Search This Blog

Friday 28 October 2022

KISASI - 5

 









    Simulizi : Kisasi

    Sehemu Ya Tano (5)





    SIKU MBILI BAADA YA TUKIO LA KUTEKWA KWANGU.

    Nilikuwa nimepewa likizo ya miezi sita kwakuwa sijawahi kupumzika muda mrefu sana. Hii ilinifurahisha sana kwakuwa hata Felly nayeye alikuwa ameomba likizo ya miezi sita na alipewa. Tulikuwa tuko huru na kazi ambayo Pamela alikuwa ametuajiri rasmi kumkabili Mary. Mbali na kwamba tulikuwa tukilipwa lakini mimi nilijitolea mwenye kwa gharama zangu kuhangaika na Mary mpaka nihakikishe kuwa naliona chozi lake na mwisho niwe moja kati ya watu watakaofanikisha kifo chake. Patrick alikuwa likizo ya miezi miwili na Pamela alikuwa kwenye maandalizi ya kuanzisha hospitali yake ndogo hivyo ni kama wote tulikuwa huru, maisha yetu tuliishi kama familia. Cris ambaye ni mtoto wa Pamela na Patrick alikuwa mzuri sana na Patrick alimuahidi Pamela kuwa wangefunga ndoa baada ya mambo yote kuisha. Hiyo ilikuwa ni habari ya furaha sana, lakini furaha hii ingekamilika kama Mary angekuwa hayupo duniani.

    “Tunaanzia wapi Felly?” nilimuuliza Felly wakati wa chakula cha jioni ambapo wote wanne tulikuwa nyumbani kwangu, wakati huo ndio tulikuwa tunamalizia kula na Felly aliondoka kwenda kuchomeka ‘projector’ kisha tulipomaliza alianza kuelezea juu ya uchunguzi alioufanya kwa siku nne na aliyogundua ili tuweze kujua zaidi.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tuanzie kipindi cha nyuma kidogo mpaka juzi hapa tulivyokuwa na uhakika kuwa Mary yupo hapa Fiji. Niliingia kwenye mfumo wa Urusi na kutafuta kama kwenye vitu vyao kuna jina linalojulikana kama Mary Robert, nilipata nakala nyingi sana za matukio ya Mary Robert ambaye nilihakikisha na kuthibitisha kuwa kweli ni Mary huyuhuyu, ya kwanza ni Cheti cha kuhitimu chuo kikuu ambacho Mary alipatiwa na chuo kikuu cha Altai kilichopo Urusi, hapa Mary alipewa shahada ya mfumo wa mawasiliano, ilikuwa mwaka 2003, na kwenye picha ya watu waliomaliza shahada hiyo ipo hapa lakini ukiitazama kwa makini sana utaona kabisa hii picha imepachikwa kwa ujuzi mkubwa, hii inatia shaka kwakuwa Mary alikuwa Marekani mwaka 1996 akisoma shule ya sekondari huko Tobago. Lakini pia jina na picha ya Mary inatokea mwaka 1997 kwenye chuo kikuu cha Limkokwing huko Malaysia akiwa kati ya wahitimu wa shahada ya kwanza ya Utawala wa biashara, kwenye picha ya wahitimu pia yupo sehemu ya mwisho kabisa, na picha hiyo sijaielewa pia. Mwaka huohuo kipo cheti cha Mary akiwa muhitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa watoto wa wanajeshi wa Tobago yaliyokuwa ya wiki moja huko marekani yaliyohitimishwa na sherehe ya kupongeza wanajeshi waliotoka Iran. Mary hakuwa mtoto wa mwanajeshi wala hakuwa na ndugu mwanajeshi ila aliweza kuhudhuria mafunzo na kuhitimu akiwa mwanafunzi bora wa kulenga shabaha. Hii imenipa wasiwasi mana picha za wahitimu Mary hakuwepo lakini kuna picha za mazoezi Mary yupo na ni halisi kabisa. Lakini pia kuna cheti kingine cha stashahada ya upelelezi wa makosa ya jinai ambacho Mary anacho hiki alipata mwaka 1998 chuo kikuu cha Bradford kilichopo Uingereza. Baadaye aliaajiriwa na UK Military Academy ambacho ni chuo cha kijeshi kama mpelelezi, lakini mwaka huohuo Mary anaonekana tena chuo kikuu cha Lethoto akiwa ni moja ya wahitimu wa stashahada ya Uandishi wa habari, na mwaka uliofuata Mary alifunga ndoa kwenye Kanisa la St. Petersburg huko Alaska, alifunga na mtu aliyejulika kama Francisco Domosco, katika barua pepe iliyotoka kwa Mary kwenda kwa Domosco wiki mbili kabla ya ndoa yao alimwambia kuwa hataki sherehe kubwa, anataka watu wachache tu. Fransic ana Mary inaonekana walikutana mtandaoni na mara nyingi waliwahi kuonana. Ila miezi sita baada ya Mary kufungwa ndoa Domosco alifariki kwa ajali na hivyo mali zake zilichukuliwa na Mary ambaye alizifilisi na kuondoka Alaska 2000 mwishoni. Mwaka huo huo Mary alifunga ndoa na Timoth Mobutu huko Afrika ya kusini, huyu ni mfanya biashara wa madini, lakini miezi sita mbele yule jamaa alikufa kwa kupigwa risasi na Mary alikuwa mrithi wa mali za yule mwanaume. Hapo Mary alirudi tena Marekani kwakuwa inaonekana kuna ujumbe wa barua pepe alioutuma kwa mtu aliyeitwa Derick aliyekuwa yuko Urusi kumwambia yuko tayari kuingia kwenye mafunzo, ujumbe huo haukuonyesha ni mafunzo gani, lakini Derick alimwambia anaweza kumfanyia mpango wa kuingia ila sharti ajifunze Kiurusi kwa miezi sita kwanza, hata hivyo Mary alimjibu sawa, miezi saba mbele, Mary alimtumia tena yule mtu ujumbe wa barua pepe akimshukuru kuwa amefanikiwa ila atafanya kwa miezi mitatu na kisha atatoroka kwani haitaji kufika mwisho. Sasa kwenye mazungumzo haya hakuna mafunzo yaliyotajwa, ila kwenye ujumbe wa mwisho uliotumwa ulituma kwa kompyuta yenye anuani ya utambulisho KF5642, hii kompyuta iliyotumiwa ilikuwa Kazakhstan upande wa kusini mgharibi mwa Urusi na ni kaskazini mashariki mwa mji wa Islamabad Afghanistan. Eneo ilipo kompyuta hiyo kuna kambi ndogo ya wanajeshi wa kundi la alqaida sasa ninachojiuliza je alikuwa kwenye hiyo kambi au la? Lakini majibu sikupata. Mwaka 2001 alimtumia Dany ujumbe wa barua pepe akimwambia amuandalie vijana wasio na kazi ila wasomi, wawe ni wale waliotoka JKT na ambao bado hawajajiriwa na hawajaoa, alimwambia anataka wawe wenye afya nzuri na awapime magonjwa yote, wawe imara na wenye mbavu nene. Ujumbe huu ulitumwa akiwa Djibouti sehemu inaitwa Arta, wiki mbili mbele Dany alimtumia majina na picha za vijana hao, mmoja ni yule ambaye tulimkuta kule Villa Bridge mwenye asili ya kitanzania. Wengine picha zao zimetumwa katika namna ambayo mpaka uwe na vifaa flani ndio uzisafishe uzione. Kisha wiki hiyo hiyo Mary alitoka Djibouti na kwenda Tanzania, alipokutana na vijana wale akamtumia ujumbe mtu anaitwa Chevinski ujumbe huo ulikuwa ‘Je vais vous envoyer mes hommes pour la formation que nous avons parlé, s'il vous plaît raccourcir à trois mois. tout le paiement a été effectué’, ujumbe huu ulioandikwa kwa lugha ya Kifaransa ilikuwa ikimaanisha kuwa ‘ninawaleta vijana wangu kwako kwaajili ya mafunzo tuliyoongea, tafadhali fupisha mafunzo na yawe miezi mitatu. Malipo yote yameshafanyika.’ Huo ndio ujumbe ambao Mary aliutuma na hapo inaonekana vijana wale walikwenda Urusi.” Alimalizia hapo Felly na mimi nilikuwa nimechoka sana, sikujua kama Mary anaweza kuwa mtu asikuwa na hadithi moja tu, mambo mengi sana juu yake inaonekana hatukuwa tukiyajua, na hiyo pia inaamisha kuwa itatuchukua muda sana kumuweza Mary lakini kwangu mimi nitamkamata tu kwakuwa sina cha kupoteza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hivyo hapo tunatakiwa kufanya nini Felly?” nilimuuliza Felly ambaye hata yeye alionekana kama kukata tamaa vile.

    “Hapa Dany ndiye ataongea ukweli wa kila kitu, inaonekana kuna mengi sana ameyaficha ambayo sisi hatuyajui, tunatakiwa tumjue Mary kwa uzuri sana na mtandao wake ni upi ili tujue namna ya kuenenda. Lakini pia Dany ni moja kati ya watu waliokwenda Urusi kwenye hayo mafunzo, na baada ya yale mafunzo aliporudi alikuwa na wale vijana wakaenda mpaka Kabul ambapo walikutana na mtu anayeitwa Mahamoud ambaye pia mawasiliano yake ya barua pepe na Mary yapo ambapo aliambiwa awape kazi ya kufanya na kama wakishindwa awaue, lakini hakuna aliyeuawa na wala kazi waliyopewa haikuelezwa. Na kingine ambacho hamkijui ni kwamba Mary aliwahi kutembea na Dany wakiwa Qala-e-Fathullah, eneo hili liko kaskazini mwa mji wa Kabul na liko karibu kabisa na Khaje Burga. Na baada ya hayo Dany aliondoka kurudi Tanzania na Mary alimtumia ujumbe wa barua pepe akimwambia kuwa walichokifanya kiwe ndo mwanzo na mwisho ili wasiharibu kazi na Dany asijiweke pabaya.” Aliongeza Felly.

    “Sasa kama dany alikuwepo kwenye mafunzo kwanini alimtumia ujumbe Paul, yule muuaji wa Tanzania na kumwambia nashukuru kukufahamu na nimetambulishwa kwako na Mary nategemea tutafanya wote kazi pale itakapobidi.” Nilimuuliza Felly.

    “ule ujumbe haukuwa unaanisha hayo, nimejaribu kujiuliza pia lakini niliona herufi zake zikimaanisha kitu kingine, kulikuwa kwenye kila neno kuna majina ya mahali, mfano kwenye ‘Nashukuru’ ambayo kwa mujibu wa Pamela maana yake kwa kingereza ni kutoa asante, neno hilo lilikuwa limeandikwa NashuKuRu, ukichukua hizo herufi kubwa na ndogo yake inayofata utapata neno NAKURU, hii ni sehemu ipo Kenya ambapo Mary alishawahi kumtumia ujumbe Paul akiwa huko, ukichukua neno lingine ‘kukufahamu’ lilikuwa limeandikwa KukuFahamU, hii inasimama badala ya KFU, ambapo niliiona kwenye ujumbe pia toka kwa Paul kwenda kwa mtu anaitwa Rajab neno hilo lilikuwa likimaanisha KING FINANCIAL ASSOCIATION, hii ni taasisi moja ya fedha iliyopo Nakuru, ambayo ilivamiwa siku nne baada ya hawa watu kutumiana ujumbe na kiasi cha pesa kilichoibwa kilikuwa ni dola laki 6.Hivyo maneno mengi waliyokuwa wakiongea haikumaanisha vile ambavyo wanamaanisha. Baada ya tukio hilo Mary alimtumia ujumbe mtu anaitwa Apolo akimwambia amemuwekea pesa kwenye akaunti namba hii 23456’6753 aliweka kialama katikati katika namba hizo ionekane ni makosa, lakini haikuwa makosa hiyo sio akaunti namba ni namba za kijiografia za eneo la Iringa huko nchini Tanzania, ukiangalia kwenye ramani zinazopatikana kwenye satelaiti utagundua kuwa kwenye namba hizo kuna benki ya biashara na siku hiyo ambapo ujumbe huo ulitumwa kesho yake kulikuwa na taarifa kuwa benki ile ilivamiwa na kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia 7.” Alieleza Felly lakini bado nilikuwa naona mambo yanazidi kuwa mengi sana.

    “Patrick unasemaje.” Nilimtazama Patrick ambaye alionekana kuchoka sana, ilionekana kabisa alikuwa anajuta kukutana na Mary, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba alikuwa amepambana na gaidi.

    “Nilitaka kujua, je Mary ni gaidi, jambazi au nani?” aliuliza Patrick.

    “hatujui chochote kuhusu hayo kwakuwa inaonekana kuna matukio mengi ya kihalifu ambayo Mary anahusika, kila wanapotumiana ujumbe kuna jambo zito linalotokea hivyo hatufahamu kabisa kuhusu mambo mengi kwakuwa bado taarifa ni nyingi sana.” Alijibiwa na Felly na hapohapo wakati bado tukiongea simu yangu iliita, ilikuwa ni namba ya Mary na hapo sikupokea badala yake niliiacha na Felly aliingiza kwenye kompyuta ili kujua mahali ilipopigiwa ile simu tuweze kumpata Mary iwapo tutajua mnara uliotumiaka. Baada ya Felly kumaliza kuiingiza niliipokea;

    “Khajat huwezi kuitafuta namba yangu ilipotokea, mimi sio mjinga hivyo, napiga toka kwenye mkondo usioweza kutafutika, hivyo usiache kupokea simu yangu ukitegemea unaweza kunitafuta kwa mtindo huo.” Aliongea huku akicheka.

    “Unahitaji nini wewe mkosaji?” nilimuuliza swali, lakini alizidi kucheka. Ile hali ya kucheka ilizidi kuniudhi sana, nilikuwa na hasira na nilitamani sana kumkamata kwa muda ule.

    “Ujue tofauti yako wewe na mimi sio tu kuwa mimi naua watu wema na wewe unaokoa maisha yao, hapana, wewe unahasira sana na unaongozwa na hasira zaidi kuliko utaalamu wa uyafanyayo, ungekuwa kama dada yako anayeitwa Felicity basi ingekusaidia, yeye hana hasira, ni mwoga na woga wake unamsaidia.” Aliongea kwa dharau huku akiendelea kucheka.

    “Mary unajichimbia shimo refu la kujifukia mwenyewe kila unapozidi kuongea, kata simu.” Nilimwambia kwa hasira na nilipotaka kukata simu aliendelea kuongea nikaamua kumsikiliza kilichomfanya apige simu.

    “Nataka kesho saa 2:00 asubuhi umuachie Dany huru na umpe simu yake ili niwasiliane naye kwakuwa ninamuhitaji. Ni lazima wewe kufanya hivyo na sio ombi. Ikifika saa mbili na dakika moja hujamuachia basi elewa kuwa utakuwa wewe na dada yako pamoja na Patrick mmejiingiza kwenye vita itakayogharimu damu ya mmoja kati yenu, mimi ni binadamu na ninakikomo cha uvumilivu, nitawavumilia nyie kukaa na Dany hadi kesho saa 1:55 ila baada ya hapo muachieni. Hii ni amri, nasisitiza ni amri.” Aliongea na kabla sijaongea chochote yeye alikuwa ameshakata simu.

    “Vipi Felly umeweza kujua namba ilipotokea?” nilimuuliza Felly ambaye hata hivyo alikuwa amekaa kimya akiwaza.

    “Hakuna kitu, simu yake haiwezi kufanyiwa hivyo.” Aliongea Felly.

    >>KESHO YAKE<<

    Ilikuwa asubuhi ya saa 2:30 bado tulikuwa hatujamuachia Dany na wala hatukuwa na mpango wa kumuachia, tulimtoa ndani na kumuingiza kwenye gari ya Felly ili tumuamishe toka nyumbani kwa Felly ili akakae kwangu na siku hiyo ndiyo nilipanga kutumia muda mwingi na yeye ili nipate kujua majibu ya maswali yote.

    “Huyu ni bora kumuweka kwenye buti.” Aliongea Felly.

    “Je akitoroka.” Nilimuuliza Felly japo niliamini kuwa asingeweza kutoroka lakini ilikuwa kama ni tahadhari tu. Tulimtoa na kumuingiza kwenye buti huku tukiwa tumemfunga katika namna ambayo asingeweza kutoroka hata awe na mazoezi vipi. Baada ya hapo niliwasha gari na kuondoka kwa kasi sana. Tukiwa njiani nilisikia kama kitu kimegonga gari kwa nyuma, nikasimamisha gari na kuzunguka nyuma lakini sikuona kitu hivyo nikarudi kwenye gari na kuodoka, nilipofika nyumbani kwangu niliingiza gari mpaka karibu na mlangoni na hapo nilishtushwa na damu zilizoonekana kuchuruzika toka kwenye buti. Haraka nikaamua kulifungua lakini nilichoka baada ya kuona Dany akiwa anavuja damu kichwani, nilipomtazama vizuri alikuwa na tundu kubwa lililopenya kichwa chake na kutokezea kwa nyuma. Wote tulibaki mdomo wazi, nilimgeuza na kumtazama vizuri alikuwa na tundu la risasi, ikabidi tufunge ule mlango wa buti na kuanza kuukagua na ndipo tulipokuta tundu la risasi moja. Nilipotazama kwenye siti ya gari kwa nyuma niliona ile risasi ikiwa imejipenyeza kwenye kiti. Ilikuwa ni risasi ya rifle na hii ilimaanisha kabisa kuwa alikuwa ni Mary. Tulichukua ule mwili na kwenda kuuchimbia mbali sana na pale na kisha tulirejea kwangu tukiwa wote wanne, Pamela, Patrick, Felly na mimi, tulikuwa tukitafakari nini cha kufanya na hapohapo Mary alipiga simu yangu na mimi nilipokea.

    “Khajat, nilikuambia mimi ni binadamu na huwa uvumilivu wangu una mwisho, sasa nakupa zoezi lingine, naomba umpe Patrick simu kwakuwa simu niliyompigia haipatikani.” Aliniambia kama alikuwa akiniamuru.

    “Simpi yeyote simu, ongea unachotaka kuongea kama huna cha kuongea basi subiri siku nikikuweka mkononi ili uongee.” Nilimwambia vile na hapo alizidi kunipandisha hasira.

    “Tumia busara ndogo Khajat, mpe Patrick simu.” Aliongea tena na mimi bado nilizidi kumkatalia.

    “Basi nitakupigia simu baada ya nusu saa, hakikisha unakuwa na uamuzi wa kumpa simu Patrick au kumwambia awashe simu yake, usichukie kipenzi, vita hii itakupelekea kifo muda ukifika.” Aliongea na kucheka kisha alikata simu. Tulikuwa kimya wote kila mmoja akitafakari ni nini tutafanya. Wote walikuwa wanakaribia kukata tamaa lakini mimi bado nilikuwa na matumaini. Baada ya nusu saa simu yangu iliita tena na sasa niliipokea na kuipandisha sauti ili kila mtu asikie.

    “Khajat nadhani uko karibu na Pamela hapo na Patrick, nataka wasikie kwanza hili kisha nitatoa maelekezo.” Baada ya kusema hivyo nilisikia kama mtu akipigwa kofi ambalo halikuwa kubwa sana kisha tulisikia sauti ya mtoto ikilia, nilishtuka kwakuwa alivyolia tu Pamela alianguka na kuzimia, ilikuwa ni sauti ya mtoto wa Pamela, nilikata kwanza simu na kumgeukia Patrick.

    “Kwani mtoto mlimuacha wapi?” nilimuuliza Patrick aliyekuwa anahangaika kumpepea Pamela.

    “Tulimuacha nyumbani na mfanyakazi, walinzi wapo pale.” Alinijibu na mimi nilizima simu yangu kwanza kisha niliwasha gari na kuondoka moja kwa moja mpaka kwa Pamela, nilipofika pale nilikuta walinzi wote wamefungwa kamba kwenye miti na mfanyakazi wa ndani alikuwa amefungiwa kwenye kabati la nguo.

    “huyo mwanamke amekuja hapa muda gani?” nilimuuliza yule mfanyakazi aliyekuwa akitetemeka.

    “amekuja asubuhi baada ya bosi kuondoka.” Alijibu hivyo na wala sikuhangaika tena kuwahoji, niliondoka mpaka kwangu tena na sasa nilikuta Pamela ameamka na Patrick pia alikuwa akimbembeleza kwani alikuwa akilia kupita kawaida. Felly alikuwa amekaa na hajui cha kufanya. Nikawasha simu yangu na kumpigia Mary.

    “Nakusikiliza.” Nilimwambia hivyo mara baada ya yeye kupokea simu.

    “Nataka uweke simu ili Patrick asikie.” Aliongea hayo na mimi niliweka simu sawa ili Patrick na wote pale wasikie.

    “Nakusikia, ongea.” Alisema Patrick na Mary alianza kuongea.

    “Patrick nataka ikifika saa saba mchana leo uende uwanja wa ndege, ukifika pale yupo kijana wangu atakupa kila kitu kwaajili ya kusafiria, utaingia kwenye ndege saa 8 na ndege hiyo itakupeleka mpa Somalia. Ukifika Somalia utatafuta gari ndogo yenye namba SMT5678, ni voxy nyeusi, ukiiona nenda mwambie dereva akupeleke Jowhaar na hapo utanikuta, hakuna simu kwenye safari yako nzima, hakuna kuwasiliana na yeyote, nikigundua umeenda kinyume na hilo basi jua kabisa mwanao huwatampata akiwa hai. Umeelewa?” aliuliza Mary na Patrick aliitika huku aking’ata meno.

    “Nimekuelewa.” Patrick alijibu na kushusha pumzi.

    “Nakupenda sana Patrick kwakuwa wewe ni msikivu, mpe Khajat simu.” Aliongea Mary na mimi niliingilia sauti ile.

    “Khajat usijaribu kumfata Patrick nyuma kwakuwa utahatarisha maisha ya Cris, ubishi wako uzingatie uhai wa huyu mtoto kwakuwa sitasita kuwaletea kichwa chake kama nitagundua mnafatilia. Ninawaona kwenye kila jambo.” Aliongea Mary na mimi nilimkatisha.

    “Tutampataje mtoto.” Nilimuuliza lakini moyo wangu ulikuwa unasononeka sana.

    “Mtoto atakuwepo sehemu salama, Patrick atakaposhuka uwanja wa ndege wa Bender Qassim basi nitakupigia simu ukamchukue mtoto sehemu.” Aliongea na kuniuliza kama nina swali zaidi.

    “Nitakuamini vipi kwamba utamleta mtoto?” nilimuuliza tena.

    “Huna chaguo lingine zaidi ya kuniamini, ukiniona huniamini basi fanya utaratibu mwingine wa kumpata ila ujue utakuwa unaweka shingo yake karibu na kisu.” Aliongea na kukata simu.





    “Watu waliofanikiwa zaidi ni wale walioyajua matatizo, waliozijua harakati za maisha yao, waliokumbana na misukosuko na taabu, waliokutana na kukata tamaa na majaribu lakini mwisho wa siku waliyakabili na kusonga mbele. Lolote ambalo haliwezekani leo, unaweza kulifanya liwezekane kesho, hiyo ni kama tu utaamua juu ya mustakabali wa njia uipitayo” HII NI SEHEMU YA KUMI NA SABA

    ***KHAJAT***

    Akili ya Mary ilikuwa inafanya kazi haraka sana, nilikuwa nimekubali kwa mpaka hapo alipofikia. Alichokifanya kilikuwa ni mbinu ya kumaliza kila kitu kwa upande wetu, alikifanya akiwa ana nia ya kuzima mbio zetu za kumuwajibisha, tusinge weza kuhangaika tena kama angemuua Patrick hivyo hiyo ilikuwa kete yake ya mwisho kuicheza ambayo alijua kabisa ingenyong’onyesha juhudi zetu. Sikuwa na lolote kichwani, kwa mara ya kwanza katika ukubwa wangu nilikaa chini na kulia, nilimuonea sana huruma Patrick lakini sikujua nitaweza kumsaidia namna gani. Kwa vyovyote vile kama Mary ameamua kumchukua Patrick basi hiyo ilimaanisha kuwa alikuwa makini kutufatilia na sisi ilikujua kama kweli Patrick alikwenda mwenyewe. Muda ulizidi kwenda na saa saba ilikuwa imekaribia. Kila mtu alikuwa akilia kivyake kasoro Felly tu aliyekuwa yuko busy kusikiliza tena ile sauti ya maelekezo ya Mary na kuyaandika pembeni. Hakuonekana kuwa na chembe ya woga wala kuhofia juu ya lile litakalokwenda kutokea kwa Patrick, hiyo ilinipa moyo kiasi na kunifanya na mimi niwaze zaidi. Sikuwahi kufikiri kuwa ingefikia huku tulikofikia hasa kwakuwa mwanzoni ilionekana kama ni kitu kidogo tu, lakini mpaka sasa hatujajua uwezo halisi wa Mary japo ameshatuonyesha matukio ambayo yametutisha kwa kiasi fulani, inaonekana ana watu kila sehemu na hiyo inamaana ni rahisi sana kwake kufanya jambo lolote. Umri halisi pia wa Mary ulinisumbua, japo alikuwa na miaka isiyozidi 30 lakini alikuwa na uzoefu wa mambo wa miaka 60, kwa muda mfupi wa maisha yake ilionekana kabisa Mary aliutumia sawia kupanga aina ya maisha anayoyataka. Moyoni nilikuwa nikijiuliza ni nini kimemfanya Mary awe vile. Nilifahamu na ninajua kabisa mazingira na matukio yatokeayo kwa binadamu huchangia kumtengeneza awe mtu wa aina gani, nisichokuwa na kielewa kwa wakati huo ni mazingira gani au matukio gani yalimtengeneza Mary kuwa mtu wa aina ile. Alikuwa ni muuaji mwenye sura nzuri usiyoweza hata kuitilia shaka. Urembo wake ungeweza kumvutia tajiri yoyote duniani kutamani kumpa kasri yake na roho yake ila umuingizapo ndani basi ni wazi kuwa umeingiza bomu ambalo ni wazi kabisa muda wowote litalipuka. Mary anafanya haya kwanini? Ni swali gumu kujijibu labda yeye tu ndiye ajuaye. Kumuua Dany ilikuwa ni ujumbe kwetu kuwa kwake hana mtu muhimu, yeyote anaweza kuwa muhimu kwa muda tu na ikitokea hakuna haja tena ya kuwa nae kutokana na muda basi ni wazi humuondoa duniani. Hakuwa mwanamke wa mchezo, japo nilimfahamu muda mfupi lakini nilikuwa nimemsoma kwa namna hiyo.

    *****

    Ilikuwa ni saa 6:25 hii ilimaanisha bado dakika 35 kutimia saa aliyoambiwa Patrick awepo uwanja wa ndege. Bado Patrick alikuwa pale akimbembeleza Pamela. Felly alinyanyuka pale alipokuwa amekaa na kutuita wote. Kisha tulipokuwa tumefika alianza kuongea kwa sauti iliyoonyesha kukata tamaa.

    “Hatuna jinsi hapa, kama tunataka tumpate Cris basi lazima Patrick aende, lazima tutimize matakwa ya Mary hasa kwa wakati huu mgumu.” Aliongea Felly huku akionekana kulengwa na machozi.

    “Lakini pia tutakuwekea kifaa maalim kwenye saa yako kwa ndani kitakachokuwa kikituonyesha kila unakoelekea ili tujue. Nakuahidi hakuna baya litakalokutokea na unatakiwa uwe jasiri. Kila nafasi ya kutoroka itakapotokea au nafasi ya kumuua Mary itakapotokea basi itumie. Unajua kutumia bastola na bunduki basi ukipata nafasi ya kuipata itumie. Sisi tuko nyuma yako kwa kila jambo, ni lazima tutakutoa kwenye hilo banio alilokuweka na Cris atakuwa salama. Usiogope, kumbuka unafanya hivi kwaajili ya Cris, huu ndo muda wa kumfanya Cris aje ajivunie ushujaa wako baadaye.” Nilimwambia Patrick na yeye alionyesha kujaa uimara na utayari wa kufanya hivyo. Patrick alikuwa mtu mzuri sana, alikuwa ni mtu anayejali sana watu na hii ilikuwa ni maumivu makubwa sana kwa Pamela. Hatukuwa na namna ya kufanya zaidi ya kumuacha akajiandae, tulimuwekea kile kifaa kilichoonyesha alipo kwa kila hatua aliyopiga, hii ingetuwezesha kujua sehemu aliyopo. Baada ya hapo gari ilikuwa tayari na tulimsindikiza mpaka nje. Alikuwa akijizuia kulia lakini tulimuona machoni kwamba alikuwa akilia. Walikumbatiana na Pamela ambaye na yeye alikuwa akilia kupita maelezo, mimi niliamua kuwaacha pale nje na kuingia ndani nikitazama kwa dirishani kwakuwa ilikuwa imeniuma sana.

    “Pamela, kama sitarudi, au kama nitakufa naomba unisaidie kumwambia Cris kuwa baba anampenda sana, mwambie nilitamani sana kumuona akiwa mkubwa na mwenye furaha huku akipata malezi yetu sote, lakini mwambie kuwa baba aliamua kujitolea ili wewe uishi.” Aliongea hayo kwa sauti ya uchungu na kumkumbatia Pamela.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Utakuwa salama Patrick usiseme hivyo, utarudi salama mume wangu, tutampata mtoto wetu, niko tayari kutumia hadi senti ya mwisho ya pesa zangu kuhakikisha kuwa unakuwa hai.” Aliongea Pamela huku akizidi kulia, ilikuwa zimebaki dakika 20 tu na hatukuwa tayari kuchelewa muda na kusababisha matatizo mengine. Waliagana na Patrick alimshukuru sana Felly na hapo Patrick alipanda kwenye gari na kuondoka, kutoka pale nyumbani mpaka uwanja wa ndege ilikuwa ni mwendo wa dakika 20 kwa spidi 80, hivyo tulielewa kabisa Patrick angeweza kufika kwa wakati. Felly na Pamela walirudi ndani na hapo wote tulikaa kwenye makochi kila mmoja akigeukia upande wake, Pamela alikuwa bado akilia lakini Felly aliendelea kuisikiliza ile sauti ya Mary alipokuwa akitoa maelekezo, mimi sikuwa nikiwaza chochote zaidi ya kupangilia kitu cha kumfanya Mary siku ambayo atajiingiza kwenye himaya yangu. Nilikaa pale kwenye kochi na baada ya muda mfupi mimi na Pamela wote tulipitiwa na usingizi. Nilikuja kushtuliwa na sauti ya Felly, nilipoitazama saa yangu ya mkononi ilikuwa ni saa 9 mchana na pale ukutani alikuwa amebandika makaratasi na picha nyingi, nikajua kabisa kuna kitu amegundua, nilitazama pale sikumuona Pamela, wakati bado nikijinyoosha Pamela aliingia akiwa na chakula na kila mmoja alipewa mfuko wake, tulikula na tulipomaliza Felly alianza kuelezea tena.

    “kile kifaa tulichomuwekea Patrick kwenye saa kitakuwa kimeharibiwa kwakuwa sioni tena kwenye kompyuta yangu. Alipofika uwanja wa ndege pale alikaa kama lisaa limoja hivi ndio hapo sikuona tena alipoelekea.” Aliongea Felly na hapo nilizidi kuchoka. Kile kifaa ndicho pekee kingeweza kutuonyesha Patrick anapokwenda na hiyo ingetusaidia kumtafuta na kumrudisha akiwa salama.

    “Hivyo hatuna namna nyingine ya kujua alipo?” nilimuuliza Felly.

    “Nahisi tunayo ila sina uhakika nayo sana.” Aliongea Felly na hapo nilikaa makini ili niweze kumsikiliza.

    “Kwenye maelezo yake Mary amesema kuwa Patrick akifika uwanja wa ndege wa huko Somalia atapanda voxy nyeusi yenye namba SMT5678, lakini gai yenye namba hizo sio gari za Somalia ni gari za Suva, nimejaribu kuingia kwenye tovuti ya idara ya usajili wa magari ya Suva na kuwaomba kusajili gari langu kwa namba hiyo wakaniambia kuwa namba hiyo tayari ina mtu, na nilipotafuta gari yenye namba zile kwenye kamera za barabara za Suva zinazoelekea uwanja wa ndege wa pale mjini sikuona, ila gari hiyo yenye namba hizo za usajili zilionekana juzi zikielekea barabara ya Natovo ambayo ni barabara ya kuja Fiji kupitia msitu wa Ravo, nilipoitafuta gari hiyo tena kwenye kamera za uwanja wa ndege wa hapa kwetu halikuonekana lakini lilionekana leo asubuhi kwenye kamera za barabarani mitaa ya bandarini na saa hizi limeonekana uwanja wa ndege wa Vunesia, uliopo kwenye kisiwa cha kusini mwa hapa tulipo. Dereva wa gari hilo aliyejiandikisha pale bandarini ili gari yake ivushwe anaitwa Johari Qasim, hii inaonyesha kuwa Patrick hapelekwi Somalia, Patrick anakwenda Kisiwa cha kadavu kilichopo kusini mwa hapa tulipo ambacho kukifikia kinachukua lisaa limoja na nusu tu. Patrick ameambiwa akifika huko Somalia uwanja wa Bender Qasim amwambie dereva wa gari hiyo ampeleke Jowhaar, ni kweli kwamba Jowhaar ni eneo lililopo Somalia, lakini kwakuwa jina la huyu dereva linamajina mawili ambayo yote yanatokea kwenye maelekezo ya Mary basi hapa tujue kuwa huko ndiko anakopelekwa Patrick na sio Somalia.” Aliongea felly na muda sio mrefu simu yangu iliita na alikuwa ni Mary, nilitazama saa yangu ya mkononi ilikuwa ni saa 10 na dakika ishirini, nikapokea;

    “Ndio, unataka nini?” nilimuuliza Mary na yeye alicheka kabla ya kusema lolote.

    “Sina cha kutaka kwako kwakuwa mimi na wewe tumemalizana, nasubiri muda ukifika nitakuja kukunyamazisha na mwambie dada yako nitamtumia barua ya kazi, kama atakuwa tayari nimuajiri kwa pesa nyingi basi nitafanya hivyo.” Aliongea huku akicheka na mimi sikumjibu chochote.

    “Okey, sasa sikiliza vizuri, mwambie Pamela aende Pilmira Hotel, akifika pale aseme amekuja kwenye chumba namba 548 na ajitambulishe kama Patronila Mkesi, atapewa funguo na atamkuta mwanae.” Aliongea Mary na kutaka kukata simu lakini nilimuwahi.

    “Kwanini yeye na sio mimi au mwingine yeyote.” Nilimuuuliza na kama kawaida alicheka.

    “Yeye ndiye mwenye mtoto, ndio maana nilimwambia yeye. Ingekuwa mtoto ni wako basi wewe ndio ungeenda kumchukua, lakini mmmmhh, unaweza kumsindikiza.” Aliongea kwa dharau na kuendelea kucheka.

    “Kama mtoto umemdhuru nitakukamata na kukukata vipandevipande.” Nilikuwa na hasira sana na sikudhani kama atakuwa amemuacha mtoto akiwa hai.

    “Mimi ni mtu wa ahadi, niliahidi nikishampata Patrick mtoto atakuwa salama hivyo nimetimiza ahadi yangu kama nitakavyotimiza ahadi niliyokuahidi ya kukuua.” Aliongea huku akiendelea kucheka.

    “Ni bora ukawahi kuitimiza kabla mimi sijatimiza ya kwangu.” Nilimwambia na kumkatia simu. Nilimgeukia Pamela na niliona dhahiri kuwa alikuwa akitetemeka, hii inawezekana ni kwakuwa tu alikuwa anahofia juu ya mtoto wake. Kabla sijafikiria lolote nilisikia Felly akiongea na simu na muda si mrefu sana alikata simu na kuingia ndani.

    “Khajat nimeongea na rafiki yangu mmoja anaitwa Babra anafanyakazi kitengo cha madawa ya kulevya pale uwanja wa ndege ambapo ndio tunadhani kuwa Patrick atakuwa amepelekwa, amesema ameliona hilo gari na alilikagua yeye ni kweli kuna mwanamke, na pia kuna ndege imetua hapo uwanjani muda si mrefu sana na kwamba ilitoka Fiji saa nane, gari hiyo yenye huyo dada wa Kiarabu ilikuwa inaondoka muda huo ambapo nilikuwa naondoka naye na ndio anaifatilia, hii inamaana inawezekana kwamba Patrick alipofika uwanja wa ndege wa huku alipandishwa kwenye ndege ya kwenda kisiwa cha kadavu.” Aliongea Felly kwa haraka haraka huku akiweka visu kwenye mkoba wake, hiyo ilimaanisha kuwa safari ilikuwa inaanza lakini bado nilikuwa sijajiridhisha.

    “Sasa tuna uhakika gani kuwa Patrick yuko huko wakati bado hajaonekana huko.” Nilimuuliza Felly.

    “Kwenye maelezo ya Mary alisema kuwa atapiga simu kumrudisha mtoto pale ambapoPatrick atakuwa amefika Somalia, sasa Somalia na hapa ni zaidi ya siku moja, hapa na Kadavu ni lisaa limoja na nusu kwa ndege na amepiga simu muda mfupi baada ya ndege kutua huko Kadavi, na tayari gari aliyotoa maelekezo kuwa Patrick akapande ilikuwa hukohuko, na msichana anayeiendesha gari hiyo anamajina mawili ambayo yanaendana kabisa na maneo mawili yenye majina matatu aliyoyataja Mary. Hii inamaana kuwa ni kwa asilimia mia moja kuwa Mary yuko Kadavi.” Aliongea na hapo alikuwa ameshamaliza kuweka vitu vyake sawa.

    “Kwahiyo tunafanyaje?” nilimuuliza huku na mimi nikifata kisu changu.

    “Tunakwenda kumfata mtoto kwanza kisha mimi na wewe tutakwenda Kadavi, tunafanya vamizi baridi, hakuna risasi, ni mkono na kisu au kitu kingine kisicho cha moto.” Aliongea Felly na hapo tuliondoka mpaka kwenye hoteli tuliyoelekezwa na tulipofika pale tulimtanguliza Pamela na yeye aliulizia kama alipoambiwa na kupewa ufunguo kisha sisi tulikuwa tumetangulia kule juu, alipokuja alifungua na tulimkuta Cris akiwa salama kabisa japo alikuwa na wekundu mguuni ulioonyesha kuwa lile kofi nililolisikia ilikuwa alipigwa Cris mguuni. Hatukupoteza muda badala yake tulimrudisha Pamela na sisi tuliwahi uwanja wa ndege na kukodi ndege ndogo ya kasi iliyochukua lisaa limoja.

    “Babra umefikia wapi na hiyo gari?” Felly alimpigia huyo rafiki yake wakati tukiwa tumeshashuka uwanja wa ndege.

    “wameingia kwenye gofu moja liko kilomita kumi toka hapo uwanjani, kuna kijana hapo nilimwambia mkifika awape gari, mtapita barabara ya kwenye Hoolu Park kisha mkifika Pier mtakuta nimeegesha gari barabarani, mkishafika hapo tu mimi mtanikuta.” Aliongea Babra na muda sio mrefu tuliletewa gari na safari ya kwenda kule ilianza. Nilikuwa naendesha mimi gari kwakuwa nilihisi nina haraka kuliko kawaida, tulifanikiwa kufika pale kwenye eneo alilotuambia na yeye alitokea.

    “Sasa kuna geti pale na gari limeingia kule ndani kabisa, pale getini kuna walinzi wawili, kule mbele kidogo kuna walinzi wawili na ndani kule sijaweza kujua, ila tunatakiwa kuhangaika na hawa kwanza ili tupitie getini kwa hapa kwanza, hivyo nitajifanya nimeng’atwa na nyoka na nitakwenda kwa wailinzi pale nitawaeleza kuwa nyoga bado yupo hapa kichakani ili watoke pale na nyie mtangoja kule kwenye kile kichaka pale karibu na geti ambapo ndipo nitamuelekeza kuwa nyoka yupo, kisha wakija mtamaliza.” Aliongea Babra na hapo alivua viatu na kuanza kupita vichakani akienda kule kwenye kichaka cha upande wa pili ili atokee kule karibu na geti, na sisi tulikuwa nyuma tukimfata, alipofika maeneo yale alianza kulia na kuchechemea kuelekea kule getini na alipofika pale wale walinzi walimfata;

    “Unatatizo gani.” Mmoja wao alimuuliza na Babra aliyekuwa bado akilia pale chini.

    “Nimeng’atwa na nyoka, yuko pale bado ni mkubwa sana.” Baada ya kuwaambia hivyo walitoka na kwenda pale kichakani kuangalia kama huyo nyoka bado yupo na Babra aliwafata kwa nyuma kisha alipokaribia Babra alichomoa waya mfukoni na kumrukia mmoja shingoni kisha alipitisha ule waya kwa nyumba na kuupitisha kwa nguvu na moja kwa moja ulikata koo na wakati huo Felly alimkamata yule mwingine na kukata shingo, kisha wote tuliondoka mpaka geti la pili kwa kupita upande kwa upande kwenye maua na tulifanikiwa kuwaweka chini walinzi wale wawili na mmoja Babra alimchinja kwa kutumia waya. Hapo tulifanikiwa kumaliza orodha ya walinzi pale nje na sasa tulielekea ndani ya lile jengo, Babra yeye hakuwa muongeaji, alikuwa kama jini, yeye ni dam utu, anachinja kila anayekutana naye. Alitangulia yeye kuingia ndani na ndiye aliyetupanga, baada ya kuvuka mlango tukakuta walinzi wengine na hapo kama kawaida kila mtu alikamata wakwake, ila nilizidi kushangaa jinsi ambavyo Babra alikuwa akiwachinja kwa waya. Alipochungulia ndani aliwaona watu wanne na sisi tulipochungulia tulimuona Patrick akiwa amefungwa na Mary alikuwa anaongea na simu na kuna mlinzi mwingine alikuwa pale na yule dada ambaye kwa mujibu wa Babra ndiye aliyekwenda uwanja wa ndege, tulivamia na mimi nilimrukia mlinzi na Felly alimrukia yule dada lakini hakumuua bali alimzimisha, wakati tumeshawadhibiti hawa tulishtuka kuona Babra ashamuweka Mary waya shingoni na sasa alikuwa anataka kuvuta ndipo Felly alipopiga kelele.

    “Babra acha.” Alipaza sauti na Babra aliacha.

    “Mary nilikuahidi.” Nilimwambia hayo na hapo nilimpiga ngumi ya pua iliyomfanya alewe na kuzimia.





    “Umaskini wa fikra ni mbaya zaidi kulikoni umasikini wa kipato. Fikra sahihi kwa wakati sahihi ndio njia ya kupata suluhu ya kila limfikalo mwanadamu.



    ******



    **KHAJAT**

    Nilimshukuru sana Felly kwakuwa umakini wake umenifanya nijione mtu tena. Hatukukaa sana, tulipohakikisha kuwa Patrick hana tatizo lolote tuliamua kumchukua na Mary tayari kwa kurudi Fiji. Baada ya kuingia kwenye ile ndege ndogo tuliyokodisha tuliweza kuondoka moja kwa moja mpaka Fiji bila tatizo lolote na tulifika mpaka nyumbani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nini kinafuata?” nilimuuliza Felly ambaye mara zote alionekana kama kuzuia ili nisimfanye Mary chochote.

    “Kwanza lazima Mary arudishe vitu vyote vya Patrick lazima alipe gharama ya kila kitu, na kitakachofuata ni kwenda Tanzania kesho asubuhi.” Aliongea Felly na mimi nilikuwa nikimtizama kwa mshangao.

    “Unaakili vizuri wewe? Tanzania kufanya nini?” nilimuuliza na yeye wakati huo alikuwa akitembea kuelekea kule alikokuwa Mary na Patrick.

    “Nataka tupate nyaraka zote za kampuni ya Patrick alizobadilisha ili kusaidia kurudisha mali ya Patrick na mambo mengine yatafata.” Aliniongelesha hayo na hata hivyo sikuwa nimemuelewa.

    “Mengine yapi? Unataka kumuachia huru si ndio?” nilimuambia na yeye alionekana kuchoshwa na maswali yangu.

    “Khajat yametosha maswali, tukubaliane kwa pamoja, tumsaidie Patrick arudishe kwanza mali zake kisha utamfanya chochote utakacho. Jiandae kesho tunaondoka.” Alimaliza na hapohapo niliamua kurudi kwenye kochi na kukaa, muda wote huo Mary alikuwa amepoteza fahamu bado. Felly aliwaita kina Patrick na Pamela pale na wote tulikaa kama kikao kidogo;

    “Kila mmoja anisikilize kwa makini, huyu hapo mnayemuona, anaitwa Babra ni rafiki yangu, tulikuwa naye jeshini lakini yeye ni mwalimu wa mafunzo ya kivita pia ni mpelelezi wa kitengo cha madawa ya kulevya na ugaidi wa uwanja wa ndege wa huko kidava.” Alitambulisha na wote tulishukuru kumfahamu. Babra aliendana sana na mimi na nilipenda jinsi alivyokuwa, alikuwa ni mshap na sio mzungumzaji sana.

    “Kesho tutaondoka kwenda Tanzania, nimeshafanya mawasiliano na watu wa ndege na tumepatiwa tayari sehemu za kukaa, ila sijajua Mary tutaondokaje naye bila kuleta shida njiani.” Aliongea Felly na hilo wala halikuwa shida kwangu.

    “Hilo sio tatizo, ukimaliza kuongea nitakuwa tayari nimekuonyesha njia ya kuondoka naye.” Nilimjibu Felly na yeye alikubali kisha aliendelea na maelezo.

    “Tunakwenda Tanzania kama watalii, kila kitu kimeshaandaliwa na Babra anawatu wake kule watakao weka mambo sawa, tunaenda watu wanne, mimi, Khajat, Patrick na Babra. Pamela utabaki na Cris na usiogope wapo watu watakaokulinda muda wote. Kazi ya kwanza tufikapo Tanzania ni kuhakikisha nyaraka zote za kampuni zinarudi kwa Patrick, kisha Mary atalazimika kubadilisha nyaraka zote majina na kwenda kwenye jina la awali ambalo ni la Patrick, mashtaka juu yake yatafunguliwa akiwa nchini Tanzania na sisi tutawatumia watu wa kule kupenyeza ushahidi wote ili kesi ifike mwisho kwa haraka. Tunavyoongea hapa tayari shehena ya biskut ambayo ilitoka Tanzania imekamatwa na wameitizama na kugundua ilikuwa ni pembe za ndovu zimesagwa, polisi wa kimataifa (Interpol) wanatafuta kampuni iliyotengeneza ule mzigo na hakuna nakala inayoonekana toka kwa Mary. Hii inamaana kuwa tunatakiwa kuwahi haraka kabla hawajagundua kuhusu Mary na kumtafuta. Taarifa za uhakika zinasema kiwanda cha biskuti hizo kimeungua moto jana chote na haieleweki chanzo cha moto, usajili wake pia una utata. Sisi ndio tuna ushahidi wa yote na ni juu yetu kufanikisha mambo kwa wakati. Khajat dada yangu kipenzi kwasasa punguza jazba, tuhakikishe tunafanikisha haya yote kisha mengine yatajipanga yenyewe.” Aliongea Felly na hapo niliona kabisa nia yake ya kumkimbiza Mary mbali na mikono yangu lakini mimi nilielewa njia ya kumpata. Nilichomuahidi ni lazima akipate. Baada ya maelekezo yale kila mtu alianza kujitayarisha na mimi niliondoka na kwenda mjini kisha baada ya muda mfupi nilikuwa tayari nimerudi.

    “Unapeleka wapi jeneza wewe Khajat.” Alikuwa ni Felly akishangaa baada ya kuona nikishusha jeneza pale nyumbani.

    “Mary atakaa humu kwenye jeneza, piga simu kwa watu wako waambie watuwekee sehemu ya kusafirisha maiti.” Niliendelea kulishusha lile jeneza na kumuomba Babra anisaidie tulipeleke ndani. Nilipoingia nilikutana uso kwa uso na Mary aliyekuwa tayari amekwisha zinduka.

    Alinitazama na mimi nilimsogelea, alionekana kuchoka lakini hiyo haikunifanya niache kuwa ha hasira na yeye. Felly aliingia pale na aliponiona nimesimama mbele ya Mary alikuja na kusimama mbele yangu na kuniomba nijiandae kwanza kuongea na Mary. Walimuweka Mary vizuri na kisha Felly alianza kumuongelesha. Muda wote huo nilikuwa bado nikimtazama kwa hasira usoni na yeye alikuwa akinitazama pia.

    “Mary tunakwenda Tanzania kesho, nia ya safari ni wewe kwenda kurudisha kila kitu ulichochukua kwa Patrick, tunataka tumalizane kwa namna hiyo kwa hatua za awali kabisa kabla hujalipia machozi na maumivu ya kila mmoja uliyemsababishia usumbufu.” Aliongea Felly lakini Mary hakujibu chochote badala yake alikuwa kimya tu akinitizama mimi.

    “Mjibu Felly acha kunitazama.” Nilimuambia hivyo na Mary hakujibu chochote zaidi ya kunitazama. Niliondoka pale na kwenda kuchukua waya ule ambao Babra huutumia, nikaunyoosha vizuri na kurudi nao pale, Mary alikuwa bado akinitazama tu.

    “Mary, sababu ya mimi kukuacha wewe hai mpaka sasa ni kwakuwa tu kuna mambo inabidi utimize kabla sijakuaga rasmi, hatua ya kwanza katika maisha yako ya mwisho ni kusafiri kwenye jeneza ukiwa hai, hatua ya pili na ya mwisho utaijua kadiri muda utakavyotutuma. Hivyo umeelewa tulichokuambia au unahitaji maumivu ili kuelewa?” nilimuuliza lakini alizidi kutoa tabasamu. Felly alinitazama kama vile akinipa ishara ya kwamba nihangaike naye. Nilimtoboa mkono na ule waya na yeye alikuwa kimya huku akiguna kwa maumivu kisha nilikuwa nikimuuliza huku nikiuingiza ule waya taratibu kwenye mwili wake, zoezi lile huwa linachana nyama ndani kwa ndani na kusababisha maumivu makali sana, niliupeleka na yeye alianza kulia, nilipoufikisha umbali wa sentimita 30 alianza kuongea.

    “Naumia, niache.” Alilia kwa uchungu, ile ilikuwa ni adhabu ya kumfanya aongee.

    “Nia yangu ni wewe uumie, siko hapa kukufurahisha.” Nilimwambia huku nikiendelea kuongea. Patrick alikuwa pembeni akimtazama kwa hasira na wala hakumsemesha kitu.

    “Niko tayari kurudisha, niko tayari, tukifika Tanzania nitafanya mtakalo.” Aliongea hayo na alipomaliza kuongea nilichomoa ule waya na kumchoma sindano ya kumpunguzia maumivu. Alikuwa ametokwa na jasho kama mtoto mdogo. Kila nilipomtazama nilitamani nimkatekate kama kachumbari.

    ******

    Mpaka usiku wa saa 8 wote tulikuwa macho, muda huo ndio Felly alipigiwa simu kuwa nafasi ya kuweka maiti haitakuwepo kwakuwa tayari ndege imeshajaa. Tulichanganyikiwa kwakuwa ndege ilikuwa iondoke saa 11 asubuhi na mpaka muda huo hatukujua ni wapi tutamuweka Mary.

    “Piga simu waambie watuongeze nafasi moja kwenye ile sehemu ya peke yetu, Mary tutaondoka naye akiwa mzima hivihivi.” Aliongea Babra na hicho ndicho kitu ambacho niliona hakitawezekana. Tukimfunga pingu lazima itakuwa ni tatizo tayari kwenye ndege, tukisema tumuache atembee na sisi kama kawaida itakuwa tumemuaga bila ya sisi kutumia akili.

    “Babra haitawezekana, ni bora tutafute namna nyingine au hata kuahirisha safari ili tupate pa kumuweka.” Felly alimwambia Babra, lakini hata hivyo Babra alitikisa kichwa akimaanisha hatuwezi kuahirisha safari, kisha alitoka pale na kuondoka, nje tulisikia akiwasha gari na kuondoka kwa kasi sana. Tulikuwa tumechoka mpaka muda huo, kila mmoja alikuwa akitafakari ni nini tutafanya, hatukujua Babra alikoelekea lakini kwa zaidi ya lisaa limoja alikuwa bado hajarudi.

    “Khajat, mbona naona kama tutashindwa kwa hili?” aliuliza Felly huku akionekana kukata tamaa.

    “Tumsubiri Babra tuone atakuja na mbinu gani.” Nilimweleza Felly lakini hakuwa tayari kunisikiliza kuhusu Babra badala yake alizua kicheko.

    “Babra atakuwa amekwenda kuvuta bangi labda, ujue anamsongo wa mawazo, baba yake na mama yake waliuwawa kwa kuchinjwa na waya toka kipindi akiwa mdogo, alishuhudia lile tukio, sasa ile picha bado huwa inamuijia kichwani ndio mana katika miaka yote nimekaa naye sijawahi kuona akicheka, si muongeaji sana na hajui kumbembeleza mtu, hana mpenzi na hata siku moja hamnyenyekei mtu. Sasa sidhani kama anaweza kuwa na njia yoyote.” Niliguna kwa yale maelezo, na kabla sijauliza jambo linalofata alikuwa ameingia pale ndani na kimfuko. Ni kweli alipoingia nilisikia harufu ya bangi lakini niliamua kukaa kimya tu.

    “Vipi umepata njia gani?” nilimuuliza kwa haraka lakini alitazama saa yake na muda huo ilikuwa saa 10 kasoro, alivua nguo pale mbele ya Patrick na sisi bila aibu, na kuondoka kwenda bafuni, nilitamani sana kucheka lakini sikuweza. Hatukufungua ule mfuko tulisubiri mpaka alipokuja, alipewa nguo zake na Felly kisha alivaa na kutuambia twende kile chumba ambapo Mary yupo. Alipofika alimfungua zile kamba na kumchukua kisha alimpeleka bafuni na kumsimamia aoge.

    “Jamani ni saa 10 inaelekea na nusu sasa, tujiandaeni kuondoka.” Aliongea Babra na sisi tulimshangaa, lakini yeye hakuonekana kama kushangazwa na kutokushangaa kwetu. Ilibidi Felly amuulize kwa lugha kwa lugha ambayo hata hivyo mimi sikuifahamu;

    “conas is féidir linn taisteal léi gan a bheith faoi deara.” Aliongea Felly na wakati huo Babra alikuwa akimsikiliza.

    “Tá gach rud faoi smacht, ach fan agus a fheiceáil.” Alijibu na hapo Felly aliondoka pale, nilimfata Felly na kumuuliza ni lugha gani ile waliyokuwa wakiongea na yeye alinijibu kuwa kilikuwa ni ki ‘Irish’, nikamuuliza nini walikuwa wakiongea na yeye alinyamaza kidogo na kunitazama.

    “Nilimuuliza tutawezaje kuondoka naye bila kuleta shida? Na yeye akanijibu kuwa nitulie kila kitu kitakuwa sawa.” Alinijibu Felly na wakati huo Babra alikuwa amemtoa Mary bafuni na kumshikilia akiwa uchi, Mary alikuwa na michubuko kidogo usoni hivyo alimfuta akiwa amemfunga pingu na kumpaka poda na sasa alionekana vizuri, tulishangaa kuona akimlaza Mary pale kitandani na kumfunga mikono huku na huku na miguu yake pia akaitanua. Mary aliogopa ni nini alikuwa anafanyiwa, wote tulibaki midomo wazi, Babra aliondoka pale na kuchukua ule mfuko aliokuja nao, alimtizama Mary akiwa katika ile hali ya kupanua miguu kitu kilichofanya sehemu zake za siri kuwa nje, alifungua ule mfuko na kuchomoa bomu dogo la saizi ya mwisho kama kiazi na kulipaka mafuta kisha alichomoa kipini chake na hapo Felly alishtuka, Mary alikuwa anatoaka machozi na alishindwa hata kuongea.

    “Babra unafanyaje?” Felly alimuuliza lakini Babra hakujibu, alimtanua Mary na kuanza kuliingiza lile bomu taratibu, Mary alipiga kelele sana lakini Babra hakujali wala kuongea kitu chochote, alitoa kitu kama uume mmdogo wa plastiki na kuutumia kusukumiza lile bomu mpaka alipohakikisha na ule uume umezama wote, Mary aliendelea kulia na baada ya hapo Babra alinyanyuka na kumuinua na kuchomoa ule uume wa plastiki lakini lile bomu lilibakia ndani.

    “Hutapata maumivu yoyote, hilo bomu limekwenda kukaa kwenye mfuko wa uzazi, rimoti yake mimi ndio ninayo, hivyo hakuna atakayekushika wala kukufunga wakati wote tutakapokuwa safarini kuelekea Tanzania na hata tutakapofika Tanzania, ila ukijaribu kuondoka mbele ya uso wangu jua wewe ni bomu na utalipuka.” Alimaliza kuongea Babra na Mary alionekana kukubali kushindwa. Tulikwenda uwanja wa ndege na Mary akiwa hajafungwa kamba wala pingu, alikuwa na nidhamu sana, hatukuwa na bastola kwakuwa hazikuruhusiwa na hasa kwamba tulikuwa tunasafiri kama watu wa kawaida. Lakini cha kushangaza tulipofika ndani ya ndege Babra alitoa vichumachuma vingi kwenye kiatu na sehemu nyingine za mwili akaviunganisha na ikatokea bastola, hiyo ilinikumbusha mafunzo tuliyopewaga kipindi nikiwa jeshini ya namna ya kuunganisha silaha.

    *****

    Safari iliyoanza pale Fiji ilitufikisha mpaka Misri ambapo tulishuka ili kubadilisha ndege. Tafrani ilianzia pale ambapo baada tu ya kushuka tuliona watu ambao hatukuwaelewa. Mary alikuwa bado akionekana kufadhaika sana na muda wote ule alikuwa akimwangalia Babra. Nilikuwa makini sana na mimi kumtazama ili asiondoke mbele ya macho yangu. Wale watu walikuwa ni wanaume wawili ambao niliwaona. Walikuwa na asili ya kiarabu na wengine wengi tu kama sita walikuwa wametapakaa kila kona ya pale uwanja wa ndege.

    “Felly mnaona lakini hapa kuna dalili nisiyoielewa?” nilimuuliza Felly na yeye alitazama na kugundua kweli kulikuwa na shida pale.

    “Babra, hawa watu lazima watakuwa na uhusiano na Mary sasa lazima tujipange vizuri hapa, kuna uwezekano kabisa kwamba kipo kilichofanyika kinachoweza kuwa kimewapa watu wa Mary taarifa. Hapa tusipokuwa makini tutapotezwa.” Felly alimnong’oneza Babra na hapo walinichukua na wote tukaenda kwa pembeni na kumuacha Mary akiwa pale kwenye viti amekaa kimya. Hakuwa amefungwa popote lakini lile bomu alililoingiziwa ndani ya mwili wake ndilo lililomfanya akae kama vile amefungwa pingu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kila mtu achukue nafasi yake hapa. Hawa watu hawawezi kufyatua risasi hapa uwanjani, tumeowaona walipo, hivyo hakikisha kila mtu anakamata wake kwa kadiri awezavyo. Felly unakwenda upande wa kulia wa uwanja huu, Khajat wewe utakwenda upande wa kushoto, mimi nitakuwa mbele pale. Utaratibu wa hapa utatofautiana sana na sehemu nyingine zenye kificho. Hapa ni kimyakimya. Hivyo nashauri ni bora kutumia waya zaidi kuliko kisu au silaha nyingine za moto. Hakikisha mtu anakuwa mbele yako akiwa na yeye anaangalia mbele, kisha unamuwahi na kumvisha waya na unavuta kwa nguvu zote ili umnyonge, kisha akiishiwa nguvu unaivuta waya na mkono mmoja huku upande mwingine umeachia na hii itakata shingo bila wasiwasi. Weka mwili sehemu ambayo haitakuwa na matatizo kwa muda huu. Kaeni mbali na kamera za uwanja huu. Kama ukishinda kutumia waya basi tumia mkono, piga ngumi moja tu itakayomzimisha mtu ili kusiwe na purukushani zisizo za lazima.” Aliongea Babra na kutoa waya tatu mfukoni kisha akatupatia lakini mimi nilimrudishia kwakuwa niliuamini zaidi mkono wangu, Felly yeye pia alirudisha na alitaka kutumia zaidi mkono wake.

    “Khe!” nilisikia Babra akishangaa baada ya yeye kugeuka.

    “Mary hayupo pale.” Alitueleza hivyo na tayari nafsi yangu ilianza kusikia joto tena. Hayupo?! Nilijiuliza moyoni lakini ukweli ni kwamba Mary hakuwepo pale na nilipotazama kwa mbali niliona akitokomea na vijana wawili waliovalia nguo za kiaskari.







    “Usilale kwa kujiachia kama bado mafanikio yanakukimbia. Amka panga namna ya kuyakabili matatizo yako kwakuwa matatizo yameshapanga namna ya kukukabili. Amka na ujiulize utalala mpaka lini na kuamka ukiwa na hali ile ile na mawazo yaleyale? Jiulize ulivyokuwa mwaka jana na ulivyo mwaka huu. Je kwanini hamna tofauti ya mafanikio yako wakati kuna ongezeko la umri??? GUNDUA KIPAJI CHAKO…KITUMIE…ELIMU YAKO SI KITU KAMA ITASHINDWA KUKUTATULIA CHANGAMOTO ULIZONAZO.”



    **BABRA**

    Tulikaa pale tukitafakari na kila mtu akiwa amepigwa na butwaa juu ya kilichotokea, nikakumbuka juu ya ile rimoti niliyokuwa nayo ambayo hata hivyo nisingeweza kuitumia pale kwenye eneo lenye watu wengi. Tulisogea kando zaidi na tulipogeuka tena nyuma tuliona polisi watatu wakija upande wetu na sisi tuliondoka pale na kuanza kutembea haraka kule mbali na uwanja. Tulipofika mbali kidogo na pale watu walipokuwepo walituambia wao ni maafisa wa polisi na kutuamuru tusimame. Tukasimama na kugeuka, wale ndio tuliowaona mara ya kwanza pale uwanjani wakiwa wamevaa nguo za kiraia.

    “Nyoosha mikono juu.” Aliongea yule askari mmoja kwa lugha ya kingereza. Wale wawili nao walikuja na kuanza kutupekua. Walinikuta na ile Rimoti na hapo wote walicheka na kutuambia tulale chini. Wakati tunalala chini nilimuona Khajat akitutazama kisha alitupa ishara kwamba tuwarukie wale jamaa ili kuwadondosha. Kila mmoja alianza kuhesabu ndani yake moja mpaka tatu kisha tuliwavamia kwa kasi na kuanguka nao. Hapakuwa na mtu aliyetuona kwakuwa pale ilikuwa ni mbali kidogo na uwanja. Tulizungushana nao pale lakini baada ya kuwapiga sana walilegea. Yule mmoja aliyekuwa na Khajat alikuwa ameshauwawa kwa kuvunjwa shingo. Walibaki wawili na Felly alimnyonga mmoja na kusema tunayemuhitaji pale ni mmoja tu. Tulimuweka sana yule jamaa na hapo Khajat alianza kumuhoji.

    “Mko wa ngapi na Mary yuko wapi?” aliuliza Khajat lakini yule jamaa hakujibu kitu. Alimuuliza kwa mara ya pili na ya tatu lakini yule jamaa alikuwa bado tu yupo kimya. Kilichofata Khajat alichukua ule waya na kuanza kuuingiza puani kwa yule jamaa. Aliuchomekana kwa nguvu mpaka damu zilianza kutoka na yule jamaa aliongea.

    “Tuko tisa, watatu ni sisi na wengine sita wako na Mary kwenye gari ndio wanasubiri tupeleke rimoti.” Aliongea kwa sauti ya kulia yenye maumivu ndani yake. Alipomaliza tu kuongea simu yake ya mkononi iliita, na hapo ndipo Khajat alipomuonya kuwa akitoa ishara yoyote ya kwamba amekamatwa atamuua palepale.

    “Kama unataka kufa kikatili basi jaribu kuonyesha hata ishara. Ongea kwa ukakamavu. Mwambie upo huku ili wakufate na mwambie kuwa umemkamata mmoja na wengine wamekimbia.” Alipewa maelekezo hayo na yeye alisema kama alivyokuwa ameambiwa. Mimi na Felly tulikuwa tumeondoka na kwenda kukaa pembeni ya pale tulipokuwa kwa muda ule, tukajificha vizuri na muda kama wa dakika mbili tuliona gari nyeusi ikija kwa kasi upande ule. Yule jamaa alikuwa amemshikia Khajat bastola kwa nyuma na ile miili mingine ya wale wawili tulikuwa tumeificha. Ile gari ilipofika walishuka wale vijana sita na kwenda moja kwa moja pale aliposhikiliwa Khajat, taratibu mimi na Felly tulinyata na kulisogelea gari na kufungua mlango kwa haraka tukakutana na Mary, kabla hajaongea kitu Felly alikuwa ameshamuwahi na kumziba mdomo. Kule Khajat likuwa ameshawabadilikia wale wengine sita na mimi nilikwenda kuongeza nguvu. Tulifanikiwa japo kwa tabu sana kuwakabili na kuwaondoa duniani kisha muda huo ndege tuliyokuwa tuondoke nayo ndio ilikuwa inatuhitaji ndani. Tulimchukua Mary na kuondoka mpaka kwenye ndege bila ya kushtukiwa kuwa kulikuwa na tukio limefanyika. Tulipofika ndani ya ndege nilikuwa namtazama Mary kama nilitaka kumng’ata, alikuwa amenichefua sana na nilianza kumchukia kwa moyo wote. Nilitamani yeye ndiye awe aliyemuua baba yangu lakini haikuwa hivyo.

    Kina Felly hawakujua kwanini niliwasaidia kwa moyo wote. Hawakujua kuwa nilikuwa nawekeza kwao ili waje kunisaidia katika mipango yangu ya baadaye. Mpango ambao ni siri ndani ya moyo wangu, mpango niliouota kwa muda na kujipanga juu yake kwa zaidi ya miaka ya nusu ya uhai wangu. Nilikuwa nimeng’ata meno nikitafakari kwanini Mary alitaka kumaliza kila kila mtu aliyejitokeza mbele yake. Nikamwangalia kwa makini sana lakini aliamua kunitazama pia usoni, alikuwa haamini ni kwa namna gani ameweza kuzipita mashine zote za viwanja vya ndege bila kujulikana kuwa alikuwa na bomu ndani yake. Hakuna aliyejua, ni mimi tu, ni mimi na mimi pekee.

    Niliamini kila binadamu alikuwa na sababu ya kumfanya awe vile alivyo, lakini nilitamani zaidi kujua kwanini Mary alikuwa vile alivyo. Historia ya maisha yangu ilinichukua na kunifinyanga ikanifanya kuwa mtu mpya kabisa katika jamii ya wasio nijua. Nilibadilika kabisa na kuwa mtu wa kuua na kufanya unyama, lakini huyu Mary ambaye nimemfahamu kwa muda mfupi tu si muuaji kama mimi ila ni zaidi ya hivyo. Msichana mdogo mwenye matukio ya kigaidi, alikuwa ni mkavu wa macho na fikra na hicho ndicho kilichonifanya nimuoene kama asiye na cha kupoteza.

    “Mary uko kwenye siku za mwisho kabisa za uhai wako, unaweza kuelezea historia ya maisha yako japo tukakuheshimu kwa hilo.” Nilimsemesha Mary ambaye alikuwa amekaa pembeni yangu huku jasho dogo likimtoka. Hakuongea chochote kile bali alinitazama tu kwa macho yaliyoonyesha kuwa angekuwa na uwezo wa kunifanya chochote basi pengine angenigeuza kibiriti. Hakusema chochote kabisa na mimi nilimuonea huruma nikaamua kumuacha asiongee chochote.



    ******

    Ilikuwa ni safari ndefu na yenye vikwazo vingi lakini hatimaye tulifanikiwa kutua uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, ilikuwa ni mara ya kwanza kukanyaga Tanzania na maelekezo yote tulitegemea kuyapata toka kwa Patrick na Mary lakini zaidi mambo ya kiintelijensia tulitegemea kuyapata toka kwa watu wangu ambao walikuwa tanzania.

    “uvítací” (karibuni) ilikuwa sauti ya Marcus Diero, kijana wa ubalozi wa Slovakia, alikuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi ambaye nilikutana naye nchini marekani kwenye mazoezi ya jeshi la majini yaliyokuwa yakiendeshwa na jeshi la marekani. Alikuwa ni mpelelezi wa ujasusi wa Slovakia lakini pia kulikuwa na tetesi kuwa alichukuliwa na shirika la kijasusi la marekani.

    “vdaka”(asante)

    “zariadil som všetko, co pre vás, ako dlho bude u zostanem tu” (nimewaandalia kila kitu, na je mtakaa hapa kwa muda gani)

    “tak dlho, ako je potreba”(kwa muda wowote ikaochukua). Tuliondoka na Marcus mpaka kwenye nyumba moja iliyokuwa kando kidogo ya mji. Ilikuwa ni nyumba iliyojitenga kidogo na makazi ya watu na hapo tulikuwa na uhakika kabisa wa kila kitu kwenda kama kilivyopangwa. Baada ya kutufikisha yeye aliondoka na sasa mwenyeji wa kila kitu chetu alikuwa ni Mary na Patrick, ilikuwa ni usiku wa saa sita na hatukuwa na muda wa kufanya lolote zaidi ya kukaa na Mary ili atueleze tunaanzia wapi na kuishia wapi.

    “Mary tuna masaa 72 tu ya kumaliza kila kitu, tunataka kujua tunaanzaia wapi na tunaishia wapi.” Khajat alimuuliza Mary huku akimtazama kwa macho makali. Mary hakuonekana kuogopa kitu, alikuwa amechoka lakini bado asili ya kiburi chake ilikuwa imeujaza moyo wake.

    “Sijui pa kuanzia, nyie ndio mniambie.” Aliongea hayo na kunyanyuka huku akitembeatembea pale ndani. Khajat alimfata na kumpiga kibao kilichomfanya apepesuke na kuanguka chini, damu zikaanza kumtoka puani na na Khajat akamnyanyua kwa roho ya kikatili kisha akamkalisha kwenye kochi.

    “Mary tunataka hati za vitu vya Patrick, tunataka kila ulichochukua kwa Patrick kirudishwe kwake”. Aliongea Khajat kwa upole, wakati huo Patrick alikuwa ameketi kwa mbali huku akimtazama Mary kwa huruma.

    “Naombeni niongee nae labda atanisikiliza.” Aliongea Patrick kwa upole na unyonge kisha Khajat alimuacha na hapo Patrick alijisogeza mpaka pale na kuanza kumfuta zile damu puani. Mary alianza kulia kwa kwikwi na kuanza kumtazama Patrick huku akimuomba msamaha, ghafla wote tulijawa na huruma.

    “Nisamehe Patrick”. Aliongea Mary huku machozi yakizidi kumtoka.

    “Nini kimekutokea Mary.” Patrick alimuuliza Mary.

    “Hakuna kilichonitokea ila hukunijua kabla.” Aliongea Mary lakini wakati bado akiendelea kuongea pale, simu ya mkononi ya Patrick iliita, namba ya simu ilionyesha kuwa ilikuwa ni namba ya simu ya Tanzania, kitu cha kushangaza ni nani alikuwa anapiga wakati namba ile ni mpya kabisa na Patrick alinunua line yake tuliposhuka tu pale uwanja wa ndege. Khajat aliichukua ile simu na kuileta pale alipokuwa Patrick, alipoipokea tu sauti ikasikika.

    “Muachieni Mary, nawapa nusu saa vinginevyo Pamela na mwanae watakufa.” Aliongea yule mwanaume aliyesikika upande wa pili wa simu. Mary alishtuka haraka na kunyanyuka, kuja mpaka pale na kisha alimnyang’anya Patrick ile simu.

    “We ninani unayetaka mimi niachiliwe?” aliongea Mary na hapo sauti ya upande wa pili ilisikika ikicheka kwa muda kidogo kisha Mary alikata simu. Haikuchukua muda simu nyingine ya iliingia na hapo ilikuwa ni namba ya Pamela.

    “Patrick, Patrick wamemchukua mtoto wetu.” Sauti ya Pamela ilisikika ikiita huku akilia kwa sauti ya juu. Wote tulijiuliza ni wapi Pamela alitoa ile namba ya Patrick lakini hatukujua, kabla Patrick hajaongea kitu ilisikika sauti ya mwanaume mwingine kwenye ile simu akiongea.

    “Do as u were told and your family will be safe.” (fanya kama mlivyoambiwa na familia yako itakuwa salama).





    “Kuna sababu ya kila kitu kinachotokea kwenye maisha yako, ingawaje kuna muda kwa upeo wa fikra zetu au kwa ukungu wa uelewa wetu mdogo, tunajikuta tukilaani kutokea kwa kitu hata kama sababu yake inakuwa yenye manufaa kwetu. Upendo wetu juu ya wengine hutufumba macho na kutufanya tusahau kuwa tuna jukumu la kujitazama wenyewe pia pale wengine wanaposhindwa kujali hisia na machozi yetu.”





    **MARY**

    “Sikuamini kama siku moja ningekuja kuishia hivi. Sikuwahi kufikiri maisha yangu yangekuja kuwa ya namna hii. Ndoto zangu zilikuwa ni kufikia sehemu ambayo ningeweza kuionyesha dunia kuwa kuna wanawake wanaoweza kufanya mambo yakatokea. Nilitaka kuonyesha kuwa ndoto ya mtu yeyote ile inaweza kutimizwa katika namna ambayo yeye mwenyewe ataamua.” Nilimtazama Patrick na kusikia machozi yakianza kunitoka tena. Ni kwasababu yangu leo hii Patrick anataabika na dunia. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nilimuonea huruma mwanaume.

    “Nisamehe Patrick.” Nilizidi kumsihi lakini haikusaidia, mwili wangu ulikuwa ukivuja damu, Patrick alikuwa bado amenishikilia huku akilia kwa uchungu, nilipomtazama usoni niliona kabisa kuwa aliumizwa na ile hali yangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usiondoke Mary, usiondoke tafadhali.” Alizidi kulia kwa uchungu na mimi sikuweza tena kujizuia, nilizidi kulia. Picha ile ilinipeleka nyuma kabisa kipindi ninakutana na Patrick kwa mara ya kwanza. Nilikuwa nina hisia naye lakini ndoto na mipango yangu haikuzipa hisia za mwili wangu nafasi ya kusema akili yangu. Nilikuwa bado nikitazama juu wakati Patrick amenibeba na kunirudisha ndani. Haikujulikana popote ile risasi imetokea wapi, Felly alichukua vitambaa na kisu na kuja mpaka pale nilipo kisha aliniweka sana na kuniwekea kipande kidogo cha mti mdomoni ili aweze kunitoa ile risasi iliyopiga ubavuni mwangu. Nilisikia uchungu sana lakini hakukuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali maumivu yale yakae ndani mishipa yangu ya damu. Muda wote huo Patrick alikuwa pale pembeni huku jasho likimtoka. Zoezi lile liliendelea kwa muda wa dakika kumi na lilimalizika salama kisha nilifungwa vizuri na ile damu ilikatika.

    “Mary, nahitaji kujua kila kitu sasa.” Aliongea Patrick huku akionekana kuchoka na kila kilichokuwa kikiendelea pale.

    “Nipe simu kwanza.” Nilimuomba simu yake ya mkononi na hapo alinipatia kisha nilimuomba apige simu ya mkewe, baada ya sekunde kadhaa sauti ya mwanaume ilisikika kwenye ile simu. Hakuwa Pamela tena alikuwa ni yule mwanaume aliyeteka familia ya Pamela.

    “Rajan waachie huru.” Nilimpa maelekezo yule kijana aliyekuwa upande wa pili na yeye aliitikia kisha nikakata simu. Felly alikuja mpaka pale na kuchukua ile simu kisha alipiga tena na muda sio mrefu niliona akirudi pale na kumwambia Patrick kuwa mambo yameshakuwa sawa.

    “Mary, nini kimekutokea?” Aliuliza Patrick tena.

    “Patrick, mimi nilizaliwa miaka 30 iliyopita…” Nilianza kumuhadithia Patrick na wale wengine waliokuwa pale lakini nilikatishwa na sauti ya Patrick.

    “Miaka 30?” Aliuliza kwa mshangao, nilijua kuwa Patrick hakuwahi kuujua umri wangu sahihi kwakuwa nilimficha.

    “Ndio, nina miaka 30, nilipokuwa na miaka mitano, nilishuhudia baba yangu akimuua mama yangu kwa mziba pumzi kwa mto, ni ugomvi wao wa siku nyingi ndio uliopelekea yote hayo. Ile picha ilikuwa ikinirudia sana nilipofika umri wa miaka saba nilimuua baba yangu. Hakuna aliyefahamu juu ya hilo, kila mtu alidhani ni kifo cha kawaida tu. Tangu kipindi kile nilivaa roho ya kinyama. Nilichukuliwa na baba yangu mdogo na kwenda kuishi naye nchini Marekani, yeye hakuwa na mke, hakuwa na mtoto hivyo tuliishi mimi na yeye tu huko Tobargo, nilikuwa nikienda shule kama kawaida na jirani yetu kulikuwa na kambi ya jeshi, nilikuwa nikipenda sana kwenda pale na kuna baadhi ya vijana nilizoeana nao na hapo nikaanza kuwa nafanya mazoezi ya wasichana wadogo waliokuwa kwenye ile kambi. Walinipenda kwakuwa nilikuwa mwepesi na msikivu. Nikiwa kule nilibahatika kukutana pia na baba yangu mkubwa aliyekuwa akiishi Los Angelos.

    Mambo hayakuwa mazuri nilipofika miaka 12 kwakuwa baba yangu mdogo alianza kuniingilia kimwili wakati nikiwa nimelala na muda mwingine hata kuninyesha pombe na kuniingilia, hiyo iliniharibu sana lakini, nilikuwa nikitafuta namna ya kufanya. Miezi sita baada ya kutimiza miaka 12 ndiyo nilirudi tena Tanzania nikiwa na baba yangu mdogo, sikujua kuwa alikuwa na mke wake huku Tanzania. Tulipofika ndio nilikuja kujuana na mdogo wako Mark. Tulikuwa marafiki sana na kutaniana kwetu kulifanya tuwe kama wapenzi watoto.

    Wengi walidhani kuwa nilikuwa mtoto wa yule mama, lakini haikuwa hivyo. Mwanae alikuwa sehemu nyingine kabisa. Kipindi nikiwa na yule mama nchini Tanzania, alikuwa akinitesa na sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kumuwekea sumu kwenye chakula na ndipo alipokufa na wengi walijua kuwa yule mwanamke alijiua. Tulirudi tena Marekani na huko niliendelea na maisha yangu, lakini kipindi hiki sikuwa nikisoma tena, nilitoroka kwa baba mdogo na kwenda kuishi na mtu mwingine aliyekuwa mwanajeshi wa Marekani. Nia yangu kubwa ilikuwa ni kujifunza mambo ya kijeshi, huko nikajiunga na shule ya Lee Hyun aliyekuwa mwalimu wa mchezo wa Karate, nikafudhu na kumaliza mikanda yote. Sikujua ni nini nilikuwa nikiwaza, nilipofika miaka 16 nilianza kusihi kinyumba na Peterson Anglimayo, huyu alikuwa ni muuza madawa ya kulevya aliyekuwa akiishi Toronto, nilifoji vyeti vyangu vya kuzaliwa na miaka yangu ilionekana kuwa mbele zaidi hivyo alinioa japo nilionekana kuwa na mwili mdogo, mwaka mmoja mbele nilimuua Peterson na kufanikiwa kurithi akaunti yake iliyokuwa na dola milioni tano. Nilikutana na Hasheem Feisal ambaye alikuwa ni rafiki wa Peterson na ndiye aliyeanza kunifundisha mambo yote, nilienda Urusi na kuanzisha kampuni iliyokuwa ni kivuli tu lakini ilikuwa njia ya kuficha yetu ya biashara ya madawa ya kulevya.

    Nilirudi kwa baba yangu mdogo tena na kumuomba msamaha lakini alinielewa ila aliharibu pale aliponitaka tena kimapenzi na hapo ndipo nilipouondoa uhai wake. Nilirudi Tanzania na kufikia kwa baba yangu mkubwa ambaye ndiye mliyekuwa mkiishi naye karibu pia. Lakini kipindi hicho nilipata tenda ya kupeleka pembe za ndovu nchini Australia na kwingine.

    Wakati huo wote jina langu lilikuwa likitokea kwenye mitandao mingi ya vyuo vikuu kama muhitimu na msomi mahiri, mfano Shahada ya mfumo wa mawasiliano niliyopata Altai nchini Urusi haikuwa ya kweli bali ya kutengeneza, shahada ya utawala wa biashara niliyopata Limkokwing haikuwa ya kweli bali ni ya kughushi japo kweli nipo kwenye majina ya wahitimu, shahada ya Bradford ni ya kweli niliisoma mtandaoni. Ni kweli niliajiriwa kwa miezi michache kama Mpelelezi kwenye shule ya jeshi nchini Uingereza, nilikuwa nina uraia wa Uingereza na wa Marekani, shahada ya Uandishi ni ya kweli nayo nilisoma mtandaoni na niliipata Lesotho.

    Katika maisha yangu baada ya ndoa yangu ile ya kwanza, nilikuja kufunga ndoa na Fransisco Domosco huko Alaska, alikuwa ni tajiri, na mimi nia yangu ilikuwa ni kuja kuwa mwanamke mwenye mali nyingi za kutosha, miezi sita baadaye Fransisco aliandika wosia na siku mbili mbele alipata ajali niliyoitengeneza, alifariki na nilibahatika kuchukua asilimia 40 ya mali yake yote. Nilifungua kampuni Msumbiji na nchi nyingine na wakati huo bado nilikuwa na nina ndoto za kuwa tajiri kuliko nilivyokuwa wakati huo. Sikuwa na mapenzi na yeyote, sikuwa na mzazi wa kumfikiria, nilitazama jinsi watu walivyoishi kiumasikini nikaona sitaweza kuwa hivyo, nilijua niko duniani kwaajili ya kuhakikisha namiliki kila kitu kilicholetwa hapa duniani. Nilijifunza kuwa ili uwe na uwezo wa kutosha lazima uwe na roho mbaya. Niliamini wanaume ni watu ambao kama hutawawahi wao, basi ipo siku watakuwahi na itakuwa ndio mwisho wako. Kilichomtokea mama yangu sikutaka kinitokee mimi, sikutaka kuja kumnyenyekea mwanaume katika maisha yangu, nilitaka kutengeneza msingi bora wa maisha yangu ili nije kuingia kwenye orodha ya wanawake tajiri duniani.

    Nilikuja kuolewa mda mfupi mbeleni na Timoth Mobutu aliyekuwa mfanyabiashara wa madini huko Afrika ya kusini, lakini pia nilimuua baada ya kuhakikisha kuwa kila kitu chake nilijua kilipokuwa. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu. Lakini nilipofika Tanzania tena na kukukuta nilitokea kuvutiwa na wewe, lakini nilijizuia kwakuwa nilikuwa na lengo la kutimiza, ni kweli nilianzisha kampuni nyingine lakini nia yangu ni kujenga mtazamo wako juu yangu. Hukuwa tajiri sana hata kunifikia mpaka kwa wakati huo, lakini tamaa yangu haikuwa na kipimo maalum, kila kitu kwangu kilichoongeza hata shilingi 50 kwenye mabilioni niliyokuwa nayo kilikuwa ni muhim. Nilimshirikisha mdogo wako ambaye naye alionekana kuzimendea mali zako mda mrefu sana, japo tulifanikiwa na kuwa pamoja baada ya wewe kuaminika kuwa umekufa lakini Mark alikuwa mwenye papara, sikuzaa na Mark, nisingeweza kuzaa naye kwakuwa alikuwa ni mdogo wako. Mark hajawahi kufanya mapenzi na mimi. Ni vigumu kuamini lakini huo ndio ukweli, hata kifo cha Mark kilitokana na kung’ang’ania vitu nisivyovitaka. Nilijifanya kuwa mjamzito lakini sikuwa hivyo, mtoto niliyekuwa naye nilimnunua kwa mtu tu aliyemuiba toka hospitalini, nia ilikuwa ni kuficha kila kitu nilichokuwa nikikifanya. Dany alikuja kwenye mchakato huu baada ya mimi kuwa na nia ya kufungwa ndoa na wewe, mama yake na Mark pia alikuwa ndani ya mpango huo, lakini siku zote faida ndogo haiwezi kuliwa na walio wengi. Walikufa wote.” Haikuwa historia nzuri sana kuhadithia lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kumueleza Patrick kila kitu. Isingeweza kumsaidia chochote lakini ilitosha kumueleza na kumuondolea maswali mengi sana aliyokuwa nayo.

    Nilimtazama Patrick nikazidi kumuonea huruma, sikujuta kwa kumuingiza kwenye haya matatizo yote, lakini kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nilipata hisia ambazo sikutaka kuzizuia juu yake. Nilitamani muda urudi nyuma nipewe nafasi ya ku kusahihisha makosa yangu lakini hakukuwa na muda huo. Pale utendapo kosa ndipo muda wa marekebisho huishapo, muda wa majuto huja mbele kama matokeo ya uvivu wako wa kufikiri kutenda mema katika muda ambao nilikuwa nao. Sikuwa tu nikilipa kisasi kwa yale niliyokuwa yametokea katika udogo wangu bali nilikuwa nikitengeneza misingi imara ya furaha yangu mwenyewe. Sikufahamu Patrick alipanga kunifanya nini lakini nilikuwa niko tayari sasa kwa lolote alilotaka kunifanya. Lile bomu waliloniwekea lilikuwa likinipa maumivu makali ya tumbo lakini sikuwa na jinsi. Nimekuwa katili kwa miaka mingi ya maisha yangu na nimekutana na watu wengi makatili lakini sikuwahi kukutana na mtu katili kama Khajat. Kila mtu anajua kwanini yuko vile alivyo.

    “Kwanini ulinichagua mimi Mary, kwanini usingeniacha niishi maisha yangu tu, kwanini Mary.” Alizidi kuongea Patrick huku akilia, hapo alinifanya nizidi kusikia uchungu ndani ya moyo wangu. Sikuwa na jibu la swali lake, nilimchagua yeye kwakuwa alikuwa ndiye pekee ambaye alikuwa anaweza kuzoeleka haraka.

    ******

    Kesho yake asubuhi nikiwa bado sijapelekwa hospitali nilichukuliwa na Patrick na kuingizwa kwenye gari ambapo walikuwa pia kina Khajat.

    “Hati za mali zangu ziko wapi?” Aliongea Patrick ambaye alionekana kama amebadilika. Nilinyamaza kidogo nikitafakari juu ya kubadilika kwake ghafla lakini nilishtuliwa na mdomo wa bastola uliokuwa mbele ya paji langu la uso.

    “Sitauliza mara ya pili.” Aliongea hayo na hapo ndipo nilipomjibu.

    “Zipo Mkuranga, kuna sehemu niliweka kila kitu changu.” Nilimjibu na hapo bado aliendelea kuninyooshea ile bastola.

    “Na huyo aliyeenda kuteka familia yangu ni nani?” aliuliza kwa hasira.

    “Ni mtu ambaye aliwekwa anifatilie nyendo zangu.” Nilimjibu lakini sikutamani aniulize swali la pili.

    “Aliwekwa na nani.” Aliuliza swali ambalo sikutaka kabisa aniulize kwakuwa sikuwa tayari kumjibu. Ingemuumiza au kuona kama mimi ni mpuuzi zaidi ya alivyokuwa akifikiria sasa hivi.

    “Mume wangu.” Nilimjibu kwa kifupi huku nikiangalia chini, hasira zilinijaa kwakuwa mtu wa mwisho ambaye nilipanga kuja kumuua kwa mikono yangu ni Idrisa Eljabr. Alikuwa ni tajiri wa kiarabu mwenye visima vya mafuta huko Oman, alinioa kwa ndoa ya lazima na sikuwa na jinsi, akanifanya mtumwa mpaka pale nilipoamua kutoroka kwake lakini bado alikuwa akinisaka kila kona. Nilimuahidi kifo na kama ningepata nafasi ya kurudi tena kwake basi ningeweza kumfanya kitu ambacho kingebeba maumivu ya kila mpuuzi mwenzake aliyewahi kupata maumivu.

    “Una mume tena?” aliuliza kwa mshangao na hata hivyo sikuwa na la kumjibu, aliwasha gari kwa kasi na safari ya kuelekea Mkuranga ilianza. Hakuna aliyeweza kuniuliza chochote au kuongelea yale niliyokuwa nimehadithia jana yake. Tulitumia masaa kadhaa na baadaye tulishuka kwenye shamba kubwa lenye vichaka na kuanza kuingia ndani kwa mguu. Mpaka katikati ya lile shamba kulikuwa na kaburi, hakuwa amezikwa mtu, tulilifukua kwa muda wa nusu saa, na ndipo tulipokutana na sanduku lililokuwa na zile hati za kila kitu. Nilitoa na kumkabidhi Patrick, nilikuwa na moyo mweupe na nilihisi kupunguza mzigo ndani ya moyo wangu. Baada ya Patrick kuhakikisha amepata kila kitu aliniingiza ndani ya gari na tukarudi mpaka Dar. Usiku wa ile siku nilitolewa lile bomu kwa mkono. Yalikuwa maumivu makali makali ambayo sikuyategemea. Siku mbili mbele nikafunguliwa kesi ya mauaji na makosa mengine kama 9 hivi. Kesi yangu ilienda kwa muda wa miaka miwili na kwa muda wote huo sikuwahi kuona Patrick, nilihukumiwa kifungo cha maisha jela na sikuwahi kumuona yeyote aliyekuja kunitembelea.





    RIWAYA: KISASI

    MTUNZI: Frank Mushi



    SEHEMU YA MWISHO PART 03



    “Mtu DHAIFU hawezi KUSAMEHE, kitendo cha kusamehe ni cha watu JASIRI wenye uwezo wa kupuuzia machungu nakuamua kuonyesha kutojali kwao. Ni mpaka utakapo samehe na kuasahau ndipo utaweza tena kuendelea na maisha yako. Kwa kushindwa kusamehe unaweza tengeneza tatizo kubwa kuliko lile alilotengeneza aliyekukosea.”

    HII NI SEHEMU YA MWISHO.



    **MWANDISHI**

    Yule jamaa aliyenihadithia kuhusu hadithi hii aliyoisikia kupitia kituo cha radio aliniacha na maswali mengi sana ambayo nilidhani kuwa ni muda muafaka wa kuikamilisha hadithi hii kwa kutafuta kiundani juu ya wahusika kwenye mkasa huu wa kutisha. Nilifunga safari mpaka Gereza la Segerea upande wa wanawake ili niweze kuonana na Mary aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha gerezani. Safari yangu haikuzaa matunda baada ya kukuta Mary akiwa hoi hospitalini, nilibahatika kuruhusiwa kuonana naye akiwa hospitali huku amefungwa pingu kila upande wa mikono na miguu yake.

    “Mimi ni mwandishi wa habari, nimebahatika kusikia masimulizi yako ambayo naamini uliyatoa kwa mwandishi ambaye alikuwa akikusanya makala kuhusu mkasa wako na Patrick. Nimebahatika kusikia, japo ni kupitia kwa mtu juu ya kilichotokea na pande zote mbili mlitafutwa mkaelezea kilichotokea, lakini nilitaka kujua hali yako kwa sasa na maisha yako baada ya yale mambo kuishia, na unavyojisikia baada ya Patrick kukuacha bila kukufanya chochote kibaya”. Nilimweleza Mary nia yangu hiyo, japo alikuwa akionekana kabisa kuwa alikuwa kwenye dakika za mwisho kabisa za maisha yake. Alionekana akiongea kwa shida sana. Nilimgeukia yule askari aliyekuwa karibu na kile kitanda na kumuomba amfungue mikono kwani asingeweza kabisa kuwa na hata nguvu ya kutoroka. Afya yake ilikuwa imedhoofika vya kutosha, sikuamini kama kweli yule ndiye Mary niliyemsikia kwenye yale masimulizi ya yule jamaa. Yule askari alikataa kumfungua huku akinisisitizia kuwa ilikuwa ni taratibu ya kazi kuwa lazima afungwe pingu. Nilirudi tena na kumgeukia Mary, alikuwa akitaka kuniambia kitu lakini sikuweza kuisikia sauti yake vizuri. Nikazidi kumsogelea kwa karibu na hapo ndipo niliposikia sauti yake japo ilikuwa kwa mbali.

    “Nenda kwa mkuu wa gereza kuna vitu vyangu nimeweka kule, mwambie akupatie bahasha ya kijani, hakikisha unamfikishia ujumbe Patrick, tafuta namna ya kuwafahamisha watu wengi zaidi juu ya hali yangu na majuto yangu.” Aliongea hayo na kabla hata sijatoka Mary alianza kuhangaika na kurusha miguu huku na kule, akakata roho mbele ya macho yangu.

    *****

    Niliondoka mpaka kwa mkuu wa gereza nikiwa na askari yule aliyekuwepo pale wakati Mary akinipa maelekezo ya kuchukua hiyo bahasha ambayo ina ujumbe niliotakiwa kumfikishia Patrick ambaye hata hivyo sijui alipo wala sijawahi kukutana nae. Nilibahatika kupata ile bahasha iliyokuwa nyepesi sana, niliifungua ndani na kukuta ujumbe mrefu ulionifanya nikae chini na kuanza kuusoma taratibu kama vile ulinihusu, ulisomeka hivi;

    Mpenzi Patrick, na ulimwengu kwa ujumla,

    Nafahamu ya kuwa nimekuwa mnyama wa kushindwa kusamehewa na hii dunia, sijui kama naweza kuja kusamehewa na yeyote mwenye akili timamu. Natamani ningeweza kuumbwa tena upya nikasawazisha makosa yangu lakini hakuna tena muda.

    Nimeandika huu ujumbe kwako ili kukuambia sababu ya mwisho ya kwanini nilikuwa hivi nilivyo. Kila kitu kwenye maisha hutokea kwa sababu Patrick, lakini katika maisha yangu vitu vilitokea kwasababu ambayo sikuitaka katika maisha yangu wala sikuipenda kabisa. Nilitendewa unyama ulionifanya niwe mtu wa kuhangaika kila mara hasa pale nilipogundua kuwa mimi si kitu tena. Nilijidharau kwakuwa nilifanywa mtu wa kudondoka muda wowote.

    Baba yangu alimuua mama yangu nikishuhudia, lakini chanzo cha ugomvi wao sikukifahamu mpaka pale nilipofikisha miaka saba. Nilikuwa mdogo lakini nilikuwa na akili sana, niliunganisha matukio na kutafuta ushahidi na ndipo nilipokuja kugundua chanzo cha kifo cha mama yangu. Aliuawa kwaajili yangu, aliuawa kwa kitu ambacho hakikuwa cha kweli.

    Miaka mingi iliyopita baba yangu alikuwa akisoma shahada ya udaktari nchini Urusi. Kuna wakati karibu kabisa na akiwa anamaliza masomo yake alirudi nyumbani, kwa wakati wote huo mama yangu alikuwa akimsubiri tu, walioana na kisha aliondoka na kwenda Urusi kwa miaka sita, baada ya yeye kurudi ndipo mama yangu alipopata ujauzito na miezi tisa mbeleni nilizaliwa. Maisha yalikuwa mazuri lakini tafrani ilianza pale ambapo nilifikisha miaka mitatu. Baba yangu alikuwa akimtuhumu mama kuwa mimi sio mtoto wake na kwamba mama yangu alikuwa Malaya. Lakini mama alisisitiza kuwa wakanipime DNA ili iweze kujulikana ukweli. Aliyeleta maneno ya kwamba mimi sio mtoto wa baba yangu ni baba yangu mdogo ambaye alikuja kutembea na mimi baadaye, ambaye ndiye aliyekuja kuharibu maisha yangu kabisa. Nilisimuliwa haya na shuhuda ambaye alifahamu kila kitu na alinipa njia za kupata ukweli kuhusu kifo cha mama yangu. Baba zangu wadogo walikuja juu pia na baadhi ya watu lakini kila mama alipohimiza kwenda kuangaliwa DNA hawakutaka kabisa.



    Nilichomwa sindano ya sumu aina ya ‘dimethylmercury’, hii ni sumu ya kutengenezwa na binadamu, ni sumu inayoua taratibu na kwa muda mrefu. Nilichomwa kiasi cha 0.3 Mils na hichi ndicho kilichonifanya nione hakuna haja ya kufanya chochote. Nilianza kuumwa lakini haikuweza kugundulika mapema niliumwa nini. Baada ya kifo cha mama yangu na hata baada ya baaba yangu kufa pia niligundua kuwa mzee wangu alikuwa akifanya tafiti juu ya ile sumu aliyonichoma. Hapo ndipo nilipogundua ni sumu ya aina gani nimechomwa. Nilivurugika akili lakini hakuna yeyote niliyewahi kumwambia. Katika umri wangu nilianza kuua wanaume hovyohovyo, lakini hasira yangu haikuwa kwa wanaume tu, ilikuwa ni kwa kila binadamu na kiumbe cha dunia hii. Mpaka leo hii nikiandika ujumbe huu, nimeshaua wanaume zaidi ya 300, na wanawake wachache, wapo watu ambao nao niliwachoma sindano ile kwakuwa nilibahatika kuitafuta mpaka nikaipata. Nia yangu nikuona kila binadamu akihangaika kama mimi, kila binadamu akiwa na hofu ya kufa muda wowote. Lakini katika wote, sikuwahi kukuchoma wewe tu, japo nakiri kukuchoma sindano iliyopoteza akili yako kwa muda mrefu. Sio tamaa tu ya fedha bali roho ya kisasi iliufunga moyo wangu.

    Pamoja na pesa nilizokuwa nazo lakini nilishindwa kabisa kutoa ile sumu mwilini, najua itaniua siku moja hasa kwakuwa sina tena vile vidonge vya kupambana nayo na kuniongezea nguvu. Lakini najuta sana. Najuta yote niliyoyafanya.

    Naomba uniombee kwa mungu, naomba kila mmoja kwa wakati wake aniombee kwa mungu, nimefanya mengi mabaya lakini sikuyafanya kwa raha. Niliyafanya kwa uchungu na nilikuwa nikilia kila muda ulipopita mbele yangu. Nisameheni sana, nisamehe sana Pamela, nisamehe sana Cris, naomba nisameheni wote mliopata usumbufu kwa mimi kuishi duniani. Mnisamehe ndugu zangu, niliua baba zangu wadogo wote na mashangazi zangu kwakuwa walichangia sana kumnyanyasa mama yangu. Hakuna aliyefahamu kuwa walikuwa wakiuliwa, wengi walijua kuwa walikufa kifo cha kawaida lakini mimi ndiye nijuaye ukweli zaidi wa yaliyotokea. NISAMEHENI.



    NAKUPENDA PATRICK. NIKIFA BASI TUTAKUTANA MBELE YA HAKI KAMA IKITOKEA NIKAFIKA HUKO.

    Mungu akulinde wewe na familia yako.

    AMANI NA SALAMA.

    Ni mimi MARY.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******

    Huo ndio uliokuwa ujumbe wa Mary kwa watu wote na kwa Patrick. Nilihangaika sana kupata mawasiliano na Patrick lakini mwishoni nilibahatika kupata namba yake ya simu, nilimueleza juu ya ule ujumbe na alinitumia tiketi ya ndege akitaka kuonana na mimi. Nilisafiri hadi Australia ambapo ndiko anakoishi kwasasa na mkewe na watoto wake wawili, Cris na mtoto wao mwingine mdogo aitwaye Qwinzel. Wanamiliki hospitali maarufu ya Pamela Mental Clinic, na pia ukumbi mkubwa wa sinema wa Qwinzel Cinemax huko nchini Australia, na Patrick kwa sasa ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Swirnbune.



    MWISHO.









0 comments:

Post a Comment

Blog