Search This Blog

Monday, 24 October 2022

FAMBO - 5

 http://pseudepigraphas.blogspot.com/2019/12/fambo.html

    Simulizi : Fambo

    Sehemu Ya Tano (5)





     “NGO,NGO NGO HAYA, HAYA HAYA WAFANYA USAFI TUMEFIKA FUNGUA MLANGO” mlango wa nyumba ya Sebastini uligongwa huku sauti kali ikisika ikikoroma kwa amri kali,. Kimya.., “Ninyi mbwa humo ndani hamtusikii fungua huu mlango upesi”,.kamanda wa interahamwe alisema tena kwa ukali huku wanamgambo wengine wakiwa na mori kubwa ya kuuwa. Kimya kingine,.! Ndani kwa Sebastiani,Sophia alisimama wima akiwa anatetemeka, jasho lilimtoka, hakuna aliyeweza kuendelea na maombi tena. Sophia alielekea chumbani kwake na kuinama chini ya uvungu wa kitanda na kumchomoa Richard aliyekuwa amejikunyata akitetemeka mwili mzima,. “Njoo mwanangu,haya njoo baba kwa mama hakuna baya lolote litakalo kukuta” “mimi naogopa nimewasikia interahamwe wamefika, wako mlangoni” “shiiiiiii..!!, nyamaza interahamwe hawawezi kukuuwa mimi nipo, baba yupo, na yesu yupo, wote tuna kulinda wewe, unatakiwa utulie,.baba anakuja kukuficha mahala pazuri” alisema
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Sophia akimpa matumaini mtoto wake japo ukweli hata yeye aliujua moyoni kuwa kifo chao dakika chache zijazo kitawafikia,. “Haya haya haya!.hakuna kushangaa upesi tunatokea mlango wa nyuma tunatimka tokeni upesi mwiteni na huyo Magdalena naye sijui yuko wapi,..!!!” sauti kali ya Sebastiani alizungumza akitokea sebureni,. Kabla hajamaliza sauti nyingine kali ya kishindo kikubwa ilisikika mlangoni,. Wanamgambo wa interahamwe alivunja mlango kwa kombora zito wakaingia ndani kwa kasi,. Sebastiani na Sophia walibaki wamebung’aa ulikuwa ni uvamizi wa ghafla wakiwa hawajafanya jambo lolote la kujikomboa,. “Ingia kabatini Richard utulie kimya usipige kelele wala kutoka nje” alisema Sophia kwa wahka huku macho kayatoa pima,. Richard aliingia katika kabati la nguo na kujikunyata kimya,. Ninyi mende ninyi,. haya kuja hapa,. yanii muda wote sisi tunawataka mfungue hili lango la bangaluu lenu mnaleta mishauo!. Sasa leo mtajua kuwa maharagwe ni mboga na mchuzi wake ni mtamu!. mafisadi wakubwa ninyi,." alisema kamanda wa intarahamwe wakijichoma ndani zaidi kuwatafuta wenyeji wa nyumba ile “Haya kuja hapa mende ninyi” alisema kamanda baada ya kuwaona “Jamani sisi hatuna kosa lolote”alisema Sebastiani, kauli hiyo ilitosha kumpeleka akhera mbele ya macho ya mke wake na mtoto wake Richard aliyekuwa akishuhudia kupitia nyufa za mlango wa kabati, mauwaji mmoja alinyanyua juu upanga mkubwa na wenye makali na kutwisha nao Richard kichwani,. Taharuki!. Uwiiiiii jamani mumemuuwa mume wangu!., uwiiiiii Sebastiani wanguuuuuuu!. Sophia alilia, aliruka ruka juu kwa kupagawa,alipatwa na kimuhemuhe,. Damu zilimiminika katika kichwa cha Sebastiani kama koki ya bomba iliyo ng’olewa,. Sebastian alitulia kimyaaa! Panga moja la kichwa lilitosha kukamilisha safari yake hapa duniani,. uhai wake iliishia hapo!,. “Haya wanaume nyonyeni maziwa ya huyo mwanamke, mkimaliza UA” amri alitolewa,.wanamgambo wanne walimvaa Sophia,. Wakamdhibiti,wakamvua nguo akiwa ameelekezewa mitutu ya bunduki na panga,..wakamalazimisha kulala chali kisha wakambaka kwa zamu,. Walikuwa kumi na nne walimbaka wote kiasi cha kwamba Sophia alipoteza fahamu,haikuwa kigezo cha walio kuwa hawajabaka, kutobaka,walibaka mpaka miili yao iliposema basi, “Haya UA” amri alitolewa, Sophia alichomwa singe ya bunduki tumboni ikatokezea mgongoni,. mguno hafifu wa maumivu ulimtoka,. macho akayafumbua kwa mbali huku midomo yake ikimcheza,.hakuwa na nguvu kabisa katika mwili wake na wakati huohuo kifo kibaya kilikuwa kinamkabili,. Mchomaji alichomoa singe kwa nguvu damu zilitapakaa katika singe ya bunduki, kisha kwa nguvu akamdunga tena kifuani mwa mwanamke yule asiye kuwa na hatia,. singe ilitokezea tena upande wa pili wa mgongo.,.aiseee!,. Hali ilitisha!. “Kosa lako ni kuzaliwa mtusi!.” alisema kiongozi kisha akatoa tusi kali kumtukania mama yake,. Hapo nyimbo za kisiasa za kabila la kihutu zikaimbwa kwa shangwe nderemo na hoihoi,. “Hivi mmetafuta mende wengine humu ndani mmekosa kabisa?” kiongozi aliuliza kwa ukali. “Hakuna mende” “Haya mwagieni petroli nyumba nzima kisha tia kibiriti kusafisha vema,.tunataka Kigali ibaki nyeupee peeeee! pasina mende wa aina yeyote” alisema kiongozi kisha mafuta yaliyo kuwa katika madumu yakaanza kumwagwa katika nyumba ya Sebastiani,. Richard alishuhudia kila kitu alitamani awe Rambo apambane na watu wale, lakini ukweli haukubadilika,.yeye ni Richard na hawezi kuwa Rambo kamwe. Kwa macho yake alishuuhudia namna wazazi wake walivyo kufa kikatili, sasa zamu hii, ilikuwa ni zamu yake kufa kwa moto akiwa ndani ya kabati la nguo lililo fungwa kwa nje na kufuli,. Akiwa ndani ya kabati tumbo lilimchemka,mashaka makubwa yaligubika nafsi yake, maumivu ya kuungua na moto mpaka kufa yalimtia hofu kubwa alitamani apige kelele lakini kitendo kile ilikuwa si salama kwake badala yake kama interahamwe wangegundua uwepo wake angebadilishiwa staili nyingine tu ya kifo, kutoka kuunguzwa kwa moto kwenda kuchinjwa shingo kwa panga. Alitulia tuli!,. Baada ya interahamwe kumwaga petroli nyumba nzima wote walitoka nje ya nyumba, kisha ikatiwa kibiriti!. Moto mkubwa ulilipuka, nyumba ya Sebastiani ikaanza kuungua kwa kasi kubwa. Kwa mara nyingine wakashangilia kwa kitendo hicho huku risasi nyingi zikitoka katika bunduki zao. Looh! Ujinga gani huu!. Magdalena alikurupuka mafichoni baada ya joto kuwa kali na moshi kumwelemea, moto ulikuwa ukiwaka kwa kasi kubwa,alipiga kelele nyingi za kuomba msaada,. Lakini wapi!. Akili yake ikamwongoza kujaribu kujinasua katika moto mkubwa uliokuwa ndani ya nyumba ile badala ya kuendelea kumaliza nguvu zake kwa kupiga kelele za kuomba msaada,. Alipiga hatua kubwa akiwa makini kuukwepa moto ulio kuwa ukiwaka kwa kasi na kunguza vitu, Alinyata mpaka usawa wa chumba cha Sebastian mlango ulikuwa wazi,hapo mianga ya mioto ikamwezesha kuona maiti mbili zikiwa zimelala zikiwa zimeuwawa kikatili,.alipata mshutuko mkubwa hofu kubwa ikazidi kumjaa, Maiti ya Richard hakuiona!. Akazidi kuingia ndani zaidi,ni vile mungu alimwongoza tu kuingia ndani zaidi pasina kujua kwanini anazidi kuzubaa mule ndani badala ya kutimka,.hapo sauti ya Richard aliye kuwa ndani ya kabati ikapenya katika masikio yake,. Magdalena hakutaka kujiuliza mara mbili zaidi alikwisha elewa fika Richard alifichwa humo kabatini na wazazi wake kabla ya wao kuuwawa,. Upande wa kulia chumba hicho aliona pasi ya mkaa iliyo tumiwa kunyooshea nguo, upesi aliichukua ile pasi na kuikamatilia vizuri kwa mbele kisha pigo moja la nguvu lilitosha kusambaratisha kufuli dogo la kabati, Richard alitoka upesi akamrukia Magdalena na kumkumbatia huku akilia kilio cha huzuni kubwa,. Moto ulizidi kupamba moto,. “Twende nifuate huku hatuna muda wa kupoteza humu ndani vinginevyo tutateketea kwa moto” alisema Magdalena kwa sauti kali., kilichofuata ilikuwa ni kutimua mbio kupitia mlango wa uwani ambako huko moto ulikuwa hauja kolea, wakatokea katika geti dogo kisha wakatokomea nje gizani wakiwa salama salimini,. Wakati huo ulikwisha timu saa saba kasoro za usiku ama kwa hakika ulikuwa ni usiku usio sahaulika katika vichwa vya wananchi wa Rwanda,usiku wa mauwaji,usiku wa maumivu, usiku uliopeteza ndoto za maelfu ya watu, haya ndio mauwaji ya kimbari,. Basi ikawa Magdalena na Richard wanatembea kwa tahadhali kubwa wakipita pembezoni mwa barabara hata wasijue wanakoelekea!. watu kadhaa walipishana nao wakiwa na kimuhemuhe cha kuwa mbali na mji wa Kigali,. Walitembea umbali wa kiometa nne kwa mguu wakawa mbali kabisa na makazi yao, Walifika katika eneo la keiza katika kanisa kubwa la katholiki watu wengi walionekana kuingia humo ni eneo kidogo lililo onekana kuwa salama., Watu walikuwa wengi katika kanisa lile kubwa kwikwi za kilio zilisikia kwa kila mtu, Kwa namna nyingine huduma ya kwanza dhidi ya watu walio jeruhiwa na mapigano ilikuwa ikitolewa na watumishi wa kanisa lile,********************

    Richard alistushwa katikati ya kumbukumbu ya maisha yake na mtu aliye kuwa akigonga mlango kwa kasi,. Alijinyanyua kivivu huku akipiaga miayo akajinyoosha, mifupa ikalia “ka,kaa,ka” kisha akauendelea mlango na kufungua akatoa shingo nje huku robo tatu ya mwili ikibaki ndani na kutizima mgongaji wa ule mlango,. Macho yake yakakutana na macho ya msichana aliyekuwa amebeba beseni la mboga za majani mwenye urembo uliofichika kutokana na aidha hali ngumu ya kimaisha ama adha nyingine za kimaisha., “Nauza Mbogamboga kaka” alisema yule dada huku akimtupia Richard jicho lenye utafiti fulani wa siri,. “Huwa sina desturi ya kupika dada,simply mboga sihitaji” alisema Richard huku akionekana kutopenda hali ile ya kutembelewa na mgeni wa dizaini ile hasa katika nyakati zile ngumu kwake,. “Heee! Samahani kaka!, kumbe wewe bado msimbee!! Hahahaha,.. sikujua hilo!…” alisema kibwege yule dada muuza mbogo huku akijichekesha pasina sababu ya msingi,. Richard hakujibu kitu alitikisa kichwa huku akiludi kwa ndani akimuaacha yule muuza mboga mwenye ugonjwa wa ‘chekelea’ pale nje,. Yule dada alikamatilia vizuri beseni lake la mbogamboga akipiga hatua kuiacha nyumba ile ya yule msimbe mwenye kupenda kula hotelini,. Alipita katika mitaa miwili mitatu akaingia vichochoroni akiwa na beseni lake la mboga kichwani,. hapo aliangaza macho huku na kule kisha akalitua beseni na kumwaga mboga zote ardhini na kuzifunika kwa beseni lake, Haraka haraka akajiweka vema, akavuta kifaa kidogo cha mawasiliano kilicho unganishwa na waya mwembamba uliopita katika nywele zake ukitokea ndani ya ukingo wa gauni lake chakavu, kisha akasogeza mkabala na mdomo wake akasema.; “one step remain is over,. muwaji amepatiaka mpaka kufikia kesho atakuwa mikononi mwa serikali ya Rwanda,.alisema yule dada muuza mboga,. Tobaaa!! Kumbe alikuwa ni shushushu kutoka serikali ya nchi ya Rwanda,..************



    MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Blog