Search This Blog

Monday, 27 March 2023

LAITI NINGEJUA - 5

  


Simulizi : Laiti Ningejua

Sehemu Ya Tano (5)



“Sana, kitu kingine mama yangu ni mzungu, siyo mtu wa kufuatilia fuatilia mambo…” alisema Rehema huku akiachia kicheko hafifu. Nikashusha pumzi.


Kinapita tena kitambo kifupi cha ukimya, nikainywa ile juisi yote iliyobakia kwenye bilauri huku nikiwaza namna ya kumuanza Rehema maana pepo mbaya wa ngono alikuwa ananisumbua sana. Rehema alinitazama kwa makini kama aliyehisi kitu.


“Vipi maisha?”


“Maisha ni kama hivi, namshukuru Mungu kwa kuwa nipo hai, vinginevyo…” nikasita kidogo na kubaki kimya. Rehema akanitazama kwa macho ya udadisi.


“Vinginevyo kitu gani mbona huendelei?” aliuliza baada ya kuona siendelei kuongea. Nikajifanya natafakari kidogo kisha nikashusha pumzi ndefu.


“Rehema, naomba nikuulize,” hatimaye nikamwambia Rehema kwa sauti ya utulivu.


“Niulize tu kaka yangu.”


“Je, wewe umeolewa?”


Rehema akaniangalia kwa makini kwa kitambo kirefu kisha akaachia tabasamu huku akitingisha kichwa chake kukataa.


“Ningekuwa nimeolewa nadhani usingenikuta naishi hapa kwa mama yangu. Hii inaonesha kuwa bado sijaolewa!”


“Mchumba je, huna mchumba?”


“Hapana sina mchumba!”


“Boyfriend?”


“Pia sina! Ila kwa sasa Mungu amenipatia friend boy na siyo boyfriend, na si mwingine ni wewe Bilali.”


Nikashusha pumzi za ndani kwa ndani huku nikihisi faraja baada ya kujua kuwa hakuwa ameolewa na wala hakuwa na mchumba, alikuwa tofauti na Jameela ambaye alikuwa mbioni kuolewa. Nikajiegemeza kwenye kochi.


“Kwa hiyo huna mume, huna mchumba, huna boyfriend, je mvulana ambaye labda… unampenda au…”


Rehema akanikazia macho kwa mshangao huku akikunja uso wake. Ni dhahiri alionekana kukerwa na maswali yangu yaliyomjia mfululizo.


“Samahani Bilali, kwani unatakaje! Sipendi kukulazimisha kusema kwa namna ninavyopenda, lakini naona kama nimekwisha jibu vya kutosha maswali yako kuhusu uhusiano wangu na wanaume. Sina uhusiano na mwanaume na wala sijawahi kuwa na uhusiano na wanaume yeyote, sijui unahitaji nini zaidi?”


Maneno yake yakanifanya nibaki kimya kwa muda nikimkodolea macho huku nikijilaumu sana kwa kukosa uvumilivu na kuporomosha maswali mfululizo kana kwamba nilikuwa polisi ninayehitaji taarifa muhimu za kiintelijensia.


“Naomba usinielewe vibaya, Rehema, unakumbuka niliomba tuwe marafiki, ukweli ni kwamba nilikupenda tangu siku ya kwanza tu nilipokuona! Ingawa najua kuna tofauti kubwa ya kipato kati yetu lakini hii hainizuii kukupenda…” sikukata tamaa, nilimchombeza Rehema huku nikizidi kumkazia macho.


Muda huo nilikuwa nahisi msisimko wa aina yake ndani yangu ingawa ukweli kulikuwa na sauti ndani yangu iliyonieleza kuwa sikuwa nampenda kutoka moyoni bali nilimtaka kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa… yaani nilimtamani tu kwa ajili ya ngono… nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu ingeisha na ningeachana naye.


Ndiyo, ningeachana naye kwa sababu nilidhani sikuwa nikihitaji kuishi na mwanamke mrembo wa aina ya Rehema ambaye sikuwa na uhakika kama ningeweza kumuoa na kuishi naye bila kupata ugonjwa wa presha.


“Ni kweli unanipenda?” sauti tulivu ya Rehema ilinizindua kutoka kwenye mawazo yaliyokuwa yakipita kichwani kwangu, nilimtazama nikamuona akinikazia macho, na kabla sijajibu akaendelea, “Kwanza ni upendo wa aina gani huo unaouzungumzia ambao unazuiwa na kipato?”


“Wa mke na mume. Yaani… nahitaji kukuoa Rehema, sijui unasemaje?” nilijikakamua kuzungumza ingawa moyoni niliamini kuwa ule ulikuwa uongo mtupu.


Rehema alishusha pumzi ndefu na kuinamisha uso wake chini, alionekana kufikiria sana.


“Una hakika unanipenda na unataka kunioa, Bilali?” aliniuliza akiwa kanikazia macho.


“Ndiyo, tena niko tayari siku yoyote, na ndiyo maana nilikuwa tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako!” niliongea kwa kujiamini huku nikimtazama Rehema bila kupepesa macho.


Rehema alinitazama kwa makini sana kwa kitambo kirefu, ilikuwa ni kama vile alikuwa akiyasoma mawazo yangu kisha alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.


“Sijaelewa, mwanzo ulitaka tuwe marafiki lakini sasa unataka kunioa, hivi haya unayoyasema yanatoka wapi, au unataka kunichezea tu umalize haja zako kisha…”


“Najua ni vigumu kuniamini, sijui niseme nini ili uniamini,” nilimkata kauli wakati alipokuwa akiendelea kuongea.


“Okay, naomba nikuulize maswali machache,” Rehema alisema huku akiendelea kunikazia macho.


“Niulize tu,” nilijibu kwa kujiamini.


“Kwa nini unadhani kuwa unanipenda?”


“Kwa sababu nakupenda, penzi halina sababu,” nilijibu kwa kujiamini.


“Una uhakika kuwa hunipendi kwa sababu yoyote ile nyingine?”


“Kama zipo sababu, basi nakupenda kwa sababu unazo sifa zote za mwanamke ninayetaka kumuoa.”


“Asante!” Rehema alisema huku akiachia mguno na baada ya hapo kikapita kitambo kirefu cha ukimya. Nilimuona akiwa anawaza mbali na sikujua alikuwa anawaza nini. Nikawa najiuliza ni wapi nilikotoa ule ujasiri wa kuyatamka yale yote niliyoyatamka kwa Rehema.


“Lakini, hujaniambia bado kama inawezekana au vipi!” nilivunja ukimya baada ya kuona Rehema yupo kimya.


“Unataka kuniambia hujaoa hadi sasa?” Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa udadisi.


“Sijabahatika,” nilimjibu kwa sauti tulivu.


“Kwa nini?”


“Kwa sababu Mungu bado hajanijaalia”


“Na wala huna girlfriend?”


“Ninaye!” nilijibu huku nikimkazia macho Rehema, nikamuona kashtuka kidogo ingawa hakutaka kuuonesha mshtuko wake.


“Sasa… kama una girlfriend nini tatizo hadi uanze kutanga tanga?”


“Wala sijatanga tanga kwani leo ndiyo mara ya kwanza naongea naye na hajui ni kiasi gani nampenda. Girlfriend wangu ni wewe Rehema!”



“Unataka kuniambia hujaoa hadi sasa?” Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa udadisi.


“Sijabahatika,” nilimjibu kwa sauti tulivu.


“Kwa nini?”


“Kwa sababu Mungu bado hajanijaalia”


“Na wala huna girlfriend?”


“Ninaye!” nilijibu huku nikimkazia macho Rehema, nikamuona kashtuka kidogo ingawa hakutaka kuuonesha mshtuko wake.


“Sasa… kama una girlfriend nini tatizo hadi uanze kutanga tanga?”


“Wala sijatanga tanga kwani leo ndiyo mara ya kwanza naongea naye na hajui ni kiasi gani nampenda. Girlfriend wangu ni wewe Rehema!”


Endelea...


Rehema akataka kusema neno lakini nikamuona akisita. Aliyakwepa macho yangu yaliyokuwa yakimtazama kwa makini na kuangalia kando, kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Jambo unalohitaji kwangu ni jambo linalohusu maisha… yangu na yako vilevile, kwa hiyo halihitaji uamuzi wa papara,” alisema Rehema na alionekana kumaanisha kile alichokisema na kuendelea.


“Nahitaji muda wa kutafakari zaidi, nahitaji kukufahamu zaidi na kuufahamu ukoo wako kabla sijakubali au kukataa proposal yako. Najua hata wewe hunifahamu vya kutosha…”


“Ni kweli,” nilikubaliana na maneno yake ingawa moyoni sikuona sababu ya kuanza kuchunguzana wakati nilijua kabisa sitaweza kumuoa bali nilitaka kushiriki tendo tu na kumwacha kama wengine.


“Samahani, hivi wewe mwenzangu ni mzaliwa wa wapi?” nilijikuta nikimtupia swali.


“Kigoma.”


“Kigoma?” Nilimaka kwa mshangao huku nikiachia kinywa changu wazi.


“Ndiyo Kigoma… mbona umeshtuka?”


“Wewe ni kabila gani?” Nilimuuliza tena huku nikimkazia macho.


“Mmanyema, kwani vipi?”


“Ni mshtuko wa furaha kwa kuwa imeniongezea sifa nyingine nisiyoitegemea kwako wewe!”


“Sifa gani hiyo?”


“Wewe ni msichana wa kwetu, mimi pia kwetu ni Kigoma, mimi pia ni Mmanyema. Huwezi kujua, nimefurahi mno, Rehema!” nilisema huku nikihisi msisimko na ubaridi ukinitambaa mwilini mwangu.


Rehema alitabasamu tu bila kusema neno. Nikataka kusema neno lakini nikasita baada ya kumuona Bi Aisha akiingia pale sebuleni na kuketi kwenye sofa, kisha kisha mazungumzo ya kawaida ya kufahamiana zaidi yakatawala maongezi yetu.


Niliaga ili niondoke lakini Bi Aisha hakuniruhusu, aliniomba nisubiri chakula nile ndipo niondoke. Kwa kweli yule mama alikuwa mcheshi na mzungumzaji mzuri. Nilipoondoka pale ilikuwa yapata saa kumi za alasiri na moja kwa moja nilirudi nyumbani nikiwa nimefarijika sana.


Zilipita siku tatu tangu siku nilipokwenda nyumbani kwa kina Rehema na kukutana na mama yake, Bi Aisha, katika siku hizo tatu nilikuwa nashughulikia kongamano maalumu la kibiashara ambalo niliamini kuwa niliamini lingetengeneza fedha nyingi ambazo hatimaye zingenipa heshima zaidi mbele ya Rehema.


Siku ya nne nilikutana na Rehema na aliomba anitembelee nyumbani ninapoishi ili apafahamu. Sikupinga, nilimchukua hadi nyumbani na kumkaribisha ndani.


”Hapa ndipo ninapoishi, Rehema,” nilisema mara tu Rehema alipoingia ndani kwangu. “Ni padogo sana, lakini uwezo wangu ndipo ulipoishia.”


“Una maana gani?” Rehema aliniuliza huku kanikazia macho yake. Japokuwa nilishikwa na haya, lakini nilimudu kuunda tabasamu.


“Nyumba hii ni ndogo tofauti na ile ya kwenu, japo ninatamani sana kuishi maisha ya juu lakini siwezi kuishi kama mkurugenzi, ndiyo maana yangu,” nilisema na kushusha pumzi.


“Pia hii ni nyumba ya familia ambayo tumeachiwa mimi na brother wangu ambaye kwa sasa yupo South Africa. Nina hiki chumba kimoja na sebule, vyumba vingine tumepangisha,” nilizidi kujitetea mbele ya Rehema.


“Kupanga ni kuchagua, na sidhani kama huwezi kuishi kama hao wengine wakati wewe pia umesoma na huna kasoro yoyote!” alisema Rehema huku akiniangalia kwa makini.


“Ni kweli,” niliafiki. “Ila itabidi uvumilie tu maana pana joto kidogo, ila kwa huu mji wetu hilo si jambo la kushangaza.”


“Usijali…” alisema huku akiketi juu ya kochi dogo la sofa pale sebuleni kwangu. Kikakipita kimya cha kitambo kifupi.


“Kwani wazazi wako wapo wapi?” Rehema alinishtua kwa swali lake.


“Wapo Kigoma, wanaishi Mwanga mtaa wa Lumumba,” nilimwambia.


Tuliongea mengi sana siku ile na Rehema aliamua kushinda pale kwangu. Aliniuliza maswali mengi kuhusu maisha yangu binafsi na maisha ya familia yangu, nami bila ajizi nilimjibu kila swali alilouliza kwani nilijua alichokuwa akikitafuta.


Pamoja na kuwa na wakati mzuri wa kuongea na kufurahi nilijaribu sana kumuonesha kuwa nilimhitaji kwa ajili ya kushiriki tendo lakini Rehema alionesha msimamo wa kutokuwa tayari, nami niliheshimu msimamo wake kwa kuogopa kuonekana nilikuwa na papara.


Siku ile ukawa ndiyo mwanzo wa kuwa karibu zaidi na Rehema. Baadaye tukawa tukiwasiliana sana kwa simu, lakini siku moja Rehema alikuja tena nyumbani kwangu ingawa safari ile alinishtukiza maana alikuja bila kunitaarifu kama angekuja.


Ilikuwa ni siku ya Jumamosi na alinikuta nikiwa nafanya usafi ndani kwangu. Aliniambia kuwa alikuwa anapita tu akaona si vibaya akishuka kunisalimia, nikamkaribisha ndani kwa bashasha.


Hakuonesha kukaa sana lakini nami sikutaka kuipoteza nafasi ile hivyo tukiwa katikati ya maongezi nikaanzisha tena mazungumzo yaliyohusu uhusiano.


“Unajua Rehema, sifurahii aina ya maisha ninayoishi, ni ajabu kwamba katika maisha ni vitu vichache kati ya unavyovitaka ambavyo unavipata, vingi huvipati!”


“Hebu niambie Bilali, ni vitu gani katika maisha yako ambavyo hujavipata?”


Niliinamisha uso wangu kidogo nikijifanya kutafakari ingawa kimsingi sikuwa natafakari chochote, kisha nikanyanyua uso kumtazama.


“Nashukuru Mungu nimesoma kiasi cha haja, nimehitimu digrii ya Biashara katika Masoko, nimefungua kampuni na kufanikiwa kuajiari watu kadhaa na ninapata mahitaji yangu yote muhimu, lakini bado zipo haja nyingine zilizomo ndani ya nafsi yangu ninashindwa kuzipata!”


Rehema akacheka kidogo. “Kama zipi hizo?”


“Upendo…” nilijibu huku nikimtazama kwa makini.


“Unataka kuniambia kuwa familia yako hawakupendi?” Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa mshangao.


“Familia inanipenda, lakini pendo ninalozungumzia hapa, ni lile ambalo ni tofauti na la baba, mama, dada au kaka!” nilisema huku nikiachia kicheko hafifu.


Rehema aliguna na kuangalia kando akijaribu kuyakwepa macho yangu, hata nilipojaribu kumchunguza sikuiona tashwishwi usoni kwake. Kisha nikamuona akiinuka kisha akaaga na kuanza kuondoka.


“Keti kwanza,” nilimwambia Rehema huku nikimzuia asiondoke.


Rehema alinitazama kwa makini kwa kitambo kisha alitii na kurudi kuketi kwenye kochi. Akabaki akinitumbulia macho.


Nilivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku nikiuma midomo yangu, nikajifanya nafikiria kidogo kisha nikamkabili Rehema kwa sauti tulivu.




Rehema aliguna na kuangalia kando akijaribu kuyakwepa macho yangu, hata nilipojaribu kumchunguza sikuiona tashwishwi usoni kwake. Kisha nikamuona akiinuka kisha akaaga na kuanza kuondoka.


“Keti kwanza,” nilimwambia Rehema huku nikimzuia asiondoke.


Rehema alinitazama kwa makini kwa kitambo kisha alitii na kurudi kuketi kwenye kochi. Akabaki akinitumbulia macho.


Nilivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku nikiuma midomo yangu, nikajifanya nafikiria kidogo kisha nikamkabili Rehema kwa sauti tulivu.


Endelea...


“Najua umenisisitiza kuwa na subira, lakini naomba tu nikwambie ukweli, moyo wangu umeshindwa kufanya hivyo ingawa umekuwa mvumilivu mno… Nilihisi kuna wakati pamoja na matendo yangu kwako ningefanikiwa kubadilisha hisia zako lakini naona unazidi kunikatisha tamaa!”


Rehema akaniangalia kwa umakini sana na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Niwie radhi… ninakuthamini, ninakuheshimu na ninakupenda vile vile, lakini siko tayari kwa jambo hilo kwa sasa… huo ni msimamo wangu na sidhani kama unaweza kubadilika,” alisema Rehema kwa sauti yenye utulivu lakini akimaanisha kile alichokisema.


“Lakini…” nilitaka kusema lakini Rehema alinikatiza kwa ishara.


“Suala la kufanya ngono kwa sasa halipo moyoni mwangu na wala halipo akilini mwangu… nasikitika Bilali!”


“Naheshimu msimamo wako, lakini nimeomba jambo ambalo naamini limo ndani ya uwezo wako… nikiamini mimi na wewe ni wachumba! Sasa… bado hujanipa sababu za wewe kukataa!”


Rehema aliinamisha uso wake chini akaonekana kutafakari sana kisha akainua uso wake kunitazama kwa makini. Kulikuwa na huzuni iliyoonekana wazi kwenye macho wake.


“Sababu… sababu zipo, kwanza dini hairuhusu!” alisema huku akiuma mdomo wa chini.


Nikatingisha kichwa changu kukataa. “Hicho ni kisingizio tu. Kwa vyovyote utakuwa na mtu wako, ila mimi unanizuga tu!”


“Sina mwanamume na wala sifikirii kuwa na mwanamume mwingine yeyote. Nimetokea kukupenda wewe tu… wewe ndiye mwanamume wa maisha yangu!” aliniambia. Nikamtazama kwa makini na kuuona ukweli wa maneno yake kwenye macho yake.


Hata hivyo, niliamua kumsogelea karibu zaidi nikamtazama moja kwa moja machoni huku nikimkazia macho.


“Thibitisha kama kuna ukweli katika maneno yako vinginevyo nitaamini vipi?”


Rehema akanitazama kwa makini kwa kitambo kirefu kidogo, kisha akashusha pumzi zake huku akinyanyua mabega yake juu.


“Sioni kwa nini niongope. Kama huniamini sawa, sina namna ya kukufanya ukubaliane na kila kitu nisemacho. Ila ninachojua ni kuwa wewe ndiye mwanamume wa maisha yangu, basi.” Rehema alisema na kuinuka.


“Kwa heri!” alisema na kuondoka akiniacha nimepigwa butwaa.


Donge la hasira lilinikaba kooni, nikarusha mikono yangu hewani kama ishara ya kukata tama kisha nikajibwaga juu ya kochi na kushusha pumzi ndefu huku nikisonya kwa hasira.


“Aende zake asinibabaishe. Kwani yeye nani hadi nimbembeleze sana!” nilijiambia na kusonya kwa hasira.


Japo Rehema alikuwa amenikasirisha lakini ukweli ni kuwa sikuwa mtu sahihi kwake, pamoja na kunihakikishia kuwa alinipenda bado nilimhitaji kwa sababu moja tu… ngono… nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu ingeisha na ningeachana naye.


Yaani nilitaka kuwa katika uhusiano na Rehema kwa sababu ya ngono tu lakini kilichoniudhi ni yeye kutokutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi huenda alikuwa ana mtu mwingine.


Sasa nikajikuta katika pepo mbaya, nikaamua kumwonesha hadharani kuwa nilikuwa na wanawake wengine. Jioni ya siku ile Rehema alinipigia simu lakini sikupokea, hata alipotuma meseji sikuzijibu, nilitaka kumuonesha kuwa nilikuwa nimechukia kutokana na kitendo chake.


Kitendo cha kutokupokea simu wala kuzijibu meseji zake kilinifanya niwe na uhakika kwamba kingemuumiza sana Rehema na kwa vyovyote kesho yake angekuja nyumbani kwangu, hivyo nilimpigia simu Tausi kumuomba aje nyumbani kwangu.


Tausi hakuwa na pingamizi lolote kwani aliisubiri nafasi ile muda mrefu ndiyo maana hakupinga na bahati nzuri siku ile alikuwa ameanza mapumziko baada ya kumaliza zamu ya usiku.


Tausi alikuwa anafanya kazi ya uuguzi katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), tulifahamiana wakati nilipokuwa nimelazwa pale baada ya ule mkasa uliotokea kule porini Kibiti.


Tausi ndiye mara nyingi aliniuguza nilipokuwa nimelazwa na alijitolea kwa kila hali kunihudumia hata pale alipokuwa hayuko zamu, jambo lililonivutia sana.


Ukawa mwanzo wa kufahamiana zaidi, kisha urafiki ukazaliwa na baadaye tukawa wapenzi. Nilipotoka hospitali tuliendelea kuwasiliana na alikuja nyumbani mara mbili ingawa hatukuwahi kushiriki tendo.


Tausi alikuwa mwanamke wa miaka kati ya ishirini na nane na therathini, alikuwa na umbo kubwa la kuvutia. Alikuwa mweupe kwa asili lakini pamoja na urembo wa asili bado alijiongezea kwa mapambo mengine ya gharama yaliyomfanya kuvutia zaidi.


Hakuwa mwanamke wa kumtizama mara moja tu ukamwacha kwani alivutia sana kutokana na umbo lake lililokuwa na mfano wa umbo la nyigu.


Usiku wa siku ile niliupitisha nikiwa na Tausi nyumbani kwangu na asubuhi ya siku iliyofuata tuliamka kama saa tatu tukiwa hoi.


Tausi aliandaa chai kisha tukaketi sebuleni kwa ajili ya kifungua kinywa, na tulipokuwa tukinywa chai, nilishtushwa na mlio wa gari lililosimama ghafla huko nje. Nikajua tayari mambo yalikwenda kama nilivyopanga.


Tausi alinishtukia akaniuliza, “Vipi baby, kuna nini?”


“Hakuna kitu… Vipi kwani?” Nilimjibu huku nikijaribu kusikilizia vizuri kama ni Rehema au alikuwa mtu mwingine.


“Nimesikia muungurumo wa gari, sitaki wageni saa hizi miye. Tukimaliza kunywa chai tukalale maana bado nina hamu na wewe. Kama kuna mgeni wako umwondoe mapema,” aliniambia Tausi kwa utani.


Nilimtazama nikatabasamu bila kusema neno. Mara nikaisikia sauti ya Rehema akisalimia na wapangaji pale kwenye korido kisha hatua za haraka zilikuja hadi kwenye mlango wangu, kisha zikasimama.


“Nani?” Tausi aliniuliza kwa sauti ndogo huku akifinya macho yake. Nilibetua mabega yangu na sikusema neno japo nilikwisha mjua aliyekuwa kasimama mlangoni.


Taratibu mlango wa pale sebuleni ulifunguliwa. Rehema akiwa amevaa sketi fupi nyeusi yenye miraba myeupe, blauzi ya bluu ya mikono mirefu na viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio akaingia.




Nilimtazama nikatabasamu bila kusema neno. Mara nikaisikia sauti ya Rehema akisalimia na wapangaji pale kwenye korido kisha hatua za haraka zilikuja hadi kwenye mlango wangu, kisha zikasimama.


“Nani?” Tausi aliniuliza kwa sauti ndogo huku akifinya macho yake. Nilibetua mabega yangu na sikusema neno japo nilikwisha mjua aliyekuwa kasimama mlangoni.


Taratibu mlango wa pale sebuleni ulifunguliwa. Rehema akiwa amevaa sketi fupi nyeusi yenye miraba myeupe, blauzi ya bluu ya mikono mirefu na viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio akaingia.


Endelea...


Mkononi alikuwa amevaa bangili nyingi za pembe na alikuwa amejimwagia mafuta mazuri yaliyosambaa chumba kizima. Alipoingia alisimama akitutazama kwa makini.


“Karibu Rehema,” niliongea huku nikiachia tabasamu. Sauti yangu ilikuwa tulivu sana. “Kutana na best wangu, Tausi…” nilimwambia Rehema kisha nikageuza shingo kumtazama Tausi, “Huyu ni dada yangu mpenzi, Rehema.”


Rehema aliachia tabasamu japo nilihisi halikuwa tabasamu halisi ila lilificha kitu ndani yake, alipiga hatua akaja kuketi kwenye kiti tupu karibu yangu huku akinitazama kwa makini kisha akayahamishia macho yake kwa Tausi.


Tausi akageuza shingo yake kunitazama kwa jicho la kuuliza lakini hakuthubutu kusema chochote. Niliachia tabasamu nikionekana kutobabaika kabisa, kikapita kimya kirefu, huku wanawake wote wawili wakinitazama kwa makini.


“Sijauelewa vizuri utambulisho wako, unaweza kunitambulisha tena huyu ni nani?” Rehema aliniuliza kwa sauti tulivu.


“Mwanamke,” lilikuwa jibu langu.


“Najua kuwa ni mwanamke, lakini nataka kujua yeye ni nani?”


“Nimeshakwambia anaitwa Tausi, hayo mengine wayatakia nini?” niliongea kwa kufoka.


Rehema alinitazama kwa makini, nikayaona machozi yakimlenga lenga kwenye macho yake, hakutaka kuendelea kukaa pale aliinuka na kuondoka haraka, akafungua mlango na kutoka kisha nikasikia muungurumo wa gari yake ilipokuwa ikiondoka na kupotelea mtaani.


Kwa kiasi fulani moyo wangu uliridhika kwa kitendo nilichomfanyia Rehema nikiamini kuwa baada ya siku ile angeniheshimu, maana nilijua kuwa alikuwa ananiona bwege. Moyoni mwangu nikaahidi kuendelea na vimbwanga vya hapa na pale hadi anyooke.


Tausi alinitazama kwa kitambo bila kusema neno, nilijua kuwa alikuwa amejisikia vibaya sana kwa kile kilichotokea kwa mwanamke mwenzake, japo sikujali, nilijitahidi kumsemesha lakini alibaki kimya akinitazama kwa makini. Kisha alishusha pumzi ndefu.


“Bilali, najua wewe ni kijana mtanashati sana na kila mwanamke angependa kuwa na wewe, lakini nimehuzunika sana kwa kuwa sipendi kugombanisha wapendanao, usingefanya uliyofanya, mimi ningeweza kuwapisha badala ya hiki kilichotokea,” Tausi alisema kwa uchungu.


Nilimtoa wasiwasi kuwa Rehema hakuwa mpenzi wangu bali tulizoeana tu kwa kuwa nilimsaidia kwenye lile tukio la kule Kibiti. Nilimsimulia kuhusu tukio zima lilivyokuwa na jinsi nilivyomuokoa Rehema hadi pale polisi walipokuja na mimi kupoteza fahamu.


Tausi aliamua kukubali yaishe lakini hakuonekana kuridhika na maelezo yangu.


Baada ya siku ile ilipita wiki nzima nikiwa sina mawasiliano na Rehema ingawa ukweli sikutaka uhusiano wetu uishie katika hali ile, niliamini kuwa Rehema alikuwa ananipenda ingawa sikujua kwa nini hakuwa tayari kushiriki tendo, bila sababu zozote za msingi.


Japo chozi la Rehema liliniumiza sana siku ile lakini sikujali. Kwa nini alikuwa ananinyima penzi? Nilijiuliza nikakosa majibu. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye. Lakini tatizo lilikuwa ningeachana naye vipi bila kumjua ladha yake?


Nilijiapia kuwa jambo hilo lisingewezekana hata kidogo, mimi kama mwanamume kamili angenitangaza kwa marafiki zake, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo. Ingekuwa aibu kubwa kwangu!


Ndiyo maana ilipopita wiki na Rehema hakuwa amenitafuta niliamua kujishusha, niliacha shughuli zangu na kwenda kwao kumtafuta. Nilipokuwa nakaribia nyumbani kwa kina Rehema mita chache mbele yangu nikawaona wanawake wawili waliokuwa wanatokea upande niliokuwa naelekea.


Nilishtuka kidogo nikiwa siamini macho yangu kuwa niliowaona mbele yangu ni Jameela na mwanamke mwingine wa makamo aliyekuwa na umbo kubwa lililovutia. Mwanamke yule alikuwa mrefu kama alivyokuwa Jameela na alikuwa mwarabu.


Mara moja nikagundua kuwa huyo ndiye yule shangazi yake aliyekuwa akinielezea habari zake. Mwanamke yule alikuwa na macho makubwa mazuri yaliyoambatana na kope nyingi nyeusi ambazo zilizoachia nafasi kwa nyusi ili zipate kujidai, na midomo yake ilikuwa minene yenye kingo nyepesi na mikunjo midogo midogo.


Jameela aliponiona aliongea kitu kwa yule mwanamke kwa sauti ya chini kisha akainua mikono yake kunipokea kwa uchangamfu.


“Wow Bilali,” alisema kwa bashasha huku akinipokea na kuongeza, “habari za nyumbani kwako?”


“Nzuri tu Jameela, sijui nyinyi?”


“Sisi tu wazima… kutana na shangazi yangu, Bi Aisha…” alinitambulisha kwa yule mama kisha alimgeukia, “Shangazi, kutana na Bilali Ibrahim, yulee…” alisema na kuachia kicheko hafifu, wote wakacheka.


Bi Aisha akanyoosha mkono wake na kunisalimia kwa bashasha huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.


“Nimefurahi sana kukufahamu, maana kila siku nilikuwa najiuliza huyu Bilali yukoje maana tulikuwa hatuli wala hatulali, kila siku Bilali, Bilali!!” yule mwanamke aliongea kwa sauti ya kishambenga na kuendelea.


“Pole sana kwa mkasa uliokupata.”


“Nimekwisha poa, shikamoo,” nilimwamkia yule mama huku nikiwa na haya usoni kwangu.


“Marhaba… karibu nyumbani kwetu,” aliitikia huku akinikaribisha kwa ukarimu mno na kunionesha kwa kidole ilipo nyumba yao.


Nilishtuka sana maana nyumba aliyonionesha ilikuwa imepakana na nyumba aliyokuwa akiishi Rehema na mama yake mkubwa. Pia nilishtushwa sana kwa kuwa hata yeye pia aliitwa Bi Aisha.


“Twende ukapaone nyumbani kwetu, au kuna sehemu ulikuwa unaelekea?” aliniuliza Jameela baada ya kuona nipo kimya nikiwa nimenywea.


Nilishusha pumzi za ndani kwa ndani, nikatingisha kichwa. “Kuna mtu ninakwenda kumuona mara moja, ni muhimu sana maana muda wote ananisubiri mimi,” niliamua kuongopa ingawa ukweli nilikuwa nakwenda kwa Rehema.


Waliridhishwa na uongo wangu, lakini Jameela alisema kuwa baadaye angekuja nyumbani kuniona. Niliondoka nikiwa na maswali mengi kichwani, sikuwa nimefikiria kabisa kukutana na Jameela katika mazingira yale, nikawaza sana kuwa kumbe Jameela na Rehema walifahamiana!


Na kweli baadaye Jameela alikuja nyumbani na kuniambia kuwa alikuja kuniaga kwa kuwa harusi yake ilikuwa imekaribia, alisema kuwa alitafuta kila njia ya kuja ili tuagane na alikuja kulala kwangu na kesho yake angerudi Kibiti kwa ajili ya kukaa ndani kama ilivyokuwa desturi yao.


Nilipomuuliza kuhusu shangazi yake Jameela aliniambia kuwa anajua kila kitu na ni msiri wake, hivyo sikutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.


Aliichukua simu yangu na yake akazifungia ndani ya kabati. “Sihitaji simu yoyote saa hizi, leo ni mimi na wewe tu hadi lyamba,” alisema Jamila huku akitoa kila kitu na kubakiwa na nguo ya ndani tu, kisha akajibwaga juu ya kitanda.



Na kweli baadaye Jameela alikuja nyumbani na kuniambia kuwa alikuja kuniaga kwa kuwa harusi yake ilikuwa imekaribia, alisema kuwa alitafuta kila njia ya kuja ili tuagane na alikuja kulala kwangu na kesho yake angerudi Kibiti kwa ajili ya kukaa ndani kama ilivyokuwa desturi yao.


Nilipomuuliza kuhusu shangazi yake Jameela aliniambia kuwa anajua kila kitu na ni msiri wake, hivyo sikutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.


Aliichukua simu yangu na yake akazifungia ndani ya kabati. “Sihitaji simu yoyote saa hizi, leo ni mimi na wewe tu hadi lyamba,” alisema Jamila huku akitoa kila kitu na kubakiwa na nguo ya ndani tu, kisha akajibwaga juu ya kitanda.


Endelea...


Nami nilitoa nguo zangu nikabakiwa na boksa tu kisha nikamfuata pale kitandani. Niliisikia simu yangu ikiita lakini Jameela alinizuia, akanisukumia kitandani kisha alikuja akakaa juu yangu na kuanza kunibusu, nami nikijibu mapigo kwa kumpapasa nyama za mgongo.


Jameela akaanza kutweta kwa ashki huku akionekana kuhisi faraja iliyopenya hadi kwenye mishipa yake ya damu.


Tulichukua muda mrefu tukipapasana na kugusana hapa na pale, na nilimgeuza na kumweka chini kisha nikakaa juu yake na kuendelea kumpapasa, alitulia akiwa amefumba macho yake huku akihema kwa nguvu. Nikapeleka ulimi wangu kwenye sikio lake, Jameela akaonekana kusisimkwa na kuachia kicheko.


Mara nikahisi kama mlango wa sebuleni ukifunguliwa taratibu, nikashtuka na kutulia nikisikiliza kwa makini. Sikusikia chochote maana ukimya ulitawala, nikadhani labda yalikuwa mawazo yangu tu na hakukuwa na chochote.


Nikapeleka tena ulimi wangu kwenye sikio la Jameela, akaonekana kusisimkwa tena na kucheka, muda ule ule mlango wa chumbani kwangu ukagongwa na kukatiza kicheko cha Jameela.


Mimi na Jameela tukashtuka sana na kukodolea macho kwenye ule mlango, kisha Jameela akanitazama katika namna ya kuniuliza kama nilikuwa namjua aliyekuwa anagonga ule mlango. Sikuwa na jibu.


Kwa sekunde kadhaa mle chumbani kukawa na ukimya mzito. Mlango ukagongwa tena, safari hii kwa nguvu zaidi.


“Nani?”


Hakuna aliyejibu. Nikashangaa zaidi na kumtupia jicho Jameela ambaye alibaki kimya akinitazama kwa makini.


“Wewe nani?” niliuliza tena huku hasira zikianza kunipanda.


Lakini mgongaji aliendelea kukaa kimya, kisha nikaona kitasa cha mlango kikinyongwa na mlango ukasukumwa na kufunguka. Bila kusita Rehema akaingia chumbani na kusimama akituangalia pale kitandani, akapigwa butwaa.


Jameela naye alishtuka sana kumuona Rehema, wakabaki wametazamana kwa mshangao kama majogoo yaliyotaka kupigana. Nilimuona Rehema akiwa katika mshtuko mkubwa, midomo yake ilikuwa inamtetemeka.


Kwa nukta chache moyo wangu ulisahahu mapigo yake na yalipoanza tena nilivuta pumzi ndefu, nikazishusha. Nilimtupia jicho Rehema huku nikijaribu kujibaraguza.


“Jameela!” Rehema aliita kwa mshangao mkubwa huku akimkodolea macho Jameela na kubaki mdomo wazi akiwa haamini kumuona pale.


“Rehema!” Jameela naye aliita huku akionesha mshtuko mkubwa sana, kisha akageuza shingo yake kunitazama akionekana kuwa na maswali mengi.


Mimi nilibaki kimya nikiwa nimetahayari sana. Ingawa sikushangaa sana kuona kuwa Rehema na Jameela walikuwa wanafahamiana lakini sikutegemea kuwa wangekutana nyumbani kwangu.


“Unasemaje?” hatimaye nikajikakamua na kuumuliza Rehema.


Rehema alibaki kimya, midomo yake ilikuwa inamtetemeka. Machozi yakaanza kumtiririka mashavuni. Jameela alishindwa kusema chochote na kubaki anashangaa, alitutazama mimi na Rehema kwa zamu akiwa haelewi kilichokuwa kinaendelea, kisha akajiinua na kuketi kitako kitandani huku akiufunika mwili wake kwa shuka.


“Bilali, mbona sielewi, kwani kuna nini kinaendelea hapa? Au…” Alishindwa kumalizia sentensi yake akashusha pumzi akiwa hajui aseme nini.


Nilibaki kimya nikiwa nimetahayari. Rehema akashusha pumzi za ndani kwa ndani, alijaribu kuyazuia machozi yaliyokuwa yanaendelea kumtiririka bila mafanikio. Akajikuta akilia kwa uchungu mbele yangu na Jameela.


“Bilali kwa nini hukuniambia kama wewe na Jameela ni wapenzi, kwa nini siku zote ulikuwa unaniongopea kuwa unanipenda kumbe una mpenzi?”


Niliendelea kuwa kimya nisijue la kufanya. Jameela alinitupia jicho akiwa amekasirika sana, lakini alikuwa akiyakwepa macho ya Rehema.


“Ndiyo maana nakupigia simu hupokei! Ni bora ungenieleza ukweli wala nisingesumbuka hata kuja hapa…”


Rehema alikuwa analia kwa uchungu mbele yangu, kisha aliniambia kwa uchungu kabla hajatoka, “Nakupenda sana Bilali na wewe unajua hilo… wewe ni mwanaume wa maisha yangu, ila kwa hiki ulichonifanyia nashukuru sana na kwa heri.”


Rehema alisema na kugeuka, akatoka taratibu na kuufunga mlango nyuma yake. Chozi lake liliniumiza sana, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilihisi hatia moyoni mwangu lakini sikuweza kuonesha chochote mbele ya Jameela.


Rehema alipotoka tu Jameela akasimama huku akiniangalia kwa hasira na kushika kiuno. “Naomba uniambie ukweli, nini kinaendelea kati yako na Rehema?”


“Sina uhusiano wowote na Rehema. Huyu ni mtu niliyemuokoa siku ile ya mauaji kule Kibiti basi lakini hakuna kinachoendelea, naona anajigonga kwangu hadi kero!”


“Anajigonga? Siyo kwa Rehema ninayemjua! Rehema huwa hana mpango na wanaume, kwanza nimeshangaa kumuona hapa!”


“Kwa hiyo huniamini au vipi, nakwambia sina uhusiano wowote na Rehema…” nilikuwa naongea kwa sauti bila kujua kuwa kumbe Rehema hakuwa ameondoka, alikuwa amesimama sebuleni nje ya mlango.


“Nashukuru sana, kumbe mimi najigonga kwako!” Nikashtushwa na sauti ya Rehema iliyosikika kutokea pale sebuleni. Kisha nikausikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa na kubamizwa kwa nguvu.


Nilijisikia vibaya sana ingawa nafsi nyingine ilinikumbusha kuwa nilikuwa katika uhusiano na wasichana wale kwa sababu moja tu… ngono… na kwa kuwa Rehema hakutaka kushiriki ngono na mimi na alionesha kunikwepa sikuona kwa nini nisiwe na wengine.


Niliinuka na kufungua mlango wa chumbani nikachungulia pale sebuleni lakini nilipotazama sikumuona Rehema kwani alikuwa amekwisha ondoka.


Wakati huo Jameela alisimama nyuma yangu akinitazama kwa hasira huku machozi yakimtoka. Alianza kuvaa nguo zake lakini nikamzuia.


“Jameela, naomba unisikilize basi…”


“Sina haja… mfuate Rehema labda atakusikiliza!”


Nilimsogelea Jameela nikaupeleka mkono wangu wa kulia kwenye uso wake kwa uangalifu huku nikiachia tabasamu la kumlainisha, si kwa kulazimisha. Jameela aliusukuma mkono wangu kwa hasira na kurudi nyuma hatua moja huku aking’aka. “Usiniguse!”


Niliminya midomo yangu huku nikimtazama Jameela kwa uchungu. Jameela alisonya kwa hasira na kuuendea mlango, akaufungua na kutokea sebuleni lakini nikawahi kumzuia asifungue ule mlango wa sebuleni na kutoka nje.


“Sikiliza Jameela,” nilianza kusema huku nimejiegemeza kwenye ule mlango kumzuia Jameela asitoke. Jameela alibaki kimya akinitazama kwa chuki.


“Ukweli ni kwamba, unajua mimi ni bachela na wewe tayari una mtu na siku si nyingi mtafunga ndoa na kwenda kuishi Uarabuni…” nilisema huku nikimkazia macho. Jameela alinitazama kwa makini bila kusema neno.


“Hivi umejiuliza nitaishi vipi bila wewe au unadhani mimi sina wivu? Nimekubali matokeo na sioni sababu ya kuona wivu, kwa nini wewe ufanye hivi? Kumbuka umekuja tuagane, sasa kama kuagana kwenyewe ni kwa staili hii sawa, nakuruhusu uende,” nilisema kwa uchungu huku nikimpisha aondoke.


Jameela alinitazama kwa makini nikauona uso wake ukikunjuka na zile hasira zikaanza kuyeyuka, alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kujipweteka juu ya kochi.




“Ukweli ni kwamba, unajua mimi ni bachela na wewe tayari una mtu na siku si nyingi mtafunga ndoa na kwenda kuishi Uarabuni…” nilisema huku nikimkazia macho. Jameela alinitazama kwa makini bila kusema neno.


“Hivi umejiuliza nitaishi vipi bila wewe au unadhani mimi sina wivu? Nimekubali matokeo na sioni sababu ya kuona wivu, kwa nini wewe ufanye hivi? Kumbuka umekuja tuagane, sasa kama kuagana kwenyewe ni kwa staili hii sawa, nakuruhusu uende,” nilisema kwa uchungu huku nikimpisha aondoke.


Jameela alinitazama kwa makini nikauona uso wake ukikunjuka na zile hasira zikaanza kuyeyuka, alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kujipweteka juu ya kochi.


Endelea...


Nilimfuata pale kwenye kochi nikambembeleza na kuanza kuzitoa tena nguo zake na kuzitupa pale sakafuni moja baada ya nyingine hadi alipobakiwa na nguo ya ndani tu, kisha nikaanza tena kumpapasa.


“Bilali, nisamehe ni kwa kuwa nakupenda sana, unajua kuna wakati nafikiria kutoroka nyumbani, tutafute sehemu yoyote ambayo watu hawatujui tukaishi,” Jameela aliongea huku akinitazama machoni. Nikagundua kuwa alikuwa analengwa na machozi.


“Hata mimi ningetamani hivyo lakini…” nilishindwa kumalizia sentensi yangu baada ya kusikia muungurumo wa gari likifunga breki nje ya nyumba. Kumbe Jameela naye aliusikia ule muungurumo, tukatazamana.


“Rehema huyo karudi,” Jameela aliongea kwa sauti ya chini huku akinikazia macho kwa makini.


“Sidhani,” nilimjibu kwa wasiwasi huku nikijiuliza kama si yeye basi angekuwa nani?


“Na kama atakuwa ni yeye utafanyaje?” Jameela aliniuliza huku akiendelea kunitazama machoni kwa makini.


“Nitamtimua bila...” nilimjibu Jameela lakini sikuweza kumalizia sentensi yangu nikakatishwa na sauti ya mtu aliyekuwa anagonga mlango wangu kwa nguvu.


Aina ya ugongaji wa mlango ilinishtua kidogo, nikajiuliza ni nani aliyekuwa akigonga ule mlango. Mimi na Jameela tukatazamana katika hali ya kuulizana lakini hakuna aliyethubutu kuuliza. Ule mlango ukagongwa tena, lakini safari hii kwa nguvu zaidi.


Nilihisi donge la hasira likinikaba kooni kwangu, hasa nilipokumbuka kuwa huenda alikuwa ni Rehema aliamua kuja kunifanyia vurugu japokuwa alikuwa hataki kufanya ngono na mimi.


Niliinuka haraka nikiwa nimechukizwa na kuusogelea ule mlango nikiwa nina boksa tu tayari kwa kumkabili Rehema, nikaapa kuwa nitamfundisha adabu ili asisahau maishani mwake, nikashika kitasa cha mlango na kuufungua ule mlango huku nikiangalia nje kwa mategemeo ya kumuona Rehema akiwa kasimama mlangoni.


Nilichokiona kikanifanya kupigwa na butwaa, nilijikuta nikiganda kama sanamu nisijue nini nifanye. Adnan alikuwa amesimama nje ya mlango wangu akinitazama huku tabasamu pana la kirafiki likichanua usoni kwake.


Nilijikuta nashindwa kufanya lolote, nikabaki nimekodoa macho yangu kama nilikuwa nimeona mzuka au kitu cha kutisha, nilitamani ardhi ipasuke ili niingie ndani yake kuepuka aibu amabayo ingenikuta muda mfupi baadaye.


Adnan alinitazama kwa makini kuanzia chini hadi juu na kuangua kicheko hafifu huku akiongea kwa sauti ya kunong’ona. “Samahani ndugu yangu kwa kuvuruga starehe yako, kumbe upo na shemeji...”


Nilitaka kusema neno lakini sauti ilikuwa haitoki, nikaishia kufumbua mdomo tu huku nikiendelea kumkodolea macho.


“Basi ngoja niende kwanza kwa shangazi nitarudi baadaye,” Adnan alinong’ona tena na kuanza kupiga hatua kutaka kuondoka.


“Baby, kwani ni nani huyo?” nilisikia sauti ya Jameela ikiniuliza na hapo hapo nikamuona Adnan akisita na moja kwa moja macho yake yakatazama kwa makini kitu kilichokuwa nyuma yangu. Nami nikageuza haraka shingo yangu kutazama nyuma.


Lahaula! Niliishiwa kabisa nguvu baada ya kumuona Jameela akija na kusimama nyuma yangu huku akilalia mgongo wangu na kuchungulia nje ya mlango kumtazama mgeni aliyekuwa akiongea kwa sauti ya chini pale mlangoni. Pasipo kujua kilichokuwa kinaendelea Jameela alikuwa amekuja kuchungulia.


Macho ya Jameela na ya Adnan yalikutana na Jameela akashtuka sana kama aliyekuwa amepigwa na shoti ya umeme, aliruka kurudi nyuma lakini tayari alikuwa amechelwa, kwani Adnan alikuwa amemuona na kumtambua.


Assalale! Mwili wangu ulizizima kwa hofu kama uliopatwa ganzi, kilichotokea pale ilikuwa ni songombingo ambalo liliniachia aibu kubwa isiyoelezeka pale mtaani, Adnan alikasirika sana huku akiwa hayaamini macho yake.


Kama mtu aliyepandwa na wazimu Adnan alirudi nyuma hatua moja na kuruka kwa nguvu zote, alinivamia na kunipiga kikumbo kilichoniangusha chini. Msukumo wa nguvu wa kikumbo hicho ulinitupa chini kwa mshindo mkubwa na kunifanya kugaragara pale sakafuni kama mtu mwenye kifafa.


Wakati huo huo na yeye alianguka kwa kishindo katikati ya sebule kutokana na ile nguvu kubwa aliyoitumia. Jameela alipoona kuwa kaka yake ameanzisha vurugu alipiga kelele ya hofu na kukimbilia chumbani, akajifungia kwa funguo.


Adnan alinirukia tena, mapigano na tifu la aina yake lililozuka pale vilisababisha watu kujaa mlangoni na madirishani na hivyo kujionea sinema ya bure.


Sikukubali, huku nikiwa na boksa tu niliamua kupambana kiume ili nisije kuadhirika, hivyo niliinuka haraka lakini Adnan alikuwa mwepesi, aliruka kama mkizi akanikumba, wote tukapiga mweleka sakafuni. Nikiwa bado nipo sakafuni Adnan aliwahi kusimama huku hasira zikiwa zimempanda kichwani kama mbogo aliyejeruhiwa.


Aliwahi akanikwida shingoni na kiunoni kisha akaninyanyua juu juu kama Joh Cena, yule mcheza mieleka na kunibwaga juu ya meza ya kioo iliyokuwa pale sebuleni. Vioo vilipasuka vipande vipande na kuniumiza mgongo, nilihisi maumivu makali yasiyoelezeka na kupiga yowe kali huku nikijitahidi kusimama.


Hata hivyo, Adnan alionekana kuwa mpiganaji wa kiwango cha juu huku akionekana kuwa makini sana akizisoma nyendo zangu. Akiwa amepandwa na hasira aliruka na kunivaa akanipiga kichwa kikavu kilichonipata katikati ya macho na pua.


Damu zikaanza kunitoka puani utadhani mrija wa maji uliopasuka! Nilisalimu amri na kushika pua yangu nikaiminya nikijaribu kuzuia damu isiendelee kunitoka, na wakati nikiizuia damu isitoke Adnan alinirukia na kunikaba kabali ya nguvu.


Nilijitahidi kukukuruka kutaka kujitoa kwenye ile kabali lakini Adnan alizidisha kabali yake na kunifanya kuanza kuishiwa nguvu. Mwisho wa siku mchezo uliisha huku Adnan akiibuka mshindi na kuondoka na Jameela huku wakiniacha naendelea kuvuja damu.




Damu zikaanza kunitoka puani utadhani mrija wa maji uliopasuka! Nilisalimu amri na kushika pua yangu nikaiminya nikijaribu kuzuia damu isiendelee kunitoka, na wakati nikiizuia damu isitoke Adnan alinirukia na kunikaba kabali ya nguvu.


Nilijitahidi kukukuruka kutaka kujitoa kwenye ile kabali lakini Adnan alizidisha kabali yake na kunifanya kuanza kuishiwa nguvu. Mwisho wa siku mchezo uliisha huku Adnan akiibuka mshindi na kuondoka na Jameela huku wakiniacha naendelea kuvuja damu.


Endelea...


Usiku wa siku ile sikupata kabisa usingizi, niliwaza mengi kuhusu lile tukio la kufumaniwa na Adnan nikiwa na dada yake. Niliwaza kuhusu lile gari nililoahidiwa na Adnan ambalo aliamua kuondoka nalo baada ya sakata lile. Dah! Nilijilaumu sana kwa tama zangu na kutokuwa mwangalifu.


Nilimkumbuka Rehema, nikatamani nimtafute ili nimuombe msamaha maana niliamini kuwa machozi yake yalikuwa yamebeba laana fulani iliyosababisha nifumaniwe na kupata aibu ya karne pale mtaani. Usiku mzima nikawa namuwaza Rehema tu.


Ilipofika saa nane za usiku uvumilivu ulinishinda, nilichukua simu yangu na kupiga namba ya Rehema, simu iliita kwa muda mrefu na kukata bila majibu, nikapiga tena, baada ya muda mrefu wa kuita nikasikia simu ikipokelewa upande wa pili.


“Hello… Rehema!” nilisema mara baada ya simu kupokewa upande wa pili.


“Unasemaje?” Rehema aliniuliza kwa sauti tulivu.


“Rehema, samahani sana kwa yote yaliyotokea… naomba…” simu ikakatwa kabla sijamaliza kuongea! Nilipiga mara ya pili lakini simu ilikuwa haipatikani, nikasonya na kuitupa ile simu kando.


Kwa kweli sikuweza kupata usingizi, niliinuka nikaelekea sebuleni na kuwasha runinga, hata hivyo, pamoja na kukodoa macho yangu kwenye runinga lakini sikuwa naelewa chochote. Kulipoanza kupambazuka niliamka na kuelekea bafuni nikaoga na baada ya jua kutoka nilikwenda Ilala Sharif Shamba kumtafuta Rehema.


Nilifika nyumbani kwa Bi Aisha na kusimama nje ya fensi karibu ya lango la mbele la kuingilia nikiwa na wasiwasi, nikaangalia huku na huko kwa wasiwasi na kushusha pumzi za ndani kwa ndani kisha nikabonyeza kitufe cha kengele kilichokuwa kando ya lile geti.


Nilipoona kimya nikabonyeza tena kile kitufe cha kengele na muda ule ule nikaisikia sauti ya Bi Aisha kutoka ndani ikinikaribisha.


Mara geti dogo lililokuwa kando ya lile geti kubwa likafunguliwa na Bi Aisha akachungulia nje na kuniona, nikamuona akiachia tabasamu.


“Karibu, baba,” alinikaribisha huku akisogea kando kunipisha niingie. Nilishusha pumzi huku nikibabaika kidogo.


“Sh’kamoo!” nilimsalimia nikiwa bado nimetahayari.


“Marhaba. Karibu ndani, Bilali!” alijibu huku akinitazama kwa udadisi.


Nilionekana kusita sana kuingia nikatupa macho yangu kuangalia ndani ya ule uzio kupitia upenyo wa geti lililokuwa wazi nikijaribu kuangalia kama Rehema alikuwepo mazingira yale. Bi Aisha alizidi kunitazama kwa udadisi zaidi.


“Vipi, kuna tatizo, Bilali?” aliniuliza huku akinikazia macho.


Nilitingisha kichwa changu kukataa huku nikiendelea kuchungulia ndani ya fensi. Bi Aisha aliguna huku akinitazama kwa udadisi zaidi kisha akageuza shingo yake kutazama ndani ambako macho yangu yalikuwa yameelekea.


“Rehema yupo?” hatimaye nilimuuliza Bi Aisha.


“Hayupo, amekwenda hospitali ya Amana,” alinijibu huku akinikazia macho. Jibu lake likanishtua sana.


“Hospitali… kuna nini?” niliuliza kwa wasiwasi.


“Tangu jana aliporudi alikuwa analalamika kuwa hajisikii vizuri,” alinijibu huku macho yake yakionekana kuficha kitu, sikujua kama ilikuwa ni hasira, chuki au huruma.


Sikutaka kuendelea kusimama pale, niliondoka haraka nikashika njia ya kuelekea Amana bila hata kuaga, nilimsikia Bi Aisha akiguna lakini sikujali wala kugeuka, niliendelea na safari yangu nikimwacha akinisindikiza kwa macho yenye mshangao.


Nilitembea haraka hadi Amana, na nilipokuwa naingia kwenye geti la kuingilia katika hospitali ya Amana nikamuona Rehema akiwa anafungua mlango wa gari lake ili aingie, kabla hajaingia aliniona na kushtuka sana. Nilimsogelea na kusimama mbele yake.


“Umefuata nini hapa?” aliniuliza huku kakunja uso wake.


“Nimekufuata wewe! Ni nani anayeweza kuendelea na kazi zake wakati ampendaye yuko hospitali?” biliongea kwa utulivu huku nikijitahidi sana kutabasamu.


Rehema hakujibu kitu, alinitazama kwa dharau kuanzia chini hadi juu, akinishusha na kunipandisha kisha akaangalia kando kwa muda akionekana kuwaza mbali.


“Rehema, najua nimekuudhi sana, nimekukosea sana na nimekuumiza sana… lakini sasa nimetambua kuwa kweli unanipenda kwa dhati, hivyo naomba unisikilize, usinihukumu kabla hujanipa nafasi nikuelezee…”


Rehema alionesha ishara ya kunitaka nisiendelee kuongea. “Huna unachoweza kunieleza, bwana… au unadhani sijui kilichotokea huko nyuma baada ya mimi kuondoka nyumbani kwako? Please leave me alone!”


Nilishtuka sana kusikia yale maneno kutoka kwa Rehema lakini sikutaka kuonesha mshtuko wangu, nikamkazia macho. “Kilitokea nini?”


“Hata ukijidai kuficha lakini najua, na kila mtu anajua hata mama yangu mkubwa pia anajua. Kwa kuwa umefumaniwa na kupata aibu ya mwaka kwa hiyo umeona ukimbilie kwangu ili kuficha aibu yako, siyo?” alisema Rehema huku kanikazia macho. Nikaduwaa.


“Wewe siyo wa kutembea na dada wa rafiki yako, tena unajua kabisa kuwa siku si nyingi anaolewa,” aliongeza Rehema na kuingia ndani ya gari yake.


Nilishtuka sana lakini nikaamua kujikaza kisabuni huku nikimzuia asiondoe gari lake. Rehema akanitazama kwa makini huku akionekana kuzuia hasira zake kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Naomba nikuulize jambo, Bilali,” alisema huku akitoka ndani ya gari na kusimama mbele yangu huku akinitazama moja kwa moja usoni kwa macho makali yaliyokuwa yakiwaka kwa hasira.


“Ruksa, niulize!” nilijibu huku na mimi nikimtazama moja kwa moja usoni kwa makini. Kwa kitambo kifupi tukabaki tumetazamama kama majogoo yaliyotaka kupigana.


“Hivi, wewe unaamini kama kupenda kupo?” aliniuliza akiwa anaendelea kunitazama moja kwa moja machoni pasipo kupepesa macho.


Nilitulia kwa sekunde kadhaa nikimtumbulia macho huku nikijaribu kufikiria kidogo, kisha nikashusha pumzi ndefu.


“Mapenzi yapo, wapo wanaopenda na wapo wanaopendwa… yule anayependa huwa yumo mashakani, kwani anao uwezo wa kuyafanya mambo yasiyowezekana yakawa ya kweli kwa sababu ya kupenda, na yule anayependwa… yeye nadhani, mara nyingi… apendwaye huwa hajali!”


Rehema aliminya midomo yake na kushusha pumzi.


“Ni kweli, mara nyingi anayependwa huwa hajali! Lakini unajua kama kuna tofauti kati ya mtu anayependa na anayetamani?” aliniuliza tena akiwa bado ananitazama moja kwa moja machoni pasipo kupepesa macho.


“Mimi namzungumzia mtu anayependa, siyo anayetamani,” nilisema na kumfanya Rehema aangue kicheko cha dharau kisha akaingia ndani ya gari lake na kufunga mlango.


“Sidhani kama mimi na wewe tunasafiri kwenye boti moja. Ingawa nakupenda sana lakini sioni namna nyingine ya kufanya, kama ni uvumilivu nimefika mwisho, kwa heri Bilali na ninaomba usinitafute tena!” alisema na kuwasha injini ya gari lake kisha akaanza kuliondoa taratibu.





“Ni kweli, mara nyingi anayependwa huwa hajali! Lakini unajua kama kuna tofauti kati ya mtu anayependa na anayetamani?” aliniuliza tena akiwa bado ananitazama moja kwa moja machoni pasipo kupepesa macho.


“Mimi namzungumzia mtu anayependa, siyo anayetamani,” nilisema na kumfanya Rehema aangue kicheko cha dharau kisha akaingia ndani ya gari lake na kufunga mlango.


“Sidhani kama mimi na wewe tunasafiri kwenye boti moja. Ingawa nakupenda sana lakini sioni namna nyingine ya kufanya, kama ni uvumilivu nimefika mwisho, kwa heri Bilali na ninaomba usinitafute tena!” alisema na kuwasha injini ya gari lake kisha akaanza kuliondoa taratibu.


Endelea...


Nilibaki nikiwa nimesimama nikilisindikiza gari la Rehema kwa huzuni huku nikiwa nimekata tamaa. Nilihisi donge la uchungu likinikaba kooni na kunifanya nishindwe kupumua vizuri, machozi yakaanza kunitoka machoni na kuwafanya watu waliokuwa wakipita jirani na eneo lile wanitazame kwa mshangao.


Niliangusha kilio kilichomfanya Rehema ageuke kunitazama kwa mshangao ingawa bado macho yake yalionesha chuki dhidi yangu, kisha nikamuona akisita na kukanyaga breki, gari likasimama.


Alishusha kioo cha gari na kutoa kichwa chake nje kisha akaniashiria kwa mkono nimfuate, nilimfuata kwa unyonge huku nikipangusa machozi, akaniambia niingie ndani ya gari, nami sikujivunga niliufungua mlango wa mbele wa gari kushoto kwa dereva na kuingia.


Rehema alinitupia jicho na kuliondoa gari lake bila kusema chochote, gari likatoka kwenye geti la kuingilia la hospitali ya Amana na kukata kushoto kisha tukaifuata barabara iliyokwenda kuungana na barabara ya Uhuru katika ukumbi wa Amana Vijana, akakunja tena kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Uhuru.


Aliendesha gari lake na kuvukaa vibanda vya wasusi wa Kimasai kisha akakunja kuingia mtaa wa Mafao akiyapita maghorofa ya Ilala na kwenda moja kwa moja hadi akatokea katika barabara ya Kawawa, hapo akakata kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Kawawa kama anaelekea Magomeni.


Hadi wakati huo sikujua tulikuwa tunaelekea wapi, nilibaki kimya tu nikimtazama kwa kuibia bila kusema lolote.


Rehema aliongeza mwendo wa gari na mbele kidogo akalivuka jengo la hoteli ya Lamada na alipofika mwisho wa lile jengo nikamuona akipunguza mwendo na kukunja akaingia upande wa kushoto, kisha akaliingiza gari lake kwenye geti la kuingilia katika ile hoteli ya Lamada.


Tulipoingia ndani ya ile hoteli Rehema akazima injini ya gari na kunitazama kisha akashuka, nami nikashuka kumfuata. Nilimfuata kimya kimya na tukatafuta sehemu nzuri ya kukaa kwenye mgahawa uliokuwa ndani ya hoteli ile ya Lamada.


Kwenye mgahawa ule tulikuta wateja wachache wakiwa wameketi, Rehema akaagiza mchemsho wa kuku wa kienyeji na chapatti moja. Mimi niliagiza maziwa ya moto, sambusa mbili na soseji moja.


Mhudumu alipoondoka kwenda kuleta oda zetu takabaki tukiwa kimya kila mmoja akiwaza lake, na baada ya kitambo tulipoletewa chakula, tukaanza kula taratibu huku kila mmoja akiwa kimya.


Wakati tunakula Rehema alikuwa akinitupia jicho mara kwa mara akionekana kuwa makini zaidi na mimi.


“Rehema… najua nimekukosea sana, lakini ni vizuri kama tutazungumza kuhusu matatizo yetu kuliko ukimya huu! Ni pepo mbaya tu alinipitia lakini naahidi sitorudia tena…”


“Kwani ulikuwa unatakaje?” Rehema alinikata kauli.


“Tafadhali naaomba uniahidi kuwa umenisamehe,” nilisema huku nikimkazia macho.


“Nimekwisha kusamehe hata kabla hujaniomba msamaha, ingawa siwezi kusahau yote uliyonifanyia,” aliniambia huku akiendelea kula chakula taratibu.


“Nashukuru kama umenisamehe, na ninashukuru kwa kuwa unanipenda lakini naomba ubadilike kidogo ili na mimi nibadilike, kama kweli unanipenda kwa nini uendelee kukataa kunanihii?” nilimuuliza tena huku nikiwa siyatoi macho yangu kwenye uso wake.


“Je, ni lazima swali lako nilijibu sasa hivi?” Rehema aliniuliza huku na yeye akinikazia macho.


“Ikikupendeza unaweza kunijibu sasa hivi, vinginevyo naweza kukupa muda!” nilisema kwa sauti tulivu nikiendelea kumtazama.


“Basi nipe muda, kwani ni swali gumu lililoulizwa katika wakati mbaya na mahali pagumu!” alisema huku akitafuna nyama ya kuku.


“Hebu tuwe wakweli, Rehema, msichana mrembo kama wewe unaweza kuishi bila kufanya mapenzi? Hii hainiingii akilini… Wanaume wangapi, tena wenye mali zao wanakutongoza, kwani wewe ni nani hadi usiingie majaribuni?” nilimuuliza kwa wasiwasi huku nikimkazia macho kujaribu kuyasoma mawazo yake.


Rehema alinitazama kwa makini kwa kitambo kirefu na kuonekana kukerwa sana na kauli yangu.


“Kwa kweli unanikosea sana heshima, Bilali, kwa nini uongeee vitu usivyovijua? Naomba uelewe, mimi siko kama unavyodhani!” Rehema aliongea kwa huzuni.


“Kumbuka ni wewe pekee niliyeamua kukuweka kwenye moyo wangu wa nyama. Najua huwezi kuamini ila siku nikipotea jumla ndiyo utajua kuwa nilikuwa nakupenda kiasi gani,” Rehema alisema na kuinamisha uso wake chini akionekana kuwaza mbali sana. Machozi yalikuwa yakimlenga.


Nilishtuka sana kwa maneno yale. Nilitaka kusema neno lakini nikasita baada ya kuhisi kulikuwa na mtu aliyeingia na kusimama nyuma yangu. Nikageuza shingo yangu na kumuona mwanadada mmoja aliyekuwa na umbile kubwa lakini lililovutia.


Kwa yeyote awaye mwanaume rijali hapana shaka kama angemuona angekiri kuwa alikuwa na umbo zuri sana la kibantu na alikuwa ni moto wa kuotea mbali.


Kwa mlingano wa macho tu, alitoa tafsiri ya kuwa na ule uzuri usiomithilika, uzuri kama wa mdoli.


Nywele zake zilikuwa nyeusi tii zilizotumwa vema sambamba na sura yake ya kitoto yenye mvuto wa asilimia mia moja. Nyusi na kope zake zilikuwa ndefu zilizong’ara na kuyafanya macho yake yawe wazi nusu.


Pua yake ilikuwa ndefu kiasi, nyoofu ya wastani na midomo yake ilikuwa minene. Alikuwa na rangi angavu yenye ung’avu wa kuteleza.


Japo alikuwa na umbo kubwa lakini kifua chake kilibeba matiti ya wastani na tumbo lake lilikuwa flati huku kiuno chake kikiwa chembamba mithili ya dondola. Miguu yake ilikuwa mizuri mno iliyotazamika.


Mwanadada yule alikuwa amevaa gauni zuri la kitenge na alikadiriwa kuwa na miaka kati ya 25 na 28. Alikuwa amesimama pale akimtazama sana Rehema kama aliyekuwa akimfananisha.


Mara Rehema akainua uso wake na kumtupia jicho yule mwanadada kisha akanitazama kwa makini.





Japo alikuwa na umbo kubwa lakini kifua chake kilibeba matiti ya wastani na tumbo lake lilikuwa flati huku kiuno chake kikiwa chembamba mithili ya dondola. Miguu yake ilikuwa mizuri mno iliyotazamika.


Mwanadada yule alikuwa amevaa gauni zuri la kitenge na alikadiriwa kuwa na miaka kati ya 25 na 28. Alikuwa amesimama pale akimtazama sana Rehema kama aliyekuwa akimfananisha.


Mara Rehema akainua uso wake na kumtupia jicho yule mwanadada kisha akanitazama kwa makini.


Endelea...


Nilimtazama tena yule mwanadada kwa makini lakini sikumfahamu kabisa hivyo sikuwa na hofu kama angeweza kuwa mmoja wa wasichana niliofahamiana nao. Nikageuza tena shingo yangu kumtazama Rehema ambaye aliendelea kumtazama yule mwanadada katika namna ya kumfananisha. Wakaendelea kutazamana kwa makini zaidi kwa kitambo kirefu.


“Unamfahamu?” nilimuuliza Rehema huku nikimkazia macho.


“Namkumbuka, lakini sura yake inanijia na kutoka,” alisema rehema huku akiendelea kumtazama yule mwanadada.


Yule mwanadada akatafuta kiti akaketi huku akigeuka tena kumtazama Rehema, kisha akaachia tabasamu pana na kuinuka akitufuata pale tulipoketi.


“Rehema, umenisahau?” yule mwanadada aliuliza huku akiketi kwenye kiti karibu ya Rehema.


Rehema akaachia tabasamu. “Sura naikukumbuka lakini umen’toka kidogo. Nikumbushe basi.”


“Miye Joyce.”


Rehema akamtazama kwa makini na kuonesha kumkumbuka. “Joyce… Mgaya, siyo?”


“Ee… Joyce Mgaya. Si tulikuwa pamoja pale Forodhani Secondary au umesahau?”


“Ndiiiiyooo! Mtumeeee! Ndiyo uko hivi, babu wee! Umekuwa bonge!”


Joyce akacheka sana huku akimshika Rehema begani. “Ndiyo hivyo tena! Nimeridhika mwenziyo!” alisema Joyce na kugeuza shingo yake kunitazama kwa makini huku akiangua kicheko cha kishambenga. Rehema akatabasamu tu.


Nilimtupia jicho la wizi Joyce hukunami nikitabasamu.


“Vipi, ndiye shemegi huyu?” Joyce aliuliza kwa bashasha huku akinikazia macho.


“We nawe! Hujaacha tu, hata hungoji kutambulishwa?” Rehema alisema huku akiguna na kugeuka kunitazama kisha akaachia tabasamu.


“Aa babu, ngoja ngoja yaumiza matumbo ati!”


“Okay… ni shemeji yako mtarajiwa,” Rehema alisema huku akinishika mkono wangu na akuviminya minya vidole vyangu vya mkono.


Joyce akanyoosha mkono wake kwa bashasha kunisalimia. Na mimi nikanyoosha mkono wangu na kukutanisha na mkono wake. Tukasalimiana.


“Ooh shemegi, nimefurahi sana kukufahamu!” alisema Joyce kwa uchangamfu. Nikaachia tabasamu huku nikibetua kichwa changu bila kusema neno.


“Umeshaolewa, Joyce?” Rehema alimuuliza Joyce huku akimtazama kwa makini.


“Hee! Zamani gani! Lile balaa lilipokwisha tu nikaolewa. Si uliyasikia yaliyonikuta mwenziyo baada ya kifo cha mama yangu?”


“Niliyasikia! Pole sana mwaya! Halafu nikasikia sakata lile lilikufanya ukalazwa Muhimbili. Ni kweli?”


“Kweli! Yule mama aling’ang’ania mpaka baba akanileta bila ya miye mwenyewe kupenda. Lakini sikukaa siku nyingi nikatoroka,” alisema Joyce na kuachia kicheko cha kishambenga.


“Lo! Pole sana, na yule kaka’ko… Michael, yuko wapi siku hizi?”


“Alikwenda zake Sauzi Afrika! Yule ndiyo basi tena, nasikia ana jimama la Kisauzi linamlea!” Joyce alisema na kuachia tena kicheko cha kishambenga.


Waliendelea kuongea na kukumbushana mengi tangu walipokuwa shule, wakati huo mimi nilikuwa kimya tu nikiwasikiliza. Joyce alikuwa mcheshi na muongeaji sana, kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumchoka.




* * * * *




Jioni ya siku ile baada ya kuachana na Rehema nilikuwa nimetulia sebuleni kwangu juu ya sofa nikiwa nawaza sana, kwani pamoja na juhudi zote za kumshawishi sana Rehema lakini aliendelea kusisitiza kuwa mbali nami.


Pale sebuleni nilikuwa nimewasha runinga na muda ule nilikuwa nimeweka chaneli iliyokuwa ikionesha kipindi cha wanyama. Japo nilikuwa nimetulia na macho yangu yalikodolea kwenye runinga lakini ukweli sikuwa nikiona chochote kwenye ile runinga.


Muda wote nilikuwa namfikiria Rehema tu na sikujua nifanye nini ili kuurudisha moyo wake kwangu.


Mbele yangu juu ya meza kulikuwa na chupa kubwa ya konyagi, chupa ya soda Sprite na bilauri moja. Tayari nilikuwa nimeshakunywa nusu na niliendelea kumimina pombe kwenye bilauri na kuchanganya na soda, kisha nikanyanyua bilauri na kuinywa pombe yote iliyomo ndani yake na kuikita ile bilauri juu ya meza huku nikisisimkwa.


Kijasho kikaanza kunitoka usoni, nikaijaza tena pombe ile bilauri na kuitazama kwa makini lakini kabla sijainywa nikasikia sauti ya mtu akigonga mlango. Nilinyanyuka na kwenda kuufungua ule mlango kisha nikachungulia nje.


Rehema alikuwa kasimama mbele yangu huku akiniangalia kwa wasiwasi jinsi ambavyo jasho lilikuwa linanitoka usoni kutokana na ile pombe niliyokunywa. Nilibaki nikimkodolea Rehema kwa macho ya kilevi. Rehema alinitazama kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


Nilimpisha nikikaribisha ndani, bila kujivunga Rehema aliingia ndani na kuketi kwenye kochi huku akinitazama kwa makini. “Unakunywa pombe?” aliniuliza kwa mshangao mkubwa.


Sikumjibu, niliinua tena ile bilauri nikaigida ile pombe yote na kuikita ile bilauri juu ya meza huku nikisisimkwa sana. Rehema alitingisha kichwa chake kwa huzuni huku akiinuka na kuichukua ile chupa ya konyagi akaiondoa pale mbele yangu.


“Kwa nini unakunywa pombe? Ni kipi kibaya nimekifanya hadi uchukue uamuzi huu wa kunywa pombe?” Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa makini. Sikumjibu bali nilitulia tu kama sanamu huku nikimwangalia kwa matamanio.


Akiwa bado amezubaa akinitazama kwa mshangao nilimsogelea nikapeleka mikono yangu na kuipapasa shingo yake. Rehema aliendelea kunitazama, nikashusha mikono yangu na kuanza kumgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi.


Nikamgusa huku na kule akiwa ametulia tu akinitazama. Nilipotaka kumvua nguo akanizuia na alipogundua nilichokuwa nataka kufanya akagutuka na kujaribu kujitoa kwenye mikono yangu. Sikutaka kumpa nafasi, nikazidi kumng’ang’ania.


Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu, nikaamua kutumia nguvu, niliamua kumbaka kama angeendelea kushikilia msimamo wake na kutoniruhusu kuzitoa nguo zake kistaarabu.


Pepo mbaya wa ngono alikuwa amefanikiwa kuikamata nafsi yangu, sikutaka tena kungoja, nikazirarua nguo zake kisha nikaichana sidiria yake, na hatimaye nikaiondoa nguo yake ya ndani, sasa akabaki mtupu kabisa kama alivyozaliwa huku harufu nzuri ya manukato yake ikinishawishi kuendelea na hatua inayofuata.


Nilipouona mwili wake mtupu msisimko wa mapenzi ukanitambaa mwilini na sasa mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda mbio isivyo kawaida. Nilimtazama kwa uchu kama vile fisi atazamavyo mzoga. Rehema alihaha huku na kule asiamini kile kilichokuwa kinatokea mbele yake.


“Please, let me go. Leave me please!” (Tafadhali, niache niende. Niache tafadhali) rehema alilia kwa uchungu huku akinibembeleza. Sikutaka kabisa kumsikiliza.


Akajitahidi kujitoa mikononi mwangu na kufanikiwa. “Have you gone crazy?” (Umechanganyikiwa?) Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa hofu.


Akataka kukimbilia nje uchi lakini nikamdaka mkono na kumsukumia juu ya kochi ili niweze kutimiza lengo langu… Kamwe sikuwahi kumwona binti yule akiwa katika uoga namna ile! Alikuwa amekodoa macho yake… na alikuwa anatetemeka.


Niliitoa fulani niliyokuwa nimeivaa na kuitupa chini kisha nikafungua mkanda wa suruali na kuivuta suruali yangu nikiiacha idondoke chini, ikadondoka na kubakiwa na boksa.


Muda ule sikuwa na huruma hata kidogo, nilichotaka ni kitu kimoja tu, ngono. Nifanye naye ngono kisha akinichukia na achukie. Nikazidi kumtazama kwa matamanio huku nikihema kwa nguvu kutokana na ashki, nikamrukia.


Mara akatokwa na kelele kubwa zilizonishtua sana ambazo sikuwa nimezitegemea kabisa. Sikujua kama angeweza kufanya kitendo kile.


“Ananibakaaaaa! Nisaidieeni ananibaaaka!” Alipiga kelele kubwa, nilimshika nikajaribu kumziba mdomo lakini alining’ata na kunifanya niugulie kwa maumivu. Kisha akaendelea kupiga kelele ambazo ziliwafanya wasamalia wema kukimbilia pale zilipokuwa zikisikika kelele.


Mara mlango wangu ukapigwa kumbo na watu wakaingia na kunikuta nikiwa juu ya Rehema, wakaninivagaa na kuanza kunishushia kipigo. Nilijaribu kujitetea lakini walizidi kunishushia kipigo hadi nikapoteza fahamu na sikujua tena kilichoendelea baada ya hapo.




Mara akatokwa na kelele kubwa zilizonishtua sana ambazo sikuwa nimezitegemea kabisa. Sikujua kama angeweza kufanya kitendo kile.


“Ananibakaaaaa! Nisaidieeni ananibaaaka!” Alipiga kelele kubwa, nilimshika nikajaribu kumziba mdomo lakini alining’ata na kunifanya niugulie kwa maumivu. Kisha akaendelea kupiga kelele ambazo ziliwafanya wasamalia wema kukimbilia pale zilipokuwa zikisikika kelele.


Mara mlango wangu ukapigwa kumbo na watu wakaingia na kunikuta nikiwa juu ya Rehema, wakaninivagaa na kuanza kunishushia kipigo. Nilijaribu kujitetea lakini walizidi kunishushia kipigo hadi nikapoteza fahamu na sikujua tena kilichoendelea baada ya hapo.


______


Nilipozinduka nilijikuta nikiwa katika hospitali ya Amana nikiwa na majeraha mwilini huku nimefungwa pingu mkononi iliyounganishwa na kitanda. Nilikuwa na maumivu makali sana mwili mzima. Nikajaribu kukumbuka kilichonitokea na mara nikakumbuka kuwa nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji.


Nilipogeuka kutazama upande mwingine macho yangu yalikutana na macho ya ofisa wa polisi aliyekuwa na cheo cha Sajenti ambaye alikuwa kaketi pembeni kwenye kiti akinitazama kwa makini huku kakunja sura yake.


Niliendelea kuwepo pale hospitali kwa siku tatu na baada ya nguvu kunirejea mwilini niliondolewa pale hospitali nikapelekwa mahabusu ya kituo cha polisi cha Buguruni. Nilikaa pale mahubusu nikisubiri kufunguliwa kesi mbaya ya ubakaji.


Siku iliyofuata wakati nikiwa nimejikunyata kwenye kona ya chumba cha mahabusu nilishuhudia lango la mahabusu ile likifunguliwa na askari mmoja ambaye aliita jina langu. Kwa unyonge niliinua shingo yangu kumtazama yule askari ambaye alikuwa na cheo cha Koplo.


“We mbakaji, inuka unifuate!” alisema baada ya kuona namtazama kwa wasiwasi.


Mahabusu wote katika kile chumba walinitazama kwa makini, baadhi yao walinihurumia lakini wengine walitabasamu kwa kejeli. Niliinuka kwa unyonge nikamfuata yule askari, aliniongoza tukipita kwenye korido hadi kwenye mlango wa ofisi ya mkuu wa kituo.


Tulipoingia ndani ya ofisi ile ya mkuu wa kituo nilipigwa butwaa baada ya kumkuta mama yake mkubwa na Rehema, Bi Aisha akiwa kwenye ile ofisi na Mkuu wa Kituo kile, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Shaban Mungi, ambaye alikuwa kajiegemeza kwenye kiti chake cha kuzunguka. Wote waligeuka kunitazama kwa makini nilipokuwa naingia.


Nilijikuta nagwaya baada ya kuhisi uwepo wa hali ya majonzi na ukimya mzito sana ndani ya ile ofisi. Nilipowatupia jicho la wizi niliowakuta mle ofisini niliona huzuni kwenye macho yao. Mkuu wa kituo alinionesha kiti, nikaketi nikiwa na wasiwasi mkubwa.


Mkuu wa kituo aliendelea kunitazama kwa macho yaliyokuwa yameficha kitu nyuma yake. Sikuweza kujua nini kilichokuwa kikiendelea pale, nikajiuliza, yuko wapi Rehema?


Nilianza kuingiwa wasiwasi, hata hivyo, nilibaki kimya nikiwatazama wote kwa makini ingawa nilianza kuhisi kuwa kulikuwa na jambo lisilo la kawaida lililokuwa limetokea. Niliogopa kuuliza. Bi Aisha alinitazama akashindwa kuvumilia, nilimuona akiinuka na kutoka nje huku akilia kwa uchungu mkubwa.


Mkuu wa kituo alishusha pumzi na kufungua droo moja katika meza yake, kisha akatoa bahasha ndogo iliyokuwa na barua ndani yake, akaishika vizuri ile bahasha mkononi mwake huku akinitazama kwa huzuni.


“Bilali, kuanzia sasa uko huru, shika barua yako!” aliniambia huku akinyoosha mkono wake kunipa ile bahasha.


Kauli ya yule mkuu wa kituo cha polisi ikanishangaza sana, nilidhani labda nilikuwa ndotoni na mara ningeamka ningekuta mambo hayapo hivyo, lakini yule mkuu wa kituo aliendelea kunyoosha mkono wake kunitaka nichukue ile barua.


Nilimtazama usoni kutaka kuona kama kweli hatanii kisha nikaipokea ile barua huku mikono yangu ikitetemeka, ilitetemeka kwa sababu sikujua ilitoka wapi na ilihusu nini. Niliitazama ile barua kwa wasiwasi.


“Unaweza kusoma hapa hapa ukipenda!” yule mkuu wa kituo aliniambia huku akifuta machozi yake. Nikiwa na wasiwasi niliifungua ile bahasha na ndani yake kulikuwa na barua ndefu iliyotoka kwa Rehema.


“Mpenzi Bilali, haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa mbakaji, bali nimefanya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni na ninapenda uishi miaka mingi…


“Bilali ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa nawe kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba yako japo ulijaribu sana kuniumiza kihisia lakini bado sikuacha kukupenda…


“Ni kweli sikutaka kulala na wewe kwa kuwa nina kasoro kubwa ambayo hainipi hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe, sikutaka kuwa muuaji kwa kuruhusu unibake… hivi, Bilali unadhani mpapaso wako haukunisisimua? Nilisisimka hasa na nilitamani nikutimizie kwa hiari kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi, lakini… lakini nisingeweza kukuua…


“Bilali, wala usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake. Kifo hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa nilikupenda sana…


“Nilitaka kukwambia lakini nilishindwa, nimekuwa nikiishi na virusi vya UKIMWI kwa muda mrefu baada ya kuambukizwa na wazazi wangu… nilizaliwa nikiwa na Virus vya Ukimwi, na mama kabla ya kufa alinikanya kuwa ni heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia…


“Kwa kuwa utaalamu umeongezeka nilikubali unioe kwa kuwa tungefuata ushauri wa kitaalamu ili nisikuambukize, maana wewe huna hatia na haustahili kufa… laiti kama ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa muuaji…


“Ninafurahi kuwa nakufa kama shujaa. Ninayaandika haya huku chupa ya sumu ikiwa pembeni yangu, nakufa leo lakini nimewaomba wakuache uwe huru. Bahati nzuri mkuu wa kituo ni baba yangu mdogo hivyo naamini atakuacha uwe huru, huru kabisa, wakati mimi nikiungana na mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili siku moja nisije kuua yeyote. Buriani Bilali, mpenzi wa moyo wangu…”


Sikujua kilichoendelea baada ya pale kwani niliishiwa nguvu, moyo wangu ukashikwa na mfadhaiko, mikono yangu ilikuwa inatetemeka na jasho jingi likaanza kunitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu.


Macho yangu nayo yakaanza kupoteza nguvu ya kuona na hatimaye shughuli mbalimbali za mwili wangu nazo nikazihisi kuwa zilikuwa mbioni kusitisha utendaji wake.


______


Siku mbili baadaye nilikwenda kwenye makaburi ya Kisutu ambako Rehema alikuwa amezikwa, nilisimama mbele ya kaburi jipya la Rehema na kulitazama kwa huzuni, nikafuta machozi yaliyokuwa yakinilengalenga.


Haikuwa ndoto, ni kweli ilitokea kuwa Rehema alijiua kwa sumu na kuzikwa… barua ile niliyopewa ilikuwa imetwa kando ya mwili wake chumbani… sasa macho ya watu yalikuwa yakinitazama kwa kunisuta, wapo waliokuwa na hasira juu yangu, wapo ambao walinitazama kwa dharau na baadhi walinitazama kwa huzuni. Kwa kweli sikujua nifanye nini!


Nilitamani ardhi ipasuke ili nijifiche chini ya ardhi kukwepa macho ya jamii. Nilitamani kunywa sumu ili nami niondoke hapa duniani, hasa baada ya kuujua ukweli kuhusu maisha ya Rehema, mwanamke aliyenijali na kunipenda kwa dhati!


Niliendelea kusimama nikilitazama kaburi la Rehema kwa kitambo kirefu huku machozi yakinitoka. Nilifuta machozi nikashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.


“Upumzike pema peponi Rehema… kamwe sitakusahau mpenzi!” nilisema kwa huzuni kisha nikainamisha kichwa changu mbele ya kaburi la rehema kama ishara ya kutoa heshima zangu za mwisho. Sikuweza kuendelea kusimama pale nikaondoka taratibu kwa huzuni, mikono yangu ikiwa nyuma.


MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog