Simulizi : Jino Kwa Jino (2)
Sehemu Ya : Nne (4)
“Weka wewe yako pia lasivyo fyatua nami nifyatue sote tuisalimie akhera!” Inspekta Pena akaongea akimkazia macho anayemuona na kuamini ni mzungu wa kibrazil.
“Sote ni wanaume.. Tuweke chini silaha kwa pamoja kisha tuongee kistaarabu nini kilichonileta kwako usiku huu”
“Unafanya kosa kubwa sana, kosa ambalo utakuja kulijutia muda si mrefu.. Mimi ni afisa wa polisi wa ngazi za juu katika jiji hili.. Nakuomba mara ya mwisho weka silaha chini!”
“Nimesema kama wanaume tuweke wote chini..Kwanini niwe mnyonge kwako Ispekta kana kwamba nakuogopa sana au naogopa mavazi yako ya kipolisi uliyovaa… Nainama kuweka silaha chini nawe weka yako chini”
“Sawa! Fanya nami nifanye hivyo”
“Moja…. Mbili… Tatu!” ‘TSC’ alihesabu hivi macho yake yaliyo ndani ya miwani yenye kazi maalumu kuangalia macho ya Inspekta Penambucano akizitumia kope za mpinzani kusoma nia ipi iliyo ndani yake.
Wote wakaanza kuinama kwa pamoja hili waweke bastola zao chini wakitizamana kila mmoja akiamini katika uwezo alionao kuwa kitakachofuata ni kumdhibiti adui kwa asilimia mia moja.
Hatimaye wote wakaweka silaha (bastola) chini kisha taratibu wakaanza kuinuka mwili kwa pamoja wakiendelea kutizamana.
“Sukuma kwenye kona ya baraza kwa mguu wako ziwe mbali” Akaongea Kai kisha akausogeza mguu wake pembeni ya bastola yake tayari kuisukuma upande anaoulekeza.
Inspekta akawa wa kwanza kutekereza hili akaisukuma bastola upande husika ikifuatiwa kwa nyuma na bastola ya ‘TSC’ iliyosukumwa zikiserereka kwa kasi zikaenda jipiga ukutani lakini hakuna aliyejisumbua kutizama zimeenda kugonga vipi ukuta wa baraza bali kila mmoja alikuwa makini kumtizama aliye mbele yake hatua nne tu toka alipo.
Polisi mwenye cheo cha uinspekta akacheza karata yake kwa kupepesa kichwa chake mara mbili upande akijifanya anaangalia kitu kwa wizi (stahili kama ya mpiga penalti anayemzuga kipa wakati anajiandaa kupiga pigo lake la penalti), janja yake ni kama ilifanikiwa kumteka Agent Kai akageuza kichwa kuangalia upande husika aliozugwa (kosa la jinai).
Mkono wa kulia wa Inspekta Fred De Luis Penambucano ulizunguka kwa kasi nyuma ya kiuno chake na ukaibuka na bastola ndogo lakini pia haikuwa hali zubaifu kwa mwanadamu aliyepewa jina la nyayo za paka toka kwa mwalimu wake mmoja wa mafunzo ya kunyata kiustadi na weledi wa hali ya juu katika moja ya kambi za mafunzo huko Marekani, mkono kabla haujanyooka vizuri wakati unainuka kwa kasi, teke kisu (dochi la kubutua juu) lilifyatuka toka mahala aliposimama Agent Kai likifyatuka kwa kasi ya umeme nukta kumeta ukatandika mkono ulioshika bastola, shambulizi kali la ghafla lilifanya mkono ule kuachia bastola iliyoikamata na pia teke likiacha athari ya kupeleka maumivu katika eneo la kifundo cha kiganja na pia kumyumbisha Inspekta akarudishwa mpaka ukutani akijizuia kwa mkono mwingine ambao haukushambuliwa asipigize kisogo ukutani.
Uso ukakusanya makunjamano akang’ata meno kwa hasira na maumivu kisha akajisogea upande mkabala na mlango kisha akakunja ngumi bila kujali maumivu maana Kai alimsogelea baada ya shambulizi la teke kisu.
Wanaume hawa wote wakakaa mkao wa mapigano, ngumi ziliashiria wanataka wapigane mtindo huru usio na stahili maalumu, hapa ndipo Agent Kai upend asana kucheza napo akiamini anautunza ujuzi wake zaidi anapokuwa anapata fursa ya kupigana ngumi na mateke (kick boxer).
Pena akatisha anamsogelea mwamba aliye mbele yake ambaye naye alijifanya katishika akarudisha mguu wa kushoto nyuma, Pena akaja kasi na kutupa shambulizi la ‘mawashi teke’ ‘TSC’ aliliona lakini akaacha limpate hili amuaminishe jambo adui likatua kwenye paja, likatupwa teke lingine likilenga lishambulie hazina kuu ya ukoo wa ‘TSC’ hili hakuliacha litue akakutanisha magoti yake kasi teke dochi likakutana na kigingi cha mwamba, likafuatishwa gumi zito la mkono wa kushoto toka kwa Inspekta hapa likakuta hewa likitoa mvumo wa kutisha, kama kichwa nyoka swila ‘TSC’ aliinama konde likapita papo hapo akatoa ‘jebu’ (ngumi ya pembeni) ya mbavu changa za Inspekta zilizomstua akainuka kama kapigwa jeki akaona itakuwa noma haraka naye akarusha ngumi iliyokuta kigingi tena cha Kai kwa kupanguliwa mpanguo ambao ulimjuza Inspekta kuwa hapambani na mtu boya, aliyumba kwa mpanguo huu angekuwa hana balansi za miguu basi angepigiwa mlangoni.
Haraka akawaza hapa barazani ni padogo na kawekwa ukutani yeye na adui yake mvamizi wa nyumbani kwake, akajifanya kama anataka kumvamia Kai kwa nguvu kisha kwa wepesi wa hali ya juu aliruka akatua juu ya kiti kati ya viti vitatu vilivyo barazani ambapo napo akajifyatua na kutua uwanjani mwa eneo la mbele la nyumba hatua chache toka lilipo gari.
Kimoyo moyo Agent Kai akatabasamu akiwa kashageuka upande wa adui yake, yeye akashuka ngazi kawaida akitembea kwenda uwanjani.
Inspekta akakaa mkao wa mchanganyiko mkono wa kushoto uliotangulia mbele akiwa kauachia kiganja kidole gumba kikikunjwa kubana (karete) na huku mkono wa kulia ukiwa umekunjwa ngumi na kuwekwa kando ya kifua na miguu ikiwa katika stahili pia (patamu hapo).
Mwisho wa sehemu ya mia moja na nane (108)
Salvador imechangamka sasa!
Inspekta wa jeshi la polisi la Brazil kanda ya jimbo la Bahia katika mji mkuu wake amekutana na mtu ambaye kama angekuwa ameiona sura yake ya halisi labda angeweza kuhisi kitu kama alishawai kusikia habari zake hata kama hakuwa amewai kumuona lakini kupewa kwake taarifa kuwa kuna watu wanahisiwa kuwa wameingia ndani ya Brazil basi huyu mtu angemuhisi kuwa ni fundi flani asiye na masihara lakini hapa haikuwa hivyo kwani yeye aliamini mtu huyu ni mmoja wa wahalifu flani wa kibrazili waliovamia kwake pengine kwa kutumwa na mtu anayemlipa hili amuue yeye au amekuja kwa nia ya kutaka kumpora gari yake nzuri ya kifahari aliyoinunua hata wiki moja bado.
Mpambano utakuwaje?
Kwa majibu zaidi twende mbele kwa kufahamu kilichojiri
ILIPOISHIA SEHEMU YA 108…!!
Uso ukakusanya makunjamano akang’ata meno kwa hasira na maumivu kisha akajisogea upande mkabala na mlango kisha akakunja ngumi bila kujali maumivu maana Kai alimsogelea baada ya shambulizi la teke kisu.
Wanaume hawa wote wakakaa mkao wa mapigano, ngumi ziliashiria wanataka wapigane mtindo huru usio na stahili maalumu, hapa ndipo Agent Kai upend asana kucheza napo akiamini anautunza ujuzi wake zaidi anapokuwa anapata fursa ya kupigana ngumi na mateke (kick boxer).
Pena akatisha anamsogelea mwamba aliye mbele yake ambaye naye alijifanya katishika akarudisha mguu wa kushoto nyuma, Pena akaja kasi na kutupa shambulizi la ‘mawashi teke’ ‘TSC’ aliliona lakini akaacha limpate hili amuaminishe jambo adui likatua kwenye paja, likatupwa teke lingine likilenga lishambulie hazina kuu ya ukoo wa ‘TSC’ hili hakuliacha litue akakutanisha magoti yake kasi teke dochi likakutana na kigingi cha mwamba, likafuatishwa gumi zito la mkono wa kushoto toka kwa Inspekta hapa likakuta hewa likitoa mvumo wa kutisha, kama kichwa nyoka swila ‘TSC’ aliinama konde likapita papo hapo akatoa ‘jebu’ (ngumi ya pembeni) ya mbavu changa za Inspekta zilizomstua akainuka kama kapigwa jeki akaona itakuwa noma haraka naye akarusha ngumi iliyokuta kigingi tena cha Kai kwa kupanguliwa mpanguo ambao ulimjuza Inspekta kuwa hapambani na mtu boya, aliyumba kwa mpanguo huu angekuwa hana balansi za miguu basi angepigiwa mlangoni.
Haraka akawaza hapa barazani ni padogo na kawekwa ukutani yeye na adui yake mvamizi wa nyumbani kwake, akajifanya kama anataka kumvamia Kai kwa nguvu kisha kwa wepesi wa hali ya juu aliruka akatua juu ya kiti kati ya viti vitatu vilivyo barazani ambapo napo akajifyatua na kutua uwanjani mwa eneo la mbele la nyumba hatua chache toka lilipo gari.
Kimoyo moyo Agent Kai akatabasamu akiwa kashageuka upande wa adui yake, yeye akashuka ngazi kawaida akitembea kwenda uwanjani.
Inspekta akakaa mkao wa mchanganyiko mkono wa kushoto uliotangulia mbele akiwa kauachia kiganja kidole gumba kikikunjwa kubana (karete) na huku mkono wa kulia ukiwa umekunjwa ngumi na kuwekwa kando ya kifua na miguu ikiwa katika stahili pia (patamu hapo).
ENDELEA NA MAPIGO..!!
FUNGA KAZI IV
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
“Unataka nini kwangu?” Swali liliulizwa na Inspekta huku anajiweka sawa na kila anavyojiweka sawa anaona kama hajakaa vizuri wakati huo huo ‘TSC’ anakaa mkao wa mcheza kick boxer baada ya kuitoa miwani yake machoni mwake kisha kuiweka kwenye mfuko wa mbele ya koti la suti aliyovaa.
“Nakutaka wewe” Akajibu Kai.
“Kwa shida gani? mpaka unijie kinyemela”
“.. Khah! Kinyemela sababu usingenisikiliza na kukubali niku..!” Aliishia hapa kwani ilimbidi arudishe kichwa chake nyuma kwa kasi, teke dochi lilirushwa kisha kwa wepesi Inspekta akazungusha teke la kuzunguka (round kick) lililomkumba ‘TSC’ upande wake kulia akayumbishwa lakini hakuanguka bali alisogea kama chura aliyepigwa teke papo hapo naye akajizungusha teke la kuzunguka la chini (down round kick), inspekta akaruka juu kulikwepa teke la Kai likapita napo hakuruka tupu kwa wepesi akarusha ngumi iliyompata begani Kai mzee baba akayumba tena, mashambulizi ya kushtukiza na kasi yalimfanya nywele zake kusisimka.
Haraka Agent Kai akapiga hatua za kurudi nyuma mbili kujiondoa karibu na adui anayemshambulia kwa kasi akiamini kwenye kasi hiyo aliyomstukiza itamfanya kumzidi maarifa, Pena alipoona Kai anarudi nyuma akasogea kasi asimpe nafasi ya kujipanga.
Alimgundua mpinzani wake ana ujuzi lakini aliamini ujuzi wake si wa kumfikia yeye, Pena ni mtu anayejiamini sana pale anapokuwa katika mapambano ya kupimana ubavu wa ngumi, kimtizamo wake alivyomuangalia Agent Kai alimuona ni mzungu wa kibrazil mwenye sura soft yenye mashavu ya kuvutia warembo na si kuonyesha amewai kupigana ngumi na mtu mjuzi na mjanja kama yeye askari mzoefu aliyeingia katika kazi ya upolisi akitokea kwenye kuwa bingwa wa kick boxer jimbo la Bahia miaka iliyopita akiwa katoka kumaliza masomo yake ya sekondari.
Agent Kai kwa uzoefu wa kumsoma mtu alitambua Inspekta Pena anajiamini sana na hiki ndicho kitu alimpendea, alikuwa kashajua anadharaulika kwa jinsi alivyoshambuliwa kwa kasi, akakunja ngumi na kukaza mikono akikaa stahili ya kawaida kana kwamba anamuelekeza mpinzani sehemu za kumpiga adui, miguu ikiwa kasimama kawaida kabisa hili kumvutia adui na kweli mbinu hii ilimfanya adui kuamini anapigana na boya.
“Sogea mchumba.. Unavamia kwa Inspekta wa polisi.. Kama inaweza kutokea bahati mbaya ukakimbia hapa nafikiri utaenda kuuhadithia kwa aliyekutuma hapa kuwa si mahala salama kabisa ila naamini hautaweza kupata nafasi hiyo ya kuondoka hapa ukiwa salama..!” Akaongea Inspekta kisha akasogea kwa hatua mbili mbele karibu na TSC ambaye sasa alishaamua kuwa aweke umakini amfunze huyu Inspekta hivyo akurudi nyuma hata hatua moja.
Ngumi ya mkono wa kulia toka kwa Pena ikavuma na kukuta hewa kwa ‘TSC’ kuinama kwa kasi yake, Pena akutaka kuzubaa tena akarusha ngumi ingine ya mkono wa kulia hii ikabidi Agent Kai aipangue kwa nguvu hili kumyumbisha adui yake na kweli akayumba papo hapo akatumia fursa kumpiga futi goti la kende (pumbu) lililompata kijuujuu Pena kwani alijitahidi kurudi nyuma lakini maumivu aliyapata ikambidi kibinadamu apoteze umakini kidogo hapa ni mahala ambapo kwa Agent Kai uwa kama kapewa penati katika soka, akaunganisha kwa kufaytua ngumi akilenga chembe ya adui (eneo la chini ya kifua na juu ya tumbo), Pena akakinga kwa mkono lakini ilitereza na kupenya ikamstua tena ingawa si kwa makali kama ingetua bila kuguswa kwa minajili ya kuepeshwa uso wake ulisogea mbele karibu na kichwa cha Kai ukasikika mlio wa kama nazi zilizokomaa kugongana, kichwa cha Agent Kai eneo la juu ya paji la uso kilitua katikati ya mwamba wa pua ya kizungu ya Inspekta Pena kana kwamba Christiano Ronaldo ‘CR7’ anapiga kichwa kufunga goli la kusawazisha baada ya timu pinzani kutangulia bao moja maana kilikuwa kichwa cha nguvu kilichobeba uzito wa mrukio, msamba wa pua ya Inspekta wa polisi Penambucano ulivunjika kwa ndani na kwa nje ukapasuka damu ziliruka na kumkuta hadi mpiga kichwa usoni huku naye ngozi ya sura ya bandia aliyovaa iliondoka kwa kuchanika eneo lote lililotua kwenye pua ya mwenzake.
Maumivu makali yaliyoambatana na kuona nyota nyota kwenye macho yake vilimfanya Inspekta Pena kutaka kujishika eneo aliloathirika (kosa lingine) mkono wa kushoto, ambao ni mkono wa dhahabu wa Agent Kai ambao ana pete mbili anazovaa vidoleni moja ya ndoa yake na ingine ambayo niliwai ielezea katika riwaya ya mshangao kisa cha yeye kuwa anaivaa kama hujaisoma tafuta usome, ngumi nzito toka mkono huu wenye nguvu za ajabu ilitua katika eneo la pembeni la paji la uso la mheshimiwa inspekta Pena na pete moja iliyo kubwa isiyo ya ndoa ikatoa adhabu mpya kwake kwa kumchana pakubwa hapa hakuweza stahimili alikwenda chini kilazima tena kwa kasi kama gunia la mkaa lililokosa balansi akatoa mguno wa kuwa ameumia amekubali.
Mwamba wa kiafrika unaohudumu kazi zake Marekani ulisogea kwa kasi kisha kama anapiga shuti mpira kwa mguu wa kushoto aliachia teke dochi kwa nguvu zote za mguu huu ambao nao usapoti sana nguvu zake safari hii akilenga tumbo la Inspekta Pena ambaye hata kama anaona nyota nyota alitambua ubaya wa teke alilokuwa katupiwa akajigeuza lisimpate tumboni akiweka na mkono ikawa bahati mbaya mpya kwake mono ule wa kushoto haukuweza himili nguvu za mpiga teke ulivunjika huku ukitoa mlio wa kukatika kwa kuni kubwa iliyokauka hapa hakuguna tena Pena bali alipiga yowe kubwa tu, ni kama kichaa cha mbwa mwitu kwa Agent Kai hakutaka kuelewa kama anayegaragara chini kwenye nyasi ni binadamu alimtizama kama anaona kivuli cha mtu akaruka juu kwa miguu yote miwili kisha miguu ile yote miwili ikatua kwa nguvu kwa mikito katika mgongo wa Pena na kumvunja pingili kadhaa za uti wa mgongo mheshimiwa huyu ambapo sekunde hii aliona giza alitamani kupiga yowe lingine akashindwa giza likachukua hatamu machoni mwake akazirai.
Mlango mkuu wa nyumba ya Inspekta Pena ukafunguka kwa nguvu ukifunguliwa na mtu aliyekuwa ndani kwa kasi Agent Kai akaruka sarakasi moja ya mtupu mtupu kiupande iliyomfanya atue kibarazani kisha akaserereka kwa kasi hadi ilipo bastola yake kasi ambayo ilienda sambamba na mfungua mlango alipotokeza tayari yeye Agent Kai alikuwa anajigeuza kuelekea upande ule akiwa na bastola mkononi ila hakuwa ameiinua kuielekeza kwa mtoka ndani ndiyo anataka kuruhusu kilimi wakati huohuo anaiinua.
“Mume wanguu. Mume wangu uuu…!!” Kelele za mwanamke wa kizungu mwenye mwili tipwatipwa ilitangulia wakati mfungua mlango anajitokeza macho yake yakiwa yamechanganyikiwa kwa kuona maajabu ambayo hajawai kuyaona hata mara moja kwa mtu aliyekuwa akipigana na mumewe kuyeyuka wakati yeye anafungua mlango alimuona ndiyo anamrukia na kumkita mgongoni mume wake, aliacha kupiga kelele ghafla na kuacha kuwa anaangalia tu alipolala mumewe akageuza kichwa chake huku na huko kutafuta wapi alipo mtu aliyekuwa anamsulubu mumewe na yeye akishuhudia ngumi za wawili hawa kana kwamba kalipa kiingilio kuangalia ngumi ukumbi wa Bahia Arena, alishuhudia ngumi hizi kwa kutokea dirishani baada tu ya mumewe kuwa kafika na kupaki gari yeye alibaki akiendelea kumbembeleza mwanae alale lakini alistuka aliposikia sauti ya mumewe ikimuonya mtu kwa vitisho hivyo yeye akasogea na kufungua dirishani ndipo akawakuta wanaumea hawa wakiwa wamekinga ngumi tayari kupambana kwakuwa anamuamini mumewe alitulia ajionee sinema ya bure, sinema ya bure ilimtokea puani ndipo akakurupuka kuchukua funguo afungue mlango.
“Sitahitaji uendelee na kelele zako.. Mume wako mzima.. Amezirai tu hajafa..” Agent Kai akaongea kwa kireno chao watu hawa mkono alioshika bastola akiwa kauelekeza kwa mwanamama huyu tipwatipwa.
“Wewe ni nani? Kwanini umempiga mume wangu hivi?” Akauliza mwanamke huyu akitetemeka macho yake makubwa yakitisha kwa jinsi alivyoyazidisha kuyapanua kana kwamba yanataka kwenye fremu yake.
“Mimi ni askari wa upelelezi.. Mumeo ana jambo amenifanyia nilipotaka kumuuliza kabla sijauliza akataka kuniua nikamuwai kumpokonya bastola ndipo tukaanza kupigana kwa bahati mbaya imekuwa hivi kama hujuavyo hasira zilivyo mbaya …. Utanisamehe sana… Niko tayari tumuwaishe hospitali, tusaidiane kumuweka kwenye gari tumpeleke hospitali, humu ndani mwako kuna nani mwingine?” ‘TSC’ akajibu maswali aliyoulizwa kwa mtindo huu.
“Leo nilikuwa peke yangu… Mdogo na mume wangu ambaye uwa anakuwepo hapa mara kwa mara muda kama huu amesafiri kwenda Gremio”
“Sawa.. Sogea tumbebe mumeo kumuweka kwenye gari.. Funguo ya gari hiyo ipo karibu na uliposimama ilete tufungue milango ya gari”
Walimnyanyua Inspekta Pena akiwa hajitambui kazi iliyofanyika kwa ushirikiano wa wawili hawa huku mwanamama mwili tipwatipwa mke wa Inspekta Penambucano akitokwa machozi, walipomaliza kumuweka siti za nyuma za gari hii ya Mr. Pena, mwanamama akamuangalia Agent Kai ambaye walipotizamana tu mkono wake wa kulia kwa kasi ulifyatuka na kumtwanga karete nyepesi ya sehemu nyeti shingoni ambayo yeye fundi wa mapigo ya sehemu za mwili alitambua akipiga hivi basi anayempiga atakuwa katika hali gani, pale pale mwanamama bila kuinua hata mdomo aliotamani kuuinua alijikuta akidondokea juu ya mwili wa mumewe.
Kai akashuka toka ndani ya gari akafunga mlango wa gari, mkononi alikuwa na rimoti ya kufungua geti akalengesha getini kufungua geti kisha akaingia ndani ya gari akaiwasha na kuiondoa kasi kwa nje napo akasimama na kulifunga geti gari likaondoka akiliendesha kwa kasi ya kawaida akiwa anawaza wapi anaenda na watu hawa.
Akiwa anakaribia mzunguko wa makutano ya barabara ya BR-116 na BR-117 kama jinamizi fulani alipishana na gari ya polisi inaendea alipotoka yeye na wazirai wake walio siti za nyuma wakiwa dunia isiyojulikana na sisi wanadamu tunapozimia, hakubadili mwendo aliendelea kuendesha kawaida wakapishana hivyo akazunguka mzunguko huu akiondoka barabara ya BR-116 kisha akaingia BR-117 hapa akaongeza mwendo wa gari kisha akatoa simu yake toka mfuko wa suruali akaiwasha kwakuwa alikuwa ameizima wakati ananyapia nyapia kuingia kupitia ukutani katika eneo la nyumba ya Inspekta Penambucano.
Simu ilipokuwa na uzima tayari kufanya kazi (active) akatafuta namba za Special Agent Rebecca Smith anazotumia alipozipata akaruhusu kupiga, ikaita miito kama mitatu tu ikapokelewa.
“Halloo Reby!” Akaongea baada ya kupokelewa simu aliyopiga na upande wa pili.
“Boss! Nakupata nakupata..!” Rebecca akajibu kwa haraka huku akisogea mbali na kelele za spika za muziki zilizokuwa zikikita mshindo mkubwa muziki wa aina ya Carribien.
“Bado huko club?”Kelele za muziki zilimfanya aulize hivi Agent Kai huku umakini wa kushika usukani wa dreva na kuongea ukiongezeka maradufu maana alikuwa anasikia makelele zaidi kuliko sauti ya Rebecca.
“Ndiyo boss ila ndiyo nilikuwa natoka”
“Toka nje kisha nipigie nikuelekeze jambo la haraka” Agent Kai akaongea hivi kisha akakata simu na kuitupia katikati ya siti ya abiria iliyo kulia kwake.
Haikufika dakika moja mbele simu yake ikaanza kuita mlio mzuri wa moja ya muziki wa mwanamuziki wa kitanzania aliye kati ya wasanii wanayemvutia sana yeye Kai.
“..Yah! hapo sawa…. Sikia! Niko na wateja wawili muhimu kwenye njia, mmoja ambaye ni mume kazima kwa kichapo na mwingine ambaye ni mke kazima sababu ya kumfumba mdomo, wote ni muhimu kwakuwa wanabebana mke na mume hawa, sijui nawapeleka wapi? Hivyo naomba uchukue taxi tukutane barabara kuu ya BR-101 Transcoastal Highway kwenye makutano ya mzunguko wa Feira De Santana, tutaenda kuwahoji nje ya jiji, wai kufanya hivyo wakati tunaongea uwe unaita taxi! Usisahau kununua maji ya baridi chupa kadhaa hapo club” Maelekezo ya kasi ya kuongea yalitoka kwa Agent Kai.
Anapotokea Agent Kai ni umbali wa kilometa kadhaa kufika barabara kuu ya BR-101 Transcoastal wenyewe wabrazil wanaotumia lugha ya kireno uwa wanaita BR-101 Translitoranea pia inaitwa ‘Rodovia Governador Mario Covas’ (Rodovia ni kireno kwa kiingereza ni Highway) hii ni barabara kubwa kabisa kuliko barabara zote zilizo jiji la Salvador na jimbo la Bahia na nchi ya Brazil kwa ujumla ikiwa imeunganisha miji mikubwa 12 ya majimbo 12, imekatiza kutoka kaskazini mwa nchi jimbo la Rio Grande Do Norte mpaka kusini mwa nchi jimbo la Rio Grande Do Sul na miji mingine ya majimbo yaliyo katikati ya majimbo haya ya kaskazini na kusini.
Rebecca Smith alikuwa wa kwanza kufika kwenye makutano ya mzunguko wa Feira De Santana, akamuomba dreva wa taxi amuache hapo akamlipa na kushuka toka ndani ya gari, alichepuka upande wa pili akajisogeza karibu na alama ya pundamilia kusubiri ujio wa Agent Kai na hao aliowaita wateja.
Muda huu wa saa tano na nusu usiku barabara hii kulikuwa na magari makubwa ya mizigo ndiyo yanapita zaidi hivyo makelele ya miungurumo ya magari ilikuwa kubwa masikioni mwa watu waliokuwa wanapita maeneo haya.
Dakika tatu toka akanyage alama za kuvuka barabarani alistuka gari mpya ya kisasa aina ya Volkswagen Atlas toleo jipya, ilichepuka toka katika barabara ikiacha gari lililo mbele yake na nyuma yake yaendelee na safari zao lakini hii Volkswagen Atlas ilienda ikasimama hatua chache mbele ya Rebecca Smith hapo Kai akashusha kioo.
“Twende zetu” Akaongea sauti ya kupaza Agent Kai, Rebecca akazunguka kwa haraka upande wa pili akaingia ndani ya gari. Bahati nzuri kwake ikatiwa gea mara moja na kuondoshwa.
“Eeeeh! Kweli wateja.. Umewatoa wapi? Ni kina nani?” Akauliza Rebecca baada ya kutulia kitini ksiha akageuza kichwa kuangalia upande wa pili na kuwaona mume na mke.
Agent Kai ‘TSC’ huku anaendesha gari kwa mwendo fanana na magari yanayopita muda huu ambayo yalikuwa si mengi sana kiuhalisia, alichukua fursa hii kumuhadithia kila kitu Rebecca wake mpaka walipokaribia makutano ya mzunguko wa barabara kuu hii ya BR-101 na barabara ya BR-415 uliopo eneo la Itabuna ambako walijikuta hawajaongozana sana magari mengine wameachiana nafasi wao wakafuata barabara ya vumbi iliyokuwa inachepuka kuingia ambako kwa pembeni ya barabara hii ya vumbi kulikuwa na makaravati yanayotengenezwa ikiashiria hapa ni kituo cha kutengeneza makaravati haya kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii ya vumbi huko inakoelekea au kwingineko wao hawajui zaidi na hata mimi sijui zaidi, gari ilipelekwa huko na kuingia mita mia moja na zaidi kidogo pande zote kukiwa na miti miti na vichaka vya pembezoni mwa barabara giza nalo lilikuwa si haba kwakuwa kulikuwa hakuna nyumba zilizopo eneo hili, hapa ‘TSC’ akasimamisha gari na wote wawili wakashuka toka siti za mbele wakafungua milango ya siti za nyuma ya siti za dreva.
“Huyu mwanaume amevunjika mgongo na mambo mengine lakini ni muhimu kwa mahojiano yetu hivyo hatuna budi zaidi ya kumzindua ni afisa wa polisi ndiyo maana unamuona kavaa sare za jeshi la polisi la Brazil” Agent Kai akaongea huku anamfungua vifungo vya shati ya sare za polisi Inspekta Penambucano.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na tisa (109)
Inspekta wa jeshi la polisi amekutana na kisago cha kutoka kwa mtu ambaye awapo kwenye mapambano akili zake uwa anazijua yeye mwenyewe maana uwa ni akili za yeye awe mzima ila adui yake ateseke kwa maumivu bila kujali anampimia vipi icho kipimo cha maumivu.
Mambo ni mengi tumeyasoma, twende mbele!
Dakika tatu toka akanyage alama za kuvuka barabarani alistuka gari mpya ya kisasa aina ya Volkswagen Atlas toleo jipya, ilichepuka toka katika barabara ikiacha gari lililo mbele yake na nyuma yake yaendelee na safari zao lakini hii Volkswagen Atlas ilienda ikasimama hatua chache mbele ya Rebecca Smith hapo Kai akashusha kioo.
“Twende zetu” Akaongea sauti ya kupaza Agent Kai, Rebecca akazunguka kwa haraka upande wa pili akaingia ndani ya gari. Bahati nzuri kwake ikatiwa gea mara moja na kuondoshwa.
“Eeeeh! Kweli wateja.. Umewatoa wapi? Ni kina nani?” Akauliza Rebecca baada ya kutulia kitini ksiha akageuza kichwa kuangalia upande wa pili na kuwaona mume na mke.
Agent Kai ‘TSC’ huku anaendesha gari kwa mwendo fanana na magari yanayopita muda huu ambayo yalikuwa si mengi sana kiuhalisia, alichukua fursa hii kumuhadithia kila kitu Rebecca wake mpaka walipokaribia makutano ya mzunguko wa barabara kuu hii ya BR-101 na barabara ya BR-415 uliopo eneo la Itabuna ambako walijikuta hawajaongozana sana magari mengine wameachiana nafasi wao wakafuata barabara ya vumbi iliyokuwa inachepuka kuingia ambako kwa pembeni ya barabara hii ya vumbi kulikuwa na makaravati yanayotengenezwa ikiashiria hapa ni kituo cha kutengeneza makaravati haya kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii ya vumbi huko inakoelekea au kwingineko wao hawajui zaidi na hata mimi sijui zaidi, gari ilipelekwa huko na kuingia mita mia moja na zaidi kidogo pande zote kukiwa na miti miti na vichaka vya pembezoni mwa barabara giza nalo lilikuwa si haba kwakuwa kulikuwa hakuna nyumba zilizopo eneo hili, hapa ‘TSC’ akasimamisha gari na wote wawili wakashuka toka siti za mbele wakafungua milango ya siti za nyuma ya siti za dreva.
“Huyu mwanaume amevunjika mgongo na mambo mengine lakini ni muhimu kwa mahojiano yetu hivyo hatuna budi zaidi ya kumzindua ni afisa wa polisi ndiyo maana unamuona kavaa sare za jeshi la polisi la Brazil” Agent Kai akaongea huku anamfungua vifungo vya shati ya sare za polisi Inspekta Penambucano.
ENDELEA NA NONDO..!!
FUNGA KAZI V
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
Alipomaliza kumfungua vifungo vya shati alimkagua maeneo ambayo alikuwa anajua ndiyo ana maumivu ukaguzi wa kutafuta jambo fulani ulipotimia akachukua mfuko wa nailoni (Rambo) aliokuwa kaingia nao kwenye gari S.A Rebecca humo akatoa chupa moja ya maji ya baridi akafungua mfuniko kisha akammwagia kidogo tumboni maji yale Inspekta Fred De Luis Penambucano ambapo akastuka kwa kuutingisha mwili wake, Kai akamuongezea kwa kummwagia kichwani sasa hapa macho yakafunguka akayatoa kama anataka kuyaondoa kwenye fremu yake yasogee mbele.
Maumivu makali aliyoyasikia alipotaka kukiinua kiwiliwili chake yalimfanya akunje uso kama kalamba krolokwini.
“Usistuke kwa nguvu hivyo utazidi kujiumiza mheshimiwa..!” Agent Kai akamwambia macho ya mkurupuka toka kwenye zirai yalipokutana na yake ana kwa ana, Pena akanyanyua mkono wake na kufikicha macho yake kisha akafumbua macho yake tena kuhakiki anachokiona kwenye sura ya aliyemuinamia akimtizama.
Hapa Agent Kai alikuwa ameivua sura ya bandia aliyovaa sababu ilishamchosha sana kukaa juu ya sura yake na ilivyo yeye si mpenzi wa kuwa na sura ya bandia katika sura yake kwa muda mrefu uwa inampa karaha sana.
“..Hiii shiiii khaa haaaa…Na.. Naan ni nyi eee?” Kwa tabu akitumia kireno chao aliuliza baada ya kuugumia maumivu sura akiikunja kana kwamba anakatiza kwenye vumbi kubwa kwenda kusiko na vumbi.
“Pindua kichwa chako uangalie kulia kwako” Kai hakumjibu wao ni kina nani bali alimuelekeza jambo kwa maneno na vitendo kuwa Pena aangalie upande anaoelekezwa.
“Mm.. mke, mke wangu kwani..Kwa ni nini yu..Shiiii khaaah..Kwa kwani kwanin yuko hapa?” Akauliza kwa tabu Inspekta Pena baada ya kumuona mke wake akiwa amelala kwa kuegemezwa kwenye kiti cha gari huku shingo yake ikilalia upande wa bega.
“Yuko hapa kwa sababu wewe huko hapa Inspekta..!” Akajibu Agent Kai huku anafunga mfuniko chupa ya maji.
“Khaaah! Tafadha..Tafadhali nisaidieni kuniki.. Kunikimbizaa hospital.. Ni nina mau..mivu makalii saaana!” Alilalamika Inspekta wa polisi uso ukiwa umekunjwa kupitiliza (hapana chezea maumivu).
“Sawa.. Tutakupeleka hospitali muda si mrefu, vumilia kidogo Inspekta kuna jambo unalijua tunataka utusaidie haraka.. Ukisumbua kutujibu au kukataa kabisa kutujibu tunavyotaka basi tutatafuta mahala ambapo hawezi fika mtu mwingine kirahisi tutakuacha hapo ufe taratibu kwa maumivu makali unayoyasikia..!” Agent Kai akaongea tena akiwa kamsogelea karibu wanaangaliana bila kupepesa ingawa macho yake alikuwa kayaweka katika hali ya kumfanya anayemuangalia aogope ya Inspekta yalikuwa ya kuogopa na kuhitaji kuonewa huruma.
“Mke wangu.. Sama, samahani nataka.. Nataka kujua amefanyaje?” Inspekta akauliza tena baada ya kutizama tena pembeni yake alipo mkewe.
“Mkeo mzima… Sikia Inspekta! Unachelewa kwenda hospitali kwa maswali yako mengi mengi yasiyo na msingi hii unatuonyesha haujali uzima wako kabisa... Jioni ya siku iliyoisha uliwasiliana kupitia ‘facebook messenger’ na mtangazaji wa Redio Periodical FM iliyopo Chilpancingo mji mkuu wa jimbo la Guerrero, kuna taarifa alikuwa anakupatia kwa njia hiyo ya meseji ni ujumbe gani aliokupatia?” Agent Kai alimtoa kwenye hitaji lake la kutaka kujua mke wake ana hali gani? Akampachika swali murua ambalo uso wa muulizwa swali uliokuwa umeweka tege kufuata kichwa kilivyoweka ulirudishwa sawa na kumuangalia Agent Kai macho yakiwa yamefunuliwa kope zake uzuri sasa maana mshtuko uliofichwa ulijionyesha machoni mwa majasusi hawa wanaomtizama kwa umakini ingawa kama ingekuwa mtu asiye mzoefu asingeuona mshtuko husika.
“Unase.. Sielewi mkuu?” Akauliza akibabaika akitamani huu muda awe kwenye ndoto maana swali aliloulizwa likitanguliwa na ufafanuzi aliofafanuliwa wa mawasiliano aliyofanya ulimfanya ajihisi yuko katikati ya uwanja wa mpira wa miguu akiwa uchi huku watu (watazamaji) wamejaa majukwaani.
“Ina maana hujasikia Inspekta.. Au unatuektia msanii?” Rebecca akajikuta anaongea kwa ukali baada ya kuangalia saa yake ya mkononi iliyomuonyesha ni saa sita na dakika ishirini siku mpya ya jumanne ikiwa imeanza, hakuwa anajua haswa ni nini kinaendelea kwakuwa Agent Kai hakuwa amemfafanulia kiurefu zaidi yaliyotokea mpaka kumuita afike kutokea club alipokuwa na hata alipohoji aliambiwa avute subira atajua muda si mrefu nini kimejiri.
“Labda nirudie tena ndugu Inspekta Fred De Luis Penambucano a.k.a Laza Blocks.. Siku iliyoisha muda wa jioni ukitumia akaunti yako ya facebook inayotumia jina lako la bandia la Laza Blocks ulifanya mawasiliano na mwanadada mtangazaji aliyekupa taarifa fulani za siri mlitumia facebook messenger.. Taarifa alizokupa tayari mimi nazijua na sitaki tena uniambie chochote maana tutacheleweshana tu hapa… Tafadhali usitake nikuongezee maumivu mapya kwenye mwili wako au kuzidisha majeraha juu ya majeraha uliyonayo.. Naomba kuwa muungwana maana askari polisi wote ni waungwana sana hata kama wapo wanaojihusisha na mambo ya kijinga lakini si wabishi inapofika wakati wa kuongea ukweli utakaosaidia upelelezi juu ya jambo fulani ambalo si la kiserikali bali la wahalifu wanaomlipa.. Naomba tufahamishe yuko wapi Madam Millian Codrado?” Kwa kirefu ‘TSC’ akaongea akimkazia macho muhusika huku paji lake la uso likikusanya ndita chache za kishikaji.
“Si.. Sijuii… Sijui unaong.. unaongeeleea ni ni?” Akajibu akiwa kafumba macho kusikilizia maumivu aliyonayo ambayo ni kama kunapwita mgongoni na mbavuni jinsi alivyokuwa akijiskia hata kuhema kulikuwa kwa tabu sana.
“Unamaanisha? Unamaanisha hujui nachokiongelea? Kwahiyo mimi ni kichaa?” Kai akauliza huku anakunja ngumi taratibu hasira zake zikiwa zinajikusanya taratibu kwa jibu atakalopewa basi afanye jambo.
“..Sijui.. Simjui huyo huyo uuuwi shiiii.. Mtangazaji mnayesema na waa..!” Hakuachwa aendelee kumaliza alichohitaji ‘TSC’ kama mnyama alimpiga ngumi kama anakita chini ikatua kwenye mbavu zilizovunjika za Inspekta Pena ambaye alitoa yowe kali la maumivu lakini ‘TSC’ alichofanya alikunjua ngumi pale pale kisha akamkamata maeneo ya mbavu akaanza kumminya kwa nguvu huku anakandamiza.
“Ongea mbwa weee.. Nitakuua mbwa weeeeh! Usinichezee mbwa weee mi siyo mtu wa mchezo mchezo mimi ni nusu mnyama mtoa roho nisiye na huruma kazini… Nasema ongea kabla sijakuacha wewe nikampeleka jehanamu mkeo asiye na makosa kwa upumbavu wako!” Kai aling’aka alikuwa kama anabweka kwa hasira maneno ya kuongea haraka kwa nguvu akifoka yalimtoka tayari alikuwa na hasira kali ambapo akiwa hivi kutoa roho ni sekunde tu.
“..Ooooh! naku nakufa nakufa! Pumzi inakata mnanionea buree.. Si wajui unao unaose maaa!” Kwa tabu akajibu tena baada ya kuona anapiga kelele haachiliwi kubinywa mbavu zake na mkono unaojua wapi unaminya na unaminyaje.
Agent Kai alimuangalia Special Agent Rebecca, wakaangaliana macho yao yakaongea jambo, Rebecca akakamata kichwa cha mke wa Inspekta Pena kwa viganja vyake akibana huku na huku tayari kuzungusha amvunje shingo.
“Nahesabu mpaka tano.. Ikifika tano vunja shingo hiyo afie mbele mkewe kwanza kisha mimi nitavunja shingo yake mbwa huyu sitakuwa na cha kutaka kujua kuhusu yeye na hao anaowaficha.. Askari polisi anayeficha wahalifu kwa ubishi hatakiwi kuishi duniani makazi yake ni jehanamu…. Umenisikia wee mpuuzi” Akaongea Agent Kai aliposimama naye mikono yake ikakamata kichwa cha Inspekta Pena kama alivyokamata Rebecca cha mkewe lakini bado Inspekta alitaka kuendeleza msimamo ila moyo wake ukafikiria jinsi mkewe alivyo hana kosa akataka kuona jambo kwanza.
“Tayari Reby.. Moja!... Mbili…. Tatu… Nn..!” Aliishia hapa baada ya Pena kujitingisha kichwa kisha kuinua mdomo.
“Usimuueeee… Msituueee jamani… Naongea…Naongea mkuu..!” Aliongea akihema kwa nguvu kana kwamba hana maumivu aliyokuwa nayo katika mwili wake na usoni alikopasuka pua kwa nje na kuvunjika mwamba wake kwa ndani.
“Reby! Muachie.. Haya eleza haraka yuko wapi Madam Millian Codrado?! Mke wa Feca” Akatoa amri Kai kwa Rebecca amuachie mwanamke mke wa Inspekta Pena kisha akaomba Pena aeleze naye akimuachia kichwa chake.
“.. Madam Millian Fernandes Codrado…. Ni kweli, ni kweli… yu, yupoo hapa Salvador kwa ajili ya bia.. Biasha raa za ke, mimi, mimi, mimi ni m mtu ambaye hiiii shiiii, maumivu yana maumivu yanani..!” Inspekta Pena alianza kueleza wanachotaka kujua Kai na Rebecca wake lakini maumivu yaliongezeka ukali akshindwa endelea kuongea, ujasiri wa askari shupavu ulimuisha machozi yakaanza mporomoka kama maji yanayofuata mkondo baada ya boss wa kipolisi kuibiwa.
“Jitahidi Pena.. Jitahidi kutujibu haraka, nakuahidi kukukimbiza hospitali haraka iwezekanavyo.. Anapatikana wapi Madam Millian?” Kai akasogeza mdomo wake kwenye sikio la Inspekata Pena ambaye alianza shindwa vumilia maumivu ya mgongo uliovunjwa pamoja na mbavu mbili za upande wa kulia kwake ambazo zimevunjwa kikatili na Agent Kai, alipomaliza kumwambia akaweka kichwa upande kuweza kusikia Pena anachotamka.
“… Block.. Block.. Blooock namba.. Block namba 7thBA… M..Mta.. M taa wa Lelia Dourad..!” Kwa tabu alijitahidi kuongea ikiwa kwa sauti ndogo sana mabayo aliisikia Kai peke yake kwakuwa alikuwa amesogeza sikio karibu kabisa na mdomo wa Inspekta Fred De Luis Penambucano, maumivu yalimkata akashindwa malizia akajikuta giza linaishinda nuru katika mboni ya macho yake Israel mtoa roho hakuwa karibu lakini Pena alienda kunakopatikana nusu ya kukutana na Israel (alizimia).
Haraka hili asisahau Agent Kai akatoa simu yake na kuandika alichoweza kukisikia kwa mbali sana toka kwa Pena.
“Amezimia tena..!” Akaongea Agent Kai macho yake yalipogongana na macho ya S.A Rebecca.
“Lakini umeweza msikia nafikiri..”
“Ndiyo nimesikia ingawa kwa mbali naamini nimemsikia vizuri katika tunalohitaji toka kwake”
“Vizuri boss”
“Hii gari ni ya kwao.. Huyu mwanamke hana makosa kabisa”
“Eeeeh! Lakini huyu naye katusaidia ingawa hatujui kwa kiasi gani? Hatuna budi kutoa msaada wa kumfikisha huyu mwanaume hospitali”
“Sawa.. Ila kwa msaada wa haraka mwanaume tukamtupe karibu na hospitali na huyu mwanamke toka namchukua na mashaka naye kuwa ananyonyesha ananuka shombo ya maziwa ya mtoto hivyo yeye tutampeleka kwao akizinduka atajikuta yuko kwao” Majasusi hawa walijadili kisha wote wakashuka toka siti za nyuma kila mmoja na upande wake wakaenda siti za mbele, gari ikawashwa na kuondoka.
Karibu na geti la hospitali ya Ana Nery iliyopo mtaa Tribuna Da Bahia kuna nguzo kubwa za zege ambazo zimeshikana na ukuta mfupi uliojengwa kwa mawe huku juu yake ukipangwa vyuma nondo kufanya uzio uliozunguka hospitali hii kuwa na urefu wa mita kadhaa kwenda juu, usiku huu wa saa saba kasoro dakika kumi usiku kulikuwa hakuna anayepita pita kama inavyokuwa mchana na hata magari yanayopita hayakuwa yakipita kwa mfululizo ilikuwa ni kuachana kwa muda fulani ndipo linatokea lingine, Agent Kai akiwa anaendesha gari aliendesha mwendo mdogo sana wakati wanakaribia geti la hospitali kisha mlango wa siti za abiria nyuma ya siti za cabin (mbele) ulifunguka na Inspekta Pena akasukumwa nje kwa nguvu akadondoka kwa kishindo papo hapo dreva Agent Kai akaongeza spidi zaidi kukimbiza gari kwakuwa tayari walishahisi walinzi wa getini watasikia kishindo na misuguo ya kulalamika kwa tairi za gari wakati gari inaongezwa spidi matairi yalilalamika.
“Hakumalizia kauli yake lakini naamini hatutapata tabu kujua zaidi juu ya alichonieleza kwa tabu.. Tunaenda liacha gari hili kwenye geti la nyumba huyu mwanamke akiamka atajikuta pale itakuwa tumewapa msaada tosha sisi tutatafuta taxi” Agent Kai akaongea baada ya Rebecca kuruka kutoka siti za nyuma kuja za mbele.
“Tukishafanya hivyo ratiba inaendelea kwa msako?” Rebecca akauliza.
‘Hapana tunaenda kulala kisha asubuhi tukikutana tutaendelea na tulipoishia”
“Kwanini boss? Kwanini tusiendelee kabisa tukamaliza kabla hakujakucha au umechoka?”
“Inawezekana lakini itabidi tupate mtu tumuulize vizuri hiyo nyumba ilipo”
“Kama umechoka boss nipe maelekezo niende au tunaweza tukaenda ukanisubiri nje mi nikaifanya kazi vizuri tu”
“Basi sawa.. Kama ni hivyo tutamuingiza ndani huyu mwanamke kisha tukaondoka na gari lao maana hofu yangu ilikuwa kwenye usafiri tu wa kutufikisha huko aliposema Inspekta”
“Yah! Mchuzi wa mbwa unywewa wa moto acha tumalize hatua hizi pengine tunaweza jikuta tumemaliza kazi kirahisi usiku wa kwanza ndani ya Salvador” Akaongea Rebecca wakaangaliana na Kai wakajikuta kila mmoja anaachia tabasamu pana.
“Ndiyo maana napenda kufanya kazi na wewe..” Kai akajikuta anaongea huku anatabasamu.
“Hata mimi… Wewe kazi ngumu uwa ni nyepesi kwako na ndicho kinachonifanya niamini hakuna kama wewe pande zote za dunia hii”
“Usinipake mafuta kwa mgongo wa chupa.. Hahahaha hahahaha! Sitaki mimi..!!!!” Kai akaongea wote wakacheka gari ikazungushwa mzunguko wa barabara ya kwenda bandarini kisha ikakamatwa barabara ya kuelekea stendi kuu ya mabasi Iguatemi.
Walienda kumuacha mke wa Inspekta Penambucano nyumbani kwao mtaa wa Lafayette Velos 7th Street uliopo eneo la Pelourihno kisha wao wakaondoka na gari, ikiwa linaendelea kutumika bila idhini ya mwenye gari.
“Inspekta Pena alieleza kwa tabu kuwa Madam Millian yupo kwenye nyumba namba 7thBA ila mtaa aliosema hakuumalizia vizuri hivyo twende kituo cha madreva taxi karibu na stendi tukamuulize dereva wa taxi yoyote juu ya kirefu cha Lelia Dourad..!!” Agent Kai ‘TSC’ akamueleza S.A Rebecca.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi (110)
Mambo yanazidi kunoga!
Agent Kai na swahiba wake mkubwa katika kazi mwanadada Rebecca Smith usiku wa kwanza kufika ndani ya jiji kuu la Salvador jimboni Bahia nchini Brazil wanakutana na kinachoitwa hakuna kupumzika kazi imeanza.
Nini kitafuata? Nini hitimisho la yote haya?
ILIPOISHIA SEHEMU YA 110…!!
“Tukishafanya hivyo ratiba inaendelea kwa msako?” Rebecca akauliza.
‘Hapana tunaenda kulala kisha asubuhi tukikutana tutaendelea na tulipoishia”
“Kwanini boss? Kwanini tusiendelee kabisa tukamaliza kabla hakujakucha au umechoka?”
“Inawezekana lakini itabidi tupate mtu tumuulize vizuri hiyo nyumba ilipo”
“Kama umechoka boss nipe maelekezo niende au tunaweza tukaenda ukanisubiri nje mi nikaifanya kazi vizuri tu”
“Basi sawa.. Kama ni hivyo tutamuingiza ndani huyu mwanamke kisha tukaondoka na gari lao maana hofu yangu ilikuwa kwenye usafiri tu wa kutufikisha huko aliposema Inspekta”
“Yah! Mchuzi wa mbwa unywewa wa moto acha tumalize hatua hizi pengine tunaweza jikuta tumemaliza kazi kirahisi usiku wa kwanza ndani ya Salvador” Akaongea Rebecca wakaangaliana na Kai wakajikuta kila mmoja anaachia tabasamu pana.
“Ndiyo maana napenda kufanya kazi na wewe..” Kai akajikuta anaongea huku anatabasamu.
“Hata mimi… Wewe kazi ngumu uwa ni nyepesi kwako na ndicho kinachonifanya niamini hakuna kama wewe pande zote za dunia hii”
“Usinipake mafuta kwa mgongo wa chupa.. Hahahaha hahahaha! Sitaki mimi..!!!!” Kai akaongea wote wakacheka gari ikazungushwa mzunguko wa barabara ya kwenda bandarini kisha ikakamatwa barabara ya kuelekea stendi kuu ya mabasi Iguatemi.
Walienda walimuacha mke wa Inspekta Penambucano nyumbani kwao mtaa wa Lafayette Velos 7th Street uliopo eneo la Pelourihno kisha wao wakaondoka na gari, ikiwa linaendelea kutumika bila idhini ya mwenye gari.
“Inspekta Pena alieleza kwa tabu kuwa Madam Millian yupo kwenye nyumba namba 7thBA ila mtaa aliosema hakuumalizia vizuri hivyo twende kituo cha madreva taxi karibu na stendi tukamuulize dereva wa taxi yoyote juu ya kirefu cha Lelia Dourad..!!” Agent Kai ‘TSC’ akamueleza S.A Rebecca.
ENDELEA NA PIGO NONDO..!!!
FUNGA KAZI VI
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
“.. Simu yangu inaweza kutusaidia bila kwenda huko kwa madreva wa taxi, hili ni jiji haliwezi kuwa kama majiji ya huko kwenu Afrika Boss wangu” Rebecca alimchekesha boss wake na kiongozi wake wa kikazi, wote walicheka kwa sauti kinachoitwa kicheko laini si kikavu maana hadi machozi yalimtoka Kai wakati anajicheka kutaka kufuata njia ndefu wakati njia fupi ipo.
“Hahahah! Hahaha! Unapokuwepo wewe najiona kama nipo na Lizy.. nashukuru nimejenga ukaribu nawe mpaka umeshanizoea sana na kuzoeana ufanya kazi ifanyike kwa raha baina yetu, haya fanya unachotaka mpendwa wangu”
“Je? Hufurahi mimi nilivyokuzoea, kuliko kipindi kile tulipokutana kwa mara ya kwanza Malaysia”
“Nafurahi sana na nimeeleza hilo au sijaeleweka mpendwa?”
“Nimekuelewa boss wangu..Sijiombei mabaya ila kama itakuwa nimepangiwa kufa nikiwa kikazi basi naamini nitafia mikononi mwako na waliothubutu kuniua hawataendelea kuvuta pumzi wote utawapeleka jehanamu”
“Ajali kazini wanasema wahenga lakini naamini si mimi wala wewe aliyepangiwa kufa kabla ya kufika wakati wetu wa kustaafu… Khaaah! Kufa hatufi ila chamoto tutakiona si tumezoea kutesa wengine nasi mateso tukisogezewa hili kupimwa imani zetu tusilaani na kumkufuru Mungu”
“Tayari nishaipata ramani ya mitaa ya jiji la Salvador na hata picha ya satelaiti ipo hapa..!”
“Mtaa unaoitwa Lelia Dourad, tizama..!”Agent Kai aliongea huku anapunguza mwendo wa gari wakiwa katika barabara ya BR-099, barabara hii ya njia mbili zilizotenganishwa katikati na minazi, barabara ambayo kwa wao wanavyoelekea ilikuwa ikiwapeleka beach inayosemekana kuwa ni beach ya maajabu kwa jinsi ilivyo beach ya kuvutia inayovutia watalii kufika jimbo la Bahia kutalii kwa wingi kutoka nchi mbalimbali, ukiipita hii beach kuna eneo ambalo ni feri likiitwa ‘fishing village’ huku eneo hili lote la mitaa hii na barabara hii likiitwa ‘Praia Do Forte’.
“Hatuko mbali na huo mtaa na hili eneo, kumbe hili eneo linaitwa Praia Do Forte mita mia tatu toka hapa kuna fukwe ya bahari ya beach ya maajabu na mita mia tatu toka hapo kuna soko la samaki linaloitwa fishing village.. Mtaa aliosema Inspekta ambako kuna hiyo nyumba namba namba 7thBA ni mitaa ambayo katika satelaiti kunaonekana wanaishi watu vibopa kwa jinsi nilivyo mzoefu wa mikato ya viwanja vikubwa kama hivi unielekeza hivyo, mtaa unaitwa Lelia Dourados unapatikana eneo la Ondina ila kwa ilivyo inabidi usimame tuitafute barabara hii ya BR-114 kwa kutokea hapa BR-099, tukishapita kanisa kuu la katoliki la Palacio Arquiepiscopal Da Se lililopo eneo la Praca Da Se ndipo tutaipata hii barabara” Maelekezo marefu yalitolewa na S.A Rebecca punde google ilipomletea ramani mitaa na satelaiti ya mitaa ya jiji la Salvador katika simu yake aina ya Samsung A10, moja ya toleo bora kati ya matoleo kadhaa ya simu za aina ya Samsung.
“Sawa.. Utakuwa unanisomea ramani” Agent Kai alisimamisha gari sehemu inayoruhusu kupindua na kuingia njia ya upande wa pili, akapindua gari safari ya kuitafuta kwanza Praca Da Se ikaanza.
Iliwachukua dakika ishirini na tano kufika eneo la Ondina kwa mwendo wa kasi usiku huu kukiwa hamna magari mengi barabarani na gari hii kuwa inakimbizwa kwa spidi, hatimaye sasa gari ikapunguzwa mwendo wakaanza kuutafuta mtaa wa Lelia Dorados kwa kusoma vibao kila wanapoanza mtaa, shukrani kwa manispaa ya jiji hili kuweka utambulisho wa vibao hivi hili kurahisisha mtu asiulize kwa watu ovyoovyo bali anajisomea tu vibao.
“..Naam! kumekucha” Agent Kai akaongea huku anasoma kibao kilichowekwa kwenye nguzo ya chuma iliyopandwa juu ya kimuinuko kilicho pembezoni mwa mtaro wa maji wa pembeni mwa barabara ya mtaa.
“Pana umbali kidogo… Kumetulia sana na majumba yote mazuri..” Akaongea Rebecca huku anaanza kusoma namba iliyo kwenye geti la nyumba ya kwanz unapoanza mtaa upande wa kushoto kwake.
“Utasoma namba nyumba za upande wako nami nasoma za huu upande wangu wa kulia..”
“Sawa ila punguza tena kidogo mwendo..!”
Gari ikapunguzwa tena mwendo na kila mmoja akachukua jukumu la kusoma namba za mageti uwa au kuta zilizozunguka nyumba hizi, ambako kulikuwa hakuna nyumba iliyokosa kuzungushiwa uzio wa ukuta tofauti ikiwa mingine mirefu zaidi mingine si mirefu na mingine ikiwekwa vyuma juu na mingine hamna iliyo hivyo.
“Nimeiona hii hapa..!” Agent Kai aliiona nyumba wanayoitafuta akamwambia S.A Rebecca wote wakageuzia shingo huku kulitizama geti na kuta iliyozunguka huku kwa ndani paa ya kisasa iliyoezekwa kwenye nyumba ilionekana kwa muundo ambao hata kama unakuwa hujaiona nyumba yenyewe bati tu linakufahamisha kuwa nyumba ni ya kisasa.
Walipita na kwenda mwisho wa mtaa ambako kuna kona ya barabara inayoendea mtaa wa pili Agent akakunja kuelekea mtaa wa pili hili wapate sehemu ambayo watapaki gari na kurudi mtaa husika kuona wanaingia vipi ndani wakati anaweka sawa usukani ikatokea gari aina ya Mitsubishi Pajero Sport 2.5 AT rangi nyeusi ikiwa na vioo vya giza na hata taa zake za ndani zote zikiwa zimezimwa kama wao kina Kai walivyozima katika gari lao, nywele za Agent Kai zilisisimkwa wakati wanapishana na hili gari akashawishika kugeuza shingo kuangalia vizuri lakini hakuambulia kuona hata vivuli vya watu waliopo ndani ya gari ikizingatiwa usiku wa siku hii ulikuwa ni usiku uligubikwa na giza zito sababu ya wingu la mvua lililopo angani.
“Natamani tugeuze gari kulifuatilia hili gari tulillopishana nalo.” Akaongea Agent Kai bila kumtizama S.A Rebecca ambaye naye aligeuka kuangalia kwa nyuma gari anayoambiwa.
“Umehisi kitu?” Akauliza Rebecca baada ya kurudisha kichwa sawa.
“Naam.. Ukiwa umebobea sana katika hii michezo ya hatari kunakuwa na vitu vinakujia ingawa si mara zotelakini uwa vinaendana na hali halisi.. Nimehisi kuna jambo katika gari hili na nafikiri siko mbali na hisia zangu.. Acha nipaki nyuma ya gari hizi mbili, hizi nyumba zinaonekana hazina maegesho ya magari hivyo wenye nyumba hizi wanapaki magari yao eneo hili” Aliongea Agent Kai kisha akafanya kwa vitendo anachosema.
Walishuka kwenye gari wakiwa wamechukua kila mmoja bastola yake baada ya kuzicheki cheki kuwa ziko tayari kwa kazi kama ujuavyo usiku huu wote hawakuwa wametoka na silaha za kazi nyingi kwakuwa kila mmoja aliona hawezi kutoka na vitu mbalimbali zaidi ya bastola hasa kwa Special Agent Rebecca aliyetoka na bastola tu pamoja na miwani yake ya kijasusi huku yeye Agent Kai akiwa ametoka na bastola pamoja na kisu alivyovificha vyote katika mkanda nyuma ya kiuno bastola na kisu kwenye kamatio la soksi mguuni na miwani kama alivyo Rebecca zikiwemo na simu zao ambazo si silaha ya dhahiri shairi ni silaha ukipenda iwe silaha inaua na kujeruhi (simu).
“Twende mbio kidogo, mbio zisizo tiliwa shaka na mtu endapo atatokea naamini si mgeni wa mbio hizo” ‘TSC’ akatoa maelekezo wakiwa wanaangaliana na wote wakatabasamu kwa kauli hizi.
“Sawa boss.. Ila kwa hili umenikosea!” Akajibu Rebecca wakiwa washaanza kwenda mwendo wa nusu kimbia nusu tembea kwa hatua ndefu za kuruka msingi wenye kaupana.
“Nimekosea? Nisamehe kama nimekosea.. Hahah hahahaha hahahaha Reby”
“Ndiyo.. Umenikosea.. Mimi siyo Shufania mwanafunzi wa chuo cha habari na utangazaji”
“Khahah! Oooh... Mhh! Shufania tena? Kaja tena, haya mama!”
Mbio za nusu kimbia nusu tembea huku wanaongea kwa furaha ziliwafanya wafike mtaa husika wakifuata barabara iliyoenda gari waliyopishana nayo.
“Haah! Turudi kwenye usawa wa miti haraka.. “ Walipotokeza macho tu mbele akiwa katangulia ‘TSC’ aliiona ile gari aliyohisi tofauti ikiwa imepaki kwenye geti la nyumba namba 7thBA urefu wa mita kama sabini za mraba toka walipo.
Pembezoni mwa barabara ya mtaa huu wa Lelia Dorados kulikuwa na miti iyopandwa kwa safu kuleta vivuli kwenye mtaa, mti mmoja waliutumia kujibanza wasionekane na watu waliokuwa wao wakiwaona tokea pale walipo, watu ambao walikuwa kama watano wanaongea kwa pamoja na mmoja wao akiongea kwa simu.
“Nilihisi kitu maana mwili wangu hasa nywele zangu zilisisimkwa wakati tulivyopishana nao.. Tusogee karibu kuona kwa ukaribu pengine tunaweza nasa mambo kadhaa” Kai akaongea tena kisha akatoa miwani yake ya kazi akaivaa na Rebecca akaiga kufanya kama alivyofanya anayemuita boss wake.
“Nitatoka mimi kutangulia kituo kitakuwa kwenye mti unaofuata tutatembea kufuata vivuli.. Pole kwa kukuelekeza mtaalamu.. Hahahah!” Maelekezo mengine yakatoka kwa ‘TSC’.
“Hahahah hahahah! Sawa boss mwenye pua zake za kunusa visivyonusika” Rebecca akakubalia akitumbukiza na utani, utani uwa muhimu sana nyakati kama hizi maana uleta hali ya kujiamini na kuondoa uoga kama ubongo unakuwa una kauwoga fulani.
Walipeana ‘tano’ kwa kugonganisha ngumi zilizo ndani ya gloves kwakuwa wote walikuwa wamevaa gloves kwenye viganja vyao.
‘TSC’ akatoka akiwa kainama kama anataka kutembelea magoti au ana ‘rukuu’ akipiga hatua mnyato mpaka kwenye mti unaofuata toka waliokuwa wamejibanza kwa pamoja sekunde tatu toka afike Rebecca akaibuka kama alivyofanya kaka wake wa kazi wakakutana tena kwenye pembeni ya mti mmoja, ambako hawakuongeleshana bali walichungulia walipo wanaowasogelea kwa sekunde kumi hivi kisha kama ilivyokuwa mwanzo akaondoka Kai mpaka mti unaofuata.
Kulikuwa na miti sita iliyoachana hatua kama kumi toka mti na mti kukaribia karibu na gari walilopishana nalo, majasusi hawa walifanya nyatia mpaka mti wa karibu kabisa na gari lililopo pande ya pili barabara, wakijiweka kwa nyuma na kutokeza kidogo sehemu ya kuchungulia kuona kunani pale.
Bastola zao walizozifunga viwambo vya kuzuia sauti zilikuwa mikononi mwao na kabla hawajavuta pumzi zao vizuri zilizokuwa zikitoka kwa pupa kidogo kutokana na mijongeo yao waliyojongea geti la nyumba lilifunguliwa kisha wakatoka watu watatu kwa mpigo kisha nyuma yao akatoka mwingine, wale wa mbele walikuwa mmoja kwenye macho ya kina Agent Kai ambayo yalikuwa na msaada wa miwani ya kijasusi waliweza kumuona ni mwanamke akiwa kabeba begi dogo na wengine walikuwa ni wanaume ila hawa walikuwa wamebeba begi kubwa la mizigo kwa kila mmoja wao na wa mwisho kutoka ndani ambaye alikuwa ni mwanamke hakuwa amebeba kitu na alipotoka yeye hakusimama kama wale wengine waliomtangulia yeye haraka haraka aliingia ndani ya gari siti za abiria, kwa upande huu walipo kina Agent Kai walikuwa wakiona vizuri kwakuwa milango ya gari yote ilikuwa wazi hivyo mlango mmoja wa siti za abiria waliutumia vizuri kuona kwa kutokea walipo mpaka kwenye geti.
“Aiseeh! Madam Millian anaondoshwa hapa” Akanong’ona Agent Kai akisogeza mdomo wake karibu na bega la S.A Rebecca hili amsikie vizuri.
“.. Ni yeye kweli?”
“Ndiyo! Amejiziba uso kwa kitambaa cha kilemba alichovaa lakini ni yeye hakuna la kuona si yeye”
“Wamejuaje kama tunakuja hapa?”
“Hahaha! Hahaha…. Na wao ni wataalamu si wahalifu wa hali ya chini hawa Reby, tunatakiwa tufanye kitu haraka sana..”
“Unataka tuwashambulie?”
“Inawezekana.. Tuko makomando wawili hapa hatuwezi shindwa”
“Sawa boss.. Lasivyo tutamkosa mtu muhimu na hata kama tungekuwa na gari hapa tusingeweza kuweka mkia kuwafuatilia usiku huu hakuna magari mengi mitaa hii kama unavyoona hivyo tutastukiwa mapema na kuharibu kazi”
“Shida iliyopo hapa hatujui ndani kama kuna walinzi ukiacha hawa watu watano waliofika hapa ambao tumewaona kabla ya waliotoka ndani… Ni fumbo kwetu na kamari pia..! hakuna njia hapa, tukubali wametuzidi kete kwa leo acha waondoke naye”
“Boss! Huoni tutapoteza fursa muhimu na kushindwa kumaliza lililotufanya tuwe macho mpaka muda huu.. Hahah! Sawa kama unaona ni sawa”Alilalamika Rebecca akiwa na mshangao alichokisikia toka kwa Agent Kai ambaye alitabasamu kisha akamuangalia akamsogelea wakawa kama wamekumbatiana mkono ulioshika bastola ukairudisha nyuma ya kiuno mahala salama kwake kwa kuhifadhi hiki kitendea kazi chake kama ilivyo peni na chaki kwa walimu.
“Jumla ya waliopo pale itatusumbua kwa silaha tulizonazo.. Ningeruhusu tushambulie kama tungekuwa na mashine kubwa kama bunduki si hizi bastola maana kumbuka kuna kutupa risasi na kumkosa mtu je una magazine hapo ulipo?” Aliongea Agent Kai kwa kunong’ona karibu kabisa na kichwa cha S.A Rebecca huku mkononi mwake akiwa na simu anaitoa ‘lock’ (kizimba) akainua na kupiga picha ikiwa kaondoa mwanga kwa umbali huu waliopo hii simu yake aina ya Samsung Galaxy A20 Ikiwa ni zalisho maalumu kwa kazi zao kitengo cha ‘Special Activities Divion’ (SAD) kutoka moja kwa moja kwenye kampuni ya Samsung hivyo si sawa na yako msomaji kwatika utendaji wake wa kazi ingawa ungeiona ungedhania kiuwezo iko sawa na yako.
Alifanikiwa kupiga picha kadhaa za watu aliokuwa akiwaona huku Rebecca akifuatilia tukio lile kwa kuangalia simu iliyo mkononi mwa boss wake na pia kuangalia kule, geti lilifungwa watu wote wakaingia ndani ya gari ikaondolewa kwa kugeuzwa ilipotokea kisha ikaondoka kasi ikiacha Agent Kai akipiga picha vioo vya gari kwa ukaribu zaidi na kisha kumalizia kwa ‘plate number’ ya gari.
“Kuna haja ya kuingia ndani ya hii nyumba?” Akauliza S.A Rebecca walipojitokeza na kupiga hatua kujongea kunako barabara.
“Tukalale tupumzishe akili na mwili.. Asubuhi tutaanza na kujua nani mmilki hii gari iliyoondoka hapa” Akajibu kiufafanuzi kidogo Agent Kai kisha wakatembea wakiwa wameongozana kama mtu na mpenziwe usiku huu kuelekea walipoacha gari ya Inspekta Pena.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na moja (111)
Maswali na majibu yaliweza kuwafikisha Agent Kai na Special Agent Rebecca katika nyumba ambayo ni kweli alikuwa ameweka makazi ya muda Madam Miliian Carlos Codrado.
Kipi kimesababisha kwa Madam Millian kuondoshwa katika nyumba aliyofikia?
Ni nani kasababisha hili?
Majibu ya maswali haya na mengineyo mengi kwa ujumla wake fanya kusogea sehemu ya inayofauta!
“Jumla ya waliopo pale itatusumbua kwa silaha tulizonazo.. Ningeruhusu tushambulie kama tungekuwa na mashine kubwa kama bunduki si hizi bastola maana kumbuka kuna kutupa risasi na kumkosa mtu je una magazine hapo ulipo?” Aliongea Agent Kai kwa kunong’ona karibu kabisa na kichwa cha S.A Rebecca huku mkononi mwake akiwa na simu anaitoa ‘lock’ (kizimba) akainua na kupiga picha ikiwa kaondoa mwanga kwa umbali huu waliopo hii simu yake aina ya Samsung Galaxy A20 Ikiwa ni zalisho maalumu kwa kazi zao kitengo cha ‘Special Activities Divion’ (SAD) kutoka moja kwa moja kwenye kampuni ya Samsung hivyo si sawa na yako msomaji kwatika utendaji wake wa kazi ingawa ungeiona ungedhania kiuwezo iko sawa na yako.
Alifanikiwa kupiga picha kadhaa za watu aliokuwa akiwaona huku Rebecca akifuatilia tukio lile kwa kuangalia simu iliyo mkononi mwa boss wake na pia kuangalia kule, geti lilifungwa watu wote wakaingia ndani ya gari ikaondolewa kwa kugeuzwa ilipotokea kisha ikaondoka kasi ikiacha Agent Kai akipiga picha vioo vya gari kwa ukaribu zaidi na kisha kumalizia kwa ‘plate number’ ya gari.
“Kuna haja ya kuingia ndani ya hii nyumba?” Akauliza S.A Rebecca walipojitokeza na kupiga hatua kujongea kunako barabara.
“Tukalale tupumzishe akili na mwili.. Asubuhi tutaanza na kujua nani mmilki hii gari iliyoondoka hapa” Akajibu kiufafanuzi kidogo Agent Kai kisha wakatembea wakiwa wameongozana kama mtu na mpenziwe usiku huu kuelekea walipoacha gari ya Inspekta Pena.
ENDELEA NA MAPIGO…!!!
FUNGA KAZI VII
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
Habari za kuingia kwa majasusi watatu kupitia usafiri wa ndege iliyotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Deputado Luis Eduardo Magalhae International Airport uliwafanya Bwana Fernandes Carlos Codrado (Feca) na wenzake kushtushwa na kuchanganyikiwa na jambo hilo ikiwa ni kuwashangaza kwanini ni mapema sana toka waingie ndani ya jiji la Salvador, walishindwa kuelewa majasusi hao wanaosemwa ni wa Mexico au ni wa Marekani? Hili lilikuwa ni swali kuu walilokuwa wakijiuliza katika maongezi yao yaliyowafanya kuchukua tahadhari kadhaa wa kadha katika kuhakikisha hawaingii katika mtego wowote utakaowaletea kuharibu nia yao kuu ya kuja katika jimbo hili la Bahia nchini Brazil kujificha mpaka itakapokuwa na hali ya usalama upande wao bila kujali ni muda mfupi au muda mrefu, imani yao ni kuwa mambo yatakaa sawa na hakuna litakalowafanya wao kuumia zaidi.
Tahadhali ya kwanza haraka iliamriwa Madam Millian aondolewe katika nyumba aliyofikia yeye na mtoto wake mmoja aliyeongozana naye pamoja na wafanyakazi wao wa kuwasaidia kazi mbalimbali za kibinadamu.
Watu waliotumwa kumfuata Madam Millian na hao niliowaelezea walifanikiwa kufika muda muafaka muda ambao walizuia jaribio la Agent Kai na Special Agent Rebecca kumfikia bila ya wao kujua kama wamezuia jaribio lililobaki robo hatua kutimia kwa wajuzi wa mambo kufanya yao.
Wakati Madam na watu wake wanafika mahala palipotolewa maelekezo wapelekwe kwakuwa ni mahala salama kwa wakati huo, simu ya taarifa toka kwa mtu aliyeko idara ya upelelezi ya jeshi la polisi iliyopigwa kwenda kwa mtu ambaye anatumika kama kiunganishi wa mawasiliano baina ya bwana Feca na wengine katika mtandao wao waliouunga ambao ulifanywa siri haswa ilikuwa ni simu ya taarifa kuwa Inspekta wa jeshi la polisi makao makuu ya jimbo la Bahia aitwaye Inspekta Fred De Luis Penambucano hii nayo iliwastua sana kwakuwa Inspekta alikuwa ameunganishwa kwa Madam na mtu ambaye yuko shirika la ujasusi la Brazil la Law Enforcement Agency (LEA) lenye matawi yake kila jimbo katika nchi hii ya Brazil, mtu huyu yuko makao makuu ya shirika hili huko jijini Brasilia, taarifa ilikuwa ikieleza amekutwa ametupwa pembezoni mwa geti la hospitali ya Ana Nery iliyopo mtaa Tribuna Da Bahia, wamekuta amepigwa kwa kipigo kinachoonyesha ni mateke mpaka kupelekea mateke hayo kumvunja pingili za uti wa mgongo na mbavu mbili za upande wa kushoto, haijulikani amepigwa na nani? au kina nani? na kwanini?.
Taarifa hizi tata zilimfanya Bwana Feca kuitisha kikao cha dharura hasa ukizingatia yupo yeye na mdogo wake ambaye si mzoefu sana kwenye mambo ya mikimbizo na pilikapilika za kiuhalifu, hawakuwa wao tu walikuwepo swahiba wake mkuu waziri wa usalama mfukuzwa katika serikali ya Guatemala mheshimiwa Rafael Ceni huyu naye alikuwa mweupe tu si mtu wa kazi kivile inapofika kipindi cha kufanya jambo linalohusiana na kazi kwa vitendo kwake yeye alikuwa ni mtu wa maelekezo tu huku akikaa kwenye kiti cha kuzunguka anagonga mvinyo mwekundu, alikuwepo swahiba wa Feca ambaye miaka mingi alikuwa kiunganishi wa genge la ‘TRJ’ huko Marekani na hata kuwa mlinzi wa familia ya Feca wakati yupo gerezani huyu ni Bwana Sergio Lopez Puto huyu kidogo kashikashi anaziweza si tuma tuma, pamoja nao pia alikuwepo Bwana Villa Nandez Guti huyu anajua mambo ya kazi za kazi lakini kuja tu huku ilikuwa ni kwa sababu Bwana Feca alihofia anaweza akakamatwa na kumuharibia mambo yake mengi sana kama angemuacha Mexico lakini kiafya hakuwa vizuri alikuwa akisumbuliwa sana na ugonjwa wa kiuno hivyo alikuwa ametoka Canada kwa ajili ya matibabu ambapo alifanyiwa operesheni huko huko katika kliniki ambayo ipo chini ya uangalizi wa watu ambao wao wamewaweka ila ni kliniki ambayo kama ingekuwa ni mambo ya uwazi si kujificha ficha basi mmiliki wake wa halisi angejulikana ni familia ya ‘Feca’ licha ya operesheni aliyofanyiwa hali yake haikuwa hali tengemaa, watu wengine ambao walikuwa hapa hawa ni vijana ambao Feca aliwaweka jimboni hapa kumlindia mambo yake na mali alizokuwa kaziwekeza hapa kisiri siri.
Kikao chao kwakuwa kilihudhuriwa na baadhi ya wanausalama ambao ni wasaliti kwa nchi yao na uwa hawakosekani katika kila nchi au vyombo vya usalama vingi tu.
Zilianza kutafutwa habari kuanzia uhamiaji, uwanja wa ndege, mahotelini na kwingineko kuliko na njia ya kuingia ya Salvador na Bahia nzima kwa ujumla, vyanzo havikukosa majibu ilionekana kuna watu watatu walipandia ndege jimbo la Guerrero jijini Chilpancingo wanatiliwa mashaka licha ya kujifanya hawajaongozana wala kufungamana kwa chochote, mmoja ni mwanamke na wawili ni wanaume, taarifa zinasema vibali vyao vya kuingia hapa Brazil vina ubabaishaji fulani ambao unatakiwa kufanyiwa kazi na laiti uhamiaji ya Brazil wangekuwa makini basi watu hawa wasingeruhusiwa kuingia jimbo la Bahia.
Kazi iliendelea ndipo zikapatikana picha za kamera za cctv kutoka kwa mmoja wa kibaraka wao aliye uwanja wa ndege ndipo wakawaona watu watatu wanaowatilia mashaka ingawa walijibadili muonekano wa sura zao kwa ghiriba mbalimbali ni Agent Kai aliyevaa sura ya bandia akitumia kitambulisho na paasport bandia katika uonekano wa kuwa yeye mzungu ambapo hata mama Kai angemuona angeweza pishana naye.
Agent Hansen Blade alifuatiliwa akiwa kwenye ukaguzi kupitia video alizotumiwa kiunganishi wa mawasiliano wa Bwana Feca, lakini Rebecca ilikuwa bahati kwake ingawa faili lake la taarifa yeye ni nani zilianza kufuatiliwa kuona kama ni jasusi kwakuwa tu kila aliyepandia ndege Chilpancingo alichunguzwa hasa kwakuwa mtu wa kwanza kuleta habari kuwa kuna watu wa kufukunyua wanaweza kwenda Bahia ni mtangazaji wa Thea hivyo shina lilianzia jimbo la Guerrero jijini Chilpancingo.
Ikaamulika watafutwe watu hawa kwa haraka ikibidi isizidi masaa ishirini na nne, boss anataka kukaa jijini Salvador kwa raha zake, haraka kazi ikaanza rasmi upande wao.
***** ***** *****
Ilikuwa kama anaota kitu kilicho kama mbao kinagongwa kisha ikifuatia na mlio wa kengele ndogo kama ya baiskeli, usingizi ulianza kukata hali ya kawaida ikaanza kujirudia kwake ndipo akasikia vizuri kengele ya mlangoni inaita kupitia spika iliyo karibu na kitanda alicholala tokea usiku uliopita, hapo alifungua macho na kujikuta kajifunika shuka mwili hauonekani (gubigubi), haraka akatoa kichwa chake toka ndani ya shuka kisha akaiangalia spika inayotoa mlio haraka kwa sekunde mbili ikaacha kutoa mlio mlango ulio huko sebuleni ukagongwa kwa migongo mitatu ya kufuatana ikigongwa kwa kinachodhaniwa kichwani mwa muamshwa ni vidole ambaye sasa alilitupa shuka pembeni na kujiinua kwa pupa kitandani.
Alikuwa amevaa ‘tracksuit’ ya michezo ya rangi ya ‘hudhurungi’ (bluu), alipojiinua aliinua mto ambao hakuwa ameuwekea kichwa chake wakati amelala hapa akakuta bastola yake ambayo haraka akaikamata na moja kwa moja akaipachika nyuma ya kiuno kwa kuinua koti lake la suti ilipotulia akalishusha na kuelekea sebuleni, akasogea malangoni na kuchungulia kwenye kitundu maalumu ambacho uwa milangoni kwa baadhi ya nyumba za kisasa kwa minajili ya aliyegongewa kuweza kuona nani anagonga.
Macho yake yakakuta mgongaji ni mwanamke muhudumu wa hoteli lakini nyuma yake alikuwa na wanaume wawili waliovaa sare za jeshi la polisi, moyo wa mgongewa ambaye ni mpangaji wa hotel hii iitwayo Pousada Solaris Hotel iliyopo eneo la karibu na beach maarufu na bora ya Rio Vermelho ambako kutoka hii hotel ilipo na beach ni mwendo wa dakika mbili kwa mtembea kwa miguu mwenye afaya yake ni moja ya hotel nzuri ya kimataifa inayopendeza katika mandhari mpaka huduma zake za kila kitu kwa ujumla.
Mgongewa mlango anaitwa Agent Hansen Nichoalaus Blade, alirudi kawaida na kusimama akiacha kuchungulia akijiuliza ‘kwanini muhudumu amekuja kugonga akiwa na maaskari?’, aliinua mkono wake wenye saa akaangalia kuona ni saa ngapi? Saa ikamtambulisha ni saa kumi na mbili na nusu kwa saa za hapa Bahia nchini Brazil.
Mlango ukagongwa tena safari hii ukigongwa kwa nguvu zaidi ikamfanya Agent Hansen kuchungulia tena kitunduni huku mkono wake wa kulia ukipapasa nyuma ya kiuno ilipo bastola yake akarudi kawaida akatoa pumzi kubwa kisha akatulia na kusugua kadi yake katika kitasa maalumu kinachofunguliwa kwa kadi maalumu kama funguo ya mlango, akajitokeza kichwa kuwaangalia wagongaji akiwa kakunja sura kuonyesha alivyochukia kugongewa mlango muda kama huu.
“Habari yako mgeni?” Mmoja wa wanaume wale waliovaa sare ya jeshi la polisi aliongea baada ya kuona jinsi jamaa alivyokasirika na kuwaangalia bila uoga wowote wa kuwa waliomgongea na wako mbele yake sasa ni maaskari, muhudumu wa kike alijiweka pembeni akitetemeka dhahiri machoni mwa Agent Hansen Blade.
“Kuna nini?” Akauliza Hansen akiwauliza maaskari bila kujibu salamu ya mmoja aliye ambele aliyeuliza habari, kiasili Agent Hansen Blade ni mtu mkorofi sana mwenye kujiamini na asiyependa mtu kumuharibia utulivu wake pale anapokuwa ametulia au anawaza jambo kwa kina na hata kuamshwa usingizini bila yeye kuona kuna sababu ya msingi yeye kuamshwa hivyo hapa alikuwa akitamani atoe bastola yake kisha awasulubu watu hawa wote bila kujali nani ni nani.
“Mbona hamsemi kuna nini mmenyamaza? Heti wewe muhudumu hawa askari umewaambia nini? Mpaka niamshwe kabla ya wakati niliopanga kuamshwa..” Kwa hasira akahoji tena akimtizama dada wa kizungu wa kibrazil mwenye nywele za blonde akiwa kavaa sare ambazo kiukweli zilimpendeza sana.
“..Mimi sijui kuna nini ila wamesema wana kibali cha kuomba kuongea na watu ambao wameingia kupanga hoteli yetu kuanzia muda wa saa kumi jioni..!” Akajibu muhudumu akipepesa macho yake huku na huko.
“..Kwanini? usumbufu huu mmeufanya na kwa wateja wengine tayari au mimi ndiyo nimeanza?” Akahoji Hansen uso ukizidi kurindima kwa ndita babu kubwa mpaka askari nao wakashangaa wakijiuliza mtu huyu vipi kukasirika hivi hadi ngozi yake ya kizungu kuanza kuwa nyekundu na macho kuongezeka rangi ya bluu katika mboni yake.
“Mkuu! Samahani kwa usumbufu huu.. Hili jambo ni kawaida kwa ajili ya usalama wa nchi yetu.. kuna jambo limetokea usiku uliopita si la kawaida na tunahisi limefanywa na wageni si wenyeji wa hapa na ndicho kilichotufanya tupite katika mahoteli kuangalia tunachoangalia kutokana na taarifa zetu za kiintelejensia.. Kuna maswali machache ambayo tutaomba utujibu kisha utaendelea na mambo yako kama kawaida utatusamehe kwa hili sababu si ombi ni lazima mkuu” Askari wa polisi wa mbele aliyetoa salamu ambayo haikujibiwa akatoa maelezo marefu kidogo.
“Mimi si muhalifu na pia mimi si mgeni katika nchi hii hivyo sitakuwa na jibu la hayo mnayotaka kujua toka kwangu, nafikiri busara mngeendelea kutafuta kwenye vyumba vya wageni wengine walioingia huo muda mnaosema” Akajibu tena jeuri ikiendelea kama kawaida.
“Naitwa Sajenti Bruno na mwenzangu anaitwa Koplo Maxilian, sote tunatokea makao makuu ya jeshi la polisi jimbo la Bahia hapa jijini Salvador, tumeku..!” Alitoa utambulisho bila kuombwa askari aliyekuwa mbele uso kwa uso na Agent Hansen lakini wakati akiendelea kuongea alikatiziwa kauli zake na Agent Hansen aliyeamua kufanya kitu kupitia uzoefu wake wa kazi za kazi.
“Nimekuelewa Sajenti wa Polisi Bruno na mwenzako mlioongozana. Tusipishane kauli na kuleta tofauti sisi sote ni vijana, je nitawaamini vipi kama nyinyi ni polisi? Si kuwa mnataka niwaamini hivyo kwa mavazi tu mliyovaa, nafikiri utaratibu mzuri mnaujua” Agent Hansen akaongea akiwaangalia kwa zamu polisi hawa.
“Ooooh! Samahani, hiki kitambulisho changu” Akaongea askari polisi mzungumzaji ambaye kashatujuza jina lake anaitwa Bruno! Sajenti Bruno wakati yeye akionyesha kitambulisho chake mwenzake ambaye alikuwa kimya toka wafunguliwe mlango naye alionyesha kitambulisho chake.
“Ahsanteni sana.. Huu ndiyo utaratibu wakuu wangu.. Lakini mmenikurupusha kitandani mnaonaje mkiniacha nipate haki zangu za asubuhi kuhusu usafi?” Hatua ya kwanza Hansen alianza na kuomba apate kuswaki na kuoga kama ilivyo ada kwa mtu yoyote anayejali afya yake.
“Nafikiri tungefanya maongezi kwanza na kwakuwa ni dakika chache tu utapata muda ya kufanya hayo utakapomaliza mahojiano yetu” Sajenti Bruno akaongea.
“Kama ni mazungumzo mafupi nafikiri tunaweza kwenda ongelea kwenye mgahawa huku tukipata kahawa” Akaweka ombi lingine Hansen.
“Ujumbe ambao tumefika nao hapa kuwa tukuchukue mpaka kituo kikubwa sisi wajumbe tu mfanya mahojiano nawe yuko huko anakusubiri..”
“Mnajifunga katika hili.. Wakti nilipofungua mlango mliniambia mna oda ya kufany mahojiano na kila mtu ambaye ameingia katika hotel hii kuanzia muda wa saa kumi ebu nifafanulieni hapo tafadhali..!”
“..Hata tukikwambia kuwa tumeshamaliza kufanya mahojiano na watu wote sita waliofika kuchukua vyumba katika hotel hii utatubishia ila ukweli ni kuwa wewe ndiyo wa mwisho” Afande akaongea uongo wake ambao Hansen aliuelewa ila akajifanya hajang’amua chochote.
“Mmh! Sawa kwahiyo natakiwa kwenda kituoni? Je siruhusiwi kumpa taarifa mwenyeji wangu hili anifuatile huko kituoni maana mimi mgeni na nina mwenyeji wangu hapa Salvador”
“Sawa ila utatumia simu tukiwa ndani ya gari.. Hivyo tuingie ndani uvae viatu tuondoke” Afande muongeaji akaendelea kumwaga sumu katika ubongo wa kuamka wa Bwana Agent Hansen.
“Dada! Ahsante na kaendelee na kazi maana tusikucheleweshe ni muda wako wa kutoka kazini huu.. pole sana sisi tunatimiza wajibu wetu tu, hatupendi kuonekana kama tunanyanyasa wapangaji wenu na kuwaingilia uhuru wao, ila tatizo lililotokea halina namna” Askari ambaye hakuwa muongeaji sana toka wafike aliongea kwa mara ya kwanza kumwambia muhudumu wa vyumba vya hotel vilivyo korido ya flour hii.
Agent Hansen aliamua kuwa mpole hili aone wataishia wapi na watu hawa, alikubali kuingia nao ndani walipofika chumbani alishangaa akivamiwa na askari mwenye jina la Koplo Maximilian na kuanza kusachiwa kwa nguvu mwilini katika nguo alizovaa hapa kengele ya tahadhali ikagonga kichwani mwake kwakuwa aliyekuwa akifanya naye mahojiano alishika bastola mkononi akamuelekezea hili atulie asachiwe.
“Jamani vipi tena? Nishakuwa mtu wa hatari mpaka mnafanya hivi..” Akaongea wakati bastola yake ikiamia kwenye mikono ya Koplo Maxi.
“..Bastola hii ni yako?” Akauliza Sajenti Bruno huku anaipokea toka mikononi mwa mwenzake.
“Ndiyo yangu, mimi ni mmiliki halali najilinda kwa ajili ya biashara zangu nazofanya” Akajibu Hansen huku akitizama hesabu za anachofikiria kufanya.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na mbili (112)
Kazi zimekutana juu ya kazi!
Nini kitakujia katika sehemu inayofuata?
Agent Hansen yuko katika taratibu za kuingia katika mikono isiyojulikana kutoka wapi?
Kwa kazi yenye pigo za hatari!
“Mnajifunga katika hili.. Wakati nilipofungua mlango mliniambia mna oda ya kufanya mahojiano na kila mtu ambaye ameingia katika hotel hii kuanzia muda wa saa kumi ebu nifafanulieni hapo tafadhali..!”
“..Hata tukikwambia kuwa tumeshamaliza kufanya mahojiano na watu wote sita waliofika kuchukua vyumba katika hotel hii utatubishia ila ukweli ni kuwa wewe ndiyo wa mwisho” Afande akaongea uongo wake ambao Hansen aliuelewa ila akajifanya hajang’amua chochote.
“Mmh! Sawa kwahiyo natakiwa kwenda kituoni? Je siruhusiwi kumpa taarifa mwenyeji wangu hili anifuatile huko kituoni maana mimi mgeni na nina mwenyeji wangu hapa Salvador”
“Sawa ila utatumia simu tukiwa ndani ya gari.. Hivyo tuingie ndani uvae viatu tuondoke” Afande muongeaji akaendelea kumwaga sumu katika ubongo wa kuamka wa Bwana Agent Hansen.
“Dada! Ahsante na kaendelee na kazi maana tusikucheleweshe ni muda wako wa kutoka kazini huu.. pole sana sisi tunatimiza wajibu wetu tu, hatupendi kuonekana kama tunanyanyasa wapangaji wenu na kuwaingilia uhuru wao, ila tatizo lililotokea halina namna” Askari ambaye hakuwa muongeaji sana toka wafike aliongea kwa mara ya kwanza kumwambia muhudumu wa vyumba vya hotel vilivyo korido ya flour hii.
Agent Hansen aliamua kuwa mpole hili aone wataishia wapi na watu hawa, alikubali kuingia nao ndani walipofika chumbani alishangaa akivamiwa na askari mwenye jina la Koplo Maximilian na kuanza kusachiwa kwa nguvu mwilini katika nguo alizovaa hapa kengele ya tahadhali ikagonga kichwani mwake kwakuwa aliyekuwa akifanya naye mahojiano alishika bastola mkononi akamuelekezea hili atulie asachiwe.
“Jamani vipi tena? Nishakuwa mtu wa hatari mpaka mnafanya hivi..” Akaongea wakati bastola yake ikiamia kwenye mikono ya Koplo Maxi.
“..Bastola hii ni yako?” Akauliza Sajenti Bruno huku anaipokea toka mikononi mwa mwenzake.
“Ndiyo yangu, mimi ni mmiliki halali najilinda kwa ajili ya biashara zangu nazofanya” Akajibu Hansen huku akitizama hesabu za anachofikiria kufanya.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI VII
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
“Wewe ni mfanyabiashara?” Akauliza afande Sajenti Bruno huku anaendelea kumpapasa mwilini kana kwamba anampapasa mpenzi wake hali hii ilimchefua sana Agent Hansen anayechukia sana kupapaswa mwili wake na mwanaume mwenzake, kabla alipanga wakishatoka nje ya hotel hii tu basi atawafanyia kitu hawa askari ambacho kama kitawapelekea wote kukutwa na umauti basi wataenda hadithia kama riwaya huko jehanamu wanakostahili kwenda.
Wakati Sajenti Bruno anaendelea kumpapasa akishusha mikono yake eneo la makalio yake ikiwa anafanya marudio tu tena akipapasa kihuni sana ilimkera kupitiliza Hansen akamtizama kwa chati kisha akatizama umbali wa hatua toka alipo na alipo Koplo Maxi akaona hakuna namna hawezi zalilishwa komandoo wa Navy Seals na jasusi mbobezi wa kitengo cha ‘Special Activities Divion’ (SAD) kilicho ndani ya CIA, hata wenzake kama wangemuona hapa anafanyiwa hivi wangejiuliza lini Hansen kaanza ushoga huu kuruhusu mipapaso toka kwa mwanaume mwenzake.
“Mphxxiiiiiih!!!!!” Akatoa msonyo kisha akafanya kama anataka kugeuka kwa nguvu upande wa nyuma alipo bingwa wa mipapaso Sajenti wa polisi Bruno, ilikuwa ghiliba! Koplo Maxi akasogea mbele kidogo hili amtulize kwa msisitizo kuwa kuna yeye kashika bastola, kosa! Tena kosa la kimataifa! Mkono ulioshika bastola ulijikuta ukipigwa teke zito la mguu wa kulia lililotua kwenye kifundo cha mkono na mkono ukaachia bastola bila kupenda toka kiganjani ikamruka Koplo kama imemvisha kanzu ikaenda tua kwenye mwisho wa kitanda ambako nako ikakosa balansi kukaa pale ikadondokea chini ya kitanda huko kilicho ukutani mwisho wa chumba, mguu wa Agent Hansen uliporudi chini tu mguu wa kushoto ukakunjwa kinyume nyume kisigino kikatua katikati ya miguu ya Sajenti Bruno ulipo uume na kende (korodani/pumbu), miguuni Agent Hansen hakuwa na viatu hivyo makali ya vitu hivi alivyovifanya kwa haraka havikuwa na makali kama ambavyo angekuwa na viatu.
Sajenti Bruno alistushwa na matukio haya ya haraka akatoa mikono yake haraka kwenye kupapasa na kutaka kuipeleka ilipo hazina kuu iliyoshambuliwa likawa kosa jipya tena, Hansen akapiga kipepsi (kiwiko) kwenda nyuma ambacho hiki sasa kilipeleka madhara makubwa kwenye pua ya mpapasaji, mfereji wa kutokea zilipo tundu za pua kuja mdomoni ulipasuka maana kiwiko kilikita juu ya ngozi nyama ya nje huku ndani mgongano ukakutana na meno ikawa bahati hayakuvunjika ila njemba likaguna na kujirudisha nyuma kwa nguvu.
Koplo Maxi alishuhudia yote haya kwa kasi naye akasogea kusaidia ambako alipokuwa anataka kurusha ngumi kabla mkono wake huu wa kulia haujanyooka vizuri kwa wepesi Hansen akaipiga teke la kurukia ngumi ile hapa napo kama ingekuwa kuna kiatu kwenye mguu huu nafikiri mpigwa teke angetoa chochote kati ya aibu fulani lakini maumivu aliyapata akaguna tu na kutaka kujiweka sawa asiyumbe tena Hansen akazungusha teke la kuzunguka mwili wote likaenda kutua pembeni ya kichwa cha mlengwa kwa uzito wake wa kushindwa kuhepa lakini kwa watu wepesi lilikuwa ni teke lililoonekana hivyo angeinama na kulikwepa kwake haikuwa hivyo kama mzigo akadondoka kichwa kikijipigiza kwenye kiti kilicho pembeni ya kitanda kama ujuavyo kwenye vyumba vya mahotelini kulivyo huku kofia yake ya upolisi ikiwa imetangulia juu ya kiti, kwa wepesi kama hajaamshwa kwa nguvu usingizni aligeuka kwa kasi baada ya kuhisi aliye nyuma kashasogea na kweli akakuta jamaa linakuja kasi kama mbogo mjeruhiwa.
“Unatushambulia maaskari.. Unatuzuia tusitimize wajibu wetu” Sajenti Bruno akaongea domo lake likiwa limezungukwa na damu zinamtoka alipopasuliwa uso aliukunja na kofia naye hakuwa nayo.
“Pumbavu zako.. Unajua mimi ni nani? mbwa weeeh!! Nitawaonyesha leo mimi ni nani!!” Agent Hansen akamjibu na kumpa maswali na yeye.
Sajenti Bruno alikuwa amepaniki akasogea kasi lakini wakati anasogea nyuma ya Agent Hansen aliyedondokea kiti kichwa chake kikijipiga alijaribu kuinuka aendelee na kupambana lakini kizunguzungu kilimshika akajikuta kabla hata hajashika vizuri kiti hili kimsapoti kuinuka anakiangusha naye kuanguka hii ilimfanya Bruno kuzubaika kumuangalia mwenzake, hakuwa anajua kwenye mapambano kama haya umakini unatakiwa kuwa kwa asilimia mia moja lilikuwa kosa ambalo huko alipo sasa atakuwa analijutia sana kwani Agent Hansen alitisha anataka kumpiga teke la kwenye ukoo tena ambako kwa jinsi alivyokuwa amepigwa mara ya kwanza ilikuwa kama mng’atwa na nyoka kuguswa na unyasi jamaa alirudisha macho yake kuangalia nini kinakuja akaruka kwa uwoga huku mikono yake ikikinga eneo nyeti akiacha uso ameuanika kama kaanika mpunga, ngumi nzito ya mkono wa kulia ilitua puani na kumpaisha nyuma hatua tatu toka aliposimama na alipotua kwa mgongo akaserereka hadi ulipo mlango ambako hakuwa umerudishwa (kufungwa) kichwa kikagonga kwenye mlango na kusababisha urudi kwa kasi kujifunga.
Hansen akasogea kwa mruko mmoja mpaka alipo Sajenti alikuwa na hasira naye sana aliinua mguu wake akaupindua na kufyatua teke la pembeni (outer kick) likatua shingoni na kuivunja shingo ya muhusika, akawa ameua askari wa jeshi la polisi la kibrazil, akamgeukia aliyedondokea kiti na kumkuta amepigwa na mshangao macho kayatoa kama anaota amekaa kwenye malumalu za chumbani miguu kainyoosha mbele kama yupo kwa mganga wa kienyeji anatolewa jinni.
“.. Mlitumwa na nani kwangu? na aliwaambia kwanini mje mnichukue?” Akauliza Agent Hansen baada ya kuona bwege tayari kasalimu amri kwa kipigo alichopewa na pia kushuhudia mwenzake akirudisha namba ya uhai kwa mwenyezi Mungu.
“Mimi niliombwa na Sajenti Bruno kuja huku nimsindikize tu.. Kwa kweli sijui kitu na ndiyo maana hukuwa unaona naongea lolote wakati anakuhoji, sijui kitu kaka” Akajibu Koplo Maxi.
“.. Unafahamu sihitaji utani ndiyo maana nilipowageukia nimewageukia kwa kasi na kichapo babu kubwa kupelekea mwenzako kwenda jehanamu kuwai nafasi ya kuwa kuni ya motoni, naomba nijibu vizuri swali langu lasivyo na wewe unaenda kuwa kuni ya akiba muda si mrefu” Akafoka Agent Hansen kijasho kikiwa kinaendela kumtoka baada ya kazi aliyoifanya.
“Ni kweli mkuu, mimi sijui kitu chochote, unaweza ukaniua lakini utakuwa unaniua mtu niliyeletwa hapa kama matairi ya gari yanavyokangaga kila sehemu ambayo muendesha gari husika yametaka yakanyage.. Tafadhali nionee huruma juu ya hili mkuu.. Uliyekwisha muua ndiye aliyekuwa anajua kila kitu” Akajibu Koplo Maxillian akiwa kakaa chini vile vile mbele yake kasimama Agent Hansen.
“Nitakuacha hai ukiniambia ni nani aliyemtuma Sajenti Bruno mpaka akakuchukua na wewe mkaja hapa hili umsaidie kunichukua na kunipeleka kwake?” Akauliuza Agent Hansen akiwa katanguliza mkataba mbele wa maneno.
“Hili suala limekuja kwa sababu ya askari mwenzetu Inspekta Fred De Luis Penambucano kukutwa amepigwa na kuvunjwa vunjwa mbavu na mgongo wake na mtu au watu wasiojulikana kisha kutupwa pembeni ya geti la hospitali ya Ana Nery mpaka sasa hivi tunavyoongea hajazinduka…Jambo lililotokea katika muda wa saa nane za usiku hivyo maaskari wote wa operesheni maalumu tuliitwa kituoni mi nilichelewa kufika kwa wakati nikafika kikao cha dharura kikiwa kishafanyika nikaambiwa natakiwa kuongozana na kutafuta mtu anayehisiwa amefanya tukio alilofanyiwa Inspekta Pena hivyo sikuwa najua mengi kati yaliyoongolewa katika kikao” Akafunguka kwa urefu mdogo Koplo akimtizama kwa macho ya kuogopa aliye mbele yake.
“Huyo mtu anayehisiwa ni mimi?” Akauliza Hansen.
“Katika picha ambazo tumepewa kila askari katika simu yake miongoni mwake ni yako na ndiyo maana tulivyokuona tukakung’ang’ania tuondoke kwenda kwa mahojiano zaidi lakini si picha iliyowekewa msisitizo zaidi ya moja kwakuwa hiyo ni ya mtu ambaye mchoraji wa michoro ya wahalifu wa polisi aliichora akifuata maelekezo ya mke wa Inspekta”
“Mke wa Inspekta alimuona huyo mtu?”
“Ndiyo alimuona wakati anapigana na mkewe ila na yeye anasema alipokuwa akimsaidia mtuhumiwa wa uvamizi kumuingiza mumewe kwenye gari tu akajikuta anashambuliwa shingoni kupelekea kupoteza fahamu mpaka alipokuja kuzinduka akajikuta kalazwa mlango wa ndani ya sebule yake”
“Kwahiyo kwa maelezo yake tu mkaweza kumchora huyo mtu ni mwanaume au mwanamke?”
“Mwanaume wa kizungu aliyevaa vazi aina ya suti lakini maelezo ya mke wa Inspekta yaliweza kukolezwa na jibu lingine toka kwa maaskari wa ulinzi wa getini wanasema mtu yule alifika getini akiomba kutoa taarifa kuwa kapoteza begin a kila kitu chake kwa kuibiwa na dreva wa taxi ambao nao walipoonyeshwa mchoro wakasema ndiye mwenyewe”
“Naomba simu yako niione hiyo picha” Hansen akaomba aonyeshwe picha ya mtu anayezungumzwa hapa na Koplo.
“..Hii hapa..!” Koplo akatoa ushirikiano bila shuruti zaidi aliona atumie fursa kujiondoa matatizoni na yeye kunyofolewa roho kwa kile anachokiona yeye bila sababu akiwa hajui nini haswa kinaendelea katika jeshi lao la polisi toka usiku mpaka muda huo, aliona ni kama anapelekwa pelekwa kama ng’ombe tu.
Agent Hansen akachukua simu akiwa kachukua tahadhari zote kama jamaa akitaka afanye jambo jipya asilolijua yeye basi amdhibiti haraka kwa risasi moja tu ya kichwa, picha ilikuwa ni ya mzungu usoni na ni picha ya Agent Kai wa bandia akichorwa vizuri na mchoraji aliyeichora picha hii akifuata maelezo ya anayesemekana ni mke wa Inspekta Pena ambaye yeye Hansen hamjui huyo Inspekta na hajui kwanini Agent Kai amemfanya alichomfanya ikiwemo kutokujua kwanini alienda kwenye geti la kituo kikuu cha jeshi polisi akijieleza kaibiwa begi lake na vitu vingine vyote lakini alijua tayri ndugu yake ameshaanza hatua zaidi katika kazi yao iliyowaleta katika jiji hili.
Alipomaliza kuiangalia ile akasogeza pembeni kwa minajili ya kuona zingine ndipo alipojiona yeye mwenyewe katika picha inayoonekana kuchukuliwa katika video ambayo imefanyiwa ‘screanshoot’, video ambayo kwa uzoefu wake yeye Agent Hansen alitambua imechukuliwa katika ‘cctv camera’, akalichunguza eneo akagundua ni uwanja wa ndege wa Deputado Luis Eduardo Magalhae International Airport, hapo akatambua cctv camera zimechua jana wakati wameingia katika jiji hili lililopo ndani ya jimbo la kujitawala la Bahia nchiNI Brazil, hakukomea hapo akasogeza tena kushoto na kukuta ya Special Agent Rebecca nayo ikiwa imepigwa ‘screanshoot’ toka kwenye video za cctv camera zilizopo uwanja wa ndege, aliinua macho kumtizama Koplo kisha akaiweka kwenye ‘dressing table’ simu.
“Jina la aliyetoa maagizo haya tafadhali?” Akamuuliza kwa sauti ndogo ya upole baada ya kumtizama kwa sekunde kadhaa.
“Kamanda Meja Lazarous Antonio Luna, mkuu wa operesheni za dharura jimbo la Bahia..!”
“.. .. Oooh! Vizuri sana.. Kamanda Antonio.. Nitamtafuta ni mtu muhimu sana..!” Akaongea Agent Hansen akirudia jina “Inuka!” akaongea tena akimwambia Koplo.
Koplo aliinuka na kusimama pale pale akiwa kama kuku anayesubiri amri ya mfugaji kama achinjwe au ale pumba zinazosogezwa kwake.
“Geuka nyuma yako..” Amri ingine ikatoka na kutekelezwa haraka papo hapo kitako cha bastola kikakitwa katika kichogo chake akadondoka Koplo kama mzigo akiwa kazirai kwa kipigo cha ghafla.
Haraka haraka kama abiria aliyechelewa ndege Agent Hansen akabadili nguo kwa kuvua ‘tracksuit’ alizovaa akavaa suruali ya jeans bluu nyeusi ya kuiva na shati kubwa kubwa la maua maua (kama bawama) na refu linalokuja mpaka kwenye mwisho wa zipu ya suruali, alipomaliza akapaki vitu vyake katika begi akasogea mpaka dirishani akalifungua na kuchungulia kuona umbali wa toka ‘floor’ aliyopo mpaka chini alipoona akautokeza uso wake kuangalia uzuri akaliona bomba la kupitisha maji ya taka ngumu tokea ’floor’ za juu kuja za chini mpaka kwenye mashimo ambayo kwa nyuma huku ndiyo yalikuwa yapo huku kuendelea mbele kukiwa na bustani nzuri za maua na nyasi zilizokatwa kiustadi na kulifanya eneo kupendeza sana kimandhari.
Muda huu wa asubuhi inayoingia saa moja ya asubuhi toka saa kumi na mbili kulikuwa hakuna watu kabisa katika bustani hizi na hata wafanya usafi hawakuwepo hivyo haraka mwamba Agent Hansen alivuka kupitia dirishani akatokea kwenye korido nyembamba inayopita nyuma ya jengo kisha ya hapo hakuremba hakutaka atokee mtu amuone anafanya jambo hili lisiloruhusiwa litakalofanya ashukiwe na kumuingiza katika matatizo zaidi alinyosha mkono akakamata bomba ambalo lilikuwa na vumbi viganja vyake vikapokewa na vumbi hili lakini hakujali akaufyatua mwili wake toka kwenye kikorido, miguu ikanasa kwenye bomba akajiachia kutereza kuelekea chini kutoka ‘floor’ (losheni) ya sita aliyokuwepo.
Alifika chini salama wasalimini bila yoyote kumuona akajifuta vumbi kwa kukung’uta viganja vyake akaweka begi lake vizuri mgongoni akafuata yalipo maegesho ya gari ambako kulikuwa na magari kadhaa hapo akaendelea kupita kikawaida mpaka kwenye korido pana iliyomuongoza mpaka kwenye geti ambako hakumjali mlinzi aliyekuwa kalaza kichwa chake kwenye meza huku kakaa kwenye benchi kama ujuavyo kukesha usiku na mpokea zamu wake hajafika, Agent Hansen akafungua komeo la mlango mdogo kiulaini na kutereza nje ya eneo la hotel.
Hatua kumi mbele akifuata barabara kuu akatoa simu yake na kupiga namba ya Agent Kai iliyoita muda mrefu kisha ikakata akarudia tena mara mbili huku anaendelea kutembea kwa miguu kufuata barabara linavyoelekea upande wa kusini na mara simu ilipokelewa alipofanya marudio ya kama mara nne mbele.
“Nisamehe ndugu yangu.. Najua umechoka sana” Akaongea punde tu alipofahamu imepokelewa.
“hakuna shida.. Nisamehe wewe kuchelewa kupokea simu yako.. Usingizi kiboko hahaha hahahah.. Vipi kwema huko?” Akajibu Agent Kai.
“..Nimelazimika kuikimbia hotel niliyofikia kuna wateja wamezingua… Kama ujuvyo salama si salama katika simu za wateja hivyo nielekeze tukutane saa ngapi na wapi?”
“Oooh! Basi sawa.. Timu iko karibu kutimia kwa ajili ya mechi nakujulisha kwa meseji wapi tuonane kwa ajili ya maandalizi ya mechi husika nina hamu ya kujua na mengine juu ya wateja wetu kutoka kwako”
“Hata mimi nina hamu kujua juu ya mteja wako mwenye kofia..!”
“Hahaha hahaha.. Wee kweli mkali kumbe ushajua kama ana kofia.. Hatari sana lakini salama..!”
“Utanijuza basi kwa meseji wapi na wapi?” Maongezi baina yao yalifanyika kwa mafumbo kisha simu zikakatwa nami naamini msomaji hawajakuacha sana na kama wamekuacha basi yajayo yatakujulisha nini ni nini?.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na tatu (113)
Agent Hansen komando huyu wa kitengo cha ‘Special Activities Divion’ (SAD) kikosi maalumu kilichopo ndani ya shirika la kijasusi la CIA, kitengo chenye kazi ya operesheni maalumu zinazohitaji makomandoo kufanya kazi kwa siri au kwa uwazi, anafanya kazi ambayo inamfanya kumuamisha kinguvu katika hoteli aliyofikia.
Tusipoteze muda zaidi katika kupeana maana ya tayari kinachoonekana maana, twende mbele tukamalizie episode chache za dodo letu.
Alifika chini salama wasalimini bila yoyote kumuona akajifuta vumbi kwa kukung’uta viganja vyake akaweka begi lake vizuri mgongoni akafuata yalipo maegesho ya gari ambako kulikuwa na magari kadhaa hapo akaendelea kupita kikawaida mpaka kwenye korido pana iliyomuongoza mpaka kwenye geti ambako hakumjali mlinzi aliyekuwa kalaza kichwa chake kwenye meza huku kakaa kwenye benchi kama ujuavyo kukesha usiku na mpokea zamu wake hajafika, Agent Hansen akafungua komeo la mlango mdogo kiulaini na kutereza nje ya eneo la hotel.
Hatua kumi mbele akifuata barabara kuu akatoa simu yake na kupiga namba ya Agent Kai iliyoita muda mrefu kisha ikakata akarudia tena mara mbili huku anaendelea kutembea kwa miguu kufuata barabara linavyoelekea upande wa kusini na mara simu ilipokelewa alipofanya marudio ya kama mara nne mbele.
“Nisamehe ndugu yangu.. Najua umechoka sana” Akaongea punde tu alipofahamu imepokelewa.
“hakuna shida.. Nisamehe wewe kuchelewa kupokea simu yako.. Usingizi kiboko hahaha hahahah.. Vipi kwema huko?” Akajibu Agent Kai.
“..Nimelazimika kuikimbia hotel niliyofikia kuna wateja wamezingua… Kama ujuvyo salama si salama katika simu za wateja hivyo nielekeze tukutane saa ngapi na wapi?”
“Oooh! Basi sawa.. Timu iko karibu kutimia kwa ajili ya mechi nakujulisha kwa meseji wapi tuonane kwa ajili ya maandalizi ya mechi husika nina hamu ya kujua na mengine juu ya wateja wetu kutoka kwako”
“Hata mimi nina hamu kujua juu ya mteja wako mwenye kofia..!”
“Hahaha hahaha.. Wee kweli mkali kumbe ushajua kama ana kofia.. Hatari sana lakini salama..!”
“Utanijuza basi kwa meseji wapi na wapi?” Maongezi baina yao yalifanyika kwa mafumbo kisha simu zikakatwa nami naamini msomaji hawajakuacha sana na kama wamekuacha basi yajayo yatakujulisha nini ni nini?.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI VIII
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
Hali ya Pousada Solaris Hotel ilikuwa ni hali tete kwa wingi wa maaskari wa jeshi la polisi la Brazil kanda ya jimbo la kujitawala la Bahia katika jiji la Salvador waliofika hapa baada ya kupokea taarifa ya kukutwa yamefanyika mauaji ya askari wa polisi na mwingine ambaye walioanza kuona yaliyotokea katika chumba hiki walifikiri naye amefariki lakini kumbe amezirai kwa kupigwa na kitu kichwani mwake ikiwemo kutanguliwa na kugongwa gongwa kichwa chake kwa kipigo.
Maiti alitolewa ndani baada ya kushushwa toka ‘floor’ (losheni) ya sita ya ghorofa hili la hoteli ya Pousada Solaris ikiwa tayari majeruhi ambaye ni Koplo Maxillian kashaondoshwa kukimbizwa hospitali.
Simu ya kiongozi wa msafara iliita akiwa kaishika mkononi akaiinua kuangalia mpigaji ni nani ndipo akaona mpigaji ni Kamanda Antonio mkuu wa operesheni za dharura katika jeshi la polisi la jimbo la Bahia makao makuu ya jimbo hapa jijini Salvador.
“Halloo mkuu!” Akaongea baada ya kupokea huku anapiga hatua kujiondoa karibu na yalipo magari ya polisi waliyokuja nayo hapa Pousada ambako kulikuwa na kelele za kimaongezi za maaskari wengine waliokuwa kila mmoja akiongea hili na mwingine anajibu hili yote kwa yote ilikuwa ni mazungumzo juu ya yaliyotokea usiku uliopita kwa Inspekta wa polisi Fred Penambucano na haya ya mauaji ya askari mwenzao ikiwemo operesheni ya baadhi yao kupita hoteli mbalimbali zilizopo hapa jijini Salvador kusaka watu watatu ambao kila askari anayeshiriki hii operesheni alipewa picha mnato za kutembea nazo katika simu zao zenye sura za wahusika wanaohitajika na jeshi lao la polisi wakiwa wanahisiwa kuwa wanahusika na jambo lililomtokea Inspekta Penambucano.
“Halloo Koplo Jo! Mmemaliza mahojihano ya kwanza?” Swali la mpigaji lilikuwa hivi.
“Ndiyo Kamanda Antonio.. Tunataka kutoka kupeleka mwili mochwari”
“Kamera za cctv za hapo hotelini ulizoniambia mnazichunguza imekuwaje?”
“Tume copy kila tukio katika flash na jamaa anaonekana wakati anafika kuomba chumba na pia akiwa kwenye lifti yeye na muhudumu aliyekuwa anaenda kumuonyesha chumba na pia wakati anatoka kinyemela getini kamera za getini zilimchukua vizuri akiwa na begi lakeakiondoka kwa kujiamini kabisa kama hajafanya tukio baya”
“Vizuri… Nami huku nimeshapokea majibu huyo mtu ni nani? Si mbrazil kama alivyodanganya katika daftari la mapokezi na wala si mmexico ila wamepita njia ya Mexico kufika hapa Bahia, watu hao ni majasusi wa Marekani, inashangaza wenzetu hawa wamekuja katika jimbo letu bila sisi polisi kujulishwa na wala LEA, tuko katika taratibu za kujua majina yao kwa ukamilifu na wako shirika gani la kijasusi katika mashirika ya Marekani,…Hivyo nakusubiri ufike hili sote twende kwenye kikao na wenzetu wa shirika la ujasusi LEA, mkurugenzi ameomba tufike haraka pale nikamuomba asubiri niende na baadhi ya ushahidi juu ya muhusika wa mauaji haya na kujeruhi”
“Sawa mkuu! Nakuja muda si mrefu nitakuwa hapo..”Alimalizia na kukata simu Koplo Jo.
Msafara wa magari matano ya polisi yaliyofika hapa hoteli ya Pousada uliondoka na kuondoa hali ya taharuki miongoni mwa wapangaji waliokuwa wakihofu sana juu ya kulivyo.
Kwa mwendo wa kasi msafara wa magari ya polisi yote aina moja ya Land Cruiser ubavuni kukiwa na maandishi makubwa ‘POLICIA MILITAR’, walitumia dakika ishirini kutoka eneo la Rio Vermelho hadi eneo la Avenida Tancredo Neves ulipo mtaa wa Parque Bella Vista Street kunakopatikana makao ya jeshi la polisi jijini Salvador na jimbo la Bahia jengo linalofahamika kama ‘Flagant Central Civil Police Of Bahia’ pia kukiwa na makao makuu kadhaa ya majengo mengine ya kiusalama kama jengo la tawi la shirika la kijasusi la Brazil ‘Law Enforcement Agency’, kifupi mtaa huu na eneo hili kwa ujumala lilikuwa ni moyo wa usalama wa jimbo la kujitawala la Bahia lililo chini ya serikali kuu ya Brazil.
Gari ziliingia maegshoni kisha zikafanyika taratibu za kiheshima kushusha maiti ya Sajenti Bruno na kupelekwa katika chumba maalumu cha kuhifadhia (mochwari) maiti kilichopo nyuma ya jengo hili kubwa.
“Tunaweza kwenda kwenye kikao.. Tumebakiwa sisi tu kufika katika kikao cha dharura mpaka mkuu wa usalama wa raia na mali zao wa jimbo ameshafika kwa helkopta akitokea Minas Gerais kwenye mkutano wa wafanyabiashara wakuu wan chi.. Mambo mengine yote atayasimamia msaidizi wangu.. “ Maneno haya yalitoka kinywani mwa Kamanda mkuu wa jimbo la Bahia, Meja Lazarous Antonio Luna akimwambia Koplo baada ya kumalizika baadhi ya taratibu za kupeleka mwili wa marehemu katika mochwari ya kipolisi.
“Sawa mkuu niko tayari!” Koplo Jo akajibu na mara moja wakabeba baadhi ya nyaraka muhimu na kuondoka kwa miguu tu kutoka makao makuu ya jeshi la polisi mpaka ofisi za tawi la shirika la kijasusi la LEA ng’ambo ya pili tu ya barabara toka ofisi zao ambako walipofika moja kwa moja wakelekea kilipo chumba cha mikutano ambacho kwao si kigeni.
“Karibuni waheshimiwa..!” Walipewa ukaribisho punde mlango ulipofunguliwa.
“Ahsanteni sana..!” Alijibu Meja Antonio kisha kila mmoja kati yao akaenda kukaa mahala ambapo kwa cheo chake atakaa na wa rika lake kivyeo kama inavyojulikana protokali na itifaki hii kuzingatiwa katika majeshi yote duniani.
“Nianze kikao kwa kuwaombea askari waliokutwa na matatizo kuanzia usiku wa jana na mmoja kuuliwa leoi asubuhi hii na watu wasiojulikana” Alianza kuongea hivi mwenyekiti wa kikao hiki ambaye ni mtendaji mkuu wa shirika la kijasusi la Brazil LEA kanda ya tawi la jimbo la Bahia.
Wajumbe wote walioitwa kuhudhuria kikao hiki toka polisi, jeshi na hata wao wa ujasusi waliinuka na kusimama kikakamavu kuwaombea majeruhi wapate kupona haraka na marehemu pia, walifanya hivi kwa dakika moja wote wakiwa kimya kila mmoja anasali kwa imani yake kwa sauti ya ndani kwa ndani vifuani mwao kisha likapigwa kofi moja katika viganja vya mwenyeji wao kuashiria sala, swala na dua zao tayari zimefika ukomo kwa muda huu.
“Ahsanteni sana wote kwa ujumla.. Na mara moja nafikiri itakuwa busara tukianza kwa kusomewa ripoti ya mambo haya ya ajabu ya kushtukiza toka kwa Kamanda wa polisi Meja Lazarous Antonio Luna, karibu Meja!” Mwenyeji akaomba kikao kianze kwa kusomewa ripoti ya yaliyotokea huko jeshi la polisi.
Kamanda! Alieleza akisoma katika nyaraka alizoandaa zikiwa na maelezo ya kutoka kwa wasaidizi wake juu ya kilichotokea jana akianza na uendaji wa mtu asiyefahamika ukweli wake aliyejitambulisha kwa jina la Feylan Casemiro akifika katika geti la makao makuu ya polisi ambako aliwaambia aliowakuta hapo walipotaka kujua anataka nini? Kuwa anahitaji msaada kwakuwa ameibiwa begi na vitu vyake vyote, stori inayosomwa na Kamanda iliendelea kutoka kwenye maelezo ya mke wa Inspekta Fred De Luis Penambucano akieleza mapambano ya ngumi baina ya mume wake na mtu aliyevamia nyumbani kwao akitoa na wajihi wa mtu huyo yeye Mrs. Penambucano akieleza wajihi wa mtu huyo kuwa ni mzungu (ghiliba ya kuvaa sura ya bandia kwa Agent Kai lifanikiwa hapa), maelezo ya Kamanda Meja Antonio yaliendelea mbele akieleza yale ambayo mengi alikuwa ameyapata toka kwa mtu aliye shirika la ujasusi la LEA lakini yeye akiwa makao makuu ya shirika hili huko Brasilia mji mkuu wa nchi ya Brazil, huyu mtu alikuwa ni mtu mwenye mawasiliano ya moja kwa moja kutoka kwa mtu ambaye naye anafanya mawasiliano na Bwana Feca.
“..Nafikiri wote tulikuwa makini kusikiliza maelezo ya mwenzetu Kamanda mkuu wa polisi.. Naomba tujadili maelezo haya pia mwenye kuwa na swali basi atamuuliza Kamanda hapa kwa majibu sahihi maana yeye anajua zaidi yetu… Tungependa kusikia maelezo ya kutoka kwa mkurugenzi wa idara ya uhamiaji wa jimbo letu Mr. Christian Pete, je katika nyaraka zako kuna majina ya wahusika ambao kila mmoja katika meza mbele yake kuna picha za wahusika tunaowahisia wanafanya mambo haya ya kutilia mashaka usalama wa wetu kwa ujumla?” Baada ya maelezo marefu ya kutoka kwa Meja Antonio mwenyeji wa kikao hiki aliomba maelezo mengine toka kwa mkurugenzi wa idara ya uhamiaji.
“Ni kweli katika kumbukumbu zetu zinaonyesha wahusika walio katika picha hizi waliingia jana saa kumi na moja kwa ndege ya kutoka nchini Mexico jimbo la Guerrero katika mji mkuu wake wa Chilpancingo lakini watu hawa kila mmoja ana taarifa tofauti na aliyotoa mwingine, mmoja huyu ambaye inasemekana alifika makao makuu ya polisi kutoa taarifa kuwa kaibiwa na kisha kwenda nyumbani kwa Inspekta Penambucano na kufanya aliyofanya maelezo yake yanasema ni mwandishi wa habari za kimichezo wa kujitegemea wa kimexico toka jimbo la Guerrero aitwaye Manuel Mendoza amekuja hapa kwa ajili ya kuandika habari juu ya mechi ya timu taifa ya Brazil inayochezwa mwishoni mwa wiki hii na wageni wao wa timu ya taifa ya Mexico mechi ambayo imeletwa jimboni hapa Bahia katika uwanja wa soka wa Fonte Nova Stadium na huyu wa kike yeye ametoa maelezo kuwa amekuja Brazil jimbo la Bahia kumtafuta mchumba wake aliyeondoka nchini Mexico miaka miwili iliyopita, mchumba wake huyo anayemtafuta ameandika anaitwa Willian Beto Bargos huku yeye akiandika anaitwa Kelsi Maria Miguel, wote hawa passport zao zinaonyesha si mpya zimetumika mara kadhaa ndani ya nchi yao Mexico na hata nchi jirani na nchi yao kama Guatemala, Bolivia na Canada na mtu wa mwisho ambaye yeye ndiye amemuua Sajenti Bruno, passport yake inaonyesha anaitwa Alexis Silvestre Mundo huyu naye kilichomleta hapa ni mechi ya mwishoni mwa wiki lakini yeye si mwandishi wa habari za kimichezo bali yeye ni kiongozi wa shirikisho la soka jimbo la Guerrero akijipachika cheo kuwa ni makamu wa Rais wa shirikisho la soka jimbo lao…”Alitoa maelezo marefu mkurugenzi wa idara ya uhamiaji jimbo la Bahia Mr. Pete alisimama hapa ili kulainisha koo lake kwa kunywa kinywaji aina ya juisi kilichokuwa tayari kwenye glasi iliyo mbele yake kisha akatizama baadhi ya watu wanaomuangalia yeye akajifuta papi za midomo yake kujiweka tayari kuendelea na maelezo yake.
“.. Wakati napokea maswali kwa njia ya email toka kwako mtendaji mkuu wa LEA hapa jimboni kwetu juu ya watu hawa tayari uchunguzi ulikuwa umefanyika kutokana na vyanzo kugundua jamaa hawa watatu wametumia passport za bandia kuingia nchini mwetu, hivyo mpaka nakuja hapa timu yangu ya vijana watano inaendelea kuchunguza hawa watu ni kina nani? Na kwanini wameingia kinyemela jimboni mwetu na nchini mwetu kwa ujumla hivyo muda si mrefu watatupa majibu juu yao kabla hata hatujatoka hapa maana wanafanya mawasiliano na wenzetu wa Mexico na …..!” Alisimama kuongea simu yake iliyo kwenye kiganja chake muda wote ilionyesha kupokea ujumbe toka mahala kwa njia ya intaneti.
“Yah! Niliacha kuongea nikifahamu inaweza kuwa ni kile tulichotaka kusubiri toka kwa wenzetu idara ya uhamiaji Mexico… Naam! Ujumbe umefika… Awa jamaa wenzetu wa Mexico wanasema katika vitabu vyao vya kumbukumbu za kiraia hakuna sura zao wala majina yao yenye kuendana na sura hizo hivyo wao walichosema bado wanaendelea na uchunguzi ilikuwaje waghushi passport zao kuwa ni wamexico na pia wanasema siku hii ya leo mpaka jioni watakuwa washapata jibu ilikuwaje kuwaje” Mr. Pete akamaliza kuielezea meseji ndefu aliyotumiwa kwa njia ya mtandao wa whatssap, alipomaliza akainua kichwa kuwaangalia ndugu wasikilizaji wanaomsikiliza kwa umakini.
“Kesi ni ya kijasusi.. Watu awa ni majasusi na sisi hatujui kitu gani kimewaleta hapa… Lakini siku zote tunaohusika na usalama wan chi kazi ni kwetu kuzuia wahalifu kama awa kuvamia nchi yetu na kufanya vile wanavyojisikia… Uchunguzi uendelee kwa kasi juu ya watu awa nahitaji hadi usiku wa leo tuwe tushawadhibiti” Akaongea mtendaji mkuu wa LEA.
“Kazi ni kwetu kama usemavyo .. Hii ni pasua kichwa sana ila lazima tufanye jambo.. Askari polisi wanaohusika na kesi za kiuchungzi watatakiwa kutapakaa kila kona kwa ajili ya kupeleleza pia na mimi nitateua vijana wangu wawili kwa ajili nao wafanye hii kazi, nitaomba nawe mtendaji wa LEA uteue watu wa kazi angalau watatu waungane na wa kutoka ofisni mwangu, tuwape siku mbili kuifanya hii kazi kwa ushirikiano baina yao… Watatakiwa kupekua kila kona ya Salvador kuwapata watu hawa kisasi cha jino kwa jino..” Mkuu wa watu wote waliopo hapa ambaye kama ingekuwa jimbo hili ni nchi basi yeye angekuwa waziri anayehusika na usalama wan chi kwa ujumla lakini bwana huyu hapa jimboni ni mwakilishi wa waziri wa mambo ya usalama wan chi akiwa amechaguliwa kushika cheo hiki na gavana anayetawala jimbo hili la Bahia na kila jimbo lina mtu kama yeye kisheria hapa akiitwa mkuu wa usalama wa raia na mali zao, hili aliloongea hapa lilikuwa ni amri sasa kwa wanaomsikiliza.
“Sawa mkuu! Binafsi nitatelekeza kila kitu kwa wakati na kama bado wapo ndani ya mipaka ya jimbo hili haraka tutawatia mikononi mwetu..!!” Mtendaji mkuu wa LEA alikubaliana na walichoambiwa akaendelea mbele kwa kuwashukuru wahusika wote kutii amri kufika katika kikao hiki kilichofanyika katika chumba cha mikutano kilichopo katika majengo ya ofisi zake.
Wahusika wa kikao walitoka kikaoni wakiwa na shuhuku ya kutimiza kila kitu kilichoongolewa na kutolewa na maamuzi akiwemo Kamanda Lazarous Antonio Luna ambaye yeye ni mmoja wa watu wa malipo walioingizwa ndani ya mkumbo mmoja na Inspekta Peaambucano ila yeye alikuwa akiwasiliana na Pena au afisa wa LEA aliyeko huko makao makuu ya nchi Brasilia mabaye naye sasa ilikuwa hapeleki mawasiliano kwa Inspekta kwa kuwa ni majeruhi bali alipata mtu ambaye aliweza kuwa anawasiliana naye akiwa ni rafiki yake aliyeko LEA Bahia.
Hivyo Kamanda Lazarous Antonio alipotoka kikaoni aliagana na Koplo Jo aliyetakiwa kurudi naye makao makuu ya jeshi la polisi kuwa anaelekea hospitali kumuona Inspekta Penambucano ikiwepo na nia ya kupata wasaa wa kutuma ujumbe wa kikao walichotoka kwa afisa wa LEA aliye Brasilia.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na nne (114)
Vikao vya kutaka uchunguzi ufanyike kujua nini ni nini katika jiji la Salvador vimefanyika katika ofisi za ‘Bahia Law Enforcement Agency’ umefanyika na kupitishwa maamuzi kuwasaka watu wanaosemekana ndiyo haswa wanahusika na mauaji ya askari mmoja wa polisi na pia kutoa kipigo kilichowaumiza maaskari wawili na kuwa hoi bin taabani.
Je? Vikao hivi vitaleta tija kwao kutimiza kutumika kwao kuwalinda wahalifu waliokuja kujificha nchini mwao bila ya wao kujua wala kupenda.
Nini kitatokea kwa kikosi kazi kinachoongozwa na Agent Kai?
Twende tumalizie dodo asali kwa mapigo ya kisasa katika sehemu chache zilizobaki kumaliza ‘JINO KWA JINO’.
“Kazi ni kwetu kama usemavyo .. Hii ni pasua kichwa sana ila lazima tufanye jambo.. Askari polisi wanaohusika na kesi za kiuchungzi watatakiwa kutapakaa kila kona kwa ajili ya kupeleleza pia na mimi nitateua vijana wangu wawili kwa ajili nao wafanye hii kazi, nitaomba nawe mtendaji wa LEA uteue watu wa kazi angalau watatu waungane na wa kutoka ofisni mwangu, tuwape siku mbili kuifanya hii kazi kwa ushirikiano baina yao… Watatakiwa kupekua kila kona ya Salvador kuwapata watu hawa kisasi cha jino kwa jino..” Mkuu wa watu wote waliopo hapa ambaye kama ingekuwa jimbo hili ni nchi basi yeye angekuwa waziri anayehusika na usalama wan chi kwa ujumla lakini bwana huyu hapa jimboni ni mwakilishi wa waziri wa mambo ya usalama wan chi akiwa amechaguliwa kushika cheo hiki na gavana anayetawala jimbo hili la Bahia na kila jimbo lina mtu kama yeye kisheria hapa akiitwa mkuu wa usalama wa raia na mali zao, hili aliloongea hapa lilikuwa ni amri sasa kwa wanaomsikiliza.
“Sawa mkuu! Binafsi nitatelekeza kila kitu kwa wakati na kama bado wapo ndani ya mipaka ya jimbo hili haraka tutawatia mikononi mwetu..!!” Mtendaji mkuu wa LEA alikubaliana na walichoambiwa akaendelea mbele kwa kuwashukuru wahusika wote kutii amri kufika katika kikao hiki kilichofanyika katika chumba cha mikutano kilichopo katika majengo ya ofisi zake.
Wahusika wa kikao walitoka kikaoni wakiwa na shuhuku ya kutimiza kila kitu kilichoongolewa na kutolewa na maamuzi akiwemo Kamanda Lazarous Antonio Luna ambaye yeye ni mmoja wa watu wa malipo walioingizwa ndani ya mkumbo mmoja na Inspekta Peaambucano ila yeye alikuwa akiwasiliana na Pena au afisa wa LEA aliyeko huko makao makuu ya nchi Brasilia mabaye naye sasa ilikuwa hapeleki mawasiliano kwa Inspekta kwa kuwa ni majeruhi bali alipata mtu ambaye aliweza kuwa anawasiliana naye akiwa ni rafiki yake aliyeko LEA Bahia.
Hivyo Kamanda Lazarous Antonio alipotoka kikaoni aliagana na Koplo Jo aliyetakiwa kurudi naye makao makuu ya jeshi la polisi kuwa anaelekea hospitali kumuona Inspekta Penambucano ikiwepo na nia ya kupata wasaa wa kutuma ujumbe wa kikao walichotoka kwa afisa wa LEA aliye Brasilia.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI IX
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
“Mpango wetu unaweza kuwa sawa lakini sisi hatuwezi kuwa sawa katika hali kama hii.. Hoteli zote zimekuwa zikifanyiwa misako kila muda ya kusaka watu wasiotujua vizuri hasa katika sura zetu halisi hivyo kufika kwenu imekuwa msaada kwetu kwakuwa nyinyi si watu shukiwa kama ilivyo kwetu sisi.. Ahsanteni sana kwa kufika kwa wakati pia karibuni kazi imeanza karibuni tufunge kazi ndugu zetu..!” Maneno toka kwa mtu ambaye ungemuona ungesema na mmama fulani kama si bibi aliyevaa gauni refu jekundu lenye madoa madoa madogo dogo meusi kichwani akiwa kavaa kiremba kilichofungwa kama hijabu na kuacha uso wak tu unaoonekana kama mama mtu mzima, mtu huyu kiundani ni Special Agent Rebecca akiwa kajibadili uso wake kuwa uso wa mama anayekimbilia kwa kasi uzee.
Watu sita walikuwa wapo kwenye kikao katika moja ya mkahawa maarufu kwa utoaji huduma bora katika vinywaji vya vifungua vinywa asubuhi kama kahawa, chai na juisi za aina mbalimbali, mkahawa huu uitwao Coffee Town Salvador uliopo mtaa wa Sete De Setembro ulio eneo la Vitoria, eneo lililo kando kando ya fukwe za bahari.
“Unamaanisha hata mkiwa katika sura hizi mlizozivaa leo wanaweza kuwashtukia? Nafikiri inaweza kuwa ni njia sahihi kwa nyie kubadilika badilika na kubadili badili hoteli katika sura hizo za kubadilika.. Hongera kwenu nyote kwa kazi iliyofanyika usiku uliopita kiasi ya kulitia katika hali ya taharuki jeshi la polisi la hapa ambalo kwa maelezo aliyoeleza Agent Kai wanaonekana wanahusika katika kulinda uwepo wa TRJ hapa Bahia..!” Aliongea mwanadada mrembo mchanganyiko wa damu ya kizungu na afrika (chotara) Agent Jade Poul Brown, Jasusi mfika asubuhi hii kutokea Mexico akiwa kaongozana na wenzake wawili ambao wote pamoja nao walisafiri kwa pamoja na kina Agent Kai kutokea Marekani kisha kushushwa kwa kujirusha angani kwa parachuti katika misitu ya milima Tuxtla nchini Mexico lakini ilipofika wakati wa kuja huku Brazili waliamua kwa pamoja kujigawa katika makundi mawili ya watu watatu watatu, watatu wa kwanza kutangulia kwa usafiri wa ndege wa moja kwa moja toka jimboni Guerrero hadi hapa Bahia na hawa kina Jade walipitia safari ya ndege ya abiria shirika lingine iliyowatoa Guerrero hadi Mexico City ambako napo wakachukua ndege ingine toka pale mpaka Rio De Janeiro ambako wakapumzika kidogo kisha alfajiri ya siku hii wakachukua usafiri wa treni ya mwendokasi iliyowaleta hapa Salvador, Bahia na sasa wako kikaoni hapa Coffee Town Salvador.
“Kwa haraka kilichopo mbele yetu ni kufuata vile connection inavyohitaji… Kwa maelezo aliyokuja nayo mwenzetu Agent Hansen jinsi alivyopambana na askari wa jeshi la polisi na ukijumlisha niliyokutana nayo mimi utaona ni kuwa njia iliyopo kufika tunapotaka ni maaskari wenyewe na ni kwa sababu wanashirikishwa katika hili kwa makusudi au kwa bahati mbaya… Kwa kuanzia tutahitaji kuendelea na pale tulipoishia usiku uliopita na asubuhi hii.. Tutagawana majukumu kwa haraka kwa kila mmoja au kwa watu wawili wawili” Alianza maelezo kamanda wa msafara wao kutoka Marekani mpaka Mexico kisha kuja hapa Salvador, Bahia Mr. Kai Hamis jasusi na mpelelezi wa CIA mwandamizi na mbobezi, alisimama kuongea kisha akazungusha shingo huku na huko kuwaangalia wanaomsikiliza.
“…Nawaamini wote na ndiyo maana kila napopata kazi ambayo mimi au mwingine kati ya waanzilishi wa operesheni fulani ikiwa ambapo tunaona kuna ugumu wa kazi uwa nateua mmoja au wawili kati yenu au hata watatu na mara nyingine wote kati yenu kutegemea na ukubwa wa operesheni au ugumu wa kazi ya wahusika tunaotakiwa kuwachunguza na kupambana nao… Na pia nashukuru kwa jinsi mnavyoniamini mimi pia pale mmoja wenu au kati yenu anapokuwa na usumbufu wa kazi fulani anayohisi ina umuhimu wa Kai kuwemo basi uwa hamsiti kuniambia kwa kutaka ushauri au kuingia kufanya kazi hiyo… Nimesema haya kwa sababu nataka tugawane majukumu ili ifikapo kesho ama keshokutwa tuwe njiani kurejea Marekani na hadithi ya ushindi tukiwa tumempiga pingu za kijasusi adui mkuu wa sakata ili.. Katika kazi yetu hii kuna mwenzetu ambaye mimi ndiyo najua umakini wake pamoja na ufanisi wake wa kazi huyu ni Special Agent Joseph Simone Silla kama nilivyokwisha wafahamisheni mwanzo kuwa tutakuwa naye hivyo yoyote atakayepangwa atambue amepangwa na mtu mzoefu wa kazi na fundi kama yeye” Aliendelea Agent Kai alipoona wote wanamtizama kwa umakini ingawa watatu kati yao walikuwa wamevaa miwani meusi unayoweza idhania ni miwani ya jua ikipendwa sana kuvaliwa na watu wanaokuwa wameenda kupumzika ufukweni, kunyamaza kwake iliwapa fursa wengine nao kulowanisha makoo yao kwa vinywaji ambavyo kila mmoja alikuwa ameagiza kile ambacho ataona ni muhimu yeye kunywa asubuhi hii.
“Upande wangu Bwana Kai! Kiukweli navutiwa sana na ufanisi wako kazini hivyo shukrani na wewe kwakuwa unavutiwa kufanya kazi na kila mmoja kati yetu… Weka mkakati mchana wa leo tu tutakuwa tushapiga hatua ndefu kumkaribia adui.. Karibu!” Akaongea Detective Omar Chilamwena kijana wa makamo yanayolingana na Agent Kai na mtu wa asili ya bara la Afrika kama alivyo Kai akitokea nchi ya Kongo ambapo akiwa mdogo kabisa waliamia na wazazi wake kama wakimbizi watafuta hifadhi hivyo huyu bwana ni mkongomani mmarekani kwakuwa alifika Marekani akiwa mdogo kabisa akasoma na kupita mafunzo mbalimbali ya kijeshi mpaka walipokutana na Kai katika mafunzo ya ukomandoo na ndipo urafiki wao ulipoanza.
“Sawa sawa!... Mbele yetu kwa muda huu tuna kazi tatu za kuanza nazo… Kwanza kila mmoja aangalie hizi picha nilizoweka katika ipad yangu” Aliongea tena nahodha wao kisha akampa mkononi S.A Rebecca apokee Ipad yakekuangalia hizo picha ambaye naye alipomaliza kuangalia kwa dakika moja alipasia kwa aliye pembeni yake.
“Angalieni zote zilizoongozana kisha nitarusha picha hizo kwa watu ambao tutawapa kazi ya kufuatilia watu iwe mimi mwenyewe au mwingineyo yoyote kati yetu timu.!” Aliongea tena TSC kisha akanywa kahawa chungu isiyochanganywa na chochote hii ikiwa anapunguza makali ya usingizi ikizingatiwa usiku uliopita ulikuwa usiku mrefu kidogo.
“Tayari kila mmoja kawaona hao watu… Hao watu ndiyo watu waliotuwai mimi na Rebecca kumchukua mke wa Feca dakika chache za mbele yetu kabla hatujafika mtaa husika.. Awa watu watakuwa muongozo wetu kufika tunapopataka hivyo kwa muonekano wao wa haraka nafikiri tutatakiwa kupita mitaa ya wahuni tukiwa na picha hizi kununua habari zao na kwa ushauri wangu wa haraka naomba kazi hii ifanywe na Agent Jade Poul Brown na Agent Hansen, mtajibandika tattoo za stiker ambazo uwa tunajibandika kwa kazi kama hizi za kujichanganya na wahuni kuteka habari zao, nitarusha picha hzi kwa kila mmoja wenu” Maelekezo yaliendelea kutolewa.
“Jukumu letu lingine lililo katika mgawanyo wa kazi ni kuwa tutatakiwa kumpata Kamanda wa jeshi la polisi wa jimbo hili, huyu mtu anaonekana anajua jambo kwakuwa jina lake ndiyo jina tajwa lililohusika kusemwa kwa Agent Hansen kuwa alitoa taarifa sura za watu watatu walioingia jioni katika jimbo hili watafutwe, kazi hii nafikiri itafanywa na Detective Omar pamoja naye Special Agent Silla lakini mimi na Rebecca tutakuwa na kazi ya kila mmoja wetu kuwa tayari muda wote kuongeza nguvu kwa makundi yenu mawili kwa dharura ya aina yoyote ile itakayowatokea wakati mnatimiza wajibu..!” Nahodha alisimama akawaangalia kwa zamu watu walio kimya kumsikiliza huku wengine midomo yao ikitafuna nyama na mara nyingine kunywa kidogo vinywaji vyao.
“Kama kuna mwenye swali juu ya kazi hizi liulizwe mara moja..!” Alimalizia kuongea hivi Agent Kai na kujiweka vizuri katika kiti cha kulala chenye kitako cha kitambaa kizito (turubai).
Wanaume hawa waliendela kukaa hapa kwa nusu saa mbele wakiongea mambo ya kazi na kupanga mengi zaidi itakavyokuwa kisha timu mbili zinainuka zikiwaacha timu moja iliyozoeana sana (Agent Kai ‘TSC’ na Special Agent Rebecca ‘Reby’.
***** ***** *****
Salvador De Bahia Nightlife Club, Bar & Tips hapa ndipo moyo wa birudani ndani ya jiji la Salvador na jimbo la Bahia kwa ujumla, hakuna sehemu ambayo muda wote uwa imechangamka huwezi kupakuta kumefungwa zaidi ya kupungua tu kwa watu katika mida ambayo ni asubuhi kwenda mapaka saa sita ya siku husika, ipo katikati ya eneo maarufu la Pelourihno.
Kama utafika jimbo la Bahia hususani mji mkuu huu wa jimbo wa Salvador na wewe ni mtu wa kupenda burudani na starehe mbalimbali bila ya kufika hapa basi itakuwa umefika kisha ukafungiwa ndani ya nyumba na wenyeji wako usitoke kwenda popote, hapa ndipo ambapo kunakuwa na madj wakali na bora sana katika kutoa burudani ya miziki kuna Dj wawili maarufu sana ndani ya Brazil kwa ujumla kwakuwa walishashinda mara kadhaa mashindano ya kuwashindanisha madj kama DJ Sankofa na DJ Vasco wakipiga miziki ya wanamuziki bora duniani na mizki mingine kama miziki ya Carribean na mengineyo iliyo maarufu ulimwenguni.
Watu wa jinsia mbalimbali wakiwemo machangudoa (wadada wauza miili yao) na hata mashoga wenye laana waliokuwa hawakosekani karibu kila mshale wa saa unavyosogea iwe mchana iwe usiku walikuwa wapo hapa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wao wanaume wapenda mambo ambayo wao wanayauza kupitia miili yao waliyoigeuza kuwa kitega uchumi, wakiwa katika ukumbi mkubwa kati ya miukumbi mbalimbali iliyo katika floor mbalimbali zinazounda hii casino ambazo zimejipanga kwa ‘grade’ maana hii ya kwanza inayopatikana ukiingia tu baada ya kulipa kiingilio huwezi kukuta mtu anacheza uchi.
Wakiwa wanaendelea kucheza michezo ya pool na mengineyo inayohusika na kamari, wengi wao waligeuza shingo kuangalia walipoona wenzao wengine wanaangalia, katika lango kuu waliingia mwanamke mrembo akiwa kaongozana na mwanaume ambaye naye si haba machoni mwa kila anayewaangalia aliona wamependeza sana, mwanamke akiwa kavaa sketi nyekundu fupi ya kumfika magotini kikoti cha jeans kisicho na mikono (kawoshi) kikiwa cha rangi ya bluu panapo na vifungo hakukufungwa hivyo kumuonyesha kitovu chake kizuri kwenye tumbo lake pamoja na sidiria yenye rangi ya kufanana na kisketi chake cha rangi nyekundu, mwanaume naye akiwa na michoro karibu mwili mzima (tattoo) kama ambavyo vijana wengi wa kihuni na hata baadhi ya wengine walio wastaarabu upenda kujichora michoro na imekuwa kama tamaduni katika nchi za Amerika Kaskazini, kusini na hata kati.
Mwanamke akitembea kwa mwendo wa maringo akiwa amependeza haswa mkono wa mwanaume aliyeongozana naye ukiwa umekamata kiuno ulifanya baadhi ya watu walio mule ndani katika ukumbi wa kwanza uingiapo katika club hii, kuchukuliwa muda wao kwa macho yao kugeuka kuwaangalia watu hawa walioonyesha dhahiri shahiri kuwa ni wapenzi, walitembea wakiwa wanaamini wameteka ‘attention’ ya robo ya watu waliokuwa hata kama wanaendelea na mambo yao lakini kwa chati walilazimika kuchungulia kijicho pembe wapendanao hawa.
Walisogea hadi kwenye viti vilivyozunguka meza moja yenye mtu mmoja mwanaume aliyekalia kiti kimoja akiwa kageuza mgongo walipotoka wao hivyo yeye hakuwa amewaona watu hawa lakini walipokuwa wakivuta viti wapate kukaa akageuka kuwaangalia.
“Habari yako?” Akasalimu mwanaume punde alipokaa kwenye kiti na papo hapo akaondoa miwani yake toka machoni.
“Safi… Karibuni!” Akajibu mtu huyu kisha akanyanyua glasi yenye kimiminika akanywa kilichomo chote.
Muhudumu alifika kuwauliza wageni wanahitaji kitu gani kati ya vitu ambavyo vinapatikana katika club hii muda huu wa saa tano na robo asubuhi inayoishia.
“…Mliipenda hii meza au mlikosa meza nyingine za nyie kwenda kukaa mkaongea kwa utulivu zaid?” Swali likaulizwa na waliyemkuta kwenye meza.
“Kwanini? Kwanini bwana mkubwa?”Baada ya kujibu swali muulizwa swali naye aliuliza swali akiwatizama kwa zamu anaowauliza.
“Tumevutiwa na kukaa hapa kuliko kukaa katika meza nyingine… Utusamehe kwa hili lakini pia vile vile ni muhimu kwetu kama wanadamu kujuana na kupeana ushauri wa kimawazo.. Samahani sana mkuu..!” Akajibu mwanaume huku anatabasamu tabasamu ambayo ilikenua mdomo na meno yakiachwa yaonekane dhahiri ikiwa ni mkausudi alitaka mtu yule asiishie kuona madini yake aliyovaa shingoni nia yake ilikuwa aone meno yake aliyoyapachika vito vya madini aina ya almasi yaking’aa na kuwaka waka.
“..Sawa karibuni ila sitawapisha kamwe kuongea mambo yenu mi napumzika zangu hapa na sitaki karaha kama mtaongea ongeeni taratibu msiharibu fikra zangu na ndiyo maana mnaona nimeachwa peke yangu bila mtu mwingine kuwepo karibu hapa..!!” Onyo lilitoka kwa mwenyeji wa meza akiwa ‘serious’ na anachoongea.
“… Hatari lakini salama.. Sawa tutajitahidi kufanya hivyo utakavyo.. Naitwa Eder Vinicius na huyu mpenzi wangu anaitwa Lina Oriola, sisi ni wageni katika jiji ili la Salvador hususani hapa Club, tunaomba uagize chochote utakacho kwa bili yetu pia si vibaya tukikujua mwenzetu unaitwa nani? Kisha ya hapo utaendelea na utulivu wako hatutakubughudhi kwa chochote” Mwanaume aliona afanye utambulisho wao, huu ulikuwa ni utambulisho wa majina ya uongo kama zilivyo sura zao kuwa ni za uongo kutokana na kuwa walikuwa wamevaa sura za bandia usoni mwao, mwanaume akiwa ni Agent Hansen Blade na mwanadada anayesababisha wanaume wengi wakware kuwakatia shingo kila wakati alikuwa ni Agent Jade Poul Brown.
“Nyie mna pesa nyingi sana? Mnatokea jimbo gani hapa Brazil?” Mtaka utulivu pamoja na kuwa alitakiwa kujibu jina lake aliloulizwa yeye aliomba kujua mengine kabisa kwa kuuliza hivi.
“Tunatokea Sao Paolo.. Lakini hata hivyo mimi binafsi natokea Colombia mji wa Cali nafanyia biashara zangu huko huku Brazil ndipo nyumbani kwa wazazi wangu nyumbani kwangu kiuraia na mpenzi wangu yeye anaishi huko Sao Paolo nimekuja kwa ajili ya sherehe ya kumvisha pete ili tuelekee kwenye ndoa yetu mwakani” Akajibu Agent Hansen au Eder Vinicius wa bandia.
Jamaa alitoa miwani yake ya rangi ya kijani aliyovaa machoni mwake na kumtizama vizuri anayeeleza akavutiwa na jambo akanyanyua glasi ya kinywaji akanywa funda mbili tatu za kuongozana.
“Sawa! Naitwa Alvaro Mendes.. Mimi pia si mkazi wa hapa Salvador ingawa ni nyumbani kwa kuzaliwa, nimekuja hapa Club kupoteza mawazo kidogo sababu sitaki kuonekana huko mitaani kuna mambo yananichanganya kidogo” Sasa jamaa hakuona sababu za kuzunguka na kuwa mbishi mbishi akaongea hivi akijitambulisha kwa jina aliloona kwake sahihi kujitambulisha hivyo lakini kiukweli haitwi jina hilo na pia ni mkazi wa hapahapa Salvador, Bahia.
“..Oooh! safi sana.. Pole sana kwa kutokuwa sawa” Akatoa pole Hansen, wakati huohuo mwanadada Jade alijifanya yuko bize katika simu yake akichat na mtu kisha akamuangalia mpenzi wake wa bandia, walipoangaliana wakatabasamu wote.
“.. Hivi huyu mtu tutampataje? Maana sasa naanza kuchoka mpenzi wangu..!” Akaongea Agent Jade akimuuliza swali Agent Hansen wakiwa wanaangaliana.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na tano (115)
Kikosi kazi kinachoongozwa na Agent Kai tayari kimekamilika na tayari wamegawana majukumu kuona kazi inafanyikaje.
Agent Hansen na Agent Jade wako Salvador De Bahia Nightlife Club, Bar & Tips wakianza kuwinda bila kujua windo lao ni lipi haswa lakini wao wanapapasa kuona kipi watashika huku wakitegemea hasa picha walizopewa na Agent Kai.
Nini kitafuatia?
“Nyie mna pesa nyingi sana? Mnatokea jimbo gani hapa Brazil?” Mtaka utulivu pamoja na kuwa alitakiwa kujibu jina lake aliloulizwa yeye aliomba kujua mengine kabisa kwa kuuliza hivi.
“Tunatokea Sao Paolo.. Lakini hata hivyo mimi binafsi natokea Colombia mji wa Cali nafanyia biashara zangu huko huku Brazil ndipo nyumbani kwa wazazi wangu nyumbani kwangu kiuraia na mpenzi wangu yeye anaishi huko Sao Paolo nimekuja kwa ajili ya sherehe ya kumvisha pete ili tuelekee kwenye ndoa yetu mwakani” Akajibu Agent Hansen au Eder Vinicius wa bandia.
Jamaa alitoa miwani yake ya rangi ya kijani aliyovaa machoni mwake na kumtizama vizuri anayeeleza akavutiwa na jambo akanyanyua glasi ya kinywaji akanywa funda mbili tatu za kuongozana.
“Sawa! Naitwa Alvaro Mendes.. Mimi pia si mkazi wa hapa Salvador ingawa ni nyumbani kwa kuzaliwa, nimekuja hapa Club kupoteza mawazo kidogo sababu sitaki kuonekana huko mitaani kuna mambo yananichanganya kidogo” Sasa jamaa hakuona sababu za kuzunguka na kuwa mbishi mbishi akaongea hivi akijitambulisha kwa jina aliloona kwake sahihi kujitambulisha hivyo lakini kiukweli haitwi jina hilo na pia ni mkazi wa hapahapa Salvador, Bahia.
“..Oooh! safi sana.. Pole sana kwa kutokuwa sawa” Akatoa pole Hansen, wakati huohuo mwanadada Jade alijifanya yuko bize katika simu yake akichat na mtu kisha akamuangalia mpenzi wake wa bandia, walipoangaliana wakatabasamu wote.
“.. Hivi huyu mtu tutampataje? Maana sasa naanza kuchoka mpenzi wangu..!” Akaongea Agent Jade akimuuliza swali Agent Hansen wakiwa wanaangaliana.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI X
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
“.. Na ulisema ndugu yake alikwambia muda mwingi uwa anapatikana hapa au?” Agent Hansen alikuwa fundi wa maneno ya uongo uongo anapokuwa anataka lake pia hata Agent Jade Poul alikuwa fundi kwa mambo haya, hapa walikuwa wanajaribu kete ambayo itasababisha kutega ulimbo hatimaye kumnasa wanayetamani kumnasa.
“Ndivyo alivyosema..Tuvute subira kumsubiri kwakuwa mzigo wake hatutakiwi kumpa mtu mwingine zaidi yake na hapa Club hii ndipo anapopenda kuja mara kwa mara, acha tupige vinywaji… Kaka samahani kwa kukiuka makataba wako nasi uliosema hatutakiwi kukupigia makelele kwa mazungumzo yetu, sisi…!” Agent Jade alijibu swali aliloulizwa na mwenzake kisha akaamisha mazungumzo kuelekea kwa kijana wa kibrazil aliyewakareibisha kwenye meza huku akiwaongopea kila kitu walipotaka kujua kuhusu uwenyeji wake lakini hakuweza kumalizia alichohitaji kumalizia muhudumu aliyeitwa na bwana huyu wa kibrazil alifika, ikabidi achukue maagizo toka kwa wote kisha akaondoka.
“Usijali kaka… Huduma ya kila kitu tutakulipia kwakuwa umekuwa kama mwenyeji wetu sasa” Jade akaendelea kusambaza ulimbo.
“Shukrani sana dada yangu, sijui shemeji yangu..!” Akashukuru mwenyeji.
Haikuchukua dakika nyingi muhudumu akarudi akiwa na chano yenye vinywaji alivyoagizwa na watu hawa watatu.
Dakika mbili mbele ukimya ulivunjwa kwa mtu mmoja aliyekuwa kapita pembeni ya meza yao akampungia mkono huyu mwanaume aliyejitambulisha jina anaitwa Alvaro Mendes, jamaa hakukaa hapa bali alisogea kwenye stuli ndefu za kaunta, Agent Jade alijifanya anamtizama sana kana kwamba kamfananisha na mtu kisha akageuka kumtizama Alvaro, wakaangaliana.
“Kuna mtu namtafuta amefanana na huyu aliyekusalimia, huyu anaitwa nani jina lake?” Jade akamuuliza Alvaro akimkazia macho bila kupepesa huku sura yake ikionyesha uhitaji mkubwa wa kupata jibu zuri toka anayemuuliza.
“Huyo unayemtafuta anaitwa nani?” Alvaro hakujibu swali bali naye alileta kama zile tabia walizonazo watanzania wengi ‘kutojibu swali aliloulizwa anataka yeye naye aulize swali kwanza ndiyo ajibu swali’.
“Marcos Bernado! Vipi ndiyo yeye?”
“Si yeye! Sababu huyu ni mdogo wangu anaitwa Ricardo Emanuel..!” Akajibu huku anaelekeza kidole upande alipo jamaa bila kujali amekaa stuli ndefu akiwaangalia wao.
“Dah! Unaongea na kidole mpaka mwenyewe ajue namuongelea yeye, rafiki vipi bwana, huoni unatuuza kwa ndugu yako?”
“Siwauzi! Mdogo wangu hana tatizo yuko poa sana usihofu.. Mnayemtafuta ni nani? Maana kabla sijaamua kuwa niongee na nyinyi vizuri tu licha ya kuingilia kikazi chetu mimi na mdogo wangu ambapo tulikuwa na makubaliano tukutane hapa muda huu wa saa tano, nilikusikia ukisema kuwa ndugu yake kakwambia uwa anapatikana hapa mara kwa mara..!” Taratibu Alvaro kwa jina alilojitambulisha aliingia kwenye mstari ambao Agent Jade alikuwa akimpeleka bila yeye kujua, aliinua simu yake ya mkononi iliyo juu ya meza waliyoizunguka kisha akaondoa ‘pattern’ akafungua ‘gallery’ na kuchagua moja ya picha ambazo alirushiwa na Agent Kai zikiwa na watu waliofika kumuokoa mke wa Feca, Madam Millian.
Alikuza kwa vidole vyake akitanua katika skrini kisha akamuonyesha mmojawapo bila kujali wala kuweka chaguo maalumu.
“Huyu hapa, huyu hapa Marcos Bernado…!” Akaongea Jade akijifanya ana shauku vidole vikimsaidia kugonga juu ya kioo cha simu yake.
“… Sasa dada! Huyu ndiyo kafanana na ndugu yangu?” Alvaro akauliza akiendelea kuangalia katika skrini simu ikiwa katika viganja vya Jade, swali lake lilifanya majasusi hawa kuangaliana kwa chati kisha kila mmoja kurudi ilivyokuwa.
“Huoni? Urefu na wanavyonyoa kipara.. Kama unamjua nisaidie kujua nampata wapi? Nitakulipa kidogo dogo sababu mume wangu amechoka kuzunguka nami kunisaidia kumpata huyu kaka yangu”
“..Katika picha hii nawajua watu watatu kati yao watano.. Huyu pia nishawai muona hapa mara mbilli mara tatu..!” Chaguo la Jade lilikwenda mrama kwakuwa aliyemlenga hakuwa anafahamika au kujulikana kisura kwa ‘Alvaro’.
“Lakini hakijaharibika kitu kunielekeza mmoja tu kati ya hawa anaweza kutusaidia mimi na mume wangu kujua tunampataje Marcos nitakulipa vile vile kama nilivyoahidi..!” Akabembeleza Agent Jade akimuangalia machoni ‘Alvaro’.
“Je naweza kuwauliza swali moja tu?” ‘Alvaro’ akaongea akiacha angalia kioo cha simu kisha kuupweteka mgongo wake kwenye kiti, nywele zake nyingi za kizungu zikamwagika nyuma ya kiegemeo alichoegemea.
“Uliza tu!” Kwa mara ya kwanza Agent Hansen akaingilia maongezi ya wawili hawa kwa kujibu yeye haraka akiwa na shauku kubwa sana kuona yanatimia haraka katika anayotaka yatimie, mwanaume huyu kuwatambua watu watatu katika picha yao ni mafanikio makubwa kwao.
“Mnamtakia nini huyo mnayemtafuta?” Akauliza akiwatizama kwa zamu kisha kinywaji kilicho kwenye glasi kikabugiwa chote wakati anabugia kimiminika hiki ikatumika fursa kwa majasusi hawa kuangaliana kwa wizi na kupeana ishara katika macho yao ambayo sasa wote hawakuwa na miwani waliyokuwa wameivaa wakati wanaingia hapa Nightlife Club.
“Kikawaida tu.. Kawaida tu kwani hatutakiwi kumtafuta ndugu yetu?” Akajibu na kuuliza Agent Jade huku anafungua kipochi kidogo cha kike ambacho wanawake wengi upenda kuwa wanavibana chini ya makwapa yao wanapotembea kwa madaha na maringo, ndani ya kipochi alitoa noti mbili za dola mia mia akaweka juu ya meza kisha akakifunga kipochi chake (uchawi huu).
“..Dola mia mbili! Dola mia mbili nikisema wanapatikana wapi hawa watu?” Akahoji ‘Alvaro’.
“….Ndiyo rafiki! Au unaonaje? Tuna siku mbili tuko ndani ya jiji hili la Salvador tunamtafuta huyu mtu… Mama yake amepatwa na pararaizi huko nyumbani Sao Paulo na amesisitiza anataka amuone mwanae kwa kuongea kwa tabu sana na ishara na huyu ni mtoto wake pekee wa kiume” Akaingilia tena Agent Hansen akiunyoosha uongo kiurefu kidogo mpaka kimoyomoyo (kifuani) Agent Jade akatabsamu kichwa chake kikatingishika kuunga mkono.
“Hawa watu ni genge dogo lakini ni hatari sana hapa Salvador ni watemi kupitiliza wenye kuogopewa na ni miaka mingapi toka huyu mtu aondoke huko kwa mama yake?” Akajibu kimatumaini zaidi kisha akauliza swali akijua ni kweli aliyoambiwa na Hansen.
“Zaidi ya miaka mitatu hajafika Sao Paulo na kama anafika basi hafiki kwa mama yake ambaye ni mama yangu mdogo na ni mama mlezi wangu aliyenilea mimi ni dada wa marehemu mama yangu mzazi huyo mama yake” Agent Jade naye si haba katika mambo ya uongo na kwakuwa kazi yake ni kazi aliyo na uzoefu nayo wa miaka mingi uongo kwake ni sekunde tu kuuunda bila kupepesa macho.
“Kama nilivyokwisha kusema, ndugu yako hapo alipo si mtu wa kawaida tena ni mtu ambaye ana roho ya kiuaji na nimeshangaa kuona mna picha inayoonekana mmeipiga kwa njia ya simu na kwa kuibia kwa uzoefu wangu wa mambo kihalifu” Akaongea ‘Alvaro’ na kuwafanya majasusi hawa kushtuka ndani kwa ndani wakaangaliana bila kificho lakini hawakufanya mawasiliano ya moja kwa moja.
“Picha hii nilitumiwa na rafiki yake mmoja mwezi mmoja uliopita lakini kwa sasa huyo mtu sina mawasiliano naye toka kwa wakati huo sababu kila nikipiga au kutuma meseji na mambo mengine ya kimawasiliano tuliyokuwa tukiwasiliana simpati lakini alikuwa ni mmoja wa rafiki yake mkubwa sana kiasi ya kwamba yeye ndiyo alikuwa anawasiliana zaidi na mimi kuliko Marcos mwenyewe” Jade akaporomoka tena kisha kwa kutumia ncha za vidole vyake vyenye kucha ndefu za kubandika alizozinakshi nakshi kwa rangi nyekundu inayoendana na ‘lipstick’ aliyopaka, kusukuma noti za dola mia mbili karibu na mikono ya ‘Alvaro’ aliyoiweka mezani ikichezea chupa ya pombe na glasi anazotumia.
“Hawa watu wote watano ni watu wanaounda genge la ulanguzi wa madawa ya kulevya ni hatari hata kuwaongelea sababu wana mapusha wao katika kila club na macasino hapa Salvador na miji mingine ya karibu, ninaposema ni hatari hata kuwazungumzia watu hawa uwa namaanisha hivyo nitaomba nisihusishwe na chochote pale mtakapokutana naye ingawa siwaoni kama mnaweza kuwa hammaanishi mnachokisema na pia hamuelekei kuwa ni maaskari maana hakuna maaskari wenye ma tattoo kama nyie.. Muda kama huu si rahisi kwa wao kuwa wako macho kwakuwa dili za biashara zao za ulanguzi wa madawa ya kulevya pamoja kuseti mambo juu ya usalama wa maisha yao ufanya usiku hivyo kwa sasa hakuna anayekuwa hajalala kati yao” Aliongea kirefu kidogo ‘Alvaro’ klisha akanyamaza akaangalia upande alipo aliyemsema kuwa ni mdogo wake na kumtaja jina anaitwa Ricardo Emanuel.
“Humu club muda kama huu mapusha kidogo wanakuwa hamna hasa katika ukumbi huu wa kwanza wa bar na casino club, mapusha wengi unaowaona jiji hili ni watu wa genge hili, genge lililo na ukaribu mkubwa na baadhi ya maafisa wa polisi ambao ulipwa kwa kazi ya kuwalinda hawa watu, wana pesa za kusumbua na hata huyo kaka yako naye ni miongoni mwa watu wachache wanaotembelea gari aina ya Bentley katika jiji hili… Almaarufu kwa jina la Cambiasso hapa Salvador hasa wanawake warembo hakuna asiyemjua Cambiasso wakimfananisha na mchezaji mmoja wa msimu kadhaa iliyopita aliyokuwa akicheza ligi ya Italia Serie A klabu ya Inter Milan na ni kwa sababu ya kuwa na kipara kama cha mchezaji huyo ndivyo yeye akaitwa hivyo ikizingatiwa inasemekana anashabikia Inter Milan katika vilabu vya ulaya.. Hapa hakuna anayejua jina hilo lenu la Marcos Bernado” Hapa alinyamaza akaangalia watu walio karibu na meza yao kama kuna ambaye anawaangalia sana akaona kila mmoja yuko bize na mambo yake hasa waliokuwa wakicheza mchezo wa ‘pool table’, alipoona mambo shwari akaangalia upande wa mdogo kisha akamuonyesha ishara aje kwenye meza yao, ikabidi Agent Jade na Agent Hansen waangaliane wakakonyezana kumaanisha jambo kisha wote wakalalia mgongo wa kiti walivyokalia kana kwamba wameambiana kusubiri nini kitafuata kwa mwenzao anayewapasulia mayai ya kisasa sasa (siri).
“Chukua pesa hii uagize unachotaka mi bado na maongezi na marafiki hawa ni wageni wangu wanatokea Sao Paulo” Akaongea ‘Alvaro’ baada ya ndugu yake kufika kwenye meza, alipokea noti moja ya dola mia moja aliyopewa mpaka akashangaa na kujiuliza swali hasilo na jibu nalo ‘kapataje hii pesa’ na hasa akiwa anatambua kaka yake alikuja hapa club kumfuatilia mwanamke wake anayejiuza katika club hii huku wao wote wakiwa wanajua lakini waliliridhia mwanamke huyo kujiuza hapa kwa wanaume wakware kisha pesa anazopata wanatumia wote hivyo ‘Alvaro’ alikuwa na kibarua cha usiku kumleta na kuondoka naye huku mara nyingine akimuacha kukesha kabisa na kuja asubuhi mida kama hii kuchukua alichoingiza au kuondoka naye kwenda naye kwake, hali hii zoeleka ilifanya mwanaume awe bweteka kwa kutofanya kazi yoyote (king’asti).
“Tunaweza endelea.. Mdogo wangu ana virafiki vyake viwili vitatu ni vipusha vya tunaowaongelea, nimeona akinitizama sana hivyo nimeonelea nimtoe wasiwasi kidogo kwa kumpa hii pesa aanze kutumia na yeye… Watu hawa inasemekana wanapewa nguvu na mtu mmoja maarufu sana na bilionea wa huko Mexico kiongozi na mmiliki wa genge la The Red Jaguar ambalo nalo nimesoma kwenye magazeti juzi juzi tu hapa kuwa genge lao limesambaratishwa na wafuasi wao wengi kuuwawa katika moja ya ngome yao iliyokuwa ya siri huku Guatemala, anatafutwa kiongozi wa genge lao huyo bilionea Feca.. Huyu bwana ndiyo anawapa jeuri watu hawa hapa Salvador na Bahia kwa ujumla wao ndiyo vidume wasioshindwa jambo yaani hata wakiingia hapa saa hivi wakisema watu wote amieni ukumbi mwingine wao watabaki ukumbi huu basi amri inatekelezwa mara moja hapo ndipo unafanyika ufuska wa hali ya juu kwa kweli jamaa starehe wanaijua na kazi zao pia wanazijua” Aliendelea kuongea ‘Alvaro’ hapa alinyamaza alisikia kiu ya kuvuta sigara na mchezo ulisomwa machoni mwa Agent Hansen haraka alitoa sigara katika paketi ya sigara zake aina ya ‘cigar’ kisha akamnyoshea akitambua wavuta sigara wengi wa Brazil hakuna anayegoma kuvuta haina hii ya sigara na kweli jamaa akaipokea na kuipachika mdomoni hapo Agent Hansen akamuwashia sigara kwa kiberiti chake kidogo cha gesi.
Mikupuo kadhaa ya sigara ilipulizwa na kufanya na Agent Hansen kupatwa na hamu na yeye avute akajiwashia yake naye hivyo akabaki asiyekuwa mvutaji mwanadada Jade Poul Brown akitamani ahame meza lakini hakuna jinsi hakuweza fany hivyo ilikuwa lazima aendelee kukaa hapo avumilie moshi wa sigara toka kwa wanaume hawa.
“Sigara nzuri sana hii! Dada wewe huvuti?” Akaongea ‘Alvaro’ sigara ikiwa mdomoni kisha akamtupia swali la ghafla Jade.
“Sivuti kwa sasa.. Ila nilishawai kuwa mvutaji kabla sijashika mimba ya binti yangu.. Endelea tunahitaji kujua tunampataje. Anaishi wapi Cambiasso?”
“Ooooh! Cambiasso anaishi ghorofa moja na wenzake wote lenye floor mbili tu, ghorofa hilo lipo mtaa wa Largo uliopo eneo la Old Quarter Pelourihno, ghorofa lao ndiyo ghorofa pekee ambalo ukifika tu unatambua kuwa ni ghorofa la kifahari zaidi licha ya kuwa si refu kama maghorofa mengine, wahuni hawa wanaishi kama familia pale lakini hakuna aliye na mke kati yao ni mahala pa laana sana kwa ufuska unaofanyika pale kwa dada zetu wa hapa Salvador kuumizwa kwa matumizi ya kuwastarehesha wanaume hawa, nafikiri kwa maelezo haya inatosha mkifika msije mkasema mmeelekezwa na mimi kwa ndugu yenu..!” Alimalizia kutoa lililotakiwa kusikiwa kwa hamu katika ngoma za masikio ya majasusi hawa ambao furaha yenye matumaini iliwajaa kiasi ya kwamba walikuwa wakitabasamu mioyoni mwao bila kuonyesha dhahiri kwa muungwana wao.
“Ahsante sana Alvaro… Umetusaidia kwa kiasi kikubwa kutupa mwanga wa maisha aliyoyachagua ndugu yetu kuishi hapa Salvador kiasi cha kumsahau mama yake mzazi aliyemuweka tumboni miezi tisa.. Na kwa hili mi naomba nikushukuru sana kwa niaba ya mke wangu ingawa naye yupo hapa na ninaamini atashukuru pia, naomba nikuongeze dola mia mbili zingine..” Akaongea Agent Hansen kisha ya hapo akatoa wallet toka mfuko wa suruali aliyovaa aina ya jeans, akachana wallet na kutoa noti mbili za dola mia mia akampa ‘Alvaro’.
“Ahsante sana, ahsante sana.. Naomba tu nisisitize nisitajwe huko kama mtaenda na muda kama nilivyoelekeza watakuwa wamelala kama ratiba zao zinavyosoma kila siku..” Akasisitiza ‘Alvaro’ tabasamu likiwa limeweka skani usoni mwake.
Agent Hansen na Agent Jade hawakuona kama kuna umuhimu wa kuendelea kuwepo pale club wakaaga baada ya kulip vinywaji vya ndugu hawa wote wawili bila kujali kuwa walitoa pesa za malipo ya taarifa, wakaondoka club hapa kwenda kupanga nini kifanyike baada ya habari walizopata.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na sita (116)
Katika sehemu hii tumesoma tukiwa eneo moja tu la Nightlife Club ikiwa kulikuwa na kazi maalumu ya kupata taarifa zitakazowasogeza majasusi waliofika hapa Bahia kwa ajili ya kazi moja tu ya ‘operesheni maliza kazi’.
Tusipige porojo na longolongo twende mbele!
ILIPOISHIA SEHEMU YA 116…!!.
“Ooooh! Cambiasso anaishi ghorofa moja na wenzake wote lenye floor mbili tu, ghorofa hilo lipo mtaa wa Largo uliopo eneo la Old Quarter Pelourihno, ghorofa lao ndiyo ghorofa pekee ambalo ukifika tu unatambua kuwa ni ghorofa la kifahari zaidi licha ya kuwa si refu kama maghorofa mengine, wahuni hawa wanaishi kama familia pale lakini hakuna aliye na mke kati yao ni mahala pa laana sana kwa ufuska unaofanyika pale kwa dada zetu wa hapa Salvador kuumizwa kwa matumizi ya kuwastarehesha wanaume hawa, nafikiri kwa maelezo haya inatosha mkifika msije mkasema mmeelekezwa na mimi kwa ndugu yenu..!” Alimalizia kutoa lililotakiwa kusikiwa kwa hamu katika ngoma za masikio ya majasusi hawa ambao furaha yenye matumaini iliwajaa kiasi ya kwamba walikuwa wakitabasamu mioyoni mwao bila kuonyesha dhahiri kwa muungwana wao.
“Ahsante sana Alvaro… Umetusaidia kwa kiasi kikubwa kutupa mwanga wa maisha aliyoyachagua ndugu yetu kuishi hapa Salvador kiasi cha kumsahau mama yake mzazi aliyemuweka tumboni miezi tisa.. Na kwa hili mi naomba nikushukuru sana kwa niaba ya mke wangu ingawa naye yupo hapa na ninaamini atashukuru pia, naomba nikuongeze dola mia mbili zingine..” Akaongea Agent Hansen kisha ya hapo akatoa wallet toka mfuko wa suruali aliyovaa aina ya jeans, akachana wallet na kutoa noti mbili za dola mia mia akampa ‘Alvaro’.
“Ahsante sana, ahsante sana.. Naomba tu nisisitize nisitajwe huko kama mtaenda na muda kama nilivyoelekeza watakuwa wamelala kama ratiba zao zinavyosoma kila siku..” Akasisitiza ‘Alvaro’ tabasamu likiwa limeweka skani usoni mwake.
Agent Hansen na Agent Jade hawakuona kama kuna umuhimu wa kuendelea kuwepo pale club wakaaga baada ya kulipa vinywaji vya ndugu hawa wote wawili bila kujali kuwa walitoa pesa za malipo ya taarifa, wakaondoka club hapa kwenda kupanga nini kifanyike baada ya habari walizopata.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XI
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
“Tumefanikiwa kupata habari ambazo zimetuvusha mbele kidogo.. Unaniskia vizuri?”
“Ndiyo nakusikia bila shaka ingawa upo mahala kuna kelele nyingi za watu, ungeongeza kidogo sauti yako kama hapana tatizo, mpo wapi?”
“… Tupo katikati ya jiji, karibu na Museu Da Cidade eneo la Jorge Amado..!”
“Sawa na endeleeni na mpango wa kuelekea huko kutizama kama wateja wanaohitaji mzigo wako kiasi gani na wanaweza kutulipa kwa namna gani? Kuweni makini maana biashara ya bidhaa kama zetu usumbufu unakuwa mwingi sana”
“Sawa! Ahsante kwa maelekezo, acha sisi twende huko, nitakupa location nikishafika”
“Vizuri! Utanipa kwa kuweka taarifa katika group kwakuwa nina kazi ngumu naifanya kuingiza data fulani katika kompyuta ya kampuni hivyo sitakuwa na muda wa kuongea mpaka nimalize hii kazi.. Nitawasiliana na jamaa zetu waliopeleka mzigo kwenye maduka ya karibu na Parque Bella Vista Street kujua nao wamefikia wapi katika kuwashawishi wateja wetu wa pande zile kuchukua mzigo angalau nusu yake.. Niwatakie kazi njema yenye umakini ndugu zangu”.
“Ahsante sana na nyie kazi njema kwenu nyote”
Simu zilikatwa wakiwa wameongea lugha ya kibiashara wakitumia lugha ya kireno ingawa si kweli kama walikuwa wakiongelea biashara kama mazungumzo yao yalivyokuwa.
Agent Kai aligeuka upande wa pili alipo Special Agent Rebecca aliye kwenye umakini katika Ipad yake akiwasiliana kwa njia ya mtandao wa whatssap na kina Special Agent Simone Silla.
“Kazi inaelekea pazuri, kina Hansen wamesogea karibu kwa mujibu wa maelekezo yao, muda huu wanaenda kuchunguza jambo mahala muda si mrefu watatuma ujumbe kwenye group kuwa niaje huko.. Tuwe tayari kwa kazi” Agent Kai akaongea kumwambia S.A Rebecca wakakutanisha macho na Reby akakubali ujumbe kwa kutingisha kichwa.
***** ***** *****
Eneo la kitongoji cha Old Quarter Pelourihno mtaa wa Largo ardhi yake ilikuwa inakanyagwa na watu wawili wa hatari wenye hadhi ya ukomandoo wote mwanamke na mwanaume, wakiwa wameshuka toka kwenye gari ambayo asubuhi ya siku ya leo waliikodisha kwa utaratibu maalumu uliowawezesha kupata gari katika hotel aliyofikia Agent Jade Poul Brown waliona ni vizuri wakaliacha gari hii ndogo aina ya Toyota IST 150X rangi ya kahawia (brown) kwenye kona ya kuingia kwenye mtaa huu na si kama wote waliipenda haina hii ya gari lakini iliwalazimu kwakuwa huduma nyingi za magari ya kukodishwa kwa mtu binafsi kujiendesha yeye mwenyewe katika makampuni yanayofanya kazi ya kukodisha magari haya katika jimbo la Bahia asilima tisini walikuwa wanatumia magari kama haya au mengine yanayofanana na haya kutoka nchi ambazo wanaunda magari ya bei rahisi inayoweza kuimiliwa na mtu yoyote wa kipato cha saizi ya kati na hata cha chini kwa wengineo.
Pilika pilika kwenye mtaa za watu wanaopita kwa miguu pembezoni mwa barabara na wengine wakiwa wanatumia baiskeli ikiwemo kwenye barabara yenyewe magari aina mbalimbali na mapikipiki yalikuwa yakipishana yanayoenda mbele kusini na yanayorudi kaskazini.
Jamaa hawa majasusi wa kimarekani walio ndani ya sura za bandia na mavazi yanayowaonyesha wao ni vijana wa kihuni fulani ikiwemo miili yao kuchafuka kwa matattoo , walikwenda kwa mwendo wa kawaida wakijifanya wako bize kuelekezana jambo katika simu zao wakiongea kwa furaha na mara kwa mara baada ya vicheko vyao walikuwa wakigonga viganja vyao kuonyesha jinsi wanavyofurahia maongezi yao huku wanatembea lakini si kama walikuwa wako makini na wanayozungumza hawakuwa katika umakini huo walikuwa wakifanya maigizo tu wote wawili walikuwa wakichunguza jengo waliloelekezwa na bwana waliyemlipa pesa (sijui kwanini walimuamini).
“Bila shaka mahala tunapopataka ni jengo jirani hapo.. Punguza mwendo kidogo tukishaanza kufika kwenye ukuta unaolizunguka jengo kisha tutajifanya stori zimekolea tukifika kwenye ule mti ulio karibu na geti hili tuweze kidogo kuchunguza” Agent Hansen aliongea huku anaweka vizuri ‘earphone’ ya simu yake.
Walikwenda kama walivyokubaliana wakasimama karibu na geti pembeni ya mti hapo Agent Jade Poul akajifanya ameingiwa na mdudu jichoni akaomba aangaliwe akitoa sauti kana kwamba anaumia ikabidi wasimame, dume likajifanya linampekua kope na kisha anampuliza huku jicho lingine likifanya uchunguzi mujarabu kuanzia getini hadi jengo lenyewe linaloonekana vizuri kuanzia ‘floor’ losheni ya pili nay a mwisho kati ya floor mbili zinazounda jengo ikiwa ya chini nay a juu.
“Tayari! Twende zetu” Akaongea Agent Hansen akimalizia kwa kumbusu kwenye paji la uso mshirika mwenza bila kujali wapiti njia wenzao.
Waliendelea na safari yao hii ya kama wanatembeza mwenge uliokwisha fika eneo la wakimbizaji kupumzika.
“Nilitega kamera yangu ya peni ebu tuangalie itakuwa imechukua vizuri..!” Agent Jade naye akaongea wakiwa washapiga hatua kama kumi toka jengo husika wakawa wanaenda, peni husika ikatoka toka katika kimfuko kidogo kilichopo kwenye kikoti alichovaa Jade, alipoitoa akaiunganisha na kiwaya cha usb kisha akachomeka kwenye simu yake kifaa chenye uwezo wa memory kilichofungwa ndani ya ‘peni kamera’ peni za kijasusi hizi zao la wenyewe wamarekani katika vifaa vyao vya kazi za kijasusi zilizo na teknolojia ya hali ya juu, kifaa kikasoma kwenye simu hapo akai ‘cut’ video na kui ‘paste’ (kuiamishia) katika simu yake, alipomaliza wakaanza kuiangalia video katika kioo cha simu huku wanaendelea na mwendo wa kutembea.
Ni kweli kamera ndogo iliyofungwa katika peni hii ambayo wewe au mimi nikiiona sitaweza kujua kama ina kamera na inafanya kazi kama video kamera nyingine ndogo ndogo, tungeweza shangazwa na taarifa toka kwa anayejua kuwa hii si peni tu iliyo na wino ndani ikiwa na kazi ya kuandika tu bali ina mambo mengine ya zaidi ya uwezo wake wa kimuonekano (ahsante teknolojia).
“Kuko kimya kabisa, madirisha yote ni madirisha yaliyowekwa tinted.. Tunatakiwa tuingie ndani kuchunguza, mtaarifu Agent Kai kuwa wasogee karibu ikiwa tutahitaji msaada wao basi watoe haraka..!” Ikiwa inaishia video ya dakika mbili iliyochukuliwa kwa peni kamera Agent Hansen hakuacha iishe akatoa maamuzi.
“Mchana huu tunapitia wapi?” Agent Jade akahoji akimuangalia machoni mwenzake aliye bize kuangalia huku na huko kama anamtafuta mtu katika wapiti njia wanaopita kwenda huku na huko wengine wakiingia katika baadhi ya nyumba za mtaa huu ikijuza ni wenyeji wa mtaa.
“Jasusi, kachero, komandoo wa Navy Seal! Unaulizaje swali dogo kama hilo? Una wasiwasi na uzoefu wako usiniangushe mpendwa.. !” Akajibu akitabasamu Agent Hansen wakajikuta wanagonga viganja vyao kufurahia kilichosemwa na Hansen.
“Wee mtaarifu Kai… Mimi natafakari tunaendaje ndani ya jengo kwa jinsi jengo lilivyo katikati ya majengo mengine” Akatoa elekezo kisha akatizama magari yanavyokuja yalipoachi nafasi ya yeye kufanyanachotaka akavuka kwenda upande wa pili akikimbia kuwai kuvuka akimuacha Agent Jade akichati kupitia mtandao wa whatssap na Agent Kai kumpa taarifa kazi ilipofikia pia kumuomba yeye na Rebecca wake kuja mtaa huu akimuelekeza kila kitu hadi jengo shukiwa lilivyo.
Upande wa pili baada ya kuvuka barabara Agent Hansen alisogea mahala ambapo kuna duka la kuuza vyakula na vitu vingine vilivyo muhimu kwa binadamu na visivyo muhimu sana kwa binadamu (luxury needs) likiwa katika fremu ya nyumba ya ghorofa la floor (losheni) tatu, fremu ya duka ilikuwa ikiangalia geti la jengo wanalohitajika kuingia na kufanya uchunguzi wa watu wanaowatafuta.
Aliingia dukani akaulizia kama anaweza kupata sigara aina ya ‘cigar’ ilikuwa bahati kukuta zinapatikana akanunua pamoja na kiberiti cha gesi kisha akamuomba muuzaji kama anaweza akavuta akiwa kakaa kwenye benchi lililo nje duka kuliko na kibaraza kidogo muuzaji akakubali, alipotoka nje na kukaa akaja Agent Jade ambaye naye alivuka barabara kuja upande huu.
“Karibu mke wangu.. Nimeona kuna vinywaji unaweza agiza mi nilikuwa na kiu ya sigara tu..!” Akaongea Agent Hansen baada ya kuona mwambata wake Agent Jade amemsimamia mbele, hakujibu kitu akaingia dukani haikuchukua dakika mbili akarudi mkononi akiwa na pepsi ya chupa ya plastiki maarufu kama ‘pepsi take away’.
“Karibu! Pole kwa kukuacha nikavuka upesi kuja huku dukani… Ni kweli nilikuwa na kiu ya sigara lakini pia wakati tumesimama pale kwa dirishani niliona kivuli cha mtu kisha mtu huyo akafungua dirisha ndipo nikatupa macho upande huu akili ya kazi ikanisukuma nije kwa ajili ya subira zetu za kawaida sehemu muhimu, tutafanya mambo taratibu tukiangalia kwa chati na uzuri wa hii baraza imeinuka kwa juu tunaona uwani mwa nyumba vizuri kwa juu juu” Kwa sauti ndogo isiyoenda mbali Agent Hansen akaongea huku anavuta sigara yake kwa mbwembwe.
“Nilishajua nini ulichofikiri mara nyingi siachwi mbali na mawazo ya watu wa kazi za kazi awe kachero au mhalifu.. Huko sahihi dakika ishirini mpaka thelathini zitatutosha hapa kupata mambo kadhaa wa kadha yaliyo muhimu” Akajibu Agent Jade akiwa anazungusha kifuniko cha chupa ya soda kiweze kufunguka apate kuanza kunywa.
Funda mbili tatu za soda kwa mnywaji soda Jade huku wanaongea mambo ambayo hayahusiani na kazi yao ili kupumbaza watu wengine waliokuwa wakiingia na kutoka dukani kupata huduma ziliweza kufanya zipite dakika tano tu wakati gari jipya la kifahari aina ya Jeep Wrangler rangi nyeusi ilifika na kufunga breki pembezoni mwa geti kisha akashuka mtu mmoja toka ndani ya gari upande wa dreva.
Alisogea lilipo geti kisha akatoa funguo mfukoni mwake akafungua geti akilisukuma upande toka kushoto kwenda kulia, alipomaliza kusukuma akarudi ndani ya gari akatia gia na kuingia ndani. ya uwa wa jengo husika.
Majasusi wawili waliweza kuona ndani kulivyo kwa kiasi chake kupitia geti lililofunguliwa na jamaa yule, gari lilipowekwa maegeshoni akashuka tena na kwenda kulifunga geti hapo kina Hansen hawakuweza kuona kinachoendelea.
“Umeona hali halisi ya tunapotakiwa kuingia, unafikiri kwa muda huu tutaingiaje? Maana kwa haraka kwa akili zangu nafikiri ni kwenda kugonga mlango tu” Agent Jade akaongea akiwa anamuangalia kwa umakini mshirika wake.
“Sikia nimefikiria kwa haraka na jibu limekuja nikuji risk tu kwa wewe kwenda getini kugonga wakikuona mwanamke hawatasita kuja kukusikiliza ila utafanya hivyo baada mimi kuondoka hapa kwenda kuona kama naweza kupita kupitia mtaa wa nyuma hivyo tutawasiliana nikishapata namna ya kusogea karibu kutokea kwa nyuma ndipo utaenda kugonga geti ukijifanya unamuulizia mwanaume wa jina lile tulilotajiwa kule na jamaa yetu kule club..!” Maelekezo yakatoka kwa Agent Hansen akitaka watumia mbinu ambayo wanajua uwa mara nyingine inafeli na mara nyingine inakuwa mbinu isiyofaa kwao majasusi.
“Sawa hamna shida nitafanya hivyo, nenda kaangalie uwezekano huo!” Jade na kunywa kidogo soda.
Agent Hansen aliunyka pale walipokaa kwa pamoja kwa benchi kisha akaenda kuelekea kusini inakoelekea barabara akitembea mwendo wa kasi alipotembea hatua za mita ishirini toka dukani upande wapili ulimvuti avuke barabara kutoka upande alipo kwenda upande wa pili kwenye safu ya jengo wanalolihitaji wao kuingia na kufanya uchunguzi wao wanaoamini utawafikisha mahala husika kama kikosi chao chote kilichofika hapa Salvador kumaliza kile kilichoanzwa Guatemala.
Alivuka barabara pale gari zinazopita barabaraniu zilipompa fursa hiyo, kilichomfanya aje upande huu kwa haraka ni uchochoro ambapo baadhi ya watu walikuwa wakipita kuja mtaa huu na wengine wakienda mtaa mwingine kupitia uchochoro huu.
Macho yakapachikwa miwani juu yake, miwani ya kazi za kazi wakati akienda ilikuwa kama bahati kwake kulikuwa na mtu mmoja mwanaume aliyekuwa kamtangulia mbele yake naye akiwa na safari zake hivyo ilimpa wakati mzuri kwenda huku akichunguza kila hatua anayopiga aliipiga ikidavua jambo.
Kati ya nyumba na nyumba za aina ya ghorofa zilizopeana mgongo kulikuwa na uwazi ulioacha kama inavyokuwa ramani nyingi za mipango jiji au miji kuacha eneo hili, uwazi huu haukuwa na matumizi ya kawaida kibinadamu iwe kwa watu kuwa wanapita kama njia au matumizi mengine hivyo kulikuwa na mifereji iliyojengewa zege kufunikiwa pamoja na chemba zake huku mabomba yanayotoka katika majengo haya yakiingia humo kwa uzoefu wa miji na majiji yaliyo katika mipango bora kutoka kwa serikali husika uwa inajuza huu ni mfumo wa mtandao wa maji taka.
Macho yaliyo ndani ya miwani yaliangalia huku na huko mbele mtu aliyetangulia mbele yake alikuwa amimalizia kutokea mtaa wa pili lakini kulikuwa na wanawake wawili wanakuja mbele ya macho yake Agent Hansen wote wakiwa wabrazil weusi waliojiremba kwa kuvaa mawigi ya rangi rangi wakipendeza kwa kujinakshi nakshi kwa mavazi yao ya suruali ya jeans kila mmoja lakini nao hawakuwa na muda wa kuangalia mbele zaidi ya kupiga kwao soga kwa furaha na simu zao kila mmoja macho yake yalikuwa yakiangalia simu huku wanakwenda.
Fursa uwa haiji mara mbili kutoangalia mbele kwa wadada hawa ilimpa nafasi Agent Hansen kuchepukia uchochoro wa nyuma kwa kasi na hili asiweke maswali zaidi alisogea kwa kasi na kwenda kujificha kwenye moja ya kimti kidogo kilichojiotea lakini matawi yake yangeweza kumficha asionekane kama wadada hawa watapata shahuku ya kutupia macho upande huu baada ya kushangazwa na kutomuona machoni mwao.
Wadada walifika na kweli wote wakaangalia upande huu wakiwa na wasiwasi walipokutana na kisichoonekana machoni mwao waliongeza mwendo kisha wakaunga mbio kichwani kwa kila mmoja maswali kibao kama waliona kama mtu lakini mara hawamuoni hivyo walidhania itakuwa ni mauza uza.
Walipopita! Agent Hansen mwanaume wa kizungu hakutaka kuremba alijiinua akatembea mwendo wa anakimbia lakini kwa tahadhari kubwa kwakuwa licha ya kuwa ni nyuma na nyuma ya majengo haya madirisha ya baadhi ya vyumba vya floor (losheni) yalikuwa wazi yakiachwa na wakazi wa maghorofa haya hivyo kutokuwa kwake na tahadhari kungeweza mletea matatizo endapo ataonekana na mmoja tu wa wakazi kwakuwa atahofia usalama wake.
Hesabu zake zilikwenda sawa akafika nyuma ya jengo husika akiwa amehesabu kwa mpangilio wa jengo na jengo kama alivyoyapigia hesabu kwa mbele, kulikuwa na kimti kingine kidogo kwa ujumla eneo hili lilikuwa na vimti kama hivi kila baada ya jengo na jengo hii ilimjuza Agent Hansen kuwa pengine ni alama fulani, alivipenda vimti hivi vilivyopandwa pembeni ya zege za mfumo wa mtandao wa majitaka kwani vilimfanya awe anajificha kwa nyuma yake kukwepa kwa wapiti njia kule alipotoka kumuona, akainama chini lakini macho yakitizama madirisha ya floor (losheni) ya kwanza ya ya jengo hili la ghorofa lenye ‘floor’ mbili.
Akatizama saa yake pia macho yake pia yakacheza kuangalia huku na huko kucheki usalama wake, ukuta ulikuwa ni ukuta mrefu kwa futi kumi kwenda juu, komandoo Agent Hansen si urefu tatizo kwake alishaupigia hesabu anaukweaje mpaka juu.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na saba (117)
Zamu ya Agent Hansen tena kuonyesha alichonacho, kuonyesha anaweza kufanya nini? Kwanini Agent Kai amemchagua kati ya aliowachagua kuambatana nao kumalizia kazi katika operesheni hii ndogo.
je nini kitatokea kwenye jengo hili?
Kwa majibu ya yote tuvute hatua kusogea sehemu inayofuata huku tukikaribia mwisho wa safari hii ndefu.
Wadada walifika na kweli wote wakaangalia upande huu wakiwa na wasiwasi walipokutana na kisichoonekana machoni mwao waliongeza mwendo kisha wakaunga mbio kichwani kwa kila mmoja maswali kibao kama waliona kama mtu lakini mara hawamuoni hivyo walidhania itakuwa ni mauza uza.
Walipopita! Agent Hansen mwanaume wa kizungu hakutaka kuremba alijiinua akatembea mwendo wa anakimbia lakini kwa tahadhari kubwa kwakuwa licha ya kuwa ni nyuma na nyuma ya majengo haya madirisha ya baadhi ya vyumba vya floor (losheni) yalikuwa wazi yakiachwa na wakazi wa maghorofa haya hivyo kutokuwa kwake na tahadhari kungeweza mletea matatizo endapo ataonekana na mmoja tu wa wakazi kwakuwa atahofia usalama wake.
Hesabu zake zilikwenda sawa akafika nyuma ya jengo husika akiwa amehesabu kwa mpangilio wa jengo na jengo kama alivyoyapigia hesabu kwa mbele, kulikuwa na kimti kingine kidogo kwa ujumla eneo hili lilikuwa na vimti kama hivi kila baada ya jengo na jengo hii ilimjuza Agent Hansen kuwa pengine ni alama fulani, alivipenda vimti hivi vilivyopandwa pembeni ya zege za mfumo wa mtandao wa majitaka kwani vilimfanya awe anajificha kwa nyuma yake kukwepa kwa wapiti njia kule alipotoka kumuona, akainama chini lakini macho yakitizama madirisha ya floor (losheni) ya kwanza ya ya jengo hili la ghorofa lenye ‘floor’ mbili.
Akatizama saa yake pia macho yake pia yakacheza kuangalia huku na huko kucheki usalama wake, ukuta ulikuwa ni ukuta mrefu kwa futi kumi kwenda juu, komandoo Agent Hansen si urefu tatizo kwake alishaupigia hesabu anaukweaje mpaka juu.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XII
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
Jengo la ghorofa lililopeana mgongo na jengo la ghorofa ambalo ukuta wake ndiyo Agent Hansen anataka kuukwea hili aweze kuingia kwenye upande wa nyuma wa uwa lilikuwa ni jengo ambalo lilikuwa na ukuta kama jengo hili la ghorofa lenye floor mbili, hii ilimfanya Agent Hansen kukamata bomba linaloshusha majitaka kwenda kwenye chemba akalitumia kukwea mpaka usawa unaowiana na ukuta wa upande wa pili hapa akaweza kuona kwa ndani ya uwa akiwa katika tahadhari iliyo katika kiwango cha juu kwa jinsi alivyokuwa akipepesa macho kila upande akashuka toka juu kwa kutereza kwa kasi alipotua katika kasi kasi ileile kwa kudunda miguu aligeuka haraka na kuunga mbio za hatua mbili tu kisha ya hapo kwa wepesi mikono akiwa kaiinua juu kama stahili ya ‘mateka mikono juu’ akaruka kwenda juu mikono ile ikakamata kingo ya ukuta hapo hakutulia akajivuta juu miguu ikijipinda mguu wa kulia ukitangulia kwenda juu nao ukakamata kingo mwili ukajikuta umejivuta kwa kufuata amri na utashi wa ubongo wake na kwakuwa alikuwa kashachunguza kupitia bomba alilokwea haikumfanya agande kucheki usalama bali alipitiliza moja kwa moja mpaka ndani ya uwa akitua salama salimini mbio zenye vishindo vya wastani mpaka usawa wa jengo husika akatulia.
Macho yake yaliyo ndani ya miwani ya kazi maalumu yalizunguka huku na huko huku anaitoa simu yake toka mfukoni ambapo ilipotulia kiganjani akatoa ‘lock’ na kuingia mtandao wa whatssap akaandika meseji moja kumjulisha Agent Jade kuwa yeye tayari yuko eneo la ndani ya uwa wa jengo kusudiwa, hakusibiri jibu akairudisha simu yake mfukoni.
Upande wa Agent Jade! Alivuka barabara kwa mwendo wa hatua nusu mbio nusu tembea mpaka lilipo geti alipolifikia akalichunguza kidogo pande zote mbili ikiwemo juu na chini, hapo akarudisha macho yake kushoto muda huu akiwa katoa miwani yuko kawaida tu, hatua mbili zikamsogeza nguzo ya upande wa kushoto ambako kuna swichi ya kengele za mlangoni/getini akainua mkono wake wa kulia akabonyeza kitufe kisha akatulia kusubiri sekunde thelathini kisha ya hapo akarudia tena akibo nyeza kwa kufuatana mara mbili halafu akatulia tena.
Dakika mbili mbele nyayo za mtu anayekuja getini kwa ndani ya jengo zilizisikika zikija tena zikiwa ni nyayo za mtu aliyevaa ndala au kandambili (malapa).
Geti lilifunguliwa baada ya mtu yule kuchungulia kwenye kiuwazi kidogo kilicho juu kidogo ya komeo za mlango mdogo (mtoto wa geti).
“Habari yako?!” Akauliza mwanaume wa kichotara (aliyechanganya damu ya kiafrika na kizungu) aliyefungua mtoto wa geti (geti dogo ndani ya geti kubwa), akiwa amevaa mavazi ya kimichezo (tracksuit) rangi nyeusi ikiwa na mistari mekundu kwa pembeni na miguuni ndala zilikuwa kama vile miguu yake ilivyowakilisha wakati anakuja kufungua na kujuza mjaji kufungua amevaa ndala.
“Nzuri! Za kwako?” Agent Jade akiwa ndani ya sura yake ya bandia aliyoivaa siku hii alijibu huku akimuangalia kiutalii kunasa mengi ndani ya macho yake na anaingilika vipi kwa jambo ambalo yeye alifika nalo muda huu wa asubuhi inayoukimbia uasubuhi wake na kuualika mchana.
“Mimi niko poa tu! Nikusaidie nini dada yangu..!”Akauliza mfungua geti mwenyeji wa jengo hili macho yake yakifanya udadisi katika kila kilicho katika mwili wa kiumbe wa kike aliyesimama hatua tatu toka yeye aliposimama huku mwili wake nusu ukiwa ndani ya uwa wa na nusu hasa mguu wake wa kulia ukiwa nje
“.. Eeeh!.. Mi nina jambo linalohusu mmoja wa wakazi wa jengo hili..”
“Kivipi? Jambo lipi linalohusu?”
“Naitwa Nikita Crawley.. Nafanya biashara ya mwili wangu, nikijiuza katika casino club mbalimbali zilizopo ndani ya jiji hili nimek..!” Alikatiza kuongea kwakuwa msikilizaji aliposhtuka waziwazi na kuongeza uangaliaji usahili kwake huku dalili za kutaka kuhoji jambo zikidhihiri machoni mwa mwanamke (Agent Jade) akiwa amejitambulisha yeye ni ‘Nikita Crawley’.
“Nikita!… Nikita Crawley! Unahitaji nini sasa hapa?”
“Siku tano zilizopita mwanaume mmoja alinichukua katika kiwanja cha 30 segundos club mtaa wa R.Iliheus 21 huko eneo la Rio Vermelho kisha akaenda nami hotel Monte Rei huko akanilala usiku mzima bila kunipumzisha akinitumia kotekote bila huruma kwa makubaliano atanilipa kiasi fulani zaidi ya kawaida endapo anganitumia mbele tu kitu ambacho niliridhia kwa dau tamanisha aliloniahidi lakini ilipofika alfajiri aliomba tulale kidogo nami nikamkubalia nilipokuja kushtuka ilikuwa saa tatu asubuhi nilijikuta peke yangu, sikumkuta yeye pembeni yangu, nikajua labda yupo bafuni nikaamua kwenda kuchungulia labda yupo maliwato sikuona mtu ndipo niliporudi na kuangalia alipoweka nguo zake usiku nikagundua hazipo hapo ndipo nikapatwa na mashaka kuwa nimeachwa kwenye mataa nikavaa nguo zangu upesi na kutoka nje kumuulizia kwa wahudumu ndipo nao wakasema walimuona akiondoka asubuhi ya saa moja wakajua tushamalizana nami mpenzi wake.. Siku ile niliondoka zangu kurudi kwangu jioni yake nikaanza kumtafuta anipe malipo yangu ndipo jana usiku nikakutana naye mahali bila yeye kuniona nikamfuatilia akaja kuingia kwenye ghorofa hili, uchunguzi wangu ukagundua anaishi hapa na vijana wenzake wengine kama wewe hivyo nimemfuata anipe changu” Alitoa maelezo marefu kidogo akisikilizwa na mwenyeji wake aliyeacha kumkaribisha ndani wakisimama pale pale getini, mwenyeji akishikilia kiambaza cha geti na mgeni akisimama pale pale karibu na swichi ya kengele.
“Una uhakika huyo mtu wako anaishi hapa?” Swali likatupwa kwake.
“Ndiyo na uhakika na hilo sababu mimi uwa sidhulumiki kirahisi na wahuni kama yeye uwa nawafuatilia kwa mbinu zangu kisha napata haki yangu.. Kwanini niache nyumba zote nije hapa?.. Angalia maghorofa yote yaliyopo eneo hili kwanini niyaache nije hapa? Au mimi naonekana chizi kaka yangu?” Alijibu changudoa feki Agent Jade aliye katika sura ya kimueonekano tofauti na yake ikiwa ni sura ya kahaba haswa jinsi alivyojiweka na ni sura ya mrembo wa sura matata na ukileta umbo lake la uhalisia ambalo ni umbo la kimazoezi lakini lililokaa kikike haswa.
“Yukoje?” Swali lingine likafuata mwanaume akiuliza huku akionyesha uso wa kukasirika ingawa moyoni mwake aliamini ni kweli anachosema mwanamke huyu mrembo changudoa kwakuwa hii tabia wao wote yaani yeye na wenzake uwa wanaitumia mara kwa mara ni kama Jade alilenga kwa maneno yake ya uzushi yaliyo na ukweli kwa msikilizaji wake aliye mbele yake.
Taswira ya picha mojawapo aliyopewa na Agent Kai ilimjia kwa haraka machoni mwake na haraka akamlenga mmojawapo alivyo wajihi wake na bila kufikiri sana akaanza kumvavadua.
“Mrefu, kifua kipana cha mazoezi na mikono iliyojaa vivyo hivyo ana sura pana ananyoa ndevu zote akiacha mustachi sehemu ndogo ya katikati na macho yake ya kusinzia.. Mengine nayajua ambayo nikieleza sidhani kama yatakusaidia kaka” Alieleza Jade akipatia vilivyo wajihi wa mtu aliyeamua kumpa kesi isiyo yake.
“Mmmh! Sasa dada mbona hatuna mtu kama huyo.. Hilo lisilo nisaidia ni nini? Labda hilo linaweza sababisha nikavumbua ni nani? Kati ya wenzangu wengine” Akajibu uongo mwanaume huyu ilihali akijua dhahiri tayari kashamjua mwanaume huyo lakini siku hiyo yeye alikuwa naye na walilala hapo wote baada ya kazi ya kuwapokea wageni wao fulani toka Mexico lakini aliamini inaweza ikawa mwanamke kakosea hiyo siku akataka kujua zaidi huku naye akimtamani mwanamke huyu mrembo.
“Ana lidude likubwa sana yaani ni kwa sababu kazi tu lakini poooh mwanaume yule muuaji halafu anataka kunidhulumu kutonipa haki yangu siwezi kukubali na sitatoka hapa mpaka kieleweke.. Nasema mpaka kieleweke” Aliongea kwa sauti ya kupazwa iliyovutia hadi wapita njia wanaopita kwa miguu barabarani wengie wakaanza kusimama kuona kulikoni hapa.
Mara kwa ndani kuna mwanaume mwingine akafungua mlango ikafanya huyu aliye getini kugeuza shingo kuangalia ni nani aliyetoka asije kuwa anayeongelewa na huyu mwanamke, bahati ikawa si yule mzungumzwa.
“Vipi hapo Olivas? Kuna nini? Maswali mawili yakaulizwa kwa kufuatana na mtu aliyefungua mlango wa lango kuu la kuingilia ndani ya jengo hili la ghorofa.
“Dada ana malalamiko yake lakini namwambia kapotea mtu anayemtaka hakai hapa yeye anang’ang’ania mtu huyo yupo hapa…!” Akajibu aliyeitwa Olivas na mtoka ndani.
Wakati wao wakiwa wanaendelea na mahojiano na mwanamke aliyeamua kuwazuga wajiwekeza katika kumuweka kipaumbele yeye, Agent Hansen fundi huyu mwenye mambo ya kariba moja na Agent Kai karibu mengi tu alikuwa tayari yupo katika sebule kubwa yenye thamani kadhaa za fenicha akinyata kuelekea zilipo ngazi zinazokwenda ‘floor’ ya pili.
Kabla hajazifikia ngazi akiwa anapita pembeni ya fenicha zilizo kati ya sebule nyayo za mtu anayekimbia kushuka ngazi kutokea juu zilisikika hapo ikamfanya mtaalamu Hansen kujilaza nyuma ya sofa alilokuwa nalo karibu, mshuka ngazi kwa mbio alitokea na hakuangalia upande wowote zaidi ya mlangoni anakoelekea alipoufikia aliufungua na kutoka nje, wakati huo kwa kipembe cha chini kabisa Agent Hansen alikuwa akila chabo kwa chati bastola yake ndogo aina ya Glock 47 ilikuwa mkononi, alitulia sekunde 30 kisha akainuka tena taratibu safari yake ikaendelea katika mwendo wa mnyato.
Alizifuata ngazi mpaka mwisho wake na kumfikisha kwenye korido hapo akasimama kuangalia mandhari ndipo masikio yake yaliposikia mtu anaongea sauti ikitokea katika moja ya mlango wa chumba kwa ndani katika korido hii kulikuwa na safu ya milango iliyojipanga ikifuata korido inavyosogea kwa urefu wake, maongezi yaliyokuwa yakisikika yalikuwa ni hatua mbili toka aliposimama Agent Hansen ikamvutia asogee zaidi aweze kusikia kinachosikika toka kwa muongeaji ndipo akagundua muongeaji anaongea kwa kutumia simu kwa lugha yao ya kireno lugha zungumzwa na wenyeji wa nchi hii ya Brazil.
“… Tunakuja boss!.. Ratiba haikuwa hivyo unavyosema na ndiyo maana sote tumelala kwa muda mrefu hivi ila hapo ni karibu tu dakika 15 tu tupo hapo..!” Maneno haya toka kwa muongea kwa simu ndiyo maneno ambayo Agent Hansen aliweza kuyasikia punde aliposogeza kichwa chake na kukindamiza eneo la sikio sambamba na mlango eneo la kitasa, ukimya wa sekunde 10 ukachukua nyakati kisha vikasikika vitu vinachakachuliwa chuliwa kama ni nguo au vitu vinavyofanana na hivyo hapo macho ya Agent Hansen yakawa yanatafuta kwa kasi wapi apate hifadhi iliyo salama ikiwa korido yote hakuna chochote cha kumficha anayehitaji ajifiche na mara masikio yake yaliyo makini kusikia chochote kile aliskikia kwa kutokea chini ilipo sebule kuu watu wakifungua mlango mkuu kwa fujo huku vicheko na maneno mbalimbali yakiingia navyo hapo ikawa kama kengele ya hatari inagongwa kichwani mwa Hansen.
Akapiga hesabu za haraka kisha akatoka aliposimama mbio za kunyata hadi mlango wa pili kutoka huu aliokuwa akinyapia kusikiliza maongezi ya muongea kwa simu, nyuma yake ngazi zikaanza kusikika zikianza kupandwa sasa na wanaume waliokuwa wameenda kumsikiliza mwanamke aliyewapa taarifa kuwa yeye ni dadapoa anahitaji chake.
Kwa akili ya kazi iliyokuwa inachemka kwa kasi na hisia kwa haraka mwamba bastola mkononi akaminya kitasa cha mlango wa chumba cha pili ukakubali kufunguka akausukuma na kuchungulia hapo akakutana na chumba kikubwa cha kulala chenye kitanda na vitu vingine vilivyo mahususi kwenye chumba cha mtu aliye msela asiyehitaji vitu vingi katika chumba chake kulikuwa hakuna kiumbe kinachovuta pumzi akauvuta wote na kuzama ndani kimya kimya, tendo hili lilipofanyika tu nyuma yake yalitokea mambo ambayo ubongo wake uliamini akichelewa kuchukua maamuzi tu anaingia katika mapambano bila kutaka kwa wakati huu, wapanda ngazi walifika na muongea kwa simu akafungua mlango sekunde wakipishana na anayewakimbia.
“Tunatakiwa haraka sana kwa boss kuna maelekezo anataka kutupatia sote hivyo wote tunaondoka kwenda huko..” Akaongea aliyesikika vizuri hadi kwa Agent Hansen aliye ndani ya chumba asichojua ni cha nani kati ya wenyeji wake aliowavamia bila wao kujua kama kuna mgeni ndani yao.
“Haya kila mmoja ajiandae haraka mi niko tayari nawasubiri chini..!” Sauti ile ile ikaendelea tena kuelekeza na mara nyayo za watu waliokuwa wamesimama tu zilianza kusikika upya kwa fujo, hapo Agent Hansen akatambua mwenye chumba anakuja na yeye hatakiwi kuingilia mpango wao wa kwenda kwa boss wao haraka aliondoka pale nyuma ya mlango mpaka kilipo kitanda baada ya kuona anaweza akaingia uvunguni bila shaka na kweli alipofika akainua shuka lililokuwa limetandikwa likiziba mpaka chini kusionekane hapo akazama kwa kasi na mlango ukafunguka mwenye chumba akaingia.
Akiwa chini hapo akipumua kwa kujipunja hili asiweze sikika hata kidogo katika mihemo yake ya kawaida kibinadamu, alitoa simu yake akatoa ‘lock’ kisha ‘pattern’ akatafuta uwanja wa meseji kwa njia ya mtandao wa whatssap kasi kama vile vidole vyake vina mota jinsi alivyokuwa akifanya, alipoupata uwanja moja kwa moja akaenda kurasa ya Agent Jade akacharaza meseji fupi lakini ya kueleweka ikiwa na maelekezo kuwa watu hawa wanatoka wameitwa kwa mtu waliyemuita kuwa na boss wao hivyo afanye ima kurudi lilipo gari lao kwa ajili ya kuwaungia mkia, meseji ikafika kwa mlengwa na ikajibiwa ameelewa, ikiwa pia ni ngumu yeye kuweza kumsubiri Agent Hansen atoke ndani kwenda mpaka alipo hili wafanye wote kazi ya kuwa mkia.
Ujumbe ulimfikia Agent Jade akiwa ameondoka pale getini baada ya wanaume waliotoka kumsikiliza madai yake kumwambia watampiga risasi au kumuitia mwizi aondoke haraka na kama anamtaka huyo mtu wake kama kweli yupo katika jengo lao hili basi amvizie akimuona club yoyote amdai anachodai si kufika hapo na kuwavunjia heshima zao kwa majirani zao, Jade aliona hana haja ya kuendelea kung’ang’ania pale kwakuwa kwa dakika zilivyo imani yake kwa Agent Hansen na anavyomjua aliamini muda huu ule atakuwa tayari yumo ndani ya jengo husika, alijifanya bado analeta ubishi akitukana kwa matusi machache ya kireno anayoyajua, wanaume wakafunga geti naye akaona hana jinsi aondoke kusubiri maelekezo ya ndugu yake aliyeamini sasa yuko ndani ya mjengo husika.
Kupokea kwa meseji kulimfanya naye aendelee kubaki katika uwanja wa mtandao wa whatssap kupitia simu yake aina ya Iphone X, akatuma meseji taarifa kwa Agent Kai akiomba na wao wajiandae tayari na gari kufuata maelekezo yake wakati yeye anaunga mkia, alikwenda akichati kwa kasi isiyoshtua watu mpaka pale walipopaki gari lao akaingia ndani ya gari kisha taratibu akarudi mtaa husika kwa mwendo ambao hesabu zake aliamini utakuwa mwendo ambao anaowahitaji kuwaundia mkia watakuwa wanatoka kwenye mjengo.
Alipokuwa akikaribia ghorofa la wahusika geti likafunguliwa na kufuatia kutoka kwa gari aina ya Cadillac XTS 2016 rangi nyeusi ikasimama mbele mtu mmoja ambaye hakuwa ndani ya gari akalifunga geti naye kukimbilia ndani ya gari kisha dreva akaliingiza barabarani gari kwa mwendo wa ambao ni wa kasi wakimpita Jade iliyembidi avute pembeni kidogo asije kugongwa na gari hili.
Mkia ukawekwa sawa ukiacha gari mbili zitangulie kisha na wao ukaongeza kasi ya kuendana na wahusika anaowafukuzia.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na nane (118)
Kasi ya kumsogelea ‘KINGPIN’ Feca bila ya yeye kujua kuwa anasogelewa inazidi kushika kasi ya moto uliowashwa katika nyasi zilizokauka.
Agent Hansen na Agent Jade wamejikuta wamefanya kazi ambayo kwao ni nyepesi lakini ni kazi ambayo tutaona umuhimu wake katika sehemu inayokuja.
Agent Jade ameunda mkia kuwafuata vijana wa kazi ambao muda si mrefu alikuwa ametoka kutupiana maneno baada ya wao kumuona wa Malaya anayewazingua.
Kwa uhondo zaidi wa mwisho mwisho twen’zetu mbele..!
Ujumbe ulimfikia Agent Jade akiwa ameondoka pale getini baada ya wanaume waliotoka kumsikiliza madai yake kumwambia watampiga risasi au kumuitia mwizi aondoke haraka na kama anamtaka huyo mtu wake kama kweli yupo katika jengo lao hili basi amvizie akimuona club yoyote amdai anachodai si kufika hapo na kuwavunjia heshima zao kwa majirani zao, Jade aliona hana haja ya kuendelea kung’ang’ania pale kwakuwa kwa dakika zilivyo imani yake kwa Agent Hansen na anavyomjua aliamini muda huu ule atakuwa tayari yumo ndani ya jengo husika, alijifanya bado analeta ubishi akitukana kwa matusi machache ya kireno anayoyajua, wanaume wakafunga geti naye akaona hana jinsi aondoke kusubiri maelekezo ya ndugu yake aliyeamini sasa yuko ndani ya mjengo husika.
Kupokea kwa meseji kulimfanya naye aendelee kubaki katika uwanja wa mtandao wa whatssap kupitia simu yake aina ya Iphone X, akatuma meseji taarifa kwa Agent Kai akiomba na wao wajiandae tayari na gari kufuata maelekezo yake wakati yeye anaunga mkia, alikwenda akichati kwa kasi isiyoshtua watu mpaka pale walipopaki gari lao akaingia ndani ya gari kisha taratibu akarudi mtaa husika kwa mwendo ambao hesabu zake aliamini utakuwa mwendo ambao anaowahitaji kuwaundia mkia watakuwa wanatoka kwenye mjengo.
Alipokuwa akikaribia ghorofa la wahusika geti likafunguliwa na kufuatia kutoka kwa gari aina ya Cadillac XTS 2016 ikasimama mbele mtu mmoja ambaye hakuwa ndani ya gari akalifunga geti naye kukimbilia ndani ya gari kisha dreva akaliingiza barabarani gari kwa mwendo wa ambao ni wa kasi wakimpita Jade iliyembidi avute pembeni kidogo asije kugongwa na gari hili.
Mkia ukawekwa sawa ukiacha gari mbili zitangulie kisha na wao ukaongeza kasi ya kuendana na wahusika anaowafukuzia.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XII
SALVADOR, BAHIA – BRAZIL
Akiwa katika umakini mzito wa kuifuatilia gari aina ya Cadillac XTS 2016 rangi nyeusi iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi ambayo yeye Agent Jade ilikuwa lazima amalize gia zote za mwendo kasi ili kwenda sambamba kwa angalau fulani kutokana na kagari wanachokitumia aina ya Toyota IST 150X yeye na mwenzake Agent Hansen ambaye kwa hapa hakuwepo alikuwa bado yupo ndani ya jengo la ghorofa mbili, aliamua aendeshe huku anatumia simu yake kuongea, haraka aliinua pale alipokuwa ameitupia siti ambayo kikawaida ukaliwa na abiria asiye dreva punde alipoingia ndani ya gari kwa wakati huu anaoendesha yeye kisha akatoa ‘lock’ akifuata na ‘pattern’ akapata kwenye majina akapiga kwa Agent Hansen.
“Halloo Hans!.. Nikizubaa naweza kuwapoteza ila najitahidi kwa kila hali huku nikimuomba Mungu lisitokee hilo, vipi umeshatoka ndani ya jengo?”Akaongea akiwa ameweka ‘bluetooth earphones’ sikio lake la kushoto ilipopokelewa tu simu na upande aliopiga.
“Naangaika kufungua mlango.. Mbuzi alinifungia kwa nje wakati anaondoka hapa kijasho chapa kila mbinu nimetumia unanizingua amebana komeo kwa nje mlango hautumii funguo..”
“Shiiit.. Itabidi uwasiliane na kina Chilamwena wafike kukupa msaada hapo..”
“Muda mfupi nimetoka kuongea na ‘sole’ kuhusu hili la mimi kukwama humu ndani naye amemuagiza Chilamwena afike hapa mara moja kunipa msaada wa kuufungua huu mlango” Akajibu hivi akitumia jina la ‘Sole’ (nyayo) kwa maana ya Kai ambaye anatumia a.k.a ya ‘The Sole Cat’ hivyo yeye Agent Hansen alichukua neno moja la kati ili kujenga fumbo kama kuna mtu au watu wanadukua maongezi wasipate urahisi wa kuelewa nini kinazungumzwa.
“Pole sana, mko kwa wapi?”
“Umejisahaulisha kama mimi na wewe na hata wengineo sote sisi ni wageni hapa Brazil hususani jimbo hili la Bahia.. Kwa mbali naziona paa za uwanja mkubwa wa mpira ila barabara hii tunayopita ni highway tena upande wa mwendokasi”
“Kama mpo hapo mnaelekea kaskazini magharibi kwa vile usiku nilisoma ramani ya jiji na unasema unaziona paa za uwanja wa mpira basi mpo kwenye muinuko wa barabara ya BR-101 punde mtaingia mzunguko wa Feira De Santana na kama watanyooka bila kwenda barabara ya kushoto wala kulia baada ya kuzunguka basi mtakuwa mnaelekea maeneo ya nje ya jiji hili na kama mtakunja kuelekea barabara ya kushoto mtakuwa mmeingia BR-116 barabara inayoelekea uwanja wa mpira wa miguu wa kimataifa wa jimbo la Bahia uitwao Fonte Nova Stadium na mkiupita huo uwanja mtaingia mitaa ya watu wenye pesa zao ikiwemo na viongozi wa kiserikali wa jimbo eneo la Metropolitan kuna fukwe pembezoni mwa eneo hilo fukwe maarufu ya Lauro De Freitas.. Utanijulisha kama mnanyooka tu” Agent Hansen komandoo aliyekwama ndani ya chumba akiwa ameshindwa kufungua na wala kuvunja mlango alitoa ufafanuzi mrefu kwa Jade na kusubiri Jade ataongea nini.
“Sawa.. Acha nitumie maelekezo yako kumuelekeza TSC, naomba ukate simu yako maana anapiga kwangu” Jade akaongea na kuomba Hans akate simu ambapo hakuchelewa hata sekunde kauri kukatwa tu naye akakata simu.
“Hallooo!”
“Vipi huko?”
“Salama kabisaa.. Msiwe na wasi najaribu kujitahidi kukikimbiza kimkebe kiendane na spidi ya mashine kali Cadillac XTS..!”
“Pole sana! Jitahidi kwa kila hali wasikupotee… Mko wapi?”
“..Mh!.. Hii barabara ni highway kwa mujibu wa Hans na uelewa wake wa jiji hili anasema hii ni barabara ya BR-101 Highway kuna maelekezo mengine amenipa naomba usikate simu wamezunguka muzunguko wa Feira De Santana kama wataenda vile alivyoeleza Hans nitapata hisia wapi tunakoenda..!”
“Sawa… Sisi pia tupo kwenye kigari cha kufanana na chenu ambacho alikiacha Hans wakati mnatoka tunakuja barabara ya BR-101” Akaongea Kai upande wa pili kisha ukafuata ukimya wa sekunde 32 ikisikika miungurumo ya gari wanazoendesha.
“Unanisikia Sole?” Akaukata ukimya Jade.
“Yes! Jade…Nakupata!”
“Ni kama alivyotarajia Hans… Wamezunguka na hawakunyooka moja kwa moja, wameingia barabra ya ya upande wa kushoto nafikiri ndiyo BR-116 sasa nauona vizuri na maandishi yake yakimulika tutokapo uwanja wa mpira wa miguu wa Fonte Nova Stadium”
“Vizuri.. Hivyo sisi tutafuata moja kwa moja ramani ya kutuleta uwanja wa Fonte Nova.!” Alipomaliza kuongea hivi Agent Kai akakata simu huko alipo.
Gari inayofukuzwa kimya kimya bila kujua, mawazo yao yakiwa kuwai walikoitwa ilitembea ikipita kwenye barabara hii ya BR-116 inayotumiwa kuwafikisha watu uwanja wa mpira wa miguu wa Fonte Nova Stadium kisha ikienda mpaka eneo la beach ya Lauro De Freitas, fukwe inayotumiwa na mahotel kadhaa ya nyota tano pamoja na majengo mengine ya makazi ya watu wenye pesa zao, Cadillac XTS toleo la 2016 ilianza kupunguzwa mwendo na dreva anayeendesha kisha ikachepuka toka barabara kuu na kusimama kwenye moja ya geti lililoshikana na ukuta uliozunguka ghorofa la floor (losheni) tano, Jade hakupunguza mwendo hili kuzuia kushtukiwa alipita kwa kasi ileile akiyapita majengo kadhaa ya mtaa huu kisha ndiyo akapunguza mwendo alipoliona jengo la hotel iliyo msafara mmoja na msafara wa wawindwa wake waliposimamisha gari mbele ya geti ikionyesha ndiyo mwisho wa safari yao.
Agent Jade aliingiza gari maegeshoni, maegesho ya hotel ya Wish Hotel Da Bahia, hotel ya nyota tano ya ghorofa lenye urefu wa losheni (floor) tisa kwenda juu ikiwa toka uwanja wa Fonte Nova hadi mtaa huu ni kilometa 2.3, hakushuka kwa haraka alitulia ndani ya gari akijifanya anapanga vitu vyake ndani ya pochi lake kumbe akili na mawazo yake ilikuwa kuangalia mita mia nyuma na mara gari ile aina ya Cadillac ilizama ndani ikimaanisha geti lilifunguliwa kuwaruhusu kuingia ndani.
“Halloo!” Simu aliyopiga haikuita miito hata miwili aliyepigiwa haraka alipokea kana kwamba mtu aliye na hofu pengine mpigaji atakata hivyo amuwai na kuongea.
“Windo la mteja kilometa mbili kutoka Fonte Nova Stadium kwa hesabu za kagari haka tulikoingilia mita mia mbele maegesho ya hotel ya nyota tano ya Wish Hotel Da Bahia pembezoni mwa fukwe namaanisha nyuma ya majengo haya kuna fukwe ya Lauro De Freitas… Njooni tupate upepo mwanana na burudani za kibrazil..”
“Chukua chumba..!” Akajibu hivi Agent Kai na kisha kukata simu akiwa kaelewa mafumbo ya kifundi ya Jade.
Aliposhusha simu chini Jade haikumpa nafasi ya hata kuangalia pengine ikaita jina likitoka kwa maandishi ya kigiriki akiwa kalisevu likimaanisha ni ‘Hans’.
“Hans!” Akaongea baada ya kuruhusu kuwa hewani.
“Wamefika Chila na Silla mapacha wa majina awa.. Vipi huko?”
“Kilometa 2.3 kutoka Fonte Nova Stadium.. Mita mia moja tu kwa kuingilia maegesho ya hotel ya nyota tano ya Wish Hotel Da Bahia” Akajibu na kukata simu.
Alipomaliza kuongea na simu hii ilimbidi ashuke toka kwenye gari kwakuwa moja ya muhudumu wa pale maegesho mwenye kazi ya kupokea wateja wanaofika katika maegesho ya hoteli alikuwa amesimama pembeni kusubiri mteja yeye ashuke toka ndani ya gari.
“Karibu Wish Hotel Da Bahia, hoteli yetu nzuri ya nyota tano zinakopatikana huduma nzuri sana..!’Akaongea muhudumu mpokea wateja akibabaika kama anaweza kupokea nini pengine kwakuwa Agent jade aliye katika muendelezo wa muonekano wa sura ya bandia hakuwa na mzigo wowote zaidi ya kipochi kidogo maarufu kwa jina la ‘kipima joto’ kwa madada wa mjini.
“Ahsante sana kaka yangu.. Sina mzigo wowote niko kama nilivyo tu..” Alijibu ukaribisho ule huku macho yake yaliyo ndani ya miwani ya kazi za kazi yakiwa yameelekea mita 100 toka pale.
Aliona hana jinsi ya kuweza kuendelea kuwa pale maegesho sababu kule kwenye jengo waliloingia aliokuwa anawafuatilia kulikuwa na taa kubwa ziizofungwa pembezoni mwa ‘kenopi ya geti’ kwa uzoefu wake wa shughuli hizi anazofanya Agent Jade ilimjuza zilikuwa ni taa zisizo taa za kawaida zilikuwa na mfumo wa kamera za cctv zikichukua katika pande zote za mbele na pembeni ya ukuta huu uliojengwa kulizunguka jengo husika la urefu wa floor tano kwenda juu zinazoonekana ikiwa pia ipo floor ingine ya chini, aliingia mapokezi mwa hoteli hii na kusogea kwenye dirisha la mapokezi.
Meseji katika njia ya mtandao wa whatssap ilimfanya asisogee zaidi akafungua kuisoma meseji husika ambapo ilikuwa ikisomeka hivi > ‘Chukua chumba katika hotel unayosema upo hapo kisha tusubiri tunakuja mimi na Reby’, meseji hii ilikuwa ni kama Agent Kai ameingia mawazoni mwake.
Alifuata taratibu zote akachukua chumba katika alichopenda kuchukua katika floor ya mwisho kabisa akisema atakaa siku moja, muhudumu anayehusika kutoa huduma katika vyumba vya hoteli vya floor ya mwisho alimpeleka mpaka juu wakitumia lift na kumuacha katika chumba.
Dakika kumi mbele Agent Kai akiwa ndiyo dreva wa gari aina ya Toyota IST 1.5S L EDITION rangi ya samawati (silver) ambayo kimsingi ni gari ambayo ilikuwa imekodishwa na Detective Omar Chilamwena katika hoteli aliyofikia ambayo nayo kuna kampuni tanzu inayojishughulisha na huduma za kukodisha magari madogo haya kwa wateja wanaotaka kujiendesha wenyewe na hata wanaotaka kuendeshwa na madreva wa kampuni, walifika maegeshoni wakiwa wamepita mahala ambapo wakipiga hesabu za kimaelekezo ziliwajuza ni jengo lipi la urefu wa floor (orofa) tano linalozungumziwa ndimo walimoingia wanaume watano waliopigwa picha usiku uliopita kwa simu ya Agent Kai.
“Karibuni sana! Wish Hotel Da Bahia, hoteli yetu nzuri ya nyota tano zinakopatikana huduma nzuri sana.. Kama kuna mzigo katika gari ningependa kuwapokea mizigo yenu!” Muhudumu yule yue wa kiume aliyempokea Agent Jade Poul allitoa ukaribisho kwakina Agent Kai punde waliposhuka na kufunga milango ya gari wakiwa pamoja na mshirika wake kipenzi Special Agent Rebecca Smith kitukuu cha ukoo maarufu kwa ufuaji wa chuma ulimwenguni ukoo wa ‘Smith’.
“Ahsante sana muhudumu mtanashati.. Kwa bahati nzuri kwetu vibegi tulivyo navyo tunavimudu kuvibeba wenyewe.. Ahsante sana kwa ukarimu wako na tumekaribia hoteli nzuri kwa huduma nzuri tulizosikia toka huko tulipo juu ya hii hoteli” Akajibu akiwa kaachia tabasamu murua na matata S.A Rebecca akionyesha meno yake jinsi yalivyo meupe nay a kuvuti katika sura yake iiiyo na ulimbo kwa vidume wakware a.k.a pendapenda.
Waliongea mawili matatu na mwanaume huyu wa huduma maegeshoni kisha wakaingia mapokezi.
“Karibuni wateja..!” Wakiongozana kama vile wapenzi wote kimuonekano wakionekana kama ‘couple ya wazungu’ kwakuwa wote walikuwa wamevaa sura za plastiki zinazowaonyesha katika muonekano wa mtu mwingine wasio wao huku Agent Kai mtu mwenye asili ya Afrika (mbantu) alikuwa amevaa sura ya kizungu imuonyeshao kama mvulana fulani kwa mbali waweza mfananisha na wazungu wa kilatin nywele nyeusi na weupe wa kuiva wekundu, kwake ikimlazimu kuvaa shati la mikono mirefu lenye mifuko mingimingi kama mashati ya wafuasi wa chama fulani cha upinzani nchini Tanzania, mikononi mwake akivaa ngozi laini kufunika viganja vyake viziwe katika muonekano wa kirangi tofauti na sura aliyovaa kwakuwa kiasili yeye ana rangi ambayo waswahili tumezoea kuiita ‘maji ya kunde’.
“Ahsante sana” Wote kwa pamoja wakaongea sauti iliyo katika ulingano kana kwamba wameambiana mpaka wote wakatabasamu ikwemo muhudumu wa mapokezi aliyewakaribisha.
“Mmependeza sana.. Couple au?” Akaongea muhudumu akiwa bado Kaunda tabasamu lake usoni mwake.
“Ndiyo couple.. Tumefika hapa tuna kikao na mshirika mwenzetu wa kibiashara anaitwa Nikita Crawley yuko chumba namba 118 orofa ya nane..!” Akajibu swali la kuwa kama wao ni walio katika mahusiano kisha akaeleza sababu iliyowapeleka pale.
“Ooooh! Ni kweli amefika hapa muda si mrefu na alieleza wafanyabiashara wenzake watafika kwa maongezi, karibuni na rukhsa kwenu kwenda kumuona”Muhudumu wa mapokezi akawakaribisha tena na kuwaelekeza upande lifti itakayowafikisha orofa ya nane ilipo nao bila ajizi wakaelekea ilipo lift wakaingia ikawafikisha orofa ya nane wakatafuta chumba namba 118 walipokipata wakagonga mlango ukaja kufunguliwa na Agent Jade mwenyewe akiwa ametabasamu.
“Karibuni.. Nilishawamisi wapendanao nyie..!” Akawakaribisha, wote hakuna aliyemjibu wakabaki wanatabasamu tu kisha wakaingia ndani.
“Sasa tunaweza kuongea vizuri na kupanga mikakati ya kazi kwa uzuri.. Jamaa wameitwa kwa boss?” Agent Kai alianza kuongea baada tu ya kukaa kwenye sofa lililo karibu na dirisha pana la sebuleni ambalo waliinua pazia upande kidogo upande wan je ilikuwa kwa nyuma ya hoteli hii ambako kuna fukwe ya bahari mita kadhaa tu kutoka kwenye ukuta unaozunguka jengo la hoteli hii, swali lake hili alilomaliza katika kuongea kwake lilikuwa limeenda kwa Agent Jade.
“Kwa mujibu wa aliyewasikia wakiongea amenieleza hivyo” Alijibu Agent Jade kisha ya hapo alianza kueleza kwa urefu jinsi walivyoenda Salvador De Bahia Nightlife Club, Bar & Tips wakafanya maongezi mtego na mtu waliyemkuta kakaa meza ya peke yake ambapo aliwapa muelekeo wa wapi wataweza kumpata waliyesema wanamtafuta kama ndugu kaka wa Agent Jade, aliendelea kueleza walivyoenda mtaa wa mtaa wa Largo uliopo eneo la Old Quarter Pelourihno ambako waliamua kufanya ambayo yaliweza kumsaidia Agent Hansen kuingia ndani ya jengo hilo la ghorofa lenye ‘floor’ (orofa) mbili na hapo ndipo Hansen akaweza kumsikia mmoja ya ambao hawakutoka nje kumsikiliza yeye Jade kuwa wameitwa haraka sana na boss wao ambaye hakutajwa jina lakini kwa ilivyo inaweza kuwa wao wamerahisishiwa kazi.
“Oooh! Nimeelewa na ninasikia harufu ya marashi ya mtu tunayemsaka aliyetufanya tuje Bahia bila kupenda kuwa anaishi pale, itakuwa furaha kubwa sa..!” Kabla hajaendelea zaidi kuzungumza simu yake iliyo mfuko wa suruali ika ‘vibrate’ akaitoa kutoka mfukoni kioo kikamuonyesha anapigiwa na Detective Omar Chilamwena haraka hakuiacha iendelee ku vibrate akasugua kioo kwenda kulia kwa dole gumba lake.
“Haloo Chila!”
“Tunakaribia mtaa wenye zizi mkuu!”
“Vizuri msiingie zaidi papo hapo mwanzo wa mtaa jengo la kwanza tu lina urefu wa orofa mbili kuna mkahawa mdogo tu wekeni makazi hapo macho yawe makini kuangalia kwenye zizi.. Tutawajuza tulichoamua baada ya kikao mkakati tunachofanya muda huu hapa..!” Agent Kai akaongea kisha mpigaji huko alipo akakata simu.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na kumi na tisa (119)
Kusogea kwa majasusi awa karibu na jengo ambalo wanafikiri atakuwa yumo aliyewafanya wafike hapa Bahia ni sawa na kufuka moshi unaotaka kuwasha moto.
Muda mchache mambo mengi, twende kazi mbele!
“Karibuni.. Nilishawamisi wapendanao nyie..!” Akawakaribisha, wote hakuna aliyemjibu wakabaki wanatabasamu tu kisha wakaingia ndani.
“Sasa tunaweza kuongea vizuri na kupanga mikakati ya kazi kwa uzuri.. Jamaa wameitwa kwa boss?” Agent Kai alianza kuongea baada tu ya kukaa kwenye sofa lililo karibu na dirisha pana la sebuleni ambalo waliinua pazia upande kidogo upande wan je ilikuwa kwa nyuma ya hoteli hii ambako kuna fukwe ya bahari mita kadhaa tu kutoka kwenye ukuta unaozunguka jengo la hoteli hii, swali lake hili alilomaliza katika kuongea kwake lilikuwa limeenda kwa Agent Jade.
“Kwa mujibu wa aliyewasikia wakiongea amenieleza hivyo” Alijibu Agent Jade kisha ya hapo alianza kueleza kwa urefu jinsi walivyoenda Salvador De Bahia Nightlife Club, Bar & Tips wakafanya maongezi mtego na mtu waliyemkuta kakaa meza ya peke yake ambapo aliwapa muelekeo wa wapi wataweza kumpata waliyesema wanamtafuta kama ndugu kaka wa Agent Jade, aliendelea kueleza walivyoenda mtaa wa Largo uliopo eneo la Old Quarter Pelourihno ambako waliamua kufanya ambayo yaliweza kumsaidia Agent Hansen kuingia ndani ya jengo hilo la ghorofa lenye ‘floor’ (orofa) mbili na hapo ndipo Hansen akaweza kumsikia mmoja ya ambao hawakutoka nje kumsikiliza yeye Jade kuwa wameitwa haraka sana na boss wao ambaye hakutajwa jina lakini kwa ilivyo inaweza kuwa wao wamerahisishiwa kazi.
“Oooh! Nimeelewa na ninasikia harufu ya marashi ya mtu tunayemsaka aliyetufanya tuje Bahia bila kupenda kuwa anaishi pale, itakuwa furaha kubwa sa..!” Kabla hajaendelea zaidi kuzungumza simu yake iliyo mfuko wa suruali ika ‘vibrate’ akaitoa kutoka mfukoni kioo kikamuonyesha anapigiwa na Detective Omar Chilamwena haraka hakuiacha iendelee ku vibrate akasugua kioo kwenda kulia kwa dole gumba lake.
“Haloo Chila!”
“Tunakaribia mtaa wenye zizi mkuu!”
“Vizuri msiingie zaidi papo hapo mwanzo wa mtaa jengo la kwanza tu lina urefu wa orofa mbili kuna ka glocery kadogo tu wekeni makazi hapo macho yawe makini kuangalia kwenye zizi.. Tutawajuza tulichoamua baada ya kikao mkakati tunachofanya muda huu hapa..!” Agent Kai akaongea kisha mpigaji huko alipo akakata simu.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XIII
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
“..Huu mtaa ni mtaa ulio na majengo wanayoishi watu wenye pesa kwa jinsi ramani ya jiji hili inavyoonyesha hapa hivyo kiharaka haraka nimefikiria kuwa inawezekana tukachunguza lililo na uhakika zaidi kama adui yetu yupo ndani ya jengo lile na ndiyo huyo boss aliyetamkwa”Kikao cha watu watatu kilikuwa kimeshika hatamu ndani ya chumba chenye hadhi ya VIP katika hoteli hii, kauli hii ilizumgumzwa na Agent Jade Poul Brown akiwa kakaa katika sofa la kukaa watu wawili katika sebule hii.
“Hatuwezi juwa kiurahisi juu ya yote haya sisi tunachotakiwa ni kwenda ndani ya jengo kuona kama yaliyomo yamo boss aliyetamkwa ni Feca au lah!.. Ni vizuri Agent Kai ulivyofikiria na kuona kuna umuhimu wa kina Chila kuweka ulinzi wa kuona kila jambo, itatusaidia sana na hisia zangu zinanisonga kuwa pale alipo Feca ni kwenye jengo lile tu..!” Akaongea Special Agent Rebecca yeye akiwa kakaa sofa moja na sofa alilokaa Agent Kai kaka na boss wake kikazi kama yeye anavyopenda kumuita ‘boss’.
“Muda huu ni muda wa unaokaribia au ulio tayari kwa ajili ya chakula cha mchana nafikiri ni vizuri tukaagiza vyakula tule tushibe kisha tuje na mkakati tufanyeje maana naona sote tunahisi Feca yuko pale ingawa ni hisia zetu za kazi zinazotusukuma hivyo… Mimi nathubutu kusema Feca yumo mule ndani katika moja ya orofa na muda huu naye anaendesha kikao cha mkakati kazi wa kujilinda, naomba nitahadharishe kwetu sote kuwa Feca ni komandoo mwenye mafunzo ya juu yaliyompelekea kuwa mwalimu wa kijeshi katika mafunzo ya kijeshi ngazi ya ukomandoo katika nchi ya Mexico mpaka pale alipokutwa na hatia ya kufanya biashara ya ulanguzi wa madwa ya kulevya katika kambi za jeshi ingawa waliokutwa na mzigo wa ushahidi walimficha na kukubali wafungwe wao ni ushahidi wa audio zilizonaswa katika maongezi yake ndizo zilizomtia hatiani na kupelekea kufungwa miaka aliyofungwa… Umri wake umesogea kwa sasa hivyo ufanisi wake katika mipango, kutumia silaha aina zote na kupambana kwa mapigano ya ana kwa ana itakuwa umepungua kidogo lakini beberu lililozeeka ndiyo uwa lina harufu kali zaidi ya kuogofya katika kila hali na hata kutisha kwa jinsi linavyokuwa nachelea kusema hivi nikimaanisha kuwa tusimuingie kana kwamba tunamuingia mwanafunzi wa kazi za kijeshi na ujasusi ni mtu wa hatari ni beberu lililokomaa mjanja sana kukwepa mikono ya sheria na kukwepa maadui zake.. Hivyo naomba tuamue tunakula kwanza au tunaweka akili zetu kwa kuimaliza operesheni hii kwa ushindi?” Aliongea kwa kirefu kaka jasusi na kachero Agent Kai akiwatizama kwa zamu wenzake.
“Hatuwezi tukaweka mbele kula wakati pua zetu zimenusa harufu ya beberu unalosema kaka.. Sitakula mpaka tuwe tumeweka mkakati sawa si ndivyo shosti wangu?” Agent Jade aliongea na kumalizia kwa swali kwa mwanamke mwenzie Special Agent Rebecca.
“..Basi naweza nikasema walio nje waendelee kuwepo huko wakitizama nyendo zote kwa umakini.. Nilieleza uzoefu wa kazi wa beberu la mbuzi Feca kwa sababu nilitaka kila mmoja kati yetu atambue ndani ya jengo lile kuna komandoo wa jeshi hivyo havamiwi kama wanavyovamiwa watu wengine walio na ujuzi mdogo… Muda huu ni mchana na kazi za kijasusi zinakuwa kama mlo mtamu wa chakula cha usiku zinapofanyika muda wa usiku, sote tunajua kazi yetu ni kazi ya gizani kuanzia uchunguzi hadi mapambano yetu.. Tunasema gizani sababu uwa tunachunguza vilivyojificha hivyo uwa tuko gizani tukichunguza nini vilivyo gizani kisha kuvileta kwenye mwanga lakini tunatambua upinzani tunaopata wakati tunapambania tunayopambania huko gizani… Acha mchezo wa giza upewe heshima yake tutapumzika tukichunguza kikawaida kama tutaona kuna ulazima kufanya hivyo kukiwa na uhakika hatuharibu chochote na ifikapo usiku mnene tutavamia kwenye jengo kumalizia kilichokuwa kimetangulizwa” Aliongea Agent Kai huku anatabasamu baada ya kuona warembo awa walio katika sura zao za bandia wametingisha vichwa vyao kukubaliana na anachokizungumza.
“Na kubaliana na wewe.. Je tutafanyaje sasa kwa wakati huu?” Akaongea na kuuliza swali S.A Rebecca akiwa ana wazo lakini wazo hilo alilonalo kifuani mwake aliamini ndilo lililo kwa wote hapa kwa uzoefu wake wa kazi za kazi za gizani.
“Niko na Ipad yangu hapa si kama nachat kwenye social media nikitafuta mrembo wa kibrazil wa kubarizi naye usiku wa leo au baada ya siku ya leo baada ya ushindi ninaoamini huko njiani lah hasha! Niko online naelekezana jambo na fundi Lizy Roby, yuko kwenye mitambo anafanya udukuzi wake wa cctv kamera za mtaa huu kuona kama anaweza kunasa picha ya mke wa Feca, mtu yoyote aliye karibu na Feca au hata Feca mwenyewe na taratibu anasema mambo yanaweza kamilika na kutupa majibu kwa video au picha za ushahidi utakaotupa mwanga ni nini!” Akajibu kiufafanuzi Agent Kai huku anaionyesha Ipad yake, kiukweli katika maisha yake ya kazi mtu huyu toka Afrika nchi ya Tanzania kiuhalisia kama mzaliwa akihudumu kikazi katika nchi ya Marekani aliko na uraia wake, anatakiwa kumshukuru sana mwanadada Elizabeth Robert “Lizy Roby’ kwakuwa umrahisishia kazi zake kiteknolojia kama ujuavyo kazi za ujasusi na teknolojia kwa dunia ya sasa ni mapacha wanaofanana.
“Hahahah! Unatafuta mrembo wa kibrazil.. Kaka kwa mwarabu umekolea unatafataje mwanamke mwingine? Hahahaha hahahaha haaaa!” Agent Jade akaongea akicheka kwa furaha kubwa kisha akainuka na kusogea dirishani.
“..Vueni hizo sura zenu nataka niwaone warembo wangu halisi niliowazoea.. Aisee CIA yote nawajua baadhi ya madada makachero na majasusi walio wa siri na wa kazi za kazi lakini nyie ambao nawajua kwangu mimi ndiyo wazuri sana napenda pia mna ubongo wa kazi ulio makini na kazi sijui kwa nisiowajua hasa maajenti wa siri.. Mungu awalinde..” Aliongea Agent Kai huku anavua sura ya bandia aliyovaa inayomuonyesha kama kijana wa kizungu anayefanana na wanaume wa kireno, brazil au latin amerika.
“Akitokea muhudumu au tukitaka huduma ikiwa alituona hapo kabla si atajua kakutana na majini wanaojibadili sura zao kwa mwendokasi ila masura haya kukaanayo muda mrefu ni kipaji..!”Agent Jade mpenda stori zaidi kuliko Rebecca aliongea lakini hakuwa ameacha kufanya vile wanavyofanya wenzake kuondoa misura feki.
Waliendelea kwa kila mmoja kuongea utani utani kumtania mwenzake kwa kila anachoona ni utani usioumiza kwakuwa wote awa ni watu waliozoena kikazi hasa S.A Rebecca na Agent Kai na Jade pia kiukweli amemzoea sana Kai pia kwakuwa amefanya naye mafunzo mbalimbali katika elimu mbalimbali za mafunzo mbalimbali ya kijasusi na jeshi.
***** ***** *****
Muda mmoja unaorandana na majasusi watatu walio ndani ya moja chumba cha VIP cha hotel ya Wish Da Bahia Hotel na wengine watatu wakiwa katika mkahawa ulio karibu na kona ya kuingilia mtaa huu katika jengo wnalolilenga majasusi awa kulikuwa na kikao bila wao kujua kuwa hatua chache toka walipo kuna watu wameweka kambi wakipanga mikakati kazi ya kuvamia katika jengo lao baada usiku wanaotamani uingie utakapoingia, kikao kilichokuwa kimeitishwa kwa haraka na ‘Kingpin’ Feca mwenyewe na watu ambao wanamlinda yeye na wenzake wanaotakiwa kulindwa kwa umakini mkubwa.
“Nimewaita hapa nyote kutaka kuwapeni taarifa ambayo si nzuri kwetu… Nimepokea taarifa muda si mrefu kupitia njia zangu za kimawasiliano juu ya mpuuzi aliyeharibu mambo yetu huko GTL na Mexico ndiyo anayeongoza tena kikosi cha wamarekani wa shirika la kijasusi la CIA kuhakikisha wananitia nguvuni mimi na wenzangu hapa kwa oda ya mkurugenzi wa ujasusi wa Marekani.. Hapo awali tulikuwa tumelishwa uyoga pori kuwa waliofika hapa ni DTO kumbe si kweli waliofika hapa Bahia ni CIA tena wakiongozwa na adui yetu namba moja Agent Kai Hamis kikaragosi mweusi mwenye ujasiri unaokolezwa na uchawi wa bibi yake kama baadhi ya watu wengine walio katika mtandao wa kiuhalifu wanavyomnadi..!”Alianza kuongea Kingpin Feca kisha akanyamaza kuwaangalia wanaomsikiliza ambao karibu kila mmoja kati yao alikuwa na kamshtuko kusikia CIA wako hapa Bahia ukizingatia kilichowashwa huko Guatemala kiliwaogopesha na kuwafanya mpaka waishi kwa wasiwasi bila familia zao ilipokuwa hakuna budi zaidi ya kuzikimbia na wengine bila hata taarifa.
“Msinyong’onyee.. Natambua wale walio na roho za upambanaji katika genge letu miaka sita mpaka mitano iliyopita karibu wote wameteketea katika operesheni hii iliyotukumba tukiwa tumelemaa tukiamini hakuna baya la kutukumba hili ni kosa la kifundi tulilolifanya kama genge baada ya kuwa tumesambaratisha magenge mengine na kutawala soko kwa ukubwa na upana wake katika kusini na kaskazini mwa mabara ya amerika, tulibweteka sana na ndicho kilichotuharibia, nathubutu kusema hivyo lakini sitaki tujutie yaliyopotea sababu tuna nafasi ya kuinukia tena lakini tutainukia baada ya kufanya kile ambacho naamini kama tutatuliza akili zetu kabla ya siku mbili mbele tutakuwa tushaweka funzo kwa wamarekani na CIA yao kwa ujumla kwa stahili ya jino kwa jino nasema jino kwa jino sababu tutawafyeka wapuuzi wao wote waliofika hapa Salvador kisha tutaandaa shambulizi la kigaidi ndani ya nchi yao kama kisasi chetu cha jino kwa jino wameng’oa letu nasi tutang’oa lao kichwa kwa kichwa maiti kwa maiti, naapa sitawaacha wawe na raha kwa waliyotufanyia.. Nilifikiri kupata kwa watu wao waliowapata katika operesheni yao ya kutaka kuwarejesha kwao mateka tuliokuwa tunawashikilia Tajumulco itakuwa wamemaliza, wanakuja hadi huku kwa oda hiyo niliyosema heti Feca anatakiwa akajibu mashitaka nchini kwao in my body dead si hai kama wazaniavyo nitapambana mpaka tone la mwisho la pumzi zangu na ninaamini huyo Kai litarudi jina nchini kwao si mwili wake maana nitahakikisha anazikwa katika matumbo ya wanyama kama mnyama maana nitamkata kata vipande kama nyama nguruwe buchani… Tunatakiwa tuitumie siku ya leo vizuri kuwapata watu awa wakiwa hai au wakiwa katika miili iliyokufa.. Wanatembea katika sura zisizo zao ni waoga na wao wanaogopa mtu aliye na umri wangu umri wa wazazi wao.. Mkakati wa kwanza ni kuwawinda sababu mpango wao kutaka kumtumia mke wangu hili kunifikia nimeshaudhibiti wamefeli kwa asilimia mia moja ni sisi sasa tunaotakiwa kuwawinda wao si wao kutuwinda sisi na kutukaribia kama walivyowakaribia kina Zuantejo huko GTL”Aliongea kwa hisia kali Kingpin Feca mkononi akiwa kashika bastola yake aina ya Tokarev TT-30 anaichezea chezea kwa kuizungusha kifundi mzee huyu, moja ya bastola bora sana kwa matumizi ya kutoa roho na kutia majeraha watu zao la kutoka nchini Russia iliyotengenezwa kwa jumba lililonakshiwa dhahabu kana kwamba ikiua inaua bila kuacha maumivu kwa muhusika, bastola iliyomgharimu mamilioni ya pesa kwa pesa za kibongo ikiwa ni oda maalumu kutoka kwake kwenda kiwandani moja kwa moja.
“Ilivyo ni kwamba polisi na mamlaka zingine za kiusalama na wao wanawasaka watu awa kwakuwa wamefanya madhara kwa jeshi la polisi, hivyo tuko nao bega kwa bega kuna fungu nililitoa kwa Kamishina wa polisi usiku uliopita nilimtuma mtu kupeleka alipoenda hospitali na maongez yao yamefanyika vizuri hakuna shida juu ya hili hivyo tuna mamlaka ya kuwafanya chochote watu awa, popote pale tunapokutana nao bila kusita tunaruhusiwa kuwavamia na kuwachukua iwe mmoja au wakiwa katika kikundi… Watu awa kama nilivyoeleza awali kuwa tulilishwa uyoga pori hawako wawili tu kama tulivyopokea taarifa watu awa wako sita hivyo hawakuja wakitudharau ndiyo maana wamekuja wengi wanajua Feca si mwepesi na ninaahidi nitawaonyesha kama mimi ni nani?... Mkakati wa kwanza nataka mpitie katika hoteli ambazo nimepenyezewa taarifa hapa na mtu ambaye usiku kucha alikuwa akipita pita kupeleleza katika mahoteli mbalimbali ya nyota tano, nne mpaka tatu amepata majibu ya watu ambao wanafanana na watu awa kimuonekano wa miili maana kwa ujanja wao wa kutumia sura za bandia imebidi tutumie mbinu mbadala wa kufananisha miili yao katika kimo na mengineyo si sura tena.. Watakaotoka hapa kwenda huko ninawaomba muende kiakili katika hizo hoteli pia nimeomba msaada wa vijana wa nguvu kazi toka Argentina hadi saa kumi jioni watafika hapa kutuongezea nguvu maana awa watu si watu wa kawaida na wametupania sana kuharibu TRJ na kila kitu chake..” Alieleza tena kwa kirefu kwa sasa munkari wa kuongea kwa hasira ulikuwa umeshuka akatoa miwani yake toka machoni akainuka na kumimina kinywaji akipendacho katika glasi kutoka kwenye chupa ya mvinyo huo, akagonga funda tatu za kufuatana zenye ujazo mpaka mashavu yakatuna na kupungua kila anavyoweka mdomoni na kumeza.
“Umesema mtu wako amegundua hoteli walizofikia watu awa.. Je unaonaje kama ungesubiri nguvu kazi uliyoiomba toka Argentina ndiyo wavamiwe? Maana tunatambua hapa Salvador mtu aliyefika akiwa na uzoefu na mikiki ya kazi hizi ukiacha wewe mwenyewe ni mimi na walinzi wetu watano tuliofika nao hapa Salvador wengine wote ni watu wa kawaida ambao si wazoefu katika hili na hata vijana awa wa kibrazili si wazoefu kama tunavyoweza kudhania pia kumbuka hawapambani na watu walio wanafunzi katika kazi za ukachero, ujasusi na uhalifu wa kimataifa.. Wazo langu naomba kazi hii ingesogea mpaka kuanzai jioni ya leo na tena itakuwa vizuri sababu kiuhalisia na uzoefu wangu majasusi na makachero uwa wanaanza kuranda randa kunusa taarifa wanazozitafuta kwa watu wanaofikiri watawasogeza mbele… Langu ni hili mkuu!” Aliongea Puto Sergio Lopez huyu ni rafiki mkubwa wa Feca ambaye alikuwa ameshika mipango ya genge lao nchini Marekani alirudi Mexico baada ya kupata taarifa juu ya hali ya hatari iliyotokea nchini Guatemala na ni kweli alilokuwa akiliongelea juu ya watu walio hapa katika jiji la Bahia kuwa si watu wa kazi sana kama ilivyokuwa awali wakati genge la TRJ linaanza watu kama kina Ivan ‘alto genius’ mtu makini mwenye akili za kutosha kuchanganua mambo ambaye alikufa akiwa kwenye helkopta kwa kombora la lililoidungua wakati wanaenda jimboni San Marcos kutoa msaada baada ya taarifa ya uvamizi wa kina Agent Kai, walikuwepo watu makatili mmexico mwenye asili ya ujerumani Wolfs Klauben Gend (Mnyama), Cisco Murlindo a.k.a Tocon (kisiki) na wengineo kama awa walio na ukatili na ujuzi.
Kingpin Feca kabla hajaanza kuijadili hoja iiyotolewa na rafiki yake simu yake iliingia meseji katika mtandao wa whatsapp akaonyesha ishara kwa mkono wake usiokuwa umeshika bastola kuwa watulie asome meseji kwanza.
“Brigedia Grannell amenitumia meseji amefika hapa Salvador yuko kwenye katika maduka ya katikati ya jiji, naomba Marcelo umfuate uwe makini sana maana mtu huyo alikuwa ni mkurugenzi wa uhamiaji hivyo anaweza kuwa anafuatiliwa nitaomba umpeleke kwenu baada ya kuhakikisha kuko salama salimini itakapofika usiku ndiyo ataletwa hapa kwa usalama zaidi ndiyo maana nimeweka hiyo taratibu isije kusogeza nzi..!”Alitoa maelekezo huku anamuangalia aliyemtaja jina anaitwa Marcelo.
“Nitamjuaje?”Akauliza.
“Nimemuelekeza ulivyovaa pia naye amenielekeza atakapokaa kwenye duka la kuuza bidhaa za Samsung kwakuwa wewe mwenyeji utakuwa unapajua, sawa nenda sasa na utabaki naye huko kwenu mpaka nitakapowajuza mje” Akafafanua Feca.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini (120)
Ndani ya chumba cha VIP katika hotel ya Wish Da Bahia mkakati kazi umepangwa kuwa ifikapo usiku utakuwa usiku wa kumaliza kazi, usiku wa kumuonyesha Feca kuwa ukiujua huu wapo wanaoujua huu pia.
Ndani ya ghorofa lenye urefu wa orofa tano kwenda juu nako kuna mikakati inapangwa wakiwa hawajui kuwa mkia gari wa gari aina ya Cadillac XTS 2016 umewasogezea hatari na nusu ambayo inaweza kuwa nzima kama itafanywa kwa usahihi na mafundi awa, wakijipanga kuwa wanataka kufanya nini na nini kuhusu timu pinzani kumbe na timu pinzani wanayoipangia imekaa kwenye mstari mwekundu ikisubiri kitufe chekundu kubonyezwa.
Tuweke stori ufafanuzi kando twende kazi!
“Umesema mtu wako amegundua hoteli walizofikia watu awa.. Je unaonaje kama ungesubiri nguvu kazi uliyoiomba toka Argentina ndiyo wavamiwe? Maana tunatambua hapa Salvador mtu aliyefika akiwa na uzoefu na mikiki ya kazi hizi ukiacha wewe mwenyewe ni mimi na walinzi wetu watano tuliofika nao hapa Salvador wengine wote ni watu wa kawaida ambao si wazoefu katika hili na hata vijana awa wa kibrazili si wazoefu kama tunavyoweza kudhania pia kumbuka hawapambani na watu walio wanafunzi katika kazi za ukachero, ujasusi na uhalifu wa kimataifa.. Wazo langu naomba kazi hii ingesogea mpaka kuanzai jioni ya leo na tena itakuwa vizuri sababu kiuhalisia na uzoefu wangu majasusi na makachero uwa wanaanza kuranda randa kunusa taarifa wanazozitafuta kwa watu wanaofikiri watawasogeza mbele… Langu ni hili mkuu!” Aliongea Puto Sergio Lopez huyu ni rafiki mkubwa wa Feca ambaye alikuwa ameshika mipango ya genge lao nchini Marekani alirudi Mexico baada ya kupata taarifa juu ya hali ya hatari iliyotokea nchini Guatemala na ni kweli alilokuwa akiliongelea juu ya watu walio hapa katika jiji la Bahia kuwa si watu wa kazi sana kama ilivyokuwa awali wakati genge la TRJ linaanza watu kama kina Ivan ‘alto genius’ mtu makini mwenye akili za kutosha kuchanganua mambo ambaye alikufa akiwa kwenye helkopta kwa kombora la lililoidungua wakati wanaenda jimboni San Marcos kutoa msaada baada ya taarifa ya uvamizi wa kina Agent Kai, walikuwepo watu makatili mmexico mwenye asili ya ujerumani Wolfs Klauben Gend (Mnyama), Cisco Murlindo a.k.a Tocon (kisiki) na wengineo kama awa walio na ukatili na ujuzi.
Kingpin Feca kabla hajaanza kuijadili hoja iiyotolewa na rafiki yake simu yake iliingia meseji katika mtandao wa whatsapp akaonyesha ishara kwa mkono wake usiokuwa umeshika bastola kuwa watulie asome meseji kwanza.
“Brigedia Grannell amenitumia meseji amefika hapa Salvador yuko kwenye katika maduka ya katikati ya jiji, naomba Marcelo umfuate uwe makini sana maana mtu huyo alikuwa ni mkurugenzi wa uhamiaji hivyo anaweza kuwa anafuatiliwa nitaomba umpeleke kwenu baada ya kuhakikisha kuko salama salimini itakapofika usiku ndiyo ataletwa hapa kwa usalama zaidi ndiyo maana nimeweka hiyo taratibu isije kusogeza nzi..!”Alitoa maelekezo huku anamuangalia aliyemtaja jina anaitwa Marcelo.
“Nitamjuaje?”Akauliza.
“Nimemuelekeza ulivyovaa pia naye amenielekeza atakapokaa kwenye duka la kuuza bidhaa za Samsung kwakuwa wewe mwenyeji utakuwa unapajua, sawa nenda sasa na utabaki naye huko kwenu mpaka nitakapowajuza mje” Akafafanua Feca.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XIV
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Detective Omar Chilamwena alikuwa macho yake hayatembei mahali pengine zaidi ya akiinama kichwa kunywa kinywaji chake sekunde tu anainua kuangalia umbali wa mita zaidi ya mia mbili toka walipo, anaangalia lilipo geti lililoshikana na ukuta unaozunguka jengo la ghorofa lenye urefu wa orofa tano kwenda juu huku ya geti juu ya geti lile rangi nyeusi kukiwa na kenop.
Gari aina ya Cadillac XTS 2016 ambazo ni gari zilizo zaidi ya nne ambazo ni aina hii zilizo katika banda la kuwekea magari lililo katika ndani ya kuta zinazozunguka jengo hili viziwa sasa na majasusi awa wa CIA, gari hizi aina moja zilinunuliwa ili kuzuia maadui kujua mtu wanayemlenga yuko kwenye gari gani kwakuwa zote zilifanana hivyo ilitakiwa uzijue namba za hizi gari ndipo ungeweza elezea gari ya mtu yupi unayemuhitaji endapo kutatokea tatizo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment