Sehemu Ya Tano (5)
“ Najua ni vigumu kuamini lakini huo ndio ukweli.Kama hamuamini ninachowambia hebu jaribu kutafuta mawimbi toka katika ile saa ambayo tulimpa Kigomba iliyokuwa na kifaa maalum kilichotiuwezesha kufahamu kila mahala alipo.” Akasema Mathew.Anitha akaanza tena kucheza na kompyuta yake na baada ya dakika kadhaa akatikisa kichwa.
“ Mathew can be right.Hakuna tena mawimbi yoyote toka katika ile saa.Inawezekana kabisa saa ile tayari imekwisha haribiwa baada ya kugundua tulichokifanya.”
“ Jaji Elibariki tayari amewaeleza kila kitu na ndiyo maana mnaona wamechukua kila aina ya tahadhari.Ili kuwafikia akina Kigomba ilimlazimu kutafuta njia ya kuweza kumfikisha huko na ndiyo maana akaamua kumtumia Rosemary Mkozumi kwani huyu mama aliwahi kuwa mke wa rais na anafahamika kwa viongozi wote kwa hiyo ingekuwa rahisi kwa yeye kumsaidia kuonana na Kigomba” akasema Mathew na kuvuta pumzi ndefu
“ What are we going to do ? akauliza Anitha
“ Baada ya kufahamu mipango yetu yote lazima wamebadilisha mipango yao yote na nina wasi wasi tunaweza kuchelewa kukipata kirusi hicho au tusikipate kabisa.Right now we have one option and one option only.” Mathew akanyamaza..
“ What option Mathew? Akauliza Peniela
“ To kill Dr Joshua” akasema Mathew
Peniela na Anitha wakapatwa na mstuko mkubwa hawakutegemea kabisa kusikia kitu kama kile.Zaidi ya dakika moja wote wakawa kimya
“ Najua mmestuka sana” Mathew akauvunja ukimya
“ Kwa hatua tuliyofikia sasa hatuna namna nyingine ya haraka ya kukinusuru kirusi kile kisitoke ikulu zaidi ya kufanya hilo nililolitaka.Kwa muda huu ambao hatukufanya lolote tayari wamekwisha buni mbinu mpya za kuweza kuikamilisha biashara yao na kwa wakati huu sisi hatuna mbinu ya haraka ya ku kutuwezesha kukipata kirusi Aby.Njia pekee ninayoiona mimi ambayo ni ya haraka ni kumuua Dr Joshua .Kumbukeni kwamba Dr Joshua ndiye anyefahamu mahala kirusi hicho kilipo kwa hiyo tukimuondoa mipango yote itavurugika na sisi tutapata nafasi ya kuweza kukipata kirusi hicho toka mahala kilipofichwa huko ikulu” akasema Mathew na ukimya ukatanda tena mle chumbani
“ Anitha na Peniela ,huu ni uamuzi mgumu mno kwangu na sitegemei kabisa siku moja nngeweza kufikria kitu kama hiki cha kumuua kiongozi mkuu wa nchi lakini kama nilivyowaeleza kwamba hakuna njia ya haraka ya kuweza kuzuia mipango ya Dr Joshua na wenzake kwani nina uhakika mkubwa tayari mipango yetu yote wanaifahamu,njia pekee hapa ni kumuua rais ambaye ndiye mhusika mkuu katika jambo hili .Kirusi hiki kama nilivyowaeleza ni hatari mno kwa nchi yetu na dunia kwa ujumla na tunatakiwa kutumia kila njia kuhakikisha kwamba kirusi hicho hakitoki ikulu na kama kikitoka basi kitue katika mikono yetu na si kwa watu wengine.Kumbukdeni vile vile kwamba John Mwaulaya alipambana kufa na kupona kuhakikisha kirusi kile kinahifadhiwa sehemu salama na msisitizo wake kwetu ni kwamba tusikubali kwa namna yoyote ile kirusi Aby kitue katika mikono ya watu waovu.Kwa hiyo basi naombeni mnikubalie wazo hili nililolitoa.” Akasema Mathew
“ Mathew, binafsi si kwamba ninakupinga na ninaiona mantiki ya ulichokisema lakini moyo wangu unakuwa mzito sana kufanya kitu kama hicho.Huu ni uhalifu wa kiwango cha juu kabisa na endapo ikitokea tukajulikana adhabu zake ni mbili tu,kifo au kifungo cha maisha gerezani.Cant we find another option? Akasema Anitha
“ Right now,thats the one and only option we have .If we want to save our country and the world we need to kill Dr Joshua.Nakubaliana na nawe kwamba kweli nchi itatikisika kwa kuuawa kiongozi wake mkuu lakini itabaki salama .Hata kama tutagundulika kwamba sisi ndio tuliotekeleza mauaji hayo watanzania na dunia watatushukuru kwa tulichokifanya” akasema Mathew
“ Mathew na mimi naungana na Anitha” akasema peniela
“ Mpango wako ni mzuri lakini naingiwa na shaka sana namna ya kuutekeleza.Kumuua rais si kitu kidogo.Ni mpango unaochukua muda mrefu na unaohusisha watu wengi.How are you going to do it? Akauliza Peniela
“ Sikieni ,suala hili halihitaji muda mrefu wala kushirikisha watu wengine .I know the simple way to do that.Naifahamu ikulu. Magharibi mwa ikulu kuna chumba cha kulala rais.Upande huu wa magharibi pia kuna jengo moja refu lenye ghorofa zaidi ya 15 .Jengo hili lipo umbali wa kama mita 360 au zaidi toka chumba cha rais.jengo hili ni la kibiashara ba makazi na tunaweza kulitumia kumdungua Dr Joshua akiwa chmbani kwake.Kwa njia hii tutaepusha nchi yetu na dunia dhidi ya maangamizi ya kirusi Aby” akasema Mathew .Pamoja na maelezo yale ya Mathew bado Anitha na Peniela walikuwa na woga mwingi
“ Pamoja na maelezo hayo Mathew lakini bado moyo wangu unakuwa mzito sana kukubaliana nawe kufanya hivyo.Mimi kwa ushauri wangu ,suala hili la kumuua Dr Joshua liwe ni la mwisho kabisa lakini kwa sasa tutafute namna nyingine ya kufanya kwa haraka kuzuia kirusi Aby kisitoke ikulu.Nasema hivyo kwa sababu hatuna uhakika kama biashara hiyo imeshafanyka ama bado.Tunaweza kumuua Dr Joshua halafu kumbe tayariik irusi kimekwisha toka.Kama tukipata uhakika kwamba kirusi kipo basi tunaweza kuchukua hatua za haraka kuzuia kisitoke na kama ikishindikana kabisa basi hatutakuwa na njia nyingine zaidi ya kumuua Dr joshua” akasema Anitha
“ Anitha yuko sahihi ,ninamuunga mkono” akasema Peniela
“ Tutafute njia nyingine ya kufanya kabla ya kuamua kumuua Dr Joshua .Kuna kitu nimekifikiria.Kwa siku ya leo Flaviana anazikwa kwa hiyo Dr Joshua lazima atakuwa na shughuli nyingi kwa hiyo sina hakika kama anaweza akajihusisha na mambo ya kirusi.Tuitumie nafasi hii vizuri kufahamu mipango yao na kujipanga namnaya kukichukua kirusi hicho.Kuna mtu ambaye nahisi anaweza akawa na msaada kwetu.Anna mtoto wa Dr Joshua” akasema Peniela
“ Anna ??!! Mathew akashangaa
“ Ndiyo.Ana anaweza akawa na msaada mkubwa kwetu .Naamini mpaka sasa hivi hafahamu chochote kuhusiana na mambo anayoyafanya baba yake .Haelewi kama baba yake ndiye aliyemuua mchumba wake Edson ,mama yake na dada yake Flaviana .Nina hakika endapo tutampata Anna na kumueleza ukweliwa mambo anayoyafanya baba yake atatuelewa na ataungana nasi.Mimi na yeye ni maadui kwani niliwahi kuwa na mahusiano na mchumba wake Edson lakini ninaweza kumpata kwa kumtumia Kareem”
“ Kareem ? Who is he ? akauliza Mathew
“ Huyu ni mlinzi wa Dr Joshua ambaye anamuamini sana na ambaye ninaelewana naye sana.Nitamtumia huyu kumpata Anna”
“ Una mawasiliano yake huyo Kareem? Akauiza Mathew
“ Siikumbui namba yake lakini ninafahamu mahala ninakoweza kuipata.Kuna mwanamke mmoja anaitwa Zaituni ninafahamiana naye.Huyu Zai ni mke wa mtu lakini ana mahusiano ya siri na Kareem na mimi ndiye niliyemuunganishia..Zai ana duka kubwa la urembo ninaweza kumfuata dukani kwake na kupata mawasiliano ya Kareem.”
“ Unadhani Kareem anaweza kukubali kukusaidia kumpata Anna? Akauliza Mathew
“ Kareem anafahamu mahusiano yangu na Dr Joshua lakini kwa muda mrefu amekuwa ananitaka kimapenzi.Kareem ni mtu anayependa mno wanawake.Nitampa anachokihitaji ili naye atupatie tunachokihitaji ambacho ni Anna.”
“ What ?!!.Mathew akastuka
“No you can’t do that. I won’t let you do that” akasema Mathew.
"Mathew we’re in a war and we have to use every weapon we have .Binafsi siwezi kumfuata Anna kwa sabau tuna uadui niliwahi kuyavunja mahusiano yake na mchumba wake Edson laini Kareem yuko karibu sana na familia ya rais kwa hiyo anaweza kumpata Anna kirahisi.” Akasema Peniela
“ Hakuna namna nyingine ya kumshawishi Kareem akusaidie tuweze kuonana na Anna zaidi ya njia hiyo unayotaka kuitumia?
“ Itachukua muda mrefu hadi alifanikishe hilo na sisi hatuna muda mwingi wa kusubiri.Kumpa anachokihitaji ni njia rahisi ya kumfanya afanye kazi yangu kwa haraka.Dont worry I’ll be fine” akasema Peniela.Mathew na Anitha wakatazamana na Anitha akamfanyia ishara akubali
“ Ok let’s do that.” Akasema Mathew japo kwa shingo upande.
“ Nashukuru kwa kukubaliana nami.Naona nisiendelee kupoteza muda ngoja niende mara moja kwa Zai ili niweze kuzipata namba za simu za Kareem.Jioni ya leo natakiwa pia kwenda katika ile nyumba aliyonipa Dr Joshua nilikolihifadhi lile kasha alilonipa John Mwaulaya” akasema Peniela
“ Tutaongozana wote.Kuna magari ya kutosha hapa.Mimi na Anitha tutatumia gari lingine tukikufuatilia ili kuhakiki usalama wako.Hali si nzuri kiusalama kwa sasa na hatujui team SC41 wana mipango gani hadi sasa kuhusu wewe”
“ Don’t worry about me I’ll be fne.I can do this on my own” akasema Peniela
“ No Penny we’re going with you,that’s an order” akasema Mathew kwa sauti iso masihara kisha wakaanza kufanya maandalizi kila mmoja akaweka sikioni kifaa kidogo cha mawasiliano .Mathew akampatia Peniela bastora moja.
“ Take this.You may use if necessary” akasema na kumgeukia Anitha
“ Anitha najua umechoka sana na bado una maumivu .kama hujisikii vizuri unaweza kubaki ukapumzika
“ Ni kweli nina maumivu makali lakini hii si sababu ya kunifanya nishidwe kuungana nanyi .I’ll go with you” akasema Anitha
Baada ya kujiandaa,Peniela akaingia katika mojawapo ya magari yaliyokuwapo katika gereji ,Mathew na Anitha wakaingia katika gari lingine na wote wakaondoka
“ Pole sana Mathew kwa yote yaliyotokea” akaanzisha maongezi Anitha wakiwa garini
“ Wewe ndiye ndiye unayepaswa kupewa pole kwa mambo yaliyokupata ila nashukuru Mungu uko hai.Sisikitiki kwa vitu vilivyopotea kwani ninaweza kuv ipata vingine ila sijui ingekuaje kama ningekupoteza.Nisingeweza kupata Anitha mwingine hapa duniani.Nakuhakikishia Anitha wale wote waliohusika na suala hili lazima walipe tukianzia na jaji Elibariki.I trusted that bastard but….” Mathew akashindwa kuendelea akapandwa na hasira
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Japokuwa yeye na hao anaoshirikiana nao wameturudisha nyuma sana lakini bado hawataweza kutuzuia kufanya kile tulichodhamiria kukifanya.Hata kwa kumwaga damu zetu lazima tuhakikishe tunakipata kirusi Aby” akasema Mathew .Safari iliendelea hadi katika duka moja kubwa la vipodozi
“ Mathew tumefika “ Peniela akawataarfu akina Mathew ambao walikuwa mita kadhaa nyuma yake
“ Sawa Peniela tuko nyuma yako” akasema Mathew.Peniela akashuka garini na kuingia dukani na muda wote macho ya Mathew hayakubanduka katika mlango mkubwa wa kuingilia dukani akajaribu kumsaili kila aliyeingia dukani.Kw a kuwa walikuwa wamevaa vifaa vya mawasiliano masikioni Mathew na Anitha waliweza kuyasikia maongezi yote ya Peniela na Zai.Peniela alitumia zaidi ya dakika kumi mle dukani na baadae akatoka akiwa ameongozana na mwanamama mmoja mrembo wakaagana akaingia katika gari lake.
“ I’ve got the numbers.” Peniela akawataarifu akina Mathew
“ Ngoja nimpigie simu Kareen sasa hivi“ akasema na kwa kutumia mojawapo ya zile simu walizopewa na askofu Edmund akampigia Kareem.
“ Hallow” ikasema sauti ya kiume upande wa pili
“ Hallow Kareem it’s me Peniela”
“ Peniela ?!! Kareem akauliza kwa mshangao
“ Yes its me.Mbona mestuka?
“ Nimestuka kidogo kwani sikutegemea kabisa kupokea simu toka kwako” akasema Kareem
“ Kareem ninashida na ninahitaji kukuona”
“ Una shida gani Peniela?
“ Ninashida binafsi.Tunaweza kuonana sasa hivi?
“ Hapana Peniela.Kwa sasa haitawezekana.Leo yanafanyika mazishi ya Flaviana yule mtoto wa Dr Joshua kwa hiyo kuna viongozi wengi wa kitaifa hapa nyumbani kwa Dr Joshua kwa hiyo tuna heka heka ya kuimarisha ulinzi wa rais na viongozi wengine wote.Labda tuonane kesho”
“ Hapana Kareem nataka tuonane leo tena sasa hivi” akasema Peniela
“ Sasa hivi haiwezekani Peniela.Nimekwisha kuambia kwamba nina kazi nyingi siku ya leo.Nisubiri hadi kesho”
Peniela akavuta pumzi ndefu na kusema
“Kareem find a way to meet me ,I have something for you”
“ Whats that you hhave for me?
“ Kitu ambacho umekuwa unakitaka kwa muda mrefu .Me”
“ You??
“ yes me.Umekuwa unalitaka penzi langu kwa muda mrefu leo nitakupa penzi but in exchange to what I want”
Kareem akacheka kidogo na kusema
“ What exactly do you want Peniela?
“ Nitakwambia tukionana ni kitu chepesi tu ninachokitaka unisaidie.kama uko tayari tafadhali fanya hima tuonane haraka”
Kareem akabaki kimya kwa sekunde kadhaa
“ Kareem are you there? Akauliza Peniela
“ Unataka tukutane wapi Peniela?
“ Sema wewe unataka tukutane wapi? Sehemu unayoamini ni salama”
“ Tukutane pale katika mkahawa wa wachina karibu na White Panda lodge” akasema Kareem na kukata simu.Peniela akawasha gari na kuondoka
“ Tunaelekea karibu na White Panda lodge kwenda kukutana na Kareem” Peniela akawataarifu akina Mathew.
“ Peniela are you sure you want to do this? Akauliza Mathew
“Relax Mathew let me do this” akajibu Peniela na safari ikaendelea hadi walipofika mahala alikoelekeza Kareem.Peniela akashuka na kwenda kuketi katika meza moja ambayo haikuwa na mtu akampigia simu Kareem ambaye alimfahamisha kwamba yuko karibu kufika.
“ He’s on the way” Peniela akawataarifu akina Mathew
“ Anitha wewe baki humu garini mimi ngoja niende ndani,I cant leave Peniela alone” akasema Mathew na kushuka garini akaelekea ndani ya mkahawa,akatafuta meza ambayo angeweza kumuona vizuri Peniela
“ Sijui kwa nini Peniela na Anitha wameonyesha wasiw asi kuhusu mpango nilioufikiria wa kumuua kabisa Dr Joshua.Bado naamini ile ingekuwa ndiyo njia pekee ya kuzuia kirusi Aby kisitoke ndani ya ikulu. Lakini ngoja kwanza tuone mpango huu aliousema Peniela kama utafanikiwa.Ikishindikana the only solution will be to kill Dr Joshua” akawaza Mathew
Zilipita dakika kumi na mbili Kareem akatokea Peniela akainuka wakakumbatiana
“ Nimefurahi sana kukuona Peniela.Mambo yako yanakwendaje? Akasema kareem
“ mambo yangu yanakwenda vizuri.Vipi wewe unaendelaje?
“ Hata mimi ninaendelea vizuri “
“ Mazishi ya Flaviana yamemalizika? Akauliza Peniela
“ Ndyo yamemalizik.Tayari Flaviana amezikwa.It’s so sad.She was still very young.Anyway tuachane na hayo nimetoroka mara moja kuja kuitika wito wako.I’m here now tell me what do you want? Akauliza Kareem
“ Nashukuru kwa kuja Kareem.Bila kupoteza wakati kuna mambo mawili nayahitaji” akasema Peniela na kutulia akamtazama Kareem
“ kwanza nataka nikufahamishe kwamba watu wasiojulikana wameiteketeza nyumba yangu juzi usiku kwa hiyo kila kitu kimeteketea .Nimepoteza mawasiliano na Dr Joshua kwa hiyo naomba namba za simu za Dr Joshua”
“ Nani waliokufanyia unyama huo? Tayari wamekamatwa? Dr Joshua anafahamu kuhusu tukio hilo lililokupata?
“ Sina hakika kama Dr Joshua anafahamu kwani sikuweza kumfahamisha .Yawezekana akasoma katika magazeti au kusikia katika taarifa za habari.Kuhusu ni nani kanifanyia vile siwezi kufahamu kwani nina maadui wengi ambao lengo lao ni kuhakikisha ninapotea kabisa.Hata hivyo naviachia vyombo vya uchunguzi vifanye uchunguzi wao.Naomba tafadhaliunipe mawasiliano ya Dr Joshua .”
“ Pole sana Peniela .Sikujua kama umepatwa na janga kubwa namna hii kwa sasa unakaa wapi?
“ Kuna rafiki yangu mmoja amenisaidia makazi ya muda”
“ Good .If you need anything please let me know” akasema Kareem na kumpa Peniela namba za Dr Joshua
“ Jambo la pili ni lipi? Akauliza Kareem
“ Nina shida na Anna mtoto wa Dr Joshua”
“ Anna ? Una shida naye gani?
“ Kwa ufupi si mimi ambaye nina shida naye bali kuna mtu anahitaji kumuona kuna jambo la muhimu anataka kuongea naye.Mimi na Anna hatuna maelewano mazuri na si rahisi mimi kumshawishi aonane na huyo mtu kwa hiyo nataka utumie kila njia unayoweza ili Anna akubali kuonana na mtu huyo jioni ya leo .Can you do that?
Kareem akafikiri kwa muda kidogo na kusema
“ Ni nani huyo mtu anayetaka kuonana na Anna? Anataka kuongea naye mambo gani?
“ Kareem huna haja ya kumfahamu mtu huyo ni nani na wala ni jambo gani anataka kuongea naye hayo hayakuhusu.Ninachokihitaji mimi ni wewe kufanikisha Anna aonane na huyo mtu”
“ Peniela ninao uwezo wa kumkutanisha Anna na huyo mtu anayehitaji kumuona lakini kama ujuavyo yule ni mtoto wa rais na chochote kikimtokea kibaya ,mzigo wote utakuwa juu yangu na ndiyo maana nahitaji kujiridhisha kwanza kwamba anakwenda sehemu salama”
“ Trust me Kareem.Hakuna chochote kibaya kitakachomtokea.Nisingeweza kukuomba jambo hili kubwa kama ningefahamu anakokwenda Anna kuna hatari
Kareem akafikirii kidogo na kusema
“ Sawa nitafanya kama ulivyoomba.Vipi sasa mimi na wewe tunamalizana vipi?
“ usihofu kuhusu hilo.Wakati Anna anaongea na huyo mtu ,mimi na wewe tutakuwa katika chumba cha pili tukifanya yetu.” Akasema Peniela akamfinyia Kareem jicho na kumfanya atabasamu
“ Lakini uwe muangalifu kwa mali za mkuu wako.Nadhani unafahamu adhabu yake pindi akigundua unakula mali zake” akasema Peniela
“ Oh !!! C’mon Peniela ,unampendea nini yule mzee ambaye hana nguvu za kukuridhisha? Siku moja atafia kifuani chako.Achana naye na uwe na vijana kama sisi.Malaika kama wewe hupaswi kabisa kumuonyesha utupu wako Yule mzee” akasema kareem na Peniela akaangua kicheko na kusema
“ I love him .Ananijali sana.Ninyi vijana hamuwezi kunimudu gharama zangu.Hata wewe nitakupa tu penzi kwa sababu bila hivyo usingekubali kunisaidia.Anyway tuachane na hayo,muda unakwenda haraka .Nenda kafanye kazi niliyokutuma halafu nitakupa maelekezo sehemu ya kukutana.Nataka umlete Anna mwenyewe sitaki aongozane na mtu mwingine yeyote” akasema Peniela huku akiinuka na kuagana na Kareem akaelekea katika gari lake.Mathew naye akarejea katika gari lao wakaondoka kurejea nyumbani
“ Mathew endapo Kareem atafanikiwa kumpata Anna,nimuelekeze amlete wapi? Akauliza Peniela wakiwa njiani kurejea nyumbani
“ Sehemu pekee yenye usalama kwa sasa ni katika makazi yetu.Utamuelekeza amlete Anna pale.”
“ Are you sure ? akauliza Anitha
“ Usihofu Anitha ,hakutakuwa na tatizo” akajibu Mathew na safari ikaendelea kimya kimya
Profesa Savatory Ulomi mjomba wa Flaviana ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyoshughulikia mazishi ya Flaviana alitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia ya rais baada ya shughuli ya mazishi kumalizika na waombolezaji walianza kuondoka taratibu kwani tayari jua lilianza kuchwea.
“ lazima nionane na Elibariki.I need to know what’s real going on” akawaza Anna huku macho yake akiwa ameyaelekeza kwa jaji Elibariki aliyekuwa amezungukwa na watu wakimpa pole.Wakati Anna akisubiri watu waliokuwa wakimpa pole jaji Elibariki wapungue ili apatae nafasi ya kuonana naye ,akatokea mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam ambaye aliwataka radhi watu wale waliokuwa na jaji Elibariki na kuondoka naye
“ Amechukuliwa tena,nitamtafuta hata baadae.Leo lazima nifahamu ni kitu gani hasa kinachoendelea kwa sababu mambo yaliyotokea ndani ya kipindi kifupi yamenipa wasi wasi mwingi lazima nijue kin….” Anna akastuka baada ya kuguswa bega ,akageuka na kukutana na Kareem mlinzi wa baba yake
“Kareem “ akasema Anna
“ Anna naweza kuongea nawe kidogo? Akasema Kareem wakasogea pembeni
“ Unasemaje Kareem,?
“ Anna nimeelekezwa na rais nikupeleke sehemu Fulani kuna mtu unatakiwa kuonana naye”
“ Anataka tukaonane na nani? Mbona hajanitaarifu ? Akasema Anna huku akionyesha mshangao kidogo kwa safari ile ambayo baba yake hakuwa amemtaarifu
“ Sifahamu unakwenda kuonana na nani lakini inaonekana ni mtu muhimu sana” akasema Kareem.Anna japokuwa alibaki anajiuliza maswali juu ya nani anayekwenda kuonana naye lakini hakuwa na wasi wasi hata kidogo na Kareem kwani ni mtu ambaye anaaminiwa sana na baba yake.Bila kupoteza muda wakaongozana hadi katika gari la Kareem wakaondoka.Kareem akamtumia Peniela ujumbe katika simu akimtaka amuelekeza mahala ambako Anna atakutana na huyo mtu anayehitaji kuonana naye.Mara tu baada ya kuyaacha makazi ya Dr Joshua ukaingia ujumbe katika simu ya kareem uliotoka kwa Peniela aliyempa maelekezo ya mahala pa kumpeleka Anna
Hakukuwa na maongezi mengi garini,muda mwingi Anna alikuwa amejiinamia akiwaza
“ I’m all alone now.All my loved ones are gone.Edson,mama na sasa ni Flaviana.Kitu gani hasa kinachoendelea katika familia yetu? Why always us? Akajiuliza na kufuta machozi.
“ Hakuna kifo kimeniuma kama cha Flaviana.Amekwenda na uzuri wake.Halafu cha kushangaza mtu ambaye jeshi la polisi lilitangaza kumsaka kwa kusababisha kifo cha Flaviana yupo huru kana kwamba hakuhusika katika tukio lile.Ni filamu gani inayochezwa hapa? Akaendelea kuwaza Anna
“ Nikiwa afrika ya kusini niliwasiliana na Elibariki na akanihakikishia kwamba baba ndiye muhusika mkuu wa vifo vya mama na Flaviana lakini cha kushangaza ameibuka toka alikokuwa amejificha na amekuja akiwa ameongozana na baba .Hapana siwezi kuruhusu akili yangu ikubaliane na sinema hii inayoendelea Halafu kingine kinachonishangaza ni hizi taarifa nilizozisikia eti Elibariki alikuwa ametekwa na alifanikiwa kutoroka.Mimi niliongea naye kwa simu akaniambia kwamba yuko mafichoni kuna watu wanaomtafuta wamuue sasa hizi hadithi za kwamba alikuwa ametekwa na kufichwa msituni zinatoka wapi? Yeye na wote anaoshirikiana nao watawadanganya watu wengine lakini si mimi. “ akaendelea kuwaza Anna huku safari ikiendelea.
Kareem alifuata maelekezo yale aliyopewa na Peniela na kujikuta akitazamana na geti jeusi
“ Ni hapa” akawaza Kareen halafu akamgeukia Ann a ambaye bado alikuwa amejiinamia
“ Anatia huruma sana huyu binti.Imemtokea misiba mfululizo ya watu wake wa karibu.Ni nani huyo mtu anayehitaji kuonana naye? Anataka nini kwa Anna? Sehemu hii ni salama? Akajiuliza Kareem
“ Lakini sina wasi wasi na Peniela,endapo kugekuwa na hatari yoyote asingeweza kuniomba nimlete Anna .”
Mara uso wa Kareem ukachanua tabasamu baada ya kumkumbuka Peniela
“ Muda mrefu sana nimekuwa nikimtamani Peniela na leo siamini kama nitaipata nafasi ya kujivinjari naye .Japokuwa ninajiweka katika matatizo makubwa endapo Dr Joshua atagundua lakini siwezi kuiacha nafasi hii adimu “ akawaza Kareem na kumshika Anna bega
“ Anna we’re here” akasema Kareem na kushukja garini akaenda getini akabonyeza kengele
Mathew na akina Anitha Wakiwa katika ofisi yao walisikia kengele ya getini na wote wakaenda katika chumba kidogo ilimo luninga iliyounganishwa na kamera za ulinzi
“ Kareem” akasema Peniela
“ Anitha utaenda kufungua geti mimi sitaki kuonana na Anna.Akiniona tu hatakubali kuingia humu ndani.Wakishainga ndani utamuacha Anna sebuleni na Mathew halafu utamleta Kareem chumbani kwangu.Wakati mimi na y eye tukiwa chumbani ninyi mtaongea na Anna na mkisha maliza utagonga mlango na Kareem atatoka” akasema Peniela.Mathew akamtazma na kutaka kusema kitu lakini kabla hajasema chochote Anitha akasema
“ That’s a good plan.Ngoja nikawafungulie geti” Anitha akatoka akaenda kufungua geti akakutana na Kareem wakasalimiana
“ Kareem karibu sana"Akasema Anitha huku uso wake ukiwa na tabasamu kama vile anafahamiana sana na Kareem
“ Ahsante sana! akajibu Kareem
Anitha akawaongoza akina Kareem hadi sebuleni ambako walimkuta Mathew ambaye naye aliwakaribisha kwa furaha.Anna alikuwa anashangaa hakuwafahamu watu wale aliowakuta katika ile nyumba.
“ hawa ni akina nani? Akajiuliza.Anitha akawakirimu wageni wao vinywaji halafu akasema
“ Kareem na Anna karibuni sana.Mimi naitwa Anitha na Yule mwenzangu pale anaitwa Mathew ambaye ndiye anayehitaji kuongea machache na Anna.Kareem naomba tuwaachie nafasi Mathew na anna ya kuzungumza.” Akasema Anitha.Kareem naye alipatwa na mshangao kidogo lakini hakutaka kuonyesha mbele ya Anna
“ Kareem what’s this? What’s going on here? Akauliza Anna kwa mshangao
“ Relax Anna usiwe na wasi wasi.You are safe here.I’ll be just next door.”
“ No kareem you stay here !! akasema Anna.Kareem akamsogelea na kumnong’oneza kitu sikioni halafu yeye na Anitha wakaondoka pale sebuleni wakamuacha Anna na Mathew
“ Usiogope Anna.Uko salama na hakuna chochote kibaya kitakachokutokea” akasema Mathew.Anna akamtazama Mathew kwa macho makali na kusema
“ Who are you? How do you know me? Why do you want to see me? Akauliza Anna.Mathew akamfanyia ishara aketi kitini na baada ya sekude kadhaa akasema
“ Naitwa Mathew,ni mpelelezi wa kujitegemea.Nimewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa lakini kwa sasa ninajishughulisha na kazi binafsi” akasema Mathew .
“ Mimi na wewe hatujawahi kukutana na wala kufahamiana na ndiyo maana nimeamua kumtumia Kareem kutukutanisha.” Akasema Mathew.Anna akapatwa na mshangao
“ So he lied to me? Aliniambia kwamba baba alimtuma anilete huku kuna mtu ambaye natakiwa kuonana naye.Kareem must pay for this..How could he sell me like this? Akasema Anna kwa hasira huku akiinuka
“ I’m going..mwambie huyo mwenzako uliyemtumia kunidanganya kwamba nimeondoka and he is going to answer to my father.!! Akasema Anna kwa hamaki. Huku akianza kupiga hatua.Mathew akasimama
“ Anna you are not leaving!! Akasema Mathew kwa ukali na kumfanya Anna ageuke ,akajikuta anatazama na bastora,pochi aliyoishika ikamponyoka na kuanguka kwa woga
“ Oh my gosh !! Kareem set me up..This is a trap “ akawaza Anna huku akihisi miguu ikimuisha nguvu.
“Are..a..are..you..goi…going to shoot me?? Akajikaza na kuuliza
“ If I have to ,Yes !!!!..akasema Mathew kwa ukali
“ Sikiliza Anna,sijakuita hapa ili kukutisha au kukufanyia kitu chochote kibaya bali uko hapa mida hii kwa sababu moja kubwa nayo ni kuhitaji msaada wako”
“ msaada wangu?? Akauliza Anna
“ Ndiyo nahitaji msaada wako”
“ Umenielekezea bastora na wakati huo huo unahitaji msaad wangu ?? Siwezi katu kukusaidia.I’m leaving and if you want to shoot me go ahead,shoot me !! akasema Anna kwa ukali na kuinuka akaanza kuelekea mlangoni
“ Anna please help me find who killed your mother and your sister” akasema Mathew.
“ What?? Akauliza Anna na kugeuka
“ What you’ve just said?
“ Help me find who killed your mother and your sister Flaviana
"
Kwa dakika mbili Anna akasimama akimkodolea macho Mathew
“ Naomba uketi Anna.Kuna mambo mengi ya kuongea mimi na wewe” akasema Mathew na bila ubishi Anna akaketi sofani.
“ Anna najua nimekugusa sana kwa hili nililolitamka na ninapenda kwanza kutumia nafasi hii kukupa pole sana kwa misiba mizito uliyoipata.Pole sana Anna” akasema Mathew kwa sauti ya upole.
“ Do you know who killed my mother and my sister? Akauliza Anna huku akilengwa na machozi
“ Yes I know” akajibu Mathew
“ tell me please” akasema Anna na kuchukua kitambaa akajifuta machozi
“ Ni hadithi ndefu kidogo ila nitakueleza kila kitu kilichotokea na nini kinachoendelea hivi sasa” akasema Mathew
“ Kabla sijasema chochote nataka nikuombe samahani sana kama nitakuwa nimekukumbusha machungu ya vifo vya wapendwa wako”
“ Go ahead,tell me everything” akasema Anna
“ Nitaanzia mbali kidogo kwa aliyewahi kuwa mchumba wako Edson.Kabla ya kifo chake,Edson alikuwa katika mahusiano na msichana mmoja anaitwa Peniela ambaye ndiye aliyekuwa mtuhumiwa mkuu wa kifo cha Edson.Baada ya kesi kusikilizwa, mahakama ilijiridhisha kwamba Peniela hakuwa na hatia na ikamuachia huru.Jaji aliyeisikiliza kesi ile alikuwa ni jaji Elibariki ambaye ni mume wa dada yako.Wakati wa kusikilizwa kwa kesi ile ,jaji Elibariki aligundua kwamba kuna nguvu kubwa ilikuwa inatumia katika kuhakikisha Peniela aliyekuwa anatuhumiwa kumuua Edson,anakutwa na hatia na hatimaye kufungwa,jambo ambalo lilimfanya jaji Elibariki ajiulize kulikoni? .Baada ya kesi kumalizika ilimlazimu jaji Elibariki atake kufahamu ukweli wa jambo lile na kumpata muuaji halisi wa Edson kwani alimini Peniela hakumuua Edson” Mathew akatulia kidogo halafu akaendelea
“ kwa kuwa jaji Elibariki ni mbobezi katika mambo ya sheria ilimlazimu kutafuta mtu ambaye amebobea katika mambo ya uchunguzi na kwa kua mimi na yeye tunafahamiana akanifuata na kuniomba nimsaidie kufanya uchunguzi huo ili kubaini ni nani hasa aliyemuua Edson? Nilikubali kumfanyia kazi hiyo na katika kuifanya kazi hiyo niliungana pia na wenzangu wawili ambao hufanya nao kazi pamoja.Wenzagu hao ni Noah ambaye kwa sasa ni marehemu na Anitha huyu aliyewakaribisheni hapa.Vile vile nilimshirikisha pia Jason wakili aliyekuwa anamtetea Peniela” Mathew akanyamaza na kumtazama Anna aliyekuwa makini akimsikiliza
“ Uchunguzi wetu ulitupelekea kugundua mambo kadhaa ,kwanza tuligundua kwamba Peniela hakumuua Edson kama ilivyodaiwa bali Edson aliuawa kwa amri ya rais..”
“ My father ??..that cant be …” akasema Anna
“ Ndiyo Anna.Baba yako ndiye aliyetoa amri Edson auawe.”
“ Mathew I cant believe you…Baba hawezi kabisa kumuua mpenzi wangu,that’s not true !!! akasema Anna
“ Sababu kubwa iliyosabisha Edson auawe ni baada ya kuazisha mahusiano na Peniela ,kwani Peniela alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Dr Joshua”
“ What ??!! Anna akastuka sana
“ Usishangae Anna huo ndio ukweli.Peniela na baba yako wana mahusiano ya siri ya kimapenzi.Alipogundua kwamba Peniela na Edson wana mahusiano Dr Joshua alichukia mno na akatoa amri Edson auawe’
“ Siamini kama hicho unachonieleza ni kitu cha kweli” akasema Anna huku akitokwa na machozi ,Mathew akaendelea
“ Kitu kingine tulichokibaini ni kwamba Edson alikuwa na mtandao wake ambao walimtumia kuiba nyaraka Fulani ikulu.Nyaraka hizo zilikuwa na kanuni ya kutengeneza kirusi hatari kinachoweza kusababisha maangamizi makubwa.”
Anna akashika kichwa kwa mshangao.Muda ulizidi kwenda na Mathew akaendelea
“ Wakati tukiendelea na uchunguzi ,tukagundua uwepo wa kikundi fulani cha watu wachache kijulikanacho kama Team SC41.Kikundi hiki kipo hapa nchini na kinaendesha shughuli zake kwa siri kubwa na kazi zake ni kulinda maslahi ya Marekani hapa nchini.Tuligundua kwamba Peniela naye n mmoja wa Team SC41 na mahusiano yake na Dr Joshua yalikuwa ni kwa sababu maalum.Team Sc41 kuna kitu fulani wanakitafuta toka kwa Dr Joshua ambayo ni package Fulani ambayo imehifadhiwa mahala pa siri ndani ya ikulu na ndani ya package hiyo kuna kirusi hatari kinachoitwa Aby.Hiki ni kirusi hatari kwa dunia kwani hakina kinga wala tiba hadi sasa na kinaweza kuleta maangamizi makubwa duniani endapo kitaachiwa kisambae hewani.Dr Joshua kwa kushirikiana na washirika wake wa karibu akiwemo Dr Kigomba wanataka kukiuza kirusi hicho kwa pesa nyingi mno.Katika mpango huo Dr Joshua anashirikiana na washirika wake wa karibu ambao ni Dr Kigomba na Captain Amos ambaye kwa sasa ni marehemu”
“ Dr Amos is dead?? Anna akazidi kushangaa
“ yes he’s dead” akajibu Mathew
“ Oh my God ! what’s going on? Akajiuliza Anna
“ Captain Amos” Mathew akaendelea
“ Alikuwa katika kundi moja na Peniela la Team SC41na wote wawili kwa pamoja walikuwa na lengo la kukipata kirusi hicho” Mathew akatulia kidogo halafu akaendelea
“ Marehemu Dr Flora alifahamu kuhusu mpango huu wa Dr Joshua kukiuza kirusi Aby na akajitahidi sana kutaka kuzuia jambo hili lisifanyike kwani aliyafahamu madhara yake lakini akashindwa .Hatua ya mwisho aliyotaka kuichukua ni kwa kuwaelezeni ukweli wewe na Flaviana lakini hakuweza kufanya hivyo kwani alifariki ghafla kabla hajawaelezeni chochote.Kifo chake kilitokana na kuchomwa sindano ya sumu na aliyefanya hivyo kwa amri ya rais ni Captain Amos.”
Haikuwa rahisi kwa Anna kukubali moja kwa moja kama baba yake angeweza kufanya kitendo kama kile
“ No ! No ! No !...baba yangu katu hawezi kufanya kitendo kama hicho.Tafadhali naomba usizidi kunichanganya kichwa changu!! Please tell the truth who killed my mother?? Akauliza Anna huku akilia.
“ Baada ya kifo cha Dr Flora,kuliwekwa zuio la kutaka kufanya uchunguzi wa kubaini sababu za kifo chake bali ikatolewa sababu nyepesi tu kwamba ni shinikizo la damu.Flaviana hakuridhika na kilicho kuwa kinaendelea akamuomba mumewe jaji Elibariki amsaidie kupata ukweli kuhusu kifo cha mama yake.Jaji Elibariki alinifuata na kuniambia nimsaidie kuupata ukweli huo.Haikuwa kazi nyepesi lakini mwishowe tulifanikiwa kujua kilicho muua Dr Flora .Jaji Elibariki aliwasilisha kwenu ripoti ya uchunguzi tulioufanya lakini Dr Joshua kwa kufahamu kwamba ilikuwa inasema ukweli aliipinga vikali.Kutokana na ripoti ile tayari Dr Joshua akaingiwa na wasi wasi na ili siri ya Dr flora isivuje iliamriwa kwamba jaji Elibariki auawe kwani tayari alikwisha kuonekana ni mtu hatari kwao.Lilipangwa shambulio la kushtukiza na katika shambulio hilo jaji Elibariki akanusurika kufa baada ya kuokolewa na mmoja wa washirika wangu aliyekuwa naye garini .Noah alipoteza maisha wakati akimuokoa Elibariki asiuawe kwa risasi.Shambulio hilo lililopofanyika alitokea mwanamke mmoja ambaye hadi leo hatujamfahamu ambaye alimchukua Elibariki na kumpeleka kwa Peniela”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Peniela again? Akauliza Anna kwa mshangao
“ Anna I’m sorry to tell you this but Peniela na Elibariki walikuwa na mahusiano ya siri”
“ This woman is a devil!!...Mpenzi wangu ,baba yangu,shemeji yangu wote ni wapenzi wake,what kind of a woman is she?? Everywhere Peniela ,Penelal!!! Akasema Ana kwa ukali.Mathew hakumjali akaendelea
“ Kama nilivyokueleza awali kwamba Peniela ni mwanamke anayetumiwa kufanya kazi maalum na Team SC41.Ukimuona yuko na mwanaume Fulani basi fahamu kwamba si kwa ajili ya mapenzi bali kuna kitu anakitafuta.Jaji Elibariki baada ya kunusurika kuuawa yeye mwenyewe alichagua kujificha kwa Peniela na baadae akanipigia simu nikaenda kumchukua na kumuhifadhai nyumbani kwangu . Kuna mambo mengi ambayo tumeyagundua lakini kutokana na muda sintoweza kukueleza yote ila kuna jambo moja nataka ulifahamu.Tuligundua kwamba kuna mtu mmoja tajiri aishiye nchini Saudia Arabia ambaye ndiye mnunuzi wa kirusi hicho na ambaye alitakiwa kuingia nchini jana kuja kukichukua kirusi hicho.Bado sijafahamu huyu Hussein ni nani na ana malengo gani na kirusi hicho ila ninachokifahamu ni kwamba Marekani kwa kutumia Team SC41 wanakutaka kirusi hicho ili kuleta maafa makubwa hapa nchini kwa lengo la kuchota rasilimali za nchi.Kama hili litafanikiwa maelfu ya watu wataangamia kwani kirusi Aby kunasambaa kwa njia ya hewa na ndani ya muda mfupi maelfu ya watu wataangamia”
“ Oh my God…!! Akasema Anna kwa woga
“ Jaji Elibariki akiwa mafichoni ,msako mkali uliendeshwa na jeshi la polisi wakimtafuta kwa kusababisha kifo cha Flav……”
“ Hebu ngoja kwanza Mathew” Ana akamkatisha Mathew
“ Bado hujanieleza ni nani aliyemuua Flaviana ?
“ Oh sorry nilijisahau ,mambo ya kukueleza ni mengi.Kuhusu kifo cha Flaviana ni kwamba baada ya Dr Joshua kuikataa taarifa aliyoileta jaji Elibariki kuhusiana na kilichosababisha kifo cha Dr Flora, walitengeneza ripoti ambayo walidai kwamba ni ya madaktari bingwa toka katika hospitali kuu ya taifa .Jaji Elibariki alitaka kuipata taarifa hiyo ili tufanye uchunguzi kubaini ukweli kwa hiyo akampigia simu na kumuelekeza sehemu ya kukutana ili aweze kumpatia zile karatasi .Flaviana hakujua kama kulikuwa na watu waliotumwa kumfuatilia ambao dhumuni lao ni kumpata Elibariki.Baada ya kufika sehemu tulikopanga wakutane likatokea shambulio la ghafla na katika shambulio hilo Flaviana akajeruhiwa kwa risasi na hivyo ndivyo sababu ya kifo chake.Hata hivyo tulipata taarifa hiyo na tukaifanyia kazi tukabaini haikuwa na ukweli wowote kwani madaktari wale wote walioorodheshwa katika taarifa hivyo kwamba walishiriki kufanya uchunguzi kubaini kifo cha Dr Flora hakuna hata mmoja anayefanya kazi katika hospitali kuu ya taifa wala hawapo katika orodha ya madaktari nchini”
“ Jesu Christ !!!..akasema Anna.Mathew akaendelea
“ Dr Joshua alipata fununu kwamba jaji Elibariki na Peniela wana mahusiano na kwamba amejificha nyumbani kwa Peniela.Ili kupata uhakika kuhusu hilo akamtuma Dr Kigomba amchunguze lakini naye akajikuta akianguka katika mahusiano na Peniela.
“ Again???.Peniela again???.Jamani huyu mwanamke ana tatizo gani? Mbona wanaume wote mji huu ni wake? Anna akazidi kushangaa
“ Kama nilivyokueleza Anna ni kwamba Peniela akiwa katika mahusiano na mtu huwa ni kwa ajli ya jambo Fulani lakini kwa Dr Kigomba hakuwa akifanya kazi ya Team SC41 bali alikuwa anashirikiana na sisi “
“ My God !!!even you?? .. akasema Anna kwa mshangao
“ Naomba nikuweke wazi Anna kwamba kwa sasa tunafanya kazi pamoja na Peniela “
“ No ! that’s not true !!! Tell me its not true ..” akasema Anna
“ Its true Anna ila ni hadithi ndefu kidogo nitakueleza siku nyingine ila kwa sasa naomba uelewe hivyo kwamba tunafanya kazi bega kwa bega na Peniela” akasema Mathew na kwa sekunde kadhaa wakabaki wanatazamana
“ Juzi usiku nilimsindikiza Peniela nyumbani kwake na wakati tukirejea akataarifiwa na mmoja wa vijana toka Team SC41 kuwa achukue tahadhari kuna watu wanamfuatilia.Usiku huo yakatokea mapambano kati yetu na watu waliotumwa kumfuatilia Peniela.Tulizidiwa nguvu lakini tulifanikiwa kuwatoroka na tulipofika kurejea nyumbani kwa Peniela tulikuta nyumba yake inateketea kwa moto.Wakati sisi tukipambana na Team SC41 ,nyumbani kwangu pia kulitokea tukio baya.Jaji Elibariki alimpiga Anitha na kitu kizito kichwani akapoteza fahamu ,akamfungua Rosemary Mkozumi wakaiteketeza nyumba kwa moto wakamchukua mateka Anitha na kuondoka naye.Anitha alipelekwa kwa Rosemary Mkozumi ambako aliteswa sana ili aeleze mahala nilipo lakini kwa jitihada zake binafsi alifanikiwa kutoroka na kuungana nami tena.Jaji Elibariki amerudisha nyuma juhudi zetu zote za kukipata kirusi Aby.Mpaka sasa hatufahamu ni kwa nini alifanya vile .Hata hivyo baada ya haya yote kutokea tumejipanga upya na tunaendelea na operesheni yetu ya kuhakikisha tunakipata kirusi Aby na kuzuia maangamizi makubwa yanayoweza kutokea nchini kwetu au sehemu nyingine yoyote ambako kirusi hiki kingeweza kuachiwa hewani.Kwa hiyo Anna nimekuita hapa nikueleze ukweli wa kila kinachoendelea ili tusaidiane mosi kukipata kirusi Aby na kuiepusha nchi yetu na dunia dhidi ya janga kubwa linaloweza kutokea iwapo kirusi Aby kitaachiwa kisambae hewani.Pili kuhakikisha kwamba wale wote waliohusika katika vifo vya mama na dada yako wanafikishwa katika vyombo vya sheria bila kujali ni akina nani.Katika kufanikisha haya tunahitaji mno msaada wako” akasema Mathew.Anna akainama na baada ya kama dakika mbili akafuta machozi na kusema
“ First I want to tell you that I believe you” Anna akafuta machozi tena na kuendelea
“ Bnafsi nilikwisha hisi kuna jambo linaloendea na hata usiku ule Flaviana aliposhambuliwa nilikuwa naye ila aliniacha sehemu nikimsubiri na kabla hatujaachana ,tuliongea kuhusu jambo hilo na baada ya kuchambua masuala kadhaa tukapata picha kwamba kuna kitu kinachoendelea.Nikiwa afrika ya kusini nilimpigia simu jaji Elibariki na nikamtaka anieleze ukweli kama baba anahusika katika matukio yale ya vifo vya mama na dada na akanihakikishia kwamba ni kweli baba ndiye muhusika mkuu wa matukio yale yote.Tulipanga na kuongea zaidi pindi nitakaporejea toka afrika ya kusini lakini nilistuka jana usiku nilipomuona Elibariki akiwasili msibani akiwa ameongozana na baba.Sikuweza kupata nafasi ya kumuhoji yeye wala baba.Leo asubuhi nimetolewa taarifa katika vyombo vya habari kwamba kuna majambazi wameuawa usiku wa kuamkia leo katika msitu wa Makenge.Kwa mujibu wa taarifa hizo ni kwamba majambazi hao ndio waliokuwa wamemteka jaji Elibariki na ndio waliohusika katika kusababisha kifo cha Flaviana.Baada ya mazishi ya Flaviana nilitaka nimtafute nimuhoji lakini alikuwa amesongwa sana na watu wakimpa pole na baadae alifika mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam akaondoka naye.Sikuweza kumfuatilia tena kwani Kareem alifika na kunichukua akanileta huku.Mathew maelezo uliyonipa yamenifumbua macho na sasa nimeelewa kilichotokea na kinachoendelea .Nashukuru kwa kunieleza ukweli halisi bila kujali kama ukweli huo utaniumiza ama vipi.Ni kweli nimeumia mno kwa mambo uliyonieleza na hasa kwamba baba yangu ndiye muhusika mkuu wa matukio ya vifo vya mama na Flaviana.Kwa namna moyo wangu unavyosononeka kwa vifo vya watu niliowapenda na kwa sababu hiyo nitaungana nanyi katika kuhakikisha wale wote waliosababisha vifo hivyo awe ni baba au nani lazima wanafikishwa mbele ya sheria.Tafadhali naomba nieleze Mathew unahitaji nini ili tuweze kuwafikisha hawa watu mahakamani? Unahitaji nikusaidie jambo gani? Niko tayari kufanya jambo lolote hata kama ni la hatari kiasi gani ili mradi nihakikishe watuhumiwa wote wanafikishwa mbele ya sheria tukianza na baba yangu.” Akasema Anna huku akifuta machozi.Mathew akamtazama kwa makini usoni
“ She’s deeply hurt and she’s ready to do anything.Huyu atakuwa msaada mkubwa kwetu” akawaza Mathew
“ Anna kwanza nashukuru sana kwa kukubali kuniskiliza ,pili kwa kunielewa na tatu kwa kukubali kuungana nasi katika operesheni yetu.Umechagua jambo jema na ninakuahidi kwa niaba ya wenzangu kwamba hakuna yeyote ambaye amehusika katika mambo haya yote atakayesalimika.Lazima wote wafikishwe mbele ya sheria.Pamoja na hayo nataka nikuweke wazi kwamba jambo hili ni la hatari kubwa kwa hiyo utafakari kwa makini na uwe tayari kwa lolote ,muda wowote .Ukumbuke pia kwamba hapa tunazungumzia kumuangusha mtu mwenye mahusiano makubwa na wewe,Dr joshua ambaye ni baba yako mzazi kwa hiyo inahitaji moyo mgumu kuweza kukubali kumuona baba yako akienda mbele ya sheria”
“ Mathew najuta kuwa na baba mwenye roho ya kishetani kama huyu.I hate him so much.Ninakuhakikishia Mathew kwa namna nilivyotokea kumchukia baba yangu niko tayari hata sasa hivi kumuona akianguka katika mkono ya sheria.Sintaumia kabisa kumuona akisimama mahakamani kujibu kwa mambo maovu aliyoyafanya.Mtu kama yule na wenzake wanastahili kifungo kirefu gerezani.Theu are monsters.They don’t have souls! Akasema Anna kwa hasira
“ Ok good.Sasa ni hivi kuna mambo mawili ambayo nataka uyafanye ambayo yanaweza kuwa na msaada kwetu.Kwanza jenga ukaribu na Elibariki na uchunguze ni kitu gani kinachoendelea kati yake na Dr Joshua.Jaji Elibariki lazima atakuwa amemueleza Dr Joshua mipango yetu yote ili kumfanya amuamini na ninaamini kabisa kwamba taarifa iliyotolewa leo asubuhi kwamba Elibariki alikuwa ametekwa na majambazi ni mojawapo ya njia za kumsafisha Elibariki na hapo ndipo unapoweza kuona kuwa kwa sasa Elibariki ni mtu muhimu sana kwa Dr Joshua na ninahisi anaweza akamshirikisha hata katika baadhi ya mipango yake.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Jambo la pili linaweza kuwa gumu kidogo kwako lakini hatutalifanya kwanza hadi hapo tutakapofanya maandalizi”
“ Ni jambo gani Mathew? Nimekwambia kwamba niko tayari kwa jambo lolote lile hata kama ni gumu na hatari kiasi gani mimi nitalifanya.Tell me what to do and I’m going to do it” akasema anna kwa kujiamini.Mathew akavuta pumzi ndefu akamtazama Anna kwa makini na kusema
“ We need someone who can have access to President office.Can you do that?
Bila kufikiri mara mbili Anna akasema
“ Ile ni ofisi ya baba yangu na ninaingia mara nyingi sana.Unahitaji nini katika ofis ya rais? Tell me Mathew and I’m going to do it!!
“ Dah ! Nimependa sana ujasiri wa Anna.Haogopi anafaa sana kufanya naye kazi” akawaza Mathew
“ Kwa kuwa nina uhakika kwamba mpaka mida hii tayari Dr Joshua na wenzake watakuwa na mipango mipya baada ya kuelezwa kila kitu kuhusu mipango yetu na jaji Elibarki,njia pekee ya haraka ya kukipata kirusi Aby kabla ya Dr Joshua hajakikabidhi kwa Hussein ni kwa kuingia wenyewe mahali kilipohifadhiwa na kukichukua.Mpaka kesho jioni nina uhakika tayari nitakuwa nimeonana na mtu huyo na nitakuwa na taarifa kamili kuhusu mahali kilipo kirusi Aby.Kwa hiyo basi naomba ujitahidi kupata taarifa zozote zinazoweza kutusaidia kutoka kwa Elibariki na wakati huo huo mimi nikifanya taratibu za kuonana na huyo mtu ambaye anafahamu mahala kilipo kirusi hicho.Tutakapokutana tena tutapanga vizuri mpango mzima”
“ Nimekuelewa vizuri Mathew and I’m ready to find justice for my mother and my sister.I’m not scared to take down my own father!! Akasema Anna
“ Usijali Anna.Haki itatendeka na wote waliohusika kwa namna yoyote na vifo vya Flaviana na Dr Flora hakuna atakayesalimika.Wote watakutana na mkono wa sheria
“ "Thank you Mathew.Lakini bado nina maswali kama mawili au matatu kama hutajali”
“ Uliza Anna”
“ Hicho kirusi Aby kilifikaje ikulu? Kilitokea wapi?
“ Hiyo ni habari ndefu kidogo nitakufahamisha siku nyingine endapo tutakuwa na muda wa kutosha”
“ Sawa Mathew swali la mwisho,Kareem anafahamu chochote kuhusu mambo haya uliyonieleza?
“ Hapana hafahamu chochote”
“ Good.Hatakiwi kufahamu chochote .Ni mtifi sana kwa baba na akifahamu chochote kinaendelea kuhusu baba lazima atamueleza.Mambo haya yanatakiwa yawe siri kubwa.Amekwenda wapi kwani?
“ Wapo chumba kingine wakiongea ili mimi na wewe tupate nafasi nzuri ya kuzungumza bila bugudha na bila ya Kareem kusikia chochote”
“ Unaweza kumuita ili tuondoke? Mda unazidi kwenda na ninadhani tayari tumeongea mengi ya kutosha lakini kabla hatujaondoka nitaomba unipatie namba yako ya simu ili tuweze kuwasiliana “ akasema Anna ,wakabadilishana namba za simu halafu Mathew akaenda moja kwa moja katika chumba cha ofisi alimokuwamo Anitha
“ Anna yuko tayari kuondoka,mstue Kareem” akasema Mathew
“ Mambo yamekwendaje lakini?
“ Kila kitu kimekwenda vizuri.Go get him .Anna is waiting” akasema Mathew na kutoka akarejea sebuleni.Baada ya dakika tatu Kareem akatokea na Mathew na Anitha wakawasindikiza hadi katika gari lao wakaondoka
“ Mambo yamekwendaje? Akauliza Anitha wakati wakirejea sebuleni baada ya akina Kareem kuondoka
“ Tutaongea .Nitawaelezeni kila kitu but I need to see Peniela first if she’s ok”
“ Peniela is ok” akasema Anitha,wakaingia ndani na kuelekea katika ofisi yao na muda huo huo Peniela akatokea
“ How did it go? Akauliza Peniela
“ Mambo yamekwenda vizuri .It wasn’t easy lakini nashukuru amenisikia na kunielewa”
“ Good” akasema Peniela
Mathew akawaeleza kila kitu walichokiongea na Anna
“ I was right then.Anna ni msaada mkubwa kwetu atatusaidia kufanikisha mipango yetu”
“ Ndiyo.Ulikuwa sahihi.Anna atakuw ana msaada mkubwa kwetu.Nimemsoma ,ana nia ya dhati ya kulipiza kisasi kwa vifo vya mama na dada yake.Kwa msaada wake tunakwenda kuchukua kirusi ikulu ,hatuna namna nyingine ya kufanya ili kumuwahi Dr Joshua kabla hajakikabidhi kirusi hicho kwa Hussein.Kwa kuwa nyote wawili hamkuwa tayari kwa mpango wangu wa kumuua Dr Joshua kwa hiyo basi hii ni nafasi nyingine imetokea na tunatakiwa kuwekeza nguvu zetu zote kufanikisha kukichukua kirusi Aby toka mahala kilipofichwa.Tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuwasiliana na Deus Mkozumi yeye atatupa maelezo ya mahala kirusi hicho kilipo.Wakati wa uongozi wake Deus Mkozumi alihakikisha kwamba anakilinda kirusi Aby kwa nguvu zake zote kwa hiyo hayuko tayari kumuona Dr Joshua akikiuza kirusi hicho.Nina uhakika lazima ataungana nasi na atatusaidia katika mipango yetu.” Akasema Mathew
“ Mathew mpango huu ni mzuri sana kuliko ule wa kumuua Dr Joshua.Nina uhakika mkubwa tutafanikiwa .Kuhusu kuonana na Deus Mkozumi hilo halina shaka hata kidogo.Nitalifanikisha hilo.Kama mtakumbuka mara ya mwisho nilipoonana naye alionyesha wazi kuvutiwa sana nami.Huo ni mwanya ambao tunatakiwa kuutumia vyema”
“ No Peniela.You’ve done enough.This time mwili wako hauwezi kutumika kama chambo .We’re going to find another away”
“ Mathew najua unanijali sana na hupendi kuona nikiutumia mwili wangu kama chambo lakini kwa hatua tuliyofikia sasa sina budi kufanya hivyo.Bila kufanya hivyo katu hatutaweza kupata kile tunachokihitaji.Please let me do this”
“ Hapana Peniela imetosha.Safari hii tutakwenda sote kuonana na Deus Mkozumi ,tutamweleza ukweli and he will help us”
“ No Mathew.That wont work.Deus Mkozumi si mtu rahisi kama unavyodhani.Please let me do this my way.Nina hakika tutafanikiwa” akasema Peniela lakini Mathew akatikisa kichwa ishara ya kutokubaliana naye
“ Mathew trust me I’m good at this and I’ve never fail” akasema na kusisitiza Peniela
“ Mathew let Peniela do this” akasema Anitha.Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Sawa Peniela tufanye hivyo unavyotaka lakini moyoni I’m not happy .Tutafanya maandalizi baada ya kurejea kutoka kulichukua kasha alilokupa John lako.Nadhani muda huu ni muafaka kabisa wa kwenda huko mahala ulikolihifadhi
“ Kasha ?!! Anitha akashangaa
“ Ndiyo Anitha.sikukufahamisha kuhusu jambo hili lakini kuna kasha ambalo John Mwaulaya alimpatia Peniela na ambalo lina mambo muhimu sana yanayomuhusu Peniela .Kutokana na unyeti wake Peniela alilihifadhi kasha hilo katika nyumba aliyopewa na Dr Joshua na ambako ndiko tunakwenda kulichukua”
“ Mathew nitakwenda huko peke yangu ,ninyi mtabaki hapa,sintachukua muda mrefu” akasema Peniela
“ Hapana Peniela siwezi kuliruhusu hilo.Kokote utakakokwenda sisi tutakuwa nyuma yako.Tutakwenda sote huko na hakuna mjadala katika hilo.Jiandaeni tuondoke ili tuwahi kurudi” akasema Mathew na kuondoka akaelekea chumbani kwake.
*******
Mara tu baada ya shughuli za mazishi kumalizika,Rosemary Mkozumi alizungukwa na viongozi mbali mbali wakimpa pole kwa masahibu yaliyomkuta.Wengine walimpongeza kwa uamuzi wake wa kutaka kugombea urais na kumpa moyo asikate tamaa aendelee kupambana.Hiki ndicho alichokuwa anakitafuta Rosemary .Wakati akiendelea kusalimiana na watu mbali mbali ,alikuwa macho sana kuangaza huku na kule kumtafuta Dr Joshua.Alihitaji kupata wasaa wa kuongea naye mawili matatu lakini mara ghafla msaidizi wake akamfuata na kumnong’oneza kitu sikioni
“ Madam twende garini kuna jambo nataka nikueleze”
“ Not now !! Bado ninahitaji kuonana na rais..” akajibu Rosemary
“ Madam kuna dharura imetokea.”
“ Dharura gani? Nini kimetokea? Akauliza Rosemary
“ Twende garini” akasema Rita msaidizi wake.Rosemary akaagana na watu ambao bado walikuwa na hamu ya kuongea naye akaelekea garini
“ Rita nini kimetokea? Akauliza baada ya kuingia garini.
“ Kuna taarifa niliyoipokea muda si mrefu kidogo ambayo si nzuri lakini sikuweza kukufahamisha mapema kutokana na shughuli iliyokuwa inaendelea”
“ Niambie Rita nini kimetokea?
“ Ni Fernando”
“ Fernando? Kafanya nini?
“ Is dead”
“ Dead ??.Rosemary akapatwa na mstuko mkubwa
“ When? How?? Akauliza
“ Kwa mujibu wa taarifa niliyopewa ni kwamba Fernando aliondoka nyumbani akiwa na msichana mmoja ambaye alikuwa na hali mbaya na akadai kwamba anaelekea hospitali .Haijulikani nini kimetokea ila Fernando amejirusha toka ghorofa ya tano ya benki na akafariki dunia”
Dakika tatu zikapita Rosemary Mkuzumi akiwa kimya.
“ Please take me home..Hurry !! akamuamuru dereva wake naye akaliondoa gari kwa kazi
“ Ni msichana yupi ambaye Fernando ametoka naye akiwa hoi? Kuna wasichana wawili mle ndani,Anitha na Naomi,ni yupi kati yao ? Naomba isije kuwa ni Anitha kwani nitakuwa nimepoteza kila kitu.Halafu kwa nini ajirushe ghorofani? Hizi taarifa zimenistua mno. Fernando ni mtu ambaye nilikuwa namtegemea mno katika kazi zanu nyingi.Nini hasa kilichomsibu hadi akaamua kuchukua uamuzi wa kujirusha ghorofani?Hapana lazima kuna sababu kubwa,au kuna watu wamemuua?.Nitaufahamu ukweli” akawaza Rosemary Mkozumi.
Alifika nyumbani kwake na kabla hajapokea maelezo yoyote toka kwa walinzi wake akaelekea moja kwa moja katika chumba alimokuwa amefungwa Anitha,nguvu zikamuisha akataka kuanguka bahati nzuri mlinzi wake alikuwa karibu akamdaka na kumketisha kitini.Anitha hakuwemo mle chumbani
“ She’s gone.Msichana aliyeondoka na Fernando ni Anitha.Amempeleka wapi?Mambo haya mbona yanazidi kunichanganya kichwa change kila uchao?.Lazima kuna mahala alimpeleka Anitha .Nina wasiwasi kwamba yawezekana Anitha au wenzake ndio waliosababisha kifo cha Fernando.Nitamsaka kokote hadi apatikane,siwezi kumuacha akapotea hivi hivi.Kitu kingine kinachonisumbua akili kwa nini Fernando alitaka kumpeleka Anitha hospitali wakati anafahamu utaratibu kuwa kama kuna mtu anateswa hata awe katika hali mbaya vipi huwa hapelekwi hospitali na badala yake Dr Abdul huitwa hapa hapa nyumbani kuja kumuhudumia.Ilikuaje hadi Fernando akataka kumpeleka Anitha hospitali? NI kweli alitaka kumpeleka hospitali au kuna kitu kingine kilitokea? I’m confused “ akawaza Rosemary Mkozumi .Akawaomba walinzi wake wamsaidie awe kurejea chumbani kwake.
“ Sintokubali hata kidogo kumpoteza Anitha.Lazima apatikane haraka iwezekanavyo .She knows too much arleady. yeye na timu yake wanaweza kuharibu mipango yangu yote kwani tayari wananifahamu mimi ni nani” akawaza Rosemary akiwa amejilaza kitandani
“ I have to go back and talk to Dr Joshua about this.yeye anao mtandao mkubwa na itakuwa rahisi kwa kutumia vyombo vyake kumsaka Anitha kwani mwanamke Yule ni hatari kwetu sote” akawaza Rose na kuanza kujiandaa kurejea nyumbani kwa Dr Joshua.
********
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Idadi kubwa ya wageni waliohudhura mazishi ya Flaviana tayari walikwisha ondoka na hivyo kumpa nafasi Dr Joshua kuendelea na ratiba zake nyingine .Kwa usiku huo alitakiwa kuonana na mjumbe maalum aliyetumwa kutoka Marekani.Kabla ya kwenda kuonana na mjumbe huyo ambaye hakujua ametumwa kitu gani,alihitaji kwanza kuonana na Abel Mkokasule ambaye tayari alikuwa katika chumba ha maongezi ya faragha akimsubiri.
“ Siku imekuwa ndefu mno.Karibu sana Abel” akasema Dr Joshua
“ Ahsante mzee.Pole sana kwa siku ngumu ya leo.Ninafahau ugumu uliopo katika kumzika mwanao kipenzi”
“ Ni kweli Abel ,kumzika mwanao ni jambo linaloumiza sana lakini kama ujuavyo sisi wanaume machozi yetu si machoni sisi tunalia moyoni.Tuachane na hayo naomba unipe ripoti kuna chochote umekipata kutwa nzima ya leo?
“ Tumeendelea kumfuatilia Kigomba kama ulivyoagiza lakini kutwa nzima ya leo ameshinda pale nyumbani kwako ufukweni .Bado vijana wangu wanaendelea kumfuatilia.” Akasema Abel
“ Good.Hajaonana tena na Jacob?
“ Hapana mzee,kwa mchana wa leo hakuonana naye “
“ Vizuri ,najua yeye na Jacob kuna mambo wanayapanga ,leave them to me I know what to do “
“ Sawa mzee ,halafu kuna wale vijana uliiambia kwamba niwaweke tayari kwa ajili ya kazi Fulani ya kuifanya usiku wa leo”
“ Kwa usiku wa leo endeleeni kumfuatilia Kigomba ,kazi niliyotaka muifanye usiku wa leo nimeahirisha hadi kesho.Mfuatilieni Kigomba kwa karibu sana endapo mkiwaona yeye na Jacob wakiwa pamoja unitaarifu mara moja.”
“ Sawa mzee tutafanya hivyo” akasema Abel na kuinuka tayari kwa kuondoka”
“ Abel nashukuru sana kwa kazi nzuri” akasema Dr Joshua na kuagana na Abel
“ I know Kigomba and Jacob are planning something.Kuna kitu wanataka kukifanya .I wont give them a chance to do what they want t do,Im going to surprise them.Hauna wa kushindana na mimi.Yeyote ambaye ataonekana kuwa kikwazo kwangu lazima nimuondoe.Kama niliweza kumkata pumzi mke wangu ,sembuse Kigomba na Jacob? Hawa kwangu ni kama udongo tu ambao muda wowote ninaweza kuufinyanga nitakavyo.Ngoja kwanza nikaonane na mgeni wangu nifahamu ametumwa nini kwangu” akawaza Dr Joshua na kumpigia simu Dr Kigomba akamuuliza endapo maandalizi yote yamekamilika kule nyumbani kwake.Kigomba alimtaarifu kwamba kila kitu kiko tayari na bila kupoteza muda Dr Joshua akaondoka kwenda kuonana na mgeni wake.
********
Hakukuwa na maongezi ndani ya gari wakati Kareem na Anna wakirejea nyumbani.Kila mmoja alikuwa anawaza lake.
“ Baba yangu ni rais wa nchii,we’re the first family,ninaishi maisha mazuri,ninapata kila ninachokihitaji lakini pamoja na hayo yote badala ya kufurahi ninajiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa kuliko wote.Najuta kuwa na baba kama huyu asiye na hata chembe ya ubinadamu.Ana roho ya kishetani kabisa.Why could he be so cruel ?? He took away from me all the important people ,the people that I loved the most.Edson, mama na Flaviana walikuwa ni watu walioyafanya maisha yangu yawe ya furaha lakini kwa roho yake mbaya na kwa tamaa zake za utajiri amewaua kikatili bila hata huruma.Kwa hili katu sintomsamehe.Nitashirikiana na Mathew mpaka tuhakikishe baba na mtandao wake wote wanafikishwa mbele ya sheria na kujibu mashtaka ya mauaji.Mambo aliyonieleza Mathew yanaogopesha sana.Amenifumbua macho na nimefahamu kile kinachoendelea.Amenifanya nimfahamu baba vizuri ni mtu wa namna gani.Sikujua kuwa watu niliowaheshimu mno wana roho za kishetani namna hii.Mtu kama Amos sikutegemea kabisa kama anaweza kuwa anashirikiana na baba na akamuua mama yangu.Kitu kama Kigomba ni mtu ambaye ninamuheshimu mno lakini kumbe naye ni shetani tu kwa wenzake.I swear hawa wote lazima nihakikishe wanalipa uovu wao “ akawaza Anna
“ Inanibidi kuanzia sasa niwe makini mno katika kila jambo nitakalolifanya kwani endapo baba atagundua kwamba ninashirikiana na akina Mathew lazima atanifanyia kitu kibaya sana .Kama aliweza kumtoa mama uhai hatashindwa kwangu.” Akaendelea kuwaza Anna na kumkumbuka Mathew
“ Namsifu sana Mathew ni mtu jasiri mno.Amekumbana na misuko suko mingi ikiwamo kusalitiwa na Elibariki lakini bado hajakata tamaa ,amesimama imara kuhakikisha anaiokoa nchi dhidi ya janga baya kabisa linaloweza kutokea endapo baba atakitoa kirusi na kikasambaa hewani.Laiti kama ningemfahamu mapema ,yawezekana hata vifo vya mama na Flaviana vingeweza kuzuilika.Hata hivyo bado sijachelewa nitahakikisha ninampa Mathew kila aina ya msaada ili aweze kufanikisha mpango wake.Akipate kirusi hicho na vile vile kumkamata baba na mtandao wake wote.Nataka kabla baba hajamaliza kipindi chake cha uongozi basi awe mshtakiwa na mimi naapa nitasimama mahakamani kutoa ushahdi wangu dhidi ya baba yangu mzazi.Ninamchukia mno.Hii itakuwa ni funisho kwa marais wengine wajao kuwa ikulu si mali yao.wanapaswa kupaheshimu sana.” Akawaza Anna halafu kuna kitu akakikumbuka
“ Nakumbuka Mathew aliniambia kwamba anashirikiana na Peniela ambaye ni adui wangu mkubwa lakini kwa kuwa sote tuna azma moja sina namna ya kufanya zaidi ya kuweka pembeni tofauti zetu na kufanya kazi pamoja.Itanilazimu niwe mvumilivu japokuwa nitaumia sana kila nikikumbuka kwamba yeye ndiye aliyevunja uhusiano wangu na Edson.”
“ Anna !! Kareem akaita na kumstua Anna toka mawazoni,akainua kichwa na kumtazama
“ Unasemaje Kareem? Akauliza
“ Naomba unisamehe sana kwa jambo nililolifanya la kukudanganya.Sikukueleza ukweli kwa kuwa nilijua hutaweza kukubali kuja .Ukweli ni kwamba sikutumwa na rais nikulete huku bali…”
“ Its ok Kareem,usijali” Anna akakatisha Kareem
“ Anna tafadhali naomba jambo hili lisimfikie rais kwani akijua nimefanya hivi nitakuwa katika wakati mgumu sana” akaomba Kareem
“ Usijali kareem hatajua chochote ila siku nyingine usinidanganye tena,unieleze ukweli”
“ Ahsante sana Anna” akajibu Kareem na safari ikaendelea.Baada ya muda mfupi Kareem akauliza
“ Anna Yule jamaa ni nani? Kwa nini alihitaji kukuona? Anna akamtazama kwa makini na kuuuliza
“ You don’t know him?
“ Sina mahusiano naye ya karibu japokuwa tumewahi kuonana mara kadhaa ila ninayefahamiana naye ni Yule mpenzi wake Anitha Yule dada aliyetukaribisha ndani.Anitha ndiye aliyeniomba nikulete ili uonane na mpenzi wake kuna jambo la muhimu maana anataka kuzungumza nawe” Kareem akamdanganya Anna
“ Kwa hiyo ulinipeleka kwa mtu ambaye humfahamu? Vipi kama angekuwa na nia mbaya ya kunifanyia jambo baya kama ilivyomtokea Flaviana? Akauliza Anna kwa sauti ya juu.
“ Nafahamu nilifanya kosa Anna na ndiyo maana nilitanguliza samahani lakini hata hivyo ninamuamini Anitha na nilikubali kukupeleka kwa kuwa nilijua hakuna jambo lolote baya ambalo lingeweza kutokea .Akihitaji nini Yule jamaa” Kareem akazidi kudadisi
“ Yule ni rafiki wa Flaviana na kuna vitu vya Flavana viko sehemu Fulani na alitaka kunipa maelekezo ya namna ya kuvipata.” Akasema Anna kwa ufupi na kuinamisha kichwa ishara kwamba hakuhitaji tena maongezi.
“ Bado siamaini kama leo nimempata Peniela.Dah ! Yule mtoto anayafahamu mapenzi.Japo ni kwa muda mfupi lakini alinifanya nione kama nina fanya mapenzi na kiumbe mwingine asiye binadamu kutokana na raha niliyokuwa naisikia.Sasa nimegundua kwa nini Dr Joshua humuelezi kitu kuhusu Peniela.Ni kutokana na mambo makubwa aliyonayo .Wanasema bucha ni tofauti lakini nyama ni ile ile lakini kwa Peniela nyama ni tofauti.Ile ni habari nyingine kabisa.I swear I’ll come back.Kazima nimtafute tena Peniela.Amenionjesha asali lazima nirudi tena nionje tena na ikibidi nichonge mzinga kabisa” akawaza Kareem
Dr Joshua aliwasili katika nyumba yake iliyoko ufukweni mwa bahari.Nyumba hii ndiyo aliyompa Peniela aishi ili kurahisisha kuonana kwao.Tayari kulikuwa na ulinzi wa kutosha kila kona.Dr Joshua akapokelewa na Dr Kigomba ambaye alimfahamisha kwamba maandalizi yote yamekamilika na mgeni wake tayari amekwisha wasili
“ Thank you Kigomba.Thank you so much for everything .After a very long day you can go home now.Go take a rest and I’ll take it from here.” Akasema Dr Joshua .Dr Kigomba hakuonyesha kulifurahia jambo lile
“ Are you sure you want me to go Mr President? akauliza
“ Nenda kapumzike Kigomba.Umefanya kazi kubwa sana leo.Tutaonana kesho” akasema Dr Joshua na kuanza kupiga hatua kuelekea sebuleni aliko mgeni wake
“ Mr Donald McNeel“ akasema Dr Joshua baada ya kungia sebuleni.
‘ Mr President ! “ akasema Donald na kupeana mikono ,wakaslimiana
“ samahani sana kwa kuchelewa.Nilikuwa na ratiba ndefu sana siku ya leo.Mwanangu aliyefariki nchini afrika ya kusini baada ya kushambuliwa kwa risasi alikuwa anazikwa leo”
“ Pole sana mheshimiwa rais.Mungu amrehemu mwanao na ampumzishe katika ufalme wake.” Akasema Donald.
“ Amen” akasema Dr Joshua na kikapita kimya kifupi ,Dr Joshua akasema
“ Nilipata taarifa zako lakini kutokana na shughuli iliyokuwa inaendelea nisingeweza kuonana nawe hivyo nikamuagiza Dr Kigomba katibu wangu aandae ili tuonane usiku huu” akasema Dr Joshua
“ Nashukuru sana mheshimiwa rais kwa kuacha shughuli zako na kuja kuonana nami.Licha ya kwamba uko katika msiba lakini bado umekubali kuja kuonana nami.Ahsante sana meshimwia rais” akasema Donald
“ Kama ambavyo tayari umetambulishwa ,naitwa Donald McNeel,ninafanya kazi katika ikulu ya Marekani “ akanymaza kidogo halafu akaendelea
“ Niko hapa kwa niaba ya ya ikulu ya Marekani na ninadhani unanielewa ninaposema kwa niaba ya ikulu y a Marekani hii ina maana kwamba ninamuwakilisha rais wa marekani.” Akanyamaza tena kidogo halafu akaendelea
“ Mwaka 2013 mtu mmoja aliyejulikana kama Andrew Rodney aliyekuwa mfanyakazi wa shirika la ujasusi la Marekani C.I.A alitoa katika mtandao taarifa za siri za kijasui za serkali ya Marekani.Taarifa hizo zilisambaa duniani kote na zikasomwa na mamilioni ya watu .Mojawapo ya taarifa za siri aliyoiweka hadharani ni ile ya kuwafanyia uchunguzi baadhi ya viongozi wakuu wa mataifa kadhaa ambao serikali ya Marekani imekuwa na mashaka nao kwa kudukua simu zao na hata barua pepe.Jambo hili kama utakumbuka mheshimiwa rais lilizusha taharuki kubwa sana nchini Marekani na duniani kwa ujumla na uhusiano wa Marekan na baadhi ya mataifa rafiki zake ulitetereka.Si hilo tu,Andrew Rodney alitoa siri nyingi za Marekani na kuhatarisha usalama wa nchi na raia wake na kibaya zaidi aliwaweka katika hatari kubwa majasusi wa Marekani waliosambaa katika sehemu mbali mbali duniani.Kingine kikubwa zaidi ni kwamba alitoa siri za ujasusi kwa Korea Kaskazini nchi ambayo ni hasimu mkubwa wa Marekani “ Donald akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Wakati akitoa siri hizo tayari Andrew alikuwa ametoroka na alipewa hifadhi nchini Urusi ambako bado anaishi hadi leo hii.Serikali ya Marekani imeendelea kutafuta namna ya kumpata Andrew bila kuchoka na hivi majuzi majasusi wa Marekani walioko nchini Urusi waligundua kwamba hivi karibuni Andrew atakuwa na safari ya kuja Tanzania.Lengo la safari yake hii ya kuja Tanzania ni kuja kuonana na rais mstaafu wa Tanzania ndugu Deus Mkozumi”
“ Deus Mkozumi?? Dr Joshua akashangaa
“ Ndiyo anakuja kuonana na Deus Mkozumi” akasema Donald
“ Deus Mkozumi anafahamiana na Andrew Rodney? Dr Joshua akazidi kushangaa
“ Kwa mujibu wa majasusi wetu walioko Moscow wakimfuatilia Andrew,walidukua maongezi kati ya Andrew na Deus Mkozumi,inaonyesha wawili hawa hawafahamiani ila Andrew ndiye aliyeanza kumtafuta Deus na endapo wataonana basi hii itakuwa ni mara yao ya kwanza kuonana na kikubwa ambacho Andrew anakuja kuzungumza na Deus ni kuhusiana na mtu mmoja anaitwa Chang ling.”
“ Chang ling?? Dr Joshua akazidi kushangaa
“ Ni nani huyu Chang ling?
“ Chang Lin ni mwanasayansi wa Kimarekani mwenye asili ya China ambaye amebobea katika sayansi ya viumbe.Wakati wa vita ya marekani na Iraq,Chang Ling aliwahi kutengeneza kirusi kilichotumiwa kama silaha kupiga katika kambi za kijeshi za Iraq na kusababisha maangamizi makubwa hivyo kurahisisha ushindi kwa Marekani lakini baadae ilikuja kugundulika kwamba mabomu yale yalisababisha madhara makubwa sana kwa askari walionusurika si wa Iraq pekee bali hata kwa wamarekani” Donald akatulia kdg halafu akaendelea
“ Chang Ling alikuwa ni miongoni mwa abiria waliokuwapo katika ndege ya Chinair iliyokuwa inasafiri kwenda Nairobi Kenya,lakini haikuweza kufika katika kituo chake cha mwisho kwani ilipotea katika mazingira yenye utata sana na hadi leo hii bado haijapatikana.Bado haijafahamika Chang Ling alikuwa anakuja kutafuta nini Afrika lakini kwa namna inavyoonekana lazima kulikuwa na kitu anakuja kukifanya .Kuna taarifa Andrew anaitafuta na kiipata basi ataendelea na utaratibu wake wa kutoa siri za Marekani k wa dunia.Suala la marekani kutumia silaha za kibaolojia katika vita ya Iraq ni suala ambalo halijajulikana kabisa hadi leo lakini inavyoonekna Andrew analichimba kwa undani ili aweze kulianika kwa dunia .Serikali ya Marekani hatuwezi kamwe kukubali hilo litokee ndiyo maana ikulu ya marekani imenituma kwako nikueleze kwamba tunataka kumuua Andrew Rodney katika ardhi ya Tanzania.Si Andrew pekee bali na rais mstaafu wa Tanzania Deus Mkozumi kwani naye anaonekana kuna kitu anakifahamu kuhusiana na Chang Ling .”
Dr Joshua alihisi kama kuna kitu kimegonga kichwa chake.Alipatwa na mstuko mkubwa.Kwa sekunde ishirini akabaki kimya akitazama Donald halafu akasema kwa sauti ndogo
“ Andrew Rodney auawe katika ardhi ya Tanzania ? Deus mkozumi pia?
“ Ndiyo mheshimiwa rais.Hii ni fursa pekee kabisa tumeipata na tunatakiwa kuitumia vyema kwani Andrew Rodney ni mtu hatari sana kwa sasa kwa taifa la Marekani na tumekuwa tukimsaka kwa muda mrefu bila mafanikio na hatuwezi kupoteza fursa hii .Anazo siri nyingi za serikali na maadui zetu wanaweza kuzitumia kutuletea madhara makubwa.Deus Mkozumi naye anaonekana kufahamu mambo Fulani kuhusu Chang Ling kwa hiyo naye hatuwezi kumuacha hai” akasema Donald .Dr Joshua akafikiri kidogo kisha akasema
“ Marekani na Tanzania ni nchi marafiki na muda mrefu na Tanzania imekuwa ikipokea misaada mingi sana ya kimaendeleo kutoka Marekani lakini kitendo cha Marekani kutaka kumuua Andrew katika ardhi ya Tanzania hatuwezi kukikubali hata kidogo.Dunia nzima inamfahamu Andrew ni nani na endapo akiuawa hapa Tanzania lazima itajulikana kwamba nchi yangu imetumiwa na Marekani kumuua Andrew.Hii inaweza ikatuletea matatizo kama nchi katika jumuiya ya kimataifa.Sikatai kwamba Andrew asiuawe kutokana na hatari yake kwa Marekani bali siko tayari mauaji yake yafanyikie nchini Tanzania.” Akasema Dr Joshua
“ Usiogope mheshimiwa rais,kila kitu kimekwisha pangwa na kuna mambo makubwa ya faida kubwa kwako na kwa nchi endapo jambo hili litafanikiwa.Tafadhali endelea kunisikiliza hadi mwisho. “ akasema Donald.Dr Joshua akatoa kitambaa na kujifuta jasho.Donald akaendelea
“ Ili kuufanikisha mpango huu,hatutatumia watu wetu wa Marekani au Tanzania bali tutawatumia watu kutoka katika mtandao wa Kigaidi wa Alqaeda”
“ Alqaeda??? Akauliza Dr Joshua kwa mshangao mkubwa
“ Ndiyo mheshimiwa rais” akajibu Donald
“ Nashindwa kukuelewa Donald umetumwa na Marekani ipi? Serikali ya Marekani ninayoifahamu mimi imekuwa inatumia gharama kubwa sana katika kupambana na magaidi .Inakuaje leo Marekani hao hao washirikiane na magaidi wa Alqaeda katika mipango yao? Hii hainiingii akilini hata kidogo” akasema Dr Joshua
“ Ni kweli utastaajabu kuhusu jambo hili lakini pale inapolazimika kwa maslahi mapana ya nchi yetu huwa tunawatumia watu hawa kufanikisha baadhi ya mambo yetu.Si mara ya kwanza kushirikiana na hawa jamaa.Tayari mipango yote imekwisha fanyika na kinachosubiriwa ni utekelezaji tu.Hata hivyo ili makubaliano yetu yafanikiwe kuna sharti wametoa ambalo nitakueleza hapo baadae kidogo.Hilo lilikuwa ni jambo la kwanza nililotumwa kwako mheshimiwa rais” akasema Donald.
“ jambo la pili nililotumwa kwako mheshimiwa rais” akaendelea Donald
“ Si muda mrefu sana toka sasa utamaliza muda wako wa uongozi na Tanzania itaingia katika uchaguzi mkuu na kupata rais mpya. Ambaye tunaamini atatoka katika chama chako kwani katika utafiti tulioufanya inaonyesha kwamba rais mpya atatoka katika chama chako kwani bado chama unachokiongoza kina nguvu sana na kinaaminiwa na wananchi.Macho ya dunia yanaelekezwa Tanzania kujua muelekeo wake kisiasa.Uwepo wa madini mbali mbali ya thamani, ugunduzi wa gesi asilia na viashiria vya uwepo wa mafuta vinaifanya Tanzania kuwa ni ya kutolewa macho na mataifa mengi makubwa.Kwa mujibu wa takwimu ,serikali ya marekani ndiyo inayoongoza kwa uwekezaj mkubwa hapa Tanzania kupita nchi zote zilizowekeza hapa kwa hiyo basi serikali ya Marekani inaitazama Tanzania kwa jicho la pekee kabisa” akanyamaza akanywa maji kidogo kulainisha koo halafu akaendelea
“ Katika kipindi chote cha uongozi wako kumekuwa na mahusiano makubwa na mazuri kati ya Tanzania na Marekani na nchi zote mbili zimefaidika sana na mahusiano haya.Dr Joshua umekuwa mstari wa mbele sana kuhakikisha maslahi ya Marekani yanalindwa kwa hiyo tunataka rais ajaye awe kama wewe ambaye atayalinda maslahi yetu.Katika utafiti tulioufanya tumebaini kuwa wanasiasa wote waliokwisha tangaza nia ya kuteuliwa kugombea urais kupitia chama chako wanatumiwa na mataifa hasimu zetu kibiashara na endapo mmoja kati yao akibahatika kushika nafasi ya urais basi uwekezaji wa Marekani hapa Tanzania utakuwa mashakani.Hatukubali hilo litokee na ndiyo maana baada ya kuwachambua watia nia wote tumempata mmoja tu ambaye tunaamini endapo atashika madaraka basi atayalinda maslahi yetu na mahusiano baina ya nchi hizi mbili yataimarika sana .Mtu ambaye nimetumwa niliwasilishe jina lake kwako kwamba ndiye ambaye serikali ya Marekani inamtaka awe rais wa Tanzania baada yako ni Dr Lucia Mkozumi”
“ Lucia Mkozumi?? Akauliza Dr Joshua kwa mshangao mkubwa
“ Ndiyo Dr Joshua.Lucia Mkozumi ndiye ambaye serikali ya Marekani inamtaka awe rais ajaye wa Tanzania.”
“ Hapana hilo haliwezekani.Sisi tuna utaratibu wetu wa ndani wa kumpata rais na hatutaki kuingiliwa na taifa lolote lile .Marekani ni marafiki zetu na wafadhili wakubwa wa miradi mingi ya maendeleo hapa nchini lakini kitendo cha kutuchanganya hadi nani awe rais wamevuka mstari na hatuwezi kulikubali hilo”
“ Dr Joshua tunafahamu haya ni masuala ya ndani ya nchi lakini inachokitaka serikali ya Marekani ni kulinda maslahi yake na Dr Lucia Mkozumi ndiye pekee ambaye anaweza akalifanya hilo.Dr Joshua ,faida zitakazopatikana kwa jambo hili ni nyingi ,kwako binafsi na kwa taifa.Nchi ya Marekani itakuwa na uhakika wa maslahi yake kulindwa na hapa nchi ya Tanzania itanufaika kwa misaada mikubwa itakayoipata .Tanzania itapewa msaada mkubwa ambao haijawahi kupewa nchi yoyote duniani na Marekani,itasaidiwa katika kujenga na kukuza viwanda vya ndani,itaisaidia Tanzania kielimu ,kilimo na afya.Tanzania itapaishwa kiuchumi na kijeshi pia.Tanzania itakuwa ni taifa kubwa na la mfano barani Afrika Tayari mipango imeanza kuandaliwa ya kuongeza uwekezaji mkubwa katika viwanda na kilimo na suala la ajira hapa nchini itabaki historia.Mambo mengi sana yatafanyika lakini yote yatawezekana tu kwa kauli yako moja itakayomsimamisha Dr Lucia Mkozumi kuwa mgombea urais na hatimaye rais wa kwanza mwanamke Tanzania.Tukiachana na faida hizo nyingi ambazo serikali ya Tanzania itazipata ,tugeukie kwako.Serikali ya Marekani itakupa uraia wa kudumu wa Marekani na makazi ambako utapumzika baada ya kustaafu.Utapewa ulinzi mkali wewe na familia yako na utapata kila unachokitaka ikiwamo ndege maalum ambayo utaitumia kila unapoihitaji.Ukiacha hayo kuna akaunti maalum imefunguliwa yenye fedha za kitanzania shilingi trilioni tano .Vitu vyote ni vya kwako endapo utalifanikisha jambo hili.Dr Joshua umeitumikia vyema nchi yako na kupandisha uchumi kwa kiasi kikubwa na sasa ni muda wako wa kupumzika huku ukipata kila aina ya starehe unayoihitaji.Endapo pia itatokea labda wakati wa uongozi wako uliwahi kufanya jambo ambalo litakupelekea kufunguliwa mashtaka wakati umekwisha staafu,serikali ya marekani itakukingia kifua .Hizi zote ni faida ambazo utazipata endapo utakubaliana na mambo haya mawili niliyotumwa kwako.” Akasema Donald .Ikamlazimu Dr Joshua amimine mvinyo mkali katika glasi na kunywa wote akatafakari kidogo halafu akasema
“ Huyu Dr Lucia Mkozumi ni nani hasa? Sijawahi kumsikia kabisa katika media za siasa na hata katika watu ambao wametangaza nia ya kuwania uteuzi ndani ya chama ,sijamsikia .Ana mahusiano yoyote na rais mstaafu Deus Mkozumi? Akauliza Dr Joshua
“ Dr Lucia Mkozumi ni mtoto wa pili wa rais mstaafu Deus Mkozumi .Ni mtu ambaye hafahamiki sana hapa nyumbani kwani karibu sehemu kubwa ya maisha yake ameishi nje ya nchi.Dr Lucia ni bingwa wa masuala ya uchumi na kwa sasa anafanya kazi katika shirikla la fedha la kimataifa na ameonyesha uwezo mkubwa sana katika masuala ya uchumi na fedha.Ni mtu abaye anafaa kuiongza Tanzania katika zama hizi” akasema Donald.Dr Joshua akainama akawaza kwa muda halafu akasema
“ Donald uongozi si kitu ambacho anaweza akapewa mtu yeyote na hasa kwa nafasi hii ya urais .Inaniwia ugumu kutamka chochote kwa sasa kwani simfahamu huyo Dr Lucia.Isitoshe watu hawamfahamu na amekaa nje ya nchi kwa miaka mingi na sina hakika kama anazifahamu vyema siasa za hapa nchini.Inanipa ugumu kutamka chochote kwa sasa”
“ Uko sahihi Dr Joshua nafasi nyeti kama urais haiwezi kupewa mtu kiholela lakini Dr Lucia ni mtu ambaye tumemthamini tukaona anafaa sana .Tumemuita tumefanya naye mazungumo na ameonyesha utayari wake wa kuliongoza taifa la Tanzania.Suala la kutokufahamika kwake hapa nchini si suala gumu hata kidogo.Tunaweza kumfanya akafahamika na kila mtu ndani ya dakika kumi tu.” Akasema Donald.Dr Joshua alionekana kuchanganyikiwa .Alishindwa aseme nini
“ Dr Joshua jipe muda wa kulitafakari suala hili kwa kina na faida zake.Nataka hadi kufikia kesho jioni tayari tuwe tumepata majibu toka kwako kuhusiana na mambo niliyokueleza.Sasa turejee tena katika lile suala la kwanza la kuhusiana na mpango wa kumuua Andrew Rodney na Deus Mkozumi” akasema Donald.
******
Peniela alikaribia kufika katika nyumba aliyopewa na Dr Joshua.Toka kwa mbali taa zilikuwa zinawaka na hili halikumstua kwani ni kawaida kwa walinzi wa usiku kuwasha taa kwa ajili ya ulinzi.Mathew na Anitha walimfuata kwa nyuma na waliacha umbali wa kutosha kati yao.Mathew hakuwa tayari kumuacha Peniela peke yake bila kumfuatilia kwa nyuma kuhakiki usalama wake
Peniela alikaribia kufika katika geti kuu la nyumba ile na mara akajitokeza askari mwenye silaha akasimama barabarani na kumnyooshea mkono akamuamuru asimame.
“ Nimekaribia kufika getini lakini nimesimamishwa na askari mwenye silaha,on No ! Ninawaona askari watatu mbele yangu.” Peniela ambaye alikuwa ameweka kifaa cha mawasiliano sikioni akawataarifu akina Mathew
Askari wale walimkaribia na kumtaka ashuke garini
“ Habari yako dada? Mmoja wa askari wale akamuuliza
“ Nzuri ,habari zenu?
“ Nzuri.Wewe ni nani na unatafuta nini hapa mida hii?
“ Thats going on here? Kuna tatizo gani kwani? Akauliza Peniela
“ Tafadhali dada naomba utueleze haraka wewe ni nani na unatafuta nini eneo hili? Akauliza kwa ukali mmoja wa askari wale huku wakizikoki silaha zao
“ Hapa ni kwangu.Ninakuja kwangu”
“ Kwako? Akauliza mmoja wa askari
“ Ndiyo hapa ni kwangu” akasema Peniela kwa kujiamini.
“ Dada tunakupa nafasi ya mwisho ya kujieleza wewe ni nani na unatafuta nini hapa?
“ Officers,ninaitwa Peniela .Namfahamu mwenye nyumba hii rais Dr Joshua na ninaishi hapa kwa ruhusa yake.” Akasema Peniela na kuzidi kuwashangaza wale askari
“ Dada tafadhali sogea mbele hatua tano na inua mikono juu” akaamuru kiongozi wa askari wale
“ Peniela fanya kila watakachokuamuru,usibishane nao” Mathew ambaye alikuwa anasikia kila kilichokuwa kinaendelea kupitia kifaa cha mawasiliano alichoweka sikioni akamwambia Peniela.Bila ubishi Peniela akafanya alivyoamriwa ,mmoja wa askari akamsogelea akamfunga pingu kwa tahadhari ,wakalikagua gari lake lakini hawakukuta kitu chochote cha hatari wakamuita mmoja wa walinzi wa rais wakamueleza kilichotokea
“ Unadai unamfahamu Dr Joshua? Akauliza Yule mlinzi wa rais
“ Tafadhalini naombeni mnifungue hizi pingu.Mimi si mualifu na nimekwisha waelezeni kwamba hapa ni kwangu.Nawatahadharisha Dr Joshua akifahamu mnavyonifanyia mtajiweka katika matatizo makubwa.Nifungueni pingu na mniache niingie ndani nikapumzike na sintomueleza chochote lakini endapo mtaendelea kunishikilia hapa nitamueleza kwamba mlitaka kunibaka.Do you know what will happen to you? Akauliza Peniela .Askari wale pamoja na Yule mlinzi wa rais wakatazamana.Yule mlinzi wa rais akaelekea ndani akazungumza na mlinzi mwingine kama dakika mbili halafu wakaongozana hadi mahala alipokuwa anashikiliwa Peniela akaamuru afunguliwe pingu akamshika mkono akaingia naye ndani.Peniela akapatwa na mshangao baada ya kuyakuta magari ya msafara wa rais.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Dr Joshua is here? Akamuuliza Yule mlinzi
“ Yes he’s here and I’m going to ask him if he knows you.Kama umedanganya utakuwa umejiweka katika matatizo makubwa sana kwa kuhatarisha usalama wa rais.” Akasema Yule jamaa na kumkabidhi Peniela kwa mlinzi mwanamama ili amkague na alipohakikisha hana silaha yoyote akaelekea ndani
“ Stay Calm Peniela.Usionyeshe woga wa aina yoyote” Mathew akamwambia peniela kupitia kifaa cha mawasiliano Peniela alichokivaa sikioni.
MWISHO WA SEASON 4
0 comments:
Post a Comment