Search This Blog

Monday, 27 March 2023

KIZUNGUMKUTI ! - 1

 

IMEANDIKWA NA : BISHOP HILUKA

*******************************************

Simulizi : Kizungumkuti !

Sehemu Ya Kwanza (1)


“Hii ni trela tu, picha kamili keshokutwa! Hakyamungu keshokutwa hakai mtu hapa… mi naapa! Nitakunywa na nitatembea uchi ukumbi mzima kama mademu wakinimaindi poa tu, au vipi kichaa wangu?” Kabwe alipiga kelele kilevi, wakati huo huo Liston alikuwa analazimisha kumshika matiti dada mmoja aliyepita karibu yake…


Fuatilia stori hii hadi mwisho ya kusisimua kuyajua yote yanayoleta kashikashi..


KATIKATI ya jiji la Dar es Salaam hali ya hewa ilikuwa ya joto sana kama kawaida, hata katika majira yale ya saa tano za asubuhi. Asubuhi ile pilika pilika za watu zilikuwa zimeshamiri katikati ya jiji hilo kubwa zaidi Tanzania, na hivyo kulifanya kuchangamka sana kama ilivyokuwa kawaida yake.


Katika eneo la Mnazi Mmoja, barabara ya Lumumba kulionekana msululu mrefu wa magari, zikiwemo daladala zilizokuwa zikizunguka kutokea mtaa wa Uhuru katika kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja na kupita barabara ya Bibi Titi kabla hazijaingia katika mtaa wa Mkunguni na kisha kutokea barabara ya Lumumba.


Katika barabara ile ya Lumumba, gari dogo la kifahari aina ya BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati lililotokea katika barabara ya Morogoro kwa mwendo wa taratibu na kujiunga katika msululu ule, kisha lilichepuka na kwenda kusimama chini ya miti ya kivuli iliyokuwa imepandwa kando ya ile barabara.


Hata hivyo, dereva wa gari lile alionekana kutoridhika na eneo lile, akaanza kutafuta sehemu nzuri zaidi na baadaye alikwenda kuliegesha gari lake kwenye eneo lililokuwa na magari mengine mawili matatu yaliyokuwa yameegeshwa pale, na vijana kadhaa walionekana wakiosha magari.


Vijana wawili waosha magari walimfuata haraka yule dereva wa lile gari na kuonekana kumzonga, kila mmoja alionekana akitaka apewe tenda ya kuosha lile gari lakini yule dereva hakuonekana kuwajali. Alibaki ametulia kimya akiusikilizia muungurumo laini wa lile gari kwa kitambo kirefu.


Ndani ya gari lile kulikuwa na watu wawili tu, mwanamume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari na mwanadada mrembo sana ambaye alikuwa ameketi pembeni yake kwenye siti ya abiria.


Yule mwanamume alikadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka arobaini na arobaini na tano. Alikuwa mrefu wa futi sita na ushee, mweusi na shababi kwelikweli aliyekuwa na mwenye mwili uliojengeka kwa misuli.


Macho yake yalikuwa makali na alikuwa amevaa kofia ya rangi ya bluu aina ya kapelo, t-shirt ya pundamilia iliyokuwa na miraba ya bluu na myeupe aina ya form six na suruali ya jeans ya rangi ya bluu. Miguuni alikuwa amevaa buti ngumu za ngozi zilizokuwa na rangi nyeusi.


Mwanamume yule aliitwa Carlos Mwamba na aliendelea kutulia kwenye siti yake nyuma ya usukani akiwa ameibana njiti moja ya kiberiti kwenye pembe ya mdomo wake, huku akiendelea kuusikilizia muungurumo laini wa lile gari.


Kushoto kwa Carlos Mwamba, kwenye ile siti ya mbele ya abiria yule mrembo aliyekuwa ameketi aliitwa Jackline Mgaya na alikuwa mke wa ndoa wa Carlos, wakiwa wameoana takriban miaka mwili iliyokuwa imepita.


Jackline au kama alivyopenda kujulikana kwa kifupi kwa jina la Jacky alikuwa na umri usiozidi miaka therathini, alikuwa mrefu na mweupe mwenye haiba nzuri ya kuvutia sana.


Alikuwa na nywele nyeusi za kibantu alizokuwa amezikata vizuri na kubaki ndogo ndogo na hivyo kumfanya aonekane mzuri wa asili. Alikuwa na sura yake ya duara na macho makubwa ya kike na legevu yaliyokuwa yamezungukwa na kope ndefu na nyeusi.


Pua yake ilikuwa ndogo na iliyochongoka mfano wa pua ya kihabeshi na mdomo yake ilikuwa laini yenye maki na kingo pana kiasi zilizokuwa zimekolezwa kwa lipstick ya rangi ya chocolate pamoja na vishimo vidogo mashavuni mwake vilimfanya azidi kuonekana mrembo zaidi.


Jacky alikuwa na masikio madogo yasiyochusha aliyokuwa ameyatoga na kuyavalisha hereni kubwa za kitamaduni zilizokuwa na umbo la mviringo. Alikuwa amevaa blauzi nyepesi ya arangi ya pinki iliyoyaficha vyema matiti yake imara yenye ukubwa wa wastani yaliyokuwa na chuchu nyeusi imara zilizosimama kikamilifu ndani ya blauzi ile.


Shingoni alikuwa kavaa mkufu mwembamba wa dhahabu uliokuwa umeizunguka ile shingo nyembamba na kidani cha dhahabu kilichokuwa na herufi ya “J” kilikuwa kimepotelea katikati ya uchochoro mdogo wa yale matiti.


Kwenye mkono wake wa kushoto alikuwa amevaa bangili kadhaa za pembe na vidole vyake viwili vya mkono huo alikuwa amevaa pete ndogo za madini ghali ya tanzanite na green tourmaline.


Mkono wake wa kulia alivaa saa ndogo ghali na nzuri ya kike aina ya Cartier La Dona, ambayo bei yake ilikuwa si haba kama angeamua kuibadili kwa pesa za madafu, kwani ilikuwa imemgharimu kiasi cha dola za Marekani 137,000.


Cartier La Dona Watch ilikuwa ni saa ghali sana iliyotengenezwa kwa madini ya dhahabu nyeupe ya Karati 18 ikiwa na kesi imara iliyokuwa na milimita 27 kwa 29 na mkanda wake pia ulikuwa umetengenezwa kwa dhahabu nyeupe, ikiwa na gerentii ya miaka hamsini.


Alikuwa ameinunua nchini Switzerland walipokwenda kwenye fungate muda mfupi tu baada ya ndoa yao iliyoacha gumzo jijini Arusha na kwenye viunga vyake.


Gari ikiwa bado inaunguruma taratibu Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kutazama nje kwa kitambo fulani huku macho yake yakielekea moja kwa moja kwenye jengo la ghorofa la Benki ya Biashara.


Alilitazama lile jengo kwa makini akionekana kama aliyekuwa akijiuliza jambo kuhusiana na lile jengo, kisha aliyashusha macho yake kuutazama mkoba wake mzuri wa kike wa rangi ya pinki uliokuwa umelala juu ya mapaja yake mazuri.


Aliufungua ule mkoba na kutoa humo mkebe mdogo wa duara wa rangi nyekundu kisha aliinua macho yake kujitazama kwa kitambo kifupi kwenye kioo cha lile gari cha katikati kinachotumika kuangalia nyuma huku akigeuza geuza uso wake pembe zote.


Alikunja uso wake huku akiminya midomo yake mizuri yenye maki, na hapo mashavu yake yakapiga misingi, pembe za midomo yake zikafinya, akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akigeuka kumtazama Carlos aliyekuwa ametulia tuli kama maji mtungini na kuachia tabasamu bashasha.


Carlos aliendelea kutulia pale nyuma ya usukani akionekana kuwaza mbali sana, alimtupia jicho Jacky mara moja tu, kisha akayahamisha macho yake na kutazama kwenye lile jengo la Benki ya Biashara huku sura yake ikiwa haioneshi tashwishwi yoyote.


Jacky alimtazama Carlos kwa makini kisha akaufungua ule mkebe akatoa vipodozi na kuanza kujiremba akiongezea urembo kwenye sura yake huku akijitazama kwenye kile kioo cha gari cha katikati kinachoonesha nyuma.




Jacky alimtazama Carlos kwa makini kisha akaufungua ule mkebe akatoa vipodozi na kuanza kujiremba akiongezea urembo kwenye sura yake huku akijitazama kwenye kile kioo cha gari cha katikati kinachoonesha nyuma.


Aliporidhishwa na urembo wake alishusha tena pumzi za ndani kwa ndani na kuufunga ule mkebe, akarudisha kwenye mkoba wake na kuufunga, kisha akageuza tena shingo yake kumtazama Carlos aliyekuwa bado ametulia tuli kwenye siti yake nyuma ya usukani.


Hapo Carlos akaachia tabasamu jepesi usoni mwake lililoyafanya meno yake yaliyokuwa yamepoteza mng’ao wake kwa sababu ya ukungu wa moshi wa sigara na pombe kali kuonekana vizuri.


“Are you nervous, my love?” (Vipi, una wasiwasi, mpenzi?) Carlos alimuuliza Jacky huku akiendelea kutabasamu.


“No, I’m not,” (Hapana, sina) alijibu Jacky huku akijiinua kidogo akapeleka shingo yake karibu na Carlos.


Na hapo akasogeza midomo yake karibu zaidi na midomo ya Carlos, midomo yao ilipokutana Jacky akambusu Carlos kisha akashika vyema mkoba wake na kuteremka kutoka kwenye lile gari huku akimwacha Carlos ndani ya gari akiwa bado katulia akisubiri.


“Take care, my love, and try in anyway you can to make him go crazy about you,” (Kuwa makini, mpenzi, na jaribu kila uwezavyo kumchanganya atakapokuona) Carlos alisema kwa sauti tulivu.


“Don’t worry, honey,” (Usihofu, mpenzi) Jacky alijibu huku akipiga hatua zake taratibu na kwa madaha kuivuka ile barabara ya Lumumba kisha akaelekea upande wa pili akilifuata moja kwa moja lile jengo la Benki ya Biashara.


Alipokuwa akitembea ndipo umbile lake lilipoonekana vizuri, alikuwa mrefu na mwenye umbo zuri sana, kiuno chake kilikuwa chembamba kiasi chenye misuli imara kilichokuwa kimeizuia suruali yake ya rangi nyeusi ya jeans iliyolichora vyema umbo lake matata lenye kuzitaabisha vibaya nafsi za mwanaume wakware.


Miguuni alikuwa amevaa buti ngumu za kike za ngozi na kwa kweli alikuwa kapendeza sana, alitembea akiangalia huku na kule huku akiwa amening’iniza mkoba wake wa kike begani uliomfanya kuvutia zaidi. Itoshe tu kusema kuwa Jacky alikuwa mwanadada mrembo kwelikweli aliyestahili hata kutwaa taji la urembo la dunia!


“She’s so gorgeous… I’m very lucky because this is exactly the type of woman I was always dreaming for,” (Ni mrembo hasa… nina bahati sana kwa sababu huyu ndio aina ya mwanamke ambaye siku zote nilikuwa naota kumpata) Carlos aliwaza huku akimsindikiza Jacky kwa macho.


Alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akijiegemeza kwenye kiti chake na mara akaanza kukumbuka alivyokutana na Jacky kwa mara ya kwanza kabla hawajaangukia kwenye mapenzi mazito ambayo baadaye yalikuja kuzaa ndoa…


______


Ilikuwa siku ya Jumatano, Carlos alikuwa amechelewa sana kutoka hotelini kwake baada ya kukurupuka kitandani saa tatu na nusu za asubuhi akiwa chumba namba 204 cha Arusha Crown Hotel jijini Arusha!


Arusha Crown Hotel ilikuwa hoteli nzuri ya kisasa iliyokuwa katikati ya jiji la Arusha, katika barabara ya Makongoro jirani kabisa na Uwanja wa Mpira wa Sheikh Amri Abeid Kaluta.


Baada ya kuamka Carlos hakuzubaa, alifahamu nini maana ya kuzingatia muda, alielekea haraka bafuni na kujimwagia maji. Ilimchukua muda mfupi sana kuoga na muda mfupi baadaye alikuwa amemaliza kujiandaa huku akiwa katika mwonekano bomba wa suti nzuri ya gharama iliyokuwa na rangi ya kijivu, shati la rangi ya samawati, tai ya rangi ya bluu na viatu vyeusi vya ngozi.


Alipotoka hotelini aliendesha gari lake kama kichaa katika barabara ya Makongoro, akavuka Uhuru Roundabout na kusonga mbele hadi alipoipata AICC Roundabout, akakunja kuingia kushoto akilipita jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hadi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).


Alipoteremka kwenye gari lake alitembea kama mtu aliyekuwa anakimbia akiwahi kwenye mkutano wa wafanyabiashara na wadau wa madini uliokuwa ukifanyika AICC na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye alikuwa mgeni rasmi.


Mkutano ule ulikuwa umeandaliwa na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini Tanzania kujadili kero na tozo mbalimbali, na yeye alikuwa mmoja wa wafanyabiashara wa madini walioalikwa kwenye mkutano ule.


Katika jengo lile la AICC Carlos aliendelea kutembea kwa kasi ile ile na kama ingetokea angejikwaa basi angeweza kupata ajali mbaya sana. Alipokuwa akikata kona kuingia kwenye korido iliyokuwa ikielekea kwenye ukumbi ule wa mikutano, akiwa katika mwendo ule ule ghafla alishtukia anagongana na mwanadada mmoja aliyekuwa akija mbele yake na kila mmoja aliangusha vitu alivyokuwa amebeba mkononi.


Yule mwanadada aliangusha simu yake aina ya Samsung Galaxy S8 na Carlos aliangusha simu yake aina ya Iphone X na briefcase yake ndogo nyeusi iliyokuwa na nyaraka zake muhimu.


Carlos alimtazama yule mwanadada na hapo macho yake hayakuamini kile alichokuwa amekiona, alikuwa akitazamana na msichana mrefu mrembo sana aliyekuwa amevalia suti nadhifu ya kike ya rangi ya bluu iliyokolea ya ‘single button’ iliyokuwa imemkaa vyema na kumpendeza sana na viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio.


Yule mrembo alimtazama Carlos kwa hasira na kuduwaa kisha aliyapeleka macho yake kuiangalia simu yake ya Samsung Galaxy S8 iliyoanguka pale sakafuni. Wakati huo huo Carlos aliinamisha mgongo wake na kuiokota ile simu kisha akamkabidhi yule mrembo huku naye akiendelea kuokota simu na briefcase yake.


“Samahani sana, bibie, sikukusudia…” Carlos alijaribu kujitetea baada ya kumuona yule mrembo akimtazama pasipo kuonesha tashwishwi yoyote. Yule mrembo alibaki kimya akionekana kuduwaa huku akimtazama Carlos.


“Sijui simu imeumia, anti?” aliuliza huku akimtazama kwa makini. Yule mrembo alishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Usijali, ipo sawa,” hatimaye yule mrembo alisema huku akiiwasha ile simu yake iliyokuwa imezima.


Carlos alistaajabishwa na sauti laini ya yule mrembo iliyovunjika ilipenya sawia kwenye ngoma za masikio yake, ukichanganya na macho yake yaliyolegea, vyote kwa pamoja vilitoa haiba ya kike ndani mwa yule mrembo na kummwaia Carlos.


Macho ya Carlos yaliganda kwenye sura ya yule mrembo huku akionekana kusahau kabisa kuwa alikuwa amechelewa kwake kwenye mkutano wa wafanyabiashara na wadau wa madini. Yule mrembo alipohakikisha kuwa simu yake haikuwa na tatizo, aliminya midomo yake na kumtupia jicho Carlos na kuanza kupiga hatua kwa madaha kuondoka eneo lile.




Macho ya Carlos yaliganda kwenye sura ya yule mrembo huku akionekana kusahau kabisa kuwa alikuwa amechelewa kwake kwenye mkutano wa wafanyabiashara na wadau wa madini. Yule mrembo alipohakikisha kuwa simu yake haikuwa na tatizo, aliminya midomo yake na kumtupia jicho Carlos na kuanza kupiga hatua kwa madaha kuondoka eneo lile.


Ile suti aliyokuwa amevaa ilikuwa imembana kidogo mwili wake na hivyo kusababisha mistari ya chupi iweze kujichora kwenye ule mzigo wa makalio, na utembeaji wake uliwafanya wanaume waliopishana naye kumtazama kwa matamanio na wala hakuna aliyejuta kumwangalia.


Mwondoko wake na mwili wake ulivyokuwa ukitingishika ulizidi kumfanya azidi kuvutia na ilikuwa kama vile alikuwa anaamua vile kwani mwendo wake na sauti ya vile viatu vye visigino virefu alivyokuwa amevaa vilikuwa vinaendana hasa. Na ilikuwa ni bahati sana kwa macho ya mwanamume yeyote kuona kiumbe kama yule wa shani akipita mbele yake.


Carlos aliduwaa akabaki mdomo wazi akimsindikiza kwa macho hadi alipomuona akiiingia kwenye mlango mmoja uliokuwa na maneno ‘Staff Only’ juu yake na kuacha gumzo kule nyuma. Kila mwanamume aliyepishana naye alitamani angalau angeisikia hata sauti yake tu.


Carlos alizinduka na kuanza kutembea kwa kasi ile ile ili kuwahi kwenye ule ukumbi wa mikutano kwa ajili ya mkutano. Baada ya mkutano ule kumalizika Carlos alirejea hotelini alikofikia lakini akiwa na mawazo mengi kuhusu yule mrembo aliyegongana naye asubuhi.


Walipotoka kwenye mkutano alimtafuta rafiki yake, Godlove Kimaro aliyekuwa akiishi hapo jijini Arusha, alimweleza kuhusu yule mrembo na kumpa kazi ya kufuatilia taarifa zote za yule mrembo na ikibidi amlete hotelini kwake huku akimuahidi kumpa fedha nyingi kuliko ambazo amekuwa akimpa endapo angefanikiwa.


Aliazimia kutoondoka jijini Arusha pasipo kuonana na yule mrembo hata kama ingemchukua wiki mbili. Hata hivyo, jioni ya saa kumi na mbili ya siku ya pili Kimaro alimpigia simu na kumpa habari njema kuwa kila kitu kilikuwa safi.


Alimweleza yote aliyotaka kuyafahamu kuwa yule mrembo aliitwa Jackline Mgaya, alikuwa msomi aliyefanya kazi pale AICC na hakuwa ameolewa. Alimweleza mengi kumhusu Jacky ambayo yalizidi kumsisimua Carlos na kwamba baada ya kumwimbisha sana Jacky hatimaye alikuwa amekubali kuonana naye siku iliyofuata saa kumi na mbili jioni pale pale hotelini.


Kwa habari zile Carlos alijikuta akitokwa na kijasho chembamba sehemu mbalimbali za mwili wake, huku akihisi ubaridi fulani wa woga wa aina yake ukimtambaa mwilini na mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!


Siku iliyofuata saa kumi na mbili jioni Carlos alikuwa chumbani kwake amejipumzisha, akitazama runinga na pembeni yake kwenye meza ndogo ya kioo kulikuwa na chupa kubwa ya Whisky na bilauri.


Chumba chake kilikuwa kikubwa na kizuri cha kifahari, kilikuwa na kitanda kikubwa cha samadari cha futi sita kwa sita, cha mbao ngumu za mninga, chenye droo mbili kila upande kilichokuwa katikati ya chumba.


Juu ya zile droo kulikuwa na taa mbili za rangi nyekundu na mbele ya kitanda hicho kulikuwa na seti nzuri ya runinga pana aina ya LG ya inchi hamsini na mbili na chini yake kulikuwa na meza nzuri nyeusi ya kioo. Juu ya ile meza kulikuwa na simu yake ya kisasa ya Iphone X na kando ya ile meza kulikuwa na briefcase yake nyeusi.


Upande wa kulia wa kile chumba kulikuwa na jokofu dogo la vinywaji lililokuwa kwenye kona ya chumba, na hatua chache kutoka kwenye lile jokofu hilo kulikuwa na dirisha pana la kioo lililokuwa limefunikwa kwa pazia zito na refu lenye nakshi za michoro ya maua yaliyodariziwa vizuri na kuyafanya yapendeze.


Pia kulikuwa na kabati kubwa la kisasa la nguo ambalo lilikuwa limefungwa muda huo na pembeni ya lile kabati hilo kulikuwa na kochi moja kubwa la sofa na meza ya kioo mbele yake iliyokuwa na chupa kubwa ya Whisky na bilauri moja.


Kando ya lile sofa kulikuwa na meza fupi ya mbao iliyokuwa simu ya mezani na kitabu kidogo chenye orodha ya majina ya watu na kampuni zilizotumia huduma ya simu ile ya mezani na kwenye kona ya chumba hicho upande wa kushoto kabisa kulikuwa na mlango wa kuelekea kwenye chumba kidogo cha maliwato na bafu.


Chini sakafuni kulikuwa na zulia nene lililokuwa na mchanganyiko wa maua ya rangi mbalimbali yaliyolifanya kuvutia. Akiwa ameketi alisikia mlango wa chumba chake ukigongwa taratibu, Carlos aligeuza shingo yake kuutazama ule mlango kwa shauku.


Aliinuka haraka na kuufungua kidogo huku akichungulia nje, macho yake yakagongana na macho ya kimaro ambaye alimfanyia ishara kuwa alikuwa na mgeni, Carlos aliufungua mlango huku akirudi nyuma kuwapisha waingie.


Kimaro aliingia na kufuatiwa na Jacky aliyeingia mle ndani akiwa na wasiwasi kidogo. Kwa sekunde kadhaa Carlos alibaki ameduwaa akimtazama Jacky aliyekuwa amesimama huku akitazama chini kwa aibu.


Jacky alikuwa amevaa amevaa sketi fupi nyekundu iliyokuwa na miraba myeupe na bluu iliyoyashika vyema mapaja yake yaliyonona yaliyokuwa yameshikiliwa na hipsi pana na huko nyuma kukiwa na mzigo wa haja wa makalio.


Juu alivaa blauzi ya nyeupe ya mikono mirefu na viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio na begani alikuwa ametundika mkoba mzuri wa ngozi ya pundamilia ambao ulionekana kumgharimu fedha nyingi.


“Oh my Gosh! What a beautifull angel…” (Mungu wangu! Urembo wa kimalaika…) Carlos alijikuta akiwaza huku akiendelea kumkazia macho Jacky. Alizidi kuchanganywa na uzuri wa Jacky na alikiri kuwa asubuhi hakuwa amemchanganyia vizuri macho.


“Kimaro was right. Jacky ana uzuri wa kipekee mno. Katika wasichana wote ambao amewahi kuniletea kila ninapokuja hapa jijini Arusha hajawahi kumleta msichana mrembo kama huyu,” Carlos aliendelea kuwaza huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Boss, kutana na Jackline Mgaya,” Kimaro alimzindua Carlos kutoka kwenye mawazo.


“Jacky, huyu ndiye Boss wangu anaitwa Carlos Mwamba, nadhani mlishakutana asubuhi pale AICC,” Kimaro akaendelea na utambulisho.




“Boss, kutana na Jackline Mgaya,” Kimaro alimzindua Carlos kutoka kwenye mawazo.


“Jacky, huyu ndiye Boss wangu anaitwa Carlos Mwamba, nadhani mlishakutana asubuhi pale AICC,” Kimaro akaendelea na utambulisho.


Jacky aliinua uso wake kumtazama Carlos usoni kisha akanyoosha mkono wake kumsalimia Carlos kwa adabu huku akiyakwepesha macho yake yalijaa aibu.


“Hello, Mr Mwamba,” Jacky alisema kwa sauti tulivu na nyororo iliyotosha kabisa kumtoa nyoka pangoni huku akiachia tabasamu bashasha.


“Hello! Karibu sana Jacky, nimefurahi kukuona tena,” Carlos alisema huku akilamba midomo yake iliyoanza kukauka.


“Hata mimi nimefurahi kukutana tena na wewe, Mr Mwamba,” alisema Jacky huku akiangalia chini kwa aibu, alionekana kuwa hawezi kumtazama mwanamume usoni kwa sekunde tatu mfululizo bila kukwepesha macho yake na kutazama kando kwa jinsi alivyojaa haiba na aibu. Carlos akamtazama Kimaro na kumpiga ukope.


“Kimaro, asante kwa kumfikisha mgeni wangu, sasa nenda kamuone yule binti wa mapokezi ana ujumbe wako,” Carlos alisema na Kimaro akaondoka bila kusubiri kwani alikwisha elewa kuwa fedha yake ilikuwa imeachwa pale mapokezi.


Carlos akamkaribisha Jacky kwenye sofa lililokuwa mle chumbani huku yeye akienda moja kwa moja kwenye jokofu dogo lililokuwemo mle ndani aambalo lilisheheni vinywaji mbalimbali.


“Jacky, sijui unatumia kinywaji gani?” aligeuza shingo yake akamuuliza Jacky.


“Anything that you can choose for me, Mr Mwamba,” (Chochote unachoweza kunichagulia) Jacky aliasema kwa sauti laini iliyozidi kumpagawisha Carlos na kuachia tabasamu pana.


Carlos alilamba midomo yake na kuchukua bilauri, kisha akarudi pale kwenye meza ndogo na kuchukua ile chupa kubwa ya Whisky na kumimina katika bilauri akampatia Jacky.


“Karibu sana Jacky, Nina furaha kubwa mno kuwa nawe kwa usiku huu,” Carlos alisema huku akipiga funda kubwa la mvinyo na kuonesha kusisimkwa.


“Hata hivyo, ninatamani sana kukufahamu zaidi, Jacky,” alisema tena Carlos baada ya kuikita juu ya meza ile bilauri.


“Unahitaji kufahamu kitu gani kuhusu mimi, Mr Mwamba?” Jacky aliuliza huku akikwepesha macho yake na kutazama kando kwa aibu.


“Just call me Carlos. I need to know everything about you… your life, relationship, everything,” (Niite Carlos tu. Nahitaji kujua kila kitu kukuhusu… maisha yako, uhusiano, kila kitu) Carlos alisema huku akimkazia macho Jacky.


“Why do you want to know about my life and everything? Is this an interrogation,” (Kwa nini unataka kujua kuhusu maisha yangu na kila kitu? haya ni mahojiano?) Jacky alisema huku akimtupia jicho Carlos akionesha kuwa na aibu.


“Not an interrogation… (Siyo mahojiano…) ni kwamba nina sababu zangu binafsi za kutaka kukufahamu kiundani,” Carlos alisema huku akinywa funda kubwa la mvinyo.


“Can you tell me what the reasons are?” (Unaweza kuniambia ni sababu zipi) Jacky aliuliza huku akimtazama Carlos kwa macho yake yaliyolegea.


“The only reason is that, I’m looking for a wife, (Sababu pekee ni kwamba, natafuta mke) na umebeba sifa zote za mwanamke anayefaa kuwa mke wangu,”


“Wife?” (Mke?) Jacky aliuliza kwa mshtuko.


“Yes a wife,” (Ndiyo, mke) Carlos alijibu kwa sauti tulivu huku akimtazama Jacky kwa makini.


“A handsome guy like you, you are still single up to now, or you want me to be your second wife?” (Mwanamume mtanashati kama wewe bado hujaoa hadi sasa, au unataka kunifanya mke wa pili?)” Jacky aliuliza tena huku akiendelea kumkazia macho Carlos.


“Trust me, I'm not married, and if you’re ready I’ll make you the most beautifull woman in the world. I’ll give you all luxuries,” (Niamini, sijaoa, na kama uko tayari nitakufanya mrembo kuliko wanawake wote duniani. Nitakupa starehe zote) Carlos alisema kwa kujigamba na kumfanya Jacky aangue kicheko hafifu.


“Jacky, I’m serious about this. It’s not a joke,” (Jacky, niko siriazi. Huu siyo utani) Carlos alisisitiza baada ya kuona Jacky anacheka.


“You don’t have to tell me, I can see it in your eyes…” (Wala huhitaji kuniambia, macho yako tu yanaongea…) alisema Jacky.


“But, are you sure that you love me and you want to marry me?” (Lakini una hakika unanipenda na unataka kunioa?) Jacky aliuliza.


“Yes, I’m ready anytime and any day,” (Ndiyo, tena niko tayari muda wowote na siku yoyote) carlos aliongea kwa kujiamini huku akimtulizia macho Jacky bila kupepesa macho.


Jacky alimtazama kwa makini sana kwa kitambo kirefu, ilikuwa ni kama vile alikuwa akiyasoma mawazo yake.


“What you need from me is a difficult thing, it’s about my life and yours…” (Jambo unalohitaji kwangu ni jambo gumu linalohusu maisha yangu na yako vilevile…) Jacky alisema kwa sauti ya tulivu huku akimtazama Carlos kwa makini.


“Kwa hiyo, halihitaji uamuzi wa papara, tunahitaji muda wa kufahamiana zaidi,” aaliongeza na kunyanyua bilauri ya mvinyo, akapiga funda kubwa na kuusikilizia wakati ulipokuwa ukiteremka tumboni.


“So what do you say?” (Kwa hiyo unasemaje?) Carlos aliuliza kwa sauti ya chini.


“Say what?” (Kusema nini?) Jacky akauliza huku akimtazama Carlos kwa mshangao.


“About tonight, will you spend this night with me? I need you so badly!” (Kuhusu usiku wa leo, tutakuwa wote usiku wa leo? Nakuhitaji vibaya sana!).


“It’s okay, but if you need love and comfort from me I’m ready to give you but not in exchange for money,” (Sawa, lakini kama unahitaji penzi na faraja kutoka kwangu niko tayari lakini si kwa kwa fedha) akasema Jacky.


Waliendelea na maongezi na mwishowe wakajikuta wakiwa kitandani, muda ule taa mbili za rangi nyekundu zilikuwa zinatoa mwanga hafifu wenye mg’ao na kufanya nusu ya chumba kuwa kizani.


Muda huo Carlos alikuwa amefumba macho yake huku akisikia raha ya aina yake wakati mikono ya Jacky ikichezea ikulu.


“Ooh Jacky… ooh… aah...” Carlos alilalama lakini Jacky hakumjali, aliendeleza utundu wake kwa kutumia mikono halafu taratibu akapiga magoti na kuanza manjonjo kwa kutumia mdomo wake, jambo lililomfanya Carlos atamani kupiga kelele kwa raha aliyoipata.


Haukupita muda Carlos alijikuta akiwa katika hali mbaya na hakuweza tena kuvumilia, hivyo wakaingia ulingoni. Ulikuwa ni mpambano mkali kila mmoja akionesha ufundi na kutaka kuutawala mchezo.


Walibadili kila aina ya mfumo wa uchezaji ili mradi kujihakikishia ushindi mnono mwisho wa mchezo, Jacky alijitahidi kumwonesha Carlos mautundu aliyokuwa nayo na kumfanya kutoa miguno kwa raha aliyojisikia huku akimimina ahadi nyingi ambazo aliapa kuwa angezitekeleza. Hadi dakika tisini wote walikuwa hoi wakitweta kama wakimbiaji wa mbio ndefu.




Walibadili kila aina ya mfumo wa uchezaji ili mradi kujihakikishia ushindi mnono mwisho wa mchezo, Jacky alijitahidi kumwonesha Carlos mautundu aliyokuwa nayo na kumfanya kutoa miguno kwa raha aliyojisikia huku akimimina ahadi nyingi ambazo aliapa kuwa angezitekeleza. Hadi dakika tisini wote walikuwa hoi wakitweta kama wakimbiaji wa mbio ndefu.


“Thank you, Carlos, you said you wanted me so badly,” (Asante, Carlos, ulisema unanihitaji vibaya sana) alisema Jacky huku akitweta kwa nguvu.


“Jacky…” Carlos alitaka kusema neno lakini Jacky akamwekea kidole mdomoni akimzuia kusema.


“You don’t have to say anything, Carlos,” (Huhitaji kusema chochote, Carlos) alisema Jacky huku akirembua macho yake.


“Yeah, but spend this night with me, Jacky. I still need you so badly, you are wonderfull woman,” (Ni kweli, lakini kesha nami usiku huu, Jacky. Bado nakuhitaji vibaya sana, hakika wewe ni mwanamke wa ajabu) alisema Carlos kwa sauti nzito ya chini iliyokuwa na kitetemeshi.


Tangu siku ile mapenzi yao yalinoga, hasa baada ya kugundua kuwa walikuwa na vitu vingi walivyofanana, ikiwemo wote kupata mafunzo ya kujihami, wote walikuwa wasomi wenye ujasiri katika kuyakabili mambo, wote walikuwa na kiu ya kutafuta pesa kwa hali yoyote na wote walikuwa na utaalamu wa masuala ya teknolojia.


Carlos alikuwa amehitimu Shahada ya System Analysis na Jacky alikuwa amehitimu Shahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information Technology).


Kila mwisho wa wiki Carlos aliruka kwa ndege kutoka jijini Dar es Salaam na kwenda jijini Arusha, na baadaye Jacky alikuwa akija jijini Dar es Salaam na kukaa siku mbili kisha aliruka na ndege kurudi Arusha, na baada ya miezi kadhaa ya kuchunguzana hatimaye walikubaliana kuoana huku Jacky akiacha kazi pale AICC…


______


Carlos alizinduliwa kutoka kwenye yale mawazo na dada mmoja wa kampuni ya maegesho ya magari aliyekuwa akiweka karatasi ya madai kwenye kioo kikubwa cha mbele cha gari lake.


* * * * *


Jacky alikuwa ameingia ndani ya jengo lile la benki na kusimama, akazungusha macho yake kutazama huku na kule kisha alikwenda moja kwa moja hadi kwenye dirisha namba tatu la kaunta ya ile benki. Alifika pale kaunta na kusimama nyuma ya mteja mmoja mwanamume mtu mzima aliyekuwa ameegemea kaunta ile.


Nyuma ya ile kaunta kulikuwa na kijana mmoja mtanashati sana, mrefu na mwembamba aliyekadiriwa kuwa na miaka therathini. Kijana yule alikuwa amevaa sare za kazi: suruali ya rangi ya bluu, shati jeupe lenye kola ya rangi ya bluu bahari na nembo ya benki ile upande wa kushoto wa kifua chake.


Pia alikuwa amevaa koti la suti ya rangi ya bluu na shingoni alikuwa amevaa tai ndogo ya bluu iliyokuwa na nembo ya ile benki. Yule kijana aliitwa Yusuf na alikuwa ‘busy’ akimhudumia yule mteja wa benki mtu mzima aliyekuwa ameegemea kaunta.


Yusuf alimtupia jicho Jacky na kwa nukta kadhaa na kupata mshtuko, alijikuta akiuajabia uzuri wa Jacky uliokuwa mbele ya macho yake na kusahau kidogo kumhudumia yule mteja huku akiduwaa, aliendelea kukodoa macho yake kwa kitambo fulani.


Yule mteja mtu mzima aliyekuwa akihudumiwa na Yusuf baada ya kumuona Yusuf kaduwaa, aligeuza shingo yake kutazama kule ambako macho ya Yusuf yalikuwa yakitazama na kukutana na uso wa Jacky uliokuwa umepambwa na tabasamu bashasha.


Yule mzee akajikuta akiachia tabasamu zuri la kirafiki huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.


Jacky aliinamisha uso wake kuangalia sakafuni kwa aibu baada ya kuona macho ya wanaume wawili yakimtazama kwa mshangao, kisha aliufungua mkoba wake na kutoa kadi ndogo, akaishika kwa uficho mkononi mwake huku akiufunga ule mkoba, akaendelea kusubiri zamu yake ifike.


Yusuf alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuendelea kumhudumia yule mzee, muda huo huo Jacky aliamua kugeuza shingo yake kuwatazama wateja waliokuwemo ndani ya ile benki na kuhisi kijasho chembamba kikimtoka licha ya kuwa mle ndani ya ile benki kulikuwa na viyoyozi vilivyokuwa vikitoa ubaridi mkali uliowafanya baadhi ya wateja kujikunyata kwa baridi.


Moyo wake ulikuwa umeanza kupoteza utulivu kabisa huku kijasho chepesi kikizidi kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake, alianza kushangaa kukutwa na hali ile wakati alikuwa amekwisha fanya mambo makubwa na ya hatari kuliko lile alilokuwa anatarajia kulifanya.


“C’mon, Jacky, just relax,” alijipa moyo akijiambia atulie na asiwe na wasiwasi, alivuta pumzi ndefu za ndani kwa ndani kisha akazishusha taratibu huku akiminya midomo yake yenye maki, na kutoa kitambaa chake laini kilichokunjwa kwa umaridadi kutoka kwenye mkoba wake, akajifuta jasho.


Aliporudisha kitambaa kwenye mkoba akaitupia jicho saa yake ya mkononi aina ya Cartier La Dona na kushusha tena pumzi ndefu za ndani kwa ndani.


“Habari yako, dada?” Jacky alishtuliwa na salamu kutoka kwa yule mfanyakazi wa benki baada ya yule mteja mtu mzima kuondoka, yule mfanyakazi alikuwa akimtazama Jacky kwa hamu na kwa tabasamu.


“Nzuri tu, kaka Yusuf, hujambo?” alisema Jacky huku akiachia tabasamu na pembe za midomo yake zikafinya, kisha tabasamu lake likageuka kuwa kicheko hafifu.


Yusuf alionekana kushituka kidogo, akamtazama Jacky kwa makini huku akijitahidi kuwa mtulivu. Jacky aliendelea kutabasamu.


“Umelijuaje jina langu?” hatimaye Yusuf aliuliza kwa udadisi huku akizidi kumkazia macho Jacky.


Jacky aliangua tena kicheko hafifu na kunyoosha kidole chake kuonesha beji maalumu iliyokuwa imechomekwa kwenye shati la Yusuf katika kifua chake ikiwa imeandikwa jina lake.


"Si hiyo beji uliyovaa kwenye shati lako. Au wewe siyo Yusuf?" alisema Jacky huku akiwatupia jicho wateja wengine waliokuwa wakihudumiwa kwenye kaunta zingine.


"Hmm, mimi ndiye. Karibu sana, sijui nikusaidie nini, dada…?" alisema Yusuf na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


Jacky alitoa tena kitambaa chake na kufuta jasho jepesi lililokuwa likimtoka, akageuza shingo yake kuwatazama wateja waliokuwemo ndani ya ile benki kisha akampenyezea Yusuf ile kadi kwa uficho akihakikisha hakuna mtu mwingine zaidi ya Yusuf aliyeona kitendo kile.




“Umelijuaje jina langu?” hatimaye Yusuf aliuliza kwa udadisi huku akizidi kumkazia macho Jacky.


Jacky aliangua tena kicheko hafifu na kunyoosha kidole chake kuonesha beji maalumu iliyokuwa imechomekwa kwenye shati la Yusuf katika kifua chake ikiwa imeandikwa jina lake.


"Si hiyo beji uliyovaa kwenye shati lako. Au wewe siyo Yusuf?" alisema Jacky huku akiwatupia jicho wateja wengine waliokuwa wakihudumiwa kwenye kaunta zingine.


"Hmm, mimi ndiye. Karibu sana, sijui nikusaidie nini, dada…?" alisema Yusuf na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


Jacky alitoa tena kitambaa chake na kufuta jasho jepesi lililokuwa likimtoka, akageuza shingo yake kuwatazama wateja waliokuwemo ndani ya ile benki kisha akampenyezea Yusuf ile kadi kwa uficho akihakikisha hakuna mtu mwingine zaidi ya Yusuf aliyeona kitendo kile.


Endelea...


Yusuf alimtazama Jacky kwa mshangao na kuipokea ile kadi, aliiangalia kwa makini kwa kitambo kifupi kisha akainua uso wake kumtazama Jacky akiwa na uso wenye maswali.


Jacky aliachia tabasamu kabambe na kujilegeza. "Dont worry, call me anytime when you get chance, there’s something important we need to talk," (Usihofu, nipigie wakati wowote utakapopata nafasi, kuna kitu muhimu tunahitaji kuongea) alisema Jacky kisha akageuka na kuanza kuondoka eneo lile haraka kabla Yusuf hajasema lolote.


Yusuf alitaka kusema neno lakini alisita na kubaki akimkodolea macho Jacky wakati alipokuwa akitembea kwa madaha huku akili ya Yusuf ikijikuta ikipumbazika mno na mtikisiko maridhawa wa mwili wa Jacky.


Yusuf aliendelea kumsindikiza Jacky kwa macho na kwa utulivu hadi pale alipofungua mlango na kutoka nje ya lile jengo la benki, kisha aliitupia tena jicho la haraka ile kadi na kuitumbukiza mfukoni. Akaendelea kupokea hundi za wateja wengine.


Jacky alipotoka nje ya lile jengo la benki alitembea kwa madaha, tembea yake ilikuwa adimu kuipata kwa wasichana wengi ambao pamoja na kujikwatua, bado walishindwa kupata miondoko kama yake. Tembea ya Jacky iliwafanya watu wageuze shingo zao kumtazama alipokuwa akipita huku macho yao yakishindwa kuamini kile walichokuwa wamekiona, ni kama walikuwa wamemuona malaika.


Kila alikopita, wazee kwa vijana walikuwa wakibabaika, na hawakuisha kugeuza vichwa vyao ili kuustaajabia mwili wake jinsi ulivyoumbika! Alikuwa tofauti sana na wasichana wengine wengi ambao walijiona na kujikweza juu ya kila kiumbe duniani, wasiridhike hata kukanyaga ardhi.


Wakati Jacky alipokuwa akivuka barabara ya Lumumba kuelekea lilipokuwa limeegeshwa gari lao, kuna gari moja dogo lilimpita na muda ule dereva alijikuta akimshangaa na kuivamia pikipiki ya magurudumu matatu aina ya Bajaj iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara, akairusha kule.


Kidogo lizuke vurumai kubwa katika ya yule dereva na wananchi wenye hasira, akiwemo dereva wa Bajaj, vurumai ambalo lingeweza kuigeuza sehemu ile kuwa Mogadishu, badala yake watu wote walisahau kuhusu ile ajali na kujikuta wakigeuza vichwa vyao kuangalia kazi ya Mungu ilivyotendeka vyema katika mwili wa Jacky huku wengine wakipiga mbinja.


“Dah, tuacheni utani jamani, ilikuwa haki ya dereva kupotea njia!” mwanamume mmoja wa makamo alisema kwa sauti ya juu na kuwafanya watu waliokuwa na hasira kuanguka kicheko.


Hata hivyo, Jacky hakujishughulisha nao, aliendelea na safari yake kwani hali kama ile alikwishaizoea, alifika lilipo gari lao na kufungua mlango wa abiria, akaurusha mkoba wake kwenye siti ya nyuma.


Aliminya midomo yake yenye maki na kuachia tabasamu wakati alipokuwa anaingia kwenye gari na kuufunga mlango kisha alifunga mkanda wa siti na kumtazama Carlos kwa tabasamu.


"Let’s go, my love," (Twende, mpenzi) alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


Carlos alimtazama Jacky kwa makini na kuliondoa gari taratibu bila kusema neno. Kisha aliiacha barabara ya Lumumba na kushika uelekeo wa upande wa kulia akiufuata mtaa wa Mkunguni.


Baada ya mwendo mfupi wa safari yao aliyafikia makutano ya mtaa ule wa Mkunguni na barabara ya Bibi Titi Mohammed, mbele ya Soko la Kisutu. Carlos alichepuka na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara ya Bibi Titi Mohammed.


Katika barabara ile ya Bibi Titi Mohammed Carlos alilazimika kupunguza mwendo kutokana na msongamano mkubwa wa magari, alitazama nyuma kupitia kioo cha katikati cha gari kinachoruhusu kuona nyuma ili kuchunguza kama kulikuwa na chochote alichokitilia mashaka au lah!


Alishtuka sana baada ya kuhisi kulikuwa na jambo lisilo la kawaida, alitazama kwa makini na aliweza kuliona gari aina ya Toyota Land Cruiser Pick-up la rangi nyeusi likiwa katika foleni nyuma yao, alikumbuka kuliona gari lile tangu alipotoka barabara ya Lumumba na kuingia katika mtaa wa Mkunguni.


Hata hivyo, hakutaka kumshtua Jacky, aliendesha kimya kimya hadi walipozifikia taa za kuongozea magari barabarani katika makutano ya barabara za Uhuru na Bibi Titi Mohammed. Pale kwenye makutano Carlos walishindwa kuvuka kwa kuzuiwa na taa nyekundu za kuongozea magari barabarani.


Aliitupia macho saa yake ya mkononi na kuminya midomo yake huku akitazama tena nyuma yake kupitia kile kioo cha katikati cha gari kinachoruhusu kuona nyuma, hakuliona lile gari.


Alipogeuza shingo yake kutazama kando akaliona lile gari Toyota Land Cruiser Pick-up jeusi likiwa limesimama sambamba na gari lake upande wao wa kushoto, na sasa aliweza kusoma maandishi makubwa ya POLISI yaliyokuwa yameandikwa ubavuni.


Mbele ya lile gari kulikuwa na dereva na ofisa mmoja wa polisi na nyuma ya lile gari kulikuwa na maofisa watano wa polisi waliokuwa wameketi na walishika bunduki aina ya SMG zilizotundikwa begani na kulalia vifuani.


Wale askari walikuwa wakilitazama lile kwa makini sana. Hapo akili ya Carlos ilianza kupoteza utulivu taratibu kadiri lile gari lilivyoendelea kusimama pale. Jacky alishtuka na kugeuza shingo yake kutazama kule lilikokuwa lile gari la Polisi baada ya kumuona Carlos akioneshwa kubabaika kidogo.


Carlos alikuwa akihisi kijasho chepesi kikimtoka usoni, alitoa kitambaa na kufuta jasho usoni huku akiendelea kuwachunguza wale askari wenye mitutu ya bunduki kwa makini sana huku akijaribu kuyasoma mawazo yao.


Mara taa ya kijani ya kuongozea magari ikawaruhusu kupita, Carlos akashusha pumzi za ndani kwa ndani na kuingiza gia huku akiliondoa gari lake, alizivuka zile taa na kushuhudia lile gari la Polisi likifuatia nyuma yake, alipokwenda mbele kidogo akapunguza mwendo na kukata kona kuingia mtaa wa Sofia Kawawa upande wake wa kushoto ili kuona kama alikuwa anafuatiliwa.


Lile gari la Polisi nalo lilipunguza mwendo na kuingia kufuata uelekeo ule ule japokuwa lilikawia kidogo kuingia. Tukio lile lilimfanya Carlos ahisi kuishiwa nguvu ingawa hakuwa na uhakika kama wale Polisi walikuwa wakimfuata yeye, hata hivyo kwa namna nyingine ile ilikuwa ni ishara mojawapo ya kumtahadharisha kuwa alipaswa kuwa makini.



Mara taa ya kijani ya kuongozea magari ikawaruhusu kupita, Carlos akashusha pumzi za ndani kwa ndani na kuingiza gia huku akiliondoa gari lake, alizivuka zile taa na kushuhudia lile gari la Polisi likifuatia nyuma yake, alipokwenda mbele kidogo akapunguza mwendo na kukata kona kuingia mtaa wa Sofia Kawawa upande wake wa kushoto ili kuona kama alikuwa anafuatiliwa.


Lile gari la Polisi nalo lilipunguza mwendo na kuingia kufuata uelekeo ule ule japokuwa lilikawia kidogo kuingia. Tukio lile lilimfanya Carlos ahisi kuishiwa nguvu ingawa hakuwa na uhakika kama wale Polisi walikuwa wakimfuata yeye, hata hivyo kwa namna nyingine ile ilikuwa ni ishara mojawapo ya kumtahadharisha kuwa alipaswa kuwa makini.


Endelea...


Aliongeza mwendo hadi alipofika kwenye makutano ya mtaa wa Sofia Kawawa na Indira Ghandi, akaelekea upande wa kulia na kutokea katika Mtaa wa Nkrumah. Kisha aliifuata barabara ya Nkrumah akionekana kurudi kwenda kuungana tena na barabari ya Bibi Titi Mohammed.


Kwa kuwa hakukuwa na msongamano mrefu wa magari katika barabara ile, Carlos aliongeza mwendo hadi alipozifika taa za barabarani za kuongozea magari katika makutano ya barabara za Nkrumah na Bibi Titi Mohammed.


Aligeuza shingo yake kutazama nyuma na kuliona lile gari la Polisi likiingia katika barabara ile ya Nkrumah na kukata kona kuelekea upande wa kushoto likielekea kwenye mzunguko wa barabara katika mnara wa saa maarufu kama Clock Tower.


Hapo Carlos alishusha pumzi za ahueni na kuachia tabasamu huku akigeuza shingo yake kumtazama Jacky. Waliangaliana na kujikuta wakiachia kicheko hafifu.


Haikuchukua muda zile taa za barabarani za kuongozea magari pale Nkrumah na Bibi Titi Mohammed zilimuashiria Carlos kupita. Alipita akiifuata barabara ile ya Nkrumah na mara kwa mara akitupia jicho kwenye kioo cha ubavuni kutazama nyuma yake kama kulikuwa na gari lolote alilolitilia shaka likimfuatilia.


Hakuliona gari la namna hiyo, hivyo aliamini kuwa hali ilikuwa shwari, alizidi kusonga mbele katika barabara ile ya Nkrumah akikatisha katikati ya majengo ya ghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).


Wakati wakiivuka reli katika eneo la Goldstar Carlos aligeuza shingo yake na kumtazama Jacky ambaye muda wote alikuwa mtulivu sana isivyo kawaida.


“How was it? Was it successful?” (Ilikuwaje? Ulifanikiwa?) Carlos alimuuliza Jacky huku akimkazia macho.


“Oh C’mon, Carlos! What’s the hurry, my love?” (Oh Carlos, haraka ya nini, mpenzi wangu?) Jacky alijibu kwa sauti tulivu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuegemeza kichwa chake kwenye kioo cha dirisha.


Carlos aliachia tabasamu huku akiyahamisha macho yake kutoka kwa Jacky na kuyaelekeza kutazama barabarani.


Hatimaye walifika kwenye taa za kuongozea magari barabarani katika makutano ya barabara ya Nyerere na mitaa ya Msimbazi, Nkrumah na Gerezani. Gari lake likasimama usawa wa jengo la ofisi za Selous Safari Company.


Eneo lile kulikuwa na askari wa usalama barabarani waliokuwa wametanda wakisimamisha magari. Carlos alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiwatazama wale askari wa usalama barabarani waliotapakaa katika eneo lile.


Askari mmoja ofisa wa ukaguzi wa magari barabarani aliyekuwa na nyota mbili mabegani kwake akiwa amevaa koti refu alipiga hatua zake taratibu kulisogelea gari la Carlos, alifika na kuonekana akilichunguza kwa macho.


Kisha alilizunguka na kwenda nyuma huku akizidi kulichunguza kwa jicho la hadhari, hatimaye alikuja kwa mbele kwenye dirisha la Carlos na kumuashiria Carlos kwa mkono kuwa akaegeshe gari lake mbele kando ya barabara baada ya kuvukaa zile taa.


Carlos aliitazama saa yake ya mkononi na kusonya, kwani siku hiyo alikuwa na mambo mengi ya kushughulikia, hivyo kuegesha gari lake kwa ajili ya ukaguzi ilikuwa ni namna fulani ya kumchelewesha. Wakati huohuo askari wa barabari aliyekuwa akiongoza magari aliyaruhusu magari yaliyotoka Mnazi Mmoja.


Carlos aliliondoa gari lake na kuvuka zile taa kisha akaenda kuliegesha kando ya Barabara ya Nyerere, jirani na jengo zilizopo ofisi za Davis and Shirtliff (T) na Reni International. Na hapo akakuta magari mengine kadhaa yaliyokuwa yamesimamishwa kando ya ile barabara yakikaguliwa na askari wengine wa usalama barabarani.


Carlos alisubiri pale kwa kitambo kifupi huku akionekana kukerwa, hatimaye yule ofisa wa usalama barabarani alifika na kuanza kulizunguka lile gari na kwenda nyuma huku akiwa analichunguza kwa jicho la hadhari, kisha alikwenda moja kwa moja kwenye dirisha la Carlos.


“Naomba leseni yako ya udereva,” alisema yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani huku akiinaama kidogo kumtazama Carlos.


Carlos alimtazama yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani kwa makini huku akionesha kujiamini. “How are you, Officer Lutter?” alimsalimia yule ofisa kwa sauti yake nzito na tulivu huku akitoa leseni yake na kumpa.


Yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani alishtuka kidogo na kumtazama Carlos kwa makini kisha akaachia tabasamu. “Ooh, Mr Mwamba! It’s you, my boss?” alisema huku akijiegemeza kwenye mlango wa dereva.


“Kwa nini hukuniambia kama ni wewe mzee wa mishemishe! Kwema lakini?” aliongeza yule askari mkaguzi wa magari barabarani huku akiangua kicheko hafifu kabla hata Carlos hajajibu.


“Kwema tu, mimi pia sikuwa nimekutambua kabla, nimeshtuka baada ya kusikia sauti yako,” Carlos alisema huku akiachia tabasamu.


Wakati wakiendelea kusalimiana askari mwingine wa usalama barabarani mwenye cheo cha Koplo aliyekuwa ameshika mkononi mashine ndogo ya kielektroniki ya kutolea risiti papo hapo baada ya malipo alisogea.


Alifika na kuanza kulichunguza lile gari kwa jicho la hadhari, kisha alizunguka hadi upande wa pili na kusimama kwenye dirisha la Jacky, alimtazama Jacky na macho yao yakakutana.


Jacky aliachia tabasamu bashasha kumpumbaza yule askari, na kwa kweli hila yake ilifanikiwa, kwani yule askari alionekana kubabaika kidogo, alilamba midomo yake kwa matamanio huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


Yule askari aliendelea kumkodolea macho ya tamaa Jacky huku akionekana kuhemukwa na tamaa za kimwili, hata hivyo alinywea kidogo baada ya kumtazama Carlos aliyekuwa akizungumza na bosi wake, Ofisa Lutta walioonekana kufahamiana.


Japo Jacky alikwishayasoma mawazo ya yule askari wa usalama barabarani lakini aliendelea kumtazama kwa namna ambayo ilizidi kumpumbaza zaidi, kisha alijifanya kuyakwepa macho yake na kuangalia chini kwa aibu huku akiachia tabasamu la chati.


Muda ule ule yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani alimruhusu Carlos kuendelea na safari yake huku akimtaka amtafute mwisho wa wiki. Bila ya kupoteza muda Carlos aliachia tabasamu na kumuaga yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani kwa kumpungia mkono kisha aliliondoa gari lake kwa madaha kutoka eneo lile akiifuata barabara ya Nyerere.


Wakati akiondoka alitazama nyuma kupitia vioo vya ubavuni vya gari lake na kuwaona wale maofisa wa usalama barabarani wakiyasimamisha magari mengine huku wengine wakiendelea na ukaguzi wa magari yaliyokuwa eneo lile.





Muda ule ule yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani alimruhusu Carlos kuendelea na safari yake huku akimtaka amtafute mwisho wa wiki. Bila ya kupoteza muda Carlos aliachia tabasamu na kumuaga yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani kwa kumpungia mkono kisha aliliondoa gari lake kwa madaha kutoka eneo lile akiifuata barabara ya Nyerere.


Wakati akiondoka alitazama nyuma kupitia vioo vya ubavuni vya gari lake na kuwaona wale maofisa wa usalama barabarani wakiyasimamisha magari mengine huku wengine wakiendelea na ukaguzi wa magari yaliyokuwa eneo lile.


Endelea...


Carlos alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiongeza mwendo wa gari lake kulipita lori la mafuta lililokuwa mbele yao wakati wingu zito la mvua likianza kutanda angani.


Muda huo Jacky alikuwa ameanza kuchukuliwa na mawazo, alikuwa anawaza kuhusu kazi iliyokuwa mbele yao na jinsi alivyohangaika kupata taarifa za kibenki katika Benki ya Biashara tawi la Lumumba.


alikumbuka siku mbili zilizokuwa zimetangulia kabla hawajaenda pale Benki ya Biashara tawi la Lumumba, yeye na Carlos walikuwa katika chumba fulani nyumbani kwao kilichokuwa kikitumika kama ofisi maalumu na maktaba ya siri ambayo ilikuwa na kila aina ya ulinzi, na ili kuingia mle ndani ilikuwa ni lazima ubofye namba fulani za siri zilizokuwa kwenye kisanduku kidogo chenye namba pembeni ya mlango.


Ndani ya ile ofisi Jacky na mumewe Carlos walikuwa wameketi, Jacky aliketi kwenye kiti kirefu cha ngozi halisi cha kiofisi chenye magurudumu madogo yaliyokiwezesha kusogea na kilikuwa cha kuzunguka, akiwa kazini huku wote wakijipongeza kwa Whisky.


Kwa mtazamo wa kawaida tu ungeweza kudhani ilikuwa ni ofisi ya kawaida tu yenye samani chache za kiofisi ikiwa na kiyoyozi aina ya Singsung kilichokuwa kikisambaza hewa safi.


Ofisi ilikuwa na zulia zuri la rangi nyekundu sakafuni, meza kubwa ya kiofisi ambayo juu yake kulikuwa na kompyuta mbili, IMac Retina 5K ya inchi 27 na PC aina ya Acer i5 yenye kioo cha flat.


Zile kompyuta zilikuwa zimefungwa mfumo maalumu wa udukuzi wa taarifa za kibenki uliokuwa ukifuatilia taarifa mbalimbali za fedha na kuhamisha fedha kutoka akaunti moja na kuzipeleka kwenye akaunti nyingine.


Kwa kutumia mfumo ule Jacky alikuwa ametengeneza kirusi maalumu aina ya Trojans kilichofanya kazi ya kuiba taarifa za kibenki baada ya kutumwa kwenye kompyuta za benki husika kikiwa kama keyloggers na RAT (Remote Administration Tools).


Keylogger ulikuwa ni mfumo uliosimamia keys fulani ambazo kama mtu angebonyeza kwenye keyboard yake angeziingiza kwenye rekodi, na kisha bila kujua angejikuta akituma maelezo kwa wadukuzi.


Na pale ambapo Keyloggers zilionekana kushindwa kufanya kazi ipasavyo ndipo RAT iliweza kupenya kwani ilikuwa ni hatua ya juu ya keylogger iliyosimamia shughuli zote za kiudukuzi. Kwa kutumia RAT, Jacky aliweza kujiunganisha kwenye mfumo wa benki mbalimbali bila kujulikana, wakati wafanyakazi wa benki wakiwa mtandaoni.


Ilikuwa rahisi kwa kwake kufanya mashambulizi ya kimtandao kwa kutumia RAT kwenye mfumo wa intaneti kwa watu waliokuwa wakipakua programu mbalimbali au keygens mtandaoni, ingawa siku hiyo ilikuwa tofauti kidogo.


Akiwa pale kwenye meza ya kiofisi iliyokuwa na kompyuta, pembeni yenye kulikuwa na meza ya kioo ya pembe nne ambayo juu yake kulikuwa na chupa kubwa ya Whisky, na chini ya ile meza kulikuwa na magazeti na majarida kadhaa tofauti ya siku za nyuma yaliyokuwa na taarifa za kifedha. Meza hiyo ilikuwa mbele ya kochi moja kubwa la sofa lililokuwa likitazamana na ile meza ndani.


Kwa ukutani juu ya ile meza ya kioo kulikuwa na shubaka la vitabu lililokuwa na nakala chache za magazeti ya siku za karibuni na majarida machache yaliyopangwa kwa ustadi, na kulikuwa na kidau cha wino, mhuri na kichupa kidogo chenye wino mweupe wa kufutia maandishi.


Upande wa kulia kulikuwa na dirisha pana la kioo lililokuwa limefunikwa kwa mapazia mawili mepesi marefu ya rangi ya samawati, pia kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu.


Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na majarida mengi yaliyohifadhiwa pale kwa muda mrefu na mazingira ya mle ndani yalikuwa nadhifu na yaliyovutia kwa mpangilio wake. Upane wa mbele wa ile ofisi kwa juu ukutani kulikuwa na ramani kubwa ya Tanzania iliyokuwa imetundikwa ikionesha maeneo mbalimbali yenye hazina za madini na mifumo ya kibenki.


Pia kulikuwa na jokofu lenye ukubwa wa wastani aina ya LG ambalo lilikuwa limejaa vinywaji mbalimbali, moto na baridi vilivyoweza kumchangamsha yeyote aliyeingia humo hata kama angekuwa amechoka baada ya kazi ngumu.


Katika muda ule Jacky alikuwa nyuma ya kompyuta yake ya IMac Retina 5K akibonyeza bonyeza kwa kitambo kirefu huku akisoma maelezo yaliyojitokeza kwenye screen na kujaribu kuingiza code number fulani ili ku-log in kwenye SWIFT system ya Benki ya Biashara tawi la Lumumba akijaribu kupata taarifa za kifedha, lakini ujumbe uliokuwa ukitokea kwenye screen uliandikwa 'REMOTE PROCEDURE ERROR'.


Hakukata tamaa akajaribu njia nyingine kwa kutumia Open Source Intelligence (OSINT) akaingia code number fulani na mara maneno 'NOT OPERATING' yakatokea kwenye screen yake, akatweta. Kisha aka-log in kwenye mtandao maalumu wa ‘dark web’, ili kuona kama angeweza kupata taarifa na wadukuzi wengine waliofanikiwa kuvunja ngome za kiulinzi za kibenki.


Maelezo aliyoyapata kutoka katika dark web yakamfanya azidi kuchanganyikiwa, akashusha pumzi za ndani kwa ndani huku akijiegemeza kwenye kiti chake. Muda wote ule Carlos alikuwa ameketi kwenye sofa akimtazama kwa makini.


“I think I need to find the latest OSINT program, otherwise we’ve to take the risk by going there physically,” (Nadhani ninahitaji kutafuta programu mpya ya OSINT, vinginevyo tutapaswa kwenda wenyewe) Jacky alisema huku akionekana kuchoka.


“What happened?” (Kumetokea nini?) Carlos aliuliza kwa wasiwasi.


“It’s not working… tomorrow I’ll know what to do,” (Haifanyi kazi… kesho nitajua nini cha kufanya) alisema Jacky huku akichukua bilauri ya whisky na kupiga funda kubwa la whisky huku akisisimkwa.


“What will you do?” (Utafanyaje?)


“I think I’ll go to the bank and leave a USB stick preloaded with malware near a teller’s desk with the hopes someone will pick it up and plug it into an internal computer…” (Nadhani nitakwenda benki na kuacha USB yenye virusi kwenye dawati la mhudumu nikitumaini ataichukua na kuifungua kwenye kompyuta za ndani…) alisema Jacky huku akiachia tabasamu bashasha.


“If this doesn’t work?” (Kama mbinu hiyo haitafanya kazi?) aliuliza Carlos huku akimkazia macho Jacky.


“Hmm… let me think,” (Hmm… ngoja nifikirie) alisema Jacky huku aking’ata mdomo wake wa chini.





“I think I’ll go to the bank and leave a USB stick preloaded with malware near a teller’s desk with the hopes someone will pick it up and plug it into an internal computer…” (Nadhani nitakwenda benki na kuacha USB yenye virusi kwenye dawati la mhudumu nikitumaini ataichukua na kuifungua kwenye kompyuta za ndani…) alisema Jacky huku akiachia tabasamu bashasha.


“If this doesn’t work?” (Kama mbinu hiyo haitafanya kazi?) aliuliza Carlos huku akimkazia macho Jacky.


“Hmm… let me think,” (Hmm… ngoja nifikirie) alisema Jacky huku aking’ata mdomo wake wa chini.


Endelea...


“Do like this, I know there’s that handsome guy, go find him and make him fall in love with you…” (Fanya hivi, najua yupo yule kijana mtanashati, kamtafute na uhakikishe anaangukia kwenye penzi lako…) alisema Carlos. Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akifikiria kuhusu kazi ile.


* * * * *


Jioni ya saa kumi na mbili na nusu katika mtaa mmoja eneo la Tabata Segerea nyumba moja nzuri ya kifahari ya ghorofa mbili iliyokuwa imezungukwa na miti mizuri ya vivuli ilikuwa katika hali ya ukimya sana. Ilikuwa katika eneo la makazi ya kisasa ya watu wenye ukwasi, lenye majumba ya kifahari yaliyozungukwa na miti mirefu na kuta zenye usalama wa uhakika.


Nyumba ile ilikuwa imezungukwa na ukuta mrefu uliofungwa mfumo maalumu wa umeme wa kuzuia wezi juu yake usiomwezesha mtu kuona ndani, na ilikuwa na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatwa vizuri.


Ilikuwa na madirisha makubwa ya kisasa na baraza kubwa mbele yake iliyopangwa seti moja ya makochi ya sofa ya rangi nyeusi.


Ndani ya uzio wa ile nyumba upande wa kushoto kulikuwa na banda la wazi la kuegeshea magari na kulikuwa na magari madogo matatu ya kifahari, BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati, Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe na Toyota Landcruiser GX V8 lililokuwa na rangi nyeusi.


Sehemu nyingine ya mandhari ya nyumba ile ilikuwa imezungukwa na miti mirefu na mikubwa ya kivuli. Sehemu ya mbele ya hiyo nyumba ilikuwa imezungukwa na bustani nzuri ya maua ya kupendeza na katikati ya bustani hiyo kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa matofali madogo madogo yaliyokuwa yanavutia.


Pia kulitengenezwa njia kubwa ya gari iliyotengenezwa kwa ufundi mkubwa iliyokuwa inaanzia sehemu ya getini hadi mbele ya ile nyumba ili kumruhusu dereva ageuze gari pasipo kurudi nyuma.


Ndani ya ile nyumba kwenye sebule kubwa yenye samani zote muhimu za kisasa, Jacky na Carlos walikuwa wameketi wakiwa na bilauri za whisky mkononi na kwenye meza kulikuwa na chupa kubwa ya Whisky na sahani iliyojaa nyama choma za mbuzi.


Carlos alikuwa amevaa bukta ya khaki na singleti nyeupe na Jacky alivaa nguo nyepesi nyeupe ya kulalia iliyolichora vyema umbo lake la kuvutia na na kuifanya nguo yake ya ndani ya rangi ya bluu ionekane bila kificho.


Sebule ile ilikuwa imepambwa na seti mbili za makochi ya sofa ya kifahari yaliyokuwa yamepangwa katika mtindo wa kuizunguka sebule hiyo. Katikati ya ile sebule kulikuwa na meza nzuri ya kioo yenye umbo la duara.


Pia kulikuwa na mapambo mengine mbalimbali yaliyoifanya ile sebule ivutie sana huku madirisha yake makubwa ya vioo yalikuwa yamefunikwa kwa mapazia marefu.


Jacky alikuwa kimya akitafakari kwa kina, Carlos alimwangalia Jacky kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“But you haven’t answered my question, how do you see the guy?” (Lakini bado hujajibu swali langu, huyo bwana unamwonaje?) Carlos aliuliza huku akimtazama Jacky kwa makini.


“How?” (Kivipi?) Jacky aliuliza huku akimtazama Carlos kwa mshangao.


“Yaani… unadhani upo uwezekanao wowote wa kumbana na kupata taarifa muhimu?”


Jacky alimeza funda kubwa la whisky na kuweka bilauri juu ya meza kisha aliachia tabasamu. “Kumpata wala haina wasiwasi, na akishapatikana si ndiyo basi tena! Kwani unadhani kwangu atafurukuta?”


Carlos aliachia tabasamu na kuchukua kipande cha nyama choma huku akimtazama Jacky kwa makini zaidi.


“Jacky, don’t take this for granted. You can do anything with him and still get nothing. You do not know, maybe he's got a beautiful wife than you…” (Usilichukulie hili jambo kirahisi rahisi hivyo. Unaweza kufanya naye chochote na bado akafurukuta. Hujui, pengine ana mke mzuri kuliko wewe…) Carlos alisema kwa sauti tulivu.


Jacky alimwangalia Carlos kwa kitambo kirefu na kuachia tabasamu lililokuwa limeficha bezo ndani yake.


“So you know that he has a wife?” (Kwa hiyo umeshajua kama ana mke?) aliuliza huku akichukua kipande cha nyama choma na kukitumbukiza mdomoni.


“I do not know, but that’s something you should consider more carefully, to know his movements, his habits, his potential talents and his dreams,” (Sijui, lakini hilo ni jambo unalopaswa ulichunguze kwa makini zaidi, uzijue nyendo zake, tabia yake, uwezo wake na ndoto zake) alisisitiza Carlos huku akimeza funda kubwa la pombe na kusisimkwa mwili.


Jacky naye aliinua bilauri ya pombe na kuinywa pombe yote iliyobakia kwenye bilauri huku akisisimkwa mwili, alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani na kuirudisha ile bilauri mezani. Kisha akamtazama Carlos kwa makini.


“Naona sasa unataka kuniongezea kazi zingine nisizoziweza,” alilalamika Jacky huku akijiegemeza kwenye kochi.


Carlos alimkazia macho, akakunja uso wake na kutengeneza matuta madogo madogo usoni kwake. Macho yake yalikuwa yanawaka kwa hasira. “Utoto huo! Kazi zipi usizoziweza?”


“Si kama hizo za kufuatilia nyendo zake, sijui tabia yake na ndoto zake. Basi itabidi nihamie kabisa nyumbani kwake,” alisema Jacky kwa kulalamika huku akipigwa miayo ya uchovu.


“Hamia! Potelea mbali, hamia kwake hata kesho. Tunahitaji pesa, Jacky, tunahitaji bilioni moja na kuendelea! I am ready to take a knife and cut off my mother's curfew for such amount…” (Niko tayari hata kushika kisu na kumkata koromeo mama yangu mzazi kwa fedha kama hiyo…) alisema Carlos huku macho yake yakiwaka kwa ghadhabu.


“Sembuse eti kumruhusu mke wangu ahamie kwa mwanamume nisiyemjua! Hamia hata kesho,” aliendelea kusema huku akionekana kupandwa ghadhabu.


Jacky alitaka kusema neno lakini alipomtazama Carlos kwa makini akasita, alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kubaki kimya. Alianza kuhisi hofu na ubaridi fulani wa woga wa aina yake vikimtambaa mwilini, nywele zake pia zilikuwa zimemsimama kichwani kwa hofu.


Carlos aliigundua hofu aliyokuwa nayo Jacky, hivyo aliamua kumsogelea na hapo hapo mikono yake yote miwili ikaanza kufanya ziara ya kwenye mwili wa Jacky, huku mkono wa kulia ukienda moja kwa moja kwenye kifua cha Jacky.


“Please forgive me, my love, I did not intend to scare you, you know precisely how much I love you so much and I do not want to see another man navigating to this body,” (Tafadhali nisamehe, mpenzi wangu, sikukusudia kukutisha, unajua kiasi gani nakupenda sana na nisingependa kuona mwanaume mwingine akijivinjari kwenye mwili huu) Carlos alisema kwa namna ya kumbembeleza Jacky.




Carlos aliigundua hofu aliyokuwa nayo Jacky, hivyo aliamua kumsogelea na hapo hapo mikono yake yote miwili ikaanza kufanya ziara ya kwenye mwili wa Jacky, huku mkono wa kulia ukienda moja kwa moja kwenye kifua cha Jacky.


“Please forgive me, my love, I did not intend to scare you, you know precisely how much I love you so much and I do not want to see another man navigating to this body,” (Tafadhali nisamehe, mpenzi wangu, sikukusudia kukutisha, unajua kiasi gani nakupenda sana na nisingependa kuona mwanaume mwingine akijivinjari kwenye mwili huu) Carlos alisema kwa namna ya kumbembeleza Jacky.


Endelea...


Kisha aliupeleka mkono wake kwenye chuchu laini za Jacky zilizosimama kwa utulivu juu ya milima miwili isiyofahamu adha yoyote ya volkano.


“But since we need money, I have to let you go to another man, I hope you know precisely what I mean, my darling,” (Lakini kwa kuwa tunahitaji pesa, nalazimika kukuruhusu kwenda kuonana na mwanamume mwingine, natumaini unajua hasa namaanisha nini, mpenzi wangu) Carlos alizidi kusisitiza huku akiachia tabasamu pana.


Jacky hakusema neno bali alibaki kimya huku akimtazama Carlos kwa makini. Hata hivyo, Carlos hakusubiri jibu la Jacky, alipeleka mkono wake kwenye tumbo la Jacky na kuanza kukipapasa kitovu chake laini chenye kishimo kidogo kilichotengeneza ziada nyingine ya uzuri wake.


Kisha mkono wa pili ulikwenda moja kwa moja kiunoni na aliigusa nyonga yake laini iliyokuwa na mifupa miteke iliyopakana na mzigo imara wa makalio yaliyotuama vyema. Wakati akiendelea kumpapasa, Jacky akaamua kuvunja ukimya huku akimtazama Carlos usoni.


“Carlos!” Jacky aliita kwa sauti laini ya mahaba.


“Yes, my love,” Carlos aliitikia kwa sauti yake nzito iliyokuwa na kila aina ya kiashiria cha kuhemkwa na tamaa za kimwili.


“I’m tired with this life and I need to live a normal life, you don’t know what I’m going through right now…” (Nimechoshwa na maisha haya na ninahitaji kuishi maisha ya kawaida, hujui napitia magumu gani hivi sasa…) Jacky alisema kwa huzuni na kuongeza.


“Hivi kwa nini tusiachane na maisha haya na tuishi maisha huru ya mke na mume? Tuna shida gani, kama ni pesa tayari tunazo nyingi tu…” Jacky alianza kusema kwa utulivu huku akiipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Carlos na kuzifanya chuchu za matiti yake kukitekenya kifua cha Carlos.


Kitendo kile kikafanya joto kali la mwili wa Jacky limfanye Carlos ajisikie faraja ya aina yake. Carlos alimtazama Jacky machoni na kuyaona machozi yakianza kumlenga machoni.


“I understand, my love, but nobody ever felt satisfied with money. We still have many things to do so we need money…” (Naelewa, mpenzi, lakini hakuna aliyewahi kutosheka na pesa. Bado tuna mambo mengi ya kufanya hivyo tunahitaji pesa…) alisema Carlos huku kwa kutumia kiganja chake taratibu alianza kumfuta Jacky machozi.


“…so we don’t have time to rest. We need to work day and night to make sure we have more money,” (…hivyo hatuna muda wa kupumzika. Tunahitaji kufanya kazi mchana na usiku kuhakikisha tunapata pesa zaidi) aliongeza Carlos huku akiendelea kuyafuta machozi kwenye macho ya Jacky.


Jacky aliusukuma mkono wa Carlos kutoka machoni mwake kisha akajisogeza nyuma kidogo huku akimtazama Carlos kwa makini.


“You depend on me to complete this mission, so you’ll have to listen to me. This is the last mission and after this you’ll never ask me again, promise?” (Unanitegemea kukamilisha mpango huu, kwa hiyo unapaswa kunisikiliza. Huu mpango ni wa mwisho na baada ya hapo hutaniambia tena, unaniahidi hivyo?) Jacky alisema huku machozi yakianza kumtiririka kwenye mashavu yake, hakujua kwa nini alikuwa akisita sana kuifanya ile kazi.


“Promise!” (Nakuahidi) Carlos alisema.


“Baada ya mpango huu kukamilika nataka tuachane na hizi kazi. Nataka tuanze aina mpya ya maisha, I’m dreaming to have a good family and be happy,” (Nina ndoto ya kuwa na familia nzuri na maisha ya furaha) Jacky alisema na hapo Jacky akamsogelea na kuvuta karibu zaidi, kisha ndimi zao zikakutana. Kilichofuata baada ya pale ilikuwa ni sauti ya pumzi zao sambamba na miguno isiyoeleweka ya mahaba.


Kama mtu aliyepandwa na wazimu wa mapenzi, Jacky akaanza kumvua Carlos singleti yake na kuitupilia mbali kisha akapeleka mikono yake kifuani kwa Carlos na kuanza kumpapasa kwa pupa. Carlos alitaka kumzuia lakini Jacky akamng’ata mkono.


“Don’t stop me, please make my night beautiful,” (Usinizuie, tafadhali ufanye usiku wangu kuwa wa kupendeza) Jacky aliongea kwa hasira kama mwehu huku akiivuta chini bukta ya Carlos kwa pupa.


“I thought we still need to talk and plan our things well,” (Nilidhani bado tunahitaji kuongea na kupanga mambo yetu vizuri) Carlos alinong’ona.


“No, we’re done. Now I want to spend time with you, I need you so badly,” (Hapana, tumekwisha maliza, sasa nahitaji kujivinjari na wewe, nakuhitaji vibaya sana) Jacky alisema huku akihema kwa nguvu, muda ule ule alimvuta Carlos na ndimi zao zikaingia tena kazini zikitekenyana taratibu mdomoni.


Japokuwa Carlos alikuwa mtu hatari wa kuogopwa aliyekubuhu katika umafia lakini mbele ya mlimbwende yule, hasa wakati kama ule, alikuwa kama mbwa muoga mbele ya chatu mwenye njaa kali.


Jacky aliinuka na kuvua haraka gauni lake na kulitupa kando na hivyo kubakiwa na nguo yake nzuri ya ndani huku harufu nzuri ya manukato yake ikimshawishi Carlos kuendelea na hatua iliyofuata.


Carlos hakuwa na ujasiri tena wa kupingana zaidi na hisia zake, hivyo taratibu aliupeleka mkono wake ndani ya nguo ya ndani ya Jacky na kuanza kuyatomasa makalio yake laini yaliyoshiba minofu.


Jacky aliachia mguno hafifu wakati mkono mwingine wa Carlos ulipokuwa ukiyatomasa matiti yake taratibu. Kisha Carlos alianza kutembeza taratibu ulimi wake shingoni kwa Jacky na hatimaye sikioni na hapo ikasikika sauti hafifu ya Jacky ya mguno wa mahaba.


Jacky hakuweza kuvumilia tena hivyo haraka akaishusha chini nguo yake ya ndani na kuupeleka mkono wake akiichezea ikulu ya Carlos na kumfanya aanze kuhema ovyo.


Muda mfupi uliofuata walikuwa kwenye kochi kubwa la sofa pale pale sebuleni huku kila mmoja akiwa amepandwa na wazimu wa mapenzi. Mara wakajikuta wakiwa kwenye sayari nyingine ya mahaba mazito iliyokuwa kama kisiwa cha raha kwa ajili yao.


Sebule ile ikajazwa na vilio vya mahaba toka kwa Jacky vilivyoashiria raha ya aina yake aliyokuwa akiipata. Jacky alikuwa msichana mtundu sana aliyemudu vyema mitindo mbalimbali kiasi cha kumfanya Carlos ajihisi kama mvulana wa shule ya msingi.




Jacky hakuweza kuvumilia tena hivyo haraka akaishusha chini nguo yake ya ndani na kuupeleka mkono wake akiichezea ikulu ya Carlos na kumfanya aanze kuhema ovyo.


Muda mfupi uliofuata walikuwa kwenye kochi kubwa la sofa pale pale sebuleni huku kila mmoja akiwa amepandwa na wazimu wa mapenzi. Mara wakajikuta wakiwa kwenye sayari nyingine ya mahaba mazito iliyokuwa kama kisiwa cha raha kwa ajili yao.


Sebule ile ikajazwa na vilio vya mahaba toka kwa Jacky vilivyoashiria raha ya aina yake aliyokuwa akiipata. Jacky alikuwa msichana mtundu sana aliyemudu vyema mitindo mbalimbali kiasi cha kumfanya Carlos ajihisi kama mvulana wa shule ya msingi.


Endelea...


Alikuwa amezitendea vyema hisia za Carlos na raha aliyoipata Carlos iliyafanya macho yake yashindwe tena kumtazama Jacky usoni. Hata hivyo, Carlos naye hakuachwa nyuma, kwani alikuwa akimchezesha Jacky gwaride la ukweli.


“Ooh Carlos, you’re a real man!” (Carlos, wewe ni mwanamume kwelikweli!) Jacky alisema huku akitweta baada ya kumaliza mzunguko mmoja, aligeuza shingo yake kumtazama Carlos aliyekuwa amejilaza kwenye sofa akitiririkwa na jasho kutokana na shughuli ile ambayo haikuwa ndogo.


Kisha Jacky alijiinua kutoka pale sakafuni alipojikuta akiwa amelala, akachukua chupa ya whisky na kumimina katika bilauri kisha akapiga funda kubwa huku akisisimkwa mwili na kushusha pumzi ndefu.


“You’re so wonderful, my love. I swear in heaven and earth, I’ve never met a man who knows love like you!” (Wewe ni mwanamume wa aina yake, mpenzi wangu, naapa sijawahi kukutana na mwanaume anayeyajua mapenzi kama wewe!) Jacky alisema huku akitweta na kujipweteka kwenye sofa.


“Dah! Jacky mtundu sana na ana sifa zote, ni mwanamke mrembo sijapata kuona na mambo anayonifanyia kila siku yananipagawisha, ninashukuru kuwa na mwanamke huyu maishani mwangu. Ana kila kitu ninachokihitaji kwa mwanamke. Halafu yuko tofauti sana na wanawake wengine,” Carlos aliwaza huku akimtupia jicho Jacky.


“Mwili wote unaniuma kwa gwaride alilonichezesha Carlos, huyu ni kidume kweli kweli kwani muziki wake si mdogo utadhani ana mapafu ya farasi!” Jacky naye aliwaza huku akijiinua kutoka pale kwenye sofa na kuelekea maliwato.


“Dah! Mwili wote hauna nguvu hata kidogo, Carlos huwa ananikimbiza mchaka mchaka kwelikweli,” alijiambia wakati akijimwagia maji mwilini ili kurejesha nguvu mwilini.


“Lakini, ni kweli huyu mwanamume ananipenda au kanioa ili anitumie kama project yake ya kujipatia fedha? Kwa nini aniruhusu nikalale na mwanamume mwingine sababu ya fedha? Hivi nitaendelea na maisha haya ya kuutumia mwili wangu kwa ajili ya fedha hadi lini? I’m tired with this kind of life,” (Nimechoka na aina hii ya maisha) Jacky aliwaza wakati akitoka kule maliwato na kurudi sebuleni alipokuwa ameketi Carlos.


* * * * *

Ilikuwa tayari imetimia saa mbili na nusu ya usiku wakati Jacky na Carlos walikuwa wamelala usingizi kwenye kochi kubwa la sofa pale pale sebuleni na kupitiwa na usingizi mtamu wa uchovu. Walipitiwa usingizi baada ya kwenda mzunguko wa pili uliowafanya washindwe hata kuinuka na kuamua kuangusha gari pale pale.


Wote walikuwa watupu huku Jacky akiwa amekilaza kichwa chake kifuani kwa Carlos. Mguu wake mmoja ulikuwa katikati ya mapaja ya Carlos huku mkono wake mmoja akiwa ameuzungusha shingoni kwa Carlos na alikuwa akikoroma kwa sauti hafifu ya uchovu.


Mara simu ya Jacky ilianza kuita kwa fujo na kumshtua Carlos, ambaye aliinua kichwa chake kuitazama kwa makini. Hii ilikuwa simu nyingine aina ya Nexus 6P ambayo ni tofauti na ile ya IPhone X, na aliitumia kwenye dili za hatari tu.


Ile simu ilifanyia utundu kwa kumfanya mtu yeyote ambaye angejaribu kuifuatilia mahali alipo asiweze kubaini, kuna wakati ingesoma kuwa yupo Australia au Uingereza, alifanya vile ili hata kama lingetokea jambo lolote ingekuwa vigumu kumhusisha kwani hata namba iliyotumika katika simu ile ilisajiliwa kwa jina bandia la Belinda Jackson.


Ile simu ilikuwa juu ya ile meza ya duara na iliendelea kuita kwa fujo na kugeuka kero kubwa masikioni mwake. Carlos aliinua mkono wake wa kulia ambao aliutumia kuvaa saa na kuitazama saa yake ya mkononi aina ya Ferrari King Gold hublot aliyoinunua Dubai kwa dola za Marekani 43,600.


“Ooh shit! It is quarter past eight!” (Ooh! Ni saa mbili na robo!) Carlos aling’aka kwa mshangao huku akiikodolea macho kwa makini ile saa yake kisha alimtazama Jacky ambaye alikuwa anakoroma na kuanza kumpigapiga mgongoni ili kumwamsha.


Jacky alifumbua macho yake kivivuvivu na kumtazama Carlos usoni kisha alinyanyua kichwa chake na kugeuza shingo yake kuitazama ile simu iliyokuwa bado inaita huku akipiga miayo ya uchovu.


Alijaribu kuipuuza ile simu na kukilaza tena kichwa chake kifuani kwa Carlos lakini iliendelea kuita kwa fujo na kusababisha kero masikioni mwake. Aliinuka akaichukua na kuitazama namba ya mpigaji kwa makini, kisha akaipokea na kuiweka sikioni.


“Hello!” Jacky alizungumza kwa sauti laini huku akipiga mwayo mrefu kutokana na uchovu wa usingizi.


“Hello, I think I’m talking to Belinda Jackson, right?” (Halo, nadhani nazungumza na Belinda Kizito, au siyo?) sauti ya upande wa pili wa simu ilipenya kwenye sikio la Jacky na kumfanya ashtuke kidogo. Alikunja sura yake huku akijaribu kutafakari haraka haraka jibu ambalo angetoa.


“Yes, who is this?” (Ndiyo, nani mwenzangu?) Jacky aliuliza kwa mashaka kidogo.


“My name is Yusuf Akida,” (Jina langu ni Yusuf Akida) sauti ile ilizungumza kwa utulivu.


“Which Yusuf?” (Yusuf gani?) Jacky aliuliza tena huku akikunja sura yake kujaribu kukumbuka kama aliwahi kukutana na mtu mwenye jina hilo.


“You came to the bank this morning and gave me your business card…” (Ulikuja pale benki leo asubuhi na ukanipa kadi yako…) ile sauti iliongea kwa utulivu na kushusha pumzi ndefu.


“Ooh… Yusuf! How are you, my love?” (Ooh… Yusuf! Habari yako, mpenzi?) Jacky alisema kwa sauti nyororo huku akiachia kicheko hafifu kilichopenya vyema kwenye sikio la Yusuf.


“I’m fine…” (Sijambo…) ile sauti ilijibu kisha kimya kifupi kikapita.


“Samahani sana kwa kukukera kwa simu saa hizi, nilitaka tu kukusalimia nisikie sauti yako,” sauti ile ilisema.


Jacky aliachia tabasamu pana huku akigeuza shingo yake kumtazama Carlos kisha akamkonyeza. Carlos alijiweka sawa pale kwenye sofa na kusogeza sikio lake akiwa na hamu ya kutaka kusikiliza maongezi.


“Wala usijali, Yusuf, hujanikera kabisa! We nipigie muda wowote tu, ndiyo maana nimekupa namba yangu,” Jacky alisema kwa sauti laini yenye kusihi.


“Asante sana, Belinda…” Yusuf alisema na kunyamaza tena. Kitambo kingine kifupi cha ukimya kikapita huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri, na wakati hali ile ikiendelea mara Yusuf akavunja ukimya. “Bila shaka saa hizi uko nyumbani!”


Jacky aliachia kicheko cha mahaba huku akigeuza tena shingo yake kumtazama Carlos ambaye muda wote alikuwa ametega sikio lake kwa shauku ya kutaka kusikia kilichokuwa kinaongewa.


“Ndiyo, niko nyumbani,” Jacky alijibu huku akibana midomo yake yenye maki.





“Asante sana, Belinda…” Yusuf alisema na kunyamaza tena. Kitambo kingine kifupi cha ukimya kikapita huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri, na wakati hali ile ikiendelea mara Yusuf akavunja ukimya. “Bila shaka saa hizi uko nyumbani!”


Jacky aliachia kicheko cha mahaba huku akigeuza tena shingo yake kumtazama Carlos ambaye muda wote alikuwa ametega sikio lake kwa shauku ya kutaka kusikia kilichokuwa kinaongewa.


“Ndiyo, niko nyumbani,” Jacky alijibu huku akibana midomo yake yenye maki.


Endelea...


“You are in bed?” (Upo kitandani?) Yusuf aliuliza tena kwa shauku.


“Nope… I'm just sitting in the living room,” (Wala… nimeketi tu sebuleni) Jacky alisema huku aking’onga.


“Are you alone or you are with someone?” (Uko peke yako au una mtu?) Yusuf aliuliza tena kwa shauku huku sauti yake ikiashiria wivu fulani.


Jacky aliangua kicheko kingine cha mahaba, kicheko cha safari hiyo kilikuwa kicheko hafifu lakini kilichopenya vyema kwenye sikio la Yusuf na kumfanya akunje sura yake.


“Why are you laughing, Belinda, or have I asked a question that is unusual?” (Mbona unacheka, Belinda, au nimeuliza swali ambalo si la kawaida?) Yusuf aliuliza kwa sauti tulivu iliyopenya haswa kwenye sikio la Jacky.


Jacky alilamba midomo yake kwa madaha huku akijiegemeza kifuani kwa Carlos. Carlos akamkumbatia huku akizishika chuchu zake na kumfanya Jacky asisimkwe.


“No, it's a very common question,” (Hapana, ni swali la kawaida kabisa) Jacky alijibu kisha akageuza shingo yake kumwangalia Carlos na kusogeza mdomo wake kwenye mdomo wa Carlos, kisha akambusu.


“I’m all alone. Do you want to come and give me a company?” (Nipo peke yangu tu. Vipi unataka kuja kunipa kampani?) Jacky alimuuliza Yusuf swali la uchokozi huku akitoa ulimi wake na kulamba midomo.


“Where are you living?” (Kwani unaishi wapi?) Yusuf aliuliza kwa shauku.


“Naishi Masaki…”


“Aah, Masaki! Kwani ubavu wa kuja huko ninao basi! Kuja huko kwenu si mpaka nipewe Viza!” Yusuf alisema kwa utani huku akiangua kicheko hafifu.


“Viza?” Jacky aliuliza kwa mshangao.


“Ndiyo, nitaingiaje maeneo ya watu wazito kama naingia sokoni?” Yusuf alisema huku akichia kicheko kingine hafifu na kumfanya Jacky naye aangue kicheko.


“Acha mzaha bwana…” Jacky alisema baada ya kile kicheko huku akimpapasa Carlos kwenye kidevu.


“But, I’m just curious, Belinda. Be honest with me, living at Masaki all alone! I guess whoever your husband he is, he is sure a big or rich guy…” (Lakini, najaribu kujiuliza, Belinda. Kuwa mkweli tu, unaishi Masaki peke yako! Nahisi huyo mumeo, bila shaka atakuwa mtu mkubwa au tajiri sana…) Yusuf aliuliza kwa wasiwasi.


“Trust me, Yusuf, I’m not married. I’m all alone… ” (Niamini, Yusuf, wala sijaolewa. Naishi peke yangu…)


“Or maybe you're related to a very rich family?” (Au pengine unatoka katika familia tajiri sana?) Yusuf akauliza kwa sauti yenye wasiwasi


“Hmm…” Jacky aliguna.


“And they are taking good care of you…” (Na wanakuhudumia vizuri sana…) Yusuf akasema tena kabla Jacky hajasema lolote.


“Oh, Yusuf my dear, why can’t we skip this conversation and talk about our matters?” (Oh Yusuf mpendwa wangu, kwa nini tusiyaache maongezi haya na kuzungumzia mambo yetu?) Jacky alimkatisha Yusuf huku akionekana kuanza kukereka.


“Okay, I’m very sorry for…” (Sawa, samahani kwa…)


“Don’t worry, my love. Niambie uko wapi saa hizi?” Jacky alisema na kumkata kauli Yusuf.


“Nipo hapa Malapa La Promise Hotel, sijui unapajua?”


“Napafahamu sana,” alisema Jacky na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, kisha kikazuka kitambo kifupi cha ukimya.


“Do you want me to come there?” (Kwani unataka nije hapo?) hatimaye Jacky aliuliza huku akimkonyeza Carlos.


“Njoo kama unaweza,” Yusuf alisema huku akishusha pumzi ndefu.


“Okay, give me just forty-five minutes I’ll be there,” (Sawa, nipe kama dakika arobaini na tano tu nitakuwa hapo)


“I’m patiently waiting, but I’m sorry for troubling you,” (Nakusubiri kwa hamu, lakini samahani kwa usumbufu) Yusuf alisema kwa sauti ya kusihi.


“Don’t worry,” Jacky alisema na kukata simu huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani. Alipeleka mkono wake wa kulia kwenye kifua cha Carlos na kuanza kumpapasa, kisha alimbusu kwenye paji la uso kwa furaha.


“The first step towards billions,” (Hatua ya kwanza kuelekea kwenye mabilioni) Jacky alisema huku akimbusu Carlos mfululizo kwenye mashavu na mdomo wake. Muda wote Carlos alibaki kimya akimtazama bila kusema neno, uso wake haukuonesha tashwishwi yoyote.


“The way is clear, my love,” (Njia iko wazi, mpenzi wangu) Jacky alisema huku akizidi kujiegemeza kwenye kifua cha Carlos.


“But, be very careful, my love, I hope you don’t see the way to jail,” (Lakini, kuwa mwangalifu sana Jacky, nina imani huioni njia ya kwenda gerezani) Carlos alimtahadharisha Jacky kwa sauti tulivu.


“Do not worry, I'm very careful,” (Ondoa shaka, nipo makini sana) Jacky huku alisema akimtoa wasiwasi Carlos.


Kitambo kifupi cha ukimya kikapita huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri na wakati hali ile ikiendelea mara Jacky akakumbuka jambo na kumtazama Carlos.


“So what do you say, nikaoge niondoke?” Jacky alimuuliza Carlos huku akimtazama usoni.


“Nakutakia kila la heri,” Carlos alijibu na muda ule ule Jack alijiinua kutoka pale kwenye sofa na kuelekea maliwatoni.



Kitambo kifupi cha ukimya kikapita huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri na wakati hali ile ikiendelea mara Jacky akakumbuka jambo na kumtazama Carlos.


“So what do you say, nikaoge niondoke?” Jacky alimuuliza Carlos huku akimtazama usoni.


“Nakutakia kila la heri,” Carlos alijibu na muda ule ule Jack alijiinua kutoka pale kwenye sofa na kuelekea maliwatoni.


Endelea...


Alioga chap chap na baada ya dakika kadhaa alitoka bafuni na kuingia chumbani, akafungua kabati maalumu ambalo lilitumika kuhifadhi nguo maalumu kwa matukio maalumu, akajichagulia gauni maalumu kwa siku ile iliyoendana na umbo lake.


Lilikuwa gauni jepesi la rangi nyekundu la mikono mirefu lililolichora vyema umbo lake na kuishia juu ya magoti yake huku likiwa na mpasuo kwa mbele ulioacha paja lake nusu wazi na kuifichua vizuri hazina ya kupendeza yenye mvuto wa ajabu ya miguu na mapaja yake maangavu yenye misuli imara ya rangi maridhawa ya mng’ao.


Miguuni alivaa viatu vizuri vyekundu vya ngozi ya mamba vilivyokuwa na vikanyagio virefu vya mchuchumio.


Kisha alisimama mbele ya meza iliyokuwa imesheheni vipodozi vya kila aina akajipodoa na kuuremba uso wake. Midomo yake ya kike yenye kingo pana kiasi aliikoleza vizuri rangi ya mdomo na masikio yake madogo yasiyochusha aliyavalisha hereni maalumu za madini ghali ya tanzanite na kujipulizia manukato ghali aina ya Clive yenye harufu nzuri ya kuhamasisha ngono.


Alipomaliza akajitazama tena katika kioo kikubwa na kutabasamu, kwa kweli usiku ule alipendeza mno kuliko kawaida na uzuri wake uliongezeka mara dufu. Kisha akakumbuka kuchukua mkufu wake mwembamba wa dhahabu safi uliokuwa na kidani cha madini ya tanzanite, na kuuvaa.


Ule mkufu ulionekana kuizunguka vyema shingo yake nyembamba huku kile kidani kikipotelea katikati ya mfereji wa matiti yake mazuri.


“I’m so pretty. Thank you God for giving me this beauty…” (Mimi ni mrembo. Asante Mungu kwa kunipa uzuri huu…) aliwaza huku akijigeuza geuza kujitazama kwa makini.


Aliporidhika alichukua mkoba wake mzuri wa kike wa rangi nyekundu akautundika begani, kisha akatoka chumbani na kuelekea sebuleni, pale sebuleni alisimama na kumtazama Carlos kwa makini kisha alimpungia mkono na kuanza kuondoka.


“Mpaka asubuhi?” Carlos aliuliza kwa sauti yake nzito iliyokuwa imebeba wivu mkubwa.


Jacky aligeuza shingo yake kumtazama Carlos na kuachia tabasamu. “Ikibidi nitalala mpaka asubuhi, na kama kiroho kinakuuma niahirishe,” alisema huku akiangua kicheko hafifu.


“Aah, nenda…” Carlos alisema huku akijiinua kutoka pale kwenye sofa alipokuwa ameketi na kuanza kuelekea maliwatoni lakini akasita kidogo na kugeuka kumtazama Jacky. “Lakini isiwe kavukavu, sawa?” alisema huku akimkazia macho.


Jacky aliachia tabasamu na kufungua mkoba wake akatoa kondomu kadhaa na kumuonesha Carlos, kisha akazirudisha kwenye mkoba wake na kutoka huku akiangua kicheko hafifu.


Alipotoka alielekea moja kwa moja kwenye banda la magari na kuchagua gari aina ya Toyota Landcruiser GX V8 jeusi, akabonyeza rimoti maalumu iliyokuwa kwenye ufunguo wa gari, kitasa cha mlango wa lile gari kikafunguka.


Jacky aliufungua mlango wa lile gari na kufungua mkoba wake kisha akatoa simu yake ya mkononi aina ya Nexus 6P na kuurusha ule mkoba kwenye siti ya pili.


Aliingia kwenye gari na kuwasha injini ya lile gari kisha akabonyeza rimoti maalumu kwa ajili ya kufungua geti na mara lile geti likaanza kujifungua taratibu. Jacky akaliondoa lile gari na kugeuka kubonyeza tena rimoti na mara lile geti likajifunga tena. Akaingiza gia na kupotelea mtaani.


Katika muda ule wa usiku jiji la Dar es Salaam lilikuwa limetawaliwa na pilika pilika za aina yake za watu, pikipiki na magari yaliyoonekana kukatisha barabarani, hasa katika barabara kuu za jiji.


Jacky aliendesha gari lake kwa umakini lakini akiwa katika mwendo wa kasi huku akipishana na pikipiki na magari mengine na alipofika katika eneo la Barakuda aliifuata barabara iliyokuwa ikipitia eneo la Vingunguti na baadaye kwa Mnyamani.


Kwa kupita barabra ile ilimsaidia kukwepa foleni ndefu ya magari katika barabara ya Mandela, na hivyo baada ya dakika arobaini alikuwa amefika Buguruni Malapa.


Alifika katika hoteli ya La Promise wakati Yusuf akionekana kuchoka kusubiri, maana alikuwa anaitazama saa yake ya mkononi mara kwa mara na kutingisha kichwa huku akionekana kuishiwa uvumilivu.


Jacky alitafuta sehemu nzuri na kuliegesha gari lake kwenye eneo la maegesho ya magari katika ile hoteli ya La Promise, kisha aliteremka na kuingia ndani, akapandisha ngazi chapchap kuelekea ghorofa ya kwanza kwenye eneo la baa kwa mwendo wa madaha huku akitoa simu yake na kupiga zile namba za Yusuf huku akiangaza macho yake kutazama huku na kule.


Yusuf akiwa amekata tamaa aliona simu yake ikiita na kabla hajaipokea aliweza kumuona Jacky akiingia na kusimama huku akiendelea kuangaza macho yake huku na kule. Yusuf alisimama na kupunga mkono wake hewani kumwita. Jacky alimuona na kukata simu kisha akamfuata huku akiachia tabasamu.


Jacky alimkumbatia Yusuf kwa bashasha kwa namna ya kumsalimia, kisha aliketi kwenye kiti kitupu huku akimtazama kwa tabasamu kabambe.


“Pole sana, Yusuf, naona umesubiri muda mrefu, eh?” aliuliza Jacky huku akiitazama saa yake ya mkononi.


“Siyo sana. Hata hivyo jambo la muhimu ni kwamba umefika, sijui utakunywa nini?” alisema Yusuf huku akinyoosha mkono wake kumwita mhudumu wa ile baa kwa ishara.


“Hapana, twende mahali pengine pazuri zaidi ambako tutakunywa kwa raha na kuongea mambo yetu kwa nafasi zaidi,” Jacky alisema huku akiinuka kutoka kwenye kile kiti.


“Wapi?” Yusuf aliuliza huku akimtazama Jacky kwa mshangao akionekana kushtuka kidogo.


“Kuna sehemu nzuri sana nimeibuku mara tu baada ya kunipigia simu, hiyo sehemu ni maalumu kwa ajili yetu,” Jacky alisema huku akimshika Yusuf mkono wake kumuinua.


Yusuf aliinuka bila kupinga, akaanza kumfuata Jacky nyuma kama vile mbwa aliyemuona chatu.


“Umekuja na gari?” Jacky alimuuliza Yusuf mara tu walipofika chini.


“Hapana, nimekuja kwa miguu maana sikai mbali na hapa,” Yusuf alijibu lakini akasita baada ya kumuona Jacky akimfungulia mlango wa abiria wa gari la kifahari aina ya Toyota Landcruiser GX V8 jeusi. Akataka kuuliza lakini akasita na kuingia kimya kimya.




“Kuna sehemu nzuri sana nimeibuku mara tu baada ya kunipigia simu, hiyo sehemu ni maalumu kwa ajili yetu,” Jacky alisema huku akimshika Yusuf mkono wake kumuinua.

ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog