Search This Blog

Thursday, 23 March 2023

ZAWADI TOKA IKULU - 2

 

Simulizi : Zawadi Toka Ikulu

Sehemu Ya : Pili (2)

hazikunitisha. Nilirudi mpaka jengo la CCM mkoa nikaikuta gari yangu ikiwa imeegeshwa palepale nilipoiacha nashukuru ilikuwa salama niliichukua na kurudi nyumbani.


Nikiwa barabarani nilijitahidi kuwa makini maana akili yangu haikuwa sawa hivyo nilichukua tahadhari mapema ili nisisababishe ajali. Baada ya kufika niliingia chumbani kwangu kujipumzisha maana nilikuwa nimechoka na pia nilizongwa na mawazo kichwani mwangu na kusababisha kichwa kiume. Siwezi kuuficha ukweli nilikuwa nampenda Jesca lakini kikwazo ni kimoja tu cheo cha baba yake, niliwaza na kuwazua lakini sikupata jibu jepesi niliamua kulala kwakuwa nilikuwa nimechoka haikuwa taabu kuupata usingizi maana ulinichukua ndani ya dakika kadhaa.


Najaribu bahati yangu ya kukutana na mrembo Jesca kwa mara nyingine ananichukuwa na kunipeleka sehemu ambayo sikuifahamu, nakaribishwa ndani ya jengo kubwa la kifahari niliingia mpaka ndani na kuketi, ni jumba la kifahari na ni fahari kweli. Wafanyakazi wa kila aina walikuwa wakizunguka huku na kule wengine walipita na chupa ndefu na nzuri za mnvinyo wa kila aina.


Baada ya kujipumzisha kwa mda nililetewa glass yenye muonekano nadhifu ilivutia ni ya mnvinyo. Alikuwa ni mhudumu mmoja wa kiume aliyevalia shati jeupe, shingoni kafunga tai ya kipepeo nyeusi, suruali nyeusi na kiatu kizuri cha moka. Nilivutiwa na muonekano wake kweli kijana alivutia sana, nilitia glass mdomoni nikapiga funda moja nilibaki naitafakari ile radha hakika nilijiona niko peponi. Katika maisha yangu ndiyo kwa mara ya kwanza nakutana na kinywaji chenye ladha nzuri kiasi kile ni ladha tamu na harufu nzuri nilii penda sana.


Nikiwa naendelea kupata mvinyo pale sebuleni nilikuwa nimeketi mwenyewe hakukuwa na mtu katu, aliyeshughulika na uwepo wangu, maana kila mtu alikuwa bize na shughuli zake kwenye hilo jumba la kifahari. Walizunguka huku na kule wakifanya shughulizao.


Kuna wengine walipita na kunisalimia “habari mheshimwa” ndo salamu iliyotumika mle ndani nadhani kwa kila mgeni aliyekanyaga jumba lile japo sikuwa na uhakika leo na mimi kabwela naitwa mheshimiwa? Dah kweli tembea na uaridi upate bahati ya kunukia , nilijibu nzuri. Sikuwa na amani muda wote ule niliokaa pale sebuleni maana hapakuwa pa hadhi yangu kiukweli palikuwa na hadhi ya juu sana kuliko maisha ya kawaida.


Mapambo yaliyokuwa ndani ya lile jumba sikuwahi kuyaota wala kukutananayo katika maisha yangu yote. Nimehudhuria harusi nyingi za kifahari na zingine kuangalia kwenye muvi mbwembwe za wapambaji wale kwa kifupi hazitafua dafu ndani ya ule mjengo nikisema mapambo ya kifahari ni ufahari kweli. Basi mwenzenu mtoto wa kisukuma niliudhihilisha ushamba tutaniwao na watoto wa Dar-es salaam kila siku “msukuma mshamba a.k.a Ngosha”.


Baada ya kuniacha kwa muda sasa Jesca anarejea akiwa kapendeza zaidi niliongozana naye wakati tunakuja akaniacha hapa sebuleni sikujua alipokuwa na sasa karejea alikuwa kapendeza zaidi. Nilimpokea na kumkumbatia kisha mfanyakazi mmoja alituonesha kwa ishara sehemu tuliyopaswa kwenda.


Tuliongozana huku tukiwa na tabasamu mwanana, usoni na rohoni ingawa sikujua ninapelekwa wapi lakini imani yangu ilinipa furaha nikijua itakuwa sehemu salama na nzuri kuliko hapa. Basi tulitumia dakika kadhaa mpaka kufika tulikokuwa tunaenda ni mwendo kama wa dakika saba tulitembea ingawa ni mwendo wa kawaida lakini huwezi amini tulikuwa bado tuko ndani ya lile jumba la kifahari.


Mazingira tuliyopita yalivutia zaidi kuliko ya awali na kunifanya nitamani kusonga mbele zaidi. Mkono wangu ukiwa umekishika vyema kiuno cha mtoto Jesca nilijiona mfalme ndani ya jumba la kifalme, nilihisi dunia yote sasa iko mikononi mwangu.


Tulizidi kupiga hatua na kuufikia uwazi ambao pia ulizungukwa na majengo ya kifahali, lilikuwa ni eneo la wazi tulivu lililozungukwa na viyoyozi na kulikuwa na bwawa kubwa la kuogelea. Basi yule kijana alitukaribisha kwenye meza moja iliyokuwa na chupa ya mvinyo alivuta kiti huku akiinama na kuweka mkono wake kifuani ishara ya heshima kwetu, Jesca aliketi kwa utaratibu huohuo alikuja upande wangu pia nikaketi.


Alimimina kinywaji nusu glass na kunikabidhi kisha akafanya hivyo kwa Jesca na mwisho alitukaribisha kwa heshima tukagonga glass na kuendelea. Jesca alionesha ishara ya kumuomba atupishe kwa kichwa hali hii iliashilia tulikuwa na faragha, kijana alitii kwa kuinama huku mkono ukiwa kifuani kisha akageuka na kuondoka.


Jesca alinikaribisha kwa upendo tulikunywa mvinyo, tulitaniana, tukacheka na kufurahi. Basi kadri muda ulivyozidi kwenda mambo yalizidi kunoga kwakuwa ilikuwa giza tulijikuta tukijisahau na kujiachia zaidi pale nje tulibusu mara kadhaa na baadae tukajisahau kabisa kana kwamba ni wapenzi wa muda mrefu. Jesca anaonekana amelegea zaidi na alitamani niwekaribu yake zaidi hali hiyo ilisababisha tukajikuta tumekumbatiana na ndimi zetu zilikuwa vinywani huku tukikumbatiana kwa mahaba mazito.


Staki kueleza juu ya miguno na kazi ya mikono bali ni kupagawa na hisia za mahaba wote tunaonekana kuzidiwa huku Jesca jicho limemlegea lilionekana kama nusu mwezi, anaonekana kuwa fundi zaidi yangu mpaka nikajiuliza mtoto wa Ikulu kajifunzia wapi hivi vitu?. Kiukweli staki kueleza kilichotokea ila Ilikuwa ni zaidi ya raha.


Baada ya mambo kuwa mambo Jesca aliomba tutoke eneo lile na sasa alinishika mkono tukapandisha ngazi na kuifikia lifuti iliyotupeleka golofa ya kwanza tulitoka huku tukiwa tumeshikana mikono mpaka kwenye chumba kimoja alichokifungua na kunivutia ndani.


Alinibana kwenye ukuta na kuanza kubusu na kutomasana ilikuwa ni kutupa nguo bila mpangilio. Na hatimaye nilimurusha juu ya kitanda kizuri kilichotandikwa kwa ustadi na manjonjo ya kila aina. Mashuka meupe yenye mvuto wa ajabu yalivutia kuyatizama,blanketi na mito mizuri laini ya thamani ilikipamba kitanda kile. Ukiniuliza lilikuwa ni godoro la aina gani stakujibu nitakwambia nililala kwenye kitanda maridhawa kuwahi kutokea duniani, kiukweli kile kitanda ni kitanda kizuri hakuna mfano, godoro laini lakunesanesa, nilihisi niko peponi.


Marashi ya chumbani yalizivutia pua zangu na kunifanya nihisi niko mbinguni, kiukweli kitanda kile kinasahaulisha uwepo wa shida katika ulimwengu huu, nahapo ndipo nilijiuliza kama hiki ni kitanda cha mtoto cha baba kikoje? “Haki ya Mungu ndo maana watu hawataki kuachia madaraka Afrika” nilijisemea kimoyomoyo.


Basi ukawa ni utani juu ya kitanda kukimbizana na kurushiana mito wakati mwingine tulishuka na kuizunguka ile nyumba kwa furaha. “Hakika sihitaji mke zaidi ya huyu katika maisha yangu” nilijisemea. Nilijiona nimechelewa kumjua, nilijuta kutokumueleza mapema kuwa nampenda pengine hizi raha ningeanza kuzipata mapema zaidi ya hapa.


Hisia zilionekana kumuelemea Jesca akiwa kajilaza juu ya kifua changu huku akipumua kwa hisia kali, nilikuwa nikizidi kumbembeleza kwa maneno matamu ili kuufurahisha moyo wake. Jesca ndiye msichana niliyemchagua, ndiye mpenzi wangu wa pekee, nilikuwa najiona kidume na mwanaume aliyekamilika, nilijiona mwanaume pekee mwenye bahati katika dunia hii, leo hatimaye nafanikiwa kuwanaye huyu mrembo katika kitandana cha kifahari ndani ya jumba la Kitawala la Ikulu.


Tukiwa tumelala Jesca kakiweka kichwa chake juu ya kifua changu, tulianza mazungumzo juu ya mahusiano yetu. Tuliaongea mengi sana nilimuuliza Jesca itakuwaje iwapo Rais angejua juu ya mahusiano ya mwanaye? Jesca aliniambia Rais ni mtu muelewa na anamheshimu mwanaye kuliko kawaida na pia anampenda sana hivyo atamsikiliza maana ndiye mwanaye wakike pekee. Pia kama hato elewa basi mama yake Jesca angeingilia kati swala hilo na lingeisha. Kwa upande wake hakuliona kama ni tatizo alinisihi nisiogope. “Nakupenda sana Jamie handsome wangu inakuwaje unakuwa na mashaka juu yangu, mambo ya familia yangu niachie mimi” ni maneno mazuri ya kunifariji yalivutia kuyasikia na pia yalitia moyo.


Jesca aliendelea kunipa faraja kuwa hakuna mtu wakumuamulia ampende nani katika maisha yake, pia akasema hali ya mtu huamliwa na Mungu, hakuna mwanadamu apangaye juu ya maisha yake isipo kuwa muumba peke yake. Jesca alizidi kunifariji sana na kunitia moyo kuwa nisiwe na uoga kwani kila lipangwalo na Mungu hakika hakuna binadamu wakulipangua ni maneno ya faraja yaliyonifanya nijione nimezaliwa upya ndani ya hilo jumba la kifalme. Basi baada ya hayo maneno matamu tuliendelea kuliwadhana juu ya kitanda chetu tulichokichagua kwa siku hiyo natamani ungetuona bila shaka ungetamani kuwa wewe mana furaha ilitawala nyuso zetu.


Hii ilikuwa ni siku niliyoitamani toka siku ya kwanza nakutana na Jesca na leo niko naye kwa karibu zaidi, niko naye katika kitanda kimoja, niko naye tukiwa watupu, nilikuwa nikiutafakari uzuri wake na siupatii picha, ngozi yake laini kila nilipoitomasa ilinitia hamasa, staki kukizungumzia kifua chake kilicho umbwa kikaumbika, Jesca ni binti mwenye mikono laini yenye mbinu katika mapenzi.


Ufundi wake wa mchezo wa kichokozi ulizidi kunipagawisha na kunifanya nizidi kumpenda zaidi huyu mwana wa Ikulu, tabasamu na kicheko chake vilinifurahisha maradufu kila nilipo kisikia kicheko na kuliona hilo tabasamu maridhawa nilizidi kuwa teja wa mahaba, ni mwana wa Ikulu muite Jesca Jones Manguli na sasa naweza kusema ulikuwa ni muda muafaka wa mimi na Jesca kulianza penzi letu rasmi.


Siwezi kukisema kilicho endelea ninachokikumbuka ni mlango kugongwa kwa nguvu tena ilikuwa ni nguvu na siyo masihara. Kelele za mlango zinatukurupusha na kubaki njia panda baada ya Jesca kusema huyo lazima atakuwa baba yake basi tulianza kulaumiana tukitupiana maneno huku nisijue pakukimbilia. Nilikuwa nikilia huku namlaumu Jesca kwanini kanileta Ikulu mimi mwana wa masikini, maana sasa nilikuwa sijui itakuwaje iwapo nitaangukia mikononi mwa Rais.


Nilikuwa nikisali kila aina ya sala huku machozi yakinitiririka naweza kusema ni muda mfupi sana lakini niliomba mamia ya sala ambayo ukiniambia nirudie hata tatu siwezi kukumbuka. Kweli binadamu akikwama ndipo huukumbuka uwepo wa Mungu, haijalishi ni mpagani kiasi gani, huwa pia haijalishi kakwama katika tatizo gani.


Hatimaye Jesica alipata wazo alinichukua na kwenda kunificha ndani ya kabati la nguo zake, kabati lilikuwa kubwa limepangwa vizuri, nilijificha huku nikizidi kusali sala zote nilizozijua.


Basi rais aliingia na walinzi wake huku nikiwa nachungulia kwenye kitundu kidogo cha mlango waliangaza huku na kule hawakuona mtu. Basi wakaamua kutoka lakini kabla hawajatoka mmoja aliona kiatu cha kiume kikiwa karibu na kitanda aliwaita wenzake wakarudi.


Nilijua nimekwisha, na sasa nilianza kulia kwa uchungu nikimlaumu huyu mwanamke, naapa sikuwahi kulia hivyo hapo kabla tangu nizaliwe. Walirudi wakaangaza mle chumbani hawakuona mtu, kuanzia chooni, sebuleni na sasa walisimama mbele ya malango wa kabati nililojificha na mlango ukatikiswa.


Walianza kuhangaika kuuvunja mlango wa kabati lakini walishindwa na sasa waliamua kufuata nyundo ili waje kuuondoa kabisa, waligonga kwa nguvu ule mlango na hapo ndipo nilikurupuka kutoka usingizini nikiwa nimetweta kwa jasho huku nikipumua kwa hofu. Nilikuwa nahema juujuu kama nimenusurika kukata roho, nilikuwa nameza mate kwa shida huku koo limenikauka.


Wakati huohuo mlango wangu ulikuwa ukigongwa bila shaka kelele hizo ndizo zilizoniamsha. Niliamka kwa unyonge kuelekea mlangoni nilifungua nikakutana na Dominic. Nilimkaribisha ndani na tukaketi, Dominic alinishangaa mana sikuwa kwenye hali yangu ya kawaida, nilikuwa nimelowa jasho mwili mzima huku nahema juuju, alijitahidi kunihoji ili ajue ni nini kinanisibu kulingana na hali niliyokuwanayo, sikuwa na budi kumueleza kila lililonisibu maana nilikuwa natafuta suruhu na mtu pekee awezaye kunipa suruhu walau nikaridhika ni Dominic rafiki yangu kipenzi.


Nilimhadithisia Dominic, kuanzia nilipomuacha pale hotelini kwa lengo la kwenda kumtafuta Jesca na nikafanikiwa kumpata nikaenda naye mpaka hotelini alipofikia tukakaa na kuongea lakini tumeshindwana. Dominic alishitushwa na kauli ile alitaka kujua kwanini tumeshindwana, nilimueleza yule mwanamke siyo wa hadhi yangu.


Kila nilicho mueleza kiliibua swali alijenga maswali alihoji kwanini asiwe wa hadhi yangu? Nikahaba?, nitajiri kuliko familia yako?, au hajiheshimu?. Nilimwambia Dominic anaweza kujiuliza maswali mengi ila kuna moja ambalo ni gumu kulitambua na hajalihusisha kweny maswali yake. “Dominic hivi ikitokea ukapendwa na mtoto wa Rais, tena Rais huyu tuliyenaye kwasasa Mzee jones Manguli utafanyaje?” niliuliza kama mtego. “Aaah! itategemea kama kweli binti yake kanipenda naweza kukomaa ila kwa tahadhali sana mana huyo mzee mwenyewe hasomeki unaweza kujikuta unaozea segelea” Alijibu kwa uoga uoga bila kujiamini. “lakini Jamie hizo ndoto zimeanza lini?” alihoji huku.


Nilimuuliza ndoto gani “ hizo za kuota wewe unatoka kimapenzi na mtoto wa Rais mpaka uniulize?” aliniuliza. “Kaka siyo ndoto Jesca ni mtoto wa Rais” nilimjibu kwa upole. Kauli ile ilimfanya acheke sana mpaka alianguka chini huku machozi yakimtoka.


Nilihisi ameanza kuleta uchuro ni kama anageuka kuwa mnafiki, basi nilikaa kimya sikutaka kuongea nae tena. Basi mwenyewe akacheeka mpaka basi najua hajui, ndiyo maana anacheka, hatimaye alilidhika baada ya kucheka kwa muda aliohisi unamtosha “Jamie na ujanja wako wa mjini wote, yaani ujuaji wote bado unadanganywa na hivi vitoto vya mjini? Kaka watoto wa Rais wote nawajua na hawawezi wakawa wanaishi hapa nchini, kile ni kitoto cha kabwela mwenzetu mmoja hapa town kinakuzingua hebu fungua kichwa utatapeliwa ndugu yangu”.


Dominic kwa kifupi alikuwa ameesha nikera alitakiwa anisikilize kwanza lakini haikuwa hivyo, badala ya kutafuta suruhu sasa anaanza kunikejeli na kunidharau.


Basi nilijitahidi kumuelewesha juu ya ushahidi nilionao ili aamini lakini hakutaka kusikia na badala yake aliendelea kunisakama kwa maneno ya kejeli na dharau na kunikatisha tamaa. Na chaajabu zaidi alikuwa akinitolea maneno ya dhihaka kana kwamba mimi siwezi kujisimamia. “Jamie wanawake watakufanya bwege mpaka lini kaka, amka mdogo wangu amka, usiwe mpumbavu, kumbuka Maria alivyokutesa mpaka sasa unahangaika kujinasua mtegoni, alisha kugeuza ATM yake. Leo tena hiki kikalagosi nacho kinataka kukugeuza mtelemko aah! Hapana jiangalie ndugu yangu” nilimsikiliza kwa makini nikayapima maneno yake yenye kejeli ndani yake, maana haikuwa tabia yake kunivunjia heshima sasa niliona anavuka mpaka. Nilimpenda sana rafiki yangu tunapendana na tunajuana toka kitambo alipo yeye mimi nipo na nilipo mimi yeye yupo pia.


Dominic, alikuwa akizidi kuongea maneno ya kijinga yaliyonifanya nizidi kujaa sumu, lakini yeye hakuwa anajua kuwa nilikuwa nimekasirika kupita kiasi. “haya baba endelea kumwamini huyo mtoto wa Rais huenda mkapewa zawadi ya bombardier siku ya harusi yenu”. Hakuishia hapo aliendelea “Jamani mijitu mingine sijui huwa haijiulizi umetoka kwenye maisha ya dhiki bado unakubali kuendeshwa na wanawake kama gali bovu unapelekwa tuuu!, wewe niwakwenda tu, kushoto kulia, nyuma mbele. Sikia kama huwezi kuamua tushirikishe wenye maamzi huenda tukakusaidia”. Nilijitahidi kuzikusanya hasira lakini kwa bahati mbaya hazikutosha nilishusha pumzi na kuanza kuikusanya amani moyoni mwangu nilitumia dakika kama mbili kwa kiwango kilichohitajika hakika ilinitosha nilikaa kimya na ikawa kimya kweli.


Nilirudi nyuma na kuketi juu ya sofa nikaendelea kumsikiliza Dominic kwa makini, basi aliongea kila aina ya neno. Alitukana kila tusi alilohisi linanifaa, sijui mbwa asiye ng’ata kwangu sawa tu, mara aliniita nyuki wa mashineni mla unga asiyeng’ata mimi kimya, mara aliniita ATM, kwangu sawa tu, kiukweli tukiacha unafiki yale maneno yalikuwa yanaumiza sana na nilijikaza sana kuyavumilia.


Nadhani urafiki ni kusaidiana, kujengana na kushauriana, siwezi kumsema kwa mabaya Dominic maana ni rafiki yangu wa kitambo sana ila leo ninamuona mpya na ni mtu tofauti kabisa. Siyo Dominic Martine niliyemjua leo nakutana na Dominic Martine tofauti kabisa.


Kulingana na hali aliyonikuta nayo nilidhani atakuwa msaada kwangu na sasa kageuka kuwa karaha na kero kubwa kwangu. Moyo wa mtu ni pango huwezi jua umehifadhi nini ndani yake mpaka uingie ndani yake, bado nampenda Rafiki yangu hivyo nilijitahidi sana kuwa mwema na ndiyo maana pamoja na yote aliyoniambia bado nilijikaza na kuyavumilia huku nikizidi kuwa mtu mwema kwake.


Nilikuwa nimejaa hasira mpaka natweta kwa jasho, “Dominic, nimekuelewa brother nashukuru kwa ushauri wako nitafanyia kazi, sawa ndugu yangu?, ila kwasasa naomba uniache nipumzike” nilianza kutafuta njia yakumuondoa nyumbani kwangu maana nimechoshwa na kelele zake. Bado hakulidhishwa na kauli yangu “aaah! Kweli mapenzi yananguvu kuliko sumaku, leo Jamie niwakunifukuza mimi nyumbani kwako?, sababu ya yule kahaba wako anayejiita mtoto wa Rais? Ila sishangai maana nchi hii tuna marais wengi huenda ni mtoto wa Rais wa masharobaro, au Rais wa TFF huenda ni Rais wa chama cha riadha au Rais wa Monduli maana kila mtu ni Rais siku hizi.


Nashukuru bwana, mkwe mtarajiwa wa Rais mi naondoka zangu, naisubiri hiyo zawadi ya Hummer siku ya harusi yenu wewe na princes Jesca usinisahau bwana kwenye ufalme wako mi nitaridhika hata ukinipa kusimamia kamati ya vinywaji siku ya harusi yenu ili nilewe mpaka nizime data”.


Aliondoka lakini kabla hajalifikia gari lake alinigeukia na kuanza kucheka upya alicheka sana tena kwa dharau kubwa kisha akasema. “jitahidi kuota usiku ndugu yangu hizi ndoto za mchana huambatana na uchizi, eti leo Jamie na mtoto wa Rais wakati hata mkuu wa wilaya yako hakujui wapi na wapi, fungua kichwa we bwege nyie ndo huwa mnakufa kibudu huna mbele wala nyuma. Mi naondoka bwana utamsalimia Rais na shemeji yangu sawa kaka?” niliendelea kumuangalia aliwasha gari, mlinzi wangu alifungua geti na akaondoka zake.


Nilihisi miguu inaishiwa nguvu nikajikuta nadondoka, nilijitahidi kujikokota mpaka ndani kwangu nikaketi sebuleni, huku moyo ukinienda mbio mithili ya pangaboi, nilikuwa sina nguvu kabisa hasra zimenijaa. Ujasiri pekee ndiyo ilitakiwa kuwa ngao ya maisha yangu kwa wakati huo na katika maisha yangu huwa sikubali kushindwa.


Nilikuwa jasiri na kuamini kila kitu naweza kupambana nacho, niliisogelea friji iliyokuwa jikoni nikachukua maji yangu yakunywa hayakuwa ya baridi sana nilikunywa ili kuupoza moyo urudi kwenye hali yake. Ilichukua muda na hatimaye mapigo yalianza kushuka na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.


Nilirudi sebuleni na kuketi kwa utulivu huku nikiwaza na kuwazua juu ya mambo yanayozidi kuniandama kwanini ni mimi tu, sina mpenzi na naona kama hata rafiki nimempoteza sababu ya kulisaka penzi la Jesca. Siwezi kumlaumu mtu maana nimeyataka mwenyewe, huenda Dominic yuko sahihi au mimi niko sahihi hivyo hakuna jibu la moja kwa moja. Nilikuwa naongea peke yangu kama mwehu narusha mikono na kujidharau nilikuwa kama mwehu alieyeshindikana Milembe.


Maisha huwa na vituko na yakikuamualia unaweza kuwa kichekesho, katika maisha yangu sijawahi hufurahia mapenzi, kwa hilo nisiwadanganye, ni wanawake watatu niliowahi kuwa nao katika mahusiano, lakini kila mtu na vituko vyake.


Wakwanza ni Anna Mwanjerwa mtoto kutoka Mbeya huyu alikuwa anatupanga kama behewa za treni akitoka huyu anaingia huyu nikavumilia mwisho yakanishinda watu walikuwa wanamuita maharage ya Mbeya yaani maji maramoja.


Wapili Salome Mchunguzi huyu ni mhaya mmoja kutoka huko mapenzi yalikokulia. Yeye kila kitu afanyiwe, masaa yote anataka uwenaye hata ukiwa kazini anatamani ukaenae ofisini tangu asubuhi mpaka muda wa kuondoka, hapiki, hafui, hasafishi nyumba, haoshi vyombo wala kutandika kitanda pesa anatumia kama mchwa akitaka kitu mpaka kipatikane ndo amani itarejea ndani alinishinda nuikamwambia ajaribu kwingine.


Wa tatu ni Maria huyu yeye na pesa kama ATM, mdomo hauna breki ni matusi kwa kwenda mbele ungemkuta anaongea ungedhaani ni wapigadebe wa standi waliozurumiana shilingi mia maana hayo matusi yalimfurahisha mwenyewe anatokwa maneno kama kapoteza koki.


Sasa nahitaji mpenzi wa tofauti nahitaji mpenzi wakunifariji, nahitaji mpenzi atakayeniheshimu, nahitaji mpenzi atakayejali shida zangu. nahitaji mpenzi atakayeficha aibu zangu, nahitaji mpenzi atakayenitunza na kuifanya furaha hii idumu milele. Ukweli hautapingika simujui hanijui kiundani lakini maongezi yetu yananipa picha kuwa Jesca ni mwanamke pekee atakaye nifaa maishani.


Ilikuwa yapata saa tano usiku sasa nilinyanyuka kwenda chumbani nakuta simu yangu niliyokuwa nimeitoa sauti inatoa mwanga kuashiria ilikuwa inaita. Alikuwa ni mama tulisalimiana na tukaongea mambo kadhaa vilevile alikuwa analalamika mgongo unamsumbua nilimshauri aende hospital na pia nikaahidi kwenda kumtembelea siku yoyote. Baada ya kuishusha simu ile kutoka sikioni, nilikuta missed calls tisini na tisa za namba ngeni, nilishituka kidogo maana siyo kitu cha kawaida. Niliamua kupiga simu iliita kwa muda kisha ikapokelewa ni msichana mmoja aliniuliza we nani? Nilimjibu kwa jeuri kuwa mimi ndiye nilipaswa kumuuliza we nani maana amenipigia mara 96 alicheka kisha akasema ni Auntie J ngoja nimpe simu. “hallo! Ilikuwa ni sauti ya Jesca Manguli.


Ilikuwa ni sauti ya Jesca Jones Manguli ililalamika amenikosea nini mpaka niondoke kwa hasira pale Gold Crest leo mchana, “Jamie hukupaswa kufanya hivyo, hivi unahisi nilijisikiaje kipindi unaondoka?, labda nikwambie tu kuwa nimejisikia vibaya kuliko ulivyodhani, umeniumiza sana kitu ambacho sikukidhania” Jesca aliendelea kunitupia lawama, alikuwa hajapenda nilichomfanyia na nikweli hata mimi nilihisi kumkosea, tena sana. Alilaumu kwanini sikupokea simu zake nimemfanya alie kama mtoto.


Meneno ya Jesca yalinishitua sasa nahisi ananipenda na hapo ndipo niliporudi na kuitafakari ndoto niliyoiota muda mfupi uliopita, na sasa nagundua Jesca kweli alikuwa na dhamira ya dhati yakuwa na mimi ingawa hajasema moja kwa moja.


Ilikuwa yapata saa tano na robo usiku tuliendelea kunogewa na maongezi, tulipiga soga mpaka mate yakakauka, nilikuwa nikibadilisha vinywaji tu pale sebuleni. Basi tuliulizana mengi mpaka nikapata taarifa juu ya familia ya Rais na familia marafiki zilizoruhusu kupewa.


Haikuwa kazi ndogo lakini huo ndiyo ulikuwa uhalisia maana penzi limekwisha chipua mizizi mioyoni mwetu. Hatukuishiwa maneno na sikumbuki yalitoka wapi, simu ilichemka sikioni mpaka ikapoa yenyewe huku nikiendelea kupiga soga tu. Kiukweli jesca hachoshi kumsikiliza. Hakutaka kukata simu nami sikuchoka kuisikia sauti yake ya upole, ucheshi na unyenyekevu.


Nilikuwa napiga miayo na kuendelea kupiga soga mara kadhaa alinitania nitammeza kutokana na kupiga miayo mara kwa mara, penzi lilichipua bila sisi kujua na huo ndiyo ulikuwa mwanzo mzuri wa mahusiano yetu. Utani, vituko na ucheshi ulinivutia sana na kunifanya nizidi kumpenda msichana huyu.





Alam ya saa yangu ya chumbani iligonga ikinitaka kwenda kwenye mazoezi, nilishituka ni saa kumi na moja alfajiri sijalala nilishangaa, lakini sikujali maana Jesca furaha yangu alikuwa akizidi kunipa maneno matamu na sasa sauti yake ilikuwa ikikwaruza kidogo kama vile ametoka usingizini na kuifanya iwe bora zaidi.


Hakuna cha maana tulichokizungumza lakini tulikuwa bize utadhani watoa huduma kwa wateja kwenye makampuni ya simu. Basi tuliendelea kuongea hatimaye saa kumi na mbili asubuhi nilijishangaa imewezekanaje leo niwakuongea na simu masaa yote hayo? Lakini ndiyo hali halisi mapenzi hayana mwenyewe, dalili za kukwama zimeesha jidhihilisha nimenaswa kizembe, nilifanana kama nyati aliyenaswa kwenye mtego wa sungura, nakumbuka simu ilikatika saa kumi na mbili na nusu asubuhi mara baada ya Jesca kuniaga kwa busu tamu kisha akakata simu.


Nililipapasa sikio langu maana sikuamini nilichokisia lakini huo ndo uhalisia, mtoto alikuwa amejaa kweye kumi nanane. Niliingia bafuni nikiwa na furaha, sijui hata ilikotoka hiyofuraha, nilioga huku nikipiga miluzi.


Basi nilirudi nikachagua nguo kwenye zile nguo zangu mpya siku hiyo niliamua kuvaa suti. Ilikuwa ni suti nyeusi ilikaa vizuri nika vaa na kiatu changu cheusi saa ya dhahabu nilinyonga tai nyekundu nikaweka na kitambaa changu chekundu kwenye mfuko wa suti kifuani. Baada ya kumaliza nilipiga unyunyu wenye manukato safi. Nilibeba begi langu na kuliweka kiti cha nyuma cha gari yangu leo niliamua kutumia gari yangu mpya ambayo huwa ni nadra sana kutoka nayo.


Haikuchukua muda nilikuwa nimepaki gari yangu mbele ya jengo la NSSF, niliingia ndani nikaweka begi langu na kuanza shuguli zangu.Nilikuwa na furaha sana hivyo nilifanya kazi zangu kwa furaha sana, na namshukuru Mungu ziliisha haraka na zote zilifanyika kwa ufanisi. Niliiangalia saa yangu ilikuwa ni saa sita mchana nilisema ngoja nikampitie Domi maana ulikuwa ni muda wa kwenda kupata chakula cha mchana, toka asubuhi sijaonana naye.


Niliingia ofisini kwake nikiwa na furaha lakini nilidakwa na maneo ya kejeli “aisee! nakuona mkwe wa Rais naona umeanza kubadirika sasa ni mwendo wa suti, kiatu cha thamani, saa kali nimepita hata nje leo umetoka na ndinga mpya hutaki kuonekana mshamba mbele ya mtoto wa Rais, haongera bwana jitume mtoto wa kiume ule vya bure” Ni maneno ya Domi kiukweli alinikatisha tamaa huyu jamaa na rafiki yangu wa kitambo tulishibana na kupenda mno lakini inaonekana amedhamiria kuuvuruga urafiki wetu, sikuwa na hamu tena yakueleza kilichonileta mule ndani. Nilimsalimia Domi lakini hakuwa tayari kupokea salamu yangu, basi nilikaa kimya na kuamua kuondoka.


Nikiwa mwenye mawazo nilitoka moja kwa moja nje, mara nilipofika tu simu yangu iliita niliitoa na kuangalia jina alikuwa ni Jesca. “Jamie hope utakuwa ofisini kwako mimi nipo hapa nilipofikia Gold Crest natamani nikutoe lunch kama hauto jali” niliishusha simu toka sikioni na kutabasamu. “okey nipo hapa nje nakusubiri” nilimjibu kwa haraka zaidi. Moyo ulichanua kwa tabasamu na kujikuta nayasahau yote yaliyonitokea muda mfupi uliopita.


Ilimchukua dakika tano kufika nilipokuwa nimepaki gari, Jesca alikuwa kapendeza sana alikuwa kavaa gauni lake la kitenge refu halikuwa na mikono (mchinjo) lilivutia sana, juu kafunga kilemba kilicho fungwa kwa ustadi mkubwa huku kikilandana kwa karibu na gauni hilo alilokuwa kalitinga, usowake mzuri ulipambwa kwa miwani mikubwa ya jua maana jua lilikuwa kali kidogo ila hakukuwa na joto kali.


Viatu vyake virefu vya wazi vilikamilisha muonekano wake wenye umbo zuri la kupendeza. Huku tabasamu lake mwanana lililovuta hisia zangu mara tu aliponiona lilinifanya niwe taabani. Nilimkaribisha ndani ya gari alishangaa “hii ni gari yako?” nilimwambia ndiyo aliongeza tabasamu maradufu.


Alinikumbatia mara baada ya kuketi, sikusahau kumsifia maana alipendeza “umependeza Jesca sina mfano mzuri wakufananisha, natamani kuuelezea uzuri wako ila nashindwa umependeza msichana mrembo, wewe ni zaidi ya mzuri” nilimsifia bila unafiki alikuwa kalivunja kabati.


Alishukuru na kuniambia nimependeza pia na kisha akaniambia suti ndilo vazi linalonifaa na anatamani kila siku anione nimevaa suti maana kwa muonekano nilionao leo umemvutia zaidi. Basi tulicheka kwa furaha na kukumbatiana tena na safari hii tulibusu kidogo.


Baada ya kumbatio alionekana akivuta pumzi ndeefu kisha akacheka kwa furaha, Jamie usiniambie unatumia Chibu pafyum?” nilijibu “yap” huu ni unyunyu wangu toka bidhaa hii inaanza kuzalishwa nchini. Aisee nimependa sana harufu yako staki kusema inasikikaje ila umetisha sana. Mwanaume unatakiwa unukie hivi bwana siyo mwanaume unanuka shombo la samaki kama pungo kapita. Ilinibi niangue kicheko, maana ukiwa na Jesca matani na vijimaneno vya kejeri havikatiki.


Niliuliza wapi tunaelekea, alinicheka na kuniambia ananisikiliza mimi. Tulitizamana na kuangua kicheko “Jesca hebu kuwa makini bwana punguza utani tulicheka na mwisho alisema twende zetu Kapri-Point.” Sikuona haja yakumbishia na safari ikaanza.


Ni Victoria Hotel nilipoliegesha gari langu nikamsubiri mlembo akashuka kisha tukaongozana na kuingia ndani, tuliagiza ugali na samaki wa kupaka wakati tukisubiri, tuliendelea kupata juice maridadi huku tukipisoga.


Katika kupiga soga ndipo nilipouliza maswali kwanini Jesca kuna wakati anatembea bila ulinzi na wakati mwingine ana ulinzi? Jibu lilikuwa jepesi tu “Jamie kila nilipo ninaulinzi unaweza kuwa wa moja kwa moja ama usio wa moja kwa moja. Ninalindwa wakati wote ukiona niko peke yangu usiniamini jua kuna watu nyuma yangu. Kwa Mwanza kuna wakati naweza kuwa huru zaidi maana ni watu wachache wanaonijua” alimaliza lakini aliona bado nina dukuduku.


najua unajiuliza walinzi walikuwa wapi siku napanda daladala au walikuwa wapi siku tunakutana supermarket jibu ni kwamba usiniamini huenda hata hapa tulipo nalindwa tafadhali yasikushughulishe saana hayo”


Wakati tukiongea nyuso zetu zilikili kuwa hakukuwa na shaka kuwa penzi limeesha ota katikati yetu na ilikuwa ni kazi yetu kulistawisha, najua hakuna aliyemwambia mwenzake lakini kila ishara ya upendo ilikuwepo.


Stori zilitukolea, hatimaye mhudumu aliyechukua oda zetu alikuja na kijana mmoja wakiwa na sahani zetu, ziliwekwa mezani tukaanza kupata chakula. Tulilishana tukanyweshana, tulikuwa kivutio kwa kila aliyekuwa karibu yetu. Jesca sasa alikuwa kaangukia kwenye penzi zito la fukara, alikuwa haoni wala hasikii.


Tulimaliza kula akaniomba nirudi ofisini, nilikataa nikamwambia nimeesha maliza kazi zote ofisini, aliniuliza kama nimeaga nikakataa basi alinyanyuka na kuniambia tuondoke nirudi ofisini si uungwana kuondoka bila kuaga wakati masaa ya kazi bado yangali yanaendelea, tulinyanyuka ingawa sikupenda kabisa kutoka kwani nilitamani tuendelee kuwepo pale victoria.


Mkono ukiwa kiunoni mabusu kila hatua ni tabasamu na vicheko ndivyo vilipamba nyuso zetu, tulipofika nilipopaki gari pasipo kutarajia tulikuta kuna ugeni ukitusubiri ni Dominic na Maria walikuwa wameegemea gari langu.


Kwakuwa nilisha hisi lengo lao sikuwaza nilifika pale waliposimama sikuwasemesha niliwapita kimyakimya na kuwaacha wakiangua kicheko kama wanawake waliokolea umbeya wamefunga safari kwenda kumsuta shoga yao na tayari wameesha mtia mikononi. “He! he! Heee! mbona mtoto wa Rais, tutakoma mwaka huuu”. Waliongea kwa pamoja kwa sadifa, Jesca aliwasikia akageuka kisha akaniuliza kama nawafahamu nilimwambia twende aachane nao.


Nilimfungulia mlango wa gari huku nikizidi kupokea maneno ya kejeli “mwenzetu tunaona unandoto yakuoa Ikulu, jikaze baba kuhudumia mtoto wa rais wa manzese huenda ipo siku TipTop itakukumbuka” maneno hayo yote Jesca aliyasikia vyema.


Nilijikaza kama sijayasikia wakati nataka kuondoka Maria alikuja kusimama mbele ya gari yangu kisha akasema “Jamani wanaume kwa kupenda sifa hamjambo kudanganywa tu ooh! Mimi ni mtoto wa rais bila hata kuchunguza ndo huyo umeanza kuazima gari mpaka suti mtakufa masikini wapenda mitelemko nyinyi”.


Yalikuwa ni miongoni mwa maneno yaliyoniumza zaidi siku hiyo, katika maisha yangu sijawahi kumuomba mtu, wala kumuazima mtu kitu tofauti na kalamu pindi nikiwa shule. Lakini leo natuhumiwa kuazima suti mimi? Yaani niazime nguo pamoja na gari ili nipate nini? Na ili iweje? Nilijiuliza maswali hayo na majibu sikuwa nayo!, moyo ulichafuka ghafla nikajikuta nashindwa kabisa kupumua vyema.


Kilichoniuma zaidi ni gari nililoliota siku nyingi nikajikamua nikajumlisha na mikopo ambayo mpaka leo sijamaliza kulipa nalo naambiwa nimeazima, nisiwe muongo ukweli yalikuwa ni maneno ya udhalilishaji kwangu.


Tuhuma hizo kwangu halikuwa tatizo, ila tatizo lilikuwa kwa Jesca ningemueleza nini maana tayari nimejigamba hii ni gari yangu na anaelewa hivyo, na huo ndio ulikuwa ukweli na sasa anapata taarifa kuwa nimeazima hivi naanzaje kumtizama machoni. Nilijitahidi kukaa kimya niliwasha gari nikaondoka na kuwaacha wakizidi kunizonga kwamaneno yasiyo na mantiki.


Nakumbuka hatukusemeshana na Jesca mpaka nilipoegesha gari pale nje ya ofisi yangu ila kabla hajashuka aliniuliza “uliniambia hii gari niyako?” alihoji kutaka kujua. Nilichokifanya nilichukua kadi ya gari na kumpa kisha niliendelea kuwa kimya baada ya kuipitia naamini alilidhika kuwa alichokisikia sicho.


Baada ya kuisoma ile kadi ya gari na vidhibitisho vingine, alinirudishia kisha akashuka bila kuniaga akaondoka zake kuelekea jengo la jilani ilipo Hotel ya Gold crest alipokuwa kafikia.


Niliendelea kumuangalia mpaka alipoingia ndani. Nilijua kabisa nilikuwa nimemkwaza iliniuma sana, nilipaki vizuri gari nikashuka na kuingia ofisini. Nililia sana baada ya kufika ofisini kwangu, hasira zangu humalizwa na kilio ni ngumu sana kunikuta nazozana na mtu katika maisha yangu huwa naiamini amani kwanza kuliko kitu chochote na hili malanyingi watu hulitumia kama fimbo yakuni nyanyasa.


Watu huniona kama mnyonge lakini mimi si mnyonge nina kabla sijachukua hatua huwa najifikiria mimi kwanza. Mimi ni mtu hatari sana baba yangu kanilea katika malezi ya mazoezi magumu maana alikuwa anacheza kunf-u na karate, pia nimefunzwa vyema na makocha kadhaa wa mchezo huo hatari mpaka namaliza chuo kikuu nilikuwa na mkanda mweusi nimehifadhi ndani.


Sheria moja wapo ya michezo hiyo ni kutokupigana na mtu asiye na mafunzo ya michezo hiyo hata kama kakuudhi vipi ukithubutu kufanya hivyo huenda ukafia jera au ukakutana na adhabu ambayo hutaisahau maishani.


Sheria nyingine ya mchezo huu inasema huruhusiwi kupigana ila ikibidi pigana ila usiumize, sheria hiyo inaendelea kusema kwa kujilinda umiza ila usiuwe na mwisho inatoa ruhusa ya kuua. Kuna masharti magumu sana ndani ya mchezo huu amabyo sikupaswa kuyaopuuza maana mani ni tunu niliyobarikiwa tangu nikiwa mtoto.


Uvumilivu ni silaha lakini pia nilifundishwa machozi hupunguza uchungu na kunywa maji hupunguza hasira nilichukua chupa yangu ya maji ya kilimanjaro nikanywa huku nikishusha pumzi kwa nguvu.


Niliketi kwenye kiti changu cha kuzunguka nikatuliza mawazo yangu sikuwa na pupa ya kuhangaika na wajinga. Niliwaza na kuwazua kwanini Domic hataki niwe na Jesca? Inakuwaje anapambana na mimi tena kwa kushirikiana na Maria?. Uswahiba wao umeanza lini mpaka kufikia hatua hiyo waliyopo?.


Hii inanipa picha kuwa huenda hata kipindi cha nyuma yeye na Maria walikuwa marafiki na inawezekana walikuwa wakinizunguka kimahusiano. Wazo hili nilianza kuliamini kulingana na mienendo niliyokuwa naiona baina yao.


Niliendelea na shughuli zangu za kawaida maana zile za lazima nilikuwa nimeesha kamilisha hivyo sikuwa bize sana siku hiyo. Baada ya muda nasikia mlango uligongwa kwa nguvu niliruhusu “ingia” aliyeingia ni Maria tena akiwa kafura kama mbogo sura imemshuka kama turubai la msibani. Kabla hajaongea chochote nilinyoosha mkono wangu nikiashiria arudi anakotoka, alijitahidi kuongea ujinga alioujua yeye lakini nilibaki na msimamo mmoja mkono wangu uliendelea kunyooka ukimtaka aondoke maana sasa nilikuwa nimechoshwa na tabia zao. Alitoa matusi, akajigeuza geuza pale na mwisho aliondoka.


Sijui walichokwenda kuhadithiana na ndugu yake maana baada ya muda mfupi nilisikia tena mlango ukigongwa nilifungua na kuwakuta wote wawili. Nilirudisha mlango nikiwaacha wanacheka kwa dharau huku wakipeana zamu ni vicheko vya kijinga tu visivyo na maana wala sababu za msingi.


Muda wa kufunga ofisi saa kumi jioni, nilitoka ofisini nilipofika nje niliwakuta Domi na swahiba wake kipenzi sijui walikuwa wakijadili nini. Niliwapita taratibu nikaingia jengo la jirani la Gold Crest Hotel mpaka golofa ya nne nilifika kwenye chumba alichokuwa akiishi Jesca, niligonga na kusubiri kwa muda lakini kabla sijafunguliwa nilijikuta niko katikati ya watu watatu na wote walikuwa wasichana wakiwa wamevalia suti huku bastora zikielekezwa kichwani kwangu.


Nilinyoosha mikono juu nikihitaji amani “unatafuta nini kwenye chumba hiki?” mmoja alihoji. “Nilikuwa namuulizia Jesca tafadhali” nilijibu kwa uoga huku nikitetemeka. “Jesca yupi na unamfahamu kama nani?”. Sasa nilihisi mkojo unapita maana wale watu walionekana siyo wakawaida.


“Mimi? … aaah! Ni Jamie rafiki yake … ndiyo ni rafiki tu”. Niliona dada mmoja anainua mkono kuelekea kwenye sikio lake alikandamiza kile kidole huku akiinamisha kidevu chake kwenye bega lake, aliongea maneno nisiyoyajua ni mchanganyiko wa namba herufi na mengine siwezi hata kuyahadithia maana sikujua ni Lugha gani na mwisho akataja jina langu Jamie. Baada ya kushusha mkono wake yule dada, bastora tatu zilizokuwa zimekilenga kichwa change zilisogea zaidi.


Basi nilijua nimekwisha hivyo nikabaki kama nilivyo kwa dakika tano hivi. Niliwaza vitu vingi sana ndani ya muda mfupi lakini kubwa lilikuwa ningejua ambalo daima huja baada ya safari.


Nilipekuliwa kama mwizi, mikono ilipita kila kona na baada ya kuhakikisha sina kitu zaidi ya simu na waleti, walinitanguliza mpaka kwenye lifti, nilimuona mmoja wa wale wasichana akibofya kitufe chenye herufi G na safari ilielekea chini tulipofika chini haraka niliingizwa ndani ya gari na gari likaondoka kwa kasi.


Sikujua napelekwa wapi nilichokijua nilikuwa nimekamatwa, hofu ikiwa imeutanda moyo wangu. Sikujua nimekamatwa kwa sababu gani nilichokijua nilikuwa nimejitafutia matatizo mwenyewe. Nilikuwa nikiwaza mle ndani ya gari sikujua nawaza nini maana ni mlundikano wa mawazo yasiyo na mfano nikiwaza namna ya kujinasua mikononi mwa hawa watu, niliwaza hiki kabla kile hakijaisha, nimewaza hiki, hakijafika mwisho nawaza kile yaani ilikuwa shagara bagala.




.


Nilipokuwa nikiziangali sura za wale wasichana zilivyo kavu hapo ndipo nilianza kuuona umhimu wa maneno ya Domi na huyo kichaa mwenziye. Kilichoniuma zaidi mimi sijawahi kukamatwa wala kulala kituo cha polisi si hilo tu hata kesi ya kusingiziwa sijawahi kuwa nayo, lakini sababu ya mapenzi naziona dalili za kulala selo leo.


Sikuwa najua tunaenda wapi kwani ile gari ilikuwa haioneshi nje, ukiwa ndani hautaweza kuona kinachoendelea nje. Baada ya mwendo mfupi hatimaye ilifunga break eneo ambalo sikulijua, mlango wa gari ulifunguliwa nikatoka, na kwa wakati huu nikama nilikuwa huru maana hakuna aliyenizonga wala kushughulika na mimi.


Ni kapre-point kwenye lile geti la kipindi kile nilipokuja kumsaka Jesca nilibaki najiuliza kwanini nimeletwa hapa? Kuna nini kinaendelea?. Maswali lukuki yasiyo na majibu yalizidi kuniandama.


Geti lilifunguliwa nikaruhusiwa kuingia kwa bahati nzuri nilimuona Jesca akija kwa tabasamu mwanana. Jesca ndiye aliyenipokea kwa furaha tukakumbatiana huku akinikaribisha ndani kwa furaha. Tulikumbatiana na kisha akageuka kwa kutumia kidole chake alibofya kitufe kilichokuwa ukutani na geti likafunguka bila shaka lilikuwa linatumia alama za vidole.


Kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kuingia ndani ya ile nyumba nilikuwa nashangaa kila nilichokiona. Jamani kuna maua humu duniani mengine ndo kwanza niliyaona hapo. Maua mazuri na yanavutia yalipandwa kwa ustadi yalivutia kuyatazama.


Tulilifikia geti la pili ambalo Jesca alilazimika kulifungua kwa kutumia lenzi ya jicho lake kwani kulikuwa na ulazima wakuingiza uso wake sehemu maalumu na geti likafunguka. Tukaendelea na safari baada ya hatua chache kulikuwa na geti lingine ambalo lilihitaji mawimbi ya sauti hivyo kuna maneno alizungumza likafunguka pia. Kabla hatujaendelea alinipa maelekezo “Jamie hili eneo tunaloingia linalindwa na mbwa hatari tafadhari hupaswi kuonesha ishara yoyote ya kuinama narudia tena kuwa makini na hili. Naomba unyoke mpaka nitakapokwambia sasa uko salama” nilimsikiliza kwa makini na safari ikaanza.


Nilinyooka mithili ya mpapai tulitembea mle ndani huku nikiwa naangaza huku na kule sikuona mbwa wala paka waliosemwa basi nikaendelea kushangaa maana mazingira nayo yalishawishi kuyaangalia tu maana yalikuwa fahari ya acho yangu. Huku nikiendelea kujikaza mapaka nikafika tulipokuwa tunaelekea Jesca alisimama kisha akashusha pumzi.


Tulielekea karibu na mlango mmoja nilivyo mjinga si nikainama kutaka kuvua viatu vyangu, asikwambie mtu ni mbwa zaidi ya ishirini sijui walitoka wapi. Zisingekuwa juhudi za walinzi wa eneo lile kuzuia sijui kama ningebaki hai.


Hakuna mbwa aliyenigusa ila nilikuwa najuta kwanini nimeingia eneolile. Jesca alinitizama akacheka kwa maskitiko “Jamie si nimekwambia mapema usiiname? Mbona unataka kunitafutia matatizo bure?” Jesca alikuwa kakasirika sana maana nilienda kinyume na alichonielekeza. “unadhani ungejeruhiwa na hawa mbwa ningejibu nini mimi kwa baba yangu?” alikuwa akiongea kwa uchungu na alizidi kunionya “tafadhali hapa ni Ikulu si pahala salama kama maeneo mengine kutokana na ulinzi wake. Ngoja niwe wazi tu kwako ukikiuka masharti kuna gharama utalipia ambazo ni ghari mno moja ni kujeruhiwa vibaya na pili ni kifo. Sitaki kabisa tufike huko hebu jitahidi kufuata ninachokwambia mimi, sawa Jamie?” Niliitia kwa kichwa na sasa ndo nagundua kumbe nilikuwa jengo la Ikulu ndogo ya Mwanza huwa nasikia tu kuna Ikulu ndogo hapa Mwanza na sasa nilikuwa ndani ya Ikulu mtoto wa kabwela, tabasamu kwa mbaaali baada ya kauli ile sikuwaza tena kuhusu mbwa bali furaha ilijidhihirisha.


Tuliingia ndani tulipofika sebuleni kulikuwa pazuri mno na kama peponi ni pazuri zaidi ya hapa basi mbinguni kuna raha ya milele. Nilikutana na vigae vya ajabu kuwahi kukutana navyo, sakafu ilikuwa mithili ya bwawa la maji ilionekana kama blue bahari na zilionekana mikunjo ya mawimbi madogo ya majini ungechungulia ungejiona kama tufanyavyo kwenye maji.


Kila hatua ukikanyaga kulikuwa na ishara ya mistari ya duara ikisambaa kama yafanyavyo maji uyakanyagapo au kutupa kitu ndani yake, lakini huwezi amini hapakuwa na maji ni urembo tu uliofanisiwa kiustadi. Jamani Ikulu aaah! Acheni paitwe Ikulu bwana.


Jamani kwa uzuri huu hivi viongozi wa afirika wanawezaje kuachia madara? Bila shaka ni ngumu tena ngumu haswaa maana wanajiuliza wakitoka hapa wakaishi wapi tena?. Hii naambiwa ni ikulu ndogo vipi kuhusu makao makuu ya mheshimiwa huko anakoishi kila siku? Staki kuwa mnafiki mtu akikabidhiwa Ikulu akaiachia kwa amani basi ana mungu ndani yake bila hivyo lazima mmtoe kwa mabavu maana atapaganda kama kupe.


Mara tu tulipofika ndani kuna ngazi zilishuka chini, basi tuzifuata na kukuta kule chini kumejengeka ni uwazi mkubwa na eneo la kutosha kiukweli ilikuwa fahali ya macho kwangu. Tulitembea kidogo tukakutana na ngazi zingine zilizozidi kutupeleka chini zaidi na hatimaye tukakutana na eneo jingine zuri zaidi. “Jamie karibu sana ndugu yangu, jisikie uko nyumbani” basi wahudumu walikuja na kutuletea juice huku tukiendelea na maongezi.


Jesca aliniambia walinzi wake wamemwamuru kuhama kule alikokuwa kulingana na hali ndogo yakiusalama. Mle ndani wamekuwa wakiingia watu ambao huenda wanawahofia hivyo ili aendelee kuwa salama zaidi ameamuliwa kuja kuishi hapa. “Nimetolewa pale hotelini mnamo saa nane mara baada tu yakutoka kula chakula cha mchana hivyo niko hapa kwa sasa. Na ndiyo maana hata ulipokwenda kunifuata najua hawajakupokea vizuri hizo ni changamoto na huo ndiyo ukubwa.


Karibu sana rafiki yangu kipenzi hizi ni nyumba za baba yangu kwa sasa na hazitatutambua mara tu akiondoka madarakani hivyo karibu sana na ujisikie huru” alinikaribisha kwa upendo.


Nilifurahi sana na sasa sikuwa na shaka tena juu ya ukweli wa binti huyu niliamini kweli ni mtoto wa rais wala hakukuwa na shaka juu yake. Tuliendelea kuzungumza mambo mengi Jesca alitamani sana sikumoja nimpeleke akawaone wazazi wangu ingawa kwa upande wangu sikutamani hata sikumoja kukutana na baba yake maana nilikuwa namuogopa balaa.


Macho yangu hayakuchoka kuangaza maana yalikuwa yakitamani kukiona kila yalichodhani ni kizuri. Niliangaza huku na kule ili kukidhi kiu ya macho yangu, ukweli asikwambie mtu jamani Ikulu ni pazuri, Ikulu pana mvuto waajabu na nashawishika kuiunga mkono kauli ya mwasisi wetu na rais wa kwanza wa taifa hili kuwa ikulu ni mahala patakatifu.


Sikuwa na ndoto za kukanyaga Ikulu leo Jamie Justine niko ndani ya Ikulu ni furaha iliyoje?. Pamoja na kuwa ni ikulu ndogo huenda ipo siku nitakanyaga ilipo ikulu kubwa tuombeane kheri.


Tuliendelea na mazungumzo, Jesca alinieleza kuwa mimi ni zaidi ya ndugu kwake alinikumbusha jinsi nilivyomsaidia kipindi cha ile kesi yake na mpaka sasa ninavyozidi kuwa karibu na yeye. Jesca alionekana kuguswa sana na alikuwa msichana muelewa hivyo hakusita kutoa shukrani zake mara kwa mara kwangu akisema “Wewe ni rafiki yangu wakwanza katika maisha yangu kukuleta ndani ya nyumba hii” alisema Jesca.


Aliendelea kuhadithia kuwa walinzi wake walibaki Gold Crest na walipopiga simu aliwaomba wanilete, “nakuthamini sana na nimetokea tu kukuweka moyoni, najua inakuwa hivi sababu ya upole wako na ukarimu, pia thamani unayoitoa kwa watu bila kujali matabaka yao.


Mimi ni miongoni mwa watu unaowaheshimu na kuwapenda najua hukunisaidia kwasababu ni mtoto wa rais, ulinisaidia kama mtu mwingine mwenye shida ahsante sana.” Nilitabasamu huku nikiupokea mkono wake ulioelekezwa kwangu kivivu niliupokea na kuuelekeza kinywani kwangu ili niubusu maana ulivyokuwa umekunjwa ulihitaji kupata huduma hiyo. Lakini kabla sijafanya hivyo Jesca aliuchomoa kwa nguvu na kujikuta nabusu mkono wangu huku akinicheka.


Basi wote tulifurahi na nilivutiwa zaidi na tabasamu la Jesca, lilikuwa na mvuto usio wa kawaida. Jesca Jones Manguli msichana mrembo mwenye hadhi ya kiafrika na sifa za kiafrika halisi. Hana nyodo, hajisikii ni mtu anayeishi maisha ya kawaida kabisa ya kumheshimu kila mtu anajichanganya na kutumia usafiri wa umma kama tufanyavyo sisi.


Tuliendelea na maongezi lakini katikati ya maongezi ni kama alikumbuka kitu aliniuliza “Jamie yule dada aliyetukuta Victoria leo nikama niliwahi kumuona ofisini kwenu ni mfanya kazi mwenziyo?” aliuliza kwa tahadhari kubwa nilimjibu kuwa nikweli alikuwa mfanyakazi mwenzangu na ndiye aliyekujibu vibaya siku umekuja kuomba msaada wa kumtafuta George Faru.


Kisha niliendelea, Si hilo tu hata yule jamaa waliyekuwa naye nilimwambia pia alikuwa ni rafiki yangu, na pia ni boss wangu pale kazini. Alitikisa kichwa kuashiria ameelewa. Aliuliza swali jingine “unawezaje kuwa na marafiki wa aina hiyo na bado ukaendelea kuwaita marafiki mbele za watu? Watu walioweza kukuaibisha mbele ya kadamnasi na bado ukaendelea kuwatambulisha kama marafiki? Au ndo urafiki wa siku hizi ulivyo?” nilicheka kidogo baada ya swali hilo kisha nikamjibu. Unyenyekevu ni silaha katika maisha ya binadamu.


Kabla sijamaliza Jesca alidakia na awamu hii alionekana kuwa serious zaidi alitoa kauli hii “Unyenyekevu huwa ni ujinga ukikubali kunyenyekea mambo yanayokuumiza, kwa kuogopa kukosana na watu. Kumbuka hakuna mtu wakuamua juu ya maisha yako bali ni wewe mwenyewe” nilibaki kimya sikujibu kitu maana alichokisema kilikuwa kweli asilimia miamoja.


Jesca alionekana kukwazika sana na kile kilichotokea leo “Jamie wewe ni mwanaume hebu kuwa na tabia ya kukemea ujinga, unadhani mungekuwa mnaishi kwa kuheshimiana hao unaowaita wafanyakazi wenziyo wangekuja na kukudhalilisha leo pale victoria?” aliniuliza “Hapana isingetokea” nilijibu kwa aibu aibu. “Hebu badilika, kijana mzuri na mtanashati kama wewe, unahitaji heshima na siyo kukubali kudhalauriwa. Nibora akudharau asiyekujua kuliko mtu unayeishi naye kila siku na na unamuita rafiki. Lakini nibora udhalauliwe kimyakimya kuliko kuanikwa mbele za watu. Jamie sikufundishi uishi vipi ila jifunze kuyatatua matatizo yakiwa madogo usisubiri yakue maana mwisho wake huwa fedheha. Kwa picha ile inaonesha hawajaanza leo kukudharau si ndiyo?.” Yote aliyoyasema Jesca yalikuwa kweli kabisa na sasa niligundua upole wangu ndio uliokuwa ukisababisha nizidi kudhalauriwa.


Nilimuomba msamaha Jesca na kumuahidi haitajirudia na nitakuwa tayari kupambana na changamoto zote zitakazokuja mbele yangu. Nilianza kujiona sistahili kuwa na Jesca maana mpaka mwanamke ananielekeza jinsi yakuishi tena kwa kuanika madhaifu yako ni aibu ukweli nilikuwa nimepotea, niliumia sana.


Ulikuwa ni muda wa chakula cha yapata saa moja na nusu, mhudumu mmoja alikuja na kutukaribisha mezani. Nilifika na kukuta meza imeandaliwa vizuri kila aina ya mapochopocho, vyakula vya ainatofauti, matunda, mboga za majani na Chupa kadhaa za mnvinyo, majagi ya juice nakadhalika.


Tuliketi na kuchagua tulipakua na kuanza kula huwezi amini meza yote ile tulikula watu wawili tu. Katikati ya mwanga hafifu na marashi mazuri. Ni sebule kubwa naweza kuiita ukumbi huko chini tulikokuwa wala usinge jua kuwa jumba lile lilikuwa chini ya ardhi. Kama kawaida tunapokutana mimi na Jesca mara nyingi huzaliwa mizaha mingi na utani wa kimahaba. Hata leo dalili zilianza kuoneshwa na macho ya kichokozi, tabasamu na hatimaye tulianza kulishana kwa upendo taratibu tulienda tunazidi kupoteza uelekeo na hatimaye zoezi la kula lilishindikana kabisa.


Jesca alinyanyuka na kuja nilipokuwa nimeketi alinishika mabegani na kunitomasa, kilicho fuata ni mabusu kadhaa ya shavu, kwenye paji la uso na kujikuta tumepagawa. Sikumbuki ilikuwaje ila ninachokikumbuka tulikuwa ndani ya chumba kimoja cha kifahari ambacho Jesca aliwasha taa huku tukiendelea kubadilishana ndimi ndani ya vinywa vyetu. “Jamie nakupenda natamani uwe mume wangu wa ndoa tafadhali usiniache, niamini nakupenda” kiukweli sikuamini kuyasikia maneno ya Jesca na sasa alinitamkia rasmi kuwa ananipenda taratibu nilimyanyua na kumbwaga kitandani.


Nilimuangalia na kujikuta natabasamu, aliniangalia na kuniambia naisubiri kauli yako Jamie hali iliyonifanya nicheke tena na tena kwa mara ya pili. Nilikuwa nimemlaza na kuketi juu ya mapaja yake yaliyokuwa yamefunikwa vyema na gauni lake refu zuri la kaki. Niliinama na kuuelekeza mdomo wangu upande wa masikio yake, niliyachokonoa hayo masikio kwa ulimi alipagawa ni nusu apige mayowe huku akininga’anga’ania kwanguvu. Kisha nilimwambia mimi na wewe……….. mpaka kifo.


Wote tuliachia tabasamu la huba tulikumbatiana na kuendelea kula denda huku tukipagawa na kujikuta tukichomoa nguo moja baada ya nyingine na sasa tulibaki watupu kama tulivyozaliwa ni mimi na Jesca ndani ya chumba cha Ikulu ndogo kwa mara ya kwanza.


Ni asubuhi nyingine niliamka nikiwa nimechoka, nilijinyoosha kidogo na kupiga miayo huku nikifuta macho yangu ili yapate kuona vizuri. Bila shaka nilikuwa nimelala Ikulu ndogo ya Kapre- point, mazingira hayakunidanganya na huo ndiyo ulikuwa ukweli, niliamka na kwenda kuoga ilikuwa yapata saa kumi na mbili asubuhi.


Nilimuangalia Jesca pale kitandani alikuwa hoi akizidi kukoroma, alikuwa kachoka saana hili halina ubishi. Basi niliinuka na kwenda kuchukua koti la kulalia lililokuwa limening’inizwa pale kabatini.


Nikalivaa na kuelekea bafuni, nibafu la kisasa lilikuwa nadhifu mno sikuwahi kukutana nalo hapo kabla, kwani kulikuwa na sehemu ya kibwawa kidogo chakuogea. Niligusa maji yake yalikuwa ni maji uvuguvugu, lakini pia kulikuwa na sinki la kukaa au kulala kama utataka kuoga umekaa au umelala basi ingewezekana.


Mbali na sehemu hizo zote pia kulikuwa na sehemu ya mvuke kama utahitaji kuoshwa kwa mvuke ungefurahia, palinivutia sana tena sana. Kulingana na mazoea niliamua kuoga maji ya baridi maana ndiyo niliyoyazoea na ni maji ambayo hunipa nguvu kila nikiyaoga.


Narudi kutoka bafuni mwili ukiwa safi, huku tabasamu likiupamba uso wangu nilimkuta Jesca bado kajilaza. Alikuwa kapumzika ila hakua amesinzia maana alikuwa akiniangalia huku akiachia tabasamu. Najua alifurahi kuuona mwili wangu uliojengeka vizuri, najua alifurahishwa na mapenzi mazito niliyompa usiku kucha, najua hatosahau mengi tuliyoyafanya na naamini atazidi kunipenda daima.


Nilimsogelea pale alipojilaza nikampa busu la shavu aliachia tabasamu zito, nilimuuliza anajisikiaje? Alijibu anajisikia poa!. Usiku wetu ulikuwa ni usiku tofauti sana, naamini kila mtu alitamani sana kusiche ili tuendelee kuwa pamoja.


Mimi na Jesca sasa tulikuwa wapenzi, na kila mmoja wetu naweza kusema alilifurahia penzi. Nilikuwa najiandaa kuwahi kazini maana ulikuwa ni muda wakuwahi kazini. Nilimuaga mpenzi wangu maana nilitaka kuwahi kazini alicheka na kutikisa kichwa.


Basi nilisogea kabatini kwaajili ya kisha kuvaa, nilishika suluali yangu ili nivae lakini haikuwa hivyo, Jesca alikuja na kuishika akaninyanga’nya na kuitupa pembeni kisha aliniuliza “unawezaje kurudia nguo uliyovaa kutwa nzima?” swali lake lilikuwa zuri lakini sina nguo nyingine na niko mbali na nyumbani lakini pia muda umeenda sana itabidi nirudie tu. Nilijaribu kujitetea lakini alikataa katakata kunisikiliza.


Alisogea kabatini na kuchukua kibegi alikifungua kile kibegi kulikuwa na suti ya rangi ya kijivu mpya, nilishituka maana ni kitu ambacho sikukitegemea, lakini nilifurahi nilipoijaribu suruali ikanitosha aah! Asikwambie mtu nilifurahi mno maana sasa nilihisi nimepata mwanamke anayenijali na kunipenda sana.


Wakati bado nashangaa alinipa shati la rangi nyeusi nilivaa likanitosha vizuri na mwisho niliweka koti nikaonekana poa zaidi. Nilivua haraka nikamuomba pasi akanipa nikazinyoosha na kuziweka sawa wakati huo yeye akinisaidia kufuta vumbi viatu vyangu. Baada ya kumaliza zoezi hilo nilivaa zilikuwa ni nguo za thamani kubwa na nzuri zaidi kimuonekano, pamoja na kupenda kwangu nguo nzuri sizani kama ninauwezo wakuziuliza hata bei.


Nilirekebisha nywele na kujiweka sawa nilionekana nadhifu zaidi. “Jamie nilikuahidi utaanza kuvaa suti, baada ya kuachana muda ule nilipita dukani pale NSSF plaza nimekuchukulia suti mbili, kiatu pea moja na tai zipo nne staki uhoji kuhusu gharama all I need ni kukuona ukiwa nadhifu mme wangu mtarajiwa” alisema huku akinifungia tai shingoni.


Baada ya hapo alipiga simu kwa wahudumu na baada ya dakika mbili hivi walileta kifungua kinywa, nikapata supu ya samaki aina ya sato na chapati mbili huku nikishushia na Juisi ya tikiti maji. Wakati nakamilisha mlo, Jesca alikuwa anaoga badae alikuja akavaa na tulikuwa tayari kuondoka.


Nilianza kuyaona maisha yangu yakibadirika kila sekunde, suti niliyoivaa siku hiyo ilionekana kuwa aghali mno naamini kila aliyeniona lazima alitamani arudie kunitizama. Jesca alibeba begi moja kubwa akaniambi kuna zawadi zako humu utafungua ukifika nyumbani bila shaka ni zile nguo alizo niambia kanichukulia hivyo sikuhangaika nazo.


Tulifika nje ya geti kulikuwa na gari aina ya Toyota Land cruiser V8 nyeusi imepaki. Aliniambia “ingia wakupeleke kazini mume wangu” Alinisogelea na kuniaga kwa mabusu mwanana. Niliingia tukawa wawili mimi na dereva kwenye gari ile, jamaa alikuwa haongei mpaka tunafika hofi haikumithilika. Tulipofika nilipumua maana mapigo ya moyo yalikuwa yananienda mbio kuliko kawaida.


Ningumu sana kukutana na mtu asiyeongea na yuko serious kuliko kawaida unaweza kuomba ushuke popote maana hujui anawaza nini juu yako. Alipaki gari na kuzunguka mlango wa nyuma alitoa lile begi na kuliweka chini kisha alinionesha ishara ya dole gumba kumaanisha kila kitu kiko sawa. Nami nikaitikia kwa kichwa kuashiria mambo yako sawa aliondoka. Nikakibeba na kibegi change nimesimama kabla sijaanza kwenda nilipoipaki gari yangu tangu jana. Ni pale nje eneo la kupaki magari, maana imelala palepale na sikuwa na hofu kulingana na usalama uliopo hapo.


Niliikagua nikagundua haikuwa na shida. Nilifungua buti na kukiweka kile kibegi. Nilitamani sana kukifungua lakini nimeambiwa mpaka nikifika nyumbani basi nikaendelea kujikaza tu hivyo hivyo ili nisivunje maagano.


Tangu nikiwa pale nje watu wote macho yalikuwa kwangu, salamu zilikuwa nyingi mpaka nikaogopa, kila mtu alikuwa akiniangalia mimi tu. Niliijua sababu ilikuwa ni suti yangu mpya ilimvutia kila mtu.


Niliingia ndani ya jengo kila nilipopita macho yalikuwa kwangu amini usiamini kila mtu alivutiwa na suti yangu kabisa maana hakuna mtu ambaye hakunisifia kila nilipokanyaga “Jamie umependeza” ni sauti tu zilikuwa zikipishana kunipa pongezi nami bila hiyana niliitikia Ahsante.


Hatimaye nilikuwa ndani ya ofisi zetu nilikata kulia nikielekea ofisini kwangu, kwa bahati mbaya nakutana na Maria nilimpita kama sijamuona. Najua ilimuuma zaidi akaguna na kusonya kwa dharau, sikugeuka mpaka ofisni kwangu nilimuacha akizidi kuvimbiana kwa hasira kama jipu lisilo na mdomo.


Kutokana na uchapakazi wangu kuwa bora sikuwa na utaratibu wa kurundika kazi hivyo ratiba yangu haikuwa ngumu sana siku hiyo, nilifanya kazi zangu na kumaliza kwa wakati. Mbali na kupokea simu kadhaa toka mamlaka za juu za kampuniyetu, vilevile nilitoa maelekezo kwa watu wa chini ya mamlaka yangu ili kukamilisha kazi kwa wakati.


Niliondoka kazini majira ya saa kumi na moja jioni. Wakati wote huu nilikuwa na furaha kubwa mno maana nilihisi napata kila nilichokihitaji katika maisha yangu kubwa zaidi lilikuwa ni pendo. Nahisi sasa nilikuwa nimempata mwenye mapenzi ya dhati na mtu sahihi kwangu, tangu nimeyajua mapenzi.


Nilifika nyumbani na shauku ya kulifungua begi nililopewa kama zawadi, taratibu nililifungua nilikuta suti nyingine ndani ilikuwa ya rangi nyeupe kitambaa chake nadhifu, pea moja ya kiatu cha ngozi chenye rangi ya udongo kilivutia sana.


Katika kuendelea kuangaza nakutana na tai nne za rangi tofauti na mwisho kulikuwa na saa yenye mkanda wa shaba lakini imetengenezwa kwa nakshi za kuvutia ilionekana kuwa niyathamani ya juu zaidi hali iliyonifanya nizidi kupagawa kwa penzi.


Nilitabasamu na mwisho uzalendo ulinishinda na kujikuta nikicheka kwa furaha huku nikivikumbatia kifuani vitu hivyo nilivyopewa, sasa nilikuwa na furaha ndani ya moyo wangu, nilijaribu kutafakali maisha yangu ya mwanzo na sasa hakika Jesca kayabadilisha maisha yangu maana katika historia ya maisha yangu hapo kabla sikuwahi kupokea hata vocha ya shilingi miatano kutoka kwa mwanamke lakini leo nikama ninatunzwa.


Nilianza kuandaa chakula changu mapema siku hiyo nilichambua mchele huku nikipiga miluzi na kuimba nyimbo mbalimbali zilizo uliwaza moyo wangu. Ilikuwa ni siku njema sana kwangu ambayo nilihisi haijawahi kutokea maishani mwangu hapo kabla.


Simu iliita bila kuchelewa niliipokea mara tu baada ya kuliona jina la malikia wa moyo wangu. “Hallow! honey!” sauti ilisikika toka upande wa pili. Nilitabasamu na kuitia kwa kujiamini “naam! mpenzi wangu, mahabuba wangu, uwaridi la moyo wangu, nashukuru kwa zawadi nzuri malikia wangu” nilimaliza kumpamba kwa maneno ya sifa alizokuwa nazo na kumshukuru kwa zawadi nzuri aliyonipa.


Jesca alicheka sana alinimbia alichokifanya ni wajibu wake hivyo sipaswi kumshukuru bali napaswa kuliombea penzi letu lidumu milele kwani neema bado zipo nyingi zitakuja. Tulijuliana hali toka tumeachana asubuhi na kukumbushana mengi kuhusu vitu tulivyovifanya usiku uliopita, kwakweli ilikuwa faraja kubwa sana maishani mwangu.


Wakati tukiendelea kuongea na simu Jesca aliniuliza anasikia kelele nyingi kuna nini huku niliko?, nilimwambia ni kelele za mafuta niko jikoni napika alishituka na kunicheka. Alishangaa maana hakuamini kama najua kupika, nilimwahidi ipo siku nitampikia chakula kitamu akinitembelea.


Nyumbani kwangu nilikuwa nakaa mwenyewe na mlinzi wangu ambaye pia alikuwa anatoka kampuni ya ulinzi hivyo hakuwa anahusika na mambo yangu ya ndani. Basi tuliongea mengi na kubwa zaidi aliahidi atakuja nyumbani kwangu ila hata sema ni lini.


Wakati naandaa chakula changu mezani mlango uligongwa nikaamua kuachana na kazi hiyo nilikwenda moja kwa moja kufungua mlango. Nakutana na Dominic mlangoni “amefuata nini tena huyu mwanga nyumbani kwangu?” nilijiuliza kwa hasira.


Nilimkaribisha ndani ila moyoni sikuwa na furaha kama siku zingine tulizokuwa tukikutana. Alifika na kuanza kunituhumu kama kawaida yake, alianza kuzungumza maneno ya ajabu akinituhumu mara nimetekwa na kahaba wa mjini inafikia mahala mpaka naliacha gari langu linalala ofisini, alizidi kushushia lawama akidai Jesca kanikamata mpaka mbele sioni, kwani niko tayari kugombana na rafiki yangu tulieshibana, tuanefahamiana na kusaidiana sababu ya huyo mwanamke ambaye yeye alimwita malaya.


Domi alinihakikishia kuwa nikiendelea na huyo aliyemwita yeye kahaba ipo siku nitawakana hata wazazi wangu. Hakuishia hapo alizidi kufoka. “hivi huwa huwezi tu kujitathimini kuwa unapotea mpaka uambiwe? Amekupa nini huyo mwanamke mpaka usinisikilize hata mimi ambaye ni sawa na ndugu yako? Jamie usiwe mpumbavu hicho kitoto siyo cha rais wala waziri mkuu watu wanasema nika kahaba na katapeli kakubwa utakuja kuuliwa bure utuache tukiahangaika na kesi za kujitafutia. Maana inasemekana kamewaibia watu kibao mikoa ya Arusha na Dar-es-salaam ndiyo maana kakakimbilia huku” Nilijitahidi kumsikiliza maana kama kawaida yangu huwa sikurupukii mambo, uvumilivu na kupuuza ni sehemu ya nguzo zangu.


Nilimuomba Domi anisikilize japo kwa sekunde lakini hakuwa tayari kunisikiliza, aliendelea kunifokea kama mtoto mdogo aliyekomba mboga jikoni n.


Ninakipaji cha uvumilivu kwa hilo hakuna shak, niliendelea kukitumia na nilipogundua amedhamiria kuja kunitukana basi nilimuacha atukane mpaka achoke nilivuta sahani na kupakuwa chakula changu pale mezani nilimkaribisha hata hakunijibu.


Nilianza kula huku akiendelea kuimba nyimbo zake zisizo na vina wala mizani, ilikuwa ni usiku wa saa tatu sasa, nilijua nyimbo zake hazita mruhusu kukesha. Matusi, kejeli, dharau ndo ilikuwa tabia yake kwangu na nilisha mzoea sasa maana sioni mabadiriko kila tukikutana tangu ameamua kuwa msaliti.


Sikujua kama kuna mtu alikuwa akimtuma au ni yeye ndiye alidhamiria kwa matakwa yake, nilijikaza huku nikaendelea kupiga wali kwa njegele mbichi nilizokuwa nimeziandaa kwa ustadi. Hiki ni miongoni mwa chakula ninachokipenda na leo kilinoga zaidi maana mlo wangu ulikuwa ukisindikizwa na kwaya isiyo na vyombo vya mziki.


Ndugu yangu alibwabwaja wee! Na hatimaye yakamshinda akashika njia na kuondoka nilibaki nacheka maana usilolijua ni sawa na giza nene. Baada ya mlo nilimpigia simu mpenzi wangu tukaongea wee! Mpaka nikalidhika tukatakiana usiku mwema nikasogeza mto wangu nikauchapa usingizi.


Ni alfajiri ya saa kumi na moja nilikuwa niko mazoezini ndani ya chumba changu cha mazoezi, baada ya kumaliza nilioga na baadae kumpigia simu mpenzi wangu kumjulia hali. Bahati nzuri alikuwa salama salimini niliamua kutinga suti mpya tena ili roho zizidi kuwauma.


Leo niliamua kwenda na suti yangu nyeupe niliyonunuliwa kama zawadi na mpenzi wangu. Nilipoiweka mwilini bila shaka ilikaa kama matarajio yangu yalivyokuwa, ndani kulikuwa na shati ya rangi ya maziwa naamini viliendana sawa nilitupia tai yangu ya rangi ya kijivu mpauko na kuunogesha muonekano bila kukisahau kitambaa cha kijivu nilichokiweka mfuko wa suti pale kifuani. Nikiwa ndani ya gari nilikuwa nikijiangalia mara kwa mara maana nilikuwa navutia, maana nilipendeza mno.


Hatimaye nilitinga ofisini niliwasalimia baadhi ya watu huku nikielekea ofisini nilifika kwa secretary nilimkuta Domi akisaini daftari ya mahudhurio. Aligeuka baada ya kumsalimia bila kunijibu alinidaka kwa kejelii “oooh wow! Nakuona mkwe mtarajiwa wa Mzee Manguli naona ni mwendo wakubadili suti, tai, kiatu. Mmh! na hii saa vipi nilikuwa sijaiona hahahah! Haaaaa! aaaah! Utakufa wewe mbwa kwakupenda vya bure, watu wanakushauri sasa uvae suti huenda ukateuliwa ukuu wa wilaya” alinikejeli mbele za watu mle ofisini kulikuwa na watu kama saba hivi wakisubiri kusaini nilijisikia vibaya sana. “Domi tafadhali acha mambo yako bwana huo utani haufai kufanyika hapa” niliamua kukatisha mazungumzo yake maana kila mtu alisubiri kuona naamua nini niliongea huku nacheka.


Nilitarajia atatulia lakini sasa alikuja juu tena akipayuka kila mtu asikie. “kwani nini mwanaume mzima, msomi mzima umeshikwa na kikahaba, husikii hata huelewi, hutaki kuwasikiliza hata wazazi wako, umekuwa kiziwi eti kimekudanganya ni kitoto ya rais na wewe umeingia mkenge… mwendawazimu kweli wewe kila siku nakusihi ubadirike lakini hutaki kusikia. Nilazima nikufananishe na mbwa maana mbwa anatabia ya kusikia na kusahau papo hapo” watu walishika midomo kwa aibu baada ya kumsikia rafiki yangu akinidhalilisha. “Domi unaniitaje?” nilimuuliza ili nipate uhakikia “nasema wewe ni mbwa tena mbwa koko lisilo hata na meno yakung’ata” alirudia kwa msisitizo tena bila aibu akitamba. Niliamua kuondoka maana sikutaka shari.


Napiga hatua moja mbele nakutana na Maria ananisukuma kurudi huku akisema “rudi hapo wewe bwege uambiwe unaenda wapi we dume suruali?, kila siku unaambiwa husikii basi leo wacha tukukomeshe mbele ya ofisi huenda utabadirika” nilizidi kukasirika maana alinisukuma na kujikuta napalamia watu.


Nilirudi na watu wakizidi kunishangaa kiukweli heshima yangu ilishushwa mno. na hata thamani ya uongozi wangu ilianguka ndani ya dakika chache. Nilipiga hatua moja kurudi nyuma wakati huo Domi alikuwa akiendelea kuropoka sikutaka hata kusikia aliongea nini ninachokikumbuka ni teke nililolirusha kutua tumboni kwake vyema, huku ngumi ikitua vyema kwenye pua zake hali iliyowafanya watu kukurupuka mbio maana kilitokea kitu ambacho hawakukitarajia. Domi alikuwa chini katulia damu zikimtiririka puani na mdomoni na Maria alikuwa kapiga magoti kwa upole akiomba msamaha maana alijua inayofuata ni zamu yake.


Kwakweli Domi hakunyanyuka tena na hata walipokwenda kumshika hakuwa anapumua basi sauti zikasikika “Ameua!..atakuwa kafa!… kauwa! … umeua!… jamani amekufa!… hivi atapona kweli?” Na hapo ndipo nilitahamaki kutaka kukimbia lakini nilikuwa mikononi mwa watu niliwekwa chini nikabaki nawasubiri polisi maana nilikuwa ni haki yao kwa wakati huo, niliyoyatafuta hatimaye nimeyapata.


Kelele ziliendelea nilikuwa niko chini nimepiga magoti huku nikiwa nimezungukwa na wafanyakazi wenzangu wakisikitika na Domi akizidi kutiririkwa damu hapo chini. Watu walijitahidi kumpepea kwa kitambaa na kummwagia maji ili aweze walau kuzinduka arudie hali yake ya mwanzo, lakini haikuwezekana.


Wafanyakazi wenzetu walimbeba na kumweka ndani ya gari walimwahisha hospitali huku wakiniacha na mawazo chungu mzima. Nilikuwa najilaumu kwa nilichokifanya maana sikutegemea kama ningesababisha madhara makubwa kiasi kile.


Domi ni rafiki yangu na iliniuma sana kwa kile nilichokifanya maana sasa nilikuwa na hofu juu ya maisha yake. Niliamini huenda hatapona kulingana na hali aliyoondoka nayo, maana alikuwa kaangukia kisogo na inasemekana mtu akiangukia kisogo huenda ikasababisha madhara makubwa kutokana na damu kuvujia kwenye ubongo.


Amechukuliwa akiwa anapumua kwa taabu sana na sizani kama atarudi katika hali yake, hofu ilitanda maradufu. Kwa hali hiyo nilikuwa tayari kuubeba msalaba wangu mwenyewe, maana nimeyatafuta matatizo acha niyamalize.


Nikiwa pale chini polisi walifika kwani walikuwa wamesha pigiwa simu nilikabidhiwa kwa polisi na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Mwanza niliwekwa mahabusu.


Mazingira ya chumba cha mahabusu yalitia kinyaa, yalikuwa machafu yasiyo na mvuto kamwe sikupenda kuyaangalia. Ukigeuka huku ndoo ya kinyesi hapa chini mkojo, watu wamekojoa hovyohovyo. Harufu ya mle ndani haikuwa rafiki kwa afya ya binadamu, hapafai hata kupakanyaga lakini ningefanya nini mimi ambaye tayari niko matatizoni.


Nilikuwa mle ndani kimwili ila mawazo yangu sasa yalikuwa yakimuwaza rafiki yangu Domi, niliwaza juu ya afya yake maana nilijua huenda akapoteza maisha na hii ingekuwa mbaya zaidi kwangu sit u kufungwa lakini hata mahusiano mabaya na familia.


Niliyawaza maisha ya mle ndani na nikayatafakari maisha ya jera iwapo ikitokea bahati mbaya akafa, nilitikisa kichwa huku nikijiuliza kama mahabusu kupo hivi itakuwaje huko gerezani?. Nilitikisa kichwa na kumuomba Mungu aepushe lisitokee la kutokea maana nilikuwa katika hali tete ya sintofahamu iliyoniweka njia panda.


Kwa hali niliyokuwa nayo nilijaribu kumfikiria mpenzi wangu iwapo atazipata hizi taarifa itakuwaje, wakati wote huu nilikuwa nikitiririkwa machozi maana nilijuta kwa kile nilichokifanya.


Baada ya mchanganyiko wa moshi wa sigara za vijana niliokuwa nao ndani, harufu ya viroba ukichanganya na harufu ya mikojo na kinyesi, ilikuwa bangi tosha ya kuivuruga akili yangu na kunijengea ujasiri hakuna mtu aliyethubutu kunisogelea. Huku nikiwa na tahadhali ya simulizi za jera maana nilikwisha zisikia toka kitambo kuwa ukilemaa kuna ndoa hiyo nilichuykua tahadhari yakutosha.


Usiku wa siku hiyo nilikuwa nimejikunyata kwenye kona kama kifaranga yatima mwenye ugonjwa wa kideli, nikiwaza na kuwazua, mbu nao walinishughulikia ipasavyo na walifurahia uwepo wangu. Maana koti, shati langu, mkanda, viatu na suluali niliviacha mapokezi na hapo nilikuwa nimebaki na sing’iendi na kikabutula cha ndani.


Nikiwa nimejikunyata mpweke huku nikilisikilizia baridi kali lililotoka ziwa vikitoria na kupenya vyema kwenye nondo za madirisha ya chumba cha mahabusu na kuifanya sakafu na kuta kuongeza baridi.


Radi ngurumo na mvua kali ya upepo iliyonyesha usiku huo, ilizidi kuubadilisha ule usiku na kuufanya kuzidi kuwa moja ya siku mbaya kuwahi kutokea maishani mwangu, kwani upepo ulikuwa ukipuliza na maji yalipenya kwenye madirisha ambayo hayakuwa na viooo na kuingia mpaka ndani ambapo yalituosha na kutuacha tumelowa huku tukitetemeka.


Asubuhi kulikucha nikiwa nimelowa, maji yakiwa yamejitenga mle ndani tukawa tunayakanyaga, ni mchanganyiko wa mkojo na kinyesi wenzangu niliona wakikanyaga bila kujali kwa upande wangu sikulidhishwa na hali hiyo nilibaki nimejikunyata kwenye kisehemu kikavu ambacho hakikufikiwa na maji.


Kwa kweli mahabusu hapafai na kamwe hapata kuja kufaa milele. Siku ya kwanza ilipita hakuna aliyekuja kuniona, mtu wangu wa karibu ni Domi ambaye sikuwa najua kama yuko hai ama kuna lolote lililotokea. Upande wazazi wangu bila shaka walikuwa hawajapewa taarifa au walizipata kwa kuchelewa kwasababu hakuja kuniona.


Jesca niliamini hajui chochote kilichoendelea maana simu yangu ilikuwa haipatikani nimeiacha mapokezi kabla sijawekwa ndani. Siku hii ya leo ilikuwa ni siku ya matarajio makubwa kwangu maana niliamini watu wengi watakuja kuniona.

Nilirudi na watu wakizidi kunishangaa kiukweli heshima yangu ilishushwa mno. na hata thamani ya uongozi wangu ilianguka ndani ya dakika chache. Nilipiga hatua moja kurudi nyuma wakati huo Domi alikuwa akiendelea kuropoka sikutaka hata kusikia aliongea nini ninachokikumbuka ni teke nililolirusha kutua tumboni kwake vyema, huku ngumi ikitua vyema kwenye pua zake hali iliyowafanya watu kukurupuka mbio maana kilitokea kitu ambacho hawakukitarajia. Domi alikuwa chini katulia damu zikimtiririka puani na mdomoni na Maria alikuwa kapiga magoti kwa upole akiomba msamaha maana alijua inayofuata ni zamu yake.


Kwakweli Domi hakunyanyuka tena na hata walipokwenda kumshika hakuwa anapumua basi sauti zikasikika “Ameua!..atakuwa kafa!… kauwa! … umeua!… jamani amekufa!… hivi atapona kweli?” Na hapo ndipo nilitahamaki kutaka kukimbia lakini nilikuwa mikononi mwa watu niliwekwa chini nikabaki nawasubiri polisi maana nilikuwa ni haki yao kwa wakati huo, niliyoyatafuta hatimaye nimeyapata.


Kelele ziliendelea nilikuwa niko chini nimepiga magoti huku nikiwa nimezungukwa na wafanyakazi wenzangu wakisikitika na Domi akizidi kutiririkwa damu hapo chini. Watu walijitahidi kumpepea kwa kitambaa na kummwagia maji ili aweze walau kuzinduka arudie hali yake ya mwanzo, lakini haikuwezekana.


Wafanyakazi wenzetu walimbeba na kumweka ndani ya gari walimwahisha hospitali huku wakiniacha na mawazo chungu mzima. Nilikuwa najilaumu kwa nilichokifanya maana sikutegemea kama ningesababisha madhara makubwa kiasi kile.


Domi ni rafiki yangu na iliniuma sana kwa kile nilichokifanya maana sasa nilikuwa na hofu juu ya maisha yake. Niliamini huenda hatapona kulingana na hali aliyoondoka nayo, maana alikuwa kaangukia kisogo na inasemekana mtu akiangukia kisogo huenda ikasababisha madhara makubwa kutokana na damu kuvujia kwenye ubongo.


Amechukuliwa akiwa anapumua kwa taabu sana na sizani kama atarudi katika hali yake, hofu ilitanda maradufu. Kwa hali hiyo nilikuwa tayari kuubeba msalaba wangu mwenyewe, maana nimeyatafuta matatizo acha niyamalize.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog