Search This Blog

Thursday, 23 March 2023

MSAKO - 4

Simulizi : Msako

Sehemu Ya : Nne (4)

“Lakini kufuatia hali kuwa ngumu na tete, nchi hizi zote isipokuwa Iran, Iraq, Saudia na Urusi zimekubaliana kuunganisha nguvu ila kwa sharti moja kuwa apatikane jasusi mmoja ambaye ataendesha operesheni hii. Hakuna Jasusi aliyepewa taarifa ya makubaliano hayo. Ila ili kumpata Jasusi mmoja atayeendesha operesheni hii kwa niaba ya nchi saba, yaani, China, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Japan, Ujerumani, na Italia, imeamuliwa kuwa lazima afanikiwe kuwaua majasusi wangine waliokuwa wametumwa na nchi zao”

“Pili, mtu pekee ambaye anaweza kuhatarisha mpango huu ni mpelelezi Jacob Matata. Ndiyo maana mikakati mizito inafanyika ili kummaliza. Marekani, licha ya kuingia kwenye mpango huu lakini ukweli ni kuwa haikuwa imeleta Jasusi yeyote, hivyo tukaombwa tutafute mtu wa kufanya hiyo kazi. Hapo ndipo unapoingia wewe. Majasusi wengine wameshaanza kutafutana, jina lako na taarifa zako wanazo kwa hivyo na wewe utakuwa unawindwa. Ila tuna taarifa kamilifu za mienendo za majasusi wengine isipokuwa mpelelezi Jacob Matata.” Alisema Ngongoseke.

“Sikiliza Bwana Poka Kingu, una siku chache sana, nne tu, kufanya kazi ambayo imefanya wewe utolewe kule shimoni ulikokuwa. Ukimpata Jacob Matata, uko huru na hakutakuwa na kumbukumbu ya maisha yako na mikasa yako ya nyuma, ila ukishindwa unajua nini maana yake. Lazima utatafutwa na kuuawa...” Ngongoseke alisema kwa sauti ya taratibu huku akitengeneza tai yake.

“Nitamtafuta hata bila malipo, nilikuwa naitafuta sana hii nafasi. Muda ni mfupi sana kumtafuta mtu kama Jacob Matata, ila nitajitahidi kufanya kazi ndani ya muda huo. Kama ulivyosema, nikimuua niko huru nikishindwa siko huru, huo ndiyo ukweli. Maana mtu pekee ambaye akijua niko huru na anaweza kunitafuta na kunitia nguvuni ni Jacob Matata pekee. Hii inamaanisha uhuru wangu ni kifo chake na kinyume cha hapo ndiyo hivyo.” Alisema Poka Kingu

“Kwa kusema hivyo, ina maana kuanzia sasa najua napigania uhuru wangu na wala sifanyi kazi yenu, pesa zenu sizihitaji kuliko uhuru wangu. Nikiupata uhuru wangu najua pesa si shida kwangu.” Alisema Poka Kingu huku akivuta mkupuo wa kahawa.
“Hivi hapa ni vifaa vya kuanzia kazi.” Alisema huku akisukuma kwa mguu boksi la mbao lililokuwa sakafuni.

“Sihitaji, kwani ulinipa vifaa wakati nafanya operesheni ya ile ndege?!’’ Alijibu Poka Kingu huku akiminya vidole vyake ambavyo vilitoa mlio mkavu kama vijiti vikavu vinapovunjwa kwa pamoja.
“Acha utani. Au umemsahau Jacob Matata?’’ Ngongoseke alisema.
“Mwili wangu ni zaidi ya silaha, fundi hukuta silaha uwanja wa vita.” Alisema kwa kujiamini.
“Sawa, faili lako litaharibiwa mara tu tutakaposikia kifo cha Jacob Matata.” Ngongoseke alisema, kisha akamkabidhi Poka Kingu kifurushi kilichokuwa na pesa. Pesa za kigeni na shilingi.

“All the best!’’ Ngongoseke alisema.

“https://jamii.app/JFUserGuide you!” Pako alisema huku akitembea taratibu kutoka kwenye hiyo nyumba. Alitembea kwa kuchechemea.

Ngongoseki alibaki anamwangalia, halafu akajisemea; Shetani kaingia kazini!

Imetungwa na kuandikwa na Japhet Nyang’oro Sudi

Saa tatu na nusu juu ya alama watu watatu walikuwa ndani ya chumba. Watu hao ni Bi. Anita, Jacob Matata na Waziri mkuu, Silas Kiondo.

Pwaaa! Faili lilitupiwa mezani.

Faili hilo lilikuwa na jina Msako.

“Mwandishi wa faili hili ni Inspekta Msaidizi wa Polisi Lucas Mwenda ambaye ameuwa jana asubuhi kisha faili lake likaharibiwa kama utakavyoliona. Lucas Mwenda alikuwa akiongoza timu upande wa Jeshi la polisi, iliyokuwa ikisaka mtu anayehusika na mauaji ya Sabodo Msumari. Lakini kwa vile mambo yamepandana ilibidi timu yake iguse kwa kiasi kikubwa kutoweka kwa Judith Muga na pia kuanguka kwa ile ndege iliyokuwa na wale wataalam wa mambo ya gesi toka makampuni ya Magharibi. Faili hili kama unavyoliona, limefutwafutwa na karatasi nyingine zimeloana au zimelowekwa kwenye kitu ambacho inaaminika kuwa ni maji ili lisiweze kusomeka. Maiti ya Inspekta Lucas Mwenda ilikutwa daraja la Sarenda. Faili hili lilikuwa Kituo cha Polisi cha Msimbazi. Inaonyesha kuwa askari huyu alikuwa amefanikiwa kupata fununu fulani kuhusiana na mambo haya, ndiyo maana kumuua tu haikutosha ila wameharibu na faili alilokuwa akilitumia. Kwa sababu hii, Mkuu wa Kituo cha Polisi na watu wote waliokuwa zamu katika muda unaodhaniwa faili hili liliharibiwa wamewekwa chini ya ulinzi mkali sana, kupisha na kusaidia uchunguzi. Kama ukitaka kuwahoji tutaarifu tu” Ndiyo alivyoanza kuongea mhe. Silas Kiondo. Waziri mkuu.
Akamwangalia Jacob, kuona kama nafuatilia alichokuwa akisema.

Halafu ikawa zamu ya Bi. Anita kutoa maelekezo.
“Kama tulivyokuambia hapo awali, hiki ni chumba chenye mafaili yenye siri nzito za nchi. Ni watu wachache sana hapa nchini wanaojua kilipo na matumizi ya chumba hiki ambacho huitwa SAFE HOUSE. Watu wanaojua chumba hiki kina nini na umuhimu wake, hawafiki wane. Hata walinzi wanaokuja kulinda hapa hawajui umuhimu wa chumba hiki. Lakini kutokana na umuhimu wa suala lililoko mbele yetu tumefikiria namna ya wewe kuweza kujua historia hii kwa kina na tumeona hatuna njia nyuingine zaidi ya kukuleta kwenye hiki chumba. Tutakufungia humu”

“Awali tulitaka kulitoa hili faili na kukuletea. Lakini kwa hali ilivyo sasa hakuna namna tunaweza kutoa hili faili ndani ya chumba hiki. Tulitaka kutoa nakala ya ziada ya faili hili na kukuletea, lakini bado tukaona si salama sana kwako na nchi pia. Hivyo bwana Jacob Matata, ndani ya chumba hiki kuna mafaili zaidi ya elfu tatu lakini tunataka usome mafaili kumi na saba. Mafaili haya kumi na saba yako kwenye kabati lile pale. Kutokana na taarifa tulizonazo, kabati hilo lina mafaili ambayo tunahisi yatakuwa yanahusiana kwa namna moja ama nyingine na tukio hili. Lakini pia, tumekuwekea kitabu kimoja cha riwaya kiitwacho Patashika, ambacho kiliandikwa na mwandishi Japhet Nyang'oro Sudi. Utashangaa kitabu cha riwaya kinaingia namna gani kwenye mkasa huu. Ila kitabu hicho kina kisa ambacho upelelezi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha yatokeayo sasa yana muunganiko toka kwenye matukio ya kitabu hicho.” Alisema Bi. Anita mkuu wa Kitengo cha ujasusi - Ofisi Fukuzi. Kitengo hicho kilichosheheni vijana hatari wenye mafunzo ya juu katika ujasusi, upelelezi na kupigana.

“Kukuwezesha wewe kukaa humu wiki nzima huku ukifanya uchambuzi huo tumeona tukuwekee kila kitu. Kama nilivyosema hakuna mtu ajuaye juu ya nyumba hii zaidi ya watu wanne katika serikali. sasa wewe utakuwa mtu wa tano. Tutakuja hapa baada ya wiki na tutajua namna ya kuanza upelelezi mzito wa kumsaka huyo anayefanya matukio haya ya kutisha yanayohatarisha usalama wa taifa letu. Kama utagundua lolote wakati wowote ambalo unadhani haitakuwa na haja ya wewe kuendelea kukaa humu basi utanitaarifu kwa mawasiliano haya. Utachukua hiki kifaa kisha utaminya namba 00001111 utanipata. Hii ni secure line” Bi. Anita alisema. Halafu akamkabidhi Jacob kifaa Fulani kidogo kama kiberiti, kikiwa na batani zenye namba. Jacob Matata alikipokea na kukitupia juu ya meza. Kukawa kimya kwa muda.

“Jacob, najua wiki moja kwako inaweza kukufanya usome na kutafakari vitu ambavyo askari hata wapelelezi wengine wa kawaida wangetumia miezi sita kuvisoma, kuvielewa na kupembua ukweli uliko ndani ya kule kuelewa. Chukulia suala hili kwa uzito mkubwa. Kama ulivyosema, imetosha kwa washenzi wa magahribi kutaka kutuchezea. Imetosha, hebu tuwazime na kuwashikisha adabu. Kuna mengine siwezi kukuambia moja kwa moja, ila jua kuwa Taifa linatikisika hivi sasa. Rais, Mhe. Jovin Sekendu anaishi kwa wasiwasi mkubwa. Inabidi tumtafute yeyote aliyeko nyuma ya mpango huu” Bi. Anita alisema kwa uchungu. Maneno ambayo yaliuchoma moyo wa Jacob Matata na kumfanya awe tayari kwa kazi.

Baada ya hapo, waziri mkuu na Bi. Anita walimuaga mpelelezi Jacob Matata, ambaye angebaki ndani ya nyumba ile kama walivyosema.

“Nitajitahidi kufanya linalowezekana, japo naona jambo lenyewe limejifungafunga sana na muda wake ni mchache. Tuombe heri.” Jacob alisema huku macho yake yakiwasindikiza wakuu hawa waliokuwa wakitoka. Wote wawili walitembea kutoka mle chumbani huku Jacob Matata akiwa amesimama, mkono wake wa kushoto ukiwa umeshikilia lile faili. Walitoka mlangoni na wa mwisho kutoka alikuwa Mhe. Silas Kiondo, ambaye kabla hajafunga mlango nyuma yake aligeuka akamwangalia Jacob Matata, macho yao yakakutana.

"Jacob.."Mhe. Silas Kiondo aliita. Jacob akanyanyua kope kabla ya kusema, "Mkuu".

"Fanya kazi yako kwa makini, taifa hili linategemea sana matokeo ya kazi yako. Binafsi nimefurahi kuonana na wewe nimekuwa nakusikia tu." Waziri alisema, hakusubiri jibu la Jacob Matata.

Riwaya hii inaitwa MSAKO Imetungwa na kuandikwa na Japhet Nyang’oro Sudi

"Fanya kazi yako kwa makini, taifa hili linategemea sana matokeo ya kazi yako. Binafsi nimefurahi kuonana na wewe nimekuwa nakusikia tu." Waziri alisema, hakusubiri jibu la Jacob Matata.

***************

Mpelelezi Jacob Matata hakutaka kupoteza muda, alielewa kuwa safari hii alikuwa katika mazingira tofauti ya kazi. Pia alikuwa kama askari wa mwamvuli ambao hudondoshwa katika eneo la vita ambalo limetekwa na adui. Hakuwa na muda wa kupoteza, kasi, umakini na shabaha vilitakiwa kuwa kwenye kiwango cha juu.

Aliketi mezani na kuanza kusoma faili ambalo alikuwa amekabidhiwa. Aliamua kufanya hivyo kwanza ndipo ahamie kwenye kabati aliyokuwa ameonyeshwa, lenye mafaili kumi na saba. Baadae angesoma kitabu Patashika cha mwandishi Japhet Nyang'oro Sudi.
Alipoanza kusoma lile faili alishangazwa na jambo moja, sehemu kubwa ya karatasi zake zilikuwa zimefutwa kwa kupakwa rangi au kulowekwa kwenye maji. Hivyo hadi anamaliza kuangalia na kupekua lile faili alijikuta ameweza kuambulia sentensi chache sana ambazo hakuona kuwa zingeweza kumfikisha popote. Katika sentensi hizo chache moja ilisomeka kwa lugha ya kiingereza ....First Eleven..... maneno mengine kwenye ukurasa huo yalikuwa yamefutwa makusudi kabisa kwa rangi na kalamu ya Marker Pen.

Kipande kingine cha maneno kwenye karatasi moja ya kijani kilisomeka .... Upanga NHC nyumba namba 41A....... sentesi hii aliipata baada ya kufunua karatasi 11 zilizokuwa zimefutwa katika kitini kilichokuwa kimeandikwa kwa mkono.

Akiwa anaendelea kupekua lile faili akakutana na sentesi iliyokuwa imekoswakoswa kufutwa. Ilionyesha mfutaji alikuwa akifuta kwa haraka. Sentensi ilisomeka ....nikamuuliza Afande kuhusu Luteni wa Jeshi Fran.........akanionya...... Baada ya maneno hayo likafuata pori la karatasi zilizoharibiwa hadi alipofika sehemu alipokutana na vimaneno vichache tu visivyosomeka wala kueleweka. Neno la mwisho aliloambulia kwenye faili hilo lilisomeka ...Kitab.....ch..Patashika....Japhet...

Mpelelezi Jacob Matata alilibwaga chini lile faili. Lakini, ghafula, kama aliyekumbuka kitu alilichukua tena. Alipekua hadi mwishoni kabia mwa faili. Kulikuwa na karatasi ndogo sana ya njano. Aliiangalia kwa makini. Kulikuwa na maelezo kuhusu mwandishi wa faili hilo ambaye sasa alikuwa marehemu. Hivyo karatasi hio haikuwa na jipya

Si kawaida ya mpelelezi Jacob Matata kuandika maelezo. Alifundishwa na kujizowesha kuweka kila kitu kichwani. Lakini mara hii alijikuta anachukua karatasi na kalamu. Akaandika kwa namna ya orodha yale maelezo machache aliyokuwa ameyapata kwenye lile faili. Aliandika;
…Upanga NHC nyumba namba 41A..
…First eleven..
...nikamuuliza Afande kuhusu Luteni wa Jeshi Fran............. akanionya.....
....Kitab..... ch.. Patashika....Japhet...
Jacob alijikuta akirudiarudia kusoma hizi sentensi maelezo. Huku akijaribu kuunganisha mambo. Hakuweza kupata chochote cha maana kwenye maelezo hayo.

Alitumia muda wa siku uliobaki kusoma mafaili mengine kwenye kabati aliloelekezwa. Ilimchukulia muda mwingi, huku akijitahidi kuandika maelezo mafupi alipoona inahitajika. Usiku ulipokuwa mkubwa, alikuwa amechoka. Aliamua kulala halafu asubuhi ndiyo angesoma kitabu Patashika.

* * *

Asubuhi ilipofika, ilimaanisha siku nyingine ilikuwa imeshaingia. Akiwa ameshajiandaa, amekaa mezani kuanza kusoma kitabu Patashika mara wazo lilimjia. Alikumbuka kuwa wakati amelala alihisi kama kulikuwa na mtu amemtembelea mle chumbani. Hakuwa na hakika kama ilikuwa ndoto ama la, lakini alikuwa mzito sana kuweza kuamka usiku huo. Hakuwa na namna ya kuthibisha kama kweli ama zilikuwa hisia zake au njozi. Hilo akalitupilia mbali na akazama katika kusoma kitabu. Katika kitabu hicho Patashika, yeye ndiyo alikuwa mpelelezi mkuu. Kwa sababu hiyo haikumchukua muda mrefu sana kukisoma. Maana sehemu ambazo yeye alihusika aliona hakukuwa na haja ya kuzisoma sana. Lakini alitoa nakala ya vipande vichache kwenye kitabu hicho ambavyo alidhani vinahitaji uchunguzi na kuunganishwa na matukio mengine ambayo yanaweza kuunganisha na kinachotokea sasa. Alitoa nakala sehemu kama tano. Halafu akaandika tena kwenye kile kidaftari chake alipoandika zile sentensi tano za mwanzo. Alikitupia pembeni kitabu, pale alipokuwa amelitupia faili la Afande Lucas Mwenda. Sasa akaanza kupekua tena lile kabati lenye mafaili kumi na saba.

Ilimchukua saa zaidi ya kumi na mbili kusoma, akichunguza maandishi na kulinganisha matukio katika maandishi hayo. Ilikuwa kazi yenye kuchosha na iliyohitaji utulivu mkubwa. Saa sita na dakika arobaini na tisa usiku ndipo mpelelezi Jacob Matata akaamua kulala. Kulala kwenyewe ilikuwa ni sakafuni.

Akiwa amelala, kama ilivyokuwa usiku uliopita, alihisi kama kuna mtu anatembea kwenye chumba alichokuwemo. Usingizi ulimwacha taratibu. Akafungua macho taratibu. Kweli aliona kivuli cha mtu akiwa pale alipokuwa ameweka daftari alilokuwa akiandika maelezo yake madogo na nakala chache alizokuwa ametoa kivuli toka kwenye kitabu Patashika. Mtu huyo alionekana kuwa na tochi ndogo sana kama kalamu, alikuwa akisoma kwenye daftari. Jacob Matata hakutegemea kukabiliana na hali kama ile. Hasa ikizingatiwa kuwa aliambiwa kuwa sehemu hiyo ilikuwa ya siri sana na ilijulikana na watu watano tu.
Sasa huyu nani?
Anatafuta nini?
Kaingiaje humo ndani bila yeye Jacob Matata kujua? Hayo pamoja na maswali mengi yalifumuka kichwani kwake.

Toka alipokuwa amelala Jacob Matata hadi pale alipokuwa huyo mtu ilikuwa kama hatua tatu hivi. Hivyo alipiga hesabu za harakaharaka. Akajikohoza kidogo kama vile yuko usingizini. Yule mtu aligeuka akamwangalia Jacob, ambaye bado alijifanya amelala. Kuona hivyo, yule mtu akapata wasiwasi, akachukua zile nakala ambazo Jacob alikuwa amezitoa kivuli toka kwenye kitabu. Akaanza kusoma. Halafu akawa na kifaa kama kamera ndogo mfano wa kiberiti akaanza kupiga picha zile karatasi.
Kwa kasi sana, lakini akiwa amechukua tahadhari zote, Jacob Matata alikurupuka na kurukia pale alipokuwa yule mtu. Akamkumba wote wakaanguka chini.
Jamaa akawa wa kwanza kuamka akamzibua Jacob Matata teke la mbavu. Jacob akaangukia upande mwingine. Kuona hivyo yule jamaa akataka kukimbilia ulipokuwa mlango wa kutokea nje ya kile chumba. Jacob alijibiringisha kwa kasi akamkumba yule mtu. Safari hii tena jamaa alikuwa wa kwanza kusimama. Lakini badala ya kumshambulia Jacob Matata aliingiza mkono mfukoni haraka, akatoa ile kamera ndogo kama kiberiti akaibamiza chini. Ikatawanyika vipandevipande. Jacob tayari alikuwa ameshasimama. Alimtandika teke la mgongoni, nguvu ya lile teke ikamzoa na kumpeleka chini. Baadaye akampa vipigo vingine vitatu, jamaa akalegea. Wakati Jacob Matata anaenda kuwasha taa ili aweze kuongea na huyo mtu ghafla alisikia jamaa akikoroma.
"Alinimbia nisijaribu kupambana na wewe....nakufa.....!’’ Jamaa alisema kwa sauti ya taabu. Macho yake yalionyesha dhahiri kuwa hakuwa na muda mrefu wa kuishi.

Jacob aliweza kuona hilo maana alikuwa ameshawasha taa. "Nani kakwambia!?’’ Jacob alifoka huku akijitahidi kumtingisha . Lakini haikusaidia kitu, maana sekunde chache baadae jamaa alikuwa ameshakufa huku povu likimtoka kinywani.

Hilo halikuwa geni kabisa kwa Jacob, mara moja akajua kuwa yule mtu alikuwa amejiua kwa kutafuna vindonge vya sumu viitwavyo ‘L-Pill’ yaani, ‘Lathel Pill’ ambavyo huwa vidogo sana kama punje ya mchele. Vidoge hivyo hutengenezwa kwa kuta nyembamba sana za kitu kama chupa ambayo hufunikwa kwa mpira mwembamba sana wa plastiki ya rangi ya damu ya mzee. Mpira huo huzuia uwezekano wa kupasuka kwa bahati mbaya. Maana majasusi wengi hubeba kidonge hicho kwa kukiweka chini ya ulimi muda wote wanapokuwa maeneo ya hatari ambayo wanahisi wanaweza kukamatwa muda wowote. Kile kichupa kidogo ndani ya kimfuko chembamba cha mpira hujazwa mchanganyiko mkali sana wa ‘potassium cyanide’ vitu hivi kwa pamoja ndiyo hutengenezea hicho kidonge. Vingine huwa na ukubwa wa jino na hupachikwa kwenye pengo na kuonekana kama jino la bandia. Kama jasusi akikimeza kwa bahati mbaya toka chini ya ulimi, basi kitapita bila madhara na kutolewa nje kwa njia ya haja kubwa. Kile kichupa chembamba kilicho funikwa na mpira mwembamba sana hufanya ile sumu ya ‘potassium cyanide’ iliyoko ndani ya kile kichupa kutotoka na kufanya madhara. Ili kutumia kile kidonge, jasusi au mpelelezi atatakiwa kuking'ata ili kipasuke, ndipo ile sumu hufanya kazi. Kinapopasuliwa kile kidonge na kuiachia sumu iliyoko ndani yake mambo mawili hufanyika; ndani ya dakika moja ubongo hufa kabisa halafu muda mfupi baadae moyo huacha kufanya kazi. Ndicho kilichofanyika kwa huyu jamaa.

Jacob alisonya kwa hasira.

"Pumbavu sana! Nani aliyemwambia hawezi kupambana nami?’’ Jacob alisema kwa hasira. Harakaharaka alikagua mifuko ya yule mtu. Kwenye moja ya mifuko yake aligusa kitu, alipotoa, macho yalimtoka pima.
Ilikuwa ni kidole cha mtu.

Alimwangalia yule mtu aliyekufa kuona kama alikuwa hana kidole kimoja, akidhani kuwa mtu huyo alikuwa amekatika kidole. Alikuta ana vidole vyote kamili. Jacob Matata alikiweka mfukoni kile kidole. Kilikuwa cha baridi kama soseji iliyotoka kwenye jokofu.

Kutoka na tukio hilo, Jacob Matata hakulala tena. Alishahisi kuwa maisha yake yalikuwa hatarini. Akiwa bado anafikiria mara alisikia kama kishindo cha mtu akija kwenye chumba alichokuwepo. Alinyata taratibu kuelekea kwenye upenyo fulani uliokuwa ukienda vyumba vingine vya nyumba hiyo. Aliendelea kunyata hadi alipofikia mlango wa chumba kimoja ambao alikuta kitasa chake kimeharibiwa vibaya. Aliona risasi kadhaa zikiwa sakafuni chini ya mlango huo, hivyo akajua kuwa kitasa kile kilikuwa kimefumuliwa kwa risasi. Pia, ikaja akilini mwake kuwa bastola iliyotumika ina kiwambo cha kuzuia sauti na risasi zake zinaonyesha ni bastola aina ya Automatic 45. Aliusukuma mlango wa kile chumba taratibu sana, hadhari ikiwa kwenye kiwango cha juu mno. Mapigo ya moyo yakienda kasi. Alikuwa katika hali ya kupambana na tayari kwa lolote.

Mlango ulipofunguka mpaka kiasi cha yeye kuweza kuchungulia, badala ya kuchungulia akiwa amesimama alipiga magoti chini kisha akachungulia kwa kwa namna kuwa jicho liweze kuona lakini sehemu kubwa ya kichwa ibaki nyuma. Hakukuwa na kitu chumbani humo zaidi ya boksi moja la mbao lilikuwa limesambaa vipande vipande sakafuni.

Aliamua kusimama, alisimama bila kufanya kelele. Aliusukuma ule mlango hadi ulipotoa nafasi ya mwili wake wa wastani kuweza kuingia. Alitanguliza mguu, kisha kiuno halafu kichwa kikafuata. Sasa aliweza kukiona chumba vema. Sakafuni kulikuwa na nyayo za viatu zilizoacha alama ya damu. Inaonyesha mtembeaji alikuwa amekanyaga damu mahali.

Imetungwa na kuandikwa na Japhet Nyang’oro

Mlango ulipofunguka mpaka kiasi cha yeye kuweza kuchungulia, badala ya kuchungulia akiwa amesimama alipiga magoti chini kisha akachungulia kwa kwa namna kuwa jicho liweze kuona lakini sehemu kubwa ya kichwa ibaki nyuma. Hakukuwa na kitu chumbani humo zaidi ya boksi moja la mbao lilikuwa limesambaa vipande vipande sakafuni. Aliamua kusimama, alisimama bila kufanya kelele. Aliusukuma ule mlango hadi ulipotoa nafasi ya mwili wake wa wastani kuweza kuingia. Alitanguliza mguu, kisha kiuno halafu kichwa kikafuata. Sasa aliweza kukiona chumba vema. Sakafuni kulikuwa na nyayo za viatu zilizoacha alama ya damu. Inaonyesha mtembeaji alikuwa amekanyaga damu mahali.
Lakini alama ile ya viatu ilimkumbusha kitu na mtu. Ile ni alama ya viatu maalum ambavyo huvaliwa na mtu mmoja maalum sana aitwaye Poka Kingu. Lakini wazo hilo alilisukumia mbali, alipojikumbusha kuwa Poka Kingu alikuwa kwenye gereza ambalo angeozea huko.
Alisogelea kwenye vipande vya mbao vilivyokuwa sakafuni. Aliona kitu kama karatasi, aliposogea aliona vema, ilikuwa karatasi. Aliinama akaiokota, ilikuwa imeandikwa kwa mkono maandishi ya herufi kubwa yaliyosomeka KISANDUKU CHA TAARIFA- KSD067MZ. Hakuchelewa kujua kuwa boksi lililovunjwa lilikuwa na kisanduku cheusi kidogo cha kurekodia taarifa ya ndege. Akaziangalia tena zile namba KSD067MZ, akakumbuka kuwa zilikuwa namba za ile ndege iliyoanguka hivi karibuni ambayo kwa mujibu wa Bi. Anita kuna kila dalili kuwa ndege hiyo ilihujumiwa.
“Damn!, Poka Kingu kafikaje hapa?’’ Jacob Matata alinong’ona kwa sauti kiasi.
“Weka chini Jacob Matata. Ulidhani nitafia gerezani wakati bado kuna watu wananihitaji.” Sauti ilisikika nyuma yake.

“Nani akuhitaji mtu kama wewe Poka?’’ Jacob alisema taratibu huku akiwa anainama kuweka bastola chini. Hakuhitaji kuambiwa tena.

Alimjua vema Poka Kingu. Alijua anauwezo wa kufanya nini kwa namna gani. Jacob Matata aliamini kuwa inawezekana yeye ndiye mtu anayemjua vema huyu mtu-mnyama binadamu kuliko watu wengine. Kwa vile ameshakutana naye mara kadhaa na kupambana naye mara nyingi.

Jacob hakutegemea kukutana na mtu kama Poka kwa wakati huu na mazingira haya. Katika mara zote walizowahi kukutana ushindi kati yao huamuriwa na bahati na fursa za nadra sana wala si suala la mtu kuzidiwa nguvu.

“Utashangaa nikikuambia watu haohao wa serikali ndiyo wanaonihitaji. Kwani wadhani watu wote wa serikali ni wapenzi wa watu kama wewe Jacob Matata?’’ Poka alisema kwa jeuri, kisha akaongeza, “Kuna huduma wazitakazo gizani ambazo mtu kama wewe huwezi wapa na ndiyo maana hawakuona mtu wa thamani kwao kama mimi kuozea gerezani wakati naweza kuwafanyia kazi zao kwa ufanisi kuliko wewe. Safari hii sidhani kama bahati iko upande wako Jacob Matata. Unajua vema kuwa kati yangu mimi na wewe nisuala la bahati tu wala si ufundi. Mara ya mwisho bahati ilikuwa yako, lakini kwa kutaka sifa badala ya kuniua ukajifanya kunikabidhi kwa watu wanaojiita wa usalama. Nilijua umekosea lakini nisingeweza kukushauri vinginevyo kwa vile niliona unacheza na bahati na wahenga walishasema bahati haiji mara mbili....” Poka Kingu aliongea kifedhuli.

“Mwenye bahati haba....” Jacob hakuwahi kumalizia kauli yake aliruka upande wa kushoto. Poka alimimina risasi upande wa kulia. Mara hii tena Jacob alitumia kumbukumbu kucheza mchezo, mara tano zote walizowahi kukutana, Poka amewahi kumteka Jacob Matata mara tatu na Jacob Matata amewahi kumteka nyara Poka mara mbili. Mara zote ambazo Jacob amekuwa akitaka kuponyoka amekuwa akirukia upande wa kulia. Hivyo Jacob Matata alishajua kuwa kwa kiwango cha Poka Kingu angeshasoma namna Jacob anavyoruka. Hivyo alitegemea Poka angewahi kulia, lakini yeye sasa amecheza na bahati na nafasi karuka kushoto.

Hata hivyo haikuchukua hata sekunde kwa Poka kujua Jacob ameshabadili hali ya chumba hivyo akajiweka sawa kwa mpambano.
“Shenzi Jacob leo lazima tu utakufa!’’ Poka alisema huku akiruka juu.
“Misanya kahifadhi hilo boksi, lakini usilipeleke kwa mwajiri” Poka alipiga kelele wakati anatua pale alipokuwa Jacob Matata. Bila shaka alikuwa akiwasiliana na mmoja watu aliokuwa nao. Alipotua, ilibidi Jacob atumie mbinu ya ziada kuchezesha kiuno na kufanya teke la Poka kupita inchi chache sana kutoka kwenye kiuno chake. Teke lile likaishia kupalaza mkanda wa suruali wa Jacob Matata. Kama lingempata teke lile lingemtengua kiuno. Jacob alizungusha shingo kwa kasi na kuangalia jinsi Poka alivyotua, alijirusha chini na kuvingirika kama tairi akamkumba. Poka, kwa kutumia mikono akajisukuma toka sakafuni na kuangukia upande mwingine, halafu akasimama haraka na kumpa Jacob teke la mgongoni. Jacob alijigeuza haraka na kuachia kifuti cha mkono ambacho kilitua mgongoni kwa Poka.

Sasa wakawa wanatazamana.

Poka akaingia kwa karate mbili za ufundi wa hali ya juu, Jacob ikabidi abonyee kwa kupiga magoti halafu akaruka kwa upande. Poka akajivuta jirani zaidi na Jacob lakini akapoteza hesabu kidogo jinsi alivyoweka mguu wake wa kushoto, Jacob akaona hilo kosa, kosa la fundi hugunduliwa na fundi tu, Jacob aliuchota ule mguu, Poka akaenda chini. Kuona hivyo Jacob Matata akajisogeza na kumpa kisigino cha nguvu kifuani, Poka akapumua kwa fujo. Akajiviringisha kama tango lililodongoka sakafuni, Jacob akamfuata kwa kasi. Lakini wakati akiendelea kuzunguka Poka alikuwa akisoma hatua za Jacob, hivyo alipoona yuko karibu kiasi cha kutosha alisimama ghafla na sasa akawa jirani zaidi na Jacob nyuso zikitazamana. Poka alikuwa akitokwa na damu mdomoni, kutokana na kile kisigino alichopewa na Jacob kifuani. Poka alitumia ule ukaribu kwa usahihi, alimpiga Jacob kichwa kikavu cha usoni. Looh, kichwa kilipigwa kifasaha, kasi na uzito sahihi Jacob akaona nyota. Akapoteza umakini, Poka akaona hilo kosa. Akafyatua teke kali lililomrusha Jacob Matata, halafu hata kabla Jacob hajatua chini, Poka akawa ameshafika anamgonja. Ilibidi Jacob ajikunje kama nyoka kukwepa kisigino kilichokuwa kimesukumwa na Poka kwa lengo la kuvunja shingo yake. Alisimama haraka, wote walikuwa wanapumua kwa fujo. Ni ajabu hakuna aliyekumbuka kuwa kuna bastola zilikuwa sakafuni, kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzie. Poka alijisogeza ukutani kisha akainama kuashiria kuwa wabadirishe aina ya mapigano. Jacob Matata alikubali kwa kuonyesha ishara hiyo pia. Wakawa tayari, lakini mara wakasikia vishindo vya watu.

Poka alikuwa wa kwanza, aliruka kwa namna ya ajabu kuelekea mlangoni. Kuona hivyo Jacob yeye aliparamia dirisha la chumba akalifungua haraka. Akarukia nje, wakati huohuo akasikia milio ya risasi ikirindima upande wa ndani.
“Kwa herini, acha Poka awaonyeshe kazi!’’ Jacob alisema wakati akipotelea vichakani. Aliweza kuona magari kadhaa yakiwa na taa zinazomweta mweta juu, akabaini kuwa wale walikuwa ni askari. Bado Jacob Matata alikuwa na mshangao. Kuvamiwa kwenye eneo kama hilo aliona ni sawa na kuingiliwa na nyoka chumbani, kitandani kwako.

Akatokomea maana hakutaka shari na askari ambao sasa walikuwa wakirusha risasi ovyo baada ya kuona maiti eneo lile.

“Kwa herini, acha Poka awaonyeshe kazi!’’ Jacob alisema wakati akipotelea vichakani. Aliweza kuona magari kadhaa yakiwa na taa zinazomweta mweta juu, akabaini kuwa wale walikuwa ni askari. Bado Jacob Matata alikuwa na mshangao. Kuvamiwa kwenye eneo kama hilo aliona ni sawa na kuingiliwa na nyoka chumbani, kitandani kwako. Akatokomea maana hakutaka shari na askari ambao sasa walikuwa wakirusha risasi ovyo baada ya kuona maiti eneo lile.

*********************

"MAKAMANDA, nitasoma hii taarifa kama ilivyoletwa hapa na jopo la wataalam. Kama tulivyoomba, tumeletewa upembuzi juu ya ile nyumba iliyovamiwa kule porini” Alianza afisa huyu mwenye wasifa mkubwa jeshini.
“Kamanda, labda kabla hujaendelea sana, ni vema kikao hiki kikaambia ile nyumba ina kazi gani? Afisa mwingine aliuliza.
“Naomba kuwasilisha taarifa hii juu ya nyumba hiyo halafu juu ya huyu mtu aitwaye Jacob Matata. Baada ya kumaliza kusoma bila shaka tutaijadili na kuulizana maswali." Alisema afisa huyo.
"Taarifa inasema; Safe House au nyumba ya Hazina kama wengi tunavyoiita, ni nyumba inayoaminiwa kuwa na mafaili ya kihistoria na siri kubwa na nyingine zenye utata mkubwa. Uwepo wa nyumba hiyo na mahali ilipo imekuwa fumbo kwa muda mrefu sana. Ila sasa imebainika kuwa iko katika msitu mdogo wa Mabwepande ulioko katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Hadi jana, kaba ya tukio lilochukua maisha ya askari wetu watano, ni watu watano tu katika nchi hii ndiyo waliokuwa wakijua kuwa nyumba hiyo ndiyo Safe House. Wengi tumekuwa tukijua kuwa katika nchi hii kuna safe house lakini hakukuwa na hakika kuwa nyumba hiyo ilikuwa wapi. Kama ilivyo kawaida kuwa serikali huagiza Jeshi la Polisi au Jeshi la Ulinzi kutoa ulinzi sehemu nyingi ambazo hudhaniwa kuwa zinahitaji ulinzi. Mara nyingine jeshi huwa haliambiwi ni kwa nini sehemu fulani imeombewa ulinzi na sababu kubwa ambayo ukipewa huwezi kuuliza zaidi ni lile jibu lisemalo ni kwa usalama wa nchi. Afisa ukishaambiwa ni kwa usalama wa nchi basi, ulinzi hutolewa kwa sehemu au mtu husika. Kwa jinsi jengo hilo lilivyojengwa si rahisi mtu kuweza kuingia bila msaada wa hao watu watano wanaojua kuwa nyumba hiyo ni safe house. Watu hao ndiyo pekee ambao vidole gumba vyao ndiyo funguo za kila mlango katika nyumba hiyo”

“Imebainika kuwa, Jacob Matata aliingizwa humo juzi asubuhi kwa sababu alikuwa amepewa kazi maalum ndani ya nyumba hiyo. Kazi hiyo inahusiana moja kwa moja na jitihada za kutafuta ukweli juu ya kutoweka kwa Judith Muga yule mtaalam wa mambo ya gesi, kuanguka kwa ndege iliyokuwa imebeba wataalamu wa mambo ya gesi ambao walikuwa wamemaliza kazi ya kuchunguza na kupima kiwango cha gesi. Lakini pia kuuawa kwa waziri Sabodo Msumari kulisababisha Jacob Matata apewe kazi . Hivyo inasemekana na kuna mambo Jacob Matata alitakiwa kuyasoma na kisha kuyafanyia kazi katika jitihada za kujua chanzo cha mauaji haya na mtu aliyeko nyuma ya mauaji haya!!

“Leo asubuhi, iligundulika kuwa mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo ulikuwa wazi huku miili ya walinzi wawili ikiwa nje, wakiwa wamekufa. Baada ya kuingia ndani, imegundulika kuwa hakuna faili hata moja lililoibiwa, hakuna uharibifu mwingine uliofanyika. Sakafuni kwenye chumba ambacho Jacob Matata alitakiwa kufanyia kazi, kulikuwa na maiti nyingine mbili, ambazo inaonyesha muuaji hakutumia siraha ya aina yeyote kutekeleza mauaji. Haijulikani walinzi hao waliingiaje ndani ya nyumba hiyo na kwenda kwenye chumba alichokuwa Jacob Matata”

“Lakini pamoja na maiti hiyo kulikuwa na vipande vya kitu kilichovunjwa vunjwa, baada ya kukichunguza kitu hicho, wataalamu wetu wamejiridhisha kuwa kitu hicho ni ‘Vig - Spy AV Camera’ ambayo ilirekebishwa na kupewa uwezo wa kutuma taarifa mara mtumiaji anapofanikiwa kupiga picha au kurekodi tukio.Wanasema kamera hiyo huwa na ukubwa wa kiberiti. Hivyo kwenye kamera hiyo hakukuwa na kitu chochote cha maana. Haijulikani kama kamera hiyo ilikuwa ikitumiwa na Jacob Matata au yule mlinzi. Lakini vyovyote iwavyo katika mazingira waliyokuwepo hakuna hata mmoja aliyetakiwa kuwa na kamera kama ile, muda na mahali kama pale. Kingine kilichokutwa sakafuni ni kitabu cha riwaya kiitwacho Patashika kilichoandikwa na Mwandishi Japhet Nyang'oro”
ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog