika mlango wa kutokea.

    Alipomtazama, tayari walitazamana!

    Ailin alikuwa ameketi kitandani akiwa mtupu!

    Obrien akajua, akaendelea kumtazama kwanza huku taratibu akizivuta hisia kwa kurejea kumsaili utadhani ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kumtia machoni mwake!

    Alimtazama kwamba alikuwa ni mzuri wa wastani huku hisia zikivuma zaidi katika kusisimshwa na ukubali wa mvuto wa matako na mapaja yake; na si kwamba hapo aliona yote, bali mawazo pia yalifanya kwa kumchorea umbo lote kama lilivyokuwa likijulikana mbele zake!

    Alipokumbuka unyororo wa ngozi yake iliyokuwa ya maji ya kunde, ndivyo hatua za kumsogelea tena zilianzishwa; na kadri alivyomjongelea ndivyo tazama zake ziliongeza msisimko wa mwili wake kutokana na kuangalia kilafi sura yake ndefu kiasi ikiwa ni pamoja na kuikodolea pua yake ya kuchongoka ambayo alizoea kumtania kwa kumuita, ‘kipenzi mwenye pua ya kizungu’.

    Alipomfikia tayari Ailin alikuwa akihema!

    Akaitupa ile khanga, akabakia asiyevishwa!

    Kwamba, wote wakarejea wakiwa watupu!

    Huku akitetemeka na kuzidi kuhema, Ailin alijilaza ‘kifo cha mende’ huku akifumba macho katika utayarisho, kwani hakutaka kuchezea muda kwa kujua Obrien alitakiwa kumuwahi mteja wake huko tabata asubuhi na mapema; na ndivyo kwa mlalo huo, kile kifua chake kilifunikwa kiasi na matiti yake yaliyokuwa makubwa kuliko kiwiliwili lakini yaliyovimba mithili ya yule mama wa kimarekani wa kufokafoka…Qeen Latifa!

    Obrien akajilaza kiasi akitokea maeneo ya miguuni ambapo licha ya kuitomasa miguu hiyo, pia aliilambalamba; na halikadhalika, ndivyo pia alimtanua akimfungua kwa kuruhusu mikono yake kusawazisha njia huku yeye mwenyewe akiongezeka kuhema na akishuhudia mwenzake akitetemeka huku pia ishara za miguno ya hapa na pale vikitawala sehemu!



    *****

    Mihemo ya Obrien ilipozidi sana ndipo askari yule aliinua kichwa chake tena, na hivyo kumuona jinsi alivyokuwa akijinyonganyonga huku pumua zake zikisomeka mithili ya mtu aliyetetemeshwa na jambo lililochokoza hisia kali! Hata alitikisa kichwa huku akiamua kukifunga kitabu chake, maana alibaini asingeweza kukifaidi katika mazingira yale; na hivyo, sasa aliamua kumtazama ili aone mwisho wake huku hisia fulani zikimueleza ingekuwa vyema kama angekwenda kumjulisha nesi juu ya hali hiyo ya kushangaza, ingawaje, hatahivyo, jeuri yake pia ilikazana kujisimika kwa kumueleza kwamba hilo halikumuhusu sana, kwani alikumbushwa hapo alikuwepo kwa ajili ya kuhakikisha usalama na si vinginevyo!

    Ndivyo, alibaki akimtazama, akimshangaa!

    Lakini kwa upande wa Obrien, mihemo ile ilikuwa na maana ileile, kwamba, hapo alitumbukizwa mzimamzima ndani ya mawazo yake yaliyobebwa na hisia zake katika kutambulisha hali ilivyokuwa siku ile ya tarehe 21/08/1989.

    Kwamba, sio aliota tu;

    Kwamba, sio aliwaza tu;

    Kwamba, hivyo alikuwa akikumbushwa aliyofanya; kwamba, hapo yalikuwa ni matokeo ya kuudandia mwili wa mpenzi wake aliyetaka ‘ashughulikiwe’ kabla Obrien hajaondoka kumfuata Brigitte (mteja wake) huko nyumbani kwake mtaa wa Damascus, tabata.

    Hivyo, wakati akionwa kama ‘kituko’ mbele za macho ya askari; lakini Obrien hakuwa hivyo, kwamba hapo alikumbushwa akianza kuutayarisha ‘mswaki’ huku ‘mdomo’ ukijua kuruhusu utibiwe!

    Ndio, Obrien alijiona ‘akimkwea’ mpenzi wake taratibu kuelekea katika mapaja yaliyoachanishwa, kwamba hivyo alisogea mithili ya kinyonga na ulimi wake uliojua kumchota mdudu aliye mbali!

    Lakini hakutulia sana alipofika ‘makutano ya mapaja’; kwani baada ya kasheshe fupi zilizofanywa na mkono wake mmoja katika ‘kuhamasisha’, basi alipitiliza juu yake hadi kitovuni ambapo ulimi uliachiwa kuchezacheza huku taratibu akiendelea kuukwea mlima huku halikadhalika akishuhudia jinsi Ailin alivyozidisha kuhema!



    Mikono ilipoyagusa matiti, Ailin alijikuta hata akisema kwa kuweweseka, akilalama alizidiwa na kasi ya mwendo, kwasababu alikiri aliiva tayari!

    Akikiri alishindwa wasianze!

    Akikiri ashindwa asiliwe!

    Akikiri ashindwa wasilane!

    Na ndivyo Obrien hata aliteremka ‘kuteremkiana’!



    *****

    Askari alishangaa zaidi pale alipomuona Obrien akitokwa udenda uliomchomoka hata kwa sauti kusikika!

    “Kheh, jamaa linaota nini? Makubwa!” askari alijisemea kabla ya kuangua kicheko ambacho bado hakikuweza kutibua maisha ya mawazoni mwa Obrien ambaye alizidi kutumbukizwa ndani ya raha akishirikiana na mwenzake kuisaka ilipo ‘kona ya raha’ ili kupiga krosi ya kuifikia!



    “7” Obrien aliendelea kukumbuka; alikumbuka aliwasili nyumbani kwa Brigitte alfajiri na mapema ili kuwahi kumpeleka kazini kama walivyokubaliana jana yake wakati alipokuja kumchukua kwa safari ya kwenda baa ya De-paradise huko sinza.

    Alilipaki gari lake pembeni ya nyumba hiyo. Lakini hakutoka ndani ya gari; alikirudisha nyuma kiti chake. Akaiweka mikono yake yote miwili nyuma ya kichwa chake kabla ya kujilaza kidogo huku muziki tulivu ukiendelea kumliwaza kwani hakuizima redio ya gari.

    Alijilaza hivyo hadi ilipotimu saa 7.30 ndipo akakirudisha kiti chake kama kilivyokuwa mwanzo, akapiga honi mara tatu lakini akiwa ametulia humo humo garini.

    Alitulia hivyo hivyo kwa muda wa dakika kama kumi hivi bila kuona dalili ya mtu kutoka ndani ya nyumba hiyo ya ghorofa moja.

    Akapiga honi nyingine!

    Bado kukawa kimya tu!

    Akatulia kidogo na kisha baadaye akatoka ndani ya gari na kuanza kuelekea zilipo ngazi za kupandia juu ambako ndipo aliishi Brigitte.

    Alipanda hadi katika kibaraza.

    Alipofika, akakisogelea kibonyeza kengele.

    Alipokifikia, alibonyeza na kutulia ili kusikiliza…

    Alipoona alisubiri sekundi nyingi, alibonyeza tena!

    Ooh…wapi, hakupata jibu!

    Hisia zilipotaka kumueleza pengine umeme haukuwepo ndivyo macho yalisuta, kwani aliona uwakaji wa taa ndani ya nyumba!





    Akabonyeza tena na tena...bado, alijibiwa vilevile; kwamba, ukimya ulisimama imara!

    Sasa aliutazama mlango kwa muda huku akiwaza kwamba pengine kengele ilikuwa mbovu au vinginevyo hakukuwemo mtu; na ndivyo kadri alivyozidi kuwaza ndivyo hata alijikuta akikikamata kitasa cha mlango…

    Hicho, akaanza kukizungurusha taratibu huku hisia zake zingine zikitamani azuiwe kuthubutu kuendelea kufanya hivyo bila kutoa sababu zilizoshibishwa hoja...

    Kutamakia…

    Mlango ulifunguka!

    Akashangaa kwa sekunde kadhaa bila kujua alianza kuwaza nini; na baadaye alijikuta akitoa sauti kubwa ya kumuita Brigitte kwa jina la ‘dada’!

    Ndivyo huku akiendelea kumuita, ndivyo pia alianza kuingia ndani taratibu huku ile hisia yake iliyotaka asifungue mlango ikiwa mtangulizi katika kurejea mawazoni mwake huku sasa akizidisha sauti katika kuvuma kwamba halikuwa jambo jema kujikaribisha ndani bila kukaribishwa, kwamba mawazo hayo yalikuwa mithili yakitoa onyo fulani kwa njia ya ‘machale’.

    Onyo lipi? Hilo, mawazo hayakusema, isipokuwa bado yalipiga kelele abadilishe muondoko!



    Mara…ay, mawazo yalitibuliwa!

    Kwani pua zilinasa harufu! Harufu kali, harufu nzito!

    Na hapohapo macho yake yalisafiri hadi kuganda sehemu moja sakafuni ambapo kiumbe kilionekana!

    Mamaa, alimuona mtu!

    Alikuwa amelala; pia akaona damu!

    Alipotazama zaidi, aligundua sehemu yote hata alipokanyaga, damu zilitapakaa!

    ‘Amekufa!’ Sauti moja ikasema mawazoni ikiwa ni aina nyingine ya kengele ya hatari; na hapohapo, mawazo tofauti yaliyokuwa yakibishana huku mengi yakiwa ni ‘hoja za nguvu’ zilizomjia ovyoovyo yalimiminika sana kiasi kichwa kilimuuma huku akivamiwa na kizunguzungu!

    Pia ndivyo hofu ilianza kukamata nafasi kwa kasi kubwa huku mwili ukifanywa kutetemeka…lakini…mara?

    Ndivyo kama aliyekurupushwa, alitoka ndani ya nyumba kiasi alipofika nje alipitiliza kwa kuzishuka ngazi; lakini akiwa katikati ya ngazi, alitereza!

    Akaserereka hadi chini!

    Hatahivyo, maramoja aliinuka bila kusikiliza au kujitazama kama aliumia au vipi na kuikimbilia gari yake!

    Alihema sana, hofu ikizidi kusogea kushika usukani!



    Aliingia ndani ya gari na kuliondosha kwa mwendo mkali sana bila kujali ufupi wa barabara na hivyo kufanya gari kuyumba sana hata baada ya kugeuza uelekeo!

    Alipofika kwenye kona ya kuuacha barabara ya mtaa huo wa damascus, alipinda kona kali na kujikuta akimgonga kijana mmoja aliyekuwa pembezoni akiuza mikate na vitu vingine kadhaa vilivyokuwa katika meza yake kiasi kijana yule alirushwa juu kabla ya chini pembeni mwa barabara na meza yake ilipondeka vibaya!

    Watu kadhaa wakiwamo wauzaji wa pale gengeni walipigwa bumbuwazi; bado Obrien hakusimama wala kushtuka, kwani hisia zake zilikuwa tayari zimejiweka mtawala mwenye madaraka kamili kuendesha mwili wake katika kufanya; na ndivyo kutamakia, gari lilipitiliza na kujikuta hata likikwaruzana na gari jingine (toyota-markII) wakati akiingia barabara kuu ya mawenzi!

    Toyota ile ilikosa mwelekeo na hivyo iliserereka hadi pembeni kabisa mwa barabara hadi iligonga ukuta wa nyumba moja! Maskini, watu wote ndani ya gari hiyo walikufa palepale; watu hao walikuwa ni mwanaume mmoja aliyekuwa ndiye dereva akiwa na mkewe na watoto wao watatu ambapo wawili walikuwa wanaume!



    Obrien ndio kwanza alizidisha mwendo; na kwakuwa tayari alionyesha kushindwa kuidhibiti hofu yake, ndivyo alisababisha ashindwe kumiliki gari hilo kiasi hata alilitumbukiza darajani baada ya kushindwa kukata mduara katika kuupanda muinuko ili kuanza kuelekea tabata-bima!



    ****

    Ukelele mkubwa aliopiga Obrien ulifanya askari ainuke, kwani sasa ulimfanya avutwe zaidi katika kuona ulikuwepo umuhimu wa kutoa taarifa kwa daktari kuhusu hayo aliyokuwa akiyaona!

    Obrien alifungua macho huku akihema kama alivyofanya mwanzoni wakati alipokurupushwa usingizini na ile ndoto iliyokuwa chachu ya kukumbuka haya yote.

    Sasa alikubali alikuwa hatarini.

    Ndivyo alihofu sana huku akijaa maumivu makubwa moyoni achilia mbali yale maumivu yake ya kimwili ambayo bado alihisi hayakuwa yameondoka hata kama tayari alikuwa na nafuu kubwa.

    Waliangaliana na askari kwa muda si mrefu sana kabla ya kujikuta akiamua kufumba macho huku akihema zaidi ya kawaida…



    *****

    Hata baada ya wiki moja, bado Obrien hakujua mtu (akihisi alikuwa amekufa) aliyemkuta asubuhi ile nyumbani kwa Brigitte alikuwa nani. Na kwakuwa si askari wala wauguzi wake hawakutaka kujulisha, ndivyo hakuweza kujua kabisa; hatahivyo, alikuwa na uhakika hapo aliletwa kutokana na kupata ajali mbaya ya gari huku akielewa pia alilindwa vile kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya kusababisha uharibifu na pengine mauaji! Halikadhalika, hisia zilikazana kumjulisha kwamba ilikuwa ni kweli alituhumiwa kuhusika na kifo cha yule mtu aliyemkuta barazani kwa Brigitte!

    Na ndivyo kufikiri huko kulimuumiza sana, kwani hakukuweza kuwa msaada katika kumpatia majibu muafaka kuhusu ni namna gani angeweza kutenda katika kujiopoa nje ya janga hilo ambalo msingi wake alijua uliletwa na woga wa upumbavu wake kwa kule kuamua kukimbia kwa pupa bila kufikiri vyema!

    Ndivyo huku akiendelea kuumizwa moyoni, aliona hakukuwa na namna njema ya kuanza kuelewa uzito wa janga lake isipokuwa ni kusubiri kuja kuhojiwa ambako sasa alijua kulikuwa ni habari isiyoweza kuzidi wiki hivi kutokana na jinsi afya yake ilivyokuwa ikielekea mahala pa kutia matumaini katika kupona.



    *****

    KWA SIKU NZIMA ya tarehe 11 ambayo iliangukia siku ya alhamisi ndani ya juma la pili la mwezi januari katika mwaka huo wa 1990 ulioanza vibaya tofauti na miaka mingine, Hushley Collin aliamua kujifungia nyumbani kwake akiwa muda mwingi amelala pamoja na mmoja wa wanawake zake ambapo nyakati fulani huchangua mmoja wao na kumualika kumtembelea kwa ajili ya habari za kimapenzi; hatahivyo, hivi hufanya mara chache sana kutokana na tabia yake ya kutopenda kuruhusu mazingira ya wapenzi wake kujizoesha kuwasili nyumbani kwake vile wapendavyo ikiwa ni pamoja na kukwepa kujikuta hatimaye akin’gan’ganiwa kwa kugandwa mithili ya kupe katika mwili. Ndio, alipenda uhuru na upweke.

    Kipindi hiki hata mfanyakazi wake wa ndani aliyekuwa na nasaba naye alipewa nafasi ya kutembelea jamaa; na ndivyo kuachwa ndani ya nyumba wakiwa wawili tu huku nje ya jengo akiwepo Bonnet (mlinzi) ambaye licha ya kuwa na ujamaa naye lakini pia alikuwa mtu wake wa karibu sana kwa shughuli nyeti.



    Aliamua kuwa hivyo ili kujipatia nafasi nzuri katika kusubiri matokeo ya kazi aliyomtuma kijana wake huko hospitali ya Muhimbili ili kumuua Michelle Obrien ikiwa ni harakati zake za kuhakikisha akizima nafasi zote ambazo polisi wangeweza kuzitumia katika kujipenyeza hata kuweza kupata habari zitakazowafanya kujua habari nzima ya mauji ya Brigitte.

    Ndio, hakutaka polisi ipate mwanya utakaozalisha kujulikana kwa habari zao za kufanya biashara ya madawa ya kulevya chini ya mzee Kasonzo; na ndivyo ili kuhakikisha nafasi hiyo haizaliwi alipanga ijulikane Edwin hakuwepo nchini muda mrefu, jambo ambalo kwa mara ya kwanza alitenda kabla ya kumjulisha mkuu wao.



    Sasa hapo alitulia akistarehe na mmoja wa wapenzi wake huku akisubiri matokeo ambayo yalikuwa ni juhudi ya pili ya kumuondoa Obrien baada ya kushindikana ile ya awali ambayo ilitakiwa wamdunge sindano yenye sumu kama siyo kumnywesha sumu!

    Akiwa ni mwenye kusubiri hakupenda kujikumbusha habari hii wala agizo alilolitoa kwa kijana wake, kwani aliona ilikuwa ni vizuri zaidi awe katika subira huku akiburudishwa na mapenzi ya mwanamke wake akichanganya na starehe zingine kama vile kuvuta bangi ambapo walivuta wote huku wakiwa uchi wa mnyama!





    Lakini kutopenda kwake si kwamba aliweza asijikute akiwaza hali kama ilivyotokea usiku ule wa jumapili ya kuamkia tarehe 21/08/1989; ndio, nyakati fulani fulani alijiwa na kuwaza huko ambako kulimfanya kuishia kuilaani sana siku hiyo hasa pale mawazo yalipomkumbusha kwa kuchora mwili wa bosi wake (uliolowa damu) ukiwa umelala pembeni huku utumbo umetoka nje na kichwa chake kikishikiliwa na ngozi tu kama matokeo ya kuchinjwa!

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****

    NDIO, ALHAMISI HIYO, mtu mmoja aliyevalia koti jeupe na refu aliingia ndani ya chumba alicholazwa Michelle Obrien, na moja kwa moja aligeuka kumtazama askari aliyekuwa bado kaketi pembeni ya mlango akijisomea kitabu kama ilivyokuwa hulka yake kila awapo katika nafasi ya kuvuna upweke fulani hata kama si kwasababu ya kuwa peke yake.

    Wakati huo Obrien alikuwa mithili aliyekuwa usingizini kutokana na kule kufumba macho.

    Hapo ilikuwa katika majira ya asubuhi ambayo haikuzidi saa 5.30 ingawaje pia ilikuwa ni baada ya saa 3; halikadhalika, ilikuwa ni siku ya tano tangu Obrien atoke kuhojiwa na Inspekta Hughes.



    “Habari yako daktari” Askari aliwahi kutoa salamu huku akijiinua taratibu.

    Mtu yule alichelewa kujibu, kwani ndivyo kwanza aligeuza shingo na kumtazama Obrien kabla ya kurejesha tazamo lake kwa askari; na kisha ndipo alijibu taratibu na kwa sauti ya chini, “shwari Bwana askari.”

    Wakati macho ya askari yakionyesha kuingizwa kushangazwa, ndivyo pia mkono wake wa kushoto ulianza taratibu safari ya kujipeleka kiunoni ili uweze kuwahi kuchukua kitu fulani…na hivyo, alipenda mkono huo upelekwe haraka huko, lakini kwakuwa alijua kufanya hivyo ingekuwa ni kujiweka ndani ya hatari zaidi kama ni kweli hisia zake zilinena sahihi kuwa hapo iliwezekana ‘hatari’ ilikuwa ikivamia nafasi! Kwamba, askari alihisi kama hapo angeonwa na huku ‘hatari hiyo’ iwe ni jambo hakika, basi angewahiwa kirahisi tu, kwani ule mkono mmoja wa huyo mtu ulikuwa tayari ndani ya mfuko wa koti lake ukiachia hali iliyotengeneza hisia pengine ilikuwa tayari ‘kitu’ kilishikwa!

    Hivyo, mkono ukapelekwa taratibu huku akisema, “wewe pia ni daktari?”

    Mtu yule aliitikia kwa kichwa huku akikenua meno yake yalioonyesha kuchakazwa na uvutaji wa sigara; na hali hiyo ilizidi kuvuta hisia za askari kwamba dalili zilikuwa na nguvu katika kumtilia wasiwasi mtu huyo!

    Sasa mkono wa askari ulikaribia sana kufika, na ndivyo spidi ikaongezwa…

    Lakini, mara…?

    Mtu yule alisema huku akiachia tabasamu ambalo hatahivyo lilitapika kinamna ishara za dhihaka, “tafadhali inua mikono juu.”

    Kusikia hivyo, ule mkono wa askari ukasimamisha zoezi, lakini ulitulia hapohapo kwamba hakutii ile amri kwa kujifanya kama hakusikia tishio hilo; na bado, macho yake yalijifanya mithili yalipepesa ingawaje katika hali halisi yalikuwa yametulia yakikodoa hapo katika mkono uliokuwa ndani ya koti la mtu huyo!

    Kengele ya hatari iligonga rasmi!

    “Inua mikono juu, kwani hisia zako hazikudanganyi!” Yule mtu sasa alisema kwa kufoka huku akimsogelea askari, “hatahivyo, wewe si uliyefuatwa kama unathamini maisha yako.”

    Askari alianza kuinua mikono juu huku ubongoni hesabu nyingi zikipigwa, kwani sasa tayari ilidhihiri alikuwa jirani sana na mdomo wa mauti uliokuwa tayari kummeza na hivyo kuufanya ‘uhai wake’ upeperushwe kwa kuachanishwa na maumbile.

    Mtu yule sasa alikuwa jirani sana.



    Lakini ghafla…aah!

    Ndio…ghafla mtu huyo si tu alisita kujongea, bali kwa haraka sana pia alipiga hatua mbili nyuma! Ndio, hivyo alitenda kwakuwa aliliona teke la askari lilivyorushwa likiwa limelenga shabaha kuupiga ule mkono wake uliokuwa ndani ya mfuko wa koti; na ndivyo hatua zake za kurudi nyuma ziliweza kupunguza nguvu za teke hilo ambalo bado lilifanikiwa kujibamiza katika shabaha iliyokusudiwa!

    “Pumbavu!” Mtu yule alifoka huku akipepesuka na kuashiria kiasi fulani teke hilo liliweza kumuumiza licha ya kule kupunguzwa makali yake!

    Askari alijua haikutosha; na ndivyo mara moja huku akiruka hewani alizungusha mguu wake mwingine na kumtandika usoni mtu yule kiasi cha kumfanya azungushwe mithili ya mpira huku akidondoka chini!

    Askari akasimama huku akihema sana; lakini bado alichelewa, kwani mtu yule akiwa chali huko chini aliwahi kuiruhusu bastola yake itende ambayo sasa ilikuwa nje ya mfuko; na ndivyo risasi mbili zilizoachiwa zilifumua kichwa chake huku zikimrusha hadi kumfanya ajigonge ukutani!

    Obrien alifungua macho kutokana na kelele za uyowe wa sekunde uliomtoka askari, kwani bastola haikutoa sauti kutokana na kuwa na kiwambo!



    ****

    Mtu yule alijizoa hapo chini, akaamka huku akisikilizia maumivu makali katika shavu lake la kulia ambalo ndilo lilipokea kipigo kilichopelekea kudondoka chini.

    Ule mkono usioshikilia bastola uliposhika mdomo katika harakati za kujikagua, ndivyo alitanabahi kuona zilikuwepo damu zikitokea puani!

    “Bastard!” Alisema huku akitoa leso mfukoni mwa suruali yake na kuanza kujifuta huku akimsogelea askari yule ili kupata uhakika kama tayari alikuwa ni maiti kama sasa alivyotaka iwe.

    Alipomfikia, alimtazama kwa sekunde chache huku akimalizia kujifuta damu. Kisha alisema huku akianza kugeuka na halikadhalika akiirudisha leso mfukoni, “Off the plan though you worthy of it! (Umestahili hata kama hatukupanga iwe hivi!)”

    Kabla mtu yule hajamaliza kugeuka, tayari akili za Obrien zilibaini uwepo wa hatari; lakini, kwakuwa alikuwa kafungwa mkono wake mmoja katika fumbati moja ya kitanda, basi ndivyo kwanza aliona hakuwa na namna ya kuweza kuinuka zaidi ya kutulia kitandani akisubiri nini kitakachofuatia! Hatahivyo, akili iligoma kukubali; na ndivyo kazi ya ziada ilihakikisha ikifanyika kwa haraka sana!

    Mtu yule alipogeuka, wawili hao waliweza kutazamana kwa sekunde kadhaa bila neno kusemwa huku mmoja akionyesha dharau na hali za kujiamini huku mwingine akionekana kutotulia na akiwa ndani ya mashaka matupu!



    “Ndugu sielewi unachofuata.” Obrien aliweza kuuliza huku akijitahidi kuachia taswira kwamba hakuwa ndani ya hofu sana.

    Mtu yule hakujibu; na badala yake alikuwa akiigeuzageuza bastola yake.

    “Sema au fanya kilichokuleta.” Obrien alisisitiza.

    “Sitakuua kabla sijakujulisha,” Mtu yule alisema huku akivua koti lake kwa kutumia mkono mwingine, “ni kweli hujatukosea ingawaje ni sahihi nimekuja kuifukuza roho.”

    Obrien akashtuka!

    “Kifo chako ni usalama.”

    Obrien alishtuka zaidi, hatahivyo baada ya sekunde chache alijikuta akiweza kuuliza huku akili zikizidi kuzunguka sana katika jitihada za kutafuta njia za kujiokoa; “kunionea ndio usalama? Usalama wa nani? Sikuelewi kama unataka nijue!”

    “Ukiondoa ajali uliyopata, nathibitisha uhusiki na hizi tuhuma zingine!”

    “Ati…?”

    “Huku nikikuaga, napenda niseme hivi,” aliendelea kusema mtu yule huku akimalizia kuegesha koti katika ule mkono mwingine baada ya kumaliza kuivua. ‘nisamehe kwamba nakuua ingawaje sipaswi kulaumiwa, kwani mlaumiwa ni mazingira yaliyokumeza.”

    Macho ya Obrien yakatumbuka!

    Na wakati huohuo, mtu yule alianza kuinua bastola taratibu huku akiendelea kutabasamu utadhani alichokuwa akikitenda kilikuwa ni uungwana...







    “Hapana…aah, naomba nijulishe ili nijue unaniua kwa sababu zipi! Eeh…jamani, nimekosea nini?” Obrien alijaribu kujitetea akisaka muda zaidi wa kuweza kujinusuru, na hadi hapo bado hakujua atendeje ili kujinasua.

    Mtu yule akacheka kidogo huku akiteremsha silaha, na kisha alisema kwa sauti ya kuonyesha kumuhurumia, “narudia kusema, nisamehe sana kwa mwendo huu kwani hujatukosea.” Aliendelea, “ila nikikuacha, maisha yatakuwa hatarini.”

    Obrien alihema sana kwa hofu akiona kama sio kuhisi zilibakia sekunde kadhaa atenganishwe na mwili!

    Akiwa ameshusha chini mkono ulioshika bastola, mtu huyo aliendelea kusema huku wakati fulani akitazama pembeni hasa hapo katika mwili wa yule askari, “skiliza…hili tatizo limezaliwa na Brigitte, mteja wako! Bila yeye hapa nisingekuwepo!” Mtu huyo aliendelea kusema, na sasa alisema kwa harakaharaka mithili alihitaji kuwahi jambo, “Hata wewe usingekuwepo hapa bila yeye! Au?”

    “Ni kweli ndugu yangu!” Obrien alijibu bila kujua sauti na uso wake vilieleza mithili alikuwa ndani ya unyonge.

    “Laumu mapenzi, laumu mazingira! Ndio, mlaumu Brigitte kwa tamaa ya kuchanganya wanaume!”

    “Nihurumie!”

    “Kukusafirisha ni wajibu ili tusizalishe mazingira ambayo yataweza kumtumbukiza hatarini hata bosi wetu asiyehusika na upuuzi huu…mmh, Mbilikimo anachukia sana kuona bado unapumua huku Bob Collin akipenda kusikia hupumui tena baada ya mpango wa kukupiga sindano ya sumu kutofanikiwa.”

    Kijasho chembamba kilianza kumvuja Obrien huku akijitahidi kufukuza mawengewenge yaliyoanza kutaka kujikaribisha; na hivyo alifanya ili kuhakikisha mwili ulikuwa na nguvu wakati wote huku pia akiachia akili ishughulike na suala moja la kuona ni kwa namna gani angeweza kujinasua dhidi ya kifo hiki ambacho alikubali kilikuwa sentimita chache sana kumfikia kumrarua. Na bado alijua ni muendelezo wa maneno ndio ulikuwa nafasi zake za mwisho kuweza kujinusuru…vinginevyo, alijua alikuwa ni mtu wa kufa baada ya sekunde kadhaa!

    “Tunazo taarifa unayo matatizo ya kuweza kujikumbuka ila kuna nafuu fulani ambazo umeanza kuzipata ambazo sisi hatuzipendi. Kweli tulichukia ulivyozinduka, kwani tulipenda ufe sisi tusifanye!”

    Obrien alikapua macho!

    “My hands wouldn’t let you breath!”

    Akimuacha Obrien akizidi kukapua macho, mtu yule aliendelea kusema zaidi, “ kama unakumbuka vyema, basi yule uliyemkuta barazani ndiye alifanya mauaji hayo ingawaje nasikitika sana zile risasi tatu alizolishwa na Collin hazikuweza kummaliza. Nina uhakika Marlon hatapona, na hata akipona mimi ndiye nitamrudia kabla hajapata uwezo wa kusema.” Mtu huyo alitulia kidogo kabla ya kuendelea tena, “Marlon alimuua Edwin, ila Bob ndiye aliyemtoa ili polisi wasijemkuta na hivyo kuanza kupeleleza mambo yetu. Damned right, we’re real pushers, the big one with big hands from the government!”

    “Duh!”

    “Yeah, sometimes we live by human spare-parts.”

    “Na Brigitte?” Obrien aliuliza tena. Na wakati huohuo bila kusubiri majibu, ndivyo pia alijikuta amefanya kuiwahi ‘hatari’ kabla haijafanikiwa kumrarua, kwani hakika hakujua hicho alichokifanya kama kilikuwa ni mpango kamili uliojengwa na akili zake zaidi ya kule kujikuta maramoja akiwa ametumia ule mkono wake uliofungwa pingu kushikilia kwa nguvu zote mfumbati wa kitanda huku kwa wakati huohuo akiubinua mwili mzima upande aliokuwepo mtu huyo huku mguu mmoja ukirushwa kwa nguvu pia! Na ni hapo ndipo teke nzito liliwahi kuupiga mkono wa mtu huyo uliokuwa umeshikilia bastola kizembe na hivyo kufanya idondoke chini!

    Kilichofuatia, alimuangukia mtu huyo!

    Kwamba, wote walidondoka sakafuni huku kitanda kikiwaangukia pia; na hapohapo, mkono huru wa Obrien ukafanikiwa kukamata shingo ya mtu huyo na ukihakikisha ukikaba kisawasawa!

    Kweli alifanya hasa!

    Mtu huyo alijitahidi kujinasua bila mafanikio kutokana na Obrien kuhakikisha alikaba hasa huku akili zake zikimjulisha mwendo huo ndio ulikuwa usalama pekee kwamba hakutakiwa kukosea hata kiduchu!

    Ndivyo mtu huyo alitapatapa huku povu jingi likimtoka!



    Baada ya dakika kadhaa za kuona mtu huyo akiashiria kuzidiwa nguvu, ndipo Obrien alianza kumkokota kuelekea ilipokuwa imeanguka bastola ya askari (marehemu); lakini aliendelea kumkaba kwa dakika kama kumi hivi kabla ya kuamua kumuachia na kuiwahi bastola!

    Kwanza alitulia sekunde kadhaa akihema sana kabla ya kuamua kuachanisha ule mkono wake uliofungwa pingu kwa kuupiga risasi mnyororo wake!



    *****

    Ndivyo akiwa ametulia na bado akihema sana ndivyo hofu ilianza kushuka taratibu huku hasira ikijaza nafasi yake kiasi hata alifura sana!

    Naam, alifura sana huku akihisi alitakiwa kutoroka; lakini si kwamba alihisi alitakiwa kufanya hivyo kwasababu za kushikwa na hofu…la haikuwa hivyo! Ni kwamba hisia zilimueleza hivyo kwa maana ya kutengeneza nafasi ya kuwasaka wote waliomtumbukiza katika janga hili; na pia hivyo alielezwa kama tafsiri kwamba polisi hawakuwa makini katika kutimiza wajibu zao katika kutetea haki za wasiokuwa na hatia, yaani ilikuwa ni habari sahihi awakimbie kwanza kabla hajaamua nini atende katika kujibu hicho alichoita ‘uzembe wa polisi’!

    Kila sauti ya kujidai ya mtu huyo ilivyokuwa ikijirudiarudia mawazoni mwake, ndivyo alikubali alihitaji kupata muda wa kutafuta ni kwanini alikuwa anasakwa kuuawa na watu asiowajua kabla ya kujua namna za kujinasua dhidi ya tuhuma hizo za kudaiwa kuhusika katika mauaji ya damascus ambapo sasa amejulishwa si Brigitte pekee aliyekufa, bali kumbe bwana wake mpya pia aliuawa!

    “Edwin is dead…polisi hawajui!” Alisema kwa sauti.

    Lakini pia alitambua kwa kuamua kutoroka ndivyo zaidi alikuwa akijiweka hatarini katika kuonekana ni muuaji na hivyo kufanywa kuwa mtu hatari sana mbele za jamii; na halikadhalika, alitambua hatari ingekuwa jirani sana dhidi ya usalama wake kama ataendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi, kwani hao wanaomsaka bado hakuwajua!

    Hatahivyo, mawazo hayo hayakumzonga sana, kwani mwishowe alivutwa kukubali ilikuwa ni muafaka kuamua kutoroka ili kufanikisha kujenga nafasi za kuweza kuwajua waliokuwa wakimsaka ambao aliamini ndio waliokuwa na majibu sahihi ya sakata hili lililomkuta.

    Wakati hali ilibainisha ni kweli alifura kwa hasira, lakini ndivyo hali ilibainisha halikadhalika akili zake ziliweza kutafakari ingawaje kimsingi hizo ziliongozwa na hasira hiyo ambayo bado ilikuwa ikijijaza zaidi kabla ya kuzaa.



    *****

    Kwanza, aliisogelea ile bastola iliyotupwa na yule askari; na wakati akitaka kuifutika mfukoni mara baada ya kuinama na kuichukua, wazo jingine likamvaa na hata kumfanya aseme ingawaje alifanya kwa sauti ya chini sana, “hizi nguo noma!”

    Alipepesa huku na huko kwa sekunde kadhaa kabla ya kugandisha tazamo lake mbele ya mtu yule.

    Hapo alitabasamu kabla ya kuanza kumsogelea; na alipomfikia ndipo kazi ya kumvua ikaanzishwa ambayo ilichukua si dakika nyingi.

    Aliliokota koti lile na kulikagua kidogo, na kisha alilivaa huku akikubali halikuchafuka sana kiasi cha kutia shaka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alianza kuvaa suruali ya mtu yule mara baada ya kuvua pajama lake; lakini alijikuta akiahirisha zoezi hilo huku machale fulani yakichukua nafasi pana ndani ya hisia zake!

    ‘Nini?’ Alijiuliza huku mkono mmoja ukianza kuingia ndani ya mfuko wa suruali ya mtu yule ambao ulionekana kutuna; lakini, punde kidogo aliamua kuahirisha zoezi hilo kwa kuuondoa mkono mfukoni huku hisia bado zikizidi kumuwasha kwamba alipenda ajue nini hivyo vilikuwa!

    Ndipo aliendelea kumvua suruali…





    Na viatu pia alimvua huku akidharau kumvua soksi.



    Alipumua kwa furaha zaidi mara alipomaliza kuvaa mavazi yote na kuona hayakumkaa vibaya kiasi cha kumshtua mtu yoyote huku silaha ile akiifutika katika mfuko wa kulia wa koti lile. Hatahivyo, ili suruali kuweza kumkaa vyema ilibidi kuikunja kiaina kiunoni.

    Hata pumua zake zilipungua sana ingawaje ujazo wa hasira ulikuwa ukitembea vilevile lakini sasa ukiwa kwa habari ya kuhakikisha hakurudishwa nyuma tena katika kuhitaji kutekeleza kile hasira ilichoamua kitendwe hadi wakati huo.

    Mara, wazo la kutaka kujua vilivyomo katika ule mfuko lilirejea tena ili kuhakikisha aliingizwa kujua nini vilihifadhiwa; basi, ndivyo alitumbukiza tena mkono…

    Hata akavishika…pumzi ya shauku ikamdaka zaidi!

    “Nahisi…au, aah?” Alishindwa kumalizia zaidi ya kujikuta akishuhudia mkono ukitoa kitu.

    Alitoa pochi!

    Akapumua tena!

    Mkono ukazama tena baada ya mkono mwingine kukabidhiwa ile pochi; huko uliibua simu ya mkononi ambayo mara moja ilirejeshwa!

    Kisha alifanya kuifungua pochi kidogo ili kuruhusu udadisi kukamata nafasi iliyohitaji…lakini…aah, mara moja aliifunga tena bila kutaka kujua idadi ilisemaje, kwani tayari akili ilijibu hadi hapo ilitosha sawasawa kama ilivyoonwa simu!

    Kwamba, aliziona zilizojaa!

    Pumzi ya furaha ikamtoka tena huku pochi ikirejeshwa hukohuko ilipotolewa; na ndivyo hata ikawa alianza kuufungua mlango wa chumba, akifungua taratibu na kwa tahadhari kubwa…



    Alipomaliza kufungua mlango, alichungulia nje ili kuruhusu macho yake kusafiri pande zote katika kutazama kama usalama ulikuwepo. Kama ambavyo kushoto kwake kulikuwa ni utupu, ndivyo pia alibaini hata kulia ilitoa jibu lilelile; kwamba, korido lilikuwa ukiwa.

    Akitabasamu zaidi huku akiendelea kutazama huku na huko, alitoka na kuufunga mlango taratibu kabla ya kuanza kupiga hatua.

    Lakini…wakati akitaka kutembea mara alijikuta mwili ukigoma kutenda, kwani aliwaona watu wawili ambao walikuwa wakitokea katika chumba kimoja!

    Watu hao walikuwa wakijia upande wake!

    ‘Those…doctors!’ Obrien aliwaza akiwa amesimama huku akianza kujikagua kiaina ili kujipa moyo alifanana nao kimavazi; lakini baada ya kitambo kidogo sana, alianza tena kuondoka akizivuta hatua za taratibu huku kwa mbali akianza kuhisi maumivu ya ule mkono wake ambao pingu ziliukwaruza sana; na hata kiuno kilimuuma.

    ‘Run nigger run!’ Alisemeshwa mawazoni bila kujali kama ilikuwa ni hasira ndiyo iliamrisha au tayari chuki ilizaliwa ili kuanza kuumiza.



    *****

    Aliwapitiliza watu wale baada ya kurushiana salamu kwa lugha za mwili kupitia namna walivyotazamana huku wakichezesha vichwa vyao; na ndivyo, alivyohakikisha alipiga hatua kadhaa katika kuwa mbali nao, aligeuza kichwa chake na kuaangalia.

    Macho yakakutana, kwani wale watu pia walikuwa wamefanya vilevile ingawaje wao waligeuka mwili mzima na wakiwa wamesimama; na ndivyo moyo ulipwita!

    Tena mara aligeuza shingo harakaharaka huku tayari hisia zikifukuzana katika ujenzi wa dhana kwamba walimshtukia; na hata kasi ya mwendo alifanya!

    Alipofika kwenye kona ya kuingia korido jingine ambapo kushoto kwake kulikuwa na ngazi za kushuka, hapo alisimama na kugeuka tena...akatazama!

    Wale watu sasa walikuwa wakija upande wake, na wakija kwa mwendo wa kasi mithili kama walikuwa wakiwahi jambo fulani!

    ‘Kumekucha!’ Alijisemea huku taratibu akigeuka tena.

    Alianza tena kuondoka, lakini hakufanya kwa mwendo wa haraka kama mwanzo; na hivyo alifanya kwa makusudi kabisa huku akijua eneo la ngazi lilikuwa ni hatua tano hivi ambapo hawataweza tena kumuona. Hatahivyo, moyoni alitetemeka sana kiasi zile hisia za kusikia maumivu ya mkono na kiuno vilitoweka.

    ‘Damascus ulifanya papara ukaishia kuletwa hapa hospitali na ukiwa chini ya ulinzi…usifanye tena!’ Sauti jasiri ilinena mawazoni katika kumpatia nguvu za kudhibiti hofu zake kiasi ilionekana pengine ni chuki yenye kujua kujipanga na kushambulia ndio ilikuwa tayari imechukua hatamu za uongozi.

    Ndivyo, alipozifikia ngazi aligeuka tena na kutazama nyuma yake na kubaini sasa walikuwa hawaonekani; na hata pumzi ya matumaini ikamtoka!

    Kitambo kidogo…mara aligeuka na kuanza kuzishuka ngazi kwa mwendo wa kasi mithili alikuwa ni daktari au muuguzi aliyekuwa akiwahi jambo fulani…



    *****

    Ilimchukua dakika kumi au zaidi kidogo kuweza kufika eneo la majengo ya uzazi na magonjwa ya kina mama; na hata alipofanikiwa kutoka nje ya hospitali, alikenua meno kwa furaha huku akielekea njia za uswahilini huko nyuma ya hospitali. Lakini badala ya kuelekea katika nyumba za uswahilini za kinondoni, alielekea katika majaruba ya majani na miti yaliyokuwa yakitokezea Surrender-bridge bila kujali kujiingiza katika matope; hatahivyo, tahadhari mmoja alifanya kutokana na kukumbuka eneo la kuanzia karibu na majaruba hayo kulikuwa na baadhi ya sehemu angeweza kumezwa na mchanga!

    Kwa tahadhari sana alifanikiwa kuingia katika jaruba na kujituliza eneo moja kwa kuketi chini ya mizizi ya mti mmoja ambayo ilikuwa juu kidogo na maji.

    “This a good step slip off the net…thanks! (Hii ni hatua nzuri kukwepa kushikwa…ahsante!)” Alisema kwa sauti huku akivua koti, na kisha aliketi juu ya mzizi mmoja kwa kuegamia mti ule.

    Ndipo hisia zile za maumivu zilianza kumtandika tena ingawaje aliweza kujikaza ili kuruhusu kufikiri zaidi nini alitakiwa kutenda baada ya hapo; lakini hapo alipokuwa, mwili wake ulielekezwa upande aliojia, yaani macho yakifanywa kutazama njia ya wapitaji ambayo bado ilikuwa ukiwa kama alivyoikuta wakati akija huku.

    Baada ya kufikiri kidogo, tena aliinuka huku akiliweka koti lake begani, na kisha aliichomoa mfukoni ile pochi.

    Akaanza kuzitoa zile pesa na kuzihesabu.

    Majibu yalifanya aachie tena pumzi ya tumaini huku akithibitisha ukubali wake kwa kutingisha kichwa; alianza kuondoka akitokomea ndani zaidi ya majaruba, lakini hivyo alifanya huku akisogea taratibu eneo la makazi ya uswahilini, kwani alikumbuka huko kulikuwepo kijiwe kimoja cha wahuni ambao aliwahi kuwabebea mizigo fulani ya magendo.

    Huko ndipo aliazimia afike kwanza kwa kutumaini wahuni wale wangemsaidia kumficha huku akiwaomba mchango wa fedha ili kuweza kukimbia masafa marefu, kwani aliona ingekuwa ni hatari kujulisha hapo alikuwa na shilingi zaidi ya laki mbili taslimu.

    Mara…!?

    Naam, mara mawazo yake yalikatishwa kwa mtingishiko wa ile simu huko mfukoni; kwanza alisinyaa kwa sekunde chache kabla ya kuitoa simu hiyo na kuitazama usoni pake ambapo alikuja kubaini kuwa namba ya mpigaji ilikuwa imefichwa!

    “Them!” Alisema kwa sauti ndogo huku akipiga moyo konde, kisha aliipokea simu.

    “Bob Collin?”

    Hakujibiwa!

    Aliuliza tena kwa kutaja jina la Mbilikimo; na safari hii alifanya kwa kufoka!

    Bado hakujibiwa!

    Sasa alisikia uhemaji wa mpigaji ulivyoanza kuvuma kwa namna kama vile hakutegemea kujibiwa kupitia muondoko huo!

    “Hujapata habari?” Obrien alisema tena; bado alifoka.

    Vilevile…alisindikizwa na ukimya!

    “I don’t know if you’ll be next, but the count is set!”

    “Nakusikia!” Sasa alijibiwa; ilikuwa sauti nzito yenye kukwaruza ambayo iliashiria wazi aliyeimiliki alikuwa ndani ya hasira iliyojitokeza ndani ya mshangao mkubwa.

    “I’m the finisher with the number!” Kisha aliendelea tena kusema kwa kuuliza, “vipi, utauchukua mzoga?”

    Simu ikakatwa!

    Obrien hakuishia kuirejesha simu mfukoni, kwani aliizima kabisa kwa kujua mawimbi ya elektroni yangeweza kutumiwa ili kujua alikuwa maeneo gani; ingawaje, hatahivyo, bado alikuwa na imani kwa kiasi fulani ‘wauaji’ wasingethubutu kuisaidia polisi katika kumnasa kutokana na kuutamua ukweli kwamba kwa kutenda hivyo ingekuwa ni sawa na kuhatarisha usalama wao halikadhalika kama alivyoelezwa na yule marehemu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hata usiku ulipoanza kunukia zaidi, bado mwangaza wa mbalamwezi ulimfanya aweze kuona kwa kiasi hadi kule katika kinjia cha kuelekea uswahilini ambapo alifanywa shuhuda kwa kuwaona wapita njia mmoja mmoja na wasiozidi kumi hivi.

    Hapo mkono ulipungua kumuuma.

    Lakini wakati akiangazaangaza, mara tazamo lake liliganda sehemu moja katika dimbwi la maji ambalo lilikuwa mithili ya kibwawa kidogo chenye maji machafu huku kikiwa na majani sehemu kadhaa yaliyoota.







    Pembeni yake aliona kidudu!

    Kilikuwa kidudu asichowahi kukiona maishani!

    Hatahivyo, hakukiogopa; isipokuwa ndivyo alikisogelea karibu na kuchuchumaa huku akikitazama kwa makini.

    Kilikuwa kidudu kidogo sana, kilichofanana kwa kiwango fulani na nyuki ingawaje chenyewe kilikuwa na meno yaliyojidhihirisha kuwa makali sana mithili ya meno ya simba; na isitoshe, hicho kilikuwa na kitu kirefu kiasi chenye ncha kali! Halafu, hakikuwa na mabawa kama ilivyo kwa nyuki aliokuwa akiwafahamu!

    Titanic beetle!



    Kidudu hicho kilikuwa kimetulia sehemu yake huku kikiwa kimeyatupa macho yake mekundu yaliyokuwa yakitisha mahala fulani katika eneo moja juu ya maji. Sehemu hiyo au mahala hapo palionekana kuchezacheza kwa kutoa mapovu na wakati mwingine mdudu mwingine alikuwa akitokezatokeza kwa namna ya kurukaruka juu kama vile alikuwa akifanya juhudi za kujitoa majini.

    Ndio, mdudu huyo mwingine alikuwa akijitahidi katika kujitoa majini, kwani hatimaye matunda ya juhudi zake yalionekana kwa jinsi hata alipoweza kutoka humo; na ndivyo alitulia pembeni mbali kidogo na kile kidudu kidogo huku akionekana kutotambua hakuwa peke yake.

    Alikuwa ni chura!



    Kile kidudu kiliyaona yote.

    Hivyo, taratibu na kwa kusuasua kilianza kujisogeza, kikimnyemelea chura yule kwa kunyata na kujifichaficha mithili kilikuwa katika mawindo fulani...



    Ni kweli, kwani mara chura yule alishtukia amerukiwa mgongoni kwa kitendo kilichofanyika kwa ghafla na spidi ya hali ya juu!

    Kidudu kile kilikuwa kimejirusha juu kama mshale na kisha kuubamiza mwiba wake mkali katika mgongo wa chura ambao ulichanwa kwa kupasuliwa sehemu moja!

    Mwiba ulizama ndani ya nyama; na hapohapo, damu zilianza kutiririka mithili ya bomba la maji lililotoboka!

    Yule chura kwa machungu makali alijikuta akijirusha juu sana kwa nguvu huku bado mshambuliaji akiwa ameganda juu ya mgongo wake akihakikisha ule mwiba hakubanduka kamwe!

    Obrien alishangaa kiasi huku akizidi kukodolea!

    Zile kukurukakara za chura katika za kutaka kujinasua kulimfanya hata ajikute akiingia majini tena!



    Ilikuwa ni ajabu sana, yaani mshambuliaji aliye mbabe alikuwa ni kijidudu kidogo sana mbele ya mshambuliwaji aliyekuwa mdudu mkubwa lililovimbiana mara dufu!

    Baadaye, kidudu kile kilitokezea kwa kurudi kinyumenyume hadi nje ya maji huku mdomo wake mdogo sana sasa ukionekana umeuma sehemu fulani ya pua ya chura na hivyo kumfanya avutwe kibwegebwege! Naam, chura alikuwa tayari na dhahiri amesalimu amri, kwani hapo alikuwa mithili ya mlevi aliyekuwa akipepesuka huku akikokotwa na msaidizi wake!

    Yaani, chura alikuwa hoi bin taabani!

    Kidudu kile kilipohakikisha windo lilifanikiwa, ndipo mara hatua ingine ilifuatia ambapo sasa sehemu mmoja ya shingo ya chura ndiyo ilichomwa na ule mwiba wake.

    Hata…taratibu, kilianza kufyonza!

    Kwamba, kilinyonya damu!

    Uuh!



    Kitambo kifupi baadaye, Obrien alikenua meno, akikenua kwa matumaini huku ujasiri ukianza kuibeba ile chuki kwamba yeye pia alipaswa kushambulia bila kuhofia ukubwa wa hao waliomtumbukiza katika janga hili ambalo akili ilizidi kusema alikuwa kwa wakati mmoja akiwa mfukuzwaji na mfukuzaji.

    Lakini bado akiwa amechuchumaa, mara alihisi kusikia sauti ya kitu au mtu kuijia upande wake akitokea nyuma!

    Akageuka haraka huku akisimama; na tayari mkono ulikwenda mfukoni ili kuichomoa kama ingelazimu!

    Macho yakaangaza huku akili zake zikihama moja kwa moja kutoka katika kutafakari kisa cha mpambano wa kidudu kile dhidi ya chura yule mkubwa!



    Kwamba, alimuona mtu akija huku akikimbia!

    Wakati fulani, mtu huyo aligeuka nyuma mithili alikuwa akifukuzwa hivi; na ilielekea huyo alimuona Obrien huku akidhihirisha pia hakumuhofia!

    Mtu huyo (akionekana kijana) alipomfikia karibu alisimama huku akihema; bado hakuwa ametulia kutokana na kuangazaangaza.

    Mkononi alikamatilia pochi dogo.

    “Hey guy, whtsup?” Obrien alimuuliza huku hisia zikianza kukimjia kwamba huenda mtu huyo alikuwa kibaka aliyetoka kufanya vitu vyake na akimuhisi hata yeye alikuwa ni sampuli hizohizo.

    “Nimemliza kuku wa kizungu,” Kijana yule alijibu kwa kuhemahema, “duh, mara likasanuka na ndipo nikatoka nduki…vipi, mazee? Umepiga bao tayari?”

    “Mimi ni tofauti na michongo yangu ni tofauti vilevile. Usijali, tunaweza kukamua pamoja.” Obrien alijibu huku akiitoa bastola ile ili kujulisha kama alikuja ‘kimtindo’, basi aelewe shughuli nzito itabidi itembee kwanza.

    “Nakubali, wewe ni ngoma ingine…hamna noma hatahivyo, au siyo mazee?”

    Obrien hakujibu.



    Ni kwamba, kijana yule aliyejitambulisha aliitwa Chizzon, alimpora mfuko dada mmoja kutoka katika gari lake kule barabara ya jangwani baada ya foleni kubwa kutokea ambayo ilisababisha magari kutembea kwa mwendo dhaifu sana. Ndani ya mfuko kulikuwa na simu ya ‘bei mbaya’ pamoja na kitita cha shilingi alfu thelathini; pia kulikuwa na vitu vingine kama vile mkufu na heleni za dhahabu, kitambaa kidogo na vikorokoro kadhaa.



    *******

    Pamoja na Hughes kuwa na tabia ya kuchelewa kurejea nyumbani kwake mara nyingi baada ya kutoka kazini (mara nyingi hurudi usiku sana), hatahivyo, bado kwa nafasi kubwa sana bado aliweza kuendeleza desturi yake ya kuhakikisha kila ifikapo alfajiri ya saa 12 ilikuwa ikimkuta tayari ameamka huku mara chache sana akiwa bado kitandani lakini akiwa macho.

    Basi, ndivyo ilivyokuwa alfajiri ya ijumaa hii, kwani muda huo uligonga akiingia bafuni. Alivalia bukta huku taulo ikiwa imenin’ginizwa katika bega lake la kushoto.



    Akiwa bado hajafunga mlango wa bafu, sauti laini ya kitoto ilisikika; na alipogeuka, ngoma za masikio yake zilikuwa zimegongwa tena na neno ‘shemeji’ kabla macho hayajapata kutazama ingawaje tayari hisia zake zilimbashiri mmiliki wa sauti hiyo!

    Alikuwa mtumishi wa ndani, akimkimbilia!

    “Ooh, Jacky!” Hughes alisema kwa kupumua.

    Jackline alipomfikia karibu alisimama huku akihemahema, lakini macho yake yalirendemka!

    “Ooh, katotoo!”

    Macho ya Jackline yalitazama kwa huba huku ishara za huzuni zikijisemasema katika uso wake ulioonyesha pia si dakika nyingi alitolewa usingizini.

    “Wasemaje binti?”

    Jackline alifungua mdomo wake uliokuwa ukichezacheza na kusema kwa hali za masikitiko, “shem, elewa ni wiki mbili sasa nauguza!”

    Hughes hakusema neno, kwani aliachia ‘zile tazama zake’ akiwa amesimama vilevile huku akihisi mwili ukianza kujipeleka ukijivutavuta!

    Halikadhalika, alimeza mate!

    “Aah, hukuja bwana…si ulisema lakini?” Hapo Jackline alikuwa kajitanda upande mmoja wa khanga; nywele zake nyeusi na ndefu zilikuwa bado zimefumka. Aliendelea kusema zaidi kwa kuumauma maneno huku akitumbukiza mdomoni kidole cha shahada, “nimezoea shem! Nihifadhi japo nipunguze kuuguza!”

    “Mama kalala?”

    “Tulikusikia ukiamka. Nimemjulisha, leo ni zamu yangu kwasababu jana sikupewa!”

    “Uuh…katoto wewe!”

    “Sio mimi…wewe ulifundisha!” Jackline alijibia puani, “halafu khanga hii nzito…ebu nishikie!”

    Alijivua khanga, akaishika mkononi huku akianza kumsogelea Hughes ambaye macho yalilazimishwa kuukodolea mwili ulionyan’ganywa vya kusitiri eneo lote la kuanzia juu ya kiuno kilichozungushiwa ‘kadhaa zivutazo’. Kwamba, hapo ‘mtoto’ alijibakisha akiwa amevaa sketi fupi sana iliyoacha sehemu kubwa ya mapaja bila kufunikwa.

    Hughes alipofikiwa, alitupiwa khanga mabegani huku mwenyewe Jackline akijiachia kudondoka kifuani mwake!

    Ooh!

    Jackline alichezewa kidogo kwa kutomaswa huku na kule kiasi sauti za kugugumia zilivuma ijapokuwa ilikuwa ni kwa mbali sana; na alipoachiwa, tayari alihema sana!

    Hughes hakutaka kumtazama tena, kwani alipomuachia ndivyo aligeuka taratibu na kuingia bafuni; hivyo alifanya bila kuufunga mlango huku akikapuakapua macho mfano wa mtu aliyekuwa akifikiri. Ndio, alikuwa akikusanya hisia katika kuzirejesha kuratibu na kuongoza mashambulizi.

    Jackline akamfuata…



    Pamoja na ukweli kwamba Hughes alishinda na Susan ‘wakitingishana’ kuanzia jioni ya jana hadi saa nne usiku, na kuja kumalizia kwa ‘kumtelemkia mkewe‘ mara aliporejea nyumbani; bado hatahivyo, nguvu hazikuwa zimepungua kiasi cha kushindwa kumtimizia Jackline haki yake ya ‘kuraruana’!

    Hatahivyo, alijua alihitaji ‘kujipasha moto’ kabla kwa njia ya kuzidi kumlainisha Jackline ingawaje aliziona ishara zote kwamba huyo alikuwa ‘ametayarishika’!

    Na ndivyo alianza kwa kumbana Jackline katika ukuta huku akimsukasuka na kumn’gatan’gata kwa mahaba; na wakati huo, viganja vyake vyote vilimminyaminya kiunoni huku zikiparaza zile shanga alizomnunulia kama mojawapo za kumbukumbu alikuwa ndiye mfundishaji na mfunguzi rasmi wa barabara - go & return. Tena kuminyaminya huko kulikwenda pamoja na kupanda na kushuka chini ya kiuno hicho kwa hatua za taratibu.

    Huku Jackline akisikika akilalamika kwa kunon’gona ndivyo baadaye mikono ilianza kupanda juu huku ikipapasapapasa ngozi laini mithili ilikuwa ikisaka upele uliojificha; na ilipofika katika matiti ambapo yalifikiwa kwa pamoja, basi hapo iliyafumbata kwa kuyasukasuka kiasi zile lalama zilizidi, kwani Jackline alikuwa mithili alikuwa akilia kwa sauti ya chini, sauti ya hofu, sauti kama akihitaji kuhurumiwa.

    “Ahsante, nasikia raha!” Jackline alisema huku mikono yake ikipapasa mabega ya Hughes aliyekuwa akianza kuhema nje kidogo na mstari wa kawaida huku akimn’gatan’gata shingoni taratibu.



    Ndio, wakati neno moja baada ya jingine la kimahaba zikiendelea kumtoka Jackline, ndivyo alihisi akizungusha mikono yake shingoni mwa Hughes huku pumzi zikimtoka kwa fujo kiasi mengi ya maneno yake yalikuwa yakiishia njiani bila kumalizika katika kusikika vyema.

    “Hughes! Hughes!”

    Hughes alisogeza mdomo katika masikio, na kisha alisema kwa kumpulizia hewa, “nakupenda…pfuh!”

    Jackline alipagawa zaidi akijivuta zaidi kwa msaada wa mikono yake iliyojizungusha shingoni mwa Hughes huku akijikuta akiinua mguu kwa namna iliyokuwa dhahiri kabisa hapo alikuwa tayari kwa lolote, kwani ndivyo sketi ilipanda juu na kujulisha kumbe hiyo ilikuwa ndio nguo pekee aliyovaa hapo!

    Taratibu! Taratibu! Taratibu!

    Taratibu, mikono ilianza kujiondoa katika matiti, hiyo ikiteremka chini kuelekea kiunoni. Hiyo ilipofika hapo, ndipo ilikaza kiasi kabla ya Jackline kushtukia akiinuliwa juu huku yeye pia akijikuta akiitikia kwa kuivuta miguu yake na kuishia kuizungusha kiunoni mwa Hughes!

    Jackline akawa alibebwa!

    Hughes akawa alibeba!

    Bado, Jackline alibamizwa ukutani…







    CHUMBA CHA OFISI ya mkuu wa kituo cha polisi kanda ya kusini tabata kilijaza vyema meza tatu ambapo meza kubwa ya robo mduara ndio ilikuwa ikitumiwa na afisa mwenyewe huku ikionekana kujaa mafaili ambayo hatahivyo yalikaa katika mpangilio maalumu; pia katika meza hiyo kwa pembeni upande wa kushoto ilitulia kompyuta aina ya laptop iliyounganishwa na simu pamoja na mitambo mingine kadhaa kama vile printer na scanner. Halafu, kiti kilichotumiwa na afisa huyo kilikuwa chenye matairi na hivyo kumrahisishia kujizungusha katika kufikia mahala pote pa meza hiyo.

    Meza ya pili iligusana na meza hiyo ya robo mduara; hiyo ilikuwa ni ndefu na yenye kuruhusu viti vitatu katika pembe zake mbili, na haikuwa na chochote juu yake.

    Meza ya tatu ilikuwa pembeni huko mbele karibu na mlango wa kuingilia chumbani humo; hiyo ilikuwa meza fupi na ndefu ambayo ilitulia katikati ya makochi matatu ambapo mawili yalikuwa ni yenye kuweza kuhudumia watu watatu kila moja, na jingine ni nafasi kwa mtu mmoja. Ndio, kochi hilo la mtu mmoja na ambalo ndilo lilinakshiwa maradufu zaidi, hilo lilikuwa likiangalia ubao mkubwa kiasi wa compyuta uliowekwa juu ya kabati ambalo halikuwa kubwa na wala halikuwa dogo sana; na si hivyo tu, kwani, halikadhalika, kabati kama nne hivi zingine zilikuwepo ikiwa ni pamoja na jokofu dogo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika meza hiyo waliketi watu wawili; mmoja alikuwa ndiye mkuu mwenyewe ambaye aliketi katika sofa la mtu mmoja huku katika kochi la kushoto kwa karibu kabisa akiwa ameketi Inspekta Hughes.

    Sekretari alipoleta sahani ndogo iliyokuwa na chupa ya maji ya moto na biskuti kadhaa pamoja na pakiti ya kahawa bila kusahau kibakuli kidogo cha sukari, ndipo Hughes alitingisha kichwa huku akishukuru kwa mdomo; na kwa wakati huohuo, macho yake yalipepesa kiaina katika kumtazama mwanamama huyo utadhani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumtia machoni au hakuwa na mazoea ya kuonana naye mara kwa mara.

    “Bibie, usijali. Nitajihudumia.” Hughes alijibu mara baada ya kuona tayari aliweka mezani ile sahani, kwani vikombe vilikuwepo muda mrefu kitambo.



    Ni kwamba, mkuu wa kituo aliitisha kikao cha dharura akihitaji kuongea na Inspekta Hughes pamoja na kundi lake kuhusiana na tukio la jana la kutoroka kwa Obrien hospitalini na kuuawa kwa askari aliyekuwa akimchunga; lakini kabla ya muda wa kikao kufika, Hughes aliwasili ofisini akiwa na lengo la kuomba kama ingewezekana waahilishe kidogo kikao kwa kukisogeza saa kadhaa mbele kutokana na kutakiwa kufika sehemu fulani kwa nyeti za kipelelezi.

    Mkuu huyo alikuwa Mrs. Groria Maxwell, mwanamama mwenye umbo lililojazia ingawaje alinyimwa sana eneo la chini ya mapaja yake kutokana na kuwa na miguu myembamba; lakini huyo alikuwa na matako makubwa sana kiasi mtoto mdogo angeweza kukalishwa juu yake bila wasiwasi, kwani hayo yalikuwa ni zile dizaini ambazo kama ungebahatika kumkuta akisalimiana na mtu mara baada ya kuvuka mtaro mfupi, basi ndivyo macho yangeburudishwa na ‘uchokozi wa mtepeto’ kwa zaidi ya sekunde ishirini hivi kabla hayajatulia.



    Basi pamoja na ukuu wake, bado Groria alikuwa akipata shida sana kuweza kuhimili utazamaji wa Hughes kila walipokuwa wakikutana na hasa mazingira yakiwa yamefanya kujikuta wakiwa peke yao; na hiyo ilitokana na kuhisi alikuwa akivuliwa nguo na huo utazamaji ambao halikadhalika ulikuwa ukimsukuma katika ‘kukunika kindani’ ingawaje huko awali wakati ndio akiletwa ofisi hiyo (baada ya kupandishwa cheo) alikuwa akijihisi ovyo kila utazamaji huo ulipojibandika mbele zake na hivyo kujenga chuki dhidi ya Hughes.

    Ndivyo hapo alijitahidi kuudharau muonekano huo huku akitamani sana amalizane naye ingawaje kutokana na unyeti wa kazi, bado alihitaji kuzungumza zaidi. Kwani kuhisi kwake kwamba macho ya Hughes yalikuwa yakimvua nguo kulitokana na yeye kumkubali alikuwa mwenye umbo zuri na macho yenye kuzalisha raha mbele ya mtazamwa na raha zake. Ndio, hivyo ndivyo alimpokea, kwani tazamo lilifanya kujihisi alipelekwa na kubwagwa ‘kitandani’ akiwa tayari amevuliwa.

    Basi ndivyo hapo aliketi kwa wasiwasi sana huku zaidi akijihisi ni kiumbe dhahifu bila kujipokea alikuwa ndiye mkuu na wakiwa kazini mbele ya majukumu.



    “Sasa mkuu, nadhani utaona ni muhimu niende huko ili kuona ni nini tunaweza kupata.” Hughes alisema huku akimtazama mama kwa chini chini kwa namna kwamba alivutika kumtamani.

    Huku Groria akitazama pembeni, alijibu kwa sauti ya chini, sauti iliyojaa hali za aibu na udhalili, “kwakuwa imekuwa bahati tunazo taarifa za marehemu huyo, na ndivyo ninaahirisha kikao hadi utakaporejea.”

    “Nashukuru mama.” Hughes alijibu na kisha aliendelea tena kwa mwendo wa kubadilisha uelekeo wa mazungumzo huku kwa ndani akitamani sana kujenga uthubutu wa kujaribu kumtongoza kutokana na kuziona ishara fulani kwamba uwezekano wa kumnasa ulikuwepo, “halafu…mama nakupatia fununu, kwamba, mwezi huu unaweza usiondoke kabla sijapata mtoto.”

    Groria alitabasamu na kuinua kiasi kichwa chake, na kisha alijibu taratibu kwa kutumbukiza swali, “Ina maana mkeo ni mjauzito?”

    “Mkuu, ulikuwa hujui?”

    “Nani angenijulisha mwingine?”

    “Basi…ooh, samahani sikufanya!” Hughes alijibu huku akibadilisha aina za utazamaji wake katika kumfanya aonekane ni mtu wa kuhurumiwa.

    “Namtakia mkwe afya njema.”

    “Ila mama…napata ugumu sana kipindi hiki.” Hughes alisema hili huku akihisi kuwashwa na hofu fulani.

    “Ugumu? Upi huo? Au hii kesi inakuweka mbali na mkeo kwa sana?” Groria alijibu kwa namna sasa alianza kupata ujasiri wa kuzungumza ingawaje bado alikuwa akimtazama Hughes kwa mara chache sana.

    “Ugumu wa kazi ameuzoea, hili si tatizo kabisa!”

    “Sasa ugumu gani huo?” Groria aliuliza tena kisha alishusha pumzi kama vile kuna kitu fulani kiliingia ndani ya hisia zake baada ya kusema huko; na hata alibadilisha ukaaji wake kwa kupandisha mguu wake mmoja juu ya mwingine huku mikono yote ikitupwa hapo katika huo mguu uliopanda.

    “Mkuu, wewe ni mwanamke, na mimi ni mwanaume.” Hughes alitulia kidogo, kwani mara aliona uhemaji wa mama ulianza kubadilika zaidi huku akiubadilisha tena ule mguu ili kufanya miguu yote ikae kwa kubanana bila kupandiana. Kisha tena aliendelea kusema, “sote tupo ndani ya ndoa. Huu ndio ugumu ninaoupata.”

    Groria alipumua tena kwa kuzishusha pumzi kwa kasi kidogo, na kisha aliiondoa mikono yake na kuiweka juu ya mikono ya kochi.

    Hughes aliinua kikombe cha kahawa na kupiga fundo, kisha huku akikirudisha mezani kikombe hicho ndivyo pia aliendelea kusema tena, “ni ugumu…hasa ugumu kwa mwanaume, kwani sote tunayo miili dhaifu yenye tamani na tamaa zake.”

    Groria hakujibu!

    Sasa alidhihiri kushikwa na aibu!



    Waliendelea na mazungumzo mafupi kabla ya kuagana huku Hughes akiwa bado hakuweza kutumbukiza zaidi ‘zoza zake’; lakini hatahivyo, aliongeza ujenzi wake wa matumaini kuwa, mama alisogea.

    Mawazoni, sauti fulani ilimsemesha Hughes kwa kumjulisha kwamba, kwa kawaida ‘msogezwa’ husogea kabla ya hatimaye kujikuta akianza kupenda kujivuta huku pia akijua kusogeza.



    *****

    WAKATI GRORIA MAXWELL alipanga kukutana na Inspekta Hughes na wenzake katika kuzungumzia sakata la Michelle Obrien kutoroka, ndivyo halikadhalika, Hushly Collin aliitisha mkutano na vijana wake huko ‘CC’ ambako ulipangwa kufanyika kuanzia saa 6.30 mchana.

    Katika mkutano huo, Collin hakuwa wa kwanza kuwasili. Rafiki zake Dullivan na Magret ndio waliwahi hata kabla ya muda uliokubaliwa; na hao ndio walichagua chumba binafsi ambacho kiliangaliana na uso wa bandari ya DSM.

    Wawili hao walitulia mezani huku wakinywa vilevi vikali vilivyochanganywa kwa ndimu na vipande kadhaa vya barafu katika glasi.

    Dakika kumi baada ya kuwasili kwa akina Jamex, ndipo Muvan (Punch-up) naye aliwasili na akionekana tayari alivuta bangi kama ilivyokuwa desturi yake kwani macho yake makubwa yaliushibisha ukweli huu waziwazi.

    “Washikaji, nilidhani nitakuwa peke yangu…kumbe nanyi mmewahi pia?” Muvan alisema huku akivuta kiti ili aweze kuketi katika meza iliyokuwa ndefu kiasi.

    Muhudumu wa kiume alikuja mbele yao na kusema kwa sauti ya unyenyekevu, “please, nikuhudumie nini?”

    Muvan aligeuka taratibu na kumtazama muhudumu huyo kwa sekunde kadhaa bila kumsemesha, na kabla ya kumjibu alichomoa paketi la sigara kutoka mfuko wa shati lake la kadeti, “gimme the kick but must not be cold, and…” Alinyamaza baada ya kuchomoa sigara na kuiweka mdomoni ambapo Magreth alimsogezea chombo cha kuwashia moto kilichokuwa mezani tangu awali; na alipowashiwa moto, alisogeza mdomo wake na kuiwasha sigara, na kisha ndipo alirudisha paketi ya sigara mfukoni. Alipiga pafu mbili kabla ya kuanza kusema tena huku akiachia moshi mzito ambao hatahivyo ulisambazwa maramoja na upepo wa bahari uliokuwa ukipuliza eneo lote la chumba, “hapa tunahitaji samaki na…ahm, gimme fishcake.” Kisha maramoja, alimtazama Magreth na kuuliza, “The pocket is somewhat full! So say pals!”

    Muvan na Magreth walitikisa vichwa kwamba bado hawakuhitaji chakula kwa wakati huo; na si hivyo tu, Magreth alijibu, “Thanks…ooh, Punch-up. We’ll kill it later! (Ahsante mbabe. Tutaagiza baadaye.)”



    Capitol Club ni miongoni mwa kumbi chache za starehe zilizopo eneo la Sea View huku ikifahamika zaidi kwa herufi zake mbili za mwanzo – CC: jengo hilo la ghorofa tatu na lililofanywa zaidi kwa mbao huku baadhi ya sehemu zake zikiwa zimeezekwa kwa makuti, lilibebwa na nguzo kadhaa na hivyo kulifanya kuwa juu ya bahari kwa yadi thelathini hivi; na ndivyo (jengo hilo) lilifikiwa kupitia kinjia kilichofanywa kwa ukuta mrefu kidogo (a narrow jetty) ambao pia pembeni zake (ukiacha fito kadhaa za kuzuia watu wasitumbukie majini) boti ndogo ziliweza kuegemea maeneo yaliyoandaliwa rasmi ili kushusha au kuingiza watu.

    Naam, ‘CC’ ilikuwa ni sehemu iliyojulikana sana kwa unywaji pombe na vyakula vya baharini huku ikionekana kuwa na wateja wachache wenye kupenda kufanya vurugu (brawling) ingawaje mwendo huo haukuwa kwa sana na hata ulipokuwepo mara nyingi ilikuwa ni katika siku za mwisho wa juma ambapo mabaharia wa boti ndogo (wengi wao wakiwa wakorofi) walipendelea sana kujiburudisha hapo!





    Hatahivyo, vurugu hizo za wakorofi hazikuweza kufanya watu watulivu wasiweze kuacha kuja hapo, kwani kama ni usalama huo ulikuwepo wa uhakika hata pale waleta vurugu walipofanya vitendo vyao; lakini mara nyingi, ‘watulivu’ walipendelea kuwepo maeneo ya ghorofa ya tatu ambayo yalikuwa imara kuhakikisha hakukuwa na vurugu za kuhatarisha usalama wa wateja.

    Ni kwamba, eneo la juu ya jengo hilo zilikuwepo sehemu sita zilizokuwa rasmi kama vyumba binafsi vya kulia vyakula na vitafunwa; hivyo vilifikiwa kwa ngazi za nje na kufanya urahisi wa kuweka ulinzi dhidi ya wakorofi ambao walipendelea kuwepo eneo la chini hadi ghorofa mbili kutokana na eneo hizo kuwa na sehemu za kuchezea kamari ukiachilia mbali zile meza za kunywea pombe na kadhaa zake huku kahaba wengi wakifurika kwa kupitapita huku na kule katika kujiweka sokoni.

    Pia, watu wenye uhitaji wa kupata faragha zao walipendelea kuwepo huko juu huku wakipulizwa na upepo mwanana wa baharini pamoja na kufanywa wasikivu wa sauti laini na za chini za ala za mziki. ndio, mazingira haya yalikuwa ukaribisho mzuri kwa ufanyaji wa faragha zao bila kupokea sumbufu kama zile za maeneo ya huko chini.



    ****

    Hushly Collin alifika wa mwisho, lakini akiwa na mwenzao mwingine aliyejulikana zaidi kwa jina la ‘Spanner’ kutokana na namna zake za kufanikisha mipango mingi ambayo iliyodhaniwa ilishindikana kufuatilia uzembe au ugumu fulani kujitokeza katika kuziba nafasi za ufanisi.

    Dhahiri, Collin hakuwa katika hali zake za kawaida, kwani alionyesha kuwa mwenye mashaka na mwingi wa mawazo ingawaje si kwamba hali hii ilijizungumza sana; bali hivyo alionekana kutokana na uzoefu wa waliokuwa wakimjua kama hao wenzake.

    Kule kuuawa kwa mwenzao kukichangiwa na fedheha ya kushindwa mara mbili katika juhudi zake za kumuua Michelle Obrien ndiko kulizidisha hali zake za kuonekana mithili ya mkata tamaa huku akiwa hajui wapi tamati ya sakata la kifo cha Brigitte lingeweza kujimalizia.

    Ile picha, lile tukio lililosababisha hadi maisha ya Edwin Edmund kukatika kwa staili ya kusikitisha, ndio, hilo lilikuwa sasa kila mara likivuma mawazoni mwake huku akikiri alianza kushindwa kuhakikisha haliji kwa kuzisumbua namna zake za kufikiri vyema kama alivyojizoeza kila alipotatizwa na jambo.

    Sasa alikiri alianza kushindwa kumudu yatokanayo, lakini bado akili ilijulisha nafasi wakati wote huwa ipo kama angeumiza kichwa chake katika kutatua.



    Baada ya kuletewa kinywaji kikali yeye na mwenzake, ndivyo alipiga fundo moja na kisha kuanza kusema kwa sauti iliyoashiria ukunjufu fulani tofauti na mazoea yake ya kuongea mara nyingi kwa sauti ya amri, “nyote mtakuwa mnaafahamu kwanini hapa nimewaita. Inasikitisha sana tunashindwa kutatua tatizo hili dogo na la kipuuzi.”

    “Mukulu! Hakuna tatizo dogo, kwani tatizo ni tatizo hadi litatuliwe, au sivyo Spanner?” Muvan alijibu huku akijiweka vizuri katika kiti.

    Spanner aliitikia kwa kichwa.

    Collin akatabasamu.



    Hapo waliongea mengi ikiwa ni pamoja na kutakiana kuhangaika sana na kwa spidi kubwa hadi kuweza kujua alipojifisha Obrien kabla hajatiwa hatiani na polisi.

    “Ni uzembe wa kimapenzi wa Edwin, lakini ndivyo sasa unakuwa uzembe wetu kama hatutaweza kumnasa huyu jamaa ambaye…shit! He’s just a mere taxi driver!” Magreth alisema kabla ya kusonya kuonyesha alichukia sana kwamba walisumbuliwa na mtu ambaye alimchukulia kama kiumbe dhaifu sana mbele yao.

    “Halafu, kuna fununu mbaya nimepewa na Mzee Kasonzo kwamba polisi imechukua vitu fulani nyumbani kwa Edwin ili kujaribu kuangalia…aah, they’re making DNA test to march with blood found in Brigitte’s house! This cut me off! Even the boss is so worried now!”

    “We’re dead then!” Magreth alijibu huku akijishika mashavu huku pia macho yake yakitazama kwa alama za mzubao.

    Collin aliweza tena; alisimama na kusema kwa sauti ya amri yenye mamlaka, “Tukiwa imara tutavuka…we’re street smarters! Let we refuse moving back lest we’re pinned down foolishly!”

    Akiwa bado vilevile, Collin aliita jina la Muvan; bado sauti ilifanya kwa amri.

    Muvan aliinua kichwa na kumtazama Collin.

    “Nataka kesho niamke nikisikia Henry amekufa!”

    “Lakini bosi…huyu si…?”

    “Ni amri, nimemaliza!” Collin alimkatiza Muvan ambaye alionyesha kuchukizwa na amri hiyo kutokana na jinsi alivyoachia tazama zake.

    Hata wengine walipigwa butwaa!

    Ukimya ukashika nafasi…



    “Bosi!” Spanner alianza kusema kwa sauti ndogo baada ya robo dakika tangu Collin arejee katika kuketi, “makosa mengi yamefanyika. Na hapa nashuhudia makosa mengine tunaendelea kuyajenga na tukifanya kwa njia za kidikteta.”

    Collin hakujibu.

    Muvan alikenua meno kiasi na kisha akawahi kusema, “nadhani Bosi unatupeleka pabaya.”

    “Nini?” Collin aliuliza huku akikunja uso.

    “Umenisikia bosi.” Aliendelea tena Muvan bila kumtazama Collin huku akionyesha sasa hakuwa ndani ya hofu, “hapa tunazungumzia usalama wa maisha ambao ni lazima sote tushirikiane kimawazo na kivitendo…or else everybody for himself!”

    Collin alianza kuinuka tena, lakini safari hii alifanya kwa taratibu kiasi kwa namna kama hakuwa na uharaka.

    Magreth pia alisema, “hivi bosi unajua hili tatizo ni matokeo ya umalaya wako na Edwin?”

    “Unasemaje wee mwanamke?”

    “Wewe ni bosi tunayekuogopa sana, lakini kukuogopa huku kuna mipaka ndani ya binafsi za maisha. Mambo yenu yametuingiza pabaya, halafu bado unataka kutuburuza kwa kuendelea kufanya makosa zaidi!”

    “Absolutely, this uncalled for!” Dullivan aliachia sauti yake kwa mara ya kwanza huku akimtazama Collin kwa macho makavu yenye alama kadhaa za shari.



    Ilibidi Collin arejee kuketi huku akisikitika moyoni kwamba sasa mambo yalianza kubadilika kwa kumsukuma ili hatimaye awe muelemewa zaidi! Ndivyo aliilani tena ile jumapili huku hata mawazo yakijazwa tena na habari ile upya katika kuona kama vile ilikuwa ikianza kutendeka!

    Macho ya mawazo yakatazama; hayo yakawa mithili yalikuwa hapo yakijulishwa, yakikumbushwa!

    Ndivyo tazamo lilianza kwa kuuona ukiwa wa mtaa wa Damascus sawasawa ulivyokuwa katika usiku ule wa jumapili…



    *****

    Ni kwamba, wakati Collin alipopinda kona na kuingia rasmi barabara ya mtaa wa Damascus katika usiku ule wa jumapili walipokuwa wakitokea sinza katika baa ya De-paradise, ndivyo alitania huku akigeuka nyuma na kuwatazama Edwin na Brigitte, “Shemeji isiwe unatuleta katika mzozo mwingine?”

    “Hutoke wapi tena?” Brigitte alijibu huku akiwa amekumbatiwa na Edwin ambaye mkono wake mmoja ulikuwa umemzunguka nyuma ya mabega na ndivyo ukibinya na kuvutavuta matiti yake yaliyokuwa nje.

    “Na kweli…mamaa tujulishane mapema!” Edwin alitania pia, kisha akajipinda kidogo na kumpiga Brigitte busu la shavu.



    Hatimaye, walifika na gari likasimama nje ya jengo la gorofa moja alilokuwa akiishi Brigitte.

    “Karibuni.”

    Brigitte alitoka na kuwaacha wakina Collin baada ya Edwin kumueleza angeweza kutangulia ili awahakikishie kwanza kama ilikuwa ni sahihi Marlon waliyempiga kule De-paradise hakuwa ameamua kuja hapo tofauti na madai yake kwamba asingerejeana tena na Brigitte baada ya fumanizi lile lililozalisha kudhalilishwa vile.

    Ndio, Brigitte alikubali kulala nyumbani kwa Collin ili kuweza kuburudika kimapenzi na Edwin ambaye pia aliamua asingeweza kurejea nyumbani kwake; lakini kwakuwa alipaswa kwenda kazini kesho yake ndivyo aliona umuhimu wa kuja nyumbani kwake ili kuchukua nguo za kubadilisha.



    Hivyo, Brigitte alianza kupiga hatua za kujiamini hadi katika ngazi za kupandia gorofani ambapo ndipo ilikuwa sehemu aliyokuwa akiishi.

    Vilevile, alizipanda ngazi kwa mikogo huku nyakati fulani akigeuka nyuma na kuitazama gari.

    Alipofika juu katika kibaraza, kwanza alisogea na kuchungulia katika dirisha moja na kisha ndipo aliufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba huku akianza kuimba wimbo ule uitwao ‘sogea sogea’ wa mwanadada anayedaiwa kuwa na kiuno kisichokuwa na mfupa.

    Na wakati huo, mkono wake ulikuwa umeanza kuchakura katika kijimkoba chake alichokinin’giniza begani hadi alipofika mlangoni ambapo alisimama.

    ‘Ni poa tu. Ang’ang’anie kwani hapa ni kwake? Na kwanza kwa jeuri ipi hata an’gan’ganie? Hajipendi?’ Brigitte aliufurahisha moyo huku kwa kasi zaidi tabasamu lake likizidi kukunjuka na hasa alipobaini mlango ulikuwa umefungwa na funguo tofauti na inavyokuwa kila amuachapo Marlon.

    Na ndivyo, alipoufungua mlango, maramoja alijitoma ndani huku akizidisha sauti katika kuimba.

    Aliwasha taa kubwa ya sebuleni, na kisha kuanza kuangaza huku na kule.

    Aliporidhika na mazingira aliyoyakuta, alitembea hadi katika mlango wa chumba chake na kuufungua.

    Akajitoma ndani.



    Akiwa chumbani, alikibonyeza kitufe kimoja kilichokuwa ukutani pembeni kidogo ya mlango, na ndipo taa yenye mwangaza mkali ikawaka. Akapepesa kidogo macho kabla ya kuamua kutoka.

    “Naamini hii meli mpya imesheheni kinoma…lakini, aah! Maana inaonekana huyu kapteni si namba ya kuichezea bila kuweka mikakati mizito!” Brigitte alijikuta akipayuka kwa furaha ya kujiona kama alikuwa mshindi fulani tayari kwa kufanikisha kumuweka Marlon ‘dock yard’.

    Kumbe, maskini hakujua ‘sheshe la buzi lililojeruhiwa’ lilikuwa bado halijamaliza kutenda, kwani ndio kwanza zile rasmi zake zilikuwa zikitaka kutimilizwa!







    Brigitte alipotoka chumbani kwake, alipitiliza hadi mlango wa kutokea nje ambao hakuwa ameurudishia pale alipoingia; hapo alitoa ishara kwa kuinua mikono yake kabla ya kurejea tena ndani.



    Ndipo Edwin alitoka garini, lakini alisimama nje huku akitazama huku na kule na wakati huohuo akionekana kupandisha suruali yake juu ikiwa ni pamoja na kuvigonganisha kidogo viatu vyake; na baada ya sekunde chache, alizifuata ngazi kwa mwendo wa taratibu…

    Alipozifikia, alipandisha tena suruali yake kabla ya kuanza kuzipanda ngazi hizo huku nyakati fulani mkono wake wa kulia ukijipeleka katika paji la uso wake na kushikashika kidogo mahala ambapo alikuwa kajifunga plasta.

    Alipofika katika kibaraza, mara alijikuta akiamua kusimama kidogo na kuwa kama vile wazo fulani la ghafla lilimjia; na ndivyo kweli ikawa baada ya kitambo kifupi sana aligeuka na kuanza kurudi katika kuzifuata ngazi. Bado uso wake uliachia tabasamu.

    Alipozifikia ngazi, alianza kuzishuka kwa mwendo wa tofauti na alivyozipanda ingawaje bado isingeweza kusemwa alikuwa akishuka kwa spidi.



    “Bob! Naona nukumani inaniwasha kiasi nahisi itabidi nipige bao la chapuchapu.”

    Collin alitabasamu bila kusema chochote huku akimtazama kwa dirishani.

    “Hivyo, ukiona nimechelewa wala usishangae!”

    Hapo Collin aliachia kicheko kidogo; lakini bado hakujibu ingawaje kichwa kilicheza kwamba aliitikia.

    Edwin akarudi tena akizifuata ngazi.

    Na ndipo baada ya sekunde kama kumi hivi, Collin aliiwasha gari na kisha kuiondosha hadi mbele kiasi kulikokuwa na kona moja ya kuingia barabara moja iliyokuwa ikiingia eneo pana lililoashiria lilikuwa ni uwanja wa michezo. Aliifuata njia hiyo iliyokuwa nyembamba sana na hata akauingia uwanja wenyewe ili aweze kuligeuza gari.



    Hicho kilikuwa ni kipande kimoja wapo ambacho mawazo ya Collin yalikichora katika kumfanya asononeshwe sana na ule uamuzi wa kuliondosha gari hapo nje ya nyumba ya Brigitte kwani alipatwa na hisia huwenda angeweza kuin’gamua mapema hatari iliyokuwa ikimkabili Edwin na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kumuokoa!

    Ndivyo hapo alitulia kimya akiruhusu vijana wake waje na mawazo yao kama walivyoonyesha kuhitaji kuwa na nafasi zenye mamlaka kuhusu utatuzi wa tatizo hilo la kifo cha Brigitte ambacho kila kukicha kilikuwa kikihatarisha usalama wa mambo yao.



    ****

    Bado kichwa kilimuuma Collin akizamishwa zaidi ndani ya mawazo yake, akizamishwa katika kuziona alama zilizoendelea kumchorea mambo yalivyokwenda ambapo sasa aliwaza alipokuwa kule eneo la uwanja wa michezo huku Edwin akiwa tayari ndani ya nyumba ya Brigitte…

    Ndivyo alipofika kule uwanjani, alijikuta akihisi kushikwa na haja ndogo. Akasimamisha gari na kutoka nje, akatembea kidogo hadi nje kidogo ya uwanja na kisha alisimama sehemu moja iliyokuwa na majani majani kwani eneo kubwa la kiwanja lilikuwa kipara.

    Hapo akakojoa.

    Na alipomaliza, ndipo akarudi ndani ya gari lake. Akachomoa sigara ndani ya pakiti lililokuwa katika mfuko wa shati. Akakichomoa kiberiti cha ndani ya gari na kisha akaiwasha sigara.

    Alivuta moshi mwingi kama ‘puff’ mbili tatu hivi na kisha akauachia tena utoke kwa wingi kupitia mdomoni na hivyo kuruhusu kusambaa hewani kiasi hali ilibadilika kwani harufu nzito sana ilijiachia!

    Baada ya hapo aliliwasha gari na kuanza kuliondosha kwa mwendo wa taratibu sana huku akionekana kuburudishwa sana na ‘stimu’ ya sigara hiyo ambayo bila shaka ilikuwa ni bangi.



    Jinsi alivyoanza kuwa karibu na nyumba ya Brigitte ndivyo alianza kuhisi kusisikia kelele fulani ambazo baadaye zilianza kumshtua ingawaje bado haikuwa kwa kumletea alama za hatari.

    “What’s ditching what?” Alisema kwa sauti huku akiongeza mwendo.



    Alipofika mbele ya nyumba, ndipo tafsiri ya mshtuko ilibadilika kwamba sasa akili ilijipatia usahihi kuwa kelele zilitoka nyumbani kwa Brigitte huku hisia ikiendelea kumvuta zaidi kwamba kulikuwa na mtu akiomba jambo fulani hivi, au akiomba msaada fulani kwa tafsiri hapo alikuwa ndani ya hatari fulani!

    Na ndivyo mawazo mengine yalianza kumiminika katika kuibumba zaidi ile tafsiri yake!

    ‘Hapana, si bure…ipo namna!’ Alijisemea moyoni huku akichomoa bastola yake na kutoka garini na kuanza safari ya taadhari sana katika kuzipanda ngazi huku akishukuru uwepo wa mbalamwezi iliyofanya isiwe taabu kuona ingawaje hatahivyo ile taa iliyokuwepo katika kibaraza huko juu iliweza kusafirisha mwangaza wa kutosha katika kuona.



    “Boss! Boss!” Aliita kwa sauti kubwa mara tu alipomaliza kupanda juu huku sasa akiufuata mlango ambao haukuwa umefungwa jambo ambalo lilizidisha hali zake za mashaka.

    Ukimya ukamkaribisha!

    Hapohapo akaamua asiite tena lakini huku akiendelea kujongea kwa kunyata!

    Alinyata, akanyata, akanyata!

    Alipofika mlangoni, alichungulia…

    Loh, alipigwa na butwaa hata asiyaamini macho kwa kile yalichokiona, kwani hapo alimuona mtu akiwa amechuchumaa sakafuni!

    Bado, macho yalipepesa!

    Huko mbele ya mtu huyo kwa pembeni kulionekana mwili wa mtu uliokuwa umechanwa chanwa vibaya kiasi utumbo ulikuwa umemwagika!

    Akili zikatambua!

    “Sh…shiiit!”



    ****

    Collin hakujua mawazo yake yalifanya aachie ukelele fulani ambao ulisikiwa na vijana wake ambao walishangaa zaidi kwani walimjua kwa ujasiri wa kutoonyesha hali za kukata tamaa kila walipokutana na hatari katika pilika za shughuli zao.

    “Vipi mkuu?” Spanner alimuuliza Collin huku macho yake pia yakizungumza ushangao wake kwa jinsi yalivyokuwa yakimkodolea.

    “Vijana, hili balaa linaniuma sana!” Collin alijibu huku akijipigapiga mapajani na mikono yake.

    “Huwezi kutatua tatizo bila kuwa na tatizo…we’ve to solve it no matter what!”

    “The fact we should not give up!” Muvan aliongezea maelezo huku Magreth akitingisha kichwa kuashiria pia alikuwa ndani ya msisitizo huo.

    “Nakubali sitakiwi kutumia veto yangu, lakini ni lazima tupokee hili tatizo ni letu sote hata kama nyinyi hamkusababisha…ndio, hili linatuhusu kwamba tutatue kwa nguvu zote!”

    “That…yeah, absolutely!” Magreth alijibu.

    “Nilipomuua shoga wa Brigitte kirahisi huko chumbani kwake ndivyo niliona hili tatizo nitatatua mwenyewe bila kuwasumbua sana.” Alisema zaidi Collin, na alifanya kwa sauti ya chini isiyoonyesha alama zake za ukatili kila awapo ndani ya matatizo, “lakini ilivyoshindikana kummaliza Obrien ndivyo hofu na hasira viliniandama sana, kwani hata mkuu sasa namuona yupo katika hali ya wasiwasi kama nitafanikiwa kutatua hili sakata la kipumbavu.”

    “Kummaliza Janet ilikuwa ni busara, lakini hili lingekuwa sahihi zaidi kama ungefanikiwa siku ile kumuua yule nani vile…?”

    “Marlon aliyemuua Edwin.” Collin alimkatiza Spanner kwa kudakia kujulisha jina la huyo aliyesahau jina lake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok.” Spanner aliendelea kusema, “halikadhalika ulifanya makosa kutotushirikisha wote ili kuhakikisha tunamzima huyo dereva taxi ambaye sasa ndiye mwiba mkuu huku nikiwa na wasiwasi yule…nanihi..eeh, Marlon anaweza kupona na hivyo kuutapika ukweli wote!”

    Collin alikapua macho huku mawazo yakimrejesha tena katika usiku wa jumapili ile aliyodhani aliondoka nyumbani kwa Brigitte akiwa amemuua Marlon! Ndivyo aliwaza tena…



    ****

    Pale mlangoni, Collin alikanyaga kitu fulani, akainamisha kichwa chini na kutupa tazamo lake. Macho yakakiona kile kitu, akainama na kukiokota.

    Ilikuwa ni bastola ambayo hakupata shida kuitambua kwamba ilikuwa ni ya Edwin; na ndivyo alijisemea moyoni kwa masikitiko, ‘ooh, I’see you tried hard to retaliate…you died hard!’

    Na hivyo ndivyo ikawa sasa Collin alikuwa na silaha mbili mkononi.

    Alipiga hatua mbili katika kuingia ndani, na kisha alisimama huku sasa akibwata, “muuaji mkubwa!

    Ni hakika Marlon atakuwa alilisikia vizuri tusi lile lakini bado hakuamua kugeuka nyuma, kwani alionekana kuzamishwa ndani ya hisia fulani alizozipokea kwa mikono miwili; kwamba, hapo alikamatilia kisu kikubwa kilichokuwa kimetapakaa damu na akiwa akikielekezea kwake ili pengine ndani ya dhamira ya kujitoa uhai wake mwenyewe!

    Ni kweli hapo alipanga kujimaliza, kwani maneno aliyoanza kusema yalin’garisha viashiria!

    “Nasikitika kwa kukuacha peke yako kama shahidi wa haya!” Kama vile alikuwa akikieleza kisu hicho ambacho sasa kilikuwa kimeinuliwa juu; sauti ilikuwa ya upole sana.

    Collin hakupata kuyazingatia maneno yale na badala yake ndivyo alizidi kumfokea Marlon, “Kama ulivyomuua Edwin ni lazima ufe pia!”

    Inawezekana kauli hiyo ndio ilifanya Marlon ashtuke kidogo, kwani alionekana kama alikumbuka jambo kiasi hatimaye alianza kugeuka huku akiwa kakamatilia kisu kwa nguvu zaidi…

    Mbona alichelewa, kwani Marlon alipogeuka tu, mara milio mikali ilisikika kwa mfululizo; kwamba, hapo alikutana ana kwa ana na vitu vidogo na vikali vilivyojibamiza usoni mwake na kupenya ndani kiasi taya zote zilitobolewa huku mwili ukihisi kufungwa kwa kukazwa na nati kubwa iliyovunja bega!

    Ndio, Marlon aliangushwa chali baada ya kurushwa hewani na nguvu za risasi zile tatu!

    Collin alitaka kuongeza risasi zingine, lakini alijikuta akisita kwakuona hakukuwa na haja tena; na ndivyo akabakia akitazama mwili ukitapatapa!

    Damn it!



    Baada ya Collin kutafakari sana, aliona ilikuwa ni jambo zuri kutoiacha maiti ya Edwin, kwani aliona kwa kuiacha hapo ingekuwa ni sawa na kukaribisha hatari kubwa dhidi ya kundi lao na hivyo kuja kujulikana. Hivyo aliona ingefanya polisi kuanza kufuatilia uhusiano wa Edwin na watu mbalimbali akiwemo yeye mwenyewe.

    “Nitamshauri Mkuu ili Boss wangu ajulikane hayupo nchini yapata miezi mingi iliyopita. Na familia yake je?...Hilo tutaona mbele kwa mbele.” Collin alijisemea mwenyewe kwa sauti huku tayari akiibeba maiti ya Edwin hadi nje ambapo aliingiza nyuma ya buti ya gari.

    “Lakini...oh, sijui Mkuu atanifanyaje?”

    Edwin alitetemeka sana kila alipofikiria eneo hili!



    _________________________________



    MWISHO





0 comments:

Post a Comment

Blog