Search This Blog

Monday, 27 March 2023

GARI LA KUKODI (2) - 4

  


Simulizi : Gari La Kukodi (2)

Sehemu Ya Nne (4)



“Pole sana,” Bi. Pamela alisema kwa upole huku akijifuta machozi.


Wakati hayo yanaendelea Madame Norah alikuwa bado amezama kwenye dunia yake, dunia ya kisasi. Sasa alikuwa anahisi kifua chake kikiwaka moto utadhani alikuwa anataka kulipuka! Aliapa kushughulika na yeyote aliyefanya hivyo. Donge la hasira lilikuwa limemkaba kooni na alikuwa anapumua kwa shida kama mgonjwa anayepigania pumzi ya mwisho.


Alichokumbuka kuongea muda huo ilikuwa kuomba ruhusa ya kumwona Sammy kabla hajapelekwa Muhimbili. Wote waliongozana hadi nje walikolikuta gari la wagonjwa likiwa tayari kuondoka. Sammy alikuwa kalala kwenye kitanda maalumu hajitambui, alikuwa kama mfu akiwa anapumua kwa msaada wa mashine maalumu ya kumsaidia kupumua na alitundikiwa chupa maalumu ya maji aina ya Normal Saline yaliyowekwa dawa maalumu ndani yake ili kusaidia kuyafanya mapigo ya moyo yasishuke.


Wote walishindwa kuyazuia machozi, walijikuta wakilia kwa uchungu huku wakimwangalia Sammy ambaye alikuwa ametulia, hatingishiki. Madame Norah alimwita Sammy huku akibubujikwa na machozi kana kwamba ni mama aliyempoteza mwanawe wa pekee kwenye shimo refu sana, alimwita huku akilia kilio cha uchungu.




Wakati hayo yanaendelea Madame Norah alikuwa bado amezama kwenye dunia yake, dunia ya kisasi. Sasa alikuwa anahisi kifua chake kikiwaka moto utadhani alikuwa anataka kulipuka! Aliapa kushughulika na yeyote aliyefanya hivyo. Donge la hasira lilikuwa limemkaba kooni na alikuwa anapumua kwa shida kama mgonjwa anayepigania pumzi ya mwisho.


Alichokumbuka kuongea muda huo ilikuwa kuomba ruhusa ya kumwona Sammy kabla hajapelekwa Muhimbili. Wote waliongozana hadi nje walikolikuta gari la wagonjwa likiwa tayari kuondoka. Sammy alikuwa kalala kwenye kitanda maalumu hajitambui, alikuwa kama mfu akiwa anapumua kwa msaada wa mashine ya maalumu ya kumsaidia kupumua na alikuwa ametundikiwa chupa maalumu ya maji aina ya Normal Saline yaliyowekwa dawa maalumu ndani yake ili kusaidia kuyafanya mapigo ya moyo wake yasishuke.


Wote walishindwa kuyazuia machozi, walijikuta wakilia kwa uchungu huku wakimwangalia Sammy ambaye alikuwa ametulia, hatingishiki. Madame Norah alimwita Sammy huku akibubujikwa na machozi kana kwamba ni mama aliyempoteza mwanawe wa pekee kwenye shimo refu sana, alimwita huku akilia kilio cha uchungu.


SASA ENDELEA...


Muda huo Madame Norah alikuwa anatiririkwa na jasho jingi hali iliyoanza kuwapa wasiwasi mkubwa walinzi wake na watu wengine waliokuwepo mahali hapo.


* * * * *


Tunu aliufungua mkoba wake, akatoa noti moja ya shilingi elfu kumi na kumpatia mlinzi mmoja kijana aliyekuwa akilinda katika eneo la viunga vya maegesho ya magari la mgahawa maarufu wa Elli’s. alimpa ile fedha kama ‘tip’ akimwomba kumwangalizia gari lake makini ili mtu yeyote asilifikie na kupachika kifaa. Tunu alikuwa ameamua kwenda kuliacha lile gari pale Elli’s kutokana na kuhisi usalama wake ungekuwa shakani endapo angeendelea kulitumia.


Alikuwa amepata wazo la kwenda kuliacha lile gari pale kwenye mgahawa wa Elli’s wakati alipokuwa akitoka Shaurimoyo, japo alikuwa amefanikiwa kung’amua mtego wa adui zake kumwekea kifaa cha GPS lakini aliamini kuwa wangeendelea kumwandama, hasa baada ya kugundua kuwa alikwisha ng’amua mtego huo.


Sasa alikuwa akimtilia shaka kila mtu, hakutaka kumwamini mtu kirahisi hasa kila alipokumbuka kuwa hata Victor, mtu aliyemwamini sana aliweza kumsaliti, hivyo alijiambia kuwa alipaswa kuwa makini zaidi. Ndipo alipofikia hatua ya kupeleka gari lake pale Elli’s akiamini kuwa hiyo ndiyo ilikuwa sehemu pekee kwa wakati huo ingeweza kuwa salama kwa gari lake.


Eneo la viunga vya maegesho ya magari la Elli’s lilikuwa na ulinzi madhubuti likiwa limezungushiwa kamera za ulinzi kila sehemu. Hata hivyo, hakutaka kuzitegemea kamera peke yake, ndipo alipoamua kumtafuta yule kijana mlinzi ambaye kwa macho tu aliweza kutambua kuwa alikuwa mwaminifu. Akamwachia jukumu hilo na kumtaka ampigie simu endapo angehisi jambo lolote lisilo la kawaida kwenye gari lake. Muda huo eneo lile lilikuwa na magari yasiyopungua therathini, mengi yakiwa ya watu wenye vipato vya juu.


Baada ya kuachana na yule mlinzi, Tunu alitoka na kuelekea sehemu zilipokuwa zimeegeshwa taxi, upande wa pili wa barabara. Alitazama pande zote mbili kabla hajavuka barabara na kwenda kuingia kwenye taxi moja, ambayo dereva wake alikuwa mtu mzima, mrefu na mwembamba mwenye sura ya ucheshi muda wote akiwa amevaa kofia aina ya baragashia, shati la mistari ya pundamilia, suruali ya kijivu na makubazi meusi ya ngozi miguuni.


Kwa mtazamo wa haraka haraka Tunu aliona ile taxi ingemfaa sana, alipoifikia alifungua mlango wa nyuma na kuingia haraka, akaketi huku akimtaka dereva ampeleke hospitali ya Amana. Yule dereva aliwasha injini, akaliondoa gari taratibu na kuifuata barabara ya lami iliyokuwa inakwenda kutokea hospitali ya Amana. Zikapita kama sekunde tano tu tangu waondoke eneo la maegesho ya taxi, gari jingine aina ya Toyota Wish la rangi nyeusi ambalo lilikuwepo karibu na maegesho yale ya taxi, nalo likaondoka kuwafuata.


Ile taxi haikwenda mbali kabla Tunu hajakumbuka wajibu wake. Toka katika siti ile ya nyuma aliyoketi alikizungusha kichwa chake taratibu kutazama nyuma bila kumshtua dereva na hapo mwili wake ukajikuta ukiingiwa na ubaridi wa ghafla. Aliliona lile gari aina ya Toyota Wish lenye watu wawili mbele likiwa nyuma yao.


Alikumbuka kuliona lile gari likiwa limeegeshwa karibu na maegesho ya taxi pale nje ya mgahawa wa Elli’s wakati alipofika kutoka Shaurimoyo na kuingiza gari lake ndani ya viunga vya magari vya mgahawa wa Elli’s, hata alipotoka na kuvuka barabara kisha akaingia ndani ya ile taxi alikuwa ameliona tena lile gari likiwa palepale, na sasa lilikuwa nyuma yao. Aligeuka na kumtazama dereva wake kwa udadisi na kugundua kuwa alikuwa hafahamu chochote kilichokuwa kikiendelea. Tunu akageuka tena kutazama kule nyuma.


Lile gari aina ya Toyota Wish lilikuwa nyuma yao kiasi cha umbali wa mita therathini hivi na lilikuwa linakuja kwa mwendo wa kasi likionekana kutaka kuwapita. Kilichozidi kumtia hofu Tunu ni kuwa wale watu sasa walionekana wazi kuwa walikuwa wamedhamiria kumfuatilia pasipo uficho wowote. Akapanga kubadilisha mwelekeo ili kuwapoteza.


“Dereva, ongeza mwendo na uhakikishe gari lolote toka nyuma yetu lisitupite,” Tunu alimwambia yule dereva, na pasipo kuhoji chochote yule dereva aliongeza mwendo.


Kwa kitendo kile cha lile taxi kuongeza mwendo Tunu alikuwa na uhakika kuwa kingetosha kabisa kuwafahamisha wale watu kwenye lile gari lililokuwa nyuma yao kuwa tayari alikuwa ameshawashtukia hila yao, hata hivyo, hilo halikumpa shida. Akili yake sasa ilikuwa makini mno kupanga mikakati ya namna ya kuwapoteza wale watu.


Hakutaka wajue kama alikuwa anakwenda Amana, kwani alihitaji sana kuongea na Sammy ili amweleze ukweli kuwa yeye ni ofisa wa usalama na kwamba alikwisha gundua kuwa adui yake ni Mr. Oduya, hivyo alipaswa achukue tahadhari.


“Dereva, naomba ukifika mwisho wa hii barabara ingia kulia,” Tunu alimwambia yule dereva na kumfanya ashangae kidogo.


“Kwani tunaelekea wapi, bosi wangu? Mimi nilidhani tunaelekea hospitali ya Amana!” yule dereva alihoji kwa mshangao huku akimtupia jicho Tunu kupitia kwenye kioo cha kati cha gari kinachotumika kutazama vitu vilivyoko nyuma.


“Hatuelekei tena Amana kuna mtu nahitaji kuonana naye kwanza kabla ya kuelekea huko,” Tunu alimdanganya yule dereva huku akiwa anafikiria cha kufanya endapo lile gari lililokuwa nyuma yao lingefanikiwa kuwafikia au kuwapita. Alipeleka mkono wake kiunoni, akaigusa bastola yake ndogo aina ya Glock 19M ambayo hutumiwa na wapelelezi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), mwili ukamsisimka.


Inaendelea...


- (126)


“Oh! kumbe umebadili mawazo, ungeniambia ni wapi tunapoelekea sasa badala ya kusema tu ingia kulia!” yule dereva alisema kwa jazba kidogo. Wakati huo ile taxi ilikuwa inafika mwisho wa ile barabara, dereva akaingia kulia.


“Wewe fuata maelekezo yangu, suala la fedha siyo tatizo,” Tunu alimjibu kwa sauti tulivu lakini akionekana kukerwa kidogo.

“Sawa basi usijali bosi wangu, wewe kwangu siyo mfalme tu, hata ukitaka urais nakupa. Wewe sema popote nitakupeleka,” yule dereva alisema huku uso wake ukitengeneza tabasamu la kirafiki.


“Ingia upande wa kulia hapo kama unaifuata barabara ya Uhuru kisha uingie kushoto kuufuata mtaa wa Tukuyu,” Tunu alimwambia yule dereva wakati wakiifikia ile barabara ya Uhuru iliyokuwa na msongamano wa magari muda huo.


Dereva akafanya kama alivyoagizwa. Aliliingiza gari lake katika barabara ya Uhuru kama aliyekuwa anaeleka Buguruni kisha akachepuka na kuufuata ule mtaa wa Tukuyu huku gari likikosakosa kugongana na daladala linalofanya safari zake kati ya Mnazi Mmoja na Banana. Pasipo kujali matusi ya dereva na abiria wa lile daladala, yule dereva aliongeza mwendo wakapita mtaa ule uliokatiza katikati ya makazi ya watu hadi walipoufikia mtaa wa Kasulu.


Walipokuwa mwishoni mwa mtaa ule wa Tukuyu kabla hawajaufikia mtaa wa Kasulu Tunu akageuka tena nyuma kulitazama lile gari lililokuwa limewafungia mkia kwa nyuma. Bado lilikuwa likiwafuatilia na sasa lilikuwa likiufuata mtaa ule wa Tukuyu likiwa katika mwendo wa kasi. Ilionekana wazi kabisa kuwa watu waty hawakuonekana kuwapa mwanya wa kuwatoroka.


Kengele ya hatari ikalia kichwani kwa Tunu, sasa alihisi kuwa wale watu walikuwa wamedhamiria kufanya jambo baya zaidi, pengine walidhamiria kuua. Hakuona tena sababu ya kuendelea kumficha dereva wake, kwani kumficha kungemfanya kuwa na wakati mgumu sana wa kuwapoteza wale watu.


“Naomba nisikilie, sina sababu ya kukuficha kwa sababu nakuamini. Kuna gari nyuma yetu linatufuata tangu tulipotoka kule Elli’s, fanya namna yoyote ya kuhakikisha unawapoteza kwani sitaki kabisa wajue naenda wapi, sawa?” Tunu alimwambia yule dereva kwa sauti ya kuamuru.


Yule dereva akaangalia nyuma na kuliona lile gari aina ya Toyota Wish likizidi kuwasogelea, akaonekana kushtuka sana na kumtupia Tunu jicho huku wasiwasi ukijengeka usoni kwake. “Kwa nini wakufuatilie, kwani umewafanya nini, dada?” yule dereva aliuliza huku akihisi jasho likimtoka mwilini.


“Yule ni mume wangu, nimemtoroka nyumbani. Naomba fanya nilivyokwambia mambo mengine nitakueleza tukishawapoteza,” Tunu alisema huku akigeuza shingo yake kutazama nyuma. Dereva akamwelewa na kuchepuka kuufuata mtaa wa Kasulu upande wa kushoto. Muda huo Tunu aligeuka tena kutazama nyuma akaliona lile gari likizidi kuwasogelea, akatabasamu huku akijisemea moyoni, “Nyie subirini tu, dawa yenu ipo jikoni.”


Sasa dereva wa taxi alianza kuendesha gari kama aliyepandwa na kichaa, alipoufikia mtaa wa Arusha akakunja kushoto akiufuata ule mtaa kisha akakunja kuingia kulia na kuufuata mtaa wa Pangani kisha akakunja tena kuingia kulia akiufuata mtaa wa Mwanza. Mtaa ule ulikuwa mfupi, akakunja kuingia kulia kwake akiufuata mtaa wa Tanga, akawa anarudi nyuma kwenda kutokea tena mtaa wa Arusha.


Walipoingia tena kwenye barabara ya mtaa wa Arusha Tunu akageuka tena kulitazama lile gari kwa nyuma, akafarijika kutoliona likiwa nyuma yao na hapo akageuka tena mbele kumtazama dereva ambaye alikuwa anatabasamu. Katika mtaa ule wa Arusha dereva aliingia kushoto na walipofika Pangan Water, Ilala Depot akaingia kulia kuufuata mtaa mmoja wa barabara ya vumbi hadi alipoufikia tena mtaa Tukuyu.


Walipokuwa wanaingia katika mtaa ule wa Tukuyu Tunu alipogeuka tena kutazama nyuma, na hapo moyo wake ukapiga kite kwa nguvu kama aliyepigwa konde zito la kushtukiza kichwani. Lile gari aina ya Toyota Wish lilikuwepo nyuma yao. Akashtuka sana. Hata yule dereva pia alishtuka sana. Tunu alimwona yule dereva akibabaika kidogo.


“Usijali, wewe nyoosha moja kwa moja, nitakwambia cha kufanya,” Tunu alimwambia yule dereva huku akipeleka mkono wake kiunoni, akaishika bastola yake akiwa tayari kwa lolote. Dereva wa taxi aliongeza mwendo. Wakati huo akili ya Tunu ilikuwa inafanya kazi haraka sana ili aweze kujinasua kutoka kwenye mawindo ya wale watu walioonekana kuwa na uchu wa kuutoa uhai wake.


Wakati wakikaribia kwenye fremu za maduka yanayozunguka Kanisa la Anglikana, Tunu alitoa noti tatu za shilingi elfu kumi kumi na kuzirushia mbele kwa dereva, “Ukifika mtaa wa Moshi kunja kulia na kuufuata mtaa huo, kisha punguza kidogo mwendo, nishuke halafu wewe ongeza mwendo ili kuwapoteza, sawa?”


Yule dereva aliitikia kwa kichwa huku akilitupia jicho lile gari lililokuwa nyuma yao. Akakunja kuingia kulia akiufuata mtaa wa Moshi huku akimkwepa mtoto mmoja aliyekuwa anakatiza barabara. Muda ule ule Tunu aliufungua mlango akashuka haraka na kuusukuma ule mlango, ukajibamiza. Akachepuka na kujibanza nyuma ya mti mmoja mkubwa wa kivuli jirani ya nyumba moja ya wageni.


Lile gari lililokuwa nyuma yao pia liliingia barabara ile lakini kwa kuchelewa kidogo likaongeza mwendo kuifuata ile taxi. Dereva wa taxi aliufikia mtaa wa Arusha na kuuvuka, akaendelea mbele akiifuata barabara ile ya vumbi. Sasa alikusudia kuwafanya wale watu waamini kuwa yule dada alikuwa bado yumo ndani ya ile taxi.


* * * * *


Kwa mara ya kwanza tangu alipoanza harakati zake za kutaka kuingia ikulu, Mr. Oduya alijikuta katika hali ya wasiwasi na mashaka makubwa. Kwa mbali hofu ilikuwa ikitishia kuutawala moyo wake, hasa kwa hisia zilizokuwa zikimnong’oneza kuwa mambo yameanza kumwendea mrama. Alikuwa amekanganyikiwa akiwa ameketi kwenye kiti chake cha kuzunguka ofisini kwake.



Wakati wakikaribia kwenye fremu za maduka yanayozunguka Kanisa la Anglikana, Tunu alitoa noti tatu za shilingi elfu kumi kumi na kuzirushia mbele kwa dereva, “Ukifika mtaa wa Moshi kunja kulia na kuufuata mtaa huo, kisha punguza kidogo mwendo, nishuke halafu wewe ongeza mwendo ili kuwapoteza, sawa?”


Yule dereva aliitikia kwa kichwa huku akilitupia jicho lile gari lililokuwa nyuma yao. Akakunja kuingia kulia akiufuata mtaa wa Moshi huku akimkwepa mtoto mmoja aliyekuwa anakatiza barabara. Muda ule ule Tunu aliufungua mlango akashuka haraka na kuusukuma ule mlango, ukajibamiza. Akachepuka na kujibanza nyuma ya mti mmoja mkubwa wa kivuli jirani ya nyumba moja ya wageni.


Lile gari lililokuwa nyuma yao pia liliingia barabara ile lakini kwa kuchelewa kidogo likaongeza mwendo kuifuata ile taxi. Dereva wa taxi aliufikia mtaa wa Arusha na kuuvuka, akaendelea mbele akiifuata barabara ile ya vumbi. Sasa alikusudia kuwafanya wale watu waamini kuwa yule dada alikuwa bado yumo ndani ya ile taxi.


* * * * *


Kwa mara ya kwanza tangu alipoanza harakati zake za kutaka kuingia ikulu, Mr. Oduya alijikuta katika hali ya wasiwasi na mashaka makubwa. Kwa mbali hofu ilikuwa ikitishia kuutawala moyo wake, hasa kwa hisia zilizokuwa zikimnong’oneza kuwa mambo yameanza kumwendea mrama. Alikuwa amekanganyikiwa akiwa ameketi kwenye kiti chake cha kuzunguka ofisini kwake.


ENDELEA...


Mambo hayo hayakuwa yakimwingia kichwani kwake kabisa, alikuwa anajiuliza ni vipi Tunu akafanikiwa kuwatoroka watu wote waliowekwa kumfuatilia? Tena watu wenye ufanisi mkubwa katika kazi hiyo na wenye silaha? Kidogo akawa amejifunza ni mtu wa aina gani alikuwa anasumbuka naye ndiyo maana baadaye aliamua kuwatuma watu maalumu kwa kazi moja tu, kuua. Watu hao walitakiwa kumuua Tunu popote ambapo wangemwona.


Mr. Oduya aliamini kuwa Tunu hakuwa mtu wa kawaida kama alivyokuwa anamchukulia mwanzo, mbaya zaidi, hata yule dereva teksi Tom ambaye walimtegemea kwa shughuli za kuchukua watu wake na kuwakimbiza huku na kule pia alikuwa amejiunga na Tunu!


Sasa Mr. Oduya alianza kujiuliza iwapo aachane na ndoto ile ya urais kisha atoroke nchi na kukimbilia nchini Canada ambako alikuwa amewekeza kwa kiasi kikubwa, akaishi kwa raha mustarehe na mpenzi wake Zainabu, akitumia utajiri wake mkubwa. Hata hivyo, wazo hilo alilipinga kwa kuona kuwa hiyo ilikuwa dalili ya mtu mwoga. Yeye hakuwa mwoga, hivyo alipaswa kupambana hadi dakika ya mwisho.


Kichwa chake kilikuwa kimechemka utadhani ubongo wake uligeuka kuwa volcano iliyotishia kulipuka wakati wowote, aliuhisi ubongo wake ukiwaka moto na muda wowote kichwa kingelipuka na kusambaratika. Hadi muda huo hakuwa ameambua japo lepe la usingizi, kwa siku mbili mfululizo tangu alipogundua kuwa lile gari aina ya Cadillac DeVille lenye muundo wa kizamani lilionekana Mzizima TV na sasa lilikuwa linamilikiwa na mtu mwingine.


Kwa kuiamini timu yake iliyoongozwa na Spoiler, Mr. Oduya alitegemea suala la kumpata mmiliki mpya wa lile gari na kuliteketeza lile gari lingekuwa rahisi na kuchukua muda mfupi, lakini tangu kuibuka kwa yule binti, Tunu, ambaye alionekana waziwazi kuanzisha vita ili kumkwamisha, mambo yakaanza kwenda mrama.


Timu yote aliyoitegemea kuifanya kazi hiyo ilionekana kuzidiwa akili na yule binti. Mr. Oduya hakujua Tunu alikuwa ana nini hasa? Ni mara ngapi amejaribu kwa uwezo wake wote kutaka kumtia mkononi lakini binti huyo amekuwa akiikwepa mitego yote na kuwapotea katika mazingira ya utata?


Alikuwa ameketi pale kwenye kiti chake kwa takriban dakika arobaini na tano akiwa hajui afanye nini, hiyo ilikuwa ni baada ya kuongea na vijana wake aliowafokea sana kuhusiana na kitendo cha wao kuendelea kuzidiwa akili na Tunu.


“Ninaomba maelezo mafupi sasa hivi, kwa nini mmeshindwa kumnasa huyo binti?” Mr. Oduya aliwauliza Spoiler, Victor na Job waliokuwa wameketi mbele yake huku wamejiinamia.


Spoiler, Victor na Job waliinua nyuso zao, wakatazamana na Spoiler akawa wa kwanza kusema. “Nadhani, bosi hatutakuwa na maelezo ya kukuridhisha kwa nini hatujafanikiwa kumtia mbaroni hadi sasa, kwa sababu…”


“Ni wazembe tu!” Mr. Oduya alimkatiza Spoiler kwa kufoka, uso kaukunja na kutengeneza ndita usoni. “Au mna sababu nyingine?”


Spoiler aliwatupia jicho Victor na Job mara moja kisha akaketi vema kitini. Alishaanza kuingiwa na hofu iliyochanganyika na woga. Alikuwa na kila sababu ya kujisikia vile. Mr. Oduya alikuwa mtu katili sana asiyeruhusu makosa ya kipumbavu yaliyoashiria uzembe yatokee kwenye kazi zake, ingawa machoni kwa watu alionekana mnyenyekevu na mwenye kusaidia jamii lakini ukweli ni kwamba alikuwa hana tofauti na mnyama yeyote wa porini.


“Siyo wazembe bosi,” Spoiler alisema kwa sauti ya chini.


“Kumbe nini?” Mr. Oduya aliuliza huku akimtolea macho. “Mlishajua kuwa Tunu tayari amekutana na Sammy na kisha akagundua kuwa gari lake limewekwa GPS device. Hakukuwa tena na sababu ya kuendelea kumwacha akiwa hai, mlikuwa mnasubiri nini, pingu? Sasa amefanikiwa kuwatoroka, mnataka kusema nini? Ni uzembe tu!” Mr. Oduya alifoka.


Victor alishusha pumzi, akawageukia akina Spoiler na Job waliokuwa wanamtumbulia macho Mr. Oduya kwa wasiwasi.


“Inawezekana kweli kuwa ni uzembe wetu, mzee,” Victor alijikakamua na kusema, “lakini hapa tunamzungumzia Tunu Michael, shushushu mbobezi aliyepata mafunzo maalumu ya kijeshi na mwenye shahada ya umahiri ya ujasusi wa mambo ya usalama na mapambano dhidi ya ugaidi, isitoshe ni ninja na kama ilivyo kwa maninja wote ni kama wanatumia nguvu za mizimu…”


“Upumbavu!” Mr. Oduya alisema huku akishusha ngumi nzito mezani iliyowashtua watu wote. “Hatuzungumzii nguvu ya mizimu katika kazi kama hizi, Victor… wewe na Job pia ni mashushushu. Wewe umekaa miaka mitatu nchini Cuba ukijifunza upelelezi wa kisasa na bado unazungumzia nguvu ya mizimu…” Mr. Oduya alikuwa amefura kwelikweli, sasa alikuwa anaongea kama anayetaka kupiga kelele. “Au mlitakaje? Tuwachanje kwanza chale mwilini ndipo mumkamate Tunu?”


Victor alimlaani sana Mr. Oduya kimoyomoyo, alitamani kumtukana kisha ainuke na kuondoka zake lakini akaogopa, kwani yule mzee hakuwa tajiri tu wa kawaida, alikuwa na nguvu kubwa sana serikalini na ndani ya vyombo vya usalama akiaminiwa na watu wengi kama bilionea anayesaidia jamii.


“Hatuhitaji kuchanjwa chale, mzee, hilo tunalijua. Lakini Tunu, si kama unavyomjua… huyu ni shushushu hatari sana aliyepata mafunzo ambayo katika nchi hii wapo wawili tu, mafunzo hayo ndiyo humsaidia kung’amua jambo lolote hatari kabla halijatokea. Sisi si wazembe, kama unavyotutuhumu. Tumefanya kazi ngapi kubwa na za hatari, mzee?” Victor alisema kwa sauti kakamavu iliyoficha hasira ndani yake.



Mr. Oduya alishusha pumzi, akajiegemeza kitini. Ni kweli kabisa Victor na Job walikuwa mashushushu shupavu ambao serikali ilikuwa ikijivunia kuwa nao. Walikubali kukiuka misingi ya kazi yao ya usalama wa taifa ili kumtumikia katika uhalifu wake, wakifanya kazi kwa kujituma bila ya kuhitaji kusimamiwa au kuhimizwa. Mr. Oduya mwenyewe aliwategemea katika kazi zake na aliwaahidi kuwapa nafasi nyeti ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa pindi akishika madaraka ya nchi.


Sasa walikuwa wameondoka kwenda kusaidiana kumtafuta Tunu, alikuwa amewataka wasirudi hapo bila taarifa ya kifo au kichwa cha Tunu, haijalishi kama Tunu ni ninja au anatumia nguvu ya mizimu. Ni kweli Tunu alikuwa shushushu hatari, mbobezi, ninja au vyovyote ambavyo angeitwa, lakini Mr. Oduya alikuwa na uhakika kuwa pamoja na sifa zote hizo bado alikuwa na mwili wa nyama, na risasi haichagui raia, shushushu au ninja.


Jambo lililompa ahueni kidogo Mr. Oduya ni kwamba, aliamini kuwa Tunu bado alikuwa hayajui mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea kwenye harakati zake ingawa kitendo chake cha kufanikiwa kukwepa mitego yote aliyowekewa kilitosha kumpa salamu Mr. Oduya kuwa alikuwa anadili na mtu wa aina gani. Shushushu hatari, mbobezi na ninja, kama alivyosema Victor.


Hilo lilizidi kumtisha Mr. Oduya kwani pamoja na kuweka watu wake karibu maeneo yote ya mji na yale aliyodhani Tunu angeweza kufika ikiwemo hospitali ya Amana na Muhimbili, bado hawakufua dafu. Aliona kuwa anatakiwa kutafuta njia mbadala za kumpata Tunu, lakini sasa angempataje? Aliona kichwa chake kinakaribia kupasuka kwani bila kumpata Tunu mambo yake yote yangeharibika. Njia mbadala ya kumpata ilikuwa ni kwa kupitia Victor, lakini sasa wameshaitifua.


Akiwa bado amezama kwenye lindi la fikra alishtuliwa na mtu aliyegonga mlango wa ofisi yake mara moja kisha mlango huo ukafunguliwa. Aliingia mtu aliyevaa suti maridadi ya kijivu mmoja na Mr. Oduya alipomtazama akamtambua mara moja na kushusha pumzi. Alikuwa Dk. Masanja.


Mr. Oduya alishangaa maana hakuwa na miadi yoyote na Dk. Masanja siku hiyo, tangu kikao chao cha kupanga mikakati kilipovunjika usiku ule baada ya taarifa za kuonekana kwa lile gari aina ya Cadillac DeVille lenye muundo wa kizamani, hawakuweza kuongea tena. Dk. Masanja hakuwa na kawaida ya kumtembelea ofisini kwake na hata kama angefika pale ilikuwa ni mpaka wakubaliane. Dk. Masanja alijikaribisha mwenyewe kwenye kiti kisha wakasalimiana.


“Kwani ni kipi kilichotokea, naona hadi leo bado haupo katika hali yako ya kawaida!” Dk. Masanja alimuuliza Mr. Oduya huku akimtazama usoni kwa makini.


“Ni mambo ya kifamilia tu, nisingependa kuyaongelea,” Mr. Oduya alisema huku sura yake ikishindwa kuficha wasiwasi aliokuwa nao, “ni kwamba ninahitaji siku mbili zaidi ili kuyaweka sawa kabla hatujaendelea na mipango yetu.”


“Okay!” Dk. Masanja alisema kisha akajiweka sawa kwenye kiti, “Maana hatujawasiliana wala hujatokea pale Paradise Club jambo ambalo si kawaida yako, imenipa wasiwasi kidogo.”


“Uihofu juu yangu, hata hivyo nimeshangaa kidogo kwa ujio wako maana ungeweza kunipigia simu tu badala ya kusumbuka kuja huku.”


“Ni kweli, ila sikutaka kufanya hivyo maana mambo mengine hayafai kuzungumzwa kwenye simu, si unajua tena tupo kwenye ulimwengu wa teknolojia, watu wanaweza kudukua mawasiliano…” Dk. Masanja alisema na kuendelea, “Nilihitaji kujua kuhusu suala la huyu bwana mdogo Sammy!” Dk. Masanja aliuliza huku akimkazia macho Mr. oduya.


“Kuhusu nini?” Mr. Oduya aliuliza huku akionesha mshtuko usoni kwake.


“Naamini unafahamu kilichompata. Nilitaka kujua kama unahusika!” Dk. Masanja aliongea huku kamkazia macho Mr. Oduya.


“Nimesikia yaliyompata lakini si mimi niliyehusika,” Mr. Oduya alisema huku akitingisha kichwa chake kushoto na kulia kukataa.


Dk. Masanja akamtazama kwa sekunde kadhaa kabla hajashusha pumzi na kutia neno, “Mr. Oduya, mimi sipo hapa kukuhukumu ama kukutuhumu. Nipo hapa kuona namna gani tunaweza kufanya ili polisi wasiweze kugundua lolote. Labda nikwambie, nimefuatwa ofisini na maofisa wa polisi wakitaka maelezo yangu kama bosi wa Sammy.”


Mr. Oduya akashtuka kidogo, “Kwani hujawaambia kama alikwisha acha kazi katika hoteli yenu?”


“Sijawaambia lakini wanajua kuwa aliacha kazi, walitaka kujua aliacha lini na kwa nini! Hapa nipo njia panda kwa kuwa inaonekana wanazo taarifa nyingi kuliko tunavyodhani, ndiyo maana nimekuja kwako,” Dk. Masanja alisema na kumeza funda la mate kutowesha koo lake lililokauka.


Mr. Oduya alibaki kimya, alikuwa ametahayari sana. Uso wake haukuweza kuficha hofu aliyokuwa nayo.


* * * * *


Tangu aliposhuka toka ndani ya ile taxi iliyomchukua toka katika mgahawa wa Elli’s, Tunu alitembea kwa tahadhari kubwa huku akiwa na wasiwasi mkubwa. Kubwa lililomsumbua ni jinsi watu wa Mr. Oduya walivyoonekana kupania kumpata kwa gharama yoyote. Alijiuliza, ilikuwaje huko nyuma baada ya kuachana na yule dereva wa teksi? Je, walifanikiwa kumpata? Na kama walimpata walimuhoji? Aliwajibu nini?


Tunu alikuwa na wasiwasi na yule dereva kwani alishaanza kuonesha dalili za hofu na wasiwasi. Kama alihojiwa, akaudhihirisha wasiwasi wake, yawezekana waliamua kumtumia kama chambo ili kuja kumnasa Tunu, au pengine walimpeleka nyumba ya mateso. Yawezekana muda huo alikuwa anapokea mateso wakiamini kuwa alikuwa anayajua mengi.


Mawazo yalikuwa yakipita kichwani kwa Tunu wakati akiambaa na ukuta kuelekea kwenye jengo la wadi ya wagonjwa mahututi wenye kuhitaji uangalizi maalumu katika hospitali ya Amana. Muda wote alikuwa makini sana akizungusha macho yake kila pembe ili kubaini mtego wowote uliokuwa umewekwa dhidi yake. Mawazo hayo yaliufanya moyo wake uongeze kasi ya mapigo yake. Alivuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu.



Alikuwa ameingia ndani ya eneo la hospitali ya Amana baada ya kuruka ukuta, pasipo kuambiwa alitambua kuwa watu wa Mr. Oduya wangekuwepo pale hospitali kumsubiri, hivyo ilimbidi kuwakwepa na kuzunguka nyuma ya hospitali ambako alifanikiwa kuingia ndani.


Haikuwa rahisi kuingia ndani ya uzio wa hospitali ile, kwani alipotoka mtaa wa Moshi, alitembea haraka huku akiwa makini kuangalia pande zote na kuvuka barabara ya Uhuru, akaelekea kwenye vibanda vya wasusi wa Kimasai ambapo alipita, akashika njia kama anakwenda kwenye maghorofa ya Ilala. Alipofika eneo lile aliyazungusha macho yake pande zote kutazama kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia, hata hivyo hakumwona mtu yeyote hivyo aliendelea na safari yake akiyapita maghorofa ya Ilala na kuambaa ambaa na ukuta wa hospitali.


Aliporidhika kuwa hakuna aliyekuwa akimtazama alichepuka chini ya miti mikubwa iliyokuwa imepandwa kandokando ya ukuta wa Hospitali ya Amana na kwenda kwenye ule ukuta wa hospitali. Akafanikiwa kuufikia ukuta ule ambapo kwa mbinu zake za kijasusi alifanikiwa kuupanda kama anayeruka mtaro mdogo wa maji machafu. Muda mfupi baadaye akatua upande wa pili ndani ya ukuta.


Mara tu alipotua mle ndani alisimama akachunguza vizuri mazingira ya eneo lile. Kulikuwa na miti miwili mikubwa eneo lile na hakukuwapo mtu karibu, na hapo akaanza kutembea kwa tahadhari akiambaa na ukuta huo kuelekea ilipo wadi maalumu ya wagonjwa mahututi wenye kuhitaji uangalizi maalumu.


Alisimama ghafla baada ya kuona eneo lile la nje ya wadi ya wagonjwa mahututi likiwa linalindwa na askari watatu wenye silaha. Askari wale walikuwa makini sana wakizungusha macho yao pembe zote kuhakikisha usalama unakuwepo. Tunu alipochunguza kwa makini akagundua kuwa kila aliyepita eneo lile alisimamishwa na kuhojiwa, na pengine alikamatwa au alizuiwa na kutakiwa kurudi alikotoka.


Alitweta, akajiuliza iwapo alitakiwa aendelee na safari yake au arudi. Katikati ya mawazo hayo, mlio hafifu wa simu yake ya mkononi ukamshtua! Tunu aliiangalia ile simu kwa makini, akaliona jina la Tom. Alijibanza sehemu akaipokea na kuongea, “Hallo!”


“Uko wapi?” Tom aliongea kwa sauti iliyoonesha wasiwasi kidogo.


“Nipo sehemu fulani kuna kitu nafuatilia. Wewe upo wapi?” Tunu alisema huku akizungusha macho yake pembe zote kuhakikisha usalama wake.


“Pia nipo sehemu fulani nimetulia, nilitaka kukwambia kwamba, kuwa makini sana na kila mtu unayepishana naye wakiwemo baadhi ya askari polisi, kuna wauaji wawili wa kukodiwa wamepewa kazi ya kukufuatilia kokote uliko na kukuua, hawatakiwi kufanya kitu kingine isipokuwa kukuua tu,” Tom alisema kwa wasiwasi.


“Usijali kuhusu mimi, watakufa wao kabla hawajafanikiwa kuniua,” Tunu alijibu kwa sauti tulivu ingawa mapigo ya moyo wake yalikuwa yanakwenda mbio isivyo kawaida.


“Vipi umesikia kuhusu kilichompata Sammy?” Tom aliuliza kwa wasiwasi.


“Hapana, amepatwa na nini?” Tunu aliuliza huku akihisi ubaridi mwepesi ukimtambaa mwilini mwake na kuzifanya nywele zake kusisimka.


“Walimtegesha bomu kwenye gari lake, likalipuka wakati ameliegesha na kuingia ndani. Hivi sasa yupo hospitali akiwa mahututi…”


“What?” Tunu aling’aka kwa mshtuko mkubwa. Alihisi kama vile moyo wake uliyasahau mapigo yake kwa muda, na yaliporejea yalianza kwenda mbio isivyo kawaida. “Dah! Yupo hospitali gani?” Tunu aliuliza baada ya kitambo.


“Walimpeleka Amana, hali ikaonekana ni mbaya zaidi, wakamhamishia Muhimbili.”


“Okay! Vipi kuhusu wewe, bado hawajakushtukia?”


“Dah, sijui nikwambie nini! Ninasakwa kwa udi na uvumba. Nimekutana na rafiki yangu mmoja huwa tunapaki wote pale Elli’s, akanitonya kuwa natafutwa kama gaidi na watu fulani ambao wamemwaga fedha kwa siri pale kijiweni ili nikionekana tu wapewe taarifa. Ila usijali niko poa,” Tom alisema na kushusha pumzi.


“Basi nitakupigia baadaye ili tujue cha kufanya,” Tunu alisema na kukata simu baada ya kuhisi kulikuwa na watu waliokuwa wanaelekea kule alikokuwa. Hakuona sababu ya kuendelea kuwepo pale, akaondoka haraka na kurudi alikotoka akitumia mbinu ile ile ya kijasusi kuupanda ukuta na kurukia nje. Sasa alihisi kuwa eneo lile lilikuwa halifai tena, alipaswa aende sehemu akajipange kwanza kabla ya kuendelea na harakati zake.


* * * * *


Habari za kuvamiwa nyumba ya Sammy, kupigwa risasi mkewe na yeye kujeruhiwa kwa bomu lililotegwa kwenye gari na kuharibu nyumba yao zilitapakaa nchi nzima na nje ya mipaka ya nchi. Hofu ilitanda kila mahali watu wakijiuliza, huyu Sammy alikuwa na nini kiasi cha kuandamwa na watu hao walioonesha wazi kuwa nia yao ilikuwa kumteketeza.


Wakazi wa jiji la Dar es Salaam walikuwa wamezipokea habari zile kwa kitu zaidi ya mshangao, hofu kubwa. Hofu ilipenya katika fikra zao kwa kule kusikia kwamba haikuwepo fununu yoyote juu ya kupatikana kwa watu waliofanya tukio lile ambalo lilionekana ni zaidi ya uhalifu wa kawaida, lilikuwa limefikia kiwango cha kuitwa ugaidi. Kila mtu alimtazama mwenziwe kwa macho yaliyoitangaza hofu iliyojificha moyoni mwake.


Siku hiyo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Ramon Mamboleo alikuwa na hasira kali na alikuwa katika uso wa kusawajika kidogo. Hakuna kitu kilichomkasirisha kama wahalifu. Mhalifu alimchukulia kama shetani mwenyewe na alikuwa tayari kumsaka kwa ari zote ili ampate na kumpeleka gerezani alikokuita jehanamu.


Ilikuwa saa tisa alasiri alipowasili kituo kikuu cha polisi akitokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukuta watu wa habari: waandishi wa magazeti, redio na televisheni wakimsubiri. Muda wote alikuwa akipokea ujumbe mfupi wa simu na kupigiwa simu toka kwa wakuu wake wa kazi na watu wengine waliotaka kujua jeshi la polisi lilikuwa limefikia wapi katika uchunguzi wake ili kuwabaini waliofanya uhalifu huo.


Safari bado inaendelea. Taxi imezua mambo na sasa wenzi wawili wanapigania uhai vitandani, mmoja yupo Amana na mwingine Muhimbili! Tunu naye anasakwa kama gaidi, popote atakapoonekana anatakiwa auawe. Je, nini kitaendelea? Endelea kufuatilia stori hii ya kusisismua hapa hapa JamiiForums ili kuujua mwisho wake. Ciao...




Wakazi wa jiji la Dar es Salaam walikuwa wamezipokea habari zile kwa kitu zaidi ya mshangao, hofu kubwa. Hofu ilipenya katika fikra zao kwa kule kusikia kwamba haikuwepo fununu yoyote juu ya kupatikana kwa watu waliofanya tukio lile ambalo lilionekana ni zaidi ya uhalifu wa kawaida, lilikuwa limefikia kiwango cha kuitwa ugaidi. Kila mtu alimtazama mwenziwe kwa macho yaliyoitangaza hofu iliyojificha moyoni mwake.


Siku hiyo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Ramon Mamboleo alikuwa na hasira kali na alikuwa katika uso wa kusawajika kidogo. Hakuna kitu kilichomkasirisha kama wahalifu. Mhalifu alimchukulia kama shetani mwenyewe na alikuwa tayari kumsaka kwa ari zote ili ampate na kumpeleka gerezani alikokuita jehanamu.


Ilikuwa saa tisa alasiri alipowasili kituo kikuu cha polisi akitokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukuta watu wa habari: waandishi wa magazeti, redio na televisheni wakimsubiri. Muda wote alikuwa akipokea ujumbe mfupi wa simu na kupigiwa simu toka kwa wakuu wake wa kazi na watu wengine waliotaka kujua jeshi la polisi lilikuwa limefikia wapi katika uchunguzi wake ili kuwabaini waliofanya uhalifu huo.


ENDELEA...


Hakutaka kuongea na mwanahabari yeyote kwa muda ule, kwani hakuwa amepokea taarifa yoyote toka kwa wasaidizi wake. Aliposhuka garini alielekea moja kwa moja ofisini kwake. Ilikuwa ofisi pana na sakafuni ilifunikwa kwa zulia maridadi jekundu na katikati ya lile zulia likiwa na nembo kubwa ya Jeshi la Polisi la Tanzania.


Ndani ya ofisi ile kulikuwa na meza ndefu ya mikutano iliyozungukwa na viti kumi na mbili. Viti vitano upande wa kushoto, viti vingine vitano upande wa kulia, kiti kimoja mwanzoni mwa ile meza na kiti kimoja kilikuwa mwisho wa meza.


Naibu Kamishna Mamboleo aliketi juu ya kiti chake kikubwa chenye foronya laini cha kuzunguka na chenye magurudumu yaliyokiruhusu kusogea, kiti kile kilikuwa nyuma ya meza kubwa ya ofisini yenye majalada mengi juu yake. Bendera ndogo mbili zilionekana juu ya ile meza, moja ikiwa bendera za Taifa na nyingine ya Jeshi la Polisi. Vitabu kadhaa vikiwemo vya Sheria na Katiba ya Tanzania, kidau cha wino, mhuri na kichupa kidogo chenye wino mweupe wa kufutia maandishi.


Pembeni ya ile meza ya ofisini kulikuwa na mashine ndogo ya kidijitali ya kurudufu, mashine maalumu ya kuchapa barua na nyraka mbalimbali za kiofisi, mashine ya picha na mashine moja ya nukushi. Naibu Kamishna Mamboleo alishusha pumzi ndefu.


“Majaribo mawili ya mauaji katika familia moja ndani ya saa kumi na nne!” Naibu Kamishna Mamboleo alijikuta akiropoka. “Mke kwa risasi na mume kwa bomu! Ni nani hawa waliofanya hivi? Na kwa nini wafanye hivi kwa familia hii? Je, familia hii ina adui yeyote?” Naibu Kamishna Mamboleo alijiuliza.


Hata hivyo, hakutarajia kupata majibu haraka kiasi hicho kwani alikuwa anasubiri uchunguzi uliokuwa ukifanywa na vijana wake machachari wakiongozwa na Inspekta Abel wa mkoa wa kipolisi wa Ilala. Hata hivyo, kama kuna kitu kilikuwa kinamsumbua sana Naibu Kamishna Mamboleo ni kusubiri. Subira ni jambo lililokuwa likimtesa mno kama adhabu. Alihisi kila dakika aliyoendelea kusubiri ilikuwa ikimjeruhi moyo wake na kuutia jeraha. Kiti alichokalia alikihisi kilikuwa kinawaka moto.


Wazo kuu lilikuwa moja tu, awapate vipi wahalifu hao wasio na hata chembe ya huruma, wahalifu wenye kutaka kuichafua amani ya nchi hii na kufurahia kumwaga damu isiyo na hatia? Angepeda sana kuwapata wahalifu hao haraka iwezekanavyo. Tatizo lilikuwa angewapataje haraka kiasi hicho? Jiji la Dar es Salaam lilifurika watu wote: wema kwa waovu, wenye hatia kwa wasio na hatia. Ni vipi awapate watu wachache wenye hatia miongoni mwa mamilioni wasio na hatia kwa muda mfupi?


Kila alivyojiuliza alijikuta akipata jibu moja tu, jibu lililozidi kumjeruhi moyo wake, hakuwa na budi ya kusubiri taarifa ya uchunguzi! Alitakiwa asubiri hadi hapo wasaidizi wake wamalize uchunguzi wao na kukusanya taarifa zote muhimu za kiitelijensia ambazo zingewaongoza hadi mbele ya wahalifu hao.


Taarifa hizo zilitegemea sana kuifahamu mienendo ya Sammy katika siku za karibuni na watu aliokuwa anakutana nao, wapi alikokuwa usiku wa siku ambayo mkewe alipigwa risasi, alikopita kabla ya kufika nyumbani, watu gani waliokutana nao siku hiyo au alioongea nao kwenye simu na mambo gani waliyoongea.


Ni hayo ambayo yangetengeneza njia ya kuwapeleka polisi kwa wahalifu hao, lakini ilihitajika subira. Kusubiri kulimtisha zaidi Naibu Kamishna Mamboleo kuliko hata wahalifu wenyewe. Hakupenda kuketi ofisini akisubiri kwa sababu hakujua wahalifu hao walikuwa wanapanga nini katika kipindi hicho, pengine walikuwa wanajiandaa kushambulia watu wengine wasio na hatia au hata kutoroka nchi!


Sababu nyingine iliyomfanya ashindwe kusubiri ni kwamba raia wema jijini Dar es Salaam walikuwa wamejawa hofu kubwa na usalama wao, ni yeye Naibu Kamishna Mamboleo aliyekabidhiwa jukumu la kuhakikisha raia na mali zao ndani ya jiji la Dar es Salaam wanakuwa salama.


Hakupendezwa kabisa na hali ile, kama mlinzi wa amani katika jiji la Dar es Salaam, aliyepewa dhamana hiyo na taifa, asingeweza kukaa kwa amani ofisini kwake akishuhudia amani hiyo ikitoweka na hata kuwafanya raia wema kuanza kuichukia serikali yao.


Hadi muda huo jeshi la polisi lilikwisha wahoji watu wengi wakiwemo majirani wa Sammy, marafiki, jamaa wa karibu na hata wafanyakazi wa Udzungwa Beach Resort alikokuwa akifanya kazi Sammy kabla hajaacha. Katika mahojiano na msako mkali uliofanywa, wapo wengi waliokamatwa na kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi baada ya kushukiwa kuhusika, lakini bado kulikuwapo maswali mengi ya kukanganya yaliyotakiwa kupatiwa majibu ili kuwaongoza polisi mbele ya wahalifu hao.


Hata hivyo, kulikuwa na mtu mmoja tu katika jiji zima la Dar es Salaam ambaye alikuwa na majibu yote ya maswali hayo. Mtu huyo, msichana mrembo, mrefu, maji ya kunde na mwenye umbo matata lenye kuweza kuitaabisha vibaya nafsi ya mwanamume yeyote, alikuwa na sura ya duara, macho malegevu, pua ndefu na midomo yenye kingo pana.


Mtu huyo machoni kwa jamii isiyoelewa kazi yake alionekana binti mrembo aliyepaswa kuolewa na mwanamume mwenye fedha zake akatulia ndani, azae na kumhudumia mume basi. Lakini kwa magaidi na wahalifu wa kimataifa, binti huyo aliogopwa sana kwani alikuwa na uwezo mkubwa na mbinu nyingi za kumfikia adui na oparesheni alizowahi kuzifanya ziliwafanya wengi kuhisi pengine hakuwa binadamu wa kawaida.



Huyu ni mtu aliyeijua vyema njia ya kuelekea mbele ya wahalifu hao walioleta taharuki jijini Dar es Salaam na tayari alikuwa mbele ya wakati akitumia mbinu zake kuifuata njia aijuayo mwenyewe hadi ahakikishe wahalifu hao wanapokea tuzo ya uhalifu wao. Tatizo lilikuwa moja tu, alihitaji ushahidi kamili ili kuwafikisha wahalifu hao mbele ya sharia. Ushahidi huo ulikuwa umefichwa kwenye memory card ambayo sasa ilikuwa imepotelea ndani ya nyumba ya Sammy baada ya kubomolewa na bomu. Mtu huyo aliitwa Tunu Michael.


* * * * *


Elli na Jengo walikuwa wamejiinamia kwa huzuni kwenye mabenchi nje ya chumba maalumu cha wagonjwa mahututi wenye kuhitaji uangalizi maalumu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kila mmoja aliwaza lake na walionekana wamekata tamaa. Sammy alikuwa bado hana fahamu na juhudi za kuyaokoa maisha yake zilikuwa zikiendelea kufanywa na jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali hiyo.


Muda wote akina Elli walikuwa wakiwasiliana na akina Madame Norah na Bi. Pamela waliokuwa katika Hospitali ya Amana, ili kujua maendeleo ya kila upande. Hadi muda huo Joyce hakuwa ameambiwa chochote kuhusiana na hali ya Sammy, ingawa alikuwa akisumbua sana kwa maswali ya “Sammy yupo wapi?”; “Mbona haji kuniona?” na kadhalika.


Eneo lote kuzunguka jengo la wadi ya wagonjwa mahututi wenye kuhitaji uangalizi maalumu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alimokuwa amelazwa Sammy lilikuwa na ulinzi mkali wa polisi wenye silaha, nia ilikuwa ni kuzuia uwezekano wa watu wenye nia ovu ya kutaka kumuua Sammy wasijipenyeze ndani ya kile chumba alimolazwa.


Pia ilikubalika kuwa hata matibabu ya Sammy yafanywe kwa usiri mkubwa kutokana na hali ya wasiwasi iliyokuwa imelikumba jiji zima la Dar es Salaam.


Uchunguzi wa awali kuhusu hali ya Sammy ulionesha kuwa alikuwa amepatwa na tatizo la mtikisiko wa ubongo, tatizo ambalo kitalaamu lilijulikana kama brain concussion. Tatizo hilo liligunduliwa baada ya jopo hilo la madaktari bingwa watano kumfanyia uchunguzi na wasiwasi ulikuwepo miongoni mwao kuwa lingeweza kumfanya Sammy apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.


Hadi muda ule walikuwa wanaendelea na vipimo katika sehemu ya maini yake na majimaji ya machoni kuona kama ubongo wake ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo kwani mfumo wake wa upumuaji ulikuwa umeathirika. Vipimo hivyo vilikuwa vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kulikuwa na sumu au kitu kingine katika mwili wake.


Hata hivyo, walijiridhisha kwamba mtikisiko huo wa ubongo haukuwa umetokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum) kwani ingetokea hivyo asingeweza kuinuka tena, kwa kuwa hali hiyo huua haraka. Kingine kilichogunduliwa ni mapigo ya moyo wake na joto la mwili vilikuwa katika hali ya kukatisha tamaa kabisa, kwa kifupi, daktari bingwa mmoja alisema kuwa “the patient is basically dead” akimaanisha kuwa kimsingi mgonjwa alikuwa amekufa.


Hicho ndicho kilichowafanya Elli na Jengo waonekane kukata tamaa wakiamini kuwa Sammy alikuwa katika hali ambayo ni hatua moja tu kutoka kati yake na kifo, kwani ndicho kilichoonekana mbele ya wale madaktari bingwa.


Kipindi chote Elli alikuwa anajiuliza maswali yasiyo na majibu kuhusu watu waliomshambulia Sammy na hata Joyce. Je, shida yao kubwa ilikuwa nini? Kilichomtokea Sammy kilimaanisha kuwa huenda alikuwa tishio kwa watu fulani, je, ni watu gani hao? Je, kulikuwa na uhusiano wowote kati ya mashambulizi hayo na kusimamishwa kwake kazini?


“Daktari, unadhani upo uwezekano wa Sammy kuinuka tena na kuendelea na maisha yake ya kawaida?” Elli alikuwa amemuuliza daktari bingwa mmoja hapo awali wakati walipoelezwa kuhusu matokeo ya uchunguzi wa awali.


“Hilo linawezekana, tumuombe Mungu.” lilikuwa jibu fupi la daktari huyo ambaye hakutaka kuelezea kiundani zaidi kwa kuwa hakuwa msemaji.


* * * * *


Tunu alipotua nje ya ukuta wa Hospitali ya Amana alitembea haraka haraka akipita chini ya miti mikubwa ya kivuli kando kando ya ule ukuta hadi kwenye vibanda vya wasusi wa Kimasai, alipotaka kuvuka barabara ya Uhuru ili kuelekea upande wa pili alianza kusikia vishindo hafifu vya watu waliokuwa wakija nyuma yake, alipogeuka nyuma kutazama akawaona wanaume wawili wakitimua mbio kumfuata.


Hakuhitaji kueleweshwa kuwa wale watu walikuwa wakimfuata yeye kwa lengo la kumdhuru kwani alikwisha wafahamu ni watu gani na walikuwa na dhamira gani. Bila ya kupoteza muda akaanza kutimua mbio na kuvuka barabara ya Uhuru kisha akaingia katika mtaa wa Kigoma.


Wale wanaume waliongeza mwendo na kuvuka barabara ya Uhuru lakini tayari Tunu alikwisha ufikia mtaa wa Moshi na kuufuata ule mtaa akienda kasi zaidi. Wale watu walikuwa wameishtukia dhamira yake ya kutaka kuwapotea hivyo nao waliongeza mbio kumkaribia na walikuwa na kasi sana. Tunu hakutaka kuwapa nafasi hiyo wakati wao wakiufikia mtaa wa Moshi Tunu alikuwa anaelekea mwishoni mwa mtaa ule, katika mtaa mwingine wenye msongamano mkubwa wa watu, wa Utete.


Mtaa wa utete ulikuwa na wafanyabiashara ndogo wengi waliopanga bidhaa zao chini, Tunu akajichanganya na watu katika namna ya kuwapotezea wale watu waliokuwa wakimfukuza. Akautumia mwanya huo wa kujichanganya kwenye kundi lile la watu na kupotea akishika uelekeo wa upande wa kulia. Alipofika kwenye makutano ya mitaa ya Utete na Nzasa akaingia kushoto kuufuata mtaa wa Nzasa, akizidi kujichanganya kwenye umati wa watu.



Hakujua uelekeo ule ungemfikisha wapi ila alichokuwa amepanga ni kutoweka haraka eneo lile. Wakati akiharakisha kutoweka eneo lile kichwa chake kilikuwa kimetawaliwa na mchanganyiko wa mawazo. Moyo wake ulikuwa ukienda mbio sana. Alizidi kujichanganya na watu wengine na mbele kidogo akakutana na mtaa mwingine wa Morogoro uliokatisha mbele yake.


Kabla ya kujua afuate uelekeo wa upande gani; kulia au kushoto akakumbuka kutazama nyuma yake na hapo moyo wake ukapiga kite kwa nguvu. Alimwona mtu mmoja tu, mwanamume aliyekuwa amevaa suti nyeusi, kofia kubwa nyeusi ya pama na miwani myeusi ya jua akimfuatilia kwa nyuma.


Japokuwa kulikuwa na msongamano mkubwa wa watu katika eneo lile la soko lakini uzoefu wa mbinu za kijasusi ulimsaidia Tunu kugundua kuwa yule mtu alikuwa akimfuatilia yeye. Hata hivyo, kuna kitu kilianza kumchanganya, alijiuliza yule mtu alitokea wapi kwani hakuwa mmoja wa wale wawili waliokuwa wakimfuatilia tangu mwanzo.


Tunu aliamua kushika uelekeo wa upande wa kulia akiufuata mtaa wa Morogoro huku mkono wake ukiwa tayari umezama mafichoni kuipapasa bastola yake ya kijasusi. Kwa kweli alikuwa ameanza kuchoshwa sana na hali ya kufuatiliwa, hivyo alipanga kufanya shambulizi la kujihami na la kushtukiza kwa kugeuka na kumshindilia risasi za kutosha mtu yule bila kujali macho ya watu waliokuwa eneo lile kisha angepotea haraka toka eneo lile.


Aligeuka tena nyuma kumtazama yule mtu aliyekuwa akimfuatilia huku akiwa tayari amekwisha jiandaa kumfanyia shambulizi la kushtukiza lakini hakumwona! Akashangaa kidogo lakini mara akawaona tena wale wanaume wawili waliokuwa wakimfuata tangu mwanzo toka kule hospitali. Sasa walikuwa wakitimua mbio kumfuata. Tunu hakutaka kuanza kutimua mbio kwani kwa kufanya hivyo angeweza kuyavuta macho ya watu waliokuwa eneo lile, hivyo aliongeza mwendo huku akipanga namna ya kuwafanyia shambulizi la kushtukiza.


Aliufikia mtaa wa Pangani na kabla hajajua afanye nini au aelekee upande upi alimwona mwendesha bodaboda mmoja aliyekuwa anapita pale akitokea katika msikiti wa Irshaad Salafy na kuelekea upande wa Kariakoo. Tunu alikimbia kisha akarukia juu ya ile bodaboda huku akimtaka yule mwendesha bodaboda amkimbize haraka Machinga Complex, Kariakoo. Lilikuwa ni tukio la ghafla sana na wale watu waliokuwa wakimfukuza Tunu hawakuwa wamelitarajia kabisa.


Yule mwendesha bodaboda hakuwa amemtilia shaka yoyote Tunu ingawa alishangazwa na kitendo chake cha kurukia juu ya pikipiki wakati ikiwa katika mwendo. Pikipiki iliongeza mwendo na kwenda kasi kama alivyotaka Tunu, wakaufuata mtaa ule wa Pangani hadi walipoufikia mtaa wa Tabora, wakaingia upande wa kulia na safari ikaendelea. Wakati wakiingia katika mtaa wa Tabora Tunu aligeuza shingo yake kutazama nyuma, hakuwaona tena wale watu waliokuwa wakimfukuza nyuma yake.


Walipofika eneo la Machinga Complex Tunu alimlipa yule mtu wa bodaboda fedha aliyoitaja, akateremka na kujichanganya na watu wengine, kisha akachukua bodaboda nyingine akimtaka dereva wake ampeleke haraka mtaa wa Kongo. Vivyo hivyo alipofika mtaa wa Kongo na kushuka alichukua bodaboda nyingine hadi Mnazi Mmoja.


Aliendelea na mchezo huo wa kubadilisha pikipiki toka eneo moja hadi jingine na baadaye alichukua taxi katika eneo la Gerezani iliyompeleka Temeke kisha akachukua taxi nyingine, na akiwa ndani ya taxi simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Tunu aliitazama na kuliona jina la Tom, hata hivyo aliikata na kumtumia ujumbe kuwa angempigia baadaye kwani hakuwa sehemu nzuri. Tom alimsisitiza kutoacha kumpigia kwani ilikuwa muhimu.


Saa yake ya mkononi ilimwonesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa kumi na nusu wakati alipokuwa anasimama mbele ya geti kubwa jeusi la nyumba ya kifahari ya Elli katika eneo la Kurasini, huku akiiacha ile taxi ikitoweka nyuma yake. Kwa kiasi fulani alikuwa amechanganyikiwa kutokana na kuona kuwa harakati zake za upelelezi ziliingia dosari baada ya lile shambulizi la bomu nyumbani kwa Sammy.


Alibonyeza kitufe cha kengele kilichokuwa kando ya lile geti na kushangaa kuona kulikuwa na ulinzi tofauti na alivyokuwa ameacha alipokuja mwanzoni. Geti dogo kando ya lile geti kubwa jeusi likafunguliwa, mlinzi mmoja aliyekuwa wamevaa sare maalumu za kampuni binafsi ya ulinzi na mkononi akiwa ameshika bunduki akachungulia nje na kumuona Tunu.


Alimtazama kwa makini kwa kumkazia macho. Tunu alimsalimia kisha akajieleza kuwa yeye ni rafiki wa familia ya Elli na alifika hapo kuonana na Victoria. Baada ya maswali mawili matatu hatimaye Victoria aliulizwa na kuwataka wale walinzi wamruhusu Tunu aingie.


Tunu aliruhusiwa kuingia ndani ya ule uzio alikowakuta walinzi wengine wawili. Akapokelelwa na Victoria aliyemshangaa baada ya kuona akiwa hana gari. Tunu alimwabia kuwa alilazimika kuliacha kule kwenye mgahawa wa Elli’s kwa sababu za kiusalama, wakaongozana na kuingia sebuleni alikomkuta Winifrida akiwa amejikuyata kwa huzuni huku akilia kilio cha kwikwi. Winifrida alipomwona Tunu akaanza kulia kwa uchungu uchungu mkubwa na kwa sauti ya juu, mwili wote ulikuwa unamtetemeka.


“Winnie!” Tunu aliita huku akimshika Winifrida mikono, akamwinua na kumkumbatia lakini miguu ya Tunu haikuwa na nguvu hata za kusimama. Tunu akamketisha kwenye sofa huku akiketi kando yake na kuanza kumpetipeti mgongoni katika hali ya kumfariji. Tunu alikuwa amepata taarifa za shambulizi lililomlaza kitandani kaka yake Sammy.



Alimtazama kwa makini kwa kumkazia macho. Tunu alimsalimia kisha akajieleza kuwa yeye ni rafiki wa familia ya Elli na alifika hapo kuonana na Victoria. Baada ya maswali mawili matatu hatimaye Victoria aliulizwa na kuwataka wale walinzi wamruhusu Tunu aingie.


Tunu aliruhusiwa kuingia ndani ya ule uzio alikowakuta walinzi wengine wawili. Akapokelelwa na Victoria aliyemshangaa baada ya kuona akiwa hana gari. Tunu alimwabia kuwa alilazimika kuliacha kule kwenye mgahawa wa Elli’s kwa sababu za kiusalama, wakaongozana na kuingia sebuleni alikomkuta Winifrida akiwa amejikuyata kwa huzuni huku akilia kilio cha kwikwi. Winifrida alipomwona Tunu akaanza kulia kwa uchungu mkubwa na kwa sauti ya juu, mwili wote ulikuwa unamtetemeka.


“Winnie!” Tunu aliita huku akimshika Winifrida mikono, akamwinua na kumkumbatia lakini miguu ya Tunu haikuwa na nguvu hata za kusimama. Tunu akamketisha kwenye sofa huku akiketi kando yake na kuanza kumpetipeti mgongoni katika hali ya kumfariji. Winifrida alikuwa amepata taarifa za shambulizi lililomlaza kitandani kaka yake Sammy.


ENDELEA...


Ni kama vile simanzi ilikuwa imezidi baada ya Winifrida kumwona Tunu, hata pale Tunu alipojaribu kumbembeleza na kumfariji bado Winifrida alionekana hakuwa akijiweza kabisa. Kilio chake kilimshtua sana Victoria na kumfanya kuanza kumtilia shaka, alihisi labda lilikuwepo jambo fulani kati yao lililozidisha simanzi ila alikuwa hataki kusema.


Akajiuliza, ni nini ambacho kingeweza kumfanya Winifrida kulia kiasi kile, hasa baada ya kumwona Tunu? Kwa mtazamo wa kawaida, yeyote asingeshindwa kubaini kuwa kulikuwepo na jambo au siri kubwa sana moyoni mwa Winifrida. Mara kwa mara Winifrida alionekana kutaka kumweleza Tunu kitu fulani kilichokuwa moyoni mwake, alifungua mdomo wake kutaka kusema lakini maneno hayakutoka.


Kila alipotaka kusema alihisi donge fulani la uchungu likizidi kumkaba kooni na kumsononesha sana. Victoria aliwatazama kwa makini jinsi walivyokuwa wakifarijiana kama mama na mwanawe.


“Winnie, kwani kuna tatizo gani? Maana naona umebadilika ghafla!” Victoria aliuliza kwa mshangao lakini akashangaa kumwona Winifrida akiinuka na kukimbilia nje, akazunguka kueleka nyuma ya nyumba huku akiendelea kulia kilio cha kwikwi.


Wote wakapigwa na butwaa, walimtazama Winifrida kwa mshangao, kisha wakaangaliana katika hali ya kujaribu kuulizana kitu.


“Kuna nini, mbona sielewi!” Tunu aliuliza kwa mshangao. Victoria akanyanyua mabega yake juu na kuyashusha huku akibetua midomo yake. Kisha akaondoka kumfuata Winifrida kule nyuma ya nyumba.


“Winnie, kuna nini? Hivi unajua jinsi unavyolia hivi utamfanya hata Pendo ahisi labda kuna jambo baya zaidi limewatokea wazazi wake,” Victoria alimwambia Winifrida huku akipapasa kichwani.


Winifrida alitaka kusema neno lakini maneno hayakuweza kutoka, donge la uchungu lilizidi kumkaba kooni na kumfanya azidi kutokwa na machozi, kwa kweli alishindwa kuvumilia, akalia kwa uchungu.


“Winnie, naomba nisikilize mdogo wangu, kuendelea kulia hivi hakutaweza kuwasaidia kaka yako na wifi yako wapate nafuu, sanasana ni kuwachulia tu…” Victoria alisema kwa upole huku akijaribu kumfuta machozi yaliyokuwa yanachuruzika kwenye mashavu yake. “Cha msingi ni kuzidi kuwaombea kwa Mungu ili waweze kupona na, sawa?”


Winifrida alibetua kichwa chake huku akishusha pumzi ndefu na baada ya kitambo kirefu hatimaye alinyamaza na dakika tano zilizofuata waliongozwa kuelekea sebuleni. Hapo sebuleni walimkuta Tunu akiwa anaongeza na simu huku akionekana kuwa na wasiwasi kidogo. Alipowaona alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akijiweka sawa pale kwenye sofa.


“Ndiyo Tom, kwa upande wangu mimi niko poa kabisa, sijui wewe?” Tunu alisema huku akikunja sura yake kama aliyekuwa anatafakari sana.


“Nilikuwa na wasiwasi sana baada ya kuona umenipotea katika mazingira yasiyoeleweka, nikawa na wasiwasi huenda wale watu walikupata.”


“Wapi?” Tunu aliuliza huku akishtuka kidogo.


“Kule Ilala...”


“Uliniona? Wewe ulikuwa wapi?” Tunu aliuliza kwa wasiwasi huku picha ya lile tukio la kufuatwa na wale wanaume watatu kule hospitali ya Amana ikijiumba akilini kwake.


“Nilikuwa nakufuatilia nyuma nyuma ili kama wakikupata na kulianzisha balaa niweze kukulinda.”


“Kwani wewe ulikuwa umevaaje? Maana kuna mtu nilimwona lakini sikumwelewa kabisa!” Tunu aliuliza kwa mshangao huku akijaribu kuvuta picha ya tukio la kule Ilala.


“Nilivaa suti nyeusi, kofia nyeusi na miwani myeusi…”


“Ooh! Ni wewe! Unajua niliona mtu akinifuatilia kwa nyuma lakini sikuweza kutambua kama ni wewe. Nilidhani ni miongoni mwa wale watu wa jamaa yetu na kuna wakati nilipogeuka nikashangaa kutokukuona, ndiyo maana nikaamua kufanya tukio lililowaacha watu mdomo wazi wakati mimi nikiingia mitini.”


“Nilitamani sana nikuite lakini sikutaka jamaa wanishtukie hivyo nikaacha kukufuatilia mara baada ya kuwaona wakiwa nyuma yangu. Nilikuwa natumia njia za mkato kukufuatilia, hivyo nilikwenda kutokea mtaa wa pili lakini sikukuona tena, nikawa na wasiwasi.”


“Okay!” Tunu alisema kwa mshangao kisha akaongeza, “Kwani ulijuaje kama nilikuwa maeneo yale?”


“Wala sikuwa najua chochote, ilitokea tu muda huo nilikuwa kwa jamaa yangu mmoja ambaye mara nyingi huwa namtumia kama informer, ana ofisi yake mtaa wa Uhuru na Kigoma, jirani na vibanda vya wasusi wa Kimasai mara nikakuona ukipita mbiombio na kabla sijajua cha kufanya nikawaona jamaa wawili wakikufuata nyuma, kwa jinsi walivyokuwa nikajua kimenuka,” Tom alisema na kumfanya Tunu acheke.


Baada ya kile kicheko Tunu alishusha pumzi za ndani kwa ndani kisha kikatokea kitambo kifupi cha ukimya. “Basi nitakupigia simu baadaye kidogo, nipo sehemu najaribu kupata taarifa fulanifulani, si unajua tena hatuna muda.”


“Okay, nipigie mara tu utakapomaliza mambo yako!” Tom alisema na mara simu ikakatwa. Tunu alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiwatazama Winifrida na Victoria. Baada ya hapo kikatokea kitambo fulani cha ukimya. Kila mmoja alionekana akitafakari jambo.


“Nilishindwa kurudi tena kule hospitali baada ya tukio la bomu nyumbani kwa Sammy, vipi kuna taarifa gani kuhusu hali za wapendwa wetu?” Tunu alimuuliza Victoria akiuvunja ule ukimya wa ghafla uliojitokeza.


“Joyce anaendelea vizuri, ameweza kuamka na...” Victoria alisema na kusita kidogo, akamtupia jicho Winifrida. “Winnie, hebu kamletee mgeni kinywaji. Sijui utatumia nini mgeni wetu?” alisema huku akimtazama Tunu.


“Chochote kitanifaa.”


“Nasikitika kuwa hatuna chochote ila tunazo soda, juisi, bia, wine, chai na maji!” Victoria alisema kwa utani huku akiangua kicheko hafifu na kumfanya Tunu naye aangue kicheko.


“Basi naomba wine, kama ipo red wine yoyote nitafurahi zaidi,” Tunu alisema bila wasiwasi wowote huku akijiweka vizuri pale kwenye sofa.


Winifrida aliinuka huku anashusha pumzi na kuelekea kwenye ukumbi wa chakula kulikokuwa na jokofu kubwa la vinywaji, huku macho yote yakimsindikiza.


“Sikutaka asikie. Kwa kweli hali ya shemeji Sammy ni tata sana, hata madaktari wanakiri kuwa hawana uhakika kama ataweza kuamka tena,” Victoria alisema kwa huzuni huku akizuia machozi yaliyokuwa yanamlengalenga machoni.




Tunu alihisi mwili wake ukizizima kwa hofu na kuishiwa nguvu. Kikatokea kitambo fulani cha ukimya, alipotaka kusema neno akasita baada ya kumwona Winifrida akirudi akiwa amebeba trei ndogo yenye chupa kubwa ya mvinyo aina ya Pinot Noir na bilauri ndefu, aliiweka ile trei mezani. “Karibu,” alimkaribisha Tunu kwa heshima zote huku akishusha pumzi.


“Ahsante, mdogo wangu,” Tunu alimshukuru Winifrida, akaifungua ile chupa na kumimina mvinyo kwenye bilauri kisha akanyanyua ile bilauri na kupiga funda moja kubwa kisha akairudisha bilauri ile mezani, na hapo wakabaki wakitazamana kwa kitambo. Winifrida alikuwa ameketi kwenye sofa akiwa jirani kabisa na Tunu huku akimtazama kwa namna ambayo hakuna aliyeelewa nini kilikuwa moyoni mwake.


Victoria alimwangalia Winifrida kwa makini kisha akayahamishia macho yake kwa Tunu, wakaangaliana. Macho yao yaliweza kuongea mengi. Victoria akashusha pumzi na kuinuka.


“Utanisamehe kidogo, Tunu, ninakuacha na Winnie, kuna kitu nakwenda kufanya na nitarejea baada ya kama dakika kumi hivi. Jisikie huru,” Victoria alimwambia Tunu na kusimama huku akimtazama kwa makini akionekana kusubiri ruhusa yake.


“Usihofu, dada, maadam nipo na Winnie basi unaruhusiwa kiroho safi,” Tunu alimwambia Victoria huku akiachia kicheko hafifu. Victoria akaondoka akiwaacha Tunu na Winifrida.


* * * * *


“Tunu amefanikiwa kuwatoroka tena!” Mr. Oduya alimaka kwa mshangao uliochanganyika na hasira kwenye simu huku akiyakodoa macho yake mbele kwa hasira kana kwamba kulikuwa na mtu mbele yake aliyekuwa akiongea naye.


Alikuwa akiitazama picha yake mwenyewe iliyokuwa imetundikwa ukutani. Ilikuwa picha kubwa iliyotundikwa jirani na picha ya Rais wa Tanzania, Dk. Yohana Funguo. Mr. Oduya alibaki akiwa kimya ameyakodoa macho yake kwenye ile picha huku akiwa hajui aseme nini. Kwa kadiri alivyomfahamu Tunu, alijua kuwa bila ya kumdhibiti mapema basi angesababisha matatizo makubwa.


Kwa mara nyingine tena katika harakati zake Tunu alikuwa amesababisha hofu katika moyo wake, akahisi jasho jembamba likimtoka usoni. Hakujua afanye nini, kwani aliamini kuwa Tunu alipenda sana kufanya harakati za kimya kimya kwa hadhari na uangalifu zaidi.


Hata hivyo, alifarijika kiasi fulani alipojikumbusha kuwa pamoja na ujanja wote wa Tunu lakini asingeweza kuwakwepa watu wote aliowaweka kumfuatilia, Mr. Oduya aliwaamini sana watu wake aliowaweka sehemu mbalimbali za mji walizoamini kuwa Tunu angeweza kufika au kupita, watu hao walikuwa kikazi na hawakuwa na mzaha kabisa.


Kama Tunu angethubutu kurudi tena hospitali au kulifuata gari lake aliloliacha kule kwenye mgahawa wa Elli’s angekufa kama kuku. Na kama angekuwa mpumbavu kiasi cha kujitokeza ili kupambana na watu wake angekufa pia. Mr. Oduya alitamani kumpata Tunu akiwa hai ili amfundishe adabu, alitamani yeye mwenyewe aitumie bastola yake, kwa dhamira moja tu, kumuua.


Mawazo yakiwa bado yanapita kichwani kwake, alikumbuka kuwa simu ilikuwa bado ipo hewani na upande wa pili wa simu kulikuwa na watu waliokuwa wanasubiri kusikia neno lake. “Tunu ametoroka!” Mr. Oduya aliongea tena, safari hii aliongea kwa sauti ya kunong’ona kana kwamba alikuwa akimnong’oneza mtu aliyekuwa ameketi jirani yake.


“Sikieni, hakikisheni anapatikana haraka kwa gharama yoyote ile, akiwa hai au maiti. Jipangeni maeneo yote kama tulivyokubaliana na msisahau kufuatilia Sinza nyumbani kwake na Sharif Shamba, nyumbani kwa Tom. Ila kuweni makini sana maana ana hila nyingi, msikubali awababaishe,” alisema na kukata simu.


Aliketi kwenye kiti chake kikubwa cha kuzunguka kilichokuwa na magurudumu yaliyokiwezesha kusogea kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani huku akimhurumia Tunu kwa kuwa alikuwa anajihangaisha, kwani asingeweza kufika mbali wala kupata ushahidi wowote wa kumtia Oduya hatiani kuhusiana na suala la Sammy na mkewe.


* * * * *


Baada ya Victoria kuondoka na kuwaacha Tunu na Winifrida wakiwa peke yao, kilizuka tena kitambo kirefu cha ukimya. Katika kipindi kile cha ukimya Tunu alikuwa anatafakari sana kuhusu kazi iliyo mbele yake na jinsi ya kupata ushahidi wa kumtia hatiani Mr. Oduya na genge lake, kama si kwa suala la Sammy na familia yake basi kwa kile alichokifanya hapo kabla.


Alinyakua tena bilauri ya mvinyo aina ya Pinot Noir na kupiga mafunda mawili na kuirudisha bilauri ile mezani, akamtazama Winifrida kwa makini akijaribu kuyasoma mawazo yake. Kuna jambo alikuwa ameligundua usoni kwa Winifrida, jambo hilo likamfanya aachie tabasamu pana. Winifrida alikuwa ametahayari sana na hakujua aseme nini.


“Pole sana, Winnie, nafahamu ni majonzi kiasi gani uliyo nayo baada

ya mkasa huu uliowakumba kaka’ako na wifi yako. Mimi pia nimesikitika sana ndiyo maana unaniona narudi hapa mara mbilimbili,” Tunu alimwambia Winifrida huku huzuni ikiwa imemshika.


Winifrida alikuwa ameinamisha uso wake akitazama sakafuni huku anamsikiliza Tunu kwa makini halafu akashusha pumzi kwa mkupuo huku akiwa kama anayefikiria jambo fulani, kisha akainua uso wake kumwangalia Tunu huku machozi yakimlenga lenga machoni, akayafuta na kuinamisha tena uso wake kutazama chini.


“Ninaamini kuwa vyombo vya dola vinafanya kazi kikamilifu kuwasaka watu wote waliohusika, hata hivyo sina hakika sana kama watafanikiwa kwani waliofanya hivyo ni watu makini waliojipanga na wanaozifahamu vyema nyendo za maafisa wa usalama wa serikali hii, hali inayowapa mwanya rahisi wa kutopatikana. Mimi na wewe tunawafahamu wahusika, na kwa kupitia ile memory card tungeweza kuwafanya waozee gerezani lakini tatizo ndiyo imespotea baada ya nyumba kulipuliwa na bomu...” Tunu alisema kwa huzuni huku akimkazia macho Winifrida.


“Nimerudi tena kwako nikitaka kujua, pengine uliamua kunificha au sasa unakumbuka uliiweka sehemu gani. Kama uliiacha kule kule nijue sehemu, naweza kuwatumia watu wangu wa karibu wajaribu kupekua kama wataweza kuiona,” Tunu alimaliza kuongea kisha akainyakua tena ile bilauri ya mvinyo iliyokuwa mezani na kuvuta funda moja kubwa na kuirudisha tena mezani huku akiendelea kumtazama Winifrida.


“Da, Tunu, hata sijui nisemeje sasa!” Winifrida alisema kwa sauti ya chini ya kukata tamaa kama ambaye hakutaka watu wengine zaidi ya Tunu wasikie maongezi yao. Mara hii Tunu aliweza kuhisi kuwa Winifrida alikuwa mwingi wa wasiwasi na alikuwa akiongea kwa woga. Hali hiyo ikamshtua ingawaje alijitahidi sana kuuzuia mshtuko wake.


“Nafahamu kuwa pengine ikawa si rahisi sana kwako kufahamu kaka yako yupo kwenye hatari kwa kiwango gani, ila naamini kuwa ukitulia vizuri na kufikiria unaweza kuwa na hisia ya jambo fulani ambalo huenda likawa msaada mkubwa wa kuniwezesha kuwanasa wote waliohusika,” Tunu alizungumza kwa sauti ya chini huku pia akikwepa maongezi yao yasisikike na watu wengine.


Tunu alifikiria sana na kushusha pumzi, alikuwa anatazama kule alikokuwa ameelekea Victoria katika namna ya kuibia ibia, ingawa alijitahidi sana kuificha hali ile. Tunu aliona, hali hiyo ilikuwa ni ishara nyingine muhimu aliyoweza kuishtukia haraka, hivyo hakuwa na mashaka tena kuwa Winifrida alikuwa na jambo ambalo alitamani sana kulisema ila hakutaka mtu mwingine asikie.


“Ni kweli kuwa nilikuwemo ndani wakati wale majambazi wanaingia lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya mimi kufahamu yaliyokuwa yanaendelea kwa kuwa nilikuwa nimejificha ndani ya kabati,” Winifrida alimjibu Tunu kwa msisitizo.


“Sawa! lakini hebu kumbuka vizuri ulipoihifadhi memory card, naamini kabisa kuwa itakuwa pamoja na simu yako. Je, simu ipo wapi, au nayo uliiacha kule kule nyumbani?” Tunu aimuuliza Winifrida kwa sauti tulivu ya kubembeleza huku moyoni akijyapima maneno yake kama yalikuwa na ukweli wowote.


“Kwa kweli sikumbuki,” Winifrida alijibu na kumfanya Tunu asitishe mohojiano, alibaki akimtazama kwa makini ingawa Winifrida aliendelea kuyakwepesha macho yake pembeni yasikutane na ya Tunu, na kwa hali ile Tunu akajua kuwa Winifrida alikuwa akimficha jambo fulani ambalo asingeweza kumlazimisha aliweke bayana kwa wakati ule.


“Sawa kama hujisikii kuniambia, inawezekana pengine huniamini au ni kweli hujui. Lakini elewa kuwa mimi pia nimeumizwa sana na matukio haya ya kaka yako na wifi yako, nisingeweza kustahimili kuacha kazi zangu zote na kufuatilia suala hili moja tu,” Tunu alisema huku akijinyoosha.


“Basi niitie wifi yako nimuage niondoke zangu, nitaendelea kuwepo hapa jijini kwa muda wa siku kadhaa, hivyo siku ukijisikia kuniambia chochote namba zangu hizi hapa, wewe nibip tu,” Tunu alimwambia Winifrida huku akisimama na kunyoosha mkono wake kumpa business card yenye namba zake za simu.


Winifrida alionekana kusita kidogo, aliitazama ile kadi kwa wasiwasi kisha macho yake yakahamia kwenye uso wa Tunu, “Basi kaa, n’takwambia ukweli...” alisema huku akimeza mate kutowesha koo lake lililokauka. Tunu alimtazama kwa makini na kuketi tena juu ya sofa.


Mambo yanazidi kunoga. Je, Winifrida anataka kumwambia nini Tunu? Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua...





“Sawa! lakini hebu kumbuka vizuri ulipoihifadhi memory card, naamini kabisa kuwa itakuwa pamoja na simu yako. Je, simu ipo wapi, au nayo uliiacha kule kule nyumbani?” Tunu aimuuliza Winifrida kwa sauti tulivu ya kubembeleza huku moyoni akijyapima maneno yake kama yalikuwa na ukweli wowote.


“Kwa kweli sikumbuki,” Winifrida alijibu na kumfanya Tunu asitishe mohojiano, alibaki akimtazama kwa makini ingawa Winifrida aliendelea kuyakwepesha macho yake pembeni yasikutane na ya Tunu, na kwa hali ile Tunu akajua kuwa Winifrida alikuwa akimficha jambo fulani ambalo asingeweza kumlazimisha aliweke bayana kwa wakati ule.


“Sawa kama hujisikii kuniambia, inawezekana pengine huniamini au ni kweli hujui. Lakini elewa kuwa mimi pia nimeumizwa sana na matukio haya ya kaka yako na wifi yako, nisingeweza kustahimili kuacha kazi zangu zote na kufuatilia suala hili moja tu,” Tunu alisema huku akijinyoosha.


“Basi niitie wifi yako nimuage niondoke zangu, nitaendelea kuwepo hapa jijini kwa muda wa siku kadhaa, hivyo siku ukijisikia kuniambia chochote namba zangu hizi hapa, wewe nibip tu,” Tunu alimwambia Winifrida huku akisimama na kunyoosha mkono wake kumpa business card yenye namba zake za simu.


Winifrida alionekana kusita kidogo, aliitazama ile kadi kwa wasiwasi kisha macho yake yakahamia kwenye uso wa Tunu, “Basi kaa, n’takwambia ukweli...” alisema huku akimeza mate kutowesha koo lake lililokauka. Tunu alimtazama kwa makini na kuketi tena juu ya sofa.


ENDELEA...


Winifrida alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu kisha akabaki kimya huku akiminyaminya viganja vyake huku akivitazama. Tunu alimtazama kwa tabasamu kwa kitambo fulani.


“Niambie basi, shoga’angu!” Tunu alisema kwa sauti ya chini ya kubembeleza huku akitabasamu.


Winifrida alitaka kuongea neno lakini akasita, aibu ilimwingia, akajifunika uso wake kwa viganja. Tunu aliendelea kumtazama kwa makini huku akitabasamu.


“Naomba kwanza uniambie ukweli, umejuana vipi na kaka Sammy?” hatimaye Winifrida aliuliza huku aibu ikijionesha waziwazi usoni kwake


“Na wewe niambie, una boyfriend?” Tunu naye alimuuliza Winifrida huku akiendelea kutabasamu.


Winifrida alionekana kushtuka sana lakini hakuonesha moja kwa moja. Alimtazama Tunu moja kwa moja machoni huku akijitahidi kuifukuza aibu. Kisha akatingisha kichwa chake juu na chini, kushoto na kulia, alikuwa amekubali na kukataa kwa wakati mmoja, halafu akafunika uso wake kwa viganja tena na kuficha uso kwenye mapaja. Safari hii Tunu hakutabasamu. Alimtazama kwa kina. Winifrida aliinuka huku akimtazama Tunu kwa aibu kisha akajaribu kujiweka sawa kwenye sofa. Alionekana kuwa na hofu iliyochanganyika na aibu.


“Okay, kama hutaki kuniambi ngoja mimi nikwambie...” Tunu alisema kwa sauti tulivu huku akijiweka sawa kwenye sofa, “Sammy alikuwa boyfriend wangu… ndiye alikuwa mwanamume wangu wa kwanza, wakati huo alikuwa hajaoa bado. Sasa hebu fikiria, utajisikiaje pale mtu unayempenda sana anapopata matatizo kama haya!”


Winifrida alibaki kimya akionekana kumsikiliza Tunu kwa makini sana. Maneno yale yalionekana kumwingia vilivyo. Akavuta pumzi ndefu huku hofu yake ikionekana kupungua. “Niahidi kwamba hutamwambia kabisa kaka Sammy wala mtu mwingine,” alisema kwa aibu.


“Nilikuahidi na ninakuahidi tena, yote haya yatabaki kuwa siri yetu wawili,” Tunu alisema kwa msisitizo.


“Basi subiri nikuoneshe,” Winifrida alisema na kuinuka, akaelekea chumbani kwao akimwacha Tunu akimsindikiza kwa macho nyuma yake, kisha akatingisha kichwa chake huku akiachia tabasamu.


* * * * *


Katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Ramon Mamboleo alikuwa hatulii kwenye kiti chake. Kiti chake kilikuwa kama chenye moto. Hakikukalika kabisa. Mara aliinuka mara aliketi kana kwamba alikuwa amekalia makaa ya moto ambayo yalimuunguza kila alipojaribu kuketi. Alikuwa amemezwa na fikra na hakuwa na furaha wala amani kabisa.


Mkono wake wa kulia alikuwa ameshika redio ya upepo akionekana mwenye wasiwasi. Mara kwa mara aliinua mkono wake wa kushoto na kutazama saa yake ya mkononi kisha alitingisha kichwa chake. Alikuwa akiwasubiri askari wake wamletee taarifa ya kiuchunguzi ambayo ilitakiwa iwasilishwe saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo, kwenye kikao kati ya wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Ulinzi.


Naibu Kamishna Ramon Mamboleo alitamani aipate taarifa hiyo mapema ili aipitie na kurekebisha kasoro kabla hajaenda kwenye kikao hicho. Ni muda mfupi tu uliopita alikuwa amepigiwa simu na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Solomon Zirro akitakiwa kuwasilisha taarifa ya uchunguzi wa kile kilichokuwa kimetokea ili kijadiliwe kwenye kikao hicho.


Kabla ya simu hiyo macho yake yalikuwa yakiitazama chati yake ya taarifa za uhalifu katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam huku akijipongeza kwa jinsi ilivyoonesha kuwa tangu akabidhiwe jukumu hilo idadi ya vitendo vya uhalifu ilikuwa imeshuka kwa kasi. Uhalifu mkubwa ulipungua sana na kubakia udokozi mdogomdogo, wizi wa kuaminiana na ufisadi wa mali za umma. Ingekuwa ni amri yake, alitamani sana jiji la Dar es Salaam liwe jiji la kwanza duniani lisilo na uhalifu.


Lakini shambulio la bomu kwenye nyumba ya Sammy liliashiria kuwa mambo hayakuwa shwari kama alivyodhani. Sasa kichwa chake kiliwaka moto, alikuwa mtu wa kwanza aliyestahili kuwa na wasiwasi na hali hiyo kwani ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kusimamia usalama wa raia na mali zao katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Alikuwa akiumiza kichwa chake na kukesha usiku na mchana kuhakikisha hakuna tukio lolote la kutishia usalama ndani ya jiji hilo linalotokea.


Aliishukuru sana falsafa ya ulinzi shirikishi kwani ilikuwa imesaidia sana kulifanya jiji la Dar es Salaam nan chi kwa ujumla kuwa na hali ya utulivu. Hata hivyo, alijikuta akiingiwa na simanzi mara baada ya kukumbuka kwamba, kama ilikuwa imefikia hatua raia wenyewe walishirikishwa kukesha nje wakijilinda, jukumu lililopaswa kufanywa na vyombo vya usalama, basi hilo ni jambo ambalo hakulipenda kabisa ingawa hakuwa na namna nyingine ya kufanya.


Alijiuliza, kama raia walikuwa wakijilinda wenyewe, je, vyombo hivyo vya ulinzi na usalama vilikuwa vinafanya nini? Inamaana haviwezi? Havifai? Au haviaminiki? Na kama hivyo ndivyo, je, kulikuwa na umuhimu gani wa kuwa na vyombo hivyo na kuvitengea bajeti kila mwaka? Maswali hayo yalimfikirisha sana Naibu Kamishna Ramon Mamboleo, aliamua kuja na mpango kabambe wa kuhakikisha hali hiyo inakoma, kwani alikuwa askari mwaminifu aliyeipenda na kuiamini kazi yake. Alitamani kuona raia wote ndani ya jiji la Dar es Salaam wakilala usingizi wao kwa amani.




Akiwa bado amezama kwenye lindi la fikra nzito alishtushwa toka kwenye mawazo yake baada ya mlango wa ofisi yake kugongwa mara moja na kisha kufunguliwa, askari wake wawili machachari wakaingia. Hawa walikuwa Inspekta Abel na Sajenti Mapunda ambao walipoingia walisimama mbele ya meza yake kwa ukakamavu na kupiga saluti.


“Vipi, umepata kitu?” Naibu Kamishna Ramon Mamboleo aliuliza mara baada ya kujibu ile salamu huku akiwa ameyatuliza macho yake kwenye uso wa Inspekta Abel. Muda huo alikuwa amesimama kandokando ya meza yake akiwa ameshika kiuno. Uso wake ulikuwa bado umemezwa na fikra na sononeko.


“Ndiyo, afande!” Inspekta Abel aliitikia kwa ukakamavu huku akinyoosha mkono wake kumkabidhi Naibu Kamishna Ramon Mamboleo faili dogo lenye taarifa za uchunguzi alilokuwa amelishika mkononi.


Naibu Kamishna Ramon Mamboleo alilipokea lile faili kisha akaketi kwenye kiti chake huku akiwaashiria wale askari waketi. Wote wakaketi kwenye viti vilivyokuwa vinatazamana vikiwa mbele ya meza ya Naibu Kamishna Ramon Mamboleo.


Mamboleo alilifungua lile faili, akajiegemeza kwenye kiti chake na kupitia harakaharaka lakini kwa umakini mkubwa ile taarifa kisha akaziangalia nyaraka zingine kutoka kampuni ya mawasiliano iliyoonesha namba zote za simu alizopigiwa Sammy na ujumbe mfupi aliotumiwa, kisha akaziangalia picha kadhaa zilizokuwa zimeambatanishwa na taarifa ile na kuachia tabasamu. Ingalau sasa alikuwa amepata cha kuelezea, na pia mahali pazuri pa kuanzia. Ilikuwa ni kheri kwake, askari ambao aliwapa kazi ya kufanya uchunguzi wa matukio hayo walipata kitu cha ziada ndani ya muda mfupi.


Baada ya kuipitia taarifa ile kwa takriban dakika ishirini, Naibu Kamishna Ramon Mamboleo alitulia kwa dakika zipatazo mbili, akavuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.


“Ingalau tumepata pa kuanzia, hata hivyo, bado nawahitaji sasa mchimbue zaidi, hawa wote waliohusishwa humu nataka wahojiwe na wale mtakaohisi kuhusika muwatie ndani,” Naibu Kamishna Ramon Mamboleo alisema huku akilifunga lile faili.


“Sawa, afande!” Inspekta Abel aliitikia kwa sauti ya ukakamavu.


Naibu Kamishna Ramon Mamboleo aliinuka na hapo hapo Inspekta Abel na Sajenti Mapunda nao wakainuka na kusimama kwa ukakamavu. Wakapeana mikono na kuagana.


* * * * *


“Vyote ni shilingi laki moja na elfu thetathini na tano tu,” mhudumu mmoja wa kike alisema akimtazama Tom kwa makini. Hayo yalitokea ndani ya ‘supermarket’ kubwa iliyopo kwenye majengo ya Mlimani City eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, ambapo Tom alikwenda kujipatia mahitaji muhimu kwa ajili yake na Tunu.


Baada ya kutajiwa kiasi, Tom alizama mfukoni na kutoa wallet yake, akahesabu kiasi hicho cha fedha na kumkabidhi yule mhudumu na kupewa risiti yake, akaaga na kuanza kupiga hatua kutoka huku akisukuma torori dogo lililojaa bidhaa mbalimbali ambazo zilikuwa zimefungashwa ndani ya mifuko yenye chapa ya jina la ‘supermarket’ hiyo. Tom alikuwa bado amevalia suti nyeusi, kofia na miwani myeusi ya jua.


Wakati akitoka kulifuata gari lake lililokuwa limeegeshwa katika viunga vya maegesho ya magari ndani ya uzio wenye ulinzi wa Mlimani City, aliyazungusha macho yake kutazama pande zote kabla hajajivuta taratibu kuelekea kilipo chombo chake cha usafiri. Muda huohuo simu yake ya mkononi ikaanza kuita, Tom aliiangalia kwa makini na kuliona jina la Tunu, akashusha pumzi na kuipokea.


“Hello!”


“Tom, usije tena, nimewasiliana na Bob Chopa na tumekubaliana kuwa kwa sababu za kiusalama yeye ndiye atanifuata huku, halafu wewe tutakutana Kinyerezi. Sijui wewe umefikia wapi?” Tunu aliuliza kwa sauti iliyoonesha furaha isiyo kifani.


“Nimefanikiwa, sasa ndo natoka hapa Mlimani City,” Tom alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Una uhakika kila kitu kiko sawa? Hakuna shaka yoyote?” Tunu aliuliza kwa shauku.


“Yeah, hali ni shwari ila kama kitatokea chochote nitakujulisha,” Tom alisema huku akiyazungusha macho yake pembe zote kuangalia kama kulikuwa na mtu yeyote aliyemtilia shaka.


“Basi nitakukuta huko kuanzia saa mbili usiku, itanibidi kwanza nipitie nyumbani kwangu Sinza nika...” Tunu alijibu.


“Kuwa makini sana, kuna watu wamewekwa huko kukusubiria,” Tom alimuasa Tunu.


“Usihofu, Tom, ninajua... huu ni mchezo mdogo sana kwangu, wenyewe watashangaa na roho zao,” Tunu alisema huku akiangua kicheko hafifu.


“Na vipi kuhusu gari?”


“Wacha likae palepale Elli’s, lipo mahali salama.”


“Okay, see you later,” Tom alisema huku akilifikia gari lake aina ya Toyota Rav4 L jeupe, akazungusha tena macho yake pembe zote kuangalia kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia, hakumwona.


“See you,” Tunu alisema na kukata simu.


Tom akafungua kwanza mlango wa nyuma wa gari na kutia mizigo yake huko kisha akaelekea kwenye mlango wa dereva na kuufungua akaingia na kuketi halafu akatia gari moto. Alitokea kwenye geti la upande wa kaskazini kwenye barabara ya Survey, kisha akaingia upande wa kulia akiifuata barabara ya Survey. Ikapita kama sekunde tano tu, gari lingine aina ya Toyota Hilux double cabin la rangi ya bluu lililokuwa na namba bandia ambalo pia lilikuwapo kwenye viunga vya maegesho ya Mlimani City, nalo likatoka kumfuata.


Tom pasipo kujua akaendelea na safari yake, aliufikia mzunguko wa barabara za Sam Nujoma na ile ya Survey na kuingia kulia akiifuata barabara ya Sam Nujoma. Alipoifikia barabara ya Igesa iliyokuwa inakwenda kutokea Sinza akaburini, Tom akaamua kupima upepo ili aone kama kulikuwa na gari lolote lililokuwa limemuungia mkia nyuma, hivyo akakunja kushoto kuifuata barabara ile.


Lile gari aina ya Toyota Hilux double cabin la rangi ya bluu lililokuwa nyuma yake likiyaacha magari matatu katikati yao nalo likakunja kuelekea barabara ile, Tom akaanza kupata shaka kwamba huenda alikuwa anafuatiliwa. Kwa kutazama vioo saidizi vya pembeni vya gari lake alipata kuliona gari lile vizuri, akakumbuka kuwa alikuwa ameliona pale kwenye viunga vya maegesho ya Mlimani City.


Akaamua kuongeza kasi ya gari lake ili kuona kama na wao wangeweza kuongeza mwendo. Alipotazama tena kwenye vioo saidizi vya pembeni akaliona lile gari nalo likiongeza mwendo huku likijaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake. Sasa Tom hakuwa na shaka kuwa alikuwa anafatwa. Akaona afanye jambo ili kuwapoteza.




Alizidisha mwendo na alipofika Kanana Car Garage, kabla hajalifikia duka moja la kuuza keki, maarufu kama Happiness House of Cakes akakunja kushoto akiufuata mtaa mmoja fupi hadi alipokutana na mtaa mwingine wa Social uliokuwa unatokea barabara ya Shekilango na kuishia katika mtaa wa Mjiasali. Hapo akakunja kuingia kushoto kuufuata ule mtaa wa Social, sasa alikuwa anarudi alikotoka.


Kwa kuwa mtaa ule haukuwa na magari mengi aliamua kuendesha gari lake kwa mwendo wa kasi hadi alipoupata mtaa wa Mjiasali akakunja kuingia upande wake wa kulia, kisha akaingia tena kushoto akiifuata barabara ya Igesa na kwenda kutokea barabara ya Sam Nujoma. Hapo akavuka taa za kuongozea magari barabarani bila kujali kama taa nyekundu ilikuwa imewashwa kumtaka asubiri, kidogo asababishe ajali lakini hakujali, akakunja kuingia kulia akionekana kurudi eneo la Mlimani City.


Aliendesha kwa fujo aliyapita magari mengine hadi alipoufikia tena mzunguko wa barabara za Sam Nujoma na ile ya Survey, akakunja kuingia kushoto akiifuata barabara ya Survey. Ndani ya muda mchache, akawa amelipoteza kabisa lile gari lililokuwa linamfuatilia. Sasa aliazimia kupitia barabara ya Makongo kisha akatokee Mbezi Mwisho ili kwenda Kinyerezi.


Alipohakikisha kuwa amefanikiwa kuwapoteza akaona ni vyema amtaarifu Tunu juu ya jambo hilo. Akampigia simu na kumweleza yote yaliyotokea na jinsi alivyofanikiwa kuwapoteza, kisha wakaonyana kuendelea kuwa waangalifu ili wasije wakaharibu mambo wakati wapo katika hatua za mwisho kukamilisha uchunguzi wao.


* * * * *


Saa moja na nusu usiku, gari aina ya Nissan Patrol la rangi ya bluu lilimshusha Tunu katika mtaa wa pili toka barabara ya Mori, katika eneo la Sinza Mori. Eneo alilorushwa lilikuwa umbali wa takriban mita mia tano toka ilipo nyumba ya Tunu, jirani na Kanisa la Reality of Christ. Tunu hakutaka wamfikishe hadi nje ya nyumba yake kwa sababu moja kubwa ya kutotaka kushtukiwa na mtu yeyote ambaye angekuwa ameweka mtego wa kumnasa.


Aliposhuka akaamua kuingia kwenye uchochoro wenye kiza hafifu uliomchukua hadi kwenye mtaa ule wenye nyumba yake kisha akazunguka kuelekea nyuma ya nyumba yake, lakini kabla ya kufanya chochote akaamua kufanya uchunguzi ili kujiridhisha kuhusu usalama wa eneo lote.


Japo hakuweza kumwona mtu yeyote nje ya nyumba ile iliyokuwa na giza kutokana na kutowashwa taa lakini aliamua kuchukua tahadhari zote, alitumia mbinu yake ya kijasusi kuupanda ukuta na kurukia ndani pasipo kutoa kishindo, kisha akaingia ndani ya nyumba kupitia dirisha dogo la jikoni huku akiwa amechukua tahadhari zote za kukwepa kumshtua kiumbe yeyote ambaye angekuwa ameweka mtego mle ndani.


Akiwa anaifahamu vizuri ramani ya nyumba yake, mara tu alipokiacha chumba cha jiko akaingia upande wake wa kulia akiifuata korido ndogo pembeni ya sebule ili aelekee vyumbani, mkono wake wa kuume ulikuwa umeshika bastola yake ndogo ya kijasusi aina ya Glock 19M, macho yalikuwa yamemtoka kukodoa na masikio yake yamesimama kusikiliza.


Hapo akasita kwanza kusikilizia kama yu salama. Alipoona kimya, akapiga moyo konde na kuanza kusonga zaidi. Kisha akahisi kusikia sauti hafifu ya mtu akisogea, alipogeuka kutazama nyuma alikuwa tayari amechelewa kwani mtu mmoja alikuwa amemfikia karibu yake! Kabla hajajua afanye nini akasikia sauti ya kilimi cha bastola kilichovutwa ikipenya masikioni mwake kumwonya asifanye chochote. Ikabidi asitishe kile alichokuwa akitaka kukifanya na hakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuanzisha mapambano ya ana kwa ana katikati ya giza lile.


Upesi akanyoosha mkono wake wenye bastola lakini kwa kasi ya ajabu ule mkono ukapigwa teke na bastola ile ikadondoka chini! Moyo wake ulikuwa kama uliosimama ghafla kabla ya kurudia mapigo yake na kuanza kwenda mbio huku jasho jepesi likianza kutoka. Hata hivyo alijiweka sawa kwa jili ya pambano.


“Nilikuwa natarajia ujio wako, Tunu,” Victor alisema huku akimwelekezea bastola yake aina ya 45 Colt. Victor alikuwa amevalia mavazi meusi yaliyomfanya aonekane kama kivuli, shati linalobana mwili pamoja na suruali nyepesi mithili ya ‘traki’.


Tunu hakutia neno. Akili yake ilikuwa inafanya kazi haraka sana baada ya kugundua kuwa alikuwa anapambana na Victor. Wakati Victor akijiandaa kufyatua risasi alishtukia akipigwa pigo ambalo hakuweza kulielewa kwa haraka lilipigwa kwa mtindo gani kiasi cha kuweza kuipokonya bastola yake mkononi. Ile bastola ikaangukia sehemu fulani sakafuni ndani ya ile nyumba na kutokana na kiza kilichokuwemo mle ndani hakuweza kuiona.


Kabla hajajua afanye nini, Tunu alizunguka kwa kasi ya ajabu akitupa pigo la ngumi usawa wa shingo ya Victor lakini ilikuwa kazi bure kwani Victor alikuwa mwepesi kuishtukia hila yake hivyo pigo la Tunu lilikata upepo bila kutoa majibu na kumfanya apepesuke kwa kupoteza mhimili na wakati huohuo akajikuta akipokea kipigo cha ngumi mbili kavu za chapuchapu mbavuni mwake.


Victor alikuwa mwepesi sana kiasi cha kumshangaza sana Tunu, alirusha ngumi nyepesi na za haraka. Alikuwa mwepesi sana lakini mashambulizi yake hayakuwa na madhara kwa Tunu. Mara kwa mara Tunu alitabiri mwenendo wake na hivyo basi ikawa rahisi kumkabili adui yake. Alipopiga pigo jingine la teke Tunu aliwahi kulikwepa kwa kuruka hewani kwa mtindo wa samasoti na alipokuwa akitua chini alibinuka na kuachia teke farasi. Lilikuwa pigo zuri lililomfanya Victor kugugumia kwa maumivu.


Tunu hakutaka kumkawiza, akamfuata katika mtindo wa kujiviringisha sakafuni kama gurudumu na alipomfikia akajizungusha na kumchota mtama wa chini lakini Victor aliwahi kumshtukia, akamtandika teke la kifuani lililomrusha nyuma. Jambo ambalo Tunu hakuwa akilifahamu ni kwamba, Victor alikuwa ana silaha nyingine kwenye mwili wake, alikuwa na visu na alikuwa mzuri zaidi kwenye matumizi ya silaha kuliko mapigano ya kawaida.


Basi waliendelea kupimana ubavu, Tunu alikuwa anajipindua na kurusha mateke kwa haraka sana, kisha alimgeuzia mgongo Victor na kupaa juu na kujigeuza huku akiwa ametanua miguu yake na kuutanguliza mguu wake wa kulia kwa nguvu huku ukifuatiwa na mguu wa kushoto. Victor akafanya jitihada za kujikinga na shambulizi hilo huku akiwa tayari amechomoa kisu toka kwenye mguu wake na kukishika vyema mkononi.


Tunu alipotua chini akatahamaki kisu kikipita na kuuchana mguu wake wa kulia, damu ikaanza kumtoka. Tunu hakujali, akaruka hewani na kuganda ukutani huku mguu mmoja ukiwa umegota upande mmoja wa ukuta na mguu wake mwingine upande mwingine wa ukuta wa korido ile, kisha akajibetua na kuruka hewani huku akitua mbele ya Victor, na wakati huohuo akimtupia pigo moja matata la teke kifuani kwake lililomfanya apepesuke na kugugumia kwa maumivu,

Kuona hivyo, Victor akarusha kisu, lakini Tunu alikikwepa na kuruka hewani kisha akamshindilia Victor ngumi tatu mfululizo za mbavuni na kuzivunja. Victor akashika mbavu zake akiugulia huku akitema damu. Alikuwa anahisi maumivu makali sana. Hakuweza tena kuhimili kwani ngumi zile zilimfanya kuwa mdhaifu sana katika kupambana na Tunu.


Tunu aliruka tena hewani na alipotua aliachia teke mauti lililopoteza kabisa fahamu za Victor, teke jingine lilipotua Victor hakujua maumivu yake kwani tayari alikuwa amezirai.





Basi waliendelea kupimana ubavu, Tunu alikuwa anajipindua na kurusha mateke kwa haraka sana, kisha alimgeuzia mgongo Victor na kupaa juu na kujigeuza huku akiwa ametanua miguu yake na kuutanguliza mguu wake wa kulia kwa nguvu huku ukifuatiwa na mguu wa kushoto. Victor akafanya jitihada za kujikinga na shambulizi hilo huku akiwa tayari amechomoa kisu toka kwenye mguu wake na kukishika vyema mkononi.


Tunu alipotua chini akatahamaki kisu kikipita na kuuchana mguu wake wa kulia, damu ikaanza kumtoka. Tunu hakujali, akaruka hewani na kuganda ukutani huku mguu mmoja ukiwa umegota upande mmoja wa ukuta na mguu wake mwingine upande mwingine wa ukuta wa korido ile, kisha akajibetua na kuruka hewani huku akitua mbele ya Victor, na wakati huohuo akimtupia pigo moja matata la teke kifuani kwake lililomfanya apepesuke na kugugumia kwa maumivu,


Kuona hivyo, Victor akarusha kisu, lakini Tunu alikikwepa na kuruka hewani kisha akamshindilia Victor ngumi tatu mfululizo za mbavuni na kuzivunja. Victor akashika mbavu zake akiugulia huku akitema damu. Alikuwa anahisi maumivu makali sana. Hakuweza tena kuhimili kwani ngumi zile zilimfanya kuwa mdhaifu sana katika kupambana na Tunu.


Tunu aliruka tena hewani na alipotua aliachia teke mauti lililopoteza kabisa fahamu za Victor, teke jingine lilipotua Victor hakujua maumivu yake kwani tayari alikuwa amezirai.


SASA ENDELEA...


Kwa sekunde kadhaa Tunu alibaki amesimama pale akimtazama Victor huku akitweta ovyo na kijasho chepesi kilikuwa kikimtoka usoni. Japokuwa hakuwa amepata upinzani mkubwa sana kama alivyokuwa ametarajia baada ya kuwa amechomoka na ushindi rahisi katika pambano lile, lakini hakuamini kabisa kuwa Victor alikuwa peke yake eneo lile.

Hakutaka kupoteza muda, kwa harakaharaka alianza kumpekua mifukoni na maeneo mengine ya mwili lakini hakupata kitu chochote cha maana zaidi ya magazine moja ya bastola iliyojaa risasi na kifaa maalumu cha kuepeleka mawasiliano kwa wenzake.


Tunu aliichukua ile magazine ya bastola iliyojaa risasi na kisha kile kifaa maalumu cha mawasiliano alikiharibu kwa kukikanyagakanyaga kwa mguu wake pale sakafuni. Kisha alijitazama jinsi alivyokuwa amechafuka kwa damu iliyotokana na lile jeraha la kisu mguuni kwake. Aliokota kile kisu na kulichana shati la Victor, akajifunga pale kwenye jeraha ili kuzuia damu isiendelee kutoka.


Sasa alijua kuwa hakuwa na muda zaidi wa kuendelea kupoteza katika eneo lile kwa kuamini kuwa yote yaliyotokea wenzake Victor walikuwa wakiyasikia na sasa wangepatwa na wasiwasi zaidi baada ya mawasiliano kati yao na Victor kukatika ghafla. Hivyo, haraka akaanza kuitafuta bastola yake iliyokuwa imeanguka gizani.


Alitoa kurunzi yake ndogo ya kijasusi toka mfukoni na kuanza kumulika kule alikodhani ilikuwa imeangukia. Ndani ya muda mfupi akawa amefanikiwa kuipata ile bastola yake na kuirudisha tena kwenye himaya yake, akaiokota na ile bastola ya Victor na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake ili kuchukua begi lake. Kama alivyokuwa ametarajia, mlango wa chumbani kwake ulikuwa wazi.


Tunu alisita kidogo na kuyatega vyema masikio yake kusikiliza, hakukuwa na sauti yoyote iliyomtia shaka. Akaingia taratibu huku akitamani sana kuwasha taa ya mle chumbani lakini nafsi yake ilimuonya kuwa kwa kufanya vile angeweza kuyavuta macho ya adui ambayo yangekuwa jirani na eneo lile. Akaamua kuingia hivyo hivyo huku akitembea kwa kunyata, alimulika kwa kutumia ile kurunzi yake ndogo.


Alichokiona mle ndani kilimzidishia hasira na kumfanya ahisi mapigo ya moyo wake yakisimama kwa muda na yalipoanza tena moyo ukaanza kwenda mbio isivyo kawaida.


Aligundua kuwa upekuzi wa ovyo ulikuwa umefanyika ndani ya chumba chake, kabati kubwa la ukutani lilikuwa limefunguliwa na kuachwa wazi. Nguo zake chache zilizokuwemo humo zilikuwa zimetupwatupwa ovyo sakafuni na vitu vyake vilipekuliwa na kutawanywa ovyo. Droo za ndani za lile kabati zilikuwa zimevunjwa na vitu vilivyokuwa mle ndani vilikuwa vimetawanywa ovyo kila mahali. Godoro katika kitanda chake pia lilikuwa limevurugwa na kuinuliwa.


Tunu alishuka pumzi za ndani kwa ndani huku akimeza mate ya uchungu kutowesha koo lake lililokauka kwa hasira, kisha akaelekea moja kwa moja kwenye mlango wa chumba kidogo cha maliwato na kuingia mle ndani kwa tahadhari kubwa huku akimulika kwa utulivu. Aliyapeleka macho yake kutazama juu ya dari kwenye gypsum ambako kulikuwa na mlango mdogo wa siri wa kumruhusu mtu kupanda na kuingia ndani ya paa la ile nyumba.


Alitazama kwa makini na kuachia tabasamu baada ya kuuona uzi mwembemba mweupe uliokuwa umegundishwa kwa umakini sehemu ya ule mlango wa siri. Tunu alikuwa ameutegesha ule uzi kwa umakini wa hali ya juu ili endapo mtu yeyote angeufungua ule mlango mdogo wa siri wa kuelekea kule juu basi ule uzi ungekatika.


Hali ile ilikuwa ni ishara kuwa sehemu ile ilikuwa haijafikiwa na mtu mwingine yeyote na hivyo kudhihirisha kuwa vitu vyake muhimu vilikuwa salama. Tunu akajisogeza na kupanda juu ya sinki la maji, kisha akajivuta na kuusukuma ule mlango wa siri na kupeleka mkono wake ndani, vidole vyake vikagusa begi lake dogo la safari. Akashusha pumzi za ahueni na kulivuta lile begi ili kulishusha.


Lilikuwa ni lile begi lake la safafri alilokuja nalo toka jijini Mwanza likiwa na nguo zake chache na vifaa vyake vya kazi, ikiwemo laptop yake yenye program zote muhimu kwa ajili ya kazi za kishushushu, kisu maalumu kitumiwacho na majasusi (Butterfly Knife) na vifaa vingine. Begi lilikuwa vilevile kama alivyokuwa ameliacha siku iliyotangulia siku hiyo.


Tunu aliivua ile suti yake ya bluu aliyokuwa ameivaa tangu asubuhi ya siku ile na kujisafisha kwa maji harakaharaka akijaribu kuiondoa damu miguuni kwake kisha akavaa suruali ya blue ya jeans na t-shirt nyeusi. Miguuni alivaa raba za simpo nyeusi.

Alipomaliza akatoka haraka kule bafuni na kuingia chumbani huku akiipachika bastola yake kiunoni, kisha akalifungua lile begi na kutoa begi lenye laptop, akachukua vifaa vyake vyote vya kazi, ile magazine ya bastola iliyojaa risasi na bastola ya Victor na kuviweka haraka kwenye lile begi la laptop kisha akaanza kupiga hatua kwa tahadhari kuelekea nje.


Kabla hajatoka alichungulia sebuleni na kumulika kwa kutumia ile kurunzi yake ndogo ya kishushushu, hakushangaa kuona kuwa hata kule sebuleni pia walikuwa wamepekua na kutawanya ovyo vitu vyake wakivitupatupa huku na kule. Kwa kuwa Tunu alikuwa amepata vitu vyake muhimu, sasa akili yake ilikuwa mbali, alikuwa anawaza jinsi atakavyoufunga ukurasa wa kesi ile na kuimaliza kabisa jeuri ya Mr. Oduya baada ya kushindwa kuikamilisha kazi hiyo miaka mitatu iliyokuwa imepita.


Wakati akitoka nje kupitia mlango wa jikoni mara akahisi kusikia vishindo hafifu vya watu waliokuwa wakiizunguka ile nyumba kuelekea kwenye mlango wa kuingilia mle ndani. Tunu alishtuka na kuondoka haraka eneo lile kwa mwendo wa kunyata, alikwenda kujibanza nyuma ya mti mkubwa wa kivuli.




Kutokea pale aliweza kuwaona wanaume wawili waliovaa nguo nyeusi zilizowafanya wawe kama vivuli, walikuwa wakitembea kwa tahadhari pasipo kutoa kishindo na kuelekea ndani ya ile nyumba, kisha akamsikia mmoja wao akiita kwa wasiwasi kwa sauti ya chini yenye wasiwasi, “Victor! Victor!”


Tunu hakuwa na muda wa kupambana nao, alitumia mbinu yake ya kijasusi kuupanda ukuta haraka na kurukia nje pasipo kutoa kishindo. Mara tu alipotoka nje ya ile nyuma akakumbuka kuitazama saa yake ya mkononi na hapo akagundua kuwa alikuwa amepoteza takriban dakika therathini, kwani ilishatimia saa mbili za usiku.


Hakutaka kuelekea moja kwa moja barabara na kwenda kule alikokubaliana kukutana na kina Bob, hivyo akashika uelekeo wa upande wa kulia ili kumpoteza mtu yeyote ambaye angejitia kumfuatilia. Kutokea pale akaingia kwenye kichochoro kimoja na kuanza kutembea kwa tahadhari kwenye kile kichochoro huku mara kwa mara akigeuka na kutazama nyuma yake ili kuona kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia. Hakumwona.


Alipofika mwisho wa kile kichochoro alisimama na kutathmini hali ya usalama wa eneo lile na aliporidhika akachepuka na kuvuka barabara ya mtaa ule wa nyuma kisha akaelekea upande wa pili. Akiwa upande wa pili wa ile barabara akaendelea kutembea haraka haraka na kwa tahadhari kubwa chini ya miti iliyokuwa pembeni ya barabara ile kando kando ya nyumba za makazi ya watu.


Ule mtaa ulikuwa ni wenye pilikapilika nyingi za watu kutokana na uwepo baa mbili tatu. Tunu alizidi kusonga mbele pasipo kuwajali wanaume waliokuwa wakigeuza shingo zao kumtazama na wengine kumwita, akaingia kwenye kichochoro kingine kilichompeleka katika mtaa wa pili kisha akashika uelekea mwingine uliompeleka hadi alipokwenda kutokea katika barabara ya Mtatiele.


Alipofika pale alisonga mbele zaidi hadi eneo alipokubaliana kuwakuta kina Bob wakimsubiri lakini hakuliona lile gari aina ya Nissan Patrol la rangi ya bluu wala dalili za kuwepo kina Bob, akaangaza macho yake huku na huko lakini hakukuwa na dalili zozote za uwepo wao. Tunu akatweta na kuchukua simu yake akitaka kupiga lakini akajionya kuwa huenda angeweza kuingia kwenye mtego.


Sasa hakuwa na namna nyingine ya kumfanya kuondoka haraka eneo lile isipokuwa kutafuta usafiri mwingine. Alianza kutembea huku akitupa macho yake huku na kule kutafuta usafiri wowote ambao ungemtoa eneo lile, mara akaiona taxi moja ikija kufuata uelekeo wake kwa mwendo wa kawaida.


Tunu akampungia mkono dereva wa ile taxi ambaye alipomfikia alisimama na kumfungulia mlango wa mbele lakini Tunu hakutaka kuketi mbele, akaufunga ule mlango na kufungua mlango wa nyuma kisha akaingia na kumweleza dereva ampeleke Ubungo. Yule dereva alikubali, lakini badala ya kuondoa gari alishuka na kuzunguka nyuma akiyatazama magurudumu kuona kama yangekuwa na hitilafu yoyote. Aliporidhika aliingia ndani ya gari lake na kutulia kwenye siti yake akionekana kama aliyekuwa anachunguza kuona kama kulikuwa tatizo mle ndani ya lile gari lake.


Tunu alianza kuingia na wasiwasi, alipotaka kumuuliza kama kulikuwa na shida au kitu chochote kilichokuwa kinaendelea pale akashtuka kuona mlango mmoja wa nyuma na mwingine wa mbele kushoto kwa dereva ikifunguliwa na wale watu wawili wanaume wakaingia haraka ndani ya gari na kuketi.


Tunu aligeuza shingo yake kuwatazama wale wanaume haraka haraka mmoja baada ya mwingine, wote wawili walikuwa wakimtazama kwa tabasamu lililojaa kejeli. Zilikuwa ni sura zilizopambwa na tabasamu la kinafiki lenye tafsiri halisi ya ushindi na macho yao yalimwonesha Tunu jambo moja tu, kwamba alikuwa “amepatikana”.


Akiwa ameshikwa na mshtuko wa hali ya juu, Tunu alianza kuyatembeza macho yake taratibu akizikagua vizuri sura za wale watu kisha akaweka kituo akimtazama yule dereva ambaye pia alikuwa anatabasamu. Tunu alijitahidi kuumeza mshtuko aliokuwa nao moyoni, akajifanya kuachia tabasamu kidogo kujifariji na kuitowesha hasira iliyokuwa imeanza kuchemka moyoni mwake.


Yule mwanamume aliyeketi siti ya mbele kushoto kwa dereva alikuwa mrefu na mweusi kama mjaluo, alikuwa na mwili ulioshiba na alivaa suti maridadi nyeusi. Macho yake yalikuwa makubwa mekundu yenye kila dalili za unyama. Tunu hakumtambua, akayahamisha macho yake kumtazama kumtazama mwanamume wa pili aliyeketi kule nyuma pamoja na Tunu na kumtambua.


“Spoiler!” Tunu alinong’ona kwa mshtuko. Alijikuta akiingiwa na hofu kubwa sana ingawa hakutaka kuionesha. Hapo hapo akili yake ikafanya kazi haraka sana, aliupeleka mkono wake kiunoni kwake kwa uficho ili kutoa bastola yake lakini akawa amechelewa, aliuona mtutu wa bastola aina ya FNX 45 Tactical yenye kiwambo cha kuzuia sauti toka kwa yule mwanamume aliyeketi mbele kushoto kwa dereva ukimwelekea usoni kwake. Akanywea.


“Tulia hivyo hivyo kama unanyolewa,” sauti tulivu ya yule mwanamume aliyeshiba ikapenya kwenye ngoma ya masikio yake huku bastola yake ikichukuliwa na Spoiler, “Kama hautakuwa mjinga basi utaendelea kuwa hai japo kwa saa kadhaa.” Yule mwanamume alifoka huku akiikoki ile bastola.


“Kwani shida yenu nini, mbona sielewi?” Tunu aliuliza huku akijitahidi kuifanya sauti yake ionekane ya kawaida.

“Haipendezi kuuliza swali ambalo jibu lake unalijua vyema,” Spoiler alimwambia Tunu kisha akamtazama yule dereva wa taxi. “Chuku ondoa gari uelekee Kinondoni.”


“Basi kama shida yenu ni mimi mmeshanipata, naomba nipake lipstick yangu ili tuelewane,” Tunu alisema na kuchukua kibomba kidogo cha rangi ya dhahabu kilichokuwa kinafanana sana na rangi ya mdomo, alipotaka kukifungua Spoiler akamdaka mkono wake na kumpoka kibomba hicho.


Kibomba kile kwa macho ya kawaida kilionekana kama kibomba cha kawaida cha rangi ya mdomo lakini kiuhalisia ilikuwa ni bastola hatari sana ya kijasusi (lipstick gun) iliyotengenezwa kwa mfano wa rangi ya mdomo. Kwa kukizungusha tu risasi ingeweza kutoka na kuua.




“Don’t try to do anything stupid,” Spoiler alifoka huku akichomoa haraka kisu chake cha springi toka kwenye ala yake, akakielekeza kwenye shingo ya Tunu. Alikuwa ameghadhabika sana.


Tunu aliuma meno yake kwa hasira na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, ujanja wake ulikuwa umegundulika. Sasa alihisi kuwa huenda huo ulikuwa mwisho wa maisha yake. Wakati gari likikata kona kuingia barabara ya Mori, Tunu akaliona gari fulani likija nyuma yao kwa kasi na kulitambua, akaachia tabasamu huku akijiegemeza kwenye siti yake. Lilikuwa ni lile gari aina ya Nissan Patrol la rangi ya bluu. Mara akahisi kuchomwa na kitu fulani ubavuni kwake mfano wa sindano na mara usingizi mzito ukaanza kumnyemelea.


Hakutaka kulala, alijaribu kufumbua macho yake lakini hakuweza na mara usingizi mzito ukammeza kabisa. Kama ndoto alianza kusikia mabishano kati ya wale watu wawili, mmoja alisema, “Tumuue kabisa maana haaminiki huyu.”


“Hapana, hana tena ujanja. Hii dawa itamlaza hadi keshokutwa hivyo ngoja tumfikishe kwa mzee, ndiye ataamua cha kumfanya!” mwingine alisema na mara akasikia kishindo kikubwa na kuanza kuyumba huku na kule.


Lile gari aina ya Nissan Patrol la rangi ya bluu lilikuwa limeifikia ile taxi na kuipiga kumbo ubavuni kiasi cha kufanikiwa kuihamisha kabisa barabarani na kuisogeza hadi kando ya barabara kwenye mfereji wa maji machafu. Tukio lile likaifanya ile taxi ianze kupoteza uelekeo huku ikiyumbayumba ovyo barabarani. Kilikuwa kitendo cha ghafla kilichowatokea kina Spoiler wakati wakiwa hawajajiandaa.


Yule mwanamume mwenye mwili ulioshiba aliyeketi kule mbele kushoto kwa dereva aliielekeza bastola yake kwenye lile Nissan Patrol na alipokuwa akijiandaa kufyatua risasi, Bob aliyekuwa akiendesha lile Nissan Patrol akawa mwerevu wa kushtukia mapema hila yake na hivyo akaliwahi lile taxi na kuligonga tena ubavuni. Mtikisiko uliotokea ukafanya bastola ya yule mtu imponyoke mkononi na kuangukia chini siti.


Lakini kabla hawajapata ufumbuzi Dumba, aliyekuwa pamoja na Bob aliachia risasi moja iliyokisambaratisha kichwa cha dereva wa ile taxi na muda huohuo uhai ukawa mbali na mwili wake. Wote ndani ya taxi walifahamu kuwa ule ungekuwa mwisho wao kwani kilichokuwa kinafuata baada ya hapo kingekuwa hatari zaidi kwao. Kwa haraka yule mwanamume mwenye mwili ulioshiba aliyekuwa ameketi mbele akawahi kuudaka usukani ili kuiongoza ile taxi.


Muda uleule ile taxi ikaparamia ukuta wa nyumba moja iliyokuwa kwenye kona kuelekea barabara ya Kwa Mwarabu na hapo yowe la hofu kutoka kwa watu waliokuwa kando kando ya ile barabara wakishuhudia kilichokuwa kinatokea likasikika wakati lile gari likiuparamia ule ukuta na kubomoa kabisa kisha likazama ndani ya nyumba.


Lile gari aina ya Nissan Patrol lililoendeshwa na Bob lilifunga breki na kusimama kando ya barabara ya Kwa Mwarabu, na kwa haraka sana Bob na mwenzake Dumba wakashuka na kuelekea kule ndani ilikokuwa ile taxi pasipo kujali macho ya watu walioanza kukusanyika eneo lile kushuhudia ajali ile ya kutisha.


Walipoifikia ile taxi wakawakuta watu watatu tu ndani ya gari. Dereva ambaye alikuwa amekufa, yule mwanamume mwenye mwili ulioshiba alikuwa amebanwa katikati ya lile gari na ukuta pale alipojaribu kuruka ili ajiokoe na damu zilikuwa zikimtoka mdomoni, na Tunu aliyekuwa amelala kwenye siti akiwa amepoteza fahamu. Spoiler alikuwa ametoweka.


Haikujulikana kama yule mwanamume mwenye mwili ulioshiba alikuwa mzima au mfu na wala hakuna kati yao aliyejihangaisha naye. Kina Bob walihitaji kumuokoa Tunu, na walipomwona amelala akiwa hana fahamu huku akitokwa damu mdomoni na sehemu ya kichwani, begi lake lenye laptop likiwa kando yake.


Walimchomoa haraka toka kwenye siti yake. Bob akambeba na wakati huohuo Dumba alilichukuwa lile begin a kuiona bastola ya Tunu, akaichukua na kutoka haraka kumfuata Bob kwenye gari lao.


Muda mfupi baadaye lile gari aina ya Nissan Patrol liliondoka toka eneo lile kwa mwendo wa kasi huku watu waliokuwa wameanza kujaa eneo lile wakiwa wamepigwa na butwaa.


* * * * *


Gari dogo aina ya Land-Rover 110 jeupe la POLISI lilifika katika eneo ilipotokea ajali nusu saa baada ya gari la kina Bob aina ya Nissan Patrol kuondoka. Polisi walikuwa wametaarifia uwepo wa ajali ile na mmiliki wa nyumba iliyogongwa na kubomoka. Ndani ya gari lile la polisi kulikuwa na watu wane. Mbele ya gari kulikuwa na watu wawili, dereva wa gari aliyekuwa amevaa sare ya kazi ikiwa na cheo cha koplo na mtu mwingine aliyekuwa amevaa suti ya kijivu na shati jeusi akiwa ameketi upande wa kushoto.


Nyuma ya gari lile kulikuwa na askari wawili wengine waliokuwa wamebebelea bunduki na vifua vyao vimekingwa na mavazi maalumu yanayozuia risasi maarufu kama ‘bullet proof’. Askari wote walikuwa na sura ya kazi.


Wale askari wawili walioketi nyuma pamoja na yule kiongozi wao mwenye suti ya kijivu ambaye kimwonekano alikuwa mweusi wa miaka arobaini wakashuka haraka na kuuliza kilichotokea, baada ya kuelezwa kwa ufupi wakaanza kupenya kuelekea kule ndani ilipokuwa ile taxi wakipita kwenye makundi ya watu waliokuwa wamekusanyika pale wakishangaa.


Walipozama ndani wakakutana na mmiliki wa ile nyumba ambaye alijitambulisha kwao na kuwaeleza kilichotokea: tangu aliposikia mshindo mkubwa wakati yeye na familia yake wakiwa mezani wanakula kisha wakaona ukuta wa nyumba yao ukianguka na gari kupenya ndani, kisha alivyoweza kumwona mtu mmoja akitoka ndani ya lile gari akiwa ameshika kisu na kupotelea kizani, na mwisho alivyowashuhudia wanaume wengine wawili wakiingia pale na kumbeba msichana mmoja aliyekuwa ndani ya ile taxi akiwa amezirai na kuondoka naye.




Baada ya hapo yule askari mwenye suti ya kijivu ambaye alikuwa na cheo cha Inspekta akapata kuuona mwili wa dereva wa ile taxi ukiwa umelalia usukani ukivuja damu, kichwa chake kilikuwa kimechakazwa kwa risasi, na akamwona mtu mwingine mwenye mwili uliojazia aliyekuwa amebanwa katikati ya gari na ukuta huku akiugulia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata.


Inspekta akamtazama kwa makini yule mtu mwenye mwili uliojazia aliyekuwa akiugulia na kuwataka watu wenye ujasiri waliokuwepo pale wasaidiane na askari wake kumtoa pale alipokuwa amenasa, wakafanikiwa kumtoa na kumlaza kando wakati yule Inspekta akipiga simu ofisini kuomba magari mawili, moja la wagonjwa na gari jingine kwa ajili ya kuuchukua ule mwili wa dereva wa taxi.


Alipokata simu akaanza kukagua eneo zima ambapo tukio lilitokea na kupiga picha kwa kutumia kamera yake ndogo maalumu kwa kazi hiyo. Alipomaliza kufanya ukaguzi wake ikiwa ni pamoja na kupiga picha akaanza kuwauliza maswali watu aliowakuta pale ambao walikiri kushuhudia kila kitu tangu magari yale yalipokuwa yakigongana hadi ajali kutokea na kisha watu wawili kutoka ndani ya gari aina ya Nissan Patrol na kumbeba yule msichana aliyekuwa ndani ya taxi na kuondoka naye.


Baada ya mahojiano ya kutosha kwa takribani dakika therathini na tano, yule Inspekta akawa amebaini mambo kadhaa kuhusiana na tukio lile, mambo hayo aliyahusisha na matukio ya kutekwa kwa Sammy na kisha kulipuliwa kwa nyumba yake.

Wakati akitafakari mara magari mawili yakawasili eneo lile, moja likiwa gari la wagonjwa na gari la pili lilikuja kwa ajili ya kuuchukua ule mwili wa dereva. Wakashuka watu waliokuwa wamevaa glavu mikononi na kusaidiana kumchukua yule mtu mwenye mwili uliojazia na kisha kumpakia kwenye lile gari la wagonjwa na wakati huo huo wengine wakiupakia mwili wa yule dereva, kisha magari hayo yakaondoka haraka kuelekea hospitali ya Mwananyamala.


Yule Inspekta hakuonekana kuridhika, aliendelea kuuliza maswali mengine machache ambayo kwa kiasi fulani yalikuwa yamemsaidia kupata picha halisi, kisha akaaga na kuondoka huku akiwaacha wale askari wawili wenye silaha wakilinda eneo lile wakati wakisubiri gari maalumu kuja kuivuta ile taxi.


* * * * *


Saa kumi na mbili na nusu ya asubuhi ilimkuta Mr. Oduya akiwa ameketi ofisini kwake kwenye jengo lake la ghorofa kumi na mbili lililopo barabara ya Bagamoyo, eneo la Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Hakuwa ameambua japo lepe la usingizi na muda huo alikuwa amekwisha pata taarifa juu ya kile kilichokuwa kimewatokea vijana wake watatu.


Ajali ya ile taxi ilikuwa imesababisha kifo cha dereva wa taxi huku yule muuaji wake wa kukodiwa mwenye mwili uliojazia ambaye alikuwa akiitwa Casmir akiwa ameumia sana eneo la kifuani na mbavuni na kukimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala, baada ya kutokea mapambano na lile gari aina ya Nissan Patrol lililokuwa limewachukua watu wa Tunu.


Mr. Oduya pia alikuwa amepokea taarifa hizo za kusikitisha sana kwa mshtuko mkubwa na zilizidi kumnyima raha. Kilichomzidishia uchungu ni taarifa za kwamba Victor alikuwa amechakazwa vibaya na hali yake ilikuwa mbaya sana kiasi cha kukimbizwa hosipitali akiwa mahututi baada ya kuvunjwa mbavu kwenye mapambano kati yake na Tunu.


Kwa ujumla taarifa zote mbili zilimtisha sana Mr. Oduya. Alihofia kuwa sasa ingeweza kugundulika kuwa yeye ndiye alikuwa mhusika mkuu baada ya majanga mfululizo yaliyokuwa yakiwaandama watu wake wa karibu na endapo taarifa zile zingewafikia watu wa magazeti basi zingeweza kumharibia kwenye harakati zake.


Muda wote alikuwa akivuta sigara kwa fujo kama mtu asiye na akili sawasawa. Kutokana na maelezo aliyokuwa ameyapata toka kwa Spoiler kuhusu lile gari aina ya Nissan Patrol na aina ya watu waliokuwa ndani ya lile gari ilimaanisha kuwa sasa matumaini ya kumpata Tunu yalikuwa yamekufa kabisa, kwani Tunu alikuwa tayari anacho kikosi kabambe kilichojiandaa kwa ajili ya mapambano dhidi yake.


Muda mfupi tu uliokuwa umepita Mr. Oduya alikuwa amewapigia simu baadhi ya washirika wake muhimu na kuwaomba wakutane hapo ofisini kwake ili awaeleze ukweli wa kile ambacho mwanzoni hakuwa ametaka kukiweka wazi kwao, nia yake ilikuwa kuwataka wamsaidie jinsi ya kujikwamua kutoka kwenye balaa hilo baada ya maji kumfika shingoni.


Kati ya washirika muhimu sana wa Mr. Oduya ambao aliamua kuwaita walikuwemo Balozi Mageuzi na Dk. Masanja. Mr. Oduya alikuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa timu yake ya mauaji aliyokuwa ameiandaa kummaliza Tunu ikizidiwa ujanja kwa kila hali na Tunu.


Baada ya hapo Mr. Oduya aliendelea kuketi kwa utulivu kwenye kiti chake cha ofisini huku sigara zikipishana mdomoni. Baada ya kitambo fulani alionekana kushtuka, akaitazama saa yake ya mkononi na kushusha pumzi. Alikuwa anahofia sana muda huo wa kusubiri kwa kudhani lolote baya lingeweza kutokea. Kwa mara nyingine tena wazo la kutaka kutoroka nchini lilimjia, sasa hakuwa na uhakika kama alistahili kuendelea na harakati zake za kuuwania urais wa nchi ya Tanzania au atoroke nchini mara moja na kukimbilia Canada akaanze maisha mapya.


“C’mon! Urais hauji kwa starehe, ni mapambano ya kufa au kupona,” Mr. Oduya alijikumbusha maneno hayo na hapo hapo yakamtia moyo hata kicheko hafifu kikamtoka. Kilikuwa kicheko halisi cha faraja kilichoujaza moyo wake furaha na kumsahaulisha kwa muda mashaka yote aliyokuwa nayo, akaapa kupambana hadi dakika ya mwisho ili atimize ndoto yake.


* * * * *


Saa moja ya asubuhi Tunu aliyatega masikio yake kwa makini huku akijaribu kutafakari kuwa pale alikuwa wapi. Hakusikia sauti ya kitu chochote na utulivu wa eneo lile ulikuwa ni wa hali ya juu kiasi kwamba nafsi yake ilianza kuingiwa na hofu. Muda huo alikuwa amerudiwa na fahamu, na kumbukumbu juu ya yote yaliyomtokea kule Sinza alipotekwa na kina Spoiler zikamjia.




Hakuweza kukumbuka nini kilichokuwa kimemtokea baada ya kuchomwa na kitu mfano wa sindano na kisha fahamu zake kuanza kupotea huku akichukuliwa na usingizi mzito. Kitu pekee alichoambulia ni kuhisi maumivu kwenye mguu wake wa kulia na kichwa chake kilichoelemewa na uzito. Aliuinua mkono wake wa kulia na kuanza kujipapasa kichwani taratibu na hapo akagundua kuwa alikuwa amefungwa bendeji kukizunguka kichwa chake.


Hata hivyo, alipiga moyo konde na kumshukuru Mungu kwa kumweka hai hadi wakati ule kwani aliamini kuwa mambo mengine angeyafahamu baadaye.


Alikuwa na maswali kadhaa kichwani kwake lakini alijua kuwa asingeweza kupata majibu katika tafakari yake na badala yake aliyatembeza kwa siri macho yake kuyapeleleza mazingira ya mle ndani. Alikuwa amelala kitandani kwenye foronya laini na mto wa kuegemeza kichwa. Alikuwa na kila hakika kuwa alikuwa ndani ya nyumba ila hakujua nyumba ile ilikuwa ya nani na alifikaje hapo!


Alikuwa bado amevaa suruali ya blue ya jeans na t-shirt nyeusi, na alipotazama mbele ya kile kitanda alicholazwa akaliona dirisha kubwa la kioo na akaweza kubaini kuwa muda ule ulikuwa ni asubuhi kwani miale hafifu ya jua la asubuhi ilikuwa inapenya na kuingia mle chumbani dirisha hilo.


Hakutaka kuendelea kulala, alinyanyuka taratibu toka pale kitandani na kuketi kitako, na wakati akifanya hivyo alihisi maumivu makali yakipenya kwenye mguu wake wa kulia. Kichwa chake nacho kilikuwa kizito na hakikuonesha utulivu hata kidogo kutokana na kizunguzungu kilichokuwa kimemshika, hata hivyo alijitahidi akaketi na kuanza kuyazungusha macho yake taratibu kuyatazama mazingira ya chumba kile.


Lakini alisitisha uchunguzi wake baada ya kuona kitasa cha mlango wa kile chumba kikizungushwa taratibu. Tukio lile likayavuta macho yake kuutazama ule mlango huku moyo wake ukipoteza utulivu katika kiwango fulani. Mlango ulipofunguka Tunu akamwona Tom akiingia mle ndani. Wakatazamana kwa sekunde kadhaa na Tom alipomwona Tunu ameamka na kuketi kitako akaachia tabasamu.


Tom alikuwa amevaa mavazi ya michezo, tracksuit nyekundu na raba nyepesi nyeusi aina ya Kung Fu na alionekana kuwa alikuwa ametoka kufanya mazoezi ya karate, kwani alikuwa amening’iniza chain shingoni na taulo dogo la kufutia jasho begani kwake huku jasho jepesi likiwa linamtiririka taratibu mwilini.

ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog