Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

JINO KWA JINO - 2

   

Simulizi : Jino Kwa Jino

Sehemu Ya : Pili (2)


Maeneo ya kujidai ya jumba la Mr. Guti, viunga vya manispaa ya Petatlan jimboni Guerrero baada ya jana yake kuwa katika pilika pilika za furaha ya tafrija ndogo, siku ya leo ya jumatano kulikuwa na hali ya utulivu ulinzi ukiimarishwa zaidi kuhakikisha hakuna baya lolote linaloweza kutokea ukizingatia magenge mbalimbali ya mihadarati yalikuwa hayatabiriki katika biashara hii ya haramu hakuna mwenye uhakika na usalama wake na hata kuaminiana katika magenge yao kulikuwa hakuna sana.


“Karibuni Nasco… Muda si mrefu tulikuwa tukiwazungumzia kumbe mpo njiani kurudi” Nasco na kijana mwingine aliyeongozana naye kufika hapa ni moja wa vijana wa mahiri sana katika kundi kazi la Mr. Guti, kijana huyu na mwenzake aliyeambatana naye na vijana wengine wawili katika kundi hili ambao kazi yao kubwa ni kuchunguza habari za makundi mengine kama yao yaliyo mengi sana katika kila jimbo la nchi ya Mexico na manispaa zake kiasi ya kwamba katika manispaa moja unaweza ukakuta vikundi vya biashara hii ya haramu viko viwili mpaka vitatu na vikimiliki kundi la vijana wa kiume kwa wakike katika kuhakikisha bosi wao ambaye ndiye anakuwa tajiri yao ‘Kingpin’ anaishi salama bila kupatwa na bugudha yoyote toka kwa makundi hasimu na hata serikali na vyombo vyake vya usalama vya kupambana na madawa ya kulevya.


Nasco licha ya kuwa alikuwa muajiriwa wa Mr. Guti lakini hakuwa akihusika moja kwa moja kwa kujitambulisha kwa wasio husika na kundi hili kama anafanya kazi kwa kupokea maagizo ya Mr. Guti, yeye alikuwa akifika hapa kwa Mr. Guti kwa siri sana akijibadilisha sura kwa kuvaa sura za bandia aina mbalimbali endapo anakuja kwa bwana mkubwa huyu wa Manispaa ya Petatlan ila sura alizokuwa akizivaa zilikuwa sura mtambuka kwa walinzi wa jumba la Mr. Guti na hata baadhi ya wafuasi wake na si yeye tu pia hata wenzake wawili nao walikuwa wakifanya kama yeye afanyavyo yeye.


Kazi waliyopewa toka jana kisha yeye Nasco Dos Santos na mwenzake mmoja anayeitwa Joao Zabalo ikawapeleka katika jimbo la Tabasco ndiyo iliyowafanya muda huu kufika katika jumba hili lenye fahari zake ingawa si fahari ya kufikia hata nusu ya fahari ya kasri la Mr. Fanuel Miguel Mendoza analoishi huko Villahermosa, Tabasco.


Vijana hawa wenye umri rika unaorandana wote walikuwa ndani ya sura za kificho, sura zilizo tofauti na sura zao lakini hakuna kati ya sura wanazozitumia kuficha sura zao ambazo zilikuwa ni sura ngeni kwa Mr. Guti na walinzi wake hivyo kufika kwao katika jumba hili kulifanya wapokelewe kwa sura za bashasha tele na watu wote wa hapa.


“Ahsante boss.. Tumewai muda muafaka, ndiyo mko mnapata mlo…. Haha hahahaah!” Akajibu Nasco uso wake wa bandia ukilazimishwa kutabasamu na uso wake ulio ndani.


“Mmewai wakati muafaka.. Brigedia! alihitaji chakula na mimi nikaona niunge humo humo tule pamoja kwenye meza moja maana najijua nilivyo mvivu kula.. Vuteni viti hivyo msogee mezani mpate chakula nasi huku twaongea ya huko maana kwa niwajuavyo mtakuwa mmetoka safari ya huko mbali na moja kwa moja mmekuja kuripoti kwanza ofisini” Akaongea Mr. Guti.


Nasco na Joao wakachukua viti kama walivyoagizwa na bosi wao kisha wakasogea navyo kwenye meza ambayo haikuwa na Mr. Guti peke yake bali alikuwepo na Brigedia Fernandes akila huku anasikiliza maongezi ya kukaribishana kati ya wageni waliofika na rafiki yake Mr. Guti.


“Karibuni vijana wa kazi” Akatoa ukaribisho Brigedia Fernandes huku akijifuta mdomo kwa tishu nyeupe.

“Tumeshakaribia kaka mkubwa Brigedia Fernandes… Tumekuja na habari nzuri kati ya yale mliyotuagiza tukayafanye na kuyachunguza huko Villahermosa” Akajibu ukaribisho ule huku akijiwekea chakula katika sahani kutoka katika hot-pot.


“Naamini kila kitu kimeenda vile tulivyotarajia Nasco, nawaamini sana vijana wangu….!”Mr Guti akiwa na shauku ya kujua ilikuwaje huko Villahermosa akaanzisha maongezi hayo bila kusubiri wamalize kula chakula wanachokula.


“Yaah! Huku tunakula tuna shauku ya kujua kilichojiri huko.. !”Brigedia Fernandes akaunga mkono hoja.


“Mpango wetu umefanikiwa nafikiri na utekelezaji tu ndiyo wa kufuatwa sasa… Fanuel Miguel Mendoza ni kama nilikuwa sijui utajiri wake ulivyo na ukwasi mkubwa wa pesa kwa sasa, binafsi mimi Nasco na hata mwenzangu Joao tulikuwa tukisikia tu kwa watu wengine ila safari hii kwakuwa tulikuwa na masaa machache ya kujua mengi ya bwana mkubwa yule nashukuru tumeweza kujua mengi” Akaanza kueleza Nasco kisha akatupia vipande kadhaa vya nyama mdomoni mwake, akatafuana tafuna na kumeza akajifuta mdomo kwa tishu.

“Kama ilivyo kawaida ulinzi wa mtu yule ni wa level kubwa sana na kisasa kutoka walinzi mahiri alionao na wengi wao ni vijana aliowatoa Brazil, Peru na Mexico yetu…. Mkuu wa kikosi chake anayeshughulika na masuala yote ya biashara haramu na mambo mengine ikiwemo ulinzi na mikakati mbalimbali ni mwanadada aitwaye Maria Rodgruez a.k.a Baby Beauty, mwanadada mrembo sana aliyekuwa idara ya usalama wa taifa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya akishirikiana na DTO, mwanadada huyu aliachishwa kazi sababu kuna kipindi alipatwa na tatizo la ugonjwa wa kichaa ikawa haina budi zaidi ya yeye kuachishwa kazi, alipoachishwa kazi ndugu zake walimpeleka Hispania na huko alipata matibabu na kurudi katika hali yake ya kawaida” Aliendelea Nasco kisha akala tena chakula chake na kusindikiza na juisi akazungusha macho kuwaangalia mabosi zake wote wawili wanaomsikiliza kwa umakini.


“Endelea bwana! Chakula kipo icho ila sisi tuna hamu zaidi ya kujua majukumu yenu mlivyoyatekeleza huko Tabasco.. Hahahah hahahah unavyoshambulia huo msosi hatariii” Akaomba Mr. Guti na kutumbukiza kautani kidogo kwenye ulaji wa kijana wake.


“Niliishia kwa mwanadada Baby Beauty … Haya tuendelee! Ingawa haya ninayoyatoa Joao Zabalo anayajua yote ila kaamua kujifanya kama bwana mkubwa alto mzee wa vimemo.. Hahahah hahahah.. Hatukufanikiwa kuingia katika jumba lake kwa vyovyote kati ya vile tulivyopanga tutaingia kwa kujifanya tunataka mzigo… Ni kwamba katika kasri lake lililopo mtaa wa Avenida Pasco Usumancita, bwana mkubwa yule anapafanya pale kama ofisi yake ndogo na makazi yake yapo hapa yeye na familia yake… Ukiacha ofisi yake kuu ya kampuni yake ya Miguel La Plancha Compania Limitado, ambapo yeye kama mwenyekiti na mtendaji mkuu wa kampuni yake ofisi iliyopo mkabala na jengo la ubalozi wa Marekani mtaa wa Paseo de la reforma… Uzuri hatukuchelewa kupata mtu anayejua mambo mengi ya kumuhusu Mr. Fanuel Miguel Mendoza. Mtu ambaye alikuwa karibu na familia yake mwaka mmoja tu uliopita akiwa ni dereva binafsi wa mke wa Mr. Fanuel… Mtu huyu kwa sasa hayupo tena kikazi kwa familia ya Fanuel kwa sababu ni mlemavu alipatwa na matatizo ya ajali ya gari iliyosababisha yeye kutoendelea na kazi yake” Alisimama hapa kwakuwa kuna mtu aliingia pale katika sehemu ya kulia chakula walipo, alikuwa ni Ivan Alberto ‘alto’ na moja kwa moja akajumuika pale akitoa salamu kwa mikono tu bila kuongea chochote.


“Karibu alto…. Tunapokea taarifa mrejesho kutoka kwakina Nasco kama hujuavyo tuliwatuma Villahermosa” Brigedia Fernandes akamkaribisha ‘alto’ (Tall) katika kikao chao kilichokuwa kikiendelea huku wanakula na kunywa vinywaji.


“…Tuendelee Nasco…!” Akaongezea Brigedia.


“Kuna jambo mnatakiwa kujua ni kuwa dereva ninayemzungumzia kuwa tulifanikiwa kumshawishi na kuweza kuyajua mengi kuhusu Mr. Fanuel maana tulivyofika tu Villahermosa na kuanza upelelezi wetu tulipata mtu aliyetupeleka kwa dereva huyu kwa kutuambia kwa ajuavyo huyu ndiyo anaweza kutusaidia zaidi juu ya tajiri Fanuel na ni kweli katusaidia sana na pia nashukuru amekubali kuambatana nasi hapa kwa maelezo zaidi na zaidi maana anasema ni kama alidhulumiwa haki zake nyingi na familia ya Fanuel na kila akifuatiliwa anazuiliwa getini hivyo haonani na Mr. Fanuel” Akaendelea na kueleza Nasco ila ilimbidi anyamaze baada ya kuona kuna swali linataka kuulizwa na Brigedia Fernandes.


“Sasa kwanini hamkufika naye moja kwa moja hapa?” Akahoji Brigedia Fernandes.


“Yupo kwenye gari, tulitaka kwanza ruhusa yenu ya… ya!” Hakuendelea Nasco na alichotaka kuongea Brigedia Fernandes akamkatizia.


“Joao mfuate huyo mtu…Wewe endelea kutuelezea ilikuwaje na mmefika wapi katika uchunguzi wenu, akifika huyo mtu hapa atatuelekeza kuhusu tunavyoweza kumpata Mr. Fanuel” Maelekezo yakatoka kwa Feca.


“Sawa mkuu!” Akakubali Joao kisha akainuka kumfuata mtu aliyeelekeza Nasco kwenye maelezo yake kuwa wamemuacha kwenye gari.


“Sasa Nasco unaweza kuendelea ila nyie wawili mna roho mbaya sana ya kutu cha chuma lilisahaulika porini huko, mmetukuta tuna kula na mmetoka safarini mkiwa watatu mkaacha mwenzenu abaki kwenye gari bila kula wakati si mwenyeji hapa Tetaplan, dhambi nyingine ndogondogo hamtakiwi kuziendekeza, dhambi za utu kwa mtu mkarimu aliyejitolea kufikisha mengi kwetu.. Hahaha hahahah hahahah.. Ebu endelea..!” Akaongea Mr. Guti na wote pale wakacheka kwa sauti.


“Nisamehe mimi bosi! Maana Joao alipendekeza tuingie naye mi nikapinga nikisema uwa haupendi mtu yoyote aingie hapa kwako bila ruhusa yako kwani wengine ni wachora ramani.. Tuendelee… Mtu huyu ameweza kutusaidia ndiyo maana mlitupa siku tatu kuwa Villahermosa lakini kwa uwezo wake Mungu tumeweza kutumia masaa kumi na tatu tu kila kitu kikawa katika mstari na ndipo tukaamua tuingie makubaliano na mtupa maelezo yote na twashukuru hakuwa na hiyana akakubali tukamuachia fungu kidogo la kuiachia familia yake na kuondoka naye… Hivyo mengi ataeleza yeye zaidi na maswali mengi nafikiri mtapata fursa ya kumuuliza na kupata majibu yake, hizi hapa kwenye ipad ni picha tulizopiga kwa mbali kasri lake..!” Maelezo haya ya Nasco yaliambatana na kukabidhi ipad yake kwa Brigedia Fernandes.


“Maxi! Kutana na viongozi wetu… Wa kushoto ni Mr. Guti ningependa umuite hivyo hivyo tu kuwa Mr. Guti na huyu wa kulia ni Mr. Feca naye pia kama hautajali ningependa umuite tu hivyo Mr. Feca maana nasi sote hawa tunawaita hivyo…. Na wakuu zangu mnayemuona mbele yenu ni Mr. Maxi Garcia Rovirosa na kama nilivyokwsiha tangulia kuwaeleza hapo awali huyu alikuwa dereva maalumu wa mke wa mheshimiwa sana Fanuel Miguel Mendoza” Akatoa utambulisho Nasco kwa mabosi zakena kwa mgeni aliyeletwa na Joao kutoka nje walipokuwa wamemuacha kwenye gari.


“Karibu sana Mr. Maxi.. Jisikie huru sababu hapa ni mahala huru kabisa pasipo na makunjo kunjo yoyote na pole sana kwa ajli iliyokupata sikuwa najua kama imekuathiri kwa kiasi hiki cha kuwa unatembea kwa kigari cha kukokotwa na mtu” Mr. Guti akamkaribisha Mr. Maxi ambaye ni kweli alikuwa hawezi kutembea yeye mwenyewe mpaka atumie baiskeli ya walemavu wa miguu au kama hiki alicholetwa nacho humu ndani akisukumwa na Joao.


“Ahsante sana mkuu… Mambo haya ni magumu kuyazoea lakini kwakuwa imeshatokea kunakuwa hakuna jinsi uwa tunajifariji kwa kusema tunamuachia Mungu” Akajibu Mr. Maxi kijana ambaye ukimtizama unaweza kumuweka katika vijana wale wenye umri unaoenda miaka arobaini na tano.


“Muda wa wewe kulipwa stahiki zako umefika, usihofu Maxi, nakuahidi kusababisha unalipwa stahiki inayokustahili na zaidi yake” Mr. Guti akaongea tena kisha akanyamaza kumuacha muhudumu wa meza ya chakula aliyefika kuondoa vitu aondoe vyombo vichafu na kisha kamuelekeza aache na chakula kwa ajili ya Maxi.


“Mr. Maxi tunaweza kuendelea au utapendelea umalize kula kwanza ndiyo tuongee?” Brigedia Fernandes akamuuliza.


“Sina njaa ya hivyo mkuu.. Naweza nikala baada ya kumaliza maongezi yetu.. Hivyo ruksa niko tayari kueleza na kufafanua yote mnayohitaji kuyajua kutoka kwangu” Akajibu Maxi.


“Safi sana Mr. Maxi… Cha kwanza tungependa kile unachojua juu ya mali za Mr. Fanuel, boss wako wa zamani” Akaeleza Brigedia Fernandes.


“Mr. Fanuel utajiri wake kwa sasa naweza nikasema ni utajiri mkubwa sana kwa Tabasco na majimbo ya jirani ambako napo ana biashara zake za utakatishaji wa fedha anazozipata katika biashara yake kuu anayoipenda na kuiheshimu kuliko chochote kile maana anaweza asikuue ukiiba chochote kwenye viwanda vyake lakini si kumletea mchezo katika biashara yake ya mihadarati… Ni mkali kama chui akikugundua tu unakwenda tofauti na matakwa yake katika ishu ya unga na pesa zinazoingia kupitia unga.. Mali alizonazo cha kwanza kilicho kikubwa ni hiki cha siri cha biashara haramu kisha kinachofuata ni viwanda vitatu alivyonavyo vilivyo chini ya kampuni yake ya Miguel La Plancha Compano Limitado… Kama nilivyoeleza viwanda vyake vya chuma na maduka yake makubwa ya kuuza bidhaa toka kwenye viwanda vyake ndicho chanzo kikuu cha utakatishaji wa fedha haramu anapozipata katika mihadarati, basi uchukua kiasi fulani na kukipeleka huko, zinapoingia mzungukoni ndipo yeye uingiza pesa hizo kidogo kidogo kwenye akaunti za kampuni yake kupitia viwanda vyote vitatu anavyomiliki mpaka faida yake anaichukua kuipeleka kwenye akaunti za kampuni yake… Ukitizama unaweza ukaona ni kama ni kweli faida kubwa ya pesa anapata kutoka katika viwanda hivyo kwakuwa ni viwanda vinavyotengeneza nondo na vyuma vingine ambavyo vinakuwa imara haswa” Maelezo marefu yalitoka kwa Maxi kisha akapumzika kulowanisha koo mate.


“Uimara wa bidhaa za kampuni yake vinafanya hata wanaofanya mahesabu ya makampuni binafsi kumuandikia hati safi katika kampuni yake licha ya kuwa si siri katika serikali hii kama Fanuel anajihusisha na biashara za dawa za kulevya… Fanuel ni mtu wa hatari sana katika nchi yetu kwa sasa lakini nguvu kubwa aliyonayo sasa si rahisi kufuatiliwa na iwe na watu binafsi wenye kumiliki magenge makubwa kama yake na hata serikali yetu… Nimefanya kazi nikiwa dereva wa mke wake kwa miaka minne toka alipohamia tu Villahermosa toka hapa Guerrero hivyo yapo ninayoyajua juu yao na pia yapo nisiyoyajua ila yale niyajuayo ni mambo ambayo yanaweza yakawasaidia sana nyinyi mnaohitaji kumjua Mr. Fanuel angalau kwa kiasi msaada kwenu, karibuni kwa maswali niweze kuwajibu na kuleta faida itakayosaidia”. Maxi akaeleza na kwakuwa alikuwa hajui atembee vipi kimtiririko akaomba habari za Fanuel azifikishe kwa kujibu maswali.


“Jambo zuri Maxi… Ni vizuri tukakuuliza tutajua zaidi… Nasco ametueleza kuwa Mr. Fanuel ana ofisi mbili, moja ipo kwenye kasri lake analoishi na ingine ipo makao makuu ya Miguel La Plancha Co. Ltd, je mke wake anajihusha na nini?” Brigedia akaunga mkono hoja kisha akauliza huku akiwa kaambatanisha viganja vyake vya mikono anasugua kwa kushusha hiki chini na kupandisha hiki juu taratibu lakini vilitoa joto na kumfanya ajisikie vizuri zaidi. Wakati huo huo Mr. Guti alikuwa tayari dakika nyingi zilizopita sigara ilikuwa ikivutwa kwa madaha mdomoni mwake kana kwamba anasukumia chakula alichokula.


“Mke wake ni ndiye mwenyekiti msaidizi wa kampuni yao ya Miguel La Plancha Co. Ltd.. Na yeye kila siku za kazi ndiyo ufanya kazi zote za kampuni, Fanuel alimuoa huyu mwanamke kwa kufuata uwezo wa kibiashara na usomi wake wa uchumi… Ana PHD ya uchumi huyu mama ila pamoja na usomi wake anavutiwa na stahili ya mumewe kuongeza mali kwenye familia yake kupitia biashara haramu na anashiriki baadhi ya mambo hasa mahesabu” Akajibu Maxi kisha akatulia kwa kunywa kinywaji alichokuwa ameletewa na kikawa kinamsubiri yeye tu kumburudisha.


“Anaitwa nani mke wake?” Akahoji Brigedia Fernandes.


“Felister Fanuel… Madam. Felister ndivyo wafanyakazi wote umuita hivyo…!!!!”


“Kumbe wameoana… Na ndoa yao ina watoto wangapi?”


“…Wana watoto wawili… Wa kwanza wa kike na wa pili wa kiume…!”


“Sawa.. Kwahiyo Fanuel sasa ana watoto watano.. Maana tulivyokuwa marafiki miaka sita iliyopita nilifika kwenye mazishi ya mke wake wa kwanza aliyefariki walikuwa na watoto wa tano na kwa sasa nafikiri watakuwa wamesogea zaidi kiumri na kiumbo” Akajkuta anaeleza kwa sauti ndogo lakini iliyosikika Brigedia Fernandes kisha akainua macho yake yakagongana na macho ya Maxi.


“Unaweza kuujua mfumo wa Mr. Fanuel katika shuguli zake za haramu?” Akauliza Brigedia Fernandes.


“Nitaeleza vile ninapojua na sitafika ambapo sipajui kwakuwa mimi nilikuwa dereva wa mama si yeye baba… Mr. Fanuel anamiliki kikundi cha siri kama si genge la siri kama mjuavyo mfumo wa biashara ya mihadarati hapa Mexico ilivyo watu kuunda kitu kama jeshi dogo lenye kumiliki silaha kali ni inaonekana ni kawaida, icho kikundi cha siri kinaitwa MPD wakimaanisha kwa kirefu kuwa ‘Mendoza Potentia Distributio’” Akaweka kituo hapa macho akayazungusha kwa kila mtu kisha akanywa kinywaji chote kilichopo kwenye glasi.


MDP ni jina la kikundi kinachofanya kazi kwa utiifu kumtumikia Mr. Fanuel Miguel Mendoza na kufanikisha kila jambo analolihitaji liende sawa katika biashara haramu, MPD ni mkusanyo wa maneno matatu ya kilatino lugha kuu ya taifa la Mexico ikiwa urefu wake ni ‘Mendoza Potentia Distributio’ kwa kiingereza waliitwa ‘Mendoza Power Distribution’ kwa lugha yetu adhimu lugha murua na tamu lugha ya kiswahili ‘Mendoza Nguvu Ya Usambazaji’ na nguvu yenyewe ya kusambaza walimaanisha ni kusambaza mihadarati.


“Kila mtu anayejiunga ‘MPD’ uchorwa tattoo ya mjusi kafiri ameng’ata kifurushi kidogo chini ya kwapa lake la kushoto la kila mmoja wao na hii ndiyo alama ya kila mmoja katika genge hili, sijui idadi yao kamili ila miongoni mwa matajiri wa madawa ya kulevya ‘Kingpin’ mwenye kumiliki kikosi kipana chenye kufanya kazi zake kwa utiifu mmojawapo ni huyu Mr. Fanuel… Pale kwenye kasri lake mtaa wa Avenida Pasco Usumancita kunalindwa kwa ulinzi mkali sana kwa kushirikisha kamera zilizofungwa kwenye kuta na miti ya minazi na pia kuna walinzi walio na mafunzo ya kutumia mbwa wakali wenye mafunzo na si pale nyumbani tu na analindwa pia hata atembeapo iwe kwa miguu au kwa usafiri, misafara yake ya magari uwa na magari manne ukiacha gari lake na magari haya walinzi ubadili mfumo hadi magari matano mpaka sita kutegemea na sehemu anayoenda, ikiwa anaenda ofisini kwake basi uongozana na magari matatu tu, mbele moja na nyuma ufuata yeye na nyuma ya yeye uwa kuna mawili ni kama msafara wa mawaziri… Ulinzi wa nyumbani kwake si kama ndipo mahali anapohifadhi madawa yake au wanapopatikana watu wa kazi za mihadarati la hashaa! Watu wake wa kazi wana kambi yao na mara moja niliwai kumpeleka mkewe huko ni nje ya mji kuna eneo kubwa lenye maghala makubwa ambayo kwa juu ukifika utagundua ni maghala ya kawaida ya kuhifadhi bidhaa ghafi za viwandani lakini kwakuwa mama yule alikuwa ananiamini sana kuna siku alikuwa amekerwa sana na mumewe akaamua tu kuniambia kwa chini ya maghala yao kuna kambi kubwa ya ‘MPD’ na kwamba mume wake akidhidi kumchefua atawaambia ‘DTO’ juu ya jambo hilo lakini baadaye wakaelewana na mama yule namshukuru Mungu alisahau kuwa alishawai niambia jambo lao hilo la siri, watu wao ‘MPD’ karibu wote uishi mule na kuendesha shughuli kulingana na kazi wanayopewa na boss wao” Maelezo marefu toka kwa Maxi yakaweka kituo hapa akajiweka vizuri katika kiti chake kilicho katika kigari cha kusukumwa, macho yake yakamwangalia Mr. Guti kisha akayatuliza kwa Brigedia Fernandes.


Mwisho wa sehemu ya kumi na mbili (12)


Bado tupo miaka kumi iliyopita!

Mkakati kazi wa mzee wa kazi Brigedia Fernandes na kikosi kazi chake wanadhidi kuunda mkakati utakaofanikisha kupata kilicho haki yake kutoka kwa Mr. Fanuel.


Je mpango wanao uandaa utafanikiwa?



“Kila mtu anayejiunga ‘MPD’ uchorwa tattoo ya mjusi kafiri ameng’ata kifurushi kidogo chini ya kwapa lake la kushoto la kila mmoja wao na hii ndiyo alama ya kila mmoja katika genge hili, sijui idadi yao kamili ila miongoni mwa matajiri wa madawa ya kulevya ‘Kingpin’ mwenye kumiliki kikosi kipana chenye kufanya kazi zake kwa utiifu mmojawapo ni huyu Mr. Fanuel… Pale kwenye kasri lake mtaa wa Avenida Pasco Usumancita kunalindwa kwa ulinzi mkali sana kwa kushirikisha kamera zilizofungwa kwenye kuta na miti ya minazi na pia kuna walinzi walio na mafunzo ya kutumia mbwa wakali wenye mafunzo na si pale nyumbani tu na analindwa pia hata atembeapo iwe kwa miguu au kwa usafiri, misafara yake ya magari uwa na magari manne ukiacha gari lake na magari haya walinzi ubadili mfumo hadi magari matano mpaka sita kutegemea na sehemu anayoenda, ikiwa anaenda ofisini kwake basi uongozana na magari matatu tu, mbele moja na nyuma ufuata yeye na nyuma ya yeye uwa kuna mawili ni kama msafara wa mawaziri… Ulinzi wa nyumbani kwake si kama ndipo mahali anapohifadhi madawa yake au wanapopatikana watu wa kazi za mihadarati la hashaa! Watu wake wa kazi wana kambi yao na mara moja niliwai kumpeleka mkewe huko ni nje ya mji kuna eneo kubwa lenye maghala makubwa ambayo kwa juu ukifika utagundua ni maghala ya kawaida ya kuhifadhi bidhaa ghafi za viwandani lakini kwakuwa mama yule alikuwa ananiamini sana kuna siku alikuwa amekerwa sana na mumewe akaamua tu kuniambia kwa chini ya maghala yao kuna kambi kubwa ya ‘MPD’ na kwamba mume wake akidhidi kumchefua atawaambia ‘DTO’ juu ya jambo hilo lakini baadaye wakaelewana na mama yule namshukuru Mungu alisahau kuwa alishawai niambia jambo lao hilo la siri, watu wao ‘MPD’ karibu wote uishi mule na kuendesha shughuli kulingana na kazi wanayopewa na boss wao” Maelezo marefu toka kwa Maxi yakaweka kituo hapa akajiweka vizuri katika kiti chake kilicho katika kigari cha kusukumwa, macho yake yakamwangalia Mr. Guti kisha akayatuliza kwa Brigedia Fernandes.


ENDELEA NA BURUDANI…!


TETAPLAN, GUERRERO-MEXICO

“MPD ina kiongozi na kiongozi wake sikuwa namjua mwanzoni lakini pia kama bahati kuna siku alifika kuonana na Madam ofisini kwake na kwenye maongezi yao niligundua yeye ndiyo kiongozi wa ‘MPD’ kwa jinsi alivyokuwa akisemwa na kuelekezwa ya kufanya ni mwanadada aitwaye Maria Rodgruez ‘Baby Beauty’… Mwanadada huyu si mtu wa mchezo mchezo ni mwanamke wa shoka haswa, ni fundi katika mapigano ya ana kwa ana na hata kutumia silaha, hapo kabla alikuwa ni mfanyakazi wa idara ya ujasusi ya Mexico Intelligence Agency ‘MIA’…. Alifukuzwa baada ya kukutwa na kosa kumjeruhi aliyekuwa kiongozi wa idara hii wakiwa katika mapambano na moja kikundi kati vikundi vinavyojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya… Kilichomfukuzisha kazi ni hilo tukio kupelekwa katika uchunguzi wa kujua kwanini Maria amempiga risasi kiongozi wake na anapohojiwa anasema hajui kama amefanya shambulizi hilo kwa kiongozi wake.. Ikabidi apelekwa kwa madaktari kwa uchunguzi zaidi wa kidaktari na ndipo Maria Rodgruez alionekana akili zake haziko sawa ndipo akaachishwa, ndugu zake wakaamua kushughulika zaidi kwa kumpatia matibabu ya juu zaidi maana alitelekezwa na serikali! Mungu jalia upande wake akapona vizuri na ndipo hasira zake akajiunga na mambo ya biashara za madawa ya kulevya mpaka alipokutana na Fanuel aliyemsainisha katika kikundi chake kipindi anaunda kikosi chake anachokiita ‘MPD’ kikosi kazi… Huyu Baby Beauty ndiyo kila kitu kwa Fanuel kuanzia ulinzi, manunuzi ya mizigo kwa watu wao Bolivia wanakonunua mzigo mwingi Cocaine, huku Peru na Colombia uwa anachukua kwa wingi Heroin na Methamphetamine ikiwa na mizigo yote hii tofauti na magenge mengine ‘MDP’ wanachukua mali iliyokwisha sukwa tayari kwa matumizi… Kwa Mexico wao na magenge makubwa kama Los Zetas, Sinaloa na mengine machache sana ndiyo wanachukua mzigo kwa mtindo huu huku soko la Mr. Fanuel kubwa ni huko Marekani anakopitishia jimboni Frolida, New Mexico na Texas kutokana na hali ya usalama ilivyo lakini kwake imekuwa kazi nyepesi kwakuwa kikosi chake kina nguvu kubwa sana maeneo ya mipakani na ndani ya Marekani amewekwa muungano na baadhi ya vikundi vinavyojihusisha na biashara hii.. Fanuel sasa anajiona yeye ni kama ‘El-Chapo’ au Luteni Salinas kwa kweli jinsi anavyoingiza pato kubwa huku akiwa kawashika viongozi wengi wa serikalini hasa wa usalama na ulinzi… Ni haya tu kati ya niyajuayo kwa ufupi kuhusu mfumo wa biashara haramu wa Mr. Fanuel” Mr. Maxi alitiririka kuelezea aliyonayo kuhusu Mr. Fanuel taita (kingpin) mkubwa wa ulanguzi wa madawa ya kulevya katika viunga vya Tabasco na Mexico yote kwa ujumla kwa baadhi ya sehemu, akifanya kazi kwa bidii kuwaharibu vijana kwa wazee wa mataifa haya na mataifa mengine duniani.


“Nataka kujua kwa uonavyo wewe.. Mimi kama mimi nawezaje kumsogelea Fanuel? Licha ya ulinzi mkubwa uliosema anao” Brigedia akaongea kutaka kujua.


“Mr. Fanuel si mtu wa kusogelewa na mtu ambaye yeye hajataka amsogelee kwa njia yoyote ile ila unaweza kumsogelea kwa kuomba miadi naye kwa kujifanya wewe ni mfanyabiashara unayejihusisha na mambo ya ujenzi unataka labda nondo kwa idadi kubwa pengine ya hata tani moja au mbili, hapo lazima utaweza onana naye” Akajibu Mr. Maxi kisha akanyanyua bilauri lililojaa juisi nzito ya zabibu akamimina kwenye glasi na kupiga funda mbili tatu kuweka koo lake sawa.


“… Mmh! Ni kweli lakini kuna njia nimeiona… Je mke wake inawezekana vipi kumpata kwa kumteka? Nataka nijue ulinzi wake huko vipi?”Katika sehemu hii ya chakula iliyogeuka sehemu ya maongezi sauti zilizokuwa zikisikika ni ya Mr. Maxi na Brigedia wengine walikuwa wasikilizaji huku mmoja alikuwa akisikiliza huku anaandika katika karatasi, huyu alikuwa mzee wa vimemo Mr. Ivan ‘alto’.


“Huyu ulinzi ni mkali lakini njia ya kumpata ipo… Pale katika kasri lao kuna uwanja wa gofu, anapenda sana kucheza gofu nyakati za jioni hasa siku ya jumamosi… Uwanja wao wa gofu upo mbali na kasri na mbali na bustani yao iliyo kama kitalu binafsi cha wanyama wadogo wadogo na ndege kama tausi na mbuni… Lakini kote kumezugushwa ukuta mrefu wenye nyaya za ulinzi zilizowekwa kwenye mfumo wa umeme kwa juu zikiwemo na kamera… Nimechagua eneo hili kwa sababu upande wa pili kuna mabweni ya wanafunzi wa kike wa chuo cha Universidad Autonoma De Villahermosa tawi la jimbo la Tabasco…. Hivyo kama inawezekana mkajipanga vizuri ni rahisi kuingilia kwa kupitia upande huu kwakuwa pia kuna mfereji wa maji unaopitisha mkondo wake eneo la uwanja wa gofu, umezingwa kwa juu kwa zege lakini ukomo wa zege uishie unapoungana na mfereji wa maji machafu yanayotoka kwenye mabweni ya wanafunzi kisha kuna kimto kidogo kinapokea maji hayo mpaka kwenda mto mkubwa wa Grijalva… Ule mkondo wa mfereji ni wa asili kabla hata Fanuel ajajenga kasri lake ulikuwepo hivyo hakukuwa na njia ya kuudhibiti zaidi ya maji mengine uenda kwenye bwawa lake la samaki ambalo pia utumiwa na wanyama, pamoja na ndege wake walio kwenye kitalu chake na ya ziada ndiyo utokea hapa na si mara zote mfereji huu unakuwa na maji zaidi ya kipindi cha mvua, ambacho si kipindi hiki…” Akaeleza kirefu Mr. Maxi alipopumzika akanywa juisi funda mbili za kufuatana kisha akatulia akijilamba mdomoni ndani kwa ndani (raha ya utamu wa juisi).


“Ahsante Mr. Maxi… Atembeapo barabarani anatembea na walinzi wangapi?”


“Gari lake uwa yeye na dereva tu na ndivyo ilivyokuwa nilivyokuwa namuendesha na kazi yangu ilikuwa si kumuendesha tu ni hadi kumfunga mkanda wa usalama katika kiti anapoingia, kumfungua tunapofika mahali tulipokuwa tumeenda kisha haraka natakiwa nishuke nikamfungulie mlango… Yaani ni usultana aliokuwa nao… Nyuma ya gari uwa tunafuatwa na walinzi katika gari moja tu ambapo hao walinzi uongozana na daktari mmoja kwa ajili ya kumpa tiba ya huduma ya kwanza madam akikutwa na jambo baya, yeye madam hana gari la kuongoza safari mbele sababu safari zake hatowagi muongozo rasmi kwa mwingine zaidi yangu mimi ninayeendesha gari yake hivyo wale wa nyuma utufuata tu ila kaka njia rahisi ni ile ya mwanzo niliyoieleza, kule kwenye uwanja wao wa gofu!”.


“Hiyo gari ya nyuma ya walinzi wanatumia mfumo wa ulinzi wa kizamani au wa kisasa unaombatana na teknolojia?”


“Wanatumia ulinzi wa kisasa sababu wanakuwa wanaona mbele yetu sisi mita ambazo mimi sifahamu ni ngapi lakini nilikuwa nikijua kwa wao kutuamrisha kwa njia ya sauti kwa spika zilizo ndani ya gari, ambapo kama kuna hatari wameiona au njia ni mbaya basi wao uona kabla na utujulisha tubadili njia au tusimame na kweli uwa kuna kitu… Hili lilinijuza kuwa wana mtambo wa autopilot camera uliounganishwa kwa kutokea mbele ya gari nayoendesha na hata pembeni ya gari kwa mzunguko walio uunganisha kitaalamu”


“Hapa kweli hili kumpata huyu mwanamama itatubidi tumteke akiwa huko kwenye burudani yake ya kucheza gofu… Hivyo nguvu yetu kubwa tutaitumia kuchunguza jinsi tutakavyoweza kuingia na kumchukua… Kazi hii ya kumteka huyu mwanamke itatakiwa iambatane na kazi ya kumpata kiongozi mkuu wa ‘MPD’ mwanadada ‘Baby beauty’… Hawa wawili ndiyo watasababisha tumpate Fanuel kwa maongezi naye na kumlazimisha afanye nitakachotaka mimi” Akaongea Brigedia Fernandes na watu wote waliokuwa wakisikiliza wakatingisha vichwa vyao kukubali.


“Huko sahihi Feca.. Njia rahisi ya kucheza na huyu mtu ni hii aliyopendekeza Maxi.. Pia nimegundua Maxi ni zaidi ya msaada kwetu hivyo nitaomba baada ya opersheni hii tuone tunamsaidia vipi zaidi” Akaingia kwenye maongezi Mr. Guti kwa kutoa hoja aliyonayo ambayo pia ilipita kwenye kichwa Brigedia Fernandes kwani alitikisa kichwa chake kukubali tena huku akitabasamu tabasamu lake ambalo ukilitizama utashindwa kung’amua lilivyojaa majivuno fulani.


“Nitafurahi sana Mr. Guti kujumuishwa nanyi na kufanya kazi chini yenu… Pia nimefurahi kwa kuona umuhimu wa njia niliyoiona ni nyepesi kufanikisha mpango wa kumpata Madam Felister” Mr. Maxi hakuficha furaha yake akatoa shukrani na kuongezea maelezo ya kushukuru mpango maelekezo yakekuwa umewaingia wazito hawa.


“Ivan! Itatubidi kesho asubuhi tuondoke hapa kuelekea Villahermosa nikiwa na watu wangu wote wa kazi na pia utanichagulia watu sita wengine twendeni tukafanye kazi huko Villahermosa, njia ya kuingia tushaelekezwa kazi yetu ni kwenda kuihakikisha na kujua tunafanyaje haswa maana hatuitajiwi kufeli na kwa ilivyo Fanuel hata angemiliki jeshi lote la Mexico hawezi kupambana nami na sisi sote kwa ujumla lazima nikamfunze ninapokuwa nipo uraiani yeye hawezi mfalme… Ahsante Mr. Maxi.. Wewe utabaki hapa wakati sisi tukiondoka ila tutakuwa tukiwasiliana na wewe kila hatua tunayopiga kwakuwa maelekezo yako ni muhimu kila muda tutakaokuwa huko” Brigedia Fernando alitoa maelekezo kwa watu wake kisha kikao hiki kifupi kilisitishwa wakaendelea na mambo mengine ikiwemo kujiandaa na maandalizi ya kuelekea Villahermosa manispaa, jimbo la Tabasco.


***** ***** *****


MSHTUKO MPD I,VILLAHERMOSA,TABASCO-MEXICO

Ilikuwa saa tano na dakika tano usiku unaomalizia siku ya ijumaa kwa saa za Mexico katika jimbo la Tabasco, manispaa ya Villahermosa mtaa wa Avenida Pasco Usumancita.


Wanaume wapatao nane walikuwa wakisaidiana kupanda ukuta unaozunguka mabweni ya wanafunzi wa kike wa chuo cha Universidad Autonoma De Villahermosa, tawi la chuo kikuu cha Universidad Autonoma De Guadalajara.


Mabweni haya hayakuwa na walinzi wa kuzunguka pande zote kama sehemu ambazo uwa tunasema ulinzi ulioimarishwa, hapa mlinzi mmoja tu alikuwa yuko kulinda geti la kuingia katika mabweni haya wasichana watupu ambayo yapo nyuma ya madarasa ya chuo hiki cha wanafunzi mchanganyiko.


Hivyo upande wa wanaume hawa haikuwa vigumu kwao kusaidiana kuhakikisha kila mmoja anapanda ukuta.

Brigedia Fernandes alikuwa akiwaongoza wanaume wengine walio na ujasiri na mafunzo yanayokaribiana na uwezo wake, wote walikwea ukuta na sasa wakawa wako nyuma ya majengo ya mabweni ambayo yalikuwa majengo manne makubwa yaliyojengwa kwa mtindo wa ghorofa (losheni) tatu kwenda juu na kwa muda huu vyumba vingi taa zake zilizimwa na upande wa juu kabisa wa ghorofa ambalo lilikuwa umbali wa mita za mraba kama mia hivi na walipoingilia kikosi kazi kinachoongozwa na Feca, lilikuwa likwaka taa na mabinti kadhaa kwa walionekana wako mule wanajisomea masomo ya kujisomea usiku kabla muda wa kulala.


“Kwa maelekezo ya Mr. Maxi kwa kule bondeni ndipo kuna mfereji wa kupokea maji ya mvua inaponyesha katika eneo hili la mabweni ya mabinti hawa na ndipo tutaona mfuniko wa kuingia kwenye mfereji husika…Sidhani kama kuna mtu anatokea huku mida hii… Kuko poa kabisa tunaweza tembea kama kawaida kuelekea kule ila tusijiamini sana kila mmoja ashike bastola yake” Aliongea Brigedia Fernandes baada ya wote kuwa washaruka ukuta kuingia ndani ya eneo la ndani la mabweni, wamekutana chini ya mti mkubwa wa muembe.


Kikosi hiki usiku huu kiliongozwa na Brigedia Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ mwenyewe akiambatana na watu wake waliokuwa wafungwa waliotoroka wataalamu wa kijeshi waliofukuzwa jeshi kama yeye Feca, Koplo Maxiwell Zuantejo, Koplo Savatel Luca Santos, Sajenti Lara Moentes, Stafu Sajenti Morientes Jose Gudrado na vijana watatu wasio wai kuwa waajiriwa wa jeshi katili sana Wolfs Klauben Gend a.k.a Hitler, Bezela Muricho ‘Animal’ na mzee wa vimemo Ivan Alberto ‘alto Genius’ hii genius ikiwa imeongezwa siku mbili tu zilizopita sifa iliyoongezwa na Brigedia Fernandes na kutaka watu wengine wote kumuita ivan jina la ‘Alto Genius’.


Eneo hili la nyuma ya mabweni kulikuwa hakuna mwanga wa kutosha kutokana na kuwa ni

usiku, mianga ya taa za umeme isiyotosheleza kwa kuwa ilikuwa ni mianga inayotokea katika madirisha ya vyumba vya mabweni na moja kubwa inayoleta mwanga kwa kutokea mbele ya ghorofa la mbele kabisa ambako wao hawafiki huko.


“Ni hapa tumefika” Akaongea Wolfs ‘Hitler’ alipoona sehemu inayoonyesha kuna karavati linaonekana kwa chini likiwa limezibwa na udongo mzito.


“Yah! Kweli ndiyo lakini maelezo ya Maxi hayajatosheleza hakusema kama kumefunikwa na funiko kubwa hivi.. Mawazo yangu kwa jinsi nilivyomsikiliza nilijua kuko wazi kabisa..!!” Akasema Brigedia huku miguu yake yote miwili ikisogeza maudongo huku na huko na wengine nao wakajiunga kufanya anavyofanya kwa tahadhali yenye umakini mkubwa wasisikike.


“Sidhani ka ma yeye aliwai kufika siku za karibuni eneo hili, nafikiri atakuwa alifika lakini muda mrefu uliopita… Sisi tufanye tunachoweza” Akaongea Koplo Savatel Santos.


“Shida iliyopo tunaingia hapa halafu hatujui kama mtu tunayemtarajia kama kesho atafika kucheza mchezo wake wa gofu..” Sajenti Lara akaongea huku ana tabasamu akiweka kama masikhara lakini kwa kiasi alimkera Feca ambaye alimuangalia tu wakagonganisha macho na wote kuendelea na kazi ya kusogeza udongo.


“Lara… Mwanajeshi wewe.. Tumefunzwa uvumilivu jeshini… Kumbuka hapa ndipo kitovu cha kazi yetu… Tumebeba vinywaji na vyakula hili tuweze kusubiri, subira ni jambo muhimu sana kwetu kwa sheria zetu za kijeshi, wewe ukianza kulalamika, je ‘Alto’ na Wolfs ambao si wanajeshi kama wewe watasemaje?” Brigedia akaamua afunguke kwa onyo la kidizaini akihofu kuzusha mengine endapo kutatokea kubadilishana maneno.


“Maongezi tu… Usichukulie serious boss! Niko tayari kukesha hata siku tatu ndani ya karavati hili ilimradi kupata kile unachotaka wewe boss wetu… Nisamehe sana kama nimekukera” Haraka Sajenti Lara akaongea na kufanya kupite ukimya kidogo.


Waliuona mfuniko wa chemba kubwa inayounganisha maji yanayotoka ndani ya ukuta unaozunguka kasri la Mr. Fanuel Miguel Mendoza na kwa ushirikiano wa watu wawili wakaweza kuufunua na kuusogeza sehemu ambayo watapita kisha Wolfs akatoa tochi na kumulika ndani, wote kwakuwa walikuwa wamezunguka eneo lililotoka mfuniko waliweza kuona ndani.


Kulikuwa kuna maji madogo sana, maji ya kuogelea mende au unaweza ukasema maji ya unyayo na upana wa ndani ya karavati ulikuwa ni upana unaoweza kuwaweka watu wawili wakiwa sambamba na kila mmoja akwa kafika mwisho ila si wabanane.


Kwa umakini na tahadhari ya hali ya juu wote wakaingia ndani ya karavati na kisha wakaburuza mfuniko uliokuwa upande ukafunika eneo lile.


“Hapa sasa inatubidi tukachunguze huko kwenye kiwanja cha gofu hivyo hatuna budi kusonga mbele na kabla ya yote uliye mbele mulika usalama wetu kila upande huko mbele” Akatoa maelekezo Brigedia na mbele kabisa alikuwepo ‘alto genius’ akafuata maelekezo kwa kumulika ndani kona zote huku akisogea mbele na alipohakikisha hakuna chochote cha kuhatarisha usalama wao kwa eneo la karibu kuelekea kwenye kona ambayo hawakuwa na uwezo wa kuona zaidi pande za huko akawaonyesha ishara wenzake walio nyuma yake hatua kumi wasogee.


Walifuatisha kwa kutambaa kwakuwa hakuna aliyeweza kusimama wakiwa humu hivyo stahili ya kwenda humu ilikuwa ni kutambaa tu kama mwendo wa masokwe.


Mwendo wa mita za mraba kumi na mbili ulimfikisha muongoza msafara Ivan katika sehemu ambayo kama angesogea zaidi basi alichokiona kingeleta athari katika safari yao, ilikuwa ni kamera inayochukua matukio hivyo haraka yeye Ivan akazima tochi na kulala chini.


“Vipi Ivan?” Akauliza Koplo Savatel kwakuwa yeye alikuwa nyuma ya ‘alto’ na alikuwa hajui kama anayewaongoza anaongea mara chache sana tena kwa kulazimisha sana.


“Alto.. Mpishe mbele Savatel hili aone kuna nini atujuze” Ombi likatoka kwa Feca na utekelezaji ukafanyika haraka, karavati hili kulikuwa na giza totoro kuanzia mbele hivyo ilimuwia ugumu Savatel kuona mpaka alto akamuelekeza kwa mikono wakiwa gizani hivyo hivyo.


“Boss! Kuna CCTV… Ndicho kilichomkwamisha alto… Ila kwakuwa kuna giza siamini kama inaweza kuwa na nguvu ya kuchukua gizani kama hivi hivyo imani yangu Ivan hakuonekana, naisogelea nikaifanyie utundu kidogo” Akaeleza Koplo Savatel.


“…Sawa… Ifunge kifaa cha kugandisha… Ngoja nikupe..!” Akaongea Brigedia Fernandes kisha akafungua begi lake na kutoa kifaa kilicho kama sumaku lakini mahususi kwa kugandisha uwezo wa kamera za kuchukua matukio ikabaki na tukio ambalo wakati kikifanya kazi kilichukua tukio hilo.


Kwakuwa yeye Feca alikuwa wa pili kutoka nyuma katika msafara wao wanaotambaa kama masokwe ndani ya karavati ilibidi ampe wa mbele na mbele akampa wa mbele yake mpaka kifaa kile kikamfikia Koplo Savatel Santos akakichukua na papo hapo hakusubiri akaanza kutambaa kama nyoka anayevizia kukamata panya kuelekea ilipo kamera ya cctv karibu na wavu unaonekana ndiyo funiko la kutokea ndani ya uzio ukuta unaozunguka eneo lote la kasri la Mr. Fanuel.


Aliamini giza zito liliweza kuzuia yeye asionekane alifika eneo husika akapapasa papasa mpaka akashika kikonyo kinachoshika kamera husika kutokea kwenye kuta ngumu ya karavati, akacheza anavyoweza kupachika kifaa cha kupoteza uwezo kamili wa cctv na kwakuwa kifaa hiki uwa kina sumaku maalumu kwenye kitako chake hivyo akakingandisha kwenye kikonyo kikatulia na kuanza shughuli ya unafiki si shughuli kamili, yaani huko kwenye mtambo wa kompyuta unaopokea kila kitu kutokea katika kamera hii ilikuwa ikipokea kwa tofauti taarifa zisizo na muendelezo.


Koplo Savatel Santos ni mwanajeshi mzoefu wa kazi hizi hivyo uwa hasubiri maelekezo ya mtu yeye mwenyewe ufanya kazi vile akili yeke inavyompeleka na hata Brigedia Fernandes alikuwa akijua haya na kumuamini toka wako jeshini wakifanya kazi pamoja.


Mwisho wa sehemu ya kumi na tatu (13)


Kazi imeanza!


Wanajeshi wafukuzwa wenye ujuzi katika kazi zao wakiongozana na vijana ngangari wenye sifa kazi za kazi za kutisha wanasogelea kasri lenye ulinzi unaosifika kuwa ulinzi bora.


Nini kitafuata?



Kwakuwa yeye Feca alikuwa wa pili kutoka nyuma katika msafara wao wanaotambaa kama masokwe ndani ya karavati ilibidi ampe wa mbele na mbele akampa wa mbele yake mpaka kifaa kile kikamfikia Koplo Savatel Santos akakichukua na papo hapo hakusubiri akaanza kutambaa kama nyoka anayevizia kukamata panya kuelekea ilipo kamera ya cctv karibu na wavu unaonekana ndiyo funiko la kutokea ndani ya uzio ukuta unaozunguka eneo lote la kasri la Mr. Fanuel.


Aliamini giza zito liliweza kuzuia yeye asionekane alifika eneo husika akapapasa papasa mpaka akashika kikonyo kinachoshika kamera husika kutokea kwenye kuta ngumu ya karavati, akacheza anavyoweza kupachika kifaa cha kupoteza uwezo kamili wa cctv na kwakuwa kifaa hiki uwa kina sumaku maalumu kwenye kitako chake hivyo akakingandisha kwenye kikonyo kikatulia na kuanza shughuli ya unafiki si shughuli kamili, yaani huko kwenye mtambo wa kompyuta unaopokea kila kitu kutokea katika kamera hii ilikuwa ikipokea kwa tofauti taarifa zisizo na muendelezo.


Koplo Savatel Santos ni mwanajeshi mzoefu wa kazi hizi hivyo uwa hasubiri maelekezo ya mtu yeye mwenyewe ufanya kazi vile akili yeke inavyompeleka na hata Brigedia Fernandes alikuwa akijua haya na kumuamini toka wako jeshini wakifanya kazi pamoja.


ENDELEA NA MAUTAMU..!


MSHTUKO MPD II,VILLAHERMOSA,TABASCO-MEXICO

Aliujaribu kuusukuma wavu mzito uliofunika eneo linalopokea maji ya mvua kutokea eneo la ndani la ukuta wa Mr. fanuel, kwa kichwa haraka akang’amua huu wavu si wavu wa kawaida ulitengenezwa kwa nondo iliyo kamili kama chuma cha mjerumani hivyo hapa inahitajika msaada wa ziada si nguvu za mikono yake wala miguu yake, akatoa begi lake lililo mgongoni, akafungua zipu akatia mkono wa kulia na kuibuka na jeki ya gari ndogo kama chupa ndogo ya chai ya kuhifadhi vikombe viwili.


Kwenye begi lake pia alikuwa na chuma kilicho na upana na urefu wake kama pampu ya baiskeli zilizo nyingi mtaani kwa mafundi baiskeli (walijiandaa kutokana na uzoefu wao wa kazi), jeki ikawekwa chini akapachika kwa juu kiurefu chuma kile mwisho wa urefu wake ukawa umekamata nondo moja kati ya nondo zilizosukwa na kuchomelewa vizuri.


Akaanza kunyonga jeki kutumia kichuma kidogo lakini ukikizungusha kinapandisha jeki juu na mara chuma aliloliweka lipandishe mfuniko likaanza kupanda, mfuniko taratibu ukaanza kupanda juu na dakikka tatu mbele kwa juu huko kukasikika ‘nkwaaah!!!’, akaendelea na pakafunuka.


Koplo akatulia kuvuta umakini baada ya kazi, masikio yake yakiwa makini kusikia chochote hata kama kinanyata mnyato wa mnyama anayenyatia windo.


Utulivu ulitamalaki hakukuwa na chochote zaidi ya upepo uliokuwa ukivuma na kusuka suka miti ambayo wao hususani yeye Savatel aliye mbele hawakuwa wakiiona, bastola mkononi tayari kwa chochote alitoa sura mpaka eneo la katikati ya pua.


Macho yalizunguka kwa kasi huku kichwa kikisapoti kugeuka pande zote na ni kweli kwa ramani maelezo waliyopewa aliweza kuona hapa walipo wapo kwenye bonde na hili lilimjulisha Lavatel kuwa maji ya eneo lote la karibu na maeneo mengine uporomoka kufuata mdomo huu wa karavati.


Hatua kama kumi za miguu ya mtu mzima kulikuwa na muinuko unaozuia yeye kuona baada ya muinuko kuna nini kingine zaidi ya matawi ya miti mikubwa na kwengine aliiona miti yenyewe yote hivi ilijipanga vizuri kudhihirisha ni miti iliyopandwa kwa ustadi na watu wa hapa.


“Hapa kwenye mdomo wa karavati ni bondeni kuna alama za kuwa mikondo ya maji ya mvua toka kila upande unaozunguka kasri uleta maji kwenye hili karavati, kutokea hapa hatua kumi kuna muinuko, natoka kwenda kwenye muinuko nione eneo la juu zaidi…!” Akaongea aliporudisha kichwa ndani ya karavati kuwaambia waliokuwa wakimsubiri awape mrejesho.


“Wawili mlio mbele muende naye mara moja wakati sisi watatu tunasubiri taarifa zenu..!” Akaongea kiongozi wa msafara huu Brigedia Fernandes ‘Feca’.


Koplo Savatel Santos akaweka vizuri begi lake alilolipachika mgongoni mikanda ikipita makwapani kutokea mgongoni kuja hadi mabegani, akaibuka taratibu toka mtaroni akitambaa bila kujiinua, nyuma yake alifuata Sajenti Lara Moentes ambaye naye kwa nyuma alifuata mzungu wa kijerumani mwenye asili ya ujerumani, mzungu katili ambaye kwa ukatili naweza nikasema umefika kipimo cha asilimia 95% kati ya binadamu wenye mioyo ya ukatili ikiwa kipimo chao ni cha asilimia hizi, Wolfs Klauben Gend ‘Hitler’.


Koplo Savatel macho yake yakiwa yamezoa giza na wote wakiwa wamevaa mavazi aina ya ‘over roll’ aligundua kamera nyingine inayochukua matukio kuelekea eneo la mdomo wa karavati, hapa alistuka sana na kutoa pumzi nzito na kwa haraka akawapa ishara wanomfuata kisha akajiweka nyuma ya mti mmoja kati ya miti miwili midogo isiyo na mashina mapana.


Sajenti Lara na Wolfs nao wakafuatisha alichofanya mwenzao wao wakijikusanya kwa pamoja nyuma ya mti mwingine, ikawa wote wanaangalia huku na huko.


“…Chochote tutakachofanya kitakacho haribu ukimya wa eneo hili kwa njia yoyote ile kitaharibu mpango wote wa kumteka Mrs. Fanuel… Hivyo tuombe kamera ile isiwe iliyoweza kutuchukua kwa uzuri wakati tukitoka, inasikitisha sana..!” Akaongea Koplo Savatel kwa sauti ya kunong’ona ila aliyohakikisha inawafikia Wolfs na Lara.


“Giza la hapa ni zito sana Koplo, naamini kwa nguo tulizovaa kama kuna mtu anafuatilia katika chumba cha cctv atakuwa hajafanikiwa kuona chochote… Ingekuwa mchana tungeshashtukiwa na kufanya tuzingwe kwa aina ya ulinzi tulioelekezwa kuwa upo hapa”Akaongea Sajenti Lara.


“Tuombe iwe hivyo.. Tunatakiwa tuangalie pande zote za hapa kama kuna kamera nyingine ukiacha tuliyoiona ikiwa imefungwa kwa ukutani.. Kazi kwetu..!” Akaongea tena Koplo Savatel.


Dakika kumi na dakika kadhaa kwenda dakika kumi na tano kila mmoja akiwa kalala chini kabisa kana kwamba anataka kutoboa ardhi auzamishe mwili wake ndani, alikuwa akipepesa macho huku na huko kama wataona kamera iwe kwenye miti au kwingine.


“Nimeiona moja kwenye mti ule mkubwa aina ya mkaratusi na pale nafikiri ndipo uwanja wa gofu unaanzia pale” Ikasikika sauti nzito ya Wolfs ikiongea kwa kunong’ona ila muungurumo wake wenye mkwaruzo unaofanana na watumiaji vilevi vikali ilisikika.


“Inachukua kwa kuja huku au?” Akahoji Koplo.

“Imeelekezwa kwenye kona ya ukuta upande wa kulia… Nafikiri kamera hatari kwetu ni ile inayochukua kuja kwenye mdomo wa karavati”Akajibu Wolfs.


“Hatuna njia ingine zaidi ya kuipa unafiki na kisha tuombe kusiwe na mtu atakayepita karibu yake kwa kutwa yote ya kesho”Akaongea tena Koplo huku akichungulia kwa chati uelekeo ilipo kamera.

“Ipo juu.. Natatamani niipasue kwa risasi ila kufanya hivyo ni kuleta maswali kwa wahusika.. ilipo pale itatuwia ugumu sana kutimiza lengo letu kesho” Akaongezea Koplo.


“Kuna mwanga wa tochi unakuja maeneo ya huku, naona unatokea kule juu ilipo kamera iliyo kwenye mti wa mkaratusi..!”Akaongea kwa sauti ya chini Wolfs na wote wakamsikia.


“..Shiit! Hatutakiwi kuharibu hii operesheni kwa kuua au kumpoteza mtu yote aliye kwenye idadi ya walinzi wa hapa… Angalieni anavyokuja acha mi nimpigie Brigedia nimuelekeze hali halisi pengine ataleta wazo muafaka….!!” Akaongea haraka haraka lakini kwa sauti ya chini Koplo Savatel Santos kisha akajivuta kuelekea kisehemu chenye kifusi kilichotengeneza kama kijimlima cha mchanga akajilaza sambamba na kimlima kile huku kukiwa vimti vidogo vidogo vichipukizi.


Alitoa simu na kwa tahadhali mwanga wa simu usije ukaonekana kutokea mahala pale akatafuta namba haraka haraka kisha akaruhusu kupiga akaiweka chini kwenye michanga kisha akalaza sikio lake akawa kaiziba.


Muito mmoja tu ikapokelewa na anayepigiwa Brigedia Fernandes.


“Halloo!” Sauti ya upande wa pili ikaongea baada ya kupokea tu.

“Kuna kamera ya cctv inaharibu plan yetu ya kulichunguza eneo hili ingawa giza la…!” Hakuendelea Brigedia akaingilia.

“Niko hapa hapa kwenye mdomo nimetokeza robo kichwa hivyo nimeona mengi na hata kamera nimeiona, sasa sijui kwanini hukuiona? Savatel… Ok! Itabidi tuishughulikie haraka maana itakuwa kikwazo wakati kesho tutakapoanzisha mtiti wa kumteka Madam Felister.. Ebu so….!”Naye hakumaliza alichotaka kuongea, Koplo akamkatizia.

“Kuna mtu anakuja upande wetu… Wolfs amemuona kwa mbali na anazidi kusogea… Kama tulivyokubaliana kwamba tudhibiti tumizi lolote la nguvu litakalosababisha wao kesho kuongeza umakini, tumfanyaje huyu akifika hapa?”

“Jificheni, muacheni kabisa naamini hawezi kuwaon..!” Simu haikuendelea kuwa hewani Koplo akakata simu.


“Jitahidini wote kujificha kwa kila hali asituone labda awe na mbwa ndiyo itatubidi tuwadhibiti..!’ Akaongea Koplo Savatel haraka kwa sauti ya chini iliyosikiwa na walio jirani yake wote wakiwa wamelala chini sawa sawa na manyasi na michanga iliyopo hapa mwisho wa bonde kwa kwenda kwenye muinuko.


Mwanga wa tochi ulisogea taratibu zilipobaki mita kama kumi hivi toka alipolala Wolfs wakaona pia na dalili ya moto wa sigara inayovutwa na hapa waliyekuwa wanamuona kwa uzuri zaidi walikuwa Koplo na Wolfs tu na pia waliweza kutambua wakiendelea kulala vizuri mtu yule kwa uelekeo anaoenda atawapita tu kwa juu ingawa alikuwa anazungusha huku na huko mwanga wa tochi kumulika kila upande huku anasogea taratibu ana wasiwasi anaharibu tu mapafu yake kwa sigara anayoivuta kwa mbwembwe za kuuchezea moshi kwa stahili mbalimbali.


Aliendelea kuja taratibu nyayo zake zikawa zinasikika kwa wote na hakuwa na mbwa zaidi ya bunduki aina ya SMG ya kichina aiitwayo Norinko QBZ-97, silaha hii ya kivita kubwa na hatari sana kutoka kwa moja ya nchi mafundi wa kuunda silaha za kivita, nchi ya China ni silaha inayotumika hasa huko maeneo yenye vita za wenyewe kwa wenyewe hususani Afrika yetu.


Bunduki hii yenye uzito wa kilo 3.35 kgs, urefu 78 mm ina uwezo wa kubeba magazine yenye uwezo wa kubeba risasi 30 mpaka 75 huku ikiweza kushambulia kwa kupiga risasi 650 kwa dakika kama unaweza kufyatua wewe mtumiaji yaani ikiwa magazine imejaa full automatic inaweza kumaliza magazine ya risasi 30 kwa sekunde 2.7 ingawa hakuna anayeweza kushambulia kwa kasi hiyo ni katika bunduki ambazo Mr. Fanuel Miguel Mendoza alikuwa amewanunulia wafuasi wake wa ‘MPD’ wanaolinda hapa kwake na kwenye maghala yake ya kuhifadhi malighafi za kiwanda kinafiki kumbe lengo kuu ni kulinda mizigo haramu ya mihadarati.


Mlinzi huyu ndiyo alikuwa na mzigo huu ukiwa unaning’nia kwenye mbavu zake za upande wa kulia kwakuwa kamba za kuishika bunduki ilikuwa kaipachika bega la kulia na mkono wa kushoto ndiyo ana tochi na mkono wake wa kulia sigara ilikuwa ikiwekwa mdomoni anakamua anashusha hili kuzipa tundu za pua kazi zilizokuwa hazijapangiwa na muumbaji wetu, kazi ya kutoa moshi kwa mbwembwe.


Asante kwa waliokuwa wamejificha ielekee kwa Mungu! Kwani mlinzi hakuwaona wala kusikia harufu zao akawapita.


Simu ya Koplo Savatel iliita katika hali ya ku vibrate (kitetemeshi) kwa kuwa alikuwa ameiseti hivi toka wanasogea eneo hili la mtaa wa Avenisa Pasco Usumancita, haraka bila kuchelea akaitoa mfukoni kuangalia nani mpigaji? Jina lilibeba namba inayopiga lilimjuza ni Brigedia Fernandes.


Akajipindua kulalia mgongo kichalichali na kisha akapopkea simu kwa kusugua kioo kati kwenda kulia maana simu yake ilikuwa ni smartphone aina ya Samsung J7.


“Nipe muongozo ameshapita..!” Akaongea Koplo Savatel Santos huku akitumia mkono wake wa kulia akidhidi kuigandamiza sikioni kana kwamba anataka simu itumbukie ndani ya sikio.


“Nimemuona nilikuwa naufuatilia mwanga wa tochi unavyoruka ruka ingawa sikuwa namuona… Ni hivi muda huu wa saa sita nusu ni muda ambao watu wengi wanaofanya kazi za ulinzi uendelea kuwa makini kwa mujibu wa maelezo ya Mr. Maxi kutoka hapa tulipo hadi unapoanza uwanja wa gofu ni mita ishirini za mraba pia uwanja wa gofu hadi kilipo kitalu chenye misitu midogo midogo, miti mingi , wanyama na ndege ni mita za mraba hamsini kwenda upande aliotokea mlinzi na anapoelekea mlinzi huko ndiyo kuna nyumba wanazoishi wahudumu wa kasri hili zipo mita arobaini toka hapa na kasri lenyewe la Mr. Fanuel lipo katikati likiacha eneo kubwa sana lenye nyasi nzuri, bustani zenye maua na mabwawa ya kuogelea ni mita mia na hamsini toka hapa tulipo na ndipo maeneo yanaolindwa kwa ulinzi mkali zaidi.. Hivyo naomba mfanye subira huko mlipo sababu naamini mpaka sasa hamjaonekana kwenye rada zao hasa hii ambayo tunatakiwa tuidhibiti… Tusubiri mpaka muda ambao walinzi uwa wamechoka kiubinadamu muda wa saa tisa usiku, hapo tutazishughulikia kamera zote zilizo maeneo ya kiwanja cha gofu hili kazi yetu isije kuharibiwa kabla haijafanyika” Maelezo marefu ya Brigedia Fernandez yalisikilizwa kwa umakini na Koplo Savatel Santos na kumuingia hasa hakufanikiwa kupanua mdomo wake kuhoji lolote au kuitikia kuwa amekubali simu ikakatwa ikawa ngoma droo kwakuwa naye alimkatia wakati alipompigia.


Ukimya ulitamalaki eneo lile na baridi likawa linadhidi kuchukua nafasi kila masaa yanavyoyoyoma wanaume hawa waliendelea kusubiri bila kuongea ongea wala kuruhusu usingizi uchukue nafasi katika macho yao kila mmoja akiwa mfuatiliaji wa kutizama saa kila baada ya muda fulani kupita. Si waliokuwa eneo la karibu ya muinuko ambao ni watatu wakiongozwa na Koplo Savatel pia si wale walio ndani ya karavati na kaka mkubwa Brigedia Fernandes wote walibaki kimya hakuna ‘story’.


Saa tisa na dakika mbili usiku wa manane ukiwa umekolea baridi kali lililoambatana na upepo Brigedia Fernandes akajiinua mahala alipo na kutokeza kichwa akajizinga vizuri a kutoka katika karavati akitambaa chini kabisa kwenye nyasi fupi aina ya magugu zilizo hapa palipo na mdomo wa maji kuingia kwenye karavati, hakuwa peke yake nyuma yake walifuata wenzake wawili waliotoka na katika karavati wakitambaa kwa stahili ile ile anayoitumia yeye, wakijigandamiza sambamba na ukuta unavyokwenda kwa chini kabisa.


Mtambao ule uliwafikisha mahala ambapo kwa juu kuna cctv kamera, hapo Feca akajipindua bila wasi wowote kwakuwa kamera ile ilikuwa inachukua zaidi eneo la mdomo wa karavati na si hapa walipo ambapo ni mita kumi za mraba ndipo inaanza kuchukua hivyo kama wao kuchukuliwa basi watakuwa wamechukuliwa kuanzia pale kwenye karavati hadi kuja mita kumi kabla haujafika ilipo kamera yenyewe.


Begi likatoka mgongoni mwa Feca na kuamia mkononi mwake, alioongozana nao wakasimama wote kama yeye alivyosimama.


“Mnatakiwa mniwekee ngazi nifike juu nifanye kazi ya dakika tatu tu…!”Akaongea Brigedia Fernandes wakati huo huo waliokuwa wametangulia kuingia eneo hili wakiongozwa na Koplo Savatel Santos wao walikuwa wakilinda maeneo haya asitokee mtu wa kuingilia kazi inayotaka anza kufanywa na Brigedia Fernandes.


Staff Sajenti Morientes Gudrado mtu ya mbavu nene yenye kupiga mazoezi hasa kipindi chote alichokuwa gerezani yeye muda wote wa ziada alikuwa akiutumia gerezani, hapa alijiweka vizuri akijiamini vya kutosha kuwa nguvu zake hazina masikhara juu akapanda Koplo Maxiwell Zuantejo miguu yake akaisimamisha kwa kila mguu upande wake katika mabega ya mbavu mtu Morientes yakawa ngazi yake, wakiwa wameugekia ukuta kana kwamba wanajaribu kuugandamiza na vifua vyao.


Brigedia alipomaliza kazi ya kuandaa kifaa chake chenye unafiki mkubwa katika kamera za cctv hii ndiyo kiboko yake, aliwatizama wanajeshi wenzake aliotimuliwa nao kwa makosa yao ya kujihusisha na mihadarati. Kisha akaangalia juu ilipo kamera ya cctv na mara akakwea kwa kasi ya nyani anayekwea mti kumkimbia mnyama wa hatari pindi alipomfuma chini ya mti, yeye hakukwea kwenye miti bali kwenye migongo ya watu hawa waliokuwa wakijua wanafanya nini? Maana walitega viganja vyao kwa chini ya mgongo na ndivyo hivi Brigedia alikanyaga kwa kasi mpaka juu yao kisha akatulia akiwa juu kabisa kichwa kikiwa mita moja tu toka ilipo kamera, ukuta mrefu na kamera iliyowekwa juu kabisa ikawa si lolote angeweza hata kuing’oa kama angetaka.


Kazi ilifanywa kwa kasi akaitia unafiki kamera ile ikawa sasa inachukua tofauti na dhumuni la walioiweka hapa, akaseti iwe hivyo mpaka itakapofika saa kumi na mbili ibadilike ichukue muda huo kidogo kisha igande na walioko huko kwenye chumba cha kuongoza kamera hizi waone kama kawaida tu kisha baada ya masaa fulani itachukua tena, mambo haya kwa Feca ilikuwa kwake ni kama kumsukuma mlevi chini ya bonde mambo ambayo uwa yanafanywa na majasusi wa CIA, MOSSAD, FSB na mashirika mengine makubwa ya kijasusi.


“Hapa mpaka mtu apite karibu hapa ndiyo atagundua kuna unafiki umefanyika” Akaongea akiwa kashashuka toka juu Brigedia Fernandes.


Koplo Savatel na wenzake watatu pamoja na kina Brigedia Fernandes walishirikiana kukagua maeneo yote na wakapiga picha maeneo yote ya kuzunguka uwanja wa gofu ambao waliamini siku hii iliyokwisha anza ikiumaliza usiku wake wa kuanzia saa sita za usiku kwa saa za Mexico, kisha walipachika vikamera vidogo katika miti miwili katika njia inayokuja kwenye uwanja wa gofu ambavyo waliviunganisha na mtambo wao mdogo ulio kwenye kompyuta iliyokuwa ikiongozwa na mtaalamu wa kompyuta Ivan Alberto ‘alto genius’ mwisho wakapachika kamera ingine kwenye mti mmoja kamera ambayo ilikuwa ikichukua robo ya eneo la kuchezea na vyote hivi walivifanya kwa umakini sana.Wote waliamini wanakwenda fanya vile walivyopanga bila hofu kuwa watafeli.


Mwisho wa sehemu ya kumi na mbili (14)


Wawindaji wakimuwinda mke wa Fanuel walimaliza ukaguzi wa eneo ambalo kesho yake wanahitajika kufanya kazi itakayoamua hatima ya na mustakabali wa genge jipya watakaloliunda lenye madhumuni ya kupindua meza za ma ‘Kingpin’ na magenge mengine sifika ndani ya Mexico.


Mamabo mazuri zaidi yanakuja katika hatua nyinginezo zinazokuja hivyo kaa nami kwa uhondo zaidi, uhondo wa utamu wa dodo lenye ladha murua ya asali.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO, SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)


BY K M M M @2018/19


Shughuli bado ipo nchini Mexico, bado tunaendela na mikakati ya Brigedia mfukuzwa Fernandes ‘Feca’ hatua zinadhidi kusogea.


Kikosi kazi kiliingia mtaa wa wazito, mtaa wa Avenida Pasco Usumancita yanapopatikana makazi ya tajiri na kibopa mzito wa madawa ya kulevya katika Mexico ya wakati wa miaka kumi iliyopita, nguli huyu dhuluma yake ishaanza kutiliwa sumu na aliyekuwa rafiki yake Brigedia Fernandes.


Je? Nini kitatokea kwa kikosi kazi kilichofika hapa kwenye kasri la Mr. Fanuel Miguel Mendoza


Majibu ya maswali kama haya yanapatikana katika sehemu zinazofuata.



Kazi ilifanywa kwa kasi akaitia unafiki kamera ile ikawa sasa inachukua tofauti na dhumuni la walioiweka hapa, akaseti iwe hivyo mpaka itakapofika saa kumi na mbili ibadilike ichukue muda huo kidogo kisha igande na walioko huko kwenye chumba cha kuongoza kamera hizi waone kama kawaida tu kisha baada ya masaa fulani itachukua tena, mambo haya kwa Feca ilikuwa kwake ni kama kumsukuma mlevi chini ya bonde mambo ambayo uwa yanafanywa na majasusi wa CIA hasa manguli waliopo SAD, MOSSAD, FSB na mashirika mengine makubwa ya kijasusi.


“Hapa mpaka mtu apite karibu hapa ndiyo atagundua kuna unafiki umefanyika” Akaongea akiwa kashashuka toka juu Brigedia Fernandes.


Koplo Savatel na wenzake watatu pamoja na kina Brigedia Fernandes walishirikiana kukagua maeneo yote na wakapiga picha maeneo yote ya kuzunguka uwanja wa gofu ambao waliamini siku hii iliyokwisha anza ikiumaliza usiku wake wa kuanzia saa sita za usiku kwa saa za Mexico, kisha walipachika vikamera vidogo katika miti miwili katika njia inayokuja kwenye uwanja wa gofu ambavyo waliviunganisha na mtambo wao mdogo ulio kwenye kompyuta iliyokuwa ikiongozwa na mtaalamu wa kompyuta Ivan Alberto ‘alto genius’ mwisho wakapachika kamera ingine kwenye mti mmoja kamera ambayo ilikuwa ikichukua robo ya eneo la kuchezea na vyote hivi walivifanya kwa umakini sana.Wote waliamini wanakwenda fanya vile walivyopanga bila hofu kuwa watafeli.


ENDELEA NA UKALI WA MAMBO…!!


MSHITUKO KWA MPD III, VILLAHERMOSA,TABASCO-MEXICO

Makazi ya muda ndani ya karavati la maji yatokayo ndani ya eneo la himaya ya kasri la kisasa la Mr. Fanuel Miguel Mendoza kibopa mwenye ukwasi wa kutosha, mwenye nguvu kubwa sana ndani ya jimbo la Tabasco.


Zamu ya kuangalia usalama ilipewa kwa watu wawili, mmoja akiangalia kioo cha laptop ndogo iliyokuwa ikiwaka muda na kupokea kila kinachokatiza mbele ya kamera ndogo walizozitega karibu na uwanja wa gofu ulioko kwenye kasri, huku mmoja aliyebaki alikuwa karibu na mdomo unaoingiza maji kwenye karavati akiwa na bastola aina ya Astra-Unceta Model 44 zao la Hispania, hizi ndizo bastola ambazo Mr. Guti uwapa vijana wake wakitoka kwenda mahalia kufanya kazi, yeye Guti aliuziwa bastola hizi kama ishirini na tano na rafiki yake muuza silaha mwenye urafiki na mmoja wa watu wa ukoo wa muasisi wa kiwanda cha silaha cha ‘Arms’ kilichopo Guernica, Eibar-Hispania kiwanda kilichoasisiwa na Juan Esperanza kisha kuboreshwa zaidi na Mr. Pedro Unceta, wanatengeneza bastola za aina nyingi sana lakini zote uanza na jina la Astra kisha kama kubadilika ubadilika mbele ya Astra.


Saa kumi na dakika ishirini na mbili ikiwa wote washafanya mzunguko wa kulala, kulindana na kula vyakula vyepesi vyepesi pamoja na vinywaji mbalimbali walivyovibeba, kweye kioo cha laptop kamera namba moja ilionyesha wanawake wawili wenye wajihi wa kimexico haswa wa umri wa kati ya miaka arobaini mpaka arobaini na tano kwa kukadiria, wakiwa wamevaa mavazi ya kimichezo (tracksuit) wakija muelekeo wa njia ya uwanja wa gofu, nyuma ya wanawake wale walikuwepo wanawake wengine watatu wakiwa wameshika fimbo za kuchezea mchezo wa gofu kila mmoja na mwingine kati yao aliongezea kwa kushika kikapu kidogo cha plastiki ambacho wao kina Brigedia hawakuweza kuona ndani ya kikapu kuna nini? Pia kulikuwa na watoto wadogo wanne watatu wa kike na mmoja wa kiume umri ukiwa unafuatana na hata kwa baadhi kurandana, wakiwa katika mavazi ya kimichezo na wao kama walivyovaa wakubwa wao kama si wazazi wao (hatujui kwa sasa).


“Haraka Ivan, ruhusu kamera za eneo lile zichukue matokeo yote kisha ya pale maana naamini watakuwa makini kuangalia familia ya bosi inacheza mchezo katika hali ya uangalizi mzito zaidi..!” Akaongea Brigedia Fernandes na mzee wa vimemo na mtaalamu wa kuchezea program za kompyuta Ivan Alberto 'alto' alianza kwa spidi kucheza na kompyuta kubadilisha hali ya unafiki wa kamera kwenda katika uhalisia.


“Tuvumilie mpaka waanze kucheza ndipo urudishe katika hali vimitambo vyetu usifanye makosa” Akaongea tena Feca na bwana vimemo akatikisa kichwa kukubali.


Nyuma ya wanawake hawa wote ambao kwa ujumla wake walikuwa watano kulikuwa na wanaume wapatao sita wakiwa kwenye mavazi ya kufanana (sare) na kila wawili walikuwa wamevaa miwani huku wengine miwani walikuwa nayo lakini ilikuwa kwenye mifuko yao ya mashati yao waliyovaa ambayo ni mashati yenye mifuko mingimingi, wanaume hawa kila mmoja alibebelea bunduki zinazofanana aina na bunduki ya yule mlinzi aliyepita kukagua maeneo akiwa na tochi katika usiku uliopita kisha Koplo Savatel na wenzake wawili kujificha, bunduki ambazo katika watu hawa walio ndani ya karavati walikuwa wakizijua aina yake kuwa ni Norinko QBZ-97 zao la mchina hii.


“.. Heeeh!... Yah… Nafikiri…Mtu tunayemuhitaji yupo hapa ni huyu mwanadada…. Yes! Ni yeye… Picha inaendana na maelekezo niliyoyaandika kwenye simu yangu.. Yes! Ni yeye Madam Felister lakini kumbe ni bado wamo, bado anavutia sana nilifikiri ni mwanamke wa kawaida si mzuri aiseee kumbe nilikuwa nikizidanganya hisia zangu… Chombo..!” Akajikuta anasema macho yake yakiwa hayataki kupoteza hata lepe moja la kupiga ukope.


“Yes! Ni yeye na huyu mwingine namjua ni dada maarufu sana hapa Mexico ni mwigizaji wa tamthilia zetu za kimexico…!” Akaongea mtu katili sana, (a monster man) Wolfs.


“… Hahahaha hahahaha! Mpenda tamthilia wewe.. Uwa unazifuatilia nini?” Akacheka kidogo Koplo Savatel na kumuuliza Wolfs, wakaangaliana.


“Nilifuatilia sana kipindi fulani… Huyu mdada ndiye alinifanya nifuatilie.. Au mwamuonaje? Ni mzuri acheni tu, Mungu anaumba aiseeeh! Naomba tuondoke nao wote hawa namtaka dada yule ni kama kajileta kwangu, namuota sana nashukuru leo kumuona tena katika misheni”. Akaongea kwa shauku kubwa Wolfs, ama kweli mapenzi hayana mwenyewe, mapenzi ni kama njaa, njaa haina baunsa. Wolfs ‘Hitler’ ukatili wote alionao kumbe naye ana mapenzi kwa mtu anayemfikirisha juu ya jambo hilo.


“Tunawachukua wote hakuna kuremba na hata vile vitoto nafikiri ni watoto wao, aisee kazi itakwenda kuwa nyepesi sana kuipata familia yote.. hahahahah hahahahaha.. Subiri mchezo wao uchanganye, tunawazunguka kisha tunashambulia kwa kasi walinzi wao tunaondoka kupitia hapa karavatini… Acha niwapigie kina Rude wasogee kwenye geti la kuingia kwenye mabweni..” Akatoa maelekezo huku mikono yake ikifanya kazi ya kutafuta namba ya simu anayotaka kuipigia katika simu.


Muda wa dakika moja mbele simu yake ilianza kuita upande wa pili aliopiga na haikudhidi miito mitatu simu ilipokelewa na huko alipopiga ikidhihirisha mpigiwa naye alikuwa akiisubiri kwa hamu simu toka kwa Brigedia Fernandes ‘Feca’.

“Halloow! Mkuu lete habari” Mpokeaji akaongea kwa haraka ndani ya lugha yao wa mexico kilatin.

“Sogeeni na gari zote mbili mtaa kusudiwa standby! Nikibipu tu wakati ujao mtasogea kwa kasi lilipo geti hakikisheni hamuwashtui watu wa huo mtaa kwa ujio wenu kwa namna yoyote ile pia hakikisheni mnaangalia usalama wetu sote yaani hata wakitokea kutaka kuja kuzuia tusitoke nyinyi ndiyo mtawajibika kuzuia hakuna kibwengo yoyote anayefika kutuzuia kuondoka na mateka wetu… Kazi njema!” Aliongea kwa sauti ya haraka iliyo makini na msisitizo wa hali ya juu kwa aliyempigia kisha akakata simu.


Walisubiri pale kwa dakika kumi na tano kisha wakapeana mkakati wa mwisho huku ‘alto’ akirudisha mfumo wao wa kawaida waliokuwa wakiutumia kuzichezea cctv kamera na taratibu yenye umakini mkubwa sana Koplo Maxiwell Zuantejo alifunua mfuniko wa nondo waliofunika kwa kuuegesha tu, mkono wa kulia alikuwa ameikamatia barabara bastola ndogo aina aipendayo yeye katika shughuli za kazi za kazi bastola aina ya Berreta zao la italiano, ikitokea viunga vya Gardone Val Trompia ndipo kilipo kiwanda cha kuunda bastola hizi na aina nyingine ya silaha mbalimbali hapo nchini Italia, mwanzilishi wa kiwanda akiwa Mr. Bartolomeo Berreta.


Mgongoni mwake alikuwa na bunduki ambayo nayo ikiwa tayari kwa kutumika endapo italazimika kutumika na zote hizi silaha walikuwa wote kwa ujumla wamezifunga kiwambo cha kuzuia sauti hili wakianza kushambulia washambulie kwa bila kusikika milio ya risasi.


Dakika moja nzima ilimgandisha pale kwenye mdomo wa karavati Koplo Zuantejo akitumia darubini kuvuta maeneo mbalimbali ya mbali na walipo kuona hali yake iko vipi na baada ya kuona jinsi hali ilivyo akarudisha kichwa ndani akawaonyesha alama ya dole wenzake akimaanisha mambo safi na aliporudisha kichwa juu hakusubiri akachomoka kwa kasi akiwa anatambaa kwa kasi kuelekea ulipo mti wa kwanza kabisa ambao upo karibu na mdomo huu wa karavati ambako ukitoka hatua kumi mbele kunaanza miinuko na kote hapa kukiwa na nyasi aina ya magugu zinazojiotea tu kutokana na maji yanayotuhama na mengine kupita nyakati za mvua.


Sekunde ishirini mbele aliibuka Koplo Savatel Santos naye akatambaa kwa kasi kuelekea ulipo mti mwingine na haikuchukua sekunde kumi akamuona mtu anakuja eneo la huku akitokea kwenye muinuko ulio umbali wa kama mita hamsini za mraba toka wao alipo, kwa kumtizama akatambua ni mlinzi anayezunguka zunguka kuhakikisha usalama eneo hili.


Kaplo Savatel akamuangalia Koplo Zuantejo na alipoona wameangaliana akajilengesha macho yake kwa vidole cha kati na shahada kama anataka kujitoboa machoni kisha akapindua mkono ule wa kiume kule anapotokea mlinzi aliyemuona Zuantejo akaelewa na kumuonyesha alama ya dole gumba kuwa yuko makini na papo hapo akatupa macho kule kwenye mdomo wa karavati na kukutana na macho ya Wolfs akiwa katokeza kichwa anataka kujitokeza kabisa ndipo Zuantejo akamuonyesha ishara atulie na azame kwa ndani kwanza.


Wolfs akarudisha kichwa chake taratibu naye pia akawaambia wenzake wanaosubiri katika foleni ya kutoka kuwa watulie kidogo kuna jambo.


Makoplo wawili waliokuwa wanajeshi shupavu wa jeshi la wananchi la Mexico walijibanza vizuri kwenye miti waliyopo kusubiri mlinzi anayekuja ambaye alibebelea bunduki ya kama walinzi wengine wa hapa wanazobeba zikiwa tayari kutumika endapo zitahitajika Norinko QBZ-97, bunduki hatari sana kutoka China.


Akija bila wasiwasi wowote akijiaminisha hakuna jipya linaloweza kutokea mara alipoupita mti aliojificha Koplo Savatel mlinzi yule alishtuka, aliona kama kivuli kikiwa kinahama kwa kasi na ni kweli kilikuwa kivuli cha Koplo Zuantejo akifanya mjongeo wa kubadili eneo kuzunguka hili isije akaonekana.


Shtuka yake iliweza tambulika toka kwa Koplo Savatel aliye nyuma yake hatua nne tu toka alipo kwani alimuona mlinzi yule ghafla amesimama halafu mkono wake ukahamia haraka kushika kitako cha bunduki na taratibu huku kasimama alikuwa akikiangalia kile kivuli kinavyomalizia kuondoka bila mtu aliye na kivuli kujua kama kivuli kimemsaliti, ukubwa wa mwili wake pia ulichangia.


Mlinzi akaangalia kushoto na kulia kisha akainua bunduki ikawa thabiti mkononi akaanzisha mjongeo wa taratibu toka alipo kurudi kwa juu lakini hakufanya mjongeo wa pili kwani alivamiwa kwa kasi kubwa kwa kutokea kwa nyuma mvamizi akiwa Koplo Savatel.


Walienda wote chini kwa kishindo chepesi kilichozingwa na manyasi magugu yaliyoko eneo hili kabali kali sana ikiwa imekamata barabara shingo ya mlinzi ilisababisha mikono yake yote miwili itumike kuhangaika kuondoa kabali aliyopigwa maana si mchezo shingo ilishikwa ikashikika hapana chezea watu na mafunzo yao.


Taratibu nguvu zilimuisha mlinzi hakuweza piga kelele wala kufanya jingine lolote zaidi ya kurusha rusha miguu yake huku na huko kujaribu kuiokoa nafsi yake na umauti lakini wapi, makamasi yakaanza kumtoka na machozi yakianikiza, shingo ikamaliziwa kwa kuvunjwa kwa nguvu na Koplo Savatel huku kijasho chembamba kikimtoka maana nguvu ilitumika sana kwake mlinzi hakuwa na mwili wa kizeke zeke alijaa kimazoezi Israel mtoa roho alifanya yake akapitia chake.


Koplo Zuantejo alikuwa pembeni yao akishuhudia huku akihakikisha hakuna kitu kingine kinachosogea pale kwa macho yake kuzunguka huku na huko kwa kasi, bunduki ikiwa mikononi mwake maana bastola alishairudisha mahala pake.


Maiti ilifunikwa kwa majani yaliyotafutwa na kukusanywa kwa haraka na maafisa hawa wa zamani wa jeshi kisha kikarushwa kijiwe kidogo kuelekea kwenye karavati.


Wolfs akaibuka na kukutana na alama ya dole gumba toka kwa kila mkono wa kulia wa Koplo na Koplo mwenzake, haraka akarudisha kichwa chake ndani akawaonyesha na wenzake alama kama aliyoonyeshwa yeye na wote wakaelewa sasa mambo ni safi.


Wolfs akatoka akitambaa kuelekea walipo watangulizi wao ambao nao hawakusubiri wakaanza kutambaa kuelekea unapoanza muinuko na kwakuwa usiku uliopita sehemu zote walishazichunguza walikuwa wakienda kwa kupita maeneo wanayotambua fika kwanini wanapita eneo hilo.


Kikosi chote wa watu saba kikiwa kimelala chini kuzunguka uwanja wa gofu walikuwa wakisubiri ishara watayoambiwa sasa tayari waanzishe kilichowafikisha eneo la kasri hili, eneo la uwanja wa gofu.


Subira yao iliwapeleka dakika zipatazo tano toka wazinge eneo hili lenye kamera za cctv lakini wao usiku uliopita walishazifanyia michezo ya kijasusi na kuzipoteza kazi halisi na kuwa zikifanya kazi kinafiki vile wao wanavyotaka, kwani mpira wa gofu uliopigwa na mmoja kati ya wanamama wale uliruka karibu na eneo linapoanza bwawa lililo ndani ya kasri hili na kote huku kulikuwa kumepandwa nyasi zilizokatwa vizuri sana kama ujuavyo viwanja vya gofu na kama huvijui basi juwa uwa vinakuwa hivi kwa uzuri wake.


Kwa furaha ya wachezaji na waangaliaji walisogea kundi karibu lote kuja huku kuona shoot itakayopigwa kwa mbwembwe kwakuwa ilikuwa inatakiwa kwa mpigaji mmoja kufanya shoot ikitokea hapa kwenda sehemu ingine kwa wacheza gofu wenyewe wanajua mi si mchezaji wa gofu na wala si shabiki wa mchezo huunaandika tu nilichoadithiwa ndani ya ubongo wangu (lol).


Brigedia akiwa sambamba na Bezela Muricho, alizungusha kichwa chake huku na huko kutokea pale chini kwenye majani mafupi na mti kadhaa iliyozunguka huku na huko alipoona wengi wanamuangalia yeye toka walipo nao wakiwa wamelala chini alitoa ishara ya mkono wa kulia akinyoosha kidole kimoja juu cha shahada akakunja ngumi na kunyoosha tena kidole kimoja juu akakitikisa mara mbili na kuachia kiganja akikunjua ngumi hii ilimaanisha jambo pia.


Mwisho wa sehemu ya kumi na tano (15)


Kasri la kibopa mwenye ukwasi wa kutosha unaotokana na ufanyaji wake wa biashara za haramu, limeingiliwa bila wenyewe kutambua kama tayari watu wa hatari wakiongozwa na mwanajeshi mfukuzwa aliyefika cheo cha Brigedia, Brigedia Fernandes.


Nini kitatokea?

Je? Mpango utakwenda vile walivyopanga Brigedia Fernandes na watu wake.

Itakuwaje hapa katika uwanja wa gofu?

Majibu ya haya yote ni wewe kuweka subira na kusubiri sehemu ijayo kumi na nne kuona kama kutakuwa na mziki mnene unaotikisa spika bila kuzipasua au nini?..!


Mimi mwandishi na mtunzi na kuletea tu kile nilichohadithiwa na kukipokea katika ubongo wangu, ahsante sana.



Subira yao iliwapeleka dakika zipatazo tano toka wazinge eneo hili lenye kamera za cctv lakini wao usiku uliopita walishazifanyia michezo ya kijasusi na kuzipoteza kazi halisi na kuwa zikifanya kazi kinafiki vile wao wanavyotaka, kwani mpira wa gofu uliopigwa na mmoja kati ya wanamama wale uliruka karibu na eneo linapoanza bwawa lililo ndani ya kasri hili na kote huku kulikuwa kumepandwa nyasi zilizokatwa vizuri sana kama ujuavyo viwanja vya gofu na kama huvijui basi juwa uwa vinakuwa hivi kwa uzuri wake.


Kwa furaha ya wachezaji na waangaliaji walisogea kundi karibu lote kuja huku kuona shoot itakayopigwa kwa mbwembwe kwakuwa ilikuwa inatakiwa kwa mpigaji mmoja kufanya shoot ikitokea hapa kwenda sehemu ingine kwa wacheza gofu wenyewe wanajua mi si mchezaji wa gofu na wala si shabiki wa mchezo huunaandika tu nilichoadithiwa ndani ya ubongo wangu (lol).


Brigedia akiwa sambamba na Bezela Muricho, alizungusha kichwa chake huku na huko kutokea pale chini kwenye majani mafupi na mti kadhaa iliyozunguka huku na huko alipoona wengi wanamuangalia yeye toka walipo nao wakiwa wamelala chini alitoa ishara ya mkono wa kulia akinyoosha kidole kimoja juu cha shahada akakunja ngumi na kunyoosha tena kidole kimoja juu akakitikisa mara mbili na kuachia kiganja akikunjua ngumi hii ilimaanisha jambo pia.


ENDELEA NA MUENDELEZO..!!


MSHITUKO MPD IV, VILLAHERMOSA-TABASCO

Walinzi walijipanga kwa stahili ya kuwa wao wanapishana pishana kuzunguka sehemu mbali za ndani ya uwanja wa gofu na hawa ni walinzi binafsi wa mke wa Mr. Fanuel Miguel Mendoza pamoja na watoto wake ambako hapa walikuwa watoto watatu ni wa bwana mkubwa mwenyewe aliyezaa na mke wake Felister ndoa yenye miaka mitano tu lakini ilileta baraka ya watoto watatu wa kwanza wa kiume wa pili wa kiume tena kisha wa mwisho mwenye miaka miwili na nusu alikuwa wa kike, mtoto wa nne aliyekuwa hapa alikuwa ni mtoto wa shosti mkubwa sana wa Madam Felister ambaye ni mwanadada maarufu sana katika nchi ya Mexico mwenye makazi yake ndani ya jiji la Mexico City lakini kila jumamosi ufika katika jimbo la Tabasco kuja kumtembela rafiki yake na kucheza mchezo anaoupenda sana mchezo wa gofu pia ufika na mtoto wake huyu ambaye umri wake ni miaka minne kama mtoto wa pili wa Mr. na Mrs. Fanuel tajiri kubwa.


Mfumo wa ulinzi wa walinzi binafsi wa Madam na wengine walioko hapa ulishaangazwa vizuri toka kwa kikosi kazi cha kazi za kazi waliokuwa wakijikinga na miti pia wakiwa wamelala chini kwa kusaidiwa na nyasi ndefu ambazo ziko pembeni ya uwanja wa gofu hivyo Brigedia aliwagawa watu wanne wakazingire kwa ukaribu maeneo wanayozunguka na kupishana pishana walinzi wale.


Kikosi kiliongozwa na Koplo Savatel Luca Santos,akawepo katili Wolfs ‘Hitler’, Sajenti Lara Moentes, Bezela Muricho ‘Animal’ na Ivan ‘alto genius’ ambapo walitumia fursa ya Madam kusogea kona ya karibu na walipo kina Feca kujisogeza karibu zaidi na walinzi ambao walikuwa wako katika hali ya kutaka kukutana hili wapishane wawili waende upande magaharibi na wawili waelekee wanakotoka wenzao mashariki ya uwanja huku wawili wakiwa kazi kuwa karibu na alipo madam na watu wake wakiwemo madada wa kazi (wasaidizi binafsi wa kazi kwa watoto na hata yeye).


Wanaopishana walipokaribiana kikosi kazi cha kazi za kazi kilijiinua kwa mtindo goti moja chini mkao wa kupiga goti na goti moja likiinuka bunduki zilizo na kiwambo cha kuzuia risasi (sailensa) zilipiga kazi kwa ufasaha hakuna aliyeweza nyanyua hata kwato, wanaume waliwatandika risasi za vichwa tena kwenye sura ni maubongo tu yaliyokuwa yanaruka na milio ya ‘pyuuuuh, pyuuuuh, pyuuuh iliyosikika na miili kuangukiana kama magunia ya dagaa yaliyokosa balansi.


Upande wa Brigedia nao hawakuwa nyuma kwa kasi waliibuka kisha wakafyatua risasi kuelekea kwa walinzi wawili waliobaki ambao walikuwa hatua kumi hivi toka walipo Madam na wenzake, umauti ukawakumba kwa kasi ya kimbunga cha Katrina.


Makelele yakaanza kupigwa kwa wanawake kwa taharuki wa waliyoyaona, ikabidi haraka zifumuke mbio za huku walipo kina Koplo Savatel wote watano kuelekea kule walipo wanawake wale, spidi kali ya wazee wa kazi hawa kuelekea kule ambako palikuwa na umbali wa mita kama thelathini lakini sauti za wanadada na watoto zilikuwa kubwa sana.


Brigedia Fernandes akawaelekezea bunduki kisha akaweka kidole chake cha shahada katika papi (lips) zake kwa ishara wafunge midomo yao lasivyo anamtandika risasi atakayeenedelea kuhanikiza kelele na ikawa atakavyo wote walinyamaza hadi watoto nao mbele ya mdomo wa bunduki nao wakafunga midomo papi zao zikabaki zinatetemeka kama wako kwenye baridi la kipimo cha sentigredi ziro, walisogeleana na wamama wakawakusanya watoto kuwakumbatia.


Staff Sajenti Morientes Gudrado alichomoa bomba ya sindano (syringe injection) kutoka moja ya mifuko ya begi lake, bomba hili la sindano lilikuwa lishajazwa dawa anayoijua yeye na haraka akaanza kwa Madam Felister akamchoma sindano ile katika moja ya mishipa anayoijua yeye kitaalamu na madam akakukuruka kidogo lakini nyuma yake alifika Ivan ‘alto’ akamdhibiti, mwanamama dawa ndogo aliyomiminiwa ilimchukua akafumba macho na kupoteza fahamu.


Koplo Savatel na kikosi chake kilifika eneo lile na mara ving’ora vikaanza kusikika vikihanikiza vilikuwa ving’ora vya hatari spika zake zilikuwa zimefungwa sehemu mbali mbali za eneo la kasri hili.


Morientes alipitia kwa watoto wote akawachoma sindano ile akammalizia na rafiki wa Madam Felister, wale madada wa kazi watatu hawakuwa na kazi nao hivyo katili Wolfs aliwagonga kitaalamu ngumi nyepesi za shingo wakapoteza fahamu.


Kilichofuata waliwabeba na kuanza kukimbia kueleke kule kwenye mdomo wa karavati, Brigedia Feca begani mwake alimbeba mke wa Mr. Fanuel, Koplo Zuantejo akambeba shosti wa madam na vitoto viwili alivinyanyua ‘alto’ mkono wa huku na huku na viwiii akavinyanyua Morientes na mbio zao zilikuwa kana kwamba wamebeba mabegi ya kawaida.


Koplo Savatel, Wolfs, Bezela na Sajenti Lara walikuwa wakikimbia kwa kinyume kuangalia wanapotokea walinzi kama wafungwa waliofunguliwa toka ndani ya gereza lenye mateso, wakiwa na silaha mikononi mwao, mpaka Brigedia na wenzake walinzi wale licha ya kuwa wamewaona walikuwa bado hawajaanza kushambulia kwa kuhofia wale waliobebwa hivyo wataalamu hawa wazee wa kazi za kazi waliling’amua hilo, haraka mfuniko wa karavati ukafunguliwa na Koplo Savatel kisha akazama ndani kama joka kubwa linalokimbia hatari akapokea vitoto vyote akaviweka chini kisha kwa kasi wakaingia kwa kufuatana Wolfs na Koplo Zuantejo akiwa na mzigo wake akapita.


Brigedia Fernandes akageuka kule wanapotokea walinzi wakiwa wanakuja mbio maana wengi walikuwa wavuta bangi na madawa hivyo walikuwa wakifanya mambo kwa mihemko tu bila akili na laiti asingekuwepo mkubwa wao wangeweza kushambulia kwa kupiga risasi bila kujali chochote, hivyo Feca aliacha wenzake wote waingie kisha yeye akaingia kwa kutanguliza miguu akiwa kamuacha Madam kwa nje alipomaliza kuzama akamvutia kwa kumburuta huku kamshika makwapa mwanamama yule akiwa hana fahamu akamzamisha ndani ya karavati walinzi wakiwa wamesogea mita kama thelathini tu wafike pale.


Haraka akasogea Wolfs ‘Hitler’huku anatabasamu na Feca alipomuangalia akamuona ana bomu la kutegwa mkono wa kulia kalikamatia na pia ana bomu la kutupwa na mkono wa kushoto ikabidi ampishe kichaa huyu mpenda kuua kikatili.


Wolfs akavuta mfuniko na kabla hajautokeza uso wake kuchungulia zilipigwa risasi za dabodabo kama mia na zaidi toka kwenye bunduki za waliokuwa wakiwasogelea huku wakiogopa kushambulia, Risasi zililengwa kwenye mdomo wa karavati baada ya jamaa kuona mfuniko wa karavati unasogezwa kukawa vumbi tupu la kuchakazwa kwa vyuma nondo vilivyosukwa kutengenezwa mfuniko, kelele kubwa sana milio ya bunduki aina ya ‘NorInko QBZ-97’ ambazo zina sauti kali sana, Wolfs hakujali kwakuwa zilimkosa kosa alijibanza pembeni na kwa kuona hivyo akauacha mfuniko bila kuuvuta wala kuugusa kabisa.


Akahakikisha anajibinya pembeni kwa chati kisha akatoa ‘lock’ ya bomu la kutupwa kwa mdomo na kama alivyotaka risasi ziliachwa kushambulia kukawa kumebaki mabaki ya vumbi likimalizia hapo ‘Hitler’ hakusubiri kwa mkono wenye kasi akarusha bomu litoke toka ndani ya karavati tena bila kuangalia analirusha kuna watu au wameondoka ‘shenzi!!’ mlio wa bomu ukijumlishwa na wa kelele za maumivu za watu idadi ya kuridhisha zilimfanya Wolfs kutabasamu kisha akaliacha bomu kutega pale pale chini ya ya mdomo wa karavati akageuka na kuondoka mbio kulekea muelekeo wa waliko elekea wenzake.


Brigedia alipibu simu ya dreva Rude kumaanisha asogee getini kama alivyomuelekeza kisha aliongoza msafara ule uliokuwa mgumu kwakuwa ilibidi waende wameinama kwa mtambao wakiwa wamebeba mabegi yao, silaha zao mabegani na kwa kuhakikisha hawawaumizi mateka wao walitumia dakika kumi kufika hadi ndani ya eneo la nyuma la mabweni ya wanafunzi.


Wakafunua mfuniko na kutokeza ambako walisababisha taharuki kubwa eneo lile maana waliwakuta wanafunzi wengi wa kike wakiwa eneo wengine wanajisomea wengine wanapiga soga, makelele yaliibuka ndipo Wolfs aliyekuwa wa mwisho kutoka pale akapiga risasi juu na kuwaomba wanyamaze.


Pamoja na kuwa alikuwa akikimbia kainama kama ilivyo ada na sharti la karavati hili lakini kasi yake ilikuwa kubwa na hakuwakuta wenzake walikuwa washafika mwisho wa karavati, hata kabla hajatoka mlio wa bomu ulisikika na kutikisa karavati lote, sauti iliyorindima na kilio cha sauti ya mtu mmoja, akiwa ndiyo anatoka toka karavatini alitabasamu tena na kisha akageuza shingo kutizama vumbi la bomu linalokuja hadi kwa ndani ya karavati kuleta msogeo wake karibu na mdomo wa upande huu wa eneo la nyuma la majengo wa mabweni ya wasichana.


Brigedia Fernandes akiwa kambeba mke wa Fanuel aliongoza kwa kukimbia bila kujali taharuki iliyokuwepo pale na hapa sasa walikuwa wamegawana watu hawa kwa kila mmoja kubeba mtu mmoja akiachwa Wolfs aliyewai kuwafikia na kusapoti ulinzi wao alikuwa kakamatia bunduki anaongoza msafara mbele wakazunguka bweni moja wakatokea mbele ya mabweni na hata mlinzi wa getini alipowaona ilibidi atupe bunduki yake aina ya gobore pembeni kisha akanyosha mikono juu kana kwamba kaamrishwa afanye hivyo.


Wolfs akafungua geti wakatoka akiwalinda wenzake kwa kukaa pembeni ya geti gari mbili za wagonjwa (ambulance) rangi nyeupe zenye maandishi mekundu ‘Ambulancia Villahermosa’ zilikuwa zikiwasubiri getini mbele haraka waligawana magari kuingia na mateka wao, gari zikaondoka kwa kasi ziiacha vumbi la lami ya hapa ambayo ni lami iliyowekwa miaka mingi iliyopita hivyo ilikuwa baadhi ya sehemu zingine kuna mashimo na kuleta vumbi dogo.


Waliendea barabara ambayo ilikuwa si rahisi kukutana na watu wa kikosi cha Mr. Fanuel (MPD), watu hawa walikuwa wamejiandaa sababu mbio za madreva waliokuwa wakiwaendesha kwa gari la mbele lililokuwa liiongoza msafara dreva wake akiwa Maxi Anguelo Rude ‘Bwoy’ ziliwafikisha mtaa wa El Recreo nyuma ya jengo la hospitali ya General Dr. A. Rovirosa Perez iliyo pembezoni kidogo ya manispaa ya Villahermosa.


Hapa walikuwa wamewaacha Cisco na Alejandro Lopez ‘La Culebra’ wakiyalinda magari mawili aina ya Town Hiace rangi nyeusi.


Kikosi kinachoongozwa na Brigedia Fernandes kilipofika hapo haraka walishusha mateka wao wakiwagawa Madam Felister na watoto wake wawili wakiingizwa kwenye gari ambalo pia aliingia Brigedia Fernandes huku shosti wa Madam Felister akiingizwa na mtoto wake pamoja na mtoto wa pili wa Madam Felister katika gari iliyokuwa wameingia Koplo Savatel na wakali wengine gari ziliondoka kwa kila moja kufuata njia yake kutokea kwa pale nyuma ya hospitali maarufu ya General Dr. A. Rovirosa Perez.


Wakiwa wamepanga wakakutane kona ya kwanza inapoanza milima ya Tuxtla karibu na jimbo la Chiapas, milima ambayo kwa pembeni ndipo kuna barabara kuu ya kuelekea Jimbo la Veracruz kutoka Jimbo la Tabasco mwendo masaa nane kwa usafiri wa umma.


***** ***** *****


Simu iliyokuwa ikiita ilionekana kama kero katika masikio yanayosikia sauti yake na hata macho yaliyokuwa yameitizama mara moja tu katika na kuona jina la mpigaji yalidharau pia ikaita mpaka ikakata.


Ilikuwa ni saa kumi na moja na dakika kumi a saba wakati simu hii ilipoanza kuita, pembeni yake alikuwa kazungukwa na wanawake walio uchi bila kipande chochote cha kusitiri miili yao, walikuwa ni wanawake wapatao sita na wote hawa walikuwa wakiuchezea mwili wake bila kuacha sehemu, wapo waliokuwa wakimlamba kwa ndimi zao kila sehemu waliyojisikia kuilamba pia wapo waliokuwa wakimpapasa kimahaba.


Bwana mkubwa huyu ambaye naye alikuwa mwili mtupu ukiacha hereni za madini ya tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania tu dunia nzima zilizokuwa zikining’inia masikioni na cheni tatu kubwa za madini tofauti kila cheni, kulikuwa kuna cheni ya madini ya silva pana inayoning’inia kuja kwenye kitambi chake kutoka shingoni papo hapo kulikuwa na dhahabu yenye upana na urefu unaofanana na ile ya silva pia ikiwepo na ya madini ya tanzanite, saa ya bei ya aghali sana aina ya Rolex ambayo haiingii maji wala ikidondoka haivunjiki hivi ndiyo vitu pekee vilivyokuwa vipo juu ya mwili wake.


Miguu yake ilikuwa ndani ya maji yaliyo kwenye swimming pool, pembeni kukiwa na vinywaji vya pombe za kampuni kubwa ya kutengeneza pombe zinazopendwa sana na watu wa Mexico na hata Marekani katika majimbo ambayo wa Mexico wanapatikana kwa wingi ‘Tequila’.


Hapa palikuwa ni eneo la VIP ya casino maarufu sana iliyopo ndani ya manispaa ya Villahermosa, Veneto Casino inayopatikana kando kidogo ya manispaa hii.


Mr. Fanuel Miguel Mendoza ufika hapa mara kwa mara pale anapojisikia kufika hapa kwakuwa ni mahala ambapo mwanaume yoyote mwenye asili ya uhuni wa kupenda wanawake mabinti wabichi walio katika uzuri wa kiwango cha grade one kiasi waweza kudondokwa mate ukiwaona basi akifika hapa mara moja hata nyumbani kwake akiwa na mwanamke mzuri kiasi cha kufanana na mmoja kati ya hawa lazima atarudi casino hii na si kwamba mkewe mbaya la hashaah! Kitakachomfanya arudi hapa ni ujuaji wa kazi, ujuaji wa kutega na kunasua mapenzi kama yote yalijaa hapa kila binti ni hatari ukitaka sodomize hakuna binti aliyekuwa hatumiki huko na hii ndiyo michezo levya inayowaleta walio na ukwasi wao hapa Veneto.


Matajiri wenye pesa zao kama Fanuel uwa wanapewa eneo la VIP likiwa na wasichana sita wenye kujua kazi na hapo huduma uendelea kama hivi ilivyokuwa kwa Fanuel muda huu kiasi anapigiwa simu anaiangalia tu anaona karaha, anatamani aizime ilikuwa si hulka yake kuzima simu yake popote alipo.


Dakika tano baada ya simu yake kuacha kuita mlango wa kioo cha kuingia katika VIP aliyomo uligongwa stahili anayoitambua yeye ikigongwa uwa ni mmoja wa walinzi wake anagonga.


“Naomba taulo..!” Akaongea akimwambia binti aliye karibu na taulo na binti yule akachukua taulo na kumpa bosi bwana wao wanayempa huduma kamili kama inavyoitwa na watu wote wanaofanya kazi casino hii.


Alijifunga taulo lile kisha akawabusu kwenye papi (lips) zao za mdomo mabinti kama watatu akigusanisha na papi zake za mdomo vikifuatishwa na vimlio vitamu vya ‘mwaaah, mwaaah,mwaaah’ kila anapokutanisha papi kwa papi, alipowaacha akapiga hatua hadi mlango wa kioo unaotumika kuingia ndani yah ii VIP, mlango ambao mtu wan je hamuoni wa ndani ila wa ndani anamuona wa nje vizuri tu.


Alikuwa ni mkuu wa kikosi chake cha walinzi binafsi akiwa katika mavazi yake ya nguo zinazofanana kimuonekano na gwanda za kijeshi ila hizi zikiwa za rangi ya bluu nyeusi kimuonekano wake zinafanana na muonekano wa sare wanazopenda kuvaa wafuasi wa chama kimoja cha kisiasa nchini Tanzania.


Fanuel alipomtizama usoni mtu yule haraka alitambua kuwa kuna tatizo kubwa limetokea au linataka kutokea alikuwa akimjua A to Z mtu wake huyu, kiongozi mkuu wa walinzi wake binafsi popote anapokwenda iwe nje ya Mexico au kwingineko.


Kwa kasi akapitisha kadi maalumu katika swichi soketi iliyo pembeni na mara moja nayo ikapokea kwa kusensi kwa kuwaka mara mbili taa ya kijani, mlango ukajiachia kwa kujigawa katikati kila upande ukisogea upande wake.


“Vipi Mendez?” Alipotokeza tu akauliza huku akiutoa uso wake kuangalia eneo lote la korido hii akakutanisha macho yake na walinzi wake wengine walio na silaha zao aina bunduki za ‘Norinko QBZ-97’ na wote walisimama tu wakiwa wamejipanga karibu korido yote na hii ikamshangaza tena.


“Umepigiwa simu mkuu hujapokea..Hivyo nikapigiwa na nimetaarifiwa ‘Miguel Palace’ imevamiwa na familia yako kwa maana mkeo na watoto wote wametekw..!” Akaongea kwa kasi huku kihemo cha kasi kikifuatisha maneno yake.


“Whaaaat?! Unasemaje Mendez? Nani kakupigia?” Alishtuka sana Fanuel akajikuta baada ya kuuliza kistaarabu akauliza kwa kupayuka sauti ikasambaa kote kuanzia ndani ya VIP hadi koridoni.


“Kama ulivyosikia boss… Tunatakiwa tuondoke haraka sana… Maana hatujui waliofanya hivyo kama ni kina nani? Na wana nguvu gani?.. Aliyenipigia ni mkuu wa ulinzi wa kasri, Ximo” Akajibu Mendez uso wake ukiwa umeloa jasho maana hakuwai kumuona boss wake Mr. Fanuel akiwa katika hali ya mfadhaiko kama alionao.


Haraka bwana mkubwa Fanuel alirudi ndani ya chumba cha VIP akavaa suruali yake na mabinti nao wakiwa wameshikwa na butwaa walinyanyua shati lake wakamsaidia kumvalisha maana walimuona jinsi alivyobadilika wakajua kuna tatizo kamili huko si nusunusu.


“Kuna tatizo kidogo kwangu… Kuna mashoga wamechezea sharubu za simba.. Nitawaona siku nyingine” Akasema kwa haraka kisha akatoka kuungana na walinzi wake kwa mwendo wa nusu mbio nusu tembea akavaa na miwani yake yenye fremu pana ya duara na kioo cha rangi ya zambaru inayong’aa.


“Washenzi gani hao, wanathubutu kuvamia kwenye kasri langu na kuichukua familia yangu? Ina maana ulinzi wote uliokuwepo si lolote kwao? Naenda kumchinja Ximo na kiongozi wa ulinzi wa MPD Mauro simtaki naye achinjwe kashindwa kazi nawaua kwa mikono yangu.. Sitaki upuuzi na familia yangu.. Mimi muhuni pia wasiniletee ujinga familia yangu haihusiki na mambo yangu kwanini? Kwanini familia yangu” alikuwa akifoka kwa sauti wakiwa ndani ya lifti ya ghorofa inayowatoa toka juu ghorofa (losheni) ya saba.


Walifika chini na haraka gari lake la kifahari aina Mitsubishi Outlander Sport rangi ya silva likasogezwa mlango ukafunguliwa akaingia kwenye gari na dreva akaliondoa kwa kasi kufuata gari la mbele ambalo lilikuwa aina Land Rover Discover 3 rangi nyeusi ambalo walinzi wanne ambao mara zote uwa wanaongoza msafara wake walikuwa washaanza safari ya kutoka eneo hili la Veneto Casino, nyuma ya gari ya yake, magari mawili yaliyo kama lile la mbele aina ya Land Rover Discover 3 yenye walinzi watano kila gari wenye silaha za kubebeka mkononi za kivita za aina mbali mbali nao waliunga mkia katika kasi ile ile waliondoka nayo walio mbele.


Mwisho wa sehemu ya kumi na sita (16)


Hali mchafuko imeanza manispaa ya Villahermosa, hali iliyotokea miaka tisa kwenda kumi iliyopita.

Nikileta hali ile iliyotoke katika fasihi andishi sasa hili kuweza kufanya kitu ambacho pengine ni kufukua makaburi ya wale walioumia kipindi icho mpaka kupelekea kupoteza maisha yao.


Shukrani kwako msomaji, endelea kufuatilia riwaya hii ambayo utajutia kupoteza muda wako kusioma.


karibu tunarudi kule ilikoanza riwaya yetu Washington DC!



Haraka bwana mkubwa Fanuel alirudi ndani ya chumba cha VIP akavaa suruali yake na mabinti nao wakiwa wameshikwa na butwaa walinyanyua shati lake wakamsaidia kumvalisha maana walimuona jinsi alivyobadilika wakajua kuna tatizo kamili huko si nusunusu.


“Kuna tatizo kidogo kwangu… Kuna mashoga wamechezea sharubu za simba.. Nitawaona siku nyingine” Akasema kwa haraka kisha akatoka kuungana na walinzi wake kwa mwendo wa nusu mbio nusu tembea akavaa na miwani yake yenye fremu pana ya duara na kioo cha rangi ya zambarau inayong’aa.


“Washenzi gani hao, wanathubutu kuvamia kwenye kasri langu na kuichukua familia yangu? Ina maana ulinzi wote uliokuwepo si lolote kwao? Naenda kumchinja Ximo kwa mikono yangu.. Sitaki upuuzi na familia yangu.. Mimi muhuni pia wasiniletee ujinga familia yangu haihusiki na mambo yangu kwanini? Kwanini familia yangu” alikuwa akifoka kwa sauti wakiwa ndani ya lifti ya ghorofa inayowatoa toka juu ghorofa (losheni) ya saba.


Walifika chini na haraka gari lake la kifahari aina Mitsubishi Outlander Sport rangi ya silva likasogezwa mlango ukafunguliwa akaingia kwenye gari na dreva akaliondoa kwa kasi kufuata gari la mbele ambalo lilikuwa aina Land Rover Discover 3 rangi nyeusi ambalo walinzi wanne ambao mara zote uwa wanaongoza msafara wake walikuwa washaanza safari ya kutoka eneo hili la Veneto Casino, nyuma ya gari ya yake, magari mawili yaliyo kama lile la mbele aina ya Land Rover Discover 3 yenye walinzi watano kila gari wenye silaha za kubebeka mkononi za kivita za aina mbali mbali nao waliunga mkia katika kasi ile ile waliondoka nayo walio mbele.


ENDELEA NA MTIRIRIKO..!


MSHTUKO MPD V-VILLAHERMOSA,TABASCO-MEXICO

Ni kama alipandwa na kichaa Mr. Fanuel Miguel Mendoza, alishuka kwenye gari bila yale mapozi yake yaliyozoeleka siku zote kusubiri kufunguliwa mlango na mlinzi wake binafsi (bodyguard) kama utaratibu alivyojiwekea siku zote yeye alikuwa hafungui mlango wa gari yeye mwenyewe pale inaposimama bali usubiri mtu anayetokea siti ya mbele ya alipo dreva wa gari ambaye ndiyo bodyguard wake mkuu ambaye kila anapoenda ukiacha sehemu za ndani za starehe ndipo ambapo uwa hamfuati kama tulivyoona kule Veneto Casino.


Muda huu ilikuwa tofauti breki za Mitsubishi Outlander Sport ziliporuhusu tairi zisugue lami iliyo ndani ya eneo la mbele ya kasri lake na kisha kusimama tu aliondoa ujinga wake na uzembe wake uliotawaliwa na kiburi cha pesa akafungua mlango akatizama saa yake kisha akaanza kupiga hatua ndefu kuelekea eneo la mbele la kasri lake ambako kuna lango kuu la kuingia ndani.


“Haraka sana niitieni Ximo na genge lake lote la ulinzi hapa kwenye kasri na pia namtaka afisa wa ulinzi Mauro hapa.. harakaaa!” Akapaza sauti kali sana inayoogopesha maana wengi wao hawakauwa kumuona akifoka hivyo kwa kupaza sauti, mishipa ilijizinga pembeni ya paji la uso na kuonekana ilivyofura damu inayopita humo.


Hakuwa ameingia ndani bali aliishia pale pale lilipo lango kuu mkononi akiwa kashika bastola yake aina ya Titanium Gold, bastola iliyoundwa kwa jumba la dhahabu kana kwamba ikiua mtu yeye muuaji anakwenda peponi moja kwa moja (lol).


Hakuwa mtu wa kutulia alikuwa akihama kwenda mwisho wa baraza upande wa kulia kisha anarudi kwenda mwisho kushoto katika baraza yake yenye malumalu zinazong’aa kama kioo cha rangi ya dhahabu, uso umefura kama uso wa kiboko aliyekerwa nchi kavu kisha kufanikiwa kurudi majini kizalizali bila adui yake kumdhuru.


Walinzi wake nao hawakuwa mbali walikuwa wakipishana pishana kwa pembeni ya baraza ile kubwa iliyoko mbele ya lango kuu la kuingilia ndani ya kasri, nao sura zao zilikuwa kama zimerekodi na kuhakisi sura ya boss wao nao walikuwa wamefura kwa hasira na hii ni katika kuonyesha nao wameguswa na tukio lililotokea maana watu wema husema ‘lililompata mwenza wa karibu ni la mwenza wa karibu’.


Ximo hakuwa mbali alikuwa anatokea eneo la mabweni ya wasichana wa chuo kilicho mtaa wa nyuma wa mtaa huu wa Avenida Pasco Usumancita, akiwa na kikosi chake cha watu wapatao ishirini wenye silaha kana kwamba ni wanajeshi wa jeshi la serikali maana hawakuwa na wasiwasi wala kuficha silaha zao ndani ya magari manne yaliyo wazi juu aina ya Toyota FJ Cruiser Convertible rangi nyeusi gari zenye thamani kubwa lakini pesa ya bwana mkubwa Fanuel iliongea na kumiliki vitu hivi bila kuhofia lolote.


Gari zile nazo zikaingia kwa kasi ndani ya uwa wa kasri wenye ukubwa unaomiliki maegesho kubwa ya magari yenye uwezo kupaki magari mengi kwa nafasi ya kutosha na hata watu wengine kufanya sherehe ya mwanamuziki mkubwa kama 50 Cent na pakatosha vurugu hizo za kistarehe.


“Mje hapa wote na wote muweke silaha zenu chini hapo” Akafoka Fanuel waliposhuka tu kwenye magari na wote walishtuka sana kwa amri ile wakaangaliana kwa zamu kila mmoja kisha wakaona watii amri wakatupa bunduki chini.


Muda huo huo wakati kinyonge kama wamemwagiwa maji ya baridi kipindi cha baridi kali kama lile la nchini Russia, zikaingia gari nyingine zinazofanana na gari hizi aina ya Toyota FJ Cruiser Convertible walizokuja nazo hawa waliopewa amri kali na nzito kuitimiza lakini ikawalazimu kutimiza na kutii.


Gari zilizoingia zilikuwa sita zikiongozana na kila moja kuchukua mahali penye kustahili kupaki katika maegesho, gari ya nyuma kuingia akashuka mwanadada Maria Rodgruez ‘Baby Beauty’, alikuwa amefika hapa akiwa na wanaume wa kazi za kazi idadi ambayo ilikuwa karibu wote wa ‘Mendoza Potentia Distributio’ (MDP).


Haraka kwa mwendo wa kukimbia Maria alifika mbele ya boss wao Fanuel akampa heshima ambayo uwa anampa kila anapokutana naye.


“Familia yangu imetekwa Maria.. Nimechanganyikiwa sana nataka niwahoji kwanza waliokuwa wanalinda hapa.. Na Mauro utawajibika kwa hili” Akaongea Fanuel na kuficha aibu ya macho yake kutoa machozi mbele ya mwanamke akatoa miwani iliyokuwa kairudisha kwenye mfuko wa shati akaitwaa mkononi kisha akaivaa lakini Maria alikuwa kashauona uso wa boss wake ulivyo katika taharuki kubwa alikuwa kashayaona macho yaliyopoteza asili yake kuwa macho ya bluu na kuanza kuwa mekundu na hii ilimjuza boss amechanganyikiwa na kwa jinsi anavyoijali familia yake leo kazi ipo hivyo akamsogeza Mauro upande wake maana yeye na Mauro wana mahusiano ya siri ya kimapenzi.


“Cool down boss! Tafadhali jishushe boss wangu, tujaribu kuuliza vizuri na umakini, siku zote hasira ni adui wa utaalamu katika michezo hii boss, hatutakiwi kutokasirika tunapouziwa lakini tunatakiwa kudhidhibiti hasira zetu na mara zote umekuwa mstari wa mbele kutuhusia juu ya hili boss leo ni zamu yako jaribu kuvaa vitu vile vile unavyovivaa viatu vya busara… Tulia ninawahoji mimi kaa kwenye kiti” Mwanadada huyu anammudu sana hili lijamaa lenye kujua kutumia pesa na kuzitafuta, Maria alijua huu si wakati wa kutaka hasira zishike nafasi bila kujua ilikuwaje na kama kuna makosa alitaka adhabu iwafike wanaostahili adhabu kwa wakati ambao tayari mbivu na mbichi inayohitajika itakuwa ishajulikana, alitumia mafunzo yake kiintelejensia kimanufaa zaidi katika pilika zake na nyendo za kumfanyia kazi Fanuel.


Mr. Fanuel mwili ukiwa umelowa jasho alisogea sehemu ya pembeni ambapo pana kiti chake ambacho uwa hakai mtu yoyote baki zaidi ya watoto wake wanapokuwa wanacheza cheza hapa barazani na alipokaa tu wakatokea wadada wahudumu wawili wakaanza kumpepea kwa vipepeo kama vile ambavyo mimi kwa mfano uwa naviona sana kwenye movie za wachina au wajapani mabosi au makubwa wa maadui upepelewa na wajakazi wao.. Madada wakaanza kumpepea boss aliyefurwa na hasira mpaka anahema kwa mtumbo wake kuonekana unavyohakisi pumzi zinazoingia na kutoka.


“..Ximo sogea hapa… “ Akaongea mikono yake ikiwa kaipachika kiunoni Maria, miwani yake meusi ikiwa machoni mwake, mwanamke mrefu mwenye shepu ya kuvutia umbo namba nane unaweza kusema akiwa kavaa mavazi yake ya mara nyingi suruali ya jeans na kitopu kinachomuonyesha kitovu chake, pembeni akiwa na kifuko cha kuhifadhi bastola na hii ikifichwa kuonekana waziwazi kwa kikoti cha kimtindo cha jeans.


Ximo mkuu wa ulinzi na mifumo yote ya ulinzi kwenye kasri la ‘Miguel Palace’ alisogea, li baba hili lenye umri unaokaribia miaka arobaini na tano likiwa na urefu unaorandana na urefu wa ‘Baby Beauty’ alisogea akiwa haelewi hatima yake na aliokuwa akiwaongoza itakuwaje, hasira alizoziona kwa boss Fanuel ilimtumbukiza katika lindi zito la kutojielewa kama kosa hili atapewa yeye kwa kiasi cha kuhadhibiwa adhabu ya aina gani?.


“…Mmmh!..Uliponipigia simu ulinieleza watekaji walipitia chini kwa chini kupitia karavati kuu la maji ya mvua.. Inakuwaje jambo hili wakati mfumo wa kamera za cctv huko masaa ishirini na nne..!” Akaanza mahojiano yaliyokuwa yakifuatiliwa na kila aliyekuwa pale ambapo palikuwa na watu wengi wa kikosi hiki cha ‘MPD’.


“Baada ya ving’ora vilivyohanikizwa kwa taarifa kuwa kasri limevamiwa mara moja nikaongoza kikosi kilichoenda kasi eneo la tukio kwenye uwanja wa gofu kujaribu kuzuia utekaji na wakati nasogea mbio kule nilikuwa nawasilina master control room wa cctv room nikamuhoji inakuwaje tunaingiliwa bila yeye kuona ndipo akanijibu hakuona tofauti yoyote ila anahisi jambo hivyo anatizama mfumo umechezewa vipi..!” Akajibu Ximo huku macho yake yakihama hama toka kwa Maria aliyesimama sambamba na Mauro kwenda kwa boss kila anavyoongea wasiwasi tele.


“.. Torreira na wenzako wote wa chumba cctv naomba msogee hapa!” Akaongea Maria kumuita mtu mwingine ambaye huyu ndiyo alikuwa taabani kwa kutetemeka, mkono wa kulia alikuwa kashika laptop na mkono wa kushoto alishika Ipad akiwa na wenzake wote wanne wa chumba cha mawasiliano ya ulinzi wa kasri wakasogea kwa licha ya kuwa walikuwa hawajawai kuitwa hata siku moja mbele ya watu wote hawa pia hawakuwa wamewai kuingia katika tatizo lolote lile miaka miwili mitatu toka waajiriwe hapa kama wataalamu wa mambo ya kompyuta katika chumba kinachoitwa ‘master control room’.


“Mnatambua jambo lolote baya la kivamizi katika kasri hili likitokea na likafanyika kama ilivyofanyika leo mnawajibika kwa kiasi gani?” Swali la kwanza akawatupia baada ya vijana wale kusimama mbele yake yeye Maria.


“Boss ni kweli tunatakiwa kuwajibika lakini dada yangu tayari tushagundua kwamba tulizidiwa kidogo kitaalamu na wavamizi na wapi walipotuwai… Naomba nifafanue kidogo dada..”. Yaani jinsi ambavyo alikuwa akitetemeka huyu kijana huyu Torreira ungeweza kuwepo eneo hili nafikiri ungehisi labda kuna baridi kali sana lakini ungeshangazwa na jasho linalomtoka na kutambua si baridi bali ni hali kutojua nini kitafuta dakika inayofuata katika mustakabali wa maisha yake na wenzake anaishi nao kama ndugu katika chumba wanachofanyia kazi.


“Nataka kuona picha za wahusika waliofanya tukio sihitaji ngonjera zingine hapa.. Sema kipi ulichogundua mmechezewa kitaalamu lakini kiambatane na kutuelekeza sura za wavamizi wetu..” Akahoji kwa sauti ya kike lakini ukiisikia lazima uogope kama hujazoea.


“Ziko za kwanza wakati mtu wa kwanza anatoka kwenye mdomo wa karavati lakini giza lililokuwepo eneo lile na maski ya sox aliyovaa usoni vinafanya asionekane vizuri, pia anaonekana mwingine akitoka na wote ukivuta kwa karibu na kujaribu kuipa video mwanga wa kuwaonyesha wanaonekana wameziba sura zao kwa mask… Lakini kamera baadaye zilipotezwa kitaalamu uwezo wake wa kuchukua sawa video kwa vifaa ambavyo hivyo hapo kwenye box aliloshika Clautos na ndipo walipotudhidi kwakuwa vifaa hivyo uharibu uwezo wa kamera kuchukua kwa kufuata mfumo wetu na kufuata mfumo wao waliofanikiwa kufunga katika kamera zetu zikikaa mbele ya kioo na kuleta taarifa za uongo wanazotaka wao kuja kwetu…” Akafafanua Torreira kisha akaangalia upande alipo boss Fanuel ambaye aliinuka alipo na taratibu akaanza kujongea pale. Uwoga uliongezeka mara tatu kwa Torreira akitamani utokee muujiza wowote ule maana hakuwa amemzoea Mr. Fanuel ila sifa za mabosi wa unga alikuwa akizijua ni kuwa makatili na wasiopenda utani wala uzembe kwenye maslahi yao pamoja na familia zao.


“Maria… Uzembe hapa si wa hawa watu wa control room, uzembe ni wa walinzi wa pembeni ya kasri kwa sababu wao ndiyo wameruhusu.. Torreira kaa pembeni na watu wako nataka kuongea na Ximo yeye ndiyo ameshiriki tukio hili baya kabi...” Hakumalizia kuongea alichotaka simu yake iliyokuwa kwenye mfuko wa suruali ikaita.


Haraka akaitoa na bila kuchunguza kama ilivyo ada yake kuwa hapokei namba asiyoitambua na uwa anajisikilizia sana kupokea simu lakini hapa haraka akaruhusu kupokea.


“… Fanuel.. Niko njiani kuelekea mahala salama patakapofanya mimi na wewe kuonana…. Usihofu juu ya familia yako niko nayo mimi ni Brigedia Fernandes, mimi ndiyo nimevamia kwenye kasri lako na kuichukua familia yako… Wako salama salimini..!” akaongea aliyempigia huku akijinasibu kwa kujitambulisha kwa Fanuel bila wasi wowote.


“Fe..!” Upande wa pili haukuruhusu yeye Fanuel aongee lolote ukakata simu, Mr. Fanuel akaitupa chini simu yake, simu ya thamani kubwa sana iliyo na kava lilinakshiwa madini ya silva yanayong’aa sana machoni mwa watu, uzuri haikuwa simu ya kuvunjika ikitupwa kawaida chini bila kupigizwa hivyo ilikuwa salama salimini, wahudumu wa kike waliokuwa wakimpepea bosi wakaiokota wakiishika kwa kitambaa (leso) kwakuwa walikuwa hawaruhusiwi kuishika kwa mikono yao (amri ya boss).


“Sheeenzy!.. Sheeenzy! .. Mwanaharamu Feca, mwanaharamu Feca… Feca! Familia yangu, familia yangu ina watoto wadogo wasiojua lolote unaipeleka wapi mjinga weeeh!.. “ Alifoka kwa nguvu akiruka ruka kama kichaa aliyeugua kichaa ghafla.


“Vipi boss?!” Maria akamsogelea akamuuliza na kujaribu kumtuliza aache kuruka ruka atulize munkari.


“Fernandes… Brigedia Fernandes Carlos Codrado niliyekwambia ufuatilie nyendo zake ndiyo ameongoza uvamizi wa utekaji mke na watoto wangu… Naapa atanitambua mimi ni nani kama akiwadhuru sitajali uwanajeshi wake na ukomando wake.. ha haaa hahaa hah haaa inauma sana, inaumaa.. mke wangu jamani, watoto wangu Mariaaa!”Hali mbaya kwa Fanuel tajiri kubwa, ilikuwa ni ngumu kwa Maria kumtuliza yeye mwenyewe peke yake ikabidi aombe msaada kwa walio pembeni wakiangalia tu kiongozi wao mkuu akiongea na boss wao na kujaribu kumtuliza baada ya simu aliyopigiwa kuonyesha imemfungulisha kulia bila aibu.


“Tumpeleke ndani… Aitwe dokta haraka..!” Akaongea Ximo na wanaume watupu wakamnanyua bonge nyanya juu juu kwenda naye ndani kabisa ya kasri kutoka pale barazani.


“Naomba familia yangu ipatikane haraka jamani… Naipenda familia yangu kuliko chochote” Akiwa kabebwa juu juu na wanaume wapatao wanne hakuacha kuongea kimakelele huku machozi yakimiminika kwa kasi machoni mwake.


Hali aliyokuwa nayo bila busara za mwanadada Maria Rodgruez basi leo hapa Mr. Fanuel angeshamwaga uhai wa watu wake wengi sana.


***** ***** *****


Ilikuwa si kazi rahisi kumtuliza Mr. Fanuel, ilibidi kazi ya ziada itumike kwa wasaidizi wake wenye busara na ndipo alipoamua kutulia baada ya kuelekezwa mbinu ya kifundi iliyotumika kuwateka mke, rafiki wa mke wake na watoto wake.


“Bosi nafikiri hili jambo tunatakiwa kulifanya siri serikali isijue hili sisi wenyewe tumalizane na Brigedia Fernandes maana kama anavyosema mzee Perreira kuwa tuwataarifu maafisa wa polisi na tumlengeshe moja kwa moja kuwa mtu aliyemaliza kifungo chake cha miaka saba katika gereza la Acapulco ameiteka familia yako… Hii kwangu hainiingii akilini mkuu wangu”. Kilikuwa ni kikao cha viongozi wa juu wanaomsaidia Mr. Fanuel katika shughuli zake za haramu, walikuwa na Mr Fanuel mwenyewe katika chumba cha mikutano na biashara kilichopo kwenye jumba liliyo kando na kasri kuu la Mr. Fanuel.


“Shida iliyopo mpaka sasa wale watu wetu wa upelelezi tuliowatuma wafuatilie kila kitu kinachomuhusu Feca hawajajua lolote baada ya bwana yule kutoka jela alikwenda wapi?.. Na yule wa Marekani anasema familia ya Feca ilipokuwa inaishi Washington DC haipo tena katika nyumba na hata yule mtu aliyekuwa anawapa huduma hayupo pia kwake, baada ya habari ikanibidi nitoe msisitizo wazidishe nguvu kwenye kujua familia ile na bwana anayewapa huduma wako wapi ikibidi waongeze wapelelezi tutakaowalipa..” Mkuu wa idara ya intelejensia ya MPD Mr. Vicente Neto Manuela akaongea kisha akawaangalia kwa zamu wenzake walio katika chumba kile chenye masofa tupu ya rangi nyeupe yanye kung’aa na kupendeza na kukifanya chumba hiki kuwa kivutio kama ni mgeni umekitembelea.


“Inatubidi tuzidishe spidi na sisi kuipata familia yake hili iwe jino kwa jino.. Kwakuwa kama alivyokwisha tuambia boss, mtu huyu anachotaka ni kumshinikiza boss amrudishie pesa yenye thamani ya mzigo aliompa miaka saba iliyopita na nafikiri atataka na faida kubwa sana kutokana na mafanikio anayoyasikia ya boss Fanuel kuwa anayo… Tulichokikosea ni kile cha wenyewe kujinyima fursa ya kumtoa uhai wake akiwa gerezani Acapulco kwa stahili waliyotumia kuingia hapa Miguel Palace ni dhahiri amejipanga na yuko makini sana” Akaongea Maria baada ya kumsikiliza kila mtu akitoa maoni yake kati ya watu sita waliomo ndani ya chumba hiki, akiwemo yeye kiongozi mkuu wa MPD.


“… Inaweza ya kuwa mtu huyu ametoka tu ndani a tayari ana kikosi cha kufanya aliyofanya?” Akauliza Shaxi, huyu naye msimamizi mkuu wa kikosi cha MPD kinachohakikisha mzigo njiani wanapouchukua nchi yoyote kati ya nchi ambazo wao wanafuata unga iwe wa heroin, methamphetamines au cocaine, Mr. Shaxi Taxeira ndiyo kila kitu huko.


“Haijulikani ila inawezekana alivyokuwa gerezani alikuwa akimfuatilia boss nyendo zake na ndiyo maana haijapita wiki mbili toka atoke gerezani anafanya tukio la kustaajabisha kwenye kasri lenye ulinzi mkubwa unaosifika kwa magenge yote ya uhalifu na unga… Nafikiri la kufanya kwetu kwa sasa ni kuuliza watu wa magenge yote ya unga ambayo hatuna uhasama nayo juu ya mtu kwakuwa kiuhalisia hawezi kutoka gerezani halafu akae tu bila kujihusisha na genge lolote” Akajibu kiufafanuzi Maria.


Mr. Fanuel alikuwa akiwasikiliza watu wake lakini hakuwa akiongea lolote zaidi ya kila muda anaangalia saa kisha anaangalia simu yake akitarajia inaweza kuita muda wowote kati ya sehemu alizoweka mitego ya habari juu ya watekaji wa familia yake.


Saa mbili na nusu usiku kwa saa za Mexico kikao kikiwa kimefikiwa muafaka kuwa wavute subira na mambo yatakaa sawa baada ya muda kidogo kwani walishatoa taarifa za siri kwa watu wao wa serikali walio katika idara za ulinzi na usalama pia walishatoa taarifa za siri kwa watu wao wa mamlaka ya simu ambapo watu hao wote walikuwa wanafuatilia mawasiliano ya watu mbalimbali kuona kama wataweza kupata mawasiliano ya mtu yoyote atakayeongea juu ya kilichotokea kwa Fanuel.


Simu ya bwana mkubwa Fanuel iliita, alijiinua haraka na kuinyanyua upesi kisha bila kuangalia vizuri namba za mpigaji akapokea.


“Fanuel naongea…!” Akaongea kwa sauti ya haraka kisha akatega sikio kusikia sauti ya upande wa pili.


“Feca naongea… Naomba unisikilize kwa makini Fanuel… Familia yako iko mahala salama na wote wako vizuri kiafya hakuna hata aliye hata kwenye mchubuko… Unanisikia?” Sauti ya Feca ikaunguruma.


Wakati huo huo Fanuel anapokea simu, mtaalamu wake wa mambo ya kompyuta Torreira aliyepewa maagizo awe karibu na boss muda wote alikuwa akiangaika kusachi simu iliyopiga kwa bosi wake inapiga kwa kutokea wapi? Na ilikuwa kabla hata haijapigwa walikuwa washaifunga kifaa cha ‘Google Map Phone Search’ kifaa alichokinunua yeye mwenyewe Fanuel toka kwa rafiki yake mmoja afisa wa juu wa shirika la ujasusi la MOSSAD la Israel.


“Nakusikia mheshimiwa.. Sema unataka nini kwa familia yangu? Niambie nikupe nini? Watoto wangu bado wadogo sana Feca…!!” Akaongea na machozi yakaunganisha toka machozi, watu wake walishikwa na simanzi iliyochanganyika na hasira kuu.


“..Natambua unanijua vizuri mimi ni nani katika nchi hii.. Hivyo nataka kwako mambo matatu makuu.. Unanisikia? Nisikilize vizuri tajiri dhuluma wewe” Akasimama tena kuongea maana alikuwa akisikia rafiki yake wa zamani anavyovuta mafua na kuyameza akajua jamaa linalia.


“Hahahahaha hahahaha hahahaha.. Kwani Fanuel ulifikiri sitatoka jela? Hukuwa unajua kama siku hazigandi na siku moja nitamaliza kifungo changu na kuwa mtaani kama wewe ulivyo mtaani? Ukasahau yote na kuamua kuhama kutoka Guerrero hadi Tabasco ukiona kama umehama kutoka duniani kwenda kuishi mbinguni au jehanamu bila kufa… Sasa muda wako wa kulipa umefika.. Nahitaji unilipe mzigo wangu wote wa cocaine nyeupe ounces gram 5000 ukiwa na faida ya miaka saba niliyokuwa jela, hilo la kwanza. La pili nahitajiunilipe fidia ya mimi kutumikia kifungo bila wewe kufika hata mara moja ikiwa nilituma ujumbe kwako zaidi ya watu watano, fidia hii nahitaji unipatie kiwanda chako kimoja cha chuma kilichopo Jalisco au Juanhuto uchague kimoja na unikabidhi kisheria kikiwa na faida na mtaji wake na la tatu ambalo la mwisho nahitaji unipatie au eneo lako unaloishi au uninunulie kasri linalofanana na hilo lako kwenye jimbo na manispaa nitakayochagua mimi… Ukimtimiza hayo yote utaipata familia yako yote ikiwa hawajaumizwa wala kuteswa.. Nakupa siku mbili za kufikiri sitakupigia mpaka baada ya siku mbili yaani leo jumamosi mapaka jumatatu muda kama huu.. Kwaheri”. Aliongea kwa kirefu kidogo Brigedia Fernandes kisha akakata simu bila kusubiri Fanuel atajibu kitu gani? Maana hakuwa anataka kumsikia akiongea chochote.


Mwisho wa sehemu ya kumi na tano (17)


Hali inadhidi kuwa tete kwa Mr. Fanuel Miguel Mendoza tajiri mkubwa mwenye sifa zake katika jimbo la Tabasco manispaa ya Villahermosa.


Tamaa yake anajikuta ikianza kumpalia kama kavuta moshi wa pilipili kichaa.


Familia yake inaingia katika kisasi cha Brigedia Fernandes, kisasi cha kudhulumu mzigo wa unga aina ya cocaine nyeupe (white cocaine), watoto wake wote watatu, mke wake na rafiki wa mke wake mwanadada mwanamitindo na mcheza filamu maarufu nchini Mexico, Gabriela Lopez naye akiwa na binti yake wanaingia kwenye mkono wa mwanajeshi mfukuzwa, mwanajeshi aliyekuwa akitumikia kifungo kisha kukimaliza Brigedia Fernandes.


Je bwana mkubwa Fanuel atatimiza masharti aliyopewa na rafiki yake wa zamani juu ya mabadilishano ya mali kadhaa na familia yake?


Majibu ya haya tutayapata katika sehemu zinazofuata!




Wakati huo huo Fanuel anapokea simu, mtaalamu wake wa mambo ya kompyuta Torreira alikuwa akiangaika kusachi simu iliyopiga kwa bosi wake inpiga kwa kutokea wapi? Na ilikuwa kabla hata haijapigwa walikuwa washaifunga kifaa cha ‘Google Map Phone Search’ kifaa toka shirika la ujasusi la MOSSAD la Israel, alikinunua bwana mkubwa Fanuel kwa mmoja wa maafisa wa kijasusi wa Israel.


“Nakusikia mheshimiwa.. Sema unataka nini kwa familia yangu? Niambie nikupe nini? Watoto wangu bado wadogo sana Feca…!!” Akaongea na machozi yakaunganisha toka machozi, watu wake walishikwa na simanzi iliyochanganyika na hasira kuu.


“..Natambua unanijua vizuri mimi ni nani katika nchi hii.. Hivyo nataka kwako mambo matatu makuu.. Unanisikia? Nisikilize vizuri tajiri dhuluma wewe” Akasimama tena kuongea maana alikuwa akisikia rafiki yake wa zamani anavyovuta mafua na kuyameza akajua jamaa linalia.


“Hahahahaha hahahaha hahahaha.. Kwani Fanuel ulifikiri sitatoka jela? Hukuwa unajua kama siku hazigandi na siku moja nitamaliza kifungo changu na kuwa mtaani kama wewe ulivyo mtaani? Ukasahau yote na kuamua kuhama kutoka Guerrero hadi Tabasco ukiona kama umehama kutoka duniani kwenda kuishi mbinguni au jehanamu bila kufa… Sasa muda wako wa kulipa umefika.. Nahitaji unilipe mzigo wangu wote wa cocaine nyeupe ounces gram 5,000 ukiwa na faida ya miaka sita niliyokuwa jela, tena kwa thamani ya kila badiliko linaloenda na wakati, hilo la kwanza. La pili nahitaji unilipe fidia ya mimi kutumikia kifungo bila wewe kufika hata mara moja ikiwa nilituma ujumbe kwako zaidi ya watu watano, fidia hii nahitaji unipatie kiwanda chako kimoja cha chuma kilichopo Jalisco au Ocaxa uchague kimoja na unikabidhi kisheria kikiwa na faida na mtaji wake na la tatu ambalo la mwisho nahitaji unipatie au eneo lako unaloishi au uninunulie kasri linalofanana na hilo lako kwenye jimbo na manispaa nitakayochagua mimi… Ukimtimiza hayo yote utaiapata familia yako yote ikiwa hawajaumizwa wala kuteswa.. Nakupa siku mbili za kufikiri sitakupigia mpaka baada ya siku mbili yaani leo jumamosi mapaka jumatatu muda kama huu.. Kwaheri”. Aliongea kwa kirefu kidogo Brigedia Fernandes kisha akakata simu bila kusubiri Fanuel atajibu kitu gani? Maana hakuwa anataka kumsikia akiongea chochote.


ENDELEA NA DODO..!


MAKUBALIANO, MLIMA TUXTLA-MEXICO

‘Leo ndiyo siku ya mwisho wa mimi kutoa maamuzi kuhusu mustakabali wa familia yangu, watu wangu wanaonizunguka mpaka leo hawajaweza kunisaidia… Mke wangu anajua nina kila aina ya uwezo wa kuwasaidia wao katika matatizo niliyo watumbukiza, natambua Fernandes atakuwa kashamueleza sababu ya wao kuwashikilia… Dah sijui nafanyaje mimi’ Ilikuwa ni asubuhi ya alfajiri ya siku ya jumatatu, muda wa saa kumi na moja Mr. Fanuel akiwa kaka kwenye pembe ya kitanda chake kikubwa kilicho katika chumba chake chenye hadhi yake kama asemavyo mwenyewe na ni kweli kilikuwa cha hadhi ya tajiri mkubwa kama yeye mwenye majivuno na upenzi wa kuishi kwa ufahari.


Toka siku ya jumamosi bwana huyu hakuwa amewai kupata usingizi pamoja na kujilazimisha ajaribu kulala lakini hakuwa amefanikiwa katika hilo, muda wote alikuwa akiwaza hili na lile na jinsi gani anaweza kuisaidia familia yake iliyo mahala asipojua ni wapi? Alijaribu kujipoza machungu yake yaliyojichanganya na wasiwasi mkubwa kwa kunywa sana pombe kali lakini akaona si suluhisho ya yeye kuirudisha familia yake kwake ikiwa salama.


Alikuwa akijua fika jinsi ilivyo roho ya Feca, alikuwa kashamshuhudia akifanya unyama mara kadhaa kwa watu walioingia katika anga zake kipindi icho yeye akiwa karibu yake na yeye Feca akiwa mwanajeshi wa jeshi la wananchi wa Mexico.


‘Hahahahaha hahahaha hahahaha.. Kwani Fanuel ulifikiri sitatoka jela? Hukuwa unajua kama siku hazigandi na siku moja nitamaliza kifungo changu na kuwa mtaani kama wewe ulivyo mtaani? Ukasahau yote na kuamua kuhama kutoka Guerrero hadi Tabasco ukiona kama umehama kutoka duniani kwenda kuishi mbinguni au jehanamu bila kufa… Sasa muda wako wa kulipa umefika.. Nahitaji unilipe mzigo wangu wote wa cocaine nyeupe ounces gram 5,000 ukiwa na faida ya miaka sita niliyokuwa jela, hilo la kwanza. La pili nahitajiunilipe fidia ya mimi kutumikia kifungo bila wewe kufika hata mara moja ikiwa nilituma ujumbe kwako zaidi ya watu watano, fidia hii nahitaji unipatie kiwanda chako kimoja cha chuma kilichopo Jalisco au Ocaxa uchague kimoja na unikabidhi kisheria kikiwa na faida na mtaji wake na la tatu ambalo la mwisho nahitaji unipatie au eneo lako unaloishi au uninunulie kasri linalofanana na hilo lako kwenye jimbo na manispaa nitakayochagua mimi… Ukimtimiza hayo yote utaiapata familia yako yote ikiwa hawajaumizwa wala kuteswa.. Nakupa siku mbili za kufikiri sitakupigia mpaka baada ya siku mbili yaani leo jumamosi mapaka jumatatu muda kama huu.. Kwaheri’ Maneno makali yaliyolandana na sauti kavu yenye uzito sauti ya rafiki yake wa miaka kadhaa iliyopita, sauti ya Brigedia Fernandes Carlos Codrado a.k.a Feca yalikuwa hayakauki kwenye ubongo wake mara kwa mara tena bila kumruhusu kupumzika masaa matatu mpaka manne.


‘Siwezi kupata usingizi.. Haiwezekani kupata usingizi wakati Romeo, Pablo na binti yangu mrembo Happer Clarra sijui wanalala wapi? Inauma sana na kwa akili za kigerezani na milio ya risasi na mabomu aliyokuwa akisikia jeshini bwana yule mpuuzi mmoja Feca anaweza kuua mmoja mmoja kati ya malaika wale wazuri, furaha yangu, maisha yangu na akafikia kumuondoa na malkia wangu Felister.. Oooh! Mungu wangu..!’ Machozi yakaanza kumtoka, akanyoosha mkono katika meza ndogo ya kioo ambayo uwa anaweka kinywaji kinachomburudisha kabla ya kulala akiwa na mkewe kila ifikapo usiku. Pale alinyanyua picha zote zilizopo akaziweka mkononi na kuanza kutizama moja moja hapa machozi yakadhidi kuporomoka.


‘Hakuna namna.. Nishadanganywa sana.. Nafanya anavyotaka Feca, nafanya, nafanya… Utajiri na kila kitu nachotafuta ni kwa ajili yake alinipa mtaji kisha akaniongezea na mbinu kadhaa za biashara, nilipofeli akaniiunua tena na tena na mara ya mwisho akanipa mzigo ambao laiti asingeingia matatizoni nami nisingeingiwa na ibilisi wa kutaka kumdhulumu lakini mipango yote iliyo duniani ni mipango ya Mungu siwezi kushindana na kudra zake hii ndiyo ilikuwa kadiri yangu na kadiri yangu imeshafika na kufika kwa kadiri yangu si kufeli kwa maisha yangu vyote anavyosema vimo ndani ya uwezo wangu.. Felister na wanangu ni bora kuliko mali na pesa anazotaka Feca.... Niliunda Mendoza Potentia Distributio kwa ajili ya kulinda biashara zangu za haramu na kunilinda mimi na familia yangu lakini ni kama wameshindwa… Sina budi kusimama mwenyewe katika suala la kifamilia… Mtu huyu ni mjanja sana namjua Feca alivyo si mtu wa kumjaribu katika jambo lake ni mtu anayeogopwa na hata wakuu wa jeshi walio juu yake kivyeo… Anabadili namba kila anaponipigia… MPD wamenifanyia kazi nzuri sana katika kunisaidia kukuza mtaji wangu wa biashara hii ya haramu nimepata faida kubwa sana kiasi ambacho naweza kufanya jambo lolote linalohusu pesa na nisitetereke lakini kwenye kuilinda familia wamefeli na siwezi laumu sana kwakuwa ni mara ya kwanza nashambuliwa mimi binafsi na moja kwa moja athari inakwenda kwenye familia yangu hali hii iliwafanya wabweteke kabisa na kudhani kutokewa na mambo kama haya… Hii ni familia yangu, sikuwai kuwa na mwanamke ambaye nimempenda kwa asilimia zote kama nimpendavyo Felister.. Sijui wanahudumiwa vipi huko?.. Nahitaji leo iwe mara ya mwisho kutokuwaona nawapenda sana’ Akaendelea kuwaza huku akiendelea kuangalia picha ya mtoto wake wa kike HapperClarra ni binti yake wa pekee na anayempenda sana kuliko kiasi kile anachowapenda watoto wake wawili wa kiume alikuwa akimdekeza na kumfanya kama malkia wa dunia na kila akiiangalia picha hii machozi hayakukauka katika macho yake na hata usingizi ndipo ulipodhidi kugoma kumfika.


‘Kukuche nimuite mwanasheria wangu tuone tunafanyaje katika zile mali zinazojulikana anazozitaka Feca na pia kuhusu pesa… Ila sitamuacha salama kwa kosa lake kuigusa familia yangu nay eye nitamlipizia, najua akishapata vitu anavyovitaka atataka kuunda genge lake pia atataka aishi na familia yake, hata kama atakuwa hajamuua mwanafamilia yangu ila ana wajibu kulipia alichofanya.. Nitahakikisha namuadhibu kwa kumuua mmoja wa mtu wa familia yake lazima iwe jino kwa jino alichofanya ndicho nimfanyie… Angeweza kuja na kuniona hata ofisini tu kuniomba anachotaka lakini bila hata kujua kama naweza kumlipa bila kufanyiana hasadi zozote yeye kaamua kuichukua familia yangu yote.. shenzi zake’ Akaendelea kuwaza kisha akainuka kitandani na kusogea kwenye dirisha kubwa la kioo lililopo chumbani mule kisha akafunua pazia kubwa na kuanza kutizama nje ya kasri macho yakitua kwenye bustani zinazozunguka kasri pamoja na mabwawa ya kuogelea yanayopendeza eneo la nyuma la kasri lake la thamani ya juu.


Sekunde, dakika na masaa yalikwenda vile inavyotakiwa sababu hakuna kinachoweza kuganda kati ya vitu hivyo vya kiasili lakini kwa bwana mkubwa Fanuel ilikuwa kama yameganda maana hakuishiwa na kuiangalia saa ya mkononi aliyovaa inavyopepeta mshale wa sekunde na wa dakika ukisapoti kisha macho yakihama yalihamia kwenye saa ya ukutani, alihama kutoka dirishani akaenda mlangoni akarudi kitandani akakaa akainuka ilimradi tu aweze kujiweka katika hali ya kawaida, donge kuu likiwa limekaa kwenye koo lake likimereketa kiasi kikubwa.


Ilipofika saa kumi na mbili na dakika tano asubuhi ikiwa imepambazuka akaamua kuvuta muda kwa kwenda bafuni kwake bafu lililo ndani ya chumba chake kikubwa chenye mapana ya kutosha na marefu ya kukifanya chumba kionekane kama darasa la shule kwa ukubwa wake.


Alitumia dakika ishirini kucheza cheza na maji katika Jacuzzi lililopo bafuni katika hali ya muda usogee afanye anachotaka, alipotoka akavaa aina ya nguo anazopenda kuvaa, pensi (kaptura) kubwa ya jeans kutoka kampuni ya ubunifu wa mavazi ya Gucci rangi ya bluu nyeusi kisha akavaa na shati jepesi jeupe akitanguliza ndani singlend nyeupe na akivaa hivi uwa hafungi vifungo vya shati. Akakamatia miwani yake na kutoka chumbani mwake moja kwa moja akaenda ilipo ofisi yake iliyopo hapa hapa lilipo kasri lake.


“Naomba ufike kwenye kasri langu ukiwa na nyaraka zote muhimu zinazohusu mali zangu zote bila kuchelewa na moja kwa moja ukifika uje ofisini kwangu… Samahani sana mwanasheria wangu, nimetingwa sana nakuhitaji ufike tufanye jambo..!” Muda wa kupiga simu hii ulifika na kafanya hivyo ikiwa imetimia saa mbili kasoro robo asubuhi.


Saa mbili na nusu juu ya alama mwanasheria wa kampuni maarufu ya kisheria katika jimbo la Tabasco na hususani viunga vya manispaa ya Villahermosa, kampuni ijulikanayo kama Calbaros Chamber Of Law’s ikiongozwa na huyu mwanasheria aliyefika hapa ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa kampuni hii Mr. Diego Funtes Calbaros.


“Karibu mheshimiwa Calbaros…!” Akatoa ukaribisho Mr. Fanuel huku akijiweka vizuri katika kiti chake cha kujidai kinachotii mengi ayatakayo kama kumfurahisha akikaliapo.


“Ahsante sana mheshimiwa boss wangu.. Nimeitikia wito wako… Salama hapa? Maana si kawaida yako kuniita asubuhi asubuhi na hali niliyoiona hapa kwenye kasri ni lazima kuna tatizo..!” Akapokea ukaribisho na kushikana mikono.


“Ni kweli hali si kama ile unayoifahamu kila ukifika hapa… Niko katika jaribio kuu la katika maisha yangu toka nipande juu kwa miaka michache na kuwa hapa nilipo, jaribio ambalo sikuwai kuwaza kuja kukutana nalo kwa miaka yote ya neema niliyonayo katika maisha yangu na familia yangu… Sijalala siku mbili kaka yangu nina matatizo makubwa kuliko ya mambo yangu ya siri ninayoyafanya maana hayana matatizo kama haya niliyonayo sasa..!” Akajibu kwa kirefu kisha wote wakachukua siti zinazowahusu, bwana mkubwa akikaa kwenye kiti chake na mgeni wake Advocate Calbaros alikaa upande wa pili wakitengenishwa na meza nzuri ya kioo ilinakshiwa kwa pembeni kwa madini ya silva na kuifanya ofisi ipendeze.


“Nini tena mkuu wangu? Jambo gani la kuweza kukufanya ukose usingizi mtu jasiri usiyeogopa jambo kama wewe”. Akahoji Adv. Calbaros akijiweka vizuri kitini apate kusikia kunani.


“Familia yangu!... Familia yangu Calbaros… Familia yangu yote imetekwa, wako mateka kuanzia mke wangu hadi wanangu” Akajibu Mr. Fanuel twasira ya wanae na mkewe ikimjia usoni mwake.


“Kivipi?, kivipi? mkuu!” Akahoji tena akiwa katoa macho kumuangalia anayemuita boss wake wakati hajamuajiri yeye katika kampuni anayoimiliki ya ‘Calbaros Chamber O f Law’s’.


“Kama nilivyokwambia… Aliyefanya jambo hili ametuwai, ametudhidi step kafanya alichotaka akiwa kanyooshewa kila kitu… Namaanisha akiwa kashachorwa ramani ya hapa na ratiba ya hapa ya familia yangu.. Na ndiyo maana amefanikisha jambo alilofanya kiulaini sana kiasi ya kwamba hata angeeanda ikulu ya Mexico City angefanikisha mpango wa kumchukua mke wa Rais wa nchi” Akaeleza kisha akasita kidogo kumuangalia mwanasheria wake anayemsikiliza kwa umakini halafu akaendelea.

“Mtu aliyefanya hivi ni mtu aliyekuwa mshirika wangu miaka saba iliyopita kama utakuwa umewai kusikia kesi ya mwanajeshi wa cheo cha Brigedia kituo cha kijeshi cha Guerrero aliyekuwa akijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya..” Akasimama kuongea baada ya kuona mwanasheria anataka kuongea jambo hivyo akampa nafasi aongee.


“Yah.. Naikumbuka hiyo kwa sababu alikuwa akitetewa na Wakili ninaye mjua na nilisoma naye sheria chuo cha Universidad La Salle, Facult Of Law… Advocate Daniel Brayan…!” Akajibu mwanasheria.


“..Basi amemaliza kifungo chake cha miaka saba na ndipo ameamua kuitumia familia yangu kupata anachohitaji kutoka kwangu”

“Eeeh! Hivi anaitwa nani vilee?!!”

“Anaitwa Fernandes Carlos Codrado ni Brigedia wa jeshi… Kuna jambo ambalo lilitokea wiki iliyopita wakauliwa wafungwa pamoja na baadhi ya maaskari kwenye daraja la kona ya Jalisco mto wa Actopan huko Veracruz.. Jambo lile limestaajabisha kwakuwa wafungwa wale ndiyo walikuwa wafuasi wakuu wa mtu huyu kwa kilichotokea kwangu ninapatwa na hisia uenda wale waliouliwa pale na miili yao kukatwa katwa kisha kuchomwa moto pengine si wafungwa bali watu wengine ila tuyaache hayo naomba twende kwa nilichokuitia haya mengine nitayafanyia kazi nikishamaliza matatizo ya familia yangu..” Akaeleza kirefu kidogo kisha akasimama akajiweka vizuri kitini na kusababisha kiti kimtii kwa kunesanesa kwa raha zote kikimpa hali ya kiburudani mkaliaji kiti ambaye mara zote toka kitengenezwa ukalia yeye tu hakuna aliyewai kukikalia..


“Hayo pia niliyasikia.. Nchi yetu mambo kama hayo ni kawaida ingawa yanakuja na kutoweka… Biashara zenu za siri zina mambo mengi sana boss.. Endelea!”


“Brigedia.. Ame.. Amenipigia simu na kunipa masharti kama naitaka familia yangu irudi kwangu salama wasalimini basi nitimize masharti yake kadhaa na kama hujuavyo familia kwangu ndiyo kila kitu nimeona hakuna namna maana kikosi changu cha kazi kimejaribu siku mbili kutafuta wanaweza kuwa wapi na mpaka sasa hivi navyozungumza na wewe hapa hakuna jipya ni yale yale tu MPD hakuna walichoambulia zaidi ya muajiriwa kujipambanua kwa bosi wake kuwa kazi itafanyika bosi tulia lakini hakuna jipya na kwakuwa mi si mgeni kwa Feca, najua uwezo alionao ndiyo uliomuwezesha katoka jela haijafika wiki mbili tayari kashanifanyia jambo ambalo kwa genge lolote hapa Mexico au hata vikosi vya DTO vingetumia miezi kama si mwaka kujua njia wataitumia kuingia hapa kwa jinsi navyo uamini ulinzi wangu wa hapa… Nimeamua Calbaros, nimeamua siwezi kusubiri nikianza kupokea kwenye box kichwa cha mmoja mmoja wa wanafamilia yangu… Sitavumilia kuona hali hiyo na nishashuhudia unyama mwingi alioufanya mtu huyu katili na sitapenda unyama ule niuone anaufanya kwa mmoja wa watoto wangu au mke wangu.. Naomba tujadiliane tunafanyaje kumpatia anachotaka kuliko kusubiri Maria na watu waipate familia yangu kwa mbinu zao ambazo sina tena imani nazo maana kama mtu niliwaambia wajue haraka yuko wapi toka atoke gerezani lakini walishindwa, naamini hawataweza kuipata familia yangu… Ni muda wa kutimiza ayatakayo kisha kama kumgeuka na kurudisha nitakavyompa basi nitarudisha siku za mbele na hili nina hakika nalo tena kwa stahili kali zaidi ya jino kwa jino..!” Akaeleza kwa hisia kali Fanuel.


“Oooh! Pole sana boss wangu… Anataka nini?! Brigedia..!” Akahoji mwanasheria.


“Anataka nusu ya mali nilizonazo..!” Akasema na kuweka kituo kutizama uso wa mwanasheria wake ulivyohakisi mshtuko mkubwa.


“Eeeeh! Kwanini? Anawezaje kuthubutu hilo? Fanuel huyo mtu ni kichaa au?” Akahoji mwanasheria macho yakiwa yametumbuka mpaka weupe wake wa kimexico ukiwa weupe mwekundu ngozi yote.


“Siyo chizi Calbaros.. Ana haki sababu anaishikilia familia yangu.. Mali hizi nimetafuta kwa mbinu zote za kimafia hili familia yangu iishi kifalme.. Mali hizi si chochote kwa mke na wanangu acha nimpatie anachokihitaji..” Akajibu Fanuel kisha akainuka kitini akasimama kidogo halafu akakaa tena akiinamisha uso chini na papo hapo akafikicha macho yake yakaanza kuonyesha uzi wa machozi ukitamalaki kufunika mboni za macho yake yote mawili.


“Pole sana mkuu.. Tafadhali tulia wewe ni mwanaume shababi usilie kaka yangu… Ebu tulia kisha nieleze mtu huyu mlikuwa vipi? katika urafiki wenu kabla hajaenda jela hili nami nijue mengi na tuone ana haki ipi na pia hana haki ipi aktika mali zako”. Mwanasheria Calbaros akajaribu kumtuliza boss. Mteja wakena rafiki yake ashushe hali yake arudi katika hali ya kawaida licha ya uchungu alionao.


“… Mmmh! Acha tu mdogo wangu… Mtu huyu alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana akishirikiana nami katika biashara zetu kama unavyozijua wakati naishi Guerrero.. Yeye alikuwa anauza mihadarati katika jeshi kama kesi ulivyosema umewai kuisikia ni kweli alikuwa akihusika na biashara ile kwenye makambi ya jeshi.. Kuna kipindi alinipatia mzigo mkubwa sana wa unga wenye thamani kubwa, mzigo wa kipimo cha ounces gram 5000 white cocaine..! lakini wakati hukumu yake ikisubiliwa kusoma yeye akiwa rumande alinitumia ujumbe nifike kumuona ila nilifikiria mbali nikaona itakuwa ujinga mimi kwenda kumsikiliza, akatuma ujumbe wa pili kuwa basi nimsaidie hata pesa kidogo napo pia nikamjibu aliyemtuma ajifanye hajaniona nikampa pesa kidogo na kweli hakurudi tena.. Hapo sikusikia tena kunisumbua wala kusikia habari zake za kutuma watu wa kuniomba msaada ya baada ya mwezi hukumu yake iliposomwa akahukumiwa yeye na watu wake nane, yeye akienda gereza la kijeshi la Acapulco huku wenzie wakihukumiwa gereza la Tamaulipas… Bado hakuniuliuzia tena ila mimi nikaamua nihame Guerrero kuja hapa Villahermosa hili hata kama ana watu wake wasiniingilie kama hujuavyo kipindi hiko sikuwa na nguvu yoyote ya kiushindani lakini hapa sikukuta maushiundani ya kibiashara katika biashara zetu za haramu hivyo mara moja nikaweza kuuza ounces grams 5,000 na kuniingizia faida kubwa sana na ndipo neema zikaanza kufunguka mpaka nikaona na mimi nimiliki kikundi cha kulinda maslahi yangu mwaka nilipounda kikundi baada ya kukutana na Maria Rodgruez na ndipo nilikutana na wewe na kukufanya uwe mwanasheria wangu wa kunisaidia katika mambo ya biashara zangu ambazo serikali inazitambua na nakumbuka kazi yetu ya kwanza ilikuwa ni ya kununua eneo hili nililojenga hili kasri” Akasimama kuongea baada ya mlango wa ofisini kugongwa, gonga zile ambazo yeye akiisikia anakuwa anajua ni nani amegonga.

“Pita Maria..!” Akaruhusu mgongaji aingie na bila kuchelewa sura ya Maria ikatokea baada ya kufungua mlango.


“…Karibu Maria…!” Akamkaribisha na kumuelekeza akae kwenye sofa lililo pembeni kidogo ya kiti alichokaa mwanasheria Diego Funtes Calbaros ambaye yeye viwiko vyake alikuwa ameviegemeza kwenye kiti cha kunesanesa huku akipata burudani murua ya kunesanesa huku anaongea na boss wa ofisi.


“Ahsante boss.. Naona leo ofisi imekuhusu mapema na mwanasheria… Kwema?” Akauliza Maria macho yake malegevu lakini yenye nguvu ya asili ukikutana nayo yakiwa yanaangaliana na boss wake.


“Kwema tu Maria.. Vipi upande wako kuna jipya lolote?” Akajibu na kuhoji Mr. Fanuel.

“Zipo lakini sidhani kama zinaweza kutusaidia boss!”

“Taarifa hata ikiwa ndogo kwa kiasi gani inaweza kuwa na manufaa kwetu.. Sema?”

“Taarifa toka Mexico City kwa mtu wetu anayefanya mamlaka ya usalama wa jiji anasema kamera za jiji zilinasa video ya Fernandes akiwa uwanja wa ndege wa Mexico siku ya alhamisi ya wiki iliyopita saa moja jioni akiwa ndiyo ameingia kisha akachukua taxi na kuondoka akiwa peke yake na alipofuatilia zaidi kwakuwa ilibidi sasa nimuombe afuatilie alikuwa anatokea wapi? Akaniambia alikuwa anatokea jimbo la Guerrero maana ndege aliyofika nayo ilitokea huko… Lakini hakumuona tena kuondoka Mexico City kupitia uwanja wa ndege sasa sijui aliondoka kupitia usafiri gani tena mpaka kuja huku Tabasco hilo hatujui lakini ameniambia kuna teknolojia ataitumia ambayo itasababisha kama kuna kamera yoyote ambayo ilimchukua mtaa wowote basi atazipata video zake na kukusanya iwe benki, stendi za taxi za mabasi, vituo vya mafuta na hata majengo ya serikali ambayo kamera zake zinakuwa katika system ya usalama wa jiji kama ujuavyo Mexico City kuna kamera nyingi sana za cctv… Kazi hiyo ataifanya leo asubuhi na kisha kutupatia majibu tuombe iwe vile tunavyotaraji maana tutaona aliongozana na nani? Au alienda kuonana na nani huko” Akatoa maelezo marefu mwanadada Maria ‘Baby Beauty’.


“Ni kweli Mr. Fanuel… Kama mna mtu yupo mamlaka ya usalama ya jiji mdili naye vizuri itajulikana tu kama Feca yupo kimakazi Mexico City au alienda tu kuonana na mtu kama si watu wa genge fulani.. “ Mwanasheria akatoa hoja yake akiingilia katia maongezi ya Maria na boss wake.


“Sawa! Taarifa nzuri fuatlia kwa ukaribu… Lakini hapa umekuta tuna kikao na mwanasheria ukataka kujua kama ni kikao chema? Kuna maamuzi nimefikia Maria, kama ujuavyo leo ifikapo jioni Fernandez atanipigia anataka jibu la kipi nimeamua? Hivyo mi kwa upeo wangu ulivyo na ninavyomjua chizi Feca kwa sasa sina budi zaidi ya kumnyenyekea lasivyo hata mke wangu ataumia sana kwa kuwaacha zaidi ya siku tatu mikononi mwa watu nisiojua wanawafanya nini mke na watoto wangu.. Nimemuita mwanasheria hapa kisha nataka aitwe mhasibu wangu tuone hesabu ziko vipi nitoe anavyovihitaji chizi yule kuiokoa familia yangu kisha sisi kama MPD tutarudi kumlipizia kisasi kama vita na iwe vita tu na ninaamini uwezo wenu naamini tutamshinda Fernandes” Akatoa maelezo marefu yaliyolenga kumuelekeza kiongozi mkuu wa MPD mwanadada Maria.

Mwisho wa sehemu ya kumi na sita (18)


Mr. Fanuel aliamua familia kwanza kisha mambo mengine baadaye.

Ni kweli hakuna kilicho bora duniani kama familia, Mr Fanuel alikuwa sahihi kukosa raha, kulia na hata kutokula chakula na hata kunywa tena vinywaji vikali, aliona kama vinampotezea mawazo mazuri ya jinsi atakavyoona anawasaidia watoto wake? Anamsaidiaje mke wake kipenzi? Anamsaidiaje shemeji yake rafiki wa mkewe?


Maamuzi yake makuu aliyoyapitisha alfajiri baada ya usiku kucha kuwaza ilikuwa ni kumpa anachotaka Fernandes kisha kama ni kisasi basi atalipa wakati mwingine.


Je itakuwaje?


Majibu ya yote haya ni subira yako tu kisha twende sehemu inayofuata kwa ajili ya kujua mengi zaidi.



ILIPOISHIA SEHEMU YA 18…!!

“Ni kweli Mr. Fanuel… Kama mna mtu yupo mamlaka ya usalama ya jiji mdili naye vizuri itajulikana tu kama Feca yupo kimakazi Mexico City au alienda tu kuonana na mtu kama si watu wa genge fulani.. “ Mwanasheria akatoa hoja yake akiingilia katia maongezi ya Maria na boss wake.


“Sawa! Taarifa nzuri fuatlia kwa ukaribu… Lakini hapa umekuta tuna kikao na mwanasheria ukataka kujua kama ni kikao chema? Kuna maamuzi nimefikia Maria, kama ujuavyo leo ifikapo jioni Fernandes atanipigia anataka jibu la kipi nimeamua? Hivyo mi kwa upeo wangu ulivyo na ninavyomjua chizi Feca kwa sasa sina budi zaidi ya kumnyenyekea lasivyo hata mke wangu ataumia sana kwa kuwaacha zaidi ya siku tatu mikononi mwa watu nisiojua wanawafanya nini mke na watoto wangu.. Nimemuita mwanasheria hapa kisha nataka aitwe mhasibu wangu tuone hesabu ziko vipi nitoe anavyovihitaji chizi yule kuiokoa familia yangu kisha sisi kama MPD tutarudi kumlipizia kisasi kama vita na iwe vita tu na ninaamini uwezo wenu naamini tutamshinda Fernandes" Akatoa maelezo marefu yaliyolenga kumuelekeza kiongozi mkuu wa MPD mwanadada Maria.


ENDELEA NAYO…!!


MAKUBALIANO II, MLIMA TUXTLA-MEXICO

“Hakuna anayeweza kupinga juu ya ulichoamua, vyote vilivyo MPD na Miguel La Pancha Co. Ltd ni mali zako, mali ya mtu ni mali yake na matumizi yake ni matumizi yake juu ya mali yake husika… Mimi Maria napitisha lolote uliloamua na utakaloamua..!” Maria akaunga mkono kilichoongewa na boss wake ikiwa moyoni mwake akiwa na wasiwasi ni mali kiasi gani itapunguzwa katika mali alizonazo boss wao ikiwa na wao MPD wamehusika kwa kiasi kikubwa kumsaidia kufika ilipo.


“Ni kweli Maria usemavyo! sote hatuna budi kufanya akitakacho yeye..!”Mwanasheria akatoa lakekisha akapandisha briefcase lake aliloweka chini kwenye zulia mpaka mezani.


“Je hakuna haja ya kuwepo kina Mr. Vicente?!” Akahoji mwanasheria swali akilielekeza kwa Mr. Fanuel.


“… khaah!... Haina haja mwakilishi wao maria yupo hapa..” Akajibu Mr. Fanuel huku kichwa akiwa kakiinamisha kana kwamba hataki maongezi yale.


Fanuel akanyanyua simu yake iliyo pembeni katika meza yake ya ofisi akatafuta jina linalobeba namba ya mhasibu wake wa kampuni ya Miguel La Plancha Compania Limited na pia umuwekea sawa na mahesabu yake ya biashara ya genge lake la biashara haramu Mendoza Pontatia Distributio (MPD).

“Huko wapi? Nimekutumia meseji ufike hapa ofisini kwangu kwenye kasri! Mbona haufiki?” Akahoji baada ya upande wa pili kupokea simu.

“Niko getini boss.. Nishafika eneo la kasri.. Nisamehe kwa kuchelewa boss!” Akajibu mpigiwaji na boss wake hakusubiri zaidi akakata simu.


Dakika tano mbele Mhasibu mkuu wa kampuni yao inayotambulika na serikali, ya kificho (MPD) na familia yao aliyekuwa akisubiriwa alifika na kukuta kikao kikiendelea lakini na maongezi mengine ya watu walio na Fanuel kumpa maneno kadhaa ya matumaini boss wao katika hali aliyokuwa nayo.


“Samahani kwa kuwachelewesha jamani.. Nina mafua yananisumbua toka juzi hivyo yamenifanya niwe mnyonge kidogo” Akaongea mhasibu baada ya kuingia, alikuwa akiitwa Pedro Iker Pullieta.

“Pole sana mkuu.. Macho yako yameiva sana.. Naelewa uchungu wa familia na Mungu ataleta kheri mambo yatakaa sawa..!” Akaongea tena halafu akachukua nafasi ya kiti kilichokuwa hakina mtu.


“Ahsante Pedro… Nataka tuweke mahesabu sawa hili nitoe anachotaka mtekaji.. Kwanza kuna faida ya miaka sita anaitaka kutoka katika mzigo wenye thamani ya ounces gram 5000 ya white cocaine… Pia ameweka angalizo kwamba faida iendane na mabadiliko ya thamani ya sasa” Akaanza kuongea Fanuel kisha akakataa sigara aliyokuwa anapewa na mwanadada Maria.

“Sijisikii kuvuta tafadhali, nitavuta baadaye…! Ahsante!” Akaongezea na kutulia kitini.


“Boss! Mtu wako angetakiwa kuelewa kwamba hiyo ounces grams 5,000 white cocaine aliyokupa miaka hiyo kwa sasa ina thamani kubwa na ya juu zaidi ya mara tatu… Pia haitakiwi yeye aifikirie faida tu akukumbuke biashara hizi zinahitaji kulindwa kwa nguvu kubwa sana na huwezi ukalinda biashara hii kama unalinda duka la spea za magari na vile vile hii biashara inahitaji hongo kubwa sana kwa watu wa serikali hii ya hapa Mexico wanaohusika na upambanaji wa madawa ya kulevya ‘DTO’ na tunapopeleka nchi zilizo na soko letu pia tunakula nao maafisa wa mipakani nab ado mapambano makali yanatokea hasa kwa DEA ya Marekani.... Si rahisi yeye kuchukua faida tu iliyo nzima tena ya miaka yote sita.. Mkuu fikiria hili kisha tujaribu kumuelewesha mtu huyo na kwakuwa si mgeni wa biashara hizi ataelewa tu” Mhasibu akaanza kuongea kitaalamu kitu ambacho Boss Fanuel alikuwa anajua hilo lakini familia kwanza ndiyo lilikuwa neno lake kuu kisha likafuata neno la ‘kisasi’ ambacho alitaka kiwe kisasi cha ‘jino kwa jino’.


“Hilo lote nilishafikiria.. Lakini kumbuka nahitaji kuiokoa familia yangu… Naomba tupige hesabu zetu kisha atakatupigia tumpe ofa yetu kisha tumsikilize anasemaje? Miaka sita ounces grams 5,000 ya white cocaine mara sita ni ounces grams 30,000 ni pesa nyingi sana kwa kweli na anachoangalia Mr.Feca ni faida ya mali anazosikia ninazo na hata mimi ningeweza dai faida hizo kwa hasira ya kufikiri nilidharauliwa… Jambo hili kwa kweli linaniumiza sana na kunifanya nijutie upande mwingine naona pia ilikuwa jambo la busara kwa maamuzi niliyochukua..!” Akaongea boss na kufanya watu wote walio kikaoni kunyamaza kila mmoja akifikiria lake juu ya wanachokisikia.


“.. Sawa mkuu acha nicheki hesabu zinakuwaje nipe dakika ishirini.. Napiga hapa hapa nipo na laptop yangu..!” Mhasibu akakubali kuangalia hesabu zinakuwaje katika hazina yao ya biashara za haramu ambayo kila mwezi uwa wanatoa kiasi fulani kidogo kukipeleka katika kampuni yao Miguel La Plancha Co. Ltd kwa minajili ya zikiingia humo kuingia katika utakatishaji nah ii kutokana hawawezi kuingiza pesa zote mahesabu yatakataa na kampuni kuulizwa imepataje pato lisilo sawa na wanachoingiza hii stahili wanaitumia wafanyabiashara wa biashara za haramu karibu wote katika nchi zinazofanya biashara hizi na hata serikali zao zikiacha zifanywe tu kwakuwa na wao wanazitegemea kinamna moja ama nyingine kiuchumi.


Dakika ishirini zilikatika mhasibu mkuu Pedro alikuwa akiendelea kuangalia mapato na matumizi ya miaka sita ilivyokuwa huku akitizama na itakavyokuwa baada ya kiasi watakachotoa kulingana na hali halisi iliyopo wakati waliokuwepo.


“Sawa…! Hesabu zetu kwa miaka hii sita itabidi ziende na mwaka ambao ulianza kuunda kundi hili la Mendoza lililotujumuisha sisi sote, sababu na sisi tuna nguvu yetu humu licha ya wewe kuwa mwenyewe… Kumbuka kuwa uligawa hisa hili kupunguza manung’uniko kwetu kama ulivyotuambia wakati unatoa hisa zako miaka miwili iliyopita… Mr.Fanuel katika biashara ya mihadarati ambayo sisi watu wawili ulitupa hisa ambao tumetimia hapa wawili ambapo pia kuna mkeo na watoto wako, ukiacha mwanasheria wako ambaye hayumo kwenye hisa za ‘Mendoza Potentia Distributio’ (MDP). Alianza mhasibu kuelezea hali ilivyo katika biashara ya kando lakini ndiyo shina la wao kama MPD.


“Hisa zako wewe bwana mkubwa ni asilimia sitini, wakati mkeo ambaye hayupo hapa ana asilimia ishirini ya hisa hivyo kufanya nyinyi nyote muwe na asilimia themanini huku zilizobaki mimi nina kumi na Maria ana kumi, watoto wako ambao ndiyo warithi wa asilimia zako wamo kwenye mkataba kisheria katika magawanyo ya hisa lakini hawana sauti yoyote katika maamuzi wakati wewe ukiwa hai… Pendekezo langu naomba sisi wenye asilimia ishirini tusiguswe kwenye mgawo utakaokwenda kwa Fernandes… Nasema hivi kwa sababu endapo litanitokea tatizo mimi au Maria kwa mkataba wa hisa tuliouingia miaka miwili iliyopita kuna kipengele kinachosema zitatumika asilimia zetu husika katika kutatua shida ama tatizo hilo… Hivyo na sisi tunaomba wakati napiga hesabu hizi niweke kando asilimia ishirini ambazo hazihusiani na familia yako, unasemaje mwanasheria uliyetusainisha huu mkataba?” Aliendelea Pedro kufafanua kisha akapeleka swali kwa Advocate Diego Funtes Calbaros.


“… Ni kweli ninao mkataba wenu wa mgawanyo wa hisa wa biashara ya siri.. Huko sahihi kabisa…Sheria iko wazi katika gawio atakalofanya Fanuel asilimia zenu hazitaguswa”. Akajibu Calbaros.


“Niko tayari kupunguzwa utajiri wangu kwakuwa naamini nitarudisha kwa muda mfupi… Mhasibu wangu usiwe na wasi.. Weka hesabu sawa hili nitakapopigiwa na yule mtu nimueleweshe hali ilivyo na naamini atakubali kupokea kiasi nitakachompa..” Akaongea Fanuel na kutizama saa yake ya mkononi.


“Sawa! Iko hivi kwa vipimo vya sasa vya madawa ya kulevya kama tukitumia ounces kwakuwa alikupa ounces gram 5,000 itatubidi tuzidishe maana ounces grams 1360 kwa vipimo vya sasa kama mtu hataki kupima kwa paundi kama wanavyopima ulaya inauzwa dola 136,000 na katika ounces grams 5,000 tunaingiza 1360 mara tatu na kubaki ounces grams 920… Hii kama atataka mpigiane mahesabu kwakuwa ni mtu mzoefu wa mihadarati utamwambia ilitumika kulipia madhira yote ya kibiashara kama hajuavyo biashara ya mihadarati haifanikiwi bila kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa nchi kama na kwenye masoko yetu… Tuje kwenye faida anayotaka ya miaka sita..!” Aliongea kirefu kidogo akiendeleza na ufafanuzi kish akasimama kidogo akanyanyua chupa ya kinywaji alichoomba aletewe na kuletewa na muhudumu wa ofisi hii toka yeye anaingia, alipiga tarumbeta mpaka karibu na nusus ya chupa kisha akafunga mfuniko na kukisogeza pembeni, mhasibu mwenye tattoo karibu mwili mzima kana kwamba hajasoma kufika level ya kupata shashahada ya uchumi na biashara.


“Kwa kiasi ambacho kilichopo na kwakuwa yeye hajui umeingiza kiasi gani miaka yote hiyo nafikiri tukiacha kwanza na mtaji ambao sitataka uguswe tuje kwenye faida kwa nyie wanahisa wakuu, faida ya pesa za hisa za mkeo za toka umgawie hisa zake ishirini ukija kwenye faida za hisa zako toka ulipoamua kugawa hisa kwetu uliotuchagua kwa kuthamini mchango wetu kwako… Kwa kilichopo itabidi mgawe nusu kumpa mtu wako hivyo hakuna mtakachotetereka kwa ukweli na hiyo mkisema mumpe faida ya miezi sita katika kila mwaka baada ya mgawo wa hisa zako zikizokuwa asilimia 100, ambako sasa tuna miaka miwili toka tuwe na utaratibu wa hisa… Lakini tukivuka na kwenda kihalali miaka sita anayotaka yeye kwa kiasi kilichopo na mabadiliko ya biashara kila yanavyotokea basi itabidi achukue robo tatu theluthi moja ya faida yenu na nyie kubakiwa na theluthi, pesa ndogo sana kiasi ambacho hamtapendezwa nacho maana ni kiasi ambacho ni kama mtaji na faida ya asilimia zangu..” Mhasibu akaendele kueleza kiutaalamu kisha akanyanyua chupa ya mvinyo aupendao akagonga tarumbeta (kunywa bila kutumia glasi) aliposhusha akafuta mdomo wake.


“Hii ni dawa nzuri ya mafua..!” Akaongea na watu wengine wote wakacheka cheko dogo ukiacha Fanuel aliyewatizama tu akili yake ikiwa imetawaliwa na msigano mkubwa wa mawazo lukuki.


“Mmh! Hatari sana… Hivyo nimwambie nampa dola ngapi?” Akahoji Mr. Fanuel kijasho kikimuanza asubuhi hii bila kujali hali ya baridi la asubuhi ambalo kwa Villahermosa uwa linaanza kupungua makali yake saa tano asubuhi kwenda saa sita.


“Mi naona tusiweke faida yote iliyojitokeza kwenye hesabu boss… Nafikiri ungemkadiria kisha ukamtamkia kiasi tutakachokubaliana sababu lazima tujue kuwa hakutaja kiwango cha pesa kasema anataka faida ya miaka sita kwa sababu hajui wewe una kiasi gani? Anajua tu una viwanda vitatu, una ndege mbili kama kaambiwa hivyo atakuwa kaambiwa pia una majumba kadhaa na magari lukuki ila hawezi kujua una pesa cash dola ngapi ya Marekani…!” Maria akaongea macho yake na ya boss yakiwa yamekaziana bila kupepesa na hivi wote hawakuwa na miwani machoni mwao ilikuwa kama yana shauku ya jambo.


“Ndiyo boss Maria yuko sahihi… Hatuwezi fanya anachotaka, ameweka mtego anataka ujikate mwenyewe ujikaange na mafuta yako kama nguruwe kisha yeye afurahie ushindi kwa dharau kubwa sana na nataka nitoe angalizo mwanajeshi huyu akishapata pesa hizi tujiandae kuona kusikia mtu mkubwa sana mwenye nguvu kubwa katika sekta ya mihadarati.. Muda utatueleza!” Akaeleza mhasibu Pedro na watu wote wakatikisa vichwa vyao kukubali maneno yake.


“Nimewasikia jamani… Mimi nafikiri ni bora nikampatia dola milioni 10” Fanuel akaongea kiujasiri kabisa kisha akautupa mgongo wake kwenye muegemeo wa kiti chake na kufanya anesenese kwa raha zote.


“Ni sawa… Hasipo ridhika na hizo itakuwa jambo la hatari sana… Dola milioni 10 kwa pesa yetu hapa unaongelea Mexican Peso Milioni 195,618,153 na hii haitakuhathiri katika faida uliyonayo kuliko tukienda kihalali kama alivyotaka maana yake ingekubidi utoe mara tatu ya hizi na hii ingekuwa loss kubwa sana hata kama mtaji wetu usingeguswa lakini nguvu yetu ingepungua katika ushindani wa soko la ununuzi na pengine yeye ndiyo angetutoa katika soko la ununuzi katika nchi tunazonunua mizigo yetu… Moja kwa moja nikiwa kama mhasibu nahizinisha pesa hiyo kutoka hazina ya siri…” Mhasibu aliunga mkono kiasi alichoona ni sahihi kutoka baada ya Mr. Fanuel kufikiri na kuibuka na kiasi anachoona akimwambia Feca atakubali kukipokea kama faida na faini juu.


Mwanasheria alitoa nyaraka zingine zinazohusu mali zingine kisha kamkabidhi Mr. Fanuel azipitie maana aliomba aletewa na hizo.


“Mkuu umesema na jambo lingine mtu wako hajaishia kwenye pesa kuna mambo mengine anadai kama fidia yake, nyaraka hizi hapa nipe malekezo tuweze kushauriana inakuwaje?”. Mwanasheria Calbaros akaongea baada ya kuzitoa baadhi ya nyaraka na kuziweka juu ya meza.


“Anataka nimpatie mojawapo wa kiwanda changu kisheria sababu nafikiri ndiyo ile ile anajua chanzo cha yote ni mzigo wake… Hapa nafikiri itatubidi nifike naye hadi wizara ya viwanda na biashara kisha kwa msajili wa viwanda na biashara lakini kwa kuanzia atataka tuingie naye mkataba wa awali na ndiyo akatanguliza neno kisheria… Pia anataka nimunulie kasri linalofanana na kasri hili…!” Akafafanua Fanuel.


“Duuuh! Huyu mpuuzi mbona anavuka mipaka hivyo… Panakuwaje hapo?” Maria akataharuki na kujikuta anafoka kwa sauti.


“Maria! Calm down… Ni kama amenioa sina jinsi, ukiolewa huwezi kulala na suruali ya jeans kitandani wakati umelala na mumeo, ametudhidi step… Tushamchelewa ametangulia hatua nyingi mbele hatuna budi kwenda naye anavyotaka na kama kuna njia ya kurudisha vitu vyetu tutajipanga na sisi na kurudisha kilicho chetu kwa gharama yoyote..” Akajibu Mr. Fanuel na machozi yakaanza kumtoka, alishaikumbuka familia yake akakamata leso na kuanza kujifuta machozi.


“Pole boss… Basi wewe ndiyo utaamua… Mimi nitakuwa tayari tukaingia naye mkataba wa kwanza akiwa na mwanasheria wake pia tutazunguka na mwanasheria wake pamoja nasi sote kukamilisha taratibu zote za kiwanda, je utampa kiwanda cha jimbo gani?” Mwanasheria akatoa pole kwa boss wao kisha akahoji.


“Cha Jalisco.. .. Nimeonelea cha Jalisco kwa sababu mitambo yake sikuitoa ujerumani nilinunua Canada kwa mhindi aliyeshindwa kuendeleza kiwanda chake na kuhus kasri analotaka nitamwambia achague moja kati ya makasri yangu ya Jalisco na nitafanya hivyo hili kama akisema aishi Jalisco tupate urahisi wa kulipiza kisasi chetu na kurudisha mali zetu na pesa zetu..” Akafafanua tena akiwa na uchungu mkubwa sana unaojionyesha dhahiri machoni mwa wafuasi wake.


Maongezi yao yaliendelea wakielekezana itakavyokuwa katika mambo kadhaa wa kadha baada ya kumaliza mambo makuu ya msingi, waliendelea kuwepo pale pale ‘Miguel Palace’wakimpa maneno ya kumfariji na matumaini makubwa boss wao ambaye kidogo aliweza kusawajika na kuweza hata kula chakula kilichokuwa kikimshinda kabisa kula.


Walikaa hivi wakisubiri muda ambao atapiga simu mtaalamu na fundi Brigedia Fernandes Carlos Codrado, ulinzi ukiimarishwa vya kutosha kwakuwa hawakuwa tena na imani na ulinzi wa kikawaida kawaida wakijiamini kiasi kikubwa kuwa hawawezi kumbwa na tatizo lingine.


Masaa kwa wengine yalikuwa yakienda sawa sawa kama siku zote yanavyokwenda lakini masaa haya haya ya kawaida kwa Fanuel Miguel Mendoza yalikuwa kana kwamba yamesimama, moyo wake haukuacha kudunda vile udundavyo kikawaida katika mwili, mwili mkubwa, mwili wa mwanaume wa kimexico aliyeshiba pesa na jeuri kubwa ya pesa aliyonayo, moyo ulikuwa ukidunda kana kwamba umeamishwa kutoka mahala pake na kusogezwa sehemu ingine.


Huu ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwa bwana mkubwa huyu, hakuwai hata mara moja kufikiria heti siku moja ingetokea mtoto wake au mama yao siku moja anaweza kupelekwa sehemu kilazima sehemu iliyo tofauti na yeye kama baba wa familia kuijua wakati yeye yupo hai anaishi dunia hii hii ya walimwengu sisi.


Alijihisi ana mkosi mkubwa sana huku akijiona ana makosa makubwa sana ya kutowalinda ipasavyo watoto wake vipenzi na mke wake kipenzi, mwanamke anayempenda sana licha ya kuwa hakuwa anampa heshima ya kutomsaliti kwa Malaya wanaolipwa kwa ajili ya kumfurahisha lakini mara zote Fanuel aliumia napouangalia uso mkewe akiwa kalala na hata kuwaza kwanini anamsaliti na kufuata nalaya lakini ilikuwa si rahisi kwa tajiri kama yeye kuacha kwenda sehemu kama Neveto Casino kufuata mabinti wazuri, angeachaje kwenda huko? Utajiri wake ungekuwa na maana gani kama yeye si mtu wa burudani hii ya kibinadamu? Anapata kila atakacho. Anamiliki ndege binafsi ya kifahari, anamiliki meli binafsi ya mizigo, ana boti tatu ziendazo spidi na za kifahari, majumba na makasri kadhaa katika majimbo kadhaa makubwa ya hapa Mexico, magari ndiyo usiseme kwa bwana huyu.


Sasa vitu vyote hivyo alivyo navyo na anavyozidi kuongeza angeachaje kujihusisha na kuhudumiwa na mabinti sita wanaomzunguka wakimfanyia huduma ya masaji kisha wakamnyonya sehemu zake za siri na kumalizia kwa kumpa huduma ya sex (ngono), maana kama pombe, sigara, kulala sehemu nzuri kana kwamba akifa haozi vyote hivi ni hanasa hakuwai kuona ni shida kwake kumalizia na hanasa ya kuhudumiwa kimapenzi na wanawake wengi kisha anaporudi nyumbani furaha yake inaongezeka kwa kumuona mkewe na wanae wa damu yake.


Lakini sasa ndiyo anaona jambo lililomkuta halikumstahili, anaona ameonewa sana na ndiyo hakaukiwi na kulia iwe kwa machozi peke yake akiwa yupo na mtu pembeni au akiwa pke yake chumbani kwake kulia kwa sauti.


Mwisho wa sehemu ya kumi na saba (18)


Mr. Fanuel ameitisha kikao cha kamati kuu yake ya wanahisa wa kampuni ya siri anayoiongoza inayomiliki genge la ‘Mendoza Potentia Distributio (MPD).


Ndani ya kikao hatimaye anawaeleza aliloliamua kwa faida na mustakabali wa hatima ya maisha ya wanafamilia wake.


Anamshirikisha mhasibu wake ambapo baada ya ubishano na kuelekezana wanafikia makubaliano na kuunga mkono Mr. Fanuel atoe dola milioni 10, ambayo kwa pesa ya Mexico ifahamikayo kama Mexico Peso ni Mexico Peso Milioni 195,618,153 ambayo ni pesa ndefu sana kwa pesa za nchi kama yetu ya Tanzania ni tshs bilioni 23.

Pia alikubali kutoa kiwanda chake kimoja cha uyeyushaji na uundwaji wa chuma kilichopo jimbo la Jalisco.


Je upande wa Fernando atakubali ofa ya dola milioni 10?





Alijihisi ana mkosi mkubwa sana huku akijiona ana makosa makubwa sana ya kutowalinda ipasavyo watoto wake vipenzi na mke wake kipenzi, mwanamke anayempenda sana licha ya kuwa hakuwa anampa heshima ya kutomsaliti kwa Malaya wanaolipwa kwa ajili ya kumfurahisha lakini mara zote Fanuel aliumia napouangalia uso mkewe akiwa kalala na hata kuwaza kwanini anamsaliti na kufuata nalaya lakini ilikuwa si rahisi kwa tajiri kama yeye kuacha kwenda sehemu kama Neveto Casino kufuata mabinti wazuri, angeachaje kwenda huko? Utajiri wake ungekuwa na maana gani kama yeye si mtu wa burudani hii ya kibinadamu? Anapata kila atakacho. Anamiliki ndege binafsi ya kifahari, anamiliki meli binafsi ya mizigo, ana boti tatu ziendazo spidi na za kifahari, majumba na makasri kadhaa katika majimbo kadhaa makubwa ya hapa Mexico, magari ndiyo usiseme kwa bwana huyu.


Sasa vitu vyote hivyo alivyo navyo na anavyozidi kuongeza angeachaje kujihusisha na kuhudumiwa na mabinti sita wanaomzunguka wakimfanyia huduma ya masaji kisha wakamnyonya sehemu zake za siri na kumalizia kwa kumpa huduma ya sex (ngono), maana kama pombe, sigara, kulala sehemu nzuri kana kwamba akifa haozi vyote hivi ni anasa hakuwai kuona ni shida kwake kumalizia na hanasa ya kuhudumiwa kimapenzi na wanawake wengi kisha anaporudi nyumbani furaha yake inaongezeka kwa kumuona mkewe na wanae wa damu yake.


Lakini sasa ndiyo anaona jambo lililomkuta halikumstahili, anaona ameonewa sana na ndiyo hakaukiwi na kulia iwe kwa machozi peke yake akiwa yupo na mtu pembeni au akiwa pke yake chumbani kwake kulia kwa sauti.


ENDELEA NA DODO..!


MAKUBALIANO V,MILIMA TUXTLA-MEXICO

Milima ya Tuxtla ni milima mikubwa na maarufu katika eneo lote la America kuanzia kusini, kaskazini na kati, umaarufu wake unatokana na historia yake kijiografia na kuwa ni chanzo cha mvua zote zinazopatika maeneo ya mipakani ya Marekani, Guatemala na Mexico yenyewe.


Eneo la milima hii kuna vyanzo vya mito kadhaa mikubwa kama mto Grijalva ambao ni chanzo kikuu cha umeme unaopatikana nchini Mexico, mto Canyon Sumidero na mto mwingine wenyewe ukichukua muelekeo wa kuingia Marekani, mto Colorado. Pia milima hii katika historia kumeshatokea volcano miaka tofauti tofauti ya zamani kama vokano Santa Marta, Volkano San Martin Tuxtla ikitokea mwaka 1664 na volcano kubwa zaidi ikitokea mwaka 1793 ikifahamika kama volcano alkali kisha ya hapo haikutokea tena volcano lakini kwakuwa sehemu ya milima ya volkano uwa haitabiri watu huishi maeneo haya kwa tahadhari kubwa sana.


Sehemu ya juu zaidi ya safu ya milima zilipolipuka volcano za San Martin Tuxla na Santa Marta zimefunikwa na theluji ya Sierra de los Tuxtla ambayo usababisha mvua za mara kwa mara eneo na kulifanya kutokuwa eneo rafiki kabisa kwa makazi ya watu.


Eneo hili la juu ndipo linapoanza jimbo la Veracruz kusini karibu na ghuba ya Mexico lakini kote kuna misitu mizito ambayo yote ipo katika eneo la hifadhi la kiasili la mamlaka ya shirikisho ya Mexico katika milima hii inayoanza kutokea jimbo la Tabasco milima ikaendelea kwa kuunganisha majimbo mengine kama Chiapas na Veracruz yenyewe.


Ndani ya eneo la mpaka wa jimbo la Chiapas na Veracruz kando kando ya milima hii ya Tuxtla kuna kijiji kinachoitwa Coyatoc ndipo mahali ambapo kuna hifadhi ya maua yaitwayo Flora huku kukiwa na majumba kadhaa ya kizamani ya wananchi waliokuwa wakiishi eneo hili na baadaye kusogea mbele zaidi na kulifanya libaki kuwa eneo la hifadhi ya taifa na uzalishaji wa maua ya flora yanayostawi kwa wingi eneo hili kutokana na hali ya hewa yake ni eneo lililo kando ya mto mkubwa wa Sumidero unaonzia ndani ya hifadhi ya milima Tuxtla kisha wenyewe unaenda kujigawa na mgawo huo kuanzisha mto usumancita unaokatiza katikati ya manispaa ya Villahermosa mpaka bahari ya Atlantiki.


Coyatoc katika moja ya jumba lililokuwa zahanati ya kijiji miaka kadhaa kabla eneo halijageuzwa kuwa eneo la hifadhi na uzalishaji wa maua ya flora ndipo mke wa Mr. Fanuel Madam Felister, watoto wake wote watatu na rafiki yake Gabriela Lopez akiwa na mwanae walihifadhiwa eneo hili chini ya ulinzi mkali sana ikiwa ni kando kabisa ya mto huku mamlaka za kiserikali zinazolinda eneo hili kutoona jambo hili kwakuwa eneo hili lilikuwa mita kama mia tatu na hamsini toka mwisho kabisa wa shamba la maua ya Flora.


Saa kumi na mbili na dakika tano ya jioni ya siku ya jumatatu, bwana mkubwa Brigedia Fernandez alichomeka kifaa cha kusaidia kuepusha dira ya google map ya minara ya simu katika kompyuta mpakato baada ya kuwa pia akiwa kashachomeka modem ya intaneti.


Akatafuta namba za rafiki yake wa miaka nane mpaka tisa iliyopita wakishirikiana mambo mengi kisiri siri katika biashara ya mihadarati huku yeye Brigedia Fernandes ‘Feca’ akiamini anamsaidia rafiki yake wa kufa na kuzikana na kama ikitokea yeye akawa katika matatizo basi rafiki huyu ndiyo atamsaidia.


Simu iliita mara moja tu baada ya Feca kuipata namba na kupiga hii ilionyesha mpokeaji alikuwa na simu muda wote akisubiri iite tu apokee, bila kujali mpigaji ni nani?.


“Halloow…!” Mpokeaji haraka akauliza mpaka Feca akatabasamu.

“Habari yako Fanuel?” Akauliza Feca huku uso wake ukiwa na tabasamu pana lililochanua kama ua la saa nne.

“Hali yangu mbaya Feca… Unaishikiria familia yangu Feca nitakuwaje na hali nzuri…!”

“Ha ha hah ahaha! Nacheka kama mazuri… Nachotaka kwako tayari unakijua ni muda wako kuhakikisha unairudisha familia yako Avenida Pasco Usumancita katika kasri lako bomba la Miguel Palace ikiwa katika hali nzuri na afya tele au kupokea kichwa cha mtoto wako wa mwisho ifikapo saa nne usiku.. Unanijua nilivyo sina masikhara nitakuchinjia watoto wako kila siku mmoja usipotii maagizo yangu na kisha kumalizia na mkeo”

“Kwanini? Kwanini… Kwanini Feca? Niko tayari kutimiza masharti yako nielekeze nayatimiza vipi?”

“Kwanza ningetaka kujua umeripoti kwenye chombo chochote cha usalama juu ya kilichotokea?”

“Siwezi kufanya ujinga huo Feca… Mimi nafanya biashara ambayo urafiki wangu na polisi ni kulinda mali zangu na si urafiki wa kuwashirikisha katika vitu ambavyo najua ni hatari kwa familia yangu… Niamini kaka”

“…Niambie unatoa MX-Peso ngapi katika faida ya miaka sita ikiwa pamoja na mtaji niliokupa miaka saba iliyopita lakini nimetaka faida ya miaka sita tu?”

“Mambo hayako vile unavyofikiri kaka yangu… Faida haiko vile ambavyo nafikiri wapambe wasionitakia mema wamekupa.. Nitatoa kiwanda pia nitatoa kasri lililo katika eneo kilipo kiwanda nitakachokupatia pia nimekuongezea na gari mbili za kifahari katika ofa yang..”Hakumalizia sauti nzito ya kufoka ikamkatizia.


“Unachelewesha mambo Fanuel au unatafuta eneo nilipo mpuuzi wewe na hao vijakazi wako? Sikiliza niko vizuri kuliko wewe na hao wanaokudanganya… Sema unatoa kiasi gani maana unanieleza ving..” Naye hakumalizia kwakuwa Fanuel naye akafanya kama alivyofanya mwenzie.

“Dola milioni kumi… Dola milioni kumi… Tafadhali naomba upokee na tuache uhasama ndugu yangu… mambo ya familia si mambo kaka yangu..”Akaongea sauti ya upole lakini yenye mwendo wa haraka kutamka matamshi.


“Ongeza dola milioni tano…” Akaongea kisha akakata simu Feca, akitabasamu.


Alizima kompyuta mpakato na kuondoka eneo lile lenye korongo kubwa linaloonyesha mto mkubwa sana unaopita kwa bondeni hivi, eneo lenye misitu ya asili ya kijani inayopendeza.


Alisubiri pale pale akiwa na wenzake wapatao saba hivi wao wakipata burudani ya kunywa pombe na kuvuta bangi huku wakipiga stori mbalimbali kwa raha zao na umakini ukiwepo mkubwa na wa kutosha.


Saa moja kamili akiwa ameacha muda wa dakika kama hamsini upite akapiga tena simu kwenda kwa Fanuel kupitia aina ile ile ya upigaji ambayo ina usalama kwake.


“Umeamuaje?” akauliza baada ya upande wa pili kupokea.

“Nimekubali nitaongeza hiyo pesa.. Nachotaka familia yangu Brigedia na ninaomba nisamehe sana kwa kosa nililokutendea.. Si..!”

“Sawa nishakusamehe… Nataka pesa hizo cash… Na naamini hakuna ujanja wowote utakaokuwepo… Mimi sihitaji kudhuru mke wala watoto wako, najua unajua jinsi gani nilivyokuamini na kukuthamini ila wewe mwenzangu hukutaka twende sawa na ndiyo maana nikachukua hatua hizi Fanuel… Nataka usiku wa leo tumalizane kila kitu katika vitu vyote ninavyotaka kwako tena kisheria tukishamaliza hayo ndipo utaipata familia yako.. Umenielewa?”

“Nimeelewa na pia naujua utaratibu huo.. Ila kuna jambo unatakiwa utambue kiwanda unachohitaji inatakiwa nikukabidhi kisheria kama umenunua kwangu hivyo kutakuwa na kodi ambayo serikali itaitaka katika manunuzi tutakayokubaliana, huku kuhusu nyumba na magari itakuwa rahisi tu… Kiukweli nimeumia sana na mambo yaliyotokea kwa sababu kama ulivyotoka tu jela ungeamua kuja kwangu ningekupatia kila unachotaka sababu ni halali yako kaka ila umeamua kutumia njia hii kwakuwa huniamini kaka..”

“Acha uongo wako Fanuel… Mimi siyo fala, najua nilivyotoka jela ningekutafuta muda huu funza wangekuwa wanashindana kutoboa mwili wangu waweke makazi…. Utanisamehe kwa njia niliyotumia lakini imenibidi iwe ndiyo njia sahihi sababu sote tunajuana sisi ni mafia na mafia hatutabiriki.. Nafahamu ningekuja kwako ungenishindilia risasi za kutosha tu kama si kunikatakata kwa mapanga kama wafanyavyo Z ya mwisho unaoshirikiana nao kulinda baishara zako... Nachoomba ufuate malekezo yangu jinsi tutakavyowashirikisha wanasheria wetu kupeana kila kinachohitajika… Pesa na kila kitu kikishamalizika kimakabidhiano ndipo na wewe utawapata watu wako ujanja wote familia yako itakwisha yote na kubaki historia”.

“Sawa kaka! Nakusikiliza wewe”


Sekunde thelathini za ukimya zilimuacha Brigedia Feca akitathimini iweje kwa haraka.


“Acha watu wako wote wa ulinzi na wa kazi… Mimi pia nitakuwa bila watu hao.. Njoo na mtu wako wa hesabu na mwanasheria wako… Sihitaji uende tofauti na maagizo ninayotoa, nataka tukutane na kuongea kirafiki” Akaongea Feca baada wa ukimya ule wa sekunde thelathini.


“Sawa nitafanya utakavyo.. Wapi tunakutana?”

“Chiapas! Kwenye maegesho ya magari ya chini ya jengo la La Torre Chiapas Mesoamericana.... Kesho saa kumi na moja alfajiri, uje na pesa pamoja na hao watu niliosema… Zingatia na utii bila shuruti maelekezo yangu kuanzia muda hadi idadi ya utakaongozana nao..”

“Chiapas.. Sawa, nitafika bila kuchelewa ila naomba na wewe uzingatie usalama wa familia yangu, sitapenda kuwakuta wakiwa katika hali yoyote mbaya pia maswali toka kwa familia ya mwanamitindo na muigizaji Gabriela Lopez yamekuwa mengi sana ningeomba tukikutana basi angalau uwe umefika na huyo akiwa na mwanae hili nirudi naye Villahermosa nimkabidhi kwa baba yake maana leo alivyofika hapa nimemdanganya wameenda Frolida na mke wangu kuna mikataba ya kibiashara wameenda ingia huko..”

“Naweza mleta kama utamlipia dola milioni tano maana asije kuwa amegundua wapi alienda ikawa shida kwangu kabla sijamalizana na wewe… Kama huwezi mlipia hivyo vumilia utampata akiwa na familia yako kwa gharama za jumla bila hiyo dola milioni tano..!”

“Nitamlipia dola milioni mbili na nusu sababu naogopa baba yake akiendelea kutomuona ataenda toa taarifa kwenye vyombo vya usalama na media ambapo mimi sitaki jina langu au la mke wangu lichafuke katika media itaniletea shida kibiashara..”


Brigedia kidogo hapa somo lilimuingia akaona ni kweli asemavyo Mr. Fanuel hivyo alitulia kidogo akifikiri kisha akajibu.

“Sawa lete mzigo huo..”

“Nashukuru ndugu yangu…”


Brigedia Feca hakuendelea kuwa hewani akakata simu wakiwa wamekubaliana hivyo kuwa wakutane jimbo la Chiapas alfajiri ya siku inayofuata.


***** ***** *****


La Torre Chiapas Mesoamericana jengo refu lenye urefu wa mita 104 zilizobeba flour (losheni) 22 kwenda juu ni jengo refu kuliko majengo yote katika mji wa Tuxtla Gutierrez jimbo la Chiapas, Mexico, mji uliojengwa ukanda wa chini wa milima ya Tuxtla. Ni jengo la tatu kwa urefu kwa ukanda huu wa kusini mashariki mwa nchi ya Mexico.


Likipatikana eneo la makutano ya mtaa wa Libramiento Norte na Calzada Andres Secra Rojas ni sehemu yenye miradi ya kijamii, ofisi nyingi sana za taasisi mbalimbali zinazohusika na mambo mengi ya kimaendeleo katika hifadhi ya milima Tuxtla na zingine kama za elimu na vijana zinapatikana katika mtaa huu hususani jengo la La Torre Chiapas Mesoamericana.


Saa kumi kasoro dakika kumi ya usiku unaokaribia kukucha kwa majira ya saa za kimexico, Brigedia Fernandes Carlos Codrado alikuwa akiingia mtaa huu akiwa ndani ya gari anayoendesha yeye mwenyewe na watu wengine wanne na jumla yao kuwafanya wawe jumla watano ukimjulisha na yeye.


Katika gari hii aina ya Nissan Patrol Falcon rangi nyeusi aendeshayo Feca kuelekea eneo la jengo la La Torre Chiapas Mesoamericana kulikuwa na mwanasheria wa familia ya Guti, pia alikuwepo mhasibu wa Guti wote hawa wakiwa wameletwa hapa kuhakikisha kila kinachotakiwa kwenda sawa kinaenda sawa pamoja nao waliambatana na rafiki wa madam Felister akiwa na mtoto wake.


Lakini wao wakiwa wanafika tayari masaa mawili yaliyopita wazee wa kazi wapatao sita wakiongozwa na Koplo Savatel Santos, wao waliingia na kwenda maegesho ya chini ya jengo hili refu lenye maegesho ya juu kabisa ya jengo na chini kabisa ya jengo.


Wao walipofika tu walishuka wawili kwenye gari yao na kuchunguza chunguza mandhari ya eneo lile kubwa tu ambalo muda huo wa usiku kulikuwa na magari machache tu wakati ukifika asubuhi ya saa mbili saa tatu kunakuwa kunajaa mpaka wengine kulazimika kwenda kupaki magari yao juu kabisa ya jengo na wote hawa uwa ni wafanyakazi wa makampuni na taasisi mbalimbali kama nilivyotangulia kueleza.hapo juu.


Baada ya kuridhika na ukaguzi waliofanya ndipo wakashuka kwenye na kujitawanya karibu kona zote za eneo hili wakijificha vizuri na pia kutoa taarifa kwa boss wao Feca kuwa wao washafika na mazingira yaliyopo ni kama sehemu zingine zinazokuwa na huduma hii ya kuegesha magari nchini Mexico uwa hakukosi cctv Kamera hivyo wakamuelekeza eneo lipi zuri yeye kuja na kumsubiri Mr. Fanuel kwakuwa eneo hilo waliichezea kamera moja hili ichukue matokeo ya hali ya usiku ilivyo kisha igande isiendelee kuchukua ifanye unafiki wa kiwango SGR.


Brigedia Fernandes alipita kwenye geti la kuelekea maegesho ya chini ambalo muda wote uwa linakuwa wazi masaa ishirini na nne halifungwi lipo kwa ajili ya huduma limradi unalipia kiasi fulani cha Mexican Peso kiwango walichoweka hivyo uwa kabla haujapita unalipa wanaruhusu kwa kuinua mnyororo na kwakuwa ni usiku alikuwepo mlinzi mmoja tu.


Alisogeza gari upande alioelekezwa kuwa kamera ya cctv ya upande imefanyiwa ufundi na kupewa uwezo wa tofauti na uwezo wake katika kazi yake akapaki gari na wote waliomo ndani ya gari hakuna aliyeongea kitu kila mmoja akiwa katika fikira zake huku mtoto wa mwanamitindo Gabriela Lopez akiwa amelala usingizi kichwa akikilaza kwenye mapaja ya mama yake.


Saa kumi na moja kasoro dakika tatu gari aina Land Rover Discover 3 Rangi nyeusi iliingia kwenye maegesho yale ikiwa katika mwendo wa gari ya bi harusi, ikaonyesha ishara kwa kupiga taa za mwanga mwekundu mara tatu na hapo waliotangulia kufika na kujigawanya pande zote walitambua hiyo ndiyo gari husika na hata Feca pia alitambua na yeye akamjibu kwa kuwasha taa nyekundu mara tatu ishara ikaeleweka dereva wa gari iliyofika muda huo bila kuongeza spidi ikakata kona na kuelekea kule ilipo gari iliyotoa ishara ya taa nyekundu mara tatu kisha ikabaki imeachia taa zile ziendelee kuwaka.


Taratibu Land Rover Discover 3 ikapaki ubavu kwa ubavu na gari alilomo Brigedia Fernandes na watu aliokuja nao huku kisha dereva wake akashusha kioo na Feca kuona vile naye akashusha upande wake, sura mbili za watu wanaofahamiana ikiwa sura ya Feca ina mabadiliko kidogo kwa kuachia ndevu zake kiasi ya kuwa zilimeza kidevu chote na kuufanya pia mdomo wake papi (lips) zake kuonekana kwa mbali kwa jili mzigo huo ambao waswahili wameupa jina la ‘ndevu si mzigo’.


Wote wakiwa wamevaa miwani ya rangi nyesusi lakini ile yenye uwezo wa kuona gizani vizuri tu, waliangaliana kila mmoja akimtathimini mwenzie kwa lile analofikiri katika mengi ambayo watu wa kazi za mihadarati wakikutana uwa hivyo.


“Umekuja na mwanasheria wako?” Akauliza Feca bila hata kumsalimia mwenzie baada ya macho yake yaliyo ndani ya miwani kudadisi kwa tabu waliomo ndani ya gari ni watu wa aina gani kutokana na vioo vya gari aliyokuja Mr. Fanuel vilikuwa kama vioo vya gari aliyokuja nayo Feca, vioo vilivyoongezwa nailoni nyeusi (tinted) juu ya vioo vya vya madirisha yote ya milango ukiacha kioo cha mbele tu.


“Nimefanya vile ulivyoagiza… Naomba unihakikishie juu ya uzima ya wanafamilia yangu..!” Akaongea kwa sauti iliyodhihirika masikioni mwa Feca kuwa mtu huyu amechoka na ana maumivu makali sana.


“Najua umekuja na wafuasi wako wa MPD wako nyuma ya jengo hili… Sijakuita hapa tufanyiane uhuni.. Familia yako iko salama salimini mahala salama wakipata huduma zote muhimu kama walizokuwa wakipata kwako ‘Miguel Palace’.. Naomba pesa nilizotaka ziwe tangulizi kisha nataka nikupe ratiba mpya kwako kuwa hatutaachana tena baada ya hapa tutaendelea na michakato yote tukiwa pamoja hivyo nina tiketi za ndege nimekata zako na watu wako kwenda Mexico City wizara ya viwanda na tukiwa huko tutakabidhiana kila kitu nachohitaji na familia yako yote utaipata huko Mexico City ila wale uliowahitaji muigizaji na mwanamitindo maarufu Gabriela Lopez na mwanae ninao hapa na kwa kurahisha na wao nimewakatia tiketi ye ndege maana Gabriela Lopez aliniambia anaishi Mexico City hivyo tutaongozana naye… Kwa kuhakikisha nachoongea angalia…!” Akaongea kirefu Feca kisha vioo vya gari yake vikashuka vyote na watu walio ndani ya gari wakaonekana ndani ya macho yaliyo ndani ya miwani ya ‘Kingpin’ na tajiri mkubwa Fanuel Miguel Mendoza.


“Sawa nakubali uyasemayo.. Kwa hiyo familia yangu ipo Mexico City? Asante sana.. Nachotaka nipate watoto wangu na mke wangu..!” Akaongea na kisha mkono wake ukainuka na briefcase akatoa mkono dirishani kisha akalielekeza kwenye mkono wa Feca ambapo alipoliona briefcase akasogeza mkono wake wa kupokea kisha akamkabidhi mtu aliye pembeni yake Mhasibu wa Mr. Guti ambapo hapa alifika kama mhasibu wa Feca.


Mara moja alipolipokea akalifungua na macho yake kukutana na harufu ya pesa za noti za dola akahesabu kwa haraka vifungu vilivyopangwa mistari huku vikiwa vimetuna, alipomaliza kuhesabu vifungu akainua kibunda kimoja akapaka mafuta fulani vidoleni akazipitia kwa kasi kwa dole gumba na kwa alivyo mzoefu akapata idadi yake kwa dakika nne tu hivyo akawa amepata idadi kamili kwa hesabu ya vifungu vyote.


“Mzigo huko sawa boss!” Akajibu muhasibu baada ya kutizamana na Feca.


“Nashukuru Fanuel.. La kwanza umetimiza… Tuanze safari ya kwenda uwanja wa ndege, tutapumzika kwenye migahawa iliyopo pembezoni mwa uwanja wa ndege.. Naomba uwaambie watu wako kosa lolote dogo litasababisha kuchinjwa mkeo na wanao hivyo wakae kando, mchezo hauwahusu huu wakati mimi nakupatia mzigo wangu wao walikuwa hawajui kama kuna mtu anaitwa Fanuel atakuja kuwa tajiri mkubwa baada ya miwili au mitatu ijayo” Alimalizia kwa kuweka onyo kali lenye msisitizo wa kumtaka yeye Fanuel na watu wake wa MPD watulie na wafanye atakavyo, wawaache kabisa wao wawili wakifanya yao kwakuwa wao ni kama waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba.


Kwa kutumia mawasiliano ya meseji Feca aliwataarifu watu wake walio hapa maegesho ya chini kuwa safari waliyokubalina kwenda Mexico City imewiva hivyo wao wanatangulia kuja kisha watu wake wa kazi wakiongozwa na Koplo Savatel akiwa kajibadili kidogo muonekano wa sura yake watafuata nyuma wakiweka ulinzi maana magenge ya mihadarati inayongozwa na maboss wakubwa (Kingpin) kama Fanuel uwa hawatabiriki nawao kwakuwa wako kwenye biashara hii ya haramu ilikuwa wanatambua hayo.


Mwisho wa sehemu ya ishirini (20)


Hali ya makubaliano kati ya Brigedia Feca na swahiba wake wa miaka kadhaa iliyopita yameweza kuwakutanisha watu hawa na kuanza kukabidhiana yale yaliyopo ndani ya makubaliano yao.


Kulikuwa hakuna njia nyingine ya kusababisha Fanuel ‘Kingpin’ wa MPD asitoe anavyotaka Feca na sasa ndiyo makabidhishiano yameanza rasmi katika maegesho ya magari ya chini ya jengo refu kuliko majengo yote katika jimbo la Chiapas, jengo la La Torre Chiapas Mesoamericana.


Safari ya kuelekea Mexico City kutokea Chiapas…


Tusipoteze muda kwa kuelezana mengi yaliyopita twende tusonge…



ILIPOISHIA SEHEMU YA 20…!!

Mara moja alipolipokea akalifungua na macho yake kukutana na harufu ya pesa za noti za dola akahesabu kwa haraka vifungu vilivyopangwa mistari huku vikiwa vimetuna, alipomaliza kuhesabu vifungu akainua kibunda kimoja akapaka mafuta fulani vidoleni akazipitia kwa kasi kwa dole gumba na kwa alivyo mzoefu akapata idadi yake kwa dakika nne tu hivyo akawa amepata idadi kamili kwa hesabu ya vifungu vyote.


“Mzigo huko sawa boss!” Akajibu muhasibu baada ya kutizamana na Feca.


“Nashukuru Fanuel.. La kwanza umetimiza… Tuanze safari ya kwenda uwanja wa ndege, tutapumzika kwenye migahawa iliyopo pembezoni mwa uwanja wa ndege.. Naomba uwaambie watu wako kosa lolote dogo litasababisha kuchinjwa mkeo na wanao hivyo wakae kando, mchezo hauwahusu huu wakati mimi nakupatia mzigo wangu wao walikuwa hawajui kama kuna mtu anaitwa Fanuel atakuja kuwa tajiri mkubwa baada ya miwili au mitatu ijayo” Alimalizia kwa kuweka onyo kali lenye msisitizo wa kumtaka yeye Fanuel na watu wake wa MPD watulie na wafanye atakavyo, wawaache kabisa wao wawili wakifanya yao kwakuwa wao ni kama waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba.


Kwa kutumia mawasiliano ya meseji Feca aliwataarifu watu wake walio hapa maegesho ya chini kuwa safari waliyokubalina kwenda Mexico City imewiva hivyo wao wanatangulia kuja kisha watu wake wa kazi wakiongozwa na Koplo Savatel akiwa kajibadili kidogo muonekano wa sura yake watafuata nyuma wakiweka ulinzi maana magenge ya mihadarati inayongozwa na maboss wakubwa (kingpin) kama Fanuel uwa hawatabiriki nawao kwakuwa wako kwenye biashara hii ya haramu ilikuwa wanatambua hayo.

.


ENDELEA….!


MAKUBALIANO V,CHIAPAS-MEXICO

Baada ya pande zote mbili kuweka sawa watu wao kuwa watulie maana huko nje ya jengo nako MPD wakiongozwa na Maria Rodgruez walikuwa wako kama kumi na sita katika gari tatu walizoziweka kwenye maegesho ya kota za watumishi wa serikali zilizoko nyuma ya jengo refu la La Torre Chiapas Mesoamericana wakimsindikiza boss wao kufanya yale yaliyoelekezwa na mdai wake, walikuwa wakiamini linaweza likatokea lolote basi wao wataingilia (kulikuwa hakuna kuaminiana)


Safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa uuitwao Angel Albino Corzo uliopo jimbo hili la Chiapas eneo la mwinuko wa juu la Tuxtla Gutierrez. Magari mawili yakiongozana na kwa maelekezo ya boss wao Maria Rodgruez na watu wengine wa MPD hawakuendelea tena kumfuatilia boss wao kwakuwa Fanuel aliwaelekeza kwa meseji kuwa walionekana kwa watu wa Feca na hivyo kuendelea kuwafuatilia wanaweza wakaihatarishia maisha familia yake.


Wakati wale wa Feca wakiongozwa na Koplo Savatel wakaondoka pale maegesho ya chini mara baada ya kupambazuka kabisa na kwakuwa walikuwa na tiketi za ndege wao wakaondoka pale moja kwa moja wakaelekea kwenye mgahawa wa bustani ya De La Marimba uliopo karibu na uwanja wa ndege wa Angel Albino Corzo.


***** **** *****


MAKUBALIANO VI, MEXICO CITY-MEXICO

Abraham Gonzalez 49 Juara Street, mtaa iliyopo ofisi ya waziri wa mambo ya ndani wa nchini Mexico katika jiji kuu na makao makuu ya serikali ya Mexico, Mexico City.


Jiji lililojengwa kwenye bonde liitwalo bonde la Mexico ni moja ya jiji lenye wakazi wengi sana miongoni mwa majiji yaliyopo Amerika Kaskazini, jiji ambalo makusanyo yake ya pesa ni makubwa sana ikisemekana pato linaloingizwa kwa mwaka na jiji hili la kibiashara na makao makuu ya serikali ni pato ambalo linaweza kuzipita nchi nyingi za jirani na nchi ya Mexico kama Guatemala, Costa rica na Puerto Rico, nchi hizi mapato ya nchi nzima kwa mwaka hayafikii mapato wanayopata jiji la Mexico.


Ndani ya ofisi hii ya waziri wa mambo ya ndani kulikuwa na kikao cha viongozi wa juu wa ulinzi na usalama, akiwemo waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Castillo Zuguzaleta aliyeitisha tena kikao hiki baada ya cha kwanza kufanyika wiki moja iliyopita kukawa na mapungufu ya watu wengine kutofika kwakuwa hawakuonekana kama wanahusika siku hiyo.


Alikuwepo Waziri asiyehusika na wizara hii lakini mualikwa kwenye kikao hiki waziri toka wizara ya ulinzi ambaye ndiyo bosi wa wizara hii mheshimiwa Rafael Castillo Nigueto akiwa ameambatana na mkuu wa majeshi Brigedia Jenerali Moses Talvares Murillo ambaye naye alikuwa ameambatana na mkuu wa kitengo cha nidhamu jeshini Secretariat Of The Navy, Meja Sanz Manuel Fuerza.


Kwa pamoja nao hao walikuwepo mkuu wa idara ya usalama wa taifa Meja Fransisco Calisto Mugiera, mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jeneral Ernesto Manuel Calderon, mkuu wa jeshi la magereza Kamishina Nieto Luna Spreto akiambatana na msaidizi wake kamishina msaidizi wa jeshi la magereza Mr. Geraldo ALexander Muriel akiwa na wanayemuita Kamishina mdogo Mr. Fergata Maxiwell Ginger na wa mwisho kutimiza idadi ya wahudhuriaji alikuwa katibu wa wizara ya mambo ya ndani kunakofanyika mkutano huu Mr. Saul Nuahin.


“Leo nafikiri tutafanikiwa kuyapata majibu tunayostahili kuyajua kwa kuwa sote tulio na umuhimu tuko hapa tukihitaji kufahamishana ni vipi yamefanyika mambo yaliyofanyika…. Naomba niwashukuru wote mliofika katika muda muafaka hapa ofisi ya wizara ya mambo ya ndani” Alianza kuongea Waziri wa mambo ya ndani kisha akajikooza kidogo na kutupa macho yake kwa kila aliyepo pale kisha akaendelea.

“Mara mwisho tulivyokutana katika ukumbi huu wa vikao vyetu wanausalama kwa wale ambao tulifanya kikao kile tulifikia maamuzi ya kuwa kikao kitapendeza kama kitahudhuriwa na sote sisi tuliopo hapa muda huu… Naomba tusipoteze muda tuanze kikao chetu kwa kusikiliza maelezo ya mwenzetu toka jeshi la Magereza Kamishina msaidizi Geraldo Muriel, karibu”


“….Mmmh!.. Ahsante sana waziri wangu wa mambo ya ndani kwa kunipa fursa hii mimi kujieleza maana siku mbili nilizorejea kutoka Veracruz nimekuwa mtu wa kuonyeshwa vidole na hadi maaskari wa chini nikituhumiwa kupanga njama za kuwahamisha wanajeshi waliofungwa kwenye magereza yetu… Ukweli ni kuwa nilitia sahini nyaraka nilizoletewa na sekretari wangu kisha nikampa Mr. Fergata Maxiwell Ginger atume nyaraka zile gereza la Matamoros huko Tamaulipas pia afuatilie kwa ukaribu utaratibu wote hivyo yeye alisimamia zoezi hilo kwa kushirikiana na mkuu wa gereza la Matamoros… Swali kuu ninaloulizwa kuwa niliwasiliana kwa simu na afisa gani wa ngazi za juu toka jeshi la wananchi, ukweli ni kuwa sikuwasiliana na mtu yoyote baada ya kuona nyaraka zile ni zenyewe zikiwa na muhuri wa ofisi ya secretariat of navy pamoja na sahihi ya bwana mkubwa Meja Sanz Manuel Fuerza… Sasa kwakuwa naye leo yupo hapa kikaoni naomba yeye ndiyo hajibu maana nyaraka hizi hapa na zina muhuri wake pamoja na sahihi zake karibu kila nyaraka pia mimi si mgeni wa sahihi ya Meja Sanz na muhuri wa Sekretariati ya Navy kitengo cha nidhamu pia si mgeni nao sababu tunafanya nao kazi kwa ukaribu kuliko ofisi zote jeshi huko makao makuu ya jeshi” Akaeleza kirefu Mr. Geraldo kamishina msaidizi.


“Meja Sanz! Nyaraka husika hizo hapo, naomba uzipitie kisha utupatie majibu ilikuwaje.. Siyo kesi hii ni kuelekezana na kama itakuwa kesi basi baada ya kikao hiki ndiyo tunaweza kuamua kama kuna kesi ya kujibu katika hili!” Mwenyekiti wa kikao waziri wa mambo ya ndani akamtupia mzigo unaomstahili mkuu wa kitengo cha nidhamu ya wanajeshi jeshini ofisi ya secretariat of navy Meja Sanz.


Alizipokea nyaraka na kuanza na iliyo juu macho yakaanza na sahihi kutoka karatasi ya kwanza akaenda ya pili na ya mwisho ya tatu akatizama kisha akasikitika kwa kutikisha kichwa stahili ya kusikitika akalisogeza pembeni na kutwaa la pili na akafanya kama la kwanza kulipitia hakuishiwa na kusikitika mpaka anamaliza faili la mwisho.


“Wakuu zangu na wale ambao si wakuu zangu katika vyeo nasikitika kuwaambia kuna mchezo umechezwa… Si mimi niliyetia saini hizi nyaraka na wala si mimi niliyegonga muhuri nyaraka hizi zote.. Hu…!” Hakuweza kuendelea macho makali ya bosi wa jeshi la wananchi, mkuu wa majeshi Brigedia Jenerali Moses Talvares Murillo yalimfanya asiendelee kutoa maelezo hili amuache aongee.


“Meja!... Ofisi yako ina watu wangapi?” Akaulizwa na mkuu wake mkuu wa jeshi la wananchi Brigedia Jenerali Moses Talvares Murillo.


“Ofisi yangu niko mimi mwenyewe na mapokezi yupo sekretari na msaidizi wake ambaye ndiye mesenja wetu..!” Akajibu kisha akatulia kusubiri kama kuna swali jipya.


“Nani anakuletea mafaili yanayotakiwa kupitiwa na wewe?” Akauliza Waziri wa ulinzi bosi wa wao wote ingawa mkuu wa majeshi anateuliwa na Rais wa nchi kwa katiba ya Mexico lakini kazi zake anafanya akiwa chini ya mteule mwenzake mwingine kama yeye waziri wa ulinzi wote wakiteuliwa na Rais wa nchi.


“Sekretari wangu au msaidizi wake! mheshimiwa waziri..!” Akajibu Meja Sanz.


“Katika ofisi yako imeshawai kutokea kashfa kama hii kisha ukaamua tu kuifumbia macho na kuifanya ipite tu?” Mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa Meja Fransisco Calisto Mugiera akaingia na swali lake.


“Hapana sijawai kujua.. Pengine michezo yao ipo lakini sijawai kustuka kwa kweli..!”Meja Sanz akaendelea kujitetea kwa pointi ambazo zilikuwa zikishawishi kwa kila mmoja.


“Tunashindwa kuamini Meja Sanz lakini kwakuwa wewe ndiyo unasema inatubidi tuamini na kuamia katika uchunguzi wa kuujua ukweli juu ya hili jambo kwa sababu tayari lina ukakasi mkubwa.. Hatuwezi kukubishia wakati tunaona muhuri na sahihi bila kupepesa macho unasema huvitambui vitu hivi wewe muhusika…. Hofu yetu ni haya magenge yanayoendeleza ushenzi wao nchini hasa hawa Los Zetas, Gulf Cartel na lile kundi lililokuwa la El Chapo genge la Sinaloa hawa nao walitupachikia watu wao katika idara zetu za usalama na ndiyo maana unaona hatuaminiani hadi sisi ambao tuko nyadhifa za juu..!” Waziri wa ulinzi akaongea tena kisha akanyanyua glasi ya maji akanywa kidogo maji.


“Nafikiri pale ofisini kutakuwa na mchezo mchafu.. Inanibidi nikifika niwaite wasaidizi wangu wote wawili kuwahoji vizuri ilikuwaje? hizi nyaraka zimefika makao makuu ya jeshi la magereza zikiwa na muhuri wa ofisi pamoja na sahihi yangu..!”Akaongea Meja Sanz.


“Miaka saba ya kifungo cha Brigedia Fernandes halafu siku chache tu toka atoke gerezani baada ya kumaliza kifungo chake huko Acapulco, yanatokea mauaji ya kutisha ya watu waliokuwa wafuasi wake, watu waliomlinda kwa udi na uvumba yeye asifungwe wanahamishwa kwa taratibu zisizo sahihi na kisha wakiwa njiani kwenda Acapulco wanakatwa katwa na kubaki na viwili wili… Hivi hamuoni kuna kitu? Mimi kuna kitu najaribu kuunganisha dot na dot niweze kupata jibu lakini sifiki napopataka na hii inaniwazisha sana” Akaongea akizungusha macho yake kwa wote kwa ujumla mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jeneral Ernesto Manuel Calderon.


“IGP! Mchezo? Inawezekana lakini.. Basi nafikiri Meja Sanz achukue timu yake upelelezi wakawahoji vizuri masekretari wake naamini watatapika tu ukweli tukajua ilikuwaje na kwanini? Kisha majibu utanipatia mimi nitawaita waheshimiwa kuwapa taarifa yako na kama kumtafuta mtu aliyefanya mchezo huu mchafu ndani ya makao makuu ya jeshi haraka aanzwe kutafutwa huu ni uhuni, jeshi letu muhimili wa mahakama na maamuzi yake iwe ya kiraia au mahakama yetu ya jeshi” Waziri wa ulinzi akaongea kisha kujiachia mgongo wake ulalie kiti alichokalia.


“Waheshimiwa kwa mara nyingine napenda niwashukuru kwa kufika kwenu hapa. Nafikiri maamuzi yetu yataleta majibu baada ya siku moja tu kwani najua masekretari wa Meja Sanz wana majibu sahihi ya suala hili… Wiki sasa Amiri Jeshi mkuu anahitaji kujua nini kimesababisha wanajeshi waliofungwa wachinjwe kikatili na pia askari wetu wa jeshi la magereza wauliwe, asubuhi hii na tuna mambo mengi yanayotungoja katika majukumu yetu ingetosha tukafunga kikao hiki na kurejea kwenye kazi zetu huku tukisubiri ripoti ya Meja Sanz!” Mwenyekiti wa kikao Waziri wa mambo aliamua kusitisha kikao chao baada ya maongezi yao ambayo hayakula muda mwingi na maamuzi kufikiwa haraka tu.


Walipeana mikono ya shukrani na waliopiga stori mbalimbali katika kubadilishana mawazo walifanya hivyo huku wengine wakiondoka haraka kuendelea na majukumu mengine.


***** ***** *****


Uwanja wa ndege wa Mexico City International Airport (Aeropuerto Internacional de la ciudad) uliopo eneo la Venustiano Carranza ni moja ya viwanja vya ndege vilivyo bora na vikubwa sana kati ya viwanja vilivyopo katika eneo Amerika ya kaskazini, moja ya kiwanja ambacho teknolojia kila inapodhidi kukua hapa duniani na chenyewe ubadilika kuendana na teknolojia inavyotaka. Kiwanja cha kisasa kimiundombinu na ulinzi wa hali ya juu.


Muda huu wa saa mbili na robo ndege ndogo ya shirika la ndege la Aeromexico itokayo jimbo la Chiapas ilitua hapa ikiwa na abiria sitini na sita, wengi wakiwa ni wale wa genge la siri linaloongozwa katika msafara huu na Brigedia Fernandes Carlos Codrado, akiwa kaongozana na mwanasheria wa Mr. Guti


Koplo Savatel na watu wake ambao wote kati yao waliingia kwenye ndege wakiwa hawajaongozana kana kwamba si wamoja, ndege ilipotua pia walishuka vile vile kama walivyopanda kila mmoja kijifanya hayupo na mwenzie na pia hakuna hata aliyeonyesha anamjua Brigedia Fernandes, pia walichukua tahadhari ya kujibadili muonekano wa sura zao sababu hawakutaka kuamini kuwa inaweza kuwa Mr. Fanuel hawajui kabisa hata mmoja kati yao kwani kipindi cha miaka saba iliyopita kuwa kwao karibu na boss wao Fernandes kuliwafanya wawajue watu wengi wanaofanya biashara biashara za madawa ya kulevya hasa waongoza vikundi (kingpin).


Feca, Mr. Fanuel na waliongozana nao kuja Mexico walitoka uwanja wa ndege na moja kwa moja wakaelekea katikati ya jiji kwa ajili ya kumalizana kisheria mambo yaliyo katika makubaliano yao na kote walikopita kulikuwa hakuna pingamizi kwakuwa nyaraka zote zilizohitajika zilikuwepo.


Mpaka inafika saa tisa alasiri wanasheria wa serikali waliopo ofisi inayohusika na usajili wa viwanda vinavyomilikiwa na watu binafsi wakishirikiana na wanasheria wa pande zote mbili walifika makubaliano ya kisheria kiwanda cha Miguel La Plancha Jalisco Industries kukabidhiwa kwa mmiliki mpya Mr. Fernandes Carlos Codrado kutoka kwa mmiliki aliyeamua kwa hiyari kumuuzia bwana mkubwa huyu kwa kiasi ambacho serikali iliambiwa Mr. Fernandes amemlipa Mr. Fanuel, kitu ambacho hakikuwa kweli.


Walipigiwa hesabu za kodi ambayo serikali ilihitaji katika mauziano yao na hapo ilibidi Mr. Fernandez alipie gharama za kodi hii iliyoingia kwenye mamlaka ya mapato ya nchi.


Hawakuishia hapo Mr. Fanuel alimkabidhi Feca hati ya kasri lake lililopo huko huko jimbo la Jalisco pia nyaraka za gari mbili aina ya Chevrolet Camaro, ndipo wakaelekea kando ya jiji la Mexico eneo lenye hifadhi ya jiji linalojulikana kwa jina Chapultepec huko Mr. Fanuel akaikuta familia kwenye njia ya kuingilia kwenye hifadhi wakiwa kwenye vivuli vya miti mikubwa wanamsubiri.


Muda huo wote kwenye pilika pilika zote mwanamitindo na mcheza sinema maarufu ndani ya Mexico mwanadada Gabriela Lopez walikuwa naye mwisho walipofika kukutana na Madam Felister ndipo Feca akamuachia aungane na rafiki yake na hii ilikuwa kwa sababu walizoziita za kujihami maana mwanamke kama yule kumuamini ilikuwa ni kuji risk lazima kwa uwoga alionao kama wangemuacha angetoa kutoa taarifa polisi na kuharibu mipango kabla haijakamilika.


Brigedia akiwa na watu waliokuwa wakiwalinda mke wa Fanuel na watoto wake walipowashusha kina Fanuel na yeye kuiona familia yake, Feca na wenzake wakaondoka kasi wakiwaacha pale kama usafiri wa wao kuondoka kurudi Villahermosa watajiju wenyewe.


“Pole sana mke wangu.. Poleni sana watoto wangu..” Akaongea Mr. Fanuel machozi yakiwa yanamtoka kisha wote kwa pamoja wakakumbatiana (watoto, mke na mume) na wote hakuna aliyekuwa halii wote walikuwa wakitoa sauti na machozi ya kilio kwa uchungu na furaha.


“Mume wangu nini hiki? Nani yule aliyetuteka?” Akahoji Madam Felister huku akiitizama gari waliyopanda Brigedia Feca na watu wake inavyopotea.


“Usijali mke wangu, wewe mtu mzima na muelewa hutakiwi kuhoji mambo kama haya kwa sisi watu wa biashara kama zetu.. Tushukuru Mungu tumeonana, mmerudi mikononi mwangu na kuahidi alitakuja kutokea jambo kama hili maishani mwetu” Akajibu Mr. Fanuel huku akiwaachia mikononi mwake watoto wake ambao licha ya kulia walikuwa wamemkumbuka sana baba yao hivyo hawakuwa wanataka kumuachia baba yao.


“Pinto mwanangu acha kulia, nishatuma meseji kwa madreva wetu wanakuja na gari kutuchukua tunaenda panda ndege kurudi nyumbani” Akaongea Mr. Fanuel kitambaa chake kikihama kwenye macho ya mtoto huyu kwenda kwa mwingine akiwafuta machozi watoto wake wapendwa.


“Utanieleza vizuri Fanuel.. Siwezi kukubali ujinga huu uliotokea ujirudie tena.. Nimepoteza muda, nimeishi kwa woga mkubwa sana kwa siku tulizokuwa tunashikiriwa na wahuni hawa.. Muda wote wakitulinda na mabunduki yao pamoja na kutulaza sehemu mbaya kabisa ambayo sikuwai kuota wala kuwaza siku hata moja nitalala… Mshenzi yule kama wewe utamuachia ni wewe Fanuel! Mimi lazima alipie huu upuuzi aliotutendea na familia yangu na rafiki yangu wa karibu… Na wale si watu Z maana wangekuwa wao ningewajua na uwa tunalipa ushuru wao vizuri kwa Z, huyu mpuuzi yeye nani?” Kwa hasira akaongea Madam Felister kifua chake kikipanda na kushuka kwa hasira kali.


“Mke wangu unasababisha watoto nao walie… Cha muhimu mmeonekana.. Mengine naomba tukaongelee Villahermosa si hapa, tafadhali na kuomba vuta subira..” Fanuel akaendeelea kujaribu kumtuliza mke wake aliyekuwa amefura kwa hasira na hiki kisirani alikuwa anacho toka aliporudiwa na fahamu aliyochomwa wakati anatekwa uwanja wa gofu uliopo kwenye kasri lao huko Villahermosa, Tabasco.


“Ndiyo nishasema Fanuel.. Siku mbili natoa siku mbili tu washenzi waliotuteka mimi na familia yangu wanapelekwa ngome ya chini kisha wanachinjwa mbele yangu.. nimewahesabu wapo kama kumi na tano bila kujali chochote nataka oda nayotoa itimizwe lasivyo nakodisha kikundi cha kufanya kazi hiyo.. Wanangu hawakustahili mateso ya kulazwa kwenye boma la hosptali chakavu katika vigodoro vidogo visivyo na afya ya usafi.. Fanuel usinitanie katika hili mshenzi yule lazima alipe hili lasivyo utanitambua.. Ni bora angeniteka mimi peke yangu kuliko na watoto wasio na hatia..! Aliendelea kufoka Madam Felister, nywele zikionyesha alivyo zimechanguka changuka si katika mpangilio wake anaokuwa nao siku zote.


“Madam! Basi tulia.. Hapa tulipo hapafai kuzungumza maswahibu yaliyotukuta.. Sote hatujaridhika na kilichotokea, tumelipa pesa nyingi sana, tumetoa mali kumpa mtu yule hili akuachie hivyo hatuwezi muacha kijinga kwa yote aliyofanya na pia kuchukua kilaini kila alichotaka..” Akaongea mhasibu wao wa kampuni na familia Mr. Pedro Iker Pullieta.


Dakika kumi mbele magari mawili yote yakiwa aina ya Cherokee yalifika pale na wao hawakusubiri wote wakaingia ndani ya gari na safari ya kurudi katikati ya jiji la Mexico.


Njia nzima katika gari walilopanda Mr. Fanuel, mke na watoto, sauti ya mwanamama msomi na mrembo Felister ilikuwa ikisikika na kudhidi kuusukuma moyo wa mume wake kwa yale aliyokuwa akilalamika walivyokuwa mateka, Mr. Fanuel hakuwa ana mpango wa kulipiza kwa haraka kile anachoona upande mwingine ni haki yeye kumpa Feca alichostahili lakini upande mwingine kwa anavyosikia malalamiko toka kinywa cha mwanamke tena mke wake kikilalamika na machozi yakihanikiza aliamua kisasi kikapangwe kifanyike vipi punde tu wakifika Villahermosa na kukutana na Mendoza Potential Distributio (MPD).


‘Lazima nilipize kisasi, mke wangu amechukia sana… Nitawapa taarifa hii viongozi wa Los Zetas niwaombe msaada wasiruhusu mbwa huyu atanue kwa pesa yangu niliyotumia kuiweka kwenye nafasi hii iliyopo kwa akili nyingi’ Akawaza Mr. Fanuel huku gari alilomo na familia yake likiwa limeshika kasi barabarani.


Mwisho wa sehemu ya kumi na tisa (19)


Hatimaye Brigedia Fernandes Carlos Codrado alipata alichotaka toka kwa bwana mkubwa bonge la mtu Fanuel Miguel Mendoza.


Mke wa Fanuel! Madam Felister baada ya kuwa ameshaonana na mume wake kutoka walikokuwa wakishikiliwa mateka amaeongea maneo ya kumlazimisha mume wake alipe kisasi kwa Fernandes.


Je nini kitafuta kati ya mahasimu hawa wawili?



“Madam! Basi tulia.. Hapa tulipo hapafai kuzungumza maswahibu yaliyotukuta.. Sote hatujaridhika na kilichotokea, tumelipa pesa nyingi sana, tumetoa mali kumpa mtu yule hili akuachie hivyo hatuwezi muacha kijinga kwa yote aliyofanya na pia kuchukua kilaini kila alichotaka..” Akaongea mhasibu wao wa kampuni na familia Mr. Pedro Iker Pullieta.


Dakika kumi mbele magari mawili yote yakiwa aina ya Cherokee yalifika pale na wao hawakusubiri wote wakaingia ndani ya gari na safari ya kurudi katikati ya jiji la Mexico.


Njia nzima katika gari walilopanda Mr. Fanuel, mke na watoto, sauti ya mwanamama msomi na mrembo Felister ilikuwa ikisikika na kudhidi kuusukuma moyo wa mume wake kwa yale aliyokuwa akilalamika walivyokuwa mateka, Mr. Fanuel hakuwa ana mpango wa kulipiza kwa haraka kile anachoona upande mwingine ni haki yeye kumpa Feca alichostahili lakini upande mwingine kwa anavyosikia malalamiko toka kinywa cha mwanamke tena mke wake kikilalamika na machozi yakihanikiza aliamua kisasi kikapangwe kifanyike vipi punde tu wakifika Villahermosa na kukutana na Mendoza Potential Distributio (MPD).


‘Lazima nilipize kisasi, mke wangu amechukia sana… Nitawapa taarifa hii viongozi wa Los Zetas niwaombe msaada wasiruhusu mbwa huyu atanue kwa pesa yangu niliyotumia kuiweka kwenye nafasi hii iliyopo kwa akili nyingi’ Akawaza Mr. Fanuel huku gari alilomo na familia yake likiwa limeshika kasi barabarani.


ENDELEA NA DODO..!


MIEZI MICHACHE MBELE-

PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

Soledad De Maciel eneo lililopo nje ya manispaa ya mji wa Petatlan mpakani kabisa na manispaa ya Acapulco upande wa kaskazini na huku kusini kukiwa na manispaa ya Ziuhatanejo zote hizi ni miongoni mwa manispaa zinazounda jimbo la Guerrero. Eneo hili linaloendana na hali yake ya kuwa mpakani kutokana na shughuli za wakazi wa hapa kuwa wengi ni wakulima wadogo wadogo na wavuvi wadogo wadogo.


Eneo la hekta ishirini na tano lilipata mnunuzi kutoka kwa mmoja wa wamiliki wake akimuuzia tajiri mpya kabisa katika eneo hili la Guerrero, tajiri aliyeupata utajiri kwa mbinu ya kupigania chake kilichopotea.


Eneo hili ambalo kama unaweza kujenga viwanja vya kisasa vya mpira wa miguu basi unaweza ukajenga viwanja vipatavyo kumi na bado ‘square meter’ zikabaki. Bwana mkubwa huyu aliamua ndipo patakuwa mahali ambapo patamfanya kuheshimika na kila ‘Kingpin’ (mabosi wa magenge ya mihadarati) na hata serikali watampa heshima yake.


Muda wa miezi mitano mbele eneo hili lilibadilika na kuwa eneo ambalo licha ya kuzungushwa ukuta mkubwa na mrefu kwa ukubwa wa eneo lenyewe lilivyo kama ungepita kuutizama ukuta huu kwa kipande cha juu cha ghorofa kinachoonekana kikiwa na paa ya bati za kisasa nyekundu yenye weusi usingesita kugundua kwa haraka eneo hili kwa ndani kuna kasri la kisasa sana.


Mjengo ulioanzia chini ya ardhi kukijengwa ngome ya kisasa kubwa iliyokwenda mita mia moja chini na upana wa chini kwa chini huko mita mia nne na hamsini, kukiwa na vyumba vya kisasa vya kulala vipatavyo kama mia tatu tena vikiwa vya kisasa vikienea huduma zote muhimu , kumbi za disko na hata maeneo ya starehe zingine. Kifupi bwana mkubwa alijenga eneo la starehe la chini kwa chini akitumia wakandarasi wawili aliowatoa Canada na hata vibarua walioifanya kazi ya ujenzi usiku na mchana nao walitoka Canada huko huko hakutaka watakaojenga wawe watu wanaofahamika katika nchi ya Mexico.


Brigedia Fernandes ilikuwa kama ndoto zake zimeanza kuonyesha ule mwangaza aliokuwa akiuhitaji kipindi jela, alihakikisha kiwanda cha chuma kilichopo Jalisco anakiwekea wasimamizi wazuri wa kukisimamia ambao menejimenti kuu aliwaweka wasomi aliowatoa nchini Canada ambao kwa muda mfupi walisababisha kiwanda kipate sifa maradufu na hata kuleta ushindani mkubwa katika soko la bidhaa za vyuma jimboni Jalisco na majimbo ya jirani na Jalisco akikiita kwa jina la ‘Jalisco La Plancha Furantur Industria’ kwa kiingereza unaweza kuita ‘Jalisco Iron Steal Industry’.


Akiwa anazijua mbinu nyingi za michezo ya hatari aliweza kupanga safu bora ya ulinzi wake huku akiwa hajulikani anaishi wapi rasmi ikiwa hadi kasri la Jalsco alilopewa kisheria na Mr. Fanuel mpaka kuwa mali yake, Feca mjanja mjanja aliweka wafanyakazi wa kulihudumia kasri hili liwe katika hali ya usafi muda wote huku yeye akiwa amefika mara moja siku aliyowaleta wafanyakazi wa usafi.


Mpango wake ilikuwa ni kutojulikana wapi hasa anaishi lakini kuisha kwa ujenzi wa jengo la Soledad De Maciel kulimfanya ayapinge mawazo yake, apinge alichoamua. Aliamua makao makuu ya genge atakalounda yawe hapa kwenye majengo ya chini ardhi, pia akaamua majengo ya juu ndipo ataishi yeye akiwa ameimarisha ulinzi wake licha ya hivyo aliamua familia yake haitafika hapa alinunua jumba kubwa lenye hadhi ya juu huko jimbo la Puebla ambalo limepakana na jimbo la Guerrero, familia yake akaitoa Corolado na kuiamishia hapa.


***** ***** *****


KUUNDWA KWA RED JAGUAR-THE MONSTER GANG

TETAPLAN, GUERRERO-MEXICO

Sherehe za wana kikundi walioshirikiana bega kwa bega kuhakikisha Brigedia Fernandes Carlos Codrado anarudisha kile alichokuwa nacho kabla hajaenda jela zilifanyika ndani ya kasri lililopewa jina siku hiyo hiyo kuwa kasri la ‘Secreto Potentia La Feca Palacio’, (Nguvu ya siri kasri la Feca) sherehe zilifanyika watu wanaohusika na kundi lililokuwa la Mr. Guti peke yake wakichanganywa na sita waliokuwa wafungwa wa gereza la Matomoros,Tamaulipas wengine waliohudhuria hii sherehe walikuwa ni wanawake wanaojihuza waliochukulia toka madanguro mbalimbali ya katika majimbo yaliyo jirani na jimbo la Guerrero.


Siku mbili mbele ndipo Brigedia Fernandes ‘Feca’ alikubaliana na Mr.Villa Nandez Guti kuwa kiitishwe kikao kwa ajili ya kuunda umoja utakaosababisha wao watoke mahala walipo kwenda sehemu nyingine kibiashara ya mihadarati, huku wazo kuu la Fernandes kupambana mpaka kuumaliza utawala wa genge la Los Zetas genge hatari na tishio sana nchini Mexico na majirani zao au ikibidi waingie mkataba wa amani utakaogawa mipaka ya kibiashara lasivyo vita ya tatu ya magenge ipigwe.


Ndani ya ukumbi wenye upana na urefu wa kama viwanja viwili vya mchezo wa basketball kulikuwa na mabenchi ya mbao lakini juu yaliyotengenezwa vizuri kwa kuwekewa sponji na kava la ngozi nyekundu, mabenchi yakiwa yamepangwa kama ukumbi wa sinema unavyokuwa unapangwa viti vyake kwa wateja wanaofika kuangalia sinema, mbele yao ndipo kulikuwa na meza kuu ikiwa na watu watano wakiongozwa na watu wawili waliokaa viti vya katikati yao.


“Habari zenu wote kwa ujumla.. !” Kwa niaba ya walio meza kuu Mr. Guti alitoa salamu.


“Salama salimini kabisa..!” Karibu wote walio katika mabenchi walijibu salamu ya Mr. Guti huku wakiwa na furaha na karibu kila mmoja alikuwa na chupa ya mzinga wa kinywaji anachopenda kunywa vyote vikiwa ni pombe kali toka nchi za nje ya Mexico na zingine ndani ya nchi.


“Naamini sote tuna furaha kubwa siku ya leo hasa kwa jana tulivyofanya sherehe ya kupongezana baada ya kazi nzito tulizozifanya tukishirikiana bega kwa bega bila kuangushana katika yale kila mmoja aliyotakiwa kuyafanya”Akaendelea Mr. Guti, akisimama kuongea baada ya koo lake kukauka hivyo akapiga funda mbili kubwa za kinywaji anachokunywa akipiga mtindo tarumbeta.


“Mambo mengi tuliyaongea jana wakati wa sherehe sote tukimpongeza kiongozi Brigedia Feca.. Nitapenda wote kuanzia sasa tutumie jina la Brigedia ‘Feca’ tu kwakuwa amependekeza aitwe hivyo na asingependa sote kumuita jina lake lililo hasa midomoni mwetu jina la Fernandes… Siwezi kurudia pongezi zile za jana tulizofanya juu huko kwakuwa kila mmoja alipata nafasi ya hata kuongea binafsi yake juu ya upendo aliotuonyesha Brigedia ‘Feca’ kwa kipindi chote tulichokuwa naye akituelekeza katika kazi zetu na kutuongezea ujuzi wa kazi.. Feca na wenzake kuanzia Koplo Savatel Santos hadi Stafu Sajenti Morientes Gudrado wamefanya tuone vile unavyoweza kutumia nguvu vilevile unaweza tumia ushawishi wa mipango iliyopangwa kifundi kukamilisha jambo lako unalotaka liwe.. Tumeitana hapa kama jana tulivyoahidi mimi na Feca kuwa leo tutakuwa na kikao kitachotuwezesha kujua muundo wetu utakuwaje katika ushirika wetu” Akanyamaza Guti na kujifuta mdomo kwa kiganja chake cha kushoto kisha akatupa macho huku na huko halafu akaendelea.


“Mimi Guti nilikuwa na watu walio chini yangu wapatao thelathini na tano, ishirini wakihusika na uuzaji wa mizigo huku kumi na tano wakiwa ndiyo walinzi wanaolinda jumba langu mbele kwangu na leo hapa ishirini na tano mpo huku wale wengine kumi wakibaki kwangu kulinda mambo yasije yakaharibika kama ujuavyo biashara ya utekaji wa familia baina ya magenge imekuwa kubwa sana hapa Mexico kwa sasa, ila kutokuwepo kwa watu wale si kama hawasikii haya tunayoongea hapa la hashaaah! Ni kama na wao wapo hapa mkutanoni sababu asubuhi nilivyoenda kwangu niliwapatia kila mmoja vifaa ambavyo vimeunganishwa na mfumo wa ulinzi alioufunga hapa Brigedia Feca hivyo na wao tupo nao bega kwa bega na kile tutakachoamua tutaamua na wao wakisikia na kama kuna mtu ataona hajaridhika iwe huko au hapa basi atanipigia simu kueleza maoni aliyonayo katika kuhakikisha genge letu linakuwa genge bora lenye watu wajuzi, wajasiri na wenye mafunzo yaliyo sawa sawa haswa!” Mr. Guti alinyamaza kuongea na kuwaangalia wote walio katika ukumbi kwa zamu zamu akianza wanaoiangalia meza kuu kisha akamalizia walio kwenye meza kuu kwa muda mfupi tu macho yalitizama kila sura ya aliye pale.


“Niingie moja kwa moja kwa dhumuni la kikao chetu hiki cha kwanza ambacho leo wasemaji wakuu tutakuwa mimi na Brigedia Feca ila na nyinyi nyote hamtakuwa nyuma tutapokea na kusikiliza maoni yenu bila kubagua lolote na kama kutakuwa kuna mantiki basi hatutasita kuingiza katika kile tulicho kwisha kiandaa au kuahidi kuwa tutaingiza katika siku za mbele kwa maslahi ya genge lote… Naomba katika jambo la kwanza la muhimu ambalo ningependa kila mmoja asikie na kujua ni kwamba… Mimi Villa Nandez Guti kwa pamoja na Brigedia Feca tumeamua kuunganisha umoja wetu katika biashara ya mihadarati lakini kwakuwa mtaji wangu haukufika katika kiasi alichonacho mheshimiwa Feca hivyo tumegawa asilimia za hisa kutokana ana kile tulichonacho… Kimisingi kile alichonacho Feca na kile nilichonacho mimi tumekiweka katika thamani ya fedha na kuwa ni mtaji kisha tukaangalia mali na uwezo wa kuajiri rasilimali watu wenye ujuzi na nguvu pamoja na wale wasio na nguvu wala ujuzi ila wana muelekeo wa kuwa vile tutakavyotaka.. Katika haya ya kwanza naamini kila yule ambaye alikuwa ameajiriwa na mimi anaweza kupatwa na mshtuko kwa kutojua je itakuwaje?!... Nachotaka kusema wale wote waliokuwa waajiriwa wa Guti wataingia katika mfumo ambao tulijadili na mwenzangu hapa na kuona umuhimu wa wao kupata mgawo wa hisa hili kila mmoja afaidike na faida ya kuwa wamoja licha ya kuwa sote tutakuwa tukilipwa mishahara itakayopangwa kisawa bila kubagua kutokana na nafasi ya mtu huku ufanyaji kazi wa bidii wa kila mmoja ukisababisha kupanda mshahara na marupu rupu huku hisa zikifanyiwa gawio kwa kila mwanahisa kila itakapofika tarehe kama ya leo na mwezi kama wa leo kila mwaka.. Hivyo kila mmoja atasoma karatasi itakayopita kwa kila mmoja ikiwa ni sheria za genge letu, genge letu litajulikana kwa jina la ‘RED JAGUAR’ a.k.a ‘The Monster Gang’” Hapa alisimama akajilamba papi (lips) zake kwa ulimi.


Wakati amenyamaza Mr. Guti kutoka katika meza kuu alisimama Ivan Alberto ‘alto’ akiwa na makaratasi mikononi mwake akatoka pale na kuanza kugawa kwa watu wote walio kwenye mabenchi.


“Nawapa dakika kumi kila mmoja apitie kwa uzuri kila kilichoandikwa katika karatasi mbili hizo na kama umekubaliana mwisho kabisa kuna sehemu utajaza jina na kisha kutia sahihi na ndiyo utakuwa mkataba wetu ‘Red Jaguar…. Feca na mimi tumeamua kitu ambacho pengine mkikisikia masikioni mwenu hamataamini lakini itabidi muamini sababu palipo na makomando hapashindwi kitu na mimi nashawishika kusema kuwa tunakwenda teka biashara hii ya ulanguzi wa madawa ya kulevya hapa Mexico na nchi jirani tunaenda ondoa ama kupunguza nguvu na utawala wa Los Zetas sababu genge lao lilianzishwa na wanajeshi na letu pia linakwenda kuasisiwa na mwanajeshi komando na fundi zaidi yao’”Akaongea tena Mr. Guti kisha akanyakua karanga kadhaa zilizokaangwa kwa mchanganyiko na mayai na kuongezewa na vitu vingine pendezwa mpaka kuzifanya ziwe karanga zenye ladha tamu ya kuvutia (mapishi ladha ya kimexico).


Dakika kumi za kila mmoja kupitia zilifanya ukumbi kuwa na ukimya wa maneno yakisikika makaratasi yanayohamishwa kurasa kwenda kurasa nyingine na baada ya utulivu huo ikafika muda kila mmoja akawa anaandika jina lake na kutia sahini hii ilimaanisha muundo, sheria na kanuni zilizoandikwa mule hakuna zilizo na makwazo kwa kila mmoja.


‘Alto Genius’ alitoka tena meza kuu kisha kupita kwa kila mtu akizikusanya tena nyaraka zile huku minong’ono ikiendelea baina yao.


“Ahsanteni sana kwa uungwana mliouonyesha hakuna aliyeuona huu mkataba huu wa kazi na mashirikiano kuwa una makwinyokwinyo kwake… Naamini hata wale walio kwangu muda huu wakisimamia ulinzi watasaini na mara moja tutaanza kazi ambayo iko mbele yetu… Napenda nimkaribishe bwana mkubwa Brigedia Fernandes kwa maelezo zaidi” Aliongea Mr. Guti huku akipokea makaratasi nyaraka toka mikononi mwa Ivan ‘alto genius’.


Kabla Brigedia hajaongea chochote kwanza yeye alitia sahihi kwenye kila nyaraka ya mkataba na kisha ya hapo akagonga muhuri juu ya sahihi na hii ikimaanisha mkataba umekubalika kwa pande zote mbili.


“Napenda nirudie kusema neno la kiungwana, neno la shukrani, kuwashukuru nyinyi nyote kwa kukubali kuunganisha nguvu zetu na kuunda umoja wetu katika kazi… Siku zote nilizokuwa jeshini nilikuwa naamini jambo ambalo na kila mwanajeshi anaamini ya kuwa umoja ndiyo kila kitu katika jambo lolote… Pale Uingereza kuna msemo maarufu wa timu moja maarufu katika soka la Uingereza na Ulaya nzima kwa ujumla, msemo wao majogoo wale uwa wanasema ‘You will never walk alone’ na jeshini msemo huu tunautumia sana katika hali ya kuhamasishana… Sisi sasa ni Red Jaguar, kwa kuanzia tumekubaliana sisi tulioanza katika kundi hili ndiyo tutakuwa viongozi wa kundi, yaani hadi nyinyi ambao hampo hapa meza kuu pia ni viongozi sababu sote tutakuwa na watu tutakaowaongoza… Kwanini?” Akaanza kuongea kirefu kidogo Brigedia Feca kisha akauliza swali ambalo kiukweli ilitakiwa yeye mwenyewe ndiyo ajibu swali hilo hivyo wote waliokuwa wakimsikiliza na kumuangalia kuna walioangaliana tu na kuna wengine walibaki wakimuangalia Feca tu ishara ya kuwa aendelee aache pozi zake.


“Kwa sababu! Sisi kila mmoja wetu atatakiwa kutafuta watu wawili au watatu watakaokuwa chini yetu wakifuata maelekezo yetu kikazi bila kukosea… Kuna jambo ambalo kila mmoja anatakiwa kujua ni kuwa nimenunua eneo katika nchi ya Guatemala, eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na mmoja wa wakuu wa Sinaloa Cartel ambao kwa sasa wamesambaratishwa wote na genge linalojifanya hii Mexico yote iko chini yake yaani mtu hata akitaka kutengeneza kikundi cha watu watano tena kiwe hata cha kutumia viwembe kupora simu huko mitaani basi wao wanataka wakijue na wachukue ushuru… Sasa huko nilikonunua kunaenda kumaliza jeuri ya Los Zetas ni eneo ambalo litafaa sana kwa mafunzo ya watu ambao tutakwenda kuwatafuta kutoka kwenye magenge mengine hata kwa kuwanunua ama kuwashawishi kwa vyovyote vile kujiunga nasi Red Jaguar, watu hawa watakaojiunga wao tutawasainisha mkataba wa kuwalipa mishahara punde wanapomaliza mafunzo maalumu watakayoyapata huko San Marcos… Eneo lipo katikati ya milima mitatu mikubwa ya Tajumulco, ilikuwa kambi nzuri aliyokuwa akiitumia kwa mafunzo ya watu wa genge lake kabla ya Los Zetas hawajawasambaratisha na kuua karibu wafuasi wake wote ila uzuri ni kuwa ‘Z’ hawakuchukua eneo lile hawakuvutiwa nalo ila mimi nilipoliona mara moja nililipitisha majengo yake yapo katika hali isiyo nzuri kidogo na ukarabati ushaanza kuanzia majengo ya juu mpaka ya chini ya ardhi, kitakuwa kituo kikuu cha mafunzo na kambi kuu ya kuhifadhi mizigo tutakayokuwa tunapora kwa magenge yatakayotaka kutofuata masharti yetu na kufuata ya LZ… Ningependa nizungumzie hisa… Hisa katika Red Jaguar itakuwa mimi niliyekuwa na hisa sabini nimetoa hisa kumi na tano hivyo hisa ishirini na tano atabaki nazo Mr. Guti! Yeye alikuwa na hisa thelathini, ametoa tano ukijumlisha na zangu kumi na tano unapata hisa ishirini ambazo kumi wamechukua hawa walio meza kuu na kumi na tano mnachukua nyinyi wa kwenye benchi, hisa hizi ndugu zangu mnaweza kuona kama ndogo lakini mtaona faida wakati tutakapokuwa tunagawana faida za hisa zetu kwa kila mmoja… Kazi iliyopo sasa kila mmoja ataondoka hapa Secreto Potentio La Feca Palace akiwa na kiasi ambacho atapewa kikiwa kwenye bahasha, kiasi icho ni kikubwa kufanya ushawishi kwa mtu ambaye utamuona anafaa kujiunga katika Red Jaguar kwa malipo ya kama muajiriwa na kila ukimpata mtu utatakiwa uwasiliane na Koplo Zuantejo au Koplo Savatel Santos ambao watakupa maelekezo fulani ambayo yatatusaidia kufanikisha mtu huyo akaelekea moja kwa moja kwenye kituo chetu cha usahili sababu hatutataka mtu ambaye muathirika wa mihadarati ni bora akawa mlevi wa kawaida au mvutaji wa bangi tu maana shughuli zetu kama zitakuwa na watu hao basi wataharibu maana kabisa ya kazi… Shughuli yetu itakuwa kubwa sana tunataka Red Jaguar ilete mabadiliko makubwa miongoni mwa magenge ya mihadarati hapa Mexico mpaka nchi jirani, mafunzo tutakayotoa yatakuwa ya kijeshi hivyo lazima heshima tunayohihitaji itakuja na si Mexico tu mpaka nchi jirani” Maelezo marefu ya bwana mkubwa Brigedia Feca yalifanya kila mmoja aliye pale kuwa makini kusikiliza kwa hisia za juu sana huku baadhi wakivuta taswira ya kesho zao zitakavyokuwa.


“Samahani boss! Nina swali dogo?” Akaomba dreva maarufu katika timu iliyokuwa chini ya Mr. Guti maarufu kama dreva Rude Boy.


“Usiogope uliza tu!!” Brigedia Feca akatoa ruhusa iliyoombwa na Rude Boy.


“Umesema tukatafute watu tutakao waingiza ndani ya genge, je tunaweza watoa watu hao toka kwenye magenge mengine?”


“Hilo halina shida… Ila ni vizuri pia mkaangalia wasije wakawa wale ambao wametumwa na watu wa magenge mengine au mkatuingizia watu wa DTO sababu viongozi vya kupambana na magenge ya wauza unga wamekuwa na mbinu nyingi sana na wao pia vile sisi tunavyobadilika na DTO nao wanabadilika kwa kasi inayoendana nasi, hivyo sote tuwe makini na ndiyo maana kutakuwa na usahili utakaofanyika ndani ya Mexico mahala tutakapopanga kabla ya mtu huyo kupelekwa kambi ya Tajumulco, San Marcos- Guatemala na naomba kwenu Koplo Savatel na Koplo Zuantejo mkawe makini sana wakati wa usahili tusije ajiri mamluki… Nakaribisha swali lingine hili twende katika ratiba nyingine kisha tufunge kikao chetu” Alijibu kwa kirefu Brigedia Feca na pia kutoa ruksa liulizwe swali lingine.


“Boss mimi nina ombi nataka niliwakilishwe na kama likiwa sawa basi niko tayari kuchukua dhamana hiyo” Aliongea Alejandro Lopez a.k.a la culebra nyoka ndani ya hili kundi bingwa wa kung’ata akiwa na historia kali ya kuua kwa kukata makoromeo kwa meno yake.


“Leta ombi lako Cobra..!!!” Brigedia akatoa ruhusa haraka.


“Katika genge la ‘la hormiga’ lililopo Veracruz kuna mtoto wa mjomba wangu mule na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wenzake hivyo kama utanipa ruhusa niko tayari kuongea naye akatushawishia kuwapata wenzake wakajiunga nasi na itakuwa vizuri kutokana na uzoefu wao wa shughuli za unyama wa magenge kwa magenge na hata DTO, ni haya tu boss!” La Culebra akatoa wazo lake ambalo kwa haraka lilimshawishi Feca akatikisa kichwa kukubali na pia Mr. Guti akapiga makofi kukubali.


“Mimi kama Rais wa Red Jaguar sina pingamizi juu ya hilo na kwa upigaji makofi aliyopiga Guti makamu wa Rais wazo lako limepita… Au mlio meza kuu kuna mwenye wazo la tofauti juu ya wazo la Cobra?” Akaongea Feca na kuuliza swali kwa walio meza kuu.


“Upande wangu sina pingamizi juu ya vijana wa kihuni wenye sifa zao sifika toka genge la hatari sana kama ‘la hormiga’, naunga mkono na naomba mara moja tukitoka hapa Alejandro aelekee huko Veracruz akiwa na wenzake wawili na wakifika watatushirikisha maongezi yao maana kwa nijuavyo ‘la hormiga’ wako kama elfu nne ni genge kubwa sana na ndiyo maana tishio sana tena kuliko hawa mabwana wa Los Z wanaotishia watu wasiokuwa shirika nao wanawaua, sasa tukiwapata siafu naamini Los Zetas hawatatugusa kwa chochote kwa kuhofia walivyokuwa wanashindwa kuwaingilia ‘la hormiga’ na pia kwa taairfa nilizonazo vijana hawa hawana bosi maalumu wao wanafanya kazi kwa umoja kila mmoja akiwa ana amri na maelekezo kwa mwenzie na uzuri wanaheshimiana sana! Ni haya niliyonayo..” Akaongea katili Wolfs ‘Hitler’ mtu anayekubalika sana kwa Guti na Feca kwa ukatili wake akifuatiwa na mshenzi mwingine Bezela Muricho ‘Animal’.


Mwisho wa sehemu ya ishirini (22)


Tayari tumefika kuundwa kwa genge la hatari linalotisha nchini Mexico, genge la Red Jaguar ‘The Monster Gang’.


Hatua hizi zinatusogeza kuliko na JINO KWA JINO!.


Mambo mazuri na matamu yanadhidi kujongea, utamu kolea unaanza taratibu ukikolea taratibu na ladha ya embe dodo la kitanga lililopandwa ardhi yenye rutuba ya mkoa wa Morogoro.



ILIPOISHIA SEHEMU YA 22…!!

“Katika genge la ‘la hormiga’ lililopo Veracruz kuna mtoto wa mjomba wangu mule na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wenzake hivyo kama utanipa ruhusa niko tayari kuongea naye akatushawishia kuwapata wenzake wakajiunga nasi na itakuwa vizuri kutokana na uzoefu wao wa shughuli za unyama wa magenge kwa magenge na hata DTO, ni haya tu boss!” La Culebra akatoa wazo lake ambalo kwa haraka lilimshawishi Feca akatikisa kichwa kukubali na pia Mr. Guti akapiga makofi kukubali.


“Mimi kama Rais wa Red Jaguar sina pingamizi juu ya hilo na kwa upigaji makofi aliyopiga Guti makamu wa Rais wazo lako limepita… Au mlio meza kuu kuna mwenye wazo la tofauti juu ya wazo la Cobra?” Akaongea Feca na kuuliza swali kwa walio meza kuu.


“Upande wangu sina pingamizi juu ya vijana wa kihuni wenye sifa zao sifika toka genge la hatari sana kama ‘la hormiga’, naunga mkono na naomba mara moja tukitoka hapa Alejandro aelekee huko Veracruz akiwa na wenzake wawili na wakifika watatushirikisha maongezi yao maana kwa nijuavyo ‘la hormiga’ wako kama elfu nne ni genge kubwa sana na ndiyo maana tishio sana tena kuliko hawa mabwana wa Los Z wanaotishia watu wasiokuwa shirika nao wanawaua, sasa tukiwapata siafu naamini Los Zetas hawatatugusa kwa chochote kwa kuhofia walivyokuwa wanashindwa kuwaingilia ‘la hormiga’ na pia kwa taairfa nilizonazo vijana hawa hawana bosi maalumu wao wanafanya kazi kwa umoja kila mmoja akiwa ana amri na maelekezo kwa mwenzie na uzuri wanaheshimiana sana! Ni haya niliyonayo..” Akaongea katili Wolfs ‘Hitler’ mtu anayekubalika sana kwa Guti na Feca kwa ukatili wake akifuatiwa na mshenzi mwingine Bezela Muricho ‘Animal’.


ENDELEA NA DODO…!


KUUNDWA KWA RED JAGUAR

PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

“… Siwezi pinga jambo la ‘la hormiga’ kwakuwa nami pia natambua hakuna madogo wanaogopewa na magenge yote yaongozwayo na mabosi wakubwa ‘Kingpin’ hivyo sina pingamizi tukiwapata hata mia tano ni sawa tu, muhimu kuwashawishi kwa nguvu zote wajiunge nasi wao ni kete kubwa…!” Akaunga mkono hoja Koplo Savatel Santos.


Kwa muda wa dakika ishirini mbele kila aliyepata fursa ya kutoa maoni yake alipitisha wazo toka Alejandro ‘La Culebra’ la kutupa kete ya kushawishi vijana walio katika genge maarufu sana na linaloogopewa katika Mexico nzima miongoni mwa magenge hata yaliyo makubwa yanayoongozwa na matajiri wa unga (Kingpin), genge hili lisilo na uongozi rasmi wa mtu fulani lakini ni genge ambalo likitaka kitu lazima litimize iwe toka serikalini au kwenye genge lolote la shughuli za haramu lilikuwa ni genge ambalo linajiongoza katika njia ya ajabu na kufanya kazi kwa makubaliano huku wakigawana kutokana na kazi iliyofanyika, wakifanya kazi hata za kukodiwa kufanya jambo lolote linalohusiana na umafia iwe kisasi na mengineyo yanayoendana na uhalifu.


Genge linaloitwa ‘La hormiga’ kwa kiingereza unaweza kuwaita ‘The Ant’ huku kwa Kiswahili chetu unaweza kuwaita ‘siafu’ ni genge la hatari sana kwa miaka hiyo ilikuwa ukipita mitaa yao ya La Playa huko Veracruz ujiandae kwelikweli.


Wakati wakiendelea na maongezi huku wakisindikizwa kwa nyama choma za wanyama mbalimbali wanaopendwa na watu wa jamii ya Mexico, simu ya Brigedia Feca iliita alitizama kwenye kioo chake bilaa kuiinua ilipo mezani ambako aliiweka huku mikono yake akiigemeza kwenye yote miwili mezani pale.


Jina la mpigaji lilimfanya anyooshe mkono wake wa kulia kisha haraka akaruhusu kuipokea kwa kusugua kioo cha smartphones hii aina ya Huawei P8 Lite.


“..Gumendez..!!!” Akatoa salamu baada ya kupokea, simu ile ilikuwa imepigwa na Luteni Kanali Gumendez Cassilato toka kambi ya jeshi ya Base Aerea Militar No: 06 iliyoko Tuxtla Gutierrez jimbo la Chiapas.


“Brigedia! Habari yako?”

“Nzuri Luteni Kanali!.. Habari za Tuxtla?”

“Nzuri tu hakuna tatizo hapa… Ila habari zako zilishika kasi midomoni mwa wanajeshi wenzetu hasa kwa sisi viongozi na si kambi hii hadi kambi zingine umekuwa kichwa cha habari.”

“Naongelewa kwa mabaya yapi tena? Maana nimezoea kuongelewa kwa ubaya kila siku nilipokuwa huko jeshini na lita wa cost hili hao wasioliheshimu jina la Feca..”

“Kwa sasa kidogo wameanza kunyamaza ila wengi walikuwa wakikuhusisha na vifo vya kuuliwa kinyama kina Koplo Savatel na wenzake waliokuwa wanatumikia kifungo chao huko gereza la Matamoros na..!” Hakuweza kuendelea kueleza alichotaka kwani Feca aliingiza maneno ya haraka akihoji.


“Walikuwa wakisema nimewaua watu waliokuwa karibu nami?”

“Wanasema umefanya mpango waamishwe toka Acapulco kisha ukatuma watu wakawaue kikatili licha ya msaada wote waliokusaidia lakini umeona ni bora wakapotea kabisa duniani”

“Na wewe ambaye nilikugusia suala hili umewai kumwambia yoyote juu ya hili?”

“Hakuna ajuaye kama mimi na wewe tuliwai kuonana toka utoke gerezani.. Na wengi hawajui kwa sasa makazi yako wapi ingawa siku nne au tano zilizopita zililetwa habari umemilikishwa kiwanda cha chuma cha jimboni Jalisco na rafiki yako ambaye ni cartel maarufu sana anayekingiwa kifua na magavana wengi wa majimbo Mr. Fanuel Miguel Mendoza mmiliki wa kampuni ya Miguel La Plancha Compania Limited… Wengi wanasema ni malipo ya mizigo uliyokuwa ukimpatia wakati huko kikosi cha jeshi kilichokuwa kinafanya doria mpaka wa Guatemala na mpaka wa Marekani… Lakini hayo yote siyo yaliyonifanya mimi nikupigie simu… Napenda maendeleo yako na ndiyo maana nilikwambia siku tuliyokutana kuwa hakuna anayeweza kukufanya ukaishi kwa tabu.. Wewe ni mwanaume mwenye nguvu na akili.. Nilisema hivi kwa kuwa nakuamini sana Brigedia na najua upambanaji wako..”

“Nafurahi dua lako lilienda mahala sahihi na malipo yako yapo.. Nitatuma pesa kwenye akaunti yako weee utanipa namba ya akaunti tu kisha baada ya siku moja ukienda benki kuangalia salio lazima ukenue meno yako kwa furaha.. Niambie haswa kilicho katika dhumuni la kunipigia kama ulivyosema lipo lililokufanya unipigie”

“Ndiyo Feca!...Nimekupigia kutaka msaada wako kwa mwanadada aliyekusaidia kupata nyaraka zilizo ruhusu uhamisho wa watu wako toka gereza la Matamoros, Tamaulipas kwenda Acapulco, Guerrero mpaka wakakutwa na mauaji kona ya Jalisco.. Kitu ambacho hata mimi hukunielekeza kuwa wakishapewa huo uhamisho wataondoshwa duniani tena kinyama, ungeniambia hivyo pengine ningehoji kosa lao ni lipi kwako?...Nimesikitishwa sana kwakuwa mimi nimesh….!” Akasimamishwa kwa sauti ya kali yenye msisitizo kutoka kwa Feca.


“Gumendez! Unanijua vizuri nilivyo.. Nina mipango mingi sana mimi na sikutaka kukwambia lililopo lakini leo hii nataka ujue tu hapa nilipo Savatel yupo, Zuantejo yupo, Morientes yupo na wengineo wote wapo ile ilikuwa ni propaganda tu na usiulize sana tafadhali na hili liwe miongoni mwa siri zako kuu ulizonitunzia toka tuko pamoja jeshini, ipo siku utawaona wote hao… Endelea na habari unayotaka kunipa kuhusu mwanadada aliyetusaidia kupika mpango wa Matamoros!!”

“Eeeeh! Ama kweli sikuwezi.. Nilijua tu kuna jambo umefanya huwezi kuwaua kina Koplo Savatel tena kwa mauaji ya kutisha kama yale… Hapa sasa nina amani kwa asilimia zote kaka yangu… Mwanadada aliyekusaidia kupika nyaraka zile Koplo Mariana Funtes anakutafuta anahitaji msaada wako…”

“Msaada wangu? Kivipi? Mi nilishamalizana naye tena kwa malipo cash!!”

“.. Baada ya tukio lile, serikali ilitaka kujua ukweli juu ya wafungwa wale kuhamishwa toka Matamoros kwenda Acapulco ikawa kazi kweli kweli katika kutafuta nani alifanya uhuni wa kuiba sahihi ya Meja Sanz Fuerza pamoja na muhuri wake mpaka nyaraka zile zikatumika kumghilibu kamishina msaidizi wa magereza na yeye kutia sahini kuidhinisha kina Savatel waamishwe.. Hivyo uchunguzi ulipochachamaa haraka Mariana akashtuka kuwa anaweza kuingia hatiani baada ya kujulikana baadhi ya shahidi toka kwa mamesenja wa pande zote mbili kama ujuavyo barua zetu za mamlaka za usalama na ulinzi nchi hii uwa tunatumia mamesenja kiusalama kwa kuogopa utapeli wa kughushi nyaraka kwa kupitia mitandao au posta, Mariana akaamisha familia yake kwenda anapopajua kisha na yeye akaenda anapopajua yeye mwenyewe mpaka sasa hata mimi na wasiliana naye lakini sijui yuko wapi katika Mexico hii… Anahitaji kuonana na wewe haraka sana hivyo toka juzi alinipa kazi ya kupata namba unayotumia sasa ikabidi nianze kutafuta na nashukuru leo asubuhi Guti alinitumia baada ya kumbembeleza sana maana mimi nilikuwa nayo ya Guti kwakuwa ulinipigia kwa simu yake siku ile ulivyokuwa unanitafuta, hivyo sasa kama huko tayari nikutumie namba zake anazotumia kila anaponitafuta kisha mtaelekezana vizuri wenyewe..” Maelezo marefu yalitoka kwa Luteni Kanali Gumendez Cassilato akimalizia kwa kutoa pumzi ndefu.


“Mr. Guti alijuza kuwa unataka namba yangu na nikampa ruhusa akupatie…Nitumie namba zake.. Atanifaa sana kwenye shughuli zangu Koplo Mariana Funtes mjanja sana yule.. Mwambie asihofu nitamlinda na hakuna wa kumgusa katika nchi hii kwa sasa na kwa uwezo wangu… Ahsante sana kwa taarifa nzuri kwangu… Pia usisahau kunitumia namba ya akaunti yako ya benki pia” Akamalizia Feca na kwa pamoja wakakata simu zao baada ya kuagana.


***** ***** *****


VILLAHERMOSA, TABASCO-MEXICO

Avenida Pasco Usumancita mtaa lililopo kasri la kifahari la tajiri bonge la mtu Mr. Fanuel Miguel Mendoza katika bustani iliyopo kwenye uwa wa kasri walikuwa wamepumzika mume, mke na watoto wao wakicheza cheza kwa furaha ikiwa ni miezi sasa imepita toka watokewe na tatizo lililokuwa kwao kama jinamizi, tatizo la kutekwa.


“Miezi sasa imepita na tunakaribia kumaliza mwaka toka uniambie mnajipanga kulipa kisasi kwa yule mwanaharamu, mmefikia wapi?” Sauti nyororo toka kwenye kinywa cha Madam Felister ilihoji huku akipapasa kitambi cha mumewe kilichotuna na manyoya mengo tumbo lote kama manyoya ya ndezi.


Wote walikuwa wamekaa kwenye viti vya kulala pembeni ya swimming pool (bwawa la kuogelea) kubwa lililonakshiwa kwa malu malu za kung’aa kama dhahabu, bwawa ambalo lilikuwa likitumika kwa kuogelewa na wanafamilia hii tu hasa Mr. Fanuel mwenyewe na mkewe. Haikuruhusiwa kwa mtu mwingine kugusa maji ya bwawa hili labda kwa mfanya usafi anayelihudumia kwa usafi na si kuogelea.


Mavazi yao ya kuogelea kwa wote yakiwa na rangi ya kufanana kwa bukta ya Fanuel huku kivazi (swimming cost) ya bibie kikimuonyesha mwili mzima kikiziba maziwa na matako yake tu.


“Watu wangu wanaendelea kumuwinda yeye na hata kujua ilipo familia yake hili tufanye lipizo lakini kazi imekuwa ngumu tofauti na tulivyotarajia sababu mara ya kwanza nilidhani ataweka makazi kwenye kasri nililompatia la Jalisco lakini pale wapo wafanyakazi wanao lifanyia usafi kasri na pia walinzi.. Familia yake mara ya kwanza ilikuwa inaishi Columbia, Washington DC lakini kwa sasa familia haijulikani ilipo na yeye mwenyewe hajawai kanyaga kwenye kasri toka niweke mtego na pale ilikuwa rahisi kumfanyizia kwakuwa nyumba ya jirani na pale ni nyumba yetu niliinunua muda mfupi baada ya makabidhiano yetu kule Mexico City, hivyo kwenye ile nyumba niliyonunua nimewaweka vijana kazi yao muda wote kuangalia kwa umakini siku atakayofika kulala pale nasi tufanye kazi yetu” Akaongea Mr. Fanuel huku naye akipapasa mkono wa mwenza wake.


“MPD! MPD yako wako kwa kazi gani? Naomba uvunje uongozi wote wa MPD tuchague viongozi wapya, sababu wameshindwa kazi watu wako unaowaamini… Hivi Fanuel unajua nimeumia vipi kwa tukio lile?” Akaanza kufoka mwanamke kwa sauti ambayo alihakikisha anaidhibiti watoto wake walio mita kama ishirini wakicheza ndani ya bwawa la kuogelea.


“Ngumu sana Felister kuvunja uongozi wa MPD… Kazi unayotaka usifikiri ni ya kitoto au kazi kama kazi ya kukivamia kigenge cha kipuuzi kilichopora mzigo wetu, Feca ni mwamba na hivi tunavyoongea hapa nataka nikwambie nimepewa taarifa kuna mambo makubwa sana yanakuja kutoka kwake katika biashara ya unga… Jamaa ni hatari sana mke wangu naomba utilize hasira zako kama ulivyotuliza siku za hapa katikati, tushukuru naye ametulia haendelei na sisi ameridhika na alichopata.. Siku za mawanzo nilikuwa na hasira sana juu yake lakini kwa sasa sitaki tena nionyeshe uadui naye si mtu mzuri kabisa” Mr. Fanuel akaongea macho yake yaliyo ndani ya miwani ya rangi ya kijani inayongaa yalikuwa yakimuangalia mkewe ambaye naye pia alikuwa kavaa miwani inayofanana na aliyovaa mumewe.


“Kuna jambo nahisi lipo kati yako na Maria Rodgruez…. Na icho ndicho kinachokufanya ushindwe kuvunja uongozi anaouongoza huyu mwanamke mnayemuita Baby Beauty.. Tumetekwa chini yake, tumeteswa huko tulipokuwa tunashikiliwa sababu yake na hata pia kulipa kisasi cha jino kwa jino anashindwa kabisa mume wangu.. Hivi huoni kasoro zake? Ameshindwa kutulinda, ameshindwa kuongoza genge lake kutuokoa mpaka ukatoa pesa na mali zetu na hata sasa miezi mingi anaendesha kinachoitwa kisasi cha jino kwa jino lakini hakuna cha jino lililoanguka wala ufidhi uliovimba kila siku ngonjera tu ninapomuuliza kafikia wapi?, nafahamu anafanya kazi nzuri kwenye manunuzi na mauzo salama lakini huku amefeli… Nakupeni mwezi mmoja, mwezi mmoja narudia tena mwezi mmoja nipewe majibu ya kuridhisha aidha mtoto wa Feca ametekwa au mke wake kama si Feca mwenyewe ni hayo tu, mkishindwa nitafanya mwenyewe kazi hiyo, makundi ya kukodishwa yapo mengi msinizingue kabisa..” Alimalizia neno la mwisho ‘msinizingue’ akiwa kainuka toka alipo kwa mwendo wa kasi lakini wenye mbwembwe za kike alisogea zilipo ngazi kisha akaanza kuzipanda kuondoka eneo la swimming pool iliyotengenezwa kwa kuchimbwa ardhi kwenda chini mita kumi kisha eneo likapanuliwa kupandwa miti ya mikokoni (miti iliyo kama minazi inapokwenda juu huku makuti yake yakiwa pia kama minazi lakini si minazi) na katikati ndipo pakachimbwa bwawa hili kubwa la kuogelea la familia, pakipandwa na maua mazuri ya kunukia.


Mr.Fanuel alibaki kaganda mdomo kauachia asiamini yale aliyoyasikia toka kwenye kinywa cha mama watoto wake mpendwa Madam Felister, macho yake yaliduwaa kana kwamba ndiyo mara ya kwanza anaona mara ya kwanza maeneo ya nyuma ya mkewe.


***** ***** *****


PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

“Halloow!” Upande wa pili uliopigiwa simu ilisikika sauti ya kike.

“Koplo Mariana Funtes” Akaongea Brigedia Feca.

“Ni mimi!..Nani mwenzangu?”

“Feca… Brigedia!! Nimepewa taarifa unanitafuta mrembo”

“Fernandes? Ni kweli ni wewe?”

“Ndiyo Mariana.. Ni mimi, usiogope, sema huko wapi nitume mtu akufuate uje nilipo”

“Niko Guerrero, niko mahala nimejificha sitoki hata nje ya nyumba niliyopo… Nilikuja huku kujificha nkitaraji kukutana na wewe unisaidie kwakuwa kilichonikuta kimetokea kwenye pesa za mkononi mwako, tafadhali nahitaji msaada wako kaka yangu..!!”

“Oooh! Kumbe upo hapa hapa Guerrero.. Sawa kwa usalama zaidi wa sisi pia na wewe mwenyewe nitatuma mtu aje mahala ambapo nawe utajulishwa mukutane hapo kisha atakuchukua mpaka nilipo, usiwe na wasi siwezi kukutupa na hata haki zako za msingi zote huko serikalini nitahakikisha unazipata.. Vumilia mpaka saa mbili usiku nitakupigia kukujuza usogee wapi utakapokutana na watu watakaofika kukuchukua, endelea kujificha papo hapo”

“Ahsante sana Feca nitausubiri huo muda” Akakubali alichoelekezwa.


Brigedia Feca akakata simu na kumgeukia rafiki yake, makamu wake wa Rais Mr. Villa Nandez Guti na wote wakatabasamu kwakuwa Guti naye alikuwa akisikiliza anachoongea Feca na Mariana Caro Funtes, ikiwa hapo awali walikuwa wamemjadili na hata kufanya uchunguzi wao wa awali kujua mengi juu ya Koplo Mariana na wote kwa pamoja wakakubaliana katika genge lao la Red Jaguar watahitajika wanawake kadhaa wenye roho za kijeshi zenye ujasiri kama alivyo Mariana.


“Itakapofika saa mbili tutamtuma Ivan ‘alto’ akamchukue akiongozana na Wolfs…!” Akaanza kuongea Feca kisha akanyanyua glasi ya mvinyo mwekundu aina ya tequila akapiga funda tatu za kufuatana.


“Ni mwanamke mjanja anayeyajua magenge mengi sana yenye kuongozwa ma cartels wakubwa wakubwa hapa Mexico yote kwa ujumla hivyo katika operesheni tutakayoanza nayo baada ya kumalizika kwa mafunzo ya watu tutakaowapata huko Tajumulco Camp… Natambua atatuongezea wanawake wenzake walio na akili za kijasiri kama zake kama ulivyosema kuwa tutatakiwa tuwe na wanawake tutakaowatumia katika kuwatia kwenye mikono yetu maadui zetu kwa vishawishi vyao” Akaongea Mr. Guti kisha akavuta sigara kwa mbwembwe kama ilivyo kawaida yake.


“Sahihi kabisa, wanawake wazuri sana tena tukiwapata kwa wakati sahihi wakaanze mafunzo na wengine watakaingia kambini Tajumulco na ik…!” Alisimama kuongea simu yake iliita na mara moja akainyakua toka kwenye stuli ndogo ya kioo iliyo pembeni ya kiti alichokaa hapa kwenye baraza ya nyuma ya kasri jipya kabisa ambalo juzi tu walifanya sherehe ya kuzindua kasri hili lenye kambi chini ya ardhi na jana wakifanya mkutano wa kuanzishwa kwa genge jipya ndani ya Mexico ‘The Red Jaguar’.


“La Culebra anapiga… Natumaini ni habari njema kwetu maana nina hamu na habari za La hormiga kuliko chochote kwa sasa toka nipitie habari zao kwenye mitandao nimeshwishika sana juu yao” Akaongea Feca kisha akasugua kioo cha simu hili kupokea.


“Hallow! Cobra..” Akaongea haraka baada ya upande wa pili kuwa hewani.

“Boss… Mambo yameenda vizuri mdogo wangu Timotheo amekubaliana na ombi letu pia mpaka sasa tushapata vijana wa kazi walio katika mstari unaouhitaji mia tatu na ishirini ambao hawana miaka zaidi ya miwili katika la hormiga… Muda huu naokupigia simu nimetoka kwenye kikao nao ila ilitubidi tufanye kwa siri kwa sababu siku hizi kuna watu kama kumi hivi wanajifanya kama wao viongozi na uwa wakali sana wanapokuja watu waliotumwa na Cartel kutoka magenge mbalimbali kutaka vijana wa hapa”

“Eeeh! Kwahiyo walikuwa wananunuliwa kwenda kwenye magenge mengine?”

“Ndiyo mkuu hasa Los Zetas na Sinaloa kabla haijasambaratishwa lakini kwa siri sana.. Timotheo anasema yeye hakuwa anakubali kwenda sehemu zingine kwa sababu ya maslahi madogo waliyokuwa wakiambiwa wakijiunga watapata na mara nyingi tu ma cartel wa magenge kadhaa wamefika bei kumuhitaji maana mzuri sana kwenye mambo ya kipelelezi, amekubali kujiunga nasi kutokana na hitaji lake la siku nyingi kufanya kazi nami katika genge moja maana sisi ni pacha pia maslahi”

“Sasa tutawapata katika ile idadi tuliyohihitaji?”

“Inawezekana sababu kuna watu walienda kufanya kazi fulani kwa kukodiwa na mtu mmoja huko Nuevo Luredo kwenye ngome ya Los Zetas watu hao wako njiani wanarudi ndiyo tumaini letu wakifika tukiweza kuwashawishi tu basi na wao kila mmoja ataweza kushawishi watu wengi sababu wana ushawishi mkubwa sana pia wanaaminiana sana na Timotheo… Wanatarajia kufika hapa saa mbili usiku ni watu wa kazi haswa boss!”

“Basi jitahidi sana juu ya idadi… Tunataka mafunzo yetu yaanze na watu mia tano na zaidi hili tukianza kazi tuwe wengina kwa ujuzi wa mafunzo tutakayoyatoa naamini tutafanya Mexico yote itetemeke kwa muda mfupi..Mwambie Timo asiwe na wasiwasi malipo yake kwa ajili ya ushawishi yapo maradufu ya vile ulizompa kabla..”

“Usihofu boss kwa pamoja tunajitahidi kufanya kwa weledi mkubwa kama ulivyotutuma”

“Kazi njema na mafanikio tele”


Simu zikakatwa kwa pande zote kama waliweka makubaliano wakate kwa pamoja.


“Cobra anasema kuna nusu ya mafanikio huko mpaka sasa… Amenifurahisha sana kwa hata hayo nusu mafanikio waliyofikia” Akaongea huku akimkazia macho Mr. Guti.


“Naamini tutafanikiwa Feca… Kesho asubuhi Savatel atawafanyia usahili watu zaidi ya mia tano na hili itabidi tuliangalie vizuri kwa kumpunguzia walau watu fulani kwa idadi hiyo ya watu mia tano kama ujuavyo siafu ni siafu tu lazima watakuwa na nidhamu ya tofauti na hawa tulio nao hivyo watahitajika kunyooshwa kidogo upande wa nidhamu” Mr. Guti akaongea kisha wote wakagonga mikono yao kufurahi.


“Hahahaha hahahahah!!! Mambo yanakwenda kwenyemstari ulionyooka.. Shenzi miezi sita ya mafunzo tutakuwa na jeshi lililo na makomando watupu nakwambia… Nina furaha sana kwa hatua tunazopiga… Nia yangu nataka cartels wote ndani ya Mexico wapige magoti chini yetu hahahah hahahaha hahahaha… Ndoto niliyoota jumapili moja nikiwa gerezani Acapulco inakwenda kutimia kama malaika wa mungu kufyatua mbawa zake kupaa… Hahahaha hahahaha hahahaha!!” Walicheka sana kwa pamoja kisha wakagonganisha glasi zao kwa furaha na vinywaji vikaendelea huku wakiwa pale pale baraza ya nyuma ya kasri la‘Secreto Potential La Feca Palace’.


“Cartels na Kingpin wa magenge mengine watahemea mipira ya gesi kuwasapoti waheme vizuri maana kama kunyanyaswa haswa mimi nilinyanyaswa sana hapo kabla na ndipo wakati wa malipo umefika.. Mafunzo yetu kwa vijana hao itabidi na mimi nijifunze kidogo maana siko vizuri sana kwenye kazi na wewe mwenzangu tayari umeiva na kuiva” Mr. Guti akaongea baada ya kicheko kupungua kwa pande zote.


“Tutaweka program maalumu kwa ajili ya nyinyi msio na mafunzo yoyote angalau muweze hata kutumia silaha vizuri lakini hili najua huko vizuri kwenye kutumia bastola..”

“Si sana kwa kweli… Natembea na bastola kutishia tu maadui zangu… Nataka nikupe siri yangu ambayo sipendi watu wengine waijue katika maisha yangu ni kuwa sina idadi ya watu kudhidi wawili katika niliowaua na hili kwa mtu niliyekuwa muongoza genge ilikuwa inaniuma sana.”

“Eeeeh! Hilo halina shida… Ni bora zaidi sababu hauna dhambi za kuua zilizo nyingi… Usiwe kama mimi mpaka sasa sijui nimewaua watu wa idadi gani.. Hahaha hahahah hahahah! Siku zote juwa ya kuwa ukikaa karibu na ua waridi lazima utanukia… Jiandae kuwa mbwa mwitu asiye na huruma kwa kupitia kioo chako ambaye ni mimi Brigedia Feca komandoo!” Akajisifu Feca kisha akanywa pombe yote iliyo kwenye glasi akifumba macho kwa uchungu wa Tequila anayotupia chupa kwa chupa bila kupumzika lakini inampelekea kucheka cheka tu na si kulewa ki mbwa.


Mwisho wa sehemu ya ishirini na moja (23)


The Red Jaguar inadhidi kujiimarisha kwa kuongeza sajili mpya baada ya uzinduzi rasmi wa kikosi kazi, kikosi tishio kinachotisha ukanda wote wa Amerika Kaskazini.


Mke wa Mr. Fanuel naye ameendelea kung’ang’ania walipize kisasi cha yeye na watoto wake kutekwa.


Kudhidi kufurahia na kuielewa zaidi riwaya hii na magenge ya wauzaji wa unga yanayoongozwa na mabosi wakubwa wanaoitwa ‘Kingpin’ kaa nami kwa burudani kali zaidi huku tukidhidi kusogea kule tulipoanza mwanzao kabisa kwa Agent Kai ndani ya Washington DC akiwa ndiyo amemaliza fungate yake ya miezi mitatu na mkewe.



“Cartels na Kingpin wa magenge mengine watahemea mipira ya gesi kuwasapoti waheme vizuri maana kama kunyanyaswa haswa mimi nilinyanyaswa sana hapo kabla na ndipo wakati wa malipo umefika.. Mafunzo yetu kwa vijana hao itabidi na mimi nijifunze kidogo maana siko vizuri sana kwenye kazi na wewe mwenzangu tayari umeiva na kuiva” Mr. Guti akaongea baada ya kicheko kupungua kwa pande zote.


“Tutaweka program maalumu kwa ajili ya nyinyi msio na mafunzo yoyote angalau muweze hata kutumia silaha vizuri lakini hili najua huko vizuri kwenye kutumia bastola..”

“Si sana kwa kweli… Natembea na bastola kutishia tu maadui zangu… Nataka nikupe siri yangu ambayo sipendi watu wengine waijue katika maisha yangu ni kuwa sina idadi ya watu kudhidi wawili katika niliowaua na hili kwa mtu niliyekuwa muongoza genge ilikuwa inaniuma sana.”

“Eeeeh! Hilo halina shida… Ni bora zaidi sababu hauna dhambi za kuua zilizo nyingi… Usiwe kama mimi mpaka sasa sijui nimewaua watu wa idadi gani.. Hahaha hahahah hahahah! Siku zote juwa ya kuwa ukikaa karibu na ua waridi lazima utanukia… Jiandae kuwa mbwa mwitu asiye na huruma kwa kupitia kioo chako ambaye ni mimi Brigedia Feca komandoo!” Akajisifu Feca kisha akanywa pombe yote iliyo kwenye glasi akifumba macho kwa uchungu wa Tequila anayotupia chupa kwa chupa bila kupumzika lakini inampelekea kucheka cheka tu na si kulewa ki mbwa.


TWENDE KAZI…!


MIEZI SABA MBELE

TAJUMULCO MOUNTAINS, GUATEMALA

Mambo mengi yalipita katikati kabla haijafika miezi saba ya ‘The Red Jaguar’ chui wekundu wa Amerika hawa, kwa muda huu wote genge hili liliweza kukuza mtaji wake kwa kutumia rasilimali watu walioingia wakiwa wazoefu zaidi ukiacha vijana wa kiume na wa kike wapatao mia tano hamsini na tano walioingia kundini baada ya kufudhu mafunzo katika kambi hii iliyopo katikati ya milima ya Tajumulco, San Marcos mpakani mwa nchi ya Mexico na Guatemala pembezoni mwa mashamba ya kahawa yaliyo mpakani upande wa Guatemala.


Siku ya jumapili ikiwa imebaki wiki moja kusherehekewa kwa sikukuu ya Christmass, sikukuu ambayo watu wenye imani ya kikristo usherehekea kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo, hapa katika kambi hii kulikuwa kukifanyika sherehe ya kumalizika kwa mafunzo yaliyochukua miezi saba, mafunzo haya ya vijana wenye umri kati ya miaka ishirini hadi ishirini wengi wakitokea genge lisilo na mwenyewe genge la ‘la hormiga’ ukipenda unaweza kuita ‘siafu’ wa la playa kama wanavyoitwa na watu wengi wa Mexico wanaowatambua hawa vijana waliopinda na maisha na kuamua kuwa na magenge ya kufanya matukio ya kihalifu.


Mafunzo yao yalikuwa yakisimamiwa vikali chini ya wakufunzi waliobobea kwenye mafunzo yote ya kijeshi, wakiwa na weledi wote katika mafunzo, kanuni na sheria zake ukiwa mafunzoni, mafunzo yote yalikuwa chini ya watu wawili mmoja ambao sote tunaofuatilia riwaya hii tunajua walikuwa ni wanajeshi wenye sifa zao toka wakiwa ndani ya jeshi la Mexico Koplo Maxiwell Zuantejo na Koplo Savatel Santos wote hawa wakiwa wamepata mafunzo yao ya ukomando katika kikosi maalumu cha kijeshi cha nchini Israel (Israel Special Forces Unit) na hata wasaidizi wao katika mafunzo Sajenti Lara Moentes na Staff Sajenti Morientes Gudrado wao walikuwa wamepata mafunzo kwa nyakati tofauti katika jeshi la Marekani (American Special Forces) hivyo mafunzo kwa vijana toka ‘la hormiga’ yalikuwa makali wakifundishwa ‘ushushushu’ (intelligence gathering) ‘utekaji’ (kidnapping) ‘utesaji’ (torturing) ulinzi maalumu (boardguard) kutumia silaha za aina yoyote, kutega na kufyatua mabomu na hata namna ya kudhibiti eneo wanapovamia mahali.


Huku katika wale mia nane na kumi walioingia hapa Tajumulco, mabinti wakiwa mia moja na ishirini na mbili (122) na wanaume mia sita themanini na nane wengine wakikutwa na mauti mafunzoni ikiwemo sita wakiliwa na wanyama walioko katika maeneo ya karibu na milima ikwemo majoka makubwa kama Anaconda.


Kati yao sasa wakawa wamepatikana waliofudhu wanaume mia nne tisini na tatu na wanawake sitini na mbili wakiwa wameiva na wakiwa tayari kugawanywa kufanya kazi kwa malekezo ya boss mkuu na msaidizi wake.


Hii kambi ilikuwa ni kambi ambayo unaweza kusema ni kambi ya jeshi ya kiserikali maana ilienea vifaa vyote vya mafunzo ya kijeshi na hata magereza ya watu wanaokosea ilijengwa hapa ikiwa imezungukwa na maji pande zote. Pia pembeni kukiwa na bwawa dogo la mateso ambako walifungwa mamba na jamaa hawa wakawa wanatumia mamba hawa kuwatupia binadamu walioleta matatizo juu yao na kuwageuza chakula cha mamba.


“Habari za leo mabibi na mabwana?” Akiwa kasimama mahala palipojengwa jukwaa alianza kwa salamu Brigedia Feca akiwa katika mavazi ya suti ya rangi nyeusi, miwani ya kijasusi na fimbo mkononi iliyotengenezwa kwa madini ya silva.


“Nzuriii mkuuu!!!!” Sauti ya kujibu ikahanikiza kwa pamoja ikijibiwa kwa mwangwi kwa mbali huko iliko sambaa milima hii ya Tajumulco iliyolizunguka eneo hili la kati lenye miinuko na mabonde kadhaa.


“…Wote mnafahamu kama genge letu linaitwa Red Jaguar! si ndiyoo…?!!” Akaendelea kuongea Brigedia Feca kwa kuwauliza watu waliokaa uwanja mkubwa ulio mbele yake, wote wakiwa wamekaa chini ardhini bila kujali lolote na wote pia mapajani mwao walikuwa wamezipakatia bunduki zinazofanana aina, bunduki toka nchini china Norinko QBZ-95, mzigo ulioingia wiki tu toka kwa watu aliowatuma kufuata bunduki hizi kwa mawakala wa kuuza silaha kwa magenge ya wauza unga na uhalifu.


“Ndiyo mkuu uu uuu!!!” Sauti za kupazwa toka kwa watu zaidi ya elfu moja zikasikika na kurudiwa kwa mwangwi toka pande za milima iliyozunguka eneo hili.


“Natangaza kuanzia sasa tunapokutana hapa tutakuwa na salamu yetu ya kwanza ya utambulisho ambayo pia itatumika iwe kwa siri yaani kwa vitendo maeneo ya watu lakini mnahitaji kutambuana kuwa mlioko hapo ni The Red Jaguar…. Salamu yetu mimi nikisema TRJ nyie mtakuwa mnajibu TGM… Na pale tutakapokuwa tunakutana mahala kwakuwa sisi ni wengi basi vidole vya shahada vya mikono yote miwili vitagusanishwa kwenye ncha zakena wewe utakapoona hivyo nawe utajibu kwa siri kwa kusugua viganja mara mbili haraka basi mtakuwa mshatambuana maana si rahisi kwa watu wote tuliopo hapa kujuana tutapoingia kwenye harakati zetu kwakuwa kila mmoja kuna kitengo atawekwa, kutakuwa na walinzi wa maeneo yetu, kutakuwa na watu wa kupeleleza maadui zetuambao ni magenge kama yetu na hata serikali za nchi mbalimbali ambazo tutakuwa na maslahi ya biashara zetu ni maadui zetu haswa vitengo vyao walivyoweka kupambana juu ya mihadarati… Genge letu litakuwa kubwa sana lakini nyote mtapata maslahi yote ya posho na mishahara mikubwa zaidi ya watu wa magenge yote yaliyopo ukanda huu nyinyi ni jeshi kamili kwangu kama lilivyo jeshi la Mexico, natambua kwa mafunzo mliyopitia hakuna genge lolote la kutusumbua katika Mexico na ukanda wote wa Amerika Kaskazini yakiwemo hata yale magenge yaliyo ndani ya Marekani nathubutu kusema hivyo kwa dhati kabisa ya moyo kwa jinsi miezi sita hii mlivyokuwa mkifanya mafunzo kwa spidi kubwa moyo wote na kiukweli acha niseme tumetoa mafunzo kwa program wanayopewa makomando waliopo hapa Mexico katika jeshi letu… Hongereni sana..!”Hotuba ilianza hivyo akapumzika kidogo bwana mkubwa Feca, eneo lote likiwa kimya kabisa kusikiliza hotuba na kuonyesha nidhamu waliyofunzwa imewaingia.


“Tiii Araaa Jeiiii” Akapaza sauti kwa salamu aliyowafundisha huku akiisindikiza na ngumi akiitupa hewani kwa nguvu kwenda juu ikiwa inawakilisha ‘The Red Jaguar’ (TRJ).


“Tiii Emm Jiiii!!!!” Sauti za wafuasi zikajibu zikipazwa kwa nguvu na kama kawaida mwangwi toka kando kando ya maeneo ukajibu ukifuatisha nah ii ilikuwa ikimaanishwa ‘The Monster Gang’ (TMG).


“Safi sana… Kila mmoja kati yenu atachorwa tattoo mgongoni katikati ya mabega, tattoo ya jaguar aliyekenua mdomo ambao ndani ya kinywa kilichotanuka kutaandikwa maandishi madogo trjtmg… Na pia mkono wa kulia itapigwa chata ya maandishi madogo ya trjtmg na kama utaongeza tattoo zako basi tutataka ziwe tattoo zisizochafua eneo ambalo wachoraji wetu watachora zetu… Wakati wa kuchorwa alama hizi za genge letu ndipo kila mmoja atasaini mkataba wa kuajiriwa nasi na akishausoma na kuusaini kabla hajaanza kuchorwa na endapo hajaridhika na kilichoandikwa kwenye mkataba basi hatachorwa tattoo zetu na sisi tutajua cha kumfanya na hakika naamini kama ulisaini mkataba wa kwanza wa mafunzo sidhani kama utagomea mkataba wetu wa kuwa ndani ya TRJ.. Karibuni sana katika genge letu na mjisikie huru kabisa kama una tatizo lolote katika mkataba wa kila mtu kuna maelekezo yeye atakuwa kitengo gani katika kazi hivyo jina la kamanda anayeongoza kitengo chake atalikuta humo humo… Nisingependa kuwachosha kwa kunisikiliza sababu kiukweli mimi si msemaji sana kama mjuavyo sisi wanajeshi si wanasiasa ambao wao ndiyo wana vipaji vya kuongea kwa mwendo kasi… hivyo namalizia kwa kuwaruhusu muendelee na ratiba nyingine ambayo inawasubiri na hakika itakuwa ndefu sana hivyo natanguliza poleni na pia kiukweli huo ndiyo uvumilivu… Kuna wachora tattoo ishirini tuliowapata miongoni mwenu hivyo wao watatangulia jengo la zahanati yetu ambako timu nzima ya kushughulikia mikataba yenu inawasubiri” Alimalizia hivyo kwa maneno marefu kisha akatulia na kunywa maji kidogo yaliyoko kwenye chupa ya maji.


“…Tiiii Araaa Jeiiii!!!!” Akawapa salamu yake akiihanikiza na ngumi ya kushoto juu.


“Tiiiiii Emm Jiiiii!!!!...” Wakajibu wafuasi nao wakitupa ngumi ya kushoto juu wakiwa wamekaa chini vile vile kama ilivyokuwa.


Mkutano wa hotuba ya Rais wa ‘The Red Jaguar’ ulimalizika kwa mtindo huo na kila mmoja akaondoka pale uwanjani kuelekea kwenye muendelezo wa ratiba zao hasa waliokuwa wanatakiwa kwenda kusaini mikataba na kuchorwa tattoo za utambulisho wa kuwa ni (TRJTMG).


***** ***** *****


MIAKA MIWILI MBELE

Miaka miwili mbele baada ya uzinduzi rasmi wa ‘THE RED JAGUAR’ ilikuwa imekaa juu, imekaa ndani ya midomo ya magenge mengine ikiwemo genge tawala la Los Zetas kiasi ya kwamba wakaamua kuwekeana mipaka ya kibiashara, ndani ya wananchi wasiohusika na uhalifu wowote ukanda wote wa Amerika kaskazini na ndani ya vyombo vyote vya usalama na ulinzi vya nchi ya Mexico na hata zile za jirani hakuna ambaye alikuwa halijui hili genge hatari sana.


Taharuki kubwa ilifumuka kama volcano iliyoruka toka kwenye mlima ulioacha kurusha volcano kwa karne nne nyuma wakati ni kawaida kwa mlima huo kurusha volcano, kazi nzito ilifanywa na ‘The Red Jaguar’.


Mara kadhaa mapigano baina ya genge hili na genge kubwa na tishio la Los Zetas yaliibuka na mara karibia zote vita yao haikuisha mapema, watu walichinjwa, risasi zilipigwa na kusababisha athari kubwa sana ikiwemo kuharibika kwa mali zinazowahusu na hata zile zilizokuwa haziwahusu za wananchi wa kawaida na hata za serikali.


Hakuna wiki ambayo ilipita bila mapigano yaliyosababishwa na genge jipya la ‘Red Jaguar’ambalo lilipindua meza za magenge mengine chini juu pakubwa na kuyafanya yawe yanaheshimu sheria wanazotaka hawa ikiwemo hadi kulipa ushuru kwa magenge mengine yaliyokuwa yakilipa kwa Los Zetas wao The Red Jaguar walitia ngumu na ngumu yao ikakubalika maana Kingpin wa Los Zetas waliogopa kihisia jinsi genge hili lilivyo kubwa na viongozi wenye ujuzi na ufundi wa hali ya juu, mara kadhaa vijana wao walipigwa, kuuliwa na hata kuporwa mizigo yao na fedha ikiwa wao ndiyo walikuwa wakifanya hivi.


Ilikuwa ni siku ya jumapili wakati vijana saba wa Mr. Fanuel Miguel Mendoza ‘Kingpin’ mmiliki wa genge la Mendoza Pontetia Distributio (MPD) walipokuwa ndani ya eneo la uwanja wa michezo wa American School Academy ambao umezungushiwa uzio wa senyenge ya waya zilizosukwa stahili ya vibox box kiasi ya kuwa aliye nje alikuwa akimuona aliye ndani na pia aliye ndani akimuona vizuri aliye nje, uwanja unaotumika kwa michezo mbalimbali na wanafunzi wa shule hii ya upili (sekondari) ya kimataifa inayofundisha wanafunzi wake wa mchanganyiko wakitumiwa lugha mbili kubwa zinazotumika nchi hii ya Mexico‘Kilatino’ lugha kuu ya taifa na ‘kiingereza’lugha ya kibiashara kwakuwa wanafanya sana biashara za muingiliano na nchi jirani ya Marekani.


Pia ni shule iliyotoa mafunzo kwa wanafunzi wapendao michezo hivyo kuwa ni shule yenye wanafunzi wenye vipaji vya michezo mbalimbali hasahasa mpira wa miguu (soka) na mpira wa kikapu (basketball), hivyo wazazi wengi wenye watoto wanaovutiwa na michezo uwaleta shule hii hili kuua njiwa wawili kwa jiwe kupata elimu ya kitaaluma na michezo wanayovutiwa nayo.


Ni shule iliyopo mtaa wa Durango Madero Street barabara ya Pasco Colon Road manispaa ya Nuevo Laredo jimboni Tamaulipas, kulikuwa na ruhusa kwa wanamichezo wengine walio vijana toka katika shule zingine kufika uwanja huu wa shule kufanya mazoezi na wanafunzi wa hapa siku za wikiendi na hata kujenga ukaribu wa kirafiki hasa kwakuwa wengi wa wanafunzi wa hapa walikuwa ni wageni wa maeneo ya Nuevo Laredo.


Vijana hawa walifika eneo hili wakiwa na mipira ya kuchezea katika mfuko mkubwa wa kamba kamba za manila zilizofumwa kutengeneza mfuko spesho kwa kubeba mipira, idadi ya mipira kumi ya kuchezea ikiwa ndani ya mfuko huu uliwekwa pembeni huku mpira miwili waliitoa wakawa wanacheza kwa kupasiana wakiwa wamevaa nguo zisizo za michezo na hili halikuwashangaza vijana wengine hasa wanafunzi walioko pale sababu pia inatokeaga watu wanafika kwenye uwanja uliopo eneo la shule lakini ni rukhsa kutumika na vijana wengine wa mtaani wakihitaji kufanya hivyo.


Muda huu wa saa kumi na moja kasoro ulifanya eneo hili kuwa na watu wengi kwakuwa kuna viwanja vingi kama nilivyokwisha eleza walikuwa wapo wanaocheza soka wakiwa wao wamewai eneo la kati la kuchezea mpira wa miguu (pitch) pia walikuwepo waliokuwa wakicheza mchezo wa volleyball eneo la uwanja wake wa volleyball na hapa walichanganyika mabinti na wavulana, wapo waliokuwa kwenye mchezo wa mpira wa kikapu (basketball) nao pia wakiwa mchanganyiko na pia walikuwepo mabinti waliokuwa wakicheza netball na kulifanya eneo lote kuwa changamfu haswa kelele za furaha katika michezo kama hujuavyo wanafunzi wa umri huu wengi wakiwa umri wa kupevuka hivyo mgeni ukifika hapa utaamua mchezo upi uuangalie lakini raha na furaha ilikuwepo na watazamaji walikuwepo pia.


(MPD) ‘Mendoza Potantia Distributio’ vijana saba toka genge hili wao walijitenga kwa pembeni kidogo wakicheza mpira kati ya mipira miwili waliyoitoa ndani ya mfuko wa kamba kamba huku mmoja wao akionekana mara nyingi akiandika meseji kwenye simu yake kisha anarudisha simu mfukoni anaendelea na mchezo huku zikipita dakika fulani anatoa tena simu anasoma ujumbe na kisha kujibu.


Katika barabara inayoelekea eneo hili la uwanja wa shule hii ya upili mita kama sabini toka zilipaki gari mbili moja aina ya Nissan Dualis 2006 rangi ya silva na huku nyuma ya gari hii kulikuwa na gari aina ya Toyota Prado hili likiwa la rangi nyeusi.


Magari haya yote mawili ndani yake kulikuwa na vijana wa ‘The Red Jaguar’ kila gari kulikuwa na vijana sita jumla yao kuwafanya wawe kumi na mbili eneo hili, wakiwa na silaha zao aina ya bunduki pendwa ya genge hili hatarishi la bwana mkubwa Brigedia Feca, bunduki kutoka nchini China, bunduki ambazo magenge mengi ya kazi hizi za mihadarati imekuwa rahisi wao kuzipata silaha hizi kali za kivita ‘Norinko QBZ-95’ ingawa wengine huenda mbele na kumiliki ‘Norinko QBZ-97’lakini kwenye ufanyaji kazi ufanana kwa kiasi kikubwa kama ilivyo umbo kufanana lakini bei yake ni tofauti katika manunuzi kutokana na matoleo yake ikiwa kwa mtumiaji wa hizi bunduki akishika utofautisha haraka katika uzito na upakiaji wa risasi kwa ajili ya kufanya kazi husika iliyofanya kiwanda husika cha silaha hizi kutengeneza.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog