Search This Blog

Thursday 23 March 2023

MTOTO WA KIGOGO - 2

   

Simulizi : Mtoto Wa Kigogo

Sehemu Ya : Pili (2)


Zabi alikuwa kafunga taulo jeupe saafi huku kichani akiwa na kofia ya kulalia ambayo pia ilikuwa nyeupe. Alikuwa kajilaza kitandani akiwa ndani ya usingizi mzito sura yake ilionekana niya upole na ni upole haswaa maana kwake ilikuwa ni tabia mtoto mrefu mwembamba mwenye umbo lililo kidhi vigezo vya kuitwa mwanamke hakika alikwa mzuri mno. Kutokana na zahama alizokutana nazo wakati amelala yuko usingizini mimi nikawwa ninawaza anatafuta nini kwa Tom huyu binti pamoja na kashikashi anazokutana nazo kila kukicha ? Zabi inaonesha kwao kuna uwezo mkubwa tu na inaonesha anakila hadhi ya kuitwa mwanamke na akaishi na watu wenye uwezo mkubwa kielimu na kifedha, wenye mapenzi ya kweli na wanaijua thamani ya mwanamke lakini kwaini Tom ? kijana anayeonekana hanaa mbele wala nyuma hana pakuishi na hata hitaji lake la chakulaa tu kwa siku moja ni bahati kulitimiza. Lakini niliona ya Ngoswa hayanihusu ni kumuachia Ngoswa mwenyewe.


************************************************************

Swala la kodi ya nyumba mwenye nyumba alikuwa kacharuka hashikiki anaongea Lugha ya kwao tu “mura nda kutema mura” ndo kauli iliyo sikika sikutaka hata kuijua ina maana gani lakini iliashilia hali ya hatari akiwa na panga mkononi anaingia na kumchomoa Tom ndani alimokuwa kajilaza akiwepa aibu kutoka. Akiwa kamkaba shati na panga lake mkononi safari mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa. Mwenyekiti anajaribu kusuluhisha kesi inamshinda anatoa rufaa kwenda kituo cha polisi pamba. Basi njia nzima watu wakimshuhudia Tom na mwenye nyumba wake wakitembea kwa miguu huku mwenye nyumba kashika panga mkono wa kulia hao wanashuka mpaka kituo caha polisi Pamba. Kitendo cha kuonekana tu yule jamaa anakuja na panga polisi Wote wanawekwa ndani kwanza kwa masaa matatu. Na baadaye wanatolewa lakini baada ya kusikilizwa kesi yao inaonekana kwamba Tom anatakiwa kulipa kodi ya nyumba ya kipindi chote anachodaiwa ni mwaka mzima na kila mwezi anatakiwa kulipa shilingi elfu tano.


Mose anajaribu kumuwekea dhamana Tom lakini anashindwa hakukuwa na jinsi pesa yote elfu sitini ilihitajika. Mose rafiki wa kweli wa Tom kwenye shida na Raha anapigana huku na kule akitafuta walau fedha ya kuhonga ili rafiki yake aachiwe na alitamani kuizima kesi kabla Tom hajapelekwa lumande kwenye gereza la butimba. Karibia siku inakata bila mafanikio jasho linamtoka. Mose anajaribu kusoma alama za nyakati hakika alikuwa kakwama hakukuwa na jinsi anaamua kukubali matokeo huku akijuta na kumlaani baba mwenye nyumba wa Tom kwa kuwaingiza katika majaribu. Ninaiita hatua ya mwisho kimaamzi Mose anakumbuka ana namba ya Zabi. Bila kuchelewa anachukua simu yake anajaribu kitafuta namba anafanikiwa kuipatana kujaribu kuipiga iliita haikupokelewa, alirudia tena bado haikupokelewa Mose anaishiwa nguvu na kujikuta akiketi chini huku kaiweka mikono yake kichwani. Wakati akijaribu kutafakari lakufanya simu iliita alipoangalia simu ilikuwa ni namba ya Zabi. Akapokea “hallo!”………




Mazungumzo kati ya Zabi na Mose yaliendelea kama ilivyosikika kutoka kwenye simu ya Mose,

“Hallo Zabi ni mimi Mose hapa, ninataka kukujuza kuwa Tom amekamatwa yuko selo hapa Pamba kituoni tafadhali Zabi. Polisi wanahitaji alipe pesa zote anazodaiwa pango la nyumba kwa mwaka mzima, na mimi sina fedha hapa hata kidogo” Mose alimaliza kujieleza huku akionekana kukerwa na hali hiyokuwa.

“Wanadai fedha kiasi gani ? “ zabi alihoji ….. “ni karibia laki moja Zabi … Ni laki Moja” Tom alijibu harakabilakuuma maneno.

“aah sawa ila muache kwanza Tom ajifunze, aijue thamani ya binadamu wengine kuwa wanahaki ya kuheshimiwa, ninampenda saana ila muache. Mose, Tom alichonifanyia nakijua mimi kakaangu achana naye” Zabi alikuwa kama kawekewa kaa la moto kwenye kidonda na kukumbushwa maumivu wakati anaumia baada yakukupata hicho kidonda siku ya kwanza. Mose alijitahidi kushawishi lakini ilishindikana kabisa maana Zabi sasa roho ya ubinadamu ilikuwa imemtoroka imesafiri kidogo hivyo mambo yakwa ndivyo sivyo. Juhudiza Mose zinagonga Mwamba anaamua kuufyata mkia maana nguzo yake na tegemeo la mwisho alikuwa Zabi lakini tayari amekwisha mtosa.

Ni wiki imekatika tangu Tom aswekwe ngomeni kama watoto wa Kiswahili wanavyopenda kuita. Na leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa kesi yake katika mahakama ya mwanzo hapa jijini Mwanza. Mahakama iliyoko jilani na makao makuu ya idaraya maji. Ninaliona gari la magereza likuwashusha mahabusu wanatremka taratibu na hatimaye zamu ya Tom iliwadia. Anashuka kijana aliyenyong’onyea utafikri hajala ana wiki tatu. Tom alikuwa kachoka hana hamu hakuwa hata na tabasamu la kulazimisha, rafiki yake Mose alikuwa pembeni kwa mbaali akimwangalia kwa huzuni na majonzi huku akimshukurumungu angalau Tom amerudi salama, askari magereza baada ya kuhakikisha wameshuka wote walipelekwa moja kwa moja lokapu ndogo ya hapo mahakamani. Huku wakingoja kesi zao kusikilizwa. Tom aikuwa mtu wa tano kuingizwa kizimbani kwa siku hiyo lakini kesi yake haikusikilizwa maana upande wa madai hakukuwa na mtu aliyekujakuisikiliza ile kesi. Hivyo ilipangwa siku nyingine na akarudishwa lumande tena mpaka tarehe iliyopangwa ifike. Mose alikuwa kajiinamia baada ya kesi ya rafiki yake kuahilishwa aliumia maradufu. Aliona sasa ulimwengu umembadilikia, aliona tatzo linazidi kubwa ambalo kwa kawaida asinge thubutu kulitatua. Wakati mose akitoa kitambaa afute machozi anagundua alikuwa kaka jilani na Zabi muda wote huo lakini hakumuona maana alikuwa kwenye dimbwi zito la mawazo. Zabi ananyanyuka kwenda nje na Mose anamfata. Mose, Tom atakuwa ameipata shule sasa fanya maarifa tumtoe. Harakati zilianza murungula ukatumika kwa makarani na hatimaye hakimu aliyesimamia kesi Tom anaachiwa kwa shart moja tu akalipe gharama zote anazodaiwa kitu ambacho ulikwa mtihani mdogo kwa Zabi.

Masaa mawili baadae gari la Zabi lilikuwa nje ya nyumba aliyokuwa amepanga Tom, tom akijaribu angalau kuchambua chambua vitu atakavyoondoka navyo, maana Zabi amemwamuru ahame ile nyumba baada ya kumtoa mahabusu. Kweli hatimaye wanaondoka baada ya kumkabidhi madai yake mwenye nyumba sasa wanarudi ndani ya gari wanaondoka kuelekea Victoria Hotel alikokuwa akiishi Zabi. Baada ya kufika Zabi ananyanyua mkonga wa simu ya mezani anabofya namba kazaa na kisha kuupachika sikion simu iliita kidogo ikapokelewa. Zabi aliweka Oda ya chakula na akamhimza Mhusika kufanya haraka. Haikuchukua muda kweli wahudumu waliongozana sebleni pale na tray za vyakula walifika wakatenga na kuondoka zao. Hakukuwa na mazungumzo kati ya Tom na Zabi ila kulionekana kuwepo na kuogopana. Tunaiiita nidhamu ya uoga. Waliangaliana kwa kuogopana basi Zabi alipakua chakula cha Tom na kumkabidhi sahani iliyojaa Wali kuku huku jipande la samaki mkavu likiwa juu yake, harufu ya chakula ilivutia saana kilinuki vizuri na bila shaka kilikuwa kitaamu haswaa.

Baada ya chakula tom hakuwa sawa kiakrialikuwa mbaali kimawazo, alikuwa kaumizwa kisaikolojia, mara kadhaa alikuwa akiduwaa bila sababu. Hii ni kwasababu ni mara yake ya kwenza kwenda kukaa jela kwani pamoja na ujanja wake wote, utapeli, wizi na ujuaji wa kijanja kwesi zilikuwa zikiishia polisi tu na anaachiwa huru lakini hii ilikuwa kesi ndogo saana lakini ikamkamatisha mpaka ngomeni. Waswahili husema ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu. Basi Zabi anajitahidi kuwa naye karibu mbali na tom kuwa mbali kimawazo lakini Zabi anajitahidi kuwa naye karibu anamsemesh na hata kujaribu kumchekesha, Zabi aliujua wakati mgumu aliokuwa nao Tom, aliyajua mambo makubwa aliyokuwa akiwayawaza au aliyokutana nayo huko mahabusu. Zabi alijitahidi saana kuwa naye karibu kumjali na kumtunza alimfariji na kumsihi apunguze mawazo ingawa ilikuwa ngumu saana kwa Tom. Basi zabi alikuwa akiendelea kumsihi saana tom akijitolea kumpa furraha na faraja wakati wote. Zabi anamapenzi ya dhati ambayo hayajawahi kutokea kwa miaka mingi iliyopita katika ulimwengu huu.

Siku tatu zimepita tangu Tom atoke gerezana alikokuwa mahabusu, sasa amerejea katika hali yake anaonekana mwenye nidhamu na mtiifu yuko karibu saana na zabi na leo wanashindana mchezo wa kuweka uzi kwenye sindano, ulikuwa ni mchezo wa kujiburudisha kwa wapeni hawa na kweli ulileta burudai kubwa sana kwani wanataniana na kurushiana mito, kupigana kwa kutumia mito ndani kuna furaha kubwa. Hakukuwa na buguza kwani walitulia wawili hawa kama wapenzi na kwa mara yakwanza ninaona Tom amerudisha mapenzi kwa Zabi kinyume na awali. Wawili hawa wanaonekana ni wapenzi haswaa kinyume na awali ilivyokuwa Tom hakuwa na hisia zozote za mapenzi kwa Zabi. Lakini leo wanaonekana wanaongea na kusikilizana Tom alionekana kuwa muungwana anyemjali Zabi anambembeleza kwa upole saana. Hali hii inatoa nafasi ya madeko kwa Zabi akimdekea Tom haki ya nani ungewaona mnh! Ungetamani kuwa wewe ndo Zabi au Tom. Uhalisia wa Tom ambaye zabi alimtaka ndo huu., mwanamme ajue kujali, kutunza, kubembeleza na siyo tom wa awali aliyekuwa anajua kufoka, kuzira, kudharau na kuumiza hata mimi namuona Tom mpya, Tom aliyetengenezwa na kuzaliwa, Tom mnyenyekevu na mtiifu upya haya yanaitwa mapenzi.

Malaika beach iliyoko eneo la ilemela, ninawashuhudia wawili hawa wakikimbizana kando ya ziwa huku wakimwagiana mchanga na maji, Tom na Zabi wamependeza wanafuraha yakutosha tu. Nazidi kuangaza mcho kila wanapokanyaga niko nyuma yao kwasababu nilivutiwa saana na mahusiano yao. Kwenye bustani nzuri nyasi nzuri katikati ya mimea jamii ya mitendeiliyokuwa imepandwa pale Beach Tom na zabi wamejuipumzisha chini yake huku wakinyweshana juice kupitia milija wa makopo yao. Wazungu husema Wow! Kuudhihilisha mshangao wa furaha. Na ndivyoilivyokuwa kwangu. “Baby naweza kukuliza maswali?” Tom alihoji … “usijari uliza tu mpenzi wangu? .Tom alisita kidogo akamtizama usoni Zabi kisha akamchombeza kwa busu shavuni, kisha midomoni kabla ya kuzama kinywani kwa dakika kadhaa. Kisha wanaachina na hadithi ikawa hivi.

“Zabi natamani kuijua historia ya maisha yako, nataka kujua umezaliwa wapi, historia ya wazazi wako wako wapi? Kingine hapa mwanza ulikuja lini hapa na unafanya nini ?” Tom alikuwa kamaliza kuuliza maswali yake na alikuwa kimya akingoja majibu. Zabi alimtizama akacheka kidogo kisha akamjibu “kwa sasa sishangazwi na maswali yako ya busara now you’re a real Tom niliye mtaka” wote walicheka kwa furaha huku wakikumbatiana, kisha Zabi alianza kuhadithia hivi. Yeye ni mtoto pekee katika familia ya bwn Mohamed said, mtanzania mwenye asili ya kisomali, na mama yake alikuwa ni raia wa Kigali Rwanda walikuwa wakiishi Dare Es salaam maeneo ya Masaki ndiko aliko zaliwa Zainabu.


Zainabu anaendelea kusema kuwa alimpoteza baba yake akiwa na umri wa miaka minane tu katika kumbukumbu inaelezwa kuwa baba yake alikuwa ni mmoja wa wadhamini wa utekeji wa meli za mizigo za kimarekani na za ulaya katika upwa wa Mombasa. Mohamedi Said baba yake Zabi aliuwawa na serikali ya Somalia mapema alipokwenda kuzungumza na kikosi cha Al-shababu ili wampe vijana kwaajili ya kufanya kazi ya utekaji wa baadhi ya meli zilizotarajiwa kuingia katika upya huo. Ndipo habari zilivuja na akapigwa akakamatwa lakini aliuwawa kabla ya kufikishwa mahakamani kwani alikuwaakijaribukuwatoroka asikali, wa kisomali walimpiga risasi akafa. Nihadithi ambayo Zabi aliikuta baada ya kuhadithiwa na mama yake ambaye pia alimpoteza miaka miwili iliyoisha kwa ugonjwa wa moyo. Zabi anaeleza baba yake ilisemekana alikuwa mtu mzuri saana kwa familia yake kwani aliwajali na kuwekeza fedha za kutosha, hakuwa katili ila mpole na mwenye upendo kwa familia, ila hakuwa mtu mzuri katika jamii kwani ana historia kubwa na mbaya ya uvamizi na utekaji wa aina mbalimbali katika maeneo mbali mbali ya ukanda wa afrika mashariki hasa nchini Kenya eneo la Mombasa na Nairobi. “Niliachwa mimi kama nilivyo nikiachiwa makampuni makubwa ya kusambaza mafuta nchini Kenya na Uganda, nina store za vyakula afrika mashariki nzima, mimi ndiye mkurugrnzi wa makampuni ya ZabSaid Interprises. Ninakila kitu katika maisha yangu ninauwezo wa kuishi maisha niyapendayo, ingawa kuna vitu ninakosa Tom Furaha, sina ndugu, sina dada, sina kaka, sina mjomba wala shangazi katika nxchi hii” zabialifafanuahuku utulivu ukizidi kushika hatamu.


Zabi alimwambia Tom amempenda kwa moyo wake wote asifikri hawezi kupata mwingine, anauwezo wa kufanya lolote lakini haoni jipya katika ulimwengu huu “mimi ni mzuri, si kama najisifia nimekuwa na wanaume tofauti mpaka huyo mtoto wa raisi wa nchhi hii amewahi kuwa mpenzi wangu, lakini nanaamini nilikuwa sijapata nafasi ya kuenda kama nilivyoopenda kwako Tom.” Zabi alimaliza. Tom akiwa kajiinamia asijue cha kujibu aliishia kuangua kilio huku akimpa pole Zabi, maisha huwa yana changamoto zake kiukweli hadhi ya Tom haikustahili hata robo kuishi na Zabi hii ni kama bahati ya mtende kuota jangwani. Baada ya Zabi kueleza kwa ufupi sasa ilikuwa ni zamu ya Tom. Ilikuwa ni ngumu saana kuanza lakini hakukuwa na budi ilimpasa afanye hivyo. “Zabi kwanza samahani saana nimekuwa nikiishi maisha ambayo siyo halisi kulingana na Familia yangu, ninaigiza maisha yasiyo yakwangu, ninakopi maisha kinyume na uhalisia wangu Zabi ninakupenda. Kiuhalisia ni kwamba mimi nimezaliwa kkatika familia masikini, na ni masikini haswaa, masikini wakutupwa ni familia ambayo hata kuupata mulo mmoja kwa siku ni ndoto. Ninatokea kijiji kimoja kilichoko magharibi mwa mji wa sengerema kilomita zisizo pungua arobaini kutoka sengerema mjini, ni kijiji cha Lushamba ndiko niliko zaliwa. Kijiji hiki kipo ndani ya tarafa ya Buchosa na kata ya Bulyaheke. Nifamilia masikini saana iliyo na watotokumi na wawili mimi nikiwa mtoto wakwanza katika familia hiyo. Nimefika hapa mjini baada ya kukimbia matatzo ya chaa na taabu nyingine. Mama yetu ametulea katika mazingira magumu mpaka sasa anaendelea kuwalea wadogo zangu ambao hata hivyo sina msaada wowote kwake na wadogo zangu tangu nimeondoka.” Tomu alikohoa kwa kwikwi maana wakati akisimulia machozi yalikuwa yakimtoka bila kizuizi. “Zabi sikuwa nakufanyia jeuri, sikuwa nakudharau ila nilikuwa natafuta namna ya kukukwepa mimi na wewe hatuendani, kwa sababu mimi ni masikini, kapuku, sina lolote wala chochote katika maisha haya. Niligundua unanipenda saana hukuwa tayari kunielewa kwa namna yoyote ile nilijua unaamini kuwa maisha yangu na wewe yalishabihiana lakini kiuhalisia mimi sikuwa hata nakusogelea japo kwa robo” maelezo ya Tom yaliuchoma saana moyo wa Zabi alikuwa akilia na kuhudhunishwa na maelezo yale.


Baada ya maelezo hayo Zabi alimuuliza Tom hajafikakwao kwa muda gani tomu alijibu alitoka kwao akiwa na umri wa miaka 11 mpaka leo ana miaka 28, ni sawa na miaka 17 hajafika nyumbani. Zabi aliamuru “kesho asubuhi tunaenda kwenu tukamuone mama yako.” Kauli iliyo mshitua Tom….




Tom alijitahidi kupinga ila alikuwa kabanwa na Zabi hakuwa na jinsi kwani hakuwa na sababu yoyote ya kukwepa kwenda kwao, alilazimika kuwa mpole na kukubaliana na hali. Ni lavena supermarket Zabi muonekano wa Tom ukiwa tofauti saana asubuhi hii alikuwa katoka salon kuzilekebisha nywele na ndevu zake alionekana ni mtu fulani anaejiheshimu. Siku hii alikuwa katinga jeans yake ya kaki na t-shirt nyeusi. Hapa lavena wawili hawa wanaonekana na vitroli vya kubebea bidhaa kadhaa vikiwa vimejaa mapochopocho yakutosha ikiwemo Unga wa ngano, unga wa ugali, sukali, dumu ndogo za mafuta yakupikia, sabuni, dawa za meno n.k. basi baada ya haya mahemezi yaliyo chukua muda wa saa nzima na nusu siku hiyo Zabi aliamua kutumia gari yake aina ya Ford ilikuwa ni pick-up, alifanya hivi ili abebe huo mzigo, pili alifanya hivyo kutokana na njia walizotakiwa takiwa kupita kwenda eneo walilokuwa wakienda zilikuwa ni korofi, hazipitiki kiurahisi. Baada ya kuona kwamba kila kitukilikuwa sawa Zabi aliamua kupita maduka ya nguo na kuchukua nguo kadhaa za mama mkwe wake na ndugu wa mpenzi wake.


Safari inaanza na hatimaye waanza kuliacha jiji la Mwanza Zabi na Tom wakiwa ndani ya kivuko cha kigogo ferry kuelekea Busisi hatimaye wanavuka na kurudi barabarani. Ilikuwa ni safari isiyo chosha mpaka kuifika Sengerema mjini. Lilikuwa ni eneo ambalo Tom alilifajamu vilivyo lakini kwawakati huu alikuwa ni mshamba tu kwani kulikuwana mabadiliko makubwa saaana yaliyoanyika. Kuhusu miundo mbinu kama barabara na umeme, maisha ya watu nyumba zilionekana kujengwa katika ubora wa hali ya juu. Basi baada ya kutembea kidogo wakiupasua huo mji mdogo wanaifikia njia wliyotakiwa kupi ni barabara ya Nyamazugo, Zabi ndiye alikuwa kwenye usukani huku kaweka wimbo wa Nameless unaitwa Coming home (rudi nyumbani). Mbali nakuusikiliza huku akifurahi Tom alitakiwa kuijua maanaa liyokuwa ikikusudiwa na Zabi juu ya huo wimbo, Zabi alimuhimiza Tom arudi nyumbani japo ilikuwa ni kwa kutumia njia ya mafumbo. Barabara hii pia ilionekana kumshangaza Tom kwani haikuwa na kiwango hiki wakati akitoka kwao barabara ilikuwa mbovu kuliko maelezo ila leo inapitika, kwani angalau ilijengwa kwa kiwango cha molamu (changalawe). Basi taratibu wanazidi kuvipoteza vijiji mle njiani wakianza na nyamazugo yenyewe, nyakasungwa, luchiri, Nyakalilo, Ilenza na sasa wako Kakobe na harufu yakufika kwako Tomu ilikuwa imeanza kunukia kwani walikuwa karibu saana. Taratibu walee wanaingia kijiji cha Nyambeba, Bulyaheke namaanisha sasa wako ndani ya kata yao, na haimaye wanauvuka mto Chai mto mkubwa mno ulitenganisha kijiji cha Lushamba na Bulyaheke walikuwa ndani ya kujiji cha Lushamba sasa kijiji chao walihitaji dakika zisizozidi kumi kwenda kulipaki gari lao nyumbani. Ndani ya gari mwanzo kulikuwa na maongezi yakila aina lakini kadri muda ulivyozidi kwenda kulikuwa kimya na ilikuwa kimya haswaa. Taratibu Tomu alianza kukishangaa kijiji chake kilikuwa kimepiga hatua angalau kwa kujenga nyumba za kisasa, mabadiliko ya shule yake yamsingi aliyosoma hata hivyo hakufanikwa kumaliza sasa shule ilionekana namvuto kidogo kwake. Hakujua pia kulikuwa na shule ya sekondari iliyokuwa imejengwa hapo jilani. Zahanati na vitu vingi amabavyo hakuviacha. Taratibu Zabi anaoneshwa kwa kidole kuliegesha gari lake nyuma ya jumba lenye paa lililoonekana limechakaa, huku nyumba ikiwa na nyufa nyingi Tom alikuwa ameesha anza kutokwa machozi huku akiufungua mlango wa gari lake.


Tom anashuka ndani ya gari hakuna aliyemjali, maana hata ndugu zake hawakuhangaika naye watu walikuwa wakiishangaa familia ya kina Tom kutembelewa na mtu mwenye uwezo, anayemiliki gari basi watu walijaa wakishangaa kulizuka gumzo mtaanai na hadithi ikawa ni juu ya gari hilo. Tom pia hawakumbuki ndugu zake maana ukiacha dada zake aliofatana nao walikuwa wakubwa kumbuka mama yake alikuwa na watoto kumi na wawili huku akiwa amebahatika kuzaa mapacha maratatu. Tom anayaangalia mazingira hayakuwa yanamlizisha Zabi alimjua Tom hivyo hakuhitaji ufafanuzi kuwa hapo ndo kulikuwa nyumbani alipozaliwa Tom. Mama wa makamu apataye miaka hamsini alijilaza kwenye kivuli cha mti mkubwa uliokuwa katikati ya uwanja wa nyumba ile. Tom alimtizama kwa mbali mara anatoka dada mmmoja ndani alikuwa mrembo saana tu lakini kulingana na hali ngumu ya maisha na mazingira alijaribu kujikwatua lakini bado balaa la umasikini liliufukuzilia mbali urembo wake, kwani alikuwa kadhoofu bila shaka ni sababu ya lishe mbovu na mazingira moabovu ya familia yao. “Thomas” aliita dada yule baada ya kumkodolea kwa makini sana jamaa huyu hatimaye anagundua ni kaka yake waliye pishana miezi tu wakati wa kuzaliwa. “naamu ni mimi mdogo wangu Misoji.. nimerudi… nimerudi nyumbani kaka yako” Tom alimkumbatia kwa nguvu huku akitokwa machozi. “mamaaa… mamaaaa amka Thomas amekuja” ilikuwa ni sauti ya Misoji dada wa Thomas mama anakurupuka usingizini na kumkimbilia mwanawe mama hakuiona furaha bali uchungu uliuma na kuangaua kilio upya. Mama aliishika mikono ya Thomasi akitaka kuhakikisha kama kweli ni yeye bila shaka aligundua kupitia vidole ya mikono yake kwani kidole kidogo chwa mwisho Thomas aliungua uji akiwa mdogo hivyo kulikuwa na kovu lisilo futika. “nikweli ni mwanangu, niyeye … umerudi baba? … karibu saana nyumbani, karibu mwanangu” mama alitia huruma Zabi alikuwa akishuhudia huzuni na furaha iliyochanganyika na maumivu iliyokuwa imemfika mama Tom.


Basi wakakaribishwa ndani na kuketi kwenye viti vibovu vibovu huku kila kona kukionekana kuwa na matandiko yaani vilago na mikeka ilikuwa imekujwa wakati huu wa mchana ambayo ilitakiwa kufanya kazi mara tu ifikapo saa tatu usiku. Tom alikuwa kaongozana na Zabi alikuwa anashindwa aanze vipi kumtambulisha kwa mama yake maana Zabi alionekana kuwa kimya huku akimsubili mwenyeji wake amtambulishe lakini ilionekana Tom alikuwa kama anawasiwasi. “Thomas na mgeni mbona hujatuambia ni nani ?” mama alihoji “naitwa Zainabu ni rafiki wa Thomas mama”. Tom hakuwa na nyongeza basi waliendelea na mazungumzo. Huku baadhi ya wadogozake walikuwa wakija na kumsalimia Tom.. lakini pamoja na wote kuja, wengine aliambiwa wameolewa na wengine wapo katika harakati zamaisha bado Tom anawakumbuka wadogo zake wawili ambao hajapata taarifa zao walikuwa ni Kedison na Kened mapacha wa kwanza wa mama kwa mama yake. “mama Kened na Kedison wapo wapi maana hujanipa taarifa zao. Mama anaangua kilio ambacho kinamchanganya Tom anajitahidi kumbembeleza lakini ilishidikana, Tom wakati anageuka upande wa pili mlangoni alikuwepo Misoji naye alikuwa akilia kwa uchungu saana. “Tomas wadogo zako walifariki miezi miwili iliyopita walikufa kwaajali ya basi walikuwawakirudi chuoni Dar es salam walikokuwa wanasoma na ulikuwa ni mwaka wa tatu wa masomo yao ya udaktari. Ni wadogo zetu waliojitolea kuiokoa familia lakini ndo hivyo mungu amewachukua, ilikuwa ni ajali mbaya mno kiasi kwamba aliye pona kwenye ajali hiyo basi aliondoka na ulemavu wakudumu. Ni miili tu ndiyo iliyotufikia hapa Tom hatukuamini ila uhalisia ndo huo, si wao tu tunatarifa za kifo chako zaidi ya mara nne Thomas mara umechomwa moto kwa wizi, umezama majini kwenye shughuli za uvuvi n.k.” Misoji alimaliza kutoa ufafanuzi juu ya swali laTom. Tom aliumia sana kuwapoteza ndugu zake alitamani bora mungu angemchukua yeye kuliko kuwachukua wadogo zake Kedison na Kened na kizuri zaidi hakujua kuwa familia yao inaweza kuwapata wasomi wa kuikomboa kumbe mungu aliwaandaa hawa madaktari mapacha lakini wameondoka kabla hawaja itimiza ndoto, “ni changamoto za maisha zimekwamisha harakati hizi” Tom alijisemea


Majira ya saa saba Tomas na akiendelea kupiga soga na mama yake alionekana mwenye nidhamu ya hali ya juu kuliko kawaida yake. Maji ya kunawa yanatangulizwa, linasogezwa dumu la maji liliotumika kama meza hatimaye lilikuja sinia kubwa saana la viazi vitamu vilivyopikwa bila kumenywa maganda. Tom alimhurumia sana Zabi, Tom anaangaza huku na kule akiwa kaduwaa mama anamkalibisha Zabi na Zabi anakipokea kipande chakiazi alichu katiwa na mama Tom kama ishara ya kuvunja mwigo na kuundoa ugeni, mpaka hapo ugeni ulikuwa umekwisha. Tom alikuwa akihahaha na jasho jembamba lilimtoka, lakini hakuamini alichokiona. Zabi alikuwa akila viazi bila wasiwasi kupitia walichokuwa wakikifanya mama na wifi yake jinsi yakuvimenya vile viazi, mwanzo ilimpa tabu lakini kadri muda ulivyozidi kwenda hatimaye akawa mtaalamu na kumudu kuvimenya kwa ustadi mkubwa, hakuna aliyeamini, mama, Tom, Misoji na wengine walikuwa kimya wakimtizama hakuwajali aliendelea kushusha kiazi kimoja baada ya kingine taratibu hakukuwa na shaka wala wasiwasi. Maswali ya kujiuliza huu ulikuwa ni upendo toka moyoni au limbwata ?.. sikuyapata majibu… ngoja tuone hatima yao.


Basi usiku baada ya kupata pilau na kuku lililosimamiwa na Zabi kimapishi kwenye jiko la kuni, ulikuwa ni muda wa kulala. Chini kulitandikwa mkeka, hakukuwa na nyumba ya falagha hivyo kulitengwa na pazia lililoshonwa na magunia. Vijana walilala upande huu na Tom na mpenzi wake wakalala upande wa pili hakukuwa na usingizi kabisa maana matandiko yalijaa kunguni, chawa na mbaya zaidi kulikuwa na utitiri na viroboto, Tom na zabi wanashindwa kabisa kulala na waliwasikia tu wenzao wakikoroma huku wao wakiwasaidia kulinda mmbu na wakiyaumiza masikio yao na ngozi zao zilizokuwa zikipapaswa na utitili kwa kuzikuna kwa nguvu. Ni mwendo wa kujikuna mpaka inafika saana nane usiku Tom alimhurumia Zabi na kumuomba akalale kwenye gari. Zabi alikataa lakini kadri muda ulivyo zidi kwenda Zabi alishindwa kabisa kulala ilimubidi kukubali, Tom aliwasha kibatari akachukua funguo na wakaenda kulala kwenye Gari.


Asubuhi kuna pambazuka nawaona wawili hawa wakiwa bado wamekumbatiana nyuso zao za upendo, kelele za kuku na ndege wengine zilichangia kuwaamsha usingizini. Wanaamka zabi anamuagiza Tom ampe jembe kulinga na mazingira ya pale nyumbani kuchakaa, Tom anafanya hivyo Zabi ananza kurekebisha mazingira ya nyumbani yaliyokuwa machafu kupita kiasi nyasi zilikuwa nyingi zimeota mpaka mlangoni. Tom alishangazwa na kitu hapo hakuamini kuwa Zabi anweza kushika jembe? Kwa mara yakwanza anaona Zabi alipalilia eneo lote linalozunguka nyumba na kuusafisha uwanja ukawa safi kabisa. Kisha alianza kuzoa takataka akisaidiwa na mpenzi wake. Haya ndiyo yalikuwa maisha halisi ya kijijini alikozaliwa Tom, kuishi katika mazingira machafu ilikuwa ni sehemu ya maisha yao, nikwasababu hawakuujua umhimu wa usafi. Zabi anamhimiza Tom akirekebishe choo kilichokuwa kimejengwa kwa makuti ya mawese kwani hakikuwa kimefunikwa ilikuwa ni aibu mtu mzima anaingia chooni huku akioneka. Tom akishirikiana na Wadogo zake kama Ben, Luckas na james walifanya hiyo kazi kwa muda wa masaa kadhaa ilikuwa imekamilika.


Wakati huu Zabi anarudi ndani na kuanza kupangua kila kitu mwanzo walimuona kama mwehu alitoa kila kitu na kukiweka nje, humo ndani ndimo walilala, kuku, bata, paka, mbwa lakini pia kulikuwa na maatamio ya kuku waliokwisha kutotolewa siku nyingi. Lakini tusisahamu watu ndimo walilala pia. Zabi alianza usafi kutoa kila kitu nje, baadae anaungwa mkono na wifi yake Misoji sasa nae anabadilika kimawazo wanamwaga maji mengi kutoa vumbi mule ndani, na baadae Zabi anampa Tom hela akatafute dawa ya kuuwa viroboto kunguni na kadhalika Tom alifanya hivyo na akapulizia ndani kote. Wakati haya yote yakifanyika Zabi anafikri kitu na inamchukua kama dakika tano hv akiwa kaduwaa anamuita wifi yake. “Misoji” kwa kutumia ishara ya mikono alimaanisha aje kumsikiliza. “mbali na sengerema mjini wapi kuna kimji kikubwa angalau naweza kupata huduma ya mahitaji mbalimbali? Zabi alihoji ‘aaha ni kanyala au nyehunge kanyala siyo mbali ila Nyehunge ni senta kubwa ila ni mbali” Misoji alijibu “sasa naomba niondoke na Ben na Luckas” Zabi alisema, basi zabi akawaita Beni na Lucks ambao hawakutofautiana sana kiumri kwani walionekana kulingana kama mapacha Beni alikuwa na miaka 17 na Luckas akuiwa na 19. Safari ya kwenda nyehunge ilianza wakipitia Iligamba, Bulyahelu, Mizulo, Bupandwa, Buhindi, Isaka na hatimaye Nyehunge. Zabi anachukua vitanda visivyo pungua 10 magodoro kwa kila kitanda mashuka, mapazia na kila aina ya mahitaji ikiweo viti na meza pia, kisha anachukua baadhi ya vitu vya ndani hakusahau Sola na betri zake, baada ya mahemezi hayo alikodo gari ndogo ya mizigo alipandisha mizigo yate kwenye kenta na kisha kuongozana nao mpaka nyumbani safari iliyotumia takribni dakika 30. Tom alishangazwa na kitu alicho kifanya Zabi alibaki kaduwaa na asiamini aliyokuwa akiyaona. Vitanda vilifungwa mle ndani na nje kulitengenezwa hema la dhalura lililokuwa mfano wa nyumba ambalo Zabi hutembea nalo kwenye gari lake, wakati akisafirini kwa tahadhari ya kuharibikiwa na gari sasa ilibidi litumike kama nyumba yao Zabi na Tom. Familia haikuamini kila mtu alikuwa akifunika kinywa na kutumbua macho kama kama sangara aliyekanyagwa na mvuvi.


Siku hiyo sola ilikuwa imefungwa hakukuwa na haja ya vibatari, moshi wa mafuta ya taa uliagwa na kuukaribisha ulimwengu mpya wa teknelojia. Kutokana na shughuli pevu iliyofanywa na zabi Tom anaamua kuingia jikoni leo kuipikia familia chakula cha usiku. Chikolao la kuni lilikuwa limebomoka upabe na kuzibwa na vipande wa mabati mabovu hata hivyo haikusaidia kuuzuia upepo kuingia ndani Tom alihangaika na jiko lake hatimaye samaki wake aina ya sato wabichi (fresh) walikuwa wameiva, huku upande wa pili wa mafiga alikuwa kainjika sufuria kubwa la wali utafikri anapikia sherehe ya ubatizo. Kama kawida kwa mara ya kwanza nayashuhudia manjonjo ya Tom jikoni akibadilisha mwiko na mikao hatimaye naona akichukua koleo na kuchota mkaa wa moto alio uweka juu ya mfuniko wa sufuria alilokuwa akipikia. Kisha alitoka zake nje huku akipikicha macho kwa maumivu yaliyo sababishwa na moshi huku akikenua kama kalazimishwa kutabasamu.


Chakula kilikuwa tayari mezani ni majira ya saa tatu na robo usiku, kwa mara ya kwanza Zabi anakutana na chakula kilichopikwa na Tom. Alipokionja hakuamini kwanza aliachia tabasamu zito kisha akauliza nani alikufundisha kupika tom hakujibu ila alionesha kwa kutumia kijiko kilichokuwa mkononi alimaanisha Mama Tom. Zabi alicheka “ni mama kweli? … siwezi amini hili.’ Wote walicheka mama alitabasamu kisha akadakia “ kipindi baba yao yuko hai hawa watoto mbona walikuwa wakichekelea tu nilikuwa napika sizani kama kuna mtu wakunifikia katika ulimwengu huu. Mimi upishi nimesoma hotel management kabla sijaolewa na badae baba Tom alinizuia kufanya hizi kazi, Ni maisha tu mama mkwe… “ alitumia neno mama mkwe kukwepa kuliita jina Zabi maana kimaadili ya kisukuma haikuwa haki mkwe kutajajinala mkwewe. Basi wote walikula wakakifurahia chakula na baada yakula wakashukru na kwenda kulala. Ndani ya nyumba yao ya dharula upendo ulikuwa umeimalika Zabi na Tom kama kawaida ni kutomasana na kukumbatiana huku wakipeana pongezi juu ya mambo kaza wakaza ambayo Zabi kafanya ndani ya familia ya Tom na mambo kaza wa kaza ambayo Tom kafanya. Bila shaka hakukuwa na pingamizi tena kama jana leo hii walirudi kwenye hali yao kama wapenzi walijitupa kwenye jitanda lao jipya lililokuwa na godoro bora kabisa bila kiroboto wala kunguni, hakuna uvundo wala kelele. Hakika ilikuwa ni kubadili mikao tu huku wakitupa mipira iliyotumika na hatimaye wanalala usingizi mnono huku wamekumbatiana kwaupendo.


********************************************************


Upande wa pili usiku ulele kila mtu amelala kwa pozi lake Luckas alijiegesha huku miguu ikiwa chini chaa jabu ameuchapa usingizi mpaka asubuhi huku miguu ikiwa chini na kiwiliwili chake tu yaani kuanzia kiuno ndicho kilikuwa kwenye godoro, Ben naye kautandika mshazali kona kwa kona hana habari huku akiota ndoto zake za kuongea usiku kucha utafikri alikuwa na kikao mule ndani. Upande wa mama kautandika usingizi mpaka kesho yake saa sita napo kabahatika kuamshwa na Tom baada ya kuona haamki Tom akaamua kwenda kumchungulia kwa mashaka. Duh! kiukweli maisha yalikuwa yamebadilika saana nyumbani kwa akina Tom ni gumzo la zali la mentali kila mtu alihadithia. Huku watu wakikili kuwa kila mtu hutembea na nyota yake ila tatizo hatuibonyezi nyota na badala yake tunabonyeza saana alama ya reli hali inayosababisha nyota kwenda mbali. Kama ridhiki ipo ipo tu mbali na mama kuwazika wanawe aliowategemea lakini leo Tom anaonekana mkombozi ndani ya hii familia.


Ni jioni ya siku hiyo baada ya siku kwenda vizuri Tom aliamua kumtoa out Zabi kwenda bushi beach ni ufukwe wa asili uite Karaza upande huu kulikuwa na mchanga saafi, uoto wa asili hali ya hewa nzuri siku hiyo hakukuwa na wimbi kabisa ndani ya ziwa Victoria. Basi uneyaangalia maji ungetamani kutembea juu yake kwani yalitulia tulii, eneo hili walikuwa wamejiachia Tom na Zabi kwenye jiwe moja kubwa lililokuwa ndani ya maji ambalo wamelifikia baada ya kuogelea. Waliketi huku wakizitizama mashua, boti za mbao, meli ndogo na kadhalika lakini pia kulikuwa na jamaa wengi waliovua samaki kwa kutumia ndoano na boti zao zilizotengenezwa kwa maboya ma matete wao huziita Nzwenge ni ubunifu mzuri ila ni hatari saana kwa maisha ya mwanadamu kwani si salama wa siyo imala. Kalikuwa niakutalii ka ndani siku ilipendeza sana. Wakiwa wamekumbatiana kwa furahaTom hakusita kuoneha hisia zake “Zabi ningeambia nikuache wewe au niuawe kama stakuacha hakika ningetumia neno langu la mwisho katika ulimengu huu kusema…. “Zabi nakupenda” Zabi alidakia huku akimcheka. Tom aliishia kucheka tu maana hakuwa na jipya tena. Waliendelea kuogelea na kucheza ndani ya maji huku wakiigiza michezo mbali mbali ikiwemo kuchora juu ya mchanga uliokuwa umelowa baadaya kupigwa na wimbi ilionekana alama ya upendo (kopa) imechorwa juu ya mchanga huo . Zabi aliichora na kisha wote wakaketi upande na kugusianisha vichwa huku wakipiga picha za ukumbusho kupitia simu zao.


Hivi ungemueleza nini Zabi kuhusu Tom akakuelewa ?, bado nilikuwa na mashaka na Tom lakini nimeanza kumuelewa pia pengine nikweli kapenda ila sina uhakika. Basi ni majira ya saa moja usiku giza ndo kwanza linaanza kuingia. Kweli pata fedha ndugu wakukumbuke huwezi amini Tom leo anashangaa familia yao inapokea wageni watatu ambao walichangia kuivuruga familia yao baada ya baba yake Tom kufariki na baba zake waliotapanya mali na kujimilikisha huku wakiiacha familia ya Mjane mama Tom ikitabika. Tom anawakuta baba zake hawa wameketi, bila shaka wamezipata taarifa kuwa Tom karejea. Hawakuwa mbali lakini huwezi amini hata kifo cha Kenedi na kedison hawakuhudhuria mazishi mmoja yuko kijiji cha pili, mwingine mtaa wa tatu na mwingine ni kijiji cha tatu ng’ambo ya pili. Swali leo wamefata nini. Nakumbuka hawana msaada wowote katika familia hii tangu baba yao Tom amefariki, kikubwa walichofanya ni kujimilikisha mali na kuitosa familia. Basi Tom aliwasalimia kwa furaha ingawa mama Tom kwa upande wake hakuwa anakubaliana kabisa na kuendelea kuwa nao hapo nyumbani.



Basi Tom na Zabi waliingia chumbani kwao na badae Tom alitoka, “we Tom samahani njooo hapa” mzee Kibopa baba mkubwa wa Tom aliita. Tom alipofika anakutana na kizingiti, mzee Kibopa alianza kueleza kilicho waleta alisema wamesikia taarifa za ujio wa Tom na anaishi na mwanamke bila wao kuhusishwa kama wazazi hivyo wameamua kuja kumfukuza hapo mpaka atakapo fuata taratibu za kimila za kumleta mke ndani ya nyumba ya kaka yao. “Tofauti na hivyo tunaomba uondoke na huyo unayemuita mkeo maana sisi tumefika hapa hatuelewi kwanza nyupi ni mwanamke na yupi ni mwanamme maana tunaona wote mna suruali, harafu kwanini ukaoe mjini ? umeshindwa kuwasiliana nasisi wazazi wako tukakutafutia mke anaye jiheshimu hapakijijini ulipo zaliwa ? mpaka ukaokote okote jimwanamke huko mjini sijui kabila gani hilo mtaoa mpaka michaga mfirisike pumbavu zenu kazi kuokota okota tu. Kama ni kupotea wewe ni mwenda wazimu na ulipotea kweli sina chakusema mbele ya kipofu kama wewe, kiziwi kama wewe .. pengine baba zako nao waseme.” Kibopa alimaliza.. mzee Masalu akadakia “toka lini mzazi akajadili na mtoto, toka lini mtoto akawa na maamzi bila kumshirikisha mzazi ? kama mimi ni baba yako niliye zaliwa Tumbo moja na Baba yako tukaachiana ziwa achana na huyu mwanamke, bila hivyo eeeeh! Nalamba mchanga uliomfukia mamaangu hautaishi katika ulimwengu huu.” …. Mzee masalu alimaliza yakwake yaliyo mkera kwa kula kiapo. Tom akiwasikiliza kwa makini. Mzee Petro alikuwa wa mwisho ni baba yake pia ingawa hakuzaliwa tumbo moja na baba yake Tom ila babu yake Tom walichangia ziwa pia na baba yake mzee petro hivyo ni ndugu wa damu moja ‘mimi naona baba zako wamemaliza hivyo kufikia kesho asubuhi staki kuwaona ndani ya familia ya kaka yetu unatutia aibu… Thomas usiwe mjinga mwanetu hizi pesa ulizo nazo nizakutusaidia sisi baba zako, tunaona una magari bila shaka kuko mjini unanyumba .. kumbuka hata huyu mama yako ni mtu wakupita sisi ni toka nitoke na baba yako hivyo tujali sisi baba zako. Kumbuka hata katika maisha hata siku moja jina la mama yako halitakaa kweye kitambulisho daima ni baba yako. Tuthamini baba zako daima na milele na hata sasa hivi ulitakiwa uangalie japo kidogo basi baba maana mmetoka huko mjini … na kagari hahhaaaaa aaah Tomm.” Tom ana geuka na kumkuta mama yake anachungulia alikuwa kasikia kila kilicho zungumzwa. Tom anaamua kutoka nje alakini wakti akitoka nje anamkuta Misoji na Zabi pia wako dirishani wanachungulia bila shaka ujumbe wameupata.




tom baada ya kutoka nje anaenda kuketi chini ya mti mkubwa uliokuwa katikati ya uwanja wa nyumba yao akiwa kaketi kwenye miziz mkubwa ya mti ule alikuwa kajiinamia, kichwa chini sijui alikuwa anawaza nini, sikujua alichokuwa akikiwaza alikuwa kimya saana. Zabi anajaribu kumfataalipokuwa lakini Tom ananyanyuka nakuingia Ndani bado sikujua alifata nini humo ndani. Taratibu Tom anatoka na mundu akiwa kauweka begani huku panga likiwa mkononi> anapishana na Zabi mlangoni. “tafadhali Tom don’t do this ninakuomba usifanye hiki unachotaka kufanya, Zabi alizidi kutembea naye kwa kasi huku akijaribu kumzuia mpaka alipofika ndani alisimama mlangoni mkono wa kulia ukiwa umeshika mundu na mkono wa kushoto ukiwa umebeba panga. “samahani mnaweza kuondoka kwa amani au mnangoja shali ?” swali la Tom bila shaka alilielekeza kwa baba zake “wewe si wakutu fukuza hapa hapa si kwako” mzee masalu alikuwa anabwata. Taratibu Tom anamsogelea kisha anajaribu kulielekeza panga singoni huku akimpigapiga sahavuni, hakukuwa na haja yakuga wazee walinyanyuka mmoja baada ya mwingine bila neno huku wakijikaza na kuongeza mwendo walijikuta wakibanan mlangoni na hata kupalamia ukutalakini walipofanikiwa kufika nje hawakurudi kama walivyo kuja, namaanisha hakukuwa na umoja tena kila mtu alipita njia yake, hakukuwa na mazungumzo tena bali kuzidiana uwezo wa kukimbia nakumbuka aliyekuwa mzee zaidi ndiye alikuwa wakwanza kwenye hizo mbio na kijana zaidi akawa wamwisho.

Tom akiwa kafula kwa hasira Zabi anakuja na kujaribu kumtuliza anaongea naye kwa upolea taratibu hasira zilianza kushuka mpaka kufikia nyuzi sifuri. Mama analalamika saana kuhusu hawa ndugu wa mmewe anasema huwa hawataki afanikiwe lazima watie zengwe ni tabia yao. Mama alimsifu Tom kwa kuwasambaza maana alijua kama angewanyenyekea lengo lao ilikuwa ni kupoteza, nikuharibu nikubomoa, huo ndio ulikuwa uhalisia. Kwa upande wake Zabi hakufurahishwa na hayo maamzi alliwaona kuwa wale ni wazazi walipaswa kuheshimiwa pamoja na kwamba wallikuwa kinyume na matakwa ya hawa wawili wapendanao Tom na Zabi. Baada ya chakula cha usiku tom na Zabi walikuwa chumbani kwao wamejipumzisha zabi akiwa juu ya kifua cha mpenzi wake huku akijiburudisha na pipi ya kijiti iliyokuwakinywani mwake aliyopewa zawadi na tom baada ya kuingia chumbani. Zabi alikuwa akimpenda saana tom kila wakati alionekana akimkodolea kwa makini bila kuchoka huku akizichezea ndevu za Tom na kukichezea kifua chake. Walikuwa wakibadilishana mawazo mbalimbali huku Zabi mara chache aliitoa ile pipi kinywani mwake na kuitumbukiza kinywani kwa Tom. Walichangia mate kupitia hiyo pipi na ilipo malizika huku wakiendelea na maongezi yao walijikuta katikati ya mahaba mazito ambayo hawakuyatarajia usiku ulie taratibu katikataia ya hayo mahaba kulitiwa motisha na mvua kubwa iliyoanza kunyesha usiku ule kibaridi kikaleta burudani ya ajabu na kuufanya usiku upendeze zaidi.

Nje ya hema au nyumba ya Tom na zabi kunaonekana matone madogo ya mvua iliyo nyesha usiku yakidondoka kutoka kwenye majani na kutua vyema kwenye udogo, ndege nao walianza kuimba kwa sauti zao tamu zilizo liwaza mioyo ya wengi, kumepambazuka ilikuwa ni saakumi na mbili asubuhi miale ya jua kutoka masharili ilianza kutanguliza saama maana hakukuwa na wingu hata kidogo, anga lilionekana la bluu hakuna wingu hata lakusingiziwa. Zabi anashiytuka usingizini taratibu anajiondoa kwa Tom huku akijinyoosha kwa upole. Ananyanyuka na kuzitafuta kanda mbili zake anazifaa kisha analivua gauni lake la kulalia na kuvaa nguo za kawaida. Anafungu sehemu ya kutokea iliyokuwa imefungwa kwa zip. Zabi anatoka nje lakini alipotoka nje alikuta masikitika makubwa nyumba ya mama ilikuwa imeanguka sehemu ya nyuma ya ukuta. Zabi alimwamsha Tom ili aje ahuhudie ni nini kilikuwa kikiendeledelea. Taratibu Tom anatoka nje na kuikuta hali ile anajaribu kushauliana na mama bado hawakupata mwafaka maana nyumba ilikuwa imechooka. Wakati wakijadili namna ya kufanya zabi alimwambia “Tom take a car now nenda kamtafutie mama nyumba Sengerema mjini yakununua kwa garama yoyote, I’m I clear ?” Tom alishangwaza na ule uamzi Zabi alikuwa kimya. Basi tom alichukua Gari kweli mpaka sengerema mjini. Kwa msako wa siku mbili hatimaye anafanikiwa kuipata nyumba maeneo ya Nyatukala ilikuwa ni nyumba kubwa pia mwenye nyumba hakuwa na mpango wa kuiuza lakini aliamua kuiuza kutokana na dau. Tom aliambiwa hiyo nyumba itauzwa milioni miamoja na Ishilini, Kwa hofu alimpigia simu zabi “baby nimekosa nyumba za milioni Saba, kumi hakuna kabisa nimepata moja haopa naamini hatuiwezi kabisa.” Alikuwaakijaribu kujihami.. “kwani inauzwaje ?” zabi alihoji “ aaha ni bei kubwa mno zabi mi naona tuiache Tu…” Tom alionekana kukata tamaana kabisa. “tafadhali Tom kwani inauzwaje ninachotama ni bei na siyo maelezo…” Zabi alifoka maana alianza kukasilika sasa “aaha et anasema milioni 120 lakini yenyewe ni nzuri ila bei mnh!” Tom alitaja bei bado akendelea kujikanyaga kanyaga.. “ila unauhakika nyumba umeipenda?” … zabi alimtupia swali tena Tom. “nyumba yenyewe ni nzuri bati la msauzi, ina vigae ni kubwa pia kila kitu inacho maji, umeme pia lakini tatizo ni bei Zabi.. yaani hapa ningekuwa na hela dah! Lazima tu ningeichukua” Tom alikuwa akizidi kujihami huku akiota ndoto za mchana kweupe. “Tom hudred million shillings bila nyongeza, Kesho Luckas atakuletea cheque kama anakubali utamalizana nae na asubuhi sawa?” Tom alibaki mdomo wazi asijue cha kujibu wakati huo Zabi alikuwa akizidi kumpa maelekezo ambayo hakuyasikiliza hata kidogo. Linaitwa wenge kichwani mwa Tom alianza kuongea peke yake hakuwahi kuzisikia Fedha nyingi kiasi hicho hakuwahi kuota kuzishika hata siku moja. Basi Tom alikuwa akionge peke yake huku akitembea huku na kule akizunguka hukuakionekana kuchanganyikiwa.

Kesho yake asubuhi majira ya saa mbili Luckas alikuwa kafika na cheque yake mkononi, Tom baada ya kupewa ile chaque ilikuwa inamuruhusu yeye kuchukua hiyo pesa yote ilikuwa ni milioni miamoja taslimu, Tomu aliingia benki akiwa haamini baada ya kuona anakataliwa kupokelea fedha hizo dilishan alipelekwa kwenye chumba maalumu alihesabiwa fedha zote na kukabithiwa. Mawazo ya kishetani yanamuingia Tom baada ya kukabidhiwa fedha ya kumnunulia mama yake nyumba Tom anaona hakuna haja ya kumnunulia mama yake nyumba. Akiwa ndani ya gari na mdogo wake Luckas anamwamuru Luckas ashuke chini huku akiona ni bora atoweke na zile fedha kuliko kuziteketeza kwa kumnunulia mama yake nyumba. Baada ya Luckas kushuka Tom anautekenya ufunguo wa Alteza Subaru inaitika kwa muungurumo wa simba kisha anakanyaga mafuta anajiandaa kutoweka.




Tom anaondoka na zile fedha wazo lake ni kutokomea kusiko julikana ili Zabi asijue aliko na alitamani saana akazifanyie kitu cha maana zile fedha. Tom yuko kwenye mviringo wa barabara anachagua ni njia gani atumie kuelekea Mwaza aidha apite njia ya vumbi kuelekea kamanga au apite njia ya rami akavukie Busisi. Taratibu anaiacha njia ya rami na kuingia njia ya vumbi alikuwa na kasi ya ajabu haijawahi kutokea. Tom aliendesha gari kwa kasi kama kama dreva wa gari la wagonjwa anae wahisha mgonjwa mahututi hospital. Haikumchukua muda saana akiwa kaushika usukani barabara alikuwa kwenye kona ya ya Katunguru hapo alikoswa kukogana uso kwa uso na lori la mkaa akaacha njia na kuyavamia matuta umbali wa mita 80 anafanikiwa kuiweka sawa gari. Tom anashusha pumzi na kutafakari marambili. Kimoyo moyo aliaanza kuwaza. Hivi ni yeye aliyenusulika kufa kwa tama za kutaka kumdhulumu mama yake? Tom anaiona hiyo ni kama dhuluma tena dhuluma kubwa kwa mama yake kipenzi kwani mama yake amwpewa heshima na dhabi ya kununuliwa nyumba na Zabi kamuamini Tom maana ni mtoto wa huyo mama na Tom ndiye kiunganishi kati ya Mama Tom na Zabi “kwanini mim?, kila siku mimi … jamani matatizo haya yataisha lini, leo nina kioja hiki kesho ni kioja kile eeeh! Mungu wangu nisimamie” Tom alikuwa akimwaga chozi kwa uchungu, alilalamika huku akizidi kujiona mjinga, Tom anageuza jivho lake kwenye kiti utande wa pili kulikuwa na Mfuko mkubwa wa plastiki mgumu rangi nyeupe isiyoonesha huku ukiwa na nembo y CRDB Bank Tom. Akiwa na mawazo mazito anaingiza mkono wake nakuchukua bando kadhaa anazishika mononi kisha anazibusu na kuzirudisha huku akiongea polepole “mama nisamehe…. Mwovu shetani kaambali na mimi” tom anahanganika kuirudisha gari barabarani hatimaye alikuwa karudi na term hii aliigeuza gari kurudi Sengerema.


Tom anafika maeneo ya nyatukala kama alikuwepo hakuwa na mazungumzo na mtu, bali alipokea simumuda mfupi kutoka kwa Zabi ikimueleza kuwa autambue uwepo wa wanasheria wawili ambao ni Bwana Kazungu Safari na Frank Alexender wanasheria wa kujitegemea walikuwa wameitwa na Zabi kutoka jijini Mwanza waliokuwa wameesha wasili kuja kusimamia manunuzi ya hiyo nyumba taratibu zote za kisheria zilifuatwa na nyumba ilikamilika na kuwa mali ya Mama Tom. Basi Tom alisimama kama shahidi huku hati zote zikiwa ni mali ya Mama Tom. Tom alisimama na kwenda kujiegemeza pembeni kidogo mwa ukuta akaanza kuitathimini ile ajari, kisha akawaza hivi ingekuwaje iwapo angekutana uso kwa uso na lile gari la mkaa ? alishia kumwaga chozi hakuwa na namna. Pili alianza kuwaza juu ya njama aliyokuwa ameipanga “hivi ningeishi vipi na wapi iwapo ningefanikiwa kutoroka na hizo fedha ?. Tom alijuta sana na akailuaum nafsi yake kwa tamaa na kuitupilia mbali mawazo ya kishetani yaliyokuwa yakimsumbua. Kwa uchungu ule Tom anajikuta akipiga goti na kutubu chini ya aridhi huku akiomba msamaha kwa mungu wake, kisha alimshukuru mungu kwa kuepusha ile ajali na kumpongeza Zabi kwa maamzi magumu anayoyafanya ili kuibadili familia yake. Siku iliyofuata familia yote ilihamia Sengerema mjini kwenye nyumba mpya waliyonunuliwa na Zabi. Zabi alimkabidhi mama nyumba iliyokuwa na kila kitu na akaaahidi kuihudumia familia hiyo kwa uwezo wake wote. Zililipuka shangwe na furaha ya ajabu hakuna alieamini kilichotokea katika Maisha ya Tom na familia yake si majilani ndugu na hata watu wa karibu. Lakini si hao tu mama Tom alihisi ni muujiza, bado alibaki haamini kilichotokea, kwa upande wa Tom hakuwa anaamini pia kwani alimuita mara mbili mbili Zab. Tom na mpenzi wake walikumbatiana na kubusu huku wakichekelea Familia haikuwa na taabu tena bali walianza kuishi kwa furaha. Hata Zabi na Tom walipoaga na kuondoka hakukuwa na matatzo tena, baa la njaa lilikuwa limekwisha na sasa ni furaha kwani walikula na kusaza. Kuila mahitaji walipewa kuhu mama Tom akiachiwa miradi midogo midogo kama mghahawa na mashine mbili za kusaga unga na moja ya kukomboa mahindi na mpunga. Amakweli ridhiki nikama ajali hutajua siku yakuja. Familia ya Tom ilianza kutoka katika taabu za umasikini ulio kithili.


Ni wiki mbili zilipia Zabi na Tom wakiwa Sengerema sasa wanaamua kurudi Mwanza walifikia pale pale Victoria Hotel Kapri-Point. Tom na Zabi walipata maji yakuoga bafuni kwao wakiwa pamoja mbali na micehezo ya kurushiana maji, kukumbatiana na kusaidiana kuoshana mfano kusuguana mgongoni na kwingineko Tom na Zabi wanautumia muda huo kuoneshana mahaba ya dhati kwani baada ya kumaliza Tom anambeba zabi na kwenda kumtupa kitandani huku wakichekelea. Mbali na kuendeleza michezo yao walitupiana mito wakakimbizana kubebana na hata kuimba pamoja nyimbo za mahaba. Siku hii ilikuwa ni siku mhimu saana kwa hawa wawili wapendanao kwani walipata muda wa kukaa pamoja na kuzunguza. Baada ya hizo kuwa kwenye furaha sasa wanaamuna kukaa pamoja na kuzungumza Tom alikuwa kapia magoni na kukilaza kichwa chake juu ya miguu ya Zabi, Tom alimshukuru saana Zabi na kumusifu kwa kuwa na moyo wa kujali, moyo wa kujitoa, moyo yenye upendo wa kweli Tom alikili si lahisi kukutana na binadamu mwnye moyo kama wa Zabi, alisema si kama hawapo ninaamini wapo na miongoni mwao ni Zabi. “Nimejifunza mengi saana kutoka kwako Zabi tajiri unayejua masikini kuwa naye ni binadamu, tajiri uliye tayari kuishi popote na wasio nacho, tajiri uliyetayari kugawana ulichonacho na sisi makabwela. Nilikuwa na ndoto ndiyo yakuikomboa familia yangu kutoka katika umasikini ila hii inaitwa surprise ni wazungu ndo huita hivyo yaani mafanikio bila maandalizi kwakifupi mama umenifanyia shitukizi la mafanikio.” Tom ungemuona wakati akiyazungumza haya alikuwa kalowa vyakutosha, ni machozi ya uchungu alidhihirisha kweli aliumizwa na umaikini aliokuwa nao. Iliuma saana kwa kiasi Fulani hali ya familia ya Tom alipokuwa akikumbuka hakika ilimuumziza saana.


Zabi na Tom wanaondoka Mwanza kwa ndege haikuwachukua muda walikuwa ndani ya jiji la maraha, jiji la Dar es salaam. Ni mitaa ya Manzese Tip top ukipita vichochoro kadhaaa unakutana na nyumba moja ya kifari iliyopambwa na vigae vya rangi ya kijivu na dhahabu kwenye kuta zote za nyumba hiyo kwa nje , paa lake la rangi ya kijani bati zake zenye muundo wa mikunjo mithili ya vigae … Taxi inaegeshwa nje ya nyumba hiyo taratibu zabi anashuka huku akipekua mkoba wake anatoa ufunguo na kulifungua geti kisha anatoa ishara ya Dreva kuingiza gari mpaka ndani. Wote wanashuka Tom kwa mara ya kwanza amepanda ndege, kwa mara ya kwanza ameikanyaga ardhi ya jiji la Dar Es Salaam, basi zabi anafungua milango na kuingia mpaka ndani wakati huo tom akishusha mabegi taratibu na hatimaye alianza kuyaingiza ndani. Sable ilikuwa ikionekana vizuri saana hakukuwa na shida kila kitu kilivutia mule ndani kulikuwa na sofa za kisasa kabisa, runinga ya yakisasa bapa na kubwa kama tambala la sinema huku visipika vyembamba na virefu vikiwa vinaonekana vizuri zaidi mule ndani. Tom alikuwa kaachama akishangaa madhali huku akiogopa hata kulikanyaga zuria lililokuwa limetandazwa kwenyesakafu ya sable hiyo. Nyumba ilikuwa nzuri saana kiukweli Tom hakuamini kama Zabi angekuwa anaishi kwenye nyumba nzuri kiasi hicho.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog