Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

MBWA WA GETINI - 3

   

Simulizi : Mbwa Wa Getini 

Sehemu Ya : Tatu (3)


*****


Kabah alikuwa amezungukwa na vijana kama sita hivi na vijana wote hawa walikuwa na T-shirt nyeusi zenye kichwa cha mbwa alieachama,wlikuwa ni vijana wa kikundi cha mbwa wa geti wakiongozwa na Temba.


Temba alikuwa anamkabidhi Kabah majalada kadhaa alioyachukua kutoka kwa askari wasaliti waliokuwa ndani ya jeshi.


Kabah aliyatia moto huku akitabasamu.


“hakuna kosa lolote?” aliuliza Kabah.


“Hatuna huo utaratibu wa kuacha nyayo mkuu” alijibu Temba kwa kujivuna


Wakiwa katikati ya maongezi gari ya Burizozo rafiki mkubwa wa Kabah ikaingia na kisha akateremka akiwa na picha mbili kashikilia,alipokifikia kile kikundi akamkabidhi zile picha Kabah na kusema


“Hawa wameagizwa kutoka makao makuu na wataingia hapa usiku huu,watafikia hotel ya perugina”


Kabah alicheka kisha akachukua picha zile na kumkabidhi Temba,Temba akazitazama kisha akaguna jambo lililofanya macho yote yamtazame.


“Kama huyu kweli yupo basi anatakiww kufa ndani ya usiku wa leo kabla hajapiga hatua yoyote ile” alisema Temba


“unamfahamu?!”aliuliza Kabah


“Ndio”


Burizozo akamtazama Temba kisha akamsukuma kwa kidole cha shahada huku akisema


“mh unalipwa kwa kazi kama hii,sitaki kusikia unanbia upuuzi huo wafe leo ama kesho,kikubwa wafe”


Temba alimtazama Burizozo aliekuwa anamwagiza Temba kwa dharau ,alitamani amshambulie japo kwa kichwa tu lakini haikuwezekana na hakuhitaji hilo litokee kwa wakati huo.


Wakati Burizozo akiongea na vijana wa Temba na Temba mwenyewe,Kabah alikuwa anaongea na simu kutoka kenya,simu ile ilimchamganya,tayari Zedi alikuwa ameanza kuleta madhara upande wake,kwa hasira akaioki bastola yake na kumpiga risasi ya kifua kijana wa Temba na kumuua papo hapo,jambo lile likamkera zaidi Temba na hata vijana wake hawakuonekana kulifurahia ila wakapata ishara kutoka kwa Temba ya kuwa watulie wasifanye lolote wakati huo zaidi walimchukua kijana mwenzao na kuelekea kumpeleka kuzika na kikao kile kikaishia pale huku Burizozo akimchukua Kabah wakaingia ndani huku nyuma waliacha maagizo kwa vijana ya kuwashugulikia wapelelezi kutoka makao makuu.


***


Wakati Temba akiwadhani tukio lile halikuonwa na watu wengine alikosea sana.


Siku ya tukio


Watu wawili walikuwa wamekalia viti ndani mgahawa bora na wa kisasa uliokuwa pembeni kidogo ya mataa,mgahawa huu uliitwa Destination.


Walikuwa wamependeza huku muda mwingi nyuso zao zikiwa zimepambwa kwa tabasamu la upendo.

“u mzuri sana mwanamke wewe,yaani natamani uwe wangu milele” alizungumza mwanaume aliekuwa amekaa kwa kuelekea upande wa barabara.


“mh Ziga mpenzi acha kunipamba hivyo mwenzio naona aibu” aliongea mwanamke kwa madeko huku akiachia kicheko laini kilichousisimua mwili wa komando Ziga ambae kwa sasa anahudumu ofisi kuu hapo alikuwa likizo yeye na mpenzi wake huyo waliekutana kwenye hekaheka za kikosi cha pili.


“Mina sio siri umeuteka moyo wangu huwa natamani kuwa nawe kila sekunde itambaayo,pua zangu hunusa harufu ya ngozi yako hata kama ukiwa umbali wa anga ama haki…..”


Pah,pah..


Wapenzi wale haraka walisahau mideko yao na nyuso zao wakazielekeza kule walikosikia mlio wa risasi na hapo wakashuhudia mparanginyiko wa watu waliokuwa wanakatiza barabarani huku madereva nao wakinusuru roho zao kwa kuvunja sheria za mataa.


Ziga akasimama huku mkono wake ukiwa unaelekea kiunoni,lakini Sajini Mina akawahi kumshika na kumzuia na kisha akamwambia


“mpenzi sio kila muda ni kazi,tupo likizo tuwaachie wenyewe na yaezekana ni uporaji tu huo mmh”


Ziga akimtizama mpenzi wake huyo na pasi kusema kitu alikaa.


Ni wakati anakaa tu ukaanza tena mrindimo wa risasi na kitendo kile kikaibua mashaka kwenye fikra zao,maana gari moja imeshambuliwa na watu wa aina mbili tofauti.


Mrindimo ule ulipokoma,wakasimama na kuondoka maana hata wahudumu wa mgahawa ule haikujulikana walikoelekea.


Ni wakati wanaanza kundoka ndipo wakashudia magari mengi ya polisi yakifika eneo lile na ulinzi kuimarishwa.


“Hebu ngoja niangalie kuna kitu gani kinaendelea pale” alisema Ziga huku akishuka ndani ya gari na kujichanganya na raia waliokuwa wameanza kujaa eneo lile.


Katika machache alionasa ni kuhusu faili lililopotea na pia alijua walioshambuliwa ni askari wa mkoani,Ziga aliona awaachie wenyewe akarudi ndani ya gari kisha wakaondoka kuelekea kwenye hotel waliofikia.


Usiku wa siku hiyo uliwakuta wapenzi wale wakiwa wanaogeshana ndani ya hotel kubwa na ya kisasa ilioko pembeni kidogo ya mji,hotel ya perugina.



Nb:wakati huu wa Ramadan tujaribu kufungua nyoyo zetu katika kuonesha tupo pamoja kila hatua

Utaonekana mnafiki na dhambi itakuandama kama kila siku unasoma hapa afu hata hukoment wala hulike.

Ila unangoja shetani akutumie siku nikiwa kimya kwa sababu mbalimbali basi uje hapa kutukana na kukejeli......


Zika unafiki leo sapoti kazi zetu waandishi hata kama haijakufurahisha sema ili tuumize kichwa kukufanya utabasamu kila usomapo





Usiku wa siku hiyo uliwakuta wapenzi wale wakiwa wanaogeshana ndani ya hotel kubwa na ya kisasa ilioko pembeni kidogo ya mji,hotel ya perugina.


Wapenzi hawa walikuwa wanyoana via vyao vya uzazi,huku wakitomasana hapa na pale kwa uchu wa ngono.


Zoezi lao la kutomasana,kuogeshana na kusafishana,lilikamilika huku likiwa linawalazimisha kuingia kwenye zoezi lingine.


Ziga akambeba Mina kisha akaichomeka saundi na kuanza kupampu huku akipokea sauti ya wizi kuribu na masikio yake.


Zoezi lile alilifanya kutokea bafuni hadi kitandani kisha akambwaga Mina huku wololo yake ikiwa imesimama kwa uchu ikitamani kuzama kwenye sangulo ya Mina.


Ziga alipanda kitandani na akamshika Mina,lakini kwa makusudi Mina akatoa sauti ya Madeko eti anaogopa wololo ya Ziga.


Ziga nae kwa uchu akawa anataka kulazimisha maana maji yalikuwa yamezidi kingo,lakini akakuta Mina akiwa amebana upaja.


Loh wanawake wamejaliwa uwezo wa ajabu,na nguvu zote za Ziga ila alikwama kupanua mapaja ya mpenzi wake huyo aliekuwa anamfanyia kusudi ili mradi tu ilikuwa ni mbinu ya kutia hamasa kwenye mtanange ambao Mina aliamini utamwacha hoi na sangulo yake ikiwaka moto.


Ziga ikabidi awe mpole aanze kubembeleza apewe Sangulo.


“Mpenzi niachie kidogo basiii mmh!!”


“Aku sitaki leo niache mhm!!”


“Bebi niachie kidogo basi hata kichwa tu kiingie…!!”


Mina huku akitabasamu kwa mbali akajibu


“ Aha wololo yako haina mabega bwana itazama yote mh””


Ziga aliyadaka maziwa ya Mina yaliokuwa yamesimama kama papai changa juu ya mti wake akayatia mdomoni na hapo akaona miguu ya Mina ikichanua nae bila ajizi akaushika uwololo wake na kuupeleka kunako sangulo na kilichofuata si kuingiza kichwa tena ilikuwa ni watu kucheza ekibinda nkoi.

*****



Mina alikiweka kichwa chake kifuani kwa Ziga huku mikono yake laini ikipapasa kifua kile kipana na usingizi ulimpitia huku Ziga akiwa anapapasa kishudu cha Mina taratiibu na mawazo mapya yakikkfikia kichwa chake


Alimkumbuka Zedi


Taratibu akamweka pembeni Mina na kushuka kitandani kisha akaifuta simu yake na kuzitafuta namba za Zedi,lakini hazikuwa zikipatikana,akaamua kupiga namba za Tausi mke wa Zedi,nazo hazikupatikana na hakutilia shaka sana,akajivuta taratibu na kurudi kitandani huku macho yake yakiwa juu ya mwili wa mwanamke wa ndoto zake Mina.


Alikuwa hajapata hata lepe la usingizi simu ya Mina ikaita,akasonya huku akienda kuipokea ama kuizima kabisa,lakini aligairi baada ya kuona jina la mpigaji likiwa limeandikwa Chief


Haraka alimwamsha Mina.


Simu ile ikabadili kila kitu ndani ya likizo yao na ikaibua mapya na mageni masikioni mwa watanzania na waafrika kiujumla.


****


Zedi alikuwa anauacha mji wa Nyeri huku akiwa ni abiria asie maalumu ndani ya gari la kubeba mizigo aina ya fuso.


Lakini aliona tofauti nyusoni mwa wenyeji wake ambao kila mara walikuwa wakimtizama kijicho pembe kila mara huku mara chache akiwasikia wakiongea lugha ya kitaita ambayo hakuambulia neno hata moja.


Nafsi yake ilikataa kuwaamini dereva na tingo wake na kila mara alikuwa akiona utingo yuko bize kuwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi huku kila akimaliza kutuma anamtazama Zedi.


Walikuwa wamebakiza kilomita chache waingie mjini Nairobi na tayari walikuwa wanaingia sehemu maalumu ya kupimia uzito wa magari


Tingo alishuka,na dereva nae akashuka ni wakati huo Zedi aliutumia kukagua gazeti la Jambo Kenya na mwanzo tu akakutana na picha yake kubwa huku ikiwa imeambatana na maneno kadhaa juu yake,lakini pia aliona kiasi cha pesa kilichowekwa kama zawadi kwa atakae fanikisha kukamatwa kwake.


Alitabasamu na hapo akaona ndio muda sahihi wa yeye kuwaacha solemba watu wale.


Kulikuwa na foleni ya malori mengi yaliohitaji kupima uzito pale na na hivyo watu kadhaa walikuwa wapo chini wakifanya biashara zao,zedi akawatazama watu wale na kisha akatumia kioo cha upande wa dereva kuona waliko wenyeji wake na jambo la ajabu kabisa aliona dereva akiteta jambo na askari maalumu wanaokuwa wanalinda vituo vile,Zedi hakuwa mjinga.





Kulikuwa na foleni ya malori mengi yaliohitaji kupima uzito pale na na hivyo watu kadhaa walikuwa wapo chini wakifanya biashara zao,zedi akawatazama watu wale na kisha akatumia kioo cha upande wa dereva kuona waliko wenyeji wake na jambo la ajabu kabisa aliona dereva akiteta jambo na askari maalumu wanaokuwa wanalinda vituo vile,Zedi hakuwa mjinga.



Dereva yule alirudi haraka kwenye gari yake baada ya kuwa watu madereva wengine walikuwa wanapiga honi wakitaka asogeze gari lake.


Alimanusura ashindwe kuiondoa ile gari baada ya kuona mgeni wake hayumo ndani ya gari.


Wahka ukamjaa akawa anasogeza gari huku akiangalia upande wa vioo kushoto na kulia pengine ataona hata nguo ya Zedi.


Utingo wake alirudi nae kwa lugha ya kitaita akauliza alipo mgeni wao,hakupata jibu la maana zaidi ya kuchanganywa tu na majibu ya dereva wake.


Askari aliekuwa anapewa mchongo wa kumkamata Zedi nae akawa amefika huku akiwa ameongozana na askari wengine waliokuwa eneo lile .


Isuzu ile ilipaki pembeni mwa kituo kile baada ya kumaliza kukaguliwa huku dereva na utingo wakiwa hawajui waseme nini mbele ya askari wale waliokuwa na wao wamepiga simu makao makuu ili waongezewe nguvu eneo lile ili wamkamate gaidi kutoka kundi la alshabaab aliesadikika kushiriki kulipua westgate.


Wakiwa wanahaha kuulizia uelekeo alioonekana Zedi akipita mara difenda ya askari wapatao kumi na tano iliingia kwa fujo ndani ya kituo kile na hapo madereva na matingo walipata kuisoma namba,mizigo ya magari yao ilikaguliwa hovyo huku maswali yakiwa ni wapi wameona mtu yule hatari alipoelekea na hakuna aliejibu maana kila mtu alikuwa bize na mambo yake wakati zedi aliposhuka na kujichanganya na wamachinga kisha akatokomea upande wa pili wa barabara.


Zedi alikuwa anatembea kwa kufuata njia ya watembea kwa miguu iliokuwa mbali kidogo na barabara huku wazo lake likiwa ni namna gani ataweza kufika Nairobi salama.


Alivipita vimtaa kadhaa na kisha akaanza kuingia mjini sasa na huko akakutana na mapya mengine


Kila ukuta,kila nguzo ya umeme ilikuwa na sura yake ilionekana kwenye machapisho yaliokuwa yamepambwa kwa maneno kadhaa .


Zedi aliyapuuza na sasa alikuwa ameiacha hiyo njia na alikuwa anapita kufauata reli na tayari giza lilianza kushika hatamu.


Lengo lake alitaka awahi kuvuka stesheni ama kituo kikuu cha treni kisha aingie katikati ya Nairobi kwa kuivuka daraja ya Ahi River


Ni wakati akikaribia kitua cha treni cha Nairobi Railway alipata kuona barabara kadhaa zikiwa zimewekwa kizuizi huku kila gari likakaguliwa na baadhi ya raia waliokuwa wakitembea kwa mguu .


Akapiga hesabu alizozijua yeye ili aweze kuvuka barabara bila kutiliwa shaka hasa aliamini mavazi yake yametangazwa kwa kila askari,mara kwa mbali akasikia treni ikipiga honi kuashiria inaingia jijini Nairobi.


Behewa kadhaa zilimpita na yeye hakuwa na na ujanja zaidi ya kufanya awezavyo kudandia behewa moja wapo na kuingia ndani na hapo akafanikiwa kuingia ndani ya jiji la Nairobi kwa kupitia kitua cha treni na alipokwisha kushuka akaongoza njia na kutoka pale kituoni kisha akafuata barabara ya Nkrumah na kuingia kulia huko akaifuata barabara ya lusula kisha akakunja kushoto na kuingia kwenye nyumba za shirika la nyumba la kenya ndani ya Kaviba streat na hapo akaanza kukagua namba za nyumba lengo likiwa ni kukifikia nyumba namba 150 aliokuwa ameelekezwa na mateka mwenzie ndani ya ngome ya Kabah.


Akili yake tu ndo ilihisi yule mzee alitaka kumwambia kitu cha muhimu ama pengine alihitaji kumwelekeza jambo lenye kuendana na mkasa ule ambao hakujua aupe jina gani.


Aliambaa na giza lile huku macho yake yakijaribu kuzipitia namba za nyumba zilizokuwa eneo lile na hatimae akawa ameifikia nyumba namba 149 ni wakati huo ambapo aliona harakati flani zikiendelea kwenye nyumba iliofuata ambayo aliamini ni nyumba alioihitaji.


Nyumba ile ilikuwa na gorofa moja kwenda juu na wakati alipokuwa akisogea aliona taa za vyumba vya juu zikiwaka lakini gafla tu aliona zikizimwa hadi taa za nje.


Jambo lile halikufanya asite kuendelea kusogea mbele,ni wakati akikaribia zaidi ndipo akapata kusikia geti likifunguliwa na haraka akaona kuna gari iliokuwa imezimwa taa ikisogea pale na kisha kuna watu wawili walikuwa wakitoka ndani ya lile geti wakiwa na wamebeba kitu mfano wa sanduku dogo lakini ilionesha lina uzito kiasi chake.


Watu wale walipokuwa wakikaribia milango ya lile gari mara mmoja simu yake iliita na akashusha chini mzigo ule na kisha akapokea akasikiliza kidogo kisha akawambia wenzie

“Jafo anatuomba tufanye haraka maana kuna kiwingu kinakuja”


Muda huo Zedi alikuwa amewasogelea zaidi hivyo kufanya aweze kuyasikia vizuri maongezi yao na akanasa jina Jafo.


Zedi aliwapita wakati wao wakizidi kufanya jitihada za kuingiza mzigo wao ndani ya gari ni wakati huo Zedi alipata kushuhudia jambo lingine tena.


Aliona kama kivuli tu kikihitokeza kizani na kwa wepesi wa hali ya juu kikaenda hewani na kilipotua kilikuwa juu ya gari ya wale watu na kisha kikashuka na kwa aina nyingine tena ya ajabu na hapo watu wale wakajikuta wakichezea kipigo na wao wakajaribu kujibu lakini hawakuweza kuzuia nguvu ya kile kivuli kilichokuwa kinashuhudiwa na Zedi kutoka kwenye pembe ya kona ya ukuta ya nyumba za upande wa pili.





Aliona kama kivuli tu kikihitokeza kizani na kwa wepesi wa hali ya juu kikaenda hewani na kilipotua kilikuwa juu ya gari ya wale watu na kisha kikashuka na kwa aina nyingine tena ya ajabu na hapo watu wale wakajikuta wakichezea kipigo na wao wakajaribu kujibu lakini hawakuweza kuzuia nguvu ya kile kivuli kilichokuwa kinashuhudiwa na Zedi kutoka kwenye pembe ya kona ya ukuta ya nyumba za upande wa pili.


Kivuli kile kilichokuwa kimepambwa na barakoa nyeusi kilipiga mbinja na muda mfupi tu kuna gari ilikuja na kwa kasi ikitokea upande wa pili wa nyumba ile namba 150,gari ile ilikuwa ni nyeupe na ilikuwa na namba za usajili K369DLD, na ilipofika haraka wakateremka watu wanne wakiwa wamevaa suti nyeusi na kisha wakateta kidogo na kuchukua kile kisanduku kutoka kwa wale jamaa ambao walikuwa hoi hawajiwezi kwa kipigo kutoka kwa mtu mwenye barakoa nyeusi,kisha wakapanda gari lao na kuondoka eneo lile kwa kasi.


Zedi alitulia kuona kama kulikuwa hakuna mtu mwingine atakae sogea pale ilipokuwa gari nyeusi ambayo aliamini wamiliki wake wamekufa ama wamezimia.


Alipoona kumetulia akaanza kupiga hatua taratibu ili kuifikia gari ile.


Akiwa kabakiza hatua chache tu kuifikia gari ile mara ukasikika mlio wa injini kutekenywa na punde ikawaka na kutimka eneo lile,Zedi akajaribu kuiwahi aone kama atafanikiwa kuwaona waliomo,ikamzidi kasi hivyo akasimama na kupiga hesabau zingine tena.


Dakika tano baadae zilimkuta Zedi akiingia ndani ya nyumba namba 105 ambayo hakubahatika kumjua mmliki wake kwa jina ila alihisi ni yule mzee aliempa maagizo ya kuifikia nyumba ile.


Alitembea kwa tahadhari kuingia ndani zaidi huku akiwa hana hakika na usalama wake hadi muda huo.


Aliufuata mlango wa kuingia ndani ya nyumba ile ambao nao ulikuwa wazi na alipokwisha kuingia haraka akanyata na kujibanza pembeni kidogo ya mlango na kutulia ili kujipa nafasi ya kunasa mjongeo wa kitu chochote ndani ya giza la pale sebleni.


Zikapita zaidi ya dakika kumi bila kusikia chochote na hapo akafanya kunyata tena kuyafikia masofa yaliokuwa yamebebeshwa kuonesha kuna kitu kilikuwa kinatafutwa hapo ndani,alipoyafikia tena akasimama na kusikiliza kidogo huku hesabu zake zikiwa ni kupata japo hata kiberiti ili apate kuona chochote chenye kuweza kumsaidia,aliogopa kuwasha taa za pale ndani maana hakujua lolote kuhusu ile nyumba.


Akazidi kutembea ndani ya sebule ile na punde masikio yake yakanasa sauti ya mdondoko wa kitu ndani ya nyumba ile nae haraka akachumpa na kujibanza nyuma ya kabati iliokuwa ipo karibu na ngazi za kuelekea vyumba vya juu.


Mwanga hafifu kidogo ulitoka kwenye penlight ya mtu aliengia mle ndani na alionekana mwenye haraka na Kama alikuwa anatafuta kitu alichokuwa amekiangusha mle ndani maana alionekana kupekua zaidi chini ya kwenye zulia.


Zedi alimwona kwa kila hatua aliopiga mtu yule na hata alipookota kitu pale chini macho ya Zedi yalimwona pia na akili ya Zedi ikamhitaji mtu yule.


Alitoka alipo kwa kasi na kumpita mtu yule kisha akasimama nyuma yake,mtu yule alisikia akipitwa na kitu karibu yake akasimama wima na akataka kugeuka hapo akakutana na ngumi nzito iliomfanya apepesuke kurudi nyuma na ile kurunzi ya kijasusi ikaanguka mbali kidogo.


Mtu yule nae hakutaka kuwa mzembe haraka akarusha makonde mfululizo na kumpa shida Zedi namna ya kujikinga na hiyo ndio nafasi alioitaka mtu yule kwa wepesi wa karatasi akajirusha nje kupitia mlango uliokuwa wazi na Zedi alipokuwa amepata kusimama vyema akaruka kumwahi mtu yule lakini alichelewa aliishia kuona mlango wa geti ukijifunga kumaanisha kuna mtu kaupita.


Zedi haraka akageuka kurudi ndani na kama mwendawazimua akaipitia kurunzi ile na kuelekea kwenye Kabati alilokuwa amejibanza na hapo haraka akapekuwa kwenye milango ya kabati lile na punde akatoka na kadi mbili za benk akazitia mfukoni na haraka akatoka nje na kutokomea gizani.

*****


Nusu saa badae ilimkuta Zedi akiwa amesimama mbele ya mashine ya kutolea pesa kwenye Bank ya backlays ndani ya mtaa wa Namore.


Aliingiza nywila kama alivyokuwa ameambiwa na mzee Matare na alilifahamu hilo jina kwa sababu ndilo lilikuwa juu ya kadi ile ya Bank.


Akatoa kiasi cha ksh 72000 na kukitia mfukoni na kisha akachukua kadi nyingine tena (visa) akajaribu kutoa pesa lakini hapo akakutana na manaeno yalioonesha akaunti ile imefungwa,


Itaendelea


Operation jicho la paka inaenda kuanza kwenye group leo usiku huku Jicho la kuwadi ikianza kesho





Akatoa kiasi cha ksh 72000 na kukitia mfukoni na kisha akachukua kadi nyingine tena (visa) akajaribu kutoa pesa lakini hapo akakutana na manaeno yalioonesha akaunti ile imefungwa,


Kwanini ifungwe wakati ina pesa na mtumiaji hayupo,hapo akapiga akili mara mbili na kugundua kuna tatizo,haraka akatoka ndani ya kibanda kile cha kutolea pesa kilichokuwa pembeni tu ya mlango wa kuingilia ndani ya bank ile na ulikuwa umefungwa kwa sababu ilikuwa ni usiku.


Akatoka huku akijaribu kuwaza ni wapi atapata duka anunue nguo ili abadili muonekano wa mavazi hasa baada ta kugundua kila askari ameambiwa kuhusu mavazi yake.


Alietembea kwa muda kidogo na kufika hadi eneo la kupaki daladala maarufu kama matatu kwenye mji wa Nairobi,kisha akaita konda na kuuliza yalipo maduka ya nguo mitaa hiyo,akaelekezwa kisha akaelekea huko.

****


Usiku mnene ulimkuta Zedi akiwa amerudi kwenye nyumba ya mzee Matare na kisha akaikagua na kuhakikisha Hakuna mtu au kitu akaamua kwenda kujilaza huku mto aliolalia akiufunga kwa kamba ndefu ilioenda hadi kwenye kitasa cha mlango hivyo kama mtu angeliingia kamba ingelivuta mto na yeye kuamka,alipohakikisha mtego wake akaamua kupumzika ndani ya nyumba alioamini maadui wanaisakama kila muda ila ndo komando yule mzoefu akamua kuweka makazi yake.


Hatari ilioje!!!!


******


Kumekuchwa Dodoma


Lakini kuchwa huku kulikuwa na aina nyingi za mapambazuko.


Ndani ya hotel ya perugina,kulikuwa na tukio la ajabu kidogo na tukio hili lilitokea wakati ambao hakuna alietarajia litatokea ndani ya usiku uliopita.


Askari zaidi ya wawili walikuwa wanagonga vyumba vya wageni waliolala ndani ya Hotel ile na miongoni mwa vyumba vilivyofikiwa na askari wale ni chumba kilichokuwa kimekaliwa na watu wawili waliokuwa wapo kwenye tafakuri maana walikuwa na taarifa ya mauaji yale na hapo walikuwa wanajaribu kupata jibu la nani hasa aliekuwa anavujisha siri kutoka ndani ya idara yao,idara nyeti kabisa.


Ziga na Mina walikuwa wanatazamana wakati waliposikia mlango unagongwa kwa nguvu huku wakisikia sauti za askari wasiofuata misingi ya kazi yao wakikoroma ndani nyuma ya mlango.


Taratibu Mina akasimama na kuuendea mlango,akaufungua na hapo akakutana na tusi zito kutoka kwa askari wale waliokuwa wameshika bunduki zao mikononi.


Ziga akapandwa na gadhabu lakini alipomtizama mpenzi wake akaona ishara ya kumtuliza nae akatii.


Askari wale walikagua kila pahali ndani ya chumba kile na kisha wakauliza maswali kadhaa kuhusu tukio lililotokea usiku ndani ya hotel ile na maswali yote yakajibiwa na Mina aliekuwa anajua nini maana ya upuuzi wa askari wa Tanzania.


Askari wale wakatoka ndani ya chumba kile huku wakiwaacha wapenzi wale wakiwa wanarudi tena kujadili kuhusu kilichotokea.


“waliwezaje kujua kama watu kutoka makao makuu watafikia hapa?! Lilikuwa swali la Ziga kwenda kwa Mina.


“sijui kwa kweli,maana imetokea haraka mno tena wakati ambao hata sisi hatukujua kama wenzetu wapo tayari ndani ya Dodoma” alijibu Mina.


Wakaangaliana bila kusemeshana na Kama aliekumbuka kitu Ziga akanyanyua simu yake na kumpigia Chief.


“nakusikia” ilikoroma sauti upande wa pili


“Kuna kuku anakula mapandio yetu,hivyo naomba msilete tena mbegu nyingine,zilizoko zinatosha” ilikuwa ni sauti ya Ziga akiomba kwa chief kwa lugha ya mafumbo kisha akasikiliza kidogo na kukata simu na bila kusubiri akasimama na kuchukua mabegi yake na mpenzi wake na kutaka kutoka lakini Mina akawahi kumzuia


“ningojee dakika moja tu nakuja” alisema huku akiuendea mlango na kutoka nje.


Baada tu ya kutoka nje ya chumba chao,Mina akakutana na umati wa askari polisi wasiopungua kumi huku wengine wakipiga picha miili ya maiti mbili zilizokutwa ndani ya chumba kimoja.


Mina akataka kukatiza kati yao lakini askari mmoja akamfokea na kumzuia asipite


Taratibu Mina akatoa kitambulisho chake na hapo kilichofuatia ni askari yule kupiga saluti mfululizo kama kinyonga alieona chatu kwenye mti.


Mina hakumjali akasogea hadi ilipo miili ya watu wale,hakutaka kuamini ni watu kutoka kwenye kitengo chao ni watu kutoka kwenye kitengo ndani ya usalama wa Taifa (NSA) National security Agency.


Akawapekua kidogo na hapo akakutana na mchirizi mwekundu kwenye shingo zao,hiyo ikampa maana ya kuwa walinyongwa kabla ya kufa kwao,akatoa simu yake na kupiga picha sehemu kadhaa alizoona zaweza kumpa mwanga kwa aina ya mauaji yalivyofanyika.


Alirudi hadi chumbani kwao na akamkuta Ziga akiwa yupo wima na mabegi yake ikimaanisha hakuwa amekaa tangu Mina atoke mle chumbani.


“Aliefanya mauji hakuwa mmoja,yawezekana ni kikundi cha watu zaidi ya wawili na nilivyoona waliwalazimisha kusema kitu kabla hawajawaua” alisema Mina kisha akanyosha mkono na kumpa Ziga simu aliokuwa ametumia kupiga picha miili ile ya wanausalama wale waliokuwa wameuwawa.


“Walilazimishwa kusema chumba ulichopo…”alisema Ziga huku akiirudisha simu mikononi mwa Mina,hapo Mina akatoa jicho kama kumbikumbi aliebanwa na sisimizi.


“wewe umejuaje”

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog