Search This Blog

Thursday 27 October 2022

AFANDE ANAHUSIKA - 5

 







    Simulizi : Afande Anahusika

    Sehemu Ya Tano (5)







    Jitu akahoji vipi? Inspekta badala ya kumjibu swali lake, akamwambia

    “Jitu, umeisha kula mchana?” akiwa na mshangao akajibu

    “Mkuu, umesahau kuwa tumekutana hapa tangu saa mbili asubuhi na hatujaachana? Mimi hata chai bado sijanywa,”

    “Oh! Nilisahau, ujue nini? Tunaweza hata kufa kwa njaa, hebu twende kwanza nje tukatafute chakula, unaweza kujikuta umeanguka ghafla, dah! Hizi kazi hizi ni za kuzeeka kabla ya wakati,” alijibu huku akimpa karatasi kadhaa ambazo zilikuwa na majibu ya alama za vidole.

    “Watu wanakuwahisha hospitali kwa kujua kwamba huenda ikawa unaumwa, kumbe tatizo ni njaa,” wakacheka huku Jitu akiperuzi peruzi zile karatasi na kushuka ngazi taratibu.

    Wakatoka hadi kwenye kantini ya Jeshi la Polisi na kuagiza chakula, walikula kimya kimya tena kwa haraka kutokana na njaa kali ambayo ilikuwa imewanyemelea kwa kasi na walipomaliza kula tu wakatoka kurejea ofisini.

    Hapo ndio nafasi yao nyingine kwa wao kujadili juu ya ripoti toka uchunguzi wa awali, walipoifunua karatasi ile, walichoka kabisa maana ilionekana kwenye usukani kuna alama za mtu ambae kwao ni ngeni kabisa, ila kwenye upande mmoja wa gari, upande wa dereva, waliona alama ambazo hazikusomeka, maana zilifichwa na Gloves.

    Unaona kwamba muuaji anajua ni kipi anachofanya, kuna wakati unakuwa unahisi kabisa kuwa siku chache mbele kutokana na makosa yake madogo madogo afanyayo, tutamtia nguvuni, lakini anayafuta kabla ya kumtia nguvuni,” Inspekta Kalindimya aliweka wazi hisia zake.

    Hadi muda wa kazi unaisha, hakuna walicho ambulia zaidi ya kupiga soga tu na ilipofika saa 11 kamili jioni wakatoka wakiamini wanaenda kupumzisha akili kwani walikuwa wamechoka mno.

    **********

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku ulikuwa ni mrefu mno kwa Inspekta Kalindimya hasa akikumbuka tishio la mauaji toka kwa mtu huyo ambae alimtaka kuachana na kesi ile haraka iwezekanavyo.

    Akajiuliza ni kwanini muuaji amwambie hivyo? Ina maana kuwa yeye amefikia hatua ya mbali sana kuliko wengine ambao wamechunguza hizo anazo ziita ni kesi zake? Akakosa jibu na kunyanyuka kwenda kwenye meza yake ya kazi.

    Kwenye meza hiyo pindi anapokaa basi huwa yupo busy tu na kazi, wakati mwingine hata husahau kula na hata usingizi huwa unampitia akiwa ameketi hapo, suala la msingi kwake ni chai tu…

    Sasa ndio akaenda hapo kuketi kwa mara nyingine, ikiwa ni saa saba usiku akatoa zile namba na kuanza kuzifanyia kazi. Safari hii alibadili njia ya kuziangalia, akachukua zile namba na zigawa kwenye herufi.

    Alianza kwa kuzipa namba kwanza, hivyo ndivyo akili yake ilivyo mtuma, akaanza na A akiipa moja B ikiwa ni mbili hadi alipofika Z ambayo ilikuwa ni namba 30.

    Bado hakupata matunda yoyote yale, maana kuna namba zingine zilijichanganya, akaona hapo bado amefeli, akaacha na kunyanyuka, akili yake ikamtuma kwenda Mwana Nyamala kisiwani, sehemu ambayo ilionekana gari ya MwanaMtama.

    Akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake, huko akafungua draw ya kabati yake ya kitandani na kuchukua kitu Fulani ambacho alikuwa akikihitaji muda ule, kisha akatoka na kufunga mlango wake vizuri, maana wale askari wa ulinzi aliokuwa amepewa awali tayari waliisha amriwa warejee kituoni kwao na waendelee na amjukumu mengine haraka.

    Alipohakikisha kuwa amefunga vizuri mlango wa nyumba yake, akaelekea hadi garini kwake na kuingia kuelekea huko alipo panga kwenda usiku huo.

    Kwa mwendo wa taratibu tu akatoka na kuelekea Mwananyamala akiwa peke yake njiani, barabara ilikuwa imetulia sana, aliwasili ile sehemu ambayo alisoma kama ni sehemu ambayo gari lilitelekezwa.

    Akashuka akiwa makini, maana ilikuwa ni sehemu ya hatari ikionesha dhahiri kuwa na vibaka na hata mateja pia, hivyo kwa tahadhari kubwa akateremka na kusimama nje ya gari lake.

    Kwa mbali aliweza kuona kundi la vijana ambao moja kwa moja akajua hao ni wezi tu wametoka kuiba na sasa wanagawana aidha wanaficha. Akaondoka kwa tahadhari akiwa na silaha yake mkononi akisogea kule walipo huku akijificha kwenye vichaka vilivyokuwepo pale.

    Aliweza kuwasogelea na kuwakaribia kabisa, kisha akawaweka chini ya Ulinzi, walikuwa ni vijana watatu tu kumbe, tofauti na alivyo kuwa akiona kwa mbali kuwa ni wengi sana.

    Akiwa amewaelekezea bastola yake aina ya Revolver 09/80 yenye uwezo wa kubeba risasi 12 kwa wakati mmoja, vijana wakatulia, hasa kutokana na mkwara aliokuwa akiwapiga.

    “Tulieni hivyohivyo, ujanja wowote au kujidai kujua kutasababisha kupoteza maisha ya Yule ambae atajidai kujua,” akawa anatoa simu na kupiga kituoni kuomba msaada wa gari la Polisi.

    Alipomaliza tu akawaambia walale chini vile vile walivyo, wawili wakalala bila hata vurugu, ila mmoja wao akajidai yeye ni mjuzi sana, akawa kama anataka kulala vile, akamrukia Inspekta ili kumpora bastola yake.

    Kumbe tangu anajiandaa kufanya shambulizi tayari mwenzie amemuona na amejitayarishaili aweze kumdhibiti, kijana akajirusha mzima mzima pale alipo Inspekta…





    Kile kitendo cha yeye kujirusha tu akakutana na teke kali mno la tumbo na alipotua chini tu akamzima na mguu sehemu za kiuno.

    Ilitosha kabisa kumnyamazisha na kumkata ngebe zake, maana alitoa ukelele wa ajabu wa kuugulia maumivu huku akilia anakufa. Bastola yake Inspekta bado ilikuwa imewaelekea wale vijana waliokuwa pale chini.

    Akawaamuru wenye we wajifunge mashati yao, walikuwa ni dhaifu, tayari dawa za kulevya zilikuwa zime waathiri kwa kiasi kikubwa mno hawa wawili, ila Yule aliempiga, kidogo ndio alionekana kuwa na afadhali.

    Walijifunga hayo ma Tshirt waliyokuwa wamevaa huku Yule mwingine akiwa analalamika kuwaa ameumia, na baada ya muda sio mrefu sana, gari ya Polisi aliyokuwa ameiomba ikafika, haikuwa mbali sana, akawakabidhi watu wale.

    “Hawa wasitolewe na yeyote bila kuwasiliana name hiyo kesho asubuhi, mkuu akiuliza mwambieni kuwa ni nyeti, nitamtafuta mimi, sawa kuruti?” alimuuliza mmoja wa askari ambae alijibu sawa mkuu.

    Wakawaingiza kwenye Pick Up ile ya Polisi na kuanza kuondoka huku Inspekta nae akiingia garini mwake tayari kurejea kwake.

    Lakini akiwa anakaribia maeneo ya Mwana nyamala A, akakumbuka kitu, akakata kona ya ghafla na kuelekea kilipo kibanda cha simu, akashuka na kuchkua Camera maalum aiyopewa na mmoja wa wataalamu wa IT kutoka ofisini kwake.

    Hiyo alipopewa ndio akaja kuiweka nyumbani kwanza akisubiri muda kama huu ufike ili aweze kufanya hilo ambalo analifanya sasa. Aliposhuka na kwanza akakagua kama kuna mtu yeyote ambae anaweza kuwa anamtazama.

    Aliporidhika tu akaingia haraka, akaifungua simu iliokuwa mbela yake pale, alikuwa ameelekezwa kuwa afungue pale na kuifunga ndani ya Cover bila kujali kama itaonekena ama lah!

    Nae akafanya kama alivyoa amriwa kisha akategesha ware aliopewa sambamba na Camera ile na baada ya kumaliza kazi yake akaondoka ikiwa ni saa 10 ya alfajiri na kuelekea hospitali.

    Pale hakusumbuka kabisa, ilimchukua dakika chache zaidi na alipomaliza tu akaondoka na kwenda kumalizia ile ya mwisho iliopo maeneo ya Studio kisha akaelekea nyumbani kwake moja kwa moja.

    Nyumbani kwake, saa 11 alfajiri akiwa bado yupo nje hata hajaingia ndani, akahisi kuna mabadiliko, wakati akitoka alikuwa amezima taa, lakini sasa amerudi na kukuta taa zinawaka na hali hakuiacha katika hali hiyo.

    Kengele ikalia kichwani mwake, kwa tahadhari kubwa mno akateremka garini na hata kabla hajaufunga mlango wa gari, taa za nyumba nzima zikazimika kwa ghafla na kumfanya atetemeke na kujitupa chini ya gari na bastola yake mkononi.

    Taratibu akaanza kujivuta chini kwenye majani madogo madogo maarufu kwa jina la Ukoka huku akijielekeza nyuma ya nyumba yake ambapo alitegemea kuweza kujua ni nini kinaendelea.

    Kutokana na kuielewa vizuri nyumba yake, aliweza kuizunguka nyumba nzima na lakini hakuona tatizo lolote kwa nje, sasa akalazimika kujua kwa ndani napo kupo kwenye hali gani.

    Ndio sasa akaanza kuchungulia madirishani, aliporidhia ni salama, akaelekea mlango mkubwa wa mbele na kugusa kitasa cha mlango, ajabu akakuta upo wazi na hali aliufunga.

    Akarudi nyuma hatua kadhaa na kuingia kwa kasi huku akibiringita silaha mkononi. Ndani hakukuwa na mtu yeyote, bali juu ya Computer yake akakuta kisu chenye mpini wa rangi ya Pinki kikiwa na ujumbe mdogo kwenye karatasi.

    Ncha ya kisu ilikuwa imechoma karatasi kwenye ‘key board’ akawasha taa na kuikagua nyumba yake nzima kwa ndani, bahati mzuri kila sehemu mle ndani ilikuwa salama.

    Mwisho akarejea sitting room na kuelekea moja kwa moja hadi pale kilipo kisu na kukichomoa kwenye keyboard, akaichukua ile karatasi na kuanza kuusoma ujumbe ulio andikwa.

    Ujumbe ulikuwa sio mrefu sana na ulisomeka

    ‘Imebaki siku moja tu kwa ajili ya usalama wa MwanaJuma, ambae sina nia ya kumuua, ila ikinibidi nitafanya hivyo ikiwa tu nae hatokukufukuzisha kazi, kwani lengo langu ni wewe kuachana name, kwa hiari kabla ya kulazimishwa kurudi mitaani kuzurura,’ ilimaliza hiyo barua bila kuweka kingine chochote cha ziada.

    Roho ikapiga mshindo, Pah! Huyu MwanaJuma ni nani? Na ni kivipi anaweza kunifukuzisha kazi? Ina maana huyo mtuhumiwa ananijua sana mimi ama? Maswali yalikuwa ni mengi mnoakakoa majibu na kushusha pumzi kwa nguvu huku akiketi kwenye kiti kivivu.

    Alitamani iwe ni muda wa kazi ili atoke tu kwenda kazini kufanya mahojiano na wale vijana aliowakamata asubuhi ile, lakini muda ule wa saa 12 ilikuwa niu mapema sana kwa yeye kwenda kazini.

    Hivyo alicho amua kuwa ni heri tu aende akaoge na kujiandaa kwenda zake kazini. Akiwa ameshika tu mikono ya kochi lake, simu ikaita, ilikuwa ni simu yake ya mezani, ambayo ni nadra sana kuita.

    Akashtuka sana kwa wito ule, aliiangalia kama ndio mara ya kwanza kuiona, akaendelea kuitazama ahadi aliposhtuka kuwa ile ni simu imepigwa na inahitajika kupokelewa. Akaichukua na kuiweka sikioni.





    “Inspekta, pole sana kwa kuhangaika usiku huu, napiga simu kutoka hapa A kwenye kile kibanda ulichotegesha Camera, umesahau kuwa mimi nipo kama upepo, kila sehemu wewe ulipo, tambua sasa kwamba mimindio nasaidia wewe kufika hapo, nakushauri njoo uziondoe zote tatu, maana hakuna msaada kwako kwa kupitia hizo,” halafu akacheka, Inspekta Kalindimya akamuuliza kwa taratibu tu

    “Umemaliza?”

    “Bado sana, ila cha mwisho ni kuwa leo ndio siku yako ya mwisho ya kuamua kuacha kazi kwa hiari yako, chagua tu moja…” akakata simu bila kumwambia achague nini.

    Alijaribu kuita Hallow... Hallow… Lakini bado wala haikupokelewa, kwani tayari ilikuwa imeisha katika.

    Japo kulikuwa na hali ya ubaridi, lakini jasho jembamba lilimtoka, akawa ni kama mtu ambae hajielewi elewi, akampigia simu Jitu na kumtaka ampitie wakati akitoka kuelekea kazini.

    **********

    Saa moja asubuhi Jitu aliwasili nyumbani kwa Inspekta na kumkuta akiwa ameketi amatazama taarifa ya habari kupitia Televisheni ya Taifa. Hakuwa na jambo la muhimu sana kutazama bali alikuwa akivuta muda tu wa kumsubiri Jitu.

    Hivyo alivyofika tu Jitu na ratiba ya kuangalia TV ikawa imekufa rasmi na sasa alimkarimu na kumuonesha sehemu ya kukaa huku nae akijitengeneza vizuri. Akamuuliza kuhusu familia yake huko nyumbani alipotoka nae akamjibu ni njema tu.

    Sasa ndio akamueleza sababu ya kumuambia apite pale. Jitu alishangaa sana na kumuuliza kuwa wakati anatoka pale kuelekea kwenye hizo Call boxes alimueleza nani? Inspekta akamwambia kwamba hakumueleza yeyote hasa ukizingatia ilikuwa ni usiku mnene.

    "Isingewezekana kabisa kumwambia yeyote, maana usiku ulikuwa ni mkubwa san," alisisitiza zaidi Inspekta Kalindimya.

    Sawa Boss, hapo nami sasa nimehakikisha kuwa kila hatua yako unayofanya hao watu wanaifuatilia, na nina hakika wamefanya hivyo ili tu kukujulisha kwamba kila hatua yako unayopiga,"

    "Of Coz, hiyo ni kweli! kama wangekuwa wananifuatilia ili wanidhuru nafikiri wangefanya hivyo maana inaonesha kabisa kwamba walikuwa na uwezo huo," Inspekta alikubaliana na kauli ya Jitu ambae alikandamiza kwa swali

    "Sawa, tunafanyeje sasa?" huku akiegamia sofa akamtazama boss wake.

    "Jitu hiyo ndio sababu upo hapa, nimekuita ili tujipanfe tunafanya nini hata kabla hatujafika ofisini," alieleza kiurefu.

    "Lakini si umesema kuwa kuna watu umewakamata mkuu?" aliuliza Jitu na Inspekta akakiri kuwa ni kweli na muda ule wapo kituoni.

    "Sasa ndio twende kwa hao watu ili tukawahoji huenda tukajua ni kipi kinaweza kutusukuma mbele,"

    "Wazo zuri sana Jitu, ngoja nifunge milango twende hukohuko," akasimam na kwenda kufunga milango yote ya ndani kisha alipofika pale Sitting room akamkuta na Jitu ameisha simama nazima TV kisha wakatoka kwa pamoja na kisha Inspekta akafunga na huo mlango mkubwa na kutoka sambamba na Jitu.

    Walienda kazini kwa kutumia gari ya Jitu na garini walikuwa kimya wakitafakari hayo yanayotokea. Kila mmoja alikuwa na mawazo yake. Hakuna lililokuwa likimuumiza kichwakaa suala la huyo MwanaJuma ni nani ambae amekuwa akitumika kama nguzo.

    Hakuna kati yao hata mmoja aliekuwa akimjua huyo MwanaJuma, hawakuongea hadi walipowasili kituoni na bado walikuwa kimya wakielekea ofisini kwao. waliwasili ndani na kuketi kamawatu walio ambiana.

    Inspekta akanyanyua simu na kutoa maagizo ya kupelekwa kwake mara moja wale watuhumiwa aliowakamata usiku uliopita. baada ya kukata simu ile dakika mbili tu mbele wakaletwa vijana watatu wakiwa wameongozana.

    Jambo la kwanza alilolifanya ni kuomba na faili lao ambalo alilisoma na kumtupia Jitu nae akaliperuzi kwa sekunde chache na kulifunika. Inspekta akaanza kuwahoji na mwanzo walionesha kugoma kutoa ushirikiano wa kutosha lakini baada ya vitisho waliweza kufunguka.

    Walisema pale wao ni wafanyakazi tu na mida ile ndio hupata muda wa kufanya kazi zao na ndio kama vile walichomoka na kwenda kujitafutia chochote na waliporudi na chochote yeye sasa ndio akawakamata.

    Jitu akataka kujua bosi wao ni nani? wakakataa katakata kutaja na hapo Jitu akapandwa na jazba, akachukua Office pin moja Sisi tumezoea kuita Sindano urungu na kumsogelea mmoja akamuuliza atamtaja bosi wao wa kazi ama lah! Yule teja akakataa kuwa hamtaji, Jitu akasema yeye hupenda sana kukutana na watu wabishi kama huyo. akamwambia aweke mkono mmoja kwenye meza teja akaweka na ule mwingine Jitu akaukanyaga kwa mguu wake palepale kwenye kiti alichokaa na kkushika ule mkono ulioko mezani kwa mikono miwili, kisha akasema...





    “Hivi ndio tunaanza, na ikizidi kunisumbua name nitaongeza adhabu,” akaichukua ile sindano na kuanza kuiingiza chini ya kucha, teja alipiga kelele za ajabu mno, Jitu akaendelea kuisukuma taratibu huku akimtazama usoni.

    Inspekta akamshika Jitu beaga na kumwambia asubiri sasa atasema, nae Jitu akamuuliza kama yupo tayari kusema, Teja akajibu kwa pupa kuwa atasema huku chozi likimtoka.

    “Haya sasa hebu tuambie, ni nani bosi wenu?” Inspekta ndie alieuliza swali.

    “Afande mkuu wetu anaitwa Jembe,”

    “Anaishi wapi Jembe?”

    “Sinza,”

    “Sinza ile ni kubwa sana, yeye anaishi Sinza sehemu gani?”

    “Afande hatujui wote anapoishi, kwanza tu huwa hapendi kuulizwa ulizwa maswali, akihisi tu unamchimba anaweza hata kukupoteza,” sasa walielewa kuwa anasema kweli, hapo ndio Jitu akamuachia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kumbe kiustaarabu hauendi wewe hadi kiuwenda wazimu ndio unatoa ushirikiano, pumbavu wewe,” Jitu akasonya baada ya kusema maneno hayo.

    “Tofauti na hii kazi Jembe anafanya kazi gani?”

    “Kiukweli afande mimi Sijui, yaani hapo nilivyoeleza mimi ndio nimejua hadi hapo,”

    “We usilete nyodo kwenye maswali ya msingi, sasa nitakubadilishia adhabu na kukupa kubwa zaidi, tueleze kazi nyingine anayofanya ama aliyowahi kuifanya hapo kabla,” Jitu aliingilia kati.

    “Kweli afande, mimi nimemjua Jitu wakati ametoroka gerezani na akafika maghetto pale kuomba hifadhi ndio hadi leo japo baadae alianza kazi za binafsi na ndio zikamtoa hadi sasa yeye ndio amekuwa mkuu wa kundi zima,”

    “Kazi gani binafsi anafanya?”

    “Anasafiri sana kwenda huko na kule kucheza madeal,”

    “Wewe umewahi kucheza nae deal lolote hivi karibuni?”

    “Hapana afande mimi sijawahi,”

    “Wewe hebu sema kweli, nitamuamuru Jitu akushughulikie sasa hivi,” alisema Inspekta Kalindimya na Teja alipomtazama Jitu akamkuta kakunja ndita kwenye sura yake, akarudisha macho yake kwa Inspekta na kumwambia yeye huwa anaachwa kwenye deal kwani ni dhaifu huwa wanakwenda na Dega.

    “Dega ndio nani?” Jitu alihoji.

    “Ni Yule alietaka kupigana nawe,” hapo akajibu huku akimtazama Inspekta japo swali aliulizwa na Jitu.

    Inspekta akageuka nyuma na kumuonesha Jitu huyo Dega, Jitu akapiga hatua kadhaa kuelekea kule alipo na kurudi nae baada ya kumfuata. Alipomfikisha tu mbele ya Inspekta, akawa mpole.

    “Dega, nataka ujibu maswali yangu kama nitakavyo kuliza, ole wako unizungushe ama ukwepe kujibu vile nitakavyo mie, nitakutonesha maksudi,” Inspekta alimwambia hivyo.

    “Afande naomba mnipeleke hospitali, mkono unaniuma sana,” alisema kwa majonzi huku akijikunja kunja kwa maumivu, Inspekta akamwambia kuwa amefanya vile maksudi ili atakapofika yeye kwa ajili ya mahojiano, basi asimsumbue

    “Yaani ukinisumbua tu ujue nagusa mkono tu huo mie, sawa?”

    “Nitakuambia ukweli mtupu, ila nakusihi nipeleke hospitali afande, naumia mno,” machozi yalikuwa wamemtoka mpaka basi, mkono nao ulikuwa umevimba, lakini hakupelekwa hospitali kwa amri ya Inspekta.

    “Sawa, nitakupeleka, tena ni mimi mwenyewe, kwanza niambie Jembe ni nani na yupo wapi?”

    “Jembe ndio mkuu wetu wa kazi anaishi Sinza, ila hakuna anaepajua ni wapi, mimi nimekujibu, Afande nipeleke hospitali,” aliendelea kuomba.

    “Bado hujanijibu, yupo wapi mkuu wenu?”

    “Sijui alipo kwa sasa!”

    “Kwa mara ya mwisho ulicheza nae deal lini na wapi?”

    “Juzi alikuja anaendesha gari Fulani hivi akanipa nijifunzie ndio nikaendesha endesha hadi ilipoishiwa mafuta nikaiacha pale kijiweni, nikafuata mafuta, kumbe ilikuwa imeibwa,”

    “Ulikuwa umelewa eti?”

    “Ndio afande!” alijibu kiufupi huku akigugumia kwa maumivu.

    “Nilijua tu katika mazingira ya kawaida utaendeshaje gari uliyoletewa na mwizi na kujiendeshea tu wakati hujawahi kumuona hata siku moja? Sasa ndio nieleze, hiyo gari ni ipi na alimuibia nani?”

    “Inspekta mimi Sijui ni wapi na ni nani alimuibia, aliniletea tu, nisaidie afande, mimi Sijui tena zaidid ya hapo,” alijitetea Dega.

    “Wewe ulikutana na DEga wapi hadi mkaunda hilo kundi?”

    “Tulikutana nae gerezani, mi wakati naingia yeye anatoka kisha akarudishwa tena na kunikuta, mimi nikatoka na kumuacha kisha tukaja kukutana miaka mitatu iliopita akiwa yupo tu mtaani ndio nikamkaribisha maskani,”

    “Alifungwa gereza gani?”

    “Ilikuwa Keko wakati tulipokutana mimi nae kwa mara ya kwanza,”

    “Mwaka gani huo ilikuwa?” Jitu ndie alihoji hapo.

    “Miaka mitatu iliopita afande,”

    “Alikuwa akitumia jina gani?”

    “Dah! Hata silikumbuki kwa sababu hata kule alikuwa akitumia jina hili hili la Dega, kwa hiyo jina lake lilikuwa likitajwa hakuna alie shughulishwa nalo,”

    “Namba gani ulitumia ukiwa huko?”

    Mimi nilikuwa nikitumia namba 427010” Walimuelewa na kisha wao wenyewe wakajadiliana, wakaamua sasa atolewe na kupelekwa hospitali, kwani msaada huo alioutoa umekuwa ni mkubwa sana kwao.

    Wakamuita askari mmoja wa zamu na kumpa maelekezo, kisha nao wakaamua waende magereza ya Keko kwa ajili ya uchunguzi wa mtu huyo na kwa hatua zaidi.

    “Inspekta unafikiri huko tunaweza kupata fununu juu ya mtu huyu muuaji kweli?” Jitu aliuliza akiwa ndie ameketi nyuma ya usukani.

    “Amini usiamini huyu mtu bila risasi wala ngumi, tunamtia nguvuni, hana siku mbili mbele,”









    Jitu akatikisa kichwa tu kukubali, Inspekta akachukua file alilokuwa nalo mkononi na kuanzaa kulifunua funua huku akiendelea kuzungumza na Jitu.

    “Jitu amini usiamini, tunamtia nguvuni huyu muuaji ndani ya siku mbili kwa sababu ana tatizo la kukurupuka, japo anatuumiza sana vichwa lakini elewa fika kuwa hana maisha tena ya kuwa uraiani,”

    “Labda pia name nikukumbushe tu mkuu, unakumbuka ahadi yake ya leo?”

    ‘Ile ya huyo MwanaJuma Sijui MwanaEid?”

    “Ndio hiyohiyo,”

    “Mfamaji tu Yule hana lolote, angekuwa mtendaji kwa hilo si angefanya? Maana jioni haipo mbali.” Inspekta alikuwa akijiamini kupita kiasi, hadi Jitu mwenyewe akawa anashangaa.

    ‘Hivi huyu jamaa anategemea nini hadi kujiamini kiasi hicho? Ama ndio anatuhadaa? Mbona mimi simuelewi elewi?’ alijiwazia mwenyewe na wakati huo tayari walikuwa wamewasili mbele ya geti la kuingia ndani ya Fensi ya Magereza.

    Walitoa vitambulisho vyao na kuruhusiwa kuingia ndani ambapo walielekezwa hadi lilipo jengo la ofisi ya Bwana Gereza ambapo wakanyoosha hadi huko na kushuka ili kukutana nae.

    Aliwakaribisha na kuwapa siti za kukaa kisha wakajitambulisha baada ya salamu, Inspekta alielezea sababu ya wao kuwepo pale.

    "Hakika mkuu hapo ndio tulipokwama na tuna kila sababu ya kumtafuta mtu huyu na kumkamata kwa ajili ya usalama wa raia wetu, na sasa naona kama jukumu la kumjua muuaji ni letukwa kushirikiana nawe, sijui unatusaidiaje hapo?" alisema kama vile ni mtu anaejivua yeye na kumkabidhi jukumu mkuu wa gereza.

    Nae alionekana kamakufikiri kwa sekunde kadhaa kisha akawa kama amekurupuka hivi na kuuliza

    "Umesema namba yake yeye huijui wala jina alilotumia gerezani?" wakajibu wote kwa pamoja kwamba hawajui. lakini wakamtajia jina la utani tu alilokuwa akitumia. Mkuu wa gereza akaomba namba hiyo ya mtu waliemtia nguvuni.

    Jitu akavuta faili uliyokuwa mbele yake na kufunua ukurasa wa mtuhumiwa huyo na kumsogezea Mkuu wa gereza. hata kabla hajasoma jina la Mtuhumiwa, akasema mtuhumiwa huyo atakuwa alikuja pale kwa kesi ya utumiaji wa silaha za moto.

    "Hapa naona namba ya gereza letu hili, namba ya selo aliyokuwa amepangiwa na namba yake ya utambulisho kama mfungwa, kisha ndio akamtafuta jina. Baada ya kulisoma jina la huyo mfungwa akamtambua.

    "Sasa nashauri cha kufanya muende kwa huyo mliemkamata mlazimishe amtaje kwa namba ili tuweze kumtambua, na hapa kabla hamjaondoka nitawaonesha ni vipi mtamtambua huyo mtu ni nani na alikuwa gereza gani!" kisha akanyanyuka na kwenda pale walipokaa maofisa wale wapolisi.

    Pale alipofunua ilikuwa ni kwenye ile page ya mtuhumiwa walienae kituoni ambae namba.yake ilisomeka kama 427010 akaanza kuwafafanulia, akasema

    "Daima husomwa kwa namba mbili mbili kwa kuanzia mwanzo kwenda mwisho. Namba mbili za kwanza ni za gereza, yaani hiyo 42 ndio gereza leetu kama nilivyokuambia awali, namba hii huyolewa mahakamani kwani ni wao ndio hupanga gereza la mtu kufungwa, nafikiri tupo pamoja?" aliwauliza akiwatazama na wakatikisa kichwa tu kumkubalia, akaendelea

    "Namba ya kati hutolewa na gereza,kwani gereza ndio hupanga ni nani atafikia kwenye selo ipi pindi anapoletwa hapa, hivyo hiyo inayofuatia ni 70 hii ni namba ya Cell ambayo alikuwa akiishi humu ndani na kwa mujibu wa namba hiyo alikuwa yupo kusini magharibi, cijui mnanielewa?" alikuwa akifafanua kwa uhodari kabisa.

    wakamuitikia kuwa wanamuelewa vizuri sana aendelee tu.

    "Hiyo ya mwisho ni namba ya mfungwa mwenyewe, ambayo hutolewa na Nyapara na kusajiliwa kama namba rasmi ya mfungwa." alimaliza kutoa ufafanuzi ambao waliona kama haujawasaidia lolote. Jitu akauliza kaa anaweza kumfahu dega ama lah wafungwa waliokuwepo miaka mitatu iliopita.

    Mkuu alishikilia palepale kuwa ni vigumu sana kwa jambo hilo. basi kwa shingo upande tu wakaaga huku wakiwa wanasimama na kumpa mikono yao na kutoka akiwa amewashindikiza. Inspekta akamueleza kuwa atahitaji namba yake ya siku na hasa ya mkononi ili ikitokea juwa kuna chochote ambacho watahitaji msaada, basi wawasiliane.

    Upande wa pili huku Jitu alikuqa akiona kama wamepoteza muda tu bure. Aliamini muda huo wangeweza tu kufanya mambo mengine na hata kwenye upelelezi wa ndani kwa ndani wangeweza kung'amua kitu tofauti na hiyo ya kwenda huko.

    Wakiwa wamechoka kabisa na muda wao, wakaelekea garini na Jitu kama kawaida akaingia upande wa usukani huku Inspekta Kalindimya akiingia kwa dereva na kuanza safari ya kurejea ofisini kwao.

    Ndani ya gari Inspekta aliendelea tu kupekuwa pekua faili ile. Lakini katika upekuzi wake akakumbuka kittu. harakaharaka kama vile ameamriwa afanye upesi, akarejea mwanzo kabisa na kuifunua namba ile ya mauaji ya mwanaHamisi.

    Namba ile ilisomeka 426474 nae akajaribu kuiweka kwenye makundi matatu vilevile kama alivyofanya Mkuu wa Gereza, akaguna na kumshika mkono mmoja Jitu aliekuwa makini akitazama mbele, akageuka na kumtazama, Inspekta nae akamtazama na kumwambia warudi gerezani Keko.





    "Jitu faster turudi keko, muuaji tumemjua, haraka tumuwahi Mkuu kabla hajatoka," Jitu kwa kasi aliyokuwa nayo aliipunguza kidogo na kulala na gari na kurejea kulekule alipotokea.

    Kabla hata hawajafika Inspekta akakumbuka kuwa alichukua namba ya simu ya Mkuu wa gereza, akampigia simu na kumuuliza kama yupo. badala ya kujibu kwanza nae akahoji kuna nini? Inspekta akamwambia kuna dharula hivyo wapo njiani wanarejea.

    Akawaambia wajitahidi wawahi jwani anapaswa kutoka muda ule kuelekea kwenye shughuli zingine za kitaifa. Wakamjibu dakika tano tu watakuwa pale.

    Kauli ya Inspekta aliisikia Jitu, akageuza kasi.

    Safari yao iliishia getini, hawakuongea garini hadi wanafika kwenye geti la kuingia ndani ya gereza ndio Inspekta akanyanyua mdomo na kusema mwisho wake huyo muuaji umewadia.

    Jitu akashusha pumzi kwa nguvu na kumuuliza boss wake kuwa ni kwanini amesema hivyo.

    Inspekta akamwambia anmuhakikishia kwa wakitoka mle ndani tayari watakuwa na jina la muuaji na kama watatulia ofisini hadi kufikia kesho kitakuwa kimeeleweka.

    “Amini usiamini huyu muuaji wa hawa watu ni mtu ambae anakesi hapo kwetu na nina hakika kabisa tukilijua jina lake tu nae amekwisha ndio maana nakueleza hivyo,” aliongea kirefu na maneno yake kiasi yalimuingia Jitu kichwani.

    Tayari walikuwa kwenye mlango wa mkuu wa magereza, akawakaribisha Secretary wake ambae tayari alipewa habari ya kurudi kwao na kuwaruhusu waingie.

    “Tena mna bahati sana, maana mkuu alikuwa na safari, hivyo jitahidini tu muwahi,” aliongezea huku akiwaonesha mlango ambao nao tayari wanaujua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ahsante,” alijibu Jitu wakiwa na haraka ya kuingia humo ndani.

    Walimkuta akiwa ameketi kama vile anawasubiri wao tu ili atoke, maana alikuwa amekaa kama amesimama vile, haraka haraka akawauliza shida kwani alikuwa na haraka.

    Inspekta akamwambia kuwa amepata namba Fulani kutoka kwenye chanzo chake cha upelelezi na kuifananisa na namba ya awali hivyo wamerudi ili apate kuwahakikishia.

    “Naomba niione Inspekta,” alikuwa na haraka sana na kila kitu alitaka kifanyike haraka haraka.

    Alipoitazama tu akasema ile namba kweli ni ya pale, akasimama na kuanza kuwangalia kwenye mafaili yaliyokuwa kwenye Self mbele ya macho yake lakini nyuma ya migongo ya wale maaskari wa upelelezi.

    Ilimchukua dakika kadhaa hivi hadi kuweza kuipata na kuja nalo pale mezani kwake na kuanza kulifunua funua. Alifunua kama kurasa mbili tatu hivi, akachomoa picha na kuinyanyua kuiangalia.

    Baada ya hapo akampa Jitu ambae alikuwa yupo karibu nae na kasha akarudisha macho yake kwenye faili lake kama kwamba hakuna kilichotokea. Jitu alipomtazama alie kwenye picha ile akampa Inspekta Kalindimya.

    Inspekta nae aliitazama picha ile kwa sekunde kadhaa na kuiweka mezani kasha akaelekeza maco yake kwa bwana gereza amabe alikuwa wala hahangaiki nao, kwani alikuwa anashughulishwa na lile faili tu.

    Baada ya kufunua funua kidogo akalifunika lile faili na kuwaangalia wale wapelelezi wawili na kuanza kusema

    “Namba hii mliyo ileta hapa ni mfungwa mmoja aliewahi kufungwa hapa gerezani na kuishi kwenye Selo namba 74 ambayo ipo mashariki kati ya miaka mitatu iliopita ana alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano kwa kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha nzito, ila inaonekana hakikutimia kifungo hicho na akatoka,” wakashangaa.

    “Akatoka? Kivipi?”

    “Nasema akatoka kwa sababu kwa mujibu wa hii namba mliyo niletea inaonesha kwamba mtu huyo ni mzima, au sio?” Wote wakajibu ndio, wakiendelea kumtazama, Bwana Jela akaendelea

    “Lakini huku anaonekana alifariki kitambo sana, yaani hata mwili wake ulitoka humu kama unatolewa mwili wa maiti, ndio maana hata faili yake inaonekana ikiwa imepigwa ‘X” walichoka wale maafande na bila kuchelewa Inspekta akamwambia anapenda kumjua jina lake na alipoandikisha kuwa anaishi.

    “Jina lake ni Loren Malima, aliingia hapa miaka mitano iliopita akiwa na miaka 33 akiwa amehukumiwa kufungwa miaka mitano lakini ndani ya miaka miwili tu akawa amefariki na akachukuliwa na nduguze kwa ajili ya mazishi,” akliwasomea huku Jitu akiandika na Bwana Gereza alikuwa akitazama saa yake.

    Alionesha kuwa muda umemuishia sasa, nao wakamuelewa, Inspekta akatoa kamera na kuipiga picha tena ile picha na kumtaka Bwana gereza ampe nakala ya maelezo hayo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

    “Sawa, lakini samahani, nina mkutano na Waziri alasiri hii, sasa naomba nije niwakabidhi kwa Katibu wangu awashughulikie, samahanini lakini kwa kitendo hicho,” aliomba radhi kwani alihitaji kutoka.

    Wala usijali mkuu, jambo la msingi ndio hilo umetusaidia, nasi tunashukuru sana,” waljibu huku wakitoka nje na Bwana Gereza akiwa nyuma yao.

    Walipofika kwa Sekretari Yule, akamfahamisha watakacho kasha wakaagana akiwaomba wafike siku nyingine kwa maelezo zaidi, wakashukuru na kumuacha aende kwa amani,

    Dada Yule aliwasaidia kila walichohitaji, akawatolea copy kwa zile karatasi na kuwapatia, nao wala hawakukaa sana wakaaga na kuondoka, njiani ndio wakajadiliana na kuona kama bado wapo njia panda bado.







    Waliwasili ofisini kwao moja kwa moja na kuanza kupitia majina yale waliyotajiwa, kwanza walianza kumchunguza na kutaka kumjua huyo Loren ni nani.

    Hivyo wakavuta Compuuter na kuanzaakumfuatilia kumjua, ajabu hakuonekana mle kabisa kitu ambacho hata wao kiliwaumiza kichwa

    “Haiwezekani kiu hicho, yaani mtu aliefungwa gereza kubwa kama Keko akosekane kwenye kumbukumbu za Polisi? Haiwezekani!” alisema Inspekta Kalindimya huku akiuma biki yake na kumfanya Jitu asimame kutoka kwenye kiti alichokuwa amekaa.

    “Hapa yawezekana ikawa kuna siri kubwa nyuma ya pazia, wizi wa kuku wapo humu, iweje huyu akosekane?” alisema Jitu na kujikuta akiropoka tu kuwa yeye anahisi ile kazi imemchosha.

    “Unaweza kujikuta unazeeka kabla hata ya muda,” Inspekta alikuwa yupo kimya tu, Jitu sasa ndio alikuwa msemaji.

    “Mkuu ninafikiri huu ni muda muafaka wa sisi kufunika haya makabrasha na kwenda kupumzisha akili maana hata kesho nayo ni siku, tusijiumize bure leo,”

    “Hilo nalo ni neon, maana hata utumie dawa nyingi kiasi gani, mguu wa bandia hauwezi kuota vinyweleo, hebu tukapumzishe akili,” akaungana na Jitu wakakusanya makabrasha ma kuzima na Computer pamoja na AC.

    Kwenye kutoka akanza kutoka Inspekta Kalindimya, itifaki ilizingatiwa na moja kwa moja yeye alielekea garini kwake n kusimama nje akiongea na simu na baada ya sekunde kadhaa akafika Jitu na kumuaga akaelekea kwenye gari yake.

    Kabla hata hajaketi kwenye gari yake Jitu, mlango ukiwa wazi huku akimuona dhahiri Inspekta nae akifngua mlango wa gari yake, aliweza kumuona pia Sekretary wa Inspekta akajitokeza akitweta kwa kuwa alikuja mbio.

    Alimsemesha na kwa umakini na uharaka wa ajabu Jitu akamuita Jitu ambae alishtushwa na ule ujaji wa Sekretary, hata naea lihisi kuwa hakuna jema, itakuwa kuna jambo tu.

    Kwa hatua ndefu ndefu Inspekta akatangulia na kufuatiwa na Sekretary wake huku mwisho akimalizia Jitu ambae alikwenda moja kwa moja kwa Sekretary na kumshika bega kumuuliza kuna nini?

    Akamwambia kuwa wanahitajika haraka sana ofisini kwa RCO muda uleule, bila kuguna wala kuuliza tena akanyoosha moja kwa moja hadi kwenye ngazi za ghorofa ya kwanza.

    Kila alivyozidi kupanda ngazi hizo, ndio na kasi nayo iliongezeka maana alitarajia kumuona Inspekta akiwa anapandisha ngazi hizo, lakini ilionesha kabisa kuwa alienda kasi kuliko yake.

    Inspekta akafika hapo na kugonga mlango kwa muda mrefu lakini hakuitikiwa, akalazimika kuingia tu hivyohivyo kwani alisikia sauyi ya nyayo zikihama toka sehemu moja kwenda nyingine.

    Hiyo ndio ilimchelewesha na kumfanya amkute Inspekta Mlangoni ndio anamuona Inspekta akimalizia kuingia nae akaongeza kasi zaidi na kuingia muda huo huo na kuwasalimia kasha akaketi sambamba na alipoketi Inspekta Kalindimya.

    Walimkuta mzee akiwa anazunguka tu hapa na pale kama vile mtu aliechanganywa na jambo fulani na alipowaona wamekaa akawakaribisha na kuwaonesha viti kwa mara nyingine.

    Wakatazamana na kujua kuwa itakuwa kuna jambo zito linamkwaza huyo mzee hadi anafikia hatua ya kutokujielewa.

    Ghafla kama mtu aliezinduliwa, akamgeukia Inspekta na kumuuliza anashughulika na kesi gani kwa sasa? Inspekta akamjibu kuwa anashughulikia kesi ya mauaji ya wasichana wawili waitwao kina Mwana.

    "Lakini pia kwenye kesi hiyo kuna majeruhi mmoja ambae yupobbado hospitali na tunafikiria..." kabla hajamaliza kutoa maelekezo zaidi, akakatishwa na Mkuu wake na kumwambia

    "asaaa tangu sasa hizo kazi zote fungia kwenye box kwa muda kwani kuna tukio moja kubwa na baya sana limetokea leo jioni hii, hadi Rais na baraza lake lamawaziri limepiga kelele na kutupa wakati mgumu mno jeshi la Polisi," alisema na kushusha pumzi kwa nguvu.

    “Tukio gani hilo mkuu?" aliuliza Inspekta kwa shauku huku akiongeza umakini kwa RCO.

    "Waziri wa Jumuia ya Afrika na Muungano..." kabla hajamaliza Jitu akadakia

    "Bi MwanaJuma Eid,"

    "Yap! ametekwa maeneo ya Manjunju akiwa anaelekea nyumbani kwake maeneo ya Victoria."

    "Boss hilo tukio limetokea leo saa ngapi?" alihoji Inspekta.

    "Tukio hili limetokea dakika chache zilizopita na tumezuia vyombo vya habari kutangaza juu ya jambo hilo hadi pale kila kitu kitakapo kuwa kipo vizuri..." akatulia kidogo na ukimya ukiwa umetawala kisha Inspekta akavunja ukimya na kusema

    "Mkuu, ninahisi kuna muingiliano wa kesi hizi mbili, yaani hii unayotueleza sasa na ile ambayo tumekuwa tukiishughulikia tangu awali"

    "Kivipi na unawezaje kutambua hilo?" aliuliza huku akiwa anamtazama kwa umakini, kwani kauli ile aliona kama huenda ikaleta unafuu kwa kiasi fulani.

    "Kesi ninayoisimamia sasa, muuaji aliniambia napaswa kujitoa kwenye hiyo kesi kabla sijafukuzwa na pia baada ya kuona simuelewi ndio jana akanipigia simu na kuniambia kuwa ananitaka niache kazi kwa faida ya Mwana, kibaya zaidi hakutaja ni Mwana gani ambae anae mtumia kama kinga yake," aliongea kirefu Inspekta na kumfanya RCO afikirie kwa dakika kadhaa na kuhoji tena;







    "Unafikiri ni kwanini alikwambia ujitoe kwenye kesi hii?" sasa alimuuliza huku akiwa anaketi kwenye kiti chake kuonesha kuwa anepata ahueni kiasi.

    "Nahisi ni kwa sababu amejua kuwa muda sio mrefu tutamtia nguvuni, sasa maekuwa na mashaka mashaka tu ambayo yanamfanya azidi kufanya makosa," kauli hiyo ikawafanya wote wamuangalie Inspekta na Jitu akamuuliza

    "Kama lipi vile kosa ambalo amelifanya?"

    “Hiyo ya kumkamata Waziri ni dalili ya kutapatapa, na ndio kosa kubwa zaidi alilolifanya hilo Jitu,” wakakubali tu ili kujua ni muafaka gani ambao watafikia.

    “Najaribu kuchanganua maneno yako lakini hata sipati jibu, sasa hebu niambie, ni msaada gani naweza kuwapatia ili muweze kukamilisha zoezi hili ndani ya saa 24?” aliuliza Mkuu huku akiwaangalia kwa zamu.

    “Task force mkuu, naomba utuongezee uwezo,”

    “Upi huo?”

    “Ninahitaji sana kikosi kazi, kikosi maalum cha kukubaliana na uhalifu (Crime Response Team) kwani mhalifu amekuwa akitumia sana mawasiliano ili kutekeleza mambo yake,” aliomba Inspekta.

    “Sawa, nataka hadi kesho muda kama huu niwe na jibu kamili kuhusu huyo mtekaji nyara na lakini asubuhi nijulishe kuhusu Waziri, umenielewa?” alisema huku akisimama, itifaki ikazingatiwa, nao wakasimama na kukubali alichokisema, kisha nae akaongeza

    “Ninampigia simu RPC sasa hivi akuandalie hicho ulichotaka, lakini kumbuka, ninatoa masaa 24 tu uweze kumtia mbaroni huyo mhalifu na pia umuokoe Waziri akiwa yu hai, unanielewa?”

    “Sawa Mkuu,” akaitika Inspekta na kutoka kichwa kikiwa kinamzunguka, hakika alivurugikiwa akili, hasa akikumbuka hizo amri za mkuu wake wa kazi, ndio akachoka kabisa.

    Walikuwa wameongozana hadi ofisini, Jitu akiwa mpole kabisa, aliona kama wametwishwa mzigo wa mawe, walifika na kujitupia kwenye viti vyao vya kuzunguka, lakini leo wala havikuwa na staraham leo.

    Hakuna aliekumbuka kujizungusha, kila mmoja aliwaza ni wapi pa kuanzia, Jitu ndio akawa wa kwanza kupata wazo

    “Inspekta naomba niseme kitu,” Inspekta hakumjibu bali alimkazia tu jicho.

    “Nafikiri tuanze na utaratibu wa kumtambua huyo mtu ni nani na wapi tunaweza kumpata,”

    “Kivipi?”

    “Mimi sitaki kuamini kuwa Computer za Polisi zimeshindwa kumuhifadhi mtuhumiwa hadi inakosekena kumbukumbu kweli?”

    “Jitu bado hujatoa mwongozo, ni kipi tukifanye ili tuweze kulifanikisha hiyo,”

    “Sawa, mimi nilichokiwaza hapa ni kwenda kuanza na watu wa IT, tuwape jina na ikiwezekana na picha washughulikie hilo…” Inspekta nae akapata mwanga na kumkatisha Jitu.

    “Wazo zuri sana hilo Jitu, sasa name pia hapa nina wazo jingine, tukichanganya hilo lako na langu, ninaamini tutapata muafaka kwa urahisi sana,”

    “Wazo lipi Mkuu?”

    “Ninafikiria wewe uende kwa watu wa IT kisha mimi nielekee hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa Mwana,” hivyo ndivyo walivyogawana majukumuna kukubaliana kuwasiliana muda wote mmoja wao anapopata kitu kipya.

    Inspekta akatoka na kumuacha nae Jitu akijiandaa kutoka. Aliwasili hospitalini na kuingia kwa daktari kisha akajitambulisha, kwa kuwa haukuwa ni muda mzuri kwa wageni kuingia, akaomba aruhusiwe kwa sababu maalum.

    Daktari alimkubalia na kumuongoza hadi wadini na kumuacha huko wakiwa wao wawili tu. Alijitambulisha mbele ya Mwana na kumpa pole kisha akaanza mahoiano nae.

    Alimuuliza swali la kwanza kama anamfahamu aliemvamia? Mwana akakiri kuwa anamfahamu kwa sauti yake ambayo anajua fika kwamba anaitambua japo kwa upande wa sura hajui, kwani ilifichwa.

    “Wakati unavamiwa, ndani ya gari mlikuwa wangapi?”

    “Wakati nvamiwa ndani ya gari nilikuwa nipo peke yangu,”

    “Na wavamizi walikuwa wapo wangapi?”

    “Wao walikuwa wapo wawili tu, mwanamke na mwanaume,”

    “Anhaa! Ina maan a wote wawili walificha sura zao?”

    “Ndio afande, wote wawili walikuwa wamevaa mask, lakini Yule mwanaume sauti yake si ngeni kabisa kwenye masikio yangu,”

    “Na huyo mwanamke je?”

    “Yeye ni mgeni kabisa kwenye masikio yangu na hata bumbo lake kwenye macho yangu ni jipya kabisa,” akajiweka vizuri kwenye kitqanda ambacho kwa upande mmoja wa juu kiliinuliwa ili kumpa ahueni ya maumivu mgonjwa.

    “Lakini sina budi kumshukuru huyo mwanamke kwani nahisi huenda ndie alieniokoa na kifo,” aliendelea kusema Mwana.

    Habari ile ilikuwa ni mpya kabisa kwake, akamuuliza huyo mwanamke alimuokoa kivipi?

    “Baada ya kuchukua pesa, Yule mwanaume alitaka kuniua kabisa kwa kusema nimeponzwa, Yule mwanamke akamzuia na kusema kama ni pesa mbona nimetoa tena bila vurugu wala kelele? Ukatokea ubishi kidogo kati yao lakini wa muda mchache mno,”

    “Hakukuwa na mtu jirani?” alihoji Inspekta huku akiandika.

    “Hapana, kwa mbali niliona walinzi kwenye jingo la ghorofa la vioo pale karibu na makaburini, ila walikuwa ni mbali mno,”

    “Mh! Endelea, baada ya huo ubishi?”

    “Yule mwanaume akamuwekea bastola Yule mwanamke shingoni na kumwambia anipige risasi ya kichwa,”

    “Enhee! Ikawaje baada ya hapo?”

    “Hapo sasa Yule mwanamke akasogeza bunduki yake na kunipiga risasi ya bega na nakumbuka akanipiga na kitako cha bunduki kichwani, sikujua ni kipi kilicho Endelea hadi niliposhtuka nikiwa hospitali,” alimaliza kujieleza Mwana.





    Inspekta alikuwa akiandika tu yale maelezo ya MwanaMeka, sasa akamuuliza

    “Umesema sauti ya Yule mwanaume sio ngeni si ndio?”

    “Ndio japo hata siikumbuki ni wapi nilipoisikia, ila hakika sio ngeni kabisa,”

    “Je ukiisikia tena unaweza kuitambua?”

    “Naam hata niwe taabani kiasi gani, naitambua vema kabisa,” alijibu Mwana kwa kujiamini na afande akatikisa kichwa kukubali akisemacho Mwana.

    Kisha akazama mfukoni na kutoa simu yake ya mkononi na kutafuta kitu Fulani hivi, alipokipata akanyanyuka pale alipokuwa ameketi na kumsogelea, akamsikilizisha audio Fulani ambayo alikuwa amerekodi.

    Yalikuwa ni mahojiano, Mwana alisikiliza na ilipofika sauti hiyo ambayo Inspekta alihisi kuwa Mwana ataijua, ni kweli aliijua na kutaka kulazimisha kunyanyuka kitandani na kusema hiyo ndio sauti yenyewe hasa.

    Inspekta akamtuliza na kumwambia apumzike tu vilevile hadi watakapomaliza mahojiano yao. Mwana akarudi chini na kulala kama awali, kisha Inspekta akahoji

    “Kama sauti si ngeni, ina maana huyo ni mtu ambae mnafahamiana nae vizuri, sasa hebu nifumbulie hili fumbo… je unafikiri huyu mvamizi aliekuvamia, alijuwa kuwa wewe una pesa kwenye gari ama ilitokea tu?” akamtazama usoni wakati Mwana akihangaika kutafuta jibu.

    “Mh! Afande kwa kweli hapo mimi siwezi kujua wala hata kupata hisia maana kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana kwangu,” mahojiano yaliendelea kwa muda kidogo na huku akimbana kwa kila Nyanja kama ana fununu zozote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini ilionekana kama vile hakuwa akijua lolote, Inspekta akachukua bahasha aliyokuwa nayo na kutoa picha moja ya wastani na kumuonesha MwanaMeka. MwanaMeka akaiangalia na kusema hamtambui kabisa mtu Yule.

    Inspekta akamwambia ajaribu kujikumbusha vizuri kama atamkumbuka, kisha akasimama na kutoa business kadi yake na kumwambia wakati wowote akipata kumbukumbu yoyote juu ya mtu Yule aliemuona kwenye picha, basi amshitue.

    “Wewe nijulishe wakati wowote, iwe mchana ama usiku, asubuhi ama jioni sawa Mwana?” alimuuliza huku akichukua bahasha yake na kuanza kutoka.

    Mwana aliitikia sawa na Inspekta alipopiga tu hatua moja akageuka na kusema

    “Pia ukikumbuka mtu mwenye sauti ile, basi ujue kuwa ndio mwenye picha ile niliokuonesha, nijulishe haraka iwezekanavyo,” Mwana akasema sawa na Inspekta akatoka kuelekea anapo pajua mwenyewe.

    **********



    Ilikuwa ni saa moja jioni muda ambao alitoka nje ya hospitali ya Taifa, akampigia simu Inspekta Jitu kumuuliza matokeo ya huko alipokwenda na kujua ni kipi kilicho Endelea.

    Jitu akamwambia kuwa kiufupi ni kwamba data zilikuwepo na zikafutwa na haieleweki kama ni kwa maksudi ama ni bahati mbaya, lakini hakika inaonesha uwepo wa picha na jina lakini hakuna maelezo yoyote.

    “Hii inaonesha kuwa huyu msumbufu ana watu wake ndani ya Jeshi la Polisi, inatulazimu kwa sasa kuwa makini zaidi hasa kwa usiku huu wa leo,” aliongea Inspekta Kalindimya.

    “Sawa kabisa Inspekta na hata name nilikuwa na wazo kama hilo, wewe upo wapi kwa sasa?” alihoji Jitu.

    “mimi natoka Muhimbili hapa, sasa wewe fanya kila njia tukutane Ferry ili tuvuke kwenda Kigamboni, huko kuna dharula,” aliongea Inspekta huku akitazama saa yake, neon lake kwa Jitu, ambae kicheo ni mdogo na hata kiumri pia, lilikuwa ni sheria.

    Jitu akamuuliza kama yeye yupo nagari? Inspekta akamjibu ndio yupo na gari yake hivyo kama yeye anakwenda sasa hivi ni heri atumie pikipiki ya Polisi ili aweze kumuwahi na achukue dereva.

    Jitu akamwambia ampe dakika chache tu watakutana hapo Ferry, wakapanga akifika atamkuta kwenye gari yake ambayo atakuwa ameipaki getini kwa ndani, haitokuwa kwenye foleni.

    Dakika kadhaa mbele kweli Jitu alifika akiwa kwenye pikipiki ya jeshi la Polisi na kuelekea moja kwa moja ilipo gari ya Inspekta Kalindimya na kuingia, alimkuta akiwa anasoma maandishi aliyo yaandika yeye mwenyewe.

    “Tunaenda wapi mkuu?” aliuliza Jitu wakati Inspekta akiwasha gari kulielekeza kwenye njia ambayo ilikuwa inaishia ndani ya pantoni.

    “Nataka tukaanzie kituo cha Polisi Kigamboni, pale ndio safari yetu itapata muelekeo, kwa sasa hakuna muelekeo zaidi ya huo,”

    “Sawa, nipe habari za huko ulipo kwenda,”

    “Mh! Jitu… hatari sana! Amini usiamini kuwa kila mtu anamtambua jambazi lakini hamjui,”

    “Inspekta mbona sikuelewi? Inakuwaje anamtambua halafu hamjui?”

    “Namaanisha sauti yake kila mtu anaijua na lakini inapokuja suala la kumjua ni nani ndio inaingia kuwa ni shida,” akamueleza yote yaliyojiri kule kwa MwanaMeka na kumuacha na mshangao.

    “Mh! Hivi ina maana kuwa matukio haya yanashabihiana si ndio mkuu?”

    “Hicho kitu mimi ninakiamini, na hapa tulipofikia leo, ndio ilipokuwa point ya mtuhumiwa, alikuwa akimlenga waziri, kote kule alikuwa akizunguka tu,”

    “Ni kweli sasa name nimebaini, lakini je unafikiri muda huo tuliopewa unaweza kututosha kweli kumtia mikononi mwetu mkuu?” Jitu alikuwa akiuliza huku akionesha kabisa kuweka matumaini yake yote kwa Inspekta Kalindimya ambae alikuwa kijiamini mno.

    Gari ndio zilikuwa zinakamilisha utaratibu wa kutoka baada ya watu wote kuwa wameishatoka.







    Alimjibu kuwa uwezekano ni finyu lakini hiyo haiwezi kusababisha kukata tamaa, bali pale ambapo unakatishwa tamaa na jambo Fulani basi hupaswi kuvunjika moyo, bali unalazimika kujituma zaidi.

    Waliwasili kituoni na kuomba kukutana na Mkuu wa kituo kile cha Kigamboni, wakaruhusiwa kumuona na kuketi nae ofisini na kumueleza kuhusu jambo lililowateta pale na kumkumbushia tukio la siku za nyuma lililitokea kule Kigamboni.

    “Hivyo Mkuu Yule mtu alikuwa ni MwanaMeka aliekuwa akiwindwa na huyo msumbufu, na sasa tumekuja huku kwa lengo maalum,”

    “Lipi hilo?”

    “Tunataka kukutana na askari wale waliompa Escort Yule mwanadada mfanyabiashara, kwenda sehemu ya biashara na kurudi nae,” Inspekta akasema huku akimtazama, Mkuu akatikisa kichwa kukubali na kunyanyua simu kumuita Katibu wake.

    Aliingia kwa unyenyekevu, Mkuu akamwambia ampigie simu askari aliekuwa zamu siku ile, akamtajia tarehe ya siku na muda husika.

    “Mwambie afike hapa haraka na wenzake aliokuwa nao, sawa?” alitoa amri ya kijeshi ambayo Katibu alitii bila shuruti na kujibu sawa huku akiwa amekakamaa.

    Akatoka na kuwaacha wakiendelea kuongea huku Mkuu wa kituo akiwauliza kama wanaweza kumkamata mtu huyo haraka iwezekanavyo? Jitu akajibu kuwa kuna asilimia kubwa za kumtia mikononi mwa vyombo vya usalama mapema.

    Wakati story zimenoga, akarudi Katibu Muhtasi wa Mkuu wa Kituo na kupiga saluti kisha akasema amewapata wawili kati ya wale waliokwenda huko, Mkuu hakujibu kitu akawatazama Jitu na Inspekta akitegemea jibu kutoka kwao.

    Inspekta akasema kwamba wao wawili hao wanatosha kabisa, akamruhusu tu Yule dada aende kuendelea na kazi nyingine wao wakamuomba Mkuu wafanye mahojiano mafupi.

    Akawapeleka kwenye chumba maalum ambacho kilionesha kama ni ukumbi wa mikutano hivi na kuwaambia kuwa wanaweza kufanya mkutano wao mle ndani, kisha yeye akatoka na kuwaambia atakuwepo ofisini kwake.

    Mahojiano yao hayakuchukua muda mrefu sana kwani wote kazi zao zilikuwa zimefanana na kila mmoja alikua akijua ni kipi kinachotakiwa kujulikana.

    Jitu aliuliza swali la mwisho na kisha akawataka wanyanyuke na kuelekea eneo la tukio walipompeleka huyo dada.

    Kwa pamoja wote wakanyanyuka na kutoka huku waitangulia nje na Inspekta pekee ndio akaenda ofisini kwa mkuu wa kituo na kumwambia kuwa anatoka na vijana hao kuelekea eneo la tukio.

    Aliwaruhusu na kumwambia kuwa iwapo atahitaji msaada wowote asisite kumjulisha kwani yeye hatotoka pale ofisini hadi wao watakaporejea, Inspekta akamwambia kuwa asijali, wapo pamoja.

    Wakati wanawasili eneo walilokwenda, ilikuwa ni saa tatu usiku, lakini eneo hilo lilionekana kama bado ni changamfu sana, mizigo mingi ikionekana kupakuliwa kutoka kwenye meli za magendo na watu wakitumia vinywaji vikali huku bangi na vitu vingi vya anasa vikiendelea eneo hilo waziwazi.

    Wakiwa bado hawajashuka garini kwa mwendo wa taratibu waliweza kuyaona yote hayo, mbele kidogo akasimama Inspekta na kugeuka nyuma walipokuwa wameketi wale askari wawili ambao ndio wenyeji wao na akawauliza huku akiwatazama

    ‘Hivi eneo hili limeruhusiwa kuwa katika mazingira haya tunayo yaona ama hamjui kinacho Endelea hapa? Mbona mimi sielewi?”

    “Yaani unaweza kusema imeruhusiwa kuvunja sheria, hii ni hatari sana,” aliongezea Jitu na Inspekta akasema kwa kuwa leo si kitu ambacho kimewapeleka huko.

    “Kilichotuleta leo hapa ni kumtafuta na kumjua ni nani ambae alikuwa akifanya biashara na Mwana, lakini hakikisheni kuwa jambo hili mnalidhibiti mara moja,” alisema huku akishika kitasa kwa ndani.

    Waliitikia sawa mkuu na kuanza kujipanga, Jitu akawauliza kama wanamjua Yule muuaji kwa sura? Wote wakasema hawamjui kwani walikuwa nae kwa mbali wakati akifanya mazungumzo na Mwana.

    “Labda kwa kumbahatisha tu tusogee eneo ambalo niliwaona huyo mfanya biashara na Yule jamaa wakiwa wamesimama,” alisema askari mmoja kati ya wale wawili na huku akionesha kwa kidole.

    “We ulimuona vizuri?” Jitu alihoji mguu mmoja ukiwa nje na mwingine ukiwa ndani ya gari.

    “Si mimi peke yangu bali ni sote tulimuona,” alipojibu hivyo na Yule mwingine alitikisa kichwa kumuunga mkono mwenzie.

    Wakajipanga kuwa waende wale wawili na kumuulizia kwa kumtaja umbo lake na alivyo kisha wakisha mjua wao watashuka na kuendelea nae.

    “Hakikisheni mkimjua mnamtoa pale na kumpeleka pembeni, hiyo itakuwa ni ishara kwetu, sawa makamanda?” Jitu ndio alikuwa akipanga kikosi kazi nae akamuambia afande kwamba anashuka garini na kusogea ambapo anaweza kuwa nao karibu ili kudadisi mazingira yale.

    Inspekta akabaki garini peke yake lakini macho yake yakiwa yanaangalia kule wanapoelekea wale askari wawili, alitamani mno kushuhudia mtu huyo akiwa amesimama nao.

    Jitu akiwa ameacha nafasi ya hatua zisizozidi tatu, kutokana na kuwa na shughuli nyingi eneo lile, hakuna aliekuwa akishughulishwa na mwingine, kila mtu alikuwa na jambo lake.

    Hiyo iliwapa nafasi mzuri zaidi kwa wao kufanya yao kwa nafasi, mbele kidogo ya macho yake Jitu, akaona Wale maskari wawili wakisimama ghafla na kumshika jamaa mkono, jamaa akasimama na kuwatazama kwa mshangao.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walimsalimia na kumuulizia huyo mtu wanaemtafuta, alikana kumfahamu na kila walivyojaribu kumuelekeza hakumjua, wengi pia wakakana kumjua na hivyo walihisi kukata tamaa.

    Ikawalazimu kurejea garini ambapo ndio kilikuwa kituo chao, hapo ndio Jitu akatoa ushauri wa kuongea na MwanaMtama, ambae alikuwa ni mfanya biashara nyingine kabla ya kumjeruhi ikiwa kama ni kweli ndio yeye muhusika.

    Lilikuwani wazo zuri, Inspekta akampigia simu Mwana na bahati mbaya simu yake ikawa haipokelewai, ilikuwa ikiita hadi inakata, sasa hapo ikawa haina jinsi ila tu kurejea mjini.

    Waliwapitisha wale askari pale walipo watoa na wao kuelekea kwenye pantone ili kuvuka. Wakiwa ndani ya Pantoni simu ya Inspekta sasa ikaita, namba ya simu ilikuwa ni ya mezani, akamtazama Jitu na kumwambia ‘kumekucha’

    Akaweka vitu vyake sawa ili kuweza kurekodi mazungumz yao na kupokea kwa neon moja tu

    “Nakusikiliza,”

    “Inspekta sasa naona unavuka kiwango, unakumbuka ahadi yangu ya jana kwako?” sauti ya leo ilikuwa ni kali tofauti na ile ya kila siku, Inspekta akajua kuwa leo amemshika pabaya, akazidi kumkera kwa kujidai amesahau na kumuuliza ni ahadi ipi aliyomuahidi jana.

    “Nazungumzia kuhusu Mwana,” Inspekta akazidi kumchanganya tu kwa maswali ya kebehi.

    “Mwana? Mwana yupi huyo?”

    “MwanaJuma Eid ambae wakati huu nipo nae sehemu,”

    “Ok! Amefanyaje huyo Mwana?” hakika ilikuwa ni ishara ya dharau, akapanic.

    “Una kiburi sio? Umepata jeuri kutokana na vijihabari ulivyopata si ndio? Sasa leo nakata mzizi wa fitna, na kesho utalipata jibu mapema tu maeneo ya kwa mama , uende ukaokota mzoga wa Mwana, Pumbavu kabisa,” alikuwa na jazba leo.

    “Name nakukumbusha kuwa leo utalala usingizi wa mwisho uraiani na huyo Mwana atakuwa ndio mtu wa mwisho kwako kumtoa roho, lakini jiandae nawe kwenda kuozea jela,” akacheka sasa Yule mtu kwa kujilazimisha na kusema

    “Na baada ya Mwana, kama utaendelea kunifuatilia basi jua usiku wa kesho utakua ni zamu yako, nitakutenganisha kila kiungo cha mwili wako, waambie nimesema kuwa kichwa chako nitakiweka Hospitali na mikono nitaipeleka sokoni, huku miguu yako nitaiacha kwako na kiwiliwili nitakipeleka ofisini kwako ili iwe ni fundisho kwa vimbembele wengine,” sauti ya sasa ilikuwa ni nzito sana na hata kufikia kumtisha Jitu.

    Alipomaliza tu kuongea safari hii akakata simu na kuwaacha wale wapelelezi wawili wakiwa wameketi wanajipanga, Jitu akajiwahi

    “Huyu mtu mara zote huwa hatanii, tunafanyeje mkuu?” Inspekta hakusema kitu bali akanyanyua simu na kumwambia RCO kuwa anataka kuwatumia wale askari wa kikosi cha CRT yaani Crime Response Team.

    Akamueleza kuwa amepanga kukitumia kikosi hicho huko maeneo ya Kwa mama Zacharia, akaruhusiwa na kisha yeye na Jitu wakajipanga kuwa usiku ule ni hakuna kulala.

    Walizunguka kila upande wakiweka ulinzi wa kutosha wakitumia askari wa kikosi tajwa hapo juu, ambacho mara nyingi huwa hakina vazi maalum wakiwa wamelichakaza kabisa eneo lile kwa ulinzi mkali.

    Saa nane usiku, inspekta alikuwa kituo cha Polisi akiwa na watu wa IT wakijaribu kumtafuta hewani huyo muuaji kwa njia ya mtandao, ghafla kwa mshtuko mkuu, akajishika mfuko wake wa suruali.

    Ni simu yake iliyoita, ambayo wala hakuitegemea muda ule, akaitoa haraka haraka huku mapigo yake ya moyo yakiwa na kazi zaidi ile ya damu yake, akaitazama na kugundua kuwa safari hii namba iliyompigia, haikuwa ya Yule hayawani.

    Hii sasa ilikuwa ni namba ya simu ya mkononi, akashusha kidogo munkari na kujilazimisha kutulia na kumsalimia aliepiga

    “Inspekta Kalindimya upo wapi?” hakujibu salamu mtu huyo bali aliuliza kwa haraka, sauti ilikuwa ni ya kike ikiongea kwa mashaka makubwa.

    “Wewe ni nani?” aliuliza huku akiitazama ile namba ya simu na kuwaambia wale watu wa mawasiliano waiunganishe kwao, nao wakaiunga na kumwambi aendelee.

    “Inspekta huwezi kunielewa kwenye simu, tambua leo nimeshinda nyumbani kwako hujaja hadi muda huu, nikatoka na kuelekea hadi kituoni, ofisini kwako napo sijakukuta, nahitaji kuonana nawe usiku huu, maisha yangu yapo mashakani!” aliongea huku akionesha wasiwasi ukiongezeka na tena kwa sauti ya haraka haraka.

    “Sawa, upo wapi kwa sasa?” alihoji Inspekta huku jamaa wengine nao wakisikiliza.

    “Wewe ndio uniambie mimi ulipo ili nije sasa hivi, maana mimi nipo mitani tu nikikimbia huku na kule kukutafuta wewe,” ilijibu ile sauti ya kike.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hata kama nikitaka kukuelekeza mimi nilipo, kwanza ni lazima nijue upo wapi ili kuweka uzani wa kati, tuweze kukutana,” alimfafanulia Kalindimya.

    “Mimi kwa sasa nipo Manyanya, basi tukutane Studio baada ya muda mfupi,”

    “Hapana! Njoo vijana Hostel hapa kinondoni, kuna bendi ya Home alone inapiga, nitakuwa kwenye pembe ya mashariki kule nimevaa juba jeusi, ukifika mezani weka simu yako mezani mimi nitakufahamu kama ni wewe,” alitoa maelekezo marefu mtu wa upande wa pili.

    “Poa!” alijibu Inspekta na ilipokatika tu hiyo simu akampigia simu Jitu na kumwambia wakutane Vijana Hostel kisha akairudisha simu mfukoni.





    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog