IMEANDIKWA NA : BAHATI MWAMBA
***********************************************
Simulizi : Ukurasa Wa Gaidi
Sehemu Ya : Kwanza (1)
Saa nane na dakika ishirini mchana yalionekana
magari matatu yanayofanana, yakiwa na umbo
kama yale magari ya kusafirishia fedha kwa jinsi
yalivyo na mtenganisho kati ya kichwa cha gari na
'bodi' lake. Magari haya yaliyokuwa mapya yakiwa
na kichwa cha ranngi nyeusi na michirizi ya rangi
ya silva na bodi yake rangi ya maziwa,yalikuwa
katika mfuatano huku yakiongozwa na magari
mawili aina ya Nissan Patrol 'model' mpya rangi
nyeusi mbele huku yakifuatiwa na magari mengine
mawili ya aina hiyo nyuma. Magari haya aina ya
'Nissan patrol' yaliyokuwa na vioo
visivyomuwezesha mtu aliye nje kumuona aliye
ndani (tinted), yalipiga king'ora huku yakiwa
yamesheheni askari makini kabisa kutoka kitengo
maalum cha jeshi la polisi. Mbele ya msafara wa
magari haya umbali wa mita mia hivi kulikuwa na
piki piki mbili za police zilizoenda sambamba huku
zikitawanya magari ili kupisha msafara huu.
Kilichotofautisha msafara huu na misafara mingine
ni ile kasi kubwa iliyokuwa ikiendwa na magari
haya kwa muonekano wa nje kwa wananchi na
muonekano wa ndani ambao watu hawakuuona ni
wale askari maalum ambao ulikuwapo ndani ya
magari haya.
"Eeh bwana eh. Msafara wa 'mapene' huo."
Mwananchi mmoja alisikika akiongea.Na kweli ,
kwa muonekano wa nje, magari haya yalionekana
kama yale magari ya kusafirisha fedha kutoka
benki kuu ya Tanzania iliyo na makao makuu huko
jijini Dar es salaamvna kuzipeleka katika mikoa
mbali mbali. Kitu pekee ambacho watu hawa
hawakujiuliza ni kwamba mbona leo magari haya
yametokea upande wa nyanda za juu kusini.Kwa
bara bara hii ambapo magari yalikuwa yanapita,
ilikuwa dhahiri kuwa magari haya yametokea mkoa
wa Mbeya. .Labda kama magari haya yalipeleka
fedha huko na sasa yanarudi, Lakini pengine cha
kushangaza zaidi ni ule ulinzi mkali uliokuwa
katika magari haya. Kulikuwa na kitu ambacho
hakuna aliyekifahamu zaidi ya waliokuwa ndani ya
magari haya.
*************************************
Saa kumi kasorobo. Msafara huu ulikuwa katikati
ya msitu wa miti mirefu maarufu kama milingoti
kama ilivyotoholewa kutoka neno la kiingereza
'Long tree'. Miti hii ilitengeneza kichaka
kilichopakana na msitu mkubwa zaidi wa miti
inayojulikana kama mipaina au ' pines tree' nayo
pia kama ilivyotoholewa kutoka lugha ya kiingereza
na wakazi wa mkoa wa Iringa.Misitu hii ipo katika
wilaya ya Mafinga huko Iringa.
Msafara huu ulikuwa katika kasi kali sana, wakati
ambapo askari waliokuwa katika gari la mbele
waliposhuhudia pikipiki za police zilizokuwa mbele
ya msafara zikianguka chini mara baada ya askari
waliokuwa wakiziendesha, kushambuliwa kwa
risasi kutoka katika kichaka kimoja ndani ya
msitu.Lilikuwa ni tukio la kushtukiza sana
lililosababisha magari yote kufunga breki kwa
ghafla .Kutokana na ustadi waliokuwa nao
walioendesha magari haya ,haikutokea hitilafu
yoyote wakati walipofunga breki kwa ghafla.
Askari wote waliokuwa katika 'Nissan patrol'
walishuka kwa tahadhari na kuweka silaha zao
tayari kwa lolote. Lakini kabla hata hawajafanya
lolote, walishangaa kuona askari mmoja kati yao
akianguka chini huku akivuja damu nyingi
shingoni. Risasi iliyotokea msituni upande wao wa
kushoto ilimuondoa uhai askari huyu. Hapo ndipo
askari wote walifyatua risasi huku wakizielekeza
bunduki zao kutoka upande wao wa kushoto
ambako ndiko risasi iliyoondoa uhai wa mwenzao
ilitokea.
Askari mwingine akaanguka chini huku akivuja
damu katika goti mguu wa kulia. Safari hii risasi
ilitokeaupande wa nyuma yao na kusambaratisha
mguu wa askari huyu.
''We being shot by snipers.All units take
cover".Ilikuwa ni sauti ya kapteni Joshua akitaka
vikosi vyote vijifiche kutokana na shambulio la
'udunguaji'.Kisha "sniper one and two take your
position(mdunguaji namba moja na namba mbili
kaeni tayari)".Kutokana na kuwepo kwa
mchanganyiko wa askari wa weledi wa Tanzania na
Marekani katika msafara huu, ililazimika kutumika
lugha ya kiingereza ambayo wote waliielewa
vyema.
Hapo moja kati ya yale magari ya kusafirisha pesa
yakalegezwa vifungio vya milango kutokea ndani,
wakashuka askari wawili waliovalia nguo
zilizotengenezwa kwa mfano wa majani makavu ya
mgomba kwa rangi yake na jinsi matambara
yalivyoachwa kuning'inia hovyo katika nguo
hizi.Kichwani walivalia vilemba vilivyopambwa
kiustadi na aidha nyasi kavu au mfano wa nyasi
kavu. Ni kama vile walijua nini kingeweza
kuwapata iwapo wangeshuka bila uangalifu, hivyo
walichukua tahadhari kubwa sana. Askari hawa
walishuka kutoka ndani ya gari kwa kupiga
vikumbo milango kwa ghafla na kujidondosha chini
kama vifurushi.Sekunde hiyohiyo risasi mbili
zililenga usawa wa milango ambayo askari wale
waliipiga kikumbo. Zilitokea upande wa porini na
pengine zililenga kuwadhuru askari wale.
Wadunguaji hawa wawili mmoja kutoka Idara ya
kupambana na ugaidi Tanzania C.T.I (Counter
Terrorism Inteligence) na Mwenzie kutoka Idara
kuu ya ujasusi ya Marekani C.I.A (Central
Inteligence Agency) walijificha nyuma ya miti na
kuanza kazi yao mara moja.Bunduki kubwa za
kisasa maalum kwa kudungua zilikuwa kazini.
Mara walipoanza kufanya kazi yao ,wakitumia lenzi
zilizofungwa katika bunduki hizi ili waone kama
watawaona adui hawa ndipo walipopata
changamoto kubwa sana. Kutokana na msitu huu
kuwa na miti iliyoshonana sana,haikuwa rahisi
kuweza kumuona mtu aliye ndani ya msitu huu.
Miti hii ilifanya kuwe na giza ndani ya misitu hii.
itaendelea.....
Wakati huu ambapo wadunguaji walikuwa
wakijaribu kila namna ili wafanikishe kuwaona na
kuwapiga adui zao,ghafla ilisikika sauti ya helkopta
mahali hapo. Risasi kutoka helkopta mbili ambazo
zilitokea kusikojulikana zilianza kushambulia
msafara wa magari hayo.Hapo magari ya
kusafirisha pesa yakafunguliwa milango kisha
askari kadhaa waliovalia gwanda nyeusi,kofia
ngumu pamoja na fulana nzito maalum kwa kuzuia
risasi , walitoka kutoka ndani ya magari haya.Hawa
walikuwa ni askari wa weledi kutoka katika kikosi
maalum cha United States Marine Corps Forces
Special Operations Command(MARSOC ).Askari
hawa walianza kuzishambulia helkopta zile kwa
kutumia bunduki zao za kisasa kabisa aina ya HK
MP7.Lakini hawakufua dafu japo walitumia bunduki
za kisasa sana ambazo hutumiwa na Kikosi
maalum kingine maarufu sana cha makomando
kutoka katika taifa lao kijulikanacho kama Navy
Seal DEVGRU. Pengine ni kwa sababu katika
mapambano ni rahisi sana kwa aliye juu
kumuangamiza aliye chini kuliko aliye chini
kumuangamiza aliye juu. Adui waliokuwa katika
helkopta waliendelea kumwaga risasi nzito nzito
kama njugu bila kuwapa upenyo askari hawa
maalum kulenga shabaha.Vikosi vyote yaani askari
wa kitanzania na wale wa Marekani waliendelea
kupambana lakini kazi ilikuwa bado ni nzito sana.
Wakati mapambano makali yakiendelea , helkopta
nyingine ya tatu ikatokea upande wa mashariki.Hii
ilikuwa ya tofauti na hizi helkopta nyingine kiumbo
na ilikuja kwa lengo tofauti kabisa.
Helkopta hii ilikuwaimetundikwa ndoano kubwa
sana ambayo ilichomekwa minyororo minene na
imara sana minne.Minyororo hii kwa pamoja
iliunganishiwa sumaku kubwa sana iliyokuwa na
umbo la mche mraba iliyokuwa kama mita mbili za
mraba kila upande.Helkopta hii ilienda hadi juu ya
gari mojawapo kati ya yale magari yanayotumika
kusafirisha pesa, kisha ikagusisha lile sumaku juu
ya paa la bodi la gari hilo kisha ikaanza kupaa
tena.Kadri helikopta ile ilivyopaa ndivyo gari lile
lilivyoanza kunyanyuliwa polepole.Mwisho gari
lilinyanyuliwa juu zaidi na zaidi kisha kutokomea
angani.
Wakati huu ndipo adui wengine walijitokeza
kutokea porini na kuanza kushambulia.Map
ambano yakawa makali zaidi na kufanya eneo lote
kuwa kama eneo la vita kwa kelele za risasi.Askari
wa weledi wa idara ya C.T.I na wenzao wa kikosi
cha MARSOC waliendelea kupambana na adui
hawa waliokuwa wengi sana na waliopigana kwa
ari ya juu sana.Hata adui waliouawa kwa wingi
bado waliendelea kupambana kwa ari ya juu sana
kitu kilichosababisha vita kuwa ngumu zaidi na
zaidi. Kiongozi wa kikosi cha askari hawa wa
weledi wa kitanzania Kapteni Joshua na yule wa
kikosi cha Marekani cha MARSOC kamanda Lucas
Bradock waliongoza vyema vikosi vyao na
kuonesha uwezo wa hali ya juu kimapambano
.Lakini kutokana na ari na uwingi wa adui, vikosi
hivi vilianza kuzidiwa nguvu.
"We are out numbered,sergent John request for
backup". Kamanda wa kikosi cha MARSOC alitoa
maelekezo kwa askari wake kwamba afanye
mawasiliano kuomba usaidizi. "Okey Cover
me".Alijibu sajenti John akitaka kulindwa wakati
akifanya mawasiliano. Kwa kutumia kifaa maalum
cha mawasiliano alichokivaa katika sikio lake la
kushoto na kuanza kuwasiliana na makao makuu
ya muda kuomba usaidizi. Makao makuu haya ya
muda yaliweka kambi ndani. Huku makao makuu
helkopta tatu za kisasa ziendazo kasi aina ya
'Chinook' zilikuwa ziko tayari na makomando tisa
kutoka vikosi vya Navy SeAL Marekani pamoja na
makomando kutoka JWTZ Tanzania. Kikosi hiki
cha Navy Seal kilikuwepo Tanzania tangu miezi
mitatu iliyopita kwa ajili ya kufanya mazoezi ya
pamoja na vikosi vya makomando vya JWTZ ili
kuwaongezea uzoefu makomando hawa wa
Tanzania.
Kikosi hiki kilichojumuisha watanzania na
wamarekani kilikuwa tayari kutoa usaidizi tangu
walipopata taarifa za kiintelijensia kuwa msafara
ule umevamiwa.Walikuwa wanasubiri amri ya
kwenda kutoa usaidizi tu.Mara tu walipopata
mawasiliano, makomando hawa (Navy Seal na
JWTZ) walipaa na helkopta zao muda huo huo.
Uwanja wa mapambano kulikuwa na kelele za
risasi kutoka katika bunduki za wanausalama na
adui.Majibizano ya risasi yaliendelea huku idadi za
majeruhi na maiti zikiendelea kuongezeka kila
upande.Upande wa kikosi cha ' MARSOC' tayari
askari wawili walipoteza maisha na wanne
kujeruhiwa huku Tanzania ikipoteza askari wa
weledi wanne na mmoja kujeruhiwa. Upande wa
adui, walipoteza askari wengi zaidi kwa idadi
isiyojulikana. "Cease fire and take cover". Amri
nyingine ilisikika kutoka kwa kiongozi wa kikosi
cha 'MARSOC' na ambaye ndiye alikuwa mkuu wa
msafara huu kamanda Bradock.Amri hiibiliwataka
askari wote kuacha kupambana bali
wajifiche.Wakati huu ndipo kundi kubwa la adui
likajitokeza kutokea msituni na kuanza
kuyasogelea magari ya wanauslama wale kutoka
pande zote.Sura zao zilionesha kuwa ni watu walio
na asili ya somalia. Wengi kati yao walionekana
kuwa wachafu sana na wengine wadhoofu wa miili.
Lakini ni hawahawa walionekana kuvipa shida
vikosi hivi kwa muda wa saa moja na dakika
thelathini sasa.
Adui walizidi kuyasogelea magari ambayo
yaliwaficha wanausalama wale ndani yake.
Walionekana kuwa na uchu kama fisi mwenye njaa
aliyeona mzoga mahali.Sasa walizidi kusogelea
magari yale huku wakipiga kelele na kunyoosha
bunduki zao mbele.Wakiwa karibu sana na magari
yale,walisikia kelele za helkopta zaidi ya
moja.Kadri sekunde zilivyosogea ,mvumo ule wa
helkopta uliongezeka kuonesha kuwa pengine
helkopta ilikuwa inaelekea upande ule waliokuwapo
wao. Mara wakaanza kuziona helkopta zile
zikiwaelekea na wakati huo huo risasi zikaanza
kurushwa kuwaelekea adui wale . Adui walianza
kuanguka mmoja baada ya mwingine kwa kasi
kubwa.Vikosi vya uokozi vilikuwa vimefika tayari.
Bunduki aina ya FN Minimi 7.62 zilizofungwa
katika helcopter zilifanya kazi yake ipasavyo.
Makomandoo walioshuka kwa miamvuli mita
chache kabla ya kufika uwanja wa mapambano,
nao wakaanzisha mashambulizi ya ardhini na
kufanya adui kuzidiwa nguvu. Vikosi vya usalama
vilivyojificha ndani ya magari navyo vikaendeleza
mashambulizi kama mwanzo.Maadui wakaanza
kuzidiwa nguvu na kuamua kukimbilia msituni
huku wakibeba maiti za wenzao.
Hadi kufika saa kumi na mbili jioni,hakukuwa na
mapambano tena wala sauti ya risasi. Eneo
palipotokea mapambano , lilizungushiwa utepe
maalum na jeshi la polisi ili mtu yeyote asipite na
kuharibu upelelezi. Kisha askari kadhaa wakaletwa
kulilinda eneo hilo.
*********************************************
****************************************************
Mtaalamu wa teknolojia ya kompyuta ambaye pia
alikuwa mtaalamu wa kuvunjavunja ' password'
bwana Abdallah Yusoof,alifanya kila jitihada
kuhakikisha anafungua loki iliyofunga mlango wa
nyuma wa gari lile. Ni lile gari lililobebwa na
helkopta kule katika uwanja wa mapambano.
Alikwisha wahi kufungua loki nyingi sana lakini hii
ya leo ilihitaji umakini wa hali ya juu zaidi. Loki hii
ilitengenezwa kwa mfumo maalum ambapo
mfunguaji alipewa nafasi mbili za kuifungua.
Kukosea mara ya kwanza kungempa mfunguaji
nafasi ya pili.Kukosea mara ya pili kungesababisha
mlipuko kama wa bomu ambao ungeteketeza gari
pamoja na watu ambao wapo karibu na gari.
Abdallah au kama alivyozoeleka kwa ubini wake
Yusoof,alichukua waya fulani wa 'USB'
akauchomeka katika simu yake iliyokuwa na
programu maalum kisha upande wa pili wa waya
huo akauchomeka mahala fulani pembeni ya
kidubwasha kilichobeba vitufe vilivyo na namba
sifuri hadi tisa.Kidubwasha hiki kilifanana na mita
za umeme wa LUKU za TANESCO. Mara
alipochomeka waya huo, namba fulani zilionekana
zikipita na kubadilika kwa kasi katika kioo cha
simu yake kisha zikajitokeza tarakimu sita. Yusoof
akazibonyeza tarakimu zile katika kidubwasha
kile.Ukasikika mlio 'krack'. Loki ilikuwa
imefunguka.
Yusoof akafungua milango ya gari lile ,ndani ya
gari lile akaonekana mtu mwenye ndevu nyingi na
ndefu sana huku akiwa na upara wa haja. Mtu huyu
alikuwa amesheheni pingu madhubuti sana
zilizofungwa mikononi na miguuni. Yusoof
alizitawanyisha pingu hizi kwa risasi kutoka katika
bastola yake.Yule bwana akashuka kutoka katika
gari.
Naam.Labda ni kimo cha gari like kilichomfanya
atoke akiwa kainama kilichangia kumfanya
aonekane kuwa mtu wa kimo cha kawaida
tu.Aliposhuka kutoka katika gari lile alionekana
sasa kuwa mtu mwenye tambo kubwa na mrefu
sana. Japo alikuwa katika vazi kubwa la asili kama
yale yanayovaliwa na 'Wanigeria', lakini haikusaidia
kuficha kuonekana kwa misuli mikubwa
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment