Search This Blog

Thursday 23 March 2023

ZAWADI TOKA IKULU - 1

 

IMEANDIKWA NA : EMMANUEL VENANCE

***********************************************

Simulizi : Zawadi Toka Ikulu

Sehemu Ya : Kwanza (1)


Ni jumapili tulivu sana ambayo imejidhihilisha tangu jua linachoza, kwani hakukuwa hata na dalili ya wingu angani kukionekana safi na kumependeza kwa rangi ya bluu bahari.


Baada ya kutoka kanisani nilikaa nyumbani kwangu nikiwa mpweke kani nilikuwa peke yangu. Nyumba niliiona kubwa mno kwasababu kila nilipokanyaga nilikuwa peke yangu, sina wakuongea naye wala kushirikiana naye kwa lolote lile, hali iliyonipa hudhuni wakati wote.


Nimezoea kusndinda kazini na nikirejea hapa nyumbani huwa nimechoka nafikia kulala, lakini kwa siku za mwisho wa wiki huwa ni ngumu sana kwangu maana inanilazimu kushinda nyumbani, kwasababu huwa hatuendi kazini. Na leo ni moja ya siku hizo nisizozipenda katika maisha yangu.


Nilijaribu kufanya hiki na kile lakini haikuwezekana na baada ya muda mfupi kidogo niliamua kutoka nyumbani kwangu maeneo ya Busweru. Nilitaka nitafute sehemu ya kwenda kupumzika yaani kujichanganya na marafiki angalau tubadilishane mawazo.


Baada ya mwendo mfupi nilipokuwa nikitembea huku nikiwaza pakuanzia niliona ni bora nikamtembelee swahiba wangu wa nguvu bwan Domini Martin Kalyanze. Niliamua kumpigia simu kwanza ili nijue kama yupo nyumbani kabla sijaanza safari. Bila shaka majibu ya hiyo simu yalikuwa sawa na matarajio yangu rafiki yangu alikuwepo nyumbani na alikuwa tayari nionane naye.


Dominic ni mfanyakazi mwenzangu ni mkurugenzi wa Mauzo katika kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Kanda ya ziwa. Na mimi ni Meneja wa mauzo, si hilo tu lililotufanya tushibane na kuwa marafiki lakini Martin ni rafiki yangu tuliye soma pamoja Pale IFM chuo cha usimamizi wa fedha na tuliomba kazi pamoja na bahati nzuri tukaajiriwa siku moja na sehemu moja, hivyo niseme wazi kuwa huyu jamaa tunapendana sana tena sana.


Nilifika kwa Dominic nikakuta anajiandaa kwa kufuta vumbi gari lake lakini aliponiona aliniangalia sana na kutikisa kichwa, nilimuuliza “kwani vipi kaka mbona kukodoleana macho hivyo?


“mbona umekuja kwa miguu?” Dominic alihoji.Nilimjibu kwa maneno yaliyoambatana na kicheko.


“Aaah! ndugu yangu sijali, sijisikii kuendesha leo kwahiyo nimepanda daladala nikashuka hapo kituoni maana siyo mbali kuja hapa, nimeona pia niwape ridhiki makonda wetu si unajua ndiyo waliotulea toka tunasoma chekechea kwenda shule na kurudi mpaka hapa tulipo leo?. Na pia huu ni usafiri wa umma bwana, tusivimbe saana na vigari vyetu tukajisahau maana tukumbuke kuna kupanda na kushuka ipo siku tunaweza urudi kwenye haya maisha sasa yanini kujikweza” Baada ya majibu hayo wote tuliangua kicheko na tukasalimiana na kuingia ndani. Tulipiga stori mbili tatu kabla ya kupata kifungua kinywa, na baada ya zoezi hilo kuisha tuliamua kutoka.




.

Dominic anapenda sana pikipiki naweza kusema huo ni kama ugonjwa kwake. Basi siku hiyo aliamua tutoke na moja ya pikipiki yake mpya ni BMW K1300r. hii ni moja ya pikipiki aghali mno na ni nadra mno kukutana nayo kwenye nchi hizi za ukanda wa kusini mwa sahara. Jamaa hajali kuhusu bei kama kitu amekipenda huwa anajiachia kwa mikono miwili na hata ukimuuliza bei hawezi kukujibu maranyingi huwa naishia kuguna tu.


Basi nilifungua geti na kofia yangu ngumu (helement) mkononi , Dominic alitoka na pikipiki yake hadi nje akiwa pia kavalia kofia ngumu. Tulitoka kuelekea barabara kuu ili tuianze safari lakini kabla hatujaingia kwenye barabara kuu ya Mwanza, Musoma. “mzee subiri usiingie nimeona kitu hapa, alisita kidogo kuingia akashusha mguu wake wa kulia chini kisha akageuka kunisikiliza.


Nilimuonesha “Mzee angalia pale” Dom aliangalia, alikuwa ni msichana mrembo amesimama pembeni ya barabara bila shaka alikuwa akingoja usafiri. Bada ya kumuona aligeuka tena na kuniuliza vipi kaka? Nilimjibu kwa maneno mafupi ya kiingereza “she is beautiful” nikweli alikuwa mrembo sijawahi ona katika historia ya maisha yangu, narudia tena sikuwahi ona msichana mrembo kiasi kile.


“Yes! She is very beultiful, so what do you wanna do?” akimaanisha ndiyo ni murembo kweli sasa unataka kufanya nini? Wakati akiniuliza hivyo alikuwa akiegesha pikipiki pembeni huku na kisha kuvua kofia yake huku akiniangalia. Ilinibidi nisimfiche bali nimwambie ukweli.


“Dominic nimevutiwa na huyu msichana ni mzuri na sijui hapo alipo anafanya nini?”n Nilimwambia Dominic ambaye alinijibu “ nikweli ni mrembo lakini humjui na hujui hapo anasubiri nini au anamngoja nani, hivyo kuwa makini rafiki yangu” alinionya.


Safari yetu ilikuwa tayari imeingia dosari, aliyekuwa akinishauri naye niliona akizubaa na kukodoa macho. Jamani kitu kizuri ni kizuri tu asikwambie mtu. Muda ulizidi kwenda wote tukiwa tumevutiwa naye, hivyo hakuna kati yetu aliyetaka kuondoka eneo lile. Basi tukawa pale tumekodoa macho kodo kwa makini na kwa uangalifu zaidi kwani kila alichokuwa akifanya, kwetu ilikuwa furaha tu ni kuachia tabasamu maana hata yasiyo furahisha sisi yalituvutia. Basi hata akinyanyua mguu tu kwangu ni rahaaa! Msatarehe.


Nilimuomba Dominic twende japo tukamsalimie ingawa nilijua itakuwa ngumu na kweli ilikuwa ngumu mno kwani Domi kwani hakukubali, aligoma kwenda, hali iliyoleta masawali mengi kwangu kwazababu ninamjua vizuri Dominic. Rafiki yangu hakuwa anamuogopa mwanamke wa aina yeyote ile, alikuwa ni kiwembe mbaya sana kilaaikmtaka mwanamke lazima asalimu amri. Lakini hapo alionekana kutoridhia alikataa katakata, kukataa kwake hakukuonesha msimamo bali alionekana kuwa na hofu sambamba na uonga.


Nilimlazimisha sana na hatimaye akakubali, aliwasha pikipiki kuelekea alipokuwa kasimama yule msichana lakini, bahati haikuwa yetu tulipomkaribia kuna daladala iliegeshapale alipokuwa kasimama akaingia ndani ya gari na kutuacha tukibung’aa. Tulitazamana na kujicheka,


“Panda faster tuifuate hiyo gari nimeikariri namba” Dominic alitoa kauli hiyo,nami sikuwa na ubishi.


Basi aliwasha pikipiki kwa kasi na tukaifikia ile gari tukaongozana nayo mpaka kituo cha daladala cha Buzuruga, kama ilivyoada kwa daladala ikisimama ni kushusha na kupakia niliangaza macho yangu sikumuona yule binti mle ndani. Tulianza kulaumiana kama wajinga mara wewe umesababisha, lawama zilizidi lakini wakati tukilaumiana nilimuona Dominic akiwa kabaki mdomo wazi niligeuka kujua kulikoni, kumbe yule mrembo alikuwa kasimama pembeni yetu, basi kila mmoja wetu macho yalikuwa kwake, tulikuwa kama mazoba.


Yule dada alitoa simu yake kwenye mkoba na kupiga hatua kadhaa kulivuka barabara kuingia kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jilani cha Buzuruga.


Maswali yalianza kuwa mengi kichwani, itakuwaje kama huko anakoenda ana miadi na jamaa mwingine? Nilianza kuhisi wivu wa kijinga kwa mtu hata asiyenijua.


Dominic alikuwa kimya na mimi nikiwa kimya, basi akapata wazo la haraka na kuniambia “Jamie naenda kujaza mafuta pale GBP, kwahiyo wewe mfuate na hakikisha haumpotezi na pia hakikisha hajui kama unamfuatilia sawa?” nami nikajibu “okey sawa”. huku nikianza safari.


Nilikuwa nimekwisha chelewa, kwani nilizunguka sana kwenye magari yaendayo mikoani pasipo kumuona. Nilikata tamaa niliamua kuondoka lakini wakati natoka pale niliamua kuvuka barabara itokayo Mecco ili nikakutane na Dominic tuendelee na safari yetu. Kwa bahati nzuri nilimuona yule dada.


Alikuwa kaketi kwenye mghahawa mmoja maarufu kwa jina la UDIUDI akipata juice, Nilikimbia haraka nikafika pale na kuagiza juice ili niwe karibu naye na nihakikishe simpotezi tena bila kuchukua wala namba yake ya simu. Kulikuwa na ugumu kumkaribia maana urembo wake haukuwa wa kawaida, kujishitukia na hofu havikukatika kila nilipokutanisha naye macho.


Nilikuwa busy dirishani kusubiri juice na chenji yangu iliyokuwa kwa mhudumu, baada ya kuwa nimehudumiwa. Lakini nilipogeuka nakukuta kiti alichokuwa kaketi kiko wazi, na ile juice aliyokuwa akinywa ipo kwenye glass ikiwa imeshuka kwa sentimita chache tu. Daah! nilishituka na kujilaumu sana, nilishika kichwa na roho iliniuma na kujikuta nabamiza ile glass chini, watu wote waligeuka kuniangalia na kunishangaa. Sikujali nilienda kaunta na kulipia gharama ya glass niliyovunja kisha nikaondoka nikiwa nimenyong’onyea kama paka aliyelowa maji.


Nilitoka kwa hasira mpaka barabarani nikaanza kuelekea petro station nilipomwacha Dominic lakini baada ya hatua chache ghafla simu yangu iliita, niliangalia alikuwa ni Dominic akinipigia. Nilipokea huku nikitaka kumpa mkasa ulivyokuwa kabla sijazungumza chochote aliniwahi kwa lawama.


“We Jamie uko wapi?” sauti ya Dominic ilisika katika spika ya simu yangu ya mkononi. “Niko huku juu nakuja….” Nilimjibu.


“we mwehu kweli, mtoto huyu huku amekutorokaj? hebu wahi twende….. we bwege kweli” Dominic kama kawaida na lugha zake za matusi akiwa kakasirika huwa haziepukiki. Nilikimbia na kupanda pikipiki haraka tukaondoka .Dominic alikuwa kakalili namba ya daladala aliyopanda yule mrembo kwa mara nyingine.


Tulikuwa kama wendawazimu tuliokosa kazi siku hiyo. Safari yetu iliendelea tukiamini popote alipo tupo gari lililombeba lilishusha na kupakia abiria vituo kadhaa tukilingoja na kisha tuliendelea nalo bila wao kujua kama tunawafatilia kwenye kila kituokama vile Sinai, Kokoto, Mabatini, Getini, Mlango Mmoja na liliingia kituo cha Nata kushusha abria, sisi tukapaki barabarani kusubiri litoke na tuendelee na safari ya kulifuata na hilo ndilo lilikuwa kosa kwetu.


Tulijikuta tuko mikononi mwa Asikari wa barabarani kwa kufanya kosa la kuegesha pikipiki baranarani. Dominic alikamatwa na kuzuiliwa kuondoka, unawajua tena askari wetu wazee wa chochote kitu. Harakaharaka Dominic alijiongeza na kuniambi “chukua bodaboda ulifuate gari usikate tama ndugu yangu, huyo mtoto ni wako ukizembea imekula kwako. Hii issue nitatatua mwenyewe we sepa” haraka haraka nikafanya hivyo niita bodaboda huku nikizikumbuka zile namba za gari zilikuwa ni T344 DAD tuliifuatilia mpaka ilipoingia stendi ya Soko Kuu yanapopaki magari ya abiria. nilimuona yule dada akishuka na nafsi yangu ikatulia niliendelea kumfuatilia hatua kwa kwa hatua.


Aliponifikisha nilimuuliza dreva boda ananidai shilingi ngapi. Akajibu elfu mbili, sikujali nikampa noti ya shilingi elfu tano huku nikimwahi yule dada ili isiniache, nilimuachia chenji bila mimi kujua.


Basi nilimfuata yule dada alipokuwa kasimama lakini nilipo mkaribia alikuwa akiongea na bwana mmoja, nilisimama pembeni kusubiri, ulipopita muda kama dakika tano hivi niliona yule jamaa akifungua mlango wa gari na yule dada akaingia kwenye gari wakaondoka.


Ilinilazimu kuchukua tax na kumuamuru aifuate ile gari lakini wakati tukiifuata ile gari nikiwa na dereva wanguniliyemkodi aliniuliza unamjua huyo jamaa mwenye gari tunayoifuata?.. nikasema “hapana”, akadaikia yule ni tax dreva mwenzetu ingawa anatumia namba private. “Mbona unamfuata na unaonekana hauko sawa vipi kuna tatizo maana jamaa haishiwi majnga huy” alifafanua na kuuliza swali la kizushi bila shaka alihitaji mazungumzo. Nilijibu “Aliyembeba nadhani ni mteja wake ninamfuta huyo mteja wake mimi sina shida na dreva”. Safari ilielekea Kapri Point jirani na Rock Beach, gari lilifunga break eneo hilo na alishuka yule dada na kuingia kwenye mlango uliokuwa na uzio mrefu wa maua ya miiba lakini mbele yake pia kulikuwa na ukuta mkubwa ambao haukuonesha hata jengo moja mule ndani.


Huko ndani pia palionekana kuwa na msitu mkubwa wa miti mbalimbali sikulijua eneo hili kiundani, maana lilikuwa tofauti sana na maeneo mengine. Nilijaribu kuusogelea ule mlango wa geti, lakini kabla sijaugusa nilisikia sauti ikisema “tafadhari eneo hili linalindwa na mitambo maalumu usalama wako ni mhimu sana tafadhari, odoka eneo hili haraka iwezekanavyo ili kulinda usalama wako, ahsante kwa kutii”.


Niliondoka kwa hofu kubwa huku nikitetemeka, sikugeuka nyuma tena, nilikuwa nimelowa jasho ndani ya muda mfupi. Hofu na wasiwasi viliambatana kwani katika maisha yangu sikuwahi kukutana na nyumba yenye ulinzi wa aina hiyo. Katika maisha yangu yote, ujuaji wangu wote na matembezi yangu yote ndani na nje ya nchi nilizobahatika kutembea, kamwe sikuwahi kukutana na nyumba inaulinzi unaoambatana na vitisho tena kwa sauti.


Nilirudi kichwa chini na sikuwa na hamu ya kumjua tena yule dada, nikapanda gari la moja kwa moja mpaka nyumbani kwangu. Sikuwa nakumbuka Dominic nilimuacha wapi, wala sikuwa nakumbuka chochote, nilikuwa mwenye mawazo mazito, sikuwa na furaha, sikuwa na amani tena moyoni mwangu bali hofu ilinitawala.


Niliwaza huenda nimekutana na jinni, ingawa nafisi ilipinga lakini ukweli ulikaribiana. Nimesikia simulizi nyingi kuhusu majini na moja ya simulizi hizo ni kuishi majini au kando ya maji. Yumba hii iko ufukweni kabisa mwa ziwa viktoria huenda kuna ukweli maana lisemwalo lipo.


Nilifika na kukilowesha kichwa changu kwa maji ya baridi na nikashushia na maji baridi ya kunywa ili niwe sawa lakini haikuwa rahisi kurudi kwenye hali yangu. Kichwa kiliendelea kunigonga na mawazo yalinisakama nikaamua kupumzika. Niliingia chumbani kwangu nikalala ili kukipumzisha kichwa.


Nilikuwa nimechoka hivyo kwa bahati mbaya zaidi niliacha milango wazi na wakati nikiwa usingizini nilishituliwa na mtu ambaye tayari alikuwa ameingia chumbni kwangu, nilishituka sana baada ya kuhisi miguu yangu ikipapaswa.


Kumbe alikuwa ni mpenzi wangu huwa namuita pasua kichwa Maria Kimaro. Swali lilibaki ameingiaje ndani? Lakini kabla sijaenda mbali nilikumbuka nimerudi saa kumi na mbili nikafikia kulala bila kufunga milango.


Maria tunafanya kazi ofisi moja ni Meneja Uhusiano na Huduma kwa Wateja. Ni mpenzi wangu ila ni kero kwangu maana tabia zake na mdomo wake anaujua mwenyewe na muumba wake. Alikuwa yuko chumbani, tayari aliniamsha kwa kelele “wewe Malaya unajifanya umelala siyo? Nakupigia simu yangu hupokei umeshikwa na hao mahawala zako eti? Na mwisho ukazima kabisa haipatikani, na unabahati sijamkuta naamini hayuko mbali maana nimekuta milango iko wazi nabado unajifanya umelala siyo? Jamie usicheze na akili yangu nilisha kwambia mimi si wamchezo kama unavyozani jiangalie sana dume suruali wewe” Sikuwa na jibu nilibaki kujiinamia tu.




.


Alichukua funguo na kufungua droo ya kabati alichukua kiasi cha pesa alichokikuta na kisha akaondoka zake. Kabla hajatoka kumbe Dominic alikuwa anakuja aliingia moja kwa moja nilikuwa nimesimama mlangoni nikitokea chumbani kuja sebuleni. Dominic alianza kucheka kwa sauti na kusema “Jamie hufai hata kidogo kwahiyo baada ya kumpata mtoto ndo ukaondoka hata hukunijulisha mzee?, simu zangu hupokei kabisa ila wewe ni noma sana" hapo alikuwa kaharibu kila kitu.


Nilijitahidi kumkonyeza lakini hakujari aliendelea kuporomosha maneno "Umeona kukupigia nakuzingua ukazima kabisa, lakini vipi umechukua hata namba ya simu? Maana yule mtoto kakushika na umeshikika kwelikweli! Fanya mpango uoe, uachane na ule msalaba wa kichaga duh! mpenzi anapenda pesa kama mfuko wa jeans" kima kikazidi kutanda.


Domimic hakushituka aliendela kuchafua hali ya hewa "u ndo umekuja nae kabisa mtoto? Maana nimeacha ndala za kike pale mlangoni, huenda yuko chumbani.” Domic alikuwa kaharibu kila kitu, ila siwezi kumulaumu maana hakujua kama Maria alikuwepo ndani na Maria amejificha akijua ni mwanamke wangu ndiye anaingia ili aanzishe vurugu lake kumbe alikuwa Dominic. Maria alijitokeza hadharani na kusimama mbele ya Dominic.


Maria aliyadakia yale maongezi “Ndiyo amekuja naye mtoto mzuri, niko hapa, ….. Dominic wewe ndiye mshenga wa huu upuuzi unaotendeka humu ndani siyo? …” Maria alihoji kwa ghadhabu “aaaha.. haha!.. haaa! hapana shemeji unajua..” Dominic alijibu kwa aibu aibu lakini “shut up” Dominic anajaribu kujitetea lakini juhudi zinagonga mwamba baada ya kunyamazishwa na Maria. “kupenda kwangu pesa wewe kunakuhusu nini? … unazitafuta?... unanipa wewe?...” Dominic alikuwa mdogo kama punje ya ulezi, nilikuwa kimya maana ngoma tumeianzisha wenyewe hivyo hatuna budi kuicheza.


Maria alisogea nilipokuwa akaniambia kwa sauti ya juu “Jamie hukunitongoza nilijileta, hukunipenda nilikupenda, hukuwa na mipango na mimi ila ninayo mipango na wewe hivyo kaa ukijua na huyu mpuuzi mwenzio haipo siku utaniacha sahau kuhusu hilo!, ….baba fanya kusahau!, utake utanioa usitake utanioa”. Baada ya kumalizana na mimi alienda kwa Dominic “mshenga ahsante kwa kazi nzuri mmefanikiwa kunisaliti, umefanya kazi nzuri baba ila kumbuka hakuna siri, nashukuru buyu limetoboka kabla ya wakati, ahsante kwa kushindwa kuizuia furaha yako umenirahisishia kujua nini kinaendelea. Harafu mwambieni huyo mke mwenza ajiandae kaingia ligi ya mchangani refa huchezesha na panga kiunoni kuna mawili mshindi kutokwa manundu au kifo ndo mwisho wa mchezo, kufa mimi, kufa yeye au bwana kaka hapo, ili wote tukose hapo upo babaa? Salamu zimfikie bila kufanyiwa marekebisho” . Maria alimaliza na kuondoka huku akituacha tukitizamana.


Nilibaki nikiwa nimejiinamia huku Dominic akinilaum “Kaka nilikwambia mijike mingine siyo yakupalamia ona sasa unavyoishi kwa shida ndugu yangu kama mtumwa ndani ya nyumba yako mwenyewe”. Yalikuwa ni maneno ya Dominic baada ya kuumizwa na matusi ya Maria, iliniuma lakini hakuna jinsi maji nilisha yavulia ni sharti niyaoge tu.


Sikuwa na chakujibu wakati huu kichwa changu hakikuwa sawa hata kidogo, sikutaka kuzungumza chochote, nilikuwa najuta kwanini nimetoka nyumbani leo, kwanini nilimpitia Dominic, kwanini nilijiingiza kwenye uhusiano na Maria, hivi kwanini nimevutiwa na yule mwanamke, kwanini nililala mlango wazi. Kila kwanini niliyojiuliza isingekuwa kwanini pengine iwapo tu haya yote yasingetokea. Kwanini hii kwanini iwe chanzo cha hizi kwanini na kwanini? Ni swali la kijinga hata hivyo sikuumiza nalo kichwa saana ingawa lilikuwa na maana kubwa mno.


Mimi na Dominic hakukuwa na story tena, hakuna aliyetaka kuelezea nini kimetokea baada ya kuachana siku hiyo jioni kila mtu aliwaza alijualo, kila mtu alikuwa kimya kwa muda na mwisho Dominic aliamua kuondoka zake kurudi nyumbani kwake.


Usiku kucha namuwaza huyu mwanamke mwenda wazimu, hivi kanipa nini mpaka aape stamuacha, tangu nimjue, mwanzo alikuwa mwema kwangu na sasa amebadirika na kuwa kero isiyo na mfano. Siwezi ishi na mke mzigo, siko tayari kuishi kama mtumwa ndani ya familia yangu na stavumilia kuishi kama mpangaji ndani ya nyumba yangu.


Maria hakuzaliwa na mimi tumbo moja na wala hajanizaa, hivyo hatonishinda hii ni nyumba yangu. Baada ya kuwaza kwa muda niliamua kulala kwa kulazimisha na kweli nilibahatika kuupata usingizi japo nikwa muda mfupi.


Saa kumi na moja kamili alfajiri kengere ya saa iliniamsha ni muda wa mazoezi bila shaka niliamka na kuingia chumba cha mazoezi siku hii sikuwa vizuri kiakili kabisa, mwili ulikuwa umenyong’onyea sana na nilikuwa nikiishiwa nguvu kila nilipo yakumbuka matukio yaliyo nikumba jana nilijikaza kidogo walau nipate joto la kuogea, nilifanikiwa kupata jasho la uongo na kweli nikaingia zangu bafuni kuoga na nikaja kuandaa kifungua kinywa na baadae nikanyoosha nguo zangu za kazini na kuelekea kazini.


Nilifika mlangoni nikielekea ofisini kwangu nikakutana na Maria uso kwa uso aliachia tabasamu la kinafiki kama kawaida yake akijifanya kayasahau aliyoyafanya jana. Nilimpita kama simjui mbele ya rafiki zake Magreth na Ester ambao ndio walikuwa wapambe wake wa kila siku. Niliingia ofisini kwangu nikaketi na baadae nikakumbuka kitu na kwenda kumzuia Secretary asiruhusu mtu yeyeyote tofauti na Dominic kuingia Ofisini kwangu maana nilijua huyo mwenda wazimu angekuja muda wowote kunisumbua.


Nilifanya kazi zangu kwa ufanisi mkubwa nikiamini matatizo yangu ya nyumbani yasiwe sababu ya kuharibu kazi inayoniweka mjini nilipenda sana kutumia usemi wa baba yangu mzazi alioniambia kwamba “matatizo ya nyumbani kwako hasa mapenzi ni mchwa ambaye huitafuna kazi yako iwapo tu utayaruhusu yaingie kazini basi kazi itatafunwa na kubaki vipandevipande maana yake utaikosa”. Nilikuwa makini sana juu ya hili sikutaka kufanya mchezo nilikuwa makini na kazi yangu kuliko kitu chochote.


Majira ya saa sita mchana, Dominic aliingia ofisini kwangu


“mzee vipi? Alinihoji.


“Aah! niko poa Dominic, niko safi rafiki yangu, nilikuwa naweka sawa hapa kazi za watu na ninaamini nimemaliza sasa” Nilimjibu kikamilifu.


“chakula cha mchana wapi leo?” Dominic alihoji tena.


“Malikusema hapo mlango mmoja patatufaa twende zetu tukapige kuku mchemsho na ugali, itakuwa poa sana, lakini tuwahi saa saba kuna issue naiwahi, kuna simu ya boss toka makao makuu atakuwa na kikao na mimi Skype, hivyo natakiwa kuipokea muda huo bila kuchelewa hivyo tuna takiwa kwenda na muda rafiki yangu” nilimsisistiza kuwahi baada ya kupendekeza sehemu ya kwenda.


“sina pingamizi mkuu twende zetu maana hata mimi nimewakumbuka saana hao kuku mchemsho” Dominic alishabikia, tuliongozana mpaka Malikusema kwa Bonge, tulikamilisha mlo wetu pale na kuondoka kurudi kazini ofisi zetu zilipo NSSF Plaza barabara ya Kenyatta jijini Mwanza.


Dominic aliegesha gari kwenye maegesho pale nje ya jengo, alionekana ana kitu anataka kunihoji nilimsikiliza kwa makini baada ya kuniangalia “Jamie yule dada hujaniambia ilikuwaje jana” nilicheka kidogo baada ya swali lile, nami nikalirusha kwake “Dominic hivi ilikuwaje jana ule msala na wale traffic” wote tuliangua kicheko. Kulingana na tulivyozoeana Dominic aligundua nilikuwa staki kabisa kukizungumzia hicho kitu, maana ningekuwa ninataka kulizungumzia ningekuwa nisha mueleza nahii ilitokana na matukio ya kukatisha tamaa niliyokuwa nikikutana nayo kila wakati.


Kipindi tunaendelea kuongea kwenye gari nikama niliona kitu lakini sikuwa na uhakika, ilinilazimu kushuka haraka na kwenda ofisini maana nilimuona yule dada niliye muona jana akiingia ofisini kwetu. Niliwahi kumfuata na baada ya kufika ndani kweli alikuwa ni yeye. Alikuwa anaenda ofisi ya huduma kwa wateja. Nilitamani kujua amekuja kufanya nini maana sasa moyo ulianza kunienda mbiyo kwa wasiwasi, lakini baada ya kufika mule ofsini nilikuta wanazozana na Maria.


Chanzo nikwamba yule dada alikuwa katapeliwa na mtu kiasi kikubwa cha pesa kama milioni saba hivi ambazo alikituma kwa awamu, alimtumia jamaa ambaye hawafahamiani ila waliaminiana kupitia biashara zao kwahiyo huyo dada alihitaji msaada wa kumpata huyo jamaa kwani amejaribu kila njia ila imeshindikana. Ameenda mpaka polisi lakini bado kama polisi hawajali.


Kwa upande wa Maria haikuwa rahisi kiasi kile maana alikuwa na hasira za nyumbani ukijumlisha na nilivyomchunia asubuhi hivyo hasira za nyumbani akazifanya kuwa majibu ya kazini. Majibu aliyokuwa akitoa kwa wateja hakika yalikatisha tamaa. Sikutaka kuingilia mzozo wao kama sheria za kazi zinavyonitaka, nilisubiri baada ya wao kushindana, yule dada aliamua kuondoka huku machozi yakimlenga lenga, kiukweli niliumia mno. Niliamua kumuita yule dada ofisini kwangu na bahati nzuri alikubali wito alifika na kuketi karibu yangu, ni mara ya kwanza namuona akiwa karibu zaidi. Ni nafasi niliyoiota na kuitamani na sasa iko mbele yangu ukweli ni kwamba, ni msichana mdogo, mzuri, mrembo na mpole kupita kiasi hakika sina mfano wakumfananisha naye


Macho yangu yenye aibu hayakuchoka kumuangalia ingawa ilikuwa ni kwa wiziwizi. Nilipata nafasi ya kumsalimia japo kwa kumshika mkono kwa mara ya kwanza. Viganja baridi na laini vilinifanya niishiwe pozi mithiri ya fundi umeme aliyetikiswa kidogo na shoti.


Macho yangu yalianzia juu kwenye nywele zake za asili nyeusi tii, kisha yalitua kwenye uso mzuri mweusi wenye ngozi nyororo ya kuteleza, macho meupe na maangavu, tabasamu lake lilivutia kila wakati, nilipata bahati ya kuyaona meno yake meupe na maang’aavu mithili ya seruji.


Umbo lake lisinge kuchosha kuliangalia alikuwa na umbo zuri mno, mrefu, mwembamba wa wastani, alikuwa na nyonga ya kuvutia naweza kusema ni umbo la kipekee katika ulimwengu huu. Alikuwa na kifua cha wastani ambacho kilibeba matiti yenye ukubwa wa watani na umbo mchongoko. Jamie nilikuwa nimetekwa kihisia hata mbele sasa nilikuwa sioni, Kwani nilijikuta hata sikumbuki nimemuitia nini mle ndani, nilijikanyaga huku na kule walau nikumbuke ni kitu gani nimemuitia lakini bado ikawa ngumu , macho yangu yalilidhika kuendelea kumuona karibu yangu japokuwa nilijua huenda ninamkwaza lakini sikulijali hilo. Kilichonikustaajabisha ni kwamba binti huyu alikuwa akiachia tabasamu kila wakati tulipokutanisha macho hali iliyozidi kunipagawisha zaidi na kujikuta nalainika kama ugali wa mhogo uliolowekwa ndani ya mlenda.


Kichwa changu kilikuwa bize kikiwaza nianze la lipi kumueleza huyu msichana mrembo, nianze na kumuuliza tatizo alilonalo au nianze na kumueleza hisia zangu juu yake, wakati nikijaribu kupambanua lipi jema na baya tayari mlango ulifunguliwa ghafla na aliingia mtu kwa spidi kali, alikuwa ni Maria.


Nilipigwa butwaa kwa muda na kubaki nikijiuliza ni kitu gani alichokifuata Maria ofisini kwangu na isitoshe anakuja kipindi ambacho nilikuwa namsikiliza mteja. Maria alifika na kusimama pembeni huku akijibinua binua bila kusema chochote na kisha akaondoka zake huku akionesha dharau za waziwazi.


Nilijisikia vibaya sana lakini sikujali niliendelea na shughuli niliyokuwa nayo yakumsikiliza mteja “naitwa Jamie” nilijitambulisha, ni meneja wa mauzo hapa ofsini sijui Mwenzangu unaitwa nani?. Nilijitambulisha kwa majina na cheo na kisha kumrushia swali. “Naitwa Jesca J Manguli” alijitambulisha lakini jina kama lilinishitua kidogo ila niliona huenda ni kawaida maana majina hufanana.


Niliendelea kumsikiliza “Karibu naweza kukusaidia?”, baada ya kumpa nafasi, basi Jesca alinieleza mkasa mzima ilivyokuwa mpaka anatapeliwa na yule jamaa. Kupitia biashara zao walizokuwa wakifanya, Jesca alimwamini sana yule jamaa kumbe jamaa alikuwa tapeli. Lakini kwa bahati nzuri, yule jamaa alikuwa anapatikana kwenye namba yake ya simu ileile aliyokuwa akitumia na kila tulipojaribu kumpigia simu yake iliita ingawa alikuwa hapokei, hivyo haikuwa taabu saana kumtafuta. Maelezo yake aliyonisimulia nay ale niliyoyasikia wakati akimsimulia Maria hayana tofauti hivyo lilikuwa ni jukumu letu kumsaidia


Nililikabidhi jukumu kwenye idara ya kupambana na uharifu wa mtandao, nao wakafanya kazi yao mbele ya Jesca wakafanikiwa kumpata jamaa alikuwa Mwanza hapahapa mitaa ya Kiloleli. Walibaini hivyo kutokana na simu yake kuonekana ikisomeka katika minara ya mawasiliano ya eneo hilo.


Nilimwambia Jesca “jamaa amepatikana yupo maeneo ya Kiloleli” Jesca alionekana kufurahi sana huku akihoji “kwa hiyo tunafanyaje ili kumkamata?” nilimjibu bila kusita wala kigugumizi “Sisi tuna uwezo wa kutengeneza mazingira akakamatwa ila wenye jukumu la kumkamata ni Polisi, sisi hatuna uwezo huo maana siyo jukumu letu kisheria” na bila shaka aliridhika.


Jibu lile lilonekana kumkatisha tamaa Jesca na kujikuta akihoji tena kwa hofu “sasa mnajua yuko eneo fulani na mmewezaje kumpata na kumjua kama ni yeye bila mimi kuwaonesha?” lilikuwa ni swali zuri hivyo nikalitolea ufafanuzi. “Tumetumia namba yake uliyotupa kwa kuifuatiliana tukajua wapi alipo. Njia tunazotumia sisi ni za kiteknolojia hatuendi kutafuta mtu mmoja kwa mmoja bali tunatumia teknolojia ni rahisi mno na nakuhakikishia atakamatwa na hutaamini.


Jesca aliondoka na kwenda kituo kikuu cha polisi kilicho jilani na jengo la CCM Mkoa mkabala kabisa na bandari kuu ya mwanza, alitoa maelezo akapewa askari watatu aliongozana nao mpaka ofsini kwangu wakiwa na siraha nzito. Walipofika tuliwapa maelezo na baada ya kutoa maelezo na ufafanuzi sasa niliwakabidhi jukumu maana kazi ilikuwa imekwisha kwa upande wetu.


Tuliwapa mbinu itakayotumia kumpata kwa urahisi zaidi “tutatuma fedha fake kwenye simu ya mhusika, tunauhakika lazima ataenda kuzitoa kuzitoa kwa wakala haraka akiamini zimetumwa kimakosa. Kwake pesa itaonekana imetoka kwenda kwa wakala lakini kwa wakala haitaonekana hivyo itamlazimu kusubiri muamala kukamilika maana wakala hawezi kutoa pesa bila muamala kukamilika kisha nitawaelekeza muende moja kwa moja mpaka kwa yule wakala mtamkuta na kumkamata” maelekezo hayo niliyatoa huku polisi wakinisikiliza kwa makini.


Haikuwa mbinu ngeni kwao, hivyo waliondoka na walipofika Kiloleli wakanijuza nilifanya hivyo kweli baada ya dakika kadhaa tuliiona namba ile ikitoa pesa kwa wakala mwenye namba ya uwakala iliyoishia na 03. Mawakala wetu ni wachache hivyo tulijua alipo na askari walikwenda na kujikamatia kizembe kama kuku wa mdondo na kumpeleka kituo cha polisi ambako alihojiwa, na bahati nzuri alikiri kutenda wizi huo wa kuaminiwa na kuwekwa rumande akisubiri kesi yake kusikilizwa.


Baada ya pilika hizo kukamilika nilibadilishana namba za simu na Jesca kisha tukaagana. Mara baada ya kuagana na Jesca ndipo nikakumbuka nilitakiwa kuwa na kikao na boss saa nane na sasa ni saa kumi na moja jioni, nilijiona mjinga, “oooh! Mungu wangu, nimefanya ujinga gani huu?, boss atanielewaje mimi?” Nilijilaumu sana na mwisho niliamua kumpigia simu kumtaka radhi.


Nilizungumza na boss kwa upole kwa bahati nzuri alinielewa na akaniomba kikao hicho tukifanye jioni hiyo kabla sijaondoka ofisini, sikuwa na kipingamizi hivyo nilijiandaa na baada ya kuwa tayari tulifanya kikao na nilitoka ofsini majira ya saa mbili za usiku.


Nilikuwa na furaha saana baada ya kufika nyumbani kwangu niliandaa chakula changu kwa furaha nikala na kwenda kujipumzisha. Nilikuwa wakati huu wote nilikuwa namuwaza Jesca kichwani kwangu. Jesca alikuwa kateka hisia zangu, Jesca alikuwa kateka akili yangu, niseme tu kutoka moyoni nilijikuta nimependa na kuiridhisha nafsi yangu kuwa huyu ndiye mwanamke wa maisha yangu.


Kulingana na urembo alionao huyu Jesca J Manguli, ninaamini ni kutojitokeza tu kugombea taji la mrembo wa Tanzania. Lakini angejitokeza lilikuwa ni halali yake kabisa kwani alikuwa na vigezo mpaka vya ziada.


Mwanamke wa kiafrika ninayekiri kuwa ameteka hisia zangu ni Jesca Manguli, nilikuwa kama mgonjwa na sasa nilimuona kama chanzo cha matatizo ya katika akili yangu. Lakini baada ya kutafakari kwa kina niligundua kuwa chanzo cha tatizo hakuwa Jesca, tatizo ni tabasamu lake, tatizo hakuwa yeye Jesca pengine ni ulaini wa viganja vyake, tatizo ulikuwa muonekano wake na kilichonitesa ni urembo wake.


Jesca, Jesca, Jesc J Manguli anaitesa akili yangu, usiku kucha yu mawazoni mwangu, usingizi umefutiliwa mbali na dimbi la mawazo lililotililika mithili yam to mtela.


Nikiwa chumbani kwangu sikuishiwa furaha na kujikuta nikijinong’oneza mwenyewe “sijawahi ona msichana mrembo maishani mwangu kama huyu binti, pamoja na kukutana naye akiwa kwenye majonzi, lakini hali hiyo haijaharibu muonekano wake na mvuto wake. Bado anaonekana ni mrembo na mwenye mvuto zaidi je itakuwaje akiwa katika hali ya utulivu na furaha iliyo imara?” lilikuwa ni swali la kizushi nililojiuliza na kuyakosa majibu yake.


Nilikuwa nikijigeuza pasipo mafanikio nikigeuka huku mawazo nikirudi huku mawazo, na sasa ilikuwa yapata saa sita usiku. Uzalendo ulinishinda niliamua kumpigia simu, niliwasha taa ili niione simu yangu kwa bahati mbaya haikuwepo mezani, nilinyanyuka na kwenda kabatini napo nilikuta hakuna nilienda sebuleni nako jibu likawa lifelike na mwisho nilikagua nguo nilizokuwa nimevaa bado simu haikuonekana. Sasa ndiyo niligundua simu sikuwa nayo usiku huo.


Niliamua kutoka nje nikiamini itakuwa kwenye gari napo pia sikuikuta na sasa ndipo nashituka na kugundua kuwa nilikuwa nimepoteza simu kizembe. Kumbukumbu zinaniijia niliweka juu ya gari lililokuwa limepaki jirani na gari yangu kipindi nataka kuondoka, nilikumbuka kuwa nimeondoka na kuisahau pale nilipoiweka. Moyo uliniuma na kujikuta machozi yakinitoka kwa uchungu.


Sina furaha tena mimi Jamie, sidhani kama nitayapata mawasiliano mapya ya Jesca, bahati nimeichezea, bahati imepukutika kama majani ya mwembe wakati wa kiangazi, bahati nimeiharibu kwa uzembe, bahati imeyeyuka na sina bahati tena


Nilijikaza kisabuni ingawa iliniuma sana, sikuwa na namna zaidi ya kukubaliana na hali kwa kile kinachotokea.. Jesca hajanieleza chochote juu ya maisha yake, Jesca hajui chochote juu ya hisia zangu kwake, Jesca hajui kama ninaumia kwaajili yake. Mawazo yaliniandama na kuikosa suluhu. Nina mpenda sana Jesca, nampenda kutoka moyoni, sipajui anapoishi, ingawa nilimshuhudia juzi akiingia kwenye lile jumba lenye geti la kifahari huko Kapri Point, sina uhakika kama hapo ni kwake au kwao na sina hakika kama anaishi hapo kweli ama ni ofisini au alikwenda kuwatembelea ndugu na jamaa.


Kesho yake asubuhi baada ya kuwasili kazini ninakutana na Dominic rafiki yangu kipenzi tunasalimiana na kisha tunaongozana mpaka ofsini kwangu. Nilianza kumpa mkasa mzima toka siku namfuatilia Jesca na mpaka kufikia jana nilipomsaidia tatizo lake na mwisho napoteza simu yangu kizembe ikiwa na namba zake nilizozipata kwa bahati, kiukweli iliniumiza sana maana niliongea huku nikilengwa machozi.


Dominic aliumia pia alisikitishwa sana na hicho kilichotokea, alinilaumu kwa uzembe pia alinionya kwa kujifanya naficha siri na mwisho nimeharibu. Alilalamika sana akisema ningemshirikisha kwa kila jambo huenda hayo yote yasinge tokea.


Chuki zangu kwa Maria ziliongezeka zaidi ya awali nilionesha chuki hadharani bila kuogopa na bila kuona aibu. Tulianza kuishi kwa uhasama wa hali ya juu mle ofsini na nilimzuia kukanyaga nyumbani kwangu na yeye alitii amri hiyo. Maisha yangu sasa yalikuwa na stofahamu ndani yake, maana mwanamke niliyempenda kwa dhati, sijui alipo kwa sasa, sijui kama ni mke ama ni mchumba wa mtu mwingine na kilichoniuma zaidi sifahamu anapoishi, sijui anachokifanya na pia sina uhakika kama ipo siku nitakutana naye tena. Kuna wakati nilikuwa na mawazo mpaka nahisi kuumwa, kuna wakati nilikuwa nawaza mpaka nahisi kuchanganyikiwa. Chanzo ni yeye na wala si mwingine Jesca J Manguli jina nililotamkiwa na msichana mrembo niliyempenda kwa dhati lakini hajui kama naumia kwa ajili yake.


Najua aliondoka na namba yangu ya simu niliendelea kujipa matumaini ipo siku huenda atanitafuta baada ya kuwa nimeirudisha namba yangu ya simu ya siku zote iliyokuwa imepotea. Lakini ndoto zangu zikaendelea kuwa ndoto milele na kamwe hazikuonesha dalili za kutimia, nilizidi kuzihesabu siku bila simu wala sms kutoka kwa Jesca hata ya bahati mbaya.


Majonzi, kukosa furaha na kukosa amani viliniandama kila mara, kuna wakati nilifunga safari na kwenda Kapri Point, nilikaa mbali kidogo na lile geti aliloingia siku ile nikingoja huenda Jesca au mtu yeyote angetoka nikajaribu kumuuliza ili walau nipate msaada. Lakini haikuwezekana niliishia kuchoma mahindi hapo nje kuanzia asubuhi mpaka jioni pasipo mafanikio nilijiona kwli naenda kuchanganyikiwa kutokana na mapito niliyokuwa napitia.


Kuna siku nilipata wazo na nikaamini huenda litanisaidia nilienda kumtafuta yule dreva wa tax aliyembeba siku ile ya jumapili nilipokuwa namfuatilia niliamini huenda ni mteja wake wa siku nyingi au ana mawasiliano naye. Nilimpata lakini hakuwa anamjua na hakujua chochote zaidi ya kumbeba kama mteja na kwenda kumshusha kwenye lile geti. Nakumbukumbu zilimwijia baada ya kumtajia lile geti, majibu ya yule dereva tax yalinimaliza nguvu nikaamua kurudi zangu nyumbani nikiwa mnyonge.


Miezi sita ilipita tangu nikutane na Jesca nilikwisha kata tamaa ya kumpata tena jesca, matumaini ya kuwa naye yalishafutika na uhusiano wangu na Maria niliuvunja kwa nguvu na nikaamua kubaki mwenyewe.


Nakumbuka tulikuwa Adden Palace Hotel maeneo ya Iloganzala hapa jijini Mwanza tuliamua kwenda kupata chakula cha asili siku hiyo ya Jumamosi ili weekend yetu iende poa. Tuliamua kula makande ya kisukuma na juisi za mapapai chakula kilicho andaliwa kwa ustadi mzuri kamwe usingejuta kukipata.


Ni Adden Palace Hotel pekee ndipo kilipopatikana chakula hiki kitamu, siku hii ya Jumamosi ni siku ambayo Adden hujaa kupita kiasi palipendeza sana, magari yalikuwa yamejaa kila kona watu wakija kupata chakula safi cha asili.


Dominic alikuwa kaketi pembeni yangu alinishitua na kuniambia geuka nyuma yako bwana mkubwa, nilishituka na kugeuka duh! Sikuamini nilichokiona tulikutana na jamaa yetu wa kitambo sana, Victor Donian alikuwa na Pacha wake Mayala Kapinga. Hawa ni vijana tuliofahamiana sana toka tukiwa chuoni ingawa tulikuwa vitivo tofauti maana wao walisomea udaktari na sisi tukiwa upande wa uchumi lakini tulikuwa marafiki na tulitembea pamoja na kufurahi pamoja.


Mitoko ya usiku na kwenda viwanja mbalimbali hatujaanza leo ni tokea kitambo. Kuonekana kwao hapa hawa vijana halikuwa tatizo bali palikuwa pahala sahihi zaidi kwao. Ninani asiye ijua Adden palece ni nani asiyependa kuitembelea siku za jumamosi? Kwenye hii timu yetu alikuwa kakosekana kijana mmoja tu Francisco Charles huyu alikuwa ni mkuu wa ramani za viwanja vya starehe na tulimuamini sana enzi hizo tukiwa chuoni, pia tulimuita mkemia mkuu wa timu yetu kwa umahili wake wa kuchanga vinywaji na kuwafurahisha wanjwaji bila mkemia mkuu siku hiyo mtoko ulikuwa hauna mvuto.


Salamu ziliambatana na furaha, basi tulikumbushana mengi na mwisho tuliamua kukumbushia enzi zetu za chuoni tulianza kushusha chupa huku tukipiga soga kuyasogeza masaa mbele. Donian alikuwa ni mtu safi sana alisimamia huduma ile kwa kupenda sifa kwake na sisi tukapona namaanisha bili zote alizibeba yeye.


Tulikunywa sana tukapiga stori sana na mwisho tuliamua kuondoka majira ya saa moja jioni tuliagana na kubadilishana namba za simu. Nilikuwa nyuma ya usukani wa kigari changu aina ya Toyota mark X, basi nilimwambia Dominic “tunaenda Malaika Beach tukaikamilishe siku yetu”. Basi tuliongozana mpaka Malaika Beach tulifika na tukaendelea kupata kinywaji.


Malaika palichangamka, si unajua tena week-end watu walikuwa wengi hivyo tulitulizana tukaendelea kula maisha. Baada ya kukaa sana na chupa nilizozitundika nilijikuta hali inanilazimu kwenda msalani, huwezi amini nilipoukaribia mlango wa choo nakutana na Jesca ana kwa ana akitoka upande wa vyoo vya wanawake.


Niliduwaa nikamwita Jesca aligeuka kwa unyonge akaniangalia lakini sidhani kama alinikumbuka, maana aligeuka maramoja tu na kisha kuendelea na safari zake. Ilinilazimu kurudi haraka nikimfuata lakini kabla sijamfikia walikuja wasicha wawili wakiwa wamevalia suti na kunizuia huku wakiniambia niache fujo. Hali ile ilinishangaza kidogo maana ni kitu ambacho sikukitarajia. Walionekana kuwa na nguvu sana kulingana na jinsi walivyo wenza kunikabiri kiulaini baada ya kutaka kubishana nao.


Ilinibidi kuwa mpole hivyo niliwaomba wanipe nafasi niongee na Jesca maana ni mtu ninaefahamiana naye. Walikataa nikajitahidi kuwabembeleza zaidi lakini walikataa kata kata.


Baada ya kuendelea kuwasumbua hatimaye mmoja aliniuliza jina na ninakoishi na ninafahamiana vipi na Jesca. Nilimueleza lakini naikadanganya kuwa mimi ni rafiki yake tumesoma wote na sasa nafanya kazi Vodacom. Nilijua nikitaja jina na kampuni ninayofanyia kazi itakuwa rahisi kunikumbuka. Baada ya maelezo ikambidi mlinzi mmoja aende mpaka alipokuwa kaketi Jesca kujaribu kumuomba lakini alirudi na jibu hasi, Jesca alikataa katakata kuongea na mimi na akasema hanijui.


Huwezi amini machozi yalinibubujika, nilirudi na kwenda kumwambia Dominic, ambaye hakuniamini pia kilichotokea, alihisi labda ni pombe ndizo zinanizuzua nilimuomba twende naye akaone huenda hayaamini maneno yangu, kweli tuliongozana mpaka karibu na meza aliyokuwepo Jesca lakini tulizuiliwa tena na wale wasichana kumsogele.


Dominic alijitahidi sana kuwaomba lakini ilishindikana walikataa katakata. Walisema “Jesca amesema leo hahitaji kuzungumza na mtu yeyote Yule lakini mbaya zaidi kasema hajawahi kusoma na mtu mwenye jina lako na kwakifupi hakufahamu”, ni kama kichekesho lakini huo ndio ulikuwa uhalisia ilishindikana.


Nilijiuliza maswali mengi sana juu ya wasichana wale ni akina nani na kwanini wanizuie kuongea na Jesca? Lakini hilo lilikuwa swali dogo kubwa ni kwamba inawezekanaje msichana huyu awe na ulinzi mkali kiasi hiki ni nani?


Majibu ya maswali yangu hayakupatikana kiurahisi lakini kimuonekano nilihisi atakuwa mtoto wa tajiri mkubwa “bila shaka baba yake huyu binti atakuwa na pesa yakuchota kwa koleo maana si kwa ulizni huu kwa binti yake” kwa kifupi mbali na kuwaza sana nilikuwa nimeumia mno kutokupewa nafasi ya kuongea na Jesca, unaweza kuniona mjinga lakini ukweli wa mapenzi niliujua mwenyewe, hakuna aliyejua kuwa Jesca nilimpenda kiasi gani isipokuwa moyo wangu tu.




.


Malaika palichangamka, si unajua tena week-end watu walikuwa wengi hivyo tulitulizana tukaendelea kula maisha. Baada ya kukaa sana na chupa nilizozitundika nilijikuta hali inanilazimu kwenda msalani, huwezi amini nilipoukaribia mlango wa choo nakutana na Jesca ana kwa ana akitoka upande wa vyoo vya wanawake.


Niliduwaa nikamwita Jesca aligeuka kwa unyonge akaniangalia lakini sidhani kama alinikumbuka, maana aligeuka maramoja tu na kisha kuendelea na safari zake. Ilinilazimu kurudi haraka nikimfuata lakini kabla sijamfikia walikuja wasicha wawili wakiwa wamevalia suti na kunizuia huku wakiniambia niache fujo. Hali ile ilinishangaza kidogo maana ni kitu ambacho sikukitarajia. Walionekana kuwa na nguvu sana kulingana na jinsi walivyo wenza kunikabiri kiulaini baada ya kutaka kubishana nao.


Ilinibidi kuwa mpole hivyo niliwaomba wanipe nafasi niongee na Jesca maana ni mtu ninaefahamiana naye. Walikataa nikajitahidi kuwabembeleza zaidi lakini walikataa kata kata.


Baada ya kuendelea kuwasumbua hatimaye mmoja aliniuliza jina na ninakoishi na ninafahamiana vipi na Jesca. Nilimueleza lakini naikadanganya kuwa mimi ni rafiki yake tumesoma wote na sasa nafanya kazi Vodacom. Nilijua nikitaja jina na kampuni ninayofanyia kazi itakuwa rahisi kunikumbuka. Baada ya maelezo ikambidi mlinzi mmoja aende mpaka alipokuwa kaketi Jesca kujaribu kumuomba lakini alirudi na jibu hasi, Jesca alikataa katakata kuongea na mimi na akasema hanijui.


Huwezi amini machozi yalinibubujika, nilirudi na kwenda kumwambia Dominic, ambaye hakuniamini pia kilichotokea, alihisi labda ni pombe ndizo zinanizuzua nilimuomba twende naye akaone huenda hayaamini maneno yangu, kweli tuliongozana mpaka karibu na meza aliyokuwepo Jesca lakini tulizuiliwa tena na wale wasichana kumsogele.


Dominic alijitahidi sana kuwaomba lakini ilishindikana walikataa katakata. Walisema “Jesca amesema leo hahitaji kuzungumza na mtu yeyote Yule lakini mbaya zaidi kasema hajawahi kusoma na mtu mwenye jina lako na kwakifupi hakufahamu”, ni kama kichekesho lakini huo ndio ulikuwa uhalisia ilishindikana.


Nilijiuliza maswali mengi sana juu ya wasichana wale ni akina nani na kwanini wanizuie kuongea na Jesca? Lakini hilo lilikuwa swali dogo kubwa ni kwamba inawezekanaje msichana huyu awe na ulinzi mkali kiasi hiki ni nani?


Majibu ya maswali yangu hayakupatikana kiurahisi lakini kimuonekano nilihisi atakuwa mtoto wa tajiri mkubwa “bila shaka baba yake huyu binti atakuwa na pesa yakuchota kwa koleo maana si kwa ulizni huu kwa binti yake” kwa kifupi mbali na kuwaza sana nilikuwa nimeumia mno kutokupewa nafasi ya kuongea na Jesca, unaweza kuniona mjinga lakini ukweli wa mapenzi niliujua mwenyewe, hakuna aliyejua kuwa Jesca nilimpenda kiasi gani isipokuwa moyo wangu tu.


Huku akitokwa machozi ya furaha, alikuwa kanikumbatia kwa nguvu zote, nilikuwa nikivutiwa zaidi na kifua chake laini juu ya kifua changu. Jesca alinitizama na kuniambia “unamoyo wa ajabu sana wewe kaka yangu sijui nikulipe nini masikini wa Mungu? Sijui nikupe nini ili kuonesha furaha yangu kwako. Najua sina chakukulipa maishani mwangu na katika ulimwengu huu sidhani kama kuna mtu ana moyo kama wako naamini hayupo na hata kuwepo milele…Jamie ni wewe kweli na nimekuona tena? Sikuwa nakukumbuka kwa sura na hata jina nimerudi Mwanza jana ila kesho nilipanga kuja kukutafuta ofisini kwako ili nitoe shukrani zangu lakini umeniwahi ahsante Jamie” Akiwa bado mikono yake imeyashika mabega yangu akiniangalia kwa huba alinichombeza kwa busu maridhawa shavuni kwangu na kisha akaniangalia usoni huku akitabasamu.


Na mwisho anatoa kauli yenye utata “Hebu twende unisindikize sehemu kama hutojali, maana umeibadilisha siku yangu na kuwa siku bora kuliko siku zote zilizowahi kutokea maishani mwangu.” Alinishika mkono na kuongozana tukitoka ndani ya ile supermarket kama wapenzi vile….. kusema kweli nilikuwa na furaha mpaka mapigo ya moyo yalivurugika nikawa nausikia moyo ukidunda mpaka unanisukuma kwenda mbele


Mapenzi upofu nilijikuta nalisahau gari nililokujanalo pale supermarket bila hata kukumbuka nilijikuta naingia kwenye tax aliyoichukua Jesca, huwezi amini sikuwa na kumbukumbu hata kidogo kuwa nimekuja na gari pamoja na kuwa nilikuwa nimeshika funguo zangu mkononi muda wote.


Basi dreva aliwasha gari, mimi nilikuwa kiti cha nyuma na Jesca alikuwa kiti cha mbele safari yetu haikwenda mbali kumbe mbwembwe zote zile tulikuwa tunaenda Gold Crest Hotel, kutoka jengo la CCM mkoa kwenda Hoteli ya GoldCrest haifiki hata robo kilometa. Nilishangaa na kubaki nasikitika jamani hapa napo tax? lakini mshangao wangu ulibaki moyoni sikutaka kuuweka wazi.


Tulishuka na kuingia kwenye lift mpaka golofa ya nne tulielekea upande wa kulia, Jesca alichukua kadi kwenye mkoba wake na kufungua mlango wake huku akitangulia ndani, nilimfuata baada ya kunikaribisha niliingia kwenye kile chumba nikakitanzama ni uwazi mkubwa uliokuwa na kila kitu ndani yake na kiligawika kwa vioo vinavyoonesha. Ni chumba cha wazi maana unaweza ona kila kitu nje, pamoja na kugawanywa kwa vioo, zaidi kulikuwa na sofa nzuri za kuvutia seti nzima ikiwa imepangwa kwa ustadi, runinga kubwa ya bapa ilikuwa ukutani, palipangiliwa vizuri na kupambwa kwa ustadi. Macho yangu hayakuchoka kuangaza kwani fahari ya macho ni kutizama na sikuwa mvivu kufanya hivyo maana nilikuwa ugenini yanini nisitoe ushamba.


Niliketi kwenye kiti kizuri na nadhifu, kulinukia malashi mazuri mle ndani kiasi kwamba angeingia nzi kwa bahati mbaya bila shaka mauti yangemkuta kwa ubora wa utuli ule. Eeeh! Nzi wake uozo sasa angestahimili vipi sehemu nadhifu kama hii?. Kila kilichoonekana mle kilikuwa ni kitu cha thamani kubwa kuanzia dhuria, mapambo, vitambaa, kitanda na hata mapazia nadhani kwa kabwela kama mimi siwezi hata kuthubutu kuuliza bei yake waswahili husema nyumba imepambwa kwa thamani ya nyumba nadhani umeelewa vizuri usemi huu. Kama hujaelewa basi inamaanisha mapambo ya mule ndani yalitosha thamani ya nyumba nyingine mpya ya kifahari.


Nikiwa naendelea kushangaa mazingira na mwonekano wa kuvutia wa kile chumba, nilishtushwa na sauti ya Jesca iliyonisemesha Jamie karibu nimefikia hapa nitakuwepo kwa siku kumi ingawa kuna vi safari vya hapa na pale, kama hakutatokea mabadiriko basi hizo siku zitaisha nikiwa hapa Jesca alinikaribisha, nami nikajibu kwa ufupi ahsante sana Jesca.


Moyoni nilijua Jesca atakuwa ni mtoto wa tajiri mkubwa hapa nchini, si bure kukaa kwenye kile chumba cha hoteli cha hadhi ya nyota tano kwa gharama ya siku kumi si kitu kidogo maana gharama yake yaweza jenga nyumba mpya ya kawaida watu wakaishi.


Nilikuwa najikaza nisionekane mshamba lakini ukweli ulibaki kuwa ukweli mle ndani mimi nilikuwakuku mgeni ujanja wote mfukoni, kila kitu kilikuwa kipya, tena kipya haswaa. Basi tuliendelea kupiga soga za kujuliana hali na utani kidogo, lakini kuna wakati soga zilinipita maana macho yalitaka kutimiza adhima yake. Kiukweli tu macho yangu siku hiyo nili ya overdoze maana yalikuwa hayatulii mara yamwangalie Jesca huku nako yanavutiwa ilikuwa ni hovyohovyo.


Baada ya maongezi ya muda mfupi ndipo alipo amua kunihadithia juu ya kesi yake aliyokuwa akiishughulikia na hiyo kesi ndiyo iliyotukutanisha. Jesca alinishukuru sana kwa kufanikisha kupatikana kwa yule jamaa aliyemtapeli alimtaja kwa jina la George Faru, hata mimi nilipata nafasi ya kumfahamu maana jamaa ni tapeli mkubwa kila mtu anamjua hapa mjini na anajiamini sana. Jesca aliniambia hakua ameibiwa milioni saba na Mr. Faru kama alivyokuwa ameeleza awali. Sasa alinihadithia mkasa wa kusisimua kuhusiana na Mr. Faru, aliniambia kuwa Faru ni tapeli wa kimataifa tena ni tapeli aliyeshindikana, Jesca alikuwa akimsaidia rafiki yake wa karibu ambaye walishibana sana maana walisoma wote aliyejulikana kwa jina la Grace , rafiki yake huyo aliajiriwa kama meneja wa tawi kwenye benki moja kubwa huko Dar es salaam. Faru alikuwa ni moja ya wateja maarufu katika benki ile. Alikuwa na tabia moja chafu sana ambayo nirahisi sana mtu kujiingiza kama haujui huo mchezo. Mr. Faru alifika kila siku asubuhi kwenye tawi la benki hiyo alichukua kiasi kikubwa mno cha pesa kwa mfano milioni ishirini na ikifika saa nane mchana alirudisha marambili ya kiasi hicho.


Mr. Faru alivalia vizuri kila siku suti za bei ghali alionekana nadhifu usinge mdhania kuwa ni tapeli, tamaa za mafanikio ndizo zilizomuingiza kwenye mtego huyu rafiki yangu Grace. Tamaa za kupata mafanikio ya haraka alijikuta akivutiwa na biashara za Mr. Faru, alijaribu kuongea naye ili kama kuna uwezekano aanze kutengeneza faida kwa njia za mkato na siri. Kumbuka muda huo Mr. Faru hakuwa na biashara yoyote isipokuwa alikuwa akiandaa mtego wa kumtapeli mtu yoyote pale benki na sasa Grace alikuwa amejiingiza kwenye huo mtego.


Mr.Faru hakuwa na tatizo alimwambia alete kiasi alichonacho hiyo asubuhi na mchana angemletea marambili yake. Grace aliitumia nafasi ile alitoa laki tano na kumpa Mr. Faru ilipotimu saa nane mchana Mr.Faru alileta milioni moja. Basi biashara ikawa na mvuto kesho alitoa milioni zikarudi mbili, kesho kutwa akatoa milioni tano zikarudi kumi, siku iliyofuata akatoa milioni kumi zikaja ishilini, kosa kubwa alilokuwa akilifanya huyu Grace alikuwa akichukua fedha za wateja bila kuutarifu uongozi aliendelea hivyo akichota pesa na baadae analetewa faida kubwa.


Naweza kuuita mchezo mchafu na hatari ambao unahitajia akili ya ziada kuuepuka lakini Grace ulimnogea , maana alivuka mipaka na sasa alichukua kiasi cha shilingi milioni miatano akiamini kuwa saa nane angerudishiwa shilingi bilioni moja na Mr. George Faru. Grace alikuwa kajipanga kesho yake kuacha kazi maana angekuwa na mtaji wa mamilioni ya pesa hivyo hakuwa na maana ya kuendelea kuwa kibarua wa benki, lakini kinyume chake ikawa sahihi.


Baada ya kuzichukua zile pesa Mr. Faru hakurejea aliondoka jumla. Ilifika saa nane kamili Mr. Faru hakuonekana, saa nane na robo bado Mr. Faru hakujitokeza na hatimaye saa kumi muda wa kufunga ofisi bado hakukuwa na dalili za Mr. Faru kuonekana. Mr. Faru alikuwa ametokomea na kiasi hicho kikubwa cha fedha hakuonekana tangu hapo mpaka siku ile ulipotusaidia kumpata.


Huu ni mwaka wa pili rafiki yangu alikuwa jela na tayari alikuwa kahukumiwa kifungo cha miaka 25. Ililazimika kuwa hivyo maana pamoja na kufilisiwa mali zake pamoja na mali za wazazi wake na ndugu zake, lakini bado hawakuweza kupata hata robo ya kulilipa hilo deni, alikuwa gereza la Butimba alihamishiwa hapa mwaka jana mwishoni nilikuwa naenda kumuona kila nilipopata nafasi. Jesca aliongea kwa uchungu sana machozi yalikuwa yakimtoka maana alionekana kuwa na ukaribu mkubwa na mhusika, niliendelea kumsikiliza kwa makini.


Ni hadithi mbaya kuisikiliza haina mvuto na sikuipenda maana inaweza kukukera mpaka ukajikuta unalia. Maana kuna asilimia tisini na tisa ya tamaa na uzembe uliosababishwa na Grace, lakini ilikuwa ni lazima kuijua kutokana na hali ilivyokuwa niliendelea kumsikiliza Jesca. Njia pekee ya kumuokoa huyu rafiki yangu ni kumpata mhusika ili kuzirejesha hizo pesa ni milioni miatano siyo kitu kidogo tunazungumzia nusu ya bilioni moja za kitanzania kitu ambacho tumekiota kwa miaka miwili sasa bila mafanikio.


Nimekuwa nikienda gerezani kumuona ananililia na kuniomba nijaribu hata kuisaidia familia yake maana haina hata pakuishi nyumba iliuzwa na baadhi ya mali ziliuzwa pia.


Nilimuahidi kulishughulikia hilo maana ni rafiki yangu tena rafiki wakweli, sikutaka kuisaidia familia yake tu ila nilitaka kumsaidia yeye pia maana sehemu aliyokuwepo kipindi hicho haikuwa salama. Uchungu ulikuwa ukimfanya akatishe masimulizi lakini nilimtia moyo akaendelea kuzungumza.


Hakuishia hapo aliendelea kunisimulia.Jamie ulinisaidia kumpata George Faru ingawa sikuwa mkweli kwako, lakini ulinisaidia kumuokoa rafikia yangu kipenzi kutoka jela na kukiepuka kifungo cha miaka ishirini na mitano. Baada ya Mr. Faru kukamatwa alikili kuhusika, na tukakata rufaa ya kesi ya ndugu yetu Grace ikasikilizwa upya na akapata bahati ya kuachiwa huru baada ya zile pesa zote kurejeshwa mikononi mwa benki hiyo. Mwisho kesi ilienda kwa mhusika na kujikuta akitumikia kifungo cha mika 43 jela kwa kesi ya udanganyifu na wizi wa kuaminiwa (utapeli). Wote tulishusha pumzi kuashiria mafanikio, maana mapafu yalipumua kama tumetua mzigo mzito.


Niliendelea kumsikiliza Jesca kwa makini zaidi maana hadithi yake ilitia uchungu ila ilikuwa na funzo, Jamie nisamehe kwa kushindwa kukutafuta na hata kujikuta nakusahau kabisa kuwa ni miongoni mwa watu walionisaidia. Wewe ni mtu mhimu sana katika maisha yangu na ndiyo maana uliponikumbusha nimefurahi nikajikuta nakukumbatia na kukubusu, usinielewe vibaya ilikuwa ni furaha kwa mtu aliyeonesha utu kwangu nakupenda sana na kamwe stakuvunjia heshima. Aaah! Mi nilijua amekwisha ingia laini kumbe alinishobokea kisa nilimsaidia? kidogo hiyo sentensi iliupunguza uchangamfu wangu, lakini aliendelea kama ada Siwezi kusema chochote bali namshukuru Mungu kwa kila jambo hasa kunikutanisha na wewe mtu ambaye hatukufahamiana na leo umekuwa msaada mkubwa kwangu.


Nilizipokea shukurani zake na kumshukuru Mungu pia. Jesca msichana mrembo, mpole, mwerevu, mnyenyekevu, mwenye huruma, anayejali na sasa nagundua pia anajitolea na siyo mbinafsi lazima nimuoe, nilijiwazia.


Kimya kilitanda kwa muda, nilimpa pole na nikamtia moyo kwa mapito magumu ambayo anayapitia.


Baadae alitaka kujua historia ya maisha yangu nilimhadithia, naitwa Jamie Justine ni mtoto wa peke kwenye familia yangu. Wazazi wangu wapo hapahapa Mwanza maeneo ya Igoma natoka familia ya kawaida sana na ndiyo maana nikazaliwa pekee yangu ili wazazi wangu waweze kukidhi mahitaji yangu kulingana na hali ngumu waliyokuwa nayo.


Nadhani kuhusu kazi yangu aliijua hivyo sikuwa na haja ya kumwambia ni nini nafanya ili kujipatia riziki , nyumbani kwangu ni Busweru. Utambulisho wangu haukuwa umejitosheleza maana nilimuona Jesca kama anaswali lakini niliamua kumuwahi kabla hajahoji aaaah! sijaoa na sina mchumba wala mpenzi.Tulijikuta tukicheka kwa pamoja. mbona unajiwahi kabla hujaulizwa kuna nini? alichombeza kwa utani kidogo.


Baada ya utambulisho wangu na sasa ni zamu ya Jesca nitajitambulisha lakini usiogope naitwa Jesca Jones Manguli ni mtoto wa mwisho wa Rais wa jamhuri hii ya muungano


Sikukiamini nilichokisikia ilibidi nimwambie arudie lakini aliporudia haikuwa tofauti na kile nilichokisikia mwanzo. unamaanisha wewe ni mtoto wa Rais wa nchi hii ? nilihoji kwa hofu bila shaka Jamie yule ni baba yangu mzazi na mkewe ndo mama yangu mzazi na mimi ndiye mtoto wa mwisho na wakike pekee kwenye hiyo familia ya watoto wanne.


Kwa sasa ukiniuliza nyumbani kwetu ni wapi nitakwambia ni Ikulu na maanisha Magogoni. Sikuweza kuongeza hata neno moja bali nilibaki nimeduwaa huku nikijiwazia na kujihoji maswali. inawezekana je huyu binti awe ni mtoto wa Rais? Hivi mtoto wa Rais huwa yuko hivi kweli? Lakini huwa nasikia wanalindwa na mbona yeye halindwi?. Sikuwa najua chochote juu ya familia za kitawala hivyo nilikuwa nimekwama kimawazo. Lakini wakati napambana na mawazo nilirudi nyuma nikakumbuka wale wasichana walionizuia kumuona bila shaka picha ilikuja na kuniambia huenda kuna ukweli.


Kihelehele cha kuuliza swali kilinikauka sikuwa na jeuri tena, maana pamoja na urembo wake wote sasa sikustahili hata kumuwazia tu kuwa nampenda. Nakama kweli ni mtoto wa rais hawezi kuwa na kabwela kama mimi, ukweli ndo huo, siyo rahisi kiasi hicho.



.


Ilinibidi kubadilisha mikao kwanza mana sasa nilikuwa naongea na serikali, kwani ni mtoto wa rais namzungumzia mwana wa mtawala wa taifa hili, namaanisha mwana wa mkuu wanchi hii daah!. Kwa tafsiri nyepesi ni mtawala wa watoto pia katika nchi hii ana sauti kuliko spika za tamasha la mziki.


Nilianza kutetemeka ghafula maana sikuwa na amani tena moyoni mwangu, sikuwa najiamini tena niliona matatizo nayatafuta tena kwa miguu miwili. Tukiachana tu na kile cheo chake cha Urais cha baba yake, kiongozi wetu ana maamzi magumu kuliko hata chuma cha pua, ni mkali zaidi ya moto wa gesi, ukimchokoza hana huruma kama tanulu la tofali.


Ila uzuri nikwamba taarifa hutufikia sisi wananchi juu ya yale anayoyaamua kwa watu wanaokwenda kinyume na matakwa yake, kwani anastaili zake za kuwanyoosha wale wanaomchokoza. Chakushangaza zaidi nilijiona na mimi nilikuwa nimejiandaa kumchokoza, nilikuwa namtafuta ugomvi, nikama nimeamua kushusha mbendera ya taifa iliyo katikati ya kambi ya jeshi tena mchana kweupe.


Nilijiona ninagonga geti la ikulu huku nimelewa na nikitoa matusi machafu najua unakijua kitakachofuata. Bado niliona nnachotaka kukifanya ni kuweka kiganja cha mkono kwenye domo la nguruwe mwenye njaa kali na kitakachotokea ninakijua.


Niligundua nilichokuwa nakifanya ni sawa na kukwea mnazi ukweni huku nimefungamsuli na ndani pakiwa patupu kitakachotokea ni fasihi simulizi itakayodumu milele na milele.


Ulifuata ukimya na ulikuwa ni ukimya wa kustajabisha, wakati nikiyawaza hayo kumbe Jesca alikuwa akinisemesha kwa muda, sikumsikia nilikuwa mbali kimawazo, maana tayari ameesha iharibu kabisa siku yangu. Ninampenda Jesca wangu lakini naanzaje kumueleza hilo?. Mtoto wa Rais sistahili hata kukigusa kiganja cha mkono wake, hivi itakuwaje nikimwambia harafu akakataana kunikasirikia si nitafia jela mimi?. Hudhuni majonzi na kukata tama kulitanda moyoni, mawazo yangu yote yalijikita upande hasi,. Niliwaza tena au akikubali harafu yule mzee akajua itakuwaje?. Jamie we Jamie. Umekuwaje . Hivi unanisikia kweli?.. sikuwa nasikia muda wote huo Jesca alioniita sana na sasa aliamua kuja kunigusa nikashituka kama mtu aliyekuwa usingizini. Jesca alikuja karibu yangu akaketi huku akinipapasa shavuni aliniuliza vipi unaumwa?.... mbona umekuwa hivi ghafla jamani? duh! mikono laini iliusisimua mwili wangu na kujikuta naishiwa nguvu, lakini sauti laini nyembembe na tamu ikaiburudisha nafsi yangu.


Nilihisi nabembelezwa mimi, nilihisi kudeka kwa muda kitu ambacho nimekuwa sikipati kwa muda penzini, nilikuwa nikiisikia sauti yake juu ya kifua change ikiniburudisha, natamani awe wangu natamani sana, nilijihisi niko peponi.


Lakini nilipomkumbuka Mh. Rais na heka heka zake sikuwa na chakumjibu nilinyanyuka na kuamua kuondoka kabisa nikitembea kwa mwendo wa unyonge usiyoweza kuelezeka.


Kwa kifupi nilikuwa nimevurugwa, niliufungua mlango na kutoka nje nilikutana na wasichana wawili warembo waliovalia vizuri suti za kijivu na miwani myeusi. Walionekana si watu wa kawaida kimuonekano tu. Bila shaka walikuwa ni walinzi wa Jesca, sasa naanza kupata picha halisi na nilianza kuyaamini macho na masikio yangu.


Jesca kweli alikuwa mtoto wa Rais hakukuwa na swali zaidi maana nimejionea kwa macho, mbali na kusikia kwa masikio yangu akinieleza kwa kinywa chake. Niliingia ndani ya lifti nikiwa mwenye mawazo kwelikweli niliwakuta watu wawili kijana na mzee ndani ya lift nikaungana nao bila kusemeshana na mwisho walishuka nami nikashuka. Sikujua kumbe ilikuwa gorofa ya nane, niligutuka kumbe sijabonyeza namba ya wapi ninaelekea nilirudi ndani ya lift na kubonyeza herufi G iliyoniruhusu kwenda mpaka chini nilishuka nikiwa mwingi wa mawazo mana Togwa limetiwa nzi.


Nilielekea upande wa kulia jirani na Mwanza hoteli ndipo nakutana na rafiki yangu mpendwa ni dreva tax wa siku nyingi Thomas James jina la kazi wanamuita Gwaba. Gwaba aliponiona tu kama kawaida yake ni kulia hali mbaya. aah! Jamie fanya hata buku tano boss wangu mdogo wako hapa hali mbaya, tenki kavu sijanywa hata chai, mdogo wako, fanyafanya bwana kiungwana tu si unajua tena. Huwezi amini leo nimepiga bundi gizani. Gwaba ni rafiki yangu anapenda sana kutumia maneno ya mtaani hivyo kumuelewa inakuwa ngumu kwa mtu asiyemjua akikwambia kapiga bundi gizani anamaanisha kakesha patupu yaani hajapata wateja usiku mzima.


Na akisema tenki kavu anamaanisha ananjaa yani tumboni hakuna kitu. Nilimsogelea Gwaba nikionekana mwenye mawazo hata alichonieleza sikushughulika nacho ingawa nilisikia kila sentensi tena neon kwa neno, hivyo sikumjali kabisa nilipozidi kukaribia hata yeye alijua leo Jamie hayuko sawa.


Maana ni kijana aliyekuwa na mimi kwa muda mrefu kwanza tumefahamiana toka nasoma kipindi hicho alikuwa anapiga debe standi kuu ya Igoma, pili tangu nimeanza kazi hapo NSSF Plaza amekuwa akinisaidia safari za hapa na pale hasa kile kipindi ambacho nilikuwa sijanunua usafiri wangu, hivyo Gwaba ananijua vizuri sana. Alinifungulia mlango nikaingia na kuketi kisha nilimwambia anipeleke nyumbani sikuwa nahitaji bugudha maana akili yangu haikuwa sawa.


Basi tuliondoka kuelekea nyumbani kwangu Busweru, nilihitaji utulivu nikiwa kwenye gari maana nilikuwa nimechanganyikiwa, lakini haikuwa hivyo kwa upande wa Gwaba. Gwaba ni msumbufu sana mana anapenda kuongea ni mchangamfu kupita kiasi. Utamfurahia ukiwa sawa ila ukiwa unahitaji utulivu basi Gwaba si mtu sahihi maa atakuchosha.


Alikuwa akiongea njia nzima na ukimkalia kimya ni sawa na bure tu maana maana atakukomalia mpaka umpe ushirikiano utasikia Jamie mwaka kesho nitanunua gari yangu tena itakuwa kali sana, warembo watanikoma na nina mpango wakuagiza Nissan Murano, au hela ikipungua basi nitachukua kama ile yako Toyota mark X”. Hapo mfukoni hana hata mia katoka kunipiga mzinga wa buku tano lakini ndo maisha ya vijana na ndoto kubwa huku mfukoni hakuna kitu. na hana hata akiba ya senti hamsini na ana ndoto yakumiliki gari mwakani sikutaka kutukana niliendelea kukaa kimya.


Si hilo tu njiani nako kila dereva anajuana naye, yaani ni kero kwa kwenda mbele. Mara asimame kusalimiana na watu, ilihitaji uvumilivu sana kumzoea Gwaba hasa akiwa amekunywa kidogo aah! Unaweza mwambia nishushe nitembee.


Nilivumilia hizo kashikashi nikitajiwa kila aina ya gari na bei yake mengine ndo marayangu yakwanza kuyasikia. Thomas Gwaba anawajua matajiri wote wenye magari mazuri na ya thamani kubwa hapa mjini na mikoa ya jirani. Hapa nishahadithiwa mpaka nimechukia lakini sikuwa na jinsi nilivumila na baada ya dakika ishirini na tano tayari nilikuwa nyumbani kwangu niulipumua na kumshukuru Mungu ngoja niepukane na hii kero.


Nilishuka na kumlipa Gwaba akaondoka huku nikipiga ishara ya msalaba kumshukuru Mungu acha nikapumzike. Nilijikokota mpaka mlangoni kwangu ili nikajipumzishe. Niliingiza mkono mfukoni kutoa funguo za nyumba nakutana na funguo za gari, nilishituka maana kumbukumbu ilinirudia haraka kuwa gari nimeiacha supermarket, ilinibidi nijicheke kwanza.


Nilijiona mpumbavu, na mwenda wazimu kabisa mana kwa hali ya kawaida mtu huwezi ukasahau gari tena sehemu hatari kama ile na kwa muda wote huo wote zaidi ya masaa manne.


Ilinibidi nimpigie simu Gwaba arudi, nilimbembeleza maana sikuwa na jinsi ilinibidi tena kutumia usafiri wake maana sikuwa na namna kama kawaida kelele zake sasa zilikuwa za chura 

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog