Search This Blog

Friday, 28 October 2022

ASKARI JELA - 2

 









    Simulizi : Askari Jela

    Sehemu Ya Pili (2)





    Upande wa wafungwa wanawake wao walikuwa wakivunja mawe katika upande mwingine ambao haukuwa na mawe magumu sana, gereza hili lilikuwa halina jinsia kabisa katika suala la kzi ndiyo maana hata wanawake walikuwa wakifanya kazi ngumu pia. Ni ndani ya eneo la chini ya gereza hilo ambako ilikuwa ikihitajika kupanuliwe zaidi gereza hilo, walikuwa wakichakarika huku waikisimamiwa na maafande wa kike.

    Getu, Frida na Stella wale wasichna waliokamatwa kwenye kisa cha Shujaa kilichoandikwa na mtunzi Mahiri Hassan O Mambosasa. Walikuwa wapo eneo moja wakiwa wamekaa na rafiki yao Josephine mwanamke tishio aliyekamatwa ndani ya kisa cha Wito wa kuzimu baada ya kuua maelfu ya watu jijini Dar es salaam. Wote walikuwa wakivunja mawe huku wakiongea mambo mbalimbali ambayo yaliwafanya wasione kazi ngumu, wakati wakiendelea kuchakarika na kazi ilifika muda Josephine alisimama kwa muda wa dakika kadhaa akiwa ameshika kiuno huku wenzake wakiendelea kufanya kazi. Kitendo hicho kilisababisha apigwe na kirungu cha bega na mmoja wa Maafande ambao walikuwa wakisimamia eneo hilo, ilikuwa ni tendo ambalo lilimuudhi na alijikuta akifytua teke la shukrani ya punda ambalo lilimpata Afande huyo kifuani akaanguka chini. Aligeuka nyuma akaona kundi maafande watatu wakiwa wanamjia kwa kasi, hakutaka kabisa kuwahofia yeye alitupa nyundo chini na kisha akasimama akiwa hana hofu. Afande wa kwanza kumfikia alikutana na pigo la karate akaenda chini, mwingine alileta rungu ambalo lilimkosa baada ya kuyumba na kisha akamuachia ngumi nzito ya kidevu.

    Shangwe za wafungwa ziliamka muda huo kutokana na maafande hao kupewa kipigo,waliendelea kushuhudia wale maaskari ambao walikuwa wakiwanyanyasa wakipewa kipigo na mwenzao. Fujo za kelel zao ilikuwa ni jambo ambalo lilisababisha waje wale wasichana ambao walikuwa wamempokea na kumleta gerezani, wasichana hao hawakuwa wengine ila ni kina Teddy. Hakuna ambaye alikuwa hawajui walivyo wajeuri na makatili hao maafande, Josephine alijipanga kupigana nao lakini alipopangua pigo la mmoja basi alionja kirungu cha mwingine. Alipigwa sana virungu ambavyo vilimkumbusha siku ya kwanza kuingia ndani ya gereza hili alipoleta ubishi. Aliongezwa na mabuti baada ya kuanguka akiwa haonewi huruma, hakika aliingia ukanda wa wajeuri wenzake. Alipokuja kuachiwa baada ya kupewa kipigo alikuwa na manundu mengi sana, alikuwa hana tofauti na mcheza masumbwi akitoka kwenye pambano.

    Baada ya hapo aliburuza mithili ya gunia na kupelekwa eneo jingine kabisa, aliburuza hadi kuingia kwenye eneo hilo ambalo lilikuwa na kila uchafu ndani yake ambao ulimfanya yule mwenye kinyaa kutapika. Alikuja kuhisi kutoburuza baada ya kufika eneo lenye unyevu ambalo lilikuwa na harufu kali sana. Alipoangza vizuri alikuja kubaini kuwa alikuwa yupo jirani na mtaro unaopitisha kinyesi ambao ulikuwa umefunguliwa, unyevu huo ulimbainishia kabisa kuwa mtaro huo ulikuwa umeziba na muda huo ulikuwa ukitoa uchafu nje. Hapo aliinuliwa kwa nguvu sana na kisha kichwa chake kikatazamisha kwenye mtaro huo uliokuwa ukichukua uchafu vyooni, aliona takamwili za ndani miili ya mwenzake zikiwa zimejazana na kuweka taswira isiyo ya kawaida. Takawmili hizo zilikuwa zimeganda sehemu moja ambapo ziliweka taswira isiyopendeza, chepe ambalo lilikuwa kuukuu liliangushwa mbele yako hapo.

    "We si kiburi humu ndani tupo viburi zaidi yako, sasa utachota mavi na chepe hili kuahimishia upande wa pili wa mtaro huu ambako hakujaziba. Uzibuke na huo uchafu wenu ulioganda hapo nisiuone" Teddy alimuambia kwa jeuri kisha akamsukuma kungia ndani ya mtaro huo.

    Josephine na jinsi ilimbidi yeye mwenye aingie kwenye mtaro huo na kuanza kuyachota hayo yasiyopendezeka kuyatazama, alikuwa akisimamiwa hapo hadi kazi hiyo ambayo haikuwa ngumu lakini ilihitaji moyo iweze kuisha. Harufu kali ilitoka alichota koleo la kwanza tu lakini hakuwa hata na uwezo wa kuziba pua zake, alivumilia harufu hiyo akiendela kuyachota. Koleo la mwisho kulichota ndiyo alijuta kabisa kuleta jeuri yake, yale maji yaliyokuwa yamezibwa yalizibuka kwa kasi sana na kumvamia hata yeye kwenye mwili wake. Alitoka juu kwa haraka akiwa amelishiia chepe hilo, kazi aliyopewa alikuwa tayari ameshaimaliza ila alikuwa hatamaniki kwa kutoa harufu mwilini mwake. Aliondolewa eneo hilo baada ya adhabu hiyo kuisha akiwa ananuka na alienda kujiafisha moja kwa moja, alirudishwa eneo lile ambalo wenzake walikuwa wakifanya kazi baada ya kubadili nguo na aliongezewa kazi mara mbili ya wenzake.

    ****

    Usiku kama kawaida maofisa wote walikuwa wapo ndani ya Bwalo la chakula wakingalia vipindi mbalimbali vya luninga, wote wenye vyeo ngazi ya juu walikuwwepo kasoro Afande Nkongo ambaye alikuwa yuo ndani ya nyumba yake iliyomo humo gerezani. Ukimya ndiyo ulikuwa umetawala katika muda ambao walikuwa wakiangalia Luninga, ukimya huo ulikuja kuondoka baada ya mitambo kukata ghfla baada ya kuvurugika kwa hali ya hewa. Ukimya huo ulizusha maongezi mengine kabisa, ndani ya maongezi hayo ndipo walipokuja kubaini kuwa mmoja wao hakuwepo. Walipoangalia meza aliyokaa Mkuu wao hawakumuona Afande Nkongo, hapo walibaini ni yeye tu ndiye alikuwa amekosekana humo ndani.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mkuu mwano yupo wapi?" Afande mmoja wa kike aliuliza

    "Mbona unamuulizia sana Hollo au ndiyo mkwe?" Mkuu huyo aliuliza kimasihara na wote wakaanza kucheka humo ndani.

    "Lakini mkuu hujawahikutumbia kabisa sababu ya Nkongo kuwa vile zaidi ya kutuambia kila kila siku kila mtu ana historia yake katika maisha" Mwingine aliongea

    "Ni jambo ambalo ni zito sana vijana wangu msilione rahisi sana kuliongea, kwanza mna vifua?"

    "Mkuu tupo tayari kulitunza ila tujue tu kipi kinamsibu mwenzetu" Aliambiwa

    "Ok naomba hata yeye mwenyewe asijue kuhusu hili, hapendi kabisa mwingine ajue"

    "Ondoa shaka kuhusu hilo" Alitolewa hofu kuhusu hilojambo.

    "Ok sasa ngojeni niwaelezeni" Alipoongea hivyo wale ambao walikuwa wapo mbali naye walisogea karibu zaidi waweze kusikia, ukimya ulitawala wakiwa wanajiandaa kusikiliza kuhusu hilo jambo ambalo walikuwa wakitaka kulifahamu zaidi. Kila mmoja alikuwa amekaa mkao mzuri kuweza kulisubiria jambo hilo kwa hamu sana aweze kulisikia, habari za kukatika mitambo ya televisheni walikuwa wameshazitoa ndani ya vichwa vyao na kusikiliza historia muhimu ndiyo walilipa kipaumbele





    MIAKA KADHAA ILIYOPITA

    Kundi kubwa la watoto wa shule walikuwa wakitoka darasani majira ya saa nane, walikuwa ni watoto wa darasa la saba ambao walikuwa wakitoka m ndani ya msingi inayotumia Kingereza katika kufundisha. Miongoni mwa watoto waliyokuwa wakitoka darasani, James alikuwa yupo akiwa amebeba begi lake nadhifu kabisa. Makelele ya watoto hao ya hapa na pale ndiyo yalisikika katika muda huo waliokuwa wakitamani kwenda nyumba kuliko kitu chochote, wengi walikuwa wakiongea kwa sauti katika muda huo huku wengine wakicheza na kufukuzana kama ilivyo kawaida yao. James alikuwa yupo katika kundi la marafiki zake wakubwa wawili ambao alikuwa wakiwapenda sana, wote kwa pamoja walikimbilia kupanda kwenye gari la shule ambalo huwa linawarudisha majumbani mwao.

    Baada ya muda mfupi safari ya kuondoka kurudi nyumbni ndiyo ilianza, wanfunzi wote walikuwa wametulia ndani ya gari hilo kutokana na uwepo wa mwalimu mkali ambaye hakuwa akitaka kabisa makelele. Gari hilo lilizunguka mitaa mingi sana na kuwashusha wanafunzi tofauti na hatimaye likafika maeneo ya Tameko ambalo ndiyo kituo cha kushuka James. Hapo aliagana na marafiki zake halafu akashuka jirani kabisa na lango la nyumbani kwao. Alibonyeza kengele langoni hapo kisha akasubiri kwa muda hadi pale mlango ulipofunguliwa, alitokea Mwanamke ambaye alimfanya James amkimbilie na kumkumbatia kwa furaha. Alikuwa ni mama yake mzazi ambaye alikuwa akimpenda sana, alibebwa ingawa alikuwa amefikia umri wa kutobebwa na kisha aliingia naye hadi sebuleni.

    "Mama huyo mwanao unamdekeza" Mvulana mabye alikuwa ni mkubwa kiumri alimuambia mama yake baada ya kuona mdogo wake anabebwa.

    "Niachie mziwanda wangu huyu wacha nimdekeze" Alongea huku akimshusha chini na kuanza kumfungua kamba za viatu, alimvua na begi lake la shule na kisha alimpeleka kwenye meza ya chakula na akaanza kumlisha kama vile alikuwa hawezi kula

    ****

    "Hivi hizi habari ni za ukweli Philipo mbona sielewi?" Mwanaume mmoja aliyekuwa na nyota moja pamoja na ngao begani mwake aliongea

    "Hapana siyo za ukweli mkuu nafikiri wewe unatambua kazi yangu" Philipo ambaye alikuwa na nyota tatu mabegani mwake akiwa na nguo za maaskari magereza kama mwenzke alijitetea.

    "Ujue hii ni skendo kubwa sana"

    "Elius nafikiri unanijua tangu tukiwa shule hebu fikiri nitaweza vipi kufanya haya, mimi ni Philipo yuleyule sijabadilika kitu"

    "Hata fikiria jinsi Kamishna General huko alivyo mkali akisikia habari hii unafikiri itakuwaje"

    "Sasa sina hatia Elius, wewe ni mkuu wangu na pia rafiki yangu wa siku nyingi nisaidie ndugu"

    "Ngoja nikamsikilize huyo Mwandishi ambaye alikuwa ameandika kuhusu habari hii vizuri ndiyo nijue nitakusaidia vipi"

    "Sawa ndugu ila usiwaamini sana hao waandishi si unajua ni hatari kiasi gani kuzusha mambo"

    "Ngoja kwanza nikaone ana ushahidi gani huyo na tuhuma hiyo anayokutuhumu kabla hayajafika huko"

    Yalikuwa ni maongezi kati ya Mrakibu Mwadamizi wa jeshi la magereza SSP Elius Nkongo na rafiki yake kipenzi pia askari wa chini yake Mrakibu msaidizi ASP Philipo Lutonja. Tuhuma ambayo ilikuwa imemkumba ASP Lutonja kupitia gazeti pendwa maarufu nchini ndiyo lilifanya aitwe kwenye ofisi hiyo na Mkuu wake huyo. Ilikuwa imekaa kama habari ya kidaku kwa jinsi ilivyokuwa imeandikwa kwenye gazeti, habari hyo haikudharauliwa mara moja kwani ingeweza kabisa kulipa sifa mbaya jeshi la Magereza. Ilipofika ofisi kwa SSP Nkongo aliamua kuivalia njuga kwani lilikuwa likimuhusu rafiki yake, hakutaka kabisa kuona habari hiyo ikimuacha na sifa mbaya rafiki yake. Pia hakumuamini asilimia mia moja na ndiyo maana alimuita hapo na kuanza kumuuliza juu ya suala hilo, tayari alikuwa na miadi na Mwandishi aliyeandika habari ile ambaye alikuwa amethibitisha kabisa kuwa alikuwa na ushahidi wote kuhusu habari aliyoandika. Kabla hajaenda kwa mwandishi huyo ilimbidia fanye mahojiano kabisa na ASP Lutonja.

    Majira ya alasiri yalimkuta akiwa yupo ndani ya mgahawa katikati ya jiji la Dar es salaam akiwa yupo uso kwa uso na mwandishi huyo. Alikuwa ni mwandishi mkongwe ambaye alikuwa na jina kubwa ndan ya nchi hii, ndiyo huyo aliyekuwa akidai ana na ushahidi wa kila kitu juu ya jambo ambalo aliliandika kwenye gazeti alilokuwa akilimiliki. Gazeti ambalo lilikuwa limebatizwa jina na kuitwa gzeti la kidaku kutokana na habari zao walizokuwa wakiziandika, hakuna mwananchi ndani ya Tanzania ambaye alikuwa hamtambui kabisa mwandishi huyu ambaye alikuwa akisifika kwa umahiri wake katika uandikaji habari kwenye magazeti mbalimbali makubwa mbali na gazeti lake. Akiwa yupo hapo mbele alikuwa amekuja na mkoba wa kubeba mgongoni ambao muda huo alikuwa ameupakata, alikuwa akitazamana ana kwa ana na SSP Nkongo ambaye alikuwa amefuata huo aliokuwa akiuita ushidi wake.

    "Ndiyo Bwana Kizigo nimekuja nilikuwa nahitaji kujua kila kitu kuhusu ilichokiandika kwenye gazeti lako" SSP Nkongo alifungua mjadala

    "Ndiyo SSP kama nilivyokuambia ushahidi upo na niliutafiti mwenyewe, huwa siandiki habari bila ushahidi" Kizigo aliongea

    "Unao hapo hapo tuuone?" Kizigo alipoulizwa swali hilo hakujibu na badala yake alifungua mkoba wake akatoa picha ambazo alizimwaga kwenye meza.

    "Kwa muda mrefu ndani ya nchi kulikuwa na wimbi la uuzaji wa silaha kinyume cha sheria. Kipindi hicho chote kumekuwa kukitokea matukio kupungukiwa kwa silaha katika ghala zenu tofauti na hata za majeshi meingine, wasamaria wema wa kwanza kulijua hili suala walitoa taarifa kwa mwandishi mwenzangu Marehemu Kibiti ambaye alifariki siku cchache tu alipotangaza kuwa alikuwa akilifuatilia hilo swala, alikutwa amefariki kwenye kiti chake cha ofisini na haikueleweka kifo chake kilitokana na nini zaidi ya kumsikiliza Dokta Nasibu ambaye alidai alikufa kwa shinikizo la damu.. Ndugu SSP napenda utambue kuwa kabla ya kifo chake Kibiti aliwahi kuniambia kuwa maisha yapo hatarini kupita simu ya mkononi na maongezi yake niliyarekodi ni haya hapa" Kizigo aliongea na alipomaliza alitoa simu yake na kisha akafungua kwenye faili la maongezi hayo.

    Alibonyeza kitufe kuyacheza maongezi hayo mbele ya SSP Nkongo, yalisikika vizuri maongezi hayo ambapo walikaa kimya wote. Baada ya kuyasikiliza kwa umakini sana hadi yakaisha, Kizigo aliendelea na maelezo.

    Jambo ambalo halikufahamika ni kwamba picha hizo zilikuwa tayari zimeshapigwa na Kibiti mwenyewe, alizihifadhi hizo picha nyumbani kwa mdogo wake na kumpa maelekezo yote ikiwa atauawa. Alipouawa ndiyo picha hizo zikafika kwenye mikono yangu kama maelekezo yalivyomtaka. Ndugu SSP nafikiri unaona kabisa hapo ni jinsi gani hao maaskari waaminifu ndani ya jeshi la magereza wakiondoka na wafungwa majira ya usiku kwenda kuwapelekea huko kwenye biashara zao. Wengi wao wanaopelekwa huko waliingizwa gerezani hapo kwa sababu hiyo tu kuweza kufanya zao, nilipopata ushahidi huo wa awali niliamua kuingia kazini mwenyewe nikiwa sijulikani kabisa kama ninafuatilia suala hili. Wahusika waliona hili suala lilikuwa limeisha kabisa, kupunguza umakini kwenye suala hili ndiyo kulinifanya mimi niweze kufika mbali kabisa kiasi cha kujua mengi zaidi" Kizigo alieleza.

    "Sawa nimeyasikia maelezo yako na pia ushahidi wa picha nimeuona, je Lutonja anahusika vipi hapa maana sijaona ushahidi wa kumtia hatiani" Aliulizahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndugu SSP tunaenda hatua kwa hatua hadi huko utapajua kote we kuwa na subira"

    "Enhee! Ndiyo"

    "Jirani yangu ni mmoja wa maaskari wa gereza ambalo ofisi zako zipo, ndiyo aliweza kutoa siri hii. Aliniambia jinsi ambavo wafungwa huwa wanatolewa usiku na magari tofauti ya magereza ambayo huja hapo gerezani. Alieleza kuwa huwa wanaambiwa warudi nyumbani katika muda ambao wa kazi pindi yanapoingia magari hayo, yeye aliamua kunieleza hayo kutokana na kuhisi ni kinyume cha utaratibu na pia alikuwa ni mdogo kicheo alikuwa akihofia maisha yake. Hapo ndipo mimi nilipofunga safari hadi hapo gerezani muda huo wa usiku nikiwa nimevaa nguo zake za kazi, kama kawaida nilishuhudia yakija magari ya mizigo makubwa na yaliingia hadi ndani. Nikiwa nimebandika kamera yangu kwenye kifungo cha shati, tuliamriwa wote kwa pamoja tuondoke hapo gerezani kurudi nyumbani eti tulitakiwa kuwa off. Ndugu SSP napenda utambue kuwa sikutaka kuondoka hapo gerezani bali nilijibana mahali nikiwa nashuhudia jinsi ambavyo wafungwa walivyokuwa wakitolewa na kisha hupewa nguo nyingine na kupanda hayo magari na kisha kuondoka. Kwenye siku hiyo ndipo nilipoweza kumshuhudia ASP Lutonja akiwa yupo katika nguo za kiraia akiwaongoza wafungwa hao kuingia kwenye magari. Siku hiyo niliwafiatilia hadi walipifika kwenye gereza la Ukonga ambapo walichukua wafungwa wengine, safari yao hiyo iliendelea hadi Kisarawe porini. Huko nilishuhudia kukiwa na magari makubwa ya mizigo mawili, moja la jeshi la polisi na jingine la JWTZ. Yote mawali yalikuwa yana mizigo ndani yake ambayo sikuweza kuitambua hadi pale waliapoanza kuishusha. Niliweza kushuhudia kwa macho yangu silaha mbalimbali zikishushwa na kisha kuingizwa ndani ya magari hayo yalikuwa yamewachukua wafungwa hao hadi zikaisha, kazi hiyo yote walifanya wafungwa waliochukuliwa ambao walionekana kuwa na maelewano mazuri na maasakari hao kwani walikuwa wakiongea nao kama marafiki. Picha zote za ushahidi ni hizi hapa jionee mwenyewe" Alipomaliza kuongea maneno hayo alitoa picha zingine akampatia SSP Nkongo.

    Alibaki kutoamini kwa picha hizo ambazo zilimuonesha rafiki yake kipenzi ambaye alikana kabisa kujihusisha na tuhuma hizo, msaliti alikuwa ni rafiki tena zaidi ya ndugu ambaye walishibana kwa kipindi kirefu cha muda tangu wakiwa hawajijenga kimaisha. Ilikuwa ni aibu sana kuwa rafiki ambaye alikuwa akiliasi taifa pasipo kujali kiapo ambacho alikiweka. SSP Nkongo alikuwa akimpenda sana rafiki yake lakini kwa hilo jambo ni heri hata urafiki ufe kuliko kuwa na msaliti.

    "Sawa Bwana Kizigo nimekuelwa naomba uniachie hili suala nilifanyie uchunguzi, pia huo ushahidi naomba usitoke kwenye gazeti kabla sijamaliza upelelezi wangu nitakaouanza mwenyewe" Alimuambia

    "Sawa SSP hilo halina shida ushahidi mwingine video hizi hapa nafikiri ni muhimu kwako" Kizigo alimpatia na mikanda ya video ambayo alikuwa ameirekodi kuhusu tukio hilo la usaliti wa afisa wa ngazi ya juu kabisa wa magereza.

    Waliagana hapo na kisha kila mmmoja akaondoka kuelekea alipokuwa amepanga kwenda katika majira hayo, hawakujua kabisa ushahidi huo ungekuwa ni chanzo mengine ndani ya maisha yao. Pia hawakutambua kuwa walikuwa wakipambana na mtandao mkubwa kiasi gani ambao ulikuwa nyuma ya kila kitu walichokuwa wakikichunguza. Utayari wa kufanya jambo lolote katika uchunguzi huo ndiyo uliwafanya hata wasijali kuhusu uhatari wa kazi waliyokuwa wakiifanya, Askari aliyekuwa yupo tayari kufa kwa ajili ya nchi yake. Alikuwa amekutana na mwandishi ambaye yupo tayari kufa kwa ajili ya kutetea jamii yake, hakika walishabihiana kwa kila kitu.

    ****

    Jioni yake ilikuwa ni ambapo giza lilianza kuzidi kwa wafuatiliaji wa sakata hili kabla majira ya usiku wa manane hayajafika, kubisha hodi kwa giza kwa wafuatailiaji hawa. Kulianza nyumbani kwa Bwana Kizigo ambaye alikuwa hana hili wala lile na wala hakutarajia kama yangekuja kuwa hayo. Majira ya saa moja jioni akiwa anaangalia luninga nyumbani kwake, mlango mkuu wa mbele katika nyumba hiyo ambayo alikuwa anaishi uligongwa kwa taratibu sana. Ugongwaji wa mlango huo ulisababisha mke wake ambaye alikuwa yupo jikoni akiendelea na shughuli zake za upishi atoke mbio hadi mlangoni kwenda kumsikiliza huyo mgeni. Alipoukaribia mlangoni alifungua kiuwazi kidogo na kisha akaangalia nje, alipomuona mgongaji wa mlango huo aliamua kufungua kwani hakuwa na hofu yeyote kwake.

    Aliingia ASP Lutonja akiwa ameongozana na watu wawili ambao walikuwa waemvaa suti nyeusi, Mke wa Kizigo aliwatolea tabsamu akiona walikuwa ni wageni wa kawaida.

    "Karibuni" Aliwakaribisha zaidi lakini karibu yake ilijibiwa na mmoja wa wale watu waliokuwa wamevaa suti kuchomoa bastola ndani ya koti lake la suti.

    Kzigo alishuhudia kwa macho yake mawili bastola hiyo ikikohoa na kupasua kichwa cha mke wake kipenzi, aliuona mdomo huo wa bastola ukimuangalia yeye baada ya kuachia kikohozi chenye maafa.

    "Kizigo napenda nikuambie kuwa uropokaji una ubaya wake, tulianza na Kibiti kwakuwa alikuwa ni mbishi kama wewe. Sasa ni zamu yako" ASP Lutonja aliongea kifedhuli

    "Lutonja ndiyo unaniua nipo radhi uniue lakini jua hamna siku nyingi nyinyi mtaozea jela" Pamoja na kuwekewa silaha aliwajibu kijeuri

    "Tunayo miaka mingia ya kuishi vyombo vyote vya dola vipo chini yetu siku nyingi. Jiulize huo ushahidi wako utaenda wapi wewe"

    “Ndiyo mnavyojidanganya siyo tayari haupo mikononi mwangu na upo kwenye mikono ya mtu ya mwaminifu sana katika vyombo hivyo vya dola. Mkuu wako hakuniamini nimeupeleka kwingine kabisa"

    “Unachekesha wewe rafiki yangu kipenzi anayeniamini SSP Nkongo akuamini wewe na gazeti lako linaloropoka hadi tumelipakazia sifa na kuonekana la udaku linalodandia siasa"

    "Sasa tuone mtapata faida gani na kuniua mimi, nipo tayri niueni kama mke wangu ila mjue kiama chenu chaja"

    "Hebu dawa yake naona anachonga sana na huyo mwenye ushahidi tutampata" ASP Lutonja aliongea na hapohapo ile risasi ilikohoa tena, paji la uso la Kizigo lilitobolewa na na ukawa ndiyo mwisho wake.

    "Kiama ni chako kimefika sisi chetu bado hata ungekuwa na mtoto angeota mvi sisi bado hakitafika, boys chomeni nyumba yake ionekane ni tukio la ajali ya moto. Mimi nitahakikisha ripoti itayofanywa ya kifo hiko inapindishwa" Alipoongea maneno hayo alitoka hadi nje ya nyumba hiyo akiwaacha wale vijana ndani.

    Muda mfupi baadaye wale vijana walitoka nje kujongea hadi mahali walipokuwa wameegesha gari, walipolifikia tu gari lao nyumba ile ililipuka kwa moto mkubwa sana. Wao waliachia matabasamu kisha wakaingia ndani ya gari na kuondoka.

    ****

    Majira hayo SSP Nkongo alikuwa amekaa sebuleni akiwa yupo na mtoto wake wa miaka kumi na mbili ambaye ni James, kaka yake mkubwa alikuwa yupo kwenye meza akijisomea kutokana na kuwa yupo kwenye masomo ya sekondari. Muda huo alikuwa akiangalia Luninga lakini tafakari zote zilikuwa zipo kwenye ushahidi aliokuwa amepewa na Kizigo, alikuwa akitafakari jinsi mbavyo mtu mzima yule mwenye taaluma ya habari alivyojitoa mhanga ili kuweza kupata ushahidi muhimu kama huo. Macho yote yakiwa yameelekea kioo cha luninga, moyo wake ulikuwa ukimpongeza kabisa kwa kazi nzuri aliyokuwa ameifanya yeye na Marehemu Kibiti.





    Hakuwa hata na taarifa ya mwenzake ambaye alikuwa amempa ushahidi muda mfupi uliopita, hakujua alikuwa amebaki peke yake tu ambaye alikuwa akiujua ushahidi ule ambao ungewaweka wote wale matatani. Alitafakari kuhusu suala hilo ambalo lilikuwa limemfanya aanze kumchukia rafiki yake kipenzi, tafakuri hizo za ndani ya kichwa chake ziliambatana na upangaji wa jambo jingine. Hakika alidhamiria kwa nguvu zake kuhakikisha ASP Lutonja anaishia nyuma ya nondo kwa usaliti aliokuwa ameufanya hakuona umuhimu wa mtu huyo kuendelea kuwa uraiani ikiwa alikuwa amefanya usaliti mkubwa. Akiwa kwenye tafakari hizo kwa mara nyingine aliweza kulikumbuka jina ambalo lilikuwa limeanza kumtoka ndani ya kichwa chake, usaliti wa mwenzake ndiyo chanzo kikubwa cha yeye kulikumbuka jina ambalo lilikuwa limesahaulika tayari kwenye kichwa chake. Bond ndiyo jina pekee ambalo alikuwa ameanza kulisahau ndani ya kichwa chake, hatimaye lilikuwa limerudi kichwani mwake kwa mara nyingine.

    Asili ya neno Bond ilikuwa ni miaka thelathini iliyopita ndani ya Shule ya sekondari ya Usagara Tanga, jina hli lilikuja baada ya wanafunzi wa shule hiyo kusoma kitabu cha kipelelezi maarufu kilichoandika na mwandishi Ian Fleming. Urefu wa jina hili ulikuwa ni James Bond lakini lilikuja kufupishwa ndani ya shule hiyo. Jina hili lilikuja kubandikwa na kuficha jina la mwanafunzi mwingine kabisa ndani ya shule hiyo. Sifa za huyu mwanafunzi ambaye alikuwa ni kibaraka wa walimu, mwanafunzi huyu hakuweza kufahamika ukibaraka wake kwa walimu hapo shuleni. Haikuweza kufahamika jina halisi la mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akifanya upekuzi wa siri zao na hatimaye kuzianika kwa walimu na kuwapa wakati mgumu wa kukabiliana na adhabu ngumu, waliishia kumbandika jina mtu huyo kama Bond kutokana na kumtomjua na pia jinsi alivyokuwa akiwapeleleza. Ilifika kipindi wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wakawa hawaaminiani kutokana na mtu huyo ambaye alikuwa akiuza siri zao kwa walimua kila kukicha. Kila mmoja alikuwa akimuhisi mwanafunzi mwenzake kuwa alikuwa akihusika na jambo hilo ikiwa siri zao walizokuwa pamoja zikagundulika. Hakika walikuwa wakimuogopa Bond huyo waliyembatiza jina kila siku, hawakuwahi kumjua kwa sura lakini sifa zake ilitosha kuwatia hofu kabisa. Hawakujua kabisa huyo alikuwa akifanana namna gani, zaidi ya kuishia kujenga picha vichwani mwao kuhusu muonekano wake. Kila mwanafunzi ambaye alikuwa yupo makini sana katika mambo yake walikuwa wakikaa kimya kila mtu apitapo mbele yao, walihisi huenda huyo ndiyo alikuwa Bond huyo aliyekuwa akiwaharibia mambo yao yaliyokuwa yapo kinyume na miiko ya shule. Walipoweka jicho la umakini kila waongeapo kwa kuwa wamemuhisi fulani bado mipango yao ilikuwa ikiharibika kila kukicha, hakika walibaki wakichnganyikiwa wakijiuliza huyo Bond alikuwa na uwezo gani. Wengi wa wanafunzi wa mkoa wa Tanga kwa kipindi hicho walikuwa wakimuhusisha sana na ushirikina huyo mwanafunzi, hata viranja wasio waaminifu ambao walikuwa wanawaibia siri ya wanafunzi mbalimbali walikuwa hawajui alikuwa akifanana vipi. Imani za kishirikina zilizokuwa zimetawala ndani ya mkoa hu zilitosha kabisa kwa wao kumuhusisha na ulozi.

    Bond mwenyewe aliyekuwa akiwanyima raha wale wavunjifu wa sheria za shule, alikuwa ni mwanfunzi wa kawaida sana hapo shuleni. Asiye na cheo cha uongozi wa serikali ya wanafunzi wala uongozi wa darasa, hakuna ambaye angedhania kwamba huyo mwanafunzi ndiye alikuwa akiwaharibia kila siku mipango yao. Wengi walizoea kumtania kutokana na urefu aliokuwa nao, alikuwa ni mu ambaye alikuwa hakasiriki kila anaapotaniwa. Kipenzi cha watu ndani ya shule hiyo, aliyependwa na wanafunzi karibu vidato vyote kutokana na kupenda kuwajali watu pamoja na ucheshi aliona nao. Ndiye huyu aliyekuwa akiitwa Bond kutokana na kupeleleza maisha ya wanafunzi hao shuleni, hakuna ambaye alikuwa hamfahamu huyu mwanafunzi kutokana na ucheshi aliyo nao. Aliitwa Elius Nkongo kwa jina lake halisi, ndiye huyu ambaye alikuwa akiwanyima usingizi wavunjifu wa sheria za shule. Kijana ambaye alizaliwa na uwezo wa juu katika kufuatilia mambo ambao ulikuja kubainika kwa wazazi wake wenye asili ya Kagera waliokuwa wakifanya kazi mkoani Tanga, kabla walimu wa shule hiyo hawajaufahamu kuufahamu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hadi anaondoka ndani ya shule hiyo hakuna ambaye alikuja kuikaimu nafasi yake ya kupeleleza wavunjifu wa sheria za shule, alibaki kuwa historia tu jina lake ndani ya shule hiyo kwa wanafunzi wa miaka aliyokuwepo. Mwaka aliyohitimu kidato cha sita ndiyo mwaka ambao habari hizo za kukamatwa kwa watu ziliisha, wengi walijua kabisa kuwa huyu Bond alikuwa ametoka kwenye mwaka wa wanafunzi hao waliomaliza ingawa hawakumjua kwa sura. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kupooza kwa ufuatiliaji wa wanafunzi na hata ule wasiwasi ukapungua kutokana na kuondoka kwake.

    Bond huyu alikuja kuhamia kwenye mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa ya awali kabisa, yalikuwa ni mafunzo ambayo walikuwa wakikaa mwaka mzima ndani ya kambi. Mafunzo hayo nayo bado hakuacha ile asili yake ambayo alikuwa ameianza tangu kipindi akiwa yu mdogo, huko napo alipokea sifa ya aina yake akiwa yupo huko jeshini. Ilifikia hatua ya kutaka hata kuchukuliwa akimaliza mafunzo hayo lakini Mzazi wake hakupenda kabisa. Alikuwa akihitaji mwanae aendelee na masomo na si kujiunga na jeshi hilo, majibu ya kidato cha sita hayakuwa mazuri kwake jambo ambalo lilifanya ashindwe kujiunga na chuo. Hili suala lilimfadhaisha sana mzazi wake na Bond akabaki mtaani alipotoka mafunzoni, aliendelea na tabia yake ileile ambapo kwa muda aliokuwa amekaa hapo mitaa ya nyumbani kwao alifanikiwa kugundua uwepo wa kikundi cha uhalifu. Maaskari wa jeshi la polisi walimpongeza sana kwa kuweza kufanikisha huko kugundulika kwa kikundi hicho, lakini aliporudi nyumbani ilikuwa ni ugomvi mkubwa. Mzee Nkongo alikuwa hataki kabisa mtoto wake afanye huo upelelezi wake ambao alikuwa akiufanya tangu yupo mtoto, alkizidi kumuonya na hapo akaona hakusikilizwa.

    Alipochoshwa na tabia hiyo mbayo alikuwa akimuonya mwanae ilimbidi tu aongee naye kuhusu kujiunga na jeshi la polisi, aliona ndipo kunamfaa. Aliamini kuwa jambo hilo litasikilizwa na kuuungwa mkono na mwanae huyo, aliona kabisa alikuwa na mwangaza wa kuelekea huko. Ule msemo wa kuwa kipaji huonekana kwa mtu angali mdogo, aliuamini kabisa na akaamua ni bora ampeleke sehemu ambayo inamfaa kwa yeye kuendeleza hicho kipaji chake. Alikuwa na uhakika kabisa Bond angelipokea suala hilo kwa mikono mwili, muda wa jioni akiwa yupo ndani ya nyumba yake aliyopewa na serikali alimuita mwanae na kumueleza kuhusu suala hilo. Tofauti na alivyotarajia suala hilo lilipokewa kwa namna nyingine kabisa, kupingwa kwa suala la kujiunga na jeshi la polisi ndiyo alipopakea. Mzee Nkongo alichoka na hakumuelewa kabisa mwanae huyo, aliyekuwa akikaa nyumbani huku muda ukiwa unaenda sana. Alitakiwa awepo masomoni au awe na ajira yeyote kwa kipindi hicho, lakini masomo yameshindikana na ajira nayo alikuwa ameikataa. Hakuweza kumuelewa na ikambidi amuulize kile apendacho kukifanya, hapo ndipo Bond alichagua kujiunga na jeshi katika kikosi kingine tofauti ambacho baba yake hakudhania kabisa.

    Elius maarufu kama Bond hatimaye alichagua kujiunga na jeshi la Magereza kwa mafunzo mafupi kwani tayari alikuwa amepitia mafunzo imara ya kijeshi. Nafasi kipindi hicho za kujiunga na jeshi hilo zilikuwa zimetoka, alipoomba kutokana na kuwa katika jeshi la kujenga taifa kwa muda mrefu. Alipita bila kikwazo chochote na akajiunga kwa mara ya kwanza ndani ya jeshi hilo, pamoja na kujiunga kwake ndani ya jeshi hilo bado hakuacha kabisa tabia yake ya kupeleleza. Huku jeshini ndiyo alikuja kukutana na rafiki yake waliyepotezana wakiwa shuleni, huyu hakuwa mwingine ila ni Philipo Lutonja.

    Bond huyu alikuja kulala usingizi katika kipindi ambacho alikuwa amepata mchumba,tabia hii ilionekana kumkera kabisa mwanamke ambaye alikuwa amempata katika umri wake aliokuwa akihitajika kuwa na mwenza. Kipindi hicho alikuwa tayari amehamishiwa jijini Dar es salaam akiwa pamoja na rafiki yake Philipo, ajira alikuwa nayo na cheo alikuwa ameshapata japo hakikuwa kikubwa sana. Tabia hii ilikuja kujulikana na mchumba wake ambaye ilimchukiza sana, alimuonya kuhusu hiyo tabia ya kufuatilia vitu lakini haikukoma. Mwishowe alitishiwa kumuacha ndipo alipoamua kuiacha tabia, hapo ndipo Bond alilala na akabaki Elius yule mcheshi na mpenda kuzungumza na kila mtu.

    Miaka thelathini sasa imepita tangu Bond alale akimuacha Elius akiwa yupo huru, akiwa ameacha ile tabia yake ya kupeleleza. Sasa akiwa amekaa hapo kwenye kochi ndiyo aliamka tena, uamkaji huu ulikuwa ni wa kimyakimya sana bila hata kumshtua mwanae wa mwisho James akiwa yupo naye. Hakika asili haifi hata kwa kushikiwa silaha, humrudia mtu kutokana na sababu maalum. Ndiyo ilivyokuwa kwa SSP Nkongo asili hiyo ilirudi katika muda ule ambao yule Mchumba wake anaitwa mke wake na wala hakuwaza kabisa kama ingeweza kurudi, hakukaa sana hapo kwenye televisheni yeye aliinuka na kuingia ndani. Huko ndani napo hakukaa sana, alitoka akiwa mkononi na funguo pamoja na mkoba wake wa kazini, alielekea kwenye maktaba yake ambayo alikuwa akifanyia mambo muhimu ya kiofisi kipindi akiwa yupo nyumbani kwake. Kitendo cha kuketi mezani kiliambatana na utoaji simu yake ndogo ambayo haitumii kwa mawasiliano makubwa, alibonyeza vitufe vya simu hiyo na hatimaye alipata kitu alichokuwa akikitafuta.

    Alikuwa akitafuta ni faili muhimu la sauti ambayo alikuwa ameirekodi kipindi akiongea na Kizigo, alicheza sauti hiyo ikawa inasikika vyema katika muda huo aliokuwa amejifungia humo ndani. Aliisikiliza sauti kwa umakini kabisa akifuatilia hadi jinsi iliyokuwa ikizalishwa, alijenga taswira ya Kizigo na kipindi akiongea na hapo akapata akakumbuka lugha ya mwili kipindi alipokuwa akiongea naye. Lengo lake ilikuwa ni kupima kuwa huyo mtu alikuwa yu miongozi mwa ukweli au siyo, ushahidi pekee wa picha haukutosha kumthibishia kuhusu hilo pasipo yeye kuchunguza. Uchunguzi wake hakuona shaka ndani ya maneno ya Kizizo, hakika alikuwa ni miongoni mwa wakweli. Bado hakutaka kujiridhisha kuwa ushahidi wote uulikuwa umekamilika, alitaka ajithibitishie na yeye. Hakuwa mtu wa kuridhishwa na ushahidi utakaoletewa pasipo na kujiridhisha, hapo aliamua kupanga mikakati muhimu ya kazi yake. Vitu muhimu ambayo alikuwa akivifanya aliamua kuvinakili kwenye kitabu chake cha siri ambacho alikuwa akikitumia kuhifadhia mambo muhimu, usiri uliomo ndani ya kitabu hicho ulikuwa ukijulikana na yeye mwenyewe tu na hata mke wake hakuwa akijua. Aliponakili mammbo muhimu ya kuanzia alifunga kitabu hicho, alitoka na kurudi ukumbini kwani muda wa kula tayari ulikuwa umewadia.

    Siku iliyofuta kama kwaida alienda ofisini kwni ilikuwa ni siku ya Ijumaa, ilikuwa ni siku ya kazi ilimbidi awe kazini. Asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameshapata taarifa za kifo cha Kizigo mtu muhimu aliyemfumbua macho. Magazeti muhimu ndani ya asubuhi hiyo yalikuwa tayari yameshaandika habari juu ya kifo hicho, magazeti mengi yalikuwa yameandika sababu maalum juu ya kifo hicho. Alijikuta akivutika na gazeti moja kati ya magazeti mengi yaliyokuwa yameandika juu ya kifo hicho, lilikuwa ni gazeti muhimu sana ambalo huandika mambo mazito kuhusu matukiom balimbali ndani ya nchi hi.

    'KIZIGO AULIWA NA WASALITI WENZAKE Muuaji aeleza kila kitu'. Hicho kilikuwa ni kichwa cha habari kikubwa na maandishi madogo yalifuatia chini yake. Gazeti hilo lilimvutia kabisa pindi aliposhuka kutazama meza ya magazeti siku hiyo, alilipita hela na kisha akarudi ndani ya gari akaendeleana safari ya kuelekea ofisini.

    Kitendo cha kutia mguu ndani ya ofisi yake tu na kufunga mlango, alitupa gazeti hilo kwenye meza yake na kisha akaweka mkoba chini ya meza. Alipoweka kiungo cha kukaa kwenye kiti chake, alikamta gazeti hilo na kuanza kuipitia habari hiyo kwa umakini sana. Alimaliza kuisoma habari hiyo na akaona ni jinsi gani ilikuwa imetengenezwa kiufundi zaidi, alinakili vitu muhimu kwenye habari hiyo na kisha aliendelea na kazi zingine zilizomuweka kwenye jeshi hilo.

    ****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda wa kifungua kinywa ulimkuta akiwa yupo meza moja na rafiki msaliti, ilikuwa ni kawaida kwenda pamoja katika maeneo kama hayo na hakutaka kabisa kuuvunja utaratibu huo. Alijua wazi laiti angeuvunja ingekuwa ni mwanzo wa kuweka fikra mpya kichwani mwa ASP Lutonja. Hakutaka hilo litokee mapema kabisa, aliamua kutobadilisha tabia zote ambazo alikuwa akizoeleka kuonekana nazo akiwa naye. Lengo ni kuzidi kuivuta amani ya moyo wake, kuonesha hakuwa anajua chochote ili aweze kumchunguza. Bond alikuwa yupo kichwani mwake na ule umakini wake uliongezewa na hamasa za kusoma riwaya za James Bond ulikuwa umerudi tena, ucheshi ulikuwa ukitawala kwenye maneno yake. Si yeye wala ASP Lutonja aiyekuwa amegusia juu ya tuhuma iliyowasili siku iliyopita, walipomaliza kupata kifungua kinywa ndipo Msaliti wake alipoanzisha mada hiyo.

    "Elius vipi jana ulienda kukutana naye?" Aliulizwa

    "Aaaah! Nilienda hana lolote lile waandishi wa habari wanaleta janjajanja tu" Alijibu

    "Nilkwambia mimi rafiki jana hukutaka kunielwa aisee, siwezi kusaliti kiapo nilichokiweka wakati najiunga na jeshi hili"

    "Aisee nimekuamini kabisa si umesikia kumbe naye alikuwa akihusika kwenye mchezo huo"

    "Unaona sasa! Alitaka kunigeuzia mimi mpira yaani mambo yamekuwa mabaya kwake wenzake wamemuuua, si umesikia Mhusika yupo kituo cha kati kasema katumwa kumuua na kaichoma nyumba yake moto"

    "Mshahara wa dhambi ni umauti na kaupata"

    "Kabisa kabisa hata angepona bado angekuwa na kesi ya kujibu, kwanini anichafue Assistant Superintendent of prison"

    "Ujue habari ya kizigo alivyokuwa akinisimulia imenikumbusha ishu ya Bond kipindi kile tupo shuleni"

    "(huku akicheka) Aisee Elius una kumbukumbu, unajua sikuwahi kumjua ni nani yule mtu aliyekuwa akipeleka taarifa kwa walimu hadi namaliza pale shuleni"

    "Hata mimi simjuia hadi leo hii,naona huyu Kizigo ndiyo likuwa akileta ujanja huo. Bahati mbaya hata kupangilia maelzo hajui yaonekane kweli, body language imemuonesha ni muongo"

    "Achana naye huyo si wa kumsema tena, Elius unajua wiki ijayo ni Kipaimara ya Jane"

    "Sasa nitajuaje bila wewe kunifikia taarifa, nina tunguli za kunijulisha"

    "Haaaah! Huachi mambo yako, sasa ndiyo nakujulisha hivyo ni wiki ijayo jumapili sherehe nyumbani"

    "Usihofu nitaleta mangoko yangu haya nije kukusaidia kupunguza kilo za pilau ili usipate akiba ukamwaga"







    Kicheko kilimtoka ASP Lutonja kutokana na vituko vya rafiki yake, alicheka sana huku akimtazama lakini hakukuta cheko kwenye uso wa SSP Nkongo zaidi ya tabasamu. Alicheka hadi alipomaliza hakusikia kicheko chake, alikuwa amemzoea kabisa rafiki yake ambaye hupenda kumchekesha pasipo yeye kucheka.

    "Hivi Elius hivyo vituko utaacha lini?" Alimuuliza

    "Mamba akiacha kuwinda kwenye maji na mimi ndiyo nitaacha" Alipewa jibu

    "Yaani tupo shule hivyohivyo, JKT nahisi ulikuwa hivyohivyo. Tunaingia mafunzoni hivyohivyo hadi huku kazini aisee"

    "Yaani nimekuambia Mamba akiacha kutegea mawindo ndani ya maji na kuja kutega na kushika nchi kavu. Basi nitaacha pia"

    "Ushawaambukiza hadi watoto wake aisee, yaani Fred ndiyo huyo vituko James sipati picha aisee"

    "Hivi Paka kuchimba shimo kabla ya kujisaidia anaambukizwa na mzazi wake?"

    "Hamna ni tabia asili"

    "Basi Fred naye ni tabia asili kama yangu"

    "Mshindi wewe, time hii imekimbia tayari tuondoke"

    Wote walismama kwenye viti walivyokuwa wamevikalia wakiwa wanaongea na kutaniana, kila mmoaja aliingia ofisini wake na kuendelea na kazi kama kawaida.

    Muda wa kutoka kila mmoja alielekea nyumbani kwake na baadaye jioni walikutana tena, walikutana kwenye bar moja ambayo walikuwa wakipenda kukutana kila ufikapo mwisho wa wiki. Ndani ya Bar hiyo walikuwa wakipenda kupata kinywaji kutuliza machungu ya wiki nzima, walikunywa na kula nyoma choma wakiongea mambo mbalimbali. Muda huo SSP Nkongo alikuwa akitafuta kila mbinu aweze kumchimbua huyo Msaliti wake, pombe iliendelea kunyweka kwa taratibu sana kiupande wake lakini kwa mwenzake alikuwa akinywa kwa fujo san. Haikufika muda mrefu ASP Lutonja alikuwa amelewa tayari na uchangamfu mkubwa ulikuwa umemvaa na hata akafikia kupiga makelele kwa nguvu.

    Hiyo ilikuwa ni hatua mbaya sana kwao kutokana na kujulikana vyeo vyote, ili kuiokoa hatua hiyo SSP Nkongo alimchukua rafiki yake hadi kwenye gari yake ambayo ndiyo walikuja nayo pamoja. Ilikuwa ni muda ambao giza lilishaanza kuingia na kuiondoa nuru ambayo ilikuwa iking'ang'ania kuwepo ingawa muda wake ulikuwa umeisha. SSP Nkongo aliliondoa gari kwa mwendo wa wastani hadi alipofika eneo ambalo lilikuwa ni mitaa kadhaa kutoka nyumbani kwa ASP Lutonja, hapo alisimamisha gari na kisha akamtazama rafiki msaliti aliyekuwa haishiwi kuropoka akiwa yupo ndani ya gari.

    "Unajua hii kazi nishaanza kuona haina faida kiupande wangu vipi wako mzee" Alimuuliza kimtego huku akitambua kiwango cha unywaji pombe alichofikia hakikuwa na utunzaji siri.

    "Mimi nishatambua hilo kitambo sana ndiyo maana nikaungana na wakina Meja Ibrahima Salim wa JWTZ" ASP Nkongo aliropoka

    "Yaani Philipo wewe rafiki yangu upo kama ndugu yangu wa damu unanificha hili"

    "AaaaaH! Tatizo wewe Elius unajifanya mzalendo kulinda kiapo, kiapo kitu gani viongozi wa dini tu wanasaliti imani zao ndiyo sembuse sisi"

    "Nipe mpango upo vipi maisha yanapanda gharama si unajua hilo"

    "Aaaaah! Kitu simpo kabisa Elius, ni kuiba silaha za kambi zote za kijeshi na kuziuza tuna mawakala wakubwa"

    "Duh! Mtu wangu si hatari hiyo au kupo vipi"

    "Hakuna hatari yeyote ile, polisi na hata usalama wa taifa wapo viganjani mwetu hawana tabu kabisa. Umeona kama Kizigo kajifanya mjuaji jana tumemfuata na tumemuua kisha tumemuuzia kesi mwingine kabisa na kalazimishwa akakiri. Eti aje kunisemea kwako"

    "Ndiyo hapo hata mimi nameshngaa kabisa, mimi na wewe toka lini tukawekana pabaya"

    "Aaaaah! Si ndiyo hapo yule jamaa hebu muache na ujinga wake"

    "Sasa nipe ramani nipo tayari kujiunga na wewe nisogeze maisha"

    "Usijali wewe kama ndugu kwangu kesho nitakuja kukupa taarifa kila kitu"

    "Hamna shida.

    SSP Nkongo alipoondoa gari baada ya kuridhishwa na majibu ya mwenzake ambaye alikuwa amelewa, alimpeleka hadi nyumbani kwake na kisha alimshusha na kuingia naye ndani. Alipomkabidhi kwa mke wake kisha aliondoa gari na kuelekea nyumbani kwake akiwa na ushahidi mwingine, ASP Lutonja alikuwa hatambui kabisa kile ambacho kilikuwa kimetokea kutokana na kuzidwa kilevi. Hakujua sababu ambayo ilimfanya rafiki yake huyo asinywe kilevi kingi zaidi ya kunywa kidogo akiwa na kinywaji chenye kupunguza makali kilevi hicho, lengo lilikuwa limeshatimia mtegwaji alikuwa hatambui kama alikuwa ametegwa.

    SSP Nkongo alipofika nyumbani hakukaa hata kidogo aliaga na kutoka, aliongoza gari yake kuelekea kwenye eneo ambalo hisia zake zilikuwa zimemtuma. Safari yake alifuata muongozo wa aliokuwa ameukuta kwenye picha ya Kizigo mojawapo ambao ulikuwa umewekwa nyuma. Muongozo huo ndiyo ulimfikisha hadi kisarawe na alipitliza kwenye eneo alilokusudia hadi mbele kidogo ambako alikuta kulikuwa na mji mdogo. Aliegesha gari yake pembeni ya duka hio na kisha akaomba kuangaliziwa, alitoa ahadi ya kurejea muda mfupi na kisha alianza kukita hatua zake ndefu ardhini kusogea alipopakusudia. Alifika kwenye eneo alilokuwa amelikusudia na alitembea kuingia kwenye njia ya kujificha kulingana na muongozo wa picha aliokuwa ameukariri, aliingia kwenye kichaka na akajibana hapo. Alikaa kwenye eneo hilo kwa muda mrefu na hata alifikia kukata tamaa ya kuendelea kukaa hapo, muda mfupi baadaye aliweza kushuhudia gari mbili kubwa za kijeshi zikiingia kwenye njia ambayo ilikuwa ikiingia kwenye eneo la pori ambalo alikuwa amejibana. Alishuhudia watu wanne wakishuka baada ya magari hayo kuegeeshwa, watu hao walienda moja kwenye eneo lenye majani mengi. Kilikuwa ni kichaka kilichokuwa kimejifunga ambacho watu hao waliingia na hawakuonesha dalili ya kutoka. Alikaa hapo kwa muda wa dakika kadhaa ili kuhakiki kama watu hao ndani ya mgari walikuwa peke yao. Alipoona kimya kwenye magari hayo taratibu alijitoa kwenye kichaka hicho, alitembea kwa mwendo wa kunyata mithili ya simba aliyekuwa akinyatia wingo lake. Alikuwa yupo makini sana asiweze kupatwa na Yuda mmoja miongoni mwa Mayuda wengi waliokuwa wakihusika na eneo hilo, kituo cha kwanza cha mnyato wake ilikuwa kwenye magari hayo ya kijeshi yaliyokuwa yameegeshwa na kuzimwa taa. Ubond ulikuwa umempanda kichwani akajikuta akiyaangalia magari hayo vizuri aweze kutambua umiliki wake ulikuwa ni jeshi gani, pamoja na uwepo wa giza eneo hilo aliweza kutambua gari mojawapo ni aina ya Iveco na muundo wake alibaini kabisa lilikuwa ni gari la jeshi la wananchi, jingine aliona lilikuwa ni aina ya Leyland hapo alitambua lilikuwa ni mali ya jeshi la polisi kutokana na kuchunguza sehemu za bati za namba kwa macho yake makali gizani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakutaka kulala nyuma baada ya hapo alisogea hadi kwenye eno ambalo lilikuwa na kichaka, taratibu alifungua kichaka hicho akaingia akiwa na tahadhari kubwa. Alikutana na njia iliwekwa mawe ambayo ilikuwa ikishuka chini ya ardhi. Alishuka chini kuifuata njia hiyo hadi alipofika kwenye eneo ambalo lilikuwa na mlango, alijaribu kuufungua mlango lakini alishindwa kutokana na kufungwa uimara. Alipoutazama sehemu ya pembeni alibaini kuwa ulikuwa umefungwa na namba za siri, ugumu wa kufungua mlango huo alianza kuuona na hakutaka kubaki tena eneo hilo kwani hakuwa na njia nyingine ya kuufungua huo mlango. Aliondoka kwa kupitia njia aliyoingia nayo eneo hilo hadi barabarani na kisha alirudi hadi pale alipokuwa ameeegesha gari lake, alitoa noti moja ya shilingi elfu tano na kumpatia aliyemuomba kumlindia gari. Baada ya hapo aliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi awahi kufika nyumbani kwake, dakika ishirni baadaye alikuwa tayari ameshafika nyumbani kwake kwa ajili ya kupumzika na familia yake.

    ****

    Asubuhi iliyofuata AS Lutonja aliamka akiwa ni mchovu sana kutokana na kilevi cha siku iliyopita, pamoja na uchovu huo hakutaka kabisa kukaa ndani kwani ilikuwa ni muda ambao alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa pamoja na rafiki yake. Alivaa nguo za mazoezi baada tu ya kusafisha kinywa chake na kisha akatoka nyumbani kwa akiwa ameongozana pamoja na kijana wake wa kiume, wote walikimbia taratibu kuelekea nyumbani kwa SSP Nkongo. Baada ya mwendo wa takatibani robo saa waliweza kufika nyumbani hapo, walimkuta tayari akiwa amejiadnaa akiwa na kijana wake Fred ambaye alikuwa akikimbia naye mazoezi. Familia hizo mbili kwa pamoja zilijiunga na kuanza kukimbia kuelekea kwenye uwanja wa mpira ambao walikuwa wakipenda sana kufanya mazoezi hapo, muda mfupi baadaye walifika uwanjani hapo wakikimbia huku mmoja akiwa ni mwenye amani moyoni mwake lakini mwingine hakuwa na amani. Mmoja alikuwa amejawa na umakini mkubwa katika kumchunguza mwenzake, umakini huo aliokuwa amejawa nao alikuja kupata uhakika na kisha akaondoa hofu.

    Alikuwa ni SSP Nkongo alikuwa na hofu huenda mwenzake angekuwa na kumbukumbu wa kile kilichotokea usiku uliopita, kulewa haikumaanisha ndiyo ingeweza kutokuwa na kumbukumbu zote. Alihisi angeweze kukumbuka chochote. Alipopata uhakika hakuwa akikumbuka chochote aliondoa hofu yote aliyokuwa nayo, aliendelea kufanya naye mazoezi kuweka mwili sawa kwani hawakutaka kabisa kuwa na miili ya kizembe ingawa walikuwa na vyeo vikubwa ndani ya jeshi la Magereza. Mazoezi yaliwachukua muda mfupi na hadi saa moja asubuhi wakawa tayari wameshamaliza, walianza kukimbia kwa mwendo wa taratibu wakirejea majumbani mwao kwa ajili ya kujiandaa. Ilikuwa ni siku ya jumamosi na wote walikuwa wakielekea kazini kwa kufanya kazi kama kawaida, siku hii ya leo ilikuwa na masaa machache ya kufanya mazi hivyo walikuwa wakihitajika wawepo makazini kwa ajili ya kutimiza wajibu wao.

    ****

    Majira ya saa nne asubuhi ofisini kwa SSP Nkongo aliingia Inspekta, alitoa saluti kwa mkubwa wake huyo wa kazi na kisha aliamriwa kuketi kitini. Ulikuwa ni ujio ambao ulikuwa ukimaanisha kuwa kulikuwa na taarifa au shida kutoka kwa aaskari huyo ambaye alikuwa yupo chini yake kicheo. SSP Nkongo alijiandaa kusikiliza shida ya huyo Inspekta, aliacha kufanya kazi ili aweze kumsikiliza.

    "Ndiyo Mwambe" Alimpa wasaa wa kuongea

    "Afande kuna jambo sijalipenda nimeamua kuliripoti kwako" Inspekta Mwambe aliongea akiwa ni mwenye hofu

    "Kwa siku ya nne mfululizo kuna kijana wa chini yangu alikuwa akinilalamikia juu ya utolewaji wafungwa usiku Gerezani na kupelekwa kusikojulikana. Hii siyo kwake tu hata ndugu yangu mmoja ambaye ni Askari gereza la Ukonga amenithibitishia"

    "Ndiyo nipe maelezo kamili"

    "Juzi nimeamua kuja mwenyewe hapa gerezani nikashuhudia mkuu wangu akiwaondoa wafungwa wa zamu wasilinde usiku na kisha yeye huwatoa wafungwa wale wanaotuhumiwa ujambazi wa benki na kuondoka nao. Jana sikumuona Mkuu akifika lakini walikuja maafande wengine ambao nahisi siyo wa kambi hii wakawachukua wafungwa wale na kuondoka nao"

    "Mkuu ni nani maana wapo wakuu wengi hapa"

    "Ni Mkuu Lutonja" Kauli hiyo iliposikika kwenye masiko ya SSP Nkobgo alionesha kushtuka ingawa haikuwa taarifa ngeni kabisa, aliweka vignja vya mikono usoni mwake kwa sekunde kadhaa na alipovitoa alimtazama Inspekta Mwambe.

    "Mwambe hili suala ni serious, gazeti limetoa tuhuma hiyo lakini uchunguzi haujaonesha hatia yake"

    "Mkuu hata mimi nilitaka kuamini hivyo lakini hata kabla huo uchunguzi haujatoka. Tayari nimelibaini hili. je kushuhudia na uchunguzi kipi ni ushahidi sahihi"

    "Kwako wewe uliyesema umeshuhudia ila siyo kwangu Mwambe"

    "Natambua hilo Mkuu ila nakuomba tu hata na wewe uje usiku huku ujibane mahali uone mambo yanayofanyika"

    No Inspketa usiseme maneno hayo inaonesha unaona sijakuamini, lakini utafiti kwangu pia ni muhimu. Mtu mkubwa kama Lutonja hatuwezi kumkamata kienyeji, lazima nikusanye ushahidi"

    "Sawa mkuu, ukinihitaji kutoa msaada nipo tayari kukusaidia"

    "Nikikuhitaji nitakuita uwe msaidizi wangu ila kwa sasa wacha niingie kazini peke yangu kwanza. Unaweza kwenda kuendelea na kazi Mwambe"

    "Mkuu" Alinyanyuka na kwenye kiti akatoa heshima baada ya kupokea amri ya kurudi eneo lake la kazi, baada ya hapo alitoka ofisini akiwa tayari amefikisha dukuduku lake

    Alimuacha SSP Nkongo akianza kuona uhatari wa urafiki wake na ASP Lutonja, usaliti wake ndani jeshi la magereza ukigundulika basi na yeye angehusika moja kwa moja. Urafiki wake na Yuda ndiyo ungeweza kumtia hatiani jambo ambalo hakuwa tayari litokee, kufikia wakati huo alikuwa yupo tayari urafiki ufe lakini si yeye kuingia kwenye aibu. Jambo hilo hadi kumfikia Inspekta alikuwa na uhakika kwa asilimia mia moja lilikuwa limefika kwa Maaskari wengi waliokuwa wapo chini yake. Kugundulika kwa jambo hilo kwa wakubwa zake aliona ungekuwa mwanzo wa yeye kuanza kunyooshewa vidole na maaskari wa chini yake, hakika kutembea na mwizi nawe utaitwa mwizi. Ndiyo hili alilihofia kutokea, kuonekana ni ndani ya mnyororo mmoja na rafiki wa tangu shuleni. Urafiki wao ulioshibana hadi kufikia kila mmoja kuwa msimamizi wa mwenzake kwenye ndoa, aliona ndiyo ulikuwa ukielekea kumtia doa kutokana na kuambatana naye kila sehemu kama kumbikumbi. Lazima angehisiwa hata huko kwenye uhaini aliyokuwa anaufanya angeambatana naye, hata kama ushahidi wa kumtuhumu yupo kwenye hatia haukuwepo. Bado aliona angehukumiwa na hukumu ya wanadamu wasiyojua hata uhalisia wa jambo, wanadamu wasio acha kuongea kitu kinachopita mbele yao hata kama hawakukijua uhalisia wake. Hao ndiyo aliokuwa akiwahofia kabisa kuweza kumshushia heshima yake, rekodi nzuri ambayo alikuwa anyo kwenye jeshi hilo hata kiasi cha kuwa nishani kadhaa kwenye vazi lake. Alihisi zitakuja kuonekana hazina thamani kwa raia ambao walikuwa wakimuheshimu pia, pia hakutaka kuona linatokea kwani alikuwa akihitaji heshima za pande zote mbili

    "Sitokubali" Alijisemea moyoni mwake alipoyafikiria masuala hayo yaliyokuwa yakikaribia kuchafua heshima yake, akiwa hapo mezani aliiingiza mkono mfukoni mwake. Alifungua na picha ya familia yake pamoja na ile aliyopiga na rafiki Yuda zilionekana.

    "Ni bora unione sifai kwa familia yake kuliko jamii inione sifai, majukumu na heshima hazina urafiki" Alijisema huku akiitazama picha aliyokuwa yupo pamoja na ASP Lutonja, alipochoka kuitazama picha hiyo aliitazama picha aliyokuwa yupo pamoja na familia yake.

    "Ukigundulika wewe kabla ya mimi kukuweka hatiani nitaonekana nilikuwa nakufuga, hata nikitoa ushahidi hautokuwa na maana. Nitaanza kukuweka pingu mwenyewe ili familia yangu isije kudharaulika kisa urafiki wetu" Aliendelea kusema na moyo wake huku akizitazama picha hizo kama vile zilikuwa zikitambua kle akisemacho.







    Hatimaye muda wa kurudi nyumbani baada ya kutimiza majukumu ya kiofisi uliwadia, siku hii aliondoka akiwa mwenyewe tofauti na ilivyozoeleka kuondoka akiwa yupo na Yuda wake. Safari yake ilikuja kuweka kituo cha kwanza kwenye nyumba yake ambayo alikuwa akiishi na kisha alichukua kitu muhimu. Alitoka tena na kuondoka akiwa hakuaga kabisa alikuwa akielekea wapi. Alikuja kuishia kwenye nyumba nyingine ya kwake ambayo ilikuwa ipo shambani kwake, SSP Nkongo aliingia ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa na kila kitu ndani yake kasoro tu makazi ya viumbe hai. Alielekea hadi kwenye chumba kimojawapo ndani ya nyumba hiyo ambacho kilikuwa kimejaa vitabu pamoja na mafaili mbalimbli, hapo alitua mkoba wake ambao alikuwa ameubeba na kisha akasogelea kabati kubwa la vitabu.

    Macho yaliyokuwa yakizunguka mithili ya kurunzi ya ulinzi mpakani, yalitua kwenye faili jipya kabisa miongoni mwa mafaili kadhaa yaliyopo humo kabatini. Alilitoa faili ambalo lilikuwa limefungwa kamba na kisha alifungua kamba hiyo, yaligawanyika na kuwa mafaili mawili ambapo moja alilirudisha mahala pake na kisha jingine alilichukua. Faili hilo moja ambalo alilichukua alikwenda nalo mezani na kisha akalitua, macho yake yaliyokuwa yamejaa umakini yalikuwa yametua juu ya faili hilo lilipokuwa hapo mezani kabla hata ubongo haujashurutisha mikono yake kuweza kufungua.'Msaliti' ndiyo kichwa kilichokuwa kipo juu ya faili hilo, alikisoma kama vile alikuwa akikiona kwa mara ya kwanza na kisha alilifungua faili hilo kuangalia ndani yake.

    Ushahidi wote aliokuwa ameukusanya ulikuwa upo ndani ya faili hilo, alipofungua aliongezea na ushahidi mwingine kwa kuandika vitu vyote ambavyo alikuwa amevifanyia utafiti. Aliambatanisha na ushahidi wa kurekodi ambao alikuwa ameufanya kwa watu mbalimbali ambao walikuwa wamethibitisha juu ya kile alichokiona. Alipomaliza kunakili kila kitu kwenye karatasi za ndani ya faili hilo alihakiki maandishi yake, usahihi wa maandishi hayo uliporidhishwa na macho yake aliyoyapitisha juu yake aliamua kulifunga faili hilo kisha akalirudisha pale alipokuwa amelitoa. Kuliweka faili hilo kuliambatana na kuchomoa faili jingine ambalo lilikuwa limefungwa pamoja na faili hilo, nalo alilifungua na kuandika kama alivyofanya kwenye faili lililopita. Baada ya hapo alilifunga faili hilo lakini aliingiwa na utaribu mpya tofauti na utaratibu ambao alikuwa ameufanya kwenye faili la awali. Utaratibu huu ulimpelekea kutolirudisha faili hilo mahala pake na akabaki nalo mezani.

    Alipomaliza alitoka humo ndani na kisha alielekea kwenye sebule ya nyumba hiyo, alilitua faili mezani pindi tu alipofika kwenye sebuleni na kisha alijibwaga kwenye kochi. Alijipekua mfukonni akiwa ni mwenye kutafuta kitu, alijipekua kwa namna hiyo kwa sekunde kadhaa akibadili mifuko tofauti. Hatimaye alifika mfuko wa mwisho kabisa na kupata kile ambacho alikuwa akikitafuta, hakika ilikuwa ni bangili ya rangi ya fedha ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa madini magumu. Pingu za kufungia watuhumiwa ndiyo alikuwa akizitafuta na hatimaye zilikuwa zipo mikononi mwake. Aliiweka juu ya faili hiyo pingu na kisha aliinuka na kuliendea jokofu ambalo lilikuwa lipo jirani kabisa na sebule hiyo, ufunguaji wa jokofu hilo ndiyo ulifuata na aliinama kutafuta miongoni mwa cupa kadhaa ambazo zilikuwa zipo ndani ya jokofu hilo. Alipoinika mikono haikuwa mitupu kama ilivyokuwa hapo awali kipindi akilisogelea hilo jokofu, iliibuka ikiwa na chupa moja ya pombe kali ambayo alizoea kuinywa kabla hajaingia kwenye kazi ngumu tangu akiwa yu na cheo kidogo ndani ya jeshi hilo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alirudi na chupa hiyo mezani na aliifungua huku huku akilitazama faili lilipo mbele yake, kifuniko kilipotii amri ya kufunguka alipeleka chupa hiyo mdomoni na kisha alipiga mafunda kadhaa. Alipoishusha ilikuwa imepungua mililita za ujazo kutokana na kumezwa na kinywa chake, aliipeleke hiyo chupa kwa mafundo kadhaa na hatimaye ikaisha. Alipoitua alichukua faili lake na kisha alitoka ndani ya nyumba hiyo, adhma iliyokuwa ipo ndani ya kichwa chake ilikuwa ni kumtia nguvuni Msaliti wake tu.

    ****





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog