Search This Blog

Thursday, 27 October 2022

KAHABA YUAN LIANG - 5

 









    Simulizi : Kahaba Yuan Liang

    Sehemu Ya Tano (5)





    Mexic;



           Kundi la majambazi, kundi la Casabranka gang, waliendesha msako mzito, nyumba zote za kulala wageni, katika mji mdogo wa Mexic. Mkononi walikuwa na picha ya Yuan Liang, picha ambayo waliichukua katika akaunti yake ya instagramu.



    “,Nawambia tutakesha, tutakesha! mimi nashauri, angalieni kwenye akaunti yake ya instagram, bila shaka ameweka namba ya biashara yake ya ukahaba, tujifanye kama wateja,tujue yuko mahali gani,tukamfyekelee mbali…”,mmoja kati ya vijana ishirini,vijana wa Kasabranka gang walioenda kumsaka Yuan Liang alitoa ushauri,baada ya kupekua hoteli zote bila mafanikio.



    Ikulu;



         Hali ya raisi Jonsoni Mtemvu ilikua mbaya sana,chumba cha siri alichokuwa anafanyiwa matibabu awali kilikuwa kimevurugika, damu ilitapakaa kila kona, huku dirisha likiwa limepasuliwa kitaalamu na kumuwezesha adui kutokomea.Askari walimnyenyua mheshimiwa raisi, akahamishiwa chumba kingine, madaktari bingwa wanne, wawili wazungu, mmoja muhindi, na wa mwisho muafrika. Kila mmoja alikua bize akijitahidi kuokoa maisha ya raisi wa nchi ya Goshani, bwana Jonsoni Mtemvu.



    “,Ana high blood pressure,isitoshe anapumua kwa shida sanaa! “,daktari wa kihindi aliyefanya kazi idara ya afya serikalini, kwa mika takribani kumi aliongea.



    “,Vipi kuhusu picha ya X-ray aliyopigwa, majibu yanasemaje! “,daktari wa kizungu, daktari mkuu wa raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.



    “,Hana tatizo,bila shaka ameteguliwa, hajavunjwa mahala popote pale! “,daktari aliyekuwa amevalia suti nyeusi, suti iliyofanana na rangi ya ngozi yake aliongea,akatoa maelezo ya kina, wote wakatikisa vichwa, walikubaliana na ripoti aliyoitoa, wote wakiwa wamezunguka kitanda cha raisi.



    “,OK,tatizo kubwa ni hili la difficult in breathing, tuhakikishe upumuaji wake unarudi katika hali ya kawaida, blood pressure ya mwili wake iwe normal kufikia saa mbili asubuhi, bila shaka ulimwengu wote utataka kusikia ripoti kuhusu afya ya raisi wetu,! “,daktari wa kizungu aliongea,kisha wote wakaanza kazi,nje ya chumba kipya cha matibabu ya raisi, askari kumi wenye silaha nzito walikuwa makini kudumisha ulinzi,hakuna mtu yoyote aliruhusiwa kusogelea chumba hiki bila kitambulisho pamoja na sababu maalumu.



    …………………………………



    2;20am



          Kamanda Kendrick aliongoza msafara,askari wezanke wakamfuata nyuma yake,huku mwisho kabisa mama Zainath akiwa amefunga kanga yake kiunoni, akitoa ushirikiano wa hali ya juu kwa wapelelezi hawa, wenye siku moja tu nchini Goshani. Wakapanda ngazi, wakafika ghorofani, uso kwa uso na damu nzito ambayo haikusafishwa makusudi, kwa ajili ya uchunguzi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Hapa ndipo kulikuwa na maiti ya askari  wetu, alipigwa risasi kichwani! “,mama Zainath aliongea,sura yake ikiwa haina hata chembe ya tabasamu.



    “,Wakati anapigwa risasi nyie mlikua mahali gani! “,kamanda Catherine aliuliza.



    “,Tulikuwa tumefungiwa chooni, mimi pamoja na askari wawili wa ulinzi, ndipo baada ya tukio kukamilika, adui akiwa ameshatoroka, kamanda Junior pamoja na kamanda Amiry walikuja kututoa chooni kwa kuvunja kitasa cha mlango! “,mama Zainath aliendelea kuongea kwa huzuni.



    “,Hawa askari inabidi wahojiwe, inawezekana wanahusika, kuna jambo wanafahamu, haiwezekani tukio la kwanza litokee wakiwepo halafu wasijeruhiwe, tukio la pili vivyo hivyo! lazima tuwahoji kwa mara nyingine tena! “,kamanda Kendrick aliongea..



    “,Kweli kabisa afande, lakini tayali wameshakamatwa na kuwekwa rumande! “,mama Zainath aliongea.



    “,Basi ni vizuri, kesho tutafanya nao mahojiano, watapata mateso makali mpaka watasema ukweli! “,kamanda Kendrick aliongea, alikuwa na hasira sana,wote kwa pamoja wakaingia ndani ya chumba cha siri, chumba alichokuwa anapatiwa matibabu muheshimiwa raisi, kabla ya tukio.



    “,The same person, the same killer, muuaji ni yule yule, ona visigino vya viatu vyake, ona jinsi alivyokata kioo, kama alivyofanya hotelini ……”,kamanda Catherine aliongea, wote wakatikisa vichwa, viatu vya Yuan Liang vilionekana kukanyaga damu baada ya askari kupigwa na risasi,kila alipokanyaga, mpaka eneo la dirishani alipotorokea, kulikuwa na alama za visigino vya viatu vyenye damu, wakapata majibu haraka sana!



    “,Mama usjali, masaa kumi yajayo tutakua tumemtia nguvuni, aliyefanya tukio hili ndiye aliyefanya na hili tukio lililopita,ngoja tukamtafute adui, lakini tutapaswa kufanya mahojiano na mume wako akipata nafuu, inaonekana kuna siri nzito imefichwa hapa katikati, inawezekana tatizo sio diski, kutakuwa na jambo lingine kabisa linaloibua matukio yote haya! “,kamanda Kendrick aliongea, akaanza kutoka nje, askari wote wakamfuata,safari ya kumsaka adui ikaanza haraka iwezekanavyo.



    Walishuka ghorofa ya ikulu kama wendawazimu, wakatoka nje ya jengo la ikulu, wakajipakia ndani ya difenda yao, kamanda Gupta akakamatilia uskani.



    “,Kamanda Philipo pamoja na Catherine fanya majukumu yenu, tumieni kompyuta yenu kujua lokesheni ya diski kwa sasa! ,kamanda Gupta ondoa gari mahali hapa, tutajua tunaelekea wapi mbele kwa mbele, tutakapo fahamu mahali adui alipo  “,kamanda Kendrick aliongea, kila askari akatimiza majukumu yake kama alivyo elekezwa. Kamanda Gupta akawasha gari, geti likafunguliwa, akaliondoa gari kwa kasi, akawaacha midomo wazi waandishi wa habari ambao walisimama nje ya geti la ikulu kwa ajili ya kukusanya taarifa, kuwahoji watu mbalimbali walioingia  na kutoka ikulu…



    ” ,Connected!, the related disc is available in Mexic …”,(imeunganishwa, diski inayohusiana inapatikana Mexic) “,ujumbe ulisomeka kwa mara nyingine tena katika kompyuta ya the super three soldiers,mara baada ya kamanda Catherine kuunganisha saa ya raisi na kompyuta yao, wakatambua mahali diski ya raisi ilipo, mahali ambapo adui alikuwa anapatikana.



    “,Kendrick! mashine yetu inaonesha adui yuko Mexic! “,Catherine aliongea.



    “,Duuuh huyu mwanamke ni hatari sana! muda huu kafanya tukio na tayali yuko Mexic! ,anyway, Gupta nazani umesikia, kanyaga mafuta kuelekea Mexic haraka iwezekanavyo! “,kamanda Kendrick aliongea, akionekana kushangazwa na mbinu mbalimbali alizokuwa anatumia adui kwenye shughuli zake.



    “,Nimesikia afande! dakika ishirini tu,tutakua tayali tumetia nanga! “,Gupta alijibu, macho yake yakitazama mita mia moja mbele, akikwepa na kuovateki magari makubwa barabarani, akapenya katikati ya magari, huku king’ora cha gari yake kikimsaidia kuwataarifu madereva wa magari mengine kukaa mbali na gari lake. Alikuwa dereva mzuri kwenye mashindano ya olimpiki mwaka 2005,akatwaa taji kama dereva namba moja wa dunia, serikali ya Goshani ikampenda, ikampatia pesa nyingi, ikamuajiri kama dereva mkuu wa jeshi, akiwa kitengo cha upelelezi …



    …………………………………



    Mexic; Nusu saa iliyopita



                 Kundi la majambazi la Casabranka gang walitabasamu, walifanikiwa kupata namba ya simu, namba ya kahaba Yuan Liang kupitia akaunti yake ya instagramu, wakakopi namba, wakampigia.



          “,Haloo! mimi raia ya kigeni, iko toka Italiano, mimi taka penzi lako, iko lipa wewe dola mia tano kwa saa moja, this night, before morning! “,jibaba la mlango wa kasino, kasino la Kasabranka liliigiza sauti,baada ya kumpigia Yuan Liang.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Ok, kwangu nahitaji pesa tu! njoo, niko Mexic, but hata mimi nimeigiza sana drama kama hizo za kujibadirisha sauti, kubadirisha nchi yangu n. K, kwahiyo kama umetumwa, una lengo baya na mimi, nitakuua! “,sauti ya simu ilisikika.



    “,ok mama, no problem! wewe iko hoteli gani, chumba namba ngapi ?”,jambazi liliuliza tena, likijitahidi kuigiza sauti na rafudhi ya kigeni, lisije likashtukiwa.



    “,Niko chumba namba tano, hoteli ya Mtakuja,pembeni ya barabara kuu, mwanzoni mwa mji mdogo wa Mexic! “,sauti ya simu ilisikika.



    “,Ok mama, mimi kuja hapo now, wewe nipa penzi zuri, mimi kupa wewe mapesa mingi, a lot of money!……”,jambazi liliongea,likakata simu,kundi lote likatabasamu kwa furaha, wakajipakia katika pikipiki zao, wakatoka katika hoteli ya Suncity mwisho wa mji wa Mexic,baada ya kukagua bila mafanikio na kumaliza hoteli kubwa za mji wote, wakaanza kurudi katika hoteli ya hadhi ya chini, waliyoelekezwa na Yuan Liang.



    …………………………………



    Mexic; 3;01am



            Kahaba Yuan Liang alikuwa na masaa takribani mawili akiwa amekamilisha kazi na kurejea Mexic katika makazi yake, ndani ya hoteli ya hali cha chini. Alijaribu kulala, kujipumzisha katika kitanda chake, lakini malengo yake yakashindwa kukamilika,alipigiwa simu ya kwanza, akakurupuka usingizini, akaipokea, akazungumza na baada ya mazungumzo akalala tena, saa moja likapita, akapigiwa tena, akakurupuka usingizini, akapokea simu, watu wawili wenye malengo ya kufanana walimpigia kwa muda uliokaribiana, akatafakari, machale yakamcheza …



    “,Kuna kitu, huu ni mtego sio bure,siwezi kukaa hapa tena!, ngoja niondoke, napaswa kuondoka mahali hapa, napaswa kukaa sehemu ambayo itaniwezesha kuona mtu yoyote atakaye sogea hotelini hapa kunitafuta …”,Yuan Liang aliongea, huku akitafakari haraka haraka, akapata jibu.



    “,Ngoja nikakae na ombaomba hapo barabarani, nitajivika gunia, mizigo yangu na pikipiki yangu nitaipaki hapo sheli, kando ya barabara, nitalipa pesa, watanihifadhiaa katika pakingi yao,kama ni maadui nitawatandika, kisha nitaelekea kwenye sheli, nitachukua pikipiki yangu, nitatoweka! “,Yuan Liang alimaliza kutafakari,alimaliza kupiga mahesabu mazito ndani ya kichwa chake, akanyanyuka kitandani, akafungasha virago vyake, akatoka nje ya chumba chake, akiwa na kila kilicho chake mkononi …



    Mexic; 4;02



            Yuan Liang alikuwa amebeba mabegi yake,koti lake kubwa lilikuwa mwilini mwake, akatoka katika hoteli ya Mtakuja,akiwa amepania kuihama hoteli hii na kutokomea mbali,atakapomaliza kuwatandika maadui zake.



    “,usiku huu unaelekea wapi mwanangu? “,mama muhudumu na mmiliki wa hoteli ya Mtakuja, hoteli isiyokuwa na madirisha ya vioo, huku pazia chakavu zikiipamba milango yote ya hoteli hii yenye vyumba vitano tu vya kulala wageni, alimuuliza swali Yuan Liang baada ya kukutana naye uso kwa uso ,akiwa anafanya usafi, majira ya asubuhi …



    “,Naondoka! asante kwa huduma zako, lakini kuna watu wanaweza kufika hapa kunitafuta,siunajua kazi zetu za kiaskari bwanaa! watakao niulizia waambie nimeondokaa, nimehama hoteli, ikiwezekana waonyeshe hata chumba nilichokuwa nalala, usionyeshe jeuli yoyote ile, watakuua! “,Yuan Liang alimpatia maelekezo mama yule, akaisogelea pikipiki yake, akapakia mabegi yake, akawasha pikipiki, akatokomea, huku akimwachia maswali mengi mama yule yasiyokuwa na majibu.



    “,Sawa mwanangu, Mungu akulinde! “,mama yule liongea, akaendelea na shughuli zake za usafi.



    Yuan Liang aliwasha pikipiki yake, akavuka barabara upande wa pili, akaingiza pikipiki yake katika sheli, “PURE OIL “,kibao cha sheli kilisomeka,akasimamisha pikipiki yake, akashuka, akatembea kwa mwendo wa haraka, akazisogelea ofisi za sheli …



    “,Naomba mnihifadhie pikipiki yangu, shilingi ngapi bosi? “,Yuan Liang aliuliza, macho yake yakimtazama muhudumu wa kike, akiwa amevaa ovaroli la bluu, lenye chata kubwa ya “PURE OIL ” mgongoni.



    “,dola tano kwa siku! “,muhudumu yule alimjibu Yuan Liang.



    “,Sawa, nitaichukua baada ya saa moja tu, saa kumi na mbili nitakua hapa! “,Yuan Liang aliongea, akaingiza mkono mfukoni, akatoa shilingi elfu kumi na mbili, pesa halali za nchini Goshani,kisha akatokomea.



    Alitembea huku akiangaza pembe zote za barabara, akafika pembeni na hoteli ya Sun city, hoteli ya kifahari iliyoangaliana uso kwa uso na hoteli ya Mtakuja,hoteli zote zikiwa zimetenganishwa na barabara kubwa!



    “, Pesa hizi hapa, nisaidieni magunia nijifiche hapa, kuna majambazi wananitafuta, nataka nijifiche mahali hapa, nijifunge magunia, nionekane kama mwenzenu”,Yuan Liang aliongea, akachukua noti kumi za elfu kumi kumi, akawagawia omba omba kumi waliokuwa wamelala kando kando ya barabara, karibu kabisa na hoteli ya Sun city.



    Yuan Liang aliwapatia omba omba pesa nyingi sana, siku zote walipewa pesa za sarafu, leo ilikua bahati yao, walishika noti kabla hata jua halijachomoza, walimuona Yuan Liang kama mkombozi wao,kila mmoja akampatia gunia moja japo aliomba magunia matatu tu, akayachana vizuri, akajifunika,dakika moja tu ilipita, msafara wa pikipiki takribani ishirini zikapaki pembeni ya hoteli ya Mtakuja, wakaingia ndani ya hoteli, Yuan Liang aliwaona vizuri sana,…



    Dakika tano zilipita, kumi zikapita, dakika ya kumi na tano, majambazi ishirini ya Kasabranka gang yakatoka ndani ya hoteli ya Mtakuja,sura zao zikiwa zimekunjamana kwa hasira,jambazi moja lenye kiduku kichwani, midomo ikiwa imebabuka kwa kuvuta bangi bila kipimo maalumu, lilikuwa limemshika mwanamke mmiliki wa hoteli hii, mama ambaye alimpenda sana Yuan Liang tangu akanyage katika hoteli yake.



    “,Paaaaaa, twambie malaya mwenzako kaenda wapi?, bila hivyo tunakuua! “,jambazi lilifoka, lilimtandika kofi zito mwanamke yule, akajitupa mweleka, akagaa gaa chini kwa uchungu.



    Yuan Liang alishindwa kuvumilia, alishuhudia kila kitu ambacho mama mwenye umri sawa na mama yake alikuwa anatendewa, alidharilishwa sana kwa kutukanwa matusi ya nguoni, “twambie, malaya mwenzako kaenda wapi, twambie, malaya mwenzako kaenda wapi? “,maneno aliyotukanwa mama yule yalijirudia mara mbili mbili katika kichwa chake, siku zote alilichukia sana tusi hili,Yuan Liang aliibuka kama mzuka, akiwa amevaa magunia, visu viwili vikiwa mikononi mwake, akavuka barabara huku akikimbia, akawasogelea majambazi wale.



    “,Kill him fyeka vidole vyake tumpelekee bosi! “,sauti ya amri ilisikika, majambazi wote wa kasabranka gang wakamvamia Yuan Liang, aliyekuwa amejifunga magunia kama kichaa.



    “,Mnanitukana mi malaya et eee! mtajuta kunifata mahali hapa, “Yuan Liang alifoka, sura yake haikuonekana, macho yake na mdomo wake ulionekana kupitia matundu  yaliyokatwa katika gunia,alionekana zaidi ya kituko.



    “,Kwachaa! “,



    “,Yalaaa! “,



    “,Kwachaa! “,



    “,Uwiiii! “,



    “,Kwachaa, kwachaaa! “,



    “,Yalaabiii! “,



    “,Kwachaa! “,



    “,Nakufaa! “,



    Yuan Liang alipiga mapigo ya kuua mtu, kila jambazi aliyemsogelea alivujwa vunjwa mifupa ya mkono wake, huku akichanwa chanwa na visu shingoni, hakuna aliyeinuka tena baada ya kipigo kutoka kwa Yuan Liang, kahaba hatari katika mapigo ya karate.



    “,Nitakuua malaya wewe! “,jambazi moja lilifoka, mkononi likiwa limeshika mnyororo, likijiandaa kumvamia Yuan Liang.



    “,Nisogelee uone kati ya wewe na mimi nani malaya! “,Yuan Liang aliongea kwa kejeli, akipiga mahesabu kuwashambulia maadui zake  ,akiwatazama kupitia matundu madogo kwenye gunia lake.



    “,Iyaaaa! nakuuwa malaya wewe, nakuuwa! “,jambazi lile lenye mnyororo lilipiga kelele, likaruka mateke mawili hewani, Yuan Liang akapangua mateke yake, likampiga na mnyororo akakwepa, likampiga tena na mnyororo akainama chini, akaudaka mnyororo wake, akauvuta, akalipiga na vifuti, akalinyonga kwa mnyororo wake, likafa palepale.



    “,Tukimbie! kimbieniii!Yuan Liang ni shetani, hatumuwezi, atatuua!”,amri ilisikika tena, majambazi takribani kumi na mbili waliokuwa wazima, walijipakia katika pikipiki zao, wakaziwasha kwa rimoti, zikawaka, wakatokomea,kila mmoja akitaka kuiokoa nafsi yake mbele ya kahaba hatari, Yuan Liang.



    ………….………………………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mexic; dakika kumi zilizopita



           Kundi la magaidi ishirini na saba ,M27,walifika katika mji mdogo wa Mexic, kaskazini mwa jiji la Costa. Gafla msafara wao ulisimama,kulikuwa na magari takribani matano mbele yao, yakiwa yamesimama barabani, na kusababisha foleni.



    “,Bosi hatuwezi kuendelea na safari, ngoja nishuke nikaangalie foleni hii inasababishwa na nini! “,gaidi namba tisa, dereva wa mkuu wa kikundi aliongea, akafungua mlango wa gari lake, akashuka.



    “,Kuwa makini! miji hii imejaa wahuni kama wewe, ukienda kizembe utashambuliwa na vibaka …”,bosi wa kikundi cha M27 aliongea, dereva akatikisa kichwa, bila shaka alimuelewa, dereva akaanza kupenya kwenye magari, gari la kwanza, la pili, kisha la tatu,uso kwa uso na kundi la vijana wakipigana, mtu mmoja aliyejifunika magunia akipiga karate na kuwashambulia vijana takribani kumi na tano kwa mpigo, akavutiwa naye, akarudi haraka kwa bosi wake huku anakimbia.



    “,Bosi, bosi, kuna mapambano barabarani, kandokando ya hoteli mita mia moja kutoka hapa! kuna mpiganaji atatufaa kama akiungana na sisi, twende ukamuone, “dereva alifika huku akihema, bosi akatoka nje, magaidi wote wakashuka kwenye magari yao kwa ajili ya kumlinda bosi wao, wakaanza kusogea eneo la tukio, tukio ambalo lilisababisha msongamano wa magari mengi barabarani.Bosi wa kundi la magaidi la M27 alivutiwa sana na mpiganaji huyu, alitamani sana aungane naye kwenye kundi lake, akiwa tayali kumlipa pesa zozote zile, akaendelea kutazama mpambano huo huku akisubili mapigano yaishe, amweleze mtu huyo aliyejivika magunia aweze kujiunga na kundi lake.



    “,Tukimbie, kimbieni!, Yuan Liang ni shetani, hatumuwezi, atatuua …”,sauti ilisikika, ikapenya katika masikio ya bosi mkuu wa kundi la M27,jina lililotajwa halikuwa geni masikioni mwake, ni jina la mwanamke ambaye walikuja kumtafuta,akiwa anatafakari, Yuan Liang alivua magunia yake, akabaki na sura yake halisi ya kichina, akiwa amevaa koti jeusi, suruali nyeusi ya jinzi pamoja na viatu vyake vya visigino virefu, mkononi alikuwa ameshika visu vyake viwili, maadui wake wakipanda pikipiki na kutokomea kama wendawazimu, wakimkimbia msichana huyu!



    “,Mkamateni!, huyu ndiye tumekuja kumtafuta, huyu ndiye mpuuzi Yuan Liang aliyemjeruhi rafiki yetu Jonsoni Mtemvu …”,bosi mkuu wa kundi la M27 alitoa amri, magaidi wake ishirini na tano wakatoa nyundo zao ndogo kwenye mifuko ya makoti yao, wakaanza kumsogelea Yuan Liang ili wamshambulie, huku gaidi mmoja akiwa amesimama sambamba na bosi kumpatia ulinzi. Watu walikuwa wamefurika, mji huu haukua na watu waoga, ikiwa majira ya saa kumi na moja asubuhi, watu waliamshwa na kelele, wakafungua madirisha yao, wengine milango, wakashuhudia mapigano haya, wenye magari barabarani walisimamisha magari yao, hawakua na haraka,wengine walitoka nje ya magari yao kushuhudia mapigano haya, huku baadhi wakibaki ndani ya magari yao na kuendelea kuushuhudia mpambano huu mkali …



    Ikulu; 6:00am



         Waziri Januari Sasamba aliwasili jijini Goshani, hakua na muda wa kupoteza, alifika moja kwa moja ikulu, aweze kumjulia hali rafiki yake kipenzi raisi Jonsoni Mtemvu,kisha azungumze na shemeji yake, mama Zainath, aweze kufahamu kile ambacho alitaka kumweleza tangu usiku uliopita.



    “,Anaendeleaje? “,raisi Jonsoni Mtemvu aliwauliza madaktari watatu ambao walikuwa wanampatia matibabu rafiki yake.



    “,Kwa sasa anaendelea vizuri, muda mfupi uliopita nd’io amepata usingizi, akalala fofofo, akiamka tutakujulisha uongee naye! “,daktari wa kizungu alimjibu Januari Sasamba, akatikisa kichwa,kukubaliana na kile alichoelezwa, kisha akatoka nje ya chumba cha matibabu ya raisi, akashuka ghorofani, akafika sebureni, akaketi.



    “,Shemeji nimekuita hapa! bila shaka unajiuliza maswali mengi bila majibu,ukitaka kujua nini hasa nimekuitia?”,mama Zainath alizungumza,macho yake yakiwa bize kumtazama Januari Sasamba usoni, kusoma hisia na fikra zake.



    “,Ndiyo maana sikutaka kufika nyumbani kwangu, nataka nijue jambo ambalo umeniitia, maana hali sio shwari kwa sasa! “,Januari Sasamba alijibu, akikwepesha macho na mama Zainath, asije akapoteza uwezo wake wa kujiamini, akaharibu kila kitu.



    “,Mume wangu tangu apate tatizo mara ya kwanza anaongea na simu kwa wasiwasi sana, na wewe umekua naye bega kwa bega kama rafiki wa karibu, isitoshe mtu anayemvamia na kumjeruhi ni yule yule!, je unafahamu kitu chochote hapa katikati kilichojificha! “,mama Zainath aliuliza swali, akionekana kubadirika kabisa, sura yake haikuonesha tabasamu hata kidogo.



    “,Hapaana, hapana, sijui choc…hote, sijui kabisa…aa, labda um…uulize mwenyewe! “,waziri Januri Sasamba alijibu kwa kigugumizi, akiwa na wasiwasi.



    “,Muuaji yuko Mexic, ndipo alipotorokea mara ya kwanza baada ya kufanya tukio, tukio la pili kalifanya na amerudi huko huko Mexic, lakini pia, nimekupigia simu usiku uliopita ukaniambia uko Mexic, ulienda kufanya nini huko? “,mama Zainath aliuliza tena.



    “,Nilienda kwenye shughuli zangu zingine kabisa, kwahiyo siwezi kulizungumzia swala hilo! ” ,Januari Sasamba aliongea, alitambua tayali shemeji yake alianza kuhisi jambo fulani,wasiwasi wa siri zao kuvuja ukazidi kuongezeka nafsini mwake, akawa mkali kama pilipili!



    “,Sawa shemeji yangu, tusije tukakwazana bure! lakini kama kuna mambo mabaya mmeyafanya na mume wangu, yanapowageukia na kupata matatizo msinishirikishe kwa jambo lolote lile …!”,mama Zainath aliongea ,akasubili majibu kutoka kwa shemeji yake.



    “,Sawa shemeji usjali, ngoja mimi nifike nyumbani mara moja! “,waziri Januari Sasamba aliongea, akanyanyuka kwenye sofa, akausogelea mlango, akaufungua,akutoka nje na kuondoka zake.



    “,Kuna tatizo, ona alivyotoka ndani kama anakimbizwa!, anyway! mtakapo kufa kwa aibu ndipo mtakapo sema ukweli, haiwezekani kila kukicha kuvamiwa na kupigwa tena na jambazi hatari, jambazi linaloshinda nguvu jeshi la serikali, haiwezekani kabisa, kuna kitu! “,mama Zainath aliongea, akajilaza kwenye sofa, tangu usiku hajapata usingizi kabisa, muda wote aliketi sebureni na kuangalia televisheni, akisubili kupokea wageni mbalimbali walioingia na kutoka ikulu, kumjulia hali mume wake, raisi Jonsoni Mtemvu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    …………………………………



    Mexic; Nusu saa iliyopita



           Yuan Liang alikuwa ameshayatupilia mbali magunia aliyokuwa amejifunika, wakati akipambana na kundi la majambazi maarufu kwa jina la Kasabranka gang, akafanikiwa kuwashinda,majambazi nane aliwajeruhi vibaya sana, kumi na mbili wakamkimbia.



    Akiwa bado hajapumzika,kundi lingine la majambazi asio fahamu mahali walikotokea walimzunguka,wote walivalia makoti marefu na meusi, mkononi wakiwa wameshika nyundo ndogo kwa ajili ya mapambano..



    “,Nasema mshambulieni, hakikisheni mnaipata diski, kisha mnamuua! “,sauti ilisikika kutoka jambazi mmoja akiwa amesimama nyuma kabisa, pembeni yake akiwa amesimama komandoo aliyekuwa na mwili mkubwa, bila shaka alikuwa ni mlinzi wake. Yuan Liang aliendelea kuwatazama, akisubili kujibu mashambulizi, huku akiahidi kumfyekelea mbali Jonsoni Mtemvu,kwani aliamini ndiye aliyemtumia makundi ya majambazi, waweze kumuua.



    “,Nazani umesikia kauli ya bosi,kama unataka kuishi, tukabidhi diski,M27 hatujawahi kushindwa na mtu yoyote yule, tena wa kike kama wewe! “,jambazi mmoja aliongea,Yuan Liang akawahesabu majambazi wale,walikua ishirini na saba, akatabasamu, akatikisa kichwa, bila shaka aligundua kitu fulani…



    “,Kumbe nyie ndiyo magaidi wa M27,nyie ndiyo mnauziwa silaha na serikali ya Jonsoni Mtemvu, nyie ndio mnahonga serikali kupitia kivuli cha raisi Jonsoni Mtemvu pamoja na waziri mshenzi Januari Sasamba, mnapitisha madawa ya kulevya bandarini bila kukaguliwa mkitumia kibali cha raisi!, sasa leo ulimwengu wote utajua maovu yenu, siku ya leo ijumaa, dunia nzima itakua bize kufuatilia habari pamoja na vifo vyenu …”,Yuan Liang alifoka, raia waliokuwepo pembeni kwa ajili ya kushuhudia mapambano ya ngumi bila malipo yoyote, wote walikimbia kujificha,kila mmoja aliwatambua magaidi hawa kwa ukatili, japo hawakuwahi kuwashuhudia machoni uso kwa uso. Yuan Liang hakutaka pesa tena, alitaka kuipigania haki iweze kupatikana, hakuwa tayali kuitoa diski mikononi mwake na kupoteza ushahidi.



    “,Anasema nini huyo mshenzi, mkamateni tuondoke naye, akatwambie diski ameficha wapi!! “,bosi wa kikundi cha magaidi cha M27 alifoka, baada ya kusikia Yuan Liang anaweka wazi siri zao, alipaswa kunyanganywa diski na kuuawa kabla mambo hayajaharibika. Baada ya kutoa amri, magaidi ishirini na tano walimvamia Yuan Liang, kila mmoja akiwa na nyundo yake mkononi, katika mkono wake wa kulia.



    Yuan Liang aliruka mateke,magaidi yakakwepa, akaruka tena yakwakwepa, yakamtandika na nyundo, akaruka serekasi, akatua upande wa pili, yakamvamia yote kwa pamoja, akayatandika ngumi yakwepa, akatumia kisu chake, akaruka mateke manne mfululizo, yote yakapanguliwa kwa ufundi na magaidi watano waliokuwa mbele kuongoza kundi …



    “,Hawa washenzi nikizubaaa wataniumiza, isitoshe nimechoka tangu jana niko kazini!! “,Yuan Liang aliongea, akarudisha visu vyake kwenye mkanda wake, akainama, akafunga vizuri kiatu chake, akakunja ngumi, akajiandaa kutumia pigo lake la kifo, pigo ambalo siku zote liliwaacha maadui zake viwete.



    “Naomba asinisogelee mtu yoyote,nitamuua ……”,Yuan Liang aliongea, mguu mmoja alikuwa ameuning’iniza juu, mikono yake miwili ilishika chini, alikuwa kama ng’e anayejiandaa kumshambulia adui.



    “,Hahaaaaa, usijitetee malaya wewe, na leo wote tunakulala bureee!! “,gaidi moja lenye mwili ulioshiba kwa mazoezi lilimkejeli Yuan Liang, likamsogelea huku mkononi likiwa linacheza na kurusha rusha nyundo yake.



    “,Paaaa! “,



    “,Yalaaa! “,



    “,Vuuuu, puuuu! “,



    “,Yalaaa! “,



    “,Kwachaa! “,



    “„Yalaaa!, umeniumiza mseng* wewe! “,



    “,Mseng* mama yako, nimewaambia msinisogelee mkazani nawatania, leo ndio mtajua mimi na nyie nani malaya! “,Yuan Liang alifoka, huku akikunja ngumi, akijiandaa kutumia pigo la kifo kwa mara nyingine tena, baada ya kulitumia kwa sekunde tano tu, akaruka hewani na kuvunja vunja mikono ya kila jambazi aliyemsogelea,magaidi takribani watano walikuwa chini wakiugulia maumivu ya mikono yao, wengine wakitukana matusi ya nguoni, huku baadhi ya magaidi wakirudi nyuma baada ya wenzao kujeruhiwa vibaya kwa sekunde tano tu.



    …………………………………



    Mexic;



            Difenda ya polisi ikiwa na king’ora juu, ilipita barabarani na kufyatuka kama ndege, the super three soldiers walikuwa wamepania kukamilisha kazi haraka iwezekanavyo, waweze kurudi nchini Tanzania.



    “,Tunaingia Mexic, hebu angalia kama bado adui yuko eneo hili …… !”,Kamanda Kendrick alitoa amri, kamanda Catherine akabonyeza batani ya kompyuta yake,akatazama kwenye kioo.



    “,Connected, the related disc is available in Mexic, “(Imeunganishwa, diski inayohusiana inapatikana Mexic …)”,ujumbe uleule ulikuwa bado unaonekana kwenye kompyuta, akatabasamu, huku akijiweka sawa kwa ajili ya kuanza kazi.



    “,Afande, bado mtuhumiwa yuko hapa Mexic, mwanzo wa mji! “,kamanda Catherine aliongea, wote wakatoa bastola zao, wakajiandaa kwa ajili ya kuanza kazi haraka iwezekanavyo, dakika tano zijazo, watakapoingia mji wa Mexic.



    …………………………………



    Magaidi yaliendelea kumnyemelea Yuan Liang, huku Yuan Liang akimsubili yoyote yule atakayemsogelea aweze kumtia adabu, ghafla king’ora cha gari la polisi kikasikika, magaidi hawakutaka sura zao kuonekana mbele ya macho ya polisi,wakaanza kukimbia kuyasogelea magari yao waweze kutoweka haraka sana.



    “,Chukueni wenzenu walio jeruhiwa ,huyu mshenzi tutamtafuta baadae, ngoja tuwapishe hawa watoto wanaotupigia ving’ora! “,amri ilisikika, magaidi wote wakajipakia kwenye magari yao, wakatoweka, barabara ikiwa kimya, wananchi wote wakiwa wamejifungia kwenye majumba yao, uwepo wa M27 maeneo hayo uliwatisha sana.



    “,Mikono juu!ukijitikisa, au ukifanya lolote lile tunakushambulia ……”,Yuan Liang hakutaka kukimbia, alitaka kujisalimisha ili awaeleze polisi ukweli kuhusu ukatili wa raisi wao Jonsoni Mtemvu pamoja na Waziri wake Januari Sasamba.



    “,Sitaki shari na mtu, naomba mniache, nitajifunga pingu mwenyewe, nitaingia kwenye gari mwenyewe! “,Yuan Liang aliongea, bila wasiwasi wowote, akitoa masharti kwa askari wa the super three soldiers, pamoja na kamanda Gupta na Yasini waliokuwa wamemnyoshea silaha zao wakimsogelea.



    “,Nawaomba mtii masharti yangu, sina lengo baya kujisalamisha, na mimi sio mtu mubaya, nasema hivi!nitajifunga pingu mwenyewe, nitaingia kwenye gari mwenyewe! “,Yuan Liang aliongea kwa upole, akatoa maelekezo kwa mara nyingine tena, kwa askari waliokuwa wanamsogelea.



    “,Pumbavu kabisa, umeua, umemshambulia raisi, umeiba diski, halafu unatuwekea masharti ya kukumata! “,kamanda Gupta aliongea. Wote walimtambua Yuan Liang, baada ya kuitazama sura yake na mavazi yake, walimkumbuka siku alipowatoroka kwenye baa nje ya mji wa Mexic, wote walikuwa na hasira isipokuwa kamanda Kendrick. Kamanda Gupta akamvamia Yuan Liang, kamanda Catherine akafuatia, kisha wote wakafuatia, Yuan Liang alikwepa mateke matatu kutoka kwa Gupta, Catherine pamoja na Yasini, kisha akaruka mateke manne yaliyotupilia mbali bastola zao, wote wakabaki bila silaha mkononi.



    Mexic; 6:24am



          Kamanda Kendrick japo alikuwa hajapona vizuri bega lake, hakua na budi kuingilia mapigano kati ya askari wake na kahaba hatari sana, Yuan Liang. Askari wake wote walikuwa wanahema kama mbwa, piga nikupige, licha ya Yuan Liang kuwa peke yake, lakini alikuwa hapigiki kizembe.



    “,Puuuuuh “,kishindo kilisikika.



    Kamanda Kendrick aliruka teke, Yuan Liang akainama chini, akaruka tena mateke matatu mfululizo, Yuan Liang akayapangua yote kwa mikono yake ,kabla kamanda Kendrick hajatulia chini, alimpiga ngwala Yuan Liang, akadondoka chini kama mzigo! wakamvamia na kumfunga pingu pale pale chini, kamanda Gupta alishika mguu mmoja, kamanda Yasini akashika mguu mwingine, kamanda Philipo akamshika mikono Yuan Liang, kamanda Catherine akamvalisha pingu huku kamanda Kendrick akiwa ameshika bastola, tayali kwa ajili ya kumshambulia Yuan Liang atakapotaka kuleta vurugu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Tatizo nchi za Kiafrika zinatetea sana wahalifu, mnakamata wasio na hatia,haya kabla ya kwenda kituoni, naomba tuchukue pikipiki yangu hapo sheli ……”,Yuan Liang aliongea, hakuna aliyemjibu, wote walimuona kama jambazi hatari aliyestahili adhabu ya kunyongwa.



    Walimpakia kwenye gari, wakamtupa kama mzigo, difenda ya polisi ikasogezwa katika sheli ya “pure oil “,ikajazwa mafuta, kisha wakapakia kwenye difenda pikipiki ya Yuan Liang, wakatoweka kwa fujo eneo hili,raia wakafungua milango na madirisha, kushuhudia difenda ya polisi ikitoweka mbele ya macho yao!



    …………………………………



    Costa; kituo cha polisi



         Tetesi za jambazi hatari kukamatwa, jambazi hatari aliyemshambulia raisi mara mbili mfululizo, zilienea kila kona ya jiji la Costa na nchi jirani. Raia walijaa nje ya kituo cha polisi wakitaka kumshuhudia jambazi huyo wa kike, huku waandishi wa habari wakiwa bize kuchukua taarifa kwa ajili ya kupamba vyombo vyao vya habari, wengine redio, wengine televisheni.



    “,Naomba majaji wote, balaza la mawaziri, na askari wote wawe mahali hapa, washuhudie mahojiano haya,waandishi wa habari wawe hapa kurusha matangazo laivu, bila hivyo sitaongea ukweli wowote ule,”Yuan Liang aliongea, akiwa amefungwa na kutundikwa kwenye mlingoti kama yesu msalabani, mkono wake ulifungwa kaskazini, mwingine ukafungwa kusini.



    “,Dakika tano kila mtu uliyemuhitaji atakua mahali hapa! “,kamanda Kendrick aliongea, kamanda Catherine na wenzake wakatoka nje, dakika kumi mbele,mawaziri na waandishi wa habari walijaa kituo cha polisi, mahali alipokuwa amefungwa Yuan Liang,alifungwa kwa kamba na minyororo migumu, asipate upenyo,akaua watu na kutoroka.



    “,Unaweza kutwambia historia fupi ya maisha yako? “,kamanda Catherine aliuliza swali, waandishi wa habari wakiwa bize kurekodi matukio, huku majaji wakiwa makini kuskiliza kesi, watoe hukumu mara moja bila hata kuipeleka kesi mahakamani.



    “,Naitwa Yuan Liang,nililelewa na kukulia katika kituo cha watoto yatima cha mtakatifu Petro chini ya kanisa katoriki, nilipo fikisha miaka kumi na nane, niliingia mtaani kutafuta pesa, nikiwa barabarani, ghafla nilivamiwa, nikazibwa mdomo na kupakiwa kwenye gari,sikujua naelekea wapi,gari ilifika bandarini, nikapandishwa kwenye boti, mpaka kwenye kisiwa ambacho sikikumbuki jina, nikakuta watoto wengi kama mimi, wanafundishwa mapigano na mbinu mbalimbali za kujilinda, walikuwa magaidi, nikajifunza kwa miaka miwili, nikafikisha miaka ishirini,nilikuwa nimeiva,  nikatumwa mzigo wa madawa ya kulevya, sikuwa tayali kurudi tena kwa magaidi hawa, nikajitupa majini, na kuogelea, walinitafuta bila mafanikio, nikaibukia pwani ya nchini Goshani, nikaingia mtaani tena, hapo ndipo nilianza wizi, niliwaibia pesa watu wabaya hasa wafanya biashara, wanasiasa na viongozi wa dini waliotaka kuninunua kama kahaba, hapo ndipo niliwaibia na kuwatia adabu ili waache tabia zao kulingana na vyeo vyao ……”,Yuan Liang alimaliza kutoa historia yake fupi, historia iliyomwacha mdomo wazi jaji mkuu, mwenye umri wa miaka themanini.



    “,Wewe ni mtoto wa gavana wa kichina, mtawala wa Goshani enzi za ukoloni, baba yako alikua anaitwa Liang Xung, mama yako alikuwa ni muafrika, ndio maana wewe ni chotara! baba yako alitoroka na kurudi China, hakutaka kwenda na ngozi ya kiafrika huko, akamuacha mama yako, mama yako akapatwa na mshituko akafa palepale! wewe ukapelekwa kituo cha watoto yatima, ndipo ulipotoweka katika mazingira ya kutatanisha! “,jaji yule alimaliza kusimulia, watu wakazidi kuachwa midomo wazi



    “,Mungu wangu! is this true?, anyway! yameshapita, napaswa kusahau! “,Yuan Liang alishtushwa na historia kuhusu wazazi wake, akapiga moyo konde na kujikaza kisabuni,ili aweze kusahau yaliyopita.



    “,Mungu wangu, maajabu haya, jambazi kumbe alikuwa mtoto wa gavana! “,kelele zilisikika, watu walizidi kushangaa.



    “,Tuambie! kwa nini ulimshambulia na kutaka kumuua raisi Jonsoni Mtemvu! “,swali lilisikika kutoka kwa waziri wa ulinzi,ukimya ukatawala, kila mtu alitaka kujua kuhusu jambo hilo.



    “,Raisi ni muuaji, yeye na waziri Januari Sasamba, ni wauaji wakubwa na wauzaji wa silaha za serikali! “,Yuan Liang aliongea, askari wote wakamnyoshea silaha,tayali kwa ajili ya kupokea amri kumshambulia.



    “,Acha kumkashifu raisi mbele ya majaji watukufu, utahukumiwa kifo! “,jaji mkuu aliongea.



    “,Nitahukumiwa kifo, baada ya raisi na waziri mkuu kuhukumiwa, msipowahukumu, nitawahukumu mimi mwenyewe,!”,Yuan Liang aliongea, watu wote wakabaki midomo wazi.



    “,Silahaa chini! “,Kamanda Kendrick, akiwa kama askari mwenye cheo kikubwa kuliko wenzake alitoa amri, askari wote wakashusha silaha zao chini …



    “,Hujajibu swali, kwanini ulitaka kumuua raisi ?”,waziri wa ulinzi akauliza swali kwa mara nyingine tena.



    “,Raisi alininunua kama kahaba, lakini mimi sio kahaba, sijawahi kulala na mwanaume yoyote yule, mtu anaponihitaji, mimi naenda kwa lengo la kumuibia, na kumzimisha kabla hajatimiza lengo lake, akishtuka, anakuta ameshaibiwa na mimi nikiwa nimeshatoweka!! ndivyo ilivyotokea, nilimzimisha raisi Jonsoni Mtemvu kabla hajafanikiwa kulala na mimi, nikamuibia diski ya saa yake ambayo ni ya dhahabu, nilijua nikiiuza nitapata pesa nyingi, nilipoenda kuichunguza nikagundua siri na maovu yote ya raisi, ndiyo maana nasema niwauaji! naomba televisheni iletwe hapa mara moja! “,Yuan Liang aliongea, dakika mbili tu, televisheni kubwa ililetwa, ikaunganishwa, walikuwa wameshamsachi kila kona, hwakuona diski, alikuwa ameshaificha mbali sana.



    “,Askari mmoja abonyeze batani ya miwani yangu, mkono wa kushoto, kisha atazame kisigino cha kiatu changu, kikijifungua, achukue diski ya raisi wenu mshenzi kuliko wote duniani! “,Yuan Liang akaendelea kutoa maneno ya kejeli kwa raisi,akatoa maelekezo, kamanda Kendrick akasogelea miwani ya Yuan Liang, akabonyeza kama alivyoelekezwa, kisigino cha kiatu cha Yuan Liang kikafunguka, ndani ya kisigino kulikuwa na mashine ya kukata mawasiliano, akaachana nayo, akachukua diski, akabonyeza tena batani, kiatu kikajifunga, akasogelea televisheni, akachomeka diski, diski yenye ukubwa sawa na flashi, wakaanza kusikiliza sauti na kutazama  matukio ya kihalifu yaliyofanywa na Jonsoni Mtemvu pamoja na Januari Sasamba.



    “,Zima televisheni, wakamatwe mara moja, haijalishi ni mgonjwa au amekufa wote wakamatwe! “,amri ilitoka kutoka kwa waziri wa ulinzi, askari wakatoka nje haraka sana, wakiongozwa na kamanda Kendrick, kila kitu kiliwekwa wazi, ukweli ulikuwa umejulikana



    …MWISHO …

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jonsoni Mtemvu na Januari Sasamba walihukumiwa kunyongwa, Yuan Liang akapewa bilioni kumi na serikali kama zawadi, akaachana na wizi, akafungua kampuni ya ulinzi, mke wa raisi, mama Zainath alikufa kwa presha baada ya kutambua ukweli kuhusu maovu ya mume wake.







0 comments:

Post a Comment

Blog