Search This Blog

Thursday 23 March 2023

ZAWADI TOKA IKULU - 5

 

Simulizi : Zawadi Toka Ikulu

Sehemu Ya : Tano (5)




Jesca alianza kufuatilia kwa karibu huku akiwauliza wafanyakazi aliokuwa akiwaona wako bize kila kukicha wanashughulikia harusi yake nayeye mhusika hakuwa anajua lolote juu ya chochote kinachoendelea. Siku zilizidi kutoweka na kuisogelea siku iliyokuwa imepangwa harusi hii waliitambua wazazi wa pande zote mbili na Von Gao pekee ambaye ni muoaji naweza kusema ilikuwa ni siri kubwa ndani ya familia ya Manguli na pia katika familia ya Mzee Gao ni siri iliyofumbwa ndani lakini nje ilizidi kuenea kwani viongozi wengi waliarikwa na wakajiandaa kuhudhuria harusi hii ya binti wa rais.


Mzee Manguli alikuwa akiamini na kushikilia misimamo yake katu huwa hayumbishwi na binadamu wachache na huwa anaamini kuwa kamwe hatashindwa na kitu katika maisha yake. Aliamua kuisimamia harusi ya mwanae kimyakimya maana hakuhitaji majadiliano tena na mwanae maana aliona binti yake amekuwa akimchanganya na misimamo yake hasi juu ya penzi alilolijenga yeye na leo analikana tena.


Mzee manguli hakuwa tayari kuaibika na kuwa gumzo mtaani kwa kuendeshwa na binti yake. Suluhu ilikuwa ni kumuoza kwa Von Gao awe anampenda au hampendi kutokana na wao kukubaliana na kuamua kupokea mahali.


Baba ndiye kichwa cha familia kamwe hatoendeshwa na mtoto daima hiyo ilikuwa ni misimamo ya Mze Manguli mtoto hupewa haki na akiichezea humtafuna mpaka kufa, Jesca alipewa nafasi ya kuchagua na akamchagua Von Gao familia zilikaa na kukubaliana hivyo hakuna nafasi ya pili tena yakuchagua maana kama alilamba galasa basi ajiandae kuushindwa mchezo. Manguli hakuteteleka aliendelea na shughuli zake huku akiiandaa harusi ya binti yake.


*********************************


Nilikuwa bado niko mikononi mwa Kimbo, nilikuwa hoi bin taabani maumivu kila sehemu vimbe na mipasuko mwilini ilinikosesha raha, bado mikono yangu imefungwa na minyororo ya vyuma vizito nilipokuwa nimefichwa sikuwa napajua. Kimbo alikuwa bado ananishikilia na hatukuwa na mazungumzo mazuri ingawa alikuwa mtu mwenye huruma lakini hakutaka kuwa karibu na mimi.


Sikujua chochote kinachoendelea duniani zaidi ya kuwaza ninajinasua vipi katika matatizo. Kimbo alikuwa akibadilisha sigara na chupa za pombe kali kama vile konyagi na Value sigara alikuwa akiteketeza pakiti kwa pakiti na ndani palinuka moshi sigara na kusababisha ndani panuke harufu ya sigara na bangi mchanganyiko na kuifanya hali ya hewa ya pale ndani kuwa siyo nzuri kiafya.


Kimbo alikuwa kalewa chakali nilianza kumuuliza kwa upole.


“kimbo nimekukosea nini mpaka unifanyie hivi ndugu yangu?”


“huna kosa mdogo wangu na hapa natamani sana kukuachia ila najua maisha yangu yatakuwa mashakani, Mimi ni mfu tayari”


“hapana siwezi kukushitaki na sitasema popote maana utakuwa umeokoa maisha yangu”


“nikweli lakini familia ya Gao lazima itaniangamiza haitaniacha hivihivi”


“kwanini wakuangamize?”


“ninasiri kubwa ndani ya familia hiyo na wamejichanganya kunipa kazi hii nashukuru kwa kuwa hawakujua”


Mazungumzo yaliendelea kiurafiki na hatimaye Kimbo alienieleza mengi aliyotendewa na familia ya Gao, ikiwemo kutumikishwa kama mbwa tangu Gao akiwa waziri mkuu na hata alipositaafu amekuwa akimtumia kimbo kwa manufaa yake binafsi.


Alikuwa akilia kwa uchungu alisema katika hisitoria yake hana ndugu wala wazazi na hajui yeye ni nani na alitoka wapi anachokikumbuka amepata fahamu katika maisha yake akiwa kwenye kambi za jeshi na amehamishwa kambi kadhaa ambako kufikia hapo alipo ameishi maisha ya kijeshi. Alisema amezungushwa kwenye mataifa mbali mbali na vyuo kadhaa vya kivita kufunzwa mbinu za kijeshi na umahiri katika vita na mapambano.


Alilia kwa uchungu “kazi yangu ni kuua, sijawahi kufanya kazi nyingine katika maisha yangu mimi nimekuwa na kazi moja tu kuondoa roho za watu tangu nikiwa na umri wa miaka 18 na sasa nakaribia hamsini sina familia nina maanisha sina mke wala mtoto kwasababu siruhisiwi kuoa, kazi yangu hainiruhusu. Jamae wewe ni rafiki yangu kamwe sitakuuwa ila naomba uyaheshimu maamzi yangu nimekupenda sana na nitahakikisha nakusaidia umekuwa rafiki wa kweli kwangu.


Baada ya maongezi ya muda mrefu kunasimu ilipigwa Kimbo alipokea bila shaka alikuwa ni Von Gao aliweka sauti kubwa na hivyo nilisikia kila kilichozungumzwa.


“Kimbo habari” ni sauti ya mzee Gao


“salama mzee Gao”


“vipi nasikia uko naye huyo kijana uliyeambiwa kumkamata na Von?”


“ndiyo nikonaye na yuko salama”


“nasikia umegoma kumuua, kwanini?”


“kwasababu hana kosa na pia nahitaji pesa zangu”


“sasa unapaswa kumuua haraka sana maana lolote linaweza kutokea, magazeti yanahoji sana juu ya kupotea kwake na pia kunawatu wamechoma jengo la kampuni yake na akionekana yuko hai huenda siri ikafichuka na mimi siko tayari kuishusha hadhi yangu kwasababu ya mpuuzi mmoja, hakikisha anakufa mapema iwezekanavyo”


“Mzee Gao mimi nikotayari kumuua kwa sharti moja tu, nahitaji malipo yangu haraka sana yote najua naidai familia yako zaidi ya milioni 80 fanyeni kulipa pesa yangu haraka la sivyo hakuna anayejua huyu kijana alipo mkipuuza kufikia leo jioni nitamuachia na kumpa siri zenu zote na kama mnavyojua ni mpenzi wa mtoto wa rais na mtoto wa rais hataki kuolewa na Von hii ni nafasi ya mwisho mkichelewa ataichafua mitaa na haitakalika maana ataeleza kila kitu Von atakosa mke na ataishia jera Manguli mnamjua, na niko tayari kumlinda mpaka hatua ya mwisho”


“usifanye hivyo Kimbo pesa yako ipo nitakulipa hakikisha anakufa”


“Hatokufa bila kuuona muamala wangu ndani ya simu yangu simu inihakikishie akaunti yangu ya benki imewekewa pesa.”


“Kwahiyo unamaanisha hautomuua mpaka nilipe?”


“Bila shaka nakupa masaa sita huna jipya maana hujui nilipomuweka na kamwe hautajua na nzuri zaidi unanijua nikidhamilia kitu hatima yake ni nini”


Mzee Gao sasa maji yalikuwa shingoni kwani maisha ya Kimbo anayajua yeye mwenyewe na tabia zake hazitafsiriki na mbaya zaidi akichoka kuendeshwa basi kachoka hakujua hatima yake ni nini.


Majibizano yao hayakuwa mazuri kati yao kwani yalilenga kifo changu na sikuyafurahia hata kidogo nilikuwa nikisikiliza nilivyokuwa nikipigwa mnada na kufanywa kama bidhaa ya mabadilishano. Kimbo alikuwa ananisisitizia hatoniua lakini akili yake ilikuwa haiaminiki. Maana alikuwa akibadirika kila baada ya dakika moja. Huwezi amini nilikuwa nikitetemeka kwa hofu nilijua ghadhabu zikimpanda huenda akaniua na hakuna atakae niona na sasa naanza kuyaamini maneno ya Von alinionya na nikapuuza na sasa nayaona majibu yake. Kimbo alikuwa akipandwa hasira alikuwa akifyatua risas hovyo hovyo kwa hasira hali hiyo ilikuwa ikinitia hofu.


*******


Ni siku moja kabla ya Harusi taarifa inamfikia Jesca kuwa anatakiwa kufunga ndoa siku inayofuata na alikuwa chini ya ulinzi mkali hakuna kutoka kwenda popote maandalizi yalikuwa yamekamilika na wageni walikuwa wameesha wasili Ikulu na wengine wakizidi kuwasasili kwaajili ya kuishuhudia ndoa ya kifahari ya mtoto wa rais na kijana toka familia ya kitajiri ya waziri mkuu wa zamani Von Gao.


Kilio na majuto ndiyo yalizidi kumtesa Jesca alijilaumu kwanini asingeliondoka zamani pale nyumbani huenda haya yote yasingemtokea. Alijuta sana kuona akimsaliti mpenzi wake aliyempenda kwa dhati na sasa analazimishwa kuolewa na mtu asiye mpenda na chakushangaza zaidi ulinzi uliimalishwa kuanzia chumbani mpaka mlangoni. Jesca aliomba akutane na wazazi wake baada ya kugundua kuwa nilazima ndoa yake ifungwe kesho yake yaani siku iliyofuata, wafanyakazi wake walikutana na baba yake na kuzungumza naye alikubali kukutana na mwanae.


Familia ilikutana ni mama Jesca, Jesca na mzee Manguli wote walikuwa kimya kulikuwa na sintofahamu Jesca alikuwa akiwalaumu wazazi wake kwa hatua walizozichukua bila kumshirikisha. Nikweli alikubaliana na posa ya Von Gao pamoja na kuruhusu wazazi wake kuchukua mahali Jesca alitamani pia asikilizwe kwa mara nyingine juu ya maamzi yake.


Najua hakuya kubali maamzi ya kubadilishwa kwa tarehe ya harusi bila yeye kushirikishwa.


“Baba kwanini tarehe ya harusi imebadilishwa kutoka mwaka kesho mpaka kufanyika kesho, na kwanini mmenificha mpaka mama ananiambia leo tena baada ya kushitushwa na ugeni uliokuwa ukiingia hapa leo asubuhi sikujua kumbe watu tayari wamealikwa kwenye harusi. Na mmewezaje kuandaa ndoa yangu bila mimi mhusika kunijuza au mnaolewa nyinyi?”


Binti yangu umekuwa na kiburi hushikiki husikilizi na ndiyo maana unasababisha niwe na maamzi magumu juu yako. Tulipanga uolewe mwaka kesho lakini kiburi chako na dharau vimesababisha tubadili uamzi ndoa yako itafungwa kesho saa kumi na moja jioni na sherehe itafanyika usiku huohuo hapa nyumbani na utaondoka na mmeo kesho yake asubuhi”


“Ni sawa kwa mtazamo wenu ila hamnitendei haki binti yenu, hivi mmewahi kujiuliza kwanini nilikubali kuolewa na Von Gao na baadae kubatilisha uamzi wangu?”


“Hatujui!, na tunajua haunasababu za msingi zakutushawishi ”


“Nikweli lakini kumbukeni ninayeolewa ni mimi na kama maisha yakiharibika yanaharibika yakwangu, kwasasa mmedhamilia na mnaamini mmeniweza maana nikiwaangalia hawa wageni hapa wote wamekuja kushuhudia harusi yangu, ni watu na heshima zao na wameacha shughuli zao, siwezi kuwaaibisha nitafunga hii ndoa lakini kunamakosa mmeyafanya naamini huenda yataigharimu hii familia.”


“Jesca sijawahi tishwa na mtoto na kamwe statishwa na mtoto ataendelea kuwa mtoto tu ndani ya himaya yangu, kamwe hatoweza kuchezea akili yangu.”


“nikweli ila kumbukeni taarifa ni kitu mhimu, na huenda kunificha hiliswala mmesababisha kukosa taarifa za msingi sana kwa kifupi mimi ni mjamzito nina mimba ya miezi minne nina mimba ya Jamae.”


“sijakusikia vizuri unasema je?”


Hali iligeuka na kuwa tofauti katikati ya mazungumzo Mzee Manguli alikasirika na kujikuta akimshushia kipigo kizito binti yake. Hali ilikuwa mbaya na kila kitu kiliharibika mama Jesca alikuwa akitetemeka kwa uoga na mzee alikuwa kafula kwa hasira. Jesca alikuwa chini akigaagaa chini kwa maumivu huku mama Jesca akiumizwa na kilichokuwa kikifanyika. Hali inaonekana kuwa tete ndani ya familia ya mzee Manguli , wakati huo wageni walikuwa wamejaa nyumbani kwa mzee Manguli na walikuwa wakiendelea kuingia.


Upande wangu na Mr. Kimbo, Kimbo hakufikia makubaliano na familia ya Gao na sasa aliamua kunifungulia na kuniingiza kwenye gari usiku ule alienda kunishusha nje ya Jengo la ofisi zangu aliponitoa siku kadhaa zilizopita.


Nilishuka pale nikiwa na kitambaa usoni nilikifungua kitambaa na kuangaza huku na kule kulikuwa hakuna jengo tena ofisini kwangu isipokuwa palikuwa pameteketea kwa moto nyumba ilionekana kama gofu, nilishangaa sana na kuumia mno moyoni mwangu nilijivuta na kumfikia mlinzi mmoja aliyekuwa karibu niliongea naye na bahati nzuri alinitambua.


Alishangazwa sana na hali yangu kwani ananijua vizuri. Mlinzi yule alianza kunihadithia kilichotokea lakini aliniambia amesoma taarifa zagu gazetini nimepotea alinieleza kuwa ofisi zangu zilichomwa moto muda murefu kidogo na hakuna mfanya kazi amewahi kufika hapa tena. Nilimuomba anisaidie simu yake nilijaribu kumpigia Dominic maana ndiye nilimuachia ofisi yangu baada ya kupewa simu nilijaribu lakini hakupatikana. Huyu alikuwa ni mlinzi wa jilani yangu kulingana na hali niliyokuwa nayo alinitafutia usafiri nikapelekwa hospitali ya Mwananchi iliyopo Makoroboi ili nipatiwe huduma ya haraka. Nilifikishwa pale na kuanza kupewa huduma za haraka. Nilifanikiwa kurejea uraiani salama na sasa nilikuwa napokea matibabu baada ya mateso na kifungo cha zaidi ya wiki mbili.


Asubuhi kulikucha na nilikuwa najisikia vizuri angalau kwa kiasi fulani ni baada ya kuhudumiwa vizuri na kupewa chakula, madaktari waliniuliza umepatwa na nini wakitaka kujua kilichonitokea niliwajibu nilitekwa na watu nisiowajua na nimefanikiwa kuwakimbia jana usiku nikiwa salama.


Madaktari walinipa pole nikawashukuru kwa upole sana lakini ukweli niliujua mimi,kimawazo sikuwa vizuri maana nilitaka nikahakikishe kama kweli niliyoyaona jana juu ya kuungua kwa jengo la ofisi za Himaya ni kweli au si kweli picha ya jana usiku ulidhidi kuisumbua akri yangu.


Maana iliniuma sana kila nilipofikilia juu ya maisha yangu, sikuwa nataka kuvumilia baada tu ya kuhudumiwa ile asubuhi nafanikiwa kutoroka hosipital na kwenda kuhakikisha kilichotokea nilitoroka kupitia zilipo ofsi za tanesco jilani na maktaba ya mkoa wa Mwanza niliifuata barabara ya Kenyata na kwenda kuingia kwenye barabara ya Karuta, nikweli nilipoinua tu macho pindi nakata kona, majibu yalikuwa ni yale yale hakukuwa na jengo tena ila gofu.




Ofsi zangu zilikuwa zimeteketea kwa moto na mbaya zaidi Domi hajulikani alipo nahii inanipa picha ya wazi kuwa huenda Domi amehusika kwa asilimia miamoja na uharibifu huu. Iliniuma sana nilianza kufikilia nini kinaendelea kwenye maisha yangu niliumia sana na niligundua chanzo yalikuwa ni mahusiano ya kimapenzi kati yangu na Jesca.


Kuna vitu vinauma katika maisha ila hakuna kitu kinauma kama kurudishwa nyuma wakati ulikuwa umepiga hatua kubwa na leo binadamu wenye ubinafsi na hila wanapambana mpaka wanafanikiwa kunirudisha nyuma na kunifanya nianze mwanzo. Nilikuwa naliangalia lile jengo kwa huruma na upole lakini sina jinsi imeesha tokea sinauwezo wa kulirudisha kama mwanzo ingawa iliniuma mno. Nilikuwa nimeichezea bahati pekee niliyopewa na baba yangu nimeharibu pesa yote na leo sina urithi tena. Nilikuwa najilaumu sana na kujiona mjinga huku nikijihoji maswali magumu ambayo hata mimi sikuwa na majibu.


Ni nani kanifirisi huenda ni Von au Domi ndiye kahusika na hili au wote wamekula njama. Kiakili sikuwa sawa nilikuwa nateseka sana maana maisha ninayoenda kuyaanza sasa yalikuwa magumu kuliko kawaida. Jamani hakuna kitu kigumu kukiamini kama surprise ya kufirisika nawezakusema maisha yangu sasa yalikuwa ni vita tu kila kukicha kuna vita kuu mpya ya kupambana juu ya maisha yangu.


Niliondoka eneo lile huku siamini nini kimetokea lakini macho yangu hayakunidanganya nikweli Himaya haipo tena na sijui hali ya kiwanda changu lakini kiuhalisia nilikuwa unajionyesha wazi maana taarifa zote za fedha hazikuwepo ni ishara iliyoonesha kuwa nimefirisika.


***************************


Kimbo alikuwa jijini Dar na safari yake inaelekea nyumbani kwa Gao, lengo na madhumni ya Kimbo ni kuhakikisha analipwa pesa yake yote. Anafunguliwa geti na kuingia ndani na anamuagiza mlinzi wa nyumba ile kuwa anashida na mzee Gao hivyo aende akamuite.


Anafunguliwa na kuingia hadi ndani huku akijipujisha sebleni bila wasiwasi maana hakuwa mgeni kwenye nyumba ile kila mtu alimfahamu aliyekuwa wakwanza kufika pale sebuleni alikuwa Von Gao.


“Kimbo nadhani umekamilisha nilichokutuma na ndiyo maana uko hapa?”


“Hapana! Jamae nimemuachia huru na mjiandae kuunguzwa na magazeti na vyombo vingine vya habari kama radio na televisisheni, muda wowote mtateketea kama zilivyoteketea ofisi za Himaya ChapaKazi. Ujio wangu hapa Dar ni kuhakikisha nalipwa stahiki zangu zote bila kukopwa wala kupigwa tarehe, nimerekodi sauti na simu zenu zote za amri na hata maelezo mliyonipa, hivyo hamnitishi chochote”


“Lakini hayakuwa makubaliano yetu Kimbo”


“Ninajua hakuna makubaliano hayo ila pia ninajua hatukukubaliana kudhulumiana hivyo ni ngumu sana kunidhulumu”


“kimbo rudi haraka ukamuuwe huyo kijana nitakulipa pesa unayotaka tafadhali Kimbo”


“Huna pesa wewe mbwa huenda angeongea mfuga mbwa ningemuelewa, kwanza yuko wapi mzee Gao maana huyo ndo mfuga mbwa?”


“Niko hapa kimbo, tafadhali mwanangu ulichokifanya si kitu cha busara hata kidogo, huoni kama umenitia kitanzi shingoni, huyo kijana hukupaswa kumuachia sasa inakuwaje umemuacha wakati huo ukijua mimi stapona iwapo tu atazungumza na vyombo vya habari?”


“Hayo utayajua mwenyewe na naondoka, subiri jipu litumbuke”


Familia ya Gao ilibaki ndani ya mawazo mazito sikujua waliwaza nini yeye na mwanaye.


Kimbo anaondoka na gari lake lakini aliamini wazi ni lazima hatokuwa salama maana anaijua vizuri akili ya Gao, nikweli alikuwa akifatiliwa na gari lingine nyuma yake chakufanya aliendesha gari kwa kasi ya ajabu lakini waliomfuata pia walimfuata kwa kasi zaidi alichokifanya ni kupaki gari na kuamua kutembea kwa miguu.


Hakuna mtu hatari kama Kimbo unapotaka kumjaribu, waliokuwa wakimfuata ni baadhi ya maofsa wenzake watatu walioagizwa kumuua kabla hajaliacha jiji basi walianza kukimbizana barabarani na mwisho aliiingia kwenye nyumba moja na kuchomoa bastora yake iliyokuwa kiunoni, huwa hafanyikosa alinyanyua mkono alitumia risasi tatu tu kama ilivyokuwa idadi yao wote walikuwa chini na walisahaulika.


Kimbo aliendelea kutokomea kusipojulikana kwa miguu na baadae anafanikiwa kumteka kijana mwenye pikipiki aina ya Honda XXL anachukua pikipiki ile na kutokomea kwa kasi ya ajabu.


***************************


Maandalizi ya harusi nyumbani kwa rais yalikuwa yakiendelea kama kawaida bi harusi alikuwa akirembwa na upande wa Von Gao pia alikuwa akijiandaa wakiisubiri hiyo mida ya kufunga ndoa kama ilivyokuwa imepangwa. Matangazo mubashara ya televisheni na radio wakihojiwa watu maarufu waliokuwa wakiisubiri harusi hiyo toka asubuhi matangazo yalikuwa yakirushwa na vituo mbalimbali vya radio na televisheni.


Watu mashuhuri wakiwemo viongozi, wasanii wa mziki vichekesho na wafanya biashara maarufu walikuwa wameesha jaa ndani ya ukumbi ulioandaliwa maalumu kwaajili ya sherehe hiyo.


Upande wa Jesca harusi hii haikuwepo kichwani kwake lakini inambidi afanye hivyo ili kumlidhisha baba yake maana hakukuwa na jinsi, alitamani kutoroka lakini asingeweza kwani ulinzi uliimalishwa vya kutosha hakukuwa hata na upenyo maana agizo la kulindwa lilitekelezwa ipaswavyo na walinzi wa ikulu na hata kubadilishiwa walinzi na kuletwa walinzi wapya mara kwa mara ili asiwe na ushawishi wala mazoea kwao.


Wakati huu malikia wangu alikuwa kwenye chumba chake maalumu akiandaliwa kwaajili ya ndoa ambayo hakuilidhia ila kwa matakwa ya wazazi. Pamoja na marembo yote uso wake ulionekana umeng’aa lakini hudhuni machoni haikukatika.


Wakati maandalizi ya harusi yakiendelea na sasa Jesca hakuwa na jeuri tena habari zinazagaa mitandaoni juu ya kuibuka kwangu vichwa vya habari vilianza kugonga vyombo vya habari kwa kasi huku habari za dharula zikishika kasi mitandaoni “Jamae Justine aibuka akiwa hai” mtandao mmoja uliandika mtandao mwingie ukiandika “aliyekuwa tajiri mdogo zaidi Tanzania bado yu hai” chombo kingine kilitangaza “Jamae arejea uraiani” ni tarifa zilizowashitua wengi siku hiyo na siwezi kushangaa kwani muda mfupi uliopita nilijikuta nazingirwa na lundo la waandishi wa habari nikiwa kituo cha baladala ziendazo Igoma barabara ya Pamba wakitaka kujua nini kimetokea.


Walinihoji maswali mengi lakini kwa kuhofia usalama wangu sikuweza kueleza chochote, zaidi nilikuwa nikikataa kulizungumzia swala hilo na waliponibana zaidi niliwambia nikweli nilitekwa ila watekaji siwajui na mpaka nimefanikiwa kuwatoroka sikujua kwanini waliniteka.


Maelezo yangu yalihitajika polisi mara tu walipofika muda mfupi tu baada ya kusikia taarifa zangu ili kuwasaidia kumtafuta mtekaji nilipofika kituo cha polisi Pamba naamini sikupindisha maneno nilizungumza kama nilivyowaambia wandishi wa habari.


Naweza kusema siku hii iliibua maswali mengi yaliyolala. Mitandao ya kijamii ililipuka na kusababisha kila mtu ahoji juu ya kupotea kwangu na kuibuka tena nikiwa hai pia kuna maswala mawili yalihusishwa moja kuungua kwa makao makuu ya Himaya Chapakazi, kupotea kwa Mkurugenzi msaidizi wa himaya na kupotea kwangu wote katika mazingira ya kutatanisha.


Kila ukisoma kurasa za mitandao na majadiliano ya dharula redioni unagundua wazi kuwa nilikuwa ni mtu mashuhuli sana katika taifa hili na nikazidi kuwa mashuhuri ndani ya muda mfupi.


Jamae Justine alikuwa akigonga vichwa vya habari na kuwa kiini cha majadiliano katika vituo mbali mbali vya redio na televishemi. Kila mtu alikuwa na swali lake na hata mtazamo wake kuna wengine walisema ninatafuta umaarufu, wengine walisema huenda ni janja ya kukwepa kodi, wengine walisema kuna kitu nyuma ya pazia.


Kwa wakati huu nilikuwa nawaza mengi sana juu ya maisha yangu lakini kubwa kuliko ni hatima ya maisha yangu, ukweli niliujua kuwa Kimbo kaniacha salama lakini familia ya Gao haijaniacha huenda wakatuma watu wengine kuja kuniua. Nilikuwa naishi kwa tahadhali mno na sikutaka kwenda nyumbani kwangu maana nilihofia maisha yangu.


Nilikuwa nimejificha kwenye nyumba ya kulala wageni moja huko Mecco iliyofahamika kwa jina la Promise ni uswahilini niliamini hakuna mtu angejua nilipo, sikutaka kwenda nyumbani kwangu siku hiyo maana lolote lingetokea nilikuwa makini kuliko kawaida.


Kwa wakati huu sikupaswa kumuamini yeyote, siyo polisi wala ndugu maana nilihofia kuuwawa muda wowote na nilikuwa naogopa kuliko kawaida. Maisha yangu ndiyo kitu cha thamani kuliko chochote, najua familia ya Gao hainihitaji niendeleee kuishi katika ulimwengu huu, wanatamani ningekuwa nimeesha angamia na nafsi zao zingesha tulia.


Mwili wangu haukuwa vizuri sana kiafya maana ni siku moja tu tangu nimeachiwa toka mafichoni na sasa ulikuwa ni wasaa wakujipumzisha nilipitiwa na usingizi na kupumzika.


**********************


Von anamuita baba yake baada ya kuona taarifa ikirushwa kwenye Tv baba anakuja mbiyo mbiyo anafika na kusimama wote wakiwa na hofu waliamini kuwa kila kitu kimeharibika walijua nitaongea yote yaliyotokea, kila mtu alikuwa makini mno kujua nitajibu nini juu ya maswali niliyoulizwa na wandishi wa habari.


Mzee Gao alikuwa anahofu kubwa kwani aliamini huenda nitamtaja mbele ya vyombo vya habari baada ya kujiridhisha kuwa sijawataja wote walipumua kwa nguvu huku wakimshukuru Mungu. Gao hakuishia hapo alipiga simu mkoani Mwanza kujua kama kuna taarifa zozote zinazomhusu yeye kwa kamanda wa polisi,polisi walisema hapana tarifa zinazomhusu, alitupa simu kwenye kochi huku akipiga ishara ya msalaba. Baada ya zoezi hilo sasa alianza kuzungumza na mwanae.


“Huyu hawezi kusema najua anaogopa kuuawa, ila tunachopaswa kufanya ni kumuondoa duniani kabla ndoa yako haijafungwa leo jioni saa hivi ni saa sita mchana natamani ikifika saa kumi tuwe tumepata taarifa ya kifo chake”


“Sasa tunawezaje kulikamilisha hili baba na Kimbo kagoma kumuua.”


“upande wa Kimbo ondoa shaka maana hapa nasubiri taarifa ya kifo chake nimemtuma Chaha na Grey wanatimu nzuri naamini hatotoboa ni ule muda aliotoka hapa ametoka na wasindikizaji huenda alishakufa kitambo nasubiri simu tu yakuthibitisha.”


“Kuhusu Jamae nilazima afe leo, maana Jesca akijua yupo hai atakutoroka na kwenda kuishi kwake au kukuletea zengwe na ukumbuke tulichomfanyia huyu jamaa Jesca akijua na Manguli akijua basi ni maumivu, sitakubali kukuona ukiaibika mwanangu kipenzi ningali hai, Kimbo atakufa leo na Jamae nahakikisha hatoifikisha saa kumi ya leo jioni”


“lakini tunapaswa kuwa makini baba hii ni sikendo iwapo watu watagundua itakuwaje?”


“Mzee Gao ni nembo ya taifa hili hakuna moto wakunishinda kuuzima katika maisha yangu amini usiamini haya mazoezi yatakamilika na hakuna atakayehoji”


Mazungumzo yaliendelea na makubaliano yakafikiwa kati ya baba na mwana na Sapy Goro nateuliwa kuwa kijana mwingine aliyetumwa kuja kuangamiza maisha yangu, Goro ni mtu mwingine hatari kuwahi kutokea duniani ni jambazi la kujitegemea ni mtu hatari ambaye hukodiwa kwa malipo ya papo hapo. Walikamilisha miamara yote ya malipo na lilibaki kuwa jukumu la Goro mwenyewe.


Wakati huo Kimbo alifunga safari kurudi Mwanza na lengo lake ilikuwa ni kunishinikiza kuvieleza vyombo vya habari juu ya familia ya Gao kuhusika na matukio yote yaliyotokea. Safari kutoka uwanja wa ndege ilianza saa sita kamili ni watu wawili ndani ya ndege waliokaa viti jilani hawakufahamiana ni Kimbo na Gao wanasafiri mpaka Mwanza mmoja akienda kutafuta njia za kumuokoa Jamae na mwingine akiagizwa kwenda kumuangamiza.


Walishuka uwanja wa ndege wa jijini mwanza na kila mmoja aliendelea na safari zake hakuna aliyeshughulika na mwenzake. Kimbo alikuwa anajua nilipo alikua moja kwa moja mpaka Mecco nilipokuwa ujio wake ulinishangaza lakini aliniambia mimi najua uliopo muda wote maana kuna kifaa nimekiweka mwilini kwako ambacho wewe huwezi kukiona. Kimbo alifika na tukazungumza juu ya hatima yangu.


“Jamae familia ya Gao wanataka kukuangamiza ninajua maana wamenitumia watu kutaka kuniua tayari nimeesha waua walikuwa watatu.”


“unasema wewe leo umeesha ua watu watatu?”


“Ndiyo nimewaua asubuhi na nafikiri walikuwa ni usalama wa taifa walitumwa na Mzee Gao kuniuwa na usipokuwa makini huenda wapo njiani wanakuja kwako pia” maelezo ya Kimbo yananifanya nitetemeke, kwanza nilishangazwa na kauli yake yakuniambia kaua watu watatu lakini nikimuangalia hana hata jeraha na aliongea anacheka niliona ni kitu cha ajabu mno.


“Kimbo watatuua hawa, hawana utani ujue”


“Hawawezi mimi nawajua kuliko unavyowajua wewe usiogope”


“Sasa tunafanyaje?”


“Unachotakiwa nikuwatafuta waaandishi wa habari na kueleza kila kitu sasa hivi kama tutakufa tufe taifa limeesha ujua ukweli”


“Hapana Kimbo nitafanya yote ila hilo siwezi nitakufa ndugu yangu siwezi kabisa na siko tayari kufa kizembe”


“Nibora useme huenda uakajiokoa kuliko kukaa kimya maaana unasakwa kama swala aliyekatiza kariakoo sasa endelea kuficha siri utaangamia”


“Kimbo Gao na mwanae ni watu wabaya mno”


“Ni bora ungelilitambua hili mwaka kesho ila kwakuwa umelijua hili leo ni bora nikuongezee na hili lingine leo ni harusi ya Von Gao na Jesca saa kumi na moja jioni”


“unasemaje?”


“kama ulivyosikia na itafungwa saa kumi na moja jioni” ni miongoni mwa habari zilizouchoma moyo wangu na kunifanya nikose raha


“Tafuta waandishi sasa hivi tukamilishe hili swala”


Nilianza kutafuta namba za waandishi wa habari lakini sikufanikiwa kuwapata namba zote nilizokuwa nazo hazikunipa msaada tuliamua kwenda moja kwa moja kwenye kituo cha televisheni cha Nyota Tv hapa jijini Mwanza kilichopo Ilemela mtaa wa Iloganzala. Nikiwa na Kimbo tuliingia na kujiandaa kuanza kurekodi kipindi baada ya kuwaeleza hali ilivyo walihitaji maelezo yetu. Kabla sijafanya lolote kituo cha televisheni kilivamiwa na nje kulisikika milioa ya risasi ni baina ya asikari walinzi wa zamu wa eneo lile na mtu mmoja ambaye hatukumfahamu kwa wakati huo. Kulingana na ushupavu na uzoefu wake aliwazidi askari na hapo ndipo Kimbo alipojitoa mhanga kupambana naye kwa bastora yake lakini hakufanikiwa.


Alikuwa ni Sapy Goro Jambazi lililokubuhu, majibizano ya risasi ya dakika kumi bila kupumzika yanasaidi kuacha upenyo na tunafanikiwa kutoroka eneo lile mimi na Kimbo lakini wafanya kazi kadhaa wa kituo hicho cha televisheni walikuwa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa na baadhi majeraha makubwa yaliyohatarisha maisha yao.


“nilikwambia sasa unapaswa kulikamilisha hili swala mapema zaidi bila kufanya hivyo tutakufa mimi na wewe mapema tu tena bila msaada”


“sasa tunafanyaje ili tulikamilishe”


“ Subiri, Nina namba za Masafa Fm jaribu kuzipiga zikiita tu ujue tumewini maana wale wanakiherehere mno na hiki ndicho kituo ambacho hata rais anapenda kukisikiliza wakisikia jambo wanataka kuruka Live”


“Nilipozijaribu kupiga zile namba zikawa ziko bize sikuweza kuwapata”


Tuliendelea kukimbia mtaani tusijue tunaelekea wapi Goro alikuwa anakuja kwa kasi na Gari lake, maisha yangu yalikuwa hatarini Kimbo alikuwa ananieleza kuwa aliponikamata kipindi kile cha nyuma aliniwekea kifaa mwilini mwangu ambacho kinampa taarifa popote nilipo kupitia simu yake na ndiyo maana amejua mpaka nyumba nilipo hivyo hajapata taabu kunipata.


Tulikuwa tumechoka saana kutoka maeneo ya Iloganzara zilipo Ofisi za Nyota televisheni Mpaka maeneo ya Mwaloni Kirumba siyo mwendo wa kubeza lakini tulitumia muda mfupi sana kwa miguu huku tukipita njia za uchochoro kumkwepa Goro na kuupigania uhai wetu.


Goro bado anatusaka kila kona ya jiji naamini lengo lake ilikuwa ni kunipoteza mimi duniani maana hiyo ndiyo ilikuwa kazi pekee aliyopewa. Kimbo ananikumbusha kupiga tena ile namba ya Masafa Fm. Na safari hii ninafanikiwa kuipata na bahati nzuri kilikuwa ni kipindi cha kutoa maoni kuhusiana na maswala ya kisiasa kilikuwa kikiruka live simu yangu inafanikiwa kupokelewa na mtangazaji, niliingia moja kwa moja kwenye hoja bila kujua walichokuwa wakikizungumzia.


“naona tuna msikilizaji kutoka Mwaza karibu uko live sasa” mtangazaji alinikaribisha


“Jamani ninasakwa kuuawa na anaenitafuta ni Mzee Gao na Mwanae Von naitwa Jamae Justine naomba mtunze Jina hili nikifa leo ama kesho wahusika ni familia ya mzee Gao.”


“unaweza kutuambia chanzo ni nini Jamae?” mtangazaji alihoji na simu yangu ilikuwa ikisikika live.


“Chanzo ni ndoa….….” Kabla sijamaliza kusema kilisikika kishindo na nilipogeuka Kimbo alikuwa chini na nilipotaka kunyanyuka bastora ya Goro ilikuwa kichwani kwangu simu ilikuwa sikioni kwangu ikiendelea kuongea na sauti ya mtangazaj iikiita “hallo! haloooo!”…….


Hesabu ziligoma na kujikuta naishiwa nguvu kiuhalisia tu kabla hujafanya kitu huwa tunajitathimini kwanza, kwa tathimini yangu nagundua kuwa hata kwa dawa nisingeweza kupambana na Goro, ushahidi ni baadhi ya matukio aliyoyapiga ndani ya muda mfupi mbele yangu na kilichonivunja nguvu ni tukio la kumuuwa Kimbo mbele yangu na niliamini hakuna kidume wakumuua Kimbo kutokana na ninavyomfahamu Kimbo lakini leo naamini kuwa umdhaniaye kumbe siye.


Kuna miujiza hutokea katika maisha ya watu ila hakuna muujiza utakaoushangaza ulimwengu wa kuwa mimi ipo siku nitapambana na Goro ni wazi kuwa haiwezekani. Bastora yake ilikuwa bado iko kichwani kwangu huku nikiutazama mwili wa Kimbo ukiwa pale chini umelala ukisubiri kuzikwa na kwakuonesha dharau Goro anachukua simu mfukoni kwake na kuanza kumpigia mwajiri wake bila hata wasiwasi.


“eeeh! Mzee Gao nakusikia , Ndiyo Kimbo nimemuuwa na tayari Jamae nimemuweka chini yaulinzi hapa hana jeuri, siwezi kumuacha hai nadhani ukikata simu tu nae atakata roho mzee wangu”


“ahsante sana Goro Kimbo kawaua vijana wangu watatu leo asubuhi na mbaya zaidi alitaka kukuua na wewe?”


“Ndiyo ningezembea angekuwa ameesha niondoa dunuiani ni mtu hatari sana hata hivi nashukuru Mungu kwa kumuwahi tu, hapa tulipo tunasakwa maana nimepiga tukio la maana pale Nyota Tv, nimeteketeza watu bila huruma sababu ya hawa wana haramu.”


“Goro umefanya nini sasa!, taarifa zimezagaa kila kona na inasemekana umechelewa kupiga tukio na tayari Masafa FM wameesha zipata taarifa si unajua walivyo wambea na wanavyopendwa sasa mitandao yote ya kijamii imejaa picha za marehemu na majeruhi, naomba ujifiche uwezavyo usikamatwe na ukikamatwa kwa bahati mbaya usithubutu kunitaja maana ni mimi pekee ninayeweza kukutoa na si mtu mwingine na Hao wapuuzi ngoja niwatengenezee zengwe la kunisafisha, hakikisha unawaua asibaki hata mmoja.”


“sawa boss”


Alitoa simu sikioni na kuiweka mfukoni lilikuwa ni kosa kubwa kwake nilijipindua na ule mkono ulioshika bastora, nilitumia kila juhudi kuukunja lakini ulinishinda ilikuwa ni vita ya nguvu kati yetu. Lengo langu halikuwa kumuua bali kumnyanya ile siraha.


Yalikuwa ni mapambano ya wanaume shupavu vidume wa shoka tukiwania siraha moja na yalikuwa mapambano mazito huku zikitumika nguvu zaidi kuliko akili maana tuligombea kuokoa maisha yetu. Hakuna aliyekubali kulegea maana alijua huenda ungekuwa ndiyo mwisho wake. Nafanikiwa kuruka na kuubana mkono wake kwa kuukunjia katikati ya goti la mguu natua chini na kuubana vizuri huku bastora ikielekezwa juu mkono wake shingo yake niliikandamiza kwa mguu wangu wa pili.


Kwa akili ya kawaida mtu wa kawaida ambaye hana mafunzo maarumu kitendo hiki kingemvunja mkono au angehisi maumivu makali na hata kuangua kilio, lakini hali ikawa tofauti kwa Goro hakujali wala kushituka alijipindua kiustadi na kuuchomoa mkono wake miguuni kwangu huku akinishushia bonge ya ngumi sikioni kwangu.


Nilishituka na kuirukia shingo yake kabla hajaiweka sawa siraha yake nikaibana kwa mkono kama kabali hakuweza kupumua vizuri na nilijua hapa nitakuwa nimemuweza kabisa. Goro alipumua kwa taabu sana lakini ndani ya dakika chache alijichomoa na kuielekeza bastora yake kwenye paji langu la uso huku akiikoki na kutoa agizo nisali sara za mwisho.


Sikuwa na namna maana sura ya Goro haikuonesha hata ishara ya huruma na alikuwa kadhamilia huku mikono ikiwa juu na sikumbuki kama nilikuwa nasali ila ninachokikumbuka ni kishindo kikumbwa huku usoni kwangu nikihisi michirizi ya maji bila shaka sikuwepo duniani na ndamu zilikuwa zikinitoka. Nikiwa nimeyafumba macho nilihisi kama bado ninahema nilipounyanyua mkono wangu nikama ulikuwa unafanya kazi nilipofumbua macho niliiona sura ya Kimbo kwa mbali akinipa mkono, sikuwa na hakika kama ni yeye ama naota


Sikumbuki kilichotokea ila alikuwa ni Kimbo na wakati huo fahamu zinanirudia Goro alikuwa chini akiipigania nafsi yake ambayo pamoja na kujitahidi kuinusuru ilimponyoka ndani ya sekunde chache tu.


Kimbo alivua shati na kutoa jaketi maalumu la kuzuia risasi akanionesha ile risasi aliyopigwa na Goro ilinasa kwenye lile jaketi. Sikuamini kama kweli Kimbo bado yuko hai aliniambia tunatafutwa na polisi kutokana na milio hii ya risasi hatupaswi kuwa eneo hili tuondoke haraka sana mdogo wangu.


Tuliondoka kuelekea mjini lakini njia zetu hazikuwa zimenyooka tulipishana na polisi sehemu kadhaa hawakutujali ingawa tulikuwa na hofu kubwa ukituangalia tu nyuso zetu kulingana na hofu zile tukabadili mawazo hatukuelekea mjini tena, tulipita mtaa wa Nera na kutokea Isamilo na sasa tunaelekea Isamilo juu na kupita njia ya mkato karibu na kambi ya jeshi ya Nyanshana na kutokea Nyasaka.


Baada ya mwendo huo tuliamini tuko salama. “Hebu chukua hii simu upigesimu tena kwa hao wambea” Nilipiga simu tena Masafa Fm ilipokelewa na kunipa nafasi ya kueleza kila kitu kuanzia kutekwa kwangu, kuchomwa kwa makao makuu ya ofisi zangu na pia kuhusika kwa familia ya Gao katika haya matukio. Nilieleza kila kitu na nikawambia kila kitu Juu ya matukio hayo walifurahi sana na wakanipongeza kwa kuwa mkweli.


Nilijua taarifa imefika lakini kumbe Masafa Fm wameesha chimbwa mkara mzito na mzee Gao baada ya kurusha kile kipande cha taarifa yakwanza na tayari wameesha waomba radhi wasikilizaji na kuikanusha tarifa ile, lakini mimi sikujua kumbe waliishia kurekiodi tu na hakuna taarifa iliyoruka. Imani yetu kila kitu kiko poa na kimeenda kama tulivyotarajia, tulipongezana na kuanza kusonga mbele.


Tulicheka huku tukiambizana habari wanayo hawa nguruwe pori kumbe tulikuwa tunajidanganya, urafiki wangu na kimbo unanifanya kuwa karibu naye zaidi. Sikuona haja yakumficha nilianza kumhadithia kuhusu maisha yangu na Jesca kuachana na kurudiana tena, nilimueleza haya yote yananipata kwasababu Jesca bado ananihitaji mimi maana anaipenda sana anauhitaji uwepo wangu katika maisha yake lakini Von Gao hataki kusikia hizi habari na amechagua njia moja tu yakupambana na tatizo hili ni kuniua. Kimbo alicheka sana akasema Von anafunga ndoa leo jioni na Jesca na anatamani hiyo ndoa isifungwe wewe ukiwa marehemu na sasa ni saa tisa na ndoa ni saa kumi na moja jioni linda nafsi yako sana ndani ya haya masaa.


Basi tukiwa tumejipumzisha kwenye kichaka kati kati ya mlima huku tukiwa tumezungukwa na majabari makubwa huko mpakani mwa Nyasaka na Nyanshana tuliendelea kubadilishana mawazo. Kuitafuta suruhu ya hili tatizo, ilikuwa ngumu maana tunaamini vyombo vya habari huenda vikatusaidia lakini kumbe ilikuwa kinyume vyombo hivyo vikibanwa havina jipya


Wakati tukiwa pale tumeketi Kimbo anaamua kufungua redio, ni masafa Fm habari ilikuwa imegeuka tulijadiliwa sisi tunamchafua Mheshimiwa waziri mkuu wa zamani na sasa Masafa Fm ilikuwa ikituponda kwa maneno ya kejeli sana tu huku wakitoa tangazo la kusakwa kwa majambazi wawili ambao ni Jamae Justine na Evarist Kimbo taarifa tuliyoisikia inaonesha tumeua watu kumi na wawili na kujeruhi watatu maiti tatu jijini Dar esalaam zimekutwa na alama za vidole za Kimbo maiti nane kwenye kituo cha nyota Tv na maiti moja kwenye jengo moja bovu maeneo ya Kilumba.


Maiti hizi zote zinauhusiano wa kimauji. Kuhusu zire za Dar kumekutwa alama za vidole vya kimbo lakini kuhusu zile za nyota TV Kimbo na Jamae walionekana eneohilo na baadae kutoweka baada ya kufanya mauaji yakutisha, uhusiano wa matukio haya unakuja baada ya kuikuta maiti ya Goro iliyokutwa mtaa wa Kilumba ambapo baada ya kuikagua wanaikuta na alama za vidole vya watu wawili na jaketi moja la kuzuia risasi.


Kimbo anazima redio na kuangua kicheko wakati huo mimi nikiwa ninalia kwa uchungu. Sasa naangamia maisha yangu mimi kila siku ni shida tu, nilitamani dunia ipasuke ili nimezwe kuificha hii aibu wanayoipata ndugu zangu, nilimuwazia sana mama yangu huko aliko na kuyawazia maisha yake anajisikiaje anapopata tarifa kama hizi.


Nilikuwa nimetekwa kwa wiki zaidi ya mbili, mali zangu nimefirisiwa nabado mapya yanaibuka kila kukicha na leo natafutwa kwakuua watu kumi na wawili. Jamae Justine niliuona ukingo wa maisha yangu ni dimbwi la mawazo ambalo katu haliwezi kukauka. Wakati nawaza kumbe Kimbo alikuwa akinisemesha alirudia kama maratatu kuniita na bado sikumsikia na kilichofuata ni kunishushia bonge ya kofi nilishituka bila kujua nini kinaendelea.




Saa kumi kamili juu ya alama watu walikuwa wanejaa kwenye ukumbi teule uliopangwa kwaajili ya sherehe hii ya ndoa kati ya Von Pius Gao na Jesca Josefu Manguli. Wandishi wa habari na wapiga picha wachache tu ndio waliruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi huo tena kwa mwaliko maalumu.


Magari ya kifahari zaidi ya arobaini yaliongozana kuelekea eneo la magogoni yakitokea Masaki huku yakiongozwa na msafara wa asikari na ving’ora vya kila aina. Maandalizi ya harusi hayakwenda vibaya na upande wa Jesca sasa ameesha ridhika maana hana jinsi tena, juhudi za kuliokoa penzi letu zimekwama rasmi hali hii imetokea baada ya kuupata ushauri wakutosha kutoka kwamama yake na ndugu zake wa karibu hali ya amani inarejea moyoni mwake na sasa kutoka moyoni alikuwa karidhia kuolewa na Von Gao.


Muonekano wa Jesca ulikuwa mpya sura yake nzuri ilikuwa imetiwa urembo na kuifanya ivutie zaidi, gauni lake zuri la rangi ya zambarau na mapambo ya rangi mbalimbali na likiwa na muonekano wa manyoya ya kasuku lilivutia mno huko chumbani kwake. Ungemuona Jesca hakika usingeacha kumtamani kwangu mimi alikuwa ni mke niliemtarajia katika maisha yangu lakini nimezidiwa kete na anaonekana karidhia kuolewa na Von muache aolewe, acha aende!.


Familia ya Gao iliwasili muda mfupi baadae walipokelewa kwa shangwe na ndelemo, bwana harusi alikuwa kavaa mavazi mazuri mno alikuwa katinga suti yake ya blue bahari kiatu cha rangi ya kijivu shati la dhambarau na tai iliyoelekea na sana shati lake.


Von alikuwa kakinyoa vyema kichwa chake na kuongeza mvuto saa yake mkononi ilikuwa aghali mno naweza kusema ni harusi ya kushitukiza ila wamejiandaa vyema kila mtu aliyeshiriki hakika hakuijutia nafasi ile maana nikweli ilikuwa harusi ya watu mashuhuri, Von alionekana mtanashati sana wakati huu alipendeza mno kwa kila aliyemtazama na hata msindikizaji wake nae alivutia sana. Baada ya kufika walikaribishwa kwenye chumba maalumu kilichoandaliwa na waliketi huko wakiingoja saa kumi na moja itimie.


Mzee Manguli kwa muda sasa alikuwa nje ya dunia nina maanisha hakuwa anapata taarifa yoyote ile na alizuia asipewe taarifa ya aina yoyote maana huenda akavuruga harusi ya mwanaye. Akili yake yote aliielekeza kwenye harusi ya mwanaye kipenzi. Hakuwa anaangalia runinga kusikiliza redio na hata kusoma gazeti na hakushughulika nayo maana aliona ni kitu cha kawaida kabisa.


Hatimaye zilibaki dakika mbili upande wa Jesca moyo ulikuwa ukimwenda mbiyo kwa shahuku akitaka kukutana na Von ambaye kwa mara ya kwanza anahisi kumpenda sana na upande za Von Gao alitamani sana kumuona mke wa ndoto zake malikia wa nafsi yake mke aliyempenda na akaahidi kutoa hata nafsi za watu ilimradi tu alipate penzi la Jesca Manguli.


Kulingana na hali ya hewa ya mule ndani kuwa na viyoyozi Von alikuwa akivipasha moto viganja vyake kwa kuvikutanisha na kuvisugua huku nafsi yake haiamini kinachokwenda kutokea maishani mwake. Alijiuliza itakuwaje iwapo ataikamiklisha hii ndoa na Jesca binti pekee anaempenda katika maisha yake. Alikuwa akiliwaza fungate la miezi mitatu ambalo ameesha andaa nje ya bara la Afrika, sehemu za kwenda kutembelea yeye na Jesca wataanzia Marekeni baadae Dubai na mwisho watanmalizia katika mji wa kihistoria wa Roma huko Uitaliano na kila mji watakaa kwa mwezi mmoja mmoja.


Kwenye chumba alichokuwepo Jesca kunamtu aliwasha runinga baada ya kuwa na ukimya wa muda na hapo ndipo walipokutana na tangazo la kutafutwa kwa Jamae Justine na Evarist Kimbo wakitajwa kama majambazi walioua watu kumi na wawili leo.


Ni habari iliyomshitua sana Jesca na hapa anagundua kumbe familia ya Gao haijaachana na mpango wakunifatilia. Habari za Kimbo kuhusishwa na sikendo hii zinamshitua kidogo na alibaki ameduwaa “Kimbo shushushu wa serikali anaingiaje kwenye hii kesi, hapa lazima kuna kitu na si kitu kidogo bali kunatatizo lisipotibiwa hiki kidonda kitageuka kansa” alijisemea polepole. Lakini muda haukuwa rafiki kwake kwani walitakiwa kuingia ukumbini muda wa kufunga ndoa ulikuwa umewadia.


Kichwani alianza kuujutia uamzi wake wa kuolewa na kimbo na kujiona mpumbavu mbele ya kadamnasi. Zilikuwa ni cheleko, ndelemo na vifijo watu waliimba wakafurahi. Naweza kusema harusi ilipendeza mno, mavazi yalipendeza kwa kila mtu aliyekuwa hapo harusini naweza kusema kila mtu alivutiwa na kila kitu katika ukumbi ule.


Bwaba harusi alimpokea bi harusi baada ya biharusi kuletwa na baba yake na kukabidhiwa kwa mumewe mtarajiwa. Von Gao anampokea mkewe huku akitabasamu na kwambaali na kwa taabu sana lilionekana tabasamu la Jesca lakini hilo halikuwa tatizo kwa Von. Wapenzi hawa sasa walikuwa mbele ya Padre Josephat Ngalo na kwaajili ya kukamilisha ndoa yao.


***********************************


Tulikuwa bado tumeketi pale kichakani tukitafakari nini chakufanya Kimbo hakuonesha kuwa na wasi wasi aliniambia hapo hakuna kesi chakufanya tuwe makini maana hawa polisi wakitukamata kutoka itakuwa shida ila naamini hakuna kesi tunachopaswa kufanya ni kuwakwepa kama ukoma. Kiukweli maisha yangu sasa yamegeuka mikosi bundi alikuwa akiishi moyoni mwangu, bundi alikuwa katua kwenye paji la uso wangu, sina bahati tena, sina maana katika ulimwengu huu. Kimbo alinishauri hatupaswi kutoka hapa mpaka kiza kitakapo ingia maana tunatafutwa kama pesa huko mtaani. Kulingana na uchovu tuliokuwa nao tulijikuta tumejiamini kupita kiasi na kujiona tuko sehemu salama kabisa na usingizi ukatupitia.


Tulijiachia na kujiona tuko nyumbani kabisa baada ya kulala kwa muda mrefu na kujisahau kabisa tulijikuta katika matatizo. Zilisikika sauti za bunduki sikikokiwa na kilifuata kipigo kizito ndicho kilicho tutoa usingizini. Ebwana walikuwa wanajeshi, tulichezea kipigo ambacho sina kumbukumbu kama nimewahi kukipitia katika maisha yangu nilipotekwa na Kimbo nilipigwa ila hiki kipigo cha leo ni kiboko. Siyo mimi tu niliyejuta maana hata nilipomuangalia Kimbo ambaye ni tegemeo langu naye nilimuona amekwama alikuwa mdogo kama punje ya haradali, tulikung’utwa hasa na kisha kutangulizwa mbele huku tukiruka kichura chura. Tulirushwa kichura chura umbali mrefu sana na hatimaye tulifikishwa kambini kwao. Tulilowekwa kwenye pipa la oili chafu huku na kulazimishwa kukwea minazi oili inateleza lakini walitulazimisha tulipigwa sana. Tukifanyishwa mazoezi magumu na ya ajabu na hakua aliyepigwa baada ya kichapo cha muda kama wa robo saa hivi tuliambiwa tumekamatwa kwenye eneo la kambi ya Jeshi na adhabu iliyofuta tulifungwa miguu na kuning’inizwa vichwa chini kama nyama kwenye bucha siijui hatima yetu itakuwaje?.


Maumivu makali yaliutawala mwili wangu tulikuwa tukimwagiwa maji na kushushiwa viboko mfurulizo kwa takiribani dakika kumi na sasa kuna jamaa anakuja na kutukuta tumechakazwa vilivyo alisimama mbele yetu na kutuangalia kisha akauliza


“Imekuwaje hawa watu ?”


“Tumewakuta eneo la Jeshi na tulipowasachi mmoja alikuwa na bastora mbili na risasi zake kama kumi na mbili hivi na hii inaonesh wazi kuwa hawa watu ni waharifu na huenda walipania kutuvamia hapa kambini”


Nikweli kimbo alikuwa na bastora mbili na hizo risasi zilizotajwa lakini hatukuwa na lengo la kuvamia kambi ya jeshi “eti jamani tuvamie kambi ya jeshi sisi hatujipendi?” Baada ya hayo maelezo yalionesha nikweli Kimbo alikuwa nazo hizo bastora mbili na risasi zake kumi, ndoto zakujinasua ziligonga mwamba.


Kuna bwana mmoja alikuja na kusimama mbele yetu kwenye sare yake ya kijeshi kulikuwa na kitambaa cheupe kwenye mkono kuelekea mabegani kilichoandikwa kwa maandishi mekundu herufi mbili na zikasomeka MP (Miritary Police) huyu ni asikali wa jeshi nakazi yake ni kurekebisha tabia za wanajeshi pale jeshini wanapokosea aliwaamuru wale wanajeshi kutupeleka mahabusu. Kitu ambacho Kimbo hakukikubali hata, wakati tukiwa tumebaki peke yetu Kimbo aliniambia hayuko tayari kupelekwa mahabusu za jeshi kwani tutakufa mateso ya huko siyo mchezo na hapo tulipo tunahesabika kama mateka tuliotaka kuivamia kambi ya jeshi si ajabu tukakabiliwa na adhabu ya kifo hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi. Nikweli aliyoyasema lakini tutajinasua vipi mikononi mwa hawa watu? Hilo ni swali lakimiujiza.


Baada ya kukamilisha mazungumzo yao huko walikokuwa sasa wanarejea wanajeshi watano walifika wawili wakachomoa visu na kuzikata zile kamba walizotufunga huku tukianguka kama magunia, lakini baada ya kusimama kutoka chini alipoanguka Kimbo anazua balaa lingine lililoushitua moyo wangu na kubaki najiuliza maswali. Nilishangaa wakati tunapelekwa mahabusu alianza kuwatambua majina kwa kuwaita wale asikari wa kijeshi.


“Frenk Mchunguzi na wewe Samson Marwa leo hamnitambui siyo?” wale askari waligeukiana na kutazamana kwa hofu na mikono yako ikiwa imewahi kushika bastora kitendo kilichofanyika haraka zaidi, hapa sasa nagundua Kimbo alikuwa anakitafuta kifo tena kwa nguvu, lakini Kimbo hakuwa na wasiwasi hakuishia hapo akaendelea.


“MP Jackson Mkinga umekuwa kijana wangu leo unakiburi mpaka unanikabiri mimi mlezi wako siyo, nyie wote ni wanafunzi wangu mbona mnanishangaza” askari mmoja alimsogelea ili amtizame vizuri.


“kuwa makini wewe mbwa adui siyo mama yako.” Kauli ilitoka kwa askari mwenziye.


“Oooh! Generali Kimbo ni wewe” Frenk Mchunguzi alimtambua, vijana walishangaa sana na kujikuta wanampigia saluti na kubaki wameganda mpaka alipo kubali na mwisho wanamkumbatia kwa furaha.


Ndani ya ofisi ya mkuu wa kikosi Kimbo anakutana na Meja Athanas Ngayoma bila hata kuuliza Meja anapiga saluti na kushangazwa na kitendo cha Kimbo kuonekana mchafu mbele ya ofisi yake.


“Vipi Meja Jenerali Kimbo inakuwaje uko katika hali hii?”


“Ni vijana wako wamenikuta kambini kwao bwana si unajua tena sisi tunavyopenda, wamenishughulikia vyakutosha”


“Pole sana mkuu nitawashughulikia”


“hapana wape uhuru nilisha kufundisha usemi usemao usimulee adui maana..”


“siyo mama yako”


Mimi sijasema bali umesema wewe” wote waliangua kicheko, tulibadilishiwa mavazi na kupewa chakula na kuhesabika kama wageni mhimu sana ndani ya eneo hili. Na baada ya hapo Kimbo alikuwa na maongezi na meja Ngayoma, Kimbo alimuomba atupe msaada kwani tunasakwa na familia ya Gao cha kwanza ni kutuhakikishia usalama hasa mimi kwani tunasakwa kama swala. Pili alimueleza jinsi Goro alivyofanya mauaji na sasa tunasakwa sisi kama wahusika wa mauaji pale Nyota Tv. Ngayoma alisema yuko tayari kutusaidia na aliahidi atalisimamia hilo swala na kulifatilia kwa karibu zaidi. Kimbo alirudi na kuniambia mambo yote yako poa chakufanya sasa ni kurudi jijini Dar, Ngayoma ni kijana wangu huyu nimemfundisha miaka ya nyuma walipokuja kwenye mafunzo maalumu kipindi hicho nikiwa arusha, ameahidi kunipa ulinzi mpaka tufike kwa rais ili tukalimalize hili swala maana tukiliendekeza Gao atatuhamisha nchini.


Basi maandalizi yalikamilika na kusindikizwa mpaka uwanja wa ndege kwaajili ya safari. Tuliondoka Mwanza tukiwa na usindikizaji wakutosha maasikari watano wa jeshi la wananchi tena waliofuzu mafunzo maalumu wakiwa wamevaa kiraia ndio waliotusindikiza, walikuwa wakitulinda na kutuhakikishia usalama wakutosha.


*****************************


Mbele ya kadamnasi mzee Manguli akitabasamu baada ya kuwa amemkabidhi binti yake kwa Von Gao kijana wa rafiki yake kipenzi shangwe na ndelemo zikazizima ukumbi mzima ukarindima kwa furaha na sasa maharusi hawa wawili walikuwa mbele ya padre Josephat kwaajili ya kuikamilisha ndoa yao.


Nyuso zao zinaonekana za furaha kwa kuwatazama lakini hatuwezi kujua mioyoni mwao wamehifadhi nini. Lakini navutiwa na furaha mioyoni mwa watu kwani kila mtu alilifurahia penzi la hawa vijana wawili toka familia mashuhuri licha ya kupendeza lakini walivutia hata kuwatizama tu ilitosha kuilidhisha mioyo ya watazamaji. Na sasa ulikua ni wakati wa kufungishwa ndoa yao rasmi, au pingu za maisha na pia tunaweza kuita mkataba wa maisha ambao ulisindikizwa na maneno haya ya viapo…..


“Pius Von Gao. Je, unakubali kumuoa Jesca Joseph Manguli awe mke wako kwenye shida na raha, uzima na maradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha?”


“Ndiyo ninakubali mpaka kifo kitakapotutenganisha”


“Jesca Joseph unakubali kuolewa na Pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na amaradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha? ” kimya kilitanda, hakuna jibu lolote lililotolewa hali iliyomfanya Padre kurudia tena kuuliza.


“Jesca Joseph unakubali kuolewa na pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na maradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha ” bado jibu likawa ni kimya na awamu hii uso wa Jesca ulikuwa ukitokwa machozi. Padre hakukata tamaa alirudia tena.


“Jesca Joseph unakubali kuolewa na Pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na amaradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha? ”


“Hapana!” watu aaaah! Minong’ono, Padre alirudia tena kupata uhakika zaidi jibu lilibaki kuwa hapana na hata aliporudia tena bado ilibaki kuwa hapana. Mzee Manguli alikuwa kafula kwa hasira na asijue chakufanya upande wa mzee Gao alikuwa kasimama walijitahidi kuvumilia lakini wakashindwa alijaribu kujikanyaga walau kuzificha hasira lakini ilishindikana. Ni aibu, aibu ambayo haitaweza kusahaulika ni mbele ya wageni marafiki kutoka nchi mbali mbali, marafiki maarufu kutoka mataifa tofauti, wafanya biashara na watu mashuhuli ni aibu kubwa si yakusimulika.


Jesca hakuishia hapo alisogea karibu na kipaza sauti mbele ya ukumbi huku watu wakimshangaa na wakinong’ona kila mtu alichokijua yeye, maana tayari alikuwa ametibua nyongo za watazamaji na washiriki wote katika harusi hiyo alianza kuongea kwa huzuni.


“Mabibi na mabwana nasimama mbele yenu, kuzungumza nanyi najua mlijua leo ni siku yangu mhimu katika historia ya maisha yangu na ndiyo maana mmejitokeza kwa wingi kuja kuniunga mkono katika safari hii mhimu.” Alipumzika kidogo!!.


“Kinyume na matarajio yenu nimefanya uamzi tofauti ila naamini ni uamzi sahihi maana ndoa ni pingu ya maisha ukikosea kuingia kwenye ndoa nahisi utakuwa umeyavuruga maisha. Nafanya uamzi huu mbele yenu kuiahirisha ndoa niliyoilidhia mwenyewe hapo awali baada ya kuyaona mapema makucha ya mwenzi wangu aliyokuwa kayaficha. Nibora uonekane hufai katika jamii, uonekane mjinga katika jamii, usiogope aibu na kushindwa kuisimamia haki. Leo mnaona kama nimetia aibu lakini kuna kitu hamkijui, yanini niogope aibu kwa kuwafurahisha ninyi na wazazi wangu ilihali naenda kuishi maisha ya mateso kama mnyama wa mwituni?”. Alimeza mate kidogo huku ukumbi ukiwa kimya na ilikuwa kimya kweli maana Jesca aliongea maneno mazito kuliko umri wake.


Mpumbavu huu ongopa ukweli na muongo daima huwa mnafiki maana huamua asilo likusudia, najua mnanishangaa na wengine kujiuliza kama sikutaka kuolewa yanini nivae gauni la harusi. Ukweli ni kwamba Familia ya mzee Gao wanayaingilia maisha yangu binafsi na lengo lao ni kuyavuruga maisha yangu hivi leo mnafanya hivi nikiwa kwetu nakesho nitakapokuwa ndani ya familia yenu itakuwaje?. Jesca alisita kidogo na kisha kumgeukia Von Gao Mchumba wangu Von maana katu huwezi kuwa mume wangu cha kwanza tambua kuwa sikukupenda toka awali, pili acha kufanya unachokifanya kwa watu wasio na hatia au mnataka niseme kinachoendelea?”


“sema… sema… tueleze…” aliendelea baada ya kelele za watu kumtaka aseme “familia ya Gao inahusika na kuharibu maisha yangu kwanza walimteka na kumtesa na kumfirisi kijana Jamae Justine huku wakihusika na kuichoma moto Kampuni yake, pili wanamtafuta kumuua mpaka hivi tunavyoongea ni watu kumi na wawili wameesha poteza maisha wakiwemo wafanyakazi wa Nyota Tv katika msako wa kumuuwa Jamae lengo ni kuhakikisha wanayapoteza maisha ya Jamae” watu wanashika midomo kwa mshangao, Mzee Gao kajiinamia na mwanae alikuwa akipumua kwa taaabu huku akitetemeka.


“Nina ujauzito wa miezi mnne lakini baba yangu aliamuru niolewe tu na Von pamoja na kuwa na mimba ya Jamae… familia yangu haitendi haki kwangu na wala hawazijali hisia zangu juu ya kipi ninachokipenda. Nahitaji kuheshimiwa na kulindwa lakini wakwe zangu na wazazi wangu namaanisha watu wa karibu zaidi ndiyo wananiangamiza”


Watu walikuwa kimya wasiamini kilichokuwa kikiendelea.


Mzee Manguli aisimama na kwenda mbele alipokuwa kasimama binti yake alifika na kumbamiza bonge la kibao shavuni kisha alishika mike kwa hasira.


“katika kizazi changu sikuwahi kufikiria kuwa na mwana mpumbavu kama huyu binti na nahisi hawezi kuwa mwanangu pengine mama yake anapaswa kutueleza vizuri alimtuoa wapi huyu binti?” Mzee Manguli alikuwa akiongea kwa hasira sana.


“Tunasikia porojo nyingi zisizo na ukweli, yanini kumsingizia mzee wa watu maswala yako yakijinga unayoyavuruga wewe mwenyewe? Jesca binti yangu kanitia aibu tena aibu ya mwaka na mimi kamwe staikubalia aibu hii initafune. Ninajua nitafanya nini na ulimwengu utaamini kuwa sina hatia, ndani ya familia yangu siishi na makahaba, siishi na watu waongo, siishi na watu wanafiki na mwana mpumbavu biblia inatueleza ni mzigo wa mamaye bali mwana mwenye hekima humfurahisha babaye najua mmeesha jua hili ni zigo la nani” alikaa kimya kidogo huku akirekebisha miwani yake.


“kuropoka ni jambo rahisi sana oooh! Gao jambazi, mwizi , sijui tapeli unaushahidi?”


“tusipende kuchafuana na kukosana na ndugu kwa sababu ya upuuzi wetu… wahenga walisema ukilikoroga lazima ulinywe.. yanini kusingizia watu ilihali wewe ndiye chanzo?”


“Jesca sasa utalazimika kutupa ushahidi wa hiki ulichokisema bila hivyo stakubali umudhalilishe mzee wa watu, na uzuri unanijua zaidi ni nini nitakiamua baada ya hapa mana uko ndani ya himaya yangu”


“Nina taka ushahidi la sivyo askari wataondoka na wewe hapa nahesabu mpaka tatu….. moja …….. mbili …….ta..


“ushahidi tunao Mh. Rais mimi ni Evarist Kimbo hata nisipojitambulisha unanijua vizuri mno” Mzee Gao na Mwanae macho yaliwatoka baada ya kumuona Kimbo akiingia akiwa hai maana hawakutarajia kabisa


Mimi ndiye niliyetumwa na Mzee Gao kwenda kumuuwa Jamae ili Von amuoe binti yako kwasababu Jesca alitaka kubadili mawazo baada ya kukutana na Jamae ambaye ndiye mpenzi wake wa siku zote, mimi ndiye niliyemteka Jamae na kukaa naye mateka zaidi ya wiki mbili kisha nilimuachia baada ya mzee Gao kushindwa kukamilisha makubaliano yetu, ukweli ni kwamba familia ya Gao ndiyo iliyo husika na kuchomwa kwa ofisi za Himaya Chapakazi wakishirikiana na aliyekuwa mkurugenzi msaidizi aliyejulikana kwa jina la Dominic Martine walifanya hivyo baada ya Domi kukomba pesa zote na walimlipa pesa zingine akatimukia nchini Urusi, ni familia ya Gao hii uliyonayo hapa na nashangaa unavyopambana kuwapa mwano, nayaongea haya mbele yako na mbele yao na niko tayari kwa lolote ikiwa ni pamoja na kutoa ushahidi popote nitakapohitajika, ninakumbukumbu za sauti za simu walizonipigia na simu zao zote na pia ujumbe wa maandishi.


Familia ya Gao imeyaharibu mno maisha yangu na siko tayari kuendelea kuona yanaharibika. Tafadhali familia ya Gao mwacheni Jamae hana kosa mtu wa watu, najua zisingekuwa juhudi zangu leo huyu kijana angekuwa ameesha kufa maana hapa ninavyoongea na wewe wameeshatumia kila njia kuhakikisha wanamteketeza lakini si yeye tu hata mimi wamejaribu kuniua asubuhi ya leo na pia mchana walitaka kumuua Jamae na bahati nzuri nilikuwa namlinda kwa karibu mno, kwa juhudi zangu nikamuokoa. Nalitafuta kosa lake silioni lakini wanataka kumuangamiza sidhani kama wivu wa mapenzi unaweza kuwa na athali kubwa kiasi hiki.


Familia ya Gao najua mko hapa achaneni na mnachokifanya Jamae hana hatia mmeharibu maisha yake vyakutosha sasa tuseme yatosha, kumbukeni mmemnyang’anya mpenzi wake kwa nguvu, mmemfilisi na sasa ni masikini wakutupwa bado haitoshi mnataka kumuua hii sasa ni laana.” Niliingia ukumbini pale huku nikisindikizwa na Wale askari watano tulikuja nao Jesca alifurahi mno hakuamini baada ya kuniona alinikimbilia na kunirukia kwa furaha huku akinikumbatia kwa nguvu na kuanza kupata denda.


Watu walipiga makofi, wengine walinuna lakini hatukuwa jali kila mtu na maisha yake na kila mtu na furaha yake tumefanikisha kulirudisha penzi letu. Jesca alinishika mkono tukatoka nje ya ukumbi huku Von na baba yake wakitutizama kwa ghadhabu na wasijue chakufanya. Tuliwaacha na suti zao sisi tukaingia zetu ndani sijui walichokiwaza ila mtoto nilikuwa nimejibebea kiulaini bila wasiwasi hapa sikuwa nawaza kitu kingine zaidi ya furaha kutoka kwa mpenzi wangu.


Nahisi Jesca amerudi mikononi mwangu na amedhihilisha upendo wakweli na msimamo wakweli katika mapenzi na sasa tuliingia ndani. Chumba chetu kiliimarishiwa ulinzi na Kimbo akiwa mkuu wa ulinzi kwa wakati huo si Rais wala mfanya kazi yeyote hakutakiwa kukisogelea pamoja na kuwa ndani ya Himaya ya Ikulu. Tulisikia ving’ora vya gari la polisi hapo nje na tulipochungulia tunawaona Gao na mwanae mikono ikiwa imepigwa pingu huku wakiwekwa kwenye gari la polisi na ndoa imeahirishwa.


Tulikumbatiana na kufurahi pamoja Jesca alikuwa na furaha sana kwani alinihakikishia kuwa ananipenda na sasa aliniambia kuwa ni mjamzito na ameesha hakikisha tunatarajia mtoto wa kiume, ilikuwa ni furaha mpya iliyoleta na kujenga tumaini jipya katika mapenzi na sasa tunakumbatiana tena na kupiga kelele kwa furaha huku tukibusu na kupongezana. Ni mapenzi ya dhati baina yetu sasa nayadumu milele ni mimi na malikia wangu wangu Jesca Manguli tumejipumzisha ndani ya jumba la Ikulu bila wasi wasi tukila na kunywa kwa upendo.




Maumivu makali yaliutawala mwili wangu tulikuwa tukimwagiwa maji na kushushiwa viboko mfurulizo kwa takiribani dakika kumi na sasa kuna jamaa anakuja na kutukuta tumechakazwa vilivyo alisimama mbele yetu na kutuangalia kisha akauliza

“Imekuwaje hawa watu ?”

“Tumewakuta eneo la Jeshi na tulipowasachi mmoja alikuwa na bastora mbili na risasi zake kama kumi na mbili hivi na hii inaonesh wazi kuwa hawa watu ni waharifu na huenda walipania kutuvamia hapa kambini”

Nikweli kimbo alikuwa na bastora mbili na hizo risasi zilizotajwa lakini hatukuwa na lengo la kuvamia kambi ya jeshi “eti jamani tuvamie kambi ya jeshi sisi hatujipendi?” Baada ya hayo maelezo yalionesha nikweli Kimbo alikuwa nazo hizo bastora mbili na risasi zake kumi, ndoto zakujinasua ziligonga mwamba.


Kuna bwana mmoja alikuja na kusimama mbele yetu kwenye sare yake ya kijeshi kulikuwa na kitambaa cheupe kwenye mkono kuelekea mabegani kilichoandikwa kwa maandishi mekundu herufi mbili na zikasomeka MP (Miritary Police) huyu ni asikali wa jeshi nakazi yake ni kurekebisha tabia za wanajeshi pale jeshini wanapokosea aliwaamuru wale wanajeshi kutupeleka mahabusu. Kitu ambacho Kimbo hakukikubali hata, wakati tukiwa tumebaki peke yetu Kimbo aliniambia hayuko tayari kupelekwa mahabusu za jeshi kwani tutakufa mateso ya huko siyo mchezo na hapo tulipo tunahesabika kama mateka tuliotaka kuivamia kambi ya jeshi si ajabu tukakabiliwa na adhabu ya kifo hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi. Nikweli aliyoyasema lakini tutajinasua vipi mikononi mwa hawa watu? Hilo ni swali lakimiujiza.


Baada ya kukamilisha mazungumzo yao huko walikokuwa sasa wanarejea wanajeshi watano walifika wawili wakachomoa visu na kuzikata zile kamba walizotufunga huku tukianguka kama magunia, lakini baada ya kusimama kutoka chini alipoanguka Kimbo anazua balaa lingine lililoushitua moyo wangu na kubaki najiuliza maswali. Nilishangaa wakati tunapelekwa mahabusu alianza kuwatambua majina kwa kuwaita wale asikari wa kijeshi.

“Frenk Mchunguzi na wewe Samson Marwa leo hamnitambui siyo?” wale askari waligeukiana na kutazamana kwa hofu na mikono yako ikiwa imewahi kushika bastora kitendo kilichofanyika haraka zaidi, hapa sasa nagundua Kimbo alikuwa anakitafuta kifo tena kwa nguvu, lakini Kimbo hakuwa na wasiwasi hakuishia hapo akaendelea.

“MP Jackson Mkinga umekuwa kijana wangu leo unakiburi mpaka unanikabiri mimi mlezi wako siyo, nyie wote ni wanafunzi wangu mbona mnanishangaza” askari mmoja alimsogelea ili amtizame vizuri.

“kuwa makini wewe mbwa adui siyo mama yako.” Kauli ilitoka kwa askari mwenziye.

“Oooh! Generali Kimbo ni wewe” Frenk Mchunguzi alimtambua, vijana walishangaa sana na kujikuta wanampigia saluti na kubaki wameganda mpaka alipo kubali na mwisho wanamkumbatia kwa furaha.


Ndani ya ofisi ya mkuu wa kikosi Kimbo anakutana na Meja Athanas Ngayoma bila hata kuuliza Meja anapiga saluti na kushangazwa na kitendo cha Kimbo kuonekana mchafu mbele ya ofisi yake.

“Vipi Meja Jenerali Kimbo inakuwaje uko katika hali hii?”

“Ni vijana wako wamenikuta kambini kwao bwana si unajua tena sisi tunavyopenda, wamenishughulikia vyakutosha”

“Pole sana mkuu nitawashughulikia”

“hapana wape uhuru nilisha kufundisha usemi usemao usimulee adui maana..”

“siyo mama yako”

“Mimi sijasema bali umesema wewe” wote waliangua kicheko, tulibadilishiwa mavazi na kupewa chakula na kuhesabika kama wageni mhimu sana ndani ya eneo hili. Na baada ya hapo Kimbo alikuwa na maongezi na meja Ngayoma, Kimbo alimuomba atupe msaada kwani tunasakwa na familia ya Gao cha kwanza ni kutuhakikishia usalama hasa mimi kwani tunasakwa kama swala. Pili alimueleza jinsi Goro alivyofanya mauaji na sasa tunasakwa sisi kama wahusika wa mauaji pale Nyota Tv. Ngayoma alisema yuko tayari kutusaidia na aliahidi atalisimamia hilo swala na kulifatilia kwa karibu zaidi. Kimbo alirudi na kuniambia mambo yote yako poa chakufanya sasa ni kurudi jijini Dar, Ngayoma ni kijana wangu huyu nimemfundisha miaka ya nyuma walipokuja kwenye mafunzo maalumu kipindi hicho nikiwa arusha, ameahidi kunipa ulinzi mpaka tufike kwa rais ili tukalimalize hili swala maana tukiliendekeza Gao atatuhamisha nchini.


Basi maandalizi yalikamilika na kusindikizwa mpaka uwanja wa ndege kwaajili ya safari. Tuliondoka Mwanza tukiwa na usindikizaji wakutosha maasikari watano wa jeshi la wananchi tena waliofuzu mafunzo maalumu wakiwa wamevaa kiraia ndio waliotusindikiza, walikuwa wakitulinda na kutuhakikishia usalama wakutosha.


*****************************


Mbele ya kadamnasi mzee Manguli akitabasamu baada ya kuwa amemkabidhi binti yake kwa Von Gao kijana wa rafiki yake kipenzi shangwe na ndelemo zikazizima ukumbi mzima ukarindima kwa furaha na sasa maharusi hawa wawili walikuwa mbele ya padre Josephat kwaajili ya kuikamilisha ndoa yao.


Nyuso zao zinaonekana za furaha kwa kuwatazama lakini hatuwezi kujua mioyoni mwao wamehifadhi nini. Lakini navutiwa na furaha mioyoni mwa watu kwani kila mtu alilifurahia penzi la hawa vijana wawili toka familia mashuhuri licha ya kupendeza lakini walivutia hata kuwatizama tu ilitosha kuilidhisha mioyo ya watazamaji. Na sasa ulikua ni wakati wa kufungishwa ndoa yao rasmi, au pingu za maisha na pia tunaweza kuita mkataba wa maisha ambao ulisindikizwa na maneno haya ya viapo…..

“Pius Von Gao. Je, unakubali kumuoa Jesca Joseph Manguli awe mke wako kwenye shida na raha, uzima na maradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha?”

“Ndiyo ninakubali mpaka kifo kitakapotutenganisha”

“Jesca Joseph unakubali kuolewa na Pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na amaradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha? ” kimya kilitanda, hakuna jibu lolote lililotolewa hali iliyomfanya Padre kurudia tena kuuliza.

“Jesca Joseph unakubali kuolewa na pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na maradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha ” bado jibu likawa ni kimya na awamu hii uso wa Jesca ulikuwa ukitokwa machozi. Padre hakukata tamaa alirudia tena.

“Jesca Joseph unakubali kuolewa na Pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na amaradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha? ”

“Hapana!” watu aaaah! Minong’ono, Padre alirudia tena kupata uhakika zaidi jibu lilibaki kuwa hapana na hata aliporudia tena bado ilibaki kuwa hapana. Mzee Manguli alikuwa kafula kwa hasira na asijue chakufanya upande wa mzee Gao alikuwa kasimama walijitahidi kuvumilia lakini wakashindwa alijaribu kujikanyaga walau kuzificha hasira lakini ilishindikana. Ni aibu, aibu ambayo haitaweza kusahaulika ni mbele ya wageni marafiki kutoka nchi mbali mbali, marafiki maarufu kutoka mataifa tofauti, wafanya biashara na watu mashuhuli ni aibu kubwa si yakusimulika.


Jesca hakuishia hapo alisogea karibu na kipaza sauti mbele ya ukumbi huku watu wakimshangaa na wakinong’ona kila mtu alichokijua yeye, maana tayari alikuwa ametibua nyongo za watazamaji na washiriki wote katika harusi hiyo alianza kuongea kwa huzuni.

“Mabibi na mabwana nasimama mbele yenu, kuzungumza nanyi najua mlijua leo ni siku yangu mhimu katika historia ya maisha yangu na ndiyo maana mmejitokeza kwa wingi kuja kuniunga mkono katika safari hii mhimu.” Alipumzika kidogo!!.

“Kinyume na matarajio yenu nimefanya uamzi tofauti ila naamini ni uamzi sahihi maana ndoa ni pingu ya maisha ukikosea kuingia kwenye ndoa nahisi utakuwa umeyavuruga maisha. Nafanya uamzi huu mbele yenu kuiahirisha ndoa niliyoilidhia mwenyewe hapo awali baada ya kuyaona mapema makucha ya mwenzi wangu aliyokuwa kayaficha. Nibora uonekane hufai katika jamii, uonekane mjinga katika jamii, usiogope aibu na kushindwa kuisimamia haki. Leo mnaona kama nimetia aibu lakini kuna kitu hamkijui, yanini niogope aibu kwa kuwafurahisha ninyi na wazazi wangu ilihali naenda kuishi maisha ya mateso kama mnyama wa mwituni?”. Alimeza mate kidogo huku ukumbi ukiwa kimya na ilikuwa kimya kweli maana Jesca aliongea maneno mazito kuliko umri wake.

“Mpumbavu huu ongopa ukweli na muongo daima huwa mnafiki maana huamua asilo likusudia, najua mnanishangaa na wengine kujiuliza kama sikutaka kuolewa yanini nivae gauni la harusi. Ukweli ni kwamba Familia ya mzee Gao wanayaingilia maisha yangu binafsi na lengo lao ni kuyavuruga maisha yangu hivi leo mnafanya hivi nikiwa kwetu nakesho nitakapokuwa ndani ya familia yenu itakuwaje?. Jesca alisita kidogo na kisha kumgeukia Von Gao Mchumba wangu Von maana katu huwezi kuwa mume wangu cha kwanza tambua kuwa sikukupenda toka awali, pili acha kufanya unachokifanya kwa watu wasio na hatia au mnataka niseme kinachoendelea?”

“sema… sema… tueleze…” aliendelea baada ya kelele za watu kumtaka aseme “familia ya Gao inahusika na kuharibu maisha yangu kwanza walimteka na kumtesa na kumfirisi kijana Jamae Justine huku wakihusika na kuichoma moto Kampuni yake, pili wanamtafuta kumuua mpaka hivi tunavyoongea ni watu kumi na wawili wameesha poteza maisha wakiwemo wafanyakazi wa Nyota Tv katika msako wa kumuuwa Jamae lengo ni kuhakikisha wanayapoteza maisha ya Jamae” watu wanashika midomo kwa mshangao, Mzee Gao kajiinamia na mwanae alikuwa akipumua kwa taaabu huku akitetemeka.

“Nina ujauzito wa miezi mnne lakini baba yangu aliamuru niolewe tu na Von pamoja na kuwa na mimba ya Jamae… familia yangu haitendi haki kwangu na wala hawazijali hisia zangu juu ya kipi ninachokipenda. Nahitaji kuheshimiwa na kulindwa lakini wakwe zangu na wazazi wangu namaanisha watu wa karibu zaidi ndiyo wananiangamiza”

Watu walikuwa kimya wasiamini kilichokuwa kikiendelea.


Mzee Manguli aisimama na kwenda mbele alipokuwa kasimama binti yake alifika na kumbamiza bonge la kibao shavuni kisha alishika mike kwa hasira.

“katika kizazi changu sikuwahi kufikiria kuwa na mwana mpumbavu kama huyu binti na nahisi hawezi kuwa mwanangu pengine mama yake anapaswa kutueleza vizuri alimtuoa wapi huyu binti?” Mzee Manguli alikuwa akiongea kwa hasira sana.

“Tunasikia porojo nyingi zisizo na ukweli, yanini kumsingizia mzee wa watu maswala yako yakijinga unayoyavuruga wewe mwenyewe? Jesca binti yangu kanitia aibu tena aibu ya mwaka na mimi kamwe staikubalia aibu hii initafune. Ninajua nitafanya nini na ulimwengu utaamini kuwa sina hatia, ndani ya familia yangu siishi na makahaba, siishi na watu waongo, siishi na watu wanafiki na mwana mpumbavu biblia inatueleza ni mzigo wa mamaye bali mwana mwenye hekima humfurahisha babaye najua mmeesha jua hili ni zigo la nani” alikaa kimya kidogo huku akirekebisha miwani yake.

“kuropoka ni jambo rahisi sana oooh! Gao jambazi, mwizi , sijui tapeli unaushahidi?”

“tusipende kuchafuana na kukosana na ndugu kwa sababu ya upuuzi wetu… wahenga walisema ukilikoroga lazima ulinywe.. yanini kusingizia watu ilihali wewe ndiye chanzo?”

“Jesca sasa utalazimika kutupa ushahidi wa hiki ulichokisema bila hivyo stakubali umudhalilishe mzee wa watu, na uzuri unanijua zaidi ni nini nitakiamua baada ya hapa mana uko ndani ya himaya yangu”

“Nina taka ushahidi la sivyo askari wataondoka na wewe hapa nahesabu mpaka tatu….. moja …….. mbili …….ta..

“ushahidi tunao Mh. Rais mimi ni Evarist Kimbo hata nisipojitambulisha unanijua vizuri mno” Mzee Gao na Mwanae macho yaliwatoka baada ya kumuona Kimbo akiingia akiwa hai maana hawakutarajia kabisa.

“Mimi ndiye niliyetumwa na Mzee Gao kwenda kumuuwa Jamae ili Von amuoe binti yako kwasababu Jesca alitaka kubadili mawazo baada ya kukutana na Jamae ambaye ndiye mpenzi wake wa siku zote, mimi ndiye niliyemteka Jamae na kukaa naye mateka zaidi ya wiki mbili kisha nilimuachia baada ya mzee Gao kushindwa kukamilisha makubaliano yetu, ukweli ni kwamba familia ya Gao ndiyo iliyo husika na kuchomwa kwa ofisi za Himaya Chapakazi wakishirikiana na aliyekuwa mkurugenzi msaidizi aliyejulikana kwa jina la Dominic Martine walifanya hivyo baada ya Domi kukomba pesa zote na walimlipa pesa zingine akatimukia nchini Urusi, ni familia ya Gao hii uliyonayo hapa na nashangaa unavyopambana kuwapa mwano, nayaongea haya mbele yako na mbele yao na niko tayari kwa lolote ikiwa ni pamoja na kutoa ushahidi popote nitakapohitajika, ninakumbukumbu za sauti za simu walizonipigia na simu zao zote na pia ujumbe wa maandishi.


Familia ya Gao imeyaharibu mno maisha yangu na siko tayari kuendelea kuona yanaharibika. Tafadhali familia ya Gao mwacheni Jamae hana kosa mtu wa watu, najua zisingekuwa juhudi zangu leo huyu kijana angekuwa ameesha kufa maana hapa ninavyoongea na wewe wameeshatumia kila njia kuhakikisha wanamteketeza lakini si yeye tu hata mimi wamejaribu kuniua asubuhi ya leo na pia mchana walitaka kumuua Jamae na bahati nzuri nilikuwa namlinda kwa karibu mno, kwa juhudi zangu nikamuokoa. Nalitafuta kosa lake silioni lakini wanataka kumuangamiza sidhani kama wivu wa mapenzi unaweza kuwa na athali kubwa kiasi hiki.


Familia ya Gao najua mko hapa achaneni na mnachokifanya Jamae hana hatia mmeharibu maisha yake vyakutosha sasa tuseme yatosha, kumbukeni mmemnyang’anya mpenzi wake kwa nguvu, mmemfilisi na sasa ni masikini wakutupwa bado haitoshi mnataka kumuua hii sasa ni laana.” Niliingia ukumbini pale huku nikisindikizwa na Wale askari watano tulikuja nao Jesca alifurahi mno hakuamini baada ya kuniona alinikimbilia na kunirukia kwa furaha huku akinikumbatia kwa nguvu na kuanza kupata denda.


Watu walipiga makofi, wengine walinuna lakini hatukuwa jali kila mtu na maisha yake na kila mtu na furaha yake tumefanikisha kulirudisha penzi letu. Jesca alinishika mkono tukatoka nje ya ukumbi huku Von na baba yake wakitutizama kwa ghadhabu na wasijue chakufanya. Tuliwaacha na suti zao sisi tukaingia zetu ndani sijui walichokiwaza ila mtoto nilikuwa nimejibebea kiulaini bila wasiwasi hapa sikuwa nawaza kitu kingine zaidi ya furaha kutoka kwa mpenzi wangu.


Nahisi Jesca amerudi mikononi mwangu na amedhihilisha upendo wakweli na msimamo wakweli katika mapenzi na sasa tuliingia ndani. Chumba chetu kiliimarishiwa ulinzi na Kimbo akiwa mkuu wa ulinzi kwa wakati huo si Rais wala mfanya kazi yeyote hakutakiwa kukisogelea pamoja na kuwa ndani ya Himaya ya Ikulu. Tulisikia ving’ora vya gari la polisi hapo nje na tulipochungulia tunawaona Gao na mwanae mikono ikiwa imepigwa pingu huku wakiwekwa kwenye gari la polisi na ndoa imeahirishwa.


Tulikumbatiana na kufurahi pamoja Jesca alikuwa na furaha sana kwani alinihakikishia kuwa ananipenda na sasa aliniambia kuwa ni mjamzito na ameesha hakikisha tunatarajia mtoto wa kiume, ilikuwa ni furaha mpya iliyoleta na kujenga tumaini jipya katika mapenzi na sasa tunakumbatiana tena na kupiga kelele kwa furaha huku tukibusu na kupongezana. Ni mapenzi ya dhati baina yetu sasa nayadumu milele ni mimi na malikia wangu wangu Jesca Manguli tumejipumzisha ndani ya jumba la Ikulu bila wasi wasi tukila na kunywa kwa upendo.


Part I inaishia hapo

Tukutane part II ujue kiliendelea nini

Asanteni


Baada yakufunga safari kutoka Mbezi beach nilikokuwanaishi na familia yangu niliamua kwenda kumtembelea rafiki yangu Goodluck Bembe rafiki yangu kipenzi sana, aliyehamia hivi karibuni maeneo ya Kibaha Maili moja sikuwahi kufika na pia sina mawasiliano yake ila kwa alivyo nielekeza naamini ninakumbukumbu yakutosha hivyo siwezi kupotea.


Ni majira ya jioni yapata saa kumi na moja nilikuwa tayari niko eneo la maili moja wilayani Kibaha, nageuka kushoto kwangu ninauona ubao mweupe ulioandikwa kwa mandishi ya buluu na mekundu kwakukolezwa yalisomeka hivi “Mkunguni High School” bila shaka ilikuwa ni shule ya Sekondari ya binafsi iliyokuwa mashughuli sana wilayani Kibaha na Dar es salaam kwa ujumla na alama hii ni moja ya alama nilizoelekezwa na mwenyeji wangu naamini nilikuwa karibu sana kumfukia alipo.


Kushoto kwangu kulikuwa na jumba moja la kifahari ambalo hakika sina mfano wake, ni jumba lililomvutia kila mpita njia, halikuwa jumba tu bali waweza kuliita hekalu kulingana na ukubwa wake lakini pia uzuri wa muonekano wake. Hakuna mpita njia ambaye aliizuia shingo yake na kuyanyima uhondo macho yake wakuliangalia jumba hili la kifahari lililokuwa sehemu hiyo. Kuitizama tu ile nyumba ilikuwa ni ufahari, niufahari pia kwenda kuwaeleza ndugu jamaa na marafiki kuwa kuna nyumba nzuri na yakifahari katika eneo Fulani ambayo niyakwanza kukutana nayo katika taifa hili masikini. “Dar wanajenga ila kibaha aaah! wanajenga zaidi.” Nilijisemea kimoyo moyo.


Ilinilazimu kuegesha gari maana sasa sikuwa na namna, hakuna mpita njia aliye nishangaa maana ilikuwa ni jadi kwa eneo hili kukuta watu wamefurika wakiliangalia jengo hili lisilo na gorofa hata moja ila ni kivutio kikubwa kwa wapiti njia. Katika akili yangu nilijuaa wazi jengo lile ilikuwa ni hoteli wala sikuwa na shaka nikamuuliza jamaa mmoja wa makamo mpita njia mwenzangu.

“samahani kaka hii hoteli inaitwaje kaka?”

“hoteli?.. hoteli ipi unayohoji?

“si hii kaka?... “

“Au unamaanisha hii nyumba?”

“ndiyo…. Hii nyumba”

“nyumba ya mtu hiyo kaka, siyo hoteli ni nyumba yakuishi kaka”

“una maanisha kuna mtu anaishi kwenye hili jumba lakifahari?”

“bila shaka hujakosea. Watu wanapesa zao bwana”

“humu wanaishi watu?”

“kaka eeh! Unataka waishi punda siyo?, umeuliza MASWALI nimejibu sasa maswali mia nane yanini…..” Bila shaka maswali yangu yalikuwa yememkera jamaa alikuwa ameesha kasirika …. yule! alitokomea huku akinung’unika na maneno sikuyasikia.


Ukuta ulionakishiwa na rangi pamoja na maumbo ya kufinyanga yenye michoro ya wanyama mbalimbali mashughuli duniani, unakwenda kukutana na geti la rangi ya dhahabu lililokuwa na mvuto usioelezeka, ni geti lakuvutia ambalo kwa kuliangalia tu halikuwa geti lakawaida kuwahi kuliona katika taifa hili, mimi nimtembezi ila hili geti hapana sina chakusema maana lilikuwa nijipya katika upeo wa macho yangu na kumbukumbu zangu zilinielez wazi ndo kwanza nakutana nalo.


Bustani nzuri iliyotiririka maji kama chemichemi ya asili iliyojengwa kwa majabali ilionekana kupitia sehemu,mbalimbali za uwazi pembezoni mwa ukuta ule wa lile jengo huku sehemu hizo zikizibwa na nondo ngumu ila ziliruhusu kuona. Kibwawa kikubwa kilicho nakishiwa kwa vigae na marumaru pembezoni kiliifanya hiyo sehemu kuvutia zaidi. Mita kama hamsini toka bwawa lilipo ilionekana nyumba ya kifahali iliyojengwa mjengo wakimagharibi, iliezekwa kwa vigae vya kijani kwa mitindo yakuvutia, madirisha yake ya vioo yalionekana mwanana huku mbele ikipambwa na bustani nzuri ya majani ya ukoka yaliyohifadhiwa vizuri ili kuongeza mvuto.


Muonekano ule ulinifanya nisogee nikitamani kujua zaidi niliposogea nililiona eneo kubwa la wazi lililozungushiwa ukuta kushoto mwa lile bwawa niliona kuna sehemu iliyojengwa kiasili namaanisha iliezekwa kwa majani lakini ilipambwa na kuvutia na kulipangwa vinywaji vya kila aina. Nje kulipaki magari ya bei ghali kama vile Mercedes Benz, Hummer, Jeep nakadharika, hali iliyozidi kunikata nguvu. Macho yangu sasa yalitamani kushuhudia zaidi maana nilivutiwa zaidi nahii nyumba lakini pindi nageuza jicho mkono wakulia nilikutana na mashine zitumikazo kwenye sheli zamafuta zilikuwa na nembo ya kampumi kubwa ya mafuta hapa nchini GBP.


Hamaki iliongezeka na nikataka kuupata ukweli wakati nazidi kuzungusha macho nilikutana na mandishi yaliyokuwa yameandikwa kwa rangi nyeupe “Barclays Bank ATM 24hours” yakiwa na maana ya mashine yakutolea fedha ya benki ya Barclays inafanya kazi masaa 24.”bila shaka mwenye hii nyumba siyo mtanzania ….. siyo mtanzania!” Nilijisemea huku nikishusha pumzi ndefu. Hakuna mtanzania mwenye fedha kiasi hiki, toka nizaliwe sijawahi kuona mtanzania wa dizaini hii, fedha mpaka zakuweka sheli nyumbani kwake hapana hii ni zaidi ya kukufuru, lakini vipi kuhusu ATM mashine… hili sidhani hata sheria za nchi kama zinakubali.


Sasa nilishapoteza uelekeo kwanza sikumbuki nilifuata nini huko maili moja, nilikuwa nanung’unika mwenyewe huku nikitembea kurudi lilipo gari langu. Nilifungua mlango na kuubamiza kwa hasira niliiwasha kwa hasira na kuondoka zangu. Yanini kuwa na mali kiasi hiki huku watu wanakufa njaa, yanini kumiliki fedha mpaka zikakufanya mwendawazimu?, yanini! Manung’uniko haya hayakuishia moyoni tu bali yalijidhilisha wazi usoni kwangu, sikupendezwa na hali hii iliniumiza na iliendelea kunitesa ndani ya moyo wangu.


Sijui ni wivu, chuki au maumivu tu sikukubaliana kabisa na utaratibu alioutumia yule sijui bwana/bibi katika uwekezaji wa pesa yake. “hata kama unafedha kiasi gani huwezi… huwezi kuustajabisha ulimwengu kwakujifanya wewe ndiye fahari waajabu katika huu ulimwengu. Sidhani kama hata tajiri namba moja wadunia amewahi kuwaza kufanya ujinga kama huu.


Nilipokelewa na mke wangu kipenzi baada ya kufika nyumbani akiwa mwenye furaha nilijitahidi kuificha hudhuni niliyokuwa nayo maana haikumhusu, ingawa nilijua roho inaniuma balaa sikujua kwanini niliumia vile yule jamaa kuwa na nyumba nzuri, sikuiona sababu lakini niliumia sana, pamoja na kujaribu kuikwepa hali ile lakini sikufanikiwa. Jesca mke wangu kipenzi alinikaribisha ndani nikaketi na pembeni kulikuwa na kitanda kidogo kilichokuwa kimembeba mwanangu kipenzi Eric Jamae akiwa na miezi miwili tu tangu amezaliwa nilikisogelea na kumkuta akichezesha mikono nilimbusu na kumpapasa kisha nikaingia zangu bafuni kulipunguza joto na kujaribu kukituliza kichwa kilichokuwa na lundo la mawazo kwa maji ya baribi.


Baada ya kupata maji nilibadili nguo na kumfuata Jesca alikuwa jikoni akihangaika kuandaa chakula, nilifika na kuanza kumtania kidogo tulicheka nilijaribu kumsaidia lakini hakukubali alikataa kabisa akaniomba nikapumzike. Mke wangu hakupenda kuniona namsaidia kazi za jikoni ingawa mimi nilipenda sana kufanya hivyo. Haijalishi alitoka familia gani ila Jesca alipenda kuishi katika uhalisia aliamini jiko ni mahali pa mwanamke.


Na alipokuwa jikoni aliamini yuko sehemu sahihi. Niliondoka zangu na kwenda kujipumzisha sebuleni. Niliketi Tv ilikuwa ikiendelea na vipindi vyake ambavyo havikunivutia lakini sikuhangaika hata kubadili stationi maana nilijua nitapoteza muda wangu bure. Picha iliyokuwa ukutani ni picha ya Jamae Justine na Jesca Manguli vijana waliopitia mikikimiki mingi mpaka kuya vaa mavazi waliyokuwa nayo hapo pichani. Ni picha ya ndoa kati yangu na Jesca ndoa iliyopitia vikwazo vingi lakini ilifungwa.


********

KAA CHONJO KWA SEASON 2

MWISHO 


 

0 comments:

Post a Comment

Blog