Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

JINO KWA JINO - 5

   

Simulizi : Jino Kwa Jino

Sehemu Ya : Tano (5)


   “Nini kwani?” Akahoji Rebecca naye akitabasamu lakini yeye akimuangalia.

   “Unasogeza mbele cd ya kazi hili uendelee na mada yako ya waafrika wachawi… Hayo hayajibiki sababu siyajui na nishaulizwa sana na sisi wewe tu… Hahahaha hahahaha hahahaha!”

   “Khaah! Muhuni kakutana na muhuni.. Sawa bwana mkubwa umeninyima fursa niliyokuwa na itamani” Akaongea kinyonge Rebecca kana kwamba hajatoka kufurahi sekunde chache zilizopita maana alinyongeka kweli kwa sauti aliyoitoa.

   “Khaahaah! Mi mwenyewe naitamani fursa fulani juu yako nikiiomba naogopa nitatimuliwa… Lol!!”

   “Mmmmh!... Basi tule kwanza maana mi namaliza wewe bado”

Utani wao waliukatizia wakamalizia supu zao wakamuita muhudumu atoe vyombo vile kuondoa karaha kisha ‘TSC’ akatoa Bluetooth earphone toka kwenye begi lake a Rebecca naye akafanya vile katika begi lake dogo ambalo naye ni kawaida kutembea nalo kama ilivyo kwa Agent Kai.

   “Kazini sasa…. Tuzisikilize hizi kisha tutazijadili kwa pamoja sisi wawili au kama itabidi tutawaongeza na wenzetu katika mjadala kama kuna ulazima” Akaongea Agent Kai kisha karuhusu audio ya kwanza waisikilize ambapo kwanza ilianza sauti ile ambayo yeye kwake ni kama imezoeleka kuisikia maana ni ya dada anayetamani sana kujua nyendo zake akiwa akijua tu anaitwa Valentina ingawa kwa akili zakeza kazi za TSC alihisi si jina halisi.

Audio ya kwanza! Ilikuwa ya maongezi ya mtu aliyepigiwa simu na mwanadada huyu akipiga tokea Guatemala kwenda Mexico mtu yule mwanaume akipewa taarifa kuwa kuna kijana ambaye ameagizwa amfuatilie aliyetajwa mkurugenzi wa OCLA Kamanda Muniain, kijana yule ameweza kuwaona kwa pamoja mkurugenzi na kijana wake aliyeitwa Norman, hapo mpigiwa simu ambaye ni mwanaume mwenye sauti nzito sana tena ya kuonyesha ni mtu mwenye amri nyingi sana kwa mwanadada anayeongea naye alisisitiza watu hao wafuatiliwe kwa umakini na siku hii waspoteze nafasi adimu waakikishe wanawateka wote na kwenda kuwahoji wapi ilipopelekwa flash, simu ilikatwa ikawa mwisho wa audio iliyokuwa si ndefu sana.

Audio ya pili! Simu ilipigwa kutoka kwa mwanadada yule akipiga kwenda kwenye namba ambazo code number yake zilionekana ni za Guatemala ambapo mwanadada yule alisikika akimtaja mtu aliyempigia kwa jina moja la Maquez wakati anaanza tu kuongea naye, alimpa maelekezo waelekee barabara ya Jocotenango na kisha waingie mtaa wa Carratera San Felipe kuna mgahawa wa watalii unaoitwa Filadelifia ambako watawakuta Kamanda Muniain na Detective Norman wakiwa na watu wengine wawili hapo wasiogope chochote waanzishe mtiti utakaofanikisha kuwachukua Muniain na Norman, mwanadada akasisitiza lisifanyike kosa lolote na polisi wataarifiwa wafike huko ikiwa wao wamemaliza kazi hivyo wasiogope kutumia bunduki kutisha watu hata kuua watu kama itahitajika ilimradi dhamira itimie.

Audio ya tatu! Simu ya mwanadada huyu ilipigwa kuelekea kwenye namba zingine zenye code number za Guatemala tena ila mtu huyu aliyepigiwa alianza kwa kutamkwa Inspekta tu na maongezi yalipoendelea yaliwajuza wasikilizaji hawa kuwa mpigiwa ni askari wa jeshi la polisi mwenye cheo na mamlaka ya juu ya kiamri, maana alikubali alichoelekezwa na mwanadada huyu kuwa TRJ wanaenda kufanya kazi mtaa wa Carratera wanaomba wasiingiliwe wapewe dakika arobaini za kufanya kazi hivyo yeye Inspekta acheleweshe kupeleka askari ambao kikawaida wangewai eneo la tukio, makubaliano yakafanyika na kwa uzoefu wao Agent Kai na Special Agent Rebecca waliweza tambua huyu atakuwa kiongozi mkubwa kabisa katika jeshi la polisi katika mji huu wa Antigua maana usalama wa mali na wananchi upo chini yake hivyo ameingizwa katika mtandao wa genge linaloitwa TRJ ambalo wao kina ‘TSC’ washawai sikia juu ya genge la kimexico la mihadarati linaloitwa ‘THE RED JAGUAR’ (TRJ).

Mwisho wa sehemu ya arobaini na nane (48)

‘TRJ’ moja ya watu watatu wa safu ya juu wamekutana kwenye kikao na mwanadada Mariana ambaye naye ni miongoni mwa watu walio safu ya juu wa genge linalohusika na ulanguzi wa madawa ya kulevya, genge la ‘THE RED JAGUAR’ (TRJ).

Kikao cha moto! Chenye maswali ya moto yaliyoelekezwa kwa Mariana hili hawa wengine waweze kung’amua wao kama wao wanaanzia wapi katika kazi iliyowaleta ndani ya Guatemala.

Maamuzi yanapita kazi ianze mara moja kusaka kundi linaloongozwa na Kamanda Muniain na Detective Norman.

Upande wa Agent Kai ‘TSC’ na Special Agent Rebecca nao wako mgahawani wakipata supu wanaanza pia na kazi ya kusikiliza audio alizotumiwa ‘TSC’ na bibie Lizy Roby.

Nini kitafuata?




Audio ya kwanza! Ilikuwa ya maongezi ya mtu aliyepigiwa simu na mwanadada huyu mtu yule akipewa taarifa kuwa kuna kijana ambaye ameagizwa amfuatilie aliyetajwa mkurugenzi wa OCLA na kijana yule ameweza kuwaona kwa pamoja mkurugenzi na kijana wake aliyeitwa Norman, hapo mpigiwa simu ambaye ni mwanaume mwenye sauti nzito sana tena ya kuonyesha ni mtu mwenye amri nyingi sana kwa mwanadada anayeongea naye alisisitiza watu hao wafuatiliwe kwa umakini na siku hii waspoteze nafasi adimu waakikishe wanawateka wote na kwenda kuwahoji wapi ilipopelekwa flash, simu ilikatwa ikawa mwisho wa audio iliyokuwa si ndefu sana.

Audio ya pili! Simu ilipigwa kutoka kwa mwanadada yule akipiga kwenda kwenye namba ambazo code number yake zilionekana ni za Guatemala ambapo mwanadada yule alisikika akimtaja mtu aliyempigia kwa jina moja la Maquez wakati anaanza tu kuongea naye, alimpa maelekezo waelekee barabara ya Jocotenango na kisha waingie mtaa wa Carratera San Felipe kuna mgahawa wa watalii unaoitwa Filadelifia ambako watawakuta Kamanda Muniain na Detective Norman wakiwa na watu wengine wawili hapo wasiogope chochote waanzishe mtiti utakaofanikisha kuwachukua Muniain na Norman, mwanadada akasisitiza lisifanyike kosa lolote na polisi wataarifiwa wafike huko ikiwa wao wamemaliza kazi hivyo wasiogope kutumia bunduki kutisha watu hata kuua watu kama itahitajika ilimradi dhamira itimie.

Audio ya tatu! Simu ya mwanadada huyu ilipigwa kuelekea kwenye namba ingine yenye code number za Guatemala tena ila mtu huyu aliyepigiwa alianza kwa kutamkwa Inspekta tu na maongezi yalipoendelea yaliwajuza wasikilizaji hawa kuwa mpigiwa ni askari wa jeshi la polisi mwenye cheo na mamlaka ya juu ya kiamri, maana alikubali alichoelekezwa na mwanadada huyu kuwa TRJ wanaenda kufanya kazi mtaa wa Carratera wanaomba wasiingiliwe wapewe dakika arobaini za kufanya kazi hivyo yeye Inspekta acheleweshe kupeleka askari ambao kikawaida wangewai eneo la tukio, makubaliano yakafanyika na kwa uzoefu wao Agent Kai na Special Agent Rebecca waliweza tambua huyu atakuwa kiongozi mkubwa kabisa katika jeshi la polisi katika mji huu wa Antigua maana usalama wa mali na wananchi upo chini yake hivyo ameingizwa katika mtandao wa genge linaloitwa TRJ ambalo wao kina ‘TSC’ washawai sikia juu ya genge la kimexico la mihadarati linaloitwa ‘THE RED JAGUAR’ (TRJ).

ENDELEA NA UTAMU WA DODO ASALI!!

ALHAMISI

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Zimeisha?” Akahoji S.A Rebecca

   “Lizy ametuma tatu tu akasema tusikilize hizi kwanza… Ni audio zenye mnuso wa harufu nzuri upande wetu” Akajibu kirefu na kufafanua ‘TSC’.

   “Kwa ilipoishia boss haiwezekani ikawa mwisho wa namba hiyo kutumika… Tumuulize Lizy kabla hatujaanza kuzijadili kwa pamoja” Akaweka hoja Rebecca.

   “Okay! Acha nimpigie..!”Akajibu na kunyanyua simu yake iliyokuwa pembeni ya Ipad akatafuta kwenye phone book namba za Lizy Roby na alipopiga tu ilipokelewa bila hata muito wa kwanza kuita vizuri upande huo wa pili.

   “TSC!” Upande wa pili ikasikika sauti ikitaja jina la siri la Agent Kai.

   “Umepokea upesi sana…! Niko na mrembo hapa..Tunataka kujua kama audio za hii namba hujapata zingine?”

   “Nimepata… Nilituma kwako tatu ngoja nikumalizie mbili za mwisho ambazo kwa sasa hajaongeza zingine”

   “Ahsante mpendwa… Acha tufanyie kazi kwanza..!” Akamalizia hivyo Agent Kai, hakusubiri jibu akakata simu maana anamjua Lizy kwa utani unaofanania na ukweli ni kiboko.

Dakika nne mbele audio walizotaka zilitumwa na mara moja wakaanza kuzisikiliza kama muendelezo.

Audio ya nne! Hii iliwasikitisha wote mpigaji na mpigiwaji wote wakisikitika kwa kosa la kizembe lililofanywa na mwanadada kutuma kikosi ambacho wote walisema na kidhaifu na kilichowafanya wote kuumizwa na kikosi icho ni kuwa kiongozi wa kikosi alikuwa si mzoefu wa kuongoza operesheni ya kupambana na watu wenye ujuzi na uzoefu mkubwa, taarifa aliyopewa aliyeitwa boss ilisema watu wao kumi na tatu wameuliwa kwa kupigwa risasi, asilimia themanini wakiwa wameuliwa kwa risasi za vichwa, aliyeitwa mkuu alimuahidi mwanadada kuwa ataitisha kikao cha wana bodi yake kisha atatuma ujumbe kwake maamuzi yaliyoamriwa na bodi yake.

Audio ya tano! Mwanadada alikuwa akimpa taarifa inspekta wa polisi kuwa mambo hayajaenda sawa kama watakavyo na inspekta akajibu lazima apeleke askari polisi angalau wananchi waende kuwa na imani na jeshi la polisi, aliweza kumsihi aondoke upesi kama anataka mambo yake yasiwe na mapindo pindo. Mwisho mpigaji wa simu ambaye ni mwanamke ambaye yeye ‘TSC’ni mtu ambaye ana hamu kubwa ya kumuona na kumuingiza katika kivambo chake amuhoji alipo Jogre wa DEA, alifikia makubaliano yeye anawapigia watu wake kama wanashindwa kuwapata waliowafuata waondoke muda wa makubaliano umeisha.

Audio ya sita! Ilikuwa ya mwanamke akipiga tena kwenye namba zenye code number za mexico mtandao wa Sprinter ambao ni wa Marekani lakini unatumika mpaka nchi ya Mexico na nchi zingine za jirani na Marekani, hii audio iliweza kusikilizwa na majasusi hawa ambapo mwanadada alisikika akisikitika kuwa kazi imefeli na kwa masikitiko makubwa kiongozi wa msafara wa polisi aliyetumwa na Inspekta ameweza kumtaarifu yeye mwanadada kuwa watu kumi na tatu wa TRJ wamepigwa risasi hii ikimaanisha kati ya vijana wa kazi kumi na tano waliotumwa kuelekea huko ni wawili tu waliopona na wawili wenyewe ni madreva wa gari zilizowapeleka na ni kwa sababu wao walibaki kwenye magari wakiwasubiri wenzao na pengine na wao kwa sasa wangekuwa marehemu, hii audio Agent Kai ilimfanya atabasamu maana muhusika wa kuwafyeka watu hao alikuwa yeye na idadi yao alishaijua kupitia vyombo  vya habari vilivyoweza kupewa habari kamili toka kwa afisa wa habari wa polisi wa mji wa manispaa ya Antigua.

Bosi alisikika akisikitika sana na kutamani hata angekuwa Guatemala alifoka sana kumfokea mwanadada akimalumu kwa dharau na kusababisha hasara ya rasilimali watu wao, ikawa mwanadada akiomba msamaha na kusema atarudia kosa jingine tena, bosi akamwambia ataitisha kikao cha viongozi wa juu walioko eneo alilolitaja ni Mexico kisha watamtaarifu yeye mwanadada nini wameamua. Audio hii iliishia hivyo kwani upande mmoja ulikata simu.

Audio ya saba! Ilikuwa ya simu ya code number za mexico mtandao wa sprinter ulipiga kuelekea simu ya mwanadada na ilikuwa ya siku hii ya alhamisi si usiku kama zingine. Hii mpigaji mwanaume mwenye sauti nzito yenye kiburi cha madaraka fulani ilisikika ikimuuliza mwanadada kuhusu mtu aliyekuwa akimfuatilia Kamanda Muniain kwa siri kila anapoenda, mpigaji alitaka kujua yuko wapi? Ndipo mwanadada akaomba samahani kwa kushindwa kutoa taarifa zake kisha akamtaja jina mtu huyo kuwa anaitwa Gadiano Soria na akamalizia kusema mtu huyo Kamanda Muniain na kijana wake Norman waliomba kwa polisi waondoke naye hivyo yupo mikononi mwa Norman na Muniain na akamalizia mwanadada kwa kusema ‘inauma sana’. Bosi akalaumu kuwa ni uzembe mkubwa umefanywa kwa mwanadada na mtu mwingine aliyetajwa na bosi kuwa anaitwa alto akaongezea kwa kusema huyo alto yupo Canada kwa muda huu hivyo atampigia kumtaarifu masikitiko, mwanadada akakubali lawama toka kwa boss wake kisha boss akamuuliza amejipangaje? Mwanadada akajibu wamejipanga kumfuatilia kwa ukaribu Kamanda Muniain akisema amekuwa kiburi mpaka kwa mawaziri ambao yeye mwanadada na wenzake wanawategemea katika mambo yao amekuwa akiwagomea kuwasikiliza juu ya kufuata matakwa yao wao.

Hapo boss akasema amechukua maamuzi yeye ameamua kuwa ataongeza nguvu ya watu watatu wazito akawataja majina kuwa ni Aristos Mosquera, mtu mzito Koplo Maxiwell Zuantejo na Molina Qadrado kuongeza nguvu katika operesheni hii akisema baada ya masaa mawili tu watu hao watawasili alipo mwanadada, akisisitiza mpaka siku ya kesho ikifika waipate flashdisk iliyo kwa Norman. Hapo simu ikakatwa na  hii ilikuwa simu ya mwisho au ni audio ya mwisho iliyotumwa na Lizy kuja kwa Agent Kai.

   “Robo pazia imesogea pembeni sasa tunaweza chungulia kwenye upenyo mdogo tukaona kwa tabu kilichomo ndani… Audio hizi zitatufikisha mahala Rebecca…!” Akaongea ‘TSC’ akiisogeza pembeni kidogo Ipad ilipo mezani kisha akasogeza karibu bilauri ya juisi akamimina glasini kisha akanyanyua glasi na kugonga funda tatu za kufuatana, alipoitua glasi chini wakaangaliana na Rebecca wakatabasamu.

   “Je vile nilivyoweza kuchanganua ni kama vile ulivyochanganua wewe boss? Au nisubiri tu ukiamini nimeweza changanua kama ulivyo wewe fundi mkuu?”Akahoji Rebecca wakikaziana macho.

   “Naujua ubongo wako… Wewe ni chagua langu kuu katika kazi zangu kijasusi… Nakuamini sana tena sana tena kuliko kina S.A Silla na Investigator Miller na si kama napenda nisiwaamini kiasi nachokuamini laah hashaah! Nakuamini sababu wewe nakujua najua ufanyaji wako wa kazi wale siwajui sana ingawa naamini na wao ni wajuzi sana katika kazi hii… Twende katika ufafanuzi nitajitahidi kufafanua vizuri na kama nitakosea utasema usiogope lakini ilivyo muongozo wa kazi upo hapa” Akaongea Agent Kai ‘TSC’ akiweka macho ambayo hapa aliweka miwani kando hivyo walikuwa wakiangaliana macho kwa macho majasusi hawa.

  “Kwanza hapa kuna jibu la swali kuwa tunapambana na kina nani? Kina nani wanamshikilia Jogre? Jibu limekuja ni TRJ… Sasa tunaweza kufuatilia juu yao watu hawa tukikusanya habari zao katika vyanzo vyetu mbalimbali maana nasikia walipindua meza ya magenge mawili hasimu yaliyo huko Mexico, inaelekea hapa GTL kuna ngome yao kubwa sana” Akaanza ufafanuzi ‘TSC’.

  “Ni kweli boss! Nami nilielewa hivyo hivyo…. Kwakuwa tumeungana kikazi na watu wa hapa na tena kwa maelezo ya audio hizi tulizosikiliza tunaona uadui mkubwa uliopo baina yao” Akaongea Rebecca kisha akanyanyua glasi ya juisi akanywa funda mbili na kuishusha ikihitaji kuongezwa kama atahitaji kuendelea kunywa na uzuri bilauri ilikuwa pembeni ina juisi.

  “Jana wakati nilipotoka uwanja wa ndege nilichukua taxi wakati niko ndani ya taxi nilipiga simu kuuliza kina Silla wako wapi? Baada ya kunielekeza walipo wakampa simu Kamanda Muniain akanielekeza uzuri walipo” Agent Kai aliamua aanze kumsimulia vile alivyoingia Guatemala City kisha akaelekea barabara ya Jocotenango akiwa na dreva wa taxi, akaendelea kumuhadithia vile yaliyotokea kule mpaka alipofanya mauaji ambayo yalikamata vyombo vya habari vya Guatemala kiasi ya kwamba Rebecca alipata habari za waliouliwa zikisema wameuliwa na watu wasiojulikana polisi wakiahidi kufanya uchunguzi zaidi kumjua muuaji na waliouliwa ni kina nani.

   “Dah! Mwenzangu umepokelewa na kazi, pole sana na hongera kwa kazi nzito uliyoifanya, nilipokuwa nikisikia juu ya mauaji yaliyotokea nikakumbuka wosia wako mmoja uliowai kuniambia wakati wa mashambulizi ya risasi nijitahidi kulenga kichwa na waliouliwa wameuliwa kwa kulengwa katika vichwa moja kwa moja nikapata hisia kazi hii ni ya mikono ya mwanaume mmoja anayeitwa nyayo za paka” Ilikuwa furaha usoni mwa Rebecca Smith, akifurahia alichotoka kukisikia toka kinywani mwa ‘TSC’.

   “Ndiyo hivyo ndugu yangu… Polisi walipofika ilibidi sisi tujitahidi tusionekane kama tuko na Kamanda Muniain pamoja na Norman, tulikubaliana haraka tujifanye ni moja ya wateja waliojificha ndani wakati wa mashambulizi tukatoka pale ikiwa Norman akimuelekeza kiongozi wa msafara kuwa sisi ni miongoni mwa wateja wa kawaida wanaofika kwenye mgahawa maarufu unaopendwa sana na watalii.. Tulienda kuwasubiri kwenye kona ya kuingilia barabara ya Jocotenango mtaa wa Carratera San Felipe hapo wakaja na kijana ambaye katika hizi audio umesikia akitamkwa kwa jina la Gadiano Soria ingawa wakati tulipokuwa tunamuhoji aligoma kuongea chochote akisema ameonewa na hawajui wale waliofika pale na kuanza kuwashambulia kina Kamanda Muniain… Jamaa ni jeuri haswa hivyo tuliamua kwa pamoja tumuache katika nyumba ambayo inatumiwa na Norman kama kujificha kwake huko Chimaltenango karibu na Greenhouse’s mtaa wa Signs yaani sehemu nyingi za hapa Guatemala City ni sehemu zilizotulia sana lakini huko alipochagua maficho Norman kumezidi zaidi, nimepapenda sana!… Kituo cha kazi na mipango nataka nipendekeze kiwe hapo kwa Norman ni nje ya mji masaa mawili toka Guatemala centre kwa jinsi tulivyotumia muda katika gari ya Norman..” Akaeleza kwa urefu ‘TSC’ alipopumzika akanyanyua glasi ya juisi na kupiga funda mtiririko maana moja lililokuwa zito nusu glasi ikawa imeondoka.

  “Kazi nzuri boss… Hizi audio alizotutumia boss Lizy naamini zitatufikisha mahala tunapohitaji..!”Akaongea Rebecca Smith.

  “Kazi nzuri imefanywa na Lizy… Nataka ndugu zetu nao tukawasikilizishe hizi audio kisha tupange kazi mara moja, kazi ya kwanza nataka tumjue Inspekta wa polisi wa mji wa Antigua ni nani? Naye achukuliwe kwa mahojiano mara moja ana mengi ya kutujuza na ndiyo ataweza kutuvutia mwanamke hitaji letu..”Macho ya Agent Kai yenye ujanja mwingi sana ambao pamoja na kujitahidi kwake kuuficha uwa akikutana na jasusi wa kukaribia viwango vya juu basi uweza kumuhisi vile anavyoficha mengi, simu yake ilianza kuita hivyo macho haya yalikwenda kasi mahala ilipo pembeni ya meza waliyokaa, akatizama mpigaji nani katika kioo cha simu hapo akaona kuwa ni Investigator Miller ndiye anayepiga maana jina alilisevu kimafumbo katika ‘phone book’.

   “Salama huku! Vipi huko?”Akaongea kwa kasi Agent Kai ‘TSC’ baada ya kupokea kwa kusugua kioo kama ilivyo desturi ya simu za smartphone.

   “Salama kabisa… Mnafika muda gani?”

   “Nyinyi mshafika tayari huko?”

   “Ndiyo tushafika sasa tuna dakika kama ishirini toka tutimie wote..”

   “Mkurugenzi amefika?”

   “Ametujuza yuko njiani kuja huku kilichomchelewesha alikwenda ikulu kuonana na mkuu wa nchi na pia ametujuza familia yake yote yaani mke wake na watoto wake wadogo kawapeleka huko kama ulivyomshauri jana sasa yuko tayari kwa kazi rasmi..!”

   “Safi sana kama amefanikisha hili maana mara nyingi magenge utumia familia za watu walio katika misigano nao kupata wanachohitaji… Mimi niko na RS tulikuwa tunapata supu kwanza na pia nikimuhadithia mambo ya jana toka naingia GTL, naomba mtutegemee hapo baada ya masaa mawili tuje tupange jinsi gani tunaanza kazi leo maana jamaa nao wameongeza wateja wa mbolea za kahawa wameingia leo hii hii hivyo muwe tayari kwa huduma nzuri..” Akaongea Agent Kai kama ilivyo ada yake yeye kuongea kwa tafsida ni kawaida sana kwake na uzuri anaoongea nao uwa wanamuelewa sababu ni lugha ya kazi za kazi hivyo kwa majasusi wazuri haiwasumbui.

   “Sawa tunawasubiri…”

   “Tuna mengi tunakuja nayo..!”

Walimaliza hivyo na simu ikakatwa upande wa Investigator Miller.

   “Washafika Sign Street?” Akahoji Special Agent Rebecca akimkazia macho ‘TSC’.

   “Wana dakika ishirini toka wafike inaelekea wameongozana kwenda huko kwa gari moja ya kukodi… Jana niliondoka nao, Norman alitusindikiza kwa moja ya gari zake hadi huku mjini itabidi nimuombe gari moja kwakuwa nimeyaona matatu pale ambayo nahisi ni magari ambayo hayajatumika kwa muda mrefu… Tunatakiwa kuondoka hapa kuelekea huko Chimaltenango”

Walimalizia juisi zao bila kubakiza katika bilauri hapa wote hawa huyu mwanadada wa kizungu Special Agent Rebecca Smith binti aliyekulia mitaa ya jiji la Frankfort mji mkuu wa  jimbo la Kentucky, Marekani na kijana wa uswahilini haswa mitaa ya Morogoro, Tanzania aliyejikuta akiitumikia Marekani, walikuwa wakipenda sana juisi za matunda asilia iliyokamuliwa kwa blander si juisi iliyopita katika mashine za viwandani na kuwekwa makemikali.

Waliondoka wakiongozana kama mwanaume aliyeongozana na mkewe maana walishikana mikono kama ilivyo kwa watu wengi walioongozana na wenza wao.

Mwisho wa sehemu ya arobaini na tisa (49)

Audio za simu zilizotumwa na mtaalamu wa kompyuta mwanadada Lizy Roby baada ya kudukua simu ya mwanamke wanayemfuatilia namba yake ya simu bila yeye kujua zinaweza kuwaamsha morali ya kazi zaidi.

Nini kitaendelea katika sehemu inayofuata?

Majibu kamili yako katika sehemu hiyo ya hamsini na nyinginezo zinazokuja.



   “Salama kabisa… Mnafika muda gani?”

   “Nyinyi mshafika tayari huko?”

   “Ndiyo tushafika sasa tuna dakika kama ishirini toka tutimie wote..”

   “Mkurugenzi amefika?”

   “Ametujuza yuko njiani kuja huku kilichomchelewesha alikwenda ikulu kuonana na mkuu wa nchi na pia ametujuza familia yake yote yaani mke wake na watoto wake wadogo kawapeleka huko kama ulivyomshauri jana sasa yuko tayari kwa kazi rasmi..!”

   “Safi sana kama amefanikisha hili maana mara nyingi magenge utumia familia za watu walio katika misigano nao kupata wanachohitaji… Mimi niko na RS tulikuwa tunapata supu kwanza na pia nikimuhadithia mambo ya jana toka naingia GTL, naomba mtutegemee hapo baada ya masaa mawili tuje tupange jinsi gani tunaanza kazi leo maana jamaa nao wameongeza wateja wa mbolea za kahawa wameingia leo hii hii hivyo muwe tayari kwa huduma nzuri..” Akaongea Agent Kai kama ilivyo ada yake yeye kuongea kwa tafsida ni kawaida sana kwake na uzuri anaoongea nao uwa wanamuelewa sababu ni lugha ya kazi za kazi hivyo kwa majasusi wazuri haiwasumbui.

   “Sawa tunawasubiri…”

   “Tuna mengi tunakuja nayo..!”

Walimaliza hivyo na simu ikakatwa upande wa Investigator Miller.

   “Washafika Sign Street?” Akahoji Special Agent Rebecca akimkazia macho ‘TSC’.

   “Wana dakika ishirini toka wafike inaelekea wameongozana kwenda huko kwa gari moja ya kukodi… Jana niliondoka nao, Norman alitusindikiza kwa moja ya gari zake hadi huku mjini itabidi nimuombe gari moja kwakuwa nimeyaona matatu pale ambayo nahisi ni magari ambayo hayajatumika kwa muda mrefu… Tunatakiwa kuondoka hapa kuelekea huko Chimaltenango”

Walimalizia juisi zao bila kubakiza katika bilauri hapa wote hawa huyu mwanadada wa kizungu Special Agent Rebecca Smith binti aliyekulia mitaa ya jiji la Frankfort mji mkuu wa  jimbo la Kentucky, Marekani na kijana wa uswahilini haswa mitaa ya Morogoro, Tanzania aliyejikuta akiitumikia Marekani, walikuwa wakipenda sana juisi za matunda asilia iliyokamuliwa kwa blander si juisi iliyopita katika mashine za viwandani na kuwekwa makemikali.

Waliondoka wakiongozana kama mwanaume aliyeongozana na mkewe maana walishikana mikono kama ilivyo kwa watu wengi walioongozana na wenza wao.

ENDELEA NA DODO ASALI..!!

ALHAMISI MCHANA

CHIMALTENANGO, ANTIGUA-GUATEMALA

Saa nane na dakika tano mchana wa siku ya alhamisi iliwakuta Agent Kai ‘Tsc’ na msaidizi wake wa karibu Special Agent Rebecca Smith wakifunguliwa  kimlango kidogo cha geti  lililoshikana na ukuta unaozunguka nyumba na Detective Norman, walikuwa wamewasili katika nyumba ambayo usiku uliopita ‘TSC’ alifika akiwa kaongozana na majasusi wenzake wa DEA na huyu Norman Cabrera wakiwa na mateka wao.

   “Karibuni waheshimiwa… Mmefika muda muafaka sana!” Akawapa ukaribisho Detective Norman, mchana huu ‘TSC’ aliweza kumuona uzuri kijana huyu wanayerandana naye umri tofauti ikiwa ni rangi zao, Norman mzungu wa kilatini amerika na Agent Kai kama mnavyomjua ni mmarekani mweusi.

   “Ahsante sana… Tumeshakaribia, muda muafaka mlikuwa mkitaka kutoka?” Akashukuru ukaribisho waliopewa na kuhoji huku wakimpisha mwenyeji wao afunge mlango ule waliofunguliwa.

   “Chakula kilichoandaliwa na mpishi wa kiume wa ki Guatemala kimeiva tayari mapoti yapo mezani kwa ajili walaji kula” Akajibu Detective Norman akitabasamu kwa furaha sana maana meno yote yanayostahili kuonekana katika uso wa tabasamu yalionekana vizuri sana.

   “Okay! Safi sana.. Walaji tumefika tena niko na huyu mwanadada anakula kama ana tumbo mbili..!!” Akaongea kimasihara Agent Kai na hapa tena wote wawili wakampisha mwenyeji atangulie kuwaongoza kuelekea ndani ya nyumba.

Walikwenda kimya kimya lakini wote walikuwa wako kwenye tabasamu kavu, tabasamu lisilo na kicheko cha sauti yoyote zaidi ya uso kuruhusu mdomo kuchanua papi (lips) zake.

Mlango wa barazani ulifunguliwa wakaingia na kujikuta wako sebuleni hapo wote kwa pamoja wakaona kwenye meza ya chakula kuna watu wawili, Special Agent Fransis Simone Silla na Investigator Joseph January Miller.

   “..Ooooh! karibuni tushakuwa wenyeji… Na tayari tunakula ndizi na nyama hapa.. Mje tujumuike pamoja kwa chakula na maongezi..!” Sauti ya kupazwa kidogo tokea kule sehemu ya chakula ilitoka ikiwa ya Investigator Miller, macho yake yakikosa stara kwani yalikaza kwa mtu mmoja zaidi yakimuangalia Rebecca Smith.

   “Sisi naona tuyape pumzi matumbo yetu sababu muda si mrefu tumetoka kuyatumia supu nzito na majuisi, malizeni kisha njooni mezani hapa tupange kazi!” Akaongea ‘TSC’ akiwa kasimama karibu na meza iliyo katikati ya sebule ya maongezi kwa wageni wanaofika ndani ya nyumba hii ambayo kwa nje huwezi kujua kama ndani ni ya kisasa kama ilivyo maana kwa nje.

   “Sawa… Mtusubiri basi!” Norman akawajibia wenzake walio meza ya chakula kisha naye akakaa kuendelea kula kwakuwa kabla hajaenda kufungua geti kwa wageni alishaanza kula.

Dakika ishirini walaji walimaliza kula na hata kumsaidia mwenyeji kuondoa vyombo vichafu kupeleka jikoni kisha wote wakajumuika sebule ya wageni na maongezi.

   “Brother! Na wewe ni mtu wa kupenda movies?” Akauliza S.A Silla kumuuliza Agent Kai ambaye alikuwa akiangalia movie iliyo katika mtindo wa series katika Ipad yake.

   “Naam! Muda mwingine nachukua dakika nazopata kwenye u free kuangalia movie hasa hizi za kijasusi maana fani hii hivyo wananiongeza vitu fulani ambavyo hata kama havipo katika ukweli mimi uamua kuvifanyia kazi napokuwa katika kazi kama hii iliyotufikisha hapa GTL”

   “Inaitwaje hiyo?” Akahoji tena Silla.

   “The 100… Unaipata?” Akajibu na kumuuliza.

   “Ndiyo niliangalia kidogo season one.. Inabamba sana kwa kweli!”

   “Basi mimi kila nikipata dakika za free za ziada lazima niangalie vipande kadhaa kama si episode yote kisha naendelea na mambo mengine”

   “Vizuri sana.. Habari za toka usiku uliopita?” Akaongea Silla na kuhoji akiondoka katika maongezi ya movie .

   “Kwa kweli nzuri sana… Sijui nyie mna hali gani?”

   “Tunamshukuru Mungu mimi na Miller tuko poa kabisa… Tumewai mapema kufika hapa tukakuta mwenyeji anaandaa chakula hivyo kwakuwa sote ni watu tunaojua mambo ya upishi tukajumuika naye jikoni tukaandaa tulivyoweza ndipo mkatukuta tumeanza kushambulia chakula…!” Silla akaeleza tena, wakati huo huo Miller kwa wizi alikuwa akiendelea kufanya usahili kwa Rebecca Smith alionyesha kuvutiwa na mwanadada huyu alivyo kuanzia sura mpaka shepu yake.

  “Miller huko kimya sana… Salama lakini?” Agent Kai akamgeukia Investigator Miller na kumtupia swali huku akiwa amemuona mara kadhaa toka mahala pale alipokaa sofani akimuona jinsi anavyochungulia kijanja upande aliokaa Rebecca.

   “Salama mkuu… Nasubiri muongozo wako tu mheshimiwa” Miller akajibu kasha akajiweka vizuri katika sofa la mtu mmoja alilokaa akijimwaga na kujinafasi.

   “Vizuri… Norman nawe! Tushasalimiana lakini hatujaulizana… Vipi hali yako? Za toka jana?” TSC akamgeukia na mwenye nyumba Detective Norman na kumuhoji maswali mawili.

   “Niko sawa mkuu! Kwa hamu nasubiri kuanza rasmi kazi iliyo mbele yetu”

   “Naiona morali iliyo mioyoni mwenu katika nyuso zenu, Mungu atutie nguvu sote… Na ndugu yangu Rebecca hapa tuna mambo ya kuelekezana tumekuja nayo, asubuhi alinitafuta Lizy… Oooh Lizy.. Samahani Norman, Lizy ni mwanadada anayesimamia kitengo cha Tehama upande wa ujasusi katika ofisi ya makamu wa Rais wa nchi yetu ni mshirika wetu na muongoza njia wetu akifanya kazi kitaalamu zaidi kama inavyojulikana teknolojia inavyopanuka kwa kasi hivyo kwa kazi zetu nasi tunawategemea wataalamu hawa, ofisi ambayo mimi niko huko kama wakala nikiongoza wawakilishi wa CIA katika ofisi ile akiwemo bibie huyu hapa ambaye anaitwa Special Agent Rebecca Smith ” Aliongea TSC huku akiwa kakishika kiganja cha mkono wa kushoto cha bibie Rebecca kwakuwa walikuwa wamekaa sofa moja linalokaa watu wawili wakiangaliana na wenzao walio upande wa pili wa meza.

   “Nimefurahi kujuana nawe Special Agent Rebecca, karibu Guatemala” Norman akaongea akitabasamu na kufanya Rebecca naye kutabasamu na kuonyesha mwanya wake hali iliyozidi kumchanganya Investigator Miller.

   “Nami pia nimefurahi na usihofu nimekaribia nishakuwa mwenyeji tayari” Akajibu kiuchangamfu Rebecca akiendeleza tabasamu lake binti huyu wa kizungu mwenye uzuri wa kuvutia machoni lakini mwenye moyo wa kijasiri usioendana na sura yake.

   “Tuendelee!… Lizy alinitumia audio za mtu wetu ambaye tunamfuatilia kwa ukaribu mawasiliano kiasi ya kwamba leo hii tupo hapa ni kwa msaada wake bila kujielewa, audio zake nitaweka hapa kuwasikilizisha kisha kuna maswali kadhaa nitakuuliza Detective Norman ambayo majibu na hata mawasli yenyewe yatakuwa muongozo kwetu… Kwanza msikilize audio” Akaongea Agent Kai huku mikono yake ikifanya kazi haraka haraka katika Ipad yake kuruhusu audio za maongezi ya simu aliyotumiwa na kisha wao yaani yeye na Rebecca kuyasikiliza wakiwa mgahawani.

Audio zote zilisikilizwa na wote kwa umakini tena hapa wakiwa wameweka kwa sauti kubwa kwakuwa haikuwa hadharani kama ilivyokuwa kule mgahawani.

   “Kuna ambaye hajaelewa mahala pengine?” Akahoji TSC baada ya kumalizika audio ya mwisho.

   “Upande wangu mimi nimeelewa vizuri sana kila audio.. Sijui kwa wenzangu!” Akaongea S.A Silla papo hapo akiwaangalia wenzake.

   “Mimi pia hakuna nilipokwama nimeelewa sana naweza hata kufafanua kile nilichokielewa mkuu.” Akaongea Norman mgongo wake akiwa kaulaza kwenye mto wa sofa (kistarehe)

   “Mimi vivyo hivyo… Nimeelewa pia ingawa kwenye majina inaweza kueleweka vile navyofikiri kumbe si sahihi ila ni audio ambazo zimenifumbua macho na kunitoa tongotongo kwa kiasi kikubwa sana… Kuhusu kule tulipovamiwa tukiwa na Kamanda Muniain hadi cheni ilivyoenda” Investigator Miller akaongea pia akikubali kuwa ameelewa.

   “Norman!” Agent Kai akaita baada ya kautulivu ka dakika moja akiwa anaweka mambo sawa kidogo katika Ipad yake ya kazi.

   “Naam mkuu!” Norman akaitika.

   “Mexico kuna genge la ulanguzi wa mihadarati ambalo ni tishio sana linaloitwa THE RED JAGUAR  kwenye mabano (TRJ)… Nafikiri umesikia likitamkwa hilo genge katika moja hizi audio?” ‘TSC’ akamuuliza Norman.

   “Ndiyo… THE RED JAGUAR ni genge linalojihusisha na ulanguzi wa madawa ya kulevya katika nchi ya Mexico ikiwa kama makao makuu yake lakini ni genge lililojitanua na kufanya biashara zake haramu katika nchi mbalimbali za ukanda wetu na hata jirani na ukanda huu ni genge hatari sana linaloongozwa na mwanajeshi aliyefukuzwa kazi jeshini kwa kosa lililomuhukumu kwenda jela miaka saba, kosa la kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa wanajeshi wenzake… Bwana huyu alikuwa ni Brigedia wa jeshi akiitwa Brigedia Fernandes Carlos Codrado a.k.a Feca” Akajibu kirefu Norman hadi vile ambavyo angeweza kuulizwa wakati unaofuata yeye akapita kabisa humo na kufurahisha kwa kurahisisha kwake.

  “Ni genge la Mexico hii inamaanisha wao ni kama waliokuwa Los Zetas na hata magenge mengineyo yanayovuma kutokea huko Mexico lakini genge hili inaonekana pia lipo hapa Guatemala, unasemaje juu ya hilo?” ‘TSC’ akauliza tena.

   “Kama nilivyokwisha kusema jana usiku tulivyoongea kidogo sisi Organized Crime Of Latin America ‘OCLA’ ni kikosi kilichoundwa kwa muungano wa nchi zote za Latin America kwa ajili ya kupambana na mihadarati hasa chanzo chake kisha kudhibiti usafirishaji wake.. Hivyo magenge yote ya madawa ya kulevya tunakuwa tunayajua ama kwa kuyasikia au kwa kupambana nayo na kujua haa khah! kumbe hili ni genge fulani… TRJ wapo hapa Guatemala na wana nguvu kubwa sana hapa kama ilivyo nchini kwao hili ni genge ambalo limekusanya nguvu yake ya rasilimali watu wake kutoka vijana wa kimexico na vijana wa nchi zingine za Latin America..”

   “Kuja kwetu hapa GTL hakukuja kwetu kama kupiga chafya maana yenyewe uja ghafla… Naamini jana ulinielewa kwanini tulikuhitaji? Na kwanini tunahitaji kufanya kazi na wewe kuliko mtu mwingine awaye katika nchi yenu, nikakuelekeza kuwa jina lako tulilipata katika maongezi ya simu ya mtu tunayemtafuta kwa udi na uvumba sababu kama yeye anakujua kwa undani anakusaka kwa nguvu sitaamini kusikia wewe humjui yeye… Huyu ni mwanamke ambaye katika audio zake zote tulizowai zisikiliza na hata hizi tulizozisikiliza leo hakuna mahala katajwa jina lake na mtu anayeongea naye na hata yeye mwenyewe iwe kwa bahati mbaya au makusudi kujitaja jina kuwa yeye anaitwa nani? Ila namba yake inaonekana amesajili hapa Guatemala kwa jina la Valentina Aurelia  Moschi lakini cha ajabu tulivyoingia katika orodha ya waliosajili laini zao katika mamlaka ya mawasiliano ya nchi hii jina hilo aliko katika orodha ni ajabu sana kwa sababu ingetusaidia kuipata picha ya mteja aliyesajili laini… Basi tukaamua kazi iwe ya kumtafuta huyu mwanamke anayeitwa Valentina… Namba ni hii! Je hujawai kutana nayo hata kukupigia kwa bahati mbaya kwenye simu yako?” Akaongea kirefu TSC mwishoni aliinua simu yake akamuonyesha namba Norman kwa kumgeuzia kioo cha simu yake huku kidole cha shahada cha mkono wa kushoto kikimsaidia kugonga gonga kioo cha simu.

  “Hii namba sijawai kukutana nayo… Ila michezo hii hapa GTL kwenye mamalaka yetu ya mawasiliano ipo sana, mtu anasajili laini halafu anafanya mipango taarifa zake zote zinafutwa kwenye orodha ni michezo wanayocheza maafisa husika wa pale… Ila hakiwezi kuharibika kitu mkuu, hii namba ni namba muhimu sana inayofanya kazi nzito katika kufanikisha uhalifu kwa kuwashirikisha viongozi walioko katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na pia ikipokea habari maelekezo toka kwa mtu ambaye nimemsikia na ninaamini ndiye kiongozi wa genge lao akiongoza uhalifu kwa kutokea huko Mexico… Moja kwa moja nathubutu kusema THE RED JAGUAR ya Kingpin Feca inahusika kwa kiasi kikubwa kuharibu usalama wa nchi yetu” Akaongea Norman.

   “TRJ ndiyo wanaokusaka kwa udi na uvumba, flashdisk uliyosema ulipewa na kiongozi taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa iko wapi?” Akahoji TSC.

   “Ijumaa ya kesho ndiyo siku ambayo Rais wa nchi aliomba mimi na Kamanda Muniain twende Ikulu tukiwa nayo tuisikilize kwa pamoja na pia kupanga kazi kuwa iweje baada ya kuiangalia… Flash hii ninayo hapa na sote twaweza kuangalia mzee wetu aliandaa video yenye maneno gani na kwanini?” Akajibu Norman.

   “Unaweza kutugusia kilichomo pengine ikawa haina haja ya sisi kuiangalia maana jana ulisema mkurugenzi alikusisitiza ikafunguliwe na Rais wa nchi mwenyewe..” Akaomba Agent Kai.

Mwisho wa sehemu ya hamsini (50)

Agent Kai ‘TSC’ akiwa na majasusi wenzake wanaingia katika mipango kazi yenye kupanga mikakati iweje, baada ya kusikiliza audio za mwanadada ambaye mpaka sasa wao wanamjua kwa jina la Valentina Aurelia Moschi.

Mikakati yao itapangwa vipi na kazi itakuwaje?

Majibu matamu ya haya yote yanapatikana katika sehemu inayofuata na zitakazofuata ambazo kama ni barabara basi itakuwa imekamata mteremko mkali wa kitonga kwa kasi yake katika mapigano.




  “Hii namba sijawai kukutana nayo… Ila michezo hii hapa GTL kwenye mamalaka yetu ya mawasiliano ipo sana, mtu anasajili laini halafu anafanya mipango taarifa zake zote zinafutwa kwenye orodha ni michezo wanayocheza maafisa husika wa pale… Ila hakiwezi kuharibika kitu mkuu, hii namba ni namba muhimu sana inayofanya kazi nzito katika kufanikisha uhalifu kwa kuwashirikisha viongozi walioko katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na pia ikipokea habari maelekezo toka kwa mtu ambaye nimemsikia na ninaamini ndiye kiongozi wa genge lao akiongoza uhalifu kwa kutokea huko Mexico… Moja kwa moja nathubutu kusema THE RED JAGUAR ya Kingpin Feca inahusika kwa kiasi kikubwa kuharibu usalama wa nchi yetu” Akaongea Norman.

   “TRJ ndiyo wanaokusaka kwa udi na uvumba, flashdisk uliyosema ulipewa na kiongozi taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa iko wapi?” Akahoji TSC.

   “Ijumaa ya kesho ndiyo siku ambayo Rais wa nchi aliomba mimi na Kamanda Muniain twende Ikulu tukiwa nayo tuiangalie kwa pamoja na pia kupanga kazi kuwa iweje baada ya kuiangalia… Flash hii ninayo hapa na sote twaweza kuangalia mzee wetu aliandaa video yenye maneno gani na kwanini?” Akajibu Norman.

   “Unaweza kutugusia kilichomo pengine ikawa haina haja ya sisi kuiangalia maana jana ulisema mkurugenzi alikusisitiza ikafunguliwe na Rais wa nchi mwenyewe..” Akaomba Agent Kai.

ENDELEA NA DODO ASALI!

KAZI IMEANZA I

CHIMALTENANGO, ANTIGUA-GUATEMALA

   “Nilivyofika pale kwake siku ambayo aliniambia nifike kuwa ana kitu anataka kunipa kabla hatujaanza maongezi alipigiwa simu na mtu ambaye mimi simjui akaniomba msamaha aongee kwa simu nikamjibu haina shida akainuka na kwenda chumba tofauti na pale sebuleni kwake… Aliporudi alibadilika ghafla tofauti na vile wakati naingia pale kwake.. Haraka akaniomba niinuke nilipokaa kisha akanishika mkono hadi kwenye kona ya karibu na mlango akachungulia dirishani kifupi alikuwa amehamaki sana akaniambia kwa sauti ya haraka nichukue flash na niondoke nayo akiniambia inatakiwa ifike kwa Rais wa nchi bila kuifungua yaani aifungue Rais mwenyewe, akaniambia ameniamini sana ndiyo maana ameniita anipe mimi niipeleke kwa Rais atakaporudi toka kwenye ziara yake ya nchi za bara la Asia, wakati ule ananipa Rais alikuwa na ziara ndefu ya nje ya nchi bara la Asia na ilikuwa siku ya kwanza ya ziara yake iliyochukua nchi tano za bara lile… Baada ya mimi kuondoka pale nusu saa baadaye nikiwa njiani kuelekea kwangu nikapokea taarifa kuwa Mr. Fontes Jota Mariapan mkurugenzi wa Corrupt Law Enforcement Institution amepigwa risasi na kuuwawa kupitia redio yangu ya kwenye gari niliyokuwa nasikiliza ikiwa ni breaking news, nilitamani nigeuze gari kurudi kwake kupata uhakika lakini kabla sijafunga hata breki katika maamuzi yangu wakati naendesha simu yangu ikaita namba isiyo katika orodha ya namba nilizosevu katika simu yangu nikapokea haraka bila kujiuliza ndipo mpigaji akiwa analia akasema yeye ni mke wa Mr. Fontes Jota Mariapan, mumewe amepigwa risasi amekufa ila wakati anakata roho yeye mkewe na mtoto wake mdogo walikuwa pembeni yake wakijaribu kumsaidia.. Mtu aliyempiga risasi akiwa ameshakimbia ni mwanamke aliyempiga risasi ambaye pamoja na kuwa alikuwa kavaa suruali aina ya jeans wao waliweza kumuona vizuri ila tu hawamjui ni mara ya kwanza kumuona, mwanamke huyu alipokuwa akiondoka aliua na walinzi wa pale… Kabla hajakata roho Mr. Fontes aliandika namba yangu akitumia damu yake katika sakafu ya karibu na mlango kisha akaandika pia niambiwe nijifiche mpaka Rais atakaporudi natafutwa kuuliwa pia… Alipomaliza tu ndipo akakata roho na mkewe alipotoa taarifa polisi kisha akanipigia nami.. Ni hivyo nafikiri kila mmoja ameelewa uhalisia ulivyo na ni kweli mpaka leo ninayo flash na sijui imeandikwa nini kwakuwa mpango tuliopanga na Kamanda Muniain kuwa kesho Rais atakaporudi basi nasi twende tukampatie flash” Alieleza kirefu sana Detective Norman Cabrera kiasi ya kwamba alipoacha kuongea aliinuka kwenda ilipo friji ya vinywaji akafungua na kutoa chupa ya maji.

   “Humu tukiacha Rebecca wote ni wenyeji, nyumba ya kisela mwenyeji wenu kwa hapa GTL…Jana ulifika Kai na leo wamefika Silla na Miller hivyo nyote nyinyi ni wenyeji hakuna shaka na hilo mwenye kujisikia kunywa chochote asogee kwenye friji afanye kujisevia.. “ Akaongea mwenye nyumba Norman kisha mdomo wa chupa ya maji ukaamia kwenye mdomo wake akapiga tarumbeta mpaka nusu chupa hii ya lita moja na nusu ya maji.

‘TSC’ akainuka sofani naye akaenda kwenye friji akatafuta juisi akapata juisi ya apple iliyotengenezwa katika box hapo akatizama pembeni na kuibuka na glasi akafunga friji na kurudi mahala alipokaa akafungua box wengine wakimuangalia yeye akaendelea na kufanya yake akaweka glasini na kupiga funda mbili za kufuatana.

  “Inasemekana ni wiki ya pili toka ukolee katika kujificha kwako kwa mujibu ya watu wanaokusaka.. Hii ya kutompa flash Rais mpaka leo imekaaje? inanichanganya kidogo, ebu tufafanulie wote kwa ujumla!”Koo la ‘TSC’ lilipopata kitu roho inataka ubongo ukauagiza mdomo uulize huku glasi nzuri ikiwa kiganjani.

  “Rais alipomaliza ziara za nchi alizopanga kuzifikia na kufanya maongezi na marais wa huko akarudi hapa siku moja tu kwani siku ya pili alianza ziara za nchi za mataifa ya ulaya ambako leo anamaliza ziara nchini Uturuki kisha kesho mapema anarudi hapa ikiwa ni ziara ndefu sana amefanya toka ameingia madarakani ndiyo iko hivyo”Akajibu Detective Norman.

   “Ooooh! Nimeelewa.. Tuelekee kwenye kazi iliyo mbele yetu ingawa hatujui flash imebeba jambo gani mpaka… Uchunguzi umefikia wapi juu ya mauaji haya? Na hujajua Rais amechukuliaje kuuliwa kwa mteule wake?” Akahoji tena Agent Kai katika maongezi ya maswali na majibu, maswali yakitoka sehemu moja kwenda kwa mtu mmoja naye akijibu majibu ambayo yalikuwa ya kulizisha, wengine wakiwa katika utulivu mwenye kunywa maji au kinywaji kingine na hata asiyekunywa chochote pia alikuwepo pia.

   “TACCG ndiyo walikuwa wanachunguza hii ni kikosi cha usalama wanaoaminiwa sana na Rais katika uchunguzi wa jambo lolote lililomkwaza Rais huyu wa awamu hii, ameweka watu ambao walikuwa intelejensia ya jeshi la wananchi, mimi walifika kunihoji kwakuwa mke wa marehemu aliwaeleza nilifika kuonana na marehemu mumewe muda mchache kabla hajafa na ninashukuru hakuwaeleza habari za flashdisk hivyo mahojiano yetu hayakuongelewa juu ya flash… Kuhusu uchunguzi umefikia wapi ukweli sijui chochote sikuwai kuuliza wamefikia wapi” Akajibu Norman.

   “Ila wanajua muuaji kama ni mwanamke?” Akahoji tena ‘TSC’.

   “Ndiyo wanajua hilo sababu waliniambia wameambiwa hivyo na mke wa marehemu”

   “TACCG wameshashindwa maana hawajamgusa mwanamke muhusika wa mauaji mpaka leo, mwanamke huyu ndiyo huyu ambaye tuna audio zake hapa na kama si yeye basi atakuwa mratibu wa mauaji haya ni yeye”

   “Ndiyo nami nilichofikiri icho… Mwanamke huyu ndiyo kiongozi wa TRJ katika Guatemala, amekuwa akipanga mambo mengi akisaidiana na viongozi wa serikalini hasa wanaohusika na mambo ya usalama katika kufanikisha mambo yake”

   “Tamaa ya viongozi wengi wa usalama wa hapa na nchi nyingine za jirani katika ukanda huu ni tamaa inayoharibu maisha ya watu wengi katika dunia yetu… Kimsingi Marekani inatumia bajeti kubwa kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya pamoja na kuwatibu waathirika wa madawa haya haramu kwa sababu ya nchi hizi zinazozunguka eneo hili tunatakiwa kupambana haswa kuwaokoa ndugu zetu si tu kina Jogre wanaoshikiliwa mateka na watu hawa pia na wanaoathirika kwa angalau kuvunja mguu mmoja kama si miwili ya magenge haya yenye nguvu kubwa zaidi… Unawezaje kulielezea eneo la milima ya Tajumulco?” Aliongea kirefu ‘TSC’ kisha akamalizia kwa swali alilolipeleka kwa mara ingine kwa mwenyeji wao Norman Cabrera.

   “Eneo la milima ya Tajumulco ni eneo la kilimo cha kahawa  ni eneo ambalo mmiliki wake anawatia watu mashaka sana kwakuwa yeye ni mdogo wake na mwanzilishi na kiongozi wa genge la TRJ ingawa serikali imekuwa ikikinga kifua kuwa mtu huyu hahusiki na biashara haramu za kaka yake… OCLA tumekuwa tukifuatilia nyendo zake mtu huyu kwa miaka mitatu sasa lakini kumekuwa na ukakasi mwingi sana katika hili maana vikwazo ni vingi sana sana!”

   “Anachunguzwa na timu yenu yote ya OCLA au kuna watu mmeteua wa kumfanyia uchunguzi mtu huyo? Na anaitwa nani?”Akahoji Investigator Miller.

   “Anaitwa Mr. Alexis Carlos Codrado ndiyo mwekezaji mmiliki wa shamba kubwa la kilimo cha kahawa linalozunguka eneo lote la milima pamoja na kiwanda kidogo kilichopo mwanzoni mwa shamba na mwisho wa kijiji ambacho nacho amenunua maeneo na kuwaweka wafanyakazi wanao hudumia shamba lake na kufanya kazi kwenye kiwanda chake kidogo… Bwana huyu pia anamiliki kiwanda kikubwa cha kahawa kilichopo Parque Regional Municipal..!” Akaeleza tena akifafanua juu ya mwekezaji wa eneo la milima ya Tajumulco eneo la kilimo cha kahawa.

   “Sasa atachunguzwa kiundani na timu yetu si OCLA tena ingawa hatuwazuii kusema wanamchunguza au mnamchunguza Norman ila tambua kama walikunyima fursa ya kiuchunguzi sasa unayo maana hatuwezi sema tunataka kujua habari za eneo la shamba la Tajumulco bila kumjua kiundani mmiliki wake na cheni yake ya utajiri alionao” Akafafanua Agent Kai ‘TSC’.

  “Huko sahihi mkuu!” Norman akakubali.

   “Jamani sote hapa tunatakiwa kuelewa kuwa tumeingia katika kazi ya kupambana na genge la THE RED JAGUAR linaloongozwa na kingpin Fernandes Carlos Codrado maarufu kama Brigedia Feca, hawa watu wa TRJ ndiyo wanaomshikilia Jogre na wenzake hivyo tunatakiwa mara moja kujigawa katika makundi mawili… Leo hii tutaanza kwa kuhitaji kujua ni kamanda gani wa Antigua anayeshirikiana na genge hili… Tunazo namba za simu za kamanda huyo kwakuwa katika audio hizi namba hii iliyo kiini ilimpigia” ‘TSC’ aligeuka walipo wamarekani wenzake akawakazia macho akiwaelekeza anachoona ni sahihi kuwa wanatakiwa kuanza kazi kwa kumuweka katika rada zao kamanda wa polisi aliyesikika akiongea na mwanamke kiongozi wa TRJ.

   “Sawa tunaweza anza hivyo Agent.. Mnaonaje kwanza tukaichunguza namba hii ya anayeonekana ni kamishina wa Antigua” S.A Silla akaweka hoja yake.

   “Norman! Kamanda wa Antigua humjui?” Akauliza S.A Rebecca swali likienda kwa Norman.

   “Namjua anaitwa Kamishina Alvaro Conedera huyu ni kamishina mkuu wa polisi wa mji wa Antigua pia kuna msaidizi wake anaitwa Kamishina msaidizi Juan Balo Neves huyu nahisi ndiyo muhusika sababu mara nyingi ninapata taarifa zinazonitia mashaka juu ya uadilifu wake hivyo tuhakiki kwa kuitizama namba hiyo katika orodha ya mamlaka ya mawasiliano..”

Special Agent Rebecca hakusubiri amri au maelekezo yoyote toka kati ya wanaume hawa alionao hapa, alitoa laptop yake ndogo toka katika begi lake dogo akaiwasha ilipokuwa sawa kutumika akachomeka modem.

Dakika mbili tu mbele akifuata maelekezo ya Norman jinsi ya kuingia katika mfumo data wa mamlaka ya mawasiliano ya Guatemala hili aweze kudukua taarifa wanayotaka bila kuwahusisha wahusika wenyewe, akaingiza namba husika ikasachi namba ile na kuleta majibu.

  “Siyo ndezi huyu… Jina tofauti kati ya majina ya makamanda hawa… Hahaha hahaha… Janja janja.. Tunaweza pata namba zao watu hawa ukiacha hii tuliyonayo?” Akaongea Rebecca Smith na kuhoji swali kwa Norman baada ya kazi ya kusachi laini iliyotumika kwa mawasiliano na mtu aliyesemekana ni kamanda aliyefanya hila ya kuchelewesha askari polisi kufika eneo la tukio kwa maelekezo toka kwa mwanamke sakwa.

  “Inawezekana… Acha nimtumie ujumbe Kamanda Muniain aweze kunitumia namba zao popote pale”

  “Fanya hivyo! Kazi imeanza” Akachombeza Investigator Miller huku akiendelea kuchati kupitia simu yake (whatssap messenger) na mtu anayejua yeye ni nani.

Detective aliomba muda kidogo wa kuchat na Boss wake Kamanda Muniain ambaye baada ya meseji mbili tatu naye aliomba muda kidogo aziombe kwa watu anaowaamini kuwa hawawezi fikisha taarifa kwa wahusika kuwa yeye Muniain kataka namba zao.

Zilipita dakika nane mpaka kumi utulivu ukitawala katika sebule hii kila mmoja akifanya yake katika simu yake kama ujuavyo simu za smartphone zilivyo, watu hawa simu zao zilizo za kisasa sana zilikuwa ziiwapa fursa nyingi za kazi na burudani, dakika hizo nilizodokeza zilipotimia meseji toka kwa Kamanda Muniain iliingia ikiwa na namba za wahusika zilizoombwa.

   “Namba zao Kamanda amenitumia… Ni kweli ziko tofauti na hii tuliyonayo.. Nakusomea andika..” Akaongea Norman huku akimtizama Rebecca.

Alimsomea huku Rebecca akiziandika katika katika simu yake ya mkononi kisha akamuangalia Agent Kai ambaye alimtingishia kichwa chake akambinyia jicho wakaelewana, papo hapo akaizima simu yake ikiwa kashasevu namba alizopewa kisha akaifungua akatoa laini ya simu iliyokuwepo ambayo uwa anaitumia mara zote kikawaida halafu kuna laini ingine akapewa na Agent Kai “TSC’ akiitoa kwenye kifuko kidogo cha begi lake.

Laini hii aliyopewa akaipachika simuni akaiwasha simu tena ikasachi network kidogo ilipotulia akaseti baadhi ya vitu hili iweze kufanya kazi kupitia simu yake.

   “Yule askari polisi aliyeongoza msafara uliokuja pale Filadelifia unamjua?” Swali toka Kai lilielekezwa kwa Norman wakati huo huo Rebecca alikuwa amepiga tayari kwenda kwenye moja ya namba alizopewa na Norman.

   “Sikuwa nimewai kutana naye kabla ila yeye ananijua mimi lakini mimi simjui ni mara ya kwanza namuona machoni mwangu, alijitambulisha kwetu anaitwa Sajenti Ruben Felipe” Akajibu Norman.

   “Huyu naye itatubidi tupate taarifa zake” Akamalizia ‘TSC’.

   “Halloo!” Simu ilipokelewa upande ilipopigiwa kwa sauti ya kiume nzito hii namba ilikuwa ya Kamishina mkuu wa polisi wa mji wa Antigua Kamishina Alvaro Conedera.

   “Halloo.. Naitwa Monica Rojas napiga simu kutokea Chimaltenango nina taarifa nataka kukupatia Kamanda hili unisaidie ..” Akaanza moja kwa moja kwenye uongo Rebecca.

   “Monica… Unajua unaongea na nani?” Akauliza wa upande wa pili.

   “Mi nachojua wewe ni Kamishinaa wa polisi wa mji wetu wa Antigua”

   “Namba yangu umeipata wapi?”

   “Namba yako nimepewa na mtangazaji mwenzangu wa redio Antigua fm”

   “Mpya hii… Mtangazaji wa Antigua FM… Eeeeh! Makubwa… Wewe ni mtangazaji wa redio hiyo?”

   “Ndiyo mimi ni mtangazaji wa pale nina tatizo tafadhali naomba msaada wako” Akajifanya anataka kulia katika bembeleza yake Monica wa uongo S.A Rebecca.

   “Shida gani unayo? Mbona simu yako sauti kama inajirudia, umeniweka loud speaker?”

   “Hapana sijakuweka loud speaker mkuu… Shida yangu nimeibiwa gari yangu muda si mrefu nilikuwa nimeingia duka la vipodozi nilipotoka sikuikuta..”

   “Wapi hapo umesema? Gari yako ni aina gani?”

   “Chimaltenango… Gari yangu ni Cadillac XTS Vsport Premium ya mwaka 2014 bado mpya ingawa ya mwaka huo, tafadhali nisaidie mkuu.. Wameelekea  barabara ya Santa Maria De Jesus”

   “Nipe namba ya gari yako nitoe taarifa vituo vya mbele wazuie isipite gari ya aina hiyo..!”

   “G 2544 BGT… Utanijuza ukishafanya hayo.. Jitahidi nitakulipa vizuri..!”

   “Haya… Jina nani vile?” Alikubali Kamishina Alvaro Conedera na akaomba akumbushwe jina.

   “Monica Rojas!”

   “Naam… Dakika kumi nifikishe taarifa kisha nitakutaarifu kwa kukupigia simu kama tayari. Gari lako haliwezi potea kwa urahisi umewai muda muafaka mpendwa”. Akamalizia Kamishina Alvaro na hapo Rebecca hakusubiri aendelee zaidi akakata simu.

   “Kuna haja ya kusikiliza sauti ya msaidizi wake?” Akauliza Rebecca akiwaangalia kwa zamu watu wote wanaomzunguka akitabasamu.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na moja (51)

Mafundi wamekutana!

Mkakati ukipangwa wapi wanaanzia katika safari ya matumaini yao katika kuhakikisha wanatimiza wito na wajibu wao.

Kwa kujua mengi yajayo vuta uzi uendelee na sehemu inayofauata!




   “Halloo!” Simu ilipokelewa upande ilipopigiwa kwa sauti ya kiume nzito hii namba ilikuwa ya Kamishina mkuu wa polisi wa mji wa Antigua Kamishina  Alvaro Conedera.

   “Halloo.. Naitwa Monica Rojas napiga simu kutokea Chimaltenango nina taarifa nataka kukupatia Kamanda hili unisaidie ..” Akaanza moja kwa moja kwenye uongo Rebecca.

   “Monica… Unajua unaongea na nani?” Akauliza wa upande wa pili.

   “Mi nachojua wewe ni Kamishina wa polisi wa mji wetu huu wa Antigua”

   “Namba yangu umeipata wapi?”

   “Namba yako nimepewa na mtangazaji mwenzangu wa redio Antigua fm”

   “Mpya hii… Mtangazaji wa Antigua FM… Eeeeh! Makubwa… Wewe ni mtangazaji wa redio hiyo?”

   “Ndiyo mimi ni mtangazaji wa pale nina tatizo tafadhali naomba msaada wako” Akajifanya anataka kulia katika bembeleza yake Monica wa uongo S.A Rebecca.

   “Shida gani unayo? Mbona simu yako sauti kama inajirudia, umeniweka loud speaker?”

   “Hapana sijakuweka loud speaker mkuu… Shida yangu nimeibiwa gari yangu muda si mrefu nilikuwa nimeingia duka la vipodozi nilipotoka sikuikuta..”

   “Wapi hapo umesema? Gari yako ni aina gani?”

   “Chimaltenango… Gari yangu ni Cadillac XTS Vsport Premium ya mwaka 2014 bado mpya ingawa ya mwaka huo, tafadhali nisaidie mkuu.. Wameelekea  barabara ya Santa Maria De Jesus”

   “Nipe namba ya gari yako nitoe taarifa vituo vya mbele wazuie isipite gari ya aina hiyo..!”

   “G 2544 BGT… Utanijuza ukishafanya hayo.. Jitahidi nitakulipa vizuri..!”

   “Haya… Jina nani vile?” Alikubali Kamishina Alvaro Conedera na akaomba akumbushwe jina.

   “Monica Rojas!”

   “Naam… Dakika kumi nifikishe taarifa kisha nitakutaarifu kwa kukupigia simu kama tayari. Gari lako haliwezi potea kwa urahisi umewai muda muafaka mpendwa”. Akamalizia Kamishina Alvaro na hapo Rebecca hakusubiri aendelee zaidi akakata simu.

   “Kuna haja ya kusikiliza sauti ya msaidizi wake?” Akauliza Rebecca akiwaangalia kwa zamu watu wote wanaomzunguka akitabasamu.

ENDELEA NA DODO ASALI!!

KAZI IMEANZA II

CHIMALTENANGO, ANTIGUA-GUATEMALA

   “Mh! Wee unaonaje juu ya hilo maana kwangu mimi masikio yangu yananiambia jibu tushalipata au wengine mnasemaje hapa?!!..” Akaongea Investigator Miller akimalizia kwa swali kwa wote macho yakizunguka kumuangalia kila mmoja kama anavyofanya S.A Rebecca.

   “Pengine na hiyo ingine inaendana na hii nawasikiliza wakuu wangu, yawezekana mimi masikio hayana uzoefu zaidi yenu ya kufananisha sauti… Msinyamaze!” Akaongea tena Rebecca akitabasamu baada ya kuona hata mtu aliyemzoea kuongea kwa haraka ameganda anafikiri kama hayupo hapa.

   “Kwangu mimi pia natamani kupitisha mawazo yenu kuwa hii inatosha kabisa… Mtoa oda na mpokea oda ni huyu mtu aliyetoka kuongea na Rebecca na kwasababu za kiusalama naomba tumpigie tiki huyu mtu… Anayewasaliti wananchi wa Antigua na GTL kwa ujumla ni Kamishina mkuu wa polisi wa mji wa Antigua” Sasa nahodha wa kikosi akaongea maana kila mtu alikuwa akisubiri ataongea nini.

   “Kwanini umesema sababu za kiusalama?”Akauliza Rebecca.

   “Hatujui Kamishina mkuu hapo yuko wapi? Na  kama yupo mwenyewe au yupo na msaidizi wake? Au na nani? Mara nyingi tusiowaona na kuwajua kwa undani uwa hatujui watu wao wa karibu wanaoshirikiana kwa ukaribu”Akafafanua ‘TSC’.

   “Okay nimeelewa hapo… Kazi imeanza!” Rebecca akaelewa ufafanuzi na kukubali lililosemwa na Agent Kai.

   “Tunatakiwa tumpate Kamishina Alvaro Conedera mara moja aje hapa kwa mahojiano na kazi hii haitafanywa na watu wengine zaidi ya timu ya DEA wakisaidiwa na mwenyeji wetu kwa maelekezo wapite wapi na wapi kukamilisha hili… Huyu Kamanda ataweza kuturahisishia kumpata mwanamke tunayemtafuta…. Muda huu ni saa tisa na nusu alasiri hadi saa kumi na mbili awe hapa kazi ni kwenu… Mimi na Rebecca tutabaki hapa tukichunguza kitaalamu zaidi habari za hili genge la TRJ!” Maelekezo ya kazi yaliendelea ikiwa kila mmoja ameridhia kwamba sauti ya audio  ya mmoja ya watu waliofanya maongezi na mwanamke wanayemsaka ni sauti ya Kamishina mkuu wa polisi wa manispaa ya mji wa Antigua Kamishina Alvaro Conedera. 

  “Muda si rafiki… Katika audio hizi tulizozisikiliza kuna taarifa ya mtu ambaye kwa anavyotoa amri zake ni kwamba yeye ndiyo kiongozi mwenye mamlaka ya juu zaidi katika genge la TRJ na naomba moja kwa moja nithubutu kusema mtu huyu ni Brigedia Feca, tunatakiwa kui track namba yake hii iliyotumika kufanya mawasiliano na mwanamke huyu… Mara nyingi sisi DEA na hata CIA uwa hatushindwi kunasa maongezi ya laini za simu za mitandao ambayo kiuhalisia makao yake makuu  ni Marekani hivyo kazi ya kuweza kuiweka katika ufuatiliaji laini hii ningeomba umuombe Lizy atusaidie kuifanya kazi hiyo” Special Agent Silla alitoa wazo lake.

  “Ndiyo  mtu huyu bila shaka wala kuweka udadisi mwingi huyu ni Feca… Acha tuulize makao makuu ya DEA kama wana audio yenye sauti ya Feca maana pale tuna audio nyingi za watu hatari katika biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya” Investigator Miller naye alipitisha kilichosemwa na ndugu yake na mshirika wake S.A Silla.

   “Kazi hii tutaifanya sisi… Ningeomba muelekee kumchukua Kamishina, nina hamu naye sana kufanya naye mahojiano.. Ila kabla hamjaondoka kuna jambo la kufanyiwa kazi mara moja na haraka … Mawasiliano ya simu za kawaida hapa GTL yamekuwa ni ya kudukuliwa sana na hawa watu wa magenge ya mihadarati hasa ya watu ambao wao wanakuwa na wasiwasi nao, ningependekeza tungetumia mfumo wetu wa mawasiliano ya ‘small call group network’ (SCGN) mtambo mkuu utakao tuunganisha tukiufunga hapa hivyo Norman naomba utupatie chumba tufunge kimtambo chetu kabla hamjaenda mkiondoka kila mmoja aondoke akiwa na small earphones Bluetooth yake” Akaeleza Agent Kai kisha ya hapo akatoa laptop yake ndogo toka kwenye begi lake.

  “Ulikumbuka kubeba hii kitu kumbe.. Nilitamani kuongea juu ya hili lakini nikawa nahisi umeacha hotelini ulikopanga, aisee kibegi chako kumbe kilikuwa kamili kama meli ndogo” Rebecca akaongea akitabasamu.

  “Umejisahaulisha kuwa mimi nilifika jana hapa hivyo nilikuwa tayari na maamuzi kamili yaliyo katika ratiba kamili kuwa nikifika hapa baada ya maongezi kutakuwa na kifuatacho mawasiliano ya peke yetu kama wana kikundi” Akaongea ‘TSC’ akimalizia kutoa kimtambo kidogo cha kijasusi chenye uwezo wa kuratibu mawasiliano ya watu kuanzia watano mpaka kumi wakiwasiliana popote pale duniani kwenye minara ya mawasiliano na hata satelaiti kisha kusikilizana wenyewe kwa wenyewe waliounganishwa na kimtambo hiki kupitia vifaa vidogo kama kidonge cha rangi mbili vinavyopachikwa kwenye tundu la sikio kwa ndani ambapo kama utaweza mtizama mtu bila macho yako kutizama kwenye tundu la sikio huwezi kukiona huku sapoti yake uwa ni saa ya mkononi kama anayoivaa Agent Kai ikiwa imeunganishwa kwa cha sikioni na saa kwa mtindo wa Bluetooth.

Norman aliongozana na Agent Kai mpaka kwenye moja ya chumba ambacho hakitumiwi na mtu kwa kulala kati ya miongoni mwa vyumba viwili vitatu vya kulala ambavyo havina watu wanaolala katika nyumba hii yenye vyumba  vinne vya kulala,  sebule, jiko na mahala pakulia chakula ikiwemo na eneo la kufanyia mazoezi lenye vifaa vya kisasa vya gym.

Waliingia kwenye chumba hiki ambako kulikuwa na kitanda pamoja na meza isiyo kubwa sana ya wastani, kabati la nguo lililo tupu na dressing table.

  “Yes! Panafaa sana… Mimi nitafanya hapa kama ofisi yetu mpaka operesheni yetu itakapokamilika na pia nitakuwa nalala hapa kuhakikisha kila jambo linakwenda linavyostahili muda wote… Acha niunganishe kamtambo haka haraka hili muende huko..Niitie Rebecca aje tufanye hii kazi kwa pamoja, mtakapoondoka mimi na yeye tutafanya naye usafi wa chumba hiki..”  Akaongea ‘TSC’ baada ya kufanya ukaguzi wa macho ya juu juu ya chumba alipoingia tu, kulikuwa na vumbi vumbi juu ya vitu vilivyokuwemo hapa ndani.

Walishirikiana kufuta vumbi ikiwa Rebecca amefika na watu wote wakawa wako katika chumba hiki ikafanyika kazi ya kitaalamu kuunganisha laptop ndogo ya Agent Kai na kimtambo chake cha mawasiliano nilichokielezea juu hapo baada ya hapo ‘TSC’ akatoa vifaa vya kupachika masikioni akampa kila mmoja na saa pia za mkononi ambazo zinaendana na vifaa hivi vyote kwa pamoja ikiwa na maujuzi ya CIA haya katika kurahisisha mawasiliano ya majasusi wao.

Vifaa vikajaribiwa na haraka vikafanya kazi bila usumbufu wakapongezana kama wameshinda jambo fulani kumbe mawasiliano yamekaa walivyotaka.

Dakika kumi mbele Detective Norman wa OCLA, Special Agent Silla na Investigator Miller waliagana na wenzao ikiwa Miller akiumia moyoni kwanini yeye ndiye asingebaki na Rebecca hapa, alitamani yeye ndiyo angekuwa Kai abaki aweze kuzieleza hisia zake kwa mwanamke ambaye amemuona wiki hii tu ikiwa mara ya kwanza kamuona katika jengo la ofisi ya Makamu wa Rais wa Marekani, Eisenhower, Washington DC.

          *****  *****  *****

Toka eneo la Chimaltenango mtaa wa Sign mpaka barabara ya Ciudad Vieja inayoelekea makao makuu ya polisi ya mji wa manispaa ya Antigua mtaa wa Colonia El Panorama kwa gari aina ya Toyota Hilux Surf Turbodiesel mali ya Kamanda Muniain lakini alikuwa amempa kijana wake Detective Norman kulitumia katika mizunguko yake ya safari za mbali zinapotokea, ikiendeshwa na Norman mwenyewe ilifika katika maegesho ya magari ya Texaco Station mkabala na Soleil Hotel.

  “Niwaache hapa mimi naenda kuonana na afisa wa polisi niliyewaambia ukisogea kidogo mbele unaweza kuliona jengo la kituo kikuu cha polisi kama nitafanikiwa nitawajulisha nimefanikiwa na hapo itakuwa kama tulivyopanga” Aliongea baada ya gari kuzimwa injini na kuacha kuunguruma ikiwa imesimama katika maegsho haya ya kituo cha mafuta cha Texaco Station.

  “Rebecca! Rebecca!” Akaita Investigator Miller akiwa kainua mkono wake wa kushoto aliovaa saa aliyopewa na Agent Kai ikiwa wote walio ndani ya operesheni hii walipewa na akausogeza karibu na mdomo ikiwa kabonyeza kitufe cha kuruhusu yeye kuongea na upande anaotaka.

   “Nakupata… Mshafika?” Akajibu Rebecca ikiwa watu wote walio katika mfumo huu wa mawasiliano ya ‘small call group network’ (SCGN) ambao walitaka kusikiliza waliweza kusikia kwakuwa ilipotokea mtu kutaka kuongea na mwingine ilikuwa lazima aite jina la anayemuhitaji kuongea naye uwa haina mipaka haina hii ya mawasiliano.

   “Yaap! Tuko Soleil Hotel barabara ya Ciudad Vieja mtaa wa Colonia El Panorama karibu na kituo kikuu cha polisi manispaa ya Antigua… Hivyo mpigie Kamishina fanya kama tulivyopanga..!” Akaongea tena Investigator Miller.

   “Nilishamuanza na meseji na ninachati naye bado kuna dalili zote atakubali kuja nitakapomwambia… Ngoja nimpigie kabisa mtasikia naongea naye!” Upande wa Rebecca ukaongea.

   “Umemuuliza kama bado yupo ofisini kwake?” Akahoji Investigator Miller.

   ”Ndiyo amenijibu hilo dakika chache zilizopita na anaonekana ameguswa sana na tatizo langu la uongo kuibiwa gari nazidi kumuweka karibu  kupitia hizi meseji” Akajibu Rebecca kisha wote wakazishusha saa zao chini kana kwamba wanaonana.

Kilipita kimya cha dakika mbili katika earphones Bluetooth za wote katika kundi la majasusi hawa na mara wote wakawa wanasikia mlio wa simu inayoita upande mwingine hii ilikuwa Special Agent Rebecca amepiga kwenda kwa Kamishina mkuu wa polisi wa manispaa ya Antigua akiruhusu simu yake kuwa katika loud speaker.

  “Monica…! Nini tena mpendwa?” Ikasikika sauti ya Kamishina Alvaro.

  “Nimetuma meseji nimeona kwenye jibu ni kama hujanielewa mkuu..”Akaongea kimtego Rebecca.

  “Hii ya mwisho au? Mbona nimejibu.. Na hata uliyotuma picha yako nimejibu iliongozana na ile ya swali ulilouliza kuhusu kama napokea taarifa ya vituo nilivyoomba waweke ulinzi mkali..”

  “Mmmh! Au haijafika… Ebu niangalie haraka haraka kama imefika maana majibu ya hiyo picha niliyotuma nilipata” Akazuga tena Rebecca kisha akanyamaza sekunde kumi, alikuwa amemtumia Kamishina picha kwa njia ya whatssap ikiwa si picha yake ni picha ya mwanamke mwingine wa kilatino, mwanamke ambaye mashaallah! Picha yake tu ukiiona lazima kamoyo kastuke labda usiwe rijali , akiichukua katika hifadhi za picha zake kwenye simu anayotumia.

   “Oooh… Kweli… Ndiyo maana umejibu tofauti… Nilikuwa nimekwambia kuwa nakuja kituoni ofisini kwako kukuona au kama unaweza tukaonana karibu na kituo kikuu  itakuwa vizuri zaidi, nahofu fulani bado juu ya hupatikanaji wa gari yangu mkuu! Ki ukweli nakaribia mtaa wa Colonia El Panorama utanisamehe nimepaniki juu ya hili Kamishina sijui nafanyaje jinsi moyo wangu unavyoumia” Akazidi kuongopa Rebecca akiongea kilatini kwa sauti ya kuremba itokayo puani mtoto wa kike sauti ambayo mwanaume akiisikia kwenye simu hata kama ni mara ya kwanza anaongea naye kwa simu lazima atashawishika  amuone mmiliki wa sauti husika.

   “Mmh! Mtihani… Naweza tuma kijana wangu mmoja afike kwenye moja ya mgahawa uliopo katika safu za mtaa huu mkaonana na kuongea vizuri akiniwakilisha?”

   “Hapana Kamishina tafadhali naomba nionane na wewe sema tu nije wapi?”

   “Nina kazi naifanya, napitia ripoti muhimu sana na muda umeenda wakati huu ndiyo nilipanga kupitia hii ripoti ila kama kweli umesogea karibu na mtaa huu basi naweza iba dakika chache tukaonana” Dalili za kuingia laini zilianza kujongea na kufanya S.A Rebecca kutabasamu na kwakuwa alipo alikuwa na Agent Kai walikuwa wakiangaliana muda wote huku nyuso zao zikiwa zinatabasamu kufurahia jinsi Rebecca anavyoitendea haki kazi ya ulaghai moja ya kati ya  mihimili mikubwa katika kazi ya ujasusi unaokusanya ukachero na ushushushu.

   “Nitafurahi sana Kamishina… Chepuka mara moja tukutane hapa kwenye  mgahawa wa Soleil Hotel.. Niko tayari hata ukisema nichukue chumba kwa usalama wako wa kimaadili ya kazi maana mapaparazi nao hawako nyuma, mi kwangu sawa tu nimeridhia” Kete ya sauti nzuri iliendelea kutumia nguvu yake kama inavyojulikana nguvu ya mwanamke kwa mwanaume ilivyo kubwa mpaka kufikia wanawake wengi wanaojiamini udiriki kusema bila woga kuwa ‘mwanamke anatawala mwanaume wakati mwanaume anatawala mamlaka’ ikimaanisha hata kama mwanaume atakuwa anatawala nchi, anapokuwa pembeni ya mwanamke anayempenda basi utawaliwa yeye.

  “Sawa nimekuelewa… Nakuja haraka hapo nitachepuka na walinzi wangu wawili tu, kwa sababu nimekuona kwenye picha na hatujuani na isiwe usumbufu chukua chumba nikukute humo”

  “Sawa mkuu… Nimefurahi sana kusikia hivyo…”

  “Utanijulisha kwa meseji au hata kunipigia namba ngapi umechukua.. Nipe dakika ishirini tokea sasa..!” Kamishina Alvaro kiukweli ni mwanaume mwenye umri uliosogea kukimbilia miaka ambayo kisheria wafanyakazi wa kiserikali na hata baadhi ya sekta binafsi ustaafu kazi za kitumishi lakini si mtu wa kujivunga kwa wanawake hasa mabinti walioiva iva hivi karibuni tayari kwa matumizi ya starehe kwa wanaume, alikuwa ametokea kuvutiwa na picha aliyotumiwa akiamini huyu anayemuona kwenye picha ndiye mwanamke anayeongea naye akiwa anamjua kwa jina la Monica Rojas.

Simu ilikatwa kwa pande zote na papo hapo S.A Rebecca akainua mkono wake wenye saa ya kiteknolojia haswa akabonyeza kitufe na kisha akaongea.

   “Natumaini hakuna mtu kati yetu ambaye hajasikia nilichokuwa naongea naye… Haraka Silla au Miller kwakuwa mpo hapo kwenye mgahawa wa hotelini mmoja wenu achukue chumba halafu anijuze namba ngapi hili nimtumie meseji mteja wetu” Akaongea kwa sauti ya haraka.

   “Ndiyo nakaribia ofisi ya mapokezi… Nitachukua mimi Miller.. Dakika tano mpaka kumi” Akajibu Investigator Miller.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na mbili (52)

Kazi imeanza! Kamishina Mkuu wa Polisi wa Manispaa ya Antigua Alvaro Conedera yuko kwenye rada ya kikundi kazi kinachoongozwa na Agent Kai, akiwa hajui anaingizwa katika mtego.

Kusiwe na maneno mengi sana tukapoteza maana ya mkasa huu mzito wa riwaya hii ya JINO KWA JINO.

Nini kitajiri katika sehemu inayokuja na nyinginezo zinazofuata?




   “Nitafurahi sana Kamishina… Chepuka mara moja tukutane hapa kwenye  mgahawa wa Soleil Hotel.. Niko tayari hata ukisema nichukue chumba kwa usalama wako wa kimaadili ya kazi maana mapaparazi nao hawako nyuma, mi kwangu sawa tu nimeridhia” Kete ya sauti nzuri iliendelea kutumia nguvu yake kama inavyojulikana nguvu ya mwanamke kwa mwanaume ilivyo kubwa mpaka kufikia wanawake wengi wanaojiamini udiriki kusema bila woga kuwa ‘mwanamke anatawala mwanaume wakati mwanaume anatawala mamlaka’ ikimaanisha hata kama mwanaume atakuwa anatawala nchi, anapokuwa pembeni ya mwanamke anayempenda basi utawaliwa yeye.

  “Sawa nimekuelewa… Nakuja haraka hapo nitachepuka na walinzi wangu wawili tu, kwa sababu nimekuona kwenye picha na hatujuani na isiwe usumbufu chukua chumba nikukute humo”

  “Sawa mkuu… Nimefurahi sana kusikia hivyo…”

  “Utanijulisha kwa meseji au hata kunipigia namba ngapi umechukua.. Nipe dakika ishirini tokea sasa..!” Kamishina Alvaro kiukweli ni mwanaume mwenye umri uliosogea kukimbilia miaka ambayo kisheria wafanyakazi wa kiserikali na hata baadhi ya sekta binafsi ustaafu kazi za kitumishi lakini si mtu wa kujivunga kwa wanawake hasa mabinti walioiva iva hivi karibuni tayari kwa matumizi ya starehe kwa wanaume, alikuwa ametokea kuvutiwa na picha aliyotumiwa akiamini huyu anayemuona kwenye picha ndiye mwanamke anayeongea naye akiwa anamjua kwa jina la Monica Rojas.

Simu ilikatwa kwa pande zote na papo hapo S.A Rebecca akainua mkono wake wenye saa ya kiteknolojia haswa akabonyeza kitufe na kisha akaongea.

   “Natumaini hakuna mtu kati yetu ambaye hajasikia nilichokuwa naongea naye… Haraka Silla au Miller kwakuwa mpo hapo kwenye mgahawa wa hotelini mmoja wenu achukue chumba halafu anijuze namba ngapi hili nimtumie meseji mteja wetu” Akaongea kwa sauti ya haraka.

   “Ndiyo nakaribia ofisi ya mapokezi… Nitachukua mimi Miller.. Dakika tano mpaka kumi” Akajibu Investigator Miller.

ENDELEA NA DODO ASALI!

KAZI IMEANZA III

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

  “Sawa kazi njema..!” Akamalizia Rebecca na wote kwa pamoja wakashusha mikono yao yenye saa kuwa kawaida wakiendelea na mambo mengine.

Investigator Miller alisogea hadi eneo la mapokezi ambako kulikuwa na masofa makubwa mawili yaliyokaa upande wa kushoto na kulia, mbele yake kulikuwa na meza kubwa ambayo upande wa pili kulikuwa na wadada wawili waliovaa sare za kama wafanyakazi wengi wa hoteli wanazovaa zikiwapendeza sana, Miller akasimama nyuma ya mteja mwingine mwanaume aliyekuwa akihudumiwa ambaye haikuchukua muda mrefu akamaliza kuhudumiwa akakabidhiwa funguo yake na kuondoka pale akiwa anaburuza sanduku la nguo.

   “Karibu kaka!” Akaongea dada ambaye yeye hakuwa akiandika katika kompyuta kama alivyokuwa akifanya mwingine aliyekuwa kainamia keyboard ya kompyuta aina ya desktop (ya mezani) anaandika mambo ambayo yapo kiutaratibu wa hoteli mgeni anapofika, aliongea kwa lugha ya kilatin kwakuwa muonekano wa Miller haukuwa tofauti sana na watu wengine wa Guatemala.

   “Ahsante sana nishakaribia.. Nina jambo linalohitaji msaada wenu na nitalilipia jambo hilo kwa ruhusa yenu na matakwa yenu, naweza lifikisha?” Akajibu naye akitumia kilatin (hapana kujiweka nyuma) ukaribisho ule Investigator Miller na kuomba ruhusa ya yeye kuweza kufikisha neno fulani, sura yake ikichanua tabasamu kijana huyu mwenye asili ya afrika akiwa na rangi ya weupe lakini nywele zake ndiyo zingeweza kukujulisha kama yeye ni Afri-cast (chotara).

   “Jambo gani kaka? Tunaweza kukusaidia kama lipo ndani ya mipaka yetu..!”Akajibu yule yule muulizaji lakini safari hii wote wawili walikuwa wameinua nyuso zao toka kwenye viti waliv yokaa kutokana na Miller alikuwa amesimama hivyo iliwalazimu shingo zao kuziinua hili kumuangalia mtu aliye mbele yao aliyetangaza ombi la neno kwao.

   “Kuna dada yangu ameniagiza hapa nimchukulie chumba, sasa sijui sheria zenu zinasemaje hapo?” Akaongea Miller huku macho yake akiyatupia kidogo kuangalia saa yake.

   “Unaandika tu jina lake, uraia wake kama wa hapa hapa GTL na kama si wa hapa tutahitaji passport yake… Hatuna masharti zaidi ya hayo sisi hapa Soleil Hotel!” Akaeleza aliyekuwa anaandika kwenye kompyuta huku wote wakitabasamu kulipa tabasamu zuri la Miller, wote kati yao hakuna aliyekuwa wa kikawaida wote walikuwa warembo wa kuvutia machoni mwa mwanaume yoyote yule.

   “Yeye bado hajafika anatokea eneo la Scuintla hapa hapa Guatemala City… Ana kikao na mtu wake anayeishi hapa hapa manisapaa ya Antigua, sijajua kikao chao kinahusu nini? Ila mimi ni mjumbe tu pengine wao ni wapenzi ilo mimi silijui nimeambiwa nije nichukua chumba tu na nikilipie wao wakija kama watafika pamoja sawa na kama kila mmoja atafika kivyake ni sawa ila naandika jina lake na hata likitakiwa na langu pia nitaandika” Akaeleza kiufafanuzi kidogo Miller yakiwa ni maelezo ya kisanii ndani ya ujasusi kama ujuavyo majasusi uongo kwao katika maongezi wanapotaka uwa haisumbui sana kwao kuongopa.

   “Hamna wasiwasi sisi tupo kwa ajili ya huduma bora kwa wateja wetu pia tunahudumia watu wengi wa vificho kama wao na wala haitushangazi… Karibu ujaze mkataba na ulipie kama watakaa siku moja au mbili wewe tu ulivyoelekezwa..”Akaongea tena dada mwandikaji kisha akamsogezea kitabu kilicho na sehemu za kujaza.

Investigator Miller akakivutia upande wake kwa karibu kisha akaangalia saa yake ya mkononi na kuanza kuandika uongo tupu unaofanana na ukweli akijaza mtaka chumba ni Monica Rojas anatokea manispaa ya Scuintla moja ya manispaa zinazounda jiji kuu la Guatemala City, alipomaliza uongo wake akiweka na yeye jina lake la uongo.

Akarudisha kitabu kwa muhudumu ambaye naye akajaza sehemu ambazo anahusika nazo akamtajia gharama ambazo zilikuwa za siku moja kama yeye Miller alivyojaza kuwa mgeni aliyemuagiza anataka chumba kwa siku moja.

   “Yoyote atakayewai kufika kati yao utamtaarifu aende chumba iko namba 12… Kama atawai mwanaume msimwambie kama mgeni wake wa kike hajafika mwambieni aende anasubiriwa watajuana wenyewe kwakuwa wanawasiliana kwa simu hivi sasa tunavyoongea hapa.. Hii hapa pesa yenu ya asante yangu kwenu!” Akaongea Miller akitoa maelekezo yenye angalizo ndani yake na mwisho alimalizia kwa kutoa pesa ya shukrani ikiwa sawa na pesa ya kulipia chumba ambayo iliwafanya wahudumu wale kuangaliana kwa furaha kisha wakacheka kicheko kidogo kilichobakiza tabasamu la furaha kwenye nyuso zao.

   “Ahsante sana kaka… Ubarikiwe sana na siku nyingine tunaomba urudi kuchukua chumba wewe mwenyewe hata kama hauna wa kulala naye sisi tupo utachagua mmoja wa kukuburudisha kaka mzuri kama wewe na mwenye roho nzuri kama wewe roho isiyo na choyo lazima kwenye mapenzi uwe mzuri mwenye kujua wajibu wako kwa mwanamke..” Dada mwandikaji hadi sauti iliongezeka vionjo akaongea kwa mbwembwe, sauti nyororo hadi macho yakihakisi unyororo wa sauti yake, sauti iliyobadilika ghafla kiasi cha kumshangaza kiundani Investigator Miller ikabidi amtizame vizuri akajikuta anabinyiwa jicho kukonyezwa na muongeaji.

   “Naahidi kurudi tena siku si nyingi… Nimepapenda hapa nafikiri dada yangu ni mtu wa kufika mara kwa mara hapa au amesikia uzuri wa huduma zenu hapa… Haya kwaherini mkae salama na kazi njema kwenu nyote..” Akamalizia Miller akiwapiga kope wote kwa ujumla.

Madada walibaki kama wamepigwa na butwaa waliangaliana na kugonga kikofi cha ushindi, wakifurahi kuingiza posho ya bila kuitaraji kwa wakati huu.

Investigator Miller aliondoka pale mapokezi akashika korido kama anaelekea nje kabisa kwa kupitia lango kuu la kuingilia hapa hotelini lakini alipofika usawa wa njia ya kuendea mgahawa wa hotel akafuata huko kisha nako hakufika akashika ngazi zinazopanda juu ambazo uwaleta watu wanaofuata huduma za chakula hapa mgahawani wakitokea flour (losheni) za juu.

Alipanda ngazi kana kwamba yeye ni miongoni ya wapangaji waliofikia katika hotel hii akafika ambapo ngazi za flour (losheni ya pili zinaishia hakuzunguka hili kufuata zinakoanza zinazoenda flour ya tatu kati ya flour tano zinazounda jengo la hotel la ghorofa hii, akashika korido ambayo yeye alipotokea hakukuwa na mtu anayepita wala aliyekaa mwisho kabisa wa safu ya korido hii ambako kuna masofa, macho yake yakaanza kuangalia namba zilizo juu ya milango inayongozana ikiachiana nafasi ya vyumba kwa vyumba.

Hakusogea hatua za zaidi mbele, mlango wa kwanza tu kuupita akiwa ananyooka kuifuata korido akauona mlango wa chumba namba kumi na mbili.

Macho yakazunguka huku na huko kwa haraka kisha akatoa funguo ya smart key kutoka mfukoni moja ya funguo bora za kiintelejensi ambazo wao watu wa DEA uzitumia kufungua milango iliyo katika mfumo wa automatic card, yaani milango inayofungwa na kufunguliwa kwa kadi maalumu inayopitishwa katika uwazi mwembamba kisha mlango unafunguka au kufungwa.

Kadi ilipitishwa pale kwenye uwazi ukatoka mwanga mwekundu kwenye kitasa pale pale kijisehemu kidogo kwa mara moja tu ikimaanisha umegoma kufunguka, hapo hakusubiri akasoma aina ya kitasa alipopata jibu akarudisha  kadi ya kwanza akazama tena mfukoni akaibuka na kadi tatu zinazofanana lakini zikiwa za kampuni zinazotengeneza vitasa hivi vya automatic ukanda wa latini amerika, akapata jina la kampuni aliyosoma hapo hakuremba akapitisha na papo hapo ukatokea wa kijani (mwanga kubali), macho yakazungushwa huku na huko shingo ikisapoti wakati mlango unajichia mtu kupita, kidume kikazama ndani na kujifungia.

   “Tayari.. Mpe taarifa unamsubiri namba 12, wahudumu wa mapokezi nimeshawalegeza kwa mchawi pesa hivyo akifika akiuliza kama ushafika atapewa jibu upo juu umejaa tele kama pishi la njegere” Miller akatoa taarifa iliyosikika vizuri kwa pande zote zinazotumia mtandao wao wa kundi lao.

Dakika nne mbele ukasikika mlio wa kuita simu katika vifaa vyao vya masikioni Rebecca alikuwa akipiga simu kwa Kamishina.

  “Niko namba 12 ghorofa ya pili… Nakusubiri usichelewe!” Akaongea hivyo tu na haikusikika sauti ya kujibu zaidi ya wote wakakata simu hii ilimaanisha Kamishina ameelewa.

   “Kazi kwenu na kazi njema” Ikasikika sauti ya Agent Kai ambaye muda wote alikuwa kimya akifuatilia mambo yanavyoenda kiufasaha akiwa pembeni ya Rebecca katika chumba walichokifanya kuwa chumba cha mawasiliano.

Zilipita dakika zipatazo kama kumi na nne hivi gari aina ya Toyota Land Cruiser Prices toleo la mwaka 2015 rangi ya kijani nyeupe (mpauko) ikiwa na vioo vyeusi (tinted) na mbele mkonge mrefu wa mawasiliano iliingia maeneo ya maegesho ya Soleil Hotel, ilisimama ikiwa bado inaunguruma kwa muda wa dakika tatu bila mtu yoyote kati ya watu watatu waliokuwa hawaonekani vizuri ni kama vivuli walivyokuwa wanaonekana kwa watu walio pembeni wakiwa katika bustani mbalimbali za eneo hili la nje ambalo wengi wa wapangaji wa hotel upenda kukaa kupumzika wakipata vinywaji.

Kwenye kiota kimoja kilicho karibu na maegesho haya alikuwepo Specila Agent Simone Silla akipata kiburudisho cha soda aina ya pepsi huku macho yake yaliyo ndani ya miwani ya kazi yakifuatilia kwa siri yanayojiri katika gari iliyopaki hatua nane tu toka alipokaa yeye.

Bila injini kuzimwa alishuka mtu mmoja akitokea mlango wa mbele anaokaa abiria ukiacha siti ya dreva haraka akaufunga mlango na kisha akatizama huku na huko, alikuwa kavaa kiraia tu lakini suti aliyovaa isingeshindwa kukujulisha mtu huyu aliyeshuka kwenye gari hii na kuwaacha wenzake ndani ya gari ni ama ni askari au ni mwanajeshi jinsi alivyo mkakamavu na makini machoni.

Alipotosheka na usahili wa macho yake kwa sekunde kadhaa alivyokuwa anayazungusha kwa kasi shingo yake ikisapoti alianza kupiga hatua kuelekea lango kuu la jengo la hotel alipokuwa akiukaribia lango kuu ambalo mtu akiwa anasogea karibu lenyewe ujiachia katikati mtu apite hii ni milango yenye ‘sensor’ maalumu inayoendana na binadamu, alitoa miwani meusi toka kwenye moja ya mifuko yake akaivaa machoni.

S.A Silla alikuwa akiendelea kucheza na macho yake akifuatilia yote anayohitaji kufuatilia huku anaendelea kunywa pepsi kwa mrija taratibu kana kwamba hana habari na zuga yake ilikuwa kujifanya anasoma gazeti kumbe hata anachosoma hakielewi.

Mtu yule alienda hadi mapokezi akauliza alichouliza kisha akaanza kupanda kuelekea korido ya ghorofa (losheni) ya pili alifanya aliyoona kwake sahihi kisha akaongea kwa simu akipiga mahala, alipomaliza akaenda hadi mwisho wa korido ambako katika hii hotel kuna masofa mawili marefu yamepangwa hapa kukiandikwa kwa juu ukutani ‘hospes/visitors’ maneno ya kimaandishi mawili la kwanza ni la kilatini na la pili ni la kiingereza ikimaanishwa ni sehemu ya wageni kusubiri mtu anayehitaji kuonana naye ambaye yupo miongoni.

Jamaa huyu aliyevaa suti nyeusi ya mikono mifupi ambazo kwa ukanda wetu wa Afrika Mashariki toka miaka iliyopita pengine hata mimi mwandishi wa riwaya hii sikuwa nimezaliwa waliipa jina suti hii kuwa ni ‘Kaunda Suit’ na kwa mawazo yangu ya haraka wakati naanza kujielewa na kuelewa baadhi ya mambo nikiwa mdogo nilijua sababu ya kuitwa hivi pengine ni kwa sababu lilikuwa vazi pendwa la Rais wa taifa la Zambia aliyekuwa akiitwa Keneth Kaunda ‘KK’, alijiweka kwenye sofa zuri mojawapo lenye rangi nyeusi likiwa la ngozi  linaloweza kukaliwa na watu watatu wasio wanene na hata wanene wa wastani bila kubanana.

Huko maegeshoni akashuka mwanaume wa makamo ambaye umri wake ni tofauti na umri wa yule wa kwanza aliyeshuka na kuingia ndani, huyu alikuwa amevaa kiraia suruali nyepesi rangi ya kijivu juu akiwa kavaa shati jeupe linalong’aa kwa weupe wake hakuchomekea licha ya kuwa lilikuwa la mikono mirefu, pengine hapendi kuchomekea, kichwa chake juu kabisa alivaa kofia kubwa aina ya marliboro rangi inayofanana na suruali aliyovaa na machoni mwake kulikuwa na miwani ya kioo chenye frem pana ya duara rangi nyeusi.

Naye alitupa macho yake huku na huko licha ya kuwa yalikuwa ndani ya miwani aliyovaa huku shingo yake ikisapoti kwa kupeleka kichwa huku na huko kama yule wa umri wa chini yake aliyeshuka mara ya kwanza, alipopiga hatua mbili mbele akatoa pakti ya sigara kisha kikafuata kiberiti kidogo cha gesi akawasha sigara yake akapiga hatua mbili tatu mbele na kuanza kupuliza moshi wa sigara uliokuwa ukipulizwa kwa wingi kiasi ya kwamba usingeweza kumuona vizuri usoni hapo akaanza mwendo wa kasi ya kawaida kuelekea lango kuu.

Watu hawa walimzubaisha kidogo Special Agent Silla kwakuwa kwa mara ya kwanza katika ubongo wake aliweza kuunda kitakachotokea kuwa gari itakayofika hata kama haitaonekana dhahiri shahiri kuwa ni gari ya polisi lakini watakaoshuka hawatakuwa wamevaa kiraia hivyo alimtizama yule aliyebakia ndani ya gari upande wa dreva kisha akabonyeza kitufe cha saa yake kuruhusu aongee.

   “Rebecca nipe mrejesho maana kuna mkanganyiko kidogo hapa” Akaongea Silla akizuga anajipapasa kidevuni kwa mkono wake wa kulia wenye saa ya mawasiliano.

    “Ameni text amefika hivyo endeleeni na kazi…. Nawatakia mafanikio mema..” Akajibu Rebecca na kuzima kitufe cha kuongea katika saa yake.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na tatu (53)

Mtego wa kumnasa Kamishina Mkuu wa Manispaa ya mji wa Antigua moja ya manispaa zinazounda jiji la Guatemala City unaendelea.

Je? Kamishina aliyejizatiti kwa kuchukua tahadhari kama ilivyo ada yake kwake kila mahala anapokwenda uwa ni mtu wa kuchukua tahadhari sana, atanaswa kwenye mtego huo.

Kila hatua ina maana ndani ya riwaya, tuendelee kufuatilia mkasa huu wa kutungwa nami!




Huko maegeshoni akashuka mwanaume wa makamo ambaye umri wake ni tofauti na umri wa yule wa kwanza aliyeshuka na kuingia ndani, huyu alikuwa amevaa kiraia suruali nyepesi rangi ya kijivu juu akiwa kavaa shati jeupe linalong’aa kwa weupe wake hakuchomekea licha ya kuwa lilikuwa la mikono mirefu, pengine hapendi kuchomekea, kichwa chake juu kabisa alivaa kofia kubwa aina ya marliboro rangi inayofanana na suruali aliyovaa na machoni mwake kulikuwa na miwani ya kioo chenye frem pana ya duara rangi nyeusi.

Naye alitupa macho yake huku na huko licha ya kuwa yalikuwa ndani ya miwani aliyovaa huku shingo yake ikisapoti kwa kupeleka kichwa huku na huko kama yule wa umri wa chini yake aliyeshuka mara ya kwanza, alipopiga hatua mbili mbele akatoa pakti ya sigara kisha kikafuata kiberiti kidogo cha gesi akawasha sigara yake akapiga hatua mbili tatu mbele na kuanza kupuliza moshi wa sigara uliokuwa ukipulizwa kwa wingi kiasi ya kwamba usingeweza kumuona vizuri usoni hapo akaanza mwendo wa kasi ya kawaida kuelekea lango kuu.

Watu hawa walimzubaisha kidogo Special Agent Silla kwakuwa kwa mara ya kwanza katika ubongo wake aliweza kuunda kitakachotokea kuwa gari itakayofika hata kama haitaonekana dhahiri shahiri kuwa ni gari ya polisi lakini watakaoshuka hawatakuwa wamevaa kiraia hivyo alimtizama yule aliyebakia ndani ya gari upande wa dreva kisha akabonyeza kitufe cha saa yake kuruhusu aongee.

   “Rebecca nipe mrejesho maana kuna mkanganyiko kidogo hapa” Akaongea Silla akizuga anajipapasa kidevuni kwa mkono wake wa kulia wenye saa ya mawasiliano.

    “Ameni text amefika hivyo endeleeni na kazi…. Nawatakia mafanikio mema..” Akajibu Rebecca na kuzima kitufe cha kuongea katika saa yake.

ENDELEA NA DODO ASALI..!

KAZI IMEANZA IV

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Miller, Miller.. “ Aliita baada ya kubonyeza kitufe kidogo kilichopo pembeni ya saa kisha akainua mkono wake wenye mpaka usoni kujifanya kama anatumia kitambaa cha leso kujifuta usoni akizunguka uso na kujifuta kumbe anaongea na mwenzake maongezi ambayo uwa wanajua yanakuwa si siri kwa wana kikundi kwakuwa wote walio kwenye mfumo huu wanasikia.

   “Nakupata, nakupata.. Lete habari?!” Akajibu Investigator Miller.

   “Mteja ameingia tayari.. Cheza na step, mi naangalia uwezekano wa kuwadhibiti wa nje!”

   “Bila shaka… Naamini Norman anatusikia.. Norman huko ulipo jiandae kwa msaada wa dharura hivyo sogea karibu!”Aliongea kujibu Silla kisha akaunganisha na maagizo akiyaelekeza kwa Detective Norman ambaye aliwaacha maegesho ya hotel hii kisha yeye kuelekea aliposema anaenda kuonana na rafiki yake anayemuamini sana licha ya kuwa yuko jeshi la polisi ambalo lina mkanganyiko sana.

   “Nimekupata na tayari niko njiani nakuja huko… Nawaamini sana” Sauti ya Norman ikasikika kwa wote ikijibu.

Mwanaume wa umri wa kumkadiria miaka hamsini na tatu ama na nne lakini akiwa na kimwili cha ukakamavu, mrefu na mwembamba na jinsi alivyovaa ikiwa nishaeleza uzuri hapo juu aliingia na kuelekea mapokezi lakini kabla hajaongea kitu kwa wahudumu akijitahidi kofia yake yake imzibe zaidi katika simu yake iliingia meseji haraka akasimama bila kujongea kwa karibu kabisa na meza ya wahudumua wa mapokezi iliyo hatua tatu toka aliposimama.

Meseji ilikuwa ikitoka kwa Special Agent Rebecca Smith anayemtambua yeye kama ni Monica Rojas mtangazaji wa Redio Antigua Fm, redio maarufu sana katika jiji la Guatemala, meseji ilikuwa ikimuelekeza achukue funguo kwa wahudumu yeye kashafika ila anaingia bafuni kuoga kuondoa vijasho kidogo vilimtoka wakati anapanda ngazi kuja kwenye chumba.

Kamishina Mkuu wa Polisi wa manispaa ya mji wa Antigua alifika pale na kwa kuhofia kuwa anaweza kuwa anafahamika sana na watu kutokana na umaarufu wake kwenye vyombo vya habari pale anapotangaza habari fulani ya kipolisi, ulinzi na usalama, hivyo basi alikuwa anapofika maeneo kama haya anaogopa kuchafuliwa heshima yake ikizingatiwa yeye ni mwanandoa, hakutaka kuongea mengi aliwapa salamu mabinti wale nao wakamjibu kisha akawaomba funguo ya namba chumba namba kumi na mbili.

Akaondoka pale mapokezi akiwa kakabidhiwa funguo ya kisasa ya ‘automatic card” inayotumika kufungua na kufunga vitasa vyote vya vyumba vya hotel hii, haraka aliondoka kwa mwendo wa kipolisi haswa akamaliza korido akakamata ngazi na kupanda mpaka flour (losheni) ya pili.

Alipotokeza kwenye korido mbele kabisa ilipo mwisho wa korido ndefu yenye vyumba kadhaa wa kadha akakutana macho yake yaliyo ndani ya miwani na aliyemtanguliwa kuingia ndani ya hotel wakaonyeshana alama ya dole, yeye akaanza kusoma namba za milango mpaka alipoiona namba kumi na mbili hapo hakujiuliza akatoa funguo kadi na kuisugua katika mwanya wa kitasa mara moja saini ya kijani ikatokea mlango ukajifungua akazama ndani ambako cha kwanza akapokelewa na sauti ya maji yanayomwagika bafuni (kazi ya Miller hii).

Baba wa watu akatabasamu mlango ulipojifunga akasogea hatua mbili mbele kisha akasimama hili afanye usahili wa chumba lakini kabla hajageuza shingo vizuri alijikuta akipigwa na kitu kizito kichogoni, ilikuwa ni kitako cha bastola kilichopigwa kwa kutokea nyuma na Investigator Miller, pigo takatifu lilitosha kumkata fahamu haraka sana Kamishina Alvaro Conedera mwili ukalagea akadakwa asidondoke kwa kishindo na kuwekwa chini taratibu.

  “Nimemaliza kazi ya kwanza wakuu!... Nimemzimisha kwa muda usingizi” Akaongea Investigator Miller.

  “Ameingia peke yake?” Akahoji Silla.

  “Ndiyo!yuko mwenyewe tu…!”

   “Alitanguliza mtu mmoja kuja huko.. Acha nipande nione ameenda wapi? Mtu aliyekuwa wa kwanza kushuka kwenye gari, hapa kwenye gari walimuacha dreva peke yake huyu ataangaliwa kwa ukaribu na Norman, ameingiza gari maegeshoni amesimama… Norman kushoto kwako gari aina ya Toyota Land Cruiser Prices angalia usalama mi naelekea juu kwa msaada wa kwanza!” Aliongea S.A Silla kwa sauti ya  haraka huku akijifanya anatembea mwendo wa kawaida kulisogelea lango kuu la kuingilia hotelini, Norman alikuwa kashafika na gari anayoendesha akawa ameiweka kwenye maegesho karibu na mahala ambapo walikubaliana atasimama hapo kusubiri ni mahala watakapoweza ingiza mtu au mzigo kwenye gari bila watu wengine kuona kwa urahisi.

   “I get you!” Akajibu kifupi Norman akimaanisha amempata.

Miller alimburuza Kamishina Alvaro aliye katika kuzirai hadi kitandani akamlaza juu kisha akamsachi mifukoni akachukua simu yake akiipata katika mfuko wa mbele wa suruali, ilikuwa simu aina ya HTC smartphone rangi nyeupe, aliitizama akaminya swichi yake ikatoka kwenye kusinzia na kuleta mwanga akasimama sababu ilihitaji pattern, hapo Miller akaisogeza karibu na macho yake kuangalia kioo chake kwa ukaribu kuna alama zilimfanya avutiwe kuileta karibu na macho yake akatoa miwani aliyovaa kwakuwa hakuihitaji.

Hakuwa mbali na alichofikiri na kuamua kukifanyia kazi alama ya vidole vinavyochora pattern haikuwa inajificha kwenye macho makali kama yake ambayo hayajaharibiwa kwa mchezo wa kujisugua mwenyewe hili kuita utamu (punyeto) na wala hayajaharibiwa kwa moshi wa sigara yoyote iwe sigara kubwa (bangi) wala sigara ndogo, alizungusha alama ya L simu ikafunguka kiulaini kana kwamba ipo kwenye mikono salama ya mmiliki.

Haraka akaifungua kwenye meseji na kukuta ina meseji nyingi zikiwemo zilizotumana kwa namba tupu ambazo hazipo kwenye phone book na ambazo zimetumana zikiwa na majina yaliyohifadhiwa kwenye simu hii.

Hakuwa na shida na meseji za muda mrefu uliopita yeye aliangalia ambazo zimetoka kuingia muda ambao unakaribiana na muda huu ambao yeye yumo katika chumba hiki, alikutana na zote ambazo majina yake yamehifadhiwa kwenye simu akafungua ya kwanza ambayo nayo ikakubali hakukuwa na kizuizi chochote, chumba hiki (inbox) ilikuwa imehifadhiwa kwa jina la ‘Double T’.

Kwakuwa  yeye Miller si mgeni wa lugha iliyohusika katika chatting za simu hii aligundua mwenye simu alikuwa akieleweshana na jamaa aliyeseviwa kwa jina la ‘Double T’ mambo yanayohusu hii safari iliyomfikisha katika chumba hiki, hapo Miller aligundua meseji chatting zilikuwa za bosi na mtu ambaye anahusika naye katika usalama wake, Kamishina mkuu wa jeshi la polisi manispaa ya mji wa Antigua Alvaro Canadero.

Akili ikafanya kazi haraka na akaamua kutunga meseji ya uongo ambayo ilielekeza kwa mtu huyo kuwa aje haraka katika chumba hiki kuna tatizo limemtokea mwanamke aliyemuita yeye Kamishina kuja hapa kisha akaituma, meseji ikafika na kupiga tiki mbili (delivered).

Kikapita kimya cha sekunde tatu tu toka ifike kwa muhusika aitwaye ‘Double T’ meseji ikarudishwa jibu kuwa ‘sawa’ kikitumika kilatin, Miller akapiga alama ya msalaba kushukuru kwa Mungu (kwa imani yake ya kikatoliki).

Haikupita sekunde nyingi mlango ukasikika unagongwa hodi, Miller akaikoki bastola yake na kushusha kilimi chake tayari kwa matumizi kama itahitajika kisha akachukua kadi funguo ya kitasa akasugua mahala husika mlango ukatoa mwanga wa kijani ulipotoa nafasi ya yeye kuonana na aliyegonga haraka alimuelekezea bastola.

   “Pita ndani bila fujo.. Mimi ni mwanausalama kama wewe!” Akaongea sauti ya kawaida akitumia kilatini, sauti aliyohakikishia inasikika eneo hili tu la mlangoni hamna kwenda mbali. 

Muitwa ‘Double T’ alistuka na alishindwa la kufanya alijikaza kiaskari asitetemeke, uso wa Miller ulimfanya asijihusishe na kufanya ujanja mwingine kwa wakati huo, uso ulionyesha huko makini na unachoongea, taratibu kama anasukumwa na mtu nyuma yake alinyanyua miguu yake iliyokuwa mizito ghafla akavuka kizingiti cha mlango na kuzama ndani, bastola ya mtu aliye makini akiwa anarudi nyuma ilikuwa ikimlenga eneo ambalo kwa vipimo vyake ‘Double T’ ni katikati ya pua na paji la uso.

   “Simama hapo.. Kisha toa kila kitu unachokifahamu wewe ni hatarishi kwa maisha ya mwingine.. Yaani kama una bastola, kisu hata peni naomba utoe urushie juu ya sofa lile pale..!” Akaamrisha Miller akiwa makini kumuangalia machoni mtu huyu.

Mlinzi wa Kamishina Mkuu wa jeshi la polisi akafanya kama alivyoamriwa maswali mengi yakizunguka kichwani mwake.

   “Usishangae sana kijana mwenzangu, mambo yetu ya kiusalama ndivyo yalivyo… Kaa hapo kitandani pembeni ya mkuu wetu kwanza kuna watu wanafika muda si mrefu hapa tunavyoongea mimi nawe wako njiani kupanda ngazi” Akaongea Miller! Bastola yake ikifanya kazi ya kuelekeza akae kwa ishara.

   “Umemfanyaje mkuu?” Akahoji ‘Double T’ huku anakaa, macho yamemtoka kama yanataka kumrukia Miller.

   “Busara iliyopo kwa sasa ni wewe kutouliza swali lolote.. Muda si mrefu utajua kila kitu..!” Akajibu kimaelekezo Miller.

   “Nawezaje kukaa kimya? Siwezi kuwa kimya wakati nimewekwa chini ya ulinzi na boss wangu ambaye muda wote natakiwa kuwajibika juu ya usalama wake.. Tafadhali nijibu wewe ni mwanausalama gani?” Akahoji tena akiongea kwa sauti ambayo ilimkera Miller, uso wa Miller ukakunjika zaidi lakini kabla hajafanya lolote mlango ukagongwa ikiambatana na sauti iliyofika katika mawasiliano yao ikiingia katika sikio la Mller.

  “Fungua tupo mlangoni!!”

Hakungojea akasogea na kadi mlangoni na kufanya inavyotaka mlango ukafunguka akaingia Detective Norman akitangulia mbele kisha akafuata Special Agent Silla na wa mwisho akaomba kadi na kufunga mlango.

   “Weweeeh! Wewe ndiyo umeshirikiana na wenzako kufanya haya?” Akapayuka ‘Double T’ baada ya kuangaliana na Norman.

   “Kufanya nini?” Akauliza Norman kumuuliza.

   “Si wakati wa maswali na majibu kwa hapa tulipo… Kinachotakiwa kujua tunaondokaje hapa, kumbukeni Kamishina Alvaro  anatakiwa mahala pakuu kwa maswali na majibu ya kazi” Akaongea Miller na Silla akajibu kwa kutingisha kichwa kuunga mkono kilichosemwa na Miller.

   “Unaitwa nani?” Silla akamuuliza mlinzi wa Kamishina wakati huo huo akiwa amesogea dirishani kuchungulia nje kutokea hapa.

   “Mmesema si muda wa maswali na majibu.. Sina la kujibu juu ya hilo!” Akajibu kijeuri.

   “Achaneni naye… Tulichotaka ni kumzuia yeye kutuzuia sisi kufanya kazi zetu… Kamuona Norman yuko hapa hivyo kifupi anajua wako mikononi mwa kina nani!” Miller akaongea huku bastola yake ikizungushwa zungushwa kitaalamu kwenye kiganja chake kimchezo mchezo.

   “Huko sahihi… Nafikiri kwa haraka hatutaweza kuondoka bila mashaka na watu hawa bila kumzindua Kamishina, hivyo basi cha kwanza tumzindue pia kule chini kuna dreva wake aliachwa naye pia ni askari kama hawa naye pia tumfikirie na kumpangia tunamfanyaje kwa haraka sana…!” Baada ya kumaliza kuchungulia alichokuwa akikichungulia huko chini kupitia dirishani Silla alirudi na wazo hili.

   “Sawa… Tumzindue kwa haraka… Wa huko nje tutajua cha kumfanya ikibidi na yeye tutaondoka naye..!” Akaleta alilonalo Norman, wote wakatazamana kisha Miller akasogea alipolazwa Kamishina akiwa katika hali kuzirai kitandani, akamshika shingoni kutumia vidole viwili sehemu ambayo kitaalamu yeye au hata watu wowote wale wanaojua masuala ya kiuzima kwa sisi binadamu.

   “Norman… Upo karibu na friji.. Naomba cheki kama kuna barafu..!” Akaomba Miller kwa Norman ambaye naye hakuremba akasogea lilipo friji akafungua na uzuri wake ni kweli alikuta kuna maji yameganda yakiwa katika chupa ya maji ya kunywa, akayachukua.

Dakika mbili tu zilitosha kumrudisha katika hali ya ufahamu wake Kamishina Alvaro akazinduka mikono yake ikikimbilia haraka kushika kichwa chake eneo la nyuma, uso akiwa kaukunja kama kalamba kitu kichachu, akafikicha macho na haraka akajiinua kukalia matako yake macho kayatumbua kama chura bibi kizee.

   “Kuna nini hapa?” Akahoji macho yakifanya usahili kwa kuzunguka kwa kila mmoja aliyepo hapa, yalipofika kwa mlinzi wake akastuka tena mdomo wazi.

   “Haaaah! Trent nini hapa? Kina nani hawa?” Akamuhoji kwa sauti iliyotoka ikipanga maneno kwa kasi iliyo na pupa ya kutaka kujua kunani.

   “Mimi mwenyewe sijui mkuu…. Nilitumiwa meseji kwa namba zako kuwa nije haraka ulipoingia kuwa umekuta tatizo, nikajua ni wewe, sikuwa najua kama mtego… Nilipofika nikawekwa chini ya ulinzi… Nisamehe mkuu sina makosa kwa kweli” Akajibu Trent ‘Double T’ wakiangaliana kwa shauku kubwa.

Kamishina akataka kusimama lakini akakutana na ishara arudi kukaa kutoka kwa watu wawili walio mbele yao kati ya watu watatu ambao wao walijua sasa kuwa ndiyo wamewateka na kuwaweka chini ya ulinzi.

   “Kama sikosei.. Wewe ni Norman?” Akahoji Kamishina swali lililomuelekea Detective Norman waliyekuwa wakiangaliana yeye akiwa kakaa pale pale kitandani alipo na Norman amesimama mbele yao na kina Silla wakiwa wamejipanga vizuri bastola zao zikiwa mikononi mwao.

   “Kamishina… Mimi ndiyo ni Norman wa OCLA lakini kama unavyotuona hapa hatuna swali juu yako kwa sasa hivyo nawe hautakiwi kuuliza lolote, la muhimu lililo mbele yetu kwa sasa ni wewe kutupa ushirikiano tukaondoka hapa… Hivyo usiulize lingine lolote zaidi ya kusikiliza maelezo yetu unatakiwa kufanya nini” Norman akamjibu kimaelekezo.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na nne (54)

Kamishina Alvaro Canedero ameingizwa katika mtego uliomnasa kwa tamaa ya kuhitaji kuonana na mwanamke aliyemtumia picha ikiwa ameanza kuandaliwa kuwa huyo mwanamke ameibiwa gari anahitaji msaada wake.

Bila kujua ni hila na hadaa hasa ikizingatiwa alikuwa akijiamini hana uadui mkubwa na watu ambao wanatishia maisha ya wanausalama walio wema katika nchi yake ya Guatemala, yeye anaingia mtegoni.

Je wataondoka vipi eneo la Soleil Hotel?”

Twende pamoja nami, twende nikupe fasihi andishi ya kile nilichohadithiwa toka ndani ya kifua chenye kuona mengine kwa wakati mwingine katika ubongo wa uhalisia wenye kutungwa ndani kwa ndani mpaka kufikia kuitwa ‘utunzi’, shukrani zikienda kwenye vidole vya mikono yangu vikifanya kazi ya kuyaandika na kuyafikisha kwako msomaji.




Dakika mbili tu zilitosha kumrudisha katika hali ya ufahamu wake Kamishina Alvaro akazinduka mikono yake ikikimbilia haraka kushika kichwa chake eneo la nyuma, uso akiwa kaukunja kama kalamba kitu kichachu, akafikicha macho na haraka akajiinua kukalia matako yake macho kayatumbua kama chura bibi kizee.

   “Kuna nini hapa?” Akahoji macho yakifanya usahili kwa kuzunguka kwa kila mmoja aliyepo hapa, yalipofika kwa mlinzi wake akastuka tena mdomo wazi.

   “Haaaah! Trent nini hapa? Kina nani hawa?” Akamuhoji kwa sauti iliyotoka ikipanga maneno kwa kasi iliyo na pupa ya kutaka kujua kunani.

   “Mimi mwenyewe sijui mkuu…. Nilitumiwa meseji kwa namba zako kuwa nije haraka ulipoingia kuwa umekuta tatizo, nikajua ni wewe, sikuwa najua kama mtego… Nilipofika nikawekwa chini ya ulinzi… Nisamehe mkuu sina makosa kwa kweli” Akajibu Trent ‘Double T’ wakiangaliana kwa shauku kubwa.

Kamishina akataka kusimama lakini akakutana na ishara arudi kukaa kutoka kwa watu wawili walio mbele yao kati ya watu watatu ambao wao walijua sasa kuwa ndiyo wamewateka na kuwaweka chini ya ulinzi.

   “Kama sikosei.. Wewe ni Norman?” Akahoji Kamishina swali lililomuelekea Detective Norman waliyekuwa wakiangaliana yeye akiwa kakaa pale pale kitandani alipo na Norman amesimama mbele yao na kina Silla wakiwa wamejipanga vizuri bastola zao zikiwa mikononi mwao.

   “Kamishina… Mimi ndiyo ni Norman wa OCLA lakini kama unavyotuona hapa hatuna swali juu yako kwa sasa hivyo nawe hautakiwi kuuliza lolote, la muhimu lililo mbele yetu kwa sasa ni wewe kutupa ushirikiano tukaondoka hapa… Hivyo usiulize lingine lolote zaidi ya kusikiliza maelezo yetu unatakiwa kufanya nini” Norman akamjibu kimaelekezo.

ENDELEA NA DODO!

KAZI IMEANZA IV

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Mkuu samahani kwa hili linalotokea lakini tumekosa njia sahihi ya sisi kukuchukua wewe kistaarabu kisha tukafanya nawe mazungumzo ambayo yanahitajika kikazi lakini sote unaotuona hapa ni maafisa wa usalama tunaohusika na vikosi vya kupambana na madawa ya kulevya eneo lote la Latin Amerika na pamoja na Kaskazini… Sisi wawili tunatokea Drug Enforcement Administration ‘DEA’ shirika la kuzuia na kupambana madawa ya kulevya la Marekani na mwenzetu huyu mmoja ambaye si mgeni machoni mwako anatokea Organized Crime Of Latin America ‘OCLA’, majina yetu utayajua mbele tukijaliwa kuondoka nawe salama hapa kama tunavyotarajia itakuwa hivyo… Hivyo usihofu kwakuwa wewe ni mwanausalama mwenzetu ila tu kuna katofauti kadogo tumegundua ndiyo maana tunahitaji kujua jambo kutoka kwako muhusika!” Akaeleza Investigator Miller kwa kirefu kidogo na pia alikuwa akihitaji kuendelea kueleza akakatiziwa na Kamishina kwa swali alilouliza.

   “Maafisa wa vikosi vya kupambana na madawa ya kulevya… ndiyo! Sasa hapo mimi naingiaje? Mimi ni kamishina wa jeshi la polisi naheshimika sana na si….” Akahoji kiukali Kamishina Alvaro lakini naye hakuendelea alikatiziwa kwa sauti ya ukali pia.

   “Funga mdomo wako.. Shiit!” Alifoka S.A Silla uso ukikunjamana mpaka akawa mwekundu zaidi ya weupe wake mzungu huyu.

   “Bosi! Umesahau kidogo… Hapa kwa sasa upo chini yetu haupo tena chini uhuru uliokuwa nao na wala haupo na watu unaoweza kuwaamrisha na hata kuwauliza wakajibu vile wewe unataka sababu ni kiongozi wao… Chunga ulimi wako tafadhali Alvaro Conedera… Nakuelekeza jambo sijamaliza unauliza swali, usirudie tena nikakung’oa kende zako!..... Tunaondoka na wewe hapa pamoja na mlinzi wako mkiwa chini ya ulinzi wa siri… Kumbukeni hamko na watu wa saizi ndogo katika masuala haya hivyo ujanja wowote kati yenu utagharimu roho zenu bila kujali chochote na popote” Akamalizia Miller baada ya Silla kumkanya Alvaro.

   “Shika simu yako wee bwana mkubwa… Kisha mpigie dreva wako aondoke maegeshoni aende akakuchukulie kitu chochote pale ambacho wewe unapenda na uwa unamtuma… Haraka fanya hivyo!” Maelekezo mengine akayatoa Silla huku akipokea simu ya Kamishina Alvaro kutoka mikononi mwa Miller ambaye alikuwa kushoto zaidi wakati yeye Silla alikuwa karibu na Kamishina, hivyo mkono ukanyooka kumpa simu Alvaro.

Kamishina Alvaro Conedera alipiga namba za dreva wake kama alivyoelekeza na mara ikapokelewa.

   “Zreyis… Naomba uende kituoni ukamwambie sekretari wangu kuwa akitoka ofisini apite kwangu amwambie mke wangu nitachelewa kurudi, mimi nampigia simu hapatikani mke wangu na wala hapatikani sekretari wangu, fanya haraka kasha kama pia una safari nyingine nenda tu mi nitatoka usiku kabisa hapa, nitakujulisha unifuate” Kamishina Alvaro akaongea uongo mzuri mpaka hadi kina Kai huko walipo wakiwa wanafuatilia mazungumzo haya walifurahi sana mpaka kugonga viganja vyao na si wao tu hata hawa waliopo hapa pia walifurahishwa na uongo wa Kamishina.

Simu ilikatwa akanyoshewa mkono wa kulia ampatie Silla naye bila hiyana akakabidhi simu yake kana kwamba si yake.

  “Norman utatangulia mbele kuongoza msafara… Tukitoka hapa kirafiki kabisa bila kuzionyesha silaha zetu zitatumika endapo masharti yetu yatakiukwa na yoyote kati yao hawa ndugu zetu… Pale mapokezi tutatakiwa wote tuchangamke kwa maongezi hili nalo msisahau hasa nyinyi mateka wetu” Miller akaeleza kisha amri za vitendo zikaanza.

Norman akafungua mlango akiwaongoza kwa nyuma yake walikuwa wako sambamba Kamishina na mlinzi wake Trent Tabaros “Double T’ nyuma yao wakifuatwa na wataalamu wawili wakiwa wameweka mikono yao mifukoni ikiwa imekamata chuma cha kazi (bastola).

Walikwenda wakiongozana kupitia njia ambayo alipita Investigator Miller wakati anapanda kuja flour hii ya pili, msafara wao ukatokea mgahawa wa hotel ambako hapa walijifanya kama wanaongea kwani Silla alianzisha mazungumzo ya swali alilotupia kwa Norman aliye mbele.

Msafara wao ulifika maegeshoni na kama nilivyoeleza awali kuwa gari alilokuwa nalo Norman alilipaki karibu na mlango hivyo haraka wakaingia wao na mateka wao kisha ya hapo gari ikawashwa na Dreva yule yule mwenyeji wa nchi wakaondoka Soleil Hotel wakiwa wamekamilisha misheni ndogo ya kumteka Kamishina wa jeshi la polisi katika manispaa ya mji wa Antigua, moja ya manispaa kubwa na maarufu zaidi katika jiji la Guatemala.

    *****  *****  *****

KAZI IMEANZA V

CHIMALTENANGO, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Hatuwezi kufanya naye mahojiano katika chumba chetu cha mawasiliano… Naamini kuna chumba kingine kitakachoweza kufaa kwa kazi hiyo” Alikuwa Agent Kai akiongea karibu na sikio la Norman, akiwa amemvutia kwa pembeni Norman mwenyeji wa nyumba hii iliyopo Sign Street. Mtaa uliopo mji wa manispaa ya Chimaltenango ikiwa watekaji wa kamishina wakiwa wamewasili ndani ya nyumba hii.

   “Huko sahihi… Kipo chumba kinachofaa kwa kazi hiyo ni ambacho yule mjinga aliyegoma kuongea tumemuhifadhi huko” Akajibu Detective Norman wa OCLA.

   “Wapelekeni huko… Mimi namalizia kusikiliza audio nilizotumiwa na Lizy anayemfuatilia mwanadada tunayemtafuta, andaa kila kitu unachoona kitatusaidia katika mahojiano endapo itahitajika nguvu ya kumtapisha tunayoyataka… Nakuja!” Akamaliza maelekezo ‘TSC’ kasha yeye akarudi chumba cha mawasiliano alikomuacha mshirika wake wa karibu Special Agent Rebecca Smith.

   “Cheni ya hapa GTL imekuwa ndefu sana… Vigogo wa serikali hii wanaiuza nchi yao bila Rais wao kujua amezungukwa na wanafiki wengi sana katika suala la upambanaji na madawa ya kulevya” 

   “Ndiyo umefika nchi hiyo sasa, hatuna njia ingine zaidi ya kuzuia mambo hayo kuendelea tena sababu yanatusumbua pia na sisi wamarekani katika njia moja ama nyingine kama ujuavyo DEA, FBI na CIA wanavyojitahidi kupambania watu wetu tena tukitumia bajeti kubwa sana.. Imefika muda wako kukata mzizi mkuu pengine itatusaidia kupunguza makali yake, wewe ni shujaa wetu”

   “Siko peke yangu! Wewe humo, Rebecca yumo na ndugu zetu waliojitolea kuwa nasi bega kwa bega wamo kwa pamoja tunatakiwa kupigana mpaka ulipo mwisho wa uwezo wetu, watu hawa wamejipanga vilivyo… Nimesoma kidogo historia ya TRJ uliyonitumia ukiwa umekusanya habari zao kwa undani ni hatari sana… Itahitajika nguvu ya ziada na kujitolea kuangusha genge kama hili”

   “Kai! Sawa na tingatinga, umepambana vita nyingi sana hivyo nakuamini sana, nitaendelea kutafuta kona zote msaada wa kiteknolojia za kiitelejensia kujua mengi zaidi, mwisho wao umefika kama ilivyokuwa kwa El-Chapo na Feca anakwenda kudondoka kwa kishindo kikuu..!”

   “Sawa Lizy.. Acha nifanye mahojiano na mgeni wetu aliyefika hapa… Kazi nzuri sana tutafanyia kazi kila unalokusanya kutokea Eisenhower”.

Yalikuwa ni maongezi ya simu ya njia ya whatssap iliyopigwa na Lizy Roby kutokea Marekani akipiga kwenye simu ya Agent Kai ikiwa alikuwa amemtumia audio tatu za mawasiliano ya simu aliyofanya mwanamke wanayemtambua wao kwa jina la Valentina, wakati Norman alivyofika katika mlango wa chumba hiki kuleta taarifa kuwa washafika yeye Agent Kai aliacha kuongea kwa simu akaenda kumsikiliza na alilpomaliza pokea ujumbe naye kutoa maelekezo akarudi kuendelea kuongea kwa simu hii ya njia ya whatssap.

Walitoka katika chumba hiki wakaelekea sebuleni ambako kulikuwa kunasikika maongezi ya kina Silla wanaongea maongezi yao ya kawaida wakifurahi.

   “Vipi jamani?” Akasalimu Agent Kai akitabasamu kwa jinsi stori alizozikuta hapa za marafiki hawa washirika toka DEA wakiwa wenyewe wanapata vinywaji aina ya bia, Norman hayupo.

   “Safi.. Lete habari?” Wakajibu kwa pamoja kana kwamba wanaimba nyimbo fulani wanayoipenda jinsi maneno yalivyojipanga kwa kasi moja. 

   “Kazi inaenda vizuri kwa pande zote mbili.. Hapa GTL na kwa mwenzetu wa Eisenhower amekuwa akifanya kazi nzuri sana mpaka inanipa hamasa sana kuwa nafanya kazi na watu wa kazi haswa kuanzia upande wetu na wenu wote DEA na Norman, tufanye mahojiano na Kamishina kwanza kasha nitahitaji kikao ya nini tunaenda kufanya usiku wa leo pengine unaweza kuwa usiku mzuri zaidi kikazi” Akajibu kwa maelezo marefu kidogo.

Norman alitokea kutoka chumbani kwake na waliopo hapa ambao walikuwa wamekaa kwenye masofa wakipiga stori na kunywa walipomuona Norman wakasimama kama walivyosimama Agent Kai na Rebecca wakiwa kwenye kona ya korido iliyowaleta toka chumba cha mawasiliano na ofisi yao ya dharura.

   “Tulikuwa tunataka kwenda kuongea na Kamishina… Jiunge nasi tukamsikie na kumjua mwanamke Valentina ni nani?” Agent Kai akamwambia Norman, wote wakaongozana kuelekea chumba ambacho Silla, Miller na Norman walikuwa wakifahamu kilipo ila Rebecca na ‘TSC’ hawakuwa wakijua kipo wapi? Walitembea wakiwafuata wenzao wanaojua.

Ukafunguliwa mlango ulio mwisho ya korido huko wakatokea katika eneo la stoo ya vyakula na vitu vingine vinavyotumika jikoni, ambako Norman alisogea zilipo swichi za ukutani ambazo zilijipanga kama tano hivi, akabonyeza moja iliyo katikati papo hapo ukuta uliokuwa hauonekani kama una kijiuwazi chochote kwa pembeni ya swichi ukajiachia hapo Norman akageuka kumuangalia Agent Kai na wote wakatabasamu kisha kimya kikaendelea.

Norman akaingia na wengine wote wakamfuata ikawashwa taa iliyo ndani ya korido wakajikuta wako katika chumba, mbele yao kuna meza kubwa ya bati aina ya mstatili ikiwa na vifaa mbalimbali ambavyo mafundi wa shughuli za kijasusi na wahalifu wakiona hivi iwe wametekwa au wameingia tu kwa bahati mbaya ujua vifaa vilivyo katika meza hii ni vifaa vya nini?.

Upande wa kona ya  kushoto  mwa chumba kulikuwa na kiti cha chuma kikiwa kimekaliwa na mtu aliyefungwa kwa kamba waya za umeme ikiwa alivyofungwa si kumzungusha mwili wote, alikuwa amefungwa mikono na miguu tu sambamba na kiti sehemu zingine akiwa huru, Agent Kai akamuangalia vizuri na yule mtu mwenye umri uliowazidi wao wote anaweza akawa baba yao bila shaka kama angekuwa mtundu wa mambo matamu, akiwa kakunja uso kwa hasira macho yake aliyakaza kwake akiwa na maswali mengi yasiyo na majibu juu ya sura ya kijana mwenye asili ya Afrika anayoiona mbele yake.

‘TSC’ macho yake yakiongozwa na shingo yake alitizama kulia nako kulikuwa na kiti kama kile cha upande wa kushoto, nacho kikiwa na mtu aliyefungwa kama yule wa kushoto lakini huyu sasa umri wake ulishabahiana na wao (kijana mwenzao).

   “Huyu kulia ndiyo mlinzi wa mheshimiwa bila shaka” Akaongea Agent Kai akitumia lugha ambayo wote hapa wanaisikia vizuri kilatin.

Silla, Miller na Norman wakatikisa vichwa vyao kukubali kilichosemwa na kiongozi wao katika misheni hii.

   “Huyu anaweza kuulizwa swali ambalo litaingia kilazima kutokana na boss wake kuyumba kujibu, na huyu mliyemlaza chini tutajua cha kumfanya baadaye atatapika tu.. Moja kwa moja tunakuja kwako mheshimiwa Kamishina Mkuu wa jeshi la polisi Manispaa ya mji wa Antigua” Akiwa kasogea karibu yake Agent Kai alianza kumuongelesha Kamishina anayetizamana naye yeye akiwa kakunja sura kama anasikia maumivu makali kumbe ana hasira kwa watu hawa wliopo mbele yake.

   “Hivi vijana mnajua kosa mnalolifanya ni kosa gani? Na kubwa kiasi gani?” Akahoji kwa sauti yenye kuhakisi hasira alizonazo Kamishina Alvaro Conedera. Macho yake ya kutisha akiyatumbua kumtizama Agent Kai, macho ya rangi ya bluu ya mzungu huyu yalitisha kama paka.

  “Hayo macho unavyoyatumbua kana kwamba mbele yako kuna majambazi wamekamatwa na vijana wako wa kipolisi hivyo majambazi wako chini yako hayawezi kukusaidia kwetu ni macho yaliyojaa uwoga mkubwa uliojificha ndani ya ushujaa wa muda, msaliti wa jeshi la polisi… Mambo unayoyafanya hayafanani na viapo tunavyoapa wana usalama katika nchi yoyote pale tunapomaliza mafunzo na kukabidhiwa vyeti vyetu” ‘TSC’ akampa maneno ya kumuonya juu ya macho yake Kamishina ambaye alistuka kusikia yeye ni msaliti wa kiapo alichoapa baada ya kuwa amemaliza mafunzo yake kiuaskari polisi.

  “Niliambiwa nikae hapa kusubiri kuongea na kiongozi… Wewe ndiyo kiongozi wa watekaji?” Akahoji Kamishina.

  “Wakati wanakuchukua hawakukupa rulling zetu?”

  “Mimi ni mwanausalama mkubwa katika nchi hii… Mimi ni mkuu wa usalama na ulinzi wa wananchi wote wa watu wa Manispaa ya Antigua, najua mnazijua sheria za kumkamata mtu kuwa kuna utaratibu hasa mtu ambaye si mhalifu kama mimi na mlinzi wangu, nahitaji kujua nyinyi ni kina nani? Na kwanini nimechukuliwa kama mhalifu wakati mkiwa kama wanausalama mnaweza fanya utaratibu wa kufanya mazungumzo nami, kati yenu namjua Norman wa OCLA naye ananijua kwakuwa mara kadhaa tumegongana sehemu mbalimbali katika kuhakikisha usalama wa wananchi wetu na mali zao ikiwa yeye nimekutana naye mara nyingi katika mambo yanayohusu mihadarati” Akaongea kirefu kidogo Kamishina akisikilizwa na majasusi hawa walioenea katika idadi yao yote walio katika misheni hii nchini Guatemala.

  “Naitwa Agent Kai Hamis natokea shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani lijulikanalo kama Drug Enforcement Administration kwa kifupi ‘DEA’ na hawa wenzangu wote unaowaona ambao wewe huwajui wanatokea DEA pia, tupo hapa Guatemala kwa operesheni fupi na ndogo ambayo wenyeji wetu ni Organized Crime Of Latin America kifupi ‘OCLA’ tukiwa na kijana huyu unayemjua Detective Norman Cabrera kijana mzalendo mwenye kujituma katika mapambano ya madawa hatarishi katika nchi yake lakini akaikatishwa nguvu yake ya kupambana na watu kama wewe… Hatujakuchukua wewe kimakosa, tumekuchukua kwa sababu zenye mashiko yote… Hivyo tunaomba u relax ujibu maswali yetu kwa ufasaha hili kama tutaona ushirikiano wako ni mzuri tutakujumlisha katika operesheni hii bila kukufikisha katika vyombo vya sheria vinavyofanya kazi kwa maelekezo ya OCLA” Agent Kai ‘TSC’ akaamua kujitambulisha kwa jina lake la ukweli ila akijiamisha kituo cha kazi kutoka shirika la kijasusi la CIA kwenda shirika la upambanaji na madawa ya kulevya la DEA, hakukosea sana sababu DEA ndiyo haswa wahusika wa hili jambo walilonalo sasa.

   “Ndiyo  bwana mkubwa… Mimi nimeingiaje mpaka nipewe shutuma kubwa kama mnayonipa kuwa mimi si mzalendo? kama alivyo Norman” Hapa kidogo sura ya Kamishina ilisawajika kusikia walio mbele yake ni maafisa wa DEA, moyo wake uliweka mstuko ambao aliuzuia kwa kiasi kikuu asiuonyeshe kwa watu hawa wanaomtumbulia macho wote kwa pamoja, aliuliza swali.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na tano (55)

Kamishina ndani ya chumba cha mahojiano, chumba chenye meza ambayo macho yake yalipotizama vifaa vilivyo juu yake aligundua ama kweli ana kazi kubwa mbele yake, taratibu hisia zake zilianza kuhisi nini watu hawa wanataka kwake.

Je itakuwaje upande wake?

Mahojiano baina yake na aliyeambiwa ndiyo kiongozi ya waliomteka Agent Kai ndiyo yameanza.

Je Kamishina atafunguka yanayotakiwa kufahamika kwa majasusi walio mbele yake?




  “Wakati wanakuchukua hawakukupa rulling zetu?”

  “Mimi ni mwanausalama mkubwa katika nchi hii… Mimi ni mkuu wa usalama wa wananchi wote wa watu wa Manispaa ya Antigua, najua mnazijua sheria za kumkamata mtu kuwa kuna utaratibu hasa mtu ambaye si mhalifu kama mimi na mlinzi wangu, nahitaji kujua nyinyi ni kina nani? Na kwanini nimechukuliwa kama mhalifu wakati mkiwa kama wanausalama mnaweza fanya utaratibu wa kufanya mazungumzo nami, kati yenu namjua Norman wa OCLA naye ananijua kwakuwa mara kadhaa tumegongana sehemu mbalimbali katika kuhakikisha usalama wa wananchi wetu na mali zao ikiwa yeye nimekutana naye mara nyingi katika mambo yanayohusu mihadarati” Akaongea kirefu kidogo Kamishina akisikilizwa na majasusi hawa walioenea katika idadi yao yote walio katika misheni hii nchini Guatemala.

  “Naitwa Agent Kai Hamis natokea shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani lijulikanalo kama Drug Enforcement Administration kwa kifupi ‘DEA’ na hawa wenzangu wote unaowaona ambao wewe huwajui wanatokea DEA pia, tupo hapa Guatemala kwa operesheni fupi na ndogo ambayo wenyeji wetu ni Organized Crime Of Latin America kifupi ‘OCLA’ tukiwa na kijana huyu unayemjua Detective Norman Cabrera kijana mzalendo mwenye kujituma katika mapambano ya madawa hatarishi katika nchi yake lakini akaikatishwa nguvu yake ya kupambana na watu kama wewe… Hatujakuchukua wewe kimakosa, tumekuchukua kwa sababu zenye mashiko yote… Hivyo tunaomba u relax ujibu maswali yetu kwa ufasaha hili kama tutaona ushirikiano wako ni mzuri tutakujumlisha katika operesheni hii bila kukufikisha katika vyombo vya sheria vinavyofanya kazi kwa maelekezo ya OCLA” Agent Kai ‘TSC’ akaamua kujitambulisha kwa jina lake la ukweli ila akijiamisha kituo cha kazi kutoka shirika la kijasusi la CIA kwenda shirika la upambanaji na madawa ya kulevya la DEA, hakukosea sana sababu DEA ndiyo haswa wahusika wa hili jambo walilonalo sasa.

   “Ndiyo  bwana mkubwa… Mimi nimeingiaje mpaka nipewe shutuma kubwa kama mnayonipa kuwa mimi si mzalendo? kama alivyo Norman” Hapa kidogo sura ya Kamishina ilisawajika kusikia walio mbele yake ni maafisa wa DEA, moyo wake uliweka mstuko ambao aliuzuia kwa kiasi kikuu asiuonyeshe kwa watu hawa wanaomtumbulia macho wote kwa pamoja, aliuliza swali.

ENDELEA NA DODO ASALI!!!

KAZI IMEANZA VI

CHIMALTENANGO, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Jana wakati tumeingia nchini Guatemala kulitokea mauaji ya watu kumi na watatu katika manispaa yako Antigua unayoiongoza… Mpaka sasa ukiwa kama kiongozi wa usalama wa mji huo umeshajua wahusika wake?” Maswali ya kimitego toka kwa fundi maswali ‘The Sole Cat’ yakaanza.

   “Niko tayari kujibu maswali yenu lakini kwanza ningeomba kuelezwa kwanini mimi?”

   “Unataka kujua kwanini wewe? Nijibu tu kiwepesi kwa sababu ni wewe ndiyo huko hapa wewe na si mwingine mheshimiwa… Tafadhali usichelewshe muda jibu maswali nayokuuliza askari unajua kabisa sheria hizi!”

   “Sheria zina mipaka pia… Naitwa Kamishina Alvaro Colnel Conedera ni kamishina mkuu wa polisi wa mji mkubwa kabisa katika jiji la Guatemala kuna taratibu za mimi kuhojiwa na si kama unavyotaka wewe kijana toka Marekani… Sina jibu bila kujulishwa niko hapa kwanini? Na kwanini hamkutaka kufuata taratibu husika kunipata kiusalama tukaongea vizuri kiusalama” Akajibu tena kijeuri ingawa kwa sasa sauti yake ilikuwa na nidhamu lakini jeuri ya maneno yake haikujificha.

   “Kiongozi… Hauoni huyu anatuchelewesha hasa ikizingatiwa kuna kazi zimejitokeza mbele yetu… Au?” Akauliza Special Agent Rebecca Smith akimtizama Agent Kai ambaye yeye alikuwa anamtizama Kamishina na kwa mbali hali ya hasira ikijisogeza katika kifua chake toka mahali inapoishi mwilini mwake.

   “Tulia Rabecca… Huyu pia ni muhimu sana kwetu kabla hatujaenda kwa hao wengine… Kumbukeni huyu pia anafanya mawasiliano moja kwa moja na wahusika tena akipokea maelekezo anayatekeleza hivyo hapa alipo ang’oke meno ang’oke kende zake mpaka aseme anayoyajua juu ya yale yaliyofungwa kwetu kwa kitambaa cheusi..!” Akaongea ‘TSC’ kujibu hoja ya Rebecca.

   “Usiwe  na haraka mpendwa.. Kama anavyosema TSC.. Mtu huyu ni afisa wa polisi tayari machoni mwake kwa sisi majasusi wabobezi tushajua nini alichonacho hivyo uvumilivu muhimu sana hata kama nao una kikomo chake” Special Agent Silla akapooza munkari ya Rebecca licha ya kuwa kiongozi wao alishafafanua.

   “Kamishina mbele yako tuko watu ambao tuna roho kama za watesaji wako unaowatumia kuwatesa wahalifu wafunguke katika yale yanayohitajika na pengine sisi tunaweza kuwa makatili zaidi ya hao watu wako.. Tunaomba ushirikiano wako… Jana sisi majasusi wa DEA kutokea Marekani tuliingia hapa Guatemala na tukafanya kikao cha kwanza katika mgahawa wa kitalii wa Filadelifia Coffee Resort and Tours uliopo mtaa wa Carratera San Felipe barabara ya Jocotenango karibu na hotel ya Casa Madelaine Hotel… Mpaka hapa nafikiri nitakuwa nishajibu kwanini wewe? Kwanini huko hapa nasi katika chumba hiki maalumu na tena ukiwa umefungwa kama muhalifu na si afisa mkuu wa polisi wa mji mkubwa wa Antigua” Akaongea Agent Kai kwa sasa akifafanua kwa uzuri zaidi kiasi ya kwamba nguvu za asili anazokuwa nazo mwanaume yoyote mwenye kujiamini ilipungua kwa asilimia ishirini mpaka thelathini katika mwili na akili yake Kamishina Alvaro Conedera.

  “Sasa mnataka kujua kuhusu nini? kuhusu icho kikao chenu ambacho wahusika wa kikao ni nyinyi wenyewe” Akajitutumua kuuliza Kamishina Alvaro kana kwamba hajui kitu wakati akiwa kama mtaalamu wa mambo haya kiuchunguzi na kiusalama alikuwa kashajua kwanini ameletwa kwa nguvu hapa na watu hawa wanaojihusisha na upambanaji na madawa ya kulevya.

   “Boss! ebu msikilizishe audio ya simu yake aliyokuwa akiongea na mtu wake pengine anaweza kuturahisishia kujibu alilonalo kwa ufasaha..!” Rebecca akaweka ombi kwa ‘TSC’.

Ni kama ombi la Rebecca lilieleweka kwani Agent Kai aliinua Ipad yake aina ya Samsung aliyokuwa kaishika mkononi muda wote ikiwa ime sinzia tu, akaiwasha swichi yake kurudi katika hali kuwaka kisha haraka akacheza cheza kutafuta audio husika inayohusika, alipoipata akairuhusu kusikika.

   “Namba hii ni yako na sauti iliyosikika ikipokea maelekezo toka kwa mwanamke ni yako… Hapa sasa tutaelewana, sisi tunataka kumjua huyu mwanamke ni nani na tunampataje? Ni hivi tu Kamishina ingawa nawe unashiriki katika masuala haya, tunaomba kupata taarifa za tunapoweza kumpata kisha wewe hatutakuwa na mpango nawe katika kadhia hii tutakuacha ukaendelea na mambo yako” Akaongea Rebecca akiwa kamkazia macho mdanganya wake aliyemuingiza ‘king’.

Kimya kilitanda kwani Kamishina alishikwa na aibu ya kuweza kuwa na hata ujasiri wake wa kawaida kuwaangalia wanaume na mwanamke mmoja aliye mbele yake, alibaki kainamisha uso wake chini kwa sekunde kadhaa, alipouinua uso wake baada ya mmoja ya watu walio mbele yake kufanya msogeo hivyo sauti ya viatu alivyoviburuza vikamfanya awe kama karejewa na fahamu, aliwatizama wote kwa kasi kisha akaigeuza shingo yake kulia kwake akayatupa macho yake alipo mlinzi wake ‘Double T’ macho yao yakagongana yeye kamishina akakwepesha kana kwamba hakutaka yeye shingo igeukie huko upande alipo mlinzi wake.

   “Naomba mnisamehe vijana wangu… Naomba nikiri sauti hiyo inayosikika ni yangu… Naona aibu na nashindwa nianzie wapi kwakweli!” Akaanza kueleza Kamishina akiwa uso wake kauinamisha chini wakati huo huo S.A Rebecca aliingia haraka sehemu ya simu yake kurekodi akaruhusu ianze kurekodi.

   “Anzia unapoona ni sahihi na itakuwa bora kwako na kwetu tunaotaka kukuondoa katika utumwa maana jambo unalofanya ni utumwa kwa Kamishina mkubwa kama wewe unayeaminiwa na jeshi la polisi pamoja serikali yako”. Investigator Miller kwa mara ya kwanza toka waingie katika chumba hiki akaongea.

   “Kwanza nasikitika kusema mmeingia katika jambo ambalo kimsingi katika nchi yetu ni jinai lakini kulifuatilia ni kama jinai pia kwa jinsi lilivyo katika usimamizi wa ajabu kama si kosa katika sheria za kimataifa… Nafikiri Norman anajua hili kwakuwa naye ni mhanga wa suala hili akiwa anaishi katika mazingira ya mnyama mdogo aina ya digidigi asiyeonekana kirahisi iwe mchana au usiku hasa katika nchi zetu za ukanda wa Amerika…. Si kama mimi au mwanausalama mwingine yoyote kiguateamala anapenda kuhusishwa katika mtandao maana si amri yetu tunaingizwa kama lazima hivyo nitashangaa sana kama nyinyi moja kwa moja mtataka kupambana mpaka kuondoa utumwa mnaosema upo miongoni mwetu” Alianza kutiririka kile ambacho kilifanya ukimya kuongezeka zaidi miongoni mwao wote walio mbele yake na hata yule mlinzi aliye kulia kwake hatua kama saba toka kona kwa kona ya chumba hiki kidogo, alipumzika akawaangalia majasusi walio mbele yake kwa macho yaliyojaa kupooza maana yalijiona msaliti haswa lakini alihitaji huruma ya watu hawa.

   “Mimi nilipopanda cheo miaka miwili tu iliyopita kutoka katika cheo changu cha Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mji wa Iztapa nililetwa hapa Antigua na kuwa Kamishina Mkuu… Siku ya kwanza tu nilipokanyaga ofisini niliitwa kwenye kikao nilichoelekezwa cha maelekezo ya kazi kwa makamishina wote wapya katika ofisi ya waziri wa usalama wa nchi… Kikao kile kilifanyika katika ukumbi wa ndani wa mikutano tukiwa tumehudhuria makamishina wapya wakuu wote na hata wa zamani kutoka miji yote yote inayounda jiji la Guatemala, nakumbuka katika kikao kile waziri wa usalama mwenyewe alikiongoza walikuwepo na watu wengine sita ambao sikuwa nimewai kuwaona kabla wote wa rangi kama yetu namaanisha wazungu wanawake wakiwepo wawili tu katika watu wote walio hudhuria kikao kile ambacho onyo la kwanza lilitushangaza licha ya kuambiwa ni kikao kilichoambatana na tafrija ya kutupongeza makamishina wapya hivyo ni kikao cha furaha ambacho kikawaida kila mmoja wetu angependa abaki na kumbukumbu ya hata picha tu kupiga na mheshimiwa waziri ila onyo lilikuwa hakuna kupiga picha wala kushika simu mkononi, simu zote ziliachwa mlangoni kwa mlinzi tuliyemkuta akiangalia na kufanya ukaguzi kwa kila mtu anayefika pale akiwa amealikwa..” Aliongea kirefu Kamishina Alvaro alipofika hapa alinyamaza kidogo akawaangalia wanaomsikiliza macho yao wote yakiwa makini kwake, yeye akajiweka sawa kidogo akiwa kafungwa mikono anatamani ajifute mdomo lakini hakuweza.

   “Mkuu! Naomba mnipe uhuru angalau mdogo wa kunifungua kamba za mikono..” Akaweka ombi macho yake makubwa yakimtizama Agent Kai ambaye naye bila kujiuliza katika halmashauri ya kichwa chake alimgeukia Norman aliye upande wa kushoto kwake.

   “Mfungue kamba zote… Pia mpatieni maji ya kunywa halafu aendelee kutueleza…!” ‘TSC’ akamueleza Norman, kijana huyu haraka akasogea alipo Kamishina Alvaro na kumfungua kamba za waya umeme walizomfunga alipomaliza Rebecca akawa kafika na bilauri kubwa iliyojaa maji pamoja na glasi akammininia glasini na kisha kumpatia, mzee akayafakamia yote kuja kushusha glasi ikawa nyeupe peee.

Mlinzi wa Kamishina naye akafungua mdomo toka kwenye kona yake alipofungwa na kukalizwa kitini kama ilivyokuwa boss wake, aliomba asaidiwe maji na yeye.

   “Mfungue na yule apate maji kisha msogeze huku awe pembeni ya boss wake awe chini ya uangalizi wetu sote.. Kwenye kiti mtamfunga huyu anayejifanya anajua kufuatilia watu” Akaongezea tena ‘TSC’ baada ya ombi la ‘Double T’

Huduma ya haraka zilifanywa kwa mateka hawa wakipewa huduma walizoomba kwa usahihi ilikuwa hafadhali yao kuwa Agent Kai ni mmoja wa watu walio na pande mbili za uhakika kabisa miongoni mwa majasusi walio juu katika kazi zao, alikuwa mtu wa huruma ikiwa anaona inahitajika huruma pia ni mtu wa hatari sana tena kuliko hatari zote ambazo umewai zishuhudia pale anapoona mambo hayaendi sawa inahitajika kazi ya ziada isiyo na huruma au pale anapoona anatakiwa kujiokoa katika hatari uwa anafanya lolote ilimradi awe huru.

   “Endelea Kamishina, kiu ishakata na muda si rafiki..!” Akaomba Agent Kai baada ya kuona sasa washatulia mateka wao.

   “Mwanamke mmoja ambaye mimi nilikuwa namjua ni Kamishina Mkuu wa polisi wa manispaa ya mji wa Sacatepequez lakini mwanamke mwingine ambaye nilimkuta tayari yupo na kaka safu ya mbele alipo waziri wa usalama sikuwa namjua na ndiyo huyo mnayesema mnamtafuta, sisi tulioingia tukiweka viti vilivyozunguka meza ambazo zilikuwa mbele ya viti vya safu mbele nao wakituangalia hii ikimaanisha kuwa walio mbele wana maagizo juu yetu katika maongezi tuliyoitiwa hapa… Pale ndipo niliwajua viongozi wa ngazi za juu wa genge la mihadarati la The Red Jaguar kwa kifupi TRJ katika nchi yetu ikiwa miongoni mwao ni mwanamke niliyekuwa napokea maagizo yake jana wakati Norman na Kamanda Muniain wapo mgahawa wa Filadelifia, huyu mwanamke kwa sura namjua vizuri lakini ni mara moja ile niliyoonana naye tukiwa ofisi za wizara ya usalama zilizopo Chinautla…” Akaeleza kwa mtiririko ambao Agent Kai na wenzake walielewa vizuri.

  “Nina haraka ya kujua… Umesema viongozi wa TRJ katika nchi hii ni hao waliokuwa na mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani akiwemo mwanamke tunayemtafuta kwa udi na uvumba, je waziri wa usalama wa nchi naye ni mmoja wa watu wanaounda genge la TRJ akiwa kiongozi wao hapa GTL au?” Akauliza Special Agent Rebecca ikiwa wengine wawili walitingisha vichwa vyao kuunga mkono swali lililoulizwa.

   “Kwa bahati mbaya naye yumo… Na nataka niwaambie ukweli ujio wenu hapa GTL unafahamika.. Asubuhi nililetewa ujumbe mfupi wa barua pepe ikiwa na taarifa juu ya watu wanne kutoka Marekani wameingia na kwa pamoja wanafanya ushirikiano na watu wawili wa OCLA ambao ni Kamanda Muniain Salivita Muniero na Norman Cabrera hivyo tulipewa taarifa tuwe makini wakati TRJ wanachunguza watu hawa wamefuata nini nchini kwetu au wameombwa msaada na Kamanda Muniain… Kazi hii ya kujua kila anayeingia hapa nchini na kujulikana ni nani watu hao ufanywa na watu wa uhamiaji ambao nao kama sisi wapo chini ya wizara ya usalma wa nchi” Akajibu kirefu mzee kamishina.

   “Tuna audio hapa ilinaswa asubuhi na mtaalamu wetu wa kudukua mawasiliano, mtu ambaye ndiyo muongoza njia yetu kufika lilipo jibu letu aliongea na mtu aliyeanza tu mawasiliano akamuita mheshimiwa waziri… Kumbe ni huyo waziri wa usalama… Jibu limekuja tayari, naomba nijue huyu mwanamke ni kweli anaitwa Valentina Aurelia Moschi?” Agent Kai akamuuliza Kamishina.

   “Hapana sijajua ukweli kuhusu jina lake sababu mimi na hata watu wengine tusiohusika moja kwa moja na genge lao uwa tunamuita ‘Madam’ sijawai juwa kama yeye ni Valentina Moschi kama usemavyo” Akajibu Kamishina Alvaro.

   “Waziri wa usalama anaitwa nani?” Akahoji Investigator Miller kwakuwa yeye shauku yake kubwa ilikuwa kujua huyo waziri wa mambo ya ndani ambaye ni kiongozi mwambata wa TRJ.

   “Anaitwa mheshimiwa Rafael Valdes Ceni ni rafiki mkubwa wa Rais wa nchi yetu ndiyo maana kamuweka katika wizara ya usalama wa nchi akiwa anamuamini sana lakini kiukweli si mtu mzuri kwa Rais wetu kabisa na ndiyo maana alitoa amri mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa auliwe na madam kwakuwa Mr. Fontes Jota Mariapan alizidisha kuwa tishio kwa biashara zao akiacha mambo ya ofisi yake juu ya rushwa anaingia hadi katika unoko juu ya mihadarati” Akajibu Kamishina.

   “Tunahitaji msaada wako kimaelekezo jinsi ya kumpata huyu mwanamke usiku wa leo” Agent Kai akaongea huku anasoma ujumbe wa meseji kwa njia ya whatssap ulioingia kwenye simu yake.

   “Ukweli mimi sijui anapatikana vipi sababu sijawai kuwa naye karibu kimaongezi ya ana kwa ana zaidi ya yeye kunitafuta kwa njia ya simu pale anapokuwa na tatizo kwakuwa ni maelekezo ya mkuu wa wizara yetu basi mimi uwa natekeleza tu anachohitaji ingawa toka waniweke katika mipango yao ovu nimehusishwa na matukio matatu ikiwa la jana limetimia la tatu… Wanatutumia makamishina wakuu wote katika miji yetu” Akajibu Kamishina.

   “Mnalipwa katika hili?” Special Agent Silla akauliza.

   “Ndiyo tunalipwa nasikitika sana kwa hili.. Sababu najutia sana kwakuwa mimi pia ni mhanga wa madawa ya kulevya, mwanangu wa kike amekuwa mraibu mpka kuepeleka kuwa kama zezeta sasa inaniuma sana kwa kweli” Akajibu na kuendelea kuongea kwa masikitiko makubwa ni kweli Kamishina alikuwa akifanyishwa kazi ya kufunika kombe mwanaharamu apite huku akiwa hapendi kabisa.

   “Unamuelezeaje mtu anayeitwa Alexis Carlos Codrado mwekezaji wa shamba kubwa la kahawa lililopo milima ya Tajumulco huko San Marcos?” Akauliza Agent Kai.

   “Mmmh..Mh!... Huyu ni mdogo wake na mtu anayesemekana ndiye kiongozi mkuu wa genge la TRJ… Nafahamu mtu huyu mtaji alionao una nguvu kubwa nyuma yake ya kingpin Feca, namfahamu Alexis kama mwekezaji mkubwa mwenye kumiliki kiwanda kikubwa cha kahawa kilichoajiri watu wengi pia namfahamu kwakuwa anafadhili miradi mingi ya serikali ni mtu anayependwa sana na Rais wetu kati ya wafanyabiashara waliowekeza hapa GTL akutoka nchi jirani hususani nchi ya Mexico” Akajibu Kamishina.

   “Mh! Basi tuishie hapa kuhusu huyu Alexis nafikiri anaweza kuwa si mtu mbaya kama alivyo kaka yake.. Mtaji aliopewa na kaka yake ni kama mtaji wa pesa haramu lakini pengine kwa nchi hii si pesa haramu wamekubali utakatishaji wa pesa ingekuwa Marekani muda huu kusingekuwa na hata jina la Alexis Carlos Codrado..! Akaongea Agent Kai huku akizungusha macho yake kuwaangalia wenzake walio pande zote wote wakiwa wamesimama wakiwaangalia waliokaa Kamishina na mlinzi wake.

   “Hapa serikali haikuangalia hilo ilichotaka ni kupata mwekezaji” Akaongea Kamishina Alvaro.

   “Naomba niandikie namba za simu za makamishina wote waliopo manispaa za jiji hili pamoja na namba ya simu ya usalama wa nchi hili tuone kama ni zile zinazoendana na tulizozinasa tunataka kuona kama tunaweza kuzi track zote hizo tukafuatilia mawasiliano yao tuweze fanya kazi zetu kiurahisi na usalama.. Pia naomba niandikie namba ya kiongozi mwingine kama si wengine ambazo unazo walio ndani ya genge la TRJ” Agent Kai aliongea kisha akatizama saa yake ya mkononi kujua ni muda gani na ikawa kama kosa sababu wote waliangalia saa zao kasoro mateka walio chini ya ulinzi wao hawakuwa na saa mikononi mwao zilishavuliwa mapema kwa kilichoitwa usalama.

Mwsiho wa sehemu ya hamsini na sita (56)

Matumaini ya kazi kuwa nzuri sana upande wao Agent Kai na wenzake ulikuwa mkubwa sana, maelezo marefu yenye tija toka Kamishina Mkuu wa polisi wa manispaa ya mji wa Antigua ameweza kufunguka mengi kiasi ya kwamba wao kina TSC ilikuwa faida kubwa sana wakitamani hata wangemlipa mzee huyu kwa jinsi alivyowasaidia.

Nini kitafuta baada ya mahojiano haya?



   “Unamuelezeaje mtu anayeitwa Alexis Carlos Codrado mwekezaji wa shamba kubwa la kahawa lililopo milima ya Tajumulco huko San Marcos?” Akauliza Agent Kai.

   “Mmmh..Mh!... Huyu ni mdogo wake na mtu anayesemekana ndiye kiongozi mkuu wa genge la TRJ… Nafahamu mtu huyu mtaji alionao una nguvu kubwa nyuma yake ya kingpin Feca, namfahamu Alexis kama mwekezaji mkubwa mwenye kumiliki kiwanda kikubwa cha kahawa kilichoajiri watu wengi pia namfahamu kwakuwa anafadhili miradi mingi ya serikali ni mtu anayependwa sana na Rais wetu kati ya wafanyabiashara waliowekeza hapa GTL akutoka nchi jirani hususani nchi ya Mexico” Akajibu Kamishina.

   “Mh! Basi tuishie hapa kuhusu huyu Alexis nafikiri anaweza kuwa si mtu mbaya kama alivyo kaka yake.. Mtaji aliopewa na kaka yake ni kama mtaji wa pesa haramu lakini pengine kwa nchi hii si pesa haramu wamekubali utakatishaji wa pesa ingekuwa Marekani muda huu kusingekuwa na hata jina la Alexis Carlos Codrado..! Akaongea Agent Kai huku akizungusha macho yake kuwaangalia wenzake walio pande zote wote wakiwa wamesimama wakiwaangalia waliokaa Kamishina na mlinzi wake.

   “Hapa serikali haikuangalia hilo ilichotaka ni kupata mwekezaji” Akaonge Kamishina Alvaro.

   “Naomba niandikie namba za simu za makamishina wote waliopo manispaa za jiji hili.. Kisha naomba niandikie namba ya kiongozi mwingine kama si wengine ambazo unazo walio ndani ya genge la TRJ” Agent Kai aliongea kisha akatizama saa yake ya mkononi kujua ni muda gani na ikawa kama kosa sababu wote waliangalia saa zao kasoro mateka walio chini ya ulinzi wao hawakuwa na saa mikononi mwao zilishavuliwa mapema kwa kilichoitwa usalama.

ENDELEA NA UTAMU WA DODO ASALI!!

SAA MBILI USIKU

SAN MARCOS-GUATEMALA

Pembezoni mwa pwani ya ziwa Atitlan moja ya ziwa linalovutia sana watalii wanaotembelea nchi ya Guatemala lililopo mkoani San Marcos, eneo la La Laguna kuna Hotel iitwayo LA PAZ & Restaurante Vegeterano De La Huerta ikiwa pembezoni kabisa mwa ziwa hili, usiku huu wa saa mbili kulikuwa na meza moja kubwa ikiwa katika baraza iliyozungushiwa kingo za miti iliyonakshiwa vizuri kuizunguka baraza hii, upande wa juu kidogo hatua kama kumi na tano toka katika baraza kwenda kwa hotelini kulikuwa na mgahawa ambao kwa usiku huu kulikuwa kumechangamka sana kwa watu wanaopata vinywaji na nyama choma lakini hapa katika baraza hii kulikuwa na utulivu mkubwa licha ya meza hii kubwa kuwa ilizungukwa na viti kama kumi vilivyokaliwa na watu wapatao idadi hii ya viti.

Meza ilikuwa na vinywaji baridi (visivyo na kilevi) pamoja na vinywaji vikali (pombe) na vyote hivi vilikuwa vimajipanga kwa safu kadhaa mchanganyiko lakini katikati kulikuwa na kitu kama karai kubwa lililojazwa mabarafu na chupa kadhaa za bia na vinywaji baridi, ilifanyika hivi sababu watu waliopo hapa walikuwa hawataki usumbufu wa kuita muhudumu kuja kuwahudumia watakapo anza mazungumzo yao hivyo waliagiza iwe hivi.

   “…. Imekuwa ni heri kwetu sote kwa mheshimiwa kuitisha kikao hiki kwa haraka sana katika wakati muhimu sana… Sababu habari za DEA kutuma watu wao hapa hatukuwa tumetaraji kwa wakati huu.. Karibu sana mheshimiwa waziri utupe maelekezo uliyosema” Baada ya utulivu uliohitajika kuruhusu mazungumzo ya kikao kuanzwa alianza kuongea Koplo wa zamani wa jeshi la wananchi la Mexico ‘Koplo’ Maxiwell Zuantejo.

  “Mambo si shwari sana hali inanishangaza… Kamanda Muniain amekuwa mtu wa kusumbua sana vichwa vyetu na sijui kwa sababu yuko karibu na Rais wetu, nimetoa taarifa mchana wa leo mtu huyu awe tayari mikononi mwetu… Mariana mmefikia wapi?” Mheshimiwa waziri wa usalama wa nchi ya Guatemala mtu muhimu na muaminiwa sana na Rais wa nchi ya Guatemala ndiyo mtu aliyeitisha kikao hiki cha siri kilichokuja kufanyika hapa pembezoni mwa pwani ya ziwa Atitlan katika beach maarufu ya hotel ya LA PAZ, aliongea na kuuliza akikuna kuna ndevu zake nyingi kwa mbwembwe zilizoshuka toka mashavuni mwake mpaka kufanya kama mkia wa kidevuni.

   “Niliagiza vijana wafanye kama ulivyotaka lakini mitego yote waliyoiweka ilitega hewa sababu mpaka sasa nakuja huku hawajamuona mahala kote ambako wao wakitaka kumuona uwa wanamuona kirahisi tu” Akajibu Mariana mwanamke pekee aliyeko kwenye kikao hiki hapa LA PAZ Hotel.

   “.. Haaaahaaah…Shit! Hivi Mariana mara ngapi unakosea? Koplo gani mzembe hivi? Hivi Brigedia Feca anajua kwamba toka Alto aende kwenye matibabau Canada umeharibu mambo mengi ya msingi… Unatambua uzembe wako unaharibu TRJ yote na mustakabali wa maisha yetu?!!” Alifoka kwa sauti uso wake akiuzungusha huku na huko kuangalia pande za karibu na mbali ya pale kuhofu sauti yake isiende mbali.

   “… Mheshimiwa waziri mi naona naenda sawa… Mimi nimepewa watu wa kufanya kazi mimi ni muelekezaji tu, shutuma unazonipa zinanipa ukakasi na kunifanya niwe mnyonge sana kwakuwa mambo yakiharibika naambiwa mimi nina makosa hii si sawa jamani… Nilikabidhiwa kwa alto hapa tukiwa chini ya Savatel kabla Savatel hajapelekwa kushughulikia masoko yetu Asia, wafuasi wote ninaowatumia ni wafuasi waliokuwa wakitumiwa na Savatel sasa pengine wananidharau mimi mwanamke wanakosea maelekezo yangu ninayowapa” Mariana aliongea kujibu tuhuma anazopewa za uzembe kwa sauti ya kuonyesha hajaridhika naye kwa anayoshutumiwa na mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani.

   “Mheshimiwa waziri! Samahani kwa yote ila naomba kama hautajali tufanye mazungumzo hapa bila kuanza kupeana lawama zozote sababu hazina mantiki kwa sasa… Kinachotakiwa ni kuona tunafanyaje na si kuanza kurushiana lawama sisi ni timu moja tukianza kuvurugana tu tutaharibu kila kitu” Aristos Mosquera akaingilia kati maana uso wa Waziri ulionyesha makunyazi ya hasira na macho yalibadilika kwa kasi akataka kuanza kufoka tena hivyo Aristos alimkatizia kibusara.

   “Nimeelewa… Ila kosa moja tu litaharibu heshima yangu kwa taifa… Eleweni kesho Rais anarudi hapa nchini baada ya ziara ndefu katika mataifa ya Asia na Ulaya hivyo kuna ripoti mbalimbali atazipokea punde atakapotulia, hofu yangu ni flashdisk je Marehemu  Jota Mariapan hakutaka iende kwake? Na kama alitaka hivyo haijamfikia Rais mpaka sasa? Na ina nini? Kumbukeni Mariapan anajua kama mimi ni muuzaji wa mihadarati wa siri nikishirikiana na TRJ kwakuwa tuliwai kumualika kwenye kikao chetu wiki mbli tu baada ya yeye kukalia kiti cha ukurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa.. Flashdisk iko mikononi mwa mtu tulielekezwa ni Norman, je mmewai kujiuliza Norman akiwa haonekani mtaani wala kwenye maficho mbalimbali ambayo mnahisi anaweza kuwa anajificha hawezi kwenda mpa Rais huko nje ya nchi?” Aliuliza maswali mengi huku pia akifafanua mambo mbali mbali mheshimiwa waziri.

Ukimya ulitawala kila mmoja akitafakari maswali aliyouliza na maneno mengine aliyoongea mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani bwana Rafael Valdes Ceni.

   “Nimekuwa nikitegemea makamishina wa polisi kunisaidia kwa kuwarahisishia kina Mariana na wao kiukweli wanacheza sehemu yao vizuri tu shida imekuja kwetu wenyewe ambao tunapewa uhuru wa kazi tunashindwa kuutumia ipasavyo… Uwa najiuliza je tusingekuwa na watu wengi katika sehemu mbalimbali tungepata tabu ya aina gani katika kutekeleza majukumu yetu ya msingi? Jibu tungepata tabu sana… Sijaja hapa kutoa lawama ila nimekuja hapa kutoa angalizo juu  ya kazi yetu na hatari inayoweza kutokea tusipoziba ufa unaotokea sasa hakika nawaambieni hatutaweza zuia ukuta usidondoke pale dhoruba litakapotufika sote tutaangamia… Naomba tuwe makini sana na mambo haya yanayotokea, angalieni mauaji yaliyotokea usiku wa jana ni mauaji ya kitaalamu sana mpigaji risasi amefanya mauaji ya kisasa kabisa akionyesha ufundi wa kucheza na silaha tena akitumia silaha ambazo kama genge tuliamua kila mtu aliyemo humu atatumia bunduki aina hiyo, hivyo muuaji ameua watu wetu kwa kutumia bunduki tulizonunua wenyewe kwa pesa zetu… Muda ambao nilikuwa niko njiani naletwa hapa San Marcos kutoka Guatemala City nilifanya mazungumzo na boss wetu Feca kwa kweli ameonyesha kuchukizwa sana na hili jambo, yeye anasema ni dharau kubwa sana kwa TRJ” Akaongea tena mheshimiwa waziri kisha akasimama kuongea kupoza koo kwa kunywa kinywaji anachokipenda.

   “Kamanda Muniain ni sumu kubwa sana tuliyoiacha ijiunde katika ukubwa wa kutisha… Mara zote nilikuwa nikiuliza kwa Boss Feca kwanini TRJ wa hapa inafyeka watu wote wenye kuonyesha kuwa kikwazo kwetu lakini Muniain anaachwa? Joka lenye sumu tumelidharau likiwa change sasa haya ndiyo madhara yake…” Maxiwell Zuantejo akaongea analoona ni kosa lao.

   “Tulimuacha kwa sababu! hatukuamuacha hivi hivi tu… Tuliamini muda wowote atakuwa upande wetu na kutusaidia lakini undugu wake na Rais umemfanya awe mbishi kufanya vile tutakavyo na sasa naunga mkono hoja kuwa sababu yetu haikuwa na mashiko joka limeota meno linataka kutung’ata… Atafutwe kwa udi na uvumba popote alipo kabla Rais hajaingia hapa GTL, Kamanda Muniain na Norman wake wawe tayari chumba cha mahojiano wakipata haki yao stahili… Tutawapataje? Ndicho nilichojia hapa LA PAZ Hotel!” Kwa mbwembwe akaongea tena mheshimiwa mkono wake wa kulia ukichezea sharubu zake, huyu alikuwa ni mmoja wa wale wazungu wa kilatino wenye majivuno sana kiburi kilichoongezewa na pesa zake za haramu anazozitakatisha kwa kumiliki Bureau Change zenye matawi kila kwenye miji ya nchi ya Guatemala.

   “Unajua mheshimiwa unavyotuona hapa karibu sote si watu wa Guatemala ingawa wenzetu wawili watatu kazi wanafanya hapa lakini wote si wazawa wa Guatemala, wewe ndiyo mtu pekee katika Guatemala hii ambaye ni mzawa na una kila kitu ambacho unaweza kufanya na kikawa msaada mkubwa kwetu…. Mara zote sisi tunategemea uwepo wako katika TRJ kuwa ni msaada mkuu kwetu, ilikuwa kazi rahisi kukubali uingie katika genge letu kwakuwa tuliona faida yetu kwetu kama wewe ulivyoona faida yako ni ipi kuwa ndani ya TRJ, hivyo kwa niaba ya boss wetu wote Feca naomba niseme kazi hii inakutegemea wewe hapa GTL mustakabali wa TRJ hapa upo juu yako, unamiliki jeshi la polisi na vyombo vyote vya usalama vinapokea maagizo toka kwako… Tamko lako moja tu katika vyombo vilivyo chini yako vinaweza sababisha kupatikana kwa haraka watu tunaowataka” Koplo wa zamani wa jeshi la Mexico Maxiwell Zuantejo alitiririka wenzake wakimsikiliza huku wakitingisha vichwa vyao kukubaliana na anachoshusha kuwa ni nondo waliyoihitaji.

   “Ni kweli Maxiwell uliyoyasema lakini watu walio hapa GTL wanajua nilivyowarahisishia kazi kwa kuwaunganisha na mitandao ya walio juu kimamlaka katika jeshi la polisi na hata walio ndani ya usalama wa taifa wa nchi hii, Mariana nimempa uwezo wa kumpigia Kamishina wowote wa katika mji wowote, nimempa mamlaka ya kuwaomba na kuwaamrisha pia.. Napokuwa mkali ni kwa sababu ya hili jamani, hivi mnafikiri Feca likitokea jambo la kuharibu lolote kati ya mambo yetu lawama za kwanza anampa nani? Mimi si kiongozi mkuu hapa ila nina mamlaka na wajibu wa kujibu lawama tutakapo haribikiwa kwa namna yoyote ile…. Nisilaumu sana kwenye hili ingawa naumia sana pale ninapotoa maagizo yanaposhindwa kutekelezwa kwa wakati” Mheshimiwa waziri akajibu hoja akimtizama Maxiwell Zuantejo.

   “Hatupo kulaumiana tena… Tumefika GTL jana lakini nasi tumeshiriki uzembe tayari baada ya maelekezo kazi yakinifu toka kwako kuwa Kamanda Muniain atekwe haraka sana kabla hata ya saa saba mchana wa leo bila kuogopa chochote, tukapanga wa kwenda huko kutekeleza kazi husika lakini wamerudi kwenye hotel waliyopanga wakiwa hawajafanikisha mpango wanatupa majibu rahisi kabisa kuwa wamemtafuta kila kona ya jiji la Guatemala hawajamuoana yeye wala walinzi wake wanaowajua… Huu ni upuuzi wetu kuwategemea watu ambao tunaamini wanaweza kumbe hamna kitu kabisa, bure kabisa” Aristos Mosquera akaongea kwa kujiamini na kama kawaida ya kikao hiki cha watu hawa waliokaa kwenye viti kuzunguka meza kuu iliyojaa vinywaji vingi vikiwa aina ya bia zenye alcohol kali kabisa hapana chezea kabisa za kuweka mbali na watoto ilikuwa kukubali jambo kwa wote kutingisha vichwa vyao.

   “Hapana sisi si wazembe… Sisi ni kama watengeneza njia si lazima ukiitengeneza njia basi ni wewe peke yako utakayekuwa unapita… Sisi tunaelekeza na ikibidi ndiyo tunaenda wenyewe kufanya kazi… Hivyo kwa hili tusinyosheane vidole tunatakiwa tujue OCLA ni shirika ambalo tulikuwa tumelishikilia kimaelekezo wakifanya kazi kwa kufuata maelekezo yetu katika kila kitu shida ya hapa GTL alipoingia Muniain tu mambo yakaanza kwenda tofauti na tunavyotaka jamaa hakutaka kuwa kama mrithi wake Kamanda mstaafu Matheaus Chaves, tulifanikiwa kuwateka wasaidizi wake na hata watu wengine katika OCLA kuwa chini yetu wakifuata mengi tuyatakayo akibaki yeye mkuu wao na huyu Norman ambaye mara nyingi amekuwa akiharibu mipango yetu akishirikiana na watu wake ambao tulijitahidi sana kuwapunguza mpaka sasa amebaki yeye tu anajifanya jeshi la mtu mmoja… Naomba nisilaumiwe kwa vyovyote jamani nachokifanya mimi ni kupokea maelekezo kwa Feca na mheshimiwa waziri hapa kisha nami nafanya kuelekeza na kufuatilia kwa ukaribu linalotakiwa kufanyika” Mariana Caro Funtes akaona ni wakati wa kufafanua pia kuondoa zana aliyonayo mheshimiwa waziri kuwa yeye amekuwa mzembe sana.

   “Mheshimiwa waziri! Hii ni vita baina ya waliopania kujua kuna nini hapa GTL na sisi TRJ… Kamanda Muniain si kama hatambui nguvu tuliyonayo lakini anajipa moyo kuwa undugu wake na Rais kutamaliza hila zozote kwake… Naomba hapa tupange safu yetu watu tuliokubuhu katika medani… Tuliowapa kazi wanasema njia zote walizopita hawajawaona sisi sasa ni kazi kwetu kusema tunatengenezaje njia kumaliza hili suala ambalo limekuwa kero sasa kwetu… Cha kwanza tunatakiwa tujue maafisa wa DEA waliokuja hapa GTL ni kina nani kwa majina”Maxiwell Zuantejo akaongea akisisitiza kwa kidole chake cha shahada kukitingisha.

   “Si kazi rahisi kuwajuwa moja kwa moja wao kimajina na … Hakuweza kuendelea alichotaka kuongea mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani Mr. Rafael Ceni maana mlio mkali wa simu yake iliyokuwa kwenye mfuko wa juu kushoto wa suti aliyoivaa uliwafanya hata wengine kumkazia macho kumtizama.

Aliitoa toka mfukoni akaangalia kwenye kioo jina la mpigaji alipoliona akawatizama wanaotizama kisha akainuka toka kwenye kiti akajisogeza kwa pembeni kidogo.

   “Halloo! Habari?” Akasalimu baada ya kusugua kioo kuruhusu apokee.

   “Si nzuri sana mheshimiwa… Kamishina mkuu wa manispaa ya mji wa Antigua inasemekana ametekwa”

    “Unasemaje?” Akauliza kwa mshtuko Waziri Rafael Ceni.

    “Tumepokea  taarifa kutoka ofisi ya kuu ya polisi ya Antigua kuwa Kamishina Mkuu wa Antigua Alvaro Canedero ametekwa katika hotel ya Soleil Hotel..!”

   “Anatekwa vipi wakati anapotoka uwa ana walinzi wake zaidi ya watano wanaomfuata katika gari ya nyuma ya gari yake na pia licha ya kuwa na dereva wake anakuwa na mlinzi wake wa karibu wakati wote.. Nieleze ilikuwaje?”

   “Walinzi wake wanasema aliwaomba kuwa anafika mtaa wa pili tu kuna mtu anaenda kumuona hivyo wamsubiri anatoka na bodyguard wake binafsi pamoja na dreva wake tu lakini baada ya masaa mawili kupita dreva wake alirudi kuwapa taarifa kuwa Kamishina Mkuu Alvaro ametoweka hayupo ndani ya hotel na hata wahudumu wanasema walimuona kaongozana na watu ambao wao hawakutitilia maanani kujua idadi yao wala ni kina nani? Na pia alivyofika hawakumjua kama yeye ni Kamishina Alvaro alifika kuwauliza akiwa kavaa kofia inayomziba kwa juu kwa kiasi kikubwa”

   “Jenerali! Naomba fuatilia kwa makini juu ya kupotea kwake Kamishina Alvaro… Kama ujuavyo jana kulitokea mauaji pale Antigua hii inatishia nyendo zetu kiusalama”

   “Najua mheshimiwa na tayari nimeunganisha jambo juu ya tukio hili.. Naomba tusiongee sana kwenye simu kesho asubuhi ya mapema tuonane kabla hatujaingia maofisini”

   “Sawa Jenerali… Mimi bado nipo kwenye kikao nilichokwambia nitakuja San Marcos kuweka mkakati sawa juu ya mpuuzi mmoja na anayemuita mwanae wanaotaka kutuharibia sifa na heshima zetu” Alimalizia kuongea mheshimiwa waziri kisha akakata simu akaitupia mezani pembeni ya chupa za vinywaji.

Alihema kwa nguvu mheshimiwa waziri kisha akamtizama kila mmoja ukimya ukiwa umetanda pale maana na wao walikuwa wakitaraji neno toka kwake.

   “Mambo yanazidi kuharibika…. Kamanda Muniain katuletea majanga makubwa sana na sijui imekuwaje mpaka watu hawa wa DEA wameingia nchini kwetu bila kujulikana kabla… Ngoja nimpigie mkurugenzi wa uhamiaji Brigedia Donald Granell anipe jibu ambalo tunaweza kuanzia hapo..!” Akaongea Mheshimiwa kisha akanyanyua tena simu yake akaikamata kiganjani mwake akaanza pekua namba alizohitaji, alipoziona akapiga.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na saba (57)

Kikao cha viongozi wa THE RED JAGUAR (TRJ) wanaopatikana ukanda wa Guatemala pamoja na waliofika kuongeza nguvu ya kilichoitwa kuzuia hila za watu wawili wa Organized CrimeOf Latin America (OCLA) kilichoitishwa na Mheshimiwa Waziri wa Usalama wa Nchi katika mji wa San Marcos eneo la LA PAZ Hotel kilikuwa na majibishano yenye kutupiana lawama miongoni mwao kuwa kuna uzembe unafanyika katika kuharibu kazi yao na mipango yao.

Mpaka hekima za ziada zilitumika kumpooza hasira mheshimiwa waziri ambaye naye ni miongoni mwa watu hatari katika nchi ya Guatemala kwakuwa anajihusisha na mtandao wa genge la TRJ tena akipewa cheo cha siri cha kimaamuzi katika genge.

Walipokea taarifa ya kutekwa kwa Kamishina Mkuu wa Polisi wa mji wa Antigua wakiwa wanaendelea na kikao chao hii taarifa ikimchanganya sana mheshimiwa waziri maana aliunganisha matukio na kuona sasa ama kweli kama sharubu zimekusanywa kiganjani mwa mtu anataka kuzing’oa.

Nini kitaendelea?



Aliitoa toka mfukoni akaangalia kwenye kioo jina la mpigaji alipoliona akawatizama wanaotizama kisha akainuka toka kwenye kiti akajisogeza kwa pembeni kidogo.

   “Halloo! Habari?” Akasalimu baada ya kusugua kioo kuruhusu apokee.

   “Si nzuri sana mheshimiwa… Kamishina mkuu wa manispaa ya mji wa Antigua inasemekana ametekwa”

    “Unasemaje?” Akauliza kwa mshtuko Waziri Rafael Ceni.

    “Tumepokea  taarifa kutoka ofisi ya kuu ya polisi ya Antigua kuwa Kamishina Mkuu wa Antigua Alvaro Canedero ametekwa katika hotel ya Soleil Hotel..!”

   “Anatekwa vipi wakati anapotoka uwa ana walinzi wake zaidi ya watano wanaomfuata katika gari ya nyuma ya gari yake na pia licha ya kuwa na dereva wake anakuwa na mlinzi wake wa karibu wakati wote.. Nieleze ilikuwaje?”

   “Walinzi wake wanasema aliwaomba kuwa anafika mtaa wa pili tu kuna mtu anaenda kumuona hivyo wamsubiri anatoka na bodyguard wake binafsi pamoja na dreva wake tu lakini baada ya masaa mawili kupita dreva wake alirudi kuwapa taarifa kuwa Kamishina Mkuu Alvaro ametoweka hayupo ndani ya hotel na hata wahudumu wanasema walimuona kaongozana na watu ambao wao hawakutitilia maanani kujua idadi yao wala ni kina nani? Na pia alivyofika hawakumjua kama yeye ni Kamishina Alvaro alifika kuwauliza akiwa kavaa kofia inayomziba kwa juu kwa kiasi kikubwa”

   “Jenerali! Naomba fuatilia kwa makini juu ya kupotea kwake Kamishina Alvaro… Kama ujuavyo jana kulitokea mauaji pale Antigua hii inatishia nyendo zetu kiusalama”

   “Najua mheshimiwa na tayari nimeunganisha jambo juu ya tukio hili.. Naomba tusiongee sana kwenye simu kesho asubuhi ya mapema tuonane kabla hatujaingia maofisini”

   “Sawa Jenerali… Mimi bado nipo kwenye kikao nilichokwambia nitakuja San Marcos kuweka mkakati sawa juu ya mpuuzi mmoja na anayemuita mwanae wanaotaka kutuharibia sifa na heshima zetu” Alimalizia kuongea mheshimiwa waziri kisha akakata simu akaitupia mezani pembeni ya chupa za vinywaji.

Alihema kwa nguvu mheshimiwa waziri kisha akamtizama kila mmoja ukimya ukiwa umetanda pale maana na wao walikuwa wakitaraji neno toka kwake.

   “Mambo yanazidi kuharibika…. Kamanda Muniain katuletea majanga makubwa sana na sijui imekuwaje mpaka watu hawa wa DEA wameingia nchini kwetu bila kujulikana kabla… Ngoja nimpigie mkurugenzi wa uhamiaji Brigedia Donald Granell anipe jibu ambalo tunaweza kuanzia hapo..!” Akaongea Mheshimiwa kisha akanyanyua tena simu yake akaikamata kiganjani mwake akaanza pekua namba alizohitaji, alipoziona akapiga.

ENDELEA NA UTAMU WA DODO ASALI..!

SAA MBILI USIKU

SAN MARCOS-GUATEMALA

   “Halloo! Mheshimiwa” Aliyepigiwa hakuremba kupokea hii ilimaanisha hakuwa na simu mbali kana kwamba alikuwa akijua kuwa atapigiwa.

   “Nilikupigia debe kwa mheshimiwa Rais akuweke hapo uhamiaji nilikuwa nataka mtu muelewa wa kazi ambaye atafanya kazi kwa umakini kulinda maslahi yetu hasa kwa watu wanaoingia nchini”

   “Natambua hilo mheshimiwa… Kwani imekuwaje?”

   “Ina maana Brigedia Granell hujui uhamiaji mmepokea watu wa aina gani toka Marekani jana tu?”

   “Aiseeh! Siku ya jana na hata leo sikuwepo ofisini nilikuwa idara ya usalama wa taifa nashughulikia wageni ambao wataongozana na mheshimiwa Rais kuja hapa nchini… Kama ujuavyo kesho mheshimiwa Rais anarudi na anaongozana na watu aliowaomba waje kuangalia uwezekano wa kuwekeza nchini kwetu sasa idara yetu ya uhamiaji na idara ya usalama wa taifa uwa tuna kazi ya kujua kila anayesema anavutiwa kuwekeza nchini kwetu tunashirikiana kuwachunguza na hili mheshimiwa waziri unalijua hivyo kama kuna wageni ambao kuna mashaka juu yao kwa kweli sijajua”

   “Lakini nilitoa angalizo uhakikishe unachunguza zaidi na kwa umakini majina ya watu wa Marekani wanaoingia nchini mwetu, nakumbuka uliniambia kwa watu wa Marekani umeweka kitengo maalumu kwa kazi hiyo. Je hujataarifiwa kuwa kuna watu watatu wameingia nchini kutokea huko?”

   “Sijataarifiwa lolote kwa kweli… Inasikitisha.. Acha niwasiliane na kiongozi wa kitengo icho kisha nitakujibu… Ningeomba unielekeze unahitaji nini kwa kuanzia?”

   “Nilitaka ujue habari zao wameingia kwa kibali gani kinachowaruhusu kufanya kazi hapa nchini kwetu? Maana na wasiwasi Kamanda Muniain kawaombea kibali kwa mheshimiwa Rais moja kwa moja bila wewe wala mimi kuhusishwa”

   “Sawa! Ila mheshimiwa Rais hayupo… Sidhani kama atakuwa kasaini watu hao kufanya kazi yoyote hapa nchini. Kwani wanafanya kazi gani?”

   “Ni maafisa wa DEA… Wanashirikiana na watu wawili wa OCLA kujaribu kuharibu mambo yetu.. Kamanda Muniain amekuwa jeuri sana kwakuwa shirika lake la upambanaji na madawa ya kulevy ani shirika lisilohusika na wizara yangu hivyo kiburi chake ni kikubwa sana anajifanyia maamuzi ayatakayo”

   “Nimekuelewa mkuu lakini mambo haya kwenye simu si mazuri kuyaongelea kwakuwa sumu ishaanza lazima tuwe makini sana… Acha nifanyie kazi swala lako kisha nitakupigia kukujulisha kwa njia ya whatssap call!” Alimalizia aliyepigiwa simu akiahidi kufanyia kazi jambo aliloelezwa na mkuu wake mhesimiwa waziri kisha wote wakakata simu.

   “Ndiyo maana sikuwa na taarifa juu yao watu hawa walioingia kinyemela hapa nchini… Sasa naomba niachieni kwenye mawindo makuu mimi mwenyewe…. Nyinyi mtataarifiwa tu wapi muelekee baada intelejensia kufanya kazi kwa usahihi, nimeamua kulivalia njuga hili suala la Norman na Muniain… Nataka kabla Rais hajafika saa tisa alasiri watu hawa wawe kwenye gereza la ardhini huko Tajumulco ikibidi na hao wapuuzi wao waliowaleta toka DEA” Mheshimiwa waziri akaongea kisha akanywa kinywaji chake alichokuwa kakimimina kwenye glasi.

   “Haya ndiyo maneno ya kishujaa tuliyokuwa tunayataka toka kwako kwa sababu hatuwezi tafuta shilingi kwenye kina cha maji ya bahari wakati hatuna vifaa vya kusaidia macho yetu” Akaongea Maxiwell Zuantejo akiwa kafurahi na kuona mwanga fulani.

   “Mi narudi Guatemala City… Nafikiri kwakuwa mambo yanafanyika huko hatuna budi sote tukaenda huko kutoka hapa San Marcos, mtatumia nyumba zangu kwa kazi hii maalumu… Na hiki ndicho kilichonileta hapa” Aliongea tena Mheshimiwa Waziri.

Kikao chao kiliisha kwa mtindo huu kwa wote kukubaliana waondoke usiku huu uliokuwa sasa ushatimia saa tatu na robo usiku kuelekea mji mkuu wa nchi hii ya Guatemala.

   *****  *****  *****

SAA TANO USIKU

CHIMALTENANGO, GUATEMALA CITY

Eneo maarufu la Peatonal 6 Avenida ni eneo ambalo mitaa yake yote uchangamka sana muda wa usiku kwakuwa ni eneo la biashara kubwa za maduka ya jumla na hata Bar na ma club ya usiku yanapatikana kwa wingi eneo hili ndani ya mji wa Chimaltenango.

Ndani ya gari aina ya Toyota Hilux 4x4 Double Cabin rangi ya nyeusi walikuwemo Special Agent Silla na Detective Norman ambaye yeye ndiye alikuwa akiendesha gari na kuja kusimama kwenye maegesho ya bar ambayo usiku huu wa saa tano ilikuwa kama mji wote wa Chimaltenango umeamia hapa, muziki mkubwa uliokuwa ukipigwa kutokea kwa ndani ya Bar ulifanya hadi watu walio nje ya bar nao kuufurahia muziki huo wa kimexico uliokuwa ukisikika na kufurahiwa sana na watu waliofika usiku huu hapa kupata burudani ya vinywaji na muziki.

   “… ..Alisema atakuwa wa kwanza kufika hapa kisha atatusubiri lakini mbona simuoni?...!!” Akaongea S.A Silla huku wote kwa pamoja licha ya kuwa walikuwa hawajashusha vioo vya miliango ya gari yao lakini wote shingo zao zilikuwa zikizungusha vichwa vyao huku na huko kumtizama mtu waliyemfuata hapa.

   “Tumpe subira kidogo kwakuwa mbona dakika tulizosimama hapa ni dakika tatu au nne tu..!” Norman akajibu huku anatizama saa yake ya katika simu yake na aliporidhika akauinua na mkono wake wa kushoto uliovaa saa napo akaangalia na kufanya ulinganisho wa muda.

   “Lakin…!” Kuongea kwakeSilla kulikatishiwa na jambo alilovutiwa nalo kuliangalia, simama hiyo pia ya kuongea ilimfanya Norman amtizame hili aone mwenzake jambo gani limemfanya anyamaze.

Kumtizama usoni Silla kulisababisha naye avutiwe na macho ya mwenzake yanapoangalia kwa umakini ndipo Norman alipoangalia alistuka sana.

Watu anaowajua yeye Norman kuwa ni watu wa usalama wa taifa kutokana na wawili kati ya watano alikuwa akiwajua kwa kila kitu mpaka majina yao, walikuwa wameongozana na mtu ambaye wao walikuwa wakizungusha macho yao kuona yuko wapi?.

   “Mh! Kamanda Muniain yule..” Alijikuta anaongea Norman kwa sauti ndogo sana.

Ni kweli! Upande wa kushoto kwao kwenye maegesho hii hii ya magari waliopo wao hatua kama ishirini za mtu mzima kulikuwa na gari aina ya Lennock Volkswagen, gari zinazotumiwa na majasusi wa usalama wa taifa hili la Guatemala ofisi kuu ya taasisi ya usalama wa taifa iitwayo Guatemala Intelligence and Security (GIS). Gari hizi hizi ni kama Noah zilivyo lakini zenyewe ziko ngumu zaidi ya Noah na ni maalumu kwa kazi za kazi (ujasusi).

   “GSI wanamchukua Kamanda Norman… Wanamteka kwa jinsi inavyoonekana..!” Norman akaongea haraka umakini wa macho yake ukiongezeka kuangalia kule, ambapo Kamanda Muniain alionekana akifunguliwa mlango na mmoja wa vijana wa GSI kisha akasukumwa kwa mgongoni hapo kina Norman haraka wakapata jibu sahihi kuwa hawako njia tofauti ni sahihi mkurugenzi wa OCLA kanda ya Guatemala anatekwa na vijana wa GSI.

   “GSI si watu wazuri?” Akauliza S.A Silla kwa sauti ya haraka bila kumuangalia anayemuuliza.

   “Hakuna uaminifu… Kama tulivyowai kuwaambia jamaa wanaojihusisha na mihadarati wameharibu nchi yetu, mtu anayeaminiwa sana na Rais wa nchi yetu ndiye anayeharibu nchi yetu kwa kiasi kikubwa sana…”

    “Rais wenu hayupo makini… Intelejensia yake haifanyi kazi vizuri.. Mimi nilipoiona picha tu waziri wa mambo ya ndani, macho yake yalinipa majibu mengi sana, kwanini? Kwanini? Inamaanishaje hii? Kumteua waziri mchafu kama yeye katika serikali yake tena akimuweka katika nyadhifa inayohusika na usalama wa nchi yake?”

   “TACCG kitengo kilicho ndani ya taasisi hii kuu ya usalama wa taifa GSI inayokusanya vitengo mbalimbali vya kijasusi lakini wao TACCG wanahusika moja kwa moja ikulu wakimlinda Rais na kumsaidia mambo mengi sana ikiwemo kuwachunguza wabunge, magavana na watu wengine walio ndani ya serikali kuu katika usafi wao katika mambo ya ovyo ovyo lakini hao hao TACCG kuna ambao hawako safi wanafanya kazi kwa matakwa ya watu wachafu si boss wao ambaye ni Rais wetu..!”

   “Inatubidi tuwafuate watu hawa tujitahidi tumuokoe Kamanda Muniain sababu hatujui wanamteka kwa minajili gani?” Akaongea Silla baada ya Norman kunyamaza kufafanua juu ya kitengo cha kijasusi kinachofanya kazi kwa ukaribu na Rais wa nchi yao.

‘Alarm’ ya saa ya Silla ikaita kwa alama ya taa nyekundu iliyowaka mara moja hapo akatambua kwenye laini yupo mmoja kati yao katika kikosi chao anataka kuongea naye kama si kuongea nao wote.

   “Naam!” Akakubali kwa kubonyeza kitufe kilicho pembeni ya saa na kuongea.

   “TSC! Nimetumiwa audio na Lizy muda si mrefu kuwa Valentina Moschi amempigia mtu ambaye hakumtaja jina kuwa kapokea ujumbe toka kwa mheshimiwa kuwa vijana wake wamemtia mikononi Muniain… Mko wapi?” Alikuwa ni Agent Kai anatoa ujumbe kwao kina Silla na kisha kuwauliza kuwa wako wapi.

   “Tuko eneo la Peatonal 6 Avenida katika mji wetu wa manispaa ya Chimaltenango…Ni kweli Kamanda ametekwa, ametekwa na majasusi wa GSI.. Na ndiyo wanatoka eneo la geti ya bar tuliyopanga na Kamanda kuwa tukutane hapa.. Acha tuwafuatilie tuone kama tutaweza muokoa” Akajibu Silla mkono ukiwa pembeni ya papi (lips) za mdomo wake.

   “Muone kama mtamuokoa? Mnatakiwa mmuokoe si kuona kama mtamuokoa… Misheni hii ndiyo imeanza hatutakiwi kupunguza nguvu ya yoyote katika kikosi chetu” Akaongea Agent Kai kwa kasi na kuzima kitufe.

   “Twende wasitupotee..!” Akaongea Silla macho yake yakitizama mkono wa kulia wa Norman anavyoingiza gia kwa kasi hili gari irudi nyuma aweze kugeuza kuondoka pale na kuanza kuwafuatilia walioondoka na Lekkon Volkswagen.

Walitokea bara bara kuu ya 6 Avenida na kwakuwa gari inayotumiwa na vijana wa GSI ilikuwa inaelekea upande wa magharibi ilipo manispaa kuu ya jiji hili ya Antigua, magari yalikuwa bado yapo kwa wingi licha ya kuwa ni saa tano usiku hivyo mwendo ulikuwa si wa kasi sana, wao kina Silla waliweza kuwaona ikawa wameachana kwa mita kama themanini hivi.

   “Kimya kimya au wajue kama wanafuatwa?”Akauliza Norman.

   “Wasijue ingawa si rahisi sana lakini jitahidi wasijue tunaweza faidika zaidi.. Hasara wakijua kwakuwa wao wanajulikana kama wanafanya jambo lililo halali wanaweza kuomba msaada wa haraka kwa polisi na polisi wa hapa mmmh!”

   “Watakuwa wanaenda Antigua… Tuwape taarifa kina Agent Kai kwakuwa wao walienda huko kwa ajili ya kwenda nyumbani kwa mheshimiwa waziri wa usalama tuwaombe watege mahala watakapoona sahihi..” Norman akatoa wazo.

   “Wazo zuri sababu njia hii mpaka Antigua haina mchepuko.. Hii itatusaidia sisi kwenda tukiweka kava tu wasitupotee tu… “ Norman akakubali na papo hapo mtoa wazo S.A Silla akabonyeza kitufe cha kuomba mawasiliano na wenzake.

Haraka wote walio katika system yao katika ‘small call network group’ (SCNG) wakakubali kumsikiliza.

   “TSC! Jamaa wanakuja Antigua.. Ningeomba msaada wenu kabla ya makutano ya Scuintla, Jocotenango na Chimaltenango tuwafanyie kitu mbaya tumuokoe mzee!” Silla akatupa wazo lililosikika vizuri na wote.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na nane (58)

Pande zote zimejipanga kujibu mapigo ya pande nyingine endapo yatatokea kwa namna yoyote huku pande moja ikiwa inajua inapambana na watu wa aina gani? Pande ingine ikiwa haina uhakika kama ni kina nani haswa wanaoshirikiana na Kamanda Muniain pamoja Detective Norman.

Kamanda Muniain ametekwa na vijana wanaosemekana ni kutoka Guatemala Intelligence and Security (GIS).

Kwanini vijana toka GIS wamteke mkurugenzi wa OCLA kanda ya Guatemala?

Majibu ya yote haya twende kazi sehemu inayokuja na zinazokuja kwa majibu mengi zaidi.





   “Twende wasitupotee..!” Akaongea Silla macho yake yakitizama mkono wa kulia wa Norman anavyoingiza gia kwa kasi hili gari irudi nyuma aweze kugeuza kuondoka pale na kuanza kuwafuatilia walioondoka na Lekkon Volkswagen.

Walitokea bara bara kuu ya 6 Avenida na kwakuwa gari inayotumiwa na vijana wa GSI ilikuwa inaelekea upande wa magharibi ilipo manispaa kuu ya jiji hili ya Antigua, magari yalikuwa bado yapo kwa wingi licha ya kuwa ni saa tano usiku hivyo mwendo ulikuwa si wa kasi sana, wao kina Silla waliweza kuwaona ikawa wameachana kwa mita kama themanini hivi.

   “Kimya kimya au wajue kama wanafuatwa?”Akauliza Norman.

   “Wasijue ingawa si rahisi sana lakini jitahidi wasijue tunaweza faidika zaidi.. Hasara wakijua kwakuwa wao wanajulikana kama wanafanya jambo lililo halali wanaweza kuomba msaada wa haraka kwa polisi na polisi wa hapa mmmh!”

     “Watakuwa wanaenda Antigua… Tuwape taarifa kina Agent Kai kwakuwa wao walienda huko kwa ajili ya kwenda nyumbani kwa mheshimiwa waziri wa usalama tuwaombe watege mahala watakapoona sahihi..” Norman akatoa wazo.

   “Wazo zuri sababu njia hii mpaka Antigua haina mchepuko.. Hii itatusaidia sisi kwenda tukiweka kava tu wasitupotee tu… “ Norman akakubali na papo hapo mtoa wazo S.A Silla akabonyeza kitufe cha kuomba mawasiliano na wenzake.

Haraka wote walio katika system yao katika ‘small call network group’ (SCNG) wakakubali kumsikiliza.

   “TSC! Jamaa wanakuja Antigua.. Ningeomba msaada wenu kabla ya makutano ya Scuintla, Jocotenango na Chimaltenango tuwafanyie kitu mbaya tumuokoe mzee!” Silla akatupa wazo lililosikika vizuri na wote.

ENDELEA NA UTAMU WA DODO..!

SAA SABA USIKU

ANTIGUA, GUATEMALA

Mpaka wanafika barabara ya kuingia Jocotenango wakitokea Chimaltenango vijana wa GIS walikuwa hawajastukia kuwa katika moja ya magari yanayokuja kwa nyuma yao toka wanaingia barabara kuu inayotoka mji wa Chimaltenango hadi Jocotenango, Antigua.

Bara bara ya Jocotenango inayoingia katikati ya mji ilikuwa katika muundo wa barabara mbili kushoto na mbili kulia, wao walitaka kuingia itakayowawezesha kuelekea Santa Callina Arch.

Dreva anayeendesha gari hii ya vijana wa GIS aliingia kwa kasi ile ile iliyoongezeka kutoka kwenye gari punde tu walipoingia hii barabara kuu ya mji huu lakini kwa ghafla alishangaa gari iliyokuwa mbele yao ambayo iliingia  kwa mbele katika msafara wakiwa wanaingia barabara mchepuko ya kuelekea Santa Callina Arch, gari haina ya Toyota Hilux Surf Turbo Diesel ilipunguza ghafla ikiwa wote walikuwa kasi haina moja na hatua za kufikiana zikiwa chache.

Lekkon Volkswagen ilisota tairi zikasugua lami haswa lakini haikuwa dawa ilivamia ngao zake zikikita katika ngao ya nyuma ya Toyota Hilux Surf Turbo Diesel, ukatokea mshindo mkubwa sana ambao waliokuwa katika gari iliyosababisha ajali walijua nini wanafanya, mshindo huu ulizidi zaidi kwakuwa Lekkon Volkswagen ilivamiwa kwa nyuma na gari ingine haina ya Land Cruiser iliyokuwa ikija kasi mfanano na wao.

Ajali sababishwa! Walio katika gari ya mbele kwakuwa wao walikuwa wakijua wanafanya nini walishuka haraka kwenye  gari yao ambayo kwa nyuma iliharibika eneo kubwa mpaka katikati na hawa wasababishi wa ajali waliwai kufungua milango ya gari baada ya dreva wa gari hii kumaliza kukanyaga breki kwa kasi hivyo walishuka kirahisi sana.

Walikuwa ni Agent Kai ‘TSC’ na Investigator Miller wakiwa mikononi wameshika bastola mmoja akishuka kutokea mlango wa kushoto na mwingine akishuka kutokea kulia ambaye ndiye alikuwa dreva wa gari bwana mtaalamu Miller.

Kwa kasi walisogea ilipo gari iliyokuwa ikitumiwa na vijana wa GIS, Agent Kai alikuwa wa kwanza kufika kwa wepesi wake akiwa maeneo kama haya, kabla hajachungulia kupitia vioo vya gari vya mlango wa mbele ambavyo kama kioo cha mbele vilikuwa vimevunjika kiasi cha kuonyesha walio ndani, alistuka na kusimama ghafla mlango wa gari ulipokitwa kwa nguvu kwa miguu ya mtu aliye ndani ambaye wakati anafika hakuwa anamuona, ilibidi ‘TSC’ ajisogeze pembeni kwa kasi. Mlango uling’oka kutokana na mkito ule.

Miguu iliyokita mlango ikashushwa toka kwa ndani kisha miguu ile kana kwamba ilikuwa ikifuatilia nyendo za mtu aliye karibu ilipotua tu mtu yule akaurusha mwili wake kwa nguvu kutokea ndani ya gari hii iliyo katika hali mbaya kwa mminyo iliyopata ya magari mawili mbele na nyuma, alijirusha kwa chini akadondokea mgongo kwa wepesi wa ajabu kana kwamba hajatoka ndani ya gari iliyopata ajali, akili yake ilikuwa nyepesi sana ilimstaajabisha hadi ‘TSC’ aliyekuwa akimtizama kila hatua anayofanya.

Kijana yule akiwa kakamata bastola kwa mikono yake yote miwili alinyoosha mikono ile akiwa pale pale chini kuelekea alipo Agent Kai ‘TSC’ lakini naye hakuwa anajua vitendo vile anavyofanya katika wepesi wa kustaajabisha ulikuwa unazidiwa na wepesi na anayetaka kumchalanga risasi, kabla hajaruhusu kilimi hili risasi zikae kwenye njia yake alijkuta akipigwa yeye risasi ya kiganja chake cha mkono ambao ndiyo kidole chake cha shahada kilikuwa kimezama katika kifyatulio (trigger), alijikuta akiachia bastola yake ikimdondokea kifuani lakini bado hakuwa bwege hakutaka achalazwe risasi zaidi bila kuijtetea maana alijua mtu aliyesimama akiwa kaegemea gari iliyowasababishia ajali lazima atataka kuendelea kumchapa risasi hivyo yeye alijizungusha kwa kutumia matako yake akitaka asogee karibu zaidi alipo Agent Kai hili kusababisha ukaribu utakaozuia asipigwe risasi vizuri kisha naye akafanya lolote la kumsaidia.

Bado hakuwa anajua mtu anayemuona kwa taa za sola zilizo katika milingoti iliyo kando ya barabara hii ni mtu wa aina gani? Kabla hajafika lilipo lengo lake alirukiwa na kukitwa kwa ‘outer kick’ (teke lililopindwa mguu ukiwekwa upande), shingo ilivunjika sekunde tatu mbele roho yake ilikuwa ikishindana nguvu na mwili kuuachia alikuwa akipaparika kwa kasi pale chini, TSC alimtizama akatabasamu kisha akaacha aendelee kuupigania uhai wake ambao yeye alishajua kwa pigo lile labda awe na roho isiyo ya kibinadamu ndipo atapona.

Haraka yeye alisogea na kuchungulia ndani ya gari ambapo sasa aliweza kuona vizuri alimuona ndugu yake katika misheni Investigator Miller akiwa amekabana koo kwa koo na mtu mmoja aliye chini huku Miller akiwa juu yake, ni nguvu zilikuwa zikitumika kila mmoja akizidisha kumkaba mwenzake, hapo TSC akiwa pale pale aliposimama alitizama huku na huko akagundua watu muda si mrefu watawazunguka na kuwaletea wingu jeusi asillolitaka, kwa wepesi alisogeza siti na kumfanya yule aliye chini akiwa anakabana na Miller kukosa balansi akarudishwa kwa chini na mikono yake ikaachia shingo ya Investigator Miller ambaye alimuona aliyefanya hivyo alipotizama kwa kasi kwa mlangoni, kabali yake sasa ilikuwa haina haja ya kutumia nguvu nyingine kukaza shingo yake kuzuia asiingie matatizoni pale alipokuwa kakabwa, nguvu zilizidishwa akamkaba koromeo vizuri vidole gumba vya mikono yake yote miwili ilizama na kulizinga koo jamaa aliyekuwa anakabwa ukijumlisha alikuwa kabanwa miguu yake yake na siti alijikuta akiona nyota nyota tu jasho likazidi kumtoka usoni taratibu akajiona anaondoka duniani huku akipenda kuendelea kuishi, aliaga dunia huku anaona maana macho yalimtoka kama ngumi.

   “Kamanda! Kamanda… Muniain..!” Agent Kai akaita akiwa kaingia kwenye gari hii iliyobonyezwa na kuwa inaleta ufupi uliowafanya wao wote kuinama zaidi wakawa kama wanatambaa, vioo vilikuwa vimetapakaa kwa ndani hivyo walikuwa pia wakichukua tahadhari juu yake.

Walio siti za nyuma ilionekana gari iliyovamia kwa nyuma iliwaathiri sana tofauti na waliokuwa wapo siti za mbele dreva na yule mwingine aliyauliwa kwa kukabwa na Miller hawa waliona ajali ikitokea hivyo kuna kamsaada walijisaidia kiasi ya kina ‘TSC’ walipofika wakafikia mapigano nao wakitaka kujiokoa.

   “Kamanda huyu hapa katikati lakini naye kiti kimembana kama wenzake tunatakiwa tung’oe kiti cha mbele kilichombana” Aliongea Agent Kai kwa kasi hapo kwa haraka wakarudi chini na watu akama watatu wasiohusika walifika hapa na kufanya Kai na Miller kuangaliana nao.

   “Poleni jamani… Mnahitaji msaada wowote?” Mmoja kati yao aliuliza huku uso wake ukionyesha uwoga wa dhahiri kwani waliona maiti iliyo pembeni ya gari ambayo Agent Kai muda si mrefu alikuwa amempa nauli ya kwenda mahala ambapo kila mmoja kati ya sisi binadamu anakuwa hana hakika anapokutwa na hali hii anaenda wapi rasmi.

   “Ahsanteni sana.. Ndugu zetu hawa.. Tusaidieni kung’oa siti hii..” Haraka Kai akawajibu hili kuwaondoa katika mshangao wao uliokuwa umewapumbaza watu wale kuangalia maiti ya kijana wa kiume wanayemuona kalala akiwa kajishika shingo.

Dakika moja mbele siti iliyokuwa imeelekezwa na ‘TSC’ ikawa imeng’olewa na kutupwa pembeni kabisa ya gari toka ndani.

   “Kati yao mzima huyu mzee.. Hawa wengine sina hakika” Akaongopa Agent Kai kuwaambia watu wale baada ya kujifanya anawashika shingo zao kiukaguzi wa uongo uongo watu waliokuwa dhahiri wamezimia na hata kuna aliyekuwa kafa basi ni mmoja kati yao ambaye alikuwa nyuma kabisa tena akiwa nyuma ya siti ambayo inaoneakana ndiyo alikuwa amekalizwa Kamanda Muniain.

Walipokuwa wakianza kumuinua Kamanda Munian ambaye alikuwa akihema lakini kwa mbali gari haina ya Toyota Hilux 4x4 Double Cabin iliyokuwa inatumiwa na Special Agent Silla na Detective Norman ilifika kwa kasi na kupaki kwa pembeni milango mmoja wa mbele wa upande wa abiria ukafunguka akashuka Silla hakuremba akasaidia kubeba mwili ulio ndani ya zirai wa Kamanda Muniain wakafungua mlango wa nyuma wa gari hii iliyofika wakamuingiza na watu wawili wakaingia kwa kufuata kwa wepesi ‘TSC’ akirukia upande wa pili na kumfanya Kamanda Muniain kuwa katikati.

S.A Silla akarudi siti yake ya mbele milango ikafungwa gari ikaondolewa ikiwaacha watu waliofika eneo lile wengi wakiwa ni madreva wa gari wakiwa na kigagaziko wasijue nini kinaendelea kwa hakika.

   “Tunatakiwa tuwai kumpatia huduma ya kwanza Kamanda… Kisha tumpate daktari wa kutusaidia juu ya kuirudisha afya yake kitaalamu… Kimbiza gari Norman, hali si nzuri kivile kwa Kamanda..!” Akaongea Agent Kai.

   “Yupo daktari wa familia yake… Tutampigia atafika camp mara moja..!” Akajibu Norman.

   “Vizuri! Kazi nzuri tumefanikiwa kuzuia udhalimu ambao angeenda kufanyiwa Kamanda wetu… Nina maswali mengi juu ya Guatemala Intelligence and Security, kwanini taasisi kuu ya idara ya ujasusi imetaka Kamanda achukuliwe kwa kutekwa tena wakimvizia usiku akiwa katika mipango yake?” Akatoa pongezi za jumla Agent Kai kisha akaeleza kile anachofikiri kikiwa katika mfumo wa swali lakini ni kama alikuwa analielekeza kwa Norman aliyekuwa kazama kwenye kukimbiza gari kuelekea ilipo kambi yao.

   “Nafikiri majibu tutayapata akishapata fahamu mkurugenzi wetu Kamanda… Sidhani kama itakuwa iliwezekana wakati wanamteka bila kumwambia kwanini wanamchukua” Akajibu Norman bila kumuangalia Agent Kai aliye siti za nyuma yake lakini akipindua tu uso wanaonana.

   “Ni kweli… Vipi mlifanikiwa kwenda makazi ya waziri wa usalama?” Special Agent Silla akamuunga mkono Norman katika jibu lake kisha akamuuliza swali Agent Kai.

   “Ndiyo… Ila nyumbani kwake tuliwakuta walinzi tu… Tulifanikiwa kuwakwepa kuingia ndani kupitia nyuma sababu tulikata umeme wa mtaa mzima tukaingia kabla ya jenereta kuwashwa lakini ndani ya nyumba hatumkuta yeye wala mke wake tulikuta watoto wake na wafanyakazi wao wakiwa wamelala hivyo tulipekua katika maselfu yake napo hatukuona cha maana ndipo tulipopata simu yenu ikatubidi tutoke haraka kuja kuona tunafanyaje katika ombi lenu…!” Akajibu Agent Kai.

    *****  *****  *****

SAA MBILI ASUBUHI, IJUMAA

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Simu binafsi ya mkononi ya mheshimiwa waziri wa usalama wa nchi ya Guatemala iliita na kumtoa mawazoni mara moja akaiangalia simu ile kwa jicho la haraka sana mahala alipoiweka juu ya meza ya ofisi yake akaona kioo kikimjuza kuwa mpigaji ni mmoja wa watu wake wa karibu walio katika ofisi ya GIS ndiye anayepiga, moyo wake ulibadili mapigo ukapiga tofauti na ilivyo, haraka akanyoosha mkono kuichukua na kisha akasugua kioo katikati kwenda kulia kwa kidole chake cha shahada simu ikawa tayari kusikilizana.

   “Grandine…!” Akaongea kwa sauti kavu kidogo macho yakiwa yanaangalia juu ya paa lilipo pangaboi linaloleta upepo kwenye hii ofisi endapo yeye mwenye ofisi ataamua kuliruhusu lifanye kazi hiyo.

   “Mheshimiwa! Habari za asubuhi?’ Akakumbana na salamu ya kuulizwa.

   “Nzuri… Mbona sikupata maelekezo kamili toka kwenu… Vipi hali?”

   “Hali si shwari mkuu… Vijana walimchukua vizuri Kamanda Muniain lakini  wakiwa wamefika bara bara ya Jocotenango nilikuwa nimeshawasiliana nao wampeleke Santa Callina Arch kwenye jengo letu la siri kabla hawajasogea mbele likatokea gari aina ya Toyota Hilux Surf Turbo Diesel ambayo ilikuwa mbele yao na ilikuwa katika mwendo kasi unaofanana na wao ilisimama ghafla kwa makusudi na kusababisha ajali ya gari kadhaa barabara ile lao lililosababisha na lingine lililokuwa nyuma liliwavamia na kuwaumiza wote waliokuwemo ndani ya gari tunayoitumia kwa mambo yetu mara nyingi ingawa wote walizirai tu hakuna aliyekufa kwakuwa wewe mwenyewe unajua vijana wale wako vizuri kwa lolote ni bahati mbaya tu wamechezewa mchezo ambao hawakuutarajia kabisa… Katika watu sita niliowatuma kwa kazi ya kuhakikisha wanamtia mkononi Muniain wawili wanaonekana wameuliwa na watu waliomuokoa Kamanda Muniain kwa mmoja kukabwa huku mwingine amevunjwa shingo kwa kitu kinachoonekana kitaalamu nI teke maana shingo inaonekana imekitwa kwa kiatu mpaka kupelekea kuvunjika vibaya… Hii inaonekana wenzetu uliotuelekeza tuwasake na wao wamejipanga vilivyo kuzuia lolote lile kuwatokea katika hali yoyote..” Maelezo marefu toka kwa aliyepiga simu ambaye mheshimiwa alimuita kwa jina moja la Grandine.

   “Ooooh..Puuuuh… Mungu wangu!! Shiiit… Aisee! Mbona kazi inataka kunichanganya hii.. Eeeeh! Majeruhi wako wapi?”

   “Tuliwai kufika kabla polisi hawajafika.. Hivyo wapo hospital ya jeshi… Niliomba msaada kwa Jenerali atusaidie..!”

   “Hawakuwaona waliofanya kazi hiyo?”

   “Waliowaona ndiyo waliouliwa…. Hawa majeruhi walizirai pale pale ilipotokea ajali hivyo wakati anachukuliwa Muniain hawakuona, wote walizinduka baada ya msaada wa daktari… Ila gari iliyosababisha ajali hawakuweza kuondoka nayo watu hao.. Ni gari mali ya Kamanda Muniain..!”

   “Hakuna mashuhuda wowote?”

   “Pamoja ilikuwa saa saba usiku walikuwepo mashuhuda… Wanasema walioshuka kwenye gari ya mbele iliyosababisha ajali ni watu wawili ambao wote ni watu wenye asili ya watu weusi lakini wakati wanamtoa mtu wao ilifika kwa kasi gari aina ya Toyota Hilux 4x4 Double Cabin wakawachukua wenzao na kuondoka kwa kasi wakiwa na mtu wao Kamanda Muniain… Lakini hata hii gari aina ya Toyota Hilux 4x4 Double Cabin kama mara mbili hivi vijana wanasema waliwai muona nayo Norman wa OCLA hivyo moja kwa moja tunajumlisha matukio moja kwa moja kuwa mchezo umechezwa ipasavyo na Norman akishirikiana na wageni tulioambiwa wameingia hapa nchini kwa uongo uliotungwa na ubalozi wao kuwa wamekuja kuandaa usalama wa makamu wa Rais wa Marekani atakayekuja baada ya miezi miwili ijayo kwa ziara ya siku mbili..!” Akajibu kirefu Grandine.

   “Rais wetu anarudi leo… Itatubidi tuwe makini sana… Nitaomba baadaye tuonane hapa ukiwa wenzako wote wa katika mtandao wetu… Nitawapa taarifa walinzi kuwa tuna kikao cha ulinzi wa Rais atakapoingia hapo jioni hivyo hatuhitaji usumbufu..!”Alimalizia hivyo mheshimiwa Waziri wa usalama Bwana Rafael Ceni, simu zilikatwa.

Ilikuwa ni asubuhi yenye hali ya kiubaridi kama kawaida ya nchi ya Guatemala ubaridi asubuhi uwa ni kawaida sana mpaka inapofika saa tano ndipo hali ya jua kuchanganya na kuondoa kaujoto uweza kufika ikitawala hali hii mpaka jioni ya saa kumi na moja ambapo hali ya ubaridi uanza kurejea tena ikikolea kila muda unaposogea, lakini kwa bwana mkubwa huyu hali ilikuwa tofauti kajasho kalikuwa kametamalaki katika paji lake la uso.

Ofisi hii ya jengo la wizara ya usalama wa nchi iliyopo eneo la Chinautla mtaa wa Ciudad De Guatemala ilikuwa si ofisi ya furaha kwa mheshimiwa kwa siku mbili sasa alikuwa akiwaza zaidi ya ilivyokuwa awali wakati alipokuwa kapata habari za kuwa kuna flash imeandaliwa na mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Mwisho wa sehemu ya hamsini na tisa (59)

Timu inayoongozwa na ‘The Sole Cat’ inafanikiwa kuzuia jaribio la vijana toka taasisi kuu ya ujasusi nchini Guatemala ambao pamoja na kuwa wameapa kuwa wazalendo lakini wapo waliokuwa wakitumika vibaya na kufanya kazi ambazo kiuhalisia hawakutakiwa kufanya, kazi ambazo hazina tofauti na uharamia kama si ujambazi katika nchi maana na wao wanatumiwa uzoefu wao, ujuzi wao, elimu zao kufanya uhalifu unaofana na watu wanaofanya hayo niliyoyataja juu.

Mheshimiwa Waziri wa usalama anazidi kujiona yupo katika wakati mgumu sana kwakuwa yeye ndiyo haswa ni mtu ambaye amesababisha kwa kiasi kikubwa genge la TRJ kutamalaki na kuzikamata sekta nyingi za usalama nchini Guatemala, anajaribu kutumia vile anavyoviona vitamsaidia kuzuia kila analoliona lina harufu ya hatari.

Je katika pande zote zinahasimiana kwa sasa hapa Guatemala. Pande ipi itakuwa katika hali hatarishi zaidi?

Twende katika hatua inayofuata kusoma zaidi toka kwa mtunzi wako.





   “Ooooh..Puuuuh… Mungu wangu!! Shiiit… Aisee! Mbona kazi inataka kunichanganya hii.. Eeeeh! 

Rais wetu anarudi leo… Itatubidi tuwe makini sana… Nitaomba baadaye tuonane hapa ukiwa wenzako wote wa katika mtandao wetu… Nitawapa taarifa walinzi kuwa tuna kikao cha ulinzi wa Rais atakapoingia hapo jioni hivyo hatuhitaji usumbufu..!”Alimalizia hivyo mheshimiwa Waziri wa usalama Bwana Rafael Ceni, simu zilikatwa.

Ilikuwa ni asubuhi yenye hali ya kiubaridi kama kawaida ya nchi ya Guatemala ubaridi asubuhi uwa ni kawaida sana mpaka inapofika saa tano ndipo hali ya jua kuchanganya na kuondoa kaujoto uweza kufika ikitawala hali hii mpaka jioni ya saa kumi na moja ambapo hali ya ubaridi uanza kurejea tena ikikolea kila muda unaposogea, lakini kwa bwana mkubwa huyu hali ilikuwa tofauti kajasho kalikuwa kametamalaki katika paji lake la uso.

Ofisi hii ya jengo la wizara ya usalama wa nchi iliyopo eneo la Chinautla mtaa wa Ciudad De Guatemala ilikuwa si ofisi ya furaha kwa mheshimiwa kwa siku mbili sasa alikuwa akiwaza zaidi ya ilivyokuwa awali wakati alipokuwa kapata habari za kuwa kuna flash imeandaliwa na mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa.

ENDELEA NA DODO ASALI..!!

SAA TATU ASUBUHI, IJUMAA

CHIMALTENANGO, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Alikuwa ameshaamka mapema licha ya kulala muda mbaya, muda wa saa tisa usiku kutokana na pilika pilika za kazi za kazi akiwa na timu yake, saa tatu ya asubuhi ilimkuta tayari ameshafanya mazoezi ambayo alijipangia kufanya mpaka alipotosheka akaoga kisha kuja chumba hiki cha mawasiliano akiwa na juisi ya embe akaanza kuinywa kisha akawasha Ipad yake akaiweka katika mfumo WI-FI ambayo mwenyeji wao Norman alikuwa akiitumia ikiwa kaunganishiwa na mkuu wake wakati anakuja kuweka maskani ya siri eneo hili la wakulima wa ndizi wadogo wadogo.

Alipitia meseji kadhaa wa kadha zilizotumwa kwa njia mbalimbali kuja kwake, nyingi zikiwa za kifamilia kisha akaingia katika mtandao wa skype akamtafuta mkewe wakachati huku wanaonana furaha ikiwa tele kwa wanandoa hawa.

Wakati anaendelea kuchati akasikia hodi ikigongwa mlango bila wasiwasi akainuka akaenda kufungua mlango akakutana na uso wa Special Agent Rebecca Smith, sura ya kupendeza ya binti wa kizungu, meno meupe ya kung’aa yalikuwa yamechanua kutokana na tabasamu alilokuwa amelichanua ikambidi Agent Kai arudishie tabasamu na hakuna aliyetoa sauti kana kwamba wanaogopa au wanasikiliziana nani amuanze mwenzie.

‘TSC’ akavuta mlango zaidi kwa pembeni kisha akageuka kurudi ndani zaidi kule alipotoka ilipo meza kuu ya kazi, Rebecca akaunda tela kuingia kisha akaurudisha mlango akaenda kukaa kiti kingine miongoni mwa viti zaidi vya plastiki zaidi ya sita vilivyopo katika chumba hiki kisicho na kitanda lakini Agent Kai alilala akitandika kigodoro kidogo cha kumtosha urefu wake akikiweka chini sakafuni kisha akapiga usingizi wake vizuri tu.

   “Kana kwamba hujalala boss..! imekuwaje?” Akahoji Rebecca ambaye amezoea kumuita Agent Kai kuwa ni boss wake popote walipo.

   “Kulikuwa na lawama kadhaa katika simu yangu hivyo nikawa nazi clear zisije nifanya nikafanya kazi nikiwa sina baraka.. Hapa nishachati na mama, Lizy na mke wangu pia… Ila nimelala kidogo pia, masaa  matatu ni mengi Alhamdulillah, vipi ulivyoamka?” Akajibu na kuuliza na yeye.

   “Mmmh! Mwarabu akijua siku unamsaliti atakunywa sumu…!” Akatania Rebecca kitu ambacho si kawaida yake kutania kuhusu mke wa Kai.

Agent Kai alistuka akamtizama usoni aliyeongea kama ni Rebecca kweli au kuna mtu mwingine pembeni yake.

   “Nitamsaliti siku nikimpata mwanamke ambaye nampenda lakini yeye hajui kama nampenda.. Naogopa kumwambia huyo mwanamke sababu naye yupo CIA na pia sitaki aumie nimemchezea sipendi kuumiza wanawake inauma sana kuona machozi yao” Akaongea Agent Kai na mara wakasikia mlango unagongwa kwa kichwa TSC akamuonyesha ishara Rebecca akafungue mlango.

Kwa hatua za haraka binti wa kizungu mwenye umbo tata la kuvutia aliinuka kitini na kuelekea mlangoni huku nyuma Boss wake ‘TSC’ alimeza mate akitamani angeona vya ndani vya mwanamke huyu mwenye umbo lililokamilika na sura ya kuvutia lakini si mchezo katika masuala ya kazi za kazi si mtu wa kuchezewa au katika sanaa zote za mapigano na matumizi ya silaha.

   “Samahani kwa kuwaingilia faragha yenu..!” Aliyekuwa amegonga mlango alijihami kwa maneno haya punde tu macho yake yalipokutana ana kwa ana na macho ya Rebecca Smith.

   “Bila samahani Norman… Hii ni ofisi si faragha yetu..!” Akajibu Rebecca akitabasamu jinsi kijana huyu mzungu wa kilatino akiona aibu kuangaliana macho kwa macho na macho ya bibie.

   “Karibu..!” Sauti ya Agent Kai ikasikika ikitokea kwa ndani, Rebecca akarudi kitini na Norman aliingia kisha naye akaurudisha mlango na kuzama ndani ya ofisi hii.

   “Habarini za asubuhi jamani?” Akasalimu Norman akiwa anajiweka kitini baada ya kuwa kakikweka sawa.

   “Nashukuru Mungu mimi niko sawa salama salimini..” Akajibu Agent Kai kwa haraka akitabasamu.

   “Hata mimi vivyo hivyo niko sawa kabisa… Vipi wewe ulivyoamka?” Rebecca naye akajibu na kuuliza hali yake mgeni aliowavamia wakiwa katika kutaka kusogezana katika mipaka waliyonayo kati yao maswahiba wa nguvu.

   “Nimeamka salama kwa kweli… Nimetoka kuuweka sawa mwili kwa mazoezi, maji yakafuata na sasa hata kale kauchovu nilichoamka nacho kutokana na kuchelewa kulala hakuna kabisa… Nimekuja kuleta habari Kamanda Muniain ameamka na anataka kuongea nasi timu nzima..!”Akajibu na kumalizia kueleza lililomfanya kugonga mlango wa chumba hiki kuwa ni kuleta taarifa juu ya boss wake wa OCLA, mkurugenzi  Kamanda Muniain ameamka kutoka katika hali ya kuzirai baada ya kupata huduma usiku na daktari wa familia yake ambaye aliletwa usiku ule ule akiwa kafungwa kitambaa cheusi na kisha kurejeshwa kwake baada ya kumaliza kumchunguza na kumtibu majeraha Mr. Muniain.

   “Sawa tunakuja… Vipi kina Silla, nao washaamka?” Akauliza TSC.

   “Wako chumba cha gym wanafanya mazoezi, walinikuta namalizia wao sasa wanaendelea..!”

   “Okay! Mimi niliingia mapema zaidi… Wastue tuelekee chumba alicho Kamanda!” Akamalizia Agent Kai kisha akazima laptop iliyokuwa ikiwaka tu toka aiwashe.

Dakika kumi mbele wote watano walikuwa wamezunguka kitanda cha kitabibu alichokilalia Kamanda Muniain.

   “Pole sana mkuu! Utusamehe vijana wako kwa yaliyotokea!” Akaanza kuongea Agent Kai baada ya kumuwekea vizuri mto aweze kuulazia kichwa chake kwa uzuri Kamanda Muniain.

   “Ahsante na hamna haja ya kuniomba samahani sababu ya kufanyika kilichofanyika ni nzuri zaidi ya majeraha haya madogo niliyoyapata… Naomba niwashukuru sana wote timu nzima kwa kazi nzuri ya kuzuia nisiingie mikononi mwa wadhalimu ambao sijui wangenifanyaje mpaka muda huu… Shukrani nyingi sana na za dhati wote kwa ujumla kwa kujitolea kwenu” Akajibu Kamanda Muniain kishujaa kabisa, aliponyamaza akanyanyua glasi ya maji akanywa nusu

 glasi.

    “Ahsante kwa kutushukuru timu nzima kwa kazi nzuri iliyofanyia kuzuia utekaji wako… Na ni kweli hatuwezi juwa ingekuwaje mpaka muda huu, tumshukuru Mungu maamuzi yetu yalikuwa ya hatari lakini yalikuwa sahihi pia…!”Akaongea tena nahodha wa timu.

Kila mmoja kati ya wote katika watu wa kikosi hiki walitoa pole ya mdomo wakimshika mkono Kamanda Muniain kumfariji katika kilichotokea naye akashukuru sana na sana.

   “…Kazi iliyopo mbele yetu vijana ni kazi nzito sana na kujitoa kwa asilimia kubwa ikitegemea ushirikiano wa kila mmoja aliyeamua kuwa anataka kuifanya hii kazi…!” Alianza kuongea Muniain kisha akawaangalia waliosimama kwa mbele yake kwakuwa ilikuwa ngumu pale alipolaza kichwa chake juu ya mto kuweza kuangalia kwa pembeni pande zote, shingo yake ilikuwa imefungwa pop(bandeji ngumu) ya shingo.

   “Nchi yetu kwa sasa si salama zaidi katika mapambano dhidi ya mihadarati, kumekuwa na hali hii kwa miaka zaidi ya mitano sasa tokea genge la TRJ liamue kuifanya nchi hii kuwa njia kuu ya kupitisha mizigo yao ya mihadarati haina zote kama methamphetamines, cocaine na heroine kuna uchunguzi ambao kama OCLA tuliuanza miaka miwili iliyopita juu ya ukweli unaosemwa na baadhi ya watu kuwa hapa GTL kuna mahala kuna kiwanda kidogo kinachosaga unga huu wa haramu… Habari za kuwepo kwa kiwanda hiki tulizipata kwenye duru za kiintelejensia toka DTO ya Mexico, wakati mimi naingia kushika nafasi ya niliyemrithi nilikuta faili la hilo jambo ikiimizwa kufanyiwa uchunguzi wa kina ndipo tulipoanza kulifanyia uchunguzi mambo yakaanza kuharabika kwa vijana wetu mwaka ule tu tulioanza kila anayepewa kazi anakutwa amekufa… Tumepoteza vijana wa OCLA 26 kwenye hili suala mpaka mheshimiwa Rais aliniita kuniuliza kulikoni nikamwambia hofu tuliyonayo na jitihada zetu zinavyokatisha tamaa huku tukipoteza rasilimali watu kwa wingi sana mp..!” Aliishia hapo akanyamaza akameza mate kidogo kisha akanyoosha mkono wa kulia kuomba asogezewe glasi iliyokuwa na maji, Rebecca aliyekuwa karibu na glasi akainyanyua na kumsogezea mzee huyu ambaye licha ya kuwa  ni asubuhi ya mapema yenye ubaridi kama ilivyo ada ya nchi hii kiu kilimshika akaona anywe maji.

   “Ahsante!” Akaongea huku anampa glasi tupu Rebecca ambaye aliipokea na kuirudisha mezani, kamanda akawaangalia vijana kisha akatabasamu tabasamu la matumaini.

   “Vijana kama Norman katika OCLA nayoisimamia kwa sasa hakuna maana wale wote waliokuwa wamejitolea kwa hali na mali walishauliwa na makatili hawa hili wazuie kila jitihada zetu… Asubuhi nilipoamka mke wangu alinikumbusha kuwa leo ijumaa Rais wa nchi yetu anarejea toka kwenye ziara zake ndefu alizozifanya mwezi mzima katika nchi za Asia na Ulaya, kikawaida mheshimiwa Rais anaposafiri kwenda nje kwa ziara zake uwa familia zetu zote tunaenda kumuaga viwanja vya ikulu na hata anaporudi pia uwa tunafika kumlaki kwa furaha.. Basi kwakuwa wao mke wangu na watoto waliona ni vizuri wakaenda mapema ikulu hili kuongea na ndugu zao wengine kama watoto wetu na watoto wa mheshimiwa na mimi niliona ni jambo la heri wawai kwenda tu hasa moyo wangu ulikuwa ukiniambia kuwa kufika kwa nyie maafisa wa DEA na mauaji ya kuua watu kumi na tatu wa TRJ ni hatari maana ni kawaida kwao kutumia msemo wa jino kwa jino wanapopoteza watu wao tu basi wao ulipiza kisasi mara mbili ya watu waliowapoteza… Hivyo nilifurahi na kuona mke na watoto wangu wamecheza kama Messi kuomba niwai kuwapeleka ikulu.. Niliamua kuwasindikiza mwenyewe mpaka huko kisha nikaelekea ofisini kwangu na nilipofika tu nikapewa taarifa na mtu ninayemuamini sana anatokea GIS kuwa kuna kikao cha siri wamekaa baadhi ya maafisa wakuu wa GIS katika ofisi ya waziri wa usalama na wakaamrishwa kuwa mimi natakiwa nisifike siku ya leo nikiwa hai ila ukawa umesukwa mpango niuliwe nikiwa na waziri wa afya kwakuwa huyu waziri ametoa hotuba siku tatu zilizopita kuhusu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja akiweka karipio zito sana juu yao na kusababisha makundi yanayotetea haki za binadamu kumkosoa sana kwa hotuba yake ambayo akiwa kama waziri wa afya amehusisha vitendo vyao vya kisodoma vinaleta ongezeko la wagonjwa wa ukimwi katika nchi yetu na kuipoa mzigo mzito wizara yake katika kuagiza ARV, hivyo kukutwa mimi nimekufa nikiwa na Waziri Mitchell Arlitiz kungewekwa katika kuwa marafiki wawili tulikuwa pamoja tukashambuliwa na watu waliochukizwa na hotuba ya waziri wa afya… Niliambiwa nasubiriwa kutekwa nikiwa natoka kwenye jengo la ofisi kisha nitapelekwa mahala ambapo ningekutanishwa na Waziri Mitchell kisha tungeuliwa hapo kwa stahili ambayo wangepanga wao kwa wakati huo… Mtoa habari alinitahadharisha niwe makini kuanzia muda huo sababu mpango unaratibiwa na mheshimiwa Waziri Rafael Ceni akishirikiana na genge lake la TRJ pamoja na maafisa wa usalama wa taifa waliopo taasisi kuu ya kijasusi ya GIS… Ilinibidi nitumie akili ya ziada kuondoka katika jengo la ofisi yangu baada ya kuomba msaada kwenu na Norman akanijulisha kuwa mnaweza kunifuata na kunichukua ndipo nilipopewa taarifa na mtu mwingine si yule aliyenipa habari huyu ni tofauti aliniambia kuwa nje ya jengo kuna maafisa wengi wa GIS wanasubiri nitoke  wanichukue na wako tayari kutumia hata nguvu endapo itatokea kikundi au mtu atakayezuia dhamira yao chafu kwangu..!” Alinyamaza tena na kumeza mate akiwa kafumba macho kwa kuyakaza uso wote ukaonyesha jinsi anavyosikia maumivu fulani fulani katika baadhi ya sehemu za mwili wake.

   “Pole sana mkuu… Vumilia utumalizie..!” Akaongea Investigator Miller.

   “Bahati nzuri kwangu.. Ofisi yetu ina njia ya kwa chini inayotokea mtaa wa pili basi niliamua kupita njia hiyo bila kumshirikisha mtu yoyote maana inaanzia chumba cha masijala ni wachache wanaoijua njia hii ni waaminifu haswa ambao kwa jana hakukuwepo na mtu wa haina hiyo zaidi ya wafanyakazi wa huduma  za kiofisi tu… Nilipotoka tu mtaa ule nilikodi taxi ikanipeleka hotel niliyowaita mje kunichukua lakini wakati nipo pale dah! Ama kweli nchi hii kwa sasa inanuka uvundo mkubwa sana.. Ceni na TRJ wameigeuza nchi yao kabisa muda niliopanga ndiyo mtakuja kunifuata ndiyo muda ambao kuna binti mmoja anayehudumia hoteli ile alinichomea kwa watu wa GIS kuwa nipo pale nimechukua chumba… Nilijkuta nimetekwa wakati nashuka kwenye ngazi kuja nje hili nicheki mazingira kama yako sawa au kuna tatizo la kiusalama” Aliongea tena kirefu kidogo lakini napo alinyamaza akameza mate kisha akajivuta juu kidogo akiurudisha mto aliolaza kichwa chake kwa chini alipoona amekaa alivyotaka akameza mate tena lakini kabla hajaanza kuongea tena akaona midomo ya Agent Kai ina swali au inataka kuongea jambo.

   “Walisema wao GIS kwanini wanakuchukua na wanakupeleka wapi?” Akahoji Agent Kai.

   “Niliambiwa mkuu wao anataka kuonana nami pia na waziri wa usalama ana mambo anataka kujua kutoka kwangu” Akajibu Kamanda Muniain.

   “Mheshimiwa Waziri Ceni hatakiwi kuendelea kuhudumu akiwa waziri wa usalama kwa faida ya nchi hii si mtu anayefaa kwenye jamii, amekuwa akimuharibia sana Rais kwa matendo yake ya ovyo kabisa kwa nchi hii” Norman akaongea uso akiwa kaukunja.

   “Anapotembea na magari ya walinzi kana kwamba ni msafara wa Rais ulidhani anafanya vile kwa kupenda? La hashaa! Anafanya vile sababu anajijua ni mtu wa maasi makubwa muda wowote anavamiwa na watu anaosimiana nao kibiashara na hata kivingine tu kama wanausalama wangekuwa hawashikiwi akili na yeye muda kama huu angekuwa gerezani au chini ya ardhi” Akaongea Kamnda Muniain.

   “Kwetu imekuwa rahisi na tumeweza kujua mengi leo juu ya mtandao huu wa mihadarati.. Naona sasa ni muda wa mashambulizi non-stop umefika, tayari tushajua tunapambana na kina nani? Tumekuja GTL ilikuwa kwa kazi ya kumuokoa toka kwenye makucha ya shetani tuliyekuwa hatumjui lakini kazi imeingiliana na kazi… Sasa tuna jukumu zito zaidi la kupambana kuondoa shida kuu katika nchi za ukanda huu wa Amerika ya kati, kusini na kaskazini, shida ya mihadarati… Rais wa GTL leo anaingia na kuna flash inatakiwa kufika mikononi mwake hivyo basi leo iwe isiwe flash itamfikia Rais kama marehemu rafiki yake alivyotaka, tutaenda ikulu kuipeleka flash muda ambao utakuwa sawa kwa kazi hiyo… Muda mfupi ujao mimi au mwingine yoyote ataelekea nyumbani kwa Alexis Carlos Codrado nataka pale tukatege vinasa sauti hili uchunguzi wa shamba la Tajumulco uanze kwa mwenye shamba.. Na pia kwakuwa tuko as a team naomba pia tujue tutagawana majukumu kiuchunguzi na kimapambano lakini kila mmoja akiwa mlinzi mwenye kulinda usalama wa mwingine..!” Alieleza Agent Kai.

   “Na ndiyo maana ya timu.. Niko tayari kupangiwa lolote, muda ni mdogo lakini mambo ni mengi sana..!” Akaongea Norman hisia zake zikiwa juu sana juu ya kufany kazi hii.

   “Alexis! Anaishi wapi? San Marcos au hapa Guatemala City” Akauliza Agent Kai.

Detective Norman na Kamanda Muniain wakaangaliana  kuweza kukumbuka jambo na Norman aliweza kukumbuka.

   “Anaishi eneo la Galarias Del Sur mtaa wa Calzada Aguillar Batres bara bara ya Zone 11… Mtaa huu ndipo ilipo ofisi ya ubalozi wenu, nimekumbuka maana nimeona wote mmeangaliana, mtaa huu ni mtaa wanaokaa watu wa hali ya juu na hata maofisi yaliyopo mtaa huu ni maofisi ya wafanyabiashara wakubwa ndipo ilipo nyumba ya Alexis Carlos siijui ni nyumba namba ngapi lakini ni nyumba ya nne upande wa pili wa ubalozi.. Yaani ukiwa unatokea Zone 10 ukiupita ubalozi unahesabau nyumba nne ndipo unafika kwenye kasri la bwana mkubwa huyu” Akaeleza Norman.

   “Kama hautajali utanipeleka mi nitaingia kufunga vinasa sauti vyetu.. Kwa sasa mzee wetu naomba tukuache upumzike ila tunakuomba uzingatie dawa hili upone upesi..!” ‘TSC’ akaongea na watu wawili kwa mpigo akianza na Norman kisha akamalizia na Kamanda Muniain.

Mwisho wa sehemu ya sitini (60)

Timu ya ukombozi inazidi kuweka mikakati sawa hili kuanza kazi ya kusaka ushindi, ushindi wa kulitokomeza genge la TRJ na watu wao wote kwa ujumla ndani ya Guatemala.

Je kuna mafanikio katika yote haya?

Majibu uwa hayajibiwi hapa mwisho wa episode (sehemu) majibu uwa yanakuja kwa ujumla yakiwa yametoka mwanzo wa riwaya mpaka mwisho wa riwaya, vuta muda wako soma utamu huu wenye raha ndani yake.




   “Kwetu imekuwa rahisi na tumeweza kujua mengi leo juu ya mtandao huu wa mihadarati.. Naona sasa ni muda wa mashambulizi non-stop umefika, tayari tushajua tunapambana na kina nani? Tumekuja GTL ilikuwa kwa kazi ya kumuokoa toka kwenye makucha ya shetani tuliyekuwa hatumjui lakini kazi imeingiliana na kazi… Sasa tuna jukumu zito zaidi la kupambana kuondoa shida kuu katika nchi za ukanda huu wa Amerika ya kati, kusini na kaskazini, shida ya mihadarati… Rais wa GTL leo anaingia na kuna flash inatakiwa kufika mikononi mwake hivyo basi leo iwe isiwe flash itamfikia Rais kama marehemu rafiki yake alivyotaka, tutaenda ikulu kuipeleka flash muda ambao utakuwa sawa kwa kazi hiyo… Muda mfupi ujao mimi au mwingine yoyote ataelekea nyumbani kwa Alexis Carlos Codrado nataka pale tukatege vinasa sauti hili uchunguzi wa shamba la Tajumulco uanze kwa mwenye shamba.. Na pia kwakuwa tuko as a team naomba pia tujue tutagawana majukumu kiuchunguzi na kimapambano lakini kila mmoja akiwa mlinzi mwenye kulinda usalama wa mwingine..!” Alieleza Agent Kai.

   “Na ndiyo maana ya timu.. Niko tayari kupangiwa lolote, muda ni mdogo lakini mambo ni mengi sana..!” Akaongea Norman hisia zake zikiwa juu sana juu ya kufany kazi hii.

   “Alexis! Anaishi wapi? San Marcos au hapa Guatemala City” Akauliza Agent Kai.

Detective Norman na Kamanda Muniain wakaangaliana  kuweza kukumbuka jambo na Norman aliweza kukumbuka.

   “Anaishi eneo la Galarias Del Sur mtaa wa Calzada Aguillar Batres bara bara ya Zone 11… Mtaa huu ndipo ilipo ofisi ya ubalozi wenu, nimekumbuka maana nimeona wote mmeangaliana, mtaa huu ni mtaa wanaokaa watu wa hali ya juu na hata maofisi yaliyopo mtaa huu ni maofisi ya wafanyabiashara wakubwa ndipo ilipo nyumba ya Alexis Carlos siijui ni nyumba namba ngapi lakini ni nyumba ya nne upande wa pili wa ubalozi.. Yaani ukiwa unatokea Zone 10 ukiupita ubalozi unahesabau nyumba nne ndipo unafika kwenye kasri la bwana mkubwa huyu” Akaeleza Norman.

   “Kama hautajali utanipeleka mi nitaingia kufunga vinasa sauti vyetu.. Kwa sasa mzee wetu naomba tukuache upumzike ila tunakuomba uzingatie dawa hili upone upesi..!” ‘TSC’ akaongea na watu wawili kwa mpigo akianza na Norman kisha akamalizia na Kamanda Muniain.

ENDELEA NA NONDO..!!

SAA SABA MCHANA, IJUMAA

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Barabara ya Zone 11 ni miongoni mwa barabara ambazo inapokuwa mchana katika jiji la Guatemala City  mji  wa manispaa ya Antigua, mji mkuu wa jiji hili kuna muda inakuwa moto sana kwa pilika pilika za magari ya kifahari ya bei kubwa kuingia katika barabara hii inayoleta watu wanaofika kikazi au kimakazi katika eneo hili, mida ya pilika pilika hizo ikiwa ni siku za kazi uwa ni asubuhi ya kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa mbili na nusu asubuhi basi pilika pilika hupungua kwa kadiri muda unavyosogea mpaka utakapoona magari moja moja sana yanayokuja huu mtaa unaomiliki hii barabara inayoitwa Zone Eleven Road, pilika pilika za magari yanayotoka huu mtaa kuondoka kwenda sehemu zingine za jiji uanza tena muda wa kazi unapokuwa umeisha ambao kikawaida uwa ni saa kumi na nusu mpaka saa kumi na moja jioni.

Mtaa huu wenye majengo makubwa na mengine marefu yaliyoshika viwanja vikubwa unaitwa mtaa wa Calzada Aguillar Batres upo eneo maarufu sana ndani ya nchi ya Guatemala linalofahamika kama eneo la Galarias Del Sur, umaarufu wa eneo hili ni kuwa ni eneo linalokusanya maofisi mengi ya kiserikali na watu watu binafsi (wafanyabiashara) na pia makazi ya watu wenye pesa zao ambako kuna nyumba za shirika la nyumba la Guatemala na pia kuna walionunua majumba haya toka serikalini na kuwa wao ndiyo wamiliki halali.

Mtaa huu muda huu wa saa saba na dakika tano ulikuwa tulivu lakini utulivu huo ulivurugwa kwa mbali sana na muungurumo hafifu wa gari haina ya Mercedes Benz 2010 ML300 CDI toleo la Mercedes Benz la mwaka 2010 ikiwa ya rangi nyeusi mali ya kampuni ya kukodi magari iitwayo Parramos Car Rent & Tour’s Iiliyopo mji huu huu wa Antigua ikiwa imekodiwa na Detective Norman Cabrera siku mbili zilizopita baada ya kuona anaweza kutaka kutembea na gari ambayo haijulikani na hata watu anaofanya nao kazi katika OCLA. Aliiokodi kwa matumizi ya mwezi mzima akalipia kabisa kwa pesa ambayo alipewa na mkurugenzi wake kwa shughuli hii kabla hata kina Agent Kai hawajawatafuta wao na kuomba msaada wa kikazi.

Dreva wa gari hii alikuwa ni Norman mwenyewe ila pembeni kwenye siti ya abiria iliyoko kushoto kwake alikuwepo Agent Kai ‘TSC’, macho yake yakitupwa huku na kule bila kutulia katika majengo yaliyoko pembeni mwa barabara.

Walisogea kwa mwendo ule walioingia nao dreva akiendesha kwa mwendo ambao si wa kasi wala si polepole sana walipofika karibu na jengo kubwa la ubalozi wa Marekani dreva alimuangalia Agent Kai kisha akakunja kona kuelekea ulipo muelekeo wa geti kuu la kuingilia ubalozini.

   “Tutaomba hifadhi ya gari yetu hapa..!”Akaongea Agent Kai na mara mlinzi mmoja wa getini kwa nje alitoka kwenye kichumba kama kibanda akiwa kavaa mavazi ya jeshi la Marekani (full ngwamba) mkononi akiwa kakamata bunduki ambayo iko tayari kutumika muda wowote kukiwa na tatizo.

‘TSC’ alipoona jamaa anakaribia kwenye gari akachukua fursa aliyoona ni busara yeye kushuka ndani ya gari hivyo akafungua mlango na kushuka, mlinzi yule akamfikia kwa ukaribu.

   “Habari yako?!” Akauliza mlinzi yule uso wake ukionyesha alivyo makini na kazi yake, alitumia kilatin kuuliza imani yake ikiwa mtu huyu aliyetoka ndani ya gari anaongea lugha hiyo zaidi.

   “Habari zangu  nzuri mheshimiwa..” ‘TSC’ akajibu kwa kiingereza salamu ile na kumfanya mwanajeshi huyu mlinzi wa geti la kuingilia ikulu kumtizama vizuri Agent Kai, macho yake yakiwa ndani ya miwani yake mikubwa, miwani ya kijeshi ya jeshi la Marekani.

   “Amerikani?” Akauliza mlinzi akifanya ukaguzi wa macho toka chini miguuni kuliko na viatu kwa ‘TSC’ mpaka kichwani.

   “Naam… Natokea Drug Enforcement Administration!” Akajibu ‘TSC’ akikataa kujitambulisha kuwa anatokea CIA kwa sababu alizohisi yeye mwenyewe ni sahihi.

   “Kitambulisho tafadhali..!” Akaomba kitambulisho mlinzi na hapo ilikuwa kama mtihani kwa mtu mwingine asiye ‘The Sole Cat’ lakini kwa huyu ilikuwa si mtihani tayari alikuwa anacho kitambulisho cha kuonyesha yeye ni afisa wa DEA, alikitoa toka kwenye wallet yake akamuonyesha jina likiwa ni sawa si la uongo ni ofisi tu ndiyo ilikuwa ya uongo.

Mlinzi alikichukua akakisoma kidogo na kulinganisha picha na mtu anayemuangalia alipohakiki akageuka walipo wenzake hatua nne tu toka aliposimama na Agent Kai, akawaonyesha kitambulisho akiwa kakifunua waweze kukiona uzuri tokea walipo nao walitingisha vichwa vyao kuwa wameona na kuridhika na kile walichokiona.

   “Ndiyo unaingia GTL?”Akahoji mlinzi tena sasa akiwa amerudisha begani bunduki yake na hata wenzake waliokuwa nao pale kwenye kibanda cha geti nao walirudisha bunduki zao mahala panapostahili na kuwa wanaangalia na kusikiliza maongezi yanayoendelea.

  “Ndiyo… Kuna kazi imenileta hapa… Niko na mwenzangu tunahitaji msaada wa kuacha gari letu hapa kuna nyumba tunaenda ifanyia uchunguzi mdogo kama mjuavyo kazi zetu za ujasusi” Kai akafunguka kilichowapeleka mtaa ule, mlinzi aliangaliana na wenzake kisha akamgeukia Agent Kai akitabasamu.

   “Boss wa hapa getini anaongea na mtu ambaye amekuona kwenye kamera kutokea ndani… Hivyo subiri kidogo kuna maelekezo” Aliongea mlinzi ambaye alikuwa yupo katika mlango wa kuingilia kwenye  kichumba cha ulinzi wa nje ya geti kuu la ubalozini.

Jamaa aliongea na simu kama mlinzi yule alivyoeleza kisha huyo muongeaji akatoka nje kabisa alipoangaliana tu na Kai akasimama imara kisha akapiga saluti kumuonyesha heshima yake kwake.

   “Katibu wa balozi anaomba kuonana na wewe mkuu..!” Akaongea mtu huyu kumwambia Agent Kai baada ya kupiga saluti kiasi ya wengine kushangazwa na kilichotokea.

    “Katibu wa hapa ni nani?” Akauliza ‘TSC’ huku anaangalia saa kuwaonyesha ana haraka maana ukitaka kumjulisha mtu kimafumbo kuwa una haraka basi wakati yeye akitaka sana kuendelea kuongea na wewe wewe angalia saa.

    “Sajenti Yossef Benson Candreza… Afisa mstaafu wa jeshi.. Anasema mnafahamiana wewe ni Sajenti mwenzie wa jeshi letu..!” Akajibu kwa heshima baba huyu wa kizungu ambaye naye alikuwa katika mavazi ya jeshi la Marekani.

   “Sajenti Yossef Benson Candreza.. Yossef Candreza… Ooooh! Nimemkumbuka… Aisee yuko hapa?” Agent Kai alirudisha kumbukumbu nyuma kwa kasi akiwakumbuka watu mbalimbali aliowai kufanya nao kazi jeshini ni kweli alimkumbuka mtu huyu kuwa alikuwa naye jeshini kipindi fulani katika operesheni kadhaa za kijeshi ila mtu huyo alikuwa amemzidi yeye umri hivyo kwa hapa na kwa miaka waliyoacha kuonana lazima atakuwa mzee anayekaribia kustaafu kazi.

   “Ndiyo huyo… Basi njoo uongee naye kwa simu kama una haraka sana.. Maana ni boss mkubwa hapa ubalozini” Akaongea kimsisitizo mlinzi na hpao tena Agent Kai akatizama saa yake ya mkononi kisha akageuza uso wake kuangalia ndani ya gari alipomuacha Detective Norman wa OCLA.

Alikubali kwenda kuongea naye kwa simu mtu aliyetajiwa jina na yeye kumkumbuka kuwa ni kweli walikuwa wakifahamiana wakiwa washafanya kazi ya operesheni moja miaka zaidi ya kumi iliyopita wakati yeye Agent Kai akiwa katika kikosi cha US Navy Seals.

Dakika tatu zilipita kwa yeye kuongea kwa simu tena wakiwa na furaha sana kisha mtu huyo akampa namba yake ya simu ya mkononi wakaishia hapo.

   “Ahsanteni sana maafisa wangu…Tunaomba msaada wenu wa kile nilichoomba hili sisi tukafanye kazi iliyotuleta mtaa huu…” Akaongea Agent Kai, haraka jamaa walifungua geti kisha Norman akaliingiza gari akashuka na kuja kuwasalimu walinzi, walipomaliza maongezi mafupi wakawaomba walinzi kuwa wanaondoka watarudi baadaye kidogo punde watakapo maliza kazi yao.

Waliondoka wakiongozana ‘TSC’ na Norman mpaka barabara kuu wakiacha inayochepuka kuja eneo la ubalozi wakapandisha kushoto kuliko na mteremko mdogo wa barabara, wakienda wanahesabu nyumba mpaka Norman alipoliona jumba la mfanyabiashara na mwekezaji wa kilimo cha kahawa huko San Marcos, Mr. Alexis Carlos Codrado mdogo wake tokea nitoke wa kiongozi na Kingpin wa ‘THE RED JAGUAR’ (TRJ).

   “Nyumba yake ni hiyo inayofuata..!” Norman akaeleza wakiwa wako sambamba wameongozana kijana wa kilatin (kizungu) na kijana mng’avu mng’avu (maji ya kunde) lakini mwenye asili ya Afrika.

   “Tutapita kwa nyuma kwa jinsi navyoiona hata kabla hatujafika kwa ukaribu.. Hivyo nitaanza mimi kuchepuka kupitia kwa ubavuni huu ubavu wa kwanza tunaoukaribia wa ukuta wa nyumba… Wewe utapitiliza ukilipita eneo la mbele ya jumba husika kisha utaangalia hali ilivyo kama kuna uwezekano na wewe utapitia ukutani kwa upande wa pili kule…!” Maelezo ya mwamba Agent Kai yalipokelewa vyema na haraka Norman akamuangalia usoni kisha akatingisha kichwa kukubali wote wakatabasamu na kwakuwa walikuwa washakaribia kulipita eneo la nyumba ya jirani na nyumba kusudiwa Norman akazidisha mwendo akimuacha ‘TSC’ akipelemba sheria anawezaje kufanya jambo.

Hakuwa amevaa miwani muda huu, miwani yake ya kijasusi inayokuwa msaada sana kwake hasa nyakati anapohitaji msaada wake alikuwa ameiacha ndani ya gari na si kwa makusudi bali kwa bahati mbaya isiyokusudiwa kutokana na hakurudi ndani ya gari baada ya kuwa anaongea na walinzi kisha na aliyesemwa kuwa ni katibu ‘Sajenti Yossef Benson Candreza’.

Macho majanja janja mwingi yalimtizama Norman anayesonga mbele kisha akajifanya anatoa simu yake papo hapo wakati anatoa simu kisu kidogo cha mkunjo kilimdondoka akiwa kakidondosha kwa makusudi pia, mtaa ulikuwa mtaa mpana ulioachiana nafasi ya katikati ya ilipo barabra kwa pakubwa sana mita za mraba kama ishirini na tano upande kwa upande kulikuwa hakuna pilika pilika kabisa kwa muda huu kama ungekuwa unaingia huu mtaa iwe kwa kutokea juu inakoelekea barabara kisha kukutana na Zone 12 ungeweza kuwaona watu hawa wawili tu mtaa mzima na hata ungekuwa umeingilia walipokuwa wameingilia wao Agent Kai na Detective Norman kwa chini ukitokea barabara ya Zone 10 napo pia macho yako  yasingekupoteza ungeona watu hawa wawili wakiwa wameongozana ila mmoja akiwa mbele kabisa hatua ishirini hivi.

Hakuinama kwa haraka kukiokota kisu kile alijifanya kana kwamba amepigiwa simu akajifanya anasugua kioo kupokea simu kisha akaipachika sikio la kushoto akiwa kasihikilia na mkono wa kushoto ,  ‘TSC’ kiungo muongo muongo kama ni kwenye ‘soka’, akajifanya anaongea kwa simu ana laumu kitu fulani  alikwenda akisogea hadi kwenye pembe ya kona ya nyumba waliyokuwa wameipita kwa pamoja na Norman macho yake yakazunguka haraka kucheki pande zote kisha akayatuliza kuangalia ukuta wa nyumba anayotaka kuingia.

Kwa haraka alijifanya kana kwamba maongezi ya simu yamekolea sana kumbe haongei na mtu yoyote alikuwa kila sekunde anasogea kisha anasimama anarudia tena vivyo hivyo anasimama sekunde mbili kisha ya hapo anajivuta kusogea mpaka alipohakisha yupo chini ya mnazi na mikokono iliyojipanga kwa ndani ya ukuta, yeye alishakuwa  sasa anapiga hatua ndefu za nusu anakimbia kuelekea nyuma kwakuwa alishaona hakuna mtu anayemfuatilia ingawa aliiona cctv kamera na ndiyo aliyokuwa akiikwepa kwa kuhakikisha halandi kwenye muelekeo wake ilipoelekezwa.

Mbio kavu zilimfanya ausogelee ukuta na kupunguza mwendo wake akaegemeza mgongo ukutani, hapa hapakuwa na uchochoro unaopitwa na watu lakini ni uchochoro unaotenganisha hatua stahili zinazoachwa kwa ajili ya mipaka baina ya nyumba na nyumba, ilikuwa bahati watu wa nyumba hizi majirani walikuwa wamepanda miti kwa ndani ya kuta zao zinazozunguka majumba yao makubwa ya kifahari na hapa uchochoroni alipo Agent Kai kwa sasa kulikuwa kumepandwa miti mikubwa kama miashoki na miti mingine midogo midogo kwakuwa kulikuwa na eneo la kutosha kufanya hivyo.

Safari yake akiwa sambamba na ukuta mchana huu ilimfikisha nyuma ya nyumba ambapo katika maelekezo na Norman alimwambia anahitaji yeye aingilie kupitia nyuma ya nyumba.

Kulikuwa shwari kabisa ingawa mimaji michafu ikitokea nyumba ya iliopeana mgongo na nyumba ya Alexis Carlos Codrado, mimaji ilikuwa kero ikitoka kule bomba ndogo inayoonekana inatokea bafuni au sehemu ingine inayofanana na hali hizo na kisha maji yakatumbukia kwenye mtaro ulio karibu na aliposimama Agent Kai pua yake ikijisikia karaha kutokana na harufu mbaya.

 ‘TSC’ akaangalia huku na huko kuhakiki usalama wake kisha akajitoa pale kwenye kona mzima mzima na kuwa sasa yupo nyuma ya ukuta unaozunguka nyumba ya Alexis Carlos Codrado, macho yakapanda ukuta mpaka ilipo kingo yake juu akakutana na nyaya zinazojulikana ukiziona zimepangwa vile uwa ni umeme unaoshirikishwa katika ulinzi wa nyumba husika, ukuta huu kwa vipimo vya haraka ulikuwa na urefu wa kama futi kumi na mbili kwenda juu si rahisi kuruka juu na kukamata kingo yake kama inavyoweza kufanya kwenye kuta za futi saba mpaka nane kwa mtu mwenye mafunzo ya kazi za kazi na utundu mwingi kama ‘TSC’.

Akatoka alipo sambamba na ukuta hili aone vizuri juu akiwa ni mtaalamu atakwea vipi? Jibu likaja haraka kwakuwa kuta hizi kwake ni mazoea kuzikwea, mtaalamu akatoa begi lake dogo mgongoni akafungua zipu na kuibuka na gloves za mikononi kama wanazovaa waendesha baiskeli za mashindano au hata waendesha pikipiki za mashindano lakini hizi zikiwa tofauti hizi ni za kijasusi (magnetic intelligence gloves), akazivaa kisha akaingiza tena mkono ndani ya begi hapa akatoka na kamba hii akaiweka begani ikawa inaning’inia, hakuacha kuingiza tena mkono kwenye kibegi na sasa aliingia na kuibuka na fimbo kama ya chuma ni nyembamba iliyokunjwa kunjwa na na kuifanya iwe kama kisu kikubwa cha mkunjo, hapa sasa akafunga zipu na kulirudisha begi mgongoni alipolitoa.

Mwisho wa sehemu ya sitini na moja (61)

Nahodha wa kikosi Agent Kai akiwa na Detective Norman wa OCLA wamesogea kwenye mtaa ilipo nyumba ya mdogo wake na Brigedia Fernandes ‘Feca’.

Nini kitafuata katika sehemu inayofuata?

Kwa mengi ya kujua na utamu zaidi tukutane sehemu inayofuata ya muendelezo wetu…



Safari yake akiwa sambamba na ukuta mchana huu ilimfikisha nyuma ya nyumba ambapo katika maelekezo na Norman alimwambia anahitaji yeye aingilie kupitia nyuma ya nyumba.

Kulikuwa shwari kabisa ingawa mimaji michafu ikitokea nyumba ya iliopeana mgongo na nyumba ya Alexis Carlos Codrado, mimaji ilikuwa kero ikitoka kule bomba ndogo inayoonekana inatokea bafuni au sehemu ingine inayofanana na hali hizo na kisha maji yakatumbukia kwenye mtaro ulio karibu na aliposimama Agent Kai pua yake ikijisikia karaha kutokana na harufu mbaya.

 ‘TSC’ akaangalia huku na huko kuhakiki usalama wake kisha akajitoa pale kwenye kona mzima mzima na kuwa sasa yupo nyuma ya ukuta unaozunguka nyumba ya Alexis Carlos Codrado, macho yakapanda ukuta mpaka ilipo kingo yake juu akakutana na nyaya zinazojulikana ukiziona zimepangwa vile uwa ni umeme unaoshirikishwa katika ulinzi wa nyumba husika, ukuta huu kwa vipimo vya haraka ulikuwa na urefu wa kama futi kumi na mbili kwenda juu si rahisi kuruka juu na kukamata kingo yake kama inavyoweza kufanya kwenye kuta za futi nane mpaka kumi kwa mtu mwenye mafunzo ya kazi za kazi jumlisha na utundu mwingi wa kuzaliwa kama ‘TSC’.

Akatoka alipo sambamba na ukuta hili aone vizuri juu akiwa ni mtaalamu atakwea vipi? Jibu likaja haraka kwakuwa kuta hizi kwake ni mazoea kuzikwea, mtaalamu akatoa begi lake dogo mgongoni akafungua zipu na kuibuka na gloves za mikononi kama wanazovaa waendesha baiskeli za mashindano au hata waendesha pikipiki za mashindano lakini hizi zikiwa tofauti hizi ni za kijasusi (magnetic intelligence gloves), akazivaa kisha akaingiza tena mkono ndani ya begi hapa akatoka na kamba hii akaiweka begani ikawa inaning’inia, hakuacha kuingiza tena mkono kwenye kibegi na sasa aliingia na kuibuka na fimbo kama ya chuma ni nyembamba iliyokunjwa kunjwa na na kuifanya iwe kama kisu kikubwa cha mkunjo, akazama tena na kutoa kiboksi kidogo nacho akakiweka chini kama vingine vyote alivyovitoa, macho hayakuacha kufanya kama kichwa chake kinavyofanya kugeuzwa huku na huko kana kwamba mgoni anaogopa kufumaniwa baada ya kuingia chumbani kwa mwenye mali, hapa sasa akafunga zipu na kulirudisha begi mgongoni alipolitoa.

ENDELEA NA NONDO…!

SAA SABA MCHANA, IJUMAA

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Kwa kasi mikono yake ilifanya kazi iliyohitajika kufanyika kwa wakati huu alitoa alinyanyua kiboksi toka chini akakifungua na kutoka na kifaa kama betri ndogo za rimoti ambacho chenyewe kwa juu kulikuwa na lenzi hapa akakifunga mwisho kabisa ya fimbo niliyoelezea sehemu ya juu kuwa iko kama chuma au antenna ya redio iliyorudishwa ndani isirefuke alipomaliza kufunga akatoa kifaa kingine ambacho nacho kilikuwa kidogo lakini kina kama kioo ‘screan’ na keypad kadhaa za kufanya kifaa kile kifanye kazi akaipachika antenna kwenye tundu maalumu kwa kazi hii akakaza upesi mpaka ikawa inavyotakiwa hapo akatupa macho kwenda juu ya ukuta.

Aligeuka akawa ameupa mgongo ukuta kisha akabonyeza swichi ya kuruhusu kifaa chake hiki kifanye kazi hapo antenna ikaanza kunyooka ikitoka kwenda juu ilinyooka ikimpita urefu wake ikapanda mpaka juu ilipo kingo ya ukuta akiiangalia na kidole kikibinya na kila anavyobinya inazidi kupanda juu yake kukiwa na kile alichokifunga kikiwa na ukubwa wa kama betri.

Cha juu kilipofika usawa wa juu kukaribia kupita kingo ya juu aliacha kubinya kidole akatupa macho huku na huko kisha yaliporudi katika kifaa alichokishikilia akabonyeza kitufe kimoja kioo (screan) ndogo yenye upana wa kama kioo cha simu baadhi za smartphone kama Samsung J-7.

Hapo aliweza kucheza na batani mbili tatu tu katika kioo kukawa kunaonyesha ndani ya uwa uliozungukwa na huu ukuta karibu kila anavyocheza na batani za kupeleka huku na huko basi aliweza kulikagua eneo vizuri tu kana kwamba amekwea juu anaangalia ndani, hii ndiyo kazi ya kifaa hiki cha kijasusi, hakukuwa na walinzi kwa ndani kama alivyoweza kuhisi kabla.

   “Halloow! NC! Kwa ndani ya ukuta huku kwa nyuma hakuna ulinzi zaidi ya huu ulinzi shirikishi wa umeme..! Huko kwa wapi?” Akaongea na kuuliza Agent Kai akiwa kasogeza saa yake iliyo mkono wa kulia karibu na mdomo wake.

   “Nimekupata mkuu… Upande ulionielekeza nipite hakuna namna yoyote nyumba mbili zilizo jirani kwa upande huu hazikuacha nafasi kuna kuta kubwa zimeunganishwa..” Akajibu Detective Norman.

   “Nisubiri mahala ambapo hautawapa walakini watu.. Mimi naingia ndani kufanya kazi iliyotuleta hapa.. Acha on Bluetooth yako kunisikiliza nami naacha on saa simu… Na wengine kama mnanisikia huko mlipo fuatilieni mchezo nazama ndani ya nyumba ya Alexis!” Akaongea kwa kasi Agent Kai kumpa taarifa Norman na hata wengine walio katika mfumo wa ‘SCNGS’ huku akirudisha kifaa alichokwisha kifungua katika begi lake.

Hapa sasa ilikuwa zamu ya kamba iliyokuwa ya kwanza kutoka ndani ya begi, kamba hii ilikuwa na imezungushwa katika kichuma kidogo ambapo alipokifungua kilikuwa ni kinanga kidogo lakini kinachoonyesha vile kilivyo kigumu haswa machoni tu.

Haraka akakamata mwisho wa kamba mkono wa kushoto na kinanga kwa mkono akazungusha kwa kasi kisha akaachia kinanga kikapaa kutoka mkono wa kulia kwenda juu kwa muongozo wa mkono wa kushoto, kwakuwa mambo yapo katika chimbo lake haikuwa tofauti na anavyotaka nanga ilikwenda mpaka alipohitaji ikanasa akaivuta kuhakikisha uimara wake.

Sekunde ishirini zilizofuata kama mashine tayari ‘TSC’ alikuwa yupo juu kwa kutumia gloves alizovaa alikuwa kakamata nyaya alizokuwa tayari amezijua zina umeme ukifanya ulinzi anaouita ‘ulinzi shirikishi’.

Nyaya hizi zilikuwa zimewekwa kwa laini tatu kwenda juu naye mtaalamu wetu alikuwa kakamata laini ya pili kamba ikimpa sapoti kwa kasi aliyoenda nayo juu ilimfanya awe na moto sana wa kuondoka pale juu kwa haraka, akavuta kamba toka chini ikabaki pale ilipokuwa imenasa napo hakusubiri akajivuta na kulala juu ya ukuta waya wenye umeme akiuzuia kwa nguvu akitumia mkono wa kulia na mguu wa kulia ukisapoti lakini alikuwa akijua hatari ya yeye kuendelea kuwa pale juu kwa muda huu wa mchana.

Alizidisha nguvu kwa kuutanua waya huu  wa kwanza akitumia mguu wake kulia na mkono wake wa kulia mpaka ukaenda kugusana na waya wa pili, kichwa kikageuka kuangalia chini akaangalia kwa haraka kwa chini kulivyo alipoona wapi atatua akanasua nanga iliponasa akakamata kamba kwa mkono wa kushoto kisha akabingirika mwili mbiringiko mmoja tu akajikuta yuko hewani kwa kukusudia akitokea juu ukutani kwa kasi kuelekea chini.

Alipotua tu ilikuwa kama tairi tupu lisilo na rim iliyotua pale chini kwani alijiviringisha kwa kasi kuelekea kwenye bustani ya maua iliyo nyuma ya eneo la nyumba kubwa ya kifahari, alipotulia hakusimama akachuchumaa macho yakizunguka huku na huko, sekunde kumi zilimtosha kuuweka utulivu akaondoka kwa kasi ya kicheche kuelekea inapoanza baraza ya nyuma ya nyumba hapa akatulia tena na kihisia tu mkono wake ukatambaa hadi kwenye pindo la suruali ya jeans aliyovaa akaipandisha juu hapo kuna kimkoba cha kuhifadhi bastola akaikamata na kuinasua ilipo akaibuka suruali ikarudi ilivyokuwa.

Akaingia barazani akinyata kama kawaida akilibeba maana ya jina lake la utani kwa asilimkia mia moja maana ilikuwa kama hakuna kinachokanyaga chini kwa wakati huo (ajabu), uwepo wa vioo katika madirisha yaliyopo hapa barazani yaliweza kumfanya aamini anaweza kuwa katika tahadhari lakini si ile ya kujifanya hadi ajifiche sana (kosa), hakuwa ameiona kamera ya cctv iliyokuwa kwa ndani kabisa ikichukua kwa nje kupitia katika vioo vya madirishani iliweza kuchukua kila anachofanya toka anatua toka juu ya ukuta ilimpoteza kidogo alipojiviringisha kwenda eneo la bustani lakini aliposogea barazani ikaanza kumchukua tena ikirekodi na kutuma kwenda kwa mtu anayetaka kamaera hii ifanye kazi hii maalumu ya kiufundi.

‘TSC’ aliendelea na mwendo wake akasogelea kilipo kitasa cha mlango wa alluminium na vioo akakiminya na kusukuma kwa ndani kiushahidi tu kwakuwa alikuwa akijua tu si rahisi kuwa atakapokisukuma baada ya kuminya kitafungua mlango, alipohakiki tarajio lake akasogeza macho na kusoma aina ya kitasa kama kinaweza kufunguka na funguo na aina gani? Jibu likaja akatoa begi mgongoni kulileta mikononi mbele yake.

Zipu ndogo ya kimfuko cha juu cha begi ilifunguliwa kwa kasi na kisha kifurushi cha funguo kikatoka ndani, hapo akazipitia akizipindua pindua kutafuta ‘master key’ inayoendana na kitasa hapa kwenye kutafuta aliliwa muda wa sekunde kumi na tano hivi, akaipata ikiwa katikati hapo akaitumbukiza kwenye tundu la funguo la mlango akazungusha mara mbili mara tatu mpaka nne ndipo ukasikika mlio hafifu kuonyesha mambo yamejipa.

Vifaa kazi vya funguo vikarudi kwenye begi, macho yakazunguka tena huku na huko kisha akausukuma mlango ukajiachia kidogo na kutoa mlio wa ukavu wake ‘TSC’ akang’ata meno kisha akautuliza mkono kwa sekunde chache halafu akausukuma sasa akiwa kaujua huu mlango huu ni mlango uliokosa simile au tunaiita ‘milango umbeya’ , milango isiyo na siri inapofunguliwa utoa milio kana kwamba imeambiwa itoe taarifa kuwa kuna mtu anataka kupita.

Alifanikiwa kuusukuma akijitahidi usitoe mlio lakini ilikuwa si kazi rahisi sababu ulishindwa kukaa na siri mlango huu ukawa unalalamika mpaka ‘TSC’ akaona ilipobaki uwazi wa kuweza kuingia yeye akapita ndani na kuushikilia urudi taratibu mpaka na wenyewe ukakubali kurudi mahala pake.

Macho ya Agent Kai yalijikuta yanaangalia mahala ambapo ni kama korido pana na kubwa ambayo ilikuwa na masofa mawili makubwa ya ngozi yenye  rangi nyeupe ya kung’aa ya kuweza kukaliwa na watu watatu kila sofa moja yote yakiwa yanaangalia upande wa mlangoni lakini pembeni ya masofa haya kuna stuli ambayo nayo imewekwa ngozi nyeuepe ya kama masofa yote, juu ya kila stuli hizi kulikuwa na vitu, stuli moja ikiwa na stray (kikasha) cha kuwekea sigara na chupa mbili za pombe aina ya bia iitwayo Gallo bia maarufu na kongwe zaidi kuliko bia zote zinazotengenezwa na viwanda v ya ndani ya Guatemala, chupa zote zilikuwa zimemalizwa kinywaji kilichokuwa ndani na hata glasi zilizotumika zilikuwa mbili ikiwa ni muda mrefu limefanyika tukio kama hili.

‘TSC’ akafuata  korido inayoonyesha itakamata ngazi kwenda kuondoka hapa kwenye hii sehemu inayoonekana ni mahala maalumu kwa wavutaji wa sigara kupumzika hapa na kuvuta sigara zao kwa raha zao.

‘TSC!” Bastola mkononi akasongesha kwenye kona karibu na zinapoanza ngazi hapo kwanza alisimama baada ya tumbo lake kuminya kidogo (ishara ya hatari) a.k.a michale ikamcheza, umakini uliongezeka akasimama kwenye kona  kwa utulivu mwingi akiugemeza mgongo wake kwenye kingo ya papi za ngazi, macho yakaanza kuangalia kwanini anabanwa na tumbo sehemu zilipo six packs.

Kila kona kuanzia juu ya dari pembe zake mpaka katikati ya dari zilipo taa za urembo wa maua maua alipita kasi akiangalia kwa umakini kwa jicho lake makini lisilo na shaka wakati anapoangalia alipofika katika dirisha hapo aliona jambo ambalo moyo ulipiga mkumbo mdogo ukisema ‘swadakta’ ni sahihi, aliweza kuona nyaya inayotoka ndani ya bomba ya alluminium inayokamata vioo vya dirisha akaifuatilia kwa macho mpaka mahala ambapo aliona kamera ndogo ya kisasa ya cctv ikiwa imeelekezwa kuchukua habari zote za nje kupitia hapo dirishani hapo ‘TSC’ alitingisha kichwa kisha akatabasamu kana kwamba kuna uzuri katika lile.

Hakuishia hapo akaamia dirisha lingine napo akaona vile vile kama lile tofauti ikiwa hili kamera yake ilikuwa ikichukua kwa uzuri sana pale pale alipojiegemeza kwenye kingo ya papi za ngazi hapa tena akatingisha kichwa chake kukubali mwenye nyumba ujan ja mwingi alionao, akazidi kujifunza kitu katika kazi yake akiongeza mbinu nyingine ya ulinzi wa majumba haya ya watu wa kazi.

Mtu mwenye nyumba hakuwa ameweka kamera za ulinzi wa cctv kamera huko nje kwenye kuta zinazozunguka jumba hili bali aliweka kwa ndani zikiwa zimefungwa na madirisha ambapo ukiwa kwa nje huwezi kuona kama kuna kitu hiki, Agent Kai hakuwa na jinsi alikubaliana na hali kuwa tayari kaonekana kwa wanaohusika na nyumba hii au kwa mwenyewe Alexis Carlos, alitabasamu tena kisha akaonyesha alama ya dole gumba kuelekea kamera inayomchukua kuwa amekubali yuko tayari kwa lolote.

Aligeuka akiacha ziendelee na kazi yake akapanda ngazi kuelekea flour (losheni) ya pili akiwa ameamua liwalo na liwe na pia alishakuwa na hisia nyumbna hii muda haina mtu na kama yupo kwa utulivu uliopo atakuwa amelala, mwisho wa ngazi kipando alikuta korido fupi akaifuata inapoelekea huku napo macho yake yakitembea kwa kasi kuona kama napo kuna kamera kama alipotoka huku hakukuwa na dirisha, hatua zilimfikisha kwenye uwazi mkubwa uliowekwa pazia kubwa hapo akapenua upande wake alipo sehemu ndogo akachun gulia na kuona amefika varandani pia hakukuwa na mtu wala kiumbe kingine chochote ni fenicha za thamani ya hali ya juu pamoja na marashi mazuri sana yaliyokuwa yakinukia kwenye varanda hii pana na ndefu.

Hakutaka kuingia bila kuhakikisha usalama wake kwa asilimia fulani hata kama alishakuwa kaonekana kuwa ameingia katika mjengo huu kupitia cctv kamera, hapa varandani palikuwa na utulivu lakini si wa kumdanganya yeye mtaalamu kuna kitu alishuku hivyo kilimfanya aendelee kuangalia kwa umakini sekunde kumi mbele akagundua mawazo yake yako sahihi kwenye sofa la karibu na alipo kulionyesha mkandamizo ambao unarudi lakini polepole halafu mbele yake kuna meza ambayo juu yake kuna rimoti mbili ambazo kwa uzoefu wake alitambua muda si mrefu alikaa mtu hapa sofani na alikuwa akiangalia luninga ni mtu wa namna gani? Hili ndiyo lilibaki swali kuu kichwani mwake.

Kabla hajaamua aendelee na lipi saa yake iliwaka mtindo wa kuwa kuna mtu anataka kuongea naye kupitia mawasiliano yao, akabonyeza kitufe cha kukubali kisha mkono wake uliovaa saa akausogeza mdomoni.

   “Naam!” Akaongea kwa sauti ya chini kweli kweli lakini kwa mawasiliano yao kuwa ‘bluetooth earphone’ zinakuwa ndani ya tundu za masikio ni sauti kubwa na inayokuwa inasikika vizuri kutegemea na saa ambayo ndiyo ina spika ya kupokea sauti inavyosogezwa karibu na mdomo.

   “Si shwari… Zimefika gari tatu na zote zimesimama upande wa pili wa nyumba wameshuka kutoka katika kila gari watu watano jumla wako watu kumi na tano..!”

   “Kuna cctv kamera zimefungwa sehemu ya kuvutia sigara zikuwa nimeziona ndizo zilizonichoma… Humu kuna mtu pengine ni mmoja tu alikuwa anaangalia luninga hapa varandani nilipo sikumkuta ila nimeona ishara… Hao watu waliofika hawajakuona kweli?”

   “Hapana.. Huku mbele nilipo kuna glocery ya vinywaji ndogo… Nipo hapa”

   “Inabidi niondoke hapa lakini msaada wako pia utahitajika..!”

   “Hilo halikwepeki kwangu.. Nafikiri na wengine wanatusikia watakuwa wanakuja haraka..”

   “Haina haja ya wao kuja… Kumi na tano ya watu hawa inaweza zimwa kwa msaada toka kwa wanajeshi wa ulinzi wa ubalozini… Nakurushia namba kwa meseji kwenye simu yako utampigia huyo nayekupa namba zake ni katibu wa ubalozini tulipoacha gari utamuelekeza hali halisi kisha umwambie naomba aizingire nyumba kwa watu wake..” Akaongea kwa kasi ‘TSC’ ikiwa sauti yake ikiwa ile ile ndogo ya kunong’ona.

  “Sawa fanya hivyo.. Wanagawana kuizunguka nyumba, nafikiri wengine wataingilia kwa getini.. Sasa sijui kule nilikoshindwa pita wao watapita vipi?.. !” Alimalizia Norman na upande wa Agent Kai haukusubiri ukakata simu.

Pazia ikasogezwa pembeni kidogo kisha mwamba akapiga hatua mbili kukanyaga zulia la manyoya nyoya rangi jekundu lililotandikwa varanda yote juu ndipo kuliko na fenicha mbalimbali zinazotakiwa kuwemo katika varanda ya mtu mwenye pesa zake na mwenye kujali unadhifu wa kujipenda yeye na vilivyo karibu yake.

Hatua zilimpeleka hadi kwenye dirisha kubwa mojawapo katika ya madirisha yaliyo hapa varandani ambayo yalikuwa na mapazia makubwa, alipofikia akafunua sehemu ndogo macho yakaweza kuona mbele ya jumba hili la kifahari ambapo kulikuwa na pande ambayo kuna bustani za kuvutia sana jinsi zilivyo pangiliwa pamoja na matunzo yake, upande wa pili karibu na geti kulikuwa na kichumba ambacho kwa ndani aliweza kuwaona watu wawili waliofaa sare zinazofanana zenye rangi ya bluu nyeusi hawa walikuwa walinzi wa getini ambao hawakuwa wanajua kipi kinaendelea ndani na nje ya jumba hili.

Kushoto kabisa kulikuwa na eneo kubwa lililofunikwa juu kwa turubai lililoenea eneo lote likianza ulipo ukuta uliozunguka jengo hadi karibu na jengo husika mashikizo yake ya nguzo za chuma yakiwa yamepigwa kwenye  zege inayounganisha flour ya kwanza na ya pili ya jumba hili la ghorofa lenye flour (losheni) mbili, chini yake kulikuwa na magari manne ya kifahari mawili rangi tofauti na mawili rangi nyeusi.

Mwisho wa sehemu ya sitini na mbili (62)

Kamera za cctv zimeweza kufanya Agent Kai kuwa katika hali tete ambayo haijulikani nini kitafuata katika sehemu inayofuata.

Umakini wake wote kazini lakini hapa aliweza kuwezwa na kuingia katika sintofahamu kuu..!

Je? Ni kina nani waliopeana taarifa na kuweza kuja haraka katika jengo hili ambalo Agent Kai alikuwa ameingia kwa ajili ya kutaka kuweka vinasa sauti na hata kamera ambazo zitaweza kuwasaidia wao kujua ni nini muhusika wa nyumba hii anafanya hasa kwakuwa ni mdogo wake na Feca pia mmiliki wa eneo ambalo barua pepe aliyotumiwa Agent Kai inaonyesha ilitumwa na mtumaji akiwa eneo hilo.

Majibu ya mambo yote ambayo kwa sasa ni kama mafumbo kwetu yatapatikana katika sehemu zinazofuata.



  “Sawa fanya hivyo.. Wanagawana kuizunguka nyumba, nafikiri wengine wataingilia kwa getini.. Sasa sijui kule nilikoshindwa pita wao watapita vipi?.. !” Alimalizia Norman na upande wa Agent Kai haukusubiri ukakata simu.

Pazia ikasogezwa pembeni kidogo kisha mwamba akapiga hatua mbili kukanyaga zulia la manyoya nyoya rangi jekundu lililotandikwa varanda yote juu ndipo kuliko na fenicha mbalimbali zinazotakiwa kuwemo katika varanda ya mtu mwenye pesa zake na mwenye kujali unadhifu wa kujipenda yeye na vilivyo karibu yake.

Hatua zilimpeleka hadi kwenye dirisha kubwa mojawapo katika ya madirisha yaliyo hapa varandani ambayo yalikuwa na mapazia makubwa, alipofikia akafunua sehemu ndogo macho yakaweza kuona mbele ya jumba hili la kifahari ambapo kulikuwa na pande ambayo kuna bustani za kuvutia sana jinsi zilivyo pangiliwa pamoja na matunzo yake, upande wa pili karibu na geti kulikuwa na kichumba ambacho kwa ndani aliweza kuwaona watu wawili waliofaa sare zinazofanana zenye rangi ya bluu nyeusi hawa walikuwa walinzi wa getini ambao hawakuwa wanajua kipi kinaendelea ndani na nje ya jumba hili.

Kushoto kabisa kulikuwa na eneo kubwa lililofunikwa juu kwa turubai lililoenea eneo lote likianza ulipo ukuta uliozunguka jengo hili hadi karibu na jengo husika mashikizo yake ya nguzo za chuma yakiwa yamepigwa kwenye  zege inayounganisha flour ya kwanza na ya pili ya jumba hili la ghorofa lenye flour (losheni) mbili, chini yake kulikuwa na magari manne ya kifahari mawili rangi tofauti na mawili rangi nyeusi.

ENDELEA NA NONDO…!

SAA SABA MCHANA, IJUMAA

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Akiwa kwenye tahadhali ya hali ya juu aliendelea kusimama pale dirishani umakini ukiwa umetamalaki thabiti kabisa kuhakikisha hakuna kinachosikika wala kujongea kote kote kuanzia hapa alipo hadi nje anakochungulia bila yeye kujua.

Akiwa bado pale masikio na macho yakiwa makini aliona kwa chini mbele ya nyumba kwenye kijumba cha ndani ambacho mara nyingi ukikiona pembeni ya geti utaweza tambua ni kichumba anachostahili kukaa mlinzi wa sehemu husika ya nyumba, aliona mwanaume wa makamo aliyevalia mavazi ya kimgambo maana ni gwanda lakini halina alama ya cheo chochote, akitoka kwa kasi na kuelekea lilipo geti mlango linalokuwa mara nyingi kwenye geti kubwa kwa ajili ya mtu kama hayuko na gari kupita kuingia ndani ama kutoka.

Mlinzi yule alionekana akichungulia sehemu maalumu ambayo angeweza kumuona mtu wa nje akaongea naye kuulizana jambo ambalo ‘TSC’ hakuwa analisikia, lakini hisia zake zilihisi maongezi yale kwani mtu yule ambaye mlinzi alistuka akageuka kuangalia huku na huko kisha akarudi kwenye chumba alichotoka akaingia ndani kwa kasi akatoka na mtu mwingine aliyevaa kama yeye (walinzi wazembe wote wawili walijiweka sehemu moja), walitoka wakiwa na bunduki ambazo ni ngumu kujua haina zake zaidi ya kusema ni za wale watu wanaotengeneza kienyeji si kisasa (viwandani).

Mmoja ambaye ndiyo alikuwa wa kwanza kutoka na kuchungulia nje kupitia tundu la kuchungulia getini alikimbia hadi getini akafungua geti dogo na kupisha pembeni wakaingia wanaume wanne na mwanamke mmoja wote wakiwa na bunduki ambazo ni za kisasa hapo Agent Kai akatambua ile cctv kamera ya kule chini imepelekea mwenye nyumba kuomba msaada ambao haijulikani hawa ni watu wa usalama au ni watu wa TRJ wanaowashuku wanafungamana na mdogo wake na muasisi wa genge hilo sifika ukanda wote wa Amerika zote.

Mtu ambaye ‘TSC’ hakuwa amemkuta hapa sebuleni lakini alitambua kuwa alikuwepo alimchanganya sana Agent Kai kuwa yuko kwa wapi? Na kumfanya asifanye mambo mengine kwa uhuru zaidi kuwa nasikilizia usalama wake huku na huko kama paka aliyeingia matatizoni na mwenye nyumba baada ya kudokoa kitoweo, kule chini wale watu macho yao karibu wote yalikuwa yakiangalia kwenye madirisha huku wakitembea kwa tahadhari kila mmoja kukaa sehemu ambayo wanaamini ni kujikinga na shambulizi lolote kama watashambuliwa kitu ambacho hakikuwa nia kwa ‘TSC’ kwa dakika hizi.

Moyo wake ulistuka mtaalamu wetu maana ni kama kustuliwa hii ilikuwa kali sana kwake hakuwa amehisi jambo hili linaweza kutokea, pale pale alipo ambako ni karibu sofa moja kubwa la watu watatu ilisikika sauti.

   “Kijana wa kiniga.. Umefuata nini ndani mwangu?” Sauti ile iliuliza ikitoka kwa karibu kabisa na alipo ikitumia lugha ya kilatino.

   “Usiogope… Maana nimeona umestuka na kupunguza ushujaa wako uliokuwa nao wakati unaingia kwa mbwembwe ukiruka toka juu ukutani… Jibu papo hapo ulipo kuna spika za kupokea sauti huwezi kuziona… Kijana umeingia nyumba iliyo nja mfumo bora kabisa wa ulinzi ambao laiti kama ingekuwa hakuna ulinzi kama huo muda unafika usingepata urahisi kuingia bila kuonekana kwa walinzi maana ningewajaza wa kutosha sababu pesa si tatizo kwangu, tatizo jinsi ya kuzitumia..” Ikaongea tena sauti hiyo hapa ikifanya Agent Kai aelewe anaonekana vizuri tu toka kwa huyo muongeaji ikabidi ajitoe eneo alipo akasogea karibu na sofa inapotokea sauti akalishika kwa juu akitabasamu.

   “Unatabasamu nini? Unafikiri unaweza kutoka humo ndani ulimo tena? Sahau hilo hakuna aliyeingia ndani ya nyumba yangu bila ruhusa yangu halafu akatoka salama bila mimi kutaka atoke salama… Wewe si wa kwanza kufika ndani ya nyumba hii ya Alexis Carlos Codrado ‘kompyuta’ kinyemela tena wakijifanya mashujaa kweli kama ilivyo kwako lakini hawakutoka mbuzi wenzio wote.. Ni vizuri kuanzia sasa ukaweka bastola yako uliyonayo mkononi pale mezani wewe ukikaa mbali nayo kusubiri wanaoingia.. Heti ulikuwa unanyata kweli wewee mpuuuzi! Unanyata ndani ya nyumba yangu? Hahahahaha!” Sauti ilisikika ikiongea kwa dharau kubwa mpaka ikamfanya Agent Kai abadilike ghafla na kukunja sura yake maana si kawaida yeye kuruhusu dharau.

   “Niue kutokea huko ulipo unapoongea kwa uwoga kama mwanamke malaya aliyefumaniwa gizani lakini ngumu sana kwa mtu kama mimi kuweka bastola yangu chini au mahala popote bila kuifanya irushe hata risasi moja kumuondoa uhai mtu mmoja… Wee kama mwanaume unajiamini kama mimi nilivyojiamini kuja hapa toka ulipojificha uje mbele ya macho yangu uongee upuuzi wako… Alexis Carlos Codrado unajiita kompyuta mdogo wake na Fernandes Carlos Codrado brigedia mjinga aliyefukuzwa kazi kijinga kwa kuwaharibu wanajeshi wenzake kuwauzia madawa ya kulevya na..!” Aliishia hapo simu yake ikatoa mtetemo ikiwa ndani ya mfuko wa suruali aliyovaa, mtetemo wa mara moja tu ulimjulisha kuna meseji akaitoa na kutoa lock kisha kwa haraka akaisoma meseji ilikuwa ikitoka kwa Norman kumfahamisha wanajeshi toka ubalozini wako kwa barabarani wanaelekea zilipopaki gari za waliofika kutaka kumdhibiti yeye Agent Kai wakiwa wameelekezwa na mwenye nyumba hii.

Simu ikarudi mfukoni kwa kasi kisha akaangalia sofa linaloleta mawasiliano ya sauti kati yake yake na bwana majivuno lakini kwake akimuona kunguru wa Zanzibar.

  “Unaomba msaada? Nchi hii ukishaingia ndani ya nyumba ya Alexis huwezi tena kupata msaada.. Au wewe niggaz mgeni wa GTL?” ikaongea sauti toka kwenye spika zilizo ndani ya sofa.

   “Shoga wewe… Acha tupambane ndiyo utajua mimi mgeni GTL kama wewe au mwenyeji GTL..”

Kwa mbali masikio ya ‘TSC’ yalisikia nyayo za kunyata zikitokea zilipo ngazi zinazokuja kwenye korido iliyomleta yeye hapa sebuleni , hakusubiri haraka akapiga hatua ndefu mpaka kwenye kizingiti ilipo pazia kubwa ya eneo lililo wazi linalofanya mtu aingie kwenye varanda hii alipofika akachungulia vikaonekana vivuli viwili vya binadamu vikiongozana taratibu kimoja kikiwa kimetangulia mbele na kingine kinafuata kwa ukaribu kutokea kwenye ngazi walizokuwa wanazipanda zinazokuja kwenye korido na bunduki nazo zikiwa zimetangulia mbele nazo zikionekana zinajongea kama waliozishika wanavyojongea.

‘TSC’ akasimama sawasawa na kizingiti kuliko na pazia kubwa lakini macho hayakuacha kufuatilia vivuli vile.

   “Nigga!.. Unataka kunionyesha sinema gani? Nakiona kila unachofanya hapo ulipo hapawezi kukusaidia kuondoka kwako zaidi ya kujibu maswali yangu na tukafanya maongezi angalau naweza kukuelewa pengine nikaacha uende tu…  Natambua njaa ndiyo iliyokuleta humo” Sauti ya dhihaka iliendelea kutokea mahala pale pale alipoondoka ‘TSC’ hakujibu akaonyesha alama ya dole la kati likimaanisha alichoamini mtu huyo anayemuangalia kupitia kamera ambazo kwa sasa yeye hakujali ziko wapi aliamini anaelewa nini maana ya dole la kati.

Vivuli vile vya watu vilifika mwisho na vyote viwili vilisimama vikigawana upande ukimya ukashika hatamu, ‘The Sole Cat’ aliinua bastola kulenga alipoamini kuna kitu kitatokea, akaruhusu kilimi na kidole cha shahada toka mkono wake wa kushoto mkono shabaha wa dhahabu ulinasa kwenye kifyatulio (trigger).

Sura ya mtu ilianza kutokeza taratibu kama kivuli kisha fremu ya miwani ilitokea taratibu ilipotokeza zaidi hili macho yaone risasi iliyotoka kwenye bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti ilikohoa kama chafya ndogo sana ya mtoto mchanga, risasi haikufanya makosa ilipasua fremu ikakita kwenye jicho la kushoto la mtu aliyechungulia akarushwa na kujipiga kwa mwenzake kelele zilizisikika akadondoka na kuanza kupaparika kama kuku aliyechinjwa kisha mchinjaji akamuachia bila kumdhibiti.

Agent Kai akakaa tayari kwa lolote lingine tena lakini akaona vivuli vikiuvuta mwili unaopaparika kurudi kwenye ngazi.

Mara kwa nje ikisikika milio mingi ya bunduki za kivita risasi zikipigwa kwa kujibishana papo hapo ‘TSC’ akajua kumekucha na makucha kucha yake, mapambano yameanza jeshi la uokozi limeanza kazi yake.

   “Umeona boss kilichomkuta nyumbu wako mmoja… Nasubiri atokee mwingine nimpeleke akhera kwa bei nafuu.. Amerikani wako nje wanawadhibiti wahuni wako kisha utafuata wewe nyumbu malkia..!” Akaongea Agent Kai akiendelea kuangalia kule kwenye ngazi kama kuna kivuli au kitu kinachosogea.

Hakukusikika jibu wala ongea ingine toka mahala pale bali ilisikika sauti ikitangaza kupitia kipaza sauti cha matangazo.

   “Naitwa Koplo Marcel Lino wa jeshi la Marekani ninayehudumu katika ubalozi wa Marekani uliopo jirani na nyumba hii… Tumepokea taarifa inayohatarisha usalama wa raia wa kimarekani pamoja na ubalozi wetu ukitokea katika nyumba hii…Nyumba imezingirwa na wanajeshi wa Marekani wote mliokuwa ndani ya nyumba mnaamrishwa kujisalimisha bila kujali bila sharti.. Watu wote waliokuwa nje wameweka zuio la kudhibiti nyumba hii wote wameshajisalimisha walioleta kiburi wamepata kilicho wastahili na sasa tunakuja ndani kwa ukaguzi aliyegoma kujisalimisha hatutamuonea huruma..” Sauti kubwa ambayo ilikuwa ikitokea nje kabisa ya jengo ilisikika ikipazwa kutokea kwenye spika ya matangazo.

‘TSC’ alirudi dirishani akachungulia kwa chini akaziona maiti kama tatu za watu zikiwa kwa mbalimbali ikionyesha walijaribu kujizuia wasiingie matatizoni kwa mapambano ya kujibizana kwa risasi ndipo umauti ukawakumba lakini pia aliwaona watu wawili wakiwa wamepiga magoti mikono juu kujisalimisha lakini wanajeshi ambao alihisi atawaona hakuwaona hapo tena akatambua wataalamu wako mahala wamejificha ila waliopiga magoti wanawaona, akatoa simu yake ya mkononi kisha akapiga namba za katibu wa ubalozini.

  “Sajenti..!” Akaanza kuongea baada ya simu kupokelewa na upande wa pili.

  “Naam kijana.. Vipi hali yako?”

  “Niko salama kabisa.. Nashukuru umewai kutuliza hili…!”

  “Ulifuata nini hapo?”

  “Mwenye nyumba hii ndiye aliyenileta hapa.. Hata hivyo sijamkuta, ingekuwa hali ya nchi hii ni ya kuomba msaada kwenye vyombo vya usalama basi ningekuomba unisaidie popote alipo awekwe chini ya ulinzi lakini hali ya hapa GTL si hali salama ni ya kutia mashaka na kutoamini katika jeshi la polisi hadi wanausalama wengine… !”

   “Mwenye nyumba hiyo ni mfanyabiashara na mwekezaji mkubwa sana unaposema hivyo nashindwa kuelewa kwa uzuri ila naweza kusaidia kupatikana kwake kwakuwa ofisi yake pia haipo mbali na mtaa huu na muda huu atakuwa yupo ofisini kwake”

   “Hivi navyoongea nawe ananisikia mimi kwakuwa ameweka mfumo wa kusikia na kuona kila kinachofanyika hapa… Ngoja nitoke nje tuongee”

   “Nipo nje hapa getini niko na Detective Norman Cabrera… Tayari vijana washadhibiti kila kitu unaweza toka tu na nyumba hii kwakuwa umeelekeza ina tatizo basi ubalozi tutaipa taarifa serikali ya hapa tumegundua mambo ya hatari kwa usalama wetu ubalozi yakitokea hapa kwa bwana Alexis hivyo hataruhusiwa kuingia wala kutoa chochote mapak uchunguzi ukamilike…” Alimalizia katibu na kukata simu.

‘TSC’ akageuka lilipo sofa halafu akalipita kisha akaonyesha alama ya dole la kati tena akirudia kama anagusa gusa kitu hewani ilikuwa ishara ujumbe tena kwa aliyekuwa akiamini anamtizama muda huu na tabasamu alikukauka’

   “Siku zako na nyendo zako ni fupi sana… Nitakupata Alexis… Chukua picha zangu wasambazie wahuni wenzao uwaulize hii sura ya nigga ya nani?” Akaongea kimajigambo Agent Kai. 

   “Amerikani… Amerikani!” Sauti nzito ikitokea kwenye korido ilimstua akajua anaitwa yeye.

   “Naam!! Mmefika wakombozi…!” Akajibu akitabasamu tabasamu la dharau kisha akachungulia kwenye kizingiti akawaona wanajeshi wa Marekani wamesimama na silaha bunduki mikononi mwao, akajitokeza wakamuona haraka wakapiga saluti kuonyesha heshima yao kwao.

   “Pakueni kila kitu humu ndani na kuna mtu yumo humu akikisheni mnampata na msimuachie anatakiwa naye kufanyiwa mahojiano… Lakini kabla hamjaanza lolote fumueni makamera ya cctv na mifumo mingine ya mawasiliano maana kila kinachofanyika humu ndani kinaonekana mahala na mtu fulani ..!” Alitoa maelezo Agent Kai ‘The Sole Cat’ jamaa walimsikiliza na wakaongezeka wengine na wengine mpaka wakawa kama saba hivi akawapisha waendelee na kazi yeye akashuka ngazi kwa njia tofauti iliyompeleka mpaka kwenye lango la mbele ambalo tayari napo makamanda wa jeshi la Marekani walikuwepo wakapiga saluti walipomuona akawajibu na kutokomea nje, akatoka mpaka nje kabisa kote huko ulinzi ulikuwa umeimarishwa uzuri wa balozi za Marekani nchi yoyote wao wanakuwa na kikosi kikubwa cha wanajeshi na maafisa wengine lolote likitokea wanalidhibiti kama hivi.

Macho ya watu wanaofahamiana yalipoonana tu wote walisogeleana kwa kasi na kukumbatiana ‘TSC’ alikuwa kakutana na rafiki yake wa miaka kadhaa iliyopita wakiwa jeshini ingawa si katika kombania moja, umri wao ukiwa umepishana padogo sana mzungu huyu akiwa kamuacha Agent Kai miaka kama mitano tu lakini umri wala kuwa kombania tofauti haikuwafanya kutokuwa marafiki wa karibu miaka hiyo mpaka walipopoteana kila mmoja kwenda kwenye mambo tofauti na jeshi.

   “Za siku mkuu?” Akauliza Agent Kai baada ya kuachiana toka kwenye kumbatio.

  “Salama kabisa… Imekuwaje tena? Nimeshangaa kukuona ubalozini na mara kumbe upo katika mambo yako kunani tena?” Akauliza Katibu kisha wakashikana mikono kujiondoa mahala ambapo kuna watu wamewazunguka hili wengi wakiwa ni wanajeshi lakini na Norman pia alikuwepo, walijisogeza hatua kama kumi tokea eneo la geti lilipo wakawa wamefika barabarani kabisa.

   “Niko na DEA siko mwenyewe tu hapa lakini pia tuliingia kinyemela tukimshirikisha balozi wako tukiahidi kufika kuonana nanyi pale tutakapoona mazingira yanaruhusu kufanya hivyo.. Naomba utusamehe kwa hili sababu ni kosa kubwa sana tumefanya kiusalama..!” Akajibu kimaelezo TSC.

   “CIA na DEA mko hapa kwa operesheni inayohusu mihadarati?”

   “Ni kama hivyo ingawa sisi lengo lilikuwa ni kuwaondoa katika mateka maafisa wa DEA.. Kama utakuwa unamkumbuka mtu mmoja alikuwa akiitwa Sajenti Johnson Greg Ramautollaye kwa kifupisho na pia ikiwa jina lake la siri tulikuwa tukimuita ‘Jogre’, watu hawa wanashikwa mateka zaidi ya miaka saba sasa mpaka uchunguzi juu ya kupotea kwao ni kama ulishafungwa miaka mitano iliyopita..”

   “Jogre… Simkumbuki vizuri nafikiri haukuwa naye karibu sana au? Maana rafiki zako wengi nawajua mpaka leo”

   “Okay! Nimechanganya madawa… Huyu nilikuwa naye Navy Seals!” Akajibu Agent Kai.

Mwisho wa sehemu ya sitini na tatu (63)

Bahati ya mtende imemuangukia Agent Kai kuingia katika jengo  la Alexis Carlos Codrado, jengo likiwa mtaa mmoja na ubalozi wa Marekani, ubalozi wa nchi yao.

Anazingirwa na dalili kuonyesha ameingia mahala hatari kwa usalama wake lakini anatumia kete ya kuwa karibu na ubalozi wao kuomba msaada wa askari jeshi ambao muda wote uwa kamili kwa lolote nao wanafika wakiongozwa na katibu mwenyewe wa ubalozini wanafanikiwa kuwadhibiti wanaume wa kazi waliofika kwa maelekezo ya Alexis Carlos Codrado.

Nini kilifuata baada ya hapa?



Macho ya watu wanaofahamiana yalipoonana tu wote walisogeleana kwa kasi na kukumbatiana ‘TSC’ alikuwa kakutana na rafiki yake wa miaka kadhaa iliyopita wakiwa jeshini ingawa si katika kombania moja, umri wao ukiwa umepishana padogo sana mzungu huyu akiwa kamuacha Agent Kai miaka kama mitano tu lakini umri wala kuwa kombania tofauti haikuwafanya kutokuwa marafiki wa karibu miaka hiyo mpaka walipopoteana kila mmoja kwenda kwenye mambo tofauti na jeshi.

   “Za siku mkuu?” Akauliza Agent Kai baada ya kuachiana toka kwenye kumbatio.

  “Salama kabisa… Imekuwaje tena? Nimeshangaa kukuona ubalozini na mara kumbe upo katika mambo yako kunani tena?” Akauliza Katibu kisha wakashikana mikono kujiondoa mahala ambapo kuna watu wamewazunguka hili wengi wakiwa ni wanajeshi lakini na Norman pia alikuwepo, walijisogeza hatua kama kumi tokea eneo la geti lilipo wakawa wamefika barabarani kabisa.

   “Niko na DEA siko mwenyewe tu hapa lakini pia tuliingia kinyemela tukimshirikisha balozi wako tukiahidi kufika kuonana nanyi pale tutakapoona mazingira yanaruhusu kufanya hivyo.. Naomba utusamehe kwa hili sababu ni kosa kubwa sana tumefanya kiusalama..!” Akajibu kimaelezo TSC.

   “CIA na DEA mko hapa kwa operesheni inayohusu mihadarati?”

   “Ni kama hivyo ingawa sisi lengo lilikuwa ni kuwaondoa katika mateka maafisa wa DEA.. Kama utakuwa unamkumbuka mtu mmoja alikuwa akiitwa Sajenti Johnson Greg Ramautollaye kwa kifupisho na pia ikiwa jina lake la siri tulikuwa tukimuita ‘Jogre’, watu hawa wanashikwa mateka zaidi ya miaka saba sasa mpaka uchunguzi juu ya kupotea kwao ni kama ulishafungwa miaka mitano iliyopita..”

   “Jogre… Simkumbuki vizuri nafikiri haukuwa naye karibu sana au? Maana rafiki zako wengi nawajua mpaka leo”

   “Okay! Nimechanganya madawa… Huyu nilikuwa naye Navy Seals!” Akajibu Agent Kai.

ENDELEA NA NONDO NZITO…!

IJUMAA, MCHANA 

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Wanashikiliwa mateka na Bwana Alexis?” Akahoji katibu wakiwa wanaangaliana na Agent Kai.

   “Kwa muoneakano ulivyo pamoja na hisia za kiufundi itakuwa wanashikiliwa na genge la The Red Jaguar la mexico lakini genge hili limesimika na kukita mizizi yake katika nchi kuliko hata walivyosimika kwenye nchi yao ya Mexico… Wasiwasi wetu na hisia zetu zimetufanya tutake kumchunguza huyu mtu mwenye nyumba hii sababu kama nilivyokwisha kukwambia awali kesi ya uchunguzi wa kupotea kwa watu hao miaka saba iliyopita ilifungwa miaka mitano iliyopita ikihisiwa Jogre na wenzake wamefariki kwa kuuliwa na wliowateka… Wiki moja iliyopita nikiwa nimetoka kumaliza likizo ya miezi mitatu ya fungate la ndoa yangu nikakuta barua pepe ya kimchoro ikiwa na maelekezo ya mtu aliyeandika kutaka msaada wangu yeye bado anaishi, mtu huyo ni Jogre alituma barua pepe kupitia kwenye simu ya mtu ambaye baadaye tulikuja kujua anapatikana sana eneo hili la Guatemala ni mwanamke”

   “Je mshamuona huyo mwanamke?”

   “Hapana bado tunamsaka hatuna hakika wapi tutampata ndani ya GTL hii… Shida ni kuu pia hatuna picha yake wala jina lake kamili hivyo tunamsaka kwa kutumia plan c ya kiintelejensia nafikiri nikisema hivi unafahamu nini namaanisha”

   “Yaah! Nafahamu hilo…. Lakini umesema mna namba yake, vipi haiwezi kutumika kwenye kujua jina lake?”

   “Ni rahisis sana kujua watu wajanja wajanja uwa hawatumii laini walizosajili kwa majina yao kamili kama ilivyo katika vitambulisho vyao pamoja na passport uwa na walakini sana.. Jina la kusajili ametumia Valentina Aurelia Moschi ikiwa imesajiliwa hapa hapa GTL”

   “Alexis ameingiaje? Au kuwa kwake ndugu na Fernandes wa TRJ kumemponza?”

   “Shamba la Tajumulco analolimiliki mtu huyu kwa kilimo cha kahawa ndipo barua pepe niliyotumia mtumaji wakati anaituma kwa njia ya simu aliituma kutokea hapo.. Na ..!!” Alinyamaza kwakuwa mwanamke mmoja mzungu wa kilatini aliletwa mbele yao akiwa kafungwa mikono kwa nyuma, alikuwa amevaa suruali ya trucksuit ya kitambaa rangi nyeusi na juu jezi ya wacheza basketball ya timu ya Milwaukee Bucks ya ligi ya mpira wa kikapu ya NBA, Marekani. Waliokuwa wakimsogeza hadi pale kwa kumuamrisha atembee kwenda walipo ‘TSC’ na katibu wa ubalozi walikuwa ni wanajeshi wa kike wawili walipofika karibu wote wakapiga saluti kwa pamoja ikajibiwa na mabwana hawa.

   “Huyu mwanamke ndiyo mtu pekee tuliyemkuta ndani nyumba nzima ya bwana Alexis..”Akaongea mwanadada mmoja aliyesimama karibu na Katibu wa ubalozini.

   “Safi.. Unaitwa nani dada?” Akaongea kushukuru Agent Kai kisha akamuuliza kwa kilatino mwanadada mrembo mrefu mwenye umbo zuri la kuvutia nywele nyeusi na sura ya kuvutia akionyesha kama si mwanamitindo basi ama anavutiwa na kuwa mwanamitindo na stahili ya maisha yao.

  “Angelica… Angelica Linares” Akajibu akitetemeka sana.

  “Kwanini ulikimbia varandani ulipokuwa ukiangalia luninga?… Ukiwai kuizima na kisha kutoweka” Agent Kai akamuuliza tena.

  “Bwana wangu alinitumia meseji kuwa nyumba imevamiwa na mtu asiyemjua hivyo akaniomba nielekee chumbani kwetu kujificha”Akajibu Angelica akiwatizama kwa zamu wanaume waliosimama mbele yake.

  “Bwana wako ni Alexis?” Akauliza Katibu.

  “Ndiyo!.. Mimi ni mchumba wake..!”

  “Simu yako unayo hapo?”’TSC’ akamuuliza

  “Wameichukua wadada hawa..!” Akajibu na kusindikiza neno lake kwa kidole kuwaonyeshea wadada waliomleta hapa kisha kurudi nyuma kusimama hatua kama tano kuacha Kai na boss wao kuongea na mwanamke waliyemtoa ndani ya mjengo.

   “Naombeni simu yake… Mchukueni huyu mkamuweke kwenye gari niliyokuja nayo iko maegeshoni ubalozini lakini simu naomba nikabidhiwe sasa… Shemeji yetu usiwe na wasi ongozana na walinzi wako watakupeleka kwenye gari muda si mrefu nami nitafika nikiwa na mwenzangu hapo kisha nitakuja tuondoke mahala salama…!” Akaongea Agent Kai akiwa amenyoosha mkono wake mbele kuomba apewe simu ya mwanadada huyu mrembo haswa wa kilatini mwenye uzuri wa kipekee mtu anayeitwa Alexis Carlos alikuwa amefanya chaguzi la mwanamke mrembo sana watoto wa mjini wanasema kiwango cha SGR.

   “Salama?! Mahala salama? Kuna mahala salama zaidi ya hapa kwa bwana wangu?” Akauliza mwanadada huyu akiwa kayakaza macho yake makubwa ya kurembuka kumtizama Agent Kai, yaani alijitahidi kukunja sura lakini ndiyo kwanza alionekana kama anaongeza madoido ya uzuri mpaka katibu alitizama kwa kasi watu wote waliopo pale kisha akameza mate.

   ‘Duh! Mtoto kama huyu hivi mzee kama mimi nikimpata si ananirudisha ujanani… Natamani nimwambie Kai asiondoke naye nibaki naye… Sasa namwambiaje?’ Aliwaza Katibu wa ubalozi kisha akajilazimisha kuangalia pembeni isije akamstua mkuu wa usalama wa maungo yake akaleta mushkeri kwa chuchu dodo zilizokuwa zinaonekana zimeisimamisha jezi ya basketball ya Milwaukee Bucks. Kama ujuavyo jezi za mchezo huu uwa za mtindo wa kuacha makwapa yaonekane (kawoshi).

   “Haukuwa mahala salama kama mwenyewe unavyohisi kuwa ulikuwa salama…. Je unafikiri tungekukuta huko na huyo bwana wako halafu yuko na walinzi wake wangeanza kutushambulia nasi tungejibu mashambulizi unafikiri asingetokea mtu wa kukudhuru kwa vyovyote ingekuwa si hatari ambayo ingeharibu usalama unaosema?”akauliza Agent Kai kumuuliza mwanadada mrembo Angelica.

   “Kwani Alexis amefanyaje?”Binti naye akahoji huku karibu watu wote wakiangalia inapoanzia barabara ya Zone Eleven inayoingia huu mtaa, kulikuwa na gari tatu za polisi zikiwa zimeongozana.

   “Katibu! Samahani naomba uongee nao wewe hao wanaokuja… Mimi hawatakiwi kuongea nami wala kunijua mimi ni nani, hivyo naondoka nikiongozana na Angelica, naomba na nyie kina dada msiongozane nasi wanaweza leta swali vichwani mwao endeleeni kujifanya mnaelekezana jambo na katibu… Pia naamini katibu utajua cha kuwaambia lolote lile” Aliongea Agent Kai kwa kasi kisha akamshika mkono mwanadada mrembo Angelica ambaye alisita kushikwa mkono akausogeza pembeni kuonyesha hataki kuongozana na Agent Kai.

   “Tafadhali usilete ubishi naomba ufuate nachotaka lasivyo nina uwezo wa kufanya jambo ambalo hutarajii bila kujali lolote” Agent Kai akamuonya na mara Norman akaonekana kwa mbele yao akiondoka kuelekea jengo la ubalozini huku akijitahidi kukandamiza kofia yake ya kapero kichwani mwake maaskari wanaokuja wakiwa kwenye magari wasimuone vizuri.

   “Sikujui tatizo kaka… Nina haki zangu za msingi kukataa kuchukuliwa na wewe pia si vizuri mimi kuwekwa chini ya ulinzi na wewe mwanaume wakati askari wa kike wapo hapa..” Akaongea dada yule akiwa ameongea pointi mpaka ikamfanya Agent Kai ageuke nyuma kuwangalia wanajeshi wa kike ambao bado walikuwa pembeni ya Katibu wakiwaangalia wao pia wakiangalia msafara unaokuja kwa kasi.

   “Mmoja atusindikize mpaka ubalozini amuongoze mrembo..” Akaongea Agent Kai na bila kuchelewa askari jeshi mmoja wa kike alipoangaliwa tu na Katibu wake akafanya kile alichosema ‘TSC’, gari za maaskari polisi zilifika karibu nao zikaenda kupaki pembeni upande wa pili.

Agent Kai kabla maaskari polisi wale hawajashuka kwenye magari yao yeye alikuwa ametanguliwa mbele nyuma wakifuata Angelica na askari jeshi wa kimarekani, uzuri eneo hili lote lilikuwa na wanajeshi wa Marekani wametapakaa baada ya kazi ya kumsaidia Agent Kai kutoka salama ndani ya mjengo wa mdogo wake na Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’.

   *****  *****  *****

IJUMAA, ALASIRI

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Ciudad De Guatemala mtaa uliopo eneo la Chinautla zinakopatikana ofisi za wizara ya usalama muda huu wa alasiri mara nyingi umkuta mkuu muhusika wa ofisi hii waziri wa usalama Bwana Rafael Ceni amemaliza nusu ya kazi kama si kazi zote za siku hiyo ambazo zinatakiwa kupitiwa na yeye ukiacha naibu wake au katibu wa wizara, lakini ijumaa hii hakuwa amepitia faili lolote kati ya mafaili zaidi ya kumi aliyowekewa mezani na masekretari wake na hata maombi mbalimbali yaliyoandikwa katika mfumo wa vimemo na barua hakuwa amepitia mheshimiwa huyu, muda mwingi alikuwa akiongea ana simu kwa mtindo wa bandika bandua katika simu zake tatu moja ya mezani ya kiofisi na zingine mbili zake za mkononi.

Aliwaomba wahudumu wake wote wasimpigie simu kuomba kuwa kuna mgeni anahitaji kuongea naye ana kwa ana, alitoa amri akifika na kujitambulisha yeye ni nani? Basi ajulishwe kwa simu na kisha yeye kama ataona umuhimu wa kuongea naye ataruhusu kuongea naye kusikiliza shida hiyo.

   “….Feca!...”Simu yake ya mkononi aina ya Tecno Camon i2x moja ya simu bora sana toka kampuni ya utengenezaji simu ya Tecno iliyopo Hong Kong, simu ambayo anaruhusu kupigiwa na namba chache sana ikiwa yeye hajataka umpigie hata ukipewa namba yake kwa mara ya kwanza na ukapiga huwezi kuipata hewani iliita kwa haraka akaipokea na kuongea.

   “Mnanichanganya sana mheshimiwa.. Nashindwa kuamini kama mipango chini yako haiendi sawa wakati una kila kitu cha kuweza kufanya kila kitu kikaenda utakavyo kikaenda nitakavyo kikaenda tutakavyo, niambie unakwama wapi? Una watu wa kazi walio chini yako kiserikali na pia unao walio chini ya watu wangu” Feca brigedia mfukuzwa wa jeshi la wananchi la Mexico moja kwa moja hakwenda kwenye salamu alienda kwenye lawama na kufanya moyo wa mpokeaji simu kuongeza uchungu mwingine akabaki anakunja uso zaidi ya alivyoukunja wakati anapokea simu na si kama anamchukia aliyempigia la hashah! Alikuwa ameudhiwa na taarifa alizopokea dakika arobaini tu zilizopita akiwa kapigiwa simu na mdogo wake huyu aliyempigia sasa.

   “Brigedia! Nashindwa kuelewa wapi tunakwama… Kila kitu naandaa katika ubora wa hali ya juu lakini mitego haiendi sawa hii inanishangaza ni kwa mara ya kwanza napatwa na jaribio la hatari ambayo naiona inakwenda kutokea lakini nashindwa idhibiti” Akajibu mheshimiwa waziri Ceni.

   “Ceni! Mtu ambaye nimerushiwa video zake zilizochukuliwa na cctv kamera ya nyumbani kwa Alexis alipoingia ni mtu ambaye nimestuka sana kuona yuko Guatemala… Ametustua genge zima maafisa wangu wote wa juu wamestuka… Kwanza si afisa wa DEA bado yuko CIA kitengo cha siri cha Special Activities Division (SAD) kilichomo ndani ya shirika hilo la kijasusi ni mtu king’ang’anizi asiyetaka kushindwa si mtu wa kuja kwenye operesheni za kusaka madawa ya kulevya au kuzuia njia za uzalishaji madawa ya kulevya pamoja na njia zake za usafirishaji, huyo mtu amefika Guatemala kwa kazi ya kutuangamiza sisi binafsi hii ni vita Ceni ni vita baina yetu na Marekani sasa sababu mtu huyo anapoonekana nchi yoyote basi anakuwa ametumwa na Rais wa Marekani au makamu wake wa Rais… Swali gumu tunalojiuliza sasa ameombwa na OCLA msaada yeye kama yeye binafsi? au ameombwa na DEA ikiwa OCLA wameomba msaada kwao? Au serikali ya Marekani imeamua kuvalia njuga suala la kutuharibia?” Feca akaongea tena kwa kirefu kidogo akapumzika na kumeza mate huko alipo.

   “Mtu huyu wakati anakuja hapa nchini amekuja kwa ndege ya shirika la ndege la Air Canada akitokea Washington DC alipo kimakazi na kiofisi ambapo anahudumu katika ofisi ya makamu wa Rais wa Marekani anaongoza kikosi cha kijasusi cha pale kinachohusika na mambo yote ya kijasusi chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa ofisi ya makamu wa Rais… Lakini pia kabla ya yeye kuja hapa nchini juzi kuna watu wawili tunawatilia mashaka nao waliingia wakija kwa treni ya umeme kutokea nchini Canada, taarifa za kufika kwao nimezipokea muda si mrefu toka kwa mkurugenzi wa uhamiaji anasema watu hao ni wa kufuatiliwa sana sababu majina yao na hati zao za kusafiria zinaonyesha ni raia wa Canada lakini inahisiwa nao wamo katika watu walio katika walakini… Nimetumiwa picha zao na muda si mrefu nimezituma kwa watu wetu wa Marekani na Canada kuona kama ni raia wa Marekani au Canada kweli au lah!, nasubiria majibu nafikiri muda si mrefu nitapata majibu kama na wao ni kama Agent Kai Hamis…” Akatoa maelezo marefu ya kiufafanuzi kwa boss wake hili asionekane kama alilala tu hafuatilii lolote katika kusaka ukweli wowote juu ya maswahibu wanayoyaona lakini kama maji kuzuia na tenga ubaya wanauhisi lakini kuzuia kwa haraka imekuwa ugumu kidogo.

   “Vipi na kuhusu kikosi cha ulinzi cha mdogo wangu?” Akauliza swali Feca kwa sauti ya ghafla kana kwamba anamuuliza mwanae kwanini hajaenda shule.

   “Mchumba wa Alexis yuko mikononi mwa hayawani mwanaharamu Agent Kai mahala alipo bado hatujajua msako unaendelea… Watu watano waliuliwa na vikosi vya kijeshi vya Marekani kutoka ubalozini ambapo ubalozi wao kuwa karibu Agent Kai alitumia nafasi hiyo kuomba msaada alipoona tayari kikosi cha Alexis kinakaribia kumtia mikononi kama video ulizotumiwa zinavyoonyesha kijana mmoja ni majeruhi alipigwa risasi na Agent Kai imempasua jicho lote lakini haikuzama ndani ya kichwa imeondoa eneo la kingo ya jicho kisha ikaenda pembeni huyu yuko hospitali nafanya mpango nimtoroshe au nimmalizie pale hospitali… Kuhusu wengine tisa nimezuia mtu yoyote kuwahoji kwa kisingizio tusubiri Rais afike pilika pilika zikipungua mkuu wa upelelezi ataenda kuwahoji akiwa na IGP, nimewambia lazima wasingizie kuwa umakini unahitajika katika kujua kwanini ubalozi wa Marekani umefanya mashambulizi katika nyumba ya Alexis? Na kwanini katibu wa ubalozi wa Marekani anasingizia kiwepesi tu kuwa intelejensia yao iliwafahamisha kuwa kuna genge la madawa ya kulevya linaitumia nyumba ya Alex kwa mazoezi ya uhalifu wao nimeandika barua kwa balozi kuwa maelezo ya katibu wake hayajaniridhisha bado..” Akajibu kirefu tena mheshimiwa Ceni.

   “Akikisha watu hao usiku wa leo ionekane wametoroka au kutoroshwa na wenzao.. Wanaweza kuwa ngazi ingine ya kutuharibia… Eeeh! Niambie mmefikia wapi mpango wa kuzuia flashdisk kumfikia mheshimiwa Rais? Maana Rais yuko angani anarudi nchini mwenu..!” Swali lingine likatandikwa kwenda mheshimiwa Ceni.

   “Ikulu leo imejaa vijana wetu wa GIS na wengine tulionao katika kikosi cha kijasusi cha Rais cha TACCG nimewaambia wana fursa mbili wakimuona Kamanda Muniain au Norman anataka kuingia viwanja vya ikulu ni kumteka au kumuua tu kisha kama atauliwa asachiwe haraka ushahidi uchukuliwe” Akajibu mheshimiwa Rafael Ceni.

Mwisho wa sehemu ya sitini na nne (64)

Mambo yanazidi kuwa bam bam kama tumechanganya damu, Guatemala inaanza kutetema mwendo wa tetema.

‘TSC’ anafanikiwa kuondoka nyumbani kwa Alexis akiwa na mchumba wa bwana mapesa huyu mdogo wake na Feca, askari polisi wanafika eneo la tukio wanapewa maelezo na katibu ambayo hata kama hayakuwalizisha sana lakini iliwabidi wakubali tu, wanafanikiwa kuwachukua watu waliokabidhiwa kwao na katibu wa ubalozi pia wanaondoka na maiti zilizoingia katika mfumo wa kubadilika toka uzima hadi ufu kutokana na mashambulizi ya kujibishana silaha na vikosi vya kijeshi vya ubalozi wa Marekani nchini Guatemala.

Feca na Ceni nao hali ya wasiwasi imeanza kuwapata wakihisi hatari inayokuja, hali imezidi kuwa tete baada ya kugundua mtu wanayepambana naye ni nani, wakiwa hawajui haswa ni nini kilichofanya mpaka aje Guatemala.

Nini kitafuata?





   “Mchumba wa Alexis yuko mikononi mwa hayawani mwanaharamu Agent Kai mahala alipo bado hatujajua msako unaendelea… Watu watano waliuliwa na vikosi vya kijeshi vya Marekani kutoka ubalozini ambapo ubalozi wao kuwa karibu Agent Kai alitumia nafasi hiyo kuomba msaada alipoona tayari kikosi cha Alexis kinakaribia kumtia mikononi kama video ulizotumiwa zinavyoonyesha kijana mmoja ni majeruhi alipigwa risasi na Agent Kai imempasua jicho lote lakini haikuzama ndani ya kichwa imeondoa eneo la kingo ya jicho kisha ikaenda pembeni huyu yuko hospitali nafanya mpango nimtoroshe au nimmalizie pale hospitali… Kuhusu wengine tisa nimezuia mtu yoyote kuwahoji kwa kisingizio tusubiri Rais afike pilika pilika zikipungua mkuu wa upelelezi ataenda kuwahoji akiwa na IGP, nimewambia lazima wasingizie kuwa umakini unahitajika katika kujua kwanini ubalozi wa Marekani umefanya mashambulizi katika nyumba ya Alexis? Na kwanini katibu wa ubalozi wa Marekani anasingizia kiwepesi tu kuwa intelejensia yao iliwafahamisha kuwa kuna genge la madawa ya kulevya linaitumia nyumba ya Alex kwa mazoezi ya uhalifu wao nimeandika barua kwa balozi kuwa maelezo ya katibu wake hayajaniridhisha bado..” Akajibu kirefu tena mheshimiwa Ceni.

   “Akikisha watu hao usiku wa leo ionekane wametoroka au kutoroshwa na wenzao.. Wanaweza kuwa ngazi ingine ya kutuharibia… Eeeh! Niambie mmefikia wapi mpango wa kuzuia flashdisk kumfikia mheshimiwa Rais? Maana Rais yuko angani anarudi nchini mwenu..!” Swali lingine likatandikwa kwenda mheshimiwa Ceni.

   “Ikulu leo imejaa vijana wetu wa GIS na wengine tulionao katika kikosi cha kijasusi cha Rais cha TACCG nimewaambia wana fursa mbili wakimuona Kamanda Muniain au Norman anataka kuingia viwanja vya ikulu ni kumteka au kumuua tu kisha kama atauliwa asachiwe haraka ushahidi uchukuliwe” Akajibu mheshimiwa Rafael Ceni.

ENDELEA NA NONDO…!

IJUMAA, ALASIRI

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Mpango umekaa vizuri… Tunatakiwa kwa njia zote kutojiingiza katika mgogoro na Rais wa hapo.. Pia nitaongea na Koplo Zuantejo juu ya umuhimu wa wao kuwepo katika maeneo ya karibu na ikulu kwa msaada wa lolote ambalo litatokea”

   “Mimi pia nitakuwepo muda si mrefu nitaondoka hapa kwenda kusubiri ujio wa Rais lakini si kusubiri Rais nitakuwa makini kuzuia mbwa jike hawa kumpatia Rais hiyo flashdisk”

   “Vizuri sana… Acha niongee na Zuantejo kisha baadaye tutachekiana kwa lolote lile..”

Maongezi yao yaliishia hapa simu zikakatwa kwa pande zote kwa mara moja na ikawa kama kitu kilichopangwa alipoweka mezani tu ikaita tena na safari hii ikiwa na code namba za kutoka Marekani.

   “Shakur..!” Akaita baada ya kuipokea kisha kuiweka sikio lake la kulia..

   “Mheshimiwa.. Za muda mfupi uliopita?”

   “Nzuri kidogo… Lete habari?”

   “Majibu tayari… Mwenye asili ya uchotara ni Investigator January Joseph Miller na wa kizungu ni Special Agent Simone Silla huyu nimetumiwa majina yake hayo mawili tu… Wote ni majasusi wa Drug Enforcement Administration kifupi DEA, mara ya mwisho pasi zao kusafiria za ukweli zinaonyesha walisafiri kutoka Springfield,Virginia makao makuu ya DEA kuelekea Washington DC wakiwa na mkurugenzi wao wakaenda ofisi ya makamu wa Rais wa nchi hii Eisenhower walichofuata huko ndicho sikuweza kuambiwa ni nini? Lakini toka wafike Washington DC mpaka sasa haionyeshi kama walitoka tena kwenda sehemu ingine hivyo inamaanisha waliondoka Washington DC kwa majina tofauti na majina yao kuelekea Canada kisha ndipo wakaingia GTL” Akajibu kirefu mtu aliyeitwa Shakur.

   “Ahsante kwa majibu ya haraka Bwana Shakur… Nami acha niwataarifu wenzangu juu ya majibu haya mazuri… Mr. Muniain kafanya mambo ya ajabu sana katusogezea majanga makubwa sana tena bila kutushirikisha wizara, hatakiwi kuishi” Akaongea kwa jazba baada ya kuwa ameshukuru kwa aliyoyaita majibu mazuri kujua habari za kina Investigator Miller na S.A Silla.

  “Kupambana na watu kama hao wakiongozwa na huyo mtu anayeitwa Agent Kai inahitaji akili kubwa sana ikibidi msiruhusu kupambana nao ana kwa ana namaanisha hawafai kuwawinda heti muwateke muwaulize maswali wao kina nani? Hao ni kuwavizia na kuwaua tu..” Akatoa ushauri Shakur.

   “Ndicho kitu nilichopitisha kwa sasa… Toka asubuhi nimepokea simu mbalimbali za ushauri juu ya mtu huyu anayeonekana ndiyo kinara wa kikosi kilichofika hapa GTL huku kirusi Muniain na mwanae Norman wakiwapa msaada.. Naomba nikushukuru tena kwa kazi nzuri na ushauri nifanyaje na kuahidi kesho watu hawa kufika itakuwa ngumu sana, nitatumia akili zangu zote kuzuia flashdisk isimfikie Rais pia nitahakikisha na wao hawaendelei kupumua na kujaribu kutukosesha raha na amani ndani ya nchi yetu..!” Akaongea mheshimiwa waziri.

Waliagana wakikubaliana watatafutana kwa kazi nyingine zaidi pamoja na msaada wa kiushauri ambao kwa mheshimiwa waziri ndiyo kitu muhimu sana kutoka Shakur Armani mwanaume wa kizungu anayefanya kazi katika ofisi za CIA makao makuu Langley, Virginia akiwa katika kitengo kinachohusika na mambo ya Cyber Crime, ni mmoja wa watu ambao pamoja na viapo vya kazi walivyoapa juu ya kazi wazifanyazo unafiki ulikuwa wa grade A akiwasaliti waajiri wake kwa kutumia fursa aliyonayo kuwemo ndani ya shirika hili kubwa la kijasusi kudukua habari za watu wengine wanaohudumu katika shirika hili la kijasusi na mashirika mengine ya usalama wa Marekani yakiwemo yale ya ndani akitumia urafiki wake kwa watu wengi alionao huko kuharibia wengine kisiri kuuza ka makundi ya kigaidi na magenge mengi ya kihalifu yaliyopo nchi mbalimbali duniani (cheefu).

Waziri Ceni hakuona anatakiwa kuendelea kuwa ofisini muda huu huku pua zake zikinusa hatari inayomnyemelea yeye binafsi ingawa kiukweli hakuwa anajua katika flash aliyopewa Norman kuna habari gani ila hisia tu zilimzonga kuwa katika flash kuna hatari kubwa, yeye kama waziri hawezi kupambana na taasisi kuu ya Rais wan chi na hata kukimbia kwenda kujificha haitawezekana kwake kwa amri moja ya Rais hata wanaomsikiliza na kumuheshimu hawawezi zuia lolote.

Alifunga vitu vyake muhimu ikiwemo kompyuta yake mpakato yenye siri nyingi zinazomuhusu akamuita sekretari wake mkuu na kumpa taarifa yeye anaondoka kwenda ikulu ya Rais kwa ajili ya mapokezi ya mheshimiwa Rais.

   *****  *****  *****

CHIMALTENANGO, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Haikuwachukua muda mrefu toka barabara ya Zone 11 mtaa wa Calzada Aguillar Batres eneo la Galarias Del Sur kurudi mji wa Chimaltenango kwenye makazi na ofisi za muda za kikosi kinachoongozwa na Agent Kai chini ya mkufunzi Kamanda Muniain, Mercedes Benz 2010 ML300 CDI inayoendeshwa na Detective Norman ilifunga breki na hatua moja tu linapoanza geti linalozunguka nyumba kisha dreva akapiga honi stahili inayowajulisha walio ndani kuwa wao wamerudi.

Geti haikuchelewa likaja kufunguliwa Special Agent Silla, gari ikaingizwa ndani kwa mwendo wa taratibu iliposimama Agent Kai akashuka akiwa na kamtanguliza mwanadada mrembo wa haswa Miss Angelica mchumba wa bwana mkubwa Alexis Carlos Codrado mwenyewe akipendwa aitwe kompyuta na watu wake wanaomjua umafia wake wa sirisiri ukiiona sura yake kama hahusiki na mambo ambayo ukiyasikia yanafanywa na yeye.

   “Karibuni..” Akakaribisha S.A Silla macho kodo kwa mrembo ambaye alikuwa kakunja uso lakini uso ndiyo kwanza unahanikiza uzuri aliobarikiwa na Mungu huyu binti wa kilatini.

   “Huyu ni shemeji yetu kwa bwana mkubwa Alexis Carlos hivyo taratibu na macho hayo..” Akaongea lugha ya kiingereza kiutani Kai kumtania Silla na wote wawili kucheka kwa pamoja hali ya kuwa mwanadada Angelica hakuwa ameelewa zaidi ya kusikia tu, hakuwa anajua kiingereza kwa ufasaha, Norman akaja kujiunga nao wakaongozana kwa pamoja binti akiwekwa kati kuingia ndani ya nyumba.

Walikwenda sebuleni ambapo walimkuta Kamanda Muniain anaangalia luninga akiwa pamoja na Rebecca na Miller pia huku vicheko na stori vikiendelea.

   “Ooooh! Jamani! Mmekuja na malaika wa urembo… Karibu binti… Jiachie ujione kama upo nyumbani kwa raha zako” Akaongea kwa lugha ya kilatini akiwa kasimama toka sofani Rebecca Smith ambaye naye mashaallah ni mzuri kiasi ambacho mpaka TSC uwa anamtamani lakini kwa Miss Angelica ilikuwa ni moto fire!.

   “Angelica! Kwa leo utakuwepo hapa… Kuna masuala kidogo tunahitaji utusaidie kisha ya hapo utarejea kokote ulipopanga kuwa utaenda, unaweza ukaona ni kitu cha ajabu lakini si jambo la ajabu kwakuwa wewe unaweza kujua au kutojua kati ya mengi yanayofanywa na Mr. Alexis Carlos..!” Akaongea Agent Kai kisha akamuonyesha sofa ambalo anaweza kukaa mwanadada huyu asiyeacha kuumua mdomo wake kuonyesha aridhishwi na yeye kuwepo hapa.

Angelica alikaa na hata watu wengine nao walikaa kwenye masofa mbalimbali yaliyo hapa sebule nzuri ya kupumzika iliyopangiliwa fenicha zake kwa uzuri wa kuvutia mtu kupaona ni mahala bora kwa uwezo wake.

   “Vipi hali yako Kamanda Muniain?” Akauliza Agent Kai baada ya utulivu kuchukua nafasi yake na watu kuwa wanaangaliana tu kwa zamu kama wanatamani kusikia mwingine anaongea nini?.

   “Naendelea vizuri kwa kweli daktari alifika hapa muda si mrefu kabla wewe hujafika na kuniomba nianze kujinyoosha nyoosha viungo angalau kwa kutembea tembea humu ndani na hata huko mbele ya nyumba… Nimehadithiwa hali ilivyokuwa huko ulipotoka kwa waliokuwa wanafuatilia kupitia mtambo wenu wa mawasiliano, nashukuru umefanikiwa kurudi salama salimini ukiwa mzima wa afya kwa kweli huko makini na kazi na naamini huko walipo si TRJ wala vibaraka wao wana wasiwasi juu ya uwepo wako hapa GTL na usalama wa biashara zao za haramu pamoja na uhalifu wao wa kiwango kikubwa sana wa wananchi wetu” Akajibu kuhusu afya na kutoa maelezo marefu Kamanda Muniain.

   “Nimefurahi unaendelea vizuri Kamanda! Uwepo wako katika misheni hii unakutegemea kwa asilimia nyingi sana kwa pamoja naamini tutaweza kama tulivyowai kuweza mengi huko nyuma mara zote uovu hauwezi kusimama mahala pamoja na wema unaomtanguliza Mungu wetu mbele… Mashetani wako wengi sana tuna kikosi kidogo lakini kikosi kidogo si kigezo cha kusema hatuwezi kupambana na mashetani walio wengi… Tunakwenda futa ushetani unaoendelea ukanda huu kwa mpango madhubuti tunaoenda uandaa muda si mrefu..” Akitumia lugha ya kiingereza ambayo kwa sasa ilikuwa uhakika inaeleweka kwa watu wa kikosi chao chote ikwemo wa Guatemala wawili Norman na boss wake Muniain, aliongea akiwaangalia wote waliokuwemo mule kwa zamu sura yake ikibeba anayoyasema kwa uzito mkubwa.

   “Ndiyo boss! Mpango madhubuti utaenda dhibiti mbinu ovu zilizokwisha andaliwa kwa muda mrefu na kuumiza vijana wengi wa ukanda huu nakuamini sana boss wangu” Rebecca Smith aliongea akiwa amekaa sofa moja na mwanadada Angelica aliyekuwa akisikia lakini akinasa (kuelewa) machache sana kutokana hana uzoefu wa  katika utumiaji lugha ya kiingereza hivyo anajua maneno machache katika maana na mengine anayasikia tu akiwa hajui nini kinamaanishwa.

  “Leo Rais wa nchi ambaye ndiyo mtu mzito zaidi katika nchi anarudi … Kamanda Muniain kuna mpango gani unaoweza kutuelekeza? kabla mimi sijasema tunatakiwa tupite wapi na wapi kumaliza misheni hii katika hali ya ushindi wa wema na haki”Akauliza Agent Kai akimuuliza Kamanda Muniain.

   “Unajua mpaka sasa hivi nimeshangazwa na jambo moja kutoka kwenu.. Kwanini mnaogopa kuangalia kilichomo katika flashdisk aliyoiandaa mkurugenzi marehemu Funtes Jota Mariapan, nimemuuliza Norman na tukajadili hili haoni kama kuna umuhimu wa kuangalia kilichomo… Jibu lake si la mtu aliye jasusi akiwa amepitia mafunzo ya ujasusi kwa ufasaha” Aliongea akitabasamu mzee Kamanda Muniain akanyamaza kila mmoja akafanya kama afanyavyo yeye kumuangalia Norman ambaye naye aliunda tabasamu kavu akajikohoza kidogo.

   “Mzee umejisahau kuwa wewe ndiyo uliniomba kuwa tutaenda kuiangalizia kwa mtu aliyeandaliwa flash hiyo… Flash ina maelekezo kuwa ina password ambazo anazijua Rais mwenyewe kwakuwa marehemu Mr. Mariapan na Rais wana utaratibu wa kujuzana habari mbalimbali kwa mtindo wa flash hivyo walikubaliana kutumia password ambayo mimi na wewe tukisema tuifungue tuangalie tunashindwa bila wao… Hivi mkuu wangu kwa unavyonifahamu unafikiri naweza kukaa na kitu nikikiangalia tu bila kujua kina nini ndani?” Alijibu kiufafanuzi Detective Norman akimalizia kwa swali kwa boss wake ambaye alionekana kuinamisha kichwa chini tu akikuna kipara chake ambacho kinakosa nywele hadi katikati ya utosi wake kiking’aa sana.

   “Niliamini uwepo wa wataalamu hawa unaweza kuleta ufumbuzi wa suala hili maana wana uwezo mkubwa wa teknolojia wa mambo makubwa na madogo” Akajibu Muniain akitabasamu macho yakizunguka kuwaangalia vijana wake kwa zamu.

   “Ni kweli tungeweza fanya hivyo kama Norman angeomba tufanye hivyo sisi pia tuliuliza kwanini mpaka leo flashdisk hakijulikani kilichomo maana kwa upande wangu na naamini hata kwa wenzangu tunajua laiti kama Norman angeweza kuvamiwa na wahuni wa waziri wa usalama au TRJ humu kwake na kuweza kuibiwa au kupokwa flash kwa kulazimishwa au hata kwa mtu kuichukua akiwa yeye hayupo humu lazima asingeweza kujua kuna kipi mule pengine angetakiwa kukifanyia kazi ama kukiwakilisha kwa mdomo yeye mwenyewe kwa mheshimiwa Rais… Hivyo tuliomba tuiangalie siku ya kwanza tu baada ya kujua ni jambo muhimu sana na linalowaumiza sana vichwa timu ulanguzi wa mihadarati, nilihoji ni jambo gani mkurugenzi wa ‘CLEI’ ameandaa na akaona ni muhimu moja kwa moja kufikishiwa Rais wa nchi… Majibu yalinifanya mimi binafsi nifuate utaratibu mliouandaa ambao tumeukuta hatukupenda kuingia ndani ya mipaka yenu ni hilo mzee kwa upande wetu” ‘TSC’ akafafanua upande wao wageni wa nchi hii.

   “Naomba nami niongezee kuwa tunaweza kutumia ufundi na ujuzi wetu kuiangalia hiyo flash lakini tukakuta ukishaifungua tu haiwezekani kurudi katika hali yake… Naunga mkono apelekewe mwenyewe sisi tufanye ambavyo viko mezani mwetu kama hivyo vitaongezeka vitakuja kwa maelekezo yake na pengine inaweza kuzidisha uamnifu uliopo kati yenu na Rais” Akaeleza Investigator Miller.

   “Mheshimiwa Rais anaingia saa ngapi?” Agent Kai akauliza swali likiwalenga Norman na mzee Muniain.

   “Saa kumi kamili jioni ndiyo atafika uwanja wa ndege wa kimataifa wa hapa Guatemala…!” Akajibu Kamanda Muniain.

   “Mlishapanga juu ya kwenda kumpatia hiyo flash?” Akauliza tena Agent Kai.

   “Tulipanga mimi na kijana wangu siku zilizopita hata bila nyie kuingia hapa GTL kuwa tutaenda kumkabidhi sisi wenyewe huku tukimpa na maelekezo juu ya mauaji ya marehemu Mariapan ilikuwaje aliuliwa huku akimpatia Norman flashdisk… Hii inatokana kuwa siku ya pili tu ya kifo cha mkurugenzi Mariapan alinipigia kuniuliza kulikoni yeye kutokuwepo kwake nchini mtu wetu wa karibu anauliwa na watu wasiojulikana, pia alitaka maelezo nahisi kuna nini nyuma yake kinachojificha katika mauaji yale… Niliweza kumueleza kifupi nachowaza pia nikasema ameacha flash ambayo anataka tumkabaidhi yeye mheshimiwa Rais… Hivyo makubaliano yetu baina yetu na yeye ni kumpatia hiyo flash tukiwa wote wawili ikulu pale pale katika hafla ya kurejea kwake salama itakayofanyika kuanzia saa kumi na mbili na nusu” Akajibu mzee kamanda Muniain.

  “Ulinzi wa Rais unaundwa na taasisi yake ikishirikisha vyombo vyote vya usalama wa nchi kuanzia jeshi la wananchi mpaka askari polisi na vyombo vyao vyote vya kiintelejensia, nafikiri vyombo vilivyo chini ya wizara ya usalama ambayo tunamuhusisha moja kwa moja waziri wa wizara hii na genge la TRJ kwa maelezo aliyotupa Kamishina Salivita Muniero, vyombo vinaweza kutumika katika kuwazuia nyinyi kumsogelea Rais kwa namna yoyote tusiyoweza sisi kuifahamu kwa njiia zetu.. Hivyo basi nina wazo ambalo likipita litaweza fanya kukwepa mambo ambayo naweza kuhisi yanaweza kutumika kuwazuia nyie kuonana na mheshimiwa” Agent Kai alieleza kirefu katika yale aliyokuwa akihisi katika halmashauri ya ubongo wake iliyo vizuri sana katika mambo ya sanaa inayoitwa na wajuzi wa mambo ya kijasusi kuwa ni ‘sanaa ya gizani’ lakini si giza lile la sanaa ya kichawi (washirikina laanakum) hii ikimaanishwa ni sanaa ya mambo yaliyojificha chini ya wengine kisha wewe unatakiwa kuyajua kwa kuyachimba iwe kwa siri au kwa nguvu utaalamu ukihitajika zaidi.

Mwisho wa sehemu ya sitini na tano (65)

Mheshimiwa Waziri wa usalama wa nchi kichwa kikimuuma upande mmoja kama kimejigawa katikati, upande akiwaza nini kitatokea Rais akikabidhiwa flashdisk ambayo pamoja na kuwa hana hakika kuna nini mule? Hofu yake kuu ikiwa uovu wake kuwa umeanikwa mule. Upande wa pili akifikiria upande wa aliopewa heshima na nguvu ambayo kwa mwingine hawezi kuiona ila yeye aliithamini na kuona bila nguvu aliyopewa upande huo yeye Ceni si lolote chochote, upande huo ni bwana mkubwa ‘Kingpin’ Feca na TRJ yake itakuwaje akionekana mzembe wa kazi?

Nako timu pinzani! Wakiwa wameongeza watu wanaowashikilia kutoka upande wanaouona ni upande pinzani, wao pia wako katika mpango mkakati wanafanya nini kusogea mbele?

Kwa mengi zaidi fanya kusogea mbele kuyajua mengi na mengi zaidi.



MWISHO WA SEASON 1, ENDELEA KUFUATILIA SEASON 2





0 comments:

Post a Comment

Blog