Search This Blog

Thursday, 23 March 2023

MTOTO WA KIGOGO - 4

  

Simulizi : Mtoto Wa Kigogo

Sehemu Ya : Nne (4)


Ni jioni nyingine Tom akiwa kachoka balaa, njaa kali na Joto la kutisha ndani ya shimo lile, hakukuwa na hewa safi nabado ilizidi kuwa hewa chafu kwa uozo hatari. Tom anasimama chini huku siafu wakimpandilia hakuwajali alilitizama lile shimo akaifuta miguu yake kwa viganja ili kuto utelezi uliosababishwa na uozo mbali mbali ndani ya shimo hilo. Taratibu anajaribu kupanda tena anapiga hatua mbili lakini alikosa pakushika akaanguka na kwa bahati mbaya aliangukia mzoga na kujikuta akipiga mweleka mwili wote ulijibwaga chini. Alipotua chini alisikia mlio tofauti alitulia kidogo na kuanza kugonga kwa mkono wake anagundua sehemu ile ilikuwa kama ina ubao. Hakutaka kusubiri Tomu alianza kufukua sehemu ile na kweli akagundua kulikuwa na dilisha lililokwenda chini ya shimo hilo halikuwa na kufuli wala kitasa alilifungua na likafunfunguka bila shaka alichungulia hakuona chochotealijitosa na kuibuia upande wa pili aliona ngazi ikishuka zaidi kwenda chini aliifata kwa hofu na baadae akaibukia sehemu nyingine ambako ngazi zilizidi kumpeleka chini kwenye handaki na kwa upande huu taa zilikuwa zikiwaka kwa mwanga hafifu. Tom alichukua tahadhari zaidi alizidi kusonga mbele, taratibu alianza kupishana na mabaki ya viungo vya binadamu kama vile mathalia ya nyonga, uti wa mgongo, mbavu na hatimaye fuvu Tom anazidi kugundua kuwa alikuwa sehemu hatari zaidi. Jasho, hofu, njaa na uchovu unamfanya aishiwe nguvu na kujikuta akikata tama na kuketi chini.


Mawazo yasiyo na majibu, Tom analia na kujilaumu ameichezea bahati ya kupendwa na mwanamke bora, Zabi na sasa ameangukiwa na jumba bovu. “asiye bahati habahatiki, na bahati ikija mlangoni hukuta bundi” alijisemea na kusonya kwa hasira kisha akanyanyuka na kuchukua kipande cha chuma kilichokuwa jilani alikitumia kama siraha na safari ikaendelea. Ni mwendo wa nusu saa bila kuona chochote, wala kukutana na mtu ndani ya lile handaki Joto, kiu ya maji sasa ilikuwa ni tatizo kwa Tom kwani koo lilimkauka alitamani hata akutane na jani lenye umande angalau kupoza kiu ile lakini haikuwezekana. Miguu haikuwa na nguvu tena alikuwa kachoka nyakanyaka hakujua anenda wapi alichokijali ni kujiokoa, Tom alikuwa akijivuta taratibu huku akisaidiwa na ukuta aliouegemea alizidi kushuka ngazi taratibu ndani ya lile handaki huku yakiyawaza mamisha ya raha msitarehe aliyoyapoteza kizembe kwa mpenzi wake Zabi. “nilikuwa napewa kila kitu, nilikuwa naheshimiwa, alikuwa anaithamini familia yangu bila kujali hali niliyokuwa nayo…… ni upuuzi wangu…. Ni upumbavu wangu, ni tamaa zangu ndizo zilizo niponza acha nilipwe hapa hapa duniani, acha nife kwa tamaa za maisha ya muda mfupi….. ha! Haaaahaaaa! Katika dunia hii sijawahi nona, stawahi na haitatokea kuona mwanamme mpumbavu kama Tom mimi”. Alimaliza kuwaza huku akisonga mbele taratibu na kuyafuta machozi yake kwa kiganja.


Baada ya mwendo alioukadilia kuwa wa saa moja Tom anaibukia kwenye chumba kingine kilicho kuwa na ngazi ya kwenda juu ambako kulikuwa na mulango wa chuma. Alipanda na alipoufungua alijikuta yuko katikati ya shamba la mahindi yaliyositawi vizuri, anajaribu kuanganza huku na kule huku kapigwa na butwaa kwani hakuamia kwani hakuona mtu hivyo ana mshukuru mungu maana alijua tayari kafanikiwa kuwatoroka wale watu wabaya, tom anashusha pumzi na kupiga ishara ya msalaba, lakini bila kutarajia alijikuta yuko katikati ya majibaba mawili yaliyokuwa yameshiba vilivyo ni miili mikubwa iliyo shiba mazoezi. Hakuwa na chakujibu ila kufuata alichoelekezwa, Tom anakutana na kipigo cha adabu kilicho mfanya akitamani kifo, mbali na kupoteza jino lake moja bado alikuwa hajitambui tena kwani kipigo kilipoteza fahamu. Wale mabaunsa walimbeba na kwenda kumuweka kwenye buti ya gari.


Kichwa kinawaka moto, shavu limevimba ni damu tu ndo zilizokuwa zikimtililika toka kinywani huku midomo ikiwa imemtepeta kama supu ya konokono. Kung’olewa jino bila ganzi inahitaji ujasili na kujitoa isitoshe huna hata dawa ya maumivu kiukweli inahitaji kipaji cha ziada nilimpongeza Tom kwa kipaji hicho hadimu ni wachache wanaweza kuhimili mziki huo. Lakini si kwakupenda kwake ni matatizo ndiyo yamesababisha. Tom alikuwa kawekwa katikati akiwa anavuja damu nyingi uso umemuumka kama kapiga funda la hamira ni dhahili kwamba maumivu aliyokuwa akiyapata ni makali na hatari zaidi ya uvimbe aliokuwa nao. Tom anajiwazia kimoyomoyo “kweli asiyefunzwa na mamaye ulimwengu ndiye darasa”. Watu waliokuwa wamemzunguka wakikuwa na sura za ajabu, roho zilizojaa ukatili na walionekana kukosa hata punje ya huruma jibu lililokuwa kichwani kwa Tom ni kumuomba mora wake amsamehe dhambi zake kwani ni wazi kuwa safari yake ya duniani ilikuwa imefika Tamati. Kila mtu alikuwa kimya wale watu wapatao watano walikuwa wakitizamana na kupeana ishara bila kuzungumza. Jamaa mmoja aliyekuwa kachomekea vizuri, miwani mieusi na tai nyeusi huku mkononi akiwa na saa yake iliyoonekana kuwa ya gharama kubwa, taratibu anavua saa yake na kuikabidhi kwa jamaa aliyekuwa karibu yake kisha akachukua jambia na kulielekeza shingini kwa Tom kama analenga pa kukata ananyanyua juu na wakati akitaka kulishusha kwa kasi ili kuigawanya shingo. ………………………..“Stoooop” wote waligeuka na kutazama nyuma alikuwa Jimmy Radi akiongozana na Love. Ndiye aliyezuia Tom asiuawe……………………



Jimy Radi mfanyabiashara maarufu jijini Dar-es salaam sambamba na majiji mengine ya jirani kama vile Arusha, Mwanza , Nairobi, Kampala na Kigali, Jimmy ndo jina maarufu saana katika majiji haya. Jamaa huyu hufanya biashara za madini, maduka, usafirishaji wa mizigo na biashara zingine kemukemu. Jimy anafika na kusimama pembeni kisha akageuka na kumwangalia Love huku akitabasamu. “mtoto wa kigogo wewe ni zaidi ya mwelevu …. Haha nimempenda huyu kijana sitaki kujua uliko mtoa anaonekana kuwa strong maana leo ni siku ya nne hajala , pamoja na hekaheka zote bado anaonekana shupavu…… ameweza kutoka kwenye chumba cha kifo ambacho zaidi ya watu miamoja wamepoteza maisha kwenye chumba hicho kwa kukosa njia ya kutoka na kujikuta wakikata tama hali iliyosababisha mauti kwao lakini yeye kaweza, kapita njia hatari pamoja na maumivu na mateso kahimili mwacheni huyu ni kijana wangu ni kijana mhimu katiak shughuli zangu. Tom karibu kwenye himaya ya Radi ….” Radi alimkaribisha huku akigeuka na kutoa agizo jingine …. “Hakikisheni anapata chakula haraka.” Tom baada ya kusikia kauli ya Radi kuwa hajala siku nne ndo anashituka “ha! Kumbe sijala siku nne?” yeye alijua ni siku mbili kwa kauli hiyo inamaanisha alizimia kwa siku zaidi ya moja, njaa iliongezeka maradufu. Lakini wakati huo walikuwa wakitizamana na Love Tom akionekana mtu mwenye hasra na aliyekata tamaa huku Love akionekana kutomjali kana kwamba ndo mara yao ya kwanza kuonana katika hisitoria nzima ya maisha yao. Love alionekana kuwa karibu zaidi na Jimmy na bila shaka walikuwa wapenzi hali hiyo haikumshangaza Tom kwani alikuwa kapata picha halisi ya Love hakushangazwa na usaliti huo wala hakuuona waajabu kwake.


Tom anaonekana mwenye mawazo aliletewa chakula n,i uji wa moto ulikuwa kwenye kikombe cha chuma kikombe kilikuwa kimechemka haswaa, bila shaka ndicho kilichotumika kuuchemsha uji huo jikoni . “nakupa uji huu uwe umeisha ndani ya dakika mbili” ni amri ilitolewa na mleta uji. Tom alikuwa na njaa yakufa alijaribu kukisogeza kikombe kinywani lakini kilikuwa cha moto alishindwa , alijikaza tena kiligusa kingo za midomo na kumuunguza alihisi maumivu makali, uji ulikuwa wa moto mno, kikombe ndo usiseme, lakini Tomu alikuwa na vidonda mdomoni isingekuwa rahisi kwake kunywa uji ule maana kang’olewa jino kwa kipigo nabado alizidi kushushiwa mkong’oto akilazimishwa kunywa uji wa moto. Lakini kama tujuavyo Kipigo huwa hakishindwi kitu huwezi amini Tomu aliumaliza ule uji japo ulimi, kinywa, koromeo na utumbo vilimulaani vikali kwani viliwaka moto kama vimepigwa pasi. Mateso ni sehemu ya maisha kila kukicha alikuwa akikumbana na mateso mazito aliishi na watu wasioongea, ni watu wa ishara na vitendo. Hakuwahi kusikia sauti ya mtu hata mmoja, kila siku aliona sura ngeni zenye maumbo yaleyale yakutisha na chaajabu hata wao kwa wao walikuwa hawaongei. Tom alijiuliza ni watu wa aina gani hawa? Kiuhalisia mtoto wa kiume alikili wazi kuwa kakwama na wokovu wake ni kuwa mpole na kufuata kila alichoambiwa.


Hakuwahi kulala tangu aingie kwenye hiyo himaya kila kukicha mpaka kunakucha tena ni suruba , mateso na hatimaye akayazoea na kuyaona kama mazoezi, Tom alibebeshwa taili za gari na kuzivuta kwa masaa kadhaa, wakati mwingine alisomba magogo kutoa sehemu moja kwenda nyingine chini ya uangalizi mkali na mwisho aliamuliwa kuyarudisha tena hayo magogo sehemu alipoyata. Baada ya wiki tatu Tom alikuwa mzoefu na mwepesi hakuna shughuli iliyomshinda na hata mwili haukuwa ukimuuma tena kama mwanzo. Ratiba ya chakula sasa ilibadilishwa na kuanza kupewa chakula kizuri lakini shughuli zikiongezeka maradufu hali iliyofanya hata hicho chakula kuonekana si chochote, ni mazoezi hatari aliyo fanyishwa Tom kama vile kupita juu ya kamba kukwea miti kwa haraka zaidi, kuruka viunzi vyenye miiba, kupita kwenye kuta zenye misumari na seng’enge ni mazingira magumu mno katika mazoezi aliyo yapitia Tom na ni hatari mno kwani hata akiumia hakuana aliyejari.


Miezi mitatu badae Tom anaunganishwa na kundi jingine la vijana ambao hakujua kuwa walikuwa katika eneo hilo, ni vijana wapatao 29 walikuwa wakiishi katika jingo hilo na hakuwahi kuwaona wala kusikia sauti ya hao watu hata siku moja. Siri ya jengo hilo ni ukimya, hupaswi kuzungumza ila ishara na ukithubutu kutoa sauti safari yako hapa duniani ndo itakuwa imeisha hayo ni maelekezo aliyokuwa akiyajua na kuyaheshimu kila mtu aliyeishi katika jengo hilo. Baada ya kuchanganywa na vijana wengine Tom alikamilisha idadi ya vijana 30 na wakaendelea na mazoezi hatari, katika jengo hilo kulikuwa na vifaa mbalimbali vya mazoezi na vingine ni hatari kama vile mashine za kupiga mishale na mtu anatakiwa kupita bila kujeruhiwa, kupita kwenye springi na hata michezo ya vizu na mapanga. Kila kukicha ni zoezi jipya, mwanzo ilikuwa ngumu kwa Tom na baadae alizoea na kuona ni kitu cha kawaida. Vijana wote walifahamiana pasipo kujuana majina wala kuzungumza ndo yalikuwa maisha yao kambini hakukuwa na lelemama.


Mateso yalizidi hakuna uhuru, hakuna kuongea na wala kuomba msaada Tom aliona njia pekee ni kutoroka . Alinza maandalizi yake na kujiweka sawa hakujua atapitia wapi ila aliamini ataweza kutoroka. Tom aliamka mapema akaanza usafi ndani ya jengo kama kawaida lakini alishitushwa na kipyenga kilicho pigwa kikiwaita paredi alipofika alikuta vijana wawili ambao ni wenzake wamewekwa chini ya ulinzi, kesi ilikuwa ni jaribio lao la kutoroka liligonga mwamba na hivyo hakukuwa na mjadala bali kifo Tom ndiye alikuwa pekee hajawahi kutoa roho ya binadamu hivyo alikabidhiwa kisu ili kuwashughulikia. Alikuwa na uoga lakini ilimbidi kufanya hivyo maana kuzembea kwake kungesababisha yeye apoteze maisha. Kwa mara ya kwanza Tom anatoa roho za watu wawili kwa upanga na kunyweshwa gilasi nzima ya ndamu ili kuongeza ujasili. Halikuwa jambo dogo ni mateso yaliyotesa nafsi ya Tom kila kukicha, aliwaza na kuwazua alitamani kutoroka lakini watu aliowauwa bila shaka damu yao itarudi kwake. Bila shaka kutoroka kwake kungeambatana na kifo mkononi , Tom hakuwa na budi kubaki. Kubaki kwake kukakutana na kikwazo kingine kwani siku hiyo waligawiwa katika makundi ya watu saba saba na kati ya hao watu saba alitakiwa kubaki mmoja tu kwa kila kundi ni mtihani ambao haukuhitaji maswali. Kundi la kwanza walitupwa msituni , kundi la pili walibaki hapo na visu vyao kundi la tatu walikuwa nje na kundi la nne wao walitupya kwenye bwawa la kuogelea. Kila mmoja na kisu chake harakati zilianza ni unyama wa hali ya juu damu zilitapakaa kila mahali vijana walijeruhiana kwa visu na kuumizana vibaya, siyo nzuri kuhadithia ila haifai pia kuonekana ilikuwa ni kama sinema lakini ni uhalisia, kila mtu alikuwa akipigana kuyaokoa maisha yake, ni visu tu vilivyo zungumza, ilikuwa ni kuwahiana kipindi ukiwaza kumuua huyu mbavuni kwako kinazama kisu kutoka kwa jilani yako, kulia kwako kinazama kisu na tumboni kisu wakichomoa huna maisha, idadani ya vijana ilizidi kupungua kutoka kwenye saba kila kundi, wengine wamesalia wawili, huku kuna wanne, hawa nao watatu na wale kule ni watano. Kwa damu zilivyokuwa zimewatapakaa sizani kama kuna hata mmoja aliyekuwa hana jeraha la kisu. Si kwa mapenzi yao ni amri iliyoambatana na kukosa huruma ya kibinadamu kifo ndiyo ajenda kuu, aliyejisahau ndiye aliyekuwa wakwanza kupoteza maisha na kifo kilichelewa kulingana na uwezo wako na kujituma kukwepa, wepesi wa kumuona adui mapema ni moja ya bahati iliyo wanusuru vijana wengi. Upande wa akina Tom shughuli ilikuwa pevu watu wane walikuwa chini walibaki watatu akiwemo Tom, kitendawili cha nani anafuata kilichukua muda kidogo kwani wote walionekana kuwa wajanja na kuchukua tahadhali kali lakini kwa bahati mbaya mmoja wao alikanyaga vibaya damu iliyokuwa ikivuja kwa kasi toka kwenye maiti ya mwenzao aliteleza kwa haraka Yule kija na mwingine alikimbia na kumshindilia kisu cha kifua na hilo lilikuwa kosa kubwaa maana hakuweza tena kukichomoa kisu hivyo ikawa mungu saidia kwa Tom aliye mmaliza adui yake kwa kumchinja wakati akihangaika kutoa kisu kwenye kifua cha mwenziye. Tom aliaguka chini huku akitokwa machozi na kukilaani kitendo kile lakinini hakukuwa na jinsi ilikuwa ni lazima iwe hivyo ili kuokoa waisha yao. Kundi la pili lilikosa mshindi kwani hata aliezaniwa kushinda alikuwa kajeruhiwa vibaya haikumchukua hata dakika kumi baada ya wenzake kuaga dunia nae akafata, kundi la tatu ni watu waliokuwa msituni anarudi kijana mmoja hodari ambaye hakuwa hata na jeraha, na kundi la mwisho aliibuka kidedea dada mmoja ambaye aliokolewa na uwezo wake wa kuzama kwenye maji kwa muda mrefu hivyo wapizani wake wengi aliwauwa kwa kuzama nao ndani ya maji wakikosa hawa alimaliza kwa kuchoma visu vya koromeeo.Washindi watatu tu waliopatikana na watu ishirini na watano walikuwa wamepoteza maisha siku hiyo, ni dhambi kubwa ambayo kila mshiriki wake aliitizama kwa upana anaodhani anasitahili kuibeba.


Hakukuwa na pongezi bali walikuwa wamefuzu kwa hatua nyingine ya mafuzo, hatua hii ilikuwa ya matumizi ya siraha za moto kama vile, bunduki, bastora, mabomu ya kurusha kwa mikono na mabomu ya kutega aridhini. Ni kulenga shabaha, jinsi ya kujificha, kukwepa na kadhalika kwa kipindi hiki mazungumzo yalianza kuruhusiwa lakini ni wakati wa mazoezi tu Tom anapata bahati ya kuwafahamu wenzake wawili amabo ni John Licko na Annet Rehan timu ilikuwa imekamilika. Watu hawa watatu walikuwa ni watu hatari kuliko unavyo wazania, maana ni zaidi ya mwaka sasa wako mafunzoni sijui waliandaliwa kwa kazi gani.


Jimmy alitua kwa helkopita huku akiogozana na Love (Mtoto wa kigogo) walifika na mavazi mbalimbali ya gharama kubwa waliwapa vijana wale na wakavaa na kwaasilimia idadi kubwa ya mavazi yale zilikuwa ni suti, mashati mazuri, tai na viatu vya ngozi. Walipewa mavazi walivalia na mwisho yalichaguliwa mavazi baadhi kwaajili ya kupigia picha walifanya hivyo. Na mwisho Jimmy na Love wanaondoka na kuwaacha vijana pale pale kambini Tom lilimuuma sana swala la kumuona Love akiongozana na Jimmy alitamani azungumze na John lakini ilishindikana maana alihofia siri kuvuja na baadae kujikuta wakiwa matatani. Ni ukimya ulizidi kutawala na sasa yalikuwa ni mazoezi madogo madogo ya kuficha siraha kama vile visu, sindano za sumu, bastora na kulenga shabaha sehemu tete. Waliendelea kufanya hivyo kwa siku kadhaa huku wakisubiri maelekezo toka kwa viongozi wao wakati huo wote walikuwa chini ya wakufunzi mahili wa kivita.


Ni zoezi la kugawiwa hati za kusafiria hawakujua wanaenda wapi kila mtu alipokea hati mbili za Tom moja ilikuwa ni ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania ya pili niya Sudani ya kusini, kwa upande wa John ilikuwa tofauti alipewa hati ya Nigeria na Kenya upande wa Annet yeye alipewa hati ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania naya pili ilikuwa ya DRC Jamhuri Ya Kidemokurasia Ya Kongo. Mara baada ya kumaliza kutoa hizo hati Jimmy aliagiza “Tom nakupa miezi sita uweze kuongea kiingereza na kiarabu, Annet, kazi yako inahitaji ujue Kifaransa na Kilingara na John Kiingereza uko vizuri natamani sana kiwe cha lafudhi ya naijeria kwa Kenya unaweza kuigiza…..” walibaki wameduwaa maana hawakujua nini kinaendelea. Love alipiga hatua mbili mbele kisha akasimama na viatu vyake vizuri na virefu. “mtaondoka kesho jioni kila mmoja atakwenda pasipoti yake ya pili inakomtaka kwenda isipokuwa John ambaye toka awali tuliandaa kuwa siyo raia wa Tanzania hivyo John utaanzia Mombasa Kenya, ukifika uendako utatakiwa kubadili jina na kutumia lililoko kwenye paspoti ya nchi uliyopangiwa, mapokezi na sehemu za kufikia zote ziko tayari, shughuli mtazikuta huko na maelekezo yote” baada ya kusema hivyo aligeuka nyuma na kufungua begi kubwa aliwapa simu kila mmoja aina ya Samsung Galaxy Edge 7 na kisha akawaaga. Tom alikuwa kavimba kwa wivu baada ya kumuona Jimy akiondoka na Mtoto wa kigogo ambaye katu hatolisahau penzi lake lililomsababisha mpaka leo kapoteza uelekeo wa maisha aligugumia na kujipa moyo ipo siku atamrudisha Loveness mikononi mwake.

********************************************************

Irene (Zabi ) alikuwa na watoto wawili wa kiume aliowapata katika Hospital ya mhimbili wiki mbili zilizopia aliamua kuwapa majina yaliyoshabihiana na jina la baba yao, wakwanza alimuita Tommy na wapili alimuita Tonny, watoto walifanana sana na baba yao ambaye alikuwa ni mume kipenzi na chaguo sahihi kwa mama yao. Irene anakitizama kitanda kilicho wabeba pacha hao anatamani Tom angekuwepo kuungana na mpenzi wake katika mapokezi ya baraka hii maalumu waliyopewa na mwenyezi Mungu Irene anaangaza huku na kule anajikuta akiachia tabasamu lililoambatana na machozi. “Tom mme wangu uko wapi? na unafanya nini?, tafadhali muogope mungu wako njoo uwaone wanao, njoo tuwalee watoto mme wangu wa pekee, acha kuniadhibu kwa kuona nilikupenda na usiniadhibu kwa kuwa unajua sitapenda mwingine zaidi yako…. Wanangu ni wiki ya pili sasa hamjamuona baba yenu kipenzi si kwa matakwa yangu bali ni mapenzi ya mungu baba anawapenda atarudi………. Tommy na Tonny baba atarejea soon” yalikuwa ni maneno ya kuchoma mioyo japo hayakuwa na maana yoyote kwa watoto hawa wachanga ambao hawakusikia chochote bali ni maumivu kwa mama yao. Mbali na utajili alionao Irene(Zabi) haukuwa na maana kwake kila kukicha alimuwaza Tom, “nilikukosea nini Tom wangu? Nilikukosea nini baba wa watoto wangu?… ulitaka nifanye nini ili uamini nakupenda? Sizani kama kweli hunipendi bali kuna mtu nyuma yako ipo siku atakuacha na utarejea mikononi mwangu....” ni maumivu ya makali ya moyo ambayo hakika kila mtu yangemgusa.

Toka ametoka labour Irene hakai mbali na kitanda cha watoto wake kutwa nzima anataja amajina ya watoto hao ili kuufariji moyo wake alikuwa kama mtu aliyechanganywa na mapenzi, mtu aliyepagawa kwa mahaba na sasa dalili za uchizi zilimunyemelea kabisa, kila kukicha utasikia akibadili majina tu “Tom, baba Tonny au baba Tommy rudi nyumbani mmume wangu kipenz .. rudi baba ……..rudi honey ” . hali hii ilianza kumtia hofu hata dada aliyekuwa akimsaidia kazi za nyumbani hakikuwa kitu cha kawaida sasa alianza kupata hofu maana Irene hakuwa sawasawa kila siku alionekana mwenye mawazo mazito, mwenye hasra asiyependa kushirikiana na wengine na hata kuongea kidogo hali ile ilimpa wakati mgumu sana Teddy. Teddy alikuwa ni msaidizi wa Irene kwa kazi za nyumbani sasa hali ilizi kumtatanisha aliamua kuwasiliana na dakitari wa Irene kwani hali hali sasa ilianza kumchanganya hata yeye Teddy. Irene anatoka ndani kwa kasi na kupitia ufunguo wake sebuleni, hakusema chochote anapishana na Teddy teddy anahoji “dada unaenda wapi?” Irene anageuka na kumjibu “is non of your business” Irene alijibu kwa mkato, “tafadhali dada bado hujawa na uwezo wa kuendesha gari nakuomba uache nibora unitume mimi huko uendako tafadhali nakuomba usihatarishe maisha yako, maana inaonekana hauko sawa najua unahasira hizi ni changamoto za dunia ni mapito tu” baada ya maelezo haypo Irene alikuwa ndani ya gari na tayari alikuwa kawasha jibu la mwisho lilikuwa “nakwenda kumtafuta mmme wangu, najua niliko mtoa, naujua umhimu wake kwangu siko tayari kumpoteza kiurahisi, ninamfata baba wa wanangu maana wanangu siyo yatima wana baba yao acha nimfuate auchuae uchungu wa mme ni mke na mke ni mimi Teddy acha niondoke mdogo wangu nitarudi” gari lilianza kutoka sehemu linapoegeshwa kuelekea getini na Teddy hakuwa nachazida bali kubaki kinywa wazi.




Hakiuwa rahisi hata baada ya kuliondoa gari ndani ya geti, Irene hakujua anaelekea wapi, hakujua Tom anaishi wapi na atampata wapi, hana tetesi wala taarifa zozote kuhusiana na Tom wala huyo mpenzi wake Tom wanakoishi kwa wakati huo na isitoshe ni muda mrefu umepita alikuwa amemkatia tamaa Tom ingawa moyo ulimuuma kila kukicha. Kabla hajaingia barabarani Irene anafunga breki na kuanza kujihoji anakwenda wapi na anakwenda kufanya nini? Jibu halikuwa rahisi, zaidi alianza kujuta na kujilaumu akiwa anajaribu kutafakali kichwa kilianza kumuuma na kujikuta akipoteza uwezo wa kuyahimili mawazo, alikuwa na msongo wa mawazo sasa anaanza kuropoka maneno mengi yasiyo na mpangilio wala tija, hii inadhihilisha ni kiasi gani Irene alikuwa na upendo wa dhati kwa Tom. Mwanzo Teddy hakuelewa lakini kadri muda unavyo zidi kwenda gari la Irene lililokuwa limeegeshwa palepale barabarani alishikwa na mshituko, haraka haraka alilisogelea na kugundua kuwa ndani ya gari hakukuwa na mtu alipogeuza jicho upande wa pili anagundua kuwa Irene ndiye alikuwa akipiga kelele upande huo. Alimfata na kujaribu kubembeleza kwani alikuwa kachanganyikiwa sizani kama alisikia hata alichokuwa akielezwa, basi Teddy aliwaomba baadhi ya vijana wamsaidie kumkamata huku akilia kwa huruma, vijana walijitahidi kufanya hivyo na wakafanikiwa Irene akakamatwa na kurudishwa nyumbani. Baada ya kufika nyumbani haraka haraka Teddy anachukua simu ya Irene na kumtafuta dakitari wa familia ambaye hakuchelewa kuianza safari mara tu baada ya kupata tarifa za mgonjwa wa mteja wake.


Ni dakitari Tuntu ndiye alikuwa dakitari wa Irene alipowasili nyumbani kwa Irene na kuiona hali aligundua mteja wake alikuwa na tatizo kubwa la kisaikolojia lilisababishwa na msongo wa mawazo, hivyo alimtafuta dakitari mwenza kitengo cha saikolojia hakuchelewa kuja alifika haraka na alipomuona aligundua anahitaji msaada wa kitabibu zaidi hivyo wakamchukua Irene ambaye alikuwa akipiga kelele na kuongea maneno asiyo yajua na wakaondoka naye. Kwa hali aliyokuwa nayo Irene haikuwa rahisi kurejea nyumbani hivyo alilazimika kubaki hospitali kwa uangalizi wa dakitari kwa siku kadhaa, hivyo jukumu la kulea watoto sasa lilibaki mikononi mwa Teddy.


Taarifa za kuugua kwa Irene hazikukawia maana zilivuma kwa kasi watu wengi walikuja kumtembelea hospitali karibu kila siku alipokea makumi ya watu wakija kumjulia hali, na baada ya siku mbili mama mke wake ambaye ni mama Tom sasa alikuwa yuko nyumbani kwa Irene baada ya kuwasiri muda mfupi kwa ndege akiongozana na mwanae kipenzi Luckas, ni mulango wa chumba cha wodi aliyolazwa irene anawaona wageni wawili waliokuja kumjuli hali ni mama mkwe wake kipenzi na shemeji yake. Irene aliwapokea kwa furaha maana sasa hali yake ilikuwa afadhari kidogo aliketi na kumuita mhudumu alipokuja alimuagiza asipokee wageni tena kwani yuko na mtu mhimu sana ambaye ni mama mkwe wake. Mama alitanguliza hongera kwa mkwewe kwa kumpatia wajukuu, pili alimpa pole kwa kuugua na tatu mama alikuwa akilia kwa uchungu akilaani tabia za mwanae Thomas za kutoshikika “huwa najiuliza hii laana aliitoa wapi? …. Ni mtu gani huyu asiye bebwa akabe beka?.. mama achana na huyo shetani atakusababishia matatizo na ukashindwa kulea watoto wako kwa amani kumbuka kwa sasa hajulikani yuko wapi ? na anafanya nini, tafadhali mama yangu wewe ndiye baba na wewe ndiye mama wa hawa wanao, kuwa makini nahii familia………… piga konde moyo najua una mapenzi ya dhati lakini kumbuka si kila kitu kimeandikwa ndiyo kuna vingine hata ukifuta kwa msasa bado neno hapana litaonekana Tom ni miongoni mwa viumbe visivyo badilika katika dunia hii, ni mwanangu ila kwa dalili hizi naogopa kusema hafai ila nafsi inanilazimu kusema kuwa Thomasi siyo mtu mwema kwako ni muuaji” mama alimaliza huku akimfuta machozi Irene.

Nyumbani kwa Irene, Irene alikuwa nyumbani karuhusiwa kutoka hospitali na sasa wako na mama Thomasi (mama mkwe wake) kipenzi walikuwa wakizungumza Irene alisema katu hawezi kuacha kumtunza mama huyo maana kwa sasa ni kama rafiki yake hivyo atamthamini na kuilinda familia hiyo mpaka mwisho wa uhai wake, “nashukuru sana unavyonijali mama yangu Toka nimetambulishwa kwako najiona kama wazazi wangu wamefufuka, unanijali na kuonesha mapenzi ya dhati kwangu, ulikuwa katika hali duni lakini hukujali hali yako bali ulijali mimi na mwanao tunaamkaje na tunaishi je, sina ndugu Mama yangu wewe ndiye ukoo wangu, ninyi ndiyo familia yangu upande wa baba na mama yangu. Nakupenda sana mama ayangu … yanayotokea acha ayatokee ila uhalisia ni kwamba kwa sasa mama Hutarudi Mwanza naomba ubaki hapa na utakaa hapa na mimi tulee hawa wajukuu zako naamini uko tayari kwa hili?” hakukuwa na mjadala zaidi kwani makubaliano yalifikiwa na mama aliamua kubaki nyumbani kwa Irene kumpa faraja na kusaidia kulea wajukuu wake vipenzi.

*****************************************************


Sudani ya kusini mji mkuu wa juba Tom anapokelewa na vijana wawili waliojitambulisha kwa majina kama ifuatavyo wakwanza aliitwa Burhan Nasri na wapili alijulikana kama Mohamed Swalehe, wanampokea tom aliyejulikana kwa jina la Said Omary kama maelekezo ya hati yake ya kusafiria yalivyomtaka kufanya, walitembea umbali kidogo kutoka mji mkuu wa Juba wakaishia kwenye nyumba moja ya udogo iliyo kuwa pembezoni mwa barabara burhani aliegesha gari walilokuwa wakilitumia aina ya Nisan Murano na kuufata mulango wa jengo hilo la jumba bovubovu waliingia baada ya kufika ndani hakukuwa na matumaini ya kuishi mtu hali ambayo ilimshitua kidogo Said (Tom) wenzake hawakujali Mohamed alikuwa akihangaika kuwasha sigara wakati huo Burhan alikuwa akifungua mulango uliowaelekeza kwenda chini walitembea umbali kama wa mita 100 chini ya aridhi huko ndiko walikutana na geti walipolifungua kulikuwa na nyumba nzuri iliyopambwa vizuri, ni nyumba ya chini ya ardhi, Burhani alimkaribisha Tom “sayeed welcome home bro………………. na mimi ni mtanzania pia but kwa sasa naishi hapa kwa zaidi ya miaka saba. Usishangae kuiona nyumba chini ya aridhi kiuhalisia haya ndiyo maisha ya Juba kutokana na vita watu wengi hasa matajiri waliamua kubadili mfumo wa ujenzi na kutumia mfumo wa chini kwa chini maana karibu kila siku nyumba zilibomolewa na watu kuuwawa kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea hapa” . Baada ya kukaribishwa Tom sasa anajulikana kama Said Omary mtihani wake ilikuwa ni kujifunza kiarabu hivyo hakupaswa kusubili zoezi lilianza mara moja kwa kukabidhiwa vifaa vya kujifunzia kama vile kanda za video, sauti, vitabu vyenye tafsiri nyepesi, walimu walipishana kama upepo. Baada ya miezi mitatu alikua kaanza kuimudu Lugha hiyo, juhudi ziliongezwa na kuwekewa mkazo wa kutotumia Lugha nyingine tofauti na Kiarabu. Alilazimika kujichanganya na kufanya mazoezi kwa tahadhari alifanya hivyo taratibu na mwisho aliimudu kabisa Lugha ya kiarabu baada ya miezi sita. Si kitu haba ulikuwa ni muda mrefu sana kwa Tom kwani alikuwa mwepesi katika matamshi bila shaka alikuwa ameimudu lugha sawa sawa.


Baada ya kuwa mmahili katika Lugha Side anakutanishwa na wafanya biashara wa dawa za kulevya na siraha, alioneshwa kila mmoja na kufahamiana nao, utambulisho ulienda sambamba na angalizo juu ya kutokumuamini mtu yeyote ukizembea kifo kitakukuta, utambulisho ulichukua siku kama tatu, za mizunguko kutoka kwa tajiri mmoja kwenda kwa mwingine, Said alikutana na watu hawa na kufahamiana nao kwa utambulisho wa mwanzo Tomalielezwa kifo au kuuwa ni swala la kawaida hapa hivyo usishituke. Biashara ilikuwa ni kubadilishana bidhaa na fedha au bidhaa kwa bidhaa, dola za kimalekani diyo fedha iliyotawala katika mabadilishano ya biashara hiyo Said, Burhan na Mohamed ni timu ya watu watatu waliotakiwa kufanya biashara hiyo hatari na vikundi vingine biashara iliyojaa ubabe,dhuruma, ubabe, utaperi na unyang’anyi wa nguvu.


Katikati ya mji wa juba kwenye nyumba moja ya kifahari Said na wenzake wanaingia na mzigo uliokuwa kwenye Bagi wanafika ndani na kuushusha mezani mbele ya jamaa mmoja wa makamo aliyekuwa kaketi karibu na meza hiyo huku akivuta sigara kubwa (sigger) , baada ya ukaguzi wa mali anaridhika na kutoa ishara ya mabadilishano ya mizigo Burhan anaukagua mzigo anaonekana kutoridhika anapiga hatua nyuma na kuzungumza na Mohamedi lakini Said hakushirikishwa. Ghafla Burhani analifuata begi lao lililokuwa mikononi mwa mmoja wa mabaunsa katika nyumba ile. Ghafla silaha zilifunguliwa na kuelekezwa kwenye kichwa cha Burhan, Said alishituka na kukimbilia kiunoni ili ashike bastora yake lakini ishara iliyotolewa na Mohamed ikasidia kumzuia na kusubiri kuona nini kinafauata.


Ni takribani dakika mbili zilipita bila mwafaka na dalili zilionesha kuwa ni dhuruma ndiyo ilitakiwa kutendeka eneo hilo, Mohamed alihoji “Sultan kuna tatizo gani? Hii ni biashara umeridhika na mzigo Toa pesa hujaridhika rudisha mzigo na ndivyoilivyo kwetu, tafadhari rudisha mzigo maana hatujaridhika na fedha uliyotoa” kiongozi wa vijana wale alikiegemea vyema kiti chake “oooh! Nimetoa pesa kulingana na thamani ya mzigo wenu so sizani kama kuna haja ya kuhoji…. Kwa kifupi vijana mko kwenye himaya yangu mtake mstake mtaniuzia mzigo kwa gharama hiyo maana Jimmy kanidhurum pesa zangu nyingi hivyo kwa mtindo huohuo aliokuwa akifanya kwasasa namimi nitafanya hivyo kama yeye alivyofanya… nibora mkapokea hiki kuliko kwenda mikono mitupu” alimaliza kujibu huku akiwatizama usoni na kuisogeza sigara yake kinywani huku akipiga funda la moshi alilolipliza vyema usoni kwa Said. Mohamed kwa wakati huu alikuwa na wasi wasi na uwezo wa Said wa kupambana na wakati huo Burhan alikuwa chini ya ulizi. Wakati mohamedi akiwaza hayo Said alikuwa akisubiri rukhusa ya kushambulia tu, maana alikuwa tayari kwa chochote maana hekaheka kama hizi sasa ni sehemu ya maisha yake. Ulikuwa ni mchezo wa dakika moja tu bada ya Mohamedi kuchomoa bastora kabla hata hajaitumia alishangaa vijana wane wakiwa chini huku yeye akiwa haja kukua hatua yoyote na wa mwisho anashushwa na Burhan bastora iliyofanya kazi hiyo ya haraka sasa ilikuwa kichani kwa kiongozi wa kundi hilo ni kazi ya Tom (Said). Kila mmoja alibaki midomo wazi kutokana na uwezo wa haraka aliokuwa nao Saidi katika mapambano . Walimkagua na kumnyang’anya siraha aliyokuwa nayo kisha wakamuacha na maiti zake huku wakitokomea na dawa za kulevya walizokuja nazo pamoja na fedha na kumuacha hana kitu.


Maisha ya kikosi hiki cha watu watatu kilikuwa ni hatari, kazi yao ni mabadilishano ya bidhaa kama vile madini, siraha, madawa ya kulevya na fedha ni biashara iliyotawaliwa na ubabe wa kila upande, ushupavu na uharaka wa kupambana aliokuwa nao Said ulifanya vijana hawa wajiamini na sasa walikuwa na uwezo wa kufanya chochote na popote iwe serikalini na hata eneo lolote lenye ulinzi wa hali ya juu. Hadithi katika vyombo vya habari ni vifo kila kukicha maana hawa jamaa walikuwa hawajaribiwi walikuwa na uwezo wakusambaratisha kundi la watu 10 ndani ya dakika moja na asipone hata mmoja . Habari zilizagaa kwa kila mfanya biashara wa dawa za kulevya na waingizaji wa siraha nchini humo, mbali na kupeana tahadhali wafanya biashara hao walikuwa pia wanajaribu kuandaa mtego utakao wanasa vijana hawa. Kuwanasa hakikuwa kitu rahisi, ilikuwa ni marufuku kwao mtu mmoja kutoka peke yake, ni marufuku mmoja kujichanganya na wengine wakawa mabali kidogo, haikuruhusiwi kuwa na mahusiano na mwanamke yeyote. Utaratibu huu uliwasaidia sana vijana hawa kukamilisha kila shughuli zao kwa wakati na kurudisha faida kwa tajiri yao bila kuingiza hasara. Jimmy Radi mmiliki na mwanzilishi wa kundi hili alikuwa akizipata habari kutoka kwa rafiki zake na wafanya biashara wenzake, wengine wakilaumu na wengine kumpongeza juu ya shughuli ya vijana wake. Said na wenzake walitekeleza mauaji ya kinyama kwa kila waliyeelekezwa kumfanyia hivyo na kwa kila mtu waliyegundua hakuwa mwema kwao. Mtu yeyote waliyefanya nae kazi na wakagundua ni msaliti mikono yao haikurudi nyuma kuhakikisha maisha yake yanafika mwisho.


Mauaji ya mwasiasa ambaye pia alikuwa mfanyabiashara wa mafuta na uingizaji wa siraha chini Sudan ya kusini, mauaji haya yalitokea kimakosa kutokana na shambulizi la kumuua mtu aliyekuwa amelengwakuuwawa na vijana hawa kwa dhuruma za kibiashara, mtu huyo kuwa pamoja na mbunge huyo maarufu wa Juba kwenye gari iliyoshambuliwa na wote wanakufa lakini kusudio lilimlenga huyo mmiriki wa gari aliyeuwawa pamoja na mbunge ni Husein Monga ndiye mbunge aliyeuwawa, mfanyabiashara aliyekuwa amelengwa kuuwawa ni Dhahiri Yasin . Serikali inalivalia njuga swala la kuwasaka waharifu hawa kwa nguvu zote, haikuwa kazi rahisi maana waliokuwa wakitafutwa walikuwa ni watu makini kupita kiasi, njia zote zilikuwa zimefungwa Mohamed na Buruhani ndio waliotajwa kwenye vyombo vya habari huku kila taarifa ikihitimisha wa mwenzao ambaye hajafahamika. Kila kituo charadio, Tv na magazeti vyote vilitangaza kusakwa kwa waharifu hawa raia wa Sudani, vikosi vya serikali vilikuwa vikitoa taarifa mbalimbali kuhusu maendeleo ya msako wao, ikiwemo uvamizi wao wa nyumba waliyokuwa wakiishi na kumkamata msichana mmoja aliyekuwa akiwasaidia kazi za nyumbani, nyumbani hapo kisha kulichukua gari walilokuwa wakilitumia na siraha mbalimbali za kivita walizozikuta eneo hilo. Ni mchezo hatari na wakishetani waliokuwa wakiufanya vijana hawa, kila bango la matangazo liliandikwa kwa maandishi makubwa yaliyo kolenzwa WANTED (ikimaanisha wanatafutwa), hali hiyo iliwatia hofu sana. Waliamua kumtafuta Jimmy Radi na kumueleza kilichotokea, Radi alishituka maana hakuwa na Taarifa hivyo ilimbidi kutuliza akili kwanza na baadae alipowapigia simu alikuwa kapata jibu sahihi, Jimmy aliwambia wasambae, “hamfai kukaa katika kundi tena vijana wangu hali imechafuka maana taarifa zimefika mpaka BBC na CNN hivyo kuweni makini, maana mtakamatwa kizembe hivyo tawanyikeni kila mmoja njia yake” Said baada ya kuishusha simu toka sikioni anageuka upande wa pili anakutana na heka heka za polisi wakija kwa kasi. Bila shaka kuna mtu kawaelekeza tulipo, uchochoro haukuwa na njia mbadala, walitizamana na kuulizana tunafanyaje Burhani aliingiza mkono wake kiunoni na kuchomoa bastora, jibu lilikuwa kila mtu ataponywa na juhudi zake. Polisi wanazingira eneo lile na kuwaweka kati kati vijana hawa watatu, Amri ya kutoka walipokuwa wamejificha ilitolewa na hakuna aliye itii kwa muda wa dakika 15 polisi waliamua kulivamia eneo walilokuwepo Said na Wenzake.


Mashambulizi ya polisi hayakuwa na macho walipiga risasi hovyo eneo hilo bado lilikuwa kimya, ni mashambulizi kama ya dakika 5 hivi bila majibu, polisi walisitisha na kutaka kujua kama kweli bado kuna watu eneo hilo, na hilo ndilo likawa nikosa kubwa ambalo hawata lisahau. Dakika saba zilitosha kuwateketeza asikali polisi na kumbakiza asikali mmoja kati ya 12 waliokuwa eneo hilo. Pamoja na kusalimika kwake alinyang’anywa siraha na pia aliwasaidia sare za polisi na gari la kutorokea hukua akiachwa mtupu pingu miguuni na mikononi na gundi kwenye mdomo wake kuzuia asipige kelele. Haikuchukua muda habari za kuuwawa kwa asikali 11 zilienea kila kona ya dunia huku wazili wa ulinzi wa nchi hiyo akikili wazi “hawa watu ni hatari sana, naweza kusema wanamafunzo mazuri hivyo tunahitaji kuimarisha ulinzi na naamini hawataukwepa mkono wa dora, leo niko kwenye mazungumzo na mkuu wa majeshi nazani sasa oporesheni hii ya kuwasaka nibora ikaendeshwa na Jeshi la wananchi na siyo polisi tena, poleni sana watu wa Sudani kusini na poleni sana familia zilizopoteza” maneno hayo yaliyosemwa kwa Lugha ya kiingereza yaliwafikia vizuri sana Burhani na wenzake kupitia Radio iliyokuwa ndani ya gari la polisi.


Baada ya kutembea kwa umbali kama wa kilometa ishirini waliona mbele kulikuwa na kizuizi ghafla kilichowekwa na wanajeshi, walikuwa na gari la polisi, ghafla ubishi ukaanza ndani ya gari, Said anakataa kabisa wasipite eneo hilo lakini Burhani analazimisha huku akionya kuwa tayari wameesha onekana na wakigeuza gari tu ujue wamefahamika. Baada ya mzozo wa kama dakika moja walikuwa wamekaribia sana eneo lile, sasa kila mmoja mkono ulikaa tayari bastora ilipo na kukaa tayari kwa lolote, kila mmoja alianza kusali kwa dini yake na maneno yake mpaka wanalifikia lile eneo kila mtu alikuwa kalowa jasho. Walipaki gari kwa kujitoa mhanga, taratibu mwanajeshi mmoja alikuja kuwasalimia na kuwahoji, Buruhani alimweleza bila kumung’unya maneno kuwa wako patro haikuwa rahisi kwa wanajeshi kujua maana wao wameshitukizwa kwenye hii oparasheni hivyo aliamini kila alicho ambiwa. Waliruhusiwa kuondoka haraka haraka Burhani alikanyaga mafuta na kuondoka huku wakishindwa kuamini kilichotokea, lakini baada ya kuondoka askari mmoja wa jeshi anashituka na kuwambia wenzake namba za hili gari walilopita nalo hawa jamaa ni namba tulizotumiwa hapa kuwa tulikamate ni gari la polisi lililoibiwa. Hawa kupoteza hata sekunde walikuwa tayari wamejaa ndani ya magari yao na walianza kulifatilia gari hilo la polisi. Mwendo waliokuja nao haukuwa wa kawaida unamshitua Burhani aliongeza mwendo ikawa ni mtafutano barabarani, ni kasi ya ajabu, hakuna aliyekubari kushindwa na hatimaye inafika mahara Burhani na wenzake wanazidiwa baada ya dreva wao kubabatizwa risasi ya mkono wakati akiendesha anapiga kona na kuingia kwenye jengo moja la hoteli. Mule ndani wanashuka kwa haraka lakini Burhani alikuwa kaumia hivyo alikutana na risasi nyingine ya kifua, akaaunga chini na hakuweza kuamka tena. Said na Mohamed ndani ya jingo la hoteli pamoja na kukimbia sana lakini jingo lilikuwa limeesha zingingirwa kote, lakini hali ilikuwa mbaya kwao kwani mashambulizi yalivyokuwa yakifanywa na wanajeshi yalikuwa ni hatari zaidi. Wanafanikiwa kijichanganya na kundi la watu ili watoke nao Mohamed anapiga risasi juu watu wanakimbizana wao wakiwa katikati wakijaribu kutoroka. Bahati mbaya Mohamed alikuwa anafahamika maana pivha yake ilienea kila mahali hivyo walimuona haraka na kumjuza mdunguaji aliyekuwa eneo la jilani alipewa maelekezo na mwanajeshi mmoja aliyekuwa kitengo cha mawasiliano ilikuwa ni rahisi kumtambua maana alivaa sare za jeshi la polisi, ilikuwa rahisi kwa mdunguaji kumuona na haikuchukua hata sekunde moja baada ya mdunguaji kumuona Mohamed kwenye dira yakena Mohamedi alikuwa chini Huku Said akilowa kwa damu iliyomwagika kutoka kwa Mohamedi na kushindwa kujua ni nini kimetokea.


Akionekana mwenye kukata tamaa watu wote wanasambaa na Saidi (Tom) anabaki kapigwa na bumbuwazi aliamini kuwa siku yake ya mwisho imetimia, akiwa kasimama palepale bila hata kupiga hatua akikisubiri kifo wanajeshi walikuja wakamzunguka huku wengine wakiichukua maiti ya Mohamed na kuiweka kwenye gari.

Je, huu utakuwa ni mwisho wa Tom? Ngoja tuone nini kitafuata? 



Irene sasa alikuwa yuko poa na leo anaona ni vyema akaendelea na biashara yake ya duka, mbali na kuwa na biashara zingine zilizomuingizia kipato lakini aliona ni bora pia duka liendelee maana alikuwa ameanza kuwapoteza baadhi ya wateja wake. Akiwa dukani akisaidiana na Teddy siku hiyo waliamua kufanya usafi kila kona ya duka hilo kuanzia stoo mpaka kwenye chumba cha duka. Haikuwa kazi ndogo lakini wanafanikiwa kumaliza na kuviweka vitu sawa. Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya kuanza kazi rasmi basi Irene anaamkia dukani kwake na kuanza shughuli mara moja. Wateja walimiminika walipata huduma zao kwa furaha, huku wengine wakiuliza maswali yaliyomuumiza moyo Irene kuna wateja waliuliza Tom alikwenda wapi mbona haonekani , wengine waliuliza au alikuuzia duka akahama mji? Ni maswali ya watu amabao hawakuujua mchezo hivyo mbali na kuuma lakini yalimpa faraja Irene kuwa Tom wake alikuwa ni kipenzi cha wateja, siku ilikwenda vizuri sana maana mauzo yalimtia moyo na kutoa faraja hivyo hakufa moyo. Huku akijiwazia kimoyo moyo “hivi Tom asingeondoka dukani tungekuwa wapi leo kibiasahara?’” ni swali lisiro na majibu Irene anafunga duka majira ya jioni na kurejea nyumbani kwake.


Anaonekana mwenye furaha nyumbani kwake yeye na familia yake, anaongea na watoto wake akiamini wanamsikia kwa furaha kabisa Irene alisema. “ nawapenda sana wanangu nawapenda sana, hakuna kitu kinanipa faraja maishani kama ninyi wanangu, kumbukeni nyie ni faraja pekee niliyoachiwa na baba yenu kipenzi baada ya kunikimbia, nampenda sana baba yenu sizani kaama nimewahi kupenda hivi katika ulimwengu huu najua Thomas ni mtu mwema tatizo ni ujana, tamaa za maisha na mafanikio ya haraka …. Atarudi baba yaenu …atarudi.. Ombi langu mimi mama yenu mkawe watoto wema msiwe viruka njia msiobebeka katika ulimwengu huu mtaishia pabaya, nawapenda sana wanangu wapendwa” bada ya kuwaeleza hayo aliwabusu kwenye mapaji ya uso kisha akawafunila shuka lao na kuwaacha walale huku akiwatizama kwa uso wa furaha nyuso zao na nywele nyeusi zilimvutia sana Irene akajisemea “hii siyo kopy baby bali uliskani” akimaanisha jinsi watoto walivyofanana na baba yao basi hakupiga kopi ila alisikani.


Kwenye meza ya chakula usiku Irene anazungumza na mama mkwe wake, wanazungumza mambo mengi wakishauriana marafiki hawa ambao sasa walifanana kitabia. Siku hiyo mazungumzo yalijikita zaidi kuhusu familia ya Tom, Irene alitamani sana familia hiyo aitoe sengerema na kuja kuishi nayo jijini Dar es salaam, ombi hilo lilikuwa zuri ila mama hakulilizia hata kidogo kwani aliyajua madhara yake ni kumbebesha mzigo Irene ambaye hata kwa sasa bado ana mzingo mzito. Mama alisema anawatoto wengi kila mtoto anatabia yake hivyo kukaa hapa wote utakuwa ni mzigo ambao hutauweza mama, aliendelea kuonya kwa kusema anazijua hulka za vijana wanatabia tofauti za kuiga na zingine hujitengenezea wenyewe, “usiwaamini sana hawa shemeji zako maana hatujui kesho yao nikiwepo hivi wanakupenda maana huwa nawakumbusha ulikowatoa, lakini wakifika hapa na tamaa zikawaingia iposiku sitakuwepo wataanza kukuwazia mabaya. Kuwa makini mwanangu najua unawapenda ndugu wa mmeo ila kwa hili mwanangu nisamehe, ni watoto wangu ila kwa hili sirikubali waache wahangaike kivyao atakaepata akili msaidie ajisaidie atakaeshindwa basi atakuwa kama kaka yao Thomas. Wakati huo wote Irene alikuwa kimya akiyapima maneno ya mama mkwe na inaonesha yalimwingia haswaa.


Mama aliendelea “niliolewa na babamkwe wako nikiwa mdogo sana miaka 18 tu na nilianza kuzaa nikiwa na miaka 19. Tulipendana sana na mme wangu, tuliwapenda sana ndugu wa pande zote mbili mme wangu aliwapenda sana kaka na dada zangu wa ndani ya familia lakini hata ndugu wa karibu na mimi pia nilifanya hivyo kwa ndugu zake wote. Tuliishi maisha ya furaha sana tulisaidia kila lililowezekana kuhakikisha tunaonekana watu wema katika maisha. Nilihakikisha kila ndugu anatoka na sifa bora atakazo zipeleka huko aendako tulifanya hivyo tukijua tunawajali ndugu kumbe, tuligeuzwa daraja la watu kurahisisha shida zao. Basi ikawa kila ndugu akipata shida kimbilio nyumbani kwangu, wengine walihamishia makazi na familia zoa wakaja kukaa nyumbani kwangu, basi nikawa mulezi wa familia za wenzangu, wengine walikuwa wakikumbuka kula kuku tu! waanafunga safari kuja nyumbani kwangu. Mama sikutaka kujishusha basi maisha yakaenda hivyo, namsifu mme wangu alikuwa na roho ya uvumilivu na alikuwa mchapa kazi alijituma usiku na mchana hatukuteteleka kiuchumi maana mme wangu alikuwa mbunifu kila kukicha alibuni mbinu mpya ya kumpatia kipato na mimi nikiwa mshauri bora kabisa mungu alituona na kutusimamia. Ni kuugua ghafla kwa mme wangu kulikomfanya asiwe na uwezo tena wa kufanya kazi ndo chanzo. Akiwa hospitali mzozo wa mali ulianza wakiamini hata pona, waligawana kila kitu wakauza mpaka nyumba huku mali zingine zikigawanwa utafikri zao. Wema wangu wote unaonekana siyo kitu mbele zao, wema wa mme wangu unaonekana hauna maana mbele zao. Basi familia yangu inageuka adui kwa wote, nikawa wakupanga kwenye nyumba za watu, nafukuzwa napanga nafukuzwa, mpaka mme wangu alipotoka hospital bada ya miaka miwili maisha ya mjini yalikuwa magumu familia ilikuwa kubwa hivyo aliamua turudi kijijini tutoke mjini ndo tukaenda kujificha huko Lushamba sengerema. Na mpaka baba yenu anafariki sizani kama kuna ndugu anajua ndugu yao alipozikwa pamoja na kuwa nataarifa za kifo chake ingawa wengine ndo hao uliwaona siku Thom amekuja kukutambulisha pale nyumbani shida yao ni pesa tu” Irene anashusha pumzi …” unamaanisha mama hayo maisha niliyoyakuta kule nyumbani hamkuwa mnaishi hivyo toka awali?” lilikuwa ni swali liliulizwa na irene “haswaaa” mama alijibu bila wasiwasi. Irene aliliona ni kama swali kwa upande wake ila lilikuwa jibu kwa upande wa mama Thomas. Tafakari ilichukua muda na ukimya ukatawala huku wakitizamana usoni mwisho mama ananyanyuka na kumshika bega Irene huku akimtakia usiku mwema. Ni mtihani ni hadithi ya kusisimua, inauma na inafunza …… sikumbuki Irene alitumia masaa mangapi kuyawaza yaliyozungumzwa na mama mkwe wake ila ninacho kikumbuka ni Teddy ndiye aliyemwamsha pale sebleni majira ya saa tisa usiku kwani watoto walikuwa wakilia. Irene anakurupuka na kwenda kuwahudumia wanawe waliokuwa na njaa usiku huo na kuwapa huduma kama ya kuwabadilishia nguo zilizokuwa zimelowa mkojo. Bada ya zoezi hilo analala mpaka asubuhi


Akiwa na furaha dukani kwake Irene anahudumia wateja wa kila aina huku akiachia Tabasamu mwanana, “dada tafadhali huyu kaka mwenye hili duka kaenda wapi?” ni sauti iliyosikika vyema masikioni mwa Irene. “hayupo kasafiri ni muda mrefu yuko nje ya nchi” Irene alijibu kwa upole bila kumwangalia aliyekuwa akiuliza. Yule dada hakuishia hapo “na wewe ni kama nani humu dukani?” Yule dada alihoji “mkewe” na mara hii hili swali lilimlazimu amjue anae muuliza hapo ndipo walikutana uso kwa uso Love (Mtoto wa Kigogo) na Irene, ghafla Irene anavuta kumbukumbu huyu dada sura yake siyo ngeni alipotafakari zaidi anagundua amewahi kuona picha zake kwenye simu ya Tom. Alikuwa amehisi kuna kitu lakini hakutaka kujishughulisha nacho alimhoji kwa wema … “vipi dada nikusaidie chochote?” Love alijibu kwa nyodo huku akiondoka “hapana mke mwenza nilitaka kujua tu kama na wewe unajua kuwa mmewetu yuko nje ya nchi nilijua hajakujuza ahsante byeeee!” Love aliondoka na kuingia kwenye gari lake la kifahari akaketi na kumwangalia Irene aliyekuwa kaduwaa kwa hasra alimcheka na kutekenya ufunguo akaondoka. Hasra zilimpanda Irene anaamua kuchukua funguo za gari ili amfute Love.

*********************************************************************


Wanajeshi wenye siraha nzito walikuwa wamemzunguka na kumuweka kati, Said (Tom) alikuwa kakata tamaa kabisa ya kuishi kwani alijua hawezi pona na hata akipona basi maisha yake yote yaliyosalia angeyaishi ngerezani huko Sudani ya kusini. Katika mizunguko yao yote pale hakuna aliyemjali Tom amri ya kusambaa kufanya msako ndani ya jengo ili wamkamate mtuhumiwa wa tatu baada ya wale wawili kuuwawa amri hiyo iliambatana na amri nyingine iliyoagiza ni lazima akipatikana auwawe. Tom analowa kwa jasho lililo changanyika na baridi kali, tumbo la kuhara lilimshuka ghafla na kujikuta alilowanisha nguo, hakua na chakusema wala kujitetea maana alikuwa ndani ya mdomo wa simba na kuchoropoka hapo haikuwa kazi rahisi. Ni kamanda wa kikosi kilichokuwa eneo lile alisogea na kumtazama Tom, anamshika bega na kuuliza “unajisikiaje...” Tom huku akitetemeka midomo anajaribu kujibu lakini ulimi unakuwa mzito kama umebandikwa kwa gundi ya mbao. Kamanda hakumjali aliendelea na shughuli zake, vikosi vya jeshi vilizidi kuongezeka eneo lile wakiendesha msako wa nguvu hata katika maeneo Tofauti ni Tom na baadhi ya watu walioumia na kujeruhiwa wakati wa mapambano ndiyo walikuwa wamebaki eneo lile. Kuongezeka kwa vikosi vya kijeshi kulizidi kumtia hofu Tom. Kichwa cha Tom ungekifungua sizani kama ungepata jibu sahihi ni nini alikuwa akikiwaza kwa wakati huo, mambo yalikuwa mengi kuliko uwezo wa kawaida wa kufikili. Kutokana na kuchafua hali ya hewa ya eneo hilo watoa huduma wa kijeshi wanamchukua Tom na kumpeleka kwenye gari ya kubebea wagonjwa wanambadilishia nguo na kumpa zingine, kisha akafanyiwa ukaguzi wa kitabibu kama kaumia, waligundua hajaumia, walimpa chakula na kumpa muda wa kupumzika na baadae kumwachia huru.


Haikuwa kazi rahisi, haukuwa mtihani mdogo kwani Tom haamini ni nini kimemtokea aligeuka kila kona huku asiyaamini macho yake, aliwaza sana imekuwaje ameachiwa huru? Jibu hakulipata ila alikumbuka na kukili wazi kuwa mungu yuko pamoja naye, Tom alikuwa akitembea huku akiongea peke yake, marakadhaa aliapa kwa jina la mungu katu hatorudia hiyo kazi, alijuta na kujuta huku akihoji ni shetani gani aliyemtuma kufanya hiyo kazi. Pamoja na kuwakumbuka wenzake waliouwawa lakini haikumuuma sana kama ambavyo aliumia yeyekunusurika kifo akiwa mikononi mwa wanajeshi ambao hawakuwa hata na chembe ya huruma. Alikuwa anatemebea mikono kichwani kama mwehu, mara aitandaze na kusimama kama anaongea na mtu hakuwa sawa. Anafika sehemu anaketi chini ya mti anajaribu kufikilia lakini kiuharisia Tom alikuwa haamini kama kapona kweli. Kwakuwa ilikuwa joini sasa analazimika kwenda hoteli moja analipia chumba cha faragha na anatoa maagizo kwa wahudumu hakuna mtu yeyote ataruhusiwa kuja kumuona. Tom anaingia na kupumzika hakukumbuka chakula wala kinywaji. Na baada ya kuusotea sana usingizi hatimaye Tom anabahatika kuupata usingizi baada ya kuusotea kwa muda mrefu, alilala usingizi wa pono. Mpaka kesho yake kunakucha majira ya saa 12 asubuhi. Baada ya kuamka Tom anawasha Tv na kuingia bafuni lakini kipindi anarudi anakuta tarifa ya kuuwawa kwa watu waliotajwa kama magaidi wawili na mmoja ametoroka baada ya kuachiwa na Maasikari wa jeshi wakizani ni raia mwema kutokana na wao kukosa taarifa za picha za awali za kuwatambulisha mtu huyo, lakini wameligundua hili baada ya kuona picha ya vijana hao wote watatu baada ya kupekua taarifa walizozichukua kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi, picha ya Tom inaoneshwa akiwa kazungukwa na asikari wa jeshi na nyingine akiwa na wenzake Mohamedi na Burhan, tangazo linamalizia kwa kumtaka Tom ajisalimishe haraka au atakaye wezesha kupatikana kwake atoe taarifa haraka kitua cha polisi au wizara ya mabo ya ndani pia dau la dolla za kimarekani laki moja zitatolewa kwa atakae toa taarifa za siri. Tom anajaribu kuwaza afanye nini hapohapo mlango wake unagongwa kwa fujo hofu inapanda upya, anajaribu kulifungua dirisha na kuchungulia alikuwa chumba kilicho gorofa ya nne na jingo lilikuwa flati halina kingo kwenye madirisha, aligeuka na kuanza kutafakari lakufanya, mulangu nao ulizidi kugongwa na baada ya kuona haufunguliwi mmoja wa watu wale aliamuru zifatwe funguo za akiba mapokezi ili waje wafungue, funguo zinafuatwa huku Tom asijue lakufanya na baada ya funguo kuletwa na kuanza kuchokonolewa kwenye kitasa Tom anaamua liwalo naliwe sasa anafungua mlango kwa hiari yake na anakutana uso kwa uso na……………………………………………


……



Ni uso kwa uso na mhudumu wa hoteli akiongozana na meneja, Tom akiwa na wasiwasi makubwa moyoni ….”aaah! samahani bwana Said kwa kukusumbua tulikuja kukuangalia maana ukimya ulizidi toka uingie jana hujatoka kwenda kula na hata kuagiza chakula tulikuwa na hofu pengine umepatwa na jambo baya” meneja alieleza dhumni lao la kuja kumgongea Tom majira yale ya asubuhi. Tom alikuwa bado kajawa na hofu hakuwa anayaamini maneno ya meneja aliangaza huku na kule kutaka kujua kama wameongozana na polisi lakini hakufanikiwa kuwaona. “hapana niko salama ila nilikuwa nimechoka tu kwa sasa namshukuru mungu niko sawa” Tom alijibu kwa hofu huku akiona aibu hata kuwatizama usoni watu wale. Basi meneja na mhudumu waliondoka na kurudi zao kwenye shughuli zao za kila siku. Ndani palikua hapakaliki Tom anatembea huku na kule akijaribu kuiweka sawa akri yake lakini anashindwa maana alihisi amewekewa mtego ni muda wowote polisi wangefika eneo lile na kuja kumkamata basi akajiaandaa haraka haraka na akafungua mlango lakini kipindi akitoka anamuona askari polisi akiwa mapokezi, alikuwa akizungumza na mgudumu Tom alihisi pengine walikuwa wamepiga simu polisi, basi akajibanza sehemu na baadae anatafuta njia ya mlango wa nyuma nafanikiwa kutoroka.

Mtaani hakukuwa shari ni vurugu tupu kwani kila kona walitapakaa askari polisi na wanajeshi kila mmoja akiangaza huku na kule, habari kubwa mtaani ni kutafutwa kwa Tom (Said). Haikuwa kazi ndogo kuvitambua vichohcoro ili kuwakwepa polisi, lakini pamoja na kujitahidi kupita njia ngumu bado hofu haikuisha alipokuwa akikutana na watu. Bada ya kuzunguka kwa muda akitafuta njia sasa anakitafuta kituo cha mabasi lengo lake ni kufika angalau Nirobi au kampala kazi ilikuwa ngum sana maana kila sehemu kulijaa msako kituo cha mabasi alikuwa kakikaribia lakini alipofika eneo lile aliamini wazi kabisa asingeweza kuingia, pamoja na juhudi zote lakini alikosa njia hivyo aliamua kurudi kutafuta njia mbadala. Pale kidume anapokwama kwenye matatizo huumia mara mbili Tom anatembea hatua kadhaa mbele yake a namuona polisi akija anampa mgongo na kujifanya anaongea na simu. Yule asikali naye anafika na kusimama palepale alipokuwa Tom(Said) anatoa sigara yake na kuanza kuvuta, anavuta kwa muda kasha anatoa salamu kwa Tom(said), Tom hakuitikia basi Yule asikali akaendelea kuvuta sigara yake ikaisha, akanza kuchezea simu yake. Lakini akiwa pele mara simu yake ikaita, alikuwa akiongea Lugha ya kiarabu ambayo haikumpa shida Tom alisikia kila kitu, Yule asikali alikuwa akitoa taarifa kuwa kwenye eneo lao hajaonekana mtu kama huyo na wameimarisha ulinzi kwenye kituo cha mabasi kila anaeingia anasachiwa na kuhakikisha siyo mahalifu aliendelea kusema kuwa tumewashikilia baadhi ya watu kuhusiana na tukio hilo kwa leo ambao tuna mashaka nao ila usijari atapatikana na naamini hakuna atakae muacha maana amri inasema akipatikana auwawe. Tom alisikia kila kilichosemwa hofu inazidi kutanda hakuweza kuondoka maana alihisi Yule askari atamshitukia hivyo alijikaza sana ingawa hali kwa upande wake haikuwa nzuri. Ilimchukua kama daika kumi Yule asikali kuongea na simu muda amabao kwa Tom aliuona kama ni siku nzima baada ya kumaliza mazungumzo Yule askali aliondoka. Tom anapumua pumzi ndeefu na kujisemea uhimidiwe uliyejuu kwa kuendelea kuyalinda maisha yangu.


Baada ya tafakari ya muda mfupi Tom anaamua kuondoka eneo lile hukua akiamini Yule askari hakuwepo maeneo yale, lakini kwa bahati mbaya Yule asikali naye alikuwa kasahau kiberiti chake eneo lile, wanakutana uso kwa uso Yule askari anamwangalia mara mbilimbili Tom wakati wakipishana wala haikuhitajki ushahidi ni wazi kuwa huyo ndo mtu aliyekuwa akimtafuta haswaa. Haikuhitaji ujasiri tena Tom anavuta hatua chache anakunja kulia na kutoka mbio, haikupita hata dakika basi vingora vikazizima mtaa ule na msako ulianza rasm, Tom anajaribu kujiokoa kwa kadri alivyoweza mbaya zaidi askali hawakuwa na lengo la kumkamata walizamilia kuuwa hivyo kila alipoonekana alikutana na risasai za kutosha hali iliyomfanya Tom kukata tama kabisa, muda wote alikuwa akilia lakini hat roho mtakatifu sasa alikuwa amemwacha kwani yaliyokuwa yakimtokea kwa wakati huo hakuna aliye yaamini. Kwa upande wa Tom ilikuwa ni kuruka kuta na kuvamia vyumbani kwa watu huku askari wakimfuata kwanyuma, ni juhudi binafsi ndizo zilizokuwa zikimsaidia kuendelea kuwa hai mpaka muda huo. Kitu ambacho kilimshangaza Tom anaingia kwenye nyumba moja na kutokea dirishani polisi waliamini yuko ndani hibvyo wakatega bomu na kuishusha nyumba ile kwa mlipuko huku tom akiwa eneo jilani hakuamini ni kiasi gani hawa watu walikuwa wamedhamilia kumuua.


Baada ya juhudi za muda mrefu hatimaye tom anafanikiwa kujificha kwenye kidaraja kidogo na kifinyu cha maji taka Toka majira hayo wa saa sita mchana, huwezi amini alikaa mule ndani mpaka saa saba usiku sasa ahali alihisi angarau ilikuwa shwari. Anajichomoa na kuanza kutembea usiku ule kwa tahadhari. Lakini baada ya muda mfupi anabaini kuwa alikuwa ni yeye tu aliyekuwepo mtaani usiku ule zaidi ni walizi na gari za polisi zilizokuwa zimetepakaa kila mahali. Anajaribu kuikatisha mitaa kadhaa lakini kabla hajafika popote gari dogo la polisi linasimama mbele yake wanashuka haraka na kumfuata juhudi zake za kukimbia zinaishia mikononi mwa askari polisi, wanajaribu kumhoji ili wapate maelezo ya uhakika na hilo ndilo likawa kosa kwao, Tom alijipindua na kutoa kipigo kibaya sana kwa hao askali hali iliyosababisha mmoja wao kuangusha siraha anaichukua na kumuweka chini ya ulinzi mmoja wao kasha akawaamuru wale wawili kushusha siraha chini mmoja aligoma wakaanza kutambiana kwa ghazabu na mwisho Yule asikari anafyatua risasi na kusababisha kifo kwa mwenzake aliyekuwa akirumiwa kama kinga na Tom. Askali mmoja alikuwa chini lakini Yule askali hakuishia hapo anafyatua risasi tena na kumkosa Tom hali iliyosababisha Tom kumuwahi kwa risasi ya kichwa naye pia akawa yuko chini.


Tom baada ya kosa hilo kubwa nafanikiwa kutoroka tena, habari zinatapakaa usiku ule kila mahali na msako sasa unaimarishwa kila kono, kumbuka tom alikuwa kaanza siku yake ya tatu ya mapambano bila kupumzika hakujali sasa anapita njia hatari ambazo si rahisi kuzipita anakatisha kwenye sehemu zisizo na watu na hatimaye anaucha mji kwa kama umbali wa kilomita kumi ilikuwa yapata saa kumi. Alijiegesha barabarani gari la mizigo lilikuwa linapia Tom anadandia na kuzama upande wa nyuma safari alijificha katikati ya magunia, hakujua kilichokuwa kikiendele kwa siku mbili mpaka gari ilipapaki na mizigo kuanza kupakuliwa Tom anafanikiwa kuchomoka kwani ilikuwa jioni. Ananjaa ya ajabu anatoroka eneo lile kwa kuvaa sare za wafanyakazi wa eneo lile anafanikiwa kutoka. Lugha iliyokuwa ikizungumzwa eneo lile asilimia kubwa ni Luganda tom hajui anababaisha kiingereza lakini baadae anagundua wakazi wa eneo wanajaribu kuongea Kiswahili, anatafuta chakula anafnikiwa kupata ndizi na samaki. Baada ya hapo anakwenda kupumzika kwenye nyumba moja ya kulala wageni.


Usiku ulikuwa mgumu sana kwa Tom, matukio yalianza kumrudia kichwani shida zote alizozipitia aliumia sana, pamoja na kutolala kwa siku tatu lakini anakosa usingizi kabisa kwani picha zi vifo ziliutawala ubongo wake anakumbuka watu aliowauwa maana kila akikumbuka anajiona yeyey ndiye alikuwa kinara mauaji alijihisi hana roho ya ubinadamu aliumia sana lakini kubwa zaidi alijilaumu sana kwa tamaa maana tamaa zake ndizo zimesababisha haya yote. Tom sasa anajiona yuko kwenye mikono salama aliishi kampala kwa muda wa siku tatu na alianza maandalizi ya kurudi Tanzania lakini swali lilikuwa angepita njia gani maana kila mahala alikuwa anatafutwa uzuri jina lake halikufahamika ila alifahamika kwa sura , mitandao ya kijamii, magazeti na vyombombalimbali vya habari vilikuwa vikimtangaza. Asubuhihii kunakucha Tom anaaamkia kwenye mgahawa mmoja lakini kuna mzee mmoja allikuwa kaketi pembeni yake bila shaka analikumbuka tangazo la dola laki moja aliloliona kwenye mitandao siku kadhaa zilizopita anaonekana kuficha kitu ananyanyuka haraka na kuacha chakula, lakini Tom machale yalikuwa yamemcheza alimfuata hukohuko chooni haikuchukua hata dakika akagundua alikuwa akijaribu kwasiliana na polisi basi hakuwa na budi kuvunja shingo yake kwa viganja. Kasha alotoroka na sasa aliamua kutafuta usafiri wa boat kutoka Uganda kuja mwanza. Aliitafuta sehemu iliyokuwa na boat zinazokuja mwanza anafanikiwa kuipata bandali hiyo ni siku iliyofuata anazungumza na wamiliki anawalipa na safari ilitakiwa kuanza siku iliyofuta. Hivyo tom alikaa kwenye hiyo boat alkalala humo mpaka kesho yake asubuhi.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog