Search This Blog

Monday 24 October 2022

DHIHAKA - 2

 

    Simulizi : Dhihaka

    Sehemu Ya Pili (2)







    Asubuhi, Hija aliondoka akiwa amechelewa kidogo tofauti na siku nyingine anazoondoka kwenda kazini. Hakuna yeyote aliyemuuliza, wazazi wake wote wawili walikuwa wamekwishaondoka kwenda makazini wakati alipokuwa akijitayarisha.

    Badi naye aliondoka nyumbani saa moja kabla muda wa ahadi haujatimia. Aliamini muda aliondoka ulikuwa mzuri kuondokea nyumbani kwa matumaini asingechukua muda mrefu kukaa kumsubiri Hija wakati atakapokuwa amefika RM Hotel.

    Akiwa ametangulia kufika RM Hotel, Badi hakumwona Hija alivyoingia. Alikuwa ameliinamia gazeti, akashtushwa na mlio wa kusogezwa kiti kilichokuwa kwenye meza aliyokuwepo. Akauinua uso na kuangalia, akamwona Hija. Akaliacha gazeti alilokuwa akilisoma na kuliweka juu ya meza, kisha alijiweka vizuri kwenye kiti.

    “Karibu,” Badi alisema.

    Hija alivuta kiti na kukaa. Badi akamwita mhudumu kwa kumpungia mkono.

    “Niletee chai,” Hija alimwambia mhudumu.

    “Utakunywa na nini?”

    Hija akaonekana kutokuwa na uhakika na kitafunwa anachokihitaji. Akajaribu kutafakari huku akisubiriwa na mhudumu.

    “Basi nitengenezee Spanish omlette!” hatimaye Hija alitaja anachokihitaji. “Lisiungue!” alitoa angalizo.

    Baada ya mhudumu kuondoka, wote wawili wakaangaliana na kutabasamu.

    “Mh? Za toka jana?” Badi aliuliza.

    “Safi.”

    Wakazungumza hili na lile kupoteza muda kwa ajili ya kusubiri kifungua kinywa kilichoagizwa na Hija kiletwe. Hatimaye kifungua kinywa kililetwa na mara tu Hija alipomaliza, hawakuwa na kingine cha kuwaweka hapo. Wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa Badi.

    “Unaishi peke yako?” Hija alimuuliza Badi baada ya kuiona nyumba aliyoingia ikiwa na ukimya mwingi.

    “Naishi na mdogo wangu, ameenda shule,” Badi alijibu.

    Uwepo wa peke yao humo ndani ukawapa uhuru mpana zaidi. Hawakuhitaji kwenda chumbani. Mambo yakaanzia sebuleni!

    Baada ya tukio hilo, ikawa kama limewapa nafasi ya kila mtu kujiona yuko huru kwa mwenzake. Mazungumzo yaliyohusu undani wao yakatawala.

    “”Nico hajanipata na wala hatanipata!” Hija alimwambia Badi baada ya kuulizwa kama uhusiano kati yake na Nico umefikia hatua ya kuwafikisha hapo walipofika wao.

    “Una hakika gani kama hatokupata?”

    “Nico siyo aina yangu!”

    “Mi’ ni aina yako?”

    Hija akamwangalia Badi usoni, kisha bila ya kutabasamu, akasema kwa sauti ya chini, “Nadhani.”

    Kauli hiyo ikamwacha Badi kwenye sintofahamu ya maana halisi ya Hija kutamka hivyo.

    “Nasikia baba yako anamiliki kiwanda?” Badi aliuliza.

    “Baba yangu mimi?” Hija aliuliza huku akionyesha mshangao.

    “Ndiyo. Ndivyo wanavyozungumza.”

    “Akina nani?”

    “Wafanyakazi.”

    “Hamna kitu kama hicho,” Hija alisema na kutingishwa kichwa.

    “Unakataa?”

    “Baba yangu hamiliki kiwanda chochote!”

    “Bali?”

    “Ninachojua ni mkurugenzi wa kampuni…” Hija akasita na kumwangalia Badi usoni. “Kuna ulazima wa kujua?”
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Siyo vibaya ukinielezea.”

    “Huwa sipendi kuzungumzia watu wengine. Nadhani yapo mengi ya kuzungumza yanayotuhusu wenyewe.”

    “Bado kuna ulazima wa kumzungumzia baba yako.”

    “Kama upi?”

    “Nadhani ni lazima kuijua familia yako, mojawapo ni hili la kujua baba yako ana shughuli gani. Huwezi kujua, pengine nina mpango wa kukuoa.”

    “Nakuona kama unakwenda kasi.”

    “Vyovyote na iwe, baba yako ni mkurugenzi wa wapi?”

    “Kampuni ya Mawasiliano.”

    Badi akataka kuendelea kuuliza kutokana na jibu alilopewa kutomtosheleza. Alitaka kujua ni mawasiliano ya nini. Akapuuzia, lakini nafsi yake haikuridhika.

    “Kwa hiyo unataka kunioa?” Hija aliuliza ghafla.

    “Eti?” Badi aliuliza kwa kushtuka.

    “Basi achana nalo!” Hija alisema.



    ***



    Kitu kilichokuwa kikimkosesha amani Nico ni kule kuona ukaribu wake na Hija ukiwa hauna matunda yoyote kati yao. Hilo lilikuwa likimwumiza akili. Siku chache zilizopita katika kile alichokuwa akijaribu kuulazimisha ukaribu huo uwe wa mapenzi, Nico alifanikiwa kuambulia kuunyonya ulimi wa Hija wakiwa ofisini kwake. Hayo yakawa ni mafanikio yake ya kwanza na makubwa tokea awe karibu na msichana huyo! Kitendo hicho kikamjengea matumaini kuwa angempata binti huyo ndani ya siku chache zijazo.

    Ndani ya siku tatu mwendelezo wa tabia hiyo ya kunyonyana ndimi zao wakiwa ofisini uliendelea. Nico akanogewa, akataka kuifanya tabia hiyo iwe ada kila wanapokuwa ofisini pamoja. Ghafla Hija akambadilikia. Akawa anakwepesha uso wake, na alipokuwa akilazimishwa kwa nguvu, akawa anaubana mdomo wake huku akilalamika kuwa ana mchumba wake na asingeweza kuendelea kufanya kitendo hicho.

    Kama hilo halikutosha, Hija akaanza kukataa kwenda ofisini kwa Nico kila alipoitwa!

    Uhusiano wake mpya aliouanzisha na Badi, ukachochea kuwa mbali na meneja huyo. Akaanza kubeza amri za Nico kila alipokuwa akimwita! Ubezaji huo akaufikisha kwa kumtumia ujumbe wa simu Badi. Eti Nico ananiita ofisini! aliutuma ujumbe wa aina hiyo. Wakati mwingine kwa kuongeza makali zaidi kwa kuandika, fala ananiita!

    Usiende! Badi naye alimjibu kwa jazba ya kimaandishi. Wivu wa kumlinda Hija asiingie mikononi mwa Nico ukaanza kujenga himaya kwa Badi!

    Madai ya Hija ya kuwa ana mchumba yakawa hayakumwingia Nico. Badala yake akaingiwa na shaka. Wasiwasi huo ukampa hisia huenda kuna sababu nyingine iliyomfanya Hija abadilike ghafla, lakini sio mchumba kama anavyodai! Hofu yake ikawa, huenda Hija anatembea na mmoja wa wafanyakazi wa hapo hotelini! Akaingiwa na dhana huenda mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Uhasibu anatembea naye. Aliamini idara hiyo ndiyo ingekuwa na watu wa daraja la kutembea na msichana kama Hija. Pamoja na kuiwazia idara hiyo ya uhasibu, lakini mtu mwingine aliyemwekea wasiwasi kuwa anaweza akawa anatembea na Hija ni Badi! Idara za Restaurant, Baa au Jikoni, aliamini wafanyakazi wa idara hizo wasingeweza kutembea na Hija kutokana na kumwogopa yeye kwa kuwa ni meneja wa idara hizo.

    Wazo la kuwa ametemwa ghafla na Hija lilimwumiza, ingawa hakulikubali. Kumbukumbu za kunyonyana ndimi wakiwa ofisini angalau zilimuweka kwenye uhakika kuwa hajatemwa na msichana huyo. Lakini pia, kumbukumbu hizo zikawa kama mshale wa kipimo cha joto uliokuwa ukipanda kulipandisha joto la mapenzi dhidi ya binti huyo. Wakati mwingine alikuwa akijilaumu kwa kutokuwa mwepesi wa kuitumia nafasi hiyo ya kunyonyana ndimi kumalizia mchezo wote wakiwa humohumo ofisini! Aliulaumu woga wake wa kutofanya mambo hayo kwa hofu ya kufukuzwa kazi endapo angekamatwa. Aliamini, laiti angefanikiwa japo mara moja, Hija asingemletea dharau anayomfanyia sasa!

    Nico alitamani kujitafuna vidole kila alivyokumbuka kuzipoteza nafasi hizo zilizoishia kushikanashikana, na matokeo yake, sasa anatumikia adhabu ya dharau kutoka kwa msichana huyo! Wazo la kuwa anataka kumtema likampagawisha! Mikwara, vitisho na manyanyaso kila alipomwona Hija akifanya kosa japo dogo na wakati mwingine bila ya kosa vilianza kumwandama binti huyo.

    “Kwani lazima usomee umeneja wa hoteli?” Nico alimwambia Hija wakati akimnyanyasa. “Mbona kuna kazi nyingi tu mjini za kufanya! Au unadhani wale makahaba wanaohaha usiku kucha wakitafuta wanaume, wao hawakusoma? Kama kazi ya hoteli inakushinda kwa nini usijiunge nao?”

    Unyanyasaji huo, Hija akawa anaulalamikia kwa Badi“Mjinga kama yule hawezi akakufanya uache mazoezi yako ya vitendo kwa ajili yake,” Badi alimsihi Hija. “Anachotaka wewe uondoke ili baadaye ajisifu amekuondoa! Usikubali! Wewe kamilisha uzoefu wako wa kikazi. Ukishakamilisha unaachana naye!”

    “Kwa nini aendelee kuninyanyasa kama vile nimetoka kwenye familia duni?” Hija alilalamika.

    “Ukiondoka utampa ushindi!” Badi alisisitiza.

    Hija akamsikiliza Badi.



    ***





    ***



    BADI alichanganywa na penzi la Hija! Msichana huyo aliujua utundu katika shughuli nzima ya kitandani. Pamoja na uzoefu aliokuwanao Badi kuhusu wanawake, lakini kwa Hija alionekana akifundishwa. Hija akawa mwalimu, yeye akawa mwanafunzi. Alivyokuwa havijui, akavijua!

    Mara zote za kufanya mapenzi zikawa zinamchanganya Badi kutokana na utukutu aliokuwa akifanyiwa na Hija. Ikawa kama vile, Hija ndiye aliyemtoa ushamba Badi! Siku chache tu za mapenzi yao, Badi akadata! Kule kukaushiana kwao wakiwa kazini kwa hofu ya kujulikana uhusiano wao, ukaanza kutoweka. Dalili za kuwa ni wapenzi wakaziachia zionekane na wafanyakazi. Mwonekano wao wakiwa pamoja ukawa huru.

    Taarifa za kuwa Badi amempindua Nico zikasambaa kwa kasi. Zikamfikia Nico, naye akapeleleza, akagundua ni kweli watu hao wana uhusiano! Huyu ndiye aliyedai ni mchumba wake? Akauona huo ni usaliti aliofanyiwa na Badi! Akatamani amwite ofisini kwake, amuulize kwa nini amemfanyia kitu kama hicho? Lakini akasita kuuchukua uamuzi huo kwa sababu Badi hakuwa chini yake kiidara. Alihofu Badi angekiri kwa dharau kuwa ni kweli Hija ni mpenzi wake. Alijua hakuwa na mamlaka yoyote ya kikazi kuchukua dhidi ya Badi, na hilo lingempa nafasi Badi ya kumtambia!

    Fikra za uovu wa kumfanyizia Badi zikaanza kuchukua nafasi kichwani kwake. Lengo lilikuwa ni kumwonyesha kuwa, yeye pia ni mtoto wa mjini! Kuna wakati aliingiwa na ushawishi wa kutaka kupuuzia kuichukua hatua hiyo, lakini kitendo cha kunyang’anywa msichana huyo na kushuhudiwa na kadamnasi ya wafanyakazi, ilimwuma! Alikumbuka alivyokuwa akiwawekea mikwara ya vitisho wafanyakazi wa chini yake waliokuwa wakijaribu kuwa karibu na msichana huyo, akafanikiwa kuwatenganisha kwa kutumia nguvu zake za kimadaraka, lakini mwisho wa yote ni yeye aliyenyang’anywa na mfanyakazi mwenzake!

    Aibu ilimwumiza!

    Ikazidi kumwumiza baada ya kugundua kitendo hicho cha kunyang’anywa kilifurahiwa na wafanyakazi wote! Ilikuwa sawa na kuumbuliwa na akakiri aliumbuka! Ikawa kama vile wawili hao walimtangazia uadui mbele ya hadhara, Badi akiwa adui namba moja! Akili ya kisasi bin kisasi ikachukua nafasi kubwa kichwani mwake!

    Akajipanga kumtafutia Badi watoto wa kihuni ambao ukiwalipa ujira wao, hukufanyia kazi unayoitaka. Angewapa maelekezo ya nini cha kumfanyia Badi. Angewataka wamfanyizie wakati Badi akiwa yuko na Hija. Wamsulubishe kwa kipigo, kisha wamwingilie kwa kumlawiti huku Hija akishuhudia! Huo ndio unyama aliokusudia kumfanyia, akiamini kitendo hicho kingemdhalilisha Badi, na aibu hiyo ingesambazwa na kuwa wazi kwa kila mtu.

    Kwa kashfa ya aina hiyo, ikamuweka Nico kwenye matarajio ya kuwadhalilisha watu hao wawili kuliko alivyodhalishwa yeye!

    Hata hivyo, wazo lake hilo likapata kikwazo. Alikuwa hajui wapi angewapata wahuni wa aina hiyo, wanaoaminika na wasio waropokaji. Uzoefu wa kuwa karibu na wahuni wa mitaani hakuwa nao. Na hii ilitokana na mfumo wa maisha aliyokulia nayo. Alilelewa kwenye mfumo wa ‘mtoto wa mama’ wenye malezi ya kudekeza yanayomfanya mtoto awe wa kushangaa wenzake wakati wote. Wazazi wake hawakumpa nafasi ya kujichanganya na watoto wengine aliokuwa akiishi nao mtaani. Hao ndio waliokuwa na usugu wa kuzijua sulubu za kitoto kama vile kucheza mpira wa miguu kwenye viwanja vya mchangani ambako matukio ya kutukanana, kuzinguana kwa jambo dogo na kukabiliana kwa kupeana vitisho vilivyojaa kauli za kitemi yalikuwa mambo ya kawaida. Aina ya maisha hayo, Nico hakuyapitia!

    Hali hiyo ilimfanya ashindwe kujua wapi pa kuanzia. Ingawa walikuwepo wafanyakazi wenye kutazamwa kwa mitazamo kuwa ni watoto kihuni, lakini aliogopa kuwatumia hata kwa kuwatafuta wahuni wenzao. Hofu yake ilikuwa ni kuvujishwa siri hiyo na kuingizwa kwenye matatizo yatakayomvunjia heshima yake, ingawa aliamini kitendo cha Badi kulawitiwa mbele ya macho ya Hija ingekuwa ni adhabu anayostahili kuipata.

    Kusudio hilo akaliona ni gumu kulitekeleza, kukwama kushindwa kuutimiza uovu huo kwa Badi kukazidi kumwongezea hasira! Suluhisho pekee aliloliona limebaki, akaamua kumnunia Badi! Akawa hazungumzi naye, labda litokee suala la kazi, na alipolizungumza, alilizungumza kwa kujionyesha yeye ni zaidi kwa sababu yupo kwenye ngazi ya umeneja wakati Badi ni mkuu tu wa idara! Kinyume na hilo, watu hao wawili wakawa hawana mazungumzo mengine. Kupishana bila ya kusalimiana ikawa ni aina mpya ya maisha yao ya kikazi!

    Wafanyakazi wakanusa, wakagundua Badi na Nico hawazungumzi! Kisa? Hija!

    Likawa gumzo hotelini kote!

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    5



    ILIKUWA asubuhi wakati Badi alipokuwa akiwahudumia watalii wa kigeni wote wakiwa Wazungu waliokuwa wamewasili hotelini hapo. Aliwaelekeza baadhi yao namna ya kujaza fomu za hoteli na za vyumba watakavyokaa. Wakati akiwa kwenye hekaheka hizo, mmoja wa wafanyakazi wa hapo mapokezi ambaye ni msichana aliyekuwa ametoka mara moja, alirudi na kujumuika na wafanyakazi wenzake. Msichana huyo alianza kumlalamikia mfanyakazi mwenzake.

    “Jamani yule baba, mbona yuko vile!” alilalamika kwa sauti ya chini ili isilete bughudha kwa wageni.

    “Baba yupi?” mwenzake alimuuliza.

    “Meneja Nico!”

    “Ana nini?”

    “Nimemwona anavyomtukana yule msichana mwanafunzi anayeitwa Hija…jamani yule baba anajua kunyanyasa!”

    Badi akayanasa mazungumzo hayo! Akavunga kama hakuyasikia.

    Hata hivyo, msichana yule alishindwa kuendelea kuzungumza baada ya kuwasili mgeni wa hoteli hapo mapokezi. Akakatisha mazungumzo yake na kwenda kumhudumia mgeni huyo.

    Kauli ile iliacha athari kwa Badi na kuifanya akili yake iyumbe. Akajaribu kuilazimisha itulie kwenye masuala ya kazi ili asije akafanya ndivyo sivyo kwa wageni anaowahudumia.

    Mgeni aliyekuja na kuhudumiwa na yule msichana wa mapokezi aliondoka, Badi akamwangalia huyo msichana kwa jicho la pembeni la mara moja, akamwona akishughulika na nyaraka zilizokuwa mikononi mwake. Badi akamaliza kuwahudumia wageni na kuagana nao kwa vicheko vya hapa na pale, kisha wageni wale waliondoka na kuelekea vyumbani.

    Badi akamwangalia tena yule msichana. Ushawishi wa kumfuata ili aelezwe tukio la Nico na Hija lilivyokuwa, ukamjia. Hata hivyo hakuutekeleza, lakini pia hakukutuliza akili yake.

    “Naenda restaurant!” ghafla Badi aliwaaga wenzake huku akiondoka.

    “Sawa bosi,” mmoja wa wafanyakazi wenzake alijibu.

    Badi alifika katika mgahawa huo na kumfuata mkuu wa idara hiyo.

    “Hija yuko wapi?” Badi aliuliza baada ya kumaliza kusalimia. Uhusiano wake na Hija ulikwishafahamika kwa wafanyakazi wote na hata kumuuliza kwake Hija hakukuleta mshangao wowote kwa mkuu huyo wa idara.

    “Nimemwambia akatulie kidogo,” mkuu huyo aliyeitwa Amin alimwambia Badi. Kauli hiyo ikamdhihirishia Badi ni kweli kulikuwa na kasheshe lililomhusu Hija.

    “Hivi ilikuwaje?” Badi aliuliza kwa utulivu.

    “Aa, huyu jamaa ovyo sana!” mkuu huyo alisema huku akiamini Badi atakuwa anaelewa ni nani aliyekuwa akimmaanisha. “Aisey!” alisema tena na kutingisha kichwa “Jamaa ana matatizo! Kamtolea Hija maneno yanayoudhi…kwa kweli inakera!”

    Badi akahisi kifua chake kikifura kwa hasira. “Kwani kamwambiaje?” aliuliza huku akijaribu kutoionyesha jazba iliyokwishamwingia.

    “Badi! Wee achana naye huyu jamaa! Si unamjua ni mjinga fulani?” Amin aliendelea kusema na kumsihi tukio hilo Badi asilichukue kwa jazba. Akamwomba arudi akaendelee na shughuli zake za kazi.

    “Hija yuko wapi?”

    “Canteen.”

    “Wacha nikamwone!” Badi alisema na kuondoka.



    *

    Badi alikwenda moja kwa moja mgahawani ambako kwa muda huo hakukuwa na huduma yoyote ya chakula iliyokuwa ikitolewa kwa wafanyakazi. Alimkuta Hija yuko peke yake akiwa amekaa kwenye kiti huku ametulia. Alionekana kuwa mbali kimawazo na alikuwa amejiinamia. Mara Badi baada ya kuingia, Hija aliuinua uso na kuangalia mara moja mlangoni. Alipomwona ni Badi ndiye aliyeingia, akaurudisha uso wake na kuendelea kuwa kimya.

    Badi alimsogelea Hija, na kadri alivyomkaribia ndivyo kasi yake ilivyozidi kupungua. Hija hakugeuka kumwangalia!

    “Hija!” Badi aliita kwa sauti ya chini.

    Hija akamnyooshea mkono Badi wa kumzuia asimzungumzishe. Badi akanywea kwa sekunde chache kama aliyekuwa akisikilizia kitakachotokea. Alipoona kimya kinazidi kati yao, akakivunja kimya hicho kwa kusema, “Huyu fala amekwambia nini?” sauti yake ilijaa shari.

    Hija hakujibu. Alitulia vilevile na kuwa kama sanamu ya binadamu iliyojengewa humo ndani.

    “Hija!” Badi aliita tena.

    Hija hakuitikia!

    “Huyu mpumbavu amekwambia nini?” safari hii sauti ya Badi ilipanda juu.

    Ghafla Hija akainama na kuuziba uso wake kwa viganja na kuangusha kilio cha kimyakimya.

    “Niambie alichokwambia!” mzuka wa jazba ulimpanda Badi.

    “Badi naomba uniache!” Hija alisema kwa sauti yenye kilio.

    “Hivi huyu mpumbavu…” Badi alisema na kutamka tusi la kumtukania Nico mama yake. Akageuka ghafla. “I’m gonna fix him mpumbavu huyu!” alisema na kuondoka kwa kasi kutoka humo mgahawani.

    Moja kwa moja aliongoza ofisini kwa Nico. Mwendo wake haukuwa wenye haraka, lakini nafsi yake ilitawaliwa na hasira. Aliufikia mlango wa ofisi hiyo, akaufungua bila ya kugonga. Akamwona Nico yuko mezani akiandika.

    Nico akashtuka kumwona Badi ameingia bila kupiga hodi. Palepale ghadhabu ya kunyang’anywa Hija ikamkumbusha uadui wake na mtu huyo aliyeingia.

    “Unaingiaje bila ya kugonga...” Nico alianza kuuliza kwa sauti yenye kiburi na uso uliojenga ujivuni, lakini aliishia njiani.

    Badi aliinamia meza aliyokuwepo Nico, akainyosha mikono yake yenye nguvu na kulikwida kwa mbele koti alilovaa Nico, kisha akamwinua kutoka kwenye kiti na kumkaba kisawasawa.

    “Nakuomba uachane na Hija!” Badi alisema kwa sauti kavu huku akimvuta Nico. Wakawa wanaangaliana ana kwa ana. Kisha akamwachia kwa kumsukuma.

    Nico aliyumba na kurudi kwenye kiti akitua kama mzigo. Akakaribia kuanguka na kiti hicho cha kuzunguka. Ghafla akaiondoa usoni taharuki iliyomkuta, akatengeneza tabasamu alilotaka aonekane kuwa hajali, lakini likakosa ujivuni aliokusudia uwepo.

    “Nakupa onyo!” Badi alisema huku akirudi kinyumenyume. “Ukimnyanyasa tena Hija, utanijua mimi nikoje pumbavu wewe! Kama mwanamke hakutaki, hakutaki tu! Usilazimishe penzi!” Baada ya kusema hivyo, Badi aliugeukia mlango aliokuwa ameukaribia na kuufungua. Akatoka na kuitengeneza vizuri suti yake kwa kulivuta chini kidogo koti lake na kuiweka sawa tai kama vile yeye ndiye aliyetoka kukwidwa. Akarudi sehemu yake ya kazi.

    Siku iliyofuata Hija hakutokea kazini!



    ***



    KUTOKUFIKA kazini kwa Hija kukawa ni pigo kwa Badi. Lilikuwa pigo kwa sababu baada ya ile jana kutoka ofisini kwa Nico na kurudi sehemu yake ya kazi, Badi alipanga itakapokaribia muda wa kutoka kazini awasiliane na Hija na kisha amwombe amsubiri ili waondoke pamoja kwa kutumia gari lake.

    Dhamira yake ya kutaka aondoke naye kwenye gari lake ilikuwa ni kumtuliza kwa kumwambia alichokifanya kwa Nico baada ya kutoka mle mgahawani. Aliwaza angeitumia nafasi hiyo kumweleza jinsi alivyochukizwa na kitendo kilichofanywa na Nico kumnyanyasa. Nafasi hiyo aliamini ingempa ujivuni wa kumwonyesha Hija ni jinsi gani anavyomjali, lakini pia angemhakikishia kuwa, Nico asingeweza kurudia tena kumnyanyasa, vinginevyo atampa kichapo!

    Hata hivyo, muda wa kumaliza kazi ukiwa umekaribia, alipompigia simu Hija; Hija hakupatikana kwenye simu! Akajaribu tena, matokeo yakawa yaleyale, hakupatikana! Hali hiyo ikamshangaza, akampigia simu Amin, Mkuu wa Mgahawa.

    “Uko na Hija?” Badi aliuliza kwenye simu baada ya Amin kupokea.

    “Hija ameshaondoka muda mrefu!” Amin alisema. “Baada ya kumruhusu kwenda canteen akapumzike, baadaye alirudi na kuniomba nimruhusu arudi nyumbani. Nikamruhusu. Kwani hakukuaga?”

    Badi alihisi akinyong’onyewa na viungo vyote vya mwili. Hija ameondoka bila ya kuniaga? alijiuliza. Na kwa nini azime simu yake?

    “Basi nitawasiliana naye,” Badi alimwambia Amin na kukata simu.

    Unyonge ukamtawala mwilini na akilini. Maswali lukuki yakarindima kwenye kichwa chake. Kitendo cha kutoagwa kiliendelea kumsumbua, lakini kitendo cha kutopatikana kwa Hija kwenye simu kikawa ni kizungumkuti kingine kilichoifanya akili yake ichoke haraka. Alijikuta akimtupia lawama Nico, alimwona ndiye chanzo cha yote!

    Akiwa ndani ya gari alijikuta akikosa shauku ya kurudi nyumbani. Akaendelea kuendesha bila ya kupata jibu aelekee wapi. Upo wakati aliwaza aelekee baa akaitulize akili kwa bia mbili au tatu, lakini ushawishi mwingine ukamtuma aende Tabata nyumbani kwa kina Hija. Ushawishi wa kumwendea Hija nyumbani kwao ndio ukawa na nguvu kuliko ule wa kwenda baa. Alimhitaji Hija awe naye, amwonyeshe kuwa anampenda na kwamba yuko pamoja naye kwenye wakati mgumu kama huo.

    Alijua Hija angeendelea kuwa mnyonge kutokana na unyanyasaji aliopewa na Nico, unyonge ambao alihitaji akauondoe kwa kumpa matumaini mapya kuwa asijali, na angesisitiza kuwa, yaliyotokea yasingejirudia tena. Akauona umuhimu wa kuwa karibu na Hija kwa siku hiyo! Akalipeleka gari lake kituo cha mafuta, akaliongezea petroli, alipomaliza akaelekea Tabata!



    *



    *

    Alilisimamisha gari lake kwenye mwembe ambao kwa mara ya kwanza alipomleta Hija alimshushia na mwembe huo ukaendelea kutumika kama kituo cha kumshushia kila alivyokuwa akimleta. Kabla ya kuteremka akajaribu kumpigia tena simu. Matokeo yakawa ni yaleyale, simu ya Hija ilikuwa haipatikani! Badi akaduwaa ndani ya gari, ushawishi wa kumwendea ndani kwao ukamjia. Akawa anajiuliza kama ingekuwa busara kufanya kitendo hicho. Akajiuliza, atakapogonga geti, akatoka mtu mwingine tofauti na Hija na kumuuliza shida yake, angejibu nini?

    Ingawa alipatwa na kigugumizi cha kwenda kwenye nyumba hiyo aliyokuwa akiiangalia, lakini ushawishi wa kumsukuma kwenda ukawa unamshinikiza aende. Aliamini muda ambao Hija aliondoka kazini, kwa muda huo angekuwa ameshawasili nyumbani. Matumaini hayo mapya ya uwepo wa Hija nyumbani yakamsukuma ateremke kutoka kwenye gari, akaufunga mlango na kuliweka sawa shati lake baada ya koti analolitumia kazini kulivua na kuliacha humohumo ndani ya gari. Kwa mara ya kwanza akaifuata nyumba anayoishi Hija ambayo ilikuwa kama umbali wa mita thelathini na tano kutoka sehemu alikolisimamisha gari lake.

    Akaiona kengele ya getini, akaibonyeza na kuitikiwa na ukimya. Akashindwa kuelewa kama ilikuwa ikifanya kazi. Ukimya huo na sintofahamu iliyomwingia kuhusu kengele hiyo ikamsukuma kuligonga geti kwa kutumia vifundo vya vidole vyake vya mkono. Akasikilizia tena.

    Alipotaka tena kubonyeza kengele na kisha amalizie kwa kuligonga geti akiamini kimojawapo au vyote hivyo vingesikika, ghafla akasikia mlango wa nyumba unafungwa kutoka ndani. Akajua kuna mtu anakuja. Akaomba kimoyomoyo, anayekuja awe ni Hija!

    Akiwa na wasiwasi huenda anayekuja ni mmoja wa wazazi wa Hija, Badi alizisikia kukurukakara za mlango mdogo wa geti unaofunguliwa. Akatokeza msichana, Badi alivyomwangalia akaiweka dhana kuwa anafanana na Hija. Akahisi huenda akawa ni mdogo wake.

    Mara tu baada ya kusalimiana, Badi akamuulizia Hija.

    “Hajarudi kazini!” msichana alijibu kirahisi.

    Jibu hilo likamfanya Badi apigwe na butwaa la muda, lakini alipohisi alikuwa akitazamwa na msichana huyo, akalitengeneza tabasamu la haraka mdomoni. “Ahsante nashukuru,” alisema huku mzinguo wa akili ukiendelea kumzingua ni wapi alikoishia Hija jioni hiyo.

    “Akija nimwambie nani?” msichana aliuliza.

    Akiwa amejua angeulizwa swali hilo, Badi akajibu, “Mwambie Badi!” Akataka kuongezea kuwa wanafanya kazi pamoja, lakini palepale akajiuliza, maneno mengi ya nini? Akaaga.

    Hija amekwenda wapi? Na kwa nini aendelee kutokuwepo hewani? Dalili za wivu akazihisi. Lakini akajipoza kwa kujipa imani huenda simu anayotumia Hija imeishiwa nguvu ya betri na kujizima. Wazo hilo angalau likaonekana kumridhisha kwa kuamini kuwa, kama angekuwa hewani angeweza kujua yuko wapi na angemfuata. Hata hivyo, pamoja na kujiridhisha huko, sintofahamu ya wapi msichana huyo alipo iliendelea kumtesa!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaifikiria safari ndefu aliyoifanya ya kuja hapo Tabata na kisha anarudi kwake Tegeta bila ya mafanikio ya kumwona na Hija. Akakiri ni safari ndefu inayomkabili, lakini akajiuliza ni haraka gani inayomrudisha nyumbani mapema? Akapata wazo la kutafuta baa yenye utulivu kwenye maeneo hayo ya Tabata, ajigidie bia zake huku akivuta muda ili baadaye arudi tena nyumbani kwa kina Hija. Ghafla akajihisi mnyonge kwa kutomwahidi msichana aliyemfungulia geti kuwa angerudi tena.

    Alipata baa iliyomridhisha. Haikuwa mbali na anapoishi Hija ingawa ingemlazimu kukata mitaa kadhaa kabla ya kurudi tena nyumbani kwao. Akanywa bia zake taratibu huku kila wakati akiangalia saa yake ya mkononi kana kwamba kulikuwa na muda alioupangia wa kuondoka hapo. Hatimaye akaridhika na kiwango cha unywaji aliokunywa na muda alioutumia hapo baa. Akarudi tena nyumbani anakoishi Hija, akiamini kwa muda huo angekuwa amesharudi nyumbani.

    Alilisimamisha gari lake kwenye mwembe, akazima taa zote na kuzima injini. Alipotaka kufungua mlango ili atoke, kukawa na mwanga wa gari uliotokea nyuma yake. Akasitisha kutoka. Hakujua ni kwa nini alipatwa na hisia hizo, lakini hisia zake zilimwambia gari hilo linakwenda nyumbani kwa kina Hija.

    Likampita, akagundua ni teksi. Akaliona likielekea ilipo nyumba anayoishi Hija, likasimama nje ya geti la nyumba hiyo. Akawa makini kuangalia ni nani angetoka kwenye teksi hiyo. Akamwona Hija akiteremka na kufunga mlango kisha teksi ikageuza na kurudi kupitia njia iliyokujia.

    Wakati teksi hiyo ikipita ubavuni mwa gari lake, Badi hakuhangaika kuiangalia, macho yake yaliendelea kumwangalia Hija. Alimwona akibonyeza kengele ya getini na kusubiri. Kitendo cha kusubiri kufunguliwa geti, akakiona ungekuwa ni muda mzuri wa kumuwahi palepale nje, lakini hakufanya hivyo! Akili yake iliyokuwa tayari imepata msukumo mpya wa bia alizokunywa, ilikataa kumshauri hivyo.

    Alikuwa amechomwa na mchomo wa wivu. Kitendo cha kurudishwa na teksi kilimtia shaka, akakichukulia ndiyo sababu ya kutopatikana kwake kwenye simu kwa muda wote aliokuwa akimpigia. Dhana yake ililenga kuwa, teksi hiyo alikuwa amekodishiwa na bwana aliyekuwa naye muda wote wakati yeye akihangaika kumtafuta kwenye simu. Akaamini, Hija alikuwa amedhamiria kuizima simu yake kwa sababu hakutaka kusumbuliwa wakati yupo kwa mwanamume aliyekuwa naye.

    Pamoja na kuingiwa na dhana hiyo, lakini hakuondoka hadi alipomwona Hija akifunguliwa geti na kuingia ndani.

    Badi akaliwasha gari lake kwa unyonge na kuligeuza. Safari ndefu ya kurudi Tegeta, kwake ikawa kama safari ya kurudi nyikani!



    ***



    SIKU ya pili akiwa amewasili kazini, Badi aliufikiria usiku uliopita alivyohangaika kitandani kwake kutokana na kumbukumbu za kimahaba zilizomhusisha Hija. Aliyafikiria mahaba mapya aliyofundwa na msichana huyo, kisha akalifikiria tukio la kumwona akiteremka kutoka kwenye teksi. Akajiuliza, kama ni kweli Hija alikuwa ametoka kwa bwana, je, mtu huyo naye alipewa mahaba yaleyale aliyofundwa yeye?

    Wivu ukamchana. Ukaendelea kumwadhibu huku taswira ya umbo zuri la Hija lililokuwa halina nguo nalo likimtesa. Aliamini kwa siku ya jana lilikuwa likitumiwa kumstarehesha mwanamume mwingine. Umbo hilo lenye mvuto usioisha hamu akakumbuka jinsi anavyojivinjari nalo kitandani huku akilifaidi kwa vionjo tofauti. Kumbukumbu hizo ndizo zilizomtesa na kumchelewesha kulala.

    Akiwa na matumaini ya kukutana naye tena kazini, pamoja na ule wivu uliotokana na dhana yake kuwa Hija kwa siku ya jana alikuwa na mwanamume mwingine, lakini alijiona bado ni shababi dhidi ya Nico kwa kumpora msichana huyo mzuri. Akapanga, pindi atakapomwona asubuhi hiyo hapo kazini, aitumie nafasi hiyo kumlalamikia jinsi alivyohangaika kumtafuta kwenye simu na hatimaye ajifanye aliingiwa wasiwasi uliomfanya aende kwao kujua kama yuko salama. Hata hivyo, akajipa angalizo la kutogusia tukio la kumwona akishuka kwenye teksi. Alihofu hoja hiyo ingeweza ikamshusha hadhi kwa kuonekana ana wivu wa kibwege. Hakutaka aonekane kama Nico.

    Akiwa anaendelea na kazi, Badi alianza kuziona dalili za kutoonekana Hija kazini. Dhana hiyo ikaisumbua nafsi yake, ikamkosesha amani kiasi cha kushindwa kuvumilia. Akampigia simu Amin.

    “Hija amekuja kazini?” Badi aliuliza

    “Leo sijamwona, sidhani kama amekuja!” Amin alijibu.

    Jibu hilo likamwondoa Badi kwenye ari ya kufanya kazi, likaiharibu siku yake. Akaingiwa na hofu huenda Hija ameamua kutokuja kazini baada ya kukasirishwa na Nico. Hakuamini kama angeichukua hatua hiyo bila ya kushauriana naye. Wazo hilo likamfanya ajiulize kama ana umuhimu wowote kwa Hija endapo ni kweli ameamua kutofika kazini kwa ajili hiyo na kisha asimfahamishe?

    Swali hilo likaendelea kumuweka kwenye unyonge baada ya kuhisi kuna kasoro kwenye penzi lao. Isingewezekana kwa watu wanaopendana na wanaofanya kazi sehemu moja, kisha mmoja akafanya uamuzi wa kutokuja kazini bila ya kumwambia mwenzake! Hilo aliliona kama ni kituko cha aina yake.

    Tukio hilo likamfanya ajihoji kama Hija yupo kwenye mapenzi ya dhati na yeye? Au yupo kwenye kupita njia? Akazirudisha kumbukumbu za wakati akifanya mapenzi naye. Akayakumbuka matukio ya kumwona Hija akiwa kwenye kupandisha mdadi wakati wakiendelea na starehe hiyo huku akitokwa na maneno yenye kumsifia umahiri aliokuwanao katika shughuli hiyo.

    Kumbukumbu hizo zikawa kama zimemtia utumwani! Kutomwona Hija kazini asubuhi hiyo, akakuchukulia kama aliyekosa kitu muhimu kwenye uhai wake kwa siku hiyo. Akaamua kumpigia simu. Badi hakuamini pale alipoambiwa kwenye ujumbe wa simu kuwa simu anayopiga haipatikani!

    Kutompata Hija kwenye simu kukazidi kumchanganya. Palepale akajipanga atakapotoka kazini alasiri, lazima aende tena Tabata! Lazima akajue kama Hija ana matatizo mengine zaidi ya lile la kugombana na Nico? Na kama litakuwa tatizo ni hilo la Nico ndilo lililomfanya asije kazini, angeichukua nafasi hiyo kumshawishi asiendelee kuchukua uamuzi huo, angemhakikishia Nico asingethubutu tena kumghasi na angemweleza sababu ya kwa nini anamwambia hivyo! Angemwelezea jinsi alivyomwingilia Nico ofisini kwake na kumpa onyo baada ya kumkunja.

    Angekuwa amemwonyesha jinsi anavyomjali!



    *

    Ilipofika alasiri, Badi alijitosa kwenye gari lake na kuianza safari ya Tabata, lakini alipokuwa njiani akapata akili ya kutaka kujaribu tena kumpigia simu Hija. Akapiga, safari hii simu ikaita! Akashangaa!

    “Hai, Badi!” Hija alisema kwenye simu baada ya kupokea.

    Badi akajenga utulivu ndani ya gari. “Hija uko wapi?” aliuliza kwa sauti yenye upole.

    “Niko mjini.”

    “Kwa hiyo hauko nyumbani?”

    “Sipo nyumbani.”

    Badi akataka kumuuliza Hija kwa nini hakuja kazini siku hiyo, lakini bila sababu ya msingi akabadilisha swali hilo. Badala yake akasema, “Nilikuwa nipo njiani kukufuata nyumbani.”

    “Oh, maskini! Mbona sipo nyumbani mpenzi.”

    “Aisii,” Badi alisena kwa sauti iliyonyongea. Aliamini hoja aliyomwambia kuwa yuko njiani kumfuata nyumbani kwao, ingeweza kumkumbushia kuhusu ujio wa jana usiku wa yeye kwenda kwao. Lakini akashangaa kuona Hija hakugusia kitu hicho! Akaingiwa na shaka huenda msichana aliyemfungulia geti, hakumpa salamu hizo.

    “Jana nilikuja kwenu,” ilibidi Badi ajieleze.

    “Mdogo wangu aliniambia!” Hija alisema kwa sauti iliyoonyesha kama ameongea jambo la kawaida.

    Mungu wangu! Badi alihamanika. Hakuamini alichokuwa amekisikia. Kumbe alikuwa nazo! Kwa nini asizigusie mpaka nilivyomuuliza? Akasikitika peke yake.

    “Basi poa,” Badi alisema kwa sauti iliyonyongea tena. “Nilitaka tu kukusalimia.” Mdadi wote aliokuwa nao wa kutaka kumwona Hija, ukamwishia!

    “Badi umekasirika?” Hija aliuliza ghafla.

    Swali hilo likamyumbisha Badi kwa sekunde chache. Hakujiandaa nalo na asingekuwa tayari kukiri kuwa ni kweli alikuwa amekasirika!

    “Ee..e..kwa nini unaniuliza hivyo?” Badi alibabaika na kujikuta akiuliza swali badala ya kujibu.

    Ikawa kama vile alimdhihirishia Hija ni kweli alikuwa amekasirika!

    “Najua umekasirika!” Hija alisema.

    Badi akataka kukiri kama njia ya kumtambulisha Hija kuwa amechukia, lakini palepale akajiuliza, atakiri kwa kipi alichokizungumza hadi Hija ajue kuwa amekasirika?

    “Nikasirike kwa ajili ya nini?” Badi alipotezea.

    “Najua umekasirika!” Hija alisema kwa msisitizo. “Hata kama hutaki kukiri…lakini sawa kama umeamua hivyo!” alimalizia kwa sauti iliyokata tamaa.

    Badi alishtuka baada ya kugundua simu ilikuwa imekatwa! Tukio hilo likamsumbua kiakili. Kukatwa kwa simu kukamfanya ajiulize, Hija alikuwa akimlaumu au alikuwa akimlalamikia? Kama ni kumlaumu, alimlaumu kwa kitu gani? Ni wazi alikuwa akiyajua makosa yake!

    Badi akataka kumpigia tena Hija ili aweke mambo sawa kwa kusisitiza kumwambia kuwa hajakasirika. Lakini palepale akajipa angalizo kuwa asiwe mwepesi wa kukiri kabla hajapata ufafanuzi kutoka kwa Hija kwa nini amwone yeye amekasirika?

    Akaghairi kupiga simu aliyotaka kupiga baada ya kuingiwa na wazo lililoanza kumsumbua. Alihofu alikuwa amejiingiza kwenye uhusiano wa mapenzi na msichana ambaye si mwaminifu!



    ***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ILIKUWA kama sumu aliyoinywa, ikawa inamwadhibu kabla ya kumuua.

    Badi alibadilisha mwelekeo wa awali aliokuwa nao wa kwenda Tabata, akaamua kwenda Kinondoni walipo wazazi wake, kisha akaenda kwenye baa ya hapo Kinondoni ambayo kabla ya kuhamia Tegeta aliitumia sana kunywea na rafiki zake.

    Alikutana na rafiki zake wa zamani na kunywa nao bia. Wakazungumza hili na lile, kuanzia mambo ya kisiasa na hatimaye ushabiki wa kimpira wa vilabu vya nyumbani na vile vya Ulaya huku oda za vinywaji zikimiminika. Wakati wote huo, Badi alishindwa kumpotezea Hija mawazoni!

    Kuna kipindi alikuwa akishiriki vizuri ubishano unaojitokeza kwenye meza yao kwa kujenga hoja za hapa na pale, lakini kuna wakati alionekana kuhama kimawazo na kujikita kumfikiria Hija! Kulikuwa na ukweli nafsini mwake ambao aliupinga. Aliupinga kwa sababu alikwishajionya kuwa asiendelee kuwa na uhusiano na Hija, lakini upande wa pili wa onyo lake ulikuwa ukikinzana na hofu ya wazi iliyomwogopesha kuwa, alikwishazama kwenye penzi la msichana huyo!

    Badi alirejewa na kumbukumbu za mahaba waliyokuwa wakipeana kitandani na Hija. Alikiri ni kweli msichana huyo alikuwa mtundu kwenye shughuli hizo na kulikuwa na burudani aliyokuwa akiipata kutokana na vionjo ambavyo hakuwahi kufanyiwa na mwanamke mwingine. Lakini upande wa pili wa fikra zake ukawa unamthibitishia kitu kimoja, kwa umri wa Hija na utukutu wa kitandani aliokuwanao, vilikuwa vitu viwili tofauti! Hija alikuwa akiyajua mambo yaliyomzidi umri wake. Hilo ndilo lililomuweka kwenye taswira ya kumwona Hija huenda si mwaminifu!

    Kwa kipindi kifupi tokea aanze kujuana na Hija, aligundua msichana huyo alikuwa akivaa mavazi ya gharama kubwa na vito vya thamani huku manukato anayonukia ni yale yenye kuuzwa bei ghali. Vitu vyote hivyo vilikuwa haviendani na mwonekano uliopo. Hija alikuja hotelini hapo akiwa mwanafunzi aliyetoka kwenye Chuo cha Utalii kinachofundisha taaluma za kihoteli, akisomea mafunzo ya umeneja. Na kutokana na maelezo yake mwenyewe Hija, ni kwamba alijiunga na chuo hicho baada ya kuhitimu masomo yaliyomfikisha kidato cha sita. Hii ilidhihirisha kitu kimoja; Hija hakuwahi kuingia kwenye ajira hadi anakuja hapo hotelini! Kwa vigezo hivyo, pamoja na kwamba baba yake ni mkurugenzi wa kampuni, bado asingeweza kumiliki mavazi ya thamani anayovaa bila ya kuwepo kwa chanzo kingine cha pesa! Ni kipi?

    Huo ulikuwa ni mlinganisho wa kuwa mwanafunzi na thamani ya mavazi yake! Lakini kwa upande wa tabia, hisia za kwanza kumuweka Badi kwenye shaka ni kule kwenda nyumbani kwa kina Hija usiku wa jana, siku ambayo Hija alikuwa hapatikani kwenye simu yake. Kilichomshangaza ni kule kumwona Hija akirudi na teksi nyumbani kwao usiku ukiwa umeshaingia. Alikuwa wapi mchana kutwa? Swali hilo likamuweka kwenye shaka huenda Hija alikuwa na mwanamume kwa muda wote aliokuwa hapatikani!





    Hofu hiyo ya kuwa Hija ana bwana haikumsumbua sana. Kuanzisha naye uhusiano wa mapenzi hakukumaanisha angemkuta bikira, lakini kilichomshtua ni umri wa msichana huyo na utundu wake kwenye mambo ya mahaba vilikuwa vikitofautiana. Badi alikiri ni kweli umri aliokuwanao Hija ulimruhusu awe na uamuzi wake, hakuwa chini ya umri. Umri huo ulimruhusu ajihusishe na mambo ya mapenzi, lakini kilichomshangaza ni uzoefu wa msichana huyo kwenye mambo hayo ambao ulikuwa ni wa kiwango cha juu kiasi cha kumchanganya mwanamume yeyote kama anavyochanganyikiwa yeye! Kwa haraka haraka, Badi akahisi upo uwezekano Hija akawa anajihusisha na ukahaba wa kutembea na raia wa kigeni kwenye mizunguko yake! Hapo ndipo alipojionya awe mwangalifu naye!

    Badi alikiri, kiumri yeye ni mkubwa kuliko Hija, lakini kwenye suala la mahaba, Hija alikuwa gwiji kuliko yeye!



    ***



    BADI aliondoka Kinondoni akiwa amelewa, aliagana na rafiki zake na kuingia kwenye gari. Muda alioondoka aliufurahia kutokana na kutokuwepo kwa foleni barabarani, akaliendesha gari lake kwa kasi na kuchukua dakika chache kuwasili nyumbani kwake. Akalisimamisha gari nje ya geti na kupiga honi.

    Mdogo wake anayeitwa Hassan akalifungua geti huku akiwa kifua wazi na chini amevaa bukta. Badi aliliingiza gari ndani na kuliegesha huku mdogo wake akilifunga geti.

    Badi alitoka kwenye gari, akayumba kidogo kutokana na ulevi, lakini alimudu kujirudisha kwenye mhimili wa kuwa sawa. Hakuyumba tena. Akamwona mdogo wake akija, lakini hakumsubiri. Alijua wangezungumza baada ya kufika ndani.

    “Kaka!” Hassan aliita wakati Badi akielekea mlangoni.

    Badi akageuka na kumwangalia mdogo wake bila ya kutamka lolote.

    “Yuko ndani!” Hassan alisema.

    “Nani?” Badi aliuliza akiwa amesimama.

    “Hija!”

    Badi akawa kimya kwa sekunde kadhaa kama mwenye kutafakari.

    “Amekuja saa ngapi?” Badi aliuliza akiwa bado amesimama vilevile.

    “Kwenye muda wa saa mbili hivi.”

    Badi akaangalia kwenye mlango kama vile alitarajia angemwona Hija amesimama hapo mlangoni. “Ameletwa na usafiri gani?” aliuliza.

    “Sijui. Nilimsikia alipogonga kengele, nikaenda kumfungulia. Lakini sikuona gari.”

    “Sawa,” Badi alisema na kuelekea mlangoni.

    Alimkuta Hija akiwa chumbani. Akatambua alipewa ufunguo wa chumbani na Hassani aliyekuwa na ufunguo wa akiba. Mara alipoingia chumbani, chumba kilitawaliwa na harufu ya manukato anayopendelea kujipaka Hija.

    Hija alikuwa amevaa gauni la kulalia jeupe lililoonyesha maungo yake ya ndani ambalo alikuja nalo. Chupi yake ilionekana wakati alipoinuka kutoka kitandani baada ya Badi kuingia. Macho ya Badi yakaiona chupi hiyo, lakini hayakuishia hapo, yakaangalia matiti yaliyosimama na yaliyotuna. Mng’ao wa ngozi ya juu iliyolainika ya matiti hayo ulionekana kama maembe dodo mawili yaliyobadilika rangi kutokana na kuiva huku sehemu ya nguo eneo la kifuani likiwa limeinuliwa na chuchu zilizosimama. Badi akameza mate kama vile alikuwa akimeza kitu kigumu.

    Hija akamwangalia Badi machoni. Badi akayakwepesha macho yake.

    “Mbona umechelewa?” Hija alimuuliza Badi kwa sauti ya kudeka, hafifu iliyokuwa kama ikipata tabu ya kupumua huku akivifungua vishikizo vya shati kwa taratibu na kwa uangalifu kama vile anakunjua karatasi laini ya kujifutia mdomo iliyokuwa imelowana na maji.

    “Tena umelewa!” sauti ya mahaba ya Hija ikamalizia.

    Badi aliyekuwa amesimama wakati shughuli hiyo ikiendelea, ghafla alijikunja na kukikwepesha kifua chake kwa kukirudisha ndani baada ya vidole viwili vya Hija kuzikamata na kuzifikicha kwa ulaini chuchu zake.

    Hija akaendelea na shughuli hiyo baada ya mkono wake mmoja kuuzungusha mgongoni kwa Badi na kumzuia asiendelee kujikunja. Badi akaanza kuzitafuta pumzi zake kwa shida, akajaribu kuuondoa mkono wa Hija kutoka kwenye chuchu iliyokuwa ikichezewa. Hija akauzuia mkono uliokuwa ukimzuia kwa kutumia mkono wake mwingine. Badi akatii mkono wake kuondolewa, akaviacha vidole vya Hija viendelee na shughuli iliyokuwepo huku yeye mwenyewe akizipandisha na kuzirudisha pumzi kwa kugugumia. Hatimaye akashindwa kuvumilia, akaupeleka mdomo wake kinywani mwa Hija na ndimi zao kunyonyana.

    “Niache kwanza nikaoge!” Badi alisema kwa sauti iliyokwishapoteza dira baada ya kuutoa ulimi wake.

    “Utaoga baadaye!” Hija alijibu na kuurudisha ulimi wake kinywani mwa Badi.

    Kama hiyo haikutosha, mkono wa Hija ukaenda kuufungua mkanda wa suruali ya Badi, kisha akaivuta chini zipu ya suruali hiyo na yeye mwenyewe akapiga magoti huku kiganja chake kikipenya kwenye nguo ya ndani aliyovaa Badi…

    Sekunde chache baadaye, Badi alihisi kama anayezamishwa kwenye maji!



    ***



    KUKWIDWA akiwa na suti yake na kisha kusukumwa na kutua kama mzigo kwenye kiti chake cha ofisini ni kitendo kilichomwumiza Nico kila alipokifikiria. Laiti angekuwa amekulia kwenye maisha ya kujichanganya udogoni mwake, kitendo alichofanyiwa na Badi angekijibu palepale kwa kurusha ngumi. Lakini hakuweza kufanya hivyo kwa sababu hakujiamini. Laiti angejiamini, angeweza hata kujibu mkwara aliowekewa na Badi mle ofisini.

    Unyonge wake wa kutojua kupigana hata zile ngumi za mitaani ukamtia kinyaa. Alijisikitikia kujiona ni kijana ambaye alipaswa angalau awe na uwezo wa kujitetea kiugomvi japo kwa sekunde chache za kuchachamaa. Woga aliokuwa nao wakati akikunjwa alihisi huenda Badi aliugundua! Wazo hilo likamzidishia unyonge, akajisikia vibaya baada ya kugundulika na mwanamume mwenzake kuwa ni mwoga!

    Hilo likampa hofu. Kubaini kuwa Badi amegundua amemwogopa, huenda udhaifu huo Badi angeendelea kuutumia kumwonea. Wazo hilo lilimwumiza kila alipolifikiria na kumhadharisha kwamba, endapo hilo litatokea, basi asingekuwa na tofauti yoyote na mwanamume ambaye ni shoga! Na si kwamba angemwogopa tu Badi, lakini pia angekuwa mwenye aibu popote pale ambako wangekutana uso kwa uso!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaapa hilo halitoweza kutokea! Wazo hilo likamtia ujasiri wa kutaka kuuondoa unyonge huo, ujasiri ambao Badi atautambua! Akajiapiza lazima awe anafanya mazoezi ya kubeba vitu vizito, lakini pia akafikiria kujifunza karate kwenye chuo kinachofundisha mchezo huo kilichopo maeneo ya Upanga. Kusudio likawa ni kupambana na Badi!

    Yote hayo yalimjia kichwani kwake, lakini pia akatamani ungetokea muujiza wa kuhitimu mazoezi hayo ndani ya siku chache wakati hasira zake zikiwa bado zingalipo! Alijua Badi angemwelezea Hija tukio hilo, tena kwa tambo za ujivuni kuwa amemkomesha! Lakini akatambua tambo hizo hazitaishia kwa Hija peke yake, bali zingesambaa hadi kwa wafanyakazi wa hotelini! Fedheha!

    Wazo hilo likamchanganya! Akajiapiza, lazima alipize kisasi! Akayaona mazoezi anayotaka kuyafanya yangemchukua zaidi ya mwezi mmoja kumwezesha kuwa mahiri wa kuja kupambana na Badi. Akautafakari muda huo utakavyokuwa mrefu kwake kwa kuendelea kudharauliwa na watu hao wawili, Hija na Badi! Lakini pia na wafanyakazi! Asingeweza kuvumilia kwa muda wote huo! Ungekuwa ni muda mrefu wa kusanifiwa na watu hao!

    Lazima atafute njia mbadala na ya haraka kumwonyesha Badi kuwa, alikosea kumchezea!



    ***



    BADI aliamka mapema asubuhi kama ilivyo kawaida yake, lakini asubuhi hii akiwa ameamka tofauti. Hakutamani kwenda kazini! Aliamka akiwa amechoka, Hija alimchosha!

    Aligeuka na kumwangalia Hija aliyekuwa bado amelala. Akamwamsha. Hija akaitikia kwa kugugumia, lakini hakuamka. Badi akamwangalia Hija kwa sekunde chache ambaye aliendelea kulala na kuonekana kuwa na usingizi mzito. Akatabasamu peke yake na kuiondoa shuka mwilini, akateremka kutoka kitandani.

    Akapanga kumwamsha tena atakapomaliza kuoga. Usiku uliopita walikubaliana asubuhi waende pamoja kazini baada ya Badi kumshawishi kwa kulielezea tukio la kumkunja Nico ofisini kwake na kuielezea taswira ya Nico ilivyokuwa baada ya kumuwekea mkwara.

    “Hatokugusa tena!” Badi alimhakikishia Hija.

    “Mi’ nilishaamua nisiwe nakwenda tena!” Hija alisema.

    “Usiende kwa ajili ya bwege yule?” Badi aliuliza kwa dharau. “Mimi nakuhakikishia hatorudia tena kukuparamia-paramia. Wewe kesho asubuhi twende kazini kama kawaida na hatokufanya lolote!”

    Wakakubaliana usiku huo kuwa asubuhi waongozane pamoja kwenda kazini.

    Badi alirudi kutoka kuoga, akamkuta Hija akiendelea kuchapa usingizi.

    “Hija! Hija!” Badi alimwamsha Hija huku akimtingisha.

    Ilikuwa mbinde, lakini hatimaye Hija aliamka huku akilalamikia kuamshwa. Akaenda kuoga huku akiendelea kulalamika.

    Hatimaye watu hao wawili wakaingia kwenye gari na kuelekea kazini.



    *

    Ujio wa Hija wa kurudi kazini ulikuwa wa kimyakimya ingawa baadhi ya wafanyakazi walimsikitikia kutokana na unyanyasaji aliokwishaupata. Lawama zikawa zinamshukia Nico waliyemwona analazimisha penzi. Tukio la Badi kumkunja Nico halikuzungumzwa kwa sababu hakukuwa na mfanyakazi yeyote aliyeliona au kuambiwa.

    Akiwa kazini, Hija alikutana na Nico kwenye bwawa la kuogelea. Moyo wa Hija ukalipuka! Akayakwepesha macho yake na kutaka kumpita Nico. Nico akamzuia kwa kumshika bega.

    “Nataka uniletee breakfast yangu ofisini!” Nico alimwambia Hija. “Mwone Amin anayo oda yangu!”

    Ilikuwa amri! Hija hakujibu, akaondoka kimyakimya.

    Akionyesha kuridhika na agizo lake alilotoa, Nico alitembea kwa mikogo ya kutumbukiza mkono mmoja mfukoni huku mkono mwingine ukichezesha kichanja kilichobeba funguo nyingi alizozibeba kiganjani mwake na wakati huohuo akipiga mruzi mwembamba wenye mirindimo ya nyimbo ya Kizungu.

    Baada ya kupiga hatua kadhaa, Hija aligeuka na kumwangalia Nico aliyekuwa akitembea kandokando ya bwawa hilo huku akiyaangalia maji ya kuogelea kwa kuipindisha shingo yake kijivuni.

    Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na hali hiyo ya kutaharuki kwa sababu ya kukutana na Nico ana kwa ana. Kabla ya hapo hakuwahi kumwogopa. Hakujua kwa nini alitaharuki wakati alishatolewa wasiwasi na Badi. Hata hivyo akagundua hali hiyo imetokana na hisia za uadui zilizojijenga dhidi yake.

    Oda aliyopewa ilikuwa lazima aipeleke kwa sababu aliyemwagiza ni bosi wake. Hakujua ni kitu gani alichokusudiwa kufanyiwa na Nico wakati atakapoingia ofisini kwake. Pamoja na kutojua, lakini aliamini kuna dhamira inayokusudiwa kufanywa na mtu huyo!

    Msukumo wa kutaka kumwelezea Badi jambo hilo ukampata. Akataka kumwendea mapokezi, lakini nafsi yake ikasita. Aliihofia dhana aliyokuwanayo dhidi ya Nico huenda haiko sahihi na taarifa ambazo angemweleza Badi zingeweza kuleta rabsha hapo kazini na zingemgharimu yeye na Badi. Akaamua kutomhusisha Badi kwenye suala hilo la oda aliyopewa. Akapanga kutoipeleka oda hiyo!

    Hija alifika mgahawani na alijua anapaswa kuufikisha ujumbe aliopewa na Nico kwa Mkuu wa Restaurant, Amin. Akaamua alipotezee suala hilo huku imani yake ikimwaminisha kuwa, wakati Amin akipewa oda hiyo na Nico, Amin hakuelekezwa ni mhudumu gani wa kumpa kuipeleka ofisini kwa Nico, hivyo akaona autumie mwanya huo kukaa kimya!

    “Hija!” kiongozi mwingine wa wahudumu wa mgahawa alimwita Hija baada ya kumwona.

    Hija akaitikia.

    “Bosi Amin ametoka kukuulizia sasa hivi!”

    Kabla Hija hajajibu, Amin akatokezea kutoka jikoni. “Hija!” aliita. “Kuna oda yako iko jikoni, nenda kaichukue uipeleke ofisini kwa meneja Nico!”

    Hija akaishiwa nguvu zote!



    ***





    ***



    Ofisi za Utawala zote zilikuwa kwenye korido moja. Ni ofisi mbili tu kati ya hizo zilizokuwa na Makatibu Muhtasi, moja ikiwa ni ofisi ya Meneja Mkuu na nyingine ni ofisi ya Meneja wa Vyakula na Vinywaji ambaye pia alikuwa ni Meneja Mkuu Msaidizi. Ofisi ya Meneja wa Vyakula na Vinywaji Msaidizi ambaye hutumiwa na Nico, haikuwa na Katibu Muhtasi.

    Akiwa ofisini kwake, Nico alimsubiri kwa hamu Hija aje na oda aliyomwagiza huku akikumbuka muda mfupi uliopita baada ya kuonana na Hija na kurudi ofisini kwake, alimpigia simu Amin na kumwagiza kwa msisitizo kuwa, oda aliyomwachia ya kifungua kinywa chake apewe Hija na ailete ofisini!

    Awali alipokuwa ameiagiza oda hiyo kupitia kwa Amin, alitarajia Amin angemtuma mhudumu yeyote kuileta ofisini. Lakini akiwa yuko kwenye maeneo yanayozunguka bwawa la kuogelea kwa ajili ya kuangalia mazingira ya eneo hilo hasa usafi, ndipo akamwona Hija akija upande lilipo bwawa hilo. Hapo akajiwa na wazo la kumtumia Hija ailete oda hiyo kwa sababu maalum!

    Alipanga kumtumia Hija kama ngao yake dhidi ya uovu aliodhamiria kumfanyia Badi! Nico aliamini uovu anaotaka kumfanyia Badi ungeweza kufanikiwa vizuri endapo Hija angetumika na ingemwepusha kuja kunyooshewa kidole pindi njama hizo zitakapofanikiwa!

    Akiwa amejiridhisha na uamuzi wa kumtumia Hija, Nico alijiweka vizuri kwenye meza yake na kuanza kujipanga namna ya kumpokea msichana huyo pindi tu atakapowasili humo ofisini!



    ***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    HIJA alishusha pumzi kwa nguvu na kujiona yupo kwenye mtihani mpya baada ya kuona kuna mwingilio wa mkuu wake wa kazi kumhimiza aipeleke oda hiyo kwa Nico! Alijua uhimizaji huo ulisukumwa na Nico mwenyewe kumtumia Amin kuhakikisha oda hiyo anapewa yeye! Kwa maana nyingine, asingeendelea kuikacha oda hiyo!

    Kilichomwingiza hofu Hija ni kutoijua dhamira ya Nico kuhimiza oda hiyo apewe yeye. Alikuwa na uhakika kuwa Nico anafahamu kuwa yeye anajua kuwa Badi alimwingilia ofisini na kumkunja kutaka kumpiga! Hakuelewa kwa nini kama angekuwa anafahamu hilo kisha bado aendelee kumfuatafuata? Anataka alipize kisasi kupitia kwake? Hija alijiuliza. Anataka kumbaka? Hija akaingiwa na hofu huenda mtu huyo angeweza hata kumpiga akiwa ofisini kwake!

    Akataka kuielezea hofu yake kwa Amin. Alitaka pindi akiipeleka oda hiyo, basi kuwepo na watu wa kusikilizia wakati atakapokuwa ofisini kwa Nico. Hata hivyo alishindwa kulitekeleza hilo baada ya kujiona angekuwa na wakati mgumu wa kujieleza na kueleweka!

    “Oda yako ipo jikoni inaandaliwa,” Amin alimwambia Hija.

    Baada ya dakika chache, oda hiyo ikawa imeshaandaliwa jikoni na Hija akatakiwa kwenda kuichukua tayari kuipeleka ofisini.

    Hija alikwenda jikoni, akakabidhiwa tray yenye kifungua kinywa cha kupeleka kwa Nico.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog