Search This Blog

Monday 27 March 2023

LAITI NINGEJUA - 4

  


Simulizi : Laiti Ningejua

Sehemu Ya Nne (4)



“Bilali, hivi hujawahi kabisa kufikiria kumiliki gari?” Adnan aliniuliza baada ya ukimya ule.


“Hakuna asiyependa kumiliki gari, ila wakati mwingine mtu unajikuta ukiwa na mambo mengi ya kufanya na kushindwa uanze na kipi kwanza, lakini Mungu akinijaalia huenda mwakani inshallah nitakuwa na gari,” nilimwambia Adnan huku tabasamu likiumbika vizuri usoni mwangu.


Adnan alinitazama kwa muda akionekana kama aliyekuwa anafikiria jambo fulani kwa kina lililokuwa linamtatiza sana, kisha nilimuona akishusha tena pumzi ndefu za ndani kwa ndani.


“Kama mambo yangu yatakwenda vizuri nadhani nitakuletea zawadi ya gari. Sijui unapenda gari aina gani?” Adnan aliniuliza swali lililonifanya kupigwa butwaa kidogo.


Kwa kitambo fulani nilijikuta nikipata kigugumizi na kubaki nikimtumbulia macho Adnan kwa muda kana kwamba nilikuwa nimeona kitu fulani cha kushangaza sana. Kwa kweli sikujua niseme nini kwa wakati huo, ingawa moyoni nilikuwa natamani sana kumwambia kuwa nilipenda gari aina ya Toyota Lexus RX.


“Niletee gari yoyote tu utakayoona inanifaa, zawadi huwa haikataliwi,” hatimaye nilimudu kusema baada ya kitambo kirefu huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Basi sawa, ngoja nikuache upumzike na mimi niende uhamiaji, nitajitahidi tuonane kabla sijaondoka, tuombe uzima tu,” aliniambia Adnan huku akiitazama saa yake ya mkononi.


“Ahsante sana, ndugu yangu, kwa kuja kuniona,” nilimshukuru Adnan huku nikinyoosha mkono wangu kumpa, “Nakutakia kila la kheri ufanikiwe katika mipango yako.”


“Ahsante sana, na wewe Mungu akuponye haraka. Naamini tutaonana panapo majaaliwa,” Adnan alisema huku akinyoosha mkono wake kunipa, kisha akanishika begani katika namna ya kunitoa hofu juu yake na kuanza kuzitupa hatua zake kwa utulivu kuelekea nje ya ile wodi.


Nilimsindikiza kwa macho wakati akitembea hadi alipofika mwisho wa ile wodi, na kabla hajatoka kabisa mlangoni aligeuka kunitazama na kuachia tabasamu la kunifariji, kisha akatoka na kwenda zake.


Nilibaki nikiwa natafakari kuhusu lile tukio la mauaji kule porini Kibiti huku nikijiuliza ni nini kilichokuwa nyuma ya yale mauaji.


Je, ni kweli yalikuwa mauaji yaliyobeba kisasi? Au yalikuwa mauaji ya kisiasa? Au ni ugaidi? Na kama si ya kisasi, siasa wala ugaidi basi yalikuwa yamebeba ajenda gani zaidi? Nilijaribu kujiuliza maswali yale na mengine mengi lakini sikuweza kupata jibu.


Nilipokosa majibu niliamua kuachana na mawazo yale na hapo hapo mawazo yangu yakahamia kwenye kuifikiria zawadi ya gari niliyoahidiwa na Adnan. Nilikuwa nimepanga kununua gari mwaka huo, kwa kuwa Adnan aliniahidi kuniletea sikuwa tena na mpango wa kununua gari.


Mara nikajiona nikiwa ndani ya gari aina ya Toyota Lexus RX ya rangi nyeusi nikiwa naendesha taratibu na pembeni yangu alikuwa ameketi yule mrembo ‘the most wanted’.


Wakati nikitafakari mara nikajikuta nikipatwa na mshtuko mkubwa, nilijikuta nikihisi ubaridi fulani wa aina yake ambao sikujua tafsiri yake ukinitambaa mwilini na mapigo ya moyo wangu yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!


Nilibaki mdomo wazi nikimkodolea macho Jameela aliyekuwa akiingia mle wodini huku akiwa ameongozana na Jonas na mara moja wakaanza kupiga hatua kuja pale kitandani nilipokuwa nimelala.


Nilimtazama kwa makini nikiwa siamini macho yangu kama yote niliyokuwa nikiyaona yalikuwa yakitendeka wakati nikiwa nipo ndotoni. Nilimtazama wakati akizidi kupiga hatua zake za ki-miss kwa madaha akija pale kitandani nilipokuwa, huku mtikisiko wa umbo lake zuri la kike na matata ukizimeza haraka hisia zangu.


“Jameela!” nilijikuta nikimwita kwa mshangao uliochanganyika na furaha huku nikitamani kuinuka kutoka pale kitandani ili nimkumbatie.


“Bilali!” Jameela naye aliniita kwa mshangao huku akiharakisha kuja pale kitandani nilipokuwa nimelala, alipofika aliinama na kunibusu kwenye paji langu la uso kwa furaha.


Kisha alisimama akanitazama kwa kitambo kirefu huku macho yake yakishindwa kuficha huzuni kubwa aliyokuwa nayo, kisha nikamuona akitoa kitambaa laini na kuanza kufuta machozi yaliyokuwa yakimlenga machoni.


Jameela alikuwa katika muonekano tofauti kabisa wa kupendeza uliozidi kuichanganya zaidi akili yangu na kuamsha hisia zisizoelezeka na kunifanya kuyasahau kabisa yale maumivu niliyokuwa nayo. Niliendelea kumtazama Jameela na kwa kweli alikuwa amependeza sana.


Nilimkodolea macho kwa muda huku nikibabaishwa kidogo na harufu nzuri ya utuli aliokuwa amejipulizia mwilini mwake. Tuliendelea kutazamana kwa kitambo kirefu huku kila mmoja akionesha hisia za furaha kwa mwenzake.




Jameela alikuwa katika muonekano tofauti kabisa wa kupendeza uliozidi kuichanganya zaidi akili yangu na kuamsha hisia zisizoelezeka na kunifanya kuyasahau kabisa yale maumivu niliyokuwa nayo. Niliendelea kumtazama Jameela na kwa kweli alikuwa amependeza sana.


Nilimkodolea macho kwa muda huku nikibabaishwa kidogo na harufu nzuri ya utuli aliokuwa amejipulizia mwilini mwake. Tuliendelea kutazamana kwa kitambo kirefu huku kila mmoja akionesha hisia za furaha kwa mwenzake.


Endelea...


Tuliendeelea kutazamana kitambo kirefu huku nikihishi shughuli za mwili wangu zikisimama kwa muda na wakati huo huo macho yangu yalikataa kabisa kuamini kama taswira ya mlibwende yule ilikuwa mbele yangu ikiwa imejengeka vizuri machoni mwangu.


Baada ya kitambo nikamuona Jameela akiachia tabasamu jepesi la matumaini na kunipa pole huku akinieleza jinsi alivyoshtushwa sana na taarifa za kuvamiwa kwetu kule porini Kibiti baada ya kusoma kwenye mitandao ya kijamii.


“Nilipooneshwa picha za watu waliouawa kwa kweli sikuamini kabisa kama wewe ulisalimika kwenye ule mkasa wa kutisha… hivi ilikuwaje hasa?” Jameela aliniuliza kwa shauku baada ya kitaambo huku tukitazamana kwa hisia.


Nilishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku nikifumba macho yangu kujaribu kulifikiria lile tukio la mauaji kule porini Kibiti. Nilipofumbua macho yangu nilimtazama Jameela na kutabasamu.


“Ni hadithi ndefu sana, kwa kweli ule ulikuwa unyama wa kutisha ambao sijawahi kuushuhudia katika maisha yangu, na hapa siamini kama bado nipo hai,” nilimwambia Jameela huku nikivishikashika taratibu vidole vyake vya mkononi, hali iliyomfanya azidi kutabasamu na kufuta machozi ya furaha kwa mgongo wa kiganja chake.


“Kama taarifa nilizozisikia ni sahihi, basi ni vigumu sana kuamini kama uliokoka lakini ni Mungu tu ndiye aliyekuokoa,” Jameela alisema kwa utulivu huku akiendelea kutabasamu.


Ukimya kidogo ukapita huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri, Jameela alionekana kuwaza mbali na mimi nilikuwa nawaza juu ya mambo yote yaliyotokea tangu nilipoondoka kule Ikwiriri kisha nikakutana na Adnan na kupewa lifti, hadi nilipoachana nao pale stendi ya Kibiti.


Kisha nikakumbuka nilivyopata usafiri na safari yetu ilivyokuwa kabla hawajatokea wale wauaji na kutenda unyama wao. Ukimya ule ulipoelekea kushika hatamu Jameela akaniuliza huku akiwa ameketi kando yangu pale kitandani, “Vipi unajisikiaje kwa sasa?”


“Kwa sasa najisikia nafuu kidogo, hasa baada ya wewe kuja kuniona ndiyo nahisi kupona kabisa,” niliongea kwa utani kwa sauti tulivu huku nikiachia kicheko hafifu.


“Usijali, kwa kuwa nipo naamini sasa utapona kabisa na Mungu atazidi kukusaidia,” Jameela naye alisema kwa utani huku akiachia kicheko hafifu, alinitazama kwa utulivu huku akitabasamu.


Nami niliruhusu tabasamu langu jepesi kuchanua usoni kwangu kisha nikageuza shingo kumtazama Jonas, ambaye muda wote alikuwa kimya kabisa akitutazama kwa zamu.


“Halafu, muda mfupi tu uliopita kaka yako alikuwa hapa,” nilimwambia Jameela huku nikimtazama moja kwas moja machoni. Jameela alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku akiachia tabasamu.


“Najua,” Jameela alinijibu kwa kifupi.


Jibu lake lilinifanya nishangae kidogo, nikageuza shingo yangu kumtazama tena Jonas huku nikiwa bado nashangaa, kisha nikayarudisha macho yangu tena kwa Jameela.


“Na yeye anajua kuwa umekuja kunitembelea?” nilimuuliza huku nikiwa bado namtazama kwa mshangao.


Jameela alizidi kutabasamu huku akitingisha kichwa chake kukataa kisha akasema jambo lililozidisha mshangao wangu. “Hajui chochote kuhusu uwepo wangu hapa na wala sitaki ajue.”


“Sasa umeaga vipi nyumbani?” nilizidi kumdodosa Jameela kwa maswali.


“Hmm! Mbona maswali mengi kama polisi?” aliniuliza Jameela huku akikunja ndita usoni kwake.


“Kwani kuna ubaya wowote kutaka kujua, maana nina uhakika kaka yako hawezi kukuruhusu kuja peke yako kuniona…”


“Unajuaje?” alidakia Jameela huku akinikazia macho kwa mshangao.


“Mimi ni mtu mzima, nilichokishuhudia siku ile ndani ya gari pale Ikwiriri kilitosha kabisa kunionesha ni kwa kiwango gani Adnan asingependa uwe huru kuongea mwanaume yeyote,”


Jameela alinitazama kwa kitambo akionekana kufikiria sana juu ya ile kauli yangu, ilionekana maneno yangu yalikuwa na ukweli fulani, alishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Ni kweli kama usemavyo, Adnan asingeweza kuniruhusu lakini kwa sasa mimi nipo hapa Dar es Salaam, kule Ilala Sharif Shamba kwa shangazi,” aliniambia Jameela na kunifanya nishangae kidogo.


“Upo Dar es Salaam! Umekuja kwa shughuli gani, wewe si ulitakiwa ukae ndani kusubiri ndoa?” nilimuuliza nikizidi kushangaa.


“Kwani umesahau kuwa nipo chuo? Au unadhani nilipoomba namba yako siku ile ilikuwa ni kwa ajili ya nini?” aliniuliza Jameela huku akinikazia macho.


“Nilijua kuwa kesho yake ningekuja Dar es Salaam na ningekutafuta, ingawa kiukweli sikujua kama haya yangetokea. Nilipopata taarifa za mauaji nilichanganyikiwa sana, kwa siku mbili sikuweza kula kwani hata nilipojaribu kukutafuta kwenye simu ulikuwa hupatikani,” alisema Jameela kwa huzuni.


“Ila namshukuru sana shangazi, amekuwa akinitia moyo sana na bahati nzuri yeye ni tofauti na mama au kaka yangu, anathamini hisia zangu na ndiye ameniruhusu kuja kukuona,” alimaliza Jameela na kushusha pumzi ndefu.


“Umejuaje kuwa nipo hapa, na umefahamiana vipi na Jonas?” nilimuuliza Jameela na kugeuza shingo yangu kumtazama Jonas. Jameela naye aligeuza shingo yake kumtazama Jonas kisha akashusha pumzi.


“Adnan alipita kwa shangazi wakati anataka kwendaa uhamiaji, akawa anamweleza kuwa lazima apitie kwanza Muhimbili kumuona rafiki yake kalazwa MOI wodi namba kumi na saba ya jengo la Sewa Haji. Alipoondoka tu na mimi nikapaanga kuja, nilipofika nikawa naulizia na bahati nzuri nikakutana na huyu kaka aliyeniambia anakufahamu na anakuja kukuona,” alisema Jameela huku akigeuza tena shingo yake kumtazama Jonas.


Niliachia tabasamu huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani, hata hivyo, nilishangazwa sana na maneno ya Jameela kuwa alishindwa kula kwa sabau ya kusikia nimevamiwa, nikaanza kuhisi kuwa huenda alikuwa amekwisha nasa kwenye mapenzi, jambo nililolihisi tangu siku ile nilipopewa lifti na kaka yake.


* * * * *


Ilikuwa imepita miezi mitatu tangu lile tukio la mauaji ya kutisha kule porini wilayani Kibiti, mguu wangu ulikuwa umepona na nilikuwa naendelea na mishemishe zangu kama kawaida, ingawa nilikuwa nasikia maumivu kwa mbali na madaktari walinishauri nisifanye kazi ngumu kwa muda wa miezi sita.




Niliachia tabasamu huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani, hata hivyo, nilishangazwa sana na maneno ya Jameela kuwa alishindwa kula kwa sabau ya kusikia nimevamiwa, nikaanza kuhisi kuwa huenda alikuwa amekwisha nasa kwenye mapenzi, jambo nililolihisi tangu siku ile nilipopewa lifti na kaka yake.


* * * * *


Ilikuwa imepita miezi mitatu tangu lile tukio la mauaji ya kutisha kule porini wilayani Kibiti, mguu wangu ulikuwa umepona na nilikuwa naendelea na mishemishe zangu kama kawaida, ingawa nilikuwa nasikia maumivu kwa mbali na madaktari walinishauri nisifanye kazi ngumu kwa muda wa miezi sita.


Endelea...


Siku moja nikiwa nyumbani Adnan alinipigia simu akinielekeza kuwa alitaka kuja nyumbani kuniaga kwa kuwa ile safari yake ilikuwa imekamilika. Nilifurahi sana kwa kuwa nilijua kuwa angesafiri na baada ya kurudi nami ningemiliki gari langu.


Nyumba niliyoishi ilikuwa katika eneo la Buguruni nyuma ya kituo cha daladala cha Rozana, ilikuwa ni nyumba kubwa ambayo wazazi wetu walituachia mimi na kaka yangu, Hassan, ambaye kwa wakati huo alikuwa anaishi Afrika Kusini alikohamishia makazi yake.


Wazazi wetu walituachia na kurudi Kigoma ambako ndiko walikokuwa wakiishi na kuendesha miradi yao, hasa baada ya baba yetu kustaafu kazi ya utumishi wa umma.


Nyumba ile ilikuwa kubwa yenye vyumba vitano, sebule, jiko, stoo, choo na bafu, vyote vikiwa ndani ya nyumba na pia ilikuwa imezungukwa na ua mpana uliojengwa kwa matofali.


Katika nyumba hiyo mimi niliishi kwenye chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na sebule, na vyumba vingine vinne tulikuwa tumepangisha.


Adnan alipokuja kuniaga sikutaka kumwacha aende pasipo kumsindikiza, hivyo alipokuwa akiondoka nilimsindikiza hadi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Baada ya Adnan kuondoka, jioni ya siku iliyofuata Jameela alikuja nyumbani kwangu akiwa amependeza sana.


Alikuwa amevaa suruali ya jeans nyeusi na blauzi ya rangi ya samawati. Zile nguo zilikuwa zimembana kiasi cha kulichora vyema umbo lake refu lenye kiuno chembamba na tumbo flati, na begani alikuwa amening’iniza mkoba mzuri wa rangi nyeusi wa thamani kubwa.


Alipoingia ndani alinitazama kwa utulivu huku akiachia tabasamu kabla ya tabasamu lake halijageuka kicheko cha kirafiki. Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa Jameela kufika nyumbani kwangu, niseme tu ukweli kuwa ujio wake ndiyo ulikuwa mwanzo wa kubadilika kabisa kwa tabia yangu.


Kama nilivyosema kabla, watu wengi walidhani labda nilikuwa na matatizo makubwa mwilini mwangu kwa kuwa licha ya kupapatikiwa sana na warembo lakini sikuwa nikijihusisha na uhusiano na msichana yeyote kati yao, nadhani hata Jameela alionekana kunifikiria hivyo.


Nilidhani hivyo kwa kuwa baada ya zile safari zake mbili alizokuja nyumbani kwangu kunitembelea, alichokiona pale nyumbani kilimfanya kuwa na wasiwasi nami. Mara hii ya tatu alipokuja nikaona isiwe taabu, kama mtoto akililia wembe mwache umkate. Lakini sikujua kuwa ndiyo ulikuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa sana ya tabia yangu.


Alipokuja siku hiyo ni mimi niliyekuwa nimempigia simu kumuomba aje nyumbani, hasa baada ya kuona ile safari ya pili alipokuja nyumbani kwangu aliondoka akiwa amenuna sana kwa sababu pamoja na kunionesha jinsi gani alikuwa amejikabidhi kwangu lakini nilijifanya sioni.


“Sina muda mrefu, nina saa mbili tu za kuwepo hapa kwako,” Jameela aliniambia mara tu alipoingia ndani kwangu huku akiitazama saa yake ya mkononi, wakati huo ilikuwa yapata saa kumi na moja za jioni na alipoingia alikwenda moja kwa moja kuketi kitandani.


Chumba changu kilikuwa kikubwa kikiwa kimepambwa vyema kwa kitanda kikubwa cha samadari nilichokuwa nimekiweka katikati ya chumba. Kilikuwa kitanda cha futi sita kwa sita, cha mbao ngumu za mninga, chenye droo mbili kila upande na juu ya droo hizo kulikuwa na taa mbili za rangi ya bluu.


Kulikuwa na kabati la nguo la kioo na pembeni ya kabati hilo kulikuwa na kochi moja dogo la sofa na meza ya kioo mbele yake. Sakafuni kulikuwa na zulia pana la rangi ya bluu.


Chumba kilikuwa na dirisha pana lililokuwa limefunikwa kwa pazia zito na refu lenye nakshi za michoro ya maua yaliyodariziwa vizuri na kuyafanya yapendeze.


Jameela alipoketi pale juu ya kitanda changu, nilisimama nikimtazama kwa matamanio, kisha nikamsogelea na kumshika mikono yake, nikamvuta nikimwinua na kuanza kumbusu. Hata hivyo, Jameela aligeuza kichwa chake akijaribu kuiepuka midomo yangu.


“Mbona una haraka hivyo!” nilimsikia akilalama kwa sauti yenye kitetemeshi huku akiachia kicheko hafifu.


“Aliyesema ana saa mbili tu za kuwepo hapa nani kama si wewe?” nilimuuliza huku nikizidi kumvutia kifuani kwangu na kumporomoshea mabusu mfululizo. Jameela alijigandamiza kwenye mwili wangu na kutulia huku akihema kwa nguvu.


Kisha niliamua kumsukumia juu ya kitanda, akaanguka kama mzigo na kutulia huku akinitazama kwa makini, nikaliendea dirisha na kulishusha pazia kisha nikageuka kumtazama Jameela bila ya kusema lolote.


Wakati ule mle ndani kulikuwa na mwanga hafifu sana. Nilihisi Jameela alikuwa akiniona kama kivuli tu pale nilipokuwa nimesimama.


Taratibu nilifungua vifungo vya shati langu na kulivua kisha nikalitupia kwenye lile sofa, nikaenda kuketi karibu yake huku nikihisi kijasho chembamba kikinitoka mwilini. Nilimshika na kugandisha midomo yangu kwenye midomo yake. Na hapo nikamuona akiyafumba macho yake na kukunja uso wake kama mtu aliyekuwa anahisi kizunguzungu na kuanza kutokwa na jasho kupita kiasi.


Nilijitupa kitandani na mara mikono yangu ikaanza kupita mwilini mwake, na hapo nikamshuhudia pumzi zikianza kumpaa! Na kilichofuata baada ya pale ilikuwa ni sinema kali ya kusisimua iliyotuacha tukiwa hoi bin taaban.


Kufumba na kufumbua ilikuwa tayari imeshatimu usiku wa saa sita, Jameela hakuweza kuondoka tena hivyo akaamua siku ile asirudi chuo bali aupitishe usiku mzima pale pale nyumbani kwangu hadi asubuhi. Asubuhi ile baada ya Jameela kuondoka aliniacha nikiwa hoi na siku ile sikutoka kabisa nyumbani, nilipooga ile asubuhi na kunywa chai nilirudi tena kitandani.


Hapo kitandani nikiwa na uchovu mwingi lakini mwenye furaha mno nilijikuta nikimwaza Jameela muda wote. Kwa kweli alikuwa mtundu mno na alikuwa amenionesha ulimwengu mpya ambao sikuwa mjuzi kabisa. Alikuwa binti mwenye busu za kusisimua sana na aliniachia maswali kibao, nikijiuliza ni wapi alikuwa amejifunzia yale mambo?


Japo sikuwa mzoefu sana wa yale mambo lakini niliamini kuwa Jameela alikuwa wa aina ya pekee, mwenye majibu yote ya maswali yahusuyo mapenzi. Na kama kungefanyika mashindano nilikuwa na imani wasichana wengine wasingefua dafu kabisa kwa Jameela.


Baada ya siku ile Jameela alikuja tena mara tatu, na kila alipokuja kazi ilikuwa ni moja tu, kisha aliniambia kuwa wiki iliyofuata angebanwa sana na mitihani ya mwisho, hivyo aliniomba radhi kuwa asingeweza kuja kwa kipindi kile hadi amalize chuo.




Japo sikuwa mzoefu sana wa yale mambo lakini niliamini kuwa Jameela alikuwa wa aina ya pekee, mwenye majibu yote ya maswali yahusuyo mapenzi. Na kama kungefanyika mashindano nilikuwa na imani wasichana wengine wasingefua dafu kabisa kwa Jameela.


Baada ya siku ile Jameela alikuja tena mara tatu, na kila alipokuja kazi ilikuwa ni moja tu, kisha aliniambia kuwa wiki iliyofuata angebanwa sana na mitihani ya mwisho, hivyo aliniomba radhi kuwa asingeweza kuja kwa kipindi kile hadi amalize chuo.


Endelea...


Kwa kuwa tayari alikuwa amekwisha amsha hamu yangu ya ngono nikajikuta nikienda mbio huku na kule isivyo kawaida kutafuta amtu ambaye angekidhi kiu yangu ya mapenzi, na kwa kipindi kifupi tu tayari nilishajihusisha katika uhusiano na wasichana wengine watatu. Lakini bado sikuweza kumuona aliyefikia utundu wa Jameela.


Taratibu akili yangu ikaanza kumsahau yule mrembo ‘the most wanted’ niliyesafiri naye kabla hatujapatwa na janga kule porini wilayani Kibiti, na muda wote nikajikuta nikimfikiria zaidi Jameela.


Siku moja nilikwenda kumuona rafiki yangu pale Amana, na nilipoacha naye sikutaka kupanda gari hivyo nikawa natembea taratibu nikiifuata barabara ya lami iliyokuwa ikitokea hospitali ya Amana ikipitia eneo la Sharif Shamba na kwenda kutokea zilipo ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).


Wakati natembea mara macho yangu yakavutwa kumtazama msichana mmoja mrembo aliyekuwa akikatiza mbele yangu kuelekea kwenye dukani moja upande wa pili wa ile barabara. Nilisimama ghafla na kumkodolea macho yule mrembo wakati akinunua bidhaa ndogo ndogo kwenye lile duka.


Wakati ule nimesimama nilikuwa najiuliza kama niliwahi kumuona sehemu yule mrembo na hapo hapo nikakumbuka kuwa ni yule mrembo ‘the most wanted’ tuliyekuwa safari moja kule Kibiti kabla ya lile tukio la mauaji halijatokea.


Nilipogundua hivyo nikajikuta naanza kuchanganya miguu yangu kuelekea pale kwenye lile duka, nilipofika nilimsalimia yule mrembo ‘the most wanted’ huku nikiagiza soda.


Yule mrembo ‘the most wanted’ aliitikia salamu yangu pasipo hata kugeuza shingo yake kunitazama usoni, na wakati yule muuzaji alipokuwa ananipatia ile soda na kuendelea kumhudumia yule msichana, nilikuwa namtazama yule mrembo kwa makini, hivyo nikawa nakunywa soda yangu taratibu huku nikiendelea kumtazama kwa makini nikiwa siamini macho yangu.


Yule mrembo yule ‘the most wanted’ alipokuwa anafungasha bidhaa zake pasipo kunitazama wala kunijali nikaamua kujikohoza kidogo na kumfanya yule mrembo ‘the most wanted’ ageuke kunitazama usoni kwa makini na hapo hapo nikaachia tabasamu, hata hivyo sikuona tashwishwi usoni kwake wala hakuonesha kabisa kunikumbuka.


“Samahani bi mdogo, nimegundua kuwa nilikuwa sijakukaribisha, karibu soda,” niliongea kwa sauti tulivu ya chini huku nikiendelea kumtazama kwa tabasamu.


Alinitazama mara moja tu na kutingisha kichwa chake kukataa huku akiendelea kukusanya vitu vyake. “Asante sana, lakini samahani mimi sinywi soda!”


Japokuwa alikataa ofa yangu lakini nilijikuta nikifarijika kidogo baada ya yule mrembo ‘the most wanted’ kunijibu pasipo kuonesha maringo yoyote kama walivyo wasichana wengine waliojiona warembo. Nikajikakamua na kumchombeza tena. “Sasa, sijui nikununulie nini ambacho unakunywa, bi mdogo?”


“Hakuna chochote uwezacho kuninunulia, bwana mkubwa…” alisema tena yule mrembo ‘the most wanted’ bila hata kunitazama.


“Okay! Naitwa Bilali Ibrahim, sijui unanikumbuka?” nilimuuliza tena, safari hii niliongea kwa msisitizo.


Yule mrembo ‘the most wanted’ alinitupia jicho mara moja tu na kutingisha kichwa chake huku akimalizia kufungasha vitu vyake na kuanza kupiga hatua zake kuondoka. “Wala sikufahamu, hata hivyo kwa heri, Mr Bilali Ibrahim!”


Nilitaka kusema neno lakini nikasita na kubaki kimya nikimsindikiza yule mrembo kwa macho huku nikiwa nimekata tamaa, nilibaki nikimtazama huku nikipeleka chupa ya soda mdomoni na kuinywa soda yote iliyobakia kwa mkupuo mmoja tu.


Kisha nikatoa pesa kwenye pochi yangu na kumpa yule muuzaji pale dukani huku nikimdadisi, “Samahani, bro, hivi huyu binti anaitwa nani?”


“Anaitwa Rehema,” alinijibu yule muuzaji wa dukani pasipo kuwa na wasiwasi wowote na mimi.


“Ooh, Rehema! Na anakaa mtaa gani kwa hapa?”


“Anakaa kwenye ile nyumba pale kubwa ya kisasa. Kwa Bi Aisha,” aliniambia yule muuzaji wa dukani huku akinielekeza kwa kidole.


Nilibetua kichwa changu huku nikiitazama ile nyumba kwa makini kisha nikamtazama yule muuzaji kwa tabasamu. Moyoni nilimshukuru sana yule muuzaji wa dukani kwa kunipa taarifa ambazo hakujua kuwa zilikuwa muhimu sana kwangu na nilikuwa nimehangaika kwa takriban miezi sita kuzitafuta.


Niliondoka pale dukani na kutembea taratibu huku hamu yangu ya kumtafuta mrembo ‘the most wanted’ ambaye sasa nilijua kuwa jina lake aliitwa Rehema na alikuwa anaishi Ilala Sharif Shamba, ikiibuka upya.


Usiku wa siku ile sikupata kabisa usingizi, niligaagaa kitandani kwangu usiku kucha nikimfikiria Rehema, na kulipokucha kitu cha kwanza nilichokifanya ilikuwa ni kuingia jikoni, nikawasha jiko na kuinjika sufuria ndogo ya chai, kisha nikaanza kusafisha chumba changu.


Nilijisikia njaa kali sana siku hiyo, na ilipotimu saa tatu asubuhi nilikuwa nimekwishamaliza kazi zangu zote. Nikaketi kitini katika sebule yangu na kuanza kunywa chai.


Wakati nakunywa chai akili yangu haikuwa imetulia kabisa, hadi wakati ule nilikuwa nawaza jinsi ya kumpata Rehema. Nilidhani kuwa endapo ningempata basi angetosha kabisa kuniweka katika hali ya furaha. Nilijilaumu kwa kutokugundua mapema kuwa alikuwa akiishi Ilala Sharif Shamba, eneo ambalo ningeweza kufika pasipo hata usafiri.


Na laiti ningejua mapema wala nisingehangaika na ‘visungura tope’ wengine, ukimwacha Jameela maana hakuwa na mpinzani hadi wakati huo. Hata hivyo, tatizo kubwa la Jameela lilikuwa moja, alikuwa mchumba wa mtu akisubiriwa amalize chuo tu aolewe. Pia alikuwa ni dada wa rafiki yangu, Adnan.


Sikujua kwa nini nilikuwa napata msukumo mkubwa sana ndani yangu kumtafuta Rehema, nadhani ni kwa sababu sikuwa huru kuwa na Jameela.


Hata hivyo, ndani yangu kulikuwa na sauti iliyonieleza kuwa sikumpenda Rehema kwa dhati kutoka moyoni bali nilimtaka kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa, kwa kifupi nilimtamani tu. Yaani nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na ningeachana naye.


Ndiyo ningeachana naye kwa sababu sikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye sikujua kama ningemuoa, hasa wasichana warembo kama yule sikuwa na mpango wa kuwaoa.


Wakati naendelea kuwaza nikasikia sauti ya mtu aliyekuwa akibisha hodi, kabla sijafanya chochote niliuona mlango ukifunguliwa na Jameela aliingia akinikuta nikiwa mezani nakunywa chai.


Alisimama akanitazama huku akiachia tabasamu pana lililovinjari usoni pake. Kwa sekunde kadhaa macho yangu yakajikuta yakipumbazwa na uzuri wake.


Jameela alikuwa msichana mrembo sana, japokuwa alikuwa amevaa hijabu iliyokuwa imefunika mwili wake wote kasoro sehemu ndogo ya uso wake, lakini bado uzuri wake haukujificha kabisa. Mdomo wake laini wenye kingo pana kiasi ulikuwa umeupakwa rangi ya mdomo ya chocolate.


Huku akiendelea kutabasamu, Jameela alilivua lile hijabu na kunisogelea taratibu. Nywele zake nyeusi za Kiarabu alikuwa amezisuka mtindo wa mkiwa wa pweza.




Alisimama akanitazama huku akiachia tabasamu pana lililovinjari usoni pake. Kwa sekunde kadhaa macho yangu yakajikuta yakipumbazwa na uzuri wake.


Jameela alikuwa msichana mrembo sana, japokuwa alikuwa amevaa hijabu iliyokuwa imefunika mwili wake wote kasoro sehemu ndogo ya uso wake, lakini bado uzuri wake haukujificha kabisa. Mdomo wake laini wenye kingo pana kiasi ulikuwa umeupakwa rangi ya mdomo ya chocolate.


Huku akiendelea kutabasamu, Jameela alilivua lile hijabu na kunisogelea taratibu. Nywele zake nyeusi za Kiarabu alikuwa amezisuka mtindo wa mkiwa wa pweza.


Endelea...


Alikuwa amevaa fulana nyepesi nyeupe iliyoyaficha vyema matiti yake imara yenye ukubwa wa wastani na hapo hapo nikakiona kidani cha dhahabu chenye herufi ‘B’ kikiwa kimenasa vyema kwenye shingo yake ndefu na kupotelea katikati ya kichochoro hafifu katikati ya matiti yake.


Chini alikuwa amevaa pensi nyepesi ya rangi nyeusi iliyoishia juu ya magoti yake na kuonesha minofu ya mapaja yake yaliyonona.


“Ooh! Karibu Jameela,” niliinuka kumkaribisha Jameela mara tu aliponisogelea karibu kabisa na kusimama mbele yangu.


“Una mguu mzuri, umewahi chai,” nilisema huku nikimkumbatia na kumbusu kwenye paji la uso wake.


“Miguu ya mkulima hii,” Jameela alisema huku akiachia kicheko hafifu, kisha akaketi kwenye kiti kimojawapo kwa chai.


Siku ile alipokuja Jameela sikuweza kutoka kabisa, ile mipango ya kwenda kumtafuta Rehema ilikufa kabisa kwani Jameela aliniambia kuwa alikuwa amekuja kupumzika pale kwangu kwa siku mbili baada ya kumaliza mitihani yake ya mwisho, kisha angekwenda kwao Kibiti.


Kwa zile siku mbili tulishinda ndani tu, hata nilipopigiwa simu za kiofisi Jameela alinitaka niwatake radhi au nisipokee kabisa, na alivyoona watu wanazidi kunipigia simu aliichukua ile simu akaizima kabisa.


Kiukweli Jameela alionesha kunipenda sana na hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, kwani aliwahi hata kudanganya nyumbani kwao kuwa alikuwa na matatizo makubwa chuoni akatumiwa pesa nyingi ilimradi anipatie mimi, hasa nilipomwambia kulikuwa na mtu fulani alikuwa ananidai shilingi laki tano na alikuwa akisumbua kwelikweli.


Siku ya tatu asubuhi ndipo Jameela aliondoka nyumbani kwangu, na mchana wa siku ile nikaona nipite mitaa ya Ilala Sharif Shamba nikamtafute Rehema.


Nilitoka nyumbani kwangu Buguruni Rozana nikatembea taratibu nikiambaa ambaa kando kando ya makaburi ya Malapa, hadi nilipolifikia jengo la ghorofa tatu zilipokuwa ofisi za kampuni ya kisimbuzi cha StarTimes.


Hapo nikaambaa ambaa tena na Barabara ya Uhuru nikiyapita majengo ya Malapa Hostel na kituo cha daladala cha Malapa Hostel na mbele yake nikakipita kituo cha kujazia mafuta cha Lake kabla ya kuvuka daraja.


Nilizidi kuambaa kando kando ya barabara ile ya Uhuru nikizivuka nyumba kadhaa kisha nikaufikia msikiti uliokuwa upande ule ule wa kushoto kwangu na kabla sijaifikia hoteli ya Ya Mungu Mengi nikaamua kukata kuingia kushoto nikiufuata mtaa mmoja huku nikiuacha ule msikiti upande wangu wa kulia.


Katika mtaa ule uliokuwa na barabara ya vumbi niliwapita watoto watatu waliokuwa wakikimbizana na kunipita huku mmoja akijigonga mguuni kwangu na kuanguka. Sikuwajali, niliendelea kutembea taratibu na mbele kidogo nikaukuta mtaa mwingine uliokuwa unaingia upande wangu wa kulia kuifuata barabara ya lami.


Hivyo nikauacha ule mtaa wa barabra ya vumbi uliokuwa unaelekea kwenye jengo moja refu la ghorofa tisa lililokuwa linaendelea kujengwa, nikakata kuufuta ule mtaa wa barabara ya lami ulioelekea upande wa kulia.


Wakati naingia kwenye ule mtaa nikaendea mbele kidogo na mara nikashtushwa na sauti ya breki kali za gari nyuma yangu. Niliogopa sana nikajikunja na kuruka juu huku nikitua kando ya ile barabara nikiwa nimefumba macho yangu, kisha nikageuza shingo yangu kutazama nyuma yangu.


Nikaliona gari ndogo aina ya Toyota Mark X la rangi ya bluu bahari likiwa linaserereka huku dereva akijitahidi kunikwepa, kisha lile gari likasimama kando mbele yangu. Nilisimama huku nikiwa nahema kwa hofu nikamtazama yule dereva ambaye muda ule alikuwa akinitazama kwa hasira.


Macho yangu yakatua kwenye uso wa yule dereva na mshtuko nilioupata ulikuwa hauelezeki. Dereva wa lile gari alikuwa ni Rehema. Tuliangaliana kwa kitambo kifupi kila mmoja akiwa kimya, kisha nikamsogelea na kusimama usawa wa mlango wake.


“Rehema!” niliita kwa mshangao huku nikimkazia macho yangu, lakini hofu ilikuwa bado inanitambaa mwilini mwangu kutokana na kukoswa koswa kugongwa.


Rehema alishtuka sana na kunikazia macho kwa mshangao, hata hivyo, nikaachia tabasamu laini. “Nadhani sijakosea jina, wewe ni Rehema…” nilisema tena huku nikiendelea kumtazama Rehema kwa tabasamu pana.


Nikamuona Rehema akishusha pumzi ndefu. “Ndiyo hukukosea… ni mimi…” alisema lakini akasita kidogo na kunikazia macho huku akinitazama kwa makini, “Lakini, ni nani amekuambia naitwa Rehema?”


“Niliambiwa na yule kijana wa pale dukani siku ile ulipokataa ofa yangu ya soda,” nilisema huku nikiachia kicheko hafifu.


Rehema aliguna na kuachia tabasamu kisha akasema, “Asante kwa kuonekana kunijali, Mr Bilali.”


“Na wewe ahsante kwa kulikumbuka jina langu!” nilisema huku moyoni nikifarijika sana baada ya kuona kumbe Rehema alikuwa akilikumbuka jina langu.


“Hamna shaka, Mr Bilali, na pole sana kwa kutaka kukusababishia ulemavu.”


“Usijali, yote ni mapenzi ya Mungu,” nilisema huku nikiendelea kutabasamu, nikavuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku nikijikuna kidevu changu.


Rehema aliniangalia kwa makini na kuachia tabasamu kisha akaingiza gia akitaka kuondoka, lakini nikamzuia kwa ishara. Hakuizima gari lake bali alinitazama kwa mshangao huku akionesha wasiwasi kidogo usoni kwake.


“Vipi kuna nini tena, au bado unataka kuninunulia soda?” alisema kwa utani huku akinikazia macho.


“Ni hivi… eer… mimi na wewe tuna bahati sana ya kukutana mara kwa mara katika maisha yetu, kwa nini basi tusiwe marafiki?” nilisema huku nikimtazama Rehema kwa makini.


“Urafiki wa vipi unaoukusudia?” aliniuliza Rehema akiwa amekunja uso wake, hakuacha kunitazama kwa makini.


“Unajua Rehema… amini usiamini, tangu siku ile ya kwanza nilipokuona kule Kibiti, nimeshindwa kabisa kukutoa akilini mwangu,” nilisema huku nikimkazia macho, nikamuona akishtuka sana na kunitazama usoni kwa mshangao mkubwa.


“Lini mimi na wewe tumeonana Kibiti?”


“Siku ile ya mgomo wa madereva wa mabasi kisha mimi na wewe tukasafiri kwenye gari moja tukiwa tumeketi nyuma ya gari na baadaye yakatokea mauaji kule porini wakati mimi na wewe tukijificha kwenye kichaka…”


“Oh my God!” Rehema alishtuka sana na kuachia yowe kubwa la mshangao usioelezeka. Nilimuona akiinua mikono yake juu na kushika kichwa chake huku akinitazama kwa mshangao mkubwa kana kwamba alikuwa ameona kitu cha ajabu sana.


“Usishangae, Rehema, ni mimi niliyekuokoa siku ile na kukushauri ujifiche pale kwenye kichaka, ni mimi niliyekulinda siku ile hadi pale polisi walipokuja,” nilizidi kuongea maneno yaliyomfanya Rehema azidi kuchanganyikiwa.


Nilimuona akibaki mdomo wazi akiwa bado amenitumbulia macho yake kwa mshangao. Kisha nikaiona michirizi ya machozi yaliyomtoka machoni kama vile bomba lilikuwa limepasuka. Rehema alijaribu kuyazuia machozi lakini akashindwa, akabaki kimya akinitumbulia macho yake bila kusema chochote.


Kisha akatoa leso yake laini na kufuta machozi na kupenga kamasi zilizoanza kumtoka, akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akijiegemeza kwenye siti yake. Hadi muda huo hakuweza kabisa kuongea neno lolote zaidi ya kusema.



Nilimuona akibaki mdomo wazi akiwa bado amenitumbulia macho yake kwa mshangao. Kisha nikaiona michirizi ya machozi yaliyomtoka machoni kama vile bomba lilikuwa limepasuka. Rehema alijaribu kuyazuia machozi lakini akashindwa, akabaki kimya akinitumbulia macho yake bila kusema chochote.


Kisha akatoa leso yake laini na kufuta machozi na kupenga kamasi zilizoanza kumtoka, akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akijiegemeza kwenye siti yake. Hadi muda huo hakuweza kabisa kuongea neno lolote zaidi ya kusema.


Endelea...


“Nashukuru sana kwa kunijali,” hatimaye alimudu kusema huku akiendelea kufuta machozi.


Niliachia tabasamu na kuangalia kando. Rehema alizidi kuniangalia kwa namna ambayo sikuijua akiwa bado haamini macho yake. Tulibaki tukiwa tunaangaliana kwa kitambo kirefu, kisha Rehema alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.


Hakuweza kusema chochote bali alikuwa akishusha pumzi za ndani kwa ndani na kunyanyua mabega yake juu kisha akaliondoa gari kwa mwendo wa kasi akiniacha nimepigwa butwaa. Gari halikwenda mbali nikaliona likisimama, kisha likaanza kurudi nyuma na kuja kusimama pale pale lilipokuwa mwanzo.


Rehema alipenga kamasi kwa kutumia kitambaa chake laini na kuniashiria niingie ndani ya lile gari, sikujivunga, nilizunguka upande wa pili nikaufungua mlango wa mbele wa abiria kushoto kwa dereva na kuingia bila kusita, kwani ile ndiyo ilikuwa nafasi muhimu niliyokuwa naingoja siku zote.


Kisha Rehema akaliondoa gari lake taratibu kutoka eneo lile bila kuongea huku akinitupia jicho mara kwa mara akiwa bado haamini alichokisikia kutoka kwenye kinywa changu. Hakuna aliyeongea chochote kati yetu, rehema aliendesha hadi tulipofika kwenye ile nyumba kubwa na nzuri ya kifahari iliyozungukwa na miti mizuri ya kivuli.


Ilikuwa ni nyumba iliyozungukwa na ukuta mrefu usiomwezesha mtu kuona ndani ambao ulikuwa umefungwa mfumo maalumu wa umeme wa kuzuia wezi juu yake.


Hiyo ilikuwa ni moja ya majumba makubwa ya kisasa ya watu wakwasi katika eneo lile la Sharif Shamba yaliyokuwa yamezungushwa uzio na mageti makubwa yenye vifaa vyote vya usalama vya kuwahakikishia wakazi wake ulinzi na usalama wa hali ya juu.


Mbele ya lile geti kubwa jeusi Rehema alipiga honi na mara mlango mdogo wa lile geti ulifunguliwa kidogo, nikamuona mdada mmoja ambaye kiumri alikuwa amemzidi kidogo Rehema akichungulia na kuliona lile gari. Akaachia tabasamu na kulifunga lile geti dogo, kisha akalifungua lile geti kubwa.


Rehema akaliingiza lile gari ndani ya uzio wa ile nyumba na kuliegesha kwenye eneo maalumu la maegesho, jirani na gari jingine aina ya Toyota Hilux double cabin lililokuwa na rangi nyeupe.


Alitulia kidogo kisha akazima injini ya lile gari na kushuka huku akiniashiria nami nishuke, nilishuka kisha Rehema akaifunga vizuri milango ya lile gari kwa rimoti na kuniashiria nimfuate ndani ya ile nyumba.


Yule mdada aliyetufungulia geti alitusalimia kwa unyenyekevu mkubwa, nikamwitikia salamu yake, na hapo nikagundua kuwa alikuwa ni mdada wa kazi.


Wakati nikimfuata Rehema nilikuwa natupa macho yangu kuangalia huku na huko kuyatazama mandhari ya kupendeza ya ile nyumba. Ilikuwa ni nyumba kubwa ya kisasa ya ghorofa moja.


Ilikuwa na madirisha makubwa ya kisasa na baraza kubwa mbele yake iliyopangwa seti moja ya makochi ya sofa. Nje ya nyumba hiyo upande wa kushoto kulikuwa na banda la wazi la kuegeshea magari.


Tulipofika kwenye mlango wa kuingilia nililazimika kupiga piga miguu yangu kwenye zulia dogo lililokuwa pale nje mlangoni ili kukung’uta vumbi kwenye viatu vyangu kisha nikavivua na kubaki na soksi miguuni, nikaingia ndani nikimfuata Rehema.


Niliingia sebuleni, nikatulia kidogo huku nikiyatembeza macho yangu kuitazama ile sebule kubwa yenye samani zote muhimu za kisasa.


Ilikuwa ni sebule kubwa iliyopambwa na seti mbili za makochi ya sofa ya kifahari yaliyopangwa katika mtindo wa kuizunguka sebule ile. Chini kulikuwa sakafu ya vigae vya tarazo vyenye maua mazuri sana na zulia zuri la rangi nyekundu katikati ya sebule.


Juu ya lile zulia kulikuwa na meza nzuri ya kioo yenye umbo la yai iliyokuwa imezungukwa na stuli ndogo nne za sofa. Upande wa kulia wa ile sebule kwenye kona kulikuwa na runinga pana aina ya Samsung iliyokuwa imefungwa ukutani na chini yake kulikuwa na meza fupi nyeusi yenye sistimu ya muziki, decorder ya DSTv yenye chaneli za kimataifa.


Upande mwingine wa ile sebule kwenye kona nyingine kulikuwa na meza fupi ya mapambo na jokofu. Pembeni ya meza ile kulionekana rafu kubwa iliyopangwa vitabu na majarida mengi na juu ya rafu hiyo kuna vinyago vya Kiafrika vilivyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu.


Upande wa kushoto kulikuwa na ukumbi mdogo wa chakula wenye meza kubwa ya chakula yenye umbo la duara iliyozungukwa na viti sita nadhifu vyenye foronya laini. Pia kulikuwa na jokofu kubwa na kabati kubwa la vyombo.


Jirani na ukumbi ule wa chakula kulikuwa na mlango mwingine upande wa nyuma wa hiyo sebule uliokuwa unaelekea jikoni.


Kisha nikauona mlango mwingine wa kioo ambao nilihisi ulikuwa unaelekea kwenye korido ya kuelekea vyumbani na kwenye ngazi zilizokuwa zinaelekea juu ya ghorofa. Sebule ile ilikuwa imependezeshwa na madirisha mapana ya vioo yaliyofunikwa kwa mapazia mazuri marefu.


Rehema alinitazama kwa makini nilipokuwa nimeduwaa kustaajabu na kuachia tabasamu, akaniashiria niketi kwenye kochi. Niliketi pale sebuleni juu ya kochi dogo la sofa, Rehema naye akaketi kwenye kochi lililokuwa mkabala na lile nililokuwa nimeketi na kunitazama kwa makini.


“Karibu sana, Mr Bilali, hapa ndiyo nyumbani kwetu,” hatimaye Rehema alinisemesha kwa mara ya kwanza tangu aliponichukua kule mtaani kwa gari lake na kuja pale nyumbani kwao.


“Nashukuru kupafahamu,” nilijibu huku nikiendelea kuzungusha macho yangu kuyatazama mandhari ya kupendeza ya ile sebule. Rehema alishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Sijui utatumia kinywaji gani?” Rehema aliniuliza huku akinikazia macho yake ya upole.


“Chochote.”


“Nasikitika kuwa tunazo soda, juisi, kahawa, chai, maji… lakini hatuna chochote!” alisema Rehema kwa utani huku akiangua kicheko hafifu na kunifanya nami niangue kicheko.


“Basi nipe juisi na itapendeza zaidi kama itakuwa ya passion,” sikutaka kujivunga, nilisema bila wasiwasi wowote.


Rehema hakusema kitu bali aliinuka na kwenda kwenye ule ukumbi wa chakula, akafungua jokofu na kutoa jagi kubwa la juisi, kisha alifungua kabati na kutoa bilauri moja ndefu, boksi lenye mirija na trei.


Akaweka lile jagi la juisi, ile bilauri na boksi lenye mirija kwenye lile trei na kupiga hatua kuja nilipokuwa nimeketi. Aliweka lile trei juu ya ile meza ya kioo na kuisogeza mbele yangu, kisha akamimina ile juisi kwenye ile bilauri na kutoa mrija mmoja, akauweka ndani ya ile bilauri ya juisi na kunitazama kwa tabasamu. “Karibu, bwana mkubwa.”


“Starehe,” nilijibu huku nami nikiachia tabasamu kabambe.


Jibu langu likamfanya Rehema anitazame kwa mshangao, alitaka kusema neno lakini nikamuona akisita na kuamua kuondoka, akaelekea jikoni.


Nilijua nini kilichokuwa kimemshangaza, ni mimi kujibu ‘starehe’ badala ya neno lililozoeleka kwa wengi la ‘asante’. Kitu ambacho wengi hawakujua ni kwamba neno starehe ndilo neno fasaha pale mtu anapokukaribisha chakula, kwani neno asante hufuatana na kupewa kitu.




“Starehe,” nilijibu huku nami nikiachia tabasamu kabambe.


Jibu langu likamfanya Rehema anitazame kwa mshangao, alitaka kusema neno lakini nikamuona akisita na kuamua kuondoka, akaelekea jikoni.


Nilijua nini kilichokuwa kimemshangaza, ni mimi kujibu ‘starehe’ badala ya neno lililozoeleka kwa wengi la ‘asante’. Kitu ambacho wengi hawakujua ni kwamba neno starehe ndilo neno fasaha pale mtu anapokukaribisha chakula, kwani neno asante hufuatana na kupewa kitu.


Endelea...


Nikiwa natafakari mara nikamuona Rehema akirudi pale sebuleni huku akiwa amebeba sahani yenye sambusa mbili na soseji mbili na kuiweka pale juu ya ile meza ya kioo.


“Samahani, Bilali, nitakuacha kidogo na nitarejea baada ya kama dakika mbili hivi, jisikie huru,” aliniambia na kusimama akisubiri ruhusa yangu.


“Usihofu juu yangu, unaruhusiwa kiroho safi,” nilimwambia huku nikiachia kicheko hafifu. Rehema akaiwasha ile runinga na kuniwekea chaneli ya filamu kisha akaondoka haraka na kuufuata ule mlango wa kioo, akaufungua na kupotelea ndani.


Nilibaki pale sebuleni nikiwa nakunywa juisi na “vitafunwa” taratibu huku nikiwa natazama ile sinema iliyokuwa ikioneshwa kwenye ile runinga pana, ilikuwa ni sinema nzuri sana ya ‘Catch Me If You Can’ iliyosimulia kisa cha tapeli mmoja mwenye akili sana ambaye hajawahi kutokea duniani.


Niliwahi kuiona sinema hiyo mara kadhaa lakini sikuwahi kuishiwa hamu, kwani huyo tapeli aliyekuwa akifahamika kwa jina la Frank W. Abagnale Jr. alikuwa amefanikiwa kuwakwepa FBI na askari wengine kwa miaka mingi kiasi cha kuamua kumpa ajira alipoamua kuachana na utapeli.


Baada ya muda Rehema alitokea tena akiwa kabadilisha nguo na kuketi juu ya kochi jingine huku akinitazama kwa tabasamu. Safari hii alionekana kuchangamka zaidi na mkononi alikuwa kashika simu yake kubwa ya kisasa.


“I hope you are not bored, maana nimekuacha peke yako muda mrefu. Si unajua tena…” Rehema alisema huku akijiweka vizuri kwenye lile sofa. Nikaachia tabasamu huku nikijiweka vizuri pale kwenye sofa.


“Hapana… infact I’m enjoying! Maana hii ni sehemu tulivu sana tofauti na kule kwetu Uswahilini,” nilisema huku nikiachia tabasamu.


Rehema naye aliachia tabasamu na kuinuka akafuata bilauri nyingine na kuja kujimiminia juisi, kisha akafyonza ile juisi kidogo huku akiisikilizia jinsi ilivyokuwa ikipita kwenye koo lake na kutua tumboni huku akionekana kutafakari jambo.


Nilitamani sana kujua alichokuwa akiwaza lakini sikujua aliwaza nini, nilimuona akifyonza tena juisi kisha akapiga mwayo mrefu huku akijinyoosha akionekana kuchoka.


Nami nikafyonza funda kubwa la juisi kinywani mwangu na kuisikilizia juisi ilivyokuwa inaingia tumboni mwangu kisha nikashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.


“Unaonekana umechoka sana au pengine hukupata usingizi usiku!” nikamwambia Rehema huku nikimtazama kwa makini.


Rehema aliguna huku akiachia tabasamu pana. “Ni kweli sikupata usingizi usiku, hata hivyo usijali sana, nipo sawa!”


“Punguza mawazo,” nilisema huku nikimtazama kwa makini katika namna ya kutafuta mazungumzo zaidi.


“Ahsante! Mawazo ni sehemu ya maisha ya binadamu, sometimes unajikuta unawaza tu na hauna namna ya kukwepa. Hata hivyo nashukuru kwa ushauri wako, nitauzingatia.”


Alisema hivyo kisha kikafuata kipindi kingine cha ukimya mrefu, Rehema alionekana kuwaza mbali sana. Nilimtazama kwa makini kisha nikashusha tena pumzi na kujiweka sawa.


“Halafu hujanieleza chochote kuhusu siku ile ya tukio kule Kibiti… Maana sijajua ilikuwaje baada ya mimi kupoteza fahamu!” nilisema huku nikimkazia macho Rehema.


Rehema alinitazama kwa kitambo kirefu kisha akaachia tabasamu lililoonekana ni la kulazimisha na lililoficha huzuni ndani yake.


“Kwa kweli sipendi kabisa kukumbuka lile tukio maana halikuniacha salama…” Rehema aliongea kwa huzuni.


“Unajua nilichanganyikiwa kabisa na ilibidi nipewe tiba maalumu ya kisaikolojia kutoka kwa wataalamu wa saikolojia na afya ya akili ndipo nikaweza kukaa sawa. Nisamehe sana Bilali sikukumbuka tena kuja hospitali kukuona,” Rehema alizidi kuongea kwa huzuni huku machozi yakimlenga machoni.


“Usijali, hata hivyo Mungu kaniponya na katukutanisha tena tukiwa hai,” nilimwambia Rehema katika namna ya kumfariji.


Muda huo huo nikaona mlango mkubwa wa barazani ukifunguliwa na mwanamke mmoja wa makamo, mnene wa wastani, akaingia pale sebuleni akitokea nje. Hakuwa mfupi wala mrefu bali alikuwa na kimo cha wastani na alikuwa mweupe.


Hakuwa mwanamke wa kumtazama mara moja tu. Ingawa alionekana kuwa na umri mkubwa wa takriban miaka hamsini, lakini ilikuwa ni vigumu mno kumtofautisha na wasichana wenye umri mdogo kutokana na jinsi alivyoonekana.


Umbo lake lilisheheni vema na kunesanesa, lilikuwa ni umbo ambalo lingeweza kulifanya kila jicho lililomuona kumtazama mara mbilimbili. Wakati namtazama nikawa najiuliza kama aliweza kuonekana mrembo kiasi kile katika umri huo, je, alionekanaje enzi za usichana wake?


Kisura alifanana sana na Rehema na alikuwa na macho makubwa na mazuri sana yaliyokuwa ya aina yake, ni aina ya yale macho yaliyoita kwa mng’aro sadifu, yakiambatana na kope nyingi nyeusi ambazo ziliachia nafasi kwa nyusi ili zipate kujidai. Midomo yake ilikuwa minene yenye kingo nyepesi na mikunjo midogo midogo.


Na hata tembea yake ilikuwa ya aina yake kabisa, ilishindwa kumtofautisha na wasichana vigoli. Ilikuwa ni adimu kuipata kwa wasichana wengi ambao pamoja na kujikwatua vilivyo, bado walishindwa kupata miondoko mizuri kama yake!


Yule mama alisimama na kuachia tabasamu pale alipotuona tumeketi sebuleni, akashusha pumzi ndefu na kwenda moja kwa moja alipokuwa ameketi Rehema, naye akaketi. Nikamuona Rehema akimuegemea yule mwanamke kama kitoto kinachodeka kwa mama yake.


Nilibaki kimya nikiwa nimeganda nikimkodolea macho pasipo kusema neno lolote, kama niliyekuwa nimepigwa na shoti mbaya ya umeme, na bila kuambiwa nikahisi kuwa yule alikuwa ni mzazi wa Rehema.


Rehema alinitazama kwa makini na kuachia tabasamu kisha akaweka mkono wake mmoja juu ya paja la yule mama.


“Kutana na Bi Aisha, mama yangu mkubwa,” Rehema aliniambia kisha akamgeukia Bi Aisha, “Mama, kutana na Bilali…” akasita kidogo huku akinikazia macho.


“Bilali Ibrahim,” nikawahi kusema.


“Ni rafiki yangu ambaye Mungu kanikutanisha naye katika mazingira ya ajabu sana. Huyu ndiye yule kijana aliyeniokoa kule porini Kibiti siku ile yalipotokea mauaji,” alisema Rehema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


Bi Aisha alionekana kushtuka sana, alinitumbulia macho na kuanza kulengwa na machozi, alisimama na kunyoosha mkono wake wa kulia kwa bashasha, akaukutanisha na ule wangu huku machozi yakizidi kumlengalenga machoni.


“Nimefurahi sana kukutana nawe mama… shikamoo!” niliwahi kumsalimia kwa bashasha huku nikiachia tabasamu.


“Marhaba baba, nami nimefurahi sana kukufahamu na pole kwa yote yaliyotokea…” alisema, sauti yake ilikuwa ya upole sana alipoongea nami.


“Nimekwisha poa, mama,” nilijibu kwa unyenyekevu.


“Karibu sana mwanangu, niliambiwa kuwa ulilazwa Sewa Haji pale Muhimbili, lakini tusamehe sana hatukuweza kuja kukuona,” alisema Bi Aisha kwa huzuni huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.



“Nimefurahi sana kukutana nawe mama… shikamoo!” niliwahi kumsalimia kwa bashasha huku nikiachia tabasamu.


“Marhaba baba, nami nimefurahi sana kukufahamu na pole kwa yote yaliyotokea…” alisema, sauti yake ilikuwa ya upole sana alipoongea nami.


“Nimekwisha poa, mama,” nilijibu kwa unyenyekevu.


“Karibu sana mwanangu, niliambiwa kuwa ulilazwa Sewa Haji pale Muhimbili, lakini tusamehe sana hatukuweza kuja kukuona,” alisema Bi Aisha kwa huzuni huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.


Endelea...


“Usijali mama,” nilijibu huku nikihisi mwili wangu ukinisisimka sana. Mbali na urembo aliokuwa nao yule mama lakini niligundua kitu kingine kikubwa zaidi kilichokamilisha uzuri na mvuto wake, ni upole wake.


Alikuwa ni mpole pindi aongeapo, alionekana mpole atembeapo na pengine hata alipokuwa katika shughuli zingine.


“Maana ule mkasa ulimfanya dada yako kuchanganyikiwa kabisa, wazimu si wazimu basi ni shida tupu, hata hivyo tunamshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea,” aliongea Bi Aisha kwa upole.


“Ni kweli mama, tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo, maana ni mapenzi yake hadi leo tuko hai,” nami nilisema kumuunga mkono yule mama.


Yule mama alirudi kuketi na kukatokea ukimya wa kitambo kifupi, niliwaona Bi Aisha na Rehema wakiwa wamezama kwenye mawazo kila mmoja akiwaza mbali, kisha kama aliyegutuka, Bi Aisha aliitazama saa yake ya mkononi na kuinuka.


“Karibu mwanangu, jisikie huru mimi nipo ndani kuna kitu nafanya,” alisema huku akiondoka.


“Nashukuru, mama,” nilijibu huku nikimsindikiza kwa macho hadi alipopotelea ndani. Kisha niligeuka kumtazama Rehema kwa makini.


“Inaonekana mama yako ni mcheshi sana?” nilimuuliza nikiwa nimekazia macho.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog