Search This Blog

Thursday, 23 March 2023

MTOTO WA KIGOGO - 3

   

Simulizi : Mtoto Wa Kigogo

Sehemu Ya : Tatu (3)



Zabi alimkaribisha Tom mpaka chumbani ndugu yangu alizi kuachama hakuwa na jipya zaidi ya kubung’aa huku mimacho imemtoka na domo limemshuka kama kama kabeba kila saba za nyama kwa mdomo. Tom anakutana na kitanda kilimuwa na muundo wa kipekee ni ngodoro zuri la spilingi lilikuwa limetandikwa vizuri na mabulanketi meupe na kuleta kamvuto kazzuri machomi. Kitanda kilikuwa katikati ya chumba kikubwa ambacho kwa mkono wa kushoto kulikuwa na meza ya kuvalia iliyokuwa samabamba na kabati lake. Huku kushoto ni mlango ambao ulikuwa niwabafu iliyokuwa imeundwa pamoja na choo hakika unge papenda tu palikuwa ni pazuri sana. Tom anaonekana kutokuwa huru na kushindwa kujiamini. Zabi anafungua sehemu iliyokuwa imefungwa kwa chini na kulingana kama sakafu ilionekana ngazi ikishuka kwenda chini Zabi anamwambia Tom ashuke Tom alimfata walipofika huko ufunguo wa Zabi ulikuwa ukihangaika na kitasa cha mlango na hatimaye wanaingia ndani ya chumba ambacho Tom kilizidi kumchanganya. “Tom hapa ni kwangu ni nyumba mpya nimeamua kuja kuishi na wewe hapa kuanzia leo mpaka tutakapo badilisha uamzi, kwa kifupi mwanzo nilikuwa naishi masaki ila pia nina nyumba mbezi na pia mwenge ninanyumba lakini hii ni mpya ndo nimemaliza kuijenga hivi karibuni pia nalipenda eneo hili kwahiyo tutaishi hapa mpenzi wangu”. Upande wa Tom alikuwa kama anaota lakini huo ndiyo ulikuwa uhalisia, Zabi alimsihi tom kutulia kwani Zabi anampenda alimuomba ajiheshimu na kumuamini kwani hajamjua bado, laity kama angejuaZabi anachomuwazia basi wala asingekuwa anatabika kwani kila anachokihitaji yeye na familia yake angepewa. “niamini mimi ndo nilivyo kwa kifupi kama hunijui usipokuwa makini kamwe huwezi nijua, Tom nataka uwe na msimamo nilisha kupenda mimi ni msichana mzuri sina kasoro ninajiamini ninakupenda sijalazimishwa hivyo kuwa na amani.” Zabi alikuwa akijaribu kumuweka sawa Tom.


Land cruiser Tx ilikuwa ni gari aliyokuwa akiitumia Zabi leo nyuma ya usukani alikuwepo Tom taratibu wanaingia barabarani baada ya kuvuka kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo, wanasonga na kukata kulia , safari yao ilielekea mlimanicity, haikuchukua muda walikuwa ndani wakichagu bidhaa za kila aina. Tom aliruhusiwa kuchagua mavazi apendayo na Zabi hivyo hakujinyima naye aliutendea haki huo msaada aliopewa hakika alichagua nguo nyingi, viatu vingi na saa kama tatu hivi.baada ya hao wlifanya mahemezi ya vitu vya ndani kama mboga, vinywaji, matunda na vitu vingine vingi. Zabi alikuwa akizungumza na Tom. “T’ alimuita kwa ufupi hivi kwamfano nikakwambia ubadili dinina kuwa muislamu tufunge ndoa uakubali” Zabi aliuliza kwa masihara…. Tom hakujibu ila jicho alilomuangalia Zabi lilitosha kuonessha kuwa hakuna muujiza utatokea wakubadili dini. Basi zabi akabadili maongezi ili asimuuzi Tom wake. Walikuwa jikoni wanapikazabi na tom zabi akakumbushia tena “Tom nataka tuoane na niko tayari kwa lolote hutaki kubadili dini nitabadili nataka unioe sawa ?” anajaribu bahati tena kwa mara nyingine. Kama utabadili dini mbona asubuhi tu wala hata usijari. Kauli hiyo iliufurahisha moyo wa zabi na kujikuta akiruka na kumkumbatia Tom.

Sikujua kama ilikuwa kweli maana namuona Zabi akiwa kwenye heka heka za harusi mara ukumbi, sijui gauni, mara kadi za mwaliko alikuwa ni yeye alijipigia ngoma na kuicheza mwenyewe. Taratibu siku ziliyoyoma na hatimaye kubaki siku mbili harusi ilitakiwa kufanyika Mulimancity conference Center, ni ukumbi wa kimataifa wa mikutano Zabi aliuandaa kwa sherehe hiyo. Sherehe hii ilikusanya watu maarufu na wenye uwezo mkubwa kifedha walikuwa wamealikwa maana ilikuwa ni harusi ya mtu mzito, tajiri na mtu maarufu zaidi hapa jijini dare s salaam tofauti na walivyo mzania kipindi akiwa Mwanza. Maandalizi ya sherehe yalikuwa yakielekea ukingoni Zabi alikuwa bize mno kiasi kwamba hata kuongea naye haikuwa rahisi. zIlibaki siku mbili kabla ya harusi Tom anaishuhudia familia yake ikiingia nyumbani kwke majira ya saa 5 usiku. Tom anaongea na mama yake wanasalimiana na kuwakaribisha. Kesho yake Zabi anarudi nyumbani na gauni lake la harusi na suti ya Tom. Tom anaitizama ile suti na gaauni kisha akahoji “Zabi hivi ulikuwa serious na ishu ya kuoana mbona mapema na hatujazungumza tukafikia mwafaka … sassa nashangaa unafanya kimyakimya sijui unamaana gani?” huyu anaitwa Tom ….

Tunazani Tom atakubali kufunga ndoa na zabi au ndo ilisha kuwa doa tena 





Zabi anageuka na kumtizama Tom kwa mshangao .. “unasemaje ?” Zabi alihoji kana kwamba hajasikia. “Tom I’m not a kid you know?” jitahidi kutokuniudhi kilamara na mimi ni binadamukumbuka ninakupenda ..isiwe sababu ya kuzusha visa kila kukicha ninaomba uniambie kitu kimoja ambacho ni rahisi tu. Je, unanipenda ?”Zabi alihoji huku akionesha kukerwa na tabia ya Tom yakukaa akizusha mambo na kutengeneza visa kila siku. “Nina kupenda Zabi tena saana tu, sina wakukulinganisha naye, wewe ni mkombozi wa maisha yangu, mwanamke wa ndoto zangu laazizi wa moyo wangu ninakupenda my dear.” Tom alijibu kwa ufasaha huku akienda na kumkumbatia zabi aliyekuwa kasimama kwa hasra huku akionekana kutokuridhishwa na ishara ya kukumbatiwa na Tom kwani ilikuwa kama ni kumpoza. Hakuhangaika naye kiukweli Zabi alikuwa ni mtu muelewa saana, na mbaya zaidi alimfahamu Tom vizuri kuliko Tom alivyo mjua Zabi.

Majira ya saa kumi jioni Zabi na Tom wakiwa wameketi juu ya kivuko au daraja la Ubungo wakitizama watu waliokuwa wakitoka na kuingia ndania ya kituo cha mabasi ya ubungu mkono wao wa kulia wakati huohuo wakiyatimam magari mbali mbali yaliyokuwa yakipita chini ya darajahilo yakitoka sehemu mbali mbali za jiji hilo. Ikiwa ni pamoja na mabasi yaendayo kasi ambayo hubeba abilia wengi zaidi na ilikuwa ni huduma ya kwanza kutolewa ndani ya jiji la Dar-es Salaam. Tom na Zabi walikuwa wakizungumza mengi kuhusu harusi yao kwani walikuwa wameesha fanya vipimo vya viviu na kukutwa hawana. Walikuwa wakisubili kufunga ndoa. Majira hayo ya jioni yaliambatana na furaha ya kulikagua jiji la daresalaam wakiwa jii ya kivuko hicho cha watembea kwa miguu ubungo Zabi na Tom wanabusiana na kufurahia paoja walikimbizana huku wakipiga picha za pamoja. Watu walikuwa ni wengi wakiingiia na kutoka ubungo kituoni na nje kulifurika vijana wapiga debe wa mabasi na wamachinga wakiuza bidhaa ndogo ndogo kama vile maji na vitu vingine kama vyakula nakadhalika.

Ni ndoa ya kipekee saana kuwahi kutokea ni ndoa ya ajabu kuwahi kufungwa ni ndani ya mlimani City conference Centre ni ukumbi wa mikutano wa kimataifa uliopo ndani ya majengo ya mlimani City. Tom alikuwa kalamba suti nyeupe na kiatu cheupe kulingana na ubunifu wa mbunifu wake alitupia shati jeusi ndani na Tai nyeupe .. asikwambie mtu ulikuwa ni muonekano mzuri uliovutiwa na Nywele zake nyeusi tii …penye kutenda haki tutende Tom alikuwa kama amezaliwa na Suti kiukweli alipendeza saana. Usinge mjua kama amezaliwa familia masikini. Katu usinge mjua kuwa ni kapuku wakutupwa. Tom alikuwa kapendeza akinyata taratibu kuku akiwa kaongozana na mrembo Zabi ambaye kwasasa alikuwa ameesha batizwa jina na kuitwa Irene, alikuwa ni mkristu sasa siyo mulisilamu tena. Taratibu mbele ya ukumbi ule ambao uliombwa kwa shughuli nzima hivyo uliandaliwa vizuri. Tom na zabi wamerejea kutoka kanisani baada ya kufunga ndoa yao na sasa walikuwa ni mke na mme. Bila shaka matajiri wakubwa na viongozi walishiriki lakini hawakumjua Tom kwani alikuwa mgeni eneohilo, michango ilitolewa huku kamati ya maandalizi ikitoa fedha nyingi na samani za ndani kaam vile meza makabati na makochi. Lakini watu walijitolea kwa cheque, fedha tasilimu, ahadi na zawadi zingine.sataki kuizungumzia saana sherehe hii kwani ilikonga nyoyo za watu wengi. Sherehe ilifana saana kila mtu alifurahia mwanzo mwisho kiukweli hakuna aliye ichukia.

Fungape lilifanyika CapeTown nchiniAfrica kusini Zabi na Tom walikuwa wamejiachia huko kwasiku saba wakipata raha na kuifurahiandoa yao. Kwa maisha waliyokaa Africa ya kusini hakika Tom sasa alikuwa ndiye mme bora wa Zabi, Tom alionesha kupmpenda saana Zabi kinyume na mwanzoo inaonesha sasa Tom ana mapenzi ya dhatti kutoka moyoni. Kama tunavyokumbuka Tom akakuliia katika mazingira magumu saana hasa mtaani hali hii ilimfanya aishi kila aina ya maisha, alijaribu kila alicho zani kinaweza kumsaidia. “mama African Hoteli katikati ya jiji la Cape Town ndiyo hoteli iliyo wavutia watalii wengi na ilikuwa ni hoteli ya nyota tano iliusanya kila aina ya wageni kutoka uarabauni, mashariki ya mbali, ulaya, marekani ya kusini na kasikazini, Australia, uhidi na hata wenyeji nikiwa na maana ya waaafrica. Tom na Zabi ukipenda muite Irene kwa jina kipya la kikristu alilobatizwa baada ya kufunga ndoa. Tom wakati akishuka ngazi anakutana na vijana wakijaribu kuweka sawa vyombo vyao vya mziki. Tom walimkumbusha mbali anakumbuka Enzi hizo akiwa na vujana wenzake juu ya milima ya igogo na nyakato jijini mwanza wakijaribu angalau watoke kwa mziki lakini ilishindikana kutokana na sababu mbali mbali. Tom anamuomba gitaa kijana mmoja na kuanza kupiga gitaa huku akiimba wimbo wa Jux I’m looking for you uongo dhambi Tom anajua kuimba, Tom anajua kulichezea gitaa, tom ni fundiii. Kila mytu alikuwa akitikisa kichwa wakati tomu akiimba hali iliyowafanya wapiga kinanda na dams kujikuta wakichalaza pila kuambiwa na kufanya mziki moja hatarii ulioamsha hisia za watu na kujikuta akijaza ukumbi maana watu walitaka kujua nini kimetokea, Basi Tom alizidi kushusha nyimbo kibao za bongo fleva na mwisho aliwaaga na nyimbo ya barnaba inaitwa I’m sorry. Dah Tom Tom Tom weweee! Zabi alijikuta akimkumbatia wakati Tom akilalamika zaidi ya barnaba kwenye wimbo wa I’m sorry. Majonzi na machozi yalimtoka kwa huzuni Zabi akihisi anaombwa msamaha na Tom kwa visa ambavyo viliwahi kupita. Hatimaye Tom anashusha uzi wa msho wagitaa lake anaushangaa umati uliomzunguka wakipiga makofi kwa kumshangilia Tom aliondoka na kwenda kumkumbatia Zabi wanaondoka pamoja kuelekea kwenye lifuti wanabonyza kitufe na kusubili. Sekunde kadhha mlango unajifnuga wanaingia na kubonyeza namba 25 ndo gorofa walipokuwa.


Ndani ya chumba chao Zabi haamini kama Tom anaweza kuimba basi tom anaamua kumuimbia tena Zabi wimbo wa mahaba kutoka Ismail wa b-band “unaitwa ninachota nikuwa nawe” sauti ya mayai, vocal hakika kijana alikuwa fundi. Hakukuwa na mabadiliko zaidi tangu wamefika Cape town upendo uliongezeka na mapenzi yakazidi kunoga kiukweli Zabi na Tom walipenda saana kama wapenzi. Ndani ya chumba chao ni Q1024 ndi ya Mama Africa hotel Zabi na Tom awamejila kwenye Sofa lenye muundo wa kitanda huku zabi akiwa na limoti mkonono wanaangalia trace for stars. Hii ni television maarufu kwa watu maarufu duniani hivyo walikuwa abize wakicheshwa na vituko vya Kevin hart. Alikuwa akitia mbwembwe zake kwenye runinga hakukuwa na shida yoyote. Lakini ikumbukwe kuwa ilikuwa ni siku ya mwisho ndani ya CapeTow walikuwa wakijiandaa kurudi nyumbani.

Asubuhi safari ilianza ambayo ulichukua masaa machache tu wakatua jijini dar wakitokea Afrika kusini. Tom anashuka kaongozana naZabi taratibu baada ya kufika nje anakuta kuna gari aina ya hummer yenye rangi nyekundu imepaki nje ya uwanja wa ndege bila shaka alijua niya Boss Fulani. Tom alivutiwa na ile Gari saana aliiangalia mara mbilimbili hivi hakumjua mwenyewe basi akiwa kakimata vizuri kiuno chembamba cha zabi huku awakinyanyua mguu pamoja na kuutua pamoja nikimaanisha walipiga kila hatua wakiwa pamoja. Zabi na miwani yake mikubw ilimfanya pendeze vizuri ndani ya gauni lake zuri. Safari yao inaishia kwa dreva mmoja aliyekuwa kapaki gari lake pembeni, zabi hakuuliza alifika na kunyanua buti na kuweka mizigo nyuma taratibu Tom naye akafanya hivyo na kisha Zabi aliingia ndani ya gari mlango wa nyuma. Tom akijiandaa kuingia kwa bahati mbaya alikuwa kalipenda saana lilegari anageuka kuliangalia anakutana na sura nzuri yenye tabasanu mwanana haijawahi kutokea, mtoto akikuangalia tu utazani kakukonyeza, midomo yake nikama inangokakukubusu, macho yake utazani kaonewa, ananywele laini na ndefu harafu nyeusi tii, uso wake mzuri, hayo yote tisa kumi alikuwa ni mtoto mrembo mweupe mithili ya mwarabu mrefu kaenda hewani sekunde kumi. Alikuwa kava kikabutula cha jeans mithili ya jeans mapaja yalikuwa wazi huku akiwa kavalia T-sheti nyekundu aliyokuwa kavalia na kuifunga kwa chini kifundo hali iliyo kiacha kitovu chake nje. Honi za Dreva zilipigwa hazikusikika kichwani mwa Tom mawazo na macho yake yalikuwa kwa yule dada “my God is so professional engineer…. To creat a great and beuliful one in this world” Tom alikuwa akijisemea peke yake sijui kama hicho kingereza kilinyooka lakini nilimuelewa. Tom alikuwa kapagawa. Basi Tom anashituliwa na mkono wa Zabi uliomgusa anashituka na kuingia ndani ya gari huku akihema juu juu. Aliketi akiwa katweta kwa tama, aibu na uchu hakujua alichokuwa anakiwaza. Basi waliondoka hukua akigeuka geuka asijue ni wapi anatamuona tena yule dada. Taratibu mpaka mitaa ya Manzese TipTop. Nyumbani kwa Tom walifika na kushusha mizigo.

Ni miezi mitatu sasa imepita tangu warudi toka fungate mambo hayakuwa haba naona kama mungu amejibu maombi baada ya wiki mbili za kula udongo, ndimu, ukwaku na ubuyu hatimaye daktari kadhibitisha Tom na Zabi huenda wakaitwa wazazi hivi karibuni. Ilikuwa ni furaha kwa wote wawili. Tena furaha kubwa mno basi wakiwa kwenye mazungumzo zabi anaahidi kumpa zawadi Tom. Basi wanaendelea na mazunguzo yao mengine ya kifamilia na kujenga familia yao. Wow! Tom sasa anamlea Zabi kaam mtoto kuitwa baba raha ni mazoezi ya kila asubuhi na jioni kupika nachotaka, kukwepa kumkela na asichokipenda. Zabi na mimba yake change hataki tom apake mafuta wala pafyumu kwa Tom ahalikuwa Tatizo, haya nyama, samaki na haziwa havikutakiwa kuonekana. Basi zabi ni mulenda kaam kalogezewa kabadili sana maharage duh Tom ni mwendo wa kucheka tu maana alifulahishwa saana na tabia za Zabi alimpenda saana mkewe. Kila alichokifanya Zabi kilikuwa burudani kwa Tom, kupenda ukapendwa raha.

Mtaa wa Msimbazi kariakoo jilani na tawi dogola CRDB Bank . zabi anaegesha gari lake upande wa pili kulikuwa na gorofa kubwa juu walionekana vijana wawili wakijaribu kufungua bango lililokuwa limefunikwa kwa kitambaa cheupe kizito wakitumia ngazi ndegu. Zabi hakuhangaika nao Tom alikuwa bize na simu huku akihoji “baby umepaki tunaenda wapi au unataka kuchukua nini mama maeneo haya” Zabi hakujibu kitu tartibu nawaona wale vijana wanafanikiwa kukitoa kile kitambaa huku chini mageti yakifunguliwa na kuonekana Duka kubwa. Zabi anamgusa Tom begani na kumuonesha kwa kidole. Tom anageuka na kuona Sura yake akiwa katinga suti huku maandishi makubwa yakisomeka Tom electrical & HD material. Tom anaachama na kubaki akijishangaa. Taratibu haamini macho yake anashuka kwenye gari akimkumbatia zabi huku akilipapasa tumbolaZabi taratibu wanavuka barabara na kuingia ndani wee!. Kulipendeza saana lilikuwa ni Duka la jumla na rejereja la vifaa vya umeme kama vile radio, tv, mashine za kufulia, compyuta, simu, camera na vitu vingine vya umeme. Tom alikabiziwa duka hilo na Zabi kama zawadi yakukubali kuwa mme wake wa maisha katika ulimwengu huu. Maisha yanasonga na sasa Tom akisimamia baishara yake huku akimsaidia mkewe katika kusimamia makampuni mbali mbali, mbali na hayo yote Tom alipenda saana kusoma na kujiendeleza alikuwa akisoma kwenye chuo cha IFM. Siku hii inaonekana kuwa bora zaidi kwa Tom kibiashara kwani hakukuwa na shida yoyo mapatotoka asubuhi yaienda vizuri akiwa kapaki gari yake mpya aina ya Range Rover yenyeRangi ya maziwa. Taratibu ni hammer nyekundu inapaki nyuma ya Gari la Tom kisha dada yule yule ambaye Tom alimuona Airport anashuka huku akijiandaa kuvuka barabara bilashaka alikuwa anakwenda dukani kwa Tom. Tom alikuwa kamuona oooh! Nguvu zilikuwa zimeanza kumuishia. “habari ya saa hizi kaka” Yule dada alisalimia kwa sauti nyembamba nzuri na nyororo. “aah poa habari” Tom alijibu kwa aibu aibu huku akikosa uvumilivu na nguvu yakumtizama Yele dada. “sorry bro unaweza ukawa na Iphone 6 hapa” dada aliuliza. “Yah zipo hizi hapa rangi mbalimbali NI kulwa alidakia kijana aliyekuwa msaidizi wa Tom dukani pale.

Dada alipita nakuzitizama zile simu kwa makini kisha akachukua moja ya rangi ya dhahabu bei yake ilikuwa milioni bili na laki sita. “kaka niwekee hii” dada alimuonesha kulwa hukua akirudi mezani kulipia. Baada ya kuhakiki fedha kwa mashine ya kuhesabia Tom ana andaa rist. Huku akiwa bado amekaliwa kooni na uzuri wa yule dada Tom anakwepahata kukutanisha naye macho walitizamana kwa kuibiaibia. “unaitwa nani?” Tom alihoji… “naitwa loveness a.k.a Mtoto wa kigogo.” Yule dada alijibu kwa mbwembwe. “Tafadhali sister nataka jina kamili maana naandaa listi yako hapa” Tom alimkatisha na kumtaka aache mzaha “Ninaitwa Loveness Patrick ni mwenyeji wa Dodoma” vasi tom alimkabidhi stakabadhi yake yule dada akaaga huku akimkonyeza Tom alikuwa Hoi.



kichwani kwaTom kulivurugika Love alikuwa kapavuruga, tom alikuwa akijaribu kuifuta fikra ya Loveness kwa Lazima lakini haikuwezekana. Alijikuta yuko katikati ya mawazo mazito mno ni umbo la Loveness siyo yeye, ni sura ya Loveness ndiyo ilimtesa, ni sauti ya Loveness ndiyo ilimpagawisha na uzuri wa Loveness ndio uliomchanganya. Tom akiwa kajiegemeza kwenye kiti chake cha kuzunguka ndani ya duka kubwa alilokabidhiwa na Irene. Kichwa chake kiliangalia juu lakini alikuwa kafumba macho. Tom alishusha pumzi marakadhaa akiwaza afanye nini lakini haikuwezekana. Wazo la mwisho lililo mwijia ni yeye kufunga safari kuifata ile Hummer alijaribu kuikatisha mitaa kadhaa lakini foleni ilikuwa suluhisho hakuwa na ujanja alikutana na foleni iliyokwamisha ndoto zake zote na kujikukuta zikiyeyuka. “mara yapili nakutana naye sijachukua hata numba duh! Si ubwege huu” Tom alijiseme huku akikilaani kitendo kilichotokea mbele yake. Taratibu ana hangaika kugeuza gari lake na mwisho anafanikiwa anarudi dukani kwakwe na kuendelea na shughuli.

Alikuwa Tom ili si Tom wa mwanzo anaonekana Tom ambaye mwili wake umejengeka vizuri, umenawili huku ukigazanyika vipandevipande sehemu za mikono zilijaa vizuri na kujika, kifua kikiwa kimejaa vizuri pia kwa upande wa tumbo lilikuwa limegawanyika vizuri na kutengeneza vipandevipande vya matuta. Tom alikuwa mwenyeji Dar, alikuwa tayari ameijua biashara alikuwa tayari anawajua matapeli hivyo kutokana na tahadhali nyingi alizopewa na Irene mkewe alijifunza mengi saana kuhusu biashara na umakini. Tom alikuwa mwaminifu na msimamizi mzuri. Irene alikuwa akimfanyia ,majaribio ya kumuachia biashara zote kwa muda hata wa weeki tatu bila yeye kujihusisha kwa kisingizio kuwa anaumwa lakini hakukuwa na Tatizo. Sasa zabi alikuwa kamuami tom sana. Joto lilipamba moto kila kona ya jiji ilikuwa ni kutokwa jasho tu Tom anaingia barabarani taratibu lakini anabahatika kuiona li Hummer nyekundu, hakutaka kujiuliza marambili aliifata baada ya kutoka ubungo wanafuata barabara ya kweenda mwenge Tom alikuwa nyuma hakuwa na haraka na Range Rover yake. Hatimaye maeneo ya Mwenge ITV ile Hummer iliingia kulia na mbele yake kulikuwa na jengo lililo pambwa picha za wanamichezo, wanasoka maarufu, wacheza kikapu, ndondi, wacheza tenesi, kick-boxing nakadhalika. Tom naye anaegesha hapo Taratibu Loveness anashuka kwenye ile gari yake aina ya Hummer taratibu alikuwa akinyanyua mguu wake uliovalia kiatu kirefu kama hataki vile hatima ye aliiingia kwenye lile jengo. Tom alikuwa akipiga hesabu kwa kutumia alama zote, si kujumlisha , kutoa wala kuzidisha, pengine aligawanya mwisho jibu likakosekana namaanisha hakufata kanuni za mahesabu. Baadaa ya kujihoji kwa muda mrefu Taratibu saana Tom anaufungua mlango wa gari lake na kuianza safari kuingia kwenye lile jengo ambali kwa nje lilisomeka kwa maandishi makubwa Supa bet.

Tom alikuwa aking’aa sharubu mana alijikuta yuko katikati ya lundo la watu ambao kila mmoja alikuwa bize na karatasi na wengine wakipekuwa mitandaoni kupitia kompyuta zisizo na idadi zilizokuwa hapo ofisini. Tom anaangalia kila ukuta ulikuwa na Television kubwa iliyopambwa ukutani, hakuna aliye mjali mwenzake kila mtu yuko bize na kupiga mahesabu. Tom kwa harakaharaka alijua watakuwa ni wanafunzi pengine wanafanya kazi ya mwalimu au ni mtihani mtandaoni lakini kilicho msangaza watu walikuwa wakimiminika kuingia na kutoka aliamua kumsogelea mmoja wao karibu kulikuwa na komyuta moja iliyokuwa wazi. Alifika na kuketi karibu yake akauliza. “kaka hapa mnafanya nini?” . “hapa bro ni mikeka tu” yule kijana alijibu. “Mikeka?” Tom alihoji huku akiangaza huku na kule lakini asipate hata hiyo bahati ya kuiona hiyo mikeka inanyo semwa. “yah! Unaona hiki kikaratasi huu ni mchezo wa kamali wa kubahatisha michezoni tunatumia fedha kidogo ila tuna piga fedha nyingi saana kwenye huu mchezo” sasa Tom alikuwa ameelewa lakini wakati akitaka kujuzwa zaidi aligeuza shingo yake na kumuona Loveness akitoka Tom alinyanyuka kama mwehu. “Love.. Love… Love” pamoja na kuita kote Love wala hakugeuka Taratibu alikuwa akifungua mlango wa gari lake kabla hajaingia Tom alikuwa karibu yake sana. Love anageuka na kujibu “ tafadhali hilo jina huwezi nipata utakesha ukiliita huwa sichangii jina hilo ni jina lakila mtu” Love alijibu kwa kejeri. Okey samahani nikuiteje sisita “niite Mtoto wa Kigogo au Binti wa Kigogo hilo ndo jina pekee ” Tom alianza kuwaza Duh nibinti wa kigogo neno kigogo ni sawa na neno sonko nchini Kenya ni ni mtu tajili, tena anaweza kuwa si tajili tu bali ni mtu mwenye nguvu serikalini, Tom anakumbuka Mtoto wa kigogo aliwahi kumwambia kuwa anatokea Dodoma na kiuhalisia katikanchi hii Dododoma ni makao makuu ya nchi wabunge, mawazili na makatibu wakuu wa wizara mbali mbali hukaa dododma. Tom aliamini wazi kuwa Loveness alikuwa ni mtoto wa kiongozi mkubwa serikalini na kwaharaka haraka alijua anaweza akawa mtoto wa waziri mkuu. “basi kwa tahadhali sana Tom alimpa mkono na kumsalimia “habari za saa hizi Mtoto wa Kigogo” Mtoto wa kigogo akajibu kwa nyodo “Nzuri sana kakaangu” basi Tom alikuwa hoi baada ya kukutana na kiganja cha mtoto wa kigogog kiganja laini alihisi kama kashikwa mkono na malikia kutoka mbinguni. Basi kwa kummaliza kabisa mtoto wa kigogo anamkumbatia Tom ana kumbusu huku akimuaga “byee see you Tom” Mtoto wa kigogo alikuwa akitabasam mithili, tabasamu ambalo lilioneha wazi kuwa Yes kabula hajaambiwa chochote na Tom. Basi Tom aliomba Tafadhali love ooh! Sorry binti wa Kigogo nipe namba” Tom aliomba japo namba Binti wa kigogo alimpa kikadi kidogo kilichokuwa na kila aina ya mawasiliano.


Tom anarudi ndani ya Range yake akiwa na furaha hakuchelewa kuhu akiimba ndege mjanja kanasa kwenye tundu bovu. Safari yake ilielekea kariakoo dukani kwake. Ni dusu saa aliitumia njiani kutokana na foleni hatimaye alikuwa msimbazi kaliegesha gari lake na kumkuta Kulwa akiendelea na shughuli zake. Majila ya jion Tom anamuomba mbinti wa kigogo watoke kwa chkula cha usiku hakukuwa na pingamizi. Ni ndani ya Mic Hotel Ubungo bint wa kigogo alipachagua maana hakuta kuingia hoteli kubwaa maana alifahamiana na watu wengi maarufu alifanya hivyo kukwepa usumbufu. Basi wakiwa kwenye meza mja ya duara walianza kushusha vinywaji kabla ya chakula cha usiku. Tom alijitahidi kuzungumza naye walau apate tarifa Zake lakini haikuwezekana alionekana ni mtu makini saana. Basi walieendelea na mazungumzo Tom alikuwa akishusha Heineken na mtooto wa kigogo alikuwa akichanganya vinywaji vikali mbalimbali. Hatimaye saa tano za usiku Binti wa kigogo alimuita mhudumi na kumwambia apewe chumba mhudumu alimpa chumba na baadae alimwambia Tom hawezi kuondoka kwani atalala palepale kama kweli anampenda. Basi Tom akiwaza nyumbani itakuwaje na Irene mkewe atamfikiliaje? Basi alichukua simu yake iliyokuwa kaiondolea mtetemo na mlio ilionesha missed call kama kumi zote ziliandikwa wife alimaanisha mke wake ambaye ni iren pasi Tom anaizima ile simu huku akishusha pumzi na kujisemea liwalo naliwe katu siwezi kupoteza bahati kama hii.

Haikuwa ngum kwani Tom alikabidhiwa kila alicho kitaka na akasahau mateso yote na utu aliotendewa na Zabi mkewe leo anaonekana kajiachia kitandani baada ya safari kadhaa na Mtoto wa kigogo wakiwa uchi wa mnyama mbali na kujuta kwa namna moja ama nyingine lakini Tom alijisifu kwa kumpata mrembo yule. Juu ya meza ndani ya hoteli ile kulikuwa na madini ya kila aina yaliyo tingwa shingoni na binti wa kigogo saa ya thamini kubwa na viwalo vingine vinaonekana kuwekwa kihasala hasala. Ufundi wa kitandani wa binti yule unampagawisha Tom na kujiona alikuwa kachelewa sijui alicho mfanyia ila ninacho kikumbuka Tom alikuwa akiangua kilio tena kwa sauti kubwa kama mtoto, si kilio cha machunu ni kilio cha mahaba, mahaba yalimchanganya na kumpagawisha Tom. Asubuhi inafika tom anzidi kumpenda Binti wa kigogo na anaamini yule ndiye alikuwa chaguo lake sahihi katika maisha yake.

Asubuhi Tom anaingia nyumbani kwake Zabi anamfungulia Geti bilahiyana na kumkaribisha ndani mmewe. Tom alikuwa akinuka pombe achilia mbali anasa alizofanya na yule mwendawazimu mwenziye. “Tom umetajirika mme wangu? , tom umepata ulicho stahili kupata.. naoona umesahau yote na vyote tulivyofanya umesahau ulikotoka leo unazima simu na kulala nje bila taarifa, Tom mlevi mpya naanza kukuona leo. Kunakupanda nakushuka, maisha ni sawa na hatuwa za mlevi Tom unaweza kupiga hatua tatu mbele ukarudi nyuma saba ila kuiwa umelewa utzijumlisha tu na kuona umepiga hatua kumi kumbe ni saba ongeza tatu tunatoa kumi na kuona hakuna ulichokifanya. Siwezi kusema chochote najua niliko kutoa sikusimangi ukweli tunausema. Una muda wa kutosha kufikri ahsante” zabi aliondoka kwa hasra baada ya kumaliza kuzungumza Tom hakuw na lakujibu alikuwa kajiinamia kaama mwenda wazimu. Hakujua aseme nini hakujua nini akifanye hakujua. Baada ya kuoga Tom anavalia na kutoka Zabi alimuaga na kumwambia awe makini, Zabi hakuonesha kuwa na kinyongo basi Tom alienda mpaka dukani kwake. Alifika akiwa ndani ya dimbwi la mawazo anajaribu kukumbuka kama kweli alikumbuka hata kutumia kinga wakati akizini na Mtoto wa kigogo. Jibu lilikuwa gum hakumbuki. Wakati akiwaza hayo Tom alisikia kama kuna mtu anamsemesha kwa mbali taratibu anavuta hisia ni kama mtu aliyetoka usingizini. Tom anashituka kumuona mtoto wa kigogo akiwa dukani kwake kasimama. Tom alitoka akijaribu kumtoa kisiasa ili Kulwa asigundue ninikilikuwa kinaendelea kati yao. Lakini kitendo cha kumsogelea tu mbele ya macho ya kulwa Tayari Binti wa kigogo alimbusu Tom shavuvi na kumuachia alama ya rangi za midomo.

Tom alimuomba binti wa kigogo wakaongeee ndani ya gari alikubali walipofika tom alianza kumuomba ladhi saana kwa yote yaliyo tokea na kumwambia kuwa tayari anamke so kama binti wa kigogo atajuwa tayari kuendelea naye ajiheshimu wafanye kwa kujificha na kama hayuko tayari basi waachane. Binti wa kigogo alicheka saana “Tom mimi siyo mjinga wa kukuvulia nguo zangu kiurahisi kiasi kile, naamini niliku nakupenda ila ulichokosea Tom ni kukubali kulala na mimi na ukanionesha ufundi wa hali ya juu kwa mapenzi yale sahau kusikia nimekuacha. Nitafanya nitakavyo any time anywhere nitakuja kama ni mkeo basi jiandae tu kumtambulisha bi mdogo nipo.” Tom alionekana kuchanganyikiwa “please Love ninakuomba saana usinifanyie hivyo” Tom aliongea kwa upole huku akijaribu kuisaka amani. “haiwezekani Tom unaujua mwili wangu una thamani gani kuna wenzako wamehonga mpaka magari hapa lakini wakaambulia kuniona nimevaa nguo tu, hukunitongoza lakini umepata bahati ya kuvuliwa mpaka nguo ya mwisho na mtoto wa kigogo una bahati kijana usiiacheipite na mimi sitakuacha kulia kuongea baby unapoteza muda tu kuwa huru honey I’m yours” Tom alionekana kukosa chakusema waswahili husema ameuvaa mkenge kuuchomoa akatambike. Mazungumzo yaliendelea lakini hayakuwa na mwafaka Basi Tom pamoja na juhudi zote basi alimuomba walau achukue kitu chochote dukani ila siyo kumharibia ndoa yake tom aliomba saana. Binti wa kigogo alimjibu kuwa haharibu ndoa ila anapigania ndoa maana wanawake ni wengi kuliko wanaume Tanzania hivyo si ajabu mwanamme mmoja kuwa na wake wawili hivyo hata yeye binti wa kigogo hana mme na anategemea Tom amuoe. Tom kichwa kilikuwa kimechemuka kilikuwa kinawaka moto, alikuwa akiwaza mpaka anapitiliza. Basi binti wa kigogo alimuomba Tom ashuke ili aondoke kwani ombi lake lilikuwa limekataliwa. “Tom baba tuzungumze kuhusu maisha kuwa tutaishije mpenzi wangu tuzae watoto wangapi ila habali za kuniacha sijui nijifiche hapa zisahau na haziina nafasi.”



Tom aliachwa dukani kwake akiwa kama mjinga akitafakali lakufanya, Tom dunia ilikuwa imemuelemea na mzigo mzito wa mawazo wa mawazo hakukuwa na suluhisho la haraka kwanialiwaza na kuwazua kuanzia muda ule ilikuwa majira ya saa nne asubuhimpaka jioni bila kula hakukuwa na suluhisho. Tom alikuwa kama mgonjwa hakuwa anawaza chochote zaidi ya kujilaumu na kujiona mjinga hayo yote tisa kumi aliwaza jinsi atakavyo weza kumueleza Irene siku akiumbuka kuhusu uhusiano wake na love. Majira ya jioni anarui nyumbani akiwa mnyonge kaama mgonjwa alikuwa na msongo ambao hakuwahi kukutana nao katika maisha yake yote. Irene alimpokea mmewe baada yakutoka kazini alijitahidi kuzungumza naye ili ajue kinacho msibu lakini Tom alisingizia anaumwa basi Irene au zabi kwa jina maarufu alimuruhusu mmewe akapumzike huku akimpa dawa aina ya dicroper ilikupunguza maumivu ya kichwa ambapo Tom pamoja na kuvimeza vile vidonge hakuna kilicho pungua zaidi ya kuongeka. Tom alikuwa kavurugwa akiwa kajilaza na simu yake akiwa kaitolea mlio na mtetemo ilianza kuonesha mwanga alipoitizama ilikuwa ikiita jina Binti wa Kigogo, tom anaingalia ile simu kwa muda hofu na hasla hatimaye anaipokea. Sauti ya mwanamke upande wa pili ilikuwa ikimwamuru Tom aende “Tom njoo nakuhitaji mara moja nimekumiss mme wangu mtarajiwa” Tom alipandisha hasira ingawa hakuwa na lakufanya alizidi kuwa mpole huku akiikata simu kwa hasira. Lakini pamoja na kuikata simu bado haikuwasidi wakati akijiandaa kuizima simu anakutana na ujumbe mfupi wa maandishi “Tom usithubutu kuzima hiyo simu ukizima tu ujue ninakuja nyumbani kwako na nitajitambulisha mbele ya mkeo sasa amua unitambulishe au uiache simu tuzidi kuwasiliana” kizungu mkuti Tom alikuwa kakalia kuti kavu.

Pamoja na kujifaragua kujibu ujumbe ule kwa matusi lakini ni dhahili kuwa Tom alikuwa kabanwa sehemu nyeti alikuwa hawezi kuchomoka. Basi Tom anafika sehemu anakubali wajadili na Loveness ili kuupata muafaka. Tom alitoka chumbani kwake akaangaza huku na kule anapandisha ngazi kutoka cchumbachake kilichokua chini ya usawa wa Ardhi anatembea na kutoka nje nyuma ya nyumba alianza kuzungumza na Love akijaribu kumshawishi huku akimueleza ukweli juu ya Irene mkewe alivyo msaada kwake, aliko mtoa yeye na familia yake kwa hiyo hayuko tayai kumuacha, kumsaliti, kumuumiza na hata kumdhalilisha. Love alicheka sana “Tom haya ni masikio yangu… mwanaume mzuri kama wewe unaolewa na mwanamke, anakupeleka atakavyo .. eti amenisaidia sana sikuwa na lolote yeye ndiye mkombozi .. ujinga mkubwa fungua akiri usiwe mpumbavu Tom think like a man ulimwengu huu niwakuamua. Nilikuona ni mtu Fulani mjanja kumbe bwege, lofa, jinga na lipumbavu Tom aliye kwambia kwangu hivyo vitu hutapata ni nani?” Tom alikuwa kaiweka simu sikioni huku jeuri ya kufoka ikikatika kama mbwa aliye rushiwa kipande cha nyama ya kukaaangwa iliyojazwa vinguo kuifanya inukie vizuri. Mazungumzo yaliendelea kwa upande watom yalizidi kumpa wakatimgumu na kumfanya bado aonekanekane mbishi na hakuwa tayari kuwa na Love hali iliyo sababisha Love aongee mazito. “Tom utakuwa na mimi utake usitake .. kama unampenda mkeo na hauko tayari kumsaliti kamwe usinge thubutu kunifatilia, kamwe usinge thubutu kushiriki na mimi tendo la ndoa usiku kucha ninajua unatengeneza mazingira ya kunikwepa lakini umeesha chelewa hautaweza Thomas amini nakwambia na kama huaamini leo ipo siku utaamini kuna siri kubwa ninayo ijua mimi kama huamini mkeo anaweza jua tarifa zote kuhusu mimi anye timu maana ninakila kitu na ili kuokoa huyu mama wa watu asjue be with me Tom” love alikuwa akizidi kutengeneza mazingirayaliyo mbana toma na kumkosesha kabisa nafasi ya kutamba na kujaribu kujetetea Love alikata simu na kumuacha tom kajiinamia kwenye nguzo fupi za kenopi nyumbani kwake.

Irene alikuwa nyuma ya Tom na Tumbo lake likiwa limeanza kuchomoza alikuwa akimuangalia mmewe aliyeonekana kuwa na wakati mgumu hali iliyomuuma sana. Tom hakujua kama Irene alikuwa nyuma yake taratibu alijikuta akiguswa mabegani na kukumbatiwa kwa nyuma na Irene huku kitumbo kilicho kuwa kimembeba kijacho wao kikimgusa Tom ambaye hakuwa na furaha yoyote kwa muda huo. “mme wangu umeanza biashara haramu zitakuumiza, kama umemdhulumu mtu tafadhali nieleze tulipe ninakujua unahali mbaya na si kwakupenda inaonesha kuna mtu anakushinikiza ufanye kitu na si bure inaonekana kuna kosa umefanya na ndilo analolitumia kukunyanyasa. Fikiri malambili mme wangu nificheuendelee kusoto auuniambie ukweli tutatue tatizo” Irene au muite Zabi alikuwa ni mtu wa ajabu alikuwa ni mke kweli aliyeletwa na mungu kwaajili ya Tom anajitahidi kutafuta suluhu ya matatizo ya mmewe maana kamuona mmewe hayuko katika hali nzuri. Mmewe anatabika na kusulubishwa. Pamoja na kubembelezwa kote Tom hakuwa tayari kusema ukweli alificha na akakataa kulizungumzia kabisa swala hilo basi kinafiki nafiki aliilazimishafulaha ili kumdanganya Zabi mkewe lakini haikuleta maana hata kidogo kulingaa na kwamba uhalisia kichwani kwake uliwaza ni jinsi gani atauvua huu mkenge alioingia huku usoni akilazimisha tabasamu la mnywa gongo.

Tom aliamua kutoaline kabisa na kuivunja makusudi majira ya usiku baada ya chakula cha usiku alikuwa kaketi na Irene, tom akilipapasa tumbo lililo beba kichanga chao kitarajiwa walikuwa wakipiga stori za hapa na pale huku wakibishana Irene aliamini na alihitaji saana mtoto wakiume alikuwa na sababu ya msingi kwenye familia yake alizaliwa peke yake na alikuwa mtoto wa kike hivyo hamu yake ilikuwa kuanza na mtoto wa kiume. Basi usiku ule walisinzinzia usingizi mzuri uliokuwa na tabasamu mioyoni. Asubuhi kunakucha majira ya saa 11 alfajiri Tom kama ilivyo ada kwakeulikuwa ni muda wa mazoezi alimwamsha mkewe wakaingia chumba cha mazoezi kilichokuwa kimejengwa hatua chache toka kwenye nyumba yao Irene alikuwa akifanya mazoezi mepesi ili kumsaidia kuwa na nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha ujauzito amabopo akiwa legelege magonjwa yange muandama na kumkosesha amani. Basi walifurahia pamoja mazoezi yale kwa angalau saa moja na baada ya hapo waliingia jikoni kuandaa kifungua kinywa kwa dakika kadhaa Tom ndiye alikuwa kalishika jahazi ndiye nahodha baada ya kuwa tayari akamkaribisha mamaa waendelee kupata kifungua kinywa. Baada ya kifungua kinywa Tom alikuwa anajiandaa kuiwahi foleni japo alikuwa tayari ameesha chelewa kisha alimuaga mkewe kwa kumbusu na kumkumbatia asubuhi ile kisha akaondoka. Aliingia ndani ya gari aliiondoa na kuingia barabarani wakati akisonga mbele aliona kuna gari ndogo aina ya Toyota Raum ilikuwa imepeki mbele yake lakini gahfula kabla hajaifikia iliingizwa barabarani na kuegesha Tom alifunga break kwa hasra alishuka na hasra lakini ziliyeyuka ghafula alipokutana uso kwa uso na Love kabla hajalishusha Tusi alilolitarajia alilimeza na kubaki kinywa wazi huku asijue chakusema. “Tom nimekuja kukuonya nilikwambia ukizima simu nitakuja nyumbani kwako na nitajitambulisha kwa mkeo sawa baba? Naomba hiyo simu irudi hewani maramoja haraka iwezekananvyo” agizo kutoka kwa Loveness au muite mtoto wa kigogo. Tom alibaki domo limemshuka kama kitambi cha fukala, Tom alikuwa na haya ya kujiuliza Love amejuaje kama naishi mtaa huu, hivi shida yake ni penzi tu au kuna kingine? “hapana lazima kuna chaziada Tom alijisemea huku akiiona ile Toyota Raum ikitokomea huku asijue lakifanya.

Tom anarudi na kuketi kwenye kiti chake ndani ya gari huku mikono kaiegemeza kwenye usukani wa gari lake. Tom alikuwa akifikiri sana juu ya hatima yake, alitamani dunia ugawanyike katikati na immeze kuliko kukutana na haya matatizo yanayoibuka kila kukicha. Tom alikuwa akilia kwa uchungu huku akijuta tamaa zilimponza aliamini ameharibu maisha yake na akajua wazi kuwa hakuna kuwa yeye ndiye chanzo cha kuingia katika haya matatizo alikuwa akiwaza sana huku alkilia kwa uchungu alitamani kulitakua hili tatizo lakini haikuwezekana. Tom alikuwa ndani ya duka lake akifanya kazi kwa bidii alijitahidi kupambana na matatzo yaliyokuwa yakimkabili na kutokuyaruhusu yaitawale nafsi yake akiwa bize kwenye kompyuta yake ofisini akikagua hesabu na uwiano wa bidhaa na thamani katika biashara zake mbalimbali yeye na mkewe aligundua hakuna tatzo biashara zote zilikuwa. Kulwa anakuja na kumuita Tom kuna mteja alimuhitaji alikuwa ni love. Tom akiwa kakunja ndita uso ulimchakaa ghafula kama magofu ya wakoloni kule kilwa alifika na kusimama mbele ya Love. “tom nataka hiyo simu irudi hewani sina ugomvi na wewe, ombi lanu ni simu yako kuwa hewani basi.” Tom alikuwa kajaa kifua mithili ya mcheza mieleka lakini kimawazo alikuwa mdogo kama punje za ulezi. Tom alitoka na kumfata Love tratibu aliomba kuzungumza naye basi wakaingia ndani ya gari na kuketi na mazungumzo yao yalikuwa hivi

“Love nimekukosea nini mama? …Kwanini unakuwa chanzo cha kutaka kuharibu maisha yangu ? huwezi kujua Zabi alikonitoa amini nakwambia ninamheshimu na nitaendelea kumheshimu kama mke wangu mpendwa naomba utuache ninakuomba pleas” tom alikuwa akijitetea huku akionekana kukerwa na tabia ya Love.

“nashukuru sana kwa maneno yako Tom hivi kuna mtu alikulazimisha kunipenda?” swalili lilimhusu Tom.

“hapana Love ni basi tu nilijikuta nimekupenda” tom alijibu kwa unyenyekevu

“basi kama ulijikutaumenipenda ndivyo hivyo hivyo utajikuta unanioa sawa mpenzi wagu?” love alimjibu kwa huku akimtizama kwa dharau.

“hapana Love usinifanyie hivyo, nikweli nilifanya kosa kila binadamu hukosea pengine ni shetani alinipitia nisamehe” Tom alikuwa akiongea huku akilia.

“kama shetani kakupitia na ukakubali kwenda basi yakubali na ulidhike nayo na anayookueleza maana umemuchagua kuqa rafiki yako, maana nijuavyo mimi mpaka mtu akaupitie mmekubaliana basi kubaliana pia na anachokushauli huyo rafiki yako shetani” hayo ndiyo yalikuwa majibu ya Love yalijaa kejeri dhalau yalikera na kuudhilakini hakukuwa najinsi.

“Tom umezaliwa kijiji cha Lushamba wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza miaka 28 iliyopita si ndiyo” Love alihoji

“umeyajuaje yote hayo ?” Tom alishituka baada ya kuyasikia hayo maneno.

“ninakujua kuliko unavyojijua ulitoka kwenu ukiwa na miaka 11 baada ya baba yako kufari, familia yenu ilikuwa na watoto 12 na sasa mko 10 wawili walifariki kwa ajali, familia yenu ni masikini saana tu na Zabi ambaye leo unamuita Irene au mkeo au mimi nimuite mke mwenza anajifanya kukusaidia sindiyo? Nikikosea uniambie” Love alizidi kumchanganya Tom na kumfanya aduwae

“mkeo yuko kama alivyo hana mzazi wala ndugu, baba yake alikufa miaka mingi iliyopita na mama yake ni kama miaka mitatu tu iliyopita, staki kuendelea *umeeesha jua niko hapa kukusaidia basi tusaidiane” Love aliponyeza kitufe kwenye gari yake dro ikafunguka alitoa bahasha ya njano akamkabidhi Tom akamwambia jitahidi mtu asiioni harafu kaangalie ukiwapeke yako kisha nitafute.


Tom alifunguliwa mlango akatoka taratibu mpaka ndani alifika akaingia stoo akafungua ile bahasha kulikuwa na mabando kazaa ya dolali haikuwa rahisi kuyahesabu lakini alipoendelea kukagua alikutana na tembe kama kumi hivi za madini yanye rangi nzuri hakuyajua hivyo akili yake ilichanganyikiwa kabisa katika maisha yake hakuwahi kushika dola na hakuwahi kushika madini. Ni nusu apige kelele alijua ameokota dodo chini ya mbamia haraka haraka anatoka dukani na kuondoka aliingia ndani ya gari lake akiwa na ule mfuko. Wakati akizunguka alipita kwa sonara mmoja lafiki yake jilani na uwanja wa Kaunda jamaa alipouona ule mzigo akamwambia “kaka hii ni tanzanite sijui utaiuza wapi hakuna sonaraanaweza kuinunua hapa mpaka wakimataifa au nenda sehemu wanazo nunua madini” sasa huyu jamaa ndiye aliharibu kila kitu alimfanya Tom azidi kudata maana aliuona utajiri ukimnyemelea alikuwa akiongea maneno ya kejeli “Zabi ananitesa na vijisenti vyake sasa nauona utajiri uko mikononi mwangu nikizipata tu breaki ya kwanza ni kutafuta gari yangu kali na nyumba ya kununua”. Tom alikuwa akijisemea huku akizunguka huku na kule kutafuta sehemu gani angeuza yale madini. Lakini Tom alikumbuka kitu akaamua kuegesha gari na kuipiga ile namba aliyopewa na Love. Alimueleza anatafuta sehemu kuuza yale madini. “Tom tumia akiri hayo madini huwezi kuuza kijinga kiasi hicho utakufa kama huniamini jaribu kama hujui hiyo ni Tanzanite ukikosea tu ujue umedhulumika au umeuwawa chukua tahadhali tuulize wazoefu tunafanyaje kwanza kabla ya kuuza nenda katunze hayo madini nitakuelekeza namna ya kufanya” Tom alikuwa kabadilika kabisa kimawazo Love alikuwa akimwendesha apendavyo.


Ni siku kasha zimepita Tom hajaonekana nyumbani Zabi ameesh choshwa na tabia ya Tom alikuwa kaka kimya maana simu ilikuwa haipatikani wala hakukuwa na mawasiliaono. Zabi alicho kifanya aliingia dukani na kukagua mali zake zilikuwa sawa hakukuwa na hasara hakutaka kuhangaika alifunga duka lake na kurudi nyumbani. Akakaa kimya ingawa moyoni ilimuuma na alitamani sana kuwa na Tom karibu lakini tabia ya Tom sasa ilikuwa haishikiki. Tom anaonekana yuko na love muda wote mitaani wakipanga mipango yao wakati huo walikuwa wakiishi kibaha nyumbani kwa Love haiikuwa mbali saana nakibaha mjini lakini siku ya leo Love anaonekana alikuwa na swala mhimu sana alilotaka kumueleza Tom. “Tom nataka nikufundishe kazi utafute pesa kama mwanaume ufanye kazi na siyo kulelewa kama jike fikri kiume uache kuishi kwa kutegemea mtu kama changudoa.. je, uko tayari?” Tom alikuwa kamuamini saana Love basi hakukuwa na mazungumzo zaidi Love aliingia ndani ya gari yake aina ya hummer taratibu alianza kuongoza njia ni kama dakika kadhaa walikuwa nje kidogo ya kibaha mjini love alikata kulia wakazidi kutokomea mashambani na hatimaye maporili hali iliyoanza kutoa hofu kwa Tom taratibu anakutana na kijimsitu kikubwa wanaingia katikati na hatimaye nje ya jumba moja la kifahari lililokuwa polini huku likiwa limejaa walinzi waliovalia miwani mieusi ya jua huku kila mmoja akiwa na bunduki aina ya A.k 47 fupi. Tom alianza kutetemeka baada ya kushuka wanawekwa kati huku Tom akiambulia kitaka cha bunduki hiyo kilichopigwa kwa ufundi na pande moja la baba lenye sura mbaya ya kutisha. Tom alikuwa yuko chini kazilahi nini kitafuata. 



Ni ndani ya chumba kidogo kilichokuwa na giza nene akiwa peke yake Tom anazinduka taratibu, huku akijitahidi kupambana na mwanga hafifu uliokuwa ukipenya kwenye chemba za uwazi wa kidilisha cha mbao kilichokuwa juu ya chumba hicho. Tom huku akifumba macho anajaribu kujiinua kutoka chini lakini anashindwa kichwa kilikuwa kizito maumivu mazito, lakini kila alipojaribu kujipapasa kila kona ya mwili wake, bado maumivu yalikuwa makali mno. Tom anajaribu kujivuta taratibu mpaka kwenye kingo ya chumba kile kidogo anajiegesha kwa taabu sana kwenye ukuta kisha anashusha pumzi ndefu kwa nguvu. Anajaribu kujiweka sawa huku aking’ata midomo yake kwa meno akigugumia maumivu ya mwili.


Akiwa kaketi anajaribu kupepesa macho huku na kule anagundua alikuwa kwenye chumba kichafu, kilichojaa taka za kila aina mizoga ya paka walioharibika vibaya, vinyesi vya binadamu, maji machafu, utumbo wa samaki ni takataka za kila aina zilizolichafua hilo eneo. Mwanzo hakugundua kuwa chumba kile kilikuwa na harufu kali lakini sasa mwili wake unashituka na kugundua ndani ya kile chumba hakufai kuishi binadamu kwani hata alipokuwa amekaa anagundua baada ya kushusha macho na kuona alikuwa kakalia mzoga wa mbwa ambao karibu unateketea kwa kuoza na kwani hata nzi sasa walikuwa wamemtapakaa Tom mithili ya nyuki kwenye mzinga, anajaribu kupambana kutafuta msaada lakini haikuwezekana kwani arijaribu kuita lakini sauti haikutoka kutokana na maumivu ya koo kwani kulikuwa na maumivu kila upande, Tom pia anahisi njaa iliyopitiliza, ni njaa kwelikweli na siyo masihara lakini hakukuwa na matumaini ya kukipata chakula. Swali kuu kwa Tom alijiuliza amefikaje humo ndani? Na majibu ya swali lake yakabaki kitendawili.


Ndani ya shimo hilo masaa yalizidi kukatika shingo ilimuuma kwa kuangalia juu pasipo kuona mtu atakae msaidia, Tom hakujua nje nini kinaendelea, hakujua nani kamtupa humo shimoni na hakujua ilikuwa ni saangapi kutokana na kutoliona jua kabisa , muda ulizidi katika kwa sipidi ya ajabu, hatimaye kiza kilianza kuingia na baadae kiza totoro, milio ya Bundi ndege na wanya mwengine ilisikika, Tom alijitahidi kuita walau mtu amsikie lakini haikuwezekana maana chumba kile kilikuwa kirefu kidogo na kimesakafiwa kilifanana sana na shimo la maji taka tutumiayo majumbani. Usiku ule mbu, kelele za nzi ndio walikuwa rafiki zake, njaa ndiye alikuwa jilani na mfuasi wake wa karibu lilikuwa joto kali “nimewahi kuishi maisha ya taabu ila haya ni mapya kwangu” Tom alijisemea. Kutokana na na takataka zile hakikuwa kitu cha ajabu kwani Tom anavamiwa na wageni usiku huo nao si wengine ni siafu walikuwa wakidondoka toka juu ya mlango na kumwangukia huko ndani, mwanzo hakujua lakini baada ya kushugulikiwa kama na wawili hivi alikuwa kapata akili sasa anashituka na kugundua siafu walikuwa wakimiminika kwa wingi mulendani. Uchovu ulimwisha ghafula na kuanza kupambana ni namuna gani angeweza kujitoa mule shimoni shimo lilikuwa pana kutoka ukingo mmoja na mwingine, Tom anajaribu kujinasua lakini hakuweza kuzishika kingo za shimo kwani lilijengwa kwa muraba, kumbuka wakati akijaribu kutafuta njia siafu waliendelea kumshughulikia ipasavyo kwani walikuwa wakimiminika kwa wingi kutoka juu ya shimo hilo. Hatimaye kulikucha bila mafaniko Tom alikuwa kavimba mwili na siafu sasa aliwaona kama ni sehemu ya maisha yake. Alikuwa kawazoea maana hakuwa na njia mbadala sawa na mtu alaliae kitanda cha kunguni.


Ni siku cha pili Tangu Tom azinduke njaa ni wimbo wa taifa Tom vita yake na siafu likijita sehemu za kichwa tu alihakikisha hawagusi mdomo, pua, masikio na macho kwani ndizo sehemu nyeti kwake sehemu zingine za mwili alizitoa sadaka. Tom alikuwa kalia machozi yamemkauka, hakuwa na jinsi lakini hakukata tama alikuwa akijaribu kila mara kujiokoa lakini alishindwa ukuta uliteleza hakuweza kupanda juu, siafu walikuwa wametapakaa kila mahali. Tom anakumbuka mara ya mwisho ametekwa akiwa na Love anashituka na kukumbuka mpenzi wake yuko wapi? Hapo ndipo harakati za kujiokoa ziliongezeka alijaribu kila mara bila mafanikio, alijaribu sana kupanda ule ukuta lakini haikuwezekana.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog