Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

MSHANGAO - 3

   

Simulizi : Mshangao 

Sehemu Ya : Tatu (3)

kutabasamu kichwani akiwa na viulizo vingi visivyo na majibu.

“Kuna mlinzi ambaye uwa anajua apartment gani Mr Logan atafanya kikao nasi, sababu uwa anabadili sehemu kila anavyokuja huko kwenye VIP… Nafikiri atatuona, tusogee mpaka ukumbi wa disco akiniona atatufuata”. Akasema Damia huku akimuelekeza Jeong wapi wapiti kuelekea kwenye ukumbi wa disco, kwa mwendo wa haraka wakaingia kwenye ukumbi kisha Damia akakata tiketi mbili za kuwaruhusu kuingia kwenye ukumbi wa disco kwakuwa ni lazima.


Watu walikuwa si wengi sana hapa kwenye kukata tiketi kutokana wengi waliowai kufika walishakata tiketi na kuingia muda tu. Ila walipoingia ukumbi wenyewe wa disco ndipo walipokutana na maana halisi ya Nightlife, watu waume kwa wakike wa marika ya tofauti na rangi za mataifa mbalimbali walikuwa wakiponda raha wapo wenye kucheza muziki, wenye kunywa pombe na vinywaji vya aina mbalimbali, madada poa hadi makaka poa wakijitahidi kufanya vishawishi kwa wanaume hili wawape huduma haramu wakifanya yao.


Wakiwa kwenye kushangaa shangaa kutafuta mtu aliyemsema Damia, Jeong akamuona mtu anayekuja upande walipo kwa kasi. Na Damia alipogeuka kumtizama tu akatabasamu na wote wakatabasamu.


Alikuwa ni yule waliyemtaraji naye akawaonyesha ishara kwa mkono wamfuate na papo hapo akageuka na kuanza kuongoza hadi kwenye lifti, Damia na Jeong wakajiunga naye jamaa akabonyeza kitufe cha kufungua mlango wa lifti kisha wote wakazama ndani mlango ulipofunguka, jamaa akabonyeza tena vitufe kwa namba kadhaa na alipoacha tu lifti ikaanza kupanda juu.

Dakika mbili mbele lifti ikafika floor (losheni) waliyotakiwa kufika mlango ukajifungua wakatokea koridoni jamaa kwa mwendo wa kasi akawaongoza kuipita milango miwili mpaka mwisho wa korido wakakuta mlango mwingine. Jamaa akabonyeza swichi kwa mipigo mitatu hazikupita sekunde thelathini mlango ukafunguliwa ikiwa walio ndani washahakikisha usalama wao.

“Wageni wa boss hawa”. Akasema kumwambia aliyekuja kufungua mlango kisha yeye akageuka kuondoka kurudi alipotoka kazi yake ikiwa imeisha kwa kina Damia.

“Piteni…!” Hakuwa na maneno mengi mfunguaji zaidi ya neno alilotoa huku akiwapisha mlangoni na walipopita tu bila kuchelewa akaufunga mlango.

Jeong na Damia macho yakapokewa na machoya watu zaidi ya ishirini na nane hii ilimaanisha sebule ile ya VIP ya hii Nightlife ya Chakit Bukit Bintang ilikuwa na watu kumi na nne, ilikuwa sebule pana sana yenye malumalu za kung’aa sakafuni na juu darini gypsum iliyotengenezwa kisasa na mafeni yanayoning’inia kama maua fulani ya kupendeza, masofa ya kukaa watu wawili wawili yaliyokaa kila baada ya hatua fulani kila upande ndipo walipogawana kukaa watu waliowakuta mule ndani wakiwa ni wanaume watupu hivyo kuongezeka kwa Damia na Jeong kuliongeza idadi ya watu mule varandani mwanamke akiwa ni Damia peke yake.


Walioingia walitoa heshima yao kwa waliowakuta na kisha kila mmoja akaenda kukaa alipoona ni nafasi kwake kukaa.

Dakika tatu mbele toka waingie Jeong na Damia kulikuwa kimya kimaongezi vikisikika vinywaji vinavyohama toka kwenye chupa kuingia kwenye glasi kisha kwa wengine vikisikika wanavyopokea vinywaji vyao kwenye makoo yao.


Mara mlango wa chumba kilichopo pembeni kushoto mwa sebule ulifunguka akatoka mtu ambaye alivaa suti ya rangi kijivu yenye madoadoa meupe viatu vya rangi nyeusi vyote suti na viatu vikiwa toka kampuni kubwa ya kutengeneza mavazi ya DOLCE&CABBANA, mtu mrefu wa kutosha ule urefu wa wastani kichwani akiwa kava kofia ya maribolo wanazopenda kuvaa wakimbiaji wa farasi, machoni miwani ya ki FBI Kama kwamba yeye ni mtu shirika hilo la kipelelezi, usoni hakuwa yule waliyemjua kati ya wote walio pale. Umbo halilo nalo na kimo cha urefu walionao kilimfanya kutowadanganya wote kwa sura aliyovaa ya bandia, alikuwa ni Mr Logan Puter a.k.a Master plan alipenda kuitwa hivyo kijina la siri pale anapoongelewa na watu wake ikiwa wapo na watu wengine wasiomjua.


“Yes! Naona idadi niliyoagiza ifike hapa imetimia ile ambayo nilihitaji iwepo hapa kusikiliza nini naongea… Nitapenda kila mtu awe makini kusikia chochote kile nitakachoongea kwa manufaa yetu sote…!”. Akaongea huku akisogea kati kati ya sebule na glasi yake yenye kinywaji aina luc belaire kutoka ufaransa.

“Kwenye kikosi chetu hiki kuna wageni watatu niliwaomba muda mrefu leo hii wameingia hapa Kuala Lumpur na kwa taarifa nilizopewa wako njiani kufika hapa kwa maelekezo niliyowapa muda si mrefu… Wote wanatokea Mongolia ni watu wa hatari sana wenye uwezo wa juu sana katika kutumia silaha na mapigano, wamekuja kipindi ambacho ni muhimu sana kwetu”. Akaendelea kuongea kisha akapiga funda moja kubwa la wine yake hii aipendayo sana.


Mara alipogeuka wakasikia hodi ikigongwa kwa stahili ile ile ya ugongaji ambayo kwao huwajulisha ni mtu wao anayegonga.

Haraka mtu mmoja akasogea na kuchungulia kwenye tundu akawaona wanaume wanne akageuka kumuangalia Mr Logan Puter na kumuonyesha ishara kuwa watu wanne wamesimama mlangoni naye akamjibu kwa ishara fungua mlango. Jamaa akafungua mlango na kuwaruhusu walioletwa na yule mletaji watu pale wapite.

“Waooh! Waoooh! Waooh… Wageni wetu ndiyo hawa jamani, hawa ndiyo muda wa dakika chache zilizopita niliwaongelea… Karibuni majabali na hawa ndiyo wenzenu mtakaokuja kushirikiana nao, naomba wajitambulishe wenyewe na wao watawajueni nyiye wote kwa muda wenu”.

“Ahsante sana kwa kutukaribisha kwa moyo mkunjufu na mimi kwa niaba ya wenzangu naahidi tutafanya kazi zote kwa ufanisi wa hali ya juu na tupo tayari kuanza mara moja kazi ambayo boss bwana Logan Puter umetuambia ipo mikononi mwenu”. Akaanza mmoja kuongea na huyu hakuwa mwili mkubwa kuliko wenzake lakini alionekana ana kile ambacho mtu wa kazi yeyote akimuangalia tu anakiona mara moja. Kisha wote wakifuatana walizunguka kutoa mkono wa salamu kwa watu wote waliomo mule varandani, walipomaliza kila mmoja alikwenda alipoona kuna nafasi ya kukaa.

“Naamini tumefika katika wakati uliostahili mkuu na kwa utaalamu wangu naziona sura za kazi tupu… Naitwa Istqal Saanjin jina langu la kikazi mnaweza kuniita ‘the iron’” Akaongea mwingine huku akipokea kinywaji alicholetewa na mtu aliyekuwa akiwahudumia mule ndani kisha yule mtu aliondoka akiwa kashagawa vinywaji kwa watu wote waliokuwa wapo na kuacha zingine za ziada kama alivyoagizwa na boss bwana Logan.


Huyu aliyejitambulisha alikuwa na mwili uliokaa kimazoezi katika kukomaa kwake utagundua ni mtu wa hatari licha ya kuwa mwili huo ulikuwa ndani ya suti.

“Karibu sana ‘the iron’”. Baadhi ya watu walijikuta wakiongea kwa pamoja kumkaribisha.

“Mtanisamehe jamani sikujitambulisha naitwa nani?.... Naitwa Khorloogin Bayari watu wangu wa nguvu wa Mongolia upenda kuniita ‘Mongolia Damme’ sababu ya sifa kubwa niliyonayo kupiga round kick kama anavyofanya Jean Claude Van Damme, ikitokea bahati nzuri siku tukakutana na mtu anayejitia kuingilia maslahi yetu nitaomba tusimuadhibu kwa silaha nitaomba nipigane naye hili muweze kuona kama wa Mongolia wako sahihi au hawako sahihi”. Akasema yule aliyeanza kuongea kwanza kushukuru kukaribishwa na nikamuelezea kuwa alikuwa ni mtu asiye na mwili ule wa kutisha lakini urefu wake na umbo lake havikuficha kuonekana yeye ni mtu wa aina gani hasa machoni kwa watu wa kazi zilizo kazi haswa si kazi za kuandika andika kama mimi niandikavyo hapa.


Kingine aliwavunja mbavu watu wa pale aliporuka sarakasi ya kujibetua toka kwenye sofa alilokaa kisha kuzungusha round kick za kuunganisha hewani mara mbili kisha akakaa vile vile alivyokaa bila kuiathiri suti aliyovaa na hata kuangusha miwani ya macho aliyovaa. Mr Logan akatikisa kichwa kukubali kisha akapiga makofi wengine nao wakaunga mkono kupiga makofi kukubali huku karibu nusu yao na zaidi kidogo wakitabasamu.

“Itabidi uwe mwalimu wetu wa siri ya uwepesi huo”. Akasema Nawaz Patrash ambaye katika kundi hili la siri akiwa ni kiongozi msaidizi kutoka Mr Logan mwenyewe basi huyu ndiye muaminiwa zaidi na zaidi kuliko watu wote kati ya alionao. Akimfunika kwa kumfanya kuwa mhasibu wa kampuni yake maarufu katika biashara nchini Malaysia iitwayo Puter Group of Business. Kiliibuka kicheko kingine tena kwa baadhi ya watu.

“Haya mambo ni magumu kuyajua ukubwani, mi nilijifunza nikiwa mtoto kabisa na nilifundishwa na babu yangu mzaa mama yangu”. Akajibu muombwa ‘Mongolia Damme’.

“Mimi naitwa Bayan-Uugun Bayar uwa sina a.k.a napenda kuacha brand yangu kila niendapo kwa kukuza jina langu ningependa wote mniite ‘Uugun’ ni mdogo wake na jamaa aliyetoka kujitambulisha, mimi sina maneno mengi ila nikipewa kazi mtayaona majibu yake, nipo hapa kuongeza ujuzi wangu nilionao katika kuwasaidia nyinyi nyote na nyie kunisaidia mimi kuongeza ujuzi…. Naamini siku tatu tu kwa idadi tuliyonayo tutakuwa tushawaondoa nchi hii watu ambao tunatakiwa kuwaondoa na kuwapeleka wanapotakiwa”. Akasema ambaye yeye ndiye mtu pekee kati ya watu watatu waliofika muda huo toka Mongolia hakuvaa suti yeye alivaa kaptura pensi aina ya timberland na raba simple na fulana yenye nyekundu kama rangi ya raba alizovaa kichwani akiwa bonge la upara linalong’aa mafuta.

“Karibuni sana tena sana na ahsanteni kwa utambulisho wenu mzuri mliofanya…. Kwangu mimi nina siri nzito juu yenu maana nikianza kuhadithia hadithi ya vipi niliwajua kila mmoja hapa atashangaa mkiwemo nyinyi wenyewe…. Kidogo nachoweza kusema na sitakuwa na haja ya kuendelea na icho nitakachosema ni kuwa wote nyinyi majina yenu nilipewa na mtu mmoja rafiki yangu mkubwa sana na ni mkuu wa kitengo cha ujasusi cha nchini kwenu Mongolia akaniambia nikiwapata nyinyi mtanirahisishia kazi zangu nyingi sababu nyinyi ni vipaji anavyovikubali na kuviogopa sana”. Akasema Mr Puter na kutoa ishara ya saluti kwa kila mmoja ya wageni wale.

“Eeeeh! Kumbe adui yetu nchini kwetu anatupenda sana, mbona uwa anatukosakosa kila mara tena bila kuchoka akituwinda yeye, majasusi wenzake na shirika la upelelezi la Mongolia?... Hahahahah! Nimefurahi kujua hivyo”. Akasema huku akicheka ‘Mongolia Damme’.

“Istqal atakuwa anajua maana amefanya kazi idara ya ujasusi ikulu miaka ishirini na kafanya kazi na Alexander Zabel mkuu wa idara ya jasusi miaka yote mpaka walipotaka kumuua kwa kugundua mipango ya siri ya waziri wa ulinzi”. Akaongea Uugun huku ile habari waliyopewa na Mr Logan ikiwafurahisha sana sura zao zikiwa hazijajificha furaha waliyonayo.

“Ahsanteni sana… Nafikiri tunatakiwa turudi kwenye dhumuni la kikao chetu… Nikishamaliza nilichokuja nacho hapa kikaoni itakuwa muda wa watu wengine kujitambulisha kwa wageni wetu” Akaongea Mr Logan kisha akapiga hatua kwenda meza ya kioo ambayo kikawaida mara nyingi wahudumu wa club hii uwa wanaiweka katikati ya varanda hii ya VIP lakini leo hii ilisogezwa pembeni, alipofika aliiweka glasi ya kinywaji alichokuwa anakunywa na kunyanyua Ipad.

“Napenda kwanza nitoe pole kwa watu tuliokuwa tukishirikiana nao kikazi ambao jana mtu anayeitwa Agent Kai Hamis Mussa amewaua… Huyu Kai Hamis Mussa ni jasusi wa CIA ambaye taarifa zake za kuingia nchini hapa nilizipata siku nne zilizopita toka kwa mtu wangu wa CIA aliye makao makuu ya CIA, nikaweka mtego wangu kwa watu wangu walioko idara ya uhamiaji wakaniwezesha kujua mtu huyo ataingia kwa ndege gani na muda gani, niliuandaa mtego wa kumnasa vizuri na uzuri tulifanikiwa kumteka nyara mwanamke ambaye yeye nilichelewa kupewa taarifa za uingiaji wake sababu nayemtegemea alikuwa anaumwa hivyo aliniambia wakati huyo mwanamke tayari kashaingia hapa Kuala Lumpur ikabidi niwatumie wahudumu wa pale ubalozi wa Marekani kuzijua nyendo zake… Bahati nzuri katika kufanya kwake upelelezi wa kwanza kina Nawaz walikutana naye akitoka kuchunguza eneo lile tulilowateka wanasayansi wao wanaowatafuta kwa udi na uvumba kiasi cha kuvuruga mipango yetu ya kuwaondoa kwa jinsi walivyoweka ulinzi wao”. Hapa alisimama kidogo akawatizama baadhi ya watu walio mbele yake kutokea pale katikati ya varanda aliposimama kisha akageuka upande wa kulia.


Mwisho wa sehemu ya kumi na nne (14)


Mwisho wa sehemu moja utupa nafasi ya kujua mengi yafuatayo katika sehemu inayofuata, twende tufunue sehemu inayofuata.


Sehemu ilyopita tumeona ‘The Sole Cat’ akienda kupumzika huku upande wa pili katika zile pande mbili za mtafutano zikiwa na kikao katika club ya Changkat Bukit Bintang Nightlife mtaa wa Berrangan city centre kikiongozwa na ‘Master Plan’.


Nisigusie yajayo, naomba muda wako tu uendelee na utamu kolea..!



“Eeeeh! Kumbe adui yetu nchini kwetu anatupenda sana, mbona uwa anatukosakosa kila mara tena bila kuchoka akituwinda yeye, majasusi wenzake na shirika la upelelezi la Mongolia?... Hahahahah! Nimefurahi kujua hivyo”. Akasema huku akicheka ‘Mongolia Damme’.

“Istqal atakuwa anajua maana amefanya kazi idara ya ujasusi ikulu miaka ishirini na kafanya kazi na Alexander Zabel mkuu wa idara ya jasusi miaka yote mpaka walipotaka kumuua kwa kugundua mipango ya siri ya waziri wa ulinzi”. Akaongea Uugun huku ile habari waliyopewa na Mr Logan ikiwafurahisha sana sura zao zikiwa hazijajificha furaha waliyonayo.

“Ahsanteni sana… Nafikiri tunatakiwa turudi kwenye dhumuni la kikao chetu… Nikishamaliza nilichokuja nacho hapa kikaoni itakuwa muda wa watu wengine kujitambulisha kwa wageni wetu” Akaongea Mr Logan kisha akapiga hatua kwenda meza ya kioo ambayo kikawaida mara nyingi wahudumu wa club hii uwa wanaiweka katikati ya varanda hii ya VIP lakini leo hii ilisogezwa pembeni, alipofika aliiweka glasi ya kinywaji alichokuwa anakunywa na kunyanyua Ipad.

“Napenda kwanza nitoe pole kwa watu tuliokuwa tukishirikiana nao kikazi ambao jana mtu anayeitwa Agent Kai Hamis Mussa amewaua… Huyu Kai Hamis Mussa ni jasusi wa CIA ambaye taarifa zake za kuingia nchini hapa nilizipata siku nne zilizopita toka kwa mtu wangu wa CIA aliye makao makuu ya CIA, nikaweka mtego wangu kwa watu wangu walioko idara ya uhamiaji wakaniwezesha kujua mtu huyo ataingia kwa ndege gani na muda gani, niliuandaa mtego wa kumnasa vizuri na uzuri tulifanikiwa kumteka nyara mwanamke ambaye yeye nilichelewa kupewa taarifa za uingiaji wake sababu nayemtegemea alikuwa anaumwa hivyo aliniambia wakati huyo mwanamke tayari kashaingia hapa Kuala Lumpur ikabidi niwatumie wahudumu wa pale ubalozi wa Marekani kuzijua nyendo zake… Bahati nzuri katika kufanya kwake upelelezi wa kwanza kina Nawaz walikutana naye akitoka kuchunguza eneo lile tulilowateka wanasayansi wao wanaowatafuta kwa udi na uvumba kiasi cha kuvuruga mipango yetu ya kuwaondoa kwa jinsi walivyoweka ulinzi wao”. Hapa alisimama kidogo akawatizama baadhi ya watu walio mbele yake kutokea pale katikati ya varanda aliposimama kisha akageuka upande wa kulia.


ENDELEA NA UTAMU……..!


MTAFUTANO PANDE MBILI VIII

“Nawaz Patrash, Gary Yong na Doctor Zhing Lae walipomuona Detective Marie na nilipowapa sifa za huyo Agent Kai walishauliana waitumie sura ya Detective Marie kumtia nguvuni Agent Kai…. Nashukuru Mr Zhing Lae na msaidizi wake waliitengeneza sura ya bandia haraka sana inayofanana na Detective Marie kisha wakamvisha Language Girl.. Shida ilikuja mimi na kina Nawaz tulipewa mwaliko wa kwenda Korea Kaskazini kwa haraka sana na kwakuwa wao ndiyo wameshika ishu hii ya operesheni tuliyonayo, tulikwenda karibia wote tulio ngazi ya juu, wakibaki wale wanaoshughulikia jinsi gani tunawaondoa mateka wetu na kwenda kumaliza biashara… Kosa kubwa sana tumefanya kuacha kazi ya kumkamata Agent Kai kwa vijana wa SDB… Kiukweli najutia sana kilichotokea sababu nilishapewa taarifa kuhusu uhatari wa huyu mtu Mmarekani mweusi, jamaa ni komando wa hali ya juu kabisa si mtu kumchukulia poa kabisa. Nimefurahi leo kuongezeka kwa watu watatu katika kuakikisha tunamtia mkononi mtu huyu”. Akapumzika kuongea na kusogea meza ya vinywaji akachukua chupa yake wine ya luc belaire akamimina kinywaji kwenye glasi kisha akagonga funda mbili tatu na akaishusha na kuiacha pale pale juu ya meza na moja kwa moja akarudi katikati ya varanda.

“Maji yakishamwagika hayazoleki, tumeshateleza na siku zote mi uwa nasema sihujutii wakati uliopita hata kidogo kwangu mimi past is gone! Tunao muda wa kumalizana na huyu mtu sababu kwanza bado yupo nchini mwetu, ametumwa kwa kazi ya kututafuta sisi… Nasikitika sana kuwa wakati yeye akitutafuta hili aweze kukamilisha aliyotumwa na sisi tunamtafuta kukamilisha mpango wetu. Kwa wengine ambao hawajui itabidi niwaeleze kidogo mpango ulivyo… Hapa kuna watu wanne kwa mara ya kwanza wanashiriki kikao nilichokiandaa mimi Master Plan, Jeong hakuwai hata siku moja kuhudhuria vikao kama hivi sababu hakuwa mwanachama wa Puter Group Of Business ambayo ni kampuni inayofanya biashara zote zenye kuingiza pesa ikiwemo biashara hii ya kuuza watu wanaohitajika na watu fulani au kikundi fulani…. Istqal ‘Iron’, Mongolia Damme na Uugun nyinyi pia mnajua kuhusu nini kimenifanya niwapandie dau kujiunga nami ingawa nilikuwa nawasumbua toka mwaka jana mjiunge nami tupige kazi lakini katika kazi niliyowaambia ndiyo kazi kubwa sana kwetu ya kuondoa mitego ya kuwasafirisha watu tunaowashikilia imeingiliana na kazi ya kuhakikisha tunampata jasusi anayeitwa Agent Kai..!”. Alinyamaza kuonyesha msisitizo kwa kuzunguka pande zote kuwaangalia wanaomsikiliza yeye akajikooleza koo kidogo kisha akaanza tena kuongea.

“Wakati nikiwapa taarifa wateja wetu kuwa kuna wapelelezi wa Marekani wamefika hapa hili kujaribu kuwaokoa wanasayansi maprofesa tunaowashikilia walinipa oda ingine kuwa wanataka kuwapata na hao watu na nilipoletewa majina kamili ya hao watu ndipo wakasema kwenye list lao hawamo lakini watawasaidia kuwapata watu wanne walio katika list lao la majasusi wa Marekani wanaowataka na tunashukuru kazi kwetu ilikuwa nyepesi tukawapata… Alipofika yule mwanamke naye pia wakasema pia watamlipia lakini mshangao ulikuja nilipowapa taarifa kulekule tena tukiwa kikaoni kuwa kuna mtu nimepewa taarifa anafika kwa kazi ileile iliyowaleta wenzake, kiongozi wa kile kikao tulichoitwa akaniuliza anaitwa nani huyo mtu nilipolitaja jina lake walistuka na kuniuliza mara mbili mbili kuwa nina uhakika na jina ninalolitaja nikamwambia ndiyo, ndipo cha kwanza akafunua tumbo lake na kutuonyesha kovu kubwa kisha akasema lile kovu alikatwa na panga na huyo mtu.. Kwa taarifa ni kwamba huyo Agent Kai ni mtu namba moja anayetafutwa na shirika la kijasusi la Marekani katika majasusi wanaowahitaji kuwapata wakiwa ni wazima kisha wao watatoa hukumu wanazozijua, inasemekana alishawai kuingia N.K akafanya ujasusi na kuiba kitu flash disk yenye siri nzito za nchi ya Korea Kaskazini kiasi ya kwamba hawakuamini kama mtu mmoja anaweza kuingia na kufanya alichokifanya… Alisababisha Raisi wa Korea Kaskazini aagize viongozi wa juu wa idara nzima ya ujasusi ya nchi wauliwe kwa kupigwa risasi hivyo kama Marekani walivyowatafuta kwa kila hali magaidi na majasusi wa nchi mbalimbali basi naye wakorea kaskazini wnamtaka huyu mtu kwa kufa na kupona… Wanasema washamtega mitego kibao katika nchi anazotembelea lakini ananasua mitego.. Nataka leo niwape taarifa nimefanya dili nyingi sana lakini dili la kuwauza hawa watu walio mikononi mwetu kwa serikali ya N.K ni dili kubwa sana kuliko dili zote, pesa ya kuwapa Profesa mmoja ni pesa ambayo timu moja huko Ulaya ilimnunua mchezaji aliyewai kuwa mchezaji wao wakati anachipukia ni rekodi ya pesa lakini wale wapelelezi watatu dau lao likijikusanya linakaribia dau la huyo mchezaji…. Mshangao upo kwa huyo Agent Kai, aisee imeniuma sana wakati waziri mwenyewe wa idara husika ya N.K aliponipigia na kuniambia pesa itatoka ikulu yao na ni dau la paundi milioni mia moja…. Jamani hawa wakorea wanaweza wakatuma majasusi wao na kumpata huyu mtu lakini wamenipa heshima ukubwa ya kutaka nifanye hiyo kazi hili serikali ya Marekani isitambue kama kazi hii ina mkono wao”. Alitoa maelezo marefu Mr Logan Puteri.

“Tuna fursa nzito ipo mikononi mwetu, tuna siku tatu za kukamilisha dili ambalo litatufanya tupae juu na ikibidi tukapumzika kufanya shughuli zingine mbaya kwa muda mrefu, taarifa inasema jamaa huyu ni kipusa hatafutwi na wakorea peke yao wapo magaidi na vikundi vya kigaidi vingi vinamuhitaji huyu mtu si kipusa tu ni mgodi uliojaa mali unaotembea… Hofu ipo ni kwamba anapokwenda nchi fulani na mashirika mengine ya kijasusi au vikundi kigaidi kujua basi utuma watu wao kujaribu kumtia nguvuni sababu huyu jamaa yeye anapopambana uwa anawafyeka wenzie kama kuku hana huruma hata kidogo hivyo tunatakiwa kuwa makini anaweza akaingia kwa watu wengine ingawa kiuhalisia ni mtu wetu sababu naye anatutafuta… Hapa nimefika na mpango wa kazi ukiwa na mgawanyo wake kwa watu wote, hivyo nahitaji umakini katika kusikiliza mpango niliokuja nao..”. Aliongea kisha akaminya sehemu moja ya Ipad yake na kuifanya Ipad yake iwake.

“Safari yetu nchini Korea Kaskazini ilikuwa safari yenye mafanikio makubwa upande wetu katika mafaniko ya tunachotarajia kufanya… Tulienda kuweka sawa mipango kutokana na hali kuwa ngumu sehemu zote tulizoweza kupitisha mambo yetu mengi siku za nyuma zimedhibitiwa zote na kila kinachotakiwa kupita huko mpakani kinasachiwa, hivyo kile tulichoitiwa ni jinsi gani tunaweza kukwepa mitego yao na usafiri gani tutautumia..!”. Akameza mate kidogo kisha akaendelea.

“Jumla ya watu tulionao ambao tunatakiwa waondoke ni watu kumi na moja wale maprofesa ambao ndiyo cha yote haya kila mmoja wapo wanne kifamilia yaani Profesa mmoja yupo na mke wake na watoto wao wawili, nimejaribu kushawishi watupunguzie mzigo wa watu kwa sisi kuwaachia wale watoto na ikibidi hata na wake zao lakini kiongozi wa misheni hii bwana Ri Choe-sik amekataa katakata amesema wanawataka wote kumi na moja na akiwemo Agent Kai hivyo list yetu ina namba ya watu kumi na mbili… Na hawatainua ndege yao waliyoiandaa kwa kazi ya kuja kuwachukua watu tuliokwisha kuwa nao mpaka tumpate huyu mtu anayeitwa Agent Kai… Ndege zao wao zimezuiliwa kuruka kupita anga ya kimataifa kutokea kwenye nchi yao hivyo viongozi wa nchi yao wanapotaka kusafiri wanatumia usafiri wa maji au ardhi hadi China ndipo wanapopata usafiri wa ndege, hivyo kwa kazi hii wamekubaliana kukodi ndege binafsi ya tajiri mmoja wa mafuta kutoka nchini Iran.. Kilichopo kuna mkanganyiko kidogo wa wao sehemu ya kutua ndege ya itakayofanya hiyo kazi hapa Malaysia kama mnavyojua saivi kuna mzozo kati ya Malaysia na Korea Kakazini… Hivyo wanafanya maongezi na huyo tajiri hili ajifanye yeye mwenyewe anakuja kutalii hapa Malaysia au hata ndugu zake wakiwa wawili au vinginevyo, baada ya mazungumzo hayo ndiyo watajua wapi ndege hiyo itaenda kutua sababu ingine imefanya kazi iingie ugumu kidogo ni kuchelewa kwetu kuwaondoa wale watu kule mafichoni kwenda Sarawak laiti tusingechelewa tungeweza kuwavisha sura za bandia kisha tukawachanganya na wale wakorea kaskazini waliofukuzwa kisiwani Borneo kwa kuishi bila kibali hapa Malaysia na mzozo uliozuka ndiyo kabisa umeharibu uhusiano wa nchi hii na N.K, haya masuala saivi tungekuwa na kazi ya kumtia kwapani mtu huyu aliyefika jana tu lakini serikali ya Malaysia inajifanya kibaraka wa Marekani inakumbatia maadui, wameshaishiwa mpaka wamemfukuza balozi wa N.k na kusababisha mpaka sisi tuitwe N.k wakati uratibu wote wa mambo haya ungefanywa na ubalozi wenyewe wa N.K sisi tungeingiza pesa kiubwete kabisa… Kilichopo sasa jamani ni suala la sisi kupanga tunampataje Agent Kai na kuhusu masuala mengine kesho nitasubiri simu au email ya maelekezo toka kwa bwana Ri Choe-sik kisha nitakuja na mpango inakuwaje hapo kesho..”. Yalikuwa ni maelezo marefu toka kwa Master Plan wa pesa haramu Mr Logan Puteri.

Ni kama mapumziko fulani sababu alisogea hadi meza ya vinywaji na kuanza kunywa wine yake kisha akamimina tena wine na kunywa mpaka nusu glasi na kurudi eneo lake.

“Operesheni tunayoamka nayo asubuhi ni ‘operesheni Agent Kai’ nahitaji tukaongeze umakini katika kumsaka huyu mtu naahidi kama atapatikana kesho basi usiku tutakapokutana kila mtu ataondoka na cheki ya dola elfu kumi na yule aliyefanikisha mpango wa kumtia mkononi kama watakuwa kundi la idadi fulani kati yetu basi nitaongeza kwao dola elfu kumi ingine huku tukikamilisha operesheni naahidi nitagawa pesa tutakayopata kwa haki ya kila mtu kwa jasho alilovuja… Ninafanya hivi sababu malipo kidogo ya kazi hii nishaingiziwa na bwana Ri na ni pesa ya kufanikisha kazi tu maana kazi hizi zinahitaji pesa…. Hivyo basi hapa kila mtu nitampatia dola elfu moja aitumie katika kurahisisha kazi huku kiongozi wa operesheni hii atakuwa Mr Nawaz Patrash, wewe bwana kwa kuongoza operesheni sitapenda ushindwe katika suala la pesa wala kunipigia simu kuwa fulani wa ubalozi wa Marekani anataka kiasi fulani hili afanye hivi no! nataka pesa iongee ikifika saa kumi basi mtu yupo mikononi mwetu hata kwa kuwatumia polisi au watu wa usalama wa taifa wawe wa DSID, MSB, RDPMD hata CGSO hawa wote nitasema nao asubuhi viongozi wao hili waturahisishie kazi, Sitaki kuwakera N.K kwa jinsi walivyoniamini na hata kunipa msaada”. Alinyamaza baada ya mtu mmoja kati ya wale wageni kuonyesha ana kitu anataka kuongea.

“Uliza Uugun”. Akampa ruhusa aulize anachotaka kuuliza.

“Shida ni haijulikani mpaka sasa wapi amefikia au?”.

“Asubuhi ya usiku uliopita ndiyo alitoroka kule Nadau na kufanya mauaji kwa watu wetu wawili wa kikosi cha pili, mchana sisi tulirudi hapa KL toka N.K ni mchana wa usiku huu na ndiyo nikapewa taarifa na Damia…. Damia ni huyo binti unayemuona… Alinipa taarifa ya kilichotokea kwa ujumbe wa meseji ndipo nikampigia akanipa maelezo yote ya kilichotokea, sitaki kuwalaumu kama nilivyosema awali past is gone ni uzoefu wa kazi ndiyo uliwafanya kumpoteza mtu wetu, sasa kazi ipo kwetu sisi si kwao tena wao nitawahamishia katika idara ya ulinzi kule maficho yetu tulipohifadhi mali…. Hivyo mpaka sasa hatujui kafikia wapi, labda ubalozi wao au labda hotel fulani au labda nyumba fulani ya mtu fulani lakini tunachojua pekee kwa sasa yupo hapa KL na anatusaka sisi anatutamani kama tunavyomtamani yeye”. Akajibu kwa kirefu ikiwa na mwanzo alionyesha kidole alipokaa Damia.

“Sawa sawa mkuu nimeelewa… Ni vizuri tukamjua kwa picha huyo mtu maana sisi wengine hatumjui kabisa..!”

“Natuma picha kwa kila mtu aliye humu ndani, muda si mrefu zitafika picha zake tano za tofauti tofauti…. Passport yake aliyoingilia nchini ninayo maana Damia aliichukua ameingia nchini kwa jina la Ramsey Bronze mfanyakazi wa idara ya ulinzi wa viongozi wa Marekani, hivyo ameletwa hapa kuongeza ulinzi kwa balozi wao Kapteni Jones Lebrons kutokana wanaona hali si nzuri kwa balozi wao hapa Malaysia icho ndiyo kibali cha kuingia nchini hapa kinavyosema ambacho nimeletewa kopi na mtu wangu wa uhamiaji… Picha yake katika Passport na hata iliyo uhamiaji hajajibadili sura sana kama walivyofanya wale wa kwanza tuliowakamata na tunao, yeye ameongeza nyusi kidogo machoni na pia ameweka ndevu za kuzunguka mdomo wakati nilitumiwa picha yake ya siku moja kabla hajaondoka Marekani hana ndevu hizo, hivyo tuna picha mbili za sura yake. Pia tuna picha moja akiwa mazoezini amevua shati yupo na bukta, pia kuna ingine yupo beach ana kichupi tupu na pia ipo kava koti kubwa la baridi na miwani kama hii yangu, hizi ndiyo picha muhimu kwetu kutufikisha kwenye kumpata… Picha zote ni muhimu sana kila mmoja kuwa nayo”. Maelezo hayo yalienda huku akizunguka kuwaonyesha picha iliyo kwenye karatasi kubwa ya 4 pieces ikiwa ni picha iliyokuzwa toka kwenye kibali cha Agent Kai cha kufanya kazi kama bodyguard wa balozi wa Marekani nchini Malaysia kisha akabonyeza sehemu kwenye Ipad yake na kukuza picha kubwa pia akaanza kuzunguka kila upande pale pale aliposimama akionyesha picha ya sura ya Agent Kai iliyo kwenye Ipad.

“Hii kwenye Ipad ndiyo sura yake halisia kabisa, zote nitatuma kwenu kila mmoja awe nazo… Uugun na wenzako nyinyi moja kwa moja mnaingia kwenye operesheni kutokana na uzoefu wenu makuwa kama viungo mkitembea na gari yetu ya mawasiliano ambayo uwa anaitumia Mr Nawaz Patrash, mtakuwa naye yeye mkiwasiliana na watu wengine kokote walipo, asubuhi tu kazi ianze… Najua Nawaz unajua kipi cha kufanya na kwangu utatakiwa kuniambia nini kimetokea tu si msaada tena, wewe ni kiongozi mwenye ujuzi na kuongezea na watu wenye ujuzi hivyo asubuhi utaanzisha utakachoona ni sahihi kwa kupanga watu wako na kuweka sawa mawasiliano kwenu wote, mi naamini saa saba tu atakuwa mikononi mwetu KL ipo chini yetu kila siku hakitusumbui kitu kama kwingine uwa wanamshindwa ni wao si sisi… Mmbo yote mtatiririka nayo jinsi yatakavyokuwa yanakuja”. Alisimama hapo, vinywaji vikapita kwenye makoo ya baadhi ya watu akiwemo Mr Logan.

“Mwenye swali?”. Akawauliza huku anazungusha machoyake makubwa kiasi yaliyo ndani ya miwani aliyovaa kwa kila aliyemo pale varandani.

Jamaa waliangaliana tu huku wenye sura za kutabasamu wakiwemo, pia wenye sura za kawaida wakiwemo.

“Jamani mwenye swali tafadhali aulize… Yupi hajaelewa?... Au niruhusu tukapumzike?”

“Mi acha niongee kwa niaba ya wenzangu, nafikiri kila mmoja ameelewa vizuri vyote ulivyoeleza, nachotaka kusema ni kukupa hongera kwa maelezo ulivyoyaweka sawa.. Naamini jumapili tunakwenda kumaliza hii biashara na kuanza mambo mengine hasa ya kupumzika kwa raha na familia zetu wakifurahia mafanikio yetu kwa pamoja”. Nawaz Patrash kiongozi wa operesheni akaongea kwa niaba ya wenzake.

“Yah! Mkuu umeeleweka kwa kweli sisi sote hapa ni watu wa hizi kazi tena waelewa wakubwa wa mambo… Naamini katika anavyoamini Patrash, jumapili tunakwenda kuwa tumemaliza kila kitu”. Mhindi Ghulam Sabry akaongea huku akitamani kikao kiishe haraka akavute sigara maana kiu ilimshika haswa.

“Basi nafikiri ni vizuri nikachukua fursa hii kugawa pesa nilizoahidi dola elfu moja kwa kila mtu kisha tukapumzike… Asubuhi sitawaacha katika kazi nami nitakuwa naseti mambo kisha nawasiliana na Mr Nawaz.

Kikao kiliisha kwa Mr Logan Puter kugawa pesa na wageni kutambulishwa majina ya watu wengine na wakatawanyika.


** *** **

Hakutaka kwenda Alamanda Hotel, hotel aliyopanga. Baada ya kwenda kumkabidhi mwanamke aitwaye Saky katika ubalozi wa Marekani ulioko mtaa wa Taman u Thant, Hakutaka kuivua sura ya bandia aliyovaa, sura imuonyeshayo kama wanaume wengi ionekane Alamanda Hotel sababu alihisi kitu ambacho kilimfanya asitake kwenda huko Alamanda Hotel. Alitizama saa yake ya mkononi ilikuwa imetimia saa kumi na nusu ya alfajiri kwa masaa ya Malaysia.

Akakanyaga gia ya Nissan Frontier kichwani akilenga kufika katika hotel ambayo aliiona mchana na kuitamani kuwa itamfaa kuwa moja ya hotel zake atakazokuwa anahama hama akiwa katika sura mbali mbali na uzuri wake kule Alamanda Hotel alilipa pesa ya kukaa siku tano.

Akakanyaga gia ikaongeza mwendo akaupata mtaa aliouhitaji unaoitwa mtaa wa Chow Kit Street moja ya mtaa maarufu ulio eneo la Petaling katikati ya jiji la Kuala Lumpur wilaya ya Persekutuan barabara ya Jalan Sultan Ismail ni hotel iliyo mwendo wa dakika tano tu kwa gari kutoka ilipo hotel ya Alamanda. Mtaa wote ulikuwa kimya watu bado wamelala hawajaamka na baadhi ya misikiti ilikuwa ikasikika adhana, haikupita muda akaiona hotel aliyohiitaji hotel ya nyota tano iitwayo Sheraton Imperial Palace Hotel. Akapunguza mwendo wa gari kisha akaingia uelekeo wa geti la hotel, mlinzi alifungua geti kuruhusu Agent Kai aingie baada ya kusikia honi ya gari.

“Habari yako?” Akampa salamu mlinzi baada ya kuzima injini ya gari na kushuka kwenye gari lake akiwa begi lake lenye mambo yote ya kazi.

“Nzuri tu kijana, mgeni hapa au tayari upo humu?”.

“Mgeni….. Nahitaji chumba”

“Pole kwa safari… Karibu, pita mapokezi utakuta vijana wenzako wakakupatia huduma”

Agent Kai aliingia mapokezi baada ya mlango mkubwa wa kuingia mapokezi ulio wa kioo na automatic sensor , ambao ikiwa binadamu amesogea tu basi wenyewe hujiachia kwa katikati pande mbili kuacha uwazi.

“Habari zenu warembo?” Salamu aliyotoa iliunganika na kugonga gonga meza kubwa iliyowatenganisha baina yake na wadada wale wa mapokezi ambao wote walikuwa wamejilaza kwa vichwa vyao kuviegemeza juu ya meza. Wote wawili walikurupuka kana kwamba wameamshana.

“Karibu kaka… Samahani kwa kutukuta tumelala”. Akasema binti mmoja kwa sauti ya woga iliyochanganyika na usingizi.

“Usiku huu dada… Kila binadamu anahitaji kupumzika, muda kama huu ni muda wa kupumzika ingawa inakaribia asubuhi iliyo kamili.. Poleni sana!”

“Ahsante kaka kwa huelewa… Ni mgeni hapa?”.

“Yah! Ni mgeni natokea jimbo la Pokok Sena, nahitaji chumba…”.

“Ok! Ndiyo unaingia Kuala Lumpur alfajiri hii?”.

“Niliingia saa tatu ya usiku nikafikia kwenye kikao, tumemaliza kikao icho saa kumi usiku”.

“Pole sana kwa uchovu wa safari na kikao kwa ujumla… Unahitaji chumba cha kawaida au VIP?”.

“VIP kitapendeza”.

“Hahahaha! Umenifurahisha sana kaka, hahhahaha na kweli VIP uwa bora zaidi… Una kitambulisho ama passport au hata leseni ya udereva?”

“Subiri niangalie…!” Akasema Agent Kai na kisha akalipandisha begi lake juu ya meza na kufungua zipu ya ubavuni mwa begi akatoa kadi ya leseni ya udereva wa gari ambayo iliandaliwa na balozi Kapteni Jones Lebrons ikiwa na picha yenye sura hii aliyoivaa (kazi ya balozi, siku zote jasusi hata akizeeka ni jasusi tu), kila kitu alikuwa kakipanga katika mstari ulionyooka kabisa.

Muhudumu akaipokea na kuanza kuandika daftarini huku akisoma anavyoviona kwenya kadi kwa sauti.

“Jina …. Faheem Ramji”. Anasoma kwa sauti kisha anaandika kwenye daftari la taarifa za wageni.

“Umri… Miaka 33!”

“Uraia… Malaysian, jimbo Pokok Sena”.

“Kazi… Mhasibu wa kampuni ya utalii ya Pok & Lebo Tours!”.

Alipomaliza hapo aliendelea kuandika kwa utulivu alipomaliza akainua uso kumuangalia Kai.

“Siku moja tu au siku ngapi utakuwepo hapa?”. Akamuuliza.

“Nalipia siku tano lakini kama nitaondoka kabla ya hapo usijali ila nitajitahidi kuwaaga maana vikao ndiyo vimeanza hatujui baada ya siku ngapi tunamaliza pengine naweza kuongeza siku ila kwa sasa jaza nalipia siku tano”.Akajibu Agent Kai.

“Ok! Unalipa kwa cash au check?”.

“Cash itapendeza zaidi maana ninazo hapa zinataka kutumika”.

“Hahahaha… hahahah.. ahsante sana mgeni wetu mcheshi sana na una maneno matamu kama ulivyo”. Akaonyesha kufurahishwa dada wa mapokezi.

“Kwenye utamu umenidanganya… Haya niambie namba ngapi niende au nipelekwe nikaubutue usingizi maana umejaa kwenye kona”.

“VIP namba 105! Shyrose mpeleke kaka yetu mtamu mtamu”. Akaongea na wote watatu wakacheka.

“Nikitaka mtu wa kuniliwaza nitakutafuta maana kwa uchangamfu ulionao basi watoto wabichi wo jiji wamejaa ndani yako”.Akasema Kai.

“Kwani sisi tumeiva? Na sisi watu babuu”.

“Haya bimdogo nimekusikia”. Kai alipojibu hivyo tayari alishaanza kumfuata nyuma dada aliyeelekezwa ndiyo atampeleka huko namba 105.


Mwisho wa sehemu ya kumi na tano (15)


Katika sehemu hii ya muendelezo wa mtafutano ulio wa pande zote za kishindani kutafuta tumeshuhudia kikao cha ‘Master Plan’ na watiifu kwake kikipokea wageni toka Mongolia na kisha kumalizika kwa mipango kadhaa kadhaa.


Huku mtaalamu wetu naye akiendelea na mipango yake ambayo hakuwa anaona ina kasoro, aliamini kila kitu kipo kwenye mstari anaohitaji kwa uzoefu wake wa kazi hii ya kijasusi.


Nini kitafuata katika muendelezo wetu?


Ni muda wako tu mahali hapahapa ulipoikuta hii kitu ya kijasusi yenye mitwangio ya kisasa..!




ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA…….!

Muhudumu akaipokea na kuanza kuandika daftarini huku akisoma anavyoviona kwenya kadi kwa sauti.

“Jina …. Faheem Ramji”. Anasoma kwa sauti kisha anaandika kwenye daftari la taarifa za wageni.

“Umri… Miaka 33!”

“Uraia… Malaysian, jimbo Pokok Sena”.

“Kazi… Mhasibu wa kampuni ya utalii ya Pok & Lebo Tours!”.

Alipomaliza hapo aliendelea kuandika kwa utulivu alipomaliza akainua uso kumuangalia Kai.

“Siku moja tu au siku ngapi utakuwepo hapa?”. Akamuuliza.

“Nalipia siku tano lakini kama nitaondoka kabla ya hapo usijali ila nitajitahidi kuwaaga maana vikao ndiyo vimeanza hatujui baada ya siku ngapi tunamaliza pengine naweza kuongeza siku ila kwa sasa jaza nalipia siku tano”.Akajibu Agent Kai.

“Ok! Unalipa kwa cash au check?”.

“Cash itapendeza zaidi maana ninazo hapa zinataka kutumika”.

“Hahahaha… hahahah.. ahsante sana mgeni wetu mcheshi sana na una maneno matamu kama ulivyo”. Akaonyesha kufurahishwa dada wa mapokezi.

“Kwenye utamu umenidanganya… Haya niambie namba ngapi niende au nipelekwe nikaubutue usingizi maana umejaa kwenye kona”.

“VIP namba 105! Shyrose mpeleke kaka yetu mtamu mtamu”. Akaongea na wote watatu wakacheka.

“Nikitaka mtu wa kuniliwaza nitakutafuta maana kwa uchangamfu ulionao basi watoto wabichi wa jiji watakuwa wamejaa ndani yako”.Akasema Kai huku anatabasamu tabasamu la ulimbo nasa.

“Kwani sisi tumeiva? Na sisi watu babuu”.

“Haya bimdogo nimekusikia”. Kai alipojibu hivyo tayari alishaanza kumfuata nyuma dada aliyeelekezwa ndiyo atampeleka huko namba 105.


ENDELEA NA DODO..!


HATUA MOJA MBELE I

Mlio wa simu iliyokuwa pembeni ya mto aliolaza kichwa chake kitandani ndiyo uliomstua toka usingizini. Si kawaida kwa mara nyingi kwa Agent Kai awapo kazini kama ilivyo hapa Kuala Lumpur kuacha simu yake mlio zaidi uacha iwe ina vibrate lakini alfajiri ile alipofika kwenye chumba 105 VIP, Sheraton Imperial Palace Hotel na kuagana na muhudumu aliyempeleka na alipojifungia mlango wa kuingia tu alivua nguo na moja kwa moja kwenda kujimwagia maji.


Aliporudi akanywa wine nyepesi isiyo na kilevi kisha akalala na muda huu ndiyo mlio wa simu unamstua maana alikuwa amepandisha volume ringtone mpaka mwisho kwa kuwa alitega alarm ndiyo imuamshe lakini simu hii ilimuamsha kabla hata ya alarm aliyotega.


Simu hii aina ya Iphone X rangi nyeupe kutoka kampuni Apple kampuni ya simu ambazo uwa ndiyo kazoea kutumia ilikuwa haina mlio wa kukera sana. Ni simu ambayo ilienda kununuliwa na Shufania, huku ikiendelea kuita yeye hakufungua macho alipapasa pembeni ya mto na kuipata alipoitia kiganjani tu akapinduka kutoka kifudifudi alivyolala hadi chali akafumbua macho na kwa kutumia mkono wa kushoto akajifikicha kidogo machoni hili auzoee mwanga wa mchana huo uliokuwa umechomoza kwelikweli na alipoachia akasoma saa iliyo kwenye simu ilikuwa ni saa tano na dakika tatu ikiwa bado dakika hamsini na tatu kabla ya muda aliotega yeye alarm imuamshe.


Siku ya alhamisi. Jua lilikuwa limechomoza kiasi ya kwamba mapazia yaliyoko pale chumbani alipo likidhihirisha dhahiri na kutokana na chumba kipo ghorofa ya 49 ukitoa pazia unauona minara mitatu iliyo mirefu sana mmoja wa DELUXE KL Tower upo mita chache na mingine ya Petronas Tower inayoonekana kwa mbali. Alitizama namba ya mpigaji, ilikuwa imetokea jina alikuwa ni Shufania binti Mahamud, Kai akatabasamu kuonyesha kufurahi kuona anapigiwa na binti huyo mrembo wa haja.

“Hallow!”. Akasugua kioo cha simu kwenye mstari wa kijani kuelekea kulia na kuruhusu kupokea simu kama ilivyo kawaida ya simu nyingi za smartphone unapotaka kupokea na kisha akaongea ikiwa tayari kashaipeleka kunako sikio la kulia analopenda kusikilizia simu yeye anapotumia simu, huku jitihada za kutosha zikienda katika kuhakikisha inakuwa sauti isiyoonyesha inatoka kwa aliyetoka kulala muda huo.

“Asallam aleykuum!”. Sauti tamu kama kinanda kinachopigwa na mtaalamu wa kupiga kinanda, sauti ya kichokozi ambayo imetoka kwenye kinywa chenye sauti mororo ya kike haswa ilipasua ngome ya sikio lake kimawimbi na kwenda kukita kwenye ubongo wake ikimpa salamu, sauti ya binti wa kiarabu wa Kisyria.

“Aleykuum salaam warahmatullah wataallah wabarakatuh!” Kwa furaha aliyonayo ya kuamshwa na mtu ambaye alitamani kusikia sauti yake akarefusha salamu ya kujibu huku akitabasamu kana kwamba yupo naye binti mbele ya macho yake.

“Jamani nimefurahi kusikia sauti yako lakini mbona ulipo ni kama umelala vile?” Sauti ya binti wa kiarabu ikatoka ikiwa ina lalamika kama kubembeleza fulani (mashaallah mtoto kajaliwa sauti ya kike)

“Sijalala.. Ningekuwa nimelala usingekuwa unaniuliza best, mzima wewe?”.

“Mmmmh! Mwanaume huishiwi visa vya maneno mpaka wanifanya usikauke kichwani mwangu, mimi mzima tu, vipi hali yako?”.

“Nashukuru Mungu niko poa kabisa, moyo wangu bado unaruka kichura chura sehemu yake ya kujidai huku ukisukuma damu kwa ufundi toka pale Allah alipoumrisha ufanye hivyo, sema nilidamkia kikaoni ubalozini saivi ndiyo tumepumzika nikaona nijipumzishe kidogo kwenye vyumba vya mapumziko hapa hapa ubalozini sasa wakati unapiga nilikuwa niko kwenye safari tamu ya usingizi, lakini ndiyo nishaamka hivyo”.

“Ooooh! Jamani nisamehe nimekukatizia usingizi, kwa kweli nisamehe sana… Ukweli nilimisi sauti yako nikashindwa kuvumilia pia kuna kitu kimenifanya nipige hili nikuulize kwanza wewe mwenyewe Ramsey”.

“Usijali… Mi mwenyewe nimefurahi kukatiziwa usingizi na sauti yako ndiyo kabisa imenifanya niondokane na usingizi uliokuwa unaninyemelea kunipeleka kuwa zezeta fulani… “.

“Ahsante sana kwa kunisamehe pia ahsante sana kama kweli umefurahi kusikia sauti yangu naamini kama umeipenda sauti yangu basi haikeri kabisa”.

“Sijawai kusikia sauti nzuri kama yako, nimezisikia nyingi kwa umri huu lakini sikuwai kukaa karibu wala kuwa na rafiki wa kike wa kiarabu labda ningeweza kuisikia sauti nzuri yenye kujua kuyaremba maneno ya lugha tunayoongea hapa… Eeeeh! Niambie Shufania binti Mahamud”.

“Narudia tena ahsante sana Ramsey Bronze… Samahani naomba kukuuliza kama hautajali!”

“Bila samahani unaweza kuniuliza hakuna tatizo Shufania”.

“Haukulala hapa hotelini?”.

“Nililala lakini niliwai kutoka saa kumi na mbili asubuhi kuja ubalozini kwa ajili ya kikao na viongozi maafisa wetu wa ubalozini na sisi wageni tulioingia jana”.

“Kweli Ramsey? .. Mbona kuna mtu ametuambia hujalala hapa hotelini!”.

“Eeeeh! Nani huyo?... Atakuwa anaota, mi nimelala hapo… Siwezi lipia hotel halafu nisilale, itakuwa nafanya kitu gani na ninamaanisha nini?, maana nimelipa siku tano hapo”.

“Mlinzi wa magari alitoa taarifa kwa watu waliojitambulisha ni wenyeji wako, walifika hapa kukuulizia… Mi nikajiuliza wametokea wapi? na nina kuuliza wewe mwenyewe sasa, hivi wewe hapa KL una ndugu?”.

Agent Kai kusikia hivyo haraka aliinua mgongo aliokuwa kaulaza chali na kukalia matako, akanyanyua mto na kuulaza kwa urefu ukutani kisha yeye akajiburuza kwa matako kurudi nyuma na kuuegemea ule mto aliousimamisha kwa kuuegemeza kwenye ukuta ulio nyuma yake.

“Wameniulizia mimi?”. Akauliza kwa sauti aliyojitahidi kuifanya iwe ya kawaida kuficha mshtuko wake.

“Yes! Walifika hapa mida ya saa tatu na nusu asubuhi, nikashangaa naitwa na bosi wetu kisha akaniambia wasikilize hao… Walianza mapokezi wakakuulizia wakitaja jina lako walipojibiwa lipo jina lako wakauliza upo ndani, dada wa mapokezi pale ni rafiki yangu sana akawaelekeza waniulize mimi akiogopa kuwaambia upo au haupo wakti kadi yako ya chumba haukuacha na kawaida ya hoteli yetu mtu anayehudumia vyumba vya losheni kumi pengine uwa anahudumia tisa na kumi na moja hivyo mimi ndiyo uwa na taarifa zote za wapangaji wetu waliopanga floor hizo… Hao watu walikuwa wawili lakini si wamarekani kama sikosei, waliponifuata nikawaomba tutumie simu ya mapokezi kupiga chumbani kwako wakaniambia basi watarudi baadaye na hawakurudi mpaka sasa”. Akatoa maelezo Shufania yaliyofanya Agent Kai atikise kichwa kukubali kitu fulani.

“Huko wapi saivi?”.Agent Kai hakutaka aendelee akamuuliza hivyo.

“Niko jikoni nimefuata chakula cha mteja aliye losheni ya tisa”.

“Ok! Sasa ni hivi mi nahitaji tuonane ukitoka kazini, inawezekana hao watu watakuwa wananijua lakini kwa hali ilivyo nchi hii si vizuri kuwaamini watu ovyo… unatoka saa ngapi hapo kazini?”.

“Tunatoka saa kumi… Ni kweli kama unavyosema na ndiyo maana nikapenda nikuulize kwanza”.

“Na hamu ya kujua walikuulizaje lakini simuni si pazuri tukiongea juu ya hao watu, tuonane muda huo utakaotoka kazini saivi kikao chetu na balozi wetu kiko mapumziko tutaingia tena kikaoni saa nane mchana hivyo nitatoka kwenda kutafuta mgahawa wowote mzuri nikapate juisi na chakula maana sijanywa chai, kikao kilikuwa kizito sana na bado kitaendelea”.

“Pole sana kwa kikao na pole kwa kukosa hata muda wa kupata breakfast ila muda bado unaweza ukawai kupata chochote… kama hautajali tunaweza kuonana muda huu ambao huko free?”. Akaongea Shufania na kumfanya Kai afinye macho kutengeneza kitu ambacho anahitaji ajijibu haraka kwenye ubongo wake ‘Mmmh! Kai nini hapa?’ Akajiuliza mawazoni. ‘Ngoja nikubali tuone’

“Shufania si upo kazini na unatoka saa kumi, unawezaje kufanya hivyo?”.

“Naweza kufanya hivyo usiwe na wasiwasi… Nikubalie utaniona utakapotaka twende kwa luch time”. Akajibu kwa kujiamini kwa sauti isiyo na mashaka wala badiliko masikioni mwa Kai.

“Lunchtime wote? Kweli? Basi mwenyeji utanichagulia sehemu nzuri utakayoona wewe inafaa”.

“Mi si mtokaji sana lakini wadogo zangu maisha yao ni wapenda kwenda sehemu mbalimbali hapa KL zenye misosi ya kila aina nitawauliza wapi sehemu nzuri kisha nitakupeleka”.

“Sawa… Nitashukuru kukuona tena maana nimekumisi sana… Saa ngapi kwahiyo utakuwa tayari mimi nisubiri hadi muda huo utakaokuwa wewe tayari”.

“Saivi ni saa tano na dakika kumi, napeleka mahitaji ya mteja kisha naenda kuomba ruhusa kwa boss kuwa naumwa nataka kwenda hospitali kupima nikishatoka nitakupigia, nafikiri itakuwa saa sita kamili ndiyo nitakuwa tayari kwa hilo”.

“Ok! Basi tutaonana muda huo mwarabu wangu, nakutakia maandalizi mema ukiwa poa nipigie nitakupa maelekezo wapi unikute”.

“Mimi pia nimefurahi kwa ulivyonipa muda wa kuongea nami pia naomba nikutakie muda mzuri huko ulipo, tutaonana muda mfupi ujao”. Akamalizia Shufania akiwa na furaha tele mpaka alijishangaa kwanini amefurahi hivyo.

“Haya kwaheri!”. Kai akamuaga wakakata simu zao.

‘Wanawake, mabinti ni watu wasiotabirika siku zote, jana alikuwa akiongea nami macho yake hataki hata yakutane na macho yangu. Leo amenitafuta na kirahisi ameomba tuonane kwa luch …. Hahahahah! Kai shilingi ina pande mbili, nijiandae na mshangao ila moyo wangu huko baridi juu yake sina wasiwasi juu yake, pia najisikia kuna kitu juu ya binti huyu, twende nikaone na uzuri siendi na sura yangu ya Kai anaenda kuchukuliwa na sura ya Faheem Ramji kama kuna mauzo yatafanyika vizuri na bwana Faheem’. Aliwaza Kai akiwa bado kaugemeza mgongo wake kwenye mto. ‘Natamani ningenyanyua uzito kidogo lakini nitaenda wapi?... Acha nipige push-up na niruke kichura chura’ Akawaza tena kisha akajiondoa kitandani kisha bila kupoteza wakati akaanza mazoezi kwa kasi akianza na kupiga push-up.


***** ***** *****


Akiwa usingizini aliusikia mlio wa simu yake ya mkononi lakini akawa anaamini ni ndoto, mlio ule aliokuwa anausikia na kudhani ni ndoto ulikata na kisha ulijirudia tena na mara akatingishwa mwili wake katika hali ya kuamshwa na ndipo alipojua si ndoto na hii ilimaanisha mke wake ameashwa na ule mlio wa simu na sasa anamuamsha yeye, hapo alikurupuka haraka na moja kwa moja mkono wake wa kulia akaunyoosha kunyanyua simu iliyokuwa pembeni kidogo na mto upande aliolala yeye, akasoma jina la mpigaji kisha akamuangalia mkewe na papo hapo akajiinua pale kitandani.

“Nani anayekupigia?”. Mkewe akamuuliza huku naye akijiinua kitandani.

“Nawaz… Nahisi kuna tatizo”. Akajibu huku akimuonyesha jina lililo kwenye kioo linaloonekana inavyoita.

“Pokea sasa!... Wewe unahisi kuna tatizo lakini unajisikilizia kupokea, au unaniogopa nitasikia hilo tatizo? Ok nenda kaongelee ofisini kwako huko”. Akaongea Mrs Zahra Logan Puter na kisha akatoa ruhusa jamaa aondoke pale chumbani aende kuongelea huko.


Simu ilikata na Mr Logan akaondoka mule chumbani kwa kasi, safari ilimpeleka sebuleni kisha akateremsha ngazi zilipofika mwisho akaingia chumba cha gym na alipofunga tu mlango kujifungia simu ikaanza kuita tena na mara moja akapokea.

“Hallow! Nawaz… Vipi hali?!”. Akaongea kwa sauti ya kasi.

“Si salama mkuu… Nyumba yetu ya Broga Hill imeunguzwa moto na vijana wako wote wa SDB na kijana wangu aliyekuwa ananichekia nyumba ile wamefyekwa na gari mbili moja yao SDB Na ingine nilimpa kijana aliyekuwa anaiangalia nyumba na kuitunza zimewaka”.

“Eeeh! Atakuwa Agent Kai? Au unaonaje?”.

“Mi ndiyo nipo hapa ila polisi, kikosi cha zimamoto na baadhi ya waandishi wa habari wapo hapa… Kwa nilivyotizama kwa jinsi walivyouliwa moja kwa moja muhusika ni yeye sababu mtu mmoja amemuua kwa kipigo na wengine kawapiga risasi kwa kutokea kwa nyuma ingawa kiufundi alikuwa yupo mita chache wakati anawashambulia sababu risasi zinaonekana kapiga kwa kuwavizia kutokea kwa nyuma ila huyu wa kipigo inaonekana amemvunja shingo akiwa kamuinamisha… Pia inaonekana ameingilia kupitia ukutani sababu mbwa waliuliwa kwa kupigwa risasi zilizotokea juu bado tunaendelea na kuchunguza kila kitu”. Akatoa maelezo marefu Nawaz.

“Yah! Ni huyo mshenzi inaelekea aliwafuatilia na hatukuwa makini juu ya hilo, kosa lingine hili. Mjinga mmoja anatuzidi maarifa… Wewe alikufahamisha nani juu ya jambo hili na umeenda peke yako huko bila mtu mwingine wa kikosi chetu?”.

“Alinipigia simu kiongozi wa zimamoto baada ya yeye kupewa namba na kiongozi wa mtaa huu, niliwai kumpa namba yangu aliniomba nikiwa mwenye nyumba ni mimi kama sheria za mtaa zinavyosema… Mara moja nilikimbia kufika hapa nikiwa peke yangu na kwakuwa hamna msongamano nilifika wakiwa wanamalizia kuzima moto sababu uliwaka kwenye eneo tu la nyumba na yalipo magari”.

“Nawaz! Imekuwa bahati wote hao hakuna anayejua mengi juu yetu hivyo sidhani kama atakuwa anatukaribia kiasi ambacho mi ninatilia shaka ila siku hii ya leo nataka huyu mtu awe mikononi mwetu sitaki afikie kuua au kumuumiza mtu yeyote kati yetu… Endelea kuwepo hapo mimi acha nianze mara moja mchakato wa kuweka sawa hii kazi… Inasikitisha sana kwa alichofanya atajuta na kulipia hili”.

“Kumekucha! Kazi ianze mara moja mkuu”.

Simu zilikatwa pande zote… Mr Logan Puter akatoa pumzi ndefu kisha akaenda lilipo benchi la mazoezi ya kifua na kukaa juu yake macho kwenye dari na kwa mara ya kwanza katika maisha yake akajikuta ana uwoga fulani.

‘Mmmh! Jana niliongea na Omar Kaken na akaniambia maneno ambayo kidogo kidogo yananiingia akilini, huyu mtu tuliyeletewa ni next level na akanionya hajawai shindwa operesheni yoyote anapopewa toka atoke US Navy Seals na kuingia CIA… Mbona natishika juu ya hili, hapa itabidi nijaribu leo na nikiona bado hatari inatunukia nitajilipua kwa kumfuata mkuu wa kitengo cha ujasusi cha ofisi ya waziri wa mkuu na nitamwambia ukweli wote ingawa nilishamkatalia sihusiki na utekwaji nyara wa wanasayansi… Najua sababu ya urafiki wetu atanisaidia tu na hawezi kusumbua ugenini mbwa huyu… Nitamshawishi Mr. Zahid Abdul Ghani na ninaamini atanielewa maana pesa haijawai kushindwa hasa kwake ambaye namjua pakumuanzia’ Aliwaza na kuinuka kuondoka kwenye kile chumba cha gym moja kwa moja akapanda juu ghorofani kilipo chumba chake cha kulala.

“Kuna habari gani huko?”. Mke wake akampokea kwa swali.

“Nyumba yake ya Broga Hill 1st Hiltop imeungua moto na walio ndani ya nyumba wameungua kwa moto huo”. Akajibu huku akivua fulana ya kulalia aliyoivaa kwa dhumuni aelekee maliwatoni.

“Eeeh! Nini chanzo cha moto?”. Akauliza kwa pupa mke.

“Uchunguzi unaendelea… Naomba tuongelee baadaye hili jambo nikiwa na uhakika na kila nitakalokwambia… Nataka nioge kisha nijiandae kwenda huko kuonana naye”. Akajibu jibu aliloamini litamfanya mke wake kuacha kumuuliza swali lingine na papo hapo akazama maliwatoni.

Saa moja kasoro robo asubuhi ilimkuta Mr. Logan akiwa ofisini kwake mtaa wa Rodger street barabara ya Jalan Hang Kasturi baada ya kuondoka nyumbaani kwake eneo la Dewan Negara, eneo maarufu sana kihistoria katika nchi ya Malaysia sababu ndipo lilipo jengo la mikutano ya bunge la nchi hii. Muda wote alikuwa katika tafakuri ya hali ya juu akitathimini mambo mengi katika halmashauri ya ubongo wake wa kufikiri, mara mlango uligongwa na kumstua toka mawazoni, hakutaka kufikiri sana akainuka na kwenda kufungua mlango.

“Karibu Mr. Nawaz…”. Akamkaribisha mgongaji na wote wakaongozana kwenda kwenye meza ambayo kila mmoja alikaa panapomuhusu (mwenye ofisi na mgeni).

“Lete habari… Vipi huko?”. Akampa ruhusa ya kuongea mgeni wake aliyeingia ofisini kwake.

“Katika maiti zilizopo pale hakuna maiti ya mwanamke”.

“Una uhakika?”.

“Ndiyo boss, ulivyonitumia meseji ukiniuliza juu ya kuwepo maiti ya mwanamke sikukujibu sababu nilitaka kuhakikisha kwanza maana katika wote waliokufa walikufa wakiwa eneo moja”.

“Ina maana aliwatoroka au ametoroshwa?”.

“Kama alikuwepo pale na una uhakika walienda naye basi aliwatoroka… Maana sidhani kama yeye ndiye amefanya tukio lile”.

“Inamaanisha Agent Kai amemchukua kuondoka naye?… Yah! Amefanya hivyo sababu mara ya mwisho nilipiga simu kuongea nao na nikawapa msisitizo juu ya umuhimu wa kumuua yule mwanamke”.

“Iko hivyo… Yupo mikononi mwake, una uhakika hajui lolote juu yako?”.

“Sidhani kama ananijua ingawa mara mbili hivi nishaonana naye nikiwa kwenye sura yangu na mara tatu nimewai kukutana naye nikiwa kwenye sura yangu ya bandia, mara zote hizo ni zile nilizowai kufika pale, ila sina hakika kama ananijua mimi kama boss wa matukio ya tofauti na anavyoamini”.

“Si wa kumuacha yeye aingie moja kwa moja katika kifo… Atakiwi kuishi”

“Wakati nakuja huku nikiwa njiani nilimpigia simu Jeong kumueleza kilichowapata wenzake na yeye jambo la kwanza aliniuliza juu ya yule mwanamke nikamjibu nilitoa oda auwawe na nikamjibu sina hakika kama ni mzima au lah!... Unaponiambia hakuna maiti yake basi yupo mikononi mwa muhusika wetu”.

“Ok! Jeong atafute picha zake pia tutafute ndugu zake wanaishi wapi hapa KL”.

“Sawa sawa.. Pia nishamwambia aondoke kwenye jengo la Nadau akakae kwingine… Kazi imekuwa ngumu bila kutarajia mtu mmoja anatupa mshangao… Nafikiri asubuhi hii hii iwe na majibu yote tunayoyahi…!”. Hakumaliza kuongea simu yake ya mkononi iliita na kumfanya atoe mikono yake iliyokuwa juu ya meza kaka mkao wa kuiegemea meza.

Alipotizama jina la mpigaji akainua macho pia kumtizama Mr. Nawaz na papo hapo akapokea.

“Hallow!”.

“Mr. Rafael Khamdushin hapa, Alamanda Hotel”.

“Yah! Rafa lete habari”.

“Mtu uliyenitumia picha yake yupo hapa Alamanda Hotel ni mgeni wetu amechukua chumba”.

“Yupo hapo Alamanda?”. Ni kama mshtuko fulani vile Mr Logan Puter taarifa ilimstua na pigo za moyo zilienda tofauti mpaka mwenyewe akashangaa kwanini, macho yake aliyakaza kumuangalia bwana Nawaz na wote wakawa wanaangaliana kwa shauku.

“Ndiyo bosi… Lakini usiku wa kuamkia leo hakulala hapa… Kwa jinsi nilivyochunguza hakulala, nilimuhoji mlinzi anasema alichukua gari aliloletewa na mzungu mmoja kisha akaondoka jumla hakumuona kurudi tena”.

“Ahsante kwa taarifa… Sasa kuna watu nawatuma watakuja hapo naomba uwape ushirikiano kuna mambo watataka kuyajua zaidi… Ninawapa na bahasha yako, vitu vingine watajua wenyewe wewe uwape msaada wowote wataokuomba”.

“Sawa mkuu… Na ahsante kwa yote”.

“Haya ahsante na wewe, naomba ukimuona asubuhi hii tu nipigie lakini uwe makini unaponipigia kuongea nami asigundue… Watakaokuja watakupigia wakifika nakuomba uwasiklize wao wapi watakapoona ni sahihi wewe kuongea nao”.

Simu ikakatwa akatoa pumzi ndefu kama kashusha mzigo mkubwa kichwani.

“Amefikia Alamanda Hotel, pumbavu… Muda wa kulipa umefika, shida hakulala pale usiku wa kuamkia leo, alikwenda kututia hasara Broga Hill”.

“Hatujajua amelipa siku ngapi pale Alamanda, patakuwa ni mahali kwetu pa kuanzia kazi sababu lazima leo atarudi kinyemela hivyo umakini unahitajika”.

“Kazi ipo mikononi mwako chukua wazee wa kazi watano leo kambi yetu itakuwa pale… Wawili watachukua vyumba, utaomba mtu wetu wa pale atusaidie kupata chumba kilicho flour moja naye… Bila kuchelewa muende muda huu huko, wengine tutawaweka tayari kwa lolote lile, hao watakuwa kule nyumba ya siri sitaki hata mmoja aondoke kwenda sehemu yoyote mpaka misheni ikamilike”.

“Sawa mkuu! Mara moja nikitoka hapa nawapitia hao watu watano moja kwa moja tunaelekea Alamanda, nakuahidi hakuna kosa litakalotokea”.

“Ukitoka tu hapa nitapiga simu kwa kila mmoja kumpa muongozo na umuhimu wa kazi hii”

“Usijali mkuu kila kitu kitaenda sawa siku ya leo haitaisha bila kumtia mbaroni, ngoja tufike kwanza Alamanda tukafanye upelelezi wetu naamini tutayajua mengi kwa muda mfupi”.

“Nakuamini sana Nawaz na ndiyo maana ukawa kiongozi, namba za mtu wa pale ni hizi hapa mkifika pale kabla hamjaingia eneo la hotel hakikisheni mnaonana nje ya hotel, sitaki muache alama zozote kama ilivyo kawaida yetu sisi, hakuna kuacha alama”. Akasema Mr Logan akiwa kaandika namba ya mtu ambaye kina Nawaz wataenda kuonana naye hotel ya Alamanda.

Maongezi yao yaliishia hapo Mr. Nawaz akaondoka pale ofisini na kumuacha mwenye ofisi yake Mr Logan Puter akiendelea kula kiyoyozi.


Mwisho wa sehemu ya kumi na sita (16)


Shufani Bint Mahamud amemtafuta Agent Kai wote wakaweka makubaliano waonane mahala atakapopanga Agent Kai kwa maongezi ambayo upende wa ‘The Sole Cat’ ni maongezi ambayo ni kazini wakati kwa Shufania ni nafasi ya kuzidi kujiweka karibu kwa mwanaume ambaye amejikuta ana hisia naye kwa mara ya kwanza toka apevuke na kuwa mwanadada.


Mr. Logani Puteri na msaidizi wake Nawaz Patrash wameingia katika mshtuko mkubwa baada ya taarifa ya kuvamiwa na kuuwawa kwa vijana wao wa SDB.

Mipango kwao wanaona kama ina ganzi, wanahisi kama adui yao wanayemtamani ni kama anafanya anachojisikia katika ardhi waliyoizoea, ujanja wao ni kama unafunikwa.


Nini kitajiri katika yote ambayo ni kama yako fumboni?


Muda wako ndiyo haswa ninaouhitaji, endelea kuwa nami nifanye kukupa burudani ya ubongo ya kijasusi.



Simu ikakatwa akatoa pumzi ndefu kama kashusha mzigo mkubwa kichwani.

“Amefikia Alamanda Hotel, pumbavu… Muda wa kulipa umefika, shida hakulala pale usiku wa kuamkia leo, alikwenda kututia hasara Broga Hill”.

“Hatujajua amelipa siku ngapi pale Alamanda, patakuwa ni mahali kwetu pa kuanzia kazi sababu lazima leo atarudi kinyemela hivyo umakini unahitajika”.

“Kazi ipo mikononi mwako chukua wazee wa kazi watano leo kambi yetu itakuwa pale… Wawili watachukua vyumba, utaomba mtu wetu wa pale atusaidie kupata chumba kilicho flour moja naye… Bila kuchelewa muende muda huu huko, wengine tutawaweka tayari kwa lolote lile, hao watakuwa kule nyumba ya siri sitaki hata mmoja aondoke kwenda sehemu yoyote mpaka misheni ikamilike”.

“Sawa mkuu! Mara moja nikitoka hapa nawapitia hao watu watano moja kwa moja tunaelekea Alamanda, nakuahidi hakuna kosa litakalotokea”.

“Ukitoka tu hapa nitapiga simu kwa kila mmoja kumpa muongozo na umuhimu wa kazi hii”

“Usijali mkuu kila kitu kitaenda sawa siku ya leo haitaisha bila kumtia mbaroni, ngoja tufike kwanza Alamanda tukafanye upelelezi wetu naamini tutayajua mengi kwa muda mfupi”.

“Nakuamini sana Nawaz na ndiyo maana ukawa kiongozi, namba za mtu wa pale ni hizi hapa mkifika pale kabla hamjaingia eneo la hotel hakikisheni mnaonana nje ya hotel, sitaki muache alama zozote kama ilivyo kawaida yetu sisi, hakuna kuacha alama”. Akasema Mr Logan akiwa kaandika namba ya mtu ambaye kina Nawaz wataenda kuonana naye hotel ya Alamanda.

Maongezi yao yaliishia hapo Mr. Nawaz akaondoka pale ofisini na kumuacha mwenye ofisi yake Mr Logan Puter akiendelea kula kiyoyozi.


ENDELEA NA UHONDO…!


HATUA MOJA MBELE II

“Hallow!”

“Hallow! Habari, naitwa Rafael…. Nani mwenzangu?”.

“Mr. Nawaz, Nawaz Patrash wa Mr. Logan Puter”

“Oooh!... Tayari nilijulishwa utanipigia, huko wapi?”.

“Madam Stang’s Stall hapa China town, unaweza kufika haraka hapa kuna mambo tunayahitaji toka kwako pia tuna bahasha yako ni vizuri ukija kuichukulia huku”.

“Dakika kumi nitakuwa hapo”.

“Tupo ndani ya gari aina ya Toyota Hiace Van rangi nyeupe, tumepaki upande wa pili wa huu mgahawa wa Madam Stang’s Stall”.

“Okay nafika muda si mrefu”.

Simu ikakatwa kwa pande zote, Mr Nawaz akawageukia wenzake waliokuwa kimya wakifuatili maongezi yake aliyokuwa akiongea kwenye simu.

“Anakuja mtu ambaye atakuwa ndiyo msaada kwetu… Bwana Ghulam Qaresh na Mosin Lee mtachukua vyumba pale Alamanda, wakati huo huo Istqal Saanjin, Bayan-Uugun, Johome Meloo na Mongolia Damme mtakuwa around pale kuhakikisha lolote linalotokea mnafika haraka ku clear kila kitu… Huyu mtu anayekuja atatusaidia mtaingia na hii gari mpaka mahali atakapowaonyesha pale kuna kazi wataifanya Hassan Saddiq na Takasho kuhakikisha eneo lote la hotel mtakaokuwa ndani ya gari mnaliona, kisha wao wakishamaliza kazi wataondoka na kuwaacha nyie niliosema mtakuwa around pale…”. Akaongea kwa kirefu kidogo Bwana Nawaz Patrash.

Hakuna aliyeongea chochote sababu wote walielewa walichoambiwa na kiongozi wao.

Dakika kumi mbele walimuona mtu waliyekuwa wakimsubiri pale mkabala na mgahawa maarufu kwa vyakula vya kitamaduni vya asili ya Asia mgahawa unaoitwa Madam Stang’s Stall. Gari hii aina ya hiace ilikuwa maalumu kwa kazi za aina wanayoifanya ilienea vifaa mbalimbali vya kisasa kama kompyuta zilizounganishwa na kamera pamoja na mawasiliano ya kisasa, pia ilikuwa kubwa iliyowekwa viti aina ya benchi kulia na kushoto katikati kukiwa na meza.

“Tupo hapa mheshimiwa”. Bwana Nawaz alishusha kioo cha dirisha la gari na kutoa uso wake akimuita mtu ambaye licha ya kuwa aliiona hiace van rangi nyeupe lakini aliogopa kusogea sababu hakuwa anaona chochote kilicho ndani ya gari sababu ya vioo vya rangi vya dirishani (tinted)

Walimfungulia mlango wa nyuma akaingia ndani na kustuka sana baada ya kukutana na nyomi la wanaume wa kazi.

“Karibu Mr Rafael… Wote hawa unaowaona ni kama wewe sababu wote sisi tunalipwa na Mr Logan kama anavyokulipa wewe, hivyo tafadhali usituogope kwa vyovyote vile, tunaomba uwe huru kabisa”.

“Ahsante…. Ahsanteni sana, nimefurahi kuwaona”. Akajibu huku akijitahidi kuupoza moyo wake unaodunda kasi.

“Naitwa Nawaz Patrash ndiye yule uliyetoka kuongea naye kwa simu dakika kumi na tano zilizopita na hawa hapa unaowaona ni wenzangu kama vile nilivyokwisha kuambia sote sisi ni ndugu… Nafikiri unatambua hapa tumekuitia nini”.

“Hilo usijali mzee, najua kipi kilichonifanya nikawa hapa saivi, ninayo ya kusaidia naamini hilo”. Akajibu Rafa akiwa tayari kashapewa nafasi kwenye benchi la upande wa kushoto.

“Vizuri… Tuna mengi tunatamani kuyajua hili iturahisishie katika kazi yetu lakini sidhani kama tutayapata kwako… Nafikiri wewe unachojua ni kuwa mtu tunayemuhitaji yupo hotelini kwenu lakini hujui tunaweza tukampata vipi… Je wewe kama wewe ushamuona kwa macho?”.

“Sijamuona kwa macho ila jina ndiyo lilinijulisha kuwa ni mwenyewe na picha niliyotumiwa na Bwana Logan nilipomuonyesha mlinzi wa magari alinijibu ni yeye aliyeongea naye jana saa tatu”.

“Basi tusipoteze muda… Kuna vitu tunataka utusaidie cha kwanza gari yetu ikae sehemu bila bugudha yoyote, pili utupe msaada watu wetu wawili wapate vyumba vilivyo karibu na mgeni wetu na maana flour moja, pia muhudumu anayehudumu kwa kufanya usafi chumba alichofikia atusaidie tupate kadi ya chumba cha mgeni wetu hili mtu wetu aingie aweke vitu vitakavyotusaidia katika kazi na mwisho tupate video record za kamera ya hotel yenu za toka muda aliofika mtu huyo”.

“Sawa vipo nitakavyoweza lakini kwa msaada wenu si kuniacha mwenyewe nifanye maana pesa pia itahitajika mi nitakachikuwa nafanya ni kutia tu ushawishi kwa wafanyakazi wenzangu wanaohusika na kila mtakachohitaji… Sababu mimi ni kiongozi wa usafi wa maeneo ya mazingira ya nje ya hotel tu na yupo ambaye ni kiongozi wa usafi wa ndani ni mwanadada hivyo lazima tutumie kilainishi kufanya yote hayo lasivyo tutakwama”.

“Sawa nimekuelewa… Kwa sasa wewe rudi hotelini haraka kaandae mazingira ya gari kupata sehemu tutakayokaa bila kufuatiliwa na walinzi wenu kwanini tumeweka gari hapo… Vingine watakaokuja watakuwa wanakuelekeza papo hapo nawe unaangalia kinawezekana vipi kinafanyika tu”

“Ok! Inabidi niongee na meneja mkuu wa hotel gari mpaki wanapopaki gari wamiliki wa hotel na uzuri wamesafiri kwenda Japan hivyo naamini hakutakuwa na pingamizi nitamuelekeza kitu nachoamini atakubali sababu ni rafiki yangu na tunaheshimiana sana… Ila ombi langu naomba yasitokee mauaji pale naomba iwe ni kumchukua kitaalamu kama alivyoniambia Bwana Logan”.

“Kila alichokueleza Logan ndivyo itakavyokuwa usiwe na wasi kabisa hatutakuingiza matatizoni bwana Rafael… Wewe nenda na ukifika na ukawa ushaweka mambo sawa utapiga namba hizi za Bwana Ghulam Qaresh kumuelekeza ni vipi”.

“Wawe wananifuata kwa nyuma sababu najua haitashindikana na nitaomba gari itakapokuwa inaingia waonekane watu wawili au mmoja tu”.

“Sawa tu… Vioo hivi havionyeshi kama tumo humu hivyo hilo limepita, bahasha yako hii hapa na nakutakia kazi njema yenye mafanikio”.

Bwana Rafael alimalizana na kina Bwana Nawaz Patrash akashuka toka ndani ya gari na kwenda alipopaki pikipiki yake na kuondoka kurudi Alamanda Hotel akiwa na mpango mkakati madhubuti wa kuhakikisha Agent Kai anatua mikononi mwa adui zake.


** ** **

Kama ni ahadi basi hii ilikuwa ni ahadi iliyokuwa ahadi kamili au kwa sisi waswahili tumezoea kusema tukimsifia aliyetimiza ahadi kwa wakati kuwa ana ahadi ya kizungu.

Simu ya mkononi ya Agent Kai iliyokuwa kaiweka juu ya dashboard ya gari ilimstua kutoka kwenye kazi aliyokuwa akiifanya kwenye internet kupitia kompyuta yake mpakato (laptop), lilikuwa jambo muhimu akilifuatilia baada ya kugundua simu yake iliyochukuliwa na vijana wa SDB iliwashwa muda wa saa tano asubuhi lakini aliamisha macho yake kutoka kazi ile anayoifanya akiwa ndani ya gari aina Nissan Frontier na kuyatupia ilipo simu kisha akainyakua na haraka akatizama upande wa juu wa kulia mwa kioo cha simu akasoma saa na ikamfanya kutabasamu ndani ya sura yake ya bandia inayomfanya aonekane kama miongoni mwa wanaume wengi wa rika lake wa nchi hii ya Malaysia tofauti ikiwa yeye akiwa ni wale wenye rangi isiyokolea weupe mkali (maji ya kunde), alitabasamu kwakuwa ilikuwa ni saa sita na nusu barabara juu ya mshale.

“Asallaam aleykuum miss!”. Akatoa salamu mara tu alipogusa kioo kuruhusu kupokea simu huku furaha kubwa ikidhihiri katika uso wake na moyo wake kutokana na tabasamu kana kwamba wanaangaliana na muhusika.

“Walaikuum salaam warahmaturah wataallah wabarakatuh”. Sauti nyororo ya kumtoa chatu pangoni ilipasua himaya ya ngome ya masikio ya Agent Kai ikijibu salamu, sauti ambayo ilikuwa kisu kikali kwa kila mwanaume rijali ambaye angeisikia nikiwemo mimi mwandishi.

“Hivi ulitega simu yako sambamba na saa?”.

“Kwanini? Ramsey!”. Baada ya kujibu naye akauliza, wakajikuta wote wanacheka kicheko kifupi.

“Kwa sababu ilipofika saa sita na nusu tu tena iliyo kamili juu ya alama simu yangu imeita na kumbukumbu zangu zilizo sahihi nakumbuka uliniambia utanipigia simu saa sita na nusu”.

“Ukweli kusema na mimi kuficha si hulka yangu, nilitamani saa sita na nusu ifike kuliko mara zote ya vitu nilivyowai kuvitamani, nikawa naona kama muda umeganda hauendi kama ilivyo kawaida yake”. Akajieleza Shufania huku akidhidi kuyafurahia maongezi.

“Mmmh! Usiniambie pengine kuna sehemu tunarandana au umetoka kwenye ubavu unaonihusu”.

“Hahahah! Ahahah! … nyie wanaume toka muambiwe Eva alitoka kwenye ubavu wa Adamu basi mmekariri kweli, kwa taarifa yako hakuna ukweli humo zaidi ya ukweli wa nyie kuwa mnatoka kwenye matumbo ya kina mama”.

“Utanivunja mbavu wee mrembo… Maana ucheshi wako inabidi tuwe tumekaa sehemu moja ndiyo uniletee maneno yako… Huko wapi saivi?”.

“Niko hospitali kuu ya rufaa ya Kuala Lumpur (HKL)… Wewe huko wapi?”.

“Hospital!... Hospital kufanya nini?”.

“Hahahaha, hahahah hah hah hah!.. Ramsey usihofu mi siumwi, nililetwa na gari ya kazini… Ni kwamba ilivyofika saa tano na nusu nilienda kwa meneja utumishi wa hotel yetu nikajifanya jino linauma sana na sihitaji kung’oa nahitaji lizibwe na hapa KL hospital hii ya rufaa ndiyo kuna clinic ya huduma ya kuziba meno. Basi kwakuwa meneja wetu wa utumishi tunaelewana sana ruhusa niliipata na akatoa amri dereva wetu wa wafanyakazi anilete, ndipo ilipofika saa sita kasoro tukaondoka hotelini nakuja hapa, tulipofika nikamuomba dereva aniache yeye arudi kazini mi sitarudi tena… Ni hivyo yaani”.

Kicheko kikaungwa pande zote mbili.

“Aiseeeeh! Wewe ni mkali zaidi yah!.. Tufanye mpango tukutane unipatie raha hizo za maneno mubashara… Mi bado nipo ubalozini hapa lakini nakaribia kumalizana na niliokuwa na kikao nao kwa leo, hili usiwe mwenye kukerekwa na lolote lile namtuma mtu akufuate, naomba uchukue taxi hadi garden ya Tamal Maxwell iliyopo Pudu Street. Utamkuta yeye kashafika amepaki gari aina ya Nissan Frontier rangi nyeusi karibu na lango la kuingilia bustani… Nielekeze umevaaje hili asipate tabu kukuona na sitampa namba yako ya simu ukitaka mawasiliano utakuwa unapiga kwangu kisha mimi nampigia yeye uwa sipendi kumuamini mtu kumpa namba ya mrembo kama wewe haitakiwi kujulikana kwa watu ovyo”.

“Oooh! Poa mtaa huo ndiyo njia yangu ya mkato nikiwa naelekea msikitini kila ijumaa nayokuwa mapumziko, nimevaa baibui ya rangi ya bluu pamoja na mtandio wa rangi nyeusi, niko na pochi la rangi nyeusi na viatu nimevaa vyeusi pia”.

“Ok! Utamkuta huyo mtu kama nilivyokwambia amevaa kanzu fupi ya mikono mirefu rangi ya zambarau pia amevaa miwani ya jua”. Akatoa muongozo Agent Kai kisha wakaagana na kukata simu kila mmoja akiwa na shauku ya kumuona mwenziye.

Na wakati wakiongea na simu Agent Kai alikuwa yupo hapo hapo karibu na lango la kuingilia moja ya kati ya bustani maarufu kati ya bustani zilizopo katika jiji la Kuala Lumpur iitwayo Tamal Maxwell, alikuja eneo hili mtaa wa Pudu baada ya signal za simu yake iliyochukuliwa na vijana ambao asilimia tisini na tisa alikuwa kashawafuta wa SDB, signal kuonyesha mara ya kwanza iliwashwa ikiwa mtaa huu.


Lakini alipofika ilionyesha aliyekuwa kaiwasha aliondoka mtaa huu na kisha kuizima wakati akiendelea na kujaribu kufuatilia ajue ni nyumba gani ilipowashwa kwa mara ya kwanza ndipo simu ya Shufania ikapigwa na moja kwa moja akaona amwambie afike hapo na kwakuwa yupo kwenye sura ya bandia akaamua atamchukua na kwenda naye hotel ya Sheraton Imperial Palace kwa kumwambia huko ndipo atamuona Ramsey Bronze.

Agent Kai aliposhusha simu toka sikioni akasachi namba na kuruhusu ipige, ikaita upande wa pili.

“USA First!”. Upande wa pili ukaongea baada ya kupokea simu.

“USA First1!... Heshima yako Kapteni”.

“Itakuwepo milele kijana wangu… Niambie?”.

“Umeonana na mwanamke niliyemleta?”.

“Nimeonana naye na niliongea naye kidogo sababu alikuwa katika hali ya ukimya muda wote”.

“Safi… Naamini masharti yangu yatafuatwa kama nilivyoomba usiku”.

“Usijali mwanangu kila kitu kiko katika mstari uliouhitaji… Muda si mrefu radio ya taifa ya hapa imetangaza kile kilichotokea broga”.

“Kazi yao kufuatilia hayo… Kuna jina la mtu nililisikia jana likitajwa sana na wale marehemu ebu , utakuwa ushawai lisikia au lah!, jina la mtu anayeitwa Mr. Logan?”.

“Mr. Logan… Mmmh! Kwa kweli sijawai lisikia jina hilo ila nitalifanyia kazi baadaye baadaye nitakuwa na jibu ni nani”.

“Ok! Nitashukuru sana… Jana nilivyotoka ubalozini niliamua kubadili hoteli kutokana ningewachanganya kule Alamanda kwa sura hii niliyovaa, imekuwa faida kwangu sababu wateja wetu wameanza kufika pale kuulizia mbolea… Hii ni faida kwetu kwa wao kujisogeza kwangu wakijua mimi ni wa kipolepole wasubiri iwatokee puani niwaachie mshangao wenye afya ya kutosha, kuna mtu muhimu sana namsubiri mahali hapa huyo akifika atanipa maelezo kamili ilikuwaje wateja hao kuuliza kuhusu mimi”

“Safi sana mwanangu naamini katika kila hatua unayopiga na naamini katika uwezo wako wa kila jambo katika kazi”.

“Usihofu Kapteni…. Muda si mrefu nimemtumia taarifa chifu!”. Ghafla aliacha kuongea zaidi sababu aliiona taxi ikisimama mita kama kumi toka alipopaki yeye gari na kwa chati aliweza kumuona Shufania akilipa pesa kumpa dereva bila kushuka ndani ya gari.

“Kapteni! Niliyekuwa namsubiri amefika acha nifuatilie usalama wetu, tutaongea vizuri baadaye”

“Ahsante sana mwanangu, uwe makini”.

“USA First!”.

“Always USA First!”.

Simu zikakatwa kwa pande zote.

Mrembo wa kiarabu kutoka nchi ya Syria, nchi iliyo kwenye janga la vita ya wenyewe kwa wenyewe alishuka toka kwenye taxi.

Moyo wa Kai uliongezeka mapigo ya kudunda kwa jinsi uzuri kwa binti aliyekuwa ameshuka toka kwenye taxi maana uzuri wake haukujificha kwa kila jicho lililomuona, Shufania alizungusha macho huku na huko kutizama magari machache yaliyokuwa kwenye maegesho kutokana na kutokuwa na uzoefu na magari alichotaka kuona ni rangi tu ya magari akikariri rangi nyeusi ya gari.

Licha ya kuwa amemuona toka taxi inaingia na mpaka anashuka, Agent Kai alitaka kuhakikisha usalama wake kwa binti na sababu kubwa ilikuwa wakati taxi ile inakunja kuingia kwenye maegesho ya pale aliweza kuiona gari moja ndogo aina ya RAV 4 L rangi ya bluu ikija kwa nyuma na kutokana na uzoefu wake wa kazi aligundua watu wale watakuwa wanamfuatilia Shufania kwa stahili ya kunyapia.


Baada ya taxi kupaki tu wao walipitiliza wakaenda kupaki upande wa pili wa barabara kwenye maegesho ya Mini Market inayoitwa Rahma Mini market.

Agent Kai alitamani kumuita Shufania lakini kwanza alitaka kujihakikishia kama hisia zake ziko sahihi, hivyo alitoa lock kwenye simu yake na kufyatua pattern na moja kwa moja akapiga namba za Shufania ambaye naye gari aliloelekezwa sasa alishaliona baada ya kusoma juu ya kioo cha mbele kulikuwa na stika iliyoandikwa Nissan Frontier, alitamani kulisogelea lakini alitaka dereva aliye ndani ya gari ndiyo amstue yeye licha ya pia alimuona.

Simu yake ilipoita hakuipokea kwanza akageuka kuangalia upande wa gari aliyoilenga na akili zake kuwa ni yenyewe lakini akataka uhakiki na hakuona aliyekuwa ndani ya gari akiwa ameshika simu wala kuweka sikioni na wala hakumuona na kamba za earphones, hapo hakuwa sahihi kwani sikio la kushoto la Kai alikuwa kaweka kifaa kidogo kilicho kama punje ya hindi (small earphone speaker) na alikizamisha kwenye tundu la sikio la kushoto, hapo Shufania akaitizama simu yake na kupokea.

“Hallow!”. Akaongea

“Hallow! Umeshafika?”.

“Ndiyo..”.

“Ok!.. Pita ndani utamkuta niliyemtuma akufuate anakusubiri kwenye viota vilivyo karibu na swimming pool, nishampa maelekezo umevaaje hivyo akikuona tu atakuita halipo”. Papo hapo Kai akakata simu hakutaka jibu. Akili yake ilishakuwa kazini akaweka miwani yake vizuri machoni.

Shufania alishangaa akageuka kuangalia upande wa gari ya Nissan Frontier akakata shauri afuate maelekezo aelekee ndani kama alivyoambiwa kwenye simu muda si mrefu.

Macho yaliyo ndani ya miwani ya kijasusi yalikuwa makini kuusoma mchezo akiangalia kule ilipopaki kijigari kidogo cha escudo kuona kitendo gani kinafuata, vioo vya tinted vilivyo kwenye madirisha ya ya gari yake na vile vilivyo kwenye escudo vilimfanya asione vizuri ndani ya gari ingawa kwa uwezo wa miwani aliweza kujua kwenye gari ile kuna wanaume wawili.

Shufania alipopotea tu ndani ya lango kubwa la kuingilia Tamal Maxwell Garden, milango ya gari alilokuwa analishuku wakashuka wanaume wote wawili aliokuwa akiwaona kwa tabu na wakaifunga milango ya gari kwa kasi kisha wakavuka barabara katika kasi ya mwendo tena wakikwepa magari na moja kwa moja Agent Kai akawa sasa amehakikisha Shufania anafuatwa na wale watu.


Akawaacha wapite kwenye geti naye akashuka haraka kwenye gari akafunga milango vizuri na yeye akazama ndani na mita kama thelathini hivi akawaona washukiwa wake wakielekea upande aliomuelekeza Shufania kuwa ndipo atamkuta aliyemfuata.

Bustani muda huo haikuwa na watu wengi sana kutokana na mida ya kazi, alipokunja kona fulani aliyohisi anaweza kuwa anafanya mkatizo wa haraka kumuwai Shufania kabla hajafika lilipo swaimming pool alimuona Shufania akisogea alipoelekezwa kwa mwendo wa taratibu huku kichwa chake akikizungusha huku na huko kuangalia viota mbalimbali akilenga ajionyeshe kwa mtu aliyemfuata hili ampeleke kwa Agent Kai ambaye naye akili yake ilitaka kuhakisha wale watu hawapo na Shufania au wapo naye wanamchezea shere.

Agent Kai akitembea kwa mwendo kasi akaenda njia za mkato mpaka Shufania anakaribia swimming pool naye akawa amefika na Shufania alipomuangalia haraka akakumbuka maelekezo ya mtu anayemjua kama Ramsey Bronze swadakta ni yeye akaachia tabasamu na kisha wote wakatabasamu.

“Asallaam aleykuum!”. Agent Kai akampa salamu huku anamsogelea na papo macho yake yaliyo ndani ya miwani yakiwatizama kipembe wanyapiaji ambao nao si haba walionyesha ujuzi wao wa mambo wakijifanya wanamtafuta mtu katika viota vilivyo karibu yao.

“Wallaikuum sallaamu!”.

“Habari yako?”.

“Nzuri tu kaka… Nilielekezwa una short kanzu ya rangi ya zambarau”. Akasema Shufania tabasamu likiwa limechanua usoni mwake na kidole cha shahada akiwa kakielekeza kwa Agent Kai kwa stahili ile ya ni wewe.

“Oooh yes! Nami nikaambiwa umevaa gauni refu aina ya baibui kama ulivyovaa na jina nikatajiwa unaitwa Shufania”. Akajibu Kai huku muda wote akiwa kaigeuza sauti yake kutoka ile ya Agent Kai au Ramsey Bronze ile ya kawaida kwenda ingine.

“Ndiyo mimi wala hujakosea!”.

“Naitwa Ramji… Ni dereva katika ubalozi wa Marekani hapa Malaysia… Naomba tusipoteze muda twende nikupeleke alipo Ramsey, amenitumia meseji kuwa ndiyo wamemaliza kikao kuna mtu anamsindikiza Sheraton Imperial Palace Hotel hivyo na sisi twende pale tutamkuta”. Hakuwa amesubiri jibu bali aligeuka nyuma na kuanza hatua za kuzunguka maua yaliyokuwa nyuma yao safari ya kutoka kuelekea nje ya garden ikaanza wakifuatana.

Wale jamaa kwa chati (kificho) kila mmoja alitoa simu yake ya mkononi smartphones wakajifanya wanapiga picha mazingira na wakafanikiwa kuwapiga picha Agent Kai aliye kwenye sura fake na Shufania na kila mmoja alifanikiwa kupata picha tatu nne hivi na mara zote walizopiga picha, Kai aliligundua hilo ila akaacha wafanye wanachojisikia kufanya, miwani yake ilifanikiwa kufanya kazi walikuwa ni wanaume wenye umri uliomuacha yeye kidogo sana kwa kifupi ni vijana wenzake ambao wanaingia utu uzima sasa kwa kadiri alivyowakadiria, ni watu wa kazi wa Mr. Logan Puter walipewa kazi ya kumfuatilia Shufania kila anapokwenda na kila anayekutana naye wakihisi atakuwa yupo karibu na mtu wanayemtafuta kwa udi na uvumba Agent Kai.


Mwisho wa sehemu ya kumi na saba (17)


Nawaz Patrash na kikosi chake, wamesogea Alamanda Hotel, hotel ambayo ni moja kati ya hotel mbili alizopanga Agent Kai.

Wamefika mgahawa ulio karibu na hotel hii kuonana na mmoja wa mfanyakazi wa hotel hii kwa ajili ya kupewa msaada fanikishi utakaowasaidia kuweza kufanya mambo yao kiulaini katika hatua yao dhumuni kumnasa Agent Kai.


Je mipango yao itakwenda sawa?

Jibu litakuja katika mfululizo wa muendelezo wa riwaya yetu tamu.


Agent Kai naye akiwa katika sehemu anafuatilia simu yake iliyoonyesha signal kuwa iliwashwa maeneo Pudu, anapigiwa simu na Shufania na kukumbuka ahadi waliyoahidiana kukutana muda wa saa sita na nusu, hivyo kwa haraka kwakuwa anahisi kufeli kuendelea kufuatilia simu yake anaamua amuite Shufania eneo hili kwa maongezi yao.

Mwanadada Shufania alipofika eneo la mgahawa Tamal Maxiwell, yeye Agent Kai anagundua kuna mkia unafuata nyuma ya Shufania, hivyo kwa tahadhari anaamua kuucheza mchezo wa giza katika mchana huu.


Nini kitawajia?


Muda wako hapa hapa ulipokutana na riwaya hii ndipo muendelezo unapopatikana.




Agent Kai akitembea kwa mwendo kasi akaenda njia za mkato mpaka Shufania anakaribia swimming pool naye akawa amefika na Shufania alipomuangalia haraka akakumbuka maelekezo ya mtu anayemjua kama Ramsey Bronze swadakta ni yeye akaachia tabasamu na kisha wote wakatabasamu.

“Asallaam aleykuum!”. Agent Kai akampa salamu huku anamsogelea na papo macho yake yaliyo ndani ya miwani yakiwatizama kipembe wanyapiaji ambao nao si haba walionyesha ujuzi wao wa mambo wakijifanya wanamtafuta mtu katika viota vilivyo karibu yao.

“Wallaikuum sallaamu!”.

“Habari yako?”.

“Nzuri tu kaka… Nilielekezwa una short kanzu ya rangi ya zambarau”. Akasema Shufania tabasamu likiwa limechanua usoni mwake na kidole cha shahada akiwa kakielekeza kwa Agent Kai kwa stahili ile ya ni wewe.

“Oooh yes! Nami nikaambiwa umevaa gauni refu aina ya baibui kama ulivyovaa na jina nikatajiwa unaitwa Shufania”. Akajibu Kai huku muda wote akiwa kaigeuza sauti yake kutoka ile ya Agent Kai au Ramsey Bronze ile ya kawaida kwenda ingine.

“Ndiyo mimi wala hujakosea!”.

“Naitwa Ramji… Ni dereva katika ubalozi wa Marekani hapa Malaysia… Naomba tusipoteze muda twende nikupeleke alipo Ramsey, amenitumia meseji kuwa ndiyo wamemaliza kikao kuna mtu anamsindikiza Sheraton Imperial Palace Hotel hivyo na sisi twende pale tutamkuta”. Hakuwa amesubiri jibu bali aligeuka nyuma na kuanza hatua za kuzunguka maua yaliyokuwa nyuma yao safari ya kutoka kuelekea nje ya garden ikaanza wakifuatana.

Wale jamaa kwa chati (kificho) kila mmoja alitoa simu yake ya mkononi smartphones wakajifanya wanapiga picha mazingira na wakafanikiwa kuwapiga picha Agent Kai aliye kwenye sura fake na Shufania na kila mmoja alifanikiwa kupata picha tatu nne hivi na mara zote walizopiga picha, Kai aliligundua hilo ila akaacha wafanye wanachojisikia kufanya, miwani yake ilifanikiwa kufanya kazi walikuwa ni wanaume wenye umri uliomuacha yeye kidogo sana kwa kifupi ni vijana wenzake ambao wanaingia utu uzima sasa kwa kadiri alivyowakadiria, ni watu wa kazi wa Mr. Logan Puter walipewa kazi ya kumfuatilia Shufania kila anapokwenda na kila anayekutana naye wakihisi atakuwa yupo karibu na mtu wanayemtafuta kwa udi na uvumba Agent Kai.


ENDELEA NA MUENDELEZO..!


HATUA MOJA MBELE III

Walifika kwenye gari wakiwa wameongozana Agent Kai mbele na Shufania nyuma, hapo Kai akamfungulia binti mrembo kama mwenyewe alivyopenda kumuita mara kwa mara lakini hapa akiogopa kumuita hivyo kutokana hapa yupo kama bwana Ramji, kisha naye akazunguka upande wa dereva na kuwasha injini ya gari.

Katika list ya watu wa kazi wa Mr. Logan alikuwepo mtu mweusi mmoja tu mwenye asili ya nchi ya Afrika ya kusini anayeitwa Johome Meloo ndiyo alikuwa mmojawapo kati ya watu hawa wawili waliopewa kazi ya kumfuata kila anapokwenda binti wa kiarabu Shufania, mwingine alikuwa bwana Daus Bilik mmalayasia huyu, wao walifanikiwa kumuona Kai akifungua mlango wa gari upande wa dereva na kuingia wakati wao ndiyo wakiwa wanachomoza kwenye lango kubwa la kuingilia Tamal Maxwell Garden walipita pale kana kwamba wanaelekezana kitu ambacho kwa mtu wa kawaida ukiwaona utajua labda kuna mtu au watu waliahidiana kuwa wakutane pale lakini hawakumkuta au hakuja (hila), moja kwa moja wakapitiliza kwenda kuvizia wavuke barabara kuelekea upande walipoiacha gari yao aina ya RAV 4 L ambayo Kai uwa anasema ni gari za watoto au wanawake.

Agent Kai alitia gia mafuta yakaruhusu gari iondoke akaomba kuingia barabarani kwa ishara ya taa pembeni na alipopata nafasi akaliingiza gari barabarani Nissan Frontie gari ya kiume. Kwa kupitia site mirror akawaona wateja wake wa mbegu wakiwa nao wanaomba kuingia barabarani na kisha wakaingia barabarani kwa kasi akiwa amewaacha gari nne toka walipo. ‘Kazi imeanza, nitawaonyesha kuwa hawafuati nyuki bali wanafuata mzinga wa nyuki’ Akawaza kisha akatabasamu na mwili ukamsisimka.

“Lete habari dada yangu mdogo, naona huko kimya kabisa… Au kwa sababu huko na mimi garini hauko na Ramsey”.Akaamua kuuvunja ukimya pindi alipokaribia mzunguko wa bara bara ya Cheng Lock Road ambao unaungana na barabara ya Tuanku Abdul Razak Road.

“Niko sawa tu! natamani turuke tuwai kufika Sheraton Hotel… Sijawai kuwa kama hivi nilivyo, rafiki yako ametawala hisia zangu… Ila naomba usije ukamwambia hivi naona aibu,yaani ni mcheshi kweli nimemisi sana ucheshi wake na ongea yake ya kuchomekea utani kila anapoongea ni lazima mtu ufurahi…”. Akaongea Shufania bila kujua aliye naye hapo ndiyo Ramsey Bronze anayemjua yeye.

Wakati anazunguka hili aingie barabara ya juu ya Tuanku Abdul Razak akawaona wateja wake na kimkebe chao wakizidisha spidi hili angalau waendane na spidi ya Nissan Frontier. Hapo kwa alichoongea Shufania akajua hayupo nao hawa watu katika mfumo mmoja bali wanamfuatilia. Je? Kawakosea nini, akajijibu papo hapo watakuwa wamehisi huyu binti yupo karibu naye kutokana na jana yake kuwa karibu naye.


Kwa chati akamchungulia binti ile kipembe na jibu la haraka likaja kichwani mwake kuwa binti hakuwa miongoni mwa wale watu kivyovyote vile, akaikumbuka kauli ya mwalimu wake wa kwanza katika mafunzo ya kutambua wahalifu pale tu unapokutana naye {‘Kai usimuamini sana mwanamke lakini penda kumtumia mwanamke sababu mwanamke kwenye kazi yoyote inayohusu duru za kijasusi ukaa katikati kama kiungo’}. ‘Siwezi kumtumia huyu mwanamke katika kazi hizi, moyo wangu umempenda tayari nafikiria kumfanya mama watoto wa wanangu, nitamuweka mbali kabisa na hatari yoyote’. Akawaza.

“Hata na yeye inaelekea umemgusa sehemu maana aliniambia jana alikutana na mrembo ambaye hakuwai kukutana naye hapo kabla na nilipokuona kwa kweli mashaallah mtapendezana mkiwa Mr na Mrs”. Akamchombeza kidogo na binti akaonyesha kufurahi kwani aligeuza uso wake kumuangalia Ramji fake na akaachia tabasamu lililomuacha hoi Agent Kai maana meno yanayong’aa yakiwa na mwanya ulikuwa ni ugonjwa wake mkubwa sana akajikuta naye akitabasamu.

“Kweli?!.. kweli amekwambia hivyo?... Nikimuona nitaona aibu kweli, natamani nimjue zaidi kaka yangu, nitaomba unisaidie sababu wewe ni wa Malaysia hapahapa nitaomba nizijue habari zake zote toka kwako, nitakupa namba yangu kisha nitakutafuta kabla sijapiga hatua zaidi unipe habari zake… nakupa kazi uanze kunikusanyia kabrasha la habari zake”. Akasema kisha wote wakacheka kwa sauti.

“Kweli kabisa .. Usijali nitakusaidia kwa yote dada yangu”.

“Nitashukuru sana kaka yangu maana kumuwarukia mtu ovyo kwa dunia ya sasa ni hatari sana hisia za kumpenda mtu ni nzuri lakini pia ni mbaya”.

“Samahani naomba nikuulize”. Akamwambia baada kufikiri na kuona itafaa amshirikishe kitu katika wakati huu walio ndani ya gari na wakiwa wamekaribia Sheraton Imperial Palace Hotel barabara ya Jalan Alor.

“Niulize tu usihofu kaka”.

“Ushawai kuwa na maadui?”. Alimuuliza hivi hili amuweke sawa kisaikolojia kabla ya kumwambia alichotaka kumwambia.

“Sina maadui mimi katika dunia hii, adui yangu ni shetani tu… Kwanini umeniuliza hivyo Ramji”. Akajibu kisha akauliza huku akimuangalia Kai a.k.a Faheem Ramji wa bandia.

“Naomba nitakachokwambia kisikustue na kukufanya ukahamaki kugeuka nyuma kwa kasi au ghafla, kama utakuwa unataka kuyaona ya nyuma ya gari kwa nje tumia site mirror… Kuna watu nahisi wanakufuatilia , hao watu umekuja nao wapo kwenye gari aina ya RAV 4 L rangi ya bluu wanatufuata na hata ulipoingia ndani kwa maelekezo uliyopewa na Ramsey walikufuata mmoja ni mtu mweusi amevaa fulana aina lacrosse ikiwa ya pundamilia yenye mistari ya rangi kijivu na nyeusi na mwingine kavaa shati mikono mifupi rangi ya bluu .. Nikuhakikishie hakuna baya litakalokukuta mbele yangu, nimetaka ujue tu na usishangae utakapoona kuwa tunaendelea mbele badala ya kuingia barabara ya kwenda Sheraton”. Akaongea huku hamuangalii Shufania macho yake yaliyo kwenye miwani yalikuwa makini na barabara huku akili yake ikichanganua afanye nini?.

Shufania alistuka sana kusikia maneno yaliyotoka kwa mtu aliyejitambulisha kwake kama Mr Ramji, alitamani sana kugeuka lakini onyo lilishamtosha hivyo macho yake yalipohama kumtizama Ramji akayatupia kwenye site mirror huku kutetemeka kukidhihiri machoni mwake. Mawazo yakavamia kichwani mwake[‘Kwanini wanamfuata? Amewafanyaje? Au wametokea Syria, wana shida na baba yake Dokta Mahamud sababu alikuwa daktari mkuu wa mji Deir El Zour mji uliokuwa wa kwanza kutekwa na kikundi cha dola ya kiislamu’] hakuwa na jibu hapo, akageuka kumtizama Ramji fake wakagongana macho ikabidi Agent Kai ampe tabasamu kumtia moyo.

“Usiogope Shufania … Hawana shida na wewe hawa”.

“Unamaanisha nini kusema hivyo? Umejuaje? Si umesema wananifuata mimi”. Tayari binti wa kiarabu Shufania alikuwa ndani ya taharuki na kijasho kikijidhihiri machoni mwa Agent Kai.

“Iko hivyo… Niko sahihi navyokwambia hawana shida na wewe niamini Shufania wanalolitaka halitakuwa”. Agent Kai alijibu kama mtoto anavyojibu swali la mtoto wake. Hakujua amemkumbusha miaka mitatu iliyopita wakati wanakimbia vita kutoka mji wa Deir EL Zour,Syria akiwa na familia yake na kuacha kila kitu walichokuwa wakikimililki.

“Samahani kaka yangu unaonaje tukienda polisi hili waache kutufuatilia na pia tuwape namba ya gari hili nao wadili nao sababu ndipo kwenye usalama na mahali tulipo ukiingia barabara hiyo unatokea kituo cha polisi”. Hali haikuwa nzuri kwa Shufania alipaniki na jasho lilizidi kushika hatamu mwilini mwake hali iliyowai kumkuta akiwa nchini Syria na kutowai kufuatiliwa kama yeye binafsi, aliamini watu wale wanamfuata yeye na anachofanya huyu bwana Ramji ni kumpa moyo kama ilivyo wanaume wengi wafanyavyo sehemu yenye mashaka wakiwa na mwanamke, ukizingatia baba yake alikuwa mmoja wa watu waliowai kutishiwa sana na watu wa kundi la dola kiislamu kipindi alipokuwa yupo serikalini kutokana na ukaribu aliokuwa nao mke wa rais wa Syria.

“Ramsey ananiamini sana mimi na ndiyo maana akanituma nikufuate ananijua nina mbinu nyingi sana kukwepa watu kama hawa… Inawezekana kufanya hivyo unavyotaka tufanye kukimbilia kituo cha polisi, lakini je kama wao ni polisi itakuwaje?... Na pia tunaweza kufanya kitu kingine ambacho kitakuwa funzo kwao na kuwafanya wasitufuate tena… Ila ningependa huelewe kuwa hawa ni kati ya wale uliomtaarifu Ramsey kuwa walikuja kumuulizia pale hotelini kwenu, hivyo mia kwa mia ondoa hofu na mashaka kabisa, shida yao ni wewe uwasaidie kuwafikisha alipo Ramsey Bronze sababu Ramsey Bronze ni miongoni mwa wanasayansi wanaotafutwa na vikundi mbalimbali kutokana na uwezo wake wa kutengeneza silaha za kibaiolojia… Nafikiri ushawai kusikia habari za kupotea kwa wanasayansi wa Marekani hapa Malaysia?”. Aliongea Kai huku akikunja kona kuingia mtaa wa Jalan Berangan.

“Ndiyo nishawai kusikia maana ilikuwa ni habari iliyovuma sana mitandaoni kwa watu wanaopenda tumia mitandao hapa Malaysia… Je? Hawa ndiyo wanahusika na kuwateka hao wanasayansi maprofesa?”.

“Tunaweza tukawahisi sababu toka ulivyompa taarifa ile Ramsey umetufanya tuwe makini sana na ndiyo maana ya mimi kutumwa kukufuata hili ukaonane na Ramsey sehemu salama zaidi”.

“Eeeh! Kumbe nilikuwa namuingiza Ramsey wangu katika matatizo… Mungu yupo upande wake kwa kweli ninaogopa sana”.

“Sisi kwa ujumla tunashukuru sana kwa ulichomsaidia Ramsey kwa taarifa uliyompa na mengine mtaongea wenyewe mkikutana kwa sasa tuangalie jinsi gani tunawakwepa hawa watu”.

“Naomba mpigie simu umtaarifu tupo kwenye hali gani kwa sasa”. Shufania akasema huku akishangaa gari kupunguzwa mwendo huku ikiomba kuingia kwenye maegesho.

“Mbona unapunguza mwendo kaka?”. Mstuko ulionekana dhahiri machoni mwa Shufania hakuamini kama dereva angepunguza mwendo badala ya kuongeza mwendo hili kuwakimbia wafukuzi wake hakujua tayari Agent Kai alikuwa kashaamua la kufanya katika halmashauri ya kichwa chake.

“Nishaanza taratibu za kuwaacha… Naomba usihamaki ndiyo tupo kwenye procces nachokuomba relax na uangalie nafanya nini pia ufuate nachohitaji… Amini, amini hakuna atakayekugusa hata unywele wako na hata Ramsey wako hakuna watakachomfanya wala kumsogelea”. Akamjibu huku anaingiza gari kwenye maegesho ya Shopping Mall iliyo mkabala na night club ya Changkat Bukit Bintang Nightlife ambayo usiku wa jana tu Mr. Puter Logan na wenzake walifanya kikao chao hapa wakipanga mikakati mbalimbali.

“Shuka kwenye gari tutaingia kwenye duka hilo la bidhaa za Hitachi”. Akasema Agent Kai kumwambia Shufania baada ya kuingiza gari kwenye maegesho ya kulipia ya eneo hili. Wote wakashuka kwa pamoja na mtoza wa maegesho yale haraka akafika na kumpa Agent Kai kijikadi kidogo cha kufanya malipo ya kuegesha gari.

Jamaa walipitiliza wakiogopa kusimama na hilo Kai alishalifikiri kabla sababu jamaa walikuwa wanakuja kifundi wakiamini bado hawajastukiwa na wanaowafuata na pia waliacha gari tatu kati yao kulifikia Nissan Frontier na wakati Kai anapunguza mwendo kuingia kwenye maegesho ya duka la bidhaa za Hitachi, wao ndiyo wakastuka kuwa wanaowafuatilia wanaingia maegeshoni hivyo ikabidi wapitilize.


Kwa ustadi na ujuzi wao walikwenda wakasimama kwenye maegesho ya jengo moja refu sana kuliko majengo mengine yaliyo mtaa huu maarufu sana kwa maduka makubwa yanayouza vitu kwa gharama zaidi, lililo mita kama sabini kutoka walipoingia Kai na Shufania.

Agent Kai akamshika mkono Shufania na kuingia kwenye duka hili wakiongozana kama wapendanao waliofika kufanya shopping.

“Nimepotea step lakini usijali sana lazima tuwaache… Sikujua kama hawakuoana taa za ishara kuwa naingia hapa, kwa jinsi walivyopitiliza tulikuwa tunaingia kisha hatushuki tunapindua gari na kuondoka… Sasa hakuna cha kupoteza muda humu tutoke tuvuke barabara tutakapoona magari yamesimama kwenye mataa, wao watakachofanya watabaki kusubiri tutakaporudi kwenye gari hili tuondoke waendelee kutufuata hapo ndipo tutakapowaacha kwa wewe kuondoka na taxi na mimi nitabaki nazunguka humu madukani mpaka watakapokata tama ya kusubiri nalifuata gari na kuondoka”. Akaongea Ramji fake kwa sauti ya haraka sana huku mpango wake ukiwa tofauti kidogo na anachokisema wakati huo huo akijifanya anaandika meseji kwenye simu yake ya mkononi.

“Sawa Ramji… Nakuamini”. Akajibu Shufania huku macho yake yakiwa kwenye milango ya vioo ya kuingilia kwenye duka waliomo.

Wakatoka dukani wakijifanya hawajaona kitu wanachokihitaji na walipotoka tu mmoja wa wale wanyapiaji mwenye asili ya Malaysia Daus Bilik hatua kama kumi tu alionekana akijia huo upande na kwa ukweli alibabaika kidogo kwenye watu wanaojua kazi za kijasusi alionekana lakini si rahisi kwa watu wa kawaida wasio na uzoefu na kazi ya kijasusi hivyo Agent Kai macho yakiwa ndani ya miwani alimgundua akatabasamu kwa mbali sana huku akijitahidi kumziba Shufania asimuone akaharibu mambo kwa uwoga alionao.

Hawakusimama kwa dakika nyingi gari zikasimama na wao wakavuka kuelekea upande wenye night club, wakati wanavuka Agent Kai aliiona taxi moja ikiwa imesimama nayo ikiwa na dereva peke yake papo hapo akili ikafanya kazi kwa kasi kama ilivyo kawaida yake.

“Sikiliza Shufania! Usiogope chochote tumeshawaacha wale… Ramsey nimemtumia meseji kumpa hii taarifa, amenijibu nijitahidi tuwakwepe hawa watu…. Hii ni funguo ya chumba cha Ramsey aliniachia kwa madhumuni tukamsubirie hotelini wakati yeye anamalizia mambo yake ubalozini na ameniomba kwa usalama zaidi nimfuate mimi ubalozini hivyo unaiona ile taxi pale?”. Akaongea Agent Kai huku wakiwa ndiyo wanamalizia kuvuka kwa mwendo wa haraka.

“Ndiyo nimeiona”. Akajibu Shufania huku anaipokea funguo kadi aliyopewa kifichoni kama alivyopewa na Ramji fake.

“Ok! Ingia kwenye ile taxi nafikiri ukigonga kioo tu atafungua na ukiingia tu mataa yatakuwa yasharuhusu… Mi hawa hawaniwezi nawachenga chenga kidogo kisha namfuata wako nakuja nay, naamini haitachukua muda mrefu tutafika … Ukiingia kwenye chumba jifungie vizuri na usimfungulie mlango mtu yeyote awaye sisi tukifika tutagonga mlango mara tano kwa ugongaji unaofuatana uwe makini kuhesabu sababu hatutatumia kengele ya mlangoni”.

Shufania alikubaliana na wazo akapiga hatua ilipo taxi na bahati nzuri dereva alipomuona alitamani awe abiria akapewa ishara afungue mlango naye bila kusita akafungua mlango wa taxi na kuzama ndani ya gari.

“Sheraton Imperial Palace Hotel haraka”. Kama bahati na kama alivyohisi mtaalamu Agent Kai binti wa kiarabu alipokaa tu taa za barabarani ziliruhusu magari kuondoka.

Kitendo kile kilishuhudiwa na wanyapiaji na kuwaacha mdomo wazi, kazi waliyopewa na Mr. Nawaz Patrash ya kuhakikisha wanamfuatilia Shufania kila anapokwenda na endapo watamuona na Agent Kai basi haraka sana watoe taarifa kwake haraka ilionekana kuwashinda maana kama kuwakimbia basi aliwakimbia kwa stahili ambayo hawakufikiri kama itafanywa na watu waliokuwa wakiwafuata wakiamini hawajastukiwa haraka Bilik akapiga namba za simu za Nawaz.

“Aisee Nawaz! Binti katuponyoka”.

“Unasemaje wewe?”. Akahamaki Mr. Nawaz maana mpaka muda huo walikuwa hawajui wapi pa kumpata Agent Kai na hata kina Bilik walipompa taarifa kuwa Shufania muongo haumwi alipoingia hospital akamvizia dereva wa aliyempeleka aondoke kisha akatoka eneo la hospitali halafu akaonekana akiongea na simu kwa furaha sana na mtu fulani na alipomaliza akakodi taxi, yeye Nawaz akaunda jambo kichwani mwake na akaamua kina Bilik wasimuache hata tone.

Jamaa walijitahidi kwenda naye na hata kutuma picha za mtu aliyekutana na Shufania (Ramji) na wakazituma kwake Nawaz na alipoona si Agent Kai kama picha zilivyomuonyesha akawaambia wasiwaache waone wanaenda wapi.

“Tuliongozana nao bila wao kujua hadi Changkat Bukit Bintang wakasimama ghafla kwenye duka la Hitachi wakashuka na kuingia dukani kisha wakatoka ghafla na kuvuka barabara kama wanaelekea upande wa night club hapo ndipo tulipoona yule binti akipanda taxi kuondoka akimuacha yule mtu aliyemfuata Tamal Maxiwell”.

“Kwahiyo hamkuwa kwenye gari yenu wakati taxi inaondoka?”.

“Hatukuwa ndani ya gari wote… Meloo peke yake ndiyo alikuwa kwenye gari na mimi nilikuwa nawafuatilia wasije wakatupotea kama wakiingia kwenye maduka yaliyo hapa”.

“Huyo mwanaume bado yupo hapo?”

“Yupo anasubiri gari zisimame avuke kuja upande alioacha gari yake”.

“Sasa naomba mumfuatilie kisha mumteke mumpeleke jumba la nyoka yeye ndiyo tutamtumia kumpata huyo binti kisha tutampata Agent Kai kupitia hao wawili… Tafadhalini nawaomba muwe makini sana nisisikie mmekosea tena na mnakoseaje wakati nyinyi wajuzi wa vitu hivi?... Haya haraka msubirieni aingie kwenye gari yake mumfuate mpaka mtakapoona sehemu salama kwenu kumchukua mchukueni haraka… Mpaka saivi huko Alamanda kuko kimya na sehemu zingine vivyo hivyo kasoro kwenu tu ndiyo nahisi kuna jambo, ninaamini hawezi kuwasumbua huyo mtu kwa nilivyomuona kwenye picha haonekani kuwa mtu wa kuwasumbua”. Akaongea Mr. Nawaz akitoa amri.

Agent Kai alivuka barabara kisha akaingia kwenye gari yake akaitoa maegeshoni na kuingia barabarani sababu haraka aliuona upenyo wa kufanya hivyo.

Aliondoka na mwendo wa kawaida hili asiwatie wasiwasi wowote jamaa zake au kama anavyopendaga kuwaita watu kama hawa kuwa ‘wateja wa mbolea’

Kabla hajakinja kona kuingia barabara inayoelekea ubalozi wa Marekani mtaa wa Taman u Thant kwa chati alichungulia kwenye site mirror na kuwaona wateja wake wa mbolea wakiteremka mteremko unaoshusha kufuata yeye naye anapoelekea. Hapo Agent Kai akatabasamu.

“Eeeh! Kumbe wananifuata?” Akajiuliza kana kwamba anamuuliza mtu mwingine aliye kwenye gari wakati yupo mwenyewe tu.

“Nafikiri siku yao ishafika… Sidhani kama wanaweza kuwa wamejua mimi ni nani? Wanachotaka wao niwasaidie wampate Shufania baada ya kuwapoteza kwa vumbi kali pale Night club”. Bado akaendelea kuongea peke yake huku akiupita ubalozi wa Marekani kwa mwendo ule ule.

“Safari Hulu Langat kuna maeneo nimeyaona mazuri kule yana misitu naenda kuwafunza adabu kabla sijawapoteza duniani kwa stahili wasiyofikiri”.


Alipiga mwendo hadi barabara ya Jalan Engag mchana huu kukiwa na magari mengi yakiwa nayo yapo kwenye mwendo kasi sababu ilikuwa barabara ya kwenda mwendo wa kasi alikwenda hadi barabara ya Jalan Taman Putra akapunguza mwendo na kuingia kisha akatia gia Nissan Frontier ikaongeza spidi akapiga mwendo mpaka barabara ya kuelekea wilaya ya Hulu Langat iitwayo Jalan Hulu Langat akaikamata na muda wote huo hakuacha kuwacheki kwenye site mirror jamaa wanaomfuata wakiwa wameacha gari mbili tu nyuma yake nao wakijitahidi RAV 4 yao irandane mwendo na Nissan Frontier.

Hakuna kitu Agent Kai uwa anakichukia kama yeye kukimbizwa na watu kama muhalifu na ana ubinafsi wa kujiona yeye ndiyo mwenye haki ya kufukuza hivi na ingawa mara nyingi humtokea hali lakini hakuwa anaipenda hata kidogo.

Mbio zilikolea jamaa hawakutaka kumuachia kama walivyopewa oda na walishahisi sasa washaonekana na mlengwa na mlengwa anawahofia na kutokana na hofu ya Nissan Frontier kuwa ina kasi kuliko gari yao ilibidi Meloo akamue gari kweli kweli wakiamini kama nongwa na iwe nongwa lolote liwe lazima wampate mtu waliyeamini ni mtu wa kawaida na hana lolote.

Agent Kai alikwenda hadi walipokipita chuo cha The Unniversity of Nottigham (Malaysia Camp) akakipita chuo kile kisha akaingia kushoto barabara inayoingia kushoto akazipita hostel na sasa hapo RAV 4 ikawa peke yake inayomfuata barabara hii ya vumbi, hapo Agent Kai akaruhusu kichwa chake kifanye mambo yake kwa kasi, akatoa simu yake na kupiga namba za Shufania.

“Vipi umeshafika Sheraton Hotel?”.

“Ndiyo nimefika muda tu na nipo kwenye chumba ulichomwambia Ramji, huko wapi wewe?”.

“Nipo na Ramji, alichelewa kunifuata hapa ubalozini sababu alitumia muda mrefu kuwakwepa waliokuwa wanawafuata maana walikomaa kumfuata tena si kwa kificho, jamaa si watu wazuri kabisa… Naomba tupe nusu saa tutafute usafiri wa kuja huko maana hatutatumia tena gari ya Nissan Frontier na hatutaongozana tena kila mmoja atakuja hapo hotelini ulipo kivyake kwa usalama wetu si vizuri tukiongozana… Naomba uwe mvumilivu kidogo na usitoke mpaka tufike pia usitumie simu yako kumpigia mtu mwingine na ikiwezekana izime”.

“Sawa sawa Ramsey… Tafadhali kuwa makini sana … Maana Ramji aliniambia wana shida na wewe”. Somo lilimuingia Shufania.

“Relax! Muda si mrefu utaniona hapo chukua kinywaji unywe pia kuna keki humo kwenye friji naomba ule”. Akamwambia na kukata simu, Akachungulia kwenye site mirror vumbi lilikuwa likitimka wakipita barabara ambayo haikuwa na magari zaidi ya wapita kwa miguu wachache pamoja na baiskeli wanaotokea eneo liitwalo Taman Desa Pelang nao walipoziona gari zile zikiwa kwenye mwendo ule waliogopa na kupisha pembeni.

Wakaipita hotel iliyojengwa kiasili kwa apartment zake kuwa ya vijumba vilivyoachana hatua kadhaa hotel hii inaitwa Bamboo Village Kuala Lumpur ikiwa kama kwenye msitu sababu miti vitu vingi vya asili viliizunguka, hapo Agent Kai akaitizama saa yake na kukunja sura kwa uchungu taratibu akaanza kupunguza mwendo bila wale jamaa kujua kutokana na vumbi lilokuwa likitimka.


“Hapa hapa!”. Akaongea kisha akatoa lock za mlango wa gari upande wake.

Breki ya ghafla ya Nissan Frontier ilisababisha utokee mlio wa mseleleko wa matairi ya gari ya kisha ukatokea mshindo mkubwa wa gari kugonga nyuma ya gari ya gari. Hatari! Lakini salama kwa mafundi wakali wa hizi kazi.

Tayari Agent Kai alikuwa nje ya gari wakati mshindo ule ukitokea na RAV 4 ikipaa juu na kudondokea pembeni mita saba ikiwa matairi juu bodi ikiwa imeminyika kiasi cha kutisha kulikuwa na watu watatu wanaokuja na njia hii nao walipatwa na mshtuko mkubwa uliochanganyikana na mshangao kushuhudia ajali iliyosababishwa makusudi.

Kwa kasi Agent Kai alikimbilia ilipoangukia RAV 4 L ambayo moshi ulianza kutokea kuashiria muda wowote itawaka moto, akawachungulia wahanga wa ajali kwa kuinama chini (kwa kweli gari ilibinywa), waliokuwa ndani ya gari licha ya uzoefu wao wa mambo ya kishenzi hawakutegemea kabisa kutokea kwa tukio lile mawazo yao yalikuwa wanayemfukuza anawaogopa na pia anaogopa kukimbiza gari kwa mwendo ambao RAV 4 yao isingeweza kuwakaribia hivyo walichotaka na kupeana moyo ni kumfukuza na kumdhibiti kama walivyopewa maelekezo. Hakuna aliyekuwa mzima muda huo wote walivunjika viungo vyao na mwili kwa ujumla ikiwemo Meloo kupasuka kichwa maana maubongo yalionekana dhahiri.

Agent Kai akatabasamu alipowaona katika hali ile ‘ndicho mlichostahili hamna adabu nyie’ Akawaza kisha akauvuta mlango wa upande wa dereva kwa nguvu hadi ukang’oka hakuogopa damu zilizokuwa zikiruka na kutapakaa akakaingiza kichwa na kutizama vitu vilivyodondoka kwa pale chini juu na akakiona alichokuwa akikitaka, simu aina ya Techno W6 ikiwa imeumia kioo kidogo akainyakua na kutoka mbio kuelekea ilipo gari yake baada ya watu wasiotaka kupitwa na jambo wakisogea kwa kasi eneo lile kama ilivyo kawaida kwa binadamu ingawa wakati wanakuja barabara hii kulikuwa hamna watu zaidi ya wanaume watatu tu waliopishana nao mita chache.

Aliporudi alitizama nyuma ya gari yake Nissan Fontier mbonyeo wake wa sehemu yote ya nyuma na kufanya vioo vya nyuma yaani cha nyuma na ubavuni kuvunjika huku hakuna taa iliyosalimika, hakutaka kuremba kuangalia vizuri akaingia ndani ya gari kisha akalizungusha kasi iliyotibua vumbi kubwa sana na kuliondoa kwa kasi ambayo si kama ile aliyokuja nayo hii ilizidi, bila kujali watu waliopo pale wanaongea ongea nini. Akawaacha waendelee kujadili yasiyowahusu.

“Hii gari polisi watazingua nisipokuwa makini ngoja nikaiache maeneo ya chuo nitajua nitakavyoondoka mbele”


Mwisho wa sehemu ya kumi na nane (18)


Shufania bint Mahamud anakutana na Faheem Ramji wa bandia ambaye sisi tunaofuatilia riwaya tunamjua ni Agent Kai.


Wakati akienda alipoelekezwa hakujua kama kuna mkia unamfuata.

Agent Kai anaugundua huo anaouhita kuwa ni mkia unatambaa na mwendo wa binti wa kisyria hivyo haraka anaamua kuchukua hatua ya kitahadhari na kufanikisha mpango wa kumuondoa kijanja Shufania.


Anawapeleka wilaya ya Hulu Langat na kufanya kile alichoona ni sahihi kuwafanyia kama tulivyoshuhudia.


Nini kitaendelea katika sehemu inayofuata?

Niazime muda wako msomaji hili twende sawa katika sehemu inayofuata..



Kwa kasi Agent Kai alikimbilia ilipoangukia RAV 4 L ambayo moshi ulianza kutokea kuashiria muda wowote itawaka moto, akawachungulia wahanga wa ajali kwa kuinama chini (kwa kweli gari ilibinywa), waliokuwa ndani ya gari licha ya uzoefu wao wa mambo ya kishenzi hawakutegemea kabisa kutokea kwa tukio lile mawazo yao yalikuwa wanayemfukuza anawaogopa na pia anaogopa kukimbiza gari kwa mwendo ambao RAV 4 yao isingeweza kuwakaribia hivyo walichotaka na kupeana moyo ni kumfukuza na kumdhibiti kama walivyopewa maelekezo. Hakuna aliyekuwa mzima muda huo wote walivunjika viungo vyao na mwili kwa ujumla ikiwemo Meloo kupasuka kichwa maana maubongo yalionekana dhahiri.

Agent Kai akatabasamu alipowaona katika hali ile ‘ndicho mlichostahili hamna adabu nyie’ Akawaza kisha akauvuta mlango wa upande wa dereva kwa nguvu hadi ukang’oka hakuogopa damu zilizokuwa zikiruka na kutapakaa akakaingiza kichwa na kutizama vitu vilivyodondoka kwa pale chini juu na akakiona alichokuwa akikitaka, simu aina ya Techno W6 ikiwa imeumia kioo kidogo akainyakua na kutoka mbio kuelekea ilipo gari yake baada ya watu wasiotaka kupitwa na jambo wakisogea kwa kasi eneo lile kama ilivyo kawaida kwa binadamu ingawa wakati wanakuja barabara hii kulikuwa hamna watu zaidi ya wanaume watatu tu waliopishana nao mita chache.

Aliporudi alitizama nyuma ya gari yake Nissan Fontier mbonyeo wake wa sehemu yote ya nyuma na kufanya vioo vya nyuma yaani cha nyuma na ubavuni kuvunjika huku hakuna taa iliyosalimika, hakutaka kuremba kuangalia vizuri akaingia ndani ya gari kisha akalizungusha kasi iliyotibua vumbi kubwa sana na kuliondoa kwa kasi ambayo si kama ile aliyokuja nayo hii ilizidi, bila kujali watu waliopo pale wanaongea ongea nini. Akawaacha waendelee kujadili yasiyowahusu.

“Hii gari polisi watazingua nisipokuwa makini ngoja nikaiache maeneo ya chuo nitajua nitakavyoondoka mbele”


ENDELEA…….!!


HATUA MOJA MBELE IV

Watu walioagizwa wafike Alamanda Hotel baada ya Mr. Rafael mwanaume mwenye umri ambao kwa kukadiria ulikuwa umri wa miaka 44, meneja wa usafi wa mazingira ya nje ya hotel kuweka mambo sawa. Walifika eneo la hotelini na kwa kufuata maelekezo ya Mr. Rafael walikwenda kupaki mahali walipoelekezwa gari yao aina ya Toyota Hiace Van.

“Eeeh! Lete habari Mr Rafael Khamdushin, maana hapa sasa wewe ndiyo unatakiwa ucheze kama Messi”. Akaongea Mr. Ghulam Qaresh aliyeongoza msafara wa watu wa kazi wa Mr. Logan Puter baada ya bwana Rafael Khamdushin meneja wa mazingira ya hotel ya Alamanda kuingia kwenye gari ilipopaki tu na kisha kufunga mlango.

“Mipango yote nimeshaiseti iko vile kama alivyonielekeza Mr. Nawaz Patrash na hata Mr. Logan alinipigia kuna mambo naye kanielekeza na nimeyafanyia kazi kwa haraka”.

“Oooh! Vizuri sana… Vyumba vitapatikana kama ilivyo au tayari vina watu?”.

“Vyumba tumepata kimoja cha jirani naye na kingine cha nne kutoka alipo… Amechukua VIP apartment nafikiri itakuwa hamna shida, nimeshamuelekeza dada wa mapokezi kuhusu hilo mkifika mtasema nyie ndiyo wageni mlionipigia mimi simu muwekewe apartments za VIP flour ya ishirini apartment namba 104 na 99”.

“Ok! Hatua nzuri sana… Kuhusu picha za video za camera za ulinzi za hapa nimeshaongea na Ayzeen muhusika wa chumba cha camera security room kuna pesa amehitaji nishamwambia bwana Nawaz kuhusu hilo kaniambia mtakuja nazo, hivyo mmoja kati yenu nitaongozana naye hadi camera security room kwenda kumpa pesa halafu atatutolea kila tunachohitaji”.

“Mpango mzuri Rafael… Nafikiri iwe kama alivyosema Nawaz mimi na Mosin Lee tutachukua hivyo vyumba, Hassan Saddiq utakuja tutakapopata funguo kadi hili utege vitega sauti na camera zetu ndogo katika chumba kile, usisahau na kutega unga wetu kwenye koki za bomba bafuni… Huko kwenye camera security room tutaenda wote Mr. Rafael nitakapomaliza taratibu za chumba”

“Sawa sawa mpango huko poa kwenye reli yake… Ila nina swali dogo naomba kuuliza”. Akaongea bwana Rafael na kuomba.

“Uliza bwana Rafa!”.Akatoa ruhusa bwana Ghulam Qaresh.

“Nimesikia unaongea kuhusu unga wenu kwenye koki za bomba, mtu akigusa koki inakuwaje?”.

“Kwani kuna mtu mwingine anaingia kwenye chumba kile?”. Akauliza naye baada ya kujibu.

“Mtu wa usafi uwa anaingia kubadili mashuka na mataulo kila asubuhi ikiwa mwenye chumba hayupo na kama akiwepo uwa wanamsubiri anapoamka wanamuomba wafanye usafi, sasa hofu yangu wakiishika hiyo koki ya bomba mliyosema”.

“Mmmh! Mtu uwa anaishiwa nguvu anapoushika huo unga na baada ya dakika tano anapoteza fahamu na ndiyo maana ya sisi kuchukua vyumba vilivyo karibu na muhusika maana akiingia camera zetu tutakazotega ndani zitakuwa zinatuonyesha kila anachofanya na atakaposhika tu koki ya bomba tutaona na baada ya dakika kumi tunaingia kumchukua”.

“Hapo kazi kweli kweli maana tunaweza muingiza mtu mwingine kwenye tatizo na kusababisha maswali… Je hakuna njia ingine?”.

“Ipo!… Njia ingine ni kumzuia mtu huyo wa usafi kuingia na kugusa mabomba yote yaliyopo bafuni na chooni”.

“Kivipi tutamzuia?”.

“Pesa itaongea, pesa haishindwi na kila mtu anataka pesa hata akiwa tajiri”.

“Naogopa sababu cheni itakuwa kubwa… Hamuoni hilo?”.

“Ni mwanamke au mwanaume?”.

“Nilisahau kuwaambia…. Kuna binti mmoja jana alikuwa karibu sana na huyo mtu na ndiyo yeye anamiliki vyumba vyote vya apartments vilivyopo flour ya ishirini, yeye ndiyo uangalia kama vyumba vinatakiwa usafi basi anampa funguo mtu wa usafi aingie kusafisha na ndipo ugumu ulipo”.

“Sasa kumbe kuna mtu alikuwa karibu yake jana kwanini ulinyamaza kuhusu hili?... Ok! Umekosea hakuna kurudi nyuma huyo binti ni muhimu sana kwetu, yupo saivi hapa hotelini?”

“Ndiyo yupo”.

“Anaitwa nani?”.

“Shufania Mahamud ni mwarabu anayetokea Syria kwa mujibu wa watu wanaomjua walikimbia vita huko ni binti mzuri haswa ambaye mwanaume yeyote rijali na mkware wa mabinti akimuona tu lazima avutiwe naye kwa urembo wake”.

“Alikuwa naye karibu kivipi?”.

“Kwa uchunguzi mdogo niliofanya alimtuma jana akamnunulie nguo na vitu vingine kama simu na laptop hizo habari alinipa dada wa upishi ambaye ana urafiki wa karibu na Shufania”.

“Mr. Rafael ulitaka habari hiyo ukampe nani?... Huoni kama ndiyo habari muhimu sana hiyo… Je anaingilika huyo binti?”.

“Si rahisi kama ninavyofikiria sababu hata kumsogelea kumuuliza chochote niliogopa ni binti ambaye mstaarabu asiye na tama kabisa nadhani kama kumuingia itumike njia ingine si pesa kwake”.

“Basi atakuwa chini ya uangalizi wetu utamuonyesha huyu Daus Bilik na Johome Meloo wakiwa hapa around basi watakuwa wanafuatilia nyendo zake pia kingine utusaidie kuipata namba yake hili tudukue mawasiliano yake… Mtu wa usafi ambaye yupo chini yake yuko vipi?”.

“Wote ni wanaume nafikiri tukidili nao wanaweza kutusikiliza sababu mmoja alikuwa chini yangu kwenye mazingira ya nje na sikuwai kwenda naye tofauti”.

“Basi hapo tutadili nao, wanaume wa Malaysia siku zote hawakatai pesa, cha kufanya wasiliana na huyo aliyekuwa chini yako tumpe dili dogo tu lakini atapata pesa anachotakiwa kutufanyia asiguse koki za bomba kwa siku mbili tatu pia amuombe na mwezie asifanye hivyo”.

“Sawa sawa nitashughulikia yote, nyie elekeeni kwenye kuchukua vyumba ukiwa tayari nistue nikupeleke chumba cha camera..!”.

“Sawa… Nafikiri na wengine wote mmenielewa maana tumeongea kwa uwazi na mmesikia kila kitu… Hassan, Daus na Meloo mtabaki humu kwenye gari sisi watatu tunaelekea kushughulikia kila tulichoongea hapa ikipatika funguo kadi au hata kivuli chake basi nitakupigia Hassan uje ushughulike na kilichopo”.

Wote walitingisha vichwa vyao kukubaliana na bwana Ghulam Qaresh.


*** ***** *****

Fundi Agent Kai akiwa kwenye mwendo wa kawaida aliingia eneo la geti la chuo cha The Unniversity Of Nottigham tawi la Malaysia ambako palikuwa na magari kama matatu yanayotaka kuingia eneo la chuo yamesimama zikitumika taratibu za kimahojiano kisha ndiyo yanaruhusiwa kuingia eneo la chuo, alitizama saa yake ya mkononi na kuona ni saa tisa na dakika kumi na tatu haraka akashuka kwenye gari akiwa na begi lake pamoja briefcase akatizama huku na huko kuangalia kama watu walioko eneo lile wako bize na mambo yao au wanamuangalia akaona hakuna anayemuangalia kutokana hakuna aliyeona hali ya gari ilivyo kwa nyuma.


Haraka akavuka upande wa pili wa barabara na kuanza kuondoka kwa hatua za kawaida kuelekea inakoelekea barabara aliyojia akiangalia magari yanayokuja upande alipo kama ataona taxi isiyo na abiria, alipoenda hatua kama ishirini akatoa simu yake na kubonyeza namba za balozi Kapteni Jones Lebrons.

“USA First!”. Simu ilipopokelewa upande wa pili akasikia neno lao la kawaida wakimaanisha Marekani kwanza.

“USA First… Habari za muda uliopita?”.

“Safi kijana wangu!... Lete habari”.

“Niko barabara ya Hulu Langat, nilikuwa na wateja wamenikimbiza hadi huku baada ya kukimbilia lakini kwao haikuwa salama wamepoteza maisha nilipowasababishia ajali takatifu… Gari yetu imeumia kwa nyuma hivyo nisingeweza kupita nayo maeneo yenye askari hivyo nimeitelekeza kwenye geti la chuo kikuu cha The Unniversity Of Nottigham ikiwa kwenye foleni kama dereva wake anataka kuingia chuo, nadhani dakika hii tayari watakuwa washajua gari imetelekezwa .. Naomba msaada wako wa usafiri mwingine”.

“Pole sana na hongera kwa muendelezo wa kazi, naamini kuna mafanikio katika yote hayo… Hakuna uwezekano wa kupata taxi huko au hata bajaji?”

“Yah! Nimeiona taxi hapa na nimeipungia imesimama, utaniambia wapi nitalikuta gari.. Baadaye”. Akaongea haraka huku akikimbia mbele alipoisimamisha kwa kuipungia mkono taxi na ikasimama.

Wote wakakata simu.

“Persekutuan,barabara ya Jalan Alor, Sultan Ismail Street haraka kuna mtu namuwai jitahidi kukimbia salama nitakulipa mara mbili”. Akamwambia dereva baada ya kukalia siti tu.

Dereva akatia gia na kuondoa kwa kasi.

Kama alivyoahidi Agent Kai aliyevaa wajihi wa kumfanya aitwe Faheem Ramji kuwa atagonga hodi ya kuugonga mlango mipigo mitano ya kufuatana, hapa alitimiza ahadi hakutumia kengele maalumu ya kubonyeza kitufe kilicho kama swichi ya kuwasha taa hili kumtaarifu mtu aliye ndani kuwa kuna mtu yuko mlangoni anahitaji umfungulie mlango, aligonga kwa kutumia pete yake pekee iliyo katika mkono wake wa kulia kidole cha kati ambayo ni miaka zaidi ya tisa ipo kidoleni, uwa nayo kama kumbukumbu ya kaka yake wa kikazi na upande mwingine ni kama mwalimu wake katika mambo ya kutegua mabomu aina zote.


Alifariki akiwa katika kichwa chake kakilaza katika paja la kulia la mguu wa Agent Kai wakati wakiwa katika mapambano ya kuwaokoa wanajeshi kumi wa UN waliotekwa na kikundi cha dola ya kiislamu (Islamic State) ilikuwa katika eneo la mpaka wa uturuki na Syria, alifyatukiwa na bomu alilokuwa akilitegua hili wao wapite njia ya chini kwa chini. Agent Kai alijaribu kutaka kuondoka naye jamaa yake huyo ambaye naye alikuwa ni komando katika kikosi maalumu cha makomando wa US Navy Seals, akifahamika kwa jina Major General Paul McNair ni miaka tisa sasa toka litokee tukio hilo lakini limebaki kumbukumbu katika maisha ya Kai na hii pete anayovaa aliivua kutoka kwenye kidole cha Major General McNair kisha akaivaa na toka siku hiyo akiivua basi uwa ni kuisafisha tu ina mchanganyiko almasi na silver na ni pana kiasi.

Shufania aliyekuwa na wasiwasi mwingi alifungua haraka sana mlango tena bila hata kuchungulia kwenye tundu la chungulia agongaye baada ya kumaliza kuhesabu ugongaji na alipotokea tu akaganda mlangoni akiwa na mstuko wenye uoga.

Hakutegemea kumuona mgongaji mlangoni akiwa peke yake, matarajio yake aliamini atakutana na sura za watu wawili yaani Agent Kai na bwana Faheem Ramji.

Lakini ni mtu mmoja tena ni yule aliyeachana naye barabara ya Jalan Alor mtaa wa Berangan.

“Assalaam aleykuum!”. Ikabidi Agent Kai amsalimu huku akijaribu kuunda tabasamu.

“Waleikuum salaam!... Vipi mbona huko peke yako?... Yuko wapi Ramsey?”. Shufania alishikwa na mshangao kutoiona sura ya Kai.

“Relax! Ramsey utamuona tu”. Kai akamjibu huku akionyesha kama naye anaangalia inapotokea korido.

“Umemuacha wapi?”. Shufania alitokeza kwenye korido na kutizama labda aliyekuwa anamsubiri kwa hamu sana pengine kajificha kiutani.

“Nikaribishe ndani kwanza halafu ndiyo nikueleze nimemuacha wapi Ramsey wako, hapa mlangoni si mahala pazuri kusimama, usiwe na wasiwasi”.

“Lazima niwe na wasiwasi, muda mrefu toka anipigie kuniambia mpo wote mnakuja halafu kufika hapa huko peke yako na uliniambia anatafutwa na waliokuwa wananifuatilia”. Akasema Shufania ilihali akipisha mlangoni Kai aingie huku kijasho chembamba kikimtiririka.

Walipita ndani kisha Kai akaufunga mlango na kutangulia mbele kuelekea kwenye sofa lililokuwa linaangalia mlango wa kuelekea chumba cha kulala akaweka begi lake juu ya meza na kujibwaga sofani.

“Mwenyeji mbona umesimama?”. Akaongea baada ya kuinua macho kumtizama.

Shufania ilikuwa kama kapigwa shoti ya umeme maana alistuka sauti iliyotoka kwa mtu aliye mbele yake ilibadilika kabisa na kuwa sauti ambayo ameimisi sauti ambayo hata usiku wakati analala ilikuwa ikimjia na akawa ameishika vya kutosha, sauti ambayo ana upendo nayo wa tofauti aisikiapo.

“Samahani!... Mbona umeongea kama Ramsey?”.

“Yes! Hujakosea ni sauti yake… Karibu uketi Shufania”. Akaongea tena kwa sauti yake ya asili, sauti ya Agent Kai halisi baada ya muda wote aliokuwa na Shufania toka Tamal Maxiwell Garden hadi mtaa wa berangan alikuwa akiongea sauti isiyo yake, sauti nyembamba isiyo na uzito lakini ya kiume.

Sauti ilimstua sana Shufania na akamkazia macho mtu aliye mbele yake akimtizama juu mpaka chini kisha akakaa kwenye sofa linaloangaliana na alilokaa Agent Kai, moyo wake ulizidisha mapigo ya kudunda.

“Umeiga sauti ya Ramsey? Unamaanisha nini?”. Akampachika swali.

“Sijaiga ni sauti yangu Shufania… Ilinibidi nikufuate nikiwa kwenye sura isiyo yangu kuwakwepa walio na nia mbaya juu yangu… Mimi si Faheem Ramji kama nilivyojitambulisha kwako”.

“Mbona sikuelewi… Wewe si Ramji, wewe ni nani?”.

“Mimi ndiye yule Ramsey unayemjua ukinitizama mwili wangu upana na urefu unapata jibu lakini kwenye sura niko tofauti… Nimevaa sura ya bandia”.

“Sura ya bandia… Kivipi? kaka yangu!”.

“Nitaivua hili uamini na kukufafanulia kwanini imekuwa hivi ila baadaye itatakiwa kuvaliwa wakati tunatoka hapa”.

Shufania alizidi kushangaa akiwa aamini anayoyasikia kwa kuhisi ni ulagahai unaotoka kwenye kinywa cha mtu aliye mbele yake.

Agent Kai akaamua kujidhihiri mbele ya macho ya Shufania, aliinua briefcase lake akalifungua kisha akaibuka na kichupa kidogo cha plastiki chenye maji maji ndani akakifungua na kumimina kimiminika kilichomo mule katika kiganja chake cha kulia, mkono wa kushoto ukaenda shingoni inapoanzia kanzu (kwenye kola) akafungua kifungo cha juu cha kanzu aliyovaa akapaka mafuta kwenye maungio inapoanzia shingo taratibu lakini kwa mgandamizo wa kutosha ngozi ikawa inajiachia eneo lile papo hapo akaivuta ngozi laini ya plastiki ikajiachia akazunguka nayo akipeleka kwa nyuma ya shingo zinapoanzia nywele huko akaikuta zipu nyembamba sana iliyofichwa kwa nywele za kisinga zilizo undwa na sura ile ya bandia, akaivuta zipu kupanda juu kupitia kisogoni mpaka utosini karibu na mwisho wa nywele. Paap! Kinyago sura ya plastiki kikawa mkononi, Shufania mdomo wazi akiwa ahamini anachokiona.


Macho sasa yakawa yanaiangalia sura aliyoimisi kama hajaiona miaka kumi kumbe ni jana tu na hapa ikiwa imechanua tabasamu pana.

“Hivi naona au naota?”.

“Huoti! Huko sahihi, mimi ndiye yule ambaye niliandika jina hotelini kwenu Alamanda Hotel kuwa naitwa Ramsey… Ramsey Bronze”.

“Kwahiyo muda wote toka Tamal Maxiwell Garden hadi kule duka la Hitachi mtaa wa Jalan Berangan mpaka unaniambia niingie kwenye taxi ulikuwa unaniigilizia tu?... Niko na wewe?.. Kwanini imekuwa hivyo?”.Shufania akasema kwa haraka kama anakimbizwa.

“Ndiyo ni mimi na ninaomba unipe nafasi nifafanue hili tafadhali usipaniki na kupaza sauti cool down and relax!”. Akamuomba ashuke chini kisauti kutokana Shufania aliongea kwa sauti ya ukali.

“Sawa lakini nimekuogopa Ramsey”.

“Unaniogopa! ndiyo nafahamu hilo na ni ngumu sana kwa mtu yeyote kuona hivi asistuke… Kifupi hakuna mtu anayeitwa Faheem Ramji ambaye mimi namjua zaidi ya hii sura ya bandia ndiyo inabeba jina hilo la Faheem Ramji”.Akaanza kujieleza huku akimuonyesha sura bandia aliyoikusanya mkononi.

“Kwahiyo wewe ni mwanasayansi na si afisa wa ulinzi wa ubalozi wa marekani hapa Malaysia?... Na kwanini unatafutwa na wale waliokuwa wanatufukuza kwa gari na pia wale waliokuja kukuulizia Alamanda Hotel?”.

“Ni kweli wananitafuta kwa dhumuni la kunizuia kufanya kazi yangu lakini na mimi nawatafuta na wao kwa mengi tu… Hii sura ya Ramsey nayo nimeongeza vitu viwili ambazo ni wingi wa nyusi hapa machoni na nimebadili mnyoo naonyoa mara kwa mara… Jina la Ramsey Bronze si jina langu halisi ni jina la bandia nililolitumia kuingilia hapa Malaysia”.Akaongea lakini alikatizwa kimaongezi baada ya Shufania kuonyesha ishara ya mdomo anataka kuongea kitu naye akamruhusu.

“Eeeh! Na Ramsey si jina lako?”.Akauliza kinachomshangaza.

“Ndiyo si jina langu na kila unachokiona kwangu kina sababu mpaka marafiki naokuwa nao hawawi marafiki zangu bila sababu pale ninapokuwa nchi yoyote kikazi, Naitwa Kai Hamis Mkarambati ni Mmarekani mweusi mzaliwa wa Afrika nchi ya Tanzania iliyopo Afrika Mashariki ambako ndipo mama yangu alipo mpaka leo. Mimi ni jasusi wa shirika la kijasusi la CIA la Marekani, nikiwa ni Agent wa CIA katika ofisi ya makamu wa Rais wa Marekani. Nipo hapa Malaysia kwa operesheni maalumu ambayo nimekabidhiwa na nchi yangu ya Marekani ikiwa ni kutafuta wapi walipo wanasayansi wetu maprofesa wawili waliopotea nchini hapa wakiwa na familia zao pia kuna watu wetu wa intelejensia nao wakapotea katika hali ya utata walipofika kufuatilia mkasa huo…. Naomba nisamehe kwa yote ila usinilaumu kwa mimi kuwa hivi kutokuwa wazi kwako toka ulivyoniona kwa mara ya kwanza, kazi nayofanya haina itikadi ya kuwa mkweli kwa kila mtu unayekutana naye sababu ni kazi ya siri… Naomba usiogope kwa kuwa kwetu karibu, nimetokea kukuamini na ndiyo maana nimefunguka kwako”. Alitoa maelezo marefu Agent Kai akijitambulisha kwa Shufaniahuku akimkazia macho bila kupepesa anayempa maelezo.

“Umesema jina lako ni nani?”

“Naitwa Agent Kai Hamis Mkarambati… Nimefurahi naiona nuru machoni mwako nakuona Shufania yule wa ndoto zangu, nimefurahi ulivyokuwa ukimwambia Ramji kuwa umetokea kuvutiwa nami… Hata mimi navutiwa nawe lakini nakuomba nimalize kazi iliyonileta kisha niingie kumaliza kazi yako”.

“Naomba msamaha kwako sababu nimefunguka mengi bila kujua kwako… Na .. Naona aibu kwa kweli… Nahisi kama nimekutongoza Ram.. No ni Kai, hadi nakosea nimezoea jina la bandia la Ramsey Bronze”.

“Usijali kuhusu hilo.. Mi nimefurahi sana tena furaha toka ndani ya vilindi vya moyo wangu, ni nani asiyefurahi kupendwa na mrembo mwenye urembo wenye mvuto uliopitiliza kama wewe, kifupi una kila sababu ya kuwa Malkia wake Kai”.

Kicheko kidogo cha furaha kilichojichanganya na aibu ya kuinamisha sura kilimtoka Shufania na kumfanya Agent Kai afarijike sana.

“Ahsante! Kama nitapata nafasi ya kuwa malkia wake Kai… Vipi wale watu uliwaachaje kule baada ya mimi kuondoka kwa stahili ya kijasusi, maana mmmh siku moja tu umeanza kunifunza ujasusi najiona nami jasusi wa kike… Ukafanya njia nzima mpaka nafika nilikuwa nawaza huyu Ramji mbona katengeneza mazingira mepesi sana ya mimi kuwakwepa wale watu, kumbe siyo hata Ramji ni Kai Hamis.. Wewe inaonekana ni mtu wa hatari sana”. Taratibu Shufania alianza uchangamfu akawa haachi kuwa na tabasamu usoni.

“Nilikimbia nao mpaka Hulu Langat district eneo la broga hill nilipopita chuo cha The Unniversity of Nottigham nikaingia Desa Padang Road wakawa wanakuja kimbuzi kwa kasi ambayo sasa haikuwa inajificha nikafuata barabara inayoingia Bamboo Village Hotel nilipopapita Bamboo nikavutiwa na ukimya wa barabara ile ya vumbi na hapo ndipo nilipopata wazo niwasababishie ajali hili wasiendelee kunifuatilia nikuwai mrembo anagalau tuongee kidogo mambo yetu na kwa bahati mbaya nilipofunga breki kwa ghafla wao wakavamia kwa nyuma na ikawa ajali mbaya iliyowafanya si tu niwe nimewazuia bali na uhai wao uishie hapo kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata”.

“Mmm! Jasusi wewe ulitaka kuwazuia kweli au ulitaka kuwakatiza uhai wao kabisa? Maana nyinyi majasusi nasikia mnatoa roho za watu wanaowavurugia mambo yenu bila kuogopa haki ya wanadamu ys kuishi na anapokosa kuhukumiwa kwa adhabu”.

“Wamejiua wenyewe kwa kosa la mimi nisiye na kosa kwao kama wanafukuza jambazi fulani aliyewaibia mabilioni na wa kilanga hawaliliwi hivyo wasiisumbue akili yako elekeza furaha yako kuniona mimi niko hapa mzima sijachubuka hata ufidhi wa jino”.

Wote wakaangua kicheko cha furaha.


Furaha ikaanza kuupamba uso wa Shufania ukawa uso mng’avu wenye kuvutia machoni kwa Kai ambaye aliukataza moyo wake usitamani anachotamani. Ukweli kusema Mungu aliumba, huyu binti alikuwa na sura nzuri sana macho yanayong’aa yakiwa nanguvu yenye mvuto wa sumaku kama utabahatisha kuyakutanisha, mdomo mtamu wenye lips za saizi ya kati, mashavu yenye vishimo (Dimples) na meno meupe yenye mwanya pamoja na shingo ndefu vilimuongezea maksi mtoto wa dokta Mahamud. Alikuwa ngozi mororo yenye rangi nyeupe inayovutia ni mmoja wa mabinti ambao akipita sehemu hata kama yupo ndani ya juba chini mpaka juu kwa umbo lakelililojengeka kwa stahili ya umbo namba nane lilivyo hutakosa kugeuka kumuangalia pale mtakapopishana pointi za juu zilikolea kwake haswa.

“Agent Kai! si ndiyo sijakosea?”. Akauliza Shufania.

“Hujakosea… Agent ni jina la kikazi na kila mtu wa CIA ananiita hivyo hivyo huko sahihi”.

“Umeoa?”. Swali la kizushi likaulizwa tena na Shufania huku kainamisha uso wake kwenye miguu yake, Kai hakujibu aliinuka toka kwenye sofa akaenda kwenye friji akatoa jagi lenye juice ya embe kisha akarudi na kumimina kwenye glasi mbili zilizokuwa juu ya meza iliyowatenganisha.

“Karibu juice Shufania… !”. Akasema huku anamsogezea glasi.

“Ahsante… ninaomba unijibu swali langu jasusi”.

“Mi niko mwenyewe kwa sasa mimi si mume wa mtu”. Akaongea Agent Kai bada ya kupiga funda moja la juice.

“Imekuwaje mpaka uwe single? Au kazi yako ya ujasusi inakufanya uwe hivyo?”.

“Hapana, hapana kabisa…. Kazi yangu hainifanyi mimi niwe single”.

“Kwahiyo si mume wa mtu Lakini unaye mpenzi? Maana wamarekani hamuogopi hivyo I mean mahusiano kabla ya ndoa”.

“Wamarekani hawaogopi hivyo, Kai anaogopa hivyo sababu Kai ni muislamu na dini yake hairuhusu kufanya hivyo… Ni kwamba miaka kumi iliyopita nilioa ndoa yangu ya kwanza ya kiislamu nikimuoa mmarekani chotara aliyechanganya uafrika na ulatino wa kizungu lakini ndoa yetu ilidumu miaka minne tu na bahati tukaachana, mke yule alikuwa hataki kazi yangu nayofanya, kipindi icho nilikuwa nafanya kazi kitengo cha kikosi maalumu cha makomando wa US Navy Seals hivyo tulisigana sana mara kwamara kutokana kikosi chetu licha ya kuwa tunapumzika muda mrefu lakini inapotokea operesheni fulani inayotuhusu tulikuwa tukipotea tunapotea haswa ingawa mara nyingine ilikuwa tunamaliza operesheni hizo kwa haraka, mwanamke yule aliamua kwenda kuandikisha taraka bila mimi kujua na niliporudi toka Darful nikakuta suala liko mahakamani basi tukatalikiana na kugawana tulichochuma wote kama sheria isemavyo na kwakuwa yeye ni mwanasheria sikuweza kufurukuta alijipanga haswa, ndoa hii ilituletea binti yangu binti Kai anayeitwa Nuraiya Kai… Miaka miwili iliyofuata nikaoa binti wa kizungu ambaye yeye alikuwa ni jasusi wa CIA wakati huo ndoa yetu haikuwa masigano yoyote hasa ukizingatia tulikuwa katika fani moja tunajua magumu na machungu ya kazi na pia nilikuwa nishatoka US Navy Seals na kupelekwa CIA Ofisi ya makamu wa Raisi yeye akiwa CIA jimbo la Washngton. Tukapata mtoto mmoja wa kiume anaitwa Junior. Lakini mke wangu huyu bahati mbaya akiwa kikazi Bogota, Colombia akapatwa na umauti baada ya kupigwa risasi mtaani na watu wa kikundi cha kihalifu alichokuwa anakifuatilia…. Sasa ni miaka miwili niko mwenyewe”. Alitoa maelezo marefu Agent Kai kisha akanywa juice kidogo.

“Pole sana kwa yote yaliyokukuta… Mmmh! Kazi zenu mko hatarini sana… Watoto wako wapi?”.

“Watoto wote ninao nyumbani kwangu Wahington DC, nipo na dada yangu na wasaidizi wa kazi wanawaangalia kwa uangalifu mzuri tu watoto wangu”.

“Je? Unafikiri kazi uliyonayo ya ujasusi utaendelea nayo mpaka lini”.

“Bado sijawai kufikiria nitaifanya hii kazi mpaka lini ila naamini siko matatizoni sana kiduniani”.

“Natamani niulize mengi lakini si mazuri sana nafikiri nikupe muda ufikirie maana kiukweli si kazi nzuri sababu unakuwa hatarini na si wewe tu mpaka familia yako kwakuwa unagusa maslahi mengi ya watu na unakuwa adui baada ya kugusa maslahi ya watu au vikundi vya watu na hata serikali zilizo na upinzani na nchi yako ya Marekani”.

“Ni kweli uyasemayo na mara nyingi nafikiria kufanya hivyo lakini pale ninapopumzika kazi basi uwa nahisi natamani kufanya kitu kwa ajili ya nchi yangu iliyotumia mbinu nyingi kunitengeneza mimi mpaka nikawa hivi nilivyo na bado ninajiona nina deni kwa wamarekani…. Nafikiri tutalijadili vizuri hili jambo pale nitakapokuwa nimemaliza kazi iliyonileta hapa Malaysia”.

“Mmmh! Kama mliachana na mke wako wa kwanza kwa ajili ya kukuzuia kufanya hii kazi, acha niwe mpole tu”

“Usijali tutalijadili hili suala na ninaomba uniamini mimi ninavyoamini hili ndiyo dhumuni nililojia hapa duniani bila kujali lina hatari gani… Acha tuagize chakula tule maana langu alipo vyema ninaamni na wewe huko hivyo hivyo mpendwa wangu”.

“Ni kweli… Muda umeenda tunahitaji kula bila kujali tayari saa kumi na moja jioni”.

“Sijui nikuagizie chakula gani?”. Akamuuliza huku kashika kifaa cha risiva ya simu.

“Chakula ambacho wewe utapenda my dear”.

“Shauri lako mimi mwafrika tena mwenye asili ya Tanzania, nikiuliza chakula kimoja kinaitwa ugali na wakinijibu kipo nawaambia waniletee… Sasa sijui kama utaweza kula ugali”.

Waliangua kicheko kikubwa huku bado kiaibu fulani kikiwa bado kimetawala kwa mtoto wa kiarabu hivyo kicheko chake akawa anacheka huku anainamisha uso wake akitizama miguu yake.

Hapo Agent Kai aliinuka toka kwenye sofa na kwenda ilipo simu ya hotelini iliyoko kwenye chumba kile VIP(apartment) kisha akabonyeza namba zilizoonyesha ataongea na chef(mpishi) mkuu wa hotel.

“halloo!”.

“Halloo! Namba 105 VIP,tunahitaji huduma ya chakula… Viazi mviringo losti bakuli mbili, nyama ya kuku wawili wa kuchemshwa na juice ya matunda aina mbalimbali birauli mbili”.

“Dakika kumi na tano tu vitakuwa mlangoni”. Akajibu Chef.

Kai akakata simu na kurudi karibu na sofa alilokaa Shufania.

“Sasa mimi naenda kuoga hili wakileta chakula upokee wewe wasimuone Kai, wao waendelee kumjua Faheem Ramji wao, nikitoka tutaanza kazi tuliyoianza asubuhi wakati unanipigia simu”.

“Sawa Jasusi Agent Kai”. Akasema Shufania akijaribu kumzoea zaidi Kai.

Agent Kai akaelekea chumba cha kulala ambako huko kuna ndiko kuna huduma za maliwato.

Shufania akwasha luninga.MWISHO WA SEHEMU YA NANE (??

Tumeshuhudia mambo yanavyozidi kuwa mambo!

Baada ya kuwafuta SIX DANGEROUS BOYS katika ramani ya dunia ikiwa imebakiwa na mtu mmoja aitwaye Jeong, Agent Kai ameanza kuingia katika ramani ya Mr. Logan Puter kwa kuwaondoa watu wake wawili kati ya watu wake wa karibu anaowaamini na kuwalipa vizuri sana akiwasababishia ajali iliyowapa umauti wa kikatili.

Taratibu akili inaanza kuwakaa sawa wafuasi wa bwana Logan Puter ikiwemo yeye mwenyewe bwana mkubwa tajiri mwenye njaa ya pesa Master Plan.

MTAFUTANO unadhidi kushika kasi unadhidi kupasua anga huku Agent Kai akifanya mabo yanayoleta MSHANGAO kutokana na mguu wake kuwa hatua moja mbele kuwasogelea adui na hata kujua mengi ya ndani…!

Twende tukashuhudie nini kinafuata katika sehemu yetu bomba ijayo ya ishirini (20)


TUKUTANE SEHEMU YA ISHIRINI

BY K M M M


Riwaya: MSHANGA0

(Bewilderment)

Sehemu Ya Ishirini (20)

Mtunzi: Kaichi M Mussa

Wtssp: +255 652 202560

Location: Moro Town


ILIPOISHIA…..!!!

Hapo Agent Kai aliinuka toka kwenye sofa na kwenda ilipo simu ya hotelini iliyoko kwenye chumba kile VIP(apartment) kisha akabonyeza namba zilizoonyesha ataongea na chef(mpishi) mkuu wa hotel.

“halloo!”.

“Halloo! Namba 105 VIP,tunahitaji huduma ya chakula… Viazi mviringo losti bakuli mbili, nyama ya kuku wawili wa kuchemshwa na juice ya matunda aina mbalimbali birauli mbili”.

“Dakika kumi na tano tu vitakuwa mlangoni”. Akajibu Chef.

Kai akakata simu na kurudi karibu na sofa alilokaa Shufania.

“Sasa mimi naenda kuoga hili wakileta chakula upokee wewe wasimuone Kai, wao waendelee kumjua Faheem Ramji wao, nikitoka tutaanza kazi tuliyoianza asubuhi wakati unanipigia simu”.

“Sawa Jasusi Agent Kai”. Akasema Shufania akijaribu kumzoea zaidi Kai.

Agent Kai akaelekea chumba cha kulala ambako huko kuna ndiko kuna huduma za maliwato.

Shufania akwasha luninga.


ENDELEA NA UTAMU…!


HATUA MOJA MBELE I

“Hallow!”.

“Hallow Patrash.. Habari si nzuri tena upande wetu”.

“Imekuwaje tena boss?”.

“Nina picha hapa nimetumiwa na Kamishna Yuvraj Bhuto afisa mkuu wa polisi wa wilaya ya Hulu Langat … Picha ya ajali iliyosababishwa … Daus Bilik na Johome Meloo wamefariki katika ajali hiyo”.

“Oooh my God! Nimechoka kaka… Unasema wamekufa katika ajali iliyosababishwa?”.

“Ndiyo…. Kwani uliwatuma wapi?”.

“Wao ndiyo niliowapanga wawe wanamfuatilia binti wa kisyria muhudumu wa Alamanda hotel, ambaye tulikubaliana hata na wewe awe anafuatiliwa nyendo zake kila anapoenda hili tuone kama anakutana na Agent Kai na kama ikishindikana kumuona naye basi tumlazimishe atuitie mahali tutakapopataka sisi lakini wakati wanamfuatilia baada ya yule binti kuomba ruhusa kwa boss wake kuwa ana matatizo ya jino tukazipata hizo taarifa toka kwa Rafael ndipo nikawaambia kina Daus wamfuatilie… Binti yule alikwenda hadi hospital kuu ya rufaa kisha akamvizia dereva aliyempeleka ameondoka halafu naye akatoka na akapiga simu mahali na kina Daus wakanipigia kuwa binti ni muongo hakuna kung’oa jino wala kuziba jino hapo nikawaambia wasimuachie hata nukta katika kumfuatilia, binti akakodi taxi ikampeleka Tamal Maxiwell Garden huko ndipo akakutana na mwanaume mmoja ambaye picha zake zilitumwa kwangu ni kama mwarabu hivi hivyo sikumchunguza sana pale Tamal Maxiwell hawakukaa hata kidogo wakatoka na kuingia kwenye gari na kuondoka kina Daus nao wakawaungia msafara ukaenda hadi Changkat Bukit Bintang hapo wakasimama na wakaingia duka la Hitachi napo waliingia na kutoka tu wakavuka barabara halafu yule binti akaingia kwenye taxi na kuondoka akimuacha jamaa.. Kina Daus waliponipa taarifa hiyo nikawaambia wasimuachie huyo mwanume wamfuatilie, lakini kwa unavyosema yamewatokea hayo najilaumu sana mimi”.

“Uzembe mkubwa umefanya Nawaz… Kamishina Bhuto amenipigia hadi picha ya gari iliyofanya tukio maana jamaa alilitelekeza kwenye geti la kuingilia chuo kikuu cha Unniversity of Nottigham, gari ni lile ambalo tulipewa taarifa zake toka asubuhi kuwa ni gari ambalo aliletewa mtu wetu Alamanda Hotel, aina ya Nissan Frontier rangi nyeusi… Hivi kwanini ukujiongeza juu ya hilo?”.

“Sikuwauliza aina ya gari baada ya wao kunipa taarifa mtu aliyekutana naye ni mtu mweupe na si mtu mweusi…. Nafikiri hapa ametughilibu ghilba nzito sana”.

“Iko wapi akili yako Nawaz?... Hivi hujui watu wa michezo hii tunavyojibadili tutakavyo… Unafikiri tunacheza na mtoto? Picha ulitumiwa ya huyo mtu je hukuona haja ya kuchunguza urefu na hata upana wa mtu huyo kimuonekano na picha nilizowapa jana usiku?”

“Inasikitisha sana tumemkosa alikuwa ni yeye na kama tungeenda kwa ushirikiano basi tungemnasa tena asingefikia kuwaua ndugu zetu”.

“Basi tumeshateleza Nawaz… Mlinzi aliturahishia kazi kabisa kwa kumtajia Rafael aina ya gari na hata rangi ya gari licha ya kuwa hakufanikiwa kujua namba za gari… Jamaa yupo hatua moja mbele lakini nafikiri nitoe muda hadi usiku pengine kutakuwa kuna jipya… Nimempigia simu Sergio, huyu ni mtu wangu anafanya kazi ubalozi wa Marekani anichunguzie mtu huyu amelala wapi jana usiku baada ya kutokurudi Alamanda lakini sikupata jibu kwakuwa ameniambia hajui chochote kuhusu huyo mtu ila ameniambia hadi saa moja usiku atakuwa ana jibu kuhusu mtu huyu… Sergio ndipo lilipo tumaini letu la mwisho kujua habari za huyu mtu sababu huyo binti kiufundi msitarajie tena kumpata jamaa si mtu wa kipolepole anajua kila kitu na ndiyo maana nadiriki kusema yupo hatua moja mbele…. Nimesema tumaini letu la mwisho kwakuwa akili yangu imeamua kuwa nitatumia uwezo wa pesa na marafiki nilionao serikalini upande wa usalama kumpata mtu huyu ifikapo kesho ikiwa usiku tutamkosa na hiyo ni plan B”.

“Yes! Tumeteleza jamaa yupo hatua moja mbele… Sikukaa kibwege Boss, nilipopata picha za mtu yule nilimtumia mtaalamu wangu mmoja wa usalama wa taifa ambaye anawajua wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani karibu kwakuwa anaenda sana pale lakini akanijibu hamjui… Shida ni yangu kuchelea kuuliza gari aliyokuwa anaitumia mlengwa… Inatubidi tuwe makini jamaa kaanza kuingia kwenye safu yetu kuu… Na simu aliyokuwa akiitumia Daus ni simu isiyo ya finger print kama ameichukua nafikiri itakuwa hatari kwetu sababu ina namba zetu… Naona tusubiri saa moja ukishapata maelekezo toka kwa huyo Sergio itatuletea mwangaza”.

“Nina wasiwasi halafu sijui unatokea wapi bwana Nawaz na hii ni mara ya kwanza mi kutokewa na hali hii, muda mfupi kaifuta SDB na muda mfupi katutia misiba kadhaa wa kadhaa… Hii kidogo lazima itutishe na kutufanya tujizatiti na wote tuondoe dharau huku tukifanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu”.

“Ok! Nawaz tuonane kule jumba la nyoka ifikapo saa mbili usiku… Hapa kwenye simu yangu ingine Inspekta wa polisi wa kituo kikuu cha Persekutuan ananipigia ngoja niongee naye pengine ana habari anataka kunipa juu ya mlengwa wetu”.

“Ok! Baadaye tutaonana”.

Mazungumzo yao waliyakatizia hapo kisha Mr. Logan Puter akapokea simu ya Inspekta wa polisi.

“Halloow! Inspekta Kamal”.

“Hallow Mr. Logan… Daus Bilik na Johome Meloo ni waajiriwa wako katika kampuni yako unaweza nieleza kwa kifupi historia zao? sababu waziri wa ulinzi ameniuliza kama tumeshafuatilia juu ya uhalali wao kuishi nchini hapa nikampa majibu lakini akaniambia inasemekana walikuwa wakimfukuza kwa nyuma aliyekuwa akiendesha gari ya Nissan Frontier hatuoni kuna ukakasi kwenye jambo hilo… Ndipo ametaka ajue mengi maana toka vifo vilivyotokea usiku na nyumba kuchomwa moto tena ikiwa ya mfanyakazi wako imekuwa ni jambo linalowatia wasiwasi wakuu wetu”.

“Ni kweli lazima tuwe na wasiwasi hata sisi wakuu wa kampuni yangu kwanini mambo haya yanatokea kwetu tena kwa kuongozana hivi… Namtuma meneja muajiri wangu afike hapo Persekutuan Police Post akiwa na faili zao hao watu waliotutoka”.

“Sawa sawa aje moja kwa moja kwangu na awai kufika … Hamna kisasi bwana Logan na watu fulani fulani?”.

“Hakuna inspekta.. Mi sina adui wangu wala adui wa kampuni yangu nafikiri upepo mbaya umeikumba kampuni yangu… Acha niitishe kikao na wafanyakazi wangu nipate kuulizana nao vizuri”.

“Kachero wa polisi bwana Hamdani Ismail alifika eneo la tukio na akafanya mahojiano na mashuhuda wa tukio… Mashuhuda wanasema jamaa alitumia kasi tena ya kiufundi kufanya aliyoyafanya ikiwemo kuruka toka kwenye gari yake wakati ajali inatokea alikuwa tayari yupo nje kisha akaenda kwenye gari ya marehemu aliowasababishia ajali mahala ilipodondokea akachukua baadhi ya vitu kwa marehemu wale… Huyu mtu ana jambo gani na watu wa kampuni yako? Sababu kiakili ndiye atakuwa amefanya mauaji ya jana usiku kwenye nyumba ya mfanyakazi wako na kisha kuichoma moto”.

“Inspekta naomba nipe muda ifikapo saa tatu nitakupigia nikiwa na majibu… Kichwa kinaniuma sana kuwaza watu wangu matatizo gani yanawatokea”.

“Sawa… Nitampa taarifa waziri baada ya afisa muajiri wako kufika hapa na nikaongea naye… Nikutakie jioni njema Bwana Logan, Inspekta akaaga na kukata simu.


** ** ***

Dakika ishirini zilimtosha Agent Kai kupata huduma zote za kibinadamu zinazopatikana maliwatoni kisha akatoka akiwa amevaa kimtoko suruali ya jeans nyeusi na fulana aina ya lacrosse rangi ya kijani pamba zilimkubali akapendeza sana.

Ile kutokeza sebuleni alipomuacha Shufania bint Mahamud alikutana na jambo ambalo lilimfanya apigwe na butwaa na ujasiri wa kikomando alionao. Alimkuta mrembo Shufania ametoa hijabu yake kichwani na kufanya nywele zake ndefu nzuri kumwagika hadi mgongoni huku uso wote ukionekana kwa hali ya dhahiri shahiri.


Agent Kai alikuwa hajawai kumuona hivi huyu binti, kuganda kwake huku katumbua macho kulimfanya mtoto mtamu kutabasamu tabasamu tamu la kupagawisha hapo ndipo kwa mara ya kwanza Agent Kai akawa ameona mrembo anavyobonyea mashavuni (dimples) .

“Eeeh! Hivi naota ama ni nini?... Mashaallah! Wewe ni mzuri sana sisemi umewapita wote lakini humo katika wazuri wa hali ya juu… Ninatamani nikuahidi mengi sana lakini si muda huu”. Agent Kai alijikuta amesogea hatua nne tu toka alipo Shufania na kisha kujikuta maneno hayo yanamtoka.

“Ahsante kwa sifa unayonipa… Allah aisimamie nia yako iwe thabiti ukamilishe kusudio kama ni haki yake kukamilika… Inshaallah!”. Akajibu Shufania huku viganja vyake akiwa kavikutanisha kimaombi.

“Amen!”. Akajibu kimapokeo Agent Kai kisha akatupa macho kwenye meza ya chakula na kuona kishaletwa.

“Twende mezani tukale jasusi!”. Akasema Shufania huku anainuka kwa pozi la uchokozi vurugu mpaka kidume akameza mate huku akijikuna kichogoni.

Walielekea mezani na kila mmoja kuanza kujiwekea chakula katika sahani yake kutoka kwenye mapoti.


“Kwenye televisheni imetangazwa habari ya tukio ulilonihadithia lakini wao wameeleza tofauti kidogo na vile ulivyonieleza”.

“Wao wamsemaje?”.

“Kamishina wa polisi anasema… Mtu mmoja mwanaume asiyejulikana akiwa anaendesha gari aina Nissan Frontier namba MLJ 37368 KL amewasababishia ajali ya makusudi watu wawili wanaume waliokuwa katika gari ya RAV 4 L namba MLT 22345 KL Baada ya kufunga breki ya ghafla wakati wakiwa wanafukuzana katika barabara ya vumbi kutoka mita kama tisini toka kwenye geti la Bamboo Village Hotel, anasema waliokuwa kwenye tukio hawakuchukua picha kwa simu zao ila wameelekeza mtu alivyokuwa kavaa na wajihi wake ulivyo hivyo polisi wapo katika kufuatilia mtu aliyefanya ni nani? Na kwanini walikuwa wakifukuzana kwa magari yao? Msako mkali umeanza kumjua kwanza mmiliki wa gari aina ya Nissan Frontier na hapo ndipo watakapoanzia uchunguzi wao, sababu muhusika alikwenda kuliacha gari geti la chuo cha nottigham… Sasa jasusi niambie ile gari ya nani?”.

Aliongea kwa kirefu Shufania akifuatilia maelezo aliyoyasikia kwenye luninga kisha akamuuliza Kai swali wakiwa tayari wapo kwenye meza ya chakula.

“Kuhusu hilo usihofu hawawezi kumpata mmiliki wa gari na wakamtangaza kuwa ni mtu fulani ndiyo mmiliki wa gari itaishia kuwa siri yao maana balozi atasafisha kila kitu… Ile gari ni ya ubalozi wetu”.

“Mmmh! Kumbe upo ki ruhusa… Basi sihofu tena, na wasiwasi wote umepotea kwa maji”.

“Una kitu kimoja ambacho mimi nimekigundua kwako ambacho wewe bado hujakijua”.

“Kitu gani?”.

“Nimegundua unafaa kuwa mtangazaji wa luninga… Kama hautajali yale tunayoombea yatokee Mungu akaamua na yeye yatimie Inshaallah! Nitakupeleka chuo cha habari na nitahakikisha unapata kazi moja ya kituo kikubwa cha televisheni miongoni mwa vituo vingi vikubwa vilivyopo Marekani”.

Waliangua kicheko na kugonga viganja vyao vya kushoto.

“Kwanini umejua hivyo?”.

“Sababu umetiririka na taarifa uliyoisikia kwenye luninga kama umeiandika sehemu unanisomea tena kwa mtiririko husika”.

“Hahahaha ahahhah! Niliweka umakini jamani si unajua inatuhusu ndiyo maana ikabidi niwe makini na habari wakati inasomwa…. Ila ofa yako naikubali sababu kweli ni ndoto zangu uandishi na utangazaji kwa pamoja na itakuwa vizuri nije kuwa naandika vitabu vinavyohusu mambo yako katika ujasusi”.

Furaha ilitawala kama vile wana miezi mingi toka wajuane kumbe ni juzi tu.

“Kama kweli ni ndoto basi fumbua macho amka maana inakwenda kutimia sasa”.

“Kweli?”

“Yes! Ahadi iko kwenye nyumba ya ahadi, tuombe uhai mrembo hili tutimize”.

“Sawa sawa.. Basi! Acha tule kwanza”.

Maongezi yao yalinoga sana wote walikuwa kwenye kilele cha furaha kubwa.

Msosi uliendelea kushughulikiwa huku wakiangaliana kwa kuibiana na mara nyingi macho yao yaligongana.

“Mbona kimya mpendwa”. Shufania akaongea baada ya kuwa ameanza kushiba.

“Uislamu umetukataza tusizungumze wakati wa kula”. Akajibu Agent Kai huku anatabasamu.

“Mmmh! Unajifanya unafuatilia makatazo… Uislamu pia umetukataza tusifanyiane ujasusi… Na wala msifanyiane ujasusi!”. Wote walicheka kwa sauti.

“Umenikamata… Hahahahah hahahahah! Ni sunna unapoona udhia njiani kuuondoa, mfano unapopita njiani ukaona kuna chupa zilizovunjika unatakiwa kuziondoa zisije zikamchoma mtu mwingine ambaye anaweza asiuone wakati anapita na kuna thawabu unajiongezea hapo… Mimi kazi nikuondoa miiba njiani pamoja na chupa kwakuwa nina uwezo wa kuondoa hili watu wengine wasije kukanyaga na kuumia”.

“Jana wakati unakula kule Alamanda ulikuwa unakula huku unaniongelesha halafu mimi nilikuwa sijakuzoea nikawa najibu kwa tabu lakini wewe hukuacha kuniongelesha licha ya dalili zile nilizokuonyesha kuwa sitaki tuongee… Leo hapa unataka tunyamaze”.

“Umeshinda wewe… Zamu yako na wewe kujibu maswali yangu”.

“Niulize tu… Ila usiniulize kama nimewai kuwa na mwanaume… Khakuuu mi naogopa kuulizwa juu ya hilo”.

Agent Kai kusikia hivyo alijikuta anacheka mpaka akainuka kitini mwake alipokaa.

“Wewe upo huko mi niko tofauti na ulipo… Mi nataka nikulete kambi yangu, kambi ya Agent Kai, kambi kiboko ya uchunguzi, upekuzi na ufukunyuzi yenye macho ya tai… Kambi Mungu akiwa upande wetu shetani, majini na vikaragosi hawana nafasi.. Upo tayari kuingia kambi hiyo?”.

“Kama nakuwa na mwalimu kila sehemu nipo tayari kuingia kambi ya Agent Kai jasusi”. Akajibu kwa kudeka Shufania.

“Vipi chakula, nimechagua kisahihi au?”.

“Yah! Nimelipenda chagua lako ila umefagia kuku wako na umepiga nuzu na robo niliyemuacha ama kweli wewe kiboko”.

“Usinitanie kwenye kula… Napiga ngumi watu wenye kilo za kutosha nikiwa sili kisawsawa nitakuwa nawapapasa tu”.

Maneno hayo yalisababisha wote walicheka sana na kugongesha viganja navyo vikatoa mlio wa furaha pwaaah!.

“Nimekushindwa tabia mpendwa”.

Walitosheka na chakula wakatoka kwenye meza ya chakula na kuelekea ilipo sebule na wakakaa sofa moja linalokaliwa na watu watatu kila mmoja akiwa kwenye kona ya sofa katikati wameacha.

“Hivi ndiyo vitendea kazi”. Akasema Agent Kai huku akifungua begi lake kisha akaitoa laptop akaiwasha, ilipowaka akaingia intaneti sababu hotel ilikuwa na intaneti ya bure.


Akafunga mtambo mdogo kama rimoti ya tv kisha akaseti seti anavyojua yeye na mara ikaanza kusikika milio ya matukio yanayoingia pale alipoacha kuseti.


Mwisho wa sehemu ya ishirini (20)


Hatua moja mbele!


Hali mbaya upande Mr. Logan Puteri kimawazo.

Hajui wapi vijana wake wanakosea katika mtafutano wa jiji walilolizoea kwa kila hali.


Agent Kai katika mapumziko ya jioni akiwa na mwanadada wa kiarabu toka Syria, tayari urafiki wao unataka kuleta dalili ya kuvuka mipaka.


Nini kitaendelea?


Acha muda uongee, tenga muda wako vizuri uweze kupita nayo riwaya yetu katika muendelezo wa sehemu inayofuata.


Agent Kai kusikia hivyo alijikuta anacheka mpaka akainuka kitini mwake alipokaa.

“Wewe upo huko mi niko tofauti na ulipo… Mi nataka nikulete kambi yangu, kambi ya Agent Kai, kambi kiboko ya uchunguzi, upekuzi na ufukunyuzi yenye macho ya tai… Kambi Mungu akiwa upande wetu shetani, majini na vikaragosi hawana nafasi.. Upo tayari kuingia kambi hiyo?”.

“Kama nakuwa na mwalimu kila sehemu nipo tayari kuingia kambi ya Agent Kai jasusi”. Akajibu kwa kudeka Shufania.

“Vipi chakula, nimechagua kisahihi au?”.

“Yah! Nimelipenda chagua lako ila umefagia kuku wako na umepiga nuzu na robo niliyemuacha ama kweli wewe kiboko”.

“Usinitanie kwenye kula… Napiga ngumi watu wenye kilo za kutosha nikiwa sili kisawsawa nitakuwa nawapapasa tu”.

Maneno hayo yalisababisha wote walicheka sana na kugongesha viganja navyo vikatoa mlio wa furaha pwaaah!.

“Nimekushindwa tabia mpendwa”.

Walitosheka na chakula wakatoka kwenye meza ya chakula na kuelekea ilipo sebule na wakakaa sofa moja linalokaliwa na watu watatu kila mmoja akiwa kwenye kona ya sofa katikati wameacha.

“Hivi ndiyo vitendea kazi”. Akasema Agent Kai huku akifungua begi lake kisha akaitoa laptop akaiwasha, ilipowaka akaingia intaneti sababu hotel ilikuwa na intaneti ya bure.


Akafunga mtambo mdogo kama rimoti ya tv kisha akaseti seti anavyojua yeye na mara ikaanza kusikika milio ya matukio yanayoingia pale alipoacha kuseti.


ENDELEA NA DODO..!


HATUA MOJA MBELE II

“Hapa wapi?”. Akamuuliza Shufania huku anamuoyesha ishara asogee ilipo laptop, Shufania akasogea karibu na kutupia macho kwenye kioo cha laptop.

“Vyumba vya hotel yetu ndiyo viko hivi… Umechukua lini hii video na huyu ni nani?”.

“Nimetega kamera katika chumba changu cha Alamanda Hotel… Huyu mtu amepewa funguo yangu nafikiri kutoka katika funguo za akiba za hoteli yenu”.

Video ya mtu akiwa kaingia katika chumba alichopanga Agent Kai ilikuwa ikionekana katika kioo cha laptop.

“Mmmh! Wamepataje funguo? Mbona funguo za akiba za hotel yetu flour iliyo na chumba ulichopanga namiliki mimi na Dada Siti nayepishana naye zamu”.

“Hii video ilijirekodi saa saba na robo mchana, wewe ulikuwa umeshaondoka.. huyo mwenzio anaingia saa ngapi?”.

“Anaingia saa kumi na kamili jioni..Ebu rudisha nyuma nione vizuri”.

Agent Kai akairudisha nyuma video ianze upya.

Video ilionyesha mwanaume wa makamo mwenye rangi inayoonyesha asili yake ni Japan mwenye kipara (uwaraza) akifungua mlango wa chumba cha sebule ya vyumba viwili vilivyo mtindo wa chumba cha kulala na sebule ambavyo Agent Kai amepanga Alamanda Hotel. Alikuwa ni Takasho Kamado mjapani mtaalamu wa mambo ya teknolojia wa Bwana Logan Puter akiwa kama msaidizi wa Hassan Saddiq katika kikundi chao kisichokuwa rasmi kwa maana ya jina na mambo ya kukifanya kifahamike kwa jamii kikundi cha siri.

Alifungua mlango akiwa na uhakika kuwa ndani hakuna mtu hivyo aliingia kama mtu anayeingia kwenye chumba chake hakuwa ananyata alipoingia tu alijifungia kwa ndani kisha akapiga hatua mbili hadi yanapoanza masofa ya sebuleni hapo akasimama kama dakika moja hivi akitizama huku na huko katika hali iliyomuonyesha anajiamini sana.


Alipoona ameridhika alichokuwa akikiangalia akapiga hatua na kuelekea ulipo mlango wa kuingilia chumbani napo akaufungua hapa kamera ilimnasa kwa mgongoni tu kutokea kwa juu lakini alipozama chumbani tu kioo cha laptop kilibadili camera 1 ikaingia camera 2 na akaonekana yupo chumbani sasa hapo alisimama mlangoni dakika kama mbili akitizama sehemu mbalimbali kisha akafanya maamuzi akaelekea mlango ulionganisha chumba cha bafu na chumba cha choo hapo akavuta mlango wa kioo na alipoingia tu camera 2 ikahamia camera 3.


Akapiga hatua kuelekea kwenye sinki la bomba la kunawia mikono mtu anapotoka chooni alipolifikia akavua begi lake dogo alilokuwa kalibeba mgongoni na kuliweka juu ya sinki hapo akafungua zipu ya begi na kisha akatoa gloves za viganja vya mkono taratibu bila haraka yoyote akazivaa viganjani kisha akaibuka na kikopo kidogo cha plastiki ambacho hakikuwa na maandishi yoyote alipofungua ndani ikaonekana poda iliyo na rangi ya silva inayofanana na koki la bomba lililokuwa lipo kwenye sinki lile.


Akachukua unga kidogo toka kwenye kikopo kile kwenye vidole kisha akapaka sehemu ya kufungulia bomba na unga ule kwakuwa ulifanana na rangi ya koki haukuonekana kabisa kwenye camera zile.


Alipohakikisha ameweka katika alioona ni umakini kwake akageuka na kikopo chake mkononi akasukuma mlango wa chooni napo camera 3 ikahama na kuingia camera 4 napo akapaka kwenye koki sehemu ya kufungulia kisha akatoka nacho kikopo chake akaingia bafuni pia akapaka poda ile kama alivyopaka sehemu zingine.


Alipomaliza yote hayo akatoka na camera hazikumuacha zikawa zinarekodi tu akarudi kilipo kibegi chake akarudisha kile kikopo kisha akaibuka na kimkebe akakifungua kisha akatoa vifaa toka ndani ya kimkebe akaingia navyo chooni akaangalia angalia kidogo kama anayetafuta kitu kisha akapata jibu akaenda dirisha la chooni lililo dogo tu na la kioo.


Hapa ndipo hasa palionekana Agent Kai ametega camera yake maana uso wake ulionekana kwa ukaribu zaidi lakini hakuiona hiyo camera ambayo ilipachikwa kiustadi sana kwenye pachipachi ya maungio ya dirisha na ilikuwa ndogo sana kama ukubwa wa punje ya hindi, Takasho akapachika sehemu ambayo naye alihisi haitaonekana kiurahisi huku kwa jinsi alivyoiweka kwa Agent Kai ilimjulisha ameweka iweze kuchukua kwa uzuri zaidi mtu anapofungua koki kwa ajili ya kupata huduma ya chooni, alipohakikisha imekaa salama kwa kuganda vizuri sababu camera hizi uwa zina visumaku vinavyonasa kwenye chuma/bati na hata simenti, alichukua kimtambo chake akaseti seti kisha akatoa simu yake ya mkononi akabonyeza namba na kuanza kuongea kwa lugha ya kiarabu na camera alizotega Agent Kai zilikuwa na uwezo wa kuchukua sauti na video.

“Umewasha kompyuta?”. Akauliza na kutulia hii ilitokana alikuwa akisikiliza jibu toka upande wa pili ambao haikuwa rahisi kwa video ile kuchukua sauti ya upande wa pili, akainua mdomo tena.

“Vizuri… Kwa hiyo mimi unaniona hapo?”

Kimya kikapita.

“Okay! Nishaweka poda … Fuatilia vizuri navyotega camera hizi pale nitakapowasha tu na ukaona haionyeshi utaniambia usikate simu”. Akasema na kuingiza simu yake mfuko wa suruali aliyovaa.

Alitoka mule bafuni akaelekea chooni napo akatega camera na akaiwasha na kuonyesha ilikubali vizuri huko alipopiga simu maana hakuongea na simu napo hakufanikiwa kuiona camera ya mtaalamu na ndipo hapo walipokuwa wameachwa hatua moja nyuma katika mambo yao bila wao kujua kuwa kama ni ligi basi Agent Kai anaongoza kwa pointi nne mbele wakati wakati mechi za ligi zimebaki nne.

Alirudi chumbani napo akatega camera dirishani wakati Agent Kai yeye alitega juu ya kabati la nguo, hapo akatoka na kurudi sebuleni ambako akaitega kwenye kona ya mlango wa kuingilia chumbani ikichukua kwa mtu atakayeingia tu wakati Agent Kai yake aliitega kwenye picha ya waziri mkuu wa Malaysia iliyopo sebuleni ambayo nayo ipo juu ya mlango wa kuingilia chumbani. Napo akaijaribu kisha akatoa simu yake akaishika mkononi na kusogea kama anataka kutoka pale sebuleni kwenda nje.

“Vipi hapo Istqal?”.

Kikapita kimya kidogo akisikiliza jibu toka upande wa pili.

“Ok! Kazi imeenda vizuri.. Nakuja!”. Akaongea na kuonekana anakata simu.

Video ikakata alipofungua mlango na kutoka sebuleni tu mlango ukaonekana ukifungwa.

“Duh! Sasa na ile poda ya rangi ya silva aliyopaka kwenye koki za bomba ya nini?”. Akauliza Shufania.

“Sumu ile… siwezi juwa kwa hapa nilipo kuwa ni sumu ya nini lakini ni sumu… Mara nyingi inaweza kuwa ni kwa ajili ya kuua au kumfanya mtu alewe hapo inategemea na aina yake pamoja na dhumuni la muwekaji… Uzuri tumeona hivyo haiwezi kuwa na madhara tena kwetu”. Akajibu Agent akiwa hajaonyesha kustushwa na jambo lile wakati Shufania kwake alikuwa na uoga na kila alichokiona.

“No… Dada Siti akimtuma mtu wa usafi aingie asafishe chumba si atazurika?”.

“Hahaha hahahah… Unafikiri wanavyofanya hivi wao ni mbumbumbu? Unafikiri kupata funguo za apartment kama ya hotel yenu ni rahisi?... La hashaah! Wanapofanya vitu kama hivi uwa wanaweka mnyororo wao uhakikisha hawafanyi kosa, huwezi pata mtu anayeweza tengeneza kadi funguo kama unavyoweza chonga funguo kiurahisi… Basi elewa wameshaweka weka sawa jambo hili na ambaye hujashirikishwa ni wewe tu sababu waliona jana ulikuwa karibu yangu, usiwe na wasiwasi juu ya Siti wala wafanya usafi wenu”. Akasema Agent Kai huku akitabasamu akiwa macho yake kayaelekeza kwenye laptop kuangalia vitu vingine alivyovinasa ambapo kulikuwa taarifa ikionyesha laptop yake iliyo mikononi mwa adui zake iliwashwa muda wa saa nane mchana eneo la merdeka square na ikazimwa saa tisa. Pia kulikuwa na barua pepe toka sehemu mbalimbali zikiwemo za marafiki zake akajibu baadhi alizoona zinatakiwa kuzijibu huku Shufania akiwa amekaa karibu yake tu akiwa na amani tele mara kwa mara akimuangalia Agent Kai kwa kuibiaibia huku moyo wake ukijadili vingi na halmashauri ya ubongo wake yakiwa ni mambo mazuri tu yasiyo na ubaya wowote.

Kimya kikapita kidogo akatoa simu aliyochukua kwa dereva aliyokuwa akiendesha RAV 4 L ambaye sasa ni marehemu Daus Bilik.

Alitoa wa USB akauchomeka kwenye simu ikiwa hajaiwasha simu yenyewe kisha waya ule wa USB akauchomeka kuunganisha na laptop yake hapo kuna program akaiwasha na ilipokubali alivyotaka ndipo akaiwasha simu na alipogeuka kumuangalia akamuona anafuatilia kwa umakini anachofanya huku anakunywa juice yake.

“Hahahah hahahah… Taratibu tu utakuwa jasusi wa mtandaoni muda si mrefu… Hapa nimeweka program inayopoteza mnara yaani ninapoiwasha hii simu basi hamna atakayejua inapatikana mnara upi hapa KL ikiwa inafuatiliwa na sisi tunaweza kuitumia tutakavyo na kuchukua tunavyovihitaji…. Kwana tunatakiwa kujua alikuwa akiongea na namba ipi iliyokuwa ikimpa maelekezo wakati wanatufuatilia mpaka pale umauti ulipomfika”.

“Ndiyo mnaenda shule kusomea hivi vitu”. Akaongea Shufania.

“Yah! Hapa nishaiona namba ambayo alikuwa anaongea nayo kwa muda mrefu… Na bahati ina jina kabisa kalisevu alikuwa akiongea na Mr. Patrash … Pia kuna muda aliongea na jina linaloitwa Mr. Qaresh.. Chukua karatasi hiyo andika namba hizi”. Akasema Agent Kai kisha akamtajia namba na majina ya wamiliki wa namba alizotaka Shufania aandike baada ya peni kuwa mkononi mwake.

“Huyu mtu meseji zake nazo anajitahidi kuzifuta kwa wakati, ukitizama na simu moja ambayo niliipata mikononi mwa watu wa kwanza niliowapoteza wale inaonyesha walikuwa wakiwasiliana sana na mtu anayejiita Language girl… Kihesabu za kijasusi inaonekana hawa wanafuta haraka meseji au hawatumiani meseji, ngoja niangalie kama nitaweza toa pattern za whatssap pengine kuna meseji itakayotusaidia”. Akaongea Agent Kai huku kwa kutumia program zilizo kwenye laptop yake akaanza jitihada za kutoa pattern za whatssap.

“Mmmh! Yangu macho wee endelea tu maana leo ni kama naambulia kitu huku siambulii kitu”. Akasema Shufania.

“Waoooh! Pattern imeshindwa kubamba kwa mtaalamu imefunguka”. Akashangilia Agent Kai kujaribu kuzidi kumchangamsha zaidi Shufania ambaye naye alizidi kuvutiwa na ukaribu wao.

“Hongera… Unaamini huko ndiyo kuna mengi zaidi?”.

“Yah! Ukiona mtu anaificha sana whatssap basi ujue kuna jambo, ngoja tuone”.

Akajibu na kufungua ukurasa wa whatssap wa simu wanayoishughulikia kujua mambo yanayoweza kuwasaidia angalau kidogo.

“Mmmh!... Shufania”.

“Beeeh!”.

“Ulisemaa…. Ulisema.. Hapa Malaysia mna miaka mingapi toka mmefika toka Syria ?”.

“Miaka mitatu hivi na miezi kama mitano kama sikosei”.

“Vipi umeshawai vutiwa na lugha ya watu wa hapa?”.

“Unamaanisha nini?”.Akauliza Shufania baada ya kujibu swali aliloulizwa.

“Namaanisha katika muda wa miaka mitatu na miezi kadhaa umewai kujifunza ki-melau bahasa?”.

“Okay! Najua kidogo si sana, kuongea nasumbuka zaidi ila kusoma kilichoandikwa nakujua maana naweza”.

“Huko kwenye kuongea usijali tutajua cha kufanya tukikutana na shida kama hizo sababu naamini unaweza ukajaribu jaribu … Kujua kwako kusoma kunaweza kutusaidia kujua baadhi ya meseji za humu zinasemaje hasa zitakazokuwa na majina ambayo tumeayaona yamepiga sana kwenye hii simu au yeye kupiga”.

“Okay! Lete nizione”.

Kai akampa simu akiwa amefungua namba ya whatssap iliyoonyesha imetuma picha kama tano zinazomuhusu yeye.

“Hii namba nafikiri jina limeseviwa kwa ki-melayu bahasa… Kwanza soma hapo na ulitafsiri jina hilo kabla haujasoma meseji tukaona wamechat juu ya nini”. Akaongea Agent Kai.

“Plan Master… Jina lililoseviwa namba hii limeandikwa hivyo”. Akajibu haraka Shufania baada ya kusoma tu kilichoandikwa.

“Ina maana huyu ndiyo ana plan kila kitu… Okay! Tuendelee, soma meseji za juu kabla ya picha zilizotumwa”.

“Meseji ya kwanza jamaa ametumiwa na huyo Plan Master na inaonekana ilitumwa wiki moja iliyopita inasema… Kikao nyumba ya nyoka…. Ya pili ilitumwa juzi inasema tena … Kikao Chakit Bukit Bintang Nightlife ukifika atakupokea Nazrim na kukuelekeza tunafanyia VIP namba ngapi…. Halafu chini ya meseji hii ndipo zinafuata picha zako, moja imewekewa namba moja kisha comment inayosema… Hii ndiyo sura yake halisi kabisa achana na zingine alizoongeza baadhi ya vitu”. Alimaliza hivyo Shufania na kumpa simu Agent Kai.

“Ahsante sana jasusi mtarajiwa”. Akasema Kai huku anapokea simu.

“Kwa muda sitaki tena kuwa hivyo huko mbele… Naogopa”. Akaongea Shufania huku anatabasamu.

“Wateja wa mbolea wataelewa tu kuwa wewe ni nani? Weee ngoja tu kuna mtu nilikuwa nifanye naye kazi aliwai kuishi hapa haraka wamemtia nguvuni wakifikiri wamenikomesha kumbe wamenisogezea kifaa kingine hatari zaidi ya yule waliyemchukua….. Hahahahahah… Nacheka sana”.

“Mtu wenyewe nani?”.

“Si wewe hapo”. Akamjibu huku anamuangalia machoni binti akavunga kwa aibu.

“Wee jasusi una matatizo sana… Ndiyo maana mkuu wa polisi aliongea kuwa wana mengi wanayohisi kwako”.

“Kasemaje tena?”.

“Wana wasiwasi wewe ni muhalifu uliyeamua kufanya uhalifu wa kikatili maana mashuhuda walimwambia ulichukua simu na vitu vingine kama viwili kwa marehemu… Navyoijua Malaysia kwa habari za mitandaoni saivi itakuwa zina trend (vuma) habari zako tu tena kwa kasi ya moto wa gesi”.

“ Na ndiyo maana nilikuwa makini kuangalia hakuna mtu anayechukua tukio kwa dizaini yoyote”.

“Haya bwana mkubwa”.

“Nina majina mawili natakiwa kuyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa zaidi… Ngoja nitume na haya niliyoyapata kwa balozi… Turudi kwako niambie nani alikuhoji asubuhi mpaka ukatia shaka juu ya uulizaji wake?”. Mtaalamu akarudi kikazi kwa Shufania.

“Kiongozi wa kitengo cha usafi wa mazingira ya nje ya hotel, anaitwa Mr. Rafael”.

“Si mtu mzuri, anatumika na watu waliowateka wanasayansi wetu na familia zao pamoja maafisa usalama wenzangu”.

“Mi sikujua kama nakosea hata kumjibu hata kile kiasi kidogo nilichomjibu kwa baadhi ya mambo niliyojua juu yako jana.. Naomba nisamehe kwa hilo… Nilishangaa alivyonifuata na kujifanya kuna ndugu zako wanakutafuta wakati wewe uliniambia ni mgeni Malaysia na hauna ndugu na ndiyo maana umenituma nikanunulie vitu, pia kiukweli sikumjibu vizuri sana sababu hatujazoeana hata kidogo zaidi ya salamu”.

“Kawaida hiyo wala usiogope ilivyo huwezi juwa habari za mtu anayefanya kazi kama yangu kama si yeye kutaka kujua hivyo isikusumbue akili kabisa… Tunatakiwa kwa hali yoyote leo tumpate huyu mtu, kiongozi wa usafi wa mazingira… Unafahamu anaishi wapi?”.

“Kama nilivyosema sijawai kumzoea huyu mzee… Labda nivae ujasusi nipeleleze wapi anaishi”.

“Hilo ndiyo lililopo itabidi tujue wapi anaishi anaweza kutusaidia kina nani wanamtumia na kwakuwa ni mfanyakazi mwenzio nafikiri tutafanikiwa kupajua”.

“Kwahiyo mimi leo sirudi kwetu?”.

“Si mahali salama mpaka tutakapomaliza kazi hii, pia kuanzia leo hutakiwi kutembea ukiwa bila nikabu”.

“Kwanini?! Kwanini si salama? Wazazi wangu itakuwaje?”. Shufania alistuka sana kusikia nyumbani kwao si salama tena. Agent Kai mara nyingi alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kung’amua yanayoweza kutokea mbele hasa upande wa hatari.

“Mpaka sasa niko hatua moja mbele ya hawa watu… Mpaka sasa hata kama sina uwezo wa kujua wayawazayo lakini kiuzoefu wangu najua tayari wameshapaniki na kutojua kwao watanipataje kuniua au kuniteka kama wengine yaliyowakuta… Mpaka sasa nimeshakwepa mitego yao midogo waliyoitega hivyo katika mbinu kuu wanayoitegemea ukiacha mbinu zingine ambazo sizijui kutokana sijui uwezo wao kwenye mchezo huu mtamu wa hatari, ni wewe… Wewe ndiyo daraja lao kuu la kunifikia mimi hivyo watakusaka kila kona na kila watakayekuona naye kwa yaliyotokea leo Tamal Maxiwell na kumalizikia Bamboo Village tena kibabe basi watajua huko na mimi …. Kwa akili ya kiufundi Shufania… Si kama nakutisha ni lazima tuchukue tahadhari mimi si mwanafunzi wa mchezo huu wa wateja wa mbolea na wazalishaji wa mbolea… Wahalifu wakichanganyikiwa uwa wanafanya lolote kujitetea iwe kwa jasho hata na damu”.

“Naogopa wazazi wangu na ndugu zangu itakuwaje jamani?”.

“Lazima tuchukue hatua za haraka kujua sasa hivi wako wapi?.... Pale kazini kwenu nani anapajua kwenu?”.

“Shost wangu tu… Ni Sheila peke yake ndiyo anapajua nyumbani kwetu”.

“Itabidi umpigie kumuuliza kama kuna mtu yeyote kamuulizia juu ya hili kwa sasa itabidi tutoke hapa twende tukapate gari ingine ya kuitumia pia kushughulika juu ya wazazi wako na mahali mtakapokaa kificho mpaka mambo haya yatakapokaa sawa”.

“Sawa ila tuombe wawe salama maana nilizima simu hili nisisumbuliwe na mtu yeyote nikiwa hapa na wewe naogopa hata kuiwasha kwa kweli”.

“Itabidi uiwashe tukishatoka hapa hili uongee na Sheila”.


Mwisho wa sehemu ya ishirini na moja (21)


Sehemu hii tumeshuhudia Agent Kai akiwa Shufania wakifuatilia mambo yaliyofanywa na wateja wake wa korosho kama anavyowaita.


Twende mbele tukadhidi kufunguka na kitakachojiri.




“Mpaka sasa niko hatua moja mbele ya hawa watu… Mpaka sasa hata kama sina uwezo wa kujua wayawazayo lakini kiuzoefu wangu najua tayari wameshapaniki na kutojua kwao watanipataje kuniua au kuniteka kama wengine yaliyowakuta… Mpaka sasa nimeshakwepa mitego yao midogo waliyoitega hivyo katika mbinu kuu wanayoitegemea ukiacha mbinu zingine ambazo sizijui kutokana sijui uwezo wao kwenye mchezo huu mtamu wa hatari, ni wewe… Wewe ndiyo daraja lao kuu la kunifikia mimi hivyo watakusaka kila kona na kila watakayekuona naye kwa yaliyotokea leo Tamal Maxiwell na kumalizikia Bamboo Village tena kibabe basi watajua huko na mimi …. Kwa akili ya kiufundi Shufania… Si kama nakutisha ni lazima tuchukue tahadhari mimi si mwanafunzi wa mchezo huu wa wateja wa mbolea na wazalishaji wa mbolea… Wahalifu wakichanganyikiwa uwa wanafanya lolote kujitetea iwe kwa jasho hata na damu”.

“Naogopa wazazi wangu na ndugu zangu itakuwaje jamani?”.

“Lazima tuchukue hatua za haraka kujua sasa hivi wako wapi?.... Pale kazini kwenu nani anapajua kwenu?”.

“Shost wangu tu… Ni Sheila peke yake ndiyo anapajua nyumbani kwetu”.

“Itabidi umpigie kumuuliza kama kuna mtu yeyote kamuulizia juu ya hili kwa sasa itabidi tutoke hapa twende tukapate gari ingine ya kuitumia pia kushughulika juu ya wazazi wako na mahali mtakapokaa kificho mpaka mambo haya yatakapokaa sawa”.

“Sawa ila tuombe wawe salama maana nilizima simu hili nisisumbuliwe na mtu yeyote nikiwa hapa na wewe naogopa hata kuiwasha kwa kweli”.

“Itabidi uiwashe tukishatoka hapa hili uongee na Sheila”.


ENDELEA NA SEHEMU YA 22


HATUA MOJA MBELE III

Agent Kai alivaa tena sura ya bandia imtambulishayo kama Faheem Ramji ‘fake’ kisha akavaa miwani yake kama kawaida, akatupia kitambaa vya shingoni (skafu). Shufania akamuongezea kwa kumfunga kilemba cha kiarabu kwa wanaume. Kisha naye akajifunga nikabu usoni akawa ninja. Kikabebwa kila kitu walichoona kinafaa kubebwa kwa wakati huo kikatiwa ndani ya begi ambalo uwa halibanduki kuwa mbali na Agent Kai. Wakatoka katika apartment yao moja kwa moja wakaingia kwenye lift na kuanza kushuka chini baada ya kumaliza taratibu za kubonyeza namba za kuwaruhusu kuteremka chini kabisa ya hotel (mapokezi).

Wakiwa ndani ya lifti Agent Kai akatoa simu yake toka mfukoni kisha akabonyeza namba za balozi Kapteni Jones Lebrons, simu ikaanza kuita.

“USA First!”. Kama kawaida yake Balozi kutumia maneno hayo kila aanzapo kuongea na Kai.

“USA First… Habari za toka muda mfupi uliopita Kapteni?”.

“Safi kijana wangu, lete habari?”.

“Vipi kwako kuna chochote kati ya vile nilivyokupa kufanyia kazi?”.

“Nafikiri si vizuri kwenye simu…. Ninayo kiasi ambacho kinaweza leta mwanga au kisilete mwanga nimejitahidi kufuatilia vile nilivyoweza hasa kutokana na tulivyoamua tusimuamini mtu basi ikabidi nifanye mwenyewe uchunguzi”.

“Nina imani leo tutaonana kama kawaida hata ikiwa alfajiri…. Sitatuma ripoti kwa chifu bila kwanza kuongea na wewe… Nipo kwenye lifti ya hotel nateremka na mgeni wangu niko naye hapa, naomba unielekeze wapi nitaikuta gari niliyoomba”.

“Nilishaiandaa! Lipo katika maegesho ya jengo liitwalo River Bank mtaa wa James Mosque, funguo ameachiwa mlinzi anayelinda ATM Card room za pale ya benki ya Western Union yule mlinzi ni mtu wangu nimemchomeka pale kufuatilia mambo fulani yanayohusu maslahi ya nchi yetu hivyo usiwe na shaka naye kabisa sababu hakujui na ukifika utajitambulisha kwa jina la Faheem Ramji”.

“Ahsante sana mzee! Kuna jambo nalifuatilia lakini katika kulifuatilia naamini itakuwa kama navyotarajia naomba katika muda unitafutie nyumba watayoweza kukaa watu nitakaokuelekeza muda huo, iwe nyumba nzuri kubwa sababu wako familia pia hata yule aliyopo ubalozininitapenda aende huko si hapo tena na hili pia nitapenda liwe la siri baina yetu na kama kuna mwingine basi awe mtu mwenye kuijali USA”.

“Okay! Nalifanyia kazi muda utakaonipigia nitakuwa tayari nishaweka sawa juu ya hilo”.

“Ahsante sana Kapteni”.

“Okay! Kazi njema kijana wangu… uwe makini tunakutegemea sana”.

“Okay! USA First!”.

“USA First!!”


Simu zikakatwa pande zote mbili na lifti ikawa imeshafika mwisho Agent Kai na mrembo Shufania wakatoka ndani ya lifti.


***** ***** *****


Kiti kilikuwa kama kaa la moto kwake muda mwingi alikuwa akifikiri, kwanini kitu kidogo kwake kinamuwazisha? Kwanini mzee wa mjini anawazishwa na kuwa na wasiwasi kwa mtu mmoja? Logan Puteri mjanja msomi asiyesumbuliwa na chochote kujiamini kwake kuko wapi?. Aliitizama saa yake iliyomfahamisha ni saa moja kasoro dakika tisa na haikuwa mara hiyo tu kutizama saa hii ilikuwa zaidi ya mara tano akiitizama saa kwa wakati tofauti tofauti.


Akili yake ilikuwa ikiutamani muda wa saa moja jioni ufike, alitamani muda uruke ifike muda huu. Alikuwa kasimama kwenye dirisha linalotizama eneo la nje la moja ya jumba lake zuri kabisa kati ya majumba yake manne ambazo anayoyamiliki akiwa ameweka kila kitu ambacho kinahitajiwa na mtu anayeishi kifahari lakini alikuwa hakai yeye kama yeye au mtu mwingine zaidi ya wafanyakazi wanaokuja kusafisha mazingira ya nje na ya ndani kisha wanaondoka.


Hizi nyumba alikuwa akizitumia kwenye masuala yake mbalimbali kama akimpata mwanamke ambaye alipenda kumtumia basi alichagua kati ya moja ya majumba haya kisha akaja naye na kumalizana naye hakuwa anapenda mambo yake mengi kujulikana kwa watu hakupenda upande wake wa pili wa shilingi ujulikane, hakutaka achafuke kabisa na kuharibu jina lake safi kwa serikali na jamii inayoamini yeye ni mtu mwema asiye na matatizo. Hizi nyumba mke wake hakuwa hakizijua kabisa kwakuwa kulikuwa na majumba mengi ambayo alikuwa akiyajua na waliweka wapangaji.

Aliitizama simu yake eneo lilipo saa na ilipofika saa moja kasoro tatu akapiga namba alizokuwa anasubiri pengine ndiyo aone kwenye simu yake zinaita.

“Michael…. Nimeshindwa kusubiri upige”. Akaongea kwa sauti ya chini kama anaogopa kusikika na mtu mwingine wakati jumba lote alikuwa peke yake.

“Kwanini umekuwa hivyo Mr. Logan Puteri?”

“Nimekuwa hivi mpaka najishangaa ndugu yangu”.

“Sauti yako imebadilika kabisa Logan…. Ebu jiamini bwana… Nielekeze tuonane wapi? Hili tuongee vizuri na tuone nakusaidiaje”.

“Huko wapi saivi?”.

“Nilikuja mazoezini Tasik Puteri Golf kwa ndugu yako ndiyo tumemaliza mazoezi leo yalikuwa mazuri sana tulienea wadau wote tunaoshindana kasoro wewe tu mzee wa kulenga…. Ndiyo tulikuwa tunaagana hapa na mheshimiwa Tasik”.

“Oooh! Sijaonana naye siku nyingi ndugu yangu huyo, jiji kubwa sana hili na kila mtu anajifanya yuko bize na mambo yake mi nisipokuja huko Tasik Puter Puteri Golf and Country club basi ndiyo sionani naye… Msalimie sana!”.

“Nyie ndugu bwana mnavyoishi mnajuana wenyewe mi siwezi ingilia maisha yenu… Okay! nitampa salamu zako”.

“Hamna shida nitamtafuta nikimaliza mambo niliyonayo kaka yangu huyo sina noma naye hata kidogo ni siasa ndiyo zinatutenganisha sababu itikadi zetu za vyama zinasigana… Mi nipo Batu Caves bara bara ya Jalan Kepong nina mjengo niliununua kama miezi miwili iliyopita unaweza ukaja tukaongelea hapa niko peke yangu na ni eneo salama tu”.

“Okay! Utanitumia meseji ya maelekezo nafika muda si mrefu, siku hizi nina Chevrolet inatimua mpaka raha”.

“Hahahahahah hahahahah! Hongera kaka kwa kununua Chevrolet naona umefuata nyayo za rafiki yako kaka Tasik…. Nitawajibu wiki ijayo”.

“Wee umezoea ma hammer yako hayo kazi kununua yenye rangi tofauti amia Chevrolet ule raha za dunia”.

Walimalizana wakakata simu kwa kila mmoja na maongezi hayo yakamfanya Bwana Logan Puteri aanze kujiamini upya.

Michael Joram Shweinsteiger ni mmarekani mwenye asili ya Ujerumani ikiwa babu na bibi zake waliamia Marekani miaka ya nyuma huko, anayefanya kazi ubalozi wa Marekani kama msaidizi wa ofisa wa kidiplomasia wa ubalozi wa Marekani nchini Malaysia, akiwa ameshikilia nafasi zaidi ya miaka ishirini wakibadilishwa maafisa wakuu lakini yeye akibaki sehemu hiyo sababu ya uzoefu wake na kuijua vilivyo Malaysia.


Wanabadilishwa mabalozi, maafisa mbalimbali na hata wakuu wake katika ofisi yake ya kidiplomasia yeye alibakizwa hapo hivyo alikuwa ni mtu mwenye marafiki wengi sana nchini Malaysia hususani viunga vya jiji la Kuala Lumpur.


Kudumu kwa muda mrefu ofisi ya ubalozi na hata kujenga urafiki na wanasiasa wengi wa kimalaysia toka vyama mbalimbali hasa kinachotawala Malaysia chama cha Malaysia Liberal Democratic Party (MLDP) Chama kinachofuata itikadi za kiliberali ambazo ndiyo itikadi za chama cha Liberal cha ujerumani ilipo asili ya Michael ilimfanya akipende sana chama hiki na hata kutia michango yake ya kimawazo na pia kuwafanya wawe na ukaribu na chama kile cha Ujerumani ambacho nacho kilikuwa kikimtumia Michael katika maslahi yake dhidi ya nchi ya Marekani.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog