Search This Blog

Thursday, 23 March 2023

MSAKO - 3

  

Simulizi : Msako

Sehemu Ya : Tatu (3)

“Sasa kulikuwa na ulazima gani kwa hao watanzania kupata mafunzo ya kijasusi na mbinu za mapigano?” Jacob Matata akahoji.

“Kama unavyojua, sehemu kubwa ya dunia inaendeshwa kwa uamuzi, ambao chimbuko lake ni taarifa za kijasusi. Upatikanaji wa taarifa za kijasusi siyo jambo rahisi, kwa vile taarifa hizo hupatikana kwenye vyanzo vinavyolindwa sana."

"Hivyo isingekuwa sahihi kuwachukua watu muhimu ambao taarifa zao zinategemewa, halafu uwaweke na majasusi wenye uwezo mkubwa wa mapigano. Vinginevyo ni sawa na kuwachanganya kondoo na mbwa mwitu kwenye zizi moja. Hivyo ili kutafuta usawa kwenye kamati hizo, ilibidi kuwaandaa watu wetu kwa namna hiyo. Nadhani sasa umenielewa?”

“Naam! Nimekupata vyema.” Jacob Matata akaitikia huku akitikisa kichwa kuafiki.

“Baada ya miaka kadhaa, hofu ya viongozi wa kijamaa ilikuja kuthibitika kuwa kweli. Baada ya miaka kadhaa, nchi nyingi za kijamaa, ilibidi zifungue mlango kwa mfumo wa uchumi wa kibepari. Ndiyo maana sasa hivi unaona nchi nyingi duniani zinafuata uchumi wa kibepari. Lakini maandalizi yalishafanyika miaka mingi iliyopita.” Bi. Anita akaweka kituo na kushusha pumzi ndefu akifikiri. Baada ya kitambo kifupi cha ukimya wa tafakuri akaendelea.

“Sasa turudi kwenye kisa chetu, kilichokupelekea uniite hapa siku ya leo. Hayo uliyosema yanauhusiano gani na wito wangu?’’ Jacob akauliza huku akipiga mkupuo mkubwa wa sharubati iliyokuwa kwenye bilauri.



Imetungwa na kuandikwa na Japhet Nyang'oro

Hivyo isingekuwa sahihi kuwachukua watu muhimu ambao taarifa zao zinategemewa, halafu uwaweke na majasusi wenye uwezo mkubwa wa mapigano. Vinginevyo ni sawa na kuwachanganya kondoo na mbwa mwitu kwenye zizi moja. Hivyo ili kutafuta usawa kwenye kamati hizo, ilibidi kuwaandaa watu wetu kwa namna hiyo. Nadhani sasa umenielewa?”

“Naam! Nimekupata vyema.” Jacob Matata akaitikia huku akitikisa kichwa kuafiki.

“Baada ya miaka kadhaa, hofu ya viongozi wa kijamaa ilikuja kuthibitika kuwa kweli. Baada ya miaka kadhaa, nchi nyingi za kijamaa, ilibidi zifungue mlango kwa mfumo wa uchumi wa kibepari. Ndiyo maana sasa hivi unaona nchi nyingi duniani zinafuata uchumi wa kibepari. Lakini maandalizi yalishafanyika miaka mingi iliyopita.” Bi. Anita akaweka kituo na kushusha pumzi ndefu akifikiri. Baada ya kitambo kifupi cha ukimya wa tafakuri akaendelea.

“Sasa turudi kwenye kisa chetu, kilichokupelekea uniite hapa siku ya leo. Hayo uliyosema yanauhusiano gani na wito wangu?’’ Jacob akauliza huku akipiga mkupuo mkubwa wa sharubati iliyokuwa kwenye bilauri.

"Swali zuri! Miaka kadhaa iliyopita, mchakato wa kutafiti na kupima uwepo na kiwango cha gesi mkoani Mtwara ulianza. Ili kuridhia matakwa ya kimataifa, kuhusiana na nishati zenye mlipuko. Serikali ililazimika kutafuta makampuni makubwa ya kimataifa, yenye uzoefu na kazi ya upimaji na uchimbaji wa gesi Mtwara. Serikali ya Tanzania ikatangaza tenda. Kampuni tatu za kimarekani na mbili za ulaya zikaomba kupewa fursa ya kufanya kazi hiyo. Baada ya kupima na kujulikana kiasi cha gesi inayopatikana hapa nchini, thamani yake ingepatikana. Hapo sasa makampuni ya uchimbani yangeanza kuomba tenda ya kuchimba gesi hiyo.

Kwa vyovyote vile ilivyo, mchakato huu ni mkubwa na hautakuwa na maslahi kwa Tanzania na nchi washirika peke yake. Bali kuna nchi nyingi sana ambazo kwa vyovyote zitaweka mikono yake katika mchakato huo. Hapo ndipo matumizi ya wale watu wetu wawili waliosomeshwa na Mwalimu Nyerere yanapokuja.” Bi. Anita akaweka kituo kabla ya kuendelea.

“Watu wetu hao wanaheshimika na kusifiwa ndani ya Umoja wa Mataifa. Tayari serikali imeshawapa taarifa kuhusu hili suala la kugunduliwa kwa gesi hapa nchini. Taarifa ziliwafikia kupitia Idara ya Usalama wa Nchi yetu. Halikuwa jambo jipya kwa vile tayari walikuwa na tetesi za mchakato huo. Hivyo mapema baada ya kupata taarifa, wakaanza maandalizi ya chini kwa chini.”

“Kwa bahati nzuri mmoja wa hao watu wetu, aliombwa na kampuni moja ya Marekani. Wakimtaka awe kwenye timu yao ya wataalamuu, ambayo ingekuja kufanya kazi nchini. Endapo serikali ya Tanzania ingewapa zabuni ya kupima kiwango cha gesi iliyopo. Mtu huyo ni mwanamke, anaitwa Judith Muga. Mara moja alipotakiwa kuingia kwenye timu hiyo ya kigeni, aliamua kuitaarifu serikali yetu. Kwa kuzingatia hilo, serikali ikaamua kwa makusudi, kuichagua kampuni hiyo kuongoza mchakato huo. Huku wakijua fika kuwa kampuni hiyo itatoa nafasi kwa mtu wetu kufanya nayo kazi. Kampuni hiyo ingefanya kazi na makampuni mengine kutoka nchi kumi, ambazo zingekuwa waangalizi huru wa mchakato mzima.” Bi. Anita akaweka kituo kabla ya kuendelea.

“Kwa sababu hiyo, Judith Muga amekuwa hapa Tanzania kwa zaidi ya mwaka mmoja. Akishirikiana na wataalamuu wa kampuni hiyo ya kigeni pamoja na washika dau wengine muhimu. Amepewa mkataba wa awali, mwaka mmoja uliyopita.” Bi. Anita akaweka kituo kama anayefikiri jambo, kisha akasema.

“Nilikwambia watanzania waliopandikizwa walikuwa wawili. Tayari nimemwongelea Judith Muga. Mtanzania mwingine Ivan Mabala, yeye aliingizwa kwenye Kamati ya Baraza la Umoja wa Mataifa, ambayo inashughulika na usalama wa raia katika matumizi ya nishati. Umoja wa Mataifa kwa kuhofia kuwa malengo ya kibiashara yanaweza kusahau kutazama usalama wa raia, uliweka kitengo hiki. Kazi kubwa ya kitengo hiki ni kuhakiki na kuwakilisha maslahi ya raia popote kunapoanzishwa mradi mkubwa wa kuchimba na kuchakata nishati. Kamati hii ndiyo ambayo huangalia mambo kama vile; uharibifu wa mazingira na kuhakikisha hakuna madhara kwa raia, kutokana na taka zitakazozalishwa na miradi ya kuchakata na kuchimba nishati.” Bi. Anita akaweka kitoa na kumtazama Jacob. Haraka akaridhika kuwa maelezo yake yalimuelea vyema. Kisha akaendelea.

“Hivyo basi, wawakilishi wa kamati hiyo, ilikuwa ni lazima wawepo kwenye shughuli ya Mtwara. Unaweza kujiuliza kisa chetu kinaingiaje hapa? Ni hivi! Kuna mambo matatu yametokea ndani ya wiki tatu zilizopita. Mambo hayo yanatia shaka sana, kiasi kwamba waziri mkuu ameomba kitengo chetu kiingilie kuchunguza. Nimefikiri kwa kina alichosema na nimekubali kuwa, sisi tukiwa kitengo cha ujasusi cha nchi hii, hatutakiwi kunyamaza na kuendelea kusubiri.”

“Nini kimetokea?” Jacob akauliza kwa shauku.

“Hatua ya kupima kiasi cha gesi iliyopo imeshafanyika. Ripoti ya awali ilishaandaliwa. Kilichobaki ni serikali kuipitia rasmi ripoti hiyo na rais kutia saini. Rais akishatia saini, ripoti hiyo itasambazwa kwenye soko la kimataifa kama tangazo rasmi la serikali ya Tanzania, kukaribisha wawekezaji wa kuchimba gesi iliyoko mkoani Mtwara. Hapo ndipo wadau watakaporusha vyema karata zao.” Bi. Anita akaweka kituo na kumtazama Jacob Matata kwa makini. Kisha akaendelea.

“Shida iliyojitokeza sasa, baada ya kazi ngumu ya mwaka mzima, ya kuchunguza na kupima upatikanaji wa gesi ya Mtwara, ripoti hiyo ilikamilika. Japokuwa Judith alikuwa anafanya kazi kwa niaba ya kampuni iliyomuajiri, lakini Tanzania ilikuwa ikimtegemea sana katika maoni yake kabla ya rais hajatia saini. Judith angeshirikiana kwa siri na maafisa wengine wa wizara ya Nishati na Madini, kupitia ripoti hiyo na kisha kuiwasilisha kwa rais. Ushiriki wa Judith, kama mtu muhimu wa serikali, ulikuwa kwa siri kubwa. Lakini ilikuwa wazi kuwa, katika Wizara ya Nishati na Madini, hapakuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kitaalamuu na uzoefu wa kusimamia mchakato huo. Hivyo kazi hiyo ilimtegemea sana Judith. Sasa jambo la kushangaza ni kuwa, hadi wakati huu tunavyoongea, ripoti ya gesi ya Mtwara imetoweka kwenye mazingira ya kutatanisha.”

“Unamaanisha nini? Kama ripoti halisi haionekani, wadau muhimu wa mchakato huo, kama Judith na wawakilishi wa makampuni shiriki. Si watakuwa na nakala kwenye compyuta zao?’’ Jacob akahoji kwa namna ya kuonesha kuwa hapakuwa na tatizo kubwa.

“Hiyo ndiyo sababu iliyonipelekea kukuitaka uingilie kati kisa hiki cha kusisimua. Judith Muga, ambaye ndiye alikuwa na nakala ya mwisho ya ripoti hiyo. Akiwa na jukumu la kuisoma na kuihakiki, kabla ya kuiwasilisha na hatimaye kupitishwa na rais. Ametoweka, huku juhudi za kujua alipo, zikigonga mwamba.” Bi. Anita akaweka kituo na kupiga mwayo hafifu. Jacob Matata akabaki ametumbua macho huku akili yake ikijenga shauku. Wakati huu, maswali mengi yalipita kichwani mwake na kuibua hoja zenye maswali lukuki. Bi. Anita akaendelea.
“Kuna kosa limefanyika mahali fulani.” Bi. Anita akaongea huku akifikiri.
“Kosa gani?” Jacob akadadisi.
“Hakuna afisa mwingine wa serikali aliyekuwa na nakala ya ripoti hiyo na bahati mbaya haikuwahi kuchapishwa. Sehemu pekee ripoti hiyo ilipokuwa imehifadhiwa ni kwenye kompyuta ya Judith. Hivyo kutoweka kwa Judith, kumetokea sambamba na kutoweka kwa ripoti hiyo ya gesi ya Mtwara.” Bi. Anita akaweka kituo.
“Kwanini tusiwaombe wataalamuu wengine, walioshirika mchakato huo watupatie nakala zao?’’

“Hapo ndiyo suala lingine linapoibuka. Ndege iliyokuwa imebeba wataalamuu, waliokamilisha uchunguzi na mchanganuo wa gesi ya Mtwara, imeangushwa siku kadhaa zilizopita. Bila shaka taarifa unazo, kwani hiyo ndiyo habari ya mjini kwa sasa. Jambo la kushangaza, yule mtanzania mwingine aliyepewa uraia wa Urusi. Bwana Ivan Mabala, ameuawa wiki moja iliyopita. Wakati ambapo taifa linategemea sana uwepo wake kwa siri.” Bi. Anita akaweka kituo, huku macho yake makali yakimtazama Jacob Matata kwa utulivu. Mara hii aliweza kubaini jinsi uso wa Jacob ulivyobadilika na kuchukua uzito unaostahili, kutokana na kile alichokuwa akimwambia.

“Ulisema uhusiano wa Judith Muga na serikali, ulikuwa wa siri sana. Umewahi kufikiri kuwa Judith anaweza kutusaliti? Halafu pamoja na ndege hiyo kuanguka yenyewe ama kuangushwa, bado hainiingii akilini kuwa, hatuwezi kupata ripoti hiyo kutoka kwenye kompyuta za watu hao!’’ Jacob akatia shaka huku akifikiri.

“Judith Muga alitoweka baada ya kutoweka kwa Waziri wa Ulinzi, Sabodo Msumari. Hapo awali haikuwa wazi kama alikuwa ametekwa au ameuawa au vyote kwa pamoja. Lakini baada ya Judith kutoweka, inaonekana Sabodo alitekwa na watu waliotaka kujua taarifa za Judith. Sabodo ndiye mtu pekee aliyekuwa akifahamu mahali anapoishi Judith. Hivyo inawezekana Sabodo aliuawa baada kuhojiwa juu ya wapi alipokuwa akiishi Judith. Hadi sasa hatuwezi kujua, watu hao walifanikiwa kupata taarifa gani kutoka kwa Sabodo.”. Bi. Anita akafafanua zaidi.




“Hapo ndiyo suala lingine linapoibuka. Ndege iliyokuwa imebeba wataalamuu, waliokamilisha uchunguzi na mchanganuo wa gesi ya Mtwara, imeangushwa siku kadhaa zilizopita. Bila shaka taarifa unazo, kwani hiyo ndiyo habari ya mjini kwa sasa. Jambo la kushangaza, yule mtanzania mwingine aliyepewa uraia wa Urusi. Bwana Ivan Mabala, ameuawa wiki moja iliyopita. Wakati ambapo taifa linategemea sana uwepo wake kwa siri.” Bi. Anita akaweka kituo, huku macho yake makali yakimtazama Jacob Matata kwa utulivu. Mara hii aliweza kubaini jinsi uso wa Jacob ulivyobadilika na kuchukua uzito unaostahili, kutokana na kile alichokuwa akimwambia.

“Ulisema uhusiano wa Judith Muga na serikali, ulikuwa wa siri sana. Umewahi kufikiri kuwa Judith anaweza kutusaliti? Halafu pamoja na ndege hiyo kuanguka yenyewe ama kuangushwa, bado hainiingii akilini kuwa, hatuwezi kupata ripoti hiyo kutoka kwenye kompyuta za watu hao!’’ Jacob akatia shaka huku akifikiri.

“Judith Muga alitoweka baada ya kutoweka kwa Waziri wa Ulinzi, Sabodo Msumari. Hapo awali haikuwa wazi kama alikuwa ametekwa au ameuawa au vyote kwa pamoja. Lakini baada ya Judith kutoweka, inaonekana Sabodo alitekwa na watu waliotaka kujua taarifa za Judith. Sabodo ndiye mtu pekee aliyekuwa akifahamu mahali anapoishi Judith. Hivyo inawezekana Sabodo aliuawa baada kuhojiwa juu ya wapi alipokuwa akiishi Judith. Hadi sasa hatuwezi kujua, watu hao walifanikiwa kupata taarifa gani kutoka kwa Sabodo.”. Bi. Anita akafafanua zaidi

“Kutekwa kwa Judith Muga na kutokuwepo kwa ripoti ya awali ya gesi ya Mtwara. Kuna maanisha kuwa, uwekezaji tulioufanya kwa miaka mingi, hauwezi kutekelezeka!

“Siamini kuwa kutoweka kwa Judith, kuuawa kwa Ivan na kupotea kwa ripoti ya awali, ni jambo la bahati mbaya. While this is not impossible to be coincidence, it is not a very attractive option since there is something troubling about the idea of systematic coincidences. Hali ya kimazingira na muda matukio yanayotokea, vinanifanya nihisi kuna jambo kubwa linaloendelea sirini.” Bi. Anita akaweka kituo na kukohoa kidogo, kusafisha koo lake.

"Inavyooneka watu hawa hawataki ripoti ya gesi itoke. Kama hilo ndiyo lengo lao wawaue Judith na Sabodo? Kwa nini inadhaniwa kuwa ile ndege iliangushwa kwa hila? Kulikuwa na ulazima gani wa kuwaua wataalamuu wa makampuni yaliyotaka kupata zabuni ya kuchimba gesi?’’ Jacob akajipa tafakuri yenye maswali kichwani. Bi. Anita akafikiri kidogo kabla ya kusema.

“Haina chembe ya shaka kuwa mradi wa gesi yetu ni wa fedha nyingi. Hii inapelekea mradi huu kuwa wa muhimu sana karne ijayo kwa taifa letu. Halafu unaweza kuleta hali tofauti kwenye soko la dunia. Nguvu ya pesa ndiyo hupelekea maamuzi makubwa ya kiuchumia. Hatuwezi kulifumbia macho suala hili. Miaka zaidi ya thelathini imepita lakini Mwalimu Nyerere aliona umuhimu wake, ndiyo maana akaandaa mkakati huu. Tutakuwa wajinga kama tutaamini kuwa, wazungu wanaweza kutupa taarifa sahihi, na kufanya mikataba sahihi na sisi, katika hili. Tunahitaji mtu tunayemwamini, ambaye anaweza kutupa taarifa sahihi na thamani halisi ya gesi tuliyonayo. Ndiyo maana hapo awali ulishangaa, nilipokwambia kuwa tuna wataalamuu wengi duniani. Ni kweli tuna wataalamuu wengi tu, lakini kwa dunia ya sasa, tunahitaji mtu awe mzalendo na mtaalamuu. Akiwa mtaalamuu tu bila uzalendo, ataishia kufanya uamuzi wa kujinufaisha, katika dunia hii inayoendeshwa kwa nguvu ya pesa.

Kuwa na mtaalamuu ambaye siyo mzalendo, ni sawa na kuwa na bunduki isiyokuwa na risasi. Mtu akiwa mzalendo tu bila utaalamuu, vilevile hawezi kutusaidia kitu. Kutoweka kwa hawa watu wawili, kunatufanya tusiwe tofauti na wale babu zetu wa zamani, machifu. Ambao walifanya mikataba na wakoloni, pasipokuwa na ufahamu sahihi. Matokeo yake wakajikuta wanadhulumiwa haki zao bila kupenda.” Bi. Anita akaweka kituo akifikiri kidogo, kisha akaendelea.

“Jambo lingine la ajabu, limekuja kugundulika baada ya ile ndege kuanguka. Ndiyo ikawa wazi kuwa, kuna watu wako nyuma ya mchezo mchafu unaoendelea. Kwenye dunia ya sasa, kuanguka kwa ndege kumekuwa ni jambo la kawaida. Hata hivyo kutokana na mazingira yetu, tunajiridhisha kusema, jambo hili ni hatari, kwa sababu kuu mbili. Moja, ndege ile ilikuwa imebeba wataalamuu, ambao walikuwa wamemaliza kuandika taarifa za upembuzi wa awali, kuhusiana na gesi ya Mtwara. Wataalamuu hao kumi na tano, kutoka makampuni mbalimbali duniani. Walikuwa wakirudi kwenye nchi zao, tayari kuwasilisha ripoti juu ya tathmini yao kuhusu mradi wa gesi ya Mtwara. Baada ya hapo, viongozi wao wangewaanda na kuwatuma kwa mara ya pili, kwa ajili kushindania zabuni ya kuchimba gesi hiyo. Kulikuwa na mvutano mkubwa juu ya ukweli kuhusu, kiasi na thamani halisi ya gesi hiyo. Bila shaka taarifa hizo ulizisikia. Ilifikia wakati ambapo baadhi ya wataalamuu waliikataa taarifa ya awali, juu ya upembuzi yakinifu wa gesi hiyo”

“Bahati mbaya wakati wakirudi, ndege yao ikaanguka. Jambo la ajabu ni kuwa, siku tatu kabla ya taarifa hiyo ya awali kukamilika. Imegundulika kuwa, watu hao walikosa mawasiliano ya mtandao na makampuni yao. Hivyo hawakufanikiwa kutuma taarifa hiyo ya awali…”
“Sijakuelewa! Unaposema walikosa mawasiliano?’’ Jacob akamkatisha Bi. Anita.
“Inasemekana kuwa, kompyuta zao zilikuwa zimeunganishwa na utunzaji wa taarifa wa moja kwa moja, kwenda makao makuu ya kampuni zao. Yaani, disc za kompyuta zao, zilikuwa zimeunganishwa moja kwa moja, kwenye server za makao makuu. Hivyo, chochote walichokuwa wakikifanya kwenye kompyuta zao, kokote wanapokuwa. Kilikuwa kinahifadhiwa moja kwa moja kwenye stoo ya taarifa, yalipo makao makuu ya kampuni zao. Hivyo basi, ikitokea kuwa wamepotea, kuibiwa au kuharibikiwa na kompyuta zao. Taarifa zote zilizokuwa kwenye kumpyuta zao, zinaweza kupatikana makao makuu ya makampuni zao. Sasa, tangu walipoanza kuandika taarifa ya gesi ya Mtwara hadi wanasafiri kurudi kwao, kulitokea hitilafu ambapo mawasiliano kati ya kumpyuta zao na zile za makao makuu yalikatika.” Bi. Anita alijaribu kufafanua.
“Hii ilikuwa kwa watu wote kumi na tano?’’ Jacob akauliza kutaka ufafanuzi.
“Ndiyo! imegundulika kuwa, tukio hilo lilitokea kwa watu wote, na kwa wakati mmoja. Baada ya ndege hiyo kuanguka, wataalamuu wetu walipewa taarifa na makampuni hayo. Tukaombwa kwenda eneo la ajali, kutafuta kompyuta za wataalamuu wao, ili waweze kupata kilichokuwemo. Wataalamuu wetu walipofika eneo la bahari, kulipotokea ajali hiyo ya ndege. Walifanikiwa kupata vitu vyote muhimu, lakini jambo la kushangaza, hawakupata hata kompyuta moja.
Ikumbukwe kuwa, ndege hiyo ilianguka dakika chache baada ya kuruka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Hii ina maanisha kuwa, ndege hiyo haikuwa umbali mrefu angani, kutoka usawa wa bahari.
Kwa vile ndege hiyo haikulipuka baada ya kuanguka baharini. Mizigo na miili ya abiria wengi ilitambulika. Kitu kingine cha kushangaza ni kwamba, mizigo ya wataalamuu hao haikupatikana. Jambo la ajabu zaidi ni kuwa, ushahidi unaonesha kuwa, miili ya wataalamuu hao, ilikuwa imepekuliwa ikiwa majini.” Bi. Anita akaweka kituo na kupiga mwayo hafifu, huku akifikicha macho yake kwa vidole.

“Hapo kweli kuna jambo limefichika. Kisanduku cheusi cha kurekodi taarifa ya safari ya ndege, kimepatikana?” Jacob akahoji huku akimtazama Bi. Anita kwa makini.

“Kisanduku cheusi kimepatikana na kipo sehemu salama. Tunatarajia taarifa zake zitasomwa siku chache zijazo.” Bi. Anita akaongea kwa hakika.
“Okay! sasa nimeanza kujenga hoja kichwani!’’ Jacob alisema huku akishusha pumzi ndefu. Baada ya ukimya mfupi wa tafakuri humo ndani akaendelea.
“Mimi ningeshauri jambo.”
“Jambo gani?” Bi. Anita akauliza kwa udadisi




“Hapo kweli kuna jambo limefichika. Kisanduku cheusi cha kurekodi taarifa ya safari ya ndege, kimepatikana?” Jacob akahoji huku akimtazama Bi. Anita kwa makini.

“Kisanduku cheusi kimepatikana na kipo sehemu salama. Tunatarajia taarifa zake zitasomwa siku chache zijazo.” Bi. Anita akaongea kwa hakika.
“Okay! sasa nimeanza kujenga hoja kichwani!’’ Jacob alisema huku akishusha pumzi ndefu. Baada ya ukimya mfupi wa tafakuri humo ndani akaendelea.
“Mimi ningeshauri jambo.”
“Jambo gani?” Bi. Anita akauliza kwa udadisi.
“Kama tunaona hakuna mtu wa kumwamini kufanya zoezi hili, kwa nini tusisitishe kwanza, wakati tukifikiria namna ya kufanya? Vilevile, huenda Judith Muga akapatikana, hivyo mchakato ukaendelea.’’
“Hapo ndiyo ugumu unapojitokeza Jacob. Wengi tulifikiria kama wewe lakini mheshimiwa Rais, Jovin Sekendu. Amekataa katakata kurudi nyuma kwenye dhamira yetu.
Amesisitiza tuendelee na mchakato. Sababu kubwa ni kwamba, wiki mbili zijazo, kuna nchi mbili za kiarabu, zinatarajiwa kutoa taarifa juu ya upatikanaji wa gesi katika nchi zao. Kupatikana kwa gesi ya Tanzania, kumekuwa tishio kubwa la biashara kwao. Hivyo wanafurahia kuona mchakato wa upatikani wa gesi Tanzania unachelewa, ili wawavutie wawekezaji nchini kwao. Kupatikana kwa gesi yetu kwenye soko la kimataifa, kunaweza kuwafanya wanunuzi waje kwetu badala ya kwenda kwao.
Judith Muga asipopatikana, kazi yote iliyofanyika itakuwa bure. Badala yake itabidi kuanza mchakato upya huku gharama mara mbili ikitumika. Hicho ndiyo wanachotaka wapinzani wetu.” Bi. Anita akaweka kituo kabla ya kuongeza.

“Mbali na hayo…” Bi. Anita akaweka kituo kifupi kufikiri.

“Endelea nakusikia.” Jacob akasisitiza huku amejenga shauku.

“Kitendo cha ile ndege kuangushwa, ni ujumbe tosha kwa nchi za magharibi, kuwa Tanzania siyo sehemu salama kwa uwekezaji. Hivyo tukio hili naliona kama ujasusi wa kiuchumi. Adui zetu wamepanga kutuchafua na kututoa mchezoni haraka.” Bi. Anita akaweka kituo na kuendelea.

“Kuna kitu hapa Jacob Matata. Tunataka kupata ukweli wa mambo. Nahisi kama kuna jambo baya linafanyika ndani ya nchi yetu. Tutakuwa tumeshindwa kutimiza wajibu wetu, kama tutakaa kimya bila kuchunguza. Hakuna nchi inayofurahia kuhujumiwa. Tunatakiwa kulichukulia suala hili kwa mtazamo wa kina zaidi. Tukikaa kimya ni sawa na kuonesha kuridhishwa na hujuma hizi. Ingawa hatuna hakika na hisia zetu lakini ni muhimu kujiridhisha. Hivyo lazima upelelezi wa kina ufanyike na kuja na majibu yasiyo na maswali.” Bi. Anita akaweka mkazo.

Jacob Matata hakutia neno, badala yake akabaki akimtazama bosi wake kwa utulivu. Akili yake ilishatia shaka juu mambo aliyoyasikia. Moyoni akahisi kuumia. Mara hii akahisi watu wake wanaonewa. Alipokohoa kusafisha koo lake, akavunja ukimya.

“Nahisi kuna mchezo mchafu unaoendelea. Kuna washenzi nyuma ya mchakato huu. Sijui kwa nini wanadhani wao ndiyo wana haki ya kuendelea kufanikiwa. Kila nchi masikini zinapopata mlango wa kutokea, wao hutafuta namna ya kuuziba. Washenzi sana hawa watu wa magharibi!”Jacob akalaani vikali.

“Sasa upele umempata mkunaji.” Bi. Anita akasema moyoni huku akimtazama Jacob kwa hamasa. Alimfahamu vyema Jacob Matata, kuwa akishaamua kuvalia njuga suala fulani, majibu ni lazima yapatikane. Alifurahi kuona maelezo yake yalikuwa yamemuelea vyema Jacob, hadi akaona uzito wa hatari iliyopo. Baada ya ukimya mfupi wa tafakuri Bi. Anita akavunja ukimya.

“Kama nilivyokwisha kusema hapo awali, Waziri Mkuu, Mhe. Silas Kiondo. Amenipigia simu usiku wa jana. Amesema anataka kuona kitengo chetu kinashughulikia hili suala kikamilifu. Najua hawezi kutoa amri hiyo bila kukubaliana na mkuu wake wa kazi. Kama ujuavyo kuwa wao wawili ndiyo wanaofahamu, juu ya uwepo wa kitengo hiki cha siri. Hivyo saa tatu na nusu asubuhi hii, tutaenda kuonana na Mhe. Silas Kiondo. Tunataka kupata maelezo zaidi juu ya jambo hili.
Nimeona ni vyema nikazungumza na wewe kitaalamuu, kabla hatuajenda kuonana na Mhe. Silas Kiondo. Kitaalamuu, nadhani jambo hili kwa sasa linaweza kutatuliwa kutokea pande mbili. Mosi, ni kufanya jitihada ili Judith Muga apatikane. Au kuhakikisha watu wote walio nyuma ya mpango huu, wanapatikana na kutiwa nguvuni. Ili kuidhihirishia jamii ya kimataifa kuwa Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza”
“Huenda tutakapoonana na Mhe. Silas Kiondo usipate maelezo kama haya. Kwa vile sitokuwa mzungumzaji mkuu. Jambo moja…” Bi. Anita akaweka kituo na kumtazama Jacob kwa makini.
“Jambo gani?” Jacob akauliza kwa udadisi.
“Ni vyema ukazingatia kuwa, kwa hali ilivyo sasa. Haitakiwi kumwamini mtu yeyote, aliye ndani au nje ya serikali.” Sauti ya Bi. Anita ilikuwa kavu na thabiti. Ilikuwa wazi kuwa Bi. Anita alikuwa amefanikiwa kumfanya mpelelezi Jacob Matata. Aone uzito wa suala lililokuwa mbele yao, na umuhimu wa kulitafutia ufumbuzi kwa haraka.

"Labda ni vyema ukafahamu kuwa, Judith Muga, alikuwa akiishi Masaki. Mtaa wa Chakechake, nyumba namba 0713C. Mlango wa nyumba hiyo ulikutwa umevunjwa. Uchunguzi uliofanyika, unaonesha kulitokea patashika kabla Judith hajachukuliwa.” Bi. Anita akaongea kwa utulivu, huku akiitazama saa yake ya mkononi. Hatimaye akasimama.
“Sasa tunaweza kwenda kuonana na Mhe. Waziri Mkuu, sehemu tuliyokubaliana kuonana.”

Jacob Matata akashusha pumzi ndefu. Tukio hilo likampelekea Bi. Anita apishe tabasamu jepesi usoni mwake. Mara hii alikuwa na furaha, kuona Jacob Matata alikuwa tayari kuingia kazini.

“Lo! Sasa naelewa kuwa, kutekwa kwa Judith Muga na kuuawa kwa Ivan Mabala. Ni mpango wa kuifanya Tanzania ipate kigugumizi, katika kukamilisha ripoti yake juu ya gesi ya Mtwara. Matokeo yake, ni kucheleweshwa kwa mchakato wa upatikanaji wa gesi hiyo. Kwa vile mchakato wote lazima uanze upya. Hii inazipa nafasi zile nchi mbili za kiarabu, kuingia sokoni kabla yetu.” Jacob Matata akaweka kituo akifikiri kabla ya kuendelea.

“Kitendo cha ile ndege kuanguka, tafsiri yake ni sawa na kusema, hakuna usalama wa kutosha eneo hili. Hivyo siyo eneo salama la kufanya uwekezaji mkubwa. It is clear now!. Ili ripoti hiyo ipatikane, ni lazima Judith Muga apatikane. Halafu ni lazima ijulikane, kama ndege ile ilianguka kwa hitilafu ya kawaida au ilihujumiwa. Ili kufahamu ukweli huo, ni lazima kisanduku cheusi cha kurekodi matukio na taarifa ya safari ya ndege, kipatikane. Mh! Hapo kazi ipo! tena si ya kitoto.” Jacob akasema huku akisimama tayari kuondoka.

“Naam! Sasa umenielewa vyema Jacob. Najua inaweza kuwa kazi ngumu, na ya hatari. Hii inatokana na namna watu hao wasiojulikana, walivyopanga vyema matukio yao na kuyatekeleza kwa ufundi wa hali ya juu, tena ndani ya muda mfupi. Watu hawa ni dhahiri wamejiandaa na wako tayari kwa lolote.” Bi. Anita akaonesha wasiwasi wake.

“Najisikia heshima kubwa kupewa nafasi hii. Nimekaa likizo ndefu bila kujishughulisha na mambo ya hatari. Siwezi kukataa kazi ninayoipenda. Yeyote aliyeko nyuma ya mpango huu ni lazima aoneshwe cha mtema kuni.” Jacob akasisitiza.

Ilikuwa tayari imetimu saa tatu kasoro dakika chache asubuhi, wakati mpelelezi Jacob Matata na mkuu wa kitengo cha kijasusi, kiitwacho Ofisi Fukuzi, Bi. Anita. Walipoondoka kwenye chumba walichokuwa wakiendelea na mazungumzo yao. Tayari kwenda kuonana na Waziri Mkuu, Mhe. Silas Kiondo.




Ilikuwa saa tatu kasoro dakika nne asubuhi wakati mpelelezi Jacob Matata na Bi. Anita mkuu wa kitengo cha kijasusi kiitwacho Ofisi Fukuzi walipoondoka kwenye chumba walichokuwa wanafanyia maongezi yao tayari kwenda kuonana na Waziri Mkuu Mhe. Silas Kiondo.

* * *

WAKATI ambao Jacob Matata na Bi. Anita walikuwa wamemaliza kikao chao, kuna watu wengine wawili walikuwa wana kikao chao cha siri sehemu nyingine ndani ya jiji hilohilo la Dar es salaam. Watu hao ni Ngongoseke na Poka Kingu. Ngongoseke ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wa nyumba hii ambayo kikao kilikuwa kinafanyika, alimwangalia tena mgeni wake. Mgeni aitwaye Poka Kingu. Alimwangalia kuanzia juu akamshusha hadi chini, halafu macho yakapanda taratibu hadi juu. Poka Kingu alikuwa na kichwa kikubwa cha mviringo kilichobeba macho madogo mekundu. Pua pana isiyoendana na ukubwa wa mdomo na macho yake. Macho ambayo yalifanya kichwa kionekane kama boga la kiangazi lililotobolewa matundu mawili. Alikuwa kama mtu aliyekuwa kwenye shimo chafu kwa muda mrefu. Nywele zake fupi, chafu, zenye udongo ukiokaa kama ukungu kwenye chumba cha kuhifadhia ndoo za mafuta ya kupikia. Alishuka shingoni, hakusubiri kuambiwa kuwa shingo hiyo ilikuwa sugu sana na misuli iliyoonyesha kuwa ilikuwa dhaifu kwa kukosa matunzo. Ilikuwa kama mti wa mnazi uliozeeka. Chini kidogo ya shingo hiyo ambapo inaunganika na kifua aliweza kuona mapigo ya moyo wa mtu huyo yalivyokuwa yakiinua na kuiachia ngozi ya mahali hapo. Ilikuwa wazi kuwa mapigo hayo ya moyo yalikuwa dhaifu sana ambayo hayakwenda sawa na kasi ya kawaida ya mapigo ya moyo.

Ngongoseke alijikuta akimhusudu Poka Kingu. Tangu alipomtoa gerezani, tayari Poka alikuwa ameshafanya mambo mengi makubwa aliyoagizwa na Ngongoseke bila kujali kujua kiini cha mambo. Na sasa ndiyo walikuwa wakionana rasmi kwa makubaliano na mkataba wa kazi.

“Kahawa tafadhali.” Hatimaye Poka alisema katika sauti ya kukwaruzakwaruza huku akiangalia kwa yale macho yake madogo. Ngongoseke hakubisha, aliinuka kwenda kuandaa kahawa kama alivyokuwa ameombwa na mgeni wake huyu.
“Kali, kati au hafifu!” Ngongoseke aliuliza.
“Inayofaa kunywewa na mtu kama mimi.” Poka alijibu bila kuinua kichwa wala kujitingisha. Mwenyeji hakuuliza swali zaidi. Dakika tano baadaye Kahawa ilikuwa tayari, ilikuwa imewekwa kwenye kikombe cha glasi cheupe, hivyo iliweza kuonekana jinsi ilivyokuwa nyeusi sana kama lami.

“Haya niambie kilichofanya mnitoe gerezani. Maana najua si bure kuna kitu?’’ Hatimaye Poka Kingu alihoji, akimwangalia mwenyeji wake usoni. Macho ya Ngongoseke, yalikuwa yametuama kwenye kifua cha mgeni wake huyo. Poka alikuwa kifua wazi, kilionekana dhahiri. Hakikuwa kikubwa wala kujazwa na minofu. Lakini mishipa iliyokuwa imetapakaa kwenye kifua hicho ilimwambia Ngongoseke kuwa Poka Kingu hakuwa wa kucheza naye.

“Kwanza nikushuru kwa kazi uliyofanya hadi sasa. Maana ilikuwa dharula lakini umeweza kusimamia vema timu yangu iliyokuwa chini ya Frank Misanya hapo kabla. Ni matumaini yangu kuwa mmefanikiwa kufuta kila ushahidi na lolote linalohusiana na kuanguka kwa ile ndege.” Ngongoseke alisema kwa tuo. Halafu akaongeza, “Mambo mawili tu ambayo kwa nikujuavyo wewe ni kazi nyepesi tu. Kifo cha Jacob Matata na kupatikana kwa kisanduku cheusi cha kurekodia taarifa za ndege. Sijui utafanyaje na itagharimu kiasi gani lakini kufanyika kwa haya mawili thamani yake ni kubwa kuliko unavyoweza kudhani. Kwa kifupi kuna mpango mkubwa sana unafuatiliwa hapa nchini. Nchi kumi na moja zimetuma majasusi wao ili kuhakikisha mambo yanawaendea vema na wanafanikiwa kwenye hili suala la gesi kwa namna moja ama nyingine. Iran, China, Urusi, Marekani, Uingereza, Saudia, Ufaransa, Japan, Ujerumani, Iraq na Italia zimeleta watu wao. Nchi hizo ziko katika makundi mawili japo hawajijui. Kuna wanaotaka kile nifanyacho na wasiotaka kile nifanyacho”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog