Search This Blog

Thursday 23 March 2023

ZAWADI TOKA IKULU (2) - 3

  

Simulizi : Zawadi Toka Ikulu (2)

Sehemu Ya : Tatu (3)


Ni usiku wa giza totoro yapata saa saba kamili na sekeseke likiendelea ndani ya nyumba ya Jamae kipigo juu ya kipigo kilizidi kushushwa kwa Jamae na hakuwa na jinsi zaidi ya kukipokea bila kuhoji maana hakuwa na jinsi ya kujitetea mbele ya umati huu uliokuwa na siraha nzito. Jamae mbele ya macho yake anashuhudia kisu kikizamishwa ndani ya tumbo la mwanae Eric mtoto mdogo alisiye na hatia anatoa kilio kimoja kilichotia huruma kinamtoka mtoto aliyekuwa kaning’ inizwa kwa mkono mmoja kisha anatetema kuikata roho na mwisho anatulia tuli kisha mwili wake unarushwa kama jibwa koko bila huruma huku Jamae na mkewe wakishika vichwa wasijue lakufanya.


Yalikuwa ni maumivu zaidi kwa mama mzazi Jesca ambaye amehangaika kukilea kichanga hicho ndani ya tumbo lake kwa miezi tisa na kufanikiwa kujifungua salama lakini leo watu wasio na huruma wanakiangamiza bila sababu za msingi inauma sana machozi yanaweza yasiwe suluhisho lakini maumivu hayatasahaurika katu .


Maiti ya Eric ilikuwa mbele yao baada ya kutupwa kama mzoga wa mpwa au paka na sasa Von alikuwa kashaitupa suluali yake pembeni anamsogelea Jesca kwa lengo moja tu lakutimiza alichokitaka hakujali maumivu waliyonayo juu ya mtoto wao bali alichokitaka ni kulipiza kisasi ili kuyajibu maumivu aliyoyapata yeye baada ya kuachwa na Jesca kisha akaolewa na Jamae.


Mabaunsa watatu wanamkamata Jesca na kumvua nguo kwa nguvu kisha wanamshikilia akiwa uchi wa mnyama ili bosi wao asiweze kupata taabu juu ya kile alichodhamiria kukifanya. Masikini wa Mungu Von anambaka Jesca mbele ya macho ya Jamae…. Nawezakusema Jamae angefanya nini ilhali katiwa kamba mikononi na kaelekezewa mitutu miwili usoni kwake. Ilimbidi kukubaliana na hali kwa macho yake alilishuhudia tukiozima lililotendeka mbele yake. Ni maumivu yasiyo na mfano kumuona mkeo akitendewa unyama mbele yako na maadui zako.


Pia Jamae aliiwaza hatima ya maisha yake maana sasa familia yake ilikuwa imevurugwa mno na hili kundi linaloongozwa na Von Gao, mtoto kauwawa mbele ya macho yake na sasa mkewe anabakwa mbele ya macho yake pia unadhani Jamae atafanya nini iwapo atanusurika kwenye hili tukio.


Ni mwanga wa radi uliofuatiwa na ngurumo kali ndiyouliomwamsha Jamae na kukatisha ndoto ya ajabu ambayo ilikuwa ikiitesa nafsi yake usiku ule. Baada ya kuamka anajikuta yuko kitandani anageuka kushoto anamkuta mkewe kalala fofofo, bado aliona kama haimuijii akilini anampapasa na anagundua mkewe alikuwa kalala na alikuwa hai na salama salmini.


Anajiangalia vyema na kupapasa mwili wake bado aliona kama muujiza ukitendeka kwenye maisha yake kwani hakuwa na dosali maumivu wala kovu. Jamae anashuka haraka kwenda chumbani kwa Eric anamkuta Eric pia kalala kwenye kijitanda chake kidogo akiwa kapiga usingizi mwanana kabisa. Anapitisha mkono ili kujiridhisha ni kweli alikuwa akipumua na hakuwa na tatizo lolote.


Jamae anashusha pumzi na kujikuta akiishiwa nguvu, mwili wote ulimtetemeka huku akipata taabu katika upumuaji wake. Jamae anapiga hatua kadhaa na kwenda kuuegemea ukuta maana mapigo ya moyo yalikuwa yanamwenda mbio haamini kama familia yake ilikuwa salama, bado haamini kuwa matukio yote aliyoyaona kwa macho ilikuwa ni ndoto. Jamae haamini tena kuwa mwanae anaweza kuwa hai nabado anashangaa kuona kuwa mkewe yupo usingizini hajabakwa wala kufanyiwa kitendo chochote kibaya ambacho yeye anaamini kuwa amekishuhudia kwa macho yake mawili. Bila hofu alijikuta akipiga magoti na kumshukuru mungu, hakika aliuona kama ni muujiza wa kihistoria katika maisha yake.


Mwanaume anarejea kitandani huku akipumua kwa taabu usingizi umempotea ghafla kutokana na hiyo ndoto ya ajabu, anajaribu kuwaza na kuwazua kwa yale yaliyomtokea lakini asipate jibu la moja kwa moja. Ilikuwa yapata saa tisa usiku mvua ikizidi kuchalaza ipasavyo. Ngurumo, radi na upepo mkali vikidhidi kumwagika. Naweza kusema ulikuwa ni usiku mbaya mno maana mvua ilinyesha kwa vurugu, pili hakukuwa na umeme kutokana na mvua kuwa kali mno katika jiji la Dar Es Salaam.


Jamae alikuwa kajilaza usingizi umekimbia amejikunja ndani ya shuka kwa uoga uliosababishwa na vitu viwili cha kwanza ni ndoto mbaya aliyoiota muda mfupi uliopita na pili zilikuwa ni radi zilizopenyeza vyema mwanga wake kwenye penyo za madrisha na mwisho kumaliza na ngurumo za kutisha hali iliyoleta hofu moyoni mwake lakini wakati huohuo mama watoto wake Jesca yeye alizidi kuuchapa usingizi pasipokuwa na hofu wala wasiwasi wa aina yoyote ile.


Zilikuwa ngurumo za radi na sasa kulisikika milio ya siraha nzito nje ya nyumba yake, ni kama majibizano ya risasi aliyoyasikia vyema Jamae anakurupuka kutoka kitandani na bila shaka masikio yake hayakumdanganya. Ndiyo ni risasi zilikuwa zikilindima kati ya askari polisi waliokuwa lindo pale nyumbani na kundi la magaidi waliokuwa wanaivamia nyuma hiyo.


Jamae anamshika mkono mkewe wanaongozana mpaka chumpa cha mtoto wanamchukua na kujiandaa kwaajiri ya kutoroka. Jamae wakati yote haya yakiendelea alijua wazi kabisa kuwa yaliyomtokea kwenye ndoto sasa yanaekwenda kutimia katika akili yake aliamini hivyo ingawa hakupata hata sekunde yakumshirikisha mkewe bali kila mmoja kwa wakati huu alikuwa akitafuta namna yakuiokoa familia yao. Giza lilitanda ndani wanajaribu kuutafuta mlango gizani kwa bahati nzuri wanafanikiwa kuupata wanatoka na korido kuelekea ulipo mlango wa dharura nyuma ya nyumba yao. Haikuwa kazi ndogo maana giza lilitanda kila mahali iliwawia vigumu hata kupaona pakukanyaga. Wanajisogeza mpaka lilipo geti la mlango huo wanafungua na kufanikiwa kutorokea mlango wa nyuma.


Majibizano ya risasi yalizidi kushika kasi asikari watatu wanaoilinda nyumba ya Jamae hawakutegemea kukutana na upinzani huo walionao kwa wakati huo kutoka kwa watu waliodhaniwa kuwa ni majambazi kuwavamia na siraha nzito na njia pekee yakujinusuru iliwabidi wapambane kadiri wawezavyo ili kuziokoa nafsi zao na nafsi ya mwajili wao.Baada ya kutoka ndani Jesca alimwambia mumewe ni vyema akibonyeza kengele ya hatari ya nyumba yao ili kuomba msaada lakini Jamae alikataa akasema kengele itawasaidia kujua kuwa Jamae na familia yake hawapo ndani au wameesha jua kuwa wamevamiwa.


Polisi waliendelea kupambana ili kujihakikishia usalama wao pamoja na bosi wao ambaye waliamini yupo ndani ya nyumba wanayoilinda. Wawili walizidi kujibizana risasi na na majambazi na mmoja alijitahidi kuomba msaada kutoka makao makuu ya polisi kwani walikuwa wamezidiwa mno. Majambazi walionekana kuwa na siraha nzito kuliko polisi pia walionekana kuwa wengi kuliko polisi hivyo pambano lilichukua sura mpya baada ya asikari mmoja kuchapwa risasi ya kichwa anaanguka chini lakini kwa bahati mbaya mwenziye aliyeenda kumsaidia pia alikula risasi za kifua na kupoteza maisha palepale.


Mzigo ulibaki kwa askari mmoja aliyepaswa kupambana na hao majambazi na mmoja alikuwa hoi kando huku kushoto kwake kukiwa na maiti ya mwenzao aliyepigwa risasi za kifua.


Jamae amefanikiwa kutoroka na familia yake wanajaribu kukatisha vichochoro usiku huo wa giza nene ukisindikizwa na radi, ngurumo na upepo mkali bila mafanikio. Mvua ilikuwa kubwa mno na hivyo kuwafanya kuwa na hofu juu ya afya ya Eric mtoto wao kutokana na baridi na mvua iliyokuwa ikiendelea na hivyo iliwalazimu kujiegesha kwenye kibaraza cha nyumba ya jirani moja usiku huo. Hakukuwa na mazungumzo kati yao kwani kila mmoja aliwaza lakwake wakati wakiisikia milio ya risasi sehemu waliyotoka na walijua sehemu hiyo si salama tena kwa maisha yao.


Baada ya muda upepo ulipungua hivyo wakaamua kuendelea na safari walipiga hatua chache lakini kulikuwa na gari linakuja nyuma yao kwa mwendo wa haraka walijua huenda ni tax hivyo Jesca alijibanza na mtoto Jamae alisimama barabarani kulisimamisha aliamini huenda wakapata msaada lakini baada ya kulisimamisha lilikuwa ni Gari aina ya Toyota Mark X. na likiwa na watu wawili waliomnyoshea bastora huku wakiuliza “mkeo na mtoto wako wapi?. Lakini kabla hajajibu sauti ya kilio cha Eric ilisikika.



Jesca anajitahidi kumziba mdomo mwanaye lakini haikusaidia kitu maana tayari sauti imeesha sikika kwa maadui zao, taratibu wale jamaa wawili wanashuka kwenye gari na siraha zao mkononi zikiwa zimeelekezwa vyema kwenye uso wa Jamae hawakumpa nafasi hata ya kukohoa, mmoja anabaki na mwingine alianza kuelekea kilipokuwa kikitokea kilio cha mtoto.


Jesca alijaribu kukimbia ili ajinasue mikononi mwa wale watu wabaya lakini hakufanikiwa. Anaamua kujisalimisha baada ya kusikia mlio wa risasi ambao bila shaka ulimkosa alijua wazi kabisa kuwa angefanya makosa basi wale watu wangeondoka na roho yake na mwanaye ambaye alikuwa kampakata kifuani huku akikimbia. Aliamua kusimama na kujisalimisha mikono juu ili kuokoa maisha yake na mwanae Eric.


Ni vijana wawili waliofunika sura zao kwa soksi nyeusi zenye matobo machoni kuwapa uwezo wa kuona, walivaa soksi hizo ili wasitambulike kiurahisi maana tukio walilokuwa wanakwenda kufanya lilikuwa ni tukio hatari. Baada ya yule mmoja kurudi akiwa kawakamata Jesca na Eric majambazi hawa, wanamuamuru Jamae kuingia ndani ya gari yeye pamoja na mkewe na waliondoa gari kwa kwasi na kutokomea kusikojulikana usiku huo.


Asubuhi kunakucha nje ya nyumba ya Jamae zilipaki gari za polisi zisizo pungua kumi nje ya geti huku polisi wakitapakaa kila kona ya mji kwa doria na msako wa mkali wa kihistoria kuwahi kutokea katika jiji la Dar. Barabara zote zilifungwa na ukaguzi mzito ulikuwa ukiendelea. Na ukiingia ndani polisi walitapakaa kila kona huku pembeni akionekana mkuu wa jeshi la polisi akiwa na mawaziri wawili wenye nyadhifa kubwa nchini na dhamana ya ulinzi na usalama wa raia ni waziri wa ulinzi wa kipindi hicho Mh. Sai Kakonko na waziri wa mambo ya ndani Mh, Katongole Bwanga walionekana wakiteta jambo kwa pamoja. Wandishi wa habari walikuwa wako nje wakisubiri kufanya mahojiano na viongozi hawa wakubwa wa serikali kuhusiana na tukio hili. Naweza kulizungumzia tukio hili ni tukio la kinyama nala kihistoria kwani liliteka masikio ya watu duniani kote kwa muda mfupi. Kila mtu alikuwa akishangazwa na tukio hili jinsi lililotokea pale nyumbani kwa Jamae kwani nyumba ilikuwa imeshambuliwa vilivyo na askari wote waliokuwa lindo usiku huo walikuwa wamepoteza maisha. Ilionekana miili mitatu ya askari wakiwa wamelala chini huku siraha zao zikiwa zimetoweka, lilikuwa ni tukio la ajabu na la kinyama sana kwa vijana hawa wadogo. Baada ya kupiga picha na kufanya upelelezi wa awali, Mawaziri hawa wanasimama mbele ya vyombo vya habari na kulaani vikali tukio lililotokea nyumbani kwa Jamae Justine wanaahidi kupambana mpaka mwisho na kuirejesha familia ya Jamae ikiwa salama kuhusina na tukio waliomba kutoa muda ili uchunguzi ukamilike.


Ni familia ya Jamae iliyopotea lakini ni sehemu ya familia ya rais Manguli iliyotekwa hivyo habari zinasambaa na kutapakaa kila kona ya dunia magazeti ya lugha zote yakaandika nyumba ya binti wa rais imevamiwa na watu wasiojulikana na kuiteka familia nzima, redio nazo zikatanganza, TV Zikaandaa vipindi maalumu namubashara na vilivyorekodiwa na kurushwa kwa lugha mbalimbali, wasemaji wa jeshi la polisi na upande wa upelelezi walisimama na kuahidi kwenye vyombo vya habari kuwa wauwaji waliouwa polisi watatu watapatikana na vyombo vya dora vitawashughulikia, lakini hawakuacha kuaahidi kuwa familia ya Jamae itarejea ikiwa salama.


Ni hadithi iliyolisisimua taifa kwa muda mfupi na kuwaacha watu wakiwa na presha, hofu na hudhuni ya hali ya juu mioyoni mwao huku wasiwasi ukizitawala nafsi zao. Na hili linakuwa ni tukio lingine ambalo ni moja ya matukio makubwa ambayo yanamkumba Jamae tangua ajaribu kuingia katika familia hii ya kitawala kwa mara ya kwanza siku nyingi zilizopita.


Familia ya rais ilikuwa kimya kulizungumzia tukio hili, maana liligusa moja kwa moja masirahi ya familia hivyo rais alishauriwa kuwa haitakuwa busara kujitokeza na kulizungumzia tukio hilo mbele ya kadamnasi ilhali polisi na vyombo vingine vya dora vikiendelea na upelelezi.


Ingawa kurugenzi ya mawasiliano ya utawala wake ilituma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliouwawa siku hiyo wakati wakitekeleza majukumu yao na pia salamu hizo zikatumwa kwa jeshi la polisi huku zikiwatia moyo na kuwaongezea nguvu katika majukumu yao. Ni siku ya hudhuni kwa taifa ndugu jamaa na marafiki waliokuwa wameguswa na tukio hilo moja kwa moja walikuwa wakitoa salamu za faraja kwa familia za wafiwa na familia ya rais.


Von Gao na Dominic walikuwa wameketi na chupa lao kubwa la mvinyo lililokuwa na chapa ya JackDaniel, wakiwa na glass fupi na nzito zenye nembo hiyohiyo ya JackDaniel mkononi walikuwa wakibadilishana mawazo huku wakiwa wamevalia mavazi yao ya thamani kubwa, Von alikuwa na suti yake ya rangi ya kaki na tai nyeusi huku kwa ndani alitupia shati jeusi lenye kola mwanana likisindikizwa na Tai nyeusi iliyofifia na miwani yake ya macho ilimfanya aongeze mvuto maradufu. Saa yake yenye rangi ya dhahabu ilikamilisha mvuto na kumfanya mpya zaidi. Kiatu chenye rangi ya ugoro kilivutia zaidi mguuni kwake na kumfanya aonekane nadhifu kuliko kawaida. Upande wa Dominic yeye alivaria vazi la kiafrika zaidi kwani alivalia vazi la rangi nyeupe lenye marembo meusi na njano lenye asili ya Nigeria na lilionekana kuwa na mvuto zaidi fimbo yake ya mpigo iliyochongwa vyema na kunakshiwa kwa mapambo iliongeza mvuto, kibaragashia kidogo kama kibakuli cha mlenda alikipachika kichwani kwake huku chini akitia viatu vyake vya wazi vilionekana kuwa vya gharama kubwa na suluari yake nyeupe fupi alimaarufu kama njiwa au ruka umanbe au wazungu waiitavyo “I’m not sure” ilimpendeza zaidi .


Mazungumzo yao yalionekana kuwa ya furaha sana na sasa walionekana kuwa ni watu walioshibana vilivyo na malengo yaliyofanana.

“Ndugu yangu Domi tumefanikiwa kumpata huyu mwana haramu na bahati nzuri zaidi tumemkamata yeye pamoja na familia yake yaani kuku na vifaranga vyake, nadhani kilichobaki ni kumuangamiza tu hakuna njia nyingine.”

“Von umekuwa rafiki mzuri kwangu ndani ya muda mfupi na kati ya vitu ambavyo uliniahidi utavikamilisha na vikakamilika kwa wakati bila kuleta shida ni hiki kilichotendeka jana. Ni lazima nikupe pongezi ndugu yangu hongera sana wewe ni mwanaume wakweli”

“hili ni swala dogo mno Domi… dogo sana”

“Hivi iliwezekanaje mkafanikiwa kuwauwa askari watatu na kuchukua siraha zao kirahisi hivyo bila kushitukiwa wala kukamatwa?”

“serikali Domi…….. mimi ni serikali… ukiitaja serikali unaanza na familia ya Gao”

“kwahiyo tunauwezo wakufanya lolote lile nikiwa na familia ya Gao?”

“Bila shaka Domi….. huwezi kushindwa serikali iko mikononi mwetu”

“duh! Mungu ni mwema uhusiano wetu niwabahati mno ni sawa na mtende kuota jangwani”

“Domi, sasa una mpango gani nahii familia ya huyu mwendawazimu maana tayari tuko naye na polisi bado wanapuyanga kwa kukamata watu hovyo huko nje?”

“ninaiona neema ndani ya familia hii”

“unaiona neema? .. ndani ya familia hii… unamaana gani kusema maneno hayo Domi?”

“subiri utanielewa.. sasa hivi”

“tafadhali kaka unazidi kuniweka njia panda hebu kuwa wazi zaidi”

“Von hii michezo nimecheza sana na sasa mchezo umefika patamu, waswahili wanasema mchezo ndo kwanza umenoga sasa nakupa bonge la aidia …”

“unamaanisha una dili jipya kwenye huu mchongo?”

“Bila shaka hujakosea ndugu yangu ….. Von Jamae ni dhahabu”

“unamaana gani kusema Jamae ni Dhahabu?”

Mara mlango unagongwa,na mazungumzo yanasitishwa …. Wanaingia vijana wawili waliojazia kwelikweli kwa kutumia ishara wanaashiria kuwa watu hawa walikuwa wanahitajika namaanisha Von Na Dami basi wanaongozana.


Wanafika kwenye chumba kimoja kilichojificha kukiwa na giza nene huku taa za mwanga hafifu zikimlika huku huku ndiko alikokuwa kawekwa Jamae kwenye chumba kidogo na chumba kingine alikuwa kawekwa mkewe Jesca na kando ya jesca alikuwepo Eric mtoto mdogo wa miezi isiyozidi mitano akiwa amelazwa chini sakafuni huku akilia kwa uchungu. Von alikuwa kasimama akimuangalia kwa dharau Jamae wakati huo Dominic akiwa amesimama kando akitabasamu kwa madaha.

“Jamae Justine kijana jeuri, bingwa wa mapenzi uliyejigamba na kumdatisha mwana wa rais huku ukinisababishia maumivu na aibu kwa dunia nzima. Niwewe uliyefanya nikaachwa siku ya harusi kwa sababu yako siku ambayo dunia nzima ilijua Von Gao anaoa na kila mtu akajiandaa kuisubiri harusi ya kifahari kutoka familia tajiri na zenye historia ya kweli ya taifa hili. Lakini akaibuka kapuku na masikini asiyejielewa akaingilia kati na kuivuruga ndoa yangu huku akijinasibu kuwa na mapenzi yakweli. Jamae ulichonitenda siku hiyo ya harusi dunia yote ikajua na kutikisika na kuandika historia mbaya historia hiyo ni mimi Von kaumizwa na kuachwa nikilia mbele ya kadamnasi. Hakika niliapa lazima utayalipa machozi yangu nilisema haya machungu niliyoyapitia nilazima uyalipe kwa gharama yoyote ile na leo nilazima niandike historia ya kukuteketeza wewe, mkeo na kizazi chako chote katika uso huu wa dunia kamwe Jamae hatakuwa na familia tena.”

“ Bila shaka Von fanya lolote utakaloona ni sawa ili kuilidhisha nafsi yako”

“Von anaweza kukujibu atakavyo lakini akumbuke kuwa sisi sasa ni nguvu moja na tulikuwa nguvu moja toka awali na tutabaki kuwa nguvu moja mpaka mwisho. Chakumkumbusha ni kwamba Jamae hukupaswa kuniamini toka mwanzo, kwa bahati mbaya uliniamini nikakomba fedha zote na kutokomea kusikojulikana. Nimetengeneza pesa nyingi kwa mtaji wako ulionikabidhi na wewe ukakalia kupigania mapenzi wakati wenzako tunatengeneza pesa…mr. lavalava. Chakufurahisha ni kwamba mimi ni tajiri sasa ahsante kwa msaada wako wa mtaji.”


Von aliomba bastora kwa ishara kutoka kwa kijana aliyekuwa jirani yake alipokea bastora kutoka kwa kijana aliyekuwa jirani yake, anaikagua mara baada ya kugundua iko sawa anaamua kuielekeza kwenye paji la uso wa Jamae. Jamae hakuwa na namna bali alianza kusali sala zake za mwisho kwa sauti kubwa akikabidhi nafsi yake kwa mwenyezi mungu muumba wa mbingu na nchi kwani aliamini waziwazi kuwa maisha yake yalikuwa yamefikia tamati hapa duniani. Mwanzo ilionekana kama masihara kwa watu waliokwa wakimwangalia Von Gao usoni lakini kiuhalisia Von alidhamiria kuua tena pasipo kuwa na huruma. Jesca alikuwa kafunika sura yake kwa viganja vyake ili asione kitakachotokea kwa mumewe huku akiingoja zamu yake ambayo pia isingechukua hata sekunde aliamini hivyo, maana alijua wazi kuwa mwisho wa maisha yao ulikuwa umefika. Kama utani na sasa mshindo wa bastora unasikika watu wakaduwaa na wakiwa ndani ya taharuki hiyo unasikika mshindo wa pili.



Jamae akiwa ameinama chini baada yakushitushwa na milio ya risasi zilizosikika muda mfupi uliopita huku akiwa kakata tamaa kabisa maana alijua wazi kuwa milio ile ingetua vyema kwenye mwili wake, Jamae anataharuki kwani hakuamini baada ya kujikuta bado anapumua, kwani aliamini wazi kuwa angekuwa ameesha poteza maisha tayari maana Von alidhamiria kuondoka na roho yake. Jamae aligeuka upande wa pili na kumuona mkewe pia akiwa hai ingawa alikuwa akilia kwa uchungu maana pia alijua risasi zilizopigwa hakika zitakuwa zimeondoka na uhai wa mumewe.


Macho ya Jesca yanakutana na macho ya Jamae tabasamu ndani ya kilio liliibuka maana wanagundua kuwa bado wako hai. Hii ilikuwa ni faraja kubwa kwao pia sauti ya kilio cha mtoto wao Eric inazidi kuwaongezea matumaini kwani walijua wazi kuwa familia nzima sasa ilikuwa hai hakuna aliyedhurika hali hii ilizidi kumfanya Jamae afarijike zaidi kwa kuamini kuwa mwanae pia yuko hai shukrani kwa Mungu ziliongezeka maradufu. Jamae ananyanyua uso taratibu na kuangaza huku na kule huku akiwa na hofu kubwa moyoni watu walikuwa wamemzunguka kama ilivyokuwa awali hakutaka kabisa kuinua uso wake maana alikuwa na hofu huenda watu wabaya wakabadili msimamo na kuondoka na nafsi yake, huku mapigo ya moyo yakimwenda kasi kuliko kasi ya pangaboi lizungukavyo wakati wa Joto. Shaka ilizidi kutanda kwa jamaa maana alikuwa haamini kama kweli inawezekana hawa maadui wakamuacha salama.


Baada ya muda wa dakika kama mbili hivi akiwa kainamisha uso wake sasa Jamae ananyanyua uso wake na anakutana na sura ya Von Gao akiwa palepale alipokuwa kasimama toka awali na alipogeuza shingo yake upande wa kulia kwake aliona matundu mawili ya risasi yaliyotoboa ukuta na kupenya mpaka ndani ya ukuta , Jamae anashusha pumzi na kugeuka upande wa pili huku asiamini alichokiona.


Nikweli familia ya Jamae ilikuwa salama na maadui wote walikuwa wamesimama kando yao bila shaka kunakitu kinaendelea pamoja na kuwa na ukimya wa muda mfupi.

“Von nadhani unaweza kunisikiliza sasa”

“ndiyo nakusikiliza Domi”

“huyu bwana na familya yake ni mtaji, ninasema ni mtaji kwasababu amemuoa mtoto wa rais mpaka sasa anatafutwa na hajulikani alipo, sasa Jamae nahii familia yake tunaweza kupiga pesa kubwa sana iwapo tutawatumia vyema”

“unamaanisha tuendelee kuwashikiria wakiwa hai tuagize kulipwa pesa tuitakayo?”

“naona unaanza kunielewa Gao ni mchezo mdogo tu wala hutumii nguvu”

“hapana Domi hili ni kosa ambalo tukijaribu na tukakwama naamini tutakuja kuaibika milele na hakutakuwa na mtu wakutusaidia”

“nimecheza hizi michezo toka zamani haijawahi kutokea nikakwama”

“vipi kuhusu mawasiliano tutakayotumia wakiyafuatilia na kujua tulipo”

“Kazi ndogo sana ninavijana wangu wawili mmoja Muislaeli na mwingine anatoka Korea ya Kaskazini kwenye swala la mtandao wanauwezo wa kuingia mpaka tovuti za Ikulu na kuchukua nyaraka tutakazo bila shida yoyote sasa ije iwe kuzuia namba ya simu?”

“Aisee unaonekana ulijiandaa kaka, kawaida kaka unajua kadri unavyopiga hizi dili za kizembe ndiyo unavyozidi kuwa imara. Tangu nimekaa Kanada kwa muda mfupi huu nimejifunza mambo mengi na naijua dunia kuliko kawaida, unadhani ningeweza kuingia kwenye biashara ya Dawa bila kuwa na mtandao imara? Hapa nilipo Mmarekani mwenyewe alishanyoosha mikono hana hamu na Domi”

“kwahiyo ulitaka atulipe kiasi gani kaka akitupa trioni nane siyo mbaya”

“eight trion ya Kitanzania?, sidhani kama inawezekana Domi”

“Hahaaaa! Unapaniki na hiyo pesa kidogo unaogopa kama utazilipa wewe kaka, amini ninakwambia atatoa, hana ubavu wakutugomea”

“Si rahisi kama unavyodhani, trioni nane ilikuwa ni bajeti ya nchi tulipokuwa na utawala wa awamu ya tatu, na sasa hizi ni pesa nyingi nadhani inaweza kuwa ni bajeti ya wizara kama tatu au mbili ambazo ni nyeti sana”

“hujakosea ndugu yangu kumbuka Dominic Martine, ni wizara ya kwanza na nyeti na Von Gao ni wizara ya pili ambayo ni nyeti pia hivyo kama ulivyosema fedha hizi zinapewa wizara nyeti nami nakuhakikisha wizara hizi zitakabidhiwa hiyo fedha haijalishi zitatokana na jasho la wananchi walipakodi, misaada ya mashirika ya kimataifa na hata kama ni mikopo kutoka mashirika ya kimataifa nilazima tulipwe hiyo pesa”

Domi anaonekana kumshawishi Von kwa kadri alivyoweza na sasa Von Gao anajikuta anamuamini kabisa Domi na kujikuta wanakuwa kitu kimoja bila shaka wamefikia mwafaka na kilichobaki ni kuyatekeleza makubariano.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog