Search This Blog

Thursday, 27 October 2022

KAHABA YUAN LIANG - 1

 









    IMEANDIKWA NA : HAKIKA JONATHAN



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kahaba Yuan Liang

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ikulu; 9:30pm,



       Usingizi uligoma kabisa, alijigeuza upande huu, akarudi upande ule, hali ikabaki ileile usingizi kumgomea.Hakuona sababu ya kuendelea kuteseka, alimgeukia mama Zainath, na kumgusa mabegani kwa mara nyingine tena.



    “Nimesema niache!, sitaki, kwa leo sijisikii, labda siku nyingine “,mama Zainath alifoka kwa hasira.



    “Sawa mke wangu, unayosema ni sahihi kabisa, lakini……”,



    “Lakini nini ?,nimesema sitaki! niache nipumzike “,



    Raisi Jonsoni Mtemvu alijitetea,lakini mke wake aliendelea kusimamia msimamo wake wa kutokidhi haja za mume wake. Alijifunika shuka, na kuuchapa usingizi.



    Bwana Jonsoni Mtemvu, raisi kijana kabisa,moyo wake ulikata tamaa ya kupata penzi la mke wake kwa usiku huo, alitazama saa yake ya mkononi, saa ya dhahabu ambayo aliinunua kwa mamilioni ya pesa.



    “Saa tatu na nusu!  bado mapema sana, kanikomoa na mimi namkomoa mara mbili zaidi, “raisi aliongea, huku akionekana kufikilia jambo. Akiwa na nguo ya kulalia, alishuka kitandani, akatembea hatua chache kulisogelea kabati lake, kabati ambalo lilisheheni suti za bei kali, suti ambazo zilimtofautisha yeye pamoja na wananchi wake.



    “Hii itanifaa, lakini ngoja nimpigie bwana Januari Sasamba, anipe mwongozo! bila hivyo usiku huu utakua mrefu kwangu ……”,Jonsoni Mtemvu alizungumza peke yake, bila mke wake kutambua. Mkono wake wa kulia ulizama mfukoni na kutoka na simu, iPhone7 ilisomeka kwenye kioo cha nyuma.



    Alibonyeza namba kadhaa, bila shaka alikuwa akiitafuta namba ya mtu huyo. Waziri January, namba ilisomeka kwenye sehemu ya majina. Alibonyeza sehemu ya kupiga, kisha akaisogeza simu yake katika sikio lake la kulia.



    “Kulikoni mheshimiwa, mbona usiku usiku! “,sauti ilisikika upande wa pili, baada ya kupokelewa.



    “Usiku una mambo mengi ndugu, anyway! naomba unijibu haraka sana ujumbe wa sms ninao kutumia “,mheshimia Jonsoni Mtemvu, raisi wa nchi ya Goshani aliongea.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sawa boss, nitafanya hivyo! “,upande wa pili wa simu ulizungumza, kisha simu ikakatwa, na kumuacha na shauku kubwa ya kutaka kufahamu ni nini ambacho kilimfanya mkuu wake wa kazi, raisi Jonsoni apige simu wakati wa usiku, tena mida ya kupumzika!



    “Samahani waziri na rafiki yangu kipenzi,mke wangu kanigomea na ninataka kukidhi haja zangu, wewe ni rafiki yangu na hatufichani kwa chochote kile, nahitaji msaada wako. “,ujumbe wa meseji uliingia kwenye simu ya waziri Januari Sasamba, waziri mkuu wa nchi ya Goshani, cheo ambacho alikipata kwa kuteuliwa na rafiki yake ambaye walisoma wote chuo kimoja, chuo kikuu cha “Goshani university “,miaka kumi iliyopita.



    “Kazi ndogo sana,sijawahi kukuangusha, ngoja nikusaidie bila hivyo unaweza kujikuta umembaka mkeo …”,mheshimiwa January Sasamba alizungumza peke yake, aliwasha data, akaingia katika ukurasa wa instagram, macho yake yakaishia sehemu ya kutafuta jina la mtu unayemuhitaji.



    “Changudoa Goshani”,aliandika, kisha akabonyeza kitufe cha kuruhusu kutafuta mtu anayetumia jina hilo. Msururu wa majina ulitokea, macho yake yakaishia kwenye jina la kichina, Yuan Liang, akiwa na shauku ya kutaka kujua mengi kuhusu jina hilo, akaenda kwenye taarifa zote kuhusu ukurasa huo.



    “Yuan Liang,chinese girl, Living in Goshani, self employed as a prostute, call; 0248698653”,(Yuan Liang,binti wa kichina,nimejiajiri kama malaya,piga;0248698653) ,



    Macho ya mheshimiwa Januari yalimtoka,mapigo ya moyo yakaongezeka,moyo ukamjaa tamaa.Hakuamini kama kuna mtoto mzuri na mrembo kiasi kile,isitoshe raia wa kigeni,anajiuza katika nchi ya Goshani.Haraka haraka alikopi namba ya Yuan Liang,akaenda upande wa meseji ,na kuanza kulitafuta jina la mheshimiwa raisi.



    “Raisi Jonsoni”,jina lilisomeka,bila kuchelewa alimtumia ujumbe,kisha akaendelea na shughuli zake za kutazama mpira,starehe ambayo aliipenda kwani alikuwa bado hajaoa,licha ya kuwa na cheo kikubwa nchini Goshani.



    “Huyu mwanamke mbona simfahamu,siku zote nachukua wanawake lakini sijawahi kukutana naye?,mchina kweli anaweza kuwa maskini kiasi hiki,tena ajiuze katika nchi maskini,nchi ambayo hawezi kupata mteja wa kumlipa dola kumi kwa usiku mmoja?anyway,ngoja nijue  mwisho wake,mkuu akifanikiwa,nitamfahamu tu binti huyu

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “, akiwa mwenye mawazo,waziri mkuu bwana Januari Sasamba aliendelea kunywa wisky taratibu,huku macho yake yakiwa bize kufuatilia mpira kati ya Real Madrid na Livrpool,fainali ya ligi ya mabigwa barani Ulaya.



    …………………………………



    “Ni msichana mrembo wa kichina,anaitwa Yuan Liang, yuko hapa Goshani,kwa mawasiliano 0248698653,kazi kwako mkuu,usiku mwema!”,ujumbe wa sms ulisomeka,katika simu ya mheshimiwa raisi,bwana Jonsoni Mtemvu kutoka kwa waziri Januari Sasamba.



    Akiwa amepigilia suti nzuri ya kifahari,suti iliyopambwa kwa mistari ya kupanda na kushuka,alitoka nje bila kumsemesha mke wake,huku mapigo ya moyo wake yenye uchu wa kingono yakienda kasi.



    “Mkuu unahitaji ulinzi?,safari ya wapi?”,kamanda mkuu,kamanda aliyeongoza jopo la walinzi katika ikulu ya raisi aliongea.



    “,Makamanda wawili wanatosha,naelekea Serena hoteli kuna mtu muhimu nahitaji kuzungumza naye”,mheshimiwa Jonsoni Mtemvu alizungumza huku akiwa bize na simu yake.



    “,Sawa bosi!,Inspekta Amiry,”,kamanda yule alizungumza.



    “,Nipo afande,”inspekta mwenye bunduki kubwa ya smg aliitikia.



    “,Inspekta Junior”,kamanda mkuu aliita tena.



    “,Nipo afande” ,inspecta mwingine mwenye bastola kiunoni aliitikia.



    “Hakikisheni usalama wa raisi,kazi ikiharibika ,kifungo au kunywongwa halali yenu…”,kamanda mkuu aliongea,huku sura yake ikiwa haioneshi utani hata kidogo.



    “,Sawa afande,tuna ahidi atarudi salama,kibaya kikitokea tunakubali kufa au kunyongwa”,inspecta Amiry pamoja na inspecta Junior waliitikia.



    “,Nafurahi kuskia hivyo,kazi njema”,kamanda mkuu aliongea,huku vijana wake wakitembea kwa ukakamavu kulisogelea gari la kifahari aina ya V8,gari ambalo mheshimiwa raisi alikwisha pakizwa ndani yake.



    …………………………………



    Green pick hotel; 10;30pm



         Mikono yenye uzoefu mkubwa wa kuchezea kompyuta, ilikuwa bize kucheza na kompyuta ya kifahari, maarufu kama “macboock air “,kioo cha kompyuta kilionesha watu mbalimbali duniani, watu ambao waliibiwa vitu vya thamani kisha kuuawa kikatili.



    “Nina masaa arobaini na manne ya kuishi hapa Goshani,kwa sasa ninapaswa kwenda China nikafahamu ukweli kuhusu wazazi wangu,kwani pesa tayali nimekusanya ya kutosha “,msichana mrembo,aliyeimudu vizuri lugha ya Kiswahili,lugha maarufu  Afrika mashariki,aliongea huku akitazama kompyuta yake yenye matukio mbalimbali ambayo amekwisha yafanya.



    “Ndrii,ndrii!ndrii!ndriii!”,mlio wa simu ulisikika.



    “Nani tena huyu,meseji za nini usiku huu nimechoka!,kama ni kazi yenye pesa za madafu sifanyi mimi siku ya leo…”,msichana mrembo wa kichina aliongea,huku akinyanyuka kutoka kwenye kitanda alipokuwa ameketi,na kuisogelea simu yake juu ya meza.



    “Aim president Jonsoni Mtemvu,the president of Goshani ,i want to be with you this night, i promise to pay u well…”,(Mimi ni raisi Jonsoni Mtemvu,raisi wa Goshani,nahitaji kuwa na wewe usiku huu,nakuahidi nitakulipa vizuri…”,) meseji ilisomeka katika kioo cha simu,huku akisoma mara mbili mbili ujumbe huu uliotumwa kwa sms.



    “Sawa mheshimiwa,nikukute wapi?”,Yuan Liang akiwa mwenye wasiwasi,huku machale yakimcheza,alijibu meseji bila  kuchelewa,huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio.



    “Oooh kumbe unajua Kiswahili, Niko Serena Hotel,chumba namba 20,karibu sana “,mheshimiwa raisi, bwana Jonsoni Mtemnvu alijibu ujumbe wa sms.



    “Dakika kumi nitakua hapo, sasa hivi ni saa nne na nusu, saa nne na dakika arobaini nitakua hapo, onyo!! polisi wakae umbali wa mita tano na eneo la chumba …”,Yuan Liang aliandika ujumbe wa sms wenye masharti mazito ndani yake, kisha haraka haraka alianza kujiandaa kwa ajili ya kazi.



    “Nimeshawaibia watu wa kubwa duniani na kuwaua, leo naenda kufanya historia nyingine, nachohitaji ni pesa tu, ukahaba ni kuficha uhalisia tu, ole wake avunje masharti, atakufa yeye na ukoo wake, ikiwezekana serikali yote, watakufa! “,kwa malingo, mwanadanda mrembo sana, mwenye asili ya kichina, aliongea huku akiivaa sura ya bandia usoni mwake.



    Alichukua mkanda wake, mkanda wenye visu vidogo vidogo takribani ishirini na kuupachika kiunoni mwake, kisha alivaa koti kubwa na jeusi, mkononi alivaa gloves nyeusi, zenye sindano ndogo ndogo zisizo onekana kwa macho ya kawaida. Mguuni alivaa kiatu chenye kisigino, kisigino kilichofungwa kifaa kidogo maalumu kwa ajili ya kukata mawasiliano ya simu pale kitakapotumika kwa kubonyeza kibatani kilichofungwa kwenye miwani ya Yuan Liang.



    “Ooooh shit! nimesahau miwani, !!ilikua kazi bure ” ,alizungumza baada ya kupiga hatua kadhaa, kisha alirudi chumbani, aliangaza huku na kule hakuona chochote kile.



    Ghafla tabasamu liliipamba sura yake, miwani yake ilikua kitandani, aliifata na kuivaa, kisha alitoweka haraka sana kutoka chumbani mwake.



    …………………………………



    Serena hotel;. 11;00pm



         “Sikilizeni vijana,kuna mgeni wangu muhimu anakuja, pesa hizi hapa, agizeni kinywaji! kuhusu ulinzi msijali sana, mgeni mwenyewe ni mwanamke, sizani kama atakua mtu mbaya kwangu, akizingua hata mimi naweza mdhibitii ……”,raisi Jonsoni alizungumza na vijana wake, umbali wa takribani mita nane kutoka chumba namba ishirini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Hahahaa, sawa bosi! ,sisi tupo, kuhusu kukulinda tutakua makini pia, tumekula kiapo cha kifo au kifungo kwahyo usjali …”,inspecta Junior pamoja na inspecta Amiry walicheka, huku wakiwa makini kuangaza huku na kule kudumisha ulinzi.



    “Sawa vijana, asisogelee chumba mtu yoyote mpaka nitoke “,mheshimiwa Jonsoni aliongea, huku akielekea chumba namba ishirini.



    “,Sawa mkuu, kuwa makini “,vijana waliitikia, huku macho yao yakimsindikiza raisi wao, raisi wa kwanza kijana kati ya watatu, tangu nchi ya Goshani ipate uhuru kutoka kwa Wachina mwaka 1994.



    …………………………………



    Pikipiki kubwa aina ya baja, ilipaki nje ya geti la Serena hoteli. Mtoto wa kike mwenye sura ya kizungu alishuka, kisha kuwasogelea walinzi ambao walionekana kuwa na wasiwasi sana.



    “Mimi itwa Elizabeth, iko kuja Gosheni toka Uingereza, kuja ona geni wangu, wewe angalia motorcycle yangu, mimi kupa wewe dola kumi “,Yuan Liang aliongea, huku akiwa amevaa sura bandia ya kizungu.



    “Sawa mzungu, karibu sana, ukihitaji chakula cha kimataifa na vyumba vya kisasa vinapatikana, pikipiki yako nitakuangalizia mpaka kesho “,mlinzi mmoja, miongoni mwa walinzi wa nne waliokuwepo getini, mlinzi mwenye tamaa ya pesa aliongea, bila kutambua kuwa mgeni anayemkaribisha alikuwa na sura ya kondoo, lakini moyo wake ulikua mubaya uliojaa ukatili kupita kiasi..

    .



    Serena Hotel;



          Yuan Liang aliruhusiwa kuingia hotelini, hakuna mlinzi yoyote aliyekuwa na mashaka naye, alibonyeza batani kwenye miwani yake upande wa kulia, kuruhusu kifaa kilichofungwa kitaalamu kwenye kisigino cha kiatu chake kufanya kazi yake, mawasiliano ya simu yakakatika eneo lote la hoteli.



    Aliangalia saa yake ya mkononi, “Saa tano na nusu! “,Yuan Liang alizungumza, akaongeza mwendo, “RECEPTION “(MAPOKEZI “) ,kibao kilisomeka katika chumba kidogo cha vioo, akasogea ili kuongea na muhudumu,



    “,Welcome! tukusaidie nini? “,muhudumu wa mapokezi alizungumza.



    “,Mimi iko nenda chumba namba twenty, taka ona mgeni wangu “,Yuan Liang alizungumza kwa rafudhi ya kizungu.



    “,Ohooo! kumbe ni wewe, karibu sana, karibu, panda juu ghorofa ya pili, kunja kushoto, kisha kulia, utaona chumba kikubwa chenye vioo vya rangi ya dhahabu “,muhudumu alizungumza, baada ya kugundua mgeni wa raisi aliyesubiliwa kwa hamu tayali aliwasili, alinyenyua simu ya mezani, akabonyeza namba kadhaa, akaweka sikioni, “Dear customer, there is network error, try again later, “(Ndugu mteja, kuna matatizo ya mtandao, jaribu tena baadae) “,upande wa pili wa simu ulizungumza …



    “,Oooh shit! hakuna mtandao, anyway! hakijaharibika kitu, nenda tu chumbani utamkuta “,muhudumu alizungumza, kwa ishara ya mkono, akamuelekeza Yuan Liang  njia ya kupita kuelekea juu ghorofani.



    “Kazi imefanyika! mawasiliano hakuna tena!”,Yuan Liang alizungumza peke yake bila sauti kusikika, tabasamu lilionekana usoni mwake, safari ikaanza, akapanda ngazi taratibu kwa umakini wa hali ya juu, huku macho yake yakiangaza huku na kule kuangalia kamera za ulinzi na njia za kutorokea baada ya kukamilisha kazi.



    “,Sorry sister, my name is Amiry, the police inspector “,(Dada samahani, naitwa Amiry, inspecta wa jeshi la polisi) “,inspecta Amiry alizungumza.



    “,My name is Junior, the police inspector “,(Naitwa Junior, inspecta wa jeshi la polisi) “,inspecta Junior alijitambulisha.



    “,Mimi itwa Elizabeth, kuja ona mgeni wangu ,chumba hiyo hapo ……”,Yuan Liang alijitambulisha, mara baada ya kuzuiwa na walinzi alipojaribu kusogelea mlango wa chumba namba ishirini.



    “,Ohoo! kumbe ni wewe, samahani sana bosi! tuko kazini, ni wajibu wetu, samahani kwa usumbufu ……”,inspecta Junior pamoja na inspecta Amiry waliomba samahani baada ya kutambua mwanamke huyu wa kizungu hakuwa adui, bali mgeni wa mheshimiwa raisi aliyesubiliwa kwa hamu. Walisogea pembeni, Yuan Liang akapita, baada ya hatua kadhaa, akafika mlango wa chumba, akabonyeza kengele ukutani, sekunde mbili tu, mlango ukafunguliwa, akatumbukia ndani …



    …………………………………



    00;00pm



          Mheshimiwa raisi alikosa usingizi,pepo la ngono liliendelea kumsumbua,alitazama saa yake,muda ulikimbia,alilala kidogo,akashuka kitandani,akatembea huku na kule ndani ya chumba,akaangalia saa tena,”saa sita kamili…!,hee!au haji?,kanidanganya mwanamke huyu,nita……”,kabla hajamaliza kuzungumza,alihisi hatua za mtu kuusogelea mlango wa chumba,akatega masikio kusikiliza kwa makini.



    “,tiririii!tiririi……”,mlio wa kengele ulisikika,mapigo ya moyo ya raisi yakaongezeka,furaha ikarejea tena.Akausogelea mlango,akazungusha kitasa cha mlango chini na juu,mlango ukafunguka…



    “,Mpenzi,mimi penda wewe sana,leo kupa wewe penzi nzuri……”,Yuan Liang alizungumza baada ya mlango kufunguliwa,alimsogelea raisi,akamkumbatia…



    Raisi Jonsoni Mtemvu alisahau kuwa mgeni aliyepaswa kuonana naye  ni mchina na wala sio mzungu,huku akizungumza kiswahili kilicho nyooka.Hakuwa na hofu juu ya mwonekano mpya wa mgeni wake pamoja na kiswahili kibovu cha rafudhi ya kizungu alichozungumza mgeni wake,Jonsoni Mtemvu alihitaji penzi na wala sio kitu kingine.Alimsogelea Yuan Liang,akamkumbatia na kumtupia kitandani.



    “O…oo…oo…oh”,Jonsoni Mtemvu alilalamika na kupoteza fahamu, pua na mdomo wake vilibanwa ghafla,mshipa wa fahamu ulipigwa kifuti cha mkono,pigo ambalo lilifanywa kwa sekunde moja tu,kitanda kikageuka uwanja wa mauaji…



    “,Pumbavu!mnakula pesa za walalahoi,pesa zote mnanunua makahaba,kufa mpuuzi wewe!”,Yuan Liang alizungumza,huku akimsachi raisi Jonsoni Mtemvu,kwenye mifuko wapi!kwenye waleti wapi!,hakuna kitu!



    “Raisi gani unatembea bila pesa!ungenilipa nini sasa?”,Yuan Liang alifoka,mkono wake ukiwa bize kukagua waleti ya mheshimiwa Jonsoni Mtemvu.



    “Free of charge,special card for president” ,(Hakuna malipo,kadi maalumu kwa ajili ya raisi)”,kadi ilisomeka,kadi ya raisi iliyomuwezesha kupata huduma bure mahala popote pale.



    “,Ohoo!ndio maana,kwahiyo hata mimi ulitaka unifanye bure?,stupid president!”,Yuan Liang alibwatuka,akatupilia waleti kule! kadi kule!,akachukua saa ya raisi kwenye mikono yake,akaichunguza kwa makini,akabonyeza batani mbili za saa ya kifahari kwa wakati mmoja,taa ya saa ikabadilika rangi,nyekundu!kijani,njano!,kisha ikawaka nyeukundu tena,memory card(diski) ikatoka!



    “,Yes!nitajua mengi kupitia diski hii,siri zote za nchi nitazifahamu,nitapata mabilioni ya pesa!”,Yuan Liang alizungumza kwa furaha, akaitelekeza saa, akaingia chooni, akachomoa visu viwili kwenye mkanda wake, akakata kioo cha dirisha, akapenya na kuruka kwa serekasi hewani mpaka chini.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ” ,Kazi imekwisha! “,Yuan Liang alizungumza, hakuna aliyemshuhudia wakati akitekeleza tukio hilo, alitoka getini, akawapatia dola ishirini walinzi, wakachekelea kwa furaha, akawasha pikipiki yake, akatokomea kusikojulikana …



    …………………………………



    08;00am



          Taharuki ilitanda nchini Goshani, kila kona watu walikaa makundi, tukio la raisi Jonsoni Mtemvu kuibiwa na kuvunjwa shingo kiligusa hisia za wengi, huyu alisema hili, yule akasema lile.



    “,Hotelini alifata nini usiku, au mikataba mibovu ya madini wanaifanyia huko eee?? “,raia mmoja aliongea.



    “,Hapana! raisi huyu hana shida kabisa,anawajali wananchi na kupiga vita mauaji ya albino pamoja na ufisadi katika nchi yetu, tumwombe Mungu amjalie afya njema, japo hatujui kaibiwa nini?na walinzi walikuwa wapi? “,raia mwingine wa pili alizungumza.



    “,Kweli kabisa! raisi hana shida, lakini tuache serikali ifanye uchunguzi, lazima tutafahamu kila kitu ……”,raia wa tatu alizungumza, huku mchezo wa karata ukiwa umepamba moto,miongoni mwa kundi la wazee watano waliokaa kwenye kijiwe kupata kahawa,kabla ya kuelekea kwenye shughuli zao…



    …………………………………



    Ikulu;9;30am



         “,Jambo la kwanza,inspekta Amiry pamoja  na Junior wawekwe mahabusu,bila shaka wameshiriki kwa namna moja au nyingine!jambo la pili,hakikisheni mtuhumiwa,anakamatwa!fanyeni uchunguzi,aletwe kwangu akiwa hai au amekufa,diski iliyoibiwa ina siri zote za taifa,zikiwekwa wazi,usalama wa nchi yetu utakua matatani”,raisi Jonsoni Mtemvu alitoa amri kwa askari wapelelezi,askari wa serikali ya Goshani wakiongozwa na inspekta  Gupta.



    Askari watano walitoka nje ya chumba cha siri,katika ikulu ya raisi,mahali ambapo matibabu ya Jonsoni Mtemvu yalikuwa yakifanyika.Mheshimiwa Jonsoni Mtemvu hakua na amani ,hofu ya maovu yake kufichuliwa ilimtawala,mikataba yote ya biashara haramu alizojishughulisha nazo ,kuuza siraha,madawa ya kulevya,kuuza viungo vya albino,mikataba yote ya biashara hizi ilirekodiwa katika saa ya mheshimiwa Jonsoni Mtemvu kwa siri kubwa,wananchi walimwamini,hawakutambua chochote kile,aliwaza ,akawazua,kichwa kikamuuma!,alijilaumu kutokuwa makini siku iliyopita,hakujua aanzie wapi kumtafuta adui yake,yote aliwaachia askari wake……



    Green pick hotel; Masaa tisa nyuma ,



            Pikipiki aina ya baja ilifunga breki, Yuan Liang aliwasili katika hoteli aliyoweka kambi, akakusanya kilicho chake kutoka katika chumba namba kumi na tano, “muhudumu amelala?  ,funguo za chumba ataziona mezani akiamka “,Yuan Liang aliongea, akiwa na sura yake halisi ya kichina, aliweka funguo za chumba chake juu ya meza ya mapokezi, akatoweka!



    Begi lake lenye kila kitu chake alilipakiza kwenye pikipiki yake,akapiga stata pikipiki yake,ikagoma kuwaka!, akapiga tena, ikakubali, akavuta moto, akaachia, ikaacha vumbi eneo lote na kuwakera walinzi wa geti la hoteli kwa moshi mzito. Alinyosha barabara kuu kuelekea nje ya jiji la Costa, kaskazini mwa nchi ya Goshani. Alidhamiria kutoka nje ya jiji, kabla raisi hajapata fahamu na kuanza kumsaka muhusika aliyemuibia na kumjeruhi.



    …………………………………



    Huwei; masaa sita nyuma



            Pikipiki kubwa aina ya baja liliwasili mji mdogo wa Huwei, nje kidogo ya jiji la Costa,kaskazini mwa nchi ya Goshani, baada ya kumaliza masaa matatu njiani.



    “,Karibu! utapata vinywaji, chumba, na starehe za kila aina mahali hapa ……”,mzee wa makamo aliongea, umri wake yapata miaka hamsini,heleni zilikua nasikioni, shingoni alivalia cheni,chini alivalia jinsi, juu akavalia tisheti iliyoandikwa jordani na kuchorwa mpira wa kikapu, bila shaka mzee huyu alipenda ujana japokuwa alikula chumvi nyingi.



    “,Casabranka Casino “,kibao kilisomeka, huku taa katika kibao zikiwaka kufuatana na mdundo wa wimbo wa “sorry “ulioimbwa na mwanamuziki wa rnb Justin Bieber kutoka Amerika. Yuan Liang alipotosheka kusoma kibao, akaridhika na makazi yake mapya ya muda, kama kawaida yake siku zote, huhama kila wakati anapotekeleza tukio la wizi au mauaji.



    “,Nahitaji chumba cha ghorofani, lakini dirishani! “,Yuan Liang alimjibu muhudumu yule, huku akiisogeza pikipiki yake mahali salama pa kuhifadhia magari ya wateja. Siku zote alitumia vyumba vya dirishani, vyumba rahisi kutoroka anapovamiwa na polisi.



    “,Kimebaki kimoja, chumba namba therathini, kiko ghorofa ya tatu, maana ghorofa ya pili kuna ukumbi na klabu ya muziki! “,muhudumu yule alimjibu Yuan Liang,kichwa chake kikishangazwa na utofauti wa mchina huyu, alikuwa mswahili haswaa licha ya ngozi nyeupe na macho madogo aliyokuwa nayo.



    “,Ewala! hicho kitanifaa, sitasumbuka kutembea hatua nyingi kutafuta muziki, napenda sana kucheza disko! “,Yuan Liang aliongea kwa utani mwingi ndani yake,alipaki pikipiki yake, wakatembea mpaka mapokezi, akalipia, akakabidhiwa funguo, akaanza kupandisha kuelekea juu kwa kutumia lifti ya umeme.



    …………………………………



    Jiji la Gosta; 11;00am



           Makao makuu ya nchi ya Goshani, msongamano uliendelea kama kawaida, huyu alifanya hili, yule akafanya lile, kila mmoja alikuwa bize kutafuta ridhiki bila kumfatilia mtu mwingine, siunajua mjini bwana!



    “,Woouu! woou! woou! “,Kingo’ra cha polisi kilisikika, kamanda Gupta akiwa kama dereva,kamanda Yasini alikuwa ameketi pembeni yake,nyuma walikaa polisi wa kawaida watatu wenye silaha,walikamatilia mikononi bunduki aina ya smg.



    Difenda ilikimbia kwa kasi, magari mengine yalipisha pembeni, watembea kwa miguu walisogea mbali na barabara waliposikia sauti ya king’ora. Kamanda Gupta aliendelea kukanyaga mafuta kuwahi kabla mtuhumiwa hajatoweka.



    “,Watalaamu wa mawasiliano wa kujitegemea, watunza siri za muheshimiwa raisi, wanasema ujumbe wa mwisho, raisi akiwasiliana kuhusu mgeni wake halisi,ulitoka chumba namba kumi na tano katika hoteli ya Green pick, kwahiyo ndiyo tunaelekea huko, mkifika ni kuonesha vitambulisho na kuzama ndani, sawaa? “,kamanda Gupta alitoa maelekezo.



    “,Ndio afandee! “,askari wote wakiongozwa na kamanda Gupta waliitikia, safari ikaendelea.



    …………………………………



    Green pick hotel; 12;05pm



             Difenda ilifinya breki kwa fujo, vumbi likatimka, askari wakalukia nje wakiongozwa na kamanda Gupta, wakaonesha vitambulisho kwa walinzi getini, wakaingia ndani.



    Askari watatu wenye bunduki walibaki nje, kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini wakaingia ndani. ” ,Reception “(Mapokezi) “,maandishi yalisomeka, wakasogelea dirisha la chumba cha mapokezi.



    “,Sisi ni maafande wa jeshi la polisi kutoka makao makuu, “,Kamanda Gupta alizungumza, akatoa kitambulisho akaonyesha, kamanda Yasini na yeye akafuatia, akatoa kitambulisho akaonyesha.



    “,Karibuni sana, sijui tuwasaidie nini? “,muhudumu wa kike, akiwa amevaa shati nyeupe, tai nyekundu ya kipepeo shingoni, usoni alijirembea na kuvutia mteja yoyote yule, aliongea kwa tabasamu zuri kwa makachelo hawa wawili wa jeshi la polisi.



    “,Raisi alivamiwa jana usiku, akaibiwa katika hoteli ya Serena,tetesi zimeenea kila kona, nazani unatambua hilo,,kabla ya tukio alifanya mawasiliano na simu kutoka chumba namba kumi na tano katika hoteli yenu! “,kamanda Gupta alifafanua kwa kina.



    “,Jana usiku tuliamka na kukuta funguo za chumba mezani, ambazo ni hizi hapa, mteja tayali ameondoka, mnaweza kwenda kufanya uchunguzi! “,muhudumu aliongea.



    “,Itapendeza zaidi, lakini sijui mwenye chumba alikuwa anaitwa nani? “,kamanda Gupta aliuliza.



    Muhudumu akapekua karatasi, wiki mbili nyuma, siku ya jumanne, akaliona jina la mtu aliyechukua chumba hicho.”anaitwa Yweon Lee “,anatokea Japan, hata rafudhi yake inadhibitisha hilo, anaongea kiswahili cha kigeni ambacho hakijanyooshwa vizuri.”,muhudumu aliongea.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamanda Gupta akatikisa kichwa, wakaelekea juu ya ghorofa, baada ya dakika tano wakafika, wakakiona chumba, chumba cha mwisho, upande wa kushoto, karibu na dirisha. Wakafungua na kuingia ndani. Dakika kumi mbele, walikuwa wamepekua kila kona, hawakutambua chochote kile, wakafunga chumba, wakarudi mapokezi, wakakabidhi funguo na kutoweka.



    …………………………………



    Kituo kikuu cha polisi jijini Costa; 2;20pm



         “Poleni sana, lakini ndio majukumu yalivyo, mtusaidie ,na sisi pia tuwasaidie! “,Kamanda Gupta aliongea, aliketi kwenye kiiti, karatasi ya maswali ikiwa juu ya meza, mbele ya meza waliketi inspekta Junior pamoja na inspekta Amiry, baada ya kutolewa mahabusu kwa mahojiano. Mkono wa kulia wa kamanda Gupta, aliketi kamanda Yasini.



    “,swali la kwanza, mnaweza kutwambia ni nani aliyemvamia mheshimiwa raisi nyinyi kama walinzi wake siku hiyo?, “kamanda Gupta alihoji.



    “,Hatumfahamu muhusika, lakini tunamuhisi mwanamke mmoja wa kizungu aliyeitwa Elizabeth,alisema anatokea Uingereza na alikuwa mgeni wa raisi, kwakuwa awali raisi alitupatia maelekezo kukaa mita tano mgeni wake akifika tulifanya hivyo, kwakuwa alituonya tusiingie chumbani kwake mpaka asubuhi, tulifanya hivyo na kumgongea asubuhi, tulipo ona kimya, tuliingia ndani, tukakuta amezimia, muhusika alitoweka kupitia dirishani, tukatoa taarifa serikalini, huku sisi tukiwekwa mahabusu! “,kamanda Amiry alitoa maelezo mazuri kwa kina, huku kamanda Gupta akilinganisha majina aliyoambiwa, raisi alimtajia mgeni wake aliitwa Yuan Liang, hotelini aliambiwa muhusika wa chumba aliitwa Yweon Lee kutoka Japan, lakini katika hoteli ya Serena, anayehisiwa anaitwa Elizabeth kutoka Uingereza.



    “,Kimbembe hapo!, kazi hii ngumu kwelikweli! ,asante kwa ushirikiano wenu,msijali tutawasaidia,mtakua huru”,kamanda Gupta hakuona haja ya kuendelea kuhoji,kazi haikuwa rahisi kama alivyofikilia,aliwashukuru inspekta Amiry pamoja na inspekta Junior kwa muda mfupi wa mahojiano,wakanyanyuka,wakapigiana saluti za heshima,wengine wakarudishwa mahabusu,wengine wakatoka kuendelea na majukumu kumsaka muhusika.



    …………………………………



    Chumba cha siri, Ikulu; 05:00pm



            Shingo ilifungwa bandeji,kichwani aliegemea mto kunyoosha shingo yake, nesi alikua bize kutimiza majukumu yake, alimpatia dawa, akampatia na maji.



    “,Inatosha!, nitafanya mwenyewe, nipishe nizungumze na vijana wangu “,Jonsoni Mtemvu, raisi wa nchi ya Goshani aliongea, huku akipokea maji pamoja na dawa,akiwatazama kwa shauku ya kutaka kujua upelelezi ulipofikia kutoka kwa kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini, wakiwa wameketi sentimita chache, kutoka katika kitanda alicholazwa mheshimiwa raisi ,bwana Jonsoni Mtemvu.



    “,Sawa, haina shida mkuu! “,kwa sauti yenye nidhamu ya kazi, nesi aliyejulikana kwa jina la Upendo aliongea, akachukua makolokolo yake, akatoka nje.



    “,Bosi kazi ni ngumu! Green pick hoteli wanasema muhusika wa chumba cha simu iliyokupigia anaitwa Yweon Lee kutoka Japan,wewe unasema anaitwa Yuan Liang, kilichonifanya nichoke zaidi, Amiry na Junior tumewahoji wanasema mgeni wako wa Serena hoteli anaitwa Elizabeth kutoka Uingereza, ndiye wanamshuku maana alipotea ghafla baada ya tukio, nashindwa kuelewa mkuu! “,Gupta aliongea, huku kamanda Yasini akitikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maneno ya askari mwenzake.



    Raisi Jonsoni Mtemvu alichoka, nguvu zikamuishia, lakini akapiga moyo konde na kujikaza kisabuni. “,Sawa, inabidi niwaongezee nguvu, nitawasiliana na waziri mkuu Januari Sasamba, aombe msaada haraka sana wa wapelelezi wa kundi la “the super three soldiers” kutoka Tanzania, nina imani watawaongezea nguvu!, “raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.



    “,Ndio mkuu, itakuwa vema zaidi na kazi itakamilika kwa wakati! “,kamanda Yasini aliongea, akakubaliana na wazo raisi.



    “,Kweli kabisa, wakifika hata kesho hapa nchini, siku moja tu inatosha kurudisha nyaraka za nchi zilizoibiwa mikononi mwako! “,kamanda Gupta aliendelea kukazia.



    “,Sawa, nitafanya hivyo! “,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea,kamanda Gupta pamoja na Yasini wakapiga saluti kwa heshima, kisha wakatoweka kusikojulikana.



    Ikulu; Costa, Goshani



            Mama Zainath, mke wa mheshimiwa Jonsoni Mtemvu, raisi wa nchi ya Goshani alikosa furaha, alijuta kwa kitendo alichokifanya cha kumnyima unyumba mume wake na kumsababishia matatizo, alijuta, kila wakati alijilaumu, alijiona hajui kutunza mume.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Lazima nikamuombe msamaha, nampenda mume wangu, sio vema ahudumiwe na manesi wakati mimi nipo,hata kama alitaka kunisaliti nakosea, napaswa kusamehe na kusahau ili kuinusuru ndoa yangu ……”,mama Zainath alijishauri, akanyanyuka sebureni alipokua ameketi, sebure iliyojaa kila aina ya samani, samani zenye hadhi na heshima. Akaelekea kwenye chumba cha siri, chumba ambacho mume wake alifanyiwa matibabu.



    “,Karibu mke wangu, nafurahi kukuona, nisamehe kwa yote niliyotaka kukufanyia,naomba tusahau yaliyopita na tugange yajayo ……”,Jonsoni Mtemvu akiwa ameketi kitandani, alimuangalia mke wake upande upande, shingo lake lilipinda kuelekea kulia mwa jicho lake, kifuti alichopigwa na Yuan Liang alimanusura kivunje mfupa wa shingo lake. Aliongea kwa sauti ya upole yenye kujaa busara kama kawaida yake, sifa ambazo zilimwezesha kuficha maovu aliyoyafanya, alifanya biashara haramu ya viungo vya albino, kuuza silaha na madawa ya kulevya, yote hayo hakuna aliyefahamu zaidi yake na rafiki yake waziri Januari Sasamba.



    “,Nimekuelewa mume wangu, sitarudia tena, nakupenda baba Zainath …”,mama Zainath aliongea kwa huzuni,akadondosha chozi, Jonsoni Mtemvu akamfuta chozi lake kwa kutumia mikono yake, wote wakakumbatiana.



    …………………………………



    Huwei;Casabranka Casino



            Msichana mrembo wa kichina, asiyechosha kutazamwa alikuwa ameketi kwenye kitanda chake,chumba namba therathini katika hoteli ya Casabranka.



    “,Shit! Kumbe raisi Jonsoni Mtemvu ni mtu mubaya kiasi hiki, anaua albino, anauza silaha za serikali, isitoshe anauza madawa ya kulevya, kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye,mimi naua watu wenye hatia, watu wabaya kujipatia pesa, siui viumbe wasio na hatia kama albino, lazima Jonsoni Mtemvu alipie damu hizo ……”,Yuan Liang alikasirika, japo alikuwa muuaji lakini alikuwa na moyo wa huruma, siku zote aliua watu wabaya na kuwaibia pesa, ndiyo maana hata raisi hakumuua, alizani ni mtu mzuri kumbe mubaya.



    Alichomoa diski kwenye kompyuta,diski aliyoiba na  kuichomoa kutoka kwenye saa ya raisi,alimaliza kusikiliza sauti na maongezi mbalimbali yaliyorekodiwa, akaweka pembeni kompyuta yake, akabonyeza namba kadhaa, kisha akaweka simu sikioni.



    “,Unaongea na Doungso! ,diski yako iko mikononi mwangu, nahitaji bilioni kumi kesho jioni, saa tano kamili usiku, nitakuelekeza mahali pa kunikuta, ukipuuzia nafichua maovu yote kwa serikali na wananchi wako, utanyongwa, onyo! polisi yoyote yule asije akanifuatilia, nitawaua nyote ……!”,kama kawaida yake ya kudanganya majina, alimpigia raisi Jonsoni Mtemvu, akampatia maelekezo namna ya kuirudisha diski mikononi mwake, kisha akakata simu.



    “,Ole wake asifuate maelekezo, nitamuua, huyu sio mtu mzuri wa kumwacha hai “,Yuan Liang aliongea peke yake, akarudi kitandani, akaendelea na shughuli zake za kuchezea kompyuta yake.



     …………………………………



    Ikulu; Costa, Goshani.



            Simu yake ikiwa pembeni ya kitanda chake ilianza kuita, akaitazama kwa jicho lililojaa maswali, hakumfahamu aliyekuwa anapiga simu, namba ilikua mpya mbele ya macho yake. Akamtoa mke wake mwilini mwake,mama Zainath akaacha kumkumbatia, akamruhusu apokee simu, akasimama akaanza kutoka chumbani kumpatia uhuru mume wake, aliamini simu ilihusu maswala ya kiofisi na serikali kwa ujumla.



    “,Unasema??,we ni nani?, uko wapi?, haloo, haloo!, “,Jonsoni Mtemvu hakuamini alichokisikia, akauliza aweze kumjua zaidi aliyempigia, alichelewa sana,Yuan Liang alikuwa tayali amekata simu.



    “,Kuna nini mume wangu?,”,mama Zainath alikuwa hajafika mbali,alirudi haraka,alitaka kujua kitu ambacho kilimshtua mume wake baada ya kupokea simu.



    Jonsoni Mtemvu alishindwa amjibu nini mke wake,alitafakari, akaamua kudanganya,”,Nyaraka za serikali kuhusu mikataba ya madini imepotea, sijui serikali itanielewa vipi, nimesaini juzi tu! “,alidanganya, jasho jembamba lilimtoka usoni,mke wake akamfuta jasho kwa kanga yake, aliamini maneno ya mume wake, akamuondoa shaka, “Usjali mume wangu, nyaraka zitapatikana, kila kitu kitakua sawa, ngoja upone kwanza, “mama Zainath aliongea, huku fikra za mume wake zikiwaza mbali sana.



    “,Nimekuelewa mke wangu!,nakuomba uniache nipumzike!!,”Jonsoni Mtemvu alizungumza.



    “,Sawa mume wangu! “,mama Zainath akaongea, akambusu shavuni mume wake, kisha akatoka chumbani.



    …………………………………



    Tanzania;



         Askari watatu wa kundi la wapelelezi nchini Tanzania, “the super three soldiers ” walikubali kutoa msaada nchini Goshani, ili kumnasa mtuhumiwa aliyemuibia na kumjeruhi raisi wa nchi hiyo bwana Jonsoni Mtemvu.



    “,Msaada wenu ni muhimu kwa nchi yetu, mtuhumiwa kaiba diski yenye siri za nchi yetu, kunaswa kwake ni faida kwenu na kwetu, kwani mtaokoa usalama wa raia wetu kwa namna moja ama nyingine, karibuni sana Goshani, ni mimi waziri mkuu wa nchi ya Goshani, Januari Sasamba ……”,Kamanda Kendrick alisoma barua iliyotumwa kwa njia ya barua pepe (email), huku wenzake wawili wakimtazama na kumsikiliza kwa makini.



    “,Inabidi tukawasaidie, hiyo ni hatari sana, nchi yao iko hatarini! “,kamanda Philipo, kamanda namba mbili na mtaalamu wa kompyuta na mawasiliano aliongea..

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Lazima usiku huu wa leo tukanyage ardhi ya Goshani, misheni ifanyike masaa matano tu, kisha kesho jioni turejee Dar es Salaam ……”,kamanda Catherine aliongea,kamanda namba tatu, mtaalamu wa mawasiliano na tehama, taaluma moja na kamanda Philipo.



    “,Asanteni sana, nafurahi kuskia hivyo, tukutane saa tano kamili usiku, mahali hapa “ofisi ya ukombozi ” ,saa tano na nusu tutapanda chopa na kuelekea nchini Goshani. “,kamanda Kendrick aliongea, wote wakanyanyuka, wakapigiana saluti, kila mmoja akaelekea alikokujua yeye.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog