Search This Blog

Monday 27 March 2023

HEKAHEKA! - 4

  


Simulizi : Hekaheka!

Sehemu Ya Nne (4)



Nilikuwa na hakika kabisa kuwa katika macho ya serikali nilionekana ni jasusi hatari sana kwa usalama wa nchi niliyekuwa na taarifa muhimu zilizotakiwa na idara ya ujasusi ili kusaidia kumaliza uhalifu nchini.


Wale makamanda waliendelea kunitazama bila kusema chochote huku macho yao makubwa yenye kila dalili ya ukatili yakionekana kunionya kuwa nisijaribu kuleta aina yoyote ya ufedhuli.


Tangu nilipofikishwa kwenye kile chumba sikuwa nimeulizwa chochote hadi muda ule, kitambo kirefu cha ukimya kilipita nikiwa bado nimesimama pale huku chumba kikiwa kimezingirwa na maofisa usalama na makamanda walionileta ambao walikuwa wakisubiri kupokea amri kutoka kwa wale makamanda wawili.


“Wakuu wanahitaji mtu huyu atapishwe taarifa zote muhimu anazozifahamu kwa namna yoyote ile,” ofisa usalama mmoja miongoni mwa wale maofisa walionileta mle ndani alivunja ukimya.


“Vipi kama dozi itamzidi na akapoteza maisha?” mmoja wa wale makomandoo tuliowakuta mle ndani akauliza huku akinitupia jicho kali.


“Roho ni ya kwake, sisi tunachohitaji ni taarifa zote muhimu,” alijibu yule ofisa usalama na kunifanya kuogopa sana.


“Okay! Tuachieni kazi hiyo tutajua namna ya kufanya,” yule komandoo akasema huku akionekana kutafakari jambo. Kisha nikamuona akiwapa ishara fulani wale maofisa usalama walionileta kuwa waondoke.


Niliwashuhudia wakiondoka na hatimaye tukabakia watu watatu tu, mimi na wale makomandoo wawili, hapo nikahisi mapigo yangu ya moyo yamesimama, hasa nilipoyafikiria maneno ya yule komandoo kuwa: ‘Sasa itakuwaje kama dozi itamzidi na akapoteza maisha’.


Hata hivyo nilijipa moyo kidogo kwa tukio lile la kuondoka kwa wale maofisa usalama kwani niliamini kuwa wale makomandoo wa idara ya ujasusi jeshini wangeweza kunielewa kwa kuwa walikuwa wamepitia mafunzo ya hali ya juu mno ya intelijensia ili kuweza kumbaini mhalifu na asiye mhalifu.


Kitambo kifupi cha ukimya kikafuatia nikiwa bado nimesimama huku tukitazamana, kisha nikawaona wale makamanda wakiinuka na kuanza kuzitupa hatua zao kunifuata wakitembea kikakamavu huku buti zao ngumu miguuni zikiitetemesha sakafu ya kile chumba kwa kiasi kikubwa.


Nilitamani nikurupuke na kuanza kutimua mbio. Lakini hilo halikuwezekana kwa kuwa muda haukuniruhusu kufanya vile na wale watu walikuwa ni kama tayari wameshanifikia pale niliposimama.


Wale makamanda walipofika pale niliposimama wakajigawa katika mtindo wa kunizunguka. Komandoo mmoja akaja na kusimama nyuma yangu na mwingine akasimama mbele yangu.


Yule kamandoo aliyesimama mbele yangu alinitazama kwa kitambo na kuonekana kama aliyekuwa akinionea huruma kwa yatakayonipata kisha akaniashiria kwa mkono niketi kwenye kile kiti cha chuma kilichokuwa upande wa pili wa ile meza kubwa ya chuma.


Sikutaka kuleta ubishi wowote, nilikifuata kile kiti kisha nikaketi huku nikiwatazama kwa wasiwasi wale makamanda waliokuwa bado wamesimama wakinitazama kwa makini.


Kwa mara ya kwanza nilianza kuhisi kuwa akili yangu ilikuwa ikishindwa kufanya kazi, hasa nilipofikiria kitu gani kingefuatia kama wale makomandoo wasingefanikiwa kupata taarifa walizozihitaji kutoka kwangu.


Hata hivyo, bado nilipiga moyo konde huku nikijiambia ni lazima niwaaminishe kuwa nimefananishwa na mtu mwingine kwani mimi ni Maximilian Banda na si Brown Senga ili kujiokoa na adhabu ambayo wangeweza kunipa, vinginevyo ule ndiyo ungekuwa mwisho wangu.


Yule komandoo aliyekuwa amesimama mbele yangu aliendelea kunitazama kwa kitambo kisha nikaliona tabasamu likijitokeza taratibu usoni mwake.


Nami nikatabasamu kidogo kujifariji na kujaribu kuuondoa wasiwasi uliokuwa umetanda moyoni mwangu na hapo nikamuona yule komandoo akirudi kule kwenye kiti na kuketi bila kusema neno lakini yule mwenzake alibaki akiwa amesimama nyuma yangu.


Nikiwa bado nimeshikwa na mshtuko, niliyatembeza macho yangu taratibu nikizikagua vizuri sura za wale makomandoo huku nikijitahidi kuumeza wasiwasi niliokuwa nao moyoni.


Mara nikamuona yule komandoo aliyerudi kuketi kwenye kiti akimpa ishara fulani yule mwenzake aliyekuwa amesimama nyuma yangu.


Sikujua maana ya ile ishara ila nilishangaa kumuona yule kamanda aliyekuwa nyuma yangu akinisogelea na kuanza kunifungua zile pingu mikononi kitendo kilichonifanya nistaajabishwe sana na upendo ule wa ghafla.


Yule kamanda alipomaliza kunifungua zile pingu akanivua ile saa niliyokuwa nimevaa mkononi kisha akarudi nyuma hatua kadhaa na kusimama kama mwanzo.


Nikiwa bado nimeketi kwenye kile kiti mawazo mengi yakawa yanapita kichwani mwangu. Nilianza kumlaani mtu aliyeitwa Brown Senga au Godwin Sengerema kwa kuniponza huku pia nikiilaani siku ile.


Niliukumbuka vyema ule wasifu wa Brown Senga uliotolewa na Babra na baadaye Madame Pamela, kisha nikajaribu kuyafikiria mateso yaliyokuwa mbele yangu nikidhaniwa kuwa mimi ndiye huyo Brown Senga na hivyo kutakiwa kutapika taarifa zote muhimu zilizotakiwa na serikali.


Nilihisi akili yangu ikipoteza uwezo wake, nikaamua kuikabidhi roho yangu kwa Mungu huku nikifumba macho na kufanya maombi kimya kimya kumuomba Mungu aninusuru na mateso makali ambayo yangenisababishia kupoteza uhai, hasa nikiamini kuwa mateso ambayo ningepewa na wale makomandoo wa idara ya ujasusi jeshini yangekuwa makali sana.


“Brown…!” Sauti nzito ya yule kamanda aliyekuwa ameketi kwenye kiti ikayarudisha mawazo yangu mle ndani. Hata hivyo sikuitikia kwani niliamini hilo halikuwa jina langu.


“Wewe!” aliniita tena yule komandoo, safari hii kwa ukali kidogo.


“Naam!”


“Unajua kwanini tumekufungua pingu? Tunataka uwe huru na tuzungumze kiurafiki, ila usidhani kama unaweza kutoroka…” yule kamanda akasema huku tabasamu zaidi likichanuwa usoni kwake.




Nilihisi akili yangu ikipoteza uwezo wake, nikaamua kuikabidhi roho yangu kwa Mungu huku nikifumba macho na kufanya maombi kimya kimya kumuomba Mungu aninusuru na mateso makali ambayo yangenisababishia kupoteza uhai, hasa nikiamini kuwa mateso ambayo ningepewa na wale makomandoo wa idara ya ujasusi jeshini yangekuwa makali sana.


“Brown…!” Sauti nzito ya yule kamanda aliyekuwa ameketi kwenye kiti ikayarudisha mawazo yangu mle ndani. Hata hivyo sikuitikia kwani niliamini hilo halikuwa jina langu.


“Wewe!” aliniita tena yule komandoo, safari hii kwa ukali kidogo.


“Naam!”


“Unajua kwanini tumekufungua pingu? Tunataka uwe huru na tuzungumze kiurafiki, ila usidhani kama unaweza kutoroka…” yule kamanda akasema huku tabasamu zaidi likichanuwa usoni kwake.


Endelea...


“Sasa tuambie taratibu na bila kificho chochote kuhusu misheni yenu, nani washirika wenzako na wapi mlipoficha silaha,” aliniambia akinikazia macho.


“Kwa kweli sifahamu kitu chochote kuhusu hizo silaha unazosema, ningekuwa najua kwanini niwasumbe?” nikaongea kwa utulivu.


“Naona umejitolea kufa peke yako huku wenzako wakiendelea kustarehe mafichoni, siyo? Au unadhani utasifiwa kwa upuuzi huu?” aliniuliza kwa sauti ya upole na tulivu lakini iliyokuwa imebeba kitu fulani kilichonionya kutoongopa.


“Kweli kabisa sielewi chochote, kwa miaka yote hii mimi naishi nchini Uholanzi na sijui chochote kilichokuwa kinaendelea hapa nchini zaidi ya yale niliyoyasoma kwenye mitandao,” nilisema nikiendelea kushikilia msimamo wangu.


Yule komandoo akanitazama kwa kitambo kirefu huku akiendelea kuruhusu tabasamu pana kuchanua usoni mwake. Sikujua kwanini alitabasamu na lile tabasamu lilikuwa likiashiria nini, hivyo hali ile ikanisumbua sana akili yangu.


“Kwa hiyo, hujui wenzako wako wapi wala silaha zimefichwa wapi?” yule komandoo akaniuliza tena kwa kujiamini kana kwamba alikuwa na hakika na anachokizungumza.


“Wenzangu akina nani?” niliuliza huku nikionekana kuanza kuchoshwa na maswali yasiyo na kichwa wala miguu niliyokuwa naulizwa tangu nilipokamatwa kule uwanja wa ndege.


“Brown, labda nikwambie kitu, wengi wanaoletwa katika chumba hiki na kushikilia misimamo yao huishia kuongea ukweli huku wakiwa na hali mbaya sana na wengine huwa tayari wamepata ulemavu wa kudumu. Sidhani kama utapenda tufike huko!” aliniambia yule komandoo huku akinitazama kwa makini.


“Wala sipendi tufike huko ingawa sijui kwanini hamtaki kuniamini,” nikamjibu yule komandoo huku nami nikimtazama kwa makini.


“Kama hupendi tufike huko basi tuambie ukweli kisha uombe msamaha ili tukusamehe… vinginevyo kitakachokupata ni dhambi hata kusimulia.”


“Nimekwisha waambia kuwa sifahamu chochote…” nilisema kwa hamaki.


Muda uleule nilijikuta nikitulizwa kwa kuzabwa kofi zito kutoka kwenye kiganja kilichokomaa kwa mazoezi cha yule komandoo aliyekuwa amesimama nyuma yangu na hivyo kunisababishia maumivu makali sana kichwani. Japo kile kilikuwa kipigo cha mara moja tu lakini maumivu yake yalikuwa hayasimuliki!


“Sasa mbona unanipiga?” nikamuuliza yule komandoo aliyekuwa amesimama nyuma yangu kwa hasira huku nikigeuka kumtazama.


“Hapa bado hujapigwa, nilichojaribu kufanya ni kukukumbusha kuwa unatakiwa kujibu maswali unayoulizwa, usitulazimishe kutumia nguvu kisha ukajuta,” akasema yule komandoo kwa namna ya kunionya.


“Nimesema sijui lolote lakini hamniamini, na hiki mlichokifanya ni utekaji nyara na uvunjaji wa haki za binadamu. Ninaweza kuwafungulia mashtaka kwa unyanyasaji kwani mnanitesa wakati sijafanya kosa lolote,” nilijaribu kujitetea, hata hivyo moyoni nilishaanza kuhisi juu ya hatari kubwa iliyokuwa ikininyemelea.


“Tunayo haki ya kumkamata mtu yeyote ambaye mienendo yake inaonekana kutishia usalama wa nchi yetu na kama hutozungumza ukweli idara haitalaumiwa kwa kifo chako, hivyo usijaribu kututisha,” yule kamanda aliyeketi akanionya huku akinitazama kwa macho makali yenye kuonya.


“Kwa hiyo mnadhani kuniua ndiyo mtakuwa mmetatua tatizo au kupata ufumbuzi wa haja yenu?”


“Huenda lisiwe suluhisho lakini angalau hutoweza kupanga tena mikakati ya ugaidi au kutishia usalama wa nchi yetu.”


“Kwani mipango gani ya ugaidi ambayo mimi nimeipanga?” nikauliza huku nikijaribu kununua muda.


“Acha maswali yasiyo na msingi wewe, unachotakiwa ni kujibu maswali unayoulizwa, basi!” yule komandoo aliyekuwa amesimama nyuma yangu akanionya huku akinisukasuka mgongoni.


“Sasa nitajibu nini wakati sifahamu chochote kuhusu ugaidi mnaousema! Au kosa langu ni kuja Tanzania kusalimia jamaa zangu?” niliuliza kwa hasira huku nikizidi kukerwa.


“Ooh… kwa hiyo unadhani kuwa umeletwa hapa ili tupige stori siyo? Kama unafikiri tunafanya utani basi subiri uone,” yule komandoo aliyekuwa nyuma yangu akaniambia huku akikisukasuka ovyo kichwa changu na kunipigapiga nyuma ya shingo yangu kwa dhihaka.


Kuona vile nikaamua kuinuka kutoka pale kwenye kiti nikiwa nimepandwa na hasira, na hapo ikaonekana kana kwamba nilikuwa nataka kupambana naye. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana.


Kilichofuatia hapo nilitamani ardhi ipasuke ili niangukie ndani na kupotelea humo. Kwa kasi ya umeme yule komandoo aliruka juu, akajiviringisha hewani, hapo nikajua akitua chini ingekuwa balaa hivyo nilijiandaa kwa pigo lolote ambalo lingefuata.


Kwa kuwa nami sikuwa nyuma kwani nilikuwa nimepitia mafunzo ya kujihami ya karate na kufikia hatua ya mkanda mweusi, haraka nikajibetua na kuyakwepa mapigo ya haraka ya yule komandoo.


Kuona hivyo, yule komandoo alikusanya nguvu za kutosha kisha kufumba na kufumbua akajibetua na kuuzungusha chini mguu wake wa kulia akinichota ngwala maridadi yenye ufundi wa hali ya juu.


Niseme tu ukweli, sikutegemea kabisa hali ile, hivyo nilishikwa na taharuki ya aina yake wakati nilipokuwa nikitupwa hewani na kuweweseka kama niliyekuwa nimepagawa na mapepo.


Nilipotua chini nikashtukia napigwa ngumi tatu mfululizo za tumbo zilizonifanya nijipinde huku nikisikia maumivu makali sana yaliyosambaa haraka hadi mgongoni.


Nikiwa bado nimejipinda yule komandoo alinichapa pigo baya la kareti mbavuni na maumivu yake yakanifanya niachie mguno mkali wa maumivu, nikayumba ovyo huku nikirudi nyuma lakini kabla sijaanguka aliruka na kunidaka kisha akaninyanyua juu juu kama kishada kwa nguvu zake zote na kunibwaga chini.


Hali ile ilinifanya nitue pale chini sakafuni kwa matako na hivyo kufanya maumivu makali yanisambae mwili mzima. Nikapiga yowe kali la maumivu huku nikijitahidi kuwahi kusimama lakini ilikuwa kazi bure.


Yule komandoo aliniwahi kabla sijasimama sawasawa akanikwida tena na kuninyanyua juu. Nilijitahidi kujitetea kwa kila namna lakini bado haikunisaidia kitu, yule komandoo alikuwa na nguvu nyingi zisizo za kawaida, hivyo alinibeba mzegamzega na kwenda kunibwaga juu ya ile meza ya chuma iliyopo katikati ya kile chumba kama furushi.


Muda wote yule komandoo mwingine aliyekuwa ameketi kwenye kiti alikuwa ametulia tuli bila kutingishika akiniangalia huku uso wake ukiwa bado umepambwa kwa tabasamu pana.


Baada ya kutua juu ya ile meza ya chuma kama furushi nilipiga tena yowe kali huku maumivu makali yakizidi kusambaa mwilini, nikajikuta nikianza kuingiwa na hofu kubwa.


Kisha yule komandoo alinijia kwa mapigo ya mateke ya haraka ambayo nilijitahidi kwa kila namna kuyapangua kwa mikono yangu bila mafanikio.


Nilitaka kuinuka lakini kizunguzungu kikanishika na kunifanya kutapika na hapo nikaanza kuishiwa nguvu na sikuona tena kama kungekuwa na namna nyingine ya kujiokoa kutoka kwenye mikono matata ya yule komandoo, hivyo niliamua kunyoosha mikono yangu juu kuashiria kwamba nilikuwa nimesalimu amri huku nikihema ovyo.


Yule komandoo alisimama akanitazama kwa makini na aliporidhika kuwa kile kipigo kilikuwa kimenilegeza kiasi cha kutosha, akaninyanyua na kunikalisha kwenye kile kiti cha chuma nilichokuwa nimeketi mwanzo, kisha akaniacha na kusogea kando huku akinitazama kwa makini.


Damu ilikuwa ikinitoka puani na mdomoni huku sehemu ya juu ya jicho langu la kushoto ikiwa imevimba na kuchanika na ilikuwa inavuja damu taratibu.


Moyo wangu ulikuwa unakwenda mbio na uliunguruma sana kama uliokuwa ukipambana na kazi isiyo ya kiasi chake. Mwili wangu nao ukawa mzito kama uliofungwa na tani kadhaa za mizigo huku jasho likinitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu.




Damu ilikuwa ikinitoka puani na mdomoni huku sehemu ya juu ya jicho langu la kushoto ikiwa imevimba na kuchanika na ilikuwa inavuja damu taratibu.


Moyo wangu ulikuwa unakwenda mbio na uliunguruma sana kama uliokuwa ukipambana na kazi isiyo ya kiasi chake. Mwili wangu nao ukawa mzito kama uliofungwa na tani kadhaa za mizigo huku jasho likinitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu.


Endelea...


“Sasa tueleze, Brown, silaha mlizoiba ziko wapi na watu unaoshirikiana nao ni akina nani?” yule komandoo aliyekuwa ameketi kwenye kiti akaniuliza huku akinitazama usoni kwa makini.


“Nimekwisha waambia kuwa mimi siyo Brown na wala sifahamu lolote kuhusu silaha, kama vipi bora mniue tu, maana nimechoka kuulizwa maswali yasiyo na kichwa wala miguu,” nikafoka kwa hasira huku nikimeza funda kubwa la mate kuitowesha hasira kifuani mwangu.


Yule komandoo hakunijibu badala yake nikamuona akiinuka huku akitabasamu kisha akaonesha ishara fulani kwa yule mwenzake aliyekuwa amesimama karibu yangu.


Yule komando aliyekuwa amesimama karibu yangu alifanya kama anainama kisha alichomoka kwa kasi ya umeme na kurusha teke la nguvu la mguu wake wa kulia lililokuwa linaelekea sehemu za mbavuni kwangu.


Hata hivyo aliambulia patupu kwani nililiona na kulikwepa kwa namna ambayo wale makomandoo hawakutegemea kabisa kwani ilimshangaza hata yule komandoo aliyekuwa akinihoji, lakini nilijikuta nikipigwa pigo jingine la nguvu lililotua kwenye tumbo langu na hapo nikajikuta nikikabiliana na maumivu makali zaidi ya tumbo yaliyosambaa haraka mwilini.


Niliruka haraka nikijitupa kando huku nikikwepa mapigo mengine matatu yaliyokuja kwa kasi lakini kabla sijatua chini yule komandoo akawahi kunichapa teke jingine hatari la tumbo lililonivuruga vibaya na kunitupa nyuma.


Nikaangukia matako na kuugulia kwa maumivu, lakini kabla yule komandoo hajanifikia nikanyanyuka haraka na kusimama sawa, tukabaki tukitazamana kwa hasira. Nilitamani kumchapa ngumi maridadi za uso lakini sikuthubutu kabisa kurusha ngumi wala teke kwa kuhofia kuwa katika mazingira yale wangeweza kuniua, hivyo nilichokuwa nikikifanya ni kujihami tu ili wasiniumize.


Yule komandoo akanifikia tena, akatupa ngumi tatu makini kichwani kwangu lakini nilizikwepa kama mchezo na hivyo zikakata upepo na kumpunguza nguvu. Kuona vile akabadili mtindo na kunitupia pigo baya la kareti lililopita milimita chache sana kutoka shingo yangu lakini nikifanikiwa kulikwepa.


Kabla sijajua nifanye nini yule komandoo akawahi kunichapa kofi moja la usoni lililonipa kisulisuli na kudondoka sakafuni, kisha nikaanza kujiviringisha nikienda mbali naye. Lakini yule komandoo alikuwa mwepesi sana, nilipotaka kusimama nilishangaa nikichotwa mtama kwa ufundi mkubwa mno.


Nikarushwa hewani na nilipotua chini aliwahi kunidhibiti kwa kabari matata shingoni mwangu. Nikajitahidi kufurukuta bila mafanikio nikitupa mikono na miguu yangu huku na kule.


Yule komandoo hakuniachia badala yake akaendelea kukaza mikono yake kwa nguvu zote na kunifanya nianze kuhema kwa shida. Hali yangu ikaanza kuwa mbaya sana baada ya kuanza kukosa hewa na hofu ya kifo ikaanza kuniingia taratibu.


Nilianza kuhisi kuwa hali yangu ilikuwa ikizidi kuwa mbaya kadiri sekunde zilivyokuwa zikiyoyoma. Kichwa changu nacho kikawa kizito mno kama niliyekuwa nimebebeshwa mzigo mzito kichwani nisioumudu. Nilitaka kusema neno lakini nikajikuta nikiishia kufumbua mdomo tu huku sauti yangu ikigoma kabisa kutoka.


Macho yangu nayo taratibu yakaanza kupoteza nguvu ya kuona, wingu zito likatanda kwenye mboni zangu na hapo nikaanza kuhisi shughuli mbalimbali za mwili wangu nazo zikiwa mbioni kusitisha utendaji wake.


Yule komandoo aliporidhika kuwa ile kabari ilikuwa imenilegeza kiasi cha kutosha akaniachia, nikajibwaga sakafuni kama zigo. Kisha akaushika mguu wangu wa kushoto kwa nguvu na kuanza kuniburuta kuelekea kwenye ule mlango mkubwa wa chuma uliokuwa nyuma.


Sikuweza kuleta upinzani wowote kutokana na hali yangu ya kiafya kuzidi kuzorota. Yule komandoo aliendelea kuniburuta na hapo hapo yule mwenzake akaufungua ule mlango wa chuma kisha tukashika uelekeo wa upande wa kushoto huku akiendelea kuniburuta, hata hivyo eneo lile lilikuwa na sakafu laini hivyo sikuchunika sana.


Baada ya umbali mfupi tukafika sehemu yenye mlango mfupi wa chuma upande wa kulia. Tukasimama na hapo yule komandoo mwingine akaanza kuufungua ule mlango.


Baada ya muda mfupi ule mlango ukafunguka na kuturuhusu kuingia mle ndani kisha ukafungwa nyuma yetu na hapo nikaendelea kuburutwa hadi katikati ya kile chumba kisha nikabwagwa pale chini sakafuni.


Nilijizoazoa na kuinuka kisha nikaketi kitako huku nikiyakodoa macho yangu kuyatazama mandhari ya kile chumba lakini sikuweza kuona chochote mle ndani kwa vile chumba kilitawaliwa na giza. Baada ya kitambo kifupi taa zenye mwanga hafifu za mle ndani ziliwashwa na hapo nikapata kuyaona vizuri mandhari yale.


Nilipoyatembeza macho yangu kuchunguza mle ndani nikagundua kuwa kilikuwa ni chumba kama kile tulichotoka lakini hiki kikionekana ni chumba cha mateso makali zaidi ambacho pia kilikuwa chini ya ardhi kikiwa hakina dirisha.


Kilikuwa ni chumba kilichoogopwa hata na wafanyakazi wenyewe wa idara ile ya ujasusi, kwani kilitisha kwa mambo yaliyokuwa yanafanyika humo.


Katikati ya kile chumba kulikuwa na bomba refu la chuma lililotoka upande mmoja wa kile chumba hadi upande wa pili ukutani. Juu ya dari kulining’inizwa vyuma vifupi vilivyokunjwa na kuchongwa mbele yake mfano wa vyuma vya kuning’inizia nyama buchani.


Upande wa kulia wa kile chumba kulikuwa na tangi kubwa lililokuwa limejengwa kwa vioo ambalo ndani yake lilijazwa maji, mara nyingi lilikuwa likitumika kuwasulubisha watuhumiwa hatari kwa kuwazamisha ndani au kama mtuhumiwa akionekana hataki kuongea ukweli, walichofanya ni kufungulia umeme uliyoungwa ndani ya tangi hilo na kuanza kumpiga shoti mtuhumiwa huyo.


Na kando ya lile tangi kulikuwa na beseni kubwa ambalo pia lilikuwa limejazwa maji.


Upande mwingine wa kile chumba kulikuwa na kitanda chembamba cha chuma chenye mikanda imara, mnyororo mfupi na pingu za miguuni na mikononi za chuma.


Kando ya kile kitanda kulikuwa na kiti cha umeme kilichotumika kuwasulubu watuhumiwa hatari na wakati mwingine kuwaua kabisa.


Mbele ya kile kiti cha umeme kulikuwa na meza ya kioo ambayo juu yake kulikuwa na sinia dogo lenye kisu, waya mwembamba lakini imara, koleo, nyundo na misumali. Pia niliona mabomba mawili ya sindano yaliyokuwa na dawa maalumu ambayo kwa uelewa wangu ni kuwa mtuhumiwa akichomwa basi huufanya ubongo na akili yake iwaze kusema ukweli tu.


Nilipotazama vizuri nikaona pia kitu mfano wa betri kubwa ya gari yenye kufua umeme na vishikizo vyake. Pia kulikuwa na mtungi wenye gesi, kamba imara na vifaa vingine vya mateso ambavyo sikuvielewa sawasawa.


Nikiwa pale chini nimeketi wale makomandoo wakanizunguka na hapo nikaanza kuvuliwa nguo zangu na kubaki mtupu kama nilivyozaliwa kisha nikafungwa kamba miguuni na mikononi na baada ya hapo nilijikuta nikibebwa na kutundikwa kichwa chini miguu juu.


Yule komandoo aliyekuwa akinihoji mwanzo akanisogelea na kunichapa kofi usoni kisha akaanza kunihoji huku nikiwa bado nimening’inizwa.


“Bila shaka sasa upo tayari kutueleza silaha mlizopora ziko wapi na watu unaoshirikiana nao ni akina nani?” aliuliza yule komandoo huku tabasamu la kinyama likiwa halimtoki usoni kwake.



Nikiwa pale chini nimeketi wale makomandoo wakanizunguka na hapo nikaanza kuvuliwa nguo zangu na kubaki mtupu kama nilivyozaliwa kisha nikafungwa kamba miguuni na mikononi na baada ya hapo nilijikuta nikibebwa na kutundikwa kichwa chini miguu juu.


Yule komandoo aliyekuwa akinihoji mwanzo akanisogelea na kunichapa kofi usoni kisha akaanza kunihoji huku nikiwa bado nimening’inizwa.


“Bila shaka sasa upo tayari kutueleza silaha mlizopora ziko wapi na watu unaoshirikiana nao ni akina nani?” aliuliza yule komandoo huku tabasamu la kinyama likiwa halimtoki usoni kwake.


Endelea...


“Laiti ningekuwa nafahamu kuhusu hizo silaha mnazozizungumzia ningekwisha waambia mahali zilipo kuliko adha hii ya mateso ninayoyapata,” nikaendelea kujitetea huku nikihema kwa taabu.


Yule komandoo alinitazama kwa makini sana kisha akashusha pumzi zake na kutazama kando na kukunja sura yake huku akionekana kama aliyekuwa akisoma kitu fulani kando.


Mara nikamuona akipiga hatua na kwenda kuchukua kibubu chenye gesi kisha aliiwasha ile gesi na kuonekana akijaribu kurekebisha ule moto wa gesi, baada ya kuweka moto fulani kwenye kile kibubu cha gesi, akanifuata na kuanza kunipitishia usoni bila kunidhuru, nia ilikuwa kunisikilizisha lile joto lililotoka mle kwenye kibubu.


“Umelisikia joto lake, basi kama hutaki kushirikiana nasi joto hili litakwenda kwenye sehemu zako za siri,” aliongea yule komandoo huku akinitazama kwa makini. Kisha aliuzima ule moto wa gesi na kukiweka kando kile kibubu cha gesi.


“Haya, sasa niambie ili tusije kuumizana. Ni swali rahisi tu: unashirikiana na kina nani na silaha mmezificha wapi?”


Nilibaki kimya kwa kuwa muda ule nilikuwa nahisi kizunguzungu, sauti nyembamba mfano wa sauti itokayo kwenye filimbi ilikuwa ikilia kwenye masikio yangu na giza zito lilianza kutanda kwenye mboni zangu za macho. Yule komandoo alinitazama kwa makini na kusonya.


“Nimejitahidi sana kuongea kwa upole ili tusije tukaumizana lakini naona bado hutaki kushirikiana nasi, sasa kama unadhani tumekuleta hapa ili kupoteza muda wetu basi subiri,” alisema yule komandoo akinionya.


Muda uleule yule komandoo akaanza kunishushia kipigo. Kilikuwa kipigo hatari sana kwangu, japo nilikuwa nimepitia mafunzo ya kujihami ya karate lakini sikuwahi kushuhudia kipigo cha aina ile.


Baada ya dakika tano nilikuwa nimechakaa vibaya huku uso wangu wote ukiwa umetapakaa kwa damu.


“Basi mwache, naamini sasa yupo tayari kusema ukweli,” nikasikia sauti ya kike ikimwambia yule komandoo asiendelee kunisulubu na hapo yule komandoo akasitisha kipigo huku akinitazama kwa ghadhabu.


Nilipojaribu kufumbua macho yangu kumtazama mtu aliyemzuia yule komandoo asiendelee kunisulubu nilijikuta nikimwona kama kiumbe cha ajabu kisichoeleweka huku lile eneo nikiliona kama tufe fulani lililokuwa linazunguka angani.


“Hebu mshusheni hapo, nahitaji kuongea naye,” yule mwanamke alisema tena, na mara nikawaona wale makomandoo wakianza kunishusha kutoka pale juu walipokuwa wamenitundika na kuniacha nikijibwaga pale salafuni.


Nilipomtazama kwa makini yule mwanamke nikagundua kuwa ni Madame Pamela na sikujua alikuwa ameingia saa ngapi mle ndani. Madame Pamela alisimama mbele yangu akinitazama kwa makini huku akionekana kama aliyekuwa akijishauri kitu nafsini mwake. Kisha alinisogelea na kuninong’oneza sikioni.


“Unajua, wanataka kukuua lakini mimi nimewaambia tusifanye hivyo, ila kama utaendelea na ukaidi wako kwa kweli sitasita kuwaruhusu wafanye hivyo,” Madame Pamela aliongea kwa upole katika namna ya kunishi, jambo ambalo lilinishangaza sana.


“Haya tueleze, silaha mmezificha wapi na watu gani unaoshirikiana nao?” Madame Pamela akaniulza kwa sauti huku akiendelea kunitazama kwa uyakinifu zaidi.


“Jamani mtaniua bure, mimi sifahamu chochote,” niliongea kwa taabu sana kwa sababu mdomo wangu ulikuwa umevimba, kwa kweli nilikuwa nikitia huruma.


Madame Pamela alinitazama kwa tabasamu kisha lile tabasamu likageuka kicheko huku akimpa ishara mmoja wa wale makomandoo. Na kabla sijajua nikashtuka nikivalishwa mfuko mweusi wa nailoni kichwani ambao ulikazwa barabara kisha nikaanza kuburutwa kibabe sakafuni kuelekea eneo ambalo sikulifahamu.


Hatukwenda mbali mara tukasimama na hapo nikabebwa na kuinamishwa chini kwenye beseni lililojaa maji nyuma yangu.


Hapo nikaanza kuhisi kuwa mambo hayakuwa shwari kabisa na muda uleule nikaanza kumiminiwa maji mengi usoni huku nikiwa bado nimevikwa ule mfuko mweusi kichwani na kunifanya nishindwe kuvuta hewa ya kutosha.


Waliendelea kunimiminia maji mengi usoni, nikajaribu kufurukuta bila mafanikio, mapafu yangu yakaanza kusumbuka kutafuta hewa safi ya oksijeni lakini sikufanikiwa kirahisi.


Kwa kweli yalikuwa mateso makali sana, hivyo nikaanza kutapatapa huku taratibu nguvu zikiniishia mwilini, hali yangu ikazidi kuwa mbaya zaidi na mwishowe nikahisi mapigo yangu ya moyo yakianza kudorora.


Nilijaribu kufungua kinywa changu ili niwaambie wasitishe yale mateso lakini sikufanikiwa. Kwa mbali nikasikia sauti kutoka kwa Madame Pamela akiwataka waache kunimiminia yale maji na hapo mateso yale yakasitishwa.


Kisha sikuweza kusikia kitu kingine chochote kilichokuwa kikiendelea eneo lile.




________




Nilikurupuka baada ya kuminywa kwa nguvu tumboni, hivyo kufanya nitapike maji niliyokuwa nimeyanywa wakati nikimiminiwa maji mengi usoni, nikaanza kuhema kwa nguvu huku maumivu makali yakizidi kusambaa mwilini. Nilikuwa nimelowa chapachapa kufuatia yale maji niliyomwagiwa.


Wale makomandoo walikuwa wamesimama mbele yangu wakinitazama kwa makini na hapo nikagundua kuwa haukuwa umepita muda mrefu tangu nilipopoteza fahamu zangu hadi kuzinduka.


Nikiwa bado nashangaa nikashtukia Madame Pamela akinimwagiwa ndoo nzima ya maji baridi ambayo yalinipa uchangamfu kiasi fulani mwilini, kisha aliwaambia wale makomandoo waninyanyue na kuniketisha kwenye kiti cha umeme.


Nikawashuhudia wale makomandoo wakininyanyua kwa nguvu na kunikalisha juu ya kile kiti cha umeme kilichokuwa kikitumika kuwasulubu watuhumiwa hatari mle ndani ya kile chumba cha mateso huku mikono na miguu yangu ikifungwa pingu.


Madame Pamela alinisogelea na kusimama mbele yangu huku akinitazama kwa makini. Niliitupia jicho saa yake ya mkononi alipokuwa amenisogelea na hapo nikagundua kuwa ilikuwa inaelekea kuwa saa kumi na moja ya alfajiri.


Hapo nikaanza kuuona mwisho wangu ulikuwa karibu mno kuliko nilivyofikiria, hata hivyo nilimuomba sana Mungu aniepushe na kifo kile cha mateso.


Hadi kufikia muda ule sikutaka tena kuamini kuwa ningeweza kutoka salama ndani ya lile jengo, kwani ni dhahiri kuwa waliamua kuniua baada ya kuona nimeshindwa kuwapa taarifa walizokuwa wakizihitaji, ambazo kiukweli sikuwa nazo.


Nilianza kumuwaza mchumba wangu Susan na mwanetu Pamela, hivi watakuwa na hali gani baada ya kugundua kuwa sipatikani na wala hakuna taarifa zozote kunihusu tangu nilipofika jijini Dar es Salaam kutoka Amsterdam?


Vipi kama nitakufa, je, watakabidhiwa maiti yangu au ndiyo nitatupwa kwenye kiroba na kifo changu kubaki siri? Dah! Nilijiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa sana…


“Brown, sema ukweli vinginevyo utakufa kifo cha mateso makali sana,” alisema Madame Pamela na kunizindua kutoka kwenye mawazo.


“Mtaniua bure, sina kitu chochote ninachokijua,” nilisihi huku machozi yakinilengalenga machoni kisha nikashindwa kujizuia, nikaanza kulia kwa uchungu.


Nililia kilio cha kwikwi na hatimaye nikalia kwa sauti kubwa. Kilio changu hakikuwa cha kutaka nihurumiwe bali kilikuwa kilio cha hasira kutokana na kusingiziwa jambo ambalo sikulifanya. Pia kilikuwa kilio kutokana na njaa na mateso ambayo binadamu mwenye afya ya kawaida asiye na mazoezi lazima angekuwa amekwishakufa.


Madame Pamela alinitazama kwa makini lakini hakutaka kuamini chochote katika maneno yangu. Alinikazia macho huku uso wake ukiwa umebadilika na kuwa mbali na mzaha. Hakuwa tena akitabasamu kama mwanzo.




Nililia kilio cha kwikwi na hatimaye nikalia kwa sauti kubwa. Kilio changu hakikuwa cha kutaka nihurumiwe bali kilikuwa kilio cha hasira kutokana na kusingiziwa jambo ambalo sikulifanya. Pia kilikuwa kilio kutokana na njaa na mateso ambayo binadamu mwenye afya ya kawaida asiye na mazoezi lazima angekuwa amekwishakufa.


Madame Pamela alinitazama kwa makini lakini hakutaka kuamini chochote katika maneno yangu. Alinikazia macho huku uso wake ukiwa umebadilika na kuwa mbali na mzaha. Hakuwa tena akitabasamu kama mwanzo.


Endelea...


Nilitishika sana, kilichonitisha ni kuwa Madame Pamela alisifika kama ‘mwanamke wa chuma’ baada ya kuongoza kikosi cha kuwahoji watuhumiwa wa matukio ya ugaidi waliohusishwa na kundi la Al Shabab, matumizi ya mbinu zake za kuhoji watuhumiwa zilivyokuwa za kipekee, mbinu za ukatili na utesaji za kuwaweka watuhumiwa kwenye maji, kuwakosesha usingizi, kuwapiga na kila aina ya ubabe ili kupata siri.


“Una uhakika kuwa huna unachokijua?” sauti ya Madame Pamela ikanizindua tena kutoka kwenye lindi la mawazo.


“Kwanini niongope? Ningefahamu ningekwisha waambia kuliko adha hii ya mateso,” nilisema huku nikiendelea kulia kilio cha kwikwi.


Madame Pamela alinitazama kwa kitambo kirefu kisha nikamuona akimwonesha mmoja wa wale makomandoo ishara fulani kwa kichwa.


Yule komandoo alitoka haraka na baada ya kitambo kifupi alirudi akiwa ameongozana na makomandoo wengine wawili ambao pia walikuwa wamevaa kombati za rangi ya hudhurungi na kofia nyekundu za bereti.


Mbele yao walikuwa wamemtanguliza mwanamume mmoja ambaye sikuweza kumfahamu mara moja, walimleta na kumsimamisha mbele yangu. Yule mwanamume alinitazama kwa makini na kuonekana kushtuka sana.


Niliinua uso wangu kumtazama kwa makini yule mwanamume ambaye alionekana mnyonge sana. Alikuwa mwanamume mfupi mnene na mweusi aliyekuwa amevaa shati la kitenge lililodariziwa vizuri shingoni kwa nyuzi za njano, ingawa lile shati lilikuwa limeanza kupauka.


Alivaa suruali nyeusi ya kitambaa na miguuni alikuwa na sendoz nyeusi za ngozi. Umri wake ulikuwa kati ya miaka arobaini na tano na hamsini hivi kutokana na mwonekano wake na alikuwa na ndevu nyingi zilizokuwa zimeuzunguka mdomo wake.


Nikahisi kuwa haikuwa mara yangu ya kwanza kumuona yule mwanamume, ila nilimuona wapi? Wakati nikitafakari ili kukumbuka nilikokutana na yule mwanamume mara nikakumbuka kuwa nilimuona kwenye moja ya picha nilizooneshwa kule kwenye chumba cha mahojiano cha uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.


“Unamfahamu huyu mtu mbele yako?” Madame Pamela akaniuliza huku akiwa amenikazia macho.


“Simfahamu,” nikajibu mara moja nikionesha kuwa na uhakika na lakini jibu langu, hata hivyo jibu hilo halikuonekana kumridhisha Madame Pamela. Aligeuka kumtazama yule mwanamume.


“Unamfahamu huyu mtu aliyekaa mbele yako?”


“Ndiyo, madam, namfahamu,” alijibu yule mwanamume mfupi.


“Unamfahamu kivipi?” Madame Pamela akauliza tena huku akimkazia macho yule mwanamume mfupi.


“Namfahamu kwa jina la Godwin Sengerema, ni mfanyabiashara wa madini, mwanzoni sikujua kuwa asili yake ni Rwanda ingawa yeye aliniambia kuwa ni Mtanzania halisi mwenyeji wa Mwanza…” alisita kidogo na kunitazama kwa wasiwasi.


“Elezea kila kitu unachokijua kuhusu huyu mtu, vinginevyo na wewe utaonja joto ya jiwe!” alifoka Madame Pamela kiasi cha kumfanya yule mwanamume mbele yangu aanze kutetemeka.


“Kwa kweli sikujua kama huyu bwana ndiye mhusika mkuu wa lile tukio la uporaji wa pesa katika Benki ya Wananchi, ambayo mimi nilikuwa meneja, ni yeye aliyesuka mikakati yote namna ya kufanikisha wizi ule…” alisema yule mwanamume.


“Hebu nieleze ukweli, mista meneja, na ole wako ukijaribu kuficha kitu… maana kuficha ni kujichongea…” alisema Madame Pamela na kunyamaza kidogo huku akimkazia macho yule mwanamume mfupi, ambaye sasa nilitambua kuwa ndiye Lister Manda, meneja wa Benki ya Wananchi.


“Ni wewe uliyempa taarifa zote za namna pesa zinavyohifadhiwa pale benki?” Madame Pamela alimuuliza yue meneja wa Benki ya Wananchi.


Mwanamume yule alionekana kunywea sana, alibaki kimya huku akimtazama Madame Pamela kwa unyonge mno.


“Jibu swali wewe!” mmoja wa wale komandoo aliingilia kati huku akimsukasuka mgongoni yule meneja.


“Hata sijui alizipataje, madam, ingawa baadaye na mimi nilimweleza,” yule meneja alijibu kwa sauti ya unyonge huku akitazama kando.


“Kwani mlikuwa mnafahamiana?” Madame Pamela alizidi kuhoji.


“Hapana, nilikuwa simfahamu na tuliwasiliana kwa simu tu. Ilitokea kuwa yeye alikuwa na taarifa zangu ingawa sikujua alizipata wapi, siku moja alinipigia simu na kunitaka nitekeleze mpango wake huku akitishia kuwa angetoa siri zangu na kuniharibia maisha yangu endapo nisingeonesha ushirikiano,” alisema yule meneja kwa uchungu na kuendelea.


“Alisema hata nikitoa taarifa polisi bado asingefanywa kitu na angeniharibia zaidi kwa kuwa anao mtandao mkubwa wa viongozi serikalini, jeshini na hata wafadhili waliopo nje ya nchi, hivyo nikawa sina namna ya kufanya,” alisema yule meneja huku akilengwa na machozi.


“Siri zako zipi alizotishia kutoa?” Madame Pamela aliuliza akiwa amemkazia macho yule meneja.


Yule meneja alibabaika kidogo na kutazama kando huku akifuta machozi.


“Ni siri zipi hizo?” Madame Pamela alizidi kumhoji yule meneja.


“Ni kama nilivyoeleza mwanzo kwenye maelezo yangu, siri za kujihusisha na masuala ya kishirikina,” alijibu kwa unyonge.


“Hebu kuwa muwazi, ushirikina kivipi?”


“Mauaji ya albino.”


“Okay, kisha ikawaje?”


“Nikawa sina namna nyingine ya kufanya isipokuwa kushiriki kwa kuwa aliahidi kunilinda endapo kungetokea lolote na ningepata mgawo mkubwa wa pesa.”


“Unaweza kunikumbusha, kiasi gani kiliibiwa?”


“Zaidi ya dola milioni tatu za Marekani ambazo ni mabilioni ya shilingi.”


“Baada ya wizi ule wewe ulipata mgawo wa kiasi gani cha pesa?”


“Dola laki mbili na ushee ambazo ni sawa na shilingi milioni mia tano, lakini sikuwa peke yangu kwenye mgawo, walikuwepo wengine ambao mimi sikuwafahamu.”


“Sasa kama hukuwahi kukutana naye umejuaje kuwa ni yeye aliyekuwa nyuma ya mpango wote?” Madame Pamela akamuuliza.


“Nilimjua kupitia mwanamke wake aliyeitwa Jasmine, kabla ya hapo nilimfahamu kama mmoja wa wateja wa benki yetu na nakumbuka kuwa kuna wakati alikuja ofisini kwangu mara mbili kama mteja wa kawaida wa benki ambaye alitaka kujua utaratibu wa utoaji mikopo. Sikuweza kufahamu kama ndiye mtu niliyekuwa nawasiliana naye kwenye simu, na namba alizokuwa anatumia hata ukizifuatilia huwezi kujua ni za nchi gani.


“Kwa kweli ilikuwa vigumu kabisa kumdhania huyu bwana kama ndiye aliyekuwa akipanga mipango yote ile kutokana na tabia yake ya upole, ucheshi na ustaarabu, niliamini kuwa bosi wa matukio haya angekuwa mtu tofauti kabisa, kuna wakati alikuwa kama mzuka, alitembea kutokana na kubadilika kwa majira na angeweza kukufuata popote uendapo bila wewe kujua, kama akiamua kufanya hivyo. Na mbaya zaidi, sisi wenyewe tulioshirikishwa wengi wetu tulikuwa hatujuani wala kumjua zaidi ya kusikia sauti yake tu… na zipo tetesi kuwa ndiye aliyewaunda hata wale watoto waliokuwa wakijiita Panya Roads,” alisema yule meneja.


Duh! Maelezo ya yule meneja yalisababisha nihisi mwili wangu ukifa ganzi, moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu na kijasho chembamba kikaanza kunitoka mwilini.


“Zipo taarifa kuwa hata wewe ulishiriki katika matukio ya kigaidi, unaweza kutueleza washirika wengine ni kina nani?” Madame Pamela alimuuliza yule meneja.


“Hapana madam, mimi sijui lolote kuhusu huo ugaidi,” yule meneja aliruka kimanga.


“Wakati mwingine mnapotuona tupo kimya si kwamba hatujui kinachoendelea bali tunakuwa tunafanya kazi, na hizi taarifa si tu ni confidencial au secret bali ni top secret, hivyo hatujakurupuka,” alisistiza Madame Pamela.


Yule meneja aligwaya na kuanza kutetemeka.




Duh! Maelezo ya yule meneja yalisababisha nihisi mwili wangu ukifa ganzi, moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu na kijasho chembamba kikaanza kunitoka mwilini.


“Zipo taarifa kuwa hata wewe ulishiriki katika matukio ya kigaidi, unaweza kutueleza washirika wengine ni kina nani?” Madame Pamela alimuuliza yule meneja.


“Hapana madam, mimi sijui lolote kuhusu huo ugaidi,” yule meneja aliruka kimanga.


“Wakati mwingine mnapotuona tupo kimya si kwamba hatujui kinachoendelea bali tunakuwa tunafanya kazi, na hizi taarifa si tu ni confidencial au secret bali ni top secret, hivyo hatujakurupuka,” alisistiza Madame Pamela.


Yule meneja aligwaya na kuanza kutetemeka.


Endelea...


“Ni kweli madam, mimi sikushiriki na wala siwajui hao washirika wa matukio ya ugaidi. Ni kweli huyu bwana alinishawishi lakini nilimkatalia.” alijitetea yule meneja.


“Muongo mkubwa, sijawahi kukutana na huyu mtu,” nilisema kwa hasira baada ya kushindwa kuuvumilia ule uongo, nilikuwa nimesingiziwa sana kiasi kwamba sikufahamu hata nijitetee vipi.


“Anajaribu kujitetea tu ili kuficha ukweli, muulizeni vizuri awaeleze watu alioshirikiana nao kwenye wizi wa benki lakini siyo mimi,” niling’aka kwa hasira lakini kibao kimoja cha usoni kutoka kwa Madame Pamela kikanifanya nione vimulivuli machoni.


“Utanisamehe sana Godwin, sina namna nyingine isipokuwa kusema ukweli, ni mara ngapi ulinifuata lakini nilikukatalia?” aliniambia yule meneja kisha akageuka kumtazama Madame Pamela.


“Yote ninayayosema hapa ni ya kweli kabisa, madam, sina sababu ya kumsingizia mtu,” alisisitiza yule meneja na kuniacha nikiwa mdomo wazi kwa mshangao usioelezeka.


“Mista meneja, una mke?” Madame Pamela alimuuliza yule meneja huku akiwa amemtulizia macho yake usoni.


“Ndiyo, na watoto watatu,” aliongea yule meneja kwa utulivu huku akimtazama Madame Pamela kwa huzuni.


“Utaipa shida familia yako,” Madame Pamela alisema huku akimtazama kwa umakini zaidi na kutingisha kichwa chake.


“Lakini mimi sikuhusika kabisa kwenye tukio la ugaidi, wala sijui lolote, madam,” alizidi kujitetea huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Sijasema kuwa lazima wewe unahusika au unajua lolote kuhusu ugaidi, lakini nina kila sababu ya kuamini kwamba kama umeweza kushiriki kwenye wizi mkubwa wa benki unashindwaje kushiriki kwenye ugaidi wakati mratibu wa mikakati hiyo ni mtu yuleyule!”


“Madam, naomba uniamini, kama ni wizi wa benki ni kweli nimeshiriki lakini siyo ugaidi…”


Madame Pamela alimpuuza yule meneja kisha alitoa ishara fulani wale makomandoo waliokuwa wamekuja na yule meneja wa Benki ya Wananchi kuwa waondoke naye na mara nikawaona wakimchukua yule meneja na kuondoka naye na kutuacha watatu mle ndani.


Madame Pamela akanitazama kwa makini kwa kitambo kirefu akionekana kama aliyekuwa akifikiria jambo fulani.


“Sasa tueleze vizuri, Brown, washirika wenzako katika ugaidi ni kina nani na wako wapi, na silaha mlizopora mmezificha wapi?”


“Sijui kwanini hamtaki kuniamini? Ningekuwa najua ningewaambia, kwanza hali yangu imeshakuwa mbaya sana,” nililalamika kwa sauti dhaifu.


“Hatutajali kuhusu kifo chako, ikiwa hutaki kusema ukweli ni lazima utakufa tu,” alisema Madame Pamela huku mzaha ukiwa mbali na yeye.


“Basi niueni tu kama hilo ndilo kusudio lenu, sina kingine cha kueleza,” nilisema kwa hasira huku nikiwa nimekwisha kata tamaa ya kuishi. Nilikwisha anza kujihesabu kuwa mfu.


Madame Pamela alinitazama kwa kitambo na mara nikaliona tabasamu pana likichanua usoni kwake, kisha akanichapa kofi la nguvu lililonifanya kupoteza fahamu kwa sekunde kadhaa na kujiona kama vile nilikuwa naelea angani.


Kisha akasogea kwenye swichi fulani iliyokuwa ukutani jirani na kile kiti na kugeuza shingo yake kunitazama akiwa amekunja uso wake.


“Hii ni nafasi yako ya mwisho, sema washirika wenzako wako wapi na silaha mlizopora ili kutekeleza uhalifu wenu mmezificha wapi?”


Nilifumbua mdomo wangu ili niongee lakini maneno yakawa hayatoki kwa sababu sikuona niongee nini kipya ili niaminike, mara akili yangu ikakumbuka jambo moja tu, kuomba toba kwa Mungu anisamehe makosa yoyote niliyowahi kuyafanya.


Katika maisha yangu sikuwa mtu wa kusali wala kwenda kanisani, hivyo nilijiona ni mtu mwenye hatia kubwa.


Nilianza kuomba Mungu na wakati huo kidevu changu kilikuwa kimeanguka kifuani kwangu, msirimbi wa kipaji cha uso wangu uliumuka, milizamu ikatutusika chini ya masikio yangu kama iliyopulizwa, shingo yangu ikavimba na mara michirizi ya machozi ikapasuka machoni mwangu.


Kwa kweli nilishindwa kujizuia hivyo nikajikuta nikianza kulia kwa sauti, nikalia japo nilijaribu kuyazuia machozi yasitoke lakini nilishindwa.


Madame Pamela aliniangalia kwa mshangao mkubwa kwa kitambo, kisha akashusha pumzi.

ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog