Search This Blog

Thursday, 23 March 2023

HUJUMA NZITO - 5

  

Simulizi : Hujuma Nzito

Sehemu Ya : Tano (5)

Hivyo wakati anaoga bafuni Ngwenyama yupo dirishani anafuta vumbi la madirisha habari hana. Hamadi weeh Ghafla bin Vuu, Catherine akawa anatoka kuoga akiwa amevaa kanga moja tu nyepesi ya Mombasa huku imemnatia mwilini na kulichora vilivyo umbile lake lenye mvuto wa aina yake.

Alikuwa ana umbo lenye kumtetemesha kiimani hata yule Mchamungu mwenye vilemba saba kichwani kama tu atakubali pepesi na tashwishi ya macho yake kushuhudia maajabu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

Catherine alikuwa hana hili wala lile amejitawala chumbani mwake, anajikausha maji mwilini sasa akiwa mtupu kama alivyozaliwa akiwa amelipa mgongo dirisha analosafisha Shamba-Boi wao huku akitikisa makalio yake yenye umbile la kifuu cha nazi kimadoido.

Ngwenyama alibaki mdomo wazi huku ameganda pale dirishani kama amenaswa na umeme. Macho yake aliyakodoa upeo wa mwisho wa kuyakodoa bila kufumba macho asije akapoteza fursa hiyo adhimu na ya bure ya kutalii mwili wa mtoto wa Kibosile wake, Catherine.




Catherine alikuwa hana hili wala lile amejitawala chumbani mwake, anajikausha maji mwilini sasa akiwa mtupu kama alivyozaliwa akiwa amelipa mgongo dirisha analosafisha Shamba-Boi wao huku akitikisa makalio yake yenye umbile la kifuu cha nazi kimadoido.

Ngwenyama alibaki mdomo wazi huku ameganda pale dirishani kama amenaswa na umeme. Macho yake aliyakodoa upeo wa mwisho wa kuyakodoa bila kufumba macho asije akapoteza fursa hiyo adhimu na ya bure ya kutalii mwili wa mtoto wa Kibosile wake, Catherine.

Alipomaliza kujikausha maji mwilini, akiwa bado hajavaa libasi yoyote ile kugeuka tu wakakutanisha macho yao ana kwa ana na Ngwenyama. Catherine akapatwa na mshtuko na kupiga kelele za uoga hakutegemea tukio kama hilo la kupigwa chabo dirishani.

Haraka haraka akakimbilia mahali ilipo kanga yake na kujifunga mwilini. Lakini alipogeuka bado akamkuta amenasa pale dirishani kama ndege aliyenasa kwenye ulimbo anamsubiria mtegaji wake aje kumnasua.

"Ngwenyama wewee...! Ngwenyama wewe...! Mbona una tabia za kishenzi, kishamba na mbovu za kuchunguliana madirishani. Akija mama nakusemea mwanahizaya mkubwa wewe, akufukuze kazi" alilalama Catherine kwa hasira.

Sauti hiyo ndio ikamzindua toka kwenye mfadhaiko huo hakujibu kitu chochote na moja kwa moja akatupa chini kitambaa cha kusafisha madirisha na kuondoka zake kurejea chumbani mwake.

Catherine safari ya kanisani ikaota mbawa alikuwa anaona aibu sura yake ataitundika wapi akikutana nae uso kwa uso. Ilipofika majira ya adhuhuri wakati wa mlo wa mchana, Catherine akamuuliza dada wa kazi kama Ngwenyama ametoka siku ya leo. Jibu lilikuwa ni kuwa toka asubuhi hajatoka na hata chai hajanywa anasema ameshiba.

Catherine moyo wa huruma ukamtembelea na kuanza kujilaumu kwa nini hata alimtolea lugha ya kebehi na matusi kiasi kile. Huenda amekasirishwa na lugha nilizomtolea hasa ikichukuliwa alikuwa anampenda sana.

Majira ya Alasiri ikabidi Catherine akimbilie dukani akanunua kadi za mapenzi kuomba msamaha huku akichora makopakopa mengi kuonyesha anampenda. Akaenda kuitumbukiza chini ya mlango wa chumba cha Ngwenyama.

Lakini mbinu hiyo haikusaidia kitu mpaka wakati wa usiku wakiwa wanapata mlo wa chajio kwa ajili ya kujiandaa kulala bado kijana wa watu alikuwa hajatoka chumbani mwake. Catherine tayari alishapanda kitandani akiwa amevalia nguo yake nyepesi ya kulalia, lakini usingizi ulipaa kabisa.

Alikuwa anamuwaza Ngwenyama. Akajikuta uzalendo unamshinda anasimama toka kitandani mwake na kufungua mlango wa nyumba kubwa kimya kimya ili dada wa kazi asishtukie dili. Akaenda mpaka chumbani kwa kwake na kugonga mlango. Aligonga sana mpaka akakaribia kukata tamaa ndio akafunguliwa.

Akaingia chumbani mule huku ameinamisha macho chini kwa aibu. Ngwenyama alikuwa amevaa bukta fupi nyeupe na singlendi nyeupe yupo pekupeku. "Unataka nini?, sema shida yako, nataka kulala" aliongea kwa hasira bila kujua anazidi kuziumiza hisia za Catherine.

"Nimekuja kukuomba msamaha, kwa maneno makali yasiyo na adabu za ukumbi niliyokuropokea asubuhi. Nisamehe kwa kuumiza hisia zako, nakupenda sana sipendi kukuona ukiteseka mpaka unasusa kula kwa ajili yangu!" aliongea Catherine huku mashavu yake yakiwa yamelowana kwa mvua ya machozi iliyokuwa inanyesha kutokea machoni mwake.

Hakuna mkate mgumu mbele ya chai ya mkandaa, kijana wa watu alishalegea. Sasa ilikuwa ni muda wa kupindua meza kibabe, matusi na kebehi za asubuhi aliyotukanwa na Catherine ilikuwa ni wakati wa kuizungumzia kesi hiyo, kwenye mahakama ya samadari ya fundi seremala. Kwa jinsi umbile la Catherine lilivyojichora kwenye vazi lile la kulalia, Ngwenyama akajikuta anamvamia Catherine na kumtupa kwenye kizimba cha mahakama tayari kwa kuanza kesi.
Kilichofuatia hapo ikawa ni historia tena, kesi ilihukumiwa usiku kucha.

Kulipopambazuka Catherine aliwahi kurejea chumbani kwake kabla hata dada wa kazi hajaamka bado.
Majira ya Alasiri wazazi wa Catherine wakawa wamerudi tayari. Ngwenyama na Catherine ikawa ndio mwanzo na mwisho wao wa kukutana kimwili, huku Catherine akiwa ndio kavunjwa kizinda chake na Ngwenyama kwa mara ya kwanza tokea aingie duniani.

Baada ya wiki moja tu kupita akaanza kujihisi hali isiyo ya kawaida. Kichefuchefu, kizunguzungu na hata kutapika wakati mwingine. Akaanza kuogopa kuwa huenda amenasa mimba lakini mawazo hayo nilikuwa anayafukuza na kuyalaani kichwani mwake kwa nguvu zote. Mama yake hakufanikiwa kumgundua mpaka alipoenda kubambwa shuleni kuwa ni mjamzito.

Kumbukizi ilipofika hapo pa kufukuzwa shule akaanza kulia kwa kwikwi Catherine, hasa akifikiria kama angesoma huenda angekuwa mtu mkubwa sana serikalini au hata kuwa mtu muhimu katika jamii ya Watanzania. "Mamaaaa....Mamaaa...una nini? Mbona umeniamsha huniambii kitu halafu unaanza kulia tu!" Asante-Rabbi alimgutusha mama yake kutoka kwenye lindi la mawazo.

"Nisamehe mwanangu kwa kukuficha miaka mingi sana, Baba yako ni Mnyasa wa Malawi anaitwa Ngwenyama. Tunamfahamu kwa jina moja tu hilo hilo na hata sifahamu yupo wapi. Alikuwa ni mfanyakazi wetu hapa nyumbani!" Catherine alijikaza kisabuni akafuta machozi akamwaga upupu wa maneno kwa Asante-Rabbi ajiwashe mwenyewe.

Asante-Rabbi akaendelea kumdodosa mama yake kwa maswali lukuki mpaka akajiridhisha. Kulipokucha akarejea zake shuleni huku akiweka nia ya kumsaka baba yake pindi atakapopata fursa.
Alipomaliza kidato cha nne kama kawaida yake akawa kinara tena kwenye matokeo ya kitaifa. Furaha yake Babu yake akaamua kuvunja kibubu chake cha mafao kumpeleka nchini Uingereza kwa masomo ya kidato cha tano na sita mpaka Chuo Kikuu.

Huko nchini Uingereza ndiko alipokutana na Dr.Pius Chilembwa wote wakiwa wanasoma Chuo Kikuu kimoja. Asante-Rabbi alipofahamu Dr.Pius Chilembwa naye ni Mnyasa kama yeye alivyo akajiona ni zaidi ya ndugu kwake. Ndipo Kapteni Wandawanda baba mlezi wa Dr.Pius alipozidi kuwaunganisha na kuwapa fikra zake hadi za kulifuta jina la Tanzania na kuisimamisha Dola ya Nyasa kupitia sanduku la kura ili kukwepa vikwazo vya Umoja wa Afrika "AU" kama wangefanya mapinduzi ya kutumia silaha.

Hivyo akawapa kazi ya kuketi pamoja na kubuni kwa kutumia elimu zao, waje na mpango mkakati wa kupata pesa za kuendesha harakati hizo za kuisimamisha Dola ya Nyasa "Nyasa Empire". Wakati Wanachuo wenzao wanaosoma nao Uingereza toka nchini Tanzania, kwenye muda wao wa ziada walikuwa wanautumia kwenye starehe na kutalii nchi mbalimbali za Ulaya ili wapate picha na simulizi za kuja kuringishia wenzao wakirejea nyumbani, wao Asante-Rabbi na Dr. Pius Chilembwa walikuwa wanajifungia ndani, wakisugua bongo zao, wanapanga mikakati ya kuichukua nchi pindi wakimaliza masomo yao.

Waliporejea nchini, Asante-Rabbi akaajiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mhadhiri katika idara ya Uhandisi wa Kompyuta huku Dr Pius Chilembwa akirejea Benki Kuu kama Mchumi Mwanadamizi. Mpango wao ulipokamilika kwa ajili ya utekelezaji, Asante-Rabbi akaacha kazi ghafla akiwa tayari ni Profesa na kwenda kujichimbia nchini Afrika ya Kusini. Huko akawa anakula pensheni yake tu huku akisubiria mpango wa kusimamisha Ufalme wa asili ya Baba yake na Babu zake usimame Tanzania.

Ufalme ambao utawapa Wanyasa wote kutembea kifua mbele na hadhi yao kuwa juu sio hadhi ya kufanya kazi za nyumbani tena.
Baada ya miaka mitano tokea kuacha kazi kwa Profesa Asante-Rabbi kupita, ndipo nae Dr Pius Chilembwa akaandaa igizo la kifo chake nchini Afrika ya Kusini. Sasa Kachero Manu ndio alipata fursa ya kwenda kuonana na Profesa Asante Rabbi ambaye sasa anaitwa Professor Potchefstroom.




SURA YA KUMI NA MBILI

Kachero Yasmine alizinduka majira ya saa 1:30 asubuhi mwanana, huku miale ya jua lisiloumiza ikianza kupenya kwenye dirisha la chumba alichohifadhiwa. Kichwani alikuwa amezungushiwa bandeji nzito kuzunguka kichwa chote. Bandeji ambayo ilikuwa na matone ya kutosha tu ya damu, iliyotonwa kutoka kwenye mishipa yake ya damu ya kichwani.

Alipotupa macho yake pembeni akaliona dripu la damu linashuka mwilini mwake huku pembeni yake kukiwa na meza chakavu iliyokuwa imetapakaa madawa mbalimbali na vifaa tiba kama sindano, pamba, mikasi na vifaa vinginevyo. Kilikuwa ni chumba kizuri wastani wake si haba ingawa kilikuwa bado hakijaisha vizuri matengezo yake.

Ukuta wa chumba hicho ulikuwa haujapigwa plasta wala juu yake kuwekwa silingibodi. Aliona taa ya Mchina ya kuchaji ndio inaangaza mwangaza mle ndani kuonyesha hamna umeme. Alipoendelea kutupa macho zaidi akaona buti za jeshi pea kama mbili na sare ya jeshi la wananchi JWTZ imetundikwa mlangoni.

Hofu ikaanza kumtawala mwilini mwake huku akishangaa na kuanza kujiuliza kuwa "yupo wapi hapa alipo na amefikaje hapo!". Akaanza kuvuta hisia ya kumbukizi kujua alipatwa na maswaibu gani mpaka ameletwa humo. Akaanza kuhisi maumivu makali sana ya kichwa yalioanza kumbangua vilivyo.

Ghafla akiwa ndani ya lindi la mawazo akaanza kusikia sauti ya ufunguo unagombana na kitasa mlango. Baada ya sekunde kadhaa mlango ukawa upo wazi akaingia mama mmoja wa makamo, amevalia sare nyeupe. Kwa muonekano ni nesi wa kike akiwa amebeba mkoba wake. Alipoingia moja kwa moja akaja pale alipo Kachero Yasmine na kumsalimia.

"Umeamkaje? pole sana kwa maumivu!" aliuliza nesi yule kwa uso wa bashasha. Kachero Yasmine akajibu kwa ishara ya kichwa kuwa yupo vizuri na kujilazimisha kutabasamu. Hakutaka kumuonyesha sana kuwa ana nguvu maana alikuwa hajui yupo wapi na kwa madhumuni gani ameletwa hapo.

"Usiwaze sana, pumzika ili mwili upate nguvu yake kwa haraka. Haya nataka nikuchome sindano ya kupunguza maumivu na itakupa usingizi muruwa". Akazungumza yule nesi na kuelekea juu ya ile meza akautua mkoba wake. Akaufungua na kutoa chupa za dawa mbalimbali. Akaanza kuchanganya michanganyiko yake kisha akaivuta dawa kwenye sindano yake kisha akaanza kumjongelea tena mgonjwa wake na kumdunga sindano ya kwenye kalio la kushoto. Alipomaliza kazi yake iliyomleta chumbani mule, akafungasha virago vyake na kuondoka zake.

Kachero Yasmine baada ya matibabu yale aliyopewa, akapitiwa tena na usingizi mzito raundi ya pili uliomlaza kwa zaidi ya saa sita mpaka majira ya adhuhuri alipozinduka toka usingizini. Alishaanza kupata nguvu kabisa, alijeruhiwa kichwani tu ambapo tatizo kubwa lilikuwa ni upotevu wa damu. Sasa kumbukumbu zake zilianza kurejea vizuri kabisa. Akakumbukia mtiririko wote wa matukio mpaka akapigwa kiti cha kisogoni na mahasimu wake.

Kilichokuwa kinamtatiza ni je bado ametekwa na mahasimu zake au yupo kwa msamaria mwema. Maana alishangaa hamna ulinzi wowote uliowekwa dhidi yake wa kumdhibiti asitoroke. Na kama kweli yupo kwa msamaria mwema kwanini asingempeleka hospitalini anampa tiba za vichochoroni anakwepa nini?. Hayo yalikuwa ni maswali yanayomtatiza Kachero Yasmine. Akawa anatamani kweli akutane na huyo msamaria mwema wake.
Adhuhuri hiyo hiyo akaletewa chakula na yule nesi, akakipiga kisawasawa kutokana na ubao aliokuwa nao. Yule nesi alipoondoka zake na kufunga mlango wa chumba, akaamka kitandani na kuanza kusogelea dirishani ili achungulie mandhari ya nje ya chumba.

Macho yake yakakaribishwa na fensi kubwa yenye urefu wa zaidi ya meta saba za waya imara, nyuma ya fensi hiyo kulikuwa na msitu mzito ulioshonana miti yake wenye nyasi ndefu, huku kwa mbali zikisikika sauti za ng'ombe wakiswagwa malishoni.

Pia sauti za ndege ndio zilikuwa kiburudisho kitamu masikioni mwake, huku akiwaona wakiruka toka mti mmoja kwenda mwingine kwa madoido. Bila kuwasahau tumbili nao walikuwa wanajivinjari katika uwanja wa nyumbani. Kwa ufupi yalikuwa ni mazingira ya porini sana sio Mjini kabisa.

Akaanza kuzunguka mle chumbani kuona huenda atakuta kitu chochote zaidi ya hizi pajama nyepesi za wagonjwa alizovikwa hakukuta chochote. Akajua ameshapoteza kila kitu chake kuanzia simu ya mkononi, funguo ya gari lake, bastola yake, flashi ya kuhifadhia nyaraka zake, mpaka nguo zake.

Alichoshukuru Mungu yupo mzima na hajabakwa kama walivyotia nia wale maadui zake. Maana kama wangemla mande sasa ingebidi apelekwe ANGAZA kwenda kupima kama ameambukizwa virusi vya UKIMWI au laa. Akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuzidi kumpigania huku akishukuru kitabu chake cha uradi wa “Yasin Mubin” aliousoma pale Sinza huenda unemuokoa na majanga yote hayo.
Baada ya utalii huo mfupi akarudi zake kitandani na kuketi yake huku akianza kutafakari namna ya kuchomoka chumbani mule. Alijua tu gari yake ataikuta tu salama pale maegesho nje ya yale maduka ila itabidi akafuate ufunguo wa akiba nyumbani. Ila kilichokuwa kinamtatiza kuwa akitoroka ataelekea wapi maaana hajui yupo Mkoa gani na sehemu gani ya nchi.

Pia hana hata senti tano nyeusi mfukoni yupo yeye kama yeye, atafikaje nyumbani kwake?. Akafanya maamuzi magumu kuwa liwalo na liwe lakini hawezi kukubali kulala tena usiku mwingine, ni upotevu wa muda tu atatoroka na kujua huko huko msituni kitu cha kufanya mpaka akatakavyojiokoa.

Akaanza kukumbukia suluba waliozokuwa wanazipata porini enzi yupo kwenye mafunzo ya ukomandoo, jinsi walivyokuwa wanapambana na wanyama wakali wa mwituni lakini alifanikiwa kumaliza mafunzo hayo kwa usalama. Mafunzo ambayo yalimjengea ujasiri wa mapambano bila uoga kwa binadamu wa sampuli yoyote ile.

Mpaka majira ya magharibi yanaingia na kuanza kuyoyoma zake kwa kuukaribisha usiku mbichi wa saa usiku, bado hakuna mtu yoyote aliyekuwa amekuja tena kwenye kichumba kile. Tumboni bado alikuwa yupo vizuri hana hisia za njaa kabisa kwa sababu mlo alioletewa adhuhuri ulikuwa kabambe kwelikweli. Hivyo tatizo halikuwa njaa, ila alichokuwa anahitaji ni kujua yupo wapi na amehifadhiwa hapo kwa minajiri gani.

Akanyanyuka tena na kwenda kuwasha taa ya kuchaji iliyopo mezani hivyo nuru ikaanza kuenea ndani ya chumba. Kisha akasogelea dirishani tena, macho yake yakapokewa na kiza kizito na sauti za wadudu wa usiku wa porini. Kwa mbali sana akawa anasikia sauti za mbwa kubweka ovyo, akaanza kufurahi.

Zilikuwa ni dalili ya kuwa sehemu hiyo sio mbali na maeneo wanayoishi watu hivyo hatopata shida kupata msaada pindi akitoroka. Wakati anapanga mipango ya namna atakavyotoroka akasikia sauti ya gari linavuma kwa nguvu kukaribia uelekeo wa kwenye chumba alichohifadhiwa.
Kachero Yasmine akakimbilia mpaka kwenye mlango na kuchungulia kwenye tundu la ufunguo na kuchungulia nje.

Akaona gari aina ya Jeep-New Model rangi nyeusi inaegeshwa, ikiwa imewasha taa zake zote. Wakashuka watu wa wawili, mmoja mrefu sana lakini amejazia kimtindo amevalia kombati za jeshi, zilizo chafuka vyeo mabegani. Akiwa ameambatana na mwenzake mwenye mwili wa kawaida tu.

Wakawa kama kuna kitu wanajadiliana kwa muda kisha wakaanza kuja uelekeo wa chumba kile huku wamewasha kurunzi zao. Kachero Yasmine himahima akachomoka nduki kwenda kuzima taa kisha akarukia kitandani kwake.
Ikabaki kazi ya funguo wao kugombana na kitasa kugombania kuuacha mlango wazi pindi walipoufikia mlango wa chumba. Funguo wao ukashinda vita hiyo na kufanikiwa kuuacha wazi mlango. Wakaingia kwa tahadhari kubwa huku wakipiga tochi chumba kizima.




Alipofikishwa moja kwa moja akapokewa na watumishi wa jumba lile ambao walishataarifiwa ujio wake hivyo kila kitu kilienda kiulaini. Bahati yake Kachero Manu ni kutekwa kwa Man-Temba hivyo taarifa zilizopo kwa Profesa ni zile zile za kuwa hamna mawasiliano mpaka ipite wiki moja na huyu Kachero Manu ndio kijana aliyetumwa na Man-Temba.

Pia taarifa itakayopelekwa kwa Profesa na Dr.Pius Chilembwa ni kuwa sasa hamna mawasiliano tena mpaka itakapopangwa upya mipango. Kinyume chake angeweza kucharangwa mapanga na kufukiwa ndani ya jumba hilo maiti yake isionekane kabisa.
Kama kawaida Profesa alikuwa amelala baada ya mkesha wa usiku, hivyo nae Kachero Manu akashauriwa apumzike maana mwenyeji wake ataonana nae usiku.

Alikuwa na mshawasha na kimuhemuhe cha kukutana na Profesa. Hamu yake ilikuwa ni kutaka kumuona huenda akawa anamfahamu. Saa zikayoyoma mara ikafika saa 4 usiku akaitwa kwenye chumba maalumu kilichopo roshani ya 4.
Akaingia kwenye chumba huku kiroho cha uwoga kinamdunda. Kile chumba kilikuwa kina kompyuta zisizopungua 10 huku zikiwa na majina ya nchi tofauti tofauti duniani. Akaelekezwa akae kwenye kwenye Kompyuta iliyoandikwa Tanzania. Akapewa maelekezo ya kuvaa vifaa maalumu masikioni mwake. Ghafla mazungumzo yao yakaanza kupitia vifaa alivyovaa masikioni.

Profesa alikuwa nae yupo kwenye chumba chake maalumu ndipo anapotoa maelekezo hayo. Kachero Manu akayakumbuka vilivyo maelekezo ya Mr.Okworonko ya kuwa amekaa chini ya Profesa miaka kadhaa lakini hajawahi kumtia machoni. Ghafla kuna kitu Kachero Manu akakumbuka, akauchomoa mkebe wake maalumu, mdogo sana na mwembamba toka kwenye mfuko wake wa suruali.

Ndani ya mkebe huo kulikuwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki. Akauchomoa waya mmoja aliouhifadhi kwenye mkebe mdogo akaaunganisha kwenye kompyuta anayoitumia. Kisha akauweka mkebe huo pembeni ya ukingo wa kompyuta.
Sasa akawa anamrekodi sauti Profesa yule wakati wanazungumza bila hasimu wake kung'amua. Baada ya nusu dakika tu ya kuutumia, akauchomoa huo waya na kuurudisha akiwa ameinasa vilivyo sauti ya Profesa.

Alishajua kitu atakachofanya kwa kutumia hiyo sauti aliyoidukua kuweza kuiona sura ya Profesa mubashara bila chenga wala mawenge. Alikuwa anaelekezwa kwenye mafunzo hayo njia ya kisasa ya kukwapua pesa kwenye mashine yoyote ya ATM. Alichagizwa kuwa ni aibu kwa mtaalamu wa mifumo ya kompyuta kulalamika hauna ajira wakati pesa zote za kwenye mabenki ni zako.

Kwanza alipewa lengo la yeye kuletwa pale kuelekezwa kuwa pesa zilizoibwa Tanzania zinataka kurudishwa zikafanye kazi husika. Hizo pesa zitakapotolewa zitasafirishwa kwa njia ya barabara mpaka Tanzania na kuwekwa mafichoni. Kisha kuna tangazo limetoka tayari la kuhakikisha wamiliki wote wa VICOBA wote na SACCOSS nchi nzima wafungue akaunti benki.

Hivyo kwa kutumia mtandao huo wa VICOBA uliosambaa mpaka vijijini nchi nzima itakuwa rahisi pesa hizo kusambazwa nchi nzima kwa kuweka kwenye hizo akaunti. Kisha wao kwa kutumia njia za wizi wa kimtandao watakuwa wanazitoa pesa zao kinyemela kutoka kwenye akaunti za VICOBA kwa kutumia kadi za benki bandia na kuzitumia watakavyo.

Profesa akazidi kufunguka kuwa katika pesa zilizoibwa, ni nusu yake tu ndio zitarudi Tanzania huku zingine zikiwa ni mgao wa watu wote waliofanikisha zoezi hilo la utoroshwaji na gharama zote zilizotumika kukamilisha zoezi zima.
Kachero Manu alishtushwa kusikia karibia nusu ya pesa zimeshapigwa na vigogo wa Nyasa Empire Supporters (NES). Akajiapiza kimoyomoyo kuwa pesa hizo lazima watazitapika hata kama ikibidi kwa kuwakata mafigo yao na kupelekwa nchini India yakauzwe.

Baada ya hapo sasa akaanza kuelekezwa namna ya kuongeza mapato mapya ya chama pia kwa kutumia kutumia ATM-kadi. Kwenye mbinu hii ni Kachero Manu atahitajika kutumia Kadi feki ya ATM (Clonned cards) maalumu zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana, ambayo ina uwezo wa kuiba taarifa za kibenki za wateja na kumwezesha mhalifu kupakua pesa kutoka kwenye akaunti mbali mbali kwa kutumia mashine ya ATM. Kadi hizi zilikuwa zimeunganishwa na programu ya MRS606 pamoja na 'malicious softwares' zingine za wizi wa mtandaoni.

Kwa maelezo ya Profesa ni kuwa hizo kadi zilikuwa zimeagizwa toka nchini Marekani kutoka kwenye magenge rafiki ya uhalifu ambayo yeye Profesa ni mwanachama pia. Gharama ya kila kadi moja ni dola za kimarekani (USD) 150,000. Hivyo akaelezwa kuwa anachotakiwa kufanya yeye ni kupambana kupata tarakimu halisi za akaunti ya benki za watu wenye uwezo wa kipesa kama Wabunge, Mawaziri, Wakurugenzi, Wafanyabiashara na hata Wafanyakazi wa umma.

Akashauriwa kuwa hizo namba za akaunti za walengwa wanaweza kuzipata kwa kuwawinda wanapokuwa benki wanajaza fomu za kutoa pesa anatakiwa ale chabo kwa kunakiri namba hizo. Pia wakiwa kwenye ATM-mashine vigogo hao kama wakitupa risiti kwenye pipa la taka. Pia alielekezwa mbinu ya kufungua taasisi ya mikopo na kujitangaza kukopesha mikopo ya riba nafuu ya chini ya asilimia 5% kwa Watumishi wa Umma na Wafanyabiashara wakubwa.

Masharti ya mikopo hiyo ni kuandika jina lako, namba ya akaunti ya benki unayoitumia mara kwa mara katika miamala yako ya kipesa na anuani ya kituo chako cha kazi au ofisi zako za kibiashara. Profesa akasisitiza kwa mbinu hizo lazima tu utapata akaunti namba ya walengwa wako.

Baada ya kuzipata akaunti namba hizo, ataichukua kadi feki maalumu zilizonunuliwa Marekani na kuziingiza kwenye mashine maalumu ambayo anaiunganisha kwenye Kompyuta. Hiyo kadi itasoma kama kadi huru. Baada ya hapo ataingiza zile tarakimu za akaunti alizopata toka kwa walengwa wake.

Muda tu ambao yule mteja mwenye akaunti halisi atakapoitumia ATM kadi yake basi 'Software' maalumu iliyopo ndani ya kadi feki, kompyuta na mashine itaweza kutoa taarifa zote za kibenki ikiwemo salio lililobaki pamoja na nywira ya akaunti namba iliyoingizwa. Baada ya hapo bila wasiwasi wowote ataenda kwenye ATM-Mashine kuchomoa pesa anazotaka kupitia kwenye akaunti ya yule wanayemtapeli.

Mafunzo ya siku ya kwanza kwa Kachero Manu yakaishia ya majira saa nane za usiku. Akaahidiwa kesho yake kuanza kufundishwa mbinu zingine kabambe ili mradi mipango ya “Nyasa Empire Supporters” (NES) isije kufeli kwa kigezo cha pesa, bali ifeli kwa uzembe mwingine tu. Kachero Manu alibaki mdomo wazi kwa jinsi Profesa huyo alivyokubuhu kwa akili za utapeli.

Akatoka kwenye kile chumba maalumu na kuelekea kwenye chumba chake huku sasa Profesa akiendelea na maelezo yake kwa vijana wengine toka nchi mbalimbali ambao nao walikuwa foleni nje ya chumba kusubiri zamu yao ya kupata maelekezo. Alipishana mpaka na waarabu na wazungu wanaosubiria kuingia kwenye kile chumba maalumu kwa mafunzo ya utapeli.


Nathanieli aliegesha gari kwenye nyumba ya jirani na nyumba anayoishi Yasmine. Nyumba ambayo Yasmine kwa maelezo yake alidai kuwa ni nyumbani kwa Baba yake mdogo. Gia aliyopanga kuingia nayo kama kweli akimkuta huyo Baba yake mdogo ni kujieleza kuwa amekuja kumtazama Yasmine kwa sababu ni mgonjwa. Na hapatikani kwenye simu yake hivyo yeye kama Mkuu wake wa kazi amekuja kufuatilia maendeleo yake ya kiafya.

Alipofika getini akaegesha gari pembeni kisha akaanza kubisha hodi kwenye geti. Baada ya kugonga mara kadha, ukimya ukatawala bila kupata muitikio wowote. Akajaribu kuangalia kama kuna kengele ya kubonyeza pembeni mwa geti, lakini hakufanikiwa kuitia machoni. Alipochunguza vizuri, kigeti kidogo kilikuwa kimeegeshwa hakijafungwa na ufunguo wala kukandamizwa vizuri.

Akapiga moyo konde na kuamua kujiongeza kwa kuingia bila kukaribishwa. Akaingia ndani ya fensi ya nyumba hiyo na kukaribishwa na mandhari ya nyumba kubwa mbele yake na upande wake wa kulia una nyumba ndogo ya mtumishi. Nathanieli akawa anaelekea nyumba kubwa kwa mwendo wa pole bila kuzalisha vishindo vyovyote vya miguu.

Mpaka akapanda kwenye ngazi za barazani, akaona madirisha yapo wazi huku kwa mbali anasikia watu wawili sauti ya mwanamke na mwanaume wanaongea kimahaba na kutoa sauti za miguno ya kubembelezana, wakionekana ni wapenzi walioshibana.

Kifua cha Nathanieli kikaanza kuchemka kwa joto kali la hasira. Joto la wivu lilimvaa mwilini, jasho jekejeke likaanza kutiririka mwilini mwake. "Ina maana huyu malaya ananibania mimi kumbe kuna mjinga kapuku tu hata gari hana tena anakuja kumbanjulia ukumbini kwake!" alinong'ona taratibu Nathanieli huku akitaka kushuhudia kabisa. Akazidi kujisogeza dirishani akajibanza kwa pembeni ya wavu wa kuzuia mbu wa dirishani asikilize kinachoongelewa humo ndani kati ya anayedhaniwa kuwa ni Yasmine na huyo mpenzi wake.

"Hans...nakupenda sana kupita maelezo, yule Bosi wangu zoba kweli ananitaka kwa gharama zote mie simpendi, na mtambi ule kama chura mwenye mimba mie nitamuweka wapi" aliongea kwa sauti ya upole ya kutokea puani yule mwanamke kueleza hisia zake kwa huyo mpenzi wake.
Nathanieli hamaki ikamvaa mwili wote huku akijiangalia tumbo lake namna lilivyoumuka akaona kabisa Yasmine ameamua kumnanga yeye kwa kebehi za uzalilishaji. Uzalendo ukamshinda baada ya kuona mihemo na makelele ya mahaba inazidi hasa kwa mwanamke ampendae sana kama Yasmine.

"Ngo...Ngo..Ngo....Ngo..., hodiii...hodiii...hodi humu ndani..!" aligonga kwa nongwa haswa ili hasimu wake asiendelee kumfaidi Yasmine. Kimya kizito cha ghafla kikatawala pale sebuleni kama vile hamna mtu. "Ngo..Ngo...Ngo..", "Karibuuu...!" sauti ya kiume ya kiunyonge ilijibu baada ya kusikia mlango unagongwa tena kwa mara ya pili. Baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa.



Ngo...Ngo..Ngo....Ngo..., hodiii...hodiii...hodi humu ndani..!" aligonga kwa nongwa haswa ili hasimu wake asiendelee kumfaidi Yasmine. Kimya kizito cha ghafla kikatawala pale sebuleni kama vile hamna mtu. "Ngo..Ngo...Ngo..", "Karibuuu...!" sauti ya kiume ya kiunyonge ilijibu baada ya kusikia mlango unagongwa tena kwa mara ya pili. Baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa.


"Karibu Mzee, Shikamoo" aliongea yule kijana aliyefungua mlango huku akiwa ametawaliwa na wasiwasi usoni mwake. "Ina maana Yasmine anakamuliwa na Kiben-10, kweli huyu hamnazo" aliwaza Nathanieli baada ya kumuona kijana mwenyewe anayemlaki mlangoni hapo hata kwenye kiganja cha mkono hajai. "Marahaba Yasmine nimemkuta hapa kwake?" alijitutumua kuuliza swali la jambo lililomleta.


"Hapana, hayupo, Bosi Yasmine toka jana hajarudi nyumbani sifahamu alipo, akija nimwambie nani alikuja?" alijibu kwa sauti ya hasira akionekana hajapendezwa na ujio wa mtu aliyekuja kumkatia stimu ya starehe zake huku akionekana anajiandaa kufunga mlango, hataki usumbufu. Nathanieli fikra zake zilimtuma Yasmine yupo ndani ila anataka kufichwa kitu, akaupiga kikumbo mlango na kujilazimisha kuingia kwa kushtukiza.

Hamadi...! Akamkuta binti mdogo tu yuko pale ukumbini ana sura ya wasiwasi, uso umejaa soni kwa aibu tele ya kufumaniwa. "Shikamoo..Baba..!" alisalimia kwa aibu yule msichana huku ameinamisha kichwa chake chini. Nathanieli hakujibu kitu, alishagwaya kwa sababu alichokikuta ni kinyume na matarajio yake. Hapa kilichokuwa kinaendelea ni paka akitoka panya hutawala, picha ikionyesha kuwa ni kuwa Shamba-Boi wa Yasmine alimvuta dada wa kazi wa jirani kujivinjari nae kimapenzi.

Nathanieli hakuitikia salamu aliyotunukiwa zaidi ya kuondoka eneo lile kwa hamaki bila hata kuaga. Ingawa aliondoka shingo upande kwa kutomkuta Yasmine, lakini hisia zake kuwa Yasmine ni kirusi cha Makachero kilichopandikizwa ofisini kwao zikazidi kustawi na kumea akilini mwake.
Dalili zote zilionyesha ile nyumba sio ya kifamilia kabisa hamna cha baba mdogo wala mama mdogo anayeishi pale. Pia mashaka yalizidi zaidi inakuwaje mtu mgonjwa asishinde nyumbani apite kuzurura tu mpaka nyumba yake inageuzwa danguro.

"Kuanzia sasa namuwekea vijana wa kumwinda na kumfuatilia nyenzo zake, kifo ni halali yake kwa mikono yangu" alijiapiza nafsini mwake huku anaondoka na gari lake maeneo yale. Tayari alishahukumu kuwa Yasmine sio mtu anayestahili kuendelea kung'ara sura yake katika mgongo wa dunia.

Kwa upande wake Yasmine akiwa hana hili wala lile, aliingia nyumbani kwake majira ya saa 3:30 usiku akitokea hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye matibabu. Majibu huko ya daktari wake yalikuwa ni mazuri sana. Hakugundulika kuwa na matatizo yoyote makubwa ya kiafya hivyo alitakiwa tu auguze jeraha lake la kichogoni.

Alipofika nyumbani kwake kijana wake, Shamba-Boi alionekana kama ana wasiwasi na kama vile ana kitu anataka kumuambia lakini anaficha. Yule kijana alikuwa anataka kutoa taarifa za ujio wa mtu pale nyumbani, lakini alikuwa anahofia huyo mtu atakapoongea na Bosi wake Yasmine atamueleza kila kitu kuhusu yeye kuingiza ghashi ndani ya nyumba ya Bosi wake itakuwa msala kwake. Yasmine alishamsoma kisaikolojia kuwa kuna kitu anamficha.


Mara tu baada ya kuoga zake akaingia kwenye chumba cha CCTV-Kamera, kuangalia mienendo ya pale nyumbani kwake wakati hayupo. Yule Shamba-Boi alikuwa hajui kama matukio pale yote yanarekodiwa masaa 24. Kwa mshangao mkubwa sana akamuona Nathanieli amekuja nyumbani kwake na kaingia mpaka ukumbini kwake akawa anazungumza na Shamba-Boi wake.
"Amekuja kunifanyia taftishi, kanishtukia tayari kama nimewadukua?", Kamwambia Shamba-Boi wangu Hans asiseme ujio wake, mbona kakaa kimya?" ni baadhi ya maswali lukuki aliyokuwa anajiuliza Yasmine bila kupata majibu.

Mambo mengine aliyoyashuhudia kwenye CCTV-kamera ya Hans kumleta dada wa kazi wa nyumba jirani ndani ya nyumba kuu hakujali sana. Ulikuwa sio wakati wake kujadili upuuzi ule kulikuwa na mambo makubwa zaidi mbele yake ya kufuatilia kwanza.

"Zege halilali, nitakwenda usiku huu nyumbani kwake kumuuliza alifuata nini kwangu mchana kweupe kama sio mwanga ni nini sasa, kifo ni halali yake kwa mikono yangu..!" Yasmine alijiapiza huku akibadili nguo zake za kulalia na kuvaa za kazi ili aingie tena mzigoni. Alipanga akirudi huko kwa Nathanieli ndio atafanya mawasiliano na Kachero Manu ili wapeane taarifa wapi wamefikia katika taftishi zao za kuisambaratisha “Nyasa Empire Supporters (NES).

Akaingia kwenye gari lake na kupiga honi ishara ambayo ilimkurupusha kijana Hans chumbani kwake kuja kufungua geti ili kumruhusu Bosi wake atoke. Yasmine alipotoka tu akapita kama nyumba tatu hivi ya nne kutoka pale kwake kulikuwa na Baa maarufu tu katika mitaa ile.
Baa hiyo tayari ilikuwa imejaza watu lukuki wanafurahia maisha kwa namna wanavyoona wao inafaa kuyafurahia.

Akasimama mbele kidogo ya eneo hilo na kushuka nje ya gari, baada ya kujikuta amebanwa na kiu na hajabeba maji. Nyuma kidogo tu ya pale alipoegesha gari lake kulikuwa na gari nyingine aina ya 'Subaru-Forester' rangi nyeupe imeegeshwa kwa kujitenga kidogo na gari zingine.

Akaizunguka gari hiyo huku akimuona kijana mmoja akiwa amevalia fulana nyeupe na miwani nyeusi akiwa ameegemea kwa nje, mlango wa upande wa kushoto, kiti cha abiria anavuta sigara macho yote yapo uelekeo wa nyumba ya Yasmine. Yasmine hakumjali akampita lakini akiwa tayari ameshaikariri namba ya gari hilo kichwani mwake na kuelekea moja kwa moja kwenye njia ya kuingilia pale Baa akaenda mubashara mpaka kaunta.

Akazungumza na muuzaji baada ya sekunde kadhaa akakabidhiwa chupa kubwa ya maji. Akailipia na kuondoka zake huku akiifungua chupa hiyo njiani na kuanza kuinywa kabla hata hajafika kwenye gari yake. Alipotoka nyumbani alijigundua hajanywa maji ya kutosha, na kutokana na hali yake ya kiafya ilikuwa inamlazimu afanye hivyo kila anapopata wasaa.

Alipoingia kwenye gari yake, kabla hajaanza kuondoka, akawasha taa ya ndani ya gari kwa lengo la kukagua kilemba chake cha kichwani kama kimefungwa vizuri kusitiri jeraha lake lililozingushiwa bendeji. Akajiridhisha kuwa yupo sawa. Akaanza kuliondoa gari lake toka eneo hilo kwa mwendo mdogo mdogo na kutimka kuja maeneo ya Bamaga anapoishi Nathanieli.

Alikuwa anakwenda tu kwa mwendo wa wastani mpaka alipofika maeneo ya Tegeta Kibaoni eneo la mataa, wakati anasubiri taa za kijani zimpe ruhusa ya kuendelea kuitumia barabara hiyo ya Mwai-Kibaki alipotupa jicho kwenye kioo tu, akashtuka kidogo.

Gari ya tatu yake kutoka nyuma yake ilikuwa ni “Subaru-Forester” nyeupe ile ile aliyoitia machoni pale Baa ya jirani na kwake, na namba zake za gari ndio hizo hizo. Huku dereva ni yule yule jamaa aliyevalia fulana nyeupe aliyekuwa ameegemea mlango anajiburudisha na sigara.

Taa ziliporuhusu magari yanayoelekea Mwenge, Kachero Yasmine akachomoka nduki kwa spidi ya hatari akitaka kuwapima kama kweli wanamfuatilia yeye au wapo kwenye safari zao tu. Akajithibitishia bila mashaka kuwa wanamfuatilia yeye kwa sababu kila akiongeza kasi nao hawa hapa, akipunguza nao wanapunguza.

Walipovuka eneo la Bondeni tu, Kachero Yasmine akaongeza kasi huku akiwa yupo upande wa kulia wa barabara kuonyesha kama anaelekea Mwenge halafu ghafla tu akahamisha gari kuja kushoto na kukatiza kwa haraka sana kuja njia ya Kawe.

Kitendo hicho cha ujanja wa hali ya juu, kiliwachanganya wale maadui zake walijua anawatoroka. Nao wakatamani wahamie upande wa kushoto ili wamfuate njia ya Kawe. Dereva wao akakosa umakini alipohama hakupiga mahesabu vizuri akajikuta anakula dafrao kutoka kwenye Lori la nyuma yao lililosheheni mzigo wa makabichi likitokea Wilayani Lushoto, Tanga.

Ilikuwa ni moja ya ajali mbaya kuwahi kutokea kwenye eneo lile. Yasmine haraka haraka akaegesha gari kwenye miti pembezoni mwa barabara na kuja kushuhudia kwa macho yake, dafrao hiyo ya kutisha. "Wawaishwe hospitali haraka hawa huenda wakapona hao" yalikuwa ni baadhi ya makelele ya mashuhuda wa ajali ile.

Yasmine alipowaangalia vizuri wale majeruhi, akawakuta wapo watatu, lakini mmoja wapo ambaye hali yake ilikuwa nafuu alivunjika miguu yote, ila wale wengine walikuwa wamepata majeraha mazito ya kifuani na usoni kiasi kwamba wakati wowote walikuwa wanarejea akhera kwa Mola wao.

"Nisaidieni huyu mmoja kumpakiza kwenye gari yangu nimuwahishe Muhimbili" alipayuka Yasmine kwa sauti ya juu akijifanya ni msamaria mwema akiomba msaada wa raia wema kusaidiwa kumbeba yule mwenye nafuu kati yao. Yule jamaa kumuona Kachero Yasmine ambaye ni hasimu wao, yupo mbele yake ndio anataka kumpa msaada, akaanza kupiga kupiga kelele za kuwa wasimpeleke kwenye gari ya Yasmine.

Wale raia wema ndio kwanza hawaelewi kitu wanajua majeruhi akili zake zimefyatuka kidogo maana katika hali ya kawaida utakataaje msaada wa kuokoa uhai wako. Kumbe yule majeruhi alitambua kuwa ameshaingia choo cha kike mikononi mwa adui yake ambaye hana jema hata chembe na yeye.

Alivyopakizwa tu yule majeruhi, Kachero Yasmine akaliondoa gari lake kwa kasi akijifanya anamkimbiza hospitalini huku akiwa anatabasamu. Alikuwa akielekea kutafuta sehemu tulivu akambinye kwelikweli mpaka aropoke katumwa na nani amfuatilie.


"Nisemehe dada yangu nisamehe sirudii tenaa...Nakufaa jamani!" alikuwa analalamika yule majeruhi kwa maumivu ya ajali na mateso anayopewa na Yasmine. Aliamua kuja nae viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo maeneo ya Kawe ili amfundishe adabu.

"Nani kakutumeni mnifuatilie nyenzo zangu nitajie haraka sana sasa kabla sijakubadilikia tena!!" akiongea Yasmine huku amechomoa bisu lake kubwa lenye ncha kali anachofanya ni kuchomachoma kwenye yale majeraha yake ya ajali kikatili sana. Hali ambayo ilikuwa inazalisha maumivu makali sana kwenye mwili wake.

"Mie simfahamu vizuri, ila Cobra yule mwenzangu aliyevaa fulana nyeupe ndio anamjua vyema nilisikia akimtaja kwa jina Nath-Masterminder ndio mwenye kazi hii" alijibu kwa haraka haraka huku anahema kwa nguvu ya kupata afueni kidogo. "Mlitaka kuniua kwa dau la shilingi ngapi? kenge nyie..!" aliuliza Yasmine huku akimtishia kutaka kumtoboa jicho kwa kisu.

"Wooooooooh....tobaaa, hapana dada sisi tulikuwa tunakufuatilia tu, afu tumpe ripoti yeye mwenyewe ndio alitaka akuue kwa mikono yake ya sisi ni visarata tu...!" alijibu kwa uoga yule mjuba mpaka Kachero Yasmine akajikuta ameshindwa kujizuia na kicheko. Alipozidi kumbinya na kuona hana lolote alijualo akamtelekeza pale pale kiwanjani anaagaragara na maumivu na kutimka zake anaelekea nyumbani kwa Nathanieli.

Barabara ilikuwa ipo safi muda huo haina msongamano kiasi ya kwamba ndani ya nusu saa tu alikuwa ameshafika karibia na anapoishi Nathanieli. Kwanza alipitiliza njia ya kuingilia nyumbani kwa Nathanieli akiwa anatokea Mwenge. Gari yake alienda kuiacha Hongera Bar, kisha akaanza kurudi mashimashi akitembea pembezoni mwa barabara upande wa kulia. Mgongoni alibeba begi lenye dhana za kazi anazohitaji usiku ule. Barabara hiyo aliyokuwa anatembea daima huwa ni yenye giza kuja uelekeo wa Chuo cha Ustawi wa Jamii.

Kabla hajaifikia fensi ya Chuo hicho akapenya kwenye ushoroba mwembamba. Akaanza kukiacha Chuo Cha Ustawi wa Jamii upande wa kushotoni kwake, akazidi kwenda uelekeo wa mkono wake wa kulia. Akatembea kama umbali wa makadirio ya dakika 5 akizipita nyumba kadhaa, mpaka akafika kwenye transfoma ya umeme iliyokuwa imejitenga kando. Alipofika hapo akasimama kwenye nguzo zile mbili za umeme zilizoshikiza transfoma hiyo.

Akaangalia kushoto na kulia kama mkwapuzi anavyofanya, hakuona mtu yoyote. Akaanza kutoa vifaa vyake vya kazi alivyobeba toka garini. Akaisogelea transfoma hiyo na kuanza kuikorokochoa kwa msaada wa kurunzi yake. Haikichukua hata dakika 3, transfoma ile ikabutuka kwa sauti ya kishindo kizito kilichosikika eneo lote lile la Bamaga linalohudumiwa na trasfoma hiyo.

Giza totoro likatawala eneo lote, hima hima akafyatuka nduki mpaka nyumba ya 3 mbele yake yenye roshani mbili. Nyumba ambayo nayo ilikuwa imetawaliwa na giza. Alipofika hapo kwa mbinu zake za kimedani za vita akafanikiwa kuruka ukuta wa nyumba hiyo na kutua salama bila kishindo chochote. Akaganda kwa dakika kama 2 hivi akashangaa hamna hata mbwa. Muda huo huo akasikia jenereta linaunguruma na umeme ukawaka.

Akashukuru Mungu kwa kufanya haraka kuingia kabla ya kuwashwa kwa umeme. Kwa sababu ni mara yake ya pili kuingia ndani ya nyumba ile hakupata tabu njia za kupita kuingia ndani huku akijikinga na kamera za ulinzi. Taa za ndani ya nyumba zilikuwa zimezimwa kuashiria hamna mtu. Ni taa za nje pekee ndio zilikuwa zinawaka kipindi hiko kwa ajili ya kiusalama na kung'arisha mazingira ya nje.

Akafanikiwa kukwea mpaka ghorofani kupitia bomba la Kupitisha maji taka toka juu ya roshani kushusha chini. Kwa zana zake makini za kazi akafanikiwa kuingia ndani ya nyumba kupitia dirisha la jikoni. Moja kwa moja bila kuwasha taa akaenda mpaka mlango wa chumba kulala cha Nathanieli. Kwa kutumia mkungu wa funguo malaya bandia alizonazo akafanikiwa kufungua chumba hicho na kuingia.

Alipoangaza chumbani mule kwa kurunzi akakuta hakuna dalili za uwepo wa mtu yoyote. Kwa kutumia kurunzi yake hiyo akaangaza kwenye meza ndogo ya kujisomea iliyopo pale chumbani akakuta kuna daftari yenye ganda gumu jeusi kwa nje likiwa limefunguliwa.

Akavutika kwenda kuangalia nini kilichokuwa kinasomwa muda mfupi uliopita na Nathanieli. Akakutana na dondoo za kikao cha Nyasa Empire Supporters (NES) kilichofanyika asubuhi yake. Tabasamu lenye bashasha mpwitompwito likajengeka usoni mwake. Akazisoma dondoo hizo kwa umakini zikielezea mpaka safari ya marehemu Dr.Pius Chilembwa ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini nyumbani kwa Profesa. Alipomaliza kusoma dondoo hizo kwa umakini mkubwa ndipo akatanabahi kumbe walimgusia yeye kwenye kikao chao hicho lakini bila kumtaja jina lake.

Aahaaaaah...Kumbe ndio maana Nathanieli kawatuma wahuni wake wanifatilie nyendo zangu..!" alinong'ona peke yake, huku akijiapiza lazima amtangulize akhera Nathanieli kabla hajamharibia kazi yake iliyomleta Benki Kuu. Kazi ambayo ilikuwa inakaribia ukingoni kumalizika. Siku za washirika wa Nyasa Empire Supporters (NES) kuishi raha mustarehe wakivuta hewa safi ya uraiani zilikuwa zinahesabika kwa vidole.

Haraka haraka kwa kutumia mtandao wa simu yake akampasha taarifa hizo mpya Bosi wake, Kachero Manu ikiwemo ya ujio wa Dr Pius Chilembwa nchini Afrika ya Kusini. Akamtumia pia picha za Dr. Pius Chilembwa alizoziskani kazini kwake kule Benki Kuu.

Alipomalizana na Kachero Manu akaanza kujisikia kichwa kinagonga kwa mbali. Akakumbuka kuwa amesahau kunywa dawa zake alizoshauriwa na Daktari wake. Ikabidi hapo hapo achomoe tembe zake kwenye mfuko wa suruali yake ili afanye maarifa ya kuzimeza.

Akaelekea mpaka ilipo friji ndogo iliyomo ndani ya chumba kile na kuifungua kisha akaichomoa chupa ya maji ambayo ilikuwa bado haina ubaridi wa kutosha. Akameza tembe zake huku akisukumizia na maji.
Baada ya hapo akaelekea moja kwa moja ukutani na kuwasha kiyoyozi ili kuleta ubaridi wa kutosha ndani ya chumba kile. Akaelekea kwenye kitanda na kukalia huku amening'iniza miguu yake chini ya sakafu. Akavua koti lake lililokuwa linampa joto na kuliweka pembeni.

Akabakia na fulana nyepesi iliyomkaba vyema na kukichora vyema ramani ya maeneo ya kifua chake. Akaichomoa bastola yake na kuikamata vyema mkononi akimsubiria mbaya wake afike. Alitaka ampe mshtuko wa ghafla Nathanieli, mshtuko ambao utamfanya asiyaamini macho yake. Ataona kama mzuka wa Yasmine umeshuka ghafla jumla jamala mpaka chumbani kwake bila kutoboa popote.

Kachero Yasmine akatupia jicho simu yake ya mkononi akakuta ni saa 5:00 za usiku. Akaamua kuulaza mgongo wake kwenye mto pembeni ya kitanda huku anachezea simu yake ya mkononi bastola kaegesha kwenye mapaja yake.
Kile kiyoyozi alichowasha kilikuwa ni kosa kubwa la mwaka kwake. Kiliupoza vyema mwili wake na joto la nje, na kuupa starehe muruwa isiyomithilika. Akajikuta anaanza kusinzia bila kupenda, ghafla akaanza kukoroma usingizi mzito ulimvaa bila kupenda akiwa juu ya kitanda cha Nathanieli.

"Yasmiii...Yasmii.... njoo giza linaingia let's go...baby time is over...!" Kachero Manu alikuwa anamuita pacha wake kwa sauti ya kudekeza akimchombeza kwa lugha ya kimombo, wakiwa wapo kwenye kisiwa cha Bongoyo, kilichopo kaskazini mwa Jijini la Dar es Salaam. Kisiwa hicho kilikuwa kipo karibu na Msasani Peninsula.
Walikuja hapo Kisiwani kwa kutumia boti ya kukodi toka “Slipway Hotel” wakiwa wanaendesha wenyewe boti hiyo. Walikuwa wamefika tokea saa 5 asubuhi na sasa ilikuwa ni saa 12:37 jioni.

Waliogelea, walikula maakuli anuwai mbalimbali na mashrabu tofauti tofauti kuanzia Soda, juisi mpaka mvinyo. Walicheza kila aina ya michezo kuanzia riadha, mpira wa mikono mpaka mieleka.
Ili mradi mtoko wao siku hiyo ulikuwa na madhumuni ya kusahau shida zao chini. Walitaka kubanjuka kwa furaha zote kama vile dunia ni pepo ndogo, hamna kifo, hamna kuugua wala umaskini wala tabu na mateso yoyote.

Kachero Manu alishachoka vibaya sasa alikuwa anahitaji kurudi nyumbani tu magharibi hiyo akaupumzishe mwili. Wakati huo Kachero Yasmine kwa jinsi alivyokuwa anayakata maji bila kuchoka utasema ndio amekuja pale Kisiwani muda mfupi tu uliopita. Kuogelea Kachero Yasmine kwake ilikuwa ni zoezi analolipenda sana na kajifunza kuogelea kwao Zenji tokea ana umri wa miaka 4.

Kachero Yasmine aliposikia wito ule wa Bosi wake Kachero Manu akatii bila shuruti na kuanza kurudi nchi kavu. Kachero Manu alikuwa amevaa bukta yake nyepesi ya kijani huku juu amevalia singlendi nyeupe. Chini alikuwa amevaa sendo nyeusi zenye ufito wa chata ya 'Adidas'. Aliposimama Kachero Manu uelekeo wake wa macho ulikuwa kule anakotokea Yasmine.

Kwa uchokozi tu na kwa jinsi alivyozoea kumtia shemere Bosi wake, Yasmine alipotoka tu nje ya bahari akawa anatembea kwa mikogo mithili ya mlimbwende wa Miss Tanzania juu ya jukwaa anategemea kupata maksi za majaji. Juu Yasmine alikuwa amevalia kitopu maalumu cha kuogelea kilichoshindwa kabisa kusitiri tumbo lake dogo na kukiacha wazi kitundu cha kitovu chake.

Pedo yake ya rangi ya pinki ilimchora vyema umbo lake namba 8 la mahaba. Pedo hiyo kamwe haikuzuia makalio yake laini yaliyokuwa yakitikisika kimahesabu yasionekane. Miguuni alikuwa yupo peku peku na kuviacha wazi vidole vyake virefu vilivyobanana vizuri.
Kachero Manu kila siku yupo na pacha wake wa kazi Yasmine miaka nenda rudi lakini kila uchao alikuwa anamuona ni mpya machoni mwake. Sasa hii leo ilikuwa sifa bin makusudi kwa jinsi macho yake yalivyokuwa yanamthaminisha pacha wake akiwa amelowana maji tepetepe mwilini.

Nywele zake za singa, Kachero Yasmine ambazo kila siku anazifungaga mchicha, leo zilikuwa zimemwagika mwa mwa mwa mpaka mgongoni zikiwa zimetota maji. Kadri alivyokuwa anasogea karibu ndipo Kachero Manu mapigo yake ya moyo yalipokuwa yanazidi kumdunda kwa hawaa ya kufanya mapenzi.
Moja ya miiko yao Makachero ilikuwa mkiwa kazini, kazi na dawa ni marufuku kabisa. Lakini leo uzalendo ulikuwa unataka kumshinda Mzee mzima.

Ibilisi wa ngono alikuwa anampa tashwishi za kupupia maovu, amempanda kichwani anamwambia "hamna Bosi Mtanika hapa, mpo wawili tu, mkomalie kweli huenda akakutunuku penzi".
Alipofika karibu tu katika umbali sifuri, Kachero Manu akajikuta anaropoka bila kuangalia, maneno yanabubujika tu kinywani huku tayari ameshakibambia kiuno cha Yasmine anakitomasatomasa.


"Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika,
Japo mbinguni sijafika lakini na uhakika kwa kila mwanaume rijali akikuona lazima udenda churu churu churu utamchuruzika.
Naomba japo yako dakika nipate kukueleza moyoni yaliyonifika!
Kwani siwezi tena kuficha jinsi navyokuhusudu mtoto Yasmine".

Kachero Manu alijua kuilenga hiyo siku ya kujinadi kwa kumwaga sera zake. Kwani Yasmine alikuwa nae amezidiwa haswa na ashki, ndio maana muda mrefu alikuwa yupo majini kujiliwaza, huku akimkumbukia mpenzi wake Dr.Rishedy Shareefy anayefanya maisha yake huko Arabuni nchini Qatar.

Kwa mwaka mpenzi wake huyo huwa anakuja nchini Tanzania si chini ya mara 4 lakini safari hii alikuwa amekaa muda mrefu sana hajaja kwa muhibu wake Kachero Yasmine kutokana na janga la ugonjwa hatari wa "Covid-19" lililoitikisa dunia.

Hali hiyo ilikuwa inamuweka kwenye mazingira magumu sana, kujizuia na mihemko ya mwili wake. Yasmine alipotupa macho kwenye kifua cha Bosi wake kilichoumbika kutokana na mazoezi na lishe bora anayekula, akazidi kulainika kama mlenda.

Akajikuta anakubali kila anachofanyiwa na Kachero Manu. Kachero Manu akaona fursa ndio hiyo, asije akachekwa akaambiwa shamba la mahindi limepandwa karibu na jirani Kibogoyo anashindwa hata kuiba hindi la kuchoma. Akawa sasa anamkunja na kumuangusha chini ya mchanga pacha wake Yasmine. Kulikuwa hamna maneno tena, bali vitendo ndio vinaongea zaidi.

Kachero Yasmine alikuwa yupo ndotoni pale kitandani kwa Nathanieli alipojilaza na kupitiwa usingizi wa ghafla usio hata na adabu. Akawa anaota yupo kwenye mahaba mazito na Bosi wake Kachero Manu katika kisiwa cha Bongoyo kumbe hakujua yupo chumbani kwa adui yake na yupo kwenye hatari.

Ilipofika saa 5:30 za usiku Nathanieli alikuwa ndio anawasili pale nyumbani kwake. Akapiga honi na kufunguliwa geti akaingia na kuegesha gari lake. Baada ya kuongea mambo mawili matatu kuhusu matukio ya pale nyumbani na Shamba-Boi wake akapandisha juu ya nyumba yake. Akiwa hana wasiwasi wowote akafika na kufungua mlango wa chumba chake.

Alipowasha taa tu ya chumbani mwake alipigwa na mshtuko wa ghafla nusra aanguke chini kwa presha. Alichokiona kitandani pake kilimstaajabisha sana. Mwanamke mrembo akiwa amejifunga kilemba kichwani mwake, juu kavalia fulana iliyochongoa chuchu chake ndogo alikuwa amejilaza kitandani mwake.
Mwanzoni aliogopa kumsogelea akijua huenda ni Jini mahaba amejigeuza mwanamke kuja kumtega.

Lakini alipomuangalia vizuri akaona ana bastola mapajani mwake. Akapata nguvu kujua huyu ni adui yake. Akachomoa bastola yake kiunoni, akavaa ujasiri na kuanza kumsogelea kwa tahadhari kubwa akiogopea isije ukawa ni mtego kwake.
Alipomkaribia kabisa na kumgeuza sura yake, ndipo akamgundua kuwa ni Yasmine. Alipomuona ni yeye tena akiwa amebeba silaha akajua asilimia 100% kabisa kuwa ni adui yake. Alikuwa anataka kumuamsha usingizini ili apambane ana kwa ana, lakini akili na mwili vilikuwa vinakosa ushirikiano




Alipowasha taa tu ya chumbani mwake alipigwa na mshtuko wa ghafla nusra aanguke chini kwa presha. Alichokiona kitandani pake kilimstaajabisha sana. Mwanamke mrembo akiwa amejifunga kilemba kichwani mwake, juu kavalia fulana iliyochongoa chuchu chake ndogo alikuwa amejilaza kitandani mwake.
Mwanzoni aliogopa kumsogelea akijua huenda ni Jini mahaba amejigeuza mwanamke kuja kumtega. Lakini alipomuangalia vizuri akaona ana bastola mapajani mwake. Akapata nguvu kujua huyu ni adui yake.

Akachomoa bastola yake kiunoni, akavaa ujasiri na kuanza kumsogelea kwa tahadhari kubwa akiogopea isije ukawa ni mtego kwake.
Alipomkaribia kabisa na kumgeuza sura yake, ndipo akamgundua kuwa ni Yasmine. Alipomuona ni yeye tena akiwa amebeba silaha akajua asilimia 100% kabisa kuwa ni adui yake. Alikuwa anataka kumuamsha usingizini ili apambane ana kwa ana, lakini akili na mwili vilikuwa vinakosa ushirikiano.

Mwili ulikuwa haujiwezi tayari umeshashikwa na matamanio, hasa alivyokuwa anakiangalia kifua cha Yasmine, chuchu zilimtoa udenda. Alikuwa haamini kama umri wake ni juu ya miaka 27, alikuwa na kifua cha binti wa darasa la 5B aliyevunja ungo karibuni tu. Akajikuta anaingiwa na tamaa za kutaka kumbaka usingizini kisha akimaliza haja zake ndio apambane nae.

Akajikuta tayari ameshasaula suruali yake, Nathanieli amebakia na chupi yake tu huku mkononi amekamatia bastola yake.
Akaitanua miguu ya Kachero Yasmine akajibana katikati ya miguu na kuanza kumpapasa Yasmine kifuani. Mpaka akajikuta bastola inamporonyoka pembeni hakujali tena.

"Pliiiz...Manu, acha banaaa, sitaki kuvunja heshima yangu, namheshimu mpenzi wangu Dr.Rishedy Shareefy...!" alijikuta anajilazimisha kuzungumza wakati anamtoa kifuani mwake Manu wa ndotoni ambaye kiuhalisia yupo nchini Afrika ya Kusini.


Aliposhtuka usingizini na kufumbua macho yake taratibu, alishikwa na mzumbao. Alimuona adui yake Nathanieli anafanya utalii haramu kifuani mwake kadri anavyojisikia yeye, akiwa ameshazidiwa na mihemko ya ngono hajitambui.
Akakusanya nguvu zake za miguuni na kumpa kifuti kimoja matata sana cha sehemu za siri.

"Mamaaaaaah...nakuf....a... aaah...!!" aligugumia kwa sauti kubwa huku akiwa ameshaanguka sakafuni juu za zulia anagaragara kwa maumivu.
Hakutaka kumchelewesha akamrukia pale pale chini kama chui mwenye njaa kali na kuanza kumsukumizia makonde yasiyo na idadi hasa akichukizwa na kitendo cha kumpasulia sidiria yake na kumpapasa kimahaba bila ridhaa yake. Ndani ya dakika mbili na nusu Nathanieli alikuwa hoi hatamaniki usoni.


Sura yote imevimba manundu huku macho yamebonyea ndani na kuwa madogo kama Mchina vile. Alipomuongelesha akawa akijaribu kuongea anabubujikwa na damu mdomoni hawezi kuongea kitu. Usicheze na ngumi za komandoo wewe, watu ambao wakiwa mazoezini ndoo ya ugali ya lita 10 ikijaa pomoni anaikata mtu mmoja tu.
Makomandoo ambao wakiwa mafunzoni wanapanda milima huku wamebeba matairi ya trekta kichwani. Wakitaka kuoga, wanatumia maji ya baridi kutoka kwenye friza, acha Bwana usicheze na hao watu, wana roho za ujasiri na miili ya chuma.


Kachero Yasmine alishajua jamaa hana maisha marefu na akimuacha hai atakuja kumsumbua kazini na kwa washirika wake. Akanyakua bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti akamtwanga risasi tatu za kichwa ikawa habari ya Nathanieli duniani hapa imekwisha.


Ugavana wa kinjozinjozi aliokuwa anauota kila siku kuwa ataukwaa pindi Dola ya Nyasa ikitangazwa ukawa umeota mbawa. Siku zote chambilecho tamaa mbele mauti nyuma, alisahau kabisa usemi huo.
Nathanieli akawa anatapatapa sakafuni kwa kutupa miguu huku na kule, yamini wa yasari uchungu wa sakarati mauti. Kachero Yasmine hakuchelewa akapiga simu kwa watu wa kitengo maalumu waje kuhamisha ushahidi muhimu uliopo kwenye maktaba ya Nathanieli kuanzia kompyuta na vikorokoro vingine vitakavyosaidia mahakamani kuwatia hatiani mabaradhuli hawa wa Nyasa Empire Supporters(NES).


Wakati anawasubiri wenzake waje, alipokuwa anamungalia Nathanieli kwa umakini kifuani akaona kajichora tatoo ya mwenge wa uhuru umeshikiliwa na mikono miwili iliyochomoza juu ya ziwa Nyasa huku chini yake kuna namba 8019. Akaanza kuitafakari hiyo namba 8019 ina maana gani haswa lakini hakuwa na jibu na anayepaswa kumpa maana ya hiyo namba tayari kashatangulizwa jongomeo.


Ile tatoo aliyojichora mjuba Nathanieli kwa uwelewa wake wa haraka haraka alielewa kuwa mwenge unawakilisha uhuru, na huo uhuru wa kweli utapatikana baada ya kusimamishwa Dola ya Nyasa, na vuguvugu la uhuru huo limeasisiwa na watu wenye asili ya ziwa Nyasa.


Walipokuja wenzake tu na kuwakabidhi lindo, kisha kwa njia za Kininja kama alivyokuja ndivyo alivyotoweka eneo lile. Aliwapa uhuru wenzake wa kutimiza wajibu wao. Akawa anakatisha mitaani giza totoroo majira ya saa 6 usiku.
Akaomba msamaha kwa Mola kwa kuwasababishia giza la makusudi wakazi wa eneo lile lakini ni kwa lengo zuri tu wapate kuishi kwa amani na usalama katika nchi yao ya Tanzania.


Akalifikia gari lake akaliwasha na kutimka eneo lile kurejea Mbweni nyumbani kwake kujipumzisha huku akisubiria asubuhi inayofuata kupewa taarifa za msiba wa Bosi wake Nathanieli. Pia alishapanga kutafuta makazi mapya Safe House” ya kuhamia kwa sababu hapo tayari maadui zake wameshapajua hivyo hamna usalama tena.


SURA YA KUMI NA NNE

Kulipokucha tu, Profesa akatuma ujumbe kwa Kachero Manu kuwa leo watakutana mara mbili. Wakutane kwanza asubuhi hiyo na kisha watakuwa na kikao cha mwisho usiku na sio usiku pekee kama walivyokubaliana jana yake.

Kachero Manu akajua lazima kuna jambo la dharura limetokea. Kachero Manu alikuwa ameshapata taarifa zote za kifo cha Nathanieli na ujio wa Dr.Pius Chilembwa nyumbani kwa Profesa. Taarifa hizi alitumiwa na Kachero Yasmine kwa mfumo wa mawasiliano wa kijasusi unaitwa 'Morse Code'.

Mfumo ambao ulikuwa unatumia nukta na alama za dashi katika kutengeneza herufi wanazojua wao tu Makachero. Wakati mwingine walikuwa wanawasiliana kwa mfumo wa herufi maalumu zinazochapwa kwa kutumia mashine inaitwa 'Enigma', mashine maalumu iliyokuwa inatumika sana na mashushushu wa Kijerumani wakati wa vita kuu vya pili vya dunia.

Walijua kwa vyovyote ulinzi nyumbani kwa Profesa kwa upande wa mambo ya kuthibiti mawasiliano utakuwa mkubwa, hivyo lazima wachukue tahadhari zote. Pia alishafanikiwa kuinasa sura ya Profesa Asante-Rabbi kimafia.
Alichofanya ni kuichukua ile sauti aliyoirekodi jana yake na kuingiza sauti hiyo kwenye 'App' maalumu ya utambuzi wa sura za watu maarufu duniani kwa kutumia sauti zao. Ilikuwa ni 'App' ambayo ukiingiza sura ya mtu yoyote maarufu katika kila nchi duniani ina uwezo wa kukupa pia sauti yake.


Kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza kupata staftahi akakutanishwa ndani ya chumba kimoja na Profesa. Lakini alikuwa bado amejifunika uso wake kwa barakoa maalumu.

"Leo nina huzuni kuliko kawaida, mwili wangu ni dhaifu na roho yangu imekuwa nyepesi sana. Nimempoteza kijana wangu mpambanaji Nathanieli ambaye alikuwa anafanya kazi kwa ukaribu zaidi na Bosi wako Newton Temba" alifungua mazungumzo Profesa akiwa anamhadithia Kachero Manu bila kufahamu huyo anajua kila kitu na ndio mhusika wa kifo cha Nathanieli kupitia pacha wake Yasmine.

Kisha Profesa akaendelea, machungu ninayoyapata ni kama siku kijana wangu Hamza Bendelladji wa Algeria alipokamatwa". Alipofikia hapo kwenye maelezo yake ya kumtaja Hamza, Kachero Manu alipigwa na butwaa na kuachwa mdomo wazi kwa sekunde kadhaa akiwa haamini kumbe Hamza, mhalifu nguli alipikwa kiuhalifu na Profesa.

Huyu Hamza Bendelladji ni mhalifu aliyefanikiwa kuiba pesa nyingi zaidi za mabenki kwa njia ya mtandao. Alikuwa ni kijana mdogo sana (25) raia wa Algeria, ambapo miaka kadhaa iliyopita alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani kwa uhalifu wa kuiba zaidi ya Bilioni 500 (Tsh) kutoka kwenye benki 217 za Ulaya na Marekani.

Mashirika yote ya habari duniani kuanzia televisheni mpaka redio yaliripoti taarifa zake kijana huyo.
Kachero Manu akaanza kuomba kimoyomoyo Mwenyezi Mungu aweke baraka zake wamtie mbaroni Profesa ili dunia nzima iweze kujua kuwa Tanzania ina mashushushu bobezi kama wale waliopo katika mashirika makubwa kama CIA, FBI, MOSSAD, KGB na mengineyo yenye heshima ya kutukuka duniani.



Leo nina huzuni kuliko kawaida, mwili wangu ni dhaifu na roho yangu imekuwa nyepesi sana. Nimempoteza kijana wangu mpambanaji Nathanieli ambaye alikuwa anafanya kazi kwa ukaribu zaidi na Bosi wako Newton Temba" alifungua mazungumzo Profesa akiwa anamhadithia Kachero Manu bila kufahamu huyo anajua kila kitu na ndio mhusika wa kifo cha Nathanieli kupitia pacha wake Yasmine.


Kisha Profesa akaendelea, machungu ninayoyapata ni kama siku kijana wangu Hamza Bendelladji wa Algeria alipokamatwa". Alipofikia hapo kwenye maelezo yake ya kumtaja Hamza, Kachero Manu alipigwa na butwaa na kuachwa mdomo wazi kwa sekunde kadhaa akiwa haamini kumbe Hamza, mhalifu nguli alipikwa kiuhalifu na Profesa.


Huyu Hamza Bendelladji ni mhalifu aliyefanikiwa kuiba pesa nyingi zaidi za mabenki kwa njia ya mtandao. Alikuwa ni kijana mdogo sana (25) raia wa Algeria, ambapo miaka kadhaa iliyopita alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani kwa uhalifu wa kuiba zaidi ya Bilioni 500 (Tsh) kutoka kwenye benki 217 za Ulaya na Marekani. Mashirika yote ya habari duniani kuanzia televisheni mpaka redio yaliripoti taarifa zake kijana huyo.


Kachero Manu akaanza kuomba kimoyomoyo Mwenyezi Mungu aweke baraka zake wamtie mbaroni Profesa ili dunia nzima iweze kujua kuwa Tanzania ina mashushushu bobezi kama wale waliopo katika mashirika makubwa kama CIA, FBI, MOSSAD, KGB na mengineyo yenye heshima ya kutukuka duniani.


"Hongera sana Profesa na sisi tunatakiwa tujue mbinu ulizompika nazo Hamza tukazitumie Tanzania" alijitia kupongeza kinafiki Kachero Manu huku akimtia shemere azidi kufunguka.


"Ha.. ha... ha...! Ahsante umenifurahisha sana kwa sifa unazonipa, mimi Tanzania kwa uwezo wangu wa kiakili wakati nafundisha Chuo Kikuu ilitakiwa niwe na eskoti ya ving'ora kunipeleka Chuoni na kunirudisha nyumbani, lakini hata heshima tulikuwa hatupewi.

Afadhali kidogo sasa hivi wasomi wenzangu wanakumbukwa na wanasiasa wanapewa vyeo vya kuteuliwa" alicheka kwa majigambo na majivuno bila kujua kuwa Kachero Manu ni popo, yupo nao kimagazigazi tu kuwapekenyua taarifa zao nyeti.


"Yule Hamza alikuwa na akili za kuzaliwa, kwanza alikuwa anaitambuka mashine husika ya ATM, kisha kwa kutumia "boot CD" ama "boot flash" anaathiri mfumo mzima wa mashine, hii ni diski maalumu yenye uwezo wa kutunza mafaili makubwa sana kwa kufanya mashine isinzie kwa muda. Baada ya hapo kirusi kiitwacho 'Tyupkin' kinaingizwa kwenye mfumo huo wa ATM, kazi ya kirusi hiki ni kukata mawasiliano ya kimtandao kati ya mashine ya ATM na seva za benki.


Baada ya hapo mfumo wa mashine unaanza kufuata masharti ambayo mtumiaji anaamuru na si maelekezo ya benki tena. Mpaka Hapo sasa unaweza kuingiza namba za siri ambazo zimetegeshwa tangu awali na kukupa uwezo wa kupakua kiasi chochote cha pesa kilichopo katika mashine. Njia hii huiba pesa zilizopo kwenye ATM mashine bila kuathiri akaunti za benki za mtu mmoja mmoja.

Na pia ni njia inayoitaji ujuzi wa juu sana wa Kompyuta. Njia nyingine aliyokuwa anaitumia kuwaliza wazungu wa Ulaya ni kuvamia ulinzi wa Kompyuta za benki za wale wa madirisha ya wateja na maofisa wao, kisha akawa anarusha kirusi cha 'Spying software'.


Kirusi hiki kinaunganisha taarifa zote za maafisa wa benki na wewe mvamizi ikiwemo namba za siri kadhaa, hivyo kumpa uwezo wa kuendesha mifumo ya benki kama afisa wa benki husika. Baada ya hapo sasa mvamizi anaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti za watu wengine na kuweka kwenye akaunti yake binafsi. Na hii njia ya pili ndio tumeitumia sana kwa hizi pesa zilizopo hapa nchini Afrika ya Kusini". Alizidi kufunguka Profesa akiwa sasa ameanza kupata uchangamfu tofauti na mwanzoni walivyoanza maongezi yao.

Baada ya maongezi hayo Kachero Manu akakabidhiwa rasmi nywira za siri za kuwasiliana nae pindi atakapokwama akiwa kazini. Huku akiahidi kuwa watakutana Tanzania siku chache zijazo mara pesa zitakapokuwa zimefika. Pia usiku aliahidiwa kuwa atasaini mkataba rasmi wa kuhakikisha Dola ya Nyasa inasimamishwa na akifanikisha malengo yake aliyopewa atapewa nyadhifa gani kwenye hiyo serikali mpya.

Pia alipewa jukumu la kutafuta wataalamu wa kufoji nyaraka 'Cobbler' watakaowatumia sana wakati wa kuhamisha pesa taslimu kuirudisha Benki kwenye akaunti za VICOBA na SACCOS. Wakaagana Kachero Manu akarudi chumbani kwake kupumzika.
Wakati amejipumzisha chumbani kwake, akaamua kuingia kwenye barua pepe yake akakutana na taarifa za kupendeza kutoka kwa rafiki yake Dr.Edson Nkube.


Vipimo vya DNA vya mama mzazi wa mwendawazimu, marehemu Van-Dubbe vilishatolewa huku vikithibitisha pasina kuacha mashaka kuwa Van-Dubbe ndio aliyezikwa Tanzania na ndio mtoto wake. Hivyo akataarifiwa kuwa tayari leo mchana Mama yake Van-Dubbe anasafirishwa kwa ndege kuelekea nchini Tanzania tayari kwa ajili ya kutoa ushahidi mahakamani pindi mambo yakikamilika.


Akafurahishwa na kazi nzuri na ya kutukuka iliyofanywa na Dr.Edson Nkube, Afisa Usalama wao wa siri ambaye hata ndani ya usalama wenyewe wengi wao hawamjui "Deep Cover". Hasa akikumbukia namna alivyomuokoa kwenye hatari alipotegewa mtego kwenye nyumba ya kulala wageni siku ya kwanza kukanyaga nchini Afrika ya Kusini.

Kachero Manu baada ya kuperuzi jumbe mbalimbali alizotumia, akaanza kupanga namna ya kuwatumia kwenye sakata hili raia wa Tanzania wanaoishi Jijini Johanesburg na kulipwa na kitengo cha Usalama Tanzania, hasa kuchunguza nyendo za namna hizo pesa zitakavyosafirishwa kwa njia ya barabara.


Taarifa alizopata ni kuwa Jijini Johanesburg pekee kulikuwa na Maafisa Usalama Waliolala "Sleeper Agents" zaidi ya 20, wanaolipwa mshahara na serikali. Ambao wengi wao kati ya hao 20 walikuwa wanakula shushu hawajawahi kupewa kazi yoyote toka waajiriwe.

Hawa mashushushu walikuwa wanajichanganya mitaani hawajulikani na watu shughuli zao halisi. Wengine walikuwa wanafanyakazi saluni za kiume za kunyoa nywele, wengine wakiuza matunda mitaani, na shughuli kedekede zilizokuwa zinatumika kuwapoteza maboya watu wasiwajue kazi zao.


Walikuwa wamewekwa kama akiba ya kutumika siku wakihitajika. Na sasa wakati ulifika wa kutumika ambapo jukumu lao litakuwa ni kuchukua ushahidi wa kutosha uwe na video au picha wakati pesa zinatolewa mlundi kwa mlundi na kupakizwa kwenye magari.


Mawasiliano yake yote wakati yupo kwenye jumba hilo la Profesa gwiji wa Kompyuta alikuwa anayafanya kwa kutumia simu yake yenye programu maalumu ya kuzuia udukuzi. Hakutaka kabisa kugusa Kompyuta za ndani ya jumba lile, akiogopea 'Carnivore Computer', ambazo ni kompyuta maalumu zinategeshwa kwa ajili ya kufukua taarifa za mtumiaji.


Majonzi na huzuni vilitawala msibani, nyumbani kwa Nathanieli. Ndugu, jamaa wa karibu na majirani walikuwa wamefurika kwenye kilinge cha nyumba hiyo. Askari polisi tayari walishaiondosha maiti ya Nathanieli. Wafanyakazi wenzake wa Benki Kuu nao hawakujivunga, walikuwa mstari wa mbele pale msibani kuhakikisha mambo yanaenda sawia bila kuharibika. Kila mtu alikuwa anasema lake pale msibani.

Penyenye za nguvu zilizoenea ni kuwa amevamiwa na majambazi usiku wa manane akauliwa. Wengine wakavumisha ni kifo kinachotokana na kisasi cha ugoni. Wakanyetisha kuwa alikutwa chumbani na mke wa mtu ndio mwenye mke akajichukulia sheria mkononi. Wakatilia nguvu nadharia yao kwa kuwa marehemu kakutwa yupo na chupi tu mwilini mwake, huku boksi kadhaa za kondomu zikifumwa chumbani mwake.


Hizi habari za uzushi zilikuwa zinaenezwa kwa kasi pale msibani na mitaani na vidinga popo na wale habari kuuzwa. Bila wenyewe kufahamu kuwa hizo habari zote ni propaganda zilizopikwa na kusambazwa na watu wa kitengo, mashushushu ili mradi kuwapoteza maboya mahasimu wao na pia ndugu, jamii na marafiki ili wasije kuharibu ushahidi wakati muda umekwenda matiti.

Maneno hayo ya ndarire yalizaa matunda chanya yaliyokusudiwa hasa ile dhana ya pili ya kushikwa na ugoni ndio ilishika kasi na kuaminiwa na wengi pale msibani. Huku dhana hiyo ikichagizwa na maisha binafsi ya Nathanieli ya kuishi bila mke wala kuwa na mtoto hata wa kusaga mkungu.


Vikundi mbalimbali vya kwaya vilikuwa vinatumbuiza nyimbo za maombolezo pale msibani. Kachero Yasmine nae alikuwa yupo pale msibani sako kwa bako na shoga yake kipenzi wa kazini Flora Tarimo. Alikuwa anawachora tu, huku akikumbukia vuta n'kuvute, patashika nguo kuchanika ya usiku wake alipokuwa anapambana na marehemu Nathanieli.



Vikundi mbalimbali vya kwaya vilikuwa vinatumbuiza nyimbo za maombolezo pale msibani. Kachero Yasmine nae alikuwa yupo pale msibani sako kwa bako na shoga yake kipenzi wa kazini Flora Tarimo. Alikuwa anawachora tu, huku akikumbukia vuta n'kuvute, patashika nguo kuchanika ya usiku wake alipokuwa anapambana na marehemu Nathanieli.


Shoga yake Flora alikuwa hajiwezi kwa kilio cha Bosi wake, huku Yasmine akifanya kazi kubwa kumliwaza. Ushoga wao ulikuwa wa kinafiki hasa kwa upande wa Yasmine. Kuna kitu Yasmine alikuwa akikitafuta kwa Flora bila yeye mwenyewe kufahamu.


"Shosti Shemeji yangu anasafiri kwenda Afrika ya Kusini leo, hivyo nataka nichomoke nimuwahishe Uwanja wa Ndege halafu nitarudi..!" Flora alimnong'oneza rafiki yake Yasmine sikioni. "Twende wote na mie sibaki hapa nitakuja baadae maana hata ratiba bado, wanasubiriwa ndugu wa marehemu toka Mkoani Ruvuma waje ndio kila kitu kitaeleweka". Kachero Yasmine alisema huku akijionyesha kubwa ni mtu aliyekabwa na huzuni kuu.


Flora kwa shingo upande akakubaliana na ombi la Yasmine kuwa waende wote, wakanyanyuka kwa pamoja huku wakiwaomba udhuru Wafanyakazi wenzao wa Benki Kuu na kwenda kwenye maegesho ya magari kisha kila mtu akaondoka ene lile na gari lake, Flora mbele, Yasmine nyuma yake linafuata.


Flora alikuwa anaishi Mbezi Tangibovu kwenye nyumba yake ya roshani mbili, jirani kabisa na shule ya msingi Mwalimu Nyerere. Kwa mtazamo tu wa jumba la Flora kwa nje lilikuwa linakuonyesha ukwasi wa mmiliki wake. Lilikuwa limetiwa nakshi za gharama zenye asili ya Asia na Mashariki ya Kati. Yasmine akilini mwake alikataa katakata kuwa hili kajenga kwa ngwenje zake mwenyewe Flora.

"Hapa kuna mkono wa danga, umenyooshwa kusimamisha huu mjengo" aliwaza Yasmine wakati anakaribishwa ndani ya nyumba hiyo wakiwa tayari wameyaacha magari yao kwenye eneo la maegesho. Alithubutu kuwaza hivyo kwa sababu alikuwa anajua dhahiri shahiri kiasi cha mshahara anaoupata sahibu wake Flora.

"Karibu sana Shosti jisikie upo nyumbani, nimefurahi sana ujio wako, maana kila siku kukutaniana kwenye Mahoteli marafiki kama sisi haipendezi. Nimekufahamu muda mfupi tu lakini nakuchukulia ni kama ndugu kwangu sio rafiki tena.." alizidi kujibaraguza Flora bila kufahamu anamkaribisha shushushu 'Birdwatcher' hatari sana.

Mtu aliyekuja hapo kwa malengo maalumu ya kuhakikisha uwepo wa marehemu Dr.Pius Chilembwa ndani ya nyumba hiyo. Hasa akikariri maneno ya marehemu Nathanieli aliyowahi kumpasha Yasmine kuwa Flora alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Dr.Pius.

"Ahsante sana Shosti, nimejaa kama pishi la mchele, huu ni mwanzo tu, nitakuja mpaka utanichoka" akajibu Yasmine mpaka wote wakaangua kicheko huku wanagongesha viganja vya mkono na kuingia ndani ya nyumba. "Tena mjengo kama huu unanitia hasira na wivu wa maendeleo, uliwezaje kujenga jengo la watu tabaka a'ali kama hili? Nimegee siri kidogo" alianza kumfukunyua undani huku usoni mwake ameunda tabasamu la uongo na kweli.


"Mhh...nilipunguza anasa zote, nikilipwa masurufu ya safari zote zinakuja saiti, marupurupu yangu yote nilikuwa nayaleta huku bila kusahau kibubu cha nyumbani nilikuwa naweka fedha akiba nikivunja mwisho wa mwaka sikosi milioni 10 mpaka 15" alijifaragua Flora majibu yenye ushobo ndani yake, majibu ambayo uso wake ulikuwa unaonyesha fika kuwa anaongopa mchana kweupe.

"Daah...hongera sana, Shosti hivi ndio tunataka, Wanawake tufanye mambo ya maendeleo tumiliki uchumi, kuondoa dhana ya kwamba hatuwezi mpaka tuwezeshwe na Madanga" alimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa wakati mawazoni mwake alikuwa anamng'ong'a kuwa thubutu yako, kibubu kwio gani hicho cha ajabu kwa mtumishi wa umma cha kuweza kuweka akiba mpaka milioni 10-15, wakati wananuka madeni mpaka ya sembe huko mitaani kwenye vigenge.


Wakapiga soga mbili tatu kisha wakaelekea mesini kutia riziki kinywani maana walikuwa bado hawajaiona asubuhi yao kutokana na hekaheka na taharuki za msiba huo wa ghafla. "Sasa Shosti huyo Shemeji yako, mbona unamficha, muweke hadharani huenda na mie nikampenda nikaopoa mchumba, tukaolewa wote kwa mkubwa na mdogo!" Kachero Yasmine alichomekea akiwa na hamu ya kumuona huyo anayesemwa ni shemeji ili ahakikishe kama sio kweli Dr.Pius.

"Mmhhh...Shosti nawe una vibweka, haya twende ukamuone maana tayari yupo kwenye gari akinisubiri mimi tu nipate staftahi nimkimbize Uwanja wa ndege" aliongea huku akiwa na wasiwasi mkubwa usoni mwake akijitahidi kuuficha kwa tabasamu. Wakaanza kushuka toka roshani ya pili wanaelekea maegesho ya magari huku tayari Yasmine akivaa miwani yake maalumu aina ya "Kestrel 1080p HD Camera Eye Glasses".

"Shosti mbona miwani tena una matatizo ya macho?" aliongea Flora akimshangaa rafiki yake kuvaa miwani ghafla maana hajawahi kumshuhudia amevaa miwani tokea wamefahamiana.
"Aaaah....macho yangu kwa sasa hayapatani kabisa na jua pia nipo kamili kumtega Shemeji yako anione ni mrembo!" alitoa jibu la uongo na kuchomekea utani ndani yake ili kumzubaisha, wote wakafa kicheko huku wamekamatana viganja vyao wanaelekea kwenye maegesho ya magari.

"Shem...kutana na rafiki yangu tupo nae ofisi moja anatokea Zanzibar anaitwa Yasmine, amenisumbua sana anataka walau akuone tu....! " Flora alifanya utambulisho mfupi huku Yasmine akichezea mkono wa upande wa kushoto wa hiyo miwani akijifanya kuiweka sawa, kumbe anafanya vitu vyake bila wao kung'amua.

"Ahaaa...vizuri nashukuru kukufahamu nadhani tutazidi kufahamiana zaidi nikirudi safari yangu maana sasa nina haraka, poleni sana na msiba uliokufikeni" aliongea yule jamaa aliyejifanya Shemeji wa Flora baada ya kusalimiana huku machozi yakimlenga mpaka akashindwa kabisa kuyazuia machozi yake, yakaanza kumdondoka. Akatoa hanchifu yake kutoka kwenye mfuko wa suruali yake na kuanza kujifuta.

"Tumepoa, nashukuru pia kukufahamu, mbona unalia sasa kumbe unamjua Bosi Nathanieli...?" Yasmine akashukuru na kuchomekea swali baada ya kuona hali sio ya kawaida katika uso wa Shemeji.

"Aah..Aah...OK.. OK....I'm fine usiwe na wasiwasi simjui ila kanisimulia Shem Flora jinsi alivyokuwa mwema kazini kwenu, nimejikuta nimeshindwa kujizuia kabisa, ama kweli wema hawadumu" alijing'ata, huku anajikany'aga katika kujieleza akijua fika tayari ameshaharibu kwa kuruhusu machozi yale. Lilikuwa ni swali lililomtia kitumbo uchungu, hakulipenda kabisa. Jambo lilizidi kumtia mashaka Kachero Yasmine kuwa huyu mtu anaficha uhalisia wake.

Baada ya hapo Yasmine wakaagana na Flora huku Flora nae akipakia kwenye gari la anayejidanganyia ni shemeji yake, akimpa ahadi rafiki yake kuwa hatochelewa kurudi nyumbani ili mradi waweze kurudi tena msibani. "Usichelewe basi mie nakungojea twende wote" alijifaragua Yasmine kujifanya ana haraka sana wakati kiuhalisia alikuwa anatamani achelewe ili aweze kuyasoma mazingira yote ya pale nyumbani.

"Sichelewi kuwa na subira, si unajua waswahili tusipoonekana tunaweza zushiwa tukio tumekula njama Bosi afe ili tupate Cheo chake ndio maana hatuonekani msibani, hatuna uchungu" alitilia msisitizo Flora mazungumzo yao wakati tayari ameshaanza kulitoa gari eneo lile. Shemeji mtu akiwa amekaa kiti cha mbele cha abiria akawa anampungia mkono Yasmine kisha akamkonyeza. Yasmine nae akapunga mkono kurudisha maagano hayo huku anatabasamu. Hivyo Yasmine akaachwa, solemba peke yake pale nyumbani.

Mungu ampe nini Yasmine!, upele ajikune? Kwake kuachiwa jumba analohisiwa kuishi adui yake ilikuwa ni kama mbuzi kufia mlangoni kwa muuza supu usiku wa manane au ngedere aliyesusiwa shamba la mahindi ajipocholee atakavyo. Kabla hajaingia ndani akaingia kwenye gari yake na kuitoa kompyuta yake ya kazi pamoja na mkoba wake maalumu wa vifaa vya kazi, wenye dhana zote anazohitaji, akaingia navyo ndani ya nyumba.




Mungu ampe nini Yasmine!, upele ajikune? Kwake kuachiwa jumba analohisiwa kuishi adui yake ilikuwa ni kama mbuzi kufia mlangoni kwa muuza supu usiku wa manane au ngedere aliyesusiwa shamba la mahindi ajipocholee atakavyo. Kabla hajaingia ndani akaingia kwenye gari yake na kuitoa kompyuta yake ya kazi pamoja na mkoba wake maalumu wa vifaa vya kazi, wenye dhana zote anazohitaji, akaingia navyo ndani ya nyumba.



Ile miwani yake aina ya 'Kestrel' haikuwa ni miwani ya kawaida kama udhaniavyo zile miwani za jua halisi. Ilikuwa ni miwani maalumu ya kijasusi yenye uwezo wa kurekodi video mpaka masaa 8 ikiwa na uwezo wa kuhifadhi wa '64GB'. Wakati anaongea na yule anayejifanya Shemeji wa Flora alisugua upande wa kushoto wa mshikio wa miwani, lengo ilikuwa ni kuiweka tayari kumrekodi mshukiwa wake.


Alipoingia sebuleni na kutulizana, akaichomoa chipu ya kuhifadhi video toka kwenye miwani na kuichomeka kwenye kompyuta yake na kuanza kuangalia video hiyo huku akiisimamisha mara kwa mara wakati ametingwa na zoezi la uchoraji picha hiyo kwa kutumia kalamu ya risasi na karatasi nyeupe.


Baada ya nusu saa alikuwa tayari ameshamchora yule Shemeji wa Flora. Akaifungua toka kwenye Kompyuta yake picha halisi ya Dr.Pius Chilembwa aliyoidukua kazini kule Benki Kuu na kuilinganisha na picha ya yule Shemeji wa Flora. Akaanza kulinganisha picha hizo kwa kuondoa zile ndevu, sharubu na masharafa ya kwenye picha aliyoichora toka kwenye video. Kadri alivyokuwa anapunguza vitu kwenye ile picha ya kuchora ndivyo alivyokuwa anaanza kufurahi mpaka tahamaki zikawa picha mbili za watu wanaorandana.


Shabaashi..! Nimekushika Dr.Pius Chilembwa, hatimaye mbio zako za sakafuni zimekaribia kuishia ukingoni. Kitanzi kinakuita kwa uhaini uliouandaa. Ni aibu kubwa mtu kama wewe uliyetopea na kutabahari katika elimu, kushiriki ujinga kama huu. Kumbe machozi yako kwa kifo cha Nathanieli ni machozi halisi ya kufiwa na kijana wako wa kazi!.


Sasa napata picha nzima kuwa unasafiri kwenda nchini Afrika ya Kusini kama nilivyosoma dondoo za moja ya mikutano yenu nyumbani kwa Nathanieli. Huko unakokwenda unaenda kukutana na pacha wangu hatari sana katika kazi, Kachero Manu nina imani utarudishwa maiti au atafanya kitu ambacho kitazidi kukuacha uchi zaidi ewe Marehemu mtarajiwa uliyejichuria kifo kabla ya siku zako..!" Yasmine alikuwa anaongea na Dr.Pius Chilembwa pale kwenye picha huku anamsoza na kidole cha shahada utasema anamsemesha mtu halisi mbele yake kumbe picha tu.


Kazi aliyobakiza kwenye nyumba ile ikawa ni kupandikiza vifaa mbalimbali vya kunasa mazungumzo na video, kitaalamu walikuwa wanaita Black Bag Operation (BBO). Kwa kutumia vifaa hivyo vya maalumu akafanikiwa kufungua mlango wa chumbani kwa Flora. Akafunga vifaa vyake chini ya kitanda na vingine bafuni. Alipokuwa bafuni ndipo alipogundua kuna njia nyingine ya kutokea bafuni kushuka chini ya jengo. Kati ya makutano ya kuta mbili kushotoni kwa choo cha kukaa aligundua kuna uwazi uliofungwa kitaalamu sana, sio rahisi kwa mtu wa kawaida kugundua. Kwa utundu wake wa kishushushu akafanikiwa kufungua uwazi huo na kushuka chini kwa chini mpaka alipokutana na chumba kingine.


Alipofanikiwa kukifungua akakuta ni chumba ambacho ni kama kipande cha chumba cha Hoteli, chenye hadhi ya nyota tano kikiwa na kila kitu kwa mahitaji ya mwanadamu. Hakutaka kukaa sana huko zaidi ya kupandikiza vitu vyake anavyotaka kisha akafunga chumba hicho na kurudi juu. Akafanikiwa kukamilisha zoezi hilo kwa umakini mkubwa.


Punde si punde sahibu wake Flora akarejea toka Uwanja wa ndege alipomsindikiza marehemu Dr.Pius Chilembwa. Wakakaa sebuleni wakaendelea mazungumzo yao mengine, kisha wakakata shauri kurejea msibani huku moyoni Kachero Yasmine ana furaha sheshe ya kukamilisha bila purukushani lile alilolikusudia kulifanya nyumbani kwa Flora.


SURA YA KUMI NA TANO

Majira ya adhuhuri wakati Kachero Manu anajiandaa kwenda mesini kupata maakuli kabla hajatoka chumbani kwake akachungulia nje ya dirisha la chumba chake. Moyo wake ghafla ikampiga paaah..! akiwa haamini ambacho macho yake yanacho mshuhudisha.

Alistaajabishwa na kuona ulinzi maradufu ukiimarishwa katika jumba lile huku walinzi hao wakiwa na silaha nzito za kijeshi.
Pia kulikuwa na helikopta ndogo si chini ya tatu zikiwa nazo zimekaa mkao wa kupaa wakati wowote. Kwa ujumla kuuvuka ulinzi ule bila ruksa yao ilihitajika nguvu za Mungu tu na si vinginevyo.

Ghafla bin vuu akiwa bado yupo pale pale dirishani hajachomoka, akaanza kusikia sauti ya ving'ora kuashiria punde tu msafara mzito unaingia eneo lile nyumbani kwa Professor Potchefstroom, au ukipenda muite Profesa 'Asante-Rabbi' mwenye Mji wake.


Akashikwa na wahaka na tashiwishi ya kushuhudia mchezo mzima unaoendelea pale nyumbani kwa Profesa mubashara kupitia dirishani. Yalikuwa magari yasiyopungua 10 ya kifahari yenye rangi nyeusi yanayofanana kila moja kimuonekano, yanaingia eneo lile. Yaliposimama tu wakashuka mabausa zaidi ya 50 kwenye magari yale yote, wakiwa wamevalia sare mithili za kijeshi. Mabaunsa hao hawakukaa sambejambe, bali walijipanga kiutaratibu maalumu kuonyesha wamefunzwa wakafunzika.

Kisha kwenye gari ya katikati akashuka mtu mmoja ana mwili mdogodogo mrefu wa wastani amefuga ndevu za kutosha na masharubu hali iliyomfanya aonekane umri wake umekimbia. Alikuwa amevaa pensi ya kaki na sendo nyeupe miguuni huku juu akivalia sweta la kumuwezesha kuhimili baridi ya nchini Afrika ya Kusini.

"Hatimaye hayati Dr Pius Chilembwa amefufuka toka kaburini kwake na kutua nchini, karibu sana kama kweli wewe ni mvuvi wa pweza tukutane mwambani" alijikuta anaropoka Kachero Manu bila kutarajia baada ya kumuona Dr Chilembwa anasaidiwa mizigo na mmoja wa watumishi wa nyumbani pale ili aingie ndani.

Kachero Manu akatoka zake nje ya chumba, akakifunga na kuelekea mesini kwa ajili ya chakula. Huko mesini alikutana na baadhi ya mabaunsa aliowaona chini ya jengo, wameingia kula kwa zamu zamu huku wenzao wakikaa ange kama washika doria. Hakuwajali, akaketi kitini na kuanza kufakamia maakuli ipasavyo mchana huo ili kuupa mwili virutubisho vyote muhimu.

Alipomaliza kula akawa anarejea chumbani kwake kusubiria wito wa kikao tena cha baadae. Alikuwa anapenda safari yake ya kurejea Tanzania iwe ya haraka alishachoka kukaa kitawa kwenye jumba lile. Alitamani waungane tena na pacha wake Yasmine kwanza ampongeze kwa kazi nzuri aliyoifanya, pili walianzishe varangati la pamoja la kuwatia mbaroni wahalifu. Maana siku zote Yasmine alikuwa anaishi katika kivuli cha Kachero Manu, hata afanye uhodari gani sifa zilikuwa zinammiminikia kwake Kachero Manu.


Alipokanyaga tu korido ya kuelekea chumbani kwake, chumba cha pili kushoto kwake akamuona Dr Pius Chilembwa anatokeza kwenye hiko chumba huku anaongea na mtu kwenye simu. "Hellow...yeah! sasa naenda kupata mlo wa mchana baada ya hapo nitaenda chumba cha kujisomea kuweka mambo sawa kisha baadae ndio nitakuwa na mkutano na Professor Potchefstroom..!" alikuwa anaongea na simu huku amerudishia tu mlango wake hajaufunga vilivyo. Akapishana na Kachero Manu kwenye korido wakasalimiana kwa kupeana ishara ya kupungiana mikono tu.


Kachero Manu alishashtukia mchezo mzima kuwa Dr Chilembwa kasahau kubana mlango na anatokomea zake kwenda mesini. Akawa anamsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yake. Jasiri haachi asili yake hata akiwa ugenini, Kachero Manu alijikuta ameshageuka na tayari na yupo mlangoni mwa chumba cha Dr Pius Chilembwa. Salama yake ni kuwa korido zote hazikufungwa kamera za usalama kutokana na Profesa kuamini sana ulinzi wa nje ya nyumba yake.


Kachero Manu alikadiria kuwa kasi ya kula kwa mtu mzito kama Dr. Pius Chilembwa haitokuwa si chini nusu, hivyo muda huo unamtosha sana kufanya vitu vyake. Akafungua mlango na kutoma ndani ya chumba hicho. Kilikuwa ni chumba kikubwa chenye kitanda, kabati kubwa la kuhifadhia nguo na mizigo. Pia kulikuwa na seti la runinga pamoja na birika la kuchemshia maji ya moto kwa ajili ya chai. Pia kulikuwa na choo cha ndani kwa ndani cha kisasa. Akaurudishia mlango kwa kuubana vizuri, haraka haraka akakimbilia kwenye mizigo ya Dr.Chilembwa kwa ajili ya kufanya speksheni.




Kachero Manu alikadiria kuwa kasi ya kula kwa mtu mzito kama Dr. Pius Chilembwa haitokuwa si chini nusu, hivyo muda huo unamtosha sana kufanya vitu vyake. Akafungua mlango na kutoma ndani ya chumba hicho. Kilikuwa ni chumba kikubwa chenye kitanda, kabati kubwa la kuhifadhia nguo na mizigo. Pia kulikuwa na seti la runinga pamoja na birika la kuchemshia maji ya moto kwa ajili ya chai. Pia kulikuwa na choo cha ndani kwa ndani cha kisasa. Akaurudishia mlango kwa kuubana vizuri, haraka haraka akakimbilia kwenye mizigo ya Dr.Chilembwa kwa ajili ya kufanya speksheni.


Akaanza upekuzi wake wa himahima kuogopea asije akabambwa bure ukawa msala mpya kwake. Begi la kwanza halikuwa na vitu vingi zaidi ya nguo za kuvaa, na baadhi ya madawa yake binafsi ya magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, kisukari, moyo, pumu na mengineyo. Alishangazwa sana kwa mtu mmoja kupewa lundo la magonjwa peke yake anataabika nayo peke yake.


Akajisemea moyoni peke yake "Enyi Walalahoi wenzangu, katu msitamani maisha ya vigogo, hatujui magumu wanayoyapitia katika maisha yao". Alipopekua katika begi lingine akakutana na nyaraka mbalimbali ikiwemo ya orodha ya majina ya washirika wakuu na vyeo watakavyopata pindi Dola ya Nyasa ikisimama.


Alistaajabishwa na kuona majina ya wasaliti hao wengine wakiwa ni vigogo wazito tena wapiga vuvuzela maarufu katika chama na serikali iliyopo madarakani. Hii ilikuwa ni nyaraka muhimu sana yenye majina ya vigogo wote washirika wa 'Nyasa Empire Supporters' (NES) zaidi ya 300 wakiwa wamegawanywa kimikoa ya kiutendaji. Akaisunda nyaraka hiyo ndani ya nguo yake ya ndani.


Nyaraka ambayo alijua fika itawasaidia sana vyombo vya dola kuwasaka na kuwachunguza kwa karibu mienendo yao. Akalifunga begi hilo vizuri kabisa na kulirudisha mahali pake. Akiwa anajiandaa kutaka kutoka nje, akasikia mchakato wa viatu unaokaribia chumba kile. Hapo hakufanya ajizi, haraka haraka akakimbilia kwenye kabati na kulifungua kisha akajifungia. Akajikunja na kujibanza vizuri kabisa sehemu ya chini ya kabati.
Hisia zake zilimtuma kiusahihi kabisa, alikuwa ni Dr Pius Chilembwa akirejea chumbani mwake.


Akasikia sauti ya mlango kufunguliwa na kibati malumu ya plastiki chenye sensa. Kachero Manu kijasho chembamba kikaanza kumvuja, huku makwapa yote mawili yakivuja jasho. Alikuwa anaomba kila aina ya dua simu yake kwanza isipigwe akiwa mule kabatini ataumbuka mchana kweupe. Atakamatwa kirahisi kama kuku mwenye mdondo. Pili alikuwa anaomba hasimu wake huyo asije kulifungua kabati maana kuna mkoba ulikuwa umewekwa kwenye rafu ya juu ya kabati lile alilojificha.


Dr.Pius alivyofungua ule mlango akaufunga na kupitiliza moja kwa moja chooni. Kwa mara ya kwanza toka afikie ndani ya jumba lile Kachero Manu akaingiwa na uwoga wa kifo. Alikuwa anatafakari akikamatwa tu, ndio waje wale walinzi mabaunsa wenye nguvu mithili ya simba wa nyika aliyechokozwa habari yake itakuwa imekwisha. Mabausa ambao aliwashuhudia kwa macho yake mmoja wao akiwa pekee yake anam nializa kuku wawili wa kienyeji na beseni la ubwabwa fyuuu.


Mpaka Kachero Manu alikuwa anajiuliza hawa wana matumbo ya kawaida au matumbo yao ni kama mapipa ya taka yanapokea tu bila kukataa.
Akatoka kule msalani na kuanza kupekenyua vifurushi vyake. "BullShit....this is stupidity......nakumbuka kama nilikuja nayo hii document..!" aliropoka kwa nguvu Dr.Pius Chilembwa huku akiporomosha mvua ya matusi. Kachero Manu jasho jekejeke likazidi kumtiririka huku akifahamu fika nyaraka aliyoisunda ndani ya chupi yake ndio inayosakwa sasa hivi. Akasikia michakato ya sauti ya viatu vya Dr. Chilembwa sasa inasogelea kwenye kabati alilojificha.


Haja ndogo na kubwa zote zikawa kama zinataka kumtoka kwa pamoja akijua fika dakika zake za kukamatwa zinahesabika. Akawa anajibana asije kujikojolea hasa ukichukulia ametoka mesini amekula mapochopocho tofauti tofauti na vinywaji bila kwenda msalani.


Kabati likafunguliwa sasa likawa wazi kabisa. Macho ya Kachero Manu yakawa yanakodolea ugoko wa miguu ya Dr.Pius, huku akiona jasho la mgongoni mwa Dr.Pius likiwa linatiririka na kuchuruzika kwenye miguu ishara ya kuonyesha kupotea kwa nyaraka hiyo kwa ghafla ni jambo lililomtingisha haswa. Baada ya dakika kama moja unusu kabati likafungwa tena. Kachero Manu akashusha pumzi nzito za ahueni akishukuru kwa kutokuonekana ndani ya kabati lile.


Ghafla bin vuu bila kutarajia akajikuta ameachia shuzi kali kutokana na mvurugiko wa tumbo lake alilokuwa amelibana muda mrefu. Simu yake marehemu Dr.Chilembwa ikaanza kuita mfululizo kwa nguvu zote. Akasukwasukwa na harakati za kuitoa mfukoni simu yake hiyo. "Mungu wangu anataka nini tena huyu mtu hivi sasa mbona balaa leo" alijikuta anatamka kwa sauti ya juu yenye kitetemeshi Dr Pius Chilembwa.


Alipokea hiyo simu, na kuanza kuongea na mtu aliyempigia hiyo simu.
"Ndio hamna shida nilikuja kuiangalia hiyo nyaraka siioni nahisi nimeisahau nyumbani...Eeh nimekuelewa sana, watume tu watu wako nyumbani wakamuulize Flora vizuri itakuwa nimeiangusha pale sebuleni, OK..bye utanijuza" alimaliza mazungumzo yake kwenye simu na kuikata.



Alipigiwa simu hiyo na Chew-Master toka Tanzania akihitaji nae nyaraka ya washirika wote ili wapitie kwa mara ya mwisho. Baada ya kupita muda wa dakika kama 5 hivi akaondoka ndani ya chumba kile, huku akiwa amemfungia ndani Kachero Manu.
Ndipo nae Kachero Manu akapata nafasi ya kutoka kabatini. Na kufanikiwa kuchomoka salama kwa kuufungua mlango kwa kifaa chake maalumu akiwa tayari amefanikiwa kuiba moja ya nyaraka muhimu sana ya siri, ambayo alikuwa anatembea nayo Dr.Pius Chilembwa peke yake. Hii ilikuwa ni kwa sababu za kiusalama. Kila mmoja alikuwa anawajua wenzake wachache, ili kuleta nidhamu ya uoga miongoni mwao ya kuogopa kusalitiana.


Kachero Manu alikuwa sasa yupo chumbani kwake anasubiria kupigiwa simu ya mkutano lakini muda ukawa unayoyoma haitwi kwenye kikao hicho cha ndani kama alivyoahidiwa. Mpaka ukafika wakati wa mlo wa chajio baada ya magharibi, akaenda kula na kurudi chumbani mwake.
Saa zikaanza kukatika, na sasa ilishatimu saa 6:00 usiku bado ngoma nzito, akazima taa za chumbani mwake na kusogelea dirisha lake chini ya jengo. Akaona ulinzi ndio kwanza umezidi kuimarishwa huku kuna gari mpya mbili. Zilikuwa ni Lori za kisasa zikiwa zimeegeshwa pale chini. Gari zilikuwa zimezungukwa na kulindwa ipasavyo na walinzi waliotapakaa kila pande. Kachero Manu akafunga pazia huku akiwa na tabasamu pana. Moja kwa moja akaelekea bafuni kuoga huku akifahamu fika safari ya Tanzania imeshawadia.


Dr Pius Chiilembwa alileta taarifa ngeni yenye kuleta taharuki juu ya kupotea kwa Bwana Newton Temba kwa Profesa. Taarifa ambayo ilizidi kumchefua ndani ya wiki moja tu kashapoteza wafuasi wake muhimu wawili aliowapika wakapikika. Hivyo wakaamua Profesa arudi mwenyewe nchini kwa muda akishirikiana na Kachero Manu wakaweke mipango sawia, ili harakati za kuisimamisha Dola ya Nyasa zisikwame.


Hivyo kikao kati ya Profesa na Kachero Manu kikawa kimezikwa rasmi, kilichobaki ni wao kesho yake kurejea Tanzania tu. Pesa zilipangwa kusafirishwa kwa njia ya barabara kwa ulinzi mzito. Walikuwa tayari wameshasafisha mazingira yote barabarani kwa kuzunguka mbuyu kwa Maafisa wote wa polisi wa nchi husika ambazo magari hayo yatapitia kwenye barabara za nchi zao. Magari hayo yalipangwa kutua nyumbani kwa Flora Tarimo anapoishi kwa mficho mpenzi wake, marehemu Dr.Pius Chilembwa.


"Tumebakiza mwezi mmoja tutimize azima yetu ya kuibadilisha Tanzania kuwa Dola ya Nyasa kupitia sanduku la kupigia kura. Dola ambayo itakuwa huru na kutambua mchango wa Wanyasa wote katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Leo mashujaa wetu kama Oscar Kambona, Denis Phombeah na Wanyasa wenzetu waliopigania uhuru huwezi kusikia wakitajwa wala kuandikwa kwa wema katika historia ya mapambano ya uhuru wa Tanganyika.


Wanyasa kwa ujumla ndio waasisi wakubwa katika kuanzisha vuguvugu la ukombozi wa bara la Afrika. Katika harakati za ukombozi wa Afrika, mashariki na kusini mwa bara hili, ni Wanyasa ndio waliokuwa juu zaidi kuliko watu wa makabila mengine ingawa ka nchi ka Malawi asili ya mababu zetu ni kadogo na idadi ya watu wake ni ndogo ikilinganishwa na wengine.


Afrika hii nani asiyekumbuka Katika mwaka 1925 kiongozi wa ICU- 'Industrial and Commercial Worker Union'- chama cha wafanyakazi viwandani kule Afrika ya Kusini, ambaye alikuwa ni Mnyasa, Clement Kaadalie, akihutubia ktk mkutano uanzishwaji wa chama hicho alitamka wazi kuwa Waafrika wanachotaka ni milki ya mali zao katika bara lao na serikali ya 'aboriginals' yaani watu wa asili wa bara hili. Huyu alikuwa Mnyasa akiwa nchini Afrika ya Kusini.


Nchini Zambia, Kenneth Kaunda, ambaye ni Mnyasa aliyehamia nchini humo akiwa na mama yake, naye alianzisha harakati za ukombozi katika taifa hilo. Hapa kwetu, kuna orodha ndefu sana ya Wanyasa ambao walioshiriki katika ukombozi wa taifa hili, wakiwemo kina Kambona, Michael Kamaliza, hata Karume sisi tunadai ana asili ya kwetu Nyasa.


Kwa hiyo ndugu wajumbe mkitafakari kwa makini utaona kuwa 'Nyasaland', pamoja na kuwa ka nchi kadogo, haina bahari na uchache wake wa malighafi kuliwafanya watu wake kutoka kwenda nje ambako walijiendeleza na kushiriki katika mapambano ya harakati mbalimbali za ukombozi wa Afrika kuliko watu wengine waliotokea kwenye nchi kubwa na zenye rasilimali nyingi.


Narudia, ni "Nyasaland" zaidi na si nchi nyingine katika bara la Afrika ilitoa watu walioshiriki katika ukombozi sehemu nyingi barani Afrika. Ingawa Rais wao wa kwanza, Hastings Kamuzu Banda, alikuja kuuasi mtazamo huu mpana wenye lengo la kuikomboa Afrika na kuwakumbatia makaburu wa Afrika ya Kusini baadae". Mkutano huo wa kusisimua uliokuwa na malengo ya kuisimika rasmi Dola ya Nyasa ulikuwa unaendelea katikati ya bahari ya Hindi, katika moja ya Hoteli ya kisasa inayoitwa 'The Pride of Indian Ocean' iliyojengwa baharini na mwekezaji wa Kiitaliano.


Ilikuwa ina vyumba vya kulala 300 vilivyopo chini ya bahari na kumbi za kisasa za mikutano na starehe mbalimbali. Kupata nafasi kwenye Hoteli hiyo ulitakiwa uweke oda si chini ya miezi 6. Na gharama ya kulala chumba kimoja kwa siku ilikuwa ni zaidi ya milioni 3 za Kitanzania. Nyasa Empire Supporters (NES) walilipia Hoteli nzima kwa ajili ya huo mkutano wao maalumu wa kihistoria.


Mtaalamu wao wa propaganda katika chama hicho Dr Mathew Chirwa, aliyepata digrii yake ya kwanza mpaka ya uzamivu ya mambo ya propaganda nchini Urusi alikuwa ndio anawalisha sumu ya hatari wajumbe hao. Sumu ya ukabila na kuwafanya wajione wao ni kabila tabaka a'ali sana katika jamii ya Kitanzania kuliko makabila mengine yote.


Wataalamu wa mambo ya propaganda wenyewe wanakiri kuwa Dr.Chirwa alikuwa na uwezo wa kumtia ndimu hata mgonjwa mahututi aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwa ana uwezo wa kupambana na bondia mkali kama Tyson au Mohammed Ali na mgonjwa huyo akajikuta anaamka kitandani na kukunja ngumi tayari kwa mpambano.


Siku ya mkutano huo wa siri Ilikuwa ndio siku ya uzinduzi rasmi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Tanzania nzima. Huku chama tawala wakizindulia kampeni zao katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam, chama cha upinzani cha "National Movement Party" (NMP) cha Dr Patrick Ndomba kilikuwa kinajimwayamwaya katika viwanja vya Jangwani. Maajabu ni kwamba mpaka saa 10:00 jioni kadamnasi ya wafuasi wa chama tawala walikuwa hawazidi hata watu elfu ishirini (20,000) katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watu elfu sitini (60,000) huku wafuasi waliohudhuria mkutano wa chama kikuu cha upinzani cha NMP walikuwa ni zaidi ya laki moja (100,000).


Dalili ya mvua ni mawingu, kama uchaguzi ungekuwa unafanyika siku hiyo chama tawala kilikuwa kinadondoka madarakani asubuhi na mapema tu, habari yao kwisha kabisa. Walikuwa wanapumulia kwa kutumia mipira ya gesi kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Mkutano wa chama tawala ulipooza kama mkojo wa ngedere na wananchi walitokea tu kukichukia ghafla chama tawala kutokana na ukwapuaji wa mabilioni ya pesa katika mabenki uliofanyika.


Wizi ambao ulisababisha baadhi ya mabenki kufunga matawi yao nchini na kuhamia nchi za jirani. Hali ambayo ilisababisha ugumu wa maisha kwa walalahoi kutokana na ukosefu wa mikopo midogo midogo kwa wajasiriamali wa kipato duni. Wajasiriamali ambao mabenki hayo ndio yalikuwa mkombozi wao.
Chama cha upinzani cha "NMP"' wao walikamatia hapo hapo kwenye nukta ya ufisadi. Wao walishikilia ajenda hiyo hiyo tu, hawakubali kutolewa nje ya mada.

Kampeni zao na porojo zao kutwa kucha zilikuwa zinazungumzia ufisadi wa ukwapuaji wa zaidi ya bilioni 560 uliotokea katika mabenki. Huku wakipayuka kwenye maspika ya uwanjani hao waziwazi kuwa zimeibwa na vigogo wa chama na serikali ya chama tawala, ndio maana mpaka sasa hamna mtu aliyetiwa mbaroni.


Wakati mkutano wa hadhara wa chama cha Dr Patrick Ndomba unaendelea kurindima, huko katika viwanja vya Jangwani, nyuma ya pazia huko baharini kulikuwa na kikao haramu kinaendelea. Kikao ambacho kina mkono wa chama cha NMP bila wananchi kufahamu chochote. Nyasa Empire Supporters (NES) walikuwa ndio washika dau wakuu wanaotaka kuingia madarakani kupitia mgongo wa chama cha siasa cha National Movement Party (NMP).


NES ndio walikuwa wanalipa mishahara na marupurupu ya waajiriwa wote wa chama cha NMP, walifadhili ujenzi wa makao makuu ya kisasa ya chama hicho, na kugharamia gharama zote za kampeni nchi nzima za chama hicho.
"Pindi ukiisha tu uchaguzi na chama chetu pendwa cha NMP kushika hatamu ya madaraka, jambo la kwanza ni kubadili jina la chama, nalo ni kutoka 'National Movement Party' na kuwa 'Nyasaland Movement Party' (NMP). Aliposema hivyo ukumbi mzima ukaripuka kwa shangwe, mayowe na vigeregere.


Pili kitakachofuatia kwa kutumia wingi wa Wabunge wetu bungeni tutabadili katiba ambayo sasa itamfanya Waziri Mkuu awe ndio mwenye mamlaka ya juu ya kiutendaji kuliko Rais. Kwa mnasaba huo Rais mtarajiwa Dr Patrick Ndomba atakuwa pale juu kama nyoka la kibisa 'Figurehead'. Kisha Professor Potchefstroom ambao wengi hamumjui wala kumfahamu kuwa ni Mnyasa wao wanajua ni Mchaga ndio atakuja kushika madaraka ya Uwaziri Mkuu. Hapo ndipo Tanzania itageuka kuwa nchi mfadhili maana huyo jamaa ana akili za kuzaliwa nao atawapeleka mpwito mpwito wababe wa kiuchumi wa dunia.


Jambo litakalofuata baada ya hapo ni kubadilisha makao makuu ya nchi kutoka Dodoma na kuhamishia Ruvuma, huku Kinyasa kikitangazwa rasmi kuwa ni lugha kuu ya mawasiliano na kufundishia mashuleni. Pia tutamtangaza rasmi Bwana Oscar Kambona kama Baba wa Taifa namba mbili baada ya Mwalimu Nyerere.


Tutamjengea upya kaburi lake linaloendana na hadhi yake huku tukiweka mnara mrefu sana utakaoangaza nuru yake mpaka kwenye ardhi ya Mababu zetu huko Malawi. Hatuishii hapo, bali jina la nchi nalo litabadilishwa na kuwa "Nyasa Empire", huku harakati na juhudi za kuziunganisha nchi ya Malawi na Tanzania zitafanyika ili kupata dola moja ya "Nyasa Empire" yenye nguvu.


Mikakati hatari na mizito ya uhaini ilikuwa inapangwa huku si Kachero Manu wala Kachero Yasmine aliyefanikiwa kuingiza pua yake kwenye mkutano huo. Walikuwa wamepigwa chenga kali ya mwili, wakatepeta tepetepe kama chapati za maji. Bado walikuwa wanahanjahanja kutafuta mbinu za kupenya waweze kuingia mkutanoni.


Huko Ikulu nako mambo yalikuwa mazito, ugali moto, mchuzi moto kwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bwana Omega Mtanika. Mheshimiwa Rais alikuwa amempa masaa 24 ahakikishe watuhumiwa wote wanakamatwa na kufikishwa mahakamani vinginevyo kibarua chake kinaota nyasi mara moja.


Kachero Manu alishawasili eneo la tukio tayari kwa kuhudhuria mkutanoni. Siku hiyo ya mkutano Hoteli hiyo ya "The Pride of Indian Ocean" ilikuwa inalindwa na askari wa kike warembo waliokodishwa toka nchini Ethiopia wakiitwa kwa lakabu ya "Black-Guard". Askari ambao kama watavua gwanda zao na kuvikwa libasi za ulimbwende basi mmoja wao anaweza kushinda taji la "Miss World"'. Walikuwa ni visura haswa ambao nmoja wao akikubali uwe nae unaweza kuuza hata nyumba yako ya urithi ili mradi tu upate pesa za kumhudumia yeye asije kukuacha kwenye mataa.

Walinzi hao zaidi ya 20 walijigawa kivitengo kwa ajili ya kulinda Hotelini pale. Walinzi wa kila siku walipewa mapumziko maalumu siku hiyo wasitie mguu eneo hilo. Ni wafanyakazi wa usafi na wapishi tu wa Hotelini hapo ndio walikuja kazini kama kawaida yao. Yasmine taarifa zote za mkutano kufanyikia hapo alikuwa anazipata kupitia vifaa vya siri alivyovifunga nyumbani kwa Flora kupitia mazungumzo ya Dr Pius Chilembwa na washirika wake. Kizuri zaidi hata Professor Potchefstroom nae alifikia nyumbani kwa Dr Pius Chilembwa.

Yasmine kupata kibali cha kuingilia hapo Hotelini, alimsaka dada mmoja muajiriwa wa kitengo cha usafi hapo Hotelini na kumtongoza ampe kitambulisho chake cha kazini. Pia alimtaka siku hiyo asikanyage kabisa ofisini. Alielekezwa nia na madhumuni ya Kachero Yasmine Hotelini hapo, akafanikiwa kukipata kitambulisho chake cha kazi. Yasmine akapewa Alifu Bee Tee za mazingira na utamaduni ya usafi Hotelini hapo ili asije kuyaboronga mambo.


Yasmine habari yake ikawa imeshawezekana ya yeye kutinga pale Hotelini "The Pride of Indian Ocean".
Pia Yasmine kupitia idara iliyopo chini ya Wizara ya Ardhi inayohusika na upitishaji wa ramani za majengo, akapata mchoro mzima wa jengo hilo la Hoteli ya kisasa lililojengwa na kampuni ya kigeni na mkandarasi tokea Uisraeli. Kufanikiwa kufika Hotelini hapo ni mwendo wa nusu saa kwa boti yenye kasi kutoka Ufukwe wa Kunduchi.


Kachero Manu yeye kufika Hotelini nae haikuwa tatizo, ila tatizo kubwa ni kwake ni namna ya kuingia katika ukumbi wa mkutano. Katika kuimarisha usalama wao zaidi kwa ajili ya kuhofia mamluki kupandikizwa kutokana na kupotea kwa 'Man-Temba', kifo cha kutatanisha cha Nathanieli, kupotea kwa nyaraka za siri za Dr Pius Chilembwa na mengineyo yaliyowafanya vigogo wa juu watumie mtindo wa kuingia kwa kutumia nywira ya siri. Nywira ambayo kila mwanachama wa 'Nyasa Empire Supporters' (NES) aliitumia pindi aliposajiliwa kwa mara ya kwanza kundini.


Tangazo la ghafla lilitoka hapo hapo kabla ya kuingia ukumbini wakiwa katika foleni za kuingia ukumbini. Kifaa maalumu kiliwekwa kinachokutaka uingize nywira ya siri ndio mlango ufunguke uingie ndani. Mwanachama ulikuwa unapewa nafasi ya kujaribu namba yako ya siri mara tatu tu ukikosa, unakamatwa na kwenda kuhojiwa.


Kachero Manu jasho jekejeke lilikuwa linamtiririka akiwa katikati ya foleni hawezi tena kuchomoka huku walinzi wakiwa makini kutaka kuwatia mbaroni washukiwa wowote wale. Ikafika zamu yake Kachero Manu ya kubonyeza namba za kitufe kile ili mlango umruhusu kuingia ukumbini. Alishajua habari yake imekwisha atageuzwa kuwa asusa ya mkutano huo wa 'Nyasa Empire Supporters' (NES).


Akawa anawaza hasira atakazokuwa nazo Dr. Pius Chilembwa na Professor Potchefstroom jinsi watakavyomshukia kama kipanga anavyokishukia kifaranga cha kuku. Hasa kwa kutambua kumbe alikuwa ni kirusi kilichopandikizwa kwao na Usalama wa Taifa. Akajipa moyo, chambilecho 'tumbo la shari huzaa heri'.


Akaanza kubofya mara ya kwanza, mashine ikapiga kelele ya kukataa kuwa namba ya siri iliyoingizwa sio yenyewe. Akajitutumua kubahatisha tu kwa kubonyesha namba yoyote ile huenda fali njema ikamuangukia mlango ukafunguka. Mashine ikagoma kwa mara ya pili huku ikimpa nafasi ya mwisho ya kujaribu. Walinzi wale sasa wakamsogelea kwa ukaribu zaidi kumbana ili asije akawatoroka tayari walishamtilia mashaka.


Kachero Manu uso wake ulishapigwa na fedheha na soni huku akijua tayari kashakamatika kirahisi bila hata kunusa ukumbini. Akajitutumua tena kwa mara ya mwisho kujaribu kuingiza namba, huku akiomba kila aina ya dua. Kilichotokea alishtukia tu kashapigwa mtama wa nguvu na wale walinzi wa kike. Tayari akabebwa mzobemzobe kama mpira wa kona anagombaniwa anapelekwa sehemu kusikojulikana.


Tenge tehanani ikaibuka zogo mtindo mmoja wakifurahia mfumo huo utakaosaidia kukamatwa kwa mamluki wote waliopandikizwa.
Washirika wote wakafanikiwa kuingia kwenye mkutano huo kasoro Kachero Manu pekee. Mkutano huku ukiwa unaendelea baadhi ya vigogo wa NES wakawa wapo na Kachero Manu wanamdodosa kwa undani.


"Hongera sana Kachero Manuel Yosephu kwa kazi nzuri uliyoifanya mpaka sasa" alifungua maongezi yake Chew-Master kwa sauti nzito, akiwa ameficha uso wake kwa kitambaa maalumu. Hakutaka Kachero Manu atambue anaongea na mtu gani. Walikuwa ni watu wanaotambuana kiundani kabisa kutokana na kukutana katika vikao mbalimbali vya ulinzi na usalama wa nchi.

"Lazima nikubali uwezo wako hasa kutokana na kwamba hamna mtu aliyejaribu kuitikisa ngome yetu akabakia salama. Nadhani ulisikia kilichompata Inspekta Mengi Matunda kashabakia mifupa mitupu huko kaburini pindi alipochaguliwa kufanya taftishi ya kundi letu la Nyasa Empire Supporters (NES)" akaweka kituo cha maongezi yake akawasha sigara yake kisha akasimama na kuelekea mpaka kwenye kiti alichofungwa Kachero Manu. Akapiga pafu ndefu kisha akamuinamia Kachero Manu kisha akampumulia moshi wa sigara usoni mwake.

"Koh..koh..koh...stupid, stop this you coward...!" aliongea kwa shida Kachero Manu huku akiwa anakohoa kutokana na kupaliwa na moshi wa sigara. "Ha..Ha... Ha ..Ha....Kachero namba wani wa nchi ya Tanzania, tulitamani uwe Kachero namba wani kwenye utawala wa Dola ya Nyasa kama ungetulia tuli na kuacha kiherehere chako. Hivyo kimbelembele chako cha kujifanya mtu wa kazi kimekuponza, umetukwepa sana kuanzia kule Arusha kwenye ajali ya bomu kwenye gari ulivyookolewa kimiujiza na mizimu ya babu zako wa Kimwera" aliendelea kumsomea risala yake ya kifo yenye kebehi ndani yake.
"Stop talking non-sense....kama kidume cha mbegu vua hiyo maski usoni, vinginevyo mie naona unaniimbia taarabu tu, kwa sauti yako nyororo" aliongea Kachero Manu kwa kumkatisha maongezi huku akiombea itokee fursa ya wafanye makosa aweze kuwageuzia kibao.

Askari wale wa kike ambao hawajui lugha ya kiswahili hata ya kupapasia waliweka silaha zao za kivita, mkao wa kushughulika. Wao wakati wote walikuwa wanawasiliana kwa lugha ya Kiingereza tu. Maneno yale ya dharau yaliyotamkwa na Kachero Manu dhidi yake yalimchoma vilivyo Chew Master. Uso wake ulibadilika na paji lake kutengeneza matuta. Akapiga mluzi uliosababisha ajitokeze kipande cha mtu mwenye miraba minne mweusi tii.
Mtu huyo alikuwa amebeba pasi ya umeme mkononi mwake.

Haraka haraka bila kuambiwa chochote akaenda kuichomeka ukutani kwenye soketi ya umeme, kisha akamvamia Kachero Manu na kuanza kuirarua singlendi yake, akimuacha kidari wazi. Pasi ikawa imeshashika moto kisawasawa. Akaikamata pasi na kumuwekea kifuani Kachero Manu.

"Aaaaaaaaah....Aaaaaaah....Aaaaah..". Kachero Manu alikuwa analalamika kwa maumivu makali. Chew-Master alikuwa anacheka mbavu hana jinsi Kachero Manu anavyoteseka kwenye moto wa pasi.
"Yule nyau mwenzako wa kike anayejifanya muajiriwa wa Benki Kuu, nae muda sio mrefu atakamatwa, amechoropoa nyaraka muhimu nyumbani kwa rafiki yake Flora, hivyo huna msaada leo, tutaondosha roho zenu na kukutupa baharini miili yenu iwe chakula cha samaki" aliendelea kubwabwaja Chew-Master maneno ya kumtia hasira.

Baada ya mateso ya moto wa pasi, ikaanza adhabu ya mijeledi ya mgongoni toka kwa wale walinzi wa kike toka Ethiopia. Kipindi chote wakati atateswa alikuwa anarekodiwa video kwa kutumia simu ya mkononi. Huku 'Chew Master' akimchagiza kuwa atakapokufa video yake itakuwa inaonyeshwa kwenye vipindi vya televisheni kila siku kabla ya kusomwa taarifa ya habari kama mmoja wapo wa maadui wa Dola ya Nyasa.

Baada ya muda fulani, likaja agizo la Kachero Manu kupelekwa kwenye ukumbi wa mkutano ili ashuhudiwe na watu wote, wafuasi wote wa 'NES'. Akafunguliwa kamba kutoka kwenye kiti na kukokotwa akiwa sasa amefungwa pingu za mikononi. Mwili wote ulikuwa unavuja damu, huku akitembea kwa kuchechemea kutokana na maumivu ya vipigo. Kachero Manu kifo alikiona kabisa kipo mbele ya uso wake kinakaribia kumvaa kimuondoshe duniani.



Kachero Yasmine alikuwa tayari ameshatinga Hotelini yupo upande wa maeneo ya chooni anafanya usafi. Lakini akili yake yote ilikuwa inawaza na kuwazua namna gani atafanikiwa kuingia ukumbi wa mkutano, ambao kwa bahati ulikuwa kama meta 25 kutoka eneo la vyoo analofanyia usafi. Kingine kilichokuwa kinampa mawazo ni kujua je Kachero Manu kafanikiwa kuingia ukumbini? Ni moja ya maswali yaliyokuwa yanamsumbua sana kichwani mwake.


Ghafla bin vuu wakati bado anapiga deki kwenye korido nje kidogo ya vyoo akamuona Kachero Manu anakokotwa kidari wazi huku damu zinamvuja mwilini wakiwa wanatokea chini ya jengo wakimpandisha roshani ya juu. Alikuwa anasindikizwa na walinzi wa kike watatu huku mmoja wao akionekana kama ndio kiongozi wao akiwa yupo nyuma amefuatana na Chew Master wanabonga simulizi mbili tatu. Akawaangalia kwa makini mpaka wanatokomea ndani ya jengo lile.

Kachero Yasmine alishikwa na uchungu usiomithilika hasa baada ya kumuona Bosi wake yupo kwenye dhahama na nakama isiyoelezeka. Sasa alijua jukumu lote la kubutua kombolela lipo mikono mwake. Akiwa bado amepigwa na tahayuri anawaza jambo la kufanya ili apindue upande wa pili wa shilingi.


Akiwa kwenye hali hiyo akamuona yule mkuu wao wale walinzi wa kike kutoka nchini Ethiopia, 'Black Guards" akiwa anakuja kwa kasi upande wa chooni alipo Kachero Yasmine na sare zake za watumishi wa usafi wa Hoteli ile ya "The Pride of Indian Ocean". Tayari akili ya kuzaliwa ya Kachero Yasmine ikafanya kazi haraka sana, akajua kitu cha kumfanyia yule Afisa Mkuu, pindi akiingia kwenye anga zake.


Yule Afisa akampita na kumsalimu kwa tabasamu jepesi huku akimpungia mkono halafu akaharakisha kufungua mlango wa kuelekea chooni, akionyesha fika amebanwa na haja. Alimpa sekunde zisizozidi 35 akamfuata upande wa chooni kwa mwendo wa kunyata usiotengeneza michakato ya sauti za nyayo.
Kwanza akaufunga mlango mkuu wa kuingilia vyoo vile maalumu kwa watu VIP huku nje ya mlango akaweka kibao cha kuonyesha kuwa havitumiki kwa sasa kutokana na usafi unaoendelea. Alipotupa jicho lake kule ndani ya choo akaona kuna choo kimoja mlango wake umefungwa kuonyesha kuna mtu anakitumia. Akakipita choo hicho na kujibanza nyuma ya mlango wa choo kinachofuata.


Punde si punde akasikia sauti ya maji yanatoka kwenye flashi ya chooni kuashiria kuwa ameshamaliza kushughulika kule chooni hivyo anajiandaa kutoka. Alipofungua tu mlango, yule Mkuu akachomoa simu yake mfukoni na kuanza kuiperuzi bila kuangalia usalama wake. Akawa amempa mgongo Kachero Yasmine.


Likawa kosa kubwa kwake, Kachero Yasmine akamfuata taratibu na kisha akarusha karate ya shingo ili ammalize pale pale bila kupata muda wa kuomba maji wala kutoa sala ya toba. Kumbe yule dada hakuwa Afisa machejo, kazi yake alikuwa anaziweza haswa.
Kwa kutumia hisia tu akainamisha shingo yake chini bila kuangalia nyuma jambo ambalo lilimsabisha Kachero Yasmine ayumbe kidogo kutokana na nguvu alizokusanya za kurusha karate ile.


Yule Afisa hakumchelewesha Kachero Yasmine, akageuka kama umeme na kumtwanga konde la juu ya jicho la kushoto na kumsababisha Yasmine alambe sakafu bila kupenda.
Alikuwa ni komandoo wa kundi la Oromo Empire Supporters (OES), kundi ambalo walikuwa na malengo pacha yanayofanana na Nyasa Empire Supporters (NES) ya kujitenga kutoka nchi ya Ethiopia. Walikuwa wanataka kuunda nchi mpya ya kabila la Oromo wanaoishi kaskazini mwa nchi ya Ethiopia.


Kachero Yasmine akajizoazoa sakafuni, aliposimama na kugusa jicho lake akalikuta linachuruzika damu. Yule Afisa Mkuu hakuwa na papara akawa anamsubiria Kachero Yasmine aamke, wafirigisane kiukweli.
Kitendo cha kuona damu yake mzalendo wa nchi inamwagika tena imemwagwa na watu mamluki hasira zake zikachemka. Alimfuata kwa kasi na kuanza kumrushia mateke na mangumi mfululizo katika mitindo mipya kabisa ya sanaa za mapigano ambayo yule komandoo toka Oromo alikuwa hajawahi kuishuhudia.


Baada ya dakika kama 3 tu yule Afisa Mkuu alikuwa amechakazwa vibaya sana hatamaniki, amekula dafrao sakafuni.
Haraka haraka akamvua nguo zake na kumsachi mifukoni akamkuta ana ufunguo wa pingu pamoja na bastola moja ya kisasa. Akamburuta mpaka chooni kisha hima hima akazivaa yeye nguo zake kisha akamfungia mule chooni. Akaenda kwenye sanduku la huduma la kwanza lililomo chooni mule mule, na kutoa dhana za kitabibu anazohitaji. Akasogelea kwenye kioo na kuanza kujishona jeraha la juu ya jicho lake la kushoto. Baada ya muda mfupi tu akawa ameshamaliza kujishona, akafunika jeraha lake kwa kutumia plasta ndogo.


Akajiangalia kwenye kioo na kutabasamu baada ya kujiona amefanana vilivyo na yule Afisa Mkuu, hasa kutokana na rangi yake ya Kipemba alionekana mithili ya wadada toka nchini Ethiopia. Akafungua mlango wa kutokea kwenye korido akaishushia kofia yake upande wa kushoto kidogo kuficha plasta iliyofunika jeraha lake.
"General General....you are needed urgently General..!" mmoja wa walinzi alikuwa anakuja kwa kasi uelekeo wa chooni kumuita Afisa Mkuu akidhania Kachero Yasmine ndio Afisa wao Mkuu.


Yasmine hakujibu kitu zaidi ya kuitikia kwa kichwa kuonyesha amekubaliana na maelezo aliyopewa. Akachomoa simu yake toka mfukoni na akaanza kupiga simu mbili tatu za haraka kisha akakata simu na kuiweka mfukoni mwake na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha mkutano kuitikia wito.
Kabla hajafungua mlango, akasita kuingia kama vile kuna kitu amekumbuka. Akamuita mmoja wa wafanya usafi wa kiume aliyekuwa ana hanjahanja na kumnong'oneza kitu. Walipokelewa na maagizo aliyompa, akachomoka mbio mbio kama mwehu, mpaka Kachero Yasmine akaachia tabasamu pana. Akakamata kitasa na kuingia ukumbini, tayari kwa mapambano.


Alipoingia na kutupa macho yake pembeni, akamuona Kachero Manu kwa mbali kawekwa pembezoni mwa meza kuu. Machozi ya hasira yakiwa yanamtiririka Kachero Manu akitamani muujiza utokee awashughulikie wabaya wake. Kachero Yasmine bila kusema chochote moja kwa moja akaenda mpaka alipo Kachero Manu na kuanza kumfungua pingu zake, halafu akaziegesha huku akimnong'oneza kuwa yeye ndio Kachero Yasmine. Aliwazuga kama anahakikisha amefungwa zile pingu kisawasawa.


Wana kikao walikuwa wanaendelea na mkutano wao huku wakimsubiria Profesa aingie wamuadabishe Kachero Manu. Kachero Yasmine akaona moja ya siti ipo tupu, akaenda kukaa kwenye kiti nyuma ya Chew-Master huku akijinuiza nafsini mwake kuwa wa kwanza kumtia adabu atakuwa huyu Chew-Master. ambaye ndio mzizi wa ulinzi wao mahasimu zake.


Punde si punde ghafla wote wakasimama ukumbi mzima wakati Profesa akiingia ukumbini akiwa katika sura yake halisi bila kujificha uso. Walikuwa wanapiga makofi ya pongezi kwa kishindo kuonyesha kufurahishwa na ujio wake mkutanoni. Wengi wao macho yaliwatumbuka kumshangaa Profesa Asante-Rabbi ikiwa ni mara yao ya kwanza kwao sura yake kudhihiri mbele yao. Walikuwa wanamsikia tu simulizi zake za kustaajabisha ila leo wamefanikiwa kumuona mubashara.


Alipoketi kitini, mara moja mipango mbalimbali ya namna pesa zitakavyowafikia huko Mikoani za kuhonga wapiga kura kwa ajili ya kukichagua chama cha 'National Movement Party' (NMP) ikaanza kupangwa. Malengo yao yalikuwa ni kupata kura milioni 8 tu za kununua huku wakijumlisha na wale wafuasi kindakindaki walikuwa na uhakika wa kupata kura milioni 10. Kura ambazo zingewatosha kuingia Ikulu na kuunda serikali.


Ajenda yao ya mwisho ikaanza kumjadili Kachero Manu, huku ikiamrishwa asogezwe mbele ya meza kuu. Kachero Yasmine alitoa amri mmoja wa askari wake wa kike ndio akae jirani na Kachero Manu ili awe chambo cha kupokonywa silaha kirahisi na Kachero Manu ili wakilianzisha wote waanzishe vagi kwa pamoja wakiwa na silaha.
Profesa sasa ukawa uwanja wake wa kujimwayamwaya kwa kujifunga kibwebwe uwanjani dhidi ya adui yake Kachero Manu.


"Nitakuchinja mbele ya umati huu wa watu iwe fundisho kwa wasaliti wengine" alizungumza Profesa huku akiwa anafoka kwa hasira.
"Umenidanganya kuwa umetumwa na kijana wangu Man-Temba kumbe wewe ndio umempoteza, na kijana wangu Nathanieli pia mmemuua. Umekaa nyumbani kwangu nimekupa mbinu zote za medani za udukuzi kumbe unanidhihaki ukinifanya zuzu tu eeh...sasa nitakuonyesha kilichomtoa kanga manyoya..!". Akaanza kumkaribia Kachero Manu huku ameshachomoa bisu kubwa lenye makali toka kiunoni amekaa nyuma ya shingo la Kachero Manu.


Kachero Manu hakusubiri kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara, fujaa bila kutarajiwa, alijirusha hewani toka kitini na kufanikiwa kumpokonya silaha yule mlinzi mwanamke kisha akiwa bado hewani akafanikiwa kumbana Profesa roba ya miguu kwenye shingo. Wote kwa pamoja wakaanguka chini kwa kishindo cha tii!.
Kachero Yasmine nae hakulaza damu akaanza kuchakaza meza kuu kwa risasi akianzia na Chew Master.


Kishindo kikubwa cha mlango kuvunjwa na bomu kikasikia huku wakiingia makomandoo 5 wa jeshi la wananchi, JWTZ. Walipata wito wa Kachero Yasmine waje kuongeza nguvu wakawasili kwa kutumia nyambizi.
Ndio hao makomandoo alimtuma yule mtumishi wa usafi ahakikishe anawaelekeza mkutano ulipo kwa haraka. Makomandoo wengine walipigiwa simu na Yasmine wakati anatoka chooni wakawa wameshaizunguka nyumba ya Flora Tarimo.


Papatu papatu ya mapigano ilirindima vilivyo. Washirika zaidi ya 20 walishapoteza maisha, huku wengine wote wakijisalimisha na kutiwa mbaroni.
Profesa Asante Rabbi na Chew Master walikuwa wapo hoi kwa mkong'oto kabambe wa paka mwizi walioupokea siku hiyo. Walinzi wa kike karibia wote walikuwa wameuliwa. Tayari zilishaitishwa boti za kutosha za kuwapakiza washirika wote wa NES tayari kwa ajili ya kuwafikisha katika vituo mbalimbali vya polisi.


Kachero Manu na Kachero Yasmine wakakumbatiana kwa furaha, wakipongezana. "Ahsante Yasmine, kazi imekwisha!" alisema Kachero Manu. "Bosi bado kazi mbichi, pesa bado hatujazikomboa na marehemu Dr.Pius Chilembwa bado hatujamtia mbaroni. Anatakiwa akafufuliwe alipojizika aje kusimama mbele ya vyombo vya dola kujibu mashitaka yake" Kachero Yasmine alimgutusha Bosi wake wajibu wake uliobakia. Wakati makomandoo wale wakiwaswaga washirika wale kuwaingiza kwenye boti, Kachero Manu na Kachero Yasmine walitoweka kimaajabu Hotelini pale bila kujulikana wanapoelekea.


Kachero Yasmine alikuwa tayari ameshatinga Hotelini yupo upande wa maeneo ya chooni anafanya usafi. Lakini akili yake yote ilikuwa inawaza na kuwazua namna gani atafanikiwa kuingia ukumbi wa mkutano, ambao kwa bahati ulikuwa kama meta 25 kutoka eneo la vyoo analofanyia usafi. Kingine kilichokuwa kinampa mawazo ni kujua je Kachero Manu kafanikiwa kuingia ukumbini? Ni moja ya maswali yaliyokuwa yanamsumbua sana kichwani mwake.
Ghafla bin vuu wakati bado anapiga deki kwenye korido nje kidogo ya vyoo akamuona Kachero Manu anakokotwa kidari wazi huku damu zinamvuja mwilini wakiwa wanatokea chini ya jengo wakimpandisha roshani ya juu. Alikuwa anasindikizwa na walinzi wa kike watatu huku mmoja wao akionekana kama ndio kiongozi wao akiwa yupo nyuma amefuatana na Chew Master wanabonga simulizi mbili tatu. Akawaangalia kwa makini mpaka wanatokomea ndani ya jengo lile.
Kachero Yasmine alishikwa na uchungu usiomithilika hasa baada ya kumuona Bosi wake yupo kwenye dhahama na nakama isiyoelezeka. Sasa alijua jukumu lote la kubutua kombolela lipo mikono mwake. Akiwa bado amepigwa na tahayuri anawaza jambo la kufanya ili apindue upande wa pili wa shilingi.
Akiwa kwenye hali hiyo akamuona yule mkuu wao wale walinzi wa kike kutoka nchini Ethiopia, 'Black Guards" akiwa anakuja kwa kasi upande wa chooni alipo Kachero Yasmine na sare zake za watumishi wa usafi wa Hoteli ile ya "The Pride of Indian Ocean". Tayari akili ya kuzaliwa ya Kachero Yasmine ikafanya kazi haraka sana, akajua kitu cha kumfanyia yule Afisa Mkuu, pindi akiingia kwenye anga zake.
Yule Afisa akampita na kumsalimu kwa tabasamu jepesi huku akimpungia mkono halafu akaharakisha kufungua mlango wa kuelekea chooni, akionyesha fika amebanwa na haja. Alimpa sekunde zisizozidi 35 akamfuata upande wa chooni kwa mwendo wa kunyata usiotengeneza michakato ya sauti za nyayo.
Kwanza akaufunga mlango mkuu wa kuingilia vyoo vile maalumu kwa watu VIP huku nje ya mlango akaweka kibao cha kuonyesha kuwa havitumiki kwa sasa kutokana na usafi unaoendelea. Alipotupa jicho lake kule ndani ya choo akaona kuna choo kimoja mlango wake umefungwa kuonyesha kuna mtu anakitumia. Akakipita choo hicho na kujibanza nyuma ya mlango wa choo kinachofuata.
Punde si punde akasikia sauti ya maji yanatoka kwenye flashi ya chooni kuashiria kuwa ameshamaliza kushughulika kule chooni hivyo anajiandaa kutoka. Alipofungua tu mlango, yule Mkuu akachomoa simu yake mfukoni na kuanza kuiperuzi bila kuangalia usalama wake. Akawa amempa mgongo Kachero Yasmine.
Likawa kosa kubwa kwake, Kachero Yasmine akamfuata taratibu na kisha akarusha karate ya shingo ili ammalize pale pale bila kupata muda wa kuomba maji wala kutoa sala ya toba. Kumbe yule dada hakuwa Afisa machejo, kazi yake alikuwa anaziweza haswa.
Kwa kutumia hisia tu akainamisha shingo yake chini bila kuangalia nyuma jambo ambalo lilimsabisha Kachero Yasmine ayumbe kidogo kutokana na nguvu alizokusanya za kurusha karate ile. Yule Afisa hakumchelewesha Kachero Yasmine, akageuka kama umeme na kumtwanga konde la juu ya jicho la kushoto na kumsababisha Yasmine alambe sakafu bila kupenda.
Yule Afisa alikuwa ni komandoo wa kundi la Oromo Empire Supporters (OES), kundi ambalo walikuwa na malengo pacha yanayofanana na Nyasa Empire Supporters (NES) ya kujitenga kutoka nchi ya Ethiopia. Walikuwa wanataka kuunda nchi mpya ya kabila la Oromo wanaoishi kaskazini mwa nchi ya Ethiopia. Kachero Yasmine akajizoazoa sakafuni, aliposimama na kugusa jicho lake akalikuta linachuruzika damu. Yule Afisa Mkuu hakuwa na papara akawa anamsubiria Kachero Yasmine aamke, wafirigisane kiukweli.
Kitendo cha kuona damu yake mzalendo wa nchi inamwagika tena imemwagwa na watu mamluki hasira zake zikachemka. Alimfuata kwa kasi na kuanza kumrushia mateke na mangumi mfululizo katika mitindo mipya kabisa ya sanaa za mapigano ambayo yule komandoo toka Oromo alikuwa hajawahi kuishuhudia. Baada ya dakika kama 3 tu yule Afisa Mkuu alikuwa amechakazwa vibaya sana hatamaniki, amekula dafrao sakafuni.
Haraka haraka akamvua nguo zake na kumsachi mifukoni akamkuta ana ufunguo wa pingu pamoja na bastola moja ya kisasa. Akamburuta mpaka chooni kisha hima hima akazivaa yeye nguo zake kisha akamfungia mule chooni. Akaenda kwenye sanduku la huduma la kwanza lililomo chooni mule mule, na kutoa dhana za kitabibu anazohitaji. Akasogelea kwenye kioo na kuanza kujishona jeraha la juu ya jicho lake la kushoto. Baada ya muda mfupi tu akawa ameshamaliza kujishona, akafunika jeraha lake kwa kutumia plasta ndogo.
Akajiangalia kwenye kioo na kutabasamu baada ya kujiona amefanana vilivyo na yule Afisa Mkuu, hasa kutokana na rangi yake ya Kipemba alionekana mithili ya wadada toka nchini Ethiopia. Akafungua mlango wa kutokea kwenye korido akaishushia kofia yake upande wa kushoto kidogo kuficha plasta iliyofunika jeraha lake.
"General General....you are needed urgently General..!" mmoja wa walinzi alikuwa anakuja kwa kasi uelekeo wa chooni kumuita Afisa Mkuu akidhania Kachero Yasmine ndio Afisa wao Mkuu. Yasmine hakujibu kitu zaidi ya kuitikia kwa kichwa kuonyesha amekubaliana na maelezo aliyopewa. Akachomoa simu yake toka mfukoni na akaanza kupiga simu mbili tatu za haraka kisha akakata simu na kuiweka mfukoni mwake na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha mkutano kuitikia wito.
Kabla hajafungua mlango, akasita kuingia kama vile kuna kitu amekumbuka. Akamuita mmoja wa wafanya usafi wa kiume aliyekuwa ana hanjahanja na kumnong'oneza kitu. Walipokelewa na maagizo aliyompa, akachomoka mbio mbio kama mwehu, mpaka Kachero Yasmine akaachia tabasamu pana. Akakamata kitasa na kuingia ukumbini, tayari kwa mapambano.
Alipoingia na kutupa macho yake pembeni, akamuona Kachero Manu kwa mbali kawekwa pembezoni mwa meza kuu. Machozi ya hasira yakiwa yanamtiririka Kachero Manu akitamani muujiza utokee awashughulikie wabaya wake. Kachero Yasmine bila kusema chochote moja kwa moja akaenda mpaka alipo Kachero Manu na kuanza kumfungua pingu zake, halafu akaziegesha huku akimnong'oneza kuwa yeye ndio Kachero Yasmine. Aliwazuga kama anahakikisha amefungwa zile pingu kisawasawa.
Wana kikao walikuwa wanaendelea na mkutano wao huku wakimsubiria Profesa aingie wamuadabishe Kachero Manu. Kachero Yasmine akaona moja ya siti ipo tupu, akaenda kukaa kwenye kiti nyuma ya Chew-Master huku akijinuiza kuwa wa kwanza kumtia adabu atakuwa huyu Chew-Master. ambaye ndio mzizi wa ulinzi wao mahasimu zake.
Punde si punde ghafla wote wakasimama ukumbi mzima wakati Profesa akiingia ukumbini akiwa katika sura yake halisi bila kujificha uso. Walikuwa wanapiga makofi ya pongezi kwa kishindo kuonyesha kufurahishwa na ujio wake mkutanoni. Wengi wao macho yaliwatumbuka kumshangaa Profesa Asante-Rabbi ikiwa ni mara yao ya kwanza kwao sura yake kudhihiri mbele yao. Walikuwa wanamsikia tu simulizi zake za kustaajabisha ila leo wamefanikiwa kumuona mubashara.
Mipango mbalimbali ya namna pesa zitakavyowafikia huko Mikoani za kuhonga wapiga kura kwa ajili ya kukichagua chama cha 'National Movement Party' (NMP) ikaanza kupangwa. Malengo yao yalikuwa ni kupata kura milioni 8 tu za kununua huku wakijumlisha na wale wafuasi kindakindaki walikuwa na uhakika wa kupata kura milioni 10. Kura ambazo zingewatosha kuingia Ikulu na kuunda serikali.
Ajenda yao ya mwisho ikaanza kumjadili Kachero Manu, huku ikiamrishwa asogezwe mbele ya meza kuu. Kachero Yasmine alitoa amri mmoja wa askari wake wa kike ndio akae jirani na Kachero Manu ili awe chambo cha kupokonywa silaha kirahisi na Kachero Manu ili wakilianzisha wote waanzishe vagi kwa pamoja wakiwa na silaha.
Profesa sasa ukawa uwanja wake wa kujimwayamwaya kwa kujifunga kibwebwe uwanjani dhidi ya adui yake Kachero Manu. "Nitakuchinja mbele ya umati huu wa watu iwe fundisho kwa wasaliti wengine" alizungumza Profesa huku akiwa anafoka kwa hasira.
"Umenidanganya kuwa umetumwa na kijana wangu Man-Temba kumbe wewe ndio umempoteza, na kijana wangu Nathanieli pia mmemuua. Umekaa nyumbani kwangu nimekupa mbinu zote za medani za udukuzi kumbe unanidhihaki ukinifanya zuzu tu eeh...sasa nitakuonyesha kilichomtoa kanga manyoya..!". Akaanza kumkaribia Kachero Manu huku ameshachomoa bisu kubwa lenye makali toka kiunoni amekaa nyuma ya shingo la Kachero Manu.
Kachero Manu hakusubiri kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara, fujaa bila kutarajiwa, alijirusha hewani toka kitini na kufanikiwa kumpokonya silaha yule mlinzi mwanamke kisha akiwa bado hewani akafanikiwa kumbana Profesa roba ya miguu kwenye shingo. Wote kwa pamoja wakaanguka chini kwa kishindo cha tii!.
Kachero Yasmine nae hakulaza damu akaanza kuchakaza meza kuu kwa risasi akianzia na Chew Master. Kishindo kikubwa cha mlango kuvunjwa na bomu kikasikia huku wakiingia makomandoo 5 wa jeshi la wananchi, JWTZ. Walipata wito wa Kachero Yasmine waje kuongeza nguvu wakawasili kwa kutumia nyambizi.
Ndio hao makomandoo alimtuma yule mtumishi wa usafi ahakikishe anawaelekeza mkutano ulipo kwa haraka. Makomandoo wengine walipigiwa simu na Yasmine wakati anatoka chooni wakawa wameshaizunguka nyumba ya Flora Tarimo. Papatu papatu ya mapigano ilirindima vilivyo. Washirika zaidi ya 20 walishapoteza maisha, huku wengine wote wakijisalimisha na kutiwa mbaroni.
Profesa Asante Rabbi na Chew Master walikuwa wapo hoi kwa mkong'oto kabambe wa paka mwizi walioupokea siku hiyo. Walinzi wa kike karibia wote walikuwa wameuliwa. Tayari zilishaitishwa boti za kutosha za kuwapakiza washirika wote wa NES tayari kwa ajili ya kuwafikisha katika vituo mbalimbali vya polisi.
Kachero Manu na Kachero Yasmine wakakumbatiana kwa furaha, wakipongezana. "Ahsante Yasmine, kazi imekwisha!" alisema Kachero Manu. "Bosi bado kazi mbichi, pesa bado hatujazikomboa na marehemu Dr.Pius Chilembwa bado hatujamtia mbaroni. Anatakiwa akafufuliwe alipojizika aje kusimama mbele ya vyombo vya dola kujibu mashitaka yake" Kachero Yasmine alimgutusha Bosi wake wajibu wake uliobakia. Wakati makomandoo wale wakiwaswaga washirika wale kuwaingiza kwenye boti, Kachero Manu na Kachero Yasmine walitoweka kimaajabu Hotelini pale bila kujulikana wanapoelekea.

MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog