Simulizi : Peniela (3)
Sehemu Ya Tatu (3)
“ I think I’ve got something “akasema Anitha na kumuonyesha Mathew barua pepe ile ambayo Rosemary alimwandikia mtu mmoja anaitwa Samir hasaad.
Katika barua pepe hiyo Rose alimfahamisha Samir kwamba wanategemea kuupata mzigo muda wowote kwani wanaye mtu wa karibu sana na rais na ambaye anawapa taarifa zenye uhakika kuhusu mzigo huo kwa hiyo wana hakiak wa kuupata muda wowote”.
“ Samir hasaad ni nani? Mathew akamuuliza henry
“ Mimi simfahamu.Hao ni watu wa Rose ambao mimi sihusiani nao.Kuna mambo ambayo mimi na Rose tuna mashrikiano na kuna mambo ambayo hatuna mashirikiano.kwa ufupi simfahamu huyo Samir “ akasema henry
“ Nimzigo gani ambao Rose anamuhakikishia Samir kwamba wanategemea kuupata? Na zaidi anamuhakikishia kwamba wana mtu wa karibu sana na rais ambaye anawapa taarifa zenye uhakika ni nani huyo? Akauliza Mathew
Ghafla Henry aliyekuwa ameelekeza macho dirishani akaonekana kustushwa sana na jambo.Mathew akaligundua hilo na kumuuliza
“ Vipi? Mbona umestuka sana?
“ Rose amerudi.Tayari amejua ofisi yake imefunguliwa”
“ What ?! amejua vipi? akauliza Mathew huku naye akichungulia nje.Ni kweli mwanamama mmoja mnene alishuka katika gari akaanza kupiga hatua kwa kasi kuelekea ndani.
“Ofisi hii ina mfumo wake maalumwa ulinzi na wenye uwezo wa kuufungua mlango wa ofisi hii ni mmi na Rose pekee.Mlango ukifunguliwa lazima itaonyesha katika simu ya Rose .”akasema Henry
Haraka haraka Anitha akachomoa kila kitu alichokuwa amekichomeka katika kompyuta ya Rose na kisha Mathew akachomoa bastora yake na kumuelekezea Henry kichwani
“ Ukitaka uwe salama wewe na mwanao ,kaa pale mezani na ujifanye ulikuwa unafanya kazi zako na usimwambie chochote kuhusu uwepo wetu humu.Ukithubutu kumweleza chochote Rose kwamba tuko humu nitakufumua kwa risasi.Tumeelewana? akasema Mathew.
“ Tumeelewana” akasema Henry kwa wasiwasi.
Rosemary Mkozumi baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea katika ofisi yake ambako aliamini ndiko aliko Henry.Mara tu alipofungua mlango wa ofisi yake kikatokea kitu ambacho hakuwa amekitarajia.Henry aliruka toka katika meza aliyokuwa amekaa na kupiga ukulele akimzuia Rosemary kutokuingia mle ofisini.Wakati Rosemary akishangaa kitendo kile ikasikika milio ya risasi zilizotoka katika bastora yenye kiwambo cha kuzua sauti na henry akaanguka chini akaanza kutapa tapa huku akivuja damu nyingi.Kutahamaki Rose akajikuta aakitazamana na basora mbili toka kwa Mathew na Anitha.Aliishiwa nguvu akaanguka chini.
Haraka haraka Mathew akamshika mkono Rosemary mkozumi na kumvuta akamuingiza mle ofisini kisha akafunga mlango.Akamfuata Henry pale chini alipolalia dimbwi la damu akamgeuza
“ Henry !! akaita Mathew.Henry hakuitika na alionekana kupumua kwa shida sana.
“ Henry ! henry !!.Mathew akamtikisa.Henry akafumbua macho na kwa sauti ndogo akasema
“ Nao..nao…Naom……!! akashindwa kumalizia alichotaka kukisema akakata roho.Anitha akafumba macho alisikia uchungu sana .Mathew akainuka na kumsogelea Anitha
“ He’s gone” akasema kwa sauti ndogo.
“ I’m so sorry” akajibu Anitha.Kwa sekunde kadhaa walibaki kimya wakimtazama Rosemary aliyekuwa amelala chini hana nguvu huku jasho likimtiririka
“ What are going to do? Akauliza Anitha
“ Mtu tuliyekuwa tunamuhitaji sana ni Rosemary ambaye amejileta mwenyewe na hatuwezi kumuacha.Lazima tuondoke naye.We must do something to get us out of here” akasema Mathew na kuchukua simu yake akampigia Eva akamfahamisha kilichotokea na kumuomba alete gari la wagonjwa haraka sana pale nyumbani kwa Rosemary .Kisha ongea na Eva akamgeukia Anitha
“ Eva anakuja na gari la wagonjwa.Najua kama gari lile la wagonjwa likifika hapa ni lazima walinzi watataka kujua kilichotokea kwa hiyo basi lazima tumtoe Rosemary humu ndani na tuifunge hii ofisi kwa nje .Mlango huu wa ofisi ukifungwa kwa nje ni watu wawili tu wanaoweza kuufungua.Rosemary na Henry pekee kwa hiyo hata walinzi wake hawataweza kuufungua huu mlango na kujua klichotokea humu hadi hapo tutakapoondoka na kuwapigia simu na kuwataarifu kuhusu Henry.“ akasema Mathew na kumshika mkono Rosemary ambaye hakuwa na nguvu hata kidogo akamvuta na kumtoa nje ya ofisi yake.Anitha akaichukua kompyuta ile ya Rosemary pamoja na simu yake kisha akatoka mle ofisini na kuufunga mlango.Taa nyekundu ikawaka juu ya mlango kuashiria kwamba hakuna anayeweza kuufungua tena mlango ule kutokea nje zaidi ya Henry na Rosemary pekee.
“ Is she going to be ok? Akauliza Anitha kwa wasi wasi akimtazama Rosemary aliyekuwa akihema kwa taabu na jasho jingi kumtirirka
“ Don’t worry .She’ll be ok.Anaonekana amepatwa na mstuko wa ghafla kwa hiyo anahitajika daktari haraka kuweza kumsaidia.Mungu atusadie tufanikiwe kumtoa mama huyu salama humu ndani” akasema Mathew .Anitha akapiga magoti na kumfuta Rosemary jasho lililokuwa linamtiririka.
Baada ya dakika kama ishirini hivi simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Eva.
“ Mathew tumezuiliwa hapa getini na walinzi kwamba hakuna gari inayoruhusiwa kuingia hapa bila kibali cha bosi wao Rosemary na hawana taarifa zozote za kuitwa kwa gari la wagonjwa” akasema Eva.
“ Naomba umpe simu mmoja wa walinzi niongee nao” akasema Mathew na baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti nzito ya kiume ikiita
“ Hallow”
“ Hallow ndugu yangu kuna tatizo limetokea humu ndani.Rosemary amepatwa na na mstuko wa ghafla na anahitajika kukimbizwa hospitali haraka sana.”
“ Mstuko wa ghafla? Nini kimesababisha akapatwa na mstukohuo? Mbona amepita haap getinimuda mfupiuliopita akiwa mzima wa afya? Henry yuko wapi ? Yule mlinzi akaulzia maswali mfululizo.
“ Kumetokea kutokuelewana kati ya Henry na Rose na Rose alipatwa na tatizo hili.Sisi ni wale wageni tuliokuwa na Henry na hatufahamu mpaka sasa aliko Henry .Tafadhali naomba mliruhusu gari hilo haraka sana la wagonjwa ili tumkimbize Rose hospitali.Endapo mtaendelea kulizuia gari hilo na hali ikazidi kuwa mbaya lawama zote zitawaangukia ninyi” akasema Mathew na simu ikakatwa.
Baada ya dakika tano wakaingia kwa kasi walinzi watatu na nyuma yao wakafuata Eva na watu wengine wawili waliovaa makoti meupe wakiwa na machela .
“ Henry kaelekea wapi “akauliza mmoja wa walinzi
“ Stop asking questions.Tusaidiane kwanza kuokoa maisha ya bosi wenu” akasema Mathew wakasaidiana kumpakia Rosemary katika machela na kumshusha chini .Gari la wagonjwa likasogezwa karibu na mlango wakampakia Rose.Mathew akawagukia wale walinzi.
“Endeleeni kumtafuta Henry,sisi ngoja tumuwahishe mgonjwa.Tutawafahamisha maendeleo yake.” Akasema Mathew na kuingia katika gari lile la wagonjwa wakaondoka kwa kasi wakiwawaacha watumishi wakishangaa kilichotokea.Ndani ya gari madaktari wale wawili waliendelea kumpatia Rose .
“ Finally we got her” akawaza Mathew
“ Vyombo vya usalama vimekuwa vikimuogopa sana huyu mama lakini leo imefika arobaini yake.Ametua mikononi mwangu na lazima atanieleza kila kitu.Ni heri angekutana na shetani kuliko kukutana na mimi” akawaza Mathew.
“ Mathew tunaelekea hospitali gani? akauliza Eva
“ Eva we need to talk” akasema Mathew na kuwatazama wale madaktari
“ Samahani ndugu madaktari.Ninahitaji dakika mbili niongee faragha na Eva” akasema Mathew na mmoja wa wale madaktari akamuomba dereva asimamishe gari pembeni ya barabara,Mathew na Eva wakashuka
“ Mathew what happened? Akauliza Eva
“ Eva kulitokea rabsha kidogo na kusababisha Rose apatwe na mstuko huu.”
“ Henry yuko wapi?
“ Henry is dead”
“ Ouh my God!!.. Eva akastuka
“ Kwa hiyo tunaelekea wapi ? akauliza Eva
“ Tunaelekea nyumbani kwangu.”
“ No ! Mathew hali ya Rose ni kama unavyoiona si nzuri hata kidogo anatakiwa apelekwe hospitali akakae chini ya uangalizi wa madaktari.”
“ Eva,huyu mama ana taarifa za muhimu sana na kwa sasa ameua mikononi mwangu siwezi kumuachia hata sekunde moja.”
“ Mathew unarudia tena ubishi wako kama wa kipindi kile uliosababisha kifo cha Yule msichana.Nakushauri kama rafiki yangu tumpeleke Rosemary hospitali na hali yake ikiwa nzuri tutamchukua na kumuhoji kama unavyotaka lakini kwa sasa bado hali yake si nzuri na huwezi kumuhoji chochote” akasema Eva
“ Eva,siwezi kamwe kufanya kosa la kumpeleka Rose hospitali.Wewe mwenyewe ndiye uliyenihakikishia kwamba huyu mama ni hatari na ana mtandao wake mkubwa kwa hiyo basi kitendo cha kumpeleka hospitali tutampoteza na hatutaweza kumpata tena.This is the only chance we have and we cant loose it”
“ Mathew nakubaliana nawe lakini bado naendelea kukushauri kwamba tumpeleke hospitali.Hawa madaktari wote wanafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa na tutampeleka Rose katika hospitali zetu ambazo huwa tunazitumia kuwahifadhi watu kama hawa wakahudumiwa bila ya mtu kufahamu .Please Mathew,naomba unisikilize na tukubaliane katika hili.” akasema Eva
“ Eva tusiendelee kupoteza muda.Rosemary anapelekwa nyumbani kwangu na atahudumiwa pale.”
“ Itakuwaje iwapo atapoteza maisha akiwa nyumbani kwako? Mathew suala hili ni la hatari kubwa sana .Muda si mrefu itagundulika kwamba Rosemary ametoweka na utaanza msako mkali sana wa kumtafuta.Hii itakuwa mbaya sana kwako Mathew” Akasema Eva
“ That’s the risk I have to take Eva.Ikitokea hivyo I’ll know what I’ll do .Get in the car” akasema Mathew wakangia garini na safari ikaendelea
“ Katu siwezi kumpa nafasi huyu mama ya kutoroka japokuwa haliyakeni mbaya ,lakini kumpeleka hospitali hata kama inamilikiwa na usalama wa taifa bado ni kumpa nafasi ya kutoroka kwani kwa mujibu wa Eva hata ndani ya idara ya usalama wa taifa mtandao wa Rose umekita mizizi yake .I have to take this risk.Kama akipoteza maisha nitajua nini cha kufanya lakini naomba Mungu jambo hilo lisitokee kwa sasa “ akawaza Mathew .Anitha aliyekuwa amekaa mbele na dereva akamuelekeza njia ya kupita hadi walipofika nyumbani kwa Mathew.Rosemary akashushwa na kuingizwa katika chumba kimoja kikubwa ambacho kina vitanda vitatu kama vya hospitali na vifaa mbalimbali vya tiba.Chumbakile kilionekana kama zahanati ndogo.Rose akalazwa katika mojawapo ya vitanda vile .Madaktari wale wakaelekeza baadhi ya vitu vinavyotakiwa kupatikana haraka ili kufanikishamatibabu ya Rose.
Gari lile la wagonjwa lililotumika kumbeba Rose likabadilishwa namba ili kuzuia kutambulika kisha Eva na dereva wa lile gari wakaondoka .Eva alikwenda kutafuta baadhi ya vifaa vilivyohitajika . Mathew alimkumbusha pia kumchukua Naomi na kumleta pale nyumbani.Wakati madaktari wale wawili wakiwa na Rosemary wakimuhudumia,Anitha akaelekea ofisini kuendelea kuifanyia upekuzi kompyuta ya Rose,Mathew akamfuata Elibariki chumbani.
“ Hallow Elibariki.Unaendeleaje? akauliza Mathew
“ Ninajitahidi Mathew lakini bado kichwa changu kizito sana.Nimekuwa na mawazo mengi mno nahisi kama ninataka kuchanganyikiwa.Kuna taarifa zozote mpya kuhusiana na msiba wa Flaviana?
“ Anitha yuko ofisini sasa hivi akiangalia kama kuna taarifa yoyote mpya.” Akasema Mathew
“ Nini kinaendelea sasa hivi Mathew? Akauliza jaji Elibariki
“ Tumefanikiwa kumpata Rosemary Mkozumi.”
“ Mmefanikiwa kumpata? Hongereni sana.”
“ Ahsante sana Jaji lakini hali yake si nzuri sana na madaktari wako naye chumbani wakimuhudumia na hali yake itakapokuwa nzuri tutamfanyia mahojiano .Tutafahamu mambo mengi kutoka kwake.” Akasema Jaji Elibariki na mara Anitha akaingia mle chumbani
“ Mathew kuna kitu nimekigundua..” akasema Anitha
“ Umegundua nini Anitha? Akauliza Mathew huku akiinuka na kuongozana na Anitha kuelekea ofisini.
“ Wakati nikipekua kompyuta ya Rose nimekutana na barua pepe hii ambayo inaonyesha Rose alimtumia mtu anayeitwa Captain Amos akimtaka ampatie taarifa zenye uhakika kwani anategemea kwenda kuonana na Samir Asaad aliyefikia 7 angels hotel.Kilichonistua ni kwamba Peniela aliwahi kumtaja Captain Amos ambaye naye ni mshirika wa karibu sana wa rais na ambaye pamoja na Dr Kigomba wanashirikiana katika biashara ya hiyo package .” akasema Anitha
“ Ni kweli Anitha.Rais Dr Joshua anashirikiana na watu wawili katika biashara ile.Kuna Dr Kigomba na huyu Captain Amos.Kama utakumbuka katika ile barua pepe ambayo Rosemary alimuandikia Samir alimueleza kwamba anategemea kuupata mzigo muda wowote kwani ana mtu wa karibu sana na rais.Ni kweli Captain Amos ni mtu wa karibu sana na Rais na kwa maana hiyo basi picha ya haraka tunayoipata hapa ni kwamba Rose na Captain Amos ni washirika na nina wasiwasi kwamba huo mzigo anaouongelea Rose kwamba wana hakika ya kuupata wakati wowote ni hiyo package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza.”
“ Exactly!! Akasema Anitha
“ Hakuna ubishi kwamba mzigo huo anaouongelea Rose ni hii package ambayo Dr Joshua na wenzake wanataka kuiuza.” Akasema Anitha
“ Ukumbuke vile vile Captain Amos yuko pia Team SC41 na wanamtegemea sana katika kupata package hiyo.Anaonekana ni mtu mwenye tamaa sana ya fedha kwani anachukua fedha toka Team SC41,anachukiua fedha kwa Rose na bado anategemea mgawo mkubwa wa fedha toka kwa Dr Joshua .Huyu ni mtu hatari sana na tunatakiwa kumpata haraka sana."
“ Hiyo package ina kitu gani ndani kiasi cha watu wengi namna hii kuitaka? Halafu kwa nini wanunuzi wake wengi wanatokea katika nchi za kiarabu? Akauliza Anitha
“ Nadhani Rose anaweza kutupa majibu ya nini kilichomo katika hiyo package lakini kwa sasa tunatakiwa kumpata Captain Amos.Endapo Amos akipotea ghafla basi Team SC41 na hata huyu Rose hawataweza kupata taarifa zozote kuhusiana na package kwa hiyo sisi tutapata nafasi nzuri ya kuweza kuichukua.” Akasema Mathew
“ Ni Peniela pekee anayeweza kutuelekeza mahala pa kumpata Amos.Nashangaa mpaka mida hii hajanipigia simu wakati nilimuachia maagizo Josh kwamba mara tu atakapozinduka anitafute .” akasema Mathew huku akiitoa sumu yake mfukoni na mara kengele ya getini ikalia.
“ Ngoja nikaangalie yawezekana Eva amerudi.” Akasema Mathew huku akitoka kwenda getini
“ Baada ya kazi hii kukamilika itanilazimu niwarudishe wale walinzi wa getini walikuwa wananisaidia sana
“ akawaza wakati akielekea getini.Alifungua geti na kukutana na Peniela
“ Peniela !! akasema Mathew kwa mshangao kidogo
“ Hello Mathew.Mbona umestuka?
“ Tulikuwa tunakuongelea sasa hivi hapo ndani kumbe uko getini.Mbona silioni gari lako? Umekuja kwa miguu? Akauliza Mathew
“ Nimekuja na taksi.Sikutaka watu wafahamu mahala ninakoenda.” Akasema peniela na mathew akamkaribisha ndani
“ Pole sana Peniela.Unajisikiaje sasa hivi? Nilishindwa kuonana nawe tena baada ya watu ambao nahisi ni Team SC41 kuwasili pale hospitali” akasema Mathew.
“ Kifo cha John kimenipa simanzi kubwa lakini baada ya kuzinduka nikakumbuka kuna jambo zito linalotukabili na ndiyo maana nimekuja hapa ili tujue kinachoendelea.”
“ Pole sana Peniela.Una hakika una nguvu za kutosha kuweza kuendelea na mapambano? akauliza Mathew
“ John amekwenda na maisha lazima yaendelee.Jambo kubwa lililoko akilini mwangu kwa sasa ni kuhakikisha package inapatikana kwa gharama zozote na kisha kuifunga kabisa Team SC41.Kukujibu swali lako ni kweli nina nguvu za kutosha kuendelea kupambana hadi mwisho.” Akasema Peniela
“ Good.Nafurahi kusikia hivyo.” Akasema Mathew
“ Elibariki yuko wapi? Akauliza Peniela
“ Peniela kuna jambo sikuwa nimekufahamisha .Nikiwa pale hospitali nilipigiwa simu na Anitha akanifahamisha kwamba Dr Joshua amempigia simu Dr Kigomba na kumfahamisha kwamba Flaviana amefariki dunia.”
“ What ?!!! Peniela akastuka sana
“ Flaviana amefariki dunia.” Akasema Mathew
“ Oh my God ! Yuko wapi Elibariki? Akauliza Peniela
“ Elibariki yuko chumbani anapumzika kwa mstuko alioupata” akajibu Mathew na bila kupoteza muda Peniela akainuka na kuelekea chumbani kwa jaji Elibariki akaufungua mlango na kuingia ndani.Elibariki alikuwa amekaa kitandani amejiinamia akiwaza na mara tu alipomuona Peniela akajikuta akipata nguvu na kusimama.Wakakumbatana kwa nguvu.
“ Pole sana Elibariki.Pole sana my love”akasema peniela huku akimpiga piga mgongoni.
“ ahsante sana Peniela.Ahsante sana kwa kuja kunifariji.Pole nawe pia.Mathew ameniambia kwamba John amefariki dunia. “ akasema Elibariki
“ Ndiyo amefariki dunia.”
“ Pole sana Peniela.Kifo hakizoeleki hasa kwa mtu wako wa karibu lakini lazima maisha yaendelee.”
“ Ni kweli Elibariki na ndiyo maana nimekuja hapa ili kuweza kuendelea na mikakati yetu “ akasema Peniela. Mara Mathew akasimama mlangoni na kusema
“ Peniela kama hutajali nakuomba ofisini mara moja”akasema Mathew na Peniela na jaji Elibariki wote kwa pamoja wakaelekea ofisini kwa Mathew
“ Peniela kuna jambo limetokea asubuhi ya leo ambalo huna budi kulifahamu.Ni kwamba tumefanikiwa kumpata Rosemary Mkozumi mke wa rais wa zamani wa Tanzania.”
“ Roemary Mkozumi? Akauliza Peniela kwa mshangao
“ Ndiyo Peniela.Katika uchunguzi wetu tumegundua kwamba huyu mama amekuwa na mawasiliano ya karibu na Habib soud ambaye anatajwa kutaka kuzinunua karatasi zile ambazo Edson aliziiba ikulu.Tunaamini kwamba huyu mama ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango ule na Edson alitumiwa tu katika kuziiba karatasi hizo.Tumekwenda mbali zaidi katika kumfanyia uchunguzi Rosemary na tumegundua kwamba amekuwa na mawasiliano na mtu mmoja anaitwa Samir asaad na katika mawasiliano hayo Rosemary anamuhakikishia Samir kwamba mzigo utapatikana muda wowote kwani tayari ana mawasiliano na mtu aliyeko karibu sana na rais.Tumeendelea kuchunguza na kugundua kwamba Rosemary amekuwa na mawasiliano na Captain amos.”
“ Captain Amos?!! Peniela akashangaa
“ Ndiyo peniela.”
“ This is weird. Captain Amos yuko team Sc41,kumbe anatumiwa tena na huyu mama? The whole game is full of betrayals” akasema peniela
“ We need to get him as soon as possible” akasema Mathew
“ Tukitaka kufanikiwa katika kuipata hiyo package lazima tumpate Captain Amos ili hao wanaomtumia wakose taarifa sahihi za kuhusiana na kinachoendelea katika biashara hiyo.Katika hili utatusaidia sana tuweze kumpata kwani wewe unaweza kuwasiliana naye muda wowote” akasema Mathew.Peniela akatoa simu yake na kuzitafuta namba za Amos akapiga
“ Hallow Peniela,pole sana na matatizo.Nimepata taarifa za kifo cha John.Zimenistua sana” akasema Amos
“ Amos uko wapi? I need to see you.” Akasema peniela
“ Kuna tatizo gani Peniela?
“ Kuna jambo la muhimu sana la kuongea nawe”
“ Cant we talk on phone?
“ No .I have to meet you face to face” akasema Peniela.Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa kisha Amos akajibu
“ Tukutane pale Mlimba restaurant,upande wa nyuma kuna vyumba,nenda hadi chumba namba kumi na nne huwa ninakitumia kwa dharura.Sitaki watu wajue nina mawasiliano nawe” akasema Amos na kukata simu
“ Anitha nitaongozana na Peniela kwenda Mlimba Lodge kumchukua Captain Amos.Wewe utabaki hapa kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri na kufuatilia mawasiliano yoyote kati ya Dr Joshua na Dr Kigomba.Vile vile endelea kufuatilia hali ya Rosemary Mkozumi .Eva ameenda kuvifuatilia baadhi ya vifaa na atarejea hapa muda si mrefu.Hakikisha unakuwa karibu na wale madaktari na kuhakikisha Rose anapata nafuu haraka kwa ajili ya kumfanyia mahojiano_One more thing,usimruhusu Eva afahamu jambo lolote lile tunalolifuatilia na wala usimruhusu akaingia humu ofisini na wala asifahamu chochote kuhusu uwepo wa Elibariki hapa ndani” akasema Mathew
“ Who is this Eva? Akauliza jaji Elibariki
“ Ni rafiki yangu anafanya kazi usalama wa taifa” akajibu Mathew
“ Are you sure you want to go there alone? Akauliza tena jaji Elibariki
“ I’m not alone.Peniela will be there with me” akajibu Mathew.
“ Sawa Mathew,jitahidi kuwasiliana nasi mara kwa mara kutujulisha kila kinakachojiri ili kama kutahitajika msaada wa haraka basi tujue namna ya kujipanga” akasema Anitha
Jaji Elibariki na Peniela wakakumbatiana
“ Please take care Peniela” akasema jaji Elibariki
“ I will” akajibu Peniela halafu Mathew akatoka na kwenda katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi ambaye kwa sasa hali yake ilianza kuleta matumaini.Mathew akatoka na kuingia chumbani kwake akachukua baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kumsaidia katika shughuli ile kisha akatoka na kuongozana na Anitha wakaingia garini kuelekea Mlimba Lodge.
“ Nilimuamini sana Captain Amos na kumuona kama mwenzangu ninayeweza kumtegemea kumbe ni mtu mbaya sana.Sikuwahi kufikiria kwamba anaweza akatumiwa pia na Rosemary Mkozumi . Kinachoniuma zaidi ni kwamba anatumiwa na Rosemary kupata taarifa za operesheni kubwa kama hii tunayoendelea nayo ya kuipata package toka kwa Dr Joshua.Amos ametuzunguka na kutoa taarifa kwa Rosemary ambaye naye pia anaonekana kuitafuta package hiyo.Jambo hili limeniumiza sana sana.Mathew nashukuru kwa kuligundua jambo hili mapema.Sisi tungeendelea na mipango yetu bila kujua kama mtu tunayedhani ni mwenzetu tayari ametuzunguka na anashirikiana na watu wengine ambao nao wanajipanga kwa ajili ya kuipata package hiyo na tungeweza hata kuuawa kwa kutolijua hili…Damn you Amos kwa nini ukatufanyia hivi? Akasema Peniela kwa hasira
“ Imekuwa vizuri sana tumewahi kulifahamu jambo hili mapema.Tusingeligundua hili mapema tungeweza kupata upinzani mkubwa sana toka kwa watu tusiowafahamu na hili lingetupa ugumu katika kuichukua hiyo package.Kwa sasa kwa kuwa tayari tunaye Rosemary Mkozumi ambaye naye anaitaka package hiyo basi tunatakiwa kwa kila namna tuweze kumpata pia Amos ambaye ndiye mtoa taarifa wake ili tuwe na uhakika kwamba kuna kundi moja tu ambalo tunapambana nao katika kuipata package hiyo nalo ni Team Sc41.Baada ya kumpata Amos kazi kubwa utakayobakiwa nayo peniela ni kuhakikisha unafahamu mikakati yote ya Team SC41 waliyoiweka katika kuhakikisha kwamba wanaipata hiyo package ili tuone namna ya kupambana nao na kuwawahi kabla hawajafanikiwa .” Akasema Mathew
“ Usihofu kuhusu hilo Mathew.Nitafalinyia kazi.Tutakuwa na kikao cha Team SC41 wote ili kujadili kuhusu suala hili nanitawafahamisheni kila kitu” akasema Peniela
“ Kuna chochote kilichopangwa kuhusiana na mazishi ya John Mwaulaya?
“ Mpaka sasa hakuna chochote kilichopangwa.Kutakuwa na kikao cha pamoja nadhani jioni ya leo kufahamishana kuhusu suala hili na hapo ndipo tutakapojua nini kinaendelea na namna tutakavyomzika John Mwaulaya” akasema Anitha
“ Ok Good ! akasema Mathew na kukawa kimya kidogo
“ Nilisikia ukimpa maelekezo Anitha kuhusiana na Eva.Who is she? Akauliza Peniela
“ Eva anafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa na ndiye aliyenisaidia nikampata Rosemary Mkozumi.” Akasema Mathew
“ Don’t you trust her? Akauliza Peniela
“ Eva amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu na mara kwa mara amekuwa akinisaidia kufanikisha baadhi ya mambo lakini kusema ukweli bado sijafikia hatua ya kuweza kumuamini.” Akasema Mathew
“ Sawa Mathew,Kuna taarifa zozote kuhusiana na kinachoendelea katika msiba wa Flaviana?
“ Mpaka sasa hivi bado hatujapata taarifa za kinachoendelea ila nina hakika mpaka jioni tutajua nini kinachoendelea.” Akasema Mathew
“ Mathew now that John has gone,kuna mambo ambayo natakiwa niyakamilishe.Yeye mwenyewe alinipa maelekezo kwamba niyakamilisha pindi atakapokuwa amefariki.amenisisitiza sana nisiache kuyakamilisha” Akasema Peniela
“ Tutayakamilisha yote Peniela lakini kwa sasa kitu kikubwa ni kuelekeza nguvu katika suala hili lililoko mbele yetu .Tunatakiwa kwa kila tuwezavyo kuhakikisha kwamba package inatua mikononi mwetu ” akasema Mathew
Walikarbia sana kufika Mlimba Lodge,Mathew akasimamisha gari katika kituo cha basi na kusema
“ Peniela tumekaribia sana kufika.Kutokea hapa itakulazmu uchuke taksi hadi Mlimba lodge.Mimi nitakuwa ninakufuatilia kwa nyuma.Utakapoingia ndani kukutana na Amos tafadhali usionyeshe kwamba unafahamu mambo anayoyafanya.Tafuta namna ya kuongea naye ili kuvuta muda wakati nikijiandaa kuvamia ndaniya chumba ” Akasema Mathew na kufungua droo ya gari akatoa kijimtambo Fulani akakiwasha halafu akachomoa vidude viwili vidogo na kumpatia kimoja peniela akamwambia akiweke sikioni.
“ Hiki ni kifaa cha mawasilino .Nitasikia kila utakachoongea na Amos ” akasema Mathew halaf akampatia Peniela bastora iliyofungwa kiwambo cha sauti. Peniela akashuka garini na kuchukua taksi kuelekea Mlimba Lodge Mathew akafuata kwa nyuma.
Taksi alilopanda Peniela likafika katika megesho ya Mlimba Lodge akashuka na kupiga hatua za haraka haraka kuelekea katika chumba alichoelekezwa na Amos.
“ Ninaelekea chumbani kwa Amos” Peniela akamtaarifu Mathew
“Ninakutazama.Peniela be carefull,this man is very dangerous” akasema Mathew
“ I will” akajibu Peniela
Peniala akafika chumba namba kumi na nne akasima mlangoni kwa sekune kadhaa halafu taratibu akakinyonga kitasa cha mlango na kuingia ndani.Ndani ya chumba kile Captain Amos alikuwa amekaa katika sofa akiwa na chupa ya bia pembeni pamoja na bakuli la supu.
“ Peniela,karibu sana” akasema Amos huku akitabasamu.Peniela akageuka kwa dhumuila kuufunga mlango na ghafla akachomoa bastora na kumuelekezea Amos
“ I trusted you son of a bitch…why you did that ? Why you betrayed us Amos ? Akauliza Peniela huku uso wake ukiwa umejikunja kwa hasira.Captain Amos akabaki anashangaa.hakuwa ametegemea kitendo kile cha Peniela
“ Peniela !!..what happened? Please calm down ! Akasema Amos huku akijaribu kutaka kuinuka
“ Sit down Amos !! akasema kwa hasira Peniela na Amos akagundua kwamba peniela hakuwa akitania akaketi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ peniela !!.akataka kusema kitru amos lakini peniela akamzuia.
“ Shut up….!! Akafoka Peniela huku akimuangalia Amos kwa hasira kali.
“ why Amos ? Why you betrayed us? Akauliza Peniela
“ Peniela I dont understand what you are talking about”
“ You don’t know ?? akauliza Peniela kwa ukali
“ Peniela tafadhali weka silaha yako chini…tafadhali weka silaha tuongee..Sielewi unazungumzia kitu gani..”
“ Toka lini umekuwa ukishirikiana na Rosemary Mkozumi na kumpa habari zetu? Akauliza Peniela
Captan amos akastuka sana .
“ How do you know that? Akauliza Amos
“ Ulidhani hatutajua? Kwa nini Amos ukafanya vile? Kwa nini ukaingiwa na tamaa ya pesa kiasi hicho? You sold us all.Sote tungeuawa kwa sababu yako.Huna thamani tena kwangu Amos.!! I hate you !
“ Forgive me Peniela..I did that on purpose.!!
“ On Purpose? Hustahili msamaha kabisa mwanaharamu wewe.”akasema Peniela huku akiuma meno kwa harsira
“ Peniela ! Peniala! …..akaita Mathew kupitia kile kifaa kidogo Peniela alichokiweka sikioni.
“ Today you’ll tell me everything .Ukikataa kunieleza ninachokitaka I swear in heaven and earth I’m going to kill you with my own hand.!! akasema peniela.Captain Amos alogopa,hakuwahi kumuona Peniela akiwa amekasirika namna ile. Macho yake yalionyesha wazi kwamba alidhamiria kukifanya kile alichokuwa anakisema
“ peniela !! ..Peniela !!..akaita Mathew
“ Peniela don’t do that please! Don’t kill him , I’m on the way coming there.Dont shoot him.We need him alive”akasema Mathew .
“ Peniela don’t shoot me..If you do that,you’ll be doing a very big mistake..Me and you we’re all in the same team and everything I’m doing is for you peniela !” akasema Amos .
“ For me ?!! Kutoa siri za mipango yetu ndiyo kufanya jambo kwa ajili yangu? Akafoka peniela
“Peniela kuna mambo mengi ambayo bado huyafahamu but we want to make you and Elibariki very powerfull.. “ akasema Amos na kuzidi kumchanganya peniela.
“ You use the word We ? wewe na nani? Rosemary Mkozumi? Akauliza
“ Peniela najua sio wakati wake kukweleza kuhusu jambo hili lakini sina ujanja lazima nikueleze kila kitu kuhusiana na mipango iliyopo juu yako na Elibariki” akasema Amos lakini ghafla mlango ukapigwa teke na kufunguka,akatokea mwanamke mmoja aliyevaa mavazi meusi na miwani mikubwa myeusi kufunika macho yake ,aliyekuw ana bastora mbili mkononi zilizofungwa kiwambo cha kuzuia sauti .Kama chura Peniela akaruka na kujificha nyuma ya kabati na mwanamke yule akaanza kummiminia risasi Captain Amos.Peniela akaachia risasi mbili toka katika bastora yake kuelekea mlangoni lakini tayari mwanamke Yule alikwisha toweka na Captain Amos alikuwa amelala sakafuni damu nyingi ikimtoka.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ouh My God !!..akasema Peniela kisha akamfuata Amos
“ Amos ! Amos !.akaita Peniela lakini tayari Amos alikwisha fariki kitambo na mara akaingia Mathew.
“ Peniela what happened? Akauliza Mathew huku naye akishangaa
“ Are you ok ? akauliza Mathew
“ I’m ok Mathew.” Akajibu peniela
“ He’s gone Mathew !..Amos is dead” akasema Peniela.
“What happened? Akauliza Mathew
“ Mlango ulipigwa teke ukafunguka ghafla na mwanamke mmoja aliyekuwa na bastora mbili akammiminia Amos risasi.Mathew I’m so scared” akasema Peniela.Mathew akamtazama Amos na kuhakikisha ni kweli amefariki akamsachi na kuchukua simu yake .Akaangaza angaza kwa haraka kuona kama kuna chochote wanachoweza kuondoka nacho hakukuwa na kingine zaidi ya mkoba wa kompyuta,Mathew akauweka begani .
“ Lets get out of here” akasema Mathew wakaufunga mlango na kutoka kwa kasi hadi katika gari wakaondoka
“ I’m sorry Mathew ,Amos ni mtu niliyemuamini kupita kiasi na siri zangu nyingi nilimweleza.Kitendo alichokifanya cha kutusaliti kimeniumza sana na ndiyo maana mara tu nilipomtia machoni nilipandwa na hasira kali na nikashindwa kuwa mstahimilivu nikamtolea bastora.I’m so sorry I failed you.” Akasema Peniela
“ Its ok peniela.Mambo kama haya hutokea.We wanted him alive na ndiyo maana baada ya kusikia maongezi yenu mle chumbani nikagundua ulipandwa na hasira na ukashindwa kujizuia naukiwa na hasira kitu chochote kingeweza kutokea ndiyo maana nikakuita ili kujaribu kukuzuia usifanye chochote.Kuna mambo mengi ambayo tulihitaji kuyafahamu kutoka kwake.” Akajibu Mathew
“ I’m so sorry Mathew.” Akasema Peniela
“ Usijilaumu sana Peniela.Imekwisha tokea na tuangalie yajayo.lakini bado najiuliza mwanamke Yule ni nani? Kwa nini kamuua Amos? Akasema Mathew
“ Inavyoonekana Yule mwanamke alikuwa karibu akifuatilia maongezi yetu mimi na Amos lakini nashindwa kuelewa ni kwa nini amuue Amos hasa pale ambapo alikuwa trayari kunieleza jambola muhimu?
“ Jibu hapa ni rahisi tu.hakutaka Amos akueleze kile alichotaka kukweleza na ndiyo maana suluhisho pekee lilikuwa ni kumuua.But this woman ,who is she? Anaonekana ni mwanamke hatari na mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kutumia silaha.kwa namna alivyomuua Amos anaonekana ni muuaji mzoefu sana.We need to find out who is she? Katumwa na nani amuue captain Amos? Na kuna siri gani ambayohakutaka Amos akueleze? Akasema Mathew.
“ Ninaskitikika sana kwa amos kufa namna ile lakini ukweliutabaki wazi kwamba Amos hakuwa vile tulivyomdhania.Alikuwa na mtandao wake wa siri .Wait ! I remember something…..” Peniela akanyamaza ghafla kwamba kuna kitu alikikumbuka
“ Umekumbuka kitu gani? Akauliza Mathew
“ Nimekumbuka usiku ule Elibariki aliposhambuliwa nilipigiwa simu na mwanamke mmoja nisiyemfahamu na akanifahamisha kwamba nikutane naye ili nimchukue elibariki.Ulikuwa ni usiku na kichwani alivaa kofia lakini nilifanikiwa kuiona sura yake.Nimeikumbuka vyema ..Nihuyu mwanamke aliyemuua Amos...Yes it was her. Yule mwanamke aliyemuoka Elibariki ndiye huyu aliyemuua Amos” akasema Peniela
“ are you sure Peniela? Akauliza Mathew
“ I’m sure Mathew.Sura ile nimeikumbuka kabisa na hasa sehemuya mashavu...Its her” akasema Peniela.Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ who exactly is this woman? Akauliza Mathew.
“ I don’t know her.Lakini nina hakika kabisa ndiye Yule ambaye alikuwa na Elibariki usiku ule aliposhambuliwa.”
“ Tunatakiwa tumfahamu mwanamke Yule na ndipo tutaweza kumfahamu yeye ni Nani.Anahusikaje katika shambulio lile la Elibariki na kwa nini amemuua Amos? Akasema Mathew
“ How are we going to find her” akauliza Peniela
“ I don’t know how but we must find her.Huu unaonekana ni mtandao hatari.Kama mwanamke Yule alikuwepo usiku ule Elibariki aliposhambuliwa basi yeye na mtandao wake wanafahamu mambo mengi na kuna sababu kubwa ya Amos kuuawa.Amos alikwamba kwamba wana mpango wa kuwafanya wewe na elibariki kuwa na nguvu kubwa.Ni mpango gani huo? Ni akina nani hawa wenye kupanga mipango hiyo ?
“ Mathew hili suala si la kupuuzia hata kidogo.Nina uhakika mkubwa kwamba ni kweli lazima kuna kuna jambo linaloendelea chini kwa chini kuhusiana na mimi na Elibariki.Ni jambo gani hilo na ni akina nani ambao wanapanga mipango hiyo ? Tunahitaji kulifahamu suala hili.Tukifanikiwa kumpata Yule mwanamke tutafahamu kila kitu”akasema Peniela.
Sura ya mwanamke Yule aliyepishana na Mathew huku akikimbia ikaendelea kuzunguka kichwani kwa Mathew.
“ who is this woman? Akajiuliza bila kupata jibu
“ anaonekana ni mwanamke mwenye kufahamu mambo mengi .Nakumbuka Elibariki aliniambia kwamba usiku ule lilipofanyika lile shambulio aliokolewa na mwanamke ambaye alimkabidhi kwa Peniela.kwa mujibu wa peniela ameikumbuka sura ya mwanamke Yule kwamba ni huyu aliyemuua Amos leo.Ninahakika mtandao aliomo utakuwa unafahamu mambo mengi sana kuhusiana na Elibariki na ninahisi kuna mambo mengi wanayafahamu pia kuhusiana na package ile toka kwa Dr Joshua.Lazima tumtafute mwanamke Yule kwa kila njia.Suala hili linazidi kuwa kubwa kila uchao” akawaza Mathew wakiwa garini
“ Unawaza nini Mathew? Akauliza Peniela.
“ Ninawaza mambo mengi sana na kubwa ni namna mambo mapya yanavyozidi kuibuka kila uchao..Hili la kuuawa amos limeniwashia taa nyekundu kuashiria kwamba mapambano haya kwa sasa yamefikia sehemu ya hatari zaidi” akasema Mathew
“ nakubaliana nawe Mathew.hata mimi sikutegemea kabisa kama suala hili lingeweza kufika hapa lilipofika.hata hivyo nawapongeza kwa hatua kubwa iliyofikiwa hadi hivi sasa.Mmegundua mambo mengi makubwa na mazito.Kinachotakiwa kwa sasa nikushirikiana kuhakikisha kwamba mambo haya yanafika mwisho na tunaizika kabisa mitandano hii ya hatari hapa nchini na hasa team SC41”
“Uko sawa Peniela lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya mbeleni.watu tunaopambana nao niwatu hatari na wenye nguvu lakinininwahakikishia kwamba tutapambana hadi tone la mwisho la damu na nitaongoza mapambano kuishinda vita hii” akasema Mathew safari ikaendelea hadi walipowasili nyumbani kwa Mathew.Anitha akawafungulia geti.
“ What happened? Kuna tatizo Mathew ?akauliza Anitha baada ya Mathew na Peniela kushuka garini
“ yes there is a problem.Eva amekwisha rejea?
“Ndiyo amerejea yuko na madaktari chumbani.”akasema Anitha.
“ Naomi yuko wapi? Akauliza Mathew
“ Yuko nyuma bustanini anapumzika.who is she? Akauliza Anitha
“ Nitakufahamisha baadae.kwa sasa muandalie chumba cha kulala ataishi nasi hapa.Vile vile mpeleke peniela chumba cha mapumziko akapumzike kwa muda.”akasema Mathew kisha akaongoza hadi katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi.hali yake ilikuwa nzuri na alikuwa amekaa kitandani akionge ana madaktari wale wawili pamoja na Eva.Mara tu Rosemary alipomuona Mathew akamkumbuka
“Its you..Its you who shot henry..its you…!!..akapiga ukulele na kutaka kuinuka pale kitandani madaktari wakamzuia kwanialikuwa na pingu mguuni..
“ Anaendeleaje? Mathew akawauliza madkatari
‘Kwa sasa hali yake imetulia na anaendelea vizuri”
“kwa hiyo ninaweza kumfanyia mahojiano? Akauliza Mathew
“ Nadhani ungesubiri kidogo kabla ya kumfanyia mahojiano ili hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri kabisa. “akashauri mmoja wa wale madaktari
“ Thank you doctor ..we’ll take it from here” akasema Mathew
“ what ?! akauliza Eva
“Your job here is done you can go now.! Akasema Mathew
“ You are kidding Mathew.Huyu mama bado anahitaji usimamizi wa madaktari na hawezi kuhojiwa kwa sasa” akasema Eva
“ Thank you so much for your help but you job is done here too,so you can go now.Naomi atabaki hapa kwetu na kama kutakuwa na tatizo lolote nitakutaarifu” akasema Mathew.Eva akaonekana kukerwa sana na kauli ile ya Mathew akamtazama kwa hasira na kusema
“ Mathew can we talk for a minute?
Mathew na Eva wakatoka nje ya kile chumba
“What are you doing Mathew? Akauliza Eva
“ I’m doing my job Eva” akajibu Mathew
“ Mathew mbona unajiweka katika hatari kubwa . Huyu mama bado anaumwa na anatakiwa uangalizi wa madaktari kwa nini unakuwa mbishi Mathew?
“ Eva this is my job and I’m going to do it the way Iwant.Huyu mama ana taaifa za muhimu sana ambazo ni lazima tuzipate.we don’t have that time to wait so if you don’t mind can you please go and let me do my job? Akasema Mathew
“ Ok I’m going but don’t you ever find me again for any help” akasema Eva huku akiingia ndani ya kile chumba kwa hasira na kuwaomba wale madaktari waondoke zao.
Baada ya Eva na madaktarikuondoka Mathew akarejea ndani ya chumba alimokuwamo Rosemary mkozumi akamtazama kwa sekunde kadhaa
“ Now its just me and you..Today I’m your angel of death..” akawaza Mathew na kuufunga mlango akatoka
Moja kwa moja akaelekea nyuma ya nyumba alikokuwa amekaa Naomi akipung a upepo.Mara tu alipomuona Mathew akainuka na kumfuata
“ Naomi karibu sana.Hapa ni nyumbani kwangu na wewe utaishi hapa pia.Nina rafiki zangu ambao ninaishi nao hapa ambao wengine tayari umekwisha onana nao.” Akasema Mathew
“ Nashukuru sana .Nimeipenda nyumba yako nzuri sana.Imetulia na sikamalile gereza nililokuwa nimefungiwa.Habari ya kule ulikokwenda? Ulifanikiwa kukipata ulichokuwa unakitafuta? Akauliza Naomi.Mathew akasita kidogo kumweleza chochote kuhusiana na kile kilichotokea kule nyumbani kwa Rsemary Mkozumi
“Naomi ninashukuru sana kwa msaada wako mkubwa .Ninaomba kama hutajali twende ndani tukaongee.Kuna mambo mengi ya kufahamishana ikiwamo kukufahamisha kwa watu ” akasema Mathew kisha akaongozana na Naomi hadi ndani Sebuleni akawaita Anitha ,Peniela na jaji Elibariki.
“ndugu zangu nimewaiteni hapa kuna mambo muhimu ninataka tuongee.Imekuwa ni bahati tumepata fursa nyingine ya kukutana sote pamoja.”akasema Mathew akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“ Siku ya leo imekuwa ni siku ngumu na chungu sana kwetu sote.Tumewapoteza watu wetu wa muhimu katika maisha hyetu.Tukianza na Elbariki,umempoteza mkeo mpendwa Flaviana.Hili ni jambo zito sana na inauma sana japokuwa kama mwanaume lazima ujikaze na ukubaliane na hali halisi .Ninayafahamu machungu ya kuondokewa na Yule mtu w a karibu yako sana na uliyempenda kwani hata mimi niliwahi kuondokewa na familia yangu yote kwa hiyo ninafahamu jaji Elibariki anapitia kipindi gani kwa sasa.Msiba huu si wako peke yako ,ni wetu sote na sote tumeumizwa na jambo hili.kwa niaba yangu , Anitha na Peniela tunakupa pole sana na binafsi ninakuhakikishia kwamba sintalala usingizi hadi nihakikishe kwamba wale wote waliosababisha kifo cha mkeo Flaviana wanapatikana na kufikishwa mbele ya sheria ili haki itendeke.Ninachokuomba jipe moyo,tuko pamoja na tushirikiane katika jukumu zito lililoko mbele yetu na tuhakikishe kwamba tunaikamilisha kazi hii vizuri”akasema Mathew na kunyamza kidogo halafu akaendelea,
“ Peniela leo hii umempoteza mlezi wako ambaye alikuwa ni mtu wa muhimu sana katika maisha yako.Japokuwa alikuwa na matattizo yake ya kibinadamu lakini nina hakika kifo chake kimekuumiza sana .Kwa niaba yangu,Anitha na jaji Elibariki tunakupa pole nyingi sana kwa kumpoteza mtu wako wa muhimu sana na tunakuahidi ushirikiano mkubwa hasa katika kipindi hiki kigumu.Ulimpenda sana John na njia pekee ya kumuenzi kwa yale mema yote aliyokufanyia ni kwa kuhakikisha kwamba tunaikamilisha operesheni ya kuzuia uuzwaji wa package ya Dr Joshua na kuhakikisha inatua mikononi mwetu.Kabla ya kifo chake John alisisitiza sana kwamba lazima tuhakikishe jambo hili linafanikiwa kwa gharama zozote na tusiiache package hiyo ikachukuliwa .Kwa hali hiyo basi ninakuomba sana Peniela kwa muda huu mchache yasahau machungu yote ya kifo cha John na tuelekeze nguvu zote katika kuhakikisha tunaikamilisha operesheni hii.”akasema Mathew.
“ Mathew ninashukuru sana kwa kusimama pamoja nami katika wakati huu mgumu. Lakini pamoja na yote yaliyotokea ninawahakikishia kwamba niko imara na akili yangu yote nimeielekeza katika suala lililoko mbele yetu.Ni kweli john alikuwa mtu muhimu kwangu lakini kifo chake hakiwezi kunifanya nipoteze muelekeo katika suala zito linalotukabili.Naomba msiwe na shaka yoyote kuhusu mimi niko vizuri kabisa kuifanya kazi” akasema Peniela
“ Ahsante sana Peniela kwa kutuhakikishia kwamba uko imara.Binafsi ninawaahidi kwamba nitawongoza katika mapambano haya na tutashinda.” Akasema Mathew
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ jambo lingine ambalo ninataka niwafahamishe ni kwamba leo tumepata mgeni.Anaitwa Naomi.Huyu ni mtoto wa waziri wa zamani wa kilimo anaitwa Henry.Naomi ametoa mchango mkubwa sana sikuya leo katika kumpata Rosemary Mkozumi.Kwa hiyo basi kwa sasa ataendelea kukaa nasi hapa kwani bado anahitaji sana msaada wetu sisi ili aweze kuendelea na maisha yakeya kawaida.” Akasema Mathew kisha akamgeukia Naomi
“Naomi hawa uwaonao hapa ni wenzangu na wote shughuliyetu ni moja.Sisi ni watu tunaoshughulika na masuala ya usalama kwa hiyo kwa hapa uko sehemu salama kabisa.Mimi ninaitwa Mathew,Yule pale anaitwa jaji Elibariki,Yule pale ni Anitha na yule pale anaitwa Peniela.” Mathew akafanya utambulisho
“ Peniela ?!!..akasema Naomi huku akitabasamu
“ Sura yako si ngeni sana machoni pangu.Nilipokuona nilikuwa najiuliza nimewahi kukuona wapi nimekumbuka nilikuona katika Luninga .Uliwahi kuwa na kesi mahakamni na ukashinda ,right? Akauliza Naomi
“ Ndiyo Naomi” akajibu Peniela huku akitabasamu
“ nakumbuka pia uliwahi kuwa na maduka maarufu sana ya mavazi ?
“ Ndiyo Naomi niliwahi kuwa na maduka ya mavazi lakini baada ya kupatwa na yale matatizo ya ile kesi niliyafunga maduka yangu.”
“ Nilikuwa mnunuzi mzuri sana wa nguo navipodozi kutoka katika maduka yako.Leo nimefurahi sana kukuona Peniela.Kumbe ni mrembo hivi”akasema Naomi na wote pale sebuleni wakacheka.Naomi na peniela wakakumbatiana..
“ Naomi utakaa hapa pamoja na sisi kwa muda wakati tunaendelea kulifanyia kazi suala lako na chochote utakachohitaji usisite kutuambia.Kwa sasa Anitha atakupeleka chumbani kwako ukapumzike wakati sisi tunaendelea na maongezi yetu ya kikazi” akasema Mathew
“Nashukuru sana Mathew kwa msaada wako na kunitoa kule kifungoni.Hapa kwako nimekaa mwa muda mfupi lakini ninajiona ni mwenye furaha sana na amani tele moyoni mwangu.Nilipokuwa ndani ya lile jumba sikuwa na tumaini kama siku moja na mimi nitakuwa huru tena lakini Mungu ni mwema siku zote na amenikutanisha na ninyi watu wema.Ahsante sana.Endapo kuna lolote mnalotaka kulifahamu kuhusu baba yangu mimi niko tayari kuwasaidia muda wowote kwani ninayafahamu mambo yake mengi sana” akasema Naomi
“ Ahsnate sana Naomi.Tutakufahamisha tukihitaji msaada ako ”akajibu Mathew.
Anitha akainuka kwa lengo la kumpeleka Naomi chumbani lakini akakataa
“ Dada Anitha,Mimi nimekuwa kifungoni kwa miaka zaidi ya minne na sitaki tena kuendelea kukaa kaa chumbani .Nataka niyafurahie maisha ya uhuru hivyo ninakwenda kule nje kuogelea” akasema Naomi na kutoka nje.
“ She’s so happy” akasema Peniela baada ya Naomi kutoka
“ Naomi ni mtoto wa pekee wa Henry waziri wa zamaniwa kilimo ambaye kwa sasa ana mahusiano ya kimapenzi na Rosemary mkozumi.kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba Henry ndiye aliyesababisha yeye kujitumbukiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.Naomi anadai kwamba anazifahamu siri nyingi za baba yake na aliwahi kumtisha kwamba siku moja anaweza akatoa siri zake jambo lililomuogopesha sana Henry na akaamua kumtumia kijana aliyekuwa katika mahusiano na Naomi ambaye alimshawishi na akakubali kujiingiza katika dawa za kulevya.lengo lilikuwa ni kumfanya Naomi aelekeze akili yake katika unga na asikumbuke chochote kuhusu mamboya baba yake. Naomi alijikuta akiboea katika madawa ya kulevya na maisha yake kuharibika kabisa.Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya,Henry akamfungia ndani ya jumba na kumuwekea kila kitu na ulinzi mkali sana.kwa takribani zaidi ya miaka mine sasa Naomi hajawahi kutoka nje ya jumba almofungiwa.Tulimuahidi kumsaidia na kumtoa katika kifungo kile na ndiyo maana alikubali kwa moyo mmoja kushirikiana nasi na akatusaidia tukampata Henry ambaye alituingiza ndani ya jumba la Rosemary .Kwa hiyo Naomi anahitaji sana ushirikiano wetu sisi katika kumrejesha katika maisha yake ya awali.Kwa sasa amekwisha achana na matumizi ya dawa za kulevya na kinachofanyika sasa ni ingawa bado hajarejea katika ile hali yake aliyokuwa nayo awali i.” Akasema Mathew
“ usijali kuhusu hilo Mathew.Tutashirikiana kuhakiksha kwamba Naomi anarejea katika hali yake ya kawaida.Huyu ni mdogo wetu na hatuna budi kumsaidia.Baada ya kuikamilisha kazi hii iliyoko mbele yetu ninakuahidi kumshuguhulikia sana Naomi.”akasema Peniela.
“ Ahsante sana Peniela.Ila kuna jambo nimemficha na sijamweleza ukweli hadi hapo baadae.Her father is dead ”
“ henry is dead? How?
“ Alifariki katika purukushani iliyotokea nyumbani kwa Rose.Alijaribu kuzuia tusiweze kumpata Rose kwa hiyo sikuwa na namna nyingine ya kufanya.I shot him” akasema Mathew na sebule yote ikawa kimya
“ kwa sasa tusimweleze chochote hadi hapo baadae “akasema Mathwe
“ na vipi iwapo jambo hili litatangazwa katika luninga je itakuwaje? Akauliza Peniela
“ Tutamweleza ukweli wa kilichotokea na nina imani atatuelewa” akasema Mathew na kuendelea
“ Pamoja na siku ya leo kuanza vibaya lakini kuna mambo mazuri pia yametokea.Tumefanikiwa kumpata mtu ambaye tunadhani ndiye aliyekuwa nyuma ya wizi wa karatasizile zilizoibwa toka ikulu zenye kanuni za kutengeneza kirusi hatari.Rosemary natajwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Habib Soud ambaye ndiye aliyetaka kuzinunua karatasizile na kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka wa mtu wangu ndani ya C.I.A ni kwamba Habib anachunguzwa na C.I.A kwa kufadhili makundi ya kigaidi.Ninahisi lengo lake la kutaka kununua karatasi zile ni kutumia kanuni zile kutengeneza kirusi ambacho wangeweza kukitumia katika mambo ya kigaidi.Rosemary amekuwa akipokea pesa nyingi kutoka kwa Habib na ninahisi kuna mambo mengi wanashirikiana na ninahisi kwamba yawezekana hata Rosemary naye pia akawa na mafungamano na makundi ya kigaidi.” akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Rosemary pia amekuwa na mawasiliano na mtu mmoja aitwaye Samir asaad na katika mojawapo ya mawasiliano tuliyoyapata,Rosemary alimuhakikishia kwamba mzigo utapaatikana muda wowote kwani ana mawasiliano ya karibu sana na mtu aliye karibu na rais.Tulipochunguza zaidi tukagundua kwamba Rosemary alikuwa na mawasiliano ya karibu na Captain Amos ambaye ni mtu wa karibu sana na rais Dr Joshua.Hii inatupa picha kwamba mzigo ambao Rosemary alimuhakikishia Samir kuupata muda wowote ni hiyo package ambayo hata sisi tunaifuatilia.Tulitaka kupata uhakika toka kwa Captain Amos na tukaweka mtego wa kumpata ,tukaenda na Peniela kuonana naye mahala walikopanga wakutane.Peniela akaonana naye na baada ya kumbana na kumtolea vitisho Amos kuna mambo alitaka kuyasema kabla ya kuuawa.Peniela hebu simulia nini Amos alikisema?
“ Nilipokutanana Amos nilishindwa kujizuia nikapandwa na hasira na kumtolea bastora.Nilimtaka anieleze ni kwa nini alitusaliti na kutoa taarifa za kuhusiana na package kwa Rosemary ? aliniambia kwamba nikimuua nitafanya kosa kubwa sana kwani tayari wana mpango mkubwa kwa ajili yangu na Elibarii wa kutufanya wenye nguvu.Nilimuuliza yeye na nani ambao wana mpango huo na akawa tayari kunieleza lakini ghafla mlango ukapigwa teke na mwanamke mmoja akajitokeza akiwa na bastora mbili akamchakaza Amos kwa risasi kisha akatoweka.Lilikuwa ni shambulio la haraka sana na ambalo hatukuwa tumelitegemea.Captain Amos alifariki dunia palepale.Baada ya tukio lile nikaikumbuka sura ya Yule mwanamke.Ni Yule ambaye alikuwa na Elibariki usiku ule aliposhambuliwa.”
“ What ?! akauliza jaji Elibariki kwa mshangao.
“ Are you sure Peniela?
“ Ndiyo Elibariki.Japokuwa ulikuwa ni usiku lakini niliweza kumuona vyema Yule mwanamke sura yake na baada ya kumuona leo hii nimekumbuka ni Yule Yule uliyekuwa naye usiku ule”akasisitiza Peniela
“ Nikweli usiku ule niliokolewa na mwanamke ambaye aliniondoa toka pale kwenye eneo la tukio naakanikabidhi kwa Peniela..Hakunieleza jina lake na wala sababu ya kuniokoa.Nimestuka kidogo kusikia kwamba leo hii amejitokeza tena.Ni nani huyu mwanamke? Akauliza jaji Elibariki
“ Hilo ndilo swali tunalotakiwa kulitafutia majibu.Tunatakiwa kumfahamu Yule mwanamke ni nani .Inaonekana wazi kwamba kuna mpango Fulani unaandaliwa na watu au kikundi cha watu unaowahusisha jaji Elibariki na Peniela.” Akasema Mathew
“ Who are these people? How do they know about us? Akauliza jaji Elibariki
“ Kwa sasa ni mapema mno kulijibu swali lako lakini tunayo sehemu ya kuanzia kutafutia majibu yetu.Tunaye Rosemary Mkozumi.Huyu ana majibu ya maswali yetu mengi tu.Nadhani ni wakati sasa wa kuweza kuyapata majibu ya maswaliyetu.I’m going in there to find answers.Anitha wewe utaendelea kuifanyia uchunguzi simu na kompyuta ya Amos.Elibariki na peniela mnaweza kwenda kupumzika kwa muda .”akasema Mathew na kuinuka akaelekea chumbani kwake.
“ Namuonea huruma sana huyu Rosemary kukutana na Mathew.Kwa usalama wake ni bora akamueleza ukweli kwa kila atakachomuuliza bila ya kumficha.”akasema Anitha baada ya Mathew kuondoka pale sebuleni
“ Mathew hata mimi ninamuogopa sana.Ni mtu mzurilakini awapo kazinihuwa nimtu tofauti kabisa ”akasema jaji Elibariki
“ By the way ninaomba kukuuliza Peniela.Ulikuwa na Mathew siku alipoitwa na John Mwaulaya hospitali.unaweza kufahamu waliongea jambo gani? Akauliza Anitha
“ Kilichotokea usiku ule kilikuwa cha kushangaza sana.John aliomba aonane naMathew na maadui wa siku nyingiwalikutana na waliongea kana kwamba ni marafiki wa muda mrefu.Waliongea kwa zaidi ya dakika hamsini na mpaka leo hakuna anayefahamuwaliongea kitu gani.Mazungumzo yao yamebaki kuwa siri ya Mathew ”akasema Peniela.
“lazima kuna jambo zito waliongea na ninatumai iko siku Mathew atatueleza waliongea kitu gani”akasema Anitha kisha akainuka na kuelekea ofisini, jaji Elibariki akamshika mkono Peniela wakaelekea chumbani.
“ Pole sana Peniela kwa kilichotokea.Nimestuka sana kusikia kuhusu kilichotokea ulipokwenda kuonana na Amos.Sijui ningefanya nini kama kwa bahati mbaya ungeshambuliwa” akasema jaji Elibariki akiwa chumbani na Peniela.
“ Lilikuwa ni shambulo la ghafla sana ambalo hata sisi hatukulitarajia kabisa.Mini nilitanguliwa kuingia chumbani kuonana na Amos naMathew akabaki nje .Mara tu nilipoingia ndani na kukutana uso kwa uso na Amos hasira zikanipanda nikachomoa bastora nikamuuliza ni kwa nini anashirikiana na Rosemary Mkozumi na kutoa taarifa zetu? Amos akanijibu kama nilivyowaeleza na nilipomtisha zaidi alikuwa tayari kabisa kunieleza nimpango gani huo walio nao juu yetu na mara tu alipoanza kunieleza akatokea Yule mwanamke na kummiminia risasi.Shambulio lile limetokea kwa haraka sana na katika muda mfupi.Mwanamke Yule alikuwa katika nafasi nzuri sana ya kuweza hata kuniua na mimi kwani sikuwa nimejiandaa kwa rabsha zozote lakini aliniacha na inaonekana kabisa kwamba lengo lake lilikuwa ni kumuua Amos tu.”akasema peniela.jaji Elibariki akashika kichwa chake akatafakari kidogo na kusema
“lakini watu hawa ni akina nani? Wametufahamuje sisi? Wana mpango gani na sisi? Akauliza jaji Elibariki
“ kama alivyosema Mathew kwamba maswali hayo ni magumu sana kujibika kwa sasa hadi hapo utakapofanika uchunguzi na tutafahamu kila kitu lakini tukae kwa tahadhari kubwa kwanikuna watu wanaotufahamu na kutufuatilia na wana mipango juu yetu.Umakini mkubwa sanaunahitajika kwa kila tunachokifanya.Elibariki sikutegemea kabisa kama suala hili lingeweza kufika hapa lilipofika.Kuna wakati najikuta nikiogopa kutokana na namna jambo hili linavyochukua sura mpya kila uchao,namna mambo mazito yanavyoibuliwa kila siku.”akasema Peniela
“ Hata mimi sikufikiria kama tunaweza kufika hapa tulipofika.Nilimpa Mathew kazi ya kumtafuta muuaji wa Edson na nilitegemea kwa uwezo wa Mathew ingechukua siku chache tu kuikamilisha kazi ile na kumfahamu muuaji na nilifanya hivi kwa lengo la kulisafisha jina lako .Nilitaka muuaji halisi apatikane iliumma wote ujue kwmba ulisingiziwa ile kesi na kwamba sikukuachiahuru kwa makosa bali hukuwa na hatia,lakini mambo yaliyoibuliwa na yanaoendelea kuibuliwa katika uchunguzi huu yanaogopesha sana.Ni mambo mazito na sijui nini mwisho wake.Kila siku unalala hujui kesho nini kitaibuka.Sikuwahi kufahamu kama hapa nchini kuna kitu kinaitwa team SC41.Kuna mambo mengi ambayo sikuyafahamu hadi lilipoanza sakata hili.” Akasema jaji Elibariki
“ usihofu Elibariki kila kitu kitafika mwisho.Anyway tuachane na hayo,unaendeleaje? Akauliza peniela
“ Kusema kweli sijielewi Peniela.Siwezi kusema kwamba ninaendelea vizuri wala vibaya,kiujumla naona akili yangu kama imefika kiwango cha mwisho cha kufikiri .Ninawaza mambo mengi sana .Hapa nilipo sifahamu hatima yangu ni nini..Sijui lini nitatoka ndani ya jumba hili na kuendelea na maisha yangu ya kawaida .sijfahamu maisha yangu yatakuaje baada ya kutoka humu ndani,ninawaza mambo mengi mno” akasema jaji Elibariki.Peniela akamtazama na kumuonea huruma sana.
“ Pole sana elibariki lakini nina kuhakikishia kwamba tutafanya kila linalowezekana ili kulifikisha mwisho suala hili na maisha yako yatarejea kuwa ya kawaida.” Akasema peniela
“ ahsante sanaPeniela.Ahsante kwa kunipa moyo.Vipi kuhusu wewe unaendelaje? Akauliza jaji Elibarki
“ John was a bastard na kifo chake kimeniumiza sana lakini kutokana na mambo yaliyoko mbele yangu nimeamua kuwa jasiri na kuendelea kukabiliana na mambo mazito yaliyoko mbele yetu.John is gone na maisha lazima yaendelee.Ni wakati wangu sasa wa kutafuta uhuru wangu.Nataka nihakikishe nimiangusha team SC41.Sitaki kusikia tena kikundi kama hiki kikiendelea.Nikifanikiwa jambo hili nitakuwa huru na nitaweza kuendelea namaisha yangu ya furaha .Nataka nianze upya maisha yangu nikiwa nawe Elibariki mwanaume wa maisha yangu ambaye ninakuwaza kila sekunde..”akasema Peniela na mara akastuka baada ya kukumbuka kitu
“ Elibariki I’m so sorry.Nimebebwa na hisia na kutamka maneno ambayo sikupaswa kuyatamka kwa wakati huu ambao unaomboleza kifo cha mkeo.Nisamehe sana Elibariki sitaki nionekane kwamba nimefurahia kifo cha Flaviana ” akasema Peniela
“Peniela ulichokisema ni ukweli ulio wazi na hakuna sababu ya kuficha.Sifurahii kwa kifo cha mke wangu Flavana lakini kwa vile kimetokea basi hii ni fursa yetu sisi kuweza kuikamilisha mipango yetu ya kuwa pamoja.Wanasema kwamba kila jambo hutokea kwa sababu maalum na inawezekana kabisa hata suala hili la kifo cha Flaviana limetokea kwa sababu maalum na sababu yenyewe ni mimi na wewe kuwa pamoja.” Akasema jaji Elibariki
“ Elbariki usiseme hivyo tafadhali.Haipendezi kuongelea masuala haya kwa wakati huu wa majonzi tunapoomboleza kifo cha Flaviana.”akasema Peniela
“ Peniela hakuna ubaya wowote wa kuliongelea suala hili.Flavana is gone and she will never come back.Hakuna ubaya kwa sisi kuanza kuyapanga maisha yetu ya mbele.Tunapendana kwa dhati na hakuna sababu ya kuficha tena kuhusu suala hili.” Akasema jaji Elibariki.Peniela akamtazama akatabasamu na kusema
“ usijali jaji Elibariki .Tutapata muda mzuriwa kuongea kuhusu mambo haya lakini kwa sasa tuelekeze nguvu katika suala lililoko mbele yetu ili tuhakikishe kwamba tunapoanza maisha mapya tunakuwa huru na hatufungwi na kitu chochote”akasema Peniela
“ Uko sawa peniela.Vipi kuhusu John mwaulaya anazikwa lini?
“ Mpaka sasa bado hatujaamua atazikwa lini na wapi .”akasema peniela.Jaji Elibariki akainama na kuzama mawazoni
“ unawaza nini Elibariki?
“ Peniela najitahidi sana kujizuia nisiwe na mawazo lakini ninashindwa.Kuna mambo yanaumiza mno,kwa mfano sintaweza kuhudhuria mazishi ya mke wangu.Jambo hili linaniumiza mno.” Akasema jaji Elibariki
“ Ni kweli inauma sana lakini nitakwenda mimi kukuwakilisha na nitahakikisha nimetupia ua kwa niaba yako.Ntasema maneno yale ambayo ungetamka wewe kwa mdomowako kama ungekuwepo wakati Flaviana akizikwa “ akasema peniela
“ Ahsante sana peniela”
*******
Geti jesi linafunguliwa katika jumba moja kubwa la ghorofa tatu na gari nyeusi aina ya BMW likaingia kisha geti likafungwa.Toka ndani ya gari lile msichana mmoja mwenye mavazi meusi akashuka garini akavua miwani yake na kisha akaanza kutembea kiukakamavu kuelekea ndani ya lile jumba.Mbele ya mlango wa kuingilia ndani walisimama walinzi wawili waliovaa suti nyeusi .Yule msichana akasalimiana nao na kisha mmoja wao akamfungulia mlango na kumuongoza ndani,wakapanda hadi juu kabisa ya ghorofa ambako kulikuwa na sehemu nzuri sana ya kupumzikia .Mlinzi akamuelekeza Yule msichana sehemu ya kukaa na kisha akafika msichana mmoja aliyevaa suruali nyeusi na shati jeupe aliyeonekana kama mtumishi wa ndani akamsalimu Yule dada kwa adabu na kumuuliza kinywaji anachotumia.Yule dada akagiza mvinyo wowote mkali .Baada ya dakika kama nne mvinyo ukaletwa na Yule dada akanywa funda kubwa.Akatoa pakiti ya sigara na kuchomoa moja akaiwasha akavuta huku akipuliza moshi mwingi .Baada ya dakika kama kumi hivi akatokea mzee mmoja mwenye umbo kubwa aliyevaa shati refu jeupe lililofingwa nusu na kukiachawazikifua chake kikubwa kilichoibeba mikufu miwilimikubwa ya dhahabu..
“ Jesica ! akasema Yule mzee aliyekuwa na sauti ndogo tofauti na mwili wake
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Hallo Vincent” akasema Jesica huku akisimama na kusalimiana na Yule mzee
“ Karibu sana Jessica” akasema Vincent
“ Nashukur u sana Vincent.” Akasema Jesica
“ Sikutegemea kabisa kama ningeweza kukuona hapa mida hii.Kuna tatizo lolote Jesica? Akauliza Vincent
“ Vincent Kuna jambo limetokea “
“ Jambo gani Jesica?
“ Amos is dead..I shot him” akasema Jessica,Vincent akamtazama kwa makini na kusema
“ How it happened?
“ They discovered him.Peniela na kundi lake la Team SC41 tayari wamegundua kwamba Amos amewasaliti.Wamegundua mawasiliano yake na Rosemary Mkozumi na kwamba alikuwa akitumiwa na Rose kupata taarifa za kuhusiana na package iliyoko ikulu inayotaka kuuzwa na Dr Joshua.Nilipata taarifa ambazonadhanihata wewe tayari umekwisha zipata kuhusu tukio lililotokea nyumbani kwa Rosemary Mkozumi ambapo Henry waziri wa zamani wa kilimo ambaye kwa sasa ana mahusiano ya kimapenzi na Rose amepigwa risasi na kufariki na Rosemary Mkozumi bado hajulikani alipo.Baadae Amos alinipigia simu na kunieleza kwamba Peniela amempigia simu na kumtaka waonane kuna jambo la dharura hivyo Amos akanitaka tuongozane wote mpaka Mlimba lodge kwenda kuonana na peniela na baada ya hapo tuelekee hospitali tukafahamu nini kinachoendelea kuhusiana na msiba wa John Mwaulaya. Kwa kuwa ninafahamu ushirika wa Rosemary na Amos,na tayari nilifahamu kilichotokea kwa Rose nilihisi lazima kuna jambo lisilo la kawaida katika mwito ule.Nilikuwa sahihi kumbe Team SC41 waligundua kwamba Amos na Rosemary ni washirika.Peniela alifanikiwa kumuweka Amos chini ya ulinzi na sikutegemea kabisa kama Amos anaweza kuwa muoga kiasi kile kwani alipotishwa kidogo tu akataka kuanza kutoa siri.Nilikuwa mlangoni na niliyasikia maongezi yao yote na Amos alianza kumueleza Peniela kuhusu mipango inaopangwa juu yake yeye na Elibariki .kwa kuelekezewa bastora tu Amos alikuwa tayari kutoa siri nikaogopa iwapo angeteswa angeweza kusema kila kitu na hata kuhusu sisi hivyo nikaona njia pekee ni kumuua tu.” akasema Jesica.Vincent akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Congratulations Jesica.You did a wonderfull job.Ulifanya vizuri sana kumuua Amos.kwa ufupi hata mimi na wenzangu ambao ni wafadhili wakuu wa chama tulikuwa na mpango kama huo kwani hatujaridhishwa kabisa na maamuzi ya Deus Mkozumi kutaka kumuweka mtu kama Elibariki kugombea nafasi kubwa ya urais.Sisi tuna mtu wetu ambaye tuna imani endapo akishika madaraka atatusaidia sana lakini Deus amekuwa akishikilia msimamo wake wa kutaka kumpigania jaji Elbariki agombee urais kupitia chama chetu .Anataka kumtumia Elibariki kwa manufaa yake mwenyewe.Hatuko tayari kwa hilo na jambo hili ulilolifanya leo umeturahisishia sana kazi yetu kwani Deus alikuwa anamtegemea sana Amos kwa hiyo kama Amos amefariki sina hakika kama Deus atakuwa na nguvu ya kutosha kuweza kuikamilisha ndoto yake kwani ni Amos pekee aliyekuwa na uwezo wa kumunganisha na Elibariki..By the way hukuacha nyayo zozote katika eneo la tukio kwa sababu nina hakika lazima uchunguzi utafanyika.”
“ Hapana hakuna nyayo yoyote iliyoachwa.Nilifanya jambo hili kitaalamu sana”.
“ Good.Umefanya vizuri sana. “ akasema Vincent na kumuita mlinzi wake aliyekuwa amesimama mbali kidogo na pale walipokuwa wamekaa,akafika haraka akamnong’oneza jambo na Yule mlinzi akaondoka
“.Jesica kuna jambo nataka kulifahamu , ukiacha John Mwaulaya na Amos kuna mtu mwingine ambaye anafahamu kwamba wewe uko team Sc41? Akauliza Vincent
“ Niliingizwa Team SC41 na Amos na nilitaka ushiriki wangu uwe ni wa siri kwa hiyo wanaofahamu ushiriki wangu katika kundi hili ni hao wawili tu.Japokuwa nimemuua lakini Amos alikuwa mtu wangu wa karibu sana na nilijiunga na Team Sc41 kwa sababu yake baada ya kuniomba niwe nikimsaidia katika baadhi ya majukumu yake aliyokabidhiwa na Team SC41.Nilimsaidia kazi kadhaa na mojawapo kubwa ilikuwa ni ile niliyomuokoa jaji Elibariki usiku ule alipotaka kuuawa.Baada ya watu hao wote wawili wawili kufariki ambao ndio waliokuwa wakinilipa I’m no longer a part of Team SC41. ”
“ Good ! nimefurahi kusikia hivyo.” akasema Vincent
“ Kwa hiyo Vincent nini kitafuata bada ya hapa? Akauliza Jesica
“ Kwa sasa endelea na kazi zako kama kawaida wakati tunaangalia upepo unavyokwenda baada ya kifo hiki cha Amos.Unajua Yule alikuwa mtu mkubwa alikuwa daktari w a familia ya rais kwa hiyo lazima uchunguzi utafanyika kubaini sababu ya kifo chake na aliyemuua lakini usihofu endapo kamakutakuw ana hatari yoyote sisi tutashughulika nayo.Nchi hii ni ya kwetu.” akasema Vincent.Mlinzi wake akareje ana kitabu ,akakichukua na kuandika cheki akampatia Jesica.
“ Nitakuwa nikikufahamisha kila kitu kuhusiana na kinachoendelea lakini kuna jambo nitaomba ulifanyie uchunguzi.Ninataka unisaidie kufanya utafiti Rosemary Mkozumi yuko wapi ? Idara yenu ya usalama wa taifa mnazo nyenzo za kuweza kupata taarifa mapema sana kwa hiyo nisaidie kufahamu mahala aliko Rosemary .Can you do that for me? Akauliza Vincent
“ Niachie suala hilo nitalifanyia kazi .Nitafuatilia ofisini ili nione kama kuna taarifa zozote zimepatikana kuhusu mahala alipo Rose.” akasema Jesica
“ Ahsante sana Jesica.Lifanyie kazi suala hilo kwani nina wasiwasi sana na kutoweka huku kwa kutatanisha kwa Rose .Yule ni mtu anayetufahamu sana sisi na anayafahamumamboyetu mengi kamasisi tunavyoyafahamu yak wake “: akasema Vincent akaagana na Jesica.
“ Sasa kidogo ninaweza kuvuta pumzi baada ya kuwa na uhakika Amos ametoweka.Huyu alikuwa ni mtu muhimu mno kwa Deus na ndiye alikuwa anamtegemea sana katika mpango wake.Kwa sasa mipango yake haitaweza kufanikiwa tena na ni nafasi yetu kumuandaa mtu wetu ambaye atatusaidia sana endapoatashika madaraka “ akawaza Vincent.
Mathew akaingIa chumbani kwake akalifungua kabati ambao huhifadhi baadhiya vifaa vyake mbalimbaLi.Akachukua sanduku moja la kijani pamoja na vifaa kadhaa akatoka mle chumbani na kuelekea katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi.Akakinyonga kitasa na kuingia ndani.Rosemary alipomuona akainuka na kukaa kitandani.Alikuwa na hasira kali sana “ Who are you? Kwan in umeniweka humu? Nani kakutuma ufanye hivi? Akauliza kwa ukali Rosemary.Mathew hakumjibu kitu akaviweka vifaa vyake mezani akavuta kiti na kuketi akamtazama Rosemary kwa sekudne kadhaa kisha akasema
“ Hello Rosemary! “ Sina haja ya salamu yako.Tafadhali kijana naomba usijitafutie matatizo zaidi.Mpaka sasa tayari umekwishajiingiza katika matatizo makubwa.Umemuua Henry na kama vile haitoshi umeniteka na kunifungia humu chumbani.Unadiriki kumteka nyara mke wa rais? Umelipwa shilingi ngapikijana wangu hata ukakubali kujihatarisha namna hii? Tafadhali naomba uniachie huru haraka sana na nitaangalia namna ya kukusamehe na kukusaidia kukutoa katika janga hili ulilojitumbukiza bila kujua....” akasema Rosemar y Mkozumi kwa sauti ya juu .Mathew akamtazama kwa makini na kusema
“ Rosemary Mkozumi just relax…”
“ Kijana naomba tafadhali usiendelee na upuuzi wako unaotaka kuufanya.Nani lakini kakutuma unifanyie hivi? Unashirikiana na akina nani? Hao waliokutuma wamekuingiza katika tanuru la moto na wewe kwa tamaa zako ukakubali kuingia na kuungua .Ninakuonya kwa ara nyingine kijana tafadhali naomba unifungue haraka sana miguu yangu inaumia” akasema Rosemary.
“ Rosemary tafadhali naomba uniskilize kwa makinisanana sihitaji mzaha hata kidogo” Akasema Mathew.
“ Ninaitwa Mathew,ni mchunguzi wa kujitegemea.Nimewahi kufanya kazi katika idara ya usalama wa taifa Tanzania idara ya kupambana na kuzuia ugaidi na baadae nikaacha kazi hiyo na kuanza kufaya kazi zangu binafsi za kiuchunguzi.Mwezi wa pili mwaka jana kijana mmoja aitwaye Edson aliyekuwa akifanya kazi katika idara ya mawasiliano ikulu aliuawa na watu wasiojulikana lakinikesi hiyo ya mauaji ikamuangukia mpenzi wake aliyeitwa Peniela.Mahakama ilimuachia huru Peniela baada ya kuridhika kwamba hakuw ana hatia na hakumuua Edson kama ilivyodaiwa.Nilikabidhiwa jukumu la kumtafuta muuaji halisi wa Edson .Katika uchunguzi wangu niligundua kwamba Edson alishiriki katika uibwaji wa nyaraka nyeti sana toka ikulu.Niligundua kwamba ili kulifanikisah jambo lile Edson hakuwa peke yake alikuwa akishirikiana na watu wawili Mzee Kitwana na Mzee Matiku ambao kwa sasa wote ni marehemu.Nyaraka hizo zilizoibwa zilikuw ana kanuni za kutengeneza kirusi hatari sana ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa sana kwa binadamu.Nimelichimba suala hilikwa undani zaidi na kugundua kwamba mtu aliyetaka kuzinunua karatasi hizo anaitwa Habib Soud raia wa Saudi Arabia .Habib anatajwa kuvifadhili vikundi kadhaa vya kigaidi nahivyo kunifanya niamini kwamba yawezekanaalizihitaji karatasizile kwa ajili ya kutengeneza kirusi kile ili wakitumie kwa mambo ya kigaidi.Sikuishia hapo nilimchunguza Habib na kugundua kwamba amekuwa na mawasiliano nawe ya mara kwa mara .Nimegundua pia kwamba wewe ndiye uliyeratibu na kufanikisha mpango mzima wa kuibwa kwa karatasi hizo ikulu kwa kumtumia Edson na baadaya kuzipata karatasi hizo uliwazunguka washirika wako na kuwamaliza ili ubaki na karatasihizo na pesa yote itokanayo na mauzo ya karatasi hizo uipate peke yako.Ili kuendelea kuuficha uhusika wako katika suala hili kumbu umbu za mawasilianokatiyako na washirika wako wakuu katika suala hili yaani mzee Kitwana na matiku zilifutwa kabisa .” Akasema Mathew na uso wa Rosemary ukabadilika .Mathew akaendelea.
“ Kwa bahati mbaya pamoja na kuwaua washirika wako lakinihukufanikiwa kuzipata nyarakazile kwani ziifichwa na mmoja wa washirika wako.baadaya kuona jambo lile limeshindikana hukukata tamaa ukaingia tena katika biashara nyingine namtu mmoja anaitwa samir Asaad.Umekuwa ukiwasiliana na Samir na katika mojawapo ya barua pepeuliyomtumia Samir umemuhakikishia kwamba muda si mrefu toka sasa utafanikiwa kuupata mzigo anaoutaka kwani una mawasiliano ya karibu na mtu wa karibu na rais .Baadae tukagundua kwamba mtu uliyemtaja kuwa karibu na rais ambaye umekuwa na mawasiliano naye ni Captain Amos ambaye ni daktariwa familia ya rais.Tulimpata Captain Amos na wakati tukimfanyia mahojiano ,alitokea mtu na kumpiga risasi akamuua na hili lilifanyika makusudi ili Captain Amos asiweze kutoa siri.” Mathew akanyamaza akamtazama Rose ambaye matone ya jasho yalionekana usoni pake.
“ Amos is dead?! Akauliza Rosemary kwa msahngao mkubwa
“ yes ..he’s dead” akasema Mathew.Rose akainamisha kichwa kwa masikitiko
“ Rosemary kuna mambo mengi ambayo ninyafahamu kuhusu wewe namtandaowako nasitaki kpoteza muda kuyaongelea hapa.Ninachokihitaji toka kwako nikunipatiamajibu sahihiya kila nitakachokuuliza kaini kama hutanipa ushrikiano wa kutosha na kuniletea jeuri sahau kabisa kutoka hapa ukiwa hai.” Akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akasema
“Kitu cha kwanza ninachotaka toka kwako nataka kufahamu ,ukiacha wale washirika wako walikwisha fariki,nani mwingine ambaye umeshirikiana naye katika kuziiba karatasi zile ikulu? akaulizia Mathew .Rosemary Mkozumi akasonya na kubetua midomo kwa dharau akasema
“ You go to hell,wewe na huyo aliyekutuma!! .Mathew akamuangalia na kusema
“ Rose ninakukumbusha kwa mara nyingine kwamba hapa ulipo ni nusu ya jehanamu kwa hiyo nataka unijibu kiufasaha kila nitakachokuuliza na kitakachokuokoa ukaweza kutoka humu ndani ni ukweli..Tell me the truth and you’ll get out of here alive..Ninarudia tena nilichokuuliza mwanzo,nina kila ushahidi kuthibitisha kwamba ulihusika katika kuratibu mpango wa kuziiba karatasi zile ikulu.Ninataka kufahamu ni akina nani wengine ulioshirikiana nao kulifanikisha jambo hili ukiacha wale ambao wamekwisha fariki? Akauliza Mathew.
“ You go to hell you witch..nakuhurumia sana wewe kijana kwa nini unakubali kutumiwa kirahisi namna hiyo ? tafadhali achana na huu upuuzi unaoufanya.Mwambie aliyekutuma kwamba hawezi kupambana na Rosemary..” akasema Rosemary kwa dharau
“ Hakuna mtu aliyenituma bali ninafanya kazi hii kwa niabaya serikaliya jamhuri ya muungano wa Tanzania na si mtu binafsi kama unavyodhani..” akasema Mathew.Rose akacheka kwa dharau na kusema “ Serikali !! Unafahamu serikali ni nani? Poor boy hujui hata unachokiongea.Tafadhali naomba unifungue niondoke zangu na nitakusamehe,lakini ukiendelea kunishikilia hapa kwako kwa dakika kumi zijazo ninakuapia kijana sintakusamehe hata kidogo.”akasema Rosemary
“ Vitisho vyako havitaweza kukusaidia hata kidogo Rose.Nakuonya kwa mara ya mwisho kwamba utatoka humu ndani ukiwa salama endapo utanipa majibu ya kile ninachokitaka.Ukileta jeuri ninakuapia Rose hautatoka humu ndani salama.” Akasema Mathew na Rose akaukunja uso wake
“ Kijana kwa nini unakuwa mgumu kunielewa? Kwa nini unaendelea kuhatarisha maisha yako na kujiweka katika matatizo makubwa? Ninakwambiwa kwamba ndani ya muda mfupi ujao utajutia hiki unachokifanya .Sintokusamehe kabisa na wala usidhani kwamba h iyo serikali unayodai unafanya kazi kwa niabayake watakusaida kitu .Iam the government! ….Akasema kwa ukali Rose. Mathew akainuka na kumsogelea karibu. “ Rose ninafahamu kwamba unalengo la kugombea urais na kwa sasa mimi ndiye nitakayeamua kama jambo hilo litafanikiwa ama vipi.Endapo sintaridhika na majibu yako ndoto hiyo kubwa haitatimia kamwe.Nita…” Ghafla Mathew akastuka baada ya kutemewa mate usoni
“ I’ve told you go to hell you black devil !! akasema kwa ukali Rosemary.Mathew akamtazama Rosemary kwa hasira na kusema
“ umefanya kosa kubwa sana.Ni bora ungekutana na mtoa roho kuliko mimi.Sasa kwa kuwa umekataa kunijibu kwa hiari yako na umeonyesha kiburi ,nitakulazimisha kunijbu kwa nguvu” akasema Mathew na kuchukua ndoo ya maji akammwagia Rosemary na kumloanisha chapa chapa
“ Are you crazy?!!.I swear I’ll never forgive you for this ”akafoka Rose.Mathew akalifungua lile sanduku halafu akatoa vifaa kadhaa akaviweka mezani.Akachukukua vyuma Fulani viwili vyenye nyaya akavichomeka katika lile sanduku halafu akaliunganisha katika umeme kisha akavigusanisha vyuma vile vikatoa cheche.Rosemary Mkozumi akatumbua macho “ Unataka kufanya nini? Akauliza.Mathew hakumjibu kitu akarekebisha kiasi cha umeme anaouhitaji na kisha akasogea kitandani na kugusisha vyuma vile vyenye umeme katika pingu aliyofungiwa Rosemary mguuni.. "Aaaaaggggghhhhh!!!!!!!!!!!!!!!...”Rosemary akapiga kelele kubwa..Mathew akatulia kidogo halafu akarudia tena zoezi lile..Rose akaendelea kupiga kelele kubwa
“ Give me the names!!...akasema kwa ukali Mathew.Halafu akatulia
“ Give me the names!! nani u nashirikiana nao? Akauliza .
“ There is..there..iiii..there are no names..” akasema Rosemary huku akitetemeka mwili.mathew akagusisha tena vyuma vile katika pingu na kuendelea kumtesa Rosemary..
“ Stop that.!!.please stoooop !!!!!..” akalia Rose.Mathew akasimama
“ Ni akina nani ulishiriana nao katika mpango ule? Akauliza Mathew. “No one..sijashirikiana na mtu yeyote na wala siufahamu huo mpango unaousema..” akasema Rose huku akitweta.
“ This is not working…!!! Akasema Mathew kwa sauti ndogo.Akavua shati na kubakiwa na fulana ya ndani akamshika Rosemary kwa nguvu akamfunga mikono yake kwa pingu.
“ Nilikuonya toka mwanzo kwamba usiombe ukutane na mimi lakini ukapuuza.Utanieleza kila kitu leo ”akasema Mathew halafu akachukua kisu na kukata kijisehemu kidogo katika kidole cha mguu wa kulia wa Rose halafu akachukua bomba la sindano akavuta dawa fulani nyeupe toka katika kichupa kidogo na kudondoshea matone kadhaa mahala palipokuwa panatoa damu.Rose akagalagala pale kitandani huku akipiga kelele kubwa kwa maumivu aliyoyasiki..Mathew akachukua gundi na kumfunga mdomo ili asiweze kutoa ukelele halafu akadondoshea tena matone kadhaa mahala alipopakata..Rosemary akaendelea kugugumia kwa maumivu makubwa.Mathew akamfungua ile gundi aliyomfunga nayo mdomo akamuuliza
“ Uko tayari kuniambia ninachokihitaji?Akiwa ndani ya maumivu makali sana akasema
“ You go to hell you devil !! Mathew akamfunga tena mdomo na kumkata kidogo shingonihalafu akadondoshea matone kadhaa mahala alipokata..Rose akaruka ruka kana kwamba anakata roho.Mathew akamuangalia halafu akamfungua ile gundi mdomoni. “ Utanijibu nilichokuuliza? Akauliza Mathew lakini Rose hakumjibu kitu akabaki analia kwa maumivu makali.
“ C’mon Rose ..nijibu haraka nilichokuuliza !!!! akasema Mathew kwa ukali Rose akaendelea kulia kwa maumivu makali sana aliyoyasikia.
“ Dah ! sijawahi kukutana na mwanamke mwenye roho ngumu kama huyu mama.Lakini leo hii atanieleza kila kitu ninachotaka.”akawaza Mathew.Akaelekea mezani kwake na kuchukua kifaa kidogo cha kukatia akakiwasha na kukijaribu
“R ose umetaka mwenyewe tufike hapa tulipofika na nilikuonya toka mapema kwamba usiombe ukutane na mimi.I’ m a monster na ninachokwenda kukufanyia kitabaki katika kumbu kmbu za uzao wako daima.Nitakukata kidole kimoja kimoja nikianzia na vidole vya miguu na halafu nitakuja mikononi na halafu nitanyunyiza dawa hii inayouma na utajihisi kamaumetupwa katika shimo la moto kwani mwili wote utawaka moto kwa maumivu utakayoyasikia..Utasikia maumivu makali mno ambayo hujawahi kuyasikia toka umezaliwa.Ukitaka nisifanye hivyo nijibu haraka kile nilichokuuliza” akasema Mathew lakini Rosemary hakujibu kitu bado aliendelea kulia kwa maumivu makali.Mathew akachukua kile kifaa akakiwasha na kisha akakishika kidole cha mwisho cha mguu wa kulia wa Rosemary na kukikata. Rosemary akapiga ukulele mkubwa sana
“ C’mon Rose,usinilazimishe nikakufanyia hivi.Niambie kile ninachokitaka” akasema Mathew kwa ukali.Bado Rose aliendelea kugalagala huku akilia kwa maumivu makali mno.
“ Bado anaendelea kuwa na kiburi ..leo lazima nimbadilishe sura yake..Atanieleza tu .” akawaza Mathew na kukishika tena kidole kinachofuata akakata.Rose akapiga ukele mkubwa hadi sauti ikaanza kumkwama..
“ Please stop !!.stop hurting me !!!!!!!!!!..akasema Rosemary..
“ Are you ready to tell me what I want? akauliza Mathew
“ I will tell you..i will tell you everything ..stop hurting me…” akasema Rose huku bado akiendelea kulia kwa maumivu makali.Mathew akachukua bandeji na kufunga mguu ule wenye majeraha halafu akamchoma sindano ya kupunguza maumivu.
“ Now tell me everything” akasema Mathew
“ I will tell you everything you want..please don’t hurt me
“ Ni kweli mimi ndiye niliyeratibu mpango ule wa kuziiba nyaraka zile toka ikulu.Nilifahamiana na Habib Soud alipokuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama.Wakati huo mume wangu Deus alikuwa katika kujiandaa kuhitimisha awamu ya mwisho ya uongozi wake na kumuachia Dr Joshua.Akiwa katika mapumziko yake Habib akatembelea ofisi za taasisi yangu na akadai kwamba amefurahishwa na kazi ninayoifanya kupitia taasisi yangu ya kuwainua wanawake kiuchumi na hivyo anataka kunipa sapoti.Ni kweli alianza kutoa misaada mingi sana ya mamilioni ya fedha na akawa ndiye mfadhili mkuu wa taasisi yangu.Tulijenga urafiki mkubwa .Siku moja aliniomba tukutane Dubai ili anitambulishe kwa matajiri wakubwa ambao wako tayari kuendelea kuifadhili taasisi yangu.Ni kweli alinitambulisha kwa mabilionea wakubwa sana ambao sikuwahi kuota kama siku moja ningeweza kukaa nao na kula nao chakula.Matajiri wale waliniahidi kunisaidia sana ili taasisi yangu iwe ya kimataifa na kusaidia wanawake sehemu mbali mbali za dunia.Baada ya kuachana na matajiri wale wakubwa,Habib akanifuata na kuniomba tuongee faragha akaniambia kwamba matajiri wale wako tayari kunisaidia sana na watamwaga pesa nyingi sana kwa taasisi yangu lakini kuna kitu kidogo wanakihitaji toka kwangu. Aliniambia kwamba kuna nyaraka Fulani za siri zinahifadhiwa ikulu na ambazo natakiwa kufanya juhudi nizipate.Hakunieleza kwa nini wanazihitaji karatasi zile ila alisema ni za muhimu sana kwao.Alinihakikishia kwamba endapo ningefanikiwa kuzipata karatasi zile basi ningeingia katika ulimwengu wa mabilionea.Ili kunithibitishia kwamba hawakuwa wakitania muda ule ule nikaingiziwa katika akaunti ya taasisi yangu kiasi cha shilingi milioni mia mbili.” akasema Rosemary na kuuma meno kwa maumivu makali aliyoyasikia. “ Please do something on my leg..I feel pain like hell !..umeniumiza sana wewe kijana I swear utanijua mimi ni nani ndani ya muda mfupi nikitoka hapa!! Akasema kwa ukali Rose huku akigugumia kwa maumivu makali.Mathew akachukua tena kichupa kingine cha dawa akaivuta katika bomba la sindano na kumchoma Rose katika mguu wake ule uliokuwa unavuja damu na mguu wote ukawa na ganzi hakusikia tena maumivu.
“ Sasa endelea na maelezo yako” akasema Mathew
“ Damu yote hii iliyomwagika haitakwenda bure lazima utailipa tu..How a handsome guy like you could be such a monster!!..
“ Rose naomba tafadhali usiendelee kunipotezea wakati wangu.Endelea kunipa maelezo au unataka nianze tena kazi yangu? Akasema Mathew kwa ukali.
“ Ok ! Ok!..dont hurt me any more you monster.nitakueleza unachotaka.” Akasema Rose akamtazama Mathew kisha akaendelea
“ Nilirejea Dar es salaam kwa lengo moja tu la kuzitafuta hizo karatasi mahala zilikofichwa.Niliishi ikulu kwa miaka kumi lakini kuna sehemu za siri ambazo sizifahamu.Suala lile nisingeweza kumuuliza mume wangu Deus ambaye kwa wakati huo tayari alikwisha staafu kwani ninamfahamu Yule mzee ni mtu muadilifu sana na asingeweza kunipa siri kama hiyo kwa hiyo nikaanza kutengeneza mtandao wa watu wa karibu na rais ambao niliamini wangeweza kunipatia taarifa za mahala zilipo hizo karatasi na nikafanikiwa kumpata Captain Amos.Huyu ndiye aliyeweza kunisaidia kufahamu mahala zilipo hizo nyaraka na ndiye aliyefanikisha mpango mzima wa kuzipata .Kwa bahati mbaya baada ya kufanikiwa kuzipata karatasi hizo watu niliowashirikisha katika mpango huu wakaingiwa na tamaa na kuzungukana wao kwa wao wakauana bila sababu . Taarifa za upotevu wa nyaraka zile zilifika hadi ikulu na Edson akauawa.Aliyemuua Edson ni Captain Amos ili kuuficha uhusika wake katika wizi ule kwani endapo rais angefahamu kwamba naye alishiriki katika wizi ule basi asingeweza kumuamini tena “
“ Wait !..” akasema Mathew
“ Kwa hiyo unaniambia kwamba Captain Amos ndiye aliyemuua Edson na si Dr Joshua? Akauliza Mathew
“ Ndiyo ! Edson aliuliwa na Amos ..” akasema Rose
“ Ok endelea…..
“ Kutokana na sintofahamu ile baina ya washirika wangu,karatasi zile zilipotea katika mazingira ya kutatanisha sana na mpaka leo hii sifahamu ziko wapi na biashara yetu ilishindwa kufanikiwa” Akasema Rose.Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Uliwahi kufahamu nini kiliandikwa katika nyaraka zile?
“ Sikuwahi kuzitia mikononi nyaraka zile na wala sifahamu nini kiliandikwamo.Nimesikia kwa mara ya kwanza leo hii toka kwako kwamba nyaraka zile zilikuwa na kanuni za kutengeneza kirusi” akasema Rose
“ Ndiyo.Karatasi zile zilikuwa na kanuni ambazo zinaelekeza namna ya kutengeneza kirusi hatari ambacho kinaweza kutumika katika maangamizi makubwa.” Akasema Mathew
“ Unafahamu kama Habib anahusishwa na kufadhili vikundi vya kigaidi? Akauliza Mathew
“ Hapana sikuwa na habari hizo.Mimi nilimfahamu Habib kama mfanya biashara wa mafuta na sikujua kama alikuwa anajihusisha na kufadhili vikundi vya kigaidi.”
“ Ukiacha karatasi hizo ambazo ulitaka kumuuzia Habib kuna mambo gani mengine ambayo amewahi kukuomba umsaidie? Au mliyoshiriiana kuyafanya?
“ Hakuna” akajibu Rose
“ Rose naomba ufahamu kwamba Habib na kundi lake walikuwa wanakutumia kwa faida yao na mitandao yao ya kigaidi na endapo wangefanikiwa kuzipata karatasi zile walizokuomba uwatafutie basi wangeweza kutengeneza kirusi hatari na wangefanya mashambulizi makubwa sana ambayo yangesababisha maangamizi makubwa duniani.Kwa kitendo hicho ulichokifanya uliiweka nchi yetu katika hatari kubwa na kukuweka wazi , hata wewe kwa hivi sasa unachunguzwa na mashirika makubwa ya ujasusi duniani kama C.I.A kutokana na ukaribu wako na ukaribu wako na Habib Soud.” Baada ya kusikia vile sura ya Rose ikajikunja.Alistushwa sana na taarifa ile ya kwamba anachunguzwa na C.I.A
“ To be honest I didn’t know if Habib is a terrorist “ akajitetea Rose
“ Lazima ulifahamu ,laini kwa tamaa ya fedha ukaamua kushirikiana naye.Kwa kushirikiana na mshukiwa wa kufadhili ugaidi ni wazi kwamba hata wewe mwenyewe unashiriki katika mambo hayo.Na kama suala hili likifahamika kwa umma basi taswira yako nzuri uliyoijenga katika jamii ya ndani na nje ya nchi itaharibika na mpango wako wa kugombea urais hautafanikiwa.All that you’ve worked hard for all these years will lost because you cant escape a very long sentence.Hebu jiulize Rose ungejisikiaje kama ungesikia maelfu ya watu wameuawa kutokana na kirusi kilichotengenezwa kwa karatasi zile ambazo wewe uliziuza kwa magaidi? Akauliza Mathew
“ I swer I didn’t know anything.Habib hakuwa tayari kunieleza kwa nini alizihitaji karatasi hizo na mimi sikuhoji kwani shida yangu kwa wakati huo ilikuwa ni fedha tu kwa hiyo sikujali hata kidogo kujua nini kimeandikwamo.Tafadhali naomba uniamini ninachokwambia” akasema Rose
“ Siwezi kukuamini hata kidogo Rose.You are a professional liar.Maisha yako yametawaliwa na uongo mkubwa. Unawadanganya watu kwa kuwapa misaada ya fedha ambazo zinatoka kwa magaidi.Unadhani wakilifahamu jambo hili watakufanya nini? Ndiyo maana nilikueleza toka mwanzo kwamba hatima ya maisha yako iko mikononi mwangu kwa sasa kwa hiyo ninahitaji maelezo yenye kuniridhisha ama sivyo I will destroy you” akasema Mathew
“ Please help me.Nimekuamini wewe ni mchunguzi makini sana na ndiyo maana nimekueleza kila kitu bila kukuficha kwa hiyo tafadhali naomba sana sala hili lisitoke nje ya kuta za nyumba hii.Lets put this between us.I ‘m giving you a chance to make a deal ”
“ A deal !!..Mathew akacheka kidogo
“ Rose lazima ukutane na mkono wa sheria lakini endapo ukinieleza ukweli mambo ambayo ninayataka basi ninaweza kulifiria ombi lako” “ Kitu gani unataka kufahamu?
“ Ni mambo mengi ambayo ninahitaji kuyafahamu toka kwako lakini nataka kwanza kumfahamu kiundani huyu Habib Soud na kama kuna mambo mengine ambayo umewahi kushirikiana naye.Ukinisaidia kumpata Habib nami nitakusaidia katika suala hili na hakuna atakayefahamu chochote.” Akasema Mathew.Rose akafumba macho na baada ya sekunde kadhaa akafumbua macho na kutazama mguu wake na damu iliyokuwa imetapakaa pale kitandani na kusema
“Ok kuna jambo lingine .Baada ya ule mpango wa mwanzo wa kuzipata karatsi zile kushindikana Habib alinikabidhi kwa binamu yake anaitwa Samir Asaad.Huyu naye ni kijana tajiri sana na ni mmoja wa mabilionea niliokutana nao Dubai.Huyu alinieleza kwamba kuna mzigo Fulani ambao rais wa Tanzania yaani Dr Joshua anataka kuwauzia watu Fulani ambao hakunitajia ni akina nani.Alinieleza kwamba kama nikifanikiwa kuupata mzigo huo ambao rais anataka kuuza basi nitakuwa bilionea.Nilikubali kwa kuwa ninao mtandao wa kutosha hata ndani ya ikulu.Kuwa kumtumia Amos ambaye ni mtu wa karibu na rais niliweza kufahamu mambo mengi kuhusiana na biashara hiyo anayotaka kuifanya rais na tayari kuna mikakati mikubwa ya kuweza kuipata. “ akasema Rose
“ Amos au Samir waliwahi kukueleza kwamba ni kitu gai hicho ambacho Dr Joshua anataka kuuza?
“ Hakuna anayefahamu kuna nini ndani yake lakini inaonekana ni kitu chenye thamani kubwa sana kiasi kwamba Samir yuko tayari kutoa fedha nyingi mno kukipata kifurushi hicho.Sikuhitaji kujua ndani kuna nini mimi shida yangu ni fedha tu .Nahitaji sana Fedha kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kampeni ya kunipeleka ikulu.“ akasema Rose na mara mlango ukagongwa kwa nguvu .Mathew akainuka na kwenda kuufungua akakutana na Anitha jaji Elibarki pamoja na Peniela
“ What ! Kuna nini mbona wote mko hapa akauliza Mathew
“ Tulisikia kilio kikubwa tukaja hapa mlangoni kujua kinachoendelea.Whats going on ? akaulizia jaji Elibarikihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Hamkutakiwa kuwa hapa Elibariki.Ninapotafuta taarifa Fulani wakati mwingine ninalazimika kwenda mbali zaidi na kutumia kila aina ya mateso kuweza kuipata taarifa hiyo.”
“ Mathew tuachane na hayo.Nilikuwa ofisini nikiendelea kucunguza simu na kompyuta ya Amos pamoja na ile ya Rosemary.Kuna mambo nimeyagundua.Naomba twende ofisini” Akasema Anitha kisha wakaongozana kuelekea ofisini.
“ Kuna nini Anitha? Akauliza Mathew
“ Jambo la kwanza nimegundua kwamba kuna mawimbi yasiyoya kawaida yanatoka hapa ndani.”
“ Sijakuelewa Anitha unazungumzia mawimbi gani? akauliza Mathew Anitha akaanza kuwaelekeza kwa kutumia luninga kubwa iliyokuwa ukutani
“ Kompyuta yangu ina mfumo wa kuweza kutambua aina mbali mbali za mawimbi yaliyoko katika eneo nilipo.Mfumo unanionyesha kwamba kuna mawimbi Fulani yasiyo ya kawaida yanatoka ndani ya nyumba hii ambao si mawimbi ya simu.Ulimchunguza vizuri Rose kama hana kifaa chochote cha kielektroniki ambacho kinaweza kuelekeza kufahamu mahala alipo? Akauliza Anitha
“ Nilimsachi vizuri na sikukumkuta na kitu chochote zaidi ya simu yake” akasema Mathew
“ wait ! “ akasema Peniela
“ ninavyohamu mimi marais na wake zao huwekewa vifaa fulani vidogo ndani ya miili yao kwa ajili ya kuwafuatilia kila mahala waliko.Huyu aliwahi kuwa make wa rais yawezekana bado kifaa hicho kipo mwilini mwake” akasema Peniela .Mathew akamtazama na kusema
“ Peniela can be right” akasema na kulifungua kabati akatoa kifaa Fulani na kwa kasi akeelekea katika chumba alimo Rosemary Mkozumi na kuanza kukipitisha kifaa kile katika sehemu mbalimbali za mwili wa Rose na mara alipofika katika mkono wa kushoto kidude kile kikatoa mlio wa kengele na kuwasha taa ya kijani
“ Got it! Akasema Mathew
“ Ndiyo maana Rose alikuwa anajiamini sana kamba muda wowote watu wake wanaweza wakafika kumuokoa kumbe alifahamu kwamba ana kifaa kinachowaelekeza watu wake mahala alipo.Ahsante sana Anitha kwa kuligundua hili.Tulikuwa katik ahatari kubwa” Akawaza Mathew akachukua kisu kidogo na kuushika mkono wa Rose ambaye alikuwa ametumbua macho asiamini kilichokuwa kinatokea
“ Unataka kufanya nini? Akauliza Rose kwa mshangao.Mathew bila kumsemesha kitu akapasua sehemu ya mkono akaingiza mkasi mdogo na kutoa kidude Fulani kidogo .Rosemary akabaki anashangaa huku akigugumia kwa maumivu makali.Haraka haraka Mathew akalitibu lile jaraha akalifunga na kutoka mle chumbani.
“ Ahsante sana Anitha kwa kuligundua hili. kifaa hiki katika mwili wa Rose watu wake kumfuatilia kila mahala aliko.Tunachotakiwa kukifanya hivi sasa ni kwenda kukitupa mbali kifaa hiki.Ngoja niende nitarejea ndani ya muda mfupi” akasema Mathew na kuingia katika nyumba ya gari akachukua piki piki yake kubwa na kutoka mbio
“ Rose hakusita kunieleza kuhusu mambo yake ya siri kwa kujua kwamba muda si mrefu watru wake wangeweza kutuvamia na kumuokoa. Namshukuru sana Anitha kwa kuligundua hili” akawaza Mathew
“ Hata hivyo maelezo aliyonipa yamenipa mwanga kidogo kuhusu suala hili ingawa bado ninahitaji kufahamu zaidi.Kupenda kwake pesa kumemtokea puani na amejikuta akitua katika mikono yangu.” akawaza Mathew na mara akajikuta ametokea katika kijikanisa kimoja kidogo kikuu kuu ambacho hakikuonekana kama kinatumika kwa ibada.Akashuka katika piki piki yake na kuchungulia ndani ya lile kanisa hakukuwa na mtu yeyote nyuma ya kanisa lile kulikuwa na kijito cha maji ,akakitupia kile kifaa ndani ya kanisa halafu akarejea mahala alikopaki piki piki yake Akapanda na kabla hajaondoka gari mbili zikawasili kwa kasi eneo lile wakashuka watu watano na mmoja wao akiwa na kifaa Fulani kilichoonekana kumpa malekezo.Mathew akawatambua watu wale walikuwa ni kutoka usalama wa taifa kutokana na magari yao
“ Ouh thank you Lord. Kama tungechelewa kidogo wangeweza kutuvamia pale nyumbani kwani kifaa kile kilikuwa kinawaelekeza mahala Rose alipo” akawaza Mathew akiwa juu ya piki piki yake.Wale jamaa wakaelekea hadi katika mlango wa kanisa na kwa kasi ya aina yake wakavunja kufuli wakaingia ndani na wote wakapigwa na butwaa. Kanisa lile lilikuwa tupu. Mathew akatabasamu na kuwasha piki piki yake akaondoka.
“ Anitha Thank you so much for saving us” akasema Mathew baada ya kurejea nyumbani.
“ Kama usingegundua mapema kuhusu kuwepo kwa kifaa kile chenye kurusha mawimbi na kumuwezesha Rosemary kuonekana kila mahala alipo tungevamiwa na sijui nin kingetokea hapa leo.” Akasema Matheq
“ Nilipofika tu katika kile kijikanisa kikuukuu karibu na njia panda ya kwenda kiwanda cha sabuni nikakitupa kile kifaa ndaniya lile kanisa na haikuchukua muda zikatokea gari mbili ambazo zote ni za usalama wa taifa wakashuka watu watano ambao na walikuwa na kifaa Fulani mithili ya kompyuta ndogo ambacho kiliwapa maelekezo ya mahala kifaa kile tulichokitoa mkononimwa Rosemary kilipo.Walivamia kanisani na kumkosa Rose wote wakapigwa na butwaa wasijue wafanye nini.Niliwaacha hapo wakishangaa nikaondoka zangu.kwa hiyo ahsante sana Anitha.Good job” akasema Mathew na kumpongeza Anitha
“ Ahsante sana Mathew.” Akasema Anitha
“ Ulipomuhoji Rosemary ulifanikiwa kupata chochote kutoka kwake? Akauliza jaji Elibariki
“ Rosemary alifahamu fika kwamba watu wake walikuwa wanamfuatili ili kufahamu mahala alipo kwa hiyo nina hakika alichonieleza hakikuwa cha kweli hata kidogo.Alitaka kuvuta muda ili kuwapa nafasi watu wake waweze kufika na kumchukua.Guys huyu mama ana mtandao mkubwa sana.Sasa ninayaamini maneno aliyonieleza Eva kuhusu huyu mama.Hata hivyo nitakwenda tena kumuhoji kwa mara ya pili .This time she will tell the truth” akasema Mathew
“ Mathew please don’t hurt her anymore.Amekwisha umia sana” akasema jaji Elibarki
“ kama atanieleza ukweli sintamfanya chochote .Yule mama ana roho ya ujasiri sana na bila kutumia nguvuna ukatili kidogo hawezei kutueleza chochote.Naombeni dakika kumi nikamuhoji tena na safari hii tutafahamu kila kitu..” akasema Mathew na kuelekea tena katika chumba alimo Rosemary mkozumi.Akamtazama kwa hasira na kusema
“ Now its just you and me..Watu wako uliowategemea waje wakuokoe hawatakuona tena.Mipango yako imeshindikana.Ninachokihitaji toka kwako sasa hivi ni ukweli.Awali uliniambaimambomengi lakini yote yalikuwa ni uongo mtupu.Nitalianza zoezi langu upya hadi pale utakaponieleza kile ambacho ninakihitaji.Kabla sijafanya hivyo tafadhali naomba unieleze kwa undani kuhusu habib Soud na kuhusiana na karatasizile zilizoibwa ikulu” Akasema Mathew .Rosemary hakumjibu kitu .Mathew akakiwasha kile kifaa cha kukatia.
“ Please don’t hurt me.Umekwiha niumiza sana npaka sasa.” Akaomba Rose
“ I’ll continue hurting you hadi pale utakaponieleza kile ninachokitaka.Nilikukata vidole viwili sasa ninaendela na vilivyobaki.Nitakukata kimoja kimoja hadi utakapokuwa tayari kunieleza ukweli” akasema Mathew na kuanza kuifungua bandeji aliyoifunga katika mguu wa Rose wenye majeraha ya kukatwa vidole
“ Ok Ok tusifike huko tafadhali. Let me tell you one thing.You need me” akasema Rose
“ Ninachokihitaji toka kwako ni majibu ya maswali yangu tu na si vinginevyo..”akasema Mathew
“ You need me because I know so many thing than anyone and I’ll tell you everything I know “
“ Ok tellme” akasema Mathew
“ We must have a deal first”
“ a deal? Siwezi kuwa na makubaliano yoyote na wewe Rose” akasema Mathew
“ kama hutaki makubaliano na mimi then you wont know anything.” Akasema Rosemary.Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Ok tellme everything na kama utakachoniambia kitaniridhisha basi nitaona kama nitakubaliana nawe” akasema Mathew.Rosemary akanyamaza kidogo na kusema
“ It’s true I lied to you about Habib…Ninamfahamu vizuri habib.Ninafahamu kwamba anahusika na mambo ya kigaidi .”akasema Rose na Mathew akamuangalia kwa macho makali
“ Ninafahamu Habib anawindwa sana na mataifa ya kigeni na hasa marekani.C.I.A wanamuwinda usiku na mchana lakini mpaka sasa hawajawahi kugundua chochote kuhusu Habib.Ninafahamu mipango yake ya sasa na baadae ,ninaufahamu mtandao wake,ninafahamu mambo mengi sana ya habib kuliko mtu mwingine.I’m an asset you can’t afford to lose. Accept the deal” akasema Rose
“So you are working with terrorist!! You Devil !! Akasema Mathew kwa hasira
“ If you want to know everything please accept the deal otherwise I’m not going to tell you anything” akasema Rose
“ Rose you know I don’t work like that..above all siwezi kufanya makubaliano na mtu anayeshirikiana na magaidi.How could you do that Rose?
“ are you accepting my deal or not? Akauliza Rose
“ Rose mimi sifanyi kazi kwa shinikizo.Kama hutaki kunieleza kwa hiari yako utanieleza kwa lazima” akasema Mathew na kuiwasha ile mashine yake ya kukatia
“ Nitaendelea kukukata kidole kimoja kimoja na utanieleza kila kitu” “ Go ahead.kill me.Do you think I’m afraid of death? I’m not afraid of death so go ahead and kill me but if you kill me you’ll never know anything that you need to know.” akasema Rose.Mathew akamuangalia kwa makini akataka kusema kitu na mara mlango ukagongwa,Mathew akaufungua ,alikuwa ni Anitha
“ Mathew there is something you need to know ”akasema Anitha kisha wakaongozana na Mathew hadi ofisini.
“ Kuna nini Anitha? Akauliza Mathew
“ Kuna mambo nimeyapata.Amos na Deus mkozumi walikuwa na mawasilaino”
“ What?!! Wanafahmaiana?! Mathew akashangaa
“Ndiyo walikuwa wanafahimiana.Kumbukumbu zinaonyesha kwamba leo asubuhi ,Amos alimpigia simu Deus Mkozumi mara tatu bila Deus kupokea hivyo akamtumia ujumbe mfupi uliosomeka hivi
“ mzee shikamoo.Nimekupiga simu lakini haipokelewi.Naomba unipigie ukipata ujumbe huu ni muhimu sana”
“ haikuishia hapo” Anitha akendelea
“ Baadae Deus akamtumia Amos ujumbe uliosomeka hivi
” Anitha akamuonyesha Mathew ujumbe ambao Deus alimtumia Captain Amos ambao ulisomeka hivi
“ Amos nimeshindwa kukupigia niko katika kikao kizito cha viongozi wa Chama .naomba tuonane saa moja jioni Rozina Hotel kuna mambo ya muhimu sana ya kuongea kuhus ule mpango wetu”
“ Amos was a bastard !! akasema peniela kwa hasira “ Sikutegemea kama yuko namna hii.Nimsaliti mkubwa sana Yule “
“ Nimeshangaa sana kusikia kwamba Amos na Deus ni washirika.kwa sasa nimepata picha Fulani.Kabla hajauawa Amos alisema alimwambia Peniela kwamba wana mipango mikubwa kuhusiana na Elibariki na peniela na ilionyesha wazi kuna kikundi cha watu aliokuwa anashirikiana nao katika kupanga mipango hiyo lakinihakuweza kuwataja,sasa ninaamini Deus ni mmoja wa watu waliokuwa wakishirikiana na Amos.Kumbukeni pia katika maelezo yake dr Joshua alimtaarifu Kigomba kwamba mmoja wa watu hatari sana katika mpango wao ni Deus ambaye aliwahi hta kumpigia simu na kumtahadharisha kuhusiana na mpango wake wa kuiuza hiyo package.Ni wazi dues alikuwa anamtumia Amos katika kupata taarifa kutoka ikulu na kufanikisha mambo mbalimbali.” aKasema Mathew
“ Deus ni rais mstaafu kwa maana hiyo nashawishika kuamini kwamba anafahamu kilichomo ndani ya package hiyo ndiyo maana amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba package hiyo haiuzwi.Mzee huyu anaonekana kufahamu mambo mengi sana.Dont you think its time to find him? Akauliza peniela
“ Hata mimi nilikuwa na wazo kama lako Peniela.We need to find Deus.Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kufahamu kutoka kwake.Tatizo ni namna ya kumpata.Tutalijadili baadae jambo hili tuone namna tutkavyoweza kumpata”akasema Mathew
“ Kuna jambo lingine vile vile nimeligundua kwa Rosemary..” akasema Anitha
“ Nimechunguza pia mawasiliano yake ,nimegundua amekuwa na mawasiliano ya karibu sana na mtu aitwaye Hasheem Abdullah.Taarifa zinaonyesha kwamba Rose amekuwa akituma kiasi kikubwa cha pesa kwa huyu mtu mara kwa mara .Hasheem ana akaunti katika benki mbali mbali za hapa nchini na nje ya nchi.Baada ya kuligundua hio nimetafuta taarifa za hasheem ni nani nikagundua kwamba huyu ni mmoja wa watu walio katika orodha ya watu wanaotafutwa kwa kuratibu matukiombalimbali ya kigaidi katika eneo la afrika mashariki na kati..” “ Oh my God!! Akasema Mathew kwa mshangao
“ Huyu hasheem ni raia wa nchi gani? Akauliza Mathew
“ taarifa hazijaonyesha uraia wake” akajibu Anitha
“ Nilihisi toka awali kwamba Rosemary Mkozumi lazima anajihusisha katika mambo ya kigaidi.Kama amekuwa na ushirika na magaidi basi lazima hata yeye mwenyewe atakuwa anajihusisha kwa namna moja au nyingine na mambo hayo.dah ! Nivigumu sana kuamini kama mke wa rais anaweza kujihusisha na mambo kama haya.Hii ni aibu kubwa kwa taifa.”akasema Mathew
“ Tayari suala hili limebadilika tena na sasa limeingia katika ugaidi.Lini mambo haya yatafika mwisho na tuvute pumzi? akauliza jaji Elibariki akionekana kukata tamaa
“ usihofu Elibariki,wanasema giza linapokuwa nene ujue kunakaribia kupambazuka.Na hata sisi tunapoanza kukabiliana magumu mengi tujue tunakaribia kufika mwishoni..Tusikate tamaa.Tuendelee kupmbana.Kuna mambo kadhaa ambayo tunatakiwa kuyafanya lakini kabla hatujafanya chochote,tunatakiwa kumuhoji Rosemary atueleze huyu Hasheem ni nani na tuufahamu mtandao wote anaoshirikiana nao.Anitha na Elibariki endeleeni kuchunguza zaidi kompyuta ya Rosemary na Captain Amos.Nadhanibado kuna mambo mengi tutayafahamu . Peniela twende ndani tukaendelee kumuhoji Rose.”akasema Mathew wakarejea tena katika chumba alimo Rose.Mara tu Rose alipomuona peniela akastuka.
“ You ?! akasema Rose kwa mshangao
“ Hello Rose.Do you know me? Akauliza Peniela
“ Yes I know you.You are Peniela.Kumbe na wewe uko na huyu kijana? Who are you guys? Akauliza Rosemary
“ Usijali utatufahamu tu sisi ni akina nani” akasema Peniela
“ Gosh ! sikutegemea kabisa kama siku moja nitaonana nawe ana kwa ana.”akasema Rose
“ Rose nimekuja hapa kwa jambo moja tuna ninataka kufahamu Hasheem Abdullah ni nani? Akauliza Mathew huku sura yake ikionyesha kwamba hakuhitaji masihara.
“ Hasheem Abdullah? Rosemary akaonyesha mstuko mkubwa
“ Ni nani Hasheem Abdullah? Umekuwa ukimtumia pesa nyingi mara kwa mara” Rosemary akanyamaza kimya “ Rose nakuuliza kwa mara ya mwisho hasheem Abdullah ni nani? “ hakuna chochote ambacho ninaweza nikakueleza kijana .Fanya unachokitaka na hata kama ni kuniua fanya hivyo haraka lakini sintakueleza chochote kama sintapata kile ninachokihitaji” akasema Rose.
“ Rose nadhani bado hujanielewa.Hakuna chochote nitakachojadiliana nawe .Utanieleza kila kitu ninachokihitaji” akasema Mathew na kuichukua mashine yake ya kukatia akaiwasha. “ tayari umenikata vidole viwili umekwiwha nitia ulemavu .Endelea kukata na vingine vilivyobaki ukimaliza njoo katika shingo yangu uniue kabisa lakini katu sintakueleza kitu chochote kama sintapata kile ninachokitaka “akasema Rose.Mathew akaushika mguu wa Rose ule alioukata vidole viwili.Peniela akaona namna vidole vya Rosemary vilivyokatwa akastuka.
“ Mathew ,Rosemary anataka nini? Akauliza Peniela
“ hajanieleza bado anahitaji kitu gani lakini siko tayari kufanya makubalino yoyote naye.She will talk” akasema Mathew kwa hasira huku akijiandaa kuendelea kukata vidole vya mguu.
“ Mathew wait!!..akasema Peniela na kumuomba Mathew watoke nje ya kile chumba wakaongee . “ Mathew hata ukimtesa vipi huyu mama hataweza kusema chochote.Muulize anataka nini na kama analolitaka liko ndani ya uwezo wako accept the deal.” Akasema Peniela
“ Peniela we cant accept any deal ..”
“ Listen to me Mathew,msikie kwanza anataka nini.Rose ana taarifa muhimu sana ambazo hatuwezi kukubali kuzikosa.Huyu ni msaada mkubwa kwetu “ akasema Peniela.Mathew akainama akafikiri kidogo na kusema
“ Ok ngoja tumsikie anataka kitu gani” akasema Mathew na kuingia tena ndani
“ Ok tell me what do you want? Akauliza Mathew
“ are you ready to accept the deal? Akauliza Rose
“ Ninataka kwanza kusikia ni kitu gani unachokihitaji” akasema MathewRose akamgeukia Peniela na kumfanyia ishara atoke nje
“ No she stays” akasema Mathew
“ Fine “ akajibu Rosemary
“ Nitawapa taarifa zote mnazozitaka kuhusiana na Habib na mtandao wake wote lakini kuna mambo ambayo ninahitaji kufanyiwa.” akasema Rose na kunyamaza kidogo kisha akasema
“ Ninataka kinga ya kutokukamatwa kwa kosa lolote lile iliyosainiwa na rais wa Tanzania na vile vile ninataka nipelekwe katika nchi ambayo nitaichagua mwenyewe. …”
“What?!!!!.....Mathew akauliza kwa mshangao
“ Nimesema kwamba ninataka kinga ya kutokukamatwa kwa kosa lolote lile iliyosainiwa na rais wa Tanzania na vile vile ninataka nipelekwe katika nchi ambayo nitaichagua mwenyewe pamoja na ulinzi kama ukilifanikisha hilo nitakueleza kila kitu..” Mathew akamsogelea na kumtazama
“ You are crazy…Siwezi kukubali jambo kama hilo litokee.I cant accept the deal.” Akasema Mathew
“ Hayo ndiyo masharti yangu .Kama hutaki kuyakubali basi sintafumbua mdomo wangu tena.I’m ready to die” akasema Rosemaryhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ You are going to tell me everything I want ” akasema Mathew na kuelekea katika meza iliyokuwa na vifaa vya kutesea
“ Mathew can we talk outside?akasema Peniela.Wakatoka ndani ya kile chumba
“ Mathew accept the deal” akasema Peniela
“ Peniela !! akasema Mathew
“ Please Mathew Accept the deal…mpaka hapa hakuna namna unayoweza kafanya ili aweze kukueleza kile unachokitaka.Chaguo ni moja tu Mathew ,tukitaka atueleze kile tunachokitaka lazima tukubaliane na matakwa yake.Rose ni mjanja sana anafahamu kwamba taarifa alizonazo ndizo kinga yake ya mwisho kwa hiyo anaicheza vizuri karata yake ya mwisho .Anafahamukabisa kwamba hawa watu anaoshirikiana nao wakigundua kwambaametoa siri zao watamuua ndiyo maana anataka aende mahala kusikojulikana akajifiche.”akasema peniela
“ Peniela hapana hatuwezi kufanya hivyo…We cant let her go just like that” akasema Mathew
“ Mathew tafadhali nisikilize.Rose anashirikiana na magaidi na anazifahamu siri zao nyingi kwa hiyo tukikubaliana na matakwa yake na akatueleza kile tunachokitafuta atakuwa ameokoa maisha ya watu wengi.Kumbuka nyaraka zile ziliibwa toka ikulu ambazo ni nyaraka hatari sana,ni vipi iwapo watakuwa tayari walizipata karatasi zile na wamekwisha zitumia kutengeneza kirusi hicho? Mathew accept that deal ili tuweze kufahamu mengi kutoka kwa Rose.” Akasema Peniela.Mathew akainama akafikiri na kusema
“ hata kama tukikubali matakwa yake how are we going to do it? Anataka hati ya inga iliyosainiwa na rais,tutafanyaje kuweza kuipata hati hiyo?
“ Hilo ni suala dogo kwangu.Kama ukikubali niachie mimi kila kitu nitakifanya.” akasema peniela
“ How are you going to do it? Rais yuko nje ya nchi hivi sasa na wakati huo huo ana msiba wa mwanae na sisi tunahitaj taarifa toka kwa Rose haraka iwezekanavyo na kingine hatakiwi kabisa kufahamu kuhus kinachoendelea ..I’m confused !! akasema mathew
“ Leave everything to me Mathew.Ninajua nitakavyofanya na rais atasaini hati hiyo” akasema peniela
“ sawa peniela nimekubali kwa sababu yako lakini roho inaniuma sana kumuacha mtu huyu anayeshirikiana na magaidi aondoke….”akasema Mathew na kisha wakarejea chumbani kwa Rose “ Ok Rose.I accept the deal” akasema Mathew
“ Good..”akajibu Rose
“ Suala lako litashughulikiwa na litakapokuwa tayari hati hiyo unayoitaka italetwa hapa.Lakini wakati tunasubiri hilo lifanyike,nataka unipe maelezo ya kuhusiana na huyu mtu Hasheem Abdulah ni nani ? akauliza Mathew
“ Save your breath ..Siwezi kukwambia kitu chochote bila ya kuona kile ninachokihitaji.And please find me a doctor immediately umeniumiza sana.!! Akasema kwa ukali Vicky.Peniela akamtazama Mathew na kusema “ Mathew she can’t tell us anything.” Mathew akamtazama Rose kwa hasira na kusema
“ I’ll be right back.” “ Tafadhali naomba mnifungue hizi pingu mlizonifunga “ akafoka Rose huku akilia Mathew na Anitha wakatoka mle chumbani na kumuacha Rose akilia kwa maumivu wakarejea ofisini walikokuwapo Anitha na jaji Elibariki
“ Amesema chochote? Akauliza jaji Elibariki
“ hapana hajasema chochote but we made a deal with her ”
“ a deal ? akauliza Elibariki kwa mshangao
“ Yes .Tumefanya makubaliano naye ili atueleze mamboya muhimu anayoyafahamu kuhusiana na habib na mtandao wake wa kgaidi.Hakuna namna tunayoweza kumfanya akatupa taarifa hizo zaidi ya kukubaliana na anachokitaka.”akasema Mathew
“ Anataka nni? Akauliza Elibariki ambaye hakuonekana kufurahishwa na kitendo kile cha Mathew kufanya makubaliano na Rose.
“ Anataka hati ya kinga ya kutokushtakiwa kwa kosa lolote iliyosaiwa na rais, na vile vile anataka apelekwe katika nchi anayoitaka pamoja na ulinzi.”
“ That’s impossible.We can’t do that” akasema jaji Elibariki
“ Elibariki hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kumtimizia matakwa yake ili aweze kutupa taarifa za muhimu sana.” Akasema Peniela
“ hata kama ana taarifa za muhimu lakini huyu mama anashirikiana na magaidi na anazifahamu siri zao nyingi ,we cant just let her go like that..Anatakiwa ateswe na atasema ukweli”
“ Elibariki,jambo tulilolifanya halikuwa rahisi hata kwangu mimi .Rose anashirikiana na magaidi na tayari amekwisha pata ujasiri wa kigaidi wa kutokusema chochote hata akiteswa vipi.Siku zote magaidi wako tayari kufa kuliko kusema chochote.Hata tukitumia njia gani Rose hataweza kusema chochote.Njia pekee ya kupata taarifa toka kwa Rose ni kumtimizia kile anachokitaka.”
“ how are we going to do that? Tutaipataje hiyo hati iliyosainiwa ana rais? Akauliza jaji Elibariki
“ I’ll do that “ akajibu Peniela.Jaji Elibariki akamgeukia na kumkodolea macho “ Peniela hili si suala dogo kama unavyolichukulia..Hili ni suala kubwa na hawezi kulifanya yeye mwenyewe ,atashirikishwa pia mwanasheria mkuu naye alifahamu suala hili na aweke sahihi yake.Endapo jambo hili likifika huko kote halitakuwa siri tena.Kila kitu kitakuwa wazi na chochote tunachokifanya.” Akasema jaji Elibariki
“ Kwa hiyo jaji Elibariki wewe ndiye mjuzi wa sheria hapa unatushauri tufanye nini? Akauliza Mathew.
“ Mimi kwa ushauri wangu ni kwamba suala hili la Rosemary tuliweke kwanza pembeni kisha tuendelee na suala letu la awali. La kuitafuta package toka kwa Dr Joshua.Tukifanikiwa kuipata package na kupata ushahidi unaojitosheleza wa kutuwezesha kumuangusha Dr Joshua tutapata nafasi ya kuonana na mtu atakayeshika nafasi ya urais na atatusadia katika kulifanikisha suala hilo.lakini kwa sasa ninashauri kwanba tusichanganye mambo mengi kwa wakati mmoja tutajikuta tumekwama.” Akasema jaji Elibariki
“ Elibariki anaweza kuwa sahihi..Tuliweke pembeni suala hili la Rosemary.Tuendelee kumshikilia Rosemary na kuhakikisha anakuwa chini ya ulinzi mkali hadi hapo tutakapolifanikisha kwanza suala la kuipata package.”
“ Rosemary kwa sasa lzima atakuwa anasakwa kial kona na vyombo vya usalama. kuendelea kumuweka hapa kwa muda mrefu inawezakuwa ni hatari kubwa kwa usalama wetu.Wewe mwenyewe umetuhakikishia kwamba watu uliokutana nao waliokuwa wakifuatilia taarifa za kile kifaa tulichokigundua mwilini mwa Rose ni watu wa usalama wa taifa basi ni wasi kuna juhudi kubwa sana zinafanyika kuweza kumpata Rose..Tukisema tusubiri mpaka hapo tutakapokamilisha kwanza suala la kuipata package toka kwa Dr Joshua tunaweza tukajikuta tumempoteza na tukashindwa kupata taarifa za muhimu toka kwake.Guys let us finish this once and for all..” akashauri Peniela
“ Nakubaliana nawe Peniela kwamba watu wa Rosemary kwa sasa hawalali wakimtafuta na leo hii nusura wangeweza kumfikia kama tusingefanikiwa kugundua kifaa kile cha kuonyesha kila mahala alipo .Hata hivyo nadhani tukubaliane na jaji Elibariki kwamba tuliweke pebeni kwanza suala la Rosemary na tuendelee na mipango yetu ya awwali ya kuipata package toka kwa Dr Joshua.Kuhusu usalama wa Rosemary naoba niwatoe wasiwasi kwamba hapa kwangu kuna sehemu salama kabisa ambayo hakuna mtu anayeifahamu na tutamuweka huko na atakuwa salama hadi hapo tutakapokuwa tayari kulishughulikia suala lake”akasema Mathew
“ Damn you Mathew umejiandaa sana katika jumba lako hili.Umekamilika kwa kila kiru” Akasema Peniela
“ Ninafahamu ugumu wa kazi zangu na ndiyo maan nikajitahidi kujikamilisha kwa kila kitu.Tukiachana na hayo kuna kitu kingine ambacho tunatakiwa tukijadili..Rosemary alikuwa anashirikiana na Captain Amos na walikuwa katika mpango wa kuipata package kutoka kwa Dr Joshua.kwa sasa Captain Amos amefariki na Rosemary tunaye hapa kwa maana hiyo mipango yao yote kuhusiana na Package imevurugika.Tumegundua pia kwamba Captain Amos alikuwa ana mawasiliano na Deus Mkozumi rais wa zamani wa Tanzania na ambaye alikuwa ni mume wa Rose.Katika maelezo yake kabla hajapigwa risasi alimueleza Peniela kwamba wana mpango mkubwa unaomuhusu Peniela na jaji Elibariki kwa maana hiyo basi ninashawishika kuamini kwamba Deus Mkozumi atakuwa akifahamu mpango huu aliousema Amos.Inaonekana wazi kwamba huku nako kuna mtandao mwingine .Mkumbuke pia kwamba Dr Joshua alimtaja Deus kama mmoja wa watu ambao ni maadui wakubwa katika kufanikisha uuzwaji wa hiyo package kwa maana hiyo Dues atakuwa akilifahamu vyema sana suala hili.Nadhani ni wakati muafaka sasa wa kumtafuta mzee huyu na kufahamu mambo mengi kutoka kwake” akasema Mathew
“ Deus Mkozumi ni rais mstaafu,ana ulimzi mkali kila aendapo na nyumbani kwake pia,kumpata mtu kama huyu haliwezi kuwa jambo rahisi hata kidogo.Huyu naye ana mtandao mkubwa wa watu wenye nguvu na hatari na wana mipango mikubwa juu yetu kwa hiyo si watu wa kuwafuata kirahisi rahisi.” Akasema jaji Elibariki
“ Ni kweli kumpata Deus Mkozumi si rahisi lakini jambo hili haliwezi kutushinda.Tunaweza kumpata”akasema Mathew
“ Tutampataje Deus?akauliza jaji Elibarii.Mathew akamgeukia Peniela
“ No ! Mathew we cant use her ..”akasema Elibariki “ Hatuna namna nyingine ya kufanya Elibariki ili kumpata Deus zaidi ya kumtumia Peniela.” Akasema Mathew
“ Mathew ,we cant put her at risk again.Peniela amenusurika leo hii katika shambulio,I’ve lost my wife today,and I cant lose Peniela again” akasema jaji Elibariki.Mathew akamtazama na kusema
“ Eli Can we talk outside?Wakatoka nje ya kile chumba
“ Elibariki tuko kati kati ya vita.Tunatakiwa tutumie kila aina ya mbinu na silaha tulizonazo katika kupambana.Wewe na Peniela kuna mipango inapangwa juu yenu na kikundi cha watu ambao wanawafuatilia.Maisha yenu yako hatarini kwani hatufahamu watu hao wana mipango gani juu yenu.Kwa hali halisi ilivyo ni wazi kwamba hatuwezi kumfikia Deus Mkozumi isipokuwa kwa kumtumia Peniela Pekee.She can penetrate any where.She’s good at this.She was trained for this .Kwa hiyo usiwe na wasiwasi hata kidogo kuhusu usalama wake..Kitu kingine nafahamu unampenda sana Peniela lakini tunapokuwa katika kazi kama hizi ,masuala ya mapenzi tunayaweka pembeni na hutakiwi kabisa kuonyesha hisia zako hata kama unampenda mtu yeyote .Peniela mwenyewe yuko tayari kuifanya kazi yoyote ile na haogopi lakini kitendo ulichokifanya cha kuingilia kati na kumzuia kwamba asishirikishwe katika kumtafuta Deus kimemshangaza hata yeye pia.Wanawake wale mle ndani wanatutegemea sisi kuwaongoza katika kulimaliza suala hili lakini kama tutashindwa kuonyesha namna bora ya kufanya maamuzi tutawavunja moyo kwani tayari wamekwisha jitoa maisha yao katika kuhakikisha tunalifanikisha jambo hili.” Akasema Mathew
“ Mathew I’m sorry kama nilikukwaza kwa kauli ile lakini nilijikuta nikishindwa kujizuia .Ninampenda sana Peniela na tukio lililotokea mchana alipokwenda kuonana na Amos lilinistua na kuniogopesha sana .Please forgive me and lets do what needs to be done” akasema jaji Elibariki
“ Are we good? Akauliza Mathew
“ We’re good”akajibu jaji Elibariki kisha wakarejea tena ndani ya ofisi
“ Are you guys ok? Akauliza Peniela
“ we’re fine.”akajibu jaji Elibariki
“ kwa hiyo nini kinachoendela saa hivi? Akauliza Peniela
“ Kitu kinachotakiwa kufanyka kwa sasa ni kumtafuta Deus Mkozumi.Yeye anafahamu mambo mengi sana na kama tukimpata basi atatusaidia kupiga hatua kubwa.Peniela utaifanya hii kazi.You will go meet Deus Mkozumi” akasema Mathew
“ Ni jinsi gani ataonana na Deus? Akauliza jaji Elibariki
“ Usihofu Elibariki,they call me an insect because I can penetrate anywhere. Kwa kuwa namba za simu za Deus tunazo hapa,I’ll call him and set a meeting.Kuhusu nitakwenda kuongea naye nini hilo ni nyie mtapanga.”akasema Peniela
“ say something Anitha “akasema Mathew
“ Peniela atakapokwenda kuonana na Deus tutamuwekea kifaa cha mawasiliano sikioni .Atavaa gauni la rangi nyeusi na sehemu ya kifuani katika titi la kulia tutaweka ua jeusi na ndani ya ua hilo kutakuwa na kamera ndogo ambayo itatuwezesha sisi kutazama kila kitu kinachoendelea kati yako na Deus.Tutayafuatilia maongezi yenu na tutakuwa tunakueleza nini cha kufanya.Endapo tutaona kama kuna tatizo lolote la kiusalama tutakutaarifu “ akasema Anitha
“ Hata hivyo hatutakuwa mbali na mahala utakapokuwa kwa ajiki ya msaada wa dharura pindi ukihitajika” akasema Mathew
“ Ok guys.muda umekwenda sana Nipeni namba za Deus nimpigie.”akasemaPeniela.Anitha akaziandika namba za simu za Deus katika simu yake halafu akapiga kisha akampatia Peniela akaiweka simu sikioni
“ hallow”ikasema sauti nzito ya kiume upande wa pili “hallow” akasema peniela
“naongea na nani? “ Unaongea na Peniela hapa.Naongea na nani?akauliza Peniela
“Kwani wewe umempigia nani? Akauliza tena Yule jamaa upande wa pili
“ Ninahitaji kuongea na Mr Deus Mkozumi tafadhali.” Kimya kifupi kikapita halafu yule jamaa akauliza
“ Umeipata wapi hii namba? Nani kakupatia namba hii?
“ It doesn’t matter nimeipata wapi ila kama Deus yupo ninaomba niongee naye“ akasemaPeniela.Kikapita kima kifupi tena Yule jamaa akauliza
“ Umesema unaitwa nani vile?
“Peniela.mwambie Peniela anahitaji kuongea naye” Baada ya dakika mbili Peniela akasikia sauti nyingine ambayo haikuwa nzito sana kama ile ya mwanzo
“ Hallow” ikasema sauti ile
“Hallow”akasemaPeniela
“ Are you Peniela?
“ Yes I am Peniela.Are you Deus Mkozumi? Akauliza Peniela
“ Yes Iam Deus..Umeipata wapi namba hii? Akauliza Deus
“ Mzee Deus nina shida na wewe ndiyo maana nikaitafuta namba hii hadi nikaipata.”
“ Una shida na mimi ! Shida gani hiyo?akauliza Deus “ Siwezi kukueleza simuni mzee.Nahitaji kuonana nawe tuongee”
“Peniela ,ingekuwa vizuri ungenieleza suala ambalo unataka tukune tuliongelee ili niweze kupima na kuona kama lina uzito gani.Unajua mimi ni mtu mwenye shughuli nyingi kwa hiyo kama ukitaka kuonana na mimi lazima nivunje baadhi ya mipango yangu kwa hiyo naomba unieleze ili nipate walau picha.”
“ Deus ninafahamu wewe ni mtu mwenye shughuli nyingi lakini hadi nimeamua kukupigia basi fahamu suala lenyewe ni kubwa hivyo naomba usilipuuzie tafadhali.Nahitaji sana kuonana nawe” Kikapita kimya kifupi kisha Deus akauliza
“ Unataka tuonane lini na wapi?
“ Tuonane leo hii jioni kuanzia saa mbili za usiku..Kuhusu mahala pa kukutana utaamua wewe mwenyewe tukutane wapi mahala ambako unaamini ni salama.”akasema Peniela.Baada ya sekunde kadhaa Deus akasema
“ Tukutane Iyumba country club saa mbili kamili. Katika geti la kuingilia jitambulishe kama mgeni wa namba ishirini na saba utapelekwa mahala nitakapokuwepo.Ila hakikisha kwamba jambo unalotaka kunieleza ni jambo kubwa .”
“ Ahsante sana mzee.Nitafika mida hiyo bila kukosa “akasema Peniela na kukata simu.
“ Good.You did great! Akasema Mathew
“ Deus hajaonyesha kustushwa kabisa na ulivyompigia simu na hii inadhihirisha wazi maneno ya Amos kwamba they know you already .Ok hatua muda mwingi sana hivyo maandalizi yaanze mara moja.Anitha anza kuandaa program zako halafu ukamchagulie Peniela gauni zuri la kuvaa usiku wa leo .”
“ Anitha ninaomba simu niwasiliane na josh kumpa taarifa kwamba sintakuwepo jioni ya leo.Nina hakika watakuwa wamenitafuta sana mpaka mida hii kwani hata simu yangu nimeizima kabisa ili wasiweze kujua mahala niliko” akasema Peniela akachukua simu na kumpigia Josh “hallow Josh.Its me Peniela” akasema peniela baada ya Josh kupokea simu “ peniela where are you? Kila kitu kimesimama hapa hawa watu wanakusubiri wewe.wanahaha wanakutafuta lakini hakuna anayejua uko wapi na simu yako umeizima kabisa.Tafadhali naomba uje hapa mara moja ili taratibu za msiba wa John ziweze kufanyika”akasema Josh
“Josh I cant come right now.I’m at the middle of something.” Akasema Peniela “kwa hiyo itakuwaje?akauliza Josh
“waambie nimekupigia simu na nimekutaarifu kwamba sintaweza kufika leo tuonane kesho”akasema peniela
‘ Ok peniela ngoja niwataarifu”akasema Josh na kukata simu
“kwema huko? Hakuna tatizo lolote?
“ hakuna tatizo ila kila kitu kimesimama wananisubiri mimi ili tuweze kupanga kuhusiana na suala la msiba wa John.” “ sawa utalishughulikia suala hilo kesho lakini kwa leo lazima tushughulikie kwanza suala la Deus.”akasema Mathew kisha akageuka kutaka kutoka mle ofisnini lakini Anitha akamuita.
“Kuna simu inapigwa katika namba ya Dr Kigomba.Inaonyesha ni simu kutoka afrika ya kusini.Yawezekana akawa ni Dr Joshua”akasema Anitha na wote wakatega sikio kusikia simu ile.
“ hallow Mr President”akasema Dr Kigomba
“ Kigomba nipe taarifa za huko.mambo yanakwendaje? Akauliza Dr Joshua “Huku kila kitu kinakwnda vizuri.Maandalizi yanaendelea.Vipi ninyi huko?
“ Huku hakuna habari mpya .Nimekupigia ili kufahamu umefikia wapi na maandalizi ya msiba”
“Kila kitu kimekwenda vizuri na tayari shughuli zinaendelea pale katika nyumba ya familia.Taarifa zimesambaa haraka sana na mpaka hivi sasa waombolezaji ni wengi mno.Kifo hiki cha Flaviana kimewagusa watu wengi sana na ndiyo maana wamejitokeza kwa wingi namna hii ndani ya muda mfupi.”akasema Dr Kigomba
“ kwa kweli kifo cha Flaviana kinaumiza sana na hata mimi kimeniumiza sana lakini yote hii ni katika kuhakikisha kwamba mpango wetu unafanikiwa.Anyway tuachane na hayo tutajadili kwa undani nikirejea.Tutawasili na mwili esho saa tano asubuhi.Watangazie.”akasema Dr Joshua.
“ Sawa Mr President.Tumekwisha fahamishwa hilo na mwenyekiti wa kamati ya mazishi na kila kitu kwa ajili ya kuupokea mwili kimeandaliwa...”
“ sawa Kigomba sina mengi ya kukwambia kwa sasa ila tutaongea mambo mengi nikishafika huko kesho.Ila nimeongea na Hussein atafika kesho saa mbili za usiku tayari kwa kuuchukua mzigo wake.Nataka tulimalize suala hili ili maisha mengine yaendelee.Nimechoshwa na kuwapoteza watu wangu kila kukicha kwa sababu ya biashara hii.Nitakupigia baadae Dr KIgomba”
“ Dr Joshua before you go,kuna jambo ambalo sina hakika kama umekwishapata taarifa zake”
“jambo gani?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment