Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

MSHANGAO - 5

Simulizi : Mshangao 

Sehemu Ya : Tano (5)

“Madam kuwa huru usiniogope mimi ni mtu mwema tu kwako kama nawe utakuwa mwema wangu hakuna jambo baya litakalokukuta… Chumba hiki kinaweza kuwa kama chumba cha hotel ya hali ya chini katika moja ya nchi za kiafrika huko iwapo tutakwenda sawa lakini pia kinaweza kuwa jehanamu kati jehanamu zilizo duniani kama itakuwa tofauti na nitakavyo, kaa kwenye kiti icho hapo au kakae kwenye godoro hapo chagua utakapo”. Agent Kai akamwambia baada ya wote kuingia katika chumba hiki na yeye kuurudisha mlango.

“Sasa nitaongeaje na wewe kwa amani? Ikiwa huwezi kunifungua mikono yangu na moyo wako kuridhika mimi kuondoka na maumivu ya waya hizi ulizonifunga kwa nguvu”. Akaongea LG na kwenda kukaa kwenye kiti cha plastiki kilichokuwa ndani ya chumba kile.

“Hahahah! Usinichekeshe madam… Ngoja nikuonyeshe kitu hili na wewe ukumbuke kitu”. Akamwambia kisha akavua fulana ya aina ya lacrose alilovaa maana sura ya bandia aliyovaa ilikuwa ni sura ambayo ni ya kuvaa mpaka tumboni hivyo akalivua plastic lile.

Wakati anatoa kwa usoni Agent Kai alistuka akipigwa teke la kurukiwa miguu yote miwili (double kick) wakati naye alijitahidi kujiweka pembeni baada kiti kutoa mlio wa mtu anainuka kwa kasi hivyo double kick haikufika yote bali mguu wa kushoto ndiyo ulikita mkono wake wa kushoto, kwake alikuwa teke la kumfanya apate maumivu hasa kwakuwa lilitua kwa juu ya mkono kwenye (byceps).

Akili sehemu kama hizi kwa Agent Kai ufanya kazi kama mamba anapoliwinda windo lake lililoingia ndani ya maji haraka aliivuta sura yote ya bandia akaitupa kwenye godoro na papo hapo akajisogeza kwa kasi kwa kurukia juu ya godoro akisogea mbali kihatua na alipotua LG ambaye naye alikuwa karusha round kick (teke mzungusho likitokea kwa nyuma) likakuta kidume kashahama yupo juu ya godoro, kwa pupa iliyojichamganya na uoga LG aligeuka kusimama sawa na kumkuta Agent Kai amesimama anamuangalia anataka kufanya nini.

“Ushawai kupigana madam ukiwa umefungwa mikono? Au ndiyo unataka kujifunzia kwangu?”. Akamuuliza huku damu yake ikiwa inachemka mpaka anaisikia maana mwili wake ulihakisi mapambano na kusisimka.

“Mbona umeacha kupambana? Mbona huongei kitu? Mimi siyo mbuzi asiyeng’ata, ushaikumbuka hii sura hivyo sina shida ya kujieleza mimi ni nani kwako… Rudi kakae kwenye kiti na utafanya kile nachotaka tu”. Akamuamrisha na kumuonyeshea kwa kidole, LG alikuwa mdogo kama punje ya mchele akajikokota hadi kwenye kiti ingawa tayari alishajua anatekwa na Agent Kai toka kule katikati ya jiji ila kufeli kwa jaribo lake kulimpa hofu kubwa sana.

“Okay! Madam, umeshanipima na kwa haraka nimejitambulisha kwako tayari kuwa mimi ni nani? Naomba uwe mstaarabu sihitahi kukudhuru nisaidie na mimi nitakusaidia kukuacha ukiwa na sura yako nzuri kama ilivyo”. Akaongea Kai kisha akatoa simu yake mfukoni na kufungua kamera.

“Inua sura yako vizuri nikupige picha kwanza”. Akampa amri LG akataka kukaidi na papo hapo akajishauri awe mtiifu ainue sura apigwe picha, Agent Kai akampiga picha nne za haraka haraka.

“Wewe si ulikuwa na picha yangu wakati uliponifuata Airport, nami nimependa kuwa na yako mrembo wa KL.... Tunaweza endelea na mengine sasa… Cha kwanza nataka kujua Detective Marie yuko wapi?”. Kazi imeanza.

LG alinyamza kimya akijifanya kama hajasikia anachoulizwa,macho yake yakibwenza bwenza kama mtu anayetaka kuanza kulia baada ya kukutwa na hali ambayo hana uwezo wa kuivumilia.

“Malkia wa lugha unaniektia hujasikia au ndiyo unanionyeshea kiburi?”

.

Bado mwanamke alinyamaza akajilazimisha kujikamua machozi yakaanza kumtoka.

“Pole sana …. Naitwa Agent Kai Hamis, jasusi wa CIA, natokea Washngton DC kitengo maalumu cha ujasusi kilichopo chini ofisi ya makamu wa Raisi…. Uwa siogopi machozi… Tafadhali naomba nijibu kistaarabu bila shuruti, machozi yako si dawa ya mimi kukuacha kawaida tu ukaondoka kwenye mikono yangu”.

“Kaka mi sielewi unasema nini?”. Akajibu LG machozi yakiendelea kumtoka.

“Inua sura yako mwanamke… Mi sijakuleta hapa kukuangalia ukitoa machozi yako ya kimaigizo… Huku nilipokuleta hakuna mtu anayeweza kupajua hapa ni kama nusu jehanamu ukitaka pawe jehanamu kamili panakuwa haraka tu…”. Akamuonya tena.

“Sijawai kukuona kaka… Kweli nachozungumza kaka ndicho cha kweli, sijawai kusikia jina ulilolitaja.. Umesema unaitwa Agent Kai Hamis ni jina geni kabisa kwangu”. Damia akaongea huku anatizama chini sura kaivuta kwa uchungu wa kuekti anaumia.

“Uwa sipendi kabisa kutesa wanawake, unataka kunilazimisha… Okay inuka kitini ukae sakafuni”. Akamuamrisha huku sasa uso wake ukionyesha unabadilika, LG alipomtizama haraka aliinuka kitini na kukaa sakafuni miguu yake akiivuta magoti usoni mwake.

Kai akatoa simu yake na kupiga namba fulani kati ya namba zilizo kwenye uwanja wake wa majina.

“Halloow!”. Akaongea baada ya upande wa pili kupokea.

“Halloow! Habari?”. Upande alioupigia ikasikika sauti ya kike.

“The Sole Cat! Hapa..”. Akajitambulisha Kai kwa jina la a.k.a yake anayoikubali baada ya kuitwa sana na wenzake na yeye kuamua kuikubali.

“Eeeh! Huko wapi wee mwanaume? Code namba siijui ya nchi gani hii”.

“Duh! Hadi wewe miss hujui niko wapi? Kweli CIA safari hii mmeamua…. Niko Malaysia, Cathy… Nina shida inayohitaji msaada wako”.

“Upo kikazi huko?”. Cathy Chris au kama wengine walivyopenda kumuita kwa kumkatizia wakimuita ‘DC’ wakimaanisha Double C, alikuwa ni mmoja wa wataalamu wa kompyuta walio katika ofisi kuu ya CIA iliyopo Langley, Virginia. Mara nyingi Agent Kai alipokuwa ana shida inayohusu siri za watu wengine wanaochunguzwa na CIA basi alimuuliza huyu.

“Hivi unajifyatua akili, unajisahaulisha kuhusu Malaysia kuna tatizo gani?”.

“Si kama najifyatua mpenzi… Si nilisikia walishatumwa watu huko na si wewe, wameshindwa au kukoje?”

“Kumetokea tofauti kidogo kwao hivyo nimekuja kusafisha kidogo uchafu… Nina haraka DC, nakutumia picha za mwanamke mmoja niko naye hapa nahitaji haraka uniangalizie katika orodha yenu kama yumo”.

“Okay! Mpenzi nitumie whatssap”. Akakubali Cathy baada ya kuhisi anayemuita mpenzi wake yuko serious.

Alivyokata simu akakutana na uso wa LG ukiwa unatia huruma sana kiasi ya kwamba angekuwa ana roho ile nyepesi nyepesi angegairi alichokuwa anatamani kumfanyia.

“Unaitwa nani?”. Akamuuliza.

“Zaynab Yussuph!”. Akajibu kwa mkato jina hilo la uongo.

“Ukiwa umenidanganya jina tu itakuwa adhabu yako kuu ya karne, maana usiku wa kuamkia jana niliambiwa unaitwa jina tofauti na hili unalonitajia na nina asilimia zote ni wewe… Picha yako ishaenda Langley, Virginia. CIA headquarter labda uwe local lakini hisia zangu zinaniambia nishawai kuiona picha yako mahali na ndiyo maana nimestuka na kuamua kutuma picha yako huko… Na hii itanipa muangaza nashughulika na watu gani… Nashukuru mimi uwa na kumbukumbu nzuri sana toka niko mdogo, sura yako nimeshakutana nayo mahali soon nitajua wapi”.

“Ukweli mimi naitwa Zaynab Yussuph na sijui kwanini umenichukua kunileta hapa”. Akaendelea kudanganya LG.

Kabla Agent Kai hajaongea kitu, simu yake ikaita alikuwa ni mtaalamu wake Cathy Chris ‘DC’.

“DC!”. Akaongea baada ya kupokea Agent Kai.

“Anaitwa Damia Abdulrahman a.k.a Language Girl kwa kifupi wanamuita LG wanapofupisha jina lake wakiwa wanawasiliana naye ni Mmalaysia dini yake muislamu, ameshawai kuwa katika kikundi cha Al Qaeda wakati Osama Bin Laden yupo Afghanistan kipindi Taleban inatawala kule, ameshawai kuwa IS kipindi fulani na pia ameshawai kuishi Colombia lakini hakuna habari zake alikaa kule Colombia kwa ajili ya nini… Ila katika hivyo vikundi vya kigaidi inaonekana alikuwa humo kwa ajili ukalimani, inasemekana anajua lugha nyingi sana pengine kukushinda hata wewe lol!... Ndiyo iko hivyo Sajenti wa zamani Agent Kai mpenzi wa mimi unayenisahau mpaka uwe na shida”. Maelezo marefu kidogo yalitoka kwa DC.

“Daah! Ahsante sana sina la kukuambia kwa sasa… Nitakupigia siku nyingine”.

Haraka wakaagana na kukata simu zao.

“Damia Abdulrahman a.k.a Language girl, swadakta ni jina nililotajiwa na mwenzako mmoja ambaye ametangulia mbele za haki baada ya kukutana nami bahati mbaya. Nilisema nishawai kuona picha yako sehemu na ni kweli ingawa sijakumbuka ni wapi lakini ni katika picha za magaidi wa kikundi fulani… Sina tena muda wa masikhara sababu nishakujua wewe ni nani, utanisamehe nahitaji kutumia nguvu uongee nitakacho au ujiue mwenyewe kama magaidi wenzako wengine wanavyofanya, nitakutoa kiungo chako kimoja kimoja mpaka unijibu nachotaka kwa usahihi… Je upo tayari nitumie nguvu?”.

“Kitu gani unachotaka kaka?”. Akajibu kwa haraka LG baada ya kumuona Agent Kai anatoa kwenye begi lake kifaa anachokitambua ni kwa ajili ya kung’oa meno na kisha akatoa mkasi mdogo.

“Yuko wapi Detective Marie? Usijifanye hujui sababu natambua fika wewe ndiyo ulikuja Airport kunipokea na kisha mkaniteka wewe na wenzako ambao nishawafyeka karibia wote kwa hesabu zangu zilizo sahihi”.

“Lakini hata nikikwambia ukweli kaka sidhani kama utaniacha salama”.

“Mimi hamna kitu ambacho uwa nafanya lakini sipendi kama kuua watu, sitakuacha huru lakni nitakuchia uhai wako”. Akamwambia huku akimkazia macho kisha akasimama toka kwenye kiti alichokuwa kaka mkononi akiwa na kifaa cha kung’olea meno na mkasi.

“Nitakukabidhi kwa serikali yako, nakuahidi ila nijibu yote nitakayokuuliza na unielekeze niyatakayo kwa usahihi kwa sasa chumba hiki kitakuwa ndiyo nyumbani kwako”. Akasema Agent Kai akitoa ahadi kwa LG, papo hapo akatega simu yake kwenye recording hili kuchukua mazungumzo atakayoyatoa Damia a.k.a Language girl.

“Nina mtoto mdogo ndiyo kwanza yupo mwaka wa kwanza shule ya msingi tena wa kike… Si kama napenda kufanya kazi hizi ila sina mbinu ingine ya kutafuta pesa kaka yangu zaidi ya hii kazi”.

“Kwa hiyo unataka nikusaidie nini?”.

“Wewe ni jasusi mkubwa sana duniani, nafikiri kwa sasa ndiyo jasusi na mpelelezi hatari sana mpaka vikundi vingine vya kihalifu na kigaidi uwa wanafikiri unatumia dawa… Naomba nisaidie kaka yangu namI nikusaidie”.

“Haya niambie malkia unataka nikusaidie nini?”.

“Niko tayari kuwasaliti wenzangu lakini na wewe unisaidie mtoto wangu naogopa nikifungwa atateseka sana baba yake alikufa Syria”.

“Hauna ndugu?”.

“Sina ndugu ninaishi na mama wa kazi anayenisaidia kazi za nyumbani na kumlea mtoto wangu ikiwa kumfuata shule mtoto ninapokuwa sipo nyumbani, nilizaliwa na baada ya umri kufikia kujijua mimi nani nikajikuta nalelewa katika kituo cha kulelea watoto mji wa Sarawak”. Aliongea na machozi yakajaa kuzunguka macho yake, mbinu hizi magaidi wa kike wengi aliowai kukutana nao Agent Kai huitumia kujifanya wanalia sana kujutia.

“Damia mi nawatambua nyinyi wajanja wajanja sana, naomba nikuahidi mwanao atakuwa salama salimini atateseka kipindi utakachokuwa hapa… Utabaki hapa kwa usalama wa kikazi”.

“Natoa machozi haya kaka najutia sana … Ni kweli nilikuwa gaidi wa Al Qaeda, Janjaweed, Al Shababy na mwisho nilikuwa Islamic State.. Lakini niliacha ugaidi nikakimbilia Colombia nilipokaa miaka mitatu hili wajue nimekufa sababu mimi huko kote walinitegemea sana katika kufanya ukalimani, Colombia niliishi kwa tabu mpaka nilipoamua kufanya kazi na kikundi kilichokuwa kinajihusha na dawa za kulevya cha Sergio Almarez napo nilitumika kama mkalimani tu ilipofika miaka mitatu watu wote wa kikundi waliuliwa na kikosi cha kupambana madawa ya kulevya ukanda wa Amerika, ndipo nikarudi Malaysia kwakuwa sikuwepo eneo la tukio”. Akaongea huku kwa utaalamu wa Agent Kai alitambua anayeongea naye ameamua kufunguka na hii ni kutokana na kuwa ana mtoto, watoto ubadilisha sana watu.

“Hapa KL nilijitahidi kuanza maisha ya kawaida ya kuishi katika bila kushiriki katika uhalifu wowote lakini nilipokutana na mtu mmoja anaitwa Anwar Mansour ambaye tulikuwa wote katika kundi la kigaidi la Al Shababy kwa shughuli maalumu nchini Ukraine na kwa sasa ni marehemu alinikutanisha na mtu mmoja anayeitwa Nawaz Patrash ambaye nilipata kusikia habari zake kipindi niko Al Qaeda lakini yeye hakuwa Afghanistan alikuwa Pakistan hivyo tulivyokutana na kwakuwa anazijua sifa zangu wakanishawishi kunipeleka kwa boss wetu ambaye ndiye kila kitu katika kile ambacho wewe kimekuleta hapa Malaysia na akaniomba nijiunge nao katika masuala mazima ya kufanya dili kubwa za kuipiga serikali ya hapa na hata nchi za jirani… Nikakubali kujiunga huko sababu ya kupata pesa ya kumlea binti yangu vizuri, hii ilitokana kikundi hiki si cha kigaidi ni kikundi cha kutafuta pesa zinazozagaa bila umakini wa muhusika mwenye pesa”. Akaanza kufunguka Damia.

“Tunakwenda vizuri malkia… Kikundi chenu kinaitwaje? Na boss wenu ni nani?”. Akampachika swali.

“Hatujawai kukaa na kukipa jina kikundi hiki, boss wetu anaitwa Mr. Logan Puteri”.

“Ni gaidi?”. Alimuuliza swali lingine bila kusubiri hata sekunde moja ipite.

“Hakuna mahali unapoweza kukuta historia ya yeye kuwai kujihusisha na kikundi chochote cha kigaidi ila rafiki zake wengi ni magaidi wa vikundi mbalimbali pamoja na vikundi vya kihalifu na hata huduma za kimsaada ya kipesa uwa anatoa kwa baadhi ya vikundi alivyo na marafiki nao”.

“Turudi kwenye swali kuu nalotamani kujua ni nini hasa kilicho ndani yake… Yuko wapi uliyemuwakilisha kuja kunipokea ukivaa sura ya bandia inayolandana naye?”.

“Tulimteka usiku wa jumapili iliyopita wakati wewe ulifika jumatatu usiku”.

“Mlijuaje kama ameingia hapa KL na ni yeye aliyewaambia juu ya ujio wangu?”.

“Boss ana mtu wake ambaye yupo ndani ya CTU huko Marekani ndiyo umpa habari zote zinazohusu Marekani, huyo mtu ni mfuasi wa IS wa siri, sababu inasemekana anajishughulisha na watu wanaofanya biashara za siri za kuwauzia silaha vikundi mbalimbali vya kigaidi”. Akajibu jibu ambalo lilimstua Agent Kai, habari mpya ya kimshangao akabaki mdomo wazi na kutamani kumjua huyo mtu ni nani aliye ndani ya Counter Terrorism Unit (CTU), kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kinachpfanya kazi kwa ukaribu zaidi na CIA, lakini wenyewe wanadili na ugaidi tu wakati CIA wanafuatilia mambo yote ya kiuhalifu, ugaidi na mengineyo juu ya usalama na maslahi ya Marekani.

“Mpya hii! Unamjua jina huyo mtu wa CTU?”.

“Sikuwai kumuuliza Mr. Logan kuhusu huyo mtu ni nani.. Sababu sikuwa na sababu ya kumuuliza hivyo”.

“Nitamjua tu huyo mtu hivyo tuachane naye kwa sasa… Wako wapi wamarekani mnaowashikilia mateka? Na kwanini mnawashikilia mateka watu wetu hao?”.

“Ni pesa ndiyo sababu”. Akajibu bila kuongeza chochote.

“Yaani kuwashikilia wamarekani ni pesa?”. Jibu lilimshangaza Agent Kai ikabidi naye aulize haraka.

“Chanzo kilikuwa ni wanasayansi wenu wa silaha za kibaiolojia, kinyuklia na kikemikali… Ilikuwa ni biashara hiyo tu kati ya mtu mmoja mkorea kaskazini aliyempa dili hilo boss wetu Mr. Logan kuwa serikali ya Korea Kaskazini ikipata wamarekani walio muhimu sana kwa nchi hiyo inatoa pesa kulipa hili iwapate, Mr. Logan hili hakuwai kunificha sababu mimi ndiyo mtu pekee niliyekuwa mkalimani wake wakati anaanza mazungumzo na huyo mkorea… Yalifanyika mitego kadhaa ya kutaka kunasa raia za Marekani wanaokuja kutalii hapa Malaysia lakini kila aliyekuwa anafika hapa toka tupewe dili hilo walikuwa si watu muhimu kiserikali kwa taifa la Marekani mpaka miezi miwili iliyopita mtu wa CTU alipompa taarifa boss kuwa kuna wanasayansi maprofesa wawili wastaafu waliofanya kazi kwa kipindi kirefu katika maabara ya Manhattan Project wanakuja kiutalii nchini hapa hivyo ni fursa kwetu sababu Korea Kaskazini na hata Iran wanataka watu wa aina hii hili wapate kuwabana wakubali kutoa siri zinazohusu silaha nilizokwisha kuelezea… Hivyo swali lako jibu lake lililo kamili profesa mmoja kati ya wale tunaowashikilia kama tukifanikiwa kuwakabidhi mikononi mwa majasusi wa Korea Kaskazini tu tunapata zaidi ya dola milioni mia moja… Wale wapelelezi walipoingia katika mikono yetu mkuu wa kijasusi pamoja na waziri wao aliomba kuwa tusiwaangamize wanawahitaji wote na watawalipia pesa pia na ni kiasi kikubwa kwa mujibu wa Mr. Logan, hivyo wote wapo salama mikononi mwa Mr. Logan… Tulipoletewa taarifa kuwa wewe Agent Kai unakuja Malaysia kujaribu bahati yako kama siku zote inavyokuwaga ni bahati kwako kufanya uchunguzi wako na ikiwezekana kuwaokoa wale wamarekani toka mikononi mwetu taarifa ikaenda kwa mkuu wa ujasusi wa Korea Kaskazini ndipo napo wakatoa oda yenye msisitizo kuwa ni bora wakapoteza watu wote si wewe… Wewe umepandiwa dau kubwa kama alilonunuliwa mchezaji Neymar toka Barcelona kwenda Psg”. Maelezo marefu yenye kueleweka yalitoka mdomoni mwa Damia huku Agent Kai akiendelea kumrekodi kwenye simu yake.

“Ooh! Shit.. kumbe ni mpango wa serikali ya Korea Kaskazini kutaka kutukomoa taifa letu.. Sidhani kama wataalamu wetu wa silaha hizi za kihatarishi wanaweza kutoa siri ya jinsi teknolojia ya Marekani inakwendaje? Hawa ni watu waliokula kiapo kikubwa sana kwa taifa.. Ukija kwa wapelelezi wetu wameingia matatizoni kwakuwa wanataka kulisaidia taifa na familia za maprofesa walio katika huzuni kupotea kwa wapendwa wao.. Upande wangu ni sahihi sababu nishafanya mambo kama matano mpaka kufika hapa nilipo nikipiga maslahi yao, wako sahihi kunihitaji wako sahihi kuhitaji nilipe walichopoteza kama rasilimali watu na hata vyombo kama ndege na vinginevyo lakini si wengine”. Kwa uchungu na masikitiko akaongea Agent Kai huku akiangalia dirishani kuona nje ya pale ambapo kwa mbali lilikuwa likionekana ziwa Metropolitan.

“Kwa ujumla kundi lenu mosi halina jina, pili mpo kipesa hamna ugomvi na wamarekani… Nimefurahi kujua hilo… Wapi wamefichwa mateka wenu?”. Akaongea tena Kai na kuuliza.

“Mimi ni mkalimani tu katika kundi letu sishiriki chochote zaidi ya kuwa chambo mara kadhaa kwa watu ambao tunahitajika kuwapata kwa maslahi ya kundi letu na boss wetu Mr. Logan… Hivyo nikwambie ukweli tu mi sijui walipo hao watu ungeonana na mkuu mwenyewe au msaidizi wake Mr. Nawaz Patrash na wengine ambao ameshirikiana kuwapeleka watu hao sehemu ya siri wanaoijua wao”. Akajibu Damia (LG) akiongopa kuhusu hilo sababu aliona kama atasema atakuwa amesaliti kwa ukubwa sana na ni bora Agent Kai akajue kwa wahusika wakuu wenyewe, kiukweli alikuwa akijua wako wapi hao wanasayansi na mashushushu wa Marekani.

“Simu yako inaita… Sitaruhusu upokee kwa sababu za kimnara”. Akasema Kai baada ya mlio wa simu kusikika ukitokea katika pochi la LG ambalo lilikuwa kwenye godoro, alichofanya alifungua pochi lile na kuitoa simu kisha akamuonyesha screan ya simu hili LG asome jina.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na tatu (33)

Agent Kai kazini na wasiwasi na mashaka unadhidi kutanda kwenye mioyo ya wapinzani wake, twen’zetu tukashuhudie nini kinaendelea katika sehemu inayofuata.

“Ooh! Shit.. kumbe ni mpango wa serikali ya Korea Kaskazini kutaka kutukomoa taifa letu.. Sidhani kama wataalamu wetu wa silaha hizi za kihatarishi wanaweza kutoa siri ya jinsi teknolojia ya Marekani inakwendaje? Hawa ni watu waliokula kiapo kikubwa sana kwa taifa.. Ukija kwa wapelelezi wetu wameingia matatizoni kwakuwa wanataka kulisaidia taifa na familia za maprofesa walio katika huzuni kupotea kwa wapendwa wao.. Upande wangu ni sahihi sababu nishafanya mambo kama matano mpaka kufika hapa nilipo nikipiga maslahi yao, wako sahihi kunihitaji wako sahihi kuhitaji nilipe walichopoteza kama rasilimali watu na hata vyombo kama ndege na vinginevyo lakini si wengine”. Kwa uchungu na masikitiko akaongea Agent Kai huku akiangalia dirishani kuona nje ya pale ambapo kwa mbali lilikuwa likionekana ziwa Metropolitan.

“Kwa ujumla kundi lenu mosi halina jina, pili mpo kipesa hamna ugomvi na wamarekani… Nimefurahi kujua hilo… Wapi wamefichwa mateka wenu?”. Akaongea tena Kai na kuuliza.

“Mimi ni mkalimani tu katika kundi letu sishiriki chochote zaidi ya kuwa chambo mara kadhaa kwa watu ambao tunahitajika kuwapata kwa maslahi ya kundi letu na boss wetu Mr. Logan… Hivyo nikwambie ukweli tu mi sijui walipo hao watu ungeonana na mkuu mwenyewe au msaidizi wake Mr. Nawaz Patrash na wengine ambao ameshirikiana kuwapeleka watu hao sehemu ya siri wanaoijua wao”. Akajibu Damia (LG) akiongopa kuhusu hilo sababu aliona kama atasema atakuwa amesaliti kwa ukubwa sana na ni bora Agent Kai akajue kwa wahusika wakuu wenyewe, kiukweli alikuwa akijua wako wapi hao wanasayansi na mashushushu wa Marekani.

“Simu yako inaita… Sitaruhusu upokee kwa sababu za kimnara”. Akasema Kai baada ya mlio wa simu kusikika ukitokea katika pochi la LG ambalo lilikuwa kwenye godoro, alichofanya alifungua pochi lile na kuitoa simu kisha akamuonyesha screan ya simu hili LG asome jina.

ENDELEA NA STORY…!

WASIWASI NA MASHAKA VII

“Nani huyu uliyemsevu Uncle G?”. Akamuuliza swali huku wanatizamana machoni.

“Moja kati ya viongozi wa kundi letu anaitwa Ghulam Qaresh ni kapteni wa zamani wa jeshi la India, nafikiri itakuwa kikao kimeanza na mimi ndiyo sipo kikaoni”.

“Mlikuwa na kikao leo?”. Akamchapa swali tena.

“Ndiyo kaka… Pale ulipotukuta kisha ukanichukua nilikuwa na maongezi na yule kijana kisha ningewai kikaoni”.

“Kikao kinafanyika wapi?’.

“Uwa hatujui wapi boss anataka tukakutane kwa ajili ya kikao ni kama kutustukiza tu uwa anatuambia muda fulani kuna kikao kisha hasemi wapi ikifika bado dakika tano ndipo anasema wapi tukakutane”.

“Kwahiyo nyinyi hamna kambi maalumu?”.

“Ndiyo hatuna kambi maalumu na mara nyingi tunakutana katika VIP Hotel, Cassino au kwenye baadhi ya nyumba za mmoja wa kiongozi wetu inaweza ikawa nyumba ya Ghulam, Nawaz au yeye mwenyewe boss, nyumba zenye utulivu kwa wakati husika”. Hapa kwenye kikao tena LG alidanganya sababu alikuwa anajua wapi wana kikao chao cha saa tano usiku.

“Nashukuru kwa maelezo yako yamenifumbua mengi na ninaamini hujanidanganya kwa asilimia sabini na zilizobaki umenidanganya lakini kwakuwa ni asilimia chache sana mi sijali… Nje ya unyambilisi wa kutafuta pesa katika njia ya siri kitu gani kinachomfanya Mr. Logan kuingiza pesa?”. Akaongea na kumuuliza swali.

“Kwanza nje ya hiki anachofanya boss wetu ni mtu safi sana, ndani ya jamii ya Malaysia ni mtu safi na maarufu sana. Hakuna anayejua kama ana kikundi anachomiliki kinachojihusisha na utekaji wa watoto wa matajiri kisha anajipatia pesa, anaingiza pesa zake serikalini kununua tenda za miradi mikubwa ya uingizaji mafuta anaiuzia serikali ana vituo vya mafuta na viwanda viwili vinavyotengeneza vifaa vya mashuleni na pia ana maduka ya kuuza bidhaa za LG yanayouza simu, tv, redio na mafriji”.

“Hii inamaanisha ana kampuni inayomiliki biashara hizo, inaitwaje hiyo kampuni?”.

“Yah! Anayo kampuni inayounganisha masuala yote hayo, inaitwa Puteri Group of Business (PGB)”.

“Unajibu nusu nusu malkia, humalizii majibu yako… Iko wapi ofisi ya kampuni hiyo?”.

“Mtaa wa Rodger barabara ya Jalan Hang Kasturi, katika mtaa huo kuna majengo ya ghorofa mengi marefu lakini jengo la pili kwa urefu ndipo zilipo ofisi za PGB floor ya kumi na tano kuna bango kubwa jeupe linaloelekeza makampuni yaliyomo ndani ya ghorofa hilo”.

“Okay! Acha nikamuone… Utapumzika humu ndani ukiwa umefungwa hivyo hivyo ni kwa usalama wangu sababu nyumba hii nipo peke yangu sina mlinzi yeyote, inuka ukae kwenye godoro”. Akamuamrisha na LG akainuka na kukaa kwenye godoro, Agent Kai akamkamata miguu kwa nguvu kisha akaiweka sambamba na kuanza kuifunga kamba huku LG akitulia tuli kuacha mtaalamu afanye anachoona ni sahihi.

“Okay! Nikuletee chakula gani?”. Akamuuliza baada ya kumaliza kumfunga.

“Chakula si kitu kwangu nakuomba usalama wa mwanangu tu maana sina kawaida ya nikiwepo Kuala Lumpur kumuachia pesa za matumizi mama wangu wa kazi za kuzidi siku mbili”.

“Kwahiyo za leo umeacha?”.

“Ndiyo nimemuachia sababu nilimuaga nitakuwa bize sana hivyo wasishangae mi kurudi usiku au hata asubuhi”.

“Sasa una wasiwasi gani? Kumbe umeaga utarudi usiku au kesho asubuhi… Nikirudi toka niendako nitakupa simu uongee nao”. Akajibu Kai na kisha kutotaka kusubiri ataongea nini akatoka na kuubamiza mlango kisha akaufunga kwa nje kwa funguo.

***** ***** *****

Saa tano na dakika tano idadi ya watu waliokuwa wanatakiwa kikaoni ‘jumba la nyoka’ kama wahusika wanavyoliita ilikuwa imekaribia kutimia akikosekana mtu mmoja ambaye ni mwanadada Damia Abdulrahman a.k.a Language Girl (LG).

Dakika mbili zilizopita mtu ambaye alikuwa kavusha muda wao wa kawaida kufika boss mkubwa Mr. Logan Puteri alifika eneo hili la Kepong Metropolitan Lake.

“Nimevusha muda kufika hapa… Foleni zimezidi sana siku hizi jiji hili mpaka muda mwingine nami Napata hamu nipande treni za umeme”. Akaongea baada ya kukuta watu wake wamekaa chumba chao maalumu ambacho uwa wanafanyia mikutano yao wakiwa hapa jumba la nyoka.

Moja kwa moja akavuta kiti chake ambacho mara zote uwa anakaa wajapo hapa, baada ya kukaa akazungusha macho kwa wote waliokuwemo pale ndani.

“LG amechelewa kama mimi nilivyochelewa… Lakini hakijaharibika tunaweza kuanza maongezi yetu sababu sidhani kama tunahitaji ukalimani hapa”. Akaongea tena Mr. Logan na kuachia tabasamu la kujilazimisha sababu kiukweli tabasamu kwake kwa siku mbili hizi ilikuwa kwa tabu sana kwa machungu ya ajabu aliyokuwa nayo moyoni inayosababishwa na wasiwasi wenye mashaka tele juu ya mustakabali wao kwa ujumla.

“Ni sawa tu tunaweza anza mazungumzo bila kumsubiri yeye”. Akaunga mkono Nawaz Patrash.

“Ni muhimu kwake kujua tunaendelea vipi na mpango ingawa si muhimu sana pia kwa sababu yeye uwa haingii sana kwenye mpango wetu kimatendo mpaka inapohitajika sana”. Akaongea Mr. Logan na kutizama saa yake aina ya Rolex aliyovaa mkono wake wa kushoto.

“Vipi siku yenu ya kwanza ya jana Uugun na wenzako? Maana hata simu hatujapigiana wakuu”. Akaendelea tena alipotizamana macho na wageni wake katika kundi lake ambao walifika siku mbili zilizopita kutokea Mongolia.

“Siku ya jana mpaka sasa kimaisha ya kawaida iko vizuri sana boss, watu wako wametufanya tuione Malaysia kama Mongolia kwa kila kitu… Lakini si kitu kilichotuleta mkuu, mikono yetu inawasha kwa kweli pua zetu zina hamu kupata harufu ya damu ya mtu”. Akajibu Uugun kwa niaba ya wenzake na watu wote waliomo ndani ya chumba hiki cha mkutano kucheka kwa sauti.

“Shida sana… Ukweli nadhani mmeuona kuwa tunamuwinda sungura ambaye kajificha kwenye mashimo, anyway! Tuendelee na mengineyo sababu naamini tunayemuwinda naye anatutamani kwa sababu tuna mali anazozifuatilia mali zilizomleta Malaysia toka Marekani maili kibao”. Akaongea Mr. Logan kisha akapumzika kumeza mate kidogo.

“Leo asubuhi Mr. Michael alifika kazini kwake na moja kwa moja akaenda kuonana na mkuu wa kitengo cha ulinzi wa ubalozi wao anaitwa Mr. Cowell, mtu wetu aliingia hapa Malaysia kwa siri sana yaani pale ubalozi waliokuwa wamehusishwa na ujio wake walikuwa ni balozi mwenyewe Kapteni Jones Lebrons na mwanadiplomasia mkuu wa ubalozi Mrs. Rose Thompson, hii inatuonyesha kuna jambo walikuwa wamejifunza jambo kuhusiana na wenzao ambao tuliwapata baada ya wao kufika tu hapa KL ingawa hawako sawa kivile sababu sisi mtandao wetu una mzizi mkuu nchini kwao na ndiyo mzizi taarifa tegemezi”. Hapa alisimama akavua koti lake la suti kisha akalegeza tai na kuliweka koti kwenye bega la kiti alichokaa.

“Kitu ambacho tulitaka kujua toka kwa mwanamke ambaye yeye huyu bwana sungura wetu kilishindikana kujua kutokana ametuwai kamuondoa usiku yule mwanamke na kumpeleka mahali kusipojulikana utafikiri pengine kwenye crew yetu tuna mtu ambaye anatusaliti na kumpa taarifa mpango huyu sungura… Michael alipouliza kwa Cowell kama anaweza kujua huyu mtu amefikia wapi maana kiukweli kabisa nataka nikwambieni hotel zote hapa KL hawana taarifa ya uhakika kuhusu huyu mtu ingawa kuna mtu mmoja kaniambia anamuhisi ni yeye kati ya wapangaji waliofika hotelini kwao usiku wa juzi, mtu huyu yupo hotel ya Sheraton Imperial Palace Hotel na jioni ya jana aliondoka na mwanamke anayeonekana kama mpenzi, nimempa taarifa amuangalie vizuri akirudi iibidi ampige picha. Sababu sungura anaonekana ni mtu anayeishi maisha ya kujibadili sura mara kwa mara toka aingie Kuala Lumpur”. Hapa tena Logan Puteri ‘Master Plan’ alinyamaza na kusogea kwenye meza ya vinywaji kisha akajimiminia mvinyo wake aupendao wa Luc Belaire katika glass na watu wengine kama watano nao wakainuka na kusogea kwenye ile meza na kila mmoja akajihudumia kinywaji anachotaka.

Dakika mbili mbele baada ya wazee wa kazi hawa kuzitumia kujihudumia vinywaji kulikumbwa na utulivu vikisika vinywaji vinavyohama toka kwenye chupa za mivinyo kuja glasini.

“Nafikiri kila mmoja yuko sawa… Usiku uliopita tulikuja hapa kuweka mipango sawa kwa kuhitaji utekelezaji wake, suala la Michael naona tuliache sababu amejikuna alipofikia na bado yupo nasi atatutonya kwa lolote ataloona ni msaada kwetu katika mpango huu.. Mpango wetu wa pili ilikuwa kuhusu wenzetu wataalamu wetu kompyuta na sura bandia Dr. Zhing Lae, Hassan Saddiq na msaidizi wao.. Nashukuru walifika Putatan na kazi wameianza kwa ufanisi na weledi mzuri, ifikapo saa kumi na moja jioni nami nitaondoka kuelekea Putatan kuweka mazingira sawa zaidi nikiwa na Khorloogin Bayari, Istqal Saanjin, Ally Kareem, Sauez Mallam na Putram Ramji tutaongozana kuelekea Putatan… Hapa mtabaki kuendeleza operesheni ya kumkamata Sungura”. Akatoa maelekezo Master plan (MP).

“Ni sawa ulivyoamua… Mimi naahidi kuhakikisha tunampata sungura na pia tunajilinda tusije kupoteza mtu mwingine kati ya watu tulionao kama timu”. Nawaz Patrash akaunga mkono maamuzi ya boss wao Mr. Logan na hata wengine wakatingisha kichwa kuonyesha kuunga mkono mawazo ya viongozi wao hawa.

“Ila boss nakumbuka jana ulisema utajaribu kurahisha jambo kabla hujaondoka kwa kuongea na mkuu kikosi maalumu cha ujasusi cha ofisi ya waziri mkuu kwakuwa ni rafiki yako atusaidie kutusogezea huyu mtu… Je? Huoni kwa jinsi anavyotufanyia usungura na siku zinakwenda tukamtumia mkuu wa Research Division of the Prime Minister’s Department (RDPMD)”. Ghulam Qaresh akatoa wazo alilonalo baada ya muda wote toka amefika hapa kuwa kimya kabisa akitafakari mambo kadhaa wa kadhaa.

“Wazo zuri lakini tunatakiwa kujua kwanza kama anajua juu ya uwepo wa huyu mtu ingawa hakuna mtu anayeweza kuingia hapa Malaysia na kuanza kufanya kazi ya kijasusi bila ofisi ya RDPMD kujua”. Akaingia kuongea Ally Kareem mtu mwenye sifa ya roho mbaya ya kikatili katika kundi hili anayehusika na mateso pindi yanapohitajika kufanyika kwa mtu wanayemshikilia ni jasusi mstaafu wa Syria.

“Mnahisi sisi wenyewe tumemshindwa Sungura? Mnataka tukajianike bila uhakika?”. Mr. Logan akaongea baada ya muda wote kuwa anakunywa kinywaji akiwasikiliza.

“Hatukurupuki tunatumia unafasi uliopo kati yako na wewe na ukimada wake na rafiki yake Damia, tunaweza kumtumia Damia akaenda kuongea naye kabla wewe hujaongea naye anatakiwa atujulishe anajua kama huyo mtu yupo hapa nchini”.Ghulam akaongea.

Wote waliokuwemo pale wakaangaliana kwa zamu na baadhi wakatingisha vichwa vyao kukubali wazo la Ghulam.

“Sawa kama mnaona hiyo ni njia itakayoturahishia acha tuifuate… Lakini kikao hiki Damia hayupo na hatujui kwanini hayupo?”. Akaongea MP huku akizungusha macho kama anatafuta kitu katika chumba kile.

“Na kweli lazima tujiulize kwanini iko hivi? Si kawaida ya kikao ambacho anatakiwa na yeye kuwepo halafu asiwepo”. Nawaz akaongea na kisha akatoa simu yake.

“Ngoja nimpigie nijue ana tatizo gani?”. Ghulam Qaresh akasema kisha akaweka simu yake sikioni hii ikimaanisha alikuwa ameshajiandaa kupiga simu.

Akiwa ameweka loud speaker simu iliweza kusikika ikiita miito yote inayotakiwa kuita kisha ikakata yenyewe, akarudia mara moja kisha akapumzika dakika mbili kisha akajaribu tena napo ikawa hivyo hivyo.

“Nini hii? Mbona hapokei simu? Si kawaida yake kutopokea simu kwa haraka inapoita na wakati huohuo akiwa anajua kuwa alikuwa anahitajika hapa kwenye kikao chetu”. Akaongea Ghulam na wengine wakiwa kimya wanatafakari.

“Ebu tusubiri dakika tano mpaka kumi kisha tumpigie tena tuone itakuwaje pengine yupo maliwato au amepitiliza usingizi maana tulichelewa kulala nikiwa naye pia tuliwai kuamka tukaenda tena kwenye windo tulilokuwa tunalifuatilia”. Akatoa alinalo Nawaz Patrash.

“Sawa tusubiri lakini nina wasiwasi na hii hali”. Akaongea Mr. Logan naye huku akiiangalia simu yake na vidole vyake vikiwa na hamu ya kupiga simu.

Dakika walizokubali kusubiria zilikwenda taratibu upande wao huku vinywaji ndiyo vikisika katika hali hii na ile kwa wote.

“Muda huu ngoja tujaribu tena kumpigia”. Boss mkulu Master Plan akaongea na haraka akapachika hearphone sikioni.

Simu yake ikakutana na anayempigia hapatikani. Wote walistuka wakashikwa na mshangao ni kitu ambacho hawakutegemea kabisa.

“Guy’s hili ni tatizo… Yah! Niko sahihi na ninacho fikiria… Nafikiri sungura sasa ametusogelea karibu zaidi”. Akasema huku kainamisha kichwa chini Mr. Logan Puteri.

“Kwanini unasema hivyo Master? Hii inaweza ikawa ni tatizo lingine tu”. Ally Kareem akasema.

“No! mara nyingi ninapoiwaza hatari basi uwa hatari Ally… Haraka Ghulam na Nawaz nendeni nyumbani kwake LG halafu mtanipigia kunijulisha niaje… Saivi ni saa sita na dakika nne, nafikiri kabla sijaondoka natakiwa nijue kila kitu kuhusu Damia, huyu ni mwanamke kumbukeni na kama ameingia kwenye mkono wa mtu hatari mwenye mbinu nyingi za kijasusi anaweza akaropoka mengi sana.. Ebu nendeni… Na Uugun naomba ongozana nao kwenda kwa Damia”. Amri ya boss ikatoka akiwa na uoga unaojidhihiri machoni mwa wafuasi wake.

Haraka Nawaz Patrash, Ghulam Qaresh na Uugun wakatoka pale kikaoni.

“Saa saba nitatoa taarifa kwenu nyote kwa njia ya meseji kuwa nini kinatakiwa kufanyika, wale wote niliowataja kuwa tunatakiwa kuondoka wote kwenda Putatan naomba nyie muendelee na mchakato wa maandalizi ya kuondoka mkiwaweka sawa wake zenu kwa wale wenye wake zao ukiacha kina Istqal, mi naelekea nyumbani kwangu Ally twende”. Mr. Logan akaendelea kuelekeza watu wake kisha kumwambia Ally Kareem waondoke naye sababu huyu ndiye anayeongoza kikundi cha watu wane ambao uwa wanamlinda walinzi wake binafsi (bodyguard’s).

Kikao chao kiliishia hapo wote waliokuwa wamefika pale jumba la nyoka wakashika hamsini zao kusubiri naelekezo nini kinafuata.

***** ***** *****

Rodger Streer barabara ya Jalan Hang Kasturi mtaa wa maofisi mengi ya makampuni binafsi ya baadhi ya kampuni nyingi zilizo katika jiji la Kuala Lumpur.

Agent Kai akiwa katika sura ya bandia, vazi ya aina ya suti ya rangi nyeupe alikuwa kwenye lifti ya ghorofa ambalo ndipo ilipo ofisi ya Puteri Group of Business akielekea floor namba kumi na tano kwa kufuatia maelezo aliyopewa na LG.

Dakika tatu mbele alitoka kwenye lifti na taratibu akawa anasogelea lango kubwa la kioo lenye kuonyesha wafanyakazi waliokuwa ndani wakiendelea na kazi, juu ya lango kulikuwa na maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa rangi nyeusi PUTERI GROUP OF BUSINESS (PGB) HEADQURTER.

Macho ya Agent Kai yalikuwa makini kuangalia walinzi wawili walio kwenye stuli ndefu mbili zilizokaa kila upande wa lango la kuingia ofisi hii huku wameshika mikononi mwao mmoja akishika kirungu kilicho kama fimbo kubwa kiunoni ana bastola na mwingine akiwa yeye hana bunduki lakini ana bunduki kubwa aina Sub Gun Machine (SMG).

Kwa mwendo wa kawaida tena wa kuonyesha jeuri Fulani ya kipesa aliwasogelea na kusogea kwa mmoja aliye upande wake (karibu).

“Habari zenu?”. Akawasalimu na wakati akiruhusu akili yake ya kijasusi kuwajadili muonekano wao.

“Nzuri mkuu.. Tukusaidie nini?”. Jamaa akajibu kwa niaba ya mwenzake aliye upande wa pili na kisha papo hapo akauliza.

“Nahitaji msaada wa kiofisi hapa PGB!”.

“Okay! Jaza daftari hilo hapo kisha utatia saini kama umeingia ukitoka utarudi tena hapa kusaini”. Akajibu mlinzi yule huku anamsogezea daftari lililoonyesha ni wageni mlangoni.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na nne (34)

Agent ameweza kumchukua katika hali utekaji mwanadada machachari mtaalamu wa lugha na mtu anayeaminiwa vya kutosha na Mr. Logan Puteri.

Anafanikiwa kumbana kwa vitisho vya hapa na bila kutarajia anajikuta amepata mtu muhimu sana, mtu anayemsogeza jirani kabisa kwa wateja wake wa mbolea.

Damia Abdulrahman anajikuta akisema vile anavyovijua kirahisi ingawa vingine alivificha kwa sababu tu ya binti yake mdogo, mtoto wake wa pekee, kabinti kenye miaka mitano.

Anajikuta anafanya hivyo hili asaidiwe na imani ya kiutu toka kwa Agent Kai, akili yake ikimlazimisha kuwa awe mkweli hata kidogo na ategemee kujiliza machozi kwa kutarajia imani ya mzazi kwa mtoto itamkuta Kai na atamsaidia yeye kurudi kulea mtoto vizuri tena bila bugudha.

Nini kitafuata katika sehemu inayofuata?

Tumeona Agent Kai akiwa kasogea mpaka zilipo ofisi za adui yake mkubwa ambaye bado hajajua hata sura yake ikoje lakini imani inamuambia ofisi ya PGB ataondoka na msaada mkubwa sana katika kazi yake.

Mwisho wa sehemu hii ndiyo mwanzo wa utamu wa muendelezo wa sehemu inayofuata na itakayofuata.

Dakika tatu mbele alitoka kwenye lifti na taratibu akawa anasogelea lango kubwa la kioo lenye kuonyesha wafanyakazi waliokuwa ndani wakiendelea na kazi, juu ya lango kulikuwa na maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa rangi nyeusi PUTERI GROUP OF BUSINESS (PGB) HEADQURTER. Macho ya Agent Kai yalikuwa makini kuangalia walinzi wawili walio kwenye stuli ndefu mbili zilizokaa kila upande wa lango la kuingia ofisi hii huku wameshika mikononi mwao mmoja akishika kirungu kilicho kama fimbo kubwa kiunoni ana bastola na mwingine akiwa yeye hana bunduki lakini ana bunduki kubwa aina Sub Gun Machine (SMG).

Kwa mwendo wa kawaida tena wa kuonyesha jeuri Fulani ya kipesa aliwasogelea na kusogea kwa mmoja aliye upande wake (karibu).

“Habari zenu?”. Akawasalimu na wakati akiruhusu akili yake ya kijasusi kuwajadili muonekano wao.

“Nzuri mkuu.. Tukusaidie nini?”. Jamaa akajibu kwa niaba ya mwenzake aliye upande wa pili na kisha papo hapo akauliza.

“Nahitaji msaada wa kiofisi hapa PGB!”.

“Okay! Jaza daftari hilo hapo kisha utatia saini kama umeingia ukitoka utarudi tena hapa kusaini”. Akajibu mlinzi yule huku anamsogezea daftari lililoonyesha ni wageni mlangoni.

Endelea na utamu wa mdundo!

MAPIGO YA KIFUNDI I

Watu wawili walikuwa wapo kwenye benchi la kusogea meza ya maulizo, Agent Kai huku akirekebisha tai yake vizuri shingoni na lengo haswa akilenga ilipo kamera yake ndogo ya kuchukua matukio ya video ambayo ilitengenezwa ikiambata na kilicho machoni mwa watu kama pini ya kubana tai, akajiunga kwenye moja ya sofa la kukaa watu watatu ambalo alikuwepo mwanadada mmoja.

Haikuchukua dakika nyingi aliyekuwa akihudumiwa kwenye meza ya wahudumu wa mapokezi, Agent Kai akageuka kumuangalia dada aliye pembeni yake macho yakagongana na dada yule akamkonyeza huku ana tabasamu kumuonyesha ishara aende yeye akahudumiwe hivyo alijibu tabasamu alilopewa kisha akainuka na kwenda meza ya huduma.

“Habari za hapa dada!”. Akatoa salamu kwa dada ambaye mpaka Kai anasogea mezani pale alikuwa bize kuandika jambo kwenye kompyuta yake ya kazi.

“Nzuri kaka… Habari zako na wewe?”. Dada akamjibu.

“Nzuri sana … Pole na kazi!”.

“Kawaida kaka yangu… Nikusaidie nini?”.

“Nahitaji kuonana na boss wa PGB!”.

“Una miadi naye kuwa utafika hapa kuonana naye?”.

“Hapana … Nimebahatisha kufika hapa kuonana naye kwa shida maalumu ya kikazi”.

“Boss uwa haonani na mtu bila miadi naye, sababu ana watu wengi sana ambao wanasumbua wakitaka kuonana naye”.

“Ni kweli sina ahadi ya kuonana naye lakini kwakuwa ni shida ya kiofisi naweza kuandika kimemo kuwa nahitaji kuonana naye na ni muhimu sana dada yangu”.

“Kama ni shida ya kiofisi unaweza kuweka miadi ya kuomba kuonana naye lakini hapa ofisini kwetu ni ofisi iliyoenea wapo wengine wanaoweza kukusaidia”.

“Sawa dada hata hilo utakuwa umenisaidia sana maana natokea nchi ya Laos na itakuwa hasara kama nitaondoka bila kuonana na mtu ambaye toka nainua mguu wangu wa kwanza nyumbani Laos nilipanga naye atakuwa ni miongoni mwa watu nitakaokuja kuonana naye”.

“Sawa! Siku za hivi karibuni boss na karibia ofisi yake yote ya seneti ya uongozi wa juu wako bize sana mpaka sisi wahudumu wa chini tunashangaa wakija ofisini wanakaa muda kidogo wanaacha maelekezo ya kazi kwa masekretari wao kisha wanaondoka, nafikiri kuna biashara kubwa zaidi wanaifuatilia ndiyo wako bize… Hapa ofisini mara nyingi tunabaki na makamu wa mwenyekiti mke boss mwenyewe ambaye ndiye mwenyekiti…. Lakini una bahati mbaya sana naye pia ametoka ameenda kwenye kikao cha wafanyabiashara wakubwa wenye makampuni makubwa zaidi, naomba uchague kwenda ofisi yake ukaonane na mmoja wa wasaidizi wake uombe ahadi ya kuja kuonana naye kesho, ngoja nipige simu kuwaatarifu wasaidizi wake kuwa kuna mgeni anayeomba kuonana nao”.

Alinyanyua mkono wa simu ya mezani (risiva) na kuipachika sikioni na papo hapo akabonyeza namba fulani.

“Hello!”. Akajibiwa na upande wa pili.

“Halloo Gwen! Kuna mgeni hapa ametokea nchini Laos anaomba kuonana na watu wa ofisi ya makamu… Kama mko sawa nimruhusu aje?”. Akaongea na kuuliza.

“Ni mwanaume?”.Upande wa pili nao ukauliza.

“Ndiyo!”.

“Anatokea Laos, okay mruhusu apite”.

Mkonga wa simu ukashushwa chini, dada akamtizama mwanaume aliye mbele yake ambaye yumo ndani ya sura ya bandia bila kujulikana.

“Ruhusa imepatikana unaruhusiwa kwenda kuonana nao”.

“Sawa acha nionane naye yeye na nibadilishane naye mawazo kama naweza kuwakilisha ombi nililonalo kwa mabosi zake… Mke wa boss, makamu wa mwenyekiti anaitwa nani?”.

“Chukua fomu hii ujaze… Makamu mwenyekiti ni mwanamama maarufu sana hapa Kuala Lumpur na Malaysia kwa ujumla anaitwa Mrs. Zahra Puteri”. Akasema mwanadada na kusukuma karatasi ambayo alisema ni fomu ambayo nayo pia ni sheria kujaza ufikapo PGB kuonana na mabosi wa hapa.

“Nashukuru kwa kunipa nafasi, nielekee mlango upi?”. Akasema na kuuliza Agent Kai.

“Fuata ukumbi huu kisha mbele utakuta korido ndipo zilipo ofisi za makamu na mwenyekiti mwenyewe, mlango wa kwanza ndipo ofisi za makamu, wasaidizi wake wapo huko”.

Kichwani alikuwa akiwaza anaenda kuzungumza nini na hawa wasaidizi wa makamu wa mwenyekiti pia alikuwa katika umakini wa kujali usalama wake, macho yake yalitambua uwepo wa cctv camera na hata kama alikuwa anatembea bila kuonyesha hofu yoyote aliyonayo lakini hakuwa mjinga kutambua ofisi kama hii kwa kipindi hiki lazima wenye ofisi wawe makini sana na kila anayefika hapo hasa mwanaume.

Aliminya kitasa cha mlango wa kioo unaoingia zilipo ofisi za makamu wa mwenyekiti Bi. Zahra Logan na kasha akatokeza ndani na macho yake kulakiwa na wanawake wawili na mwanaume mmoja waliojipanga kila mmoja na meza zilizo na kompyuta na mafaili kadhaa wa kadha.

“Karibu mgeni!!!”. Ni kama walipanga wenyeji wale wote watatu wa ofisi walitamka kwa pamoja.

“Ahsanteni sana… Nisogee kwenye meza ya nani kupata huduma?”. Akawauliza huku kasimama hatua chache baada ya kizingiti cha mlango.

“Tumepewa taarifa shida yako ni kumuona Mheshimiwa Mrs. Zahra Logan lakini unaweza kutuelekeza ni kipi unataka kwa makamu wetu wa mwenyekiti wa PGB, hili tukuombee miadi kwake ya kuja kukutana naye sababu hapa utaratibu wetu ni kuwa huwezi kuonana na makamu au mwenyekiti mwenyewe bila miadi kati yake na wewe na bila kujua nini dhumuni la wewe kuhitaji kuonana naye”. Akaongea mwanaume pekee kati yao ambaye ni kijana wa umri wa kama miaka 25 hivi.

“Hilo nalijua sababu nimeshaelezewa… Hivyo natakiwa kujua nyote mpo kwa ajili ya kunisikiliza?”

“Huko sahihi… Keti kwenye kiti icho na utupe utambulisho wako ule ambao ulijitambulisha na kule”. Dada mwingine naye kiumri akiwa mbichi tu akaongea huku mkono wake ukionyesha kilipo kiti ambacho Agent Kai anatakiwa kukaa.

“Naitwa Mr. Jayl Wang natokea Kedah ni mfanyabiashara mwenye maduka ya vifaa vya umeme Kedah na baadhi ya majimbo yaliyo kule Kedah…. Shida yangu iliyonileta hapa ninahitaji kufahamiana na mwenye hii kampuni ”.

“Karibu sana Mr. Jayl Wang, naitwa Amir Aron ni msaidizi mkuu wa mambo ya kibiashara katika ofisi hii ya makamu wa mwenyekiti, Yule pale mwisho anaitwa Mrs. Asha Malik yeye ni sekretari wetu hapa na huyu wa katikati ni Miss Verma Kapoor mesenja wetu lakini kwa ishu uliyokuja nayo wote tunaweza kukusaidia… Tungependa tujue kile ambacho tutamwambia boss wetu unachoona ni muhimu kuonana naye Mr. Jayl?!”. Akajitambulisha na kutambulisha wenzake kijana yule wa kiume.

“Nahitaji kufungua biashara ingine inayohusiana na uuzaji wa simu za mkononi, hivyo nimepita kwa mawakala wa aina za simu mbalimbali katika jiji hili la Kuala Lumpur hili nikapate kusaidiwa kupata mzigo wa uhakika kwa kiasi nachotaka na uhakika kupata nachohitaji kwa wakati na kikiwa na ubora zaidi… Nimesoma vipeperushi vyenu vya kibiashara Puteri Business Of Group nyinyi ni mawakala wa aina mbili kubwa za simu hapa duniani”. Kama kawaida yake Agent Kai uwa hashindwi kudanyanya hili kupata anachohitaji.

“Huko sahihi PGB sisi ni mawakala wa kampuni ya HTC na LG, ingawa pia tunazo na za aina nyingine kampuni karibia zote unazozijua hata zile zenye mawakala wao hapa”.

“Safi sana… Nafikiri si muhimu kuonana na wakuu wenu nyinyi tu mnatosha kuniunganisha na biashara hii nayotaraji kuanzisha, kesho nitakuja na mtaalamu wangu wa sheria hili kuingia nanyi mkataba wa kwanza kunifanya nikawa wakala wenu katika Kedah na maeneo mengine kule… Mwanzo niliogopa nikifikiri kutakuwa na vikwazo ndiyo maana sikuja na mwanasheria wangu kabisa”.

“Kampuni yetu haina matatizo kabisa linapokuja suala fursa kwa wajasiamali wadogo kama wewe… Usiwe na wasiwasi nah ii haja ya kukutana na wenye kampuni unaweza ukakubaliana na sisi kisha tutakukutanisha na meneja tu mkaingia mkataba”.

“Ahsanteni sana wote kwa pamoja kwa ukarimu wenu, kesho nitafika hapa kumaliza suala hili”. Akasema huku anainuka Agent Kai kisha akampa mkono kijana yule wa kiume ajulikanaye kama Amir Malik.

“Karibu sana mkuu… Usikose kufika kesho ufurahie huduma yetu”. Akasema dada aitwaye Miss Verma Kapoor.

Agent Kai wakati akitoka ndani ya ofisi hizi kichwani alikuwa akifikiria kama kuna umuhimu yeye kurudi tena hapa kufanya uchunguzi mwingine, alitizama saa yake ya mkononi iliyomtambulisha ni saa saba kasoro dakika kumi na nane. Lakini kabla hajafika zilipo lifti, lifti ile mlango ukafunguka na wakatoka wanaume wawili toka kwenye lifti ile na waliganda kwenye kizingiti kama wakimshangaa mtu aliyekuwa akitaka kubonyeza swichi ya lifti, walikuwa na watu waliomzidi umri kwa ukadirio ni watu wazima.

Macho yao yalimjulisha Agent Kai kuwa anaangaliana na watu walio katika huduma moja na yeye huduma ya kazi zaidi ya kazi, kazi za michezo ya gizani lakini si uchawi ingawa wapo wanaotumia uchawi katika kazi hizi za hatarishi.

Hakutaka kuonyesha amestuka lakini haraka aliruhusu ubongo wake ufanye kazi kwa haraka asije ingia katika matatizo akaamua kuwasalimu.

“Habari zenu?”. Salamu iliambatana na hatua zake za kuelekea kizingitini hili wampishe lakini alistaajabu alipozibwa asipite, hapo akakunja uso kuwaonyesha hajaridhika na tukio lile.

“Nimetoa salamu lakini hakuna kati yenu aliyejibu halafu mnasogea kuniziba nisipite nini tatizo lenu?”. Agent Kai akaongea huku kasimama karibu yao akili yake ikikinzana na moyo wa matamanio uliokuwa ukitamani atoe bastola kujihami kabla wao hawajamtolea bastola.

“Unaitwa nani?”. Mmoja aliyekuwa na mwili uliojaa zaidi kuliko mwenzake akamuuliza na papo hapo Agent Kai akahisi atakuwa amestukiwa.

“Nyinyi ni polisi?” Akajitutumua kuwauliza na uso wake akiwa kauweka katika hamaniko la hofu.

“Sisi ni wanausalama kutoka idara ya usalama wa taifa ya Defence Staff Intelligence Division ‘DSID’ tupo katika mambo ya uchunguzi wa mauaji yaliyotokea hapa Kuala Lumpur juzi na jana… Tuna wasiwasi na wewe kwa namna moja ama nyingine, hivyo tunakuomba kwa mahojiano”.

“Mimi ni mtu mwema tu ila si vibaya mkinihitaji kwa ajili ya mahojiano kama mnaona ni sahihi kwa kazi yenu… Kabla ya yote nahitaji vitambulisho vyenu”. Agent Kai akajibu huku akitafuta namna gani ataweza kujikwamua kwa watu hawa ambao mikono yao kuwa sehemu ambazo wanahifadhi silaha zao ilimjulisha anaingia matatani muda si mrefu, akaona wanaangaliana na yeye akatumia fursa hiyo kugeuza shingo yake kule kwenye lango la kuingilia ofisi ya PGB. Akapna walinzi wote wawili wanajongea wakiwa wanakuja kusikiliza kuna nini? Na mmoja akajikuta anauliza.

“Mr. Sauez… Mr. Sauez… Boss! Vipi hapo?”. Akauliza mlinzi mmoja na hapo Kai akajua kati ya watu wale walio mbele yake mmoja anaitwa Mr. Sauez na wale walinzi wanamjua. Ni kweli hapa walikuwa ni Sauez Mallam akiwa kaongozana na mtu toka idara ya upelelezi ya polisi ambaye ni rafiki yake na alikuwa ameongozana naye kuja naye hapa kwa ajili ya kuandika ripoti ya kiuchunguzi ya uongo dhidi ya ajali ya kusababishwa iliyofanywa kwa ufasaha na Agent Kai siku ya jana mchana viunga vya Broga Hill, Bambino Village Hotel.

Ripoti ilikuwa ikihitajika idara ya upelelezi sababu waliouliwa ni waajiriwa PGB na gari yao waliyokuwa wakitumia ni mali ya PGB, muda huo ndiyo ilikuwa ni muda waliokubaliana na bwana Sauez Mallam wafike hapo kwa kupika ripoti inayohitajika.

Bwana Sauez Mallam alihisi kitu wakati wanaangaliana machoni na Agent Kai pindi tu lifti ilipofunguka na kukutanisha macho na Agent Kai, umbo na urefu wa Kai ni kama nao ulimsaliti licha ya kuwa upo ndani ya suti. Afisa wa upelelezi naye alipoangaliana na Agent Kai aligundua si macho ya kawaida.

Wakati anaingia katika ofisi hizi Agent Kai alivua miwani yake ya kijasusi sababu ni miwani ambayo kwa mtu anayeijua hasa wahalifu, magaidi na hata majasusi walikuwa wakiijua sana hii miwani iliyotengenezwa kiteknolojia ya hali ya juu hasa hii ya CIA anayotumia yeye.

Hakuna jibu lililotoka zaidi ya wale watu kumkazia macho Agent Kai aliye ndani ya sura ya bandia.

“Sura yako tushaiona mahali naomba usijaribu kufanya ujanja wow..!”. Hakumaliza kuongea yule Sauez kwani lilifanyika jambo la ghafla sana, komando Agent Kai aliruka kwa kasi kumzunguka afisa wa upelelezi kwa kuwa alikuwa naye karibu kisha akamuwekea tundu la bastola kichwani huku yeye akiwa kaingia ndani ya chumba cha lifti (maajabu).

“Tulia! Lasivyo nakutawanya shingo kwa risasi”. Akamwambia, ilikuwa tendo la kasi mpaka wote waliokuwa pale waliona kama sinema. Walinzi wawili waliokuwa wanakaribia kusogea waliishia kuinua silaha zao juu kuelekezea pale kwenye kizingiti cha mlango wa lifti. Sauez Mallam naye bastola ilikuwa ipo mkononi mwake. Hakuna aliyeachwa na mshangao katika sura yake.

“Wewe! Acha kunitumbulia macho naomba hiyo silaha yako itupe chini upande ule kabla sijamdhuru mbwa mwenzako”. Agent Kai akaongea tena huku anamvuta kwa nguvu afisa wa upelelezi kuingia naye ndani zaidi ya lifti.

Lakini upande wa Sauez akiwa kajisogeza hatua tatu toka alipokuwa kasimama mwanzo alikuwa akijiuliza kama kweli anachowaza ni sahihi kuwa huyu aliye hapa ni Agent Kai au si yeye maana alikuwa akitamani kukataa anachoamrishwa anatamani atumie ujanja kumuokoa rafiki yake.

Akili yake ikawa inakinzana afuate kipi maana akiiweka chini bastola yake atakuwa karuhusu wao kufanywa atakacho mtu huyu aliye mbele yao, na je kama akiwa Agent Kai na wao ni mtu wanayemuhitaji kama bidhaa na si maiti akiwa mzima atajibuje kwa wenzake? Jasusi kama yeye tena jasusi mwandamizi aliyeasi kazi ya ujasusi kwa maslahi ya taifa na kufuata maslahi yake binafsi, atakuwa kafanya ujinga gani? Uzembe usio na majibu.

Alichokuwa akiwawaza kilisomeka machoni mwa Kai! Aliziona lugha alama za macho ya Sauez yakimuongelesha mtu anayemdhibiti, akatambua kwanini? Kwanini hataki kuitupa silaha yake kama alivyomuelekeza.

“Nilichosema hujanisikia au unafikiri nipo hapa kiutani?”. Akatoa sauti muungurumo Agent Kai hili kuipa nafasi akili yake iruhusu mwili kufanya tukio.

Mkono wa kushoto wa Sauez ulikuwa ukicheza kwa chati na kitaalamu, alichokuwa akikiongea akidhani anamwambia kiishara kificho afisa upelelezi kumbe pia na mtu wa kazi alifanikiwa kuona kwenye upenyo.

Ilitolewa ishara ya kutengenezwa ya O kidole gumba na shada vikigusana kwa kasi ya siri akavikunjua na kuleta mfano wa herufi C iliyoganda sekunde tatu kisha akatoa alama ya vidole vitatu napo akijitahidi kuiba mkono ukarudi katika hali yake, O iliwakilisha jicho na C ilimaanisha Count wakiwa na maana atahesabu mpaka tatu, Kai akatabasamu moyoni baada ya kuona kichwa cha anayemdhibiti kikikubali jambo.

Sauez akatoa ishara ya kuzuia walinzi wasisogee kisha akachezesha kopi kwa siri sana mara ya kwanza Kai naye akamuona, akachezesha mara ya pili, kabla hajaenda ya tatu likatokea la kutokea.

Kai hakutaka kusubiri itimie tatu sababu hakujua tatu itakuja na lipi? alimsukuma kwa nguvu mbele afisa wa upelelezi kisha akamuongezea teke la kukita la mgongoni ni kwa nukta tu ilikuwa, jamaa akamparamia Sauez na wote wakaenda chini Agent Kai hakuishia hapo alipiga vichwa vyao risasi na kuwatawanya maubongo sakafuni (hatari)

Wale walinzi licha ya kuwa ni walinzi wenye mafunzo ya kutumia silaha walipigwa na mshangao sababu hawakusikia mlio wa bastola ya Agent Kai, zaidi ya sauti ya kama mtu aliyepiga chafya ndogo. Wakati pale chini Mr. Mallam Sauez mwanaume wa kiarabu toka Syria na jamaa yake walikuwa wanamalizia kukamuka roho kikatilia (kimya), hapana chezea manati ya mzungu.

Kushangaa kwao walinzi wale kulimfanya Agent Kai kubonyeza namba za lifti akiruhusu zitembee kwenda chini floor ya tatu tu.

Walinzi walipostuka mlango wa lifti ulikuwa unajifunga wakafyatua risasi ambazo ziligonga kingo mlango wa lift kwani Agent Kai alijibanza pembeni na mara mlango ukajifunga. Milio ya bunduki ilistua watu wote walio ofisi ile, taharuki ikalipuka mayowe yakasikika hasa kwa wanawake.

Lifti ilitembea ilipofika floor ya kumi na mbili ilisimama na kufunguka, Agent Kai akatoka na hapakuwepo na mtu. Moja kwa moja akafuata ngazi na kuanza kuteremka mwendo wa haraka kwa kufuata ngazi zinazoelekea floor ya chini.

Masikio yake yalikuwa yakisikia makelele mengi tu huko chini na hata juu alipotoka na mara akasikia ving’ora vya magari ya polisi vikijia eneo hili. Akili yake ikafanya kazi alipokaribia floor ya nne toka chini aliweza kuona jinsi hali ya chini ilivyo na hata korido hii ambayo napo palikuwa na ofisi ya kampuni ambayo haijui alikutana na watu wengi wanaokimbia kutoka nje kufuata ngazi kama yeye, alipoona hivyo alitafuta sehemu iliyojificha chini ya ngazi.

Akavua sura ya bandia na koti la suti, tai nayo akaitoa akichomoa kamera yake na kubakiwa na shati la ndani la rangi bluu bahari, hapa akawa amefanikiwa kubadilika kubaki na sura ya Agent Kai halisi ile sura, shati na tai akavikusanya vikiizunguka ile sura na kuifanya ikawa kama mpira wa chandimu mkubwa akakamata mkononi vizuri kisha akatoka pale upenyoni bila kustukiwa na kuendelea na safari ya kukimbia akiwa kaongozana na wanawake wanne na wanaume watano waliovaa mavazi ya ofisi ya kuheshimiwa.

Uzuri bahati ingine ikaendelea kulala upande wake hakuna polisi aliyemsimamisha maana alijifanya kama kachanganyikiwa kweli kama watu wengine ambao nao walikuwa wamechanganyikiwa kwa milio ya risasi iliyosikika tena ikidabo dabo kushambulia, hivyo polisi wakawa wanaelekeza wapi waelekee huku kwa mbali aliwaona polisi wengine wakiwa wamejificha bunduki zao zikielekea ulipo mlango wa lifti, Agent Kai akatabasamu kujisifu ghiliba yake ilifaulu.

Haraka akaingia ndani ya gari yake na kuondoka eneo lile akiwa salama wasalimini.

‘Hatari sana… Nimeamini siku ikifika huwezi kukataa kuondoka , jamaa wale walikuwa wapi mpaka wakaja pale? Na je? Walinistukiaje kama ni mimi, nilivyovua sura itawajulisha kuwa ni mimi niliyefanya vile… Sasa ningetokaje bila kuvua ile sura? Cctv kamera ingewajulisha ni mimi tu maana system ya ulinzi ya majengo yote yenye maofisi makubwa ya kibiashara ipo usalama wa taifa’ Akawaza huku anaongeza mwendo. ‘Potelea mbali, shauri lao wakiamua kusambaza picha zangu napo ni tatizo, hii kazi itabidi nijitahidi niimalize mapema…Acha niende kumpelekea chakula LG, kisha nirudi Istana Negara kupumzika, nitaendelea na kazi usiku’ Akaendelea kuwaza.

Foleni ilikuwa kubwa kwa barabara hii ya Jalan Hang Kasturi hivyo ilimlazimu mara kwa mara kupunguza mwendo.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na tano (35)

Agent Kai ameweza kuingia ofisi ya Puteri Group of Business (PGB) kwa kujifanya mfanya biashara akafanikiwa kupata picha kadhaa za wafanyakazi wa PGB akiwemo boss mkuu bwana Logan.

Tumesoma akipata vikwazo wakati anaondoka wanatokea watu wawili wanajaribu kumzuia, baada ya kuona vikwazo vinazidi anatumia mbinu ya ujanja wa asili alionao ukichagizwa na ukomando alionao wenye uninja ndani yake Jasusi Agent Kai, sajenti wa zamani wa Navy Seals na mara zote hujiamini hashindwi anaruka kiwepesi wa ajabu mbele ya macho nane yaliyokuwa yakimtizama mbele manne nyuma manne, jasusi huyu hujaribu kuondoka matatizoni haraka anapohisi hatari, tumeona akiwafyeka kwa bila woga mbele ya walinzi na kisha kutokomea.

Hali ya taharuki inahumuka PGB Headqurter na wanausalama kufika.

Damia anaamua liwalo na liwe anashusha siri muhimu kwa Agent Kai na kumfanya jasusi huyu adhidi kuwasogelea watekaji.

Nini kitafuata katika hili?

Masikio yake yalikuwa yakisikia makelele mengi tu huko chini na hata juu alipotoka na mara akasikia ving’ora vya magari ya polisi vikijia eneo hili. Akili yake ikafanya kazi alipokaribia floor ya nne toka chini aliweza kuona jinsi hali ya chini ilivyo na hata korido hii ambayo napo palikuwa na ofisi ya kampuni ambayo haijui alikutana na watu wengi wanaokimbia kutoka nje kufuata ngazi kama yeye, alipoona hivyo alitafuta sehemu iliyojificha chini ya ngazi.

Akavua sura ya bandia na koti la suti, tai nayo akaitoa akichomoa kamera yake na kubakiwa na shati la ndani la rangi bluu bahari, hapa akawa amefanikiwa kubadilika kubaki na sura ya Agent Kai halisi ile sura, shati na tai akavikusanya vikiizunguka ile sura na kuifanya ikawa kama mpira wa chandimu mkubwa akakamata mkononi vizuri kisha akatoka pale upenyoni bila kustukiwa na kuendelea na safari ya kukimbia akiwa kaongozana na wanawake wanne na wanaume watano waliovaa mavazi ya ofisi ya kuheshimiwa.

Uzuri bahati ingine ikaendelea kulala upande wake hakuna polisi aliyemsimamisha maana alijifanya kama kachanganyikiwa kweli kama watu wengine ambao nao walikuwa wamechanganyikiwa kwa milio ya risasi iliyosikika tena ikidabo dabo kushambulia, hivyo polisi wakawa wanaelekeza wapi waelekee huku kwa mbali aliwaona polisi wengine wakiwa wamejificha bunduki zao zikielekea ulipo mlango wa lifti, Agent Kai akatabasamu kujisifu ghiliba yake ilifaulu.

Haraka akaingia ndani ya gari yake na kuondoka eneo lile akiwa salama wasalimini.

‘Hatari sana… Nimeamini siku ikifika huwezi kukataa kuondoka , jamaa wale walikuwa wapi mpaka wakaja pale? Na je? Walinistukiaje kama ni mimi, nilivyovua sura itawajulisha kuwa ni mimi niliyefanya vile… Sasa ningetokaje bila kuvua ile sura? Cctv kamera ingewajulisha ni mimi tu maana system ya ulinzi ya majengo yote yenye maofisi makubwa ya kibiashara ipo usalama wa taifa’ Akawaza huku anaongeza mwendo. ‘Potelea mbali, shauri lao wakiamua kusambaza picha zangu napo ni tatizo, hii kazi itabidi nijitahidi niimalize mapema…Acha niende kumpelekea chakula LG, kisha nirudi Istana Negara kupumzika, nitaendelea na kazi usiku’ Akaendelea kuwaza.

Foleni ilikuwa kubwa kwa barabara hii ya Jalan Hang Kasturi hivyo ilimlazimu mara kwa mara kupunguza mwendo.

ENDELEA NA UHONDO..!

MAPIGO YA KIFUNDI II

“Piiiii! Piiiiii! Piiiiii!”. Ulikuwa ni mlio wa honi ya gari aina ya Escudo ukipigwa nje ya geti la nyumba la mwanadada Damia Abdulrahman a.k.a Language Girl (LG) mtaa wa Taman Bukit Kalil barabara ya Jalan Bayan, eneo la Melaka”.

.

Ndani ya Escudo walikuwemo Nawaz Patrash, Ghulam Qaresh na Bayan Uugun-Bayar, honi zile zilimfanya mtu anayehusika kufungua geti muda huo kuja kufungua geti. Alikuwa ni mama mtu mzima akiwa kava baibui la rangi nyeusi na madoa meupe.

Mawazo yake ilikuwa anamfungulia bosi wake, mawazo yalikutana na kitu tofauti alikutana na sura ambazo anazijua kwa kuziona mara moja moja kwa kila mmoja kwa wakati wake wanapokuja kwa rafiki yao, mshirika wao na swahiba wao LG.

“Karibuni jamani!”. Akaongea mama yule kwakuwa wale wote walio ndani ya gari alikuwa akiwafahamu kuwa wana ukaribu mkubwa na anayemuita yeye kuwa ni mwanae yaani Damia.

“Yupo mama Cute?”. Akauliza Nawaz Patrash wote wakiwa hawajashuka ndani ya gari.

“Hayupo alitoka akituambia anaondoka kwenda kwenye kikao na wafanyabiashara wenzake na akatuambia kuna mawili anaweza akarudi usiku sana au asubuhi ya mapema”. Akajibu mama yule tena akiwa na uhakika na akizungumzacho.

“Alitoka saa ngapi?”. Safari hii akauliza Ghulam Qaresh huku akiitoa miwani yake ya jua machoni mwake.

“Alitoka saa nne kamili hapa!”.

Jibu hili liliwafanya walio ndani ya gari wote watatu kuangaliana na kisha kama wameambiana wakaangalia saa zao.

Na ghafla simu ya Mr. Nawaz Patrash ikaita na cha ajabu wote wakastuka kwa mlio ule wa simu kama ni kitu cha ajabu kwao, kabla hajapokea akiwa anaangalia jina la mpigaji, simu ya Mr. Ghulam Qaresh nayo ikaita kwa kasi na wote wakatizamana tena Nawaz na Ghulam.

“MP anapiga kwangu, wewe nani anakupigia?”. Akauliza Nawaz Patrash kumuuliza Ghulam Qaresh.

“Mlinzi wa mlangoni PGM yule Qassim, pokea ya boss kwanza huyu nitampigia acha ikate”. Akajibu Mr. Ghulam na kufanya Nawaz atingishe kichwa kukubali.

“Halloow!”. Akaongea Mr. Nawaz Patrash baada ya kupokea simu kisha akaweka loud speaker wenzake wasikie baada ya upande wa pili kuwa kimya licha ya yeye kupokea.

“Halloow! Boss?”. Ikabidi aite tena.

“Nawaz! Mjinga kavamia ofisini kaua watu wawili… Ameo.. ameondooka,… amemuondoa Sauez, amemuua rafiki yetu, swahiba wetu Sauez… Sauez marehemu sasa Nawaz!”. Sauti ya uchungu ilisikika upande wa pili, Mr. Logan Puteri alikuwa akilia, huzuni kubwa ikawakumba waliokuwa wakipokea taarifa maana simu ilisikika vizuri sana.

“Ilikuwaje? Ameweza kujua kama tunahusika… Amemteka Damia, yes! Hii inatufahamisha anamshikilia Damia…!”. Akaongea kwa sauti ya kukwaruza Mr. Nawaz Patrash huku akigeuka kuwangalia wenzake kwa zamu akianza na aliye nyuma ya siti zao wao walio mbele Uugun na kumalizia kwa Ghulam Qaresh.

“Hamjamkuta Damia kwake?”. Akauliza kwa hamaki Mr. Logan Puteri.

“Yes! Hatujamkuta hapa kwake… Na hii inahakikisi wasiwasi uliokuwa nao mkuu”.

“Haraka sana nawaombeni tukutane Rodger Street… Maafisa wa polisi pamoja na maafisa wa usalama wa taifa nao wanaelekea huko.. Itakuwa vizuri kuonana ana kwa ana na mkuu wa kitengo cha RDPMD au hata DSID maana kanipigia kachero Hamza ameniambia wanakuja wote hao sababu wanashangaa kwanini maslahi ya PGB yanaguswa kila siku kwa siku tatu mfululizo”.

Akasema Mr. Logan na kisha akakata simu bila kusubiri Nawaz ataongea nini.

“Ooooh! Puuuh! Hii hatari sana”. Akapumua kwa nguvu Nawaz Patrash na kisha kuongea na mara akajifuta jasho kwa kitambaa jasho.

“Twendeni tuwai PGB, Rodger Street!”. Akaongea tena kisha akamuonyesha ishara Ghulam Qaresh apindue gari hili waondoke.

Wote ndani ya gari ni kama walikumbwa na ganzi hasa hawa wawili bwana Nawaz na Ghulam ukiacha Uugun kijana wa kimongolia mwenye kujiamini sana katika mambo ya kiharamia.

***** ***** *****

Agent Kai akiwa bado ndani ya gari akiwa katokea kununua chakula cha kumpelekea mfungwa wake huru Damia Abdulrahman Language Girl (LG) baada ya kutoka kufanya tukio lililovuta vikosi vya kiusalama vya jijini Kuala Lumpur kuelekea mtaa wa Rodger Street barabara ya Jalan Hang Kasturi, yeye alikuwa akiweka vizuri simu yake baada ya kuchomeka kifaa chake kidogo alichokiunganisha na simu yake kisha kukipachika sikioni hili aongee kwa simu.

“Hallo! Mama yangu! Asallaam aleykhuum?”. Akasalimu huku tabasamau likijiunda usoni mwake uso ambao ulikuwa huru muda huu kutokana na kutokuwa kava sura ya bandia.

“Waleykuum Sallaam mwanangu , za huko ulipo mwanangu?”. Mama yake ajulikanaye kama mama Kai au bibi Rahman alijibu huku naye furaha ikiwa kubwa sana.

“Huku nzuri mama… Nafikiri keshokutwa jumapili au jumatatu nitakuwa nimemaliza majukumu ya huku na kisha kurudi Marekani kisha baada ya wiki nakuja huko nakuletea na mgeni wako”.

“Waooh! Mwanangu mgeni gani tena huyo?”.

“Dua zako mama ndiyo kipaumbele muhimu… Mama nimewamisi kupitiliza nakuja kukaa huko miezi miwili hili mgeni ajifunze na Kiswahili kabisa”.

“Inshaallah mwanangu nakuombea dua ufanikiwe katika kazi iliyokupeleka huko mbali na urudi kwa wajukuu zangu salama kisha uniletee mgeni wetu maana si wangu peke yangu”.

“Ahsanteee! Mama yangu, inshaallah dua lako halijawai kukwama, mashaallaah mama yangu umejaliwa dua jema kwangu mara zote… subiri nakuja mama pengine kama itapita sana haipiti wiki mbili”.

“Sawa mama! Nitakupigia kesho asubuhi, naomba usiache kuniombea dua kila dakika”.

“Inshaallah sitaacha hilo… Nashukuru leo nimeongea na kina Rahman na shangazi yao, jana walinipigia leo nimewapigia… Wanasema toka uondoke wameongezewa ulinzi mkubwa sana, kwanini imekuwa hivyo?”.

“Mama usijali kuhusu hilo…. Kila kitu ufanyika kwa maana Fulani, mimi sijajua kama ulinzi wa kawaida ambao niliuacha wameongezewa maradufu zaidi, ila ni jambo la kheri si unajua mwanao mimi ndiyo mlinzi wa wajukuu zako na familia yangu kwa ujumla sasa sipo na serikali ya Marekani ni serikali sikivu yenye kujali watu wake hasa sisi wenye kazi maalumu”.

“Haya sawa mwanangu… Naomba upendo wao uendelee kama ulivyo”.

“Sawa mama… Baki salama hapo nyumbani wasalimie na ndugu zangu wengine wote waambie nitaonana nao hivi karibuni”.

Aliagana na mama yake kisha akakata simu na kabla hazijavuka sekunde tano ikatoa muito wa kujulisha kuna mtu anapiga. Akatizama nani mpigaji na kukutana na jina la Shufania.

“Hallo! Asallaam Aleykhuum!”. Akakutana na salamu baada ya kupokea tu.

“Aleykuum Sallaam! Vipi hali mpendwa wangu?”. Akamjibu na kumuuliza.

“Safi tu… Mbona kimya mpendwa wangu?”. Naye akajibu na kuuliza.

“Nipe masaa mawili utaniona hapo”.

“Kwani huko wapi saivi?”.

“Niko Bazar Banting, fish sales kuna mteja wa mbolea nilimpata asubuhi nimemuhifadhi huku naenda kumuona na kufanya naye mahojiano kidogo”.

“Okay! Leo tumeogopa kwenda msikitini hivyo swala ya ijumaa tumeswalia hapa hapa… Vipi wewe ulipata muda wa kuswali kweli?”.

“Sikupata mpendwa… Nikija tutaongea vizuri maana nahitaji kupumzika kwa kujilaza kidogo hivyo nitakuja pumzika huko Istana Negara”.

“Sawa! Mimi sili nakusubiri ufike tule wote”.

“Sawa sawa nitajitahidi kuwai kama ndiyo hivyo… Nikuage maana nimefika nilipokuwa nakuja mpendwa”.

“Okay! Kazi njema… Nakupenda sana”.

“Nakupenda pia”.

Wakaagana na wote wakakata simu zao.

Kwa kutumia rimoti ya getini ambayo nayo ni miongoni mwa vitu alivyokuwa kakabidhiwa na mlinzi wa nyumba hii, alifungua geti baada ya kuliamrisha lifunguke kwa rimoti ile na kisha akaingiza gari huku akiwa kahakikisha usalama wake hakuna kiumbe kinachomfuatilia.

Baada ya kupaki gari vizuri akashuka na mizigo yake yote aliyokuja nayo yakiwemo mapoti mawili ya chakula, nguo aliyoviringisha kwa pamoja na sura ya bandia, akabonyeza rimoti tena na kulifunga geti kisha akafungua mlango wa mbele wa nyumba na kuzama ndani.

Alipitia jikoni akachukua sahani ya chakula kweye kabati la vyombo akaambatanisha na kijiko na akaelekea kwenye chumba alichomuacha Damia (LG).

“Habari yako?”. Akamsalimu Damia baada ya kufungua mlango na kalalia kiubavu kwenye godoro huku uso wake ukijidhihiri vile anavyojisikia vibaya kutokana na kufungwa mikono na miguu na mtu ajuaje jinsi ya kumfunga adui yake.

“Habari si nzuri kabisa”. Akajibu LG huku akijitahidi kuinua mgongo wake apate kukaa kitako.

“Kwa sababu ya mwanao? Au kwasababu ya kukufungia humu ndani?”. Akamuuliza.

“Mikono yangu haipitishi damu vizuri pia hata miguu nahisi kupoteza matumaini kaka yangu, ganzi mikononi”. Akajibu na papo hapo alikuwa kafanikiwa kujiinua akawa amekaa kwa matako.

“Ni mara ya kwanza unafungwa hivi?”. Akauliza Agent Kai na tayari alikuwa kashapanga mapoti kwenye meza na akajiweka kwenye kiti akiwa na laptop yake mkononi.

“Ndiyo kaka… Mimi sijawai shikiliwa mateka katika nyakati zangu zozote za mambo ya kihalifu na siku zote nilikuwa nikiomba isinitokee kama hivi sababu mimi ni mtu ambaye kazi yangu ni ukalimani tu, sijui kingine chochote”.

“Hujui kitu kingine chochote, je hujui kutumia silaha?”.

“Najua kutumia bastola lakini si mzuri sana kwenye shabaha.. Naomba nisaidie kaka niligeze kamba hizi”.

“Nimekuletea chakula… Tambi, nyama rosti na juisi ya matunda mchanganyiko, nitakufungua mikono hili ule lakini kabla ya yote naomba tuongee kidogo kuhusu kazi hii iliyotukutanisha”.

“Naomba kaka weka ubinadamu kidogo sura yako nzuri hailingani na unachonifanyia.. Pia naomba nile kwanza ndiyo uniulize maswali yako”.

“Sawa nitakusaidia utakula huku unajibu maswali yangu”. Akasema Agent Kai kisha akamsogelea dada yule kwenye godoro akamnyanyua kwa kumbeba mpaka kwenye meza aliyoweka chakula akamkaliza kwenye kiti.

“Nakutendea haki lakini huko walipo kina Detective Marie mnawatesa sana”. Akamwambia baada ya kumkalisha kwenye kiti na kuanza kumpakulia chakula akamuwekea kwenye sahani ikafuata juisi akamuwekea kwenye glasi.

Akarudi kwenye mikono yake aliyomfunga akafungua nyaya zile alizozifunga barabara na kumpa tabu ya kweli mwanadada huyu.

“Karibu chakula madam!”. Akamwambia yeye akasogea alipoacha kiti chake na kompyuta yake mpakato.

Haraka bila kupoteza muda akaunganisha kamera yake ndogo iliyotengenezwa kama pini ya kuibana tai akaivalisha kwenye chombo chake kilicho kama modem na kuingiza kwenye kompyuta.

Hakuwa bwege umakini ulikuwepo pia katika kumuangalia LG maana siku zote Agent Kai alikuwa hapendi kujiamini katika suala la usalama wake anapokuwa na mtu yeyote aliyewai kuwa gaidi, jasusi au hata mwenye mafunzo yoyote yale.

“Nimetoka Rodger Street ofisi za PGB… Sikumkuta Mr. Logan wala mke wake ambaye ni makamu wa mwenyekiti wa kampuni ya boss wenu anayoitumia kujificha kwenye jamii aonekane yeye mtu safi asiye na doa, wakati natoka pale nikiwa nimetoka kufanya maongezi ya uongo na wasaidizi wa ofisi ya makamu wa mwenyekiti katika kizingiti cha lifti nilikutana na watu hawa”. Aliongea Kai na kisha akageuza kioo cha laptop kumgeuzia Damia ikiwa kagandisha picha za wanaume wawili waliosimama kwenye lifti iliyofunguka kizingitini.

Damia alibaki akiwaangalia watu wale kwenye screan ya laptop.

“Mmoja hapa anaonekana anaitwa Sauez… Naomba kujua wao ni kina nani katika ofisi ya PGB?”.

Alimbandika swali.

“Mimi sijaajiriwa PGB Hivyo vyeo vya pale sivijui vipo vipi na wala siwezi juwa hao wana vyeo gani”.

“Mi jasusi na pia mimi ni komando tena niliyefudhu kwa maksi za juu sana, nimeona macho yamenijibu unawajua ni nani hapa au unamjua hata mmoja wao, niambie majina yao?”.

“Kushoto ni Mr. Sauez Mallam ni mtu mmojawapo kati ya watu wa Mr. Logan Puteri na pia ameajiriwa PGB… Huyu wa kulia ni afisa wa upelelezi wa jeshi la polisi la Malaysia ni maarufu sana hapa Kuala Lumpur na ni rafiki mkubwa wa Mr. Logan Puteri anaitwa Moussa Zamari”.

“Ahsante sana kwa majibu yako…. Bahati mbaya wametangulia kwenye haki baada ya kutaka kunichukua wakifikiri mimi ni saizi yao nikawawai”.

“Eeeh! Mmemuua Sauez?”. Damia alistuka na kuuliza kama vile hajasikia habari aliyopewa.

“Kwa bei rahisi tu sababu imelazimu… Nataka nijue anapoishi Mr. Logan Puteri, nahitaji kwenda kumtembelea nyumbani kwake… Niambie madam? Na nafikiri hii ndiyo picha yake kamera yangu ilichukua”. Akamwambia huku anamuonyesha tena screan ya laptop ikiwa ina picha kaigandisha ambayo imo ndani ya fremu.

“Ndiyo ni yeye”. Akajibu Damia kukubali mwanaume mwenye sura iliyonona nona pesa na kuonyesha ni mtu asiye na shida kabisa.

Damia alibaki akijiuliza aelekeze au asielekeze na hilo Agent Kai aliligundua wakati anamtizama kiusaili wa kijasusi.

“Unajua madam kitu ambacho wewe hujakijua ni kuwa kuisha kwa kazi hii mapema ni kukurahisishia wewe na mwanao kuonana mapema… Hivyo vyovyote unavyofanya fanya kwa manufaa ya mtoto wako”.

Maneno lainishi toka kwenye kinywa kinachojua kutumia fursa inayojitikeza mbele yake yalimfanya Damia Language girl awe njia panda, alifikiria kuhusu mtoto wake akamvuta kichwani na kufikiria jinsi gani mtoto wake anavyompenda na jinsi gani asivyowezaga kukaa mbali na mwanae zaidi ya wiki, bado akafikiria kuhusu mtego, je? Agent Kai hamtumii yeye kusaliti wenzake kisha akamkabidhi kwenye vyombo vya usalama kama alivyomwambia asubuhi.

“Kaka nitaaminije kama unanitumia tu? Mimi si chizi asubuhi uliniambia kuwa utanikabidhi kwa vyombo vya usalama vya nchi hii, hivi huoni kwa rekodi watakazokabidhi CTU, CIA na hata FBI juu ya ugaidi zitafanya mi nifungwe na kumkosa mwanangu nikamuacha aishi bila malezi yangu? Simama kama mzazi kaka yangu, angalia mi sina ndugu nimjuaye mimi nimelelewa kituo cha kulelea watoto yatima tu”. Akaongea Damia LG na kwa jinsi alivyokuwa akiongea kidogo akaulainisha moyo wa Agent Kai.

“Nitakusaidia katika hili ni kweli mtoto wako ananishawishi nikusaidie… Sijawai kuwa na ahadi ya uongo kwa watoto naahidi ukinisaidia nikatimiza kazi hii basi wewe nakuachia moja kwa moja kama kwamba ukuwemo katika kadhia hii”. Akamwambia na ikiwa Agent Kai anasema kwa kumaanisha basi uwa anamaanisha hivyo.

“Ahsante sana kaka… Mi nilishaacha ugaidi na sipendi uhalifu niko tayari kukusaidia, tena kiroho safi kabisa. Ombi langu kwako isipite siku ya kesho kutwa bila kukamilisha kazi yako nikarudi kwa mwanagu na unilinde kabisa na vyombo vya usalama”.

“Okay! Niambie yale ambayo unahisi ulinificha asubuhi”.

“Nilikuficha kuhusu kikao ambacho kilikuwa kinafanyika eneo la Kepong Metropolitan Lake kuna jumba linaitwa nyumba ya nyoka kiserikali linafahamika kama ghala la kampuni ya PGB… Kundi la Mr. Logan ni kundi ambalo ni la siri sana halifahamiki sababu lipo chini ya wataalamu ambao zamani ama siku za nyuma walikuwa ni watu wa usalama wa taifa wa nchi fulani, magaidi walioamua kuacha ugaidi”. Mwanadada Damia uzalendo ulimshinda akaanza kufunguka siri alizokubaliana na Mr. Logan kuwa hata iweje hataweza kutoa siri ya kundi hili. Imani na maamuzi hataki tena kuwa mtumwa wa uhalifu hili amlee mwanae kwa amani kwa sababu hata pesa alijihisi zinamtosha.

“Endelea madam! Harakisha mambo hili tuyamalize haya kwa haraka jamaa wakatiwa nguvuni na wewe ukawa free!”. Agent Kai aliyekuwa na haraka ya kujua mambo ya kundi hilo aliuliza kisha akaiweka simu yake juu ya meza hili irekodi vizuri maongezi hayo muhimu.

“Kampuni ya PGB imewaajiri watu wanaomsaidia katika shughuli hizo za utafutaji pesa kwa njia ya ujanja ujanja… Kile kikundi ambacho kilishirikiana name kukuteaka ni kikundi ambacho hakikuwa rasmi katika kushiriki kwao mambo ya siri kubwa ya bwana Logan, huwezi amini kile kikundi kilikuwa kikifanya kazi kupitia kwangu kama muunganishaji baina yao na Logan, walitumika kufanya mambo ambayo hata kama serikali ingestuka wahusika kuwa kina nani basi walitakiwa kutomtaja bwana Logan kwa namna yoyote ile iwayo… Walishiriki kuteka maprofesa, na hata wapelelezi toka nchini mwenu lakini kazi yao iliishia hapo hawakajua hata walipelekwa wapi sababu walipewa malipo yao na kuwakabidhi kwenye mikono ya Mr. Logan Puteri mwanaume anayependa sana kumiliki pesa nyingi, mwnye ndoto za yeye kuwa tajiri mkubwa sana katika dunia hii bila kujali kaingizaje pesa hizo”. Alisimama hapo baada ya Agent kai kumkatizia.

“Nipe majina ya watu wote anaoshirikiana nao Mr. Logan Puteri na unahisi nani anaweza kuwa anajua siri za walipo mateka anaowashikilia?”.

“Yaani unamaanisha wafuasi wote wa kundi letu?”. Akajibu kimtindo wa yeye kuuliza swali hili aunde jibu humo sababu hakuwa ameelewa.

“Yaah! Na kama simu yako ina picha zao ningetamani kuziona”.

“Picha zao sina ila majina inawezekana kukupa”.

“Sawa tiririka majina yao na kila mmoja anaishi wapi hili usiku wa leo mpaka kesho nifunge hii kazi”.

“Sawa…. Msaidizi wake ambaye pale PGB ni mhasibu mkuu anaitwa Mr. Nawaz Patrash anaishi Pangsapuri Cempeka, Merdeka villa barabara ya Jalan Merdeka nyumba namba PCM/V 555…. Mbona huandiki kwenye diary yako?”. Akaanza maelezo Damia lakini akasimama baada na kumuuliza Kai.

“Endelea tu kuna kifaa kinaandika kwa kasi zaidi hahahah! Usihofu madam!!”. Akamjibu hivyo kwakuwa maelezo alikuwa akiyerekodi kwenye simu yake ambayo ilikuwa mezani.

“Sawa mkuu… Nimeamini maelezo niliyoambiwa na rafiki yangu mmoja jasusi wa Joint Intelligence Committee ‘JIC’ ya India siku nakufuata kukupokea Airport kuwa wewe ni namba moja isiyo na mashaka kabisa na siku ya pili nilivyompigia umetutoroka akanijibu si rahisi kumpata mtu ambaye alikuwa anapambana na makomandoo wenzake wa nchi zinginewaliokubuhu… Nakubali wewe si mtu wa kawaida na hata kama usingenipata mimi naamini ungetufikia tu, sijui ni mbinu gani uliyotumia kunifuatilia na hata kunijua ni mimi niliyejifanya Detective Marie maana kati ya wale watu wa kwanza wote ulioweza kuwafyeka hakuna aliyekuwa akijua natokea wapi zaidia ya kuniona kwenye misheni zetu au kwao pale Nadau Golf… hongera kaka!”. Akaendelea kuongea maongezi ambayo Kai hakuyapenda kwakuwa aliona yanampotezea muda.

“Endelea Damia… Vyombo hivyo mi nitavitoa, yafunike tu mapoti. Nipe mtu wa pili anaitwa nani?”.

“Ni mzee Mr. Ghulam Qaresh ni mhindi na yule Nawaz Patrash ni Mpakistan… Mr. Ghulam Qaresh ni mhindi aliyeachana na jeshi akiwa na cheo kikubwa cha usajenti ni komando huyu kwa pale PGB ana cheo cha msaidizi wa mhasibu yaani yeye ndiyo msaidizi wa Nawaz Patrash hivyo ofisi yao ni moja hapa Kuala Lumpur anaishi Block A, Rumah Pangsa Kos Rendah barabara ya Jalan TP 7 Tun Perak nyumba namba BLR/JT7 409… Mtu wa tatu Na ndiye alikuwa kiongozi wetu watatu ni yule uliyemuua leo Mr.Sauez Mallam sina haja ya kumuelezea tena….Wanne ni Ally Kareem yeye ni mlinzi mkuu wa Mr. Logan Puteri huyu ni Msyria na anatokea idara ya usalama wa taifa ya kule ni mtu anayeaminiwa sana na Mr. Logan ni mtu anayesifiwa ukatili mkubwa sana na muuaji mkuu wa kikundi hiki kisicho na jina, anapotokea mtu anatakiwa kuuliwa iwe kwa siri au mbele yaw engine wote basi yeye ndiye uinua silaha kumuua huyo mtu, anaishi mtaa mmoja na anaoishi boss wetu Mr. Logan alimnunulia nyumba mtaa ule maarufu nyumba hiyo wakiishi familia mbili yeye Ally na mtaalamu wa kundi lile wa kompyuta msyria mwenzie anayeitwa Hassan Saddiq ambaye pia ni IT mkuu wa PGB wanaishi moja wa mtaa wa watu wazito sana hapa Kuala Lumpur kati kati ya mitaa kadhaa ambayo kuishi huko unahitajiwa uwe mzito mfukoni, mtaa wa Dewan Negara eneo hilo umaarufu wake ni kutokana ni eneo ambalo lipo bunge la nchi hii… Boss anaishi nyumba namba DN/KL 277 jumba lenye hekari tano kieneo, ukipita hapo linafuta jumba la waziri wa mambo ya utalli na mazingira kisha waziri wa usalama wa nchi upande wa pili inatizamana na nyumba ya Ally Kareem na Hassan Saddiq nyumba yao ni__”. Hakuendelea kuongea mlio wa simu ya Agent Kai iliyo mezani uliwastua wote.

“Shit! Nani tena anapiga?!”. Akaongea Agent Kai na kuiinua simu, alipoitizama simu namba ni za Balozi Kapteni Jones Lebrons. Haraka akainyanyua simu upesi na kisha kupokea baada ya kuibandika sikioni.

“Halloo! Kapteni”. Akaongea kwa sauti ya haraka.

“Huko wapi?”. Upande wa kapteni ukauliza kwa sauti inayoonyesha yupo kwenye haraka sana.

“Banting Bazar, fish sales… Vipi mzee?”. Naye akamjibu kwa pupa vile vile.

“Dharura… Haraka sana naomba tuonane Sungai Wang Plazza, Time Square Pavillion kuna mambo nataka kujua toka kwako kwanza… Fanya haraka sana mi natokea nyumbani kwangu nilikuja lunchtime saa kumi kamili kuna kikao baina ya waziri wa ulinzi wa hapa, waziri wa usalama wa nchi pamoja na waziri mkuu katika ikulu ya waziri mkuu… Inahusu yanayotokea baada ya mauaji ya mchana PGB”. Akaongea Kapteni.

“Sawa mkuu nitajitahidi kukimbia niwai maana muda nao umekimbia sana saivi ni saa nane na nusu”. Akajibu Agent Kai na akakata simu.

“Damia! Naomba niachie mimi kuhusu wewe, tafadhali achana na tamaa zozote kuhusu kusaidiana na Logan… Nakuacha humu ndani ukiwa huru naomba jifungue miguu yako na uwe huru ndani ya chumba, nitakufungia kwa nje tu na kama unavyoona choo na bafu vyote vipo. Angalizo usijaribu kutoroka sababu tayari nina walinzi nimewaleta”. Agent Kai aliongea kwa kasi huku akipaki vitu vyake kwenye begi lake ambalo muda wote uwa nalo bega kwa bega.

“Nashukuru kwa kuniamini kaka Agent Kai, nakuahidi hakuna baya nitakalofanya sababu sina uwezo huo”. Akajitetea Damia hili awe angalau huru wa mateso ya kutofungwa mikono na miguu.

“Tutaonana baadaye mpendwa madam..!”. Akatoka na kumfungia kwa nje akiwa kamuacha huru wa kutokumfunga kamba miguu na mkono.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na sita (36)

Hali ya taharuki inahumuka PGB Headqurter na wanausalama kufika.

Damia anaamua liwalo na liwe anashusha siri muhimu kwa Agent Kai na kumfanya jasusi huyu adhidi kuwasogelea watekaji.

Nini kitafuata katika hatua zinazofuata ambazo tunaona karata zikichangwa kwa pande zote mbili upande wa Agent Kai na upande wa Mr. Logan Puteri.

Je majasusi wa korea waliofika Malaysia kwa kuhakikisha wanaondoka na Agent Kai mpango wao utafanikiwa?

Na je? Shida yao ni Agent Kai peke yake au wana lao lingine lipi?

Majibu yote ya haya tutayapata katika sehemu inayofuata ya mtifuano huu…!

Endelea kufuatilia mapigo ya kifundi yenye Mshangao!

“Shit! Nani tena anapiga?!”. Akaongea Agent Kai na kuiinua simu, alipoitizama simu namba ni za Balozi Kapteni Jones Lebrons. Haraka akainyanyua simu upesi na kisha kupokea baada ya kuibandika sikioni.

“Halloo! Kapteni”. Akaongea kwa sauti ya haraka.

“Huko wapi?”. Upande wa kapteni ukauliza kwa sauti inayoonyesha yupo kwenye haraka sana.

“Banting Bazar, fish sales… Vipi mzee?”. Naye akamjibu kwa pupa vile vile.

“Dharura… Haraka sana naomba tuonane Sungai Wang Plazza, Time Square Pavillion kuna mambo nataka kujua toka kwako kwanza… Fanya haraka sana mi natokea nyumbani kwangu nilikuja lunchtime saa kumi kamili kuna kikao baina ya waziri wa ulinzi wa hapa, waziri wa usalama wa nchi pamoja na waziri mkuu katika ikulu ya waziri mkuu… Inahusu yanayotokea baada ya mauaji ya mchana PGB”. Akaongea Kapteni.

“Sawa mkuu nitajitahidi kukimbia niwai maana muda nao umekimbia sana saivi ni saa nane na nusu”. Akajibu Agent Kai na akakata simu.

“Damia! Naomba niachie mimi kuhusu wewe, tafadhali achana na tamaa zozote kuhusu kusaidiana na Logan… Nakuacha humu ndani ukiwa huru naomba jifungue miguu yako na uwe huru ndani ya chumba, nitakufungia kwa nje tu na kama unavyoona choo na bafu vyote vipo. Angalizo usijaribu kutoroka sababu tayari nina walinzi nimewaleta”. Agent Kai aliongea kwa kasi huku akipaki vitu vyake kwenye begi lake ambalo muda wote uwa nalo bega kwa bega.

“Nashukuru kwa kuniamini kaka Agent Kai, nakuahidi hakuna baya nitakalofanya sababu sina uwezo huo”. Akajitetea Damia hili awe angalau huru wa mateso ya kutofungwa mikono na miguu.

“Tutaonana baadaye mpendwa madam..!”. Akatoka na kumfungia kwa nje akiwa kamuacha huru wa kutokumfunga kamba miguu na mkono.

ENDELEA NA UTAMU..!

MAPIGO YA KIFUNDI III

Nje ya ghorofa lenye urefu wa floor zipatazo ishirini kwenda juu ambapo ndiyo ghorofa zilipo ofisi za Puteri Group Of Business Headqurter (PGB)H zilizo losheni (floor) ya kumi na tano kulikuwa na pilika pilika za kuhakikisha mambo yanakuwa sawa baada ya tukio la mauaji ya wanaume wawili katika ofisi hizo, wanausalama wa vikosi mbalimbali vya kiusalama vya Malaysia walikuwa wakipishana huku na huko huku wakifanya mahojiano kadhaa wanayohisi, walikuwemo askari kanzu wa vitengo vya upelelezi, usalama wa taifa ambao wako vitengo tofauti tofauti ingawa idara moja na askari polisi wa kawaida kifupi hali ilikuwa moto kweli kweli eneo lile.

Upande wa pili wa ofisi hizi kulikuwa na ghorofa linalotizamana na ghorofa hili, kwenye maegesho ya ghorofa hili lenye urefu wa losheni (floor) thelathini kulikuwa na gari aina ya Toyota Hilux double cabin new model, rangi nyeusi. Ndani ya gari ile walikuwemo wanaume wawili wenye umri unaofanana walikuwa macho yao wameyaelekeza eneo lile lenye pilikapilika la wana usalama.

Mikononi mwao kila mmoja alikuwa kashika darubini ndogo za kikorea zenye uwezo mkubwa wa kuvuta vitu vilivyo mbali, walikuwa wakiinua darubini zao kuvuta kila mmoja anayewavutia wao kumvuta kwa darubini zile kisha wanarudi kwenye makaratasi mbalimbali yaliyo katika bahasha zao zilizo katika dashboard wanatoa picha na kuzichunguza. Walifika eneo hili ikiwa muda mfupi toka Agent Kai aondoke hili eneo tena walipishana njiani bila wote kustuka.

“Yule aliyeshuka kwenye gari akiwa na Mr. Logan ni mlinzi wa Mr. Logan Puteri anaitwa Ally Kareem alikuja naye Korea Kaskazini”. Mmoja aliongea kumwambia mwenzie.

“Hatutakiwi kumuacha kila anapoenda bwana Logan… Inaonyesha kama alivyosema Chow Min haiwezekani kina Logan kumdhibiti huyu Kai na kama ameweza kuingia wanakopatikana wao basi si ajabu tusishangae kusikia helkopta ya kijeshi ya US Army kuingia hapa kuchukua watu wao muda wowote ule”.

“Huko sahihi Cheh Hohn Joo… Inatubidi tuwe makini sana kuwai kabla mambo hayajaharibika… Korean People’s Army wanatutegemea sisi katika suala hili, Marekani haiwezi kuwaachia watu wetu bila mabadilishano”. Akaongea aliyefahamika kwa jina la Komredi Pak Myong Ri kiongozi wa kikosi cha majasusi wanne toka Korea Kaskazini waliofika Malaysia kwa kazi maalumu waliyotumwa toka kikosi cha Korean People’s Army Special Operation Force and Intelligence kikosi bora kabisa kilicho ndani ya jeshi la Korea Kaskazini kikiwa na kazi ya ujasusi.

“Nimewatumia meseji kina Ki Myong Ri maana waliuliza kunaendeleaje huku… Nimewaeleza hali halisi ilivyo wamenijibu tena tuendelee kusubiri hapa hapa mpaka Logan au mwingine yoyote mkubwa tutakapomuona anatoka hapa wakati na wao wapo bado nje ya ubalozi wa Marekani”. Cheh akaongea huku akiendelea kutuma meseji kupitia simu yake wakati mwenzie Komredi Pak akiwa bize na darubini.

***** ***** *****

Mr. Logan Puteri akiwa na watu wake wote walio katika vyeo mbalimbali katika kampuni yake ya Puteri Group Of Business, kiongozi wa ulinzi wa jengo hili na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama vya jiji la Kuala Lumpur walikuwa wapo chumba kidogo cha mikutano ya wenye ofisi zilizo kwenye jengo hili ambapo tukio la mauaji ya watu wawili limetokea kwenye korido ya PGB.

“Kamera za CCTV zinaonyesha muuaji alipofika hapa alifika kwa miguu maana kamera zinachukua kuanzia mita ishirini ukikaribia maegesho ya jengo hili… Angalia hapa akiwa anafika hana wasiwasi kabisa hii inaonyesha jamaa huyu ni mtu mwenye kujiamini kwenye mambo kama huyu”. Alianza kuongea mtaalamu wa kamera za CCTV toka kitengo kinachojihusisha na kamera za ulinzi wa jiji la Kuala Lumpur, Inspekta Antony Yong huku akiwaonyesha waliokuwemo palekwa kutumia fimbo iliyopo mkononi mwake screan kubwa ambapo ilikuwa ikionyesha matukio yaliyokwisha rekodiwa muda wa masaa mawili yaliyopita hasa wakiangalia kwa mlemgwa Agent Kai aliye ndani ya sura ficho inayomuonyesha kama wenyeji wengi wa Malaysia walivyo.

“Hii sura inaonekana ni sura ya bandia kama alivyonidokeza mtaalamu wa kufahamu mtu aliye katika sura ya bandia baada ya kuivuta kwa ukaribu… Anaonekana alikuwa amejipanga kweli kweli kutokana na kamera zinavyomuonyesha akienda moja kwa moja hadi zilipo ofisi za PGB kama ionekanavyo hapa.. Mengine naona mnajionea yalivyofanyika na Inspekta Christopher Wale ambaye aliongoza mahojiano na wafanyakazi walioongea naye wanasema shida yake aliyowaambia yeye ni kuonana na Mwenyekiti mtendaji wa PGB Mr. Logan Puteri au makamu wa mwenyekiti Mrs. Zahra Logan… Kwa mujibu wa maelezo ambayo kiutaalamu tumegundua ni uongo aliwaambia wasaidizi wa makamu wa mwenyekiti anataka kufungua maduka ya kuuza simu hivyo alitaka soko la uhakika la kupata mahitaji ya simu zake kutoka kwa mawakala wa simu akisingizia ameshapitia kwa baadhi ya mawakala wakubwa katika sehemu zingine”. Aliishia hapo Inspekta Antony Yong kisha akakabidhi faili ambalo lina mambo kadhaa kwa mwakilishi wa waziri wa usalama wa nchi aliyefahamika kama Mr. Razak Zayl.

“Inasemekana alishuka kupitia lifti lakini ajabu ni kwamba lifti ilivyofika floor ya mwisho yeye hakuwepo… Uchunguzi wetu unatakiwa uwe makini sana katika watu waliokuwa wanatoka kwa kutumia ngazi… Ebu kiongozi anzia hapo tuchunguze mmoja kati waliokuwa wanashuka kupitia ngazi ingawa kamera za hapa maajabu yake nyingi zimeelekezwa kwenye lifti na moja ndiyo inafuatilia ngazi na hapa ndipo penye kitu kitakachotujulisha mtu huyu alitokaje”. Mr. Razak Zayl akatoa wazo na papo hapo bila kusubiri Mr. Antony Yong akaanza kusachi kamera inayochukua matukio ya kwenye ngazi na moja kwa moja tukio linalomuonyesha mtu aliyevaa suti nyeupe akikimbia baada ya kutoka kwenye korido ya kumi na kisha akajiunga na wengine waliokuwa wakishuka kupitia ngazi.

“Gandisha hapo huyo aliyevaa suti nyeupe siyo yeye?”. Akatoa wazo Mr. Logan Puteri ambaye muda wote alikuwa kimya na hata watu wake nao walikuwa kimya na wao walikuwa wakijua nani amefanya hivyo nia yao ilikuwa wapate msaada toka kwenye vyombo vya usalama vya kiserikali baada ya kuona kama wanazidiwa sana mbinu na Agent Kai.

“Mr. Yong gandisha hapo … Eeeh! Rudisha nyuma kidogo… hapo hapo acha kisha vuta huyo mtu”. Akasema Inspekta Christopher Wale na Yong akawa anafuata maelekezo.

“Shit! Ni yeye… Yah! Huyu kama si gaidi mzoefu basi ni jasusi mbobezi kama si mwandamizi… Alijua kutupoteza muelekeo tukawa tunasubiri atashukia kwenye lifti kumbe akacheza na akili zetu akitugeuza watoto… Endelea mbele kwenye kamera za kila ngazi za floor “. Akaongea Mr. Razak na wote wakatikisa vichwa vyao kuonyesha wanakubali anayoyasema.

“Huyu.. Huyu, huyu anapita anakimbia na watu wengine … Nenda unabadilisha kamera Mr. Yong mpaka floor ya mwisho tuone alipitaje pale chini wakati maaskari walishapewa taarifa alivyovaa”. Mr. Razak akazidi kutoa maelekezo na watu wa mule ambao wengi wao walikuwa wakiujua uwezo na huelewa wake katika mambo ya kiuchunguzi toka yupo idara ya usalama wa taifa kitengo cha Chief Goverment Security Office (CGSO) akiongoza kwa mafanikio makubwa kitengo icho.

“Hapa katika floor ya tatu hayupo mtu huyu ila kwa sisi wote tulio hapa hasa sisi tuliopitia hii michezo ya gizani tumeona hapa akiwa ameshavua suti aliyovaa”. Watu wote waliongeza umakini kuangalia baada ya mtaalamu Mr. Razak kuongea.

“Huyo hapo katikati ya watu akiwa kajipenyeza barabara ndiyo yeye, nilisema yupo katika sura kificho, alifanya tukio akiwa katika sura bandia… Mtu huyu ni mtu mweusi na kwa anayoyafanya akiwa katika umakini wa hali ya juu tena bila woga wa kutetemeka kwa aliyoyafanya hasa wakati anawaua aliowaua na jinsi alivyoweza kujificha kukwepa risasi za walinzi, huyu ni jasusi mbobezi ni mtu wa rika letu sisi tulioachana na ujasusi…. Katika nchi yetu hatuna jasusi mwenye ngozi hii”. Maelekezo yalitoka tena toka mdomoni kwa Razak Zayl.

“Logan! Siku tatu mfululizo maslahi yako na hata watu wanaotokana na ofisi hii wameuawa na sasa tumeona afisa wetu wa upelelezi leo akiuwawa… Sijajua kwanini yanakukuta, je? Mnamjua mtu huyu?”. Mr. Razak Zayl akaongea na kuuliza swali ambalo halikutarajiwa kuulizwa kwa muda huo hasa na bwana Logan mwenyewe.

Haraka Logan akaangaliana na baadhi ya watu wake kisha akamgeukia Mr. Razak na kutikisa kichwa mara tatu akimaanisha hajui lolote.

“Sijawai iona sura hii.. Ebu Mr. Yong naomba zoom sura yake maana amejitahidi sana kukwepa kamera pengine naweza kuwa nimewai muona sehemu hapa Kuala Lumpur au hata nje ya hapa”. Akajibu hivyo Mr. Logan Puteri.

Na Mr. Yong hakuwa na hiyana akajitahidi kukuza picha ile.

“Kule juu tuliweza muona vizuri sababu kulikuwa na watu wachache lakini hapa haonekani vizuri kama ilivyo pale chini kabisa ukumbini ambapo anaonekana mgongo tu… Hapa ulipogandishiwa bwana Logan ndipo hasa unapoweza angalau kuiona sura yake ingawa kwakuwa ni mtaalamu ameweza kuuinamisha uso wake mpaka ukimvuta kwa mbali unaweza kuona pua na paji la uso.. Itabidi wataalamu wa kompyuta kwenye idara ya upelelezi ya taifa wakacheze na kipande hiki tugundue ni sura ya nani lakini kifupi ni mtu mweusi kutokana na nywele alizonyoa znaonekana si nywele zetu… Kilichonijulisha ni hii suruali huku chini na viatu alivyovaa hapo anapopiga hatua cha nyuma kinaonekana vizuri, pia na hata urefu haujifichi sana waungwana hii picha ndiyo ya kufanyia kazi… Acha sisi twende idara ya upelelezi kuwaona wataalamu wa kompyuta tutawapa majibu ni nani na anatokea wapi? Sababu naamini yote yanayotokea siku tatu hizi ni mtu huyu”. Aliamua kuitimisha kikao kile Mr. Razak mwakilishi wa waziri wa usalama wa nchi aliyefika pale akiwa na baadhi ya maafisa wa usalama mbalimbali toka idara na vitengo mbalimbali.

Walipoondoka maafisa wale

Mr. Logan Puteri na crew yake waliamua na wao kuondoka pale PGB Headqurter wakiwa wameongozana na maafisa wale.

***** ***** *****

“Umepaki kwa wapi gari yako?”

“Umefika tayari?”.

“Ndiyo Kapteni nimefika eneo hili ulilonielekeza lakini ndiyo natafuta nafasi ya kupaki gari maana magari yapo mengi sana mpaka natamani twende parking ya juu”.

“Huko sahihi mwanangu… Niko parking ya magari ya juu kabisa nakusubiri huku, nilitaka sehemu salama zaidi tuongee.. Pandisha haraka juu achana na hapo chini”.

Yalikuwa ni maongezi kwa njia ya simu baina ya Jasusi Agent Kai na balozi Kapteni Jones Lebrons baada ya kufika Sungai Wang Plaza Pavillion jengo lililopo mtaa Time’s Square. Kulikuwa na maelekezo ya kuonyesha afuate njia ipi kuelekea parking ya juu sababu jengo hili lilikuwa na parking za chini pia za juu.

Alifika juu na hakupata tabu kuonana na balozi wake sababu balozi alikuwa akiijua gari anayoitumia Agent Kai hivyo alipoona gari inaingia eneo lile akapiga honi kujulisha yuko wapi.

Hapo Agent Kai akasogeza gari mkabala na gari la balozi zikiwa karibu mita mbili kisha akashuka na kuingia kwenye gari ya balozi.

“Lete habari mzee wangu… Natumaini nimewai kwa wakati”. Akaongea kabla hata hajakaa vizuri kwenye siti.

“Muda leo nahisi kama unakimbizwa kijana wangu, niambie leo kuna habari gani mpya?”. Akaanza kuongea kapteni Jones Lebrons huku hamuangalii Agent Kai usoni yuko bize kuangalia nje ya gari.

“Kazi bado inaendelea na kama itawezekana basi kesho kutwa jumapili kama tulivyopanga itakuwa imeisha”.

“Vizuri… Nimekuita hapa kwa sababu mtu wetu wa CIA tuliyemchomeka katika idara ya usalama wa taifa ya hapa amepata habari ndani ya idara yao wamejua kama wewe upo hapa Malaysia na umefanya tukio la leo mchana PGB na wanahisi matukio ya broga hill yaliratibiwa na kufanyiwa utendaji na wewe mwenyewe”. Akaongea tena Kapteni Jones na tena hakuwa akimuangalia Agent Kai pia alikuwa mtu anayeangalia nje kana kwamba mtu anayetafuta kitu Fulani na kwa jasusi bobezi Agent Kai alihisi mzee wake anahofia jambo.

“Kwanini Kapteni huko kama mtu mwenye wasiwasi?”.Ikabidi Agent Kai amuulize.

“Kuna watu walikuwa wakinifuatilia nahisi wanaweza kuwa wamekuja hadi huku… Walianza kunifuatilia toka ubalozini kwa stahili ambayo walihisi siwezi kujua ila kilichonichanganya nimewaacha wapi sijui sababu nilivyofika kwenye fly over junction ya KL Inner Ring Road nikapandisha Jalan Imbi kisha nikashuka federal route one nikawa nimewachanganya hapo nahisi ni ugeni wa jiji kwa dereva wa gari ile na ndicho kinachonitia uoga mpaka sasa”.

“Hukuwaona sura zao?”.

“Sikuwaona vizuri kwa kweli na hii inatokana niliwastukia tu kutokana na uwepo wao muda mrefu katika muongozano, toka nilipoondoa gari pale ubalozini kisha kubadili barabara kama kanuni zetu za kijasusi zinavyosema unapotoka sehemu hili kujua kama unafuatwa inabidi ubadili barabara uendayo kisha ndiyo urudi kuifuata ile barabara…”.

“Uhakika huko hivyo mzee wangu umeshawatoroka wale ingawa ingekuwa ni mimi ningependa wanifuatilie hili nijue mwisho wake na ikiwezekana niwajue na wao”.

“Basi tuyaache hayo ingawa upande mwingine najilaumu kwanini sikutoka na walinzi wangu… Nimeitwa kwenda ikulu ya waziri mkuu kuna maswali natakiwa nikajibu na kutolea maelezo juu ya uwepo wa mtu wanayeamini anafanya kazi bila kibali hapa Malaysia.. Ni kweli unafanya kazi bila kibali maalumu lakini ilibidi nisiombe kibali cha wewe kufanya kazi hapa Malaysia kwa sababu za kiusalama na kiujasusi”.

“Walitaka nifanye kazi na wao au inakuwaje?”.

“Sifikirii juu ya hilo la wao kutaka ufanye kazi hii wakiwa na wao wanatoa ushirikiano sababu nakujua nimekulea kikazi jeshini nakujua usivyopenda kuamini watu au mtu ovyo, najua watanibana nieleze ukweli lakini kama nitaweza kueleza ukweli basi ukweli huo nitaomba baina ya waziri mkuu wan chi”.

“Kazi hii inaendea mwishoni Kapteni… Watu wetu wametekwa na kikundi kinachoongozwa na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Puteri Group Of Business. Kikundi kisichokuwa na jina maalumu ni kikundi kinachojihusisha na utekaji wa watu maarufu kwa dhumuni la kupata fedha lakini wanasayansi wetu na familia zao ni oda maalumu toka kwa adui yetu namba moja kwa sasa hapa ulimwenguni, adui anayetamani kulipiza kisasi kwa yale ambayo wanahisi tuliwai kuwakosea na chuki yao dhidi yetu ambayo kila siku inazidi kumea, Korea Kaskazini”. Akaongea Agent Kai.

“Lile jina ulilonipa ndiyo jina hili unaloliongelea hapa kuwa ndiyo la mmiliki wa PGB, kijana niliyempa kazi ya kufuatilia habari za yule mtu amefanya kazi vizuri kwa nionavyo kitaalamu kwa sababu alinikabidhi ripoti fupi ingawa ilinishangaza kidogo kutokana na kukuta ana urafiki mkubwa na mwenzetu mmoja wa ubalozini”. Akaongea Balozi na kutoa bahasha yenye ukubwa wa 4 piece kisha akatoa faili lenye kurasa mbili ndani yake.

“Kila kitu kinachomuhusu Mr. Logan kipo humu kijana wetu kachero wa CIA kati ya makachero wangu pale ubalozini namuamini sana shida iliyopo vijana wetu wa pale wanamuamini sana msaidizi wetu wa mwanadiplomasia, huyu mtu si mzuri kabisa”. Akaendelea kuongea balozi kisha akamkabidhi ripoti ile Agent Kai.

“Okay! Muda umeenda sana nitautumia muda mfupi kusoma ripoti hii kisha nitakujibu tunatakiwa tufanyaje… Kuna kitu nakihisi na mimi nashukuru Mungu katika kazi hii toka niwe kule US Navy sijawai kuhisi jambo likawa tofauti, umesema ulikuwa unafuatiliwa na watu kisha ukafanikiwa kuwakwepa?”.

“Ndiyo wakati nakuja… Walikuwa kwenye gari aina ya Lexus LX 570 rangi ya kijivu zile zilizotoka 2016 niliiona vizuri kwenye site-mirror sababu kuna muda tulisimama kwenye mataa na wao walikuwa magari mawili tu toka nilipo”.

“Namba za gari hukushika?”.

“Sikushika namba kwakuwa zilifichwa na gari ya mbele”.

“Hao ni wakorea… Hao ni majasusi toka Korea Kaskazini, wamefika hapa Malaysia kwa kazi moja ya kuingilia na kuvuruga mpango wetu wa kuwakomboa wanasayansi na wapelelezi wetu toka katika kikundi cha Mr. Logan… Sababu serikali yao ndiyo ilikubaliana biashara ya kuwanunua watu wetu toka kwa Mr. Logan. Muda umekufa sana tungeongea mengi ila muda ndiyo unatugharimu, acha uende ikulu kwanza ukaonane na watu wanaokuita”.

“Duh! Natamani nisingeenda huko ikulu, kumbe nipo gizani kweli kweli… Umeweza nifungua na kuniwashia mwanga mkubwa, kwa kweli unastahili pongezi kubwa kwa ulipofikia ama kweli wewe kwenye kuchimbua habari huko vizuri sana mwanangu”. Aliongea balozi huku ameukamata mkono wa Agent Kai akiutingisha kwa nguvu kuonyesha kumkubali kijana wake.

“Nina mengi sana baba yangu ila kwanza nenda huko ukimaliza tu kikao nipigie kunijulisha imekuwaje.. Kwa sasa kwakuwa hauna walinzi utatangulia kuondoka wewe kutoka huku maegeshoni juu kisha utafuata barabara kulia nami nikishuka nitafuata kukulinda mpaka ikulu, hii ni kwa sababu majasusi waliokuwa wanakufuatilia wameshaijua hii gari yako hivyo wakikuona kwa bahati mbaya huko watakufuatilia na ndipo tutawashughulikia”.

“Sawa sawa! Basi acha niende ila pale ubalozini nahisi tuna nyoka kama Logan ameweza kuunda urafiki na Michael na huku ndiyo anahusika na utekaji wa watu wetu basi Michael atakuwa anajua lolote lile maana katika ripoti hiyo inasemekana juzi walikutana katika Mr. Logan na Mr. Michael katika jumba la Mr. Logan na wakaongea masaa mawili tena wakiwa wenyewe tu bila mtu mwingine yeyote yaani hata walinzi wa Logan hawakuwepo”.

“Kuna namna hapo, nitahitaji baadaye kijana wako muaminifu anayemfuatilia nionane naye kisha anipeleke kuonana na Michael niongee naye kidogo atakuwa na la kutujibu”.

Maongezi yao yaliyotumia kama nusu saa yaliishia hapo huku kila mmoja akiwa na kiu ya kuendelea kujuzana habari lakini muda uliokuwa ukikimbia sana na ukizingatia foleni za jiji la Kuala Lumpur ilibidi waishie hapo kwa kuahidiana kuwa balozi atampigia simu Agent Kai kumjulisha juu ya maongezi yake anayeenda kufanya ikulu ya waziri mkuu wa Malaysia ambaye kikatiba ndiye kama Raisi katika nchi zingine.

Mwisho wa sehemu ya thelethini na saba (37)

Sehemu hii tumeona majasusi toka Korea Kaskazini wameingia na kuanza nyendo zao, wakiwa wamechelewa kidogo tukio la Agent Kai kufika PGB Headquarter.

Maafisa wa usalama wa Malaysia nao walikutana katika uchunguzi kuona nini kimetokea PGB?

Mjadala mzito umefanyika.

Na upande wa Mr. Logan na wenzake napo kikao cha moto kinaendelea.

ENDELEA..!

MAPIGO YA KIFUNDI IV

Kikao cha moto!

Mr. Logan Puteri alikaa kwenye meza na leo akawa amevua kofia yake ya Marlboro anayopenda kuvaa na uwaraza wake unaong’aa ukaonekana vizuri ukivuja jasho la vidoti vidoti kisha yanajenga mfereji na kuporomoka, hakutaka hata kujifuta kwa leso ambayo alikuwa kaiweka mezani.

Na si kama kulikuwa hamna feni iliyokuwa ikipepea juu silling board la hasha kifaa icho kilikuwepo kikitoa upepo wa kutosha.

Hofu, hofu ya kushindwa kutimiza matakwa yake, hofu ya kuona na kuhisi heshima yake inaenda kushushwa, alikuwa akiwaza mengi sana na mpaka anahitisha kikao hiki alikuwa amehitisha baada ya kupata tishio baada ya kusikia Waziri mkuu amewaita mawaziri wa usalama na yule wa ulinzi kufanya kikao huku wakiwa wamemualika Balozi wa Marekani nchini Malaysia.

Kilichokuwa kikimchangaya ni taarifa aliyopenyezewa toka huko Ikulu ya Waziri mkuu kuwa mkurugenzi wa Idara ya usalama wa taifa Kanali Zubeir Hamza Abdallah hajaruhusiwa kuingia kikaoni kwa ombi la balozi mwenyewe hii ikionyesha kwa wajuzi wa mambo pengine ana siri nzito anayotaka kuisema.

“Tulitakiwa kutumia ujanja wetu wote kuzuia balozi wa Marekani kufika pale Ikulu, sababu kwa taarifa zilizopo leo hakutembea na walinzi wake na haijulikani kwanini haliwaacha walinzi wake na kwenda mwenyewe”. Alianza kuongea baada ya kimya kidogo katika chumba kile cha mikutano nyumba ya nyoka, Kepong Metropolitan Lake.

“Lakini hatukujua kama hatakuwa na walinzi, hii ni hasara kwetu. Inabidi tujaribu kuwaisha mipango kwa kadili ya uwezo wetu Mr. Logan”. Akaongea kwa utulivu Ghulam Qaresh huku macho yake yakizunguka ndani ya chumba kile kama nyoka kuwatizama wenzake.

“Hiyo ishapita kama anavyosema Ghulam.. Tatizo tupo nyuma ya mtu huyu, ametuwai kwakweli kama tunavyosema mara zote… Kumteka mtoto wa kike Damia imetuharibia sana sababu watoto wa kike hata wakiwa majasiri vipi uwa wana udhaifu wao wa kiasili kama nasi wanaume tunapokuwaga kwenye madhaifu na wanawake… Nafikiri mtu huyu amebwabwaja vya kutosha kwa adui yetu. Mi sitilii maanani kuhusu yeye Balozi kutotembea na walinzi kwenda Ikulu ya waziri mkuu sababu mtu huyu ni Kapteni mstaafu wa jeshi na kwahilo lazima hajiamini sana yeye mwenyewe kama yeye”. Akatoa maelezo marefu kidogo Nawaz Patrash.

“Matarajio ni kukaangwa na siri yetu kumwagwa ni makubwa sana… Nimewaita tufanye maamuzi ya haraka sana, kabla ya saa mbili tuondokeni wote kwenda kukamilisha dili kwa kuwaondoa wale malighafi kule Putatan na pia kuwakimbia serikali sababu kiukweli mimi binafsi nina ugomvi binafsi na Waziri wa usalama… Anachukia kila jambo ambalo mimi uwa nafanya ni kama kisasi ananifanyia mtu huyu baada ya ushindani binafsi wa kibiashara baina yetu… Huyu mtu anakwenda kuharibu kila kitu kama mpuuzi Agent Kai alivyoharibu mambo”. Akaeleza Mr. Logan lakini kabla hajaendelea Nawaz akadakia.

“Saa mbili ni mbali sana Mr. Logan…. Piga simu sasa hivi kwa watu wako walioko usalama wa taifa vitengo vyote waambie kikitokea chochote kile watutaarifu, navyojua mimi mpaka muda huu sisi sote tupo hatarini kutoka serikalini moja kwa moja… Angalia meseji hii nimetumiwa na mkuu wa kitengo cha Malaysia Special Branch anasema PGB inamulikwa na vyombo vya usalama kwa jicho la tatu anataka tuonane dakika ishirini toka muda huu”.

“Umemjibuje?”. Mr. Logan akauliza kwa sauti ya kutaka kujua kwa haraka.

“Bado sijamjibu sababu siwezi kujibu bila kuwapeni taarifa hii inayotuhusu sote”.

“Kubali akwambie yuko wapi ukaonane naye, lazima sasa tufanye mambo kama kompyuta yenye spidi kubwa… Upande wa ujasusi tumeachwa nyuma bado tuna safari ndefu sana kama kundi kukua maana nimeona hili katika kupambana na huyu mtu wa mwisho mweusi mpaka mipango yetu tuliyojitahidi kuificha kwa kila hali inaenda kuvurugwa naye”. Akaongea Mr. Logan.

“Si kama tumeachwa nyuma Master Plan, hizi shughuli ndugu yangu ni kama mpira wa miguu au michezo mingine yoyote unapovuka umri na pia uwezo wa mchezo huo kivitendo unapungua kwa kila hali… Akili inataka kutenda mwili unashindwa kutenda, umri wetu sote umeenda”.

Muda huo maongezi ya kuongelea ustadi wao kivitendo kwenye kazi hii iliendelea huku Mr. Nawaz Patrash alikuwa kashajibu meseji kadhaa na kupokea kadhaa kutoka kwa mkuu wa kitengo cha MSB (Malaysia Special Branch).

“Dakika ishirini zimebaki anataka tukutane petaling street jengo la kwanza kabla hujaingia maegesho ya nje ya ubalozi wa china”.

“Sawa… Sisi tubakini hapa wote tukisubiri habari zako sababu upande wangu mimi hakuna amabaye atawaza kwa haraka kwamba sisi wote tupo huku Kepong”. Akaingiza maneno yake haraka Mr. Logan huku akiangalia saa yake iliyo kwenye simu na kumjulisha ni saa kumi na moja kasoro.

“Anaitwa nani MSB Director?”. Ghulam Qaresh ambaye alikuwa kimya muda wote aliuliza baada ya Nawaz Patrash kusimama kwenye kiti hili aanze safari ya kwenda Petaling Street.

“Luteni Adam Nasrulhaq”. Swali hilo kwa haraka likajibiwa na Master Plan na kufanya Nawaz Patrash atabasamu kisha kupotea machoni mwao.

Dakika moja kuondoka kwa bwana Nawaz Patrash simu ya bwana mkubwa Logan Puteri iliita ikiwa ni namba ngeni kwenye simu yake, mikono ikaanza kutetemeka. Hofu! Mtu asiyependa kujulikana kwenye jamii kama ana maovu kwa vile yeye anautamani ubunge na baadaye Uwaziri mkuu wa Malaysia, alihisi sasa ndoto zinaenda kutibuka mchana peupe.

Wafuasi wake walikuwa wakimshangaa na hata waliokuwa wanakunywa vinywaji walisitisha kuinua glasi zao na kuendelea kunywa.

Na mara simu ikakata baada ya kutokupokelewa.

“Naogopa isije ikawa ni mtego jamani… Ebu Kareem tutoke nje ya eneo hili halafu tutampigia kwa simu ingine mtu huyu, hapa ndipo napomkumbuka mtaalamu Hassan na kutamani angekuwepo nasi hapa angeweza poteza mnara haraka na tukaongea”. Akaongea Mr. Logan huku tayari kashainuka kitini na safari ya kutoka ndani ya ukumbi wao wa mikutano nyumba ya nyoka ilishanganya miguuni.

Simu ikaanza kuita tena akatizama namba hii sasa ilitoa jina kuwa nani anapiga alikuwa ni Mr. Zahid Abdul Ghani ndiye anapiga kwake Logan akiwa kasevu jina kwa kifupi Mr. Ghani. Huyu ni kiongozi wa kitengo kikubwa zaidi katia ya vitengo vilivyo idara ya usalama wa taifa ya Malaysia, kitengo chake yeye kikiwa chini ya waziri mkuu mwenyewe kinachoitwa Research Division of the Prime Minister’s Department kwa kifupi RDPMD chenyewe hasa kikidili na mambo ya usalama wa waziri mkuu na vitega uchumi vinavyohusu moja kwa moja serikali kuu.

Mr. Logan alifikiri kidogo kisha akapiga moyo konde na kupokea!!”.

“Mr. Ghani”. Akaongea Mr. Logan sauti ambayo huwezi taraji inaweza toka kwake na hata jasho liliongezeka mwilini mwake.

“Huko wapi rafiki yangu?”. Upande wa pili ukatema swali.

“Batu Caves, kwani wewe huko wapi?”. Akajibu uongo alipo na kisha kuwai kuuziba uongo ule kwa yeye kubambika swali lake.

“Okay! Umeanza lini mambo ya uhalifu Mr. Logan?”. Swali hili lilimfanya atamani kuitupa simu yake chini maana anamuheshimu sana Mr. Zayid Abdul Ghani.

“Kumetokea nini tena?”. Akajikuta anapayuka kuongea huku kwa kasi akirudi kinyumenyume kilipo kiti alichokaa mwanzo kabla hajainuka.

“Tumepewa oda sisi RDPMD tukukamate haraka iwezekanavyo… Nimetuma vijana wangu ofisini kwako wakachukue vinavyoweza kutusaidia katika upelelezi wetu na wengine waelekee kwako, mimi sijaamini hiyo oda kama iko sawa sababu mpaka sasa siamini kama ni wewe uliyefanya matukio ya utekaji wa wanasayansi wa Marekani maana mara kadhaa nilikuuliza juu ya hili kama unahisi kina nani wamefanya hili tukio ambalo lilikuwa linaleta mkanganyiko na kutuvunjia heshima ya kiuaminifu kwa serikali ya Marekani… Sasa mimi kukupigia simu siyo kama najipendekeza kwako mpaka naona unadiriki kukimbia na kuniuliza mimi kuwa kuna nini, simamisha huo ujinga wako nipe ukweli nijue nakusaidiaje”.

“Ghani! Samahani sana tafadhali naomba msamaha wako kwa dhati ya moyoni… Swala hili naomba tusiliongelee kwenye simu naomba tuonane sehemu ya siri tuongee kuhusu hili”.

“Niko kwenye misheni tena si ya mimi kujiamulia ni boss kaamua ni boss wa nchi nzima Logan… Ebu nipe ukweli sasa kwenye simu naomba niamini lasivyo vijana wangu wakikuona sehemu wanakukamata haraka kuliko unavyofikiri na moja kwa moja wanakupeleka kwa boss wa nchi mwenyewe”.

“Tafadhali nilinde nitakupa kiasi kikubwa sana cha pesa… Naomba unisaidie angalau niondoke Malaysia ni kweli nahusika nilishawishiwa na serikali ya Korea Kaskazini”. Mr. Logan alijikuta anajimwaga kwenye sikio la Mr. Ghani.

Moyo wa Mr. Ghani ulilia mshindo akatamani kuachia simu idondoke mshangao mkuu upande wake, alijua siku zote katika watu wema wanaotafuta ridhiki zao huku wakimtanguliza Mungu mbele katika nchi ya Malaysia basi Mr. Logan Puteri alikuwa yumo na ni mfano haswa.

“Aiseee! Kwahiyo una kikundi kabisa Logan?... Okay! Tutaongea zaidi tukiwa wawili umenistua sana na kuna mtu anagonga mlango wa ofisini anataka kuingia, tukutane Malaysia Food Street, Merdeka kuwa makini unapokuja uje peke yako na ikibidi ujibadili kidogo muonekano maana vijana wa RDPMD nawajua umakini wao”.

“Nitajaza ndevu nyeupe kidevuni kuweka mabadiliko kidogo”.

“Nitapaki gari yangu Escudo new model rangi ya bluu maegesho ya kuingilia hivyo wewe ukifika acha gari yako mbali na jengo lile njoo kwa miguu utasogea mlangoni nitaingia kisha tutaenda sehemu ingine kuongea… Ila wewe ni mpumbavu sana mpaka sasa siamini”. Akaongea na papo hapo alipomaliza tu akakata simu bila kusubiri Mr. Logan atajibu nini.

***** ***** *****

Saa kumi na mbili na robo jioni ijumaa ikienda kumalizika na kuukaribisha usiku wakati Agent Kai alikuwa anamaliza mazoezi ya gym katika gym iliyopo nyumba ambayo inatumika kama makazi ya Shufania, mama yake na baba yake. Ilikuwa furaha kubwa sana kwake sababu toka afike Kuala Lumpur hakuwai kupata nafasi ya hata kurukaruka sarakasi zake, mchezo ulio kwenye damu yake kwa asilimia nyingi sana kuliko mchezo wowote katika maisha yake. Siku hii jioni hii mwanaume wa kazi alipata nafasi hii hapa Klang River, Istana Negara.

Alifuta jasho lililomwagika kwenye sakafu ya malumalu (tyles) sehemu ambazo zulia halikufika kisha, kiukweli anapofanya mazoezi Agent Kai basi uwa kazi kweli kweli na kama unamuangalia inaweza kuwa burudani yenye vitu adimu na vya kutisha hivyo jasho linalomwagika uwa jingi sana. Alipomaliza kufuta chumba hiki kikubwa sana cha gym iliyo na vyombo vya kisasa vya mazoezi aliamia kwenye mwili wake akajifuta jasho kwa taulo akavua nguo za mazoezi na kuvaa za kawaida kisha akatoka katika chumba kile na kabla hajapiga hatua akatokea Shufania na kuchanua tabasamu usoni ambapo mwanaume naye akalipokea tabasamu.

“Uliniambia unalala… Sasa ulalaji gani unatokea chumba cha mazoezini?”. Shufania akauliza sababu huku sura yake ikiwa kwenye mshangao fulani uliofichwa na tabasamu tamu.

“Nimelala sana tu dear! Toka saa kumi na robo mpaka saa kumi na moja na robo, lisaa limoja linatosha sana sababu usiku si nitalala wa mie”. Akajibu Agent Kai huku anasogea aliposimama Shufania.

Akaendelea kuongea!

“Wewe unaenda wapi? maana na wewe uliniambia unaenda kulala heti”.

“Nilitaka nikakae kwenye bustani pale swimming pool kuna kitabu nimekiona maktaba ya humu kizuri sana nilitaka nisome kwenye utulivu zaidi”. Akajibu Shufania.

“Okay! Twende tukakae wote tuongee ongee kidogo nipate hewa na mwili upoe kisha nikaoge”.

“Okay! Twende … Vipi leo hutoki?”.

“Natoka, nisitoke tena nitamaliza vipi kazi… Leo moto umekolea miss!”.

Kabla hawajafika eneo la bustani simu ya bwana mkubwa Agent Kai ikazizima mlio akiwa ameweka nyimbo ya kibongo kwenye mlio wa msanii mmojawapo maarufu atokaye Tanzania.

“Kapteni!”. Akapokea na bila kuremba akaungurumisha.

“Niliomba kuongea na waziri mkuu peke yake lakini akaniambia mawaziri wake wote wawili wa usalama na hata wa ulinzi anawaamini sana na hivyo nisiogope niongee pale pale… Nikawahadithia kila kitu kuhusu mambo yanavyoendelea na kisha nikawaomba msamaha kwa kutowashilikisha uingiaji wako kiukweli kama nilivyofanya mara ya kwanza wakati wanaingia Detective Caesar North na Detective Morris Hansen kuwa hawa wanaingia hapa Malaysia kwa kazi moja ya kupeleleza tukio la upoteaji wanasayansi wetu Profea Fransisco Ehud na familia yake na mwenzie waliyeongozana Profesa Martin Bender… Nikawaelekeza kwanini ulienda PGB, hapa navyoongea na wewe msako mkali unaofanywa na mashushushu wa kitengo cha waziri mkuu yeye mwenyewe umeanza wakimtafuta Mr. Logan Puteri hivyo nahitaji uchangamke kuwawai hawa RDPMD sababu hatujui nani ni nani kati yao na kwa sasa fanya kazi bila kuhofia watu wa vyombo vya usalama nimegonga muhuri kibali chako kiko wazi unafanya kazi kwa ajili ya wamarekani kutetea maslahi ya nchi yako… Lete swali?”. Aliongea Kapteni kisha alipoona maelezo aliyonayo kwa kifupi yamefika mwisho akatoa fursa ya kuulizwa swali.

“Ni vizuri ulivyopigania nipate kibali hasa katika wakati huu, nitajitahidi kukimbia haraka kabla RDPMD hawajawatia mikononi watu muhimu kati ya watu muhimu katika kundi lile… Niko istana Negara tuma yule kijana unayemuamini alete kibali hapa na pia nataka nimpange niingie naye mzigoni usiku huu tumalize misheni yote”.

“Okay! US First”.

“US First”. Simu ikakatwa.

Agent Kai akakutana macho na mrembo mtarajiwa aliyekuwa akimsikiliza aongeavyo kwa simu kama naye ni kachero au mwandishi wa asiyependa kupitwa na habari.

“Mbona hivyo miss?”.Akamuuliza huku anatabasamu.

“Si kitu! Mi langu dua tu dear”. Akajibu Shufania na Kai akatamani kumkumbatia lakini mara zote alihofia na hilo Shufania alilijua hivyo akajisogeza wakakumbatiana.

“Nakupenda”. Mtoto wa kiarabu akajikuta anasema mdomo wake ukiwa kifuani kwa mtaalamu.

“Nakupenda pia miss wangu!”. Akajibu Agent Kai kisha wakaachiana toka kwenye kumbatio lile na kubaki wanatizamana kama majogoo.

“Ngoja nikaoge kuna mtu anakuja anatakiwa anikute mkao wa tayari kwenda kazini… Tunakwenda maliza hii kazi muda si mrefu.

“Nakuamini, nakutegemea”. Akajibu Shufania huku akijitahidi kuzuia machozi yasitoke nje ya macho yake.

“Usijali miss wa moyo wa Kai”.

Mara mrembo akashindwa vumilia kwa mara ya kwanza akamwaga busu la kifuani kwa Agent Kai na kumsisimua sana mtaalamu na si kama ni mara ya kwanza yeye kupigwa busu la hasha! Busu hili lilikuwa busu la kama kumzindua simba au chui aliyelala papo hapo akuzubaa naye akabusu paji la uso la binti wa kiarabu, akatamani kukisi mdomo wa bibie lakini akatumia nguvu kujizuia hisia za mapenzi zilizoanza kutaka kuteka himaya! Wakaachiana.

***** ***** *****

Patashika, Logan house!

Kwenye geti ilisimama Land Rover Defender rangi ya damu ya mzee gari zinazotumiwa na watu wa idara ya usalama wa taifa kitengo cha ofisi ya waziri mkuu.

Ilikuwa ishatimia saa kumi na mbili kasoro dakika tano wakati dereva akipiga honi hili mlinzi wa getini afungue geti.

Mara mlinzi akafungua sehemu ya kuchungulia hili ajue ni nani anapiga honi akakutana na gari ambayo si miongoni mwa gari za boss zake wawili wanazozitumia, hivyo akasita kufungua geti lote akafungua mlango mdogo kisha akatoka nje hili aulize.

Mtaa mzima wa Dewan ulikuwa kimya kama vile ni usiku kumbe jioni ya mwisho mwisho.

“Niwasaidie nini wakuu?”. Akawauliza baada ya kufika dirisha la mlangoni upande wa dereva.

“Tunamuhitaji Mr. Logan Puteri”. Sauti yenye mikwaruzo kama spika mbovu ikaunguruma.

“Mna ahadi naye kuwa mtakuja kuonana naye hapa nyumbani kwake?”.

Hakujibiwa neon akaonyeshwa kitambulisho cha huyu dereva aliyekuwa ndiyo wanaangaliana.

“Samahani wakubwa, sikuwatambua nyie kina nani?... Mr. Logan toka atoke asubuhi hajarudi nyumbani ila mkewe yupo amerudi muda si mrefu”. Akajibu huku akitetemeka baba huyu wa makamo kiumri hafai kunyenyekea kwa hawa vijana wa usalama wa taifa lakini angefanyaje.

Akakimbia mbio hadi ndani ya geti kisha akachukua rimoti na kubonyeza namba anazozijua yeye kisha akaruhusu batani moja geti likaanza kujiachia taratibu kufunguka.

Wakati geti linafunguka na kukaribia kuacha uwazi wa kuweza gari ile kuingia mlinzi alistuka alipoona mama mwenye Mrs. Zahra Logan akiwa pamoja na mlinzi wake binafsi (bodyguard) wakiwa wameongozana na wanaume watatu na mwanadada mmoja na mshangao ukawa kwa mlinzi kutokujua wameingilia wapi watu wale.

Ukweli ilikuwa wakati wanasogea kwenye nyumba hii ya kifahari ya Mr. Logan Puteri iliyopo nyuma tu ya mtaa lilipo jengo la bunge na kufanya mitaa kuwa inakaliwa na viongozi wa serikali na watu wenye pesa eneo linalojulikana kama eneo la Dewan Negara. Watu wane walishuka karibu na eneo la upenyo (uchochoro) unaoachanisha ukuta wa waziri wa biashara, walinzi wa nyumbani kwa waziri biashara mheshimiwa Johari waliwaona walipowauliza wakawaonyesha vitambulisho na kuruhusiwa kuutumia uchochoro ule mwembamba usiofaa watu wawili kupishana bila kugusana.

Walitembea na uchochoro ule ukaweza kuwasogeza mpaka nyuma ya nyumba ya bwana mkubwa Logan Puteri na moja kwa moja bila kuchelewa wakakwea ukuta ulio mrefu na pia ukiwa na nyaya electricity security lakini kwakuwa walijiandaa waliweza kupandishana juu na kisha kukata nyaya inayopitisha umeme katika nyaya zile na wote wakavutana kuingia ndani na kwakuwa mchana bwana mkubwa huyu hakuwa anaweka walinzi zaidi ya walinzi wawili wa getini, kwao ikawa mdebwedo wakajikuta wanaingia ndani ya nyumba kiulaini kupitia mlango wa nyuma ilipo swimming pool na bustani kama paradise ya kidunia, walipofika ndani wakamkuta bodyguard sebuleni akiwa na watoto wadogo watatu wanacheza pale sebuleni huku runinga ikionyesha channel za katuni kama watoto wengi wapendavyo wakadili naye kidogo tu mwenyewe akaenda kugonga mlango wa chumbani kwa boss wake Mrs. Logan alipotoka akakutana na watu wa usalama wa taifa ikiwa anamjua mmoja kati ya wanaume wale watatu.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na nane (38)

Utamu umeishia patamu!

Majasusi wa idara ya kijasusi ya Malaysia wamevamia nyumbani kwa Mr. Logan Puteri kwa oda maalumu waliyopewa na viongozi wao.

Nini kitatokea hapo katika nyumba ya Logan?

Nipe nafasi ingine tena katika sehemu inayofuata.

Wakati geti linafunguka na kukaribia kuacha uwazi wa kuweza gari ile kuingia mlinzi alistuka alipoona mama mwenye Mrs. Zahra Logan akiwa pamoja na mlinzi wake binafsi (bodyguard) wakiwa wameongozana na wanaume watatu na mwanadada mmoja na mshangao ukawa kwa mlinzi kutokujua wameingilia wapi watu wale.

Ukweli ilikuwa wakati wanasogea kwenye nyumba hii ya kifahari ya Mr. Logan Puteri iliyopo nyuma tu ya mtaa lilipo jengo la bunge na kufanya mitaa kuwa inakaliwa na viongozi wa serikali na watu wenye pesa eneo linalojulikana kama eneo la Dewan Negara. Watu wane walishuka karibu na eneo la upenyo (uchochoro) unaoachanisha ukuta wa waziri wa biashara, walinzi wa nyumbani kwa waziri biashara mheshimiwa Johari waliwaona walipowauliza wakawaonyesha vitambulisho na kuruhusiwa kuutumia uchochoro ule mwembamba usiofaa watu wawili kupishana bila kugusana.

Walitembea na uchochoro ule ukaweza kuwasogeza mpaka nyuma ya nyumba ya bwana mkubwa Logan Puteri na moja kwa moja bila kuchelewa wakakwea ukuta ulio mrefu na pia ukiwa na nyaya electricity security lakini kwakuwa walijiandaa waliweza kupandishana juu na kisha kukata nyaya inayopitisha umeme katika nyaya zile na wote wakavutana kuingia ndani na kwakuwa mchana bwana mkubwa huyu hakuwa anaweka walinzi zaidi ya walinzi wawili wa getini, kwao ikawa mdebwedo wakajikuta wanaingia ndani ya nyumba kiulaini kupitia mlango wa nyuma ilipo swimming pool na bustani kama paradise ya kidunia, walipofika ndani wakamkuta bodyguard sebuleni akiwa na watoto wadogo watatu wanacheza pale sebuleni huku runinga ikionyesha channel za katuni kama watoto wengi wapendavyo wakadili naye kidogo tu mwenyewe akaenda kugonga mlango wa chumbani kwa boss wake Mrs. Logan alipotoka akakutana na watu wa usalama wa taifa ikiwa anamjua mmoja kati ya wanaume wale watatu.

ENDELEA NA MUENDELEZO…!

MAPIGO YA KIFUNDI V

Kwa haraka bila kutaka kupoteza muda majasusi wa kikorea walitoka eneo la nyumba wakiwa wameongozana na Bi. Zahra Logan mke wa Bwana Logan Puteri, walipofika eneo la nje kinapoanza kizingiti cha geti mmoja akatoa maelekezo.

“Natoa tahadhari Mrs. Logan… Mmoja wetu sisi hapa anawai kuondoka hapa anafuata gari sisi tutakuwa tunafuata kuelekea eneo lile taratibu na kirafiki, hivo bodyguard wako atakuwa katika hali ya kawaida kama siku zote anavyokuwa na sisi mtakuwa kama tuna maongezi na nyie ya kirafiki ama kibiashara”. Amri ile iliwafika vizuri bodyguard na Bi. Logan wakatikisa vichwa vyao kukubali , wakati huo huo tayari mkorea mmoja alishakuwa kashawaacha kwa hatua zake za kasi na kama uwajuavyuo wakorea walivyo wepesi katika kutembea kasi sababu ni maisha yao hata kikawaida nchini mwao kutembea kasi mitaani huwezi muona mtu anatembea kama anasindikiza harusi ya mtoto wa Raisi.

Walipotoka geti likarudishwa huku mlinzi akiwa ameachwa kawaida tu aendelee na mambo yake ambapo alikuwa akivizia wakiondoka tu machoni mwake apige simu polisi.

Kabla hawajamaliza kona gari iliyofuatwa ikawafikia na kugeuzwa kwa mwendo kirafiki usio tata kabisa, nafikiri hii ilitokana na hawa wakorea nao kuujua huu mtaa ulivyo na umuhimu pamoja na kuwekewa ulinzi wa uhakika karibu kila nyumba.

Wakaingizwa garini mateka wao kisha na wao wakaingia na gari kuondoka eneo hilo.

“Komredi Pak mpigie mwambie tunaye mke wake hapa tunataka kuonana naye nusu mbele”. Gari lilipokolea mwendo tu baada ya kuuacha mtaa wa Dewan Negara akaongea Cheh Hohn Joo alipotizama saa yake ya mkononi na papo hapo akampa simu Komredi, simu ya Bi Zahra ambayo walikumbuka kuichukua katika vitu walivyoona vitawasaidia kuvichukua toka Logan’s house.

“Mrs. Logan tunaomba ushirikiano wako…. Mpigie mumeo kisha nipe niongee naye”. Akatoa maneno yaliyo katika hali ya kuhimiza anachotaka.

Akaipokea simu yake ambayo mara nyingi hata mumewe uwa haishiki katika hali ya kawaida katika maisha yao lakini muda huu amekabidhiwa kama vile anaazimwa.

Akaandika namba za simu a mume wake sababu pia ilikuwa namba za mumewe hajazisevu kwenye simu sababu hakuwai kuona kama ina haja maana alikuwa anazo kichwani ni za muda mrefu, ilipoanza kuita akaipeleka mikononi mwa Komredi Pak Myong-Ri.

Haraka ilipokelewa!

“Zahra… Huko wapi mke wangu?”. Sauti yenye taharuki ikaongea kwa pupa baada ya kuruhusiwa tu kuwa hewani.

“Tuliza munkari… Unaongea na Komredi Pak Myong-Ri wa KPAOFI… Tumetumwa kufuata watu ambao tayari ushakula kitangulizi chetu”. Akajibu Komredi kwa sauti ya utulivu akitumia kiingereza chenye lafudhi ya kikorea.

Mstuko mkubwa ulimtokea tena Bwana Logan akampa ishara Kareem asimamishe gari pembeni ya barabara waliyokuwa wakipita kuelekea.

“Mr. Logan mbona kimya?”. Komredi akauliza baada ya sikio lake kutonasa chochote toka upande wa pili sekunde zikikata hewa kwa kasi.

“Natafuta parking komredi, tupo barabarani”.

“Okay! Nakusubiri”.

Dakika moja ndipo gari ikapata nafasi ya kurudi pembeni na kisha kupaki pembeni.

“Tayari Komredi… Mko wapi nyie?”. Akauliza Mr. Logan akiwa hajui kuwa watu hawa hawajaja Malaysia kirafiki kama anavyodhani.

“Tunatokea kwako, tupo kwenye gari tunataka misheni iishe kabla ya asubuhi ya kesho”. Akaongea Komredi.

“Mke wangu yuko wapi?”. Alistuka Logan baada ya kusikia watu hawa wapo kwenye gari wakati yeye kwa wazo la ghafla alifikiri wako kwake.

“Tumo naye kwenye gari… Alivamiwa na watu wa idara ya usalama wa taifa wa hapa wakataka kumchukua kuondoka naye ndipo tulipowawai na kumuokoa mikononi mwao hivyo yupo mikono salama tukutane sehemu uende ukatukabidhi wale watu kisha wewe na kikundi chako mtafute mahali mkajifiche huyo Agent Kai mtuachie sisi tumkamate kisha tuondoke naye”. Akatoa maelezo marefu kidogo Komredi Pak.

“Mmekuja na pesa yote?”. Shenzy! Mr. Logan baada ya kuwaza kuhusu mke wake kuokolewa katika mikono ya watu wa usalama yeye bila hata kusema ahsante akaulizia pesa.

“Pesa yako yote tumekuja nayo”. Akajibiwa.

“Sawa, nilikuwa na ahadi ya kuonana na mtu saa moja na ndipo nilipokuwa nawai kwenda ngoja nimpe taarifa nimepatwa udhuru mje sehemu tukutane kisha sote kwa pamoja tujaribu kuelekea huko walipo watu wenu maana nasema tujaribu sababu kuna msako mkali sana leo hapa jijini”.

“Sawa na kuhusu kufika huko haina wasiwasi mkiwa nasi tutafika tu kwani ni wapi?”.

“Putatan district, West Coast Division of Sabah!”.

“Wapi tunaonana na muda gani?”. Komredi akazidi kumbana Logan.

“Itabidi tukutane hotel zilizo karibu na feri kwa usalama wetu maana natafutwa na serikali hii baada ya balozi wa Marekani kwenda pale ikulu ya waziri mkuu na kisha kueleza anachojua juu yangu nataka ikiwezekana zipatikanike boti za kutusaidia kuondoka hapa KL”. Akaeleza Boss mkubwa Mr. Logan.

“Anza kushughulikia boti… Tukishafika Putatan mtatukabidhi sisi hao watu tutaenda nao hadi Borneo kwa njia tunazozijua sisi hata kwa miguu watafika huko”.

“Sawa naanza na ninashukuru kwa kufika kwenu kwa wakati… Acheni niweke mambo sawa hili nijue wapi tutaweza kuonana wapi huko feri bila vyombo vya usalama vya hapa kutuona”.

“Sawa na sisi tunasogea karibu na huko tukiwa na mke wako pamoja na bodyguard wake”.

Simu zikakatwa pande zote mbili.

“Kareem pesa zishafika… Tunatakiwa tuache kwenda kuonana na Mr. Ghani au twende tu?”.

“Mi nashauri twende, kumbuka tulishawatanguliza wenzetu wawili eneo lile kuangalia kama ni mtego na mpaka sasa wanasema hakuna dalili za kuwa ni mtego… Twende tukabane sehemu mpaka atakapofika tutajua kuwa hivi ni hivi kuliko kuondoka kuwakimbilia wenye pesa bila kuhakikisha usalama wetu”. Kareem bodyguard mkuu wa Mr. Logan Puteri, mshauri mkuu na msiri mkubwa sana wa master plan huyu aliyechoka katika mikakati yake mpaka anaingia katika mpango wa kutoroka nchi isivyowai kutarajiwa hapo awali na wala wakati wowote ule.

“Okay! Twende nikaongee naye hili alegeze watu wake bandarini”.

Kareem hakusubiri neno lingine akatia gari gia na kuanza kuiondoa pale pembeni ya barabara.

Barabarani hapa walikuwa kimya Mr. Logan akitamani mengi ayafanye ikafikia akawa anatamani awakimbie wenzake pale atakapopata pesa akiwa yeye, mkewe na Kareem. Hali ya tamaa baada ya kuambiwa pesa zake zipo mikononi mwa watu walio Malaysia.

Kingine alikuwa akiwaza majumba yake, magari yake na hata biashara zake anakwenda kuziacha Kuala Lumpur alitamani angekuwa anaweza amkabidhi kaka yake Tasik Puteri asimamie kila kitu chake lakini alipofikiria hivyo akakumbuka jinsi kaka yake alivyo mbinafsi na mara nyingi wanagombana sana katika mambo yao tofauti tofauti.

Akahama na kumfikiria huyu anayeenda kuongea naye sasa hivi amuachie baadhi ya mali zake azisimamie akafikiria sana kisha akaona azigawe kwa watu wawili akaamua ampe huyu anayeenda kuonana naye Mr. Ghani kiongozi wa RDPMD pia alikuwepo mwanamke aliyekuwa akimpenda sana anaitwa Aarya Bentul Rai akamfikiria sana kisha akapata jibu amuingize katika fungu la kumuachia.

Hapo akainua simu yake na kutafuta zinapohifadhiwa namba za simu za watu anaowasiliana nao mara kwa mara, alipoipata tu akaruhusu kuipiga na ikaanza kuita.

“Hallo!”. Upande wa pili ukaongea baada ya kupokea.

“Advocate Charlses! Habari za jioni”. Akaongea kwa haraka Mr. Logan.

“Nzuri tu, niambie boss wangu”. Akajibu aliyeitwa Advocate Charles.

“Naomba beba mafaili yote yanayonihusu mimi na mali zangu zote njoo hadi mtaa wa Malaysia Food Street, Merdeka ukifika piga simu hii nitakuelekeza wapi uingie tuongee”. Akaongea Mr. Logan kwa sauti ileile yenye haraka.

“Dah! Mzee muda huu tayari nishafika nyumbani na hivyo unavyosema viko ofisini”.

“Tafadhali nakuomba ni muhimu na ni haraka sana kwelikweli”.

“Naishi Sentul district na ofisi unajua zilipo…. Okay! Nipe masaa mawili nijitahidi kuweza”.

“Sawa basi… Haitakuwa tena Malaysia Food Street, Merdeka nitakujulisha utakapokuwa upo tayari wapi tuonane na hii ni saa moja hivyo saa tatu nitakupigia”.

Akaongea Mr. Logan na kisha akakata simu wakiwa washafika mtaa wa Malaysia Food Street.

***** ***** *****

“Haysen una uhakika tunaweza kumkuta Mr. Michael nyumbani kwake muda huu?”. Agent Kai alimuuliza moja ya kati ya vijana watatu ambao alikuwa nao katika nyumba aliyomuhifadhi Damia ‘LG’.

“Hata tusipomkuta nilimtegea kifaa katika simu yake kila anapokwenda naweza kujua… Nilifanya hivyo jana nilivyokwenda nyumbani kwa Mrs. Rose Thompson nikakuta naye yupo huko, wakati alipoomba kwenda chooni nikaona huo ndiyo mwanya na kwakuwa ulikuwa ni mpango wetu nilifanya hivyo mbele ya Mrs. Thompson”. Akajibu Haymes huku akijiweka vizuri kwenye sofa.

Agent Kai aliamua kumuomba balozi amsaidie vijana watatu hili wamalize kazi anayohisi wanakwenda kuimaliza kazi iliyomleta Malaysia.

Haysen Gilton Walter ni kijana wa CIA aliye nchini Malaysia chini ya ubalozi wa Marekani wa nchini Malaysia, hakuwa anapatikana mara kwa mara pale ubalozi wa Marekani sababu ni Secret Agency CIA ambaye balozi wa Marekani alimpachika katika benki ya waingereza ya Barclays. Hata majasusi wa kiingereza hawakuwa wakitambua kama kijana huyu ni jasusi wa CIA zaidi ya kujua tu ni Mmarekani na ni ndugu wa Balozi wa Marekani Kapteni Jones Lebrons.

Alipewa kazi ya kumfuatilia Mr. Logan Puteri ndipo akagundua ukaribu wa Mr. Michael afisa msaidizi wa mwanadiplomasia wa ubalozi wao akajipa kazi mbili kufuatilia nyendo za watu hao wote wawili kisiri bila wao kujua. Siku ya leo Mr. Logan aliweza kumpotea katika anga zakekutokana hakumuona kabisa toka asubuhi sababu ya kuombwa asicheze mbali kuna mtu anatakiwa kumsaidia kazi ambaye ndiye Agent Kai. Kuitega simu ya Michael lilikuwa fanikio kubwa ambapo hata Agent Kai aliona kweli kijana anajua kuona mbali.

“Kazi nzuri umefanya Haysen.. Mambo inabidi yakimbie sana lasivyo kila mimi nilichofanya na hata nyie mlichofanya kitakuwa kazi bure endapo hatutawapata ndugu zetu… Kazi hii inalenga sehemu moja lakini kwa tuliyoyaona mtaa wa Mr. Logan mimi na Haymes ni dhihirisho kuwa tuna maadui walio ndani ya maadui, namaanisha tunapambana na watu walio katika uzoefu wa tofauti mbili”.

Akaongea Agent Kai huku akiweka mezani mfano wa michoro aliyochora kitaalamu katika karatasi nyeupe.

Kabla hajaondoka Istana Negara, Klang River hapo mapema baada ya kumaliza kuoga alifika bwana mdogo Haysen ndipo ilipoingia simu ya Kapteni Jones Lebrons ikiwa na ujumbe wa kilichotokea eneo la Dewan Negara hapo Agent Kai akiwa amekabidhiwa kibali kilichogongwa muhuri na waziri mkuu wa nchi kikimruhusu yeye kufanya kazi bila woga akamuomba Haymes watoke wote kuelekea Dewan Negara.

Safari yao ilikuwa nyepesi sababu siku mbili nzima zilizopita Haysen alikuwa akipiga misele mara kwa mara akibadili magari tu. Hivyo alikuwa akijua njia gani wanaweza wakapita na kufika huko kutokea Istana Negara.

Walifika nyumbani kwa Mr. Logan Puteri na kama walivyotaraji kikwazo walichokutana nacho ni wanausalama wengi walioizunguka nyumba ile huku utepe wa mpaka ukizungushiwa kuonyesha eneo lipo chini ya uangalizi wa kipolisi.

Agent Kai alipaki gari nje ya utepe uliozungushwa kisha akampa ishara kijana wake washuke toka ndani ya gari aina ya Ford Exploler 2015 rangi nyeusi waliyofika nayo Dewan Negara gari ambayo kijana Haymes alikuwa amepewa kuitumia kwa kazi hii aliyoianza Agent Kai, kati yao katika maongezi Agent Kai na Haymes walikuwa kama wamezoeana miaka mitatu au minne iliyopita kumbe masaa kadhaa tu yaliyopita.

Vitambulisho vyao viliweza kuwasaidia wakapita mpaka ndani eneo yalikofanyika mauaji ya wanausalama sita wa RDPMD, walikuta bado miili inafanyiwa uchunguzi jinsi ilivyoshambuliwa walikuwepo wataalamu wakielekezana jinsi wanavyoona muelekeo wa mashambulizi ulivyokuwa, Agent Kai akajitambulisha kwao na kisha kuwauliza maswali kadhaa ambayo aliona yataweza kumpa mwanga yeye na hata wao anaowauliza, mwisho akaichunguza miili ile pamoja kuipiga picha kwa simu yake. Alipomaliza hayo akaulizia kuhusu kamera za CCTV za nyumba ile ndipo akakutana na jibu kigingi kuwa wauaji waliweza kuua mtambo kwa kukilipua chumba chote cha kamera, hivyo hakuna picha wala mfano wa picha.

Basi Agent Kai hakuona kama hekima wakiendelea kuwepo pale hasa kwakuwa hakuwa huru sana kuonyesha ujuzi wake wa kiuchunguzi kuchunguza kitaalamu zaidi ingawa aliondoka na majibu mengi mazuri katika ubongo wake huku sifa nyingi akizielekeza kwa waliotelekeza mpango ule kiustadi hasa wa kupigwa risasi za kichwani maiti watano ukiacha mmoja aliyepigwa risasi mbili za mbavu.

“Bosi! Pale getini nimeokota ganda tatu za risasi”. Akaongea Haysen akanyamaza kisha akaendelea tena.

“Inaonyesha mshambulizi mmoja alishambulia kutokea getini”.

“Niliona ganda moja kwa chati lakini sikujua kama utajiongeza na kuokota hasa kwa macho yale ya walinzi,umefanya la maana kuokota… Risasi aliyepigwa yule aliyefumuliwa kisogo inaonekana alipigwa kutokea umbali wa usawa wa geti na eneo alilosimama marehemu… Lete ganda la risasi moja nilione”. Akajibu Agent Kai huku akifungua mlango wa gari upande wa dereva maana walifika walipopaki gari. Haysen akamkabidhi ganda la risasi kisha yeye akazunguka upande wa pili.

Wakatulia kwenye viti vyao kisha Agent Kai akaanza kulichunguza ganda la risasi lile.

“Ganda la bunduki ya Kikorea Kaskazini ni Assault Rifle… Wale wameshambuliwa na majasusi wa Korea Kaskazini”. Agent Kai mtaalamu aliongea huku akimuangalia usoni bwana mdogo Haysen.

“Ni bunduki nyepesi sana ukiishika mkononi unaweza ukaifunga darubini na nyingi majasusi wao hutumia wakiwa wamezifunga moja kwa moja kiwambo cha kuzuia sauti”. Aliendelea Agent Kai.

“Hawa wakorea kaskazini nao ni wafuasi wa Mr. Logan?”. Akauliza Haysen.

“Hawa jamaa wana kazi mbili …. Moja ni kuondoka na mimi kunifikisha kwao nikiwa mzima au hata maiti yangu pia wao ndiyo wamekuja kuhakikisha sisi hatuharibu mpango wa nchi yao kuwapata wanaotaka kuwapata hasa wanasayansi wetu”. Akajibu Agent Kai huku akiliondoa gari kwa mwendo wa taratibu akili yake ikiwa katika mpango uendaje.

“Mmmh! Kazi ipo… Sasa tunafanyaje?”.

“CIA ya hapa jumla yenu mko wangapi?”. Akauliza swali bila kujibu swali aliloulizwa.

“CIA Agency jumla wanne ambao tunajuana sijui balozi pengine anaweza kuwa kuna wengine anaowajua”.

“Unawaamini wenzako kiuaminifu na moyo wa kuitumikia nchi yetu?”.

“Sijawai kufanya nao kazi ya karibu… Mmoja ni mzee wa umri unaokaribiana na umri wa Kapteni ni mchungaji wa kanisa, kuna dada mmoja anafanya kazi chuo kikuu cha bandari kama mkufunzi na pia yupo kijana daktari hospitali ya HKL”.

“Nawahitaji kazini siku mbili hizi… Huyu dada anaitwa nani na unavyomuona anafaa kwa kazi katika mapigano ya aina yoyote?”.

“Atakuwa anafaa ingawa kwa hapa Malaysia sisi sote hatujawai kuonana kikazi”.

“Acha nimpigie Kapteni… Wewe angalia yuko wapi Mr. Michael tukamuone baada ya kuwapata ndugu zetu wawili wa kusaidiana nao”.

Haya ndiyo yalikuwa matukio yaliyotokea kwa upande wao mpaka kuja kukutana kati ya Agent Kai na vijana watatu aliowaomba kwa Kapteni.

“Rebecca na Ferdinand mtaondoka hapa mkiwa na huyu mwanadada, mtakuwa naye huyu sababu tutamtumia katika plan yetu baada ya kumlazimisha Mr. Michael kufanya ambacho nishapanga kitakuwaje tukifika… Naomba Haysen uangalie muda huu tunampata wapi ndugu yetu huyu”.

“Tayari nimeshaona yuko wapi… Muda tuliokuwa tunakuja huku alikuwa ubalozini, saivi anaonekana yupo kwake ameingia muda si mrefu”. Akajibu Haysen.

“Rebecca! Hujafanya kazi miaka sana, wote naomba mvae bullet proof hizo kwenye meza”.

“Boss usiwe na wasiwasi kuhusu mimi nimekuwa nikifanya mazoezi kila siku na kwakuwa naenda kufanya kwa vitendo usihofu juu ya lolote kiufundi niko sawa kabisa”. Akajielezea mwanadada mrembo wa kizungu anayeitwa Rebecca Smith mkufunzi wa chuo kikuu cha bandari kilichopo Kuala Lumpur, secret agency wa CIA akiwa na kazi ya kulinda maslahi ya Marekani nchini Malaysia.

Walitoka katika nyumba ile wakiwa Rebecca ameongozana na Ferdinand Fernandez daktari katika hospitali kuu ya rufaa ya Kuala Lumpur. Wao walikuwa wameongozana na Damia a.k.a Language girl (LG) kama maelekezo ya mtaalamu Agent Kai alivyoyatoa kwao wote katika kugawana majukumu. Wakitumia gari aina ya Range Rover Sport aliyokuwa akiitumia Agent Kai. Wakati yeye mwenyewe Agent Kai aliongozana na mtu wake aliyekuwa naye toka saa kumi na mbili.

Ilishakuwa imetimia saa mbili kamili usiku.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na tisa (39)

Bi Zahra Logan! Mke wa Mr. Logan Puteri kaingia mikononi mwa majasusi toka kitengo cha kijasusi cha KPAOFI cha Korea Kaskazini, ambao nao waliona ni fursa kwao kuweza kujaribu kumlazimisha Mr. Logan kuwakabidhi watu wanaowahitaji.

Agent Kai naye kwa upande wake Anadhidi kupiga hatua.

Je nini kitatokea katika sehemu inayofuata?

Muda wako tu wa kuendelea kupita nayo na kusonga nayo riwaya itakupa majibu yote na kusogea katika mengine.

“CIA ya hapa jumla yenu mko wangapi?”. Akauliza swali bila kujibu swali aliloulizwa.

“CIA Agency jumla wanne ambao tunajuana sijui balozi pengine anaweza kuwa kuna wengine anaowajua”.

“Unawaamini wenzako kiuaminifu na moyo wa kuitumikia nchi yetu?”.

“Sijawai kufanya nao kazi ya karibu… Mmoja ni mzee wa umri unaokaribiana na umri wa Kapteni ni mchungaji wa kanisa, kuna dada mmoja anafanya kazi chuo kikuu cha bandari kama mkufunzi na pia yupo kijana daktari hospitali ya HKL”.

“Nawahitaji kazini siku mbili hizi… Huyu dada anaitwa nani na unavyomuona anafaa kwa kazi katika mapigano ya aina yoyote?”.

“Atakuwa anafaa ingawa kwa hapa Malaysia sisi sote hatujawai kuonana kikazi”.

“Acha nimpigie Kapteni… Wewe angalia yuko wapi Mr. Michael tukamuone baada ya kuwapata ndugu zetu wawili wa kusaidiana nao”.

Haya ndiyo yalikuwa matukio yaliyotokea kwa upande wao mpaka kuja kukutana kati ya Agent Kai na vijana watatu aliowaomba kwa Kapteni.

“Rebecca na Ferdinand mtaondoka hapa mkiwa na huyu mwanadada, mtakuwa naye huyu sababu tutamtumia katika plan yetu baada ya kumlazimisha Mr. Michael kufanya ambacho nishapanga kitakuwaje tukifika… Naomba Haysen uangalie muda huu tunampata wapi ndugu yetu huyu”.

“Tayari nimeshaona yuko wapi… Muda tuliokuwa tunakuja huku alikuwa ubalozini, saivi anaonekana yupo kwake ameingia muda si mrefu”. Akajibu Haysen.

“Rebecca! Hujafanya kazi miaka sana, wote naomba mvae bullet proof hizo kwenye meza”.

“Boss usiwe na wasiwasi kuhusu mimi nimekuwa nikifanya mazoezi kila siku na kwakuwa naenda kufanya kwa vitendo usihofu juu ya lolote kiufundi niko sawa kabisa”. Akajielezea mwanadada mrembo wa kizungu anayeitwa Rebecca Smith mkufunzi wa chuo kikuu cha bandari kilichopo Kuala Lumpur, secret agency wa CIA akiwa na kazi ya kulinda maslahi ya Marekani nchini Malaysia.

Walitoka katika nyumba ile wakiwa Rebecca ameongozana na Ferdinand Fernandez daktari katika hospitali kuu ya rufaa ya Kuala Lumpur. Wao walikuwa wameongozana na Damia a.k.a Language girl (LG) kama maelekezo ya mtaalamu Agent Kai alivyoyatoa kwao wote katika kugawana majukumu. Wakitumia gari aina ya Range Rover Sport aliyokuwa akiitumia Agent Kai. Wakati yeye mwenyewe Agent Kai aliongozana na mtu wake aliyekuwa naye toka saa kumi na mbili.

Ilishakuwa imetimia saa mbili kamili usiku.

ENDELEA NA DODO..!

MAPIGO YA KIFUNDI VI

Haysen akiwa kama mwenyeji wa nyumba ile alishuka ndani ya gari na kusogea kwenye geti kubwa wa wastani lililokuwa limeshikana na nguzo za ukuta mrefu uliozunguka nyumba ya Mr. Michael Joram Shweinsteiger msaidizi wa mwanadiplomasia wa ubalozi wa Marekani nchini Malaysia.

Kwa utulivu akabonyeza kengele iliyo pembeni ya geti kisha akasubiri ndipo mlinzi akafungua upenyo wa kuruhusu yeye kuona nani anayeomba kufunguliwa geti apite baada ya kusikilizwa shida yake.

“Haysen! Karibu sana”. Akaongea mchunguliaji kisha akarudisha kibati alichokivuta hili kuchungulia na papo akafungua mlango wa geti.

“Karibu ndani Mr. Haysen”. Akasema aliyeonekana bila kificho kuwa ni mlinzi wa kijeshi kutoka jeshi la Marekani kama ilivyo kawaida maafisa karibu wote wa ubalozi wa Marekani kulindwa na wanajeshi wa Marekani.

“Ahsante sana… Mr. Michael nimemkuta?”. Akauliza Haysen.

“Yah! Amerudi muda si mrefu sana akiwa ameongozana na mkewe”.

Jibu lile lilimfanya Haysen kugeuza shingo yake kuelekea ilipopakiwa gari, hapo kwa sauti aliyoisikia mwenyewe tu kutokana na kifaa kidogo sana cha mawasiliano alichovaa kwa kukichomeka ndani ya tundu la sikio.

“Ingia ndani umtoe nje”. Ilikuwa sauti iliyomwambia hivyo naye hakufanya hajizi akajitoma ndan ya kizingiti kisha mlango ule wa geti ukarudishwa na mlinzi yule.

Kuchangamkiwa kwa Haysen ilitokana na kujuana kwake uzuri kati yake na mlinzi ule wa kijeshi ingawa naye alikuwa hajui kama Haysen ni jasusi wa CIA zaidi ya kujua ni mmarekani anayefanya kazi benki ya Barclay’s na pia ana undugu na balozi wao wa Marekani kitu ambacho hakikuwa kweli Haysen hakuwa na undugu wa damu na Balozi Kapteni Jones Lebrons lakini alimuita mjomba yaani mtoto wa dada yake na yeye.

Baraza ya nyumba anayoishi Mr. Michael ilikuwa masofa ya wageni wanapofika kama wanaweza wakapenda ukaa hapo kumsubiri mwenyeji na ndicho kitu kitu ambacho Haysen alikifanya sababu sebule ya nyumba hii ilikuwa imezungushiwa kuta za vioo vigumu ambavyo wa nje anaweza kumuona wa ndani na wa ndani vivyo hivyo aliweza kumuona wan je ilikuwa ni nyumba ya isiyo kubwa sana lakini ni ya kisasa sana kwakuwa mwenye nyumba pia akitaka aliweza kubonyeza kitufe akiwa ndani mwake na kuta zile za kioo cheupe kinachoonyesha ubadilika na kuwa rangi ya bluu nyeupe ambapo hapo ni wa ndani tu anayeweza kumuona wan je hata ukichukua darubini yenye uwezo wa kupenya kwenye vioo hivi basi darubini yako isingeweza kuambulia kitu.

Haysen alibonyeza kitufe kilicho kwenye moja ya kuta zile za vioo zilizo pale barazani, kubonyeza huku ilikuwa ni kumtambulisha mwenyeji wake kuwa kuna mtu hapa barazani na yeye huko ndani Mr. Michael akaangalia kwenye luninga ndogo iliyopo chumbani kwake aliyoiunganisha na mfumo wa cctv camera na kumuona anayemuhitaji hivyo haraka akatoa taulo alilokuwa kajifunga baada ya kutoka bafuni akachukua pensi aina timberland ya khaki kisha akavaa shati jepesi aina ya bawama akanyanyua simu yake na kutoka chumbani mwake akashusha ngazi kisha akatokea sebuleni na hapo akaonyesha kutabasamu maana walionana sura na Mr. Haysen ambaye na yeye hakuwa akimjua kwa undani bwana mdogo huyu kuwa ni secret agency wa CIA ambaye sekunde zote alikuwa kazini kuifanyia kazi serikali yake katika Malaysia.

“Habari yako Haysen?!”. Akampa salamu kwa uchangamfu mkubwa sana kijana wake huku akimpa mkono wa salamu.

“Nzuri tu Mr. Michael za toka juzi?”. Akajibu Haysen wakati huo huo Agent Kai alikuwa akisikia hayo yote kupitia kifaa chake.

“Nzuri tu, vipi kazi inaendelea vizuri?”. Sasa aliuliza akiwa amekaa kwenye sofa linaloangaliana na alilokaa Haysen.

“Kazi kwa kweli namshukuru Mungu inaendelea vizuri sana tu na nyie vipi ubalozini kwetu huko mambo yanaenda?”.

“Yanaenda ingawa kazi zimekuwa nyingi sana za kidiplomasia kila siku ni vikao tu hivyo mtu unarudi umechoka sana… Lete habari? Maana sikutegemea ugeni wako kabisa”.

“Kweli hukutaraji ugeni huu na hata mimi mwenyewe sikujua kama nitafika hapa muda huu wa saa mbili usiku ila naamini hapa ni kwangu naruhusiwa kuingia muda na siku yoyote nayotaka”.

“Huko sahihi Haysen!”. Akadakia Mr. Michael.

“Mzee mi nimekuja hapa nimeagizwa nikufuate kuna mtu huko nje anataka muonane”. Haysen akapasua jipu macho akimkazia Mr. Michael.

“Kuna mtu ana shida na mimi anakuagiza wewe? Kwanini asiingie yeye humu ndani? Kwanini usingeingia naye? Yuko wapi? Na ni nani?”. Aliuliza maswali mfululizo Mr. Michael huku ka moyo kakidunda dunda kuna nini?.

“Si adui ni rafiki na ni mwenzetu, ametumwa na serikali ya nchi yetu kufanya mahojiano na wewe ya ana kwa ana lakini si hapa kwako… Ametaka yeye isiwe hapa iwe nje ya nyumba yako na huwezi kataa sababu wewe ni mwanadiplomasia wetu”. Akaongea tena Haysen kisha akampa simu Mr. Michael iliyokuwa inaita mpigaji akiwa ni Agent Kai, bwana mdogo akiwa kaisevu namba kwa jina la ‘Brother’.

“Ndiyo huyu anapiga ongea naye”. Akamwambia na kumkabidhi simu mkononi.

“Halloo!”. Huku akitetemeka akaongea Mr. Michael.

“Naitwa Agent Kai, natokea CIA ofisi ya makamu wa Raisi wa Marekani, muda si rafiki nakuomba nje ya nyumba yako haraka sana kaka si ombi ni amri na hakuna baya litakalokukuta hivyo usihofu ni kirafiki si kiofisi”. Sauti iliunguruma ikapasua anga na kukita kama nyundo kwenye ngoma za masikio yake Mr. Michael, alikuwa akitamani akatae kwa kisingizio kadharauliwa lakini kabla hajasema kitu simu ikakatwa.

“Haysen kuna nini?”. Akauliza kwa taharuki iliyodhihiri machoni mwake na alipotizama macho ya Haysen alikutana na jicho lisilo la kawaida jicho ambalo hakuwai kuliona kwenye macho ya bwana mdogo huyu hata siku moja na papo hapo akaonyeshwa kitambulisho cha kijana huyu kitambulisho cha kumtambulisha bwana mdogo Haysen kuwa ni jasusi wa CIA, mkojo ulimbana ghafla Mr. Michael yaani hata kama angekuwa hana baya kwa wamarekani lakini kwa hali aliyoionyesha ungejua tu huyu mtu hajeheshimu ana jambo lake linalokera jamii lakini ni la siri sana.

“Haysen wewe ni CIA?”.Akajikuta anauliza swali bila kutaraji kisha akatamani arudi ndani achukue hata bastola yake lakini kwa ilivyo alikiri haiwezi kutokea kuruhusiwa kurudi ndani alijua majasusi walivyo.

“Muda si mali upande wetu…. Mwanadiplomasia hujawai kuuliza majasusi wako wa ubalozi wako ni kina nani? Na kama walikuficha maboss zako hakuna uaminifu katika macho yako”. Akajibu huku akiwa kashasimama.

Ikabidi Mr. Michael aanze naye kuongoza kutoka nje hili akaonane na Agent Kai na hakuwa na imani na safari hiyo alihisi anaweza kuwa amestukiwa kuwa yeye ni jasusi wa nchi ya ujerumani au tayari kagundulika ana uhusiano wa kirafiki na Mr. Logan Puteri naye kaoneakana ameficha siri ya adui wa wamarekani kwa wamarekani wenzake? Kama hili la Logan aliamini anaweza kulihimili na kuli panchi kifundi hivyo alipenda liwe hili.

Agent Kai alikuwa kapaki gari hatua ishirini toka kwenye alama za mpaka za nyumba ya Mr. Michael hivyo walifika na Mr. Michael kuamrishwa kuingia kwenye gari na hapo ndipo alipokutana na sura ya mtaalamu Agent Kai mwanaume msumbufu pasua kichwa katika ulimwengu wa majasusi.

“Karibu Mr. Michael, jisikie huru mwanadiplomasia wetu na huna haja ya kuogopa vijana wako kama sisi sababu sisi ni kama wewe tu”. Agent Kai akampa ukaribisho kisha kumpa mkono.

‘Ahsante sana Mr. Kai, nimefurahi sana kukutana na wewe leo ana kwa ana ingawa nimeshangaa kwanini hujataka kuingia kwenye nyumba yangu”. Akajibu Mr. Michael.

“Usiwe na wasiwasi nitakuja na kuingia kwako siku nyingine pengine kwa furaha zaidi au kwa masikitiko sote tukiwa na majonzi… Amini Mr. Michael kushinda kwetu na kushinda kwa wote na kushindwa kwetu ni kushindwa kwetu”. Agent Kai alikongea maneno ambayo kwa jasusi bobezi kama Mr. Michael maneno yale kwake ilikuwa sawa na kumwambia mtoto mjanja neon la uongo hili afanye kitu Fulani.

“Nipo hapa Agent Kai… Nawasikiliza vijana wangu, niko tayari kuisaidia nchi yangu kwenye jambo lolote lenye msingi”. Akajibu Mr. Michael akijitahidi kuusawiji moyo wake usawijike uoga ujifute maana kwa hamjuavyo Agent Kai ni mtu asiye na urafiki wa moja kwa moja kwa mtu.

“Umechelewa Mr. Michael… Umejiharibia sifa yako ya kuwa mzalendo kwa taifa lako, sisi tulio nawe kwenye hii gari tayari tunajua mengi juu yako hususani mimi binafsi nakujua kuliko mtu yeyote mwingine”. Agent Kai akaongea huku akimkazia macho bila kupepesa Haysen ambaye alikuwa kaka naye Mr. Michael siti za nyuma alibaki akisikiliza kwa makini mahojiano yale.

“Nini tena Agent Kai? Nina tatizo gani kwa nchi yangu? Mbona nimekuwa mzalendo mzuri tu kwa nchi yangu”. Jicho lilimtoka na kijasho kilianza kumtoka kusikia Agent Kai anamwambia anamjua kwa uzuri kabisa kulimbadilisha akauona mwisho wake umefika.

“Mr. Michael Joram Schweinsteiger mmarekani mwenye asili ya ujerumani siku nyingine nitakwambia wewe ni nani kwa sasa nataka ujaribu kurudisha moyo wangu kwako angalau nikadharau wewe ni nani na nikajali umarekani wako unaofanana na umarekani wangu ingawa wewe mwenzangu machoni mwa watu unaonekana ni mmarekani haswa mimi sijifichi naonekana mmarekani wa kuazimwa tu”.

“Sikuelewi Agent Kai Hamis tafadhali nirudishe kwenye hali yangu ya kawaida naomba niambie ulilonalo juu yangu… Unajua watu waongo wanaweza kutuchonganisha mimi na wewe kwa faida zao binafsi”. Hakutamani kujua lakini hili asionekane kama kuna tatizo Mr. Michael akaongea hivi tena.

“Unajijua wewe nani na upo hapa kwanini? Sikiliza muda si rafiki sana, unamjua Mr. Logan Puteri mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Puteri Business Of Group?”. Haraka alimbadilishia habari na kumrudisha kwenye habari za msingi zilizowaleta wao eneo la Cheras anapoishi Mr. Michael.

“Namjua!”. Haraka akajibu Mr. Michael huku vimacho vyake vya kizungu vikizunguka kijanja kuwaangalia vijana hawa walio naye ndani ya gari.

“Unamjua kama nani kwako?”. Akamuuliza tena.

“Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya PGB”. Akajibu

“Unanijua mimi ni nani?”. Agent Kai akamuuliza huku uso akiubadilisha kwa kuukunja Mr. Michael akakwepesha macho yake yasitazamane na macho ya Agent Kai.

“Wewe? Nakujua kama nilivyowai kukujua huko nyuma kabla ya hapa leo kukutana na wewe”. Akajibu anavyofikiri kwake ni sawa kisha akanyamaza.

“Mimi nani? Mr. Michael usinitanie mimi si fala wewe nijibu vizuri lasivyo utajutia unavyonijibu kijanja janja wakati unajijua wewe nani”. Alicharuka Agent Kai.

“Mbona umekuwa mkali sana Agent Kai, nini tatizo?”.

“Hunijui wewe… Acha nikuonyeshe mimi siyo levo zako”. Akaongea Agent Kai na kuwasha gari kisha akaliondoa kwa kasi kuelekea barabara inayoingia mtaa huu.

“Agent Kai unanipeleka wapi… Tafadhali nieleweshe natakiwa nikujibu vipi, tafadhali simama tuelewane usinipeleke huko unakonipeleka”. Kwa sauti iliyoonyesha uoga asilimia mia akaongea Mr. Michael.

Agent Kai akafunga breki kali bila kupunguza mwendo na kufanya gari iyumbe yumbe kisha ikakaa sawa watu walio nje ya gari wapiti njia walishika vichwa wakiamini Ford Exploler 2015 inakwenda kupinduka.

“SItaki uchoko mzee, niko kazini na mpaka saivi sijui nafanikisha vipi kazi… Nimekuja kwako utueleze ukweli unaoujua tafadhali naomba nipe heshima yangu”. Akaongea Agent Kai hasira kali ikiwa inaonekana dhahiri.

“Nilikuwa namchunguza Logan kuwa ni nani? Sikuwai kujua hapo kabla kama anaweza kuwa vile ambavyo nimejua juzi tu kuwa yeye ni nani”. Akaanza kuongea Mr. Michael kisha akahadithia kila kitu alichoambiwa na Mr. Logan Puteri siku mbili zilizopita kule kwenye jumba lake Batu Caves bila kuacha hata neno hata moja.

“Kwahiyo alikulipa pesa hili unikamatishe kwake mbona hukufanya hivyo?”. Akauliza Agent Kai.

“Sikukubali kikweli kwake nilikuwa nikitaka kumbembeleza anielekeze kawaweka wapi watu wetu waliopotea kisha nitoe taarifa kwa balozi vijana wetu wakavamie na tukapata kuwagomboa watu wetu toka mikononi mwao”.

“Leo mmewasiliana au hata kuonana?”.

“Hapana toka niwasiliane naye jana kumjibu juu ya yale aliyotaka kujua juu yako hatujawasiliana tena, kumbuka ya kuwa alinifuata mimi hili nimsaidie sababu ya urafiki wetu si kwakuwa niko naye kundi moja sijawai kuwa miongoni mwa watu wa kundi lake na ukweli ulio wazi kabisa sifichi chochote sikuwai kujua kama anamiliki kundi la kazi ya kihalifu na ni ngumu kumjua kuhusu hilo hasa kutokana na sif ayake ndani ya jamii kuwa ni mtu safi kabisa”.

“Nahitaji utusaidie tujue yuko wapi muda huu hili tukamalizane naye”.

“Lakini Agent Kai si mnaye yule binti hamuoni mnayo kete nzuri sana ya kujua Logan yuko wapi saivi kuliko mimi ambaye bado aniamini kama naweza kuwa nipo upande wake kamili”. Akatoa wazo Mr.Michael.

“Wazo zuri sana Mr. Michael lakini kuna mpango nahisi anaukimbiza sana na wakorea wake… Basi usijali ngoja tutamtumia Damia kwa namna ambayo unataka… Ila wewe kumpigia ni lazima hili tujaribu kete yetu hii kwanza na ndiyo maana nataka upige tukiwa eneo hili hili la Cheras.

Mr. Michael akainua simu yake na kubonyeza kurasa ya majina kisha akaliona jina la Mr. Logan Puteri akagusa na kuipiga namba ile na mara moja ikaanza kuita. Haikuita sana ikapokelewa.

“Hallo! Mr. Michael”. Upande wa pili ukaongea sauti ya mwenyewe Mr. Logan ikasikika.

“Halloo! Puteri huko wapi muda huu”. Akauliza Mr. Michael.

“Niko kwenye kikao Mr. Michael, niambie?”.

“Mtu wenu nimeonana naye muda si mrefu, yupo na mwanamke nafikiri ni yule mtu wako”. Akaongea Mr. Michael.

“Wapi hapo? Yupo na mwanamke yule aliyemuhifadhi hapo ubalozini au yupi?”.

“Yupo kwenye maegesho ya ubalozi wetu na mimi nipo ndani ya ofisi, anaongea na mabosi zangu… Mwanamke aliyenaye kwenye gari ni Damia, namjua Damia nishawai kukuona naye viwanja vya Golf vya gymkana ulikuja naye mazoezini”.

“Weeeh! Yuko na Damia, ebu jitahidi kuangalia anaenda naye wapi, asije akampeleka jumba la nyoka tafadhali kuwa naye makini”. Mr. Logan alisema kwa sauti ya taharuki kubwa na kwakuwa simu iliwekwa loud speaker aliweza kusikika vyema kabisa.

“Kwani wewe upo huko jumba la nyoka?”.

“Hapana sipo jumba la nyoka, nipo hotelini nina kikao muhimu sana na kule jumba la nyoka tunaondoa vitu ushahidi hali ishakuwa mbaya sana, Mr. Michael natafutwa mimi na watu wangu wanaonizunguka sote tupo hatarini… Tafadhali nijulishe chochote atakachofanya Agent Kai ujitahidi kujua anaelekea wapi akiwa na huyo Damia, tumia hila zote kuhakikisha boss wako mmoja anakueleza kinachoendelea”.

Agent Kai alimuonyesha ishara aendelee kuongea naye yeye kuna waya wa usb alikuwa ameuunganisha na ile simu hili kutafuta eneo la alipo muongeaji na ilikuwa inasachi kwa kasi bila kuleta jibu sahihi mnara unahama hama.

Basi kufikia hivyo Agent Kai akaruhusu simu ikatwe.

“Hoteli gani ulipo? Mr. Logan nataka tuonane nikitoka hapa ubalozini nina habari zingine ambazo si vizuri kuongea kwenye simu”. Akajiongeza Mr. Michael na kuongea hivyo.

“Nitatuma mtu akufuate utakaposema akukute kisha akulete nilipo siwezi sema nipo wapi kwa mtu yeyote… Mr. Michael simuamini mtu yeyote yule hasa walio serikalini nawaogopa sana”.

“Okay! Basi mwambie anifuate mnara wa Petronas Twin Tower atanikuta pale ni muhimu sana”.

“Okay! Saa tatu na nusu wakukute pale wakifika watakuchukua kwa gari yetu… Niko bize sana Mr. Michael usiku huu utakuwa usiku mrefu sana... Okay! Baadaye tutaonana ila usikose kujua huyo mtu anaelekea wapi na Damia”.

Mara hii Mr. Logan akakata simu bila kusubiri Mr. Michael ataongea nini?.

“Usiku huu wa leo utakuwa usiku mrefu sana!” Agent Kai akayarudia maneno aliyoyasikia kisha akamuangalia Haysen, wakaangaliana kwa zamu.

“Unapajua jumba la nyoka ni wapi?”. Akampachika swali Mr. Michael.

“Sipajui kwa kweli.. Yuko wapi Damia?”. Akajibu na kuuliza Mr. Michael.

Kimya kilipita mule ndani ya gari kisha Agent Kai akaongea baada ya kubonyeza kwenye simu yake namba Fulani.

“Rebecca! Naomba kuongea na Damia, mpe simu?”.

“Sawa! Boss”. Upande wa pili ukajibu kisha kikapita kimya cha sekunde chache.

“Kaka! Damia naongea hapa”. Sauti ikasikika.

“Jumba la nyoka ni wapi?”. Agent Kai akamuuliza.

“Jumba la nyoka lipo karibu na fukwe ya Kepong Metropolitan Lake”.

“Naomba uongozane na hao vijana wangu uwapeleke jumba la nyoka, msicheleweshe muda sasa hivi mfanye hivyo”.

“Sawa kaka”. Akajibu Damia na papo hapo akairudisha simu kwa Rebecca.

“Boss! Maelekezo”.

“Tangulieni kwenda huko atakapowaelekeza na sisi tupo nyuma tunakuja sasa hivi, mkifika msianze kuvamia msubiri mpaka tufike mtakachofanya ni kuyasoma mazingira hakikisheni hatoki mtu ila aingie mtu tu”.

“Sawa sawa boss!”. Rebecca akajibu na Agent Kai akakata simu.

“Twendeni Kepong… Mr. Michael namjulisha balozi kuwa tunafanya wote kazi hii”. Akaongea Agent Kai kisha akawsha gari na kuondoa eneo walilokuwepo.

***** ***** *****

Iliwachukua dakika arobaini toka Cheras hadi Kepong Metropolitan Lake eneo la ufukweni mwa ziwa Metropolitan lililoko kando kando ya jiji la Kuala Lumpur. Agent Kai, Haysen na Mr. Michael.

“Mko kwa wapi Rebecca?”. Akauliza Agent Kai baada ya kupiga simu kwenye namba za Rebecca mwanadada wa CIA anayefanya kazi kama mkufunzi katika chuo cha bandari cha Kuala Lumpur.

“Mimi nipo chini ya vivuli vikubwa vya miti miti inayokaribia ghala hili alilotuelekeza Damia kuwa ndipo jumba la nyoka”.

“Group Private network call kwa hapa itakuwa inafanya kazi vizuri naomba uweke sikioni hili tusiwe tunawasiliana kwa simu zetu hizi za kawaida… Sisi ndiyo tunafika hapa…!”.Akaongea Agent Kai kisha akazima taa za gari.

Kulikuwa na manyunyu ya mvua ambayo dalili zilionyesha muda wowote mvua inaweza ikanyesha kubwa eneo lile.

“Ferdinand, Ferdinand unanisikia… Ferdinand itika kama unanisikia”. Akaita.

“Boss! Boss nakusikia vizuri tu sema nipo mahali ambapo si salama sana”. Akajibu kwa sauti ya chini sana Ferdinand Fernandez ‘Double F’ daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kijana mdogo muajiriwa wa CIA, secret agency.

“Huko eneo gani? Mmemuacha wapi Damia?”.

“Kwenye buti la gari.. Tulimuomba tumuache hapo akakubali”. Swali akalijibu Rebecca kwa kasi.

“Boss! Nipo hatua ishirini tu toka alipo mlinzi wa ghala hili, vipi nianze utaratibu wa kuingia ndani maana amekaa mkao wa karibisha mgeni anaomba nauli kabisa”. Akaongea Ferdinand.

“Anza kazi… tunakuja, Rebecca sogea taratibu ukimlinda mwenzio”. Akatoa maelekezo Agent Kai.

“Michael mzee wangu nafikiri tupo pamoja tunaomba usifanye ujanja ujanja wowote, wewe na Haysen mtapita upande ule kuzunguka ukuta ule mimi nitapita kule kwa nyuma naomba kila mmoja awe makini sana tutakutana ndani”. Akaongea Agent Kai baada ya wote watatu kushuka kwenye gari na milango kufungwa.

Mr. Michael alishindwa kujitetea kwa lolote ingawa hakuwa na silaha yoyote lakini mikono ya Haysen ilikuwa na bastola mkononi hivyo aliogopa kuuliza chochote akaanza kufuata nyuma wote wakienda wakiwa wameinama.

Agent Kai akiwa ameshika kisu tu mkononi alinyata kupita kwenye vivuli vya miti vilivyoongeza giza kuwa kubwa kuelekea kwenye jumba linaloitwa jumba la nyoka, alipofika nyuma ya ukuta unaozunguka nyumba alitoa mfukoni mwake block magnetic gloves kisha akazivaa kisha akaweka miwani yake ya kijasusi vizuri ibane usoni isiweze kudondoka halafu akaweka mikono vizuri kwenye kuta kiganja kikanasa safari ya kwenda juu kabisa ya ukuta ikaanza kwa kasi anagusa anaacha anagusa anaacha huku raba alizovaa miguuni zikisapoti mpaka kilele cha ukuta.

Ulikuwa ukuta mrefu lakini juu kabisa ya ukuta hakukuwa na haina yoyote ya ulinzi wa kuzuia watu wasishike juu hivyo alijivuta na kulalia tumbo usawa na ukuta kama nyoka aliyenyooka sawa na ukuta, macho yake yaliyo ndani ya miwani inayomsaidia sana awapo sehemu zenye giza kama hizi yaliweza kuona maghala mawili makubwa , hivyo hakusubiri kuona nini kinachopatikana chini ya uwa ule nyuma ya maghala yale alichofanya alijiachia na kudondokea ndani kabisa na kama ilivyo ada yake na desturi hakuna mshindo uliosikika alijiviringisha kisha akasimama katika kasi ileile yenye ubora.

Hakuna kilichosikika pale zaidi ya yeye kusikia mtu akilalamika maumivu ya kukabwa roba takatifu hii ilisikika katika kifaa alichovaa masikioni ‘The Group Private Network Call’.

“Clear! Rebecca sogea mlangoni unilinde naingia kupitia mlango mdogo nasikia sauti za watu”. Ilisikika sauti ya Ferdinand hapo Agent Kai akajua aliyekabwa mpaka akawa anatia purukushani tayari kashapewa nauli ya kuzimu na Ferdinand anaingia ndani kupitia mbele.

“Good work! Sogea nakulinda”. Sauti ya kike ikasikika alikuwa Rebecca akijibu agizo alilopewa na Ferdinand.

Agent Kai alitembea kuzunguka ghala la upande wa kulia napo hakukutana na mtu yeyote lakini masikio yake yaliweza kusikia gari ikiwashwa na mvua nayo ikawa imeongeza spidi.

“Ferdinand angalia vizuri mbele kuna watu wanatoka au mtu anatoka”. Akaongea huku akiongeza spidi ya utembeaji kufuata aliposikia mlio wa gari.

“Usiwe na wasi wasi kuna watu wanne wameingia kwenye gari aina ya Nadia nyeusi, wanasema wanatakiwa kuwai kufika haraka huko wanakoenda… Nimejibanza hapa getini na uzuri taa ipo linapoanza jengo la nyumba hivyo hawanioni… Nifanyaje mkuu?”. Akajibu Ferdinand na wakati huo Agent Kai akafika hatua nne tu toka ilipo ile Nadia kwa kutumia miwani aliweza kuwaona waliomo ndani ya gari ile.

“Piga risasi matairi ya upande wako”. Aliweza kuongea hivyo sababu dereva wa Nadia alikuwa akipindua gari”.

Nukta kumeta matairi ya ile gari yalishambuliwa kwa pande zote Ferdinand akila ya upande wake na Agent Kai akipiga ya upande wake pancha!

Waliomo ndani ya gari walijkuta wakirudi chini ghafla matairi yakakalia limu. Wakatoa bastola zao kwani haraka walijua wamevamiwa.

Agent Kai alifyatua risasi kumpiga dereva risasi ya kichwa umauti ukampa nauli ya kuzimu papo hapo, aliye pembeni yake akiwa hajui afanyaje na bastola yake akaanza kufyatua risasi bila mpangilio huku kainama kwenye siti anainuka anapiga risasi kisha anainama tena na kusababisha makelele ya risasi eneo lile hapo Ferdinand akafanya yake akampiga risasi ya sikio baada ya kuinua kichwa chake kwa kamchezo kake alikokazoea ghafla.

Wengine waliinama kwenye siti zao nyuma huku wameshika bastola zao kusubiri nini kitafuata.

“Nilinde nawasogelea njoo upande huu nilipo”. Akaongea Agent Kai na papo hapo akatokea Rebecca akitambaa mithili ya nyoka bastola yake ikiwa mkono wa kulia wakawa wamekutana wote wanatambaa mpaka wote wakatabasamu.

Rebecca alisogea kwenye kitasa cha mlango wa gari na kuminya hili afungue mlango hapo aliye ndani haraka akapiga lock usifunguke. Mchezo Agent Kai akaugundua akapiga risasi mbili kwa kutokea pale pale chini alipoinama akawa amevunja kioo cha dirisha kukawa kuko wazi.

“CIA hapa! tunawaomba mjisalimishe salama kabisa wasalimini lasivyo tunalipua gari kwa bomu la kutupwa na mkono”. Akaongea Agent Kai na mara mtu akasika akinong’ona na mwenzake jambo ambalo wao kina Agent Kai hawakuweza kulisikia.

“Msilipue tafadhali tunatoka wenyewe”. Baada ya kujadiliana kwao kwa kunong’ona akasikika mmoja akisema wanatoka toka ndani ya gari.

Wakashuka mmoja mmoja kupitia upande huu uliovunjwa kioo cha dirisha la mlango wa siti ya nyuma ya Nadia hii.

“Unaitwa nani?”. Akauliza Rebecca kumuuliza jamaa moja lililokuwa mbavu kweli kweli yaani limepiga chuma na kikapigika.

“Rebecca! Tuondokeni hapa… Risasi tano zilisikika toka katika bastola isiyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti hivyo askari watafika hapa muda si mrefu, tutaenda kuulizana nao mbele ya safari… Twendeni tuondokeni hapa”. Akaongea Agent Kai kisha haraka akaingia kwenye gari hili aone kitu gani walikuwa wanahamisha wale watu ndipo akakuta maboksi yenye mafaili mbalimbali pamoja na vimitambo vidogo vidogo mbalimbali ikiwemo mashine ndogo moja ya kutype na mashine ya moja ya kompyuta ya mezani CPU.

Mr. Michael na Haysen nao wakawa wameingia kupitia getini na hii ilimfahamisha Kai kuwa ukutani walishindwa kupita wakaamua kuja kwa mbele.

“Haysen, Michael na Ferdinand bebeni CPU Na hayo maboksi yenye mafaili twendeni nayo… Tunaelekea kambini kwetu na hawa mateka wetu…. Njiani Michael utakodi taxi na kurudi kwako utuachie sisi tuendelee na kazi kama utaamua kuendeleza usaliti wako sitasita kukumaliza hivyo unatakiwa uwe mpole.

Mwisho

0 comments:

Post a Comment

Blog