Search This Blog

Thursday, 23 March 2023

MTOTO WA KIGOGO - 5

   

Simulizi : Mtoto Wa Kigogo

Sehemu Ya : Tano (5)



Majira ya saa kumi na moja asubuhi kutoka Uganda kuja Tanzania ni mwendo wa masaa ishirini na manne, walijiandaa kwa safari toka asubuhi mpaka jioni ikawa usiku na ilipotimu saa sita basi walikuwa katikati ya ziwa vikitoria hakuna aliyekuwa na hofu maana kila mmoja alikuwa kazoea safari hizi. Lakini katika hali ya sintofahamu kuna boti ilikuja na kuwazingira walikuwa ni majambazi basi. Walikuwa na siraha nzito katikati ya maji waliagiza hiyo boati ibaki bila mtu maana walikuwa wakiihitaji hiyo boati na mali zake zote. Mwanzo ulikuwa kama mzaha na vichekesho, mmoja wa vijana waliokuwemo kwenye ile boati alihoji “jamani humu tuko majini tupishe twende wapi” baada ya swali lile walimhoji … “hujui pakwenda?” walimhoji na kasha kumwamuru asimame risasi ya kifua ilifuata akatumbukia majini kasha jamabazi mmoja akajibu “hujo ndiko mnakotakiwa kwenda na wenginme mnaweza kufuata” ilikuwa ni hali ya sintofahamu ndani ya boti ile inatanda hofu mioyoni mwao nahuu ukawa ni mtihani mwingine kwa Tom. Kelele zilizokuwa zikipigwa na watu wale zilizidi kuwapa hofu wafanya kazi wa boati ile waliokuwa wamebaki watatu bada ya mmoja kuuliwa na kutoswa majini. Kijana mwingine anasalimu amri na kujitumbukiza mwenyewe majini wanabaki watatu. Msimao wa majambazi ulikuwa palepale walizidi kutoa amri kuwa boti waliyokuwa nayo akina Tom wanaihitaji hivyo wapishe, yalikuwa ni majibizano ya kuwataka radhi wasifanye hivyo majambazi yaliyosababisha mmoja ya vijana waliokuwa wamesalia kukatwa mkono kwa panga. Ilisikitisha ila kiuhalisia inauma sana tu. Kijana alikuwa akiutizama mkono wake ukiwa kwenye boti ukivuja damu.


Muda wote tom alikuwa kimya hakujibu wala kutekeleza agizo la aina yoyote tom na nahodha wa boti ile ndo walibaki wakiwa salama, kitendo cha kinyama kilicho fuata ni kuukata mkono wa pili wa Yule kijana waliemkata mkono wakwanza. Mazungumzo hofu inazidi kutawala ilikuwa ni zamu ya Tom jambazi anaiinua shingo yake kwa upanga kasha anamwambia nakupa adhabu mbili uchague moja, yakwanza ni kukanyaga lami na yapili ni kukatwa mikono yote miwili. Wakati akiongea hayo tom hakuwa anamjali maana hiyo ni kazi yake. Sijui nini kilitokea ila ukweli ni kwamba panga alilokuwa nalo Yule jamaa lilikuwa limeesha tua kwenye kifua cha jambazi aliyekuwa na bunduki huku aliyekuwa na panga alikuwa ndani ya maji tayari sijui alifikaje ila anajaribu kupiga mbizi ili ajiokoe. Ambapo hata hizo juhudi hazikufanikiwa baada ya bastora ya Tom kukohoa alibaki akielea. Baada ya kuona hivyo wanageuza boti waliosalia huku wakilaumiana wanatokomea kusikojulikana.


Safari inaendelea ingawa Yule kijana aliyekatwa mikono hakuweza kudumu hata kwa saa moja anakata roho wanamfunika na safari inaendelea. Bada ya mwendo wa masaa kadhaa hali ya hewa inabadilika na walikuwa wamekaribia kufika upepo haujulikani ulikotoka, unazalisha wimbi kali boti inashindwa kuhimili na mwisho inapasuka na kuingiza maji wanajaribu kuziba kwa nguo lakini kasi inakuwa kubwa wanazidiwa na boti inazama, kila mtu na harakati zake za kujiokoa, wakiwa wamening’inia kwenye mbao za boti zilizokuwa zikielea mpaka kunakucha wimbi ni kali mno manaendela kujikaza, huku miili imekufa ganzi walijikaza kwa masaa kadhaa lakini baada ya masaa manne kupita Yule mmoja anakata tama na kujiachia anapoteza maisha Tom mwanaume wa shoka anaendelea kujikaza kiume. Baadae upepo unapungua na kuisha kabisa na ziwa linakuwa shari anajikaza na kufanikiwa kupanda juu ya kipande cha mbao zilizobomoka toka kwenye boti, anaanza kuelea kwa kupigwa na wimbi, majini inamchukua siku mbili bila chakula na bila msaada wa aina yoyote. Majira ya saa nne asubuhi anaokotwa na wavuvi akiwa hajitambui juu ya kiubao hicho akiwa kapoteza fahamu kwa jua kali njaa na mateso aliyoyapata.


Amepewa huduma ya kwanza baadae chakula, hakueleza ukweli ilibidi adanganye kuwa yeye ni mvuvu alikuwa na enzake wamezama hivyo hakukuwa na swali zaidi walimsaidia fedha kidogo zilizompeleka mpaka mjini anafanikiwa kuipata benki ya exim ndiyo waliyoitumia kuhifadhi fedha anaingia mpaka ndani na sasa anafanikiwa kupata kiasi cha fedha kidogo anakata tiketi ya ndege na kurejea Dar es Salaam.

Tom ndani ya dar amefanikiwa kurudi akiwa salama, je atarudi kwa Love au anarudi kwa Irene (Zabi)? Ngoja tuone itakavyokuwa. 



Uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere, Tom akiwa hana begi wala mfuko ni yeye kama yeye, akiwa katinga jinsi yake nyeusi na shati nyeupe ya mikono mifupi chini ni laba nyeupe ya air Nike, alikuwa kwenye mlango wa kutokea anatoka mpaka nje ya uwanya huo. Baada ya kufika nje zinapopaki gari anaangaza huku na kule ili apate Taksi yakumpeleka alikokuwa akifikili kwenda. Basi akapiga hatua kadhaa mbele anasimama kidogo lakini alipogeuza jicho upande wa kushoto anakutanisha macho na msichana mmoja mrembo alikuwa kavaa miwani mieusi mrefu lakini ni kama anamfahamu hivi, alipomwangalia vizuri alikuwa ni Love, lakini wakati huo Love alikuwa hajamuona Tom. Basi Tom anamwangalia kwa hasra kisha anaondoka zake, anapiga hatua kadhaa mbele inaonesha hajaridhika anaamua kurudi huku akiwa na hasra zake zimemjaa anatamani kupasuka, ni dhahili kuwa Tom alimchukia sana Love.


Basi anafika alipokuwa Love akiwa kavimbiana kwa hasra Love anakutanisha macho na Tom akiwa mbele yake, kwa hasra Tom anamsogelea huku akionekana kupandwa na hasra zaidi. Basi Lovenss anashusha miwani yake taratibu na kuishika kwa mkono wa kushoto. Anamwangalia Tom kwa tabasamu kisha anambusu shavuni na kumchombeza “Wow! Umerudi”. Tom hasra zinamjaa maradufu mithili ya paka aliyevutwa mkia basi wanatizamana kwa sekunde kadhaa bila kusemeshana. Tom alianza kufoka kwa sauti ya chini, alimlaumu sana Love kuwa yeye ndiye chanzo cha Tom kupata mateso na matatizo yote aliyokutana nayo huko alikompeleka. ‘kwa lugha nzuri nikuite shetani maana hufai hata kidogo, ulinidanganya unanipenda ili uje unitumie kama chambo katika kukamilisha mipango yako ya kishetwani, umenifanya leo naishi kwa mashaka, umenifanya leo mimi ni muuaji mtu mwenye roho ya ajabu ambaye sizani hata kama dhambi zangu zaweza sameheka” wakati Tom akibwata Love alikuwa kimya akimwangalia bila kujibu chochote, basi Tom alifoka kila aina ya tusi lakini hakufanikiwa kupata jibu hata moja. Baada ya kumuona sasa kazidi alichokifanya Love ni kuruka na kukanyaga juu ya gari ajipindua kwa sarakasi na kurusha teke la nyuma ambalo pamoja na kulipiga kwa usitadi linapanguliwa na Tom lakini pamoja na kulipangua anapoteza ustahimilifu anakwenda mpaka chini. Na tayari Love alitua kwenye kichwa cha Tom na kumkanyaga kwa kiatu chake mchongoko kilicho pasua sehemu ya kichwa upande wa kushoto karibu nasikio na kuanza kuvuja damu. Tom hakukubali anajitutumua kutoka chini anakutana na teke la kifua anarudi chini na wakati huo love alikuwa kamkalia kifuani na kumshushia ngumi moja iliyotua vyema kwenye pua na damu zinaongezeka na kulichafua shati ala Tom. Watu wanaanza kusogea eneo lile kuona kinachoendelea. Tom akiwa kajiinamia basi Love anamshika bega na kumfutafuta Tom ili kuwafumba macho watu waliokuwa eneo lile anamsaidia kunyanyuka Tom na kumuingiza kwenye gari nayeye akazunguka mlango wa dreva akawasha gari wakatoweka haraka kabla polisi hawajafika ambao nao walikuwa wakija kwa haraka baada ya kulisika tukio lile la ugomvi, lakini polisi waliambulia patupu baada ya kufika na kuambiwa zilikuwa ni vurugu za wapenzi wameesha elewana na wameondoka.


Ndani ya gari hakukuwa na mazungumzo bali ni kila mtu alikuwa kimya, Love anachukua simu yake huku akiendesha anampigia mtu mmoja na kumpa maelekezo ya kwenda kumpokea Jimmy air port kwani yeye kapatwa na dharura hatoweza kwenda. Tom anapata picha kamili kuwa kumbe Love alimfuata Jimmy airport, mbali na swali hilo bado alikuwa akigugumia maumivu makali aliyoyapata kutokana na kipigo alicho kipata huku akivua shti lake ambalo lilikuwa halitamaniki huku akijisemea kimoyomoyo “du huyu mwanamke ni kiboko nimepiga polisi nimeua majabanzi ya kila aina bila kujeruhiwa lakini leo napigwa na baby duh! Kweli polisi wa nyumbani hana mikwara”. Gari linafunga breki nyumbani kwa Love, anatoka na kumfungulia mlango Tom kisha anamshika bega mpaka ndani anamkaribisha na kumchemshia maji ya chumvi yalisaidia kupunguza maumivu, kuzuia damu na kuondoa uvimbe, sambamba na dawa za kupunguza maumivu aina ya Action zinamrudisha tom kwenye hali yake. Chakula kilikuwa tayari basi wakala pamoja na sasa walionekana kuelewana kana kwamba hawakugombana. Wakati wakipata chakula kulikuwa na mazungumzo ya hapa na pale Love anamuuliza Tom imekuwaje amefanikiwa kutoroka huku wenzake wote wakiuwawa. Basi Tom anahadithia kisa chote kilicho mtokea huko Sudani ya kusini, Uganda na mwanza na hatimaye leo yuko hapa, hadithi ilimuumiza sana Love lakini pamoja na kuumia bado alimsifu sana Tom kwakuwa jasiri asiyekubali kushindwa. Alimsifu kwa kujitolea na kuwa mvumilivu Love alimpongeza na kumwambia “kwa sasa wewe ni mwanamme wa kweli usiyeteteleka na usiyekubali kushindwa. Siyo Tom wa kipindi kile wakulelewa na wanawake tu, basi najua umeona pesa inavyotafutwa na wanaume wenziyo harafu wanawapa wanawake na wanawake wanakuletea wewe hizo ndizo shida walizokuwa wakipata wenziyo wananiletea pesa napendeza na wewe ukavutiwa na mimi kutokana na kazi hizo hizo na ungelemaa ungekufa kama hao wenziyo waliokufa toka mkiwa kambini ” ilikuwa ni kauli mbaya ila ilikuwa na maana kubwa sana kwa Tom. Love anaendele ‘ulikuwa kula kulala najua sasa hutachezea pesa tena maana unajua zinakotoka, na pia inabidi unishukru kwani sasa angalau hata ukitembea unajiona mwanaume, hapo mwanzo nilkuwa najiuliza hivi kibaka akininyanga’anya simu kweli ungepambana hata ikarudi? au angekufanya anavyotaka maana ulivyokuwa boya hadi aibu, kwa sasa unaonekana kweli kijana shupavu’. Wanaangaliana na kucheka baada ya maeneo ya Love kumchoma na kumwingia Tom.


Usiku ule ulikuwa mzuri sana kwani walikutana vijana hawa wawili wapendanao , juu ya kitanda kimoja ilikuwa ni burudani mtindo mmoja. Hata kulipokucha waliendela kula raha maana sasa Tom hakuwa na chakuuliza nyumbani kwa Love kila alichokitaka alikipata, asubuhi, mchana, jioni na hata usiku, pesa ilikuwa nyingi waliitumia watakavyo, waswahili husema niyakuchota kwa koleo. Baada ya siku hiyo basi wakawa wanabadilisha viwanja vya starehetu na ni mwendo wa kutumia pesa. Hakuna aliyelia njaa maana walijitoshereza kwa kila kitu ni magari ya kifahari ndiyo yaliyozidi kumponza Tom na kuisahau kabisa familia yake ambayo hajaonana nayo takribani miaka mitatu sasa. Hakumbuki na hajali kuwa alimuacha mkewe akiwa mjamzito hajui kama mkewe alijifungua salama au laa, hajui kama ana motto na wala haoneshi hali ya kuumia juu ya hilo kweli ukuta wa mabua hata upake rangi nzuri kiasi gani mwisho wake ni mchwa. Ni yeye na Love mguu na njia asubuhi mpaka jioni, ni kufanya matanuzi, fujo ya pesa na vurugu kila kukicha. Taarifa huwa ni rafiki mmoja mnafiki kwani hanaga siri huzagaa bila aibu na hiyo ndiyo sifa yake, basi tarifa zikawa zimezagaa mtaani na kumfikia mama wawili au Irene juu ya tabia za mme wake na jinsi watu wavyokutana naye kwenye sehemu za starehe akifanya matanuzi na kufanya mambo ya aibu kama vile matusi akiwa na mwanamke ambaye humuonesha mahaba waziwazi. Ilikuwa ni aibu alipoiwaza harusi yake na Tom mbele ya watu waliomheshimu na leo watu hao hao wanamletea habari za Tom aliyeshindikana, Tom asiyeshikika ilimuuma sana lakini alijikaza na kujifanya hajasikia. Taarifa alivyo mnafiki hakuishia hapo alitembea na kuufikisha ujumbe kwa Jimmy kuwa Tom yupo nchini na kwa bahati mbaya zaidi anaishi na Love. Hali iliyomkasirisha sana Jimmy Radi. Kwa uelewa wake alijua wazi kuwa kambi yake ya sudani iliteketea kabisa hakubaki na mtu hata mmoja wote waliuwawa na msako mzito uliofanywa na serikali, sasa chakushangaza anasikia Tom yupo Dar na chakusikitisha zaidi hajamtarifu wala kumpa ujumbe wowote juu ya ujio wake kama hiyo haitoshi anaishi na Love ambaye Tom alikuwa akijua Toka awali kuwa ni mpenzi wa Jimmy. Swali lililompa shida Jimmy ni kwanini hata Love kaficha juu ya ujio wa Tom? Swali linamtesa na asipate jibu. Mtu mzima hujiongeza si kila kitu uambiwe. Jimmy Radi tajiri mwenye jeuri ya pesa, aliye na uwezo wa kufanya lolote na likafanikiwa katika ulimwengu huu anakuna kidevu chake kilichokuwa kama kichaka kutokana na ndevu zake zilizokaa shagarabagara kama mchicha uliokosa matunzo nanatikisa kichwa ishara ya kukubali sikujua alichokiwaza kwa wakati huo.

****************************************************


Love anaegesha gari karibu na duka la Irene anashuka na kumkuta Irene akijaribu kuweka vizui hesabu zake pale dukani anasimama na kumwangalia kisha kwa dharau akahoji. “vipi mke mwenza?” lilikuwa ni swali la kichokozi Irene hakuhangaika nalo akakaa zake kimya. Love akacheka kwa dharau “hahaaaa! Eeh1 Jamani nakusalimia au ndo mwenzangu umekuwa bubu siku hizi?” kejeri zile zilihitaji moyo mpana na uvumilivu wa hali ya juu usioteteleka kuyavumilia. Love hakuishia hapo anaendelea “Okey .. naona mwenzangu ni bubu acha nitumie ishara pengine tutaelewana, anaanza kuchezesha mikono kama anawasiliana na mtu asiye na uwezo wa kusikia (kiziwi).. yaani namaanisha Tom… mmme wetu…. Niangalie basi jamani eeeh! Mnh! …. Aah!… amerudi … ndiyo karudi … anawiki sasa yuko kwangu na kanambia haji kwako ….. sawa mke wa zamani …. Kijana kapata kipya” Love alikuwa akiongea kwa vituo huku akitumia vitendo kana kwamba anaongea na mtu asiyesikia. Ni dharau iliyojidhihilisha usoni kwa Irene hakupenda makuu alijikaza ingawa moyoni ilimuuma lakini aliona kimya ni jibu sahihi kwa mpumbavu, kimya ni jibu lisilotafasrika kiurahisi, kimya huepusha shari, kimya huharibu chanzo cha matokeo tarajiwa na daima kimya huleta mshindo. Ilihitaji moyo sana kuendelea kuwa kimya lakini mungu naamini alisimama kwa upande wa Irene maana sasa kejeli za love zilivuka mipaka kwani alikuwa akimchokonoa kwa juhudi zote sijui alichokitaka lakini inaonesha kuna kitu alidhamilia. Ukimya mara nyingi ni mshindo hatimaye love anaondoka kwa kujiona kashinda na kumuacha Irene machozi yakimtoka kwa hasra na aibu alikuwa kayazuia kwa muda sasa, Toka Love alipokuwa akiropoka maneno yaliyo wafikia majilani ambao nao waliguswa tofauti wengine waliumia na wengine kufurahishwa na kitendo hicho.


hAkiwa katika majonzi makubwa Irene anaamua kufunga duka na kurudi nyumbani, alikuwa na wakati mgumu sana hata wakati akiendesha barabarani, anajikaza na hatimaye anafika nyumabani kwake, anakutana na watoto wake wenye umri wa miaka miwili na miezi kadhaa sasa ndiyo walikuwa faraja yeke pekee kelele za mama … mamaa zinampa faraja zaidi. Wanampokea kwa furaha anajitahidi pia kuilazimisha furaha lakini moyoni alikuwa na majonzi mazito. Anakwenda mpaka chumbani kwa mama mkwe wake alipofika uvumilivu unamshinda na kuangua kwikwi za kilio. Haikuwa hali ya kawaida mama Tom anajitahidi sana kumbembeleza, japo anatumia muda mwingi na hatimaye anafanikiwa anamweleza kila kitu bila kuficha. Chanzo ni Tom …. Mama anafikili kwa haraka anaamua kutumia utu uzima wake anamketisha chini Irene anazungumza naye na kujaribu kumshawishi ili aachane na hao watu. Irene anamweleza kuwa amejitahidi sana kuwaacha lakini ndo hivyo kila kukicha wanakuja na jipya, ni miaka mitatu sasa sina mpangonao wala kuonana na Tom, najua nampenda lakini niliamua kuwaacha maana walipendana zaidi sasa yanini kunifuata fuata?. Ilitia huzuni lakini ni wazi na kweli kwamba Irene alikuwa bado anampenda Tom sana tenasana na moyo wake uliuma zaidi kila alipokumbushwa swala lolote linalihusiana na Tom.walimtonesha kidonda kwani alikumbukoa alikomtoa na leo Tom kageuka kuwa msaliti.

*******************************************************

Nimwendo wa kuponda raha kila siku, kila kukicha na mpaka kunakuchwa ni ratiba za starehe, hawana mtoto, hawana ndugu wala familia nyumbani wanapoishi Tom na Love sasa penzi liliwakolea zaidi kwani walifanya kile walichoona kinawafurahisha. Na kuwafanya wao wawe na furaha, ungewakuta walivyoketi nje ya nyumba yao hakukuwa na swali juu ya uhusiano wao ungejua wazi kuwa hawa ni wapenzi wapendanao na huo ndiyo ulikuwa ukweli. Walikuwa wakila na kunywa vinywaji vya bei ghali wanacheza na kukimbizana, wakiwa kando ya bwawa la kuogelea huku wakichezea maji kama vyura wa mtoni. Wakiwa wameketi na kukumbatiana kwenye kiti kimoja cha kupumzikia kando ya bwawa la kuogelea huku mihuu yako ikichezea maji kwenye bwawa hilo. Basi kengele ya geti inagonga bila shaka kulikuwa na mgeni Love ndo alikuwa mwenyeji anakwenda kuangalia ni nani alikuwa nagonga na alifata nini, lakini katika hali ya kustajabisha anakutana na Jimmy Radi mlangoni anabaki ameduwaa Jimmy anapita na kuingia mpaka ndani huku akimuacha Love mlangoni, uso kwa uso na Tom, bila kumsemesha chochote anapita mpaka kwenye mlango wa kuingia ndani ya nyumba, wanabaki wameduwaa hakuna aliyetarajia maana Toka Love apewe hiyo nyumba na Jimmy hakuwahi kuja tena mpaka leo ndo anaonekana hiyo ilikuwa ni siri ya Love ambayo tom hakuijua kuwa alikuwa akiishi kwenye nyumba aliyopewa na Jimmy. Alichokifanya Jimmy kiliwashitua zaidi kwani alitoka na funguo za gari zake zote nne na akafunga mlango wa nyumba baada ya kutoa mabegi ya nguo za Love na Tom kisha akawapa saa moja wawe wameondoka, atakapaporudi asikute mtu kwani anakuja kufunga na geti, baada ya kusema hivyo anawaita vijana wane aliokuja nao walikuwa nje anawapa funguo na kutoa maagizo hizi gari hakikisheni mnazipeleka nyumbani kwangu mbezi kisha aliondoka na kuwaacha vijana wakihangaika na kutoa gari moja baada ya nyingine. Hakukuwa na maelezo ya awali wala maelezo ya baada ya, Love na Tom baada ya kumsindikiza kwa macho Jimmy wanayarejesha macho yao kwenye magari yaliyokuwa yakitoka moja baada ya jingine na hatimaye yakaisha yote mure ndani. Mwisho wanageukiana na kuangaliana, hakuna aliyeanza kumsemesha mwenzake na hali ikawa tete zaidi kwani love anaonekana kuchanganyikiwa zaidi.


Natamani sana kujua kitakachoendelea baada ya tukio hili hivyo ungana na mimi hapo kesho kujua nini kitafuata.



Tom hakuwa na wasiwasi maana anajua mpenzi wake ni Mtoto wa Kigogo, hivyo alitegeme maamzi ya mwisho kutoka kwa Love wanafanya nini kwa wakati huo. Love alikuwa yuko kimya na sasa anaonekana hayuko sawa maana hata baada ya Tom kumsemesha mara kadhaa alikuwa hajibu. Basi Tom aliiona hali ile ni hali ya kawaida pengine alikuwa kachanganyikiwa tu na baadae mambo yatakuwa sawa. Tom anajitahidi kumtuliza mpenzi wake ili asiwe kwenye hali ile ya wasiwasi maana hata yeye sasa alikuwa anajisikia vibaya sana love hakuwa kwenye wakati mzuri anaonekana hayuko sawa. “Love hebu achana na hayo bwana naomba tuendelee na mambo mengine hiki kimetokea inabidi tukubali kuwa kimetokea, hivyo nakuomba jikaze tuondoke hapa sawa mama maana asije akarudi tena na hasra zake?” Tom alimaliza kumsihi. “Tom hujui baba ni kiasi gani umeniweka kwenye matatizo, Jimmy ndo mtu aliyekuwa akinisaidia kila kitu hapa mjini sasa hela zote tumetumia na leo nilitegemea kumuomba pesa lakini kabla sijafanya hivyo yametokea haya, unadhani ninafanyaje?” Love alianza kuzishusha lawama kwa Tom. Lakini Tom nae hakukubali aliamua kumjibu kwa hasra “sasa Love nilipaswa nikulaumu wewe kwa kila kitu, kumbuka ulikuwa kwenye mahusiano na Jimmy lakini hukuniambie, haya hukuwahi kuniambia kuwa hii nyumba niya nani, hukuwahi kusema kuwa umepanga wala kuniambia unaishi hapo kwa mgongo wa Jimmy, hilo tisa kumi magari ulikuwa ukiayabadilisha tu hukuwahi hata siku moja kunieleza kuwa huna gari hata la wizi… unanilaumu unalaumu nini?, lakini mama kumbuka umeniingiza kwenye biashara fake kibao bila huruma hukuyajari maisha yangu nimenusurika kufa mara ngapi?, Unajua wewe?, kuna wakati nakunyamazia unaniona kana kwamba sina akili eeh?, kumbuka umeniuza kama mbuzi wa kafala sijawahi hata kuhoji maana nakupenda bad oleo unilaumu tena mimi aaaha sasa hapo mama kutakuwa na sababu zingine siyo Lawama tu” Tom alimaliza kumtolea uvivu Love na wote wakakaa kimya kwa muda huku nyuso zao zimejikunja kama wagonjwa wa meno waliokofoleni wakimsubili dakitari siku ya tatu mfululizo bila mafanikio ya kumuona dakitari.


Tom baada ya kuona sasa hakuna maelewano kati yao ananyanyuka na kuvaa nguo zake kisha alienda kuchukua bagi lake na kuanza safari hali iliyo mshitua Love harakaharaka akajiinua na kumuomba Tom amsubili, Tom anafanya hivyo bila kupoteza muda waliondoka huku wasijue wanaelekea wapi, baada ya mwendo mfupi kwa miguu Tom anaita taksi anaingia na Love anaingiza mizigo yake wanakaa. Dreva anauliza tunaelekea wapi hakuna aliyejibu kwa muda baadae Tom anajibu “Manzese Tiptop”. Love lile jibu linamshitua anashituka, Nooo no hapana! Dreva twende ubungo tafadhali basi kukawa na mkanganyiko dreva anakanyaga mafuta mpaka ubungo, walipofika akauliza tena wapi? Wanategeana tena kujibu baadae love anajibu hoteli yoyote nzuri. Basi bila kuchelewa dreva aliiegesha gari yake kwenye kihoteli cha kiana kilichosomeka kwa jina kubwa Mic Hotel walishusha mabegi yao wakaingia ndani wanalipia chumba kwa siku moja na kujifungia.


Huko ndani hapakuwa shwari hata kidogo ni vilio, lawama love alijuta sana kwanini yametokea haya? “Tom ulipanga kuniharibia maisha yangu maana wewe una mke tayari sasa mimi naenda wapi jamani?” Love anazidi kushusha lawama. Tom kunawakati anashindwa kuzitafsiri kauli za Love kabisa maana zilikuwa zikikinzana. Basi kama mwanaume alibaki kuwa mbembelezaji tu mpaka kunakucha hali ilikuwa mbaya maana aliyoyasikia ni makubwa kuliko tatzizo basi alivumilia hakukuwa na jinsi. Asubuhi ile hakukuwa n apes hata ya kifungua kinywa kidume akajitutumua kulikuwa na fedha kidogo kama laki tatu kwenye simu akaichomoa basi wakalipia chumba kwa siku mbili zaidi na iliyobaki iliwafaa kwa chakula. Lakini kumbuka fedha ni maua siku mbili hazikuwa nyingi zilikatika na walipoliangalia salio lilikuwa limelegea Tom anashauri ni bola watoke hotelini wakakae guest basi wanaikimbia ile hoteli amabayo mbali na chakula walikuwa wakilipia takribani elfu hamsini kwa siku na sasa wanachukua chumba kwenye guest house moja ambayo hata jina lilikuwa ni gumu kulitamka na ilikuwa maarufu kwa jina la guest bubu. Hapo walilipia elfu 15 kila siku na chakula walikuwa wakichukuwa magengeni. Lakini haikuwa suruhi ya kutatua tatizo kwani siku tatu baadae mifuko ya Tom sasa ikawa mikavu.


Ukaanza utaratibu wa kuweka dhamana simu ilianza simu ya Tom ikatumika mpaka na mwisho fedha zikaisha ikafuata simu ya love vilevile ilitumika kwa mtindo uleule na fedha ikaisha. Tom anashituka mpa taabu kulishugulikia swala hili. Tom anajaribu kuiingiza hiyo mada kwa Love lakini ilipanguliwa kwa hoja za msingi amabazo hata tom zilimwingia na kuamua kuachana nayo. Love alimwambia yeye na familia yake huwa hawana mahusiano mazuri kwani baba yake alimpeleka Love nje ya nchi kusoma Love akaharibu kwa kuendekeza starehe hivyo huwa hawana mahusiano mazuri na baba yake kwani baba yake Love alishaapa akimuona love atamuuwa.


Tom alishusha pumzi kwa nguvu hakujua chakufanya, wanaendelea kukaa kwa kuganga njaa, kila kukicha hali ya Love inazidi kuwa mbaya kwani hana furaha kabisa, hali iliyozidi kuibua maswali mengi kwa Tom, Tom alikuwa akijiuliza namna ya kumsaidia mpenzi wake lakini anashindwa kutokana na juhudi zake nyingi kugonga mwamba, sababu ni Love mwenyewe kutokuishiwa na mawazo kutokukubaliana na hali iliyotokea. Pengine ilimuumiza kuliko tulivyotarajia maana sasa anaelekea kupoteza uelekeo kabisa wa maisha yake. Ni mtu wa kuwaza na kulia tu kila kukicha, love hakuwa Love Yule mwenye jeuri ya pesa, siyo Love tuliyemjua na kiburi chake cha cha maisha na dharau kwa kila mtu leo anaonekana Love mpore, mwenye sura inayotia huruma, Love mwenye majonzi masaa yote hakika. Hakuna moyo mgumu usiobondeka na kila binadamu lazima ayepitie magumu . Tom alikuwa kaketi pembeni akiuangalia mwili mwembamba uliokuwa umejilaza kitandani, ni mwili wa Love uliokuwa ukipungua kila kukicha kutokana na mawazo. Tom alikuwa akiumizwa sana na hali ya kumuona mpenziwe akiteseka kwa mawazo.


Baada ya kuwaza sana Tom anakuja na wazo jipya, anamwambia Love arudi kwa Jimmy akamuombe msamaha pengine angemuelewa, Love hakuliafiki swala hilo kwani alimjua vizuri Jimmy. Love alimwambia Tom tafadhali kama umechoka kuniona naishi nibora uniambie maana kwenda kwa Jimmy nisawa na kunichimbia kaburi na kunizika mzima. Jimmy si mtu wa kawaida, usimuone kutuacha sikuile ukadhani hakuwa na uwezo wa kufanya lolote. Nibora nife kwa mawazo kuliko kwenda kujisalimisha kwa huyo mtu. Wanajaribu kuzungumza mawili matatu lakini hakuna mafanikio maana Love hakuwa katika hali nzuri. Love alikuwa akiandamwa na mawazo si kwasababu kanyang’anywa nyumba tu, bali alikuwa na aibu pia, unazani angewaeleza nini watu aliowabeza na kuwadharau, hivi angefanya nini iwapo angekutana na watu aliowatukana na kuwadharau sababu ya umasiki wao? Hayo ni baadhi ya mambo yaliyoitesa akili yake masaa yute alikuwa kwenye dimbwi la mawazo mazito. Kiuhalisia alikuwa kaporomoka kithamani baada ya kufukuzwa kama mbwa kwani sasa aliwaza nisawa na mtu aliyeshuka kwenye ndege na kuingia kwenye bajaji, thamani yake ilikuwa imeshukuka kuliko kawaida.


Sasa Tom hali ya kumulea Love inaanza kumshinda kwani hakuna mabadiliko, na sasa anagundua ni kama alikuwa anaumwa, hakulifumbia macho swala hilo kesho yake aliamua kwenda nae hospitali baada ya kuwa amemalizia vijisenti vyake vilivyokuwa kwenye akaunti yake. Foleni ilikuwa kubwa pale mhimbili lakini tom anapambana mpaka nafanikiwa kupata faili anajaribu kutumia njia za panya na hatimaye anafanikiwa kumuona dakitari, yalikuwa majira ya saa nne na ilipotimu saa kumi jioni walikuwa wamekamilisha kila kitu na tarifa hazikuwa nzuri kwa upande wa love kwani aligundulika kuwa na kansa ya ini na ilikuwa katika hali mbaya zaidi na dakitali alimwambia hali hiyo imesababishwa na utumiaji wa pombe kali kupita kiasi, alikuwa kapewa dawa kadhaa za kumsaidia lakini kwa maelezo waliyoyapata kutoka kwa dakitari kila mmoja alikuwa kachoka na wamekata Tamaa. Tom anafika na kujirusha kwenye Sofa huku Love akiwa kajiinamia kitandani, hakukuwa na mazungumzo tena mle ndani kila mmoja aliwaza kile alichokijua yeye.


Tom alitafakali kwa muda na sasa anakuja na jibu aliloamini siyo sahihi, basi hakusema aliaga anatoka nje lakini huko alikwenda kukata tiketi mbili za kwenda Dodoma kesho yake asubuhi hapo stendi kuu ya mabasi ya Ubungo. Baada ya zoezi hilo Tom alimwambia Love kuwa hana suruhu zaidi ya hiyo, hivyo ni lazima amrudishe nyumbani kwao Dodoma. Pamoja na ubishi na vikwazo alivyo viweka Love havikutosha kuweka pingamizi kwa Tom na mwisho wa siku kesho yake saa kumi na mbili asubuhi walikuwa wakilisubiri basi la Kimbinyiko lililofanya safari zake kutoka Dar kwenda Dodoma . Waliketi pamoja kwenye siti mkabala kwenye basi hilo na safari ilianza bmajira ya saa moja na nusu. Njiani hakukuwa na mazungumzo kabisa kwani kila mmoja aliwaza alichokijua yeye, Tom alikuwa akimshukuru mungu kwa kumrudisha Love kwao maana alikuwa Kautua mzigo. Wakiwa safalini Tom alikuwa akijaribu kuijenga picha ya Nyumbani kwa wazi wa Love palivyo kiuhalisia hakupata picha maana hakua amewahi kuishi Dodoma. Walifika morogoro saa saba za mchana na badae safari ikaendelea na ilipotimu majira ya saa tisa na nusu walianza kuingia Dodoma mjini taratibu basi likajongea hadi kituo cha mabasi cha Dodoma. Wote walishuka baada ya kuwa wamefika salama Dodoma.


Swali la kwamba wanaelekea wapi halikuwa na majibu kwani Love alikuwa kimya Muda wote, basi Tom alichokifanya ni kufuata love anakoelekea. Mpaka kituo cha daladala cha Jamatini ambapo Love anagoma kuongozana na Tom kwani alimshukru na kumwambia “ahsante kwa msaada wako nitakwenda mwenyewe nyumbani” Tom hakulikubali hilo ulikuwa ni ubishi uliochukua karibu Robo saa na hatimaye Love alikubali kwa shingo upande walipanga gari zilizoelekea Ng’ong’ona, basi safari iliendelea huku barabara yao ikipitia katikati ya chuo kikuu cha Dodoma na kwenda kukamuilika kwenye kitivyo cha Elimu cha chuo hicho. Wote wanashuka Tom hakuwa anajua chochote kwani mwenyeji wake alimuamini sana. Basi safari ya kutembea kwa miguu ilichukua takribani dakika arobaini na Tano kukifikia kijiji cha Iyumbu, kijiji kilichochoka kwelikweli kilichopo ndani ya manispaa ya Dodoma. Mbali na kujiuliza maswali Tom alikuwa kachoka na alikuwa na hasra pia hakujua anapelekwa wapi maana aliona wanazidi kulikung’uta vumbi tena vumbi, jekundu lililowachafua kwelikweli na majira ya saa kumi na mbili na robo jua likielekea kutwaama wanafika kwenye mji mmoja ni familia ya hali ya chini kwelikweli, Tom anaangalia hadhi ya nyumba zile na kutikisa kichwa huku akijiuliza jamani hivi humu wanaweza kuishi watu? Zilikuwa ni nyumba fupi zilizotengenezwa kwa matembe toka juu mpaka chini. Nje kulijaa mbwaa kama sita amabao nao afya zao zilikuwa zimechoka kuliko maelezo, walidhoofu kutokana na umri wao kwenda, lishe mbovu na matunzo mabaya. Pembeni kulikuwa na mzee asiyejiweza alikuwa kaketi kwenye kigoda huku akinywani akiwa kaweka sigara yake ya tumbaku iliyozima na sizani hata kama anakumbuka mwisho iliwaka lini na pia ilivyokaa sizani kama alikumbuka kama ana sigara mdomoni.


Watoto wakiwa wamechafuka kwelikweli wanaonekana wakiwa na lishe duni, mbali na mama aliyekuwa jikoni, jiko ambali nalo lilijengwa kwa mfumo ule ule wa kukandikwa juu na matembe hali iliyosababisha hata moshi usipate sehemu ya kupita na hivyo kugandamana mulemule ndani. Mama Yule natoka na kuwasalimia wageni wake kwa lugha ya Kigogo, ambapo Love baada ya salamu anajitambulisha kwa Lugha ya kikwao ambayo hata Tom alibaki kuwa msikilizaji na asiambulie chochote kama mpemba anayesikiliza kichina. Baada ya mazungumzo ya muda mfupi nazani hakuna aliyekuwa namjua Love katika familia ile basi mama akashangilia na kupiga vigelegele. Huku akirukaruka Tom alikuwa kaachwa njiapanda kwani watu hawa walikuwa wakiongea Kigogo lakini yeye hakujua. Baasi baada ya mazungumzo ya muda hatimaye mama anakuja kumsalimia Tom kwa Kiswahili chake ambacho pia hakikunyooka. Hali ya pale nyumbani ilikuwa mbaya mbaya sana. Mazingira yalikuwa duni, machafu ambayo kiuhalisia hayakufaa kuishi binadamu lakini hakukuwa na jinsi. Mama naendelea kupiga kelele akisema kwa Kiswahili chake ambacho hakikunyooka “Jamaani mwanangu ….. Malenga…. Umerudi ni miaka mingi ………………… mungu ni mkubhwa” baba kusikia hivyo naye akanyanuka na kuja kumkumbatia Love sasa ikawa ni kilio pale nyumbani, badala ya furaha kikawa ni kilio baba, mama na hata Love mwenyewe.


Chakula cha usiku kiliandaliwa, alikuwa kaandaliwa kuku aliyepikiwa kwenye chungu, huku nyanya na mafuta vikiwa vimepishana, haikuwa kazi rahisi hata kuonja lakini hakukuwa na jinsi, chungu cha pili kulikuwa na ugali wa mtama mwekundu a.k.a ugali dume mgumu ambao kulimeza Tonge kwa watoto wa mjini ni lazima upate msaada wa mtu kukushika miguu ili usinyanyuke. Haikuwa kazi rahisi kuendelea mana wanajaribu wote wawili lakini hali ikawa Tofauti kwani wanashindwa kuendelea maana chakula kinawashinda wanakaa pembeni. Tom hakuambulichochote kwani mazungumzo yaliyokuwa yakizungumzwa yalikuwa kwa Lugha ya kigogo hivyo aliambulia patupu. Picha iliyokuwa akilini kwa Tom sasa ni kwamba Love labda kaamua kuja kwa bibi yake maana tayari Alisha mwambia wanaugomvi na baba yake. Swali lingine ni kwamba kwanini bibi yake awe katika hali hii wakati baba yake Love ni Kigogo serikalini ?. wanapewa chumba cha pamoja usiku chumba kilichokuwa na kitanda cha ngoye yani kamba, vumbi kila mahali, huko ndani kulining’inizwa mahindi juu ya kitanda yani ni shida basi Tom alifika na kuketi kitandani kisha akahoji. “Loveninakusaidia lakini husaidiki kumbuka unaumwa nimeamua nikulete kwa baba yako lakini umekataa kunipeleka kwenu unanileta wapi huku?” love alifoka maana aliiona kama anadharauliwa. “Tom ukweli ni kwamba hapa ndipo nyumbani kwetu, hao uliowaona hapo ndiyo wazazi wangu halisi baba na mama yangu kwetu ni Dodoma na ndiyo hapa Iyumbu………………” Tom alishitushwa na kauli ile akahoji “unamaanisha hapa ndokwenu ulipokuwa unaniambia kwetu Dodoma mimi Mtoto wa Kigogo?” Love alijibu bila hata kupepesa macho “ haswaa kwetu Dodoma na mimi ndiye Mtoto wa Kigogo kwasababu ni mgogo ni kama wewe ulivyo mtoto wa Kisukuma maana wazazi wako ni wasukuma.”. alimaliza kujibu



Tom sasa anaanza kupata picha anatikisa kichwa kumaanisha ameelewa “kumbe kigogo hiyo haikuwa na maana ya kiongozi mkubwa ila ni kabila la wagogo?” Tom alihoji kupata uhakika zaidi, “hujakosea Tom mimi sina baba wala ndugu kiongozi au kigogo kama unavyowaita wewe Kigogo hii niliyoitumia mimi nilimaanisha Kabila la kigogo” love alimjibu vizuri na majibu yalilizisha. Tom analazimika kucheka si kwa furaha ila aliupenda mchezo aliochezewa. Kutokana na maji kumfika shingoni sasaLove alikuwa mpole alijibu kila alichoulizwa kwa usahihi bila kupindisha hata neno moja. Usiku ule hakukua na usingizi ni baridi kali harufu ya uvundo mule ndani hapakuwa mazingira rafiki kwao hivyo usiku ulikatika wakiongea.


Katika maongezi waliyo yaongea ni pamoja na Love kuelezea jinsi alivyochukuliwa kwao na mama mmoja ambaye aliwapa wazazi wake fedha na kumchukua akamsaidie kazi za ndani kipindi hicho akiwa na umri wa miaka kumi tu Love akapelekwa jijini Dar es Salaam kwenda kufanya kazi za ndani,Jina lake halisi siyo Loveness bali jina alilopewa na wazazi wake ni “Malenga” likiwa na maana ya maji kwa Lugha ya Kigogo. Jina la Loveness nilipewa na yule mama aliyemchukua nyumbani lakini hili la Mtoto wa kigogo ailipewa na wateja waliokuwa wanakuja kumchukua na kumuulizia kila wakati kwani alikuwa kipenzi chao kulingana na huduma alizokuwa akiwapa, ailikuwa maarufu kwa jina hilo maana mwanzo hakuwa anajua Kiswahili na walipokuwa wanamuuliza kabila lake aliwajibu kwa kuwambia yeye ni Mgogo na hapo ndipo jina la Mtoto wa kigogo lilipovuma. Love anaelezea mateso aliyoyapata kipindi hicho kwa kufanyishwa biashara za ngono na wanaume waliomzidi umri kwani hakuwa anafaidika chochote kutoka kwenye hiyo kazi zaidi ya kupewa chakula na mavazi tu, mpaka anafikia umri wa miaka kumi na mitano alikuwa kahaba aliyeshindikana na hapo ndipo anakutana kwa mara ya kwanza na Jimmy Radi akiwa ni mmoja wa watu waliomhitaji kuwastarehesha. Mazoea yaliendelea na hatimaye Jimmy aliamua kumnunua Love kwa thamani ya Tsh. Elfu hamsini ni miaka ya tisini hivyo ilikuwa na thamani kidogo hivyo fedha.


Baada ya biashara hiyo haramu aliyoifanya huyu mama na Jimy sasa Love akawa mali halali ya Jimmy. Anaeleza Jimmy hakuwa tajiri kipindi hicho hapo ndipo alipoanza kumtumia Love kama mtego wa kuwateka watu na kuwaibia, Love kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 17 mpaka anafikisha umri wa miaka 20, walikuwa wamefanya matukio makubwa mengi tu ya mauaji, wizi, utapeli na hata unyang’anyi. Jimmy hapo ndipo alipoanza kukuwa kibiashara akisaidiana na Love. Baada ya muda aliamua kumpeleka Love kwenye mafunzo malumu ya kung-fu huko Beijing nchini uchina kwa mwaka mmoja aliporejea ndipo walipoanzisha kampeni ya kukamata vijana na kuwaweka huko Kibaha kwa mafunzo na baadae kuwatumia katika usambazaji wa dawa za kulevya wizi, unyang’anyi , biashara za siraha na utapeli. Uzuri wa Love ndiyo ulikuwa ukitumiwa kama chambo cha kuwanasa matajiri wakubwa waliwauwa na kuwaibia kisha kutoweka lakini uzuri huohuo ndiyo uliowadanganya vijana wengi na kujikuta wanatekwa na kutupwa kwenye jumba la mauti huko Kibaha. Wamefanya kazi hiyo ya wizi na utapeli katika mataifa mbali mbali kama vile Nigeria, Kenya, afrika ya Kusini na hata Mataifa ya Ulaya na Marekani.


Jimmy alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Love toka awali ingawa baadae Love alitokea kumpenda sana Tom kuliko Jimmy na hatimaye ndo imekuwa hivyo hawawezi kuishi tena pamoja. Ni hadithi iliyoumiza na kuudhi, ilisisimua na kukatisha Tamaa. Love alikuwa akionga kwa uchungu na kuna wakati alishindwa na kuangua kilio hali iliyomfanya hata Tom atokwe na machozi. Love nakili kuwa hakupakumbuka kwao kwani alilea na starehe na aliamini hayo ndiyo maisha yake atakayoishi mpaka anafukiwa chini. Alijisahau na kuanza kujikweza na kujiona yeye ni kiumbe tofauti katika huu ulimwengu. Hakuwahi kuwaza ni wapi ametoka kutokana na maisha ya ukatili aliyolelewa na hao walezi wake wawili ambao ni Mama Zubeda mama aliye mchukua kijijini na kumuuza na Jimmy Radi mtu aliyemfundisha roho ya kinyama yakutokushirikiana na watu kutokuwa na ukaribu na ndugu wala rafiki kwani kazi walizokuwa wakifanya hazikuruhusu kuwa na ukaribu na watu kwani ingewaletea shida na urahisi wa kukamatwa. Love anakili wazi Kuwa katika maisha yake hakuwahi kuota kama anawazazi ingawa anajua kuwa familia yake aliiacha Dodoma miaka kumi na mine iliyopita. Love anasema wazazi wangu pengine ni chanzo maana kulingana na ugumu wa maisha walirubunika na kiasi kidogo cha fedha wakanikabidhi kwa mama Zubeda aliyeenda kuharibu maisha yangu na leo sikumbuki kama bado yupo duniani au alishatangulia mbele za haki.


Tom ilibidi aulize, ilikuwaje aje kumtafuta yeye na siyo mtu mwingine?. Love alieleza pia sababu za kuja kumtafuta Tom na hatimaye kumkamata baada ya kujifanya mpenzi wake kisha kumpeleka kibaha yalikuwa ni maandalizi ya kuja kuiteketeza famulia ya Irene ambayeinasemekana baba yake Waliwahi kufanya Biashara na Jimmy ila wakadhurumiana kipindi hicho wakisambaza siraha kwa magaidi wa al-shababu huko nchini Somalia. Hivyo yalikuwa ni maandalizi ya muda murefu yaliyokuwa yakifanywa ili kuja kumuangamiza Irene. Love alieleza kuwa mke wa Tom ni mtu hatari sana ni mtu aliyefunzwa mbinu zote za kigaidi kitu ambacho Tom hakukijua, Love anaeleza kuwa wamewahi kumvamia mara kadhaa ili wamuangamize lakini ilishashindikana. Zaidi huwa wanaotumwa ndiyo hurudi wameumia, ingawa hawajawahi kupoteza mtu kwenye maandalizi hayo ambao yamechukua miaka kadhaa sasa. Love anakili wazi kuwa hata yeye amewahi kutumwa na Jimmy Kipindi akitoka mafunzoni china lakini alichokiambulia ni kichapo cha hatari na katu hatomsahau. Maelezo ya Irene yalieleza kuwa kukuchukua wewe ilikuwani njia rahisi kwani ukimuua wewe kesi itaegemea zaidi upande wako na kumuacha salama Jimmy. Siri nyingine anayoisema Love ni kuwa ndani kwa Irene alikokuwa anaishi na baba yake kuna madini ya tahamini kubwa aina ya Tanzanite baba yake aliyaficha na inasemekana kuwa mzigo huo waliuteka kin a Jimmy miaka ya nyuma kwa wafanya biashara wa madini huko melelani Arusha na kuja Kuuhifadhi kwa Baba yake Irene na hiyo ndiyo sababu kubwa inayomtesa Jimmy atayapataje hayo madini Kutoka mikononi kwa Irene maana ni Irene pekee anayejua yalipo. Jimmy aliona njia rahisi ni kumkamata Tom mme wake si kwa kitu kingine bali ulikuwa ukiandaliwa kwa kazi hiyo. Love alikuwa akieleza hayo kwasababu alijua Jimmy hawezi kumpata tena maana afya yake haikuwa rafiki. Msisitizo alioutoa love kwa Tom ni kwamba Tom arudi kwa mkewe akawe mme mwema, alimwambia kitu amabcho Tom alikuwa hakijui kuhusu mkewe ujauzito aliomuacha nao alijifungua watoto wawili (mapacha) wote wakiume. Tom anashitu na kuanza kulia hakuamini kuwa hapo alipo anawatoto wenye umri wa mika miwili na miezi kadhaa bila kujua na wala kupata taarifa zozote. Love alimcheka na kumwambia “kwa picha hiyo si kitu cha ajabu ukiwa unaishi na Jimmy Radi hata mimi baada ya miaka kumi na minne jana nimekutana na familia yangu tena si kwa matakwa yangu bali kwa lazima au nguvu uliyo itumia wewe” . love alimsisitizia na kisha akatabasamu huku akimwangalia machoni.


Ilikuwa ni asubuhi yapata kama saa moja na nusu Love alimhimiza Tom aondoke arudi kwa mkewe wakalee watoto wao maana habari ya mtoto wa kigogo ilikuwa imekamilika, love alisisitiza hakuna tena mtoto wa kigogo na hatotokea. Kauli iliyoleta utata kidogo kwa Tom baada ta kuisikia ikisemwa na Love huku akilia. Love alisema “siwezi kuja kuwapa taabu wazazi wangu baada ya kuyaharibu maisha yangu mwenyewe, unazani nani atatoa msaada kwangu kwa hali unayoiona hapa?, staki kuendelea kuchuma dhambi kwa kuwatesa wazazi wangu kuanza kunilea mpaka nitakapokufa kwa matatizo niliyojitafutia mwenyewe. Ninakansa ni lazima nitakufa, kwa sasa bado ninanguvu lakini siyo sababu ya mimi kuendelea kuwapa shida baba na mama yangu. Hawajui niliko itoa ila mimi najua ni ulevi wa pombe kali uliosababishwa na starehe zisizo na nyuma wala mbele, Tom umekuwa mtu mwema kwangu Tafadhali rudi kwa mkeo anakupenda na anateseka kwaajili yako rudi kale watoto mimi nitakufa ingawa sijui nitakufa lini ingawa najua itakuwa hivi karibuni pili kabadilishe maisha yako kaombe msamaha kwa mungu wako juu ya dhmbi ulizofanya mimi najuta kukuingiza kwenye huu mlolongo wa dhambi hatari ulizoziteketeza kama vile mauaji kwa watu wasio na hatia pole sana kwa hilo.” Love alimaliza kuongea baada ya kukatishwa na hodi iliyokuwa ikibishwa kutoka mlangoni hivyo Tom anakwenda kufungu mlango bada ya kuufungua anakutana na baba yake Love lakini wakati akisalimiana na baba yake Love karibu na kijumba walichokuwa wamelala, ghafula walisikia mshindo ndani ya kile kijumba walichokuwa wamelala Tom na Love. Tom anakimbia haraka lakini alifika na kugundua alikuwa tayari kachelewa, macho ya love ndiyo yalikuwa yakiishiria kufumba huku kifuachake upande wa kushoto sehemu unapokaa moyo, kilikuwa kikivuja damu nyingi na upande wa wa kulia pembeni kulikuwa na bastora iliyokuwa imekamilisha shughuli hiyo. Vilio vilisikika na kuwaweka njia panda wazazi wa Love kwani ndo kwanza walikuwa wameonana na mtoto wao kwa siku moja tu.


Ilikuwa ni hali ya huzuni Tom aliumia sana lakini hakuwa na jinsi na mwisho mazishi yanafanyika bada ya polisi kulizika na upelelezi waliofanya na Tom anakata tiketi na Kurejea Dar es Salaam huku akiwa na majonzi tele moyoni. Love alikuwa katoweka dunian na kuacha majonzi mazito moyoni kwa aliyekuwa mpenzi wake Tom. Maumivu makali yalikuwa yakimuandama Tom, mara kwa mamra aliyakumbuka maneno na wosia mzito alioachiwa na Love. Hasa ule wa kurudi na kwenda kuitunza familia yake. Tom anawaza mengi huku akiwa na kitamba chake amacho alikitumia kufuta machozi kila yalipomtoka na kujilazimisha kujikaza kama mwanaume lakini ukweli utabaki palepale kuwa Tom alimpenda sana Love.


Basi Tom anaingia ndani ya basi kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Dodoma, lakini kipindi anaketi kwenye gari dakika kadhaa zinapita anajikuta kwenye siti aliyokaa wanakuja watu wawili mmoja akiwa ni John Licko na Annet Rehan, watu hawa wawili wanaifanya Timu ya watu watatu waliokuwa wamehitimu mafunzo ya ugaidi huko kibaha wakiwa watatu na leo wanakutana ndani ya gari moja. Licko alifika na kuketi upande wa dirishani huku Tom akakaa kiti cha mwanzo viti vilipakana, ndani ya Basi la Shabibi upande wa pili kiti cha kwanza alikuwepo Annet Rehan msichana pekee aliepona na kuonekana shujaa huko kibaha wakati wa mtihani wao wa mwisho. Baada ya salamu amabayo haikuwa hata na ishara ya tabasamu hata lakukosea watu wale waliketi na kimya kikatawala. Upane wa Tom alianza kutamani basi Ipinduke kwani yaliyosemwa na Love sasa yametimia, kwani bila hofu alijua kabisa kuwa Annet na John walikuwa wakimfatilia Tom toka ametoka Dar mpaka leo anaporejea na bila shaka kuna mkono wa Jimmy nyuma yao. Alijua lengo lao kuu ilikuwa ni kumuua na si vinginevyo.


Sasa hofu ilitawala na moyo unamwenda mbiyo pamoja na kukosa amani na kuwa na wasiwasi Tom alikuwa akigeuka huku na kule huku jasho likimtoka lakini hakuna aliyemjali. Tom anajiandaa kushuka ili aahilishe safari lakini alikuwa kachelewa na basi ndo kwanza lilianza safari na kukiacha kituo cha mabasi. Amani haikuwepo kila akigeuka hawa watu hawakuonesha hata sura ya huruma Annet alikuwa akitafuna zake big G katinga miwani yake mieusi huku sura kaikunja kwa hasira kama anakula embe change, upande wa John yeye akiwa na na Lundo la majani ya mirungi akiisaga taratibu huku katinga miwani yake mieusi. Safari ilizidi kushika kasi Tom sasa inafika wakati anakata tamaa kabisa alichokuwa akikifanya akiona mtu anajitikisa tu anashituka na kukaa tayari kwa lolote. Ikawa hivyo baada ya safari kunoga hatimaye waliiacha wilaya ya Gairo, lakini wakiwa sehemu iliyojaa vichaka na ilionekana kama pori wasiloishi watu. Jonh anamuomba dreva asimamishe gari na dreve anatii amri hiyo mara moja basi linasimama, wakati huo yeye akiwa amesimama tayari na Annet akiwa kasimama pia. Tom anatetemeka mithili ya mtu aliyetolewa kwenye friji alimokuwa kawekwa kwa takribani saa ishirini na nne, Tom aliwajua watu hawa vizuri basi alijua dakika zake za kuishi sasa zilikuwa zinahesabika, machozi yalikuwa yakimtoka huku akisali kimoyomoyo ingawa tayari alikuwa kachelewa kimuomba mungu amuokoe. Basi John Licko na Annet Rehan kwa pamoja wanasogea na kumuweka kati kati Tom.


Je nini kilitokea baada ya Tom kujikuta yuko katikati ya hawa watu wawili hatari? Mimi sijui ngoja tuone nini kitatokea kwa kuungana na mimi sehemu inayokuja. 




Tom anazidi kuhaha huku akitetemeka, uwezo wa kufikri ulikuwa mwisho na sasa Tom anashusha pumzi kwa nguvu anaamua kuwa mpole maana maji sasa yalikuwa yemevuka shingoni yakikinyemelea kidevu, akiwa bado kaketi alinyanyua uso wake kiwiziwizi anakutana na kisu kikubwa kilichokuwa kiunoni mwa Jonh kwa hisia anakumbuka watu aliowauwa kwa upanga huko kibaha kipindi wakaandaliwa kuwa majambazi na sasa zamu yake ilikuwa imetimia. Tom aliwaza mengi sana ni namna gani angeweza kujitetea au kuwatoroka hawa watu wasimuangamize kama dhamila yao ilivyojionesha. Tom anajiwazia amepambana na watu hatari tena hatari kwelikweli wakiwemo polisi, wanajeshi na majambazi walioshindikana. Lakini hakusahau kuwa aliyafanya hayo kwasababu alikuwa kafunzwa vyema. Sasa watu hawa aliokutana nao leo ni hatari kwake maana wanamjua vizuri, mafunzo aliyoyapata yeye ndiyo waliyonayo wao hivyo Tom anachoka na kulegea kama kuku wa mdondo akisubiri huruma ya nyegere.


Akiwa kasimamiwa kulia kwake na Jonh Licko huku Kushoto ni Annet wanainama kwa pamoja na Kumnong’oneza kitu kisha wanamkabidhi kakaratasi na wao wanaongozana kushukia hapo polini na safri inaendelea kama kawaida kwa wasafiri waliosalia akiwemo Tom. Maneno waliomwambia Tom ni haya “kaka tuna kakazi kidogo hapa polini hivyo kausha kama hujatuona vile ni mwendo wetu wa kimyakimya usiogope lakini chukua hii kadi ya mawasiliano tutafutane kwaheli”. Tom anashusha pumzi huku akitikisa kichwa kukichaji akili zake ambazo kidogo zilikuwa zimeanza kuganda kutokana na wakati mgumu aliokuwa kabebeshwa na hawa watu. Tom anaangalia juu na kumshukuru mungu kwa miujiza ambayo alizidi kumtendea kila siku katika siku zote za maisha yake. Tom aliwaza sana maana haamini kama kweli watu hawa wamemuacha salama . “mungu ni mwema …. Mungu wema wako hauna mfano … najua nimekukosea mengi lakini huachi kuniongoza na kunisimamia.” Ni sala aliyokuwa akisali Tom kama sehemu ya shukrani kwa muumba wake kwa mema aliyokuwa ametendewa kwa muda murefu sasa. Tom akiwa ndani ya basi safari iliendelea taratibu walifika morogoro, chalinze na hatimaye majira ya saa kumi walikuwa wamefunga breki ubungo.


Baada ya kushuka Ubungo Tom anaanza kujiuliza maswali anaanzia wapi au atawezaje kuingia nyumbani kwa Irene?, lilikuwa ni swali lililoteka kichwa chake na kumfanya akose jibu la moja kwa moja. Lakini kwa wakati huu Tom anaonekana sasa kuyarudisha mawazo kwa Irene mpenzi wake wa siku zote walietoka nae mbali hivyo hakuwa na jinsi maana aliyekuwa akai;iharibu penzi lao tayari kaiaga dunia. Taratibu anatembea na kulifikia lango kuu la kituo hicho cha mabasi anatoka nje huku akiwa na rundo la mawazo anafika nje anachukua Tax mpaka Nyumbani kwake manzese haukuwa umbali mrefu ni karibu sana. Anamlipa dreva na dreva anageuza na kuondoka zake. Nyumba ili kuwa imebadirika sana, iliezekwa upya ikafanyiwa marekebisho ya ukuta ikapakwa rangi nzuri kiuhalisia ilivutia mno na kumfanya tom nusu aisahau. Tom analisogelea geti la Nyumba ya Ya Irene anasogeza kidole ili abonyeze kitufe cha kengele lakini roho inasita basi akawa anajizungusha pale inje kwa muda kama wa dakikakumi na tano sasa. Tom aliogopa sana kuingia kwenye matatizo tena na Irene hakupenda kumuudhi tena na maswali mengi yalukuwa ni kwamba Irene angelifanya nini iwapo angekutana na Tom hapo mlangoni?. Na ndiyo maana aliogopa sana kugonga kengere ya geti hilo akiogopa shali. Pamoja na kujishauri, kujipa moyo na kujikaza lakini ilikuwa ngumu sana kwake kufanya hivyo. Tom alikuwa na sababu za msingi sana za kutokufanya hivyo. Moja aliogopa kuingia kwenye migogoro na mkewe amabaye alijuwa wazi kuwa alimuudhi nayeye ndiye chanzo cha mfarakano wao, pili ni yeye kuitelekeza familia kwa muda wa miaka mitatu bila hata kuwajulia hali hata kwa njia ya simu, tatu aibu aliyokuwa nayo Tom kwa mkewe kwani tangu kujifungua ni takribani miaka miatatu watoto hawamjui baba yao lakini hayo yote hayana sababu za msingi. Ni maswala ya msingi sana kwa tafsiri ya kawaida Tom aliyajua makosa yake vizuri mtihani uliobaki kwake ni jinsi gani ataweza kuingia ndani ili akathubutu japo kutatatua tatizo moja bada ya jingine.


Akiwa getini kasimama gafla anasikia muungurumo wa gari lililokuja kusimama mbele yake kwa gahafla ni gari aina ya RollRoyce, Tom anatoa amacho kwani haijawahi kutokea katika nchi hii ya Tanzania kukutana na gari zuri kiasi hiki na aghari kiasi kile lina thamani kubwa mno si rahisi kulimiliki anajaribu kuchungulia hakumjua aliyeliendesha ila alionekana kama ni mwanamke hakumjua moja kwa moja kuwa ni nani kutokana na ubali aliokuwepo. Tom akiwa kasimama pembeni na geti gari linapiga honi na geti linafunguliwa gari linaingia mpka ndani Tom akilikodolea macho. Tom hakuamini alianza kuhisi pengine alikosea nyumba, harakaharaka anajari bu kuingia kabla geti halijafungwa mlinzi aliyekuwa kwa ndani anamrudiha na geti linajifuga. Basi mlinzi anafunga geti Tom hakujua kilichoendela huko ndani akabaki nje na shahuku ya kuingia lakini haikuwezekana. Baada ya kukaa sana pale nje Tom anaamua kuondoka anapiga hatua kadhaa lakini uzalendo unamshinda anarudi na kubonyeza kitufe cha kengere kinafunguliwa kitundu kidogo cha kuchungulia mlinzi anachungulia na kumuuliza Tom. “kaka unashida gani? Kumbuka nimekuzuia kuingia ndani hivyo ondoka, maelezo yako hayajitoshelezi maana unaniambia wewe ni baba mwenye nyumba hii na mimi najua hapa ninaishi na mama mwenye nyumba tu sina baba mwenye nyumba” mlinzi alimaliza kufoka basi huku akimtaka Toma aondoke. Tom alikuwa kashika adabu kwa upole akaomba “namhitaji mama mwenye nyumba wako tafadhali mwambie ni Tom” . Tom aliomba kwa unyenyekevu “sawa subiri nimuulize” mulinzi aliondoka.


Mulinzi aliingia kwenye kibanda chake akachukua simu na kupiga baada ya maongezi ya sekunde kama kumi hivi mulinzi alikuwa karuhusiwa nadhani na Tom anafunguliwa geti na kuingia ndani. Ni uso kwa uso na Irene baada ya muda murefu miaka mingi imepita na leo Tom anakutana na Irene ambaye sasa alikuwa kawa mrembo mara tatu zaidi ya alivyukuwa awali, Irene alikuwa kajikoki kwenye gauni lake jekundu lenye material ya kuvutika lilimbana kidogo na kulionesha umbo lake halisi, nywele ndefu na nyeusi zilizoanguka mabegani bila kusukwa ziliongeza mvuto kwani zilikuwa ni nywele halisi, uso wake ulikuwa umerembwa na nyusi nyeusi tii, pua nzuri, macho yenye mvuto na midomo mizuri. Irene anamwangalia Tom kutoka juu mpaka chini anashindwa kujizuia anamkimbilia na kumkumbatia wote wanakumbatiana na kuanza kulia huku wakipeana mabusu motomoto ya kila mahali. Walionekana kweli ni wapenzi waliopendana sana na siyo ubabaishaji. Irene anakitoa kichwa chake begani kwa Tom alipokuwa kakiegesha kwa muda, anakiinua na kumuangalia Tom usoni huku asiamini kama kweli Tom amerejea. “ahsante … ahsante uliyejuu hakuna kinachoweza kushindikana kwa uwezo wako hatimaye mwana mpotevu leo karudi” ni maneno aliyoyasema Irene wakiwa wamekumbatiana na Tom huku akizidi kumkumbatia kwa nguvu. Irene analia kwa uchungu wote wanaangua kilio, haikuwa furaha tena bali karaha furaha inapitiliza na kuleta majonzi. Wapenzi hawa waliopendana sana na kutengana kwa sababu zisizo za msingi sasa wanakutana tena na wote wanaonekana kuwa wenye furaha zaidi kila mtu alisema maneno matamu awezavyo ili kuifurahisha nafsi ya mpenzi wake, yalisikika maneno matamu ya kila aina ambayo hata ulimwengu ulikili kuwa nikweli watu hawa wanapendana.


Tom alikuwa kama mgeni kwani kila kitu kilikuwa kimebadilika nyumbani kwakwe, kila kitu kilikuwa kipya, kuanzia rangi ya nyumba, geti liliwekwa la kisasa zaidi, huko ndani nako madoido yaliongezeka. Fahali ya macho ni kuona uzuri unaotafsirika na ndivyoilivyyokuwa kwa macho ya Tom hayakuchoka kuvutiwa na kila kitu humo ndani. Tom anakaribishwa sebureni na kuketi. Sebureni palivutia sana kwani kila kilichokuwa sebureni pale kilionekana kuwa mhimu machoni mwa Tom anzia sofa, midoli, mapazia Tv na vitu vingine vyote vilimvutia sana Tom. Irene anamkalibisha Tom chumbani ambako wanakwenda chumba cha chini walichokuwa wakikitumia toka mwanzo wa mahuiano yao, huko Tom anaoga na kubadilisha nguo. Basi wanazungumza mambo mengi Huku Irene akimuonya mapema kuwa Tom asithubutu kuzungumzia mapito, kwani hakutaka kuyajua na wala kuyasikia, basi walijikita katika mazungumzo ya kifamilia baada ya Tom kuomba msamaha, Irene alimkaribisha na akamwambia amemuandalia zawadi nzuri yakurudi kwake nyumbani. Basi walicheka na kufurahi wapenzi hawa


Tom alikuwa kajilaza, akiangalia mieleka kwenye Tv, upande wa Irene alikuwa akiweka mashuka sawa kwenye kitanda chake huko chumbani kwao. Ghafla Irene anapokea simu kisha akaondoka haraka kwenda nje, Tom hakujali baada ya muda kidogo Irene anarejea akiwa na Tommy na Tonny watoto mapacha na kuja kuwa kabidhi rasmi na kuwatambulisha kwa baba yao mpendwa. Umri wa miaka miwili si haba kwani sasa walikuwa na uwezo wa kujieleza, watoto walikuwa wachangamfu, walikuwa na vituko sana na kwa bahati nzuri walifanana sana na baba yao. Basi furaha iliongezeka kwani watoto walitokea kumpenda sana baba yao maana alipenda kucheza nao hivyo ndani ya muda mfupi kwa vituko vyaka watoto wanampenda zaidi baba yao. Baada ya utambulisho huo huko chumbani basi wanarudi sebureni Tom akiongozana na watoto wake na sasa anakutana Uso kwa uso na mama Tom. Mama alikuwa na hasra kama za bogo mara tu baada ya kumuona Tom alidakia “umerejea kwa mumeo wa ndoa siyo?, sijawahi ona mwanamke kahaba asiyejitambua kama huyu katika ulimwengu huu, nakuita mwanamke kwasababu unamambo yakike tena mambo ya mwanamke asiye jitambua ingawa nilikuzaa ukiwa kidume tena kidume kamili, mwanamke asiyeshikwa akashikika kwa mmewe, mwanamke asiyejali wapi aliokotwa na mmewe…. Tom wewe si binadamu mwanangu……. Hii shiringi unayoichezea kwenye tundu la choo ipo siku itakuponyoka na kutumbukia chubwiiii! Katu hutaiona milele utachimba choo chote na katu hutaiona.” Mama alimaliza na kujiweka sawa kwenye kiti alichokuwa kaketi.


Tom hakuwa na cha kusema wakati huo Irene akikosa aseme nini mbele ya mama mkwe wake, basi ukimya kidogo ulitanda na hapo ndipo Tom ilimbidi awe muwazi ndipo alipo amua kuporomosha hadithi ya kusisimua juu ya yote aliyokutana nayo na kuwaaacha watu vinywa wazi. Kila mtu alibaki kusikitika, mama alishika kichwa na tumbo lake kila aliposikia mateso aliyokutana nayo Tom hasa yaliyoambatana na kukoswakoswa kuuliwa na hatimaye yeye kuuwa. Mama uzalendo ulimshinda baada ya kuisikiliza hadithi iliyompata mwanaye huko Kibaha kambini walikokuwa wamefichwa, na hatimaye Sundani ya Kusini, lakini aliumizwa zaidi na utekwaji wa Tom huko ziwa vikitoria akitokea Uganda kwenda Mwanza. Wote walikuwa kimya wakitafakari na mwisho mama alisema “mwanangu Tom inatosha pole sana baba najua umejifunza tafadhali mungu anakupenda, lea familia yako ndo maana leo uko hapa naomba ulee familia yako baba nadhani umenielewa maana kama unaakili zilizo sawasawa utamshukru mungu kwa funzo hili dogo ambalo staki uendelee kutusimulia maana niliyoyasikia yanatosha kukubadilisha nimemaliza baba Mjali mkeo, lea watoto wako” . Baada ya mama kumaliza kutoa ya moyoni Irene anakuja na kumkumbatia mmewe, anampa moyo na kumwambia alisha msamehe mbali na kuomba msamaha, wanakumbatina na kubusu wote wanafurahi na mama anatabasamu.


Mazungumzo ya kawaida yalifuata, na baadae chakula maarumu kilichoandaliwa kwaajili ya mgeni ambaye ni Tom, walikula chakula na wote wakafurahi kwa pamoja na hatimaye walienda kulala wote wakiwa wenye amani tele moyoni. Usiku huo juu ya kifua kilicho mpa faraja kila kiukicha Irene alikuwa akipumua kwa furaha hakuamini kama ingetokea siku nzuri kama hiyo katika maisha yake yote. Huku akiongea kwa madeko yasiyo tafsirika kiurahisi. Raha ya kupenda upendwe na leo Irene furaha yake imerejea upya. Wakiwa wamelala Tom kwa wivu aliuza “kipindi nikiwa nje niliona mtu anaingia na ile gari nyeusi ya kifahari ni nani na imetoka wapi?” Irene alimcheka sana kisha akajibu ni gari yangu mpya mme wangu nimeipokea wiki jana na leo nimeanza kuitumia rasmi ni RollRoyce imenigharimu fedha nyingi ni kama milioni miasita shilingi za kitanzania naipenda na niliipenda hivyo niliona fedha siyo kitu Kwangu nilifumba macho nikanunua ili kuikamilisha furaha yangu na mimi ndiye uliyeniona naiendesha” Irene alikuwa kaukata umbea. Basi Tom alitabasamu na kumkumbatia kwa nguvu Irene . “wewe ni zaidi ya mke kwangu leo umeweka rekondi ya kuwa na gari la kipekee katika nchi hii nakupenda sana” .Basi wanalala usingizi mtamu kwa pembeni kukiwa na kitanda cha watoto wao.


Asubuhi na mapema ndani ya chumba cha mazoezi Tom anajirusha huku na kule kwa muda mchache alikuwa kalowa jasho mithili ya mwogeleaji aliyetoka bwawani. Tommy na Tonny wanakuja kwenye chamba hicho basi baba yao anaungana nao kwa kufanaya mazoezi na watoto wake alikimbizana nao huku na kule waliangushana na kurukaruka basi ilikuwa ni furaha ya ajabu. Irene alikuwa pembeni akiangalia na kucheka Tom sasa alianza kuuona utamu wa kuwa na familia alitokea kuwapenda sana watoto wake kwani walimpa furaha kila wakati, kila dakika aliwakumbuka Tommy na Tonny anapokuwa hatua chache kutoka walipo. Irene alivutiwa sana na Tabia ya Tomm maana iliimalika kila kukicha. Tom sasa alikuwa karibu sana na familia yake. Hakuwa anapenda familia yake ipate tatizo sasa alikuwa baba bora wa familia na kila mtu aliufurahia uwepo wake ndani ya familia.


Kadri siku zilivyozidi kwenda familia ya Tom sasa ilikuwa imekamilika, mapenzi ya dhati kwa mkewe ambayo hakuwahi kuyaonesha hapo awali sasa aliyaonesha hadharani mahali popote bila kujali kuna nini na nani yuko sehemu hiyo. Mara mojamoja alitoka na mkewe kwenda sehemu za starehe lakini pia maranyingi tu alikuwa akitoka na familia nzima kwenda kubadili upepo na mboga sehemu mbali mbali nza nchi hii, kama vile Arusha, Mwanza, Mbeya, Zanzibar na hata nje ya nchi mara mojamoja hakusita kufanya hivyo. Tom alikuwa akifanya kazi kwa bidii na uaminifu wa hali ya juu, sasa aliwaepuka marafiki wanafiki aliamua kubaki na familia yake na kila siku alihakikisha anamfurahisha mkewe. Basi Irene anamuamini na kumkabidhi miradi mingi aliyokuwa akiimiliki, Tom alikuwa akifanya kazi sana, alikuwa akijisomea sana ili kuongeza maarifa. Hali hiyo ilimsaidia kufanya kazi na makampuni makubwa hapa duniani kwa kushirikiana kibishara, Lugha ya kiarabu aliyojifunza huko Sudani unakuwa ni ufunguo wakibiahsara katika nchi za kiaarabu anafanya kazi na mashirika na pia makampuni mengi ya mafuta na bidhaa zingine Toka uarabauni. Lakini juhudi zake zinamwezesha kuimudu Lugha ya kiingereza au Kimombo na sasa Tom akuwa mtu maarufu na mashuhuri katika biashara hapa Afrika. Irene alikuwa mpaka anachanganyikiwa kwani njia zote zilikuwa zimefunguka kwa mpenzi wake hakuna kitu ambacho kiliweza kushindikana mbele ya Tom. Tom alifanya kazi kwa weledi, hakuwa na majivuno, hakuwa na dharau lakini aliweza kuwaongoza watu wenye taaruma zao kubwa na na elimu kubwa kumzidi na hatimaye kufikia mafanikio. Kampuni nyingi alizifungua na zikafanya vizuri kutokana na ubunifu wa kibiashara na uwezo wa kuyatumia maarifa yake vizuri.


Siku moja Tom akiwa aketi nyumbani kwake anakumbuka kitu ambacho anahisi ilikuwa siri kubwa ndani ya nyumba yake. Ni madini ya tanzanite aliyowahi kuambiwa na Love. Wazo hili linamtesa kwa siku kadhaa na suruhisho lake anaona ni bora akayatafute hayo madini ambayo yanasemekana yako kwenye nyumb ya marehemu baba mkwe wake huko masaki. Nyumba hiyo ilikuwa haikaliwi na mtu isipokuwa walinzi nwa mtu wa usafi ambaye alikuwa akikaa kwenye kijumba kidodo hapo pembeni. Kwa wazo hilo Tom anaona nibora akayachukue hayo madini na aondoke aende kusiko julikana, basi anaondoka kimya kimya bila kumhusisha mkewe mpaka masaki ilipokuwa nyumba ya baba mkwe wake anafungua na kuingia ndani, msako unaanza kona hadi kona akiyatafuta Hayo madini. Tom alipavuruga ndani mule bila mafanikio, hakujua yale madini yalipokuwa yamefichwa. Aliendelea kuvuruga na mwisho alichoka akaenda kuketi sebureni. Akili yake ilikuwa ikiwaza kwa haraka sana kutafuta njia ambayo ingemsaidia kuyapata hayo madini wakati huo Tom aliwaza utajiri wa haraka wakwake bila kutegemea mali za mwanamke. Tom akiwa kaketi anaangalia upande wa kulia anakutana na Irene uso kwa uso akiwa kajiegesha ukutani akimwangali. Irene alikuwa mwenye hasra kwelikweli kutokana na kitendo alichokifanya Tom. Basi kwa aibu Tom anajikaza kujaribu kumsemesha lakini, Irene alimuwahi na kuanza kumshushia vidonge kama ifuatavyo “Tom unawezaje kuingia kwenye nyumba ya wazazi wangu bila kuniambia? Na mbaya zaidi ukapavuruga hivi na mimi nisijue unachokitafuta, kumbuka tangu unioe hujawahi kuniona nikifanya hivi kama ulivyo fanya wewe na hii ni nyumba ya wazazi wangu nina mamlaka nayo inakuwaje wewe mtu baki usiyejua siri ya humu ndani uingie na kufanya utakavyo?. Naiheshimu sana hii nyumba na ndiyo maana tulipoowana sikutaka kuishi kwenye nyumba zote za wazazi wangu lakini wewe leo umeingia mpaka chumbani. Tom sijawahi kukuingiza kwenye hii nyumba toka unijue huwa tunaishia nje…. Nashangaa umepata wapi ujasili wakuchukua funguo za nyumba hii na kuja kuingia bila ridhaa yangu. Mme wangu maisha yanamipaka nilazima ifuatwe hiyo mipaka. Na mfano mzuri mimi mwenyewe sijawahi kuidhalilisha hii nyumba ulishwahi kujiuliza kwanini sijawahi kukingiza kwenye hii nyumba?. Au ndo umelewa mamlaka baada ya kuona nimekukabidhi kila kitu ninachokimiliki?. Sijui ulichokuwa ukikitafuta humu ndani na utawezaje kutafuta kitu ndani kwa mtu na mwenye nyumba asijue unachokitafuta?. ” Irene alikuwa akihoji kwa hasra na wakati huo Tom alikuwa Kimya kama kanyeshewa mvua. “Tom baba acha kuvaa viatu visivyokutosha … utajitafutaia matatizo bure.. kumbuka nimeyavumilia mengi mpaka tunafika hapa nikisema niyakumbuke najua tutaumizana, kaa mbali kabisa na maswala ya familia yangu hujui lolote na kama kuna mtu amekudanganya basi mwambie mmekwama atumie njia nyingine na siyo wewe, utanifanya sasa nianze kuishi kwa sura yangu ya pili niliyoihifadhi.” Irene alikuwa akizidi kufoka. “Tom umefuata nini kwenye nyumba ya baba yangu……? Na nani aliyekutuma…….?” Tom hakuwa na chakujibu domo lilizidi kumbaki wazi kama lango la bajaji “Tafadhari ……… sasa nimechoshwa na tabia za kishenzi maana umevuka mipaka na heshima niliyokupa sasa unajiona wewe ni zaidi ya wazazi wangu………………………. Nauliza tena umeijia nini humu ndani? …………….” Bado Tom alikuwa Kimya pamoja na Irene kuonekana mwenye hasra…………………. “sasa wakati umefika wakusema yatosha ….. Tom …. Inatosha nazani sasa unaweza kujribu na kwawengine kwangu nahisi nimetosha fanya uwezavyo ila uniache na maisha yangu” Irene alimaliza kusema huku akimsukuma Tom aondoke. Tom anajaribu japo kujitetea lakini alikuwa kachelewa kwani hakuna aliyemsikiliza tena . bai alibaki kujilaum huku akipiga mateke viti na meza humo ndani.


Penzi lisiloishiwa misukosuko, kila kukicha huibuka na jambo jipya pamoja na juhudi zote anazozifanya Irene kumsaidia Tom lakini Tom haishiwi tamaa na visa vipya visivyona maana wala mashiko, kila kukicha je, Irene sasa



Irene anatoka nje Tom anajaribu kumkimbilia huku akijaribu kujitetea lakini hakuna jibu lililotoka kwa Irene zaidi ya kuzidi kusonga mbele. Tom aliona hakuna kipya atakachokifanya Irene akamuelewa basi aliamua kurudi na kuufunga mlango na kuingia kwenye gari akurudi nyumbani. Irene baada ya kufika nyumbani alianza kujiuliza kwanini Tom alikwenda kwenye nyumba ya baba yake? Jibu hakuwa nalo ila maswali yaliongozana na kukosa hitimisho hali hiyo ilimkela sana Irene kwa hakupendezwa nayo. Tafakali ilichukua muda sana kwani sasa Irene hakuwa na imani tena na Tom alihisi siyo mtu mwema kwake, Irene anayakumbuka maneno ya mama mkwe wake kuwa Tom nimnyama si binadamu na kamwe si mtu wakumuuamini. Irene aliangua kilio akijuta kwanini mateso yahaishi kwake, kwanini kila kukicha ni visa tu, kwanini Tom habadiliki?, Yalikuwa ni maswali aliyojiuliza Irene haya yote chanzo ni Tom mmewe kipenzi, aliyemchagua bila kushawishiwa na mtu. “wanyama hufunzwa wakabadilika ila si kwaaina hii ya binadamu kweli nakili wazi kuwa Tom ni kiumbe kingine” Irene alijikuta akiropoka huku akinyanyuka kwenda chumbani.


Tom anafika nyumbani akiwa na wasiwasi mkubwa anaingia ndani kwa kunyata mpaka chumbani anamkutu Irene kaketi huku akiwa na mawazo tele. Tom alifika na kumuuliza Irene “je, naweza kufafanua kilichotokea?” Irene anamuangalia kisha anachia tabasamu la majonzi kisha akajibu huku akijiiandaa kuusikia huo utetezi aliouandaa Tom. Tom ilimbidi kueleza kila kitu jinsi ilivyokuwa kuhusiana na hayao madini, taarifa alizipata wapi na kwanini, pia anamkumbusha Irenekuwa amewahi kuvamiwa mara kadhaa na watu wakiyataka hayo madini. Ilikuwa ni hadithi ngeni masikioni mwa Irene alikuwa hajui chochote kuhusiana na Taarifa hiyo ya madini, ila katika kumbukumbu zake anakumbuka kuna kisanduku amacho aliwahi kuoneshwa na baba yake na akapewa kodi za kukifungulia. Basi Tom akamuuliza Irene kama anamfahamu mtu mmoja anaitwa Jimmy Radi na hapo ndipo Irene anashituka na kuguduka kuwa Tom atakuwa anatumiwa na watu wa Jimmy. “Tom umemjulia wapi Jimmy?, huyu ni mtu ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa sana kuuwawa na baba” Irene anahoji kwa wasiwasi mkubwa. Tom hakutaka kuficha alieleza mkasa wote kuhusiana na mahusiana yake na Jimmy kutokana na utekeji uliofanyika, alieleza kila kitu kuwa kiongozi wao kipindi akiwa huko Sudani ni alikuwa Jimmy, Tom hakuishia hapo aliweka wazi kuwa kwa sasa anatafutwa kuuwawa na Jimmy baada ya kumsaliti, pia anaongeza kuwa Jimmy alimteka Tomm ili aje kuiteketeza familia ya Irene kutokana na dhuruma zilizofanywa na baba yake Irene dhidi yake katika biashara zao za madini. Tom anaongeza kuwa baba yake Irene kuna madini aliyaficha mpaka anafaliki hayajawaki kuonekana wala kuuzwa na Tom akamwambia, Irene pekee ndiye inasemekana anajua yalipo.


Irene anarudisha nyuma kumbukumbu na kugundua kuwa anachokisema Tom yaweza kuwa kinaukweli amewahi kuvamiwa na watu kadhaa wakiwa na dai hilo la madini lakini yeye hakuwa anajua chochote. Basi Irene anamlaumu Tom kwanini anafanya mambo kimyakimya bila kumjuza, huku akijua hicho ni kitu hatari kwa familia yao. Tom aliomba msamaha na Irene akaahidi kulifanyia kazi swala hilo mpaka atakapopata jibu la mwisho. Walisameheana na kuendelea na shughuli zingine za ujenzi wa familia yao. Tom aliondoka na kwenda ofisini kwake na kuendelea na shughuli zake kama kawaida simu za ofisini zilikuwa bize kila kukicha, akipokea taarifa, akipokea mizigo, tenda, oda na kutuma mizigo na biashara ilikuwa imenoga. Tom sasa alikuwa ni mtu wa suti na tai, siyo Tom wakuweka nywele dawa wala kusuka rasta, siyo Tom wakunyoa kiduku, siyo Tom wakuvaa jinzi na tisheti za kubana. Alionekana ni mtu fulani mhimu katika ulimwengu huu. Mwili wake wa wastani usio na kitambi mikono na kifua iliyojaa kwa mazoezi ilipendeza sana kwenye kila aina ya suti aliyovaa mithili ya mwanamitindo mashuhuli duniani. Tom alizidi kufahamika na kufahamika akajulikana kila kona ya Afrika na sifa zake zilianza kuvuka mipa tangu alipoanza ubia na makampuni ya mafuta ya huko uarabuni. Sifa hizi zinamuingiza kwenye milango mingine na kufungua fursa zaidi kwa wafanyabiashara wakubwa kumtumia kama balozi wa kibiashara afrika mashariki na maeneo mengine ya Afrika.


Irene leo ameamua kulivalia njuga swala hili aliamua kwenda nyumbani kwa baba yake na kuanza kutafuta taarifa ili apate tarifa sahihi juu ya hiki kisemwacho. Siku ya kwanza anaambulia patupu siku ya pili pia anahangaika lakini anakutana na faili moja lililoandikwa kwa Lugha ya kiarabu. Irene hakujua maana yake lakini mwisho kulikuwa na sahihi ya baba yake, alilitupa na kuendelea na shughuli yake ya kutafuta alichokihitaji siku nzima inakatika bila mafanikio anarudi nyumbani huku akionekana mwenye majonzi tele. Tom anarejea nyumbani siku hiyo saa tano za usiku anamkuta mkewe akiwa na mawazo tele anajaribu kumbembeleza amwambie nini kinaendelea Irene alijibu kwa kifupi kuwa hakuna matumaini. Basi Tom alisimama lakini kabla hajaondoka analiona bokisi alilokuja nalo Irene anafungua na kukutana na faili lililokuwa na ujumbe uliandikwa kiarabu. Tom anausoma bila shida huku akionesha tabasamu aligeuka na kumuangalia Irene alikuwa kajipumzisha bila kujali kinachoendelea basi Tom alichukua faili lile na kwenda kujifungia nao chumbani. Anasoma kurasa zote bada ya kumaliza anashangilia. Ukweli ni kwamba hilo ni faili lililotabiri kifo cha baba yake Irene aliloliandika kwa mkono wake huku akiacha kamlisisha mwanaye mali zote na chakufurahisha zaidi ni Kuwepo kwa madini aliyoyaficha kwenye chumba chake cha falagha hapo nyumbani kwake mwisho alimtakia maisha marefu mwananye na awe tayari kupambana na adui wa kila aina katika maisha yake na adui mkubwa alikuwa ni Jimmy Radi.


Tom analibusu lilefaili na kulirudisha kisha anakaa kimya bila kumwambia chochote Irene. Kitu ambacho hakukijua Tom ni kwamba huwezi kuingia kwenye nyumba ya baba mkwe wake peke yako bila Irene kujua. Tom sasa alijiandaa kesho yake asubuhi aliondoka kama kawaida kuwa anaenda kazini lakini hakuwa anadenda kazini alikuwa kaiba funguo za nyumba ya baba yake Irene kwa lengo la kwenda kuyachukua hayo madini ya Tanzanite. Alifika nyumbani na funguo zake lakini kile kitendo cha kuingiza ufunguo kwenye kitasa cha mlango tayari Irene anapata taarifa kupitia saa yake ya mkononi kuwa kuna mtu kaingia kwenye nyumba ya baba yake. Haraka haraka anaingia ndani na kuseti kamera za ndani kupitia tablet yake anamuona Tom akihanganika na milango basi alichokuifanya ni kuwahi na kujificha ili ajue nini kinaendelea. Lakini wakati akitoka nyumbani kulikuwa na watu nyuma yake ambao hakuwajua na hakujua kama wanamfatili. Tom alizunguka mule ndani bila mafanikio hatimaye anaipata ngazi iliyokuwa inakwenda chini shimoni huko anakuta chumba kidogo chenye mlango mfupi anavunja kitasa na kuingia anakuta kuna kisanduku kidogo anajaribu kukibeba kilikuwa kizito anajikaza anahangaika nacho mpaka nafanikiwa kukitoa mule ndani kisha anakifunga kamba na kukivuta na anafanikiwa pia kukitoa kwenye lile shimo. Baada ya kukitoa anaaanza kuhahakukifungua kilikuwa kimefungwa vizuri na Tom hakujua kama kilikuwa kimefunngwa kwa kode maalimu yaani kwa namba maarumu yani (kode au password).

**********************************


Upande wa pili Irene anakuja haraka akimuwahi Tom lakini wakati huo hakujua kuwa wale watu wanazidi kumfuatilia Toka alipotoka nyumbani na anaongozana nao kila alipokwenda mka anafika kwenye nyumba ya baba yake. Irene anafika na kuingi ndani haraka Tom hakujua kama kawaida yake alikuwa kasimama pembeni wakati huo Tom alikokuwa kaingia vyumba vingine kutafuta kifaa kizito kitakacho msaidia kubomoa kile kisanduku. Tom anakuja haraka na shoka lake huwezi amaini alimpita Irene bila kumuo kwani mawazo yote yalikuwa yakiwaza utajiri aliokuwa akiuota. Tom alijua tayari ametimiza ndoto yake ya kuwa tajiri kwa mali zake bila kutegemea msaada wa mwanamke. Alifika na kunyanyua shoka ghafla alisikia sauti ikimwamuru “Achaaaa!!!” Tom anatupa shoka kwa mshituko na kumgeuka Irene akiwa pale pale ukutani alimwambia, Irene alimwambia Tom “kisanduku hicho ni maarumu kwa kutunzia vitu vya thamani kama hukui kodi yake tafadhari usisubutu kukifungua kwa nguvu kinatabia moja tu ukikipiga kwa lengo la kukivunja huwa kinalipuka kwani kimetengenezwa na kemikali za mlipuko namaanisha kina bomu ndani yake kitalipuka utakufa na kilichomo ndani hautakipata milele. Nakumbuka nilifundishwa na baba yangu miaka mingi iliyopia na leo nisingekufata ninahakiaka mpaka muda huu tungekuwa tusha kusahau.” Irene alimaliza huku akimwangalia Tom ambaye leo alikuwa kama zoba, kwani kaumbuka tena mara ya pili na hana sababu ya kujitetea hawezi kusema chochote mbele ya Irene, kwani amerudia kosa lilelile.


Irene alicheka na kumwambia Tom, “usimuone mtu anakusamehe kwa kosa lile lile ukamuona mwenda wazimu kuna wakati anafanya hivyo ili ajue wewe ni mtu wa aina gani, Huwa unanifurahisha sana mme wangu, unavyojua kuigiza sinema zako wewe ni nyota katika maigizo haya. Lakini kumbuka ukweli pekee ndiyo hadhina katika maisha . kuna watu huwa hawadanganywi, hawachezewi na wala hawa jaribiwi mimi ni mmoja wao. Nakupenda sana Tom ndo maana nimekuokoa ulikuwa unakufa kifo cha ajabu leo kwa tamaa za kijinga, hebu jifunze kuuliza kabla ya kufanya jambo.” Irene anakwenda na kukifungua kwa kuingiza kode kwenye kile kisanduku huku Tom akimwangalia . Anafanikiwa kukifungua wanakutana na madini mengi bila shaka hayakuwa yamekusanywa siku moja. Ilikuwa ni tanzanite Nyingi wnatabasamu. Lakini kabla Irene anageuka na kumuonya Tom apunguze tamaa kwani tama zinaua Irene aliyamwaga yale madini kwenye mkoba wake na akarudi na kuliseti lile bom kilichokuwa kwenye kikasha kwa dakika sita kisha alimwambia Tom watoke haraka. Tom hakujua kumbe tayari saa ya Irene ilikuwa imeesha mjulisha kuwa kuna watu wameingia ndani. Basi wao wanapita mlango wa nyuma na kufanikiwa kutoroka.


Ni watu watatau waliofukika nyuso zao wanaingia ndani baada ya kufika ni dakika chache tu zilipita hawakujua kama kulitegwa mlipuko humo ndani. Basi mlipuko ukatokea wale vijana watatu wakafa palepale. Hapo ndipo vurugu ilianza baada ya jamaa mmoja na msicha mmoja kuingia kwa kasi mle ndani na mapambano yakaanza. Yalikuwa ni mapambano ya hali juu sana waliyokutana nayo Irene na Tom lakini upande wa pili Tom anagundua alikuwa akipambana na John Licho na Annet Rehan, Tom aliligundua hili kutokana na staili yao ya upiganaji. Tom mwanzo alikuwa na wasi wasi na Irene lakini baada ya mapambano ya muda mfupi anagundua Irene alikuwa fiti katika mapambano. Ni mapigano ya ana kwa ana/ uso kwa uso yaliyochukua takribani dakika ishirini. Tom alijitahidi kupambana awezavyo lakini alizidiwa vibaya sana na Jonh. Lakini uapande wa Irene na Annet kidogo mambo yalikuwa tofauti kwani tayari Annet alikuwa kapokea kichapo cha mbwa mwizi na mauti yalikuwa yanamnyemelea isinge kuwa kijana mmoja kuingilia kati na kumpiga Irene na ubao wa shingo kwa upande wa nyuma na Irene kuanguka. Tom na mkewe Wote walionekana kuzidiwa sana na hapo ndipo Jimmy Radi alipojitokeza na kuanza kueleza aliyoyajua yeye. Akiwa na walinzi wake shughuli ilikuwa pevu kidogo alifika na kuomba madini Irene alisema hajui chochote kuhusu madini. Basi walimshika Tom na kumwekea bastora kichwani. Jimm aliuliza tena madini yako wapi? Mara hii Irene analazimika kukaa kimya. Kiliendelea kushushwa kipigo kwa Tom ili Irene aseme madini yalipo lakini hakuthubutu kusema. Basi Tom alikuwa kalegea hajiwezi tena kutokana na kichapo alichokuwa kapokea.


Wakati huo mkoba uliokuwa na madini ulikuwa pale karibu na Irene hakuna aliyejiuwa kuwa ndiyo mkoba wenye madini uliokuwa ukitafutwa. Hakuna aliyeuhofia huo mkoba hata kwa bahati mbaya. Waliendelea kuhoji huku wakishusha kichapo kwa Tom ambaye sasa anaonekana amekata tamaa kabisa alikuwa akishushiwa kichapo ili Irene aseme lakini Irene hakusema damu zilizidi kumtapakaa. Irene alikuwa akilia kwa uchungu lakini si kulia tu bali alikuwa akisoma alama ni namna gani angeweza kujiokoa. Kwa bahati mbaya sana wale walinzi walikuwa wamemdharau na kumuona ni mwanamke hawezi chochote maana hawakuujua mziki wake. Basi alifyatuka mikondoni mwa mabaunsa wawili waliokuwa wamemshika kizembe mpaka kwa Jimm Radi ana mkaba kabali kwa mkono wake, Jimmy anajaribu kujinasua anshindwa na kuwa mpole hapo ndipo mkono mwingine wa Irene anafanikiwa kuichomoa bastora yake ambayo aliitembeza haraka haraka na kuwashusha vijana watatu na sasa alikuwa yeye na Jimmy Radi lakini upande wa pili kulikuwa na Annet na John Licko wakiwa wamenyoosha bastora zao walionekana hawana utani lakini Irene alikuwa kadhamilia kupambana hivyo hakuvijali vitisho. Irene alikuwa akiwaamuru washushe siraha la sivyo atammaliza bosi wao. Ulikuwa ni ubushi ulichukua dakika takribani tano, wakati huo Tom alikuwa akijivuta huku akitoa ishara kwa Irene kuwa aendelee kuwazubaidha. Tom anabahatika kukiokota kisu kilichokuwa jilani yake anaruka kwa kujituma na bahati nzuri anafanikiwa kukizamisha kile kisu mgongoni kwa Jonh Irene hakufanya kosa alikuwa tayari kafyatua risasi kwa Annet na alikuwa chini. Tom anaokota bastora ya John huku akiwa hawezi hata kunyanyuka anashusha risasi na kummmaliza John Licko. Na Irene sasa hasira zake zinamalizikia kwa Jimmy Radi ananza kumsurubu Jimmy Radi kwa kumtengua miguuu kwa risasi ni mguuu mmoja baada yamwingine, Irene alikuwa hana hata senti ya huruma kwa wakati huo, Irene anayafanya hayo kwa sababu nyingi moja ni Jimmy kumtumia watu wa kujaribu kumuuwa mara kadhaa pili Jimmy ni miongoni mwa watu waliofanya maovu makubwa katika ulimwengu huu kipindi hicho akisaidiana na baba yake Irene. Mpaka polisi wanaingia walikuta miguu ya jimmy na kuanzia sehemu za mapaja mpaka kwenye unyayo ilikuwa haitamaniki. Irene na Tom wanatoa maelezo kwa polisi kisha wana beba mkoba wao na kuondoka, huku Tom akiwa hoi kwa kichapo.


Utajiri unaongezeka zaidi baada ya kuuza madini yao na sasa biashara makampuni mapya waliyazindua likiwemo la kuingiza Simu z kisasa kutoka jamhuli ya china na marekani zinaendelea. Hakikuwa kitu kidogo walipongezana na kuendelea kubuni miladi mipya, mashirika, makampuni na kutoa misaada kupitia mifuko yao ya misaada ya kifedha waliyoianzisha. Tom na Irene hawakukutana na kikwazo tena katika maisha yao bali walilea familia yao kwa furaha na amani. Tommy na Tonny walikuwa wakubwa walikuwa wakisoma kwenye shule bora kabisa hapa nchini. Tom kutoka kwenye umasikini uliopitiliza na sasa alikuwa tajiri mkubwa akishirikiana na mkewe kipenzi hakuna aliyeshangaa kutokana na mapenzi ya dhati waliyokuwa nayo watu hawa. Tom sasa alikuwa ni kijana mwema mtiivu na msikivu, alikuwa mtu wa watu, hakuwa mwenye tamaa tena bali aliamini kilicho cha Irene ni chake pia hivyo alikuwa katulia na kila mtu alimpenda sana.


************************** Mtu akikubeba bebeka***************


******************************** Mwisho


0 comments:

Post a Comment

Blog