IMEANDIKWA NA : KAICHI M MUSSA
***********************************************
Simulizi : Mshangao
Sehemu Ya : Kwanza (1)
KUALA LUMPUR, MALAYSIA
Kuala Lumpur International Airport (KLIA)kiwanja cha ndege cha kimataifa kilichopo eneo la Sepang, wilaya ya Persekutuan, kilometa 50 kutoka katikati ya jiji la Kuala Lumpur (KL Sentral), jiji la kibiashara na mji mkuu wa nchi ya Malaysia. Miongoni mwa viwanja vikubwa kabisa vya ndege na vya kisasa zaidi vilivyopo kusini mashariki mwa bara la Asia, bara namba moja kwa ukubwa kuliko mabara yote yaliyopo katika dunia yetu tunayoishi.
Ndege za abiria zilizokuwa zinaruka kuondoka kiwanjani hapo kuelekea nchi mbali mbali na zingine zikitua kuingiza abiria kutoka nchi mbalimbali wa mataifa tofauti na nchi hii wengine wenyeji wa nchi hii.
Baada ya kuwa kamaliza taratibu za kiukaguzi kama ilivyo ada, kawaida au sheria ya kila kiwanja cha ndege cha abiria kuwa na taratibu za kiukaguzi (security check)kila abiria anayetumia usafiri wa umlazimu kupitia katika kaguzi hizi kutoka kwa maofisa usalama wanaoangalia usalama wa abiria anayesafiri au kuondoka huku idara ya uhamiaji nao wakiangalia uhalali wa pasi za kusafiria za abiria hao.
Pilika pilika hizi zilizo katika utaratibu maalumu unaomlazimu anayetumia uwanja husika kuwa mpole na kufuata taratibu zote (kutii sheria bila shuruti), hali hii uwafanya wahalifu kuwa katika wakati mgumu wafikapo mahali hapa. Kutokana na teknolojia inavyozidi kukua kila siku ulimwenguni iliwapa wakati mgumu wahalifu kama wauza unga na magaidi kupita na vitu vyao hasa katika viwanja vya kisasa kama hiki cha KLIA.
Hali ilikuwa tofauti kwa kijana huyu yeye hakupata tabu katika ukaguzi licha ya begi dogo alilokuwa nalo na briefcase lake kuwa na vitu ambavyo si rahisi kwa mtu mwingine kupita, hati yake ya kibali cha kuingia Malaysia kutoka Marekani vilimtambulisha anaingia nchini Malaysia katika kuongeza nguvu za kiulinzi kwa Balozi wa Marekani nchini Malaysia ukizingatia kulikuwa na hali ya sintofahamu iliyotokea katika wiki za karibuni katika nchi ya Malaysia zikigusa maslahi ya Marekani hivyo ilileta urahisi mkubwa kwake, ukiacha watu wengine ambao kila walikopita ilichukua dakika mbili tatu hadi tano kwa mtu kuulizwa maswali mbalimbali huku hati zake zikipekuliwa kiasi cha kuwaridhisha wakaguzi.
Kwa mwendo wa taratibu huku macho yake yakiwa katika simu yake aina ya iPhone8 kutoka kampuni ya Apple ambayo toka abadilishiwe simu ilikuwa ni wiki tu, sababu kila baada ya miezi sita ofisi yao ilikuwa na utaratibu wa kuwabadilishia simu watumishi wake kwa oda maalumu waliyoingia nao mkataba kampuni ya APPLE, ambapo uwatengenezea simu, saa ambazo ni saa zilizotengenezwa zikiwa na teknolojia ya hali ya juu katika mambo ya kijasusi kiasi ya kwamba kama ungeiona ikifanya baadhi ya kazi zake usingeamini, pia walipewa na laptop nayo ikiwa ni ile ya hali ya juu sana, vyote hivi vilikuwa vikiguswa na mtu mwingine hasiye mhusika vilitoa taarifa maalumu sababu viliunganishwa na mitambo maalumu iliyopo Langley, Virginia yalipo makao makuu ya CIA nchini Marekani na hata kuonyesha wapi vilipo kwenye satelaiti maalumu.
Wakati mkono wa kulia alikuwa kashika simu akiiangalia simu hii huku akiwa kafungua upande wa gallery akiangalia picha ya mtu aliyeelekezwa toka anaondoka Washngton DC Marekani.
Kijana huyu mwenye ngozi ya asili ya watu watokao bara Afrika (watu weusi)weusi wa maji ya kunde, mwenye sura ya kuvutia pindi umuangaliapo utasita kusema unaiangalia sura ya super handsome boy, mwili uliojengeka kimazoezi kwa wastani aliouhitaji yeye mwenyewe si kama wanyanyua vyuma na watunisha misuli au wacheza mieleka wa ngazi za juu kama kina Batista, mwili wa katikati kama bondia ni wa uzito wa katikati si ule wa juu (heavy weight) au wa chini (mwepesi), urefu wake ulikuwa ni urefu uliomtosha kwa kazi zake na hata angecheza basketball basi asingesumbuka au kupingwa na makocha wa timu mbalimbali.
Alikuwa amependeza usiku huu kwa mavazi yale yapendwayo na vijana wengi hasa wa Marekani, akiwa kavaa fulana aina ya jezi, jezi ya timu yake anayoishabikia, timu ya mpira wa miguu ya Manchester united inayocheza ligi ya EPL (English premier league), jezi ya rangi nyeusi ivaliwayo na timu hiyo pindi wanapokwenda uwanja wa ugenini kucheza mechi na timu ambayo ikiwa uwanja wa nyumbani hutumia jezi za rangi nyekundu, jezi ambazo kwa wao Manchester FC ni kama alama kwao mpaka kufikia kuitwa jina la Red devils, jezi toleo jipya ikiwa na maandishi mbele Chevrolet na mgongoni jina la @Antony Martial mchezaji anayempenda sana kwa kazi aifanyayo kiwanjani namba ya jezi ikiwa namba 11. Suruali ya jeans rangi ya bluu iliyokolea, pamoja na raba nyeusi sumu (ya ukweli).
Kama nilivyotangulia kueleza hapo awali uwanja huu wa KLIA ulikuwa ni uwanja wa kisasa uliogharamikiwa na ukakubali gharama za kugharamiwa, kulikuwa na lift ngazi inayowatoa watu toka eneo la mwisho la ukaguzi ambalo lilikuwa na maaskari wapatao kama sita na kati yao watatu wakiwa ni askari wa mbwa yaani wakiwa katika sare zao huku wameshika ma-mbwa makubwa kama ng’ombe watoto (ndama).
Kijana mambo yote kati ya yale yaliyopo pale kwake hayakuwa mageni kwake, teknolojia zote zile kwa mtu anayetoka Marekani ilikuwa ni kawaida sana kwake hivyo haraka alikanyaga ngazi kisha akasimama ikiwa tayari kuna baadhi ya watu waliokuwa nao wamepanda , ngazi zile ziliwapeleka wakajikuta wanaibukia kwenye sehemu iliyokuwa kama ukumbi mkubwa sana uliokuwa na watu mbali mbali wake kwa waume, eneo lilijieleza ni sehema ya kusindikiza abiria wanaoondoka kwenda nchi mbali mbali na wengine wako pale kupokea abiria wanaoingia kutokea nchi mbali mbali (Passengers arrive), iwe ni ndugu jamaa au marafiki.
Usiku huu wa saa mbili na dakika kadhaa eneo hili lilikuwa ni kama mchana kwa jinsi mataa makubwa yaliyokuwa kwenye manguzo na paa lililo refu sana kwa kwenda juu, kuwa ni mataa mengi. Watu walikuwa wengi wakiwa wanaonekana ni wale wa mataifa mbali mbali ikiwa ngozi nyeusi kama si wawili basi ni mmoja maana kila mmoja kama si mmalaysia ambao ndiyo wenye nchi basi alikuwa ni mchina kwa muonekano, mhindi, mwarabu na wazungu wachache sana.
Ngazi iliposimama tu kijana yule alishuka huku akiwa kazi aliyokuwa anaifanya kwenye simu yake ikiwa kaimaliza kama vile kutoa taarifa kwa njia ya email kwa bosi wake kuwa kashafika salama Malaysia, pia kuikalili picha ya mwenyeji wake kwa mara ya mwisho.
Simu ilirudi kwenye mfuko wake wa suruali yake ya jeans kisha akaanza kusogea taratibu kwa mwendo ambao ni ule wa mtu asiye na haraka. Macho yake yalianza kupita kwa kila mtu anayemkaribia mawazo yake yakifikiri anajua tayari atakuwa kashaonekana na mpokeaji wake kwa uwezo wake wa kuangalia kwa haraka aliweza kumuona kila mtu aliye maeneo yale hasa wanawake sababu mpokeaji wake alikuwa ni mwanadada na hakutaraji kama hatasimama kwa dakika nzima pale bila kumuona au yeye huyo mtu kumuona yeye.
Akaamua asogee mbele zaidi akielekea sehemu zenye huduma za kifedha, akaitoa tena simu yake kisha akaitoa lock halafu akafungua kwa mara ingine tena eneo la gallery (eneo la kuhifadhia picha na video katika simu). Akagusa picha ndogo ya mwanamke kati ya picha zilizopo eneo lile, picha ile ikajikuza akaitizama kwa sekunde mbili, huku taratibu akipiga hatua kusogea kwenye huduma ya maduka ya kifedha yaliyopo pale Passengers arrives.
Hakufika kabisa eneo lile akageuza mgongo kuangalia alipotokea huku macho yake yenye ujanja mwingi wa kijasusi yakipepesa huku na huko kuangalia kwanini hamuoni mtu anayemtafuta, akarudisha tena macho kwenye simu na kuiangalia picha aliyoikuza, sababu ndiye haswa ni mtu anayetakiwa kuonana naye ingawa kiusalama haikuwa sawa kwa mshirika wake kuja kumpokea lakini wakuu wao walitaka iwe ni moja ya mbinu ya kusogeza maadui zao karibu.
Akageuza macho kushoto kisha kulia alipotaka kupiga hatua kuelekea tena upande wa kushoto hakupiga hata hatua mbili. Akageuka haraka sana nyuma tena mwili wote baada ya kuguswa bega kutokea kwa nyuma. Akakutana na tabasamu ambalo kwa haraka aliliona ni tabasamu la kujilazimisha kutoka katika sura ya mwanadada yule ambaye ndiye aliyekuwa akitafuta sura yake.
“Welcome KL! Agent Kai” (Karibu KL Agent Kai) Akasema yule binti huku akiendelea kuufanya uso wake kuunda tabasamu lile la kulazimisha ambalo kwa ujuzi wa huyu anayeitwa Agent Kai kama ulivyosoma hapo juu wakati anamkaribisha ilikuwa ni rahisi sana kutambua. Mikono yao ikakutana katika hali ya kusalimiana. Wakatingishana mikono huku mdada naye akijitahidi kuminya mkono wa Kai, hali iliyosababisha wote kufurahi kwa kucheka kicheko cha sauti.
“Thank you so much Detective Marie, how are you?” (Ahsante sana Detective Marie, vipi hali yako?”
“I’m cool, how about you are long journey in aeroplane?” (Niko poa, vipi kuhusu safari yako ndefu katika ndege?”)
“So good and so cool…. Thanks for all pirots and all in all I sending my great thanks for God” (Nzuri sana na poa sana…. Ahsante sana kwa marubani wote na yote kwa yote napeleka ahsante kubwa sana kwa Mungu”)
“So good,…! I’m really so glad to meeting with you for the first time… You are really strong man, perfect men and so most handsome! I hope you are good partner for me to doing this intelligence job” (“Vizuri sana,…! Kwa kweli nimefurahi sana kukutana na wewe kwa mara ya kwanza… Wee ni mtu mkakamavu, mwanaume kamili na mzuri sana! Natumaini wewe ni mshirika wangu mzuri katika kazi hii ya kiitelejensia”)
“Me too I’m so happy to meeting with you, also I believe for together we are going to finishing all for the right time… Inshaallah!” (Mimi pia nina furaha sana kukutana na wewe, pia naamini kwa pamoja tunakwenda kumaliza kila kitu katika wakati sahihi…Inshaallah!”)
“Don’t worry about that my great man… I trusting you…. Let’s go” (Usiwe na wasiwasi kuhusu hilo mtu wangu wa nguvu…. Twen’ zetu”)
Walishaanza kutoka kuelekea nje ya eneo lile la passengers arrive ikiwa mwanadada yule kampokea begi lake, alimuongoza hadi kwenye maegesho ya magari ya watu binafsi yanayofika na kuondoka KLIA Kupitia upande wa geti kuu la Terminal A1 KLIA.
Mwanadada mwenyeji au mtangulizi aliyetangulia Kuala Lumpur ambaye tayari tushamtambua kama kijana aliyeingia kutoka Marekani alivyomuita kuwa anaitwa Detective Marie kama alivyojionyesha kwa tuliyemtambua kwa jina la kuwa anaitwa Agent Kai. Kutokana na maelekezo kutoka alipotoka huko Marekani kuwa akifika Kuala Lumpur, airport atapokelewa na dada huyu anayeitwa Detective Marie Johson na ndiyo atakuwa mshirika mkuu katika kazi hii ngumu inayomkabili katika nchi hii ya Malaysia, sababu hasa ya kupewa mshirika huyu kikazi ni kuwa Marie alikuwa amesoma shule ya msingi katika jiji hili la Kuala Lumpur wakati huo baba yake akiwa mmoja wa maafisa wa Marekani katika ubalozi wa Marekani mpaka alipostaafu kazi na kurudi Marekani ikiwa Marie akiwa amemaliza shule ya msingi miezi miwili nyuma, hivyo mitaa ya Kuala Lumpur ilikuwa haimsumbui sana hata kama jiji lilizidi kukua kwa ongezeko la barabara mpya na majengo marefu marefu ya kupendeza.
“Gari niliipaki mbali kidogo kwa sababu niliwai kufika hili kuangalia usalama wetu wote…!” Akasema detective Marie huku akiminya remote ya gari iliyo mbele yao mpaka ikatoa mlio wa kuruhusu kuguswa bila kupiga alarm.
Kila mmoja akazunguka upande wake, Marie akafungua mlango wa upande wa dereva, Agent Kai hakusubiri kuelekezwa yeye akafungua mlango wa upande wake na kujibwaga kwenye siti wote kwa pamoja wakabamiza milango ya gari hii aina ya BMW new model.
Mwanadada akavaa mkanda wa siti yake ya udereva kama sheria muhimu ya usalama inavyoomba tufunge mikanda pale tunapotumia gari, kisha kwa jicho la chati akamchungulia Kai kuona kama atafunga mkanda ama vipi, lakini kwa Kai ilikuwa si rahisi yeye kufunga mkanda ni aghalabu kwake kuvaa mkanda na ana sababu zake ikiwemo kujiamini kuwa anakuwa salama zaidi akiwa hajajivalisha mkanda akiwa kwenye gari pia hapendi kudhibitiwa, anajiamini chochote kitokeacho basi ataweza kujisaidia akiwa huru kwa wepesi wake uliongezewa na utundu wake wa kuzaliwa, licha ya Marekani kuwa na sheria kali kwa watumiao magari kuhusu mikanda lakini kwake hii sheria aliitii mara chache tena pale anapohisi kaonekana kwa maaskari wa usalama barabarani basi kwa alivyo na kasi katika jambo analotaka kulifanya kwa kasi ufanya kuuvaa kwa kasi ya umeme kiasi ya kwamba askari wakifika dirishani hukosa ushahidi.
Mwanadada akamtizama tena kwa jicho la wizi na Agent Kai akaling’amua jicho lile kuwa lina walakini fulani ila hakutaka kulitilia maanani kimoyoni akijisemea acha avute subira atajua tu kwanini yupo katika hali ya kuhisi vitu tofauti, alichofanya akatabasamu na kumfanyia kwa ishara ya mkono kuwa ‘twe zetu’
Ilikuwa ishatimia saa nne kasoro robo gari ilipokuwa ishakamata barabara kubwa yenye njia nane kwa nne zinatoka huku wanakotoka (KLIA) na nne zinaelekea wanakotoka wao, barabara iitwayo Jalan Tun Razak road. Kijana Agent Kai alikuwa katulia kwenye siti yake akiacha mwanadada akikanyaga gia kwa mwendo unaostahili kwa magari yanayopita barabara hii kwa muda huu wa usiku.
Macho yake yakiwa yanaangalia kupitia dirishani maana alishusha kioo kutokana waliamua isiwashwe kipoza joto cha garini (Kiyoyozi) mandhari za jiji muda huu wa usiku ilikuwa yakuvutia macho ya kila mtu hasa kwa mgeni kama yeye Kai, ukizingatia barabara hii wanayoitumia inayotoka KLIA ilikuwa imeinuliwa juu hivyo ukiwa ndani ya gari unaziona sehemu nyingi zilizo maeneo ya karibu na bara bara hii na hata majengo marefu yaliyo mengi sana katika wilaya hii ya Persekutuan, KL.
Licha ya kuwa ya kuwa macho yake yakiiangalia Kuala Lumpur inavyopendeza usiku kwa mataa mbalimbali yatokayo kwenye majengo marefu pamoja taa za barabarani, kimawazo alikuwa akiwaza jinsi gani anakwenda kutimiza kazi iliyomleta hapa Malaysia, kazi ambayo kimtazamo tu wakati anapewa alijua itakuwa ina ugumu fulani katika kuimaliza kwa wakati na yeye kutopatwa na tatizo litakaloiumiza familia yake. Kazi ya kuchunguza, kupeleleza na hata kuhakikisha kama ikiwezekana yeye mwenyewe kuwapata wanasayansi wawili wastaafu waliofika ngazi ya uprofesa katika utaalamu wa silaha za kikemikali, kibaolojia na kinyuklia kutoka kituo cha Manhattan PROJECT.
Maprofesa hawa marafiki wakubwa watoka nikutoke tena tokea wako shule wakiwa na familia zao kila mmoja ikiwa baba, mama na watoto waliamua kuja kutembelea Malaysia kiutalii baada ya wote wawili kufikia umri wa kustaafu wakiwa wameitumikia Manhattan PROJECT kwa kipindi cha miaka 30 mfululizo toka wakiwa vijana, waliweka miadi na familia zao kuwa wakistaafu katika hali ya kufurahia urafiki wa familia zao watafanya ziara za kiutalii katika nchi ya Malaysia katika bara la Asia na kisha Afrika katika nchi ya Tanzania.
Walipotea katika stahili inayoonyeshwa bila kutia shaka kuwa walitekwa na kikundi cha watu fulani kisichojulikana jina ni kikundi gan?i, na je wana nia gani na utekaji wao? Hilo hakuna aliyekuwa na hakika nalo zaidi ya kuhisi hisi tu pia haikuwa inajulikana hasa hasa kama wapo hai au wameuliwa na hao watekaji.
Hali hiyo ilishtua sana si serikali ya Marekani peke yake hata serikali ya Malaysia haikufurahishwa kabisa na kilichotokea, Waziri mkuu wa Malaysia akiwa na mawaziri wake wa usalama wa taifa pamoja na waziri wa mambo ya nje kwa pamoja waliiahidi serikali ya Marekani kuwa watu hao watapatikana kwa haraka tena watajitahidi wapatatikane wakiwa katika hali nzuri na usalama.
Matangazo katika media yalipewa kipaumbele, mambo ya kiutekaji wa watalii katika nchi ya Malaysia haikuwa hali iliyozoeleka ikizingatiwa ni nchi inayotegemea katika mapato yake ikiwemo na utalii wa watu kutoka nje ya Malaysia hasa nchi za ulaya na America. Lakini siku tatu za toka kupotea zilipita pamoja na vyombo vya usalama vya Malaysia vikiweka nguvu katika kuchunguza na hata kuahidi zawadi kwa yule atakayetoa taarifa itakayosaidia kupatikana kwa Maprofesa wale maarufu wakiwa na familia zao.
Hali ya taharuki na kuogofya ikawakumba ndugu na jamaa wa wanafamilia hizo zilizopo Marekani wakihofia kuuwawa kwa ndugu zao hao. Hali iliongezeka kuwa mbaya baada ya habari za duru za kiitelejensia kufika kwa F.B.I na C.I.A kuwa maprofesa wale wanaoshikiliwa mateka wapo hai wakiwa wamewekwa mateka katika nchi ile ile waliyotekwa lakini kwa madhumuni ya kupelekwa nchi mojawapo kati ya Korea Kaskazini au Iran.
Cha kwanza serikali ya Marekani ikaiomba nchi ya Malaysia kuongeza nguvu kubwa za kiulinzi katika mipaka yake kuhakikisha hakuna watu wanaopitishwa kinyemela kwenda nchi ingine, hilo lilipokekelewa na hata jitihada zikaanza kufanywa zikionekana kwa jumuiya za kimataifa na Marekani yenyewe.
Siku ya nne toka utokee utekaji ule maofisa upelelezi watatu walio na nguvu kutoka idara ya kijasusi ya Malaysia iliyo chini ya ofisi ya waziri waliokabidhiwa kazi hii ya kufuatilia ishu hiiya upoteaji maprofesa iitwayo Research Division of the Prime Minister’s Departiment (RDPMD) walikutwa wamechomwa moto katika nyumba moja iliyokuwa katika ujenzi wa ghorofa mtaa wa Jalan Mega, old klang road.
Maofisa wa kiusalama wa kimarekani waliopo kwenye balozi ya Marekani nchini Malaysia ambao wao walianza kazi ya kufanya ushushushu mara tu baada ya taarifa kufika ubalozi wa Marekani kuwa kuna upotevu au kutekwa kwa raia wa kimarekani tena ni watu muhimu sana, lakini vijana wawili waliokuwa katika kazi ya upelelezi huo tena tegemeo walikutwa wamepigwa risasi nyuma ya shule ya msingi iitwayo SMK, Bandar Baru Ampang.
CTU ambao kiasili wao hujihusisha na mambo ya kigaidi walikubaliana na CIA kila shirika moja kati ya mashirika hayo ya kijasusi kutuma mtu wao wa kazi mmoja jumla wawe wawili lakini napo waligonga mwamba na kusababisha masikitiko makubwa sana kwa wakuu wao wa kazi pamoja na kuwa na uzoefu mkubwa waliokuwa nao katika kazi za kijasusi walipotea kimya kimya bila kuchukua hata siku tatu toka waingie Malaysia.
Kupotea bila kujulikana kwa watu wengine ndani ya Malaysia tena wakiwa ni mashushu wenye ujuzi na utaalamu wa juu haikuwa jambo dogo Habari hii ingine mbaya iliwashtua sana Wamarekani, Raisi wa Marekani aliitisha kikao ikulu ya Marekani white house kikao kilichohudhuriwa na makamu wake wa Rais wakiwa na waziri wa ulinzi pamoja na maofisa wengine wa ulinzi na usalama wa Marekani ikiwa zimeshatimia siku tano toka Profesa Fransisco Ehud na Profesa Martin Bender waingie katika mikono ya kundi la watu wasio wema na kuzusha taharuki ndani ya jamii ya wamarekani na serikali yake pamoja na serikali ya waziri mkuu wa Malaysia.
Raisi wa Marekani akiwa kama mwenyekiti wa kikao kile cha watu wachache, aliingia kikaoni akiwa mwenye sura ya huzuni sana iliyochanganyika na hasira haswa baada ya baadhi ya media za marekani pamoja na mitandao ya kijamii kuiandika vibaya serikali yake katika kulishughulikia suala hili, moja kwa moja akaweka wazo mezani kuwa anahitaji haraka sana kutumwa Malaysia kwa watu makini ikibidi kikosi cha kazi kikali kipelekwe Malaysia, kitu ambacho si rahisi kwa kikosi icho hata kama kiwe cha makomando mia bila habari za kiitelejensia ni kazi bure, amiri jeshi mkuu alijikuta hasira zake zikitulizwa na makamu wa Raisi pamoja na watu wengine waliokuwepo pale.
Makamu wa Raisi akamuomba mkuu wake kazi ile akabidhiwe yeye aisimamie yeye na baada ya wiki moja waje kwenye kikao kama hiki yeye akiwa na majibu kitu gani kinaendelea. Hasira za Rais wa nchi zilipungua baada ya kikao kile kuunguruma kwa masaa matatu, ndipo ikabidi Raisi akubaliane na wasaidizi wake kuwa ni muhimu kupisha duru za kiitelejensia zikafanya kazi, nchi ya Marekani ina mashushu wazuri na wenye uwezo kuliko mashushushu wa nchi zingine, kupotea na kuuwawa kwa baadhi ya watu waliopitia mafunzo ya kujasusi kisiwatie woga wakaacha kudharauliwa na watu wa mataifa mengine.
Maamuzi yakapita kazi ile iwe mikononi mwa ofisi ya makamu wa rais kitengo cha kijasusi. Kazi ya kutuliza mioyo ya ndugu na jamaa waliopotelewa na wengine kupoteza ndugu na jamaa zao waliokutwa na matatizo ikawa mikononi mwa makamu wa Rais na tena akiomba wiki moja tu ya kuja na majibu kipi kinaendelea huku akisaidiwa kwa ukaribu na Waziri wa ulinzi kwa pamoja na wakuu wa shirika la kipelelezi la F.B.I na shirika la kijasusi ya C.I.A, kikao kiliisha matumani yakiwa ni makubwa sana. Hakuna aliyetaka kusikia tena kuwa kuna mmarekani mwingine kapigwa risasi au kutekwa, umakini uliitajika. Kikao kikavunjwa baada ya kila mtu kuwa kaelewa kipi kinatakiwa kifanyike kuondokana na fedheha walioiona dhahiri kwa kubwa kama yao.
Mwisho wa sehemu ya kwanza (01)
Kazi imeanza ndani ya Kuala Lumpur, Malaysia!
kijana wa kazi za kijasusi zilizoshindikana ndiyo kwanza ameingia ndani ya jiji hili starehe na maraha katika eneo la Asia Mashariki.
Tumeshuhudia akipata mapokezi yale aliyoelekezwa atayapata punde atakapofika katika jiji hili.
Je? Nini kitajiri katika sehemu ya pili.
Naomba uendelee katika sehemu inayofuata ya uhondo wa riwaya hii kali yenye kusisimua na taharuki za kushtua hisia, kashikashi na ufundi wa fundi anayejulikana kwa jina la Agent Kai Hamis.
Raisi wa Marekani akiwa kama mwenyekiti wa kikao kile cha watu wachache, aliingia kikaoni akiwa mwenye sura ya huzuni sana iliyochanganyika na hasira haswa baada ya baadhi ya media za marekani pamoja na mitandao ya kijamii kuiandika vibaya serikali yake katika kulishughulikia suala hili, moja kwa moja akaweka wazo mezani kuwa anahitaji haraka sana kutumwa Malaysia kwa watu makini ikibidi kikosi cha kazi kikali kipelekwe Malaysia, kitu ambacho si rahisi kwa kikosi icho hata kama kiwe cha makomando mia bila habari za kiitelejensia ni kazi bure, amiri jeshi mkuu alijikuta hasira zake zikitulizwa na makamu wa Raisi pamoja na watu wengine waliokuwepo pale.
Makamu wa Raisi akamuomba mkuu wake kazi ile akabidhiwe yeye aisimamie yeye na baada ya wiki moja waje kwenye kikao kama hiki yeye akiwa na majibu kitu gani kinaendelea. Hasira za Rais wa nchi zilipungua baada ya kikao kile kuunguruma kwa masaa matatu, ndipo ikabidi Raisi akubaliane na wasaidizi wake kuwa ni muhimu kupisha duru za kiitelejensia zikafanya kazi, nchi ya Marekani ina mashushu wazuri na wenye uwezo kuliko mashushushu wa nchi zingine, kupotea na kuuwawa kwa baadhi ya watu waliopitia mafunzo ya kujasusi kisiwatie woga wakaacha kudharauliwa na watu wa mataifa mengine.
Maamuzi yakapita kazi ile iwe mikononi mwa ofisi ya makamu wa rais kitengo cha kijasusi. Kazi ya kutuliza mioyo ya ndugu na jamaa waliopotelewa na wengine kupoteza ndugu na jamaa zao waliokutwa na matatizo ikawa mikononi mwa makamu wa Rais na tena akiomba wiki moja tu ya kuja na majibu kipi kinaendelea huku akisaidiwa kwa ukaribu na Waziri wa ulinzi kwa pamoja na wakuu wa shirika la kupambana na ugaidi CTU na shirika la kijasusi ya CIA, kikao kiliisha matumani yakiwa ni makubwa sana. Hakuna aliyetaka kusikia tena kuwa kuna mmarekani mwingine kapigwa risasi au kutekwa, umakini uliitajika. Kikao kikavunjwa baada ya kila mtu kuwa kaelewa kipi kinatakiwa kifanyike kuondokana na fedheha walioiona dhahiri kwa taifa kubwa kama lao.
ENDELEA NA SEHEMU YA PILI..!
Faili lililokuwa na jalada la kijani lenye maelezo ya kesi hii likaondoka mikononi mwa Raisi jengo la ikulu white house na kutua mikononi mwa Makamu wa Rais na kwenda nalo ofisi yake ya makamu wa Rais Eisenhower Executive Office Building.
Kufika huko makamu wa Rais hakusubiri giza liingie, aliitisha kikao kidogo cha dharura cha watu wanne tu akiwemo yeye mwenyewe, katibu wake katika ofisi yake (Chief of Staff to the vice president), mkuu wa shirika la kupambana na ugaidi Counter Terrorism Unit (CTU) pamoja na mkuu wa shirika la kijasusi Centre Intelligence Agency (CIA).
Kikao hiki kikapitisha maamuzi ya kutuma tena makachero wawili lakini walio bora katika ufanyaji wa kazi wenye ujuzi katika mapigano na akili kubwa ya kuchanganua mambo kwa haraka. Majina mawili yaliwekwa mezani na kiongozi wa CTU (Counter Terrorism Unit) na majina mengine mawili yaliwekwa mezani na kiongozi mkuu wa CIA. Baada ya wote kupitiwa ubora wao ilionekana wote wako vizuri lakini makamu wa Rais pamoja na katibu wake (Chief of Staff to the vice Pressdent) wao walikuwa na chaguo lao na wakitaka sifa ziwaendee kwa mara ingine ofisi yao kulisaidia taifa kwenye jambo muhimu sana.
Wote kwa pamoja walikuwa wanamkubali na kumuamini kupitiliza Agent Kai, waliomba waongee pembeni wao wawili wakakubaliwa dakika kumi zilitosha kuamua wakirudi kikaoni basi wapendekeze moja kwa moja kazi ya kiitelejensia (ushushushu) itaenda kufanywa na mtu wao mtu wa ofisi yao.Wakarudi kikaoni na jina lao huku tayari mkurugenzi wa CIA na wa CTU wakiwa washaambizana jina litakalorudi kutoka kwa makamu wa Rais litakuwa jina la Agent Kai, Makamu wa Rais ulikuwa humwambii kitu kwa huyu jasusi alikuwa akimuhusudu sana kwa jinsi alivyomsaidia kazi nyingi na hata kuwai kumuokoa katika hatari wakiwa katika ziara za nchi za kiarabu zilizo Africa.
Anapopewa taarifa na katibu wake kuwa kuna tatizo fulani limeenda tofauti na wao kama usalama wanatakiwa kulishughulikia suala hilo na Agent Kai ndiyo amekabidhiwa kazi hiyo basi moyo wa makamu wa Rais uwa na faraja sana akiamini mtu wake huyo ni zaidi ya maitelejensia wote walio FBI, CTU, S.W.A.T na hata CIA. Kijana mwenye asili ya Afrika tena nchi ya Tanzania lakini aliyeangukia kwenye mikono ya kuitumikia Marekani (Tutaona mbele ilikuwaje mtz kuwa mmarekani).
Kwa majina kamili akijulikana kama Kai Hamis Mkarambati jasusi wa CIA anayefanya kazi kama wakala (Agent) wa CIA katika ofisi ya makamu kitengo cha ujasusi kinachoongozwa na Chief of Staff to the Vice Pressdent, hakuwai kufanya kazi ofisi kuu ya CIA ingawa asilimia tisini ya majasusi wa CIA ilikuwa lazima kupita na kufanya kazi makao makuu ya CIA yaliyopo Langley, Virginia.
Hii kwake ilitokea kuwa tofauti licha ya kuwa alisoma shule kuanzia sekondari zile zilizo na mafunzo maalumu ya kijasusi (Pia tutaona mbele ilikuwaje). Yeye baada ya kufanya kazi nzuri kwa miaka minne kama mwanajeshi (US, Army) akiwa katika kikosi maalumu chenye sifa za kipekee duniani, kikosi bora kabisa cha makomando waliovuka level ya juu kifaamikacho kikosi chenye makomando ambao wanahudumiwa kimazoezi na hata kimaslahi kuliko makomando wa vikosi vyovyote duniani. Kikosi kinachoitwa US, Navy seal hii seal ikifupishwa> sea, air and land> wakiwa na mafunzo ya kutumia silaha zozote, kuogelea, kutumia anga kwa kuendesha vyombo vyovyote vya anga, kupigana vita vya ardhini, kufudhu mapigano ya aina zote ni kikosi kilichotumika katika operesheni zilizohitaji uharaka na umakini mkubwa, wakishiriki hata operesheni ambayo wengi wanaijua ile iliyomuondoa duniani Osama Bin Laden nchini Pakistani. Kifupi kilikuwa ni kikosi kilichoogopewa hata na mataifa yaliyoendelea yenye majeshi yenye nguvu, inasemekana komando mmoja wa kikosi hiki cha US, Navy seal anaweza kuondoa duniani wanajeshi hata mia hamsini waliopitia mazoezi ya kutosha.
Kuna kisa kimoja ambacho kilimfanya yeye Agent Kai kuomba aondolewe US, Navy, akiwa katika moja ya operesheni iliyowahitaji wao US, Navy kuifanya nchini Afghanistan karibu na misitu iliyo katika milima ya Kandahar, ndege ndogo waliyokuwa wameipanda wakiwa makomando watatu ilipata hitilafu ikiwa juu kabisa angani, hitilafu iliyotokana wao kuwa wamefanikisha operesheni iliyokusudiwa kwa weledi wa hali ya juu wakakimbilia kwenye ndege kumbe kioo kimoja kilipigwa risasi kikavunjika pakubwa na kuwa kinapitisha hewa ndani ya ndege. Walipoona hali ishakuwa mbaya na ndege ishafeli inayumba kwa kasi kuelekea chini walichukua miamvuli ya kujirusha toka juu ya ndege kisha wote wakavunja mlango mmoja uliokuwa kwenye ndogo ile na kujirusha kwa kufuatana.
Kila mmoja alijikuta kulekule juu akipelekwa na upepo sehemu yake kutokana na hali mbaya ya hewa iliyokuwa eneo hilo ikiambatana na upepo mkali sana huku ndege ikidondokea katika moja ya nyumba ya kijiji cha watu wa jamii ya watalebani na kusababisha maafa, yeye Agent Kai alijikuta akidondokea kwenye kolongo kubwa na refu kwenda chini akipigwa pigwa kwenye miti mirefu baada ya mwamvuli wake kuchanwa na tawi la mti alijitahidi kudaka moja ya tawi la mti na kuokoka kwenda chini kudondokea kwenye mawe makubwa.
Aliposhuka taratibu hadi chini ya kolongo hali ilikuwa mbaya sana kwake alijikuta akizirai kutokana na maumivu aliyokuwa nayo. Alipokuja kuzinduka ilimchukua siku tatu kuwa katika lile kolongo na kufanikiwa kutoka kwa tabu sana akinusurika kuliwa au kudhuriwa na majoka makubwa yaliyokuwa kama ndiyo makazi yao katika kolongo lile la kutisha. Maisha yake yote hawezi kusahau mkasa wa kolongo hili na ajali ya ndege hii iliyowakumba yeye na makomando wenzake (Maelezo kamili aliondokaje katika kolongo lile na alipambana vipi na majoka na aliondoka vipi Afghanistan, utayapata katika riwaya ya ZERO MISSION.
Alipofika Marekani na kugundua wenzake kati ya wale aliokuwa nao mmoja maiti iliokotwa katika msitu ulio katikati ya milima ya Kandahar na mwingine mpaka leo hawakujua alipatwa na nini. Moyo wake ulivunjika tamaa akaona sasa huu ni wakati wake wa kupumzika na kufanya mambo mengine ya kimaisha ya kawaida, akaandika barua kwa wakuu wake wa US, Navy akiomba kupumzika.
Ikawa imetokea ofisi ya makamu wa Raisi wa Marekani kuwa wanahitaji mtu mmoja wa intelejensia aliyekamilika na bwana Kai kifani alisoma shule hadi vyuo vya kipelelezi ila aliingia tu jeshini wakamuomba kwa faida ya Wamarekani wanaona katika kupumzika kwake basi asipumzike kwa kuacha kabisa kuitumikia nchi iliyojitolea muda na akili ya hali ya juu kumfundisha yeye mafunzo ya hali ya juu, aingie CIA na akiwa humo CIA basi atakuwa ofisi ya makamu wa Rais kwa kazi za mara moja moja zitakazomlazimu yeye kufanya.
Hiyo ndiyo ikawa pumzika yake ya mikiki mikiki ya operesheni maalumu zilizoshindikana za kijeshi, ikawa ndiyo mwanzo wa kurudi alipotakiwa haswa yeye kuhudumu na kwa sasa ameshazoea kazi hii ya kishushushu, kikachero na kuifanya kwa raha zake tena akiifurahia haswa.
“Umefikia hotel gani? Na vipi hali ya hapa KL, toka ufike juzi unaionaje? Na hakuna chochote ulichoanza?” Akakatiza ukimya tena kwa kustukiza Agent Kai baada ya kutizama saa yake ya mkononi na kumuonyesha ni saa nne na robo usiku, akimuuliza mwanadada aliyekuwa yupo makini kuendesha gari huku akiwaza yake.
(Walikuwa wanatumia lugha ya kiingereza lakini kutokana na muda twende na Kiswahili pekee)
“Nimefikia hotel ya kawaida tu ipo nje kidogo ya jiji….. Hali ya hapa kwa kweli inahitaji umakini wa hali ya juu… Na kiukweli toka nimefika sijagundua kitu kikubwa cha kutusaidia kwa hali ya kuweza kuona wapi pa kuanzia kwa chochote zaidi ya kwenda ubalozini, kisha kwenda kuchunguza japo kwa kidogo eneo linalosemekana Maprofesa na familia zao walivamiwa na kutekwa… Itabidi twende wote ukapaone na wewe sababu kuna vitu nimevihisi tukitulia nitakupa hivyo vitu hili uweze kujua na vitu gani… Pia jana mchana nilifika kwenye hotel waliyopanga napo nilifanya mahojiano kidogo na baadhi ya wahudumu pia nikaingia kwenye vyumba vyao ambavyo mpaka leo ubalozi, leo mchana nilipata fursa ya kwenda hotel aliyofikia Detective Morris Hansen napo nilifanya uchunguzi mdogo nimeandika kwenye note book yangu nilivyoona vinaweza kutusaidia, kesho nimepanga asubuhi nitaanza Sheriwood Gateway Hotel alipofikia Detective Caesar North..” Alitoa maelezo marefu mwanadada ambaye kwake yeye Kai pamoja na kuwa katika hali ya kumuhisi si mtu mzuri kutokana na mambo fulani fulani ambayo aliyaona hayako sawa kimuonekano kwake toka pale tu alipomuona kwa mara ya kwanza pale Airport.
“Good, umeanza vizuri sana… Kesho tutapanga tuonane wapi utakapotoka huko Sheriwood Gateway Hotel”
“Sawa sawa”
“Tunaenda mbali sana kwanini? Mbona wakati naichunguza ramani ya mji huu niliona mahotel mengi tu yaliyo karibu na Airport” Akamuuliza tena huku akimtizama usoni.
“Ni kweli Agent…. Lakini usiwe na wasi wasi kuna hotel nimepanga ufikie kutokana na uchunguzi mdogo wa kuangalia usalama wako utakapofika nimegundua… Adui zetu walifaulu kudhuru ndugu zetu kutokana na wao kuwa na watu wao karibia mahotel yote makubwa yaliyopo hapa KL”
“Okay! Nilipenda leo kuwai kupumzika lakini sasa naona tumetembea kilometa 46” Akasema Kai huku akiangalia saa inayoonyesha pia hadi kilometa unazotembea ukiwa ndani ya gari au usafiri mwingine wowote.
“Pole sana … Ila tunakaribia kufika tukishazunguka junction Labehon tu basi tutakamata barabara iendayo ilipo hotel ndogo niliyopanga kukupeleka ni kilometa 5 tu toka hapa… Ni hotel nzuri na ni ya nyota moja lakini ni nzuri sana na si rahisi kwa adui kuhisi kuna mtu mgeni wa hadhi yetu yupo huko”
“Kilometa 5 ni mbali ila kwakuwa unaona ni salama kwangu ni sawa… Lakini sehemu isiyo salama ni nzuri na mbaya kwa kazi yetu”.
“Hahahahahaha…. Ni kweli kama usemavyo.. Ila tahadhari uwa ni nzuri zaidi….! Wee unafikiri ndugu zetu walipenda kukutwa na yaliyowakuta mapema?”.
“Natamani kujua kitu gani kimewapata, namkubali sana Detective Caesar North…. Naahidi kupigana kwa hadi tone langu la damu la mwisho kuwarudisha Marekani”.
“Kumchinja kobe kunahitaji taimingi” Akasema mwanadada msemo ambao ulimfanya Kai ageuke tena kwa chati kumchungulia vizuri ambapo kuna kitu alikiona kwenye kona za jicho lake la upande alipo yeye.
“Tutajua tu anachinjikaje…. Maana hakuna kilichowai kunishinda kukichinja kama kweli nahitaji kukichinja” Alichokiona kwenye pembe ya jicho la binti huyu kilimfanya atoe neno la kishujaa huku akitabasamu, na kujipa angalizo la kuongeza umakini na kutomuamini huyu dada. Kilichokuwa kinamuumiza kichwa imekuwaje mpaka awe katika sura ya Detective Marie.
“Toka umefika hapa KL, umeshafanya mawasiliano na Balozi wetu wa hapa au hata kuonana naye?”
“Ndiyo… Unahisi sijawai kuonana naye?”
“Sijahisi bali nilitaka kujua…. Maana hakuna kitu muhimu kama kufanya naye kazi katika ushirikiano wa hali ya juu sababu yeye ndiye mwenyeji wetu”
“Stop joking Agent… mi ni smart najua kila kitu katika ujasusi mi si mwanafunzi”
Ukweli wa hisia za Agent Kai zililenga kwenye usahihi, huyu mwanadada aliyefika kumpokea hakuwa Detective Marie kama Kai mwenyewe alivyoamini hapo awali mpaka alipoona ngozi mbili kwa mbali katika kingo za jicho na moja kwa moja kugundua mwanadada aliyenaye hapa ni mwanadada aliyevaa sura ya bandia. Hakutaka kuchukua haraka yoyote katika kushughulika na dada huyu, alitaka kuona nini mwisho wake. Akauacha muda uongee na akiamini kazi ikianza mapema basi uisha mapema.
Wakati anapewa taarifa kuwa anahitajika kuja Malaysia na atapokewa na mtu ambaye atatangulia kuja Malaysia, aliambiwa mwanadada huyo ni Detective Marie Johnson na ndiyeatakuwa mshirika wake kikazi na kwa sababu za kiusalama kati yao wakuu wameona atangulie dada kufika Malaysia si kama watangulizi wao walivyokuja kwa pamoja mpaka wakakutwa na ambacho kwao hawakujua ni kitu gani na ni jana tu alionyeshwa picha ya Marie na kupewa wasifu wakewa kikazi.
Agent Kai hakuwa anafahamiana na Detective Marie, hawakuwai kuonana hata mara moja iwe kwenye shule za kijasusi, mafunzo yoyote au hata kwenye maisha yao ya kawaida. Wote walikuwa wafanyakazi wa C.I.A lakini kila mmoja katika jimbo tofauti na jimbo la mwingine, Detective Marie Johnson alikuwa anatokea Central Intelligence Agency, headquarter (makao makuu) iliyopo Langley, Virginia. Wakati Agent Kai alikuwa akihudumu idara hiyo hiyo ya ujasusi lakini kama wakala katika ofisi ya Makamu wa Rais, kitengo cha kijasusi kilicho chini ya katibu wa ikulu hii ndogo anayejulikana kama Chief of Staff to the Vice Pressdent of America.
Gari aina ya Noah ilikuwa imeacha mbele gari tatu mbele hili kulifikia gari aina ya BMW new model walilokuwemo Agent Kai akiwa kwenye siti ya upande wa abiria na Detective Marie wa bandia akiwa kwenye usukani, tayari muda huu wa saa nne na dakika ishirini na tano msafara huu usiyo rasmi ulikuwa ushazunguka mzunguko wa Federal Highway. Katika gari ile aina ya Noah kulikuwa na takribani watu wanaume wenye umri unaokaribiana kuanzia miaka 35 kufika mpaka 45 kimakadirio miongoni mwao, walianza kuifautilia gari hii toka Jalan Pahang walipopanga na kukubaliana na Detective fake kusubiri.
“Huu ndiyo mtaa uliosema kuna nyumba ya wageni nitakayofikia?”. Aliuliza Agent Kai baada ya kuona Detective Marie feki akionyesha ishara ya kutaka kuingia bara bara ndogo ya mtaa.
“Ndiyo ni mbali sana kutoka kule Sepang, Sultan Abdul Aziz Airport… Tukishapita uwanja wa golf wa Nadau Golf Club Ground, kuna nyumba tutaenda kupaki gari halafu tutakatiza kwa miguu kwenda hiyo hotel ndogo”
Kweli mita hamsini Agent Kai aliuona uwanja wa kucheza mchezo wa golf mkubwa sana tu walikwenda mpaka walipopita kuna jengo la kwanza la ghorofa la ukubwa wa floor (losheni) tano wakalipita huku mwanadada akiwa kapunguza mwendo walipofika ghorofa lenye floor tatu Detective Marie fake akakunja kushoto na kuingiza gari maegeshoni.
Nywele zilimsisimka Kai na tumbo likaanza kumbana chini ya kitovu na inapomtokea hali kama hii basi ujuwamahali alipo si salama kwake.
“Hotel utakayofikia ipo mtaa huu ni kama kama guest bubu….Hapo mwanzo ilikuwa ni cassino club, serikali ikaifungia sababu kulikuwa na uhalifu wa uuzwaji wa unga kwa wingi sana eneo hili, mmiliki wake akaamua kuigeuza guest bubu na mimi nimefikia hotel kama hiyo huko nilikopanga ila kama utaona hapafai utasema lakini ni pazuri kwa usalama, hapa tutaliacha gari kisha tutaongozana kwa miguu ilipo hotel ni msafara huuhuu wa nyumba” Akasema huku akimuonyesha kwa mikono katika kumuelekeza Agent hili aelewe.
Gari ilikuwa imepaki kwenye maegesho yenye jengo la ghorofa tatu, ikiwa floor (losheni) ya kwanza ikiwa na lango pana juu yake kukiwa na bango lililoandikwa YOUTH MUSCLE’S & BOXING TRAINING.
“Nafikiri ni vizuri wewe ukaishia hapa na kuniacha mimi niende mwenyewe halafu asubuhi tutawasiliana kwa simu kupanga tukutane eneo gani…!
Detective Marie fake hakujibu kitu alimuangalia tu kisha akajifungua mkanda wa siti aliokuwa kajifunga akafungua mlango wa upande wake na kushuka toka ndani ya gari. Ikabidi Agent Kai anyanyue begi lake aliloliweka siti ya nyuma kisha akanyanyua na briefcase yake ambayo ilikuwa pembeni ya siti aliyokaa, kiupole akafungua mlango wa gari.
Eneo hili lilikuwa tulivu kabisa usiku huu, kukiwa na mwanga hafifu wa taa chache zilizokuwa kwenye majengo yaliyoachana umbali mkubwa tu na hata ukizingatia eneo kubwa lilichukuliwa na uwepo wa uwanja wa kuchezea golf.
Miguu yake ilipokanyaga tu chini ikatokea gari aina ya Noah rangi nyeusi kisha ikafunga breki nyuma milango yote minne ya gari ile aina ya Noah ikafunguka kwa fujo na kwa haraka ya aliposimama Agent Kai. Papo hapo Agent Kai alistuka na kubaki anababaika hajui afanyaje, wakashuka watu wapatao wanne kutoka kila mlango kisha wakamalizia wawili na kutimiza idadi ya wanaume sita. Haraka Kai akageuza macho yake upande wa pili wa gari alipo aliyekwisha mstukia kuwa siyo Detective Marie lakini akili yake ikataka kuona mwisho wake utakuwaje.
Miguu yake ilipokanyaga tu chini ikatokea gari aina ya Noah rangi nyeusi kisha ikafunga breki nyuma ya gari yao, milango yote minne ya gari ile aina ya Noah ikafunguka kwa fujo na kwa haraka ya aliposimama Agent Kai. Papo hapo Agent Kai alistuka na kubaki anababaika hajui afanyaje, wakashuka watu wapatao wanne kutoka kila mlango kisha wakamalizia wawili na kutimiza idadi ya wanaume sita. Haraka Kai akageuza macho yake upande wa pili wa gari alipo aliyekwisha mstukia kuwa siyo Detective Marie lakini akili yake ikataka kuona mwisho wake utakuwaje.
Yaah! Hakuwa mbali na alichowaza macho yake yalikutana na mdomo wa bastola ndogo aina ya Kahr ARMS zao la ujerumani ikimtizama usoni ikiwa imeshikwa thabiti kwa mkono wa kulia toka wa mwanadada aliyempokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur International Airport (KLIA) au kama unavyofahamika kwa jina lingine Sultan Abdul Aziz Airport. Uso wa Agent ukasawajika na si kama alikuwa haamini la hashaah! Katika pilika pilika zake kukutwa na jambo kama hili kwake uwa ni moja ya kazi zake,ila mapokeo ya kilichojiri yaliusononesha moyo wake kwa ubongo wake ulio makini katika kazi kutolitilia maanani jambo ambalo alilihis, mdomo hukakosa la kusema.
Akataka kuwa mpole lakini akili yake ilikataa kwa haraka mkono wake ukaenda nyuma ya kiuno chake sehemu ya kwanza na nyepesi anapohifadhi bastola yake ndogo aina ya Glock 42 zao la Marekani tena akipelekwa kama na hisia tu zilizotokana na kutoamini kama kaingia mikononi mwa adui kijinga vile, akaishia kuishika tu kitako chake tena bila hata kuinua fulana yake aina ya jezi aliyovaa.
“Usijaribu chochote mpenzi wangu mweusi,hii isikushangaze sana sababu hata wenzako tuliwapata kirahisi kama wewe tulivyokupata kirahisi…. CIA na wamarekani kwa ujumla kwa sasa ujanja hamna na kwa tulivyojipanga hamna uwezo wa kudhidi ujanja tulionao, inastaajabisha sana kama utakuwa kwenye mshangao huo ulionao” Detective Marie fake akamuonya huku akitabasamu tabasamu ambalo lilijaa unafiki,jeuri iliyojisiliba na kiburi.
Agent Kai akiwa bado anatizamana na huyu mwanadada aliyemzidi kete, mara hisia zikamjia kuwa nyuma yake kuna mtu akataka kugeuka kasi, Paaaah! Ukasikika mlio. Kitu alichokuwa anakijua ni nini kutokana na uzoefu wake wa kazi hii kilitua kwenye kisogo chake papo hapo macho yake yakakumbwa na giza akashindwa kujizuia mkono wake wa kulia ulioshika briefcase lake ukaliachia akadondoka kama gunia la dagaa huku fahamu ikimtoka. Akazimia!
Mwisho wa sehemu ya pili (02)
……NDIYO KUMEKUCHA KUALA LUMPUR….
JOGOO AMEWIKA KABLA YA SIKU MPYA…..!
JE NI KINA NANI WALIO MUWAI AGENT KAI KABLA HATA HAJAOGA MAJI YA KUALA LUMPUR?
NINI KITAMTOKEA AGENT KAI KATIKA SEHEMU INAYOFUATA?
JE NAYE ATAINGIA KATIKA HALI YA UTEKWAJI?
KINA NANI WANAOFANYA HALI HII YA UTEKAJI KATIKA JIJI HILI LA KUALA LUMPUR?
KWANINI WANAWATEKA WAMAREKANI?
…..YOTE HAYA YANA MAJIBU KATIKA SEHEMU ZINAZOFUA ZA RIWAYA YETU HII TAMU INAYOSHANGAZA YENYE MATUKIO YA MSHANGAO…!
Miguu yake ilipokanyaga tu chini ikatokea gari aina ya Noah rangi nyeusi kisha ikafunga breki nyuma ya gari yao, milango yote minne ya gari ile aina ya Noah ikafunguka kwa fujo na kwa haraka ya aliposimama Agent Kai. Papo hapo Agent Kai alistuka na kubaki anababaika hajui afanyaje, wakashuka watu wapatao wanne kutoka kila mlango kisha wakamalizia wawili na kutimiza idadi ya wanaume sita. Haraka Kai akageuza macho yake upande wa pili wa gari alipo aliyekwisha mstukia kuwa siyo Detective Marie lakini akili yake ikataka kuona mwisho wake utakuwaje.
Yaah! Hakuwa mbali na alichowaza macho yake yalikutana na mdomo wa bastola ndogo aina ya Kahr ARMS zao la ujerumani ikimtizama usoni ikiwa imeshikwa thabiti kwa mkono wa kulia toka wa mwanadada aliyempokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur International Airport (KLIA) au kama unavyofahamika kwa jina lingine Sultan Abdul Aziz Airport.
Uso wa Agent ukasawajika na si kama alikuwa haamini la hashaah! Katika pilika pilika zake kukutwa na jambo kama hili kwake uwa ni moja ya kazi zake,ila mapokeo ya kilichojiri yaliusononesha moyo wake kwa ubongo wake ulio makini katika kazi kutolitilia maanani jambo ambalo alilihis, mdomo hukakosa la kusema.
Akataka kuwa mpole lakini akili yake ilikataa kwa haraka mkono wake ukaenda nyuma ya kiuno chake sehemu ya kwanza na nyepesi anapohifadhi bastola yake ndogo aina ya Glock 42 zao la Marekani tena akipelekwa kama na hisia tu zilizotokana na kutoamini kama kaingia mikononi mwa adui kijinga vile, akaishia kuishika tu kitako chake tena bila hata kuinua fulana yake aina ya jezi aliyovaa.
“Usijaribu chochote mpenzi wangu mweusi,hii isikushangaze sana sababu hata wenzako tuliwapata kirahisi kama wewe tulivyokupata kirahisi…. CIA na wamarekani kwa ujumla kwa sasa ujanja hamna na kwa tulivyojipanga hamna uwezo wa kudhidi ujanja tulionao, inastaajabisha sana kama utakuwa kwenye mshangao huo ulionao” Detective Marie fake akamuonya huku akitabasamu tabasamu ambalo lilijaa unafiki,jeuri iliyojisiliba na kiburi.
Agent Kai akiwa bado anatizamana na huyu mwanadada aliyemzidi kete, mara hisia zikamjia kuwa nyuma yake kuna mtu akataka kugeuka kasi, Paaaah! Ukasikika mlio. Kitu alichokuwa anakijua ni nini kutokana na uzoefu wake wa kazi hii kilitua kwenye kisogo chake papo hapo macho yake yakakumbwa na giza akashindwa kujizuia mkono wake wa kulia ulioshika briefcase lake ukaliachia akadondoka kama gunia la dagaa huku fahamu ikimtoka. Akazimia!
Endelea……………..!
Mwanadada aliyekwenda kumpokea Agent Kai akiwa kavaa sura ya bandia ya Detective Marie kwa jina alifahamika kama Damia Abdulrahman akiwa na a.k.a yake ya Language girl kutokana na kuwa anajua lugha nyingi tena akiongea kwa ufasaha na kuiga mpaka lafudhi husika kwa waongeaji wa lugha kutegemea na nchi husika mfano akiongea kiingereza cha watu wa Jamaica basi ataongea utadhani ni mjamaica wa kuzaliwa katika nchi ya Jamaica na kama ataongea kiingereza cha mtu anayetokea Marekani basi unaweza ukasema huyu binti wa Kimarekani na anajua wastaarabu wanavyoongea na hata wale wa gheto, hivyo hivyo anapoongea kilatin cha mtu wa Mexico au Spain lazima atatembea nacho katika uhalisia husika wa anayezungumza naye anahitaji kuzungumza na mtu wa wapi. Kwa watu wake wa karibu wanaomjua kama yeye ni nani, walikuwa wakimuita hivyo.
Alikuwa mdada shupavu na machachari na janja janja sana akiwa na lugha tisa kichwani mwake akiongea ki-bahasa melayu baku lugha ya wenyeji wa Malaysia ilipo asili yake na ni nchi yake anayoishi, alikuwa akiongea kilatin alichojifunza Hispania akikikoleza alipokuwa nchini Mexico akitumika kama mkalimani wa muuza unga mmoja maarufu sana nchini Mexico aliyekuwa na tawi Mexico, Peru na Colombia. Alikuwa akiongea na kuandika vizuri Kireno akiwa kajifunza Brazil akiwa katika harakati zake za kiutafutaji.
Alikuwa akijua kijerumani, kifaransa, kiarabu, kiingereza tena akijua kuiga lafudhi iwe ya negros wa Marekani, kile cha kijamaica, hadi lafudhi ya mwingereza mwenyewe,na kirusi. Kifupi alikuwa ni kinyonga wa lugha mwenye uwezo mzuri sana wa kuhadaa mtu na akahadaika.
Ameshafanya kazi na kikundi cha Al Qaeda, Dola la kiislam au kama wajulikanavyo kama Islamic State (IS), kashatumikia Al Shababy na hadi vikundi vidogo kama vya wauza unga wa Mexico, Brazil na hata baadhi ya nchi za bara la ulaya kote huko akiwa kama mkalimani.
Mafunzo ya kigaidi alikuwa kayapata Sudan kwa kuanzia kasha akamalizia Afghanistan ni mwanadada mwenye umri wa miaka 45 lakini laiti ungemuona ungeweza dhani ni binti wa miaka 30, alikuwa anaweza kujitunza pia alikuwa amebahatika kupata mtoto mmoja wa kike ambaye umri wake ulikuwa ni wa miaka mitano anayempenda sana katika muda wote huo ambao kwa wasichana wengine wa umri ungeweza wakuta wana watoto wawili au watatu kama si zaidi.
Katika Malaysia alikuwa chini ya aliyeratibu mipango yote ya utekaji wa Maprofesa wa sayansi. (Tutamjua mbele) Ni muda mrefu yupo chini ya huyu mtu aliyemuomba waunde kikundi chao baada ya wote kuona ni wakati wao wa kushughulika na mambo yao huku yeye Damia akiacha kabisa mambo ya kigaidi.
Leo hii tumeona alivyotumika kumuhadaa Agent Kai komando na jasusi ambaye inasemekana kwa USA yeye ndiye jasusi mjanja kuliko majasusi wote na Jasusi namba moja kwa ubora pale wanapopangwa majasusi wa C.I.A na hata mashirika mengine ya kimarekani, akiwa anafahamika mpaka kwa Maraisi wote ambao wameitumikia Marekani ambao ni wastaafu na kila mmoja akimtamani amfanye Agent Kai kama mlinzi wake binafsi huku akimlipa binafsi
Muda wote wakiwa katika gari aina ya BMW waliyokuwemo Damia na Agent Kai, mwanadada Damia alikuwa akipanga mipango yake bara bara na asilimia za kutosha alifanikiwa, kwani aliwatumia meseji washirika wake wakakutana katika mataa mojawapo ya junction (mzunguko) mmoja kati ya mizunguko mingi iliyo katika bara bara ya Jalan Tun Razak, Damia aliwaona sababu alikuwa akilijua gari walilokuwemo licha ya kuwa gari yao haina ya Noah ilikuwa na vioo vya madirisha ya mlangoni na hata cha nyuma na nailoni nzito nyeusi kama inavyojulikana kama tinted (vioo vya tinted).
Kai hakuweza kuzing’amua hila zile za nje ya gari kutoka gari iliyokuwa inawafuatilia ingawa alishagundua hila za sura ya bandia ya Damia kuwa si Detective Marie, subira ni muhimu alitaka subira hili ajue ipi nia ya huyu dada, alitaka subira hili imfikishe kwenye kujua Detective Marie yuko wapi? lakini ndiyo hasa iliyomponza kwa kipindi hiki.
Six Dangerous Boys (SDB) walikuwa ni vijana sita miaka 15 iliyopita lakini sasa ni watu wazima si vijana tena, lakini jina lao halikufa mpaka sasa licha ya wote rika lao kusogea kutoka ujana hadi utu uzima (miaka 35 kwenda juu). Bado walifahamika kuwa wao ni Six Dangerous Boys.
Walianza kama vijana walioamua kuunda gym yao ya kimtaa wakiwa na nia ya kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma au kama inavyofahamika kwa watu wengine kuwa watunisha misuli. Walijikusanya kwa mara moja wote sita sababu walikuwa marafiki wakubwa sana tokea wakiwa shule moja ya sekondari iitwayo SMK Hulu Kelang wakiwa na nia ya kujifua wawe wapiganaji wa ubondia, walipoma;iza sekondari nguvu zote wakazielekeza katika ngumi, nia yao ilikuwa thabiti, bidii ikawa ya kweli.
Ndoto zilianza kuwa kweli kwani katika kikosi chao cha watu sita walijitokeza mabondia watatu waliotikisa sana Malaysia na bara Asia wakichukua mikanda ya ngumi ya kitaifa ya ndani ya nchi yao na ya kimataifa ya katika bara lao Asia wakitawala kila mmoja kwenye uzito wake.
Mafanikio yao yaliwapelekea kujulikana sana katika viunga vya jiji la Kuala Lumpur na hata mikoa ya jirani. Walikutana na huyo waliyekuwa wanalalamika kwa Damia kuwa ni boss lakini anawatenga miaka mitano iliyopita, kukutana kwao kulianza kama utani Fulani, kwani boss alijisogeza na kuanza kuwa nao karibu na vijana awa akijifanya kama amevutiwa nao na anahitaji kuwa mfadhili wao lakini akiwa na lake la moyoni.
Akichagizwa na pesa alizokuwa nazo ingawa si pesa nyingi za kutisha miongoni mwa matajiri wakubwa kabisa katika Malaysia, pesa za kuwa na jina kubwa sana katika Malaysia lakini alikuwa na pesa za kumfanya aweze kufanya jambo lolote kubwa la pesa linaloweza kumshinda mtu wa middle class (mwenye maisha ya kati) na hata baadhi ya matajiri.
Aliweza kuwa nao kiufadhili kisha akawaingiza katika mambo ya kuwatumia katika kupora baadhi ya vitu kama pesa na aina zingine za mali kwa matajiri wenzake ambao alikuwa nao katika dili mbalimbali kisha kutaka kudhulumiana, basi vijana awa walimsaidia na kumrahisishia Mr. Logan Puteri na kufukia nyayo kwa kutojulikana kama ndiyo yeye.
Mr. Logan Puteri mtu wa makamo mwenye umri wa miaka 58 alikuwa ni mwanaume wa shoka mjanja mjanja sana ambaye mambo mengi anayoyafanya tokea akiwa kijana mdogo kabisa baada ya kumaliza chuo cha Kuala Lumpur Unniverisity of Technology na kupata shahada yake ya mambo ya IT yalikuwa ni kuchora michongo ya kuiba pesa kwa njia za kimtandao na utapeli mbali mbali, ilikuwa bahati kubwa kwake hakuna hata mara moja katika maisha yake aliwai kukamatwa na vyombo vya dola vya Malaysia kama muhalifu.
Alikuwa ni mwepesi wa kutegua mitego hili asiingie katika mikono ya sheria, hiki kikundi cha SDB huyu bwana Logan Puteri alikuwa halitilii uzito mkubwa sababu alikifanya kama ngazi kwa yale anayoyahitaji akiamini kutokuweka karibu na yeye basi anakuwa salama kwa watu wengine wanaomuheshimu sana pamoja na serikali.
Mr. Logan Puteri alikuwa na kampuni yake yenye kukusanya makampuni mbalimbali ikiwemo kampuni za kandarasi mbili moja ya kujenga majumba na ingine ya kujenga mabarabara ambazo hazikuwa maarufu sana miongoni mwa makampuni makubwa ya ukandarasi ya Malaysia, muunganiko wa kampuni zake ndogondogo ambazo pia alikuwa na maduka makubwa shopping mall, pamoja na maduka ya kuuza simu na kompyuta za aina zote eneo la kibiashara liitwalo Putrajaya, eneo maarufu sana kwa maduka makubwa makubwa na ma-super market katika jiji la Kuala Lumpur, alimiliki na vituo vya mafuta (petrol station) katika mikoa ya jirani. Kwa ujumla kampuni zake hizo kibiashara zilijulikana kama Puter Group of Business (PGB)
Hakuwa anawatilia maanani sana vijana wa SDB licha ya kuwa walimfanyia kazi vizuri tu kwasababu aliamini walikuwa hawana ujuzi na masuala ya kihalifu hasa wa kimataifa ambako siku zote ndoto za Mr. Logan Puteri ilikuwa ni kujitanua na hata kupewa mashirikiano na vikundi vya kimtandao vya kigaidi, akiamini siku moja ataichukua serikali ya nchi ya Malaysia ikawa chini yake kidola kiuongozi akiwa waziri mkuu.
Hakuwa amejiingiza kwenye siasa kwa muda huu lakini hakupenda kujulikana kama mchafu na hata watu wanaomzunguka kuwa ni wahalifu hili atakapoingia kwenye siasa basi asaidiwe na kikundi atakachokimiliki na pia kupewa kampani na marafiki wengine aliojenga nao urafiki ambao kikweli hakuna aliyekuwa anajua siri kubwa aliyonayo mtu huyu.
SDB walikuwa wanajua jinsi bwana huyu anavyowathamini wale wanaomzunguka kwa karibu ambao siku zote Mr Puter hakupenda ijulikane kama watu waliomzunguka ni watu wa aina gani. Kampuni yake Puter Group of business kama ilivyojulikana kwenye mamlaka za serikali ya Malaysia ilikuwa ni kampuni kubwa lakini upande wa pili wa shilingi ilikuwa ni kampuni iliyoajiri watu wote wa ngazi za juu kama wahalifu.
Akianza mwenyekiti wa makampuni Mr Logan Puter, mwenyekiti msaidizi Mrs Zahra Logan mke wa Mr Puter Logan mwanamama mwenye asili ya Iran ambaye yeye ndiye pekee aliyekuwa hajui masuala nyeti yanayoendelea katika ofisi zaidi ya kuwa ndiyo mtu aliyekuwa anasimama kidete kuinua biashara za kampuni yao na hata kuajiri watu muhimu katika kiwanda na biashara zao. Kila mtu aliyeletwa na Mr Puter mwenyewe alikuwa ni mtu wa kazi lakni aliyeletwa na mwanamama huyu alikuwa mtu safi aliyepitia vigezo vya halali kuajiriwa, mwanamama huyu alikuwa ni msomi mwenye masters ya business, nyadhifa muhimu za kampuni zilikuwa zikifanyiwa uajiri na Mr Logan mwenyewe hivyo alitumia fursa hiyo kuweka watu aliotaka yeye kwa manufaa ya kazi zake za kihalifu katika utafutaji.
Mhasibu wa kampuni alikuwa ni Mr Nawaz Patrash huyu bwana alikuwa na shahada ya uhasibu ni Mpakistani aliyepitia mafunzo ya kigaidi katika kikundi cha kigaidi cha Al Qaeda baada ya kuwa kamaliza chuo tu na rafiki mmoja mmoja mtaleban kumshawishi kuingia katika kikundi icho cha kigaidi alikaa humo akipita katika kazi nyingi za hatari kutokana na kuaminiwa na viongozi wa juu, alifanikisha baadhi ya operesheni nzito ndani ya Pakistani na nje ya Pakistani kama India na nchi nyingine za jirani. Aliamua kuacha au kukaa pembeni na kikundi hiki pale operesheni ya makomando wa US Navy Seals wa Marekani ilipofanikiwa kuwasamabaratisha yeye na rafiki zake na yeye kunusurika kifo kwa kupigwa risasi iliyomchana vibaya pembeni kidogo ya moyo, alilazwa miezi sita bila kujitambua mpaka alipokuja kupona na baadhi ya ndugu zake kumshauri aachane na mambo ya kigaidi. Ndipo akachukua maamuzi magumu ya kujiondoa Al Qaeda akahama nchi na kuja nchi hii ya Malaysia ambapo alipokuwa anatafuta kazi akakutana na mtu ambaye naye alishakuwa mfuasi wa Al Qaeda akampeleka kwa Mr Logan Puter ambapo ilikuwa furaha kwake kumpata mtu aliyepitia kashikashi za kigaidi kwa kiwango kile. Katika kikundi hiki cha siri Mr Nawaz Patrash alikuwa ndiyo mtu muaminiwa sana kiasi cha kuwa kiongozi wa kikundi hiki kisichokuwa na jina rasmi.
Mtu wa pili katika kikundi hiki ambaye alikuwa ni mtu nyeti wa mambo nyeti ni Ghulam Qaresh mwanajeshi aliyefika levo ya ukomando nchini India, tamaa zilimuondoa katika jeshi la India na kuanza kujihusisha na mambo ya kijambazi mpaka alipokuwa anatafutwa na jeshi la polisi akaamua kukimbilia nchi ya Malaysia alipoendelea kufanya uhalifu wake binafsi mpaka alipokutana na Mr. Logan Puter na kuingia naye makubaliano ya kazi kazi huku akimuweka katika wadhifa wa mhasibu msaidizi wa kampuni ya Puter Group of Industries and Business, ikiwa alibebwa na shahada yake ya biashara aliyoipata hukohuko India.
Mtu wa tatu alikuwa akiitwa Sauez Mallamu akitokea Singapore pia ni mtu aliyepitia katika jeshi la Singapore, hapa aliwekwa kwenye kivuli cha meneja masoko wa kampuni.
Alikuwepo Putram Ramji naye ni msingapore kanali mstaafu wa jeshi la Singapore hapa katika kampuni alikuwa ni meneja mkuu wa kampuni.
Kulikuwa na wasyria wawili ambao walikimbia vita nchini Syria wakiwa kutoka idara ya kijasusi ya Syria ila walifanya kosa kwa kumsaliti Rais wa Syria bwana Bashar Al-Assad, ndipo wakakimbilia nchini Malaysia ambapo waziri mmoja wa zamani wa Malaysia wa mambo ya ulinzi aliwapokea kisha akawapeleka kwa Mr. Logan Puter, mmoja aliitwa Ally Kareem na mwingine Hassan Saddiq a.k.a Technical Man aliitwa hivyo kwakuwa alikuwa ni fundi mipango wa kundi kutoka bwana Logan Puter kwa mipango basi huyu ndiye alifuata.
Mtu wa sita alikuwa ni Mr. Gary Yong ni mmalaysia huyu naye aliwai fanya kazi idara ya ujasusi ya Malaysia kitengo cha ofisi ya Waziri mkuu iitwayo Research Division of the Prime Minister’s (RDPMD) kwa kipindi kirefu mpaka alipoingia waziri mkuu wa sasa aliyeamuaa kuondoa kikosi karibu chote kisha kuweka chake cha watu wake aliokuwa ana imani nao, hivyo Mr. Gary Yong akarudishwa ofisi kuu ya kikosi cha kijasusi cha Malaysia kiitwacho Defence Staff Intelligence Division (DSID) ambapo napo hakudumu sana akaacha kazi akisingizia umri kumbe alikuwa kashawishiwa na Mr Logan Puter pamoja na waziri wa ulinzi wa serikali iliyopita kabla hajaingia waziri mkuu wa sasa ambapo alimuacha nje ya serikali yake. Katika kikosi hiki cha siri yeye ndiyo huweka mipango yote sawa ya kiulinzi kutoka serikalini akiwatumia watu wake waliopo idara mbali mbali za ulinzi.
Mtu wa saba katika group hili alikuwa ni mchina lakini mwenye uraia wa Malaysia anayeitwa Zhing Lae huyu alikuwa ni daktari na mtaalamu wa plastic surgery mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza sura bandia za kuvaa au hata zile za kioperesheni kwa mtu aliyehitaji kujibadili sura, vikundi vya kigaidi vilimtumia sana bwana huyu ambaye alikuwa na Clinic yake iitwayo Lae Clinic, Mr. Puter alimshawishi daktari huyu akawa anamsaidia baadhi ya kazi zake pia akawa amemuajiri kama daktari mkuu katika kiwanda chake vifaa vya mashuleni na daktari mkuu wa kampuni zake zote kwa muunganiko.
Mtu wa nane alikuwa naye ni mtu mwenye asili ya China mtaalamu wa mapigano ya Taekwondo aitwaye Mosin Lee a.k.a Master of Taekwondo alikuja kuingia katika himaya ya Mr Logan akiwa kama mtu aliyekuwa anamfundisha mapigano binafsi.
Wa tisa alikuwa ni mjapani aliyekuwa akiitwa Makazi Takasho a.k.a Computer Man akiitwa hivyo sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuitumia kompyuta kwa kazi mbali mbali hasa zile zinazohusu ujasusi wa kimtandao (CCHS), kwenye kampuni ya kibiashara aliajiriwa kama ndiyo mkuu wa kitengo cha kompyuta.
Na wa mwisho ambaye alifunga kazi kati ya watu ambao inasemekana bwana Logan Puter alikuwa anawapendelea zaidi kwa mujibu wa vijana SDB, alikuwa akiitwa Johome Meloo ni mtu mweusi pekee katika kikundi hiki cha siri sifa kuu ya bwana huyu ambaye ni mmalaysia mwenye asili ya kutoka Afrika ile ya kusini ilikuwa ni uwezo wake wa kutumia silaha na hata mapigano ya ana kwa ana kwenye kampuni ya kibiashara aliajiriwa kama afisa muajiri mkuu katika kiwanda. Pia walikuwepo na wengine ambao tutawaona mbele kwa hapa tuishie hapa juu ya watu hawa walio top ya juu kwa Mr. Logan Puteri.
***** ***** *****
“Daktari amesemaje?” Aliuliza mmoja wa vijana waliomteka Agent Kai ambaye ndiye aliyempiga na kitako cha bunduki fupi aina KAR Shot Gun na pia ndiye alikuwa kiongozi wa kikundi cha watu sita kilichokuwa kinamfuatilia dada Damia aliyeongoza utekaji.
“Daktari anasema kwa ulivyompiga, umempiga pigo kubwa sana, ungeweza hata kumuua kama angekuwa si mtu strong… Tungeweza kulazimisha kumzindua lakini boss hayupo nchini na harudi leo hatuna haraka ya kumzindua, hivyo Dokta amemchoma sindano itakayomsaidia kumpunguzia maumivu ya kichwa taratibu na anaamini atazinduka baada ya masaa 12…! So kimahesabu saivi ni saa sita kasoro hivyo mpaka kesho saa sita mchana atakuwa kazinduka na muda huo boss atakuwa hajarudi toka Korea Kaskazini” Akajibu Damia a.k.a Language girl, binti aliyefanikiwa kumfanyia ghiliba Agent Kai kuwa yeye ni Detective Marie, aliongea huku akisogea kwenye meza iliyokuwa na begi lake kisha akalinyanyua katika ishara ya kuwa anahitaji kuondoka kwenda sehemu.
Muda huo walikuwa katika sebule kubwa iliyo katika ghorofa lenye floor tatu floor ya juu kabisa kati ya floor (losheni)tatu alizoziona Agent Kai na floor ya kwanza akaweza kulisoma bango kubwa lililoandikwa YOUTH MUSCLE’S & BOXING TRAINING.
“Anarudi saa ngapi boss wako?” Akauliza yule kiongozi jitu la miraba minne, kwenye masofa mengine yaliyopo pale walikuwa vijana wengine wamegawana kukaa na kusababisha kuwa kama wamezunguka sebule yote sababu bila kujali ukubwa wa sofa kila sofa moja alikaa mtu mmoja.
“Boss wangu ni boss wenu, kwanini hauheshimu kwa kumuita boss tu kama navyomuita mimi?.. Mara nyingi nakuona wewe Nabeel na hata wenzio hampendi kujihesabu kuwa mpo chini ya Mr. Logan …. Lakini mnaishi kwa ajili ya ujira wake pia mnafanya kazi zake tena kwa ufasaha bila kinyongo, siku zote atabaki kuwa boss wenu tu bila kujali hata kama anaonana na nyie mara moja moja sana kwa mwezi” Akasema Damia huku akionyesha dhahiri kutofurahishwa na aliyemuita Nabeel, alishakuwa kashaivua hata sura yake ya bandia iliyokuwa inamuonyesha yeye ni Detective Marie na kurudi katika sura yake ya Damia. Wanaume wote walikuwa kimya wakimsikiliza anavyoongea huku akisimama pale pale kwenye meza uso kaukunja kwa hasira kuonyesha hapendi dharau iliyoonyeshwa na Nabeel.
“Usije ukarudia tena dharau zako Nabeel… Bado hujamjua Mr. Logan vizuri, ni mtu asiyependa masikhara kabisa na anayependa heshima na sifa nyingi sana kwake.” Akasema Damia.
“Tatizo mnatutenga sana …. Tunawafanyia kazi zenu kwa faida yenu tena katika ufanisi wa hali ya juu, tumekuwa wa siri wenu kwa manufaa yenu na ninaamini mnaingiza pesa nyingi kupitia sisi. Sikia tunaomba atakapofika safari hii hatutajali ametufadhili vitu vya aina gani na anatulipa pesa ya aina gani, huyu mtu tuliyempata leo hata kama yeye kafanikisha kwa kiasi gani katika mipango hatutamtoa mpaka hatuakikishie malipo yetu kwanza ya wale makachero wawili anayatoa lini au atulipe kabisa ndiyo huyu Agent wa CIA atatoka kwenye jengo hili…! Akasema mmoja ambaye alikuwa na mwili mkubwa sana kuliko wengine wote waliopo pale ingawa wanaume wale wote walikuwa wamepiga mazoezi na yakawa yamewakubali kweli ila huyu alitisha shingo kubwa iliyojaa kuanzia kwenye maungio ya taya zake ikishuka hadi kwenye maungio ya bega na shingo kifua kilijaa kweli ukija kwenye mikono alitengeneza kuanzia try ceps, for arms alikata na kujaa kweli kweli na hata miguu squat ilikubali vigimbi na misuli ya kutosha kuzunguka miguu, miaka mitatu mifululizo iliyopita alishinda mashindano ya Mtunisha misuli bora wa jiji la Kuala Lumpur na pia miaka miwili iliyopita alishinda taji la Mr. Malaysia kwa jina alijulikana kama Jeong Low a.k.a Mr. Malaysia.
“Kwahiyo mmekaa na kupanga mnachokiongea kwangu? Mnanituma nifikishe ujumbe wenu au mnatakaje?”
“Ndiyo tulikaa na kuongea kuhusu hili suala, hujui sisi ndiyo tulishiriki kuwateka wale wanasayansi maprofesa na hata wale makachero na hadi huyu Agent Kai, hivi wewe Damia huoni kama sisi tuko hatarini zaidi kwa tunayofanya lakini sisi hatuthaminiwi kama wanavyothaminiwa wale wanaomlinda boss, amewaajiri katika ofisi yake na vyeo wamepewa… Mwingine unayefaidika ni wewe …. Nyinyi nyote ndiyo mpo karibu na boss na mnathaminiwa na kupewa kila kitu na Mr. Logan… Kinachouma akishachukua watu wake hatushirikishwi tena, SDB habari yetu inaishia hapo, hatujui hata wapi walipo na hata kati yetu hakuna anayejua anapoishi boss Mr. Logan” Akasema tena kujibu Mr. Malaysia.
“Sawa kama mnanituma kufikisha ujumbe, usiku huu kama nitaongea naye nitamwambia kabla hajamchukua huyu jamaa wa leo mna maongezi naye”.
“Ahsante kwa kutuelewa …. Tumechoka na sisi ni watu” Akakazia Mr Nabeel, kisha wanaume wote wakacheka kwa nguvu huku Damia Language girl akatabasamu tu.
“Sasa muwe makini na huyu mtu ….kamtoeni kule chumba cha matibabu mpelekeni chumba cha kuhifadhi mateka akizinduka ajikute kule, watu kama yeye uwa hawaeleweki hata kama yupo kwenye kuzirai si wa kumuamini”. Akatoa maelekezo Damia baada ya kutizama saa ya mkononi mwake.
“Sawa… Ila wewe umechukua nini na nini katika vitu vyake?” Akasema na kuuliza Nabeel.
“Nimechukua vitu ambavyo uwa naelekezwa na boss wetu nivichukue…. Laptop, simu na saa yake, hivi ndiyo vitu vya kazi vya awa CIA na FBI….. Kesho namkabidhi boss uwa wanavifanyia uchunguzi yeye na watu wake” Akajibu Damia huku tayari akikaribia mlango wa kutokea pale sebuleni kuelekea nje. Kisha akasema tena.
“Nawatakia usiku mwema , tutaonana muda nitakaokuja na Mr. Logan Puter.
Hakuna aliyejibu walimuangalia tu, yeye akafungua mlango na kuondoka akiwaacha wale majibaba mbavu pale sebuleni ambapo wawili waliinuka na kuelekea chumba cha matibabu wakamnyanyua Agent Kai aliyekuwa bado katika hali kutokuwa na fahamu kutokana na pigo la kichogo alilopigwa, wakamnyanyua na kumbeba kuelekea naye chumba kingine kilichosemekana ni chumba cha kuhifadhi mateka.
Mwisho wa sehemu ya tatu (03)
Utamu unadhidi kukolea, majibaba yamefanikiwa kumdhibiti jasusi Agent Kai..
Nini kitakachojiri, naomba nisikumalizie uhondo stay cool andaa macho na akili kupokea kinachokuja katika ubora wa hali ya juu.
SDB watamkabidhi Agent Kai kwa boss wao?
Jibu litapatikana sehemu inayokuja kwa utamu zaidi.
“Sawa kama mnanituma kufikisha ujumbe, usiku huu kama nitaongea naye nitamwambia kabla hajamchukua huyu jamaa wa leo mna maongezi naye”.
“Ahsante kwa kutuelewa …. Tumechoka na sisi ni watu” Akakazia Mr Nabeel, kisha wanaume wote wakacheka kwa nguvu huku Damia Language girl akatabasamu tu.
“Sasa muwe makini na huyu mtu ….kamtoeni kule chumba cha matibabu mpelekeni chumba cha kuhifadhi mateka akizinduka ajikute kule, watu kama yeye uwa hawaeleweki hata kama yupo kwenye kuzirai si wa kumuamini”. Akatoa maelekezo Damia baada ya kutizama saa ya mkononi mwake.
“Sawa… Ila wewe umechukua nini na nini katika vitu vyake?” Akasema na kuuliza Nabeel.
“Nimechukua vitu ambavyo uwa naelekezwa na boss wetu nivichukue…. Laptop, simu na saa yake, hivi ndiyo vitu vya kazi vya awa CIA na FBI….. Kesho namkabidhi boss uwa wanavifanyia uchunguzi yeye na watu wake” Akajibu Damia huku tayari akikaribia mlango wa kutokea pale sebuleni kuelekea nje. Kisha akasema tena.
“Nawatakia usiku mwema , tutaonana muda nitakaokuja na Mr. Logan Puter.
Hakuna aliyejibu walimuangalia tu, yeye akafungua mlango na kuondoka akiwaacha wale majibaba mbavu pale sebuleni ambapo wawili waliinuka na kuelekea chumba cha matibabu wakamnyanyua Agent Kai aliyekuwa bado katika hali kutokuwa na fahamu kutokana na pigo la kichogo alilopigwa, wakamnyanyua na kumbeba kuelekea naye chumba kingine kilichosemekana ni chumba cha kuhifadhi mateka.
ENDELEA NA SEHEMU YA NNE…!
“Tumfunge katika kiti au tumuache sakafuni tu?” Mmoja akamuuliza mwenzake.
“Tumfunge kamba ya katani vizuri…. Maana pingu zote ziliisha walivyowachukua wale makachero… Tumfunge kwenye kiti akizinduka ajikute kama kakalia kiti cha ofisini kumbe yupo nusu jehanamu..hahahha ! ndiyo kunamtosha”. Akajibu mwingine, wakacheka kwa sauti na kugogenja viganja vyao kwa furaha kisha wote wakasaidiana kumnyosha vizuri Agent Kai na wakamuinua na kumkalisha kwenye kiti cha chuma chenye muegemeo kisha wakamfunga kwa kamba ya katani miguuni wakimuweka sambamba na miguu ya kiti ya mbele na mikono wakaiweka kwa nyuma nayo wakaifunga kisha kamba ingine wakaizungusha mwilini mwake na kiti kwa kila mguu wa kiti na mguu wa Agent Kai kama mizunguko mitano.
“Mtu tumeambiwa hawezi kuzinduka hadi baada ya masaa kumi lakini tunamfunga hivi tunajipa kazi zingine bila sababu ya msingi kwa kweli, halafu chumba hiki tunamfungia kwa nje tena milango miwili…” Akasema mwingine ambaye aliingia katika chumba kile muda huohuo wakati wale wawili wakiwa wanamalizia kumfunga kamba Agent Kai. Wote wakacheka kwa sauti kuonyesha kufurahia alichoongea yule aliyeingia na wakatoka katika kile chumba kisha mmoja akafunga milango kwa nje kwa funguo.
“Hiki chumba kina joto ambalo kati yetu mmoja akizingua siku tukamfungia humu atajihisi tumemuweka jehanamu”. Akasema mfunga milango. Wakarudia kicheko kingine kikali.
“Wakuzingua ni wewe…! Hahahaha hahahah! Akatania mwingine akimtania mwenzake aliyetangulia mbele akimpigapiga begani huku wakiongozana kuelekea sebuleni.
***** ***** *****
Agent Kai alizinduka toka kwenye kuzirai ikiwa ni saa kumi kasoro dakika saba, akiwa amezimia kwa takribani masaa manne na nusu kwa kukadiria kwa haraka haraka. Ilikuwa si rahisi kwa pigo alilopigwa kwa mtu wa kawaida kawaida kuwai kupatwa na fahamu kama alivyopatwa na fahamu mtu huyu wa hatari sana.
Licha ya daktari toka Clinic ya Lae kumpima na vipimo vyake kumjulisha kuwa pigo alilopigwa bwana Kai ni pigo zito litakalomfanya mpigwaji azinduke baada ya masaa 12 lakini kwa mshangao Agent Kai alirejewa na fahamu zake muda huo. Wakati ananapimwa mapigo ya moyo wake yalikuwa yanadunda kwa mbali sana hesabu zao zao zilienda mlama hawakujua mpigwaji ni kama mzimu kwenye baadhi ya mambo yake, hawakujua Agent Kai si mtu wa kuzimia zimia ovyo anapopigwa pigo kama lile anapokuwa kaona anapigwa ilikuwa bahati mbaya kwake hakufikiri kwa haraka kuwa atapigwa na kitu kama kile alichopigwa nacho hivyo kutokana na kutokuona kwake ilisababisha akazirai lakini si kwa muda wanaofikiri wao na dokta wao.
Kichwa bado kilikuwa kizito na kinamgonga sana na kumsababishia kukunja sura huku akijitahidi kufumbua macho taratibu, maumivu ya kichwa chake yalikuwa yale ya mtu mwenye malaria kali aliyemeza dawa ya malaria bila ya kumeza panadol au dawa zingine za kutuliza maumivu ya kichwa. Licha ya kuwa alikuwa kwenye chumba chenye giza na joto kali hakuchelewa kugundua katika chumba alichokuwemo kulikuwa hamna mtu zaidi yake, akajitahidi kuyapuuzia maumivu ya kichwa aliyonayo akafumbua macho na taratibu akaanza kuyaruhusu kuzunguka katika chumba kile kidogo chenye ukubwa wa mita sita kwa urefu na mita tano kwa upana, katika nyumba yoyote ukikiona chumba hiki jibu litakujia ni stoo.
Alikuwa amefungwa lakini hata kama amefungwa kwake hakuona ni tatizo kwakuwa alifungwa na kuachwa mwenyewe kwenye chumba hivyo kubaki pale bila kujaribu chochote si kawaida ya Agent Kai, ilikuwa ni hatari lakini kwake ikitokea kama hivi uwa si hatari kama unavyoweza kudhani. Akiwa hajui ni saa ngapi lakini kutokujua saa si kumzuia yeye kujaribu kitakachowezekana.
Aligundua amevuliwa fulana yake ya jezi ya timu yake aipendayo yupo kifua wazi au kama tupendavyo kusema kitumbo wazi.
Hakuwa huru na alijua lazima atakuwa hayupo huru hata kidogo, mikono yake ilikuwa inapitisha damu kwa tabu kutokana na alivyokuwa kakazwa na kamba pale alipo. Ndipo alipojua kuwa amefungwa kwenye kiti na kwa uzoefu wake wa kazi licha ya giza totoro lililokuwemo aligundua kamba zilizotumika kumfunga ni kamba za katani.
Hapa ndipo akili zake Agent Kai uwa anazituliza na kuwa uongeza spidi kubwa sana ya kufikiri akiwa anajiamini kwa kiasi kikubwa sana.
Kwanza alitingisha mwili wake kuona ni kiasi gani kafungwa mwilini mwake kwa kamba zile za katani ikiwa tayari kashajua ni kiasi gani mikono yake imefungwa kutokana damu kupita kwa tabu mikononi, kichwa kilikuwa kikimpa kero kwa maumivu hivyo muda wote alikuwa kakunja sura, alivuta pumzi kwa nguvu kisha alijaribu kuzivuta nyayo hapo akagundua kafungwa vizuri miguu yake kila mmoja imefungwa sambamba na mguu wa kiti kwa mguu wa kushoto na mguu wa kulia. Joto nalo lilikuwa kali katika kichumba kile kiasi ya kwamba alikuwa akivuja jasho kwa kila jambo analofanya pale alipo basi jasho liliongezeka…
“Shenzy! Ni lazima nijiondoe kwanza katika kifungo hiki, nahitaji nitoke pia katika selo hii yenye joto kama hili. .!” Akasema kana kwamba kuna mtu yupo naye katika chumba kile wanaongea, shukrani kwa Macho yake yaliyokuwa yamezoea giza kiasi ya kwamba alikuwa akiona kwa uzuri baadhi ya vilivyomo mule.
“Sijawai fungwa na kamba za katani halafu nikashindwa jifungua” Akanong’ona akijiambia mwenyewe tena. Akatingisha kiuno chake akagundua hapa alikuwa huru eneo hili ila papo akagundua kiti alichofungwa akiwa kakikalia ni cha chuma.
Alijitingisha kwa nguvu bila kujali maumivu yoyote aliyokuwa akiyapata kutokana na mminyo wa kamba pamoja na maumivu ya kichwa. Haraka akapata mpango baada ya ubongo wake wa kufikiri ambao ufikiria mara tatu ya anavyofikiria kawaida akiwa katika maisha yake ya kawaida. Papo hapo akaanza kazi ambayo ungeiona usingejua kama ni kazi aliyoamini itamsaidia katika wakati mgumu huu aliokuwa nao, alikuwa akitiksa mikono kwa nguvu na mara nyingi bila kupumzika kamba zikawa zinamchuna mikononi maumivu yakawa makali pale damu ilipoanza kumtoka kiasi ya kwamba ganzi iliyokuwa imeanza kutamalaki katika viganja vyake ikakata.
Hakujali dalili alizozisikia kuwa kamba zinamtoa vidonda aliendelea kwa kasi ile ile kwa mfululizo wa dakika zaidi ya kumi, jasho lilimmwagika kama kajimwagia maji au kamwagiwa likasambaa sakafuni kama bomba linalomwga maji. Jasho lile lilifanikiwa kufanya kile alichohitaji, kamba mbili zilizofungwa kwa viganja vyake kwa stahili ya kama pingu ziliteremka na kushukia kwenye viganja ambavyo vilikuwa vimekutanishwa nyuma ya mgongo na nyuma ya kiti chenye kiegemeo.
Kazi ya kujitingisha mwili mzima iliendelea tena akiongeza kasi zaidi akawa katega viganja vyake kwa stahili ya kukinga jasho likawa linafika pale litokeapo juu mgongoni, kamba zikazidi kushuka akawa anazipokea kisha kwa kasi akaanza kuzishambulia kwa vidole stahili ya kama anafumua nywele zilizosukwa (kazi ambayo alishaifanyia mazoezi wakati yupo katika moja ya vyuo vya mafunzo ya ukomando alivyopitia)
Ilimchukua dakika ishirini kumaliza kuifumua kamba moja iliyokuwa mkono wa kulia, shukarani ziliendee jasho lake la mwili, kiganja cha kulia kikawa huru mpaka akaweza kukisogeza mkono wa kushoto ulipo papo hapo viganja vyote viwili vikaanza kufumua kamba zile dakika tatu tu zilitosha kufumua ile kamba hapo akaweza kujitanua kwa nguvu sana na kamba zilizo kwenye viwiko vyake vya mikono yote miwili zikajitanua na akazidi kuwa huru. Kwa nguvu tena akajitikisa kuanzia mgongoni hadi kwenye mikono na kufanikiwa kuzifumua kamba zote zilizofungwa mgongoni zikasalimu amri na kujiachia.
“Alhamdulillah” Akasema tena kumshukuru Mungu kwa kunong’ona. Mikono yake haikuwa inapenda kusubiri subiri awapo kama pale kwa wakati huu, haraka ikaamia mbele akaanza kutoa tu kamba kwa kuziondoa zilipozungushwa.
Tabasamu likaja usoni mwake akiwa na matumaini ya kuwa anakwenda kutoka mule anatokaje tokaje, hilo alikuwa swali kwake. Na katika kitu alichofurahi nacho sana licha ya kuwa bado hakujua atatokaje katika chumba hiki ilikuwa ni kuona amevuliwa fulana yake tu lakini suruali yake aina ya jeans pamoja na raba zake zilikuwa kama alivyozivaa wakati anaondoka nyumbani kwake Gillard Street, Northwest Washington DC.
Muda mfupi uliofuata alikuwa kamaliza kufungua kamba zote zilizozungushwa katika mwili na kiti alichokalishwa wakati hayupo katika fahamu.
Akasimama na kuanza kujinyosha nyosha kisha akatembea tembea katika kijichumba kile, kisha akarudi na kuketi tena katika kiti akiwa huru akafungua kamba za raba za mguu wa kulia, alipomaliza tu kufungua akaitoa mguuni na kuikamata mkononi. Akatoa kapeti ya raba inayofunika unapokanyaga ndani ya kiatu chochote kile, tabasamu likaupamba uso wake tena.
“Allah Akbar! Hawakufika huku, waliona hizi raba zipo kiboya boya, kosa, kosa, kosa kubwa la kujutiwa” Akanong’ona baada ya kuona amekuta alichotaraji. Kisha akaendelea tena kusema.
“Kosa, kosa …Kosa halifanywi kwa mafundi kwani ugharamika kifundi kumkosea fundi kumdhibiri kifundi hata kama unajiamini sana….” Aljinong’oneza baada kugundua katika sehemu ya siri anayoficha vitu vyake iko salama haijaguswa, alijiuliza kwanini walifanya kosa la kumuacha na raba zile alizozivaa, hawakujua kila kilicho katika mwili wake na kimevaliwa basi uwa kina baadhi ya siri za ndani ambazo kama bila kupewa maelekezo maalumu kutoka kwake basi si rahisi kujua.
Alikutwa na furaha kwa KOSA kubwa walilofanya watekaji wake, sababu aliamini hawezi shindwa kutoka katika selo ile endapo hatakuta kipingamizi cha ulinzi. Chini ya kapeti inayofunika viatu anapokanyagia kulikuwa na funguo nne ndogo ndogo (small master key) zilizofunikwa kwa pembeni kabisa katika vishimo maalumu vilivyo ndani ya raba zilizo na uwezo wa kiufundi kumudu kufungua makufuli na vitasa aina mbali mbali vya milango isiyotumia kadi, ufungua kwa kuzungushwa zungushwa pale inapotumbukizwa kwa stahili ya kimafunzo maalumu (si kibwegebwege) kwenye tundu la funguo liwe la kufuli au kitasa, na funguo zote zile zilikuwa na vichwa vya vilivyonakshiwa kwa almasi vipande vidogo hii ni kwa kazi ya kukata vioo. Hizi funguo akizipata muhalifu kama ni jambazi au kibaka halafu asiwe na mafunzo maalumu anaweza asijue atazifanyia nini lakini endapo ataweza kuzitumia makasiki ya fedha ya matajiri na milango yake itaomba poooh!
Haraka bila kuendelea kufikiri fikiri alikita kwa vidole viwili cha shahada na cha kati vya mkono wa kulia na kuchana kitambaa kinachofunika sehemu zile akazitoa funguo hizo na kuziweka kwenye mfuko wa suruali ya jeans, kisha akakaa kwenye kiti ambacho muda si mrefu kilikuwa kimetumika yeye kufungwa hapo kwa kamba kama kuni akavaa raba yake tena. Akainuka huku anamalizia kufunga kamba za kiatu hatua mbili akafika mlangoni, kwanza akaliegemeza sikio na kuanza kuvuta hisia upande wa pili wa mlango anaweza kuhisi kuna jambo gani?.
Kulikuwa kimya kabisa, akatoa funguo mfukoni na kutumbukiza moja kwenye tundu la kitasa baada ya kuzungusha zungusha anavyojua yeye aligundua funguo ile inafeli inateleza kwenye mtego hivyo akaitoa na kutumbukiza ingine ikazama vizuri bila ubishi na mizungusho minne tu lock ilitoka akaminya kitasa kwa tahadhari kiasi cha kutokufanya mchakacho wowote akauvutia mlango kwa ndani ukafunguka bila kelele yoyote kama kwamba haujaguswa… Uzuri wa ujuzi…. Uzuri wa ufundi!... Macho yalikutana na kikwazo kingine, kulikuwa na geti dogo la mlangoni lisiloonyesha ukilifungua unatokea wapi..
“Shenzi zao… Jamaa watajutia ujinga wao… Walitaka kuniua kwa joto la humu ndani, nia yao nikose hewa au ni nini? kunifunga kamba na milango miwili nayo kuifunga” Akajinong’ona huku akipiga moyo konde kutojali akifungua atatokea wapi alitumbukiza funguo ndogo zaidi kwenye tundu la funguo la geti alizungusha mara mbili tu funguo ile na lock zake zilionyesha kukubali kwa haraka akasukuma geti lile dogo kwa nje akiwa kwenye umakini mkubwa sana na kwa bahati iliyoje kwake lilikuwa geti lisilopiga kelele kwa chati akachungulia kwenye upenyo mdogo alioufungua na macho yake yakatua kwenye korido pana ambayo ilikuwa na mwanga hafifu uliotokea nje kupitia dirisha kubwa lilio upande wa kulia wa mlango wa chumba hiki kilichokuwa selo kwake.
Mwanga ule ulimtosha sana yeye kuona kila kitu hakukuwa na kiumbe chochote katika korido ile. Akijiamini kwa kiasi cha kutosha akajitoa mzima mzima kisha akalirudisha geti polepole macho yakaenda kulia kwake na kisha kushoto maamuzi yakaja ajongee upande wa kulia sababu mwisho wa korido ulionekana ni hapo pia kulikuwa na dirisha lililoonyesha upande wa pili wa jengo. Kwa mwendo wa mnyato wenye kasi, mnyato ambao ulimpa maksi za juu kuliko wanafunzi wenzake watano walipokuwa katika practical technic kwenye camp ya mafunzo kwa vitendo iitwayo Camp Pearly iliyopo Williamsburg, Virginia huko Marekani, walimu wake wa katika kambi hii walimpa jina utani wakimuita ‘The Sole Cat’ wakimaanisha ‘Nyayo za paka’ kipindi anaponyatia kitu pindi anapokuwa eneo la mapambano.
Dirisha lilikuwa kubwa la vioo, upande wa pili ulionekana ni nyuma ya jengo hili kutokana na kuwa na jengo lingine lililokuwa karibu na jengo hili na kuwa limepeana mgongo kwa kutenganishwa hatua kama tano na uchochoro. Kwa haraka alilichunguza dirisha lile na kugundua kwa lilivyo dirisha hili yeye Agent Kai angeweza kulifungua dirisha na kuruka chini kisha kujiondokea zake bila kustua mtu yoyote aliye ndani ya jengo hili, aliamini isingekuwa tabu kwake kuruka toka hapa dirishani hadi chini tena bila yeye kupata madhara yoyote sababu jengo hili masaa machache yaliyopita aliweza kuliona kwa nje kabla hajapigwa na kitako cha bunduki na kutekwa kikuku kama alivyoamini.
Alishapitia kuruka kwenda chini kwenye baadhi ya maeneo mbalimbali kama miti na hata majengo ya aina mbalimbali hivyo akiwa anahitaji kuruka sehemu kama hizi kwake uwa anaruka tu tena bila tahadhali zaidi ya kujua anapoenda kutua kuna hali gani.
Akili yake ilikuwa ikihitaji apate vitu vyake pia achunguze hili jengo ni jengo la nini na nani mmliki wake na anaweza kufanya chochote kipi kitachoweza mjulisha awa waliomteka walikuwa wanahitaji nini kwake. Hivyo alichukua maamuzi hawezi kuondoka bila kupata briefcaselake na hata begi lake pia alitaka atumie kila mbinu aweze kumuhoji mwanadada aliyejifanya yeye ni Detective Marie. Yeye sasa ni muwindaji si muwindwaji!
“Kwa ukimya huu bila shaka waliomo ndani ya nyumba hii watakuwa wamelala wote… Sijajua huu ni muda gani lakini vitu vyangu ni muhimu kwa kazi yangu kuliko kitu chochote kile kwa sasa…. Awa watu kwa jinsi walivyoweza kunighilibu kwa kutengeneza sura ya bandia ya Detective Marie ni watu wanaohusika moja kwa moja na utekaji wa watu wote ambao taarifa zao za utekaji ndiyo zinazotuhumiza kichwa kwa sasa” Alijisemea Agent Kai kwa sauti ndogo sana huku akigeuka kuelekea korido ya kutoka eneo hili inapoeleke.
Akitembea kwa mgongo wake kuuweka ukutani huku matako yakiweka sapoti sambamba alinyata hadi hadi kwenye kona ya korido hii kisha akasimama kwenye kona akinyooka kama mlingoti kichwa kikatokeza macho yakachungulia na kukutana na ukumbi mrefu wa mita kama ishirini wenye milango iliyojipanga kushoto minne na kulia minne kuashiria kuwa ukumbi ule ulikuwa ni kwa ajili ya vyumba hivi vilivyojipanga kwa kuachiana mita kadhaa, mwisho wa ukumbi huu kulikuwa na ishara iliyoonyesha kwake kuwa palikuwa na ngazi inayoteremsha floor ya chini.
Mnyato wa paka tena tahadhari ikiongezeka akaanza kunyatia kufuata mlango wa kwanza kutoka pale kwenye kona, kufika mlangoni akatega sikio kwenye tundu la funguo kwa mbali akapokewa na sauti ya mlalaji anayekoroma kama inavyowatokeaga baadhi ya watu waanapokuwa wamelala na kuwa katika usingizi mzito kukutwa na hali hii ya kukoroma.
Damu ikamsisimka!
Hatari inayoleta MSHANGAO! Huyu mtu anayeitwa Agent Kai Hamis Mkarambati muda mwingine unishangaza hadi mimi ninayemuandikia vitu anavyonihadithia unishangaza sana na kuona kama sijui ameumbwaje, anapotamani kupambana au kukaribia kupambana mapambano yatakayoanzisha kasheshe itakayopelekea mauaji au madhara kwa mtu au watu, damu umsisimka na inapomsisimka yeye utabasamu kisha ung’ata meno na baada ya sekunde mbili uyaachia basi hapo kinachofuata uwa hakina msalie kwa yoyote aliye kwenye target yake.
Yeye uamini katika imani ya juu kabisa kuwa aliumbwa na kuzaliwa kwa ajili ya kukimbizna na kuwakomesha wahalifu, ameletwa duniani kwa kazi hii ya hatari na ni kipaji chake kuwapeleleza, kuwachakua kama kuku achakuavyo chakula hili ale, kuwapekua, kupekua mambo yaliyojificha ya hatari na kuyaweka wazi, kukwepa hatari zote na hata kurushiana silaha na maadui zake huku akiwindwa na kuwindwa na hata kupimana utaalamu wa kupigana mapigano ya aina yote.
Kifupi alipenda sana kufanya kazi hii ukiacha ile aliyoomba kuiacha mwenyewe kwa hiyari yake tena akiwa kwenye kikosi cha kijanja na kitaalamu chenye vifaa bora vya kisasa, kikosi cha US, Navy Seals. Katika miaka sita aliyofanya kazi katika CIA ofisi ya makamu wa Rais kitengo cha ujasusi wa kimataifa, magaidi na wahalifu aliwanyosha kiasi kikubwa mpaka jina lake likawa kwenye top ya juu katika CIA kila kachero au bosi akipenda kufanya naye kazi sababu mara nyingi wamalizapo kazi fulani kwa ufasaha basi upewa tuzo maalumu kama ni kikosi cha watu watatu au hata watu wawili basi upata zawadi toka kwa Rais wa nchi.
‘Katika watekaji awa wengi wao watakuwa hawaongei kiingereza wala kati ya moja ya lugha ninazozijua… awa wanaongea ki-bahasa melayu sina haja na yoyote asiyejua kiingereza nachohitaji vitu vyangu na ninaamini watakuwa wamegawana kama vyao…!’ Akawaza Kai huku akiminya kitasa taratibu kisitoe sauti.
‘Yule mwanamke nina hasira naye sana sijui yupo chumba gani’ Akaendelea kuwaza huku akiusukuma mlango ule kwa ndani akiwa kang’ata meno. Akatabasamu! Mlango haukuwa umefungwa kwa ndani kwa funguo wala kwa komeo sababu ulisalimu amri, ulikuwa ni mlango wa kwanza upande wa kushoto katika ukumbi huu.
Kidume cha kazi! Akazama ndani bila kuacha mchakacho wowote akiwa katika umakini wa hali ya juu na uzuri kulikuwa na mbalamwezi inayomulika kwa kutokea dirishani iliyoweza kufanya chumba kuwa kimewashwa taa. Alimkuta mwenyeji wa chumba akiwa amelala kajiachia yupo sayari ingine anakoroma hana habari, chumba cha kisela (ghetto) kitanda, meza ya kioo na meza ya kompyuta ya iliyokuwa ya desktop na kabati dogo la nguo.
Hakuhitaji kumstua kwa sababu ya imani aliyoamini italeta lugha gongana, itakuwaje yeye anazijua lugha kuu zinazotambulikana duniani kama vile kiarabu, kiingereza, kifaransa, kijerumani, kichina kwakuwa aliishi na kusoma china shule ya msingi (tutaona mbele ilikuwaje mpaka akasoma shule ya msingi nchini China) kilatino, kiitaliano, kireno na Kiswahili lugha ya nchi yake ya kuzaliwa na taifa lake la asili na hata ndugu na wazazi wake. Kifupi alikuwa na hazina kubwa ya lugha Agent Kai tunayemfuatilia katika mkasa huu wa kusisimua wa MSHANGAO!.
Haikuwepo sababu ya kumuamsha kwa stahili yoyote mlalaji yule, sura ilikuwa ngeni machoni mwake kati ya watekaji wake wote aliyekuwa anamkumbuka na taswira yake kuja kwenye ubongo wake alikuwa ni yule aliyempiga kwa kitako cha bunduki na ni kwasababu alimuona akishuka kwenye gari akitokea mlango wa mbele wa gari. ‘Sina shida na awa zaidi ya vitu vyangu na yule mwanamke nataka aniambie yuko wapi Detective Marie, wasiwasi wangu wanaweza kuwa washamuua… lakini siwezi kumuacha hai mtu huyu wakati napekua chumba hiki’ Akawaza Kai akiwa tayari kashasogea pembeni kabisa ya yule mtu aliyelala kitandani kwa raha zake.
Damu ikachemaka na kumsisimua mwilini! Akamtingisha kichwani kama anamuamsha, ile anajigeuza tu toka alivyolala kiubavu hili awe chali, shingo yake ilitoa wa mlio kama mpira mdogo wa kindiki au wengine uita kitenesi kilichodundwa chini na mdundaji anayekichezea, karate nzito ilitua katikati ya koromeo lake na kumvunja shingo nzima misuli yote inayounganisha fahamu ya kutoka kichwani kuja mwilini ilivunjika, sekunde kumeta tu bila hata kujitingisha zaidi ya mara tatu uhai uliachana na mwili malaika mtoa roho akafanya kazi yake.
“Pumzika kwa amani, najua wewe si lolote si chochote lakini kiufundi hutakiwi kuendelea kuongeza wingi kwa wanaokutumia”. Akasema Agent Kai kwa sauti ambayo laiti ungekuwa upo naye eneo hilo angalau hatua tano ungemsikia vizuri tu.
Mwisho wa sehemu ya nne (04)
Fundi ameweza kujinasua toka katika kiti cha chuma na kamba za katani alizofungwa zikisalimu amri chini ya amri kuu iliyoundwa kifundi kupitia jasho la fundi mwenyewe.
Kosa kubwa la kukariri na kuamini kila mtu uwa kama mtu mwingine linaelekea kuwagharimu pakubwa wazee wa kazi wa kikundi kinachojiita ‘Six Dangerous Boy’s’.
Fundi wa mafundi ameweza kutoka katika chumba alichofungiwa kwa kosa la kukariri, walishindwa hisi wala kujua wanatenda kosa kutomfungua raba alizovaa mateka wao.
Nini kitawatokea SDB?
Nini anakwenda kukifanya mtaalamu ‘The Sole Cat’?
Majibu ya yote haya yanapatikana katika muendelezo wa riwaya yetu hii tamu nay a kuvutia, yenye mapigo na midundo ya kisasa toka kwa mtaalamu wako Agent Kai.
Haikuwepo sababu ya kumuamsha kwa stahili yoyote mlalaji yule, sura ilikuwa ngeni machoni mwake kati ya watekaji wake wote aliyekuwa anamkumbuka na taswira yake kuja kwenye ubongo wake alikuwa ni yule aliyempiga kwa kitako cha bunduki na ni kwasababu alimuona akishuka kwenye gari akitokea mlango wa mbele wa gari. ‘Sina shida na awa zaidi ya vitu vyangu na yule mwanamke nataka aniambie yuko wapi Detective Marie, wasiwasi wangu wanaweza kuwa washamuua… lakini siwezi kumuacha hai mtu huyu wakati napekua chumba hiki’ Akawaza Kai akiwa tayari kashasogea pembeni kabisa ya yule mtu aliyelala kitandani kwa raha zake.
Damu ikachemaka na kumsisimua mwilini! Akamtingisha kichwani kama anamuamsha, ile anajigeuza tu toka alivyolala kiubavu hili awe chali, shingo yake ilitoa wa mlio kama mpira mdogo wa kindiki au wengine uita kitenesi kilichodundwa chini na mdundaji anayekichezea, karate nzito ilitua katikati ya koromeo lake na kumvunja shingo nzima misuli yote inayounganisha fahamu ya kutoka kichwani kuja mwilini ilivunjika, sekunde kumeta tu bila hata kujitingisha zaidi ya mara tatu uhai uliachana na mwili malaika mtoa roho akafanya kazi yake.
“Pumzika kwa amani, najua wewe si lolote si chochote lakini kiufundi hutakiwi kuendelea kuongeza wingi kwa wanaokutumia”. Akasema Agent Kai kwa sauti ambayo laiti ungekuwa upo naye eneo hilo angalau hatua tano ungemsikia vizuri tu.
ENDELEA NA SEHEMU YA TANO..!
Akisaidiwa na mbalamwezi kama nilivyokwisha eleza hapo juu, aliiona wallet ambayo yeye uwa nayo kwenye mfuko wa suruali mara nyingi atembeapo na ilikuwa kwenye suruali yake hii ya jeans aliyovaa. ‘Mawazo yangu yako sahihi awa watu wamrgawana vitu vyangu tu’ Akawaza huku anainyanyua ile wallet toka pembeni ya kompyuta ya mezani (desktop).
“Shenzi!.... Pesa zangu zote wameziamisha…. Au wamegawana?” Alijiuliza tena kwa sauti ile ile ya chini baada ya kuifungua ile wallet na kukuta iko na kadi yake ya bank (ATM) ya western union haina pesa yoyote, aliiamishia wallet ile kwenye mfuko wake wa nyuma wa suruali. Haraka akaanza kuzungusha macho yake mule ndani ya chumba akaiona suruali aina jeans ikiwa ina mkanda wa kiunoni papo hapo akapata jibu alilotaka akaivamia na kuanza kuisachi mifukoni, baada ya kusachi mifuko yote akafanikiwa kukuta pesa za noti za Malaysia ziitwazo Ringiit Malay (RM) zilikuwa RM 70000 pia kulikuwa na dollar 500 ambazo zipo katika noti moja moja za dollar mia mia za marekani.
Hakutaka kuremba bora aonekane mwizi lakini kwa kitendo cha kuchukuliwa wallet hakuwa na shaka dollar zile ni zake sababu wallet yake ilikuwa na dollars 4000 na zote zilikuwa katika dollar mia mia kila noti moja, alizipanga kwenye wallet na kurudisha ile wallet ilipozoea kuishi mfuko wa nyuma wa sura yake ya jeans. Pembeni ya mto alipolala marehemu huyu wa muda si mrefu akaiona bastola na uzuri ilikuwa ni bastola inayomuhusu mali yake bastola aina ya Glock 42, alitabasamu na kuinyanyua haraka kisha akacheki risasi na kurudisha mahali pake nyuma ya kiuno.
Mara sauti ya adhana ikasikika ikiadhiniwa ikiashiria muda wa swala ya alfajiri umefika, waislamu wakikumbushwa kumekucha wanahitajiwa kujiandaa kwa ajili ya swala, ilisikika kwa uzuri kudhihirisha msikiti haupo mbali sana na maeneo haya ya Nadau Golf ‘Tayari kumekucha Kai’ Akawaza Agent Kai huku tayari akiwa nje ya chumba alichokuwemo, akipiga hatua zake za mnyato wa paka aliufikia mlango wa pili bila kuchelewa akaminya kitasa papo hapo alijikuta aking’ata meno maana mlango ulitoa kamlio kake kanakotoaga vitasa vingi vinapominywa ‘Shit Kai… Unajisahau…Tatizo lako umesahau kama adhana ni kitu cha kuheshimiwa sana kwako’ Akawaza na kubaki kaganda pale mkono wake ukiwa kwenye kitasa mpaka adhana ilipoacha kuadhiniwa.
‘The Sole Cat’ akaminya kitasa tena akiongeza umakini zaidi ya mara ya tatu ya kawaida napo kama mlango ule wa chumba alichotoka nao ulimpa taarifa huko wazi haukufungwa kwa ndani, hapo Kai alitingisha kichwa kukubaliana na kitu ambacho alikiwaza nukta chache zilizopita wakati ananyata kusogelea katika mlango huu kuwa kuna uwezekano wa kimakubaliano kati ya hawa watu ya kuacha milango yao wazi kwa sababu wanazozijua wao labda wakiwa na imani kuwa wao wako salama zaidi na hawana tatizo lolote, hasa ukizingatia jengo lao si rahisi kwa watu wa kihalifu kuwavamia.
Ukweli waliacha hivyo hili iwe rahisi kwao kuamshana kwa ajili ya mazoezi na ilikuwa ni tabia yao siku zote. Waliamini pale wanapofunga mageti na milango yao ya kuingia katika jengo hili ilitosha kwao kuwa salama. Jengo hili lilikuwa ni mali ya shirika la nyumba la taifa la Malaysia hapo kabla na walipanga floor zote tatu wakilipiwa kodi kila baada ya mwaka na Mr Logan Puter aliyejulikana mbele ya macho ya wana jamii kuwa ni mfadhili wa Gym yao na wacheza boxer wa gym hii lakini miaka miwili iliyopita mfadhili aliwanunulia likawa mali yao kwa wote kwa ujumla.
Waliishi kwa raha sana katika jengo hili tena wakijiachia na kufanya watakavyo, waligawana vyumba kama wana familia wafanyavyo. Walipopewa kazi ya utekaji basi mateka huyo jela yake ya kwanza ilikuwa lazima apite jengo hili ndiyo apelekwe sehemu ingine.
Leo waliula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua, walimpa wepesi mtu wa hatari kufanya anavyotaka, mtu waliyeamini ni mtu wa kawaida wakiamini kama kawaida bahati uwa upande wao, leo sivyo! leo walikumbwa na bahati mbaya ya bundi kila aliapo waswahili kusema ni uchuro. Ilikuwa sahihi kusema wapo hatarini, windo waliloliwinda ni windo la tofauti, sasa wanawindwa wao na muwindaji asiye na makosa anapowinda.
Kai akizidisha kasi ya mambo alizama ndani ya chumba sababu napo alishakuwa kasikia pumzi za binadamu zinazovutwa kwa kiashirio kuwa wapo watu wawili humo ndani lakini wapo kwenye usingizi mzito pumzi zinapishana tu, macho yakiwa yamezoea hali zote za pale akisaidiwa na mbalamwezi anaona kama yupo kwenye taa zenye mwanga hafifu, macho yalitua sehemu haswa aliyotakiwa kuiangalia kitandani na kutimiza kile alichokuwa akifikiri alipozisikia pumzi za watu zinazotokea chumba hiki.
walikuwepo watu wa jinsia tofauti wamelala huku wamekumbatiana haikujificha kujua waliolala ni mtu na mpenzi wake, walikuwa wamejifunika shuka moja liliwaziba kuanzia miguuni mpaka kwenye viuno vyao huku kwenda juu wakiwa hawana chochote kile, sura zao wameelekezeana kuonyesha muda wa masaa kadhaa yaliyopita walikuwa wametoka kwenye shughuli iliyowaunganisha pale, shughuli ya raha isiyoelezeka pindi inapopata wapepetaji wenye kujua kupepeta.
Wote walikuwa ndani ya sayari ya usingizi kwa raha zao pumzi zao zinapishana katika kuingia na kutoka vijana awa ambao sura zao zilijidhihiri machoni mwa Kai kuwa bila shaka ni wa Malaysia kiasili.
Kwa usalama wake na kuokoa muda uliokuwa tayari kumekucha, Agent Kai kazini hakuna kuremba kwa mwendo mnyato lakini wenye kasi akawasogelea pale kitandani. Paaaaapu! Salaleee! Kumbu kumbu za Agent Kai kumbukumbu zake ziko sawa sana huyu mtu, papo hapo kengele ililia kichwani mwake, alipoiona sura ya mwanaume aliye kwenye kumbatio murua la baby wake, aliikumbuka sura aliiona kwa muda mchache ikiongoza wengine kushuka kwenye gari aina ya Noah na ni mtu huyu wakati alipohisi kuna mtu nyuma yake alipokuwa kaingia matatani ndiyo aliyemtwanga kwa nguvu kwa kitako cha bunduki na kumfanya adondoke kisha akazirai.
Pigo lile lililomlaza asijielewe wala kujitambua mpaka alipozinduka lilimfanya kuumwa na kichwa sana kiasi ya kwamba mpaka sasa kinaendelea kumuuma ingawa kimepungua kwa kiasi, alikuwa ni Nabeel kiongozi wa kundi hili dogo la watu sita linalotumiwa na Mr. Logan Puter.
Hasira ilimpanda ghafla maradufu akang’ata meno kwa nguvu, akakunja uso kuhakisi hasira alizonazo juu ya mtu anayemuangalia, pembeni ya kitanda walicholala kulikuwa na dressing table yenye kimeza juu ambapo juu ya kimeza kile kulikuwa na bunduki fupi aina ya shot-gun na ndiyo haswa iliyotumika kumtwanga Kai kisogoni, kulikuwa na kisu kimoja kikubwa chenye makali ya wembe, funguo za mlangoni (vitasa) na funguo za makufuli zilizofungwa kwenye kamba moja na kioda kimoja pia kulikuwa na pesa aina ya noti zote za kimalaysia RINGIT ambazo zilifungwa katika kibunda kimoja kilichotuna barabara. Hasira ikiwa imemtawala akanyanyua kisu haraka, hisia za kufanya mauaji zikamuingia!
“Sheeeenzy!” Alijikuta anaropoka kwa sauti kiasi ya kwamba yule mwanaume aliacha kutoa pumzi kwa mwendo aliokuwa anatoa akanyamaza ghafla kisha akajigeuza mwili.
Kwa roho ya kikatili Agent Kai akakita kisu katikati ya koromeo la Nabeel kisha akapeleka kwa nguvu kuelekea kushoto akawa amemchinja koo lote la mwanaume yule ‘taharuki ya kutisha!’ damu za moto ziliruka, mwanamke aliyekuwa naye kakumbatia alistuka kwa kuinua mwili wake juu akataka kunyanyua mdomo kupiga kelele, papo hapo ngumi nyepesi ilipigwa chini kidogo ya taya lake na juu ya koromeo lake lisiloonekana vizuri kama alipo kabisa, kustuliwa usingizini kisha kukutana na pigo jepesi toka kwa mtaalamu wa mapigo kingumi kile kilimpelekea kuzirai.
Sekunde zilizofuata kulikuwa kunasikika kutoka kwa damu katika koo alilochinjwa marehemu Nabeel kana kwamba bata anafoka, wapenzi hawa kila mmoja alikuwa kahamia katika dunia yake, mmoja kuzimu na mwingine wanakoenda wanaozimia.
Kilichofuata Kai akachukua pesa zilizo kwenye dressing table ile kisha akaanza upekuzi kutafuta kama ataona kitu kinachomuhusu, alipofungua kabati la nguo akakutana na begi lake, pembeni kukiwa na saa yake ya mkononi pamoja na fulana yake inayozuia kuingia risasi (bullet proof), kwa haraka akalitoa begi mule na kufungua zipu ndipo alipokuta napo kuna suruali moja ya jeans nyeusi yenye mifuko mingi ambayo uwa suruali yake ya kazi na kanzu yake ya rangi ya kawahia au tuseme chocolate.
Hii ilimaanisha nguo zake nazo waligawana pamoja na laptop na vifaa vingine vya kazi, akachukua fulana yake ya bullet proof akaitia kwenye begi, akachukua saa yake saa ya kijasusi ya kisasa na kuivaa kwenye mkono wake wa kulia huku akisoma kujua ni saa ngapi, ilimuonyesha ni saa kumi na mbili kasoro kumi na nane alfajiri ya siku ya jumatano, pia kwakuwa alikuwa hana nguo ya juu, yupo kifua wazi alichagua shati la aina ya jeans rangi ya bluu lililokuwa la mwenye kabati kisha akalivaa lilimfiti kama kwamba lilikuwa lake, baada ya kumaliza hatua hizo zote alizozifanya kwa kasi na umakini wa juu akafunga zipu ya begi na akalivaa begi mgongoni. ‘Laptop na Ipad wameziondoa kwenye begi…. Briefcase hawataweza kulifungua ila kwa akili za kihalifu watataka kulivunja’ Aliwaza Kai huku akifungua mlango kutoka katika kile chumba.
Mwendo mnyato, mwendo wa kunyatia kwenda chumba kilichopo vyumba vya upande wa pili ambapo napo viliongozana katika safu inayofuatana kutoka mlango huu unasogea mwingine, akili yake muda wote ilikuwa ikimtamani Detective Marie fake (Damia), kabla hajagusa kitasa tumbo lake liliunguruma akashika bastola vizuri mkono wa kushoto, macho yalikuwa yakifanya kazi kwa haraka kuzunguka eneo lote maana alihisi kuna hatari pale tumbo lilipounguruma.
Mara mwanga wa taa Mwaaaah!
Taa ya umeme kubwa iliyo juu ya dari iliwaka kuashiria imewashwa, kwa MSHANGAO wa ajabu kwa aliyewasha taa na wenzake waliokuwa wamepangana kuwa taa iwashwe walistaajabu mpaka walihisi labda ni mazingaombwe au sinema, Agent Kai kwa wepesi mkubwa bila kufikiri wala kuacha sekunde zisizozidi kumi toka taa kuwashwa mambo mawili aliyafanya kwa ustadi wa hali ya juu, risasi moja alifyatua iliivunja taa (balbu) na kutoa mlio kama wa bomu la kutupwa na mkono huku bastola yake ikitoa mlio mdogo sana sababu ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti, giza lilirudi zito zaidi, nukta ileile taa ilipovunjika aliruka sarakasi ya stahili ya mtupu-mtupu (free-acrobatic) yaani aliruka kwenda juu kichwa na mwili vikipinduka chini miguu ikienda juu lakini anakuwa hewani na akipinduka kwa kasi kurudi nyuma (ndiyo free-acrobatic).
Jamaa waliokuwa wamejificha kwenye kona ya zinapoanzia ngazi zinazoenda sebuleni baada ya kuwa wameamshana ikiwa mmoja wao kastuka kuwa kuna tatizo, nia yao ilikuwa baada ya kuwashwa taa na kuwa wamemstukiza Agent Kai ilikuwa ni kumuomba ajisalimishe lakini walipigwa na MSHANGAO na wote kwa pamoja walijikuta wakifyatua risasi kutokea walipo kuelekea alipo Kai baada ya masikio kusikia mlio wa risasi na mvunjiko wa taa (nao pia zilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti ikawa inatokea miale tu ya moto toka kwenye midomo yao ya bastola na harufu kali ya kama baruti).
Risasi zilikuta hewa na kwenda kuchimba ukutani maana Agent Kai mruko wake wa sarakasi ile ulimfanya kupaa hewani karibu na dari amabalo lilikuwa refu na alipotua aliwaonyesha maajabu mengine kwani alijifyatua stahili iitwayo kata-shingo ambayo urukwa kwa mtu mjuzi wa sarakasi kuruka mwili ukiwa kama umelala lakini huwi umejishika popote na uchagua kimo unachotaka, hapa Agent Kai aliruka kimo cha mbuzi na alijizungusha kwa kasi akiwa hewani risasi mbili zilizofyatuliwa kwa mfyatuo wa pili toka kwa watu wawili kati ya watu wanne zilitua kwenye begi alilobeba mgongoni.
Mwili wake ulipotua chini tu alijipindua na kulalia mgongo kisha akaweka kiganja cha mkono wa kulia chini ukatokea mfyatuko wa mwili baada ya sapoti ya ule mkono mmoja akasimama wima na kujirusha kwa kasi karibu na mlango wa chumba alichotoka kumuua kwa kumchinja Nabeel papo hapo alijibu mashambulizi kwa kufyatua risasi tatu toka kwenye bastola yake iliyo mkono wake wa dhahabu, mkono wa kushoto anaoutumia kama mkono wake wenye shabaha na nguvu, wenye sifa zakutosha pindi autumapo jambo, alifaytua kuelekea ile kona walipo washambulizi wake.
Risasi moja ilitoa jibu maana lilisikika yowe la maumivu toka kwa mmoja wa watu wale wanne, risasi ilimpata kwenye bega na kumvunja. Wote walirudi ndani ya kona na kupotea huku wakitetemeka wasiamini mambo waliyaona katika giza lile lenye mwanga hafifu, bonge la MSHANGAO! Sarakasi zilizokuwa zikipigwa kwa kasi kubwa na ufundi wa hali ya juu kwao zilikuwa kama ndoto au mazingaombwe fulani.
Agent Kai alitumia fursa ile kuingia katika chumba alichotoka sababu mlango ulikuwa wazi, ilibaki sauti ya mtu anayeugulia maumivu ya kupigwa risasi kwenye kona iliyo na ngazi zinazoshuka kuelekea sebuleni.
Kichwa cha Agent Kai ni kama kompyuta yenye RAM kubwa inayofanya iwe na kasi kwa jinsi kinavyofanya kazi kwa kasi kwani alipourudisha tu mlango kwa kasi alisogea dirishani kwa hatua zisizotoa mlio kwa jinsi alivyoikanyaga sakafu kana kwamba anaiogopa.
Alipolifikia dirisha alivuta pazia kubwa ya dirishani iliyokuwa imeenea dirisha lote na kulisogeza upande mmoja wa kulia. Dirisha la kioo kama madirisha mengine yaliyo katika jengo hili la ghorofa, kioo kilichozungukwa na fremu ya alluminium pande zote, hakusubiri nini kifuate akili yake ilikuwa iifuata hisia zake za kazi zinavyomtuma kwa wakati huo.
Akafyatua vishiko (lock) zake likafunguka akalisukuma kuendea kulia alipolisukuma pazia na kuacha uwazi nusu dirisha, nukta kumeta tu akawa amedunda na kuwa amechuchumaa juu ya katikati ya dirisha macho yakitizama chini kabisa kwa kutokea pale dirishani floor (losheni) ya tatu ya jengo hili la ghorofa lenye floor tatu.
Upande wote pale chini aliona kulikuwa na magari kama matatu yaliyopaki kwa chini akaamua ajirushe kwa kutua juu ya gari. Akajiachia kwa kuruka kuelekea chini alipokaribia juu ya gari aliloamua atatua juu alijizungusha akatulia mgongo kisha kujiviringisha kwenda chini kabisa alipotua alitulia kwenye kitu kilichokuwa kama ndoo kubwa ya bati ya takataka (dustbin) ikadondondoka sambamba na mwili wake na kusababisha mlio kiasi ya kwamba kama muda huu wa saa kumi na mbili na dakika kumi na mbili ungekuwa macho na upo majengo ya jirani na pale jumlisha na ukimya uliokuwa umetawala ungeweza kusikia mlio ule wa ndoo ya takataka.
Kai akatabasmu na kuinuka haraka na kujisemea kama anaongea na mtu pembeni yake laiti ungemsikia.
“Ahsanteni sana wateja wangu… Mmenikaribisha vyema sana, mkanipa changamoto na kunipasha moto misuli… Mmenipa pa kuanzia Agent Kai”
Mwisho wa sehemu ya tano (05)
Ndiyo kwanza tumefungua kurasa chache za mwanzo za riwaya yetu tamu ya kijasusi yenye kusisimua ya MSHANGAO! Riwaya yenye MSHANGAO wenye visa vyenye ujasusi na mapigano ya kusisimua yenye taharuki.
Tumeshuhudia mambo kadhaa wa kadhaa yaliyotufungua kujua mengi tuliyotamani kuyajua baada ya kuisoma sehemu ya kwanza iliyotujuza tunasoma nini katika riwaya hii.
Tumeshuhudia Agent Kai akiingia mtegoni na kufanikiwa kujinasua kwa stahili iliyowaacha na MSHANGAO wa ajabu anaowaita ni wateja wake.
Je boss ataupokeaje ujumbe wa kwanza tu toka kwa Agent Kai?
Je Agent Kai atamuona tena Damia?
Majibu yote na mengineyo mengi ya kusisimua utayapata katika sehemu zinazofuata za hii safari yetu ndefu ya kusisimua yenye mambo ya kitaharuki na mapigo yaliyoenda shule toka kwa komando Agent Kai wa CIA.
Alipolifikia dirisha alivuta pazia kubwa ya dirishani iliyokuwa imeenea dirisha lote na kulisogeza upande mmoja wa kulia. Dirisha la kioo kama madirisha mengine yaliyo katika jengo hili la ghorofa, kioo kilichozungukwa na fremu ya alluminium pande zote, hakusubiri nini kifuate akili yake ilikuwa iifuata hisia zake za kazi zinavyomtuma kwa wakati huo.
Akafyatua vishiko (lock) zake likafunguka akalisukuma kuendea kulia alipolisukuma pazia na kuacha uwazi nusu dirisha, nukta kumeta tu akawa amedunda na kuwa amechuchumaa juu ya katikati ya dirisha macho yakitizama chini kabisa kwa kutokea pale dirishani floor (losheni) ya tatu ya jengo hili la ghorofa lenye floor tatu.
Upande wote pale chini aliona kulikuwa na magari kama matatu yaliyopaki kwa chini akaamua ajirushe kwa kutua juu ya gari. Akajiachia kwa kuruka kuelekea chini alipokaribia juu ya gari aliloamua atatua juu alijizungusha akatulia mgongo kisha kujiviringisha kwenda chini kabisa alipotua alitulia kwenye kitu kilichokuwa kama ndoo kubwa ya bati ya takataka (dustbin) ikadondondoka sambamba na mwili wake na kusababisha mlio kiasi ya kwamba kama muda huu wa saa kumi na mbili na dakika kumi na mbili ungekuwa macho na upo majengo ya jirani na pale jumlisha na ukimya uliokuwa umetawala ungeweza kusikia mlio ule wa ndoo ya takataka.
Kai akatabasmu na kuinuka haraka na kujisemea kama anaongea na mtu pembeni yake laiti ungemsikia.
“Ahsanteni sana wateja wangu… Mmenikaribisha vyema sana, mkanipa changamoto na kunipasha moto misuli… Mmenipa pa kuanzia Agent Kai”
ENDELEA SEHEMU YA SITA..!
Ule mlio wa ndoo ya taka taka (dustbin) uliwafanya vijana wawili kusogea dirishani wakiwa dirisha la sebuleni na kuchungulia kwa chini ya ghorofa.
“Aisee ameruka … Ameruka toka juu hadi chini…. Mama aaah! Hivi huyu ni mtu au jini?” Alisema mmoja kwa sauti kubwa yenye mshangao na kusababisha hadi mwingine aliyekuwa analinda ngazi za kushukia sebuleni hili Agent Kai asije akataka kuwafuata sebuleni na nia kuu ikiwa kumdhibiti abaki ndani ya chumba. Mshangao mkuu! Macho pima!
“Unasemaa aah!” Alikimbia kasi hadi pale dirishani wote wakawa wanachungulia kwa tabu kutokana na kona iliyo kali kuelekea barabarani iliyowazuia kuona vizuri uelekeo wa barabarani. Agent Kai alikuwa anapotea kwa tahadhari ya kuangalia huku na huko. Mshangao mkuu kwa jamaa.
“Eeeeh… Kama mlikuwa hamjui kuwa movie uwa ina star na maadui ndiyo mtajua safari hii” Mmoja aliye mfupi kuliko wote kati ya wale wanaume wa makamo wa kimalaysia, yaani vijana wanaoondoka kwenye ujana kwenda utu uzima miaka thelathini na tano kwenda arobaini, wote walikuwa rika moja hadi wale ambao Kai alikuwa amefupisha uhai wao muda si mrefu.
“Mbona wale wengine tuliwaweka chumba kile kile tena wote wawili na kamba hatukuwafunga tukawakuta asubuhi wako vile vile… Katokaje?... Ina maana huyu mtu mweusi kawazidi akili kwa mbali wale wazungu?” Akauliza mwingine huku kajishika kiuno kuonyesha dhahiri amechoka.
“Jamani ameshaenda… tuji ji pange tuta mwambi aje …shiiih, shiiiih… Ebu ni, nisai… idieni jamani, dam, damu inazidi kuisha mwilini” Akasema kwa tabu aliyepigwa risasi ya bega na kuvunjwa mfupa mkubwa unaounganisha bega na kifua, alikuwa akisikia maumivu makali sana maana uso wake ulijidhihiri pakubwa kile akisikiacho katika mfupa uliovunjwa.
“Itabidi tumuite daktari haraka sana aje akusaidie… kwa sasa tukufunge jeraha lisizidi kumwaga damu.. !” Akasema aliye mfupi zaidi ya wote akiwa na kichwa kikubwa chenye nywele nyingi zilizomwagika pande zote za kichwa chake na sura yenye kutisha sababu ya macho yake kuwa makali sana akuangaliapo, alifika alipo majeruhi wakiwa wamemlaza pembeni ya zulia lililo sebuleni.
“Awan chana kipande cha pazia lete tumfunge hili tuzuie damu… Damia tutampigia baada ya kufanya ukaguzi huko juu tukaona kwa macho nini kakifanya katika vyumba yule mtu mweusi” Akasema kwa sauti yake nzito inayotoa mkoromo mzito Jeong Low ama kwa jina lingine alifahamika kama Mr. Malaysia.
Awan ambaye muda wote alikuwa kajishika kiuno akiwa haamini kilichotokea muda si mrefu, sarakasi za kimiujiza na mtu kuruka kutoka dirisha lililo umbali wa floor tatu wa jengo lao hili. Aliacha kuzubaa kule akasogea dirishani lilipo pazia akachana kwa kutumia kuvuta kwa mikono kiasi alichoona kinafaa na kusogea pale walipoinama Jeong Low na kamtu kafupi kanachotisha kutokana na mazoezi ya vyuma anayopiga kwa nguvu sana alizidi kutisha.
Walifanikiwa kumfunga kiasi kilichosababisha damu isiwe inatoka kwa kasi ile ya kwanza pia wakamnyanyua na kumpeleka kumlaza kwenye sofa kubwa.
Awan ambaye kidogo alikuwa ana idea ya mambo ya utabibu akamchoma sindano ya ganzi hili kutuliza kidogo maumivu anayosikia ndugu yao katika maisha yao ya ujanja ujanja.
“Pumzika hapa Krish… Ngoja sisi tucheki juu huko kuona kipi kakifanya yule mtu kwa ndugu zetu Nabeel na Scorpion… Kisha tutoe taarifa kwa Damia aje na daktari kwa ajili aweze kukutoa risasi maana kama unavyoona imenasa mfupani na ndiyo inayokuletea maumivu makali” Akasema tena Jeong akaangaliana na Awan kisha mtu mfupi kwa pamoja wakaelewa nini kifuate? wote wakainuka na kupanda ngazi kuelekea juu kwenye vyumba ambavyo Agent Kai walimkuta akitokea chumba cha aliye marehemu sasa kiongozi wao Mr Nabeel.
Awan Razal a.k.a Fighter bingwa wa zamani wa ngumi za kulipwa ndiye aliyekuwa kastuka kuwa Kai hayupo katika chumba walichomuingiza na kumuweka kama selo yao wao SDB, Katika chumba kile kuna kamera moja inayochukua live matukio ya mule wanapomuweka mateka mtu basi uruhusu kamera iliyomo mule kuwa active, ilikuwa adhana iliyoadhiniwa toka msikiti wa jirani na eneo la Nadau Golf ilimuamsha huyu bingwa wa zamani wa ngumi za kulipwa katika Malaysia na eneo la kusini mashariki mwa bara la Asia.
Hawa wote wanne ni wapenzi wa kucheza mchezo wa Play Station Game katika screan kubwa wakifanya kama mashindano kati yao, uwa kawaida yao kila inapofika usiku kabla hawajalala kwenda katika chumba kilicho na mitambo yao mbalimbali ya kiteknolijia ikiwemo tv kubwa nchi thelathini na mbili iliyounganishwa na kamera inayoonyesha kile chumba walichomfunga kamba kwenye kiti na kumfungia Agent Kai pia ilikuwa inachukua na eneo lote la chini linalozunguka jengo lile mpaka barabara ya kuingia eneo la jengo lao.
Walicheza game siku hiyo kama ilivyo kawaida yao katika chumba ichi kilicho mkabala na sebule (floor moja) mpaka walipoamua kulala mule mule kwenye chumba kile ambacho kina masofa mawili makubwa ya kukaa watu wawili wawili pamoja na zulia lililotambaa chumba chote na kompyuta kama nne, screan kubwa za runinga nazo zikiwa kama nne kila pande ya ukuta kwa juu kati ya kuta zote nne za chumba.
Pia ilikuwa ni lazima walale hata kama hawana wasiwasi na mateka wao lakini wasingeweza kuzima screan inayoonyesha chumba kile ambapo palikuwa na giza lakini wao walipoweka kiti walikuwa wanapaona vizuri tu.
Ile adhana ilipomstua Awan Razal na kuwa kwake karibu na screan ile cha kwanza aligundua kiti hakina mtu, akawaamsha wenzake nao wakahakiki ni kweli, wakarudisha nyuma recorded ya kamera na kuona alivyovifanya Agent Kai kwa tabu kutokana na wao kufanya uzembe wa kuzima taa za chumba kile.
Haraka wakachukua bastola zao na kutoka kwa tahadhari kwenda juu vilipo vyumba vyao vya kulala waliogopa kwenda bila tahadhari wasije wakakutana na Kai mpaka walipofika kwenye kona ile yenye mwisho wa ngazi za kutokea sebuleni ndipo aliyekuwa mbele kajibanza kwenye kona alimuona Kai akitoka katika chumba alichomchinja yule aliyempiga na kitako cha bunduki ambaye alikuwa akiitwa Nabeel na pia kumgonga ngumi nyepesi na kumziraisha mwanadada mpenzi wa marehemu Nabeel.
Walipomuona wakakubaliana haraka wamstue kwa kuwasha taa kisha wamuombe ajisalimishe lakini walipigwa na butwaa ya mwaka kwa kilichotokea.
Mtu mfupi akiongoza msafara kwa kasi allingia chumba cha Nabeel, chumba cha mwisho kuingia Agent Kai na pia kukitumia kuondoka katika jengo kwa kuruka toka juu dirishani.
“Shiit!” Alipiga yowe kubwa mpaka wenzake nao wakaingia kwa kasi na pupa mpka wakawa wanagongana vikumbo kuona amestuka nini mtu mfupi.
“Vipi Mabrouk?” Akauliza Jeong huku akimsogeza mtu mfupi hili ampishe aliyemtaja kwa jina la Mabrouk.
“Ooooh…. Uuuuh…. Amemchinja Nabeel …!” Akajikuta akipayuka Jeong huku machozi yakifuatia kwa haraka sana, Mabrouk akasogea karibu zaidi na kuchungulia kwa pembeni alipo mwanadada aliyezirai.
“Saky naye sijui kamuua? Damu imemtapakaa mwili mzima!” Akasema Mabrouk.
Jeong alitoka mbio kuondoka kwenye chumba kile na kuwaacha Awan na Mabrouk, mbio zilimpeleka hadi chumba cha kwanza alichoingia Agent Kai na kumvunja shingo kwa karate mpaka kumuua mwenyeji aliyemkuta kalala katika chumba.
Jeong alifunga breki kali ya miguu yake pembeni ya kitanda alicholala marehemu na kwa pupa alimshika shingoni na ubaridi aliokutana nao ulimfanya amiminikwe na jasho mwili mzima licha ya kuwa asubuhi hii kulikuwa na baridi la kibaridi cha asubuhi. Alijikuta akidondokea matako na machozi kuongezeka maradufu, chumba kikavamiwa na kina Awan nao wakiwa kwenye kasi wakamkuta mwenzao kaka chini analia kilio cha sauti iliyojaa masikitiko makubwa.
“Amemuua mdogo wangu…. Haaah, amemuua Jack wangu” Akasema Jeong Mr Malaysia.
“Pole sana Jeong… Inauma sana … Sikujua kama siku moja kazi hii itatupotezea ndugu zetu, hii inamaanisha na sisi tungekuwa tumelala kwenye vyumba vyetu angetumaliza wote”. Akasema Awan.
“Huyu mtu jamani tusije thubutu kumfuatilia tena ni mtu wa hatari sana” Akajikuta anasema Mabrouk na wenzake wote wawili wakageuka kumtizama.
“Mab! Wenzetu wameuliwa…. Kinahitajika kisasi… Hawa ni ndugu zetu… Jack ni mdogo wangu baba mmoja… Naombeni tusirudi nyuma, huyu mtu tusimkamate na kumuweka kizuizini ni wa kumuua tu kama alivyoua ndugu zetu” Akasema kwa uchungu mkubwa Jeong huku akifuta machozi. Maajabu ya mtu ambaye alipenda kuona wasiomuhusu wakiumia kulia machozi! Mshangao!
“Lakini Mr Logan anamtaka akiwa mzima kama wale wengine tuliowakamata na kumkabidhi” Akasema Awan.
“…Sihitaji hilo tena, nchi hii ni yetu, sisi ni wa Malaysia pia tuna maamuzi… Logan anatutumia kwa faida yake….. Kwa hili atatusamehe hatutamjulisha nia yetu tutafanya kazi kwa ushirikiano na siri kubwa tukimuwinda mtu mweusi yule na tutamuua kama bahati mbaya kumbe ni kisasi, tutamtafuta kila kona za mji huu nasi tukamuonyesha kile tulichonacho… Hawezi pigana na sisi yule nasi tunavyo vya kujivunia katika mapigano hasa ya ana kwa ana”. Akaongea tena Jeong akiwa kakunja sura na kumfanya atishe jasho na machozi yakiwa yamesambaa usoni huku tayari akianza hatua za kuondoka katika kile chumba.
** *** ***** *****
Saa nane kasoro dakika kumi na mbili mchana ilimkuta Agent Kai akiwa kitandani, ndiyo anastuka toka usingizini baada ya kulala kwa takribani masaa matano na usheei hivi usingizi wa mchana siku ya alhamisi, siku ya kwanza ukiacha usiku wa saa mbili na nusu jana alioingia KL na kupokelewa katika domo la mamba kisha kuchomoka kikambale.
Saa mbili na nusu asubuhi ya siku hii ya alhamisi ilimkuta ndiyo anaingia katika viunga vya hotel hii ambayo amepanga, baada ya kuondoka mtaa wa Nadau Golf alipowatoroka kwa stahili ya kipekee watekaji wake alitembea kwa miguu mpaka alipopata taxi na kukodisha ikampeleka mpaka mtaa wa Rodger Street, barabara ya Jalan Hang Kasturi akamuomba dereva amuache hapo Rodger Street baada ya malipo akajifanya anatafuta kitu katika moja ya nyumba za mtaa ule, alipohakikisha taxi ile ishatokomea akakodi taxi ingine iliyomfikisha hadi karibu na hotel hii aliyomo sasa kitandani akijigeuza geuza kwa uchovu wa kutokulala usiku uliopita.
Ilikuwa bahati asubuhi ya siku hii kulikuwa hamna traffic jam ikamsaidia dereva wa taxi aliyemleta kumuwaisha, hotel hii iitwayo Alamanda Hotel iliyopo karibu na eneo la Sepang kilipo kiwanja cha ndege cha KLIA, wilaya ya Persekutuan ni mwendo wa dakika ishirini tu kwa gari kutoka uwanja wa ndege na ndipo hasa alipanga itakuwa hotel yake ya kwanza kupangisha atakapofika tu Kuala Lumpur ni hotel iliyojengwa kwa stahili ya majengo pacha kukiwa na jengo la kulia liitwalo Square A na jengo la kushoto liitwalo Square B, alivutiwa na hotel hii baada ya kutizama ramani ya jiji la Kuala Lumpur wakati anapewa jukumu la kuja nchi hii kufanya kazi iliyomleta.
Alijiinua pale kitandani na kumshukuru Mungu kwa dua yake anayoipenda kuiomba kila aamkapo katika imani yake ya kiislamu, kisha akashuka kitandani na kupiga push-up na mazoezi mengine ya viungo za idadi ambayo uridhika kila afanyapo mazoezi mepesi na ilimchukua takribani dakika kumi kisha akaenda maliwatoni kujiswafi kwa kuoga na kuswaki, dakika kumi na tano zilitosha kumfanya akawa msafi, mwenye nguvu mpya kutokana na maji yaliyopita kwenye mwili wake.
Alipotoka akiwa kajifunga taulo akaenda kukaa kwenye sofa moja pekee lililo chumbani mule katika hii hotel ambayo vyumba vyake vipo ki appartiment (chumba, choo bafu na sebule)alikuwa akijisikia njaa na ndiyo haswa iliyomfanya kuamka usingizini. Lakini hata akiwa katika hali gani uwa kila anapolala na kuamka katika kuianza siku yake mpya baada ya mazoezi kidogo, kuoga na kuswaki ufuata kupiga simu kwa mzazi wake aliyebakia kati ya wazazi wake wawili, mama yake mpendwa.
“Habari za mchana?”.Akasema mara tu baada ya kupiga simu ya huduma kwa wateja ya hoteli hii.
“Nzuri tu mteja wetu…. Leta habari?”
“Chumba namba 105, square A… Naomba kupiga simu nje ya nchi”
“Unapiga bara gani?”
“Nataka kuongea Afrika nchi ya Tanzania, bara la Afrika”
“Ok, dakika tano nitairuhusu utapiga” Akajibiwa na kisha simu ikakatwa. Alisubiri dakika sita kisha akabonyeza namba za simu ya mkononi ya mama yake anayeishi mkoa wa Morogoro nchi ya Tanzania barani Afrika. Simu ilianza kuita hapo Agent Kai alianza kutabasamu kabla hata haijapokelewa na muhusika ambaye ni mama yake mzazi.
“Halloo…!” Akastuliwa na sauti ya mama ake.
“Mama, mama yangu mpendwa… Asallaam aleykuum!”.
“Mwanangu mpendwa… Waleykuum sallaam warahmaturah wataallah wabarakatuh!…mzima mwanangu?”.Sauti ya furaha ilijibu toka kwa mama yake.
“Mzima mama yangu, shikamoo! Na vipi hali yako mama?”.
“Hali yangu nzuri mwanangu, leo sikuwa na raha mwananguumenizoesha vibaya miezi miwili mfululizo unanipigia simu asubuhi tena kila ifikapo saa nne kwa saa za huku afrika mashariki… Kulikoni leo mwanangu?”.
“Mama ukiona hivyo ujue hali ni tofauti… Huoni sijapiga kwa namba zangu nimepiga kwa namba nyingine tena zikiwa na code isiyo ya Marekani”.
“Eeeeh … Huko wapi tena?”.
“Nipo Malaysia mama… Nimekuja kikazi mama yangu”
“Umerudia kazi yako au kama ulivyosema umepumzishwa zile kazi zako za hatari”.
“Sijarudi tena bado nipo ofisi ya makamu wa Raisi naongoza kikosi cha ulinzi, sasa nimekuja huku naandaa usalama wa ziara atakayoifanya nchi hii lakini si salama sana hivyo naomba dua zako”.
“Mmmh! Au umerudi tena kule hatarini?.. usinidanganye jamani”
“Usihofu mama… kawaida tu si unajua mwanao nilivyo, ulinizaa na ujasiri mkubwa sana”
“Usiniambie hivyo Kai… Wewe ni msomi mwanangu kwanini usitafute kazi za kutulia ofisini, huko Marekani ulipo ajira zipo kwa wingi hasa kwa elimu uliyonayo… Au hao watu weupe wamekutisha ukiacha kazi wanakuua?”
“Hamna mama…. Lakini sipo katika hatari mama… Nimekuja hapa kwa shughuli ya kuweka mambo sawa tu halafu narudi Marekani na nikirudi nakuja huko nakuletea na wajukuu zako uwaone” Agent Kai halikuwa hapendi kumwambia mama yake kama yupo katika kazi zake kama hii iliyomleta Kuala Lumpur lakini upenda mama yake ajue yupo nchi gani na umuomba amuombee dua, mara zote umwambia mama yake yeye kaacha kazi za kijasusi na kumwambia yeye ni kiongozi wa kikosi kinachomlinda makamu wa Raisi na hapa kama tulivyoona alimwambia amekuja nchi hii kuweka sawa mambo kabla makamu wa Raisi hajaingia nchi hii.
“Upo nchi gani mpaka unasema si salama?”.
“Niko Malaysia, kusini mashariki mwa bara la Asia”
“Haya mwanangu kama una uhakika na unachoniambia ila kuwa makini sana… familia inakutegemea … Watoto wako bado wadogo sana hawataweza bila uwepo wako, watoto mpaka leo hujawatafutia mama atakayewalea katika maadili ya dini yetu”. Akasema mama huku sauti ikionyesha jinsi gani anampenda mwanae.
“Mama nakuahidi nitakuwa makini kuliko unavyonijua mwanao katika suala la kuwa makini, pia nakuahidi kuwatafutia watoto mama yao atakayewapenda kama vile ni watoto wake wa kuzaa”. Akamtia moyo mama yake.
“Nashukuru kwa ahadi, nakuombea dua na wewe usiache kujiombea dua na kumuombea dua baba yako mzazi huko alipo apumzike mahala salama”. Akasema tena mama kwa upendo wa hali ya juu.
“Sawa mama… Naomba nikuache upumzike salama, mimi nina njaa acha niagize chakula nitakutafuta kesho tukiamshwa salama wote na yule aliye muweza wa yote”
“Inshaallah mwanangu…. Mungu wetu ni mwema atatufanya tutaongea tena hiyo kesho”
Walimaliza maongezi yao wakaagana na kisha Kai akakata simu na papo hapo akapiga tena huduma kwa wateja.
“Tena chumba namba 105, square A…. Naomba muhudumu aje nina shida inayohitaji msaada wake” Akasema na kushusha risiva ya simu kwenye kipachiko chake.
Dakika kumi na moja mbele kengele iliyopo sebuleni inayojulisha kuna mtu mlangoni iliita mara mbili, haraka akaenda kufungua mlango. Harufu nzuri ya manukato ndiyo kitu cha kwanza kilichompokea toka kwa binti muhudumu aliyesimama pale mlangoni, alikuwa ni binti mzuri wa kiarabu na ninaposema mzuri ni mzuri haswa tena haswa, ni mrembo wa sura aliyevaa kistara akiacha uso pekee uonekane, umbo lake ni katika yale maumbo ya kiarabu yanayovutia sana ingawa alikuwa kavaa nguo ndefu iliyomfunika kichwani akiwa na hijabu.
Agent Kai alibabaishwa na uzuri ule mpaka akameza mate baada ya kuukubali uzuri ule alionao binti huyo.
“Asallaam aleykuum!” Binti akasalimu kwa sauti ambayo mwanaume yoyote angeisikia ingeleta shida maana iliongezwa utundu kwa kuongelewa kwa toka puani.
“Waleykuum sallaam warrahmatullah wataallah wabaraka tuh!” Ikamlazimu Kai kuirefusha salamu kwa sababu anazozijua yeye huku akitabasamu, ikamfanya binti naye kutabasamu. Aisee hatari meno ya binti yalikuwa meupe yenye kung’aa na yaliyopangika vizuri kama yeye aliyeyapanga yakiundiwa na mwanya uliofanya Kai komando na jasusi wa hali ya juu kabisa mapigo ya moyo ghafla yalipokea damu katika hali ya tofauti kidogo.
“Na… Nai… naitwa Shufania…. Shufania Mahamud…! Ni muhudumu wa hotel hii katika vyumba vya korido hii iliyopo chumba ulichopanga upande wa Square A… Kama, kama….. Kama unavyoona sare niliyovaa, nimeitikia wito wako boss!” Akajitambulisha binti kwa Kai akitumia kiingereza ambacho mimi na wewe hatuna haja nacho sana hapa labda ikilazimu {twende zetu}
Mwisho wa sehemu ya sita (06)
Six Dangerous Boys (SDB) hasira tele kwa mtu mweusi kama wenyewe walivyoamua kumpa jina lenye wasifu wa aina ya rangi ya kibinadamu aliyonayo Sajenti wa zamani wa jeshi na komando wa US, Navy Seals Agent Kai.
Jeong Low ‘Mr. Malaysia’ akiwa ni mwenye hasira kuu, akijiapiza na kumlipizia kisasi mdogo wake na kuwahamasisha wenzake kuhakikisha wanatumia kila aina ya mbinu kumpata Agent Kai na kisha naye kulipa walichoamini kuwa hawakustahili wao kufanyiwa.
Shida ya kutoamini kuwa na wao hutokea kufanyiwa iliwakwaza sana na kumkwaza zaidi ‘Mr. Malaysia’.
Je watafanikiwa katika kusudio la kisasi kwa mtu waliyemuanza wenyewe?
Subira itajibu hili, majibu yatakuja SDB vs ‘The Sole Cat’ nani anaangukia pua..!
Agent Kai ‘The Sole Cat’ bingwa wa minyapio tayari ameamka baada ya mapumziko ya usingizi akiwa katika hotel ya Alamanda.
Yajayo kwake yatazidi kukufurahisha, twende tuone itakuwaje upande wake katika msako huu wa hatari wenye Mshangao.
Dakika kumi na moja mbele kengele iliyopo sebuleni inayojulisha kuna mtu mlangoni iliita mara mbili, haraka akaenda kufungua mlango. Harufu nzuri ya manukato ndiyo kitu cha kwanza kilichompokea toka kwa binti muhudumu aliyesimama pale mlangoni, alikuwa ni binti mzuri wa kiarabu na ninaposema mzuri ni mzuri haswa tena haswa, ni mrembo wa sura aliyevaa kistara akiacha uso pekee uonekane, umbo lake ni katika yale maumbo ya kiarabu yanayovutia sana ingawa alikuwa kavaa nguo ndefu iliyomfunika kichwani akiwa na hijabu.
Agent Kai alibabaishwa na uzuri ule mpaka akameza mate baada ya kuukubali uzuri ule alionao binti aliye mbele yake.
“Asallaam aleykuum!” Binti akasalimu kwa sauti ambayo mwanaume yoyote angeisikia ingeleta shida maana iliongezwa utundu kwa kuongelewa kwa toka puani.
“Waleykuum sallaam warrahmatullah wataallah wabaraka tuh!” Ikamlazimu Kai kuirefusha salamu kwa sababu anazozijua yeye huku akitabasamu, ikamfanya binti naye kutabasamu. Aisee hatari meno ya binti yalikuwa meupe yenye kung’aa na yaliyopangika vizuri kama yeye aliyeyapanga yakiundiwa na mwanya uliofanya Kai komando na jasusi wa hali ya juu kabisa mapigo ya moyo ghafla yalipokea damu katika hali ya tofauti kidogo.
“Na… Nai… naitwa Shufania…. Shufania Mahamud…! Ni muhudumu wa hotel hii katika vyumba vya korido hii iliyopo chumba ulichopanga upande wa Square A… Kama, kama….. Kama unavyoona sare niliyovaa, nimeitikia wito wako boss!” Akajitambulisha binti kwa Kai akitumia kiingereza ambacho mimi na wewe hatuna haja nacho sana hapa labda ikilazimu {twende zetu}
ENDELEA NA DODO…!
“Ahsante sana mrembo, naitwa Ramsey Bronze natokea Marekani… Nimefurahi sana kukujua… Pita ndani tuongee kuna maelekezo kidogo nahitaji kukupa nawe ukanisaidia”.
“Samahani kama nitakukera kwa ombi langu”.
“Bila samahani mrembo, karibu” Akajibu Kai huku akimuonyesha ishara ya mikono yote miwili kuwa yupo huru kufunguka anachoomba.
“Unaweza kunielekeza tukiwa hapa hapa mlangoni?.. Samahani sana lakini”
“Inawezekana tu lakini naomba uniamini kuwa hakutakuwa na jambo lolote baya, tafadhali naomba unipe nafasi tukaongea tukiwa sebuleni… Naweza nikalipa juu ya hilo”
“Samahani sana kaka, naogopa sana sababu lilishawai kunitokea tatizo kwa mwanaume anayetoka katika nchi unayotoka si kama napenda kuogopa” Akajitetea Shufania utetezi wenye mashiko makubwa.
“Kwahiyo kila mwanaume toka Marekani ameshuka thamani kwako kwa sababu ya mwananume mmoja toka Marekani?” Agent Kai alimuuliza tena huku akionyesha sura ya masikitiko kwa binti.
“Hapana si kama nimewashusha thamani… Ukweli nina uwoga mkubwa sana… Na nimeacha kabisa kuingia katika vyumba hivi kukiwa na mtu mmoja hasa mwanaume si wa kutoka nchi unayotoka tu bali nchi zote mpendwa wangu…. Naomba nikuamini lakini tafadhali naomba nithamini mimi binti wa kiislamu nahitaji kuheshimiwa kama navyoheshimu watu wengine”. Binti aliongea maneno yaliyogusa moyo wa Agent Kai mpaka akajiuliza huyo muhuni wa kutoka nchi anayotoka alimfanyaje binti huyu mzuri wa kuvutia, akatamani ajue lakini aliona yashapita na atakuwa anafukua kaburi asiloweza kulifukia kwa namna yoyote ile.
“Pole sana … Pole sana Shufania, nafikiri ni jinsi gani uliumizwa na jambo lililotokea… Naomba msamaha kwa niaba ya wamarekani wote… Tafadhali pokea msamaha wetu, hususani wanaume wote wa Amerika” Kai aliongea huku kakutanisha viganja vya mikono yake akataka kupiga magoti papo hapo Shufania Mahamud alimkamata mkono kumzuia na kumuonyesha ishara wapite ndani ya sebule, wote wakaingia sebuleni.
“Karibu uketi kwenye sofa binti… Shufania!”. Kai akamkaribisha kwenye sofa lililo mbali mbali na sofa alilokaa yeye huku akijaribu kumuonyesha uso wa tabasamu ambapo kiukweli na yeye alikuwa anajua kutumia uzuri alionao na taratibu binti aliondokewa na uwoga akawa anaingiwa na kuvutiwa na mtu anayemuona mbele yake kwa macho yake mazuri yanayomuangalia kwa kuibia ibia kana kwamba si mfanyakazi wa hotel, maana wafanyakazi wa kike wa hotelini asilimia 95 walikuwa makauzu haswa.
“Ahsante sana… Mimi ni mwenyeji pia kwahiyo na wewe karibu Alamanda Hotel”. Akajibu na wote wakatoa kicheko kidogo.
“Unaonekana ni mwarabu… niko sahihi?”. Akaongea Kai kuuliza baada ya sekunde thelathini kupita.
“Yes! Mimi ni mwarabu wa Syria ni mkimbizi tuliyeamia nchi hii miaka mitatu iliyopita na familia yangu kukimbia vita Syria”. Akajibu Shufania huku akijitahidi kukwepesha macho yake kuangaliana na macho ya Kai ambaye anatokea katika nchi yenye tamaduni ya kimaongezi watu kuangaliana machoni muda wote wanapoongea labda itokee kitu kingine.
“Pole sana kwa masahibu hayo…!”.
“Ahsante sana … Katika kazi kama hii niifanyayo majaribu hayakosekani kaka yangu na ni changamoto kuu kwa kweli”.
“Kwa kweli … Maana yeye ndiyo upanga hili na hili tena katika ratiba anayoitaka yeye” Akasema tena Agent Kai na kujiweka vizuri kwenye sofa, macho yakiwa yanajiuliza hivi yanachokiona mbele ni chenyewe au ni nini?. Akakohoa kidogo kikohozi cha kujilazimisha kisha akameza mate maana binti alikuwa kainamisha sura yake chini mkono wa kushoto ukichezea bangili za urembo alizovaa mkono wake wa kushoto kwa kutumia vidole vyake vya mkono wa kulia.
“Kwanza napenda nitoe shukrani za dhati kwa kunikubalia kuingia hapa katika sebule hii…. Najua dini inakataza kwa binti asiye ndugu wa damu wa mwanaume husika kuwa na mwanaume katika chumba wakiwa wenyewe bila mtu mwingine… Kwa hili naomba unisamehe sana na tumuombe Mungu atusamehe kwa kosa hili”. Akavunja ukimya wa dakika mbili uliotaka kutawala kizembe mule ndani kwa yeye kuzubaa kushangaa uzuri wa binti wa kiarabu aliyekaa sofa linaloangaliana na sofa alilokaa yeye.
Aliponyamaza macho yao yaligongana maana Binti Mahamud aliinua macho yakagongana na ya Agent Kai kisha vile vile alivyo aliyaondoa haraka sana na kuachia tabasamu dogo usoni mwake akiwa na kitu ambacho uwakuta mabinti wengi wanapokutana na Agent Kai.
‘Hii sauti ya huyu mwanaume imenivutia sana, anaongea kwa sauti ambayo ni sauti ya ndoto zangu’ Alijiwazia Shufania huku akitamani ndani ya hisia zake aendelee kuwa mahala pale hivyo hakuongea kitu akainama tu kuangalia zulia zuri la rangi ya kijivu lililotandikwa pale sebuleni.
“Naamini umepokea shukrani zangu kwa moyo mkunjufu…. Kama nilivyokwisha jitambulisha kwako naitwa Ramsey Bronze nipo hapa Kuala Lumpur katika shughuli fulani muhimu katika ubalozi wa Marekani, ni Mmarekani ninayeishi jiji la Washington DC, lakini nina asili yangu ambayo ndipo nilipozaliwa pale Marekani mimi ni mhamiaji tu…!” Akatoa maelezo Agent Kai huku moyo wake ukitamani awe mkweli kwa huyu binti lakini papo hapo mawazo hayo yalijipinga yenyewe kwenye ubongo wake wenye kuchuja habari ziingiazo na zitokazo, amekutana naye dakika zisizodhidi kumi na tano pia sheria ya kazi yake inasema usimuamini mtu yeyote awaye mpaka uhakikishe kweli huko sahihi kufunguka kwa huyo mtu pengine yupo mikononi mwako na una uhakika hatoki mikononi.
“Nimepokea kaka yangu” Akajibu Shufania kwa sauti ya chini huku akiendelea kuchezea bangili zake nzuri sana na kuleta milio fulani ya kutia burudani masikioni kwa wakati fulani na ka karaha pia kama mtu anahitaji utulivu.
“Asante sana binti…. Tuje kwa nilichoomba muhudumu afike juu chumba hiki muda huu… Kwanza ningependa kujua kama hapa Alamanda hotel kuna huduma za kibenki za ATM?”.
“Ipo huduma ya Western Union na Barclays Bank kwa nyinyi wageni toka nje, pia ipo huduma ya bank ya Malaysia Bank”
“Okay! Vizuri sana, hotel yenu inajali wateja…. Ila kuna jambo nalohitaji msaada wako kama hautajali… Jana wakati nimeshuka Airport nilichukua basi treni ya mwendo kasi nikaenda shukia kituo cha KL Sentral baada ya hapo nikaenda ubalozi wetu nilipotoka kule ubalozini nikachukua taxi dereva akanipeleka hadi Batu Caves kuna kiongozi mmoja wa ubalozi wetu nilienda kuonana naye kule kwa bahati mbaya wakati nimeshuka niliacha mizigo yangu kwenye taxi wakati niliporudi kumuwai dereva kabla hajaondoka sikumkuta” Akatoa maelezo uongo Kai.
“Pole sana… Umetoa taarifa polisi?”. Kwa mara ya kwanza Shufania alimudu kumuangalia usoni Kai wakati anatoa pole yake na kuunganisha na swali ambalo yeyote mwenye busara angelipa kipaumbele kuliuliza.
“Sikulipa umuhimu wazo la kutoa taarifa polisi sababu sikuibiwa na taxi dereva bali nililisahau kwenye gari yake hivyo ningempa shida dereva yule kwa wana usalama ambapo si kitu kizuri kiubinadamu…. Muda mwingine uwa Mungu anatukumbusha kuwa makini kila tuendako na kuwa sisi binadamu hatujakamilika ndiyo maana tunausahalifu hata kama si wa mara kwa mara”. Akadhidi kutiririka uongo na kweli Agent Kai na alikuwa na kafuraha cha kupenda maongezi yaendelee ingawa kanjaa kalikuwa kanamuwanga tumboni lakini hakuijali.
“Hongera kaka kwa kuwa na utu huo, ni kweli uyasemayo” Akasema Shufania na wote wakatabsamu baada ya macho yao yaliyokuwa yanavutana katika hali isiyo kawaida kwa muda mfupi ule kugongana.
“Ahsante sana… Hii shati unayoiona nimevaa nilipewa msaada na yule afisa ubalozi wetu niliyeenda kumuona kule Batu Caves…. Shida iliyopo mbele yangu nisingependa mchana huu kuonekana mtaani nimelivaa hili shati lisilo langu hata kama aliyenipa alinipa kwa ridhaa yake lakini sijaridhika nalo bali niliridhika kama lipate kunistiri kwa usiku uliopita tu, upo hapo?”.
“Nipo na ninakuelewa vya kutosha, hivyo usihofu boss wangu” Akasema na kuingiza kautani Shufania hili apate kujipa moyo wa kumzoea Kai.
“Nakuomba unisaidie nipate laptop, simu, viatu pea mbili na nguo mbili tatu nne hivi…. Naomba wewe ndiye ukaninunulie baada ya mimi na wewe kuongozana hadi kwenye huduma ya ATM ya Western Union… Nitakulipa kwa kazi hiyo”
“Mmmh! Nisikudanganye, hilo jambo halipo ndani ya uwezo wangu… Hapa Alamanda sisi wafanyakazi tunabanwa sana kutoka nje ya hotel pale unapoingia tu zamu basi mpaka muda wa kutoka unapofika….. Hilo jambo lipo ndani ya watu wawili tu, meneja wa hotel hii au mmiliki wa hotel hii tu…. Labda ujaribu kuniombea ruhusa kwa meneja wa hotel, tena kwa kumpa pesa maana ni mtu anayependa pesa sana”
“Ahsante kwa kunikubalia ombi langu… Yupo ofisini muda huu?”.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment