Search This Blog

Thursday 27 October 2022

MVUVI BRUNO (BRUNO THE FISHERMAN) - 4

 









    Simulizi : Mvuvi Bruno (Bruno The Fisherman)

    Sehemu Ya Nne (4)





    Gari liliseleleka mpaka kule korongoni ambako hakukuwa na urahisi kwa mtu kufika huko mpaka uzungukie sehemu nyingine ya mbali. Kila mtu alikuwa hoi na wote walikuwa wakitokwa na damu.

    Bruno na Todd walikuwa kimya, damu ziliwatoka kichwani mwao na hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimeendelea mpaka kuanza kushambuliwa kwa risasi.

    Walichokifanya ni kuanza harakati za kutoka ndani ya gari lile lililokuwa limegeuka chini juu, juu chini. Wakazisogeza maiti zile na kisha kufungua mlango. Mzee Bruno akaanza kutoka, alipoanza kusimama, akashangaa akishindwa kutokana na maumivu makali aliyokuwa akisikia mguuni.

    “Aauughh..” alijikuta akipiga kelele.

    Damu zilikuwa zikimtoka mguuni, alipoangalia vizuri aligundua kwamba alipigwa risasi ambayo ilizama kabisa ndani ya mguu wake. Alisikia maumivu ambayo hakuwahi kuyasikia kabla, akashindwa kabisa kusimama, ili kusonga mbele ilikuwa ni lazima kushikwa au kubebwa.

    Haraka sana Bruno akateremka na kuanza kuelekea katika upande aliokuwa Todd na kumshika kisha kumpeleka pembeni. Akamlaza chini na kuanza kumpa huduma ya kwanza.

    Kitu cha kwanza kabisa alichotakiwa kufanya kilikuwa ni kuitoa risasi iliyokuwa katika mguu wa mzee huyo. Alishindwa kwa kuwa hakuwa na kifaa chochote kile hivyo kumwambia kwamba walitakiwa kuondoka mahali hapo kuelekea nje ya eneo la eneo hilo.

    Akamshika kwa kuupitisha mkono wa mzee huyo kwenye bega lake na kuanza kuondoka mahali hapo. Walichukua nusu saa wakafika juu kabisa barabarani.

    Hawakujua ni mahali gani walitakiwa kwenda, walichokifanya ni kuanza kuelekea upande wa Kaskazini ambapo waliamini kwamba hakukuwa na mtu yeyote hatari. Walitembea kwa mwendo mrefu, baada ya dakika ishirini na tano, wakaanza kupigiwa honi, walipoangalia nyuma, gari ndogo aina ya Vitz ilikuwa nyuma yao.

    Gari hilo likasimama na dereva aliyekuwa humo ndani kuanza kuwaangalia, kwa jinsi walivyoonekana, ilionyesha dhahiri kwamba walikuwa wakihitaji msaada, akawafungulia mlango na kuwaambia waingie ndani.

    “Nini kimetokea?” aliuliza dereva huyo huku akiwaangalia kupitia katika kioo cha mbele, aliwaweka kiti cha nyuma.

    “Tulitekwa,” alijibu Bruno.

    “Mlitekwa?”

    “Ndiyo! Bosi wangu wakampiga risasi ya mguu. Tunaomba utusadie,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo.

    “Haina shida. Nitawapeleka hospitali sasa hivi!”

    “Hospitali?”

    “Ndiyo!”

    “Hapana! Naomba utupeleke sehemu yoyote ile lakini si hospitali,” alisema Bruno.

    “Kwa nini? Mzee ana risasi mguuni, inabidi iende ikatolewe,” alisema dereva.

    “Hapana! Naomba utupeleke popote pale.”

    Bruno alimwambia dereva huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jonathan jinsi maisha yao yalivyokuwa hatarini. Alimwambia kuwa kulikuwa na mtu mwenye mkono mrefu alikuwa akiwatafuta, aliwatuma watu kwenda kuwamaliza lakini walishindwa na gari lao kupata ajali na kutumbukia korongoni.

    Hakuishia hapo, aliendelea kumdanganya kwamba kama mzee Todd angepelekwa hospitali inamaanisha kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wao kwa kuwa jamaa huyo aliyekuwa akiwatafuta alikuwa na watu wengi, kila kona alikuwa amesambaza watu wake kwa leo la kumlinda na hata kumfanyia kazi.

    Kidogo hiyo ikamuingia Jonathan, akatokea kuwaamini na kuwaambia kwamba angewapeleka nyumbani kwake. Safari iliendelea, baada ya dakika arobaini wakafika nyumbani hapo ambapo akawateremsha na kuelekea ndani.

    Akamuita mke wake aliyeitwa Magdalena na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea, jinsi alivyokutana na watu hao nje mpaka kuomba msaada wake. Hilo halikuwa tatizo, kwa kuwa mkewe huyo alikuwa na ndugu yake aliyekuwa daktari akampigia simu na kwenda nyumbani hapo.

    Baada ya dakika kadhaa, Sophiane ambaye ndiye alikuwa daktari aliyepigiwa simu akafika nyumbani hapo na kumwangalia mzee Todd aliyekuwa hoi kitandani. Akaangalia jeraha, akaandika vifaa ambavyo vilihitajika kwa lengo la kumfanyia upasuaji na kutoa risasi hiyo.

    “Inahitajika randi elfu ishirini,” alisema Sophiane.

    “Mbona kiasi kikubwa hivyo?” aliuliza Jonathan.

    “Ni vifaa vya gharama kwa kuwa ni risasi ndiyo inayotakiwa kutolewa, ila pia vifaa hivyo haiviuzwi kiholela kwani serikali ilitangaza majeraha yote ya risasi yalitakiwa kutibiwa hospitalini,” alisema Sophiana huku akiwaangalia watu hao.

    Jonathan hakuwa na pesa za kutosha ila hilo halikuonekana kuwa tatizo lolote lile, Bruno akamwambia kwamba pesa ilikuwepo na kitu kilichohitajika kilikuwa ni hivyo vifaa tu.

    Yeye, Jonathan na Sophiana wakaondoka kwenda mjini ambapo huko Bruno akaenda katika mashine ya ATM na kutoa kiasi cha pesa kilichotakiwa na cha ziada kwa ajili ya matumizi yao na kumkabidhi Sophiana ambaye alikwenda na kununua vifaa hivyo tena kwa kutumia vyeti vya udaktari.

    “Twendeni nikaanze kazi,” alisema mwanamke huyo.

    Baada ya dakika kadhaa wakafika nyumbani hapo na kuanza kazi. Risasi ikatolewa, kila mtu akafurahi na mzee huyo kuanza kutibiwa nyumbani hapo na hata alipopona, Jonathan akawaambia kwamba maisha yao yalikuwa hatarini hivyo walitakiwa kukaa mahali hapo kwa mwezi mzima jambo ambalo halikuonekana kuwa tatizo.

    “Kwa hiyo huu ni mwezi wa pili tupo Afrika Kusini! Nitarudi lini nyumbani kuwaonyesha wakina James kwamba sikufa?” alijiuliza. Mwezi huo pia wakatakiwa kukaa hukohuko Afrika Kusini.

    ***

    Maxwell alikuwa na presha kubwa, alitaka kusikia kile kilichokuwa kimeendelea nchini Afrika Kusini. Hakutulia nyumbani kwake, muda wote alikuwa akipigia simu nchini humo na kutaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea.

    Alitaka kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, na kwa sababu aliona kama kudharauliwa kwa kile alichokuwa ameagiza, alichokifanya ni kuwapigia simu vijana wake na kuwaambia wammalize Bi Juddie na mtoto wake, Martha.

    Hilo halikuwa tatizo, vijana hao walipoambiwa hivyo, wakawachukua watu hao na kwenda kuwaua na kuitupa miili yao ufukweni mpaka pale polisi walipopewa taarifa na kwenda kuichukua.

    Ilikuwa ni taarifa mbaya mno kwa kila mtu, hakukuwa na aliyejua kama kulikuwa na mtu aliyekuwa nyuma ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea, wengi walimchukulia mzee Todd kama muuza madawa ya kulevya lakini kwa kile kilichotokea kilimgusa kila mtu.

    Moyo wa Maxwell ukaridhika lakini bado kichwa chake kilimfikiria huyo Todd, hakujua vijana wake walifikia wapi kwani kila alipowapigia simu alipewa majibu ambayo hayakumridhisha hata kidogo.

    Siku zikakatika mpaka mwezi mmoja kumalizika, bado hakukuwa na kitu kilichoendelea mpaka pale alipopigiwa simu na kuambiwa kwamba vijana walikuwa njiani kwenda kutekeleza suala la kumuua mzee huyo kwani walipewa taarifa kwamba alikuwa hotelini.

    Hilo lilimfurahisha na kuahidi kulifuatilia kwa karibu sana. Walipokuwa ndani ya gari, akawapigia simu, akaambiwa kwamba walikuwa na watu hao na hivyo walikuwa njiani kwenda kuwamaliza.

    Moyo wake ukajisikia furaha ya ajabu, akakata simu, akachukua chupa ya mvinyo na kuanza kunywa huku muziki ukipiga taratibu kwenye redio yake sebuleni kwake.

    Baada ya saa moja alipoona kwamba kazi ile ilifanyika, akaanza kuwapigia simu vijana wake ili apate mrejesho kama kazi ile ilifanyika au la. Alipiga simu, haikuwa ikipokelewa, iliita na kuita lakini hali ilikuwa kimya kabisa.

    Hilo lilimchanganya, haikuwa kawaida kwa vijana wake kutokupokea simu zake, alihisi kwamba kulikuwa na tatizo na hivyo kupiga zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu haikupokelewa.

    “Nini kinaendelea huko? Mbona hawataki kupokea simu zangu?” aliuliza, hakupata jibu, kichwa chake kilichanganyikiwa kupita kawaida.

    Baada ya dakika kadhaa, akapiga tena simu, haikuita muda mrefu, ikapokelewa na sauti ya mwanamke kusikika upande wa pili. Huyo ndiye aliyemwambia kwamba kulikuwa na ajali mbaya ilikuwa imetokea ambapo watu waliokuwa ndani ya gari hilo walikuwa wamekufa wote.

    “Wamepata ajali?”

    “Ndiyo! Ila kilichowaua si ajali,” alisikika mwanamke huyo.

    “Ni nini?”

    “Risasi,” alipoambiwa hivyo, moyo wake ukapiga paa, hakuamini, aliuliza zaidi na zaidi kwa kudhani kwamba majibu yangebadilika lakini yaliendelea kuwa vilevile kwamba vijana wake waliuawa na gari kuingia kwenye korongo.

    “Haiwezekani! Haiwezekani!” alisema Maxwell huku akiwa amechanganyikiwa.



    Bruno na mzee Todd hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kuendelea kukaa nchini Afrika Kusini kwa mwezi mwingine wa pili. Hawakupenda kukaa nchini humo, kila mmoja alihitaji kuondoka kuelekea nchini mwao lakini hawakuwa na jinsi, waliendelea kubaki nchini humo nyumbani kwa Jonathan huku mzee Todd akiendelea kupatiwa matibabu.

    Siku ziliendelea kukatika, Bruno hakutakiwa kutoka ndani, alikuwa na hofu kubwa kwa kuhisi kwamba bado watu hao walikuwa wakimtafuta kila kona hivyo angeweza kuuawa.

    Alikuwa kama mwali, kila siku ilikuwa ni kuamka ndani na kubaki humohumo mpaka jioni. Yalikuwa ni maisha ya shida, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kuwasiliana na Abdul aliyekuwa nchini Kenya kwa lengo la kumwambia kuwa hakufa, ili taarifa hiyo ampe Sharifa ambaye bila shaka alikuwa na wasiwasi mkubwa huko alipokuwa.

    Kupata simu halikuwa tatizo ila tatizo kubwa lilikuwa ni kupata simu ya mtu mmoja aliyekuwa nchini Kenya ambaye angemuunganishia kuzungumza na msichana huyo.

    Kila siku alizungumza na mzee Todd ambaye alimwambia jinsi alivyokuwa akiumia kuona akiwa mbali na familia yake. Hao ndiyo walikuwa watu aliokuwa akiwategemea, hakuwa na ndugu, maisha yake tangu alipokuwa kijana mpaka alipopata utajiri, mkewe na mtoto wake ndiyo walikuwa watu pekee.

    “Unahisi tutaweza kuondoka hapa salama?” aliuliza mzee Todd.

    “Ninatumaini hilo mzee! Cha msingi ni kumuomba Mungu katika hili, ila ni lazima tuondoke salama hapa,” alisema Bruno, alimwambia mzee huyo maneno ya kumfariji kiasi kwamba akahisi kwamba Bruno alikuwa malaika aliyetumwa kwa lengo la kumtia moyo pale alipokuwa akimevunjika moyo.

    Wakati akiendelea kuugua kitandani pale ndipo alipopewa taarifa juu ya kifo cha familia yake ambapo maiti zao zilikutwa ufukweni.

    Ilikuwa taarifa mbaya iliyouumiza moyo wake, hakuamini kile alichokuwa akikiona, moyo wake ulimwambia kwamba ni Maxwell ndiye aliyefanya hivyo.

    Lawama zake zilikuwa kwa mwanaume huyo, aliuumiza moyo wake na kuhisi kabisa kwamba alifanya hivyo kwa kuwa alihitaji mali zake, aliutaka utajiri wake na hata kushikilia biashara nyingi alizokuwa akizifanya.

    Hakulia sana, hakuhuzunika sana kwani mahali walipokuwa hakutaka wenyeji wao wagundue kwa kuamini kwamba kama ingetokea hivyo basi ilikuwa ni lazima wakatoe taarifa katika kituo cha polisi na kukamatwa.

    Siku ziliendelea kukatika huku mawazo juu ya familia yake yakimuumiza moyoni mwake. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, hakuwa na watu wengine wa karibu sana kwani tangu alipokuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya hakuwa anajiamini kuwa na watu wa karibu zaidi ya familia yake, yaani hata walinzi wake hakuwa akiwaamini.

    Waliendelea kuwa hapo mpaka mwezi ulipokatika ambapo wakakubaliana kwamba ni lazima waondoke kuelekea nchini Kenya kwa kupitia njia za panya mpaka kufika huko.

    Hilo halikuonekana kuwa tatizo, alichokifanya Bruno ni kuzungumza na Jonathan na kumwambia kile walichokuwa wakikitaka.

    Jonathan akawaambia kwamba halikuwa jambo zuri kupitia njia za panya, kwa kuwa walikuwa na pesa na hati zao za kusafiria zilipotea basi lingekuwa jambo jema kama wangekwenda uhamiaji kwa lengo la kukabidhiwa nyingine.

    “Hapana! Nadhani kwa njia za panya ni vizuri zaidi,” alisema Bruno.

    “Hapana! Njia hizo si salama, mnaweza kuuawa,” alisema Jonathan.

    Walimwambia Jonathan kwamba walitaka kuondoka nchini humo kwa njia za panya lakini mwanaume huyo aliendelea kuwasisitizia kwamba hizo hazikuwa njia nzuri kwenda nazo kwani watu wengi ambao walikuwa wakitumia njia hizo walisafiri kwa hofu kubwa kitu ambacho hakutaka kuoana watu hao wakikutana nacho njiani.

    Wakaambiwa wasubiri wakati Jonathan akifuatilia hati zao za kusafiria uhamiaji. Hilo likaonekana kama kwa kosa kubwa, hawakutaka kuendelea kubaki nyumbani hapo, katika kipindi ambacho Jonathan alikuwa ameondoka kuelekea huko, huku nyuma nao wakatoroka nyumbani hapo.

    Sehemu ya kwanza kabisa ambayo walitaka kwenda ilikuwa ni katika Jiji la Pretoria ambapo waliamini kwamba safari yao ya kuelekea nchini Kenya ingeanzia hapo.

    Walipoondoka, wakaelekea mpaka katika Kituo cha Treni cha Sandton ambapo hapo wakapanda treni na kuanza safari ya kuelekea Pretoria.

    Ndani ya treni hakukuwa na mtu aliyewagundua, walivalia kofia na miwani kiasi kwamba ilikuwa vigumu sana kwa nyuso zao kuonekana.

    Ndani ya treni walikuwa kimya kabisa, hawakutaka kuzungumza jambo lololote lile. Walijifanya kufuatilia safari huku wakiwa wameviinamisha vichwa vyao.

    Kutoka hapo Johannesburg mpaka Pretoria walitumia saa mbili na dakika kadhaa, wakafika ambapo hawakutaka kukaa sana, ilikuwa ni lazima waunganishe safari mpaka Polokwane.

    Hapo hakukuwa na treni ya kwenda huko, walitakiwa kuchukua basi ambalo lingewapeleka mpaka huko. Bado hilo halikuwa tatizo, wakakata tiketi na kuanza kuelekea Polokwane.

    Ndani ya basi hilo kulikuwa zaidi ya abiria hamsini, kila mmoja alionekana kuwa na jambo lake, wote walikuwa bize huku wengine wakiwa na mizigo mikubwa, hakukuwa na mtu aliyemfuatilia mwenzake, kila mmoja alikuwa bize na mambo yake.

    Walichukua saa nne ndio wakaingia huko. Giza tayari lilianza kuingia na kulikuwa na baridi kali, wakatafuta vyumba na kwenda kulala. Huko, kila mtu aliendelea kuwa na mawazo juu ya watu wake.

    Mzee Todd alikuwa kwenye maumivu makali, bado hakuamini kama kwelii familia yake ilikuwa imeuawa kinyama, alikuwa na hasira mno na hakuona kama kweli Maxwell alistahili kuishi, kwa kuwa aliimaliza familia yake, naye ilikuwa ni lazima ammalize kwa gharama yoyote ile.

    Upande wa pili na Bruno alikuwa na mawazo yake kuhusu mpenzi wake, Sharifa. Moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kumuona kwa mara nyingine tena na kumwambia kile kilichotokea na kwamba hakufa.

    Kwa kiindi hicho, kwa esa ambazo zilikuwa katika akaunti yake aliyokuwa ameifungua hao Afrika Kusini zilikuwa nyingi mno ambazo angeweza kuzitumia kwa kufungua biashara nyingi nchini Kenya.

    Wakati mwingine alitamani hata kumkimbia mzee Todd na kupotea zake lakini kila aliofikiria hali ya mzee huyo, hatua alizokuwa akipitia katika maisha yake, hakuona kama lilikuwa jambo jema kufanya kile kilichokuwa kikimjia kichwani mwake.

    Asubuhi iliofika, wwakajiandaa kwa ajili ya kuendelea na safari yao kama kawaida. Hapo Polokwane Mjini walitakiwa kuanda basi mpaka sehemu iitwayo Mankweng ambao hao wangeunganisha mpaka Tzaneen, Nkowankowa hadi Phalaborwa ambao hao wangekutana na vijana waliokuwa wakifanya shughuli ya kuwaitisha watu miakani kwa njia za anya kuelekea nchini Msumbiji.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hawakutaka kuoteza muda, baada ya kula na kuchukua kiasi cha esa kilichoonekana kuwatosha, wakaondoka kuendelea na safari yao. Ilikuwa ndefu mno, waliondoka asubuhi lakini mpala inafika majira ya saa kumi na mbili jioni bado hawakuwa wameingia Phalaborwa ambao wangetakiwa kulala.

    Kila mtu ndani ya gari alichoka kuita kawaida, waliofika Nkowankowa, kama kilometa mia nne mpaka Phalaborwa wakaamua kulala hao.

    Hakukuwa na abiria aliyeruhusiwa kutoka ndani ya gari, walitakiwa kubaki humohuko kwani sehemu za vijiji kama hizo hazikuwa nzuri kwa usalama wao.

    Abiria wakalala usingizi wa mang’amung’amu hadi asubuhi ambao safari ikaendelea kama kawaida. Hapo, kutokana na ubovu mkubwa wa barabara walitumia saa sita kufika Phalaborwa.

    “Nyie mnataka kwenda wapi?” aliuliza kijana mmoja.

    “Msumbiji!” alijibu Bruno.

    “Msumbiji! Kwa njia za halali au?”

    “Kama ingekuwa kwa njia ya halali unahisi tungekuja huku?” aliuliza Bruno, alichoka, hakuhitaji maswali yoyote yale.

    Kijana yule akawachukua na kuwapeleka katika jumba moja chakavu ambapo huko wakakutana na vijana watatu ambapo yule kijana mmoja akawaelezea shida yao na kupewa maelekezo kwamba walitakiwa kuyafuata kama walitaka kufika nchini Msumbiji salama kabisa.

    “Yapi hayo?” aliuliza Bruno.

    “Kwanza mna randi elfu tano?” aliuliza kijana mmoja huku akiwa ameshika kipande cha bangi.

    “Pesa si tatizo,” alisema Bruno na kutoa kiasi cha pesa kilichokuwa kikihitajika na kumpa.

    Kijana yule akaanza kuwaambia kuhusu safari yao ambayo wangewaelekea mpaka katika msitu wa Kruger na wao kuunganisha mpaka nchini Msumbuji.

    Kruger ulikuwa moja ya misitu hatari sana iliyokuwa na wanyama wakali. Waliwaambia kwamba wao wangewapeleka mpaka mwanzo wa msitu huo na safari ya mbele walitakiwa kwenda peke yao ila wangewaambia njia nzuri na salama mpaka kufika nchini humo.

    Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, mchana huohuo wakaanza safari ya kuelekea katika msitu huo ambao ulikuwa ni kama kilometa kumi kutoka hao waliokuwa.

    Njiani walikuwa wakipiga stori na Bruno kuwaambia kwamba wao walikuwa maharamia ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kuteka meli Afrika Kusini na kukomba mizigo yote lakini kwa kipindi hicho walitakiwa kurudi Msumbiji kwa kuwa kule Cape Town hakukuonekana kuwa salama kabisa.

    “Na kama mimi nikitaka kuwa mharamia?” aliuliza jamaa mmoja.

    “Kwanza ni lazima ujue kuigana, uwe japo na mkanda mmoja wa karate, ujue kuua kwa kumpiga mtu sehemu hatari mwilini mwake lakini la zaidi ni lazima ujue kuambana na watu hata sita waliokuwa na bunduki,” alisema Bruno huku akionekana kuwa makini sana.

    “Wewe umefuzu?”

    “Ndiyo! Nakumbuka mtu wa kwanza kabisa kumuua alikuwa The Ruler! Mnamfahamu?” aliuliza Bruno.

    “Haana! Ndiye nani?”

    “Eeeh! Hamumfahamu mtu aliyekuwa akitisha sana kwa mauaji Somalia, yule ambaye alimteka mpaka mtoto wa rais?” aliuliza Bruno.

    “Hapana!”

    “Fuatilieni, mtajua mtu huyo alikuwa ni hatari kiasi gani. Ndiye mtu wa kwanza kumuua,” alisema Bruno.

    Kila kitu alichokuwa akiongea mahali hao kilikuwa ni uongo asilimia mia moja. Aliwaangalia vijana hao, hawakuwa wakieleweka, kwa jinsi walivyoonekana, alihisi kabisa kama wangeweza kuwageukia baada ya kuona pesa.

    Aliliona hilo na ndiyo maana alikuwa akiwaambia stori za uongo zilizowafanya vijana hao kuanza kuogoa na kuhisi kwamba walikuwa na watu hatari sana ambao wangeweza kuwapiga ndani ya dakika kadhaa tu.

    “Na huyo Mzungu?” aliuliza jamaa mmoja kwa sauti ya chini.

    “Huyo ndiye mafia mwenyewe. Muitalia, hana maneno mengi lakini ana roho ya kinyama zaidi ya Musolini,” alisema Bruno, wote wakashtuka.

    “Mmh!”

    “Huyo ni mtu hatari sana, unamuona anachechemea, alipigwa risasi tano mguuni, lakini mpaka leo bado anatembea, huyo ni mtu hatari sana,” alisema Bruno, vijana wale wakawa na hofu zaidi na kuona kwamba muda wowote ule wangeweza kugeuziwa kibao.

    Wakaona safari ikiwa mbali mno, hawakutaka kuwaamini tena watu hao, walionekana kuwa hatari na hawakuwa na mchezo hata kidogo. Baada ya saa moja, wakafika waliokuwa wakielekea na kuwapa maelekezo kuhusu njia walizotakiwa kupita.

    “Ila kumbukeni kwamba kuna wanyama wakali sana,” alisema jamaa mmoja, Bruno akaanza kucheka.

    “Wanyama wakali? Hahaha! Hawana nafasi, tuna uwezo wa kupambana na simba zaidi ya watano, usijali,” alisema Bruno maneno ambayo yaliwafanya vijana wale kuhisi kwamba mtu huyo alikuwa jasiri sana.

    “Basi sawa. Safari njema,” alisema mmojawao.

    “Sawa,” aliitikia Bruno na kuanza safari ya kuelekea katika mbuga ya wanyama ya Kruger iliyokuwa ikisifika kuwa na wanyama wakali.

    ***

    Hawakutakiwa kuogopa kuingia msituni, ilikuwa ni lazima wavuke na kusonga mbele mpaka nchini Msumbiji. Mbuga ya Kruger ilitisha mno, kila walipokuwa wakipiga hatua ni sauti za ndege na wanyama tu ndizo zilizokuwa zikisikika kila kona.

    Waliendelea kusonga mbele, walikuwa makini, mioyo yao ilikuwa ikimuomba Mungu wasiweze kuingia mikononi mwa wanyama wakali kama simba, chui na wengineo.

    Ndani ya saa tatu walikuwa wakitembea tu, walichoka lakini hawakutaka kupumzika. Njiani walikutana na wanyama wa kawaida kama nyumbu, swala, tembo na wanyama wengi wanaokula majani.

    Baada ya kutembea kwa umbali wa kilometa kama thelathini ndipo wakabahatika kuiona hoteli moja kubwa na ya kitalii iliyoandikwa King Lion kwa juu ambayo ilikuwa maalumu kwa watalii waliokuwa wakitembelea mbuga hiyo.

    Wakaanza kuifuata, walipoifikia, getini wakasimamishwa na walinzi walioonekana kuwashangaa mno. Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka watu hao kutembea katika mbuga hiyo ambayo ilikuwa ikitisha kupita kawaida.

    “Nyie mmetoka wapi?” aliuliza mlinzi mmoja huku akiwashangaa.

    “Huko mbugani!”

    “Mmewezaji kutembea katika mbuga hii?” aliuliza mlinzi mwingine.

    Kulikuwa na matukio kadhaa yaliyokuwa yakitokea huko, watalii walikuwa wakiuawa hovyo kila walipokuwa wakitembea, katika hoteli hiyo, kulizungushwa nyavu ngumu kwani hapo kabla simba walikuwa wakiingia na kuwashambulia watalii.

    Kitendo cha wao kutembea mbugani na kuonekana kuwa salama kabisa kilionekana kama muujiza fulani kwa walinzi wale.

    “Tumekuja kupanga vyumba,” alisema Bruno, aliamua kuwakatisha kwani walichokuwa wakikizungumza kilikuwa ni usalama wao tu wakati walipokuwa wakipita mbugani.

    Hilo halikuwa tatizo, wakachukuliwa na kupelekwa ndani mpaka mapokezi ambapo hapo wakachukua vyumba na kutulia.

    Kabla ya kwenda kila mtu chumbani kwake, mzee Todd akataka kukaa na Bruno kwa lengo la kuzungumza naye mambo mengi, hilo halikuwa tatizo, Bruno akakubaliana naye na hivyo kuanza kuzungumza.

    Kitu kikubwa kabisa alichokisema mzee huyo ni kumshukuru Bruno kwa kile alichokuwa amemfanyia, alipambana naye, alimsaidia pasipo kuangalia kama walikuwa wakifahamiana kabla au la.

    Walikutana kwenye meli lakini kwa jinsi alivyokuwa akimsaidia ilikuwa ni kama ndugu yake wa karibu au rafiki ambaye walikutana tangu miaka mingi nyuma.

    “Ni upendo tu! Nitahakikisha unafika nyumbani kwako salama,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo.

    “Nitashukuru sana. Sina familia, unalijua hilo?” aliuliza mzee Todd.

    “Nalijua, sitaki kukumbuka, inaniuma sana kila nikikumbuka kile nilichokuwa nikikiona kwenye televisheni,” alisema Bruno huku uso wake ukionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na huzuni moyoni mwake.

    “Kuna jambo jingine muhimu nitakwambia siku nyingine, labda baada ya kufika nchini Kenya,” alisema mzee huyo na kumruhusu Bruno kuondoka.

    Bruno hakujua ni kitu gani mzee Todd alitaka kumwambia, hakutaka kufikiria sana, kichwa chake kikaanza kumfikiria mpenzi wake, Sharifa ambaye alikuwa nchini Kenya huku akijua kwamba alikuwa marehemu.

    Alitamani sana kumpigia simu lakini hilo lilishindikana kwa kuwa hakuwa na namba ya mtu yeyote kutoka nchini Kenya.

    Hapo, wakakaa siku ya kwanza, wakakaa siku ya pili mpaka ya kumi, hawakutaka kuondoka haraka kwani waliona kuwa hiyo ilikuwa sehemu salama na ya kujificha ambapo kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angebaini kwamba walikuwa mahali hapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***

    Watalii waliendelea kumiminika ndani ya hoteli hiyo, kila siku kulikuwa kunaingia idadi kubwa ya watalii waliofika nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuangalia wanyama waliokuwa katika mbuga hiyo.

    Wakati hao wakiendelea kuingia humo, wengine walikuwa wakiondoka huku wakiwa wamelipa kiasi kikubwa cha dola kilichoifanya nchi hiyo kupiga hatua kubwa kwenye sekta ya utalii.

    Wazungu hao hao waliokuwa wakiingia ndiyo walioweza kumbaini mzee Todd. Siku ya kwanza kumuona tu, hawakutaka kujiuliza, walimfahamu mzee huyo, walikuwa wakifuatilia sana kwenye televisheni kuliko Waafrika ambao mtu huyo alikuwa barani kwao.

    Hawakutaka kuchelewa, haraka sana simu ikapigwa mpaka jijini Johannesburg ambao wao wakawasiliana na polisi waliokuwa katika mbuga hiyo na kuanza kufanya harakati za kumtia mzee huyo mikononi mwao.

    Walikijua chumba alichokuwa amepanga, wateja walisema walimuona mzee huyo akiingia chumbani kwake lakini hakukuwa na mtu aliyejua kama mwanaume huyo alikuwa mzee Todd aliyekuwa akitafutwa dunia nzima.

    Polisi hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakaelekea katika chumba alichokuwa amepanga na kuanza kugonga huku wakihitaji kufunguliwa mlango.

    Hakukuwa na mtu aliyefika kuufungua kitu kilichowapa uhakika kwamba inawezekana mzee huyo alikuwa amelala au alikuwa bafuni akioga. Kwa kutumia kadi ya kuingilia ambayo waliichukua kwa mhudumu, wakaufungua mlango na kuingia ndani.

    Humo, hawakukutana na mtu yeyote yule, kitanda kilikuwa kimetandikwa huku juu ya meza kukiwa na kikombe kilichokuwa na kahawa, walipokwenda kukiangalia, kwa jinsi mule ndani kulivyokuwa ilionyesha kabisa kwamba mtumiaji wa kikombe kile hakuwa ameondoka muda mrefu uliopita, hivyo wakazidi kumtafuta.

    Walimtafuta kila kona lakini hawakuweza kumpa. Wakatoka ndani na kuelekea nje, huko, wakaliona gari moja la watalii likitaka kuondoka mahali hapo kuelekea mbugani zaidi kwa lengo la kuangalia wanyama.

    Wakahisi kwamba mzee huyo alikuwa humo, wakalifuata na kuanza kuwaangalia watalii wote waliokuwa wamesimama na wengine kukaa kwa nyuma, waliangalia kwa makini sana lakini mwanaume huyo hakuonekana.

    Wakajua kabisa kwamba hakuwa humo, wakaondoka kurudi hotelini na kuanza kumtafuta tena. Walitumia nguvu nyingi sana lakini hawakuwa wamefanikiwa hivyo kuwauliza tena wale Wazungu kujua kama kweli mtu waliyekuwa wamemuona ndani ya chumba kile alikuwa mzee Todd au walimchanganya.

    “He was the one!” ( alikuwa yeye?)

    “Madam, we have tried to look for him i every corner but we didn’t find him,” (mama, tumejaribu kumtafuta kila kona lakini hatukumpata) alisema polisi mmoja.

    “But I saw him, he was the one,” (lakini nilimuona, alikuwa mwenyewe) alisema mwanamke huyo huku akionekana kuwa na uhakika wa kile alichokuwa akikizungumza.

    Walimwamini, wakaelekea tena na kuanza kumtafuta lakini hawakufanikiwa kumpata. Hilo liliwashangaza sana, wakatoka na kuanza kuangalia mpaka nje ya hoteli ile, walipomkosa, wakaamua kwenda kuangalia kwenye orodha ya magari yaliyoondoka na watalii kwenda kuangalia wanyama.

    “Yameondoka magari mawili tangu saa moja,” alisema mwanaume aliyekuwa akitoa ruhusa ya kuyaondoka magari hapo kuelekea ndani kabisa ya mbuga hiyo.

    “Sawa.Ila ninachokijua mimi ni kwamba magari huwa yanakwenda upande wa Magharibi, si ndiyo?” aliuliza polisi.

    “Ndiyo! Huenda huko kwa kuwa ndiyo kulipokuwa na wanyama.”

    “Sasa mbona kuna moja limekwenda Mashariki?” aliuliza.

    “Mashariki?”

    “Ndiyo!”

    “Haiwezekani!”

    “Kwani wewe unaporuhusu magari yaondoke, huwa huyaangalii?”

    “Nayaangalia. Dereva alivyopiga simu kuhitaji gari nilimwambia aende ofisini kwangu kuchukua ufunguo kwani nilikuwa nimebanwa na haja hivyo nilikwenda chooni,” alijibu.

    “Basi habari ndiyo hiyo! Kuna moja limekwenda upande wa Mashariki,” alisema polisi huyo, mwenzake akaingilia:

    “Ila si tumeangalia kwenye lile gari lililokwenda Mashariki na tukamkosa?”

    “Ndiyo! Ila kwa nini lielekee Mashariki? Nahisi kuna kitu! Hebu tulifuatilieni,” alisema polisi huyo, wakatoka kwa kasi, wakachukua gari lao na kuanza kulifuatilia gari hilo katika upande ule wa Mashariki huku kila mmoja akihisi kwamba ndani ya gari lile alikuwepo mzee Todd, ila kila walipokuwa wakikumbuka kuwa walipokwenda kuwaangalia watu waliokuwemo mule hawakuweza kumuona, walichanganyikiwa, kwa hiyo safari yao ilikuwa ni kama kwenda kubahatisha tu.



    Tangu walipoanza kukaa katika Hotel ya King Lion hawakuwa na amani kabisa, walikuwa na hofu kwa kuhisi kwamba watu waliokuwa hapo wangeweza kuwagundua.

    Hawakuwa na wasiwasi na watu weusi, waliwajua kwamba hawakuwa wafuatiliaji, hata kama wangeonyeshewa picha sasa hivi kwamba mtu huyu anatafutwa basi ndani ya dakika ishirini kama wangekutana naye ingekuwa vigumu sana kumkumbuka.

    Walichokuwa wakikiogopa ni hao Wazungu waliokuwa wakiingia na kutoka katika hoteli hiyo. Ni kweli mzee Todd alikuwa akivaa kofia na wakati mwingine miwani lakini hilo halikumfanya kuwa na amani moyoni mwake, alihisi kabisa kwamba kuna siku tatizo fulani lingeweza kutokea.

    Walikaa hapo kwa siku kadhaa, baada ya hapo, kuna mtu alionekana kumtilia shaka kwani kila alipokuwa akimwangalia, hakuwa akiyahamisha macho yake kwa haraka, ilikuwa ni kama alikuwa akimfahamu au waliwahi kukutana naye kwa siku chache zilizopita.

    Hiyo haikuwa mara ya kwanza, ilikuwa ni mara nyingi Mzungu huyo alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi naye. Walichokifanya ni kuanza kusuka mipango ya kutoroka kwani wasingeweza tena kuendelea kubaki mahali hapo.

    Hiyo ilikuwa ni mbuga kubwa ya wanyama, kwa ile iliyokuwa upande wa Afrika Kusini iliitwa Kruger ila kwa upande wa Msumbiji iliitwa Limpopo.

    Kutoka Kruger mpaka Limpopo kulikuwa na umbali wa kilometa zaidi ya hamsini, ilikuwa ni mbali mno hivyo walihitaji usafiri wa kuondoka nao kuelekea katika mbuga hiyo.

    Alichokifanya Bruno ni kuanza kufuatilia, alitaka kujua jinsi madereva wa magari yale ya kuwatembeza watalii mbugani walikuwa wakipata vipi ufunguo.

    Kwenye kufuatilia kwake akagundua kwamba kulikuwa na ofisi maalumu waliyokuwa wakienda na kuchukua ufunguo huko.

    Humo kulikuwa na meneja wao, hakuishia hapo, aliendelea kufuatilia na kugundua kwamba meneja huyo hakuwa na choo ndani ya ofisi yake, alipokuwa akitaka kujisaidia, alikwenda katika choo cha wafanyakazi na kujisaidia.

    Mbali na hayo yote, alihitaji nguo. Akapeleleza na kugundua mahali ambapo nguo za madereva zilipokuwa zikikaa. Akaanza kufuatilia ratiba za madereva hao na kugundua kwamba kwa siku kati ya magari nane yaliyokuwa mahali hapo yalikuwa yakiondoka magari sita na mawili kubaki.

    Akajipanga na mzee Todd, siku ambayo walitakiwa kuondoka, Bruno alikuwa akiangalia saa yake tu huku akiwa amemwambia mzee Todd ajiandae.

    Alikaa katika kiti kilichokuwa karibu na ofisi ya meneja wa hoteli hiyo, watu walikuwa wakiingia na kutoka ndani ya ofisi hiyo.

    Hakuwa na haraka, alichokuwa akikiangalia ni idadi ya magari yaliyokuwa kule nje, alikuwa akiyafuatilia kwa karibu kabisa.

    Baada ya saa nne kukaa katika kiti kile, mlango wa ofisi ile ukafunguliwa na meneja kutoka. Akamsalimia na kuelekea chooni kujisaidia.

    Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake, haraka sana akasimama, akachungulia dirishani, gari iliyokuwa imebaki ni Jeep moja na Toyota 110 tatu.

    Akaingia ndani ya ofisi ile, akaangalia huku na kule, funguo zilikuwa zimewekwa kwenye ubao uliopigiliwa ukutani. Akaangalia ufunguo wa Jeep, akauchukua, akaelekea katika chumba kidogo ambacho kilikuwa kikitumika kuhifadhia nguo za wafanyakazi, akachukua shati moja na kutoka harakahara.

    Alipofika nje, akamuita mzee Todd, akamfuata, Wazungu wengine walipomuona mzee Todd akielekea kule kulipokuwa na gari, wakahisi kwamba zamu yao ilikuwa imefika hivyo kuifuata gari ile na kupanda huku mzee Todd akiwa mbele na Bruno.

    “Tutafanyaje kama hawa wamepanda?” aliuliza mzee Todd huku akionekana kuwa na hofu.

    “Tunaondoka nao!”

    “Mbugani?”

    “Hapana! Mjini,” alisema Bruno.

    Hakutaka kuchelewa, hapohapo akaliwasha gari hilo, alipotaka kuliondoa tu, akashtukia akisimamishwa na polisi waliokuwa wakija kule kwa kasi, akatulia na kuwasikilizia huku akionekana kuwa na hofu nzito.

    Polisi wale walifika mahali pale na kuanza kuwaangalia Wazungu wale waliokuwa nyuma, walimwangalia mmoja baada ya mwingine, waliporidhika wakaliruhusu pasipo kuangalia mbele kwani walijua watu waliokuwa wakikaa mbele walikuwa muongozaji na dereva tu.

    Bruno akapiga gia na kuanza kuondoka mahali hapo. Hakuendesha kwa mwendo wa kasi kwa kuwa hakujua kuendesha gari vizuri, pale mbele alikuwa akipewa maelekezo na mzee Todd ambapo kila alipokuwa akiyafuatisha, gari lilikuwa likiondoka mpaka alipozoea.

    Wakaondoka mahali hapo, Wazungu wale nyuma hawakujua mahali walipokuwa wakielekea, walionekana kuwa na wasiwasi kwani walizoea kuona wakiondokea upande wa Magharibi lakini siku hiyo walikuwa wakienda upande mwingine kabisa, upande wa Mashariki.

    Hawakuuliza, gari lilikuwa kwenye kasi, njiani walikuwa wakipishana na wanyama, waliamini kwamba gari lingesimama na wao kuwaangalia wanyama hao na hata kuwapiga picha lakini haikuwa hivyo.

    Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, gari liliendeshwa kwa kasi mpaka lilipofika katika eneo lililokuwa na kibao kilichoandikwa “Welcome Limpopo” yaani wakikaribishwa katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo.

    Ulikuwa ni mwendo mrefu mno, walitumia saa moja na nusu ndani ya hilo gari huku likiwa kwenye mwendo wa kasi. Walipofika sehemu ambayo waliamini kwamba ingekuwa salama, wakateremka na Bruno kuwafuata wale watu kule nyuma.

    “Nisikilizeni,” alisema, kila mtu akawa kimya huku akiogopa.

    “Kana kuna mtu anajua kuendesha gari, aende mbele aendeshe mrudi hotelini, sisi tushafika,” alisema Bruno.

    Hawakutaka kubaki mahali hapo, wakaondoka kusenga mbele ambapo waliamini kwamba kungekuwa salama kabisa.

    Mtalii mmoja akaelekea mbele ya gari lile na kuanza kuliendesha kurudi hotelini huku kila mmoja akishangaa juu ya watu wale, walikuwa wakina nani? Na kama walikuwa wabaya kwa nini hawakuwajeruhi? Kila walichojiuliza walikosa majibu.

    Polisi wale waliokuwa wakielekea kule lilipokwenda gari lile, baada ya nusu saa wakakutana na gari la watalii likirudi hotelini kwa mwendo wa kawaida.

    Wakalisimamisha na kuwauliza kuhusu watu hao, wakawaambia kila kitu kilichotokea na kusisitiza kuwa watu wale hawakuwa hatari kwa sababu kama wangekuwa hatari ilikuwa ni lazima wawafanyizie au hata kuwaibia kila kitu walichokuwanacho.

    “Ni watu wema sana, sidhani kama walikuwa na malengo mabaya, ila ni watu wazuri mno, hawakutujeruhi wala kutuibia,” alisema jamaa mmoja huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikizungumza.

    ***

    “Ni wakina nani hao?”

    “Sifahamu.”

    “Hebu vuta kamera kwa karibu zaidi. Hapohapo, hebu waangalie vizuri!’ alisema mwanaume mmoja.

    Watu wanne walikuwa ndani ya chumba kilichokuwa na kompyuta kadhaa ambazo ziliunganishwa na baadhi ya kamera zilizokuwa zimefungwa katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo.

    Walikuwa wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kupitia katika kompyuta zao. Waliweza kumuona Bruno na mzee Todd wakipiga hatua katika mbuga hiyo.

    Walipowaangalia, kitu cha kwanza kabisa kilichokuja kichwani mwao ni kwamba watu hao walikuwa majangili. Mikononi hawakuwa na bunduki yoyote ile lakini walihisi kwamba inawezekana walikuwa wamezificha sehemu kwa kuwa tu hawakutaka kuonekana nazo.

    Haraka sana simu ikapigwa kuelekea katika kitengo maalumu cha ulinzi na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea. Taarifa iliyotolewa ni kwamba watu hao walikuwa majangili na hivyo walitakiwa kufuatiliwa haraka sana.

    Hilo halikuwa tatizo, vijana waliokuwa na bunduki nzito wakaanza kuelekea huko, upande wa Magharibi ambapo kila mmoja aliamini kuwa walipewa taarifa ya watu hao kwa kuwa walikuwa majangili.

    ***

    Bruno na mzee Todd hawakuwa na habari, walikuwa wakiendelea kusonga mbele huku wakiwa makini kuangalia kila kona. Walimuomba Mungu awalinde kwani mbuga hiyo ilikuwa na wanyama wakali na wakati mwingine walikuwa na sifa ya kuwashambulia watalii waliokuwa wakienda huko.

    Walitembea kwa mwendo wa haraka uliojaa umakini, kila walipokuwa wakiwaona wanyama wanaokula majani, waliongeza umakini zaidi kwani waliamini kwamba pembeni yao kulikuwa na wanyama wala nyama kama simba, chui na wengine wengi.

    Hawakuwa wakiongea, kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, walihisi kabisa kwamba wangesikiwa na wanyama ambao kuna uwezekano walikuwa wamejificha mahali fulani. Waliendelea kupiga hatua na baada ya kufika katika mto Mturuma, wakasimama na kuanza kujadiliana kama ilikuwa ni sahihi kuvuka mto huo au la.

    “Ila unahisi kutakuwa na mamba?” aliuliza Bruno.

    Mzee Todd akauangalia kwa makini zaidi, maji yake yalikuwa yamesimama, aina ya mito hiyo huwa hatari kwa sababu mamba hupendelea kukaa humo. Hawakutaka kuuvuka kwanza, ilikuwa ni lazima kuufanyia upekuzi kabla ya kuchukua uamuzi wa kuuvuka.

    Wakati wakiwa wanajadiliana ndiyo kilikuwa kipindi ambacho askari pori walikuwa wakija kule walipokuwa kwa kasi kubwa. Walikuwa ndani ya magari yao, walishikilia bunduki na kuona kabisa huo ulikuwa muda wa kuwakamata watu hao na kuondoka nao kwani miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikipigwa marufuku na ambavyo kesi yake ilikuwa kubwa ilikuwa ni ujangili.

    Wakati wamekaa hapo, wakasikia mlio wa magari kutoka nyuma yao, waliogopa, walijua tu kwamba walikuwa maaskari, wakabaki wakiwa wamesimama, walikuwa na uwezo wa kuingia ndani ya mto ule lakini mioyo yao ilikuwa migumu kabisa kuchukua uamuzi huo.

    Wakabaki wakiwa wamesimama, magari hayo mawili yakafika, maaskaro watano waliokuwa na bunduki wanateremka na kuanza kuwafuata, walipowafikia, hawakutaka kuzungumza nao jambo lolote lile, wakawachukua na kuondoka nao.

    “Mna bahati sana, yaani mngeingia ndani ya ule mto, tungeipata mifupa yenu tu,” alisema askari mmoja huku akiwaangalia watu hao.

    Ndani ya gari ndipo wakaambiwa kwamba walikuwa chini ya ulinzi kwa kuwa iligundulika kwamba walikuwa majangili. Walishangaa, walijitetea kwamba hawakuwa majangili lakini hakukuwa na mtu aliyewaelewa.

    Walifungwa pingu na kupelekwa mpaka katika kituo cha polisi cha hapo mbugani na kuambiwa kusubiri. Humo, hawakunyamaza, waliendelea kusisitiza kwamba hawakuwa majangili na hivyo walitakiwa kuachwa na kuondoka lakini askari hawakutaka kuwaacha.

    Ilipofika mchana, mlango wa mahabusu ukafunguliwa na kuambiwa kutoka ndani ya mahabusu ile. Wakachukuliwa na kuelekwa katika ofisi ya mkuu wa kituo kwa lengo la kuhojiwa maswali kadhaa.

    Mkuu huyo aliwaangalia, alijua kabisa kwamba watu hao hawakuwa majangili kwa kuwa walipokuwa wamewafuatilia hawakuwakuta na silaha yoyote ile ambayo ingewaonyesha kwamba walikuwa majangili.

    Aliwaweka ofisini kwake na kuanza kuzungumza nao, kitu pekee alichotaka kufahamu ni sababu ya watu wale kuwa mule mbugani, walikuwa wakitafuta nini na walikuwa wakielekea mahali gani.

    “Tulipotea njia,” alisema mzee Todd, alimwambia Bruno kwamba hakutakiwa kuzungumza kitu chochote kile.

    “Kutoka wapi?”

    Wakaanza kumwambia stori nyingine kabisa ambayo ilikuwa ni uongo mtupu, walimwambia kwamba walikuwa na wenzao kutoka nchini Afrika Kusini ambao walikuwa wakitembea katika mbuga ya wanyama kwa lengo la kutafuta dawa za mitishamba lakini wakati wakiwa huko, walikimbizwa na wanyama wakali na kupotea na hata pale walipokuwa hawakujua walikuwa mahali gani mpaka walipofikishwa kituoni.

    Kwa sababu aliongea mzee Todd, aliaminika kwa asilimia mia moja na hiyo kuambiwa kwamba warudi kwanza mahabusu kabla ya kutolea ambapo moja kwa moja wangechukuliwa na kurudishwa Afrika Kusini.

    “Ila sisi siyo Waafrika Kusini!” alisema Bruno.

    “Nyie mmetoka wapi?”

    “Kenya!”

    “Kwa hiyo mnataka mrudishwe Kenya?”

    “Ikiwezekana mkuu kwani tulikwenda Afrika Kusini kwa ajili ya hizo dawa za mitishamba tu!” alisema Bruno.

    “Basi sawa!”

    Wakati wakiwa ofisini kwa mkuu wa kituo, polisi wengine walikuwa katika chumba kingine wakiangalia televisheni. Huko ndipo walipoweza kuiona picha ya mzee Todd akiwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakitafutwa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya nyumbani kwake.

    Polisi wakabaki wakiangalia, mwanaume aliyekuwa akionyeshwa walimfahamu sana, alikuwa yuleyule ambaye walikuwa naye katika kituo hicho. Haraka sana wakainuka na kuelekea ofisini kwa mkuu wao na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haraka sana naye akafungua televisheni na kuangalia kile alichoambiwa, ni kweli alikuwa mzee Todd, mwanaume aliyekuwa akitafutwa na CIA kwa udi na uvumba.

    Wakafurahi, kiasi kilichokuwa kimetolewa kilikuwa kikubwa mno, lingekuwa kosa kubwa kama wangemuachana mwanaume huyo aondoke mikononi mwao.

    Mkuu akawaambia vijana wake kwamba hawakutakiwa kuwashtua, ili waweze kumpata vizuri na kuondoka naye mpaka mjini ambapo huko wangempeleka mpaka katika kituo kikuu cha polisi kilichokuwa Limpopo.

    Ndani ya saa moja, wakawatoa katika mahabusu kirafiki kabisa, waliwaambia kwamba walitakiwa kusafirishwa haraka sana kuelekea nchini Kenya waliokuwa wakitaka kuelekea.

    Kwa jinsi mkuu wa kituo alivyokuwa akiongea, alionekana kumaanisha alichokuwa akiwaambia na hakutaka kuwaonyeshea dalili zozote za kuonekana walikuwa na la jambo.

    Njiani, walikuwa wakizungumza, waligongesheana mikono lakini mioyoni mwao walijua kile ambacho kingekwenda kutokea mbele ya safari.

    Walipanga kupita nao mjini, kwenda sehemu fulani ambao huko wangewaweka chini ya ulinzi na kuwachukua kuwaeleka katika kituo kikuu cha polisi.

    Gari liliendeshwa kwa mwendo wa kawaida kabisa, walikuwa wakipiga mahesabu jinsi ya kuwaweka watu hao chini ya ulinzi kwani kwa jinsi mabosi wa madawa ya kulevya walivyokuwa watu hatari, walihisi kabisa kwamba kama wangefanya mchezo wangeweza kuuawa wao.

    Gari lilibakiza umbali kama wa mita elfu moja kufika katika kituo hicho cha polisi, polisi hao wakaanza kuandaa bunduki zao kitendo kilichowashtua Bruno na mzee Todd na kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichotakiwa kutokea.

    “Mmh!” aligunda Bruno, polisi hao wakawanyooshea bunduki zao na kuwaambia kwamba walikuwa chini ya ulinzi.

    “Jamani! Tumefanya nini?” aliuliza Bruno huku akiambiwa alale chini haraka sana.

    “Todd! Kila mtu anakujua kama wewe ni mtu hatari sana. Upo chini ya ulinzi, ulidhani ungeisumbua dunia kwa kipindi kirefu? Ni muda wako kwenda kuhukumiwa kwa kile kilichotokea, ila pole sana kwa vifo vya familia yako, sikuwa nimekugundua mpaka nilipoambiwa kwamba ni wewe,” alisema mkuu wa kituo huku akitabasamu, polisi wote nane waliokuwa ndani ya gari hilo waliwanyooshea bunduki.

    Simu ikapigwa makao makuu ya polisi na kuambiwa kwamba yule muuza madawa ya kulevya aliyekuwa akisumbua alikamatwa na hivyo walikuwa njiani kuelekea katika kituo kikuu cha polisi hapo Limpopo.

    Polisi wa makao makuu hawakuamini kile walichoambiwa kwamba muuza madawa huyo alikuwa amekamatwa, taarifa zikaanza kusambazwa katika kituo hicho kwamba kila polisi alitakiwa kujiandaa kumuweka chini ya ulinzi mwanaume huyo kwa kuwa alikuwa mtu hatari sana.

    “Wapo wapi?” aliuliza polisi mmoja.

    “Vasco Da Gama,” alijibu polisi mmoja sehemu ambayo haikuwa mbali sana kutoka katika kituo hicho. Polisi wote wakaweka bunduki zao tayari na walichokuwa wakikisubiria ni mwanaume huyo tu.

    ***



    Safari ya kuelekea katika kituo kikuu cha polisi ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Ndani ya gari lile polisi wote walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, kwao, kumpata mzee Todd iliwafurahisha na kujiona wakipata pesa ambazo ziliahidiwa kwa yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwa mtu huyo.

    Bunduki zilikuwa mikononi mwao, walimpa ulinzi wa kutosha kwani walichokijua ni kwamba mwanaume huyo alikuwa hatari sana, kama wasingemlinda kama walivyofanya basi hali ingekuwa ya hatari mno. Mzee huyo alikuwa na Bruno humo, walimwangalia kijana yule, hawakumjua alikuwa ni nani kwa yule mzee lakini kitu walichohisi ni kwamba alikuwa kijana wa mzee Todd ambaye alikuwa akishirikiana naye kuuza madawa ya kulevya barani Afrika.

    Wakati wakiwa wamekwishafika katika eneo maarufu kwa kuuza vitanda, Vasco Da Gama wakashtukia wakianza kumiminiwa risasi mfululizo. Hawakujua watu hao walikuwa wakina nani, walipigwa risasi lakini hawakuwaona watu waliokuwa wakiwashambulia.

    Mpaka wanainama na kujificha, polisi wanne walikuwa chini, damu zilikuwa zikiwatoka. Watu waliokuwa karibu na eneo hilo, hawakutaka kubaki mahali hapo, wakaanza kukimbia kuyaokoa maisha yao. Vijana ambao waliwashambulia polisi hao, wakatoka walipokuwa wamejificha, walikuwa vijana saba wenye silaha kali aina ya AK 47, walitembea kwa mwendo wa kujiamini huku wakiendelea kulifuata gari lile.

    Walipolifikia, wakalizunguka na mwanaume mmoja kuwatangazia polisi waliokuwa humo kwamba walitakiwa kutupa bunduki zao vinginevyo wangelilipua gari hilo. Polisi walivyosikia hivyo wakaogopa na kufanya kama walichoambiwa.

    Walifanya hivyo kwa sababu mbili. Moja ni kwamba walihisi kwamba wangelipuliwa kweli lakini kubwa zaidi ni kwamba hawakuwa wakifahamu watu hao walikuwa wangapi.

    Walipozitupa tu, wanaume hao wakalisogelea gari hilo, wakawaangalia polisi wote, walikuwa wamelala huku wakiwa na mzee Todd na Bruno ambao nao walikuwa kimya. Vijana hao hawakutaka kupoteza muda, walichokifanya ni kuwamiminia risasi polisi wote.

    “Na hawa tuwafanye nini?” aliuliza mwanaume mmoja.

    “Nao wamalize,” alisema mwingine, wakakoki bunduki zao tayari kwa kuwamaliza mzee Todd na Bruno.

    ***

    Milio ya risasi ilikuwa ikiendelea kusikika kama kawaida. Baada ya mzee Todd na Bruno kukimbia kwa kuruka ukuta, Onyango akabaki ndani ya jumba lile na wenzake. Alijua kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, hakujua ni wakina nani walikuwa wakipiga risasi hizo, alichanganyikiwa ndani ya jumba lile kiasi kwamba wakati mwingine alitamani hata ardhi ipasuke atumbukie ndani.

    Alitamani kwenda kupambana lakini kwa jinsi risasi zile zilivyokuwa zikirushwa, alijua kabisa kwamba watu hao walikuwa hatari, kwani risasi zilipigwa kwa malengo na nyingi ziliwapata wenzake.

    Hakutaka kuona akifa, alitakiwa kupambana mpaka anashinda, njia pekee ya kuyaokoa maisha yake ilikuwa ni kuingia katika dari ndani ya nyumba hiyo. Hilo ndilo alilolifanya, haraka sana akaufungua mlango wa dari na kuingia ndani kujificha.

    Huko juu, kulikuwa na harufu chafu, joto lakini alitakiwa kuvumilia kwa sababu tu alitakiwa kuupambania uhai wake. Baada ya dakika chache, mlango ukafunguliwa na wanaume kuingia ndani ya jumba hilo. Aliwasikia vilivyo, wanaume hao wakaanza kuongea ndani ya jumba hilo kwamba watu wote walikuwa wamekufa.

    Kwa jinsi Kiingereza chao walivyoongea, alijua kabisa walikuwa Wamarekani, hawakuwa Wazungu wa Afrika Kusini, hakujua sababu za watu hao kuwa mahali hapo na kuwashambulia kiasi hicho. Baada ya dakika moja tu, wanaume hao wakaondoka baada ya kuhakikisha kwamba kila mtu aliyekuwa ndani ya nyumba ile alikuwa amekufa.

    Huku akijiandaa kuteremka, akasikia mlango ukifunguliwa tena, muda huo alikuwa Bruno ambaye alifuata kadi ya ATM. Hakumuona, alichokijua ni kwamba alikuwa mmoja wa Wazungu wale hivyo akajificha kama kawaida. Baada ya sekunde kadhaa, mlango ukafungwa na mwanaume huyo kuondoka.

    Baada ya nusu saa, Onyango akateremka kutoka ndani ya dari, kile alichokiona kilimsikitisha kupita kawaida, hakuamini kama marafiki zake wote walikuwa wamekufa ndani ya nyumba hiyo.

    Hali iliyokuwa ndani ndiyo iliyokuwa na nje pia, kila kona kulitapakaa miili ya marafiki zake. Siku hiyo hapo Soweto kulikuwa na msiba mzito, watu walilia sana na kuwachukua Wazungu kupita kawaida.

    Siku iliyofuata, Onyango akawatafuta watu wengine wa kuunda kundi jingine. Alikuwa na hasira mno na hakutaka kabisa kuona wakiendelea kushambuliwa na Wazungu, ilikuwa ni lazima wahakikishe wanapambana vilivyo.

    Kundi jingine likaundwa, ingawa alikuwa Mkenya lakini kila Msauzi alikuwa akimpenda, alikuwa mkorofi sana, alijua kupambana na hata kuwalaghai watu wengine waungane naye.

    Kuunda kundi kubwa tena haikuchukua siku moja, ilichukua wiki mbili, vijana ishirini wakajikusanya na kuunda kundi jingine kubwa la wahuni. Walichokuwa wakikihitaji zaidi kilikuwa ni silaha tu.

    Walizokuwa nazo, hazikutosha, walitakiwa kujipanga na kutafuta nyingine. Baada ya kundi kutimiza mwezi, wakaamua kuondoka hapo na kwenda nchini Msumbiji.

    Walichokuwa wakikihitaji kilikuwa ni bunduki tu. Waliogopa kufanya uhalifu Afrika Kusini kwa kuwa walihofia maisha yao na kutafutwa. Hawakutaka kuharibu huko, walitakiwa kuharibu sehemu nyingine kabisa, hivyo wakaenda huko.

    Watu waliokuwa na bunduki walikuwa polisi hivyo kuanza kuchunguza na kugundua kwamba kulikuwa na gari la polisi lililokuwa likitoka katika Mbuga ya Limpopo na kuelekea mjini huku wakiwa na bunduki ndani ya gari hilo.

    Hiyo ikawa nafasi yao, wakaelekea mjini na kutafuta sehemu kujificha. Hakukuwa na mtu aliyeonekana kuwa na hofu nao, walivaa kiheshima na walikuwa wakirandaranda mpaka kipindi ambacho gari la polisi lilipoanza kuonekana.

    Hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuanza kulishambulia, watu waliokuwa mahali hapo wakakimbia kwani walijua kabisa kwamba watu hao walikuwa hatari. Kwa kuwa mule kulikuwa na polisi nane, waliamini kwamba kungekuwa na bunduki za idadi hiyo ambazo zingewafanya kuwa na idadi kubwa ya bunduki na hivyo kuendelea kufanya uhalifu.

    “Na hawa tuwafanye nini?” aliuliza mwanaume mmoja.

    “Nao wamalize,” alisema mwingine, wakakoki bunduki zao tayari kwa kuwamaliza mzee Todd na Bruno.

    Huku kijana yule akijiandaa kuwafyatulia risasi watu hao, Onyango akaamuru waache kwani alitaka kuwaona kwanza. Hilo halikuwa tatizo, kijana huyo akaacha, Onyango akasogea mpaka kule, watu aliowaona, yeye mwenyewe akashtuka.

    “Bruno!” aliita huku akionekana kushtuka.

    “Onyango!”

    “Vipi tena? Mbona sielewi?” aliuliza Onyango huku akiwaangalia kwa mshangao mkubwa.

    Bruno hakujibu kitu, kitendo cha kumuona Onyango tu kilimaanisha kwamba maisha yao yangekuwa salama. Hilo lilikuwa eneo la tukio, hawakutakiwa kukaa sana mahali hapo, walichokifanya ni kuchukua bunduki walizokuwa wakizitaka na kuondoka mahali hapo.

    Wakaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea nchini Afrika Kusini kupitia katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo. Walijua njia za panya, walijua njia ambazo hakukuwa na kamera.

    Asubuhi ya siku iliyofuata wakafika huko, wakaelekea mpaka Soweto na kupumzika. Huko ndipo Bruno akaanza kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea, kwamba walikuwa na mpango wa kwenda Kenya lakini wakajikuta wakikamatwa.

    “Mnataka kurudi Kenya?” aliuliza Onyango.

    “Ndiyo!”

    “Basi subiri nifanye mpango! Endeleeni kukaa hapa.”

    Hawakuwa na jinsi, waliambiwa kwamba walitakiwa kusubiri na hivyo kufanya hivyo. Waliendelea kubaki mahali hapo huku siku zikiendelea kukatika. Alichokuwa akikifanya Onyango ni kuwatafutia watu ambao aliwaamini ambao wangewachukua watu hao mpaka nchini Kenya.

    Bruno alikuwa na mawazo tele, kwake, siku moja ilionekana kuwa na saa arobaini na nane kwani alikuwa akisubiri sana lakini hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.

    Wakati mwingine Bruno alikuwa akimuuliza kuhusu namba za simu za watu aliokuwa akiwafahamu nchini Kenya. Kwa Onyango, hilo halikuwa tatizo, aliwafahamu watu hao kwani kulikuwa na Wakenya wengi kutoka katika Kijiji cha Guolduvai.

    Onyango akawa na kazi mbili, kwanza kuwatafuta vijana ambao wangefanikisha wao kufika nchini Kenya lakini pia vijana ambao walitoka katika kijiji hicho.

    Baada ya mwezi kukatika ndipo akafanikiwa na hivyo kuwasiliana na Onyango na kumwambia kwamba kila kitu kilikuwa tayari.

    Hata kabla Onyango hakumpelekea namba ya simu ya Alfred, mwanaume ambaye alimpata Afrika Kusini, akaamua kumpigia simu yeye mwenyewe na kuanza kuzungumza naye.

    Alimwambia kwamba Bruno, mwanaume ambaye bila shaka alisadikiwa kufariki dunia nchini Kenya alikuwa hai nchini Afrika Kusini, ila mbali na hilo, alimwambia kwamba inawezekana Bruno akaja kuwa bilionea mkubwa kwa kuwa alikuwa na bilionea mkubwa ambaye alimsaidia kwa kila kitu.

    “Bruno namkumbuka! Kijiji kizima kinajua kwamba amekufa,” alisema Alfred.

    “Hajafa! Tupo naye huku!”

    “Wapi?”

    “Afrika Kusini!”

    “Inawezekana vipi?”

    “Ndiyo hivyo, ni stori ndefu, nafikiri akija huko atakwambia nini kilitokea,” alisema Onyango.

    “Kwa hiyo nifanyeje?”

    “Amesema mtafute rafiki yake anayeitwa Abdul, umwambie kwamba yupo hai!”

    “Na nimwambie kuhusu ubilionea wake?”

    “Hilo juu yako sasa!” alisema Onyango na kukata simu.

    Baada ya hapo, akarudi nyumbani na kumwambia Bruno kwamba kila kitu kilikuwa tayari hivyo walichotakiwa ni kuanza safari siku inayofuata. Hilo halikuwa tatizo, wakajiandaa, ilikuwa ni lazima waondoke nchini humo kwani walikuwa wamekaa mno huku wakinusurika vifo na vifungo.

    Bruno hakutaka kuridhika, alihitaji kuzungumza na huyo mwanaume kutoka nchini Kenya, hilo halikuwa tatizo, akapewa namba ya simu na kumpigia lakini kwa bahati mbaya, siku ya Alfred haikuwa ikipatikana.

    Mpaka kesho yake inafika na kuondoka, bado simu ya mwanaume huyo haikuwa hewani. Vijana wanne walikuwa wakiondoka nao kuelekea nchini Kenya, hawakutakiwa kufika huko, walitakiwa kuishia njiani lakini pia hawakutakiwa kupitia Msumbiji, walitakiwa kupitia Botswana, Zambia, Tanzania na kuingia nchini Kenya.

    Waliiona hiyo kuwa safari ndefu lakini walikuwa na uhakika kwamba watu hao wangeweza kufika huko salama kabisa. Baada ya kujiandaa kwa kila kitu, wakaanza safari hiyo kwa siri kubwa sana kuelekea nchini Kenya.

    Wakati huo, tayari Bruno alikwishachukua kiasi cha dola laki moja benki ambapo dola elfu ishirini alimgawia Onyango kama shukrani huku akimuahidi kumtumia kiasi kingine cha pesa baada ya kufika nchini Kenya.

    Safari ikaanza, ilikuwa ni ndefu na yenye kuchosha sana. Waliondoka kwa kujifichaficha sana mpaka wakatoka nje ya Afrika Kusini na kuingia Botswana.

    Huko, njiani kote ni pesa tu ndiyo iliyokuwa ikitumika. Walipokuwa wakiona mambo magumu, walitoa kiasi cha pesa na kuwahonga polisi hivyo kuruhusiwa kupita katika sehemu ambazo hawakutakiwa kufika.

    Walipoingia huko nchini Botswana, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuchukua hoteli ya kawaida na kutulia. Bruno aliendelea kumpigia simu Alfred lakini hakuwa akipatikana, hilo lilimchanganya, alichokuwa akihitaji ni kuzungumza na mwanaume huyo na kumwambia kuhusu kwenda kule alipokuwa akiishi na kumwambia Abdul kwamba alikuwa hai.

    Safari hiyo ilichukua wiki tatu mfululizo na ndipo wakafanikiwa kufika Tunduma nchini Tanzania. Hapo, wakachukua basi Mbeya Mjini ambapo huo ndiyo ungekuwa mwanzo wa kuelekea nchini Kenya.

    Njiani, walichoka mno, walitamani hata Tanzania uwe mwisho wao, hawakutaka kuendelea zaidi lakini hawakuwa na jinsi. Walikuwa na pesa za kutosha, walipofika Mbeya Mjini, wakaelekea katika duka la kubadilisha pesa na kuchukua pesa za Kitanzania kiasi cha shilingi milioni sita na kuendelea na safari yao.

    Kidogo kuwepo nchini Tanzania kuliwapa amani. Watu wa huko hawakuwa wakiangalia televisheni sana, walizipata taarifa kuhusu mzee Todd lakini hakukuwa na yeyote yule aliyeonekana kujali kuhusu mzee huyo.

    Hapo Mbeya Mjini, walikaa kwa usiku mmoja na asubuhi wakapanda basi na kuanza safari ya kuelekea jijini Tanga. Safari yao ilichukua saa kumi na mbili wakafika jiji humo ambapo wakatulia katika nyumba ya wageni huku wakijiandaa safari ya kuelekea Mombasa.

    “Tunaingia Kenya kesho, ila pia tutatakiwa kuingia kwa njia za panya kama tulivyofanya huko nyuma,” alisema Bruno.

    “Ila Kenya si kwenu?”

    “Ndiyo! Sina hati ya kusafiria, nahisi litakuwa tatizo!”

    “Sawa. Basi tutatumia pesa kama kawaida,” alisema mzee Todd.

    Hilo ndilo la msingi lililotakiwa kufanywa. Walichokifanya siku iliyofuata ni kuanza safari kwa njia ya basi kuelekea nchini Kenya. Njiani, hawakuonekana kuwa na hofu, waliamini kwamba wangefika nchini humo salama kabisa.

    Basi lilitembea kwa mwendo wa kasi kuelekea mpakani mwa Tanzania na Kenya. Japokuwa huko kulikuwa na ulinzi mkubwa lakini walikuwa na uhakika wa kupita pasipo tatizo lolote lile. Ndani ya basi walikuwa wakizungumza mambo mengi, mzee Todd alimshukuru mno Bruno kwa kuwa alimsaidia sana mpaka kipindi hicho kuwa hai.

    Hakuwa na familia yake lakini kitendo cha kuwa hai kipindi hicho kilimpa uhakika wa kuendelea kuishi na kujipanga kwa ajili ya maisha yake ya mbele.

    Kulikuwa na kesi ya kuuza madawa ya kulevya, hakutaka kufikiria hilo sana kwani alikuwa na uhakika wa kulishinda, kitu pekee na cha umuhimu kabisa kilikuwa ni kuelekea nchini Marekani na kuendelea na maisha yake.

    “Nakushukuru sana Bruno, bila wewe nadhani sasa hivi ningekuwa marehemu,” alisema mzee huyo huku akimwangalia Bruno.

    “Tumesaidiana! Hata mimi nakushukuru sana! Naamini kila kitu kilitokea kwa mpango wa Mungu!” alisema Bruno huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.

    “Unahitaji nini nikufanyie?” aliuliza mzee huyo.

    “Unifanyie?”

    “Ndiyo!”

    “Mimi ni masikini sana, mkwe hanitaki kwa kuwa mimi ni masikini!” alisema Bruno.

    “Hilo si tatizo! Kuna jingine ambalo unataka nikufanyie?” aliuliza mzee Todd.

    “Labda kukitengeneza Kijiji cha Guolduvai ninapoishi, hakuna zaidi,” alijibu Bruno.

    Walikaa na kuzungumza mengi, wakati huo safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Baada ya saa kadhaa, wakakaribia katika mpaka wa Tanzana na Kenya kwa upande wa Tanga ulioitwa Horohoro.

    Siku hiyo ilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, kulikuwa na idadi kubwa ya magari yaliyokuwa yakisubiri kuingia nchini Kenya. Mbali na magari hayo, pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakitaka kuingia na kutoka.

    Kila basi, abiria walitakiwa kuteremka na kuangaliwa hati zao za kusafiria. Kwao, hawakuwa na kitu chochote kile, walichokuwa wakikitegemea kilikuwa ni pesa tu walizokuwanazo.

    ***

    Mzee Hamidu alichanganyikiwa, alimwangalia binti yake, Ashura aliyekuwa kitandani ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB), moyo wake ulimuuma mno. Ugonjwa huo ulikuwa ukimsumbua kwa kipindi cha mwezi mzima, aliambiwa na daktari hapo Mombasa kwamba alitakiwa kumpeleka Nairobi kwa ajili ya matibabu lakini hakuwa na pesa.

    Kumpeleka Ashura huko kulihitaji kiasi kikubwa cha pesa, shilingi elfu hamsini ya Kikenya ambazo zilikuwa ni kama milioni moja kwa pesa za Kitanzania. Kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho hata kama angefanya kazi kwa mwaka mzima bado asingeweza kupata kiasi hicho.

    Alimwangalia Ashura, moyo wake ulimuuma mno, alihitaji pesa kuliko kitu chochote kile. Japokuwa alikuwa mkuu wa polisi mpakani lakini bado mshahara wake haukuwa ukitosha kwa kuwa alikuwa akikatwa madeni mengi ambayo aliwahi kukopa serikali.

    Mke wake alikuwa ni mtu wa kulia tu, moyo wake ulimuuma, kila siku alikaa pembeni ya binti yake aliyekuwa akikohoa madonge makubwa ya makohozi, alitumia dawa mbalimbali lakini zote hizo hazikuweza kumtibu Ashura.

    Siku zikakatika, mzee Hamidu akawa ni mtu mwenye mawazo tele na hata ufanyaji kazi wake haukuwa kama ule ambao ulitakiwa kuwa kwa kuwa muda mwingi alikuwa akimuwaza Ashura aliyekuwa akiteseka kitandani.

    Wakati hali ya binti yake ikiendelea kuwa hivyo huku akiwa anaendelea na kazi yake ofisini ndipo akapelekewa watu wawili ofisini kwake, mmoja alikuwa Mzungu na mwingine mtu mweusi aliyejitambulisha kwa jina la Bruno.

    Watu hao walichukuliwa kutoka ndani ya gari lililokuwa likiingia nchini Kenya kupitia mpakani hapo. Hawakuwa na kitu chochote kile, walikuwa wakiingia nchini Kenya pasipo kibali na hata huyo aliyekuwa akisema kwamba alikuwa Mkenya, hakuwa na kitu chochote kile ambacho kingemtambulisha kwamba alikuwa raia wa nchi hiyo.

    Mzee Hamidu aliwaangalia, kichwa chake kilivurugika kabisa, hakuwa na hamu ya kuendelea kufanya kazi, alifikiria sana nyumbani kwake, hali aliyokuwa ameiacha kwa binti yake, ilikuwa mbaya mno.

    Bruno na mzee Todd waliogopa, walitamani sana kuingia nchini Kenya lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa, waliona kabisa wangerudishwa au kwenda kufungwa gerezani kwa kile kilichotokea.

    Walibaki wakimwangalia mzee Hamidu, alikuwa kimya huku akiwaangalia kwa zamu. Kitu ambacho kilikuja kichwani mwa Bruno kilikuwa ni pesa tu.

    Walikuwa watu watatu ndani ya ofisi ya mzee huyo, hiyo ilikuwa nafasi ya Bruno kuhakikisha anampa rushwa mzee huyo ili wavuke salama mpakani hapo. Hakuamini kama kungekuwa na Mwafrika ambaye angekataa pesa, kila mtu alihitaji pesa kwa kuwa mishahara ya wafanyakazi wa Afrika haikuwa ikitosha kabisa.

    “Mlikuwa mnavuka mpakani pasipokuwa na vibali, ni kweli?” aliuliza mzee Hamidu huku akiwaangalia.

    “Ni kweli ila...”

    “Hakuna cha ila, suala ni kwamba mlikuwa mnavuka bila vibali, tena mkajiamini kwa kuona kuwa polisi hawawezi kuwababaisha, mkaona kabisa kwamba sisi si kitu na ndiyo maana mkajiamini, si ndiyo?” aliuliza mzee Hamidu, alionekana kuwa siriazi kupita kawaida, na kila alipokuwa akizungumza, alionyesha na vitendo kabisa.

    Kwa jinsi alivyoonekana, ilikuwa vigumu kwa Bruno kuhisi kama mzee huyo angekubali kupokea rushwa, alionekana mwanaume mkakamavu ambaye aliiheshimu mno kazi yake.

    Aliwaambia mambo mengi mno, aliwatisha lakini mwisho wa siku Bruno akamuonyeshea noti ya dola mia moja na kumwambia kwamba awaruhusu kupita mahali hapo. Mzee Hamidu akatulia, aliiangalia dola ile, akasimama na kwenda pembeni kabisa ya ofisi ile, akasimama na kuuangalia ukuta.

    Hakukuwa na kitu ambacho alijiahidi kutokukifanya katika kazi yake kama kupokea rushwa, kitendo cha kuiona dola ile, kilimkumbusha mtoto wake aliyekuwa nyumbani ambaye alisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu.

    Alikaa katika hali hiyo kwa dakika moja na nusu, akayageuza macho yake kwa Bruno na mzee Todd, alikuwa akilia kitu kilichomfanya kila mmoja kumshangaa.

    Hakutaka kuwaficha, aliwaambia kwamba hakuwa na lengo la kupokea rushwa, angewaruhusu kuondoka na kuingia nchini Kenya kwani kwa jinsi walivyoonekana, walionekana kuwa na kiu kubwa ya kuingia nchini humo, ila kutokana na hali aliyokuwanayo binti yake, hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kuichukua pesa hiyo.

    “Ninaichukua kwa sababu ya mtoto wangu!” alisema mzee Hamidu.

    “Amefanyaje?”

    “Ni mgonjwa mno! Leo mnaponiona hapa, sijajua ni kitu gani kitaendelea nyumbani,” alisema mzee Hamidu, hakupanga kuwaambia watu hao suala hilo lakini alijikuta akiwashirikisha.

    Kwa jinsi alivyozungumza, alitia huruma mno, alionekana kuguswa na kile kilichokuwa kikiendelea. Bruno na mzee Todd wakajikuta wakishikwa na huruma, mioyo yao ikajawa na simanzi.

    “Tutakusaidia, atakwenda hospitali, atatibiwa na kupona kabisa,” alisema mzee Todd maneno ambayo yalimshtua sana mzee Hamidu.

    “Kweli?” aliuliza huku akionekana kutokuamini.

    “Niamini!” alisema.

    Mzee Hamidu akasimama, akawasogelea na kuwakumbatia. Kwake, kilichokuwa kikiendelea aliona kama ndoto fulani hivi ambapo baada ya muda angeshtuka kutoka usingizini.

    Hakukuwa na kesi tena, wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa mzee huyo. Walipoonyeshewa Ashura, wao wenyewe walikiri kwamba msichana huyo alikuwa kwenye matatizo makubwa na alihitaji msaada.

    Wakachukua gari na kuondoka kuelekea jijini Nairobi. Walitumia saa tatu, wakaingia jijini humo ambapo Bruno akaenda kubadilisha pesa na kuchukua pesa za Kenya na kumpeleka hospitalini.

    Walipofika huko, mzee Todd hakuteremka, alibaki ndani ya gari. Bruno, mzee Hamidu, Ashura na mke wa mzee huyo wakaingia ndani ya hospitali na kuonana na daktari, malipo yakafanyika na msichana huyo kulazwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hiki kitakusaidia wewe na familia yako,” alisema Bruno na kumpa mzee huyo dola elfu kumi na kuondoka zake.

    Mzee Hamidu hakuamini, akamsogelea mke wake na kumkumbatia, kwa kiasi alichopewa kilikuwa kikubwa mno ambacho kama angeamua kumtibu mtoto wake, basi wangempa matibabu yote na hata chenji kubaki, tena nyingi tu.

    Upande wa pili, Bruno na mzee Todd wakakodi teksi na kuanza kuelekea Mombasa katika kijiji cha Guolduvai. Njiani, mawazo ya Bruno yalikuwa yakimfikiria mpenzi wake, Sharifa, hakujua ni kitu gani kingetokea huko, moyo wake ulikuwa na furaha tele, alitaka kumuona tena, alitaka kuzungumza na mzee Jumanne na kumwambia kwamba alitaka kumuoa msichana huyo kwa kuwa tu alikuwa na pesa, hakuwa masikini kama alivyokuwa kipindi cha nyuma.

    “Siamini kama ninakwenda kumuona Sharifa, ni kipindi kirefu sana kimepita,” alisema Bruno huku akionekana kutokuamini.

    Barabara haikuwa mbaya, dereva aliendesha gari kwa mwendo wa kawaida kabisa. Ndani ya teksi, kila mmoja alikuwa kimya, vichwa vyao vilikuwa na mawazo tele na kitu pekee alichohitaji Bruno ni kufika nyumbani huko haraka iwezekanavyo.

    ***

    Sharifa alibaki akimwangalia Alfred, hakuamini kile alichokisikia kwamba Bruno alikuwa na pesa na alikuwa amemtumia kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya ya matumizi yake.

    Dola laki moja kilikuwa kiasi kikubwa sana, angeweza kukitumia mwaka mzima na pesa nyingi zingebaki, kwake, hizo pesa hazikuwa tatizo, hazikuweza kumletea furaha zaidi ya kumuona mpenzi wake huyo.

    Alimuuliza zaidi Alfred kuhusu Bruno, angefika lini kwani alikuwa amkataa kuolewa kwa ajili ya mwanaume huyo hivyo alitaka kufahamu ukweli.

    “Atafika tu,” alijibu Alfred.

    “Lini?”

    “Sijajua ila atafika tu!”

    Moyo wa Sharifa ukanyong’onyea, hakutaka kurudi nyumbani kwa kuwa tayari alikataa kuolewa kwa ajili ya mwanaume huyo ambaye moyo wake ulitokea kumpenda kwa kiasi kikubwa mno.

    Walichokifanya ni kwenda benki ambapo Sharifa akafunguliwa akaunti na kiasi kile cha pesa kuhamishiwa katika akaunti yake huku akimwachia Alfred kiasi cha dola elfu kumi kama shukrani kwake.

    Alikaa nyumbani kwa Alfred mpaka ilipofika usiku ndipo akaondoka na Abdul kurudi nyumbani kwao. Mzee Jumanne alipomuona, akamfuata na kuanza kumpiga vibao mfululizo, kwa kile kilichokuwa kimetokea, kilimdhalilisha na kumfanya kuonekana hana maana.

    Watu walitoka jijini Nairobi mpaka kijijini hapo kwa ajili ya kufunga ndoa lakini kilichotokea hapo, msichana huyo akakimbia.

    Kwake ilikuwa ni aibu kubwa, hakuamini kama binti yake wa kumzaa angeweza kufanya kitu kama kile. Sharifa alilia mno, akaondoka na kuelekea chumbani kwake. Huku nyuma mzee Jumanne alikuwa mtu wa kulalamika tu, alimwambia mke wake kwamba Sharifa aliwadhalilisha sana.

    Mke wake alimpoza lakini hakupozeka, hasira alizokuwanazo hapo zilikuwa ni za kiwango cha juu kabisa.

    Kijijini hapo, habari ikawa ni Sharifa tu, kile alichokifanya hakikuwa kitu kizuri na watu wengi walimlaumu kwa kuwa alikataa kuolewa na mwanaume mwenye pesa kisa Bruno ambaye mpaka kitu hicho hakukuwa na mtu aliyejua mahali alipokuwa, na hata kama alikuwa hai, kila mmoja alijua kwamba alikuwa masikini wa kutupwa.

    Siku zikaendelea kukatika, bado Sharifa alikuwa na hamu ya kumuona mpenzi wake, hakutaka kumwambia baba yake kuhusu pesa alizokuwa nazo kwenye akaunti, kila kitu kiliendelea kuwa siri huku akitamani kumuona Bruno akirudi kijijini hapo na kuanza maisha wote wawili.

    “Bruno! Rudi mpenzi, ninakukumbuka mno, sikutaka kuolewa kwa ajili yako, rudi mpenzi, nimekukumbuka,” alisema Sharifa. Hayo ndiyo maneno aliyokuwa akiyazungumza kila siku.

    Kiasi kile cha pesa kilichokuwa benki hakutaka kutumia pesa yoyote ile, alitulia nyumbani huku sala yake ikiwa ni kumuona mwanaume huyo.

    Siku ziliendelea kukatika, mpaka mwezi unakatika, bado Bruno hakuwa amerudi kitu kilichoanza kumtia wasiwasi moyoni mwake.

    ***

    “Bruno….Bruno…Bruno….” zilisikika kelele za watu kutoka mitaani, wanawake waliokuwa wakichota maji kisimani wakaacha na kuanza kuelekea kule kelele zile zilipokuwa zimesikika. Kila mtu alikuwa na shauku ya kumuona huyo Bruno aliyekuwa akishangiliwa na watu waliokuwa mitaani.

    Watu waliokuwa ndani ya nyumba zao wakatoka na kwenda kushuhudia kile walichokuwa wakikisikia, waliokuwa pembezoni mwa bahari nao wakaelekea kule kujionea kwa macho yao. Kila kona gumzo lilikuwa ni Bruno, alisababisha kasheshe mtaani na ndiyo maana watu walipolisikia jina lake wakatoka kwenda kujionea kwa macho yake.

    Bruno alisimama nje ya teksi huku akiwa na mzee Todd, alikuwa akikiangalia kijiji hicho, uso wake ulikuwa na tabasamu pana, hakuamini kama alirudi kijijini humo baada ya kupotea kwa miezi kadhaa. Alikuwa amekonda, hakuwa kama alivyoondoka kipindi cha nyuma.

    Watu walimsogelea na kumwangalia, walitaka kuamini kama alikuwa yeye au mtu mwingine. Wengine wakamsogelea na kumshika, walitaka kuona kama alikuwa mtu halisi au mzimu.

    Pembeni yake alikuwepo mzee Todd, watu hawakutaka kufahamu kuhusu mzee huyo wa Kizungu, walitaka kufahamu kuhusu Bruno, ilikuwaje mpaka awe hai kipindi hicho?

    Wakati watu walipokuwa wakipiga kelele za Bruno, Sharifa alikuwa nyumbani kwao akiendelea na kazi zake kama kawaida. Alikuwa mnyonge, hiyo haikuwa siku hiyo tu, hayo yalikuwa maisha yake ya kila siku.

    Akiwa anaosha vyombo akasikia kelele nje huku jina la mpenzi wake likisikika. Alichanganyikiwa, vyombo havikuosheka tena, akasimama, akavalia khanga yake na kutoka ndani huku akikimbia.

    Alichanganyikiwa, alitaka kuona kile alichokuwa amekisikia, alikimbia mpaka mahali kulipokuwa na teksi, alipoanga vizuri, alimuona mpenzi wake akiwa amesimama na mwanaume mmoja wa Kizungu, hakutaka kubaki alipokuwa, akaanza kumfuata kwa kumkimbilia, alipomkaribia, akamrukia, wakaanguka chini huku watu wengine wakibaki wakiwa wamepigwa na butwaa.

    “Bruno! Bruno...” aliita Sharifa huku machozi ya furaha yakianza kutoka.

    Kwake ilikuwa ni vigumu kuamini moja kwa moja kwamba mtu aliyekuwa amemkimbilia na kudondoka naye chini alikuwa Bruno. Alimpenda, alikuwa mwanaume wa ndoto yake ambaye hakutaka kumuacha hata siku moja.

    Machozi ya furaha yalikuwa yakimtoka, hakuamini alichokuwa akikiona, wakati mwingine alihisi kama yupo kwenye ndoto. Watu walizidi kukusanyika, kila mtu aliyekuwa akimuona Bruno, hakuyaamini macho yake.

    Hazikupita dakika nyingi Abdul akatokea, uso wake ulikuwa kwenye tabasamu pana, alichanganyikiwa kwa furaha, rafiki wake wa kipindi kirefu, aliyepotea, Bruno alikuwa mbele ya macho yake.

    Akamsogelea, akamsalimia na kumkumbatia. Siku hiyo ilikuwa ni furaha kijiji kizima, kila mmoja alionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Kabla ya kufanya jambo lolote lile, Abdul akamuuliza kilichokuwa kimetokea baharini kwani waliambiwa na akina James kwamba alizama.

    “Walinitupa baharini, sikujua lengo lao lilikuwa nini,” alisema Bruno.

    “Walikutupa?”

    “Ndiyo! Walitaka nife, nahisi walitumwa, ila sitaki kukumbuka, nimesamehe kila kitu,” alisema Bruno huku akiwa na tabasamu.

    Mzee Jumanne alikuwa nyumbani kwake, si kwamba hakusikia kelele kuhusu Bruno, alizisikia sana, moyo wake ulijawa na hasira nyingi, hakuamini kama mwanaume huyo alikuwa amerudi kijijini akiwa mzima kabisa.

    Mule alipokaa, alishindwa hata kutoka kwenda nje, uso wake ulikuwa na hasira mno na hakukuwa na kitu chochote alichohitaji kusikia kutoka kwa mwanaume huyo.

    Aliwahi kumpiga mkwara mwingi kuhusu kuachana na binti yake lakini kijana huyo hakusikia, ilimuuma sana kwa kuwa hakutaka binti yake aolewe na Bruno kisa tu alikuwa masikini.

    Kule walipokuwa, Bruno akamtambulisha mzee Todd kwa Abdul kwani aliamini kwamba hakuwa akimfahamu na baada ya hapo wakaanza kwenda nyumbani kwa mzee Jumanne huku Sharifa akiwa pembeni yake.

    Walipofika, wakaingia ndani, wakakaribishwa na kukaa kwenye makochi yaliyoonekana kuanza kuchakaa. Mama yake Sharifa alipokuwa akimwangalia Bruno, hakubadilika, alikuwa vilevile kama alivyokuwa kipindi cha nyuma.

    Nyumba nzima walimchukia, hawakumpenda kwa kuwa yeye ndiye aliyemfanya Sharifa kukataa kuolewa na kijana kutoka katika familia ya kitajiri mwezi uliopita.

    Mzee Jumanne akaitwa, akaelekea sebuleni, alipofika hapo, macho yake yakatua katika nyuso za watu hao, hakucheka wala kuonyesha tabasamu, alitaka kuonekana kwa watu hao kwamba alikuwa akimchukia Bruno kupita mtu yeyote katika dunia hii.

    Walikaa na kuzungumza, kitu ambacho Bruno alimwambia mzee Jumanne ni kwamba alitaka kumuoa Sharifa na kuondoka naye kuishi Nairobi ambapo aliamini kwamba biashara zake zingekuwa huko.

    “Umuoe Sharifa?” aliuliza mzee huyo.

    “Ndiyo!”

    “Kivipi? Huna kitu chochote kile, unataka uende kumuua binti yangu kwa njaa? Hakuna ujinga kama huo,” alisema mzee Jumanne huku akionekana kukataa kabisa binti yake kuolewa na Bruno.

    “Mzee! Mimi si Bruno niliyeondoka! Hicho ni kitu cha muhimu sana ambacho unatakiwa kukifahamu. Niambie unahitaji nini,” alisema Bruno.

    Mzee Jumanne akanyamaza, kwa jinsi Bruno alivyoongea alionekana kujiamini kupita kawaida. Hakujua sababu ni yule Mzungu au la. Alimwangalia, bado muonekano wake haukuonekana kuwa kama mtu mwenye pesa, alimdharau na aliona kabisa kijana huyo hakustahili kuishi na binti yake.

    “Baba! Nitakupa kitu chochote utakachohitaji. Nitakununulia boti za kuvulia samaki zaidi ya tano, achana na mitumbwi, hizo sitokununulia kama kujipendekeza, nitakununulia kama zawadi za kunitunzia huyu Sharifa. Na boti hizo zitaingia hapa kesho,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo.

    Mzee Jumanne hakuamini alichokisikia, akamwangalia Bruno, kwa jinsi alivyokuwa akiongea, alionekana kumaanisha mno lakini kwake ilionekana kama kichekesho fulani hivi. Hakutaka kusema kitu chochote kile, akapuuzia na kunyanyuka kuelekea chumbani kwake.

    Bruno hakutaka kujali, yeye pamoja na wenzake wakasimama na kutoka ndani, huko nje walipokwenda, watu walijikusanya nyumbani hapo, kila mtu alitaka kumuona Bruno kwa mara nyingine, walitamani hata kumgusa ili kuona kama alikuwa yeye au mzimu.

    “Bado kuna mambo mengi tunahitaji kufanya! Nitakuja ndani ya siku mbili pamoja na hizo boti za mzee,” alisema Bruno.

    “Hivi kweli unataka kumnunulia boti?”

    “Sharifa! Ninahitaji baba yako awe na furaha, amekuwa akinichukia kwa kipindi kirefu sana kwa sababu ya umasikini wangu. Nataka nafsi yake imsute kwamba yule masikini ndiye ambaye amekuwa msaada mkubwa kwake,” alisema Bruno.

    Siku hiyo hawakutaka kukaa kijijini, wakaondoka na kuelekea Nairobi huku wakiwa na Abdul. Walipofika, wakachukua chumba katika hoteli ya kawaida na kutulia humo.

    Bruno alikuwa amekwishafika nchini Kenya alipokuwa akihitaji ilikuwa ni zamu ya mzee Todd tu kuondoka na kuelekea nchini Marekani.

    Bado mzee huyo alikumbuka wema aliokuwa ametendewa na Bruno, jinsi alivyokuwa amemsaidia kwa kiasi kikubwa, alichomwambia ni kwamba alitaka kumuachia kiasi cha dola milioni mia tatu kwa ajili ya maisha yake.

    Hicho kilikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni mia sita. Kilikuwa ni kiasi kikubwa mno ambacho Bruno hakuwahi kufikiria katika maisha yake.

    Kiasi hicho cha pesa kilitakiwa kuhamishwa haraka sana kutoka katika akaunti ya mzee huyo na kuingizwa katika akaunti ya Bruno.

    Bila kuogopa kitu chochote kile, wakaondoka na kuanza kuelekea katika tawi la Benki ya Barclays. Walipofika huko, Bruno akateremka, akaelekea ndani ya benki hiyo na kuchukua kitabu cha kuandikia hundi na kurudi kwenye taksi ambapo akamwandikia hundi ya kiasi hicho na hivyo pesa hiyo kuanza kuhamishwa kwenda katika akaunti ya Bruno kitu kilichochukua dakika chache tu.

    “Bruno! Ninashukuru kwa kila kitu, pamoja na yote hayo, ninahitaji unisaidie kitu kimoja tu,” alisema mzee Todd.

    “Usijali! Kitu gani?”

    “Nitahitaji uwe shahidi katika kesi yangu inayonikabiri. Wewe ndiye umeona kila kitu kilichokuwa kikiendelea, jinsi nilivyokuwa nimetekwa na kutakiwa kuuawa, najua kwamba dunia inatamani kuona nikiuawa, ninahitaji uwe shahidi wangu, usimulie kila kitu kilichokuwa kimetokea kuanzia ndani ya meli,” alisema mzee huyo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haina shida. Nitakusaidia pale nitakapohitajika,” alisema Bruno.





    Maofisa wa CIA walikuwa makini kufuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusu mzee Todd, hawakutaka kuiambia dunia moja kwa moja kwamba bado walikuwa wakiendelea kumtafuta mzee huyo.

    Waliwatuma baadhi ya maofisa nchini Afrika Kusini, walikwenda huko mpaka sehemu ambayo waliamini kwamba mwanaume huyo alikuwepo lakini baada ya kufika, baada ya kupambana sana na watu wa hapo, hawakuweza kumpata.

    Wakarudi na kutoa ripoti juu ya kitu kilichokuwa kimetokea, kila mmoja alihuzunika lakini hawakuwa na jinsi. Siku ziliendelea kukatika, waliendelea kumtafuta kila kona lakini hawakufanikiwa kumuona.

    Baada ya siku chache wakapewa taarifa kwamba mwanaume huyo alikuwa ametoa kiasi fulani cha pesa katika akaunti yake na kukihamishia katika namba nyingine.

    Hilo likawafanya kuwa na hofu kwamba inawezekana mwanaume huyo aliamua kuhamisha pesa hizo kwa kuwa alihitaji kufanya manunuzi yake kwa ajili ya kujilinda.

    Waliwasiliana na benki ya Barclays na kuwaambia kuhusu kuifunga akaunti hiyo lakini hilo halikuwezekana kwani kwa masharti makubwa ya benki hiyo, kitu cha kwanza kabisa hakikuruhusu akaunti yoyote ya mtu kufungwa kwa maslahi ya mtu fulani au shirika fulani.

    Wakaiacha, baada ya miezi mitano wakapata taarifa tena kwamba kulikuwa na muamala ulikuwa umefanyika katika tawi la benki hiyo lililokuwa chini Kenya.

    Hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakawasiliana na vijana wao waliokuwa Nairobi na kuwaambia kufuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea huko kwani tayari walikuwa na wasiwasi kwamba mzee Todd alikuwa huko.

    Ndani ya dakika tano tu, maofisa wa CIA walikuwa katika tawi la benki hiyo na kuingia ndani, macho yao yalikuwa yakiangalia huku na kule lakini hawakuweza kumuona mzee Todd.

    Hilo likawachanganya, wakatoka hapo na kuelekea nje, walipofika huko, wakamuona kijana mmoja akitembea kwa mwendo wa kujiamini kabisa kuifuata teksi moja iliyokuwa ikimsubiri.

    Huyo alikuwa mtu pekee ambaye alitoka ndan ya benki hiyo na kufuata teksi, wakahisi kitu na kuanza kuifuatilia. Alipoifikia teksi ile, akafungua mlango na kuingia ndani.

    “Kuna nani mwingine ndani ya teksi ile?” aliuliza ofisa mmoja.

    “Naona watu kama watatu hivi!”

    “hebu twende!”

    Walitaka kuiwahi hata kabla haijaondoka mahali hapo. Mikononi walikuwa na bastola zao, walipoifikia tu, wakaushika mlango wa dereva na kumuamuru atulie kama alivyokuwa na kuufungua mlango.

    Walinzi waliokuwa mahali hapo walionekana kushtushwa na kilichokuwa kikiendelea, mawazo yao yaliwaambia kwamba watu hao walikuwa majambazi, wakaandaa bunduki zao lakini ofisa mmoja akawaonyeshea kitambulisho ambacho kilionyesha kwamba walikuwa ni maofisa wa CIA.

    “Settle down,” (tulieni) alisema mwanaume mmoja na walinzi wote kutulia.

    Wakamshusha mzee Todd, akateremka na kuinyoosha mikono yake ambapo moja kwa moja wakamfunga pingu. Haikuonekana kuwa kazi kubwa, mzee huyo hakuonyesha ishara yoyote ya kiburi kwani alijua kabisa kwamba kitu hicho kingetokea na hata kama kisingetokea yeye mwenyewe aliamua kujipeleka katika ubalozi wa Marekani ambapo huko angechukuliwa na kusafirishwa kuelekea nchini Marekani.

    Kwa jinsi kitendo kile kilivyokuwa cha haraka na siri kubwa, hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye aliona kilichokuwa kimetokea zaidi ya walinzi wawili, wakamchukua mzee huyo tu, wakampakiza ndani ya gari.

    “Help me! You have to do what I’ve told you to do,” (nisaidie! Fanya nilichokwambia kufanya) alisema mzee Todd huku akimwangalia Bruno.

    “I will!” (nitafanya)

    ***

    Mzee Todd alikuwa ndani ya ndege akipelekwa nchini Marekani. Taarifa za kukamatwa kwake zilikuwa ni za kimyakimya na hakutakiwa mtu yeyote afahamu kama mwanaume huyo alikuwa amekamatwa kwa kuogopa kuvamiwa na wauzaji wa madawa ya kulevya.

    Humo ndani ya ndege, hakuwa na raha hata kidogo, alijua kwamba kila kitu kilichokuwa kimefanyika kilikuwa ni mchezo ambao ulichezwa na Maxwell kwa ajili ya kumpoteza.

    Hakuona kama angeweza kutoka katika kesi hiyo kubwa. Mbele yake kulikuwa na ugumu lakini watu pekee ambao aliamini kwamba wangeweza kumsaidia kutoa ushahidi walikuwa wawili tu, Innocent na Bruno.

    Alikuwa akisafirishwa kuelekea nchini Marekani huku matumaini yake yakiwa kwa watu hao wawili tu. Hakuzungumza kitu chochote kile, alikuwa kimya na kichwa chake kilikuwa kikifikiria ni kwa jinsi gani angeweza kupambana na kesi hiyo ambayo dunia nzima iliamini kwamba kweli madawa ya kulevya yalikutwa chumbani kwake na kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba alihusika katika kuiteketeza familia yake.

    Baada ya saa zaidi ya ishirini, hatimaye ndege ikaingia nchini Marekani. Hapo, alikuwa akisubiriwa na maofisa wa CIA ambao walimchukua, wakampakiza ndani ya gari na kuondoka naye.

    Walipoona kwamba amefika salama ndiyo taarifa zikaanza kutolewa kwa waandishi wa habari ambao wote hawakuamini kile walichokuwa wamekisikia.

    Mwanaume huyo aliwasumbua kwa miezi sita, hawakuwa wamempata japokuwa walimtafuta kila kona, kukamatwa kwake ikawa shangwe, watu kwenye mitandao ya kijamii wakaandika sana kuhusu mwanaume huyo na kila mmoja alikuwa akimuhukumu kwa nafasi yake kama mtuhumiwa ambaye alitakiwa kunyongwa mpaka kufa.

    Kwenye vyombo vya habari, ni picha zake tu ndizo zilikuwa zikitawala. Wamarekani walijua kucheza na akili za watu, walijisifia kwamba hakukuwa na mtu yeyote ambaye angethubutu kuichezea nchi hiyo na kutafutwa asipatikane.

    Walihitaji watu wao warudishe matumaini kwao kwa mara nyingine kwani kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakitafutwa na maofisa wa CIA lakini cha ajabu kabisa hawakuwa wakipatikana.

    Kitendo cha kumkamata mzee Todd kikawahakikishia kwamba wangesifiwa kila kona kwani wangeonekana mashujaa ambao hawakulala usiku mzima kwa ajili ya mtu huyo.

    Mzee Todd akawekwa ndani ya chumba cha mahojiano na kuanza kuulizwa maswali kadhaa. Hakufumbua mdomo wake kujibu swali lolote lile, kila kitu alichoulizwa, aliwaambia kwamba asingeweza kuongea lolote lile mpaka mwanasheria wake kuwa mahali hapo.

    Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, haraka sana mwanasheria wake, Harry Donny akapigiwa simu na ndani ya dakika chache alikuwa ndani ya chumba hicho na mzee Todd kuanza kujibu kila swali alilokuwa akiulizwa.

    Aliulizwa zaidi ya maswali hamsini ambayo yote aliyajibu kwa ufasaha na hivyo kesi hiyo kutakiwa kufika mahakamani haraka sana.

    Wakati huo kila kona duniani walikuwa wakimzungumzia mzee huyo, kesi yake hiyo nzito ilizua mambo makubwa mno, kila kona, watu wote walitaka kuisikiliza na kuona hatima ya mzee huyo ingekuwa nini.

    Asilimia kubwa ya watu walitaka kushuhudia mzee huyo akifungwa kifungo cha miaka mingi gerezani kwani kwa miaka hiyo kulikuwa na idadi kubwa ya vijana waliokuwa wakipotea kutokana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya.

    Waandishi wa habari walikuwa wakimiminika mahali hapo huku wakiwa na hamu ya kutaka kuzungumza na mzee huyo au hata kupata picha zake kwani picha nyingi ambazo zilikuwa zikitumika kipindi hicho zilikuwa ni picha za zamani tu.

    Hakukuwa na mtu aliyepata nafasi hiyo, waliambiwa kwamba suala la picha walitakiwa kusubiri mpaka siku ambayo angepandishwa mahakamani.

    Mwanasheria wake ambaye ndiye huyohuyo angekuwa wakili wake akaanza kumuuliza maswali mengi juu ya kilichokuwa kimetokea. Hakutaka kumficha, alimwambia ukweli kuhusu kila kitu kwamba hakuwa ameweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba yake bali kulikuwa na mwanaume aliyeitwa Maxwell ambaye ndiye alikuwa nyuma ya mchezo wote.

    Yeye ndiye aliyeratibu kila kitu na hata alipokwenda Afrika, yeye ndiye aliyepanga mipango ya kuuawa lakini ilishindikana baada ya kukutana na kijana aliyejitambulisha kwa jina la Bruno.

    “Alisuka mipnago ya kunimaliza, nikasaidiwa kwani nilichukuliwa kwenye meli yake na kupelekwa sehemu kwa lengo la kuuawa ila tukatoroka bandarini,” alisema mzee Todd.

    “Na huyo kijana kuna uwezekano wa kupatikana?”

    “Ndiyo! Kuna uwezekano, yeye atatoa ushahidi wa kila kitu kilichotokea,” alisema mzee Todd huku akiwa na uhakika wa kumpata Bruno.

    “Sawa. Haina shida!”

    Walizungumza mambo mengi na baada ya kukamilisha kila kitu, tarehe ya mahakama ikapangwa tayari kwa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

    Mzee Todd alikuwa mtu mwenye huzuni tu, kila alipokuwa selo kichwa chake kilikuwa kikiifikiria familia yake tu, hakuamini kama aliipoteza kwa tamaa za mwanaume mmoja tu aliyetaka afutike ndani ya dunia hii.

    Alihuzunika mno lakini alijiahidi kwamba kamwe asingelipa kisasi kwa kuwa aliamini kwamba kulikuwa na Mungu ambaye alisema kwenye maandiko yake kwamba visasi vyote vilikuwa juu yake.

    Siku ziliendelea kukatika, baada ya siku kadhaa, hatimaye siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ikawadia. Zaidi ya watu elfu tatu walikusanyika katika viunga vya mahakama kwa lengo la kusikiliza kesi hiyo. Hapo, kulikuwa na waandishi wa habari ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kupiga picha kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo.

    Mashirika makubwa ya habari duniani, CNN, BBC, Sky News na mengi yalikuwa bize kuonyesha moja kwa moja kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika viunga vya mahakama huku wakijaribu kufanya mahojiano na baadhi ya watu waliokuwa mahali hapo.

    “Namkumbuka mpenzi wangu, Jericho, alikuwa mtu mwema kabisa lakini baada ya kuanza kutumia madawa ya kulevya, nikampoteza, moyo wangu uliniuma sana, ninapomuona huyo mzee, ninatamani hata nimuue kwa mkono wangu,” alisema msichana mmoja huku akionekana kuwa na hasira mno.

    “Nilimpoteza kijana wangu baada ya kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya. Nilimpa kila kitu, hakutaka kusoma, alichanganyikiwa kabisa na madawa. Halafu leo mniambie kwamba huyu mzee aachiwe huru, nadhani nitamuua hata mtaani,” alisema mwanaume mmoja, kwa kumwangalia tu isingekuwa vigumu kuamini kwamba angefanya kile alichokuwa akikisema.

    Kila mtu aliyekuwa akihojiwa alimshutumu mzee huyo moja kwa moja, hakukuwa na mtu aliyetaka kumuona mwanaume huyo akiachiwa huru, kila mmoja alitamani kuona akihukumiwa jela kwa kosa alilokuwa amelifanya.

    Baada ya saa moja, gari moja lililokuwa likiongozwa na baadhi ya magari ya CIA lilikuwa likiingia mahakamani hapo. Haraka sana waandishi wa habari wakasogea kule lilipokuwa na kuanza kulipiga picha.

    Kila mtu aliamini kwamba huyo alikuwa mzee Todd, walipiga picha nyingi mpaka mlango ulipofunguliwa na mwanaume huyo kuteremshwa huku akiwa na pingu mikononi mwake.

    Hakuuficha uso wake, alikuwa na uhakika wa kushinda kesi hiyo, alikuwa akiangalia huku na kule, hakutabasamu, alikuwa kwenye hali ya kawaida, alizungukwa na maofisa wa CIA mpaka alipoingizwa ndani ya jengo la mahakama.

    Humo ndani, kulikuwa na watu zaidi ya mia saba waliokuwa wamekaa na wengine kusimama, kila mmoja alitaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea, siku hiyo ilikuwa ni ya kusikiliza kesi lakini hakukuwa na mtu yeyote yule aliyetaka kukosa kesi hiyo.

    Baada ya dakika kadhaa, mzee Todd akapelekwa kizimbani na hakimu kuingia. Kwa heshima kila mtu akasimama, alipokaa tu kwenye kiti chake, akagonga kinyundo na watu wote kukaa.

    Kesi ikaanza mara moja. Siku hiyo haikuwa ya kusikiliza mashahidi, haikuwa siku ya kusikilizwa utetezi wake, ilikuwa ni siku ya kusomewa mashtaka, makosa aliyoyafanya na baada ya hapo kesi kuahirishwa mpaka baada ya wiki moja na nusu.

    “Ninaiahirisha kesi hii mpaka tarehe 10/08,” alisema hakimu na kugonga kinyundo chake, akasimama na kuondoka mahali hapo.

    Watu wakatoka nje lakini hawakutaka kuondoka mahakamani hapo, walitaka kumuona mzee Todd akiondolewa na kupandishwa ndani ya gari lake.

    Polisi mmoja akamfuata pale kizimbani, akamchukua na kuanza kuelekea naye nje huku akiwa amemfunga pingu. Kila kona mahali hapo kulikuwa na ulinzi mkali, walijua kwamba mwanaume huyo alikuwa na watu wengi hatari ambao wangeweza kufanya kila liwezekanalo mpaka kuhakikisha wanamtoa mahali hapo.

    Walichokuwa wakikifikiria kilikuwa tofauti kabisa, mzee Todd hakuwa na kundi lolote lile, alikuwa yeye kama yeye na hakukuwa na kitu ambacho aliamini kama mashahidi ambao wangeeleza kila kitu kilichokuwa kimetokea na hivyo kushinda kesi hiyo.

    Alipotolewa nje, watu wakachukua simu zao na kuanza kumpiga picha, waandishi wa habari walikuwa wakihangaika, hawakutulia, kila mmoja alihakikisha anapata picha ambayo ingeyafanya magazeti yao na tovuti zao kutembelewa na watu wengi.

    Mzee huyo hakuuficha uso wake kama watu wengine, hakuona kama alikuwa na hatia na muda wote alikuwa kimya tu, akachukuliwa na kupakizwa ndani ya gari na kuanza kuondolewa mahali hapo.

    Wakati akiondolewa, wakili wake, Harry alikuwa akimwangalia, moyo wake ulimuuma mno, alimuonea huruma mteja wake lakini alikuwa na uhakika kwamba hao mashahidi ambao alimtajia basi wangeweza kumsaidia kutoka katika mikono ya kifungo kilichokuwa kikimkabiri.

    Baada ya gari lile kuondoka, akalifuata gari lake na kuondoka mahali hapo. Wakati gari likiwa limefika katika Barabara ya Brooklyn, akaangalia kwenye kioo, kwa nyuma kulikuwa na gari lililokuwa likimfuata.

    Alikuwa na wasiwasi nalo kwani kila alipokuwa akijaribu kwenda huku na kule, gari lile lilikuwa likimfuata kitu kilichomfanya kuhisi kuwa watu waliokuwa humo walikuwa wabaya ambao wangeweza kumfanya lolote lile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaanza kuliendesha gari kwa mwendo wa kasi, hilo halikuweza kumsaidia kwani gari lake halikuwa na kasi kubwa kama gari lililokuwa likimfukuza kwa nyuma.

    Aliendesha lakini hakuweza kuliacha, gari hilo likamfikia na kuanza kuendesha ubavuni mwake. Mwanaume mmoja akatokeza na kumnyooshea bastola na kumtaka asimamishe gari vinginevyo angeanza kumshambulia kwa risasi.

    Harry akaogopa, hakutaka kuona akifa, mule ndani ya gari alipokuwa akaanza kutetemeka kwa hofu, akaanza kupunguza mwendo na kusimama.

    Gari lile likasimama, wanaume wawili wakateremka na kumfuata huku wakiwa na bastola mikononi mwao, baada ya kulifikia, wakafungua mlango na kumteremsha na kumpeleka ndani ya gari lao.

    “Don’t dare to open your fucking mouth,” (usithubutu kufungua wako) alisema mwanaume mmoja huku akimgongagonga na bastola kichwani. Harry akanyamaza, kijasho chembamba kikaanza kumtoka na kuhisi kwamba huo ungekuwa mwisho wake.

    ***





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog