Simulizi : Jino Kwa Jino (2)
Sehemu Ya : Tatu (3)
Ndani ya uwa ndipo waliziona selo ndogo ndogo zilizojengwa zikitumbukia kwa ndani na zingine zikiwa kubwa kubwa katika eneo la katikati ya ukuta huu ambao muda huu walikuwa wamejilaza kwa juu yake wakizilalia nyaya kama godoro Dodoma.
“Twen’zetu!” Akaongea Rebecca baada ya kuona kuna usalama wa kutosha kwa ndani wote wakajigeuza na kuning’iniza miguu kisha kwa pamoja wakajiachia mpaka chini kutokea juu bila woga walipotua kiliskika kishindo kimoja tu cha Rebecca peke yake kwakuwa alitua kwa miguu huku Agent Kai alitulia vidole kama kawaida yake kisha akajiviringisha kwa kasi kama gurudumu.
Mwisho wa sehemu ya tisini na saba(97)
Mambo yanazidi kusogea kwenye hatima ya Tajumulco Camp ikiwa moto ndiyo unazidi kuteketeza kila inachokutana nacho huku Silla na Mller wakifanya kazi ya kuzuia kwa stahili ya nyamaza moja kwa moja kila anayesogeza pua yake kutaka kwenda ilipo ‘yard’ ya magari ya zimamoto.
Agent Kai na mshirika wake wa karibu katika Special Agent Rebecca wamo ndani ya gereza la siri, nini kitatokea?
Je watamuona mtu aliyesababisha leo hii Agent Kai na wenzake kuja nchi hii ya Guatemala?
“…. Tutapanda ukuta bila kujali nyaya unazoziona kwa sababu umeme hamna hivyo hakuna madhara yoyote” Akaongea Agent Kai huku macho yake yakiwa yanaangalia juu kabisa ya ukuta zinapooneskana nyaya zimesukwa sukwa.
“Sawa boss.. Nikiuangalia ukuta huu unanikumbusha Putatan, Sabah huko Malaysia kulikuwa na mvua kubwa inanyesha tukiwa tunaangalia juu tunawezaje kukwea kwenda juu… Hahaha hahaha hatari sana.. Niambie tunakweaje na leo hapa?” Akaongea Rebecca ana kuuliza.
“Gloves zangu zenye sumaku ya ukuta ninazo.. Ila wewe nahisi huonagi umuhimu wa kuwa nazo.. Hahaha hahahah…”
“Kwahiyo mimi mbuzi nisiyejifunza? Mimi siyo binadamu?” Akaeleza Rebecca akiwa anatabasamu mikono yake ikiwa kaitumbukiza kwenye begi anatafuta cha kutafutwa.
“Ooooh! Kumbe umekumbuka kubeba safari hii… Safi sana miss wangu!”
Dakika moja mbele walikuwa wote wako juu wamezikamata nyaya ambazo kikawaida uwa na umeme lakini kwa hapa muda huu hazikuwa na umeme na hata zingekuwa na umeme mbele ya gloves walizovaa ilikuwa ngumu wao kudhulika.
Ndani ya uwa ndipo waliziona selo ndogo ndogo zilizojengwa zikitumbukia kwa ndani na zingine zikiwa kubwa kubwa katika eneo la katikati ya ukuta huu ambao muda huu walikuwa wamejilaza kwa juu yake wakizilalia nyaya kama godoro Dodoma.
“Twen’zetu!” Akaongea Rebecca baada ya kuona kuna usalama wa kutosha kwa ndani wote wakajigeuza na kuning’iniza miguu kisha kwa pamoja wakajiachia mpaka chini kutokea juu bila woga walipotua kiliskika kishindo kimoja tu cha Rebecca peke yake kwakuwa alitua kwa miguu huku Agent Kai alitulia vidole kama kawaida yake kisha akajiviringisha kwa kasi kama gurudumu.
ENDELEA NA MAPIGO NONDO..!
BUTWAA XIV
SAN MARCOS-GUATEMALA
Milio ya bunduki zilizokuwa zikifyatua risasi na milipuko mbalimbali ya mabomu na aina nyingine za milipuko iliyokuwa ikitokana na moto unaowaka maeneo yote ya viunga vya kambi ya Tajumulco ya genge la TRJ iliyopo eneo la safu ya milima ya Tajumulco, milima ambayo iko mkoani San Marcos mpakani mwa Guatemala na Mexico, milio hii mchanganyiko ilisikika vizuri hadi ndani gereza la siri la genge hili linalojihusisha na biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Wafungwa wanaotumikia vifungo visivyo vya kisheria iliyopo katika katiba ya nchi ya Guatemala inayosimamiwa na serikali halali ya kidemokrasia iliyochaguliwa, walistuliwa na milipuko husika iliyokuwa ikisikika hadi katika masikio yao ikitokea huko ilikotokea.
Agent Kai na Special Agent Rebecca licha ya kuona ni kama wamechukua tahadhari kuu wakati wanajiachia kutoka juu ya ukuta kutua ndani ya uwa wa ukuta unaozunguka eneo hili la gereza la siri haikuwa sawa na walichofikiri wako katika hali isiyotia mashaka kwao kwani karibu wafungwa wote waliopo ndani ya vyumba lakini wengi wao wakiwa wako madirishani kutamani litokee jambo lolote litakalokuwa jema kwao kutokana na mashambulizi ya majibizano ya silaha hivyo watu waliotua chini mmoja akitua na kuchuchumaa pale pale alipotua huku mwingine akiweka kitu ambacho waweza sema ufundi au mbwembwe kwa kujiviringisha kana kwamba gurudumu la tairi la gari lisilo na rim huku mkononi akiwa kakamata bunduki.
Mioyo ya wafungwa hawa ambao walishuhudia watu wawili hawa waliotua ilileta kitu ambacho toka wanaingizwa hapa kwa kila mmoja kwa wakati wake au wengine kwa uwingi wa kuanzia watu wawili mpaka watano na kuendelea, kila mmoja wao aliingiwa na hisia kuwa kuna jambo zuri linawatokea muda si mrefu shauku na mibanano ya kusukumana kila mtu akitaka aone ikiwemo kubonyezana kwa furaha ishara mbalimbali.
Agent Kai aligundua kuwa karibu kila selo wafungwa wako macho wakati akiwa amesimama karibu na ukuta wa moja ya selo iliyoko karibu na alipotua, akatizama saa yake ya mkononi yenye kazi ya kuwa saa na pia kuwa chombo cha mawasiliano na kazi zingine ambazo kwa leo chuna kidogo nisizielezee, muda ulikuwa ni muda ambao ilimbidi atingishe kichwa chake tayari ilikuwa ni saa kumi na mbili na dakika kumi asubuhi.
“Msijifiche kama mmekuja kutuondoa hapa tunaomba muendelee na mnachotakiwa kukifanya kwa haraka sababu hakuna kizuizi kwenu bali kipo kizuizi kwetu tu!” Sauti ya mtu mmoja akitumia lugha ya kilatini (kihispaniola) ambaye ni ya kiume lakini ilikuwa imekauka sana ilisikika tokea kwa dirishani hatua mbili tu toka alipo Agent Kai akiwa kauweka mgongo wake kwenye kuta ya selo husika, masikio yake na masikio ya S.A Rebecca yalisikia kwa uzuri ujumbe ulio mahususi kwao.
“…Msihofu tumekuja kwa ajili yenu… Asubuhi hii imekuwa ni asubuhi ya neema kwenu itakayowafungulia maisha mapya na familia zenu baada ya muda mrefu kutoonana nayo” Kai akajibu naye kwa kilatini ujumbe ule kwa maelezo haya kisha akasogea hadi dirishani alipofika akatokeza kichwa kidogo uso wake ukiwa umefunikwa kwa ‘mask’ akakutana na uso wa mtu ambaye kiasili yuko kama yeye ki rangi asili ya afrika, macho ya Agent Kai yaliyo ndani ya miwani yakajaribu kuweka kumbukumbu pengine anamjua, mtu yule alikuwa uso wake unaonyesha kupoteza matumaini ya kikawaida ilikuwa kama hana nyama zinazounda uso wake hadi shingoni alikuwa ni mtu aliyekonda sana na kupauka ikionyesha hata kuoga kwake ni kwa nadra sana, nyuma ya watu wale kulikuwa na wanaume wengine mchanganyiko wazungu kwa weusi wakilazimisha na wao waweze kumuona mtu anayewaangalia tokea kwa nje akiwa kaficha uso wake kwa kinyago ninja cha soksi.
“Wote mlio selo hii mnaongea kilatini tu?” Akauliza Agent Kai na mara S.A Rebecca akafika akiwa anatweta kwa nguvu wakaangaliana na boss wake.
“Vipi?” Akauliza ‘TSC’ naye akitaka kujua tweta ile inamaanisha nini.
“Nimeongea na Silla anasema moto umeshika ka..!” Hakumaliza kuanzia wao hadi walio ndani ya selo walibonyea chini kwa stahili ya kubonyea na kusimama kana kwamba wamepewa maelekezo ya pamoja wafanye hivyo, mshindo mkubwa ulisikika kana kwamba gari kubwa hivi imegonga ukuta na kulipuka papo hapo.
“Msiogope.. Nje ya hapa kuna moto unawaka lakini hatuna jinsi sisi tunachotakiwa kwa sasa ni kuangalia nyie wote humu nasi pia tunatokaje hapa” Akaongea Agent Kai tena akitumia lugha ile ile ya kilatini.
“Silla na Milller mko salama?” Mkono wake wenye saa ukiwa umesogea kando yam domo ambao wenyewe haukuwa ndani ya soksi eneo lake lilikuwa wazi, aliongea Agent Kai kutaka uhakika ya alichosema Rebecca.
“Hatari kubwa mkuu… Ule wa juu unavunja kuta za handaki eneo la lango kuu na ndicho kilichawachanganya watu hawa sasa ni mwendo wa kuokoa maisha yao tu kwa moto huu unaolipua kitu chochote kinachohusiana na mafuta, kila kona moto watu wameanza kuchakazwa na moto sasa.. Sisi tumekuja huku mlipokuja na watu karibu wote wanakimbilia huku inaelekea kuna njia ya dharura hivyo sisi tumejificha tuone wanaelekea wapi maana mbio zote wanamfuata mtu ambaye ametupita akiwa na kifungu cha funguo mkononi mwake…!” Akajibu Silla kwa haraka lakini si kwa kutumia sauti ya juu sana hivyo Agent Kai alimsikia lakini kwa tabu sana.
“Huu mshindo mkubwa wa mwisho wa nini?” Akauliza Kai.
“Moshi mzito unatokea gereji ya magari ambako tuliona magari ya zimamoto kwa ndani..!.. Vipi nyinyi? Rebecca alinijuza tayari mpo ndani mmekuta selo kama kumi zina watu wamepangwa kwa kubanana sana kila selo” Akajibu na kuhoji Silla, mshindo mwingine mkubwa ukasikika kwa karibu kabisa na eneo walilojificha S.A Silla na Inv. Miller kwakuwa mvumo wake uliweza sababisha hata Agent Kai mwenye kifaa kidogo kama punje ya harage kama ilivyo wenzake wote kikiwa ni ‘bluetooth earphones’ kung’ata meno kwa maumivu aliyoyasikia.
Mivumo ya kawaida iliendelea hakuna aliyeongea kitu hali ya kuogofya mioyo ya watu ikaendelea kidogo watu wakiangaliana tu hasa wale walio kwenye selo zote macho yao kwa wanaoweza kuwaona Agent Kai na S.A Rebecca walikuwa wakiwatumbulia macho wakitamani wafunguliwe makufuli yaliyo milangoni yanayowazuia kutoka katika selo hizi zenye mateso ambazo hata kulala ilikuwa kwa tabu sana maana mbanano wake si mchezo hata virago hawakuwa wameekewa.
“Silla! Unanisikia?” Kwa sauti ya kupayuka kwa nguvu akauliza Agent Kai.
“Naam…. Nakusikia.. Tumekoswa koswa.. Subiri namsaidia Miller ameangukiwa na kifusi cha ukuta uliovunjika.. Msihofu ila fanyeni upesi.. Watu wengine waliokuwa wanakimbia mlipuko huu umewarusha mpaka kwenye bwawa la mamba.. Hatari sana!” Akajibu Silla kisha ukimya baina yao ukafuata ikisikika mivumo ya moto tu na kelele za watu wanaolia kuomba misaada (TRJ hapa ilikuwa inapata pigo la mwaka).
“Sawa.. Kuweni makini..!” ‘TSC’ akajikuta anatoka kwenye bumbuwazi la kusikiliza yanayotokea upande wa pili na kuongea hivi kisha akabonyeza kitufe kukata simu.
“Tuvunje makufuli yote kwa haraka.. Silla na Miller wanatakiwa watusaidie jinsi ya kutoka hapa kabla moto haujaendelea zaidi..!” Akaongea Agent Kai kama anazinduka toka usingizini ksiha akahama toka pale dirishani waliposimama hadi ulipo mlango ambao ni mwembamba wa kupita mtu mmoja tu akavunja kufuli kwa kulikita na kitako cha bunduki kwa nguvu mpigo mmoja tu akakwanyua komeo mlango ukavutwa kwa ndani na mtu aliye ndani karibu na mlango ikabidi Kai arudi nyuma bunduki mkononi akiwa kaiinamisha kwa tahadhali kuu maana binadamu hatabiriki hasa binadamu ambaye yuko kwenye michezo ya giza kama hii.
“Tokeni kwa umakini na wote muelekee pale kando ya ukuta, nakuja kueleza utaratibu wa kutoka hapa.. Natambua wote mnajua gereza hili limezungukwa na nini huko nje!” Akaongea Agent Kai akiwaambia wanaotoka ndani kwa kusukumana.
Hakuna aliyeongea chochote, wote walitoka tu wakiwa wameacha kusukumana kila anayeonekana afya yake ilikuwa ya masikitiko sana na harufu kali ya jasho na vinyesi ilisikika ikitokea ndani ya selo husika, Agent Kai akasogea selo ya pili akakuta tayari Special Agent Rebecca ashazungumza nalo kufuli na watu waliomo ndani ya selo wanatoka ambao nao ilibidi wawasomee risala ya maneno machache ya kuwahatadhalisha wapunguze haraka ya kusukumana (walitilisha imani kwa kweli hali yao haikuwa si nzuri kabisa).
“Poleni sana na mateso haya” S.A Rebecca akajikuta anasema licha ya roho yake ya ujasisri na kaukatili fulani kuwaona watu hivi ilimuuma sana.
Kila anayepita pembeni ya Agent Kai alikuwa akitizamwa kwa umakini na yeye hili kuona sura ipi anaijua akiwa na hamu ya kumuona mtu aliyewafanya leo hii muda huu wa asubuhi kuwa hapa.
Selo zote zilifunguliwa katika selo zote kumi zilizojengwa kwa mtindo wa vyumba vidogo vinavyoachana hatua tatu kutoka chumba hadi chumba, waliokuwa wafungwa wa humu walielekezwa sehemu ya kwenda wakati wakielekezwa hivi Rebecca alimuona mtu ambaye alimfananisha na sifa kutokuwa na mkono mzima wa kulia Sajenti Johnson Greg Rautollaye ‘Jogre’ ila alinyamaza akawapisha waelekee kule wanakoenda wengine na hata Agent Kai alimuona mtu mmoja ambaye alimfananisha na mmoja wa maafisa kati ya maafisa waliotekwa kwa pamoja na rafiki yake ‘Jogre’ lakini alinyamaza pia kwakuwa wote wa watu walio hapa walikuwa wana ukurutu mwilini ulioambatana ‘utangatanga’ na ‘mapunye’ ikwemo kukonda sana hivyo ilikuwa ngumu sana kumtambua mtu kiurahisi hata watu hawa waliokuja kutolewa humu kwenye selo zao walikuwa hawajui hawa ni kina nani kwakuwa sura za kina Agent Kai zilikuwa ndani ya ‘mask’ walizovaa.
Watu waliouwa katika idadi ambayo bila kuwahesabu ilikuwa si rahisi kujua wako wangapi ila kwa makadirio ya haraka aliyofanya Kai aliweka kadirio la watu hawa kuwa ni watu hamsini mpaka sitini, walijipanga kwa tabu pembeni ya ukuta wakisubiri maelekezo nini kinafuata kutoka waokozi wao ambao kiukweli kati yao hakuna aliyekuwa anaamini kama watu hawa wamekuja kuwatoa humu salama si kuwamaliza kwa melekezo kutoka kwa watu wengine wa genge la ‘TRJ’.
“Tunatakiwa kwa haraka sana tutoke humu ndani… Tunashukuru hali ya taharuki ya moto unaowaka maeneo haya ya ndani chini hapa na huko juu nje kwenye majengo pia yanayomilikiwa na watekaji wenu waliokuwa wakiwaweka vizuizini imesababisha kusiwe na upinzani wa kutuzuia sisi kuendelea na mpango wa kuwaondoa nyinyi pamoja na sisi hapa hivyo changamoto kubwa kwetu jinsi ya kutoka kupitia kwenye maji kwa chombo tulichokuja nacho ambacho ni kidogo sana na hakuna njia salama zaidi ya chombo icho kwakuwa bwawa lililozunguka gereza hili ni bwawa la mamba” Alianza kutoa maelezo Agent Kai akiwa kasimama mbele ya watu wale sambamba na Special Agent Rebecca wanaangaliana na wahanga hawa wa mateso ya genge la ‘THE RED JAGUAR’.
“..Kuna wamarekani hapa?” Akauliza kisha akatulia kuwatizama “Kama wapo wasogee mbele kidogo”
Watu tisa walisogea mbele hapo ndipo Agent Kai moyo wake ulilipuka kwa furaha kuu lakini akajizuia kuonyesha furaha ile pale alipo, toka kwa nyuma ya watu wale waliojipanga alitokea mtu ambaye licha kuwa dhaifu wa mwili na uchafu wa ngozi yake alikuwa ni mtu ambaye amesababisha wao kuwa hapa leo ni Agent Jonson Greg Rautollaye ‘Jogre’ akija mbele, akisogea mbele kama ananyata.
“Nyote muwe na amani… Wote sisi hapa tutahakikisha mnatoka salama hapa.. Tufuateni” Akaongea tena Agent Kai baada ya kuona sura za wasiswasi za watu hawa ambao si wamarekani.
Waliongoza linapoonekana ni lango kuu la kuingilia ndani ya kuta unaozunguka uwa ulio na selo hizi walipolifikia lango walikuta limefungwa kwa nje na si kwa ndani hapa napo ilikuwa shughuli mpya yenye changamoto kwao ikabidi Agent Kai apande ukuta akitumia gloves zake ‘magnetic blocks gloves’ ambazo zilimfikisha hadi juu kwa urahisi kitendo ambacho kwa majasusi wawili wa Marekani waliokuwa miongoni mwa kundi lile la wamarekani walitambua jamaa yuko vizuri sana.
Upande wa pili alikuta giza lakini si giza kama lile lililo ndani ya uwa gereza na pia upande wa pili ng’ambo ya bwawa kulikuwa kila mahala moto unaosababishwa na mafuta ya mashine za kiwanda cha kuchakata na kusaga unga wa haramu pamoja na matanki ya mafuta mbalimbali kusambaa katika sakafu ambazo zimesakafiwa kwa simenti, aliangalia pande zote kisha akajirusha toka juu mpaka chini kunako baraza iliyozungushwa kwa mbele kote kuzunguka gereza hili.
Hakuchelewa akalivunja kufuli kubwa lililofungwa katika komeo kubwa la langoni kisha akalifungua lango kwa kulisukumia ndani likafunguka pande mbili walio ndani wote wakatoka.
“Umeme hamna jamani kama mnavyoona moto unavyowaka upande wa pili… Ilitubidi tuwashe moto hili tuweze fanikisha hili mnaloliona kwenu” Akaongea Agent Kai kisha akamsogelea Sajenti Johnson ‘Jogre’ wakaangaliana ikiwa ni shahuku kubwa kwa ‘Jogre’ kujua huyu mtu ni nani?.
“…Pole sana Sajenti.. Wenzako kina Agent Telizo Munde wako wapi?” Akaongea Agent Kai alipoona jamaa ana shahuku ya kuuona uso wake ikiwa tayari ameanza kuhisi yeye ni nani.
“Telizo aliondoshwa hapa mwaka juzi hatujui yuko wapi niko na Rummenige huyu hapo karibu na ngazi” Akajibu ‘Jogre’.
Kai akageuka kumuangalia alikoonyeshewa ni Agent Rummenige Brandts akiwa amejawa na mandevu kibao mpaka uso hauonekani vizuri tofauti na ‘Jogre’ ambaye ndevu zake hazikuwa ndefu kupitiliza kama wanaume wengine wote waliokuwa katika kifungo hiki kisicho rasmi kisheria na serikali husika ya nchi hii wala nchi ingine yoyote.
“Twendeni .. Boti ipo moja tu ya kutoka hapa kwenda upande wa pili tutaitumia kutoka kwa mafungu wote huko upande kuna maafisa wenzenu wa DEA wanawasubiri kwa hamu kubwa sana mtawajua huko huko” Akaongea Agent Kai na kufanya ‘Jogre’ na Agent Brandts kuangaliana.
“Wewe ni nani?” Akauliza Agent Rummenige Brandts akimuangalia Agent Kai ambaye hakujibu akageuka kuwaongoza akiwaonyesha ishara wamfuate wote kufuata baraza inavyoenda.
Mwisho wa sehemu ya tisini na nane (98)
Hatimaye Agent Kai kamuona rafiki yake Sajenti Agent Johson Rautollaye a.k.a Jogre lakini hakufunua mask aliyovaa hili wakiwa sehemu ambayo yeye ataona ni sahihi kujitambulisha atafanya hivyo hili iwe furaha sehemu sehemu salama.
Nini kitafuata sehemu inayofuata? Watatoka salama wafungwa na majasusi waliowafuata kuwapa msaada wa kutoka kifungoni?
Moto wataukwepaje?
Hakuchelewa akalivunja kufuli kubwa lililofungwa katika komeo kubwa la langoni kisha akalifungua lango kwa kulisukumia ndani likafunguka pande mbili walio ndani wote wakatoka.
“Umeme hamna jamani kama mnavyoona moto unavyowaka upande wa pili… Ilitubidi tuwashe moto hili tuweze fanikisha hili mnaloliona kwenu” Akaongea Agent Kai kisha akamsogelea Sajenti Johnson ‘Jogre’ wakaangaliana ikiwa ni shahuku kubwa kwa ‘Jogre’ kujua huyu mtu ni nani?.
“…Pole sana Sajenti.. Wenzako kina Agent Telizo Munde wako wapi?” Akaongea Agent Kai alipoona jamaa ana shahuku ya kuuona uso wake ikiwa tayari ameanza kuhisi yeye ni nani.
“Telizo aliondoshwa hapa mwaka juzi hatujui yuko wapi niko na Rummenige huyu hapo karibu na ngazi” Akajibu ‘Jogre’.
Kai akageuka kumuangalia alikoonyeshewa ni Agent Rummenige Brandts akiwa amejawa na mandevu kibao mpaka uso hauonekani vizuri tofauti na ‘Jogre’ ambaye ndevu zake hazikuwa ndefu kupitiliza kama wanaume wengine wote waliokuwa katika kifungo hiki kisicho rasmi kisheria na serikali husika ya nchi hii wala nchi ingine yoyote.
“Twendeni .. Boti ipo moja tu ya kutoka hapa kwenda upande wa pili tutaitumia kutoka kwa mafungu wote huko upande kuna maafisa wenzenu wa DEA wanawasubiri kwa hamu kubwa sana mtawajua huko huko” Akaongea Agent Kai na kufanya ‘Jogre’ na Agent Brandts kuangaliana.
“Wewe ni nani?” Akauliza Agent Rummenige Brandts akimuangalia Agent Kai ambaye hakujibu akageuka kuwaongoza akiwaonyesha ishara wamfuate wote kufuata baraza inavyoenda.
ENDELEA NA MAPIGO NONDO..!!
BUTWAA XV
SAN MARCOS-GUATEMALA
“Tuko na boti hii tu ambayo ni boti ya dharura ya wahuni wasio na chembe ya utu waliokuwa wakiwashikilia mateka kwa kuwaweka katika gereza hili la siri humu chini” Agent Kai aliongea huku anavuta kamba iliyoshika boti iweze kusogea upande wao.
“Halloo!” Upande wa pili uliitika baada ya ishara ya kuita simu yake ya mfumo wao kikundi kuita katika simu saa yake, alikuwa ni Silla akitweta na kujifuta jasho lililokuwa likimtiririka mwilini kwa joto lililopo eneo ambalo alikuwa akimvutia swahiba wake Miller aliyekuwa majeruhi sasa wa kuanzia kiunoni mpaka miguuni.
“Vipi hali hapo?” Akahoji ‘TSC’.
“Si nzuri sana… Miller ameumia sana twahitajika tutokea eneo hili kwa ajili ya matibabu yake.. Vipi na nyie huko?”
“Oooooh! Hatari sana.. Sisi huku tumewapata watu wetu wawili tumewakuta wapo lakini mmoja hayupo ila tusijadili hili kwa sasa tutalijadili baadaye.. Adui zetu sioni wakikimbia kimbia upande wapili… Hii inamaanisha nini?”
“Kama nilivyokuelekeza hapo awali walikuwa wakikimbia kuelekea eneo ambalo wataweza kutoka hapa”
“Ulikuwa bize na kumuokoa Miller! Je umefanikiwa kuona njia hiyo?”
“Sijafanikiwa kufika mahala husika ila njia inaonekana nafikiri tutatakiwa kuifuata njia hiyo itatufikisha mahala penyewe lakini moto umekuwa tishio kubwa sana sasa hata hapa tulipojificha hatujajificha kukwepa maadui binadamu tumejificha kujikinga na adui moto”
“Moto huo ni rafiki kwetu hivyo hauwezi kutudhuru Silla… Kumbuka sisi ndiyo wazazi tuliozaa huo moto hivyo usiujali sana kwakuwa unajua unafanyaje muhimu njia ya kutoka tu”
“Mmmh! Sawa baba moto.. Naona faraja imekuwa nyumbani kwako sasa.. Lete maelekezo maana nahisi joto kubwa sana hapa na kama unavyosikia vishindo vya kulipuka kwa vitu, Kai si mgeni wa mambo haya”
“Niko na watu wapatao sitini wote tunahitajika tuwatoe salama humu ndani.. Hatuwezi ruhusu kijinga jinga moto ukawala nyama za miili yao kama tulivyogoma kuruhusu mateso yao kuendelea ndani ya gereza hili… Msaada wako linda eneo la ngazi naanza kuwaleta watu hawa kwa boti hii yenye uwezo wa kubeba watu wasiozidi saba”
“Sawa nitafanya hivyo..!” Alimalizia Silla na kukata simu kuna kitu alikuwa akiwambiwa na Miller hivyo aliona amsikilize.
Boti ilianza kazi kwa kuwatoa kwa zamu wahanga wa ufungwa katika gereza hili kutoka upande wa gereza hadi upande wa pili, kazi iliyochukua dakika ishirini na nane kwakuwa boti ilikuwa na kasi ya kutosha kutumia dakika mbili watu kupanda ndani ya boti kisha mbili za kwenda na dakika mbili za kushuka na mbili za kurudi kila mmoja aliwajibika ipasavyo kuhakikisha hacheleweshi chochote katika vilivyo na umuhimu kwa wakati huu, watu wote sitini wakienda kwa mafungu ya watu kumi wakila mbanano haswa hivyo raundi za Agent Kai nenda rudi zilikuwa ni raundi sita ambazo shukrani kwao hakuna mamba aliyeweza kufanya fitina kuweza kuwageuza moja ya miendelezo ya vyakula watu walivyoweza kula kwa muda mwingi tokea alfajiri ya mapema ya siku hii ndefu sana kwa wanadamu wote waliokuwa Tajumulco tokea jana yake.
“..Shukrani kwa boti imetusaidia na adui zetu pia shukrani kwao kutuacha wenyewe wakikimbia moto mzuri uliowakimbiza.. Twendeni sasa tutoke humu moshi unazidi kuwa mzito.. Msiogope kupita kinachotakiwa na tahadhali kubwa kwa kila mmoja wetu.. Silla utaongoza msafara katika njia ambazo moto hata kama utakuwepo utakuwa si kutufanya tukawa kuni huku nyuma naomba Sajenti Jogre na Agent Rummenige mtusaidie kumbeba yule ndugu yetu aliyelala pale akiwa na maumivu ni afisa mwenzenu wa DEA na kwakuwa yeye hana mask mkifika mtamtambua yeye ni afisa gani huko DEA..” Aliongea Agent Kai akiwa anawaangalia Agent Rummenige Brandts na Agent Johnson Greg Rautollaye.
“Mheshimiwa ahsante sana kwa msaada wako nasi ni wanajeshi kama wewe hivyo acha tufanye utakavyo bila kujali afya zetu..!” Akajibu ‘Jogre’ huku akimtizama vizuri Agent Kai umbo lake katika mwangaza mdogo uliopo pale kutokana na giza lilisilokwisha katika eneo hili la chini ambalo hili kuwa na mwanga mzuri bila kujali muda iwe mchana au usiku ilihitajika umeme.
“… Naona una shahuku ya kunijua zaidi mimi kuliko chochote ‘Jogre’ usijali tukitoka tu utanijua mimi ni nani?” Kai akamkwepa ‘Jogre’ na kuanza kuongoza kufuata njia nyuma ya Silla aliyekuwa akienda katika hali ya kukwepa hatari ya moto uliokuwa umetamalaki mpaka ardhini kuna mbao na vitu vingine vingine vinawaka.
“Oooh my God.. Miller.. Ni wewe Miller.. Johnson ni Miller huyu… Ahsante Mungu mmekuja kutuokoa jamani, pole sana na matatizo yaliyokukuta umeumia ndugu!” Agent Rummenige kumuona Miller usoni tu alijikuta akipaza sauti kwa furaha bila kujali moshi na vitisho vya moto na hata Miller kuwaona watu hawa ilimfanya atabasamu tabasamu pana licha ya maumivu aliyonayo hakuyajali akatamani ainuke awakumbatie ndugu zake, washirika wenzake katika shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Marekani ‘Drug Enforcement Administration” (DEA).
“…Khaaah!... Ni mimi.. Nim.. Nim..eumia lakini.. Lakini nina furaha kubwa saana.. Nina furaha tumewapata” Alijibu Inv. Miller akitamani ainuke kuweza kufanya kumbatio la furaha kwa wenzake hawa wawili waliokuwa wanamzunguka pale alipo juu kukiwa na moshi mzito unaotokana na moto.
“Usiinuke kaka.. Inatupasa sisi ndiyo tukuinue hapo ulipo.. Ni zamu yetu sasa yako imeisha, wajibu wako umeisha” Akaonywa na ‘Jogre’ ambaye ana mkono mmoja unaofanya kazi kwa ufasaha zaidi.
Miller aliwaangalia katika hali ya moshi uliokuwepo na kuwaona vizuri watu hawa kwakuwa yeye alikuwa na miwani kavaa, miwani ambayo inavaliwa na watu wanne waliofika na kuingia ndani hapa ulipo moyo wa genge la ‘TRJ’, aliwaona jinsi afya zao zilivyo aliona huruma sana hata kama yeye yupo katika hali mbaya haikumzuia kuona imani kubwa ya kutamani yeye ndiyo angekuwa msaada kwa watu hawa.
Agent Rummenige Brandts aliinama akapitisha mkono wake kwenye mkono wa Miller kisha akamuinua hapo ‘Jogre’ akatumia mkono wake ulio mzima kukamata mkono uliobaki wakamuinua juu na kumsaidia kwa kupachika mikono yake kwenye mabega yao msafara ukaanza kuelekea wengine wanakoelekea kukiwa kuna moshi mzito mweusi.
Silla aliwaongoza hadi walipotokea katika ngema ya mwamba ulio na mawe pamoja na udongo mzito hapo ndipo wote wakatambua ni mwisho wa eneo hili la chini, majasusi hawa wakatupa macho chini wakaona alama za viatu pamoja na majivu yanayokuja kutokea walipotokea wao kuelekea mahala ambapo pana nyasi ndefu za kuanguka toka juu pamoja na miti miti kadhaa, Kai akamuangalia Silla macho yao yakakutana.
“Njia ni ile pale.. Ndiyoo!” Aliyeongea hivi alikuwa anaongoza kuelekea anaposema ndiyo njia ilipo, alikuwa ni mmoja wa waliokuwa wafungwa, Kai alitamani amzuie lakini alijikuta naye ana shahuku ya kwenda kujua mahala pale kama ni kweli waisivyo kwakuwa palikuwa na mdomo wa kama pango lakini ni mdomo uliozungukwa na vichaka vya manyasi na mengineyo.
Mtu yule aliongeza spidi kukimbilia kule nyuma yake Agent Kai akaunga akimfuata kwa hatua ndefu zenye umakini na Silla akafuata ndipo na wengine kadhaa wakawa wanawafuata kwa nyuma, alipofika eneo lile yule wa mbele alisita kidogo kisha akasogeza majani kwa kwa mikono yake aweze kuona ndani ya alichoona kuwa ni uwazi na ni kweli kulikuwa na uwazi mkubwa wa umbo la mviringo kama bomba unaoingia ndani ambako kulikuwa na giza nene, moyo wa ‘TSC’ ulisimamisha kwa sekunde kudunda kisha ishara ya kawaida yake pale anapoliendea tatizo ilivuma kwenye ngoma za masikio yake akasikia harufu ya damu, tumbo likambana lakini alishakuwa hatua mbili tu kumfikia mtu yule ambaye alishapita kwenye upenyo wa kichaka aweze kuzama ndani ya mdomo ule wa mviringo mkubwa wa mtu kuweza kupita ameinama usawa wa kiuno.
Mshindo wa mlipuko wa bomu la kukanyagwa ulisikika baada ya mtu yule wa mbele kwenda hatua moja tu mbele zaidi, mwili wake ulirushwa nje kwa nguvu na kasi kubwa akamvamia kwa vichwa vyao kugongana kwa nguvu ukitoka mlio wa kama kupasuka kwa nazi kubwa kavu iliyokomaa sana Agent Kai ambaye naye vipande vya bomu vilimrukia na kuchana mavazi yake na vingine kuzama na kuchana sehemu kadhaa za mwili wake, wakajikuta wote wanatupwa chini ikiwa mtu aliye juu tayari kashakuwa maiti. Giza likatanda machoni mwa Agent Kai miwani ikiwa imepasuka, taratibu akawa anajitahidi abaki katika hali yake lakini ‘jitihada haizidi kudra’ fahamu zilimtoka akajikuta ubongo umeacha kufikiri kikawaida ikiwa wakati anatokwa na fahamu katambua hilo ila hakuwa anajua kama anakufa au anazimia.
“Laleni chiniii!” Alipiga kelele Special Agent Silla na amri iliyoitikiwa kwa kasi na wote wakijitupa chini kwa kasi, mlipuko mwingine ukasikika tokea kwa ndani ila huu haukuwa umelipuka kwa sababu ya kukanyagwa na mtu bali ulikuwa umetegwa endapo lile la kwanza litalipuka basi hili la pili litafuata baada ya sekunde kumi na tano na ndicho kilichofanyika ila Mungu si Trump hakuna aliyejeruhika kwa hili bomu la pili.
Silla alitambaa mpaka alipo Agent Kai akamshika shingoni kuona yu hali gani nahodha wao wa ukweli hapo akatambua kuwa nahodha amezirai.
“…Shiit..!” Alijikuta akisema kwa sauti iliyosikika vizuri kwa wengine ikasababisha Special Agent Rebecca aliyekuwa mwisho kabisa wa msafara kuinuka kwa kasi toka alipokuwa kalalia tumbo lake baada ya amri ya Silla kuwa wote walale chini, mbio zilimfikisha pale alipo Silla machozi kama bomba la maji yalianza kumtoka breki ya mbio zake za mithili ya mwanariadha wa mbio za kuruka viunzi zilisimamama kwa kuserereka kwa kasi kwa magoti salama yake ikiwa suruali aliyovaa ambayo ina haina fulani ya ngozi ngumu maeneo ya goti lasivyo mawe mawe yaliyopo kwenye ardhi hii yangeondoka na nyama za magoti.
Haraka mkono wake wa kulia ulivuliwa gloves ulilovaa kwa mkono wa kushoto kulivuta kisha mkono ule uliovuliwa gloves ukapita kwenye kola kubwa ya koti alilovaa Agent Kai na kufikia shingoni kidogo hapa amani ilikuja walau kwa udogo wa tembe ya dawa ya asprini kuwa boss wake yu hai.
Wakaangaliana na Silla kisha wote kwa pamoja wakageuka kuwaangalia watu wengine walio nyuma yao ambao karibu wote ikiwemo wasiomjua mtu yule ni nani walitamani kusikia kutoka kwa watu hawa waliomzunguka kuwa aliyelala chini kifudifudi ana hali gani?.
“…Vipi jamani?... Kuna usalama?” Alihoji kwa sauti majeruhi Investigator Miller akitamani atembee yeye mwenyewe au atembezwe kwa kasi na watu walioshika mpaka pale alipo Agent Kai akiwa pembeni yake kushoto na kulia wapo Special Agent Silla na Special Agent Rebecca.
“Amezimia.. Mgongano wa kustukiza wa kichwa na marehemu umempasua juu ya jicho la kulia baada ya kuvunja miwani aliyovaa pamoja vipande vipande vya bomu lililolipuka vimemletea hali ya kuzimia..!” Akajibu Silla kwa sauti iweze kufika kwa watu wote ikiwemo aliyeuliza swali.
Watu wote wakasogea kumzunguka Agent Kai aambaye sasa alikuwa anapewa huduma ya kwanza na mshirika wake swahiba wake Rebecca aliyekuwa akimpaka dawa za kuzuia damu kutoka katika juu ya jicho na sehmu zingine zingine.
“Naomba mtulie hapa.. Mimi Naingia kuchunguza hii njia” Akaongea S.A Silla akiwaambia watu wote wanaomtizama na wasiomtizama, hakuna aliyemjibu wote walinyamaza huku wengine wakihofu naye anakwenda kulipukiwa na bomu huko.
Agent Jonhson Greg Rautollaye kwa pamoja na Agent Rummenige Brandts walimlaza mahali pazuri Investigator Miller kisha wakaenda anapotolewa huduma ya kwanza Agent Kai.
“… Eeeeeh… Nilihisis na kumbe ni kweli… Kai.. Kai.. Kai.. Kai rafiki yangu Agent Kai.. Kumbe ni wewe? Mungu mkubwa… Mungu mkubwa.. Ni kama naota miee.. Nimasheni usingizini naota… Kai umefiks kuniokoa, usife kaka, usife kaka.. Miss! Miss.. Msaidie ndugu yangu, tafadhali msaidie kama huwezi nipishe nimsaidie” Sauti ya Agent Johnson ndiyo sauti pekee iliyokuwa ikisika ikitoka kwa masikitiko ya kuumizwa na kile anachokiona na hata machozi yaliyokuwa yamejiandaa kuwa ya furaha yalikuwa ya huzuni, aliinama akapiga magoti akaanza kubusu viatu vya Agent Kai akipanda mpaka maeneo ya magoti.
“Kaka! Tafadhali.. Tafadhali tulia nampa huduma mimi.. Nafahamu una furaha kubwa sana kumuona kaka Kai lakini amezimia huduma yetu ya kwanza ndiyo itasababisha azinduke haraka zaidi, amegongana sehemu mbaya sana..!” S.A Rebecca akaongea akizuia asiendelee kutingishwa na kazi yake ya kupaka dawa ya kuzuia damu sehemu mbali mbali za mwili wa Agent Kai.
“Sawa..Sawa.. Nafahamu unaweza.. Endelea..!” Akasema ‘Jogre’ akiendeleza kubusu suruali aliyovaa Agent Kai aliye mbali kwa sasa, ulimwengu ambao sisi si rahisi kuuelezea kiuhakika zaidi ya hadithi za alinacha na kusadikika tu.
“.. Rebecca! Rebecca, unanisikia? Unanisikia Rebecca?” Ilikuwa ni mfumo wao mdogo wa mawasiliano (SCNG) simu saa baada ya kupokelewa na Rebecca sauti ikasikika kupitia ‘bluetooth earphone’ iliyo ndani ya tundu la sikio.
“Nakupata Silla.. Endelea.!” Akaitika Rebecca huku akimalizia kumfunga bandeji ya kuzunguka kichwa eneo la jicho majeruhi Agent Kai.
“Njia iko salama.. Sijajua mbele zaidi ila hapa nimekuja hadi karibu na ngazi zinazopanda kwenda juu kutokea chini nafikiri ngazi hizi zitakuwa zinapeleka huduma ya watu kutoka humu kwenda nje… Hivyo mnaweza kuja hakuna shida kama ushamaliza kazi ya huduma ya kwanza kwa Kai..” Taarifa ikatoka Silla kuja kwa Rebecca taarifa ambayo Investogator Miller naye aliweza kuisikia kwakuwa naye alikuwa na kifaa cha mawasiliano yao ya ki group (kikundi).
“Nimemaliza acha niwaelekeze tuje huko..!” Akajibu Rebecca kisha akabonyeza kitufe cha kukata katika simu saa yake.
Wakatizamana na ‘Jogre’ wote wakiwa na alama za machozi katika mboni za macho yao kila mmoja akimlilia Agent Kai.
Mwisho wa sehemu ya tisini na tisa (99)
Hali ya kuhitaji kutoka salama ndani ya ngome ya genge la TRJ imekuwa si salama sana baada ya kuongezeka kwa misuko suko ambayo inasababisha kumpoteza aliyekuwa mfungwa huku ikiacha athari ingine kwa nahodha wa kikosi kazi kuzimia kwa bomu la kutegwa lililokanyagwa na mmoja wa wafungwa aliyekuwa kimbelembele ambapo laiti kama asingejitia kimbelembele basi isingetokea kilichomtokea.
Tunakaribia kumaliza stori yetu, tusizogoe sana!
“Kaka! Tafadhali.. Tafadhali tulia nampa huduma mimi.. Nafahamu una furaha kubwa sana kumuona kaka Kai lakini amezimia huduma yetu ya kwanza ndiyo itasababisha azinduke haraka zaidi, amegongana sehemu mbaya sana..!” S.A Rebecca akaongea akizuia asiendelee kutingishwa na kazi yake ya kupaka dawa ya kuzuia damu sehemu mbali mbali za mwili wa Agent Kai.
“Sawa..Sawa.. Nafahamu unaweza.. Endelea..!” Akasema ‘Jogre’ akiendeleza kubusu suruali aliyovaa Agent Kai aliye mbali kwa sasa, ulimwengu ambao sisi si rahisi kuuelezea kiuhakika zaidi ya hadithi za alinacha na kusadikika tu.
“.. Rebecca! Rebecca, unanisikia? Unanisikia Rebecca?” Ilikuwa ni mfumo wao mdogo wa mawasiliano (SCNG) simu saa baada ya kupokelewa na Rebecca sauti ikasikika kupitia ‘bluetooth earphone’ iliyo ndani ya tundu la sikio.
“Nakupata Silla.. Endelea.!” Akaitika Rebecca huku akimalizia kumfunga bandeji ya kuzunguka kichwa eneo la jicho majeruhi Agent Kai.
“Njia iko salama.. Sijajua mbele zaidi ila hapa nimekuja hadi karibu na ngazi zinazopanda kwenda juu kutokea chini nafikiri ngazi hizi zitakuwa zinapeleka huduma ya watu kutoka humu kwenda nje… Hivyo mnaweza kuja hakuna shida kama ushamaliza kazi ya huduma ya kwanza kwa Kai..” Taarifa ikatoka Silla kuja kwa Rebecca taarifa ambayo Investogator Miller naye aliweza kuisikia kwakuwa naye alikuwa na kifaa cha mawasiliano yao ya ki group (kikundi).
“Nimemaliza acha niwaelekeze tuje huko..!” Akajibu Rebecca kisha akabonyeza kitufe cha kukata katika simu saa yake.
Wakatizamana na ‘Jogre’ wote wakiwa na alama za machozi katika mboni za macho yao kila mmoja akimlilia Agent Kai.
ENDELEA NA MAPIGO NONDO..!!
BUTWAA XVI
SECRETO POTENTIA LA FECA PALACIO
TETAPLAN, GUERRERO-MEXICO
Saa mbili na dakika kumi asubuhi ya siku ya jumatatu ndani ya makao makuu ya genge linalojihusiha na ulanguzi wa madawa ya kulevya la ‘THE RED JAGUAR’ kulikuwa na watu katika moja ya varanda kati ya varanda kadhaa za kisasa zilizopo ndani ya kasri hili linalofahamika kama ‘nguvu ya siri ya kasri la Feca’ kwa lugha yao wenyewe wa Mexico hawa wanaotumia kilatini cha wahispaniola wakipendezewa kuliita ‘Secreto Potentia La Feca Palacio’.
Watu hawa karibia wote walikuwa wametoboa kama vijana wa kihuni wanavyopenda kulitumia neno hili la kutoboa wakimaanisha ‘kukesha’, walitoboa katika varanda hii na sehemu zingine zilizoko katika korido mbalimbali zilizo flour (losheni) hii inayomiliki varanda hii waliyoko watu hawa na hakuna aliyekuwa amependa kuwa hapa muda huu wa asubuhi wala kupenda kukesha wakifuatilia yanayotokea nchi jirani, nchi ya Guatemala au kama wenyeji wa huko wanavyopenda kulikatizia jina refu la nchi yao kwa maneno matatu ya ufupisho ‘GTL’.
Kwa wengine mateso haya ya kukesha hapa yalikuwa si mepesi kuvumilika yalikuwa ni mateso makubwa sana kwao ni kama wameambiwa wasimame ndani ya tanuri la moto la makaa ya mawe lakini wengine kwao hata kama wako kama hawa wengine lakini wangewezaje kulala ilihali mioyo yao haitaki kufanya hivyo, mioyo ina wasiwasi mkubwa sana juu ya hatima yao kama kundi na hata hatima zao binafsi za maisha yao pia walikuwepo walio kama hawa wa kundi la pili lakini wao kukesha kwao ni kawaida kwakuwa mapito hayo waliyapitia mara kadhaa huko nyuma iwe kwenye mafunzo yao au katika minyato yao ya mishe (shughuli) zao.
“… Tumekwisha jamani.. Tumekwisha kabisa… Yaani siamini kama kwa miaka kumi na zaidi tuliyopigana kusimamisha genge letu heti leo hii imefikia tumeharibiwa na wapuuzi fulani kwa uzembe wao wa kushindwa kufanya yaliyo sahihi” Aliongea mtu aliyeingia varandani akiwa kavaa fulana ya kubana mwili wake (bodytight) pamoja na suruali aina ya jeans rangi ya bluu iliyoiva nyuma yake akifuatwa na watu watatu wanaonekana ni walinzi wake binafsi kwa jinsi mavazi yao waliyoyavaa ilikuwa inajulisha moja kwa moja watu hawa kuwa ni walinzi binafsi wa mtu huyu (bodyguard).
Alikwenda akipiga hatua za kasi na ndefu, maneno yake hayakujibiwa na mtu yoyote, wote walikuwa kimya wakimuangalia na kupatwa na hamu ya kujua kulikoni na nini kitafuata.
“Taarifa iliyonifikia hivi punde Mr. Ceni ni taarifa ambayo tulikuwa tukihihisi tu lakni ni thibitishwa sasa kuwa helkopta yetu iliyoondoka hapa na kina Ivan Alto imelipuliwa kwa RPG na askari wa jeshi la Marekani, operesheni iliyoteketeza kambi yetu ya Tajumulco na watu wetu nusu na robo iliendeshwa kwa ndani na hao kina Agent Kai lakini nje ya kambi yetu kulikuwa na ulinzi unaofanywa na kikosi cha jeshi la Marekani wakitokea ubalozi wa Guatemala na ubalozi wa Mexico.. Hawa walikuwa wakiweka usalama wa watu wao kufanya kazi yao.. Taarifa inaeleza uharibifu uliofanyika ni mkubwa sana eneo lote la kambi yetu.. Mheshimiwa Rais wa Guatemala amefika muda si mrefu ndipo alipotoa taarifa ya kutafutwa na kukamatwa haraka sana kwa mdogo wangu Alexis akihusihwa na kila kitu kilichokutwa pale” Mtu huyu akaendelea kuongea akiwa na hasira ambayo hakutaka ionekane machoni mwa watu hawa hivyo uso wake aliufanya uzifiche hisia zake za hasira alizonazo, mtu huyu ni ‘kingpin’ wa genge la ‘TRJ’ ambalo usiku uliopita kuja asubuhi ya siku hii wamepoteza kwa kuangamizwa nusu ya nguzo yao.
“…Simu zote za watu ambao ninaweza pokea taarifa za kinachoendelea huko zinafuatiliwa kwa ukaribu yaani kifupi kwa sasa mawasiliano yoyote tokea Mexico kuingia Guatemala yanafuatiliwa na data zimezimwa kwa baadhi ya maeneo ya jijini na mkoa wa San Marcos… Umefika wakati wa kutafuta kinga mliyosema kwa kumlipua mheshimiwa Rais” Mheshimiwa Ceni akaongea akiwa hata kutuliza miguu hawezi jinsi alivyo na muwasho washo wa wasiwasi akawa anatingisha tingisha miguu yake kitu ambacho wengi walio pembeni walikuwa wanakereka kwakuwa walipenda kuwe na utulivu.
“Petr Batromelo.. Petr hajakamatwa ndiyo mtu pekee ambaye katika watu wetu ambaye hajakamatwa na wamarekani, yaani hadi Maxiwell Zuantejo amekamatwa wakati wanatoka mdomo wa chini kambi yetu yote upande wa juu ilikuwa imeshateketea na moto ikiwemo na ndani eneo la chini” Kingpin Feca aliongea kisha akageuza kichwa chake kuangalia mezani simu yake aliyoiweka hapo ilikuwa inaita, haraka akainuka toka kwenye kiti ambacho hakikuwa kimekaliwa hata sekunde thelathini na yeye maana alipokaa tu na kuongea simu ikaita, akainyakua na kusoma jina la mpigaji ilikuwa ni private number.
Hakupokea kwanza aliinua simu akaishika huku anafikiria kama hatakosea kupokea endapo atahitaji apokee na kumsikiliza mpigaji aliyeamua kupiga simu kwa kutumia ‘private number’, lakini pia aliona itakuwa si sawa yeye kupokea simu hii hivyo akasugua kioo kupokea akiiweka sikioni bila kuongea chochote.
“Halloo.. Halloo!” Mtu huyo wa upande aliopiga akaita bila kujibiwa, Feca alitaka kuisikia sauti kwanza ya ndugu aliyepiga, ubongo wake ulikimbia haraka ukisachi sauti za watu kadhaa wanaojifunza.
“… Petr?!!” Akaongea Feca kuita jina lakini akiuliza swali akiwa hana uhakika.
“Ndiyo boss… Niko kwenye moja ya nyumba ya rafiki yangu hali ya hapa San Marcos ni hali isiyo salama kwetu kabisa niko na vijana wangu wane tu tunashukuru tumefika salama hapa kwa msaada wa usafiri wa huyu rafiki yangu” Akajitambulisha haraka mtu huyu aliyekuwa amepiga simu kwa kutumia ‘private number’.
“..Jeshi la Guatemala limeshika operesheni hii kuanzia San Marcos na Guatemala City yote na jeshi la Marekani limeongezeka kusaidia huku Mexico naona wameshiklia eneo la mipakani, nahisi hali ya hatari juu yetu hapa ndiyo maana nimechukua tahadhali ya kuiondoa familia yangu hapa na muda si mrefu tutaondoka hapa wote tuliopo maana najulikana niko hapa.. Kwa nyie naomba muendelee kujificha hapo kwa rafiki yako mpaka mambo yatakapo poa… Vipi hali ya wavamizi wetu? Umefuatilia kujua hali zao?”
“Wafungwa tuliokuwa tunawashikilia wengi wao kwa mujibu wa askari aliyenipa taarifa anasema wote wako salama ila kiongozi aliyeongoza kikosi cha uvamizi na mwenzake mmoja walitoka eneo lile wakiwa wamebebwa kwenye machela hawajielewi.. Aliyeleta taarifa ni afisa mmoja wa polisi akiwa ameambiwa na Brigedia Donald Grannell”.
“Brigedia Grannell yuko salama? Niliambiwa amekamatwa naye katika kundi la watu wote walio karibu na Mr. Rafael”
“…Hata mimi nilisikia hivyo toka jana jioni lakini si kweli yuko mahala amejificha ndiyo anatumia watu wake wa siri kufuatilia mambo yanayoendelea bila kutumia simu, ndipo nilipomuagiza Fiston atoke kwenda kunusa nusa akakutana na mtu ambaye wanajuana katika maongezi yao wakatuongelea mimi na Brigedia Grannell ikawa mawasiliano yetu yameanzia hapo mpaka sasa ndiyo tunapeana taarifa za kutoka huku nilipo mnazonipa na yeye anazopata huko serikalini katika operesheni hii… Aliniambia nimpe muda wa saa moja kasha atatuma mtu kuleta habari mbalimbali na jinsi tutakavyotoroka kuja Mexico…”
“..Mmh!.. Ningependa kwa siku mbili hizi nyote mbaki huko huko kufuatilia habari za siri na vipi tunaweza kufanya kuwasaidia ndugu zetu kina Zuantejo wasije wakaona tumewatelekeza”
“Sawa boss.. Lakini kwa haraka haraka ni kwamba wamepelekwa katika moja ya kambi ambazo ziko chini ya watu wa usalama walio chini ya mheshimiwa Rais wakilindwa na jeshi pia”
“… Kazi ya kujua zaidi itafanywa na Grannell ninataka akikutafuta haraka upelekwe ujumbe nataka mvute subira angalau siku mbili tatu kama ikishindikana kufanya lolote basi tutafanya mpango tutakaoshirikiana kuwaondoa huko”
“Sawa boss!”
Maongezi ya simu baina ya boss na mtu wake yaliishia hapo ikiwekwa ahadi ya watu hawa wawili pekee walio muhimu waliobaki bila kuwa na tatizo la moja kwa moja katika genge la ‘TRJ’ katika Guatemala kuwa wabaki wakifuatilia kwa ukaribu kwa siri mambo yanayoendelea katika operesheni ya kuangamiza genge lao na kuzipora mali zinazowahusu nchi hii yote.
“Nilikuwa nikiongea na Petr Batromelo.. Nimefurahi kuwa Brigedia Donald Grannell hakukamatwa na serikali yao kama habari za jana jioni zilivyokuwa zinasema kuwa makamishina wa polisi na mkuu wao ‘IGP’ wote akiwemo yeye wamekamatwa kwa amri ya Rais… Grannell hakukamatwa yuko mahala salama na vijana wake wa siri wasiojulikana moja kwa moja kuwa na mahusiano naye wanamfanyia kazi ya kumpatia siri ya kinachoendelea” Feca alianza kuongea alipoweka simu yake mezani akiwaambia wenzake.
“..Mr. Guti wakati naongea umeonyesha una jambo la kusema…Vipi?”
“… Na meseji ya Inspekta Raul Lavores anasema muda si mrefu wanaingia kwenye kikao ambacho kitahusu operesheni iliyofanyika huko Guatemala, matokeo yake na nini wafanye juu ya habari walizopewa juu ya genge letu hivyo anatutahadharisha tusiendelee kuwa hapa Guerrero na tusiondoke kimakundi au kimsafara kama wengi kati yetu tunavyokuwa tunafanya.. Nimemjibu kwa kumdanganya kwamba hata hivyo hatuko pamoja tayari kila mmoja yuko mahala pa usalama kwa anavyoona ni sahihi yeye kuwa hapo..” Mr. Villa Nandez Guti akaongea wakitizamana na Feca.
“..Kaka! nafikiri kwa sasa tuondokeni hapa upesi isije ikaleta majuto kwetu kwa mapuuza yetu… Tupange haraka tunaondokaje hapa bila kujali chochote ni muhimu wote tukawa salama naamini tutakuja endelea na mambo yetu kwa siri kwa kipindi kifupi muhimu ni kuona tunazikinga vipi mali zako zilizo kihalali” Alexis Carlos Codrado mdogo wake na bwana mkubwa mfalme wa wafalme ndani ya genge lao Mr. Feca aliongea akiwa amesimama toka kitini kwakuwa alikuwa na haraka kubwa sana ya kuondoka hapa akawa anaona kama anawekewa kiwingu na ndugu yake pamoja na marafiki zake.
“Ni kweli kama msemavyo… Kukesha salama hapa ni kama bahati kwetu.. Mimi nitaondoka kuelekea Brazil nimeshaweka mambo sawa huko na kama mjuavyo tuna vijana wa kazi na nyumba zetu mbili kule.. Mama wa watoto wangu nimemwambia atangulie kutokea Mexico City alipo aondoke kwa kificho kazi ambayo itafanywa na kina Martins… Nafikiri wengine kati yetu twende huko Brazil ukiwemo Mr. Ceni, Guti na Alexis lakini hatuwezi kuji risk wote kama mjuavyo hivyo mliobaki muelekee Argentina kule vijana wetu ishirini wapo watawapokea nataka sote tukawe baridi kwa muda mfupi tukiwasiliana jinsi gani tunaweza jibu mapigo kwa waliotufanyia haya” Haya yalikuwa ni maelezo ya boss wengine wakiwa kimya kumsikiliza mkali wao.
“Sawa na ni jambo la heri ulivyoamua hivyo.. Maelekezo ya jinsi tunavyoondoka umeshaandaa?” Guti akaunga mkono kisha akauliza swali mkono wake wenye saa ukiwa umeinuka aweze kuona ni saa ngapi.
“… Walinzi wetu wataondoka kwa gari moja moja kuelekea nje ya jimbo hili watatusubiri huko ambapo tutaweka kituo cha muda katika hotel ya mke wa Guti… Tushawasiliana naye aweke mazingira sawa… Hivyo mikakati yote ya safari itapangwa hapo” Maelezo ya mwisho ya boss Feca yaliishia hivi kasha akainuka kwenda zinapoanzia ngazi ambazo alishuka nazo kwa kasi huku nyuma akifuatwa na walinzi wake binafsi.
***** ***** *****
WALTER REED NATIONAL MILITARY MEDICAL CENTER
BETHESDA, MARYLAND-MAREKANI
“..Naomba kitambulisho chako tafadhali..!”
“Nimeambatanisha kila kitu hapo dada yangu”
“.. Oooh! Samahani sana sikukiona kilikuwa chini kabisa.. Pole sana.. Unaweza kukaa hapo kwenye benchi kusubiri niakiki kidogo ni dakika chache tu”
“Haina shida..!”
Maongezi baina ya dada wa kiarabu aliyevaa vazi la hijabu rangi ya bluu iliyomfanya kupendeza sana ikimuonyesha vizuri anavyopendeza kuvaa vazi hili linalopendwa kuvaliwa na wanawake wa dini ya kiislamu katika nchi mbalimbali duniani lakini pia ni vazi linalovaliwa sana nchi za kiarabu bila kujali dini zao kwakuwa ni sheria kwa baadhi ya nchi hizo kwa wanawake kujistiri hivi, dada huyu aliondoka pale dirishani kwenda kukaa kwenye benchi la kusubiri kama taratibu inavyosema akimuacha dada wa mapokezi anayefanyia ukaguzi wa vitambulisho na vibali vya kuingia katika hospitali ya kijeshi iitwayo ‘Walter Reed National Military Medical Center’ inayopatikana eneo la mtaa wa 8901 Rockville LLe Pike unaopatikana katika viunga vya eneo la Bethesda lililopo jiji la Maryland jimbo la Virginia kati majimbo kadhaa makubwa sana yanayounda nchi ya Marekani.
Hospitali hii ya kisasa na kongwe mahususi kwa kufanya matibabu ya kisasa na uhakika kwa wanajeshi wa jeshi la Marekani na taasisi nyingine zinazohusiana na usalama wa nchi ni hospitali kongwe kabisa yenye miongo kadhaa kama si karne kadhaa tokea nchi hii kujipatia uhuru wake ikiboreshwa kila hali ya kiteknolojia inavyobadilika duniani ikiwa iliasisiwa na tabibu aitwaye Walter Reed (Mwenyezi Mungu amrehemu huko alipo apumzike salama).
“Mrs. Kai.. Unaweza sogea sasa!” Sauti ilisikika na kufanya mwanadada wa kiarabu kuinuka upesi toka kwenye benchi kuja pale dirishani.
“..Samahani mdogo wangu.. Ni utaratibu wa kazi uliokutaka upitie hii hali… Pili naomba nikupe pole ni kweli Agent Kai Hamis wa CIA yupo hapa leo ni siku ya pili alifika juzi na ni kweli alitoa taarifa mke wake utaarifiwe hivyo nisikucheleweshe kuna kaka atafika kukupeleka ..Yah! ni huyo hapo pembeni yako kafika kukupeleka chumba cha mapumziko alipo, usihofu yupo salama alipatwa majeraha madogo ya kawaida utaenda jionea mwenyewe huko.. Pole sana Mrs. Shufania Mahamud Kai, karibu sana tena na tena Walter Reed National Military Medical Center..!” Dada wa dirisha la ukaguzi wa vibali na vitambulisho vya watu wanaofika hapa hospitali aliongea akiwa ameachia tabasamu ambalo hakuwa nalo wakati anaongea kabla.
Mwisho wa sehemu ya mia moja (100)
Kaa la moto huko Tetaplan jimbo la Guerrero nchini Mexico makao makuu ya genge la TRJ, wakuu waliobakia ambao ndiyo nguzo ya genge hili haramu na hatarishi kwa maisha ya binadamu likifanya shughuli zake za kilanguzi wa madawa hatarishi kwa afya za binadamu lakini licha ya uhatari wake ni biashara yenye faida ya ajabu sana.
Je mpango wao wa kukimbia Mexico kwa muda na kwenda mafichoni utafanikiwa?
Shemeji yetu naye amefika hospitali ya kijeshi ya ‘Walter Reed National Military Medical Center akiwa na dhumuni la kutaka kumuona kipenzi chake Agent Kai ambaye kwa mujibu wa maelezo madogo tuliyosoma tunaona taarifa kuwa yupo hapa.
Itakuwaje mke na mume wakionana?
Majibu yote ya haya twende hatua inayofuata kwa kujua kinachoendelea katika episode za mwisho mwisho hizi katika mkasa wetu mrefu wa JINO KWA JINO.
ILIPOISHIA SEHEMU YA 100…!!
“..Naomba kitambulisho chako tafadhali..!”
“Nimeambatanisha kila kitu hapo dada yangu”
“.. Oooh! Samahani sana sikukiona kilikuwa chini kabisa.. Pole sana.. Unaweza kukaa hapo kwenye benchi kusubiri niakiki kidogo ni dakika chache tu”
“Haina shida..!”
Maongezi baina ya dada wa kiarabu aliyevaa vazi la hijabu rangi ya bluu iliyomfanya kupendeza sana ikimuonyesha vizuri anavyopendeza kuvaa vazi hili linalopendwa kuvaliwa na wanawake wa dini ya kiislamu katika nchi mbalimbali duniani lakini pia ni vazi linalovaliwa sana nchi za kiarabu bila kujali dini zao kwakuwa ni sheria kwa baadhi ya nchi hizo kwa wanawake kujistiri hivi, dada huyu aliondoka pale dirishani kwenda kukaa kwenye benchi la kusubiri kama taratibu inavyosema akimuacha dada wa mapokezi anayefanyia ukaguzi wa vitambulisho na vibali vya kuingia katika hospitali ya kijeshi iitwayo ‘Walter Reed National Military Medical Center’ inayopatikana eneo la mtaa wa 8901 Rockville LLe Pike unaopatikana katika viunga vya eneo la Bethesda lililopo jiji la Maryland jimbo la Virginia kati majimbo kadhaa makubwa sana yanayounda nchi ya Marekani.
Hospitali hii ya kisasa na kongwe mahususi kwa kufanya matibabu ya kisasa na uhakika kwa wanajeshi wa jeshi la Marekani na taasisi nyingine zinazohusiana na usalama wa nchi ni hospitali kongwe kabisa yenye miongo kadhaa kama si karne kadhaa tokea nchi hii kujipatia uhuru wake ikiboreshwa kila hali ya kiteknolojia inavyobadilika duniani ikiwa iliasisiwa na tabibu aitwaye Walter Reed (Mwenyezi Mungu amrehemu huko alipo apumzike salama).
“Mrs. Kai.. Unaweza sogea sasa!” Sauti ilisikika na kufanya mwanadada wa kiarabu kuinuka upesi toka kwenye benchi kuja pale dirishani.
“..Samahani mdogo wangu.. Ni utaratibu wa kazi uliokutaka upitie hii hali… Pili naomba nikupe pole ni kweli Agent Kai Hamis wa CIA yupo hapa leo ni siku ya pili alifika juzi na ni kweli alitoa taarifa mke wake utaarifiwe hivyo nisikucheleweshe kuna kaka atafika kukupeleka ..Yah! ni huyo hapo pembeni yako kafika kukupeleka chumba cha mapumziko alipo, usihofu yupo salama alipatwa majeraha madogo ya kawaida utaenda jionea mwenyewe huko.. Pole sana Mrs. Shufania Mahamud Kai, karibu sana tena na tena Walter Reed National Military Medical Center..!” Dada wa dirisha la ukaguzi wa vibali na vitambulisho vya watu wanaofika hapa hospitali aliongea akiwa ameachia tabasamu ambalo hakuwa nalo wakati anaongea kabla.
ENDELEA NA NONDO..!!
MIPANGO SAWA I
WALTER REED NATIONAL MILITARY MEDICAL CENTER
BETHESDA, MARYLAND-MAREKANI
Mlango ulifunguliwa lakini watu wawili walioingia katika chumba hiki cha mapumziko walishuhudia mtu ambaye walimkuta amekaa ameulaza mwili kitandani kichwa kakiegemeza kwenye mto huku yuko makini kusoma kitabu ambacho kava ya ndiyo iliyoonekana machoni mwao hivyo uso wake haukuwa unaonekana na hakutaka kuacha kuendelea kusoma aliendelea kuwa makini kusoma hata kama haikuwa kificho kelele za mlango uliofunguliwa ulisikika vizuri tu hivyo kikawaida alitakiwa aangalie kina nani wameingia.
“… Agent Kai.. Mgeni wako amefika!” Mwanaume wa kizungu aliyevaa mavazi ya kijeshi ya jeshi la Marekani aliye mbele akimuongoza mwanamke wa kiarabu kuingia katika chumba cha kupumzka aliongea.
“Ooooh!” Agent Kai akaongea kifupi hivyo kisha akakunja kurasa ya karatasi aliyokuwa anaisoma hili kuacha alama wapi ameishia katika usomaji wake na kuinua macho yake.
“Asallaam aleykuum warahmaturah wabarakaatuh!” Akasalimu Shufania baada ya macho yao kukutana na mumewe wakatabasamu kwa pamoja kwa furaha ya kuonana.
“Waleikuum Salaam warahmaturah wataallah wabarakatuh.. Karibu mke wangu!”
“Ahasante sana… Kaka! Ahsante sana kwa kunileta mpaka hapa unaweza kwenda bila shaka..!” Akajibu ukaribisho ule kisha akaona amuombe shukrani mlinzi aliyemleta hapa ambaye ni mlinzi anayelinda kwenye korido vilipo vyumba vya kupumzikia ambacho kimojawapo ndicho hiki alicho Agent Kai.
“.. Sawa.. Karibu sana na furahini maongezi yenu wanandoa..!” Mlinzi akajibu kisha akageuka kuelekea mlangoni kuwaacha wanandoa waliomisiana kuongea yao.
“..Mume wangu habari yako?” Akaanzisha maongezi Shufania baada ya kutoa hijabu kichwani mwake ikiwa ni kawaida anapokuwa anaongea na mumewe kuacha nywele zake nzuri nyeusi zilizojimwaga pande zote mabegani mpaka mgongoni zikimfanya azidi kupendeza sana mwanamke huyu wa kiarabu mali ya jasusi mwandamizi mbobezi na komandoo wa hatari sana.
“Safi mke wangu.. Za siku mbili tatu?...Sogea lala kifuani mwangu nimekumisi sana, sogea nishike shike tumbo alilopumzika motto wetu mpendwa” Akajibu Agent Kai kisha akamuomba mkewe asogee karibu yake,ambaye bila hiyana akajisogeza kufanya alichoelekezwa akiwa kaweka kitako kitandani.
“..Imekuwaje umefikia hospitali mume wangu?” Bibie akaanzisha maongezi akiwa sikio lake la upande wa kushoto akiwa kalilaza kifuani mwa mumewe akiskiliza mapigo ya moyo yanavyopiga kila hatua.
“..Kiajali kidogo mke wangu kisikuogopeshe kabisa”
“Unathubutuje kusema kiajali kidogo? Ingewezekana vipi ufikishiwe hospitali na uachwe chini ya uangalizi wa matabibu? Naomba usinifiche ninayeumia mimi na hata wanao ingawa sikuwaambia chochote wakati napewa taarifa natakiwa kuja Maryland kuna dharura imetokea”
“…Ni ndogo sababu unaniona sina majeraha usoni wala mwilini.. Hivyo usihofu kabisa, sema chifu alitaka ufike tuonane tu akijua utakuwa umenimisi siku kadhaa hatujaonana akijua itakuwa vizuri kwakuwa umjamzito”
“Haya nieleze ajali gani ilikukuta na ni wapi?”
“..Mmmh…Sawa.. Ni hivi wakati tumeenda kuandaa ziara ya mheshimiwa makamu wa Rais nchini Mexico kama nilivyokuwa nimekwambia ilitubidi tukaandae na amambo mengine kama hayo nchini Guatemala nikaondoka Mexico na Rebecca huko ndipo tulipata tatizo la ajali ya gari sababu kuna wahalifu ambao wananifahamu mimi walipotuona niko na Rebecca wakahisi labda tunafuatilia mambo yao wakaanza kutuvizia kutufanyia jambo lisilofaa kwetu lakini kwao waliona linafaa ikabidi tujihami ndipo wakati tunawakimbia tukapata ajali tunashukuru pamoja na mimi kuzimia kwakuwa nilichelewa kuchukua hatua stahili mwenzangu hakuzulika sana zaidi ya vimichubuko kidogo, yeye ndiyo alizuia tusizuliwe na maadui wetu na pia aliomba msaada haraka ubalozini na kwakuwa hatukuwa mbali na ubalozi tunashukuru walifika wanajeshi wetu wakawasambaratisha maadui na kutuondoa eneo la tukio… Mimi sikuwa na fahamu chochote wakati huo kwakuwa nilizimia ndipo leo asubuhi nilijikuta niko chumba hiki kwa kupatiwa huduma za kitabibu kwakuwa nilijigonga kichwani nyuma na mbele yaani wakati ajali inatokea nilipigizwa mbele katika dashboard kisha nikarudishwa nyuma nikapiga eneo la chuma la mkanda wa siti niliyokaa kama ujuavyo mimi uwa sifungi mkanda ninapokuwa sehemu ya hatari na ndicho kwa bahati mbaya kilichoniponza” Aliongea uongo huu kwa mkewe Agent Kai akiupangilia kana kwamba alipanga mkewe akifika basi atampa hadithi hii ya kusadikika ambayo kwa asilimia mia moja hata angemuhadithia mama yake mzazi au hata mkuu wake wa kazi basi angeipitisha kwa tiki kubwa sana.
“Ooooh! Kumbe ni hivyo mume wangu? Pole sana.. Lakini Rebecca ngeatakiwa kunipa taarifa wakati ule ule mkiwa huko Guatemala kabla haujasafirishwa kuja huku.. Kwanini alinyamaza?” Bibie mrembo Shufania aliingia katika kujua alichoambiwa ni kweli kwa asilimia mia moja akauliza swali la kwanza lisilohitaji jibu maana aliendelea kisha akaeleza maongezi umbo lilillounda swali ndani yake.
“Nafikiri alighafirika kidogo baada ya tukio lile ambalo si la kawaida ni la kutisha sana… Tumenusurika padogo sana kuaga dunia kwa mzinga ule wa ajali.. Naomba usielekeza lawama kwake kwakuwa amewajibika vizuri kuokoa maisha ya mumeo, nipo hapa mzima sasa nasubiri ruhusa ya daktari nirudi nyumbani..!”
“… Basi tutaondoka wote mume wangu..!”
“Inawezekana… Vipi hali yako? Na mtoto wetu?”
“Niko sawa.. Jana nilienda kliniki alinisindikiza wifi pamoja na Lizy Roby..! Tulikutafuta sana kwenye simu siku ya jana mimi na wifi hatukukupata hewani namba ulizokuwa unatumia kutupigia, mambo mazuri tu usihofu juu yetu”
“Vizuri.. Na..!” Agent Kai aliishia hapa kwakuwa mlango ulifunguliwa akaingia mlinzi anayelinda eneo la vyumba vya kupumzikia upande wa chumba hiki alichomo Agent Kai.
“Samahani Sajenti Agent Kai nimewaingilia maongezi yenu…Kuna wageni wamefika wanahitaji kukuona!” Mlinzi akaongea akiwa amesimama pale pale mlangoni.
“Wanatokea wapi?” Akauliza Agent Kai.
“..Mkurugenzi wa National Security Agency akiwa ameongozana na mkurugenzi wa Drug Enforcement Administration pamoja na wasaidizi wao..!”
“Oooh!... Sikuwa najua hilo kama watafika watu wazito kuja kuniona.. Waambie wapite hili waweze mfahamu na mke wangu si kuniona tu” Agent Kai akakubali ugeni uliofika pale hospitali kwa ajili yake kuingia kumuona katika chumba hiki ambacho si haba ni kikubwa kwa kutosha sana kuingiza watu wanaoweza kuingia katika kundi la watu zaidi ya saba wakiwa wamesimama kuzunguka kitanda kilipo.
“Baba Kawthar! una uhakika naweza kubaki?” Shufania akamuuliza mumewe akiwa anamtizama anavyojiinua kukalia matako.
“..Sidhani kama kuna tatizo.. Kama watakuwa na la siri la kuniambia basi wataniambia baada ya wao kuniomba mimi wewe utoke, au hutaki kuwaona mabosi zangu?” Mume ikabidi amuondoe uoga bibie aliyekuwa ameanza ‘kumbwela’ (kuogopa bila sababu) sura za watu walioingia kuonyesha ni sura ambazo mtu mwingine ukikutana nazo lazima uhisi umekutana na watu muhimu sana serikalini, Shufania akainuka kitako alipokaa pale kitandani na kusimama kwa pembeni ya alipokaa mumewe.
“.. Karibuni wakuu zangu..!” Agent Kai akatoa ukaribisho macho yake majanja yakiwa yanawaangalia kwa zamu watu hawa walio zaidi ya watu sita, wanaume wane na wanawake wawili wote wakiwa ni wazungu.
“Ahsante sana.. Unaweza kuendelea kujilaza kama ilivyokuwa kama haujisikii kukaa kitako..!” Akaongea mwanaume mzee wa makamo ya umri unaokaribia miaka sitini au kuwa katika eneo hilo ambaye kichwani alikuwa na nywele za blonde zilizopaki upande katikati utosini mpaka mbele akiwa na kipara (uwaraza) akiwa kavaa suti nyeusi yenye tai ya rangi ya bluu, mrefu wa urefu unaorandana na karibia wote alioongozana nao kuja nao hapa.
“Niko sawa mkuu sina maumivu ninayoyasikia kwa sasa.. Nasubiri dokta apite nimuombe ruhusa ya kwenda nyumbani” Akajibu Agent Kai na kuwaonyesha kwamba hatanii aliinuka kuwapa mikono ya salamu na ukaribisho, alipitisha mkono wake kwa kila mmoja kwa zamu mpaka wote sita wakaisha.
“..Kweli huko vizuri Agent!... Bila shaka huyu ni mkeo?” Yule yule mwanaume wa umri wa karibu na kustaafu aliongea tena akiwa ameachia tabasamu pana.
“Hujakosea mkuu.. Huyu ni Mrs. Kai!” Akajibu Agent Kai akitupa macho kwa mkuu kisha aharaka akayapeleka kwa mkewe ambaye aliangalia kidogo kisha karudisha macho yak echini kana kwamba anasadifu sakafu kama ilipatiwa katika ujengwaji wake na injinia aliyejenga jengo hili la hospitali kumbe ni kawaida yake na hata watu wote wa familia yake kama si jamii yake huko alipokulia katika makuzi yake uwa hawaachi macho yao makavu kuangalia wanaume wasiohusikana nao.
“Habari yako bibie?” Huyu msemaji mwenye ucheshi na maswali mengi aliendelea kuwa yeye tu ndiyo msemaji toka waingie huku wengine wakiwa wachangamfu tu wasioongea lolote akamsalimu Shufania shemeji yetu kwa mtaalamu Kai.
“Safi mheshimiwa.. Sijui nyie?” Shufania akajibu akiwa bado ameinamisha uso wake chini.
“Sisi tunashukuru tuko vizuri… Pole na hofu juu ya mumeo” Akajibu na kutoa pole.
“Naam nami ninashukuru kumkuta yupo katika hali nzuri iliyoniondoa hofu niliyokuwa nayo wakati niko katika chombo cha usafiri kuja huku kutokea WDC!” Akajibu Shufania.
“Vizuri.. Umekuwa mwenyeji sasa binti yangu.. Naona Kai ashakufundisha kifupi cha jimbo lenu Washington DC kuwa WDC.. Safi sana na karibu sana nchini kwetu jisikie huko nyumbani na utulelee vizuri motto wetu Agent Kai.. Naam!”
“Ahsante sana na bila shaka majukumu yote hayo ninayamudu msihofu juu ya mtoto wenu mpendwa.. Naomba niwaache muongee mimi naenda nje kusubiri mmalize maongezi yenu!” Alijibu Shufania kisha akaomba atoke nje kuwapisha watu hawa waongee na mtu wao waliyemfuata hapa kumuona na kufanya maongezi kidogo wanayoona ni muhimu wao kuyajua hata kabla mtu huyu hajatoka hospitali.
“Hongera Mr. Kai.. Naona mambo tayari mazuri katika ndoa yako, nafikiri fungate ilikuwa bora sana..! Mzee huyu mcheshi aliendelea kutania akiwa anampiga pia begani Kai, watu wengine kimya wakiwatizama.
Mzee huyu ndiyo mkurugenzi mkuu wa taasisi kuu ya ujasusi ya Marekani ‘National Security Agency’ (NSA), ambaye alifika hapa kwakuwa toka jana walikuwa na kikao cha vyombo vikuu vya usalama nchini Marekani, kikao anachokiongoza yeye mwenyewe kama mkuu wa taasisi kuu ya ujasusi inayosimamia mashirika yote ya kijasusi nchini hapa.
“Ahsante mkuu.. Nimepewa taarifa mna kikao kikubwa mnafanya hapa Maryland, nafikiri kitakuwa kikao chenye faida kwa mustakabali wa nchi yetu..!” Kai alishukuru kile alichoambiwa juu ya ndoa yake kisha akaeleza juu ya habari za kikao wanachofanya wakuu wa vyombo vya usalama.
“Yah! Kesho tunamaliza kikao kwa kuhutubiwa na jemedari mkuu Rais wa nchi.. Binafsi nilifanya mahojiano na Special Agent Miss Rebecca Smith juu operesheni ndogo mliyofanya huko Guatemala na ikanifanya nije mwenyewe binafsi kuja kukupa pongezi kwa kile mlichokifanya huko… Hongera sana kijana wangu Agent Kai ikiwa ni miongoni mwa hongera zangu nyingi ambazo binafsi nimezitoa kukupatia mara nyingi toka nikiwa mkurugenzi wa CIA hadi kuwa mkurugenzi wa taasisi kuu.. Pia napenda nikupe pole kwa niaba ya serikali yetu.. Rebecca hajaacha kitu nafikiri maelezo yake yamejitosheleza hivyo sisi hatutakusumbua kwa lolote ingawa tuna ombi tumeleta na ombi hilo atalieleza mkurugenzi wa DEA!” Mkurugenzi wa ‘NSA’ akaongea.
“Ombi lenu lolote mkurugenzi kwangu ni sheria.. Niko tayari kuwasikiliza na kulifanyia kazi” Akajibu Kai.
“Naomba nitoe shukrani zangu kwako kwa kuongoza kikosi kilichoweza kuwapata watu ambao kiukweli DEA nzima tulishawasahau, mmefanya kazi nzuri sana na ya hatari lakini mkafanya kwa kutanguliza uzalendo mkubwa juu ya nchi yetu.. Hongereni sana.. Wakati ninakuja WDC kuja kwa ajili ya kuonana nanyi na kuwakabidhi Investigator Miller na Special Agent Silla nilikuwa najiuliza jinsi ambavyo umekuwa ukifanya vizuri katika kila operesheni unayoenda kuifanya ukiipa sifa kubwa CIA na nchi yetu kwa ujumla.. Kiukweli kuna faida nyingi sana kufanya kazi na wewe umekuwa mzuri kujilinda na kuwalinda wale unaofanya nao kazi nina mengi ya kusema juu yako kama ilivyo yoyote mwenye kusikia sifa zako anavyokuwa na mengi ya kutaka kujua juu yako pia kukwambia.. Ombi letu ambalo tumelileta hapa ambapo kama tutakubaliana basi tutaongea na boss wako lifanyike hilo tunaloona ni sahihi wewe kulifanya” Mkurugenzi wa DEA hakusubiri ruhusa akaeleza alilo nalo na kuingia kwenye ombi ambalo ndiyo haswa lililowaleta wote hawa hapa na si kumuona tu.
“Ahsante kwa shukrani zenu wote kwa ujumla, niko kuwasikiliza ombi lenu” Agent Kai alikuwa anahisi ombi lililoletwa na watu hawa kwake lakini alitaka awasikie wanasemaje wao wenyewe.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na moja (101)
Agent Kai anapokea ugeni akiwa hospitalini alikowekwa mapumziko huku akiwa ametembelewa na mke wake.
Mkurugenzi wa taasisi kuu ya ujasusi ya Marekani (NSA) amefika kumtembelea akiwa na mkurugenzi wa DEA.
Je hawa wakurugenzi wamefika hapa kumpa ombi gani?
Nisipoteze sana muda wako.
“Ahsante mkuu.. Nimepewa taarifa mna kikao kikubwa mnafanya hapa Maryland, nafikiri kitakuwa kikao chenye faida kwa mustakabali wa nchi yetu..!” Kai alishukuru kile alichoambiwa juu ya ndoa yake kisha akaeleza juu ya habari za kikao wanachofanya wakuu wa vyombo vya usalama.
“Yah! Kesho tunamaliza kikao kwa kuhutubiwa na jemedari mkuu Rais wa nchi.. Binafsi nilifanya mahojiano na Special Agent Miss Rebecca Smith juu operesheni ndogo mliyofanya huko Guatemala na ikanifanya nije mwenyewe binafsi kuja kukupa pongezi kwa kile mlichokifanya huko… Hongera sana kijana wangu Agent Kai ikiwa ni miongoni mwa hongera zangu nyingi ambazo binafsi nimezitoa kukupatia mara nyingi toka nikiwa mkurugenzi wa CIA hadi kuwa mkurugenzi wa taasisi kuu.. Pia napenda nikupe pole kwa niaba ya serikali yetu.. Rebecca hajaacha kitu nafikiri maelezo yake yamejitosheleza hivyo sisi hatutakusumbua kwa lolote ingawa tuna ombi tumeleta na ombi hilo atalieleza mkurugenzi wa DEA!” Mkurugenzi wa ‘NSA’ akaongea.
“Ombi lenu lolote mkurugenzi kwangu ni sheria.. Niko tayari kuwasikiliza na kulifanyia kazi” Akajibu Kai.
“Naomba nitoe shukrani zangu kwako kwa kuongoza kikosi kilichoweza kuwapata watu ambao kiukweli DEA nzima tulishawasahau, mmefanya kazi nzuri sana na ya hatari lakini mkafanya kwa kutanguliza uzalendo mkubwa juu ya nchi yetu.. Hongereni sana.. Wakati ninakuja WDC kuja kwa ajili ya kuonana nanyi na kuwakabidhi Investigator Miller na Special Agent Silla nilikuwa najiuliza jinsi ambavyo umekuwa ukifanya vizuri katika kila operesheni unayoenda kuifanya ukiipa sifa kubwa CIA na nchi yetu kwa ujumla.. Kiukweli kuna faida nyingi sana kufanya kazi na wewe umekuwa mzuri kujilinda na kuwalinda wale unaofanya nao kazi nina mengi ya kusema juu yako kama ilivyo yoyote mwenye kusikia sifa zako anavyokuwa na mengi ya kutaka kujua juu yako pia kukwambia.. Ombi letu ambalo tumelileta hapa ambapo kama tutakubaliana basi tutaongea na boss wako lifanyike hilo tunaloona ni sahihi wewe kulifanya” Mkurugenzi wa DEA hakusubiri ruhusa akaeleza alilo nalo na kuingia kwenye ombi ambalo ndiyo haswa lililowaleta wote hawa hapa na si kumuona tu.
“Ahsante kwa shukrani zenu wote kwa ujumla, niko kuwasikiliza ombi lenu” Agent Kai alikuwa anahisi ombi lililoletwa na watu hawa kwake lakini alitaka awasikie wanasemaje wao wenyewe.
ENDELEA NA NONDO…!!
MIPANGO SAWA II
WALTER REED NATIONAL MILITARY MEDICAL CENTER
BETHESDA, MARYLAND-MAREKANI
“Katika kikao chetu cha jana kuna maadhimio tuliyapitia na kuyapititisha.. Tunasikitika mkurugenzi wako wa CIA hatujaja naye hapa sababu amepatwa na dharura ana kikao asubuhi hii katika makao makuu ya jeshi letu huko Pentagon na wakuu wa majeshi yetu, kikao ambacho mkurugenzi wetu wa NSA alitakiwa kuhudhuria lakini naye saa sita ya leo anatakiwa ikulu kwa kikao na mheshimiwa Rais hivyo kwa haraka tuliona tukuone wewe na tuongee nawe katika yale maadhimio tuliyoazimia jana.. Operesheni yenu ya nchini Guatemala ilikuwa ni ile ambayo wewe uliomba ifanyike hili kumuokoa rafiki yako kipenzi hivyo ulijitolea kuifanya bila kujali lingine lolote ilimradi rafiki yako atoke alikofichwa bila sababu kwa miaka zaidi ya sita, tunashukuru adhima yako imetimia kwa kiasi kubwa ukishirikiana na watu niliokuletea na yule uliyemchagua mwenyewe tena mkirudi na ushindi mzuri mkiwa na hitilafu ndogo za mwili zenye kurekebishika… Lakini operesheni hii inatakiwa imalizwe kwa wahusika kuwajibika hivyo hamjamaliza kazi yenu, tunaomba kijana wetu kwakuwa nyiye ndiyo mliianza hii kazi mngeimalizia kwa kumsaka popote alipo na kumtia nguvuni Brigedia Fernandes Carlos Codrado aje hapa Marekani ajibu kesi ya kushikilia wamarekani wenzetu zaidi ya miaka sita bila sababu na pia kumfungulia mashitaka kwa kujihusisha kwake na biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya katika nchi yetu kwa kiasi kikubwa.. Ombi letu ni hili kwako unaweza ukaamua lini utaianza hii kazi lakini tungependa ingekuwa mapema ingependeza zaidi na wewe ndiyo utachagua watu wa kukusaidia hii kazi kama ni wale ulioenda nao Guatemala au wengine ni wewe tu nchi yetu ina watu wengi wa kazi hizi hata ukitaka wenzako walio katika Special Activities Division kama unahisi kutakuwa na ugumu hilo linawezekana boss wetu yupo hapa ataidhinisha yoyote utakayemtaka kama si wowote utakaowataka kwa idadi ya moja mpaka tano.. Tunakusikiliza wewe kazi ipo mezani kwako” Mkurugenzi shirika la kupambana na madawa nchini Marekani ‘Drug Enforcement Administration” (DEA) alitoa maelezo marefu kama anasoma gazeti.
Agent Kai aliinama chini kidogo akavuta hisia kisha akawaangalia maafisa na mabosi walio mbele yake akarudisha kichwa chini kufikiria muda na pia papo hapo akaifikiria familia yake hasa watoto wake ambao anakosa muda mwingi wa kukaa nao nyumbani lakini pia akatamani changamoto kwakuwa anapenda changamoto kuliko kitu chochote akaona ngoja awaambie wampe siku moja atakuja na jibu litakaloambatana na mpango wenyewe kama atakubali kufanya kazi hii ambayo kwake itakuwa muendelezo tu kama ataikubali lakini anaweza ikataa na haitakuwa tatizo kwake kwakuwa ametoka safarini kazini na amefanya lile aliloomba yeye kulifanya kwa kushirikiana na wenzake.
“Nimekusikia mkurugenzi.. Naomba nami nifikirie kama nyiye mlivyokaa kikao na kufikiria pia nitahitaji niongee kidogo na familia yangu hata boss wa kitengo nilichopo nitahitaji kusikia ana lipi la kuniambia kama mjuavyo niko CIA niko SAD pia niko chini ya katibu wa ofisi ya makamu wa Rais ambapo sote tunahudumu chini ya maelekezo ya makamu wa Rais hata kama mkurugenzi wetu mkuu wa NSA yupo hapa lakini hizi kazi zina taratibu zake… Naamini mtanielewa..!” Akajibu hivi Agent Kai jibu ambalo wote walio pale walilikubali vichwani mwao.
“Kwangu mimi naona ni sawa.. Ila kama alivyosema mwenzangu hapa usiache ajipange zaidi wakati tukiwa tumeziba mianya yote ya kuweza yeye kuinuka tena nguvu kazi ya watu, tunawasiliana na wenzetu wa Mexico kuhakikisha hawezi tena kufanya upuuzi wake wa kuunda kambi kubwa kama ile ya Tajumulco ambayo ilitushangaza sana” Mkurugenzi wa NSA akakubali alichoongea Kai.
“Nawaahidi siku mbili tu zitanitosha kuleta maamuzi yangu nimeimisi sana familia yangu na wao pia wamenimisi baba wa familia”
“..Basi tukuache upumzike kijana.. Mungu akufanyie wepesi kwa kila jambo.. Rekodi yako nzuri inatushawishi kuwa kazi hii utaifanya kwa ubora na ufanisi mkubwa kama ulivyofanya kazi zingine zilizopita ukitumia muda mfupi, usituangushe katika maamuzi yako na tunaamini juu ya hilo kijana wangu” Mkurugenzi wa NSA akaongea tena.
“Amini! Amini! Msiwe na wasi kabisa naamini mambo yatakuwa poa!”
Maongezi muhimu kati ya viongozi hawa na Agent Kai yaliendelea kwa wao kuagana na kutakiana kila la kheri wakamuacha Agent Kai ambapo mke wake naye akarejea na maongezi yao ya kawaida yakaendelea.
***** ***** *****
BAADA YA SIKU TATU!
WASHINGTON DC-MAREKANI
“.. Unaona ni sahihi kuondoka tena mume wangu?”
“Kiukweli inaweza ikawa si sahihi kwa familia lakini ni sawa kwa heshima ya kazi yangu.”
“Ulivyokuwa ukiniambia jioni kuwa kesho unatakiwa kwenda huko unaposema nilifikiri unatania kwakuwa mume wangu una pande mbili ambazo nilizozizoea kwa sasa”
“Pande mbili! Pande gani hizo?”
“Utani mwingi ni pande yako ya kwanza na pia u serious… Nashindwa kukuelewa kwakuwa unakuwa unaniacha njia panda kwenye masuala kama haya muda mwingine”
“Kivipi mke wangu?”
“Naona hivyo mume wangu.. Nilijua unanitania lakini umefika muda wetu wa maongezi ya kifamilia hapa kitandani kama ilivyo ada yetu mwenzangu unaniambia heti kesho unatakiwa uende Mexico safari ambayo inaweza kukufikisha Argentina na Brazil… Hivi tumelala wote usiku wa jana na usiku wa leo unakuwa usiku wetu wa pili kisha asubuhi unatakiwa uondoke narudi kwenye kulala peke yangu mimi mjamzito wa ujauzito wa kwanza katika maisha yangu baba Kawthar haututendei haki mimi na wanao.. Angalia hata mabosi zako wanajua kuwa umerudi siku tatu zilizopita ukiwa hujitambui heti siku ya nne wanakwambia uende huko ni haki kweli?”
“…Mke wangu unatakiwa name unisikilize, unafahamu kuwa mimi pia sipendi kutokuwa na nyinyi hapa WDC… Si kama sijui huu ujauzito wako ni wa kwanza unaohitaji ukaribu wangu kuliko chochote lakini kuishi bila uhakika kuwa tuko salama si vizuri, nimefanyiwa jaribio la kuuliwa huko Guatemala, haya tunapenyezewa habari za siri kuwa adui waliofanya jaribio la kuniua Guatemala wameahidi lazima waniue, unataka tukae hapa kusubiri waje kufanya wanachosema au nikawazuie kabla hawajafika? Sikiliza mke wangu mimi ni komando wa kiwango cha juu si kama najisifia lakini nastahili kujigamba hivyo, kuwasubiri maadui wanipige kofi si jadi yangu hata siku moja kawaida yangu mimi uwa ni jino kwa jino, weka mguu niweke mguu bambi kwa bambi, wamejaribu hawajafanikiwa nami natakiwa nikawajibu popote walipo”
“Lakini mume wangu wangekuacha upumzike hata wiki moja mwili wako ukae sawa zaidi… Siwezi kukuzuia kufanya kazi yako nilikukuta nayo sina budi kukubaliana nayo kivyovyote lakini kama mke wako niliyefunga ndoa na wewe nikila kiapo cha kuwa nawe katika shida na raha na kukulinda kwa kila hali sitakiwi kunyamaza kisa nikakuacha uende kazini ukiwa katika hali isiyo na uzima kwa asilimia mia moja”
“Usiwe na wasiwasi mke wangu, mimi niko fiti kwa asilimia mia moja na ninataka nikuahidi jambo moja kuwa mchoro wote huko sawa naenda kumeza tu tulichokwisha kitafuna… Ahadi yangu siku tatu mbele hazitafika nitakuwa hapa kitandani tukiongea kwa furaha kubwa sana”
“Mmmh! Mswahili wewe hujionei huruma kabisa na hili linanichanganya sana mkeo… Natamani nirudishe nyuma fungate yetu turudi Afrika ambako tulikuwa na wakati mzuri ambao kwa jinsi navyoona kazi zako sidhani kama tutarudi kuwa kama ilivyokuwa Afrika..”
“Wasiwasi wako tu… Andika moyoni mwako kisha gonga muhuri kwa ubongo wako kuwa baada ya kwenda kukimalizia hiki kiporo sitatoka nje ya Marekani mpaka utakapojifungua mtoto wetu..!”
“Siamini mume wangu”Alianza kulia mwanadada mrembo wa kiarabu, ikabidi mume aanze kibarua kipya cha kumbembeleza mke wake huku akimpapasa tumbo linaloonyesha kwa mbali kuwa limebeba kiumbe.
Wakiwa wanaendelea kubembelezana simu ya mkononi aina ya smartphone ya kampuni ya Samsung inayomilikiwa na Agent Kai ilianza kuita akiwa ameiweka juu ya meza ya vitabu vya kujisomea ambayo ipo pembeni kidogo ya droo ya pembeni ya kitanda, ilimbidi Agent Kai ainuke toka kitandani kupiga hatua mbili ilipo meza akimuacha mkewe anamuangalia kwa macho ambayo hata hanithi akikutana nayo atatamani awe mmiliki wa macho haya yaani hatari na nusu kwa urembo huu (mashaallah).
“Sijui nani usiku huu?” Akauliza Kai kwa sauti kana kwamba anataka jibu toka kwa mkewe kumbe anajiuliza yeye mwenyewe.
Aliinua na kusoma jina na namba ya mpigaji ndipo akakuta jina la boss wake ‘chief executive of the vice-president’, huyu katibu mkuu katika ofisi ya makamu wa Rais wa Marekani ambapo ndipo ofisi ya Agent Kai ipo chini ya mheshimiwa huyu, akageuka kumuangalia mke wake akakuta macho yale makali katika sekta yetu ile yamekuwa si yale tena yalikuwa ni macho ya udadisi sasa yakitamani kujua ni nani aliyepiga simu, mume hakuongea kwa sauti bali akatoa ishara ya kuweka kidole cha katikati ya papi (lips) zake akimaanisha anyamaze kisha akapokea simu.
“Halloo chifu?” Akaongea akiwa kaiweka sikioni simu mkono wake wa kushoto ukiwa umeisapoti kukaa pale lilipo sikio.
“… Mkurugenzi wako amekubali uongozane na Rebecca Smith, Hansen, Jade na Omar kama ulivyoomba pia DEA wamekupa tena Silla hivyo kesho asubuhi kama tulivyoongea leo jioni mtakutana kuweka mikakati sawa mtakapokubaliana.. Ni haya tu, pole kwa kukuvurugia mapumziko yako kijana wangu na pia salamu zako toka kwa makamu wa Rais anasema ukirudi umuone… Nikutakie usiku mwema” Hakukuwa na muda wa kupoteza toka upande wa katibu alieleza kwa haraka sababu iliyomfanya kupiga simu kisha akakata simu bila kusubiri jibu toka kwa Agent Kai.
“..Boss wako?” Kai alipoiweka simu mezani tu akakutana na swali toka kwa mkewe.
“Ndiyo..Ana maagizo ya kazi hasa juu ya safari yetu kesho” Akajibu Agent Kai.
Maongezi baina ya mke na mume yaliendelea mwisho wakafikia mufaka wakalala zao.
***** ***** *****
WASHINGTON DC-MAREKANI
‘Defending Our Nation. Securing The Future’ kauli mbiu ya wanausalama wa Marekani wanaohudumu sekta ya ujasusi na jeshi ikiwa ndiyo mwito wa taasisi kuu inayosimamia mashirika yote ya kijasusi ya National Security Agency (NSA), muda wa saa mbili na nusu asubuhi iliwakuta vijana wa kimarekani katika moja ya ukumbi ulio katika ofisi ndogo ya CIA iliyoko ndani ya majengo ya uwanja wa ndege mkubwa na wa kisasa wa kimataifa wa Washington Dulles International Airport uliopo eneo la Loudoun na Fairfax maili 26 toka katikati ya jiji la Washington DC.
Vijana hawa wote wanausalama waajiriwa wa serikali ya Marekani vitengo vya ujasusi wakiwa ni watu wanaojuana katika kazi, watano wakitokea shirika la kijasusi la CIA huku mmoja akitoka shirika la kupambana na madawa ya kulevya la ‘Drug Enforcement Agency’ (DEA), lakini katika kundi la CIA watu wawili walikuwa wanatoka ofisi ya makamu wa Rais iliyopo ikulu ya Eisenhower huku watatu wakitokea makao makuu ya CIA ila ni watu ambao Agent Kai aliyefanya chaguo la kuwachagua hawa alikuwa akijuana nao zaidi ya sana akiwa amefanya nao kazi sehemu mbalimbali hapa duniani akiwa anawakubali sana ufanyaji wao wa kazi wenye weledi mkubwa sana pia wakiwa ni miongoni ya majasusi wa juu kabisa Marekani ambao wana kitengo chao maalumu kiitwacho ‘Special Activities Division’ kwa kifupi (SAD) kikosi kilichokusanya majasusi waliofika level ya ukomandoo katika jeshi la Marekani ndiyo uletwa humu kwa ajili ya operesheni kubwa za kijasusi za siri na inapobidi za wazi.
Kikao cha siri kilikuwa kikifanyika hapa baina yao watu hawa wakiwa na mtu aliyewachagua kwa ajili ya operesheni fupi na muhimu sana kwa upande wao, operesheni iliyopewa jina ‘delete virus’ wakimaanisha ‘kufuta virusi’ ikiwa na maana ya kuwa atafutwe Feca na kuwe na mawili kwake aletwe hai Marekani au auliwe kichwa chake kiletwe Marekani kikiwa kichwa mfu tena na si mtu hai tena.
“.. Watu wa DTO huko Mexico wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya wafuasi wa Kingpin Feca wengi wao ni waliokuwa wakiwalinda viongozi wa juu wa genge lao na pia kuambatana nao.. Lakini miongoni mwao hakuna aliyeko katika orodha yetu ambaye amekamatwa” Kikao chao cha siri cha watu sita kilianza kwa Special Agent Rebecca Smith kuanza kuongea kwakuwa yeye kati yao ndiyo alikuwa anajua mengi zaidi maana hakuwa amepumzika toka watoke Guatemala akiambatana na watu wengine wa usalama waliowabeba Agent Kai na Investigator Miller katika ndege ndogo ya kijeshi, walirudi na Silla lakini Silla walipowafikisha hospitali majeruhi yeye aliondoka na kina Agent Johnson Greg Rautollaye kuelekea Springfield, Virginia yalipo makao makuu ya DEA.
“..Gazeti hili limeeleza kwa kifupi jinsi polisi walivyopigwa ghiliba na watu wa Feca kwa kutengeneza msafara wa feki wa magari anayoyatumia Kingpin Feca na msaidizi wake Guti Villa Nandez.. Nafikiri ulinzi wa mapolisi wakishirikina na maafisa wengine wa usalama huko Mexico uliamini msafara ule ni wa hao mabwana wakubwa kwakuwa ilikuwa tayari ni usiku mnene mida ambayo kwao waliamini mia kwa mia kuwa kama Feca atataka kuondoka jimbo la Guerrero basi lazima ataondoka mida ya usiku kama waliyoondokea watu hao msafara ulioanzia Tetaplan” Special Agent Simone Joseph Silla aliongea huku akionyesha nakala ya gazeti alilokuwa akilisoma kupitia mtandaoni (softpaper).
“Maboss wa madawa ya kulevya wana mbinu mpya kila siku kukicha hivyo kupambana nao inabidi kutumia ujanja mwingi… sishangai Feca kuwatoroka maafisa wa usalama kwa namna hiyo kwakuwa ana uzoefu mzuri sana na mambo ya kijeshi pia analindwa na watu mbalimbali walioko serikalini ila hakiwezi kuharibika kitu muhimu tufike kwanza Mexico, hapo tukishafika tu tutaanza uchunguzi mara moja” Agent Kai akaongea kisha akanyamaza kuangalia wenzake kwa kutupia macho kwa baadhi yao, wote na wao wakawa wanamuangalia hivyo akaendelea.
“Tutaingia Mexico kufanya uchunguzi wetu ambao tutatakiwa kuufanya kwa siku mbili, naamini timu hii ikitawanyika kwa ufasaha tutapata jibu yuko… Mavazi tutatakiwa kuvaa kiuni kama vijana wengi wa kimexico wanavyovaa… Tutaondoka kwa ndege ya kijeshi kutokea hapa WDC ikipaa mpaka anga la Colorado mpakani mwa nchi yetu na Mexico hadi kwenye milima Tuxtla pale tutashushwa kwa parachuti ambako sasa tutaweka kambi ya angalau nusu saa hapo tukipeana mikakati mipya ya kimajukumu ya kazi yetu”
Maelezo ya mwisho aliongea Agent Kai kisha ya hapo wakaletewa taarifa kuwa ndege iko tayari inawasubiri wao.
Mwisho wa sehemu ya mia na mbili (102)
Wapi walipokimbilia kina Kingpin Feca na wafuasi wake?
Kujua kinachoendelea fuatana nami katika sehemu inayofuata, mambo yanaelekea ukingoni tukiwa tumebakisha episode chache kuumalizia mkate wetu mkubwa wa kisasa.
“.. Watu wa DTO huko Mexico wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya wafuasi wa Kingpin Feca wengi wao ni waliokuwa wakiwalinda viongozi wa juu wa genge lao na pia kuambatana nao.. Lakini miongoni mwao hakuna aliyeko katika orodha yetu ambaye amekamatwa” Kikao chao cha siri cha watu sita kilianza kwa Special Agent Rebecca Smith kuanza kuongea kwakuwa yeye kati yao ndiyo alikuwa anajua mengi zaidi maana hakuwa amepumzika toka watoke Guatemala akiambatana na watu wengine wa usalama waliowabeba Agent Kai na Investigator Miller katika ndege ndogo ya kijeshi, walirudi na Silla lakini Silla walipowafikisha hospitali majeruhi yeye aliondoka na kina Agent Johnson Greg Rautollaye kuelekea Springfield, Virginia yalipo makao makuu ya DEA.
“..Gazeti hili limeeleza kwa kifupi jinsi polisi walivyopigwa ghiriba na watu wa Feca kwa kutengeneza msafara wa feki wa magari anayoyatumia Kingpin Feca na msaidizi wake Guti Villa Nandez.. Nafikiri ulinzi wa mapolisi wakishirikina na maafisa wengine wa usalama huko Mexico uliamini msafara ule ni wa hao mabwana wakubwa kwakuwa ilikuwa tayari ni usiku mnene mida ambayo kwao waliamini mia kwa mia kuwa kama Feca atataka kuondoka jimbo la Guerrero basi lazima ataondoka mida ya usiku kama waliyoondokea watu hao msafara ulioanzia Tetaplan” Special Agent Simone Joseph Silla aliongea huku akionyesha nakala ya gazeti alilokuwa akilisoma kupitia mtandaoni (softpaper).
“Maboss wa madawa ya kulevya wana mbinu mpya kila siku kukicha hivyo kupambana nao inabidi kutumia ujanja mwingi… sishangai Feca kuwatoroka maafisa wa usalama kwa namna hiyo kwakuwa ana uzoefu mzuri sana na mambo ya kijeshi pia analindwa na watu mbalimbali walioko serikalini ila hakiwezi kuharibika kitu muhimu tufike kwanza Mexico, hapo tukishafika tu tutaanza uchunguzi mara moja” Agent Kai akaongea kisha akanyamaza kuangalia wenzake kwa kutupia macho kwa baadhi yao, wote na wao wakawa wanamuangalia hivyo akaendelea.
“Tutaingia Mexico kufanya uchunguzi wetu ambao tutatakiwa kuufanya kwa siku mbili, naamini timu hii ikitawanyika kwa ufasaha tutapata jibu yuko… Mavazi tutatakiwa kuvaa kiuni kama vijana wengi wa kimexico wanavyovaa… Tutaondoka kwa ndege hadi kwenye milima Tuxtla pale tutashushwa kwa parachuti ambako sasa tutatawanyikia hapo tukipeana mikakati mipya ya kimajukumu ya kazi yetu”
Maelezo ya miwsho aliongea Agent Kai kisha ya hapo wakaletewa taarifa kuwa ndege iko tayari inawasubiri wao.
ENDELEA NA MAPIGO..!!!
MIPANGO SAWA III
MISITU YA MLIMA TUXTLA – MEXICO
“Tunakaribia eneo mnalotakiwa kuruka.. Nafikiri mlango wa chini ufunguliwe..” Rubani wa ndege ya kijeshi aina ya Gulfstream IV mali ya jeshi la anga la Marekani (United States Air Force).
Mfungua mlango alisogea mahala ambapo ataweza kubonyeza mlango wa chini wa ndege kufunguka kisha akawaangalia wanaotakiwa kuruka kama wako sawa, wote wakamuonyesha alama ya dole kuwa wako poa wako tayari kuruka, wote walikuwa wamejifunga inavyotakiwa kwa mrukaji toka ndani ya ndege wakiwa hakuna sehemu ya mwili iliyo wazi, machoni wakiwa na miwani mikubwa.
“Ruhusu” Rubani akaongea tena.
Agent Kai akiwa sambamba na Special Agent Rebecca walikuwa wa kwanza kujiachia kwa pamoja kuruka toka ndani ya ndege wakafuata wengine na kutimia idadi ya watu sita wa kazi kuruka ikiwa ni usiku wa saa saba na nusu kukiwa na giza totoro kwenye msitu ambao watu hawa walikuwa wakiuona kwa juu.
Kila mmoja kati ya watu hawa hakuna aliyekuwa si mzoefu katika miruko hii, walikuwa na mafunzo yote hivyo baada ya kuwa wamejiachia ‘tupu’(free) kutokea juu wakiwa hewani kitaalamu walikuwa wakienda kihesabu ambazo kiasi fulani kikibaki toka juu kuja chini basi mrukaji utakiwa kufyatua parachuti na ndicho kilichofanyika kati yao wote sasa wakawa wanatelemka taratibu waki control mwendo na eneo zuri la kwenda kutua licha ya kuwa ni usiku miwani waliyovaa kila mmoja ilikuwa ni miwani inayosaidia kuona vizuri tokea juu kuja kwenye msitu ambao ulikuwa ni msitu mkubwa wenye miti mbalimbali na majani makubwa.
Mungu aliwasaidia wote waliweza kutua vizuri eneo la juu ya moja ya mlima kati ya safu za hifadhi za milima hii inayoitwa mlima Tuxtla iliyo chanzo cha mito kadhaa inayotiririsha maji yake majimbo kadhaa ya nchi ya Mexico.
Kila mmoja alikusanya kitendea kazi kilichowashusha kwa usalama (parachuti), baada ya kazi hii iliyokuwa ikifanyika kwa haraka waliyakusanya kwa pamoja na kisha kuyaweka mahala ambapo kuna shimo lililosababishwa na mkondo wa maji unaopita eneo hili ila kwa sasa hakukuwa na maji ya mvua wala yaliyotuhama kwasababu zozote zile, waliyaweka maparachuti hapo wakayafunika kwa matawi ya miti waliyoyavunja katika miti iliyo karibu karibu na eneo, kazi ikifanyika kwa kasi na ushirikiano iliyowafanya watumie dakika mbili zisizotimia kufika mbili kamili (kumbuka watu hawa ukiacha Rebecca Smith na Silla walikuwa ni makomandoo waliopita mafunzo ya kila aina michezo ya akili na nguvu katika mafunzo yao).
Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa miwani waliyovaa ambayo haikuwa na kazi wakiwa hapa ardhini kwakuwa inaona tofauti na vile inavyoona ikiwa imevaliwa hewani, wote kana kwamba wanaelekezana kumbe ni hatua za kimafunzo walitoa miwani mingine wakaivaa.
“Tuondokeni haraka… Tutaenda ongea eneo la chini baada ya kuupita mlima wa pili kutoka huu” Agent Kai kiongozi wa msafara akaongea kuwaambia wenzake waliokuwa wakitupa macho huku na huko kuangalia mambo kadhaa wa kadha.
Msafara wa kuondoka eneo walilotulia ukaanza kwa kasi wakipita kwa kufuata kando ya mkondo wa maji uliotengeneza njia kutokea juu ya mlima kuteremka kwa chini wakipita miti mikubwa mikubwa na midogo midogo pamoja na manyasi magugu makubwa katika misitu ya milima ya Tuxtla iliyosambaa sehemu kubwa sana kuanzia kusini mwa Mexico, kaskazini na Mexico ya kati.
“Hapa kunafaa.. Rebecca naomba ile ramani niliyokupa WDC uiweke… Eneo lina baridi kali sana muda huu wa usiku” Agent Kai aliongea walipofika mahala ambapo ni kando ya jabali kubwa la jiwe lililojishikiza kwenye mlima na kila mmoja kutafuta mahala ambapo aliona ni sahihi kuweka kitako kusikiliza mipango toka muongoza msafara wao, Rebecca alitoa begi lake toka mgongoni mwake kisha akafanya vile alivyoombwa na boss wake.
“Historia ya eneo la milima hii kijiografia inajibu la kwanini kuna baridi hivi Bwana Kai hivyo usione ajabu ya baridi hili kuwa kali hivi tumelifuata mahala pake, mahala karibu na linapoanzia”Aliongea mtu ambaye usiku huu sura yake alikuwa ameizinga haswa kwa kitambaa cha skafu akiacha eneo la mdomo tu huku machoni akiwa na miwani isiyo ile ya kawaida miwani ya kazi (kijasusi) ni mzungu huyu mwanaume wa miaka inayokaribia thelathini na tisa sasa mtu anyeheshimika sana katika nyanja za kijasusi na kijeshi katika nchi ya Marekani akiwa amefanya kazi nyingi sana mpaka kufika umri huu alionao, alikutana na Agent Kai katika kile kikosi bora kabisa cha makomandoo wa kitengo cha US Navy Seals na baadaye wote kati yao walipelekwa katika kikosi maalumu cha ‘Special Activities Division’ (SAD), akifahamika kwa majina Agent Hansen Nicholaus Blade huku huko jeshini alikuwa akifahamika kwa utambulisho wa cheo chake cha Brigedia Hansen Nicholaus Blade a.k.a The Ghost wakimaanisha ‘mzimu’ kwa jinsi anavyofanya kazi zake kama mzimu kiasi ambacho inaogopesha kwa kweli.
“.. Nafahamu Ghost.. Milima hii imetulia karne hii lakini karne kadhaa zilizopita volcano ilikuwa inalipuka kule juu ya kilele kile niliambiwa mara ya kwanza nilivyokuja kwenye misitu ya milima hii kufanya mazoezi nikiwa mwanafunzi wa jeshi bado kachanga hahah hahaah… Mwalimu wetu tuliyekuja naye Kanali Bruno Trens alisema milima hii ina vyanzo kadhaa vya mito mikubwa” Agent Kai akaeleza kile anachokijua akivuta kumbukumbu ya miaka kadhaa nyuma akiwa mwanafunzi katika mafunzo ya jeshi waliwai fika kwenye safu ya milima hii na kuweka kambi.
“..Yah! hata nami nakumbuka tulifika kuweka kambi hapa nafikiri nilikutangulia Kai.. Kule kileleni ile theluji inaitwa theluji ya Sierra De Los Tuxtla ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha mvua za mara kwa mara eneo hili la milima na majimbo ya jirani yanayopakana na milima hii..” Agent Hansen naye akaeleza alijualo kwa haraka ubongo wake ukivuta picha miaka kadhaa iliyopita.
“… Mvumo wa maji yanayoporomoka yanayosikika kwa mbali ni chanzo cha mto Colorado tupo karibu na chanzo chake ndiyo naona kwenye ramani hapa… Hapa tukienda kwa bondeni kama mita hamsini ndipo tutafika zilipo kingo za mto Grivalja, tumeshushwa mbali sana tupo katikati ya misitu na sijui kwanini rubani alitaka tushukie hapa, ametupa kibarua cha kutembea umbali mrefu sana” Akaeleza Agent Kai akiwatizama wenzake kwa zamu kila mmoja ambao na wao walikuwa wamekaa kwa mbele yake wakiwa wanamtizama.
“Ni kweli ametupa kibarua kizito sana hakuwa amefikiria vizuri ingawa ni rubani mzoefu mwenye kulijua vizuri hili eneo” Agent Hansen akaongea tena sasa wakiwa kama wao ndiyo wameamua kuongea ukiacha wenzao waliokuwa wakiwasikiliza tu.
“Nafikiri hatutakuwa na bahati mbaya ya kutubidi kuvuka mto tukiwa tunaelekea tulipoelekezwa kuwa kuna hifadhi ya maua ya frola katika kijiji kinachoitwa Coyatoc ambapo kuna mpaka wa jimbo la Chiapas na Veracruz ambapo itakuwa vizuri tukigawana majukumu pale kuanzia upelelezi wetu” Agent Kai akaeleza tena na kisha wote wakakubaliana msafara uanze tena ikiwa ni saa nane na dakika kumi usiku unaoitwa usiku manane (usiku mnene).
***** ***** *****
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
Ilikuwa ni saa tano na dakika tano usiku siku ya jumapili inayoelekea kuisha hili kuipisha siku mpya ya jumatatu inayokaribia kuanza kama ilivyo ada ya masaa kubadili siku pale ifikapo saa sita usiku katika kila nchi ama eneo fulani kijiografia basi muda huu ndiyo uwa muda muagano na muda mkaribishwa wa siku inayoisha na siku inayokuja, saa tano hii kwa saa za nchi ya Brazil ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa uitwao Deputado Luis Eduardo Magalhae International Airport unaopatikana kilometa zipatazo ishirini na nane kutoka katikati ya jiji la Salvador, jiji kuu na jiji la kibiashara la jimbo la Bahia, jimbo linalojitawala na ni moja ya majimbo makubwa kati ya majimbo yanayounda nchi ya Brazil.
Salvador ni jiji la nne kwa ukubwa katika nchi ya Brazil ikitanguliwa na jiji namba moja Sao Paulo ambapo pia ndiyo mji mkuu wa shughuli kuu za kiserikali, mbili ikikamata jiji la Rio De Janeiro huku tatu ikienda jiji la Brasilia jiji kuu la kibiashara ndipo linafuata hili jiji la Salvador lililopo jimbo la Bahia jimbo linaloundwa na manispaa zipatazo thelathini na mbili za nguvu.
Ndege binafsi ndogo ya kubeba abiria wapatao kumi tu ilitua muda huu katika eneo ambalo uruhusiwa kutua ndege zilizobeba watu wa serikali au watu maarufu kwa watoto wa mjini upenda kuwaita watu hawa kuwa ni ‘watu wenye namba zao mjini’, watu saba walishuka toka ndani ya ndege wakatanguliwa na watu wanne walioshuka kwa kufuatana wakikuta wenyeji wao waliokuwa wanaoneka ni maafisa wa kiserikali waliokuja kuwapokea waliwalaki kisha ya hapo wakashuka watu wengine watatu usiku huu walikuwa wamevaa kofia zinazofanana aina ya pama au wengine wamezoea kuziita marliboro kutokana na ‘movie’ (filamu) nyingi za miaka ya nyuma waliokuwa wakivaa hizi katika filamu walikuwa wanavaa huku wakisukuma sigara zinazoitwa jina la Marliboro hivyo zikawa maarufu sana kwa jina hili.
“Karibu mkuu…!” Mwanaume mmoja aliye mbele Kabisa usiku huu akiwa amevaa suti nyeusi juu yake akiwa kavaa koti kubwa jeusi kama la kujikinga mvua alitoa ukaribisho baada ya kupeana mkono na mtu wa kati katika safu ya watu watatu kushuka mwisho kutoka ndani ya ndege.
“Ahsante sana.. Naamini kila kitu mmeweka sawa?”
“Yah! Kila kitu kipo sawa usihofu ila hatutakiwi kuuweka hapa gari zinatusubiri maegeshoni, walinzi wameambiwa mtoto wa Mfalme wa Hispania atafika usiku huu kwa ndege ya kukodi hivyo asibugudhiwe.. Hivyo twende bila wasiwasi sote tuko salama wa salimini”
“Vizuri sana…!” Akajibu kigogo huyu aliyepewa hadhi ya kuwa yeye ni mtoto wa Mfalme wa nchi ya Hispania katika mipango yao aweze kuingia bila kufuatiliwa na kuhojiwa hojiwa yeye ni nani.
Msafara uliondoka kwa haraka kuelekea maegeshoni, maegesho ambayo si yale ambayo yanakuwa yanatumika na watu changanyikeni haya yalikuwa ni maegesho yanayotumiwa na viongozi wa serikali au watu maarufu wa Brazil na nchi nyinginezo.
Magari matatu yanayofanana aina ya Cadillac XTS 2016 yakiwa na rangi ya mfanano pia kwa kila mojawapo rangi nyeusi yalikuwa yakisubiri watu hawa waliofika kupokea na wapokelewa kwa ajili ya kuendeshwa na kuwapeleka wahusika popote wanapohitaji kwenda katika jiji hili la manispaa ya jiji la Salvador jimbo la Bahia nchi ya Brazil.
“Mr. Ceni tuingie tu katika gari moja” Kigogo mwenye heshima zake akaongea wakati mtu mmoja alipokuwa amemfungulia mlango wa gari ambayo kimpango imepangwa katikati ya gari zingine mbele ikiwa imetangulia moja na nyuma pia ipo.
Mr. Ceni akafanya alivyoelekezwa milango ikafunguliwa yeye na kigogo mtanashati wakaingia katika gari ya katikati.
Sao Salvador Da Bahia De Todos Os Santos ni maandishi ya kireno haya yakimaanishwa kwa kiingereza kuwa ‘Holly Savior From The Bay Of The All Saints’ kwa kifupi ikifupishwa kwa kuitwa ‘Salvador’ lilikuwa ni jiji kubwa sana la kupendeza kwa majengo yake mchanganyiko kulingana na eneo kwa eneo yapo majengo ya kizamani na pia yapo ya kisasa yote yakiwa yanapendezesha jiji hili kwa taa zake usiku huu.
“.. Mlitafuta nyumba niliyosema?” Akauliza kigogo, swali lililoenda moja kwa moja kwa dreva anayeendesha gari kukata mitaa wakiwa katika barabara kuu itokayo eneo la uwanja wa ndege kuelekea katikati ya jiji.
“Ndiyo mkuu, tulitafuta nyumba kama ulivyoagiza tumepata eneo la Metropolitan karibu na beach ya jiji ya Lauro De Freitas ni jengo la ghorofa tano ni mtaa uliotulia sana sababu wakazi wa eneo hilo ni watu wenye uwezo kipesa hivyo hakuna kufuatiliana sana wote wawe wenye nyumba au wapangaji hakuna anayeweza kupamudu kama ni mtu wa hali ya chini hivyo kwa maelekezo yako uliyosema tuliona ndipo mahala sahihi kwako kukaa kwa amani ukililindwa kwa ulinzi wa serikali yenyewe bila wao wenyewe kujua kuwa wanakulinda mtu wa aina gani” Dreva akajibu bila ya kuwa anamuangalia anayemjibu akili yake ilikuwa ikifanya mambo mawili kwa wakati mmoja kuongea na kuendesha kwa umakini usiku huu ndani ya barabara hii kuu ya BR-101.
“Kazi nzuri sana Joao.. Sote tuliofika hapa Salvador tutafikia hapo na hata mke wangu baada ya mwezi mmoja nitataka aletwe hapa, nafikiri mwaka mmoja utatutosha kujipanga na kurudi kufany kinachoitwa jino kwa jino kwa wamarekani” Kigogo akaongea mkono wake wa kulia ukiwa umeachia kiganja chake kikamatie shavu lake ambapo tunaiita kujishika ‘tama’.
Msafara ulifika mzunguko wa Feira De Santana ukazunguka kisha kukamata barabara ya BR-116 ambapo walinyoosha moja kwa moja kilometa kadhaa wakafika eneo maarufu sana kwa wapenda mchezo wa soka wa jiji hili kwani ndipo wanapopata burudani ya ligi yao inayoitwa ligi ya Serie A kama inavyoitwa ligi ya Italia na pia ligi zingine za makombe mbalimbali ambazo timu za jimbo hili uwa zinashiriki ikiwemo timu kubwa ya jimbo inayoitwa Bahia FC basi eneo hili kwao ni eneo la raha ya burudani hii ya soka uwanja ukiwa unaitwa Fonte Nova Stadium, wao walipapita wakaacha barabara inayonyooka wakashuka na ingine inayoshuka chini kulia kilometa moja mbele wakafika eneo inakoanzia beach ya Lauro De Freitas lilipo jengo lililozungumziwa kuwa ni jengo la floor (losheni) tano lililotafutwa na kukodishwa lote kuanzia juu mpaka juu na watu waliopokea maagizo toka kwa ‘Kingpin’ Feca.
Gari zikaongozwa kuingia ndani ya geti kisha zikaingia barabara inayoingia ndani ya jengo kwa kwenda chini ambapo kuna maegesho ya uwanja mkubwa hapo chini ndipo wakapaki na wenyeji kuwaongoza wageni kushuka toka ndani ya magari na kuelekea ilipo lift yenye kazi kuwapandisha juu na kuwashusha chini katika ghorofa hili.
Mwisho wa sehemu ya mia na tatu (103)
Agent Kai na majasusi wenzake waandamizi wenye ubobezi katika kazi hizi za gizani wameingia Mexico kwa ajili ya kufanya kile walichoagizwa na mabosi zao.
Wakati wao wanaingia kinyemela ndani ya Mexico, mtu ambaye imesisitizwa apatikane iwe mzima au iwe maiti yake ameondoka Mexico na kuingia nchini Brazil katika jimbo la Bahia jiji la Salvador.
Nini kitatokea kati ya makundi haya yanayoasiminiana?
Kila hatua kwetu tunaenda na dua.. Timu Agent Kai najua mna hamu ya kujua nini kitajili wakati wakali hawa wanakwenda kufanya kazi isiyotabirika.
“.. Mlitafuta nyumba niliyosema?” Akauliza kigogo, swali lililoenda moja kwa moja kwa dreva anayeendesha gari kukata mitaa wakiwa katika barabara kuu itokayo eneo la uwanja wa ndege kuelekea katikati ya jiji.
“Ndiyo mkuu, tulitafuta nyumba kama ulivyoagiza tumepata eneo la Metropolitan karibu na beach ya jiji ya Lauro De Freitas ni jengo la ghorofa tano ni mtaa uliotulia sana sababu wakazi wa eneo hilo ni watu wenye uwezo kipesa hivyo hakuna kufuatiliana sana wote wawe wenye nyumba au wapangaji hakuna anayeweza kupamudu kama ni mtu wa hali ya chini hivyo kwa maelekezo yako uliyosema tuliona ndipo mahala sahihi kwako kukaa kwa amani ukililindwa kwa ulinzi wa serikali yenyewe bila wao wenyewe kujua kuwa wanakulinda mtu wa aina gani” Dreva akajibu bila ya kuwa anamuangalia anayemjibu akili yake ilikuwa ikifanya mambo mawili kwa wakati mmoja kuongea na kuendesha kwa umakini usiku huu ndani ya barabara hii kuu ya BR-101.
“Kazi nzuri sana Joao.. Sote tuliofika hapa Salvador tutafikia hapo na hata mke wangu baada ya mwezi mmoja nitataka aletwe hapa, nafikiri mwaka mmoja utatutosha kujipanga na kurudi kufany kinachoitwa jino kwa jino kwa wamarekani” Kigogo akaongea mkono wake wa kulia ukiwa umeachia kiganja chake kikamatie shavu lake ambapo tunaiita kujishika ‘tama’.
Msafara ulifika mzunguko wa Feira De Santana ukazunguka kisha kukamata barabara ya BR-116 ambapo walinyoosha moja kwa moja kilometa kadhaa wakafika eneo maarufu sana kwa wapenda mchezo wa soka wa jiji hili kwani ndipo wanapopata burudani ya ligi yao inayoitwa ligi ya Serie A kama inavyoitwa ligi ya Italia na pia ligi zingine za makombe mbalimbali ambazo timu za jimbo hili uwa zinashiriki ikiwemo timu kubwa ya jimbo inayoitwa Bahia FC basi eneo hili kwao ni eneo la raha ya burudani hii ya soka uwanja ukiwa unaitwa Fonte Nova Stadium, wao walipapita wakaacha barabara inayonyooka wakashuka na ingine inayoshuka chini kulia kilometa moja mbele wakafika eneo inakoanzia beach ya Lauro De Freitas lilipo jengo lililozungumziwa kuwa ni jengo la floor (losheni) tano lililotafutwa na kukodishwa lote kuanzia juu mpaka juu na watu waliopokea maagizo toka kwa ‘Kingpin’ Feca.
Gari zikaongozwa kuingia ndani ya geti kisha zikaingia barabara inayoingia ndani ya jengo kwa kwenda chini ambapo kuna maegesho ya uwanja mkubwa hapo chini ndipo wakapaki na wenyeji kuwaongoza wageni kushuka toka ndani ya magari na kuelekea ilipo lift yenye kazi kuwapandisha juu na kuwashusha chini katika ghorofa hili.
ENDELEA NA PIGO NONDO..!!
MIPANGO SAWA IV
CHILPANCINGO, GUERRERO – MEXICO
Holiday Inn Chilpancingo Hotel ni hoteli ya nyota 3.5 iliyopo mtaa wa Blvd Vicente mkabala na majengo ya makumbusho ya jimbo la Guerrero yanayoitwa La Avispa Museum Interactivo katika mji mkuu wa shughuli za kiserikali katika jimbo la Guerrero mji wa Chilpancingo, saa mbili na nusu asubuhi katika chumba namba 42 kulikuwa na kikao mjadala cha kujadili kazi iliyo mbele yao.
Kikao kilichowakutanisha watu ambao usiku uliopita wa saa saba usiku waliingia ndani ya nchi ya Mexico kwa njia ya kificho lakini si kama kificho ambacho wahusika wakuu kabisa wa mambo ya kiusalama wa nchi hawajui ujio wao wa kikazi la hashah! Mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Mexico alikuwa anajua na hata mkuu wa jeshi la anga la Mexico alikuwa anajua wakishirikishwa hili moja kwa moja na mkurugenzi wa taasisi kuu ya kijasusi ya NSA ya Marekani.
“Wakuu kabla ya yote acha nimpigie simu afisa wa ubalozi aliyepewa kazi ya kutusaidia jambo la nyumba ambayo tutakuwa huru kwa siku mbili tatu huku tukifanya mahala hapo kuwa makao yetu ya muda wakati tutakapokuwa katika operesheni hii!” Agent Kai aliongea huku akitafuta jina lililobeba namba ya simu anayotaka kuipiga kuongea na huyo afisa wa ubalozi wa Marekani nchini Mexico, wengine waliokuwa wakipata kahawa na vitafunwa kuondoa uchovu wa usingizi uliokuwa haujawaisha vichwani mwao na machoni mwao waliitikia tu.
“..Hallooo za asubuhi?” Agent Kai akaanza kwa salamu baada ya kusikia upande wa pili ushapokea simu.
“Safi mkuu.. Habari za huko?”
“Alhamdulillah huku tuko sawa kabisa.. Lete habari? Ondinye..!”
“Naam tumefanikiwa kupata nyumba mtaa wa Teofilo Olea Y Leyva 33 upo katikati ya mji lakini si mtaa wa watu wengi sana kwakuwa ni mtaa wa maofisi kadhaa kwa wingi kuliko makazi ya watu hivyo wapo wanaoishi hapo lakini si watu wa kusababisha kusiwe mtaa wenye utulivu unaohitajika kwa kazi zenu, upo eneo la Informacion De Sur ukimuuliza mtu wowote anayetoa huduma za taxi anakupeleka huko.. Kuna namba za mtu anayelinda nyumba hiyo nitakutumia mkifika mtawasiliana atawapokea na kuwakabidhi kila kitu kisha yeye ataondoka kuendelea na yake mpaka mtakapohitaji arudi mtanitaarifu nitamwambia atarudi pia kuna gari mbili tumetuma ziletwe mtakuta zishafika kaachiwa yeye au mnaweza mkafika mkakuta bado ila ziko njiani muda huu tunavyoonge kutokea Mexico City ni karibu tu hapo Chilpancingo city na hapa hivyo msihofu kwa kasi ya Jeep mapema tu zitafika”
“Kazi nzuri.. Mpe taarifa balozi tuna furaha kufanya kazi naye na kila tutakachokuwa tumefikia tutakupa taarifa umtaarifu na yeye.. Tuma hiyo namba tuelekee huko mara moja maana hapa tuliwaambia tunakodi vyumba kwa muda wa masaa kadhaa tu toka muda wa usiku wa alfajiri tuliofika mpaka mchana wa leo”
“Sawa nakutumia ukikata tu utakutana nayo…Mlinzi anaitwa Sergio Iago”
Neno ukikata tu utakutana na namba lilimfanya Agent Kai hata asiage akakata simu na kweli alipotizama ‘notification’ ya simu yake meseji kiboksi cha meseji kilionekana kikionyesha kuna meseji imeingia hivyo akaifungua akaisevu namba aliyotumia kwa jina atakalokumbuka mara zote, akainua uso wake kuwaangalia swahiba zake waliokuwa wakimsikiliza akiongea kwa simu na mtu ambaye aliwafahamisha kuwa ni afisa anayetokea ubalozi wao wa Marekani nchini Mexico.
“Norman amenitumia meseji wakati nikiwa nimelala nimeikuta ikiwa ni taarifa juu ya kikosi ambacho ameambiwa na Mheshimiwa Rais wao aunde kikosi kazi cha watu wanne wafanye upelelezi wao kujua waziri wao wa usalama aliyefutwa kazi na kukimbia nchini kwao Bwana Rafael Ceni anapatikana… Nimemjibu habari nzuri aunde kikosi icho na akitaka ushauri wangu au msaada wowote asisite kuniambia nitamsaidia kwa lolote lililo ndani ya uwezo wangu, sikutaka ajue juu ya sisi kuwepo hapa Mexico kwa kazi ambayo moja kwa moja itaingia na kumsaka huyo Ceni kwakuwa naamini muda huu atakuwa chini ya uangalizi wa karibu na Brigedia Feca..!” Baada ya kunywa funda kadhaa za kahawa akaongea hili Agent Kai kichwa chake kikizunguka huku na huko huku macho yake meupe majanja na makali akiyazungusha kwa kila mmoja aliyekuwa kakaa katika masofa yaliyopangwa eneo la katikati ya sebule kubwa kuizunguka meza moja ya kioo ya wastani katika apartment ya chumba namba 42.
“Samahani kiongozi! Norman ni nani?” Akauliza Agent Jade Brown mwanadada mrembo wa kizungu mrefu mwenye mwili ambao haujifichi kuwa yeye ni mtu wa mazoezi ya viungo kwa kiasi kisichojificha jasusi mbobezi komando wa US Navy Seals akiwa naye ni mmoja wa wanaounda kundi la kutumainiwa katika sekta za jeshi na kijasusi la ‘Special Activities Division’ (SAD) mwajiriwa wa shirika la kijasusi la CIA kama kwa wenzake wengine waliopo hapa.
“…Samahani na nyinyi pia.. Ni kwamba huyu ni kijana kiguatemala aliyetupokea katika kaoperesheni ka nchini mwao anaitwa Norman Cabrera muajiriwa wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Latin America la Organized Crime Of Latin America kwa kifupi OCLA na Rafael Ceni ni mmoja wa washirika wakuu wanaounda genge la The Red Jaguar ambaye alikuwa akisimamia shughuli za kiulinzi wa genge lao kwa kutokea ndani ya serikali ya nchi akitumia mamlaka yake ya kuaminiwa na Rais wa nchi kupewa uwaziri wa usalama wa nchi, vyombo vyote ulinzi na usalama kuwa chini yake…Mtu huyu alikimbia nchi ile pale tu mheshimiwa Rais alipokabidhiwa flashdisk yenye mambo kadhaa ya kuweza kumtia hatiani akakimbilia hapa Mexico hivyo kwa nihisivyo mimi nahisi alipo Feca muda huu basi yupo na Rafael Ceni”Akajibu Agent Kai Hamis.
“Vizuri… Je mnafikiri Feca bado yupo hapa hapa ndani ya Mexico au ametoka nje ya mipaka ya nchi ya mama yake?”Akauliza Agent Jade tena, swali likienda kwa watu wote waliopo pale kwa ujumla.
“Nionavyo mimi.. Kuna mawili hapo na ndipo inapoleta maana ya sisi kuitwa makachero, majasusi na watatua giza penginepo” Huyu alikuwa ni Detective Omari Chilamwena, jasusi mbobezi na mwandamizi mwenye umri ulio juu kidogo yaw engine wote huyu yeye ni mmarekani mweusi mwenye asili ya kutokea huko Kongo kwa wakongoman, umbo lake lilikuwa ni umbo mfanano kwa kiasi fulani Agent Kai na hata rangi zao za kawahia (chocolate) zilikuwa za kufanana.
“Sekretari wetu pale ikulu ya ofisi wa makamu wa Rais amenitumia ujumbe kuwa kuna jambo anafuatilia kisha muda si mrefu atatucheki kutupatia kitu ambacho kinaweza kuwa mwongozo kwetu, nafikiri tusijiumize sana vichwa vyetu kwa jambo ambalo naamini litakuwa jepesi muda si mrefu kwa maana namjua Lizy hivyo kuweni na subira kidogo” Agent Kai akaongea kisha akainuka toka kwenye sofa akaenda mezani na kunyanyua Ipad yake kisha akarudi nayo mahala alipokuwa amekaa.
Aliiwasha ilipokaa sawa kwa kazi akaunganisha na internet ya wireless ya simu yake kisha akasikilizia dakika mbili ikawa tayari kwa matumizi, alipoona iko sawa akapitia pitia akaunti zake za mitandao yake ya mawasiliano, wengine walikuwa kimya kusikiliza kiongozi wao ataongea nini? Ukimya haukuwa ukimya butu kati yao bali walikuwa wakipiga na kahawa zilizochanganywa na maziwa halisi.
“Lizy! Nakusikia! Lete habari mpendwa?” Wakati anaendelea kuangalia anaweza akapata nini habari za mtandaoni hasa vyombo vya habari vya Mexico kuhusu kutoroka kwa Feca na kulitelekeza kasri lake la ‘Nguvu Ya Siri Ya Kasri La Feca’ pamoja na mali zake nyingi katika majimbo kadhaa.
“…Nilidukua maongezi ya mwanamke mmoja mtangazaji wa Redio ya Periodical FM, namba yake niliipata wakati nafuatilia namba ya mke wa Feca, niliamua kuiweka kwenye orodha kwakuwa walikuwa wakiwasiliana sana katika mambo ya matangazo katika bidhaa za chuma zitokazo katika viwanda vyao.. Uliponipa taarifa kuwa Feca ametoroka katika kasri lake tena akiwazubaisha maaskari kwa wao kudaka msafara bandia… Nikaanza kwa kuitizama namba ya mke wa jamaa yetu mteja mkuu, namba haikuwa hewani, nikapiga namba za ofisi yake zilizopo Mexico City, muhudumu alishangaa sana kuwa hata wao hawampati na wana wasiwasi kwakuwa si kawaida ya boss wao kufanya hivyo katika mawasiliano yake.. Nikajiongeza kwa kui track namba ya mtangazaji niliyekwambia.. Muda mfupi tu akafanya mawasiliano na mwanamke ambaye alimtaja jina kuwa Frorence Zubizaleta huyu Frorence nahisi ni yule muhudumu niliyeongea naye kujifanya namuulizia boss wao mke wa Feca, Mrs. Millian Zabarelo.. Frorence akaeleza wasiwasi wake juu ya kutoonekana kwa boss wao na pia taarifa zinazosambaa juu ya mume wa boss wao, mtangazaji akamjibu asiwe na wasiwasi boss wao yuko mahala salama yeye na watoto wake na kuwa waliondoka jana jioni kwenda huko mahala salama watarudi mambo yatakapopoa… Sasa kaka ninaomba mumfuatilie huyu mtangazaji yeye ndiyo atakuwa mwanga wa kazi hii kwa kusema wapi mahala salama ni hayo bwana mkubwa” Maelezo marefu kidogo yalitoka na kwakuwa simu iliwekwa ‘loud speaker’ kila mmoja aliweza kusikia kinachozungumzwa na mwanadada Elizabeth Robert (Lizy Rob).
“Umesema mtangazaji ni wa redio hiyo uliyosema, je anaitwa nani?” Kai akauliza.
“..Ooooh… Jina lake alilosajili laini ya simu litakuwa ni jina ambalo pia linatumika kwenye kitambulisho chake cha utaifa na hata passport anaitwa Thea Mackenzie Talbaros, redio ipo mji huo mliopo sasa mtaa wa Cuauhtemoc 4”
“Sawa.. Yupo studio muda huu?”
“Nafikiri yupo sababu waliulizana juu ya hilo na akajibu yupo ofisini na ofisi yenyewe bila shaka ni studio za redio yao”
“Kazi nzuri Lizy kwa mara nyingine unakuwa mwangaza wangu.. Nauona mwanga wa ushindi mbele yetu”
“Usijali, tuko pamoja… Nahitaji sana urudi mapema kipenzi hivyo nitafanya kila ninaloweza kukusaidia katika hilo”
“Ahsante sana… Nitakujuza imekuwaje baada ya kukamilisha hili.. Nikutakie kazi njema hapo ofisini” Agent Kai alimalizia kwa maneno haya kisha upande wa Lizy ukakata simu.
“Kila mmoja nafikiri amesikia na sasa twatakiwa kulifanyia kazi jambo hili kwa haraka sana maana kama mjuavyo watangazaji kukaa kwenye vipindi uwa si kwa masaa mengi hivyo twatakiwa kumuwai mtu huyu… Akaletwe hapa mwanamke huyo” Agent Kai baada ya kuiweka simu yeka pembeni ya mtoto wa sofa akaongea mikono yake ikimsaidia katika ishara (hii uwa anamaanisha zaidi).
“..Sawa.. Kazi ndogo sana.. Nafikiri mimi na Rebecca tunaweza mfuata kama hamtajali..” Agent Hansen Blade akaongea ikiwa ni mara ya kwanza kuongea toka wakutane hapa katika kikao na kuwa amechangia mada baada ya maongezi ya kawaida kuhusu mambo ya kifungua kinywa walichokuwa wakikshambulia huku wanajadili na kupanga mikakati.
“Sawa.. Fanyeni hilo, muelekee huo mtaa kwa kazi!” Agent Kai kama kiongozi hakuwa na pingamizi juu ya ombi la rafiki yake.
***** ***** *****
PERIODICAL FM RADIO
CUAUHTEMOC 4, CHILPANCINGO – GUERRERO
Jengo la floor (losheni) mbili ndiyo jengo ambalo siyo refu kuliko majengo mengine katika mtaa huu wa Cuauhtemoc 4 wenye majengo mengi yanayotumika kama ofisi za taasisi na mashirika mbalimbali pamoja na makampuni mbalimbali, muda huu wa saa tatu na dakika arobaini au waweza sema kuwa ni saa nne kasoro dakika ishirini mapokezi ya watu wanaoingia ndani ya studio za redio hii ya Periodical FM walikuwepo mapokezini mwanamke aliyevaa kofia aina ya kapero rangi ya chungwa ikiwa na maandishi ‘MEXICO’ huku nyuma katika nywele zake nzuri aina ya blonde akifunga na kuacha kitu ambacho mimi uwa napendelea kuita ‘mkia mchicha’, koti la manyoya rangi nyeupe ndani yake akivaa fulana rangi ya chungwa ambayo ilikuwa aina andishi lolote akijihifadhi na suruali aina ya jeans rangi ya bluu ya kubana wakati mwanaume aliyeongozana naye alikuwa amevaa kofia aina ya pama koti la ngozi jeusi ndani yake akiwa na fulana ambayo haikuwa ikionekana kutokana na kuzibwa na jaketi lake pia naye pia alikuwa kavaa jeans rangi kama aliyovaa mwanamke aliye naye kasoro yeye haikuwa imebana ilikuwa ya kawaida na hata viatu vyao wote walivaa vinavyofanana aina buti aina ya buyu rangi nyesusi, mavazi haya wa Mexico wengi ndiyo mavazi wanayopenda kuvaa.
“Karibuni!” Dada aliye upande wa pili wa meza ya mapokezini aliwakaribisha punde alipoinua macho yake kuwatizama watu hawa ambao kwa akili ya haraka haraka kwake aliweza kuhisi watakuwa ni wapendanao.
“Ahsante sana dada… Habari yako?” Mwanaume akajibu ukaribisho waliopewa na kisha naye akamuuliza habari.
“Nzuri tu… Niwasaidie nini?”
“Naitwa Mr. Heritier Novat na huyu mwenzangu ni mke wangu anaitwa Mrs. Ericka Novat.. Sisi ni wamiliki wa kampuni inayojihusisha na kusafirisha watalii tunatokea nchini Canada ni wageni hapa Chilpancingo yaani ni mara yetu ya kwanza kufika hapa, tumefikia hotel ya Saint Angel iliyopo mtaa wa New Sec… Tumefika hapa tuna shida ya kuonana na mtangazaji anayeitwa Thea Mackenzie Talbaros” Jasusi Agent Hansen akajieleza kwa niaba ya mwenzake.
“Mna ahadi naye?”
“Hapana hatuna ahadi naye”
“Mkimuona mtajua?”
“… Mke wangu nafikiri yeye atakuwa anamju kwa picha.. Si ndiyo?” Agent Hansen akaongea kujibu kisha akageuza sura kumtizama Special Agent Rebecca.
“Ndiyo namjua kwa picha hivyo nikimuona nitamjua..!” Akajibu S.A Rebecca.
“Thea Mackenzie Talbaros a.k.a TMT… Yupo kwenye kipindi ambachi kinakaribia kuisha hivyo mwaweza kumsubiri kwenye masofa yale ya upande ule mnapouona mlango mkubwa wa mbao, baada ya kipindi kuisha atatokea hapo… Andikeni majina yenu kisha mtatia saini zenu”
“Ahsante..!!”
Wageni hawa wakajisogeza pembeni kidogo wakajaza majina yao ya uongo kazi iliyofanywa na Agent Hansen Blade, walipomaliza wakaenda kukaa kwenye sofa moja la watu wawili ambalo liko pembeni ya mlango wa kuingia zilipo studio za redio hii maarufu sana ndani ya manispaa ya jiji hili la Chilpancingo.
Dakika kumi na mbili tu za kusubiri zilipita mara mlango ukafunguliwa akatoka mwanadada ambaye mavazi yake yalikuwa ni suti ya kike ya rangi ya chanikiwiti au wengine wamezoea kuita kijani, kitambulisho kilichokuwa kinaning’inia kifuani mwake kamba yake ikiwa imezunguka kutokea shingoni iliweza kuwafanya watu waliogeuza sura zao kutizama mlangoni nani ametoka kutambua jina la mtu wanayemtafuta ndiyo huyu bila shaka, alipopiga hatua moja mbele akatokea mtu mwingine nyuma yake huyu akiwa ni mwanaume na wote wakawasogelea wageni hawa walipo.
Agent Hansen kwa pamoja na Special Agent Rebecca Smith walisimama walipokaribiwa na watu hawa waliotokea ndani.
“..Naitwa Thea Mackezie ni mtangazaji wa hapa redio Periodical FM.. Nimetumiwa meseji kuwa nina wageni wangu wananisubiri hapa… Na kwakuwa hakuna watu wengine walio hapa naamini ndiyo nyinyi?” Akauliza mwanadada huyu aliyevaa viatu virefu (skuna).
“Naam! Ndiyo sisi.. Naitwa. Heritier Novat na huyu mwenzangu ni mke wangu anaitwa Mrs. Ericka Novat.. Sisi ni wamiliki wa kampuni inayojihusisha na kusafirisha watalii tunatokea nchini Canada”
“Oooh! Karibuni sana.. Shida mliyonayo ni ya kikazi au binafsi yaani ya nje na kazi yangu?”
“Ni ya kibiashara.. Lakini kama itawezekana tunaweza tukaongea nje ya hapa… Kwa mfano katika migahawa au hata bar kama hautajali”
“Sawa inawezekana hilo kwakuwa muda huu nilikuwa naelekea mahala na mtangazaji mwenzangu ila tunaweza enda kuongea kwa pamoja kisha sisi tukaendelea na ratiba yetu”
“Sawa ni vizuri tu tukiwa wote na maongezi yetu naamini yatakuwa mafupi tu hivyo hatutawachelewesha kabisa..”
Walitoka baada ya kina Agent Hansen kumalizia kusaini kuwa wametoka na hata watangazaji hawa nao kujaza katika daftari linalowahusu kuwa nao wametoka katika kipindi chao wanaendelea na mambo mengine.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na nne (10$)
Kiongozi wa mipango Agent Kai anawaongoza wenzake alio nao katika timu moja nchini Mexico ikiwa ni timu iliyo na mabadiliko kiufundi ukiacha ile aliyokuwa nayo nchini Guatemala, mpango unaotiwa sukari na mwanadada kipenzi cha Agent Kai anayemuongoza kiteknolojia katika kazi yake kiasi ya kwamba kila mara akiwa yupo ofisi zao za nchini Marekani anazunguka kwenye kiti chake cha kuzunguka anatoa muongozo mzuri wa kumnufaisha Agent Kai.
Agent Hansen Blade akiwa ameongozana na mwanadada fundi kipenzi kingine cha Agent Kai wamefika redio pendwa ndani ya manispaa ya jiji la Chilpancingo mji mkuu wa jimbo la Guerrero, wanafanikiwa kutia ulimi mtamu mpaka kuwashawishi watangazaji wawili watoke nao kwenda nao mahala kwa mazungumzo.
Mazungumzo hayo yataenda kufanyika huko walipokubaliana?
ILIPOISHIA SEHEMU YA 104…!!
Dakika kumi na mbili tu za kusubiri zilipita mara mlango ukafunguliwa akatoka mwanadada ambaye mavazi yake yalikuwa ni suti ya kike ya rangi ya chanikiwiti au wengine wamezoea kuita kijani, kitambulisho kilichokuwa kinaning’inia kifuani mwake kamba yake ikiwa imezunguka kutokea shingoni iliweza kuwafanya watu waliogeuza sura zao kutizama mlangoni nani ametoka kutambua jina la mtu wanayemtafuta ndiyo huyu bila shaka, alipopiga hatua moja mbele akatokea mtu mwingine nyuma yake huyu akiwa ni mwanaume na wote wakawasogelea wageni hawa walipo.
Agent Hansen kwa pamoja na Special Agent Rebecca Smith walisimama walipokaribiwa na watu hawa waliotokea ndani.
“..Naitwa Thea Mackezie ni mtangazaji wa hapa redio Periodical FM.. Nimetumiwa meseji kuwa nina wageni wangu wananisubiri hapa… Na kwakuwa hakuna watu wengine walio hapa naamini ndiyo nyinyi?” Akauliza mwanadada huyu aliyevaa viatu virefu (skuna).
“Naam! Ndiyo sisi.. Naitwa. Heritier Novat na huyu mwenzangu ni mke wangu anaitwa Mrs. Ericka Novat.. Sisi ni wamiliki wa kampuni inayojihusisha na kusafirisha watalii tunatokea nchini Canada”
“Oooh! Karibuni sana.. Shida mliyonayo ni ya kikazi au binafsi yaani ya nje na kazi yangu?”
“Ni ya kibiashara.. Lakini kama itawezekana tunaweza tukaongea nje ya hapa… Kwa mfano katika migahawa au hata bar kama hautajali”
“Sawa inawezekana hilo kwakuwa muda huu nilikuwa naelekea mahala na mtangazaji mwenzangu ila tunaweza enda kuongea kwa pamoja kisha sisi tukaendelea na ratiba yetu”
“Sawa ni vizuri tu tukiwa wote na maongezi yetu naamini yatakuwa mafupi tu hivyo hatutawachelewesha kabisa..”
Walitoka baada ya kina Agent Hansen kumalizia kusaini kuwa wametoka na hata watangazaji hawa nao kujaza katika daftari linalowahusu kuwa nao wametoka katika kipindi chao wanaendelea na mambo mengine.
ENDELEA NA NONDO..!
MIPANGO SAWA V
CHILPANCINGO, GUERRERO – MEXICO
“Nafikiri mnaweza kutupa muda wenu wa angalau nusu saa tukaongea na kujuana zaidi kati yetu, naahidi hamtajutia muda wenu tutaulipia muda huo watangazaji wangu bora ndani ya Mexico.. Wapi? tutapata mgahawa mzuri tutakaoongea vizuri kwa utulivu zaidi..” Special Agent Rebecca akaongea kwa mara ya kwanza wakiwa wamesimama kwenye mistari ya pundamilia ya barabarani inayotumiwa na wapiti kwa miguu kuvuka kwenda wa pili wa barabara kwakuwa gari zilikuwa zikipita hivyo walisimama kusubiri zitakaposimama kwa amri ya mataa basi wao wavuke.
“Muda huu ni saa tano asubuhi.. Kama hamtajali twendeni mgahawa wa Liverpool uliopo mtaa wa Fraccionamiento Villas Vicente muda kama kunakuwa kumetulia sana na huduma zao ni nzuri sana za kimataifa” Akajibu Thea Mackezie huku akiyaangalia magari yanavyopita barabarani kana kwamba anayahesabu.
“Basi tuchukueni taxi!”
Wakakubaliana hili baada ya wanadada kuongea wanachoona ni sahihi kwa maongezi yaliyokuwa yakisikilizwa na wanaume walio pembeni yao.
Haikuwachukua dakika zaidi ya tatu ilitokea taxi isiyokuwa na abiria wakasimamisha na wote wakaingia ndani ya hiyo taxi, Thea akaelekeza wapelekwe wapi yeye akiwa kapanda siti ya mbele kwa dreva huku siti za nyuma wakikaa Agent Hansen, Special Agent Rebecca na jamaa ambaye ni mtangazaji mwenza na Thea.
Wakati safari yao ikiendelea Agent Hansen alikuwa akiwasiliana na Agent Kai walipo na wanaelekea wapi ambaye naye aliona ni bora watumie fursa hiyo kuwateka watangazaji hawa, wakaelekezana nini kifanyike na kilipofikiwa muafaka wakaacha kuchati.
Umbali wa kutoka eneo la Informacion De Sur hadi ulipo mgahawa wa Liverpool ni umbali ulio na mwendo wa dakika ishirini kwa gari lakini umbali wa kutoka mtaa wa Teofilo Olea Y Leyva 33hadi mtaa wa Fraccionamiento Villas Vicente ilipo Restaurante Liverpool kwakuwa ni maeneo yanayokaribiana ilikuwa ni dakika kumi kama mtu ataendesha kwa mwendo wa mdogo na kama ni kasi basi zinashuka zaidi ya hapo.
Detective Omar Chilamwena akiwa na Special Agent Fransis Simone Silla walifika kona ya kuingia kwenye mgahawa wa Liverpool kutokea barabara ya mtaa wakiwa na gari aina ya Jeep Wrangler-Colorado Springs toleo la mwaka 2016 rangi nyeusi lenye vioo vya giza madirishani (tinted) , wakaingia kwenye maegesho ambapo muendeshaji ambaye ni Detective Chilamwena alipofika kwenye eneo la maegesho haya akapindua kulielekeza kwa kuingilia.
Dakika moja ya utulivu akashuka Chilamwena na kurudisha mlango kisha akapiga hatua kuingia eneo la mapokezi ya mgahawa husika ambao asubuhi hii kulikuwa na watu wachache wa kuhesabika na wasifike watano katika meza ambazo ni mbalimbali mmoja kule kwenye kona peke yake wengine bibi na bwana meza ya karibu na kaunta ya huduma kwa wateja hivyo Chilamwena jasusi huyu mbobezi na mwanadamizi aliyebobea katika ujanja wa mambo ya kijasusi na vita zake za kuwindana mwenye asili ya Afrika ikisemekana mazazi ya wazazi wake ni mchanganyiko mama mkenya na baba mkongomani wa ile Kongo ya Brazaville si Kinshansa akiwa kavaa yake aina ya kapero rangi ya kijani sehemu za mzunguko juu kukiwa na rangi nyeusi, machoni miwani ya kazi za kazi ambayo sina haja ya kuielezea kazi yake sababu nafahamu msomaji wangu unafahamu kazi ya miwani hizi, alipiga hatua fupi fupi kwenda kaunta.
“Habari yako?!”Akamsalimu kwa kihispania (kilatino) muhudumu mwanadada aliye nyuma kaunta akipekua pekua daftari kubwa kuangalia yale ambayo anahusiana nayo kwa wakati huo sisi hatuna habari nayo.
“Salama kaka.. Karibu!!” Akajibu mwanadada wa kizungu mwenye nywele nyeusi.
“Naweza kupata kahawa chungu vikombe viwili vya take away?”
“Utapata kaka.. Lipia kwa aina yoyote ya malipo..!”
“Niko na cash haina shida”
Detective Chilamwena akalipia na kupewa vikombe vya kahawa vya ‘take away’ vinavyopendeza alipogeuka kuanza kutoka meseji ikaingia kwenye simu yake akaamisha kikombe cha mkono wa kulia na kuvikamatisha kwa pamoja katika kiganja cha mkono wa kushoto kisha akatoa simu mfukoni akatoa ‘lock’ na kufungua meseji akasoma haraka haraka ilikuwa ni ujumbe toka kwa kina Agent Hansen akauelewa akakaza mwendo kwenda maegeshoni.
“Wanakaribia kufika… Anasema Hansen kuwa watamuomba dreva aishie barabarani hivyo wataingia kwa miguu huku ndipo tutatokea na kuwachukua wote kama tukio la kuhalifu la kiutekaji..!” Aliongea haraka Detective Chilamwena punde alipoingia ndani ya gari akimwambia mshirika wake Silla.
Sekunde thelathini toka amalize kuongea vile ikiwa hata hajajibiwa gari inayoonekana ni taxi ilisimama kwa barabarani karibu na geti wazi la mgahawa kisha milango ya gari pande zote ikafunguka ukiacha mlango wa kwa dreva tu ndiyo hakufunguka, pande zote wakashuka watu wakitimiza idadi ya watu wanne wote wazungu wakioneakana ni wenye furaha kubwa sana kwa tabasamu zilizokuwa kwenye nyuso zao.
Waliagana na dreva taxi kwa mwendo wa aina moja wakaongozana kuja eneo la barabara inayojia mgahawani.
Paapu! Milango ya gari ya kifahari aina ya Jeep Wrangler-Colorado Springs ilifunguka pande zote mbili wakatoka wanaume wakiwa wamevaa ‘mask soksi’ rangi ya udongo wakiacha eneo la machoni na la mdomo tu wote wakakimbia kusimama mbele ya watu wanne wanaokuja mgahawani.
“Mikono juu woteee!!” Detective Chilamwena akapaza sauti bastola aliyoikama kwa mikono yake yote miwili ikiwaelekea watu ambao wawili ni washirika wenzao.
“Hakuna mtu kufanya tofauti na maelekezo yetu..!”S.A Silla akaongea na yeye kwa kufoka akawasogelea akiweka bastola yake nyuma ya kiuno eneo la mkanda wa suruali unapopita msamba wa uti wa mgongo akashusha fulana alilovaa, mikononi alikuwa na pingu za kijasusi za mikanda migumu ya plastiki akapita kwa kila mmoja akikusanya kwa nyuma mikono yao kisha anawafunga alipowamaliza kuwafunga akatoa vitambaa vyeusi akawafunga machoni akipita tena kwa mmoja mmoja alipomaliza akamsukuma kwa nguvu kwenda mbele Agent Hansen.
“Ingieni ndani ya gari upesi” Akasema Detective Chilamwena mkono wake wa kulia ukiwa umakamata bastola na wa kushoto unafungua mlango wa uapnde wa siti za nyuma za abiria katika gari yao.
Agent Hansen akijifanya kuogopa kupita maelezo alikuwa wa kwanza kuingia ndani ya gari mbio kama kafunga mota miguuni jinsi alivyorukia ndani ya gari, Special Agent Rebecca akajifanya kuacha watangulie Thea na mshirika mwenzake mtangazaji mwenzake, walipoingia ndani ya gari ndipo yeye Rebecca akafuata hii ikiwa mbinu bila watekwaji kujua kuwa wamewekwa mtu kati, Jeep ina upana wa kutosha watu hawa wote wanne kubanana na kutosha katika siti hasa ukizingatia wote walikuwa na maumbo yasiyokera kwa unene.
Watekaji wakaingia siti zao za mbele gari kwakuwa haikuwa imezimwa iliachwa sailensa muendeshaji Detective Chilamwena aliingiza gia na kuliondoa kasi mashuhuda wachache waliokuwa eneo hili la mgahawa muda huu walibaki vinywa wazi wakiachwa na maswali mengi ya kujiuliza na kuulizana juu ya tukio walilolishuhudia likitokea kwa kasi.
Dreva aliondoka akipangua gia gari mpaka gari lilipokamata lami tairi za gari zikalalamika mlio wake wa kuvutia kwa watu wa kazi za kazi, Silla akiwa siti ya mbele upande wa abiria alikuwa amewageukia mateka wao wawili wa ukweli na wawili feki akiwa kawaelekeza mdomo wa bastola iliyokamatwa kwa mkono mmoja macho yake yakizunguka kwa zamu kuwaangalia mmoja mmoja sura yake kwa asilimia themanini ikiwa imefichwa.
Mwendo kasi wa Jeep iliwachukua dakika tano toka maegesho ya Reataurante Liverpool mpaka mtaa wa Fraccionamiento Villas Vicente ilipo nyumba ambayo ubalozi wa Marekani nchini Mexico uliwatafutia majasusi hawa wa kikosi kidogo cha kazi maalumu kilichofika mji wa Chilpancingo, gari ikaingizwa kwa kasi kwenye uwa wa ukuta unaozunguka nyumba wakiwa wamefunguliwa na mwanadada wa kizungu Agent Jade Brown.
Mateka wakashushwa kwa pamoja chini ya ulinzi mkali huku ambao si mateka wakiendelea kuwa kwenye maigizo yao yasiyo na maumivu, wote wakaingizwa ndani ya nyumba machoni mwao wakiwa wamefungwa vitambaa vyeusi vilevile hivyo wakati wanatembea walikuwa wakitembea kwa kuongozwa njia.
Wakaongozwa mpaka mahala ambapo wao hawakuwa wanajua wapi lakini wenyeji walikuwa wamewaleta sebuleni ambako tayari Agent Kai alikuwa akiwasubiri kwa hamu.
“Watoeni vitambaa vyeusi machoni mwao, wameshafika walipotakiwa kufika..!” Akaongea Agent Kai akiwa bado amekaa kwenye sofa la mtu mmoja lililo kwenye kona ya sebule kubwa yenye mapana yake na marefu kama ukumbi wa disko, nyumba hii ilikuwa ni nyumba kubwa na ya kisasa ikijengwa kwa mfanano wa ramani wa nyumba nyingi za kisasa za nchini Mexico, ombi la kuwatoa vitambaa vyeusi vilivyofungwa machoni mwa watu hawa wanne ikatekelezwa haraka kwa pamoja ikifanywa na Jade pamoja naye Silla.
“Karibuni sana ndugu zangu… Mtatusamehe kwa kuwachukua kinguvu kuwaleta mahala hapa mkiwa hamjui ni nini hasa kimewaleta... Chila kwanini wanne?” Aliongea tena Agent Kai uso wake ukiwa ndani ya tabasamu ambalo kwa hawa wageni wawili wasiomjua lilikuwa tabasamu baya la kinafiki huku wale watekwaji feki wakiliona tabsamu la kawaida.
“…Ni kweli ila sidhani kama kitaharibika kitu, tusiowahitaji hapa wanaweza kupelekwa chumba kingine wakawasubiri wenzao kama hawataleta jeuri katika maswali na majibu” Akajibu Detective Chilamwena kuongezea na ufafanuzi mdogo akiwaangalia kwa zamu kila mmoja aliye pale sebuleni.
“Sawa.. Simjui yupi ni yupi.. Thea ni nani?” Akaongea na kuuliza Agent Kai, swali ambalo ilionekana ni nani anatakiwa kujibu kwakuwa alikuwa akiangaliwa na lilikuwa ni swali la kinafiki ukweli katika ile hali ya kuwapoteza maboya.
“Thea ni huyu na hawa wengine ni rafiki zake!” Akajibu Detective Chilamwena.
“..Mtatusamehe rafiki zetu.. Sisi hatuna shida na nyie kabisa, sisi ni wafanyakazi usalama wa taifa hili Mexico, tuko hapa kikazi tunatokea jiji la Mexico hivyo msituogope kabisa.. Jade chukua hawa watatu wapeleke kwenye chumba cha kupumzikia wa aina yao” Aliomba radhi Agent Kai ‘TSC’ kisha akamuomba mwanadada Jade awapeleke mateka wao wa bandia wawili na mmoja mtangazaji wa kiume wa redio Periodical FM, wakaondoka pale kwenda vilipo vyumba wakimuacha mwenzao
“..Hakuna haja yaw ewe kukunja sura yako nzuri na kuifanya iwe makunjo kunjo bila kujua hasa ni nini unatakiwa kufanya hapa, kwangu mimi na hata kwa wenzangu wote tulio hapa uwa tunaweka mbele ustaarabu wa kibinadamu kuliko chochote… Je kuna asiyependa amani? Hapana hakuna naamini pia kwako naamini uwa ndiyo kitu muhimu sana kwa kuongea kirafiki baina ya mtaka kujua na njia ya kujua ambapo njia ya kujua iko kwako… Karibu ukae kwenye moja ya sofa kati ya masofa hayo yaliyo nyuma yako.. “’TSC’ akaongea tena na taratibu Thea akarudi nyuma na kukaa kwenye sofa moja la kukaa watu wawili.
“..Mimi ni mtangazaji wa redio kubwa na sifika ndani ya mji wa Chilpancingo mji mkuu wa jimbo letu pendwa la serikali ya jimbo la Guerrero lililo chini ya mamlaka kuu ya serikali ya nchi yetu takatifu ya Mexico, napatwa na mshangao kwanini mimi na wenzangu tutekwe na kuletwa hapa mahala katika nyumba hii bila matakwa yetu kaka yangu… Naweza kujua kwanini niko hapa? Na kwanini ni mimi na wenzangu?” Mwanadada Thea alipokaa akapata ujasiri wa kuuliza maswali kadhaa kwa TSC.
“Huko vizuri.. Nimekupenda bibie.. Naitwa Detective Halland Elman kutoka shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Drug trafficking Organization kwa kifupi tunaita DTO lenye makao makuu yake jijini Mexico City na hawa wenzangu wote unaowaona hapa ni maafisa wa vyeo tofauti tofauti ndani ya DTO, tumewaleteni hapa kwa njia isiyo halali lakini si kwa lengo baya na muhusika mkuu wa nyie kuja hapa kwa njia hiyo isiyo halali ni wewe mwanadada mtangazaji maarufu wa redio Periodical FM Stereo iliyopo hapa mji mkuu wa jimbo la Guerrero na si bahati mbaya tuna hakika na tulilofanya sababu uwa hatukurupuki kwenye kazi zetu pale tunapohitaji kujua jambo kwa mtu uwa hatumuonei kwa hakika anakuwa yumo ndani ya tunalolitaka iwe kwa yeye mwenyewe binafsi kujua anachofanya au kutokujua kwa bahati mbaya akiwa kajihusisha tu” Agent Kai akafafanua macho yake yakia yanaangaliana kwa umakini na mwanadada Thea.
“Mh!..Mimi?! DTO? Kwanini jamani? Mbona mimi sijihusishi na mambo yanayoweza kutiriwa mashaka na shirika la kupambana na madawa ya kulevya, tafadhali naomba uniweke wazi nahusikaje? Mmenistusha sana kwa kweli” Mwanadada Thea alionyesha mshtuko wa dhahiri machoni mwa majasusi walio hapa sebuleni.
“Usishtuke bibie, naam utajua kila kitu acha kwanza tukufungue pingu mikono yako iwe huru… Jade! Naomba nisaidie kumfungua pingu kwenye mikono yake huyu mwanadada si mhalifu huyu ni raia mwenzetu mwema kabisa” Maneno ya kulainisha toka kwenye kinywa cha TSC uwa mara zote yana kipaumbele katika kazi yake ni dhahiri aliweka imani iliyosababisha kukunjua uso wa hasira wa mwanadada mtangazaji Thea ukasawajika na kuwa uso laini wa kirembo sasa akimtizama Agent Kai wakati Agent Jade anamfungua pingu plastiki kwenye mikono yake iliyokuwa imekusanywa kwa pamoja kwa mgongoni mwake.
“Sasa naamini tunaweza kuelewana uzuri Miss Thea MackenzieTalbaros a.k.a TMT.. Unataka kujua kwanini DTO? Sisi kama sisi kama ujuavyo aua kama haujui uwa hatufanyi kazi zetu kwa kumkomoa mtu sababu tunajua ni kosa kuu kufanya mambo kwa kumkomoa mtu hasa sisi sote wananchi wa Mexico, taifa letu ni taifa la upendo lakini kuna watu wasiopenda mshikamano wetu kwa kufanya yale wanayojisikia wa… Kwanini umeingia kwenye hili? Ni kwakuwa una urafiki na mtu ambaye tuna mashaka naye ya moja kwa moja kuwa ni mmoja wa viranja wa genge la ulanguzi wa biashara za dawa za kulevya… Genge kubwa kabisa ndani ya ukanda huu wa mabara mawili ya Amerika.. Hapana usiongee kitu, ach animalize” Aliongea TSC akakatizia kwa kuomba udhuru mwanadada Thea asiongee kitu kwakuwa alitaka kuongea kitu kwa kumakatizia yeye kisha akaendelea baada ya kuona mwanadada ametulia kusikiliza “The Red Jaguar kwa kifupi chake wanajiita TRJ hili ni genge ambalo si kwa watu kama sisi tu tulio DTO tunaojua habari zake bali hata nyie watangazaji na waandishi wa habari kifupi media zote za Mexico mnalijua jina la genge hili kinagaubaga… Kiongozi mkuu wa genge hili anaitwa bwana mkubwa Fernandes Carlos Codrado kwa kifupi wenyewe wanamuita Feca ni Brigedia mfukuzwa wa jeshi la wananchi la nchi yetu hii takatifu… Natambua huna uwezo wa kutokuwa hujawai lisikia jina hili maarufu hapa Mexico, niko sahihi?” Maelezo marefu ya TSC yaliitimishwa na swali stukiza kwa Thea.
“Siwezi kataa kuhusu kulijua jina hilo maarufu hasa kwa siku mbili tatu hizi lina vuma zaidi ya ilivyo siku nyingine zilizopita si kwenye vyombo vya dola tu bali mpaka kwenye media zetu.. Namjua Feca na pia nimeanza kuhisi kwanini DTO mmenileta hapa kwa mahojiano na mimi” Thea akajibu na kwa haraka aliweza hisi kwanini ameletwa hapa.
“Vizuri! Unaweza tuambia umehisi nini?”
“..Urafiki… Urafiki wangu baina yangu miye na mke wa Feca bibi Millian Zabarelo ndiyo uliosababisha niwepo hapa” Akajibu kwa usahihi Thea.
“..Huko sahihi.. Tunataka kujua huyu rafiki yako yuko wapi kwa sasa, tukijua hatutakuwa na budi ya kukuacha uendelee na mambo yako ingawa sikufichi tutakuwa tunafuatilia kila unachofanya mpaka tutakapowakamata mke na mume hawa.. Tusaidie hili!” Agent Kai akaongea.
“Nimejuana na Madam Millian Feca kwa ajili ya matangazo ya kampuni yake binafsi na ya familia yake yaani mali za kwa pamoja na mume wake kwakuwa Madam ndiyo mtendaji mkuu wa viwanda vyote vya chuma vya mumewe hivyo kwa hapa Guerrero mimi ndiyo mtangazaji niliyekuwa nikiandaa matangazo yote ya kuhusu kampuni zao zilizo kihalali alinipenda sana kwakuwa nilikuwa mbunifu toka tunaanza nabuni matangazo yote yanayotumika katika maredio yote maarufu katika nchi hii na hata nchi jirani na ndiyo maana na nyie mmeweza kujua hilo mkaamua kunifuata nafikiri ni kwa sababu hii… Juzi aliniaga akiwa tayari yuko kwenye mpaka wa Brazil akinipigia kwenye simu ya ofisini kwetu na yeye akitumia ya bandani na leo asubuhi nilipofika tu alinipigia kuna maelekezo alikuwa ananipa juu ya nyumba yake ya hapa Chilpancingo ambayo hata mumewe haijui leo amenipigia kwa kutumia simu ya vibandani akiwa jimbo la Bahia nchini Brazil, nafikiri yuko mji wa mkuu wa jimbo la Bahia linaloitwa Salvador” Maelezo marefu yaliwafanya majasusi walioko hapa kuangaliana kwa zamu huku wakitingisha vichwa vyao na kiongozi wa kikosi Agent Kai alikuwa akijikuna sikio maneno yanavyoingia kama msumari unaogongelewa kwenye mbao.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na tano (105)
Mambo! Mambo! Mambo kunoga taratibu!
Kazi ya kupekua na kuchunguza ikiwa inafanywa na watu walio na uzoefu katika kazi uwa haiwaii ugumu sana kana kwamba ni kazi rahisi lakini uwa si rahisi sana kama uzaniavyo uwa inahitajika uchimbaji haswa na kutumia akili hata kama kunakuwa na hali ya kulazimisha hii kufanikisha.
Kikosi kazi cha timu ya kijasusi kimefanikiwa kumpata mwanadada Thea Mackenzie Talbaros mtangazaji wa redio Periodical FM Stereo ambaye kwa mujibu wa maelekezo ya awali ya Lizy Roby ni kuwa atakuwa msaada wa kazi mkubwa sana, imekuwa vile alivyohisi Lizy ni kweli mwanadada huyu ameweza kuwajulisha majasusi hawa kuwa ni wapi alipo Madam Millian Zabarelo Fernandes mke wa boss na kingpin wa genge la TRJ.
Je? itakuwaje baada ya kujua wapi alipo mke wa Feca!
“Sasa naamini tunaweza kuelewana uzuri Miss Thea MackenzieTalbaros a.k.a TMT.. Unataka kujua kwanini DTO? Sisi kama sisi kama ujuavyo aua kama haujui uwa hatufanyi kazi zetu kwa kumkomoa mtu sababu tunajua ni kosa kuu kufanya mambo kwa kumkomoa mtu hasa sisi sote wananchi wa Mexico, taifa letu ni taifa la upendo lakini kuna watu wasiopenda mshikamano wetu kwa kufanya yale wanayojisikia wa… Kwanini umeingia kwenye hili? Ni kwakuwa una urafiki na mtu ambaye tuna mashaka naye ya moja kwa moja kuwa ni mmoja wa viranja wa genge la ulanguzi wa biashara za dawa za kulevya… Genge kubwa kabisa ndani ya ukanda huu wa mabara mawili ya Amerika.. Hapana usiongee kitu, ach animalize” Aliongea TSC akakatizia kwa kuomba udhuru mwanadada Thea asiongee kitu kwakuwa alitaka kuongea kitu kwa kumakatizia yeye kisha akaendelea baada ya kuona mwanadada ametulia kusikiliza “The Red Jaguar kwa kifupi chake wanajiita TRJ hili ni genge ambalo si kwa watu kama sisi tu tulio DTO tunaojua habari zake bali hata nyie watangazaji na waandishi wa habari kifupi media zote za Mexico mnalijua jina la genge hili kinagaubaga… Kiongozi mkuu wa genge hili anaitwa bwana mkubwa Fernandes Carlos Codrado kwa kifupi wenyewe wanamuita Feca ni Brigedia mfukuzwa wa jeshi la wananchi la nchi yetu hii takatifu… Natambua huna uwezo wa kutokuwa hujawai lisikia jina hili maarufu hapa Mexico, niko sahihi?” Maelezo marefu ya TSC yaliitimishwa na swali stukiza kwa Thea.
“Siwezi kataa kuhusu kulijua jina hilo maarufu hasa kwa siku mbili tatu hizi lina vuma zaidi ya ilivyo siku nyingine zilizopita si kwenye vyombo vya dola tu bali mpaka kwenye media zetu.. Namjua Feca na pia nimeanza kuhisi kwanini DTO mmenileta hapa kwa mahojiano na mimi” Thea akajibu na kwa haraka aliweza hisi kwanini ameletwa hapa.
“Vizuri! Unaweza tuambia umehisi nini?”
“..Urafiki… Urafiki wangu baina yangu miye na mke wa Feca bibi Millian Zabarelo ndiyo uliosababisha niwepo hapa” Akajibu kwa usahihi Thea.
“..Huko sahihi.. Tunataka kujua huyu rafiki yako yuko wapi kwa sasa, tukijua hatutakuwa na budi ya kukuacha uendelee na mambo yako ingawa sikufichi tutakuwa tunafuatilia kila unachofanya mpaka tutakapowakamata mke na mume hawa.. Tusaidie hili!” Agent Kai akaongea.
“Nimejuana na Madam Millian Feca kwa ajili ya matangazo ya kampuni yake binafsi na ya familia yake yaani mali za kwa pamoja na mume wake kwakuwa Madam ndiyo mtendaji mkuu wa viwanda vyote vya chuma vya mumewe hivyo kwa hapa Guerrero mimi ndiyo mtangazaji niliyekuwa nikiandaa matangazo yote ya kuhusu kampuni zao zilizo kihalali alinipenda sana kwakuwa nilikuwa mbunifu toka tunaanza nabuni matangazo yote yanayotumika katika maredio yote maarufu katika nchi hii na hata nchi jirani na ndiyo maana na nyie mmeweza kujua hilo mkaamua kunifuata nafikiri ni kwa sababu hii… Juzi aliniaga akiwa tayari yuko kwenye mpaka wa Brazil akinipigia kwenye simu ya ofisini kwetu na yeye akitumia ya bandani na leo asubuhi nilipofika tu alinipigia kuna maelekezo alikuwa ananipa juu ya nyumba yake ya hapa Chilpancingo ambayo hata mumewe haijui leo amenipigia kwa kutumia simu ya vibandani akiwa jimbo la Bahia nchini Brazil, nafikiri yuko mji wa mkuu wa jimbo la Bahia linaloitwa Salvador” Maelezo marefu yaliwafanya majasusi walioko hapa kuangaliana kwa zamu huku wakitingisha vichwa vyao na kiongozi wa kikosi Agent Kai alikuwa akijikuna sikio maneno yanavyoingia kama msumari unaogongelewa kwenye mbao.
ENDELEA NA MAPIGO..!!
FUNGA KAZI I
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL I
Faro Inn Hotel Salvador ni hotel ya nyota nne iliyopo manispaa ya mji wa Salvador, mji mkuu na mji wa shughuli kuu za serikali ya jimbo la Bahia moja ya jimbo kubwa kati ya majimbo thelathini na mbili yanayounda nchi ya Brazil ni hoteli ambayo kufikiwa na mgeni wa hali ya kawaida ni ngumu kutokana na ghrama zake kuwa si zile kuweza kumudu mtu wa hali hiyo ikiwa na huduma nyingi za muhimu ikiwemo za ziada kama vile gym na burudani mbalimbali ndogo ndogo inapatikana kilometa mbili toka katikati ya mji zilipo shopping mall na maofisi makubwa ya kiserikali (downtown).
Muda wa saa tatu usiku Agent Kai alikuwa katika chumba namba 32 anavua nguo aina ya suti rangi ya kijivu wenye weusi kwa mbali alizovaa, usiku huu wa saa tatu uliwakuta yeye na mshirika wake wa karibu mwanadada mrembo Special Agent Rebecca Smith pamoja naye swahiba wake wa siku nyingi jasusi mwenzao Agent Hansen Nicholaus Blade kuwa katika mji huu wakiletwa kwa usafiri wa ndege ya kukodishwa waliyoikodisha katika kutokea uwanja wa ndege mdogo wa mji wa Chilpancingo unaoitwa Chilpancingo Airport ambapo iliwaleta mpaka uwanja wa ndege wa kimataifa wa jimbo la Bahia ambao ni moja ya viwanja bora katika nchi ya Brazil uitwao Deputado Luis Eduardo Magalhae International Airport ulioko kilometa 28 toka katikati ya mji wa Salvador mji mkuu na mji shughuli kuu za kiserikali katika jimbo la kiutawala la Bahia.
Makubaliano yao kama timu inayoongozwa na Agent Kai mwenyewe baada ya kuwa wamepewa taarifa waliyoiamini kwa asilimia 95 bila ukakasi wowote kutoka kwa mwanadada mtangazaji wa redio Periodical FM Stereo na wao kujiridhisha iliwafanya haraka wakodi ndege wao watatu wakati watatu waliobaki kati yao wali book tiketi ya ndege ya abiria wote iliyowapeleka Sao Paolo mji mkuu wa shughuli kuu za serikali kuu ya nchi ya Brazil, wangeweza na wao kupanda ndege iliyokodiwa na wenzao lakini kiufundi waliona si vizuri kusafiri kwenye ndege moja hivyo wakagawana vyombo vya anga vya usafiri kwa mtindo huo ambao itawafanya waliopitia Sao Paolo kufika kesho.
Agent Kai ‘TSC’ alipanga katika hali anayohitaji vitu vyake kisha akaenda maliwato kufanya mambo mengine ya kutoa taka ngumu na ndogo kisha kujimwagia maji kuondoa uchovu wa safari, baada ya kumaliza kila jambo ambalo lilikuwa na umuhimu akatulia kula chakula alichokuwa ameagiza toka anafika katika mapokezi ya hotel kilikuja kabla hata hajaenda maliwatoni.
Alifakamia chakula inavyotakiwa huku anapitia pitia mitandao ya kijamii katika simu yake, wakati vijiko vya kukombeleza sahani vinafanya mapitio kana kwamba anaideki sahani simu yake ikaita, alipoitizama kwenye kioo alikuwa ni mshirika wake mwanadada mtamu wa kizungu mwenye utamu wake na matashititi yake ya pozi za kizungu Special Agent Rebecca.
“.. Halloo Boss!” Upande wa mpigaji uliongea haraka baada ya kujulishwa na sikio lake mpigiwa kapokea.
“Rebecca! Sema..!”
“Shwari.. Nimechukua chumba hotel ya Mansao Villa Verde, dreva wa taxi alinileta huku baada ya kumuomba anichagulie hotel karibu na beach kama ulivyonielekeza ni pazuri na pamechangamka kama tulivyotaka eneo hili ni kusini mwa wilaya ya mji huu wa Salvador mtaa unaitwa Porto Da Barra na eneo hili lote linaitwa eneo la Barra… Vipi wewe maeneo?”
“Farro Inn Hotel ni katikati ya mji..! kuna jambo nataka kuweka sawa kisha nipumzike, Hansen amenitumia meseji amepata hotel mahala ambapo ni karibu na kibanda cha simu ambacho mteja wetu aliongea mara mbili kwa simu ya pale kuongea na Tam.. Naamini asubuhi tutaanza upelelezi wetu wa kina juu ya yote hivyo pumzika sasa mpendwa wangu”
“Ahsante boss.. Ila sitapumzika muda huu nahitaji nioge kisha niende bar kunusa nusa kidogo”
“Saa nne kasoro hii ni kweli weka pua pengine kutakuwa na mnuso usisahau kujipigilia bidhaa ya kujifananisha na mionekano ile tunayohitaji..”
“Usijali.. Upande wa pili wa hii Verde kuna club ya Bahia Late Club nitaanza huko kisha nitamalizia glocery ya hotel hii”
“Kazi njema dia.. Kuwa makini sana na usisite kunijulisha lolote lile utakaloona litatusaidia” Alimalizia hili Agent Kai kisha akakata simu baada ya ukimya wa sekunde tatu upande wa Rebecca.
Simu haikurudi mezani bali yeye aliondoka eneo la karibu na meza akaenda kukaa kwenye sofa akatafuta namba za Lizy Rob alipozipata akapiga, simu ikaanza kuita.
“Mpenzi wangu!” Upande wa pili sauti ya kike ikasikika katika lugha yao zoeleka.
“Tumeshaingia Salvador.. Vipi kuna lolote?”
“Lipo.. Hivi uliwezaje kumuamini yule mtangazaji?”
“Juu ya nini?”
“Kumuachia yeye na mwenzake wawe huru..!”
“Si muhalifu hivyo sikuona sababu ya kutoamini kuwa hawezi vunja mkataba wangu na yeye ni hilo tu kipenzi, kwani kuna tatizo umelibaini?”
“Ndiyo.. Ungechelewa dakika mbili tu kunipigia simu basi mimi ningekupigia kukwambia… Nafikiri mkataba wenu ulikuwa asiongee lolote kwenye simu na anayemuita madam boss lakini ukajisahaulisha kana kwamba lena kuwa hawezi wasilisha ujumbe kwa njia ingine basi umekosea sababu ametumia mtandao wa jamii wa facebook kuwasiliana na mtu anayeitwa Laza Blocks, amefanya mawasiliano haya bila kujua kuwa mimi nime hack mawasiliano yake ya akaunti zake zote za mitandao ya kijamii amabazo amejisajili kwa kutumia email iliyomo kwenye simu anayoitumia”
“Laza Blocks umemchunguza ni nani?”
“Laza Blocks katika akaunti yake ya facebook amejisajili kwa jina hilo lakini nilipoingia kutizama zaidi kitaalamu nimefika kumfananisha na mtu anayeitwa Fred De Luis Penambucano huyu ni afisa wa polisi wa cheo cha Inspekta katika kituo cha polisi cha Salvador..!
“Mh!... Lakini umenifahamu kwanini nilimuacha huru?”
“Hapana sijafahamu mantiki yako ni nini haswa!”
“Jasusi mbobezi wa kiwango changu siwezi kumuacha mtu bila sababu… Je ningemdhibiti tu ungejuaje kama kuna huyo Laza Blocks katika mtandao wa facebook ambaye pua inanusa kuwa ni Inspekta wa jeshi la polisi hapa Salvador… Nipigie makofi kisha meza mate sema kimoyomoyo kifuani mwako kuwa mpenzi wako wa kutoka nchi ya ajabu ni noma.. Endelea, niambie ujumbe unasemaje?”
“Walianza salamu wakitumia kireno katika kuandika kwao ndipo nilihisi kitu kwakuwa uwa anachati lakini uwa sitilii maanani kama alivyotumia chati kwa lugha ya kireno, nikavutika kufuatilia majibizano yao huku naangalia anayechati naye yuko wapi? Nikastuka tena kuona mjibu chati yuko Salvador hapo umakini ukaongezeka akafunguka mwanamke kuwa kuna watu wapatao watano wa DTO walimshikilia na kumuhoji juu ya Madam M, akaendela kusema yeye alisema ukweli ajuavyo… Jamaa alistuka na kumuhoji wako wapi na wakoje mdada akaeleza wewe ulivyo, akaeleza alivyo Agent Hansen Blade na Rebecca pia alivyo hapa pamenistua sana ikiwa nyinyi ndiyo watatu ndiyo mshaingia Salvador na anatoa siri ya kuwa hivyo, alipomaliza kuchati nikaurudia zaidi ya mara ya tatu hili kuelewa kama kuna shuku toka kwa Laza juu ya nyie kuwa mmeenda Salvador lakini hakufikia kuonekana anashuku ingawa walikubaliana kuwa atamwambia madam wao juu ya hilo”
“..Je unahisi hapa yupo huyu mwanamke peke yake?”
“Inawezekana lakini pia isiwezekane maana yeye simu zake zote tulizokuwa tumezi track hazitumiki tena lakini kama hauna usingizi wa uchovu wa safari usiku huu huu kabla hakujakuchwa uwe ushaonana na Mr. Blocks wa fb”
“Vizuri sana… Endelea na umakini wako mpenzi wangu..!”
“Nawe pia baba kijacho!”
“Watoto watatu nilionao bado unaona haitoshi unaamua kuniita baba kijacho, haya ahsante mke wangu wa zamani”
Taarifa kazi! Ilifika kwa Agent Kai ambaye baada ya kuweka simu pembeni ya sofa alilokaa alitizama saa yake ya mkononi kisha akasimama.
***** ***** *****
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
“Umejuaje kama hapa yupo huyo Madam unayesema?” Lilikuwa ni swali katika lugha yao zoeleka ya kireno aliloulizwa mwanaume mmoja wa kizungu wa kibrazil aliyevaa kofia kubwa nyeusi aina ya pama (marliboro), machoni akiwa na miwani meusi licha ya kuwa ulikuwa muda wa usiku wa saa tatu kwa saa za jimbo la Bahia, mwilini mwake alivaa koti kubwa refu kama kanzu lakini lenyewe lilikuwa la ngozi na vifungo toka juu mpaka chini hvyo alivifunga kuwa limemziba hadi suruali yake ambayo nayo ilikuwa nyeusi na viatu vya moka.
“Kijana mimi si muhuni kama hujuavyo nimekwambia nmepajua hapa kwa maelekezo yake mwenyewe na ningeweza kutuma kijana wangu yoyote kuja hapa kuongea na madam lakini sijataka hivyo kwa usalama wa madam… Tafadhali naomba mpe taarifa hiyo juu yangu” Mwanaume huyu akajieleza tena ikiwa ni mara ya pili kujieleza juu ya ukaribu alionao na huyo anayeitwa Madam.
“Anasemaje?”Kwa ndani ya geti alitokea akamuuliza huyu anayeulizana na mgeni aliyefika hapa.
“Anamuulizia Madam Millian… Mimi nimemuuliza nani kamwambia kama hapa kuna mtu anaitwa Madam Millian” Akajibu korokoroni wa getini akiwa anaiweka vizuri bunduki yake.
“Mkuu! Samahani sana.. Unamuulizia Madam Millian kuna mtu aliyewai kukwambia hapa kuna mmiliki wa jina hilo?” Swali hili sasa liliulizwa na kijana aliyefika hapa getini akitokea ndani ya nyumba.
Mgeni alimtizama vizuri kijana aliyefika akamtambua ni nani hivyo akavua pama lake kichwani akifuatisha na miwani uso wake ukaachia tabasamu baada ya kijana aliyefika kustuka.
“Karibu… Karibu! Karibu Inspekta… Adofe mfungulie geti.. Yuko sahihi!” Kijana akajikuta uso wake unaona aibu punde alipogundua ni nani huyu mgeni.
Mtoto wa geti alifunguliwa mgeni akakanyaga ardhi ya ndani akaongozwa na kijana yule kimya kimya mpaka ndani alipokaribishwa sebuleni.
“Madam amerudi hapa muda si mrefu kama ujuavyo tumeingia hapa jana usiku sana hivyo hatukuwa na muda wa kupumzika na hata mchana hatukuweza pumzika sababu tulikuwa na pilikapilika nyingi sana ikiwemo Madam kuonana na mumewe ambaye yeye alitangulia toka juzi hapa Salvador… Hivyo kama una ujumbe unaosema ni muhimu sana unaweza niachia mimi kisha ukaenda nitamfikishia habari hiyo” Kijana akaongea wakiwa wamesimama bila kuketi kwenye vikalio mbalimbali vilivyopo katika seti mbalimbali.
“Surian! Surian unaitwa kama sijakosea.. Jambo nalotaka kumwambia ni muhimu kuliko usingizi aliolala tafadhali naomba umuamshe nimpe ujumbe huo.. Haustuki afisa wa cheo changu katika jeshi la polisi kuwepo hapa usiku nikiwa katika mavazi ya kujificha” Aliyetambulika Inspekta akajieleza tena akitaka aamshwe Madam Millian huyu ni mke wa Kingpin Feca ambaye naye yupo mji huu wa Salvador wakiamini wanaupita upepo mbaya tu kisha mambo yataenda vile ilivyokuwa awali.
“Sawa! Ngoja nijaribu ila hakuna kitu anachochukia kama kuamshwa anapokuwa kalala..!” Surian akaeleza kisha akaanza hatua za haraka kuelekea ngazi zinazokwenda floor ya pili.
Dakika tano zilikatika bila kijana kurudi huku ukimya ukiendelea kutawala ndani ya eneo la nyumba hii, mara zikaanza kusikika hatua muongozano zikishuka ngazi.
“Inspekta karibu..!” Mwanamke mtu wa makamo alipotokeza tu sebuleni baada ya kumaliza ngazi aliongea hivi akiwa na uchangamfu kana kwamba hajatoka usingizini.
“Ahsante sana Madam… Na pia samahani sana kwa kukuamsha usingizini” Akajibu Inspekta.
“Okay! Haina shida, sikuwa nimelala nilikuwa nikisoma soma mitandao ya kijamii inavyoendelea kusambaza ujinga wao juu ya makampuni tunayomiliki… Mbona umesimama? Keti sofani” Madam akakubali msamaha na kuomba mgeni aketi sofani.
“Utapenda mazungumzo yetu yasindikizwe na kahawa au juisi kama si kileo?”
“Hapana si lazima.. Imenilazimu kufika hapa usiku huu sababu nimeamua kutotumia simu katika kuwasiliana na wewe ila nina ujumbe wako kama si wenu wote wewe na mumeo” akaongea mgeni huyu aitwaye Inspekta Fred De Luis Penambucano au kwenye mitandao ya kijamii akitumia jina la kificho la Laza Blocks, kisha akatoa simu yake toka kwenye mfuko wa suruali yake baada ya kulibetua koti alilovaa.
Alitulia akifungua vitu anavyovijua yeye katika simu yake kisha akanyoosha mkono kumpa simu yake Madam Millian.
“..Thea amenitumia meseji hizi juu ya watu waliomteka huko Chilpancingo kisha wakamuhoji juu yako naye kwakuwa ni muoga amefunguka kuwa huko huku, sasa sielewi kama watakuja kukutafuta au washakuja kukutafuta ni watu wa DTO..” Akaongea kwa kasi Inspekta akiwa katoa miwani yake ameikamatia mkononi anaizungusha zungusha kufuatana na anachoongea.
“Duh! Inabidi haraka sana tumtaarifu Feca..! Wamejuaje kama mimi nimewasiliana na TMT? Upumbavu gani huu”
“Ni vizuri.. Ninaomba msitumie simu zenu mpaka pale tutakapokuwa tuko na uhakika kuwa kuko salama, lifanyie kazi hili swala kwa upande wako huku nami nafanya katika vyombo vya usalama ikiwemo uhamiaji juu ya kuingia kwa watu wanaotokea Mexico wote wawe wananipa taarifa zao kwa kina, pia nitakupatieni mtaalamu wa michoro atakayeweza kuwachora hawa watu kufuatana na maelezo ya Thea tukapata kujua kwa picha ya kuchorwa kuwa hawa ni nani na nani kutoka huko DTO!” Inspekta akafunguka kirefu kidogo.
“Safi sana Inspekta.. Nataka watu hawa wakifika tu wafikie vifo hili wengine wajue hatuna masihara tena tumewachekea sana wanajaribu kutufanya tuishi katika hali ngumu tusiyoijua kabisa.. Acha niende juu nibadili nguo nimchukue dogo niende naye kwa Feca..!” Madam akaongea hakusubiri neno jipya toka kwa Inspekta haraka akainuka sofani mbio mbio akakwea ngazi kupotelea huko floor ya pili vilipo vyumba vya kulala.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na sita (106)
Kikosi kazi cha kijasusi chenye majasusi nguli waliobobea katika kazi hizi za giza waliotangulia kwa njia ya moja kwa moja kuingia mji wa Salvador jimbo la Bahia nchini Brazil tayari wapo ndani ya mji.
Bingwa wa udukuzi ndani ya CIA mwenye uwezo wake anadukua chating baina ya watu walio katika target yake na kisha yeye Lizy Rob kuufikisha ujumbe wake kwa Agent Kai, je Agent Kai atafuata maelekezo ya swahiba yake kukiacha kitanda na kwenda kuanza kazi yake katika mji huu?
Muda mchache mambo mengi!
Alitulia akifungua vitu anavyovijua yeye katika simu yake kisha akanyoosha mkono kumpa simu yake Madam Millian.
“..Thea amenitumia meseji hizi juu ya watu waliomteka huko Chilpancingo kisha wakamuhoji juu yako naye kwakuwa ni muoga amefunguka kuwa huko huku, sasa sielewi kama watakuja kukutafuta au washakuja kukutafuta ni watu wa DTO..” Akaongea kwa kasi Inspekta akiwa katoa miwani yake ameikamatia mkononi anaizungusha zungusha kufuatana na anachoongea.
“Duh! Inabidi haraka sana tumtaarifu Feca..! Wamejuaje kama mimi nimewasiliana na TMT? Upumbavu gani huu”
“Ni vizuri.. Ninaomba msitumie simu zenu mpaka pale tutakapokuwa tuko na uhakika kuwa kuko salama, lifanyie kazi hili swala kwa upande wako huku nami nafanya katika vyombo vya usalama ikiwemo uhamiaji juu ya kuingia kwa watu wanaotokea Mexico wote wawe wananipa taarifa zao kwa kina, pia nitakupatieni mtaalamu wa michoro atakayeweza kuwachora hawa watu kufuatana na maelezo ya Thea tukapata kujua kwa picha ya kuchorwa kuwa hawa ni nani na nani kutoka huko DTO!” Inspekta akafunguka kirefu kidogo.
“Safi sana Inspekta.. Nataka watu hawa wakifika tu wafikie vifo hili wengine wajue hatuna masihara tena tumewachekea sana wanajaribu kutufanya tuishi katika hali ngumu tusiyoijua kabisa.. Acha niende juu nibadili nguo nimchukue dogo niende naye kwa Feca..!” Madam akaongea hakusubiri neno jipya toka kwa Inspekta haraka akainuka sofani mbio mbio akakwea ngazi kupotelea huko floor ya pili vilipo vyumba vya kulala.
ENDELEA NA NONDO
FUNGA KAZI II
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL II
Parque Bella Vista Street ni mtaa uliopo eneo la Avenida Tancredo Neves usiku wa saa nne na nusu Agent Kai alikuwa akishuka kwenye taxi baada ya dreva kusimamisha gari mahala ambapo alielekezwa asimame pembezoni mwa bustani ya jeshi la polisi, alipohakikisha taxi imeshaondoka akajiweka vizuri kisha akaanza hatua kuelekea uelekeo wa mbele ambapo hatua kumi akaliona jengo ambalo ndiyo haswa lililomleta mtaa huu usiku huu akiacha kitanda alichokuwa akikitamani sana kuliko kitu chochote ila umuhimu wa kazi nao ulimfanya asijibweteke na kulala, jengo likiwa linaangaliana na jengo lingine la ghorofa lenye urefu wa’ floor’ (losheni) la shirika la ujasusi la Brazil tawi la jimbo la Bahia liitwalo Law Enforcement Agency.
Jengo la ghorofa lenye floor (losheni) mbili likiwa na maandishi makubwa kati ya floor na floor ndipo kulikuwa na maandishi haya ‘Flagant Central Civil Police Of Bahia’ hapo ikamfahamisha Agent Kai ni jengo hili analihitaji usiku huu kufanya amabcho ni kichwa chake pekee ndicho kilichokuwa kinajua anaenda kufanya nini kwenye hiki kituo kikuu cha polisi au waweza kusema ni makao makuu ya polisi jimbo la Bahia.
Muda huu ungemuona alivyo usingejua kama yeye ni Agent Kai Mmarekani mweusi wa asili ya nchi yake ya kuzaliwa Tanzania, alikuwa anaonekana kama mzungu mwenye nywele za bonde, sura ya bandia ya mzungu fulani asiyejulikana ilimbadili muonekano wake wote kabisa ukiacha umbo lake na tembea yake ambayo hakutaka kuifanya nayo ya maigizo alikuwa amevaa suti ya rangi nyeusi inayomuonyesha kama kivuli ikiwa ni tai nyeupe aliyovaa ndiyo inayomuonyesha kwa uzuri kuwa yeye ni kiumbe, hakuwa muoga wala kuonyesha ana masito masito alipiga hatua zile zile toka anatokea eneo la mipaka ya mbele ya majengo ya polisi getini kulikuwa na walinzi watatu waliokamatia silaha aina ya bunduki.
“Habari zenu maafande?” Akawasalimu baada ya kuwa amebakiza hatua tano tu kufika getini, sura za maaskari hawa wazungu wa kibrazil zilimtisha haraka akaona awasalimu kwa kireno chao.
“Safi… Tukusaidie nini muda huu?” Akijibu mmoja macho yake akimuangalia kwa udadisi Agent Kai toka chini mpaka juu.
“Mimi ni mgeni hapa Salvador, natokea jijini Brasilia.. Bahati mbaya usiku huu wakati niko kwenye taxi niliyoikodi nilimuomba dreva anishushe katika moja ya maduka yanayouza vinywaji hili nichukue vinywaji ambavyo ningeenda kunywa nitakapofika hotelini, kumbe dreva niliyekodi gari hakuwa mtu mwema alisubiri nilipoingia ndani ya duka la vinywaji akaondoa gari na kuondoka na mabegi yangu mawili ya nguo, briefcase ya vifaa vyangu vya kazi ikwemo Ipad na laptop ndogo hivyo hivi nilivyo ndiyo nguo pekee nilizobakiza” Aliongea Agent Kai akionyesha baadhi ya vitendo kwa mikono yake.
“Unaitwa nani? Ndugu!”
“Feylan Casemiro”
“Unatokea wapi?”
“Nilishaeleza mkuu.. Natokea jijini Brasilia”
“.. Nimekuuliza unakotoka hili nipime kama kuibiwa ulikoibiwa ni halali yako.. Hahaha hahah!” Aliongea mdomo wake akiuweka kwa dharau askari huyu akimalizia na kicheko cha dharau zaidi.
“Kumbe kuna mahala ukitoka kuna kuhalalishia kuibiwa.. Hahahah hahahah sikuwa najua hilo mkuu kabla” Kai akaongea kama anataka kujua zaidi huku kifuani mwake alikuwa anabanwa kwa hasira kwa jinsi anavyoongeleshwa kwa dharau mtu mkubwa kama yeye kana kwamba anaongeleshwa muhuni flani.
“Kuibiwa ni ujinga kwa sababu mara nyingi tumekuwa tukiwaonya juu ya wizi wa ujanja kama huo toka kwa matapeli na wezi wengine wa kama ulichofanyiwa… Ukiingia jimbo la Bahia unatakiwa kuwa makini sana na ndiyo maana nimeshangaa kuibiwa ulikoibiwa wakati wewe si mgeni Brazil… Wabrazil wengi uwa hawafanyi makosa uliyofanya.. Pole sana ndugu mzembe Feylan Casemiro..”
“Sioni mkinisaidia… Hali hii inafanya uhalifu uzidi kukomaa hapa nchini mwetu sababu yenu maaskari msiojali lolote, naweza ingia kituoni nikatoe taarifa kwa waongoza dawati wa usiku huu?” Hasira za Agent Kai zingeonekana dhahiri kama asingekuwa kavaa sura ya bandia ya kizungu, alikuwa kakunja ndita ndani lakini kwenye hii ngozi ya plastiki aliyoivaa ilikuwa kuna mkunjo mdogo sana tofauti na ndani.
‘..Kaka! mi sioni sababu ya wewe kutaka kwenda kwa muongoza dawati la maelezo.. Hakuna wa kukusikiliza na kutaka kukupa msaada utakaokuwa sahihi kwako, wewe mwenyewe piga picha ungekuwa umesimama upande wetu unafikiri ungefanyaje?” Askari huyu alizidi kuzitia ndimu hasira za Agent Kai akawatizama kisha akageuka nyuma hili kuondoka.
Wakati huohuo si kama kulikuwa kote kuko pilika pilika za watu katika eneo hili la hasha! Eneo lilikuwa na hekahekaza askari waliokuwa wengine wanaingia na wengine wanatoka lakini wao walikuwana geti lao maalumu wanalolitumia likiwa mita ishirini toka kwenye geti hili ambalo linatumiwa na watu wa kawaida (raia wasio askari)
“Nenda kalale Bwana mkubwa.. Ushaibiwa umeingizwa Salvador siku nyingine ukija utakuwa makini zaidi!”. Yule yule askari anayependa kuongea maneno ya karaha alitoa maneno yake ya karaha ikiwa Agent Kai wa kizungu kashapiga zaidi ya hatua nne toka walipokuwa sambamba akiwa kafura kwa hasira ingawa hakuwa ameibiwa ilikuwa ni gia yake ya kutaka waongee kistaarabu kama alivyotarajia kisha aulize alichokuwa anaona ni sahihi.
Akiwa anataka kuvuka barabara kwenda upande wa pili aliona kuna bajaji inasogea eneo la kushusha abiria wanaotaka kufika kituoni kwa sababu mbalimbali, haraka Kai akaongeza umakini kuangalia ndani ya bajaji ile kutokea alipo huku akipiga hatua ndefu zaidi kuelekea pale ilipo mwanga wa taa za juu za barabarani zilikuwa zikimuonesha vizuri anavyopiga hatua kivuli chake kikiwa kimetangulia mbele.
Aliifikia bajaji ile kabla hata anayetakiwa kushushwa hajashuka akiwa analipana pesa na muendesha bajaji hivyo Agent Kai ‘mzungu fake’ akasimama pembeni akisubiri.
“Vipi kaka mkuu unaenda?” Dreva akauliza kwa lugha yake zoeleka (kireno) wakati abiria akishuka ambaye alikuwa ni mwanamke akiwa kavaa mavazi ya fomu za kuonyesha ni polisi.
“Naomba nikuulize kwanza kabla hatujaondoka kwenda napotaka” Agent Kai ‘TSC’ si haba kwenye kireno nako yumo humo kwakuwa ni miongoni mwa lugha ambazo kwake ni kama anakunywa uji wa ulezi anateleza tu.
“Haina tabu mkuu uliza tu”
“Kituo chako unachopaki ni karibu na hapa?”
“Ni mitaa ya juu kidogo ndipo tunapopaki.. Huku hakuna tunaporuhusiwa kupaki sababu wanazosema ni za kiusalama karibu na kituo lakini uwa tunaruhusiwa kuja kushusha hapa kwa polisi wanaotukodisha kuwaleta hapa ambao hawana magari yao binafsi..!”
“Kwahiyo wengi wao ni wenye magari yao binafsi?” Hili swali ‘TSC’ aliuliza wakati kashaingia ndani ya bajaji siti za abiria nyuma ya ‘cabin’ ya dreva.
“.. Askari wengi wa hapa kituo kikubwa wana magari lakini si wanaopenda kutumia gari zao binafsi kuja nazo kazini kwa sababu mbalimbali.. Kwani kaka wewe nae ni askari wa kituo hiki?”
“Nimehamia Salvador kutokea Brasilia.. Mimi ni askari kanzu nimeanza kazi leo hapa kituo kikuu niliripoti asubuhi kisha nikatoka kwenda kuonyeshwa nyumba ambayo nitakuwa naishi hapa kazini nilirudi tena jioni muda huu ndiyo natoka muda huu lakini kuna mkuu mmoja alinipokea asubuhi hii hatukupeana namba za simu zetu, jioni hii hatukuonana na sijui anaishi wapi nahisi kwakuwa wewe ni dreva wa bajaji itakuwa unaweza kuwa unamjua kwa namna moja au nyingine” ‘TSC’ aliingia kwenye dhumuni la kutaka kuongea na dreva wa bajaji.
“Yah! Kaka inawezekana nikamjua… Nani huyo?” Dreva aliuliza hili akiwa amegeuza uso wake kumuangalia ‘TSC’ (mzungu fake) kwenye macho ya watu wanaomuona usiku huu.
“Inspekta Fred De Luis Penambucano”
“..Ooooh! Inspekta Pena.. Ndiyo namjua ni kaka wa jamaa yangu mmoja nilisoma naye anaitwa Abbah De Luis..” Akajibu kwa furaha kubwa dreva wa bajaji akiamini amemfurahisha sana mtu anayetamani awe amteja wa bajaji siku zote atakazokuwa hapa Salvador.
“Aisee hafadhali sana nimekupata mtu sahihi..Anakaa wapi?”
“Naweza kukupeleka tu hadi anapoishi hakuna shida”
“Hapana ni usiku ulioenda kidogo si unajua jamaa ni kama boss wangu kikazi ila nafikiria nimfuate kwake hapo asubuhi na mapema hili niongozane naye kuja naye kazini.. Utanielekeza tu kwake au tutaenda wote hadi hapo muda huu utanionyesha nyumba yake kisha utanipeleka kwenye hoteli niliyofikia, nitachukua namba yako hili niwe naitumia bajaji yako kipindi chote nitakachokuwa hapa si unajua kazi za uaskari zilivyo si za kutembea tembea kwa miguu”
“Sawa twende kaka… Unajua hapa Salvador kulivyo ni mitaa hii karibu na kituo kunakuwa kumepoa poa lakini mitaa mingine kunakuwa kumechangamka sana” Dreva aliongea hivi akiwa kashatia gia hili ageuze bajaji kuelekea huko anapoishi jamaa aliyesababisha ‘TSC’ muda huu asiwe kitandani.
Maneno matamu ya jasusi mbobezi na mwandamizi mwenye mbinu nyingi kwenye ubongo wake wakati anataka anachotaka katika kazi yake uwa halengi kisha akakosa anacholenga, aliweza mlainisha dreva wa bajaji akatema mengi anayoyajua ya kijuu juu ya Inspekta Pena mpaka ‘TSC’ alifurahi sana kumlenga huyu dreva wa bajaji akaumia kwanini alienda kwenye geti la kituo cha polisi na kukerwa na askari wanaolinda geti wakijua wanaongea na bwanyenye fala tu kumbe wanaongea na jasusi wa level ambayo hapa Salvador hakuna.
Haukuwa umbali mkubwa sana kwa bajaji kutoka mtaa wenye kituo kikuu cha polisi wa Parque Bella Vista uliopo eneo la Avenida Tancredo Neves mpaka eneo la Pelourihno wenyewe upenda kufupisha kwa kuita ‘Pillory’ unakopatikana mtaa wa Lafayette Velos 7th Street, mtaa ambao kuna nyumba zilizojengwa na shirika la nyumba la jimbo la Bahia (hili linasomeka Ba’ha), nyumba zilizo katika mtindo unaofanana apartment ikiwa viwanja vyake vimepimwa kwa square mita kubwa eneo la juu umbali wa mita mia tatu toka beach ya Jaguaribe moja ya beach yenye eneo kubwa na bora kabisa nchini Brazil.
“Nyumba ya tatu toka hapa kwenye kona ndiyo nyumba ya Inspekta Pena” Alivunja ukimya uliokuwa umetawala kwa kitambo wakati yeye dreva wa bajaji anakanyaga mwendo kuja huku kumuonyesha ‘mzungu fake’ nyumba ya Inspekta Penambucano.
“Yah! Nimeiona” ‘TSC’ akaongea huku haraka anachunguza mandhari ya nyumba akiwa hajavaa miwani yake ya kazi inayokuwa inamsaidia kuona kwa uzuri maeneo kama haya nyakati za usiku lakini toka anaongea na maaskari kule makao makuu ya polisi na si kama alikuwa hajaibeba hapana alikuwa ameibeba iko kwenye mfuko wa mbele wa suti aliyovaa.
“Taa zinawaka kote kote inaonyesha hawajalala… Vipi unaweza enda muona.. Uwa anaishi na mkewe tu pamoja na watoto ambao wote wawili wa kiume wako shule ya soka ya timu ya watoto ya Bahia kipindi kama hiki wanakuwa hawapo nyumbani..!” Dreva akaongea akiwa naye ametupia jicho la wizi kisha akarudisha umakini kwenye usukani.
“Asubuhi nitakuja.. Acha unipeleke hotelini kwangu...!” Akajibu Agent Kai akiwa anauangalia mtaa kwa uzuri mawazo yake yakiwa tofauti na anachokisema kumwambia dreva wa bajaji.
Hakuwa na ramani ya jiji hili hivyo kidogo ilimuwia vigumu kudanganya wapi ashushwe hivyo akamuacha dreva aendelee kidogo lakini akapata wazo.
“Hapa karibu hakuna club ya mabinti wazuri niopoe wa kulala naye?” Akaongea baada ya kumgusa begani dreva huku anajifanya anacheka cheka.
“..Huku Pillory ndiyo mahala ambapo kuna night club nyingi sana hivyo tukiingia katikati ya pillory kuna moja maarufu sana ila hii siku kama leo muziki wa live bendi kunakuwa hakuna ni mwendo wa vinywaji na ufuska tu acha nizunguke mzunguko unaoonekana mbele yetu tuelekee huko.. Kuna watoto wazuri hatari wanatoa mambo yote pesa yako tu..” Akajibu dreva naye akachekacheka kufurahia alichoongea.
“Siyo mbali sana?”
“Hapana si mbali na mtaa huu sababu ni hapahapa Pelourihno”
“Sawa niache hapo nichukue mtoto mmoja wa kuvuta naye usiku mzima” ‘TSC’ akaongea na dreva hakuwa na hiyana akaongeza mwendo mpaka mzunguko wa makutano ya barabara ya BR-116 na BR-117 alipozunguka akaiacha BR-116 akaingia BR-117 ambayo uwa inaelekea barabara kuu inayoenda stendi ya mabasi ya jiji la Salvador iitwayo Iguatemi, Agent alikuwa akitamani ateremshiwe hata hapa wanapopita sasa kwakuwa hakuwa anataka kwenda huko club kuopoa malaya lakini haikuwa ndani ya uwezo wake, uongo wake ungebainika hata kama dreva wa bajaji asingeuliza zaidi lakini haikuwa njema kikazi.
“Jengo la katikati kati ya majengo hayo marefu yaliyo saizi sawa ndiyo club niliyosema kuwa maarufu zaidi ndani ya jiji la Salvador inaitwa Salvador Da Bahia Nightlife Club, Bar & Tips” Aliongea dreva wa bajaji huku anapunguza mwendo wa bajaji yake, ‘TSC’ akaona hana budi kujifanya anapaangalia akiinama hili aone anapoonyeshwa lilipo jengo, mawazo yake yakiwa nyumbani kwa Inspekta Penambucano.
Hakujibu kitu alitoa wallet yake toka mfuko wa suruali kisha akachana kuifungua akatoa noti moja ya dola mia moja ya kimarekani.
“Naamini dola si tatizo kwenye malipo yako best na pia naamini hii inatosha kwa mizunguko yetu mpaka hapa” Akasema huku anampa dreva ikiwa anataka kujua kama inaweza kuwa shida kwake kumlipa kwa dola na kama itamtosha.
“Si tatizo kaka.. Nyingi sana kaka nilitakiwa nikate nusu ya hii… Ahsante sana..!” Akashukuru meno yote ya mbele yakikenuka kwa kijana huyu wa kibrazil, mbrazil mweusi akiwa ametengeneza nywele zake mtindo wa bambucha.
“..Usijali mdogo wangu… Nipe namba yako kesho nikutafute” ‘TSC’ akazuga tena kuomba namba ya kijana huyu ambaye haraka alizama mfukoni mwake akatoa kikaratasi kikiwa kishaandikwa namba ya simu kwa peni, hii ilimfanya Agent Ka kutabasamu ndani ya sura yake ya bandia inayoficha uhalisia wake machoni mwa watu.
“Ahsante.. Sana kijana… Kesho nitakutafuta mchana mchana hivi.. Urudi salama Avenida Tancredo Neves!” Aliongea hivi akiwa kashashuka toka ndani ya bajaji wakaagana dreva wa bajaji akatia gia akitabasamu kwa furaha akijiona mwenye zali kukutana na mzungu huyu aliyemwambia kuwa ni askari kanzu wa jeshi la polisi la Brazil mgeni toka jiji la Brasilia.
Agent Kai aliacha dogo apotee machoni mwake kisha akaita taxi kutoka maegesho ya taxi yaliyopo upande wa pili, eneo hili lote lilikuwa limechangamka sana, taxi ikasogea haraka naye akafungua mlango wa upande wa abiria akaingia na kufunga mlango.
“Nipeleke makutano ya mzunguko wa BR-116 na BR-117.. Utaniacha mbele kidogo ya barabara ya BR-116” Akamwambia dreva wa taxi wote wakiangaliana kupitia kioo cha juu kwa dreva na kuonana vizuri ukiwaona utajua wote hawa ni wanaume wa kizungu wa kibrazil.
Mwisho wa sehemu ya mia na saba (107)
Usiku wa kwanza ndani ya Salvador ulikuwa ni usiku wa kuhitajika kupumzika kwake Agent Kai lakini haikuwa hivyo aliamua kufuata alichoambiwa na Lizy Rob kuwa asilale aakikishe anaonana na Inspekta Penambucano, njia hii haitakiwi kuachwa ikapotea kimpango maana wahalifu wana mengi ya chini chini kuwasaidia katika uhalifu wao.
Nyayo za paka zimefika kwenye mawindo zikikanyaga na pua kunusa nusa mpaka kuiona nyumba ya Inspekta Penambucano (Pena).
Hakujibu kitu alitoa wallet yake toka mfuko wa suruali kisha akachana kuifungua akatoa noti moja ya dola mia moja ya kimarekani.
“Naamini dola si tatizo kwenye malipo yako best na pia naamini hii inatosha kwa mizunguko yetu mpaka hapa” Akasema huku anampa dreva ikiwa anataka kujua kama inaweza kuwa shida kwake kumlipa kwa dola na kama itamtosha.
“Si tatizo kaka.. Nyingi sana kaka nilitakiwa nikate nusu ya hii… Ahsante sana..!” Akashukuru meno yote ya mbele yakikenuka kwa kijana huyu wa kibrazil, mbrazil mweusi akiwa ametengeneza nywele zake mtindo wa bambucha.
“..Usijali mdogo wangu… Nipe namba yako kesho nikutafute” ‘TSC’ akazuga tena kuomba namba ya kijana huyu ambaye haraka alizama mfukoni mwake akatoa kikaratasi kikiwa kishaandikwa namba ya simu kwa peni, hii ilimfanya Agent Ka kutabasamu ndani ya sura yake ya bandia inayoficha uhalisia wake machoni mwa watu.
“Ahsante.. Sana kijana… Kesho nitakutafuta mchana mchana hivi.. Urudi salama Avenida Tancredo Neves!” Aliongea hivi akiwa kashashuka toka ndani ya bajaji wakaagana dreva wa bajaji akatia gia akitabasamu kwa furaha akijiona mwenye zali kukutana na mzungu huyu aliyemwambia kuwa ni askari kanzu wa jeshi la polisi la Brazil mgeni toka jiji la Brasilia.
Agent Kai aliacha dogo apotee machoni mwake kisha akaita taxi kutoka maegesho ya taxi yaliyopo upande wa pili, eneo hili lote lilikuwa limechangamka sana, taxi ikasogea haraka naye akafungua mlango wa upande wa abiria akaingia na kufunga mlango.
“Nipeleke makutano ya mzunguko wa BR-116 na BR-117.. Utaniacha mbele kidogo ya barabara ya BR-116” Akamwambia dreva wa taxi wote wakiangaliana kupitia kioo cha juu kwa dreva na kuonana vizuri ukiwaona utajua wote hawa ni wanaume wa kizungu wa kibrazil.
ENDELEA NA NONDO
FUNGA KAZI III
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL III
“Hapa panatosha dreva.. Unaweza niacha hapa!”
“Sawa mkuu.. Unakaa mtaa huu?”
“Ndiyo naishi nyumba za nyuma ya hizi za mbele unazoziona.. Nafikiri hakuna shida nikilipa kwa dola?”
“.. Lakini nitarudishaje chenchi? Maana hesabu za dola na pesa yetu Real”
“Haina shida.. Umeniendesha vizuri tena tukiwa kimya hukunisumbua kwa maneno maneno kama madreva wengine wa taxi, keep change!”
“Ahsante sana boss.. Mungu akubariki hii inanifanya niende kwangu kulala sasa hivi..!” Ilikuwa furaha kubwa sana kwa dreva wa taxi kupewa dola mia na Agent Kai ambaye hakutaka kusubiri ngonjera za mapambio alizokuwa akipewa kama shukrani toka kwa dreva wa taxi ambapo kama angeendelea kukaa ndani ya gari basi angechelewa zaidi ya yule dreva wa bajaji, wallet ya jasusi usiku huu aliokurupushwa asilale bila kumtafuta Inspekta Pena ilikuwa imepangwa dola mia mia tu sababu alisahau kubadili baadhi yake kwenda kwenye pesa ya kibrazil iitwayo ‘Brazil Real’ (BRL).
Haraka aliposhuka alimpungia mkono dreva akimuonyesha ishara aondoke zake huku tabasamu feki toka kwake akilianikiza na kuifanya sura inayoonekana ya mzungu flani itune mashavuni (lol).
Hili kumzuga dreva wakati anapindua gari kurudi mita chache yalipo mzunguko wa makutano ya barabara (round about), yeye ‘TSC’ alifuata barabara inayoingia kwa bondeni toka barabara kuu kisha akanyoosha kidogo sababu kulikuwa na watu kama watatu wameongozana kwa miguu wanakuja kwa barabara kuu akapishana nao kimya kimya hakuna aliyemjali kila mmoja alikuwa na hamsini zake juu yake wakawa wanaendelea na maongezi yao.
Pia nao alipoona wamempotea machoni mwake akageuza kurudi kule mtaa ukiwa umetulia ambapo alipofika aliongeza spidi kulifuata barabara kuu linapoendea akipita pembeni pembeni napo alikuwa akipishana na watu mmoja wanaolekea anapotokea yeye na hata magar,pikipiki na bajaji yalikuwa yanapita katika hii barabara ya BR-116 kwa kupishana yanayoenda kaskazini na mengine kusini.
Kwa mwendo wa kasi wa kikamanda kamanda ilimla dakika sita kufika mtaa wa Lafayette Velos 7th Street ambako ikambidi apunguze mwendo na kwenda mwendo wa kawaida, akavuka barabara toka upande aliopo kwenda upande wa pili iliko safu ya nyumba zilizojipanga kuangalia barabarani mojawapo ikiwa ya Inspekta Penambucano, akapita kwa mbele sasa akiona kwa uzuri kulivyo na taa zilikuwa zikiwaka vyumba vyote kama alivyosema dreva wa bajaji wakati wanakatiza kwa bajaji dakika kadhaa zilizopita.
Nyumba hizi za mtaa huu hasa hizi zilizo upande huu ilipo nyumba ya Pena zilijengwa kwa kutoachiana vichochororo ambavyo mtu anaweza kukatiza kwenda upande wa nyuma wa nyumba hizi, nyumba husika inayonyatiwa na jasusi Kai ilikuwa ni nyumba iliyozungushiwa ukuta mfupi unaoweza kurukwa na mtu kama yeye kwa sarakasi moja tu kati ya furushi la sarakasi alilonalo mwilini mwake endapo angetaka licha ya kuwa juu kuta kuliwekwa nondo zilizopangwa kiustadi kufuata ukuta juu zikiwa zimewekwa ncha, macho ya ‘TSC’ yaliweza kufanya usahili wa haraka sana akaona kote kulivyo kuanzia maua, miti miti ya maua na nyasi zilivyopandwa kwa ustadi ikiwemo mabembea ya kubembea watoto kwa upande kulia mwa nyumba vyote hivi aliweza kuviona vizuri.
Haraka akili yake ilifanya kazi alipokuwa anaipita nyumba ya jirani kana kwamba mpita njia tu aliona taa za nyumba za ndani zikiwa zimezimwa zikiachwa za nje na ukuta uliozunguka nyumba husika ulikuwa ni ukuta wa kawaida ukiwa na urefu wa kudandiwa juu hata na mbwa mwenye mafunzo ya kurukia sehemu kama hizi, alitizama huku na huko (mbele na nyuma) kisha akaruka na kukamata kwa viganja vyake juu kabisa, hakujali hali ya kukamata kuta kavu hii bila ‘gloves’ aling’ata meno kisha akajivuta kasi hadi juu ambapo alijilaza haraka juu ya kuta kama nyoka akihakikisha gari ambayo ilikuwa inakuja kwa mbali haijasogea kwa ukaribu na kuona tendo lake la kiuhalifu kwa nyumba ya watu.
Macho yake ambayo sasa kwa tahadhari alivaa miwani ya kazi yalikagua eneo la mbele yah ii nyumba ambayo hakuwa na nia nayo kabisa bali alitaka iwe njia ya kuingia eneo la anyumba ya Pena kupitia pembeni, ukaguzi ulipokamilika tu akajiachia toka juu mpaka chini tena mwili ukiwa vilevile alivyojilaza juu hivyo alipotua alitua vile vile vitanga vya mikono yake vikitangulia kufika miguu eneo la magoti ikatoa sapoti akanata chini kana kwamba imeanguka nguo chini pale na si kiumbe.
Kabla hajaamua nini kifaute akiwa kaganda chini vile vile kama alivyotua huku kichwa kikisapoti hitaji la macho yake kwa kusukwa sukwa huku na huko katika nyasi zilizopandwa eneo la chini ya ukuta kwa ndani, mlio wa gari alilokuwa akiuona mwanga wake likika kwa mbali ulisikika ukitoa muungurumo wa kusimama mbele ya geti la ukuta unaozunguka nyumba iliyo katika mpango wake, hapo haraka ubongo wa ‘TSC’ ulifanya kazi akainuka akakimbia hatua za mnyato ndefu mpaka kwenye ukuta unaogawa maeneo ya nyumba mbili hizi hapo napo hakuweka subira ambayo ingemkosesha anachohitaji kwa wakati huo kimipango, akautizama urefu wa ukuta kisha akaruka juu kukamata kwa viganja eneo la juu ya ukuta kisha akajivuta mwili kwenda juu ambapo alipofika akatanguliza kichwa kutizama eneo la ndani ya upande wa uwa wa nyumba ya Inspekta Pena akauona usalama kwa sekunde kumi alizoganda pale ikafuata fursa ingine ya yeye kuuvuta tena mwili wake mpaka juu ambapo napo akupumzika akachuchumaa juu ya ukuta kisha akajiachia kwa ndani ya uwa huu.
Kama ilivyo ada upande wake alipotua kwenye nyasi za kupandwa zilizopandwa eneo hili huku zikipewa huduma stahili kuzifanya ziwe na afya na kupendeza, alitua pasipo kutoa kishindo cha kusikika hata hatua tano mbele baba huyu mwenye mwili mazoezi usioweza kuuzania pale anapokuwa katika kujirusha rusha kikazi zaidi si kiburudani kama ilivyokuwa miaka yake ya utotoni alipokuwa akitoa burudani za watu kulipa viingilio kwenda kumshuhudia kwenye majukwaa.
Alichomoa bastola toka nyuma ya kiuno (mahala salama) ikiwa uwa inajikamata vizuri na mkanda maalumu anaouvaa ambao kwa mbele hauna miujiza sana lakini kwa nyuma huko na kazi maalumu ya kufurahisha kwa majasusi kama Agent Kai ‘TSC’, sekunde tano mbele alikuwa tayari kavuka toke eneo la ukuta mpaka sambamba na ukuta wa nyumba husika, nyumba ya kifahari iliyopendezeshwa kwa kupakwa rangi nzuri ya kijani kwa juu huku kwa chini kukiwa na ufito wa rangi nyeusi.
Ninapoandika ndugu msomaji kuwa matendo haya yalifanyika kwa kasi na mpangilio mzuri toka kwenye ubongo makini juwa kabisa kuwa yalifanyika hivi navyoandika kwani ilimla dakika mbili kwenda tatu kuyafanya haya yote huku hiyo dakika ya tatu ikimkuta akiwa kona ya nyumba upande wa mbele akishuhudia geti likifunguka kwa kujiachia lenyewe bila mtu kuonekana akilifungua, haikumsumbua akili Agent Kai alitambua dreva anayeendesha gari kuna kifaa anakitumia kufungua geti hili lenye matairi chini yanayoliamisha toka kulia kwenda kushoto kisha ya hapo gari rangi nyeupe mpya ya kifahari aina ya Volkswagen Atlas toleo jipya kabisa liliingia ndani kwa mbwembwe likinesanesa kana kwamba linacheza muziki ule ambao unasikika ukisikilizwa na dreva kwa raha zake.
Gari ikasogezwa mahala ambapo mwenyewe muendeshaji aliona ni sahihi kulipaki akasimama na kuzima injini, akashuka mwanaume ambaye amevaa mavazi ya polisi akiwa na kifimbo mkononi pia bastola yake aina ya Glock-47 ikiwa imetulia kwenye kifuko kama pochi la ngozi maalumu kwa kubeba bastola.
Aliposhuka kwenye gari akanyoosha mkono kuelekea lilipo geti akabonyeza rimoti aliyoitoa mfukoni geti likajifunga akiwa ameupa mgongo nyumba, wakati bado mkono wake unaendelea kuamrisha moja ya vidole vyake vya kiganja chake kubonyeza rimoti aliona kivuli cha mtu kinakuja kwa nyuma yake kwa kasi kikiwa kinaonekana dhahiri shahiri huku binadamu mwenye kivuli hiki kinachojongea alipo kutokea kwa nyuma yake mkononi kakamatia bastola kumuelekea kisha kikapotea kwa kasi ilikuwa ‘TSC’ kagundua kivuli kinamuuza kwa bei rahisi, Inspekta hakuwa bwege alijifanya bado anaendelea na kazi ya kufunga mlango wa gari licha ya kuwa kimoyomoyo anatetemeka, alitaka afanye jambo aliloamini yeye kama askari mzuri mwenye mafunzo yake anaweza akafanya.
Alipomaliza kufunga mlango wa gari akapeleka mkono wake mahala anapoweka bastola yake akaseti kulegeza kifuniko cha kimfuko cha rangi ya ngozi, kisha ya hapo akaanza hatua kuelekea kibarazani akili yake ikiwa inawaza nani aliyevamia nyumbani kwake? Ni mhalifu tu? Anataka nini? Alijiweka tayari tayari akienda hatua ndefu ndefu za haraka ikiwa ‘TSC’ anamuona akiwa kajibanza kwenye nguzo moja kati ya nguzo mbili zinazishika paa ya baraza la nyumba.
Inspekta alipomaliza ngazi za kuingia kibarazani aliongeza umakini zaidi pua, macho na masikio yake vikifanya kazi maradufu, alipokaribia kitasa cha mlango mkuu, alisikia mchakacho tokea kulia kama mtu anajongea papo hapo Inspekta akatoa bastola yake kwa kasi na kugeuka haraka upande aliohisi kuna mtu ndipo hamadi kibindoni alikutana mdomo wa bastola umemuelekea na yeye alikuwa kaelekeza bastola yake kwa mtu huyu ambaye ni Agent Kai ndani ya sura ya bandia ya kizungu.
“Nani wewe? Unataka nini nyumbani kwangu?” usiku huu!” Inspekta kijasho chembamba kilianza kumtoka wakati anauliza kwa kireno maswali yake.
“Weka silaha yako chini!” Agent Kai akatoa sauti ya amri naye akitumia lugha ya kireno.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment