Search This Blog

Monday 27 March 2023

KIZUNGUMKUTI ! - 3

  


Simulizi : Kizungumkuti !

Sehemu Ya Tatu (3)


“Sawa, nitajaribu,” alisema huku akishusha pumzi ndefu kana kwamba alikuwa ametoka kwenye mashindano ya mbio ndefu.


“Usiseme utajaribu, tunachotaka ufanye kweli,” Carlos alimsisitiza kwa sauti tulivu lakini yenye kuamuru.


“Sawa, nitafanya,” Jasmine alisema na kuwafanya Jacky na Carlos watazamane na kutabasamu, kisha wakapeana ishara ya kuondoka. Walisimama wakamuaga Jasmine na kuondoka wakimwacha bado yupo katika hali ya sintofahamu.


Walipotoka nje ya ile nyumba ya Jasmine, Carlos na Jacky waliingia kwenye gari lao la kifahari aina ya Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe.


Jacky ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari, aliliondoa kwa utulivu na mara tu baada ya kuyaacha maskani ya Jasmine walishika uelekeo wa barabara ya lami iliyokuwa ikielekea kwenye machinjio ya ng’ombe ya Vingunguti.


Katika barabara ile kulikuwa na magari mengi katika muda ule wa jioni yaliyotokea katikati ya mji, hivyo Jacky alilazimika kuendesha gari lake kwa mwendo wa kawaida, japo alikuwa na haraka.


Wakati wakiwa katika barabara ile macho ya Carlos yalikuwa makini sana kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kama kulikuwa na gari lolote au pikipiki iliyoonesha ishara ya kuwafuatilia nyendo zao. Walivuka daraja la Mto Msimbazi na baada ya mwendo wa dakika chache walifika katika eneo la Barakuda.


Kisha walishika barabara ya kuelekea Segerea na baada ya mwendo mrefu hatimaye safari yao iliwafikisha katika makazi yao ya kisasa katika eneo la watu wenye ukwasi. Lile gari likafunga breki mbele ya geti kubwa jeusi la jumba moja kubwa la ghorofa mbili lililozungukwa na miti mirefu ya kivuli na ukuta mrefu wenye usalama wa uhakika.


Muda ule mvua ya wastani ilikuwa inanyesha, hata hivyo haikuwazuia kuingia ndani ya jumba lao la kifahari.


Jacky alibonyeza remote na mara lile geti jeusi likaanza kufunguka taratibu, kisha gari akaliingiza lile ndani ya uzio mrefu wa lile jumba uliokuwa umefungwa mfumo maalumu ya umeme wa kuzuia wezi juu yake.



Kisha walishika barabara ya kuelekea Segerea na baada ya mwendo mrefu hatimaye safari yao iliwafikisha katika makazi yao ya kisasa katika eneo la watu wenye ukwasi. Lile gari likafunga breki mbele ya geti kubwa jeusi la jumba moja kubwa la ghorofa mbili lililozungukwa na miti mirefu ya kivuli na ukuta mrefu wenye usalama wa uhakika.


Muda ule mvua ya wastani ilikuwa inanyesha, hata hivyo haikuwazuia kuingia ndani ya jumba lao la kifahari.


Jacky alibonyeza remote na mara lile geti jeusi likaanza kufunguka taratibu, kisha gari akaliingiza lile ndani ya uzio mrefu wa lile jumba uliokuwa umefungwa mfumo maalumu ya umeme wa kuzuia wezi juu yake.


Endelea...


Jacky aliliegesha vizuri gari kisha wote wakashuka na kuanza kutembea haraka wakiuendea mlango mkubwa wa lile jumba lao, hata hivyo, Jacky alionekana kuchoka sana. Carlos aligundua na kumwangalia kwa makini.


“My love, you seem very tired today!” (Mpenzi, unaonekana umechoka sana leo!) Carlos alimwambia Jacky huku akimtazama kwa makini kisha akafungua mlango wa mbele wa lile jumba.


“I really feel tired. I think I need a break,” (Ni kweli ninahisi uchovu mwingi. Nadhani nahitaji mapumziko) Jacky alisema huku akirembua macho yake malegevu na kuingia ndani huku akiufunga mlango nyuma yake.


Kutokana na uchovu alijitupa kwenye sofa pale sebuleni huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani. Hata hivyo, jioni ile ilionekana kuwa usiku tulivu mno, na haukupita muda tangu Carlos na Jacky waingie ndani na kuketi pale sebuleni mvua kubwa ilianza kunyesha.


“Darling, are you sure that Jasmine will help us?” (Mpenzi, una uhakika kwamba Jasmine atatusaidia?) Jacky alimuuliza Carlos kwa wasiwasi baada ya kumtazama kwa makini.


“Believe me, my love, she will help us, don’t you trust her?” (Niamini mpenzi, atatusaidia, kwani humuamini?) Carlos alimjibu Jacky huku akijiinua kutoka pale kwenye sofa.


“I don’t know, but she’s just an innocent girl,” (Hata sijui, lakini ni binti asiye na makuu) Jacky alisema huku akipiga mwayo mrefu wa uchovu.


“Jacky, you seem you didn’t get enough sleep last night. Twende ukaoge kwanza uondoe uchovu,” Carlos alimwambia Jacky kwa sauti tulivu ya upole huku akimwangalia kwa makini kisha alimshika mkono na kumuinua kutoka pale kwenye sofa.


Jacky alitii na kuinuka, kisha Carlos akamuongoza hadi kwenye ngazi za kuelekea chumbani kwao kwenye ghorofa ya kwanza kulikokuwa na chumba kikubwa cha kifahari kilichoonekana kuwa na nafasi kubwa ya kutosha.


Katika kile chumba kulikuwa na kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita cha samadari cha mbao ngumu za mninga kilichonakshiwa vizuri na kupendeza, kitanda kile kilikuwa katikati ya chumba na kilikuwa na droo mbili, moja katika kila upande wa kile kitanda, na juu ya droo zile kulikuwa na taa za rangi nyekundu.


Upande wa kulia na wa mbele wa kile chumba kulikuwa na madirisha makubwa mawili yaliyokuwa na vioo, madirisha yale yalikuwa yamefunikwa kwa mapazia marefu na mepesi. Dirisha moja lilikuwa upande wa mbele ambalo lilikuwa limeungana na mlango mmoja uliokuwa unatokea kwenye kibaraza cha ghorofani, yaani balcony.


Pale dirishani kwenye balcony kulikuwa na ua kubwa na zuri lililokuwa limepandwa kwenye chungu kikubwa cha udongo na kando ya lile ua kulikuwa na kiti kimoja cha kupumzikia kilichokuwa kinatazama nje. Pembeni ya kile kiti kulikuwa na meza ndogo na fupi ya mbao iliyokuwa na droo mbili.


Upande wa kushoto wa kile chumba kulikuwa na kabati kubwa la nguo la ukutani na kando ya lile kabati kulikuwa na meza nzuri nyeusi ya kioo. Juu ya ile meza kulikuwa na seti moja ya runinga kubwa Flat screen aina ya Samsung iliyokuwa katikati ya spika mbili za sistimu ya muziki maarufu kama Home threatre.


Upande ule ule wa kushoto wa kile chumba kulikuwa na kochi moja la kukaa watu wawili la sofa lililokuwa nadhifu na la kisasa likiwa juu ya zulia zuri la manyoya lenye rangi za ngozi ya Pundamilia.


Mbele ya lile kochi kulikuwa na meza ndogo ya mbao yenye umbo la nusu duara ambayo juu yake kulikuwa na chombo kidogo cha majivu ya sigara, kibiriti cha gesi, paketi mbili za sigara, chupa kubwa ya mvinyo mwekundu wa Kifaransa wa Navette de Marseille na bilauri ndefu mbili.


Upande wa kulia wa kile chumba kulikuwa na meza nzuri ya vipodozi iliyokuwa na vioo viwili virefu vya kujitazama na pembeni yake kulikuwa na mlango mwingine uliokuwa unaelekea kwenye chumba kikubwa cha maliwato. Ndani ya kile chumba cha maliwato kulikuwa na bafu la kisasa aina ya Jacuzzi. Pia kulikuwa na bomba la mvua kama mtu asingependa kutumia lile Jacuzzi.


Ukutani kulikuwa na picha tatu kubwa na nzuri, mbili zilikuwa ni za kuchorwa zilizokuwa zimetundikwa sehemu mbili tofauti, moja ilikuwa ni picha ya mbuga iliyoonesha wanyama wa porini na picha nyingine ilikuwa ya ua zuri la rangi nyekundu, njano na bluu lililokuwa limechorwa kwa ustadi wa hali ya juu.


Picha ya tatu ilikuwa ikiwaonesha Carlos na Jacky katika mavazi nadhifu ya harusi huku wakiwa na furaha kubwa katika siku yao ya harusi. Picha zote tatu zilikuwa zimewekwa ndani ya fremu nzuri za kioo na kuzifanya zionekane vizuri katika zile kuta safi zilizokuwa na rangi ya maziwa. Jacky alisimama pale katikati ya chumba huku akiendelea kupiga miayo ya uchovu.


“Dah! Carlos kacheza pele kweli kweli, anajua sana kumchunguza mtu na kuyasoma mawazo yake… hapa nilipo nimechoka sana na ninahitaji kupumzika, maana tangu jana nilipokimbizwa mchakamchaka usiku kucha na Yusuf na asubuhi tena nikakutana na gwaride la nguvu la Carlos sijapata kabisa wasaa wa kupumzika,” Jacky aliwaza huku akivua nguo zake akijiandaa kwenda kujimwagia maji.


Carlos alikuwa amesimama akimtazama Jacky kwa makini kama vile alikuwa akijaribu kuyasoma mawazo yake ili kujua alichokuwa anawaza, kisha akatoka na kuelekea sebuleni akimwacha Jacky anaendelea kutoa nguo zake kabla hajaelekea bafuni kuoga.


Jacky alipotoa nguo alisimama mbele ya kioo kirefu na kujiangalia kwa kitambo huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa, alijitazama akionekana kukitathmini kifua chake kilichokuwa kimebeba matiti madogo yenye chuchu ndogo zilizosimama kwa hasira zikiwa tayari kuitoboa blauzi yoyote ambayo angevaa.


Kisha macho yake yalishuka kutazama tumbo lake dogo na kitovu chake kilichotumbukia ndani na kuacha kishimo kidogo tumboni kilichoungana na mstari hafifu ambao ulikuwa umeshuka chini na kupotelea katikati ya mapaja yake huku ukikiacha kiuno chake chembamba na laini kikitanuka kwa namna ya kuvuta hisia za mwanamume yeyote hata angekuwa mgumu.


Kwa kitambo fulani Jacky aliganda pale kwenye kioo akijitazama kwa makini kisha akaachia tabasamu laini akionesha kuridhishwa na muonekano wake mzuri. Kisha aligeuka kutazama pale kwenye ile meza ndogo ya mbao yenye umbo la nusu duara iliyokuwa na chupa kubwa ya mvinyo mwekundu wa Kifaransa wa Navette de Marseille na bilauri ndefu.




Kisha macho yake yalishuka kutazama tumbo lake dogo na kitovu chake kilichotumbukia ndani na kuacha kishimo kidogo tumboni kilichoungana na mstari hafifu ambao ulikuwa umeshuka chini na kupotelea katikati ya mapaja yake huku ukikiacha kiuno chake chembamba na laini kikitanuka kwa namna ya kuvuta hisia za mwanamume yeyote hata angekuwa mgumu.


Kwa kitambo fulani Jacky aliganda pale kwenye kioo akijitazama kwa makini kisha akaachia tabasamu laini akionesha kuridhishwa na muonekano wake mzuri. Kisha aligeuka kutazama pale kwenye ile meza ndogo ya mbao yenye umbo la nusu duara iliyokuwa na chupa kubwa ya mvinyo mwekundu wa Kifaransa wa Navette de Marseille na bilauri ndefu.


Endelea...


Akapiga hatua zake taratibu akisogea pale kwenye ile meza huku kiuno chake laini kikicheza taratibu kwa kadiri alivyokuwa akipiga zile hatua, alipoifikia ile meza aliinama akanyanyua ile chupa kubwa ya mvinyo kisha akamimina mvinyo kwenye bilauri moja na kugida mafunda kadhaa ya mvinyo huku akiuacha mvinyo ukiteleza taratibu kooni mwake.


Alipiga tena funda jingine la mvinyo huku akionekana kuanza kupata uchangamfu kidogo kisha akaikita ile bilauri juu ya meza na kuingia bafuni ambako alifungulia maji kwenye lile Jacuzzi kisha akaingia ndani yake na kuzama akiacha sehemu ya juu na miguu tu huku sehemu nyingine ya mwili ikiwa ndani ya povu la maji yaliyokuwa yakichemka.


Wakati akiendelea kuoga taratibu ndani ya lile Jacuzzi mara akamuona Carlos akiingia na kusimama, Carlos alikuwa amevaa bukta ya bluu na singleti nyeupe na alikuwa akivuta sigara huku akimtazama Jacky kwa matamanio. Wakatazamana kwa nukta chache huku Carlos akiachia tabasamu la matamanio.


“Darling, what are you doing here? Please I’m really tired,” (Mpenzi, unataka kufanya nini? Tafadhali nimechoka kweli kweli) Jacky alimwambia Carlos kwa sauti yenye kukwama kwama.


“Relax, darling,” Carlos alisema kwa sauti tulivu huku akiangua kicheko hafifu kisha akaondoka na kueleka chumbani. Baada ya dakika kadhaa za kuoga Jacky alitoka bafuni na kuelekea chumbani na moja kwa moja akaelekea kwenye kabati la ukutani la nguo.


Alipokuwa akitembea kile kiuno chake chembamba kilicheza taratibu sambamba na mtikisiko wa makalio yake laini yaliyopishana taratibu wakati alipokuwa akizitupa hatua zake. Hata hivyo, usoni wake hakuonesha tashwishwi yoyote na alionekana hakuwa na furaha.


Alipofika kwenye lile kabati alisimama mbele ya kioo kikubwa kilichokuwa kwenye kabati la nguo na kujishika kiunoni akijitazama kwa kujizungusha zungusha na baadaye akaanza kujitomasa tomasa matiti yake. Aliendeleaa kusimama pale bila kujua kuwa mle chumbani kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akimwangalia kwa makini.


Carlos alikuwa ameketi kwenye sofa akimtazama Jacky tangu alipotoka bafuni hadi alipokwenda kusimama pale kwenye kabati la nguo, aliendelea kumtazama kwa utulivu muda wote huku akivuta sigara yake taratibu na kuutoa moshi taratibu huku akiuangalia kwa makini.


Japokuwa macho ya Carlos yalikuwa yakimtazama Jacky muda mrefu lakini akili yake ilikuwa imezama zaidi katika ile starehe yake ya kuvuta sigara.


Mara kikamtoka kikohozi kilichomshtua Jacky ambaye aliacha kujitazama kwenye kile kioo na hapo akafungua lile kabati haraka na kuanza kuchagua nguo. Alitoa bikini nyekundu na gauni jepesi la pinkil kulalia na alipoivaa lile gauni lililichora vizuri umbo lake zuri huku likiionesha bikini nyekundu aliyokuwa ameivaa ndani.


Kisha alielekea sebuleni ambako aliandaa meza kwa ajili ya chakula cha jioni na baada ya kumaliza alimwalika Carlos kwa ajili ya chakula. Jacky alikuwa ameandaa kile chakula mapema kabla hawajaondoka kwenda Vingunguti kumuona Jasmine.


Alikuwa amepika wali wa nazi, mchuzi mzito wa kuku ulioungwa kwa nazi pia na mchemsho wa ndizi matoke zilizopikwa kwa ufundi wa hali ya juu huku zikiwa zimechanganywa vizuri na samaki aina ya sato wa Ziwa Victoria.


Pia kulikuwa na juisi ya parachichi iliyochanganywa na passion, bakuli la mboga za majani pembeni, bakuli la saladi na matunda kwenye sinia. Licha ya urembo wake, Jacky alikuwa msichana fundi sana wa kupika na kwa kweli alikuwa amepika chakula kitamu sana.


Carlos alikuja na kujumuika na Jacky pale kwenye meza na wakati wakiwa mezani wanakula chakula taratibu mvua kubwa iliendelea kunyesha huku matone yake yakianguka juu ya paa la nyumba yao.


Jacky hakuwa katika hali yake ya kawaida, bado hakuonesha furaha na muda wote macho yake yalikuwa yakitazama chakula lakini akili yake haikuonekana kuzama kwenye kile chakula pale mezani.


Carlos alimtazama kwa makini na kuguna kitendo kilichomfanya Jacky ainue uso wake kumtazama Carlos, na macho yao yalipokutana Jacky alijitahidi kuumba tabasamu hafifu usoni mwake.


Hata hivyo, hakufanikiwa kwani badala ya kuonesha tabasamu halisi alionekana ni kama mtu aliyekuwa anataka kulia na kucheka kwa wakati mmoja.


“Are you okay?” (Uko sawa?) Carlos alimuuliza Jacky huku akiwa amekamkazia macho.


“I’m okay, why?” (niko sawa, kwani vipi?) Jacky aliongea kwa utulivu lakini maelezo yake yalikuwa hayaendani kabisa na mwonekano wa sura yake.


Alishusha pumzi ndefu kana kwamba alikuwa amekimbia umbali mrefu, kisha aliinamisha tena uso wake na macho yake kuangalia chakula ingawa hakuwa akikitazama kile chakula bali alizama kwenye tafakuri.


“Are you hiding something to me, Jacky? You’re not okay, I know you,” (Unanificha kitu Jacky? Hauko sawa, nakufahamu) Carlos alisema huku akitingisha kichwa chake kwa huzuni akionekana kutoridhishwa na jibu la Jacky.


“Don’t you trust me, darling? Why do you say that I’m hiding something to you?” (Kwani huniamini mpenzi? Kwa nini unasema kuwa ninakuficha kitu?) Jacky aliuliza huku akimkazia Carlos macho yake yaliyokuwa yamelewa kwa uchovu na usingizi.


“Jacky, we have known each other for a long time, almost three years now! Lakini bado umekuwa hueleweki…” Carlos alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Don’t worry, I’m okay… I’m just tired and sleepy, but I'm okay,” (Usiwe na shaka, niko sawa… ni uchovu tu na usingizi, lakini niko sawa) Jacky alisema huku akilazimisha tabasamu, hata hivyo, mwonekano wake usoni ulikuwa na kila dalili za mashaka na wasiwasi ingawa hakutaka kusema ukweli.


Carlos alimtazama kwa makini kisha aliinuka na kwenda kwenye jokofu, akatoa chupa ya mvinyo aina ya Pinot Noir na bilauri mbili kisha akarudi nazo pale mezani.


“I think this will make you a little stimulating to remove fatigue,” (Nadhani hii itakuchangamsha kidogo na kukutoa uchovu) Carlos alisema huku akimuonesha Jacky ile chupa ya mvinyo. Waliendelea kula taratibu na waliposhiba wakashushia na matunda.


Kisha wakahamia sebuleni kwenye masofa huku kila mmoja akiwa na kimbaka mdomoni kuondoa masalia ya nyama ya kuku pamoja na masalio mengine kwenye meno.


Moyoni, Carlos alijisifia sana kumpata mke mrembo sana kama Jacky aliyekuwa na sifa nyingine nyingi za ziada, kuanzia mapishi jikoni, utaalamu wa huduma za nyumbani hadi ufundi awapo katika katika uwanja wa futi sita kwa sita.


Kisha Carlos aliifungua ile chupa ya mvinyo na kumimina kwenye zile bilauri halafu moja akampa Jacky. Walishushia ule mvinyo na baada ya dakika kadhaa Jacky alionekana kuchangamka kidogo ingawa aliendelea kupiga miayo ya uchovu.


Baada ya kupiga mafunda kadhaa ya mvinyo Jacky aliinuka na kujikongoja kuelekea chumbani, alipoingia alijitupa kitandani huku akilala kifudifudi. Hakuchukua muda mrefu mara usingizi ukampitia.




Kisha Carlos aliifungua ile chupa ya mvinyo na kumimina kwenye zile bilauri halafu moja akampa Jacky. Walishushia ule mvinyo na baada ya dakika kadhaa Jacky alionekana kuchangamka kidogo ingawa aliendelea kupiga miayo ya uchovu.


Baada ya kupiga mafunda kadhaa ya mvinyo Jacky aliinuka na kujikongoja kuelekea chumbani, alipoingia alijitupa kitandani huku akilala kifudifudi. Hakuchukua muda mrefu mara usingizi ukampitia.


Endelea...


Muda ule Carlos alionekana kukumbuka jambo, akachukua simu ya Jacky ambayo alikuwa anawasiliana na Yusuf na kutafuta namba fulani kutoka kwenye orodha ya majina ya watu katika simu yake kisha akabofya ile namba na kuweka simu sikioni, baada ya muda ile simu iliita na kupokelewa. Kwa dakika takriban ishirini carlos alikuwa anaongea mtu, wakipanga na kupangua, hatimaye wakafikia muafaka. Alipokata simu akainuka na kuelekea chumbani.


Kule chumbani alisimama na kumtazama Jacky kwa makini jinsi alivyokuwa amelala kwa uchovu, akatabasamu na kuzima taa za chumbani na kuwasha zile taa za rangi zilizokuwa juu ya droo mbili zilizokuwa kila upande wa kile kitanda, naye akajilaza kitandani kando ya Jacky na kupitiwa usingizi.


* * * * *


Jioni ya siku ile Yusuf alirudi nyumbani kwake Ilala Bungoni mapema mara tu baada ya kufunga ofisi, ilikuwa saa kumi na moja jioni na mvua ya manyunyu ilikuwa inanyesha taratibu wakati akirudi huku akiwa mwenye wasiwasi.


Alipofika nyumbani alimkuta mkewe Mama Jasmine akiwa ameketi kibarazani na jirani yao Mama Shani wakisukana. Yusuf aliwasalimia kwa bashasha zote, Mama Shani aliitikia lakini mkewe hakusema kitu. Yusuf alimsogelea mwanawe Jasmine aliyekuwa akicheza na Shani na kumnyanyua juu huku akimrushia mabegani mwake.


Kisha alimtupia jicho mkewe na kuelekea ndani ambako alivua nguo zake na kuziweka ndani ya tenga la nguo chafu kisha alivaa bukta nyeusi na fulana nyepesi nyeupe na kuketi sebuleni, aliwasha runinga na wakati akitafuta stesheni akajikuta akiweka chaneli iliyoonesha kipindi cha katuni za “Tom and Jerry”, akataka kutoa lakini Jasmine akang’aka huku akimnyang’anya remote, “Baba usitoe.”


Yusuf alitii amri ya mwanawe, hivyo wakawa wanaangalia kile kipindi huku na Jasmine ambaye alikuwa amekaa juu ya kochi la sofa lililoanza kuchoka jirani na baba yake, akijiegemeza na kutulia tuli na mkononi alishikilia ile remote.


Kwa muda mrefu Yusuf aliketi pale sebuleni pasipo kumuona mkewe akiingia ndani kama ilivyokuwa kawaida yake kumpokea mumewe na kumpa pole kwa kazi. Kitendo kile kilimuumiza sana Yusuf japo hakuwa na namna ya kufanya.


Aliendelea kukaa kwa utulivu huku macho yakiwa yameganda kwenye ile runinga japokuwa akili yake haikuwa pale, bali alikuwa akiwaza na kuwazua hili na lile. Mawazo yalimteka na kumrudisha miaka mitano au sita nyuma akakumbuka alivyofahamiana na mkewe Mama Jasmine, ambaye wakati huo alijulikana zaidi kwa jina lake la Zaituni Malocha.


Ilikuwa siku moja wakati Yusuf alipokuwa Msamvu Morogoro akitokea nyumbani kwao Msufini pale pale Morogoro, muda huo alikuwa safarini kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza kazi katika kampuni binafsi ya masoko. Alipita kwenye duka la rafiki yake, Obedi Mkude ili kumuaga, akapishana na mwanadada mmoja aliyetoka pale dukani akiwa na haraka, Yusuf hakuwa amemtilia maanani.


Alisimama pale dukani na kusalimiana na Obedi na wakati wakiagana macho yake yakatua kwenye kitabu kimoja kinachoitwa “The Devil in Love” cha mwandishi Barbara Cartland kilichokuwa kimelala juu ya meza ya bidhaa.


Yusuf alimuuliza Obedi kama kile kitabu kilikuwa chake, lakini Obedi alikana kukifahamu ila alikumbuka kumuona nacho msichana mmoja aliyekuja pale dukani kununua soda ya “take away” akiwa anawahi basi na pengine ndiye aliyekisahau pale.


Yusuf alikifunua kile kitabu akaangalia kurasa mbili tatu, hata hivyo alivutiwa sana na maandishi yaliyoandikwa kwa penseli katika ukurasa wa kwanza tu wa kitabu kwa mwandiko mzuri wa kike yakiwa na ujumbe uliogusa hisia zake.


Chini ya maandishi yale, Yusuf aligundua jina mmiliki wa kile kitabu, “Zaituni Malocha” lililoambatana na anuani ya barua pepe. Yusuf aliamua kuondoka na kile kitabu akiahidi kumtafuta ili amrudishie baada ya kukisoma, kwani alikuwa mpenzi riwaya za watunzi Barbara Cartland na Agatha Christie.


Alipofika Dar es Salaam alimuandikia Zaituni barua pepe akitumia ile anuani aliyoikuta kwenye kile kitabu akijitambulisha kwa jina na mahali alipokuwa akiishi kisha akamweleza kuwa alikuwa na kitabu chake, na mwisho akamuomba urafiki.


“Ni urafiki wa aina gani unaouhitaji, Yusuf?” Zaituni alimwandikia ujumbe Yusuf baada ya kuona kuombwa wawe marafiki.


“Urafiki wa hivi hivi tu, wala usifikirie vibaya.” Yusuf alimjibu.


“Hata mimi ningependa kuwa na rafiki muungwana wa aina yako na ninakubali tuwe marafiki wa hivi hivi tu kama ulivyosema, lakini tafadhali, tafadhali, tusiwe marafiki wa kimapenzi, sawa?” Zaituni aliandika ujumbe ambao Yusuf hakuwa na namna nyingine ya kufanya isipokuwa kukubaliana naye.


Baada ya pale mawasiliano kati yao kupitia barua pepe yaliongezeka kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili, wakati huo Zaituni alikuwa anasoma jijini Mwanza. Kila ujumbe waliotumiana ulikuwa kama mbegu iliyoanguka katika udongo wenye rutuba na taratibu hisia za kimapenzi zikaanza kuchipuka ndani ya mioyo yao.


Yusuf aliomba atumiwe picha lakini Zaituni alikataa akimwambia kuwa kama kweli alimpenda asingejali alikuwa anafananaje, kwani kupenda ni kazi ya moyo na macho hubaki kuwa shahidi tu.


Hatimaye siku ya siku ikawadia, Zaituni alimwandikia Yusuf barua pepe kuwa angefika jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi kwa basi la Shabiby Line akitokea Dodoma ambako wazazi wake walikuwa wamehamishiwa na alitarajia kuingia Dar es Salaam saa 8:00 mchana.


“Fika Ubungo, utanitambua kwa ua waridi jekundu nitakalovaa kifuani kwangu katika titi la kushoto…” Zaituni alimwandikia ujumbe wa kumjulisha.


Hivyo, ilipofika saa 7:30 mchana Yusuf alikuwa amekwishafika katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo akiwa ameshika kile kitabu cha Barbara Cartland akimsubiri msichana mrembo ambaye moyo wake ulimpenda sana, lakini macho yake hayakuwahi kumuona.


Alikaa pale kituoni kwa muda mrefu akisubiri kwa hamu kwani alikwishachoka kuteseka na alikuwa tayari kwa lolote. Aliangaza angaza macho angani kukitazama kile alichokiona mwenyewe “muda” ambao aliuona ukivaa mbawa zake.


“Muda kitu cha ajabu sana!” Yusuf aliwaza baada ya kuitazama saa yake ya mkononi.


“Muda!” alijikuta akiwaza tena, lakini safari hii alitamka kwa sauti kama vile alikuwa akiongea na mtu.


Ni mara ngapi Yusuf alikuwa akiuona “muda” ukipita mbio mbele yake mithili ya duma mwenye kasi! Kuna kipindi aliitamani kuusimamisha ili afurahie maisha bila kuwa na wasiwasi.


Lakini siku hiyo ambayo ilikuwa muhimu sana katika maisha yake “muda” ulionekana kumnyima raha, ulikuwa ukinyiririka taratibu kwa madaha na maringo kama kinyonga. Zaituni ndiye aliyekuwa mchawi wa huo “muda”. Alikuwa na mamlaka ya kuuamuru uwe duma mwenye kasi ama uwe kinyonga.



“Muda!” alijikuta akiwaza tena, lakini safari hii alitamka kwa sauti kama vile alikuwa akiongea na mtu.


Ni mara ngapi Yusuf alikuwa akiuona “muda” ukipita mbio mbele yake mithili ya duma mwenye kasi! Kuna kipindi aliitamani kuusimamisha ili afurahie maisha bila kuwa na wasiwasi.


Lakini siku hiyo ambayo ilikuwa muhimu sana katika maisha yake “muda” ulionekana kumnyima raha, ulikuwa ukinyiririka taratibu kwa madaha na maringo kama kinyonga. Zaituni ndiye aliyekuwa mchawi wa huo “muda”. Alikuwa na mamlaka ya kuuamuru uwe duma mwenye kasi ama uwe kinyonga.


Endelea...


Yusuf alimuwaza Zaituni muda wote, mbele ya uzuri wa kiumbe huyo aliyeitwa Zaituni, Yusuf alijiona kama limbukeni wa mapenzi. Mawazo yalimpitia na moyo ulimwenda mbio kama mtu aliyekuwa na ugonjwa wa kihelehele. Alijiuliza iwapo hali ile ilikuwa ni matokeo ya kumsubiri Zaituni, ingekuwaje pindi angeingia ndani mwake?


Alijiambia kuwa kama ni mateso yalikuwa yametosha, huo sasa ulikuwa ni muda muafaka wa kumaliza utata. Aliitupia tena jicho saa yake, ilionesha kuwa saa 7:56. Wasiwasi ukazidi kwa kadiri muda ulivyokaribia. Aliendelea kusubiri lakini muda ulivyozidi kusogea ndivyo alivyozidi kuhisi mabadiliko katika akili na mwili wake.


Saa 7:57, Yusuf akaanza kupanga jinsi atakavyompokea Zaituni. Ikamjia picha akilini mwake ya Zaituni akiteremka katika basi la Shabiby na kumfuata lakini akaishiwa nguvu na kuanguka. Picha hiyo haikumpendeza kabisa Yusuf.


Saa 7:58, mwili mzima wa Yusuf ulijaa moto, alihisi joto kali sana likitambaa mwilini kwake kama vile alikuwa amewekwa kwenye tanuru la kuokea mikate. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka!


Saa 7:59, vidole vya mikono yake vilianza kutetemeka kama vile damu ilikuwa ikienda mbio kwenye mishipa. Saa 8:00 alikuwa amebadilika kabisa na yeyote ambaye angemuona kwa wakati huo asingeshindwa kubaini kuwa Yusuf alikuwa katika wakati mgumu sana.


Hata hivyo, alipiga moyo konde na kusubiri ujio wa mrembo wa shani aliyekusudiwa kuumbwa malaika lakini akateremshwa duniani kimakosa. Muda ulianza kuyoyoma na Yusuf hakukata tamaa, aliendelea kumtizamia Zaituni kwa dakika zingine ishirini huku akichungulia kwenye kila gari lililoingia pale Ubungo.


Kichwa chake kilizunguka, na ndani yake mseto wa hamu, hofu na tamaa vilianza kumtambaa taratibu na kuyafanya maungo yake yageuke. Mara akaliona basi la Shabiby kutoka Dodoma likiingia katika Kituo cha mabasi cha Ubungo.


Muda ule Yusuf alikuwa amejiandaa vyema kumkabili Zaituni, alijiandaa kwa kila hali kuanzia kimavazi, namna ambavyo angempokea na kumsalimia kisha angemkaribisha jijini na hata namna ambavyo angemweleza jinsi alivyokuwa akimpenda kwa dhati.


Alisimama kutoka kwenye benchi baada ya kuliona lile basi likisimama na abiria kuanza kushuka, akasogea karibu huku akiweka sawa tai yake shingoni kisha akakaza macho yake kuwatazama kwa makini wale abiria walioshuka kutoka ndani ya basi la Shabiby.


Mara akamuona msichana mrembo aliyeshuka kutoka kwenye lile basi la Shabiby akiwa ameshika begi dogo jeusi la safari na kuanza kupiga hatua zake kwa madaha akielekea upande ule ambao yeye alikuwa amesimama.


Yule msichana ambaye alikiri kuwa hadi wakati huo alikuwa hakuwahi kumuona msichana wa namna ile katika pitapita zake, alikuwa amevaa vazi la kitambaa cha bazee lililoshonwa na kudariziwa vizuri kwa nyuzi za dhahabu na lilikuwa limenasa vyema kwenye kiuno chake chembamba kilichoshikilia mzigo mkubwa wa makalio na minofu ya mapaja yake.


Miguuni alivaa viatu vyekundu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio na nywele zake nyeusi za kibantu alikuwa amezisuka mtindo wa rasta na kuzifunika kwa kilemba, hivyo kumfanya aonekane mzuri wa asili.


Mkono wake wa kushoto alikuwa amevaa saa nzuri ndogo ya kike iliyotengenezwa kwa namna ya kupendeza na hivyo kuongeza ziada nyingine katika uzuri wake. Begani alikuwa amening’iniza mkoba mzuri mwekundu.


Yusuf akajikuta akipiga hatua zake kumfuata yule mrembo, alisahau kabisa kuwa aliambiwa kuwa atakuwa ameweka ua waridi jekundu katika titi lake la kushoto. Alipokumbuka akasita na kusimama ghafla huku akimkodolea macho ya matamanio, na wakati huo huo yule msichana akampita kwa mwendo wa kasi passipo kumjali na kujichanganya kwenye umati wa watu.


Yusuf alibaki akiwa ameduwaa na alipokuwa bado anashangaa mara akamuona mwanamke mtu mzima aliyezidi miaka 60 akiwa amesimama akiangaza macho yake huku na kule kama vile alikuwa akimtarajia mtu. Yule bibi alikuwa amevaa gauni zuri la kitenge na miguuni alivaa viatu vya flat visivyo na visigino virefu. Yusuf alipomtazama vizuri akaliona ua waridi jekundu katika titi lake la kushoto.


Dah! Alijikuta akiishiwa nguvu, alihisi kana kwamba mwili wake ulikuwa umegawanywa katika mapande mawili, akataka aondoke zake na kumwacha yule bibi kwenye mataa, hata hivyo, hakuona kama ni busara kuondoka bila kuongea naye, hivyo akamfuata na kujitambulisha kwake huku akimuonesha kile kitabu.


"Naitwa Yusuf Akida, nimefurahi sana kukutana na wewe ana kwa ana, Bi Zaituni. Ninaomba kwanza nikupeleke ukapate chakula cha mchana kabla hatujaongea," Yusuf alisema huku akimtazama yule mwanamke kwa tabasamu.


Hata hivyo, alishangazwa sana kuona yule mwanamke hakuwa akimtambua yeye wala kile kitabu alichoshika na alimtazama kwa mshangao mkubwa kana kwamba aliona kitu kigeni cha ajabu kutoka sayari nyingine.


“Kwa kweli vijana mnazidi kunichanganya,” alisema yule bibi, “lakini kuna msichana mmoja alivaa ngyuo ya bazee na kilemba kichwani alielekea huko aliniomba nivae hili ua kwenye kifua changu. Na alisema kama mwanamume yeyote ambaye angenipokea nimuambie kuwa amekwenda kumsubiri katika hoteli ya Landmark. Alisema kuwa hili ni jaribio kuona kama kweli mwanamume huyo ana upendo wa dhati,” alisema yule bibi na kumuacha Yusuf akiwa mdomo wazi.


Haraka sana Yusuf aliondoka na kuelekea Landmark Hotel alikomkuta Zaituni akimsubiri, wakala pamoja chakula cha mchana na huo ndiyo ukawa mwanzo wa mahaba mazito na hatimaye ndoa… Yusuf aliwaza sana na mara akajikuta akipitiwa na usingizi pale pale kwenye kochi…


______


Mama Jasmine aliendelea kukaa kule nje akipiga soga na shoga zake hadi ilipotimia saa moja na ushee ndipo akaamua kuingia ndani na macho yake yakatua kwa mumewe aliyekuwa kauchapa usingizi palepale kwenye kochi, kiganja cha mkono wa kulia kikiwa shavuni.


Macho yake yalihama na kumtazama mwanawe Jasmine ambaye pia alikuwa kauchapa usingizi palepale kwenye kochi. Runinga ilikuwa bado inaonesha vipindi vya katuni.


Mama Jasmine alimfuata mwanawe na kumbeba kisha akaingia naye chumbani na kumlaza kitandani. Akarudi tena sebuleni na kusimama akimtazama mumewe kwa chuki na kuchukua remote kisha akaizima ile runinga.


Yusuf akashtuka na kufumbua macho yake, macho yake yakaanza kutambaa katika mwili wa mkewe, yakianza na mapaja yaliyonona kuelekea juu kisha yakakutana na nyonga zilizofinyangwa barabara.


Macho yake yakatuwama kwa muda katikati ya mapaja ya mkewe, kisha yakafunga safari kuelekea kiunoni yakakutana na kiuno kilichobonyea na kuacha fursa ya nyonga kuchanua zilivyotaka. Kiuno kilirembwa na tumbo dogo ambalo lilikana kuwa wakati fulani lilishabeba kiumbe kwa muda wa miezi tisa.


Hamu haikuishia hapo, macho yalielekea kwenye kifua kilichobeba matiti madogo yaliyokuwa yamesimama kana kwamba hakuwahi kunyonyesha hapo kabla. Hamu ya mapenzi ikamjaa juu ya mkewe.


Macho yake hayakuishia hapo bali yalipanda hadi kwenye uso wa mkewe, akauona uso wa mkewe ukiwa mkavu usio na tashwishwi yoyote. Yusuf akatweta na hamu ya mapenzi ikamuisha mara moja.


Mambo ndo' yanazidi kunoga, endelea kufuatilia stori hii ya kusisimua "Kizungumkuti" ili kuujua mwisho wake.




Yusuf akashtuka na kufumbua macho yake, macho yake yakaanza kutambaa katika mwili wa mkewe, yakianza na mapaja yaliyonona kuelekea juu kisha yakakutana na nyonga zilizofinyangwa barabara.


Macho yake yakatuwama kwa muda katikati ya mapaja ya mkewe, kisha yakafunga safari kuelekea kiunoni yakakutana na kiuno kilichobonyea na kuacha fursa ya nyonga kuchanua zilivyotaka. Kiuno kilirembwa na tumbo dogo ambalo lilikana kuwa wakati fulani lilishabeba kiumbe kwa muda wa miezi tisa.


Hamu haikuishia hapo, macho yalielekea kwenye kifua kilichobeba matiti madogo yaliyokuwa yamesimama kana kwamba hakuwahi kunyonyesha hapo kabla. Hamu ya mapenzi ikamjaa juu ya mkewe.


Macho yake hayakuishia hapo bali yalipanda hadi kwenye uso wa mkewe, akauona uso wa mkewe ukiwa mkavu usio na tashwishwi yoyote. Yusuf akatweta na hamu ya mapenzi ikamuisha mara moja.


Endelea...


Akiwa bado anatafakari jinsi ya kuanzisha maongezi na mkewe mara akamuona mkewe akiondoka haraka na baada ya muda akarudi akiwa amebeba jagi lililokuwa na maji ya kunawa na beseni dogo la kunawia, akaviweka pale mezani na kuondoka tena na baada ya muda akarudi akiwa amebea sahani ya chakula na kukitenga pale mezani bila hata kusema kitu, kisha akaelekea chumbani na kufunga mlango.


Yusuf alimtazama kwa kila hatua aliyopita bila kusema neno kisha akakaa pale kwa kitambo kirefu akikiangalia kile chakula, muda wote hakuwa akihisi njaa. Japo kile chakula kilikuwa kimepikwa vizuri sana lakini hakuweza kula. Alibaki kukikodolea macho akiutazama wali uliokolea nazi, samaki wa maji baridi, mboga za majani na maharage.


Baada ya kitambo kirefu cha ukimya huku akikitazama kile chakula hatimaye aliamua kula japo matonge kadhaa ili isionekane kuwa alikuwa amesusa chakula, kisha alikifunika na kuinuka akaingia chumbani kumfuata mkewe. Alipoingia chumbani alimkuta mkewe ameketi kwenye pembe ya kitanda akiwa kajiinamia anawaza na mara alipomuona mumewe alimtazama kwa jicho kali sana.


“Mama Jasmine, hivi ni mambo gani haya yasiyoisha? Nimeshakuomba samahani zaidi ya mara tatu lakini naona mwenzangu bado una kinyongo…” Yusuf aliongea kwa sauti ya chini na ya kusihi.


“Hayawezi kuisha kirahisi kama unavyodhani!” Mama Jasmine alisema kwa sauti tulivu lakini yenye hasira.


“Kwa hiyo tutaishi maisha haya hadi lini?” Yusuf aliuliza tena huku akimwangalia mkewe kwa huzuni.


“Niache bwana, nahitaji kupumzika. We nenda kwa huyo huyo malaya wako,” Mama Jasmine alijibu kwa hasira na kujilaza kitandani.


“Dah, natamani hii siku ifutike kabisa akilini mwangu. Hata kama ikibaki niione kama ndoto tu. Nahisi kama vile unanichukia sana,” Yusuf alimweleza mkewe bila kumtazama wala kusubiri jibu, akatoka zake kimya kimya.


Alifungua mlango wa chumbani akapita sebuleni na kuelekea nje hadi barazani. Muda ule alikuwa bado hajavua saa yake ya mkononi. Hivyo aliitazama na kugundua kuwa ilishatimu saa tatu na ushee.


Alisimama pale nje akainua macho yake kutazama angani. Anga lilikuwa wazi na la rangi ya samawati liking’arishwa kwa wingi wa nyota na mwezi mkubwa uliokuwa umevaa rangi nyekundu aliouona vizuri kutokea pale alipokuwa amesimama.


“Mwezi mwandamo huanza mchanga, pole pole hukua na kuwa mpevu na huweza kuonekana kwa wote hata wale waonao ukungu mbele ya macho yao, na baadaye huwa mwekundu na huogopesha manyani porini,” Yusuf aliwaza akiyakumbuka maneno ya mwanazuoni mmoja aliyemsoma kitabuni wakati akiwa sekondari.


Aliendelea kuutazama ule mwezi mwekundu, akaanza kutafakari kuhusu masimulizi aliyowahi kuyasikia kuwa ukifikia hatua hiyo huogopesha manyani porini.


Muda huo upepo wa usiku uliipuliza ngozi yake na kumfanya ajisikie vizuri na hapo ndipo alipogundua kuwa ngozi yake ilinata kutokana na jasho. Alitamani kuingia ndani akachukue maji na kuelekea bafuni kuoga, hata hivyo, hakuwa na hamu ya kurudi ndani.


Donge la fadhaa lilimkaba kooni hasa alipohisi kuwa huenda mkewe aliamua kumchukia na wala hakutaka kumsamehe. Akawaza nini cha kufanya ili kuurudisha upendo katika familia yake. Mara akakumbuka msemo kuwa “hakuna mkate mgumu mbele ya chai” hii ilimaanisha kwa Yusuf kuwa njia pekee ilikuwa ni kupata fedha nyingi ambazo zingeweza kurudisha heshima na furaha ndani ya nyumba.


Alipowaza suala la pesa mara akamkumbuka Jacky ambaye yeye alimtambua kwa jina la Belinda. Alijilaumu kwa kuiacha simu yake ndani angempigia ili ingalau asikie sauti yake ya kubembeleza, huenda ingempunguzia stress. Alitamani kuingia ndani akachukue simu yake lakini alisita.


“Dah, Belinda ameyateka mawazo yangu na akili yangu yote inamuwazia yeye tu. Katika mazingira kama haya nahitaji kuwa naye tu karibu nimkumbatie mikononi mwangu, nikimbembeleza kama mtoto mdogo huku nikiisikia miguno yake na sauti yake nyororo anapolalama kwa raha…” Yusuf aliwaza na kushusha pumzi.


“Ki ukweli Belinda yuko tofauti sana na wanawake wengine wote na ana mvuto wa ajabu mno, pia amebarikiwa vitu vya kipekee ambavyo ni vigumu hata kuvielezea…” Yusuf alizidi kusumbuliwa na mawazo juu ya Jacky, kwa muda mrefu alimuwazia Jacky tu. Mara akachoka kusimama na kuamua kukaa kwenye ngazi za baraza.


Alipoitazama tena saa yake akashtuka kuona kuwa ilikuwa imeshatimia saa sita na dakika kumi na tano usiku! Ilikuwa imeshaingia siku nyingine akiwa anapigwa na ubaridi pale nje. Aliamua kukiegemeza kichwa chake kwenye nguzo ya ukuta na kufumba macho kwani uchovu ulimuelemea sana, na mbu nao hawakumwacha salama.


Mama Jasmine akiwa chumbani amelala kitandani alishtuka na kuangaza macho yake huku na kule, Yusuf hakuwepo ndani. Akapuuzia na kufumba tena macho yake kulala, hata hivyo, alijikuta akianza kupatwa na wasiwasi.


“Mke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, lakini mwenye busara huijenga na kuiboresha nyumba yake,” Mama Jasmine alijikuta akiyakumbuka maneno hayo kutoka ndani ya Biblia ambayo aliwahi kuyasikia kutoka kwa mchungaji mmoja wa kanisa lililokuwa jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi.


Japo hakuwa Mkristo lakini maneno yale yalikuwa yamemuingia na aliyakariri japo hakujua yalipatikana wapi ndani ya hiyo Biblia. Mara akajikuta akiinuka kutoka pale kitandani na kutoka, akamwangalia mumewe pale sebuleni hakumuona, akafungua mlango na kumwangalia kule uani, hayupo!


Sasa akaingiwa na hasira akidhani kuwa labda aliondoka kwenda kulala kwa kimada wake waliyekesha wote kabla hajarudi nyumbani asubuhi, akipanga kumkomoa.


Akatoka nje na kumkuta Yusuf akiwa amejikunyata pale kibarazani kwenye ngazi akiwa chakula cha mbu, alijikuta akiingiwa na huruma, alisimama akimtazama kwa huruma na kuamua kumwamsha kwa kumpiga piga taratibu mgongoni huku akimwita. Yusuf alishtuka na kuamka, mkewe akamuinua na kumuongoza ndani.


Yusuf alipoingia chumbani alivua fulana yake na kujitupa kitandani, wala hakuwa tena na wazo la kuoga. Dakika mbili baadaye alikuwa anakoroma.


Mama Jasmine alisimama pale akimtazama mumewe kwa makini kisha akarudishia chandarua vizuri na kuzima taa halafu akapanda kitandani na kulala pembeni ya mumewe.


Akatoka nje na kumkuta Yusuf akiwa amejikunyata pale kibarazani kwenye ngazi akiwa chakula cha mbu, alijikuta akiingiwa na huruma, alisimama akimtazama kwa huruma na kuamua kumwamsha kwa kumpiga piga taratibu mgongoni huku akimwita. Yusuf alishtuka na kuamka, mkewe akamuinua na kumuongoza ndani.


Yusuf alipoingia chumbani alivua fulana yake na kujitupa kitandani, wala hakuwa tena na wazo la kuoga. Dakika mbili baadaye alikuwa anakoroma.


Mama Jasmine alisimama pale akimtazama mumewe kwa makini kisha akarudishia chandarua vizuri na kuzima taa halafu akapanda kitandani na kulala pembeni ya mumewe.


Endelea...


* * * * *


Sauti ya kengele ya getini iliyokuwa ikilia kwa fujo kuashiria kuwa kulikuwa na mtu aliyekuwa getini iliwashtua Carlos na Jacky kutoka katika usingizi mzito uliokuwa umewachukua kwa muda mrefu.


Siku ya Jumanne ilikuwa imepita ikaipisha Jumatano, muda huo ilikuwa ni saa tatu za asubuhi wakati Carlos na Jacky wakiwa bado wamelala kitandani huku zile taa mbili za rangi nyekundu zilizokuwa juu ya droo mbili kila upande wa kile kitanda zikiwa zinatoa mwanga hafifu wenye mg’ao na kufanya nusu ya chumba kuwa kizani.


Carlos alipoitupia jicho saa yake ya mkononi aligundua kuwa walikuwa wamelala kwa muda mrefu kufuatia uchovu wa siku iliyotangulia. Muda ule miale ya jua la saa tatu asubuhi ilikuwa inapenya dirishani na kutuama pale kitandani walipokuwa wamelala.


Haraka Carlos alilitupa shuka pembeni na kutega masikio yake vizuri kusikiliza na kugundua kuwa alikuwa sahihi kwani aliweza kusikia vizuri sauti ya mwanamume akiita kule nje getini. Bahati mbaya nyumba ile haikuwa na mlinzi na wala hakupenda kuajiri mlinzi.


Ile nyumba ilikuwa imewekwa mitambo maalumu ya ulinzi, lakini pia alitaka kuwa huru zaidi akiwa yeye na Jacky tu ili wafanye mambo yao bila bughudha na hakupenda kabisa watu wasiohusika wajue nyendo zao. Ndiyo maana hata ndugu aliwapeleka kwenda kuishi kwenye nyumba zake zingine zilizokuwa Mbezi Beach na Sinza.


Alishuka haraka kutoka pale kitandani na kutoka haraka akimwacha Jacky anamtazama kwa mshangao, akaelekea kwenye ngazi ambazo alizishuka haraka na kukatiza katikati ya sebule na kuuendea mlango wa barazani. Aliufungua na kutoka kisha akakatiza katikati ya ile fensi hadi kwenye geti kubwa.


Alisimama pale akachungulia nje kupitia upenyo mdogo uliokuwepo kwenye geti dogo akiwa makini kumtazama mtu aliyekuwa akibonyeza ile kengele. Alilamba midomo yake kuilainisha huku akikunja sura yake na kutengeneza matuta madogo usoni.


Kupitia ule upenyo mdogo uliokuwepo kwenye geti dogo, aliweza kumuona mwanamume mmoja mrefu aliyekuwa amepanda hewani kisawasawa na mwenye mwili ulioshiba, alikuwa mweupe kama mzungu, akiwa na umri wa miaka takriban hamsini na misuli imara ya mikononi iliyotuna kikamilifu vilimfanya aonekane kama bondia mkongwe.


Alikuwa na upara mpana uliokuwa unawaka na uso wake ulikuwa mpana na ulitulia kama maji ya mtungini, huku miwani yake mikubwa myeusi ikiwa imeyahifadhi macho yake makubwa.


Yule mwanamume alikuwa amevaa suruali nyeusi ya jeans na juu alivaa fulana mchinjo nyekundu iliyokibana vyema kifua chake kiasi kwamba ungeweza kudhani ile fulana ingetatuka muda wowote. Miguuni alikuwa amevaa buti ngumu nyeusi za ngozi imara ya mamba.


Jina lake halisi aliitwa Joram Mbezi ila alijulikana kwa jina la Kisu kutokana na ufundi wake wa kutumia kisu katika mapigano. Pia kabla hajamuua mtu kwa kisu alipenda kumuuliza, “Jina langu nani?” na kilichofuata baada ya lile swali ilikuwa ni kukizamisha kisu sehemu ambapo angeweza kuutoa uhai wa mtu huyo.


Kisu alikuwa amepata mafunzo juu ya matumizi ya silaha ndogo ndogo, na alijifunza mambo mengine mengi, alipokuwa nchini Kenya ambako aliishi na msichana mmoja wa Kikikuyu aliyeitwa Njeli, Kisu alitambulishwa kwa vijana hatari wa kazi alioshirikiana nao katika matukio mbalimbali ya ujambazi.


Kati yao, kijana mmoja aliyejiita Spoiler, ndiye aliyempa mafunzo halisi juu ya matumizi ya kisu cha kurusha, na ikafikia hatua Kisu akawa fundi kuliko hata mwalimu wake, kwani alikuwa na uwezo wa kulenga mboni ya jicho, hata la kuku, na kisu kikatua pale pale. Na hapo ndipo jina la Kisu lilipoanza kutumika rasmi huku likilifunika jina halisi la Joram.


Carlos alipotazama vizuri alimuona mwanamume yule akiwa amesimama akiliangalia lile geti kwa makini na kando yake ilikuwepo pikipiki aina ya Boxer. Mara moja Carlos akamtambua yule mwanamume, na bila kusita akakitekenya kitasa cha lile geti kwa funguo kuifyatua kabari yake kisha taratibu akalifungua lile geti huku sura yake ikipambwa na tabasamu.


“Ooh, Kisu, the devil himself!” (Ooh Kisu, shetani mwenyewe!) Carlos alisema kwa furaha huku akiachia tabasamu la makaribisho.


“Oh, Carlos, long time no see!” (Oh Carlos, siku nyingi hatujaonana!) yule mwanamume aliitikia huku akimkumbatia Carlos kwa furaha. Wakatazamana, bila shaka wakikumbuka yaliyopita.


“Umepungua kidogo, Kisu,” Carlos alisema huku akimtazama Kisu kwa makini, mkono wake wa kushoto ukiwa juu ya bega la kulia la Kisu. Kisu alimtazama kwa chini kidogo kutokana na kuwa alikuwa mrefu zaidi ya Carlos.


“Ni maisha tu ndugu yangu. Si unajua tangu janga lile kule Arusha mambo hayakukaa sawa tena hadi leo, nimekuwa mtu wa kubangaiza? Kwa kweli mkasa ule haukuniacha salama kabisa, najaribu kujisahaulisha lakini bado mawazo yananijia tu. Ni jana mchana tu nilikuwa naukumbuka mkasa wote ule, nikakukumbuka na wewe, kumbe usiku unanipigia simu.”


“Ni kweli. Maisha, maisha, maisha…” Carlos alisema na kucheka kidogo huku akitazama pembeni. Aliweka mikono yake kiunoni na kuuma mdomo wa chini.


“Maisha ni kitu cha ajabu sana! Utakuta huyu anasumbuliwa na hili, na mwingine anasumbuliwa na lile, ndiyo dunia ilivyo…” Carlos alisema, kisha kama aliyekumbuka kitu, akamtazama Kisu kwa makini. “Okay ingiza usafiri wako yako ndani.”


Kisu akakokota pikipiki yake haraka haraka na kuiingiza ndani ya fensi ya lile jumba. Alipoiegesha vizuri ile pikipiki yake akajikuta akizidi kupata mshangao, alilitazama lile jumba huku akistaajabu ukubwa wake.


Wakati huo Kisu aliendelea kuliajabia lile jumba la kifahari la ghorofa mbili lililokuwa katika hali ya ukimya sana likiwa limezungukwa na ukuta mrefu uliofungwa mfumo maalumu wa umeme wa kuzuia wezi juu yake usiomwezesha mtu kuona ndani, na lilikuwa na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatwa vizuri.


Alizitazama zile gari za kifahari, BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati, Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe na Toyota Landcruiser GX V8 lililokuwa na rangi nyeusi zilizokuwa kwenye banda la wazi la kuegeshea magari.


Kisha akazungusha macho yake haraka kutazama vizuri sehemu ya mbele ya hiyo nyumba iliyokuwa imezungukwa na bustani nzuri ya maua ya kupendeza. Carlos alitabasamu na kumkaribisha ndani.


Kisha wakaanza kuzitupa hatua zao kuelekea ndani wakipita katikati ya bustani ambapo kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa matofali madogo madogo yaliyokuwa yanavutia, Kisu alitembea kikakamavu katika namna iliyofanya hatua zake zitetemeshe ardhi kila alipokanyaga ardhi kwa buti zake ngumu miguuni.


Carlos alitangulia kuingia ndani huku akimkaribisha Kisu ambaye alipoingia tu akamkuta Jacky akiwa amesimama kwenye mlango uliokuwa ukielekea kwenye jiko, akiwa bado amevaa nguo yake nyepesi ya pinki ya kulalia iliyolichora vizuri umbo lake na kuionesha nguo yake ya ndani.




Kisha wakaanza kuzitupa hatua zao kuelekea ndani wakipita katikati ya bustani ambapo kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa matofali madogo madogo yaliyokuwa yanavutia, Kisu alitembea kikakamavu katika namna iliyofanya hatua zake zitetemeshe ardhi kila alipokanyaga ardhi kwa buti zake ngumu miguuni.


Carlos alitangulia kuingia ndani huku akimkaribisha Kisu ambaye alipoingia tu akamkuta Jacky akiwa amesimama kwenye mlango uliokuwa ukielekea kwenye jiko, akiwa bado amevaa nguo yake nyepesi ya pinki ya kulalia iliyolichora vizuri umbo lake na kuionesha nguo yake ya ndani.


Endelea...


Macho ya Kisu yalikuwa yakimtazama Jacky kiwiziwizi huku akizuga kuzungusha macho yake kustaajabia ukubwa wa ile sebule. Carlos aling’amua na kumtazama Jacky, akagundua kuwa kilichombabaisha Kisu ni lile vazi jepesi la Jacky lililokuwa likionesha umbo lake zuri.


Carlos akageuza shingo kumtazama Kisu kwa makini na mara akakiona kisu kikiwa ndani ya ala yake kilichotuna kiunoni kwake.


Carlos akajikuta akisisimkwa mwili wake huku damu ikianza kumchemka na kukimbia kwenye mishipa yake ya damu, hasa alipokumbuka ujuzi aliokuwa nao Kisu katika kutumia kisu kama silaha.


Akakumbuka siku moja alimshuhudia Kisu akionesha uwezo wake wa kutumia kisu pale alipochukua kisu na kukirusha kwenye picha yake ndogo ya ukubwa wa pasipoti aliyoibandika kwenye mlango wa pembeni wa kabati kwenye ghetto lake enzi hizo walipokutana jijini Nairobi.


“Naitoboa hiyo picha kichwani,” Kisu alisema kama utani bila kumtazama Carlos. Kufumba na kufumbua Carlos alisikia sauti ya kitu kikipenya ubaoni kwa kishindo. Alipoangalia kwa makini pale kwenye kabati akakiona kile kisu kikiwa kimezama katikati ya kifua juu ya ile picha ndogo ya pasipoti.


Carlos alitokwa na yowe dogo la mshangao. Hata hivyo, Kisu hakuonesha kufurahishwa, akasonya kwa hasira.


“Nini tena?” Carlos alimuuliza kwa mshangao.


“Nahitaji kufanya mazoezi,” nahitaji kufanya mazoezi.


“Mazoezi ya nini? Si umesema unailenga picha na kweli umefanikiwa?”


“Nilitaka kichwani, siyo kifuani. Nadhani nilichelewa kukiachia kisu mapema,” Kisu alisema huku akishusha pumzi.


“Lakini naamini hilo ni kosa dogo tu?”


“Kosa kubwa sana,” Kisu alisema na kwenda kukichomoa kile kisu, kisha alikichoma, akakirusha juu, akakidaka kwa mkono wa kushoto na kwa kasi ya umeme akakirusha tena akikipeperushia kabatini.


Carlos alichelewa nukta moja tu kugeuka na kukiona kilipokuwa kikizama katikati ya paji la uso wa ile picha. Carlos akapiga makofi huku akiachia mdomo wake wazi…


“Mbona mpo wima?” sauti ya Jacky ikamgutusha Carlos kutoka kwenye yale mawazo, akaachia tabasamu huku akimkazia macho Kisu.


“Kaa tafadhali,” Carlos alimwambia Kisu. Wote walikaa juu ya sofa maridhawa, Carlos akikaa sofa la pembeni na kushusha pumzi ndefu za kichovu huku akijiegemeza.


Macho ya Kisu yalianza kutalii tena mle ndani. Aliona kila kitu cha kifahari kilichotakiwa kuwepo ndani ya nyumba ya mtu mwenye fedha nyingi, kilikuwepo. Kuanzia samani nzuri hadi kumiliki demu mkali kama Jacky! Kisu alionekana kupatamani sana nyumbani kwa Carlos na kuisikitikia nafsi yake.


Alisikitika kwa kuwa kuna wakati alipata fedha nyingi mno kuliko alizokuwa nazo Carlos lakini akayachezea masiha, na sasa alikuwa anarudi tena kupewa kazi na Carlos ili apate fedha, jambo ambalo kama angekuwa makini na matumizi yake, pengine yeyé ndiye angemuajiri Carlos kumfanyia kazi zake.


Aliiangalia ile sebule kwa makini huku akivuta mizani ya kimawazo na kuiweka sebule yake upande mmoja na hiyo ya Carlos upande wa pili. Hapo ndipo alipoliona kwa dhahiri pengo kati ya aliyeamua kuwekeza kwenye mali na aliyewekeza kwenye starehe, kama yeye.


“Kwa nyumba hii na demu mkali kama huyo hata kama ni mgonjwa, akikaa hapa sebuleni ugonjwa ungeaga wenyewe,” Kisu aliwaza na kujikuta akiachia tabasamu.


Vitu vyote vilivyokuwemo pale sebuleni viliashiria kuleta ndani hewa mwanana yenye kutuliza hisia, huku muziki laini ukisikika kwa mbali. Muda wote wakati Kisu akistaajabia uzuri wa ile sebule Carlos na Jacky walikuwa kimya wakimtazama kwa makini.


“Shukrani kwa hao walioweza kuyageuza mawazo yao kuwa vitu halisi,” alijikuta akiwaza tena kisha akayahamisha macho yake na kumtazama Carlos.


“Carlos, mbona jumba kubwa sana namna hii, kwani humu ndani mnaishi watu wangapi?” swali la ghafla lilimtoka Kisu maana hakuweza kujizuia.


“Kwa nini? Tunaishi wawili tu, mimi na bibie hapo,” Carlos alijibu huku akigeuza shingo yake kumuonesha Kisu aliposimama Jacky.


“Wawili tu!” Kisu alionesha kushangaa huku akiendelea kupepesa macho mle ndani, sauti yake ilibeba mshangao.


“Kwani hujawahi kufika hapa?” Jacky akamuuliza Kisu huku akimtazama kwa makini.


“Ndiyo kwanza leo anafika, ila yupo makini sana, ni jana usiku ndiyo nimemuelekeza kwa simu na leo asubuhi kagonga getini,” Carlos akasema huku akimtazama Jacky kisha kama aliyekumbuka jambo akampiga ukope akimwonesha kwa ishara kwa Kisu.


“By the way, huyu ni rafiki yangu wa kitambo sana tangu kipindi kile naanza biashara ya madini kule Mirerani, anaitwa Kisu, hapa katikati tulipoteana sana, jana usiku ndo nikakumbuka nikampigia simu aje kwa ajili ya ile ishu,” alisema Carlos.


“Ooh karibu sana, bwana Kisu,” Jacky alimkaribisha yule mwanamume huku akiachia tabasamu pana.


“Asante, lakini naona kama utambulisho wenyewe wa upande mmoja tu,” Kisu aliitikia huku akimtazama Jacky kwa macho ya matamanio.


“Huyu ni mke wangu, anaitwa Jacky, nilimuoa mwaka juzi jijini Arusha,” Carlos alisema.


“Okay, nashukuru kukufahamu shem,” Kisu alisema huku akijiweka vizuri pale kwenye sofa.


“Hata mimi nashukuru kukufahamu,” Jacky alisema huku akiachia tabasamu. Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya huku Kisu akiwa anatafakari.


“Sasa mkuu, nimeitika wito wako, nipe michongo,” hatimaye Kisu alivunja ule ukimya akimwambia Carlos kwa sauti nzito na tulivu huku akiendelea kumtupia jicho la wizi Jacky akionesha kumtamani. Alifanya vile akiwa hataki Carlos ashtukie, hivyo akayahamishia macho yake kwa Carlos. Muda ule ule Jacky aliondoka akaelekea jikoni huku akiwaacha wanamume wawili pale sebuleni.


“Sijui utakunywa nini, chai, kahawa, bia au…” aliuliza Carlos.


“Shusha mzinga wa whisky hapa twende sawa,” alijibu Kisu.


Carlos aliinuka na kwenda kwenye kaunta ndogo ya baa katika jengo lile kisha alifungua kabati kubwa la vioo la ukutani na kutoa chupa kubwa ya whisky na bilauri moja na kuviweka juu ya meza.


Kwa kitambo fulani kulizuka ukimya, Carlos alikuwa akimtazama Kisu kwa makini wakati akijimiminia pombe kwenye bilauri na kugida kwa pupa huku akisisimkwa mwili.


Aliendelea kunywa ile pombe kwa kitambo kirefu akiwa kimya hadi alipoanza kuchangamka zaidi, ndipo Carlos akaamua kuvunja ukimya.


“Sasa, ni kama nilivyokudokeza jana usiku, huenda wiki hii tutakuwa na kazi moja nzito…” Carlos alisema na kuongeza.




Kwa kitambo fulani kulizuka ukimya, Carlos alikuwa akimtazama Kisu kwa makini wakati akijimiminia pombe kwenye bilauri na kugida kwa pupa huku akisisimkwa mwili.


Aliendelea kunywa ile pombe kwa kitambo kirefu akiwa kimya hadi alipoanza kuchangamka zaidi, ndipo Carlos akaamua kuvunja ukimya.


“Sasa, ni kama nilivyokudokeza jana usiku, huenda wiki hii tutakuwa na kazi moja nzito…” Carlos alisema na kuongeza.


Endelea...


“Kama unavyojua dili zangu, huwa sibahatishi katika mipango yangu, na katika matukio yote ya uhalifu niliyowahi kufanya hakuna hata moja lililofeli.”


Kisu alibetua kichwa kukubaliana naye huku akimsikiliza kwa makini zaidi.


“Ila ujue kuingia benki na kutoka na fedha ambazo si halali yenu inataka ujasiri usio wa kawaida. Nimekuchagua wewe kutokana na sifa yako ya ujasiri uliopitiliza, uhuni, wehu na ubabe ili tufanye kazi hiyo, lakini pia nikijua kuwa utaniletea vijana wawili mahiri zaidi wenye ujasiri kama ulivyo mwenyewe,” Carlos alisema akiwa amemkazia macho Kisu.


“Hili wala usikonde, kuna watu wawili kama nilivyokueleza jana kwenye simu, Kabwe na Liston,” Kisu alisema na kuongeza. “Listoni nadhani unamkumbuka, ni yule jamaa wa ile ishu ya tanzanite feki mlipompiga yule Mjerumani enzi zile…”


“Ee, huyo sawa,” Carlos alidakia.


“Basi huyo mwingine ndiyo balaa, hana spea kabisa,” Kisu alisema na kuongeza, “Ukiwataka hata sasa hivi naweza kuwapigia simu nikawaelekeza waje hapa.”


“Ngoja kwanza tuyajenge, tukishaelewana ndiyo uwaite,” Carlos akasema na kuongeza, “Kazi ya kwanza unayotakiwa kuifanya, itabidi ushughulikie bunduki na jinsi gani utaweza kupata sare ya mlinzi wa kampuni ya The Jacarandah Group.”


Kisu alibetua kichwa chake kukubali huku akiinua bilauri yake na kugida pombe yote iliyokuwemo kisha aliikita ile bilauri juu ya meza.


“Pia tunahitaji kupata gari kama lile la The Jacarandah Group kwa ajili ya kuchukulia fedha kutoka benki, halafu kazi yangu ni kuipata hundi ya kampuni ya The Jacarandah Group kwani nina uhakika wa kuipata wakati wowote kuanzia leo jioni, ninachosubiri kwa sasa ni kopi ya hundi yao yenye saini za wanaoidhinisha kutoa pesa benki,” Carlos aliendelea kumweleza Kisu.


* * * * *


Asubuhi na mapema ya saa kumi na mbili kwa mujibu wa saa ya ukutani, Mama Jasmine ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka na kupiga pasi nguo za mumewe Yusuf, kisha akazitundika kwenye henga ya nguo. Alichukua ndoo akawahi bombani na kukinga maji aliyokuwa akiyamimina kwenye dumu kubwa maarufu kama jaba.


Alipomaliza aliingia chumbani akasimama kando ya kitanda, akamtazama mumewe kwa makini. Yusuf alikuwa bado yupo kwenye lindi zito la usingizi, hajitambui na ilionesha kuwa ingemchukua muda mwingine mrefu kuzinduka.


Kando ya Yusuf alikuwa amelala Jasmine. Mama Jasmine alizitoa nguo zilizokuwa ndani ya tenga la nguo chafu na kuanza kuzikagua, kama ilivyokuwa desturi yake kabla hajazifua. Alikwenda nje akazifua chap chap na kuzianika kisha akarudi tena chumbani.


Pale kitandani Yusuf alikuwa bado kalala, alijipindua na kutafuna maneno ambayo hayakusikika akiwa bado yupo usingizini. Mama Jasmine alijenga picha akilini mwake, ingekuwaje iwapo ataamua kuachana na mumewe! Akajiuliza kwani ni mara ngapi mumkewe aliwahi kumkosea au kulala nje, hakuna, ndiyo kwanza imetokea.


Je, alikuwa na uhakika gani kuwa mumewe alilala na mwanamke na si kama alivyoelezwa na Yusuf mwenyewe kuwa alikuwa na marafiki zake? Na kama Yusuf yuko sahihi, je, hakuona kama alikuwa anamkosea heshima mumewe kwa kutomuamini? Maswali mengi yalianza kupita kichwa kwa Mama Jasmine pasipo majibu.


Alimtazama tena Yusuf pale kitandani alipolala akiwa hajitambui wala hajijui, “Hmm, isingekuwa ni mimi si angekesha na kulala huko nje kama bundi?” Mama Jasmine aliwaza huku akihisi huruma huku donge la fadhaa likianza kumkaba kooni.


Alionekana kuingiwa huruma moyoni, na mara kikohozi kidogo kilimtoka, na nyuma yake wimbi la machozi lilikuja mbio na kuyafanya macho yake yajenge malengelenge ya machozi.


Yusuf alijigeuza na kushtuka pale aliposikia kikohozi cha mkewe. Macho yake yalikuwa mekundu na yaliyovimba kidogo kutokana na usingizi aliokuwa nao. Uso wake na mgongoni alikuwa na alama za mistari zilizosababishwa na matandiko.


Alimtazama mkewe huku uchovu ukimuendesha kutokana na jinsi alivyoonekana. Alijiinua na kukaa kitandani, miguu ikiwa chini huku akifikicha macho na kupiga miayo. Mama Jasmine aliendelea kusimama akimtazama kwa makini, lakini alikwisha yafuta haraka machozi yaliyokuwa yakimlengalenga machoni, baada ya kugundua Yusuf ameamka.


Yusuf alimtazama mkewe kwa wasiwasi, hakujua nini kilichokuwa kikiendelea kichwani kwa mkewe isipokuwa alichojua ni kuwa siku iliyokuwa imepita ilikuwa ni ndefu sana kwao.


Pia hakujua ni kwa nini yote yale yalitokea kwa siku moja ingawa alichojua ni kwamba yalitokea na kuitikisa ndoa yao kiasi cha nyufa kuanza kuonekana. Yusuf aliinamisha kichwa chake chini akiyakwepa macho ya mkewe huku akiomba mtikisiko usiendelee maana hakuwa tayari kuhimili mitikisiko mingine.


Alitamani ugomvi wao ungekuwa ndoto, maana kama mkewe aangeendelea na msimamo wake kulikuwa na uwezekano wa kuzaliwa nyufa kubwa na hatimaye nyumba ingeanguka…


“Habari ya asubuhi?” sauti ya Mama Jasmine ilimshtua Yusuf na kumuondoa haraka kutoka kwenye yale mawazo, hakutegemea kama mkewe angemsalimia kwa upendo kiasi kile.


“Safi tu, wewe?” Yusuf alijibu huku akimtazama mkewe kwa wasiwasi lakini akajikuta akiachia tabasamu baada ya kuuona uso wa mkewe ukiwa ana tashwishwi.


“Mi mzima,” alijibu Mama Jasmine, kisha kikapita kimya kati yao.


“Kwa nini jana uliamua kulala pale nje au ndiyo ulisusa?” Mama Jasmine alimuuliza mumewe akimkazia macho usoni.


“Sikususa, au unadhani nilipenda kulala pale, si vile tu wewe uliniletea mapozi nikaona isiwe taabu, lakini nafikiri tumeshayamaliza, au siyo?” Yusuf alijibu huku akiitazama saa yake ya mkononi ambayo alilala nayo, kisha akashusha pumzi ndefu.


“Nilikaa pale kitandani wee kisha nikazima taa na kulala, baadaye niliposhtuka sikukuona, huruma ikaniingia juu yako. Nikatoka nikidhani umelala sebuleni lakini sikukukuta, nikaelekea uwani pia haukuwepo. Hapo hasira zikanipanda tena, nilipotoka barazani si nikakuta unaweweseka kama kifaranga kilichonyeshewa mvua. Nikakuamsha ukaamka ukaanza kupepesuka ukielekea ndani kama mlevi, kama ungejiona ungejicheka na kuona aibu,” Mama Jasmine alisema huku akitabasamu.


“Nashukuru sana, mke wangu, kwa kuonesha jinsi gani ulivyo na huruma wala huna kinyongo kabisa,” Yusuf alisema huku akijiweka sawa pale kitandani.


“Ni kweli, sina kinyongo na ni mwingi wa huruma, ila kiukweli jana hukunikera tu bali uliniumiza sana…” Mama Jasmine alisema huku akimtazama Yusuf kwa aibu.


“Aah, Mama Jasmine, si yamekwisha, sasa unataka kuyaanzisha tena?” Yusuf alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Ndiyo yamekwisha, ila tu nasema kuwa una bahati sana, kama jana ningekuacha ulale hapo halafu waje vibaka, sijui ungefanyaje,” Mama Jasmine alimwambia Yusuf huku akitabasamu.


“Jana au leo kabla hapajapambazuka?” Yusuf aliuliza mkewe huku akivuta picha, ingekuwaje endapo angevamiwa na vibaka!


“Kweli, ni leo,” Mama Jasmine alijisahihisha na kuendelea, “Siku nyingine rudia kususa halafu ulale tena hapo nje utaipata habari yake.”


Mama Jasmine alisema na kuanza kusogea kwenye meza ndogo iliyokuwa pembeni ya kitanda akitaka kuchukua kitambaa chake cha kufunika nywele, lakini kabla hajakichukua, Yusuf alimvuta na kumtupia kitandani, naye akajitupa juu yake. Mama Jasmine alilala chali.


Mambo kwa upande wa Yusuf yameanza kurudi kwenye mstari, je, atavihimili vishindo vya Jacky ili aendelee kuilinda ndoa yake au ndiyo ataharibu zaidi. Vipi kuhusu Jacky, Carlos na sasa Kisu, nini kipo nyuma yao? Jibu ni kuendelea kufuatilia simulizi hii ya kusisimu




“Jana au leo kabla hapajapambazuka?” Yusuf aliuliza mkewe huku akivuta picha, ingekuwaje endapo angevamiwa na vibaka!


“Kweli, ni leo,” Mama Jasmine alijisahihisha na kuendelea, “Siku nyingine rudia kususa halafu ulale tena hapo nje utaipata habari yake.”


Mama Jasmine alisema na kuanza kusogea kwenye meza ndogo iliyokuwa pembeni ya kitanda akitaka kuchukua kitambaa chake cha kufunika nywele, lakini kabla hajakichukua, Yusuf alimvuta na kumtupia kitandani, naye akajitupa juu yake. Mama Jasmine alilala chali.


Endelea...


Kitendo kile kilimwamsha Jasmine, aliinuka akakaa kitako pale kitandani huku akiwatazama wazazi wake kwa macho ya udadisi. Mama Jasmine alimsukuma Yusuf na kuinuka haraka, akachukua mswaki wa Jasmine na kuutia dawa, kisha akamteremsha Jasmine kutoka pale kitandani.


“Haya, twende ukapige mswaki, mtoto mzuri,” Mama Jasmine alisema huku akimpiga ukope Yusuf, akatoka na Jasmine hadi uwani, akachukua kikombe na kuchota maji yaliyokuwa ndani ya jaba na kumpa.


“Haya, kaa hapa upige mswaki vizuri na ukimaliza lazima nikukague, usiondoke hadi nije, sawa?” Mama Jasmine alimwambia Jasmine huku akianza kupiga hatua kuingia ndani, alipofika mlangoni aligeuka kumtupia jicho na kumuona akianza kujishughulisha na meno yake.


Jasmine alikuwa amechuchumaa kwenye ukingo wa ukuta wa ule ua akajitahidi kuchokonoa mswaki wake huku na huko kinywani kwake, kwani alijua baada ya kumaliza kupiga mswaki kulikuwa na ukaguzi.


Mama Jasmine aliingia chumbani ambako alimkuta Yusuf akiwa bado anamsubiri kwa hamu, alikwenda kuketi kitandani kando ya Yusuf huku akimtazama kwa aibu na hapo Yusuf akamdaka na kumsukumia kitandani. Mama Jasmine alijiangusha chali huku akiitandaza mikono kama aliyekuwa akiwambwa msalabani.


Yusuf alikuja juu yake huku mikono yake akiitandaza kuishikilia mikono ya mkewe na nyuso zao zikatazamana kwa ukaribu. Mama Jasmine alifumba macho yake kuyakwepa macho ya Yusuf, na taratibu wakajikuta wakianza kuhamia katika dunia nyingine kabisa, dunia ya mahaba… kuanzia hapo hapakuwa na kitu kingine zaidi ya kupeana mahaba mazito mazito.


Walipomaliza Yusuf alijifunga taulo kisha wote walielekea bafuni kwa ajili ya kuoga. Walipotoka nje Mama Jasmine alimkuta Jasmine akiwa bado amekaa pale pale upenuni mwa ua wa ile nyumba alipomwacha akisubiri kukaguliwa.


“Umemaliza?” Mama Jasmine alimuuliza mwanawe huku akimkazia macho. Jasmine alikubali kwa kichwa huku akikenyua meno yake kumuonesha mama yake.


“Haya nenda kanisubiri ndani kwenye makochi, nikitoka kuoga nakuja kukukagua kama umesugua vizuri,” Mama Jasmine alimwambia Jasmine huku akichota maji kwenye lile jaba na kuyajaza kwenye ndoo ya kuogea, kisha akayapeleka bafuni ambako mumewe Yusuf alikuwa amesimama anasubiri. Mama Jasmine alioga haraka haraka na kutoka akimwacha Yusuf anaendelea kuoga taratibu, yeye alikuwa akimuwahi Jasmine.


Baada ya kumaliza kuoga Yusuf aliingia ndani na kuzikuta nguo zake zikiwa tayari zimenyooshwa vizuri na kuwekwa sehemu maalumu tayari kwa kuvaliwa. Alijiandaa na kuvaa huku moyoni akiwa amefurahi sana, hasa baada ya kuonekana kuwa mkewe alikuwa amemsamehe kabisa.


Yusuf alipomaliza zoezi lile la kujiandaa alimuaga mkewe kwa kumbusu kwenye paji la uso, kisha akambusu mwanawe Jasmine na kutoka, akaelekea kituo cha daladala cha Bungoni huku akipiga mluzi wa ushindi.


* * * * *


Saa ya ukutani sebuleni nyumbani kwa Carlos na Jacky ilisomeka kuwa saa sita na robo mchana. Katika ile sebuleni kulikuwa na wanaume wanne waliokuwa wameketi wakijadiliana hili na lile huku maongezoi yao yakisindikizwa na pombe kali.


Juu ya meza kulionekana chupa kadhaa kubwa pombe aina ya whisky, Grant na mvinyo mwekundu wa Kifaransa wa Navette de Marseille na bilauri ndefu nne.


Kwenye kochi dogo la sofa Carlos alikuwa ameketi akizungumza na vijana wawili waliokuwa wameketi kwenye kochi kubwa lililokuwa mkabala na lile aliloketi.


Vijana hao ni Kabwe, ambacho kilikuwa kifupi cha majina ya Kassim Bwenzi. Huyu alikuwa na kimo cha wastani na mweusi kama Mjaluo akiwa na misuli imara ya mikononi iliyotuna kikamilifu kwa namna kuonesha kuwa alikuwa na kawaida ya kufanya mazoezi ya nguvu yasiyokuwa na kikomo.


Kabwe alikuwa amevaa fulana nyeupe iliyombana na kulionesha vyema umbo lake lililojengeka kwa misuli na alivaa suruali ya jeans ya rangi ya bluu na buti ngumu aina ya ‘safari boot’ za rangi ya hudhurungi.


Kichwani alivaa kofia aina ya kapelo ya rangi nyekundu iliyokuwa imetuama vizuri kwenye upara wake uliokuwa unawaka na usiokuwa na unywele hata mmoja.


Japokuwa alikuwa mzungumzaji mzuri na mwenye kujua mambo mengi lakini Kabwe hakupata nafasi ya kupata elimu bora kutokana na hali ya ufukara uliopindukia wa famili yake, alilelewa na mama pekee na alikuwa na ndugu zake wengine watano, huku baba yao akiwatelekeza na kwenda kusikojulikana wakati Kabwe akiwa na miaka saba tu.


Kuanzia hapo walijikuta wakiishi maisha ya ufukara uliopindukia, na hata hayo madarasa manne ya shule ya msingi ambayo Kabwe alisoma aliyapata kwa taabu sana.


Wakati akisoma ilimlazimu Kabwe na ndugu zake kwenda shuleni wakiwa na njaa, wakashinda huko na njaa na waliporudi nyumbani walilazimika kumsaidia mama yao aliyekuwa mlemavu kutafuta chakula kwa kufanya kazi za vibarua, ndipo Kabwe akajionea upuuzi kuendelea na shule. Akaachana na shule, akawa anarandaranda mitaani na watoto wengine wa mtaani.


Hapo ndipo alipoanza kujifunza uporaji madukani na mitaani ili kujipatia riziki, na ndipo pia alipoanza kujenga mzuka wa kujisikia kuua. Alianza polepole kwa kunyonga shingo za kuku na kuwatazama wakipaparika kwa maumivu makali hadi kufa. Kisha akahamia kwenye kuvizia paka akijifanya Manyaunyau, aliwakamata na kuwatenganisha miili yao na vichwa. Ukatili huu uliuburudisha sana moyo wa Kabwe.


Alipofikisha umri wa miaka ishirini Kabwe alikwisha toa roho tatu za watu waliokuwa wameingia katika anga zake.


Kijana mwingine aliyekaa pamoja na Kabwe aliitwa Liston George, huyu alikuwa mrefu na mweupe kiasi, mwenye umbo kakamavu kama wachezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani. Alikuwa amevalia shati jeupe la mistari ya rangi ya bluu la mikono mirefu, suruali ya jeans ya rangi nyeusi na raba nyeusi.


Macho yake yalikuwa makubwa na mekundu yenye uchovu lakini yaliyokuwa na kila dalili ya kuonya na muda wote alikuwa akimtazama Carlos huku tabasamu jepesi likijitokeza taratibu usoni mwake.




Kijana mwingine aliyekaa pamoja na Kabwe aliitwa Liston George, huyu alikuwa mrefu na mweupe kiasi, mwenye umbo kakamavu kama wachezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani. Alikuwa amevalia shati jeupe la mistari ya rangi ya bluu la mikono mirefu, suruali ya jeans ya rangi nyeusi na raba nyeusi.


Macho yake yalikuwa makubwa na mekundu yenye uchovu lakini yaliyokuwa na kila dalili ya kuonya na muda wote alikuwa akimtazama Carlos huku tabasamu jepesi likijitokeza taratibu usoni mwake.


Endelea...


Liston alikuwa mkimya sana, asiyependa kuongea lakini alikuwa mwingi wa vitendo. Na kama mtu angemuona asingeweza kudhani kuwa amekwisha fanya matukio makubwa sana katika nchi mbalimbali pasipo kushtukiwa.


Liston alikuwa msomi wa shahada ya kwanza aliyoipata kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alisomea Uhandisi wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na programu maalumu iliyokuwa imeanzishwa na Jeshi la Wananchi kwa ajili ya kuchukua vijana wasomi na walioko vyuoni.


Baada ya kumaliza chuo Liston alikwenda kulitumikia Jeshi kwa muda mfupi na kituo chake cha kazi kikiwa Kambi ya Mzinga na akiwa huko alipata mafunzo maalumu ya kijeshi, huo ulikuwa mpango maalumu wa kuandaliwa kama Jeshi la Akiba. Liston pia alipata mafunzo ya kujihami ya karate and judo na kufanikiwa kupata mkanda mweusi.


Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi Liston alijaribu kurudi tena chuoni kusoma shahada ya pili lakini alilazimika kukatisha masomo kutokana na matatizo makubwa yaliyoikumba familia yake.


Hakuna aliyejua ni kipi hasa kilichomsukuma kuingia kwenye uhalifu, japo alikuwa msomi mwenye taaluma ya uhandisi na hakupenda kabisa kuongea mambo yaliyohusu maisha au familia yake, nadhani ndiyo sababu ya kupenda kuwa mkimya muda wote.


Katika kochi jingine aliketi Kisu akiwa mtulivu sana huku akiendelea kugida pombe kali taratibu. Wote watatu walikuwa wakimsikiliza Carlos aliyekuwa akitoa maelekezo ya namna ambavyo kazi ingefanyika, aliwaeleza ugumu wa kazi husika uliowakabili mbele yao na jinsi ambavyo kila mmoja wao angeweza kufaidika kwa kupata mgao wake kutokana na kazi ile.


Lakini kabla hajaeendelea zaidi Jacky aliingia pale sebuleni kutokea jikoni akiwa mwenye furaha sana, mkononi alikuwa ameshika simu yake na alikuwa akimtazama Carlos kwa tabasamu. Jacky alikuwa amevaa fulana nyepesi nyeusi iliyoyaficha vyema matiti yake imara na juu yake alikuwa amevaa aproni, vazi maalumu lililotumika alipokuwa katika shughuli za mapishi.


Chini alivaa suruali yake ya rangi nyeusi ya jeans iliyolichora vyema umbo lake matata na miguuni alikuwa amevaa sandals nyepesi za kufunga na kamba.


“Darling, things have gone well,” (Mpenzi, mambo yameiva) Jacky alipaza sauti yake kumwambia Carlos na kuwafanya watu wote wageuke kumtazama kwa shauku kubwa ya kutaka kusikia kile alichokuwa anataka kuwaambia.


“Yusuf called me right now, says he has got a copy of their signed check, so I will meet him later in the evening,” (Yusuf kanipigia simu sasa hivi, anasema amepata kopi ya hundi yao yenye saini, hivyo nitakutana naye baadaye jioni) Jacky alisema huku akisimama jirani na kochi alilokuwa ameketi Carlos.


Habari ile ilikuwa njema zaidi kwa watu wote waliokuwepo pale sebuleni, walitazamana na kutabasamu huku wakibetua vichwa kuonesha kuwa tayari walishapiga hatua kubwa kuelekea kwenye ushindi.


“That's good news, I'll make sure we don't lose this opportunity,” (Hiyo ni habari njema kabisa, nitahakikisha hatuipotezi nafasi hii) Carlos alisema huku akinyanyua mkono wake na kuupitisha nyuma ya Jacky na kumpapasa mgongoni huku akiendelea kutabasamu.


Jacky alimtazama Carlos kwa utulivu, hata hivyo uso wake haukuwa na tashwishwi yoyote. Aliwatupia jicho la wizi Kabwe na Liston kisha alianza kupiga hatua zake kwa madaha kuelekea jikoni.


Kisu, Kabwe na Liston walimsindikiza Jacky kwa macho huku wakionesha kuwakwa na tamaa, hata hivyo hakuna aliyethubutu kusema chochote kumhusu Jacky kwa kuwa walimhofia sana Carlos. Hivyo, kitambo kifupi cha ukimya kikafuatia mle ndani huku kila mmoja akiwaza lake.


“Okay, nadhani kila kitu kipo kwenye mstari, sasa inakuwaje kuhusu malipo yetu?” hatimaye Kabwe alivunja ukimya huku akimkazia macho Carlos.


“Mnataka mlipwe leo leo kabla hata ya kufanya kazi?” Carlos alimuuliza Kabwe kwa mshangao huku akimkazia macho.


“Unajua nini, lazima niseme ukweli… umetutia hamasa kubwa sana kwa huu mjengo kama ikulu na asset mbalimbali unazomiliki, hata sisi tunahitaji kuishi maisha kama haya… kwa hiyo tunataka kujua tutalipwaje baada ya kazi, namaanisha malipo yetu ni shilingi ngapi?” Kabwe alisema huku akigeuza shingo yake kuwatazama Liston ambaye muda mwingi alikuwa kimya na Kisu.


Liston alibetua kichwa chake kuonesha kukubaliana na kauli ya Kabwe kisha akanyanyua bilauri yake na kugida pombe yote iliyokuwemo huku akisisimkwa mwili na kuikita ile bilauri juu ya meza.


“Ooh, nikadhani labda mnataka mlipwe kabisa pesa zenu hata kabla ya kazi haijafanyika!” Carlos alisema na kuongeza, “Kuhusu Kisu nimeshaongea naye kivyake, ila ninyi mtapata shilingi milioni hamsini, ishirini na tano kwa kila mmoja,” Carlos alisema kwa sauti tulivu huku akiwatazama kwa makini.


Kabwe na Liston walitazamana, kisha kitambo kifupi cha ukimya kikafuatia tena mle ndani, walionekana kuongea kwa ishara na kuonesha kuafikiana.


“Basi hakuna noma, kamanda, wacha sisi tusepe tukawahi mishemishe zingine, nakuaminia na ninaamini tutafanya kazi nzuri kwani Liston amenihakikishia kuwa hunaga longolongo kabisa,” Kabwe alisema huku akibetua kichwa chake kuonesha msisitizo. Aliinuka na kumpa ishara Liston waondoke.


“Ukishaweka mambo yote sawa mjulishe tu braza Kisu, yeye anajua pa kutupata, sisi tupo kamiligado,” Kabwe aliongezea huku akibeba chupa moja kubwa ya whisky, ambayo ilikuwa haijatumika ikiwa juu ya meza. Liston naye aliinuka, wakaagana na Carlos wakipeana mikono kisha Kabwe na Liston waliondoka wakiwaacha Carlos na Kisu bado wanatafakari huku wakiendelea kunywa pombe taratibu.


* * * * *


Zilikuwa zimesalia dakika chache kabla ya kutimia saa moja kamili usiku, giza tayari lilikuwa limeanza kutanda. Hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa ya baridi kidogo na manyunyu ya mvua yalikuwa yameanza kuanguka kutoka angani.


Pamoja na mvua ile lakini haikuzuia pilika pilika za watu zilizokuwa zimeshamiri katikati ya jiji hilo na hivyo kulifanya liendelee kuchangamka sana kama ilivyokuwa kawaida yake.


Wakati huo Jacky akiwa ndani ya chumba kikubwa chenye hadhi cha hoteli moja iliyokuwa katika ghorofa ya kwanza ya jengo la NSSF katika makutano ya barabara za mitaa ya Samora na Nnamdi Azikiwe, katikati ya jiji la Dar es Salaam. Ndani ya chumba kile kulikuwa na hewa safi iliyokuwa ikisambazwa taratibu na kiyoyozi kikubwa.


Alikuwa amefika pale na kulipia chumba kwa siku moja akijiandikisha kwa jina la Diana Mulenga kutoka Zambia na kwamba alikuwa jijini Dar es Salaam kuja kumtembelea rafiki yake wa kiume ambaye ni Mtanzania.




Wakati huo Jacky akiwa ndani ya chumba kikubwa chenye hadhi cha hoteli moja iliyokuwa katika ghorofa ya kwanza ya jengo la NSSF katika makutano ya barabara za mitaa ya Samora na Nnamdi Azikiwe, katikati ya jiji la Dar es Salaam. Ndani ya chumba kile kulikuwa na hewa safi iliyokuwa ikisambazwa taratibu na kiyoyozi kikubwa.


Alikuwa amefika pale na kulipia chumba kwa siku moja akijiandikisha kwa jina la Diana Mulenga kutoka Zambia na kwamba alikuwa jijini Dar es Salaam kuja kumtembelea rafiki yake wa kiume ambaye ni Mtanzania.


Endelea...


Wakati anaingia katika ile hoteli, Jacky alikuwa katika muonekano tofauti kabisa, kwa yeyote aliyemfahamu kama angemuona pale ingemchukua muda mrefu kubaini kuwa aliyekuwa akimtazama alikuwa ndiye Jacky.


Alikuwa amevaa wigi la nywele ndefu zilizolalia mgongoni na kumfanya afanane na machotara wa Kizungu huku sura yake yenye mvuto wa asilimia mia moja ikipendezeshwa zaidi kwa kope ndefu za bandia zilizong’arishwa na kuyafanya macho yake yawe wazi nusu, na mikononi alikuwa na kucha ndefu za bandia.


Alivaa miwani ya kijasusi ambayo kwa macho ya kawaida ilionekana kama ya mtu mwenye matatizo ya uoni, ilikuwa na lenzi maalumu iliyokuwa na kamera ya kurekodi matukio mbalimbali aliyoyataka. Jioni ile alikuwa amevaa gauni refu la kitenge cha wax lililodariziwa vizuri na kichwani alivaa kilemba kikubwa. Alionekana ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa kifedha, na pengine mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio.


“Now I’m ready… let me wait for Yusuf to accomplish my mission,” (Sasa niko tayari… ngoja nimsubiri Yusuf ili kukamilisha misheni yangu) Jacky aliwaza mara tu baada ya kutoka bafuni na kujibwaga kitandani kumsubiri Yusuf, kwani walikuwa wamekubaliana kukutana katika hoteli ile jioni ili akabidhiwe nakala kivuli ya hundi iliyokuwa na saini.


“When I finish this project, I’ll go back to a normal life like other married women…” (Nitakapomaliza kazi hii, nitarudi katika maisha ya kawaida kama wanawake wengine walioolewa…) Jacky alishtuliwa na sauti ya mtu aliyegonga mlangoni taratibu.


Aliinuka na kufungua mlango kidogo ilia pate upenyo wa kumuona aliyekuwa nje, na hapo akakutana na sura ya Yusuf aliyekuwa amesimama akiwa na tashwishwi. Jacky akaufungua mlango kumkabili Yusuf, lakini Yusuf alipomuona Jacky, ambaye yeye alimfahamu kwa jina la Belinda, akashtuka.


Yusuf alishikwa na bumbuwazi akidhani labda alikuwa amekosea namba ya chumba, kwani alikuwa akimuona msichana mwingine kabisa ambaye hakumtarajia. Aliinua macho yake kusoma namba kwenye kibao kilichokuwa juu ya mlango wa kile chumba.


Akiwa bado ameshikwa na bumbuwazi na kabla hajajua afanye nini akashtukia amevutwa na kuingizwa ndani ya kile chumba huku mlango ukifungwa haraka, na kilichofuata baada ya ahapo Jacky alimkumbatia na kumwagia mabusu mfululizo huku akijitambulisha kwake kuwa yeye ni yule yule Belinda aliyemfahamu.


“Nilikuwa na wasiwasi kuwa pengine usingeweza kuja baada ya kunieleza kuwa kulitokea mabadiliko ya ratiba zako baada ya kutembelewa ghafla nyumbani ya wakwe zako,” Jacky alisema huku akiupokea mkoba mdogo mweusi aliokuja nao Yusuf na kuuweka kando ya kitanda, kisha akamshika mkono akimuongoza kuketi juu ya kitanda.


“Unajua siwezi kupuuza miadi hii ya muhimu kwetu sote, hasa nikikumbuka namna ulivyonikimbiza mchakamchaka siku ile na vilio vyako vya mahaba ambavyo hadi leo bado havijanitoka akilini mwangu. Kwa ahadi hii hata kama baba yangu mzazi angefariki leo nisingeshindwa kuja kwako,” Yusuf alisema huku akizidi kumtazama Jacky kwa makini.


“Hmm! Stop joking, I know you’re not serious!” (Hmm! Acha utani, najuaa haumaanishi hivyo!) Jacky alisema kwa utani huku akirembua macho yake kwa lengo ya kuzidi kuivuruga akili ya Yusuf.


“It’s true, you are very gorgeous, more than beautiful. Your prettiness I do not know what to compare with. Every time I see you it’s like I have seen an angel pulled from above,” (Ni kweli, wewe ni mrembo sana, zaidi ya mzuri. Uzuri wako sijui niufananishe na nini. Kila ninapokuona ni kama nimeona malaika uliyeshushwa toka juu) Yusuf alisema na kumfanyia Jacky atoe tabasamu bashasha huku akimkumbatia Yusuf na kumpiga mabusu mfululizo.


“Belinda, you are a very exceptional woman I have ever met…” (Belinda, wewe ni mwanamke wa kipekee kabisa kuwahi kukutana naye…) Yusuf alimwambia Jacky huku akimkumbatia kwa nguvu.


“And since we met that day it’ll not pass even a second without thinking about you. Within a short period of time you have entered into my veins and I am wondering if there is anything you have put in my body in this way,” (Na tangu tulipokutana siku ile haipiti hata sekunde moja bila kukuwaza. Ndani ya kipindi kifupi tu umeniingia katika kila mshipa wa mwili wangu hadi najiuliza kama kuna kitu umeniwekea kiasi cha kunichanganya namna hii!” maneno mfululizo yalizidi kumtoka Yusuf.


“Yusuf, we still have a lot of time to talk about all these things but now there is only one thing we have to do,” (Yusuf, bado tuna muda mwingi tutaongea mambo hayo yote lakini kwa sasa kuna jambo moja tu ambalo tunatakiwa kulifanya) Jacky alimwambia Yusuf na kumvutia kifuani kwake kisha akapeleka mkono wake ikulu na kuanza kutomasa malighafi zake kwa ufundi wa hali ya juu, mara zikafura kwa hasira.


Jacky alitumia utundu wa hali ya juu kumfanya Yusuf aongee lugha aliyoitaka kwani Waswahili wanasema kuwa ‘kichwa cha chini kikisimama cha juu huwa hakifanyi kazi sawasawa’.


“Belinda, umeichanganya akili yangu kiasi kwamba najihisi kuwa nataka kuwa mwendawazimu kwa ajili yako…” Yusuf alisema huku akihema kwa nguvu na muda mfupi uliofuata Jacky na Yusuf walikuwa juu ya kitanda kikubwa wakiwa wamemezwa na ulimwengu mwingine kabisa, wa sinema ya mapenzi na mahaba mazito yenye kila aina ya kionjo cha kumtoa nyoka pangoni.


Kwa wakati ule hawakukumbuka kingine chochote isipokuwa kuivunja amri ya sita, huku mapenzi yakionekana kunoga kwa namna yake na miguno ya mahaba ikahanikiza kila mahali mle ndani.


Katika purukshani zile mito ya kujiegemeza pale kitandani iliangukia sakafuni, mmoja huku na mwingine kule lakini hakuna aliyejishughulisha kuiokota. Shuka lilikuwa limevurugwa ovyo wakati wazinzi wale walipokuwa wakivingirishana kwa sarakasi za aina yake pale kitandani.


Takribani muda wa saa moja ulipoyeyuka wote wawili walikuwa hoi huku kila mmoja akionekana kutosheka na mwenzake. Jacky alikuwa wa kwanza kuamka na kuketi kwenye ukingo wa kile kitanda huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa.




“Belinda, umeichanganya akili yangu kiasi kwamba najihisi kuwa nataka kuwa mwendawazimu kwa ajili yako…” Yusuf alisema huku akihema kwa nguvu na muda mfupi uliofuata Jacky na Yusuf walikuwa juu ya kitanda kikubwa wakiwa wamemezwa na ulimwengu mwingine kabisa, wa sinema ya mapenzi na mahaba mazito yenye kila aina ya kionjo cha kumtoa nyoka pangoni.


Kwa wakati ule hawakukumbuka kingine chochote isipokuwa kuivunja amri ya sita, huku mapenzi yakionekana kunoga kwa namna yake na miguno ya mahaba ikahanikiza kila mahali mle ndani.


Katika purukshani zile mito ya kujiegemeza pale kitandani iliangukia sakafuni, mmoja huku na mwingine kule lakini hakuna aliyejishughulisha kuiokota. Shuka lilikuwa limevurugwa ovyo wakati wazinzi wale walipokuwa wakivingirishana kwa sarakasi za aina yake pale kitandani.


Takribani muda wa saa moja ulipoyeyuka wote wawili walikuwa hoi huku kila mmoja akionekana kutosheka na mwenzake. Jacky alikuwa wa kwanza kuamka na kuketi kwenye ukingo wa kile kitanda huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa.


Endelea...


Alijiegemeza ukutani na kutazama juu ya dari kwa muda mrefu kiasi cha kuyavuta macho ya Yusuf pale kitandani na yeye ageuke na kutazama kule juu ya dari.


“What is it, my love?” (Kuna nini, mpenzi?) Yusuf alimuuliza Jacky huku akizifikicha chuchu zake, tukio ambao lilionekana kuamsha upya hisia za Jacky na hapo akageuka na kumtazama Yusuf pale kitandani huku akiachia tabasamu kabambe.


“Nothing, my love, I was just thinking why we’d not stay here until tomorrow morning like the other day so that we’d enjoy our love more,” (Hakuna chochote mpenzi, nilikuwa nafikiria tu kwa nini tusingelala hapa hapa hadi kesho asubuhi kama siku ile ili tufurahie zaidi penzi letu) Jacky aliongea huku akikipapasa kifua cha Yusuf.


“You know, darling, I still have things to keep in track at home, and I’d also want for something like that to happen, and not just for one day but for a whole week so that when we get out of here everyone is dog-tired. You probably told me in advance so that I’d prepare,” (Unajua bado nina mambo ya kuweka sawa nyumbani, nami natamani sana jambo kama hilo litokee, tena si kwa siku moja tu bali wiki nzima ili tukitoka kila mmoja yuko hoi. Pengine ungeniambia mapema ningeweza kujiandaa) Yusuf aliongea kwa utulivu na kutabasamu huku taratibu akizungusha mkono wake kushika kiuno cha Jacky.


“What preparations?” (Kujiandaa kwa lipi?) Jacky aliuliza huku akimtazama Yusuf machoni.


“How to explain to my wife so that she’d understand me, you know I don't want to get into another difficulties and now I have to be more smart,” (Namna ya kuongopa kwa mke wangu ili anielewe, unajua sitaki tena kuingia kwenye mtafaruku mwingine na sasa natakiwa kuwa mjanja zaidi) Yusuf aliongea kwa sauti tulivu ya kubembeleza huku akionekana kuzama kwenye tafakuri fupi.


Jacky aliachia tabasamu ambalo machoni kwa Yusuf lilikuwa tabasamu lenye bashasha na la upendo lakini nafsini mwa Jacky lilikuwa limeficha kitu ndani yake. Ki ukweli ilikuwa vigumu sana kumuelewa Jacky.


Kisha kilifuata kitambo kirefu cha ukimya, Yusuf alizama kwenye tafakari na wakati huohuo Jacky alibaki akimtazama kwa utulivu kisha akavunja ukimya.


“Yes, where is my work?” (Enhe, kazi yangu iko wapi?)


“It’s there, however, it was not an easy thing, my love,” (Ipo, hata hivyo, halikuwa jambo rahisi, mpenzi) Yusuf aliongea huku akimtazama Jacky usoni.


“What do you mean? Did you do or did you not?” (Una maana gani? Kazi umeifanya au hujaifanya?) Jacky aliuliza huku sauti yake ikionekana kuingiwa na kitetemeshi.


“Your work has been done, done very well,” (Kazi yako imefanyika, tena vizuri sana) Yusuf aliongea kwa utulivu huku taratibu akipeleka mkono wake na kukipapasa kiuno cha Jacky.


“Where is it?” (Iko wapi?) Jacky aliuliza huku akionekana kuwa na shauku. Yusuf hakutia neno badala yake taratibu aligeuza kichwa chake kuutazama ule mkoba wa ngozi uliokuwa pembeni ya kile kitanda. Kitendo kile kikamfanya Jacky na yeye ageuke na kuutazama ule mkoba huku tabasamu jepesi likichanua usoni mwake.


Jacky aliutazama ule mkoba kwa hamasa kubwa kama uliokuwa na kito cha thamani ya juu sana, hata hivyo hakuupeleka mkono wake kuuchukua ule mkoba badala yake akawa ni kama aliyekuwa anataka kushuka pale kitandani ili aufuate. Lakini Yusuf aliwahi kumzuia kwa kumshika mkono huku uso wake ukiwa mbali na mzaha kisha akamuuliza Jacky.


“So, what are the plans?” (Kwa hiyo, mipango ikoje?) Yusuf alimuuliza Jacky huku akimtazama moja kwa moja machoni.


“Everything is on the line,” (Kila kitu kipo kwenye mstari) Jacky alijibu kwa mkato.


Yusuf alimtazama Jacky kwa udadisi kabla ya kumuuliza tena. “Who coordinates all the plans?” (Ni nani anayeratibu mipango yote?).


“I am coordinating it myself, why are you worried with me?” (Ninairatibu mimi mwenyewe, kwani vipi una mashaka na mimi?) Jacky alijibu kwa kifupi na kuuliza huku akimkazia macho Yusuf.


Yusuf alitingisha kichwa chake huku akikunja uso wake, kisha aliinamisha kichwa chake akionekana kufikiria kidogo. Kilipita kitambo kifupi cha ukimya, kisha Yusuf aliinua uso wake kumtazama Jacky.


“Are you sure that the whole plan will succeed and I will not be affected?” (Una hakika kuwa mpango mzima utafanikiwa na mimi sitashtukiwa?) Yusuf alimuuliza Jacky akiwa bado amekunja uso wake na kutengeneza matuta madogo madogo usoni.


“I’ve never failed in this kind of plan, tomorrow I’ll tell you how the whole game how will be played,” (Sijawahi kushindwa katika mipango ya aina hii, kesho nitakueleza jinsi mchezo mzima utakavyochezwa) Jacky alisema huku akiangua kicheko hafifu cha mahaba, kisha aliinama na kumbusu Yusuf mdomoni halafu taratibu akajitoa pale kitandani na kuelekea bafuni.


Akiwa na hakika kuwa macho ya Yusuf yalikuwa nyuma yake yakisimsindikiza, Jacky alitembea kwa maringo kama twiga anayekatisha barabara ya mbugani huku mtikisiko wa umbo lake lisilositiriwa na nguo yoyote ukitengeneza taswira nzuri ya kuvutia machoni.


Yusuf alimtazama kwa hamasa huku akionekana kupendezwa na mjongeo ule hadi pale Jacky alipoingia bafuni. Dakika chache baadaye Jacky alirudi kutoka kule bafuni na kuchukua nguo zake, alianza kuzivaa huku akionekana mwenye haraka.


Yusuf akiwa pale kitandani alimtazama Jacky kwa utulivu huku akitabasamu kisha akajisogeza pembeni na kuupeleka mkono wake kuuchukua ule mkoba wa ngozi.


Jacky hakuonekana sana kumtilia maanani badala yake alivaa haraka haraka na alipomaliza alisogea kwenye kioo kikubwa cha kabati la mle chumbani na kuanza kujiweka sawa.


Alipomaliza kujiweka sawa na kuonekana kama Diana Mulenga kutoka Zambia, aligeuka kumtazama Yusuf huku akitabasamu. Yusuf aliufungua ule mkoba wake na kutoa bahasha moja ndogo ya khaki, kisha alinyoosha mkono wake kumpa Jacky.


Jacky aliichukua ile bahasha na kuichana kisha alitoa karatasi nyeupe iliyokuwa na maandishi.


Aliyatuliza macho yake kuiangalia kwa makini ile nakala ya hundi ya The Jacarandaha Group, na kadiri alivyozidi kuiangalia ile karatasi ndivyo tabasamu lake lilivyokuwa likichanua usoni. Muda wote huo Yusuf alikuwa bado ameketi pale kitandani akiwa kimya huku akimtazama Jacky kwa tabasamu.


Jacky aliporidhika aliirudisha ile karatasi kwenye bahasha na kuitia ile bahasha kwenye mkoba wake wa kike. Kisha aliinama akambusu Yusuf mdomoni kwa bashasha.



Jacky aliichukua ile bahasha na kuichana kisha alitoa karatasi nyeupe iliyokuwa na maandishi.


Aliyatuliza macho yake kuiangalia kwa makini ile nakala ya hundi ya The Jacarandaha Group, na kadiri alivyozidi kuiangalia ile karatasi ndivyo tabasamu lake lilivyokuwa likichanua usoni. Muda wote huo Yusuf alikuwa bado ameketi pale kitandani akiwa kimya huku akimtazama Jacky kwa tabasamu.


Jacky aliporidhika aliirudisha ile karatasi kwenye bahasha na kuitia ile bahasha kwenye mkoba wake wa kike. Kisha aliinama akambusu Yusuf mdomoni kwa bashasha.


Endelea...


“Thank you, my love. See you next time,” (Asante mpenzi. Tutaonana wakati mwingine) Jacky alisema na kutoka nje bila kusubiri neno lolote kutoka kwa Yusuf.


* * * * *


Mvua kubwa iliyonyesha kwa saa zaidi ya tano usiku uliokuwa umetangulia, ikiwaudhi hawa na kuwafurahisha wale, ikiharibu hiki na kutengeneza kile, hatimaye ilianuka ghafla asubuhi ya siku iliyofuata na kuliachia jua lenye kupunga la asubuhi likichomoza kutoka ndani ya mawingu na kuifanya miale yake kuleta uhai mpya duniani.


Mvua hiyo ilikuwa imesababisha kijibaridi cha kukera asubuhi ile, hasa kwa jiji la Dar es Salaam lililozoeleka kwa joto kali lisilo la kawaida, watu mbalimbali walionekana mitaani na barabarani wakiwa wamevalia majaketi na wengine walibeba miavuli midogo midogo kama tahadhari.


Saa mbili na nusu za asubuhi ya siku ile, katika barabara ya Lumumba eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, gari dogo aina ya Toyota Corona la rangi nyeupe lililokuwa likitumika kama taksi-bubu lilisimama kando ya Benki ya Biashara.


Benki ya Biashara tawi la Barabara ya Lumumba lilikuwa kubwa na lenye wateja wengi, ambapo wengi wao walikuwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa waliomiliki malori yaliyokwenda nje ya nchi na wamiliki wa majengo ya ghorofa na apartments katika maeneo ya Upanga, Kariakoo, Ilala na maeneo mengine yenye shughuli nyingi za kibiashara.


Jengo la Benki ya Biashara halikuwa na ulinzi wa kiwango cha usalama kamili, labda kwa sababu kulikuwa na kamera nyingi za ulinzi kila sehemu na tangu lifunguliwe hapajawahi kutokea tukio lolote la ujambazi. Au pengine ni kwa sababu waliwaamini sana walinzi wao kutoka Kampuni ya Ulinzi ya K5 Group.


Nje ya lile jengo kulikuwa na walinzi wawili vijana waliokuwa wamevalia sare maalumu za Kampuni ya Ulinzi ya K5 Group na walikuwa wameshika silaha.


“Usizime gari,” Jacky alimwambia dereva wa lile gari dogo aina ya Toyota Corona lililomleta huku akimtazama ndani ya miwani yake myeusi aliyovaa.


Yule dereva alikubali kwa kubetua kichwa pasipo kuhoji chochote, kwani pesa ilikuwa inaongea, alishalipwa shilingi elfu hamsini za kumleta Jacky pale benki na kumsubiria ili kumpeleka Mtoni Kijichi alikoacha gari lake. Dereva alibaki kwenye usukani akiwa mtulivu


Jacky alishuka kutoka kwenye lile gari na kuanza kupiga hatua kwa madaha kuelekea ndani ya ile benki huku akiuning’iniza begani mkoba wake wa ngozi aliokuja nao. Alikuwa amevaa suti maridadi ya kike ya rangi ya kijivu na miwani mikubwa myeusi iliyofunika macho yake.


Alipoingia ndani ya ile benki alikuta wateja wachache waliokuwa wamewahi asubuhi ile ya saa mbili na nusu, Jacky alijiunga katika mstari uliokuwa na watu wanne katika dirisha la Yusuf, macho yake yalikuwa yakimtazama Yusuf kwa makini, ambaye muda ule alikuwa kwenye kaunta yake, nyuma ya kompyuta akihudumia wateja waliofika muda ule.


Hata hivyo, Yusuf alikuwa akitiririkwa na jasho jingi ingawa mle ndani kulikuwa na viyoyozi vilivyotoa ubaridi mkali. Yusuf alimuona Jacky na kujikausha huku akiendelea kuwahudumia wale wateja waliokuwepo.


Ilipofika zamu yake, Jacky alichukua karatasi za benki na kuandika kiasi cha fedha shilingi laki tano alichotaka kukiingiza kwenye akaunti yake, kisha akatoa zile fedha kutoka kwenye mkoba wake na kuziweka kwenye kaunta mbele ya Yusuf huku akimnong’oneza kuwa kila kitu kingekwenda kama walivyopanga. Alipomaliza mchakato mzima wa kuweka fedha akatoka haraka akimwacha Yusuf bado anatiririkwa na jasho.


Alipotoka nje ya lile jengo la benki akatoa simu yake na kutuma ujumbe mfupi kwa Carlos, kisha aliingia kwenye ile taksi-bubu aliyokuja nayo na mara gari likaondoka huku likipishana na gari la bluu aina ya Ford Transit lililokuwa na vioo vya giza vilivyomzuia mtu kuona ndani. Gari lile lilifika na kuegeshwa mbele ya ile benki.


Lilikuwa ni gari lililotengenezwa maalumu kwa ajili ya kusafirisha fedha nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine chini ya ulinzi madhubuti na lilikuwa na nembo ya NeoVision Security, ambayo ilikuwa kampuni ya ulinzi iliyolinda mali za The Jacarandah Group.


Lile gari ndilo lililokuwa likifika pale Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba mara kwa mara kwa ajili ya kuleta au kuja kuchukua fedha.


Hata hivyo, lile gari aina ya Ford Transit lililofika hapo benki siku hiyo halikuwa lile gari la siku zote la NeoVision Security lililokuwa likitumika kusafirisha fedha bali hili liliibwa na kubandikwa stika za NeoVision Security kwa kazi moja tu ya kubeba fedha kutoka Benki ya Biashara tawi la Barabara ya Lumumba hadi mahali palipokusudiwa, basi.


Kutokana na utaalamu uliotumika kuandaa stika zenye nembo za NeoVision Security na aina ya gari lenyewe isingekuwa rahisi hata kwa walinzi na wafanyakazi wa kampuni husika kung’amua kuwa lile halikuwa gari lao, kwani liliweza kufanana kwa kila kitu kwa zaidi ya asilimia tisini, hadi namba za gari.


Ndani ya lile gari kulikuwa na watu wanne. Carlos ndiye aliyekuwa dereva wa lile gari, na kwa kuwa alikuwa mwangalifu sana kutopenda kuhusishwa na tukio lolote la kihalifu, kama alivyo kwa sura yake ya kawaida, alikuwa amevaa glovu maalumu mikononi na kubandika sharubu nyembamba, sharafu zilizo na mchanganyiko wa mvi moja moja na msitu mdogo wa ndevu.


Pia alijitumbukiza ndani ya jaketi zito lililomuhifadhi vizuri na kuvaa miwani mikubwa myeusi huku akitulia kwenye usukani kama dereva mtiifu na mwoga kwa bosi wake aliyesubiri kupewa maelekezo.


Kwenye siti ya mbele ya abiria upande wa kushoto wa dereva, Kisu alikuwa ameketi akiwa mtulivu, alivaa suti maridadi na miwani mikubwa myeusi iliyoyaficha macho yake.


Kwenye siti za nyuma za lile gari waliketi Liston aliyekuwa ameshika bunduki aina ya rifle na Kabwe aliyekuwa ametulia. Wote wawili walikuwa wamevaa sare ya ulinzi wa kampuni ya NeoVision Security.


“Kazi kwenu,” Carlos alimwambia Kisu huku akigeuza shingo yake kuwatazama Kabwe na Liston kwa makini, na hapo Kisu aligeuka kuwatazama Kabwe na Liston na kuwaashiria kushuka kutoka kwenye lile gari.


Wote watatu walishuka na Kabwe alizunguka nyuma na kufungua mlango wa lile gari kisha alitoa begi kubwa la magurudumu na kusimama kikakamavu.


Kisu, Kabwe na Liston walianza kupiga hatua za kikakamavu kuelekea ndani ya lile jengo la Benki ya Biashara, Kisu alitangulia mbele huku akifuatwa nyuma na Liston aliyetembea kikakamavu na Kabwe aliyekuwa anaburuza begi kubwa lenye magurudumu.




“Kazi kwenu,” Carlos alimwambia Kisu huku akigeuza shingo yake kuwatazama Kabwe na Liston kwa makini, na hapo Kisu aligeuka kuwatazama Kabwe na Liston na kuwaashiria kushuka kutoka kwenye lile gari.


Wote watatu walishuka na Kabwe alizunguka nyuma na kufungua mlango wa lile gari kisha alitoa begi kubwa la magurudumu na kusimama kikakamavu.


Kisu, Kabwe na Liston walianza kupiga hatua za kikakamavu kuelekea ndani ya lile jengo la Benki ya Biashara, Kisu alitangulia mbele huku akifuatwa nyuma na Liston aliyetembea kikakamavu na Kabwe aliyekuwa anaburuza begi kubwa lenye magurudumu.


Endelea...


ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog