*********************************************************************************
Simulizi : Fambo
Sehemu Ya Kwanza (1)
Wanaume nane walikuwa wakichimba shimo katika eneo la makabuli ya isevya mkoani tabora,. naam ilikuwa ni shimo siwezi kusema ni kabuli kwakuwa namna ya uchimbambaji wa shimo lile haukuwa vile kabuli linavyo takiwa kuchimbwa,.kwa haraka haraka pengine ungeweza kuhisi labda ni kwa ajili ya kufukia mzoga wa mnyama aliyekufa siku nyingi na kutoa harufu kali,. lakini swali, Je mzoga wa mnyama hufukukiwa katika makabuli? jibu ni no,. Ama labda hawa jamaa walikuwa na matambiko yao kama zilivyo desturi za jamii nyingi za kiafrika?. Sijui.,. ilikuwa ni kati ya saa moja kasorobo za jioni, kando kidogo kulikuwa na mwili wa mwanamke,.mwili ulio kuwa tayari ni maiti, mwili ule ulifunikwa kanga moja tu iliyo ishia magotini kutokea kichwani. Kulikuwa na mtoto mdogo wa kiume kati ya miaka tisa pekee ndiye aliye onekana kuguswa na msiba ule,alikuwa akilia mno alitamani kufunua uso wa ile maiti uliyo kuwa umefunikwa kwa khanga japo amtie machoni kwa mara ya mwisho lakini alishindwa, aliogopa mkwara mzito alio chimbwa na wale watu walio kuwa wakichimba shimo kwa ajili ya kuufukia ule mwili,. Mtoto alizidi kulia hakutaka kabisa mama yake azikwe akiwa hajamtia jicho la mwisho,.mahaba ya kumtizama mama yake yalizidi kumzonga,.mtoto alikuwa akihaha, Alisimama,akaketi,alipiga piga miguu yake katika ardhi kama kwamba haja ndogo imembana, mikono yake ikiwa kichwani,sauti ndogo ya kilio cha uchungu ilimtoka,akiwa mwingi wa wahka,. “liwalo na liwe” hatimaye mtoto alipata ujasiri, akavuta kanga kutoka kichwani mwa maiti ile ya 'mamae' Naam!! Harufu kali na mbaya ikatapakaa eneo lote!. Uso wa yule mwanamke ulikuwa una majeraha makubwa ya moto yalionekana katika macho ya mtoto,. mwili ulikuwa umeungua vibaya mno nyama nyekundu yenye kuvuja maji maji ilijidhihirisha katika macho ya mtoto., majeraha yale yalitoa harufu kali ya mnuko,.mtoto alipata uchungu usio mithilika. “Wewe mshenzi hebuhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ funika huo mzoga unataka tupate kipindu pindu sasa hivi, mwana haramu mkubwa wewe, na uwe mpole vinginevyo tuta kuua sasa hivi kama tulivyo muua huyu MCHAWI mwenzio,. haya funika upesi huo mzoga ” alisema kwa ukali jamaa mfupi mwenye kitambi kikubwa, akiwa amekamata sime yenye makali kote kote,. Mtoto alipatwa na joto la tumbo,hofu na huzuni vikamkamata aliinama karibu na sikio la kulia la mama yake kisha kwa sauti ya chini yenye kitetemeshi akawa anamwita mama yake amke, lakini wapi. alimtingisha kwa nguvu akimwita kwa sauti ya chini yenye mchanganyiko wa kwikwi za kilio, Yule binadamu hakuamka,tayari alikuwa ni maiti, "mama amkaa" nzi walio kuwa wakijipatia chakula chao wengi wakaruka kutoka katika kichwa cha ile maiti, Harufu kali ilizidi kusambaa,. "mamaaa uuuiwii mamaa,.mamaaa amka mamaa amkaa" mtoto alilia,. "keleleee we mbwa kelelee!.alaaa! kelele" yule jamaa mwenye kitambi alimkalipia kwa ukali huku macho yake makali akiyatumbua vibaya kwa kile kitoto kisicho elewa lolote katika hii dunia. Mtoto alinyamaza ghafura,. lile jitu katili lilimkazia macho huku mashavu yake mabaya yakiwa yamevimba kama kwamba kanyweshwa mkojo wa mlevi wa gongo,. “oyaa sogezeni huo mzoga ufukiwe hili shimo linatosha, haya mazingira ya makaburini ikifika saa moja na nusu huwa siyo pazuri huku” alisema mtu mwingie maarufu kwa jina la utani la Kibonde, “Haya wewe mchawi mtoto sogea huko” lile jitu baya la mashavu lilisema kwa dhihaka akimsukuma yule mtoto mfiwa, Mwili ile maiti ulibebwa na watu wanne wawili walishika mikono na wengine wawili walishika miguu kisha ukapelekwa katika shimo dogo na jembamba,. “moja,.mbili,.tatu., twendeeeee” walihesabu kisha ile maiti ya mwanamke ikatupiwa katika shimo kama mzoga wa mbwa, mwili ule ulijibamiza katika kuta za shimo lile kisha ukakaa kihasara hasara., mkono huku mguu kule huku baadhi ya nyama zikimenyeka vibaya,. Mtoto alizidi kulia. Baada ya hapo wakaanza kufukia kwa makoleo na majembe, ndani ya dakika kumi badae zoezi la kufukia ile maiti ya mwanamke likawa limekamilika., “Haya ulale mahala pema motoni mshenzi mkubwa wewe kaloge na huko KUZIMU shetani wewe” alisema yule mtu mwenye sura mbaya na mashavu kama mimba ya panya,.mtoto mdogo aliendaelea kupata donge rohoni mwake,alilia akiwa juu ya tuta la kabuli la mama yake,. Hakuna mtu aliye kuwa na chembe ya huruma kwa yule mtoto,. walimwacha eneo lile wao haoo wakaondoka zoa,. Maumivu makubwa yalitanda ndani yan moyo ya mtoto mdogo, Mwanamke aliye kuwa amefukiwa ndiye alikuwa kila kitu kwenye maisha yake,historia ya kile kitoto inaonyesha hakuwahi kumjua baba, mjombo bibi,wala shangazi,siku zote mama yake alikuwa ndiye baba ndiye mjomba ndiye bibi na ndiye rafiki mkuu katika huu ulimwengu, Waliishi kwa mapenzi yeye na mamaye katika nyumba ndogo ya udongo na makuti katika vitongoji vya isevya,. Hakuwahi kuona jirani ama mtu yeyote akija katika nyumba yao kuwatembelea,.hapakuwepo na ushirikiano wa aina yoyote kati yao na jamii ya watu wa Isevya,. walitengwa katika kila jambo, mama yake ailishutumiwa kwa imani za kishirikina,walimsema ni mchawi,. Kwa mika mingi tangu akiwa mtoto yeye pia hakupata nafasi ya kucheza na watoto wezake, mtaani watoto wote walimkwepa,. sumu ilipandikizwa vichwani mwa watoto wa mtaani kumwepuka kabisa yeye kwa imani kuwa yeye na mama yake ni walozi, siku zote alikuwa katika mazingira ya upweke,ni mama yake peke yake ndiye alikuwa rafikiye,. tangu anapata ufahamu ule uvumi ulikuwa kama kiitikoa cha wimbo mtaani kwamba wao ni wachawi,.katika kipindi cha miaka kadhaa alizoea uvumi ule aliishi kwa furaha yeye na mama yake tu,. “Wewe ndiyo furaha yangu na mimi ndiyo furaha yako kama watu hawatupendi mungu wetu yeye anatupenda siku zote amini hivyo,. na hawezi kutuacha peke yetu,. daima yupo nasi” ni maneno ambayo yaliyo zungumzwa na mama yake kila siku,. Leo mama yake hayupo kauwawa kikatili kwa mapanga kwa tuhuma kuwa ni mchawi kisa tu macho yake ni mekundu. looh! Ujinga gani huu! Mtoto alilia kiasi sauti ikamkauka,wakati huo ilikuwa ni saa mbili kasorobo za jioni giza lilikuwa limekwisha tanda eneo lile la makabuli ya isevya,. hakuonekana mtu yeyote kabisa eneo lile palikuwa kimyaaa! Ni sauti za wadudu na kilio cha mtoto mdogo ndicho kilicho lindima peke yake,. Pamoja na kuwepo kwa hadithi za kuwepo kwa mizimu na ushetani katika mazingira yale ya makabuli lakini Mtoto hakuogopa aliendelea kulala juu ya kabuli la mamaye kwikwi za kilio zikomtoka,. Saa nne usiku ilitimu mtoto aliendelea kuwepo makabulini hakutamani kabisa kuondoka eneo lile alilo fukiwa mama yake,. Baridi na upepo vilianza kushika hatamu,.mwili wa mtoto ulitetemeka, epepo ukaongeza kasi ya kuvuma,mvumo ukawa mkubwa hata masikioni na machoni mwa mtoto,. lakini mtoto akaendelea kuwepo pale hakuhitaji kabisa kuondoka eneo lile,hakuihitaji,. giza likiwa limetanda,. Ni kiasi cha kama robo saa tangu majira ya saa nne kutimu, Mazingira yale yalitisha,.kulikuwa na vivuli vya vitu visvyo eleweka mita kadhaa kutoka mahala mtoto alipo kuwepo,. Ila mtoto hakubanduka wala kuogopa, Miale ya radi ikamyeka ikamwezesha mtoto kuona kitu umbali wa mita mbili kutoke alipo,.akapata utulivu wa nukta kadhaa akiwa makini na kile alicho kiona kama ni sahihi ama laa! Miale ikamyeka tena huku ikiambatana na ngurumo ndogo,naam! alipata kuona barabala nyoka aina ya chatu mkubwa kwelikweli akimnyatia mahala pale taratibu,. Alikurupuka na kusimama wima yule chatu nae akasimamisha kichwa chake akijiandaa kukabiliana na kitoweo kile alicho kuwa akikinyatia!. Mtoto alianza kurudi nyuma taratibu mashaka makubwa yakiwa maoyoni mwake aliogopa lile joka kubwa,.nyoka alizidi kumkaribia akijianda kurusha mate kama siraha yake ya kwanza kwa chakula kile,. Ghafla mtoto alitimua mbio kali nyoka yule alirusha mate yake yenye sumu,. yakampata vema lakini yakiangukia katika shati la mtoto yule,ikawa bahati kwa mtoto lakini ikawa mkosi kwa nyoka yule kukosa kitoweo,. Mtoto alikimbia huku akipiga kelele lakini kelele yake haikusikika umbali japo wa mita hamsini sauti yote ilikaukia katika kilio cha msiba wa mama yake,. “puuuuuu” alipiga mweleka baada ya kujikwaa kidoleni na kutoa ukucha,.mtoto alipata maumivu makali kidoleni lakini haikuwa mwisho wa mbio zake alisimama akaendelea kujisukuma kwa mbele. mbio kali akiwa ametapakaa vumbi mwilini mwake,. Alitokea katika barabara kubwa ya kuelekea mjini hapo moyo wake ukapata ahueni,. Akatembea kwa kuchechemea maumivu yakiwa makali katika dole gumba lake lililo kuwa likivuja damu huku ukucha ukiwa unaning’inia,. alikuwa peku,.baridi na upepo iliongeza maumivu yake kisawa sawa,. Aliona ulimwengu haumtaki, aliona mungu amemsahau,alijiona mdogo zaidi ya nukta,alikosa mwelekeo,dunia ilikuwa kubwa mno kwake., Huyu ndiye Raymond Fambo Mwakabuku,. Unaweza kumwita Ray. Usiku huo Ray alitembea katika mitaaa akichechemea,kidole chake kilicho kuwa kikining’iniza ukucha kilizidi kutoa maumivu makali,.alitembea pasina kujua anako elekea,. Angefanya nini hali ya kuwa hata makazi yao yalikwisha tiwa kiberiti siku ile ile ya kusurubiwa kwa mama yake,.*******************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment