Search This Blog

Monday 27 March 2023

KIZUNGUMKUTI ! - 4

Simulizi : Kizungumkuti !

Sehemu Ya Nne (4)

Mara walipoingia tu mle ndani ya ile benki walikuta msongamano wa watu uliokuwa umeongezeka kidogo muda huo na kuwa mkubwa. Watu walikuwa wamepanga foleni kwenye mistari minyoofu kufuata huduma kwenye kauta kadhaa zilizokuwa na wafanyakazi wa benki waliokuwa wamependeza katika sare zao za kazi.

Ilichukua sekunde tatu tu kwa Kisu kumtambua Yusuf ambaye alikuwa amesimama nyuma ya kaunta yake, kama kawaida akiwahudumia wateja waliokuwa wamefika pale benki. Kisu alimfahamu Yusuf kwa kuwa alikuwa ameoneshwa picha zake na Jacky zilizopigwa kwa siri bila Yusuf mwenyewe kufahamu.

Kisu alipoingia hakutaka kupanga foleni, bali waliuvuka mstari wa wateja wengine waliokuwa wamepanga foleni na moja kwa moja alikwenda hadi kwenye dirisha la kaunta alipokuwa amesimama Yusuf. Wateja waliokuwa wamepanga foleni ndani ya ile benki waligeuka kumtazama Kisu na kampani yake kwa mshangao.

Yusuf alimuona Kisu na kampani yake walivyokuwa wakija pale alipokuwa amesimama na kuhisi mwili wake ulikuwa ukiishiwa nguvu, akiwaangalia kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio isivyo kawaida.

Kisu alipofika pale kaunta alisimama katikati ya kaunta, huku akikingwa huku na huku na walinzi wake Liston na Kabwe. Kabwe alikuwa ameshikilia lile begi la magurudumu.

Kisu alitoa ile hundi na kuiweka kwenye meza ya ile kaunta mbele ya Yusuf kwa kujiamini kisha aliwatupia jicho wafanyakazi wengine wa ile benki na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Wale wafanyakazi wengine katika kaunta zingine waligeuka kumtazama Kisu na kampani yake kwa makini huku dhahiri wakionekana kushindwa kuwaelewa. Hata hivyo, Kisu aliwasalimia kwa ishara ya mkono na wote wakaitikia kwa kubetua vichwa vyao huku wakiachia tabasamu la makaribisho na kisha waligeuka na kuendelea na hamsini zao.

Baadhi ya wale wafanyakazi walikuwa wakichambua taarifa za fedha kutoka kwenye nyaraka mbalimbali huku wakifanya uhakiki wa taarifa za fedha kwenye kompyuta zao. Wengine walikuwa wakisaini hundi mbalimbali, wakipokea na kutoa fedha taslimu kwa wateja waliokuwa wamefika pale benki kwa ajili ya kutoa au kuweka fedha zao.

Yusuf aliichukua ile hundi na kuitazama kwa makini, alionekana kushtushwa sana akiwa haamini macho yake. Alizitazama zile saini kwenye ile hundi na kushindwa kutofautisha saini halali na bandia.

Akiwa bado kwenye mshangao ule alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuwataka radhi wateja wengine ili awatoe kwanza kina Kisu. Alimtazama Kisu mara moja na kugonga mhuri kwenye ile hundi, kisha alitia saini yake.

Mambo yote yalikwenda chap chap kwani Yusuf alimaliza haraka kuingiza taarifa za kibenki kwenye kompyuta yake na bila kupoteza muda alikwenda ofisini kwa meneja wa tawi na baada ya taratibu zote kukamilika alitoka na kuwaeleza kina Kisu wamfuate kwenye chumba maalumu, ambacho waliingia na lile begi ili kwenda kuchukua fedha.

Iliwachukua takriban dakika ishirini kumaliza na baadaye walitoka mle chumbani, wakaanza kuzitupa hatua zao kikakamavu lakini kwa utulivu wakiliacha lile eneo la kaunta. Wateja waliokuwa mle ndani ya benki walibaki wameduwaa huku macho yao yakiwasindikiza kina Kisu hadi pale walipopotea kabisa mbele ya macho yao.

Walipotoka nje, haraka waliingia ndani ya lile gari lao lililokuwa nje ya jengo la benki likiunguruma taratibu kwa kuwa lilikuwa halijazimwa injini.

Carlos aliyekuwa nyuma ya usukani ndani ya lile gari aina ya Ford Transit aliliondoa lile gari kwa mwendo wa kasi mara tu watu wote walipoingia ndani ya gari na kufunga milango. Magurudumu ya gari yalisugua lami na hivyo cheche ndogo za moto zilitokea wakati gari lile lilipokuwa likiingia kwenye barabara ya Lumumba na kutokomea.

Mbele kidogo lilikata kona na kuingia mtaa wa Mkunguni kwa mwendo wa kasi, na wakati likiingia katika mtaa wa Mkunguni, gari jingine aina ya Range Rover SV Autobiography LWB la rangi nyeusi lililokuwa linatokea Barabara ya Morogoro lilifika katika lile jengo la ile Benki ya Biashara na kuegeshwa pale pale lilipotoka gari aina ya Ford Transit.

Ndani ya lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB lililofika pale benki kulikuwa na watu watatu, dereva mtu mzima aliyekuwa amevaa shati la draft la mikono mirefu, na kwenye siti ya mbele ya abiria alikuwa ameketi mwanamume mmoja mrefu chotara wa Kigiriki, Nassos Chatzopoulos na katika siti ya nyuma aliketi mwanamume mwingine wa Kiafrika aliyeitwa Cosmas Gama.

Nassos na Cosmas waliteremka kutoka kwenye lile gari na kuelekea ndani ya ile benki huku dereva akiliondoa lile gari na kwenda kuliegesha sehemu maalumu ya maegesho ya magari pale kwenye eneo la benki.

Nassos Chatzopoulos alikuwa mrefu na mweupe mwenye macho makali na mikono imara, mtu asiye na maneno mengi lakini alikuwa mcheshi. Umri wake wa miaka hamsini na ushee bado ulikuwa haujatosha kabisa kuzipokonya nguvu zake mwilini.

Alikuwa amevaa suruali ya rangi ya bluu ya jeans, buti ngumu za ngozi miguuni, fulana ya rangi nyeupe iliyokuwa na picha ya bendera ya Ugiriki kifuani na koti la rangi ya bluu.

Cosmas Gama alikuwa na kimo cha wastani, mnene na rangi ya ngozi yake ilikuwa maji ya kunde. Alikuwa amevaa suti ghali ya rangi ya kijivu, viatu vya ngozi vya rangi nyeusi na miwani.

Walipoingia ndani ya ile benki, Yusuf aliwaona na kushtuka sana. Alijikuta akigwaya sana huku koo lake likikauka ghafla na ubaridi wa hofu ulianza kumtambaa mwilini mwake. Yusuf alimwangalia Nassos aliyekuwa ameambatana na Gama kwa wasiwasi mkubwa na asijue ni nini kilichokuwa kimemleta pale siku hiyo.

Wakiwa hawana wasiwasi, Nassos na Gama walikwenda moja kwa moja hadi pale kaunta alipokuwa amesimama Yusuf kwa kuwa kulikuwa na watu wachache waliokuwa wamesimama kwenye lile dirisha tofauti na kaunta zingine zilizokuwa na foleni ndefu.

Endelea...

Yusuf alikodoa macho yake kumtazama Nassos huku akili yake ikiwa imeanza kupoteza utulivu na wakati huo huo mapigo ya moyo wake yaliongezeka kasi mara dufu, hofu ilikuwa imemwingia na kumtambaa mwili mzima. Alihisi kama vile mkojo ulitaka kumtoka pasipo hiyari yake mwenyewe.

“Good morning, Mr Akida?” (Habari za asubuhi, bwana Akida?) Nassos alimsalimia Yusuf kwa bashasha zote huku akichia tabasamu.

“I’m fine, you’re welcome,” (Sijambo, karibuni) Yusuf aliitikia huku akijitahidi kuchangamka ingawa uso wake ulikuwa umesawajika sana.

“Thank you very much… we got a new accountant who will replace Japhet Lutego who went to Sweden…” (Asante sana… tumempata mhasibu mpya ambaye atashika nafasi ya Japhet Lutego aliyekwenda Sweden…) Nassos alimwambia Yusuf katika hali ya kumtambulisha Cosmas Gama.

“He is the one who will be coming here to deposit and withdraw money on behalf of the Jacarandah Group,” (Huyu ndiye atakayekuwa akifika hapa kuweka na kuchukua pesa kwa niaba ya kampuni ya Jacarandah Group) Nassos alisema na kuongeza, “His name is Cosmas Gama.” (Jina lake anaitwa Cosmas Gama).

Kwa utambulisho ule mfupi Yusuf alibetua kichwa chake kukubali huku akimtazama Cosmas Gama kwa tabasamu pana la kibiashsara.

“I am glad to know you, Mr Gama, you’re mostly welcome, sir,” (Nafurahi kukufahamu, bwana Gama, karibu sana, bwana mkubwa) Yusuf alisema huku akijitahidi sana kuifanya sauti yake ionekane tulivu.

“I am also grateful to know you, Mr…” (Nami nashukuru pia kukufahamu, bwana…) Cosmas Gama alisema na kusita kidogo huku akimtupia jicho Nassos.

“Akida… Yusuf Akida,” Nassos alisema na kuongeza, “Now, Yusuf, I want you to print a bank statement so that we know the amount of money available to the bank so far and we compare it with the calculation I have in the office. I remember recently I put three checks with a total amount of three billion and four hundred million shillings and then we took out only four hundred million shillings. Let me have that statement so that Gama knows where to start.”

(Sasa, Yusuf, nataka utuchapishie taarifa za kibenki ili tujue kiasi cha fedha kilichopo benki mpaka sasa na tulinganishe na hesabu niliyonayo ofisini. Nakumbuka majuzi niliweka hundi tatu zenye jumla ya shilingi bilioni tatu na milioni mia nne na baadaye tulitoa shilingi milioni mia nne tu. Hebu nipatie hesabu ya kiasi kilichopo ili Gama ajue anaanzia wapi).

Yusuf alishtuka sana na kunywea, alimtumbulia macho Nassos kwa wasiwasi huku mapigo ya moyo wake yakizidisha kasi yake. Alihisi kama vile anataka kuzimia kwa sababu ya shinikizo la juu la damu lililomkabili ghafla.

Nguvu zilianza kumuishia mwilini na alitamani kukaa. Mara kikazuka kitambo kifupi cha ukimya wa aina yake kilichomshtua Nassos, ambaye alimkodolea macho Yusuf kwa mshangao, hata hivyo, Yusuf alijishtukia na kuigeukia kompyuta yake kisha akaanza kutafuta taarifa za kampuni hiyo.

Alibofya kitufe fulani kwenye kibonyezo cha ile kompyuta na mara moja zilikuja taarifa za wateja mbalimbali wa ile benki, kisha alibonyeza herufi ‘J’, mara yakatokea majina kadhaa ya kampuni na wateja yaliyoanza na herufi ‘J’.

Hapo alitumia kipanya kushusha chini zile taarifa na hakuchukua hata sekunde tano akawa ameliona jina la The Jacarandah Group, kisha alibonyeza kwenye lile jina na hapo taarifa za kibenki kuhusu akaunti ya The Jacarandah Group zikaonekana kwenye kioo cha ile kompyuta.

Yusuf alizitazama zile taarifa kwa kitambo huku akionekana kusita sana, kisha alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku akimtupia jicho Nassos na kupiga moyo konde, akaamuru taarifa zile zichapwe kwenye karatasi kupitia mashine maalumu ya kuchapa kwa kubofya kitufe fulani katika kibonyezeo cha kompyuta yake.

Baada ya taarifa zile za kibenki kuhusu akaunti ya The Jacarandah Group kuchapwa kwenye karatasi, Yusuf alizichukua zile karatasi na kuzitupia jicho haraka haraka huku akimpa Salim, mapigo ya moyo wake yalizidi kwenda kasi isivyo kawaida, japo alikuwa akijipa ujasiri moyoni mwake kuwa kila kitu kitakwenda sawa.

Nassos alizipokeaa zile karatasi na kuzitazama kwa makini, kisha pale pale alitoa karatasi alizokuwa nazo na kuanza kulinganisha hesabu zake na zile zilizokuwa kwenye zile karatasi alizopewa na Yusuf.

Muda wote Yusuf alikuwa kimya akimtumbulia macho Nassos huku mazingira ya pale kaunta yakiwa ya utulivu mno kwa dakika nzima. Baada ya kuzilinganisha zile hesabu na kugundua kasoro, Nassos alishtuka sana na kumtazama Yusuf kwa umakini mkubwa.

“I don’t understand at all!” (Sielewi kabisa!) Nassos alimwambia Yusuf huku akimkazia macho na kumuonesha zile karatasi alizompa.

Yusuf alimkodolea macho Nassos akiwa hajui la kusema, hofu ilikuwa imemtambaa mwili mzima na muda ule akili yake ilikuwa haifanyi kazi yake sawasawa, alihisi ubaridi mwepesi ukiipiga ngozi yake na nywele zake zikimsimama.

“I don't understand! Your statement indicates a deficit of one billion and three hundred million, how?” (Sielewi kabisa! Hizi hesabu zenu zinaonesha upungufu wa shilingi bilioni moja na milioni mia tatu, kwa vipi?) Nassos aling’aka huku akimrushia Yusuf zile karatasi alizompa. Tayari alikwisha kuwa mwekundu kwa ghadhabu iliyoanza kumpanda.

Yusuf alikuwa anatetemeka huku akimwangalia Nassos kwa woga kana kwamba alikuwa amemuona malaika mtoa roho. Alihisi donge fulani hivi la fadhaa likizidi kumkaba na kusimama kwenye koo lake kwa muda mrefu huku joto kali likianza kuibuka ndani yake.

“Our calculations have no defects, sir, perhaps you have forgotten that today you have taken some money,” (Hesabu zetu hazina kasoro yoyote ile, bwana mkubwa, labda ninyi mmesahau kuwa leo mmechukua fedha zingine) Yusuf alisema kwa sauti yenye kitetemeshi huku akijitahidi kuifanya ionekane ya kawaida.

“What money? No one from our office came here today or yesterday to put or take money. What do you want to tell me?” (Fedha gani? Hakuja mtu yeyote kutoka ofisini kwetu leo hii wala jana kuweka ama kuchukua fedha. Unataka kuniambia nini?) Nassos alisema kwa hasira huku akirusha mikono yake hewani. Ni wazi Nassos alikuwa ameghadhabika sana na sauti yake ilikuwa kali zaidi na iliyojaa ghadhabu.

Yusuf alianza kulihisi joto kali likimtambaa mwilini mwake na kumfanya ahangaike zaidi. Kila alilotaka kusema alihisi kama lisingeweza kumwepusha na ghadhabu ya yule Mgiriki. Nassos aliendelea kuongea, lakini safari hii sauti yake ilikuwa ni kama alikuwa anataka kupiga kelele.

“Prove to me, who came here today from our company to take money?” (Nithibitishie, ni nani aliyekuja leo kutoka kwenye kampuni yetu kuchukua pesa?) Nassos alimuuliza Yusuf kwa ghadhabu huku akiwa amemkazia macho yaliyokuwa yakiwaka kwa ghadhabu.

Muda ule wote wafanyakazi wengine wa ile benki pamoja na wateja walibaki kimya wakiwatazama kwa mshangao Nassos na Yusuf waliokuwa wakilumbana, ni dhahiri walionekana kushindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea pale.

“Three people came here, and two were wearing your company’s NeoVision Security uniform. And the checks they came with is here,” (Walikuja hapa watu watatu, tena wawili walikuwa wamevaa sare za kampuni yenu ya NeoVision Security. Na hundi waliyokuja nayo ni hii hapa) Yusuf alisema kwa kujitetea huku akimwonesha Nassos ile hundi.

Sasa endelea...

Nassos alimwangalia Yusuf kwa ghadhabu kisha macho yake yalitua kwenye ile hundi aliyoishika, alitaka kusema neno lakini akasita na kunyoosha mkono wake ili apokee ile hundi.

Pamoja na uwepo wa viyoyozi vilivyokuwa vikitoa ubaridi mkali mle ndani ya benki lakini Yusuf alikuwa akihisi kupigwa na upepo wenye joto kali sana uliokuwa ukilijaza eneo lile alilosimama na kuifanya ngozi yake kuungua huku nywele zake zikimsimama. Ilikuwa ni hisia tofauti sana ambayo hakuwahi kuihisi hapo awali na ilikuwa na nguvu kubwa.

Ukimya ulidumu kwa kitambo kifupi huku Nassos akimkazia macho Yusuf na kuipokea ile hundi aliyoishika Yusuf iliyotoka kwa kina Kisu, Yusuf hakuwa na namna nyingine isipokuwa kuitoa ile hundi, japo kwa shingo upande.

Nassos alipoikamata mkononi mwake ile hundi aliitazama kwa makini na kwa nukta chaache tu tangu alipoitia machoni alionekana kushtuka sana, macho yake hayakuamini kabisa kile alichokuwa anakiona kwenye ile hundi. Ilikuwa ni hundi halali ya kampuni yake iliyokuwa na saini zile zile za watiaji saini wa kampuni. Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akishika kichwa chake, alionekana kupigwa na butwaa na kuishiwa nguvu.

“This is robbery, and it’s too foolish!” (Huu ni wizi, tena wizi wa kipumbavu sana!) Nassos alisema kwa hasira huku akimtazama Yusuf kwa macho yenye ghadhabu. Alikunja ngumi na kugongagonga juu ya ile kaunta akiwa na hasira.

“I'm sure some of you here in the bank are involved in this robbery. I would like to see the branch manager and talk to him,” (Nina hakika baadhi yenu hapa benki mnahusika kwenye huu wizi. Naomba kuonana na meneja wa tawi niongee naye) Nassos alisema kwa hasira huku akiwa ameshika kiuno.

Sasa Nassos alikuwa anahema kwa nguvu kama aliyekuwa akipigania hewa ya mwisho kabla ya kukata roho, alitaka kusema neno lakini akashindwa na kumnyooshea Yusuf kidole chake cha shahada huku akimtazama kwa ghadhabu. Kikapita kitambo kifupi cha ukimya.

“I said I need to see the branch manager right now,” (Nimesema nahitaji kuonana na meneja wa tawi sasa hivi) Nassos alisisitiza huku akianza kuzunguka zunguka katika eneo lile jirani na kaunta kwa hasira na kuwafanya watu wote wamwangalie kwa wasiwasi.

Askari wa ulinzi katika benki ile walikwisha fika haraka na kumsikiliza Nassos, wakati huo Yusuf alikuwa ameketi kwenye kiti akionekana kugwaya sana na moyo wake ulipiga kite kwa nguvu huku kijasho chembamba kikimtoka.

* * * * *

Kwenye sebule kubwa ya jumba kubwa la kifahari la ghorofa moja katika eneo la Mtoni Kijichi, Carlos akiwa na kampani nzima ya watu waliofanikisha operesheni maalumu ya kuzipata fedha kutoka Benki ya Biashara, walikuwa wameketi sebuleni kwenye masofa wakijipongeza kwa kunywa mvinyo na kuvuta sigara.

Lile jumba lilikuwa na vyumba vitano vya kulala vilivyosheheni samani zote muhimu lakini lilikuwa halikaliwi na mtu yeyote, ingawa ndani yake kulikuwa na kila aina ya samani, tena zilizonunuliwa kwa bei mbaya. Lilikuwa na sebule mbili kubwa chini na juu, ukumbi wa chakula, ofisi na maktaba maalumu ya siri, sehemu ya ghorofani ya kubarizi yenye viti vya sofa, maliwato, jiko kubwa la kisasa, stoo na kadhalika.

Kwenye sebule ya chini, ambako ndiko Carlos na kampani yake walikuwa wameketi, mandhari yake ilipambwa kwa seti mbili za makochi ya sofa yaliyopangwa kwa kuizunguka ile sebule. Katikati ya ile sebule kulikuwa na meza kubwa lakini fupi ya kioo iliyokuwa na umbo la yai. Na kulikuwa na madirisha makubwa yaliyofunikwa na mapazia marefu mepesi ya kuvutia.

Kupitia yale madirisha makubwa ya sebule mtu yeyote ambaye angeketi pale sebuleni angeweza kuona mandhari nzuri na tulivu ya miti ya kivuli, nyasi zilizokatiwa vizuri za kijani kibichi na bustani ya maua ya kupendeza katika sehemu ya kupumzikia iliyokuwa eneo la nyuma la lile jumba kando ya bwawa la kuogolea.

Pia ndani ya lile jumba kulikuwa na gereji iliyotumika kulaza magari ikiwa na uwezo wa kulaza magari matatu hadi manne kwa wakati mmoja, lakini siku zote kulikuwa kunalazwa gari moja tu aina ya Toyota Alphard jeupe ambalo halijawahi kutumika tangu lilipoingizwa kinyemela nchini kutoka Afrika Kusini na halikuwa limesajiliwa.

Hii ndiyo nyumba ambayo baada ya Jacky kutoka kule Benki ya Biashara alimwambia yule dereva wa teksi-bubu kumleta Mtoni Kijichi, ingawa hakuletwa moja kwa moja hadi pale bali alizuga kushukia kituo cha daladala kisha akachukua bodaboda iliyomleta pale.

Alikuja katika ile nyumba kwani hapo ndipo alipokuwa ameliacha gari lake aina ya Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe na kisha kuchukua gari aina ya Toyota Alphard jeupe kwa ajili ya kutumika kwenye operesheni ya kuchukua fedha za The Jacarandah Group.

Lile jumba Carlos na Jacky walilitumia mara chache sana, hasa pale walipohitaji faragha zaidi au walipohitaji kushughulika na mambo nyeti zaidi, kwa kuwa lilikuwa halifahamiki kwa jamaa wengi.

Ki ukweli lilikuwa jumba kubwa na zuri lililokuwa limezungukwa na ukuta mrefu usiomwezesha mtu kuona ndani na uliofungwa mfumo maalumu wa umeme wa kuzuia wezi juu yake, na lilikuwa na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatwa vizuri. Mbele yake kulikuwa na geti kubwa jeusi huku likizungukwa na miti mizuri ya kivuli.

Carlos na kampani yake walikuwa kimya pale sebuleni wakinywa na kutafakari, na juu ya meza ndogo zilizokuwa mbele yao kulikuwa na mizinga mitatu mikubwa ya mvinyo na bilauri kadhaa. Hii ilikuwa ni kama sherehe ndogo baada kwa kufanikiwa kufikisha mzigo salama licha ya hekaheka za kupita huku na kule, barabara hizi na zile katika safari ya mzunguko ambao ingekuwa vigumu sana mtu yeyote kuelewa walielekea wapi endapo angejaribu kuwafuatilia.

Kwa kifupi ni kwamba, baada ya kutoka pale Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba gari lao aina ya Ford Transit lenye nembo ya NeoVision Security liliifuata barabara ya Bibi Titi Mohammed na kwenda moja kwa moja hadi makutano ya barabra ile na barabara ya mtaa wa Nkrumah.

Hapo Carlos aliongeza kasi ya mwendo wa gari huku akipiga king’ora kuyataka magari mengine yakae kando huku akikatisha katikati ya majengo ya ghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), yaliyokuwa katika pande zote mbili za barabara ile ya Nkrumah.

Alipoivuka reli katika eneo la Goldstar alikunja na kuingia kushoto akiifuata barabara ya mtaa wa Lugoda, wakapita katikati ya majengo makubwa yalikuwa na ofisi mbalimbali na kwenda kutokea katika barabara ya mtaa wa Gerezani iliyokuwa ikitokea Posta, na hapo akakunja na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara ile ya Gerezani.

Aliendelea kupiga king’ora kuyataka magari mengine yakae kando huku akiyapita kwa mwendo wa kasi na kuufika mzunguko wa barabara za Gerezani iliyotokea Kariakoo kwenda Posta na ile ya Bandari iliyoelekea Kurasini. Aliifuata barabara ya Bandari na mwendo wake haukuwa wa kubahatisha hata kidogo.

Akalivuka daraja ambalo chini yake kulikuwa na njia za treni kuelekea bandarini, hakupunguza mwendo hadi alipofika katika mzunguko ulioziunganisha barabara za Bandari, Kilwa na Mandela. Na hapo akazunguka na kuifuata barabara ya Kilwa.

Alizidi kusonga mbele zaidi hadi alipoivuka baa maarufu ya Pentagon mbele kidogo akaachana na barabara ya Kilwa na kuingia katika mtaa mmoja kushoto kwake, kisha akaivuka Meshack Automotive Solutions halafu akakata tena kushoto akiingia ndani zaidi katika eneo la Mivinjeni, kisha alikwenda kuliegesha gari lake chini ya kivuli cha miti mikubwa katika eneo lile la Mivinjeni.

Kwa muda ule eneo lile halikuwa na pilika pilika zozote, hivyo kitendo bila kuchelewa, wote walishuka haraka kutoka kwenye lile gari huku Kabwe akilishusha lile begi lenye fedha kisha wakaingia kwenye gari jingine la kifahari aina ya Toyota Alphard jeupe lililokuwa likiwasubiri pale.

Ndani ya lile gari aina ya Toyota Alphard kulikuwa na mtu mmoja tu, dereva ambaye ni Jacky, aliyekuwa ameketi nyuma ya usukani kwa utulivu.

Muda ule ule Liston alitumia utaalamu wake wa hali ya juu wa uhandishi wa umeme, kukorofisha mfumo wa umeme wa lile gari aina ya Ford Transit, na hapo gari likashika moto.

Kisha aliingia haraka kwenye lile Toyota Alphard lililoanza kuondoka taratibu, alipoingia tu likaondoka kwa mwendo wa kasi kutoka eneo lile kabla hata watu hawajang’amua nini kilichokuwa kikiendelea pale. Kitendo kile kilifanyika ndani ya muda mfupi sana sawa kitendo cha kufumba jicho na kufumbua.

Jacky alikuwa makini sana na kazi yake na alikuwa amevaa soksi maalumu za mikononi (gloves). Wakati wanatokomea mtaani waliliacha lile gari aina ya Ford Transit likiteketea kwa moto na hivyo kuvuta makundi ya watu kushuhudia na wengine wakijaribu kuuzima ule moto, na hivyo hakuna aliyeweza kuwafuatilia.

Kutoka pale walielekea moja kwa moja Mtoni Kijichi na kufika kwenye lile jumba, Carlos akabonyeza remote maalumu ya kufungua geti kubwa jeusi mbele ya lile jumba na mara lile geti likaanza kufunguka, walipoingia ndani lile geti likajifunga.

Jacky alikwenda moja kwa moja kwenye chumba maalumu kilichokuwa kinatumika kama ofisi maalumu na maktaba ya siri kilichofanana na kile kilichojengwa kwenye ile nyumba ya Segerea, alikuwa anaburuza lile begi lenye magurudumu lililojaa fedha.

Chumba hiki kilikuwa na ulinzi wa uhakika na ili kuingia mle ndani ilikuwa ni lazima ubofye namba fulani za siri zilizokuwa kwenye kisanduku kidogo chenye namba pembeni ya mlango.

Jacky alipoufikia mlango wa chumba kile, ambao juu yake kulikuwa na taa nyekundu ikiwaka alibonyeza namba nne za siri kwenye kile kisanduku kilichokuwa pembeni ya mlango kisha akaweka dole gumba la mkono wake wa kulia katika sehemu maalumu iliyokuwa ikiwaka taa ya kijani.

“Thank you, Jackline, you’re welcome…” sauti maalumu kwenye spika ndogo pembeni ya mlango ikasikika ikimkaribisha Jacky huku ikiambatana na maandishi “Welcome Jackline” na mara mlango ule ukafunguka.

Jacky aliliingiza lile begi na kulihifadhi kwenye kabati maalumu na kutoka kwenda kujiunga na watu wengine waliokuwa wameketi sebuleni wakijipongeza kwa mvinyo. Kabwe alinyanyua bilauri yake na kugida pombe yote iliyokuwemo kwa mkupuo mmoja, kisha aliikita ile bilauri mezani huku akisisimkwa mwili, alionekana kuwa mwenye haraka ya jambo fulani.

“Kwa hiyo, kamanda, inakuwaje sasa?” Kabwe alimuuliza Carlos huku akimkazia macho.

“Kuhusu nini?” Carlos alimuuliza Kabwe kwa mshangao huku akimtazama kwa makini.

“Kuhusu pesa, baba’ke… tupe chetu tusepe kwani tunasubiri nini hapa?” Kabwe alijibu huku akifinya macho yake kutokana na ulevi ulioanza kumwingia.

“Naomba tusifanye papara ya kugawana fedha, tusubiri kwanza kwa siku mbili tuone hali itakuwaje,” Carlos aliongea kwa sauti ya utulivu huku akiwatazama watu wote na kuupeleka mche wake wa sigara mdomoni.

Kabwe alikunja sura yake na kutingisha kichwa kwa nguvu akionesha kukataa na wakati huo huo hasira zilikwisha anza kumpanda.

“Aah, hiyo sasa noma, kamanda…” Kabwe alisema na kugeuka kuwatazama Kisu na Liston, “Au siyo wanangu! Eti tusubiri siku mbili, huu si ndiyo mwanzo wa kuingizwa cha kike! Siku mbili tusubiri nini, pingu?”

“Hatusubiri pingu, wala hakuna mtu yeyote mwenye kutaka kuwaingiza cha kike, kwanza siku mbili wala siyo nyingi, na kama mambo yatakuwa shwari tukutane kule kwenye nyumba ya Segerea ili kila mtu achukue chake. Kwani tatizo liko wapi?” Carlos alisema kwa sauti tulivu huku akiwatazama mmoja baada ya mwingine.

Kabwe alizidi kutingisha kichwa chake kukataa, aliwatazama Kisu na Liston kwa kitambo, kisha akamgeukia tena Carlos.

“Unajua mkubwa, hii shughuli haikuwa mchezo, na wewe unajua hilo,” Kabwe aliongea kwa hamaki huku akiwa amekunja sura yake iliyotengeneza ndita usoni.

“Najua sana, ndiyo maana nilihitaji kupata watu wa aina yenu ili kuifanya,” Carlos alisema kwa sauti tulivu akionesha kukubaliana na maneno ya Kabwe.

“Sasa kama unajua hivyo, ni lazima ujue vile vile kwamba tumejitolea roho zetu ili tutengeneze fedha itusaidie kwenye maisha yetu, au siyo, kamanda?”

“Sawa sawa!”

“Sasa fedha yenyewe si ndo hii tuliyoipata? We tukatie chetu tuondoke ili kila mtu ajue ustaarabu wake, kwani kero iko wapi?” Kabwe alizidi kusisitiza apewe mgawo wake huku akionekana kukosa uvumilivu.

Hata hivyo, muda wote wakati Kabwe akiongea, Kisu alikuwa akitabasamu tu bila kusema chochote na Liston alikuwa kimya kabisa akisikiliza kwa makini jinsi ambavyo Carlos na Kabwe walivyokuwa wakilumbana, ingawa wote kila mmoja alikuwa na yake rohoni.

“Tatizo lako Kabwe hunifahamu vizuri, mbona hushangai Kisu na Liston hawana presha? Sina kawaida ya kumdhulumu mtu, nimeshafanya nao kazi kibao za fedha nyingi kuliko hata hii na nikawapa chao bila usumbufu,” Carlos alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku akijaribu kuidhibiti hasira.

“Kabwe, Listoni na Kisu ni watu watatu tofauti na kila mmoja ana changamoto zake, huenda wao wameshiba lakini mimi nina njaa. Ninahitaji fedha ili kutatua matatizo yangu na kama sijakosea tulikubaliana kulipana mara baada ya kazi, na kazi yenyewe ndo hii imeshafanyika kwa ufanisi mkubwa, sijui haya mengine ya kusubiri siku mbili yanatoka wapi, mkubwa!” Kabwe alisema huku akirusha mikono yake juu kwa hasira.

“Okay, naomba unisikilize, niko tayari kuwapa ninyi wawili, wewe na Liston fedha kiasi za kutumia siku hizi mbili wakati tukisubiri, na kama mambo yakiwa shwari tukutane kule Segerea keshokutwa saa kumi na mbili jioni ili kila mmoja achukue chake, au vipi!” Carlos alisema kwa utulivu huku akimkazia macho Kabwe.

“Kwa nini tupewe sisi wawili tu, kwani Kisu hayumo kwenye listi?” Kabwe aliuliza kwa mshangao.

“Makubaliano yangu na Kisu ninyi hayawahusu na wala si kazi yenu kujua namlipaje,” Carlos alisema kwa utulivu huku akijitahidi kuidhibiti hasira yake.

Baada ya kauli ile kikapita kitambo kifupi cha ukimya huku Kabwe na Liston wakiangaliana kama waliokuwa wanauliza mambo ambayo hawakupenda Carlos ajue. Kisha Kabwe alibetua mabega yake juu na kugeuka kumtazama Carlos. “Kwa hiyo leo utakata shilingi ngapi, boss?”

“Nitakupeni shilingi laki tano kila mmoja, lakini hii fedha wala haimo kabisa kwenye mgao, naitoa tu kama offer kutoka mfukoni mwangu,” Carlos alisema huku akigeuza shingo yake kumtazama Jacky, ambaye muda wote alikuwa ameketi kimya kwenye kona moja ya ile sebule akiwa makini sana.

Kabwe na Liston waliangaliana tena kisha kikapita kitambo kingine kifupi cha ukimya. Liston alishusha apumzi za ndani kwa ndani na kumpiga ukope Kabwe kama ishara ya kumtaka akubali wachukue zile fedha.

“Poa, boss, basi leta hizo fedha sisi tujikatae,” Kabwe alisema huku akichukua chupa ya mvinyo na kujimiminia kwenye bilauri, kisha akapiga funda kubwa la mvinyo na kusisimkwa.

Carlos aliinuka na kupanda ngazi kuelekea ghorofani huku akisindikizwa na macho ya watu wote pale sebuleni, na baada ya muda mfupi aliteremka ngazi akiwa ameshika mabunda mawili ya noti nyekundu nyekundu na kuwarushia Kabwe na Liston, kila mtu na la kwake.

Kila mmoja alizidaka zile fedha, Kabwe alionekana kukenua meno yake kwa furaha, kisha alimkonyeza Liston akimpa ishara ya kuondoka.

“Sasa tunaondokaje, boss?” Kabwe alimuuliza Carlos huku akiwa tayari amesimama wima kwa ajili ya kuondoka.

Carlos aligeuza shingo yake kumtazama Jacky na kumpa ishara fulani, Jacky aliinuka na kuelekea juu haraka na baada ya dakika kama kumi hivi alirudi akiwa amevaa sketi fupi ya rangi nyeusi yenye miraba myeupe, blauzi nyeupe ya mikono mirefu na viatu vya kamba. Mkononi alikuwa ameshika ufunguo wa gari.

Ile sketi ilikuwa imenasa vyema kwenye tumbo lake dogo na kiuno chembamba lakini imara kilichoshikilia minofu laini ya mapaja yake makubwa na kuifichua hazina iliyotukuka ya miguu yake mizuri.

Alipotokea tu harufu nzuri ya marashi ghali aina ya Clive yenye kuhamasisha ngono aliyokuwa amejipulizia mwilini ilitamalaki pale sebuleni na kuzifanya pua za watu wote pale sebuleni kupata uhai mpya. Jacky aliwatazama Kabwe na Liston na kuwapa ishara kuwa wamfuate, na hapo wote watatu wakaanza kutoka nje huku wakiwaacha Kisu na Carlos bado wameketi.

Walipotoka waliingia ndani ya gari la Jacky aina ya Range Rover Sport L494 jeupe, Jacky akabonyeza remote na mara lile geti kubwa la nyumba likafunguka na kuruhusu gari litoke nje.

“Sijui niwapeleke wapi, mabwana?” Jacky aliwauliza mara tu alipotoka nje ya lile jumba la kifahari. Kabwe na Liston waliangalia katika namna ya kuulizana.

“Kama unaweza tupeleke Kinondoni, vinginevyo unaweza kutuacha pale Viwanja vya Sabasaba,” Kabwe aliyekuwa ameketi siti ya mbele kushoto kwa dereva alijibu huku akiachia tabasamu.

Jacky aliingiza gia na kuliondoa gari kwa mwendo wa kasi, magurudumu ya gari yalichuna ardhi wakati lilipokuwa likiingia katika barabara ya mtaa na baada ya mwendo mfupi likaingia katika barabara ya Kilwa. Hapo Jacky akaongeza mwendo na gari likaserereka.

Katika barabara ile ya Kilwa muda wote Kabwe alionekana kumtupia jicho la wizi Jacky huku akiyaangalia mapaja yake yaliyonona kwa matamanio. Baada ya mwendo wa kitambo fulani Kabwe akaonekana kushindwa kuvumilia, akajikohoza kidogo ili kusafisha koo lake, kitendo kilichomfanya Jacky ageuze shingo yake kumtazama kwa makini.

“Shem, kwa kweli nimeshindwa kuvumilia, naomba nikiri tu kuwa wewe ni mrembo mno, sijawahi kumuona msichana mrembo kama wewe…” Kabwe alisema huku akipitisha ulimi wake kulamba midomo yake iliyoanza kukauka.

“Mtu yeyote bila kujali kama ana ndoa anaweza kujikuta akichanganyikiwa na uzuri wako na pengine kutelekeza ndoa yake wallahi,” aliongeza na kuangua kicheko hafifu. Jacky alimtazama na kutabasamu pasipo kusema neno.

“Yaani wewe ni mzuri mpaka nahisi kuumwa, kwa jinsi nilivyo na wivu kama ungekuwa mke wangu nisingekubali kukuruhusu kuongea na mwanaume yeyote achilia mbali kuwasindikiza wakware kama sisi, nisingekubali hata iweje!” Kabwe alisema tena na kumfanya Liston aangue kicheko hafifu.

“Si utani! Hata mimi nisingekubali,” Liston aliunga mkono.

“Umeona eeh! Yaani mtoto amenoga mno utadhani ameteremshwa kutoka mbinguni, au pengine alikusudiwa kuumbwa malaika ila akaletwa duniani kimakosa!” Kabwe alisema kwa utani huku akigeuza shingo yake kumtazama Liston aliyekuwa ametulia kwenye siti ya nyuma.

“Hmm!” Jacky aliguna huku akiachia tabasamu laini. Hakusema neno lolote bali alibaki anawatupia jicho Kabwe na Liston huku akiendelea kuendessha gari kwa umakini mkubwa.

“I wish ningekuwa Carlos na wewe ndiye mke wangu, japo hata kwa nusu saa tu,” Kabwe alisema huku akishusha pumzi.

“Mbona wazuri wapo wengi tu, shem, juhudi zako tu,” Jacky alisema huku akiendelea kutabasamu, na mara wakawa wamefika katika eneo la Sabasaba, Jacky aliliegesha gari lake karibu na kituo cha daladala cha Sabasaba, Kabwe na Liston wakashuka.

Jacky akaanza kuliondoa gari lake taratibu akielekea mbele nia yake ilikuwa kuchukua uelekeo wa kurudi Mtoni Kijichi baada ya kufika kwenye mzunguko wa barabara mbele kidogo ya viwanja vya Sabasaba, mara akaliona gari aina ya Toyota Lexus RX la rangi nyeusi likija nyuma yake kwa mwendo wa kasi.

Jacky alipunguza mwendo ili kulipisha lile gari lipite lakini lile gari lilipokuwa likimpita ghafla likapunguza kidogo mwendo huku magurudumu yake yakiserereka kwenye barabara ya lami na baadaye gari likaanza kwenda sambasamba na gari la Jacky. Ikabidi Jacky ageuze shingo yake kumtazama dereva wa lile gari kwa jicho la wasiwasi kidogo.

Macho yake yalitia nanga kwenye sura ya kijana mtanashati aliyekuwa akiendesha lile gari ambaye alikuwa akimtazama Jacky kwa umakini sana na kuonesha kubabaishwa kidogo na uzuri wake. Sura ya yule mwanamume ilionesha uchangamfu na macho yake yalikuwa makini kuliko hata simba anayewinda.

Yule mwanamume alionekana kama aliyekuwa akihisi msisimko wa ajabu ukimtambaa mwilini mwake na kuzifanya nywele zake kumsimama baada ya kumuona Jacky. Midomo yake ilionesha kumkauka ghafla na mapigo ya moyo wake yakabadilika na kuanza kukimbia.

Alimtazama Jacky kwa umakini akijihisi kama yupo ndotoni, hata hivyo, milango yake ya fahamu ilikuwa makini zaidi kujaribu kuishirikisha akili yake kikamilifu kuhusu kile alichokuwa amekiona mbele yake.

Jacky aliligundua hilo, hivyo akaachia tabasamu laini ili kumchanganya zaidi yule mwanamume huku akimtazama kwa makini, hata hivyo alijikuta akiwa ameupita ule mzunguko wa barabara ambapo alitarajia kugeuza ili kurudi Mtoni Kijichi, na wakati huo alikuwa karibu kabisa na eneo la Uhasibu, hivyo akaanza kuongeza mwendo ili kuliacha lile gari lakini kabla hajaliacha akahisi sauti ikiliitwa jina lake.

“Jackline!” yule mwanamume alikuwa ameshusha kioo cha gari lake na kuita kwa sauti kubwa iliyopenya hadi kwenye ngoma ya sikio la Jacky, japokuwa alikuwa amepandisha vioo vya gari lake lakini aliweza kuisikia vyema ile sauti. Jacky aligeuza tena shingo yake kumtazama yule mwanamume na ndipo alipogundua kuwa hata yeye alikuwa anamfahamu.

“Jacob!” alijikuta akilitamka jina hilo kwa mshangao huku akikanyaga breki, gari likaserereka kwenye lami na kuyumba kidogo, kisha akaliegesha gari lake kando ya barabara ya Kilwa mbele ya kituo cha daladala cha Uhasibu. Jacob naye alikanyaga breki na kusimama akiliegesha gari lake mbele ya gari la Jacky kisha akateremka kumfuata.

“Hallow Jackline, how are you doing? I missed you so much, my love,” (Hallo Jackline, habari gani? Nilikumisi sana, mpenzi wangu) yule mwanamume alimsalimia Jacky mara tu alipomfikia.

“What do you want from me?” (Unataka nini kwangu?) Jacky alimuuliza yule mwanamume na mara moja akayakwepesha macho yake baada ya kugundua kuwa alikuwa akimtazama usoni kwa makini.

Yule mwanamume aliendelea kumtazama Jacky kwa kitambo huku akitabasamu kisha akavuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.

“Oh Jackline, don't you just leave your mockeries?” (Oh Jackline, hujaacha tu masihala yako?) yule mwanamume alisema huku akiendelea kutabasamu.

“Jacob, say what you want to say and leave immediately, I don’t need you anymore,” ((Jacob, sema unachotaka kusema na uondoke mara moja, sikuhitaji tena) Jacky alisema kwa sauti iliyoonesha kwamba hakuwa akitania.

“Jacky, when will you open again your heart to me? When will you be ready to sit and listen to me?” (Jacky, Hivi ni lini utaufungua tena moyo wako kwangu? Lini utakuwa tayari kukaa na kunisikiliza?) yule mwanamume alimuuliza Jacky kwa sauti tulivu ya kubembeleza lakini Jacky hakumjibu na badala yake aliachia tabasamu la dharau.

“Why did you fail even to look for me as we had planned?” (Kwa nini umeshindwa hata kunitafuta kama tulivyokuwa tumepanga?) yule mwanamume aliendelea kumuuliza huku akimkazia macho. Jacky alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.

“Mr Jacob, can you please stop this drama? It’s over between us,” (Bwana Jacob, unaweza kuachana na haya maigizo? Mimi na wewe tulikwisha malizana) hatimaye Jacky alimwambia yule mwanamume huku akimkazia macho yake.

“What?” (Nini?) yule mwanamume alimuuliza Jacky huku akimtazama kwa makini.

“We can’t go on like this, stop drama and don’t waste your time following me, it’s time to end things now,” (Hatuwezi kwenda hivi, acha maigizo na usipoteze muda wako kunifuatilia, ni muda sasa wa kusitisha mambo haya) Jacky alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Why do we need to end it so inappropriately?” (Kwa nini tusitishe mambo kienyeji?) yule mwanamume aliuliza huku akimkazia macho Jacky kisha akaendelea, “Ni hapo tu unaponiudhi…”

“Jacob…” Jacky alitaka kusema neno lakini Jacob akamzuia.

“Don’t say anything, Jacky. You know exactly how much I love you and I’ll never stop loving you no matter what,” (Usiongee chochote Jacky. Unajua kabisa ni jinsi gani nakupenda na sitaacha kukupenda hata iweje) yule mwanamume aliongea kwa sauti yenye ukali kidogo.

“Liar!” (Muongo!) Jacky naye alisema kwa sauti yenye ukali kidogo.

“I’m not a liar, I love you with all my heart,” (Mimi si muongo, ninakupenda kwa moyo wangu wote) yule mwanamume alisema kwa sauti tulivu na ya kubembeleza.

Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiinua mabega yake juu na kubetua midomo akiashiria kuwa hana namna ya kufanya.

“Jacky, why can’t we skip the past and talk about our future?” (Jacky, kwa nini tusiachane na mambo yaliyopita na kuzungumzia mustakabali wetu?) yule mwanamume alimwambia Jacky huku akimtazama machoni.

“It’s not easy, Jacob. You know exactly how much I loved you very much but you broke my heart! I was real disappointed, very disappointed,” (Siyo rahisi. Unajua hasa kiasi gani nilikupenda sana lakini ukautia moyo wangu majeraha! Nilifadhaika kweli kweli, nilifadhaika sana) Jacky alisema huku akishusha pumzi ndefu.

“I’m sorry for everything, I’m real very sorry,” (Nasikitika kwa yote, nasikitika sana kwa kweli).

“Nothing has changed. You’re still the same deceiver… by the way, can you be honest with me, Jacob, where is Diana?” (Hakuna kilichobadilika. Wewe ni yule yule msaliti… hivi unaweza kuniambia ukweli, Jacob, Diana yuko wapi?) Jacky alimuuliza Jacob huku akimkazia macho.

“She is married and living happily with her police officer, ASP Komba…” (Kaolewa na anaishi maisha ya furaha na mumewe ofisa wa polisi, ASP Komba…) Jacob alisema huku akijiegemeza kwenye gari la Jacky.

“And… I guess you’re still making love with her, right?” (Na… nihisi bado utakuwa unatembea naye, sawa?) Jacky alimuuliza Jacob huku akiwa amemkazia macho.

“Nope, how’d I do that?” (Hapana, kwa nini nifanye hivyo?) Jacob alijitetea huku akitingisha kichwa chake kukataa.

“Are you married?” (Umeoa?) Jacky alimuuliza Jacob swali jingine akiwa bado amemkazia macho.

“I am still single, all three years I have been looking for you…” (Bado sijaoa, miaka yote mitatu nimekuwa nikikutafuta wewe…) Jacob alimwambia Jacky kwa sauti tulivu ya kusihi.

“You’re a liar, by the way, I’m already married,” Jacky alisema huku akimkazia macho Jacob.

“You must be kidding! Well…” (Kwa vyovyote utakuwa unatania! Sawa…) Jacob alisema na kutoa Jacky business card akionekana mwenye haraka kidogo, akanyoosha mkono wake kumpa Jacky ile kadi.

“This is my number, please let’s keep in touch, I'm on my way to the police station, my friend has been arrested,” (Hii ni namba yangu, tafadhali tuwasiliane, kwa sasa naelekea kituo cha polisi, rafiki yangu amekamatwa) Jacob alisema na kuanza kuondoka haraka.

Jacky alionekana kushtuka sana baada ya kusikia habari za mtu kukamatwa na hakujua kwa nini alishtuka! Hata hivyo, alijikuta akitokwa na jasho jepesi mwilini na mapigo ya moyo wake yakabadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!

“His friend has been arrested! Who?” (Rafiki yake amekamatwa! Nani?) Jacky aliwaza huku akitamani kumuuliza Jacob ni rafiki yake yupi kati ya aliowahi kuwafahamu, hata hivyo aliamua kubaki kimya, alimshuhudia Jacob akiingia kwenye gari lake kisha akaliondoka kwa mwendo wa kasi kuelekea mjini.

Jacky alilisindikiza kwa macho lile gari hadi lilipopotea kwenye upeo wa macho yake, kisha mawazo mengi yakaanza kupita kichwani kwa Jacky, Mawazo yaliyompeleka mbali miaka mitatu na ushee iliyokuwa imepita, kuhusu uhusiano wake na Jacob Haule, wakati huo walikuwa wakifanya kazi pamoja katika kampuni ya simu jijini Dar es Salaam.

“I loved him very much and we spent so many beautiful moments together… but the moment I turned my back, he was cheating me…” (Nilimpenda sana na muda mwingi tulifurahia pamoja… lakini kila nilipompa mgongo tu, alikuwa akinisaliti…) Jacky aliwaza.

Jacky alikumbuka jinsi yeye na Jacob walivyoajiriwa kwa wakati mmoja katika kampuni ile kubwa ya simu nchini, Jacky aliajiriwa kama mtaalamu wa habari na mawasiliano baada ya kuhitimu Shahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information Technology), na Jacob aliajiriwa kama mkurugenzi wa masoko akiwa amehitimu shahada ya pili ya Sanaa katika Uongozi wa Masoko (Master of Arts in Marketing Management).

Kwa wakati huo Jacob alikuwa na wiki chache tu tangu aliporejea Tanzania akitokea nchini Uingereza alikokuwa akifanya kazi, baada ya kuhitimu masomo yake.

Kutokana na kufanya kazi katika ofisi moja, Jacky na Jacob walijikuta wakijenga ukaribu zaidi na haikuwachukua muda mrefu kuzoeana sana, kisha urafiki wao uliposhamiri hatimaye wakajikuta wametumbukia kwenye mapenzi mazito kiasi cha kuonewa wivu na wafanyakazi wengine walioitamani sana bahati hiyo.

Ni lini Jacky alianza kutekwa na penzi la Jacob? Hakukumbuka hasa siku, kwani ilitokea tu kama vile mtu apitiwavyo na usingizi, huwa vigumu kuitambua dakika aliyolala kwani usingizi huja kwa namna ya mwizi anayenyemelea.

Jacky alichoweza kukumbuka ni kuwa alianza kumpenda Jacob tangu siku ya kwanza tu aliyomtia machoni, kwani Jacob alikuwa kijana mtanashati kweli kweli, msomi, mkarimu na mcheshi kwa watu wa rika zote. Sifa kubwa aliyokuwa nayo Jacob ni kwamba hakujua kuringa wala kujivunia usomi wala cheo chake.

Ingawa wanasema mtu hakosi kasoro, kasoro kubwa ya Jacob ilikuwa kupenda sana vidosho. Hakupenda kupitwa na vidosho. Ila ukiachana na tabia hiyo ya kupenda vidosho hata wasiomstahili, Jacob alikuwa mpole na mkarimu sana, hata angemwamshwa saa nane za usiku na mfanyakazi mwenziye mwenye shida angeacha usingizi au jambo lolote lenye faida kwake ili amsaidie.

Tabia ya kusaidia watu haikuishia kazini tu, hata pale mtaani kwao alikokuwa akiishi wakati huo, maeneo ya Kijitonyama, watu walimpenda sana, si watoto si wakubwa.

Jacky alijikuta akimuwaza Jacob tu kila wakati na alijikuta akiwa amepata mshirika mpya katika maisha yake, akimuona kijana huyo kila mahali, tangu katika sahani ya chakula, kwenye bilauri ya maji, hadi kitandani.

Kila mara alipokutana na Jacob alijihisi kugwaya na hofu ya chini chini ilimtambaa na kusababisha maungo yake yazizime kwa msisimko ambao ilikuwa vigumu kuuelezea.

Aliwahi kumfumania Jacob mara kadhaa na wasichana wengine lakini hakuwa na uwezo wa kumwacha au kumkabili, kwani kila alipossimama mbele yake alijikuta maungo yake yakigeuka yakaingiwa ganzi, moyo wake uliunguruma sana kama uliopambana na kazi isiyo ya kiasi chake na ulimi wake uligeuka kipande cha chuma! Hakujiweza kabisa kila aliposimama mbele ya Jacob.

Mapenzi yao yalikolea na mara nyingi walitoka pamoja kwa matembezi ya jioni ama katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo au za kijamii. Ilifikia hatua walipeana ahadi ya kwenda kuwaona wazazi na kuoana huku wakiapa kulilinda pendo lao thabiti ambalo waliamini lingeweza kuvumilia raha na shida zote za ulimwengu kama chuma cha pua.

Walikubaliana kujenga pendo ambalo wangehakikisha halipwayi wala kupauka, na ilibaki siku chache tu wavishane pete ya uchumba ambayo ingekuwa mkataba wa milele usioweza kuvunjwa kwa kupwa na kujaa kwa bahari, ndipo lilipotokea la kutokea na kulifanya penzi lao libaki kuwa historia.

Ilikuwa siku ya Ijumaa jioni, Jacky alikwenda nyumbani kwa Jacob bila taarifa na kumkuta Jacob akijivinjari na Diana, tena wakitumia njia mbadala. Japo Jacky aliwahi kumfuma Jacob mara kadhaa na wasichana, lakini kilichomuumiza zaidi ni kumfumania na rafiki yake kipenzi, Diana waliyesoma darasa moja pale Jangwani Secondary School. Ni Jacky ndiye aliyemtambulisha Diana kwa Jacob.

Jacky aliukuta mpambano mkali sana pale sebuleni kati ya Jacob na Diana, walikuwa wamehama kabisa katika ulimwengu huu na kuhamia katika sayari nyingine kabisa yenye raha zisizoelezeka. Vilio na miguno kuashiria raha waliyoipata vikihanikizwa na sauti kubwa ya muziki ndivyo vilivyokuwa vikisika.

Wakati Diana na Jacob wakijivinjari katika sayari ya mahaba, tena kinyume na maumbile, Jacky alikuwa amefika nyumbani kwa Jacob pasipo taarifa, lakini alipokuwa nje alianza kusikia sauti kubwa ya muziki uliokuwa ukisikika kutokea ndani.

Jacky alishangaa sana kwani haikuwa kawaida ya Jacob kufungulia muziki kwa sauti ya juu isipokuwa wakati walipokuwa katika ulimwengu wa mahaba, hivyo alisimama nje ya nyumba akijiuliza kulikuwa na nini mle ndani bila kupata jibu. Alipokosa majibu alishika kitasa cha mlango na kukinyonga, mlango ukasalimu amri na kufunguka ukimruhusu kuingia ndani.

Aliingia ndani na kupiga hatua kwa madaha akikivuka chumba kidogo na kuingia sebuleni. Alichokiona pale sebuleni kilimfanya ahisi kama dunia yote ilikuwa imemkalia kichwani, alitamani ingekuwa ni ndoto lakini haikuwa ndoto bali kilikuwa kitu cha kweli alichokuwa akikiona mbele yake.

Alikuwa amepatwa na mshtuko mkubwa sana na kuhisi miguu yake ilikuwa inaishiwa na nguvu, akawahi kushika ukuta na kujiegemeza ukutani, kwani mwili wote ulikuwa unamtetemeka.

Katika sofa kubwa Diana alikuwa amepiga magoti na kuinama kwa mbele huku akilia kilio ambacho kilikosa kabisa tafsiri, alikuwa akichezeshwa kwata na Jacob aliyekuwa amesimama nyuma yake, na wote wawili walikuwa katika sayari ya mbali ya mahaba mazito yasiyo na staha.

Kwa nukta kadhaa moyo wa Jacky ulisahahu mapigo yake, na yalipoanza tena alivuta pumzi ndefu, akazishusha. Alijikuta akishindwa kusogea hata hatua moja na kubaki kumkodolea macho yule msichana aliyekuwa amepiga magoti kwenye sofa akichezeshwa dombolo ya solo na Jacob.

Jacky alimwangalia kwa makini akijaribu kukumbuka ni wapi alipopata kumwona msichana huyo, kwani alikuwa na hakika sura yake haikuwa ngeni machoni kwake ila hakukumbuka alimwona wapi!

“Jacob!” Jacky alijikuta akiita kwa hasira huku akiendelea kuwakodolea macho. Jacob na Diana waliokuwa wamemezwa na ulimwengu filauni walishtuka na kugeuka kumtazama Jacky, na hapo wakakutana na sura ya Jacky iliyojaa hasira.

Jacky akamuona vizuri yule msichana aliyekuwa anachezeshwa kwasakwasa na kila aina ya mitindo na kumtambua. Mshtuko wa Jacky uliongezeka mara dufu baada ya kumtambua Diana kuwa ndiye aliyekuwa akijivinjari na Jacob, na hapo mwili wake ulianza kumtetemeka zaidi kwa hasira.

Jacob na Diana walipatwa na mshtuko mkubwa sana kumuona Jacky akiwa amesimama mbele yao akiwatazama kwa hasira, hawakutegemea kabisa kumuona pale muda ule.

“Oh my God, Diana!” Jacky aling’aka huku akimkodolea macho Diana akiwa haamini macho yake.

“What are you doing here, Jackline?” (Unafanya nini hapa, Jackline?) Jacob alimuuliza Jacky kwa ukali huku jasho jingi likimtiririka. Diana alibaki akimkodolea macho Jacky pasipo kusema neno, aliogopa sana kwani alimjua Jacky kuwa mkorofi sana, na kama angeamua kuanzisha timbwili pale basi hakuna mtu ambaye angeweza kumzuia. Angeweza kuwatandika wote kama watoto wadogo kutoka na mafunzo maalumu ya sanaa ya mapigano aliyokuwa ameyapata.

Jacky hakujibu badala yake alibaki kimya akiwatazama kwa makini huku akionekana kupatwa na fadhaa kubwa, aliminya midomo yake huku akishindwa kuendelea kuwatazama na kuinamisha kichwa chake. Kisha msirimbi wa kipaji cha uso wake ukaumuka, milizamu ikatutusika chini ya masikio yake kama iliyopulizwa, na mara kikamtoka kikohozi kikubwa na michirizi ya machozi ikapasuka machoni mwake.

Sidhani kama kuna haja ya kukueleza (msomaji wangu) jinsi ambavyo Jacky alihisi moyoni mwake muda ule, bali waweza kukisia. Huenda yalikukuta kama hayo kwa mtu mmoja huko mtaani kwenu.

Je, ulihisije? Pole sana! Na kama hayajakukuta, mshukuru Mungu wako na umlaaani shetani yasikukute, maana kijasho kitakutoka na utatamani ardhi ipasuke ikumeze mzima mzima. Mambo haya ni mazuri hivi uyasomapo tu lakini yakikukuta ni mateso makubwa moyoni!

Jacky aliishiwa kabisa nguvu, hakutaka kuendelea kusimama pale akiyashuhudia yale mambo machafu ya kifilauni yakifanyika kati ya mpenzi wake Jacob na rafiki yake Diana, hivyo kwa unyonge aligeuka na kutoka nje taratibu, akaufungua mlango na kusubiri teksi yoyote ambayo ingepita.

Haukupita muda mrefu aliiona teksi moja ikija, akaisimamisha na kuingia, kisha akamwelekeza dereva sehemu ya kumpeleka.

Alichokifanya tu mara alipofika nyumbani kwake ni kuingia chumbani na kujilaza kitandani huku akihisi maumivu makali ya kichwa kutokana na kulia sana kwa uchungu. Pale kitandani alimwaza Diana tu, msichana filauni kabisa, aliyeamua bila haya kujivinjari na shemeji yake, mbaya zaidi alikuwa akimlisha Jacob ‘kisamvu cha kopo’.

“I’ve found Jacob several times with some girls and I forgave him because I love him, but to find him and the cursed Diana, I’ll never forgive them…” (Nimewahi kumfumania Jacob mara kadhaa na wasichana na nikamsamehe kwa sababu nampenda, ila kumkuta na yule mlaaniwa Diana, siwezi kuwasamehe abadani…) Jacky alijisemea kimoyomoyo alipokuwa kalala pale kitandani.

Jacky hakuishia kumlaani Diana tu bali alianza kumlaumu Jacob kwa kuanzisha uhusiano na Diana hali akijua fika urafiki wao ulivyokuwa, jinsi Jacky alivyozidi kuwaza ndivyo alivyozidi kupandwa na hasira, akataka kutoka amwendee Diana nyumbani kwake akamchambe, na ikiwezekana amtembezee mkong’oto.

“Even if I go to her, what will I do? If I’ve failed to do anything when I found her in Jacob's house, what will I do then?” (Hata nikimwendea, nitamfanya nini? Kama nimeshindwa kumfanya chochote nilipomfumania kwa Jacob huko kwake nitafanya nini?) Jacky alijiuliza na kukosa jibu.

“From now on I’ll stop Diana, I don't want to see her again, it’s clear that she’s not a good friend of mine. Even Jacob I don’t want to see him, because he doesn’t love me but he’s just using me,” (Kuanzia leo nitamkomesha Diana, sitaki kumuona tena, kanidhihirishia wazi kuwa si rafiki mwema kwangu. Hata huyo Jacob pia sitaki kumuona, kwani hanipendi bali ananitumia tu) Jacky aliendelea kuwaza.

Hata hivyo, swali moja lilikuwa linamtesa Jacky, alijiuliza angewezaje kuepuka asimuone Jacob ilhali walikuwa wakifanya kazi ofisi moja? Alifikiria sana na mwishowe akaamua kuacha kazi kwani asingeweza kuvumilia kumuona Jacob kila siku baada ya kushuhudia kitendo kile alichomfanyia.

Zilipita siku tatu Jacky akishinda nyumbani tu bila kwenda kazini na hata Jacob alipojaribu kumpigia simu alikuwa hapokei na alipoona kero imezidi aliamua kuzima simu. Pia Jacob alikuwa akituma ujumbe wa kuomba msamaha lakini Jacky aliufuta pasipo hata kuusoma.

Hatimaye siku ya tatu aliamua kuandika barua ya kuacha kazi na kumtafuta mfanyakazi mmoja wa ofisini kwao akampa ile barua ili aipeleke kwa bosi wake na yeye kuamua kuelekea Arusha, alibadilisha kabisa namba yake ya simu.

Huko Arusha hakuchelewa akapata kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), na taratibu akaanza kumsahau Jacob. Baada ya miezi mitano tu tangu kuanza kazi pale AICC ndipo akakutana na Carlos…

______

Simu kutoka kwa Carlos ndiyo iliyomzindua Jacky kutoka kwenye lindi la mawazo. Jacky aliitazama kwa makini simu yake na kuipokea kisha akaiweka sikioni.

“Yes darling…” Jacky aliongea kwa mbwembwe mara tu baada ya kuiweka simu sikioni.

“Have you seen that information on WhatsApp?” (Umeona hiyo habari kwenye WhatsApp?) sauti ya Carlos iliongea upande wa pili wa simu.

“No, what information?” (Hapana, habari gani?) Jacky aliuliza kwa wasiwasi huku akiikodolea macho simu yake kana kwamba alikuwa ameshika bomu lililokuwa lilipuke muda wowote.

“About today's theft in the bank…” (Kuhusu wizi wa leo katika benki…) sauti ya Carlos ilipenya kwenye ngoma ya sikio la Jacky na kumfanya ahisi kizunguzungu.

“What?” Jacky alijikuta aking’aka na kukata simu kisha alifungua katika sehemu ya ujumbe wa WhatsApp kuangalia. Hapo akakutana na taarifa iliyokuwa ikisambaa kwa kasi kwenye makundi mbalimbali ya WhatsApp kuhusu wizi wa mabilioni katika Benki ya Biashara:

Taarifa ile ilieleza kwa kifupi kuhusu wizi wa mabilioni ya fedha katika Benki ya Biashara na wafanyakazi kadhaa walikuwa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano. Taarifa ile ilisema Mzungu akiwa na Waswahili wawili waliingia benki na kusomba mabilioni huku ikiambatana na kipande kifupi cha picha ya video kikiwaonesha wanaume watatu ambao sura zao hazikuonekana sawasawa wakitoka benki na kuingia kwenye gari aina ya Ford Transit lenye nembo ya NeoVision Security.

Jacky alitweta, alikikodolea macho kile kipande cha picha ya video akiwa hajui afanye nini, mara akaikumbuka kauli ya Jacob aliposema kuwa alikuwa anaelekea kituo cha polisi kumuona rafiki yake alikuwa amekamatwa.

* * * * *

Kwenye chumba maalumu cha mahojiano katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam, Yusuf alikuwa ameketi kwenye kiti akihojiwa na mbele yake kulikuwa na meza ndefu yenye umbo mstatili.

Nyuma ya ile meza kulikuwa na wanaume wawili shupavu, maofisa wa polisi ambao kati yao mmoja alikuwa amevaa sare maalumu za jeshi la polisi na juu ya mabega yake kulikuwa na alama ya nyota tatu zilizoonesha cheo chake kuwa alikuwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi.

Ofisa huyo wa polisi aliitwa Ibrahim Komba, au kwa kifupi ASP Komba, alikuwa bado kijana na umri wake ulikuwa miaka therathini na mbili, japo alikuwa amevaa sare za jeshi la polisi lakini alionekana mtanashati sana.

Alikuwa na urefu wa takriban futi sita, akiwa na umbo kakamavu la kimichezo lililomfanya aonekane kama wachezaji wa ligi ya mpira wa kikapu wa Marekani.

Ofisa wa pili wa polisi alikuwa amevaa nguo za kiraia na alikuwa pembeni ya ASP Komba. Yeye alikuwa na cheo cha “V” tatu na aliitwa Venance Mapambano, maarufu kama Sajenti Mapambano, alikuwa askari wa upelelezi, maarufu kama askari kanzu.

Sajenti Mapambano alikuwa mrefu na mwembamba ila mwenye mwili ulio imara, akionekana kuwa alikuwa amepitia na kuhitimu vizuri mafunzo maalumu ya kijeshi na sanaa ya mapigano.

Wale maofisa wa polisi walikuwa wameketi kwenye viti vyao na macho yao yote yalikuwa yakimtazama Yusuf kwa makini kama yaliyokuwa yakijaribu kusoma mawazo yake. juu ya ile meza kulikuwa na mashine ndogo ya kurekodia sauti.

Yusuf aliyatembeza macho yake taratibu kuwatazama wale maofisa wa polisi kwa zamu kabla ya kuweka kituo kwa ASP Komba ambaye alikuwa ameketi mbele yake wakitazamana.

Hakuwa na shaka yoyote kuwa alikuwa amefikishwa kwenye chumba kile kwa sababu moja muhimu ya mahojiano kuhusiana na sakata la wizi wa shilingi bilioni moja na milioni mia tatu kutoka katika Benki ya Biashara aliyokuwa akifanya kazi.

Tangu alipofikishwa kwenye kile chumba hakuwa ameulizwa chochote hadi muda ule, kitambo kirefu cha ukimya kilipita akiwa ameketi pale, tumbo lilikuwa likimsokota na mapigo ya moyo wake yalikuwa yanakwenda mbio isivyo kawaida.

ASP Komba alimtazama Yusuf kwa makini kisha aliingiza mkono wake kwenye mfuko wa gwanda lake akionekana kutafuta kitu. Alipotoa mkono ulitoka na pakiti ya sigara kisha akatoa sigara moja na kuibana kwenye pembe ya mdomo wake.

Kisha alianza kuhangaika kutafuta kiberiti chake mfukoni ili ajiwashie ile sigara, hata hivyo Sajenti Mapambano akawahi kutoa kiberiti chake kutoka mfukoni na kumuwashia ile sigara kwenye pembe ya mdomo wake.

Pamoja na tukio lile la kuwashiwa sigara na msaidizi wake Sajenti Mapambano lakini hakukuwa na tashwishwi yoyote katika sura ya ASP Komba, badala yake aliivuta sigara yake kwa utulivu mno kuikoleza moto, kisha alipoitoa mdomoni akapuliza moshi wake pembeni huku akiutazama kwa makini kabla ya macho yake kuweka kituo kwenye uso wa Yusuf.

Baada ya mikupuo kama miwili hivi ya moshi wa sigara Ibrahim Komba aliinua mkono wake wa kulia kumuonesha Yusuf hundi aliyokuwa ameishika mkononi, kisha akabonyeza kitufe fulani kilichokuwa juu ya ile mashine ya kurekodia sauti.

“Tuambie, Yusuf, unakiri kwamba wewe ndiye uliyepokea hundi hii iliyoletwa na hao watu watatu unaosema kuwa hujapata kuwaona hata siku moja?” ASP Komba aliuliza kwa sauti tulivu huku akiwa amemkazia macho Yusuf pasipo kupepesa macho yake.

“Ndiyo, afande,” Yusuf alijibu kwa huzuni.

“Uliwezaje kuidhinisha kiasi kikubwa vile cha fedha kitolewe kwa watu unaokiri kuwa hukuwahi kuwaona?” ASP Komba aliuliza tena huku macho yake yakiwa bado yameweka kituo kwenye uso wa Yusuf yakimtazama kwa uyakinifu.

“Lakini sikuidhinisha mimi, afande,” Yusuf aliongea kwa utulivu akijaribu kujitetea.

“Ni nani mwingine aliyeidhinisha?” ASP Komba alimuuliza Yusuf huku akiiweka tena sigara yake kwenye pembe ya mdomo wake na kupiga mkupuo mmoja wa moshi wa sigara.

“Meneja wa tawi, hata ukiangalia utaiona saini yake iko hapo hapo.”

ASP Komba aliinamisha macho yake akaitazama ile hundi kwa umakini sana, kikapita kitambo kifupi cha ukimya kisha akainua tena uso wake na kumkazia macho Yusuf.

“Wewe na meneja wako wa tawi ni nani aliyeanza kuweka saini katika hundi hii?” ASP Komba akauliza swali jingine kwa sauti tulivu lakini iliyokuwa ikiyatetemesha maini ya Yusuf.

“Ni mimi, afande…” Yusuf alijibu huku akionesha wasiwasi mkubwa.

“Kwa nini asianze meneja wako wa tawi na badala yake ukaanza wewe?”

“Yeye mara nyingi anakuwa na shughuli nyingi huko ndani, hivyo masuala ya wateja huwa anatutegemea zaidi sisi.”

“Ndiyo kusema kama wewe usingeisaini hii hundi, yeye pia asingesaini, kweli si kweli?” ASP Komba alikuwa makini zaidi kumtazama Yusuf wakati alipokuwa akimuuliza Yusuf maswali.

Yusuf alifungua mdomo wake kutaka kujibu lakini sauti yake haikutoka, akabaki kimya akimtumbulia macho yule ofisa wa polisi kwa hofu. Kitambo kifupi cha ukimya kikapita mle ndani huku wote wakitazamana kwa makini bila kusema neno, kisha ASP Komba baada ya kukung’uta majivu ya sigara pembeni aliongea huku hasira ikionekana kuchipua taratibu machoni mwake.

“Unajua, uongo ni suluhisho la muda mfupi sana katika kutatua tatizo la kudumu… sipendi kutumia nguvu ili kukufanya uzungumze, lakini ukinilazimisha ninaweza kutumia nguvu kwani huwa siwavumilii kabisa watu waongo…” ASP Komba alisema kwa sauti tulivu huku tabasamu la kinyama likichanua usoni kwake.

Yusuf alionekana kushikwa na wasiwasi na kuinamisha kichwa chake chini huku donge la fadhaa likimkaba kooni na kumfanya ashindwe kupumua vizuri.

“Nakuuliza tena, kama wewe usingeisaini hii hundi, meneja wako wa tawi pia asingesaini, kweli si kweli?” ASP Komba aliuliza kwa sauti ya juu kidogo iliyoonesha ukali.

“Kweli!” hatimaye Yusuf alijibu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

ASP Komba alibetua kichwa chake huku akipiga mkupuo mkubwa wa moshi wa sigara, alitulia kidogo akionekana kutafakari kisha akapuliza moshi mwingi pembeni.

“Una mke?” ASP Komba alimuuliza Yusuf huku akiwa amemtulizia macho yake usoni.

“Ndiyo, na mtoto mmoja,” Yusuf alijibu kwa utulivu na unyonge huku akimtazama yule ofisa wa polisi kwa huzuni.

“Utaipa shida familia yako,” ASP Komba alisema huku akimkazia macho Yusuf kwa umakini zaidi kisha akatingisha kichwa chake kumsikitikia.

“Lakini mimi sihusiki kabisa, afande, wala sijui lolote,” Yusuf alizidi kujitetea huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani. Wakati huo machozi yalianza kumlengalenga kwenye macho yake.

“Sijasema kuwa wewe unahusika au unajua lolote, lakini nina kila sababu ya kuamini kwamba unaweza kuisaidia polisi katika wizi huu, kwani wewe ndiye uliyewaona vizuri hao wahalifu,” ASP Komba alisema huku akiminya midomo yake.

“Afande, naomba uniamini, mimi siwafahamu kabisa…”

ASP Komba aliizima ile mashine ya kurekodia sauti huku akitingisha kichwa chake kwa huzuni, aliendelea kuminya midomo yake na baada ya sekunde chache aliruhusu tabasamu la kifedhuli kuchanua usoni kwake, kisha aligeuza shingo yake kumtazama Inspekta Mapambano na kuonesha ishara fulani ya kichwa.

Sajenti Mapambano alisimama kwa ukakamavu na kuzunguka ile meza akimsogelea Yusuf, kisha alimshika na kumnyanyua kwa nguvu kama vile alikuwa akinyanyua kipeto cha sufi.

“Kabla hujamweka korokoroni, hakikisha unaorodhesha vitu vyake vyote,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akiuma mdomo wake wa chini.

Kusikia hivyo, Yusuf aliishiwa kabisa nguvu akionekana kupatwa na mshtuko mkubwa, muda ule ule aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa simu yake aina ya Tekno Spark K9.

“Afande, naomba nimpe jamaa yangu yupo hapo nje hii simu ili aondoke nayo,” Yusuf alisihi kwa sauti ya kubembeleza huku akimtazama ASP Komba kwa wasiwasi.

ASP Komba alimtazama Yusuf huku tabasamu la kifedhuli likizidi kuchanua usoni kwake, kisha aliangua akicheko hafifu. “Kwa hiyo sisi hutuamini, siyo?” ASP Komba alimuuliza Yusuf huku akiendelea kucheka.

“Nawaamini, afande, lakini…”

“Kama unatuamini iache hapa hapa, kwanza hatukuruhusu utoke tena nje,” ASP Komba alisema huku akikunja sura yake iliyotengeneza ndita.

Yusuf alionekana kunywea na kuishiwa kabisa nguvu, baridi nyepesi ya mshtuko wa hofu ikasambaa mwilini mwake na nywele zake zilimsimama kichwani huku koo lake likimkauka.

Sajenti Mapambano alimshika Yusuf kwa nguvu na kumuongoza akimtoa nje ya kile chumba cha mahojiano. Wakatoka wakimwacha ASP Komba akiwa bado ameketi katika kile chumba peke yake huku akitafakari kwa kina.

Kisha ASP Komba na Sajenti Mapambano waliwahoji watu wengine wanne wakiwemo wale askari wawili wa ulinzi waliokuwa zamu siku ile pale benki na wafanyakazi wawili walioshuhudia kwa ukaribu wakati wale watu watatu wakiingia mle Benki ya Biashara na kutoka.

Wakati akiwahoji baadhi ya wafanyakazi na wale askari wa ulinzi, ASP Komba alishindwa kuwahoji akiwa ameketi kitini pake, hivyo akawa anarandaranda mle chumbani.

“Nataka mkumbuke vizuri…” ASP Komba aliwaambia huku akiwakazia macho.

“Ninyi wawili, isipokuwa askari wa ulinzi, mlikuwamo mle benki wakati hawa jamaa watatu wanasimama pale kaunta na kumkabidhi Yusuf hundi kabla hawajatoka na fedha. Pamoja na kuwa kulikuwa na wateja wengi nanyi mlikuwa mkishughulika na wateja wengine, lakini mnaweza kukumbuka vitu viwili vitatu juu ya watu hawa, sura zao, kwa mfano, urefu wao, sauti zao… na vitu kama hivyo,” ASP Komba alinyamaza kidogo, akawatazama mmoja mmoja.

Kisha akaendelea, “Hebu wewe Pauline, umesema ulikuwa karibu zaidi, nieleze unavyoweza kuwakumbuka,” alimuuliza mfanyakazi mmoja wa kike ambaye wakati kina Kisu wanaingia benki alikuwa amesimama kaunta ya jirani na alipokuwepo Yusuf.

Pauline alitoa kikohozi cha chini chini, akaketi vema, “Wote watatu walikuwa wamevaa miwani myeusi iliyoonesha kuficha macho yao, walikuwa wakakamavu na yule mmoja wao aliyekuwa anaburuza begi la magurudumu ndiye alisimama karibu sana na dirisha langu.”

“Kwa hiyo ulimchunguza vizuri?”

“Alikuwa jasiri sana, afande, isitoshe sikujua kama hawakuwa raia wema,” Pauline alisema.

“Nimekuelewa, nimekuelewa,” ASP Komba alimkatiza. “Hebu jaribuni kukumbuka vitu vingine juu ya hawa watatu… kama kumbukumbu zenu ni nzuri.”

Kijana mmoja aliyeitwa Elibariki alijiinamia kwa dakika nzima bila kusema lolote. Alipoinua uso wake alionekana kukumbuka kitu. “Kuna yule mzungu, nahisi kama hakuwa mzungu ila ni mweupe tu, na hata zile nywele zake zilizokuwa zimelalia mgongoni nadhani zilikuwa nywele za bandia…”

ASP Komba alimtazama Elibariki kwa kitambo kirefu bila kukupesa macho. “Una uhakika?” hatimaye alimuuliza ili kujiridhisha.

“Ndiyo afande, nina uhakika hakuwa mzungu na inawezekana alikuwa na upara, ni kama nimewahi kumuona sehemu fulani hivi,” Elibariki alijibu bila hata kufikiria.

Baada ya mahojiano yaliyochukua takriban dakika ishirini ASP aliwaruhusu kuondoka lakini akawataka kufika kituoni kila watakapohitajika. Waliondoka na kumwacha akifikiria sana kuhusu yale maelezo. Kisha aliishika ile simu ya Yusuf na kuitazama kwa makini huku akiigeuza geuza katika namna ya kuichunguza kwa makini.

Kisha aliiwasha na kuanza kuzipitia namba za simu zilizopigwa na majina yaliyokuwa yameorodheshwa kwenye ile simu. Wakati akiyapitia yale majina, baadhi ya majina alionekana kuyatilia shaka na hivyo alikuwa akiyaandika pembeni kwenye notebook yake.

Alichukua muda mrefu akizichunguza zile namba kwenye ile simu, na wakati akiendelea na uchunguzi ule mara mlango wa kile chumba cha mahojiano ukagongwa na kumfanya ageuke kuutazama kule mlangoni.

Muda ule ule mlango ukafunguliwa na hapo akaingia Sajenti Mapambano akiwa ameongozana na Nassos Chatzopoulos. ASP Komba alimtazama Nassos kwa makini na kumuonesha sehemu ya kuketi. Kwa mkono

Nassos aliketi kimya akiwa na wasiwasi kidogo huku akimtazama ASP Komba kwa umakini zaidi. ASP Komba aliendelea kuzipitia zile namba za simu kwenye ile simu ya Yusuf na baadaye alifungua sehemu ya ujumbe mfupi na kuanza kusoma ujumbe uliokuwa umetumwa katika ile simu.

Alisoma ujumbe kwa umakini huku akizinakiri baadhi ya namba za simu zilizokuwa zimetumika kutuma ule ujumbe na kuandika taarifa fulani kwenye kitabu chake kidogo na alipomaliza kuandika aliinua uso wake kumtazama Nassos huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“You’re welcome,” (Karibu sana) ASP Komba alimkaribisha Nassos kana kwamba ndiyo alikuwa amemuona kwa mara ya kwanza.

“Thank you, officer,” (Ahsante, afande) Nassos alijibu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Do you know Swahili?” (Unajua Kiswahili?) ASP Komba alimuuliza huku akimtulizia macho.

“Yes, but a little, officer,” (Ndiyo, lakini kidogo, afande) Nassos alijibu kwa kujiamini.

“Are you the chief executive director of The Jacarandah Group, right?” (Wewe ndiye mkurugenzi mtendaji wa The Jacarandah Group, sawa?) ASP Komba alimuuliza Nassos huku akiwa amemtulizia macho yake usoni pasipo kupepesa.

“Yes, officer,” (Ndiyo, afande) Nassos alisema huku akilamba midomo yake iliyoanza kukauka.

Itaendelea...Kizungumkuti! - 48

Na Bishop Hiluka

“I’ve information that you went to the Commercial Bank four days ago to put a large amount of money, and the next day you took a certain amount of money… Do you remember the amount of money you took that day?” (Ninazo taarifa kwamba ulifika pale Benki ya Biashara siku nne zilizopita kuweka kiasi kikubwa cha pesa, kisha kesho yake ukatoa kiasi fulani cha pesa… Je, unakumbuka idadi ya pesa ulizochukua siku hiyo?)

“I took only four hundred million shillings, officer.” (Nilichukua shilingi milioni mia nne tu, afande).

“Since that day you’ve never signed in any check from your office?” (Tangu siku ile hujatia tena saini katika hundi yoyote ya ofisini kwenu?)

“Not yet!” (Bado!)

ASP Komba aliminya midomo yake na kushusha pumzi za ndani kwa ndani akionekana kutafakari kidogo, kisha alinyoosha mkono wake kumpa Nassos ile hundi.

“Can you look well and identify for those signatures?” (Unaweza kuziangalia vizuri na kuzitambua hizo saini hapo?) ASP Komba alisema huku kamkazia macho Nassos. Nassos aliipokea ile hundi na kuitazama kwa makini, alitingisha kichwa chake kwa huzuni huku akishusha pumzi ndefu.

“I’m very shocked, this one is my very signature, but I did not sign in this check!” (Imenishangaza sana, afande, hii moja ni saini yangu kabisa, lakini mimi sikutia saini kwenye hundi hii!) Nassos alisema kwa masikitiko huku akimrudishia ASP Komba ile hundi.

“And who’s this other sign?” (Na hii saini nyingine ni ya nani?) ASP Komba aliuliza.

“It belongs to my accountant, Japhet Lutego, but I'm sure he didn't sign this check,” (Ni ya aliyekuwa mhasibu wangu, Japhet Lutego, lakini nina uhakika pia yeye hakusaini hundi hii) Nassos alisema kwa kujiamini.

“Why are you sure that he was not the one who signed?” (Kwa nini una uhakika kuwa si mhasibu wako aliyesaini?)

“Because he has traveled to Sweden since last week, and if he’d have been involved in this scandal he’d have not left before this robbery. He’d have possibly waited for his portion.” (Kwa sababu amesafiri tangu wiki iliyopita kwenda masomoni Sweden, na angekuwa ameshiriki kwenye kashfa hii asingeondoka kabla wizi huu mkubwa haujafanyika. Kwa vyovyote angesubiri mgawo wake).

“How do you know, maybe he decided to travel before this robbery just to complicate the evidence that he was involved and he might ask them to send his portion there where he went?” (Unajuaje, pengine aliamua kusafiri kabla ya wizi huu ili kupoteza ushahidi kuwa alishiriki na huenda aliomba atumiwe mgawo wake huko huko alikokwenda?) ASP Komba aliuliza tena huku akikunja sura yake.

Nassos alikunja sura yake kutafakari kidogo, kikapita kitambo kifupi cha ukimya kisha alitingisha kichwa chake kukataa.

“I don't think so… anyway, I don't know,” (Sidhani… hata hivyo, siwezi kujua) Nassos alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Kilipita tena kitambo kifupi cha ukimya, ASP Komba alimtazama Nassos kwa huku akitafakari, kisha alikohoa kidogo kusafisha koo lake. “Tell me, who exactly is keeping your check book?” (Hebu niambie, ni nani hasa anayetunza kitabu cha hundi ofisini kwenu?)

“It's me!” (Ni mimi!) Nassos alijibu.

“Do you lock it or leave with it?” (Huwa unakifungia kabatini au unaondoka nacho?)

“I don't lock it or leave with it, it's always on my table…” (Sikifungii wala siondoki nacho, mara nyingi huwa kipo juu ya meza yangu…)

“Who enters your office regularly?” (Ni nani anayeingia ofisini kwako mara kwa mara?)

“I don't allow people to go into my office, and if a person needs a loan we have a system that he or she’d meet my accountant and then all procedures are followed…” (Huwa siruhusu watu kuingia ofisini kwangu, na kama mtu anahitaji mkopo tuna utaratibu kwamba aonane na mhasibu wangu na kisha taratibu zote hufuatwa…) Nassos alisema kwa utulivu.

Kikapita tena kitambo kifupi cha ukimya, Nassos alikuwa ameinamisha kichwa chake akitafakari kidogo, mara alionekana kugutuka na kuinua uso wake kumtazama ASP Komba.

ASP Komba ambaye muda wote alikuwa akimtazama Nassos kwa makini aliingiwa na shauku baada ya kumuona Nassos akigutuka na kumkazia macho.

“Is there anything you want to share with me?” (Kuna kitu unataka kunishirikisha?) ASP Komba aliuliza kwa shauku.

“I remember, there is only one person who is free to enter my office at any time, but I don't think if she can be involved with a big deal like this…” (Nimekumbuka, kuna mtu mmoja tu ambaye huwa yuko huru kuingia ofisini kwangu saa yoyote, lakini sidhani kama anaweza kuhusika na njama kubwa kiasi hiki…) Nassos alisema huku akikunja sura yake.

“Who is she?” (Ni nani?) ASP Komba aliuliza tena kwa shauku.

“Her name is Jasmine Kombo. She deals with the cleanliness of my office.” (Anaitwa Jasmine Kombo. Yeye hushughulikia usafi wa ofisi yangu.)

ASP Komba aliinamisha uso wake kwenye notebook yake na kuandika maelezo mafupi huku akilipigia mstari jina la Jasmine, kisha akamkazia macho Nassos.

“How long have you worked with Jasmine?” (Umefanya kazi na Jasmine kwa muda gani sasa?)

“This is the fifth year now,” (Huu mwaka wa tano sasa) Nassos alijibu baada ya kufikiria kidogo.

“Can I have an interrogation with her?” (Naweza kumpata ili nimhoji?)

“I wonder, today is the third day she has not come to work and I’ve no information, I don't know what has happened to her!” (Nashangaa, leo ni siku ya tatu hajafika kazini na sina taarifa zake, sijui amepatwa na nini!) Nassos alisema huku akinyanyua juu mabega yake juu kuonesha kuwa hajui.

Maelezo ya Nassos yakamfanya ASP Komba aweke kituo na kumtazama Nassos kwa macho yaliyoonesha kuhisi jambo lisilo la kawaida. Aligeuza kichwa chake kumtazama Sajenti Mapambano, kisha aliyarudisha tena macho yake kwa Nassos.

“Your employee has not come to work without notice for three days and you’re not worried even to look for her! Don't you see this is not normal?” (Mfanyakazi wako hajatokea kazini pasipo taarifa kwa siku tatu na wala hujahangaika kumtafuta! Huoni kama hili si jambo la kawaida?) ASP Komba aliuliza huku akivuta sigara yake kwa mara mwisho na kuupuliza moshi pembeni.

Kisha alikitupa chini kile kipisi cha sigara kilichokuwa mbioni kuunguza vidole vyake na kukizima kwa kukikanyaga na buti lake.

“I was really very busy and I didn't think anything wrong would happen.” (Kwa kweli nilitingwa sana na sikufikiria kama jambo lolote baya lingeweza kutokea.)

“Do you know where Jasmine lives?” (Je, unajua Jasmine anaishi wapi?) ASP Komba aliuliza tena huku akiwa ameyatuliza macho yake kwenye uso wa Nassos.

“No, but there is one employee who knows her location, unfortunately today she is off until tomorrow,” (Hapana, ila yupo mfanyakazi mmoja ambaye anafahamu nyumbani kwake, bahati mbaya leo hayupo kazini hadi kesho) Nassos alisema baada ya kufikiria kidogo.

“What’s her name?” (Anaitwa nani?)

“Zena Chande. They’re great friends.” (Zena Chande. Ni marafiki wakubwa).

“Okay, you can go, I’ll call you whenever I get new information or need help from you.” (Sawa, unaweza kwenda, nitakupigia simu kila nitakapopata taarifa mpya au nikihitaji msaada kutoka kwako).

“No problem, officer, I’m available at any time,” (Hakuna neno, afande, napatikana muda wowote) Nassos alisema huku akiinuka na kunyoosha mkono wake kumpa ASP Komba. Wakaagana kisha Nassos akatoka akiwaacha ASP Komba na Sajenti Mapambano wakiangaliana.

“Hapa kuna mchezo umechezwa ofisini kwake bila yeye kujua, nina wasiwasi na watu wawili, kama siyo mhasibu wake basi ni yule binti Jasmine,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano.

“Kwa Jasmine sidhani, ila kwa yule mhasibu inawezekana, maana aliyefanya wizi huu siyo mtu wa kawaida, he must be a professional bank criminal,” Sajenti Mapambano alisema na kumfanya ASP Komba abetue kichwa chake kukubaliana naye.

“Nadhani baadaye tukizitazama kwa umakini mkubwa zile clip za video kutoka kwenye kamera za usalama zilizoko ndani nan je ya lile jengo la benki tutaweza kugundua kitu zaidi, I’m very sure tutaweza kubaini kitu,” Sajenti Mapambano alisisitiza.

ASP Komba alibetua kichwa chake kukubaliana na maneno ya Sajenti Mapambano huku akizama kwenye tafakari, kisha kama aliyegutuka akamkazia macho Sajenti Mapambano.

“Sasa nenda kamlete yule meneja wa tawi la benki ulikofanyika wizi,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akitoa pakiti ya sigara kisha akatoa sigara moja na kuibana kwenye pembe ya mdomo wake.

Sajenti Mapambano aliinuka na kutoka nje huku akimwacha ASP Komba anajiwashia ile sigara na kuanza kuvuta taratibu huku akitoa moshi na kuutazama kwa makini.

* * * * *

Saa nane na robo mchana Jacky alikuwa amejilaza kwenye sofa kubwa la sebuleni nyumbani kwake Segerea, alikuwa peke yake, kimya kabisa, akijaribu kutafakari hili na lile pasipo kupata majibu. Ni dhahiri kuwa kusambaa haraka kwa taarifa zile za wizi wa mabilioni katika Benki ya Biashara zilikuwa zimemshtua kidogo.

Hakuwa ametarajia kabisa kama taarifa za wizi ule zingeweza kujulikana katika muda mfupi sana kiasi kile, na wala hakujua ni nani aliyekuwa amefichua kuhusu wizi ule. Kilichomtia hofu zaidi Jacky ni suala la kukamatwa kwa Yusuf, aliamini kuwa endapo maofisa wa polisi wangembana kidogo tu wasingepata taabu kuupata ukweli kwani angetapika siri zote akidhani kusema ukweli kungemfanya apunguziwe adhabu.

Kutokana na mshtuko aliokuwa ameupata baada ya kuona clip za video kwenye makundi kadhaa ya WhatsApp, Jacky hakujua alifikaje pale nyumbani kwake, alichokumbuka ni kuwa alijibwaga pale kwenye sofa kubwa sebuleni baada ya kuegesha gari lake kwenye eneo maalumu la maegesho. Hii ilikuwa ni baada ya kuachana na Jacob pale Uhasibu.

Carlos hakuwepo nyumbani na wala Jacky hakuwa amemjulisha kuwa hangerejea kule kwenye nyumba ya Mtoni Kijichi. Jacky alitulia pale kwenye sofa akitafakari, mara akakumbuka jambo na kuanza kuitafuta ile kadi aliyokuwa amepewa na Jacob.

Baada ya kuitafuta kwa sekunde kadhaa hatimaye aliipata kwenye mkoba wake na kuzinakiri namba za simu ya Jacob kisha akapiga na kuiweka simu sikioni. Aliisikia simu ikiita upande wa pili na baada ya kitambo kifupi ikapokelewa.

“Hello!” sauti nzito ya Jacob ilisikika ikizungumza kutokea upande wa pili wa simu. Kimya! Jacky alitaka kuitikia lakini akasita huku akijiuliza aseme nini, maana hadi muda ule alipoamua kumpigia Jacob simu hakujua alitaka kumweleza nini. Zikapita sekunde kadhaa bila ile simu kujibiwa, Jacob akaonekana kushangaa kidogo huku akiitazama simu yake kwa wasiwasi.

“Hello! Who is this?” (Halo! Nani mwenzangu?) Jacob aliuliza kwa wasiwasi baada ya kusikia sauti ya mtu upande wa pili wa simu akivuta pumzi ndefu.

“Hello, Jacob, it’s me Jacky…” (Halo, Jacob, ni mimi Jacky…) Jacky alisema kwa sauti ya unyonge sana iliyoonesha kumshangaza kidogo Jacob.

“Ooh Jackline, tell me my love! Are you okay?” (Oo Jackline, niambie mpenzi! Vipi uko sawa?) Jacob aliuliza kwa sauti yenye wasiwasi kidogo baada ya kuhisi Jacky hakuwa sawa.

“I’m alright… I need to talk to you, where are you?” (Niko sawa… nahitaji kuongea na wewe, sijui uko wapi?) Jacky alimuuliza Jacob kwa sauti yenye wasiwasi kidogo.

“Is there any problem? You sound so strange today. It seems like you’re nervous! What’s wrong my love?” (Vipi kuna tatizo? Sauti yako inaashiria kuwa hauko sawa leo. Ni kama vile una wasiwasi! Vipi kuna tatizo, mpenzi?) Jacob aliuliza maswali mfululizo kwa wasiwasi kidogo baada ya kuhisi sauti ya Jacky haikuwa sawa.

“I’m not tense, but I missed you a lot. Today I've noticed that I still love you… and I’m sure that now my happiness will be back,” (Sina wasiwasi, lakini nilikukumbuka sana. Leo ndiyo nimetambua kuwa bado nakupenda… na nina uhakika kuwa sasa furaha yangu sasa itarudi) Jacky alisema huku akishusha pimzi za ndani kwa ndani.

“Oh, I'm glad to hear that you still love me…” (Ooh, nafurahi kusikia kuwa bado unanipenda…) Jacob alisema huku sauti yake ikionesha wazi jinsi alivyofurahi, hata hivyo Jacky alimkatiza kabla hajamaliza kuongea.

“I need to see you, Jacob,” (Nahitaji kukuona, Jacob) Jacky alisema kwa sauti ya chini.

“Kwa sasa haitawezekana, nawasaidia polisi kushughulikia masuala fulani kuhusiana na wizi uliotokea leo benki, when I finish it, I will let you know, my love, maana hata mimi nimekumiss sana,” Jacob alisema.

“Wizi katika benki?“ Jacky alimuuliza Jacob kwa mshangao kana kwamba alikuwa hajui kilichofanyika.

“Yes, Kuna wizi mkubwa wa mabilioni umetokea leo asubuhi katika Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba, and very unfortunate my friend has been linked to the theft and he is now in police custody,” (…na bahati mbaya sana rafiki yangu wa karibu amehusishwa na wizi huo na sasa yupo mahabusu ya polisi) Jacob alisema na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.

“Which friend of yours?” (Rafiki yako yupi?) Jacky aliuliza huku akibana pumzi zake, kisha akakunja sura yake na kufumba macho.

“You can't know him, his name is Yusuf Akida, we were together at Tambaza Secondary School and later at IFM…” (Huwezi kumfahamu, anaitwa Yusuf Akida nilisoma naye Tambaza Secondary School na baadaye IFM…)

Jacky alihisi kuishiwa na nguvu, mwili wake ulilegea na pumzi zikampaa kisha jasho jepesi likaanza kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake, woga wa aina yake ulianza kumtambaa mwilini na mapigo ya moyo wake yalibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida! Kikapita kitambo fulani cha ukimya.

“Jackline, are you there?” (Jackile, upo kwenye simu?) sauti ya Jacob ndiyo iliyomzindua Jacky.

“Oh… yes… my love,” (Oh… ndiyo… mpenzi) Jacky aliongea kwa kusita sita huku akiwa na mashaka, “So, how do you handle police issues?” (Kwa hiyo, wewe unashughulikiaje masuala kipolisi?)

“The Police Officers have come to our company and ask us to help them explore a some phone numbers they are in doubt, that had been contacted with Yusuf, so I have them here at the office,” (Maofisa wa polisi wamekuja kwenye kampuni yetu na kuomba tuwasaidie kuzichunguza namba fulani za simu wanazozitilia shaka zilizokuwa zikiwasiliana na Yusuf, hivyo niko nao hapa ofisini) Jacob alisema na kumfanya Jacky kuhisi kizunguzungu. Kilipita kitambo kirefu cha ukimya kilichomshangaza Jacob.

“Hello!…” Jacob alianza kusema lakini Jacky akadakia.

“Jacob, I'm very sorry to bother you but I've called you because I have a little problem and I need your help,” (Jacob, samahani sana kwa kukusumbua lakini nimekupigia simu kwa sababu nina tatizo kidogo na ninahitaji sana msaada wako) Jacky alisema huku akishusha pumzi ndefu kama mtu aliyekuwa ametoka kwenye mashindano ya mbio ndefu.

“What problem do you have, my love?” (Una tatizo gani, mpenzi?) Jacob aliuliza kwa wasiwasi kidogo.

“I can't tell you on the phone, if you have time even now we can meet each other wherever you tell me.” (Sintoweza kukueleza katika simu, kama una muda hata sasa hivi tunaweza kuonana popote utakaponiambia).

“As I told you now it’s not possible, I’ll call you later when I leave the office and tell you where we’ll meet, or what do you say, my love?” (Kama nilivyokueleza kwa sasa haiwezekani, nitakupigia simu baadaye nikishatoka ofisini nikuelekeze wapi tutaweza kukutana, au unasemaje, mpenzi?) Jacob alimuuliza Jacky baada ya kufikiri kidogo.

“Okay, I’ll wait for your phone call, please it is very important,” (Okay, nitasubiri simu yako, ni muhimu sana tafadhali) Jacky alisema na kukata simu huku akionesha kukata tamaa, kisha alimeza funda la mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.

Alitafakari kwa sekunde chache akijaribu kuhisi jinsi ambavyo Yusuf alikuwa akitetemeka mbele ya maofisa wa polisi hata kueleza kila kitu alichoulizwa, hata hivyo, Jacky alijipa moyo kuwa polisi asingeweza kuhusishwa na wizi ule kwa kuwa namba aliyokuwa akiitumia haikusajiliwa kwa jina lake halisi, pili Yusuf alimfahamu kama Belinda na hakujua aliishi wapi, na mwisho namba aliyoitumia kuwasiliana na Yusuf aliiwekea uzio kiasi kwamba mtu yeyote asiyebobea katika teknolojia asingeweza kubaini ilikuwa ikipigwa kutokea wapi.

Baada ya kitambo fulani cha kuwaza hili na lile, Jacky alikumbuka kumpigia simu Carlos na kumtaarifu kuhusu yote aliyoyasikia kutoka kwa Jacob, kisha akamweleza kuwa alitarajia kutoka baadaye na huenda angechelewa kurudi nyumbani kwa kuwa ilikuwa ni lazima afuatilie taarifa zote muhimu kuhusiana na upelelezi wa polisi kwenye lile sakata la wizi wa fedha benki.

* * * * *

Jacob alipomaliza kuongea na Jacky aliingia ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ya simu aliyokuwa akiifanyia kazi, alikuwa ametoka nje ya ofisi mara moja kusikiliza ile simu, kwani muda wote alikuwa akitarajia simu kutoka kwa mke na ndugu wa Yusuf waliotaka kujua maendeleo ya dhamana baada ya mkasa ule.

Aliporudi mle ndani alitulia akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wao wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa kampuni aliyekuwa akitoa maelezo kuhusiana na mawasiliano kati ya Yusuf na namba zilizotiliwa shaka.

Hii ilikuwa ni baada ya ASP Komba na Sajenti Mapambano kwenda Makao Makuu ya kampuni ile kubwa ya simu nchini. Ingeweza kuwa rahisi kwa ASP kuzipiga namba zile za simu alizozitilia shaka baada ya kuzipata kutoka kwenye simu ya Yusuf lakini aliamua kufuatilia suala lile mwenyewe katika Ofisi za Makao Makuu ya kampuni ya simu.

Ilikuwa ni nusu saa iliyokuwa imepita ambapo ASP Komba na Sajenti Mapambano walifika kwenye Mapokezi ya ofisi hizo wakiwa wamevaa kiraia, wakasubiri mhudumu amalizane na bwana mmoja, mtu mzima wa Kiasia, kisha wakamfuata. Mhudumu alipowaona aliachia tabasamu pana la makaribisho.

“Karibuni, nikusaidieni nini?” alisema yule mhudumu wa Mapokezi huku akiendelea kutabasamu.

“Tunaomba kumwona Mkurugenzi, tafadhali,” ASP Komba alimweleza yule mhudumu huku naye akiachia tabasamu la kirafiki.

“Mkurugenzi?” yule mhudumu aliuliza kwa mshangao.

“Ndiyo.” ASP Komba alimjibu yule mhudumu huku akimkazia macho. Yule mhudumu alinyamaza kidogo, akapitisha ulimi chini ya mdomo wake wa chini, “Yupi mmojawapo, maana wapo watatu,” aliuliza huku akimtulizia macho ASP Komba.

“Yeyote tu kati yao.”

“Kwani shida yenu ni nini hasa? Kwani hamuwezi kusaidiwa na watu wengine?”

“Kama nani?”

“Inategemea na uzito wa shida yenu.”

ASP Komba aliona mahojiano yangeweza kuchukua muda mrefu, hivyo alitoa kitambulisho chake, akamwekea yule mhudumu mbele ya macho yake.

“Ni masuala ya kazi, dada’angu,” ASP Komba alisema huku akimkazia macho yule mhudumu. Yule mhudumu alipitisha tena ulimi chini ya mdomo safari hii haraka haraka, kisha akameza funda la mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.

“Ngojeni nikupelekeni kwa Mkurugenzi wa Masoko bwana Jacob Haule, nadhani mtaelewana,” yule mhudumu wa Mapokezi alimwambia ASP Komba, ambaye alionekana kushtuka kidogo.

“Ooh, sawa nadhani hata huyo ataweza kutusaidia. Hivi ofisi yake bado iko pale pale ghorofa ya pili, mlango wa tatu, au siyo?” ASP Komba alisema hyuku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ndiyo, kumbe umeshawahi kufika ofisini kwake. Basi nendeni tu, nitamjulisha sekretari wake.”

“Asante, dada,” ASP Komba alisema huku akikirudisha kitambulisho chake mfukoni kisha wakazifuata ngazi za kuelekea juu. Walizikwea zile ngazi hadi ghorofa ya pili, wakaufikia mlango wa ofisi ya Jacob iliyokuwa mkono wa kushoto mara baada ya kumaliza kupanda ngazi za kuingia ghorofa ya pili kwenye korido pana. ASP Komba aliusukuma mlango, wakaingia.

Walipoingia walimkuta katibu wa Jacob, msichana mmoja mrembo ambaye alikuwa ameinamisha uso wake kwenye kompyuta akiandaa taarifa fulani za kiofisi. Walipoingia tu yule msichana aliinua uso wake akawatazama. Ilionekana kuwa tabasamu kwa wateja ilikuwa ni kama sheria kwa wafanyakazi wa kampuni ile ya simu, yule msichana naye aliachia tabasamu bashasha.

“Karibuni sana,” alisema yule msichana huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake kwa adabu.

“Asante, binti, Habari za kazi?” ASP Komba alisema huku akiufunga mlango baada ya Sajenti Mapambano kuingia, kisha akamsogelea yule msichana huku akiachia tabasamu.

“Nzuri, shikamoo,” yule msichana aliwasalimia kwa adabu huku akiwatazama kwa makini.

“Marhaba,” wale maofisa wa polisi waliitikia kwa pamoja.

“Huyu bwana tumemkuta?” ASP Komba alimuuliza huku akiendelea kutabasamu.

“Ndiyo, yupo… subirini kidogo,” yule msichana alisema huku akienda kugonga kwenye mlango wa Jacob mara moja tu kisha akaingia akiwaacha wale maofisa wa polisi bado wamesimama. Kule ndani alimkuta Jacob na kumweleza ujio wa ASP Komba na Sajenti Mapambano.

Jacob alitoka mara moja na kuwakaribisha ASP Komba na Sajenti Mapambano huku akionesha wasiwasi kidogo.

“We are sorry to come here without information, we need your help,” (Samahani kwa kukuvamia hapa bila taarifa, tunahitaji msaada wako) ASP Komba alisema huku akimtulizia macho yake Jacob.

“It’s okay, you’re welcome,” (Haina shida, karibuni) Jacob alisema huku akiwakaribisha ofisini kwake. Wote watatu waliingia ofisini kwa Jacob.

Ilikuwa ni ofisi nzuri na pana yenye mazingira ya nadhifu na yaliyovutia kwa mpangilio wa samani za kisasa, ikiwa na zulia jekundu sakafuni na meza ndefu ya ofisini yenye viti vinne. Viti viwili upande wa kushoto na viti viwili upande wa kulia.

Juu ya meza ile ya ofisini kulikuwa na vitabu na majalada machache yaliyopangwa kwa ustadi pembeni ya kibao kidogo kilichochongwa vizuri kwa maandishi ya kutanabaisha cheo cha Mkurugenzi wa Masoko pamoja na kidau cha wino na mhuri wa ofisi.

Upande wa kulia wa ofisi ile kulikuwa na picha kubwa ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na picha nyingine ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwa zimetundikwa ukutani. Upande wa kushoto kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na majalada mbalimbali na mbele ya ofisi ile ukutani kulikuwa na ramani kubwa ya nchi ya Tanzania iliyoonesha mtandao wa kampuni ile ya simu ulivyoenea nchi nzima.

Jacob aliketi kwa utulivu nyuma ya meza yake kubwa ya ofisini mwisho wa ofisi ile upande wa kushoto akiwa katika uso wa kusawajika kidogo, kisha kwa utulivu akawakaribisha ASP Komba na Sajenti Mapambano waketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa likitazamana na ile meza yake mle ndani.

.

ASP Komba na Sajenti Mapambano waliketi huku macho ya Jacob yakiwatazama kwa udadisi kidogo jinsi walivyokuwa wakiketi kwenye viti. Jacob hakujua kilichokuwa kimewaleta wale maofisa wa polisi pale ofisini kwake, hasa kwa kuwa hakuwa akielewana vizuri na ASP Komba kutokana na Diana.

ASP Komba na Jacob Haule walikuwa marafiki wakubwa utotoni na walisoma darasa moja katika shule ya msingi huko kwao Songea mkoani Ruvuma, lakini urafiki wao ulikuja kuingia doa walipokutana jijini dar es Salaam na ASP Komba kuamua kumuoa Diana wakati akijua fika kuwa alikuwa mpenzi wa Jacob.

Jacob alimtazama ASP Komba akalazimisha tabasamu huku akijaribu kukumbuka kilichokuwa kimetokea saa takriban tatu zilizokuwa zimepita kule kituo cha polisi alipokwenda kutaka kumwekea dhamana Yusuf.

Alikumbuka jinsi ASP Komba alivyomkatalia katakata huku akitingisha kichwa chake kwa nguvu.

“Nani aliyekuambia unaweza kumwekewa dhamana mtu aliyeshirikiana na wezi wakubwa kuiba mabilioni ya fedha benki? Huyu hatoki hapa, si leo wala kesho hadi upelelezi utakapokamilika,” ASP Komba alimweleza Jacob akiwa amekunja sura yake kana kwamba walikuwa hawafahamiani.

“Bwana Komba, mbona maneno mengi, niambie tu moja, kwa hiyo dhamana hamtaki?” Jacob alimwuliza ASP Komba huku akimtulizia macho usoni.

“Hakuna dhamana,” ASP Komba alijibu kwa kifupi huku akiendelea na shughuli zake.

“Kwa nini?” Jacob aliuliza akitaka kujua.

“Kwa nini!” ASP Komba naye alimwuliza Jacob huku akimshangaa.

“Ndiyo, kwa nini? Dhamana ni haki ya kila mtu… Hata kama angekuwa mwuaji,” Jacob alisema kwa sauti tulivu huku akiendelea kumtulizia macho ASP Komba.

“Unanifundisha kazi ndugu yangu, ee?” ASP Komba alisema huku akiyasogeza makaratasi pembeni, akasimama…

______

“Sasa bwana Haule…” sauti ya ASP Komba ilimzindua Jacob kutoka kwenye mawazo yake, akamtazama ASP Komba kwa makini na kuachia tabasamu.

“Nimeshangazwa na ujio wako hapa ofisini, nilikuwa najaribvu kujiuliza sijui kampuni hii tumewakosea nini ndugu zetu wa polisi?” Jacob alisema na kuwafanya waangue kicheko hafifu!

“Wala hamjatukosea lolote, Bwana Haule, usiwe na wasiwasi, kuna jambo muhimu sana lililotulazimisha tuje kwenu kuomba msaada…” ASP Komba alisema huku akijiweka vizuri kwenye sofa. Jacob naye akajiweka vema kitini huku akimtazama kwa makini.

“Kwanza samahani kwa majibu yangu ya asubuhi ulipotaka kumwekea dhamana yule mfanyakazi wa benki, unajua wakati mwingine tunakuwa kwenye tension za…” ASP Komba alianza kusema lakini Jacob alimkatisha.

“Usijali, naelewa… Sasa kabla sijakuuliza ni msaada upi unahitaji, uniambie mpatiwe kinywaji gani?” Jacob alisema kwa sauti tulivu huku macho yake yakiwa hayabanduki kwa ASP Komba.

ASP Komba aliachia tabasamu pana lililomgusa Jacob, “Tunashukuru sana, lakini kwa sasa hatuna kiu ya kinywaji chochote, labda sijui mwenzangu hapa. Sitaki nimsemee…” ASP Komba alisema huku akigeuza shingo yake kumtazama Sajenti Mapambano, ambaye alitingisha kichwa taratibu kukataa.

“Sawa. Basi twende moja kwa moja kwenye hilo lililokuleteni,” Jacob alimweleza ASP Komba huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

ASP Komba alimweleza Jacob msaada waliokuwa wakiuhitaji katika ofisi ile, Jacob akaona suala lile halikuhusiana na ofisi yake, hivyo akawachukua hadi kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ile.

Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni, Zuberi Mwalimu, hakuwa mtu mzima sana, alikuwa na miaka arobaini na mitano hivi, mwenye macho maangavu, uso wa duara na nywele ndogo ndogo alizokuwa amezinyoa mtindo wa low cut.

“Karibuni sana,” Zuberi Mwalimu aliwakaribisha huku akinyoosha mkono wake kwa ASP Komba na baadaye kwa Sajenti Mapambano. Walisalimiana kwa furaha, kisha Jacob akamweleza sababu ya ujio wa wale maofisa wa polisi pale ofisini kwao.

Baada ya maelezo yale yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliinua simu, akamwita Jonas Maganga, mtaalamu wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambaye alikuwa tegemea kubwa katika kampuni ile, baada ya kuondoka kwa Jackline Mgaya.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog