Search This Blog

Monday, 27 March 2023

KIZUNGUMKUTI ! - 2

  


Simulizi : Kizungumkuti !

Sehemu Ya Pili (2)



Yusuf aliinuka bila kupinga, akaanza kumfuata Jacky nyuma kama vile mbwa aliyemuona chatu.


“Umekuja na gari?” Jacky alimuuliza Yusuf mara tu walipofika chini.


“Hapana, nimekuja kwa miguu maana sikai mbali na hapa,” Yusuf alijibu lakini akasita baada ya kumuona Jacky akimfungulia mlango wa abiria wa gari la kifahari aina ya Toyota Landcruiser GX V8 jeusi. Akataka kuuliza lakini akasita na kuingia kimya kimya.


Endelea...


Jacky aliliondoa lile gari kutoka pale La Promise hadi kwenye jengo la ofisi za kampuni ya visimbuzi ya StarTimes akakata kushoto na kuingia katika barabara ya Uhuru akiungana na magari yaliyokuwa yakitokea Buguruni.


Hapo alipunguza mwendo kutokana na msongamano wa magari katika barabara ile finyu, akaendesha hadi walipofika katika eneo la Bungoni akakata na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara iliyokuwa na magari machache, hasa daladala akijaribu kuikwepa foleni ndefu ya magari katika barabara ile ya Uhuru.


Aliongeza mwendo na baada ya kitambo fulani cha safari walijikuta wamefika kwenye majengo ya wafanyabiashara wadogo, maarufu kama Machinga Complex.


Hapo alikata tena na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara ya Kawawa hadi alipokwenda kuungana na barabara ya Nyerere katika eneo la Veta. Kisha alikata kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara ile ya Nyerere.


Muda wote Yusuf alikuwa ametulia kimya akimtazama Jacky kwa jicho la wizi huku akiwa hajui wanaelekea wapi.


Baada ya kuendesha gari kwa umakini wakipita barabara hii na ile hatimaye walitokea katika eneo la Posta na kuifuata barabara ya Garden, kisha Jacky alikwenda hadi kwenye hoteli ya Southern Sun iliyopo katika eneo tulivu zaidi.


Aliliegesha gari lake katika viunga vya maegesho ya magari vya jengo la hoteli ile yenye hadhi ya nyota nne ambayo ilikuwa imejengwa katikati kabisa ya jiji la Dar es Salaam.


Mahali ilipokuwepo ile hoteli ilikuwa ni mwendo wa dakika 6 tu kwa kutembea kutoka kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi na ilikuwa jirani na hospitali ya rufaa ya wagonjwa wa saratani ya Ocean Road.


Jacky aliichagua hoteli ile kwa kuwa ilikuwa katika eneo tulivu mno lisilo na bughudha ikiwa jirani na ofisi mbalimbali za kibalozi katika jiji la Dar es Salaam, ilikuwa na eneo maalumu la mazoezi [gym], bwawa la kuogelea na kituo cha biashara.


Eneo la mbele la maegesho ya magari ya ile hoteli ambalo lilikuwa ng’ambo ya pili ya barabara lilipandwa miti mizuri aina ya coconut palms pamoja na miti mingine mirefu ya kivuli.


Pia kulikuwa na bustani nzuri ya maua ndani ya uzio wa ile hoteli na taa hafifu za ardhini zilizokuwa zikimulika eneo lile na hivyo kulifanya eneo lote lipendeze zaidi.


Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kugeuza shingo yake kumtazama Yusuf ambaye muda wote alikuwa kimya, aliachia tabasamu pana huku akifungua mlango wa gari na kushuka.


“Tumefika,” Jacky alimwambia Yusuf baada ya kumuona akiwa bado ameketi kwa utulivu akiwa anashangaa.


Yusuf alishuka haraka kutoka kwenye lile gari, wakaanza kukatisha kwenye viunga vile vya maegesho ya magari taratibu na kuelekea mbele ya lile jengo, sehemu kulipokuwa na mlango mkubwa wa kioo na varanda pana yenye ngazi iliyofunikwa kwa kofia nzuri ya zege.


Walipoingia ndani walipokelewa kwa bashasha zote na wahudumu wa ile hoteli ambao sura zao zilikuwa zimepambwa na tabasamu la kirafiki muda wote.


Walipita moja kwa moja wakiuvuka ule ukumbi wa mapokezi na kuelekea upande wa kushoto wakashuka ngazi chache chini wakiuvuka mgahawa wa Baraza Grill ambao ulikuwa kwa ajili ya chakula cha kitanzania na cha kimataifa.


Ule ulikuwa ukumbi mkubwa kiasi wenye meza nyingi za kulia chakula zenye umbo mstatili zilizozungukwa kwa viti nadhifu vyenye foronya laini.


Meza zile zilikuwa zikimefunikwa kwa vitambaa visafi vya rangi nyeupe na juu yake kuliwekwa kadi ngumu za kupendeza zenye orodha ya vyakula na vinywaji vinavyopatika katika hoteli ile.


Pia kulikuwa na karatasi laini nyeupe za tishu za kufutia mikono na vifaa vyote muhimu vya kujipatia maakuli kama uma, visu na vijiko, na bila kusahau vikasha wiwili vidogo; kimoja cha kuwekea chumvi ya mezani na kingine cha vijiti vya kuchokolea meno.


Pembeni ya meza zile kulikuwa na makochi mazuri ya sofa yaliyopangwa kuzizunguka meza fupi za vioo katika mpangilio mmoja uliovutia. Pia mwisho wa ukumbi ule kulikuwa na kaunta kubwa ya vinywaji.


Madirisha makubwa ya vioo ya ukumbi ule yalikuwa yamefunikwa kwa mapazia marefu yenye rangi nzuri za kupendeza. Ukutani kulikuwa na runinga pana za bapa maarufu kama ‘flat screen’ zilizokuwa zikiendelea kurusha vipindi mbalimbali vya burudani.


Katika ule ukumbi kulikuwa na watu wachache waliokuwa wameketi wakijipatia mlo na vinywaji huku wakiendelea na maongezi yao.


Ukumbi haukuwa mkubwa na ulikuwa umetenganishwa na ile sehemu ya mapokezi kwa ukuta mdogo uliokuwa unamruhusu mtu yeyote kuweza kuona mle ndani bila usumbufu wowote.


Walipovuka eneo lile walitokea upande wa nyuma wa lile jengo kulikokuwa na mgahawa mwingine wa Kivulini ambako mara nyingi palitumika kwa ajili ya chakula cha kimataifa na ulikuwa unatazama eneo kubwa lenye bustani nzuri yenye miti mbalimbali na swimming pool.


Katika mgahawa ule wa Kivulini kulikuwa na watu wachache, Wazungu kwa Waafrika waliokuwa wakiendelea na maongezi yao ya hapa na pale katika viti vizuri na meza fupi za mbao.


Watu wale walikuwa wakijipatia vinywaji, wengine wakiwa katika maongezi ya kibiashara huku wakivuta sigara na kutazama mechi ya mpira wa miguu ya ligi ya Ulaya kati ya Manchester United na Juventus iliyokuwa ikioneshwa ‘mbashara’ kwenye runinga kubwa iliyotundikwa ukutani.


Wakati wakitafuta eneo tulivu la kuketi mara mhudumu mmoja wa kike wa baa ile aliyevalia nadhifu aliwaona na kuwafuata akiwa tayari kuwahudumia. Alipowafikia aliwasalimia kwa adabu kubwa na kwa bashasha zote.


Kabla yule mhudumu hajauliza Jacky alimnong’oneza jambo na kumfanya yule mhudumu amtupie jicho Yusuf na kuachia tabasamu. Hata hivyo, Yusuf aliyaona yote yaliyokuwa yakiendelea pale lakini alijifanya kama hajaona na kubaki mtulivu.



Wakati wakitafuta eneo tulivu la kuketi mara mhudumu mmoja wa kike wa baa ile aliyevalia nadhifu aliwaona na kuwafuata akiwa tayari kuwahudumia. Alipowafikia aliwasalimia kwa adabu kubwa na kwa bashasha zote.


Kabla yule mhudumu hajauliza Jacky alimnong’oneza jambo na kumfanya yule mhudumu amtupie jicho Yusuf na kuachia tabasamu. Hata hivyo, Yusuf aliyaona yote yaliyokuwa yakiendelea pale lakini alijifanya kama hajaona na kubaki mtulivu.


Endelea...


Kisha yule mwanadada aliwachukua Jacky na Yusuf hadi sehemu ya mapokezi ambako aliwakabidhiwa kwa mwanadada mwingine, ambaye alivuta droo na kuchukua kadi maalumu ya kielektroniki iliyotumika kufungua mlango wa chumba.


Kisha alimuashiria Jacky kwa mkono kuwa wamfuate, alitangulia akawaongoza kuelekea sehemu kulipokuwa na lifti ya lile jengo la hoteli ya kuelekea juu, walitembea taratibu wakiliacha lile eneo la mapokezi na kushika uelekeo wa upande wa kulia hadi kwenye mlango wa lifti za lile jengo.


Walipofika pale yule dada mhudumu alibonyeza kitufe fulani ukutani na mlango wa ile lifti ukafunguka kisha wakaingia ndani ya kile chumba cha lifti, na alipohakikisha wote wameingi yule mhudumu alibonyeza kitufe ukutani akiiamuru ile lifti iwafikishe kwenye ghorofa ya tano ya lile jengo.


Mlango ulipojifunga ile lifti ilianza kupanda juu hadi ilipofika katika ghorofa ya tano ya lile jengo, ikagota na mlango wa kile chumba cha lifti ukafunguka kuwaruhusu waliomo ndani watoke nje.


Yule mhudumu alitangulia kutoka, Jacky na Yusuf wakamfuata, walijikuta wametokezea kwenye korido pana iliyomezwa na utulivu wa aina yake. Korido ile ilikuwa ikipakana na milango kadhaa ya vyumba kwa upande wa kushoto na kulia.


Katikati ya ile korido kulikuwa na kitufe kikubwa chekundu cha kengele ya hatari pembeni ya mtungi mkubwa wa gesi ya kuzimia moto wa dharura.


Kwenye dari ya korido ile kulikuwa na taa ndefu za tubelight za mtindo wa kupendeza zilizokuwa zikiangaza mwanga wa wastani na hivyo kuyafanya mandhari ya ile korido yawe tulivu na ya kupendeza.


Katika korido yote kulikuwa na hewa safi iliyokuwa ikisambazwa taratibu na viyoyozi viwili, kimoja kikiwa mwanzo wa ile korido na kingine mwisho wa korido. Sakafu ya korido ile ilikuwa na tarazo maridadi zilizokuwa na nakshi za kupendeza na hapakuwa na kitu kingine cha ziada zaidi ya utulivu mkubwa.


Jacky na Yusuf walitembea taratibu katikati ya ile korido wakimfuata yule dada mhudumu aliyekuwa ametangulia mbele, waliipita milango kadhaa mikubwa na imara ya mbao ngumu iliyokuwa ikitazamana na ile korido, ambayo juu yake kulikuwa na vibao vidogo vya rangi nyeusi vilivyokuwa na utambulisho wa namba ya chumba husika.


Wakati wakipita Yusuf alikuwa akiyatembeza macho yake upande huu na ule kusoma namba zilizokuwa juu ya milango ya vyumba vilivyokuwa vikitazamana na ile korido.


Yule dada mhudumu aliwaongoza hadi kwenye mlango wa mwisho kabisa ambao pia ulikuwa mlango mkubwa na imara wa mbao ngumu. Yule mhudumu aliichukua ile kadi ya kielektroniki na kuipitisha juu ya kile kitasa cha mlango kisha akakishika na kukinyonga, ule mlango ukafunguka na hapo akausukuma taratibu na kuingia mle ndani.


Jacky na Yusuf walimfuata taratibu na kuingia ndani ya kile chumba, wakajikuta wametokea kwenye chumba kikubwa sana cha kisasa. Yusuf alisimama katikati ya kile chumba akikitazama kwa namna ya kukitathmini vizuri mandhari yake.


Kilikuwa chumba kikubwa sana chenye nafasi ya kutosha. Upande wa kushoto kulikuwa na kitanda kikubwa cha mbao chenye godoro la foronya laini lililokuwa limefunikwa kwa shuka safi za rangi ya pinki.


Kando ya kile kitanda kulikuwa na mlango wa kuelekea kwenye chumba cha maliwato.


Kulikuwa na makochi mawili ya sofa nyuma ya meza ndogo fupi ya mbao yenye kibakuli kidogo cha majivu ya sigara juu yake na pembeni yake kulikuwa na kabati zuri la nguo la ukutani lililokuwa pembeni ya dirisha kubwa la kile chumba. Lile dirisha lilifunikwa kwa mapazia marefu na mepesi yaliyoruhusu hewa safi kupenya mle ndani.


Makochi yale yalikuwa yakitazamana na seti moja kubwa ya runinga pana aina ya Sumsung iliyokuwa imefungwa vizuri ukutani na kuunganishwa na king’amuzi cha kilichokuwa na chaneli nyingi za kimataifa.


Chini ya ile runinga kulikuwa na meza ndogo ambayo juu yake ilikuwa na simu ya mezani. Pembeni ya simu ile kulikuwa na kitabu kikubwa cha rangi ya njano chenye orodha ya majina na namba za simu za watu na kampuni mbalimbali.


Pia ndani ya kile chumba kulikuwa na jokofu dogo lililokuwa limesheheni vinywaji mbalimbali ndani yake.


Yule mhudumu aliziendea swichi zilizokuwa ukutani na kubonyeza swichi moja ili kuwasha kiyoyozi kilichokuwa sehemu fulani kwenye kona ya kile chumba, na hapo hewa safi ya ubaridi ilianza kusambaa mle ndani.


Jacky aligeuka akamtazama Yusuf kwa namna iliyomweleza kuwa walikuwa wamefika sehemu tulivu kama alivyomuahidi, huku akiutupia mkoba wake kitandani.


“Welcome to Southern Sun, here is a quiet place and nice to enjoy. Have you ever been here before?” (Karibu Souther Sun, hii ni sehemu tulivu na nzuri ya kufurahia. Sijui umeshawahi kuja hapa kabla?) Jacky alimuuliza Yusuf huku akimtazama kwa madaha.


“Nope, I've never come here even once. It's my first time today. It’s a nice place,” (Wala, sijawahi kufika hapa hata mara moja. Ni mara yangu ya kwanza leo kufika hapa. Ni sehemu nzuri) Yusuf alisema huku akizungusha macho yake kuyashangaa mandhari ya kile chumba.


“Unapaonaje hapa, pako poa au siyo?” Jacky alimuuliza Yusuf ambaye muda wote alikuwa amesimama akiwa anayashangaa mandhari ya kile chumba.


Yusuf aliitikia kwa kubetua kichwa huku macho yake yakizidi kuvinjali ndani ya kile chumba. Jacky alijitupia kitandani huku akimtazama Yusuf kwa tabasamu.


“Hivi chumba kama hiki kwa siku ni bei gani?” hatimaye Yusuf aliuliza huku akishindwa kuficha mshangao wake.


“Kwa nyinyi wenzetu mnaochezea fedha kila siku wala si ghali sana. Ni shilingi laki tatu na elfu hamsini tu kwa usiku mmoja, unapata bia mbili bure na chai ya asubuhi. Unaonaje?” Jacky alisema huku akiachia kicheko hafifu.


Yusuf alitaka kusema neno lakini akasita na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku akitingisha kichwa chake taratibu na kumtupia jicho yule mhudumu wa ile hoteli, ambaye muda wote alikuwa amesimama akiwatazama kwa zamu huku akitabasamu.


Jacky aligundua kuhusu hilo na kubetua mabega yake juu huku akiendelea kutabasamu.




“Kwa nyinyi wenzetu mnaochezea fedha kila siku wala si ghali sana. Ni shilingi laki tatu na elfu hamsini tu kwa usiku mmoja, unapata bia mbili bure na chai ya asubuhi. Unaonaje?” Jacky alisema huku akiachia kicheko hafifu.


Yusuf alitaka kusema neno lakini akasita na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku akitingisha kichwa chake taratibu na kumtupia jicho yule mhudumu wa ile hoteli, ambaye muda wote alikuwa amesimama akiwatazama kwa zamu huku akitabasamu.


Jacky aligundua kuhusu hilo na kubetua mabega yake juu huku akiendelea kutabasamu.


Endelea...


“Anyway, what will you drink?” (Hata hivyo, sijui utakunywa nini?) Jacky alimuuliza Yusuf akiwa bado amemkazia macho.


“Castle baridi itapendeza,” Yusuf alijibu huku akiketi juu ya kochi mojawapo la sofa.


“Tuletee chupa mbili za castle baridi na chupa kubwa ya whisky,” Jacky alimwambia yule mhudumu aliyekuwa bado amesimama kimya akingoja kupewa oda.


“Vinywaji hivyo vyote vimo ndani ya hilo jokofu, labda kama mnahitaji huduma nyingine kama chakula,” alisema yule mhudumu huku akielekeza kidole chake kwenye lile jokofu dogo.


“Okay, basi tukihitaji chochote nitakupigia simu,” alisema Jacky huku akiachia tabasamu kisha akainuka na kwenda kufungua lile jokofu akatoa chupa mbili za Castle, bilauri mbili na chupa kubwa ya whisky.


Yule mhudumu aliachia tabasamu pana la kirafiki na kuondoka, Yusuf alimtazama Jacky kwa makini na kushusha pumzi zaa ndani kwa ndani. “Niliona nibahatishe kukupigia simu ingalau nisikie sauti yako,” alivunja ukimya.


“Yaani ulitaka usikie sauti tu, basi!” Jacky aliuliza huku akiangua kicheko hafifu kisha akaviweka vile vinywaji juu ya ile meza ndogo fupi ya mbao. Yusuf alitabasamu tu bila kujibu kisha akainamisha kichwa chake akionekana kufikiria mbali, huku akionekana kumtupia jicho la wizi Jacky kwa matamanio.


“Haya sauti yangu tayari umeshaisikia na mimi mwenyewe ndiyo niko hapa hapa mbele yako, tena tukiwa peke yetu, unasemaje?” Jacky alisema na kuangua tena kicheko hafifu.


“Kwani ninalo tena!” lilikuwa jibu fupi la Yusuf lililomaanisha kuwa alikuwa amesalimu amri huku akiinamisha sura yake kutazama chini kwa aibu.


Hata hivyo, Yusuf alikuwa akihisi joto kali la mwili lililosababisha kijasho jembamba kianze kumtoka licha ya kuwa mle ndani kulikuwa na kiyoyozi kilichokuwa kikitoa ubaridi mkali. Alianza kuhisi mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!


Aliilamba midomo yake iliyoanza kukauka huku akianza kuhisi pumzi zake zikimpaa na kuanza kuhema kwa nguvu kama mtu aliyekosa hewa safi ya oksijeni, alifungua vifungo vya shati lake na kubaki kifua wazi. Muda wote huo Jacky alikuwa akimtazama kwa makini kisha akaachia tabasamu.


“Kama unahisi jasho livue kabisa halafu njoo uketi hapa kitandani,” Jacky alimwambia Yusuf huku akimuonesha kwa mkono sehemu ya kukaa karibu yake.


Yusuf hakupinga alilivua lile shati na kulitupia juu ya kochi jingine la sofa kisha akainuka na kwenda kuketi pale kitandani sehemu aliyooneshwa na Jacky.


Jacky alifungua zile chupa za bia, akamimina pombe kwenye bilauri zote mbili, kisha bilauri moja alimpa Yusuf na nyingine aliishika mkononi. Akanyoosha mkono wake kumwelekea Yusuf, wakagongesha zile bilauri.


“Cheers!” walisema kwa pamoja wakitakiana heri na kuangua kicheko hafifu.


Yusuf aliinua ile bilauri akapiga funda moja kubwa la bia na kusisimkwa mwili wake. Alipoishusha ile bilauri alimtazama Jacky kwa tabasamu.


“Hivi una muda gani wa kazi pale benki?” Jacky alimuuliza Yusuf huku akipiga funda la bia na kuiweka ile bilauri juu ya meza.


“Nina miaka minne,” Yusuf alisema huku akiinua tena bilauri ya bia. Jacky alimtazama kwa makini kwa kitambo kifupi kisha akaitazama pete ya harusi iliyokuwa kidoleni kwake na kuachia tabasamu.


“Are you married? I can see you have a wedding ring,” (Umeoa? Naona una pete ya harusi) Jacky alisema huku akiangua kicheko hafifu.


“To be honest… I have a wife and a kid. Kwani vipi?” (Kusema kweli… nina mke na mtoto) aliuliza Yusuf huku akimkazia macho Jacky.


“Aah, napenda tu kujua nipo na mwanamume wa aina gani, mbona wewe kwenye simu uliniuliza kama nimeolewa!” Jacky alijibu kwa madaha huku akijipinda kumtazama Yusuf kwa mahaba. Walibaki wametazamana kwa kitambo fulani na kujikuta wote wakiachia tabasamu lililozaa kicheko.


“Hivi umepanga au unaishi katika nyumba yako?” Jacky aliuliza tena baada ya kile kicheko kukoma huku akimkazia macho Yusuf.


“Sijafanikiwa kujenga, pesa ngumu sana siku hizi, si unajua tena awamu hii ya hapa kazi tu jinsi inavyokaba kila kona…” Yusuf alisema na kuangua kicheko hafifu.


“Najua, ila kila kitu kinataka mipangilio. Je, una gari?” Jacky aliuliza tena lakini kabla Yusuf hajajibu, simu yake ya mkononi ilianza kuita.


Yusuf alishtuka na kuitazama kwa makini, akaonesha kusita kidogo huku akimtupia jicho Jacky. Hata hivyo Jacky alimuashiria kuwa aipokee tu, Yusuf aliichukua na kubofya kitufe cha kupokelea na akuiweka kwenye sikio.


“Eh mama Jasmine!” Yusuf alisema mara tu alipoiweka ile simu kwenye sikio.


“Uko wapi, baba Jasmine? Huku Jasmine ananisumbua sana!” sauti ya mke wake ilisikika ikilalamika kutoka upande wa pili wa simu.


“Kwani homa imemrudia tena?” Yusuf aliuliza kwa wasiwasi huku akimtupia jicho Jacky.


“Wala hana homa, ila hataki kulala mpaka akuone,” sauti ya mke wake ilisikika tena ikilalamika.


“Okay, nipo sehemu nina kikao kidogo na rafiki zangu, nitarudi mara tu nikishamaliza kikao, kama nusu saa hivi inayokuja,” Yusuf alisema na kukata simu kisha alimtupia jicho Jacky huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Is that your wife?” (Ni mkeo huyo?) Jacky alimuuliza Yusuf huku akionekana kutabasamu.


Yusuf alikubali kwa kubetua kichwa kisha akanyanyua bilauri yake ya bia na kuinywa bia yote iliyokuwemo kwenye ile bilauri huku akishusha pumzi ndefu. Jacky alimtazama kwa madaha na kummiminia bia nyingine.


“But you have not yet answered my question…” (Lakini bado hujajibu swali langu…) Jacky alimwambia Yusuf huku akimkazia macho.


“What question?” (Swali gani?) Yusuf aliuliza huku akimtazama Jacky kwa mshangao.


“I asked if you had a car.” (Niliuliza kama una gari).


“I do not have a car,” (Sina gari) Yusuf alisema huku akiweka msisitizo kwa kutingisha kichwa chake kukataa.


“Hata kagari kadogo dogo tu?” Jacky aliuliza tena huku akiachia tabasamu.



“But you have not yet answered my question…” (Lakini bado hujajibu swali langu…) Jacky alimwambia Yusuf huku akimkazia macho.


“What question?” (Swali gani?) Yusuf aliuliza huku akimtazama Jacky kwa mshangao.


“I asked if you had a car.” (Niliuliza kama una gari).


“I do not have a car,” (Sina gari) Yusuf alisema huku akiweka msisitizo kwa kutingisha kichwa chake kukataa.


“Hata kagari kadogo dogo tu?” Jacky aliuliza tena huku akiachia tabasamu.


Endelea...


“Kwani hako kadogo dogo kanapatikana bure? Napenda kujenga, napenda kumiliki gari… tena Mercedes Benz au hata Toyota Landcruiser GX V8 kama lako, lakini tatizo ni fedha,” Yusuf alisema kwa huzuni.


“Si utani tatizo ni fedha, lakini nyie watu wa benki fedha kwenu siyo tatizo kabisa,” Jacky alichombeza huku akiachia kicheko hafifu.


“Aah wapi, kakwambia nani?” Yusuf alisema huku akimwangalia Jacky kwa mshangao na kukunja sura yake, kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Kila siku si mnachezea fedha? Mnahesabu mamilioni kwa mamilioni ya fedha, sema tu nyie wenyewe mmezubaa!” Jacky alizidi kumchombeza Yusuf huku akiachia kicheko hafifu.


Yusuf ambaye muda ule alikuwa ameshika bilauri ya bia akitaka kunywa alionekana kusita kidogo na kumtazama Jacky kwa mshangao.


“Tumezubaa, ki vipi?” Yusuf alimuuliza Jacky huku akiendelea kumtazama kwa mshangao kana kwamba alikuwa ameambiwa habari ya kushangaza sana ambayo hajawahi kuisikia kabisa maishani mwake.


“We mwenyewe si unaona? Mwaka wa nne uko benki unawahesabia watu fedha zao… mamilioni kwa mabilioni lakini wewe unapata nini? Pengine mshahara wako haufiki hata shilingi milioni moja kwa mwezi…” Jacky alisema kwa uchungu huku akibetua midomo yake na kunyanyua juu mabega yake.


“Imagine, less than one million shillings per month is the salary for a guy like you? When will you build your child's future? And when will you own your own car or build a house?” (Hebu fikiria chini ya shilingi milioni moja kwa mwezi ni mshahara wa kulipwa kijana kama wewe? Utajenga lini maisha ya baadaye ya mwanao? Na utamiliki lini gari yako mwenyewe au kujenga nyumba?) Jacky alisema huku akishika tama.


Yusuf alimtazama Jacky kana kwamba alikuwa kiumbe wa ajabu kutoka sayari ya mbali, alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akijaribu kuyachuja yale maneno ya Jacky.


“Ukweli ni kwamba, chini ya shilingi milioni moja kwa mwezi si mshahara, mpenzi wangu, it's only an allowance. Tena posho yenyewe shombo tupu! Amka Yusuf, muda unapita,” Jacky alisema huku akijiegemeza kwenye kifua cha Yusuf.


Yusuf aliinamisha uso wake kwa kitambo kirefu akionekana kuguswa sana na yale maneno ya Jacky, aliwaza sana na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani. Alipoinua uso wake kumtazama Jacky kwa makini alihisi machozi kumlenga lenga. Akanyanyua bilauri yake ya bia na kuinywa bia yote iliyokuwemo.


“Hebu niwekee whisky naona bia haipandi,” Yusuf alisema huku akimpa Jacky ile bilauri. Jacky aliichukua ile bilauri na kuiweka juu ya ile meza.


Kisha akaifungua ile chupa ya whisky kisha akaijaza pombe bilauri ya Yusuf kwa whisky na kuishika ile bilauri, akaipeleka kwenye mdomo wa Yusuf kutaka kumnywesha kwa mahaba lakini Yusuf alimnyang’anya na kuishika mwenyewe, akaigida pombe yote kama maji kisha akaikita ile bilauri juu ya meza.


Jacky aliijaza tena pombe ile bilauri ya Yusuf na kumpa, Yusuf akaiangalia kwa makini kisha akayahamisha macho yake kumwangalia Jacky kwa uchungu na kufinya jicho moja.


“I love you so much, Belinda, where were you all this time?” (Nakupenda sana, Belinda, hivi ulikuwa wapi siku zote?) Yusuf alisema huku akizungusha mkono wake kumshika Jacky kiunoni bila ruhusa yake, hata hivyo hakukutana na upinzani wowote.


Jacky alimtazama Yusuf machoni kisha tabasamu maridhawa likachomoza usoni mwake na hatimaye aliachia kicheko hafifu.


“Do not laugh, Belinda, I'm not drunk yet, I’m fit… okay explain well to me about money matters,” (Usicheke Belinda, sijalewa bado, niko fiti… haya hebu nielezee vizuri kuhusu mambo ya fedha) Yusuf alisema kwa uchungu huku akionekana kuanza kulewa.


“Money matters, uh? It's like that. You really have to be awake,” (Mambo ya fedha, eh? Ndiyo kama hivyo. Inabidi uchangamke kweli kweli) Jacky aliongea kwa utulivu huku akijigeuza na kuipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Yusuf na hapo akasababisha chuchu za matiti yake kukitekenya kifua cha Yusuf.


Kitendo cha chuchu za Jacky kukitekenya kifua cha Yusuf kilimfanya Yusuf ajisikie faraja ya aina yake na alipomtazama Jacky machoni akaliona tabasamu pana likiwa limechanua usoni kwake.


“Well, I real need the money, ila huko kuchangamka ndiyo sijajua sawa sawa, nichangamke vipi?” aliuliza Yusuf huku akianza kuhema kwa nguvu kutokana na ashki iliyoanza kumpanda.


“Lakini kwanza kabla ya yote, ninataka unihakikishie kwamba ni kweli hauna uhusiano na mwanaume mwingine yeyote yule? Kama unaye naomba uniambie ukweli ili nijue kwamba ninaingia katika uhusiano na mtu ambaye ana mahusiano na mwanaume mwingine,” Yusuf alisema huku akianza kumpapasa Jacky mgongoni.


Jacky alijilegeza na kufumba macho yake huku akionekana kuhema kwa nguvu kisha akaupeleka mkono wake kwenye shavu la Yusuf na kumbusu huku akimtazama kwa makini.


“Why do you insist on that? Don’t you trust me when I told you that I’m not married?” (Kwa nini unasisitiza kutaka kufahamu jambo hilo? Kwani huamini nilipokwambia kwamba sijaolewa?) Jacky alimuuliza Yusuf huku mkono wake ukishuka hadi kifuani kwa Yusuf, akaanza kumpapasa chuchu zake.


“Because I need you so badly, Belinda. I want to spend more time with you,” (Kwa sababu nakuhitaji sana, Belinda. Nataka kuwa na wewe kwa muda mrefu) Yusuf alisema huku akionekana kuhema kwa nguvu kutokana na ashki.


“I’m all alone. That’s all I can say,” (Niko peke yangu. Hicho ndicho ninachoweza kusema) Jacky alisema huku akijilegeza kifuani kwa Yusuf.


“Thank you for reassuring me about that,” (Nashukuru kwa kunihakikishia kuhusu hilo) Yusuf alisema huku akimwangalia Jacky kwa matamanio.


Jacky aliachia tabasamu huku akizidi kujilegeza huku akimchezea Yusuf maeneo nyeti ambayo yalianza kufura kwa hasira kali. Yusuf akaanza kutoa mguno wa ashki kwa msisimko huku akimkumbatia Jacky kwa nguvu na kuanza kumpapasa maungoni kwa pupa.




“I’m all alone. That’s all I can say,” (Niko peke yangu. Hicho ndicho ninachoweza kusema) Jacky alisema huku akijilegeza kifuani kwa Yusuf.


“Thank you for reassuring me about that,” (Nashukuru kwa kunihakikishia kuhusu hilo) Yusuf alisema huku akimwangalia Jacky kwa matamanio.


Jacky aliachia tabasamu huku akizidi kujilegeza huku akimchezea Yusuf maeneo nyeti ambayo yanafura kwa hasira kali. Yusuf anaanza kutoa mguno wa ashki kwa msisimko huku akimkumbatia Jacky kwa nguvu na kuanza kumpapasa maungoni kwa pupa.


Endelea...


Kwa utundu Jacky aliipeleka ncha ya ulimi wake katika sikio la Yusuf na kumfanya azidi kutoa mguno kwa msisimko alioupata. Yusuf alishindwa kuvumilia na kumuinua Jacky kwa nguvu kisha alimtupa juu ya kitanda na kuanza kuvua suruali yake haraka na kuitupa kule.


“Oh c’mon Yusuf, not so fast my love, I’m ready to give you what you want, but we need to talk first,” (Oh subiri Yusuf, usiwe na haraka mpenzi wangu. Niko tayari kukupa unachohitaji, lakini tunahitaji kwanza kuongea) Jacky alisema huku akijiinua kutoka pale kitandani kisha akamvuta Yusuf na kumbusu huku akimpapasa sehemu mbalimbali za mwili wake akizidi kumtia wazimu wa mapenzi.


“Talk about what?” (Kuzungumze kuhusu nini?) Yusuf aliongea huku akihisi pumzi zinampaa.


“About money matters,” (Kuhusu mambo ya fedha) Jacky alisema na kumtulizia macho Yusuf. Yusuf alimkodolea macho Jacky pasipo kusema neno, alionesha wazi kuwa alikwishapandwa na mzuka wa mapenzi.


“Ni hivi, kama tukishirikiana tutafanikiwa. Kwa kweli hakuna asiyehitaji pesa. Walionazo wanataka kujilimbikizia, wasionazo wanataka wawe nazo… kikubwa hapa ni ushirikiano tu, fedha mbona zipo!” Jacky alisema kwa sauti tulivu huku akimkazia macho Yusuf.


“Zipo wapi?” aliuliza Yusuf kwa shauku huku akiketi juu ya kitanda.


“Zipo benki. Wewe unafikiri wapi penye fedha ya mkupuo?” Jacky aliendelea kusema kwa utulivu huku akiendelea kumkazia macho Yusuf.


“Fedha ya benki tutaipataje?” Yusuf aliuliza tena huku akimtazama Jacky kwa mshangao.


“Usinichekeshe Yusuf, mbona watu wanachukua pesa kiulaini kabisa tena kwenye benki za kimataifa, itakuwa hizi za hapa Bongo? Ni kwamba tukishirikiana wala haitapita wiki tutakuwa mamilionea,” Jacky alisema kwa sauti tulivu yenye msisitizo.


Yusuf alimtazama Jacky kwa kitambo kirefu bila kusema neno, kila alivyomtazama hakuona mzaha kwenye uso wa Jacky. Kikapita kimya cha kitambo kirefu wakiwa wanatazamana.


“Okay, nakusikiliza Belinda, hebu nielezee vizuri,” hatimaye Yusuf alisema na kuvunja ule ukimya ulioanza kutawala mle ndani.


Jacky aliachia tabasamu na kuanza kuishusha chini boksa ya Yusuf kisha akaivua kabisa na kutupa kule, baada ya hapo akaupeleka mkono wake katika ikulu ya Yusuf, akaanza kuzichezea malighafi zake, kitendo kile kilimfanya Yusuf aanze kutoa mguno kutokana na msisimko huku akihema ovyo.


Alimtazama Yusuf kwa makini na kujiinua kidogo akalipandisha juu gauni lake, taratibu akaanza kuishusha nguo yake ya ndani na kuiweka pembeni huku akirembua macho yake. Muda ule ule akamvuta Yusuf karibu yake na kummwagia mabusu mfululizo yaliyomchanganya.


Yusuf alionekana kuzidi kuchanganyikiwa huku akihisi pumzi zake zikimpaa na kuanza kuhema kwa nguvu kama mtu aliyekosa hewa safi ya oksijeni. Alijikuta akishindwa kabisa kuvumilia na hakuwa tena na ujasiri wa kupingana na hisia zake, muda huo alikwisha pandisha mori na kutaka kumwangusha Jacky kitandani lakini Jacky alimzuia tena.


“Ngoja kwanza…” Jacky alisema huku akijiinua na kusimama. Yusuf alimtazama kwa matamanio.


“Hebu nieleze ni akaunti gani pale kwenye tawi lenu yenye fedha nyingi?” Jacky alimuuliza Yusuf kwa sauti ya utulivu huku akirembua macho yake.


“Zipo kamaa… n…nne hivi!” Yusuf alijibu kwa kubabaika kidogo baada ya kufikiria.


“Nitajie mojawapo.”


“The Jacarandah Group,” Yusuf alijikuta akiongea bila hata kufikiri.


“Ooh, kumbe wanaweka pesa zao pale!” Jacky alionesha kushangaa kidogo.


“Ndiyo, kwani unawafahamu?”


“Sana, nasikia wana hela hao jamaa hakuna mfano, hao ndiyo wa kula nao sahani moja…” Jacky alisema huku na kumsogelea Yusuf, akamvutia kifuani kwake na kuzidi kuzitomasa malighafi zake kwa ufundi wa hali ya juu, kitendo kilichomfanya Yusuf aropoke kila alichoulizwa.


“Unakumbuka mfumo wao wa kuweka na kutoa pesa?” Jacky aliuliza kwa sauti ya kunong’ona.


“Wanaweka pesa zao kila Alhamisi, lakini hawana ratiba maalumu ya kutoa,” Yusuf alisema huku akimkodolea Jacky macho ya uchu kama fisi aliyeona mzoga.


Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani kisha akaachia tabasamu pana, “Unaweza kuniambia, ni kiasi gani cha pesa hutoa benki wanapoamua kutoa?”


“It’s between six million and one billion shillings, sometimes they withdraw up to two billions,” (Ni kati ya shilingi milioni mia sita hadi bilioni moja, wakati mwingine wanatoa hata bilioni mbili) Yusuf aliongea kwa sauti hafifu ya kirafiki.


“I see! Do they withraw such a huge amount of money?” (Kumbe wanatoa kiasi kikubwa vile cha pesa?) Jacky aliuliza huku akishindwa kuficha mshangao wake.


“Wale jamaa achana nao kabisa! Kuna tetesi kuwa hata yule tajiri mkubwa duniani, Bill Gate ana hisa kwenye kampuni hiyo, ndiyo maana huwa hakosi kuja Tanzania mara kwa mara,” alisisitiza Yusuf.


“Unadhani lini watatoa tena fedha?”


“Kati ya kesho ama keshokutwa.”


“Safi sana, sasa itabidi unitafutie saini za waidhinishaji wa fedha za kampuni hiyo,” Jacky alisema kwa sauti hafifu huku akiachia tabasamu lake maridhawa.


“Ki vipi?” Yusuf aliuliza kwa mshangao huku akimkodolea macho Jacky.


Hapo Jacky alijigeuza na kumkabili Yusuf, kisha aliipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Yusuf na kuanza kumbusu mfululizo.


“Usijali, sasa nenda kazime taa nikupe kwanza ile kitu roho inataka, mambo mengine nitakueleza vizuri baadaye,” Jacky alisema huku akilitoa gauni lake na kulitupa kando.


Yusuf aliinuka haraka na kwenda kuzima taa akionekana hakuwa tayari kucheleweshewa mambo kutokana na uchu wa ngono uliokuwa umemnasa vilivyo, huku macho yake yakiwa yamemwiva kwa ashki.


Mambo si mambo, Yusuf keshaingia




Na Bishop Hiluka


Hapo Jacky alijigeuza na kumkabili Yusuf, kisha aliipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Yusuf na kuanza kumbusu mfululizo.


“Usijali, sasa nenda kazime taa nikupe kwanza ile kitu roho inataka, mambo mengine nitakueleza vizuri baadaye,” Jacky alisema huku akilitoa gauni lake na kulitupa kando.


Yusuf aliinuka haraka na kwenda kuzima taa akionekana hakuwa tayari kucheleweshewa mambo kutokana na uchu wa ngono uliokuwa umemnasa vilivyo, huku macho yake yakiwa yamemwiva kwa ashki.


Endelea...


Ilionesha wazi kuwa alikuwa akiisubiri nafasi ile kwa muda mrefu. Alikuwa katika hali mbaya sana na hakuweza tena kuvumilia. Wakaingia mchezoni na muda mfupi uliofuata walikuwa kwenye dunia nyingine kabisa ya mapenzi yenye kila aina ya kionjo cha kumtoa nyoka pangoni.


Pale kwenye uwanja wa seremala mambo yalikuwa si mambo, mapenzi yalinoga kwa namna yake, sarakasi za kila aina na miguno ya mahaba ikahanikiza kila mahali mle chumbani. Jacky alikuwa akilia kilio kilichokosa kabisa tafsiri inayokubalika kwa haraka.


Wakati Yusuf akikaribia kumaliza safari yake ya kufika kileleni, alianza kutapatapa kama mtu aliyekuwa akitaka kukata roho, jambo lile likamfanya Jacky kupitisha vidole vyake laini kwenye masikio ya Yusuf. Kitendo kile kikamfanya Yusuf kuvunja dafu huku akilia kama mtoto mdogo.


“Thank you, darling. Thank you very much,” (Asante, mpenzi. Asante sana) Jacky alisema huku akimbusu Yusuf kwenye paji la uso baada ya kumaliza ngwe ile.


Yusuf aliinuka pale kitandani na kuketi kwenye kona ya kile kitanda akionekana kuwa mbali sana kimawazo, alijiinamia huku akitweta, kwa kweli alionekana kuwa na mawazo mengi.


Sasa alianza kuhisi hatia kubwa ikimkaba kooni, kitendo kile cha kuzini na Jacky kikaufanya moyo wake uumie sana na kupoteza utulivu huku nafsi yake ikianza kumsimanga katika namna ya kumlaumu kuwa alikuwa amefanya maamuzi yasiyokuwa sahihi kukubali kumsaliti mkewe.


“What is wrong, my love?” (Kuna tatizo gani, mpenzi?) Jacky alimuuliza baada ya kumuona akiwa kajiinamia kwa huzuni.


“I’ve betrayed my wife, you know this is my first time to cheat on my marriage,” (Nimemsaliti mke wangu, unajua hii ni mara yangu ya kwanza kuisaliti ndoa yangu) Yusuf alisema kwa huzuni huku machozi yakimlenga.


“C’mon darling, you have no reason to worry! I know you wanted to enjoy, right?” (Oh mpenzi, huna sababu ya kusikitika! Najua ulihitaji kufurahi, siyo?) Jacky alimwambia Yusuf huku akimsogelea na kuanza kumpapasa kifuani. Yusuf hakujibu kitu bali alibaki akiwa ameduwaa.


“Don’t let me down, I’m all yours, darling. I want you now so badly. Please hold me tight in your hands,” (Usiniangushe, mimi ni wako, mpenzi. Nakuhitaji mno. Tafadhali nikumbatie mikononi mwako) Jacky alisema kwa sauti nyororo ya chini iliyoshawishi huku akianza tena utundu wake.


Yusuf alijikuta akisahau ghafla kuhusu mawazo ya kumsaliti mkewe na kujikuta akiwa katika hali mbaya kwa mara nyingine, hakuweza tena kuvumilia. Wakaingia tena mchezoni kwa ngwe nyingine.


Baada ya ngwe ile ya pili kumalizika wote walikuwa hoi na hakuna aliyetaka tena waendelee kwani walikuwa hoi wakiwa wanatweta kwa uchovu. Muda ule Yusuf alishindwa hata kumwangalia Jacky kutokana na aibu.


“Belinda you are wonderful lady. Nashindwa kuelewa unatumia uchawi gani, maana nina mke wa ndoa na mtoto mmoja, nawapenda sana ila sielewi ni kitu gani kimenitokea kujikuta nikivutiwa sana na wewe. Nilipokuona mara ya kwanza pale benki moyo wangu ulivutwa kwako kama sumaku. Japo nimekuwa na msimamo mkali katika kuilinda ndoa yangu lakini kwako nimeshindwa kabisa kuwa na msimamo na kwa mara ya kwanza nimeisaliti ndoa yangu,” Yusuf alisema kwa huzuni huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Nakupenda sana Belinda, nakuahidi nipo tayari kufanya kila linalowezekana kuhakikisha unafanikiwa katika mpango wako wa kupata mabilioni na unakuwa na maisha mazuri zaidi na yenye furaha. I promise you, my love, I’m ready for anything,” Yusuf alizidi kubwabwaja baada ya kuonekana amepagawishwa na Jacky.


Jacky aliachia tabasamu laini na kumbusu Yusuf kwenye paji la uso. “Thank you very much, my love. I need someone like you. You are a person who knows how to love and care. I promise I will give you all kinds of pleasures of this world and I will not need anything from you beyond your love,” (Asante sana, mpenzi wangu. Namhitaji mtu kama wewe. Wewe ni mtu mwelewa unayejua kupenda na unayejali. Nakuahidi nitakupa kila aina ya vionjo na raha za dunia hii na wala sitahitaji kitu chochote toka kwako zaidi ya penzi lako tu) Jacky alichombeza huku akimpapasa Yusuf kwa mahaba.


“I promise, anytime you need me just call me and I’ll be right there. For you I feel the wonderful joy I’ve missed for many years,” (Nakuahidi, muda wowte utakaonihitaji nipigie tu nami nitakuwa hapo mara moja. Kwako ninahisi furaha ya ajabu niliyoikosa kwa miaka mingi) Yusuf alisema huku akimeza funda la mate kutowesha koo lake lililokuwa limekauka.


Jacky alifurahi sana na kummwagia Yusuf mabusu mfululizo, kisha kikafuata kitambo kirefu cha kupanga mipango kabambe ya namna ya kufanikisha mambo ya fedha, huku Jacky akitawala mazungumzo. Katikati ya maongezi yao Jacky alishtuka na kuangalia saa yake ya mkononi akapigwa na butwaa.


“Dah, saa tisa usiku!” Jacky alisema na kumshtua sana Yusuf.


“Oh my God, saa tisa! Sijui nitamwambia nini mke wangu! Sijawahi kulala nje hata siku moja na jana nimetoka nyumbani saa kumi na mbili jioni na sijarudi hadi saa hizi! Eeh Mungu nisamehe mja wako,” Yusuf aliwaza huku moyo wake ukijaa hofu…



Jacky alifurahi sana na kummwagia Yusuf mabusu mfululizo, kisha kikafuata kitambo kirefu cha kupanga mipango kabambe ya namna ya kufanikisha mambo ya fedha, huku Jacky akitawala mazungumzo. Katikati ya maongezi yao Jacky alishtuka na kuangalia saa yake ya mkononi akapigwa na butwaa.


“Dah, saa tisa usiku!” Jacky alisema na kumshtua sana Yusuf.


“Oh my God, saa tisa! Sijui nitamwambia nini mke wangu! Sijawahi kulala nje hata siku moja na jana nimetoka nyumbani saa kumi na mbili jioni na sijarudi hadi saa hizi! Eeh Mungu nisamehe mja wako,” Yusuf aliwaza huku moyo wake ukijaa hofu…


Endelea...


* * * * *


“Oh God, help me. What kind of life is this? Why do I live like this?” (Mungu wangu nisaidie. Haya ni maisha gani? Kwa nini ninaishi maisha kama haya?) Jacky alikuwa anawaza huku akilisikilizia tumbo lake lililokuwa dhaifu sana kwa vile usiku uliokuwa umetangulia alikuwa ametia kilevi tumboni na hakuwa amekula chakula.


Ukichanganya na mahaba mazito aliyoyapata kutoka kwa Yusuf usiku kucha yaliyochangiwa na kiu yake ya kutaka kupata taarifa sahihi za mabilioni ya pesa vilikuwa vimemchanganya sana Jacky na kumfanya asahau hata kula.


Kichwa chake kilikuwa kizito sana kutokana na mning’inio (hang over) uliotokana na uchovu wa pombe kali alizokuwa amekunywa usiku wa siku iliyotangulia. Wakati akiyawaza hayo ilikuwa tayari imeshatimia saa moja ya asubuhi, alikuwa amerudi nyumbani takriban nusu saa tu iliyokuwa imepita.


Alipofika nyumbani asubuhi ile jambo la kwanza alilofanya ilikuwa ni kukimbilia moja kwa moja bafuni kujimwangia maji ya uvuguvugu ili apate nguvu mpya, kwani mwili wote ulikuwa unamuuma kama kidonda kutokana na gwaride la usiku kucha alilokuwa amechezeshwa na Yusuf.


Kiukweli, mwanzoni alikuwa amemchukulia poa Yusuf kwa kudhani asingeweza kumudu dakika tisini za mchezo, kumbe alikosea sana kwani Yusuf aliweza kwenda hadi dakika mia moja na ishirini, na bado walipoingia kwenye matuta hakupatikana mshindi.


Jacky alikuwa amekutana na muziki wa Yusuf usio wa kitoto, kwani Yusuf alijua kucheza ngoma zote, msondo, ndekule, mdundiko, sindimba na nyinginezo pasipo kuomba poo na alikuwa hachoki utadhani alikuwa na mapafu kama ya farasi.


Asubuhi ile Jacky alipomaliza kujimwagia maji alijifunga khanga moja kifuani na taulo kiunoni na kuelekea jikoni ambako alianza kuandaa kifungua kinywa. Wakati alipokuwa mbioni kumaliza zoezi lile la kuandaa kifungua kinywa alishtushwa na mikono ya mtu iliyomshika kiunoni.


Aligeuka haraka nyuma huku moyo wake ukianza kupoteza utulivu, akamuona Carlos akiwa amesimama nyuma yake akitabasamu na hapo tabasamu jepesi likachomoza usoni kwake.


Kumbe muda ule alipokuwa akiandaa kifungua kinywa Carlos alikuwa amenyata taratibu kutoka chumbani alikokuwa amelala na kwenda kusimama nyuma yake bila yeye kujua.


Macho ya Carlos yalikuwa na kila dalili za uchovu na alisimama pale akimtazama Jacky kwa namna ambayo ilimshtua kidogo Jacky. Carlos alimtazama Jacky kwa kitambo kirefu bila kusema neno.


Alikuwa akiitazama hazina matata iliyokuwa imejificha katika umbo matata la Jacky na kujikuta akihisi donge la wivu likimkaba kooni kwake kwa kukubali kumruhusu Jacky kwenda kulala na mwanamume mwingine, eti sababu ya kutafuta pesa.


Kila alipozidi kuutazama kwa makini mwili wa Jacky jinsi ulivyoumbika vyema, ndivyo donge la wivu lilivyozidi kumkaba kooni na kuufanya moyo wake uanze kuumia sana.


“Mbona jana hukurudi nyumbani?” Carlos alijikuta akimuuliza Jacky kwa sauti nzito iliyojaa wivu na hasira. Jacky alimtazama kwa udadisi na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Kazi haikuwa rahisi kama unavyodhani, ilibidi nitumie mbinu ya ziada kumsomesha yule bwana ili anielewe,” Jacky aliongea kwa sauti nyororo yenye kusihi.


“Kwa hiyo baada ya kumaliza kumsomesha ndiyo mkaamua kukesha kabisa! Na usiniambie kuwa uliamua kwenda kavukavu!” Carlos alisema huku akimkazia macho Jacky kwa wasiwasi.


“Niende kavukavu kwani sijitakii mema!” Jacky aliongea kwa utulivu huku akiruhusu tabasamu lake kuchanua usoni kwake. Kisha alimsogelea Carlos karibu zaidi na kumkumbatia akiizungusha mikono yake kwenye kiuno cha Carlos, akambusu na kugeuka kuendelea na kazi yake ya kuandaa kifungua kinywa.


Carlos alisimama pale kwa kitambo kirefu akimtazama Jacky kwa makini, kisha alilazimisha tabasamu na kuondoka.


Dakika arobaini baadaye Jacky na Carlos walikuwa wameketi kwenye meza ya chakula wakipata kifungua kinywa. Jacky alikuwa mkimya mno wakati wote walipokuwa wakistafustahi asubuhi ile kitendo kilichomshangaza sana Carlos.


Alikuwa akila chakula lakini akili yake haikuonekana kuzama kwenye kile chakula pale mezani badala yake alikuwa akila taratibu kwa kupekua pekua chakula, huku mkono wake mmoja ukiwa shavuni, kuna wakati alikuwa akimtupia macho Carlos na kutabasamu.


Uzoefu wa Carlos kwa Jacky na wasichana warembo wa aina yake ukamwacha njia panda. Alijikuta akishindwa kula na kumtazama Jacky kwa udadisi lakini asielewe ni nini kilichokuwa katika mawazo ya Jacky, mwishowe akashindwa kuvumilia.


“Jacky, kwa nini jana usiku hukurudi, ni nini kilichokufanya ukaamua kukesha na yule bwana hadi asubuhi?” Carlos aliuliza kwa sauti iliyoonesha wazi kuwa sasa wivu kwa Jacky ulikuwa umemtawala.


“Hmm, si nimekwisha kujibu jamani, au kuna kingine? Kama hujapenda ungeniambia, ndiyo maana jana nilikuuliza kama ulikuwa unaona wivu nisiende. Sasa unaponiuliza swali lile lile mara mbili mbili nakuwa sielewi kwa nini ulinituma kufanya kazi ile kama hatuaminiani kiasi hiki!” Jacky alisema kwa utulivu lakini akionekana kukerwa sana na swali la Carlos.


“Siyo hivyo, mpenzi, wewe ni mke wangu tena wa ndoa, ni haki yangu kuhakikisha hupati madhara na unaendelea kuwa usalama, na kama ratiba ilibadilika nilitegemea ungenijulisha kwa simu kuwa hutorudi ili nijue cha kufanya…” Carlos alisema kwa sauti tulivu yenye kusihi.


“Cha kufanya kama kipi! Kwamba na wewe ungetafuta mwanamke mwingine wa kulala naye, siyo?” Jacky alimuuliza Carlos huku akiwa amemtulizia macho.


“Usinielewe vibaya, Jacky…”


“Labda nikwambie ukweli, yule bwana ni mwoga sana japo fedha anazitaka. Hivyo ilibidi nipoteze muda mwingi sana kumsomesha hadi anielewe, nimekuja kushtuka tayari ilikuwa imeshatimia saa tisa usiku, unadhani hapo ningefanyaje?” Jacky alimuuliza Carlos huku akiendelea kumtulizia macho yake.


“Okay nimekuelewa, hebu tuachane na hayo… sasa niambie umemuonaje kakuelewa?” Carlos aliuliza huku akijiegemeza kwenye kiti chake.


“Somo limemuingia sana! Tumeongea mambo mengi na kanipa data zote za kwenye tawi lao na akaunti ambayo tutaweza kuitumia kufanikisha mpango wetu. Kwa kifupi ameonesha ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa hata yeye fedha anaitaka.”


“Ni akaunti ipi hiyo aliyokuwa data zake?”


“The Jacarandah Group…”


“Wow!” Carlos alijikuta akiruka kwa furaha.


Muda ule Jacky aliinua kikombe chake cha chai ambayo tayari ilikuwa imepoa na kupiga funda kubwa akiimalizia chai yote iliyobaki, kisha alinawa mikono na kufuta midomo wake kwa kitambaa laini.


“Lakini kazi sasa ipo kwenye kuingia pale benki na kutoka na pesa yote hiyo bila kushitukiwa,” Jacky alisema huku akisukumia kando kikombe chake.


“Suala la kutoka na pesa benki wala si kazi, hilo niachie mimi. Mimi ndiye professional bank robber, nimefuzu mbinu zote za kihalifu na sijawahi kuacha rekodi yoyote ya kuwafanya polisi wanishtukie,” Carlos alisema huku akijipiga piga kifuani katika hali ya kujisifia, kisha akaendelea.


“Kwanza nimefurahi kwa kuwa ni habari muhimu sana kusikia The Jacarandah Group wanaweka pesa zao kwenye tawi lile, hapo itabidi twende kwa Jasmine tukaongee naye kwa kina sana,” Carlos alisema huku akiinuka kutoka pale kwenye kiti.


“Jasmine yupi?” Jacky aliuliza kwa shauku huku akimkazia macho Carlos.


“Mtoto wa marehemu Kombo, yule rafiki yangu tuliyemzika mwaka jana kule kwenye makaburi ya Vingunguti,” alisema Carlos.




“Suala la kutoka na pesa benki wala si kazi, hilo niachie mimi. Mimi ndiye professional bank robber, nimefuzu mbinu zote za kihalifu na sijawahi kuacha rekodi yoyote ya kuwafanya polisi wanishtukie,” Carlos alisema huku akijipiga piga kifuani katika hali ya kujisifia, kisha akaendelea.


“Kwanza nimefurahi kwa kuwa ni habari muhimu sana kusikia The Jacarandah Group wanaweka pesa zao kwenye tawi lile, hapo itabidi twende kwa Jasmine tukaongee naye kwa kina sana,” Carlos alisema huku akiinuka kutoka pale kwenye kiti.


“Jasmine yupi?” Jacky aliuliza kwa shauku huku akimkazia macho Carlos.


“Mtoto wa marehemu Kombo, yule rafiki yangu tuliyemzika mwaka jana kule kwenye makaburi ya Vingunguti,” alisema Carlos.


Endelea...


Jacky alikunja sura yake akijaribu kufikiria kwa kitambo kidogo kisha akabetua kichwa chake akionekana kukumbuka. “Okay… Kombo namkumbuka lakini Jasmine hata simkumbuki kabisa!” Jacky alisema huku akionekana kujaribu kuvuta taswira ya Jasmine bila mafanikio.


“Ukimuona utamkumbuka, tutaenda nyumbani kwake leo jioni tukamsomeshe, nina imani atatuelewa,” Carlos alisema huku akiliendea jokofu na kutoa chupa ya mvinyo aina ya Sauvignon Blanc.


Jacky aliinuka na kutoa vyombo kisha akavipeleka jikoni, aliporudi sebuleni alimkuta Carlos akiwa ameweka bilauri mbili mezani, hivyo wakashushia na mvinyo mtamu wa Sauvignon Blanc kama namna ya kujipongeza kwa kazi nzuri iliyofanyika.


Mvinyo ule ulionekana kuamsha ari mpya katika miili yao na hivyo kuwachangamsha vizuri kiasi cha kupunguza nishai machoni. Haikuchukua muda kila mmoja alijikuta mikono yake ikivinjari kwenye mwili wa mwenzake huku nguo zikitolewa na kutupwa huku na kule.


Japokuwa Jacky alipanga kupumzika asubuhi ile kutokana na mwili wake kukosa nguvu kwa kukimbizwa mchaka mchaka na Yusuf usiku kucha wa siku iliyotangulia, lakini hakuwa na namna, alijikuta akilazimika kukabiliana na gwaride jingine kutoka kwa mumewe Carlos.


“Hmm… sijui nitaendelea na maisha haya hadi lini? I’m sick and tired with this kind of life,” Jacky aliwaza wakati akipiga magoti na kuanza manjonjo yake akiisakama ikulu ya Carlos kwa kutumia mdomo wake… na muda mfupi uliofuata walikuwa wakielea angani kwenye sayari ya mbali sana isiyofikika kwa chombo chochote isipokuwa mahaba mazito.


* * * * *


Asubuhi ile nyumbani kwa Yusuf, kwenye nyumba ya kawaida ya kupanga iliyokuwa katika eneo la Ilala Bungoni, Yusuf alikuwa chumbani kwake amesimama mbele ya meza ya vipodozi yenye kioo kirefu cha kujitazama.


Alisimama pale kwa takriban dakika tano akiwa hajui afanye nini, na alipogutuka alichuku chanuo akaanza kuchana nywele zake taratibu huku akionekana kuwaza mbali.


Muda wote alionekana kuwa mtulivu sana na mwenye mawazo mengi. Asubuhi ile Yusuf alikuwa amevaa shati nzuri jeupe lililokuwa na mikono mirefu, suruali ya bluu na tai shingoni ya rangi ya bluu iliyokuwa na nembo ya benki aliyokuwa akiifanyia kazi.


Akiwa bado katika lindi la mawazo mara mlango wa chumba chake ukafunguliwa na mwanadada aliyekuwa na miaka kama ishirini na sita hivi akaingia, huyu alikuwa ni mkewe, Mama Jasmine.


Aliingia taratibu na kusimama huku akimtazama Yusuf kwa makini kuanzia kichwani hadi kwenye unyayo kisha akakisogelea kitanda na kujipwetekaa pale kitandani huku akiendelea kumtazama Yusuf.


Yusuf alionekana kushtuka sana, alimtupia jicho la wizi mkewe kupitia kile kioo cha kujitazama wakati akijifanya kuweka lile chanuo juu ya ile meza ya vipodozi.


Yule mwanamke alikuwa ni mdada mrembo sana aliyejaaliwa kuwa na uzuri wa asili, alikuwa na umbo kubwa kiasi lililovutia sana na sura ya kitoto. Alikuwa mrefu wa wastani na mweupe kwa rangi ya ngozi. Rangi ambayo ilikuwa na mng’aro wa aina yake na mvuto wa kipekee na wala hakuhitaji vikorombwezo vya aina yoyote kuinakshi ngozi ile.


Alikuwa na nywele nyingi alizokuwa amezifunika kwa kofia maalumu ya kulalia na mwilini alivaa nguo nyepesi ya kulalia ya rangi ya samawati iliyolichora vyema umbo lake zuri na juu ya ile nguo alijifunga khanga. Asubuhi ile alionekana mchovu sana kwa sababu ya kukesha usiku akimsubiri mumewe na usoni alionekana ni mwenye hasira.


Yusuf alijifanya kuitengeneza vizuri tai yake shingoni huku akimtupia tena jicho la wizi kupitia kile kioo cha kujitazama, kwa kuwa alikuwa hana ujasiri wa kumtazama moja kwa moja. Hata hivyo, aliamua kujipa ujasiri ili kuzikabili hasira za mkewe, maana kama maji yalikwisha mwagika na yasingeweza kuzoleka.


“Baba Jasmine, naomba unieleze ukweli vinginevyo leo patachimbika, jana ulilala wapi?” Yusuf alishtushwa na sauti ya mkewe.


“Jamani, si tumekwisha yazungumza! Nimekwambia nilikokuwa na sababu iliyonifanya nikashindwa kurudi nyumbani usiku, nikadhani labda tumeelewana kumbe mwenzangu bado hayajaisha?” Yusuf alijibu kwa sauti tulivu.


“Kwa nini hukunitaarifu jana hiyo hiyo kama ungechelewa kurudi ili nisiwe na wasiwasi kuhusu usalama wako?”


“Ni bahati mbaya tu nilijisahau, nimeomba samahani, nakuomba tena nisamehe yaishe ili tu…”


“Hayawezi kuisha kirahisi namna hiyo, yaani ulale nje, urudi hapa asubuhi ukiwa unanukia manukato ambayo sijawahi kuyasikia humu ndani halafu eti yaishe hivi hivi tu, haiwezekani! Mimi ni mkeo na ni lazima nijue kila kitu unachokifanya… Naomba uniambie jana ulilala wapi na ulikuwa na nani?” mkewe alimkata kauli huku akiongea kwa msisitizo, alikuwa amekasirika kweli kweli.


“I need to know everything, you are my husband and you are important to me,” (Ninahitaji kujua kila kitu, wewe ni mume wangu na wewe ni muhimu kwangu) Mama Jasmine aliendelea kuongea kwa hasira, na kila alivyozidi kuongea ndivyo sauti yake ilivyozidi kupanda na kuwa kali zaidi.


“I know that I’m important to you, and you are also very important to me…” (Najua mimi ni muhimu kwako, na wewe pia ni muhimu sana kwangu…) Yusuf alijaribu kujitetea huku akimsogelea mkewe taratibu.


“Liar! I’m not important to you at all. I’m very disappointed,” (Muongo! Mimi si muhimu kwako kabisa. Nimefadhaika sana.) Mama Jasmine alilalamika huku hasira zake zikizidi kupanda.


“Remember I'm not a little kid and not as foolish as you think,” (Kumbuka mimi si mtoto mdogo kabisa na wala si mpumbavu kama unavyofikiria) Mama Jasmine alizidi kulalamika kwa huzuni.


Yusuf alilazimisha tabasamu kisha akamsogelea na kupeleka mkono wake wa kulia kwenye uso wa mkewe kwa uangalifu huku uso wake ukizidi kuchanua kwa tabasamu, japo kwa kulazimisha.


“Don’t touch me!” (Usiniguse!) Mama Jasmine aliusukuma mkono wa Yusuf kwa hasira na kurudi nyuma.


“Kama unadhani natania basi subiri uone, yaani ulale na malaya wako usiku kucha kisha unarudi asubuhi, halafu naongea unaniona kama katuni. Au naongea upuuzi?” Mama Jasmine alisema kwa hasira na kusonya. Kitendo cha kusonya kikamkasirisha sana Yusuf.




Yusuf alilazimisha tabasamu kisha akamsogelea na kupeleka mkono wake wa kulia kwenye uso wa mkewe kwa uangalifu huku uso wake ukizidi kuchanua kwa tabasamu, japo kwa kulazimisha.


“Don’t touch me!” (Usiniguse!) Mama Jasmine aliusukuma mkono wa Yusuf kwa hasira na kurudi nyuma.


“Kama unadhani natania basi subiri uone, yaani ulale na malaya wako usiku kucha kisha unarudi asubuhi, halafu naongea unaniona kama katuni. Au naongea upuuzi?” Mama Jasmine alisema kwa hasira na kusonya. Kitendo cha kusonya kikamkasirisha sana Yusuf.


Endelea...


“Unanisonya? Yaani Mama Jasmine umefikia hatua ya kunisonya! Naona sasa unaanza kuvuka mipaka,” Yusuf alisema huku akimtazama mkewe kwa hasira.


“Mipaka ya kwenda wapi?” Mama Jasmine aliuliza kwa hasira huku naye akimtazama Yusuf kwa hasira. Kwa kitambo walibaki wakiwa wametazama kwa hasira kama majogoo yaliyotaka kupigana.


“Hivi unataka tuoneshane jeuri ya kusema, au nini? Kwa kuwa unajua nakupenda ndiyo maana unaleta jeuri siyo, lakini siwezi kukaa kimya kwa madai yako kuwa eti nimekesha na malaya wakati si kweli, una ushahidi gani kuhusu madai yako?” Yusuf aliuliza huku akimkazia macho mkewe.


“Ushahidi uliopo machoni kwa Mungu unanitosha, na ninaamini atanilipia,” alisema mkewe huku akishusha pumzi ndefu kama aliyetoka kukimbia mbio ndefu. Yusuf alitaka kusema neno lakini hatia ikamkaba koo, akabaki kushangaa tu akimtumbulia macho mkewe. Kikapita tena kitambo kirefu cha ukimya.


“Yaani hata sielewi, nimekwambia ukweli wangu hutaki kuamini, nimeomba msamaha pia hutaki kukubali, sijui wewe ni mwanamke wa aina gani? Sasa sikiliza, mimi ndiye mwanamume humu ndani, nataka mambo haya yaishe na sitaki tena kuyasikia…” Yusuf alisema kwa hasira.


“Huwezi kunizuia kuongea, Yusuf…”


“He, mara hii nimeshakuwa Yusuf na si Baba Jasmine tena?” Yusuf aliuliza kwa mshangao huku akimkazia macho mkewe.


“Kwani siyo jina lako? Usitake kutafuta sababu ya kunifunga mdomo nisiongee, nitaongea na huwezi kunifanya kitu, kwa taarifa yako ni kwamba lazima niwafikishie taarifa hizi wazee,” mkewe alifoka kwa hasira. Maneno yale yalionekana kumuumiza sana Yusuf, hivyo akamsogelea mkewe.


“Mama Jasmine, this is the last warning. Tafadhali usithubutu tena kunijibu namna hiyo,” Yusuf alisema kwa sauti tulivu huku akimnyooshea kidole mkewe kwa hasira.


“I’m not a coward to be scared, tena naomba usinitishe kabisa, Yusuf. Huwezi kunifanya lolote,” yule mwanamke alizidi kupandisha kwa kujiamini. Yusuf akamkaba shingoni kwa hasira na kumtingisha.


“I married you because I love you very much, so don’t dare disrespect me again,” (Nilikuoa kwa sababu nakupenda sana, kwa hiyo usijaribu kunidharau tena) Yusuf aliongea kwa hasira na kutoka mle chumbani huku akiubamiza mlango nyuma yake.


Japo Yusuf alikuwa amemtisha mkewe na kuondoka kwa hasira lakini ukweli ni kwamba moyoni hakuwa na ujasiri kabisa wa kusimama mbele ya mkewe na kukanusha kilichokuwa kikisemwa. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ndoa alijikuta akiogopa sana, kwani katika miaka sita ya ndoa yao hakuwahi kabisa kumuona mkewe akiwa amekasirika kiasi ile.


Baada ya Yusuf kuondoka Mama Jasmine aliketi pale kitandani taratibu, macho yake yalijenga malengelenge ya machozi kiasi kwamba kila alichokitazama mle chumbani alikiona katika hali ya ukungu. Aliinamisha kichwa chake na kutafakari sana.


Aliendelea kuganda vile kwa muda mrefu akiwaza yaliyomjia akilini na katika kutafakari akakumbuka yaliyotokea usiku uliotangulia baada ya mumewe kuchelewa kurudi nyumbani.


Ilikuwa saa nne usiku, alikuwa kasimama barazani nje ya nyumba waliyokuwa wakiishi akionekana kutokuwa katika hali nzuri, japo alijitahidi sana kuwa mtulivu. Muda ule mtoto wake Jasmine wa miaka mitatu alikuwa kamng'ang'ania mama yake khanga.


Mama Jasmine na mwanawe walisimama pale nje wakitazama barabarani labda pengine wangeweza kumuona Yusuf akirudi nyumbani na mfuko wenye zawadi kama ilivyokuwa kawaida yake pindi alipotoka kwenda kutazama mpira au kukutana na rafiki zake baa na kupata bia mbili.


Baada ya Jasmine kuzidi kumsumbua alichukua simu yake na kubofya namba za Yusuf kisha akapiga na kuongea naye, Yusuf alimwambia kuwa alikuwa anamalizia kikao na angerejea nyumbani haraka mara baada ya kumaliza.


Mama Jasmine pia akakumbuka jinsi alivyokesha sebuleni kwenye kochi akiwa na wasiwasi akimsubiri Yusuf baada ya kutorudi, aliendelea kuketi pale kwenye kochi hadi ilipotimia saa kumi usiku akashindwa kuvumilia na kujikuta akipitiwa na usingizi pale pale sebuleni kwenye kochi.


Alikuja kushtuka alfajiri ya saa kumi na mbili baada ya kusikia mlango ukigongwa taratibu, aliinuka na kuufungua akamuona Yusuf akiingia huku akionekana kuchoka sana, pia hakuwa akimwangalia machoni mkewe.


Mama Jasmine alimtazama Yusuf kwa makini lakini Yusuf alionesha kuyakwepa macho ya mkewe, jambo hilo likamfanya Mama Jasmine ashtuke na kuona kuwa huenda kulikuwa na jambo ambalo Yusuf alikuwa akilificha.


“Mbona leo umechelewa sana kurudi?” Mama Jasmine alimuuliza Yusuf huku akimkazia macho.


“Nimechelewa? Hivi mtu huwa anachelewa nyumbani kwake?” Yusuf aliongea kwa mzaha huku akijichekesha.


Mama Jasmine akamuonesha saa iliyokuwa imetundikwa ukutani. “Hebu angalia saa, ni saa ngapi sasa?”


Yusuf aliiangalia ile saa ya ukutani, kisha akaiangalia na ile ya mkononi aliyokuwa ameivaa na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. “Saa kumi na mbili na robo, lakini…” alisema lakini Mama Jasmine akamkatisha.


“Hivi huu ndiyo muda muafaka wa wewe kurudi nyumbani kwako?” Mama Jasmine aliuliza kwa utulivu huku akionekana kuzuia hasira zake.


“Samahani, mke wangu, kikao chetu kilikuwa kirefu sana na ukichanganya na pombe tulizokuwa tunakunywa si nikajisahau, nilipokuja kushtuka it was too late,” Yusuf alisema kwa utulivu huku akiyakwepa macho ya mkewe na kutazama pembeni na alionekana kuwa na wasiwasi.


“Hujanishawishi bado, kila nikiitazama sura yako na kile unachokiongea naona hata haviendani, How could you do this to me? How could you betray me?” (Unawezaje kunifanyia hivi? Unawezaje kunisaliti?) Mama Jasmine aliongea kwa uchungu huku akizidi kumkazia macho Yusuf.


“Labda nikwambie, unaweza kuongopa chochote, lakini ujue kuwa nafsi yako ndiyo inayojua ukweli na sasa inakusuta.”


“Dont you trust me? I’ve told you the truth, I didnt do anything wrong,” (Huniamini? Nimeshakwambia ukweli, sijafanya chochote kibaya) Yusuf alijaribu kujitetea.


Mama Jasmine alimsogelea karibu zaidi na kusimama mbele yake huku akimkazia macho. “Baba Jasmine, hebu niangalie machoni halafu uniambie kuwa hujanisaliti.”


Yusuf alimtazama mkewe machoni na kushindwa kuongea, akayakwepesha macho yake na kutazama pembeni. “Kama huniamini basi, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa siwezi kuisaliti ndoa yangu hata siku moja,” Yusuf alisema huku akiingia chumbani…


Itaendelea...Kizungumkuti! - 22


Na Bishop Hiluka


Yusuf alilazimisha tabasamu kisha akamsogelea na kupeleka mkono wake wa kulia kwenye uso wa mkewe kwa uangalifu huku uso wake ukizidi kuchanua kwa tabasamu, japo kwa kulazimisha.


“Don’t touch me!” (Usiniguse!) Mama Jasmine aliusukuma mkono wa Yusuf kwa hasira na kurudi nyuma.


“Kama unadhani natania basi subiri uone, yaani ulale na malaya wako usiku kucha kisha unarudi asubuhi, halafu naongea unaniona kama katuni. Au naongea upuuzi?” Mama Jasmine alisema kwa hasira na kusonya. Kitendo cha kusonya kikamkasirisha sana Yusuf.


Endelea...


“Unanisonya? Yaani Mama Jasmine umefikia hatua ya kunisonya! Naona sasa unaanza kuvuka mipaka,” Yusuf alisema huku akimtazama mkewe kwa hasira.


“Mipaka ya kwenda wapi?” Mama Jasmine aliuliza kwa hasira huku naye akimtazama Yusuf kwa hasira. Kwa kitambo walibaki wakiwa wametazama kwa hasira kama majogoo yaliyotaka kupigana.


“Hivi unataka tuoneshane jeuri ya kusema, au nini? Kwa kuwa unajua nakupenda ndiyo maana unaleta jeuri siyo, lakini siwezi kukaa kimya kwa madai yako kuwa eti nimekesha na malaya wakati si kweli, una ushahidi gani kuhusu madai yako?” Yusuf aliuliza huku akimkazia macho mkewe.


“Ushahidi uliopo machoni kwa Mungu unanitosha, na ninaamini atanilipia,” alisema mkewe huku akishusha pumzi ndefu kama aliyetoka kukimbia mbio ndefu. Yusuf alitaka kusema neno lakini hatia ikamkaba koo, akabaki kushangaa tu akimtumbulia macho mkewe. Kikapita tena kitambo kirefu cha ukimya.


“Yaani hata sielewi, nimekwambia ukweli wangu hutaki kuamini, nimeomba msamaha pia hutaki kukubali, sijui wewe ni mwanamke wa aina gani? Sasa sikiliza, mimi ndiye mwanamume humu ndani, nataka mambo haya yaishe na sitaki tena kuyasikia…” Yusuf alisema kwa hasira.


“Huwezi kunizuia kuongea, Yusuf…”


“He, mara hii nimeshakuwa Yusuf na si Baba Jasmine tena?” Yusuf aliuliza kwa mshangao huku akimkazia macho mkewe.


“Kwani siyo jina lako? Usitake kutafuta sababu ya kunifunga mdomo nisiongee, nitaongea na huwezi kunifanya kitu, kwa taarifa yako ni kwamba lazima niwafikishie taarifa hizi wazee,” mkewe alifoka kwa hasira. Maneno yale yalionekana kumuumiza sana Yusuf, hivyo akamsogelea mkewe.


“Mama Jasmine, this is the last warning. Tafadhali usithubutu tena kunijibu namna hiyo,” Yusuf alisema kwa sauti tulivu huku akimnyooshea kidole mkewe kwa hasira.


“I’m not a coward to be scared, tena naomba usinitishe kabisa, Yusuf. Huwezi kunifanya lolote,” yule mwanamke alizidi kupandisha kwa kujiamini. Yusuf akamkaba shingoni kwa hasira na kumtingisha.


“I married you because I love you very much, so don’t dare disrespect me again,” (Nilikuoa kwa sababu nakupenda sana, kwa hiyo usijaribu kunidharau tena) Yusuf aliongea kwa hasira na kutoka mle chumbani huku akiubamiza mlango nyuma yake.


Japo Yusuf alikuwa amemtisha mkewe na kuondoka kwa hasira lakini ukweli ni kwamba moyoni hakuwa na ujasiri kabisa wa kusimama mbele ya mkewe na kukanusha kilichokuwa kikisemwa. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ndoa alijikuta akiogopa sana, kwani katika miaka sita ya ndoa yao hakuwahi kabisa kumuona mkewe akiwa amekasirika kiasi ile.


Baada ya Yusuf kuondoka Mama Jasmine aliketi pale kitandani taratibu, macho yake yalijenga malengelenge ya machozi kiasi kwamba kila alichokitazama mle chumbani alikiona katika hali ya ukungu. Aliinamisha kichwa chake na kutafakari sana.


Aliendelea kuganda vile kwa muda mrefu akiwaza yaliyomjia akilini na katika kutafakari akakumbuka yaliyotokea usiku uliotangulia baada ya mumewe kuchelewa kurudi nyumbani.


Ilikuwa saa nne usiku, alikuwa kasimama barazani nje ya nyumba waliyokuwa wakiishi akionekana kutokuwa katika hali nzuri, japo alijitahidi sana kuwa mtulivu. Muda ule mtoto wake Jasmine wa miaka mitatu alikuwa kamng'ang'ania mama yake khanga.


Mama Jasmine na mwanawe walisimama pale nje wakitazama barabarani labda pengine wangeweza kumuona Yusuf akirudi nyumbani na mfuko wenye zawadi kama ilivyokuwa kawaida yake pindi alipotoka kwenda kutazama mpira au kukutana na rafiki zake baa na kupata bia mbili.


Baada ya Jasmine kuzidi kumsumbua alichukua simu yake na kubofya namba za Yusuf kisha akapiga na kuongea naye, Yusuf alimwambia kuwa alikuwa anamalizia kikao na angerejea nyumbani haraka mara baada ya kumaliza.


Mama Jasmine pia akakumbuka jinsi alivyokesha sebuleni kwenye kochi akiwa na wasiwasi akimsubiri Yusuf baada ya kutorudi, aliendelea kuketi pale kwenye kochi hadi ilipotimia saa kumi usiku akashindwa kuvumilia na kujikuta akipitiwa na usingizi pale pale sebuleni kwenye kochi.


Alikuja kushtuka alfajiri ya saa kumi na mbili baada ya kusikia mlango ukigongwa taratibu, aliinuka na kuufungua akamuona Yusuf akiingia huku akionekana kuchoka sana, pia hakuwa akimwangalia machoni mkewe.


Mama Jasmine alimtazama Yusuf kwa makini lakini Yusuf alionesha kuyakwepa macho ya mkewe, jambo hilo likamfanya Mama Jasmine ashtuke na kuona kuwa huenda kulikuwa na jambo ambalo Yusuf alikuwa akilificha.


“Mbona leo umechelewa sana kurudi?” Mama Jasmine alimuuliza Yusuf huku akimkazia macho.


“Nimechelewa? Hivi mtu huwa anachelewa nyumbani kwake?” Yusuf aliongea kwa mzaha huku akijichekesha.


Mama Jasmine akamuonesha saa iliyokuwa imetundikwa ukutani. “Hebu angalia saa, ni saa ngapi sasa?”


Yusuf aliiangalia ile saa ya ukutani, kisha akaiangalia na ile ya mkononi aliyokuwa ameivaa na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. “Saa kumi na mbili na robo, lakini…” alisema lakini Mama Jasmine akamkatisha.


“Hivi huu ndiyo muda muafaka wa wewe kurudi nyumbani kwako?” Mama Jasmine aliuliza kwa utulivu huku akionekana kuzuia hasira zake.


“Samahani, mke wangu, kikao chetu kilikuwa kirefu sana na ukichanganya na pombe tulizokuwa tunakunywa si nikajisahau, nilipokuja kushtuka it was too late,” Yusuf alisema kwa utulivu huku akiyakwepa macho ya mkewe na kutazama pembeni na alionekana kuwa na wasiwasi.


“Hujanishawishi bado, kila nikiitazama sura yako na kile unachokiongea naona hata haviendani, How could you do this to me? How could you betray me?” (Unawezaje kunifanyia hivi? Unawezaje kunisaliti?) Mama Jasmine aliongea kwa uchungu huku akizidi kumkazia macho Yusuf.


“Labda nikwambie, unaweza kuongopa chochote, lakini ujue kuwa nafsi yako ndiyo inayojua ukweli na sasa inakusuta.”


“Dont you trust me? I’ve told you the truth, I didnt do anything wrong,” (Huniamini? Nimeshakwambia ukweli, sijafanya chochote kibaya) Yusuf alijaribu kujitetea.


Mama Jasmine alimsogelea karibu zaidi na kusimama mbele yake huku akimkazia macho. “Baba Jasmine, hebu niangalie machoni halafu uniambie kuwa hujanisaliti.”


Yusuf alimtazama mkewe machoni na kushindwa kuongea, akayakwepesha macho yake na kutazama pembeni. “Kama huniamini basi, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa siwezi kuisaliti ndoa yangu hata siku moja,” Yusuf alisema huku akiingia chumbani…



“Dont you trust me? I’ve told you the truth, I didnt do anything wrong,” (Huniamini? Nimeshakwambia ukweli, sijafanya chochote kibaya) Yusuf alijaribu kujitetea.


Mama Jasmine alimsogelea karibu zaidi na kusimama mbele yake huku akimkazia macho. “Baba Jasmine, hebu niangalie machoni halafu uniambie kuwa hujanisaliti.”


Yusuf alimtazama mkewe machoni na kushindwa kuongea, akayakwepesha macho yake na kutazama pembeni. “Kama huniamini basi, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa siwezi kuisaliti ndoa yangu hata siku moja,” Yusuf alisema huku akiingia chumbani…


Endelea...


______


“Kwa kweli sijawahi kuumizwa kama alivyoniumiza Baba Jasmine leo. Hii tabia yake ya kujifanya kwenda kukutana na marafiki zake baa nilijua tu mambo kama haya lazima yatakuja kutokea,” Mama Jasmine aliwaza na kusonya kwa huzuni.


Alikuwa bado ameketi pale pale kitandani baada ya Yusuf kuondoka huku akiwaza na kuwazua lakini hakuweza kupata jibu muafaka, ingawa Yusuf alikana kufanya jambo baya lakini Mama Jasmine alikuwa na uhakika kuwa kulikuwa na jambo ambalo mumewe alikuwa akilificha.


Alitamani sana kulijua jambo lililomsibu mumewe lakini hakuwa na uwezo huo, na kutokana na maumivu makali ya moyo aliyoyapata alitamani kuondoka pale nyumbani na kurudi kwao lakini hakuwa na ushahidi wa kutosha kumhukumu Yusuf kuwa alikuwa na mwanamke mwingine…


Akiwa bado anawaza aligutushwa na sauti kali ya Jasmine aliyoisikia kwa mbali akigombana na mtoto mwingine wa chumba cha jirani kule nje ya nyumba. Mama Jasmine aliinuka pale kitandani na kujifunga khanga yake vizuri kisha akatoka nje haraka kumfuata Jasmine.


Alimkuta Jasmine akiwa amesimama aking’ang’ania andazi ambalo mtoto mwenzie alikuwa amenunuliwa na mama yake. Mama Jasmine akamchukua na kuingia naye ndani.


* * * * *


Saa mbili za asubuhi ilimkuta Yusuf akiwa ndani ya daladala lililotoka Buguruni kuelekea Mnazi Mmoja, daladala lile lilikuwa limejaza abiria kupita kiasi. Asubuhi ile abiria ndani ya daladala walikuwa wakijipepea kutokana na joto kali lililosababishwa na kujaa, hata hivyo kondakta wa daladala aliendelea kuita abiria wengine wapande kwenye kila kituo walichopita.


Yusuf alikuwa ameondoka nyumbani kwake akiwa bado ana hasira na wasiwasi kutokana na mzozo kati yake na mkewe asubuhi ile, na alikuwa akielekea ofisini kwake Mnazi Mmoja.


Yusuf alikuwa amepandia katika kituo cha Bungoni na hakuwa amepata siti hivyo kulazimika kusimama huku akiwa ameminywa na abiria wenzake, hasa wamama wawili waliokuwa na maumbo makubwa. Na muda wote aliokuwa ndani ya lile daladala alikuwa akiwaza namna ya kumfanya mkewe amwelewe na furaha irudi tena ndani ya nyumba.


Alijikuta akiwa hili na lile na kuna wakati alisonya na kuwafanya abiria wengine wageuze vichwa vyao kumtazama kwa mshangao. Aliposhtuka alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuwaangalia abiria wenzake, akawaona wao walikuwa na furaha sana tofauti na yeye.


Akajiuliza, huyu Belinda alikuwa wapi siku zote na kwa nini amekuja kwenye maisha yake sasa hivi? Je, aendelee na mpango wa kujipatia mamilioni ya pesa au ampigie simu na kumwambia kuwa hataki tena kuendelea na dili hilo la pesa ili kuokoa ndoa yake?


Alifikia hatua ya kuachana na dili aliloambiwa na Jacky ambaye yeye alimfahamu kwa jina la Belinda, lakini alipokumbuka ile adha ya kuminywa ndani ya daladala akajikuta akiwa njia panda. Alitakiwa achague kati ya dili la pesa au kulinda maadili ya kazi yake na kuiokoa ndoa yake.


Dah! Ahadi ya kupata mgao wa shilingi milioni mia mbili na hamsini baada ya lile dili kufanikiwa ikamfanya azidi kuchanganyikiwa, maana kwa pesa ile angeweza kujenga nyumba nzuri ya kisasa kule Kimara Temboni kwenye kiwanja alichozawadiwa na baba yake mkubwa siku ya harusi yake.


Pia angeweza kujenga nyumba nyingine kubwa nyumbani kwao Morogoro na angebakiwa na chenji ya kununulia gari, japo Toyota IST, na hivyo heshima ya ndoa yake ingerudi.


“Kila kitu kinamalizwa na pesa, hakuna mkate mgumu mbele ya chai nikishapata pesa amani kwenye ndoa yangu itarudi tu,” Yusuf aliwaza huku akiachia tabasamu laini, kisha aliinama kidogo kuangalia nje wakati daladala ikivuka eneo la soko la Boma.


Akaona vitu vikiwa vinapita mbele ya macho yake kwa kasi wakati daladala ikiwa inakwenda. Muda wote sura yake ilikuwa inaonesha huzuni na hakujua afanye nini ili kuirejesha furaha yake asubuhi ile.


Lile daladala lilipokuwa likivuka kwenye taa za kuongozea magari barabarani katika eneo la Ilala Boma, Yusuf aliwaona kinamama wakiwa wanafagia barabara kwenye vumbi bila hata kuwa na kitu cha kuwakinga. Hawakuwa na barakoa (masks), wala kitu chochote cha kuwakinga.


Baada ya kuvuka lile daladala lilisimama katika kituo cha daladala cha Karume, abiria wawili wakashuka na wengine wanne wakapanda baada ya kushawishiwa na kondakta wa lile daladala, na hapo daladala likaondoka tena.


Hapo sasa Yusuf alikuwa amepata siti baada ya abiria mmoja kushuka pale Karume na hivyo kumwachia siti aliyokuwa amekaa. Wakati wakiyapita majengo ya kiwanda cha bia (TBL) Yusuf aliwaona watoto wa mtaani wakigawana mkate karibu na kituo cha daladala cha Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.


Wakati huo watoto wengine walikuwa wanaomba fedha kwa abiria na madereva wa magari yaliyokuwa yanasimama. Yusuf aliwatazama kwa makini na kujikuta akimuwaza mwanawe Jasmine, alifikiria kuwa endapo hangefanya juhudi za kuinusuru ndoa yake, huenda Jasmine angeweza hata kuishia kuwa mtoto wa mtaani.


“Mungu aepushie mbali,” alijikuta akisema kimoyomoyo huku akivuta pumzi ndefu za ndani kwa ndani kisha akazishusha taratibu. Aliendelea kuwatazama wale watoto wa mtaani kwa makini wakati daladala likianza kuwaacha mbali wale watoto wa mtaani na mara wakajikuta wakivuka taa za kuongozea magari katika makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru eneo la Kariakoo.


Alishusha pumzi, akakunja sura yake na kuangalia huku na huko kwa huzuni wakati lile daladala likisimama katika kituo cha daladala cha Congo.


“Sikutegemea kabisa kama ingefikia hatua nikagombana na Mama Jasmine kiasi hiki! Hata hivyo, imenisaidia kumfahamu vizuri mke wangu, anaonekana ni mwanamke ambaye anataka kuwa na sauti ndani ya nyumba na maamuzi yake yawe ndiyo yawe ya mwisho…” Yusuf alijikuta akiwaza wakati lile daladala lilipokuwa likiondoka kutoka pale kituo cha Congo.


“Lakini mimi ndiye mwanamume ndani ya nyumba, siwezi kukubali jambo hili liendelee na siko tayari kuvumilia dharau zake. Ni kweli nimefanya kosa lakini angejaribu basi kunipa heshima yangu kama mume…” aliendelea kuwaza na mara akashtuliwa na abiria waliyekuwa wameketi siti moja baada ya lile daladala kusimama katika kituo cha Mnazi Mmoja.


Akashuka kutoka katika lile daladala na kuanza kutembea taratibu akielekea kazini kwake huku akiwa ameinamisha kichwa chake akiendelea kuwaza.


“Kichwa changu kimevurugwa kabisa, I real need someone to talk to, to comfort me,” aliwaza na mara ya Jacky ikamjia


“Oh Belinda! I need to talk to her… Dah, sura ya Belinda toka niliponana naye jana asubuhi imeshindwa kabisa kunitoka kichwani. Ninamuwaza kila dakika. Yawezekana ni kutokana na uzuri wake na kasheshe zake za usiku kucha, kwa kweli sikutegemea kama ana uwezo mkubwa kiasi kile na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimepata mwanamke ambaye amenikimbiza mchaka mchaka kiasi kile… isitoshe ni mtoto mzuri mno. Ameumbwa akaumbika…”


Mawazo ya Yusuf yalikatizwa na sauti kali za breki ya gari lililokuwa likiyumba kumkwepa. Yusuf aliogopa sana akajikunja na kuruka juu huku akitua kando ya ile barabara akiwa amefumba macho yake. Kutokana na kuzidiwa na mawazo alijikuta akivuka barabra ile ya Lumumba pasipo hata kuangalia kulia na kushoto kwake.





“Kichwa changu kimevurugwa kabisa, I real need someone to talk to, to comfort me,” aliwaza na mara ya Jacky ikamjia


“Oh Belinda! I need to talk to her… Dah, sura ya Belinda toka niliponana naye jana asubuhi imeshindwa kabisa kunitoka kichwani. Ninamuwaza kila dakika. Yawezekana ni kutokana na uzuri wake na kasheshe zake za usiku kucha, kwa kweli sikutegemea kama ana uwezo mkubwa kiasi kile na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimepata mwanamke ambaye amenikimbiza mchaka mchaka kiasi kile… isitoshe ni mtoto mzuri mno. Ameumbwa akaumbika…”


Mawazo ya Yusuf yalikatizwa na sauti kali za breki ya gari lililokuwa likiyumba kumkwepa. Yusuf aliogopa sana akajikunja na kuruka juu huku akitua kando ya ile barabara akiwa amefumba macho yake. Kutokana na kuzidiwa na mawazo alijikuta akivuka barabara ile ya Lumumba pasipo hata kuangalia kulia na kushoto kwake.


Endelea...


Lile gari lilisimama katikati ya barabara na wakati huo huo dereva wa lile gari alishusha kioo cha gari na kumtazama Yusuf huku akionekana kukasirishwa sana. Lilikuwa ni gari la zuri aina ya Toyota Lexus RX la rangi nyeusi.


“What’s wrong with you guy, how do you cross the road without looking right and left?” (We bwana una matatizo gani, unavukaje barabara bila kutazama kulia na kushoto kwako?) yule dereva alifoka kwa ukali huku akimkazia macho Yusuf.


Yusuf aligeuza kichwa chake kumtazama yule dereva huku akiwa na uso uliosawajika sana, mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kwa kasi isivyo kawaida kutokana na mshtuko mkubwa alioupata baada ya kunusurika kugongwa.


“Forgive me, brother, it’s just family problems…” (Niasamehe, kaka, ni matatizo tu ya kifamilia…)


“Do not bring your family’s problems to the road…” (Matatizo ya familia yako usiyalete barabarani…) yule dereva alimkata kauli Yusuf kwa hasira lakini akaonekana kusita ghafla baada ya kuhisi kumfahamu Yusuf. Akamkazia macho akimwangalia kwa makini.


Yusuf naye alimtazama yule dereva kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, kikapita kitambo kifupi kila mmoja akimtazama mwenzake, na kila mmoja alihisi kumfahamu mwingine.


“Yusuf!” yule dereva aliita kwa shauku huku akizidi kumkazia macho Yusuf.


“Jacob!” Yusuf aliita huku akilisogelea lile gari, wakasalimiana kwa furaha.


“What’s wrong with you, brother?” (Una shida gani, ndugu?) Jacob alimuuliza Yusuf baada ya kumtazama kwa makini na kugundua kuwa hakuwa sawa, japo alijilazimisha tabasamu lakini macho yake hawakuficha huzuni aliyokuwa nayo. Alikuwa akilengwa na machozi.


“Hmm, just leave as it is. Dunia hii ina mambo, kaka,” Yusuf alisema kwa huzuni huku akishusha pumzi.


Muda ule ule madereva wa magari mengine yaliyokuwa nyuma ya gari la Jacob walianza kupiga honi kumtaka Jacob aondoe gari lake kwani alikuwa amesimamisha gari lake katikati ya barabara na hivyo kusababisha msongamano wa magari nyuma yake.


Jacob alishtuka na kuangalia nyuma yake kupitia kwenye kioo cha gari cha katikati, akayaona yale magari ya nyuma yake yakimuwashia taa kumuashiria aondoe gari lake barabarani. Jacob alishusha pumzi na haraka kutoa business card na kumpatia Yusuf.


“If you get a chance, call me my brother, so we can talk,” (Ukipata nafasi nipigie ndugu yangu, ili tuongee) Jacob alisema na kuliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi na kusababisha kelele za msuguano wa magurudumu yalipokuwa yakiserereka barabarani.


Yusuf alibaki amesimama akilisindikiza lile gari kwa macho hadi lilipopotea kwenye macho yake. kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuitazama ile kadi aliyopewa na Jacob na kuanza kuondoka taratibu kuelekea zilipo ofisi zake.


Wakati akitembea mawazo yake yalihamia kwa Jacob, aliwaza kuhusu utofauti wa kipato uliokuwepo kati yake na Jacob, japo walisoma darasa moja na yeye Yusuf alikuwa anamzidi Jacob katika masomo ya darasani.


Jacob Haule na Yusuf walikuwa wamesoma pamoja Tambaza High School na baadaye wakaenda wote katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam. Walipomaliza Jacob alipata nafasi ya kwenda nchini Uingereza alikosomea shahada ya umahili ya sanaa katika uongozi wa masoko (Master of Arts in Marketing Management).


Alipomaliza masomo yake alifanya kazi huko huko Uingereza kwa miaka miwili kisha akarudi nchini na kuajiriwa katika kampuni moja kubwa ya simu kama mkurugenzi wa masoko na alikuwa akilipwa mshahara mkubwa mno.


“Dah, sijui na mimi nifanye nini ili nifanikiwe kama Jacob, maana haya si maisha bali inaonekana kama sisi wengine tupo duniani kwa ajili ya kuwasindikiza wenzetu tu…” sasa kichwa cha Yusuf kilionekana kujaa mawazo mengi sana, mara akamkumbuka tena Jacky.


“Hmm! Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa Belinda. Nikimtumia yule msichana naweza kutoka… yaani nashindwa kabisa kumtoa mawazoni mwangu na sikujua kama ni msichana mtundu kiasi kile. Sijui kajifunzia wapi yale mambo maana anaonekana ni mtoto wa geti kali,” Yusuf alizidi kuwaza na mara akajikuta akitabasamu.


“She’s so sweet, I didn't even expect that one day I was going to betray my marriage, for the first time I have failed to be bold in my position before Belinda,” (Mtamu sana, sikutegemea kama siku moja ningeweza kuisaliti ndoa yangu, kwa mara ya kwanza nimeshindwa kuwa jasiri wa msimamo wangu mbele ya Belinda) Yusuf aliendelea kuwaza na muda ule ule akawa amefika ofisini kwake kwenye jengo la Benki ya Biashara tawi la Lumumba.


“By the way, flies dies on the wound,” (Hata hivyo, nzi hufia kwenye kidonda…” Yusuf alitamka maneno yale na kujikuta akitabasamu huku akiwapita bila kuwasalimia wafanyakazi wenzake walioonekana kuongea na kutaniana wakiwa furaha asubuhi ile.


Wale wafanyakazi wakageuka kumtazama kwa mshangao, walimsalimia lakini alionekana yuko mbali sana kimawazo huku akionekana kuongea peke yake. Wale wafanyakazi wakapigwa na butwaa na kubaki wakitazamana bila kupata jibu.


* * * * *


Saa kumi na mbili jioni ya siku ile iliwakuta Carlos na Jacky wakiwa nyumbani kwa Jasmine katika mtaa wa Butiama eneo la Vingunguti. Jioni ya siku ile hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa imepoa zaidi kutokana na manyunyu hafifu ya mvua yaliyokuwa yakianguka kutoka angani kulikotanda wingu zito la mvua.


Lakini pamoja na hali ile ya manyunyu bado haikuwazuia watu kurandaranda mitaani huku kila mmoja akiwa kwenye pilika pilika zake.


Jasmine alikuwa akiishi katika nyumba ya kawaida aliyokuwa ameachiwa na baba yake, nyumba ile ilikuwa ya vyumba vinne, sebule, jiko, choo na bafu, na ilikuwa imezungushiwa ua mkubwa.


Alikuwa msichana wa umri wa miaka ishirini na tano, alikuwa mrefu kiasi na mwenye weusi wa kung’aa usiochusha, kichwani alikuwa na nywele nyingi mfano wa mmanga, zilizosukwa kwa mtindo wa yeboyebo na kumwagika mgongoni.


Jioni ile Jasmine alikuwa amevaa gauni fupi la kitenge lililoshonwa kwa mtindo wa pencil dress na lilionekana kumkaa vizuri sana mwilini huku likiuchora vyema mwili wake matata wenye umbo la kuvutia. Miguuni alikuwa amevaa sandals ngumu za ngozi zilizokuwa zimeshikilia kwenye miguu yake mizuri kwa kamba.


Jasmine alikuwa na uso wa mviringo na sura ya kitoto isiyoishiwa tabasamu muda wote huku macho yake makubwa na legevu ya kike yakiongezea mvuto wa sura yake. Pua yake ilikuwa ndefu na midomo yake ilikuwa laini yenye kingo pana kiasi zilizopakwa rangi nzuri ya mdomo.


Muda ule Jasmine alikuwa kaketi sebuleni kwake akiwasikiliza wageni wake Jacky na Carlos waliofika kumtembelea katika ugeni ule wa ghafla ambao hakuwa ameutarajia kabisa.


Je, Carlos na Jacky wanataka kumwambia nini Jasmine, na kwa nini wamfuate yeye? Endelea




Jioni ile Jasmine alikuwa amevaa gauni fupi la kitenge lililoshonwa kwa mtindo wa pencil dress na lilionekana kumkaa vizuri sana mwilini huku likiuchora vyema mwili wake matata wenye umbo la kuvutia. Miguuni alikuwa amevaa sandals ngumu za ngozi zilizokuwa zimeshikilia kwenye miguu yake mizuri kwa kamba.


Jasmine alikuwa na uso wa mviringo na sura ya kitoto isiyoishiwa tabasamu muda wote huku macho yake makubwa na legevu ya kike yakiongezea mvuto wa sura yake. Pua yake ilikuwa ndefu na midomo yake ilikuwa laini yenye kingo pana kiasi zilizopakwa rangi nzuri ya mdomo.


Muda ule Jasmine alikuwa kaketi sebuleni kwake akiwasikiliza wageni wake Jacky na Carlos waliofika kumtembelea katika ugeni ule wa ghafla ambao hakuwa ameutarajia kabisa.


Endelea...


Sebule yake ilikuwa ndogo yenye samani za kawaida zikiwemo seti moja ya makochi yaliyoanza kuchoka foronya na meza ndogo ya chakula iliyozungukwa na viti vinne iliyokuwa upande wa kushoto kwenye sebule ile.


Katikati ya sebule ile kulikuwa na meza nyingine fupi na nzuri ya mbao ya mti wa msonobari iliyokuwa imefunikwa kwa kitambaa cha rangi ya samawati kizuri chenye maua mekundu na kijani ya kufuma kwa mkono.


Upande wa kulia wa ile sebule kulikuwa na kabati dogo lililokuwa na vitabu, DVD mbalimbali za filamu, kisimbuzi cha StarTimes na seti ya televisheni aina ya Hitachi ya inchi 21. Pia kulikuwa na deki ya DVD iliyokuwa na vumbi ikiashiria kuwa haikuwa imetumika kwa muda mrefu.


Sakafu ya mle ndani ilikuwa imefunikwa kwa zulia kuukuu la plastiki lililokuwa na rangi ya bluu na maua yenye rangi nyekundu na njano na kuta za sebule ya nyumba ile zilikuwa nyeupe zikiwa zimetundikwa picha mbili kubwa, moja ilikuwa picha ya Jasmine na picha nyingine ilikuwa ya wazazi wake.


Pia kulikuwa na picha kubwa ya kuchorwa ya wanyama wa mwituni maarufu kama Tingatinga na kalenda ya mwaka huo iliyokuwa imetundikwa ukutani upande mwingine wa ukuta.


Jasmine alikuwa akiishi na dada yake, Zaituni Mungi, mtoto wa mama yake mkubwa, ambaye kwa wakati ule hakuwepo pale nyumbani. Aliishi na zaituni baada ya kufiwa na baba yake mwaka mmoja tu uliokuwa umepita, wakati mama yake alikufa wakati Jasmine alipokuwa na miaka kumi, akiwa darasa la nne.


Katika nyumba ile yenye vyumba vinne Jasmine aliishi kwenye chumba kimoja na dada yake pia alikuwa na chumba kimoja na vyumba vingine viwili vilivyobakia alikuwa amevipangisha na hivyo kila mwezi aliingiza shilingi laki moja kama kodi ya vyumba viwili, na alipoongezea na shilingi laki mbili alizokuwa akilipwa kama mshahara kazini kwake, zilitosha kabisa kumfanya asiukimbie mji.


Jasmine aliwatazama Jacky na Carlos kwa zamu na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani akionekana kutafakari sana. Ilionekana kuwa alikuwa njia panda na alishindwa aamue nini kutokana na maneno aliyoelezwa na wale wageni wake.


Carlos na Jacky walikuwa wametumia zaidi ya dakika ishirini wakijaribu kumshawishi akubaliane na kile walichomweleza katika mpango wao wa kupata mabilioni ya pesa lakini yeye alionekana kutokubaliana kabisa na wazo lile.


Baada ya kuonekana kuwa ameshindwa kushawishika ilimbidi Carlos atafute njia nyingine ya kumfanya akubali, alimtazama kwa makini kisha alimtupia jicho Jacky na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Jasmine, hivi unajua kuwa marehemu baba yako alikuwa rafiki yangu mkubwa na si tu tulisaidiana kwa mambo mengi bali alikuacha mikononi mwangu, kweli si kweli?” aliuliza Carlos akiwa amemkazia macho Jasmine.


“Ni kweli, baba, lakini…” alijibu Jasmine kwa sauti yenye mashaka huku akiangalia chini.


“Aah nisikilize kwanza, Jasmine… najua kuwa baba yako hakukuachia rasilimali yoyote zaidi ya hii nyumba ambayo ni ya kawaida sana. Je, unadhani kwa nyumba hii tu bila mipango mingine utaishi vipi katika karne hii? Kumbuka wewe ni mtoto wa kike na kwa umri wako unahitaji kujirusha, unahitaji kuishi maisha mazuri na pia unahitaji kuvaa vizuri… unadhani vitu vyote hivyo utavipataje?” Carlos alisema huku akizidi kumkazia macho Jasmine.


Jasmin alitaka kusema neno lakini alisita na kubaki kimya akimtumbulia macho Carlos. Carlos alitoa kibunda cha fedha kiasi cha shilingi milioni moja na kumshikisha Jasmine mkononi huku akimlainisha na tabasamu kabambe.


“Sikiliza, fedha hizi si hongo bali ni kwa ajili ya kukusaidia chakula na matatizo madogo madogo tu ya hapa nyumbani kwa hizi siku mbili tatu utakazokuwa unatafakari proposal yangu,” Carlos alisema huku akizidi kuachia tabasamu la kumlainisha.


“Lakini naogopa…” Jasmine alisema kwa wasiwasi huku akitamani kuzikataa zile fedha.


“Jasmin, hivi nikueleze mara ngapi? Hundi moja tu ya katikati itakupa shilingi milioni mia moja ya kuchunga maisha yako ya baadaye!” Carlos alimwambia Jasmine huku sura yake ikiendelea kupambwa na tabasamu.


Jasmin alimtazama Carlos kwa wasiwasi, akaziangalia zile fedha kisha akainua tena sura yake kumtazama Carlos, akataka kusema lakini maneno yakawa hayatoki na hivyo kuishia kufumbua mdomo tu, kisha alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku akigeuza tena shingo yake kumtazama Jacky.


Jacky aliachia tabasamu maridhawa ili kumlainisha Jasmine huku akimuonesha ishara ya kumsisitiza akubaliane na proposal ya Carlos. Jasmine alijikuta akichanganyikiwa, aliinamisha kichwa chake na kuanza kutafakari.


Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya wakati Jasmine akiwa amezama kwenye tafakari, muda wote Carlos na Jacky walikuwa wakimwangalia kwa makini huku wakisubiria kusikia jibu lake. Mara Jasmine akainua uso wake kumtazama Carlos huku akilazimisha tabasamu.


ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog